Вы находитесь на странице: 1из 519

MIKESHA YA PESHAWAR

(Shab'ha-ye Peshawar)

Kimeandikwa na: Sultanu 'l-Wa'idhiin Shirazi

Bookmarks have been added

Kimetarjumiwa na: Dr. M. S. Kanju

Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION


ISBN: 978 - 9987 - 512 - 02 -7

Kimeandikwa na: Sultanul-waizin Shirazi

Kimetajumiwa na: Dr. M. S. Kanju Email: mokanju2000@yahoo.com

Kimehaririwa na: Ramadhani Kanju Shemahimbo

Kupangwa katika Kompyuta na: Ukhti Pili Rajab. Toleo la kwanza: Augasti,2008 Nakala: 2000

Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.alitrah.org Katika mtandao: www.alitrah.info

YALIYOMO
Peshawar {Mikesha ya peshawar}............................................................................2

Mkutano wa Kwanza.
Uhusiano na Mtukufu Mtume...................................................................................4 Nyongeza ya ushahidi kuthibitisha kwa kizazi cha Fatma ni dhuria wa Mtukufu Mtume.......................................................................................................................6 Kwa nini Shia wanachanganya swala zao...............................................................8 Jinsi wazazi wa Allama walivyohama kutoka Hijazi kwenda Iran.........................12 Jinsi kaburi la Amirul -Muminin Ali (a.s) lilivyogunduliwa.................................12 Bani Umayya na utiaji Najisi wa Makaburi............................................................13 Matendo maovu ya ufalme huu kugunduliwa kwa kaburi tukufu la Ali.......................................................................................................................... 14 Khitilafu kuhusu sehemu aliyozikwa Amir ul-Muminin........................................15

Mkutano wa Pili - Ijumaa usiku Madhehebu ya Shia


Dhana potofu kuhusu asili ya madhehebu y Shia..................................................16 Ni upuuzi kumhusisha Abdullah bi Saba na Mashia.............................................17 Maana ya neno shia.................................................................................................17 Sifa zaidi za Shia.....................................................................................................19 Sifa za shia zathibitishwa kutoka kwenye vitabu vya Sunni................................. 21 Cheo cha Salman, Abudharr, Mikdadi na Amar.....................................................22 Sababu za wa-Iran kuupokea ushia.......................................................................23 Shukurani za wa-Iran juu ya huruma za Ali..........................................................24 Midahalo kati ya Allama Hilli na kadhi Mkuu kuhusu Uimamu .........................25 Mfalme wa Irani aliikubali imani ya Kishia...........................................................25 Uislamu unakataza kujigamba kuhusu nasaba.......................................................26 Uislamu vile vile unakataza ubaguzi( wa aina zote)...............................................27 Lawama kwa mashabiki washupavu (Magullat).....................................................28 Mashia wako Tofauti na Gullat...............................................................................29 Ufafanuzi kuhusu heshima kwa Maimamu............................................................30

Watu wa Yasin inawahusu watu wa Muhammad..................................................31 Salawat juu ya Muhammad na Aali-Muhammad ni Sunna (iliyokokotezwa), na katika swala za Faradhi ni wajibu..........................................................................32

Mkutano wa Tatu -Jumamosi usiku 25-Rajab-1345A.H.


Mashia hawakugawanyika katika Matapo.............................................................33 Zaidiyya..................................................................................................................33 Wa-Kaysaniyya na Imani yao.................................................................................34 Qaddahiyya na Imani yao.......................................................................................35 Qullat na imani zao.................................................................................................35 Shia Imamiyya Ithnashariyya na Imani yao..........................................................36 Imani katika Allah na Mitume................................................................................36 Imani katika adhabu, malipo, Jahannamu, pepo, na siku ya kiyama......................36 Imani katika kanuni za Ibada..................................................................................37 Imani katika maimamu...........................................................................................37 Kanusho juu ya Hadithi ya Marifa........................................................................38 Hadithi za Ajabu katika Sahihain-Bukhari na Muslim...........................................39 Rejea zinazoonyesha kuhusu kuonekana kwa Allah...............................................40 Quran tukufu inakataa dhana ya kuonekana kwa Allah......................................41 Hoja na Hadith kuhusu kutokuonekana kwa Allah...............................................41 Rejea zaidi ya Hadithi za ajabu ajabu katika vitabu viwili vya hadithi.................42 Hadith ya Thaqalaini (vizito viwili)....................................................................... 44 Ushirikina na aina zake...........................................................................................44 Ushirikina katika swala...........................................................................................45 Kuhusu kuomba au ahadi........................................................................................46 Nadhiri kwajina la Allah.........................................................................................47 Ushirikina ulifichika kujionyesha katika sala.........................................................48

Kwa nini Mitume walitafuta misaada kutoka kwa watu?.......................................49 Dhuria watukufu wa Muhammad ni njia (Wasyla-visababisho) neema za Mungu.50 Hadithi Ath-Thaqalaini (Hadith ya vizito viwili)....................................................51 Bukhari na Muslim wameandika Hadithi nyingi zilizosimuliwa na wazushi........53 Je, Yazid anapaswa kulaaniwa?..............................................................................70 Kuvunjwa heshima ya makaburi.............................................................................71 Dhuria wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w) ni mashahidi katika njia ya Allah na wako hai.......................................................................................................................... 72 Daraja ya Maimamu Masumin..............................................................................73

Mkutano wa Nne jumapili usiku 26 Rajab, 1345 A.H


Mjadala kuhusu Uimamu.......................................................................................73 Kuweka mipaka kwenye madhehebu manne hakuna msingi...............................74 Ushia kulinganishwa na madhehebu manne.........................................................75 Maimamu wanne wa Kisunni wametangazana kuwa makafiri..............................76 Shutuma za Maulamaa wa Kisuni kwa Abu Hanifa...............................................77 Uimam kwa mujibu wa Shia unamaana ya uwakilishi wa Allah...........................78 Cheo cha Uimam ni juu zaidi kuliko cha utume wa kawaida.................................79 Mitume wa kawaida na wale maalumu..................................................................80 Tofauti katika Daraja za Mitume ............................................................................80 Hoja za cheo cha utume kwa ajili ya Ali kutoka kwenye Hadith Manzila............82 Usahihi wa Hadithi ya Manzila kutoka kwenye rejea za kawaida.........................83 Amadi Haamini kama msimuliaji wa Hadith ........................................................85 Kuthibitishwa Hadith ya Manzila na Umar bin Khattab........................................86

Sifa za Ali...............................................................................................................87 Umuhimu wa cheo cha Ali......................................................................................88 Wakati akiwa kwenye rukuu katika sala ali alitoa pete kumpa masikini...............92 Cheo cha Harun kama Mtume kadhalika kama Khalifa........................................92

Mkutano wa Tano; Jumanne Usiku 27 Rajab 1345, A.H


Hadithi ya Manzila imesimuliwa mara nyingi.......................................................96 Harun alikuwa ni mrithi (makamu) wa Musa aliyeteuliwa....................................97 Kufanana kwa hali ya mambo kati ya Ali na Harun................................................98 Hadithi ya haramu ya ndugu na Mtume kumchagua Ali kama Khalifa wake.......99 Uthibitisho kutoka ulamaa wa Kisunni na waandishi wa Ulaya.............................99 Hadithi za wazi na dhahiri kuhusu Ukhalifa wake Ali..........................................100 Tabia za Masahaba................................................................................................103 Hadithi katika kumtukuza Abu Bakr.....................................................................104 Tabia ya Abu Huraira na laana yake.....................................................................105 Kashfa za Ibn Abd Rabbih dhidi ya Mashia....................................................... 107 Kashfa zilizotolewa na ibn Hazm........................................................................107 Kashfa zilizotolewa na Abn Taimiyya................................................................ 107 Tabia za Abu Huraira na Hadith zinazotaka Alaaniwe....................................... 109 Njama ya Abu Huraira na Busr bin Artat katika mauwaji ya waislamu..............110 Hadithi zenye kumsifu Abu Bakr na Umar na kutostahili kwao......................... 114 Hadithi ya kwamba Hasan na Husein wote ni mabwana wa Vijana wa Peponi...116 Majibu kwa Hadith inayodhaniwa kwamba Abu Bakr na Aisha walipendelewa zaidi na Mtume.....................................................................................................117 Aya juu ya mapenzi kwa familia ya Mtume.........................................................118 Kukubali kwa Shafii kwamba mapenzi kwa Ahlul Bait ni wajibu.....................119 Dhana potofu kuhusu mapenzi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w) kwa Aisha............119

Mtukufu Mtume (s.a.w.w) alimpendelea Ali kuliko watu wengine wote..............120 Hadith ya ndege aliyebanikwa..............................................................................121 Watu wenye kumbukumbu ni Ahli Muhammad dhuria wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w)................................................................................................................124 Aya za Quran Tukufu kuhusu kuchaguliwa kwa Makhalifa wanne, na majibu..124 Hoja kutokana na Aya ya Pango na majibu yake..............................................126 Kuteremshwa kwa utulivu kulikuwa kwa ajili ya Mtume wa Allah.....................131

Mkutano wa Sita Jumanne Usiku 28 Rajab 1345A.H


Aya Mia tatu zenye kumtukuza Ali......................................................................133 Imani ya Ali akiwa bado mtoto tu.........................................................................137 Imani ya Ali ilikuwa ni sehemu ya asili yake hasa...............................................140 Ali aliwapita masahaba wengine wote Umma wote katika ubora ......................141 Imani ya Ali ni bora kuliko ya Abu Bakr...............................................................141 Ali kama Nafsi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w).....................................................142 Aya ya Quran yenye kumsifu Ali kwa kulala katika kitanda cha Mtume katika usiku wa Hijra.......................................................................................................143 Ushahidi kuhusu maneno ya Umar Kama Ali asingekuwepo, Umar angeangamia.........................................................................................................146 Ushindi haukuwa kwa sababu ya sifa binafsi za Umar..................................... 148 Kushindwa kwa Abu Bakr na Umar katika vita vya Khaibar..............................149 Ali alikuwa mwenye kupendwa na Allah na Mtukufu Mtume (s.a.w.w).............152 Hadithi ya bendera katika ushindi wa Khaibar......................................................152 Tabia ya Uthman na namna ya maisha kulinganishwa na ile ya Abu Bakr na Umar.....................................................................................................................154 Utajiri wa Khalifa Uthman...................................................................................155 Khalifa Uthuman aliwapa moyo watenda maovu miongoni mwa Bani Umayya..156 Mtukufu Mtume (s.a.w.w) aliwalaani Abu Sufyan, Muawiya na Mtoto wake Yazid.....................................................................................................................159 Uthman hakukubali ushauri wa Ali......................................................................159

Uthman aliwapiga masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w) Bila huruma.........159 Ammar alipigwa kwa amri ya Uthman.................................................................160 Hadith, Masahaba wote ni kama nyota namhusu na Abu Dharr vile vile............163 Upole na Ukarimu wa Ali bin Abu Talib ..............................................................164 Upole wa Ali kwa Marwan na Abdullah bin Zaubair..........................................165 Upole wa Ali kwa Aisha........................................................................................166 Mashaka na utata kuhusu Aya ya walii na ufafanuzi wake................................168

Mkutano wa saba Jumatano usiku 29 Rajab,1345A.H


Tofauti kati ya muungano wa kuwazika na muungano halisi.............................174 Aya ya maapizano (Mubahila) inathibitisha umoja wa nafsi ya Ali na ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)..................................................................................................175 Kuwasili kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.w) kwa ajili ya maapizano....................176 Stahili ya Ali, Fatma, Hassan, na Hussein inathibitishwa naAya ya maapizano..177 Simulizi zaidi na Hadith kama ushahidi wa umoja wa msingi wa Mtukufu Mtume (s.a.w..w) na Ali ...................................................................................................179 Kwa vile Mtukufu Mtume alikuwa mbora kwa Mitume wote wengine na Ali pia alikuwa mbora kwao.............................................................................................181 Kioo cha mitume yote kama ilivyoonyeshwa na Hadith ya ufananisho............. 183 Kukubaliwa kwa Abu Bakr na watu wote............................................................184 Hoja dhidi ya uhalali wa Ijma..........................................................................185 Ali alikosa kuarifiwa kwa makusudi kuhusu mkutano wa Saqifa........................188 Hadithi -e-Thaqalain na Hadithi -e-Safina........................................................191 Hadithi Ali yuko pamoja na haki na haki iko pamoja na Ali...........................194 Hadithi ya Safina -Hadithi ya Saqifa....................................................................197 Je, Ijma inapaswa kukubaliwa kwa sababu ya kigezo cha yaliyopita?................198 Hadithi za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) zinazowahimiza waumini kumfuata Ali..198 Kulazimishwa kwa Ali na Bani Hashim kula kiapo baada ya miezi sita...............199

Ali aliburuzwa kutoka nyumbani kwake na nyumba yake ikachomwa moto.....200 Hoja kumi na mbili zinazounga mkono ukweli kwamba Ali alichukuliwa kupelekwa msikitini kwa ncha ya upanga........................................................................201 Fatma aliwaambia Abu Bakr na Umar kwamba anawalaani hao wote katika kila Salat......................................................................................................................203 Riwaya kuhusu kuharibika mimba ya Fatma........................................................205 Imamu Husein kamwe hakutamani nguvu ya kisiasa...........................................206 Imamu Husein alikataa ushauri wa kuuacha ujumbe wake..................................208 Maana halisi ya Bidaa (uzushi)...........................................................................212 Faida za kuzuru makaburi ya maimam watukufu.................................................213

Mkutano wa Nane, Alhamis Usiku (Ishaban, 1345 A.H.)


Tofauti kati ya Uslamu na Imani...........................................................................214 Kuhusishwa kwa Ushia na Imamu Jafar as-Sadiq..............................................223 Kuwalaumu masahaba haina maana ya ukafiri....................................................226 Makhalifa wenyewa hawakuchukulia kulaniwa wao kuwa ni ukafiri.................227 Khalifa Abu Bakr alimtukana Ali.........................................................................228 Khalifa Umar alishikilia kwamba kumlaani Muislamu sio Ukafiri.....................229 Masahaba wengi walitukanana wenyewe kwa wenyewe lakini hawakuchukuli kama makafiri.......................................................................................................229 Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliyajua matendo yote mabaya na mazuri ya masahaba........................................................................................................................ 230 Sifa ya kuwa mmoja wapo kwenye Baia at -e-Ridhwan.................................. 230 Mashia wanakubali ubora wa masahaba...............................................................231 Hadithi ya kuwafuata masahaba ya chunguzwa...............................................231 Suala la Aqaba na mpango wa kumuua Mtukufu Mtume (s.a.w.w) ....................232 Mtume kamwe hakutuamrisha tuwafuate waongo..............................................233 Upinzani wa masahaba huko Saqifa ....................................................................234

MKUTANO WA TISA, USIKU WA IJUMAA 2 SHABAN 1345 A.H.


Mashia wanasema kuhusu Aisha kile haswa kinacho oneshwa na wanahistoria..333 Hakuna ushahidi kwamba Aisha alitubia..............................................................333 Aisha anazuia kuzikwa kwa Imam Hassan karibu na Mtukufu Mtume...............334 Kusujudu kwa Aisha wakati wa kuuliwa kishahidi kwa Amirul-Muminin...........335 Kauli za Aisha zinazokinzana kuhusu Uthman.....................................................335 Allah ni mwingi wa huruma lakini damu ya waislamu wasio na hatia haiwezi kupita bila kuhojiwa.....................................................................................................336 Aisha hawezi kudai kupoteza kumbukumbu kwa sababu alikumbushwa na Ummu Salama................................................................................................................ 337 Hadithi ya kushona viatu ndio ushahidi mkubwa wa Uimam na ukhalifa wa Ali.339 Tofauti katika mtindo wa uteuzi wa makhalifa watatu wa mwanzo na ushahidi tosha wakutosihi kwa Ukhalifa wao.....................................................................339 Ushahidi mwingine wa ubatilifu wa Ijma.............................................................340 Uteuzi wa mtukufu Mtume juu ya Ali ulipuuzwa na uteuzi wa Abu Bakr juu ya Umarukahalalishwa............................................................................................ 340 Pingamizi kwa Abdur-Rahman bin aAuf kuw andio msuluhishi .......................341 Kwa mujibu wa Mtukufu Mtume, Ali anapswa kufuatwa kuliko wengine wote..342 Dhulma mbaya iliyofanwa na Umar kwenye Nafasi ya Amirul-Muminin.........342 Ukhalifa wa Ali uliamriwa na Allah .....................................................................343 Msingi hulisi wa Ukhalifa wa Ali sio Ijma bali ni matangazwa ya mtukufu Mtume ........................................................................................................................... 345 Ali alikuwa mbora kuliko wale Makhalifa wengine wote....................................345 Hadithi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuhusu ubora wa Ali ..............................345 Kizazi safi halisi cha Ali.......................................................................................346 Kuumbwa kwa Ali kutokana na nuru na uhusiano wake na Mtukufu Mtume.....347 Kizazi cha kima umbile cha Ali...........................................................................348 Baba yake Ibrahim alikuwa ni Azar.....................................................................349

Baba na Mama zake Mtukufu Mtume hawakuwa washirikina bali wlaikuw awote ni waumini........................................................................................................... 350 Wahenga wa Ali vivyo hivyo waliepukana na ushirikina.....................................352 Kutoeleweka kuhusu imani ya Abu Talib kwa fafanuliwa...................................352 Ijma ya Shia kuhusiana na Imani ya Abu Talib...................................................353 Ushahidi juu ya Imani ya Abu Talib ....................................................................354 Beti za Abil-Hadid katika kumtukuza Abu Talib.................................................355 Beti za Abiu Talib huthibitisha Uislamu wake.....................................................356 kukubali kwa Abu Talib imani yake juu ya Allah wakti wa kifo chake...............358 Mazungumzo ya Mtukufu Mtume na Abu Talib wakati wa Tangazo la Utume wake......................................................................................................................359 Tangazo la Ibrahim la utume na mazungumzo yake na Azar...............................359 Au Talib amhakikishia Mtukufu Mtume msaada kamili na pia asome mashairi katika kuusifu Uislamu.............................................................................................. 359 Abu Talib alikuwa msaidizi na mlezi wa Mtukufu Mtume ................................ 360 Sio sahihi kumwita Muawiya Khalul-Muminin ............................................. 361 Muawiya alitamka Takbir wakati wa kifo cha kishahidi cha Imam Hasan....... 362 Muhammad bin Abi Bakr aliuawa akiwa na kiu na kuchomwa hadi majivu kwa ajili ya mapenzi ya Ahlul-l-Bayt..........................................................................362 Muawiya hakuwa mwandishi wa wahyi bali wa barua tu...................................363 Ushahidi wa ukafiri wa Muawiya........................................................................363 Ushahidi kutoka sura za Qurani tukufu na Hadith-Muawiya na Yazid wamelaaniwa......................................................................................................................... 363 Mauaji ya waumini mashuhuri kama Imam Hasan, Ammar, Hajar bin Adi Malik Ashtar, Muhammad bin Abi Bakr, n.k. kwa Amri ya Muawiya..........................365 Mauji waumini 30,000 waliouawa na Busr bin Artat kwa amri ya Muawiya.....366 Muawiya alitoa Amri kwamba Ali alaaniwe........................................................367 Masahaba wa Mtume walikuwa katika viwango tofauti za uwelewa..................368 Quran tukufu inawasifia masahaba wema lakini pia inawalaani masahaba waovu................................................................................................................... 371 Abu Talib alikuwa muumini imara ..................................................................... 372 Ushahidi wa nyongeza juu ya imani ya Abu Talib...............................................372

Jafar Tayyar amekubali Uislamu kwa amri ya Baba yake..................................372 Nauha za Ali kwa ajili ya baba yake, Abu Talib.................................................374 Abu Talib alificha imani yake ambapo Abbas na Hamza walitangaza za kwao..374 Kwa nini Abu Talib ilikuwa ikijulikana kwa kawaida wakati wa uhai wa mtukufu Mtume...................................................................................................................375 Sunni kwa kweli ndio marafidhi na Mashia ndio Sunni hasa.............................376 Hoja za uhalali wa Muta.....................................................................................377 Ahli Sunna wazingatia uhalali wa Muta..............................................................379 Amri ya inayoruhusu Muta haikufutwa.............................................................. 380 Masahaba maarufu na Imam Malik wanasisitiza kwamba amri ya Muta haijafutwa........................................................................................................................ 381 Masharti yote ya ndoa yanatimizwa katika ndoa ya muta................................. 382 Je, amri ya Quran juu ya muta ilifutwa na mtukufu Mtume?............................383 Hoja zinazohusu kufutwa kwake wakati wa uhai wa Mtume..............................383 Je, Khalifa Umar angeweza kuifuta muta...........................................................384 Amri ya Allah au ya Mtukufu Mtume haiwezi kufutwa na Khalifa ...................386 Manufaa sio misingi kwa ajili ya ufutaji .............................................................387 Imani ya Abu Talib ilikuwa inajulikana sana wakati wa Mtukufu Mtume...........388 Mahali alipozaliwa Ali ilikuwa ni ndani ya Kaaba.............................................388 Asili ya jina la Ali ilikuw ani ulimwengu usionekana.......................................... 389 Baada ya majina ya Allah na Mtukufu Mtume jina la Ali limeandikwa juu ya Arsh..................................................................................................................... 390 Maneno yaliyotumiwa na Adam kwa ajili ya kukubaliwa kwa Toba yake yalikuwa ni majina ya watoharifu watano............................................................................392 Wahyi na Uham vilivyotolewa kwa watu wengine mbali na mitume, hata kwa wanyama...............................................................................................................392 Ufunuo wa Lawh (Uba) kwa Abu Talib................................................................394 Jina la Ali sio sehemu ya Adhana au Iqama.........................................................395 Uchamungu wa Ali...............................................................................................395 Riwaya ya Abdullah bin Rafii ............................................................................395 Riwaya ya Suwaid bin Ghafla..............................................................................396 Ali alijizui kula Halwa..........................................................................................396

Mavazi ya Ali........................................................................................................397 Mazungumzo ya Zubar na Muawiya kuhusu Ali.................................................398 Utambuzi wa Mtume juu ya Uchamungu wa Ali.................................................398 Allah na Mtukufu Mtume walimuita Ali Imamul-Muttaqin (Kiongozi wa wachamungu).......................................................................................................399 Kama Imaml-Muttaqin Ali hakuwa na mapenzi ya kujingiza kwenye anasa au Mamlaka.............................................................................................................. 400 Ukimya wa Mitume watukufu............................................................................ 403 Hali ya Ali inafanana na ya Harun.......................................................................404 Kunyamaza kwa Mitume......................................................................................404 Maelezo ya Ali juu ya kufaa kwa kimya chake baada ya kifo cha Mtukufu Mtume...................................................................................................................406 Barua ya Amirull-Muminin kwa watu wa Misr kuelezea ukimya wake wakati aliponyimwa Ukhalifa..........................................................................................407 Khutba ya Amirul-Muminin baada ya kuuawa shahidi kwa Muhammad bin Abu Bakr.......................................................................................................................408 Khutba ya Shaqshiqayya vile vile na elezea ukimya wa Ali................................409 Seyyid Razi...........................................................................................................409

Mkutano wa Kumi, Jumamosi Usiku 3 Shaban 1345 A.H


Uchambuzi wa Elimu ya Umar juu ya Sheria za Kiislamu..................................411 Mwanamke Amyamazisha Umar kaitka jambo la sheria......................................413 Kunyanganya kiasi chochote cha mahari ni kimyume cha Sheria....................414 Amri ya Umar ya kuwapiga mawe watu watano na kukatizwa na Ali................415 Umar atoa amri mwanamke punguani apigwe mawe na ali kuingilia kati...........417 Elimu na sifa za Ali .............................................................................................417 Elimu yote ilikuwa iko dhahiri kabisa kwa Ali.....................................................420 ali ndiye aliyefaa zaidi kwenye nafasi ya Ukhalifa..............................................423 Kiapo cha utii cha Ali kwa makhalifa ni cha kulazimishwa................................424 Kiapo cha utii cha Ali kwa Makhalifa ni cha kulazimishwa .............................. 425 Kusiwepo na Imani potovu) katika dini..............................................................425

Amri ya Mtume ya kumtii Ali...............................................................................426 Ulamaa wa Kisunni hawataki Ushirikiano na sisi................................................427 Tofauti ya madhehebu manne zinapuuzwa bali Shia hawavumiliwi...................429 Fatwa za wanachuoni wa Sunni zinakwenda kinyume na maelekezo ya Qurani............................................................................................................... .429 Kuosha miguuu katika udhu ni kinyume na sheria ya Qurani........................... 432 Kupaka juu ya soksi ni kinyume na sheria ya wazi ya Quran Tukufu................433 Kupaka juu ya kilemba ni kinyume na sheria ya Qurani....................................434 Shia pekee wanaolaumiw akwa tofauti kama hizo..............................................434 Kwa mujibu wa ulamaa wa Kisuni kusujudu juu ya kinyesi kikavu na kinyesi cha mnyama ni halali.................................................................................................. 435 Kwa mujibu wa ulamaa wa Kisunni kusujudu juu ya kinyesi kikavu na kinyesi cha mnyama ni halali..................................................................................................435 Shia hawachukulii kusujudu juu ya udongo wa karbala kuwa ni wajibu............436 Kwa nini tunasujudu juu ya ule udongo wa Karbala............................................437 Sifa za Hali ya udongo wa Karbala ....................................................................437 Umri mkubwa sio kigezo cha Ukhalifa................................................................439 Sababu ya kuteuliwa Ali.......................................................................................441 Hadithi ya kufuatana na Abu Bakr .......................................................................441 Mtukufu Mtume alimtuma Ali kwenda Yemen.....................................................442 Njama za maadui ..................................................................................................443 Ali alichukia siasa ya dhulma chafu.....................................................................443 Vurugu wakati wa Ukhalifa wa Amirul-Muminin zilitokana na uadui dhidi yake.......................................................................................................................444 Vita vya Ali vya Jamal, Siffin na Nahrwan vilikuwa kama vita vya Mtukufu Mtume dhidi ya makafiri...................................................................................................445 Baada ya mtukufu Mtume Ali alikuwa ndiye bingwa zaidi ya mambo ya utawala..................................................................................................................446 Ali alikuwa na Elimu ya ulimwengu wa Ghaib....................................................446 Je Elimu ya Ghaibu imetengwa kwa Allah tu?.................................................... 447 Elimu ni ya namna mbili, ya dhati (ya asili) na Arzi( ya kutafuta).................... .450 Ushahidi wa Quran kwamba Mitume walikuwa na elimu ya Ghaib..................451 Madai yakuwa na elimu ya ghaib kupitia njia nyinginezo ni ya uongo.............. 452 Waandamizi wa mitume pia walikuwa na Elimu ya ghaib................................. 453 Maimamu watukufu walikuwa ndio makhalifa wa kweli na walikuwa na Elimu ya ghaib................................................................................................................... 455 Lango la Elimu.................................................................................................... 456 Ulamaa wa Sunni ambao wamesimulia ile Hadithi ya Jiji la Elimu................457

Kusimulia sifa za Ali ni ibada..............................................................................459 Ufafanuzi wa Hadith ya Lango la Elimu...........................................................461 Ali alijua maana ya dhahiri na ya ndani ya Qurani tukufu.................................461 Kuikabidhi Elimu ya Mtume kwa Ali...................................................................464 Jafr-e-Jamia na asili yake....................................................................................465 Imam Ridhaa alitabiri kifo chake .........................................................................467 Jibril alileta kitabu kilichofungwa sili (sealed) kwa ajili ya wasii wa Mtukufu Mtume...................................................................................................................468 Tangazo la Ali la niulizeni mimi na Riwaya za Masunni...................................471 Elimu ya Ali kuhusu watu wanaongoza au wanaopotosha.................................473 Kuutabiri ule ushika bendera wa Habib bin Amamar.......................................... 474 Kutabiri ukandamizaji wa Muawiya.................................................................. 475 Kwa mujibu wa Mtukufu Mtume Ali aliwazidi wengine wote katika Elim....... 479 Ali alizimudu Sayansi zote.................................................................................. 482 Kuzaliwa kwa Imam Husain na pongezi za Malaika...........................................483 Kukubali Ushiah kwa Nawab-Sahib ..................................................................484

Jumapili Sha;ban 4,1345A.H


Wilada ya Imam Husein.......................................................................................485 Uhuru halisi..........................................................................................................485 Iman yasuni kuhusu maa ya wale waliopewa mamlaka...................................485 Njia tatu za utenzi wa ul l-Amr (wale waliopewa mamlaka)............................486 Maneno ull-Amrhayaasshirii kwa kwa watawala.............................................486 Mtawala anayetwaa madarka kwa nguvu hawezi kuitwa aagizwe na kuteuliwa na Allah................................................................................................................... 487 Kutotenda dhambi na makosa (Umasum) kwa maimam watukufu kumesimuliwa kwa jumla sana.....................................................................................................490 Elimu ya Ahlul-Bayt.............................................................................................490 Hakuna utajo wa Rakaa za swala ndani ya Qurani Tukufu..............................492 Majina ya Maimam na idadi yao (kumi na mbili)................................................495 Idadi ya Makhalifa baada ya Mtukufu Mtume ni kumi na mbili........................497

NENO LA MCHAPISHAJI
Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiingereza kiitwacho, Peshawar Nights. Asili ya kitabu hiki ni cha lugha ya Kifarsi kwa jina la, Shabha-ye Peshawar. Sisi tumekiita, Mikesha ya Peshawar. Mikesha ya Peshawar ni nakala ya mjadala kati ya wanavyuoni mbalimbali wa Kisunni na mwanachuoni mmoja wa Kishia mzaliwa wa Shiraz (Iran) aitwaye Sayyid Abdu l-Fani Muhammad al-Musawi Sultanu l-Waidhiin, ambaye wakati huo alikuwa na umri wa miaka 31 tu. Mjadala huu ulifanyika katika mji wa Peshawar ambao wakati huo ilikuwa ni sehemu ya Bara Hindi na hivi sasa ni sehemu ya Pakistan. Ulifanyika kuanzia tarehe 27 Januari 1927 na kuundelea kwa mikesha kumi ndani ya msikiti ambako watu zaidi 200 walihudhuria kila usiku. Mjadala huu ulifanywa kwa muundo mzuri wa kuheshimiana pande zote bila ya kuvunjiana heshima. Mwandishi mwenyewe amejiita katika kitabu hiki kama Dai yaani mtu anayewaombea mema watu wengine, sisi tumelitafsiri neno hilo kama Muombezi. Masharti ya mjadala yalikuwa kwamba ni vianzo vile tu vinavyokubaliwa na madhehebu zote ndivyo vitakavyorejelewa. Mjadala huu uliandikwa na kuripotiwa na waandishi wanne katika magazeti ya kila siku, na baadaye ukachapishwa kama kitabu huko Tehran, Iran. Huu ulikuwa ni mjadala uliopangwa vizuri, wa kielimu na utumiaji wa vipawa vya akili ambapo kila hoja iliyotolewa ilitumika elimu na akili kuiwasilisha mpaka pande zote zikaridhika. Katika kuwasilisha hoja zake, mwanachuoni huyu mkubwa wa Kishia alitumia rejea za vitabu vingi maarufu vya Kisunni na ambavyo si maarufu sana lakini vyenye kuaminika. Rejea na vitabu hivyo vimeorodheshwa kwa wingi sana ndani ya kitabu hiki ili msomaji aweze kuvirejelea. Lakini kwa bahati mbaya sana, mengi ya matoleo mapya ya vitabu hivyo yamefanyiwa mabadiliko na baadhi ya sehemu kuondolewa, hususan zile zinazounga mkono madai ya Shia. Ufuatao hapa chini ni mfano mdogo tu wa yanayofanywa katika vitabu hivyo: Katika ukurasa wa 301 wa juzuu ya 3 ya Tafsir al-Kashshaaf iliyokusanywa chini ya maelekezo ya Sheikh Mustafa al-Halabi (toleo la pili, 1319 A.H. liliochapishwa na Main Government Printing House ya Amiriah Bulaq ya Misir), kuna beti zinazojitokeza ambazo kwazo Jarullah Zamakhshari, mfasiri wa al-Kashshaaf, alitangaza wazi imani yake katika uhalali wa Ushia. Lakini katika chapisho la 1373 A.H. lililochapishwa na Printing House Istiqamah bil-Qahara, shairi lililotajwa halionekani tena.

Marehemu Allamah Sayyid S. Akhtar Rizvi katika kitabu chake Uimamu uk. 37, anaandika kushangazwa kwake kutokana na maneno yaliyoondolewa katika kitabu cha at-Tarikh cha at-Tabari, chapa ya Leiden (ya mwaka 1879 Masihia) ambayo imeyanakili maneno ya Mtukufu Mtume (s.a.w.) aliyoyatumia wakati wa karamu maarufu ya ndugu wa karibu aliyoitayarisha mwenyewe. Maneno ya mwisho aliyoyasema Mtukufu Mtume (s.a.w.) katika karamu hiyo yalikuwa haya: Enyi watu wangu! Huyu Ali ni ndugu yangu, wasii wangu na khalifa wangu miongoni mwenu; msikilizeni na mtiini. Lakini katika chapa ya Misri (ya mwaka 1963 Masihia) - chapa ambayo inayodaiwa kuwa imechekiwa na ile ya Leiden - maneno haya muhimu: wasii wangu na khalifa wangu yamebadilishwa na kuwa kadha wa kadha na kusomeka hivi: Huyu Ali ni ndugu yangu na kadha wa kadha. Huu ni msiba mkubwa. Sultanu l-Waidhiin, mwandishi wa kitabu hiki, amedondoa rejea nyingi kutoka katika matoleo ya zamani, hivyo, msomaji asishangae kutokuona rejea hizo katika matoleo mapya. Huu ni mchezo umefanywa na unaendelea kufanywa mpaka leo. Na lengo ni kuficha ukweli. Hata hivyo, ukweli siku zote unaelea; matoleo ya zamani yapo mengi na yamehifadhiwa kwenye maktaba zetu. Ni muhimu kufikia kila aina ya maoni katika kujaribu kuamua ukweli. Uislamu kimsingi uko dhidi ya kufuata kibubusa. Mjadala huu umefanywa ili kuwaelemisha Waislamu kwa ujumla juu ya madhehebu za Kiislamu ili kujenga maoni yao kuhusu mtazamo mzuri wa mtu mwenyewe. Ni muhimu mtu kuelewa hoja za wale ambao hakubaliani nao. Inawezekana kusemwa kwamba wale ambao hawaelewi kabisa mtazamo wa maoni tofauti, hawaelewi kwa ukamilifu (mtazamo) wa kwao wenyewe. Hili tena ni jaribio letu kubwa la kutoa kitabu kikubwa kinachohusu mjadala juu ya madhehebu za Kiislamu. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni mambo ambayo hayana nafasi tena katika akili za watu. Kutokana na ukweli huo, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeona bora kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili, kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili. Tunamshukuru ndugu yetu, Dr. M. S. Kanju kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki. Mchapishaji:

Al-Itrah Foundation S. L. P. 19701 Dar-es-Salaam, Tanzania

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU, MWINGI WA REHEMA, MWENYE KUREHEMU

Mikesha ya Peshawar

PESHAWAR
(MIKESHA YA PESHAWAR)
Sultanul-Waizin Shirazi, mwanachuo mkubwa wa Iran, alitembelea India mwaka wa 1927 (1345 A.H.) wakati akiwa na umri wa miaka 30. Alipata makaribisho makubwa popote alipokwenda. Watu walinufaika kutokana na ujuzi wake wa hadithi, historia, na tafsiri juu ya Qurani Tukufu. Alishauriwa kuingia katika mjadala wa kidini tarehe 23 Rajab, 1345 A.H., na watu wa imani nyingine katika eneo la Peshawar, eneo ambalo lilikuwa ni katika India na ambalo leo ni eneo la Pakistan. Mjadala ulifanyika kwa muda wa mikesha kumi mfulululizo. Washiriki wakubwa wawili kutoka upande mwingine walikuwa ni wanachuoni maarufu wa Kabul, Hafidh Muhammad Rashid na Sheikh Abduls-Salam. Waandishi wanne waliandika taarifa za mjadala huo mbele ya watu takirban 200 (Shia na Sunni). Magazeti ya sehemu hiyo yaliandika taarifa za mjadala huo kila siku asubuhi iliyofuatia. Sultanul-Waidhin alikusanya maelezo ya magazeti kuhusu mjadala huo katika kitabu nchini Iran, na kuchapishwa Tehran kama Shabhaye-Peshawar, au Peshawar Nights ifuatayo ni tarjuma ya kitabu hicho:

Mikesha ya Peshawar

Mkutano wa kwanza
(Usiku wa Alhamisi, 23 Rajab, 1345 A.H.) Hafidh Muhammad Rashid, Sheikh Abdus-Salam, Sayyid Abdul-Hayy, na wanachuoni wengine wa eneo hilo walihudhuria. Mjadala ulianza mbele ya mkusanyiko mkubwa. Katika majarida na magazeti, walimuita mwandishi kama Qibla-o-Kaba, lakini katika kurasa hizi nimejiita mwenyewe kama Muombezi na Hafidh Muhammad Rashid kama Hafidh. Hafidh: Tumefurahishwa sana kupata fursa hii ili kujadili nukta za msingi ambazo kwazo tunahitilafiana. Kwanza lazima tuamue jinsi tutakavyo endesha mjadala huu. Muombezi: Niko tayari kushiriki katika mjadala huu kwa masharti kwamba tunaweka kando mawazo yote tuliyokuwa nayo kabla (juu ya imani zetu), na kujadili masuala kwa mantiki, kama ndugu. Hafidh: Mimi pia niruhusiwe kutoa sharti moja: kwamba mjadala wetu uwe chini ya msingi wa maamrisho ya Qurani Tukufu. Muombezi: Sharti hili halikubaliki kwa vile Qurani Tukufu ni yenye habari nyingi katika maelezo machache ambayo maana zake za ndani lazima zitafsiriwe kwa kurejea kwenye matukio mengine na hadithi. Hafidh: Sawa, hili ni wazo la maana, lakini vile vile ni muhimu kwamba rejea zote zifanywe kwenye hadithi na matukio ambayo chimbuko lake ni juu ya ushahidi usiopingika. Lazima tujizuie kutokana na kurejea kwenye vyanzo vyenye mashaka. Muomezi: Imekubalika. Kwa mtu kama mimi, ambaye ana fahari ya kutosha kudai uhusiano na Mtume, sio haki kwenda kinyume na mifano iliyowekwa na jadi wangu, Mtume wa Uislamu. Ametambulishwa katika Qurani kama ifuatavyo:

Na hakika una tabia njema kabisa. (Qurani; 68:4) Vile vile sio vizuri kutenda dhidi ya maamrisho ya Qurani Tukufu ambayo inasema:

Mikesha ya Peshawar

Waite watu katika njia ya Mola wako kwa hikima na mauidha mema, na ujadiliane nao kwa nama iliyo bora (16:125)

UHUSIANO NA MTUKUFU MTUME


Hafidh: Samahani, unatoa rejea kwenye uhusiano wako na Mtukufu Mtume. Hiyo inajulikana sana, lakini naomba kwamba unifahamishe nasaba yako ili nipate kujua vipi jadi yako kinasaba imefikia kwa Mtume. Muombezi: Nasaba ya jadi yangu humfikia Mtume kupitia kwa Imamu Musa Kadhim kama ifuatavyo: Muhammad, mtoto wa Ali Akbar (Ashraful-Waidhin), mtoto wa Mujahid al-Waidhin, mtoto wa Ibrahim, mtoto wa Salih, mtoto wa Abi Ali Muhammad, mtoto wa Ali (ajulikanye kama Mardan), mtoto wa Abil-Qasim Muhammad Taqi, mtoto wa (Maqbulud-Din) Husein, mtoto wa Abi Ali Hasan, mtoto wa Muhammad bin Fadhullah, mtoto wa Ishaq, mtoto wa Hashim, mtoto wa Abi Muhammad, mtoto wa Ibrahim, mtoto wa Abil-Fiyan, mtoto wa Abdallah, mtoto wa Hasan, watoto wa Ahmad (Abu Tayyib), mtoto wa Abi Ali Hasan, mtoto wa Abu Jafar Muhammad al-Hari (Nazil-e-Kirman), mtoto wa Ibrahim Az-Zarir (ajulikanaye kama Mujab), mtoto wa Amir Muhammad al-Abid, mtoto wa Imamu Musa Kadhim, mtoto wa Imamu Muhammad Baqir, mtoto wa Imamu Ali Zainul-Abidin, mtoto wa Imamu Husein, mtoto wa Amirl-Muminin, Ali bin Abi Talib. Hafidh: Safu hii ya nasaba hufikia kwa Amirl-Muminin, Ali bin Abi Talib (Mungu ambariki) ingawa umesema kwamba huishia kwa Mtukufu Mtume. Kwa kweli, pamoja na nasaba hii unapaswa kujiita miongoni mwa jamaa za Mtukufu Mtume na sio miongoni mwa kizazi chake cha moja kwa moja. Dhuria ni yule ambaye moja kwa moja anaungana na Mtume. Muombezi: Safu ya jadi wetu hufikia kwa Mtume kupitia kwa Bibi Fatima Zahra, mama wa Imamu Husein. Sielewi ni kwa nini unasisitiza mno juu ya nukta hii. Hafidh: Nafikiri nimeeleweka vibaya. Ni mtazamo wangu kwamba dhuria hutambuliwa kutoka upande wa kiume tu. Nanukuu ubeti wa Kiarabu: Watoto wangu, wajukuu, na mabinti wanatokana na mimi, lakini watoto wa binti wangu hawatokani na mimi. Kama unaweza kuthibitisha vinginevyo, tafadhali fanya hivyo.

Mikesha ya Peshawar
Muombezi: Kuna ushahidi imara, kutoka katika Qurani na kutoka katika hadithi, kuthibitisha nukta yangu. Hafidh: Tafadhali usimulie ili tupata kuelewa. Muombezi: Wakati ulipokuwa unaongea sasa hivi, nimekumbuka mazungumzo kati ya Harun ar-Rashid, Khalifa wa Kibani Abbas, na Imamu wetu Musa Kadhim juu ya suala hili. Imamu alitoa jibu la kuridhisha kiasi kwamba Khalifa mwenyewe alilikubali. Hafidh: Ningependa kusikia kuhusu mazungumzo hayo. Muombezi: Abu Jafar Muhammad Bin Ali, mwenye lakabu ya Sheikh Saduq, katika karne ya nne A. H., katika kitabu chake Uyun-e-Akbar ar-Ridha (vyanzo vikubwa vya Ridha), na Abu Mansur Bin Ali Tabarsi, katika kitabu chake Ihtijajj, anatoa maelezo kinaganaga ya mazungumzo ambayo yalifanyika kati ya Harun ar-Rashid na Imamu Musa Jafar katika baraza ya Khalifa. Khalifa alimuuliza Imamu: Unawezaje kudai kwamba wewe ni dhuria wa Mtukufu Mtume? Mtume hana dhuria. Inakubaliwa kwamba dhuria ni kutoka upande wa kiume na sio upande wa kike. Wewe ni kizazi cha bint yake. Imamu akasoma Aya ya 84-85 kutoka Sura ya 6 ya Qurani Tukufu:

Na tukampa (Ibrahim) Ishaqa na Yakuub, wote tukawaongoa. Na Nuh tulimuongoa zamani, na katika kizazi chake Daudi na Suleimani na Ayub na Yunus na Musa na Harun. Na hivi ndivyo tuwalipavyo wafanyao mema. Na Zakaria na Yahya na Isa na Ilyasa, wote walikuwa miongoni mwa watu wema. (6:84-85) Imamu akamuuliza Khalifa: Ni nani aliyekuwa baba wa Isa? Harun akajibu kwamba Isa alikuwa hana baba. Imamu akasema: Kulikuwa hakuna yeyote aliyekuwa baba yake, na bado Allah alimjumuisha Isa katika dhuria wa mitume kupitia Mariamu. Hivyo hivyo ametujumuisha sisi katika dhuria wa Mtume kupitia kwa jadi wetu Bibi Fatima. Aidha, Imamu Fakhurd-Din Razi, katika kitabu chake Tafsir-e-Kabir, juzuu ya 4, uk. 124, anasema kuhusiana na aya hii kwamba, inathibitisha kwamba Hasan na Husein ni watoto wa Mtume wa Uislamu. Kwa vile katika aya hii Mungu amemdhihirisha Isa kama kizazi cha Ibrahim, na

Mikesha ya Peshawar
Isa hana baba, uhusiano huu ni kutoka upande wa mama. Katika hali hiyo hiyo, Hasan na Husein ni dhuria wa kweli wa Mtume. Imamu Musa alimuuliza Harun kama anataka uthibitisho zaidi. Khalifa akamuambia Imamu aendelee. Imamu akasoma Aya ya 61 kutoka Sura ya 3 ya Qurani Tukufu: Watakao kuhoji katika haya baada ya kukufikia ilmu, waambie: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wanawake wetu na wanawake wenu, na sisi na ninyi, kisha tuombe kwa unyenyekevu tutake laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie waongo, Aliendelea, akisema kwamba hakuna mtu hata mmoja ambaye amewahi kudai kwamba katika tukio hilo la maapizano (Mubahila) dhidi ya Wakiristo wa Najran kwamba Mtume alimchukuwa pamoja na yeye mtu yeyote isipokuwa Ali Bin Abi Talib, Fatima, Hasan na Husein. Kwa hiyo hufuatia kwamba sisi (anfusana) maana yake ni Ali Bin Abi Talib. Wanawake (nisaana) maana yake Fatima na Watoto (abnaana) maana yake Hasan na Husein, ambao Allah amewatambulisha kama watoto wa Mtume mwenyewe. Kwa kusikia hoja hii, Harun aliguta, Hongera, Ewe Abul-Hasan. Kwa uwazi mantiki hii huthibitisha kwamba Hasan na Husein (watoto wa Bibi Fatima) ni watoto wa Mtukufu Mtume.

NYONGEZA YA USHAHIDI KUTHIBITISHA KWAMBA KIZAZI CHA FATIMA NI DHURIA WA MTUKUFU MTUME.
Ibn Abil-Hadid Mutazali, mmoja wa wanachuoni wenu wakubwa, katika kitabu chake Sharhl-Nahjul-Balagha, na Abu Bakr Razi katika tafsir yake, wameionesha aya hiyo hiyo wakithibitisha kwamba Hasan na Husein wanatoka upande wa mama yao, ni watoto wa Mtukufu Mtume katika njia ile ile ambayo Allah katika Qurani Tukufu amemjumuisha Isa katika kizazi cha Ibrahim kutoka upande wa mama yake, Mariamu. Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafii, katika kitabu chake Kifayatut-Talib; Ibn Hajar Makki katika ukurasa wa 74 na 93 wa Sawaiq Muhiriqa, kutoka kwa Tabrani na Jabir Bin Abdullah Ansari, na Khatib Khawarizmi katika Manaqib kutoka kwa Ibn Abbas - wote wanasimulia kwamba Mtume alisema: Allah ameumba dhuria wa kila Mtume kutokana na kizazi chake mwenyewe, lakini dhuria wangu waliumbwa katika kizazi cha Ali. Vile vile Khatib-e-Khawarizmi katika Manaqib; Mir Seyyid Ali Hamadani Shafii katika Mawaddatul-Qubra; Imamu Ahmad Bin Hanbal, katika Musnad, na Sulayman Hanafi Balkhi katika Yanabiul-Mawadda wanasimulia katika maneno hayohayo kwa zaidi au pungufu, kwamba Mtukufu Mtume amesema: Watoto wangu hawa wawili, ni maua mawili ya ulimwengu huu, na wote wawili ni Maimamu, imma wawe ni Maimamu kwa wazi au kimya kimya wakiwa wamekaa nyumbani. Na Sheikh Sulayman Hanafi, katika Yanabiul-Mawadda, ameitoa sura ya 57 kwenye suala hili na akaonesha hadithi nyingi

Mikesha ya Peshawar
kutoka kwa wanachuoni wake mwenyewe, kama Tabrani, Hafidh Abdul-Aziz Ibn Abi Shaiba, Khatib-e-Baghdadi Hakim, Baihaqi, na Tabari - wote wanasimulia katika maneno yanayohitalifiana kidogo kwamba Hasan na Husein ni watoto wa Mtume. Kuelekea mwisho wa sura hiyo hiyo, Abu Salih anaandika: Hafidh Abdul-Aziz Bin AlAkhzar, Abu Nuaim, Tabari Ibn Hajar Makki katika ukurasa wa 112 wa Sawaiq Muhriqa, kutoka kwa Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafii mwishoni mwa jalada la 1, baada ya sura 100 za Kifayatut-Talib, na Tabari katika simulizi ya Imamu Hasan anasimulia kwamba Khalifa wa pili, Umar Bin Khattab, alisema: Nilimsikia Mtume akisema kwamba katika Siku ya Hukumu kila ukoo utatenganishwa isipokuwa kizazi changu. Kila kizazi cha binti ni kutoka upande wa baba isipokuwa kizazi cha Fatima, ambacho kimeunganishwa na mimi. Mimi ni baba yao na jadi wao. Sheikh Abdullah Bin Muhammad Bin Amir Shabrawi Shafii, katika kitabu chake Kitabul-Ittihaf bi Hubbil-Ashraf, alinukuu hadithi hii kutoka kwa Baihaqi na Darqutni kutoka kwa Abdullah Bin Umar, na yeye kutoka kwa baba yake, kwenye harusi ya Ummu Kulthum. Na Jalalud-Din Suyuti akinukuu kutoka kwa Tabrani katika kitabu chake Ausat, amesimulia kutoka kwa Khalifa Umar na Sayyid Abu Bakr Bin Shahabud-Din Alawi katika ukurasa wa 39-40 wa sura ya 3 ya RishfatusSadi min bahra Fadhail Bani Nabiul-Hadi (iliyopigwa chapa katika Maktabi Alamiyya, Misr 1303 A.H.) huthibitisha kwamba dhuria wa Fatima ni kizazi cha Mtume wa Uislamu. Kwa hiyo, ubeti ambao umeunukuu hauna nguvu mbele ya ushahidi wote huu wa kinyume chake. Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafii, katika kitabu chake Kifayatut-Talib, anathibitisha kwamba watoto wa binti wa Mtume ni watoto wa Mtukufu Mtume. Halikadhalika, kuna hadithi nyingine nyingi ambazo huthibitisha kwamba watoto wa Bibi Fatima ni watoto wa Mtume. Safu yetu ya jadi huenda mpaka kwa Imamu Husein; kwa hiyo, sisi ni dhuria wa Mtume. Hafidh: Hoja yako ni ya mantiki na kuridhisha. Watu walitawanyika kwa ajili ya Swala ya Isha. Wakati wa mapumziko Nawab AbdulQayum Khan, ambaye anatokana na familia sharifu ya Kisunni, alitaka ruhusa kumuuliza Muombezi maswali fulani.

Mikesha ya Peshawar

KWANINI SHIA WANACHANGANYA SWALA ZAO


Nawab: Kwa nini Shia wanachangana Swala ya Dhuhr na Alasir na Maghari na Isha? Hii sio sawa kulingana na matendo ya ibada ya Mtukufu Mtume. Muombezi: Kwanza kabisa, miongoni mwa wanachuoni wenu kuna tofauti nyingi za maoni kuhusu suala hili. Pili, unasema tunakwenda kinyume na mwenendo wa Mtume. Hapa umekosea kwani Mtukufu Mtume amezoea kuswali Swala zake katika njia zote, wakati mwingine kwa kuzitengenisha na wakati mwingine kwa kuzichanganya. Hapo Nawab Swahib aliwageukia wanachuoni wake, aliwauliza kama ni kweli kwamba Mtume aliswali katika njia zote. Hafidh: Ndio alifanya hivyo, lakini ni wakati tu alipokuwa safarini au wakati kama kuna vikwazo vingine fulani, kama mvua. Vinginevyo, wakati alipokuwa nyumbani siku zote alikuwa akiswali swala zake kwa kuzitenganisha. Muombezi: Imeandikwa katika vitabu vyenu wenyewe vya hadithi kwamba Mtume alizoea kusali Swala zake kwa kuzitenganisha na halikadhalika kwa kuzichanganya akiwa nyumbani na bila kikwazo chochote. Hadithi nyingi zinathibitisha ukweli huu. Muslim Bin Hajjaj katika Sahih yake, katika mlango wa Jama Bainas-Salatain fil-Hadhar, anasema kwamba Ibn Abbas alisema: Mtume alizoea kuswali Swala ya Dhuhr na Alasir kwa kuziunganisha na halikadhalika hivyo hivyo kwa Swala za Magharib na Isha bila ya kuwa na kikwazo cha kufanya hivyo, au wakati alipokuwa nyumbani. Tena Ibn Abbas alisimulia: Tuliswali rakaa nane za Dhuhr na Alasir na baadae rakaa saba za Magharib na Isha kwa kuziunganisha tukiwa pamoja na Mtume. Hadithi hiyo hiyo imesimuliwa na Imamu Ahmad Bin Hanbal katika Musnad yake jalada la kwanza, ukurasa wa 221. Halikadhalika, Imamu Muslim ananukuu idadi ya hadithi kuhusiana na suala hili. Anamnukuu Abdullah Bin Shaqiq akiwa amesema kwamba siku moja Abdullah Ibn Abbas alikuwa anahutubia baada ya Swala ya Alasir mpaka jua likazama na nyota zikawa zinaonekana. Watu wakapiga makelele, Swala, Swala, lakini Ibn Abbas hakuwajali. kisha mtu mmoja wa Bani Tamimi alipiga kelele, Swala, Swala. Ibn Abbas akasema: Unanikumbusha mimi kuhusu Sunna, lakini mimi mwenyewe nimemuona Mtume akikusanya Swala za Dhuhr na Alasir halikadhalika Magharib na Isha. Abdullah Bin Shaqiq alisema alikuwa hana hakika kuhusu maneno haya na alikwenda kwa Abu Huraira

Mikesha ya Peshawar
kumuuliza kuhusu maneno hayo. Alithibitisha kile alichokisema Ibn Abbas. Kupitia sanad nyingine ya wasimuliaji, Abdullah Bin Shaqiq alisimulia kutoka kwa Aqil kwamba siku moja Abdullah Ibn Abbas aliwahutubia watu juu ya mimbari. Alibaki pale kwa muda mrefu mpaka giza likaingia. Wakati mtu mmoja alipopiga kelele mara tatu, Swala, Swala, Swala, Abdullah Ibn Abbas alikasirika na akasema: Ulaaniwe wewe. Unathubutu kunikumbusha mimi kuhusu Swala, ingawaje wakati wa Mtukufu Mtume tulizoea kukusanya Swala za Adhuhr na Alasir na halikadhalika Magharib pamja na Isha. Zarqani katika Sharhe Mawatta cha Imamu Malik, jalada la 1, katika sura ya Jamaa Bainas-Salatain, ukurasa wa 263, anaeleza, Nisai alisimulia kutoka kwa Amru Bin Haram kutoka kwa Abi Shaatha kwamba Ibn Abbas aliswali Dhuhr na Alasir na halikadhalika Magharib na Isha kwa pamoja mjini Basra bila kukawia au kitendo chochote kati yao. Alisema kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliswali katika njia hii hii. Vile vile Muslim katika Sahih yake na Malik katika Mawatta, sura ya Jama BainasSalatain, na Imamu Hanbal katika Musnad wanamnukuu Ibn Abbas kutoka kwa Said Bin Jabir kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliswali Swala zake za Dhuhr na Alasir pamoja mjini Madina bila kulazimishwa kufanya hivyo kwa hofu au hali mbaya ya hewa. Abu Zubair akasema alimuuliza Abu Said kwa nini Mtume alikusanya Swala hizo mbili. Said akasema yeye vile vile alimuuliza Ibn Abbas swali kama hilo hilo. Ibn Abbas alijibu kwamba alikusanya Swala hizo mbili ili kwamba wafuasi wake wasije wakawekwa katika uzito na shida zisizo na sababu. Vile vile, katika hadithi nyingine nyingi, Ibn Abbas inasimuliwa kwamba alisema Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wa Uislamu alikusanya Swala za Dhur na Alasir halikadhalika na Magharib na Isha bila kulazimishwa kufanya hivyo. Hadith hizi katika Sahihi zenu na vitabu vyingine sahihi huthibitisha kuruhusiwa ukusanyaji wa Swala mbili, nyumbani au safarini. Hafidh: Hakuna nukuu kama hiyo ya hadithi katika Sahih Bukhari. Muombezi: Kwa sababu waandishi wote wa Sahih, kama vile Muslim, na Nisai, Ahmad Bin Hanbal, na wafasir wa Sahih mbili, ya Muslim, Bukhari, na wanachuoni wengine wakubwa wa ki-Sunni wamenukuu mambo haya, hii inatosha kwetu kuishindisha nukta yetu. Lakini kwa kweli Bukhari vile vile ameziandika hadithi hizi katika Sahih yake, lakini kwa hila ameziweka mbali na sehemu zao husika, ile sehemu inayohusika na ukusanyaji wa Salat mbili. Kama utaipitia ile milango ya Bab-e-Taakhirudh-Dhuhur lil-Asr Min Kitabe Mawaqtus-Salat na Bab-e-Dhikrul-Isha wal-Atma na Bab-e-WaqitulMaghrib, utaziona hadithi zote hizi humo. Hadithi hizi kuandikwa chini ya kichwa cha habari: Ruhusa na Mamlaka ya Kisheria ya kukusanya Salat mbili huthibitisha kwamba ni imani ya kawaida ya wanachuoni wa madhehebu hizi mbili. Usahihi wa hadithi hizi umekwisha kubaliwa katika vitabu vya Sahih. Kwa sababu hiyo, Allama Nuri katika Sharhe Sahih Muslim, Asqalani, Qastalani, Zakariyya-e-Razi katika sharhe ambayo ime-

Mikesha ya Peshawar
andikwa juu ya Sahih Bukhari, Zarqani katika Sharhe yake juu ya Muwatta - kitabu cha Imamu Malik, na wengine wamesimulia hadithi hizi. Baada ya kunukuu hadithi ya Ibn Abbas, walikubali usahihi wake na wakakiri kwamba hadithi hizi ni uthibitisho wa kukubalika kwa kukusanya Salat mbili. Nawab: Imewezekanaje kwamba hadithi hizi zimekuwa katika matumizi tangia wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), lakini wanachuoni wamechukuwa njia nyingine? Muombezi: Hali hii haikomei kwenye nukta hii peke yake. Utaona mifano mingi kama hii baadae. Katika suala hili, Mafaqih wa ki-Sunni, kwa wazi bila ya kufikiria kwa makini, au kwa sababu nyingine ambazo mimi sizielewi, wametoa maelezo yasiyoleweka kukinzana na hadithi hizi. Kwa mfano, wanasema kwamba huenda hadithi hizi huzungumzia hali zinazohusiana na hofu, hatari, mvua, au upepo mkali. Baadhi ya wanachuoni wenu wa zamani, kama Imamu Malik, Imamu Shafii, na baadhi ya wanachuo wa Madina wametoa maelezo kama hayo hayo. Namna hii, pamoja na ukweli kwamba hadithi ya Ibn Abbas kwa uwazi kabisa inasema kwamba ukusanyaji wa Swala mbili ulikuwa unafanywa bila kikwazo cha hofu au uwezekano wa kunyesha mvua. Wengine wamesema kwamba huenda mawingu yalikuwa yametanda angani, na wale waliokuwa wakisali hawakujua ni saa ngapi. Pengine walipomaliza kusali Swala yao ya Adhuhur, mawingu yalitawanyika, na wakaona kwamba ilikuwa ni wakati wa Swala ya Alasir. Hivyo wakalazimika kusali Adhuhuri na Alasiri kwa pamoja. Sidhani maelezo zaidi yasiyo yamkinika yanaweza kupatikana. Pengine wafasiri hawa hawakujali kufikiria kwamba mtu aliyekuwa akisali Swala hizo ni Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wa Uislamu. Mawingu hayakumaanisha kwake kile ambacho kingemaanishwa kwa wengine. Anajua sababu zote na matokeo. Mbali na ukweli kwamba maelezo haya hayaridhishi, ukusanyaji wa Swala za Mahgarib na Isha unakataa maelezo yao. Katika wakati huo mawingu hayana uhusiano na suala hili. Kama tulivyosema, hadithi ya Ibn Abbas kwa uwazi inaeleza kwamba khutuba yake iliendelea kwa muda mrefu mpaka wasikilizaji wakapiga kelele, Swala, Swala. Walimkumbusha kwamba nyota zimetokea na kwamba ilikuwa ni wakati wa Swala. Lakini aliichelewesha Swala ya Magharibi kwa makusudi ili aje kuswali zote, Magharib na Isha kwa pamoja. Abu Huraira vilevle alithibitisha kitendo hiki, akisema kwamba Mtume vile vile aliswali kwa nama hiyo hiyo. Maelezo ya uwongo kama hayo, katika mwanga wa mwongozo wa dhahiri, husikitisha. Wanachouni wenu wenyewe wameyapuuza hayo. Sheikhul-Islam Ansari, katika kitabu chake, Tuhfatul-Bari fi Sharhe Sahihul-Bukhari katika sura ya Salatuz-Dhuhr mal-Asr wal-Magharib mal- Isha ukurasa wa 292, jalada la 2, na halikadhalika Allama Qastalani, katika ukurasa wa 93 jalada la 2 la Irshadus-Sari fi Sharhe Sahihul-Bukhari, na hivyo hivyo na washereheshaji wengine wa Bukhari wanakiri kwamba aina hii ya maelezo ni kinyume na maana ya wazi ya hadithi na kwam-

10

Mikesha ya Peshawar
ba kusisitiza kwamba kila Swala iswaliwe peke yake ni mashrti yasiyo na msingi. Nawab: Basi mgogoro huu umejitokeza vipi mpaka madhehebu mbili za Waislamu kila moja inataka kumwaga damu ya mwenzake, na kulaumu kitendo cha mwenzake? Muombezi: Unasema kwamba madhehebu hizi mbili ni adui kwa kila mmoja, lakini sikubaliani na wewe. Sisi Mashia hatumdharau mwanachuoni yeyote au mtu wa kawaida katika ndugu zetu Masunni. Tunasikitika kwamba propoganda za Makhariji, Manasibi na Bani Umayyah zimeathiri nyoyo za baadhi ya watu. Kwa bahati mbaya sana, baadhi ya Masunni wanawachukulia ndugu zao Mashia, ambao wako pamoja nao kwa kuhusiana na Qibla (Kaaba), Kitabu Kitukufu (Qurani), Mtume, utekelezaji wa matendo ya dini, na kujiepusha kutokana na madhambi, kuwa kama Marafidhi (watofautishaji), waabudu masanamu, na makafiri. Amma kwa swali lako kuhusu vipi tofauti hizi zilivyojitokeza, labda hili tunaweza kulijadili katika mikutano yetu ya baadae. Kuhusu kusali Swala kwa kutenganisha au kwa pamoja, wanachuoni wa sheria wa ki-Sunni wenye kutegemewa wamenukuu hadithi ambazo huruhusu kusali Adhuhuri na Alasiri na Magharibi na Isha kama jambo la wepesi, wasaa au usalama. Sijui kwa nini baadhi ya watu hawaoni kwamba inaruhusika kusali Swala mbili pamoja pasi na kuwa na udhuru wowote. Baadhi ya wanachuo, kama Abu Hanifa na wafuasi wake wameikataza katika hali yoyote, iwe kuna udhuru au la, au Swala iwe inasaliwa wakati mtu akiwa safarini au nyumbani. Shafii, Maliki, na Hanbali, pamoja na hitilafu zao zote katika kanuni za msingi na zisizo za msingi, wameruhusu ukusanyaji wa Swala wakati wa safari ya halali. Lakini Maulamaa wa ki-Shia, wakiwa katika utii wa Imamu na kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wameruhusu bila masharti yoyote ukusanyaji wa Swala mbili kwa pamoja. Hakika kusali Swala katika wakati ulioanishwa kwa kila Swala ni bora kuliko kuzisali kwa wakati mmoja, kama ambavyo imeelezwa kwa uwazi katika vitabu vya tafsir vinavyoshughulika na matatizo ya utekelezaji wa masuala ya dini vilivyoandikwa na Maulamaa wa ki-Shiah. Kwa vile watu mara nyingi wanakuwa na shughuli nyingi katika mambo yao wenyewe na wasi wasi, wanaogopa huenda wakazikosa Swala zao. Kwa hiyo, kwa nafasi zao na kuepuka uzito na shida, Mashia wanasali Swala zao mbili katika wakati mmoja, mapema au kwa kuahirisha, katika wakati ule ule uliotengwa kwa ajili ya Swala. Sasa nafikiri kiasi hiki kinatosha kuwapa mwanga ndugu zetu Masunni ambao hutuangalia kwa hasira. Bila shaka tunaweza kurudi kwenye majadiliano yetu kuhusu misingi, ambapo baadae masuala yanayohusu ibada yatatatuliwa.

11

Mikesha ya Peshawar

JINSI WAZAZI WA ALLAMA WALIVYOHAMA KUTOKA HIJAZI KWENDA IRAN


Hafidh Sahib alimuomba Allama Sultanul-Waidhin amueleze ni vipi wazazi wake walivyohama kutoka Hijazi kwenda Iran. Alieleza historia ya wahenga wake ambao waliuawa huko Shirazi kwa amri ya mfalme wa ki-Banu Abbas. Makaburi yao mpaka sasa bado yanawavutia mahujaji kutoka sehemu za mbali. Maarufu miongoni mwao ni Sayyid Amir Muhammad Abid, Sayyid Amir Ahmad (Shah Charagh), na Sayyid Alaud-Din Husein, wote ni watoto wa Imamu Musa Kadhim. Maelezo kuhusu familia yake yanaondolewa hapa.

JINSI KABURI LA AMIRUL-MUMININ ALI (A.S.) LILIVYOGUNDULIWA.


Vile vile ulitajwa ungunduzi wa kaburi la Amirul-Muminin Ali (as). Hafidh: Lakini kaburi la Amirul-Muminin liligunduliwa katika hali gani miaka 150 baada ya kifo chake? Muombezi: Kwa sababu uonevu wa Banu Umayya ulikuwa mkali sana wakati wa mwisho wa uhai wa Ali, hivyo aliagiza katika wosia wake kwamba azikwe kwa siri wakati wa usiku, na kwamba isiachwe alama yoyote ya kaburi hilo. Ni jamaa zake wachache tu wa karibu na watoto wake ndio waliohudhuria mazishi yake. Asubuhi ya tarehe 21 Ramadhan siku ambayo ilikuwa ndio azikwe, misafara miwili ilitayarishwa. Mmoja ulielekezwa kwenda Makka, na mwingine kwenda Madina. Hii ndio sababu iliyofanya kwa miaka mingi kaburi lake lisijulikane, isipokuwa kwa jamaa zake wachache na watoto wake tu. Hafidh: Kwanini eneo la kaburi hilo likafanywa siri? Muombezi: Huenda ni kwa sababu ya hofu ya tabia isiyo ya dini ya Banu Umayya. Walikuwa maadui makhususi wa jamaa ya kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w). Wangeweza kulivunjia heshima kaburi lake. Hafidh: Lakini inawezekana kwamba Mwislamu, hata kama ni adui kiasi gani, anaweza kulifanyia vurugu kaburi la ndugu yake Mwislamu? Muombezi: Umesoma historia ya Banu Umayya? Kuanzia siku ambayo utawala huu mbaya uliposhika madaraka, mlango wa maonevu ulifunguliwa miongoni mwa Waislamu. Subuhana-LLAH! Maovu yalioje waliyoyafanya! Damu iliyoje waliyoimwaga, na heshima zilizoje walizozivunja! Kwa aibu kubwa, wanachuoni wenu wakubwa wameandika

12

Mikesha ya Peshawar
jinai zao nyingi. Allama Maqrizi Abul-Abbas Ahmad bin Ali Shafii ameandika maovu ya Banu Umayya yanayoumiza moyo kabisa katika kitabu chake Annaza Wat-takhasum fima baina Bani Hashim wa Bani Umayya.

BANI UMAYYA NA UTIAJI NAJISI WA MAKUBURI


Kwa mfano wa yale waliyokuwa na uwezo nayo, nitaonesha matukio mawili: Kuuwawa shahidi kwa Zaid bin Ali bin Husein, ajulikanaye kama Zaid Shahid, na kuuwawa shahidi kwa mtoto wake, Yahya. Wanahistoria wote wa Shia na Sunni wameandika kwamba wakati Hisham bin Malik alipokuwa Khalifa, alitenda maovu mengi. Mwishowe, Zaid bin Ali, mtoto wa Imamu Zainul-Abidin na anayejulikana sana kama mwanachuo mkubwa na mwanatheolojia mchamungu, alikwenda kumuona Khalifa kutafuta haki kwa ajili ya manunguniko ya Bani Hashim. Lakini punde tu Zaid alipowasili, Khalifa badala ya kumsalimu kama mtoto wa moja kwa moja wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), alimtukana kwa lugha ya kuchukiza sana ambayo siwezi kuirudia hapa. Kwa sababu ya kudhalilishwa huku alikofanyiwa, Zaid aliondoka Syria na kwenda Kufa, ambako aliunda jeshi dhidi ya Bani Umayya. Gavana wa Kufa, Yusuf bin Umar Thaqafi, alitoka na jeshi kubwa kumkabili. Zaid alisoma shairi lifuatalo: Maisha ya udhalilifu na kifo cha heshima, vyote ni chembe zenye uchungu, lakini kama moja wapo lazima ichanguliwe, chaguo langu ni kifo cha heshima. Ingawa alipigana kishujaa, Zaid aliuwawa katika mapigano hayo. Mtoto wake, Yahya, alichukua mwili wake kutoka kwenye uwanja wa vita na akamzika mbali kutoka mjini karibu na ukingo wa mto, na kusabibisha maji kupita juu yake. Hata hivyo, kaburi hilo liligunduliwa, na chini ya amri ya Yusuf mwili huo ulifukuliwa, kichwa cha Zaid kilikatwa na kupelekwa Syria kwa Hisham. Katika mwezi wa Safar, 121 A.H., Hisham aliamuru mwili mtakatifu wa mtoto huyu wa Mtume (s.a.w.w) uwekwe kwenye kiunzi cha kunyongea ukiwa uchi kabisa. Kwa muda wa miaka minne ulikaa kwenye kiunzi cha kunyongea. Baadae, wakati Walid bin Yazid bin Abdul-Malik bin Marwan alipokuwa Khalifa katika mwaka wa 126 A.H., aliamrisha kwamba mifupa ile itolewe kutoka kwenye kiunzi cha kunyongea, ichomwe, na jivu lake lisambazwe juu lichukuliwe na upepo. Mtu huyu aliyelaaniwa alitenda uovu kama huu huu kwenye mwili wa Yahya bin Zaid wa Gurgan. Mtu huyu mtukufu vile vile alipinga uonevu wa Bani Umayya. Yeye pia aliuwawa katika medani ya vita. Kichwa chake kilipelekwa Syria na kama alivyofanyiwa mtukufu baba yake, mwili wake ulitundikwa kwenye kiunzi cha kunyongea kwa muda wa miaka sita. Marafiki na maadui wote kwa pamoja walilia walipouona mwili wake. Waliud-Din Abu Muslim Khorasani, ambaye alipigana dhidi ya Bani Umayya kwa niaba ya Bani Abbas, aliuchukuwa mwili wake na kuuzika huko Gurgan, ambako ni sehemu ya kuhiji (Ziyarat).

13

Mikesha ya Peshawar

MATENDO MAOVU YA UFALME HUU


Kwa kuzingatia maovu ya ufalme huu uliolaaniwa, mwili wa Amirul-Muminin, Ali (as) ulizikwa wakati wa usiku, na hakuna alama ya kaburi hilo iliyoachwa. Kaburi likabakia bila kuonekana mpaka wakati wa Khalifa Harun ar-Rashid. Siku moja Harun alikwenda kuwinda katika eneo la Najaf, ambako paa waliishi kwa wingi. Wakati mbwa walipofukuza paa, walichukua hifadhi juu ya kilima kidogo (kilichotutumka juu ya ardhi) cha Najaf, kilima ambacho mbwa hao hawakuweza kukipanda. Mara nyingi wakati mbwa waliporudi nyuma, paa waliteremka chini, lakini wakati mbwa wanapowarukia tena, wale paa huchukua tena hifadhi juu ya kile kilima. Harun akatuma watu wake kwenda Najaf kuuliza. Walimleta mzee mmoja kwake na Khalifa akauliza kuhusu siri ya kwa nini mbwa hawakupanda juu kilima.

KUGUNDULIWA KWA KABURI TUKUFU LA ALI.


Yule Mzee akajibu kwamba anaielewa Siri yake, lakini alikuwa anaogopa kuitoa. Khalifa akamhakikishia usalama wake, na yule mzee akamwambia: Siku moja nilikuja hapa pamoja na baba yangu, ambaye alipanda juu ya kilima na akaswali pale. Nilipomwuuliza kuna nini pale, akasema kwamba waliwahi kuja pale na Imam Jafar Sadiq kwa ajili ya Ziara. Imam alisema kwamba hili ni kaburi Tukufu la Mheshimiwa babu yake, Amurl Muminiina Ali, na kwamba muda mfupi litakujajulikana. Kwa amri ya Khalifa sehemu ile ilichimbuliwa, na alama za kaburi zikaonekana wazi pamoja na ubao wenye maandishi ya Ki-Syria yenye maana; Kwa jina la Allah, Mwenye rehema, Mwenye kurehemu. Kaburi hili limetayarishwa na Mtume Nuh kwa ajili ya Ali, wasii wa Muhammad miaka 700 kabla ya gharika. Khalifa Harun alitoa heshima zake kwenye sehemu ile na akaamuru ule udongo urudishwe. Kisha akasali rakaa mbili. Alilia sana na akajilaza juu ya kaburi. Baadae, kwa amri yake, taarifa ya tukio lote ilitolewa kwa Imam Musa Kadhim huko Madina. Imam alithibitisha kwamba kaburi hilo ni la Mheshimiwa babu yake, Amirul-Muminin Ali, lipo mahala hapo. Kisha Harun akaamuru jengo la mawe lijengwe juu ya kaburi tukufu la Amirul-Muminin, ambalo lilikuja kujulikana kama Hajar Harun. Kwa wakati huo habari zilisambaa na Waislamu wakaizuru sehemu hiyo tukufu. Ibrahim Mujab, babu yake mkubwa wa Sultanil-Waidhin (Muombezi) pia alitoka Shiraz kwa ajili ya Ziara hii tukufu na baada ya kukamilisaha Ziara hii, yeye akafariki huko Karbala. Alizikwa karibu na kaburi tukufu la Babu yake Mkubwa, Imam Husein. Kaburi lake liko pembe ya Kaskazini Mashariki ya kuba lake tukufu na linazuriwa mara kwa mara na wapenzi wake.

14

Mikesha ya Peshawar

KHITILAFU KUHUSU SEHEMU ALIYOZIKWA AMIRUL- MUMININ.


Hafidh: Pamoja na maneno haya ya kuthibitisha na yenye nguvu, nafikiri kwamba kaburi la Ali (R.A) haliko Najaf. Wanachuoni wanatofautiana juu ya nukta hii. Baadhi wanasema liko kwenye Ikulu mjini Kufa; baadhi wanasema liko kwenye Kibla ndani ya Msikiti Mkuu wa Kufa; baadhi wanasema liko kwenye lango linalojulikana kama Ba-e-Kinda katika Msikiti wa Kufa; baadhi wanashikilia kwamba liko ndani ya Rahba huko Kufa; na bado wengine wanasema liko pembeni mwa kaburi la Fatima huko Baqi. Katika Afghanistan yetu, pia kuna sehemu karibu na Kabul inajulikana kama Kuba la Ali. Kutokana na maelezo fulani, mwili Mtukufu wa Ali uliwekwa kwenye Kasha na ukalazwa juu ya mgongo wa ngamia na ukapelekwa kuelekea Madina. Kikundi cha watu kikanyakua lile kasha, wakidhania lina vitu vya thamani. Wakati wanalifungua, wakaona mwili ule Mtukufu, wakauleta Kabul, na ukazikwa katika sehemu hii. Ndio maana watu wanaitukuza sehemu hii. Muombezi: Tofauti zilitokea kwa sababu ya maelezo ya wasia wake, ambao umeweka sharti kwamba matayarisho ya mazishi yake yatatize sehemu yake ya kuzikwa. Inasimuliwa na Imam Jafar Sadiq kwamba katika wakati wake wa kufa, AmirulMuminin alimwambia mtoto wake, Imam Hasan kwamba baada ya kumzika Najaf, atayarishe makaburi manne kwa ajili yake katika sehemu nne tofauti. Katika Msikiti wa Kufa, katika Rahba, katika nyumba ya Juda Hira, na Ghira. Shia wanakubali kwamba kaburi lake tukufu liko Najaf. Chochote walichojifunza kutoka kwa Ahli Bait ni sahihi. Watu wa nyumba wanajua vizuri zaidi kuhusu kinachohusiana na nyumba yao. Kwa hakika nawashangaa wanachuo wenu ambao wamezitelekeza simulizi za Kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika kila jambo. Hawakuuliza kuhusu mahala pa kaburi la baba kwa watoto wake wenyewe ili kuelewa ukweli. Ni hakika kabisa kwamba watoto wanajua zaidi kuhusu kaburi la baba yao kuliko wengine. Kama nadharia hizi za sasa zingekuwa sawsawa, Maimam Watukufu wangewajulisha wafuasi wao juu ya hilo. Lakini wamelithibitisha mahala lilipo Najaf, wamezuru hiyo sehemu wao wenyewe, na wamewahimiza sana wafuasi wao kuizuru sehemu hiyo. Sibt Ibn Jauz katika kitabu chake Tadhkira amezitaja tofauti hizi. Anasema: Maoni ya sita ni kwamba liko Najaf katika ile sehemu inayojulikana sana, ambayo kwa kawaida hufanyiwa Ziara. Kwa yote yaliyojitokeza, haya ndio maoni ya sawasawa. Halikadhalika, wanachuo wenu wengine kama Khatibu-e-Khawarizmi katika Munaqib, Muhammad bin Shafii katika MatalibusSuul, Ibn Abil-Hadid katika Sharhe Nahajul-Balagha, Firuzabadi katika Qamus, yake chini ya neno Najaf, na wengine, wameshikilia kwamba kaburi la Amirul-Muminin liko Najaf.

15

Mikesha ya Peshawar

MKUTANO WA PILI, IJUMAA USIKU 24 RAJAB, 1345 A.H.


Hafidh: Nilivutiwa mno na mazungumzo yako yenye maelekezo kuhusu mtiririko wa jadi yako. Nakiri kwamba wewe ni kizazi (dhuria) cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), lakini nashangaa ni vipi mtu mwenye elimu kama wewe unakuwa chini ya ushawishi wenye ushusha hadhi wa maadui. Ukiwa mwenye kuziacha njia za jadi wako Maarufu, umefuata njia za makafiri wa Iran. Ninachomaanisha hapa kwa njia za maadui wapumbavu ni yale mambo mapya ya uzushi (Bida) yaliyoingizwa katika Uislamu kupitia kwa Mayahudi. UUislaupitia Mayahud Muombezi: Tafadhali hebu elezea ni nini unachomaanisha.

DHANA POTOFU KUHUSU ASILI YA MADHEHEBU YA SHIA.


Hafidh: Historia yote ya Mayahudi imeharibiwa na hila. Abdullah bin Saba Sanai, Kabul-Ahbar, Wahhab Ibn Munabba, na wengine waliukiri Uislamu, na wakajifanya wanakubali hadith za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na hivyo kusababisha ghasia miongoni mwa Waislamu. Khalifa wa tatu Uthman bin Affan, aliwaandama na wakakimbilia Misri, ambako walianzisha madhehebu yajulikanayo kama Shia. Walieneza taarifa za uongo kuhusu Khalifa Uthman na kuandika hadith za uongo za kumaanisha kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimteuwa Ali kuwa Khalifa na Imamu. Kwa kuanzishwa madhehebu haya vurugu zilienea, ambazo zilipelekea kuuwawa kwa Khalifa Uthman na kuchukuliwa kwa cheo cha ukhalifa na Ali. Kikundi kilichokuwa na uadui kwa Uthman kikasimama juu kumpendelea Ali. Wakati wa Ukhalifa wa Bani Umayya, wakati watu wa familia ya Ali na wafuasi wake walipokuwa wanauwawa, kikundi hiki kilijificha. Bado, baadhi ya watu, kama Salman Farsi, Abu Dharr Ghifari, na Amar Yasir, waliunga mkono mwenendo wa Ali. Mashindano haya yaliendelea mpaka wakati wa HarunarRashidi, na hasa mwanae Mamun-ar-Rashidi Abbas, ambaye alimshinda ndugu yake kwa msaada wa wa-Irani, na kisha wakaeneza wazo la kwamba Ali alikuwa ni bora kuliko makhalifa wengine, Wa-Irani, wakiwa na uadui na Waarabu ambao waliwashinda, wakapata fursa ya kuwapinga Waarabu kwa kutumia jina la dini. Mashia wakapata nguvu katika kipindi cha Wadailami na Wafalme wa Ki-Safavid na hatimaye wakatambuliwa. Basi wakajulikana rasmi kama madhehebu ya Shia. Wazoroasta wa Iran bado wanajiita Mashia. Kwa ufupi, madhehebu ya Shia yalianzishwa na Myahudi, Abdullah bin Saba. Vinginevyo

16

Mikesha ya Peshawar
kusingekuwa na neno kama Shia katika Uislamu. Babu yako, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alilichukia neno hilo. Kusema kweli madhehebu ya Shia ni sehemu ya imani ya Kiyahudi. Nashangaa kwa nini umeacha njia za haki za jadi wako na ukafuata njia ya waliokutangu lia, ambao wamefuata njia za Kiyahudi. Ilikupasa ufuate Qurani Tukufu na mfano wa babu yako, Mtume (s.a.w.w.).

NI UPUUZI KUMHUSISHA ABDULLAH BIN SABA NA MASHIA


Muombezi: Ni kitu kisicho cha kawaida kwa mtu msomi kama wewe kutegemeza hoja zake katika misingi ya uongo kabisa. Hakuna maana kwako wewe kulihusisha jina la Abdullah bin Saba na Mashia. Abdullah bin Saba alikuwa Myahudi, na kutegemeana na vyanzo (rejea) vya Shia, yeye ni mnafiki na analaaniwa vikali. Ikiwa kwa wakati fulani alitokea kuwa rafiki wa Ali, ni uhusiano gani aliokuwa nao na Mashia? Kama mwizi atavaa guo ya Mwanachuo, akapanda juu ya mimbari, na akasababisha madhara kwa Uislamu, utayachukia mafundisho na kuwaita Wanachuoni wezi?** Kwa kweli Waislamu wa Madhehebu ya Shia kamwe hawajakuwa ni kikundi cha Siasa tu. Walikuwa wakati wote wanaunda madhehebu ya dini, ambayo hayakuanzishwa, kama unavyosema, katika wakati wa Ukhalifa wa Uthman, lakini lililinganiwa kutokana na maneno na maamrisho ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika wakati wake mwenyewe. Wakati ambapo wewe unajadili kwa msingi wa ushahidi wa kubuni wa maadui, mimi nitanukuu kwa ajili yako Aya kutoka Qurani Tukufu na similizi za waandishi wenu wenyewe kuonyesha hali ya ukweli halisi.

MAANA YA NENO SHIA


Muombezi: Shia kama ujuavyo, kilugha ina maana ya Mfuasi. Mmoja wa maulamaa wenu mkubwa, Firuzabadi katika kitabu chake Qamusul-lughat, anasema: Jina la Shia kwa kawaida lina maana ya kila mtu ambaye ni rafiki wa Ali na Ahlul-Bait wake. Jina hili ni lao peke yao. Maana hii hii hasa inatolewa na Ibn Athir katika Nihayatull-Lugha. Kutokana na Sharh zenu wenyewe, neno Shia lina maana ya wafuasi wa Ali ibn Abu Talib, na lilikuwa likitumika katika njia hii katika wakati wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kwa kweli alikuwa ni Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe ambaye alilitambulisha neno Shia kwa maana ya Mfuasi wa Ali bin Abu Talib. Na neno hili lilikuwa likitumiwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambaye kuhusu yeye Allah (s.w.t.) Anasema:
** Huu ulikuwa mwaka wa 1927 (1345 A.H.), katika miaka ya hivi karibuni imebainika kwamba kulikuwa hakuna mtu anayeitwa Abdullah Ibn Saba, huu ulikuwa ni ubunifu wa mtu aliyekuwa akiitwa Seif. Ukweli huu umetokana na utafiti uliofanywa na mwanachuoni mtafiti, Al-Askari. Soma kitabu chake: Abdallah bin Saba na ngano nyinginezo

17

Mikesha ya Peshawar

Wala hasemi kwa matamanio (ya nafsi yake). Hayakuwa haya ila ni Wahyi uliofunuliwa. (53: 3-4) Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwaita wafuasi wa Ali Shia, waliokombolewa na waliookolewa. Hafidh: Kiko wapi kitu kama hicho? Sisi hatujakiona kamwe. Muombezi: Sisi tumekiona na hatufikirii kuwa ni sawa kuficha ukweli. Allah (s.w.t.) Amewalaani wafichaji na hao akawaita ni watu wa motoni. Allah (s.w.t.) Anasema: Hakika wale wanaficha hoja zilizo wazi na uongozi ambao tumeuteremsha baada ya kuzibainisha kwa watu kitabuni, hao anawalaani Allah na wanawalaani wenye kulaani. (2:159) Hakika wale wafichao aliyoyateremsha Allah katika Kitabu wakafadhilisha thamani ndogo, hao hawali matumboni mwao isipokuwa moto, wala Allah hatawasemeza Siku ya Kiyama wala hatawatakasa, na watapata adhabu iliyo kali. Hafidh: Kama tunaijua kweli na tukaificha nakubali kwamba tunastahili laana kama ilivyofunuliwa katika aya hizi tukufu. Muombezi: Natumaini utaziweka akilini Aya hizi mbili ili kwamba usije ukashindwa nguvu na tabia au kutovumilia. Hafidh Abu Nuaim Isfahani ni moja wa watu wenu maarufu sana katika wasimuliaji wa hadith. Ibn Khallikan amemsifu katika kitabu chake Wafayatul Aayan kama Huffadh mkubwa (Mtu wa hikma) na mmoja kati ya wasimuliaji wa hadith aliyeelimika sana. Vile vile anaelezea kwamba jalida kumi za kitabu chake HilyatulAulya ni miongoni mwa vitabu vizuri mno vya kufundishia. Salahud-din Khalil bin Aibak Safdi anaandika katika Wafiy bil-Wafiyat kuhusu yeye: Mfalme wa wasimuliaji wa hadith, Hafidh Abu Nuaim, alikuwa wa mbele sana katika ilmu, uchamungu, na uaminifu. Alikuwa na nafasi ya hali ya juu katika usimuliaji na uelewaji wa hadhith. Kitabu chake kilicho bora sana ni Hiliyatul-Auliya katika jalida kumi, zikiwa na chimbuko kutoka Sahih mbili (Bukhari na Muslim). Muhammad bin Abdullah alKhatab amemsifu katika Rijalil-Mishkatil-Masabin. akisema kwamba ni miongoni mwa wasimuliaji hadith wa mbele ambaye simulizi zake ni za kuaminika kabisa. Kwa ufupi, Mwanachuo na Muhadithina huyu mwenye kuheshimika na fahari ya Maulamaa wenu, anasimulia kutoka kwa Abdullah ibn Abbas kupitia nyororo yake mwenyewe ya wasimuliaji katika Kitabu chake Hilyatul-Auliya kama ifuatavyo: Wakati aya ifuatayo ya Qurani Tukufu ilipoteremshwa:

18

Mikesha ya Peshawar

(Na kwa) wale ambao wanaamini na kufanya mema, hakika hao ndio wabora wa viumbe. Malipo yao kwa Mola wao ni bustani zipitazo mito chini yake, watakaa humo milele. Allah yuko radhi nao na wao wako radhi Naye, na hayo ni kwa yule amchae Mola. (98: 7 8) Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), akizungumza na Ali, alisema: Ewe Ali, wabora wa viumbe (khairil-Bariyya) katika Aya hii tukufu inakuashiria wewe na wafuasi (Shia) wako. Katika siku ya ufufuo, wewe na wafuasi (Shia) wako mtapita daraja ambayo kwamba Allah atakuwa radhi nanyi na ninyi mtakuwa radhi Naye.

SIFA ZAIDI ZA SHIA


Halikadhalika, Abul-Muwayyid Muwafiq Bin Ahmad Khawarizmi katika sura ya 17 ya Manaqib yake; Hakim Abul-Qasim Abdullah Bin Abdullahil-Haskani, katika Shawahidut-Tanzil; Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafii katika Kifayatut-Talib, uk. 119, Sibt Ibn Jauzi katika Tadhkira, uk. 31, Munzir Bin Muhammad Bin Munzir, na hususan Hakim, wamesimulia kwamba Hakim Abu Abdullah Hafidh (mmoja wa maulamaa wenu wakubwa) alisema, akitegemea juu ya ushahidi wa wasimuliaji kurudi nyuma hadi kufikia kwa Yazid Bin Sharafil-Ansari, mwandishi wa Amirul-Muminin Ali Bin Abi Talib kwamba Ali alisema kwamba wakati wa kifo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Mtume aliegema kwenye kifua cha Ali na akasema: umeisikia ile aya tukufu: Wale ambao wameamini na wakafanya matendo mema, hao ndio bora wa viumbe. (98:7) Hawa ni Shia wako. Sehemu yangu ya kukutania na wewe itakuwa ni kwenye Chemchemu ya Kauthar (katika Pepo). Wakati viumbe wote watakapokusanyika kwa ajili ya hesabu, uso wako utangara, na utatambulishwa siku hiyo kama kiongozi wa watu wenye nyuso angavu.

Jalalud-Din Suyuti katika Durrul-Mansur anamnukuu Abul-Qasim Ali Bin Hasan (anayejulikana zaidi kama Ibn Asakir Damishqi) ambaye anamnukuu Jabir Bin Abdullah Ansari, mmoja wa masahaba wakubwa wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), akisema kwamba yeye na watu wengine walikuwa wamekaa pamoja na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wakati

19

Mikesha ya Peshawar
Ali Bin Abi Talib alipoingia ndani. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: Naapa kwa Yule ambaye anamiliki uhai wangu kwamba mtu huyu (Ali) na wafuasi wake watapata wokovu katika Siku ya Ufufuo. Wakati huo huo aya hiyo hapo juu ilishushwa. Katika sharhe hiyo hiyo, Ibn Adi anamnukuu Ibn Abbas akisema kwamba wakati aya hiyo hapo juu iliposhuka, Mtume akasema kumuambia Amirul-Muminin, Ali: Wewe na waafuasi wako mtakuja Siku ya Ufufuo katika hali ambayo kwamba wote mtaridhia juu ya Allah, na Allah ataridhika nanyi. Katika Manaqib ya Khawrizmi, ifuatayo ilisimuliwa kutoka kwa Jabir Bin Abdullah Ansari: Nilikuwa kwenye hadhara ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wakati Ali alipoungana nasi, na wakati ule Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: Huyu ambaye amekujieni ni ndugu yangu. Kisha, akaelekea Kaba, Mtume akachukua mkono wa Ali na akasema: Naapa kwa Yule ambaye anamiliki uhai wangu, huyu Ali na wafuasi wake watakuwa wamepata wokovu katika Siku ya Hukumu. Kisha akasema: Ali ndiye wa mbele zaidi yenu wote katika imani, mwenye kuzingatia mno kuhusu dhamana za Allah, mwadilifu kupita wote katika kuamua mambo ya watu, na mwadilifu kupita wote katika kugawa masurufu miongoni mwa watu, na aliye juu zaidi ya wote kwa cheo mbele ya Allah. Katika wakati huo aya hiyo hapo juu ilishushwa. Katika Sura ya 11 ya Kitabu chake Sawaiq Ibn Hajar anamnukuu Hafidh Jamalud-Din Muhammad Bin Yusuf Zarandi Madani (Mwanachuo mkubwa wa madhehebu yenu) akisema kwamba: Wakati Aya hiyo hapo juu ilipoteremshwa, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: Ewe Ali, Wewe na Shia wako ndio wabora wa viumbe walioumbwa. Wewe na Mashia wako mtakuja Siku ya Hukumu katika hali ambayo nyote mkiwa mmeridhia kwa Allah, na Allah atakuwa radhi nanyi. Maadui zako watakuwa wamechukizwa mno, na mikono yao itakuwa imefugwa kuzunguuka shingo zao. Kisha Ali akauliza, ni nani maadui zangu. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akajibu, Yule ambaye ana uadui kwako na ambaye anakutukana. Allama Samhudi, katika Jawahirul-Iqdain, kwa idhini ya Hafidh Jamalud-Din Zarandi Madani na Nurud-Din Ali bin Muhammad bin Ahmad Maliki Makki, ajulikanaye kama Ibn Sabbagh, ambaye anaheshimiwa kama mmoja wa Wanachuo wenu Mashuhuri na mnadharia mkubwa wa mambo ya dini, katika kitabu chake Fusulul-Muhimma anasimulia kutoka kwa Abdullah bin Abbas, kwamba wakati Aya hii iliyo kwenye mjadala ilipoteremshwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kumuambia Ali; Ni wewe na Mashia wako. Wewe na wao mtakuja Siku ya Hukumu mkiwa mmefurahi mno na mmeridhia, ambapo maadui zako watakuja na huzuni kubwa na mikono iliyofungwa. Mir Seyyed Ali Hamadani Shafii, mmoja wa wanachuo wenu mashuhuri katika kitabu chake Mawaddatull-Qurba na mwanachuo anayejulikana vizuri sana kwa upinzani wake juu ya Shia, Ibn Hajar katika kitabu chake Sawaiq-e-Muhriqa, anasimulia kutoka Ummul-Muminina Umm Salma, mke wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kwamba Mtume

20

Mikesha ya Peshawar
alisema: Ewe Ali, wewe na Mashia wako mtaishi Peponi; wewe na Mashia wako mtaishi katika Pepo. Mwanachuo anayejulikana sana wa Khawarizm, Muwaffaq bin Ahmad, katika kitabu chake Manaqib Sura ya 19, anasimulia kutoka rejea zinazoaminika kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kumuambia Ali: Katika umma wangu wewe ni kama Masihi Isa Mwana wa Mariamu. Taarifa hii inaonyesha kwamba, kama vile wafuasi wa Mtume Isa (A.S.) walivyogawanyika katika makundi: Waumini wa kweli wajulikanao kama Hawariin, Mayahudi, na wapiga chuku (wenye kutia maneno chumvi) ambao wanamshirikisha yeye na Allah; katika njia hiyo hiyo Waislamu watakuja kugawanyika katika makundi matatu. Mojawapo litakuwa Shia, waumini wa kweli. Kundi lingine litakuwa la maadui wa Ali, na kundi la tatu litakuwa la wenye kukuza cheo chake.

SIFA ZA SHIA ZATHIBITISHWA KUTOKA KWENYE VITABU VYA SUNNI.


Kufikia hapa watu walitawanyika katika kuitikia mwito wa Swala ya Isha. Baada ya Swala Mulla Abdul-Hayy alirudi na Sherhe ya Suyuti, Mawaddatul-Qurba, Musnad ya Imam Ahmad bin Hanbal, na Manaqib ya Khawarizmi. Alisoma kutoka kwenye vitabu hivyo hadith alizokuwa amezinukuu Muombezi katika mijadala yake kwa njia ya uthibitisho. Kwa vile rejea zangu zilikuwa sawa sawa, muonekano wa nyuso za wale wote ambao wako katika kambi ya upinzani ulibadilika. Wakati huo huo walikuta hadith nyingine katika Mawaddatul-Qurba. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema, Ewe Ali, Siku ya Hukumu wewe na Mashia wako mtakuja mbele za Allah mkiwa mmefurahi mno na kuridhia, ambapo adui yako atakuja na huzuni kubwa na mikono ikiwa imefungwa. Muombezi: Hizi ni hoja zilizo wazi zinazoungwa mkono na Kitabu cha Allah, na hadith sahihi, na Taarikh. Kuungwa mkono kwa upande wangu kunakuja kutoka kwenye vitabu vya wanachuo wenu mashuhuri. Haya ni kwa nyongeza juu ya simulizi nyingi ambazo zimo katika vitabu na Sherhe za Shia. Kwa kutumia vitabu hivivilivyoko mbele yenu sasa, ninaweza kuendelea kuwasilisha hoja ziungazo mkono nukta iliyo kwenye mjadala mpaka kesho asubuhi, kwa rehema za Allah; lakini nafikiri kwamba hoja nilizowasilisha zipaswe kuwa zinatosha kuondoa mashaka yenu kuhusu Mashia. Watukufu mliohudhuria, sisi Mashia sio Mayahudi. Sisi ni wafuasi wa Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.). Mwanzilishi wa neno Shia kwa maana ya Wafuasi wa Ali hakuwa mlaaniwa huyu Abdullah bin Saba, bali ni Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe. Kamwe hatumfuati mtu binafsi bila rejea zenye hoja za kumuunga mkono. Mmesema kwamba ilikuwa ni baada ya Uthman ndio neno Shia lilipoanza kutumika kuashiria wafuasi wa Ali. Kwa kweli, hata

21

Mikesha ya Peshawar
wakati wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) Masahaba kadhaa maarufu wenye kutajika walikuwa wakiitwa Mashia. Hafidh Abu Hatim Razi katika kitabu chake Az-Zainat ambacho amekiandika kwa ajili ya kufafanua maana ya maneno fulani na Semi zinazotumika miongoni mwa Wanachuo, anasema kwamba neno la kwanza jipya ambalo lilikuja kukubaliwa na wote katika Uislamu wakati wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) lilikuwa ni Shia. Neno hili lilitumika kwa masahaba maarufu wanne: Abu Dharr Ghifar, Salman Farsi, Mikdadi bin Aswad Kindi, na Ammar Yasir. Hadith nyingi zaidi zilinukuliwa katika kuunga mkono nukta hii hii. Sasa ni juu yenu kufikiria vipi iliwezekana kwamba wakati wa Mtume (s.a.w.w.) Wanne kati ya masahaba wake wakubwa waliitwa Shia. Kama Mtume (s.a.w.w.) alifikiria kuwa neno hilo ni la uzushi (bidaa), kwanini hakuwakataza watu kulitumia? Ukweli ni kwamba watu walisikia kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) mwenyewe kwamba wafuasi (Mashia) wa Ali walikuwa ni wakazi wa Peponi. Walikuwa na fahari nalo na kwa uwazi wakajiita wenyewe Mashia.

CHEO CHA SALMAN, ABU DHARR, MIKDADI NA AMMAR


Umesimulia Hadith kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) isemayo: Hakika masahaba wangu ni kama nyota; yeyote katika wao mtakayemfuata, mtakuwa mmeongozwa sawasawa. Abul-Fida anaandika katika kitabu chake cha Tarikh kwamba watu hawa wanne, ambao walikuwa masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) walijitenga, pamoja na Ali kula kiapo cha utii kwa Abu Bakar, siku ile ya Saqifa. Kwa nini hamchukulii kukataa kwao kula kiapo kuwa kunafaa kuigwa? Maulamaa wenu wenyewe wameandika kwamba walipendwa na Allah na Mtume Wake. Sisi tunawafuata kama walivyomfuata Ali. Kwa hiyo kutokana na hadith yenu wenyewe, sisi tuko katika njia ya Mwongozo. Kwa ruksa yenu, na kutilia maanani uchache wa muda, ninawasilisha kwenu simulizi chache katika kuunga mkono hoja yangu kwamba watu hawa wanne walipendwa na Allah na Mtume (s.a.w.w.). Abu Nuaim Isfahami katika Hilyatul-Auliya, Juz. 1, uk. 172 na Ibn Hajar Makki katika hadith ya tano ya hadith arobaini zilizosimuliwa katika SawaiqulMuhriqa kwa kumtukuza Ali, iliyosimuliwa kutoka kwa Tirmidhi, na Hakim kutoka kwa Buraida, kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)) alisema: Hakika, Allah ameniamuru mimi kuwapenda watu wanne na amenijulisha kwamba Yeye mwenyewe anawapenda. Wakati watu walipomuuliza ni kina nani watu hao wanne, alisema: AIi ibn Abu Talib, Abu Dharr, Mikdadi na Salman. Tena, Ibn Hajar katika Hadithi ya 39 amesimulia kutoka kwa Tirmidhi na Hakim kutoka kwa Anas bin Malik kwamba Mtume amesema: Pepo

22

Mikesha ya Peshawar
inashauku juu ya watu watatu, Ali, Ammar, na Salman. Je, vitendo vya Sahaba hawa Mashuhuri wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) sio vya mfano wa kuigwa na Waislamu wengine? Je, sio aibu kwamba kwa maoni yenu Sahaba wamewekewa mpaka kwa wale tu waliocheza mchezo wa Saqifa, au ambao wameukubali mpango wake bila kupinga, ambapo wengine ambao wamepinga hila za Saqifa wanaonekana kama wasiokuwa waaminifu? Na ikiwa ni hivyo, basi hadith uliyoinukuu ingekuwa na maneno haya: Hakika wachache kati ya Sahaba wangu ni kama nyota .

SABABU ZA WA-IRANI KUUPOKEA USHIA.


Umekuwa sio mwema katika kusema kwamba, Ushia ni Dini ya kisiasa, na kwamba Mazoroasta wa Iran wameukubali kwa ajili ya kujiokoa kutoka umiliki wa Waarabu, umesema hivyo katika upofu wa kufuata watangulizi wako. Nimekwishathibitisha kwamba ni dini ya Uislamu, dini ambayo Mtume (s.a.w.w.) ameiweka amana mikononi mwa wafuasi wake. Kwa kweli, wale ambao bila kibali chochote kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.), wakaweka msingi wa Saqifa, walikuwa ndio wenyewe wanasiasa na sio wafuasi wa familia Tukufu ya Mtume (s.a.w.w.). Ni tabia ya Wa-Iran kwamba wao hutazama mambo kwa kuyachunguza. Wakati watakaposadikishwa na ukweli wake, wanayakubali, kama ambavyo waliukubali Uislamu wakati Iran iliposhindwa na Waarabu. Hawakulazimishwa kufanya hivyo. Waliuacha Uzoroasti na kwa uaminifu kabisa wakaushika Uislamu. Halikadhalika, wakati waliporidhishwa na mantiq na huduma za Ali zenye thamani isiokadirika, wakaukubali Ushia. Kinyume na maelezo ya waandishi wenu wengi,Wairani hawakumkubali Ali wakati wa Ukhalifa wa Harun-r-Rashid au Maamunur-Rashid. Walimkubali Ali wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Salman Farsi alikuwa mmoja wa wafuasi waaminifu kabisa wa Ali. Alifikia kiwango cha juu cha Imani. Maulamaa wa Madhehebu zote kwa makubaliano ya pamoja wameandika kwamba Mtume amesema: Salman anatokana na Ahlul Bait wetu (yaani ni mmoja wa watu wa Nyumba yangu). Kwa sababu hii aliitwa Salman Muhammad na yeye inakubalika kabisa kuwa ni mfuasi thabiti mwenye kumuunga Ali, na mpinzani mkali wa Saqifa. Kama, kutegemeana na vitabu vyenu wenyewe, sisi tukimfuata yeye, basi tuko katika njia iliyonyooka. Alizisikia aya za Qurani na maneno ya Mtume (s.a.w.w.) kuhusu Ali na kiwazi kabisa akaelewa kwamba utii kwa Ali ulikuwa ni utii kwa Mtume (s.a.w.w.) na kwa Allah (Swt). Alimsikia mara kwa mara Mtume akisema: Mwenye kumtii Ali ananitii mimi; na mwenye kunitii mimi anamtii Allah (Swt); ambaye ana uadui kwa Ali ni adui kwangu; na ambaye ana uadui kwangu ni adui kwa Allah (Swt). Kila Mu-Iran, hata hivyo, ambaye alikwenda Madina na kusilimu, iwe wakati wa Mtume au baadae, alizitii amri za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kwa sababu hii Khalifa wa pili akashindwa kuvumilia na akaweka vikwazo vingi juu ya Wairan. Shida hizi na taabu zilizaa uadui ndani ya nyoyo

23

Mikesha ya Peshawar
zao. Walihoji ni kwanini Khalifa awanyime haki za Uislamu kinyume na amri zilizowekwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

SHUKURANI ZA WA-IRAN JUU YA HURUMA ZA ALI.


Mbali na hali hizi, Wa-Irani walikuwa na shukurani sana kwa Ali kwa huruma zake kuhusiana na matendo waliyofanyiwa mabinti wa kifalme waliotekwa na Waarabu. Wakati wafungwa wa Madain (Taisfun) walipoletwa mjini Madina, Khalifa wa pili aliamuru kwamba wafungwa wote wa kike wafanywe kuwa watumwa wa Waislamu. Ali alilikataza hili na akasema kwamba mabinti wote wa kifalme ni wafungwa wa kipekee na wanapaswa wapewe heshima. Wawili kati ya wale wafungwa walikuwa ni mabinti wa mfalme Yazdigerd wa Iran na hawakuweza kufanywa watumwa. Khalifa akauliza ni nini kifanywe. Ali akasema kwamba kila mmoja yapasa aruhusiwe kuchagua mume miongoni mwa Waislamu. Kwa ajili hiyo, Shahzanan alimchagua Muhammad ibn Abu Bakar (ambaye alilelewa na Ali), ambapo yule binti mfalme mwingine, Shahbanu alimchagua Imam Husain, mjukuu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Wote walikwenda kwenye nyumba za watu hawa baada kufungishwa ndoa kisheria. Shahzanan alizaa mtoto wa kiume, Qasim Faqih, baba wa Ummi Farwa, ambaye alikuwa mama wa Imam wetu wa Sita, Jaafar asSadiq. Imam Zainul-Abidin, Imam wetu wa nne alizaliwa na Shahbanu. Hivyo mwanzo wa Ushia haukuwa na uhusiano wowote na wakati wa Harun na Maamun au na Utawala wa Ufalme wa Safavid katika Iran, kama ulivyosema mapema. Ulitangazwa wazi karne saba kabla ya Ufalme wa Safavid (yaani karne ya 4 A.H) wakati wa-Dailami (wa-Buwayyid) walipokuwa watawala. Katika mwaka wa 694 A.H. Falme ya Iran ilikuwa ikitawaliwa na Ghazan Khan Mughal (ambaye jina lake la Kiislamu lilikuwa Mahmud). Tokea wakati huo, Imani juu ya Ahlul Bait wa Mtume (s.aw.w.) ilidhihirisha kama jambo la kawaida, Ushia ulikua kwa uimara kabisa. Baada ya kifo cha Ghazan Khan Muqhal mnamo mwaka wa 707 A.H., ndugu yake, Muhammad Shah Khuda Bandeh akawa mtawala wa Iran. Aliandaa mjadala wa kidini (Mdahalo) kati ya Alama Hilli, Mwanachuo msomi wa Kishia, na Khwaja Nidhamud-Din Abdull-Maliki Maraghei, Kadhi Mkuu wa (Madhehebu) Shafii na Mwanachuo mkubwa wa Kisunni wa wakati huo.

24

Mikesha ya Peshawar

MIDAHALO KATI YA ALLAMA HILLI NA KADHI MKUU KUHUSU UIMAMU.


Nukta ya mdahalo huu ilikuwa ni Uimamu. Allama Hilli alitoa hoja zenye nguvu sana kuthibitisha kwamba Ali alikuwa ndiye mrithi alitemfuatia mara moja Mtume (s.a.w.w.) bila mwanya, na kwa kuridhisha kabisa akabainisha uwongo wa madai ya ule upande mwingine, kiasi kwamba wale wote waliohudhuria walitosheka kabisa na jinsi ya ukweli wa Allama. Khwaja Nidhamud-Din alikubali kwamba hoja za Allama haziwezi kukanushwa. Lakini akasema kwamba, kwa vile alikuwa akifuata njia za wakubwa wake waliomtangulia, haikuwa vizuri kuiacha. Aliona kwamba ilikuwa ni muhimu kudumisha mshikamano miongoni mwa Waislamu.

MFALME WA IRANI ALIIKUBALI IMAN YA KISHIA.


Mfalme alisikiliza hoja hizo kwa usikivu makini, mwenyewe akaukubali msimamo wa Shia, na akatangaza uhalali wa Ushia katika Iran. Hatimaye alitangaza kwa nagavana wa mikoa kwamba Khutuba za kila juma (zinazotolewa misikitini) zinapaswa zitangaze haki ya Ali kama mrithi wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Vile vile aliamuru kwamba Kalimah iandikwe kwenye dinari (Sarafu za dhahabu) katika njia hii:La ilaha illa llah Muhammad Rasulullah, Aliyan Waliyyullah, maana yake, Hakuna Mungu ila Allah; Muhammad ni Mtume wa Allah na Ali ni Walii wa Allah. (makamu au mlezi wa watu aliyeteuliwa ki-ungu). Katika njia hii mizizi ya Ushia ilisimama kwa umadhubuti kabisa. Karne saba baadae, wakati wafalme wa Ki-Safavid walipoingia madarakani, utando wa ujinga na ushabiki usio na maana katika dini viliendelea kuondolewa, Ushia ukashamiri kila mahali katika nchi ya Iran. Ndio, wako Mazoroasti katika Iran na wale wanaotia chimvi cheo cha Ali na kumfikiria yeye kuwa ni Mungu. Lakini haipasi kuwahusisha na watu wa kawaida wa Iran, ambao wana imani katika Allah na Mtume Muhammad kama Mtume wa mwisho. Hawa wanamfuata Ali na watoto wake kumi na moja kama ilivyoamrishwa na Mtume (s.a.w.w.). Hafidh: Ni kitu cha kushangaza kwamba ingawa kiasili umetokea Hijaz (Arabia) na umeishi Iran kwa muda mfupi, bado unawaunga mkono Wairani, na kuwaita wafuasi wa Ali, ambaye yeye mwenyewe alikuwa mtiifu kwa Allah. Lakini Mashia wa Iran wanamchukulia Ali kama ni Mungu.

25

Mikesha ya Peshawar
Hapa kuna baadhi ya beti kutoka kwa washairi wa Kiiran wakiashiria hoja hii, ambapo Ali mwenyewe alilaani imani kama hizi. Mwisho wa beti hizi unaonyesha Ali akisema: Nani anasaidia wakati wa matatizo! Ni mimi ambaye ni Mungu! Ni mimi. Ubeti wa mshairi mwengine unasema: Kulingana na iman ya wale ambao wana akili na wanamtambua Mungu, Mungu ni Ali na Ali ni Mungu. Muombezi: Nashangaa kwanini, bila kufanya uchunguzi, uweze kuwatuhumu Wairani wote kuwa wanamchukulia Ali kama Mungu. Wanachuo wenu wenyewe wamefanya madai ya kishabiki kama haya. Wamesema kwamba Mashia wanamwabudu Ali na kwa ajili hiyo wao ni Makafiri. Kwa hiyo kuwaua wao ni wajib. Matokeo yake Waislamu wa Uzbekistan na Turkistan kwa ukatili mkubwa wakamwaga damu za Waislamu wa Iran. Watu wa kawaida miongoni mwa Masunni mara kwa mara wanapotoshwa na baadhi ya Ulamaa wenu, na watu wenu wanawachukulia Wairani kuwa ni Makafiri. Katika wakati uliopita, watu wenu Wa-Turkomania wameshambulia msafara wa Wairani karibu na Khorasan, wakawanyanganya na kuwaua watu, na kusema kwamba, yeyote atakayeua marafidh saba (yaani Shia) atakuwa na uhakika wa kwenda peponi. Yakupasa uweke akilini kwamba lawama za kuhusika na mauaji haya zinakuwa moja kwa moja juu ya viongozi wenu, ambao huwaambia Masunni wasio na elimu kwamba Mashia wanamuabudu Ali.

UISLAMU UNAKATAZA KUJIGAMBA KUHUSU NASABA.


Nikirejea kwenye nukta yako ya kwanza kwamba, kwa kuwa mwanzoni nilihusiana na Arabia, Makka ma Madina, kwanini niwaunge mkono Wairani. Nakuambia kwamba mimi sina tabia ya ushabiki wa kitaifa. Mtume wetu (s.a.w.w.) amesema: Waarabu wasijigambe kwamba wao ni bora kwa wasio Waarabu na kinyume chake; na weupe wasijigambe kwa ubora kwa weusi na kinyume chake. Ubora uko tu katika elimu na uchaji. Katika Qurani Tukufu Allah (swt) anasema:

Enyi watu! Hakika tumekuumbeni ninyi mume na mke; na tumekufanyeni mataifa na makabila ili kwamba mpate kujuana; hakika aliye mbora sana miongoni mwenu mbele ya Allah ni yule amchae Allah zaidi (49:13).

26

Mikesha ya Peshawar
Vile vile katika Sura hiyo hiyo ndani ya Qurani Anasema:

Kwa hakika Waumini wote ni ndugu, basi patanisheni baina ya ndugu zenu na mcheni Allah ili mrehemiwe. (49:10). Kwa hiyo, watu wote, Waasia, Waafrika, Wazungu, Waamerika weupe, weusi, wekundu au manjano, makabila yote ambayo ni Waislamu ni ndugu, na hakuna hata mmoja anayeweza kudai ubora juu ya mwingine. Kiongozi mkubwa wa Waislamu, Mwisho wa Mitume, alitenda juu ya msingi huu. Alionyesha mapenzi yake makhususi kwa Salman Farsi wa Iran, Suhaib wa Asia ndogo, na Bilal wa Abysinia (Uhabeshi Ethiopia ya sasa). Na kwa upande mwingine alimpuuza Abu Lahab (ambaye jina lake lina maana ya Baba wa Miali ya Moto), ami yake mwenyewe ambaye amelaaniwa katika Sura ya Qurani Tukufu ambayo inasema:

Imeangamia mikono miwili ya Abu Lahab! Naye amekwisha angamia (111:1).

UISLAMU VILE VILE UNAKATAZA UBAGUZI (WA AINA ZOTE).


Ulimwengu umeshuhudia matatizo ya taratibu mbaya mno katika nchi za Maghribi ambayo yalikuwa ni matokeo ya ubaguzi wa rangi. Katika nchi hizo weusi hawaruhusiwi kwenye mahoteli, migahawa, makanisa, na sehemu nyingine za mikusanyiko iliyokusudiwa kwa weupe tu. Uislamu ulipiga marufuku taratibu hizo za kikatili miaka 1300 iliyopita na kutangaza kwamba Waislamu, bila kujali kabila, rangi, au utaifa wote ni ndugu. Hivyo Waarabu wakienda kombo, nitawalaumu, na nitakuwa rafiki wa Mashia wa Iran. Pili, umewahusisha Mashabiki (wakereketwa) wa Kiiran (Maghullat) na Mashia ambao ni Madhubuti, wenye kuabudu Mungu Mmoja (yaani Allah) na kumfuata Ali kutokana na Maamrisho ya Mtume (s.a.w.w.) Tunamchukulia Ali kama mja mcha Mungu wa Allah na aliyechaguliwa na Allah kuwa mrithi wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

27

Mikesha ya Peshawar

LAWAMA KWA MASHABIKI WASHUPAVU (MAGHULLAT).


Aidha, tunawapuuza wale ambao iman zao ni kinyume na sisi, kama Sabaiyya, Khitabiyya, Gharabiyya, Allawiyya, Mukhammasa, Bazighiyya, Nussairiyya, ambao wametawanyika nchini Irani kote, Mosul, na Syria. Sisi Mashia tuko tofauti nao na tunawaona wao kuwa ni Makafir. Katika vitabu vyote vilivyoandikwa na Maulamaa wa Kishia na Wanachuo wa Shariah, Maghulamu wamechanganywa pamoja miongoni mwa Makafir, kwa vile imani yao ni kinyume na misingi ya Ushia. Kwa mfano, wanahoji kwamba, kwa vile kuingia kwa roho katika umbo la mwili inawezekana (kama Jibril alivyoweza kujitokeza mbele ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika umbo la Dahiyya-e-Kalbi), ilikuwa ni Mapenzi ya Allah kwamba Nafsi yake tukufu ionekane katika umbo la mwanadamu, katika mwili wa Ali. Kwa sababu hii wanakiona cheo cha Ali kuwa ni kikubwa kuliko cha Mtume. Jambo kama hilo lilijitokeza wakati wa Ali mwenyewe. Baadhi ya watu kutoka India na Sudan walikuja kwake na kutamka kwamba yeye alikuwa Mungu. Mara kwa mara Ali aliwakataza kushikilia itiqadi hii, lakini hakuna athari iliyotokea (hawakuacha). Hatimaye, kama ilivyoandikwa katika vitabu vingi vya Tarekh, Ali aliamrisha wauwawe ndani ya visima vya moshi. Maelezo ya habari hii yameandikwa katika Baharul-Anwar, Juz. 7, na mwanachuoni mkubwa, Agha Muhammad Baqir Majlis. Amirl-Muminiina na Maimam wengine waliwalaumu vikali sana watu kama hawa. Ali alisema: Ee Allah ninakibeza kikundi cha Ghulat, kama vile Isa alivyowabeza Wakristo. Ikiwezekana uwatelekeze hao daima. Katika wakati mwengine alisema: Kuna makundi mawili ambayo yatapatwa na vifo vya kufedhehesha, na mimi siwajibiki nao (kwa vile ninavidharau vitendo vyao): Hao ni wale wanaozidisha mipaka halali ya mapenzi kwangu, na hao ni Ghullat, na wale ambao bila sababu yoyote ile, wana uadui juu yangu. Nawachukia wale ambao wanatukuza cheo changu kupita mipaka yake halisi. Vilevile alisema: Kuna makundi mawili yaliyojihusisha na mimi yatapata shida ya kifo cha aibu: Moja ni lile lililo na watu ambao wanasema ni marafiki na kunitukuza kupita mipaka ya halali; jingine lina maadui ambao wanatweza hadhi yangu. Mashia wanawalaumu wale ambao wanamtukuza Ali na Ahlul Bait wake kupita mipaka iliyoamriwa na Allah na Mtume (s.a.w.w.). Maulamaa wetu kwa pamoja wamewachukulia wote hao kwamba ni Makafir. Hairuhusiwi kuhudhuria mazishi yao au koleana nao. Vilevile wananyimwa kurithi mali ya Waislamu; sadaka na kodi za kidini haziwezi kupewa wao. Qurani Tukufu inawalaumu katika maneno haya: Sema: Enyi watu wa Kitabu msipite kiasi katika dini yenu bila ya haki. Walamsifuate matamanio ya watu waliok-

28

Mikesha ya Peshawar
wisha potea toka zamani, na wakapoteza wengi, na wenyewe wakapotea njia iliyosawa. (al-Maidah; 5:77). Allama Majlisi katika Kitabu chake Baharul-Anwar Juz. 3 ambacho ni ensaklopidia (kitabu cha maarifa yote) ya itiqad ya Shia, ameandika hadith nyingi kuwalaumu Ghullat. Imam Jafar Sadiq (a.s.) ananukuliwa akisema, Sisi ni waja wa Allah, ambaye ametuumba na akatufanya sisi kuwa bora kwa viumbe wake wengine. Hakika sisi tutakufa na tutasimama mbele ya Allah kwa ajili ya hesabu. Yule ambaye ni rafiki ya Ghullat ni adui yetu; na yule ambaye ni adui yao huyo ni rafiki yetu. Maghullat ni makafir na Washirikina; laana naiwe juu yao. Kiongozi mkubwa wa dini wa Mashia vilevile amemnukuu Imam huyu huyu akisema: Laana ya Allah iwe juu ya wale ambao wanadai Utukufu na Umungu kwa Ali. Kwa jina la Allah, Ali alikuwa ni mja mtiifu wa Allah. Laana iwe juu ya wale waliotukashifu sisi; baadhi ya watu wanasema mambo kuhusu sisi ambavyo sisi wenyewe hatuyasemi. Tunasema wazi kwamba hatuna uhusiano nao. Sheikh Saduq (Abu Jafar Muhammad bin Ali) Faqih mwenye kuheshimiwa sana (Mwanachuo Shariah) wa Mashia, anamnukuu Zarara bin Ayun, mwandishi wakuaminika wa Kishia, ambaye alikuwa Hafidh na Sahaba wa Imam Muhammad Baqir na Imam Jafar Sadiq, akisema: Nilimueleza Imam Jafar Sadiq kwamba mmoja kati ya watu anayejulikana kwake, huamini katika Tufiidh (uwakilishi wa mamlaka ya Mungu). Imam akasema: Ina maanishwa nini kwa Tufwidh?, Nikajibu. Yule mtu anasema kwamba, Allah alimuumba Muhammad na Ali na kisha akakabidhi Mamlaka yake kwao juu ya mambo ya watu. Hivyo wao ndio waumbaji, watoaji wa chakula, wao wahuishaji na wao ndio wenye kufisha. Mtukufu Imam akasema: Adui huyo wa Allah, anaongopa. Wakati utakaporudi kwake, msomee Aya hii kutoka katika Qurani Tukufu au wamemfanyia Allah washirika ambao wameumba kama alivyoumba Yeye, kwa hiyo alivyoviumba vikawababaisha (akili)? Sema Allah ndiye Muumbaji wa kila kitu na ni mmoja tu, Mwenye Enzi Kuu . (13:16).

MASHIA WAKO TOFAUTI NA GHULLAT.


Sisi Shia ni tofautli na Ghullat. Waache wadai kwamba wao ni Mashia, Mwenyezi Mungu, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Ali, na kizazi chao wanawachukia. Ali alimuweka mkubwa na Ghullat jela kwa muda wa siku tatu, na akamuamuru atubie kwa uovu wake. Alipokataa Ali alimfanya achomwe mpaka akafa. Kama huwezi kutoa angalau kitabu kimoja ambacho ndani yake Ghullat wametukuzwa, basi angalau uwalaumu Maulamaa wasio wavumilivu ambao wanawapotosha Masunni kuhusu Mashia.

29

Mikesha ya Peshawar

UFAFANUZI KUHUSU HESHIMA KWA MAIMAM.


Hafidh: Ushauri wako wa Kindugu unafaa kufikiriwa. Lakini tafadhali, je unaweza kufafanua nukta nyingine zaidi? Umesema muda wote kwamba hamuwatukuzi Maimam wenu kupita kiasi. Mnawaona Ghullat kama watu duni (wasiostahili heshima) na wanaofaa kwenda jahannamu, lakini unatumia maneno yasiyostahili kwa mintarafu ya Maimam wenu. Umesema Rehema za Allah ziwe juu yao, ingawa unajua kwamba, kwa mujibu wa Qurani, neno hili limetengwa kwa ajili ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) tu. Qurani inasema:

Hakika Allah na Malaika wake wanamtakia Rehema Mtume. Enyi ambao mmeamini mtakieni rehema juu yake na Msalimuni kwa (uzuri) wa Salamu. (33:56). Mwendo wako huo unakiuka kiwazi kabisa hukumu ya Qurani. Neno lako hilo ni Uzushi (bidaa). Muombezi: Aya hii haitukatazi kumuombea rehema mtu wengine yoyote. Tunaamrishwa kumuombea Rehema Mtume. Katika Aya nyingine ya Qurani Tukufu, Allah anasema. Amani na iwe juu ya watu wa Ya Sin (Ahl Ya Sin), yenye maana ya kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Ama kwa Mitume wengine wa Allah, kuombea rehema hakukutolewa pamoja na vizazi vyao popote katika Qurani. Kuombea rehema kumetolewa tu kwa Mitume wa Allah.

Amani na Salaam kwa Nuh miongoni mwa Mataifa. (37: 79).

Amani na Salaam kwa Ibrahim. (37:109)

Amani na Salaam kwa Musa na Haruni.(37:120).

30

Mikesha ya Peshawar

WATU WA YA SIN INAWAHUSU WATU WA MUHAMMAD


Wafasiri wote na Wanachuo wa madhehebu yenu wenyewe wanakiri kwamba Allah amemuita Mtume kwa jina Ya Sin. Hivyo basi Ahli (watu wa) Ya Sin maana yake ni watu wa Muhammad. Miongoni mwa wengine, Ibn Hajar Makki, Mwanachuo wa Kisunni mchungu sana kwa Shia, anasema katika Sawaiq Muhriqa chini ya aya zilizonukuliwa katika kuwasifu Ahlul Bait, kwamba kikundi cha Wafasiri wamemnukuu Ibn Abbas (Mfasiri, na mkubwa wa Waumini) akisema kwamba Ahl Yasin maana yake ni Ahl Muhammad. Kwa hiyo, Salaam, maamkuzi ya amani kwa Ahli Ya Sin yana maana Salaam kwa Ahli Muhammad. Imam Fakhrud-Bin Razi anaandika: Ahli Bait wa Mtume wako sawa naye katika mambo matano: 1) Salaam: Salaam kwa Mtume na Salaam kwa Ahli Ya Sin (Ahli Muhammad) ni kitu kimoja. 2) Salawat (kutakia rehma) katika Swala kwa Mtume na Ahlul Bait wake, ambako ni lazima. 3) Tohara: Allah Anasema katika sura ya Ta Ha (20:1): (Ewe Mtume) Msafi na tohara: Ile aya ya tohara iliteremshwa katika kuwatukuza Ahlul-Bait (33:33). 4) Uharamu wa Sadaka: Sadaka haiwezi kupokelewa imma na Mtume au Ahlul-Bait wake. Mapenzi: 5) Mapenzi: Mapenzi kwa Mtume maana yake nimapenzi kwa Ahlul Bait wake. Allah Anasema:

Sema: kama mnampenda Allah, basi nifuateni mimi, Allah atakupendeni ninyi(3:31) Na kuhusu Ahlul Bait Allah Anasema:

Sema: Sikuombeni malipo yoyote kwa haya bali Mapenzi kwa Ndugu wangu wa karibu (42:23).

31

Mikesha ya Peshawar

SALAWAT JUU YA MUHAMMAD NA AALI - MUHAMMAD NI SUNNA (ILIYOKOKOTEZWA), NA KATIKA SWALA ZA FARADHI NI WAJIBU.
Wengi wa wasimuliaji wa Hadith hususan Bukhari katika Sahih yake Juz. 3, na Muslim katika Sahih yake Juz. 1 Sulayman Balkhi katika Kitabu chake Yanabiul-Mawadda, na hata Ibn Hajar katika Kitabu chake Sawaiqi wanamnukuu Kab bin Ajza akisema: Wakati Aya: Hakika, Allah na Malaika wake wanamtakia rehema (wanamswalia) Mtume (33:56) ilipoteremshwa, tulimuuliza Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), namna gani tutaomba rehema kwa ajili yako, Ewe Mtume wa Allah,? Mtume akajibu, Ombeni juu ya rehema (Swalawat) zenu kwa namna hii. Ee Allah teremsha rehema kwa (Mtume) Muhammad na Aali Muhammad. Imam Fakhrud-Din Razi, katika Juzuu ya 6, ya Kitabu chake Tafsir-e-Kabir pia anasimulia hadithi kama hiyo. Ibn Hajar, akisherhesha juu ya hadith hiyo, anaonyesha kwamba, ni wazi kutoka katika Hadithi hii kwamba kuomba rehema kwa ajili ya Mtume ni sawa sawa na kuomba rehema kwa kizazi chake pia. Vilevile anamnukuu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema: Msiniswalie (Msiniombee) Swalawat kigutu. Alipoulizwa anamaanisha nini kwa Swalawat kigutu; akasema: Msiseme, Allahumma swali Ala Muhammad, (Ewe Allah Mrehemu Muhammad) bali semeni, Allahumma swali Ala Muhammad wa Ala Aali Muhammad. Dailami anaandikwa kwamba, Mtume alisema: Sala zetu hubakia zimezuiliwa mpaka tuombe Swalawat juu ya Mtume na Ahlul (watu) wake Imam Shafii anasema: Enyi Ahlul Bait (watu wa Nyumba ya Mtume) Allah Amefanya mapenzi kwenu kuwa ni wajib (lazima) kwetu sisi katika Qurani Tukufu. Kwa mintarafu ya ubora wenu, Cheo na Sifa zenu, inatosha kujua kwamba kama mtu hakuomba Swalawat (rehema) kwa ajili yenu, Sala yake haikubaliwi. Kama Swalawat kwa ajili ya Mtume na Dhuria (kizazi) wake inaachwa kwa makusudi, basi swala hiyo ya wajib inakataliwa. Na Mtukufu Mtume amesema: Sala ya wajib ni nguzo ya iman; kama Sala ikikubaliwa, matendo mengine yote (ya ibada) yanakubaliwa; kama imekataliwa, matendo yote mengine yanakataliwa. Kuomba Swalawat kwa ajili ya Ahlul-Bait ni Sunna iliyokokotezwa na ni namna ya ibada ambayo ilikuwa ikifanywa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe. Tunaona fahari kufanya kile ambacho Qurani Tukufu na Mtume (s.a.w.w.) wametuarimsha sisi kufanya.

32

Mikesha ya Peshawar

MKUTANO WA TATU JUMAMOSI USIKU 25 RAJAB 1345 A.H.


Hafidh: Kwa msingi wa mazungumzo yako ya usiku wa jana naona kwamba Mashia wamegawanyika katika idadi ya matapo. Tafadhali tujulishe tujue ni lipi katika hayo matapo unalikubali, ili mipaka ya majadiliano yetu iwe katika tapo hilo.

MASHIA HAWAKUGAWANYIKA KATIKA MATAPO


Muombezi: Mimi sikusema kwamba Mashia wamegawanyika katika matapo. Mashia wamejitoa kwa Allah (s.w.t.) na ni wafuasi wa Mtume na kizazi chake. Ni kweli baadhi ya matapo yamejichukulia jina la Shia ili kuwapotosha watu. Wamechukua manufaa ya jina la Shia, wakahubiri imani potofu na kueneza mkanganyiko. Watu wasio na ujuzi wamehusisha majina yao miongoni mwa Mashia. Ziko faraka nne za namna hiyo, mbili katika hizo zimebakia: Zaidiyya, Kaysaniyya, Qaddahiyya na Ghullat.

ZAIDIYYA
Zaidiyya wanamfuata Zaid bin Ali bin Husein. Wanamchukulia mtoto wa Imam ZainulAbidin, aitwaye Zaid kuwa ndiye Mrithi wake. Kwa wakati huu watu hawa wanapatikana kwa idadi kubwa nchini Yemen na majirani waizungukao. Wanaamini kwamba miongoni mwa Dhuria wa Ali na Fatima, Yeye ndiye Imam ambaye ni mwanachuo, mcha Mungu, na shujaa. Anachomoa upanga na kusimama dhidi ya maadui, Katika wakati wa Khalifa dhalimu wa Kibani Umayya, Hisham ibn Abdul-Malik, Hadhrat Zaid alisimama dhidi ya wale waliokuwa katika mamlaka na akauwawa Shahidi na kwa ajili hiyo akakubaliwa na Zaidiyya kama Imam. Ukweli ni kwamba Zaid alikuwa na cheo cha juu zaidi kuliko hicho ambacho Zaidiyya wanakidai kwa ajili yake. Alikuwa ni Sayyid mashuhuri wa ukoo wa Bani Hashim, na alikuwa akijulikana kwa ucha Mungu wake, hekima, Sala, na ushujaa. Alipitisha mikesha mingi bila usingizi akikesha kusali na alifunga mara kwa mara. Mtume (s.a.w.w.) alitabiri Shahada yake (kifo cha kishahidi), kama ilivyosimuliwa na Imam Husein: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akaweka mkono wake Mtakatifu kwenye mgongo wangu na akasema: Ewe Husein haitachukuwa muda mrefu atazaliwa mtu miongoni mwa Dhuria wako. Atakuwa anaitwa Zaid; atauwawa kama Shahid. Katika siku ya ufufuo, yeye na Masahaba

33

Mikesha ya Peshawar
zake wataingia Peponi, wakiweka miguu yao juu ya shingo za watu. Lakini Zaid mwenyewe hakudai kamwe kuwa yeye ni Imam. Ni masingizio yasiyo na msingi kwa watu kusema kwamba alidai. Kusema kweli, yeye alitambua Imam Muhammad Baqir kama Imam na alitoa utii wake kiukamilifu kwake. Ilikuwa ni baada tu ya kufariki kwa Imam Muhammad Baqir ndipo watu wajinga wakatwaa itiqad ya kwamba: Siye Imam yule akaaye nyumbani na kujificha machoni mwa watu; Imam ni yule ambaye ni Dhuria wa Hadharat Fatima, ambaye ni mwenye elimu, na ambaye anachomoa upanga na kusimama dhidi ya adui, na kulingania (kuwaita) watu upande wake. Zaidiyya wamegawanyika katika faraka Tano: Mughairiyya; Jarudiyya; Zakariyya; Khashbiyya; na Khaliqiyya.

WA-KAYSANIYYA NA IMANI YAO.


Tapo la pili ni la Kaysaniyya. Hawa ni Masahaba wa Kaysan, Mtumwa wa Ali bin Abu Talib, ambaye alimuacha huru. Watu hawa wanaamini kwamba baada ya Imam Hassan na Imam Hussain, Muhammad Hanafiyya mtoto mwingine (wa kiume) anayefuatia kwa umri, wa Amirl-Muminina, Ali (A.S.) alikuwa ndiye Imam. Lakini Muhammad Hanafiyya mwenyewe kamwe hajadai hivi. Alikuwa akiitwa Muaminifu wa Watiifu. Alikuwa akijulikana sana kwa elimu yake, Ucha Mungu, Utiifu, Ibada, na mtiifu kwenye maamrisho ya Mwenyezi Mungu. Baadhi ya watu wajinga hutoa ushahidi ambao waliuita upinzani wake kwa Imam Zainull-Abidin. Walidai kwamba Muhammad Hanafiyya alidai kuwa ni Imam. Ukweli ulikuwa vinginevyo. Hajadai kamwe kuwa ndiye Imam. Alitaka kuwaonyesha wafuasi wake wajinga cheo na hadhi ya Imam wa nne, Zaimull-Abidin. Matokeo yalikuwa kwamba, katika msikiti huohuo Mtukufu (wa Makka) wakati Hajarul-Aswad (jiwe jeusi) lilipothibitisha Uimamu wa Imam Zainull-Abidin, kama ilivyoandikwa kwa mpangilio katika vitabu vya Tarikh, Abu Khalid Kabuli, mkubwa wa wafuasi wa Muhammad Hanafiyya pamoja na wafuasi wengine, walimkubali Imam Zainul-Abidin kama Imam. Lakini kundi la watu walaghai walipotosha watu wa kawaida na wajinga kwa kusema kwamba Muhammad Hanafiyya alionyesha tu adabu, kwamba mbele za Bani Umayya ilikuwa inapendeza mno kwa Muhammad Hanafiyya kufanya kama alivyofanya. Baada ya kufariki Muhammad Hanafiyya, watu hawa walisema hakufa, na kwamba amejificha katika pango la Mlima Rizwi, na kwamba atakujatokea baadae kuujaza ulimwengu kwa haki na amani. Tapo hili lina matapo mengine madogodogo: Mukhtariyya; Karbiyya; Ishawiyya na Harabiyya. Lakini leo hakuna lililopo hata moja kati ya hayo.

34

Mikesha ya Peshawar

QADDAHIYYA NA IMANI YAO:


Tapo la tatu, Gaddahiyya, Wanajiita wenyewe Shia, lakini ni kundi la Makafiri. Kitapo hiki kilianzishwa Misri na Mamum Ibn Salim (au Disan) ajulikanae kama Qada na Issa Chahar Lakhtan (Yesu wa sehemu nne.) Walijitolea kutafsir Qurani Tukufu na kumbukumbu za Tarikh kwa kulingana na matakwa yao. Wanashikilia kwamba kuna kanuni mbili za dini: moja ya siri na nyingine ya wazi. Kanuni ya siri ilitolewa na Allah kumpa Mtume Muhammad. Mtume akaitao kwa Ali, naye akaitoa kwa dhuria wake na kwa Mashia halisi. Wanaamini kwamba, wale wanaoijua ile kanuni ya siri wamesamehewa katika Sala na kumuamudu Allah. Wamesimamisha dini yao katika nguzo saba. Wanaamini Mitume saba, na Maimamu saba, Imam wa saba akiwa yuko Ghaibuni. Wanangojea kujitokeza kwake. Wamegawanyika katika vijikundi viwili. 1) Nasiriyya ambao walikuwa Masahaba wa Nasiri Khusru Alawi, ambaye kwa mashairi yake, hotuba na vitabu alivuta watu wengi kwenye ukafiri. Walienea katika Tabaristan yote kwa idadi kubwa. 2) Sabahiyya (wanaojulikana katika nchi za Magharibi kama Assassins, yaani wauaji). Walikuwa ni Masahaba wa Hasan Sabba, mwenyeji wa Misri ambaye amekuja Iran, na ambaye alisababisha matukio ya misiba na huzuni ya Alamut, ambayo ilisababisha kuuwawa kwa idadi kubwa ya watu. Matapo haya yamehifadhiwa kwenye vitabu vya Tarikh.

GHULLAT NA IMANI ZAO:


Tapo jingine ni lile la Ghullat, ambalo ndio kundi potovu zaidi katika matapo yote. Wanajulikana kwa makosa kama ni Shia. Kwa kweli hawa wote ni makafiri. Wamegawanyika katika vijikundi Saba: Sabaiyya; Mansuriyya; Gharabiyya; Bazishiyya; Yaqubiyya; Ismailiyya na Azdariyya. Sio Shia Ithna Shariyya tu (wanoamini katika Maimam kumi na mbili), bali Waislamu wote ulimwenguni wanaikataa imani yao.

35

Mikesha ya Peshawar

SHIA IMAMIYYA ITHNASHARIYYA NA IMANI YAO.


Hili ndilo kundi Sahihi la Shia, ambalo linaamini Maimamu kumi na mbili baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Matapo haya mengine hayana kinachofanana na kundi letu; wamejichukulia tu jina la Shia.

IMANI KATIKA ALLAH NA MITUME


Kundi la Shia Imamiyya wanamini kuwepo kwa Allah Mwenye Enzi zote daima Milele. Ni mmoja, kwa maana kamilifu ya upweke wa uhalisi wa kuwako kwake. Yeye ni mmoja, hana mfano wake. Yeye ni muumba wa vitu vyote vilivyopo. Hakuna chenye kulingana au kuwa sawa na Yeye katika hali yoyote. Manabii watukufu na Mitume walitumwa kuwaeleza watu kuhusu Allah, namna ya kumuabudu Yeye, na jinsi ya kumjua Yeye. Mitume wote walihubiri na kuongoza watu kwa mujibu wa Mafundisho yaliyowekwa mbele na Mitume wakubwa watano: Nuh, Ibrahim, Musa, Issa na mwisho wa wote, Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.) ambaye dini yake itabakia mpaka Siku ya Kiyama.

IMANI KATIKA ADHABU, MALIPO, JAHANNAMU, PEPO, NA SIKU YA KIYAMA.


Mwenyezi Mungu Mtukufu ameweka malipo kwa ajili ya matendo yetu, ambayo yatatolewa kwetu katika Pepo au Jahanamu. Siku iliyowekwa kwa malipo ya matendo yetu inaitwa Siku ya Malipo. Wakati maisha ya Ulimwengu huu yatakapokoma, Allah (s.w.t.) atawafufua viumbe wa ulimwengu kuanzia wa mwanzo mpaka mwisho. Atawafanya wakusanyike katika Mashar; sehemu ya kukusanyikia Roho zote. Baada ya hesabu ya haki, kila mtu atapewa malipo au adhabu kwa kulingana na matendo yake. Mambo haya yametabiriwa katika vitabu vyote vya Mwenyezi Mungu: Taurat, Zaburi, Injili na Qurani Tukufu. Kwetu sisi Kitabu cha Mwongozo kilicho sahihi zaidi ni Qurani Tukufu ambayo imefika kwetu kutoka wakati wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) bila mabadiliko yoyote. Tunatenda juu ya amri zilizomo ndani ya Qurani Tukufu, na tunataraji malipo kutoka kwa Allah. Tunaamini katika amri zote zile za wajib ambazo zimo katika Qurani, kama Sala, Saumu, Zaka, Hija na Jihad.

36

Mikesha ya Peshawar

IMANI KATIKA KANUNI ZA IBADA:


Halikadhalika, tunaamini katika Kanuni za utendaji wa ibada, ikiwa ni pamoja na ibada za wajibu na za Suna na amri nyingine zote ambazo zimetufikia kupitia kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Tumejizatiti kushikamana nazo na kuzitekeleza kwa kadri ya uwezo wetu. Na tunajiepusha kutokana na madhambi yote, makubwa au madogo kama ulevi, kamari, uasherati, kulawiti, riba kuua, udhalimu ambavyo vimekatazwa katika Qurani Tukufu na Hadith.

IMANI KATIKA MAIMAMU:


Sisi Shia vilevile tunaamini kwamba, kama ambavyo kuna mjumbe kutoka kwa Allah ambaye anazifikisha kwetu sisi kanuni na maamrisho, na ambaye ameteuliwa na kujulishwa kwetu na Allah (s.w.t.), vilevile kuna mrithi, Khalifa, au Mlinzi wa dini, ambaye anachaguliwa na Allah na anatambulishwa kwetu kupitia kwa Mtume wa Allah. Kwa ajili hiyo Mitume wote wa Allah waliwajulisha warithi wao kwa Umma zao. Wa mwisho wa Mitume watukufu, ambaye alikuwa ndiye mkamilifu zaidi na aliye nyanyuliwa daraja ya juu zaidi kuliko Mitume wote wa Allah, aliacha kwa ajili ya wafuasi wake viongozi kusaidia watu kuepukana na matatizo. Kwa mujibu wa hadith zilizothubutu, aliwajulisha kwa watu warithi wake kumi na mbili. Wa kwanza wao akiwa ni Ali bin Abu Talib (A.s.). Imam wa mwisho, ni Mahdi (A.f) ambaye yupo ulimwenguni, lakini yuko kwenye Ghaib (amefichwa kwenye macho ya watu), atatokeza katika muda usiojulikana baadae, wakati atakapoujaza ulimwengu uliovurugika kwa haki na amani. Shia Imamiyya vilevile Wanaamini kwamba hawa Maimamu kumi na mbili wameteuliwa na Allah na wamejulishwa kwetu kupitia kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wa mwisho. Wa mwisho katika Maimam watukufu ametoweka katika macho ya watu (kwa amri ya Mwenyezi Mungu), kama vile Maimam wengine walivyotoweka katika wakati wa Mitume waliopita, kama ilivyoelezwa katika vitabu vingi vilivyoandikwa na Maulamaa wenu. Kiumbe huyu Mtakatifu amehifadhiwa na Allah (s.w.t.) ili kwamba siku moja aweze kuujaza ulimwengu na haki. Kwa ufupi, Shia wanaamini katika yale yote ambayo yamo katika Qurani Tukufu na katika hadith Sahihi. Ni mwenye kushukuru sana kwa Allah kwamba nimefuata imani hizi, sio kwa upofu tu wa kufuata wazazi wangu, bali kwa ukweli wenye mantiki na kuchunguza. Hafidh: Mheshimiwa Maulana, hakika nina wiwa na wewe kwa kuweza kueleza imani za Shia, lakini kuna Hadith na Dua katika vitabu vyenu ambazo zinakwenda kinyume na maelezo yako na kuonyesha upotofu wa Mashia. Muombezi: Tafadhali kuwa wazi zaidi.

37

Mikesha ya Peshawar

KANUSHO JUU YA HADITH YA MARIFA


Hafidh: Katika Tafsir-e-Safi, kilichoandikwa na mmoja wa Wanachuo wenu mwenye cheo cha juu, Faiz Kashi, mna hadith isemayo kwamba: Siku moja Imam Husain; Shahid wa Karbala, akihutubia Masahaba wake alisema: Enyi watu, Allah (s.w.t.) hakuumba waja Wake, bali kumjua Yeye. Wakati wakimjua Yeye, wanamuabudu Yeye, wakati wakimwabudu Yeye, wanakuwa kinyume na kuabudu kitu kingine chochote. Mmoja wa Masahaba akasema: Maisha ya Baba yangu na Mama yangu na yawe mhanga kwa ajili yako! Ewe Mtoto wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)! Nini hasa maana ya kumjua Allah? Mtukufu Imam akajibu, Kwa kila mtu kumjua Allah ina maana kumjua Imam wake wa Zama, ambaye lazima atiiwe. Muombezi: Kwanza, lazima tuchunguze nyororo ya wasimuliaji ili kuthibitisha kama ni Sahihi. Hata kama ni sawa kwa kutegemeana na wasimuliaji, bado Aya za Qurani Tukufu na Hadith halisi za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) haziwezi kueleweka vibaya kwa sababu ya madai ya mtu mmoja. Kwa nini usizichunguze hadith na simulizi za Maimam wetu Watukufu, na mijadala ya kidini kati ya viongozi wetu wa dini na makafiri, ambayo tayari imethibitisha Upweke wa Allah? Kwa nini huangalii vitabu vikuu na Sharhe hasa za Shia kama vile Tawhid-eMufazzal. Tawhid-e-Saduq, Biharul-Anwar (Kitabu cha Tawhid) cha Allama Majlisi na vitabu vingine vilivyoandikwa na Maulamaa wa Kishia ambavyo vimejaa hadith za mfululizo (juu ya Tawhid) kutoka kwa Maimam wetu watukufu? Kwa nini usiangalie katika An-Naktul-Itiqadiyya, cha Sheikh Mufid (Amefariki 413 A.H.) mmoja wa Maulamaa wa Kishia, na pia kitabu chake Awailul-Maqalat fil-Madhahib wal-Mukhtarra au Ihtajaj cha Mwanachuo wetu mashuhuri, Abu Mansur Ahmad bin Ali bin Abu Talib Tabrasi? Kama ungefanya hivyo, ungepata kujua jinsi gani Mtukufu Imam wetu Ridha (A.S.) alivyothibitisha Umoja wa Allah. Si haki kuchukua baadhi ya taarifa zenye mashaka kwa ajili ya kutaka tu kuwazulia uongo Mashia. Vitabu vyenu wenyewe vina mambo ya vichekesho na maoni yasioeleweka kiakili. Kwa kweli hadith za ajabu ajabu zimo katika vitabu vyenu Sahihi zaidi - Sahihi Sitta (yaani vile vitabu sita vya hadith vinavyokubalika kwenu ninyi). Hafidh: Kwa kweli, maneno yako ni ya kuchekesha sana maadam unaona makosa katika vitabu ambavyo umaarufu na usahihi wake si wa kutiliwa mashaka, hususan Sahihi Bukhar, na Sahih Muslim. Maulamaa wetu wanakubaliana kwamba hadith zote zilizomo humo ni za kweli. Kama mtu akivikataa vitabu hivi viwili, anaikataa Madhehebu halisi ya Sunni. Baada ya Qurani Tukufu, Sunni wanategemea juu ya usahihi wa vitabu hivi, viwili.

38

Mikesha ya Peshawar
Pengine bila shaka umeona maelezo ya Ibn Hajar Makki mwanzoni mwa kitabu chake Sawaiq al-Muhriqa, sura ya Matukio (Matukio ya ukhalifa wa Abu Bakar) kama ilivyoandikwa na Bukhar na Muslim katika Sahih zao mbili, ambavyo ndio vitabu sahihi zaidi na vya kutegemewa baada ya Qurani Tukufu kwa mujibu wa makubaliano ya pamoja ya wafuasi (yaani, Ummah). Anasema kwamba maadam ummah wote uko pamoja katika kuzikubali hadith za vitabu hivyo, chochote ummah wanachokubaliana kwa shauri moja hakiwezi kutiliwa mashaka. Juu ya msingi wa makubaliano haya, hadith zote zilizomo katika vitabu hivi zinakubalika bila kutiliwa mashaka. Kwa hiyo, hakuna mtu anayeweza kujasiri kudai kwamba vitabu hivi vina mambo ya ajabu na ya kuchekesha.

HADITH ZA AJABU KATIKA SAHIHAIN BUKHARI NA MUSLIM.


Muombezi: Kwanza, kwamba vitabu hivi vinakubaliwa na umma wote, kunapingwa kwa uwazi kabisa. Madai yako kuhusiana na rejea kutoka kwa Ibn Hajar, peke yake ni ya ajabu, kwa kuwa Waislamu milioni 100 hawaikubali nukta yake. Kwa hiyo, makubaliano ya pamoja ya umma katika suala hili ni kama makubaliano ya pamoja yaliyodaiwa na watu wenu katika suala al ukhalifa. Pili, ninayosema yametegemezwa kwenye sababu zenye msingi thabiti. Kama utavichunguza vitabu hivyo bila kuwa na mawazo ya chuki, utashangaa sana. Wengi wa maulamaa wenu wakubwa, kama vile Darqutni, Ibn Hazam, Allama Abul-Fazl Jafar bin Thalabi katika Kitabul-Imta fi Akhamus-Sama, Sheikh AbdulQadir bin Muhammad Qarshi katika Jawahirul-Mazaya fi Tabqatul-Hanafiyya, na wengineo, pamoja na maulamaa wote wa Kihanafia wamevilaumu vitabu hivi viwili (Sahihain) na wamekiri kwamba vina idadi kadhaa ya hadith dhaifu na zisizothibiti. Lengo la Bukhari na Muslim lilikuwa ni kukusanya hadith; sio kuhukumu usahihi wake. Baadhi ya Wanachuo wenu watafiti kama vile Kamalud-Din, Jafar bin Salih wamechukuwa taabu kubwa katika kuonyesha kasoro na makosa ya hadithi na wameweka misingi yenye nguvu katika kuunga mkono matokeo ya utafiti wao. Hafidh: Ningelilikaribisha suala la kama utazionyesha hoja hizo ili kwamba hadhara hii ipate kujua ukweli. Muombezi: Nitaonyesha mifano michache tu.

39

Mikesha ya Peshawar

REJEA ZINAZOONYESHA KUHUSU KUONEKANA KWA ALLAH


Kama mnataka kusoma Hadith za kupotosha kuhusu Allah kuchukua mwili wa kibinadamu (au kuingia katika mwili wa mwanadamu), ambazo zinatetea kwamba Yeye (Allah), kama kiumbe mwenye mwili, anaweza kuonekana katika ulimwengu huu, au ataonekana katika ulimwengu jao wa Akhera, (kama inavyoaminiwa na Tapo la Suni yaani Hanbaliyya na Ashariyya) mnaweza mkarejea kwenye vitabu vyenu wenyewe, hususan Sahih Bukhari, Juz. 1, uk. 100 katika Mlango wa Fadhla-s-Sujud Min Kitabul-Adhan, na katika Sahih Muslim Juz. 4, uk. 92 Babus-Sira Min Kitabur-Riqaq na vilevile tena kwenye hiyo Sahih Muslim Juz. 1 uk. 86 Sura ya Isbatul-Ruyatul-MuMinin Rabbahum Fil-Akhira; na Musnad ya Imam Hanbal Juz. 2, uk. 275. Mtapata maelezo ya kutosha ya namna hii katika vitabu hivyo. Kwa mfano, Abu Huraira anasema: Makelele na kishindo cha ukali wa moto vitakithiri, hautatulia mpaka Allah aweke mguu Wake humo. Kisha Jahannam itasema: Basi, basi! hiyo inanitosha; inanitosha. Vilevile Abu Huraira anasimulia kwamba kikundi cha watu walimuuliza Mtukufu Mtume (s.a.w.w.); Je, tutamuona Muumba wetu hiyo Siku ya Malipo? Akajibu: Bila shaka. Je, wakati wa mchana wakati anga inapokuwa haina mawingu, jua lina kuumizeni wakati mnapoliangalia? Wakasema, Hapana! Yeye akasema tena: Je, wakati wa usiku mnapoungalia mwezi mpevu wakati anga ni nyeupe, unakuumizeni? Wakasema, Hapana! Aliendelea: Hivyo wakati mtakapomuona Allah Siku ya malipo hamtadhurika, kama vile tu ambavyo hamdhuriki muangaliapo hivi (jua na mwezi). Wakati Siku ya Hukumu itakapofika, itatamkwa na Allah kwamba kila umma wamfuate Mungu wao. Hivyo kila mtu ambaye alikuwa akiabudu masanamu au kitu kingine kisichokuwa Allah, Aliye Mmoja, ataingizwa katika moto wa Jahannamu. Kadhalika kila mmoja wa watu wema na wabaya watalipwa katika moto isipokuwa wale waliomuabudu Allah, Mmoja Mkamilifu. Watalala katika moto wa Jahannamu. Katika muda huo Allah atatokeza katika umbo Makhususi mbele za watu ili kwamba wapate kumuona. Kisha Allah atawaambia kwamba Yeye ndiye Mola wao. Kisha Waumini watasema, Tunajikinga na uungu wako. Sisi ni miongoni mwa wale ambao walikuwa hawaabudu kitu chochote isipokua Allah Mwenye mamlaka ya juu. Allah atasema katika kuwajibu, Mnayo dalili yoyote kati yenu na Allah ambapo kwamba mnaweza kumuona Yeye na kumtambua? Watasema, ndio! Kisha Allah atawonyesha mguu wake uliowazi (bila kiatu). Hapo waumini watanyanyua vichwa vyao kuelekea juu na watamuona katika hali ileile kama waliyomuona nayo kwa mara ya kwanza. Kisha Allah atasema kwamba, Yeye ndiye Muumba wao. Wote kwa pamoja watakubali kwamba Yeye ndiye Mola wao.

40

Mikesha ya Peshawar
Sasa ni juu yenu ninyi kuamua iwapo maelezo namna hii ni sawa na ukafiri au hapana, kwamba Allah atajitokeza kiumbo mbele za watu na atafunua mguu Wake! Na nukta kubwa sana yenye kuunga mkono hoja yangu ni kwamba Muslim bin Hajjaj anaanza kuandika sura katika Sahih yake kuhusu uhakika wa kuonekana Allah (s.w.t.), na amenukuu simulizi za kubuni kutoka kwa Abu Huraira, Zaid bin Aslam; Suwaid bin Said, na wengine. Na baadhi ya maulamaa wakubwa wa madhehebu yenu wenyewe kama Dhahabi katika Mizanul-Itidal na Suyuti katika kitabu chake Kitabul-Lu-ualialMasnua fi hadithal-Muzua, na Sibt ibn Jauzi katika Al-Muzua; wamethibitisha juu ya hoja za Msingi kwamba simulizi (Hadith) hizi ni za kubuni.

QURANI TUKUFU INAKATAA DHANA YA KUONEKANA KWA ALLAH.


Hata kama kusingelikuwa na uthibitisho dhidi ya madai hayo hapo juu. Aya ya Qurani Tukufu inakataa waziwazi dhana ya kuonekana kwa Mwenyezi Mungu. Allah (s.w.t.) Anasema:

Macho hayamfikii, bali yeye anayafikia macho (6:103) Tena, wakati Nabii Musa alipolazimishwa na wana Israel kwenda sehemu yake ya Sala na amuombe Allah Ajidhihirishe kwake, Qurani Tukufu inaandika tukio hili kama ifuatavyo:

(Musa) akasema: Mola wangu nionyehse (nafsi Yako) ili nikuone, Akasema: Huwezi (Ukathubutu) kuniona (7:143). Seyyid Abdul-Hayy (Imam wa wa jamaat ya Ahli Sunna): Je! Hii sio kweli kwamba Ali Alisema: Siwezi kumuabudu Mungu ambaye simuoni? Wakati Ali anasema kitu cha namna hiyo, ina maana kwamba Allah anaweza kuonekana.

HOJA NA HADITH KUHUSU KUTOKUONEKANA KWA ALLAH


Muombezi: Rafiki Mheshimiwa, umeondoa sentensi moja nje ya fuo la maneno haya. Nitakusomea matini yote. Hadith hii imeandikwa na Sheikh mashuhuri, Muhammad Ibn Yaqub Kulain katika kitabu chake Usul al-Kafi, (juzuu juu ya tawhid), na hivyo hivyo

41

Mikesha ya Peshawar
Sheik Saduq katika kitabu chake juu ya Tawhid, Sura ya Ibtal Aqida Ruyatullah. Imam Jafar as-Sadiq ananukuliwa akisema, mwanachuo mmoja wa Kiyahudi alimuuliza AmirlMuminin, Ali (A.S.) iwapo amemuona Allah katika wakati wa Sala. Imam akajibu: Hawezi kuonekana kwa macho haya ya kiumbo. Ni moyo ndio unaomuona Yeye, kwa mwanga wa uhalisi wa kuamini na kusadiki. Kutokana na majibu ya Ali ni kwamba yeye anachomaanisha kwa kumuona Allah, sio kumuona kwa macho, bali kwa mwanga wa imani ya kweli. Kuna ushahidi mwingine mwingi uliotegemezwa juu ya hoja na mambo yaliyoandikwa ya kuthibitisha maoni yetu juu ya nukta hii. Zaidi ya hayo, mbali na wanachuo wa Kishia, maulana wenu wenyewe, kama Qadhi Baidhawi na Jarullah Zamakhshari, wamethibitisha katika Sharhe zao kwamba haiwezekani kwa Allah kuonekana. Yeyote ambaye anaamini juu ya kuonekana kwa Allah, katika ulimwengu huu au ulimwengu ujao, anaamini kwamba ni kiumbe mwenye mwili. Kuamini hivyo ni ukafiri.

REJEA ZAIDI YA HADITH ZA AJABU AJABU KATIKA VITABU VIWILI VYA HADITH
Mnafikiria vitabu vyenu sita vya Hadith, khususan vile vya Bukhari na Muslim, kama vitabu vya Ufunuo. Natamani kwamba mngeviangalia kwa busara na msivuke mipaka katika kuvisifu kwenu. Bukhari, katika Sura ya Kitab-e-Ghusl, na Muslim katika Sehemu ya 2 ya Sahih yake (Sura ya fadhil za Mtume Musa), na Imam Ahmad bin Hanbal katika Musnad yake, Sehemu ya 2 uk. 315, na maulamaa wenu wengine wamemnukuu Abu Huraira akisema: Miongoni mwa wana wa Israel ilikuwa ni desturi yao kuoga pamoja bila nguo, hivyo kwamba kila mmoja aliangalia utupu wa mwenziwe. Hawakufikiria kama kuna kizuizi katika hilo. Mtume Musa ndiye aliyekuwa akiingia kwenye maji peke yake, hivyo kwamba hakuna aliyeweza kuona sehemu zake za siri. Wana wa Israeli walizoea kusema kwamba Mtume Musa alikuwa na hitilafu katika sehemu zake za siri, hivyo alijiepusha kuoga nao. Siku moja Mtume Musa alikwenda mtoni kuoga. Alivua nguo zake, akaziweka juu ya jiwe na akaingia mtoni. Lile jiwe likakimbia na nguo zake. Musa akalikimbiza lile jiwe akiwa uchi, akipiga makelele: Nguo zangu! Ewe jiwe nguo zangu. Wana wa Israel wakamuona Musa akiwa uchi na wakasema: Kwa jina la Allah Musa hana hitilafu katika tupu zake. Kisha lile jiwe likasimama, na Musa akarudishiwa nguo zake. Kisha Musa akalipiga lile jiwe kwa nguvu sana kiasi kwamba lile jiwe likalia kwa sauti kubwa mara sita au mara saba kwa maumivu. Kweli mnaamini kitu kama hicho kinawezekana kwa Nabii Musa (A.S.), au kwamba jiwe, kitu kisicho na uhai, lingeweza kuchukua nguo zake? Kwa hakika itakuwa haiwezekani kwa Mtume kukimbia uchi mbele za watu.

42

Mikesha ya Peshawar
Nitasimulia Hadith nyingine iliyoandikwa katika Sahih ambayo ni ya kichekesho zaidi. Bukhari anamnukuu Abu Huraira katika Sahih yake (Juz. 1, uk. 158 na Juz. 2, uk. 153), na tena katika Sura ya Kifo cha Mtume Musa, na Muslim vilevile anamnukuu huyo huyo (Abu Huraira) katika Sahih yake Juz. 2, uk. 309 katika Sura ya Fadhila za Musa akisema: Malaika wa Mauti alikuja kwa Mtume Musa na akamtaka akubali mwito wa Mola wake. Aliposikia hivi, Musa alimchapa kofi kali la uso kiasi kwamba jicho lake moja lilingoka. Hivyo alirudi kwa Allah na akalalamika kwamba amemtuma kwa mtu ambaye hataki kufa, na ambaye amemngoa jicho lake moja. Allah akaponya jicho lake na akamuamuru arudi tena kwa Musa na amuambie kwamba, kama anataka maisha marefu, yapasa aweke mkono wake juu ya mgongo wa fahali wa ngombe. Ataishi miaka mingi kama idadi ya nywele zitakazofunikwa na mkono wake. Imam Ahmad bin Hanbal katika Musnad yake, Juz. 2 uk. 315, na Muhammad bin Jarir Tabari, katika kitabu chake chaTarikh, Juz. 1, chini ya kichwa cha habari, Kifo cha Mtume Musa, ametoa maelezo haya haya kutoka kwa Abu Hurira pamoja na nyongeza kwamba kufikia wakati wa Musa, Malaika wa mauti alikuwa akitoa roho (za watu) katika mwili kiwaziwazi. Lakini baada ya Musa kumchapa kofi la uso, alikuja bila kuonekana. Sasa ni juu yenu kuamua ni kichekesho gani hiki ambacho kimewekwa katika vitabu hivi viwili vya hadith, ambavyo mnaviita kuwa ni vya usahihi zaidi kuliko vitabu vyote baada ya Qurani Tukufu. Riwaya nilizoelezea hakika zinadhalilisha heshima za Mitume wa Allah. Ama kwa Abu Huraira, sizishangai simulizi zake. Maulamaa wenu wenyewe wanakiri kwamba, ili apate kujaza tumbo lake kwa vyakula vyenye ladha vilivyotolewa na Muawiya, alibuni hadithi za uongo. Kwa sababu ya uzushi wake, Khalifa Umar alimpiga viboko. Ni jambo la kushangaza kwamba watu wenye akili wanaamini ngano kama hizi za kuchekesha. Sasa ngoja turudi kwenye majadiliano yetu kuhusu hadith uliyonukuu. Ni dhahiri, mtu mkweli akiona hadith pekee (iliyosimuliwa na mtu mmoja) atailinganisha na hadith nyingine sahihi. Imma ataisahihisha au ataikataa moja kwa moja kuliko kuitumia kama msingi wa kuwashambulia ndugu zake wa madhehebu nyingine na kuwaita makafir. Kwa vile kitabu Tafsiri-e-Safi hatunacho hapa, hatuwezi kusema chochote kuhusu usahihi wa hadith hii. Hata kama ni kweli, yatupasa kutegemea juu ya kanuni kwamba, kama tunajua athari, tunaweza kujua sababu. Yaani, kama tunamjua Imam kama Imam, kwa hakika tunajua utambulisho wa Allah, katika njia ileile, ambayo kama mtu anamjua Waziri Mkuu, anamjua Mfalme. Ni kwa kuhusu kanuni hii kwamba Sura ya Tawhid na Aya nyingine za Qurani Tukufu zilishuka. Zaidi ya hayo, kuna Hadith nyingi kuhusu upweke wa Allah zilizosimuliwa na Imam Husain mwenyewe na Maimamu wengine. Kumjua Imam wetu ni namna kubwa ya Ibada ya Allah. Maana hiyo hiyo imetolewa katika Ziarat-e-Jamia, ambayo imefika kwetu kutoka kwa Mtukufu Imam. Tunaweza kuitafsiri pia kwa njia nyingine, kama wanachuo

43

Mikesha ya Peshawar
walivyofanya katika mambo kama haya. Mtekelezaji yoyote wa kitendo anaweza kueleweka kwa asili ya kitendo chake. Kwa vile Mtume na kizazi chake walifikia daraja ya juu kabisa katika uwezo wa kibinadamu, hakuna wengine wenye fadhila au ubora kama wao. Kwa kuwa hawa ndio njia dhahiri zaidi ya kumjua Allah, yeyote awajuaye hawa, anamjua Allah. Kama walivyosema wenyewe: Ni kwa kupitia kwetu sisi, kwamba Allah anaweza kutumikiwa. Tunaamini kwamba Ahlul Bait wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wametufundisha elimu kuhusu Allah na njia zinazostahili za kumuabudu Yeye. Wale ambao hawakuwafuata wamepotea njia.

HADITH YA THAQALAIN (VIZITO VIWILI).


Kusisitiza jambo hili hili, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema katika hadith inayokubaliwa na madhehebu zote. Enyi watu (wafuasi) wangu! Mimi ninakuachieni kwa ajili yenu vitu viwili vizito (vya rejea): Kitabu cha Allah na Ahlul Bait wangu. Mtakapokuwa mumeshikamana na viwili hivi, kamwe, kamwe hamuwezi kupotea baada yangu, kwani kwa hakika viwili hivi kamwe havitatengana mpaka vinifikiea kwenye chemchem ya Kauthar. Hafidh: Hatutegemei juu ya hadith hii, ambayo unajaribu kuirudia. Kuna uzushi mwingi katika vitabu vyenu na mifano ya ushirikina, kama vile kutafuta kutekelezewa haja zetu kutoka kwa Maimamu zaidi kuliko kutoka kwa Allah. Ushirikina ni nini? Ushirikina una maana ya kumgeukia mtu mwingine yeyote au kitu zaidi kuliko kwa Allah kwa ajili ya kutekelezewa haja zetu. Imeonekana kwamba Mashia kamwe hawamuombi Allah. Wanawaomba Maimam. Hili si chochote, bali ni ushirikina. Muombezi: Ninasikitika kwamba unapotosha ukweli. Labda ningeruhusiwa nikuelezeni ushirikina ni nini kwa mujibu wa maulamaa wakubwa wa Kiislamu na kwa mujibu wa aya za Qurani Tukufu.

USHIRIKINA NA AINA ZAKE:


Ushirikina ni wa aina mbili: Ushirikina wa wazi na ushirikina uliofichika. Ushirikina wa wazi una maana ya kumshirikisha mtu au kitu na Nafsi Kamili ya Allah au kumshirikisha na sifa Zake. Kumfanyia Allah washirika maana yake kushirikisha kitu na Upweke Wake na kuukiri ushirikishaji huu kwa ulimi, kama Sanamiyya (waabudu sanamu) au Mazorostania, ambao wanaamini katika kanuni mbili: Nuru na giza. Wakristo pia wanafanya hivyo. Wanaamini katika utatu na kuugawanya uungu katika sehemu tatu Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Wanaamini katika tabia tofauti za kila mmoja, na mpaka watatu hawa waungane, bila hivyo uungu wenyewe hautakuwa kamili. Qurani Tukufu inakataa imani hii, na Allah (s.w.t.) anaelezea upweke wake katika maneno haya:

44

Mikesha ya Peshawar

Kwa hakika wamekufuru wale waliosema: Hakika Allah ni Mmoja katika watatu; hali hakuna mungu ila Allah Mmoja. (al-Maida; 5: 73). Kushirikisha vitu na sifa za Uungu, maana yake ni kuamini kwamba sifa Zake, kama elimu Yake au nguvu ziko tofauti na, au ni nyongeza katika Nafsi Yake Kamilifu. Ashariyya wa Abul-Hasani Ali bin Ismail Ashari Basari, wanaelezewa na Maulamaa wenu wakubwa, kama Ali bin Ahmad katika kitabu chake Al-Kashf na Minhajul-Adilla fi Aqaidil-Mila, Uk. 57 kuwa wanaamini kwamba Sifa za Allah ni nyongeza katika Nafsi Yake kamilifu, na kwamba ni za milele. Hivyo yeyote mwenye kuamini kwa njia yeyote ile kwamba tabia au sifa yeyote ya Allah ni nyongeza katika Nafsi yake kamilifu, huyo ni mshirikina. Kila sifa Yake ni yenye asili kwake. Ushirikina katika matendo ya mtu, ina maana kumshirikisha mtu mwingine katika Dhati Yake Yenye kujitosheleza Daima dumu. Mayahudi wanaamini kwamba Allah aliumba viumbe na kisha akajiweka mbali na viumbe Wake. Katika kuwalaumu watu hawa, aya ifuatayuo iliteremshwa:

Na Mayahudi wanasema: Mkono wa Allah umefungwa! Mikono yao itafungwa (kwa pingu) na watalaaniwa kwa yale wanayoyasema. Bali, mikono yake yote iwazi; Hutoa apendavyo (5:64). Ghullat wanaunda kundi lingine la washirikina. Pia wao wanaitwa Mufawwiza. Wanaamini kwamba, Allah ameweka au kuaminisha Mamlaka ya mambo yote kwa Maimam watukufu. Kwa mujibu wao, Maimam ni waumbaji na pia hutupatia sisi riziki. Kwa uwazi, wale wanaomuona mtu kuwa mshirika katika Mamlaka ya Uungu ni mshirikina.

USHIRIKINA KATIKA SWALA:


Ushirikina katika Sala, ina maana ya mtu kugeuza mazingatio yake wakati wa swala kwa makusudi kuelekea kwa kiumbe aliyeumbwa badala ya kuelekea kwa Allah. Kama mtu akikusudia kuomba kwa kiumbe aliyeumbwa, huyo ni mshirikina. Qurani Tukufu inakataza haya katika maneno haya.

Anayetarajia kukutana na Mola Wake, naafanye vitendo vizuri, na asimshirikishe yeyote katika ibada ya Mola wake. (18:110).

45

Mikesha ya Peshawar
Aya hii inaonyesha kwamba sharti la msingi wa imani ni kwamba mtu lazima afanye lolote lile ambalo ni zuri na asije kumshirikisha yeyote pamoja na Allah katika kutoa utii na ibada Kwake. Kwa maneno mengine, yule ambaye anasali au kutekeleza Hija, au kufanya kitendo chochote kizuri kwa ajili tu ya kujionyesha kwa watu uzuri wake, ni mshirikina. Amewashirikisha wengine pamoja na Allah katika jambo la kutekeleza vitendo vyake. Kuonyesha kujikinai kwa matendo mazuri ni ushirikina mdogo, ambao hutangua vitendo vyetu vizuri. Imepata kuelezwa kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: Jiepusheni na ushirikina mdogo. Watu wakamuuliza, Ewe, Mtume wa Allah, ni nini ushirikina mdogo? Akajibu: Al-riya was-sama (yaani, kuonyesha watu au kuwafanya wasikie juu ya ibada yako kwa Allah). Vile vile Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: Kitu kibaya mno ninachokuhofieni kwenu ni ushirikina uliofichika; hivyo kuweni na hadhi ya juu yake kwa kuwa miongoni mwa wafuasi wangu ushirikina ni wa siri mno kuliko kutambaa kwa mdudu chungu juu ya jiwe gumu katika usiku wa giza. Tena alisema: Mtu ambaye anatekeleza ibada ya Sala kwa njia ya majivuno, ni mshirikina. Mtu ambaye anafunga au kutoa sadaka au kutekeleza Hija au kumuachia mtumwa huru ili kuonyesha kwa watu uadilifu wake au kujipatia jina zuri, ni mshirikina. Na kwa vile mistari hii ya mwisho inaelekeza kwenye mambo ya roho, umechanganywa katika ushirikina uliojificha. Hafidh: Tunaona katika maelezo yako mwenyewe kwamba kama mtu atafanya maombi kwa kiumbe yeyote aliyeumbwa ni mshirikina. Hivyo Mashia nao ni washirikina, kwa vile wanafanya maombi kwa Maimamu watukufu na watoto wao.

KUHUSU KUOMBA AU AHADI:


Muombezi: Kama tunataka kuyakinisha imani ya jumuiya moja, hatupasi kutegemea juu ya watu wasio na ujuzi wa jumuiya hiyo. Yatupasa kusoma vitabu vyao vya kuaminika. Kama unapenda kuuchunguza Ushia, usianze na Shia omba omba barabarani, wapigao makelele ya Ya! Ali, Ya! Imam Ridha, na kwa hoja hiyo, ukatangaza kwamba Mashia ni washirikina. Halikadhalika, kama mtu mjinga atafanya maombi au kiapo kwa jina la Maimamu au watoto wao, haipasi kuukashifu Ushia wote. Kama utasoma vitabu vya Sheria vya Shia, utaona kwamba hamna hata dalili moja ya ushirikina, au mambo ya upumbavu. Msisitizo juu ya Upweke wa Allah uko wazi kila mahali. Vitabu mashuhuri zaidi, Sharhe ya Luma, na Sharai, vinapatikana kwa wingi na unaweza ukavichunguza. Katika Sura ya Ahadi (ya nadhiri) maelezo sahihi ya wanasheria wa Kishia yanatajwa katika vitabu vyote vilivyotajwa hapo juu na katika vitabu vingine vingi. Kwa kuwa nadhir ni aina ya maombi, ni lazima kuwa na nia kwamba ni kwa ajili ya kujikurubisha kwa Allah (Kurbata ila llah). Kuna Sharti mbili kwa nadhiri sahihi: Nia ya moyo na kutamka au kwa maelezo ya maneno ya lugha yoyote ile itakayokuwa. Kuhusu sharti la kwanza,

46

Mikesha ya Peshawar
nia ya moyo lazima iwe kwa ajili ya Allah. Sharti la Pili hukamilisha sharti la kwanza; mtu ambaye anafanya Nadhiri lazima aseme kwa maneno kwamba, ni kwa ajili ya Allah. Kwa mfano, kama anaahidi kufunga au kuacha kunywa (ulevi), lazima aweke nia kwa kutumia maelezo ya maneno ambayo yana neno lillah (kwa ajili ya Allah) bila ya hivyo nadhiri itakuwa batili.

NADHIRI KWA JINA LA ALLAH.


Kama tunafanya nadhiri isiyo kwa jina la Allah, bali kwa mtu mwingine, ikiwa amekufa au yuhai, au tukimchanganya pamoja na jina la Allah, hata kama ni Imam au mtoto wake, nadhir hiyo si sahihi. Kama hili likifanywa kwa makusudi na kwa kujua basi huo ni ushirikina wa dhahiri, kama ilivyo wazi kutoka kwenye Aya, ...Na usimshirikishe yoyote katika ibada ya Mola Wako. (18:110). Wanasheria (mafakihi) wa Kishia wanakubali kwamba, kufanya nadhiri kwa jina la mtu yoyote pamoja na Mitume au Maimam ni kosa. Kama ikifanywa kwa makusudi ni ushirikina. Nadhiri yoyote lazima ifanywe katika jina la Allah, ingawa tumerehusiwa kufanya wakai wowote tunapopenda. Kwa mfano, kama mtu kwa jina la Allah atachukua mbuzi kumpeleka kwenye nyumba makhususi au sehemu ya ibada au kwenye kaburi la Imam au mtoto wa Imam na akamtoa dhabihu, hakuna madhara ndani yake. Vilevile, kama akiahidi na kutoa fedha au nguo kwa jina la Allah kumpa Seyyid (mjukuu wa Mtume) maalum, au kutoa sadaka kumpa yatima, au muombaji, hakuna madhara ndani yake. Kwa kweli, kama mtu anaahidi kufanya nadhiri tu kwa ajili ya Mtume au Imam, au mtoto wa Imam au kwa ajili ya watu wengine, hiyo inakatazwa. Ikifanywa kimakusudi, ni ushirikina. Ni wajibu wa kila Mtume au mwenye mamlaka ya kidini kuwaonya watu kama Qurani Tukufu inavyosema:

Sema: Mtiini Allah na mtiini Mtume, na kama mkigueka basi juu yake kinabakia kile alichobebeshwa juu yake na juu yenu hubakia kile mlichobebeshwa juu yenu (24:54). Ni wajibu wa watu kusikiliza kile anachokisema Mtume wa Allah na kukitekeleza. Walakini, kama mtu hajali kufuata mafundisho ya Kimungu na hayatekelezi, haiwezi kudhuru imani au kanuni ambazo ndani yake imani imesimamishwa.

47

Mikesha ya Peshawar

USHIRIKINA ULIOFICHIKA: KUJIONYESHA KATIKA SALA.


Aina ya pili ya ushirikina ni ule ushirikina uliofichika, kama vile kufanya kujionyesha Sala zetu au namna zingine za utiii kwa Allah. Tofauti kati ya ushirikina huu na ule ushirikina wa katika Sala, ni kwamba kuhusu suala la ushirikina katika Sala tunashirikisha kitu kingine au kiumbe pamoja na Allah. Kama mtu ataelekeza nia yake kwenye kitu kingine mbali na Allah, katika Ibada ya Sala, au kama kwa ushauri wa Shetani, akawa na picha bandia ya Mungu katika mawazo yake, au kama kiongozi wake ndio kiini cha nia yake, basi ni mshirikina. Hakuna isipokuwa Allah Ndiye apasaye kuwa mlengwa wa nia katika ibada zetu. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kwamba, kama mtu atafanya kitendo kizuri na akafanya mtu mwingine kuwa mshirika pamoja na Allah ndani yake, basi kitendo chake chote ni kwa ajili ya yule mshirika. Allah anachukia kitendo hicho na mtendaji wake pia. Vile vile imesimuliwa kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kwamba, Kama mtu akifanya ibada ya Sala, au kufunga, au kutekeleza Hija na ana mawazo kwamba kufanya kwake hivyo watu watamsifu, basi hakika, amefanya mshirika pamoja na Allah katika kitendo chake. Vilevile imesimuliwa kutoka kwa Imam Jafar Sadiq kwamba kama mtu atafanya kitendo kwa kumuogopa Allah, au kwa ajili ya malipo ya Akhera na akachangaya ndani yake ridhaa ya binaadamu, basi mtendaji wa kitendo hicho ni mshirikina.

USHIRIKINA KUHUSIANA NA KISABABISHO


Aina moja ya ushirikina ni ile ambayo huhusishwa kwenye kisababisho, kwa kuwa watu wengi huweka matumaini yao na hofu juu ya kisababisho cha pili. Huu pia ni ushirikina, lakini unasameheka. U shirikina una maana yakufikiri kwamba uwezo wote kiasili unatokana na kisababisho cha pili. Kwa mfano, jua hustawisha vitu vingi ulimwenguni, lakini kama mtu atafikiria uwezo huu ni wa msingi katika jua (yaani asili yake inatokana na jua lenyewe), basi huu ni ushirikina. Walakini, kama tunaamini kwamba jua limepata uwezo huu kutoka kwa Allah, na kwamba jua ni kisababisho cha pili tu cha ukarimu wake, basi huu kamwe sio ushirikina. Bali hasa ni namna ya Ibada, kwa kuwa kutafakari juu ya ishara za Allah ni mwanzo wa kumwabudu Allah. Utajo umefanywa katika Aya za Qurani Tukufu kwenye ukweli huu kwamba yatupasa kutafakari juu ya ishara za Allah kwa kuwa hii huongozea kwenye mazingatio juu ya Allah. Kwa njia hiyo hiyo, kutegemea juu ya kisababisho cha pili (nadhari ya mfanya biashara kwenye biashara, au nadhari ya mkulima kwenye shamba lake) humfanya mtu kuwa mshirikina kama kwa sababu hii atageuza mazingatio yake kunyume kutoka kwa Allah.

48

Mikesha ya Peshawar
Kwa msingi wa maelezo ya ushirikina ya hapo juu, ni upi katika mifano iliyoelezwa hapo ambao unafikiri unatumika kwa Mashia? Ni kwa namna gani kutokana na mtazamo wa Sala, imani au hadithi za Shia ambayo umeiona, inayoweza kuwafanya washambuliwe kwa ushirikina? Hafidh: Nakiri kwamba yote uliyosema ni sawasawa, lakini kama utachukua taabu ya kufikiri kidogo, utakubali kwamba kutegemea juu ya Maimam ni ushirikina. Kwa kuwa haitupasi kutafuta njia yoyote ya kibinadamu kumfikia Allah, yatupasa kumwomba Allah moja kwa moja kwa ajili ya kutaka msaada.

KWANINI MITUME WALITAFUTA MISAADA KUTOKA KWA WATU?


Muombezi: Inashangaza kwamba unapuuza niliyokuwa nikisema hapa wakati wote huu. Je ni ushirikina kufanya maombi kwa watu wengine kwa ajili ya kutekelezewa haja zetu? Kama hii ingekuwa kweli, umma wote wa binadamu kwa ujumla basi ni wa kishirikina. Kama kuomba msaada kwa wengine ni ushirikina, kwa nini Mitume waliomba misaada kutoka kwa watu? Yakupasa uzichunguze aya za Qurani Tukufu ili upate kujua kipi ni kweli na sahihi. Aya zifuatazo zinafaa kuzingatiwa: Akasema: Enyi wakuu! Ni nani atakayeniletea kiti chake cha enzi kabla hawajakuja kwangu, hali ya kuwa wamekwisha sslimu amri? Mjasiri mmoja miongoni mwa majini akasema: Mimi nitakuletea kabla hujainuka mahali pako hapo na mimi bila shaka ninazo nguvu za hayo (na) ni muaminifu. Akasema yule aliyekuwa na ilmu ya Kitabu: Mimi nitakuletea kabla ya kupepesa jicho lako basi alipokiona kimewekwa mbele yake alisema: Haya ni kwa fadhila za Mola wangu.. (28; 38-40) Uletaji wa kiti cha Enzi cha Bilqis (Malikia wa Sheba) kwa Sulaiman ulikuwa hauwezekani kwa kila kiumbe. Kwa kukiri kabisa, ilikuwa sio kawaida, na Mtume Sulaiman, pamoja na kujua kwake kwamba ilihitaji uwezo wa Ki-Mungu, hakumuomba Allah kuleta kiti hicho cha enzi, bali aliomba viumbe wa kawaida tu kumsaidia. Ukweli huu unaonyesha kwamba kuomba msaada wa wengine sio ushirikina. Allah, kisababisho cha kwanza, ndiye Muumba wa visababisho vya ulimwengu huu. Ushirikina ni jambo la moyo. Kama mtu anaomba msaada wa mwingine na hamfikirii yeye kuwa ni Allah au mshirika Wake, haikatazwi. Hali hii ni ya kawaida kila mahali. Watu huenda kwenye nyumba za wengine na kuomba msaada bila kuchukua jina la Allah. Kama nikienda kwa Daktari na nikamuomba aniponyeshe, je, nitakuwa mshirikina? Tena kama mtu anakufa maji, na akapiga kelele za kuomba msaada hivi atakuwa ni mshirikina? Hivyo tafadhali kuwa muadilifu na usipoteze ukweli. Jumuiya yote ya Shia inaamini kwamba, kama mtu atafikiria kizazi cha Mtume kuwa ni Allah au washirika katika Dhati

49

Mikesha ya Peshawar
(Nafsi) Yake, hakika yeye ni mshirikina. Utakuwa umewasikia Mashia wakiwa katika shida wakilia, Ya Ali, nisaidie! Ya Husain, nisaidie! Lakini ukweli ni kwamba, kwa kuwa ulimwengu ni nyumba ya visababisho vya pili, tunawafikiria wao kama njia ya kutolewa katika shida. Tunaomba msaada wa Allah kupitia kwao. Hafidh: Badala ya kumuomba Allah moja kwa moja, kwa nini muombe visababisho? Muombezi: Matarajio yetu ya kudumu kuhusu haja zetu, dhiki, na hofu yamewekwa juu ya Allah, Mkamilifu. Lakini Qurani Tukufu inasema yatupasa kumfikia Allah, kupitia baadhi ya njia (visababisho) za kupelekea.

Enyi ambao mmeamini! Mcheni Allah na tafuteni njia ya kumfikia Yeye (5:35).

DHURIA WATUKUFU WA MUHAMMAD NI NJIA (WASYLA VISABABISHO) YA NEEMA ZA MUNGU.


Sisi Shia hatuwachukulii kizazi cha Mtume kama ufumbuzi wa matatizo yetu yote. Tunawaona wao kama wacha Mungu zaidi katika waja wa Allah na kama njia za neema za Mungu. Tunajiambatanisha wenyewe kwenye ile familia bora zaidi kwa mujibu wa maamrisho ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Hafidh: Kwa nini unasema kwamba, maneno: Njia ya kumfikia (Wasyla) katika Aya hiyo hapo juu yanawahusu kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)? Muombezi: Katika hadith nyingi, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), amependekeza kwetu, kwamba katika shida zetu tuwaombe watoto wake kama njia ya kumfikia Allah. Wengi wa Maulamaa wenu, kama Hafiz Abu Nuaimi Isfahani katika kitabu chake Nuzulul-Qurani fi Ali (Ufunuo katika Qurani kuhusu Ali), Hafiz Abu Bakr Shiraz katika kitabu chake Ma Nazala minal-Qurani fi Ali na Imam Ahmad Thalabi katika Tafsir (Sharhe) yake anasema kwamba Wasilat (njia ya kumfikia) katika aya hiyo hapo juu ina maana ya watoto wa Mtume (s.a.w.w.). Maneno haya yamekuwa wazi kwenye hadith nyingi za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Ibn Abil-Hadid Mutazali, mmoja wa Mualamaa wenu maarufu, anasema katika Sherhe Nahjull-Balagha yake, Juz. 4, Uk, 79, kwamba Bibi Fatima Zahra, alitaja maana ya maneno ya Aya hii mbele ya Muhajirina na Ansari, wakati anatoa khutuba yake yenye kuhusu kunyanganywa shamba lake la Fadak, katika maneno haya: Namshukuru Allah Ambaye kwamba Ukuu Wake na Nuru Yake, Wakazi wa mbinguni na

50

Mikesha ya Peshawar
ardhini hutafuta njia ya kumfika Yeye. Miongoni mwa viumbe Wake sisi ni njia (Wasilat) ya kumfikia Yeye.

HADITH ATH-THAQALAIN (HADITH YA VIZITO VIWILI).


Miongoni mwa hoja zetu nyingi zinazokubaliwa kuhusu uhalali wa kufuata kwetu kizazi cha Mtume ni Hadith ath-Thaqalain - vizito viwili, ambayo usahihi wake umekubaliwa na Madhehebu zote. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: Kama mtashikamana na viwili hivi, kamwe, hamtapotea baada yangu. Hafidh: Nafikiri umekosea wakati unaposema kwamba hadith hii ni sahihi na kwamba inakubaliwa na wote kwa kuwa haijulikani kwa Maulamaa wetu mashuhuri. Kuthibitisha haya naweza kusema kwamba, msimuliaji mkubwa wa hadith wa madhehebu yetu, Muhammad bin Ismaili Bukhari, haisimulii katika Sahih yake, ambacho ndio kitabu sahihi zaidi baada ya Qurani. Muombezi: Sikukosea kuhusu hadith hiyo. Usahihi wa hadith hii tukufu umekubaliwa na Maulamaa wenu wenyewe. Hata Ibn Hajar Makki, pamoja na uchungu wake na chuki, anakubali ukweli wake. Yakupasa uangalie katika Sawaiq Muhriqah (Sehemu ya 2, Sura ya 2, Uk. 89-90, chini ya aya ya 4) ambamo ndani yake, baada ya kunukuu maelezo ya Tirmidhi, Imam Ahmad bin Hanbali, Tabrani, na Muslim, anasema: Elewa kwamba hadith inayohusu kujiambatanisha na Thaqalain - vizito viwili (Ahlul-Bait wa Mtume na Qurani) imesimuliwa katika njia nyingi. Wasimuliaji wa hadith hii idadi yao ni zaidi ya ishirini, wote ni Masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kisha anasema kwamba kuna baadhi ya khitilafu ya namna ambayo kwayo hadith hii imesimuliwa. Wengine wanasema kwamba ilisimuliwa wakati Mtume yuko kwenye Hija yake ya mwisho huko Arafa; baadhi wanasema ilisimuliwa Madina, wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) yuko kwenye kitanda alichofia na chumba chake kilikuwa kimejaa Masahaba wake; wengine wanasema kwamba ilisimuliwa huko Ghadir-Khum; na wengine wanasema ilisimuliwa baada ya kurudi kwake kutoka Taif. Baada ya kusema yote haya, yeye (Hajar Makki) mwenyewe anafafanua kwamba hakuna khitilafu ya wazi katika hadith yenyewe. Ama kwa tofauti ya sehemu, huenda ilikuwa kwamba Mtume amerudia kusimulia hadith hii katika nyakati tofauti na mara kwa mara (sehemu mbalimbali) kwa ajili ya kusisitiza ukubwa wa Qurani na kizazi chake kitukufu. Umesema kwamba, kwa kuwa Bukhari hakuisimulia hadith hii katika Sahih yake, basi usahihi wake ni wa mashaka. Lakini hadith hii, ingawa haikuandikwa na Bukhari, imes-

51

Mikesha ya Peshawar
imuliwa kiujumla na maulamaa wakubwa wa madhehebu yenu, pamoja na Muslim bin Hajjaj na waandishi wengine wa vitabu sita vya hadith, ambao wameziandika katika vitabu vyao kwa ukamilifu sana, na hawategemei ukusanyaji wa Bukhari tu peke yake. Kama unakubali uadilifu wa Maulamaa wako wote mwenyewe, ambao wote walitambuliwa na Masunni waliopita, yapasa ukubali hadithi hii kwamba ni ya kweli, ambayo kwa sababu fulani haikuandikwa na Bukhari. Hafidh: Hakuna sababu ya kuunga mkono kutokuiandika hadith hii. Bukhari alikuwa makini sana katika suala la kusimulia hadithi. Alikuwa ni mwanachuo mwangalifu sana, na kama aliona hadith, kwa mtazamo wa maudhui au chanzo chake, kuwa yenye madhara au kutokubalika na akili za kawaida, yeye hiyo hakuiandika. Muombezi: Kama mithali inavyosema: Kupenda sana kitu humfanya mtu kuwa kipofu na kiziwi. Waheshimiwa Masuni wamekosea hapa, una shauku kubwa katika upendo wako kwa Imam Bukhari. Unasema alikuwa mchunguzi sana wa mambo, na kwamba simulizi zilizomo katika Sahih yake ni za kuaminika na kustahiki sifa ya Wahayi (Ufunuo). Lakini ukweli ni kinyume chake. Nyororo ya riwaya zilizotajwa na Bukhari zina watu ambao mara kwa mara wameshutumiwa kama waongo. Hafidh: Madai yako sio ya kweli. Unashusha elimu na uwezo wa Bukhar, ambavyo ni tusi kwa madhehebu yote ya Sunni. Muombezi: Kama uchunguzi ulioko juu ya msingi wa elimu ni matusi, basi wengi wa Maulamaa wenu maarufu ni watu ambao wamekebehi ile nafasi ya juu ya elimu na maarifa. Ningependa kukushauri uvichunguze mwenyewe vitabu vilivyoandikwa na waandishi wakubwa na maulamaa wa madhehebu yenu ambao wameandika Sherhe juu ya Sahih Bukhari, k.m. Al-Lualil- Masnua fi hadithl-Mazua ya Suyuti, Mizanul-ibtidal na Talkhisul-Mustadraka ya Dhahabi; Tandhkiratul-Mazua ya Ibn Jauzi, Tarikh Baghdad kilichokusanywa na Abu Bakar Ahmad bin Ali Khatib Baghadad, na vitabu vingine vya Ilm Rijal (vinavyoitwa, makala juu ya sifa za wasimuliaji) vilivyoandikwa na maulamaa wenu wengi wakubwa. Kama utasoma vitabu hivi, hutathubutu kusema kwamba nimemkebehi Imam Bukhari.

52

Mikesha ya Peshawar

BUKHARI NA MUSLIM WAMEANDIKA HADITH NYINGI ZILIZOSIMULIWA NA WAZUSHI.


Nilichosema ni hiki: Vitabu hivi viwili, Sahih Bukhari na Sahih Muslim, vina hadithi zilizosimuliwa na waongo. Kama utavichunguza Sahih Muslim na Sahih Bukhari katika mwanga wa vitabu vya Rijal (yaani vitabu vyenye kuelezea maisha na tabia za wasimuliaji wa hadith), utaona kwamba wameandika hadith nyingi zilizosimuliwa kutoka kwa watu ambao walikuwa waongo wakubwa, kwa mfano Abu Huraira, muongo mwenye sifa mbaya, Ikrima Kharji, Sulaiman bin Amri, na wengine wa namna hiyo hiyo. Bukhari hakuwa makini katika kuandika Hadith kama unavyofikiri. Hakuiandika Hadith ya Thaqalain ambayo wengine wameiandika, lakini hakusita kuandika ngano za kufedhehesha na matusi kuhusu Mtume Musa akimpiga kofi la uso Malaika wa Mauti, Mtume Musa akikimbia akiwa uchi mbele za watu akifukuza jiwe, na juu ya kuonekana kwa Allah (s.w.t.). Fikiria ngano nyingine ya kudhihaki na matusi iliyoandikwa na Bukhari katika Sahih yake, Juz. 2, uk. 120, Sura ya AlLahr Bil-Harb, na Muslim katika Sahih yake Juz. 1, akimnukuu Abu Huraira akisema kwamba siku ya Idd baadhi ya mabedui kutoka Sudani walikusanyika katika Msikiti wa Mtume. Waliwaburudisha watazamaji kwa michezo na maonyesho yao. Mtume akamuuliza Aisha (Mke wake - Mama wa Waumini) kama angependa kuona hayo maonyesho. Aisha, akasema anapenda kuyaona. Mtume akamfanya (Aisha) apande juu ya mgongo wake kwa hali ambayo kichwa chake kilikuwa juu ya mabega yake na uso wake juu ya kichwa cha Mtume. Ili kumfurahisha Aisha, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akiwaomba wachezaji kuonyesha mchezo (dansa) nzuri zaidi. Mwishowe Aisha alichoka, na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamuacha ateremke chini! Amua mwenyewe iwapo ngano kama hii haifedheheshi. Kama Bukhari alikuwa makini kuhusu kusimulia mambo, je, ilikuwa inafaa kwa upande wake kuandika ngano za kipuuzi kama hizi katika Sahih yake? Lakini ni mpaka sasa unaviainisha vitabu hivi kuwa ndio sahihi zaidi baada ya Qurani Tukufu. Hakika Bukhari alichukua tahadhari maalum kuliacha jambo la Uimamu na Umakamu wa Ali (a.s.) na hivyo hivyo suala la Ahlul-Bait. Huenda aliogopa maelezo kama hayo yangeweza yakatumika siku moja kama silaha dhidi ya wapinzani wa Ahlul-Bait.

53

Mikesha ya Peshawar

HADITH NYINGI SAHIHI ZIHUSUZO AHLUL-BAIT ZILIEPUKWA KWA MAKINI SANA.


Hivyo wakati tukilinganisha Sahih Bukhari na Sahih nyinginezo, tunafikia kwenye uamuzi juu ya suala hili kwamba hadith yoyote yenye kuwahusu Ahli Bait, hata iwe sahihi vipi na kuungwa mkono kikamilifu na waandishi katika mwanga wa Qurani, Bukhari kwa makusudi alishindwa kuiandika. Kwa mfano, kuna Aya nyingi za Qurani Tukufu, ambazo zina muelekeo wa moja kwa moja juu ya Ahadith (Hadhithul-Wilaya katika siku ya Ghadir; Hadith Inzar Yaumud-Dar; Hadithul-Muwakhat; Hadithus-Safina; Hadith Babul-Hitta n.k.) ambazo zinahusu, heshima juu yao, na umakamu wao dhuria wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Hizi Bukhari ameziacha kwa uangalifu na umakini sana. Na kwa upande mwingine, zile zinazoitwa eti ni Hadith ambazo zinawatweza Mitume, hususan Mtume wetu na kizazi chake kilicho safi, zimeandikwa katika kitabu chake bila hata kufikiria kidogo kwamba zimesimuliwa na waongo.

VYANZO VYA HADITH YA THAQALAIN.


Ama kwa hadith ya Thaqalain (Vizito viwili), ambayo Bukhari hakuiandika katika kitabu chake, vitabu vingine sahihi vya madhehebu yenu vimeisimulia. Kusema kweli, hata yule mwanahadith mkubwa, Muslim, ambaye anafikiriwa kuwa sawa na Bukhari, yeye pia ameisimulia. Wanachuo wengine ambao wameisimulia hadith hii ni hawa wafuatao: Muslim bin Hajaji katika Sahih yake Juz. 7, uk. 122; Abu Dawud katika Sahih yake; Tirmidhi katika Sunan yake, sehemu ya 2, uk. 307; Nisai katika Khasais yake uk. 30; Imam Ahmad bin Hanbal katika Musnad yake Juz. 3, uk. 14-17, Juz. 4, uk. 26 na 59 na Juz. 5, uk. 182 na 189; Hakim katika Mustadrak Juz. 3, uk. 109 na 148; Hafidh Abu Nuaim Isfahani katika Hilyatul-Auliya, Juz. 1, uk. 355; Sibt Ibn Jauzi katika Tadhkira yake, uk. 182; Ibn Athir Jazari katika Usudul-Ghaiba, Juz. 2, uk. 12 na Juz. 3, uk. 147; Hamidi katika JamaBaina-s-Sahihain Razin katika JamaBaina-s-Siha-e-Sitta; Tabran katika Tarikh al-Kabir; Dhahabi katika Talkh is-e-Mustadrak. Ibn Abd Rabbih katika Iqdul-Faridh yake; Muhammad bin Talha Shafii katika Matalibus-Suul; Khatib Khawarizmi katika Manaqib Sulayman Balkhi Hanafi katika Yanabiul-Mawaddatu, uk. 18, 25, 29, 30, 31, 32, 34, 95, 115, 126, 199 na 230, pamoja na tofauti ndogo katika maneno; Mir Seyyid Ali Hamadani katika Mawadda ya pili ya Mawaddatul-Qurba; Ibn Abi-l-Hadid katika Sherh Nahjul-Balaghah; Shablanji katika Nurul-Absar uk. 99; Nurud-Din Sabbagh Maliki katika Fusulul-Muhimma uk. 25; Hamwaini katika Faraidus-Simtain; Imam Thalabi katika Tafsir Kasful-Bayan;

54

Mikesha ya Peshawar
Samani na Ibn Maghazili Shafii katika Manaqib; Muhammad bin Yusufu Ganji Shafii katika Kifayatul-Talib, Sura ya 1, katika maelezo ya usahihi wa Khutuba ya Ghadir Khum na vilevile katika Sura 62, uk. 130; Muhammad bin Saad Khatib katika Tabaqat, Juz. 4, uk. 8; Fakhrud-Din Razi katika Tafsir Kabir Juz. 3, chini ya Aya Itisma (3:103), uk. 18; Ibn Kathir Damishqi katika Tasfir Juz. 4 chini ya aya ya Mawadda (42:23), uk. 113, Ibn Hajar Makki katika Sawaiq-e-Muhriqah uk. 75, 87, 90, 99 na 136 pamoja na tofauti ya maneno. Kuna wanachuo wengine kadhaa wa madhehebu yenu ambao majina yao siwezi kuyataja katika mkutano huu kutokana na uhaba wa muda. Wengi wa wanachuo wenu wameisimulia hadith hii muhimu kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa wingi sana na kwa mfuatano usiokatika wa usimuliaji kutoka kwa mmoja hadi mwingine kiasi kwamba imepata hadhi ya hadith inayosimuliwa mara kwa mara. Kwa mujibu wa hadith hii, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema yafuatayo: Ninaacha kati yenu vitu viwili vizito; Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Ahlul-Bait wangu. Kama mtaambatana na viwili hivi, kamwe, kamwe hamtapotea. Viwili hivi havitatengana mpaka vije vinifikie kwenye Haudhi ya Kauthar. Kwa msingi wa hadith hii Sahihi, tunaona kwamba yatupasa kutafuta mshikamano kwenye Qurani Tukufu na Ahlul-Bait wa Muhammad (s.a.w.w.). Sheikh: Hadith hii ya Mtume imesimuiliwa na Salih bin Musa bin Abdullah bin Ishaq, kupitia nyororo yake ya wasimuliaji waaminifu, akisema kwamba Abu Huraira ameisimulia katika njia hii: Ninakuachieni vitu viwili vizito: Kitabu cha Allah (Qurani Tukufu) na Sunna zangu (Mwenendo). Muombezi: Unanukuu tena hadith kutoka kwa mkorofi yule yule ambaye amepuuzwa na wakosoaji wa Shia (Kama Dhahabi, Yahaya, Imam Nisai, Bukhari na Ibn Adi, n.k.). Je, hutosheki na rejea za kuaminika ambazo nimezifanya kutoka Maulamaa wenu wenyewe wakubwa kuhusu hadith hii? Unanukuu maneno yasiyokubalika ya Hadith japokuwa Mashia na Masunni wote kwa pamoja wamekubali kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ametumia maneno, Kitabu cha Allah na kizazi changu, na sio Sunna zangu. Kusema kweli Kitabu (Qurani) na Sunna (mwenendo) vyote vinahitaji tafsir. Kwa hiyo Sunna haiwezi kuelezea Qurani Tukufu. Hivyo kizazi cha Mtume ambao ndio sawa na Qurani Tukufu ndio Wafasir halisi wa Qurani Tukufu na Sunna za Mtume (s.a.w.w.) vilevile.

HADITH YA SAFINA.
Sababu nyingine inayotufanya tutafute kushikamana na kizazi cha Mtume ni hadith sahih, Hadith ya Safina, ambayo imesimuliwa na Maulamaa wenu wote wakubwa, takriban bila kuacha hata mmoja, na mlolongo usiovunjika.

55

Mikesha ya Peshawar
Zaidi ya Wanachuo wenu mia moja wenyewe wameisimulia hadith hii: Muslim bin Hajjaj katika Sahih yake, Imam Ahmad bin Hanbal katika Musnad, Hafidh Abu Nuaim katika Hilyatul-Auliya. Ibn Abdil-Birr katika Istiab. Abu Bakar Khatib Baghdadi katika Tarikh Baghdad; Mohammed bin Talha, Shafii katika Matalibus-Suul; Ibn Athir katika Nihaya Sibti Ibn Jauzi katika Tadhkira; Ibn Sabbagh Makki katika FusululMuhimma; Allama Nurud-Din Samhudi katika Tarikhul-Madina Sayyid Mumin Shablanji katika Nurul-Absar; Imam Fakhnid-Din Razi katika Tafsir MafatihulGhaib, Jalalud-Din Sayuti katika Durrul-Manthur; Imam Thalabi katika Tafsir Kasful-Bayan, Tabrani katika Ausat; Hakim katika Mustadrak Juz. 3, uk, 151; Sulayman Balkhi Hanafi katika Yanabiul-Mawadda, Sura ya 4, Mir Seyyid Ali Hamadani katika Mawaddatul-Kurba Mawadda ya 2; Ibn Hajar Makki katika Sawaiqul-Muhrikah chini ya Aya 8; Tabari katika Tafsir yake, na vilevile katika Tarikh yake; Muhammad bin Yusufu Ganji Shafii katika Kifayatul-Talib. Sura ya 100, uk. 233. Maulamaa wengine wengi wa madhehebu yenu wamesimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: Mfano wa Ahlul-Bait wangu ni ule wa Safina ya Nuh. Ambaye ataipanda ataokolewa; ambaye anaipa mgongo atazama na kuangamia. Imam Muhammad bin Idris Shafii amerejea kwenye Hadith hii Sahih katika beti zake za mashairi ambazo Allama Fazil Ajib ameziandika katika Dhakhiratul-Maal. Imam Shafii, ambaye anatambuliwa kama mmoja wa wanachuo maarufu wa madhehebu ya Suni, anakiri kwamba, kushikamana kwetu na familia iliyotoharishwa ya Mtume ni njia ya wokovu wetu kwa sababu, kati ya Madhehebu sabini za Uislam, ile madhehebu ambayo inafuata kizazi cha Mtume ndiyo peke yake itakayopata wokovu.

KUTAFUTA NJIA YA KUMFIKIA ALLAH SIO USHIRIKINA.


Umesema kwamba kutafuta njia ya kumfikia Allah ni ushirikina. Kama hii ilikuwa kweli, kwa nini Umar bin Khatib alitafuta msaada wa Allah (swt.) kupitia kwa kizazi cha Mtume? Hafidh: Khalifa Umar kamwe hajafanya hivyo. Muombezi: Katika nyakati za shida Umar alitafuta msaada wa kizazi cha Mtume, Alimwomba Allah kupitia kwao, na mahitaji yake yalitekelezwa. Ninarejea kwenye matukio mawili tu. Ibn Hajar Makki anaandika katika Sawaiq-e-Muhriqah, baada ya Aya ya 14 (kutoka kwenye Tarikh Damascus) kwamba katika mwaka wa 17 Hijria watu waliswali kwa ajili ya kuomba mvua lakini hawakufanikiwa. Khalifa Umar akasema

56

Mikesha ya Peshawar
kwamba angesali kwa ajili ya mvua siku ifuatayo kupitia njia ya kumfikia Allah. Asubuhui yake alikwenda kwa Abbas, ami yake Mtume na akasema: Toka nje ili tuweze kumuomba Allah kupitia kwako kwa ajili ya mvua. Abbas alimuomba Umar akae kidogo ili kwamba hio njia ya kufikia kwa Allah ipatikane. Basi, Bani Hashim (Ahlul-Bait) walijulishwa. Kisha Abbas akatoka nje pamoja na Ali, Imam Hassan na Imam Husein. Bani Hashim wengine walikuwa nyuma yao. Abbas akamwambia Umar kwamba mtu yoyote mwingine asiongezwe kwenye kundi lao. Kisha walikwenda sehemu ya kuombea ambapo Abbas alinyanyua mikono yake kwa ajili ya maombi na akasema: Ya Allah! Wewe ndio umetuumba sisi, na unajua kuhusu vitendo vyetu. Ya Allah! Kama ulivyokuwa Mwema kwetu mwanzoni, hivyo kuwa Mwema kwetu mwishoni. Jabir anasema kwamba dua yao ilikuwa bado haijakwisha wakati mawingu yalipojitokeza na ikaanza kunyesha. Kabla hawajafika nyumbani kwao, walikwishalowa. Bukhari pia anasimulia kwamba, siku moja wakati wa ukame Umar bin Khatib alimuomba Allah kupitia kwa Abbas bin Abdul-Muttalib na akasema: Tunatuma maombi sisi wenyewe kupitia kwa ami yake Mtume wetu; hivyo, Mwenyezi Mungu tunyeshee mvua. Kisha ilianza kunyesha. Ibn Abil-Hadid Mutazili katika Sherhe Nahjul-Balaghah (Chapa ya Misri), uk. 256, anaandika kwamba Khalifa Umar alikwenda pamoja na Abbas, ami yake Mtume, kumuomba Allah kwa ajili ya mvua. Katika maombi yake kwa ajili ya mvua, Khalifa Umar alisema: Ya Allah! Tunaleta maombi wenyewe kupitia kwa ami yake Mtume Wako, na kwa jadi yake na kwa watu wao maarufu waliobakia. Hivyo linda cheo cha Mtume wako kupitia kwa Ami yake. Tulikuwa tumeongozwa Kwako kupitia kwa Mtume, ili kwamba tutafute msaada wao na kufanya toba. Kama kuwatafuta kizazi cha Mtume na kuwaendea kwa ajili ya haja zetu katika njia ya Allah ni ushirikina, basi Khalifa Umar alikuwa mshirikina wa kwanza. Kizazi cha Muhammad (s.a.w.w.), kutoka wakati wa Mtume mpaka leo hii, wamekuwa ndio njia ya kupitia (Wasilat) katika dua na maombi yetu kwa Allah. Tunawachukulia tu kama watu wacha-Mungu sana na walio karibu mno na Allah. Kwa hiyo tunawaona wao ni njia ya kutufikisha kwa Allah. Na uthibitisho mzuri wa hili ni vitabu vyetu vya Dua zilizoelezwa na Maimam wetu Maasum. Tunakubali maelekezo ya Maimam wetu. Hapa ninavyo vitabu viwili: Zadul-Maad cha Allama Majlisi na Hidayatuz-Zairin cha Sheikh Abbas Qummi, ambavyo ninavitoa kwako ili uvichunguze. (Wote wawili Hafidh na Sheikh walichunguza vitabu vile). Waliisoma Dua ya Tawassul, na waliona kwamba Ahlul-Bait wa Mtume walikuwa ni sehemu ya dua. Kila mahali walikuwa wametajwa kama njia ya kufikia kwa Allah. Katika muda ule Mulla Abdul-Hayy alisoma Dua yote ya Tawassul, iliyoelezwa na Maimam watoharifu na kunukuliwa na Muhammad bin Babawayh Qummi.

57

Mikesha ya Peshawar

DUA YA TAWASSUL.
Haya ni maombi kwa Allah. Kama Ali ambavyo ametajwa hapa, na Maimam wote wametajwa kwa hali hiyo hiyo. Athari ya Ahlul-Bait wa Mtume inatafutwa kutufikisha kwa Allah. Wanatajwa namna hii: Ewe Bwana wetu na kiongozi wetu! Tunatafuta msaada wako wa kutufikisha kwa Allah. Ewe unayeheshimika zaidi mbele ya Allah: Tuombee sisi Kwake. Ahli Bait wote wa Mtume wametajwa katika hali hiyo hiyo.

MASHIA HAWAWASINGIZII MASUNNI.


Wakati dua hii ilipokuwa ikisomwa, baadhi ya mabwana waungwana wa Kisuni waliguta kwa mshangao na butwaa na masikitiko juu ya kutoelewana kukubwa kulikosababiwa na watu. Muombezi akauliza: Je, kuna dalili yoyote ya ushirikina katika dua hii? Je, jina tukufu la Allah halipatikani kila mahali? Ni watu wenu wangapi wasioelewa na wasio wavumilivu ambao wamewauwa Mashia wa watu masikini, wakiamini kwamba wameua mshirikina? Lawama juu ya mambo haya moja kwa moja ni juu ya maulamaa kama ninyi wenyewe. Je, umewahi kusikia hata siku moja kwamba Shia mmoja amemuua Sunni? Ukweli ni kwamba maulamaa wa Kishia hawaenezi sumu. Hawajengi chuki baina ya Shia na Sunni, na wanaona kuua kwamba ni dhambi kubwa. Katika mambo ya tofauti ya imani kati yao, wanafafanua misimamo kwa majadiliano yaliyojengeka juu ya msingi wa elimu na mantiki, na kufanya ijulikane kutokana na mazungumzo yao kwamba Sunni ni ndugu zao.

MAULAMAA WA KISUNI WANAWAITA MASHIA MAKAFIRI.


Kwa upande mwingine, matendo ya maulamaa mashabiki wa Sunni wanafaa kuangaliwa. Wafuasi wa Abu Hanifa, Maliki bin Anas, Muhammad bin Idris Shafii na Ahmad bin Hanbal, ambao wanazo tofauti za wazi kabisa, wanawaita wafuasi wa Ali bin Abi Talib na Imam Jafar bin Muhammad makafiri na washirikina. Wanachuoni wengi wakubwa na wacha Mungu wa Kishia waliuwawa mashahidi kwa fatwa zilizotolewa na Maulamaa wa Kisuni. Kinyume chake hakuna mfano wa ukatili kama huo kwa upande wa Ulamaa wa Kishia. Maulamaaa wenu mara kwa mara hutoa maneno ya kuwalaani Mashia, lakini hutaona popote laana juu ya Masunni katika vitabu vilivyoandikwa na Maulamaa wa Kishia.

58

Mikesha ya Peshawar
Hafidh: Hutendi haki. Unachochea chuki bure. Toa mfano mmoja tu wa mwanachuo wa Kishia aliyeuwawa kwa hukumu ya maulamaa wetu! Nani katika Mualamaa wetu aliyetoa maneno ya laana juu ya Shia? Muombezi: Kama ingekuwa nielezee kirefu matendo ya Maulamaa wenu au ya watu wenu wa kawaida, mkutano mmoja usingekuwa mrefu wa kutosha. Nitarejea tu kwenye mifano michache yenye kuhusiana na matendo yao ili ujue kwamba mimi sichochei chuki, bali naonyesha ukweli. Kama utavichunguza vitabu vya Maulamaa wenu mashabiki, utaona sehemu ambazo wamelaani Mashia. Kwa mfano, angalia vitabu vya Tafsiri vya Imam Fakhrud-Din Razi. Wakati anapopata wasaa tu, kwa mfano kuhusiana na Aya za Wilayat, huandika kwa kurudia rudia: Laana iwe juu ya Marafidhi, laana iwe juu ya Marafidhi, lakini maulamaa wetu hata mara moja hawajaandika mambo kama hayo juu ya ndugu zetu Masunni. Mfano wa vitendo vya kikatili vya maulamaa wenu kuhusu maulamaa wa Kishia ni zile hukumu ya Makadhi wakubwa wawili wa Syria (Burhanud-Din Maliki na Ibad bin Jamaat Shafii) dhidi ya mmoja wa Mwanasheria (Faqih) mkubwa, Abu Abdullah Muhammad bin Jamalud-bin Makki Amili. Mwanachuo yule mkubwa alikuwa akijulikana katika wakati wake kwa ucha Mungu wake na elimu ya Sheria. Mfano wa uwanachuo wake ni kitabu chake, Luma, ambacho alikiandika kwa muda wa siku saba bila kuwa na kitabu chochote mkononi mwake juu ya Sheria (Fiqih) isipokuwa Mukhtasar Nafi. Zaidi ya hayo, wanachuo wa madhehebu haya manne (Hanafi, Maliki, Shafii na Hanbal) walikuwa miongoni mwa wanafunzi wake. Kwa sababu ya maonevu ya Massuni, mara kwa mara alifanya Taqiyya (kujigeuza na kuficha mwelekeo wakati wa hatari), na hakutangaza Ushia wake waziwazi. Kadhi Mkuu wa Syria, Ibad bin Jamaat, ambaye ameweka uhusuda dhidi yake, alimzungumza vibaya kwa mtawala wa Syria (Baidmar) na akamshutumu kuwa yeye ni Rafidhi na Shia. Mwanachuo huyu maarufu akatiwa nguvuni. Baada ya kutaabikia ufungwa na mateso ya mwaka mmoja, kwa fatwa ya Makadhi hawa wawili (Ibnul-Jamaat na Burhanud-Din) yeye akauawa na mwili wake ukatundikwa kwenye kiunzi. Kwa vile walitangaza kwamba kuna Rafidh ni Kafiri yuko juu ya miti ya kunyongea, watu wa kawaida waliupiga mawe mwili ule. Baadae, mwili ule ulichomwa na jivu lake likasambazwa. Miongoni mwa maulamaa na wanasheria wa Kishia wa kujivunia wa Syria katika karne ya 10 Hijriya, alikuwa Sheikh Zainud-Din bin Nurud-bin Ali bin Ahmad Amili. Alikuwa akijulikana sana miongoni mwa marafiki na maadui kwa elimu yake na uadilifu. Akiwa mtunzi wa vitabu vingi, alijiweka mbali na ulimwengu na akaandika vitabu 200 juu ya masuala mbalimbali. Ingawa aliishi maisha ya kujitenga, bado maulamaa wa Kisunni walijenga chuki juu yake, na wivu juu ya umaarufu wake miongoni mwa watu. Mkubwa katika wapinzani wake alikuwa Kadhi Saida, ambaye aliandika kwa Mfalme Sultan Salim

59

Mikesha ya Peshawar
malalamiko yafuatayo: Hakika kuna mtu anaishi katika jimbo la Syria ambaye ni mzushi, mtu ambaye hahusiki na mojawapo ya madhehebu manne. Sultani Salim aliamrisha kwamba mwanasharia huyo aletwe mbele ya mahakama huko Istanbul (Uturuki). Alitiwa nguvuni ndani ya Msikiti Mtukufu wa Makka na alifanywa mfungwa siku arubaini mjini Makka. Katika safari ya baharini kuelekea Istanbul, alikatwa kichwa na mwili wake ukatupwa baharini. Ni kichwa chake tu ndicho kilichopelekwa kwa mfalme Waheshimiwa Mabwana! Nakuulizeni kwa shauku moyoni, kwa jina la Allah mseme iwapo mlipata kusikia tabia ya namna hiyo kwa upande wa Maulmaa wa Kishia dhidi ya Sunni kwa sababu ya kutofauta madhehebu ya Shia. Ni hoja gani mtakayoleta kuthibitisha kwamba iwapo mtu akiacha kufuata yoyote katika madhehebu manne, yeye anakuwa ni kafiri na kwamba kuuawa kwake yeye ni wajib? Je, ni mantiki kufuata madhehebu ambayo yamekuja kuweko karne kadhaa baada ya Mtume, ambapo wale wanaofuata kanuni iliyokuwepo tangu wakati wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wanaamriwa wauawe?

MASHIA NA MADHEHEBU MANNE YA SUNNI.


Tafadhali hebu semeni kwa jina la Allah, iwapo hawa Maimam wanne Abu Hanafi, Malik, Shafii na Hanbal, walikuwa hai wakati wa uhai wa Mtume. Je, waliipata misingi ya dini kutoka kwa Mtume moja kwa moja? Hafidh: Hakuna hata mmoja aliyedai hayo kuwa hivyo. Muombezi: Je, Amirl-Muminin Ali hakuwa mwenzi wa wakati wote wa Mtume, na je, hakutangaza kuwa Yeye ni lango la Jiji la Elimu? Hafidh: Yeye kwa hakika alikuwa mmoja kati ya masahaba maarufu sana wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na katika hali zingine yeye alikuwa ni mbora kuliko wao wote. Muombezi: Je, hivi hatuna haki, kwa hiyo, ya kushikilia kwamba kumfuata Ali ni wajibu? Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe alisema kwamba kumtii Ali ni sawa na kumtii yeye na kwamba yeye Ali alikuwa ni Lango la Elimu? Vile vile Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kwamba yoyote yule anayetaka kupata elimu yapasa aende kwenye mlango wa Ali. Vilevile, kwa mujibu wa Hadith ath-Thaqalain na Hadith as-Safina, ambazo zinatambuliwa na wote Sunni na Shia kugeuka kutoka kwenye njia iliyoonyeshwa na Ahlul-Bait wa Mtume itatuongozea kwenye maangamizi. Utovu wa utii, au uadui dhidi ya Ahlul-Bait wa Mtume ni sawa sawa na utovu wa utii kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe. Licha ya yote haya, Maulamaa wa Kishia hawajaonyesha ukosa subira wa namna hiyo kwa angalau hata Sunni wa kawaida, achilia mbali kwa maulamaa wao. Tulikuwa siku zote tukiwasihi Mashia kwamba Masunni ni ndugu zetu katika Uislamu na yatupasa

60

Mikesha ya Peshawar
kubakia tumeungana (yaani kulinda umoja wetu). Kwa upande mwingine mara kwa mara maulamaa wa Kisunni wamekuwa wakiwachochea watu wao, wakisema kwamba Mashia ni wazushi, Marafidhi,Ghullat, au Mayahudi. Wanasema kwamba, kwa kuwa hawa Shia hawafuati mmoja katika Maimam wanne wa Kisunni (Abu Hanifa, Malikki, Shafii na Hanbali), basi ni makafiri. Ukweli ni kwamba wale wanaowafuata Ahlul-Bait wa Mtume (s.a.w.w.) wameongozwa sawasawa.

MAUAJI YA MASHIA HUKO IRANI NA AFGHANISTAN.


Waturuki, Bani Khawarizim, Wa-Uzbeg na wa-Afghan waliwateka nyara na kuwauwa Mashia wasio na hatia. Muhammad Amin Khan Uzbeg, ajulikanaye kwa jina la Khan Khawa, na Abdullah Khan Uzbeg waliwaua kikatili na kuwapora Mashia na wakakiri kuwa wamelifanya hilo. Maulamaa wa Kisunni walitangaza kwamba Mashia ni makafiri na kwamba wanaweza kuuawa kwa mjibu wa Sharia ya dini. Ma-Amiri (viongozi) wa Afghanistani waliwatendea Mashia kwa namna hiyo hiyo. Katika mwaka wa 1267 Hijiriyya siku ya Ashura (Mwezi 10 Muharam), Masunni walishambulia ukumbi katika Qandahar, ambako Mashia walikuwa wanaomboleza mauaji ya mjukuu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Waliwaua Mashia wengi kwa ukatili mkubwa, wakiwemo watoto, na wakapora mali zao. Kwa miaka mingi Mashia waliishi maisha ya dhiki na walikatazwa kuendesha ibada zao za kidini. Katika siku ya Ashura wachache wao walikwenda kwenye kumbi za siri na waliombeleza mauaji ya Imam Husein (A.S) kisirisiri kabisa, na wale wengine walikuwa wakichinjwa kwenye nyanda za Karbala. Ilikuwa ni Mfalme Amanullah Khan aliyeondoa kikwazo hicho juu ya Shia na akawatendea upole.

KUUWAWA SHAHIDI KWA SHAHID THALIS.


Katika makaburi ya Akbarabad (Agra) India, pale amelala Mwanachuo Mchamungu mno wa Kishia, Qadhi Seyyid Nurullah Shustari. Aliuawa kishenzi sana akiwa na umri wa miaka 70 katika mwaka wa 1019 Hijiriya na Mfalme Jahangir, kufuatia fatwa kutoka kwa wanachuo wa Kisunni kwamba Yeye alikuwa Rafidh. Hafidh: Unatushambulia (kwa maneno) bila sababu yoyote. Mimi mwenyewe nimeshtushwa mno kusikia vitendo vya kuchukiza mno vya watu wajinga, lakini matendo ya Mashia pia yalikuwa yanahusika na matukio haya. Muombezi: Unaweza kunieleza ni matendo gani ya Mashia ambayo yalifanya kuwa halali kwao kuuwawa?

61

Mikesha ya Peshawar
Hafidh: Kila siku maelfu ya watu wanasimama mbele za makaburi ya waliokufa na kuwaomba msaada. Je, kitendo hiki sio mfano wa kuabudu wafu? Kwa nini Maulamaa wasikataze wakati mamilioni ya watu hao wakiweka mapaji yao ya nyuso zao kwenye ardhi wakisujudu katika kuwaabudu wafu? Nashangaa ni kwa vipi bado unayaita mambo haya kuwa sio shirki. Wakati majadiliano na Mawalana Hafidh yakiendelea, faqihi wa Kihanafi, Agha Sheikh Abdus-Salam alikuwa anakichunguza Hidayatuz-Zairin. Akasema kwa msisitizo mzito, Tazama hapa! (akikionyesha kile kitabu). Ulamaa wako anasema kwamba wakati mahujaji wanapomaliza Ziarat katika Makuba ya Maimam, wanapaswa kuswali rakaa mbili za Sala ya Ziarat. Huenda hawaikusudii Sala hii kwa jina la Allah; vinginevyo, nini maana ya Sala ya Ziarat? Huu sio ushirikina kufanya ibada ya Sala kwa ajili ya Imam? Mahujaji wanaosimama na kuelekeza nyuso zao kwenye makaburi na kusali ni ushahidi mzuri wa ushirikina. Hiki ni kitabu chenu Sahihi. Unaweza ukatetea hali yenu hii? Muombezi: Mbona unajiingiza katika mazungumzo ya kitoto! Hivi umewahi kuwako kwenye Ziarat hizo na kuwaona Mahujaji hao ana kwa ana? Sheikh: Hapana. Muombezi: Sasa ni vipi ukaweza kusema kwamba mahujaji hao wanaswali wakiwa wameelekeza nyuso zao kwenye kaburi, na kusema kwamba swala hii ya Ziarat ni dalili ya ushirikina? Sheikh: Kitabu hiki kinasema kwamba waswali Swala ya Ziarat kwa ajili ya Imam. Muombezi: Hebu lete hicho kitabu nikiangalie. Ngoja nisome maelekezo kuhusu Ziarat, mpaka tufikie kipengele cha Sala ambacho ndio hoja ya kukataa kwako. Wakati wowote ukiona dalili ya ushirikina, tafadhali ionyeshe. Na iwapo utaona alama za kuamini na kuabudu Mungu Mmoja kuanzia juu mpaka chini usije ukajisikia vibaya kwa hilo, bali sema kwamba ulikuwa umeelewa vibaya. Kitabu kiko hapa mbele yenu.

MAELEKEZO KUHUSU ZIARAT:


Maekelezo ni kama yafutayo: Wakati mwenye kufanya Ziarat afikapo handaki la Kufa, anasimama pale na kusoma kisomo kifuatacho Allah ni Mkubwa mno, Allah ni mkubwa mno Mwenye ukubwa, Utukufu, Sifa njema, na rehema. Allah ni Mkubwa Mno juu zaidi ya kile ambacho nakiogopa. Allah ni Mkubwa mno. Yeye ni msaada wangu; Kwake Yeye nategemea na Kwake Yeye yako matumaini yangu na Kwake Yeye naelekea. Wakati mwenye kufanya Ziarat akifika lango la Najaf, yampasa kusoma: Sifa zote njema ni za Allah, ambaye ametuongoza katika hili, tusingekuwa ni wenye kuongoka kama Allah

62

Mikesha ya Peshawar
asingetuongoza. Wakati akifika lango la Uwanja wa Mtukufu yampasa asome, baada ya kumtukuza Allah: Nashuhudia kwamba hakuna Mungu isipokuwa Allah, aliye Mmoja. Yeye hana mshirika. Na pia ninashuhudia kwamba, Muhammad ni mja na Mtume Wake. Ametuletea kweli kutoka kwa Allah. Na pia nashuhudia kwamba Ali ni mja wa Allah na ndugu yake Mtume wa Allah. Allah ni mkubwa mno, Allah ni mkubwa mno, Allah ni Mkubwa mno. Hakuna Mungu isipokuwa Allah, na Allah ni Mkubwa mno. Shukrani zote ni Zake kwa mwongozo na msaada Wake kuitikia kile alichofunua juu ya njia kuelekea Kwake. Wakati Mwenye kufanya Ziarat akifika kwenye lango la Quba, yampasa asome: Ninashuhudia kwamba hakuna Mungu isipokuwa Allah, aliye Mmoja. Yeye hana Mshirika pamoja Naye mpaka mwisho. Wakati, baada ya kwisha kuomba ruhusa ya Allah, ya Mtume, na ya Maimam, mwenye kufanya Ziarat hufika ndani ya Quba, husoma Ziarat mbalimbali ambazo zina maamkuzi kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kwa Amirl-Muminin. Baada ya Ziarat, husali rakaa sita (za Sunna), rakaa mbili kwa ajili ya Amirl-Muminin na rakaa mbili kwa ajili ya Nabii Adam na mbili kwa ajili ya Nabii Nuh ambao wamezikwa katika eneo hilo hilo.

SALAT-ZIARAT NA DUA BAADA YA SALA.


Je, utekelezaji wa ibada ya Sala kama sadaka kwa ajili ya roho za wazazi na waumini wengine, haikuamrishwa juu yetu? Je, maamrisho haya ni ushirikina? Vilevile ni kwa ajili ya ubinaadamu kwamba wakati mtu anapokwenda kumuona rafiki humpatia zawadi fulani. Kuna Sura katika vitabu vya Madhehebu zote ambamo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anatuamrisha kutoa zawadi kuwapa waumini. Hivyo mwenye kufanya Ziara anapofika kwenye kaburi la mpendwa bwana wake na anajua kwamba kitu alichokuwa amekipenda zaidi ilikuwa ni Sala, anasali rakaa mbili katika njia yake ya kufikia kwa Allah na anaitoa Sala ile kama zawadi kwa ajili ya roho ya bwana wake huyo. Je, huo ni ushirikina? Baada ya kusoma kanuni za msingi wa Sala hii, pia soma dua iliyoko baada ya Sala, ili kwamba mashaka yako yote yaondoke.

DUA BAADA YA SALA:


Ibada ya Dua ni kwamba baada ya kumaliza Sala katika kichwa cha kaburi la Imam aliyezikwa pale, na nyuso zetu kuelekea Kibla (sio kuelekea kwenye kaburi), tunasoma dua ifuatayo, Ewe Allah! Sala hii nimeifanya zawadi kwa bwana na kiongozi wangu, Mtume Wako na ndugu yake Mtume Wako, Amirl-Muminin Ali bin Abu Talib. Ewe Allah, teremsha rehema na amani Yako juu ya Muhammad na kizazi chake. Zikubali rakaa

63

Mikesha ya Peshawar
mbili hizi za Sala kutoka kwangu na unijazi, kama ambavyo ungewajazi watendaji wa matendo mema. Ewe Allah! Nimeitoa Sala hii (kama Sadaka) kwa ajili Yako, na nimerukuu na kusujudu mbele yako Wewe kwa kunyenyekea Kwako. Wewe ni Mmoja ambaye huna mshirika. Hairuhusiwi kusali, kurukuu au kusujudia chochote isipokuwa Wewe. Wewe ni Allah, uliye Mkuu na hakuna mungu isipokuwa Wewe. Mabwana waheshimiwa! Kwa jina la Allah, kuweni waadilifu. Kuanzia muda ule mwenye kuzuru anapoweka mguu wake juu ardhi ya Najaf, mpaka baada ya kusali sala yake ya Ziarat, yeye anajishugulisha katika kumkumbuka Allah swt. Sheikh: Inashangaza kwamba huoni yalioandikwa hapa: Busu kizingiti cha mlango na kisha ingia ndani ya haram ya Kuba. Tumesikia kwamba wakati wenye kufanya Ziarat wakifika kwenye mlango wa kuba la Maimam wao, wanakwenda Sijida kwa heshima. Je kusujudu huku sio kwa ajili ya Ali? Je, sio ushirikina wakati tunasujudia mwingine asiyekuwa Allah? Muombezi: Kama mimi ndio ningekuwa ni wewe, nisingelisema neno. Ningenyamaza kimya mpaka mkutano wa mwisho wa mjadala huu na kusikiliza mantiki ya majibu yangu. Lakini nitakuambia kwa ufupi mara nyingine tena kwamba, kubusu kizingiti au sakafu ya makuba ya Maimam sio ushirikina. Umelitafsiri vibaya neno kubusu na kuliona kuwa ni sawa na kusujudu. Wakati unasoma kitabu hicho mbele yetu unadiriki kufanya mabadiliko ya ugeuzaji maana ya maneno kama huu, sijui ni jinsi gani utatusingizia wakati utakapokuwa peke yako ukiwahutubia watu wasio na elimu. Maelekezo yaliyomo katika kitabu hiki na vitabu vinavyohusu Dua na sehemu za Ziarat ni kwamba mwenye kufanya Ziarat, kama namna ya kuonyesha heshima, inampasa kubusu kizingiti sio kusujudu. Vipi unafikiria kubusu na kusujudu kuwa ni kitu kimoja? Na, ni wapi umeona ima katika Qurani tukufu au katika hadith yoyote kwamba kubusu kizingiti cha Kuba la Mtume au Imam kumekatazwa? Hivyo kama huna jibu la maana kwa swali hili, usipoteze wakati wetu. Na, kama unavyosema umesikia kwamba wafanyao Ziarat husujudu kwa heshima. Kwa uhakika hukuwaona kwa macho yako wakifanya hivi. Qurani tukufu inasema, Enyi ambao kwamba mmeamini! Akikujieni fasiki na habari, ichunguzeni, msije mkadhuru watu kwa ujinga, kisha mkawa ni wenye kusikitika kwa yale muliyoyafanya. (49:6). Kwa mujibu wa amri hii ya Qurani Tukufu, hatupasi kutegemea maelezo ya watu waovu. Yatupasa kufanya juhudi kubwa kujua ukweli, hata ikiwezekana kufanya safari ili kupata habari ya kweli moja kwa moja. Wakati nilipokuwa Baghdadi, nilikwenda kwenye makaburi ya Abu Hanifa na Sheikh AbdulKadir Jilani na nikaona watu walivyofanya. Ilikuwa vibaya zaidi kuliko ulivyoelezea kuhusu Mashia wanavyofanya, lakini kamwe sijalizungumza hili. Nilipofika kwenye kaburi la Abu Hanifa hapo Muazzam, niliona kundi

64

Mikesha ya Peshawar
la Masunni wakirudia rudia kubusu Sakafu, badala ya kizingiti, na kujigaragaza kwenye sakafu. Lakini kwa kuwa hawakuonekana kwa mahabithi, na kwa sababu sikuwa na sababu za kuwalaumu, kwamwe sikuitaja habari hii kwa mtu yoyote. Nilielewa kwamba walikuwa wakifanya hivyo kwa ajili ya mahaba sio kama ibada. Ewe bwana mheshimiwa! Hakika hakuna Shia mcha-Mungu ambaye amediriki kusujudu kwa yeyote isipokuwa Allah. Kama, kwa vyovyote vile iwavyo, kama tunaanguka chini ya ardhi katika hali kama ya kusujudu na kusugua mabapa ya nyuso zetu juu yake (bila kuwa na nia ya kuabudu), hiki ni kitu kidogo sana. Kuinama mbele ya mtu mtukufu bila kumfikiria kuwa yeye ni Allah, au kuanguka chini juu ya ardhi na mtu kusugua uso wake juu yake, sio ushirikina. Ni matokeo ya mahaba makubwa. Sheikh: Inakuwaje kwamba tunaposhuka chini juu ya ardhi na kuweka paji letu la uso juu yake, kwamba kitendo hiki kisiweze kuwa sawa na kusujudu? Muombezi: Kusujudu kunategemea juu ya nia, na nia ni jambo la moyo. Ni Allah peke yake ndiye anayejua nia zetu za moyoni. Kwa mfano tunaweza kuona watu wamelala chini juu ya ardhi kwa hali kama ya kusujudu. Ni kweli kwamba kusujudia yeyote asiyekuwa Allah sio sawasawa, hata ikiwa bila nia yoyote. Walakini, kwa kuwa hatujui nia za mioyo yao, hatuwezi kuiita hiyo kuwa ni Sijida ya Ibada.

KUSUJUDU KWA NDUGU ZAKE YUSUFU MBELE YAKE.


Kwa hiyo, kusujudu katika hali iliyo sawa na Sijida ya ibada (lakini bila nia yake), kuonyesha heshima kwa mtu sio ushirikina. Kwa mfano nduguze Nabii Yusufu walisujudu mbele yake. Wakati huo Mitume wawili walikuwepo, Yaqub na Yusufu, lakini hawakuwakataza kufanya hivyo. Allah (s.w.t.) Anasema katika Suratul-Yusufu ya Qurani Tukufu.

Na aliwainua wazazi wake na kuwaweka katika kiti cha Ufalme, na wote wakaporomoka kumsujudia, na akasema; Ewe Baba yangu, hii ndiyo hakika ya ndoto yangu ya zamani; bila shaka Mola wangu ameithibitisha .. (12:100). Aidha, Qurani Tukufu inasema katika sehemu nyingi kwamba Malaika walifanya Sajida mbele ya Mtume Adam. Hivyo kama kusujudu namna hiyo ni ushirikina, basi nduguze Mtume Yusufu na Malaika wa Allah walikuwa washirikina. Ni Iblis aliyelaaniwa peke yake ndiye ambaye hakuwa mshirikina!

65

Mikesha ya Peshawar

KUWAOMBA MAIMAMU SIO KUWAABUDU WAFU.


Sasa napenda kumjibu Mheshimiwa Hafidh, ambaye amesema kwamba maombi mbele ya makaburi ya Maimam ni sawa sawa na kuwaabudu wafu. Unauliza kwa nini Mashia wanaomba msaada kwenye makaburi ya Maimam. Pengine unaamini kwamba hakuna maisha baada ya kifo na unasema: Kilicho kufa kimeangamia moja kwa moja. Allah (s.w.t.) anaelezea katika Qurani Tukufu mawazo potovu haya, Anasema:

Hakuna ila maisha yetu haya ya dunia, tunakufa na kuishi, basi, wala sisi si wenye kufufuliwa. (23:37). Kama mjuavyo nyote, wale wanaoamini katika Allah wanajua kwamba kuna maisha baada ya kifo. Wakati mwanadamu akifa, mwili wake unakuwa hauna uhai, lakini, tofauti na wanyama, roho na hisia ya kusema hubakia katika viwiliwili vilivyo sawa na hivi, lakini halisi zaidi na watarehemiwa au kuadhibiwa katika hali ya mpito (barzakh) au mahali pa mateso. Mashahidi na wale waliouawa katika njia ya Allah watafurahia neema maalum. Hii imesimuliwa katika Qurani Tukufu: Na usiwadhanie wale waliouawa katika njia ya Allah kuwa ni wafu; bali wahai na wanaruzukiwa kwa Mola wao, wanafurahia aliyowapa Allah kwa fadhila zake, na wanafurahia kwa hilo hilo wale ambao wameachwa nyuma yao, bado hajajiunga nao; ya kwamba haitakuwa hofu juu yao wala hawatahuzunika. (3: 169-170). Ninatafakari juu ya maneno haya: Wahai (na) wanaruzukiwa kwa Mola wao (3: 169) Wao wanatujibu, lakini kwa vile kusikia kwetu kumefunga kwa mapazia ya ulimwengu wa kimaada hatusikii sauti zao. Kwa ajili hiyo katika salaam (ziarat) kwa Imam Husein, tunasema; Ninashuhudia kwamba unasikia ninayosema na kwamba unajibu. Je, umesoma Khutuba na 85 katika Nahjul-Balagha? Kizazi cha Mtume wametambulishwa kama ifuatavyo: Enyi watu huu ni usemi wa Mtume: Yeyote anayekufa miongoni mwetu sio mfu, na yeyote ambaye anaoza (baada ya kufa) kutoka miongoni mwetu kwa hakika haozi. (Nahjul-Balaghah Tarjuma ya Kiingereza, Juz. 1, uk. 130 iliyochapishwa na Peer Muhammad Ebrahim Trust, Karachi.) Hivyo ni kwamba, katika uwanja wa mwanga na mambo ya Kiroho, Ahlul-Bait wanaishi na wanabakia wenye kudumu milele. Kwa ajili hiyo, Ibn Abil-Hadid Mutazali na Sheikh Muhammad Abdul, Mufti mashuhuri wa Misri, wakisherehesha hadith hiyo hapo juu, wanasema kwamba, dhuria wa Mtume

66

Mikesha ya Peshawar
(s.a.w.w.) hawakufa kwa namna walivyokufa wengine. Hivyo tunaposimama mbele ya makaburi ya Maimam, hatusimami mbele za wafu, na hatuzugumzi wafu. Tunasimama mbele za walio hai na kuzungumza na wanaoishi. Kwa ajili hiyo sisi sio waabuduo wafu. Tunamuabudu Allah. Je huamini kwamba Imam Ali, Imam Husain, na mashahidi wa Badr, Hunain, Uhud na Karbala walitoa muhanga maisha yao katika njia ya Allah kwa ajili ya haki? Je, hawakuwakabili madhalimu wa Kiquraishi, Bani Umayya, Yazid na wafuasi wake, ambao lengo lao lilikuwa ni kuifulitia mbali Dini. Kama vile ule uimara wa masahaba wa Mtume na mihanga ya mashahidi wa Badri, Hunain, na Uhud ulivyopelekea kushindwa kwa ukafiri, kwa njia hiyo hiyo uamuzi imara wa Imam Husain kutoa mhanga maisha yake, uliimarisha Uislamu. Kama Imam asingesimama imara dhidi ya nguvu za uovu, mwana kulaaniwa Yazid angeuharibu Uislamu na angeweza kupenyeza ukafiri wake katika Umma wa Kiislamu. Sheikh: Inashangaza kwamba, unamwita Khalifa wa Waislamu Yazid bin Muawiya kuwa ni kafir. Yakupasa uelewe kwamba Muawiya bin Abu Sufyan alimchagua yeye kuwa Khalifa. Khalifa wa Pili Umar bin Khattab na Khalifa wa tatu Uthman aliyedhulimiwa, walimchagua Muawiya kuwa Amir (Gavana) wa Syria. Kwa sababu ya uwezo na vipaji vyao, watu waliwakubali kuwa Makhalifa kwa uaminifu kabisa. Hivyo uhusishaji wako wa makhalifa wa Uislamu kuwa ni makafiri una maana kwamba hukuwatukana tu Waislamu wote ambao wamewakubali kama makhalifa, bali vile vile umewatukana Makhalifa waliopita ambao wamewaidhinisha wao kuwa makhalifa au magavana. Kwa kweli walifanya makosa, ambayo yalitokea wakati wa ukhalifa wao. Mjukuu wa Mtume, Imam Husain, aliuwawa, lakini hili lilisamehewa. Kwa vile walitubia, Allah Mwingi wa rehema, aliwasamehe. Imam Ghazali na Damiri wameshughulika na nukta hii kwa uangalifu kabisa katika vitabu vyao na wamethibitisha usafi wa khalifa Yazid. Muombezi: Kamwe sikutaraji kwamba ushabiki wako utakwenda mbali kiasi hicho mpaka kutetea kusudi la mlaaniwa Yazid. Unasema kwamba kwa vile wakubwa wao waliowatangulia waliona inafaa kuwafanya ma-Amir au watawala, basi Waislam wote iliwapasa wawakubali. Kauli hii haileti maana yoyote. Tunasema kwamba Khalifa yapasa awe safi (aliyeepukana kabisa na madhambi yote) na kuteuliwa ki-Ungu ili kwamba tusije tukadumu katika ukandamizwaji. Unasema kwamba Ghazali na Damiri wametetea nafasi ya Yazid. Lakini walikuwa mashabiki kama ulivyo wewe. Hakuna mtu mwenye akili timamu ambaye atathubutu kamwe kujaribu kutetea matendo ya mlaaniwa Yazid. Unasema kwamba Yazid alifanya kosa katika kumuua Imam Husain. Lakini kumuuwa mtoto kipenzi mno wa Mtume, kuchanganya pamoja na watu 72, wakiwemo watoto wadogo na wazee, na kuwachukua mateka mabinti wacha-Mungu wa Mtume vichwa wazi na nyuso wazi, haikuwa kosa la hivi hivi tu. Ulikuwa ni ukatili usiosemeka. Aidha, jinai zake hazikuishia kwenye chinja chinja hii ya kutisha peke yake. Kuna mifano mingi mingine ya ukafiri wake.

67

Mikesha ya Peshawar

UKAFIRI WA YAZID.
Miongoni mwa mambo yanayothibitisha ukafir wa Yazid ni beti zake mwenyewe za kishairi. Kwa mfano anaandika hivi: Kama kunywa (pombe) kunakatazwa katika dini ya Muhammad, basi na iwe hivyo; mimi nitaukubali Ukristo. Ni ulimwengu huu tu, kwa ajili yetu. Hakuna ulimwengu mwingine. Haipasi sisi kuzuiliwa starehe za ulimwengu huu. Beti hizi zinajitokeza katika mkusanyiko wa kazi zake za kishairi, na Abul-Faraj bin Jauzi ameyaandika katika kitabu chake Radd Alal-Mutaasibul-Anid. Anasema tena: Mwenye kututishia na hekaya za siku ya mwisho, muache afanye hivyo. Haya ni mambo ya uongo, yanayotunyima sisi starehe zote za sauti na muziki. Sibt Ibn Jauzi anaandika katika kitabu chake Tadhkira, uk. 748 kwamba, wakati dhuria wa Mtume walipoletwa Syria kama mateka, Yazidi alikuwa amekaa katika ghorofa ya pili ya kasri yake. Yeye alisoma beti mbili zifuatazo: Wakati machela za ngamia zilizobeba wafungwa zilipotokea, kunguru alilia (ndege mbaya katika Uarabu). Nilisema: Ewe Kunguru, kama ulie au usilie, nimelipa kisasi juu ya Mtume. Kisasi huelekeza kwenye ukweli kwamba, wazee wake na jamaa zake wa karibu waliuawa katika vita vya Badr, Uhud, na Hunain. Aliwachukulia kisasi cha vifo vyao kwa kuwaua watoto wa Mtume. Ushahidi mwingine wa Ukafir wake ni kwamba alipofanya hafla ya kusherehekea Shahada ya Husain, alisoma beti za Kikafir za Abdullah bin Uzza Bari. Sibt Ibn Jauzi, Abu Raihan, na wengine wameandika kwamba Yazid alitamani wazee wake wangekuwepo, ambao wote walikuwa makafir, na waliuawa katika vita vya Badr kwa amri ya Mtume. Yazid alisema: Natamani watu wa ukoo wangu ambao waliuawa huko Badr, na wale ambao wamewaona watu wa ukoo wa Khazraj wakilia ( katika vita ya Uhud) kwa ajili ya majeraha ya michomo mikali (ya panga, mikuki na mishale), wangekuwa hapa. Wangelinishangilia kwa sauti na kusema: Ewe Yazid mikono yako kamwe isipooze, kwa sababu nimewauwa wakuu wa ukoo wake( yaani ukoo wa Mtume). Nimefanya hivyo kama kisasi cha Badr, ambacho sasa kimekamilika. Bani Hashim walicheza mchezo tu na serikali. Hakukuja ujumbe kutoka kwa Allah, wala ufunuo wowote. Nisingekuwa wa familia ya Khandaq

68

Mikesha ya Peshawar
kama nisingechukua kisasi juu ya dhuria wa Mtume. Tumeyalipa kisasi mauaji yaliyofanywa na Ali kwa kumuuwa mtoto wake, mpanda farasi na simba mwerevu.

RUHUSA YA KUMLAANI YAZID ILIYOTOLEWA NA MAULAMAA WA KISUNNI.


Wengi wa Maulamaa wenu wanamuona Yazid kama kafiri. Hata Imam Ahmad bin Hanbal na Maulamaa wengine wengi wakubwa wa madhehebu yenu wameshauri kwamba laana juu yake zinapaswa kuelezwa. Abdur-Rahman Abul-Faraj bin Jauzi ameandika kitabu juu ya somo hili, Kitabul-Radd Alal-Mutaasibul-Anidul-Manian Lan-e-Yazid Lanatullah. Ni Maulamaa mashabiki wachache tu wa madhehebu yenu, kama Ghazali, wameonyesha upendeleo kwa Yazid, na wamebuni makinzano yasiyo na maana kwa ajili ya kumtetea. Hata hivyo, wengi wa Maulmaa wenu, wameiona tabia yake isiyo ya kidini na ya kidhalimu. Muslim anasema kwamba, kama Khalifa; Yazid alidiriki kuiangamiza dini, Masudi katika kitabu chake Murujuz-Dhahab, Juz. 2, anasema kwamba tabia ya Yazid ilikuwa sawa na ile ya Firauni, lakini ni kwamba Firauni alikuwa muadilifu zaidi kwa watu wake kuliko alivyokuwa Yazid. Utawala wa Yazid ulileta fedheha juu ya jina zuri la Uislam. Uovu wake ulikuwa ni pamoja na kunywa pombe, kumuua mtoto wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kumlaani mshika Makamu wa Mtume Ali, kubomoa nyumba ya Allah (Masjidul-Haram) na mauaji ya halaiki. Amefanya uhalifu usiohisabu dhidi ya Sheri ah ya dini, na dhambi ambazo hazisameheki. Nawab: Yazid alihusika vipi na mauwaji ya halaiki? Muombezi: Wanahistoria wengi wamelisimulia jambo hili. Sibt Ibn Jauzi katika kitabu chake Tadhkira uk. 63, anasema kwamba baadhi ya watu wa Madina walikwenda Syria katika Mwaka wa 62 A.H. Walipoyagundua matendo maouvu ya Yazid walirudi Madina na kuvunja kiapo cha utiifu kwake, wakamlaani, wakamfukuza, gavana wake, Uthman bin Abi Sufyani. Abdullah bin Hanzala ( Ghusilul-Malaikat) alisema: Enyi watu, hatukuasi dhidi ya Yazidi mpaka tulipothibitisha kwamba si mtu mwenye kufuata dini. Aliua watoto wa Mtume, alnajihusisha kinyume na sheria na mama zake, binti zake, na dada zake, anakunywa pombe, na hajishughulishi na ibada ya Sala. Habari hizi zilipomfikia Yazid, alituma jeshi kubwa la watu wa Syria chini ya Mulsim bin Uqba dhidi ya watu wa Madina. Mauaji ya Waislamu yaliendelea kwa muda wa siku tatu. Jeshi la Yazidi liliua watu 700 waungwana wa Kikuraish, Muhajirina, na Ansar, na watu 10,000 wa kawaida. Naona aibu kusema jinsi Waislamu walivyonyanyaswa. Nitanukuu

69

Mikesha ya Peshawar
kifungu kimoja tu katika Tadhkira, ya Sibti Ibn Jauzi uk. 163, kilichosimuliwa na AbulHasan Madaan: Baada ya mauwaji ya halaiki ya watu wa Madina, wanawake 1000 wasiolewa walizaa watoto.

JE, YAZID ANAPASWA KULAANIWA?


Sheikh: Madai haya yanaonyesha madhambi yake. Madhambi yanasameheka na yanaweza kufidiwa, na Yazid alionyesha hali ya kutubia. Allah ambaye ndiye Mwenye kusamehe madhambi amemsamehe. Basi kwa nini wakati wote unamlaani na kumuita muovu? Muombezi: Baadhi ya mawakili hubishana juu ya kesi ya wateja wao mpaka dakika ya mwisho kwa sababu wamepokea malipo kutoka kwao, ingawaje wanaelewa vizuri ustahili wa kesi yenyewe. Lakini nashindwa kuelewa kwa nini unapendelea mno kumtetea Yazid, mbele ya mauaji yake ya watoto wa Mtume wa Allah na kuwaua kwake watu wa Madina. Aidha, maelezo yako kwamba alionyesha kutubia hayathibitiki. Je kukataa kwake misingi muhimu ya Uislamu siku ya ufufuo, Wahyi na Utume hakustahili laana yetu kwake? Je, Allah hakuwalaani madhalimu? Kama hoja hizi hazitoshi kwa mawakili wa Yazid bin Muawiya, kwa ruhusa yako nitanukuu hadith kutoka kwa Maulamaa wenu maarufu. Bukhari na Muslim katika Sahih zao, Allama Samhudi katika Tarikhul-Madina, Abul-Faraj bin Jauzi katika Kitabur-Radd Alal-Mutaasibul-Anid, Sibt Ibn Jauzi katika Tadhkira-e-Khawasul-Umma, Imam Ahmad bin Hanbali katika Musnad na wengine wanamnukuu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema: Kama mtu yeyote atawatishia na kuwaonea watu wa Madina, Allah atamtishia (yaani Siku ya Malipo). Atalaaniwa na Allah, Malaika, na wanadamu wote. Na katika Siku ya Malipo, Allah hatayakubali matedno yake yoyote. Vilevile Mtume amesema: Laana iwe juu ya yule mwenye kuutishia mji wangu (watu wa Madina). Je, mauaji haya ya halaiki hayakuwatishia wale watu wa Madina? Kama yalifanya basi kubali pamoja na Mtume, Malaika na watu wote kwamba yule mfanya mauovu mbaya alilaaniwa na atakuwa akiendelea kulaaniwa mpaka Siku ya Kiyama. Wengi wa ulamaa wenu wamemlaani Yazid. Abdullah bin Muhammad bin Amir Shabrawi Shafii katika Kitabul-Ittihaf bi Hubbil Ashraf Rajiba Lan-e-Yazid uk. 20, anaandika kwamba wakati jina la Yazid lilipotajwa mbele ya Mulla Sad Taftazan, yeye alisema: Laana iwe juu yake na wafuasi na wasaidizi wake. Allama Samhudi katika kitabu chake Jawahirul-Iqdain ananukuliwa akisema; maulamaa kwa ujumla wamekubaliana kwamba, inaruhusiwa kumlaani aliyemuua Imam Husein, au aliyetoa amri ya yeye kuuliwa, au yule aliyeridhia mauaji yake, au yule aliyekubali kuuliwa kwake.

70

Mikesha ya Peshawar
Ibn Jauzi, Abu Yala na Salih bin Ahmad, wakihoji kutoka kwenye Aya za Qurani wanaandika kwamba: Imethibitika kwamba imeruhusiwa kumlaani Yazid. Ni wajibu wa Waislamu wote kwamba yawapasa kujua haki alizonazo Imam Husein juu yao. Na ni vipi, kwa nguvu ya kupatwa kwake na mateso ya udhalimu na uonevu, yeye alivyounyweshea mti wa Uislamu kwa damu yake mwenyewe na damu ya familia yake. Vinginevyo, mti ule uliobarikiwa ungekufa kwa sababu ya udhalimu wa Bani Umayyah. Alikuwa ni Husain ambaye aliupatia Uislamu uhai mpya. Nasikitika kwamba badala ya kuitambua huduma hii ambayo watu hawa watukufu wameitoa kwa Uislamu, mnazua makinzano kuhusu wafanya ziara ambao wanazuru makaburi yao na kuwaita wenye kuabudu wafu. Mara nyingi tunasoma kwamba katika sehemu muhimu za nchi, kama Paris, London, Berlin, na Washington kuna makaburi ya kumheshimu Askari asiyejulikana. Inasemekana kwamba, kuteseka kwa uonevu wa adui na kwa kuihami nchi yake, alijitoa muhanga maisha yake. Lakini hakukuwa na alama juu ya mwili wake au nguo kuonyesha utambulisho wa familia yake au mji anakotoka. Kwa sababu alitoa maisha yake kwa ajili ya kuitetea nchi yake, ingawaje alikuwa hajulikani, alistahiki heshima. Wakati mfalme au mtu yeyote mashuhuri anapotembelea miji hii, huzuru hilo kaburi la Askari asiyejulikana na kuweka mashada ya maua juu yake. Askari asiyejulikana anapata heshima zaidi, lakini nasikitika kwamba, badala ya kuwaheshimu wafanya Ziara wanaozuru makaburi ya wanachuoni Waislamu wacha-Mungu sisi tunawashutumu. Baadhi yao waliijua Qurani yote kwa moyo. Walitoa mhanga maisha yao kuutetea Uislamu. Watu hawa ni pamoja na mawakala (wadhamini) wa Allah, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na dhuria wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) .

KUVUNJWA HESHIMA YA MAKABURI:


Baadhi ya Waislamu wameyabomoa kabisa makaburi kama hayo na wakapika chai juu ya masanduku yaliyopangwa juu ya makaburi hayo. Tukio kama hilo lilitokea mwaka wa 1216 A.H. katika Siku ya Iddil-Ghadir, wakati wengi wa wakazi wa Karbala huenda Najaf kwa ajili ya ziara. Ma-Wahhabi wa Najaf waliishambulia Karbala na wakawauwa Mashia. Wakayabomoa makaburi ya wale waliotoa mhanga maisha yao kwa ajili ya Uislamu. Karibu wakazi 5,000 wa Karbala, ikiwa ni pamoja na Maulamaa, wazee, wanawake, watoto, waliuawa. Hazina ya Imam Husain iliporwa na vito vya thamani, taa za dhahabu, na mazulia ya thamani yalichukuliwa. Sanduku la thamani lililokuwa juu ya kaburi hilo lilichomwa moto na chai ikapikwa juu yake. Watu wengi walichukuliwa kama wafungwa. Ole kwa Waislamu kama hao!

71

Mikesha ya Peshawar
Masikitiko yalioje kwamba katika nchi zote zilizostarabika, makaburi ya wafalme, wanachuo, na hata askari wasiojulikana yanaheshimiwa, lakini Waislamu ambao wanategemewa kuonyesha hisia nzuri za umuhimu wa kuhifadhi makaburi, ya wale ambao ni fahari yao, huyapora na kuyabomoa kama washenzi. Katika mji wa Makka na Madina, Wahhabi walibomoa makaburi ya mashahidi wa Uhud, pamoja na la Hamza, na jadi zake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kama Abdul-Muttalib, Abdullah, na wengineo. Vile vile walibomoa makaburi ya familia ya Mtume, watoto wake, kama Imam Hasani, Imam Zainul- Abidin, Imam Muhammad Baqir, Imam Jafar Sadiq, Bibi Fatima binti ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na wengi wengine wa ukoo wa Bani Hashim na Maulamaa watukufu. Bado wanajiita wao ni waislamu. Hakika wao wanajenga ma-Quba makubwa kwa ajili ya watu wao mashuhuri na wafalme. Ukweli ni kwamba, Maulmaa wa madhehebu zote wamenukuu hadithi nyingi zikitutaka tuzuru makaburi ya waumini ili kwamba yasalimike kutokana na kuharibika. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe alizuru makaburi ya waumini na akamuomba Allah kwa ajili ya wokovu wao.

DHURIA WA MTUKUFU MTUME (s.a.w.w.) NI MASHAHIDI KATIKA NJIA YA ALLAH NA WAKO HAI
Je, Unafikiri familia ya Mtume iliyotukuka ambao walitoa maisha yao katika njia ya dini ni mashahidi? Kama utasema sio mashahidi, ni nini hoja yako? Kama ni mashahidi, vipi utawaita kuwa wao, ni Wafu? Qurani Tukufu inaeleza kwamba;

Wako hai ( na) wanaruzukiwa na Mola wao. (3:169). Hivyo kwa mujibu wa Qurani na hadith, watu wale watukufu wako hai, Hivyo, sisi sio waabudu wafu. Hatuwasalimii wafu, tunawatukuza walio hai. Na hakuna Shia yoyote, msomi au asiye msomi, ambaye anawafanya wao kama waondoaji wa matatizo moja kwa moja. Huwachukulia kama waja wacha Mungu na njia ya kufikisha kwa Allah. Tunaweka mahitaji yetu mbele za Maimam wanyofu ili kwamba wamuombe Allah atuhurumie waja wake. Wakati tukisema, Ewe Ali, nisaidie, Ewe Husain, nisaidie ni kama tu, mtu ambaye anataka kumfikia Mfalme. Anaweza kwenda kwa waziri Mkuu na kuomba amsaidie. Hakika hamfanyi waziri mkuu huyo wa kama kimbilio la mwisho kwa kuondoa matatizo yake. Kusudio lake pekee ni kumfikia mfalme kupitia kwake, kwa vile kwa kutokana na cheo chake, anaweza kuonana na mfalme kwa urahisi sana. Shia hawawachukuli dhuria wa Mtume kama washirika katika vitendo vitukufu; wanawachukulia wao kama waja Wake wacha-Mungu.

72

Mikesha ya Peshawar

DARAJA YA MAIMAMU MASUMIN


Kwa vile ni wawakilishi wa Mwenyezi Mungu wanawakilisha mahitaji ya shida zao Kwake. Kama ombi linastahili, Yeye hulikubali. Vinginevyo, jazaa yake itatolewa kesho akhera. Nukta moja haipasi kuachwa bila maelezo: Mashia wanachukulia cheo cha Maimam Masum kama cha juu kuliko mashahidi wengine wa Uislamu. Hafidh: Taarifa hii inahitaji maelezo. Ni tofauti gani kati ya Maimam wenu na Maimam wengine wote isipokuwa tu kwamba wao wana uhusiano na Mtume? Muombezi: Kama utaitazama nafasi ya Uimam, utoana tofauti iliyowazi kati ya dhana ya Uimam inavyochukuliwa na Mashia na ile ya Masunni.

MKUTANO WA NNE JUMAPILI USIKU 26 RAJAB; 1345 A.H Mjadala kuhusu Uimamu:
Muombezi: Ninyi watu wema mnayo habari kwamba neno Imam lina maana nyingi. Kilugha lina maana ya Kiongozi. Imam al-Jamaat maana yake ni yule mwenye kuongoza Sala za Jamaa. Anaweza pia kuwa kiongozi wa watu katika mambo ya siasa au ya kiroho. Imam al-Juma maana yake ni yule mtu mwenye kuongoza sala ya Ijumaa. Kwa hiyo, Sunni wafuasi wa madhehebu nne na sheria, wanawaita viongozi wao Maimam kama vile Imam Abu Harifa, Imam Maliki, Imam Shafii, na Imam Hanbal. Wana-itiqadi na mafaqihi hawa ni viongozi wao katika mambo ya dini na wameweka Sheria za dini kwa mujibu wa utafiti wao au kwa mujibu wa kukisia kwao kuhusu uhalali wa matendo. Kwa hiyo wakati tunapovichunguza vitabu vya Fiqih vya Maimamu hawa wanne, tunakuta tofauti nyingi miongoni mwao zinazohusu misingi ya imani na Kanuni za utekelezaji wa imani. Halikadhalika Madhehebu yote yana viongozi kama hao, na miongoni mwa Mashia, maulamaa na mafuqahaa wanashikilia nafasi kama hizo hizo. Kwa kutoweka kwa Imam wetu wa zama aliye hai, wao wanatoa matamko ya kisheria kwa kutegemea elimu yao ya Qurani Tukufu, Hadithi sahihi za Mtume, na Maimamu wa kitume. Lakini hatuwaiti Maimamu kwa sababu Uimam ni wa washika makamu (wa Mtume) kumi na wawili peke yao - dhuria wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kuna tofauti nyingine, Sunni baadae walifunga mlango wa ijtihad (juhudi ya kutafsiri sheria). Kuanzia karne ya tano A.H wakati ambapo, kwa amri ya Mfalme, maoni yaliyoelezewa na Maulamaa na Mafuqhaa yalikusanywa, huu uitwao uimamu uliishilizwa kwa maimamu wanne. Na madhehebu manne

73

Mikesha ya Peshawar
(Hanafi, Maliki, Shafii, na Hanbali) yakaanzishwa. Watu walilazimishwa kufuata kati ya moja ya hiyo, kama ilivyo desturi kwa wakati huu wa sasa. Haijulikani ni kwa misingi ipi kumfuata Imam mmoja kunapendekezwa. Sifa gani Imam wa Mahanafi alizonazo ambazo Imam wa Maliki hanazo? Ni sifa gani alizonazo Imam wa Shafii alizonazo ambazo Imam wa Hanbal hana.Na kama ulimwengu wa Kiislamu utalazimishwa wenyewe kufungwa kwenye kufuata moja ya Madhehebu manne, basi maendeleo ya Jumuiya ya Kiislamu yatakuwa yamefungwa kabisa, ingawaje kwamba Uislamu hutufundisha kwamba yatupasa kusonga mbele pamoja na nyakati. Iufanya hivi, tunahitaji uongozi wa Maulamaa. Kuna mambo mengi ambayo haitupasi kufuata hukumu ya Mujtahidi aliyekufa. (Kuanzia Jihad, kujitahidi, humaanisha katika hali hii, mtu anayejitahidi kutafsiri na kuunda taratibu na Sheria, kwa vile Ijtihad inahusika kwenye njia ya kujitahidi), bali inapasa kumgeukia mujtahid aliye hai kwa ajili ya kupata mwongozo. Mujitahidi wengi wamezaliwa baadae miongoni mwenu, ambao walikuwa na cheo cha juu katika elimu kuliko wale Maimam wanne. Sijui kwa nini upendeleo unatolewa kwa wale waliopita ili kwamba si wengine ila wao tu waweze kufuatwa na haki za wengine kupuuzwa. Katika fiqih ya Shia, Mujtahid katika kila zama, mpaka wakati wa kujitokeza kwa Mtukufu Imam wa zama zetu, wao wanayo haki ya kufanya jitihada. Katika kuhusu matatizo mapya, hatuwezi kufuata hukumu ya Mujtahid aliyekufa.

KUWEKA MIPAKA KWENYE MADHEHEBU MANNE HAKUNA MSINGI.


Ni ajabu kwamba mnawaita Mashia wazushi na waabudu wafu. Wao wanafuata amri za Maimamu kumi na wawili, dhuria wa Mtume (s.a.w.w.). Aidha haijulikani ni kwa misingi ipi mnajaribu kuwalazimisha Waislamu wawafuate Ashariyya au Mutazala kuhusiana na msingi (Usul) ya imani na mmoja kati ya Maimamu wanne katika sheria za matawi (Furu) ya imani. Wale ambao hawawafuati wanaitwa marafidhi. Kwa vile Abul-Hasan Ashari, Abu Hanifa, Malik bin Anas, Muhammad bin Idris Shafii, na Ahmad bin Hanbali walikuwa sawa na Maulamaa na mafaqihi wa Kiislamu wengine wengi, na kwa vile hakuna amri kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ya kuwafuata wao, mipaka ya kuwafuata wao tu yenyewe ni uzushi (bidaa). kama ningelileta madai haya, ungelisema nini katika kujibu? Hafidh: Kwa vile Maimamu hawa walikuwa wana daraja ya juu ya utii kwa Allah, uchaji, ukweli, na uadilifu, pamoja na elimu kubwa mno ya Fiqih imekuwa lazima kwetu sisi kuwafuata.

74

Mikesha ya Peshawar
Muombezi: Hatulazimiki na mantiki kujifunga sisi wenyewe kuwafuata wao peke yao. Wengi wa Maulamaa wenu wengine walikuwanazo sifa sawa kama hizi. Mpaka wa kuwafuata wao peke yao ni kebehi kwa Maulamaa wengine wenye sifa sawa na zao. Hatuwezi kulazimishwa kufuata mtu mmoja yeyote au watu wengine bila maelekezo ya kimamlaka kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Hakuna ruhusa kama hiyo kutoka kwa Mtume kuhusu Maimamu wenu wanne. Basi vipi muiwekee dini mpaka (kizuizi) kwenye madhehebu haya manne tu?

USHIA KULINGANISHWA NA MADHEHEBU MANNE.


Katika mikesha michache tu iliyopita uliyaita madhehebu ya Shia kuwa ni ya kisiasa na ukasema kwamba kwa vile hayakuwepo wakati wa Mtume - kwamba yalikujakuwepo wakati wa Ukhalifa wa Uthman - ilikuwa ni haramu kuyafuata. Usiku wa kabla ya jana tulithibitisha kwamba Ushia uliasisiwa wakati wa Mtume (s.a.w.w) kwa maelekezo yake mwenyewe. Kiongozi wa Mashia, Amirul-Muminin Ali alilelewa na kufundishwa na Mtume tangu utotoni na kupata elimu yake ya dini kutoka kwake. Kwa mujibu wa riwaya zilizomo kwenye vitabu sahihi vyenu wenyewe, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amemwita yeye Lango la Elimu. Kwa dhahiri kabisa alisema: Utii kwa Ali ni utii kwangu, na kutomtii Ali ni kutomtii mimi. Katika mkusanyiko wa watu 70,000 alimteua kuwa Amir na Khalifa, na akawaamrisha Waislamu wote, wakiwemo Umar na Abu Bakr, kula kiapo cha utii kwake. Lakini haifahamiki ni vipi madhehebu yenu Manne yalivyokuja kuanzishwa, wala ni yupi kati ya Maimamu wanne aliyemuona Mtume au kama kuna ruhusa yoyote iliyosimuliwa kutoka kwa Mtume kuhusu wao ili angalau kuweza kueleza ni kwa nini Waislamu waweze kulazimika kuwafuata wao. Bila sababu za kukufungeni mnawafuata wakubwa zenu na hamusemi chochote cha kupasisha Uimamu wao isipokuwa tu kwamba walikuwa mujtahid wakubwa, watu wenye elimu na uchamungu. Lakini, ikiwa sifa hizi zipo kwa kiwango cha juu sana katika kizazi cha Mtume, hivyo basi sio wajibu kwetu sisi kuwafuata wao? Hivi hizi madhehebu zisizo na kiungo na Mtume ndio za uzushi au Madhehebu iliyoasisiwa na Mtume na kuongozwa na dhuria wake ndiyo ya uzushi? Katika njia hiyo hiyo, kuna Maimamu wengine kumi na mmoja, ambao kuhusu wao kuna Hadithi mbali mbali zinazoonyesha kwamba wao ndio wanaolingana na Qurani Tukufu. Katika Hadith al-Thaqalain imeelezwa wazi kwamba: Yeyote ambaye atashikamana na viwili hivi ataokolewa na yule ambaye atakaa mbali navyo amepotea. Katika HadithusSafina. Mtume (s.a.w.w.) alisema: Yule ambaye hukaa mbali navyo ataangamia na kupotea. Ibn Hajar katika Sawaiq (Bab-e-Wasiyyatun Nabi, uk. 135) ananukuu

75

Mikesha ya Peshawar
hadithi kutoka kwa Mtume isemayo kwamba: Qurani na dhuria wangu ni dhamana zangu; kama mtashikamana wenyewe kwenye viwili hivi, kamwe hamtapotea. Kwa kuliunga mkono hili, Ibn Hajar ananukuu hadithi nyingine kutoka kwa Mtume kuhusu Qurani Tukufu na dhuria wake watoharifu: Msivuke mipaka ya Qurani na dhuria wangu; wala msiwapuuze. Vinginevyo mtaangamizwa. Na msiwafundishe dhuria wangu kwa vile wao wanajua zaidi kuliko mlivyo ninyi. Baada ya hivi, Ibn Hajar akatoa maelezo kwamba, hadithi hizo hapa juu huthibitisha kwamba dhuria wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni bora kuliko wengine wote katika elimu na katika kutekeleza wajibati za kidini.

MAIMAMU WANNE WA KISUNNI WAMETANGAZANA KUWA MAKAFIRI.


Walakini hata hivyo, inashangaza kwamba, pamoja na kujua kwamba dhuria wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni wabora kuliko wengine wote, Masunni wanamfuata Abul Hasan Ashari katika misingi ya dini na Maimamu wanne katika kanuni za utekelezaji wa Imani. Kufuata mwenendo huo ni kwa sababu ya ushabiki na kiburi. Na hata kama tukijaalia kuwa usemayo ni kweli, kwamba Maimamu wenu wanne wana haki ya ninyi kuwakubali kwa sababu walikuwa wanachuo na wachamungu, basi kwanini kila mmoja wao akamlaumu mwengine kwa ukafiri? Hafidh: Wewe umkali sana. Unasema kila kinachokuja kwenye akili. Unawasingizia Maimamu wetu. Maelezo haya ni ya uwongo. Kama kuna kilichosemwa dhidi yao, ni kutoka kwa Maulamaa wa Kishia. Kutoka upande wetu hakuna chochote kilichosemwa dhidi yao. Tumeonyesha heshima kwao. Muombezi: Ni dhahiri wewe hukusoma vitabu vya Maulamaa wako. Maulamaa wenu maarufu wenyewe wameandika vitabu vinavyohusu kukataa kwao. Hata hawa maimamu wanne wameshutumiana wenyewe kwa wenyewe kwa kukiuka sheria za dini. Hafidh: Maulamaa hao ni akina nani? Nini maelezo yao? Muombezi: Masahaba wa Abu Hanifa, Ibn Hajar (Ali bin Ahmad Andalusi aliyekufa 456 A.H.), na wengine wamekuwa kila mara wakiwasuta Imamu Maliki na Muhammad bin Idris Shafii. Kadhalika wafuasi wa Imam Shafii, kama Imamul-Haramain, Imam Ghazali na wengine wamemshutumu Abu Hanifa na Malik. Hebu ngoja nikuulize kitu:

76

Mikesha ya Peshawar
Hawa walikuwa watu aina gani Imam Shafii, Abu Hamid bin Muhammad Ghazali, na Jarullah Zamakhshari? Hafidh: Walikuwa Mafuqaha wakubwa, wanachuo wasomi, watu wachamungu, na Maimamu wetu.

SHUTUMA ZA MAULAMAA WA KISUNNI KWA ABU HANIFA:


Muombezi: Imam Shafii amesema: Hajapata kuzaliwa mtu wa kuchukiza katika Uislamu kama Abu Hanifa. Vilevile amesema: Nimeangalia katika vitabu vya wafuasi wa Abu Hanifa, na nikaona mna kurasa 130 zenye mambo yenye kukinzana na Qurani Tukufu na Sunna. Abu Hamid Ghazali katika kitabu chake Manqul-fi Ilmil-Usul anasema: Kwa hakika Abu Hanifa amepotoa kanuni ya dini, kaifanya njia yake kuwa ya mashaka, amebadilisha mpangilio wake, na amechanganya sheria katika hali ambayo kanuni iliyoelezwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) imeharibika kabisa. Mtu mwenye kufanya hivyo makusudi na kuiona hiyo kuwa ni halali; ni kafiri. Mtu mwenye kuifanya na hali akijua, ni fasiq. Kwa mujibu wa Mwanachuo huyu mkubwa, Abu Hanifa alikuwa ama yeye ni kafir au fasiq. Vitabu vingi vingine vinamshutumu Abu Hanifa. Jarullah Zamakshari, mwandishi wa Tafsirulal-Kashshaf na mmoja wa Maulamaa wenu wachamungu, anaandika katika Rabiul-Abrar kwamba Yusufu bin Asbat alisema: Abu Hanifa alizikataa karibu Hadith 400 za Mtume wa Uislamu. Yusufu akaeleza kwamba: Abu Hanifa alisema: Lau Mtume wa Uislamu angenifahamu, mengi ya maneno yangu angeyakubali. Maulamaa wenu wenyewe wametoa shutuma za namna hiyo kwa Abu Hanifa na kwa hao Maimamu wengine watatu. Zinaweza kupatikana katika Mutahawwal cha Ghazali, Nuqtush-Sharifa cha Shafii, Rabiul-Abrar cha Zamakhshari, na Muntazim cha Ibn Jauz. Imam Ghazil anasema katika Mutahawwal yake: Kuna makosa mengi katika vitabu vya Abu Hanifa. Hakuwa na elimu ya balagha, nahau, au hadith. Vilevile anaandika: Kwa vile hakuwa na elimu ya hadith, alitegemea juu ya kukisia mwenyewe. Kiumbe wa kwanza aliyetenda kwa kukisia alikuwa ni Shetani. Ibn Jauzi anaandika katika Muntazim yake: Ulamaa wote wameungana katika kumshutumu Abu Hanifa. Kuna Makundi matatu ya wakosoaji kama hao: kundi moja linashikilia kwamba imani yake katika misingi ya Uislamu ilikuwa haina uhakika; kundi lingine linasema kwamba, hakuwa na kumbukumbu imara na hakuweza kukumbuka hadith; kundi la tatu linaamini kwamba alitenda kwa kukisia na kwamba maoni yake

77

Mikesha ya Peshawar
yalikuwa siku zote tofauti na hadith za kweli. Maulamaa wenu wenyewe wemewalaumu Maimamu wenu. Maulamaa wa Kishia hawakuwahusisha na chochote, isipokuwa kile Maulamaa wenu wenyewe walichosema kuhusu wao. Kwa upande mwingine, hakuna tofauti ya maoni miongoni mwa Ulamaa wa Kishia kuhusiana na nafasi za hao Maimamu kumi na mbili. Tunawaona Maimamu watukufu kama wanafunzi wa fundisho moja. Maimamu hawa - wote walitenda kwa mujibu wa sheria za Ki-Mungu ambazo yule mwisho wa Mitume aliwapa. Kamwe hawakutenda kwa kukisia au kuafiki uzushi. Walichosema au kufanya kilikubaliana na maneno ya Mtume. Hivyo, hakukuwa na tofauti miongoni mwao.

UIMAM KWA MUJIBU WA SHIA UNA MAANA YA UWAKILISHI WA ALLAH.


Kwa mujibu wa ufafanuzi uliotolewa na Maulamaa, Uimamu au Uwakilishi wa Allah, ni moja ya misingi ya Uislamu. Tunaamini kwamba Uimamu ni uwakilishi wa Allah kwa viumbe wote na Khilafat-e-Rasul (Makamu/warithi wa Mtume) kwa ulimwengu huu na ujao. Kwa hiyo, ni wajibu kwa wanadamu wote kufuata wapangaji wake katika mambo yote, ya kidunia na hali kadhalika ya kiroho. Sheikh: Ingelikuwa vizuri kama usingelitamka kidhahiri kwamba Uimamu umeingizwa katika misingi ya imani, kwa vile Maulamaa wakubwa wa Uislamu wanakataa kuwekwa kwake humo. Umewekwa katika shuruti za matendo ya imani. Maulamaa wenu wameufanya sehemu ya misingi. Muombezi: Maelezo yangu haya, hayakomei kwenye Imam wa Mashia tu. Hata Maulamaa wenu wakubwa wanayo imani kama hiyo. Mmoja wao ni mfasiri wenu mashuhuri Qadhi Baidhawi, ambaye anasema katika kitabu chake Minhajul-Usul kuhusiana na mjadala juu ya masimulizi ya Hadithi: Uimamu ni moja ya kanuni za msingi za imani, ambazo kuzikataa na ukinzano juu yake hupelekea kwenye ukafir na uzushi. Mulla Ali Qushachi anasema katika kitabu chake Sharh-e-Tajrid. Uimamu kwa jumla ni Uwakala wa Allah kwa mambo yote ya ulimwengu huu na dini, kama Ukhalifa wa Mtume. Na Qadhi Ruzbahan, mmoja wa washupavu mno (Shabiki) wa Maulamaa wenu anaashiria kwenye maana hiyohiyo. Anasema: Uimamu kwa mujibu wa wafuasi wa Abul-Hasan Ashari ni uwakilishi wa Mtume wa Uislamu kwa ajili ya kuimarisha imani na kulinda salama maslahi ya Jumuiya ya Kiislamu. Wafuasi wote wanafungwa katika wajibu wa kufuata maamrisho yake. Ungekuwa Uimamu sio sehemu ya shuruti za matendo ya imani, Mtume asingesema kwamba: Yeyote yule anayekufa bila kujua Imamu wake wa zama, anakufa kifo cha kijahilia.

78

Mikesha ya Peshawar
Hii imenukuliwa na Maulamaa wenu maarufu, kama Hamidi katika Jami-BainusSahihain na Mulla Sad Taftazani katika Sharhe Aqaid-e-Nasafi. Kutoelewa sharti hata moja la utekelezaji wa imani hakuwezi kuwa sawa na ujinga ulioelezwa na Baidhawi kuhusu kutokujua misingi, yaani kwamba ujinga wake ni sababu ya ukafir. Kwa hiyo Uimamu ni moja ya misingi ya imani na ni hatua ikamilishayo Utume. Kwa ajili ya hiyo, kuna tofauti kubwa kati ya dhana ya Uimamu wetu na ile inayotafsiriwa na ninyi. Mnawaita Maulamaa wenu Maimamu, kama vile Imam Adhma, na Imam Maliki. Lakini hii ni maana ya mdomo. Sisi pia tunatumia neno Imam-e-Jumaa, Imam-e-Ja-maat. Hivyo wanaweza wakawepo mamia ya Maimamu kwa wakati mmoja, lakini katika maana ya kitaalamu (kiistilahi) ambayo kwayo tunatumia neno Imam, ina maana muwakilishi wa Allah. Katika maana hii kuna Imam mmoja tu kwa wakati mmoja. Sifa bora za elimu, Maadili, ushujaa, upenzi kwa Allah, na uchamungu zimekamilishwa ndani yake. Anawashinda binadamu wote katika tabia zote na hushikilia hali ya kutofanya makosa. Dunia haitakuwa bila Imam wa aina hiyo mpaka siku ya malipo. Imam wa ubora kama huo anakuwa katika kiwango cha juu kabisa cha mafanikio ya kiroho. Imam kama huyo anaidhinishwa na Allah na anateuliwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Hushinda viumbe wote pamoja na Mitume waliopita. Hafidh: Kwa upande mmoja unawashutumu Maghulat, na kwa upande mwingine wewe mwenyewe kiububusa unawasifu Maimamu na kuiona nafasi yao ya juu zaidi kuliko ile ya Mitume. Akili ya kawaida inalikataa hili, na Qurani Tukufu vilevile imeeleza kwamba Mitume wamewekwa katika nafasi ya juu zaidi. Nafasi yao iko baina ya uhuru wa ki-ungu na lile lenye kuwezekana. Kwa vile maelezo yako hayaungwi mkono na akili, hayawezi kukubaliwa.

CHEO CHA UIMAM NI JUU ZAIDI KULIKO CHA UTUME WA KAWAIDA.


Muombezi: Bado hujaniuliza ni kwa misingi ipi nimeyatoa maelezo haya, na kwa hiyo unasema ni ya bila hekima. Ushahidi mzuri kwa maelezo yangu ni Qurani Tukufu, ambayo ikizungumzia maisha ya Mtume Ibrahim, inasema kwamba, baada ya kumpa mitihani mitatu (ya maisha, mali, na watoto), Allah alikusudia kufanya cheo chake cha juu zaidi. Kwa vile Utume na Cheo cha Khalil (Rafiki) havikuruhusu dhahiri cheo cha juu, nafasi ya Uimamu ndiyo iliyokuwa nafasi pekee ya Cheo cha juu ambayo hata Mtume wa Allah anaweza kuaminishwa. Qurani Tukufu inasema: Na wakati Mola Wake alipomjaribu Ibrahim na maneno fulani, aliyatekeleza. Alisema:

79

Mikesha ya Peshawar

Hakika nitakufanya Imam wa watu. Ibrahimu akasema: Akasema ahadi yangu haiwafikii madhalimu. (2:124).

Na dhuria wangu?

Aya hii ambayo inaonyesha nafasi ya Uimamu, pia inathibitisha kwamba cheo cha Uimamu ni cha juu kuliko cha Utume. Kwa vile nafasi ya Mtume Ibrahimu ilinyanyuliwa kutoka Utume kwenda Uimamu. Hafidh: Hii ina maana, kwa mujibu wa maelezo yako, ni kwamba nafasi ya Ali ilikuwa ya juu kuliko ile ya Mtume wa Mwisho. Hivi ndivyo Maghulat walivyoamini, kama wewe mwenyewe ulivyokiri.

MITUME WA KAWAIDA NA WALE MAALUMU:


Muombezi: Sina maana ya hivyo ulivyohitimisha wewe. Kama ujuavyo kuna tofauti kubwa kati ya Utume wa kawaida na Utume maalumu. Cheo cha Uimamu ni cha juu zaidi kuliko cheo cha Utume wa kawaida, lakini kiko chini kuliko cha Utume Maalumu. Mtume wa mwisho ndiye kiwango cha hali ya juu cha utume maalum. Nawab: Nisamehe kwa kuingilia kwangu. Je; Mitume wote hawakutumwa na Allah? Hapana shaka wote wana cheo kile kile. Qurani Tukufu inasema: Hatutofautishi baina ya yeyote kati ya Mitume. (2:285). Basi kwanini umetofautisha baina yao na ukagawa Utume katika makundi mawili; kawaida na maalumu? Muombezi: Hakika, Aya hii ni kweli iko sawa sawa katika fuo lake. Yaani, kwa kiasi kufanikisha lengo la Utume kuhusikavyo (ambako kuna maana ya kufundisha watu kuhusu kuwepo kwa Allah. Siku ya Malipo na kuzifunza akili zao), Mitume wote kutoka Adamu mpaka mwisho wa Mitume, wako sawa. Lakini wanatofautiana katika sifa, mafanikio na cheo.

TOFAUTI KATIKA DARAJA ZA MITUME.


Je, Mtume ambaye ametumwa kuongoza watu 1,000 ni sawa na yule aliyepelekwa kuongoza watu 30,000, au kwa yule aliyetumwa kuongoza wanadamu wote? Hebu tuchukue mfano. Hivi, Mwalimu wa wanafunzi wa darasa la kwanza ni sawa na Mwalimu wa darasa la nne? Je, Walimu wa madarasa ya juu ni sawa na Maprofesa au Walimu wa Chuo Kikuu? Wote wako katika Utawala mmoja na kufanya kazi chini ya mpango mmoja wa jumla, lengo lao likiwa kuelimisha wanafunzi. Bado, kwa kuzingatia elimu ya Walimu hao,

80

Mikesha ya Peshawar
hawako sawa. Kila mmoja yuko tofauti na mwingine kwa mujibu wa kisomo, uwezo, na mafanikio yake. Kwa mtazamo wa lengo la Utume, Mitume wote wa Allah wako sawa sawa. Walakini, kwa sababu ya tofauti katika daraja na elimu, wako tofauti. Qurani Tukufu inasema:

Tumewafanya baadhi ya Mitume kuwazidi wengine; Miongoni mwao wako ambao Allah amesema nao, na baadhi yao Amewatukuza kwa (vyeo vingi) daraja. (2: 253). Mwanachuo wenu wenyewe Jarullah Zamakshari anasema katika kitabu chake, Tafsir-ekush-Shaf kwamba, Aya hiyo hapo juu ina maana Mtume wetu alikuwa bora katika daraja kwa wengine wote kwa sababu ya sifa zake maalumu, muhimu zaidi ni ambayo kwamba alikuwa wa mwisho wa Mitume. Nawab: Nimefurahi umelitatua tatizo hili, lakini nina swali lingine, ingawa kwa namna nyingine halihusiki hapa. Tafadhali tueleze kwa ufupi sifa makhususi za Utume maalumu. Muombezi: Kuna sifa nyingi za pekee kwa Utume Maalumu, na kuna sababu nyingi mno zinazothibitisha vipi Mtume mmoja kati yao wote ndiye Mtume maalum wa Allah. Kwa hakika hatua hiyo huishiliza duru la Utume. Lakini mikutano hii haikupangwa kuthibitisha Utume wa Allah kwa Waislamu. Kama ingekuwa tuijadili nukta hii kikamilifu, tungetoka nje ya nukta yetu ya Uimamu. Walakini kwa ufupi hata hivyo, nitajadili nukta hii.

SIFA ZA UTUME MAALUM:


Ukamilifu wa ubinadamu umo katika ukamilifu wa nafsi. Ukamilifu wa kimaadili na kiroho hauwezi kufikiwa bila kutakasa nafsi. Ukamilifu huu hauwezekani mpaka mtu aongozwe kwa uwezo wa hekima. Hapo ndipo mtu ataweza kupanda juu na juu zaidi pamoja na nguvu ya elimu na utendaji sahihi mpaka anafikia kilele cha ubinadamu, kama ilivyoelezwa na Ali. Yeye alisema: Mtu aliumbwa na uwezo wa kuongea ambayo ni asili ya ubinadamu. Kama mazungumzo yamepambwa na elimu na vitendo, hufanana na kuwepo ufalme wa ki-mbinguni ambao ndiyo asili ya kuumbwa kwa mwanadamu. Wakati mazungumzo yake yanapofikia pahala pa kujizuia na yanaondokana na mata yote ya maumbile, inakuwa moja pamoja na ufalme wa ki-mbinguni. Kisha huachana na ulimwengu wa kihayawani na kufikia hatua ya juu sana ya ubinaadamu. Uwezo wa mtu wa kuzungumza humfanya bora kwa viumbe vyote. Lakini kuna sharti moja lililoambatanishwa kwalo, kwamba uisafishe nafsi yake na uchafu wote kwa elimu na matendo sahihi. Sehemu hizi mbili ndani ya mtu ni kama mbawa mbili za ndege,

81

Mikesha ya Peshawar
ambaye huruka juu angani kutokana na nguvu za mbawa zake. Hivyo hivyo kiwango cha mtu cha mafanikio ya ubinadamu hupanda kutokana na elimu yake na matendo sahihi. Kuvuka mipaka ya hali ya kinyama na kufikia nyanja ya matendo ya kibinadamu hutegemea juu ya ukamilifu wa nafsi. Mtu ambaye hukusanya ndani yake stadi za elimu na matendo sahihi na akafikia thuluthi ya tabaka tatu za watu (watu wa kawaida, watu bora na watu bora zaidi), hufikia daraja la chini kabisa la Utume. Wakati mtu kama huyo anapokuwa shabaha ya hisani maalumu za Allah, anakuwa Mtume. Naam, kwa kweli Utume vilevile una daraja tofauti. Mtume anaweza kufikia daraja ya juu zaidi katika tabaka hizi tatu. Cheo hiki ni cha juu sana katika nyanja ya uwezekano, ambayo wenye busara (wataalamu) huiita Hekima ya Kwanza, na ambayo ni Athari ya Kwanza au Matokeo ya Mwanzo. Hakuna cheo cha juu kama hiki katika miliki ya viumbe. Nafasi hii imeshikwa na wa mwisho wa Mitume, ambaye ni wa kwanza, hakuna kama yeye isipokuwa kile Chanzo cha Awali. Wakati Mtume alipopandishwa kwenye daraja hii ya juu zaidi, Utume ulikomelezwa. Uimamu ni daraja la chini kuliko daraja ya juu zaidi ya utume, lakini ni hatua ya juu kuliko daraja zote nyingine za Utume. Kwa vile Ali alipandishwa kwenye hatua ya juu kuliko ya Utume na alikuwa mmoja katika nafsi pamoja na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), aliaminishwa kazi ya Uimamu na hivyo kuwa mbora kwa Mitume wote waliopita. Hafidh: Sehemu ya mwisho ya maneno yako inachanganya. Kwanza, unasema Ali alikuwa katika ngazi ya Utume, pili, kwamba alikuwa nafsi moja na Mtume Muhammad, tatu, kwamba alikuwa bora kwa Mitume mingine. Nini hoja zako kuthibitisha ukweli wa maneno yako?

HOJA ZA CHEO CHA UTUME KWA AJILI YA ALI KUTOKA KWENYE HADITH MANZILA.
Muombezi: Kwamba Ali amepata cheo cha Utume yaweza kuthibitishwa kwa kurejea kwenye hadith ya Manzila (Hadith inayohusu vyeo), ambayo imesimuliwa kwa kauli moja kwa kadri ya maneno yanayofanana. Wa mwisho wa Mitume watukufu amerudia mara nyingi na katika mikusanyiko tofauti. Je, huridhiki kwamba kwangu wewe ni kama Harun alivyokuwa kwa Musa, isipokuwa tu kwamba hakutakuwa na Mtume baada yangu? Na wakati mwingine aliwaambia wafuasi wake. Ali kwangu mimi ni kama alivyokuwa Hauna kwa Musa. Hafidh: Usahihi wa hadith hii haukuthibitishwa. Hata kama ingethibitishwa kuwa ni kweli itakuwa ni simulizi pekee na kwa hiyo haikubaliki.

82

Mikesha ya Peshawar

USAHIHI WA HADITH YA MANZILA KUTOKA KWENYE REJEA ZA KAWAIDA.


Muombezi: Katika kutoa taarifa kuhusu usahihi wa hadith hii, nitarejea kwenye vitabu vyenu. Hii sio simulizi ya pekee. Imethibitishwa na maulamaa wenu mashuhuri, kama Suyuti, Hakim Nishapuri, na wengine, ambao wamethibitisha kutegemeka kwake kwa vyanzo vinavyokubaliwa kwa pamoja. Baadhi yake ni hivi vifuatavyo: (1) Abu Abdullah Bukhari katika Sahih yake Juz. 111, Kitab Ghazawa, gahazawa Tabuk; uk. 54, na ndani ya kitabu chake Bidaul-Khalq, uk. 180; (2) Muslim bin Hajjaj katika Sahih yake iliyochapishwa Misri, 1290 A.H. Juz. 11, chini ya kichwa cha habari, Ubora wa Ali; uk. 236-7; (3) Imam Ahmad bin Hanbal katika Musnad Juz. 1 Sababu za kutoa jina la Husain, Uk. 98, 118, 119 na maelezo chini ya kurasa ya kitabu hicho hicho, Sehemu ya 5 uk. 31; (4) Abu Abdur-Rahman Nisai katika Khasaisil-Alawiyya uk. 19; (5) Muhammad bin Sura Tirmidhi katika Jami yake; (6) Hafidh Ibn Hajar Asqalani katika Isaba. Juz. 11, uk. 507; (7) Ibn Hajar Makki katika Sawaiq Muhriqa Sura ya 9, Uk. 30& 34; (8) Hakim Abu Abdullah Muhammad bin Abdullah Nishapuri katika Mustadarak, Juz. 11, Uk. 109; (9) Jalalud-Din Suyuti katika Tarikhul-Khulafa uk. 65; (10) Ibn Abd Rabbih katika Iqdul-Farid Juz. 11, uk. 194; (11) Ibn Abdul-Birr katika Istiab, Juz. 11, uk. 473; (12) Muhammad bin Sad Katib Waqidi katika Tabaqatul-Kubra; (13) Imam Fakhrud-Din Radhi katika Tafsir Mafatihul-Ghaib; (14) Muhammad bin Jarir Tabari katika Tafsir yake, na pia katika Tarikh yake; (15) Seyyed Mumin Shablanji katika Nurul-Absar, uk. 68; (16) Kamalud-Din Abu Salim Muhammad bin Talha Shafii katika Matalibus-Suul, uk. 17; (17) Mir Seyyed Ali bin Shahabud-Din Hamadani katika Mawaddatul-Qubra, kuelekea mwisho wa Mawadda 7; (18) Nurud-Din Ali bin Muhamma Maliki Makki, ajulikanaye kwa jina la Ibn Sabbagh Maliki katika Fusulul Muhimma uk. 23 na 125; (19) Ali bin Burhanud-Bin Shafii katika Siratul-Halabiyya Juz. 11, uk, 49; (20) Sheikh Sualyman Balkh Hanafi katika Yanabiul-Mawadda, (21) Mulla Ali Muttaqi katika Kanzul-Ummal, Juz. VI, uk. 152 153; (22) Ahmad bin Ali Khatib katika Tarikh Baghdad; (23) Ibn Maghazili Shafii katika Manaqib; (24) Muwaffaq bin Ahmad Khawarizmi katika Manaqib; (25) Ibn Jazari Ali bin Muhammad katika Usudul-Ghaiba; (26) Ibn Kathir Damishqi katika Tarikh yake; (27) AlaudDaula Ahmad bin Muhammad katika Urwatul-Wuthqa; (28) Ibn Athir Mubarak bin Muhammad Shaibani katika Jamiul-Usul; (29) Ibn Hajar Asqalani katika TahdhibutTahdhib; (30) Abul-Qasim Husain bin Muhammad Raghib Isfahani katika Muhadhiratul-Udaba; Juz. 11, uk. 212.

83

Mikesha ya Peshawar
Maulamaa wenu wengi wengine wakubwa wameisimuliwa hadith hii muhimu pamoja na tofauti kidogo ya maneno kutoka kwa Masahaba wengi wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kama vile: (1) Umar bin Khattab, (2) Sad bin Ali Waqqas (3) Abdullah bin Abbas; (4) Abdulllah bin Masud; (5) Jabir bin Abdullah Ansari, (6) Abu Huraira; (7) Abu Said Khurdri; (8) Jabir bin Sumra; (9) Maliki bin Huwairis, (10) Baraa bin Azib; (11) Zaid bin Arqam; (12) Abu Rafi; (13) Abdullah bin Ubai; (14) Abu Suraiha, (15) Hudhaifa bin Assad, (16) Anas bin Malik, (17) Abu Huraira Aslami, (18) Abu Ayyub Ansari, (19) Said bin Musayyab (20) Habib bin Abi Thabit, (21) Sharhbil bin Sad; (22) Ummi Salma (Mke wa Mtume); (23) Asma bint Umais, (Mke wa Abu Bakar); (24) Aqil bin Abi Talib (25) Muawiyya bin Abu Sufyan, na wengi wa Sahaba wengine. Kwa ufupi wote hawa wameisimuliwa pamoja na tofauti kidogo ya maneno kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: Ewe Ali, wewe uko kwangu mimi kama Harun alivyokuwa kwa Musa, isipokuwa kwamba hakutakuwa na Mtume baada yangu. Je, Maulamaa wote hawa wakubwa na kuna wengi sikuwataja hawatoshi kuthibitisha kwamba hadithi hii imekubaliwa kwa pamoja kuwa ya kweli? Je, utathibitisha sasa kwamba ulikuwa katika kutokuelewa? Kwa vile unachukua mwelekeo wa wasiwasi kuhusu ukweli wa hadith hii, yakupasa uangalie katika Kitabu Kifayatut-Talib fi Manaqib-e-Ali Bin Abu Talib, Sura ya 7, kilichoandikwa na Muhammad bin Yusuf Ganji Shafii, ambaye ni mmoja wa Maulamaa wenu Maarufu mno wa madhehebu yenu. Baada ya kunukuu hadith sita zenye kumtukuza Ali, mwandishi huyu akaisherehesha (uk. 149) hadith hii kama ifuatavyo: Hii ni hadithi ambayo usahihi wake umekubaliwa na wote. Imesimuliwa na Maimamu wenye elimu zaidi na Huffadh (wajuao Qurani Tukufu kwa moyo), kama vile Abu Abdullah Bukhari katika Sahih yake, Muslim bin Hajjaj katika Sahih yake, Abu Dawud katika Sunan yake, Abu Isa Tirmidhi katika Jami yake, Abu Abdur-Rahman katika Sunan yake, Ibn Maja Qazwini katika Sunan yake. Wote hawa kwa pamoja wamekubali usahihi wake. Hakim Nishapuri amesema kwamba hadith hii imeingia katika hatua ya Mutawatir. Nina hakika kwamba sihitaji kutoa ushahidi zaidi kuonyesha kwamba hadith hii ni Sahihi. Hafidh: Mimi sikukosa maadili ya kidini, hivyo siwezi kukataa mantiki yako ya kiakili, lakini hebu vuta mazingatio kwenye kauli ya mwanachuo na mwana itikadi mkubwa, Abul-Hasan Amadi, ambaye ameikataa hadith hii. Muombezi: Nashangaa kwa nini mtu mwenye elimu kama wewe, baada ya kusikia maoni ya Maulamaa wako mashuhuri, utaamini taarifa ya mtu muovu ambaye alikuwa hata kuswali haswali.

84

Mikesha ya Peshawar
Sheikh: Mtu yuko huru kuelezea imani yake. Kama mtu akielezea maoni yake, haitupasi sisi kumkashifu. Haipendezi kwa wewe kumzulia uongo badala ya kutoa majibu yenye mantiki kwenye maelezo yake. Muombezi: Umenielewa vibaya. Simlaumu mtu yeyote kinyume cha haki. Si kuwa ninaishi katika wakati wa uhai wa Amadi. Maulamaa wenu wenyewe wameelezea kwamba alikuwa ni mtu aliyekuwa hana dini. Sheikh: Ni wapi ambapo Ulamaa wetu wamesema kwamba alikuwa ni mtu asiyekuwa na dini?

AMADI HAAMINIKI KAMA MSIMULIAJI WA HADITHI.


Muombezi: Ibn Hajar Asqalani ameandika katika Lisanul-Mizan: Saif Amadi Mutakallim Ali bin Abi Ali, mwandishi, alifukuzwa kutoka Damascus kwa sababu ya maoni yake yasiyokuwa ya kidini, na ni kweli kwamba alikuwa hasali. Na Dhahabi, ambaye pia ni mmoja wa Maulamaa wenu Maarufu, ameandika hivyohivyo katika Mizanul-Itidal. Amesema kwamba Amadi alikuwa mzushi. Kama Amadi asingekuwa muovu na mzushi asiyekuwa na dini, asingeweza kutoa maneno ya kashfa kuhusu Sahaba wote wa Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.), ikiwa ni pamoja na Khalifa wenu wenyewe, Umar bin Khatab (mmoja wa wasimuliaji wa hadithi hii). Sio haki kabisa kwamba mnawaona Mashia kuwa na taksiri kwa sababu ya kutokubali hadith zilizoandikwa katika Sihah. Kama hadithi imetolewa kutoka vyanzo sahihi, inakubaliwa hata kama iko kwenye Sihah. Lakini hadithi iliyothibiti, ambayo imeandikwa na Bukhari, Muslim, na waandishi wengine wa Sihah inakataliwa na Amadi, hamuoni taksiri kwayo. Kama unataka kujua kwa ukamilifu hoja zinazohusu usahihi na vyanzo vya hadith hii kutoka kwenye maandishi ya Maulamaa wenu, na kama uko tayari kuwalaumu watu kama Amadi, unaweza ukaangalia jalada za Abaqatul-Anwar, zilizoandikwa na mwanachuo mkubwa na mfasiri, Allama Mir Seyyed Hamid Husain Dihlawi. Yakupasa uangalie hususan hadith ya Manzila ili uweze kujua kwamba vipi mwanachuo huyu mkubwa wa Kishia alivyokusanya vyanzo kutoka kwa wanachuo wenu wa Shariah na wakathibitisha kutegemeka kwa hadhi hii. Hafidh: Umesema kwamba mmoja wa wasimuliaji wa Hadithi hii alikuwa Umar bin Khattab. Ningetaka kujua zaidi kuhusu habari hii.

85

Mikesha ya Peshawar

KUTHIBITISHWA HADITH YA MANZILA NA UMAR BIN KHATTAB.


Muombezi: Abu Bakar Muhammad bin Jaafarul-Mutiri na Abul-Laith bin Muhammad Samarqandi Hanafi, katika vitabu vyao, Majalis, Muhammad bin Abdur-Rahman Dhahabi katika Riadhun-Nadhara, Mulla Ali Muttaqi katika Kanzul-Ummal na wengine, wamesimulia kutoka kwa Ibn Abbas akisema kwamba siku moja Umar bin Khattab alisema: Liache jina la Ali (yaani usimzungumze Ali sana kwa ubaya) kwa sababu nimesikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema kwamba Ali alikuwa na sifa tatu. Kama ningekuwa na moja kati ya sifa hizi, ningeihifadhi zaidi kuliko kitu chochote kifikiwacho na mwanga wa jua juu yake. Siku moja mimi; Abu Bakar, Abu Ubaida Jarra na baadhi ya Sahaba wengine tulikuwepo, na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa amepumzika kwa kumuegemea Ali bin Abu Talib. Alipiga bega la Ali na kusema: Ali! Kiasi imani inavyohusika, wewe ni wa kwanza wa Waumini wote, na kiasi Uislam unavyohusika, wewe umechukua nafasi ya kuongoza! Kisha akasema: Ali! Uko kwangu mimi kama alivyokuwa Harun kwa Musa. Na ni muongo ambaye anafikiri ni rafiki yangu kama yeye ni adui yako. Je, inaruhusiwa katika imani yenu kukataa maneno ya Khalifa Umar? Kama hairuhusiwi, kwa nini unaamini taarifa za ajabu za mtu kama Amadi?

NAFASI YA SIMULIZI PEKEE KATIKA MADHEHEBU YA SUNNI.


Ningali bado sijajibu moja ya madai yako. Umesema kwamba hadith hii ni simulizi pekee, na kwa ajili hiyo haikubaliki. Kama tukisema kitu hicho kwa mujibu wa mtindo wa watu ambao tunao katika maoni, tutakuwa wenye haki. Lakini inanishangaza kusikia kitu hiki kutoka kwako, kwa sababu katika madhehebu yenu hata simulizi pekee inatosha kuthibitisha ukweli wa jambo. Kama mtu akikataa kukubali usahihi wa simulizi pekee, kwa mujibu wa maulamaa wenu atakuwa si muumini. Malikul-Ulama Shahabud-Din Daulatabadi amesema katika HidayatuS-Sada: Kama mtu anakataa kukubali riwaya pekee au rai na akasema kwamba haikubaliki, huyo ni kafir. Kama akisema simulizi pekee hii sio sahihi, na rai hii haikuthibiti, atakuwa mtenda kosa, sio kafir. Hafidh: Tumetoka kwenye mada yetu ya msingi. Tafadhali hebu tueleweshe ni vipi utaweza kuthibitisha kwa Hadith hii ya Manzila kwamba Ali alishika cheo cha Utume.

86

Mikesha ya Peshawar

SIFA ZA ALI.
Muombezi: Hadith hii inathibitisha kwamba Ali anazo sifa tatu: (1) Cheo cha Utume. (2) Cheo cha Mrithi wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.); na (3) Nafasi yake ya juu miongoni mwa Sahaba wote wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kama alivyo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), wafuasi wa Ali walimfananisha na Harun, ambaye alikuwa Mtume, aliwekwa kuwa Khalifa wa Musa, na alikuwa mbora juu ya Bani Israel wote. Nawab: Harun alikuwa Mtume? Muombezi: Ndiyo. Nawab: Unaweza kuonyesha Aya kutoka kwenye Qurani yenye kuunga mkono nukta hii? Muombezi: Allah ameutaja Utume wake katika Aya nyingi. Anasema: Hakika tumekuletea wahyi kama tulivyompelekea wahyi Nuh na manabii baada yake. Na tulimpelekea Ibrahim na Ismail na Ishaq na Yakub na makabila; na Isa na Ayub na Yunus na Harun na Suleiman na Daud tukampa Zaburi. (4:163) Na halafu tena Anasema: Na mtaje Musa katika Kitabu, hakika yeye alikuwa mwenye kusafishwa, na alikuwa Mtume, Nabii. Na tukamwita upande wa kulia wa mlima, na tukamsongeza kuzungumza naye kwa siri. Nasi tukampa katika rehema zetu nduguye Harun, Nabii. (19:51-53) Hafidh: Hivyo kwa mujibu wa hoja yako, Muhammad na Ali wote walikuwa Mitume. Muombezi: Mimi sikuelezea katika njia unayoelezea wewe. Kwa kweli wewe mwenyewe unajua kwamba kuna tofauti kubwa ya maoni kuhusu ni Mitume wangapi walikuwepo. Baadhi wanadai kwamba walikuwepo 120,000 - au hata zaidi. Lakini wote hao katika nyakati zao husika walikuwa wamegawanyika katika makundi na walikuwa (daraja ya) chini kwa Mtume mkuu ambaye kwake kilifunuliwa kitabu kitukufu kikiwa na sheria mpya za dini. Watano miongoni mwao walikuwa ni Mitume wakuu: Nuh, Ibrahim, Musa, Isa, na mwisho wa Mitume wote, Muhammad, ambaye cheo chake kilikuwa ndio cha juu zaidi. Harun alikuwa mmoja wa wale Mitume ambao hawakuwa wa kudumu au wa kujitegemea. Alikuwa chini ya Sharia (mfumo wa kidini) ya ndugu yake Musa. Ali alifikia cheo cha Utume lakini hakupandishwa kwenye cheo hicho cha Mtume kwa asili yake yenyewe kwa vile alikuwa chini ya Sharia ya Muhammad. Katika hadith hii ya Manzila, madhumuni ya Mtume yalikuwa ni kuwaambia watu kwamba, kama vile ambavyo Harun amefikia Cheo cha Utume lakini alikuwa chini ya Musa, Ali alifikia cheo cha Utume. Uimamu ulipasishwa kwake, lakini alikuwa chini ya Muhammad (s.a.w.w.).

87

Mikesha ya Peshawar

UMUHIMU WA CHEO CHA ALI.


Katika Sharhe yake juu ya Nahjul-Balagha, Ibn Abil-Hadid anasema kuhusiana na hadith hii kwamba kwa kutaja cheo cha Harun katika kumlinganisha na Musa, Mtume alionyesha kwamba Ali bin Abu Talib alishika cheo hicho. Vivyo hivyo, Muhammad bin Talha Shafii, katika Matalibus-Suul, uk. 19, baada ya kuelezea cheo na nafasi ya Harun, anasema: Maana hasa ya jambo hili ni kwamba, nafasi ya Harun katika kuhusiana na Musa ilikuwa kwamba Harun alikuwa ndugu yake, muwakilishi wake, mshirika katikaUtume, na wasii wake au Mshika Makamu wakati Musa alipokuwa safarini. Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.) alikuwa vilevile katika hadith hii alionyesha kwamba, Ali alikuwa nayo nafasi ile ile kama aliyokuwa nayo Harun, isipokuwa Utume, ambao umeondolewa kwa kusema kwake: Hakutakuwa na Mtume baada yangu. Kwahiyo, imethibitishwa kwamba Ali alikuwa ndugu yake Mtume, waziri (msaidizi) muwakilishi, na mrithi au Makamu wake, kama ilivyoelezewa na Mtume katika safari yake ya Tabuk. Hadith hii kwa umoja inakubaliwa kuwa ni ya kweli. Maoni kama haya yameelezewa na Ibn Sabbagh Maliki katika Fusulul-Muhimma uk. 29, na wengine wengi wa Maulamaa wenu mashuhuri. Hafidh: Nafikiri madai yako kwamba kama Mtume wetu asingekuwa Muhuri (mwisho) wa Mitume, Ali angeishika nafasi hiyo, ni (madai) ya kipekee kwako wewe mwenyewe. Hakuna mtu mwingine aliyesema hivyo. Muombezi: Madai haya hayakuishia kwangu na kwa Maulamaa wa Kishia tu. Maulamaa wenu wenyewe wamekuwa na maoni kama haya. Mmoja wa Maulamaa wenu wakubwa ni Mulla Ali bin Sultan Muhammad Harawi Qari. Katika kitabu chake Mirqate-Sharh bar Mishkat, yeye anasema, akitoa maoni juu ya hadith ya Manzila; Kuna dalili katika Hadith hii kwamba, kama kungekuwa na Mtume wa Allah baada ya mwisho wa Mitume, basi angelikuwa ni Ali. Mwingine katika ulamaa wenu mashuhuri ambaye ameitafsiri Hadith hii kwa njia hii hii ni yule mwanachuoni ajulikanaye sana, Jalalud-Din Suyuti. Anaandika kuelekea mwisho wa kitabu chake Baghiatul-Wuaz fi TabaqatulHuffadh, akitoa Sanad (nyororo) ya wapokezi mpaka kufikia kwa Jabir Abdallah Ansari, kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimwambia Amirul-Muuminiina Ali. Angelikuwepo Mtume yoyote baada yangu, basi angelikuwa ni Wewe! Kwa nyongeza, Mir Seyyed Ali Hamadani Faqih Shafii anasema katika Mawaddad ya Pili ya Mawadda Sita katika kitabu chake Mawaddatul-Qurba, akinukuu riwaya kutoka kwa Anas bin Malik, kwamba Mtume alisema: Hakika, Allah amenifanya mimi Mkuu kwa

88

Mikesha ya Peshawar
Mitume wote, akanichagua mimi kwa ubora, na akanifanyia mimi wasii, binamu yangu Ali. Kupitia kwake yeye akaimarisha mabega yangu, kama vile mabega ya Musa yalivyoimarishwa na Harun. Yeye (Ali) ni makamu wangu na msaidizi wangu. Kama kungelikuwepo na Mtume yoyote baada yangu, angelikuwa ni Ali, lakini hakutakuwa na Mtume baada yangu. Hivyo unaona kwamba siko peke yangu katika kudai cheo cha Utume kwa Ali. Mtume na Maulamaa wenu wamelikubali hilo. Kwa vile alikuwa na cheo cha Harun na kwa vile muda wa Utume ulikuwa umefikia kikomo Ali alikuwa mwenye kufaa zaidi kwa Ukhalifa. Moja ya dalili za utukufu wa cheo cha Ali ilikuwa kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliruhusu mlango wa nyumba ya Ali kubakia kufunguka kuelekea Msikitini. Maneno haya yalisababisha mshangao na bumbuazi miongoni mwa Masunni. Muombezi akauliza kwa nini inakuwa hivyo. Nawab: Ijumaa iliyopita tulikwenda Msikitini kusali. Hafidh Sahib akatueleza kuhusu ubora wa khalifa Abu Bakar. Alisema kwamba yeye aliruhusiwa kuweka mlango wa nyumba yake kuelekea Msikitini. Tunashangaa kusikia wewe ukisema kwamba ruhusa hii ilikuwa kwa Ali pekee. Tafadhali hebu ifafanue nukta hii. Muombezi: (Akimgeukia kwa Hafidh Sahib) Ulitoa kauli hii? Hafidh: Ndio Imesimuliwa kwenye hadith Sahih zetu, kama iliyoelezwa na Sahaba mchamungu na mwadilifu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Abu Huraira. Mtume aliagiza kwamba: Milango yote ifunguliwayo kuelekea Msikitini ifungwe isipokuwa mlango wa nyumba ya Abu Bakr, kwani Abu Bakr anatokana na mimi na mimi ninatokana na Abu Bakr. Muombezi: Hakika unajua kwamba kwa sababu ya ubora wa Amirul-Muminina, Ali, Bani Ummaya walifanya juhudi endelevu kwa kupitia njia za siri na hususani kupitia kwa watu wenye kujipendekeza na kumsifu sifu mno Muawiya, kama Abu Huraira na Mughira ili kubuni hadith kama hizo. Aidha, wafuasi wa Abu Bakr, kwa sababu ya kumuunga mkono kwao yeye, waliziimarisha hadith hizi za kughushi. Ibn Abil-Hadid, katika Sherhe yake ya Nahjul-Balagha Jz. 1, na tena katika Jz. 3, uk. 17, anaeleza kwa urefu kwamba miongoni mwa hadith nyingi za kughushi ni hii ielezeayo kuhusu kufungwa kwa milango ya nyumba zote inayoelekea Msikitini isipokuwa ule wa Abu Bakr. Kinyume na hadith hii ya kughushi, ziko hadith nyingi sahihi, ambazo zimesimuliwa sio tu katika vitabu Sahih vya Shia, lakini vilevile katika vitabu vya kutegemewa vya Mualamaa wenu wenyewe, kama Sahih. Nawab: Kwa vile ni suala la ubishani, huku Hafidh Sahib akisema ni pekee kwa Abu Bakr, na wewe ukisema ni pekee kwa Ali, tungefurahia kama ungenukuu kutoka vitabu vyetu ili kwamba tuweze kulinganisha rejea zako na zile za Hafidh Sahib.

89

Mikesha ya Peshawar

HADITH AMBAYO KWA AMRI YA MTUME MILANGO YA NYUMBA INAYOELEKEA MSIKITINI ILIFUNGWA ISIPOKUWA MLANGO WA NYUMBA YA ALI.
Muombezi: Vyanzo vifuatavyo vimesimulia kwamba, Mtume aliamrisha kwamba ile milango ya nyumba zote inayofunguka kuelekea Msikitini ifungwe isipokuwa mlango wa nyumba ya Ali: Ahmad bin Hanbal katika Musnad. Jz. 1 uk. 175, Jz. 2 uk. 26 na Jz. 4, uk. 369; Imam Abu Abdur-Rahman Nisai katika Sunan na katika Khasaisil-Alawi uk. 13 14; Hakim Nishapuri katika Mustadrak, Jz. 3, uk. 117- 125 na Sibt Ibn Jauzi katika Tadhkira uk. 24 25 wameshuhudia usahihi wa Hadithi hii juu ya msingi wa Sanad za wasimuliaji wa Tirmidhi na Ahmad. Halafu, Ibn Athri Jazri katika Athnal-Matalib, uk, 12, Ibn Hajar Makki, katika Sawaiq Muhriqa, uk. 76; Ibn Hajar Asqalani katika Fathul-Bari Jz. 7, uk. 12, Tibrani katika Ausat, Khatib Baghdadi katika kitabu chake cha Tarikh Jz. 7, uk. 205, Ibn Kathir katika Tarikh Jz. 7, uk. 342, Muttaqi Hindi katika Kanzul-Ummal, Jz. 6, uk. 408; Haithami katika Majimauz-Zawaid, Jz. 9, uk. 65; Muhibud-Din Tabari katika Riyadh Jz. 2, uk, 451; Hafidh Abu Nuaim katika Fadhailus-Sahaba na katika Hilyatul-Auliya Jz. 4, uk. 183; Jalalud-Din Suyuti katika Tarikhul-Khulafaa, uk. 116, katika Jamul-Jawami, katika Khasaisul-Kubra na katika Laaliul-Masunua Jz. 1, uk, 181; Khatib Khawarizmi katika Manaqib, Hamwaini katika Faraid, Ibn Maghazili katika Manaqib, Munawi Misri katika Kunuzud-Daqaiq, Sulayman Balkh Hanafi katika Yanabiul-Mawadda, uk. 87, alitumia sura yote nzima ya 17 kwa suala hili hasa peke yake, Shahabud-Din Qastalani katika Irshad Bari, Jz. 6, uk. 81, Halabi katika Siratul-Halabiyya Jz. 3, uk. 374 na Muhammad bin Talha Shafii katika MatalibusSuul na wengine wengi, hususan kutoka miongoni mwa masahaba mashuhuri wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wamesimulia kitu hicho hicho. Kwa mfano Khalifa Umar bin Khattab, Abdulla Ibn Abbas, Abdullah bin Umar, Zaid bin Arqam, na Jabir bin Abdullah Ansari wamethibitisha usahihi wa hadith hii. Baadhi ya maulamaa wenu mashuhuri, kwa ajili ya kuepusha watu kutokana na kupotezwa na Bani Umayya wamesisitiza ukweli wa hadith hii. Muhammad bin Yusufu Ganji Shafii, katika kitabu chake Kifayatut-Talib Sura ya 50, ameshughulika na hadith hii chini ya kichwa cha habari maalum. Akinukuu kutoka vyanzo sahihi anasema kwamba, kwa vile idadi ya milango ya masahaba wa Mtume ilifunguka kuelekea Msikitini, na kwa vile Mtume amepiga marufuku watu wote kuingia Msikitini na hali ya janaba au haidh, aliagiza kwamba milango yote ya nyumba ifungwe isipokuwa mlango wa nyumba ya Hadhrat Ali. Yeye alisema: Fungeni milango yote bali acheni mlango wa nyumba ya Ali ubakie

90

Mikesha ya Peshawar
wazi. Muhammad bin Yusuph Shafii anasema kwamba ni Ali pekee yake ambaye kwamba aliruhusiwa kuingia na kukaa ndani ya Msikiti katika hali ya janaba. Aliendelea kusema: Kwa ufupi, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa kuufanya upendeleo huu wa kipekee juu ya Ali ilikuwa ni heshima kubwa mno. Inaonyesha kwamba Mtume alijua kwamba Ali, Fatima, na dhuria wao walikuwa huru kabisa kutokana na uchafu kama inavyoonyeshwa wazi na aya ya tohara katika Qurani Tukufu. Maneno haya ya mwanachuo wa Ki-Shafii yanaweza kulinganishwa na hadith iliyotajwa na Hafidh Sahib. Tukiachilia mbali vyanzo vyote Sahihi tulivyonukuu, kama mnao uthibitisho wowote wa utohara wa Abu Bakr, tafadhali utoeni. Ukweli ni kwamba hata Bukhari na Muslim katika ukusanyaji wao wa hadithi wameonyesha ukweli huu kwamba mtu aliyanajisika hawezi kukaa ndani ya Msikiti. Mtume alisema: Hairuhusiwi kwa mtu yeyote ambaye sitohara kukaa ndani ya Msikiti isipokuwa kwa mimi na Ali. Labda ningeruhusiwa hapa kunukuu hadith kutoka kwa Khalifa wa pili Umar bin Khattab, ambayo imeandikwa na Hakim katika Mustadrak, uk. 125, na Sulaiman Balkhi katika. Yanabinl-Mawadda Sura ya 56, uk. 210, na wengineo, kama Imam Ahmad bin Hanbal, Khatib Khawarizmi, Ibn Hajar, Suyuti, na Ibn Athir Jazri. Yeye alisema: Hakika Ali bin Abi Talib alikuwa nazo sifa tatu za pekee, kama ningekuwa na mojawapo kati ya hizo, ingelikuwa ni bora zaidi kwangu mimi kuliko ngamia wa manyoya mekundu:- (1) Mtume alimuozesha binti yake kwake, (2) Mtume aliagiza kwamba milango ya nyumba zote inayofunguka kuelekea msikitini ifungwe, isipokuwa mlango wa nyumba ya Ali; (3) Mtume alimpa bendera (ya Uislamu) siku ya vita ya Khaibar. Kutokana na maelezo haya, ni wazi sasa kwamba Ali alikuwa sawa kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika sifa zote, kama vile tu Harun alivyokuwa kwa Musa. Hivyo wakati Musa alipomuona anafaa kwa kazi hii, alimuomba Allah kumfanya mshirika katika ujumbe wake, ili kwamba aweze kuwa Waziri wake. Vivyo hivyo, wakati Mtume alipoona kwamba hakuna yoyote miongoni mwa wafuasi wake wote mwenye kustahiki kama Ali, alimuomba Allah amfanye Ali kuwa Waziri na mshirika wake. Nawab: Kuna hadith zaidi zinazohusu suala hili? Muombezi: Ndio, nyingi zinapatikana kuhusiana na suala hili katika vitabu vyenu wenyewe. Nawab: Niko tayari kuzisikiliza mradi ninyi pia (akionyesha upande wa Maulamaa wa upande mwingine) mtataka kusikiliza. Hafidh: Hakuna ubaya. Kusikiliza Hadith ni tendo la ibada kama simulizi yenyewe hiyo.

91

Mikesha ya Peshawar

WAKATI AKIWA KWENYE RUKUU KATIKA SALA ALI ALITOA PETE KUMPA MASIKINI.
Muombezi: Ibn Maghazili faqih Shafii katika Manaqib yake, Jalalud-Din Suyuti katika Durrul-Manthur mwana theolojia mashuhuri, Ahmad Thalabi katika KashfulBayan, Sibt Ibn Jauzi katika Tadhkiratul-Khawasul-Umma, kuhusiana na Aya ya Wilayat wananukuu kutoka kwa Abu Dharr Ghifari na Asma bint Umais (mke wa Abu Bakr) kwamba, wamesema kwamba siku moja walikuwa wanasali Sala ya Adhuhuri msikitini wakati Mtume alikuwepo. Akaja masikini akaomba sadaka. Hakuna aliyempa chochote. Ali alikuwa anarukuu (katika Sala). Wakati alipoonyesha kidole chake, masikini alitoa ile pete kutoka kwenye kidole chake. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliyaona yaliyotokea, akanyanyua kichwa chake kuelekea mbinguni akasema: Ya! Allah, Ndugu yangu Musa alikuomba: Ya! Allah, nifungulie kifua changu na nifanyie wepesi kazi yangu. Chagua kwa ajili yangu msaidizi kutoka kwenye familia yangu, Harun ndugu yangu. Ilifunuliwa Aya kumuambia Musa kwamba dua yake imekubaliwa. Allah akachagua kwa ajili yake msaidizi na akaimarisha mikono yake na akawapa uwezo na mamlaka kiasi kwamba hakuna hata mmoja aliyeweza kuwashinda nguvu. ..na Musa akasema kumwambia ndugu yake Harun: Chukua mahala pangu miongoni mwa watu, na utendee wema wala usifuate njia ya waharibivu (7: 142)

CHEO CHA HARUN KAMA MTUME KADHALIKA KAMA KHALIFA.


Hafidh: Umesema kwamba Harun alikuwa ni mshirika wa Musa katika Utume. Ilikuaje tena akafanywa kuwa Khalifa wake? Mshirika katika Utume hushikilia nafasi ya juu kuliko ile ya ukhalifa au umakamu. Kama mshirika ni Mtume, na akafanywa kuwa Khalifa, huku ni kushusha cheo chake. Muombezi: Kanuni ya Utume inahusika kwa Musa, na Utume wa Harun ulikuwa chini ya ule wa Musa. Lakini kuhusu kuhubiri alikuwa mshirika wake, kama ilivyo dhahiri kutokana na ombi la Musa, lililoandikwa katika Qurani: Musa akasema: Ewe Mola Wangu! Nikunjulie kifua changu, na unifanyie kazi yangu kuwa nyepesi, na ulifungue fundo lililo katika ulimi wangu, wapate kufahamu maneno yangu. Na unipe waziri katika watu wangu, Harun, ndugu yangu. Kwake niongeze nguvu zangu, na umshirikishe katika kazi yangu. (at-Taha; 20: 25-32)

92

Mikesha ya Peshawar
Vivyo hivyo, Ali alikuwa mmoja ambaye mbali na kuwa daraja ya Utume alikuwa ni mshirika wa Mtume katika hatua zote na sifa maalum. Hafidh: Nimeshangazwa kukusikia unavyoitia chumvi nafasi ya Ali. Wote tumeshitushwa. Umesema hivi punde tu kwamba Ali alikuwanazo sifa zote za Mtume. Muombezi: Maelezo haya sio ya kutia chumvi. Ni ya ukweli. Makamu wa Mtume, kutokana na akili ya kuwaida, yapasa awe mfano wa Mtume. Hata Maulamaa wenu wakubwa wameelezea itiqad kama hii hii. Imam Thalabi, katika Sherhe yake, aliithibitisha nukta hii. Na yule mwanachuo mkubwa wa Kisunni, Alim Fadhili Seyyed Ahmad Shahabud-Din, katika Kitabu chake Tauzihud-Dalail amerejea kwenye nukta hii kama ifuatavyo: Sio siri kwamba Amirul-Muminin alifanana na Mtume wa Allah, katika nyingi ya sifa nzuri, matendo yasiyo ya kibinafsi, tabia, maombi kwa Allah, na njia zote tukufu za maisha. Hii imethibitishwa na riwaya sahihi na vianzo vya kutegemea, na haihitaji uthibitisho wowote au hoja. Baadhi ya Maulamaa wamezihisabu kuwa ni sawa sifa zile ambazo Ali na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) walikuwa nazo. Miongoni mwa sifa walizoshirikiana wote ni nasaba yao safi. Na tukihoji kutokana na aya ya tohara, tunaona kwamba Ali ni sawa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika utohara (Aya hii iliteremshwa kwa ajili ya watu watano: Muhammad, Ali, Fatima Hasan na Husain). Ali, kama Mtume alikuwa Mwakilishi wa Allah. Kwa mujibu wa madhehebu zote, aya ifuatayo iliteremshwa kwa ajili ya Ali. Hakika rafiki yenu mlinzi ni Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na walioamini; ambao hushika Swala na hutoa Zaka nao wakiwa wamerukuu. Ali alikuwa sawa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika utendaji kazi za Utume na kuhubiri, kama suala la Suratul-Baraat linavyoonyesha. Mtume alimpa Abu Bakr baadhi ya aya za Sura hii na akamwagiza akazisome kwa watu wakati wa Hija. Mara Malaika Jibril alitokea mbele ya Mtume na akamwambia kwamba ni mapenzi ya Allah kwamba jambo la Qurani tukufu linapaswa kupelekwa ama na Mtume mwenyewe, au mtu ambaye anatokana naye. Ali alikuwa anafanana na Mtume katika wajibu wake kama Muakala wa Allah. Mtume Mwenyewe alisema: Nimeamrishwa na Allah nitangaze hivi kwenu. Kisha akakamata mkono wa Ali na kusema: Jueni nyote, yule ambaye ni mimi ni Maula kwake (yaani, ambaye mimi ni mwenye kutawalia mambo yake). Ali vilevile ni Maula (Bwana) wake. Aidha, nafsi ya Ali imetangazwa kuwa ni nafsi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Aya ya kuapizana (Mubahila) inasema:

Watakaokuhoji katika haya baada yakukufikia ilmu hii waambie: Njooni tuwaite

93

Mikesha ya Peshawar
watoto wetu na watoto wenu, na wanawake zenu na wanawake zetu, na nafsi zetu na nafsi zenu, kisha tuombe kwa unyenyekevu tutake laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie waongo. (Al-Imran; 3: 61) Tukirudi kwenye wakati ule ndani ya Msikiti, wakati Ali alipompa masikini pete yake na Mtume akamuomba Allah, akimuomba Yeye amfanye Ali kuwa mshirika wake katika Utume wake. Kisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akaomba: Ya Allah! Mimi ni Muhammad, mchaguliwa Wako na Mtume Wako. Kifungulie kifua changu. Na nifanyie wepesi kazi yangu na unichagulie msaidizi kutoka kwenye familia yangu, Ali. Imarisha mgongo wangu kupitia kwake. Abu Dharr amesimulia: Kwa jina la Allah! Dua ya Mtume ilikuwa haijafikia mwisho, Malaika Jibril akatokea na kumfunulia Aya hii: Hakika rafiki yenu mlinzi ni Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na walioamini, ambao wanadumisha Swala na kutoa Zaka huku wakiwa wamerukuu. (5: 55) Dua ya Mtume ilikubaliwa, na Ali aliteuliwa kama waziri wake. Muhammed bin Talha Shafii, katika Matalibus-Suul, uk. 19, amelishughulikia suala hili kwa urefu. Juu ya hayo, Hafidh Abu Nuaim Isfahan katika Manaqatul-Mutaharin, Sheik Ali Jafar katika Kanzul-Barahin, Imam Ahmad Bin Hanbal katika Musnad, Seyyed ShahabudDin katika Tauzihud-Dalail, Jalalud-Din Suyuti katika Durrul-Mansur, na wanachuo wenu wengine mashuhuri wa madhehebu yenu wameisimulia hii katika vitabu vyao. Baadhi yao wamesimulia kutoka kwa Asma bint Umais (Mke wa Abu Bakr), na baadhi kutoka kwa masahaba wengine. Ifuatayo imesimuliwa na Abdullah Ibn Abbas. Mtume alitushika mikono mimi na Ali. Alisali rakaa nne, na akiwa amenyoosha mikono yake Mbinguni, akasema: Ya Allah! Musa mtoto wa Imran, alikuomba umteulie msaidizi na kuifanya nyepesi kazi yake. Mimi ni Muhammad. Nakuomba ufungulie kifua changu na uifanye nyepesi kazi yangu. Ufanye ulimi wangu kuwa fasaha ili watu wapate kuelewa maneno yangu. Niteulilie msaidizi kutoka kwa familia yangu, Ali. Niimarishe mgongo wangu kupitia kwake, na mshirikishe pamoja nami katika kazi yangu! Nilisikia sauti ikisema: Ewe Muhammad! Nimelikubali ombi lako. Kisha Mtume akamshika Ali mkono na akasema: Nyanyua mikono yako kuelekea juu mbinguni na umuombe Allah ili kwamba ajaalie kitu juu yako. Ndipo Ali akanyanyua mikono yake juu na kusema: Ya Allah! Niahidi mimi kwa upande wako kwamba utanichukuwa mimi katika upendo Wako. Mara Malaika Jibril akatokea na kuleta Aya ifuatayo katika Suratul-Mariam:Hakika wale waliomini na wakatenda mema, Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehma atawajaalia mapenzi Yake juu yao. 19: 96 Wakati masahaba wa Mtume waliposhangazwa na hili, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: Kwa nini mnashangaa? Qurani Tukufu ina vigawanyo vinne: Robo moja inatuhusu

94

Mikesha ya Peshawar
sisi Ahlul-Baiti, robo moja inahusiana na mambo ya halali; robo moja ni kwa ajili ya mambo ya haramu; na robo moja inahusu maagizo na Sheria. Naapa kwa jina la Allah kwamba, kuna Aya nyingi katika Qurani ambazo zimeshushwa kwa kumsifu Ali. Sheikh: Hata kama hadith hii itachukuliwa kama ni Sahih, haiashirii cheo maalum kwa Ali. Hadith hiyo hiyo imesimuliwa kuwahusu Khalifa Abu Bakr na Khalifa Umar. Qaza bin Suwaid amesimulia kutoka Ibn Malika ambaye anamnukuu Ibn Abbas akisema kwamba, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema; Abu Bakr na Umar wako kwangu mimi kama alivyokuwa Harun kwa Musa. Muombezi: Yakupasa uangalie tabia za baadhi ya wasimuliaji wenu (wa hadith). Wakati mwingine unahoji kutokana na similizi za Amadi na wakati mwingine kutoka kwenye zile za yule mwongo mwenye sifa mbaya na mzushaji; Qaza bin Suwaid, pamoja na kwamba mualamaa wenu mashuhuhuri wamempuuza. Allama Dhahabi, katika Mizanul-ltidal, katika maelezo ya habari za Qaza bin Suwaid na Ammar bin Harun, wanaipuuza hadith hii na kusema kimkato tu: Huu ni uwongo. Wakati Maulamaa wenu wanampuuza Qaza, hadith anazosimulia inapasa zipuuzwe. Linganisha Hadith hii ya Qaza bin Suwaid na Sanad ya Hadith ambayo nimenukuu kutoka kwa maulamaa wenu mashuhuri mno wa madhehebu yenu na uamue mwenyewe ni hadith ipi unaikubali.

MKUTANO WA TANO; JUMANNE USIKU 27 RAJAB 1345, A.H.


Hafidh: Kutoka kwenye mazungumzo yako fasaha ya usiku uliopita ninahitimisha kwamba ulitaka kuthibitisha kwamba Ali alikuwa ndiye mrithi anayefuatia mara moja wa Mtume, ingawa ukweli ni kwamba hadith hii ina maana makhususi tu. Ilisimuliwa wakati wa safari ya Tabuk. Hakuna uthibitisho kwamba ina maana ya jumla. Muombezi: Katika Hadith hii neno Manzila (Cheo) linatumika katika maana ya jumla. Neno hili kwa kuonyesha upekee, huthibitsha kwa uwazi kwamba maelekezo ni ya maana ya jumla. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimtaja Ali sambamba na neno Mtume na akaelezea Manzila yake (Yaani cheo chake) akitumia usemi, isipokuwa kwamba hakutakuwa na Mtume baada yangu. Maulamaa wengi wakubwa na waandishi wamenukuu hadith hii hii kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ambaye inasemekana alimuambia Ali: Je, huridhiki kwamba kwangu wewe ni kama Harun alivyokuwa kwa Musa isipokuwa kwamba hakutakuwa na Mtume baada yangu? Muda wa kutokuepo kwake kwa siku arobaini, Musa hakuacha mambo katika uamuzi wa wafuasi wake. Alimchagua Harun, mtu bora miongoni mwa Bani-Israil kukaimu kama

95

Mikesha ya Peshawar
Khalifa wake na mrithi. Vivyo hivyo, Mtume wa mwisho, ambaye dini yake ni kamili zaidi, alikuwa na sababu kubwa zaidi za kuwalinda watu wake kutokana na machafuko ya dhamira zao huru. Alihifadhi Sheria ya dini ili kwamba isije ikapitia katika mikono ya watu wasio na ujuzi, wale ambao wangeweza kuigeuza kwa mujibu wa matamanio yao. Watu wasio na ujuzi wangetegemea juu ya kukisia kwao na kusababisha migawanyiko katika mambo ya Sheria. Hivyo, katika hadith hii tukufu Mtume anasema Ali yuko kwangu mimi kama alivyokuwa Harun kwa Musa, akithibitisha kwamba Ali alishikilia viwango vile vile vya daraja na mamlaka, sawa kama Harun alivyokuwa. Ali alikuwa bora kwa Umma wote na kwa ajili hiyo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamchagua kuwa msaidizi wake na mrithi wake. Hafidh: Uliyosema kuhusu Hadith hii hayana ubishani. Lakini kama utaangalia jambo hili kwa uangalifu, utakubali kwamba hadith hii haina maana ya jumla. Maana yake imekomea kwenye Vita vya Tabuk wakati Mtume alipomteua Ali kuwa Khalifa wake kwa muda maalum.

HADITH YA MANZILA IMESIMULIWA MARA NYINGI:


Muombezi: Ungeweza kuwa ni mwenye haki katika maneno yako kama hadith hii ingesimuliwa wakati wa vita vya Tabuk tu. Lakini Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliirudia hadith hii katika sehemu tofauti. Ilisimuliwa wakati undugu miongoni mwa watu tofauti katika Muhajirina (wahamiaji) ulipoanzishwa katika mji wa Makka. Ilisimuliwa vilevile katika mji wa Madina wakati undugu ulipoanzishwa kati ya Muhajirina na Ansar. Katika nyakati zote Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimchagua Ali kama ndugu yake, akisema, Wewe kwangu mimi ni kama alivyokuwa Harun kwa Musa isipokuwa kwamba hakutakuwa na Mtume baada yangu. Hafidh: Kadiri nilivyochunguza mimi, hadith ya Manzila ilisimulwa wakati wa vita vya Tabuk tu. Mtume alimuacha Ali katika nafasi yake hali iliyofanya Ali kuhuzunika. Mtume akamliwaza kwa maneno haya. Nafikiri umepotoshwa. Muombezi: Hapana, mimi sijakosea. Vitabu vyenu wenyewe vya Sahih vimeisimulia Hadith hii. Miongoni mwao ni Masud (Mwandishi wa kutegemewa kwa mujibu wa madhehebu zote) ambaye ameandika katika Murujudh-Dhahab, Jz. 2, uk. 49; Halabi katika Siratul-Halabiyya, Jz. 2, uk. 26 na 120, Imam Abdur-Rahman Nisai katika Khasaisul-Alawiyya, uk. 19, Sibt Ibn Jauzi katika Tadhkira, uk. 13-14, Sulaiman Balkhi Hanafi katika Yanabiul-Mawadda, Sura ya 9 na 17, na vingine vingi vimesimulia hadith hii. Wote wanasema kwamba, Mbali na sehemu mbili za kuanzisha undugu

96

Mikesha ya Peshawar
(Makka na Madina kati ya Masahaba) imesimuliwa pia katika sehemu nyingine nyingi. Kwa hiyo, hadith hii sio ya kutafsiriwa katika maana ya kukomea yenye mipaka au kwa tukio moja makhususi tu. Maana yake ya jumla ni jambo lililothubutu. Ni kupitia Hadithi hii ambapo Mtukufu Mtume alitangaza katika matukio yanayostahili umakamu wa Ali baada yake. Moja ya matukio hayo lilikuwa lile la vita ya Tabuk. Hafidh: Inawezekana vipi Masahaba wa Mtume waliisikia Hadith hii katika maana yake ya jumla, wakijua kwamba ilikuwa na maana ya kwamba umakamu wa Ali uliridhiwa na Mtume na bado baada ya kifo cha Mtume, wakawa maadui na wakamkubali mtu mwingine kuwa Khalifa? Muombezi: Nina marejeo mengi ya kuunga mkono jibu langu kwa swali lako, lakini majibu mazuri zaidi kwa wakati huu ni kuiangalia mitihani ya Harun katika hali inayqfanana kama hii hii. Qurani inaeleza kwamba, wakati Musa alipomteua Harun kuwa makamu wake, aliwakusanya mbele yake Bani-Israil (kwa mujibu wa baadhi ya taarifa watu 70,000 walikusanyika). Musa alisisitiza kwamba, wakati wa kutokuwepo kwake yawapasa kumtii Harun, Khalifa na makamu wake. Kisha Musa alikwenda juu mlimani kuwa peke yake na Allah. Kabla ya mwezi kupita, Samiri alichochea fitna miongoni mwa Bani Israil. Alitengeneza ndama (wa ngombe) wa dhahabu na Bani Israil wakiwa wamemuacha Harun, walikusanyika mbele ya msaliti Samiri katika idadi kubwa. Ilikuwa ni muda mfupi tu umepita kabla ya tukio hili, Bani Israil, hawa hawa walimsikia Musa akisema kwamba wakati wa kutokuwepo kwake Harun atakuwa Khalifa wake na kwamba yawapasa kumtii. Hata hivyo watu 70,000 walimfuata Samiri. Nabii Harun kwa nguvu sana alipinga kitendo hiki na kuwakataza wasijiingize katika matendo hayo ya dhambi, lakini hakuna hata mmoja aliyemsikiliza. Aya ya Sura ya Araf inaeleza kwamba, wakati Musa aliporudi, Harun alimwambia: Ewe mtoto wa mama yangu! Hakika watu hawa wameniona mimi mnyonge na walikuwa karibu waniuwe. (7: 150)

HARUN ALIKUWA NI MRITHI (MAKAMU) WA MUSA ALIYETEULIWA.


Bani Israil wenyewe waliyasikia maelekezo ya wazi kutoka kwa Musa, lakini Musa alipokwenda juu mlimani, Samiri akaitwaa fursa hiyo. Alitengeneza ndama wa dhahabu na kuwapoteza Bani Israil.

97

Mikesha ya Peshawar

KUFANANA KWA HALI YA MAMBO KATI YA ALI NA HARUN.


Hali kadhalika, baada ya kifo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), baadhi ya watu ambao walikuwa wamemsikia akisema kwamba Ali alikuwa ndiye mrithi wake, waligeuka dhidi ya Ali. Imam Ghazali ameelezea jambo hili katika mwanzo wa Makala yake ya nne katika Sirrul-Alamin. Anaeleza kwamba baadhi ya watu walirejea kwenye hali yao ya mwanzo ya ujinga. Kwa hali hii, kuna kufanana kukubwa kati ya hali ya Harun na ile ya Ali. Kama wengi wa wanahistoria wenu wenyewe, Abu Muhammad Abdullah bin Muslim bin Qutayba Bahili Dinawari, Kadhi maarufu sana wa Dinawar, katika Al-Imama wa Siyasa Jz. 1, uk. 14 anasimulia kwa urefu matukio ya Saqifa. Anasema kwamba, walitishia kuchoma nyumba ya Ali na wakamchukua mpaka Msikitini kwa mabavu na kutishia kumuua isipokuwa achukue kiapo cha utii kwao. Ali alikwenda kwenye kaburi tukufu la Mtume na akarudia maneno yale yale ya Qurani ambayo Harun alimwambia Musa:

Yeye (Harun) akasema: Ewe Mtoto wa Mama yangu! Hakika watu hawa waliniona mimi mnyonge na walikuwa karibu waniuwe (7: 150). Nawab: Wakati Umakamu wa Ali ulikuwa umethibitishwa, kwanini Mtume atumie maneno ambayo yalidokezea hiyo maana tu? Kwa nini hakutangaza wazi kwamba Ali alikuwa ndiye makamu wake, ili kwamba kusiweze kuja kutokea pingamizi lolote baada yake? Muombezi: Nilikuambieni kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alielezea ukweli katika njia zote. Hili liko dhahiri kutoka vitabu vyenu, ambavyo vimeandika hadith nyingi mno kuhusiana na suala hili. Watu wasomi wanaelewa kwamba kidokezo ni chenye nguvu sana kuliko maelezo ya vivi hivi tu, hususan pale kidokezo hicho kikiwa chenye mzizi wa kina mno kiasi kwamba kina maana nyingi sana ndani yake Nawab: Umesema kwamba kuna Hadith nyingi za wazi zilizoandikwa na Maulamaa wenu zinazohusu umakamu wa Ali. Tafadhali, je unaweza kutuelezea zaidi kuhusu hili? Tunaambiwa kwamba hakuna hadith ambayo inathibitisha Umakamu wa Ali. Muombezi: Ziko hadith nyingi zinazohusu Ukhalifa katika vitabu vyenu wenyewe vya uhakika.

98

Mikesha ya Peshawar

HADITH YA KARAMU YA NDUGU NA MTUME KUMCHAGUA ALI KAMA KHALIFA WAKE.


Kati ya hadith zote zinazohusu umakamu wa Ali, hadith ya Karamu ndiyo ya muhimu zaidi. Katika siku ambayo Mtume alitangaza Utume wake, alitangaza pia kwamba Ali alikuwa Mrithi wake. Maulamaa wa Madhehebu yenu, wakiwemo Imam Ahmad bin Hanbal, Muwaffaq bin Ahmad Khawarizmi, Abu Jafar Muhammad bin Jarir Tabari, Ibn Abil-Hadid Mutazali na kundi la wengine wamesimulia kwamba wakati Aya ya 214 ya Sura ya Shuara: Na waonye jamaa zako wa karibu, (26:214) ilipoteremshwa, Mtume alikaribisha Makuraish arubaini (miongoni mwa ndugu zake), nyumbani kwa Abu Talib. Aliweka mbele yao mguu wa mbuzi, mkate na kikombe cha maziwa. Walicheka na kusema: Ewe Muhammad! Hukuandaa chakula chakutosha hata kwa mtu mmoja. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: Anzeni kula kwa jina la Allah. Wakati walipokula na wakawa wameshiba vya kutosha, waliambizana: Muhammad amewarogeni na chakula hiki. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasimama katikati yao na kusema; Enyi kizazi cha Abdul-Muttalib! Allah Mwenye uwezo wote amenituma mimi kama Mjumbe kwa viumbe wote kwa jumla na hususan kwenu ninyi. Nakutakeni ninyi mutamke kauli mbili ambazo ni nyepesi na rahisi kwa ulimi, lakini katika mizani ya matendo ni nzito. Kama mtatamka kauli hizo mbili, mutakuwa mabwana wa nchi za Waarabu na wasio kuwa Waarabu. Kupitia kauli hizo mtakwenda Peponi na mtapata kinga kutokana na Moto wa Jahannam. Maelezo hayo mawili ni: Kwanza, kutoa shahada kwa Upweke wa Allah, na Pili kutoa Shahada kwa Utume wangu. Wa kwanza ambaye ataukubali wito wangu na kunisaidia katika kazi yangu atakuwa ndugu yangu, msaidizi wangu, mrithi wangu, na Makamu wangu baada yangu. Mtume alirudia maneno haya ya mwisho mara tatu, na mara zote tatu hakuna aliyejibu isipokuwa Ali, akisema, Mimi nitakusaidia, Ewe Mtume wa Allah. Hivyo Mtume akatangaza: Huyu Ali ni ndugu yangu, na yeye ndiye mrithi wangu, na Khalifa miongoni mwenu.

UTHIBITISHO KUTOKA ULAMAA WA KISUNNI NA WAANDISHI WA ULAYA.


Mbali na Maulamaa wa Kiislamu wa Kishia na Kisunni, Wanahistoria wengi walio waadilifu wa mataifa mengine wameelezea kwa kirefu Karamu hii. Walikuwa hawana upendeleo wa kidini, wakiwa wao sio Shia wala Sunni. Mmoja wa Waandishi hawa ni mwana-Historia na Mwanafilosophia wa Kiingereza wa Karne ya kumi na tisa, Thomas

99

Mikesha ya Peshawar
Carlyle katika kitabu chake Heroes and Hero-worship ametoa maelezo ya kina juu ya karamu iliyofanyika nyumbani kwa Abu Talib. Baada ya maelezo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Ali alisimama na akabainisha imani yake kwa Mtume. Kwa ajili hiyo Ukhalifa uliwekwa juu yake. Waandishi wengine wa Ulaya wamethibitisha jambo hili, wakiwa ni pamoja na George Sale wa Uingereza na Hashim, Mkristo wa Syria katika kitabu chake Maqalatul-Islam, na Bw. John Davenport katika kitabu chake Muhammad and the Quran. Wote wanakubali kwamba mara tu baada ya tangazo la Utume wake, alimuita Ali Ndugu yake, Msaidizi, Makamu na Khalifa wake. Aidha, Hadith nyingi zinathibitisha kwamba Mtume alisisitiza jambo hili katika matukio mengine mengi.

HADITH ZA WAZI NA DHAHIRI KUHUSU UKHALIFA WA ALI.


(1) Imam Ahmad Ibn Hanbal katika Musnad yake na Mir Seyyed Ali Hamadani Shafii katika Mawaddatil-Qurba kuelekea mwisho wa Mawadda ya nne, wameandika kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema; Ewe Ali! Utatekeleza majukumu kwa niaba yangu, na wewe ni makamu wangu juu ya wafuasi wangu. (2) Imam Ahmad Ibn Hanbal katika Musnad, Ibn Maghazili Faqih Shafii katika Manaqib na Thalabi katika Tafsir yake wamesimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kumwambia Ali: Ewe Ali! Wewe ni ndugu yangu, Makamu, Mrithi na Mlipa madeni wangu. (3) Abu Qasim Husain bin Muhammad (Raghib Ispahani) katika Mahadhiratul Udaba wa MuhawaratuSh-Shuara wal-Balagha (kilichochapishwa Amira-e-Shazafiyya, Seyyed Husain Afandi, 1326 A.H.), sehemu ya 2, uk. 213, ananukuu kutokea kwa Ibn Malik kwamba Mtume amesema: Hakika rafiki yangu, msaidizi, makamu na mbora wa watu ambaye ninamuacha nyuma yangu, ambaye atalipa deni langu na kutimiza ahadi yangu ni Ali bin Abu Talib. (4) Mir Seyyed Ali Hamadani katika Mawaddatul-Qurba. Katika mwanzo wa Mawadda ya sita, anasimulia kutoka kwa Khalifa wa Pili, Umar bin Khattab, kwamba wakati Mtume alipoanzisha uhusiano wa Kindugu miongoni mwa Masahaba, alisema: Huyu Ali ni ndugu yangu katika dunia hii na kesho Akhera; yeye ni mrithi wangu kutoka miongoni mwa jamaa zangu na makamu wangu miongoni mwa umma wangu; yeye ndiye mrithi wa elimu yangu na mlipaji wa deni langu, chochote anachoniwia mimi, nami nawiwa naye, faida yake ni faida yangu na hasara yake ni hasara yangu; yoyote aliye rafiki yake ni rafiki yangu,mtu ambaye ni adui yake ni adui yangu.

100

Mikesha ya Peshawar
(5) Katika Mawadda hiyo hiyo, ananukuu hadith kutoka kwa Anas bin Malik, ambayo nimeitaja mapema. Kuelekea mwisho wake anasema kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema; Yeye (Ali) ni Makamu wangu na Msaidizi. (6) Muhammad bin Ganji Shafii ananukuu Hadith kutoka kwa Abu Dharr Ghifari katika Kitabu chake, Kifayatut-Talib kwamba Mtume amesema: Bendera ya Ali, Kiongozi wa Waumini, Kiongozi wa watu wenye nyuso zenye kungara, na Makamu wangu, itakuja kwangu katika chemchem ya Kauthari. (7) Baihaqi, Khatib Khawarizmi, na Ibn Maghazili Shafii wanaandika katika Manaqib zao kwamba alisema kumuambia Ali: Sio sawasawa kwamba mimi niondoke kuwaacha watu bila ya wewe kuwa Makamu wangu kwa vile wewe ndiye bora zaidi wa Waumini baada yangu. (8) Imam Abu Abdur-Rahman Nisai mmoja wa Maimam wa vitabu sita (Siha) vya hadith, anasimulia kwa urefu kutoka kwa Ibn Abbas fadhila za Ali kuhusiana na hadith Na. 23 katika Khasaisul-Alawi. Baada ya kuelezea cheo cha Mtume Harun, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema kumwambia Ali: Wewe ni Makamu wangu baada yangu kwa kila Muumini. Hadith hii na nyingine ambazo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ametumia maneno baada yangu zinathibitisha wazi kwamba Ali alikuwa ndiye mrithi wa mara tu. (9) Kuna Hadith ya Uumbwaji, ambayo imesimuliwa katika njia mbalimbali. Imam Ahmad Ibn Hanbal katika Musnad yake, Mir Seyyed Ali Hamadani katika Mawadda-tul-Qurba, Ibn Maghazili Shafii katika Manaqib, na Dailami katika Firdaus wamemnukuu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema: Mimi na Ali tumeumbwa kwa Nuru Takatifu moja miaka 14,000 kabla Nabii Adam hajaumbwa. Kutoka kwenye mgongo wa Adam na kupitia kizazi chake kitukufu, Nuru hiyo ilirithiwa na Abdul-Muttalib, na kutoka kwake iligawanywa na kurithiwa na Abdullah (baba yake Mtume) na Abu Talib (baba yake Ali). Mimi nilipewa Utume, na Ali alipewa Ukhalifa. (10) Hafiz Abu Jafar Muhammad bin Jarir Tabari (amekufa 310 A.H.) anaandika katika kitabu chake Kitabul-Wilaya kwamba Mtume amesema mwanzoni mwa khutuba yake maarufu pale Ghadir Khum; Malaika Jibril amenifikishia amri ya Allah kunitaka kwamba nisimame sehemu hii na kuwajulisha watu kwamba Ali bin Abu Talib ni ndugu yangu, wasii wangu, na Khalifa wangu baada yangu. Enyi watu! Allah amemfanya Ali kuwa Walii (mlezi) wenu, na Imam (kiongozi). Utii kwake ni wajibu juu ya kila mmoja wenu; amri yake ni yenye mamlaka ya juu; maneno yake ni kweli tupu; laana iwe juu yake yule ambaye anampinga, rehma ya Allah iwe juu ya yule ambaye amemfanya rafiki.

101

Mikesha ya Peshawar
(11) Sheikh Suleyman Balkhi katika Yanabiul-Mawadda anaelezea kutoka katika kitabu cha Manaqib cha Ahmad, na yeye kutoka kwa Ibn Abbas, hadith inayoelezea fadhila nyingi za Ali. Ninainukuu yote hapa. Ibn Abbas anasimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: Ewe Ali! Wewe ni Mchukuzi wa Elimu yangu, Walii na rafiki yangu, Wasii wangu, Mrithi wa elimu yangu na khalifa wangu. Wewe ndiye mdhamini wa urithi wa Mitume wote waliotangulia. Wewe ni msiri wa Allah katika ardhi hii na hoja ya Allah kwa viumbe wote. Wewe ni nguzo ya Iman na mlezi wa Uislam. Wewe ni taa katika giza; nuru ya muongozo, na kwa ajili ya watu wa ulimwengu wewe ni bendera iliyonyanyuliwa juu kabisa. Ewe Ali! Yeyote akufuatae wewe atakuwa ameokolewa; yule ambaye hakutii wewe ataangamia; wewe ni njia ingaayo, na iliyonyooka; wewe ni Kiongozi wa watu wasafi, na Kiongozi wa Waumini; kwa yeyote yule ambaye mimi ni mwenye kutawaliwa mambo (Maula) wake wewe pia ni maula (bwana) kwake; na mimi ndiye Maula (Bwana) wa kila muumini; (Mwanaume na Mwanamke). Ni rafiki yako tu yule aliyezaliwa katika ndoa halali. Allah hakunipeleka mbinguni kuzungumza Naye bila kuniambia, Ewe Muhammad! fikisha salamu zangu kwa Ali na muambie kwamba ni Imam wa rafiki zangu na nuru ya waabuduo! Hongera Ewe Ali, juu ya ubora huu wa ajabu. (12). Abu Muayyid Muwafiqud-Din, msemaji mzuri wa Khawarizm, katika kitabu chake Fadhaill-Amirul-Muminin, kilichochapishwa mwaka 1313 A.H., Sura ya 19 uk. 240, ananukuu nyanzo ambavyo vimesimulia kwamba Mtume amesema: Wakati nilipofika Sidratul-Muntaha (Kituo cha juu sana wakati wa Mirraji) nilisemeshwa hivi: Ewe Muhammad! Wakati ulipowajaribu watu, ni yupi uliyemuona mtiifu zaidi. Nikasema Ali! Kisha Allah akasema: Umesema kweli Muhammad! Tena akaendelea kusema: Umechagua Makamu ambaye atafikisha elimu yako kwa watu, na kuwafundisha waja wangu kutoka Kitabu Changu yale mambo ambayo hawayajui? Nikasema, Ewe Allah! Yoyote utakayemchagua Wewe, nami nitamchagua. Yeye akasema: nimekuchagulia Ali juu yako. Ninamfanya yeye Makamu na Wasii wako. Na akampamba Ali na elimu Yake na uvumilivu. Yeye ni Kiongozi wa Waumini ambaye hakuna hata mmoja anayeweza kuwa sawa naye katika cheo miongoni mwa watangulizi wake au warithi wake. Kuna hadith nyingi kama hizi katika vitabu vyenu Sahih. Baadhi ya Maulamaa wenu waadilifu, kama Nizzam Basri, wameukubali ukweli huu. Salahud-Din Safdi katika kitabu chake Wafa-Bil-Wafiyya, kuhusiana na maelezo ya Ibrahim bin Sayyar bin Hani Basri, ajulikanae kama Nizzam Mutazali, anasema: Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.) alithibitisha Uimama wa Ali na akamchagua kuwa Imam. Masahaba wa Mtume walikuwa na habari kamili juu ya hili, lakini Umar kwa ajili ya Abu Bakr, aliufunika Uimamu wa Ali kwa pazia.

102

Mikesha ya Peshawar
Ni wazi kutoka katika vitabu vyenu, hadith na tafsiri za Qurani kwamba Ali alishika nafasi ya juu sana ya ubora. Khatib Khawarizmi anasimulia kutoka kwa Ibn Abbas katika Manaqib, Muhammad bin Yusufu Ganji Shafii katika kitabu chake Kifayatut-Talib, Sibt Ibn Jauzi katika Tadhkira yake, Ibn Sabbagh Maliki katika Fusulul-Mawadda, Suleiman Balkhi Hanafi katika Yanabiul-Mawadda na Mir Seyyed Ali Hamadani katika Mawaddatul-Qurba, Mawadda ya 5, nakala kutoka kwa Khalifa wa Pili, Umar bin Khattab wote wakithibitisha pamoja na tofauti kidogo tu ya maneno kwamba Mtume alisema: Kama miti yote ingelikuwa ni kalamu, kama bahari ingelikuwa ni wino, kama majini wote na watu wangekuwa waandishi - hata hivyo sifa za Ali bin Abu Talib zisingeweza kuorodheshwa zote.

TABIA ZA MASAHABA.
Sheikh Abdus-Salam: (Akimgeukia Hafidh Muhammad Rashid Sahib). Niruhusu niseme kitu kwa ufupi. (Akigeuka kumwangalia Muombezi). Kamwe hatuzikatai sifa za hali ya juu za Ali, lakini kuweka mipaka ya utukufu kwake peke yake sio sawa, kwa vile Masahaba wakubwa wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) walikuwa kila mmoja, ni watu wa uadilifu. Unajiingiza katika mazungumzo ya upande mmoja, ambayo yanawapoteza watu. Niruhusu kunukuu hadith moja juu ya sifa zao ili ukweli juu ya jambo hili uweze kudhihirishwa. Muombezi: Mimi sijishughulishi na mambo na watu, Aya za Qurani tukufu na hadith sahihi zinatuelekeza katika muelekeo mmoja. Ninaapa kwa Jina la Allah kwamba mimi simpendi au kumchukia yeyote kimbumbumbu. Ninawaomba wasikilizaji kunisimamisha kama wakati wowote nitakimbilia njia yoyote ambayo ni kinyume na hoja au busara. Hadithi zinazokubaliwa na madhehebu zote ziwe ndio za kutegemewa. Sizikatai sifa nzuri za masahaba waadilifu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), lakini yatupasa kutafuta miongoni mwao mmoja ambaye ni bora juu ya umma wote. Mjadala wetu sio wa kuhusu watu wema kwa kuwa wema ni wengi. Yatupasa kutafuta ni yupi aliyekuwa na sifa bora zaidi baada ya Mtume ili kwamba tuweze kumfuata yeye. Sheikh: Unaleta vikwazo visivyo muhimu. Katika vitabu vyenu hakuna hata hadith moja yenye kuwasifu makhalifa. Tutahojiana vipi juu ya msingi huo? Muombezi: Katika usiku wa kwanza wa majadiliano yetu, utakumbuka kwamba Hafidh Sahib mwenyewe aliukubali mjadala juu ya masharti kwamba hoja zetu zitegemee juu ya Aya za Qurani na juu ya Hadith zinazokubaliwa na Madhehebu zote. Kwa vile ninavyo vitabu vyenu Sahih, mimi nilikubali sharti hili. Kama ambavyo nyote mtathibitisha, sijatoka katika msimamo huo. Katika kuunga mkono hoja zangu nimesoma Aya za Qurani tu na Hadith zilizoandikwa katika vitabu Sahih vya Maulamaa wenu mashuhuri. Wakati

103

Mikesha ya Peshawar
mlipoweka sharti hili, hamkujua kwamba mtakuja kunaswa baadae. Hata hivyo, bado sitaki sharti hili lichukuliwe kikamilifu moja kwa moja. Niko tayari kusikiliza hadith zenu za upande mmoja kama ni Sahih. Kisha tutaweza kuyaamua mambo kwa haki. Mimi sina kusita katika kuukubali ukweli kwenye kulinganisha fadhail za Ali. Sheikh: Umetaja hadith inayohusu umakamu wa Ali lakini ukasahau ukweli kwamba kuna hadith nyingi kuhusu Abu Bakr. Muombezi: Kwa kuzingatia akilini kwamba Maulamaa wenu wakubwa, kama vile Dhahabi, Suyuti na Ibn Abil-Hadid wameelezea kwamba Amawi - wafuasi wa Muawiyya na wa Abu Bakr wamebuni hadith nyingi katika kumtukuza Abu Bakr, unaweza kutaja hadithi moja kutoka miongoni mwa nyingi ya hizo ili kwamba mtu muadilifu aweze kuamua juu ya usahihi wake.

HADITH KATIKA KUMTUKUZA ABU BAKR.


Sheikh: Kuna Hadith Sahihi iliyosimuliwa na Umar bin Ibrahim bin Khalid, ambaye anasimulia kutoka kwa Isa bin Ali bin Abdullah bin Abbas, na yeye kutoka kwa baba yake, na yeye kutoka kwa babu yake, Abbas, kwamba Mtume wa Uislamu alimwambia bwana huyo, Ewe Ami yangu! Allah amemfanya Abu Bakr kuwa khalifa wa dini yake. Hivyo msikilize na umtii ili kwamba uweze kupata wokovu. Muombezi: Hii ni Hadith iliyokataliwa. Sheikh: Ni Hadith iliyokataliwa kwa vipi? Muombezi: Maulamaa wenu mashuhuri wenyewe wameikataa. Kwa sababu wasimuliaji wa hadith hii walikuwa ni waongo wenye sifa mbaya na waghushaji, Maulamaa wenu hawaioni kama inastahili kukubalika. Dhahabi katika Mizanul-Itidal, akiandika kuhusu Ibrahim bin Khalid, na Khatib Baghdadi akiandika kuhusu Umar bin Ibrahim anasema: Yeye ni muongo mkubwa. Na Hadith iliyosimuliwa na muongo haikubaliki. Sheikh: Imesimuliwa kutoka vyanzo vya kuaminika kwamba mmoja wa masahaba wachamungu wa Mtume, Abu Huraira, alisimulia kwamba, Jibril alijitokeza mbele ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na akasema: Allah anakutolea salaam, Anasema, Nimemridhia Abu Bakr; muulize kama na yeye pia ameniridhia Mimi au laa. Muombezi: Yatupasa kuwa waangalifu sana kuhusu kutaja Hadith. Nataka usikilize Hadith ambayo Maulamaa wenu wenyewe, kama Ibn Hajar (ndani ya Isaba) na Ibn Abdul-Bar (katika Istiab) wananukuu kutoka kwa Abu Huraira kwamba Mtume amesema: Kuna wengi ambao huninukuu vibaya, na mwenye kunitafsiri vibaya makazi yake ni

104

Mikesha ya Peshawar
motoni. Wakati hadithi inaposimuliwa kwenu kwa niaba yangu ni lazima muipime na Qurani. Hadith nyingine inayokubaliwa na Madhehebu zote, imesimuliwa na Imam Fakhrud-Din Radhi katika Tafsir Kabir Jz. 2, uk. 271 anasimulia kwamba Mtume amesema: Wakati hadith kutoka kwangu inapoelezewa kwenu, iwekeni mbele ya Kitabu cha Allah kama ikikubaliwa na Qurani Tukufu, ikubalini. Vinginevyo, ikataeni. Vitabu vya maulamaa wenu wenyewe mashuhuri vinaeleza kwamba mmoja wa wale ambao walighushi hadith kwa jina la Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), alikuwa huyu mtu aliyekataliwa, Abu Huraira, ambaye umemuita mchamungu. Sheikh: Sikutarajia mtu wa kiwango chako kusema maneno ya kuzua kuhusu masahaba wa Mtume. Muombezi: Unataka mimi nitishwe na neno Sahaba, lakini umekosea kama unafikiri neno Sahaba lazima libebe heshima. Kweli usahaba na Mtume unaongezea fadhila za mtu, lakini hili hutegemea juu ya sharti kwamba Sahaba huyo ni mtiifu kwa Mtume. Kama anakwenda kinyume na maelekezo ya Mtume, basi kwa hakika atakataliwa. Je, Munafiqina (wanafiki) hawakuwa miongoni mwa Masahaba wa Mtume? Ndiyo, walikuwemo, na wote walilaaniwa. Sheikh: Haikuthibishwa kwamba walikataliwa. Kama walikataliwa ni uthibitisho gani kwamba watakwenda motoni? Je, kila mtu aliyekataliwa au kulaaniwa atakwenda motoni? Mtu aliyelaaniwa ni yule ambaye kwa mujibu wa Sheria ya wazi ya Qurani Tukufu, au Hadith ya Mtume ametangazwa hivyo (kuwa atakwenda motoni).

TABIA YA ABU HURAIRA NA LAANA YAKE:


Muombezi: Kuna sababu za wazi kuonyesha kwamba Abu Huraira alikuwa sio mtu wa kuaminika. Maulamaa wenu wenyewe wamethibitisha ukweli huu. Moja ya sababu ya kulaaniwa kwake ni kwamba, kwa mujibu wa maneno ya Mtume, alikuwa rafiki wa mwana kulaaniwa wa mlaaniwa Abu Sufyan. Abu Huraira alikuwa mmoja wa wanafiki. Katika baadhi ya nyakati huko Siffin alisali Sala iliyoongozwa na Amirul-Muminin Ali. Wakati mwingine alikaa katika meza ya chakula ya Muawiya kula chakula chake cha ghali. Kama ilivyoelezwa na Zamakhashari katika Rabiul-Abrar na Ibn Abil-Hadid katika Sherhe ya Nahjul-Balagha, wakati Abu Huraira alipoulizwa sababu za sera yake hii ya udanganyifu, yeye alisema; Chakula cha Muawiyya ni kitamu sana na chenye ladha, na Sala nyuma ya Ali ni bora zaidi. Maulamaa wenu wenyewe, kama vile Sheikhul-Islam Hamwaini katika Faraid Sura ya 37, Khawarizmi katika Manaqib Tibrani katika Ausar, Ganji Shafii katika Kifayatut-Talib (na kundi la wengine), wananukuu kutoka kwa huyu huyu Abu Huraira na wengine kwamba Mtume amesema: Ali yu pamoja na Haki na Haki iko pamoja na Ali. Wakati alipomuacha Ali na kwenda

105

Mikesha ya Peshawar
kubembeleza hisani za Muawiya, hakuwa wa kulaaniwa. Kama mtu si tu hanyamazi aonapo matendo maovu ya Muawiya, bali hushirikiana naye hasa na humsaidia ili kuendeleza nafasi yake mwenyewe ya kilimwengu na kujaza tumbo lake, hivi huyo sio mtu wa kulaaniwa? Abu Huraira huyo huyo mwenyewe anasimulia (kama ilivyoandikwa na Maulamaa wenu mashuhuri, kama Hakim Nishapuri katika Mustadrak, Jz. 2, uk. 124, Imam Ahmad bin Hanbali, Tibrani, na wengine), kwamba Mtume amesema: Ali yu pamoja na Qurani na Qurani iko pamoja na Ali. Viwili hivi havitatengana mpaka vinifikie katika Chemchem ya Kauthar. Ali anatokana na mimi na mimi ninatokana na Ali. Yule ambaye anamtweza Ali, hunitweza mimi. Yule ambaye hunitweza mimi, anamtweza Allah. Muawiya katika hutuba zake za Sala ya Ijumaa alimlaani Ali, Hasan, na Husein. Aliagiza kwamba katika mikusanyiko yote, watu hawa watukufu sharti walaaniwe. Hivyo kama mtu kiukamilifu amejishirikisha na watu walaanifu kama hawa na yu aridhia matendo yao, huyu si wa kulaaniwa? Na wakati anashirikiana na watu hawa, kama huwasaidia kwa kughushi hadith na kulazimisha watu watoe laana dhidi ya watu watukufu, huyu si wa kulaaniwa? Sheikh: Je, ni busara kwetu sisi kukubali masingizio haya, kwamba masahaba waaminifu wa Mtume, wanaghushi hadith na waweze kuwalazimisha watu wamlaani Ali? Muombezi: Kwa kweli ni vigumu kuamini kwamba sahaba mwaminifu angeweza kufanya kitu kama hicho. Kama yeyote katika Masahaba amefanya kitu kama hicho, ina maana kwamba hakuwa muaminifu. Kuna Hadithi nyingi zilizosimuliwa na Maulamaa wenu wenyewe kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: Yule ambaye anamtweza Ali, hunitweza mimi na Allah. Sheikh: Kwa kuwa mkweli, wakati unawasingizia masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kusema kwamba, walighushi hadith, vipi tunaweza kutumaini kwamba hutahusisha maarubu mabovu kwa Maulamaa wa vyeo vya juu wa Kisunni? Ninyi Mashia mna tabia inayofahamika ya kuwakashifu watu maarufu. Muombezi: Huna haki katika kuhusisha vitu kama hivyo kwetu. Historia ya Uislamu ya miaka 1400 iliyopita inathibitisha kinyume chake. Kuanzia mwanzo wa karne ya kwanza ya Uislamu, Bani Umayya wamewatukana Maimam Maasum, dhuria wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na wafuasi wao Mashia. Hata leo, maulamaa wenu mashuhuri wanasimulia hadith za kashfa dhidi ya Mashia katika vitabu vyao ili kuwapoteza watu. Sheikh: Ni ulamaa gani wa Sunni aliyewakashifu Mashia?

106

Mikesha ya Peshawar

KASHFA ZA IBN ABD RABBIH DHIDI YA MASHIA.


Muombezi: Mmoja wa Maulamaa waandishi wenu wakubwa, Shahabud-Bin Abu Umar Ahmad bin Muhammad bin Abd Rabbih Qartabi Andalusi Maliki (aliyefariki 48 A.H.), katika Indul-Farid yake Jz. 1, uk. 269, amewaita Mashia Mayahudi wa Umma huu. Anasema kwamba, kama vile Mayahudi walivyokuwa maadui wa Wakristo, Mashia ni maadui wa Uislamu. Anadai kwamba, Mashia kama walivyo Mayahudi, hawaukubali ukweli kwamba mke aweza kutalikiwa mara tatu kutoka kwa mtu huyo huyo, wala hawaikubali sheria ya Edda. Wote hapa, Mashia na Masunni ambao wana uzoefu na rafiki zao Shia watayacheka madai haya. Utaona katika vitabu vyote vya fiqih ya Kishia mashariti kuhusu talaka tatu na Edda baada ya talaka. Vilevile anatuhumu kwamba Mashia, kama walivyo Mayahudi, ni maadui wa Jibril, kwa sababu Jibril amewasilisha maagizo ya Allah (Wahyi) kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), badala ya Ali (kicheko miongoni mwa wasikilizaji Mashia). Sisi Mashia tunamwamini Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Tunaamini kwamba maagizo ya Allah yaliteremshwa kwake kupitia kwa Malaika Jibril, ambaye cheo chake ni cha juu zaidi kuliko kile kilichohusishwa kwake na mwandishi huyu asiye maana.

KASHFA ZILIZOTOLEWA NA IBN HAZM.


Mwingine kati ya Maulamaa wenu wakubwa ni Abu Muhammad Ali bin Ahmad bin Said Ibn Hazm Andalusi (amekufa 456 A.H.), ambaye ameandika kimakhususi dhana potofu kuhusu Mashia katika kitabu chake mashuhuri Kitabul-Fasil fil-Milal Wan-Nihal. Kwa mfano anasema Shia sio Waislamu, ni waasi, wafuasi wa Mayahudi na Wakristo. Katika Juzuu ya 4, uk. 182, anaandika kwamba: Kwa mujibu wa Mashia, ni halali kuoa wanawake tisa. Riwaya hii inaweza kukanushwa kwa urahisi sana kwa kuangalia vitabu vya Shia ambavyo kwa uwazi vimeeleza kwamba ni haramu kuwa na zaidi ya wanawake wanne katika ndoa ya kudumu, kwa wakati mmoja. Kuna tuhuma nyingi zinazofanana na hizi, zisizo na msingi wa mambo machafu yaliyohusishwa na Mashia katika kitabu chake hiki, ambayo ungeona aibu kuyasikia.

KASHFA ZILIZOTOLEWA NA IBN TAIMIYYA


Mmoja wa Ulamaa wenu mtovu wa dini zaidi ni Ahmad bin Abdul-Halim Hanbali, ajulikanaye kama Ibn Taimiyyah (amekufa 728 A.H.). Alikuwa na dhamira mbaya kupita kiasi juu ya Mashia, Amrul-Muminin Ali, na kizazi cha Mtume. Kitabu chake MinhajusSunna kimejaa uadui mkali dhidi ya Ali na kizazi cha Mtume. Yeyote yule ambaye ana ufahamu wa ukweli japo kidogo angeshangazwa kusikia uongo wake. Kwa mfano anaandika kwamba: Hakuna kundi kubwa la waongo kama madhehebu ya Shia, na ni kwa

107

Mikesha ya Peshawar
sababu hii kwamba waandishi wa vitabu vya Sahih (Sihah Sita) hawakuingiza katika vitabu vyao Hadith zilizosimuliwa na wao. Katika Juz. ya 10, uk. 23 anasema kwamba, Mashia wanaamini katika misingi minne ya dini - Tauhidi, Adili, Nubuwat na Uimam. Kwa kweli katika vitabu vya itiqad vya Shia, vinavyopatikana kila mahali, imeandikwa kwamba itiqad ya Shia ina misingi mitatu: Tauhid, Nubuwat, na Maad (Siku ya malipo); Adil ni sehemu ya Tauhid na Uimam ni sehemu ya Nubuwat. Katika juzuu ya 1, Uk. 131, anaeleza kwamba Mashia hawakusanyiki misikitini. Hawasali Sala ya Ijumaa au Sala za jamaa. Kama wakisali wanasali kila mtu peke yake. (kicheko miongoni mwa Mashia). Lakini kwa hakika tunaweka mkazo mkubwa katika Sala za jamaa. Katika miji mingi ya Iraq na Iran, ambayo ni vituo vya Mashia, misikiti yetu inajaa watu wanaoabudu wakisali sala za Jamaa. Katika ukurasa huohuo, anaandika kwamba Mashia hawafanyi Hijja kwenye Al-Kaaba. Hija yao ni ya kuzuru makaburi tu, ambayo wanaiona ni bora kuliko kwenda kuhiji Makka. Wanawalaani wale ambao hawafanyi Ziara kwenye makaburi. (kicheko). Vitabu vya dua vya Shia vina Sura maalum kwa ajili ya dua za hijja unaoitwa Kitabul-Hajj. Wanatheolojia wa Kishia, wameandika vitabu vingi wakielezea kanuni kwa ajili ya Hijja, ambamo maelekezo maalum yametolewa kutekeleza taratibu za Hijja. Hadithi nyingi kutoka kwa Maimamu wetu zinasisitiza kwamba, kama Muislamu (Shia au Sunni) anao uwezo na bado akashindwa kutekeleza Hija anatengwa katika Uislamu. Wakati akifa anaambiwa: Kufa kifo chochote unachoweza, kiwe kifo cha kiyahudi, Kikristo, au cha muabudu moto. Unaweza kuamini kwamba mbele ya maelekezo kama hayo Mashia wangejiepusha na kutekeleza Hija? Kwa nyongeza juu ya tafsiri hizi potovu, mtu huyu muovu amesema kwamba mwanachuo mkubwa wa Kishia, Muhammad bin Muhammad bin Numan (Sheikh Mufid) ameandika Manasikhul-Hajj lil-Mashahid. Jina sahihi la kitabu hicho ni Mansikhuz-Ziarat, ambacho kinapatikana kila mahali na ambacho kina maelekezo kuhusu kuzuru sehemu za Ziarat, pamoja na Ma-Kuba matukufu ya wastahiki Maimamu. Kama utaviangalia vitabu hivi vya Ziarat, utaona kwamba kutembelea kwenye makaburi ya Mtukufu Mtume na Maimamu kunapendekezwa, sio wajibu. Uthibitisho mzuri dhidi ya tuhuma za mtu huyu mtovu wa dini ni mwendo unaofuatwa na Mashia, ambao huenda kuhiji kwa maelfu kila mwaka. Shutuma nyingine bandia ya muongo huyu, yaweza kupatikana katika juzuu ya 1, uk. 11, ambako anasema kwamba Mashia wanaita mbwa wao kwa majina ya Abu Bakr na Umar na kila siku wanawalaani (hao Abu Bakr na Umar). (Kicheko miongoni mwa Mashia). Hiki ni kichekesho. Kwa mujibu wa itiqad ya Shia, mbwa ni najisi kabisa. Nyumba ya Muislam yenye mbwa hukosa baraka za Allah. Kwa hiyo, Waislamu Mashia wanakatazwa kabisa kufuga mbwa

108

Mikesha ya Peshawar
isipokuwa kwa masharti makhususi (kuwinda, kuilinda nyumba, au kuchunga mbuzi). Moja ya sababu nyingi za kutopatana kati ya Yazid na mjukuu wa Mtume, Imam Husain, ilikuwa kwamba Yazid alikuwa mpenzi wa mbwa na akiwafuga bila kuwa na sababu nzuri. Ibn Taimiyya vilevile anaandika kwamba, kwa vile Mashia wanangojea kutokeza kwa yule wa mwisho wa Maimam wao, katika sehemu nyingi, hususan katika Sardab (Sakafu chini ya nyumba) ya Samara (ambako Mtukufu Imam alitoweka), ameandaliwa farasi kwa ajili yake. Wanamuita Imam wao ajitokeze, wakisema kwamba wamejiandaa kikamilifu kumtumikia Yeye. Vilevile anaandika kwamba Mashia hugeuka kuelekea upande wa mashariki wakati wa siku za mwisho wa Ramadhani na kumwita Imamu ajitokeze. Baadhi yao huacha hata Sala zao za faradhi; wakifikiri kwamba kama watajishughulisha na kusali Sala zao na Imam akajitokeza wangeweza kukosa kumtumikia kwao. (Kicheko kwa Sunni na Mashia). Hatushangazwi sana na Hadith za kuchekesha za mtu huyu muovu. Bali tunashangazwa na tabia za maulamaa wa sasa wa Misri na Damaskas ambao, bila kuwauliza Mashia ambao wanaishi nao, wanafuata upumbavu wa mtu kama Ibn Taimiyya. Itakuwa inachosha sana kutoa orodha ndefu ya riwaya zisizo sahihi za Ibn Hajar Makki, Hafidh, na Kadhi Ruzbahan. Vitabu yao vinajulikana, ingawa katika mtazamo wa usahihi, hivyo havina thamani. Kwa mfano Milal Wan-Nihal cha Muhamma Ibn Abdul-Karim Shahrastani (amekufa 548 A.H.), katika macho ya wanachuoni, hakina thamani hata kidogo. Mtu hataweza kuona chochote ndani yake isipokuwa itiqad bandia kabisa zilizohusishwa kwa Mashia, kama kumuabudu Ali na imani ya kuhama kwa roho (baada ya kufa kuingia katika mwili mwingine). Ni wazi hakuwa mtu mwenye elimu. Akiandika kuhusu Shia Ithnashariyya, yeye anasema kwamba, kaburi la Ali Ibn Hadi Muhamma Naqi, ambaye amekuja baada ya Imam Muhammad Taqi, liko Qum. Lakini hata watoto wadogo wanajua kwamba Kuba Tukufu la Imam Ali Naqi liko ubavuni mwa kuba la Mtoto wake, Imam Hasan Askari huko Samarra. Sidhani kwamba rejea nyingine zaidi za namna hii ni muhimu kuthibitisha kwamba ulamaa wa Kisunni wamebuni riwaya za uongo kuhusu Mashia. Na siko peke yangu katika kulenga shutuma dhidi ya uaminifu wa Abu Huraira. Maulamaa wa Kisunni wamefichua tabia zake mbaya katika vitabu vyao wenyewe.

TABIA ZA ABU HURAIRA NA HADITH ZINAZOTAKA ALAANIWE.


Ibn Abil-Hadid Mutazali katika Sherhe yake ya Nahajul-Balagha, Jz. 1, uk. 358, na katika Jz. 4, anasimulia kutoka kwa Sheikh na mwalimu wake, Imam Abu Jafar Asqalani, kwamba Muawiyya bin Abu Sufyani aliandaa kikundi cha masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na watoto wa masahaba hao kwa lengo la kughushi hadith. Miongoni mwa wale

109

Mikesha ya Peshawar
waliobuni hadith chafu dhidi ya Ali walikuwa Abu Huraira, Amr bin Aas, na Mughira Ibn Shaba. Akitoa maelezo juu ya ngano hizi, Ibn Abil-Hadid anasimulia kwamba, wakati mmoja Abu Huraira aliingia Msikiti wa Kufa na kuona kundi kubwa la watu ambao walikuja kumpokea Muawiya. Alipaza sauti yake kwenye lile kundi la watu: Enyi watu wa Iraq. Mnafikiri kwamba nitasema uongo katika kumpinga Allah na Mtume Wake na kujinunulia moto wa Jahanam? Sikieni kutoka kwangu nilivyosikia kutoka kwa Mtume. Kila Mtume ana Haram (Sehemu takatifu ya kuishi) na Haram yangu ni Madina. Mtu ambaye anahusika na uzushi katika mji wa Madina analaaniwa na Allah, na Malaika Wake, na pamoja na wanadamu wote! Naapa kwa jina la Allah, kwamba Ali alihusika na uzushi. (Yaani, Ali alichochea mfarakano miongoni mwa watu, hivyo, kwa mujibu wa Mtume, anapaswa kulaaniwa). Wakati Muawiya alipolifahamu hili (kwamba Abu Huraira amefanya kitu kama hicho kwa ajili yake na amekifanya katika makao makuu ya Ali, Kufa), alimuita, akampa zawadi, na akamfanya Gavana wa Madina. Je, matendo yake mabaya hayatoshi kuthibitisha kwamba anastahili laana? Je, ni sahihi kwamba mtu ambaye amemfanyia ubaya mbora zaidi wa Makhalifa achukuliwe kama mchamungu kwa sababu tu amewahi kuwa sahaba wa Mtume? Sheikh: Ni katika sababu zipi ambazo Mashia wanamuona kuwa kalaaniwa? Muombezi: Kuna hoja nyingi katika kuunga mkono maoni yetu. Mojawapo ya hizo ni kwamba, mwenye kumtukana Mtume, kwa mujibu wa madhehebu zote amelaaniwa. Kwa mujibu wa Hadith ambayo nimeitaja mapema, Mtukufu Mtume amesema: Mwenye kumtukana Ali, hunitukana mimi, Mwenye kunitukana mimi humtukana Allah. Ni dhahiri kwamba Abu Huraira alikuwa mmoja wa wale ambao, sio tu amemtukana Ali bin Abu Talib, bali ambaye alighushi hadith kuwachochea wengine kumtukana yeye.

NJAMA YA ABU HURAIRA NA BUSR BIN ARTAT KATIKA MAUWAJI YA WAISLAMU.


Vilevile tunamlaani Abu Huraira kwa kula njama kwake na Busri Ibn Artat katika mauaji ya maelfu ya Waislamu. Imesimuliwa na wanahistoria wenu wenyewe, akiwemo Tabari, Ibn Athir, Ibn Abil-Hadid, Allama Samhudi, Ibn Khaldum, Ibn Khallikan, na wengine kwamba Muawiyya alimtuma yule katili Busri Ibn Artat pamoja na wanajeshi wa Syria 4,000 kwenda Yemen kupitia Madina kuwasaga watu wa Yemen na Mashia wa Ali. Washambuliaji hawa waliwaua maelfu ya Waislamu katika mji wa Madina, Makka, Taif, Jabala (Mji wa Tihama), Najran, Safa, na vitongoji vyake. Hawakuwaacha vijana au wazee wa Bani Hashim au Shia wa Ali. Waliwaua hata watoto wadogo wawili wa binamu yake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) Ubaidullah bin Abbas Gavana wa Yemen, ambaye alikuwa ameteuliwa na Ali. Inasemekana kwamba zaidi ya Waislamu 30,000 waliuwawa kwa amri

110

Mikesha ya Peshawar
ya dhalimu huyu. Bani Umayya na wafuasi wao walitenda ukatili huu wa kiwendawazimu. Mpendwa wenu Abu Huraira alishuhudia unyama huu na hakuwa kimya tu, bali pia aliuunga mkono kikamilifu. Watu wasio na hatia kama Jabir bin Abdulla Ansari, na Abu Ayyub Ansari walitafuta pa kukimbilia. Hata nyumba ya Abu Ayyub Ansari ambaye alikuwa mmoja wa masahaba wakubwa wa Mtume, ilichomwa moto. Wakati Jeshi hili lilipoelekea Makka, Abu Huraira alibakia Madina. Sasa naomba mtueleze, kwa jina la Allah, iwapo mtu huyu mlaghai ambaye alikuwa katika usahibu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa miaka mitatu, na ambaye amesimulia zaidi ya Hadith 5,000 kutoka kwa Mtume, hakusikia hadithi zile mashuhuri zinazohusu mji wa Madina? Maulamaa wa madhehebu zote (kama Allama Samhudi katika Tarikhul-Madina, Ahmad bin Hanbal katika Musnad Sibt Ibn Jauzi katika Tadhkira uk. 163) wamenukuu kutoka Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambaye amesema mara kwa mara: Yule ambaye atawatishia watu wa Madina na mateso, atatishwa na Allah na atalaaniwa na Allah, Malaika Wake, na wanadamu wote. Allah hatakubali kitu chochote kutoka kwake. Na alaaniwe yule mwenye kuwatisha watu wa Madina. Kama mtu yeyote atawadhuru watu wa Madina, Allah atamyeyusha kama risasi katika moto. Sasa ni kwa nini Abu Huraira alijiunga na jeshi lile ambalo liliiangamiza Madina? Kwa nini alibuni hadith zenye upinzani kwa makamu sahihi wa Mtume? Na kwa nini aliwachochea watu kumtukana yule mtu ambaye kuhusu yeye Mtume amesema: Kumtukana yeye ni kunitukana mimi? Wewe amua iwapo kama mtu ambaye amebuni hadith kwa jina la Mtume hakuwa mwenye kulaaniwa? Sheikh: Umekosa huruma, sio vyema kwako kumwita Sahaba muaminifu mno wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mtovu wa dini na mzushi.

LAANA YA ABU HURAIRA NA KUPIGWA KWAKE NA UMAR.


Muombezi: Siko peke yangu ambaye sina huruma kwa Abu Huraira. Mtu wa kwanza ambaye hakuwa na huruma naye alikuwa Khalifa wa Pili, Umar bin Khattab. Ibn Athir na Ibn Abil-Hadid katika Sherhe yake ya Nahjull-Balagha, Jz. 3, uk. 104 (iliyochapishwa Misri) na wengine wengi wameeleza kwamba Khalifa Umar alimchagua Abu Huraira kuwa gavana wa Bahrain katika mwaka wa 21 A.H., watu wakamjulisha Khalifa kwamba Abu Huraira amejikusanyia mali nyingi na amenunua farasi wengi. Kwa ajili hiyo Umar akamuondoa madarakani katika mwaka wa 23 A.H. Mara tu Abu Huraira alipoingia kwenye baraza, Khalifa akasema: Ewe adui wa Allah na adui wa Kitabu Chake! Umeiba mali ya Allah? Alijibu: Sikuiba, bali watu wamenipa zawadi. Ibn Saad katika

111

Mikesha ya Peshawar
Tabaqat Jz. 4, uk. 90, Ibn Hajar Asqalani katika Isaba, na Ibn Abdi-e-Rabbih katika Iqdul-Farid Jz. 1, wanaandika kwamba Khalifa alisema: Wakati nilipokufanya Gavana wa Bahrain, ulikuwa huna hata kiatu katika miguu yako, lakini sasa nimesikia kwamba umenunua farasi kwa dinari 1,600. umeipataje mali hii. Alijibu, Hizi ni zawadi za watu ambazo faida yake imekuwa marudufu zaidi. Uso wa Khalifa uligeuka kuwa mwekundu kwa hasira, na alimpiga viboko kwa nguvu sana kiasi kwamba mgongo wake ulivuja damu. Kisha akaamuru zile dinari 10,000 ambazo Abu Huraira alizikusanya huko Bahrain zichukuliwa kutoka kwake na ziwekwe kwenye mfuko wa Baitul-Mal. Hii haikuwa mara ya kwanza kwa Umar kumchapa Abu Huraira. Muslim anaandika katika Sahih yake Jz. 1, uk. 34, kwamba wakati wa uhai wa Mtume, Umar bin Khattab alimpiga Abu Huraira kwa nguvu sana mpaka akaanguka chini. Ibn Abil-Hadid anaandika katika Sherhe yake ya Nahjull-Balagha Jz. 1, uk. 360: Abu Jafar Asqalani amesema: Kwa mujibu wa watu wetu mashuhuri (Yaani Wanachuoni), Abu Huraira alikuwa mtu muovu. Hadith zilizosimuliwa na yeye hazikukubaliwa. Umar alimchapa na kiboko na akamwambia kwamba alikuwa amebadilisha hadith na alihusisha maneno ya uongo kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Ibn Asakir katika kitabu chake Tarikh Kabir, na Muttaqi katika Kanzul-Umma wanasimulia kwamba Khalifa Umar alimchapa viboko, alimkemea na akamkataza kusimulia hadith kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Umar alisema: Kwa sababu unasimulia hadithi nyingi kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) una uwezo tu wa kuhusisha uongo kwake. - Yaani mtu anatazamia mtu muovu kama wewe kutoa uongo tu kuhusu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Hivyo ni lazima uache kusimulia Hadith kutoka kwa Mtume; vinginevyo nitakupeleka katika nchi ya Dus. (Kabila katika Yemen ambalo kwamba Abu Huraira anatokana nalo). Ibn Abil-Hadid, katika Sherhe yake ya Nahjul-Balagha, Jz. 1, uk. 360 (iliyochapishwa Misri) anasimulia kutoka kwa mwalimu wake, Imam Abu Jafar Asqalini, kwamba Ali alisema: Jihadharini na muongo mkubwa miongoni mwa watu, Abu Huraira Dusi. Ibn Qutayba, katika Tawil-e-Mukhtaliful-Hadith, na Hakim katika Mustadrak Jz. 3, na Dhahabi katika Talkhisul-Mustadrak na Muslim katika Sahih yake, Jz. 2, wakielezea kuhusu tabia za Abu Huraira, wote wanasema kwamba Aisha alikuwa alipingana naye mara kwa mara na kusema: Abu Huraira ni muongo mkubwa ambaye hughushi hadith na kuzihusisha na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kwa ufupi sio sisi peke yetu ambao tumemkataa Abu Huraira. Kwa mujibu wa Khalifa Umar, Amirull-Muuminiina Ali, Ummul-Muuminina Aisha, na Masahaba wengine na wafuasi wa Mtume, wamesema kwamba alikuwa sio muaminifu kabisa. Kwa ajili hiyo, Masheikh wa madhehebu ya Mutazila na Maimam wao, na ulamaa wa Kihanafia kwa kawaida wanakataa hadith zilizosimuliwa na Abu Huraira. Aidha, katika Sherhe yake ya Sahih Muslim, Jz. 4, Nadwi anasisitiza nukta hii: Imam Abu

112

Mikesha ya Peshawar
Hanifa amesema: Masahaba wa Mtukufu Mtume kwa ujumla walikuwa ni wacha-Mungu na wanyofu. Ninaikubali kila hadith yenye ushahidi iliyosimuliwa na wao, lakini sizikubali hadith ambazo chanzo chake ni Abu Huraira, Anas Ibn Malik, au Samara bin Jundab. Tunamkataa Abu Huraira yule yule, ambaye Khalifa Umar alimchapa viboko na kumuita mwizi na muongo. Alikataliwa na Ummul-Muminina Aisha, Imam Abu Hanifa, na masahaba wengi na wafuasi wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Tunamkataa Abu Huraira huyo huyo ambaye alikataliwa na kuitwa muongo na Bwana wetu, kiongozi wa wenye kuabudu Mungu mmoja, Ali, na akakataliwa na Maimamu watukufu na dhuria wa Mtume. Tunamkataa Abu Huraira ambaye alikuwa muabudu tumbo, ambaye pamoja na kujua ubora wa Ali, alimpuuza. Alimpendelea mfadhili wake, mlaaniwa Muawiya, alikaa kwenye meza yake ya chakula na kula vyakula vitamu naye, na akatunga hadithi za kumpinga Ali. Kwa mtazamo wa mjadala wetu mpaka sasa, ninyi na mimi tunawajibika kuangalia kwamba wakati hadithi kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ikiwa kwenye mjadala, yatupasa kwanza kuirejesha kwenye Qurani Tukufu. Kama hadith inakubaliana na Qurani, yatupasa kuikubali, vinginevyo la.

MAJIBU KWA HADITH IDHANIWAYO KWAMBA ALLAH ALISEMA, NIMERIDHISHWA NA ABU BAKR - JE NA YEYE AMERIDHIKA NA MIMI?
Hadithi ambayo umeisimulia mapema (ingawa ni ya upande mmoja) yaweza kurejeshwa kwenye Qurani Tukufu. Kama hakuna pingamizi, hapana shaka tutaikubalia. Hata hivyo, aya moja ya Qurani inasema: Na hakika tumemuumba mwanadamu, nasi tunajua yanayopita katika nafsi yake; nasi tukaribu naye zaidi kuliko mshipa wake wa shingo. (50:16) Mnatambua kwamba Hablul-Warid (mshipa wa shingo) ni usemi wa kawaida utumiwao kuelezea ukaribu uliozidi mno. Maana ya Aya hii ni kwamba, Allah ni Mjuzi wa yote. Hakuna kinachofichika kwake, hata kiwe ndani kiasi gani katika moyo wa mtu. Allah anajua siri za nyoyo zetu. Na katika Sura ya Yunus Anasema: Na hushughuliki katika kazi yoyote, wala hasomi humo (kitu chochote) katika Qurani, wala hamfanyi kitendo chochote, isipokuwa sisi tunakuwa mashahidi juu yenu mnaposhughulika nayo. Hakifichikani kwa Mola wako kitu chochote (hata) kilicho sawa na uzito wa mdudu chungu, la katika ardhi wala katika mbingu. Wala (hapana) kidogo kuliko hicho wala kikubwa, isipokuwa kimo katika kitabu (cha Allah) kielezacho (kila kitu). (10:61). Kwa mujibu wa Aya hizi, na kwa mujibu wa akili ya kuzaliwa, hakuna kinachofichikana kwa Allah. Anajua mtu anachofanya au kufikiri. Sasa linganisha hadithi hii na Aya hizi mbili na uone kama zinaweza kupatanishwa. Itawezekana vipi kwamba Allah Mwenye Nguvu zote asijue furaha ya Abu Bakr, kiasi kwamba Yeye mwenyewe awajibike kumuuliza kama ameridhishwa

113

Mikesha ya Peshawar
Naye au la? Akili ya kuzaliwa na Qurani Tukufu vinaonyesha kwamba Hadith hii ni ya uwongo.

HADITH ZENYE KUMSIFU ABU BAKR NA UMAR NA KUTOSTAHILI KWAO.


Sheikh: Hakuna shaka kwamba Mtume alisema: Allah atajionyesha kwa watu wote kwa ujumla na makhususi kwa Abu Bakr. Vilevile alisema: Allah hakuweka kitu chochote kwenye kifua changu ambacho hakukiweka kwenye kifua cha Abu Bakr. Vilevle alisema: Mimi na Abu Bakr ni kama farasi wawili ambao wanalingana sawa katika mbio. Alisema tena: Katika anga kuna malaika 80,000 ambao huomba rehma kwa ajili ya yule ambaye ni rafiki wa Abu Bakr na Umar. Na katika usawa wa upande mwingine wa anga kuna Malaika 80,000 ambao humlaani yule ambaye ni adui wa Abu Bakr na Umar. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) vilevile alisema: Abu Bakr na Umar ni wabora wa wanadamu wote kuanzia mwanzo mpaka mwisho. Cheo cha Abu Bakr na Umar kinaweza kupimwa kutokana na Hadithi ambayo kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: Allah ameniumba mimi kutokana na nuru Yake, Abu Bakr kutokana na nuru yangu, na Umar kutokana na nuru ya Abu Bakr. Umar ni taa ya watu wa Peponi. Kuna hadithi nyingi kama hizo ambazo zimeandikwa katika vitabu vyetu Sahihi. Nimesimulia Hadithi chache tu ili kwamba ujue Cheo halisi cha makhalifa. Muombezi: Maana ya hadhithi hizi huongozea kwenye uasi na ukafiri wa kidini, ambavyo inadhihirisha wazi kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) asingeweza kusema vitu kama hivyo. Hadithi ya kwanza inaonyesha kwamba Allah ana mwili na ni ukafiri kuamini kwamba Allah ana mwili. Hadithi ya pili inaonyesha kwamba Abu Bakr alishiriki katika yale yaliyoteremshwa kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Hadithi ya tatu inamaanisha kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa hali yoyote hakuwa mbora zaidi kwa Abu Bakr. Hadithi nyingine inapingana na hadithi nyingi, ambazo zinakubaliwa na madhehebu zote, kwamba watu wabora zaidi wa ulimwengu huu ni Mtume Muhammad na kizazi chake. Mbali na ukweli huu wa wazi, Maulamaa wenu mashuhuri kama Muqaddas katika kitabu chake Tadhkiratul-Muzua, Firuzabadi Shafii katika kitabu chake Safarus-Saadat, Hasan bin Athir Dhahabi katika kitabu chake Mizanul-ltidal, Abu Bakr Ahmad bin Ali Khatib Baghdad katika kitabu chake cha Tarikh, Abul-Faraj Ibn Jauzi katika KitabulMuzua, na Jalalud-Din Suyuti katika AlLualil-Masnua fil-Abadusil-Muzua wote wamehitimisha kwamba Hadithi hizi ni zakutungwa. Zinapingana na Qurani Tukufu na akili ya kuzaliwa. Sheikh: Lakini hebu angalia hadithi nyingine, ambayo hakika ni sahihi, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: Abu Bakr na Umar ni Mabwana wa wazee wa Peponi.

114

Mikesha ya Peshawar
Muombezi: Kama utaichunguza kwa karibu zaidi Hadith hii inayotarajiwa, unaweza ukaona kwamba, mbali na ukweli kwamba ulamaa wenu wenyewe wameikataa, hadithi hii haiwezekani kuwa inatoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kila mtu anajua kwamba pepo haitaingiwa na wazee. Hakuna mabadiliko ya kidogo kidogo huko. Kuna riwaya nyingi zinazokubaliwa na madhehebu zote zinazohusiana na jambo hili. Moja ya hizo ni suala la Ashjaiyya, mwanamke mzee ambaye alikuja kwa Mtume. Katika maongezi yake, Mtume alisema: Wanawake wazee hawataingia Peponi. Yule mwanamke alihuzunika sana na akasema, huku akilia: Ewe Mtume wa Allah, hii ina maana mimi sitaingia Peponi. Alipokwisha kusema hivi, akaondoka. Mtume akasema: Muambieni kwamba siku hiyo atakuwa kijana na ataingia Peponi. Kisha akasoma Aya ifuatayo kutoka kwenye Qurani Tukufu:

Hakika tumewafanya wakuwe katika umbo (jipya), na tumewafanya vijana kama kwamba ndiyo kwanza wanaolewa, wanapendana na waume zao (walio) hirimu moja na wao, kwa ajili ya watu wa kheri. (56: 35 38). Katika Hadithi nyingine inayokubaliwa na wote ninyi na sisi, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: Wakati wakazi wa Peponi watakapoingia Mbinguni, watakuwa vijana na nyuso safi halisi, nywele za kipilipili, macho ya haiba, umri wa miaka 33. Sheikh: Maelezo yako ni kweli kama yalivyo, lakini hii ni hadithi Makhususi (yaani maalumu kwa ajili ya Abu Bakr na Umar). Muombezi: Sielewi. Una maana gani kwa kusema Hadith Makhususi. Una maana kwamba Allah atapeleka kikundi cha wazee Peponi ili kwamba Abu Bakr na Umar waweze kuwa mabwana zao? Isitoshe, ulamaa wenu mashuhuri wanaiona Hadith hii kuwa ni ya kutungwa. Mtume ametupa utaratibu kwa ajili ya kuthibitisha Hadithi. Nilisema mapema kwamba Hadithi yoyote ambayo haipatani na Qurani ni ya kupuuzwa. Wanachuoni wetu sisi wanakataa Hadithi nyingi zinazodaiwa kutokana na Mtume na Maimamu Watukufu katika misingi ya kanuni iliyotamkwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): Wakati wowote itakapoelezwa Hadith kwamba inatoka kwangu, irejesheni kwenye Qurani Tukufu; kama inakubaliana nayo, ikubalini, vinginevyo, ikataeni. Kwa ajili hiyo, wanachuoni wetu hawakubali hadith ambazo hazikubaliani na Qurani Tukufu. Nilieleza mapema kwamba Maulamaa wenu wameandika vitabu juu ya kukataa Hadithi za kutungwa. Kwa mfano Sheikh Majdud-Din Muhammad bin Yaqub Firuzabadi katika SafarusSaada (uk. 142), Jalalud-Din Suyuti katika Kitabul-Luali, Ibn Jauzi katika Muzua, Muqaddasi katika Tadhkiratul-Muzua, na Sheikh Muhammad bin Darwish (Mashuhuli kwa jina la Hul-e-Beiruti) katika Asnal-Talib - wote wamesema kwamba nyororo ya wasimuliaji wa hadith isemayo kwamba Abu Bakr na Umar ni mabwana wa

115

Mikesha ya Peshawar
wazee wa peponi humchanganya Yahya bin Anbasa. Dhahabi anasema kwamba, huyu Yahya ni msimuliaji asiyeaminika, na Ibn Jan anashikilia kwamba Yahya alikuwa akitunga hadithi. Hivyo, mbali na hoja zangu zilizopita, hata Maulamaa wenu wanaiona kuwa ni hadithi ya uwongo. Kwa kweli, inawezekana kwamba ilitungwa na wafuasi wa Abu Bakr, familia ya Umayya. Ili kuwadhalilisha Bani Hashim na kizazi cha Mtume, walikuwa wakitunga Hadith sambamba na zile sahihi zilizosimuliwa kwa kuitukuza familia ya Mtume. Mtu kama Abu Huraira, ili kupata mwanya wa kuingia kwenye kundi maalum la kiutawala la Bani Umayya, mara kwa mara alighushi hadithi. Kwa sababu ya uadui wao kwa kizazi cha Mtume, walitunga hadithi sambamba na zile zinazokubaliwa na Maulamaa wote wa Shia na Sunni. Nawab: Ni Hadithi ipi inayokubaliwa katika suala hili?

HADITH YA KWAMBA HASAN NA HUSEIN WOTE NI MABWANA WA VIJANA WA PEPONI.


Muombezi: Hadith iliyo Sahihi ni kwamba Mtume alisema: Hasan na Husein ni mabwana wa vijana wa peponi, na baba yao ni mbora zaidi yao. Maulamaa wengi wamesimulia Hadith hii. Kwa mfano Khatib Khawarizmi katika Manaqib, Mir Seyyid Ali Abu Abdur-Rahman Nisai katika Khasais-il-Alawi (hadithi tatu), Ibn Sabbagh Maliki katika Fusulul-Muhimma, uk. 159, Sulaiman Balki Hanafi katika Yanabiul-Mawadda, Sura ya 54, Sibt Ibn Jauzi katika Tadhkira, akinukuu kutoka kwa Tirmidhi, Ibn Maja na Imam Ahmad Hanbal, Sibt Ibn Jauzi katika uk. 133 wa Tadhkiratul-Mawadda, Imam Ahmad bin Hanbal katika Musnad, Tirmidhi katika Sunan na Muhammad bin Yusufu Ganji Shafii katika Kifayatul-Talib Sura ya 97, wameandika hadithi hii na huyu wa mwisho akaongeza kwamba, msimuliaji mkubwa wa hadith, Imam Abdul-Qasim Tibrani, vilevile ameiandika Hadith hii katika Muajamul-Kabir na akaorodhesha wasimuliaji wake mbalimbali wote, kama vile Amirl-Muminina Ali, Umar bin Khattab (Khalifa wa Pili), Hudhaifa Yamani, Abu Said Khudri, Jabir bin Abduullah Ansari, Abu Huraira, Usama bin Zaid, na Abdullah bin Umar. Baada ya hapo. Muhammad bin Yusufu amesema kwamba ni hadith sahihi isiyo na ubishani. Kutovunjika muala wa nyororo ya wasimuliaji wa hadith hii ni uthibitisho wa kuwa kwake Sahihi. Aidha, Hafidh Abu Nuaim Isfahani katika Hilyatul-Auliya Ibn Asakir katika Tarikh Kabir Jz. 4, uk. 206, Hikam katika Mustadrak, Ibn Hajar Makki katika Sawaiq-Muhriqa - kwa ufupi, Maulamaa wenu mashuhuri wote wamethibitisha usahihi wa hadith hii.

116

Mikesha ya Peshawar
Sheikh: Lakini hebu angalia hadith hii, ambayo usahihi wake hakuna atakayeukataa. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: Katika taifa lolote atakaloishi Abu Bakr, sio sahihi kwa mtu yoyote kufadhilishwa kuliko yeye. Hadithi hii inathibitisha kwamba Abu Bakr ni bora kwa Umma wote. Muombezi: Nasikitika kwamba unakubali hadith bila udadisi hata kidogo. Hadith hii ingelikuwa imesimuliwa na Mtume, yeye mwenyewe angetenda kwa mujibu wake. Lakini alitoa kipaumbele kwa Ali mbele ya macho ya Abu Bakr. Je, Abu Bakr hakuwepo wakati wa Mubahila pale ambapo Ali alichaguliwa kama nafsi ya Mtume? Katika vita vya Tabuk, wakati Abu Bakr mtu mzima na mzoefu zaidi alikuwepo, kwa nini Mtume akamfanya Hadhrat Ali naibu na Khalifa wake? Kwa nini Abu Bakr aliondolewa kwa amri ya Mungu na kupendelewa Ali, wakati mtu mzima huyu alipotumwa kwenda Makka kulingania Uislamu na kuzisoma Aya kutoka Sura ya tisa ya Qurani Baraat (Tawba)? Wakati Abu Bakr alikuwepo kwa nini Mtume alimchukua Ali kwenda pamoja naye Makka kuvunja Masanamu, akamfanya apande juu ya mabega yake, akimuamrisha avunje sanamu la Hubal? Kwa nini wakati Abu Bakr alikuwepo Mtume akamtuma Ali kwenda kuhubiri miongoni mwa watu wa Yemen? Mwisho, kwa nini Mtume akamfanya Ali kuwa Mrithi na Makamu wake badala ya Abu Bakr? Sheikh: Kuna hadithi yenye nguvu sana kutoka kwa Mtume ambayo haiwezi kupingwa. Imesimuliwa na Amr bin Aas ambaye amesema: Siku moja nilimuuliza Mtume. Ewe Mtume wa Allah! Ni nani unayempenda sana miongoni mwa wanawake? Akajibu: Aisha. Nikasema: Nani unayempenda sana miongoni mwa wanaume? Akajibu, Baba yake Aisha, Abu Bakr. Kwa vile Mtume amempendelea Abu Bakr juu ya watu wote, basi alikuwa mbora kwa umma wote. Ukweli huu wenyewe, peke yake ni uthibitisho wenye kuvutia zaidi wa kuonyesha uhalali wa ukhalifa wa Abu Bakr.

MAJIBU KWA HADITH INAYODHANIWA KWAMBA ABU BAKR NA AISHA WALIPENDELEWA ZAIDI NA MTUME.
Muombezi: Mbali na ukweli kwamba hadithi hii imetungwa na wafuasi wa Abu Bakr, haipatani na Hadith Sahihi ambazo zinakubaliwa na Madhehebu zote. Hadith hii inapasa kuangaliwa kwa mitazamo miwilii. Kutoka upande wa Ummul-Muminina Aisha na kutoka upande wa Abu Bakr. Mtume asingeweza kusema kwamba kati ya wanawake wote alimpenda Aisha zaidi. Nimekwisha sema tangu mwanzo kwamba hii inakinzana na Hadithi nyingi Sahihi zilizomo kwenye vitabu vyote vya Sunni na Shia. Sheikh: Ni hadithi zipi zinazopingana na riwaya hii?

117

Mikesha ya Peshawar
Muombezi: Kuna hadithi nyingi kuhusu Mama wa Maimamu; Fatima Zahra, zilizosimuliwa na Maulamaa wenu wenyewe, ambazo zinapingana na maelezo yako. Hafidh Abu Bakr Baihaqi katika Kitabu chake cha Tarikh, Hafidh Ibn Abdul-Bar katika Istiab, Mir Seyyid Ali Hamadani katika Mawaddatul-Qurba, na wengine miongoni mwa Maulamaa wenu, wamesimulia kwamba Mtume mara kwa mara amesema: Fatima ni mbora wa wanawake wote na wa umma wangu.. Imam Ahmad bin Hanbal katika Musnad, na Hafidh Abu Bakr Shirazi katika NuzululQurani Fi Ali anasimulia kutoka kwa Muhammad bin Hanafiyya, na yeye kutoka kwa Amirul-Muminina Ali, Ibn Abdul-Bar katika Istiab, katika maelezo juu ya Fatima, yaliyosimuliwa katoka kwa Ummul-Muminina Khadija, kutoka kwa Abdul-Warith Bin Sufyani na kutoka kwa Abu Dawud na Anas Bin Malik, Sheikh Sulaimani Balkhi Hanafi katika Sura ya 55 ya Yanabiul-Mawadda, Mir Seyyid Ali Hamadani katika Mawaddatul-Qurba, Mawadda ya 13 - hawa na wasimuliaji wengine wa Hadith wameelezea kutoka kwa Anas Bin Malik kwamba, Mtume alisema: Kuna wanawake wanne walioshinda wote wa ulimwengu: Mariam, bint wa Imran; Asiya, bint wa Mazahim; Khadija, bint wa Khalid; na Fatima, binti wa Muhammad. Khatib katika Tarikh Baghdad; anasimulia kwamba Mtume aliwatangaza wanawake hawa wanne kuwa ni wabora wa wanawake wote wa ulimwengu. Kisha akamtangaza Fatuma kuwa ni mbora wao wote ulimwenguni na Akhera. Muhammad bin Ismaili Bukhari katika Sahihi yake, na Imam Ahmad bin Hanbal katika Musnad yake wanasimulia kutoka kwa Aisha bint Abu Bakr kwamba Mtume alisema kumwambia Fatima: Ewe Fatima, ninakupa habari njema kwamba Allah amekufanya mbora wa wanawake wote duniani na amekufanya wewe kuwa ndiye mtakatifu zaidi wanawake wote wa Uislamu.. Vilevile Bukhari katika Sahihi yake, sehemu ya 4, uk. 64 Muslim katika Sahih yake Jz. 2, katika Mlango wa Fadhail za Fatima, Hamidi katika Jama Bainus-Sahihain yake, Abdi katika Jama Bainus-Sihahu-s-Sitta hawa na wengine wengi wamesimulia kutoka kwa Ummul-Muminiina Aisha kwamba Mtume alisema: Ewe Fatima! hufurahi kwamba wewe ni Bibi wa wanawake wote wa ulimwengu? Ibn Hajar Asqalani amenukuu maneno hayo hayo katika kitabu chake Isaba kuhusiana na maisha ya Fatima pamoja na maelezo: Wewe ni mbora wa wanawake wote wa ulimwengu. Vilevile, Bukhari, Muslim, Imam Ahmad Bin Hanbal, Tibrani na Sulaiman Balkhi Hanafi - wote wameiandika hadith hii.

AYA JUU YA MAPENZI KWA FAMILIA YA MTUME.


Kwa nyongeza, Bukhari na Muslim; kila mmoja katika Sahih yake, Imam Thalabi katika Tafsir yake, Imam Ahmad bin Hanbal katika Musnad, Tibrani katika Mujamul-Kabir,

118

Mikesha ya Peshawar
Sulaimani Balkh Hanafi katika Yanabiul-Mawadda, Sura ya 32 kutoka kwenye Tafsir ya Ibn Abi Hatim, Manaqib ya Hakim, Wasit na Wahidi, Hilyatul-Auliya cha Hafidh Abu Nuaim Isfahani na Faraid ya Hamwaini, Ibn Hajar Makki katika Sawaiq, Muhriqa chini ya Aya ya 14 kwa idhini ya Ahmad, Muhammad bin Talha Shafii katika Mutalibus-Suul uk. 8, Tabari katika Tafsir, Wahidi katika Asbabun-Nuzul, Ibn Maghazil katika Manaqib, Muhibud-Din Tabari katika Riyazun-Nuzra, Mumin Shablanji katika Nurul-Absar, Zamakhshari katika Tafsir, Imam Fakhrud-Din Razi katika Tafsir Kabir, Sayyid Abu Bakr Shahabud-Din Alawi katika Rishfatus-Sadi min Bahr-eFazail-e-Baniul-Nabiil-Hadi Sura ya 1 uk. 22 23 kutoka Tafsir ya Baghawi, Tafsir ya Thalabi, Manaqib ya Ahmad, Tafsir Kabir na Ausat vya Tibrani na Sadi, Sheikh Abdullah bin Muhammad bin Amir Shabrawi Shafii katika Al-Ittihaf uk.5 kutoka kwa Hakim, Tibrani na Ahmad, Jalalud-Din Suyuti katika Ihyau-l-Mayyit kutoka Tafsir za Ibn Mudhir, Ibn Abi Hatim, Ibn Mardawaih, na Mujamul-Kabir cha Tibrani; na Ibn Abi Hatim na Hakim - kwa ufupi, wengi wa maulamaa wenu mashuhuri (ukiondoa wafusi wachache wa Bani Umayya na maadui wa Ahlul Bait), wamesimulia kutoka kwa Abdullah bin Abbas na wengine, kwamba wakati Aya ifuatayo ya Qurani Tukufu ilipoteremshwa: Sema: Siombi malipo yoyote kwa haya bali mapenzi kwa jamaa zangu; na anayefanya wema tutamzidishia wema (42:23). Kikundi cha Masahaba wakauliza, Ewe Mtume wa Allah! ni nani hao jamaa zako ambao mapenzi kwao yamefanywa wajibu juu yetu na Allah? Mtume Akajibu, Ni Ali, Fatima, Hasan na Husein. Baadhi ya Hadith zina maneno, na watoto wao yaani watoto wa Hasan na Husein.

KUKUBALI KWA SHAFII KWAMBA MAPENZI KWA AHLU BAIT NI WAJIBU.


Hata Ibn Hajar (mtu shupavu sana asiye mvumilivu) katika kitabu chake SawaiqMuhriqa uk. 88, Hafidh Jamalud-Din Zarandi katika Mirajul-Rasul, Sheikh Abdullah Shabrawi katika Kitabul-Ittihaf, uk. 29, Muhammad Bin Ali Sabban wa Misir katika Asafur-Raghibin, uk. 119, na wengine wamesimulia kutoka kwa Imam Muhammad Bin Idris Shafii, ambaye ni mmoja wa Maimamu wenu wanne na kiongozi wa kidini wa madhehebu ya Shafii, kwamba alikuwa akisema: Enyi Ahli Bait wa Mtume wa Allah! Mapenzi kwenu yamefanywa wajibu kwetu na Allah kama ilivyokuja katika Qurani Tukufu (akirejea aya iliyotajwa hapo juu). Inatosha kwa hadhi yenu kwamba, kama mtu hatatoleeni salamu katika Sala, Sala yake haitakubaliwa. Sasa ninakuuliza, inawezekana hadithi ya upande mmoja iliyoelezwa na wewe ikasimama dhidi ya Hadith zote hizi Sahihi ambazo zimekubaliwa na madhehebu yote ya Sunni na Shia?

119

Mikesha ya Peshawar

DHANA POTOFU KUHUSU MAPENZI YA MTUKUFU MTUME (S.A.W.W.) KWA AISHA.


Kuhusu mapenzi ya Mtume kwa Aisha, unafikiri kwamba kwa sababu ya matamanio yake ya kimwili alimpenda Aisha zaidi kuliko Fatima? Ni kweli kwamba Aisha alikuwa mke wake na kwa hiyo ni Ummul-Muminina (Mama wa Waumini) kama wake wengine wa Mtume. Lakini je, inakubalika kwamba alimpenda Aisha zaidi kuliko alivyompenda Fatima, ambaye mapenzi kwake yamefanywa wajibu katika Qurani Tukufu, ambaye kwa ajili yake iliteremshwa aya ya utakaso na ambaye alijumuishwa kwenye Mubahila? Hakika unajua kwamba Mtume na warithi wake hawakushawishiwa na matamanio ya kimwili, na kwamba walimgeukia Allah peke yake. Kujifunga huku kulikuwa kwa makhususi kabisa ni halisi hasa kwa yeye mwisho wa Mitume. Aliwapenda wale ambao Allah aliwapenda. Je, yapasa sisi kuzikataa hadithi hizi sahihi ambazo zimekubaliwa na Maulamaa wa madhehebu zote, na ambazo zinakubaliana na Aya za Qurani Tukufu, au tuichukulie Hadith ambayo umesimulia hivi punde tu kuwa ni ya kutungwa? Unadai kwamba Mtume amesema alimpenda Abu Bakr zaidi kuliko mtu mwingine yoyote. Lakini dai hili vilevile liko mbali na hadithi Sahihi nyingine nyingi ambazo zimesimuliwa na Maulamaa wenu wenyewe, ambao wamesisitiza kwamba, kwa mujibu wa Mtume, mtu aliyependwa sana alikuwa ni Ali.

MTUKUFU MTUME (S.A.W.W.) ALIMPENDELEA ALI KULIKO WATU WENGINE WOTE.


Sheikh Suleiman Balkhi katika Yanabiul-Mawadda, Sura ya 55, anasimulia kutoka kwa Tirmidhi hadith ya Buraida kwamba, kwa mujibu wa Mtume, mwanamke aliyependwa zaidi alikuwa ni Fatima na mwanaume aliyependwa zaidi sana alikuwa ni Ali. Muhammad bin Yusuf Ganji Shafii katika Kifayatut-Talib Sura ya 91, anaandika kutoka kwa Ummul-Muminina Aisha kwamba alisema: Allah hakuumba mtu yeyote ambaye Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimpenda zaidi kuliko Ali. Anaongeza kusema kwamba, hii ndio hadith ambayo Ibn Jarir katika Manaqib yake na Ibn Asakir Damishqi katika tarjuma yake wameisimulia kutoka kwa Ali. Muhyid-Din na Imamul-Haramain Ahmad Bin Abdullah Shafii wanasimulia kutoka kwa Tirmidhi katika Dhakhairul-Uqba kwamba watu walimuuliza Aisha ni mwanamke yupi aliyekuwa anapendwa zaidi na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na yeye akajibu, Fatima. Kisha aliulizwa kuhusu mwanaume aliyependwa zaidi na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na akajibu, Ni mume wake, Ali bin Abu Talib. Tena alisimulia kutoka Mukhalis cha Dhahabi, na Hafidh Abul-Qasim Damishqi na yeye kutoka kwa Aisha kwamba alisema yeye Aisha: Sijaona mwanaume aliyependwa zaidi na Mtume kuliko Ali, wala mwanamke aliyependwa zaidi kama Fatima. Kwa nyongeza, Sheikh huyu anasimulia kutoka kwa Hafidh Khajandi na

120

Mikesha ya Peshawar
yeye kutoka kwa Maazatul-Ghifariyya kwamba alisema: Nilikwenda kuonana na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwenye nyumba ya Aisha ambapo Ali alikuwa nje ya nyumba hiyo. Mtume akamuambia Aisha, Huyu (Ali) ndiye kipenzi mno kwangu na mwenye kuheshimika zaidi miongoni mwa wanaume wote, Tambua haki yake na mpe heshima kwa cheo chake. Sheikh Abdullah bin Muhammad bin Amir Shabrawi Shafii ambaye ni mmoja wa Maulamaa wenu mashuhuri, ameandika katika Kitabul-Ittihaf bi Hubbil-Ashraf, uk. 9, Sulaiman Balkhi katika Yanabiul-Mawadda na Muhammad bin Talha Shafii katika Matalibus-Suul, uk. 6, kutoka kwa Tirmidhi, na yeye kutoka kwa Jami bin Umar - wote wamesimulia ifuatavyo: Nilikwenda kwa Ummul-Muminina Aisha pamoja na shangazi yangu (dada yake baba), na tulimuuliza, ni nani ambaye alikuwa akipendwa zaidi na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Yeye alijibu, Miongoni mwa wanawake alikuwa ni Fatima na miongoni mwa wanaume, ni mumewe Ali bin Abi Talib. Hadithi hii hii imesimuliwa na Mir Sayyid Ali Hamadani Shafii katika Mawaddatul-Kurba Mawadda ya 2, pamoja na tofauti kidogo kwamba Jami bin Umar alisema kwamba alipokea jibu hili kutoka kwa shangazi yake. Halikadhalika, Khatib Khawarizmi amesimulia hadithi hii kutoka kwa Jami bin Umar, na yeye kutoka kwa Aisha mwishoni mwa sura ya 4 ya Manaqib yake, Ibn Hajar Makki, katika Sawaiq Muhriqa, kuelekea mwishoni mwa sura ya 2, baada ya kuandika hadithi 40 juu ya fadhila za Ali, anasimulia hadith ifuatayo kutoka kwa Aisha: Miongoni mwa wanawake, Fatima alikuwa ndiye mwanamke aliyependwa zaidi na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na miongoni mwa wanaume ni mume wake. Muhammad bin Talha Shafii, katika Matalib-us-Suul, uk. 7, baada ya ya kuandika Hadith mahususi mbali mbali juu ya suala hili, anaelezea hitimisho lake mwenyewe katika maneno yafuatayo: Hadith hizi sahihi na zisizokifani huthibitisha kwamba Fatima alikuwa mwenye kupendwa zaidi na Mtume kuliko wanawake wote. Ni mwenye cheo cha juu zaidi ya wanawake wote wa Peponi na pia wa mbele zaidi juu ya wanawake wa Madina. Hadithi hizi za kuaminika, kwa uwazi zinathibitisha kwamba katika viumbe wote, Ali na Fatima walikuwa ndio wenye kupendwa zaidi na Mtume. Uthibitisho mwingine wa Mtume kumpendekeza zaidi Ali kuliko wanaume wengine ni ile Hadith ya Ndege (Hadith-e-Tair). Hadithi hii inajulikana sana na kukubaliwa sana kiasi kwamba hatuhitaji kutaja vyanzo vyake vyote. Nitataja tu baadhi ya hivyo.

HADITHI YA NDEGE ALIYEBANIKWA:


Wengi wa ulamaa wenu, kama Bukhari, Muslim, Tirmidhi, Nisai, na Sijistani katika Sahih zao, Imam Ahmad bin Hanbali katika Musnad yake, Ibn Abil-Hadid katika Sherhe yake ya Nahjul-Balagha, Ibn Sabbagh Maliki katika Fusulul-Muhimma, na Sulaiman Balkhi Hanafi katika Yanabiul-Mawadda, Sura ya 8, na kundi la waandishi wengine waaminifu wameiandika Hadith-e-Tair katika vitabu vyao. Wanathibitisha

121

Mikesha ya Peshawar
kwamba hadithi hii ilielezewa na wasimuliaji wa Hadith 24, kutoka kwa Anas bin Maliki. Ibn Sabbagh Maliki katika Fusulul-Muhimma anaandika kuhusu hadith hii katika maneno haya: Katika vitabu vya Hadith Sahihi na riwaya za kuaminika, Hadith-e-Tair, kutoka kwa Anas bin Malik ni haipingiki. Sibt Ibn Jauzi, katika uk. wa 23 wa kitabu chake Tadhkira na Sunan ya Tirmidhi na Masudi katika uk. wa 49 juzuu ya 2 ya Murujudh-Dhahab, wameangalia hususan katika sehemu ya mwisho ya hadithi hii ambayo ina dua ya Mtume na kukubaliwa kwake na Allah. Imam Abdur-Rahman Nisai katika hadith ya tisa katika kitabu chake Khasaisul-Alawi na Hafidh Bin Iqda na Muhammad bin Jarir Tabari, wote wamerejea kwenye nyororo isiyokatika ya wasimuliaji na kwenye vyanzo sahihi vya hadith hii, wakisema kwamba ilisimuliwa na masahaba 35 wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kutoka kwa Anas bin Malik. Kwa ufupi, Maulamaa wenu wote mashuhuri wamethibitisha usahihi wa hadith hii na wameijumuisha kwenye vitabu vyao. Allama Sayyid Hamid Husain ameweka juzuu nzima ya kitabu chake Abaqatul-Anwar kwa ajili ya Hadithi hii tu. Alikusanya vyanzo vyote vya kuaminika kutoka kwa Maulamaa wenu mashuhuri na kwa wazi kabisa akathibitisha usahihi wa hadith hii. Kwa mujibu wa Hadith hii, siku moja mwanamke mmoja alileta zawadi ya ndege aliyebanikwa kwa Mtume. Kabla ya kumla, Mtume akiwa amenyoosha mikono yake juu, akamuomba Allah hivi: Ee Allah! Kati ya viumbe wako wote, mlete mtu ambaye ni mpenzi zaidi kwako na kwangu, ili kwamba ale pamoja nami ndege huyu wa kubanikwa. Ndipo Ali akaingia ndani akala ndege yule wa kubanikwa pamoja na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Baadhi ya vitabu vyenu, kama vile Fusulul-Muhimma cha Malik, Tarikh cha Hafidh Nishapuri, Kifayatut-Talib cha Ganji Shafii na Musnad ya Ahmad Bin Hanbal, n.k. ambamo Hadith hii imesimuliwa kutoka kwa Anas bin Malik, vimeandikwa kwamba Anas bin Malik alisema Mtume alikuwa bado hajamaliza dua yake wakati Ali alipoingia nyumbani pale, lakini nikamficha jambo lile. Wakati Ali alipoingiza mguu wake mara ya tatu, Mtume akiniamrisha nimuache aingie ndani. Wakati Ali alipoingia Mtume akasema: Baraka za Allah ziwe juu yako; ni kitu gani kimekuleta kuja kwangu? Ali akamueleza kwamba alikuja kwake mara tatu lakini aliruhusiwa kuingia safari hii tu. Mtume akaniuliza ni kitu gani kimenifanya niwe hivyo, na nikajibu: Ukweli ni kwamba, niliposikia dua yako, nilitamani kwamba heshima hii ingekwenda kwa mmoja wa kabila langu. Sasa nakuulizeni enyi waungwana iwapo dua ya Mtukufu Mtume ilikubaliwa au kukataliwa na Allah. Sheikh: Ni wazi Allah aliikubali kwa vile aliahidi katika Qurani tukufu kwamba angekubali dua ya Mtume. Aidha, Allah alijua kwamba Mtume asingeweza kuomba dua isiyofaa. Hivyo Allah aliyakubali maombi yake kila wakati. Muombezi: Allah alimpeleka Ali, mtu anayestahiki zaidi katika viumbe Wake, kwa

122

Mikesha ya Peshawar
Mtume. Wanachuoni wenu wenyewe wamethibitisha tukio hili. Muhammad bin Talha Shafii katika Kitabu chake Matalib-Us-Sulu, Sura ya 1, sehemu ya 5, uk. wa 15, amethibitisha cheo cha juu cha Ali kama mwenye kupendwa zaidi na Allah na Mtume juu ya msingi wa Hadith ya Bendera (Riyat) na Hadith ya Ndege. Katika kuhusiana na hilo anasema: Nia ya Mtume ilikuwa kwamba watu waelewe cheocha kipekee na cha hali ya juu cha Ali, ambaye alifikia upeo wa juu zaidi wa kuweza kufikiwa na wacha Mungu. Vilevile Hafidh na Muhammad bin Yusufu Ganji Shafii (aliyekufa 658 A.H.) anaandika katika kitabu chake, Kifayatut-Talib Sura ya 33, akizungumzia fadhila za Ali ibn Abi Talib, kwamba hadith hii kwa uwazi kabisa inathibitisha kwamba Ali alikuwa kipenzi sana katika viumbe kwa Allah. Baadae anasema kwamba Hakim Abu Abdullah Hafidh Nishapuri ameisimulia hii Hadith-e-Tair ya Anas kutoka wasimuliaji 86 na vile vile akaandika na majina ya wasimuliaji wote 86 (Tazama Kifayatut-Talib, Sura ya 32). Ile hadith ambayo umenukuu wewe, ukiilinganisha na Hadith zilizosimuliwa na Maulamaa wenu wa daraja za juu (isipokuwa washupavu wakorofi wachache), haiwezi kutegemewa na ingekataliwa na watu wenye elimu. Sheikh: Nina wasiwasi kwamba umeamua kwa akili yako kutokubali tunayo yasema. Muombezi: Unawezaje kuhusisha chuki kama hizo kwangu? Unaweza ukatoa mfano mmoja tu ambapo umetoa hoja yenye nguvu na mimi bila sababu nikaikataa? Ninaapa kwamba katika mijadala ya kidini na Mayahudi, Wakristo, Wahindu na Wabrahmin na Mabahai wasio na elimu wa Iran, Makadian wa India na wayakinifu (wenye kuamini vitu vyenye kuonekana, kugusika na kuhisiwa tu) katika hali zote hizi mimi sijawahi kufanya ukaidi katika hoja zangu. Kamwe sijawahi kuwa mbishi kwa makafir hawa vipi nitaweza kufanya hivyo kwenu ninyi, ndugu zangu katika Uislamu? Sheikh: Tumesoma maelezo ya mjadala wako na Wahindu na Wabrahmin wa Lahore katika magazeti. Tulivutiwa mno na maelezo hayo. Ingawa tulikuwa hatujakutana na wewe, tulijisikia tumeungana na wewe kimaadili. Natumaini kwamba Allah atakuongoza wewe na sisi kwenye njia iliyonyooka. Tunaamini kwamba kama kuna wasiwasi wowote kuhusu Hadith fulani, inatupasa, kwa mujibu wa ushauri wako, kuirejesha kwenye Qurani Tukufu. Hata hivyo, kama unahoji ubora wa khalifa Abu Bakr na muundo wa ukhalifa wa makhalifa wakubwa, na kama utaziona hadith kuwa ni zenye mashaka, je, utasita vilevile kuamini hoja ambayo imetegemea juu ya Qurani Tukufu? Muombezi: Allah asitujaalie siku tutakayotilia shaka ukweli uliotegemea juu ya Qurani Tukufu au Hadith Sahihi. Walakini, wakati tutakapokuwa tumeingia kwenye mjadala wa kidini na Taifa lolote au Jumuiyya, wao vilevile wanahoji kutoka kwenye Aya za Qurani Tukufu kuthibitisha mtazamo wao. Kwa vile Aya za Qurani zina daraja mbalimbali za maana, Mtume wa mwisho, ili kuwalinda watu dhidi ya kutoelewana, hakuiacha Qurani kama chanzo pekee tu cha mwongozo. Kama inavyokubaliwa na madhehebu zote (Shia na

123

Mikesha ya Peshawar
Sunni), yeye mwenyewe (Mtume) alisema: Nawaachieni vitu viwili vizito: Kitabu cha Allah (Qurani) na kizazi changu. Kama mtashikamana na viwili hivi, kamwe, hamtapotea baada yangu. Hakika viwili hivi kamwe havitatengana mpaka vinifikie kwenye chemchem ya Kauthar. Kwa sababu hii, maana ya ufunuo wa Qurani Tukufu yapasa itafutwe ama kutoka kwa Mtume, fasir mkuu wa Qurani Tukufu, au baada yake, kutoka kwa wale walio sawa na Qurani Tukufu, dhuria watukufu wa Mtume. Qurani Tukufu inasema: Basi waulizeni wenye kumbukumbu ikiwa ninyi hamjui. (21:7).

WATU WENYE KUMBUKUMBU NI AHLI MUHAMMAD DHURIA WA MTUKUFU MTUME (S.A.W.W.).


Ahludh-Dhikr maana yake watu wenye kumbukumbu, ambao ni Ali na Maimamu watukufu, kizazi chake, ambao wako sawa na Qurani. Sheikh Sulaiman Balkhi Hanafi katika kitabu chake Yanabiul-Mawada, Sura ya 39, akinukuu kutoka Tafsir-e-KasfulBayan ya Imam Thalabi, anasimulia kutoka kwa Jabir Ibn Abdullah Ansari, ambaye amesema: Ali amesema: Sisi dhuria wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni watu wa kumbukumbu. Kwa vile Dhikr, Kumbukumbu, ni moja ya majina ya Qurani Tukufu, familia hii inajumuisha na watu wa Qurani. Kama ilivyoelezwa na Maulamaa wa kwenu na wa kwetu, Ali amesema: Niulizeni kitu chochote mnachotaka kabla sijakuacheni. Niulizeni kuhusu Kitabu kitukufu (Qurani) kwa vile ninajua kuhusu kila Aya ndani yake iwe imeteremshwa wakati wa usiku au wakati wa mchana, katika tambarare au katika milima. Kwa jina la Allah, hakuna Aya ya Qurani Tukufu iliyoteremshwa bali najua iliteremshwa kuhusu nini. Allah (S.w.t.) amenijaalia mimi kuwa na ulimi fasaha na akili yenye busara. Kwa hiyo, kutegemeza hoja juu ya Aya za Qurani tukufu, yapasa iwe kwa mujibu na maana yake sahihi na tafsir iliyotolewa na wale wenye uwezo wa kutoa tafsir ya kuaminika. Vinginevyo, kila mtu atatoa tafsir yake ya Aya za Qurani, kwa mujibu wa upeo wa elimu yake na imani, na hii itaishia tu kwenye hitilafu za maoni na mgongano wa mawazo. Pamoja na hoja hii katika akili, naomba usome hizo Aya zako.

AYA ZA QURANI TUKUFU KUHUSU KUCHAGULIWA KWA MAKHALIFA WANNE, NA MAJIBU.


Sheikh: Allah anasema kwa uwazi katika Qurani Tukufu:

124

Mikesha ya Peshawar
Muhammad ni Mtume wa Allah, na walio pamoja naye ni wenye nyoyo thabiti mbele ya makafiri, na wenye kuhurumiana wao kwa wao, utawaona wakiinama kwa kurukuu na kusujudu (katika Sala), wakitafuta fadhila za Allah na radhi (yake). Alama zao ni katika nyuso zao kwa taathira (athari) ya kusujudu (48:29). Kwanza Aya hii huthibitisha ubora wa Abu Bakr. Pili huonyesha nafasi za makhailfa wanne kinyume na inavyodaiwa na madhehebu ya Shia kwamba Ali alikuwa Khalifa wa kwanza. Aya hii bila ubishani inaelezea kwamba Ali alikuwa Khalifa wa nne. Muombezi: Hakika Aya hii haitoi dalili yoyote ya wazi kuhusu namna ya kuchaguliwa makhalifa au kuhusu ubora wa Abu Bakr. Kwa hiyo, lazima uonyeshe ni sehemu ipi katika Aya hii ambapo maana hiyo imefichwa. Sheikh: Mwanzoni mwa Aya hii, usemi (usemao) na walio pamoja naye huashiria kwa yule mtu maarufu ambaye alikuwa na Mtume usiku wa pango. Utaratibu wa kupokezana nafasi ya ukhalifa pia iko wazi katika aya hii. Walio pamoja naye ina maana ya Abu Bakr, ambaye alifuatana na Mtume kwenye Pango la Thawr katika usiku wa Hijra. Usemi, wenye nyoyo thabiti mbele ya makafir maana yake ni Umar Bin Khattab, ambaye alikuwa mkali sana kwa makafir. Usemi, wenye kuhurumiana wao kwa wao huashiria kwa Uthman bin Affan, ambaye alikuwa mpole sana. Usemi, alama zao ni katika nyuso zao kwa athari ya kusujudu huashiria kwa Ali. Ni wazi kwamba Ali ni Khalifa wa nne, sio wa kwanza, kwa vile Allah amemtaja katika sehemu ya nne. Muombezi: Nashangaa vipi nitaweza kujibu ili kwamba nisije nikalaumiwa kwa kujipendelea mwenyewe. Hakuna tafsir za Qurani, ukichukua pamoja na zile za maulamaa wenu wakubwa, ambazo zimetafsiri maneno haya kama ulivyofasili wewe. Aya hii ingekuwa inahusu utaratibu wa Ukhalifa, siku ya kwanza baada ya kifo cha Mtume, wakati Ali, Bani Hashim, na masahaba mashuhuri wa Mtume walipoweka vipingamizi na wakakataa kula kiapo cha utii kwa Khalifa, basi hoja zisizo za msingi zisingetolewa pale. Wangeweza kutoa jibu la kunyamazisha kwa kusoma aya hii tukufu pale pale. Kwa hiyo, ni wazi kwamba tafsiri yako ni mawazo yaliyokuja baadaye. Hakuna yeyote katika wafasiri wakubwa wa madhehebu yenu, kama Tabari, Imam Thalabi, Fadhil Nishapuri, JalaludDin Suyuti, Qadhi Baihawi, Jarullah Zamakhshari, Imam Fakhrud-Din Radhi, au wengine ambao wameitafsir hivyo. Nashindwa kuelewa jinsi unavyoipata maana hii. Wapi na kutoka kwa nani maana hii ilitolewa? Aya hii, kielimu na mtazamo wa kifundi, vilevile vinakwenda kinyuma na unavyosema. Sheikh: Sikutarajia kwamba utakuwa mpinzani hivyo kwenye aya iliyo na maana ya wazi kiasi hicho. Hakika kama una lolote la kusema dhidi ya hivi unaweza ukatueleza tujue ili

125

Mikesha ya Peshawar
kwamba ukweli halisi uweze kuthibitishwa. Muombezi: Ukichukulia ujenzi wa kinahau wa aya hii, kama tutaitafsiri maana yake kama ulivyofanya wewe, itakuwa na maana kwamba ama Muhammad ni Abu Bakr, Umar, Uthman na Ali au kwamba Abu Bakr, Umar, Uthman na Ali ni Muhammad! Hata wanafunzi wanaoanza wanajua kwamba aina hii ya tafsir ya kinahau sio sahihi. Mbali na hayo, kama aya hii inaashiria kwa Makhalifa wanne, kungekuwa na kiungo na kupatanisha maneno ili kupata hiyo maana yako, lakini haiko hivyo. Wafasiri wote wa madhehebu yenu wenyewe wanasema kwamba aya hii inaashiria kwa waumini wote. Aidha, sifa zilizotajwa katika aya hii kwa wazi kabisa zinaashiria kwa mtu mmoja tu, ambaye alikaa na Mtume kuazia mwanzo kabisa na sio watu wanne. Na kama tukisema mtu huyu mmoja alikuwa Amirl-Muminina Ali, itakuwa sawasawa zaidi kulingana na akili za kuzaliwa na hadith kuliko kutaja wengine wowote.

HOJA KUTOKANA NA AYA YA PANGO NA MAJIBU YAKE.


Sheikh: Ina shangaza kwamba unadai ati hujiingizi katika hoja zenye kupotosha, ingawa maoni yako ni ya kupotosha hasa. Allah anasema katika Qurani tukufu: Kama hamtamnusuru, basi Allah alimnusuru walipomtoa wale waliokufuru, yeye akiwa wa pili wake walipokuwa wote katika pango alipomwambia Sahibu y ake. Usihuzunike kwa hakika Allah yu pamoja nasi, Allah akamteremshia utulivu wake na akamnusuru kwa majeshi msiyoyaona (9: 40). Kwanza, Aya hii inaunga mkono aya iliyopita na huthibitisha kwamba usemi na walio pamoja naye, huashiria kwa Abu Bakr ambaye alikuwa na Mtume katika Pango katika usiku wa Hijra, Pili, ukweli kwamba alikuwa na Mtukufu Mtume, yenyewe ni uthibitisho mkubwa wa fadhila na ubora wa Abu Bakr kwa umma wote. Mtume aliweza kutabiri kwamba Abu Bakr alikuwa Mrithi wake, na kwamba kuwepo kwa Khalifa baada yake ni muhimu. Kwa hiyo, alitambua kwamba ilimpasa kumhifadhi Abu Bakr kama ambavyo angejihifadhi yeye mwenyewe. Hivyo, alimchukua kuwa naye ili kwamba Abu Bakr asije akakamatwa na maadui. Huduma kama hii haijafanywa kwa Mwislamu mwingine yeyote. Hii inathibitisha wazi haki yake ya ukhalifa kuliko wengine. Muombezi: Kama ungeangalia Aya hii kwa busara zaidi, ungeona kwamba uamuzi wako ni wa makosa. Sheikh: Unaweza kutoa sababu dhidi ya hitimisho ambalo tumelitoa?

126

Mikesha ya Peshawar
Mombezi: Ningekuomba uliache suala hili kwa muda huu kwa sababu maneno huzaa maneno. Baadhi ya watu wenye chuki wanaweza wakafasiri maoni yetu kwa nia mbaya. Sitaki kuchochea chuki. Mtu anaweza akasema tunataka kuwavunjia heshima makhalifa, ingawa cheo cha kila mmoja kimewekwa, na sio muhimu kufanya tafsir zisizo na maana. Sheikh: Unakuwa mkwepaji. Elewa kwamba hoja yenye maana haizai chuki; huondoa kutokuelewana. Muombezi: Kwa vile umetumia neno Mkwepaji, ninalazimika kujibu, ili uweze kujua kwamba silikwepi suala hili. Nilitaka kudumisha utaratibu wa mjadala wetu. Natumaini kwamba hutaona makosa kwa upande wangu. Umetoa utetezi wa kizembe sana kwamba Mtume alijua kwamba Abu Bakr atakuwa Khalifa wake baada yake. Kwahiyo, ilikuwa muhimu kwake kuokoa maisha yake, na hivyo akamchukuwa ili awe pamoja naye.

UKWELI KUHUSU ABU BAKR KUFUATANA NA MTUKUFU MTUME (S.A.W.W.).


Majibu kwa maelezo yako ni rahisi. Kama Abu Bakr angekuwa Khalifa pekee baada ya Mtume, maoni kama hayo yangewezekana, lakini mnaamini katika makhalifa wanne. Kama hoja yako hii ni sahihi, na kama ilikuwa muhimu kwa Mtume kulinda usalama wa Khalifa, basi Mtume angeondoka nao wote wanne kutoka mjini Makka. Kwa nini aliweza kuwaacha wale watatu, mmoja wao katika hali ya hatari ya kulala katika kitanda cha Mtume, ambavyo ilikuwa ni hatari katika usiku ule wakati maadui zake walikuwa wamekusanyika ili kumuua? Kwa mujibu wa Tabari (Sehemu ya tatu ya Tarikh) Abu Bakr hakuwa na habari za harakati za Mtume za kuondoka Makka. Wakati alipokwenda kwa Ali na kumuuliza kuhusu Mtume, alimueleza kwamba Mtume amekwenda kule pangoni. Ali akamwambia kwamba kama alikuwa na shughuli yoyote naye, alipaswa amkimbilie. Abu Bakr alikimbia na akamkuta Mtume njiani. Na hivyo akafuatana naye. Mtiririko huu wa matukio unaonyesha kwamba Mtume hakukusudia kumchuka Abu Bakr kuwa naye. Aliungana naye katikati ya njia bila ruhusa ya Mtume. Kwa mujibu wa taarifa nyingine, Abu Bakr alichukuliwa katika safari hiyo kwa kuhofia asije akasababisha matatizo na kutoa habari kwa maadui. Maulamaa wenu wenyewe wameukiri ukweli huu. Kwa mfano, Sheikh Abul-Qasim bin Sabbagh, ambaye ni mmoja katika maulamaa wenu anayejulikana sana wa madhehebu yenu, ankiandika katika kitabu chake Al-Nur-Wal-Burhan kuhusu maisha ya Mtume, anasimulia kutoka kwa Muhammad bin Ishaq, na yeye kutoka kwa Hasan bin Thabit Ansari, kwamba alikwenda Makka kufanya Umra kabla ya kuhama kwa Mtume. Aliona kwamba Maquraishi makafiri walikuwa wamewaandama masahaba wa Mtume. Mtume akamuamrisha Ali kulala katika

127

Mikesha ya Peshawar
kitanda chake, na kwa kuogopa kwamba Abu Bakr angetoa siri hii kwa makafiri, Mtume akamchukua awe pamoja naye. Mwisho, ingelikuwa vizuri kama ungeonyesha ni ushahidi gani uliopo katika Aya hii, unaoonyesha ubora wa Abu Bakr au iwapo kufuatana na Mtume katika safari ni uthibitisho kwamba mtu anayo sifa ya Ukhalifa. Sheikh: Ushahidi upo. Kwanza, usuhuba wa Mtume na kwamba, Allah amemuita sahaba wa Mtume, yenyewe ni sifa tosha. Pili, Mtume mwenyewe amesema: Hakika Allah yu pamoja nasi. Tatu, uteremshwaji wa utulivu juu yake kutoka kwa Allah, kama ilivyotajwa katika Aya hii, ni uthibitisho wa kuvutia zaidi wa ubora wa Abu Bakr. Kwa hiyo, nukta zote hizi zikiwekwa pamoja huonyesha ubora wake kwa wengine kuhusiana na ukhalifa. Muombezi: Hakuna anayesita kuikubali nafasi ya Abu Bakr, Mwislam mtu mzima, mmoja wa masahaba mashuhuri na baba wa mke wa Mtume. Hata hivyo, sababu hizi hazithibitishi ubora wake katika ukhalifa. Kama utajaribu kuthibitisha nukta yako hii kwa maelezo haya mbele ya watu waadilifu wasio na upendeleo, utakuwa unavutia lawama nzito. Watasema kwamba usuhuba na watu wema sio uthibitisho wa sifa au ubora. Kwa mfano, mara kwa mara tunaona kwamba watu wabaya hufuatana na watu wema, na kundi la makafiri hufuatana na Waislamu katika safari. Pengine umesahau Qurani Tukufu inavyosema kuhusu Mtume Yusufu ambaye amesema: Enyi wafungwa sahibu wenzangu wawili! Je! waungu wengi wanaofarikiana ndio bora au Mwenyezi Mungu, Mmoja Mwenye nguvu? (12:39). Kuhusu Aya hii, wafasiri wamesema kwamba wakati Yusufu alipopelekwa jela, siku hiyo hiyo mpishi wa Mfalme na mtunza mvinyo ambao wote walikuwa makafiri, vilevile walitiwa jela pamoja naye. Kwa muda wa miaka mitano watu hawa watatu (waumini na makafiri kwa pamoja ) waliishi pamoja kama maswahiba. Wakati akiwahubiria, Yusufu aliwaita sahiba zangu. Je, usuhuba huu wa Mtume Yusufu ulifanya hata mara moja hali ya kuwaona makafiri hawa wawili kama watu bora au wenye heshima? Je, usuhuba wao na Mtume Yusufu ulileta mabadiliko katika Iman zao? Maandishi ya Wafasiri na wanahistoria yanatuambia kwamba, baada ya miaka mitano ya usahaba, waliachana kila mmoja katika hali ile ile.Aya nyingine ya Qurani Tukufu inasema:

Sahiba wake akamuambia na hali ya kuwa anajibishana naye: Je! Unamkufuru, Yule aliyekuumba kwa udongo, kisha kwa tone la manii, kisha akakufanya mtu

128

Mikesha ya Peshawar
kamili? (18:37) Wafasiri wanakubaliana kwamba aya hii inazungumzia ndugu wawili, mmoja alikuwa muumini, ambaye jina lake lilikuwa Yahuda. Mwingine alikuwa kafir jina lake lilikuwa Baratus. Jambo hili limeelezewa vilevile katika Tafsir-e-Kabir na Imam Fakhrud-Din Razi, ambaye ni mmoja katika Maulamaa wenu. Ndugu hawa wawili walizungumza pamoja, maelezo ambayo hayataweza kutolewa hapa. Hata hivyo Allah amewaita wote wawili (Muumin na Kafiri). Masahibu. Je, yule kafiri alipata faida kutokana na usuhuba wake na Muumini? Kwa hakika hapana. Hivyo usuhuba peke yake sio msingi wa mtu kudaiwa kuwa ni bora. Kuna mifano mingi yenye kuunga mkono maoni haya.

MANENO YA MTUKUFU MTUME (S.A.W.W.) ALLAH YUKO PAMOJA NASI SIO UTHIBITISHO WA UBORA WA ABU BAKR.
Umesema pia kwamba kwa vile Mtume alimuambia Abu Bakr, Allah yuko pamoja nasi. kwamba huo ni uthibitisho wa ubora wa Abu Bakr na haki yake ya Ukhalifa! Waweza ukayafikiria tena maoni yako. Watu wanaweza wakakuuliza, kwa mfano, Je, Allah anakuwa na waumini na mawalii tu, na sio na makafir? Unajua sehemu yoyote ambayo Allah hayupo? Je, hivi Allah hayupo na kila mtu? Chukulia kwamba muumini na kafiri wako pamoja katika mkusanyiko. Qurani inasema:

Je! Huoni kwamba Allah anajua vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini? Haupatikani mnongono wa watu watatu ila yeye huwa ni wanne wao, wala watano ila yeye huwa ni wa Sita wao, wala wachache kuliko hao wala zaidi ila Yeye huwa pamoja nao, popote walipo(58:7). Kwa mujibu aya hii na wa akili ya kawaida, Allah yupo na kila mtu. Sheikh: Maelezo Allah yupo pamoja nasi Yana maana kwamba walikuwa wapenzi mno wa Allah kwa sababu wamesafiri katika njia ya Allah kwa madhumuni ya kuhifadhi dini yake. Baraka za Allah zilikuwa pamoja nao. Muombezi: Lakini hakika maelezo haya hayathibitishi kwamba mtu anazo baraka za

129

Mikesha ya Peshawar
milele. Allah Mwenye nguvu hutizama matendo ya watu. Imetokea mara kwa mara kwamba wakati fulani, watu walifanya matendo mema na wakawa ni wenye kupokea rehema kutoka kwa Allah. Baadae wakamuasi Allah na ikawapata adhabu ya Mungu. Ibilis kama unavyojua, alimuabudu Allah kwa maelfu ya miaka na akapata upole kutoka Kwake. Hata hivyo mara tu alipoasi amri yake, akalaaniwa. Qurani Tukufu inasema:

Akasema: Basi toka humo, na hali ya kuwa wewe ni mwenye kufukuzwa Na kwa yakini itakuwa laana juu yako mpaka Siku ya Malipo. (15:34-35). Kumradhi, hakuna madhara katika kutoa mifano, madhumuni yangu ni kufafanua hii nukta. Historia imejaa mifano mingi ya wale ambao walikuwa karibu na Allah, lakini ambao baada ya kujaribiwa, walilaaniwa. Balam Bin Baur, kwa mfano, wa hirimu moja na Musa, alitokea kuwa karibu sana na Allah kiasi kwamba Allah alimfunulia lile Ism-eAdhim (jina tukufu la Allah, ambalo kupitia hilo chochote kinachoombwa kinakubaliwa upesi sana na Allah). Alimuomba Allah kwa njia ya Ism-e-Adhim na akasababisha shida ikampata Musa katika Bonde la Tia! Lakini wakati wa majaribio, Balam alizidiwa nguvu na mahaba ya vitu vya ulimwengu. Alimfuata Ibilis na akalaaniwa. Wafasiri wametoa maelezo kamili ya tukio hili. Imam Fakhrud-Din Razi katika Tafsir yake sehemu ya 4, uk. 463, ameelezea habari hii kutoka kwa Ibn Abbas, Ibn Masud, na Mujahid. Allah katika Qurani Tukufu anatueleza hivi: Na wasomee habari za yule tuliyempa Aya zetu kisha akajivuna nazo. Na shetani akamuandama na akawa miongoni mwa waliopotea.

BARSISA ABID.
Au angalia la Barsisa Abid, ambaye mwanzoni alimwabudu Allah kiasi kwamba akakuwa Mustajabud-dawa (mtu ambaye maombi yake hukubaliwa). Hata hivyo, wakati muda wa majaribio ulipofika, alishindwa. Akipotezwa na Shetani, akafanya zinaa na msichana, akanyongwa, na akafa kafiri, Qurani inamzungumzia katika maneno haya:

Ni kama shetani, anapomwambia mtu: kufuru; na anapokufuru akamwambia: Mimi si pamoja na wewe, hakika namuogopa Allah, Mola wa walimwengu. Basi mwisho wa wote wawili hao ikawa waingie motoni wakae humo, na hiyo ndiyo jaza ya madhalimu. (59:16-17).

130

Mikesha ya Peshawar
Hivyo kama mtu aliwahi kufanya matendo mema wakati fulani, haina maana kwamba mwisho wake utakuwa mzuri. Ni kwa sababu hii kwamba tunaelekezwa kusema katika maombi yetu: Matendo yetu na yawe na mwisho mwema. Sheikh: Kwa hakika sikutarajia mtu mwenye heshima kama wewe kutoa mfano wa shetani, Balam Baur na Barsisa. Muombezi: Samahani, nimekwishaeleza kwamba hakuna madhara katika kutoka mifano. Kwa kweli ni lazima tuitoe katika mijadala ya kielimu ili kuthibitisha ukweli. Allah awe shahidi yangu: Kamwe sikukusudia kumtweza yeyote kwa kutoa mifano hii. Madhumuni yangu ni kuthibitisha hoja yangu tu. Sheikh: Aya hii kwa wazi kabisa huthibitisha ubora wa Abu Bakr kwa sababu inasema: Hivyo Allah akamteremshia utulivu juu yake. (9:40). Kijina hapa humuashiria Abu Bakr, ambacho huthibitisha ubora wake. Muombezi: Umeielewa vibaya, kijina kilichotumiwa baada ya Sakina (utulivu) huashiria kwa Mtume. Utulivu uliteremshwa kwake na sio kwa Abu Bakr, kama ilivyo dhahiri katika sentensi inayofuatilia ambapo Allah anasema: na akamnusuru kwa majeshi msiyoyaona (9:40) ukweli ni kwamba majeshi ya Malaika wasioonekana yalikuwa kwa ajili ya kumsaidia Mtume, sio Abu Bakr. Sheikh: Nakubali kwamba msaada wa Mungu ulikuwa kwa ajili ya Mtume, lakini Abu Bakr akiwa pamoja na Mtume, hakuwa bila rehma.

KUTEREMSHWA KWA UTULIVU KULIKUWA KWA AJILI YA MTUME WA ALLAH.


Muombezi: Kama upewaji wa rehma za Mungu umeashiria kwa watu wawili, nahau ya Kiarabu ingehitaji kwamba vijina vilivyotumika vingehusisha watu wawili katika misemo yote ya Aya hii. Lakini vijina hivi vinaashiria kwa mtu mmoja, Mtume, na rehma za Allah zilikuwa kwa ajili yake. Kama kupitia kwake yeye, upewaji wa rehma ungekusudiwa vilevile kwa ajili ya wengine, majina yao yangetajwa. Hivyo, uteremshaji wa utulivu katika aya hii ni kwa ajili ya Mtume peke yake. Sheikh: Mtume wa Allah alikuwa hana haja ya kupewa utulivu wa Mungu. Alikuwa hauhitaji kwa sababu alikuwa amehakikishiwa rahma za Mungu. Hivyo upewaji wa utulivu ulikuwa kwa ajili ya Abu Bakr.

131

Mikesha ya Peshawar
Muombezi: Kwa misingi gani wewe unasema kwamba Mtume alikuwa hategemei upewaji wa rehma za Mungu? Hakuna mtu - awe Mtume Imam au Walii ambaye anajitegemea kwa (upewaji wa) rehma za Mungu. Pengine umesahau Qurani Tukufu inasema nini kuhusu tukio la Hunain. Kisha Allah akateremsha utulivu wake juu ya Mtume wake na juu ya waliomini (9:26). Kitu hicho hicho kimesemwa katika Sura ya 48 (Fath) aya ya 26, ya Qurani Tukufu. Waumini wamejumuishwa baada ya Mtume katika aya hii, kama vile katika aya ya Pango. Kama Abu Bakr angekuwa mwenye kustahiki kupewa utulivu, ima kijina kwa ajili ya watu wawili kingetumika, au jina lake lingetajwa mbalimbali. Jambo hili liko wazi kabisa kiasi kwamba Maulamaa wenu wenyewe wanakiri kwamba kijina kilichofungamanishwa na utulivu hakiashirii kwa Abu Bakr. Unaweza kuitazama Naqzul-Uthmaniyya kilichoandikwa na Sheikh Abu Jafar Muhammad bin Abdullah Iskafi, ambaye ni mmoja wa Maulamaa mashuhuri na masheikh wa Mutazil. Mwanachuo huyu anaukana moja kwa moja uongo wa Abu Uthman Jahiz. Ibn Abil-Hadid vilevile ameandika baadhi ya majibu hayo katika Sharh yake ya Nahjul-Balagha Jz. 3, uk. 253281. Kwa nyongeza, kuna usemi katika Aya hii, ambao maana yake halisi ni kinyume na hoja yako. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuambia Abu Bakr: Usihuzunike. Usemi huu unaonyesha Abu Bakr alikuwa muoga. Je, woga huu ulikuwa unafaa kusifiwa au hapana? Kama ingelikuwa hivyo, Mtume asingemzuia yeyote kufanya tendo jema. Mwakilishi wa Allah ana sifa makhususi. Muhimu zaidi ya hizo, kama ilivyotajwa katika Qurani Tukufu, ni kwamba haogopi kubadilika kwa maisha. Anafanya uvumilivu na ushujaa. Qurani Tukufu inasema: Sikilizeni (eleweni)! Hakika vipenzi vya Allah hawatakuwa na khofu wala hawatahuzunika. (10:62).

MKUTANO WA SITA JUMANNE USIKU 28 RAJAB 1345 A.H.


Bwana Ghulam Imamain, mfanyabiashara wa Kisunni mwenye kuheshimika, alikuja katika sehemu ya mkutano kabla ya jua kuzama. Alitaja sababu yake ya kuja. Alisema kwamba yeye na watu wengine walivutiwa sana na maelezo ya Muombezi. Akasema kwamba amesikia ukweli ambao hajapata kuusikia kabla yake. Yeye na baadhi ya Sunni wengine walikuwa na majadiliano yasiyopendeza na Maulamaa wao, ambao hawakuweza kukanusha hoja za Muombezi lakini ambao kwa ukaidi wamengangania msimamo wao. Wakati wa Sala ya Magharibi ulipowadia, Bw.Ghulam Imamain alisali Sala zote Magharibi na Isha nyuma ya Muombezi. Wakati wengine walipowasili, mjadala ulianza na ushauri wa Nawab Sahib. Nawab: Tafadhali endelea na mazungumzo ya usiku wa jana. Tafsir ya ile aya ilikuwa

132

Mikesha ya Peshawar
haikukamilika. Muombezi: (Akiangalia upande wa Maulamaa wa Kisunni). Mradi na nyie mliruhusu hilo. Hafidh: (Kwa hasira kidogo). Hakuna madhara. Kama kuna kitu kimebakia kusemwa, tuko tayari kukisikiliza. Muombezi: Usiku uliopita nilithibitisha kwa mtazamo wa kinahau kwamba maelezo ya baadhi ya wafasiri wanaosema kwamba aya hii huonyesha namna ya kuamua ukhalifa yalikuwa hayakubaliki. Sasa nitaelezea kutokana na mtazamo mwingine. Sheikh Abdus-Salam Sahib alisema usiku uliopita kwamba kuna sifa nne zilizotajwa katika aya hii. Sifa hizi, alisema, zinaonyesha kwamba aya hii iliteremshwa kwa habari ya Makhalifa wanne wa kwanza na kwamba aya hii inaonyesha mpango wa ukhalifa. Majibu yangu kwa hoja hii ni: kwanza, wafasir wenye kuaminika hawajawahi kutoa maelezo kama hayo kuhusu maana halisi ya aya hii. Pili, nyote mnajua kwamba wakati sifa inapohusishwa na mtu inaenda sawasawa na tabia yake, hapo ndipo (sifa hiyo) itakuwa na maana. Kama tutayaangalia mambo kwa busara zaidi, tunaona kwamba ni Ali tu ambaye alikuwa na sifa hizo zilizoelezewa katika aya hii. Sifa hizi kwa njia yoyote haziafikiani na hizo zilizotajwa na Sheikh Sahib. Hafidh: Aya zote hizo ulizokwishasimulia kuhusu Ali hazikutosha? Unataka sasa kwa ujanja wako wa ufasaha wa kusema kuthibitisha kwamba aya hii tukufu vilevile iliteremshwa kwa kumtukuza Ali? Kama ni hivyo, hebu tujulishe ni vipi haikubaliani na ukhalifa wa makhalfa wanne wa kwanza.

AYA MIA TATU ZENYE KUMTUKUZA ALI.


Muombezi: Sijahusisha Aya ya Qurani Tukufu kwa kumtukuza Ali kwa uongo. Umechanganya mambo. Unaweza ukapuuza ukweli kwamba tafsiri zenye kujulikana vizuri na vitabu vyenye kuaminika vilivyoandikwa na Maulamaa wenu wenyewe vimetaja aya nyingi za Qurani Tukufu zikiwa ni za kumtukuza Ali? Unawezaje kuona kuwa ni kitu cha pekee kwangu? Je, Hafidh Abu Nuaim Isfahani, muandishi wa Ma-Nazala ninal-Qurani Fi Ali, na Hafidh Abu Bakr Shirazi, muandishi wa Nuzulul-Qurani Fi Ali, walikuwa Mashia? Je, wafasiri wakubwa, kama Imam Thalabi, Jalalud-Din Suyuti, Tabari, Imam Fakhrud-Din Radhi, na Maulamaa wengine wenye sifa kubwa, kama Ibn Kathir, Muslim, Hakim, Tirmidhi, Nisai, Ibn Maja, Abu Dawdi, Ahmad Bin Hanbal, na hata Ibn Hajar asiye mvumilivu, ambaye amekusanya katika kitabu chake Sawaiq Aya za Qurani zilizoteremshwa kumsifia Ali pia walikuwa Shia? Baadhi ya ulamaa kama,Tabari, na Muhammad bin Yusufu Ganji Shafii mwanzoni mwa kitabu chake sehe-

133

Mikesha ya Peshawar
mu ya 62, anasimulia kutoka kwa Ibn Abbas, na Muhadith wa Syria katika kitabu chake Tarikh-e-Kabir, na wengine wameandika Aya nyingi kiasi kama mia tatu za Qurani Tukufu zenye kumtukuza Ali. Je, watu hawa walikuwa Mashia au wanatokana na maulamaa wenu wakubwa? Hatuhitaji kuhusisha kwa uongo aya ya Qurani tukufu kwa ajili ya kuthibitisha cheo cha Amirl-Muminina Ali. Maadui zake (Bani Umayya, Nawasib na Khawarij) wamezuia fadhila zake zisitajwe na marafiki zake wakasita kusimulia ubora wake kwa kuogopa matokeo yake. Bado, vitabu vimejaa fadhila zake na vinatoa mwanga juu ya mambo yote ya kufanikiwa kwake. Kwa vyovyote inavyohusika aya hii, sikujitia katika ujanja wa ufanisi wa kusema. Nimefichua ukweli, nikitoa hoja kutoka katika vitabu vyenu. Mmeona mpaka hapo kwamba sikutoa hoja kutoka kwenye riwaya za waandishi wa Kishia. Hata kama vitabu vya Shia viwekwe kando, bado nitathibitisha ubora wa kipekee wa Ali. Niliyosema kuhusu Aya hii yanakubaliana na maoni ya Maulamaa wenu wenyewe. Muhammad bin Yusufu Ganji Shafii amenukuu Hadith ya kufanana katika kitabu chake Kifayatut-Talib Sura ya 23, kutoka kwa Mtume yenye maana kwamba Ali alikuwa anafanana na Mitume. Anasema kwamba sababu ya Ali kuitwa kwamba anafanana na Mtume Nuh katika hekima ni kwamba Ali alikuwa mkali dhidi ya makafiri na mpole kwa waumini. Allah amezitaja sifa hizi katika Qurani Tukufu. Ali ambaye siku zote alikuwa pamoja na Mtume, alikuwa mkali dhidi ya makafiri na mwenye huruma kwa waumini. Na ukichukulia, kama Sheikh Sahib anavyosema: kwamba usemi Na wale ambao wako pamoja naye unamuashiria Abu Bakr kwa sababu kwa muda wa siku chache alikuwa na Mtume ndani ya Pango, Hivi mtu kama huyo anaweza kuwa sawa na yule aliyekuwa na Mtume tangu utotoni na kupata maelekezo kutoka kwake?

ALI NI WA KWANZA KUTANGAZA IMANI JUU YA MTUME WA ALLAH.


Aidha, katika tukio muhimu la kutangaza Utume wake, hakuna aliyemuunga mkono Muhammad isipokuwa Ali. Maulamaa wenu mashuhuli, kama Bukhari na Muslim, katika Sahih zao, Imam Ahmad bin Hanbal katika Musnad yake, na wengine wengi, kama vile Ibn Abdil-Birr katika Istiabi, Jz. 3, uk. 32, Imam Abu Abdur-Rahman Nisai katika Khasaisul-Alawi, Sibt Ibn Jauzifi katika Tadhkira, uk. 63, Sheikh Suleimam Balkhi Hanafi ndani ya Yanabiul-Mawadda, Sura ya 12, kwa kunukuu kutoka kwa Tirmidhi na Muslim, Muhammad bin Talha Shafii katika Matalibus-Suul Sura ndogo - 1, Ibn Abil-Hadid katika Sharh Nahjul-Balagha, Jz. 3, uk. 258, Tirmidhi katika JameTirmidhi, Jz. 2, uk. 314, Hamwaini katika Faraid, Mir Seyyed Ali Hamadani katika Mawaddatul-Qurba, na hata yulu shabiki Ibn Hajar katika Sawaiq-e-Muhriqa, na wanachuoni wengine mashuhuri, wameandika pamoja na tofauti kidogo ya maneno, kuto-

134

Mikesha ya Peshawar
ka kwa Anas bin Malik na wengine kwamba: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipewa Utume wa Allah siku ya Jumatatu, na Ali akatangaza imani yake kwake siku ya Jumanne. Vilevile imesimuliwa tena kwamba: Utume wa Allah ulitangazwa siku ya Jumatatu na Ali akasali na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) siku ya Jumanne. Na halafu tena, Ali alikuwa mtu wa kwanza kutangaza imani yake kwa Mtume. Vilevile Tabari, Ibn Abi-Hadid, Tirmidhi, na wengine wanasimulia kutoka kwa Ibn Abbas kwamba Ali alikuwa wa kwanza kusali.

KUFUNDISHWA KWA ALI TANGU UTOTONI NA MTUME.


Ninakuombeni muangalie wanachuoni wenu, Nurud-Din Bin Sabbagh Malik, katika Fusulul-Muhimma. Sura ya Tarbiatun-Nabi, uk, 16, na Muhammad Bin Talha Shafii, katika Matalibus-Suul, Sura ya 1, uk. 11, na wengine walichosimulia. Katika wakati mmoja wa ukame hapo Makka, Mtume alimwambia ami yake, Abbas, kwamba, kaka yake, Abu Talib, ana watoto wengi na kwamba uwezo wake wa kujikimu kimaisha ulikuwa ni mdogo. Mtume Muhammad alipendekeza kwamba kila mmoja wao amuombe Abu Talib ampe mtoto mmoja ili kusaidia kupunguza mzigo mzito alionao. Abbas alikubali. Walikwenda kwa Abu Talib na pendekezo lao, na akakubali. Abbas akamchukuwa Jafar-e-Tayyar kuwa chini ya malezi yake na Mtume akamchukuwa Ali. Malik akaendelea, Ali alibakia moja kwa moja na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mpaka alipotangazwa kuwa Mtume wa Allah. Ali alitangaza Imani yake kwake, na akamfuata kama Mtume wa Allah, wakati huo Ali akiwa na umri wa miaka kumi na tatu tu. Alikuwa mwanaume wa kwanza kuukubali Uislamu. Mke wa Mtume Khadija alikuwa mtu wa pekee aliyemkubali Mtume kabla ya Ali. Katika Sura hiyo hiyo, Malik anaelezea kwamba Ibn Abbas, Jabir Ibn Abdullah Ansari, Zaid ibn Arqam, Muhammad ibn Munkadar, na Rabiatul-Marai wamesema kwamba mtu wa kwanza kumuamini Mtume baada ya Khadija alikuwa ni Ali. Anasema Ali aliutaja ukweli huu, ambao umesimuliwa na Maulamaa wenu. Alisema: Muhammad, Mtume wa Allah ni ndugu yangu na mtoto wa Ami yangu; Hamza Bwana wa mashahidi, ni Ami yangu; Fatima binti ya Mtume ni mke wangu; na watoto wawili (wanaume) wa binti yake ni watoto wangu kwa Fatima. Nani kati yenu amechangia sifa kama hizi nilivyo mimi? Nilikuwa wa kwanza kabisa katika kuukubali Uislamu wakati nilikuwa bado mtoto tu. Mtume alitangaza katika siku ya Ghadir-e-Khum kwamba ilikuwa ni wajibu kunikubali mimi kama kiongozi wenu. (Kisha akasema mara tatu) Ole kwa yule ambaye atamkabili Allah kesho (Siku ya Kiyama), kama akiwa amenifanyia mimi ukatili wowote ule. Muhammad Bin Talha Shafii katika Matalibus-Suul, sehemu ya 1, Sura ya 1, uk. 11, na wengine wengi katika Maulamaa wenu, wamesimulia kwamba maelezo haya yalikuwa

135

Mikesha ya Peshawar
ni majibu ya barua ya Muawiya aliyomuandikia Ali ambayo kwayo alijigamba kwamba baba yake alikuwa kiongozi wa kabila lake wakati wa zama za ujinga na kwamba katika Uislamu Yeye (Muamiya) alikuwa ni Mfalme. Muawiya vilevile alisema kwamba yeye alikuwa mjomba wa waumini mwandishi wa wahayi (ufunuo), na mtu sifa njema. Baada ya kusoma barua hii, Ali akasema: Mtu wa tabia hii mtoto wa mwanamke ambaye alitafuna maini - anajigamba mbele yangu! (kuhusu mama yake Muawiyya Hindi ambaye baada ya Vita vya Uhud akiwa na hasira kali alichana maiti ya Hamza, akakata ini lake, na akalitafuna). Hata hivyo, Muawiyya ingawa alikuwa mpinzani mkali wa Ali, hakuweza kuzikataa sifa hizi. Aidha, Hakim Abul-Qasim Haskani, mmoja wa Maulamaa wenu, anasimulia kutoka kwa Abdur-Rahman Bin Auf, kuhusu aya hiyo hapo juu ya Makuraishi kumi waliokubali Uislamu, kwamba Ali alikuwa wa mbele zaidi miongoni mwao. Ahmad Bin Hanbal, Khatib Khawarizmi, na Sulayman Balkhi Hanafi, wanasimulia kutoka Anas bin Malik kwamba Mtume alisema: Malaika walinitakia rehma mimi na Ali kwa muda wa miaka saba, kwani kwa muda huo hakuna sauti iliyotamka Upweke wa Allah isipokuwa yangu na ya Ali. Ibn Abil-Hadid Mutazali katika Sherh-e-Nahjul-Balagha, Jz. 1, uk. 373-5, ameandika Hadith nyingi mbalimbali zilizosimuliwa kupitia wanachuoni wenu zenye maana kwamba Ali alikuwa wa mbele zaidi katika jambo la Uislamu. Baada ya kuandika vifungu mbalimbali vya maneno na simulizi anahitimisha kwa kusema: Hivyo mukhtasari wa yote tuliyoeleza ni kwamba Ali ni wa kwanza miongoni mwa watu kuhusu Uislamu. Maoni kinyume na haya ni mara chache kuyasikia, na hayana maana kwetu kuyazingatia. Imam Abdur-Rahman Nisai, mwandishi wa moja ya vitabu sita Sahih vya hadith, ameandika katika Khasaisul-Alawi hadith sita za mwanzo juu ya suala hili na amethibitisha kwamba mtu wa mbele zaidi katika Uislamu na wa kwanza kusali na Mtume alikuwa Ali. Kwa nyongeza, Sheikh Sulayman Balkh Hanafi katika Yanabiul-Mawadda. Sura 12, ameandika hadith 31 kutoka kwa Tirmidhi, Hamwaini, Ibn Maja, Ahmad Bin Hanbal, Hafidh Abu Nuami, Imam Thalabi, Ibn Maghazili, Abul-Muwayyid Khawarizmi, na Dailami, ambayo hitimisho lake ni kwamba Ali alikuwa wa kwanza katika umma wote wa Kiislamu kukubali Uislamu. Hata shupavu mchungu Ibn Hajar Makki ameandika katika Sawaiq-Muhirika, Sura ya 2 Hadith juu ya Suala hili hili, ambazo baadhi ya hizo zimekubaliwa na Sulayman Balkhi Hanaf katika kitabu chake Yanabiul-Mawadda kuelekea mwisho wa kufunga Sura ya 2, amesimuluia hadith juu ya suala hilo hilo, baadhi yake ambazo zimekubaliwa na Suleiman Balkhi Hanafi ndani ya YanabiulMawadda yake. Zaidi ya hayo, ndani ya YanabiulMawadda, kuelekea mwisho wa Sura ya 12, amesimulia kutoka Ibn Zubair, Makki na yeye kutoka kwa Jabir Ibn Abdullah Ansari, Hadith kuhusu

136

Mikesha ya Peshawar
sifa za Ali, ambayo ningependa kuitoa hapa kwa ruhusa yenu ili kuhitimisha hoja yangu. Mtume alisema: Mwenyezi Mungu alinichagua mimi kuwa Mtume na akanifunulia maandiko matakatifu. Mimi nikamwambia, Ee Allah, Mola Wangu, ulimtuma Musa kwa Firauni, Musa akakuomba umfanye ndugu yake, Harun, Waziri wake ambaye angeweza kuimarisha mkono wake, ili maneno yake yapate kushuhudiwa. Sasa nakuomba, Ee Allah, uchague kwa ajili yangu kutoka miongoni mwa familia yangu Waziri ambaye ataimarisha mkono wangu. Mfanye Ali kuwa Waziri wangu na ndugu yangu, ingiza ushujaa kwenye moyo wake, na mpe nguvu juu ya maadui. Ali alikuwa mtu wa kwanza kuniamini na kushuhudia Utume wangu na mtu wa kwanza kutamka Upweke wa Allah sambamba pamoja na mimi. Baadae niliendelea kumuomba Allah. Kwa hiyo Ali ni kiongozi wa warithi (wangu). Kumfuata yeye ni rehma; kufa ukiwa na utii kwake ni Shahada. Jina lake huonekana katika Taurat pamoja na jina langu; mke wake, mwaminifu zaidi, ni binti yangu; watoto wake wawili wa kiume, ambao ni mabwana wa vijana wa Peponi, ni watoto wangu. Baada yao, Maimam wote ni wawakilishi wa Allah juu ya viumbe baada ya Mitume; na ni milango ya elimu miongoni mwa watu wangu. Yeyote ambaye atawafuata ameokolewa kutokana na moto wa Jahanam; yeyote ambaye atawafuata ameongozwa katika njia iliyonyooka; yeyote ambaye amejaaliwa na Allah kuwa na mapenzi kwao hakika atapelekwa Peponi. Hivyo, watu wenye akili, chukueni tahadhari. Ningeweza kunukuu hadith za namna hiyo usiku wote, ambazo zote zimeandikwa na Maulamaa wenu. Lakini nafikiri hii inatosha. Ni Ali peke yake aliyefuatana na Mtume tangu utotoni, na kwa hiyo ni sawa kwamba tunamuona ni mtu aliyeashiriwa katika maneno, Wale ambao wako pamoja naye, na sio mtu ambaye alifuatana na Mtume kwa safari ya siku chache tu.

IMANI YA ALI AKIWA BADO MTOTO TU.


Hafidh: Umethibitisha Nukta yako, na kamwe hakuna hata mtu mmoja ambaye amekataa kwamba Ali alikuwa mbele zaidi katika kuukubali Uislamu. Lakini ukweli huu haumfadhilishi yeye kuwa mwenye sifa zaidi kwa kumlinganisha na Masahaba wengine. Kweli, Makhalifa wakubwa walikubali imani katika Uislamu miaka kadhaa baada ya Ali, lakini imani yao ilikuwa tofauti na bora zaidi kuliko yake. Sababu yenyewe ni kwamba Ali alikuwa mtoto tu, na hawa walikuwa watu wazima. Ni dhahiri kwamba, imani ya watu wazima, wenye busara ilikuwa bora zaidi kuliko ile ya mtoto. Kwa nyongeza, imani ya Ali ilikuwa ya ufuataji wa kibubusa na imani ya watu hawa ilijengwa juu ya akili. Imani inayopatikana kwa akili ni bora kuliko imani ya upofu. Kwa vile mtoto ambaye hayuko chini ya wajibu wa kidini wa kutekeleza ibada, haikiri imani isipokuwa kwa kufuata kwa upofu, hivyo Ali, ambaye alikuwa mtoto tu wa miaka kumi na tatu, alikiri imani yake kwa upofu tu wa kufuata.

137

Mikesha ya Peshawar
Muombezi: Mazungumzo kama hayo kutoka kwa mtu msomi kama wewe kwa hakika yanashangaza. Nashangaa jinsi gani nitaivunja hoja kama hiyo. Kama ningekuwa niseme kwamba umechukuwa msimamo kama huo kwa ukorofi tu, ingekuwa dhidi ya tabia yangu kuhusisha sababu kama hiyo kwa mtu msomi. Ngoja nikuulize Swali: je, kuukubali Uislamu kwa Ali kulitegemea juu ya kupenda kwake mwenyewe binafsi au kwa kulinganiwa ya Mtume? Hafidhi: Kwa nini unachukuwa mtizamo mkali kama huu juu ya namna tunavyoongea, kwani tunapokuwa na mashaka ni lazima tuyajadili. Kwa kujibu swali lako, nakiri kwamba Ali aliukubali Uislamu kwa ulinganio wa Mtume. Muombezi: Wakati Mtume alipomlingania Ali akubali Uislamu, yeye hakujua kwamba mtoto hafungwi na majukumu ya kidini? Kama ukisema kwamba alikuwa hajui utakuwa unahusisha na ujinga na kama alijua na akamhubiria Ali hata hivyo, basi kitendo chake kilikuwa cha upuuzi. Ni dhahiri kwamba, kuhusiha upuuzi kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni ukafir kwa vile Mtume ni Masum (hakosei wala hatendi dhambi). Allah anasema kuhusu yeye katika Qurani Tukufu: Wala hasemi kwa matamanio (ya nafsi yake). Hayakuwa haya ila ni Wahyi uliofunuliwa (kwake) (53:3-4). Mtume alimuona Ali ni mtu wa kufaa kulinganiwa kuukubali Uislamu. Mbali na hili, ujana si lazima kutanguliwa na hekima. Utu uzima huchukuliwa maanani kuhusiana na utekelezaji wa wajbat za kidini, lakini sio mambo yanayohusiana na hekima. Imani inahusiana na mambo yanayo endana na hekima na sio sheria za kidini. Hivyo Imani ya Ali wakati wa utoto ni sifa kwa ajili yake kama vile Allah anavyotuambia katika Qurani Tukufu kuhusu Isa katika maneno haya: Hakika mimi ni Mtumishi wa Allah: Allah amenipa kitabu na amenifanya Nabii. (19:30). Vilevile katika Sura hiyo anasema kuhusu Mtume Yahaya: Na tulimpa hekima angali mtoto. (19:12). Seyyed Ali Humairi Yamani, (alikufa 179 A.H.) anaonyesha ukweli huu katika mashairi yake. Ansema: Kama vile Yahaya alivyofikia cheo cha Utume katika utoto wake, Ali ambaye alikuwa mrithi wa Mtume na baba wa watoto wake, vilevile alifanywa mwakilishi wa Allah na mlezi wa watu akingali mtoto. Sifa na heshima inayotolewa na Allah haitegemei juu ya umri. Hekima na akili hutegemea juu ya hali ya kuzaliwa. Nashangazwa na maelezo yako kwa vile hoja kama hizo zilitolewa na Manasibi na Makhariji kwa kuchochewa na Bani Umayya. Waliishusha imani ya Ali kwamba ilikuwa ya utii wa kibubusa kwa yale aliyofundishwa. Hata wanachuo wenu wameikubali sifa ya Ali kwa namna hii. Muhammad bin Talha Shafii, Ibn Sabbagh Maliki, Ibn Abil-Hadid na wengine wamenukuu mashairi ya Ali. Katika moja ya mashari yake anasema: Nilikuwa wa kwanza na wa mbele zaidi miongoni mwenu katika kuukubali Uislamu wakati nilipokuwa mtoto mdogo tu. Kama imani ya Ali katika umri mdogo kama huo haikua bora, Mtume asingeielezea namna hiyo. Sulayman Balkhi Hanafi katika Yanabiul-Mawadda, Sura ya 55, uk. 202, anasimulia kutoka kwa Ahman Bin Abdullah

138

Mikesha ya Peshawar
Shafii akinukuu kutoka kwa Khalifa wa pili, Umar Bin Khattab, ambaye alisema: Abu Bakr, Abu Ubaida Jarra na Kundi la watu waliokuwepo pamoja na Mtume wa Allah aliposhika bega la Ali na kusema: Ewe Ali! Wewe ni wa kwanza na wa mbele zaidi miongoni mwa waumini wote na Waislamu katika kuukubali Uislamu, Wewe kwangu mimi ni kama alivyokuwa Harun kwa Musa. Vilevile Imam Ahmad Bin Hanbal anasimulia kutoka kwa Ibn Abbas, ambaye amesema yeye, Abu Bakr, Abu Ubaida Bin Jarra, na wengine walikuwa pamoja na Mtume wakati alipoweka mkono wake katika bega la Ali na akasema: Wewe uko mbele zaidi katika imani ya Uislamu miongoni mwa Waislamu wote, na uko kwangu Mimi kama Harun alivyokuwa kwa Musa, Ewe Ali! Anayefikiria kwamba mimi ni rafiki yake ambapo ni adui yako, huyo ni muongo. Ibn Sabbagh Maliki ameandika hadith kama hiyo katika Fusulul-Muhimma, uk. 125, kutoka Khasa-isul-Alawi kama simulizi ya Abdullah bin Abbas, na Imam Abu AbdurRahman Nisai anaeleza katika Khasaisul-Alawi kwamba alisema: Nimemsikia Umar bin Khattab akisema, Litajeni jina la Ali kwa heshima kwa sababu nimemsikia Mtume akisema kwamba Ali anazo sifa tatu. Mimi (Umar) natamani kwamba ningelikuwa na moja tu kati ya hizo kwa sababu kila moja ya sifa hizo ni yenye thamani kubwa sana kwangu kuliko kitu chochote katika ulimwengu huu. Ibn Sabbagh amesimulia kama ifuatavyo kwa nyongeza ya walivyoandika wengine. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kuhusu Ali, Yeye ambaye anakupenda wewe hunipenda mimi, na ambaye ananipenda mimi, Allah Humpenda, na yeyote apendwaye na Allah, humuingiza Peponi. Lakini yule ambaye ni adui kwako ni adui kwangu, na ambaye ni adui kwangu, Allah ni adui kwake na humhukumu kwenda Motoni. Kujitangaza kwa Ali kuwa Mwislamu hata ambapo alikuwa bado mdogo huthibitisha ubora wa hekima na sifa yake, ambayo hakuna Mwislamu mwingine anayeweza kuipata. Tabari katika kitabu chake cha Tarikh ananukuu kutoka Muhammad Bin Saad Bin Abi Waqqas, ambaye alisema: Nilimuuliza Baba yangu iwapo Abu Bakr alikuwa wa kwanza wa Waislamu. Yeye akasema, Hapana, zaidi ya watu hamsini waliingia Uislam kabla ya Abu Bakr; bali alikuwa mbora kwetu kama Mwislam. Vilevile anaandika kwamba Umar Bin Khattab aliingia Uislamu baada ya wanaume arobaini na tano na wanawake ishirini na moja. Ama kwa aliyekuwa mbele zaidi katika Uislamu na Imani, alikuwa ni Ali Bin Abi Talib.

139

Mikesha ya Peshawar

IMANI YA ALI ILIKUWA NI SEHEMU YA ASILI YAKE HASA:


Mbali na ukweli kwamba, Ali alikuwa wa mbele katika kuingia Uislamu, alikuwa na sifa nyingine, ya kipekee kwake, na ya muhimu zaidi kuliko sifa zake nyingine. Uislamu wa Ali ulitokana na asili yake, ambapo ule wa wengine umetokea tu baada ya kuwa makafir huko nyuma. Tofauti na Waislamu wengine na masahaba wa Mtume, Ali hajawahi kamwe kuwa Kafir. Hafidh Abu Nuaim Ispahani katika Ma-Nazalul-Qurani fi Ali, na Mir Seyyed Ali Hamadani katika Mawaddatul-Qurba wanasimulia kwamba Ibn Abbas amesema: Naapa kwa jina la Allah kwamba hakuna mtu hata mmoja ambaye alikuwa hakuabudu masanamu kabla ya kuingia Uislamu isipokuwa Ali. Ali, alikubali Uislamu akiwa kamwe hajapata kuabudu masanamu. Muhammad Bin Yusuph Ganji Shafii katika Kifayatut-Talib, Sura ya 24 anamnukuu Mtume akisema: Wale ambao walitangulia kuikubali imani katika upweke wa Allah miongoni mwa wafuasi wa Mitume walikuwa ni watu watatu ambao hawajawahi kamwe kuwa washirikina: Ali bin Abi Talib, mtu aliyetajwa katika Suratu Yaa-Sin, na Muumini katika watu wa Firauni. Wale wakweli (ma-Sidiq) ni Habib-e-Najjar, miongoni mwa kizazi cha Yaa Sin, Hizqil (Sawaiq al-Muhriqah, hadith ya 30 kati ya zile 40 kuhusu sifa za Ali, Yanabiul-Mawadda, Jz. 42, Nahjul-Balaghah, Jz. 2, uk. 451) miongoni mwa kizazi cha Firauni, na Ali bin Abi Talib, ambaye amewapita wote. Mir Seyyed Ali Hamadani katika Mawadda-tul-Qubra, Mawadda ya 7, Khatib Khawarizmi katika Manaqib na Imam Thalabi katika Tafsir yake anasimulia kutoka kwa Khalifa wa pili, Umar Bin Khattab: Nashuhudia kwamba nimemsikia Mtume akisema, Kama Mbingu Saba zingewekwa pamoja katika mizani moja na imani ya Ali katika nyingine, hakika imani ya Ali ingezidi uzito ile nyingine. Nukta hiyo hiyo iliwekwa katika mashairi yaliyotungwa na Sufyani bin Musab bin Kufi kama ifuatavyo: Kwa jina la Allah, nashuhudia kwamba Mtume alituambia: Haipasi kubakia bila kutojulikana na kwa mtu yeyote kwamba kama imani za wale wote wanaishi juu ya ardhi ingewekwa katika kipimio kimoja cha mizani na ile ya Ali katika kingine, imani ya Ali ingezidi uzito ile ya wengine.

140

Mikesha ya Peshawar

ALI ALIWAPITA MASAHABA WENGINE WOTE NA UMMA WOTE KATIKA UBORA.


Mir Seyyed Ali Hamadani Shafii amendika hadith nyingi katika Mawaddatul-Qurba yake, ambazo zinaunga mkoni ubora wa Ali. Katika Mawadda ya Saba ananukuu kutoka kwa Ibn Abbas kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: Mbora wa watu wa ulimwengu wote katika kipindi changu ni Ali. Wengi wa Maulamaa waadilifu wameukubali ubora wa Ali. Ibn Abil-Hadid katika Sharh yake ya Nahjul-Balagha Jz. 3, uk. 40, anasema kwamba Abu Jafar Iskafi, kiongozi wa madhehebu ya Mutazil, alitangaza kwamba Bashir bin Muamar, Abu Musa, Jafar Bin Mubashir, na maulamaa wengine wa Baghdad wanaamini kwamba, Mtu bora zaidi miongoni mwa Waislamu wote alikuwa Ali bin Abu Talib, na baada yake mtoto wake Hasan, kisha mtoto wake Husain, baada yake ni Hamza na baada yake ni Jafar Bin Abi Talib. Anaendelea kusema kwamba kiongozi wake Abu Abdullah Basri, Sheikh Abul-Qasim Balkhi, na Sheikh Abul-Hasan Khayya wanayo imani hiyo hiyo kama Abu Jafar Iskafi kuhusiana na ubora wa Ali. Anaelezea imani ya madhehebu ya Mutazil ikisema. Mtu bora baada ya Mtume wa Allah ni mrithi (makamu) wa Mtume, mume wa Fatima, Ali; baada yake, ni watoto wake wawili Hassan na Husain; baada yao, Hamza, na baada yake Jafar (Tayyar). Sheikh: Kama ungejua maelezo ya maulamaa yenye kuunga mkono ubora wa Abu Bakr, usingesema maneno haya.

IMANI YA ALI NI BORA KULIKO YA ABU BAKR.


Muombezi: Maulamaa wote wa kutegemewa, wa Kisuni wameukubali ubora wa Ali. Kwa mfano, unaweza ukarejea Sharh Nahjul-Balagha ya Ibn Abil-Hadid, Jz. 3, uk. 264, ambamo maelezo hayohayo yamenukuliwa kutoka kwa Jahiz kwamba imani ya Abu Bakr ilikuwa bora kuliko ile ya Ali. Walakini, Abu Jafar Askafi, mmoja wa maulamaa wakubwa wa madhehebu ya Mutazil alikataa madai haya, akisema kwamba imani ya Ali ilikuwa bora kwa ile ya Abu Bakr na masahaba wengine wote. Abu Jafar amesema: Hatukatai ubora wa masahaba, lakini kwa hakika hatumchukulii yeyote kati yao kuwa mbora kuliko Ali. Ali alikuwa wa cheo cha juu sana kiasi kwamba kutaja jina lake sambamba na masahaba wengine haifai. Kwa kweli sifa za masahaba haziwezi kulinganishwa na sifa tukufu mno za Ali. Mir Seyyed Ali Hamadani anasimulia katika Mawadda yake ya 7 kutoka kwa Ahmad Bin Muhammadul-Karzi Baghdadi, ambaye amesema kwamba alisikia kutoka kwa Abdullah bin Ahmad Hanbal, ambaye alimuuliza baba yake Ahmadi Bin Hanbal kuhusu cheo cha Masahaba wa Mtume. Yeye akamtaja Abu Bakr, Umar na Uthman na akasimama. Kisha Abdallah akamuuliza baba yake. Liko wapi jina la Ali bin Abu Talib?

141

Mikesha ya Peshawar
Baba yake akajibu, Yeye ni katika dhuria watukufu wa Mtume. Hatuwezi kutaja jina lake (kwa jinsi alivyo maarufu) sambamba pamoja na watu wale. Tunaona katika Qurani Tukufu kwamba katika aya ya Mubahila, Ali anatajwa kama nafsi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kuna hadithi yenye kuunga mkono habari hii, ambayo imeandikwa katika Mawadda ya 7 hiyohiyo, iliyosimuliwa kutoka kwa Abdullah Bin Umar Bin Khattab. Alisema kwamba siku moja walipokuwa wakihesabu majina ya masahaba, yeye alimtaja Abu Bakr, Umar, na Uthman. Mtu mmoja akasema, Ee Abdur-AbdurRahman! Kwa nini umeliacha jina la Ali? Yeye alijibu Ali ni mmoja wa dhuria wa Mtume. Hawezi kuchanganywa na mtu yoyote yule. Yuko katika kundi namna moja na Mtume wa Allah. Ngoja nisimulie hadith nyingine kutoka katika Mawadda hiyo hiyo. Imesimuliwa kutoka kwa Jabir Bin Abdullah Ansari kwamba siku moja wakiwepo mbele ya Muhajirina na Ansari, Mtume alimwambia Ali: Ewe Ali! Kama mtu atatekeleza Sala zake kamili kwa Allah, na kisha akatia shaka kwamba wewe na familia yako ni bora kwa viumbe wengine wote, makazi yake yatakuwa Jahanam. (Baada ya kusikia hadith hii, wale wote waliokuwepo pale, hususan Bw. Hafidhi, walionyesha kutubu, isije wakawa miongoni mwa wenye kutia mashaka). Nimerejea hadith chache tu. Chaguo lenu linaelekea kuwa ni kuzikataa hadith zote hizi sahihi, ambazo zimeandikwa kwenye vitabu vyenu, au kukubali kwamba imani ya Ali ilikuwa bora kuliko ile ya masahaba wote, pamoja na ya Abu Bakr na Umar. Vilevile naomba muiangalie hadith hii (inayokubaliwa na madhehebu zote) ambamo Mtume alisema wakati wa Ghazawa-e-Ahzab (hujulikana vilevile kama vita vya Handaq), wakati Ali alipomuua Amru Ibn Abdu-e-Wudd kwa pigo moja la upanga wake: Pigo moja la Ali katika vita vya Khandaq limempatia fadhila zaidi kuliko malipo ya matendo mema ya umma wote (majini na watu) mpaka Siku ya Hukumu. Kama pigo moja la upanga wake lilikuwa bora katika fadhila kuliko Sala za majini na watu zikichanganywa zote pamoja hakika ubora wake hauwezi kuhojiwa na yeyote isipokuwa na mashupavu waovu.

ALI KAMA NAFSI YA MTUKUFU MTUME (S.A.W.W.).


Ingekuwa hakuna uthibitisho mwingine wa ubora wa Ali kwa Masahaba wote na Wanadamu wote kwa ujumla, Aya ya Mubahila inatosha kuthibitisha ubora wake. Inamtaja Ali kama nafsi ya Mtume. Mtukufu Mtume alikuwa kwa kukubalika kabisa ni mbora zaidi kwa wanadamu wote kuanzia mwanzo mpaka mwisho. Kwa hiyo, neno anfusana (nafsi zetu) katika aya hiyo linaloashiria kwa Ali huthibitisha kwamba pia alikuwa bora kwa wanadamu wote kuanzia mwanzo mpaka mwisho. Huenda sasa mtakubali kwamba ule usemi, Na wale ambao wapo pamoja naye, utajo wake ni kwa Ali. Yeye alikuwa pamoja na Mtume kabla ya mtu yeyote yule kuanzia mwanzo wa Uislamu.

142

Mikesha ya Peshawar
Ama kwa nini Ali hakufuatana na Mtume katika usiku wa kuhama kutoka Makka, ni wazi kwamba Mtume alimkabidhi Ali majukumu muhimu zaidi. Hakuna aliyekuwa muaminifu kama Ali. Aliachwa nyuma kurudisha kwa wenyewe mali zilizowekwa amana kwa Mtume. (Jukumu la pili la Ali lilikuwa ni kuipeleka familia ya Mtume na Waislamu wengine Madina. Na hata ingawa Ali hakuwa pamoja na Mtume katika pango usiku ule, alitekeleza jukumu muhimu zaidi kwa vile alilala katika kitanda cha Mtume).

AYA YA QURANI YENYE KUMSIFU ALI KWA KULALA KWAKE KATIKA KITANDA CHA MTUME KATIKA USIKU WA HIJRA.
Wanachuoni wenu wenyewe wametaja sifa za Ali katika tafsir zao (za Qurani). Kwa mfano, Ibn Sabi Maghribi katika Shifaus-Sudur, Tibrani katika Ausat na Kabir, Ibn Athir katika Usudul-Ghaiba, Jz. 4, uk. 25, Nurud-Din Sabbagh Maliki katika FusulilMuhimma Fi Marifatil-aimma, uk. 33, Abu Ishaq Thalabi, Fazil Nishapuri, FakhrudDin Radhi na Jalalud-Dini Suyuti, kila mmoja katika Tafsir yake, Hafidh Abu Nuaim Isphahani, muhadithina maarufu wa Ki-Shafii katika Ma-Nazalal-Quran fi Ali, Khatib Khawarizmi katika Manaqib Sheikhul-Islam Ibrahim bin Muhammad Hamwaini katika Faraid, Muhammad bin Yusuf Ganji Shafii katika Kifayatut-Talib, Sura ya 62, Imam Ahmad bin Hanbal katika Musnad, Muhammad bin Jarir kupitia vyanzo mbalimbali, Ibn Hisham katika Siratun-Nabi, Hafidh Muhadith wa Damascus katika Arbain Tiwal, Imam Ghazali, katika Ihyaul-Ulum, Jz. 3, uk. 223, Abus-Saadat katika Fadhailul-Iratit-Tahira, Ibn Abil-Hadid katika Sharhe Nahjul-Balagha, Sibt Ibn Jauzi katika Tadhikira na wengine katika maulamaa wenu mashuhuri, wanasimulia kwamba wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokusudia, kwa amri ya Allah, kuondoka Makka na kwenda Madina, alimtaka Ali ajifunike shuka lake la kijani na alale katika kitanda chake. Kwa hiyo, Ali akalala pahali pa Mtume kisha Mwenyezi Mungu akawaambia Malaika Jibril na Mikael kwamba amewafanya wao kuwa ndugu, na kwamba mmoja wao ataishi muda mrefu kuliko mwingine. Aliwauliza ni nani alikuwa tayari kumpa ndugu yake maisha yake ya ziada, ambayo kadiri yake hakuna mmoja wao aliyejua. Walimuuliza (Allah) iwapo chaguo hilo ni wajibu. Walielezwa kwamba sio wajibu. Hakuna hata mmoja wao aliyechagua kuachana na maisha yake ya ziada. Kisha yakafuata maneno haya matukufu: Mimi nimeumba undugu kati ya mwakilishi wangu Ali na Mtume wangu Muhammad. Ali amejitolea kutoa mhanga maisha yake kwa ajili ya maisha ya Mtume. Kwa kulala katika kitanda cha Mtume, anayalinda maisha ya Mtume. Sasa ninyi wote mnaagizwa kwenda duniani kumuokoa kutokana na mbinu za uovu wa maadui.

143

Mikesha ya Peshawar
Kwa hiyo, wote wakaja duniani. Jibril akakaa kichwani kwa Ali na Mikaeli miguuni kwake. Jibril akasema, Hongera, Ewe mwana wa Abu Talib! ambaye kwako Mwenyezi Mungu anajivunia mbele ya Malaika Zake. Baada ya haya, Aya ifuatayo ikateremshwa kwa Mtume. Na kuna aina ya watu ambao hutoa maisha yao kuzitafuta radhi ya Allah; na Allah ni mwingi wa upole kwa waja (wake). (2:207). Sasa nakusihini waheshimiwa, kuingalia aya hii kwa uangalifu wakati mtakaporudi nyumbani usiku na kutoa uamuzi wenu wenyewe. Je, ubora kwa haki ni wa yule ambaye alibakia pamoja na Mtume katika safari ya siku chache, akionyesha woga na huzuni, au kwa yule ambaye alihatarisha maisha yake usiku ule kishujaa na kwa furaha, kwa ajili ya usalama wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Imam Jafar Askafi, mmoja wa maulamaa wakubwa na viongozi wa Mutazil, anathibitisha, (kama ilivyosimuliwa katika Sharhe ya Nahajul-Balagha na Abil-Hadid Jz. 3, uk. 269-281), kwamba kulala kwa Ali katika kitanda cha Mtume kulikuwa bora zaidi kuliko muda mfupi wa Abu Bakr aliokaa pamoja na Mtume. Anasema: Maulamaa wa Kiislamu kwa pamoja wanashikilia kwamba, kwa ukweli halisi, ubora wa Ali katika usiku ule ulitukuka mno kiasi kwamba hakuna mtu angeweza kuufikia isipokuwa Ishaka na Ibrahimu wakati walipokuwa tayari kutoa maisha yao mhanga katika kutii mapenzi ya Allah. (Wafasiri wengi, maulamaa na wanahistoria wanaamini kwamba alikuwa ni Ismail ambaye alijitoa mhanga na sio Ishaka). Katika ukurasa wa 271 wa Sharhe ya Nahajul-Balagha, maelezo ya Abu Jafar Askafi katika kumjibu Abu Athman Jahiz Nasib yameandikwa. Anasema: Nilikwisha kuthibitisha mapema kwamba kulala kwa Ali katika kitanda cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika usiku wa kuhama kulikuwa bora zaidi kuliko kule kwa Abu Bakr kubakia pamoja na Mtume katika Pango. Ili kusisitiza hoja yangu, nitaithibitisha katika mitazamo mingine miwili: Kwanza, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wa Allah akiwa na mkuruba wa karibu na wa siku nyingi na Ali, alimpenda mno. Kwa hiyo alihisi kupotea kwa upendo wakati walipotengana. Kwa upande mwingine, Abu Bakr alipata fursa ya kwenda pamoja na Mtume. Kwa vili Ali alikuwa na uchungu wa kutengana kwao, malipo yake yaliongezeka kwa sababu jinsi maumivu yanavyokuwa makali zaidi katika utumushi, ndivyo yanavyopata malipo makubwa zaidi. Pili, kwa vile Ali alikusudia kuondoka Makka na hata aliwahi mara moja kuondoka peke yake, hali yake kama raia kule iliongezeka kuwa ngumu. Hivyo wakati akiondoka Makka pamoja na Mtume, hamu yake ya kuondoka ilitimia. Kwa ajili hiyo hakuna ubora wa kimaadili kama huo kwa ajili yake kama ulivyo kwa Ali, ambaye alivumilia machungu makali katika kuhatarisha maisha yake mbele ya panga zilizochomolewa za maadui. Ibn Saba Maghrib anasema katika kitabu chake Shifaus-Sudur kuhusu ushujaa wa Ali: Kuna umoja kamili (wa makubaliano) miongoni mwa maulamaa wa Kiarabu kwamba katika usiku wa Hijra, kulala kwa Ali katika kitanda cha Mtume kulikuwa bora zaidi ya kutoka pamoja naye. Ali alijifanya mwenyewe mwakilishi wa Mtume na akahatarisha

144

Mikesha ya Peshawar
maisha yake kwa ajili ya Mtume. Hoja hii ni wazi mno kiasi kwamba kamwe hakuna hata mtu mmoja aliyeikataa isipokuwa wale waliopatwa na uwenda wazimu au ushabiki. Nitakomeshea hapa na kurudi kwenye nukta yangu muhimu. Umesema kwamba, maneno ya Qurani Wakali dhidi ya makafir (48:29) yanamuashiria Khalifa wa pili, Umar Bin Khattab. Lakini dai hili haliwezi kukubaliwa kwa sababu tu kwamba umesema hivyo. Ni lazima tuamue iwapo sifa hii ni katika tabia yake au laa. Kama ndivyo, niko radhi kuikubali. Kwa hakika ukali unaweza kuonyeshwa katika njia mbili: Katika majadiliano ya kidini ambayo kwayo kwa nguvu ya hoja, maulamaa wa upande mwingine wananyamazishwa. Pili, unaweza kuonyeshwa katika uwanja wa vita. Kwa kadiri mijadala ya kielmu ihusikanavyo, hakuna mfano hata mmoja katika historia ambapo Umar ameonyesha ukali wowote. Katika kiwango chochote, sijaona taarifa yoyote ya kihistoria yenye kuonyesha kwamba Umar alionyesha ukali katika majadiliano ya kielimu. Nitawashukuruni kama mtanionyesha mfano wowote. Kwa kweli, maulamaa wenu, wamekubali kwamba alikuwa ni Ali ambaye aliyatatua yale matatizo ngumu ya kisheria na kufutu masala ya kidini wakati wa kipindi cha Makhalifa watatu. Ingawaje Bani Umayya na wafuasi mbumbumbu wa Abu Bakr walibuni hadithi zisizo na idadi kwa niaba yao, hawakuweza kuficha ukweli kwamba wakati watu wa imani nyingine walipokuja kwa Abu Bakar, Umar, au Uthman, kutatua matatizo magumu, makhalifa hawa waliyapeleka matatizo hayo kwa Ali. Ali aliwapa majibu ya kuvutia kiasi kwamba watu wengi wasiokuwa Waislamu waliingia Uislamu. Ukweli kwamba Abu Bakr, Umar na Uthman walikubali ubora wa Ali unatosha kuthibitisha hoja yangu. Wanachuoni wenu wameandika kwamba Khalifa Abu Bakr alisema: Niondoeni, niondoeni, kwa vile mimi sio bora kuliko ninyi alimuradi Ali yuko kati yenu. Kwa uchache kabisa, takriban mara sabini, khalifa Umar alikiri: Kama Ali asingekuepo Umar angeangamia. Mazingira mengi yenye hatari yametajwa kwenye vitabu, lakini mimi sitaki kueleza sana juu ya nukta hii. Kunaweza kuwa na mambo mengi muhimu ya kujadili. Nawab: Ni habari gani zaweza kuwa za muhimu zaidi kuliko hii? Je, mambo haya yametajwa katika vitabu vyetu? Kama yametajwa tafadhali tueleze tupate kujua. Muombezi: Maulamaa waadilifu wa madhehebu yenu wanakubali kwamba, mara kwa mara Umar alikiri kwamba Ali alikuja kumuokoa.

145

Mikesha ya Peshawar

USHAHIDI KUHUSU MANENO YA UMAR: KAMA ALI ASINGEKUWEPO, UMAR ANGEANGAMIA.


Qadhi Fadhlullah Bin Ruzbahan, yule shabiki shupavu, katika kitabu chake IbtalulBatil; Ibn Majar Asqalani katika Tihdhibul-Tahdid, kilichochapishwa Hyderabad Daccan, uk. 337; Ibn Hajar katika Isaba, Jz. 2, iliyochapishwa Misir uk. 509; Ibn Qutayba Dinawari katika Tawil-e-Mukhtalaful-Hadith uk. 201-202, Ibn Hajar Makki katika Sawaiq-e-Muhriqa uk. 78; Hajj Ahmad Afindi katika Hidayatul-Murtab uk. 146 na 152, Ibn Athir Jazari katika Usudul-Ghaiba, Jz. 4, uk. 22; Jalalud-Din Suyuti katika Tarikhul-Khulafa, uk. 66; Ibn Abdul-Birr Qartabi katika Istiab Jz. 2, uk. 474; Seyyed Mumin Shablanji katika Nurul-Absar uk.73; Shahabud-Din Ahmad bin Abdul-Qadir Ajili katika Dhakhiratul-Maal; Muhammad bin Ali As-Subban katika Isafur-Raghibin, uk.152; Nurud-Din bin Sabbagh Maliki katika Fusulul-Muhimma, uk. 18; Nurud-Din Ali bin Abdullah Samhudi katika Jawahirul-Iqdani; Ibn AbilHadid Mutazil katika Sharhe Nahajul-Balagha, Jz. 1, uk. 6. Allama Qushachi katika Sharhe-e-Tarid, uk. 407, Khatib Khawarizmi katika Manaqib, uk. 46 & 60 Muhammad bin Talha Shafii katika Matalibus-Suul Sura ndogo ya 6, uk. 29, Imam Ahmad bin Hanbal katika Fadhail halikadhalia na Musnad; Sibt Ibn Jauzi katika Fadhkira uk. 85 na 87 Imam Thalabi katika Tafsir Kafshul-Bayan, Allama Ibn Qayyim Jauzi katika Turuqil-Hakim, akiandika hukumu za Ali kuanzia uk. 41 mpaka uk. 53; Muhammd bin Yusufu Ganji Shafii katika Kifayatut-Talib, Sura ya 57; Ibn Maja Qazwini katika Sunan yake; Ibn Maghazili Shafii katika Manaqib; Ibrahim bin Muhammad Hamwaini katika Faraid; Muhammad bin Ali bin Hasanil-Hakim katika Sharh-eFathil-Mubin; Dailami katika Firdaus Sheikh Sulayman Balkhi Hanafi katika Yanabiul-Mawadda, Sura ya 14, Hafidh Abu Nuaim Ispahani katika HilyatulAuliya, halikadhalika katika Ma-Naza-lal-Quran fi Ali, na kundi la maulamaa wakubwa wa madhehebu yenu, pamoja na tofauti ndogo katika maneno, wamesimulia usemi wa Umar, Kama Ali asingekuwepo, Umar angeangamia. Mwanachuoni mkubwa, Ganji Shafii, katika sura ya 57, ya Kifayatut-Talib Fi Manaqib Ali Bin Abu Talib, baada ya kusimulia baadhi ya hadith sahihi anaelezea kutoka kwa Hudhaifa bin Yaman kwamba, Siku moja yeye Hudhaifa alikutana na Umar, akamwuliza (yeye Hudhaifa): Ulijisikiaje hali yako wakati ulivyoamka asubuhi? Hudhaifa akasema, Niliamka asubuhi nikiichukia haki, nikipenda fitina, kushuhudia kitu kisichoonekana; kujifunza kwa moyo kitu kisichoumbwa, kusali bila kuwa na wudhuu, na kujua kwamba, kilichokuwa changu hapa duniani, sio kwa ajili ya Allah katika Mbingu. Umar alikasirishwa sana na maneno haya na alikusudia kumuadhibu Hudhaifa wakati Ali alipoingia ndani. Aliona dalili za hasira kwenye uso wa Umar na akauliza kwa nini alikuwa amekasirika

146

Mikesha ya Peshawar
hivyo. Umar akamueleza (maneno ya Hudhaifa) na Ali akasema: Hakuna ubaya wowote kuhusu maneno haya. Alichosema Hudhaifa ni sawa sawa: Haki maana yake kifo, ambacho anakichukia; fitna maana yake mali na watoto ambavyo anavitaka; na anaposema kwamba anashuhudia ambavyo hakuviona, hii ina maana kwamba anashuhudia upweke wa Allah, kifo, siku ya malipo, Pepo, Moto, daraja juu yake inayoitwa Sirat, ambavyo hakuna hata kimoja kati ya hivyo alichokiona. Anaposema anajifundisha kwa moyo ambacho hakikuumbwa, hii huashiria kwenye Qurani. Anaposema kwamba anasali bila wuudhu, hii huashiria katika kumswalia Mtume wa Allah (kumtakia rehema na amani) ambako kuna ruhusiwa bila wuudhu; wakati akisema anacho kitu duniani ambacho si kwa ajili ya Allah Mbinguni, hii huashiria kwa mke wake, kwa vile Allah hana mke au watoto. Kisha Umar akasema: Umar angepotea kama Ali asingetokea. Ganji Shafii anasema kwamba maelezo ya Umar yanathibitika kwa mujibu wa riwaya za wasimuliaji wengi wa hadith. Mwandishi wa Manaqib anasema kwamba Khalifa Umar, mara kwa mara alisema: Ewe Abul-Hasan! (Ali). Sitakuwa sehemu ya jamii bila wewe. Vilevile alisema: Wanawake hawana uwezo wa kuzaa mtoto kama Ali. Muhammad bin Talha Shafii katika Matalibus-Su-ul na Sheikh Sulayman Balkh Hanafi katika Yanabiul-Mawadda, Sura ya 14, akisimulia kutoka kwa Tirmidhi, ameandika riwaya yenye kinaganaga kutoka kwa Ibn Abbas ambapo mwisho wa riwaya hiyo anasema: Masahaba wa Mtume walikuwa wakitafuta hukumu za kidini kutoka kwa Ali, na walikubali maamuzi yake. Hivyo, Umar Bin Khattab alisema katika nyakati mbalimbali, Kama isingekuwa ni Ali, Umar angeangamia. Katika mambo ya kidini na mijadala ya kielimu Umar hakuonyesha ukali wowote. Kinyume chake, alikiri udhaifu wake mwenyewe na kumkubali Ali kama kimbilio lake. Hata Ibn Hajar Makki katika sura ya 3 ya Sawaiq-Muhriqa, akielezea kutoka kwa Ibn Sad anamnukuu Umar akisema: Naomba msaada wa Allah katika kuamua yale matatizo magumu ambayo kwamba Abul-Hasan (Ali) hayupo.

USHUJAA WA KHALIFA UMAR HAUJAONEKANA KAMWE KATIKA UWANJA WOWOTE WA VITA.


Amma kuhusu ukali wa Umar katika uwanja wa vita, historia haikuandika mfano wowote juu ya hilo. Kinyume chake, wanahistoria wa madhehebu zote wanasimulia kwamba wakati wowote Umar alipokabiliana na adui mwenye nguvu, yeye alikimbia. Matokeo yake, Waislamu wengine pia walikimbia na mara kwa mara jeshi la Kiislamu lilishindwa. Hafidh: Umezidisha pole pole ukosefu wa uungwana. Umemtukana Khalifa Umar ambaye alikuwa ni fahari ya Waislamu na ambaye katika zama zake Waislamu walipata

147

Mikesha ya Peshawar
ushindi mkubwa. Kwa sababu ya Umar, jeshi la Waislamu lilishinda vita vyao. Unamuita muoga na kusema kwamba alikimbia kutoka uwanja wa vita na kwamba kushindwa kwa jeshi la Kiislamu kulikuwa ni kwa sababu yake! Je, ni sahihi mtu wa hadhi kama yako kumsingizia Khalifa Umar? Muombezi: Nina wasiwasi kwamba umekosea. Ingawa umekuwa na mimi kwa mikesha mingi, hujanielewa bado. Pengine unafikiria ni kwa sababu ya chuki kwamba ndio ninalaumu au kusifu watu. Sio hivyo. Kuna kuwiwa kukubwa katika mijadala ya kidini, ambako kumekuwa ni chanzo cha upinzani miongoni mwa Waislamu kwa karne nyingi. Mijadala kama hiyo mara kwa mara uchochea hali ya uovu, ambayo haipatani na maamrisho ya Qurani. Qurani kwa uwazi inasema: Enyi ambao mmeamini! Jiepusheni sana na dhana (kama iwezekanavyo) kwani baadhi ya dhana katika hali nyingine ni dhambi. (49:12). Unafikiria kwamba maelezo yangu yamechochewa na uovu. Ukweli ni kinyume chake. Sijatamka neno kinyume cha ambavyo maulamaa wenu wameandika. Umesema hivi punde tu kwamba nimemtukana Khalifa Umar. Lakini kulikuwa hakuna hata chembe ya dalili ya matusi. Niliyosema yanaoana na kumbukumbu za Historia. Sasa nalazimika kutoa mtazamo ulio wazi ili kunyamazisha upinzani huu.

USHINDI HAUKUWA KWA SABABU YA SIFA BINAFSI ZA UMAR.


Umesema Khalifa Umar alikuwa anahusika na ushindi wa Waislamu. Hakuna mtu anayekataa kwamba Waislamu walipata ushindi mkubwa wakati wa Ukhalifa wa Umar. Lakini kumbuka kwamba kwa mujibu wa maulamaa wenu mashuhuri, kama Qadhi Abu Bakr Khatib, katika kitabu chake, Tarikh Baghdad, Imam Ahmad Bin Hanbal katika Musnad, Ibn Abil-Hadid katika Sharhe Nahjul-Balagha na waandishi wengine wengi, Khalifa Umar alitafuta mwongozo kutoka kwa Ali katika mambo yote ya kiutawala na kijeshi. Na alikuwa akitenda kwa kufuata ushauri wa Ali. Kwa nyongeza, kulikuwa na tofauti katika ushindi wa Kiislamu kwa vipindi tofauti. Namna ya kwanza inarejea kwenye ushindi wakati wa kipindi cha Mtume mwenyewe, ambao ulikuwa kimsingi kwa sababu ya Ushujaa wa Ali. Kila mtu anakubali kwamba Ali alikuwa shujaa zaidi wa mashujaa. Kama hakupigana katika vita, ushindi haukupatikana. Kwa mfano katika vita vya Khaibar, alipata maradhi ya macho, na ilikuwa haiwezikani kwa yeye kwenda kwenye mapigano. Waislamu walirudia rudia kushindwa kila walipokwenda kwenye uwanja wa mapambano, mpaka alipotibiwa na Mtume, Ali aliwaendea maadui mpaka akaziteka ngome za Khabar. Katika vita vya Uhud, wakati Waislamu wakivunja safu na kukimbia, alikuwa ni Ali aliyesimama imara. Bila woga, alimkinga Mtume kutokana na maadui mpaka sauti iliyojificha ikatangaza, Hakuna upanga kama Dhul-fiqah, na hakuna kijana shujaa kuliko Ali.

148

Mikesha ya Peshawar

Namna ya pili ya ushindi inahusiana na vile vita ambavyo vilipiganwa baada ya kifo cha Mtume. Ushindi huu ulikuwa ni kutokana na ushujaa wa maaskari mashuhuri wa Kiislamu na ubingwa wao wa kupanga. Lakini hapa hatuhusiki na ushindi wa Kiislamu wa wakati wa Ukhalifa wa Umar. Maudhui yetu ni kuhusu ujasiri wa Umar mwenyewe. Hauthibitishwi na ushahidi wowote wa kihistoria. Hafidh: Ni matusi kudai kwamba Umar alikimbia kutoka uwanja wa mapambano, na kwamba hii ilipelekea kushindwa kwa Waislamu. Muombezi: Kama kuonyesha ukweli wa kihistoria kuhusu mtu ni matusi, basi matusi haya yameandikwa na maulamaa wenu. Hafidh: Ni wapi maulamaa wetu walipoandika kwamba Khalifa Umar alikimbia kutoka Uwanja wa mapambano? Ni wakati gani alisababisha kushindwa kwa Waislamu?

KUSHINDWA KWA ABU BAKR NA UMAR KATIKA VITA VYA KHAIBAR.


Muombezi: Kwa vile Ali alikuwa akiumwa macho katika siku ya kwanza ya vita vya Khaibar, Mtume alimpa Abu Bakr bendera ya Waislamu, ambaye aliongoza jeshi la Waislamu dhidi ya Mayahudi. Alirudi akiwa ameshindwa baada ya muda mfupi wa mapambano. Siku iliyofuata bendera ya Waislamu ilitolewa kwa Umar, lakini kabla hajafika sehemu ya mapambano, alikimbia kwa woga. Hafidh: Maelezo haya ni uzushi wa Shia. Muombezi: Vita vya Khaibar vilikuwa ni tukio muhimu la maisha ya Mtukufu Mtume, lililosimuliwa kwa kinaganaga na wanahistoria wa madhehebu zote. Hafidh Abu Nuaim Ispahani katika Hilyatul-Auliya Jz. 1, uk. 62, Muhammad Bin Talha Shafii katika Matalibus-Suul, uk. 40, kutoka katika Sira cha Ibn Hisham, Muhammad bin Yusuf Ganji Shafii katika Kifayatut-Talib, Sura ya 14, na maulamaa wenu wengi wengine wameandika tukio hili. Lakini simulizi iliyo sahihi zaidi ni ile ya wanachuoni wawili wakubwa. Muhammad bin Ismail Bukhari, ambaye ameandika katika Sahih yake Jz. 2 iliyochapishwa Misir 1320 A.H., uk. 100, na Muslim Bin Hujjaj, ambaye anaandika katika Sahih yake, Jz. 2, iliyochapishwa Misir 1320 A.H., uk. 324, kwamba, Khalifa Umar alikimbia kutoka Uwanja wa mapambano katika safari mbili. Miongoni mwa thibitisho nyingi zilizo wazi juu ya nukta hii ni beti zilizo za wazi za Ibn Abil-Hadid wa madhehebu ya Mutazila zijulikanazo kama Alawiyyat-e-Saba katika

149

Mikesha ya Peshawar
kumsifu Ali. Kuhusu lango la Khaibar, anasema: Je, umesikia hadithi ya ushindi wa Khaibar? Miujiza mingi imefunganishwa pamoja ambayo huchanganya hata akili zenyes busara! Hawa wawili (Abu Bakr na Umar) walikuwa hawana mapenzi kwayo, au maarifa, ya kubeba bendera (kuongoza jeshi). Hawakujua siri za kutunza heshima ya bendera, waliifunika na twezo na wakakimbia ingawa walijua kwamba kukimbia kutoka kwenye uwanja wa mapambano ni sawa sawa na ukafiri. Walifanya hivyo kwa sababu ya mmoja wa wanajeshi shujaa wa Kiyahudi, kijana mrefu na upanga wa wazi mkononi, akiwa amepanda juu ya farasi mwenye umbo refu, akiwashambulia kama mbuni dume aliyesisimuliwa, ambaye amepata nguvu kutokana na hewa ya msimu wa kuchipua na uoto wake wa mimea. Alikuwa kama ndege mkubwa ambaye amejipamba kwa rangi za kupendeza na aliyekuwa akienda kuelekea kwa mpenzi wake. Mngaro wa moto wa kifo kutoka kwenye upanga wake na mkuki uliangaza na kuwatishia watu wawili hawa. Ibn Abil-Hadid akizungumza nao (Abu Bakr na Umar) anaendelea kusema: Nakuombeeni msamaha juu yenu, kwa kule kushindwa na kukimbia kwenu, kwa vile kila mtu anachukia kifo na kupenda uhai. Kama wengine wote, ninyi pia hamkukipenda kifo ingawa hakuna kinga kutokana na kifo. Lakini hamkuweza kujihatarisha na kifo. Lengo langu sio kumkashifu mtu yeyote, ninasimulia ukweli wa kihistoria kuonyesha kwamba Khalifa hakuwa na ushujaa kama huo ambao angestahiki sifa ya Mkali dhidi ya Makafir. Ukweli ni kwamba yeye alikimbia kutoka uwanja wa mapambano. Sifa hii katika mjadala inamhusu Ali peke yake, ambaye katika kila vita alikuwa mkali dhidi ya makafiri. Ukweli huu umethibitishwa na Allah kwenye Qurani Tukufu. Yeye Anasema: Enyi mlioamini! atakayeiacha dini yake miongoni mwenu, basi hivi karibuni Mwenyezi Mungu ataleta watu wengine ambao atawapenda, nao watampenda, wanyenyekevu kwa waumini, na wenye nguvu kwa makafiri. Watapiganaia dini ya Mwenyezi Mungu, wala hawataogopa lawama ya wenye kulaumu. Hiyo ndiyo fadhila ya Mwenyezi Mungu, humpa amtakaye, na Mwenyezi Mungu ni Mweny wasaa, Mwenye kujua. (5:54-56). Hafidh: Inashangaza kwamba unajaribu kuhusisha aya hii na Ali. Hii inazungumzia waumini ambao wanazo sifa hizi na vipenzi wa Allah. Muombezi: Ingekuwa vizuri kama ungeniuliza ni hoja gani ningeweza kutoa kuunga mkono maneno yangu. Jibu langu ni kwamba kama aya hii ingeteremshwa katika kuwasifu waumini, wasingekimbia kamwe kutoka uwanja wa mapambano. Hafidh: Je, ni haki kuwalaumu waumini na masahaba wa Mtume (lawama) ya kukimbia kutoka kwenye hatari? Watu hawa walipigana kishujaa katika vita. Muombezi: Sio mimi niliyewaita Wakimbiaji. Historia inawaonyesha kama hivyo. Pengine umesahau kwamba katika vita vya Uhud na Hunain waumini wote na masahaba kwa ujumla, pamoja na masahaba wakubwa wa Mtume, walitafuta usalama kwa kukimbia.

150

Mikesha ya Peshawar
Kama ilivyosimuliwa na Tabrini na wengine, wao walimuacha Mtume peke yake kati ya makafiri. Je, inawezekana kwamba wale waliogeuka na kuwapa maadui migongo wakimuacha Mtume peke yake kuwakabili maadui walikuwa wapenzi wa Allah na Mtume Wake? Siko peke yangu katika kudai kwamba Aya hii iko katika kumsifu Ali. Abu Ishaq Imam Ahmad Thalabi, ambaye mnamchukulia kama mkubwa wa wasimuliaji wenu wa Hadith, anaandika katika kitabu chake Kashful-Bayan kwamba aya hii imeteremshwa katika kumsifu Ali kwa sababu hakuna mtu mwingine aliyekuwa na sifa zilizotajwa ndani yake. Hakuna mwanahistoria - wa kwetu au wa nje - ambaye ameandika kwamba katika vita 36 vilivyopiganwa na Mtume, Ali hakuserereka kamwe hata katika moja. Katika vita vya Uhud, wakati masahaba wengine wote walipokimbia, na jeshi la adui lenye askari 5000 likawashambulia Waislamu, mtu pekee aliyebakia kwenye sehemu yake mpaka ushindi ulipopatikana alikuwa ni Ali. Ingawa alijeruhiwa sehemu mbalimbali na kuvuja damu kwa wingi, aliwakusanya wale ambao walikuwa wamekimbia na kuendelea kupigana mpaka ushindi ulipopatikana. Hafidh: Huna aibu kuhusisha kukimbia kwa masahaba wakubwa? Masahaba wote kwa ujumla na hasa Abu Bakr na Umar kwa ushujaa walimzunguuka Mtume na kumlinda. Muombezi: Hukujifunza historia kwa uangalifu. Kwa ujumla, wanahistoria wameandika kwamba, katika vita vya Uhud Hunain na Khaibar masahaba wote walikimbia. Nimekueleza kuhusu Khaibar. Amma kuhusu Hunain, Hamid katika Jam-e-BanusSahihain na Halabi katika Siratul-Halabiyya, Jz. 3, uk. 123, anasema kwamba masahaba wote walikimbia isipokuwa wanne: Ali na Abbas walikuwa mbele ya Mtume, Abu Sufyan Bin Harith alishika hatamu za farasi wa Mtume, na Abdullah Bin Masud alisimama upande wake wa kushoto. Kukimbia kwa Waislamu huko Uhud hakukukataliwa na mtu yeyote. Muhammad bin Yusuf Ganji Shafii katika Kifayatut-Talib Sura ya 27, kwa vyanzo vyake mwenyewe, anamnukuu Abdullah Bin Masud akisema kwamba Mtume amesema: Wakati wowote Ali anapopelekwa peke yake katika pambano, nilimuona Jibril upande wake wa kulia, Mikael upande wake wa kushoto, na wingu likimfunika kutoka juu mpaka Allah Alipomfanya mshindi. Imam Abu Abdur-Rahman Nisai anasimulia hadith 202 katika kitabu chake Khasais-eAlawi kwamba Imam Hasan, akiwa amevaa kilemba cheusi alikuja kwa watu na akasimulia sifa za baba yake, akisema kwamba katika vita vya Khaibar, wakati Ali alipokwenda kuelekea ile ngome, Jibril alikuwa akipigana upande wake wa kulia na Mikael upande wake wa kushoto. Alimkabili adui kwa ushujaa mkubwa mpaka alipopata ushindi na akawa anastahiki mapenzi ya Allah.

151

Mikesha ya Peshawar

ALI ALIKUWA MWENYE KUPENDWA NA ALLAH NA MTUKUFU MTUME (S.A.W.W.).


Katika Aya hii Allah anasema kwamba Yeye anawapenda wale ambao wana sifa hizi na kwamba wao pia wanampenda Yeye. Sifa hii ya kupendwa na Allah ni ya kipekee kwa Ali. Kuna ushahidi mwingi sana wenye kuunga mkono mtazamo huu. Miongoni mwa hadithi nyingi zinazohusiana na jambo hili ni ile inayosimuliwa na Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafii katika Kifayatut-Talib, Sura ya 7. Anasimulia kupitia vyanzo vyake mwenyewe, kutoka kwa Abdullah ibn Abbas, ambaye amesema kwamba, siku moja alikuwa amekaa na baba yake, Abbas mbele ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wakati Ali alipoingia hapo na kumsalimia. Mtume akasimama, akamchukua mikononi mwake, akambusu katikati ya macho yake na akamfanya akae upande wake wa kulia. Kisha Abbas akamuuliza Mtume kama anampenda Ali. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akajibu, Ewe ami yangu mheshimika! Wallahi, Allah anampenda zaidi kuliko ninavyompenda mimi.

HADITH YA BENDERA KATIKA USHINDI WA KHAIBAR.


Uthibitisho wenye nguvu wa Ali kupendwa na Allah, na wa ushujaa wake katika uwanja wa vita, ni Hadith-e-Rayat (Hadith ya Bendera) ambayo ni sehemu ya mkusanyiko wenu wa Hadith. Hakuna hata mmoja wa Maulamaa wenu mashuhuri aliyeikataa. Nawab: Ni nini Hadith-e-Rayat? Tafadhali kama ikiwezekana inukuu pamoja na vyanzo vyake. Muombezi: Maulamaa na wanahistoria mashuhuri wa madhehebu hizi mbili (Shia na Sunni) wamesimulia Hadith-e-Rayat. Kwa mfano, Muhammad Bin Ismail Bukhari katika Sahih yake Jz. 2 Kitabul-Jihad Was-Siyar, Sura Duaun-Nabi, vilevile katika Jz. 3 Kitabul-Maghazi, Sura ya Ghazawa-e-Khaibar. Muslim Bin Hajjaj katika Sahih yake, Jz. 2, uk. 324; Imam Abdur-Rahman Nisai katika Khasaisul-Alawi Tirmidh katika Sunan yake; Ibn Hajar Asqalani katika Isaba, Jz. 2, uk. 508; Muhaddith-e-Sham katika Tarikh; Ahmad bin Hanbal katika Musnad; Ibn Maja Qazwini katika Sunan yake; Sheikh Sulayman Balkh Hanafi katika Yanabiul-Mawadda Sura ya 6; Sibt Ibn Jauzi katika Tadhkira; Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafii katika Matalibus-Suul; Hafidh Abu Nuaim Isfani katika Hilyatul-Auliya; Abu Qasim Tibran katika Ausat na Abu Qasim Husain bin Muhammad (Raghib Isfahani) katika Muhadhiratul-Uda-ba Jz. 2, uk. 212. Kwa ufupi, kwa hakika karibu wanahistoria wenu wote na Muhadathina wame-

152

Mikesha ya Peshawar
andika hadith hii, hivyo kwamba Hakim anasema: Hadith hii imefikia hatua ya makubaliano ya pamoja. Tabrini anasema: Ushindi wa Ali katika Khaibar unathibitishwa na umoja wake. Wakati jeshi la Waislamu lilipoizingira ngome ya Khaibar, lilishindwa mara tatu chini ya uongozi wa Abu Bakr na Umar, na wakakimbia. Masahaba walivunjika moyo sana. Ili kuwatia moyo masahaba Mtume alitamka kwamba Khaibar itatekwa. Alisema: Kwa jina la Allah, kesho nitampa bendera mtu ambaye atarudi na ushindi. Ni mtu ambaye hushambulia kwa kurudia rudia na kamwe haondoki kwenye uwanja wa mapambano na kamwe harudi nyuma mpaka apate ushindi. Yeye anampenda Allah na Mtume Wake, na Allah na Mtume Wake, wanampenda yeye. Usiku ule masahaba hawakuweza kulala, wakifikiria ni nani angepewa upendeleo huu maalum. Asubuhi, kila mmoja alivaa nguo za kijeshi na wakajitokeza mbele ya Mtume. Mtume akauliza: Yuko wapi ndugu yangu na mtoto wa ami yangu, Ali Bin Abu Talib? Walimwambia: Ewe Mtume wa Allah, yeye anaumwa na macho sana kiasi kwamba hawezi hata kusogea. Mtume akamtuma Salman amuite Ali. Salman akamshika Ali mkono akampeleka kwa Mtume. Alimsalimia Mtume na baada ya kumrudishia salaam, Mtume akamuuliza, una hali gani Ewe Abul-Hasan? Akajibu, Yote ni kheri kwa baraka za Allah. Naumwa kichwa na maumivu makali katika macho kiasi kwamba siwezi kuona chochote. Mtume alimuomba aje karibu. Wakati Ali aliposogea karibu, Mtume aliweka mate ya kinywa chake mwenyewe kwenye macho ya Ali na akamuombea. Punde tu macho yake yakawa meupe na maumivu yake yakatoweka kabisa. Akampa Ali bendera ya ushindi. Ali alielekea kwenye ngome za Khaibar, akapigana dhidi ya Mayahudi, akauwa wanajeshi wao mashujaa kama vile Marhab, Harith, Hisham na Alqama, na akazishinda ngome za Khaibar zilizokuwa hazishindiki. Ibn Sabbagh Malik katika Fusulul-Muhimma uk. 21, amenukuu taarifa hii kutoka vitabu sita vya hadith, ambapo Muhammad bin Yusufu Ganji Shafii katika Kifayatul-Talib Sura ya 14, baada ya kuisimulia hadithi hii anasema kwamba mtunga mashairi mkuu wa Mtume, Hassan bin Thabit, alikuwepo wakati wa tukio hili. Alitunga mashairi kumsifu Ali: Ali alikuwa akiumwa macho. Kwa sababu kulikuwa hakuna tabibu, Mtume alimtibia kwa mate yake mwenyewe. Hivyo wote muuguzi na mgonjwa walibarikiwa. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: Leo nitampa Bendera mpanda farasi aliye hodari mno, shujaa na muungwana, mwenzi wangu katika mapambano. Anampenda Allah na Allah anampenda; hivyo kupitia kwake Yeye Allah atatufanya tuzishinde ngome. Baada ya hili, akiwaacha wote pembeni, alimchagua Ali na akamfanya mrithi wake. Ibn Sabbagh Maliki anasimulia kutoka Sahih Muslim kwamba Umar bin Khattab amesema: Kamwe sijatamani kuishika bendera lakini siku ile nilikuwa na hamu kubwa nayo.

153

Mikesha ya Peshawar
Nilirudia rudia kujifanya nionekane mbele ya Mtume, nikitamani kwamba huenda pengine akaniita na kwamba nikaweza kubarikiwa heshima hii. Lakini alikuwa ni Ali ambaye aliitwa na Mtume na utukufu ukaenda kwake. Sibt Ibn Jauzi ameandika riwaya hii katika kitabu chake Tadhkira, uk. 15, na Imam Abdur-Rahman Ahmad Bin Ali Nisai katika Khasaisul-Alawi, baada ya kusimulia hadithi kumi na mbili juu ya habari ya Ali kushika bendera kule Khaibar, ananukuu riwaya hiyo katika hadith ya kumi na nane kuhusu matumaini ya Umar kuipata bendera. Vilevile Jalalud-Din Suyuti katika kitabu chake Tarikhul-Khulafa, Ibn Hajar Makki, katika Sawaiq na Ibn Shirwaini katika kitabu chake Firdausul-Akbar anasimulia kwamba Umar Bin Khattab amesema: Ali amejaaliwa mambo matatu na kama ningelikuwa na moja tu ningelipendelea kuliko ngamia wote walioko katika miliki yangu:Ndoa ya Ali na Fatima; kukaa kwake msikitini katika hali yoyote na hii haikuruhusiwa kwa yeyote isipokuwa Ali, na kushika kwake bendera katika vita vya Khaibar. Hoja yangu, kutegemea juu ya riwaya za Muhadithina wenu, inathibitisha kwamba maneno katika Aya - Yeye (Allah) anawapenda na wao vilevile wanampenda Yeye yanahumhusu Ali. Muhammad Bin Yusufu Ganji Shafii katika Kifayatut-Talib, Sura ya 13, anasimulia kwamba Mtume amesema: Kama mtu anataka kumtazama Adam, Nuh na Ibrahim, na amtazame Ali. Anasema kwamba, Ali ndiye yule anayesemwa na Allah katika Qurani Tukufu: Na wale ambao wako pamoja naye ni wakali dhidi ya makafiri, (na) wenye kuhurumiana wenyewe kwa wenyewe. (48:29). Ama kwa kauli yako kwamba kifungu cha maneno katika aya hii kuhurumiana wenyewe kwa wenyewe kinamhusu Uthman na huonyesha nafasi yake kama Khalifa wa tatu, hii haiungwi mkono na ushahidi wa kihistoria. Kwa kweli, tabia yake ilikuwa ni kinyume chake kabisa. Kuna hoja nyingi zenye kuthibitisha jambo hili, lakini nitasimama hapa. Mambo ambayo yangesemwa yanaweza kuchochea uhasama. Hafidh: Kama utaishia kwenye rejea sahihi tu, hakuna sababu kwa nini tuchukizwe. Muombezi: Nitataja tu baadhi ya hizo.

TABIA YA UTHMAN NA NAMNA YA MAISHA IKILINGANISHWA NA ILE YA ABU BAKR NA UMAR.


Ibn Khaldun, Ibn Khallikan, Ibn Asam Kufi (imeandikwa vilevile katika Siha-e-Sitta), Masud katika Murujudh-Dhahab Jz. 1, uk. 435, Ibn Hadid katika Sharhe NahjulBalagha Jz. 1, na wengine katika Maulamaa wenu wanathibitisha kwamba wakati Uthman Bin Affan alipokuwa Khalifa, alikkwenda kinyume na mifano iliyowekwa na Mtukufu

154

Mikesha ya Peshawar
Mtume (s.a.w.w.) na vilevile dhidi ya mwendo wa Abu Bakr na Umar. Madhehebu zote zinakubaliana kwamba katika Kamati ya Ushauri (Shura) ambayo kwayo alichaguliwa kuwa Khalifa, Abdur-Rahman Bin Auf alimlisha kiapo cha kutegemea juu ya kitabu cha Allah, Suna ya Mtume, na mwendo wa Abu Bakr na Umar. Moja ya masharti ya kiapo chake ilikuwa kwamba Uthman hatawaacha Bani Umayya kuingilia (mambo ya uongozi) wala hangewapa mamlaka yoyote. Lakini nafasi yake (ya uongozi) ilipoimarika aliyavunja masharti haya. Kwa mujibu wa Qurani Tukufu na hadith za kuaminika, kuvunja makubaliano (Mkataba) ni dhambi kubwa. Maulamaa wenu wenyewe wanasema kwamba Khalifa Uthman alivunja ahadi yake. Katika Ukhalifa wake wote alitenda kinyume na mwendo wa Abu Bakr na Umar. Aliwapa Bani Ummaya Mamlaka kamili juu ya maisha ya watu na mali zao.

UTAJIRI WA KHALIFA UTHMAN.


Hafidh: Ni katika njia gani alitenda dhidi ya mafunzo na matendo ya Mtume na mwendo wa Abu Bakr na Umar? Muombezi: Muhadith mashuhuri, Masud katika kitabu chake Murujudh-Dhahab Jz. 1, uk. 433, na wanahistoria wengine wameandika kwamba Uthman alijenga nyumba ya kipekee ya mawe yenye milango iliyotengenezwa kwa mti wa msandali. Alijikusanyia utajiri mkubwa, ambao aliutoa kiufujaji kwa Bani Umayya na wengine. Kwa mfano kodi ya kidini (Khums) kutoka Armania, ambayo ilitekwa katika kipindi chake ilitolewa kwa mlaaniwa Marwan bila idhini yoyote ya kidini. Vile vile alimpa dirham 100,000 kutoka Baitul-mal (hazina ya Umma). Alimpa Abdullah Bin Khalid dirham 400,000, dirham 100,000 kwa Hakam Bin Abil-Aas, ambaye alilaaniwa na kuhamishwa na Mtume, na dirham 200,000 kwa Abu Sufyani (kama ilivyoandikwa na Ibn Abil-Hadid katika Sherhe Nahjul-Balagha., Jz. 1, uk. 68). Katika siku aliyouawa, mali yake binafsi ilifikia dinari 150,000 na dirham milioni 20 taslimu. Alimiliki mali huko Wadiul-Qura na Hunain yenye thamani ya dinari 100,000 na kundi kubwa la ngombe, kondoo na ngamia. Kama matokeo ya matendo yake, Bani Umayya walio mbele walilimbikiza utajiri mkubwa utokanao na juhudi za watu. Kwa Khalifa wa Uislam kujikusanyia utajiri kama huo wakati watu wengi wanateseka kwa njaa kwa hakika ilikuwa ni kosa. Aidha tabia hii ilikuwa inapingana kabisa na mwenendo wa masahaba wenzake, Abu Bakr na Umar. Uthman aliahidi katika Kamati ya Ushauri (Shura) kwamba angefuata nyayo zao. Masud katika kitabu chake Murujudh-Dhahab anasema kuhusu Khalifa Uthman kwamba, wakati Khalifa Umar alipokwenda na mwanae Abdullah kuhiji, matumizi yao katika safari yao ya kwenda na kurudi yalikuwa dinari 16.

155

Mikesha ya Peshawar
Alimwambia mwanae kwamba wamekuwa wafujaji. Kama utalinganisha mwendo wa ulaji mdogo wa Umar na matumizi ya kifujaji ya Uthman, utakubali kwamba mwendo wa maisha ya Uthman ulikuwa kinyume na kiapo chake katika ile Kamati ya Ushauri.

KHALIFA UTHUMAN ALIWAPA MOYO WATENDA MAOVU MIONGONI MWA BANI UMAYYA.
Uthmani vilevile aliwapa Bani Umayya mamlaka juu ya maisha na heshima za watu. Hatimaye, machafuko yalijitokeza katika ardhi za Waislamu. Aliwachagua watu wake anao wapendelea katika nafasi za juu kinyume na matakwa ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Abu Bakr na Umar. Kwa mfano alimpa nafasi za juu ami yake, Hakam Bin Aas, mtoto wake, Marwan ambao wote walihamishwa na kulaaniwa na Mtume. Hafidh: Unaweza ukathibitisha kwamba walilaaniwa? Muombezi: Kuna njia mbili za kuthibitisha kwamba walilaaniwa. Allah aliwaita Bani Umayya Mti uliolaaniwa katika Qurani Tukufu (17:60). Imam Fakhurud-Din Razi, Tabari, Qartabi, Nishapuri, Suyuti, Shawkani, Alusi, Ibn Abi Hatim, Khatib Baghdad, Ibn Mardawaih, Hakim, Maqrizi, Baihaqi na wengine katika maulamaa wenu wanasimulia kutoka Ibn Abbas kwamba Mti uliolaaniwa katika Quan unahusu kabila la Umayya. Katika ndoto, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliona nyani wakipanda na kushuka katika mimbari yake (na kufukuza watu kutoka Msikitini). Alipoamka, Malaika Jibril akateremsha Aya hii na kumueleza Mtume kwamba nyani wale walikuwa Bani Umayya, ambao watanyanganya Ukhalifa wake baada yake. Sehemu yake ya kusalia na mimbari vitabakia katika mamlaka yao kwa miezi elfu. Imam Fakhnid-Din Razi anasimulia kutoka Ibn Abbas kwamba Mtume alitaja jina la Hakam Bin Aas. Kwa hiyo amelaaniwa kwa vile anatokana na Mti uliolaaniwa. Kuna Hadith nyingi kutoka vyanzo vya Sunni kuhusu kulaaniwa kwao. Hakim Nishapuri, katika Mustadrak Jz. 4, Uk. 437 na Ibn Hajar Makki katika Sawaiq-e-Muhriqa, ananukuu kutoka kwa Hakim hadith ifuatayo kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Hakika muda mfupi tu familiya yangu itatawanyishwa na kuuawa na Umma wangu. Bani Umayya, Bani Mughira, na Bani Makhzum ni makatili zaidi katika maadui zetu. Mtume Akasema kuhusu Marwan, akiwa mtoto wakati huo, Huyu ni mjusi, mtoto wa mjusi, mwenye kulaaniwa, mtoto wa aliyelaaniwa. Ibn Hajar anaelezea kutoka kwa Umar bin Murratul-Jihni, Halabi katika SiratulHalabiyya, Jz. 1, uk. 337; Baladhuri katika Ansab, Jz. 5, uk. 126; Sulayman Balkhi katika Yanabiul-Mawadda; Hakim katika Mustadrak, Jz. 4, uk. 481; Damiri katika Hayatul-Haiwan, J. 2, uk. 291; Ibn Asakir katika kitabu chake cha Tarikh; Imamul-

156

Mikesha ya Peshawar
Haram Muhyid-Din Tabari katika Dhakhairul-Uqba na wengine wamesimulia kutoka kwa Umar bin Murratul-Jihni kwamba Hakam Bin Aas alitaka mazungumzo na Mtume. Mtume alipoitambua sauti yake, akasema: Muacheni aingie ndani. Laana iwe juu yake na juu ya kizazi chake, isipokuwa wale ambao wanaamini, na watakuwa wachache. Imam Fakhrid-Din Razi, katika kitabu chake Tafsir-e-Kabir, Jz. 5, akiandika kuhusu Aya ya Mti uliolaaniwa....... na namna yake, anarejea kwenye kauli ya Aisha ambaye alisema kumuambia Marwan: Allah alimlaani baba yako wakati upo kwenye mbegu zake za uzazi; hivyo na wewe vilevile ni sehemu yake yule ambaye amelaaniwa na Allah. Allama Masud, anasema katika kitabu chake Murujudh-Dhahab, Jz. 1, uk. 435, kwamba Marwan bin Hakam alilaaniwa na kuhamishwa na Mtume. Alihamishwa kutoka Madina. Hakuruhusiwa kuingia Madina wakati wa Ukhalifa wa Abu Bakr na Umar, lakini Uthman alipokuwa Khalifa, alitenda kinyume cha mafundisho ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Abu Bakr, na Umar na akamruhusu kuingia Madina. Alimuweka karibu sana naye mwenyewe pamoja na Bani Umayya wote na akawafanyia upendeleo. Nawab: Hakam Bin Abil-Aas alikuwa ni nani, na kwanini alihamishwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)? Muombezi: Hakam Bin Aas alikuwa ni ami yake Khalifa Uthman. Kwa mujibu wa Tabari, Ibn Athir, na Baladhuri, ambaye anaandika katika Ansab, Jz. 5, uk. 17, yeye alikuwa ni jirani yake Mtume Zama za Jahiliyya. Alimtukana Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), hususan baada ya tangazo lake la Utume. Alitembea nyuma ya Mtume na kumdhihaki kwa kumuigiza miondoko ya utembeaji wake. Hata wakati wa Sala, alikuwa akimyooshea kidole kwa dharau. Baada ya kulaaniwa na Mtume, alibakia katika hali ya kupooza wakati wote na hatimaye akapoteza hali ya utimamu akili. Baada ya kutekwa Makka, alikuja Madina na inavyoonekana aliingia Uislamu, lakini mara kwa mara alimtukana Mtume. Wakati alipokwenda nyumbani kwa Mtume, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mara moja alitoka nje ya nyumba yake na akasema Mtu yeyote asiombe msamaha kwa niaba yake. Sasa yeye na watoto wake, Marwan na wengine wanapaswa waondoke Madina. Kwa hiyo, mara moja Waislamu wakamtoa na kumfukuzia Taif. Wakati wa kipindi cha Abu Bakr na Umar, Uthman alimsaidia, akisema kwamba alikuwa ni ami yake na kwamba inapaswa aruhusiwe kurudi Madina. Lakini hawa wengine hawakulikubali shauri hili, wakisema kwamba kwa vile alilaaniwa na kuhamishwa na Mtume hawatamruhusu kurudi. Wakati Uthman alipokuwa Khalifa, aliwarudisha wote. Ingawa watu wengi walilipinga shauri hili; Uthman alionyesha upendeleo maalum kwa jamaa zake na wengine anaowapenda. Alimfanya Marwan kuwa msaidizi wake na Afisa Mkuu wa Baraza lake. Alijikusanyia karibu yake waovu wengi wa kabila la Umayya na akawateua kushika nafasi za juu (katika serikali). Matokea yake ni kwamba, kwa mujibu wa utabiri wa Umar, wao

157

Mikesha ya Peshawar
ndio walihusika na janga lililompata Uthman. Miongoni mwa watu walioteuliwa na Uthman alikuwa Walid bin Aqaba bin Abi Muith ambaye alipelekwa Kufa kuwa Gavana. Kwa mujibu wa riwaya ya Masud katika Murujudh-Dhahab, Jz. 1, Mtume alisema kuhusu Walid: Hakika yeye ni mmoja wa wale watakaokwenda motoni. Alijitumbukiza waziwazi kabisa katika matendo maovu. Kwa mujibu wa maelezo ya Masud katika MurujudhDhahab, Abdul-Fida katika Tarikh yake, Suyuti katika Tarikhul-Khulafa, uk. 104, Abul-Faraj katika Aghani Jz. 4, uk. 128, Imam Ahmad bin Hanbal katika Musnad, Jz. 1, uk. 42 Yaqubi katika Tarikh yake Jz. 2, uk. 142; Ibn Athir vilevile katika UsudulUqba, Jz. 5, uk. 91 na wengine walisema kwamba, wakati wa ugavana wake huko Kufa, Walid alipitisha usiku mzima akifanya ufuska. Alikuja msikitini kwa ajili ya Sala ya Alfajiri akiwa amelewa na akasalisha rakaa nne za Sala ya asubuhi (badala ya mbili) kisha akawageukia watu na kusema Uzuri ulioje wa asubuhi hii! Ningetaka kuendeleza Sala hii kama mutaridhia. Baadhi wanasema kwamba alitapika kwenye kibla ya msikiti kitendo ambacho kilileta maudhi makubwa kwa watu ambao walilalamika kwa Khalifa Uthman. Mmoja wa watu hawa wanaojulikana sana ni Muawiya, ambaye alifanywa kuwa Gavana wa Syria. Walid aliondolewa na badala yake akateuliwa Said Bin Aas kama Gavana wa Kufa. Wakati watu walizipogundua sera za Uthman, sera zilizo kinyume na mafunzo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), walighadhibika. Walichukuwa hatua ambazo hatimae zilisabisha matokeo yake mabaya kama hayo. Uthman alihusika na kifo chake mwenyewe kwa sababu hakufikiria athari za matendo yake. Alipuuza ushauri wa Ali na akawa amepotezwa na wadanganyifu wenye kujipendekeza. Ibn Abil-Hadid ananukuu mazungumzo kati ya Umar na Ibn Abbas katika Sherhe ya Nahjul-Balagha, Jz. 3, uk. 106. Khalifa Umar alisema kitu kuhusu kila mmoja wa wajumbe sita wa Kamati ya Ushauri na akaonyesha udhaifu wao. Wakati jina la Uthmani lilipotajwa, baada ya kushusha pumzi mara tatu, Umar akasema kwamba, Kama Ukhalifa utamfikia Uthman atawaweka watoto wa Abi Muit (Bani Umayya) juu ya watu. Kisha Waarabu watasimama na kuasi dhidi yake na kumuua. Ibn Abil-Hadid anakubaliana na uchambuzi wa Umar. Wakati Uthman alipokuwa Khalifa aliwakusanya karibu yake Bani Umayya. Aliwateuwa kuwa magavana na wakati walipoyachezea vibaya mamlaka yao, alifumba macho. Khalifa Uthman hakutaka hata kujinasua mwenyewe kutokana na Marwan. Watu wakichemka kwa kutoridhika, waliasi dhidi yake na mwishowe wakamuua.

158

Mikesha ya Peshawar

MTUKUFU MTUME (S.A.W.W.) ALIWALAANI ABU SUFYAN, MUAWIYA NA MTOTO WAKE YAZID.
Itasaidia sana kama utasoma kitabu maarufu cha Historia cha Jarir Tabari, mmoja wa maulamaa wenu wakubwa, ambaye ameandika: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuona Abu Sufyani akiwa amepanda punda. Muawiya alikuwa anaivuta kwa mbele, na mtoto wake Yazid, alikuwa anaisukuma kwa nyuma. Mtume akasema: Laana iwe juu ya mpandaji, mvutaji na msukumaji. Maulamaa wenu mashuhuri, kama Tabari na Ibn Asam Kufi wamemuona Khalifa Uthman kuwa ni mwenye makosa kwa kutomuua Abu Sufyan wakati alipoukana Uislamu, Wahyi (ufunuo), na kuwepo kwa Jibril. Baada ya kumkemea Abu Sufyan kidogo, Uthman akalitupa kando suala hili. Nitawaomba vilevile muangalie Khutba ya 163 ya Nahjul-Balagha na simulizi ambayo Ibn Abil-Hadid katika Sherhe yake ya Nahjul-Balagha Jz. 2, (iliyochapishwa Misr) uk. 582, ananukuu kutoka Tarrikh-e-Kabir, ya Tabari kwamba baadhi ya masahaba katika majimbo mbalimbali waliandika barua wakishawishi watu kutangaza vita vya Jihad, ili kujilinda kutokana na uonevu wa kikatili wa Uthman. Katika mwaka 34 A.H. watu wenye malalamiko dhidi ya maofisa walioteuliwa na Uthman walikuja Madina kwa Ali na wakamuomba aingilie kati.

UTHMAN HAKUKUBALI USHAURI WA ALI.


Ali alikwenda kwa Uthman na akamuonya kuhusu matokeo ya kutisha ya kuendelea na sera zake hizo. Ali alisema, Nakuambia kwa ajili ya Allah, usije ukajifanya wewe mwenyewe kuwa ni kiongozi wa umma huu aliyeuawa. Imesemekana kwamba kiongozi mmoja wa umma huu atauwawa, ambapo baada yake milango ya umwagaji damu na mauaji itabakia wazi mpaka Siku ya Kufufuliwa. Lakini Marwan na masahaba wa kiBani Umayya walipuuza ushauri wa Ali. Baada ya Ali kuondoka, Uthman aliamuru watu kukusanyika Msikitini. Alikwenda kwenye mimbari na badala ya kuwatuliza watu, aliwachokoza zaidi. Matokeo yakawa kama Khalifa Umar alivyotabiri. Uthman akauawa na waasi. Tofauti na Abu Bakr na Umar ambao walifuata ushauri wa Ali, Uthman alipuuza onyo lake na matokeo yake yakampata yaliyompata.

UTHMAN ALIWAPIGA MASAHABA WA MTUKUFU MTUME (S.A.W.W.) BILA HURUMA


Aidha, Uthman aliwapiga Masahaba ambao walipinga uonevu wake. Miongoni mwao alikuwa ni Abdulla Bin Masud, ambaye alikuwa Hafidhi, Qari (msomaji Qurani) Mtunza Hazina ya Umma, Mwaandishi ambaye aliandika Aya zilizoteremshwa, na mmoja wa masahaba wakubwa wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Aliheshimiwa sana na Abu Bakr na Umar, ambao wote walichukuwa ushauri kutoka kwake. Ibn Khaldun katika Tarikh yake

159

Mikesha ya Peshawar
ameeleza kwamba, Khalifa Umar alisisitiza kwamba Abdullah abakie naye kwa sababu alikuwa na elimu kamili ya Qurani Tukufu na kwa sababu Mtume alimsifia sana. Ibn Abil-Hadid na wengine wameandika jambo hilo hilo. Maulamaa wenu wanakubali kwamba wakati Uthman alipokusudia kukusanya Qurani Tukufu, alichukuwa nakala zote kutoka kwa waandishi. Alidai vilevile nakala ya Qurani Tukufu kutoka kwa Abdullah bin Masud. Abdullah hakumpa nakala yake hiyo. Uthman alikwenda mwenyewe nyumbani kwake na akaichukuwa hiyo nakala ya Qurani Tukufu kutoka kwake kwa nguvu. Baadae wakati Abdullah alipogudua kwamba, kama ilivyofanywa kwa nakala nyingine za Qurani Tukufu, na nakala yake pia imechomwa moto, alihuzunika mno. Katika mikusanyiko ya kijamii na kidini alisimulia hadith za shutuma ambazo alizijua kuhusu Uthman. Wakati habari hizi zilipomfikia Uthman, aliamrisha watumwa wake, wakampiga sana kiasi kwamba meno yake yalivunjika na alibakia kitandani. Baada ya siku tatu alikufa kwa majeraha yake. Ibn Abil-Hadid anaandika kwa kina kuhusu ukweli huu kutoka Jz. 1, uk. 67 na 226 wa Sharh Nahjul-Balagha (iliyochapishwa Misir) chini ya Tan VI na akaendelea kusema kwamba Uthman alikwenda kumuangalia Abdullah aliyekuwa anaumwa. Walizungumza pamoja kwa muda. Uthman akasema, Ewe Abdur-Rahman! Niombee msamaha kwa Allah. Abdullah akasema, Namuomba Allah achukue haki yangu kutoka kwako. (yaani haki ifanyike). Wakati Abu Dharr, sahaba wa karibu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), alipohamishiwa Rabza, Abdullah alikwenda kumuaga. Kwa sababu hii, Abdullah alipigwa viboko arubaini. Hivyo Abdullah akamsisitizia Ammar Yasir kwamba Uthman asikubaliwe kumsalia Abdulla Sala ya jeneza. Ammar Yasir alikubali, na baada ya kifo cha Abdullah, alisali Sala ya jeneza pamoja na kikundi cha masahaba. Uthman alipogundua mpango huu wa mazishi, alikuja kwenye kaburi la Abdullah na akamuuliza Ammar kwanini alisali Sala ya jeneza. Akajibu kwamba alilazimika kufanya hivyo kwa sababu Abdullah aliusia hivyo.

AMMAR ALIPIGWA KWA AMRI YA UTHMAN.


Mfano mwingine wa ukatili wa Uthman ulikuwa ni kumpiga kwake Ammar Yasir. Maulamaa wa madhehebu zote wanasimulia kwamba wakati uonevu wa Bani Umayya ulipozidi, baadhi ya masahaba wa Mtume walimuandikia Uthman, wakimtaka awe na huruma. Walisema kwamba, kama ataendelea kuwasaidia magavana wake hao makatili wa ki-Bani Umayya hatakuwa anaudhuru Uislamu tu, bali yeye mwenyewe pia atajitia katika matokeo mabaya sana. Walimtaka Ammar Yasir kufikisha kwa Uthman ile barua ya malalamiko kwa vile Uthman mwenyewe alikubali uadilifu wa Ammar. Walikuwa wamemsikia Uthman mara kwa mara akisema kwamba, Mtume amesema kwamba imani ilikuwa imechanganyika na nyama na damu ya Ammar. Hivyo Ammar aliichukua barua ile na kuipeleka kwa Uthman. Wakati alipowasili, Uthman alimuuliza, Je, una shughuli na mimi? Akajibu , Sina shughuli ya namna ya kibinafsi. Bali kikundi cha masahaba wa Mtume wameandika katika barua hii mapendekezo fulani na ushauri kwa ajili ya ustawi

160

Mikesha ya Peshawar
wako. Wameyatuma kwako kupitia kwangu. Baada ya kusoma misitari michache, Uthman akaitupa ile barua chini. Ammar akasema: Ilikuwa sio vizuri kwako wewe kufanya hivyo. Barua kutoka kwa masahaba wa Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.) inastahiki heshima. Kwa nini umeitupa chini? Ingelikuwa vizuri kwako wewe kuisoma na kuijibu. Unaongopa Uthman alisema kwa sauti kali. Kisha akaamuru watumwa wake kumpiga, na Uthman mwenyewe akampiga teke la tumbo. Alianguka chini, akazimia; jamaa zake wakaja wakamchukua, wakampeleka kwenye nyumba ya Ummul-MuMinin Umm Salma (mmoja wa wake za Mtume). Kuanzia adhuhuri mpaka usiku wa manane alikuwa bado amezimia. Makabila ya Hudhail na Bani Makhzun waligeuka dhidi ya Uthman kwa sababu ya ukatili wake kwa Abdullah Bin Masud na Ammar Yasir. Uthman alikuwa katili vilevile kwa Jandab Bin Junada, anayejulikana kama Abu Dhar Ghifari, mmoja wa masahaba karibu mno wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na mtu mwenye elimu. Muhadithina wakubwa na wanahistoria wa madhehebu zote wamesimulia kwamba mzee huyu wa miaka tisini alihamishwa isivyo halali kutoka sehemu hii kwenda sehemu nyingine kwa fedheha kubwa - kutoka Madina kwenda Syria, kutoka Syria kwenda Madina tena, kisha kutoka Madina kwenda kwenye Jangwa la Rabza. Alipanda ngamia asiye na matandiko akifuatana na binti yake tu. Alikufa katika (jangwa) la Rabza katika hali ya umasikini na ya kutelekezwa. sMaulamaa na wanahistoria wenu wakubwa, pamoja na Ibn Sad katika Tabaqat, Jz. 4, uk. 168, Bukhari katika Sahih yake, mlango wa Kitab-e-Zaka; Ibn Abil-Hadid katika Sherhe yake ya Nahjul-Balagha, Jz. 1, uk. 240 na Jz. 2, uk. 375 87, Yaqubi katika kitabu chake cha Tarikh Jz. 2, uk. 148; Abul-Hasan Ali Bin Husain Masud, muhadithina na mwanahistoria mashuhuri wa Karne ya Nne katika kitabu chake MurujudhDhahab, 1, uk. 438; na wengine wengi wamesimulia ukatili wa Uthman. Imeelezwa kwa mapana jinsi gani alivyomfanyia ubaya Abu Dharr mtu mwenye moyo safi, mtu aliyependwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na vilevile jinsi gani Abdullah Bin Masud, Hafidh na mwandishi wa Wahyi, alivyopigwa viboko arobaini kwa sababu alikwenda kumuaga Abu Dharr Ghifari. Hali ya ufidhuli wa aina hiyo hiyo ulionyeshwa kwa Ali kwa sababu hizo hizo. Hafidh: Kama Abu Dharr alipatishwa mateso, ni kwa sababu ya maofisa wakorofi. Khalifa Uthman, ambaye alikuwa mpole sana na mwenye moyo laini, alikuwa hana habari na matukio haya. Muombezi: Utetezi wako kwa Khalifa Uthman ni kinyume na ukweli. Mateso aliyopata Abu Dharr ilikuwa ni kwa ajili ya amri za wazi za Uthman mwenyewe. Kuthibitisha ukweli huu, anachohitaji mtu ni kurejea kwa Maulamaa wenu tu. Kwa mfano unaweza

161

Mikesha ya Peshawar
ukaangalia Nihaya kitabu cha Ibn Athir, Jz.1, na kitabu chake, Tarikh-e-Yaqubi na hususan uk. 241 wa Jz. 1, ya Sharhe Nahjul-Balagha cha Ibn Abil-Hadid. Wanachuoni hawa wameinakili barua ya Uthman iendayo kwa Muawiyya. Wakati Muawiyya alipopeleka taarida yenye uovu dhidi ya Abu Dharr kutoka Syria, Uthman alimuandikia hivi: Mlete Jundab (Abu Dharr) kwangu juu ya ngamia asiye na matandiko, peke yake, na mtu katili atakayemswaga ngamia huyo mchana na usiku. Wakati alipofika Madina, miguu yake Abu Dharr ilikuwa imechubuka na kutoa damu. Na bado Maulamaa wenu wamesimulia hadith isemayo kwamba Abu Dharr alitajwa makhususi kabisa na Mtume kama mtu ambaye kila mwanadamu lazima ampende. Hafidh Abu Nuaim Isfahani katika Hilyatul-Auliya, Jz. 1, uk. 172; Ibn Maja Qazwini katika Sunan yake Jz. 1, uk. 66; Sheikh Sulayman Balkhi Shafii katika YanabiulMawadda, Sura ya 59, akisimulia hadithi ya tano kati ya hadith arobaini zilizoandikwa katika Sawaiq-Muhriqa na Ibn Hajar Makki kama sahihi, zikiwa zimechukuliwa kutoka kwa Tirmidhi na Hakim, kama ilivyosimuliwa na Buraida, na yeye kutoka kwa baba yake; Ibn Hajar Asqalani katika Isaba, Jz. 3, uk. 455; Tirmidh katika Sahihi yake, Jz. 2, uk. 213; Ibn Abdil-Birr katika Istiab, Jz. 2, uk. 557; Hakim katika Mustadrak, Jz. 3 uk. 130; na Suyuti, katika Jamus-Saghir wamesimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: Allah ameniamrisha mimi kuwapenda watu wanne; na amenijulisha kwamba Yeye pia anawapenda. Watu wakasema Ewe Mtume wa Allah tueleze majina yao. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema Ni Ali, Abu Dharr, Miqdad, na Salman. Je, haki itaruhusu kwamba watu kama hao wapendwao na Allah kutendewa ukatili hivyo na kuyaita matendo hayo kuwa ni huruma? Hafidh: Historia imesimulia kwamba Abu Dharr alikuwa mtu mvurugaji. Aliendesha propaganda kali huko Syria yenye kumpendelea Ali, akawatanabahisha watu wa Syria juu ya cheo cha Ali, na akasema kwamba alikuwa amemsikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema kwamba Ali alikuwa ndiye mrithi wake. Kwa sababu aliwaita wengine wanyanganyi na akasema kwamba Ali alikuwa Khalifa wa haki aliyeteuliwa na Allah, Khalifa Uthman, ili kulinda umoja na kuepusha matatizo, alilazimika kumuita kutoka Syria (arudi Madina). Kama mtu anajaribu kusababisha fitna miongoni mwa watu, ni jukumu la Khalifa kumuondoa kutoka sehemu hiyo. Muombezi: Kama mtu anasema kweli, ni haki kumhamisha na kumtesa kwa sababu anafanya hivyo? Je, Uislamu unaturuhusu kumlazimisha mtu mzee kupanda ngamia aliyekonda, asiye na matandiko, ikiswagwa kwa nguvu na mtumwa mwenye harara, bila kusimama kwa ajili ya kupumzika, hivyo kwamba anawasili mashukio yake akiwa amechubuka na kuvuja damu? Je, hii inaonyesha upole na moyo wa wema? Mbali na hilo kama Uthman alitaka kudumisha umoja na kuepusha matatizo kwa nini asiwaondoe Bani Umayya wahalifu, kama Marwan, ambaye alilaaniwa na kuhamishwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Walid mpotovu na fuska wa dhahiri (afanyaye maovu bila kuficha) ambaye alisalisha akiwa amelewa na ambaye alitapika kwenye kibla ya msikiti? Kwa nini asi-

162

Mikesha ya Peshawar
waondoe wanasiasa madhalimu kutoka kwenye serikali yake, watu ambao wamewaonea watu, ambao mwishowe wakaasi na kumuuwa Uthman. Hafidh: Unawezaje kusema kwamba Abu Dharr alisema kweli? Unajuaje kwamba aliyosema yako katika misingi ya elimu iliyo sawa na kwamba hakubuni hadithi kwa jina la Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)? Muombezi: Tunasema hivyo kwa sababu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe alithibitisha ukweli wa Abu Dharr. Maulamaa wenu wenyewe wameandika kwamba Mtume alisema: Abu Dharr miongoni mwa watu wangu ni kama Isa miongoni mwa Bani Israil katika ukweli, utii na Ucha Mungu. Muhammad Bin Sad mmoja wa Maulamaa wa cheo cha juu na muhadithina wa madhehebu yenu, ndani ya Tabaqat, Jz. 4, uk. 167168; Ibn Abdul-Birr katika Istiab, Jz. 1, Sura ya Jundab, uk. 84; Tirmidh katika Sahih yake Jz. 2, uk. 221; Hakim katika Mustadrak, Jz. 3, uk. 342; Ibn Hajar katika Isaba Jz. 3, uk. 662; Muttaqi Hindi katika Kanzul-Ummal, Jz. 6, uk. 169; Imam Ahmad Bin Hanbal katika Musnad Jz. 2 uk.163 na 175; Ibn Abil-Hadid katika Sherhe NahjulBalagha Jz. 1, uk. 241; kutoka kwa Mahidi; Hafidh Abu Nuaim Isfahani katika Hilyatul-Auliya na mwandishi wa Lisanul-Arab, juu ya vyanzo mbali mbali vya kutegemewa wamesimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: Ardhi haikuzaa wala mbingu haikufunika mtu muaminifu zaidi kuliko Abu Dharr. Kama Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anathibitisha uaminifu wa mtu, tunaweza kuwa na uhakika kwamba mtu yule alisema kweli. Wala Allah hamuiti mtu mpenzi wake, yule ambaye ni muongo. Kama kungalikuwa na mfano mdogo tu wa Abu Dharr kusema uwongo, Maulamaa wa mwanzo wa madhehebu yenu wangeuandika kama walivyoandika kuhusu Abu Huraira na wengine. Mtume alithibitisha uaminifu wake na vilevile akatabiri mateso yake. Hafidh Abu Nuaim Isfahani katika Hilyatul Auliya, Jz. 1 uk. 162, anasimulia kutoka vyanzo vyake mwenyewe kwamba Abu Dharr alisema kwamba alikuwa amesimama mbele ya Mtume wakati alipomuambia: Wewe ni mcha-Mungu, mara tu baada yangu utapatwa na shida. Nikauliza: Katika njia ya Allah? Akasema: Ndio, katika njia ya Allah! Nikasema: naikaribisha (naikubali) amri ya Allah! Hakika shida aliyopata sahaba mtukufu Abu Dharr katika jangwa kwa amri ya Muawiyya, Uthman na jamaa zao Bani Umayya ilikuwa ni shida ile ile aliyotabiri Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

HADITH: MASAHABA WOTE NI KAMA NYOTA INAMHUSU NA ABU DHARR VILEVILE.


Kwa kweli nashangaa kauli zako zenye kupingana zenyewe. Kwa upande mmoja unasimulia hadith kutoka kwa Mtume kwamba, Masahaba wangu wote ni kama nyota, kama mkimfuata yeyote miongoni mwao mtaokolewa. Kwa upande mwingine, wakati mmoja wa Masahaba watukufu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anateswa na kufa katika

163

Mikesha ya Peshawar
huzuni, wewe unamtetea mkosaji! Yakupasa ama upuuze maelezo ya maulamaa wenu, au ukubali sifa zilizotajwa katika aya iliyo katika mjadala kwamba hazihusiani na wale waliowatesa masahaba watukufu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Hafidh: Abu Dharr alichagua kwenda Rebza kwa hiari yake mwenyewe. Muombezi: Maelezo kama hayo yanaakisi majaribio ya maulamaa wenu mashabiki kuficha matendo mabaya ya viongozi wao. Kuhamishwa Abu Dharr kwa nguvu kwenda Rabza kunajulikana wazi sana. Kama mfano, nitaishia kunukuu riwaya moja, ambayo imesimuliwa na Imam Ahmad Bin Hanbal katika Musnad Jz. 5, uk. 156, Ibn Abil-Hadid katika Sharhe Nahjul-Balagha Jz. 1, uk. 241, na Waqid katika kitabu chake cha Tarikh kutoka kwa Abul-Aswad Duili. Abu Dharr aliulizwa kuhusu Safari yake ya Rabza. Abu Dharr akasema kwamba, alihamishwa kwa nguvu na kupelekwa kuishi porini. Akaendelea: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alinijulisha kuhusu hili. Siku moja nililala Msikitini. Mtume akaja na akaniuliza kwa nini nimelala msikitini. Nikasema kwamba usinginzi umenipitia tu. Akaniuliza nitafanya nini kama nitahamishwa kutoka Madina. Nikasema ningekwenda kwenye nchi takatifu ya Syria. Akaniuliza nitafanya nini kama nitahamishwa huko pia. Nikasema nitarudi msikitini. Aliniuliza tena ningefanya nini kama ningefukuzwa kutoka hapa pia. Nikasema: Nitachomoa upanga na kupigana. Aliniuliza kama ningependa aniambie kitu ambacho kingekuwa kwa manufaa kwangu. Niliposema Ndio yeye akaniambia: Nenda sehemu yoyote watakayokupeleka! Hivyo nikasikiliza alivyoniambia na nikamtii. Baada ya hivi Abu Dharr akasema, kwa Jina la Allah, wakati Uthman atakapokwenda mbele ya Allah atasimama akiwa ni mwenye dhambi kuhusiana na suala langu.

UPOLE NA UKARIMU WA ALI BIN ABU TALIB:


Kama utayachunguza mambo kwa akili huru iliyo wazi, utakubali kwamba Ali alikuwanazo sifa za huruma na upole kwa kiwango cha hali ya juu sana. Wanahistoria wote, pamoja na Ibn Abil-Hadid, wameeleza kwamba wakati Ali alipochukua Ukhalifa, aliondoa mambo mabaya na mazushi ambayo yaliingizwa ndani (ya Uislamu). Aliwaondoa maofisa wasiomjua Mungu wa Ki-Bani Umayya, ambao waliyakandamiza majimbo wakati wa kipindi cha Ukhalifa wa Uthman. Wanasiasa wachoyo walimshauri aahirishe uamuzi wake huo wa kuwondoa maofisa hao mpaka Ali atakapojiimarisha zaidi katika mamlaka. Mtukufu Imam akasema: Naapa kwa Jina la Allah kwamba sitaruhusu hila za kijanja kama hizo. Mnasisitiza kwamba nitumie njia za upatanisho, lakini hamjui kwamba jinsi wanavyoendelea kubakia katika mamlaka wakiniwakilisha mimi, wataendelea kutenda mabaya yale yale ya kidhalimu na ukatili ambao nitawajibika kwenye Mahakama ya haki ya Mungu. Siwezi kuruhusu udhalimu huu.

164

Mikesha ya Peshawar

Uondoaji wa maofisa uliofanywa na Ali ulipelekea uhasama kwa watu wenye uchu wa madaraka, kama Muawiyya, na wakaitayarisha njia ya vita vya Jamal na Siffin. Kama Talha na Zubair wangechaguliwa kama magavana, wasingelichochea ghasia kule Basra na kuacha vita vya Jamal kutokea. Upole na ukarimu wake ulienea sawasawa kwa marafiki na maadui. Uthman alikuwa katili sana kwake (zaidi kuliko alivyokuwa Abu Bakr na Umar), lakini waasi walipolazimisha kizuizi kwenye Ikulu ya Uthman, wakizuia maji na chakula, aliomba msaada kwa Ali. Ali aliwatuma watoto wake, Hasan na Husein, wakiwa na mikate na maji. Ibn Abil-Hadid anaelezea tukio hili kwa kina katika Sharhe NahjulBalagha. Khalifa Uthman alikuwa na sifa ya kutoa Sadaka na kusaidia wengine, lakini ilikuwa kwa jamaa zake tu, kama Abu Sufyani, Hakam Bin Abil-As na Murwan Bin Hakam. Aliwamwagia pesa na zawadi kutoka hazina ya Umma bila kibali cha kidini. Lakini Amirul-Muminina Ali kamwe hakutoa zaidi ya kilichostahiki, hata kwa jamaa zake wa karibu. Kaka yake mkubwa, Aqil, alikuja kwake na kutaka pesa zaidi kuliko kawaida ya alivyokuwa akipewa. Ali hakusikiliza ombi lake. Aqil alisisitiza na akasema kwamba kwa vile Ali alikuwa Khalifa na alikuwa na mamlaka kamiki juu ya mambo inapasa haja zake zitekelezwe. Kama onyo kwa kaka yake, Ali akapasha moto kipande cha chuma kwa siri na akakiweka karibu na mwili wa Aqil. Alipiga kelele kama mtu aliye katika maumivu makali, akiogopa kuwa ataungua. Ali akasema: Wacha waombolezaji waomboleze kifo chako, ewe Aqil! Ulinywea wakati chuma kilichopashwa moto na mwanadamu kiliposogazwa karibu yako, na bado unanisogeza mimi kunielekeza kwenye moto ambao Allah ameumba kwa ghadhabu yake. Je, ni sawa wewe utafute hifadhi kutokana na maumivu haya ya kawaida, na kwamba mimi nisijihifadhi mwenyewe na Moto wa Jehanamu?

UPOLE WA ALI KWA MARWAN NA ABDULLAH BIN ZUBAIR:


Hata baada ya kuwashinda maadui zake, Ali bado alikuwa mpole kwao. Mlaaniwa Marwan, mtoto wa mlaaniwa Hakum alikuwa ni adui muovu wa Ali. Lakini Ali alipomshinda Marwan katika vita ya Jamal, alimsamehe. Abdullah Bin Zubair alikuwa ni adui mwingine muovu. Alimtukana Ali wazi wazi, na Abdullah aliposoma Khutuba yake kule Basra mbele za watu, alisema: Hakika Ali Bin Abu Talib ni fisadi, duni, na bahili. (Allah atuepushie mbali). Lakini Mtukufu Imam aliposhinda vita vya Jamal na mtu huyu muovu alipoletwa kama mateka mbele yake, Ali hakusema hata neno kali dhidi yake. Ali alimgeuzia kando uso wake na akamsamehe.

165

Mikesha ya Peshawar

UPOLE WA ALI KWA AISHA


Mfano mzuri wa huruma ya Ali ulikuwa ni mwenendo wake kwa Aisha. Jinsi alivyokuja uso kwa uso kupigana naye na kumshutumu kungemkasirisha mtu duni. Lakini Ali alipomshinda, alimshughulikia kwa heshima. Alimpa Muhammad bin Abu Bakr, kaka yake Aisha, jukumu la kuangalia ustawi wake. Kwa maagizo yake, wanawake ishirini wenye nguvu waliovaa kama wanaume walimsindikiza Aisha mpaka Madina. Alipofika Madina, alielezea shukurani zake kwa wanawake hao na wake za Mtume. Alisema kwamba siku zote atabakia mwenye shukurani kwake. Alikiri kwamba, ingawa alikuwa katili kwake na alikuwa amehusika na ghasia kiasi hicho, hakusema neno lolote baya dhidi yake. Alisema alikuwa na lalamiko moja tu dhidi yake. Alishangaa kwa nini alimsafirisha kwenda Madina huku akisindikizwa na wanaume. Wanawake wale vijakazi mara moja walivua mavazi yao ya kiume. Ikajulikana wazi kwamba mpango huu ulifanywa kwa madhumuni ya kulinda mali zao kutokana na majambazi. Mfano mwingine wa huruma za Ali ni jinsi alivyomshughulikia Muawiyah katika vita vya Siffin. Jeshi la askari 12,000 la Muawiyah liliufunga mto wa Euphrate. Wakati jeshi la Ali lilipoona kwamba njia waliyokuwa wanaitegemea ya kupatia maji ilikuwa imeshikwa, Ali alituma ujumbe kwa Muawiyah akisema kwamba Muawiyah hapaswi kufunga njia ya kufikia maji. Muawiyah alijibu kwamba atawanyima kutumia maji. Ali akamtuma Malik Ashtar na kikosi cha askari. Alisukuma nyuma jeshi la Muawiyah na kuifungua njia ya kuufikia mto Euphrate. Masahaba wakasema: Ewe Ali! Na sisi tulipize na tuwanyime maji, ili kwamba maadui wafe kwa kiu na vita vitakuwa vimekwisha. Ali akasema: Hapana! Kwa jina la Allah, sitalipiza kwa kufuata mfano wao. Waacheni askari wao wapate njia ya kufikia mto Euphrate. Maulamaa wenu wenyewe, kama Tabari katika kitabu chake Tarikh, Ibn Abil-Hadid katika Sharhe Nahjul-Blagha, Suleimani Balkhi katika Yanabiul-Mawadda, Sura ya 15, Masudi katika Murjudh-Dhahab, na wanahistoria wengine wameandika kwa urefu kuhusu uugwana wa Ali. Unaweza ukachunguza maelezo haya na kisha ukaamua ni nani anayeelekea kulengwa na aya hii: Na wakahurumiana wenyewe kwa wenyewe Katika aya iliyoko kwenye mjadala, Muhammad, Mtume wa Allah, ndiye mlengwa na kinacho fuatilia ni arifu yake. Sifa zote zile ni kwa ajili ya mtu huyo huyo. Kuwa pamoja na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kuwa mkali dhidi ya makafiri katika medani ya vita na katika mijadala ya kielimu, kuwa na huruma kwa marafiki na maadui sifa zote hizi hurejea kwa mtu ambaye kamwe hajamuacha Mtume au hata kufikiria kumuacha. Mtu huyo ni Ali Bin Abi Talib. Nilikwisha sema mapema kwamba, mwanachuo mkubwa, Muhammad bin Yusuf Ganji Shafii ameandika katika kitabu chake Kifayatut-Talib kwamba katika aya hii Allah anamsifia Ali.

166

Mikesha ya Peshawar
Sheikh: Kuna majibu mengi kwa maelezo yako, lakini umetafsri tu visivyo aya hii. Usemi na wale ambao wako pamoja naye ni wa wingi na hauwezi kuonyesha mtu mmoja tu. Kama sifa zilizotajwa katika aya zinamuonyesha mtu mmoja tu, kwanini vijina vikawa kwa wingi? Muombezi: Kwanza, unasema kwamba kuna majibu mengi kwa maelezo yangu. Kama hiyo ilikuwa kweli, basi kwa nini usiyataje? Kunyamaza kwako ni uthibitisho kwamba hakuna mjibu mengi kwa maelezo yangu. Pili, ulichosema hivi punde tu ni hoja potofu. Unajua kwamba katika luhga zote ikiwemo Kiarabu utumiaji wa wingi kwa ajili ya mmoja ni kitu cha kawaida kama dalili ya heshima. Kuna mifano mingi ya utumiaji huu katika Qurani Tukufu kama aya hii: Hakika walii wenu ni Allah na Mtume wake na walio amini ambao husimamisha Salat na hutoa zaka na huku wamerukuu. (5:55) Inakubaliwa na wote kwamba aya hii imeshuka kwa ajili ya Ali. Wafasiri na muhadithina, kam vile Imamu Fakhrud-Din Razi katika Tafsir Kabir, juzuu ya 3, uk. 431; Imamu Abu Ishaq Thalabi katika kitabu chake Kashfu l-Bayan; Jarullah Zamakhshari katika Tafsir Kashshaf, juzuu ya 1, uk. 422; Tabari katika Tafsir yake, juzuu 6, uk. 186; Abul-Hasan Rammani katika Tafsir yake; Ibn Hawazin Nishapuri katika Tafsir yake; Ibn Sadun Qartabi katika Tafsir yake, juzuu ya 6, uk. 221; Nasafi Hafiz katika Tafsir yake, uk.496 (kwa njia ya ufafanuzi kwenye Tafsir ya Khazin Bahgdadi); Fazil Nishapuri katika GharibulQurani, juzuu ya 1, uk.461; Abul-Hasan Wahidi katika Asbabun-Nuzul, uk. 148; Hafiz Jassas katika Tafsir Ahkamul-Qurani, uk. 542; Hafiz Abu Bakr Shirazi katika Fima Nazala Minal-Qurani Fi Amirul-muminin; Abu Yusuf Abdus-Salam Qazwini katika Tafsir Kabir; Kadhi Baidhawi katika Anwart-Tanzil, juzuu ya 1, uk. 345; Jalalud-Din Suyiti katika Durrl-Mansur, juzuu ya 2, uk. 239; Kadhi Shukani Sanai katika Tafsir Fathul-Qadir; Sayyid Muhammad Alusi katika Tafsir yake, juzuu ya 2, uk. 329; Hafiz Ibn Abi Shaiba Kufi katika Tafsir yake; Abul-Baraka katika Tafsir yake, juzuu ya 1, uk. 496; Hafiz Baghawi katika katika Maalimut-Tanzil; Imamu Abu Abdur-Rahman Nisai katika Sahih yake. Muhammad bin Talha Shafii katika Matalibus-Suul, uk. 31; Ibn Abil-Hadid katika Sharhe Nahjul-Balagha, juzuu ya 3, uk. 375; Khazin Alaud-Din Baghdadi katika Tafsir yake, juzuu ya 1, uk. 496; Suleimani Hanafi katika Yanabiul-Mawadda, uk. 212; Hafiz Abu Bakr Baihaqi katika Kitab Musnnaf; Razin Abdari katika JamBainusSiha Sitta; Ibn Asakir Damishiq katika Tarikh Sham; Sibt Ibn Jauzi katika Tadhkira, uk. 9; Kadhi Azudaili katika Mawaqif; uk.276; Sayyid Sharif Jurjani katika Sharhe Mawaqif; Ibn Sabbagh Malik katika Fusul-Muhimma, uk. 123; Hafiz Abu Sad Samani katika Fadhails-Sahaba; Abu Jafar Askafi katika Nagzil-Uthmaniyya; Tibrani katika Ausat; Ibn Maghazili Faqih Shafii katika Manaqib; Muhammad bin Yusuf Ganji Shafii katika Kifayatut-Talib; Mulla Ali Qushachi katika Sharhe Tajrid; Sayyid Muhammad Mumin Shablanji katika Nurul-Absar, uk. 77; Muhibud-Din Tabari katika Riyazun-Nuzra, juzuu ya 2, uk. 247, halikadhalika na wengine wengi

167

Mikesha ya Peshawar
miongoni mwa wanachuoni wenu maarufu, wote wamesimesimulia kutoka kwa Said, Mujahid Hasan Basri, Amash, Atba Bin Hakim, Ghalib Ibn Abdullah, Qais Bin Rabia, Abaya Bin Rabi , Abdullah Ibn Abbas, Abu Dharr Ghifari, Jabir Ibn Abdullah Ansari, Ammar, Abu Rafi, na Abdullah Bin Salam, na wengine wanakiri kwamba aya hii iliteremshwa katika kumsifia Ali. Aya hii inaashiria kwenye wakati ambao Ali alitoa pete yake kumpa muombaji wakati akiwa kwenye rukuu. Hapa vile vile maneno yapo katika wingi kwa staha na heshima juu ya cheo cha Wilaya (walii), na kuthibitisha kwamba Ali alikuwa Imamu na mrithi wa Mtume (s.a.a.w.). Msisitizo wa neno Innama, hutoa maana ya uamuzi wa Allah wa mwisho na uliopangwa, yaani, uamuzi wa Allah kwamba Walii wa waumini lazima awe ni Allah, Mtume Wake (Muhammad), na waumini ambao hutoa sadaka huku wakiwa wanasali, huyu wa mwisho akiashiriwa bayana kuwa ni Ali. Sheihk: Hakika utakubali kwamba tafsiri yako haikuthubutu kwa vile kuna maoni tofauti kuhusu hilo. Baadhi wanasema huashiria kwa Ansar, baadhi wanasema ni katika kumsifia Ibadat Bin Samit, na baadhi wanasema kwamba inaashiria kwa Abdullah Bin Salam. Muombezi: Kwa hakika inashangaza kwamba mwanachuo kama wewe unaweza kupingana na ulamaa wako mwenyewe. Unachukua maoni ya wajinga wachache na wasioaminika ambao riwaya zao zinakataliwa. Wanachuoni wenu wakubwa kwa pamoja wametamka kwa dhati kuthibitisha juu ya nukta hii, watu kama Fazil Taftazani na Mulla Ali Qushachi, ambaye anasema katika kitabu chake, Sharhe Tajrid: Kwa mujibu wa maoni ya pamoja ya wafasiri, aya hii iliteremshwa katika kumsifia Ali, ambaye wakati akiwa kwenye rukuu katika Sala, alitoa pete yake kumpa muombaji.

MASHAKA NA UTATA KUHUSU AYA YA WALII NA UFAFANUZI WAKE


Sheikh: Katika mlolongo wa mazungumzo yako kuhusiana na aya hii, umejaribu kuthibisha kwamba Ali alikuwa ndiye mrithi wa mara moja wa Mtume (s.a.w.w.), ingawa neno Wali katika aya hii lina maana ya rafiki au mwenye kupendwa sana, na sio Imamu au Mrithi. Kama maoni yako ni yenye kukubalika kwamba Wali maana yake ni mrithi na Imamu, basi kwa mujibu wa kanuni iliyokubaliwa, haikomei kwa mtu mmoja, bali wengine wanakuwemo pia, Ali akiwa mmoja mionmgoni mwao. Vile vile katika aya, Hakika walii wenu ni Allah, na Mtume Wake, na wale ambao wameamini utumiaji wa (sarufi) wingi huonyesha watu kwa ujumla. Kusema kwamba muundo wa wengi ni kuonyesha heshima, haina maana bila hoja yenye nguvu, mfano wa ki-Qurani, au chanzo kingine.

168

Mikesha ya Peshawar
Muombezi: Umeulewa vibaya msemo Walii wenu Wali ni (sarufi ya) umoja, kum (wenu) ni wingi ambao huashiria kwa watu na haioneshi umoja. Naam hakika, Wali ni kwa ajili ya mtu ambaye ni mlezi kwa jamii nzima katika zama zote. Pili, katika aya ambayo iko kwenye mjadala, pale ambapo wingi umetumika, baadhi ya mashabiki wamesema kwamba haiwezi kutafsiriwa kama umoja kama katika aya wale ambao wanasimamisha Sala pingamizi hili nililijibu mapema. Nilisema kwamba, waandishi wakubwa mara nyingi wametumia umoja kumaanisha wingi. Vile vile umedai kwamba muundo wa (sarufi ya) umoja katika aya hii huashiria watu kwa ujumla. Tunasema kwamba, kwa mujibu wa msisitizo wa neno hakika, anayeashiriwa ni Ali, lakini hatukusema kwamba kuhusika huko ni kwa aina ya pekee tu kwake. Wengine kutoka nyumba ya Mtume wanakuwemo pia. Kwa mujibu wa hadithi zilizo sahihi, Maimamu wote wa kizazi cha Mtume wamejumuishwa katika aya hii. Jarullah Zamakhshari anaandika katika Kashshaf kwamba aya hii iliteremshwa makhususi katika kumsifia Ali, lakini ule wingi uliotumika ndani yake, unamaanisha kwamba wengine lazima wamfuate. Sheikh: Katika aya hii neno Wali haswa lina maana ya msaidizi. Kama lingekuwa na maana ya mlezi ambayo hujumuisha na cheo cha mrithi, basi angeliteuliwa wakati wa uhai wa Mtume (s.a.w.w.). Muombezi: Cheo cha Ali ni cha kudumu. Ujengaji wa sentensi kisarufi na neno Wali uliotumika kama sifa, huthibitisha cheo cha kudumu cha Ali. Ukweli huu unaungwa mkono zaidi na Mtume kwa kumtangaza Ali kama makamu wake wakati wa safari ya Tabuk na kamwe hakulifuta tangazo hilo. Mtazamo wetu unaimarishwa zaidi na Hadith-eManzila (Hadithi ya cheo) ambayo Mtukufu Mtume amerudia mara nyingi kuisimulia: Ali kwangu mimi ni kama Harun alivyokuwa kwa Musa, ambayo nimeilezea katika mikesha iliyopita. Hii yenyewe ni uthibitisho mwingine kwa Ali wa kuwa kwake Walii au Makamu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wakati wa uhai wa Mtume na baada ya kufa kwake. Sheikh: Kama ingekuwa tulipe suala hili mazingatio yanayostahili, tungelikiri kwamba aya hii haimzungumzii Ali. Cheo chake ni kikubwa kuliko kile tunavyotaka kukithibitsha kutoka kwenye aya hii. Haithibitishi ubora wowote juu yake, bali hukiangusha chini cheo chake. Muombezi: Sio wewe wala mimi si yeyote katika Umma pamoja na wale masahaba wakubwa wa Mtume, ambaye ana haki yoyote ya kuingilia tafsiri halisi za aya hizi. Aya za Qurani hazikuteremshwa kwa mujibu wa matakwa yetu. Kama baadhi ya watu wakitafsiri maana zao kwa kuegemeza juu ya maoni yao au wakataja tukio au habari ambayo imeteremshiwa, basi kwa hakika hao sio watu wa dini. Kwa mfano, wafuasi wa Abu Bakr wanasema kwamba kwa mujibu wa hadithi iliyosimuliwa na mghushaji mkorofi Akrama, aya hii iliteremshwa kwa ajili ya Abu Bakr. Unaweza ukatueleza ni jinsi gani aya hii inavyoangusha cheo cha Ali?

169

Mikesha ya Peshawar
Sheikh: Moja ya tabia za murwa wa cheo cha Ali ni kwamba, wakati anaposali kamwe hageuzi hadhari yake kwenye kitu kingine. Wakati fulani Ali alijeruhiwa katika vita. Kiwembe cha mshale kilibakia mwilini, na ilikuwa haiwezikani kukiondoa bila kusababisha maumivu makali. Lakini aliposimama kwa ajili sala, kiwembe cha mshale kiliondolewa, na kwa sababu ya kuzama katika ibada yake kwa Allah, hakusikia maumivu. Kama wakati wa kusali alitoa pete yake kumpa muombaji, kulikuwa na dosari kubwa katika Sala yake. Itaezakana vipi mtu ambaye amezama katika rehema ya Allah na wakati huo huo andoe hadhari yake kutoka kwa Allah kwa ajili ya kuitikia sauti ya omba omba? Aidha, katika kutenda kila jambo jema na kutoa sadaka kuweka nia ni kitu cha lazima. Wakati wa kusali hadhari ya mtu lazima iwe imeelekea kwa Allah peke Yake. Inawezekana vipi kwamba nia yake imegeuka kutoka kwenye Sala na kugeuka kumuelekea kiumbe? Kwa vile tunakiona cheo cha Ali kuwa ni cha juu sana, hatukubali tafsiri yako. Na kama alitoa chochote kwa omba omba, basi kwa hakika haikuwa wakati wa Sala, kwa vile rukuu maana yake ni kunyenyekea mbele ya Allah. Muombezi: Umejifunza vizuri jinsi ya kusoma, lakini umeikosa njia ya kuendea kwenye maombi. Pingamizi hili ni dhaifu kuliko hata utando wa buibui. Kwanza, kitendo cha Ali kwa njia yoyote hakiangushi chini cheo chake. Kwa hakika kumsikiliza omba omba ili kumpa sadaka, ni chanzo cha ubora. Katika hali hii, alikusanya sala yake ya kimwili na ya kiroho pamoja na sala ya kiyakinifu. Sala zote zilikuwa katika njia ya Allah. Ndugu wapenzi! Uharibifu ambao unanyongesha Sala ni ule ambao unatokana na fikra binafsi. Kuzingatia sala nyingine, wakati ambapo unasali Sala mahususi, ni dalili ya ubora. Kwa mfano, kama wakati wa ibada ya Sala, mtu akalia kwa mapenzi makubwa ya jamaa zake, Sala yake itakuwa batili. Lakini kama akilia kwa mapenzi makubwa ya Allah, au kwa kumuogopa Yeye, basi hiyo ni dalili ya ubora. Umesema kurukuu maana yake ni kunyenyekea kwa unyofu kwa Allah. Maana hii inaweza ikatumika kwa matukio mengine. Lakini kama ukisema kwamba kurukuu katika Sala, ambako ni hakika na lazima, kunabeba maana hiyo hiyo ya kilugha, watu wasomi watakudharau. Vile vile umejaribu kuondoa au kupuuza maana ya wazi ya aya. Umeitolea maana ya kistiari, ingawa unajua kwamba neno hilo huelezea kitendo kinachohitajika cha ibada ya Sala, ambacho ni kuinama mpaka viganja kufikia magoti. Na ukweli huu umekubaliwa na maulamaa wenu wakubwa, kama nilivyoelezea mapema. Fadhil Qushachi, katika Sharhe Tjrid, anaelezea maoni ya wafasiri kwa ujumla kwamba Ali, wakati anarukuu katika Sala, alitoa pete yake kumpa omba omba. Tukiweka kila kitu pembeni, tafadhali tueleze iwapo aya hii ilitaremshwa kwa kusifu au kwa kulaumu? Sheikh: Ni wazi ilikuwa kwa kusifia. Muombezi: Hivyo wakati maulamaa wa madhehebu zote wamesema kwamba aya hii iliteremshwa kwa kumsifia Ali, na kwamba ina ridhaa ya Allah (swt), kwa nini ulete ukin-

170

Mikesha ya Peshawar
zani usio na maana, ukubaliane na Makhawariji washabiki, ambao maoni yao yamedukizwa kwenye akili yako safi tangu utotoni? Kwa nini hukubali ukweli huu? Sheikh: Samahani! Kwa vile wewe ni mzungumzaji fasaha, mara nyingi unatumia vidokezo na rejea ambazo zinaweza kujenga mawazo ambayo yanaweza kuleta matokeo yasiyofurahisha katika akili za watu ambao hawana elimu ya kutosha juu ya masuala haya. Ingekuwa vyema kama ungejizuia kutokana na lugha kama hizo. Muombezi: Katika mazungumzo yangu hakuna chochote ila ukweli. Allah awe shahidi wangu, kamwe sijakusudia kutumia madokezo au rejea zisizo za moja kwa moja. Hakuna haja ya kufanya hilo. Chochote ninachotaka kusema, nakisema kwa wazi. Tafadhali nieleze ni vidokezo gani unavyomaanisha. Sheikh: Muda mfupi uliopita wakati wa mazungumzo yako kuhusiana na aya iliyoko kwenye mjadala, ulisema kwamba sifa zilizotajwa ndani yake ni za kipekee kwa Ali Bin Abu Talib ambaye kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa uhai wake, kamwe hajawa na shaka katika imani yake. Kwa namna hii unaonesha kwamba wengine walikuwa na hatia ya ukana mungu. Je, wale makhalifa wakubwa au masahaba kuna yeyote aliyekuwa na shaka katika imani zao? Bila shaka hao masahaba, kama alivyokuwa Ali, kamwe hawajautilia shaka ukweli wa Uislamu. Hata mara moja hawajakengeuka katika mafindisho ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Muombezi: Kwanza, kamwe sijatumia maneno ambayo wewe umeyatumia sasa hivi. Pili, unaelewa kwamba kuthibitisha kitu kwa mtu fulani haina maana ya kutothibitisha kitu hicho kwa watu wengine. Tatu, ingawa unajaribu kunikosoa, nafikiri wengine hawana kitu kama hicho katika akili zao. Allah awe shahidi wangu, sikufanya rejea yoyote isiyo ya moja kwa moja kwa kitu chochote, wala sijafikiria kufanya hivyo. Na kama kitu chochote kilitokea kwenye akili yako, ungeweza kuniuliza kuhusu kitu hicho kwa faragha. Sheikh: Namna ya uzungumzaji wako huonyesha kwamba kuna nukta fulani ambazo unazinyamazia. Nakuomba utufahamishe kilichoko akilini mwako na kutupa rejea sahihi kwa unachosema. Muombezi: Ni wewe uliyejenga kitu hicho akilini mwetu; unasisitiza kwamba suala hili lijadiliwe. Nakuomba tena, liache suala hili na uache kusisitiza juu yake. Sheikh: Kama kulikuwa na kitu chochote cha usafihi, imekwisha. Sasa huna jinsi ila kujibu. Kama hutatoa jibu la wazi, ima la kukubali au kukataa, basi nitawajibika kuamua kwamba uliyoyasema yalikuwa hayana msingi wowote. Muombezi: Hakuna chochote cha usafihi katika maelezo yangu, lakini kwa vile unasisiti-

171

Mikesha ya Peshawar
za, sina jinsi isipokuwa kuufichua ukweli. Ulamaa wenu wakubwa wanakubali kwamba masahaba wa Mtume ambao imani yao ilikuwa bado haijakamilika, mara kwa mara walionyesha kuwa na mashaka. Baadhi yao walilea shaka hiyo na uasi wa kidini. Baadhi ya aya ziliteremshwa kwa ajili ya kuwalaumu. Kwa mfano, walikuwepo munafiqin (wanafiki) ambao katika kulaumiwa kwao Sura nzima ya Qurani Tukufu iliteremshwa. Lakini masuala kama hayo hayapaswi kujadiliwa waziwazi. Nakuomba tena ujizuiye kuindama nukta hii. Sheikh: Una maana kwamba wale makhalifa wakubwa walikuwa ni miongoni mwa wale waliokuwa na mashaka. Muombezi: Kama majibu yangu yatasababisha hisia mbaya miogoni mwa watu wasio na elimu, wewe ndiye utakayebeba lawama. Umesema sasa hivi, Useme hivi au umesema kwamba. Lakini tena, ni maulamaa wenu wenyewe ndio ambao wamesimulia mambo haya. Sheikh: Wameandika kuhusu suala gani, na ni katika tukio gani makhalifa wameonesha shaka yao, na ni watu gani ambao walitia shaka? Tafadhali tujulishe. Muombezi: Watu wengi walikuwa na shaka kubwa sana, lakini wakarudi kwenye imani yao ya asili. Baadhi yao wakangangania katika shaka zao. Ibn Maghazili Shafii, katika kitabu chake Manaqib, na Hafidh Abu Abdullah Muhammad Bin Abi Nasir Hamidi katika JamBainus-Sahihain-e-Bukhari, na Muslim wanaandika: Umar Bin Khattab alisema, Sijapata kuutilia mashaka utume wa Muhammad kama nilivyofanya siku ya Hudaibiyya. Maelezo haya yanaonyesha kwamba aliutilia shaka utume wa Muhammad zaidi ya mara moja. Nawab: Samahani. Ni tukio gani katika Hudaibiyya ambalo lilimfanya awe na shaka kuhusu Mtume? Muombezi: Mtume aliona usiku mmoja kwenye ndoto kwamba alikwenda Makka pamoja na mashaba zake kufanya Umra. Asubuhi yake, aliposimulia ndoto hii kwa masahaba zake, walimuomba aitafsiri ndoto hiyo. Mtume akasema, Mwenyezi Mungu akipenda tutakwenda Makka kuitekeleza ibada hii Inshaallah. Lakini hakuainisha ni wakati gani itafanyika. Akiwa na nia ya kuizuru Nyumba ya Allah, Mtume aliondoka na masahaba zake kuelekea Makka katika mwaka ule ule. Wakati walipofika Hudaibiyya (kisima kilicho karibu na Makka), Maquraishi walikuja pale na kuwazuia wasiendelee mbele. Kwa vile Mtume hakuenda kule akiwa amejiandaa kupigana, alijitolea kufanya amani nao. Mkataba ulisainiwa na Mtume akarudi Madina. Katika tukio hili, Umar alikuwa na mashaka. Alikwedna kwa Mtume na akasema: Je, wewe sio Mtume wa Allah na mtu mkweli? Je, wewe hukutuambia kwamba utakwenda Makka na kufanya Umra kisha unyoe kichwa

172

Mikesha ya Peshawar
chako na upunguza ndevu zako? Kwa nini sasa umeshindwa kufanya hivi? Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuuliza iwapo yeye aliweka muda kwa ajili ya hilo au kama aliwaambia kwamba atakwenda kule katika mwaka ule ule. Umar akakiri kwamba Mtume hakuainisha wakati. Mtume akasema kwamba alichowaambia ni sahihi, na Mungu akipenda watakwenda Makka siku zijazo na ndoto yake itatimizwa. Hakika wakati kwa ajili ya utekelezaji wa tafsiri ya ndoto, uwe mapema au baadae utetagemea juu ya utashi wa Allah (swt). Kisha kwa uthibitisho wa maelezo ya Mtume, Jibril alijitokeza na kuteremsha aya ifuatayo ya Qurn Tukufu: Hakika Allah amemtimizia Mtume Wake ndoto kwa haki. Bila shaka ninyi mtauingia Msikiti Mtukufu, insha-Allah kwa amani, na hali mmenyoa vichwa vyenu na (baadhi) mmepunguza nywele. Hamtakuwa na hofu. Yeye anajua msiyoyajua. Basi atakupeni kabla ya haya ushindi karibuni. 48:27. Ushindi hapa una maana ya ushindi wa Khaibar. Hii ilikuwa kwa ufupi tukio la Hudaibiyya ambalo kwa kweli lilikuwa ni mtihani kwa waumini na kwa watu wanaoyumba. Kufikia hapa ulifuatia mjadala wa iwapo tuendelee na mjadala au la, kwa ajili ya ratiba ya wageni wa ki-Sunni kutoka Afghanistan na halikadhalika na Muombezi, matokeo yake ambayo ilikuwa ni uamuzi wa kuendelea.

MKUTANO WA SABA JUMATANO USIKU 29 RAJAB, 1345 A.H.


Sayyid Abdul-Hayy (Imam wa Msikiti wa jamaa wa Sunni): Mikesha fulani iliyopita ulitoa maelezo fulani ambayo kwamba Hafidh Sahib alitaka uthibitisho, lakini kwa ujanja ulikwepa kujibu au ulifanya watu miogoni mwetu wachanganyikiwe, na suala lote likawa ni lenye kukera. Muombezi: Tafadhali nifahamishe ni lipi kati ya maswali yenu ambalo limeachwa bila kujibiwa, kwani sikumbuki ni suala gani unalolirejelea. Sayyid: Wewe hukusema katika baadhi ya mikesha iliyopita kwamba Ali alikuwa na umoja wa nafsi pamoja na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na hivyo alikuwa mbora wa cheo kwa mitume wote? Muombezi: Ni kweli. Hayo yalikuwa ni maelezo yangu, na ni katika imani yangu. Sayyid: Basi kwa nini hukujibu swali letu? Muombezi: Umekosea sana. Inashangaza kwamba umekuwa ukisikiliza kwa ukaribu majadiliano yetu, lakini bado sasa unanilaumu kwa kuchukuwa njia ya ujanja au

173

Mikesha ya Peshawar
kuchanganya akili zenu. Kama utaangalia kwa makini utaelewa kwamba sijasema kitu chochote cha kupotosha, lakini ma-Mulla hawa wasomi waliuliza maswali ambayo nililazimika kuyajibu. Sasa kama una swali lolote la kuuliza, unaweza kufanya hivyo, na kwa msaada wa Allah, nitalijibu. Sayyid: Tunataka kujua vipi inawezekanaje kwamba watu wawili wanaweza kuungana kiasi kwamba muungano wao unawafanya kuwa mtu mmoja na yule yule.

TOFAUTI KATI YA MUUNGANO WA KUWAZIKA NA MUUNGANO HALISI


Muombezi: Kwa hakika, haiwezikani kwa watu wawili kuunda muungano halisi. Wakati niliposema kwamba Amirul-Muminina Ali ana muungano wa nafsi pamja na Mtume, hupaswi kuuchukualia kama muungano halisi, kwa sababu kamwe hakuna mtu aliyedai hivyo, na kama mtu yeyote akiuamini atakuwa amekosea kabisa. Muungano nilioutaja ni wa kuwazika tu, sio halisi, na unakusudia kuonesha kwamba wote wawili wana ubora ule ule wa nafsi na muruwa, sio mwili huo mmoja. Hafidh: Basi kwa mujibu wa kauli hii wote lazima watakuwa ni mitume, na kutokana na usemavyo, wahayi lazima utakuwa umekuja kwa wote. Muombezi: Hiyo ni dhana potofu ya dhahiri. Hakuna Shia hata mmoja mwenye imani kama hiyo. Nisingetegemea wewe kujiingiza katika mazungumzo kama haya na kupoteza wakati wetu. Nimekuelezeeni tu kwamba wanahusiana katika masuala yote ya sifa na ubora, isipokuwa sifa zile ambazo kuziondoa kwake kuna amri au misingi makhususi. Jambo hilo la pekee ni utume na sifa zake zote zilizoambatanishwa nao - mojawapo ikiwa ni upokeaji wa wahayi, na kwa kupitia huo ni mawasilisho ya Maamrisho ya Mungu. Pengine umesahau maelezo yangu katika mikesha iliyopita, ambamo nilithibitisha kupitia Hadithi ya Cheo (Manzila) kwamba Ali alikuwa na cheo cha utume, lakini kwamba alifuata na alipasika kwenye dini na mafundisho yaliyofundishwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Cheo chake katika utume hakikuwa zaidi ya kile cha Harun wakati wa Musa. Hafidh: Lakini kama unaamini katika usawa wa Ali pamoja Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika mambo yote ya sifa na ubora, inafuatia kwamba lazima uamini usawa wake katika masuala ya utume na sifa zilizoambatanishwa nao. Muombezi: Inaweza kuelekea hivyo, lakini kama unafikiria kwa makini utaona kwamba sio hivyo. Kama nilivyothibibitisha mapema kutoka kwenye aya za Qurani, utume ni wa vyeo tofauti, na Manabii na Mitume wa Allah wanazidiana kati ya mmoja na mwingine katika ubora wa vyeo. Kama Qurani Tukufu inavyoeleza kwa uwazi: Mitume hao

174

Mikesha ya Peshawar
Tumewatukuza baadhi yao juu ya wengine (2:253). Na kikamilifu zaidi katika cheo kwa Mitume wote ni cheo maalumu cha Muhammad, kama Allah alivyosema: Muhammad sio baba wa yeyote katika wanaume wenu, bali ni Mtume wa Allah na mwisho wa Manabii, na Allah ni mjuzi wa kila kitu (33:40). Ni kwa ukamilifu huo wa utume ambao umepelekea kwenye ukomo wa utume. Hivyo katika sifa hii ya ukamilifu, hakuna mtu yeyote anayeweza kujumuishwa humo. Katika mambo mengine yote ya ubora, kuna ushirikiano na usawa, ambao kwamba kuna uthibitisho mwingi. Sayyid: Unaweza ukaleta hoja yoyote kutoka kwenye Quan kuthibitisha madai haya?

AYA YA MAAPIZANO (MUBAHILA) INATHIBITISHA UMOJA WA NAFSI YA ALI NA YA MTUKUFU MTUME (S.A.W.W.)
Muombezi: Hakika, hoja yetu ya kwanza ni kutoka Qurani Tukufu, ambayo ni ushahidi wa ki-Mungu wenye nguvu sana, yaani aya ya maapizano (Ayatul-Mubahila) ambayo kwayo Allah anasema:

Watakao kuhoji katika haya baada ya kukufikia elimu hii waambie: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wanawake zetu na wanawake zenu, na nafsi zetu na nafsi zenu, kisha tuombe kwa unyenyekevu tutake laana ya Allah iwashukie waongo. (3:61) Maulamaa wenu wakubwa, kama vile Imamu Fakhurud-Din Razi, Imamu Abu Ishaq Thalabi, Jalalud-Din Suyuti, Qadhi Baidhawi, Jarullah Zamakhshari, Muslim bin Hujjaj, na wengine wengi, wameandika kwamba aya hii tukufu iliteremshwa siku ya maapizano, ambayo ilikuwa mwezi 24 au 25 Dhul-Hijja katika mwaka wa 9 A.H. Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipowalingania Uislamu Wakristo wa Najran, wao waliwateua watu wao wenye elimu sana kama vile Seyyed, Aqib, Jasiq, Alqama na kadhalika, idadi yao ikiwa ni zaidi ya watu sabini na wakawatuma kwenda Madina pamoja na watu 300 kati ya wafuasi wao, ili kukutana na Mtukufu Mume na kujifunza Uislamu ulikuwa ni nini. Waliingia katika mjadala wa kielimu na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na walishangazwa na hoja zake nzito. Alithibitisha ukweli wa ujumbe wake kutoka kwenye vyanzo vyao vyenye kuaminika na akasema kwamba, Isa mwenyewe alitabiri kuwasili kwake (Muhammad) kwa ishara mbali mbali, na Wakristo walikuwa wanangojea kutimia kwa

175

Mikesha ya Peshawar
utabiri wa Isa ambao kwa mujibu wake, mtu huyo atatokea akiwa amepanda ngamia kutokea milima ya Faran (katika Makka) na atahamia kwenye sehemu iliyopo kati ya Ayr na Uhud (ambayo ilikuwa ni Madina). Hoja hzi ziliwavutia sana Wakristo, lakini mapenzi yao ya heshima za kidunia yaliwazuia kuukubali ukweli. Basi Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwaeleza amri ya Allah, ambayo walikubaliana nayo kama njia ya kumaliza mjadala na kwa ajili ya kubainisha kati ya wakweli na waongo.

KUWASILI KWA MTUKUFU MTUME (S.A.W.W.) KWA AJILI YA MAAPIZANO


Kwa mujibu wa makubaliano yao ya pamoja, siku iliyofuatia kundi lote la Wakristo, pamoja na wanachuoni wao zaidi ya sabini, walimngojea Mtume nje ya milango ya Madina. Walitegemea kwamba yeye angekuja kwa fahari na idadi kubwa ya wafuasi wake ili kuwahofisha. Lakini milango ilipofunguliwa, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alijitokeza akiwa na kijana wa kiume kuliani kwake, mwanamke mwenye heshima kushotoni kwake, na watoto wawili mbele yake. Walibakia chini ya mti, wakiwakabili Wakristo. Asqaf, mtu mwenye elimu zaidi mwiongoni mwa Wakristo, aliuliza hao ni watu gani ambao Muhammad ametoka nao. Alijulisha kwamba kijana wa kiume ni mkwe wake na binamu yake, Ali Bin Abi Talib, yule mwanamke ni binti yake, Fatima, na watoto wawili ni watoto wa binti yake, Hasan na Husein. Wakati akiwahutubia Wakristo, kiongozi wao, Asqaf, alisema: Tazameni, jinsi Muhammad anavyojiamini! Amekuja pamoja na jamaa zake wa karibu, watoto, na wapenzi wake, kwenye shindano hili la kiroho la kuapizana. Kwa jina Mungu, kama angelikuwa na shaka au hofu kuhusu msimamo wake, kamwe asingewachagua hawa. Sasa siwashauri kuingia kwenye mashindano dhidi yake. Lau si kuwa na hofu na Mfalme wa Rumi, tungeikubali imani ya Uislamu. Ingelifaa zaidi kukubaliana nao juu ya masharti yao na kurudi nyumbani. Wote walikabaliana naye. Kwa hiyo, Asqaf alituma ujumbe kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), akisema: Hatutaki kushindana na wewe, bali tunataka kufanya amani na wewe. Mtume alikubali mapendekezo yao. Mkataba uliandikwa na Amirul-Muminin, Ali Ibn Abi Talib. Wakristo walikubali kulipa kodi ya mwaka katika muundo wa daraya 2,000, kila moja ikiwa na thamani ya takriban dirham 40 (dirham moja ilikuwa sawa na wakia ya dhahabu), na mithqal 1000 za dhahabu (mithqal ilikuwa sawa na 1/6 wakia ya dhahabu). Nusu ya hii ilkubaliwa ilipwe mwezi wa Muharram na nusu nyingine katika mwezi wa Rajab. Baada ya mkataba kusainiwa na pande zote, Wakristo walirudi nyumbani kwao. Wakati wakiwa njiani, mmoja wa wanachuo wao aitwaye Aqib alisema kuwaambia masahaba zake: Kwa jina la Mungu,

176

Mikesha ya Peshawar
ninyi na mimi tunajua kwamba huyu Muhammad ni Mtume yule yule wa Mungu ambaye alikuwa akitazamiwa, na chochote anachosema kinatoka kwa Mungu. Naapa kwa jina la Mungu kwamba yeyote aliyeshindana na Mtume wa Mungu aliangamia, na hakuna katika vijana wao na wazee wao aliyebakia hai. Kwa hakika kama tungeshindana nao, wote sisi tungeliuawa na asingebakia hai Mkristo yeyote ulimwenguni. Kwa jina la Mungu, wakati nilipowaangalia niliziona nyuso ambazo kama zingemuomba Mungu, wangeweza kusogeza milima. Hafidh: Ulichosema ni kweli kabisa na kinakubaliwa na Waislamu wote, lakini hakina uhusiano na suala tunalojadili, yaani, kwamba Ali alikuwa ameungana kiroho na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

STAHILI YA ALI, FATIMA, HASAN NA HUSEIN INATHIBITISHWA NA AYA YA MAAPIZANO


Muombezi: Ninahoji kutokana na neno nafsi zetu katika aya hii tukufu, kwani kutokana na aya hii masuala mengi yanatatuliwa. Kwanza, njia ya haki iliyolinganiwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) imethibitishwa. Yaani, kama asingekuwa katika upande wa haki, asingethubutu kutoka kuja kwenye shindano wala wale Wakristo maarufu wasingelikimbia kutoka kwenye uwanja wa Mubahila. Pili, vile vile aya hii huthibitisha kwamba Hasan na Husein walikuwa ni watoto wa Mtume wa Allah (s.a.w.w.) kama nilivyokwishataja katika mazungumzo yangu katika usiku wa kwanza. Tatu, huthibitisha kwamba AmirulMuminin, Ali, Fatima, Hasan na Husein walikuwa kiroho ndio watu watukufu zaidi miongoni mwa viumbe wote, na wapenzi mno wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kwani hata wanachuoni washabiki na wapinzani wakubwa wa madhehebu yenu, kama Zamakhshari, Baidhawi, na Fakhrud-Din Razi, na wengine wameandika katika vitabu vyao. Hususani Jarullah Zamkhshari, akiandika kuhusu aya hii tukufu, anatoa maelezo yanayojitosheleza kuhusu kukusanyika kwa viumbe watano hawa na kusema kwamba, aya hii ni uthibitisho mkubwa wa ubora wa Ashab-i-Ayba, watu watano ambao walikusanyika chini ya blanketi pamoja na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Nne, inaonesha kwamba Amirul-Muminin, Ali aliwapita masahaba wengine wote kwa ubora na cheo, kwa sababu Allah amemuita katika aya hii tukufu kama nafsi ya Mtume. Ni dhahiri kwamba, maneno nafsi zetu hayamaanishi nafsi ya Mtume mwenyewe, kwa sababu kuita maana yake kumwita mtu mwingine; mtu kamwe haambiwi ajiite mwenyewe. Kwa hiyo, neno hili huelekeza kwa mtu mwingine ambaye ni kama nafsi ya Mtume mwenyewe. Na kwa vile, kwa mujibu wa maoni ya pamoja ya wafasiri wa kuaminika na muhadithina wa madhehebu zote, hakuna mwingine yeyote isipokuwa Ali, Fatima, Hasani

177

Mikesha ya Peshawar
na Husein ndio walikuwepo pamoja na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika maapizano, usemi katika aya hii tukufu, watoto wetu na watoto wenu, wanawake wetu na wanawake wenu huashiria Hasan na Husein na Fatima kwa mpangilio huo, na mtu mwingine angeweza kutambuliwa kama nafsi zetu katika kundi hili tukufu alikuwa ni Amirul-Muminin, Ali. Kwa hiyo, maneno haya nafsi zetu huthibitisha muungano wa nafsi kati ya Mtume Muhammad na Ali. Kwa vile mungano halisi wa nafsi mbili hauwezikani, Allah kumuita Ali nafsi ya Mtume Muhammad maana yake ni muungano wa kutwaliwa wa nafsi mbili. Unajua vizuri sana kwamba kimsingi ni bora kulitambua neno kwa dhana ya karibu kuliko na ile ya mbali, na dhana ya karibu sana maana yake kuhusiana katika fadhila zote isipokuwa zile ambazo zimeondolewa kwa sababu fulani. Na tayari tumekuambieni kwamba ni utume maalumu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na upewaji wa Wahyi juu yake, ambavyo ni vitu vya kipekee kwake tu. Kwa hiyo, hatumchukulii Ali kama mshirika wake kuhusiana na sifa hizi mbili. Lakini kwa mujibu wa aya hii tukufu, Ali anashirikiana pamoja na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika fadhila nyingine zote, na kwa uhakika Allah (swt) amemjaalia Ali kupitia kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa baraka Zake zote. Hii peke yake inathibitisha muungano wa nafsi zao, ambao tulitaka kuuthibitisha. Hafidh: Kwa nini unasisitiza kwamba aya hii haimaanishi kuita nafsi yake mwenyewe? Kwa nini dhana hii isiwe bora kuliko dhana nyingine? Muombezi: Ni matumaini yangu kwanba hutapoteza muda katika mazungumzo yasiyo na mantiki na kutoka nje ya njia ya uadilifu. Kwa kweli uadilifu huhitaji kwamba kama tumekubaliana juu ya nukta fulani, lazima tuendelee mbele. Sikutegemea mtu wa cheo chako na elimu yako kujiingiza katika mjadala bandia. Kama ujuavyo wewe mwenyewe na kwa mujibu wa wanachuoni wote, nafsi moja inafananishwa na nafsi nyingine kwa njia ya dhana. Miogoni mwa watu wasomi ni kawaida kudai muungano wa dhana, kama nilivyoeleza mwanzo. Mara kwa mara inaonekana kwamba mtu mmoja anamuambia mwingine: Wewe ni maisha yangu na nafsi yangu mwenyewe. Hususan katika lugha ya hadith na simulizi, uhusiano huu mara kwa mara umekuwa ukielezewa kuhusu Amirul-Muminin, Ali, na kila simulizi kama hiyo ikuchukuliwa kwa peke yake ni uthibitisho wa kuonesha ukweli wa msimamo wangu.

178

Mikesha ya Peshawar

SIMULIZI ZAIDI NA HADITH KAMA USHAHIDI WA UMOJA WA MSINGI WA MTUKUFU MTUME (S.A.W.W.) NA ALI
Imamu Ahmad bin Hanbal, katika Musnad yake, Ibn Maghazili, mwanachuoni wa kiShafii katika Manaqib yake, na Muwafiq Ibn Ahmad Khawarizmi katika Manaqib yake, wanasimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: Ali anatokana na mimi na mimi natokana na Ali; yeyote anayempenda yeye, amenipenda mimi; na ambaye ananipenda mimi, amempenda Allah. Vile vile Ibn Maja katika Sunan yake, sehemu ya 1, uk. 92; Tirmidhi katika Sahih yake; Ibn Hajar katika kitabu cha Hadithi cha 5 cha Hadithi Arobaini zinazohusu fadhaila za Amirul-Muminin zilizosimuliwa katika Sawaiq kutoka kwa Imamu Ahmad Bin Hanbal, Tirmidhi, Imamu Abu Abdur-Rahman Nisai, na Ibn Maja; Imamu Ahmad Bin Hanbal katika Musnad, juzuu ya 4, uk. 164; Muhamad Ibn Yusuf Ganji Shafii katika sura ya 67 ya Kifayatut-Talib kutoka Musnad ya Ibn Samak, juzuu ya 4, na Mujim Kabir cha Tibrani; na Imamu Abudur-Rahman Nisai katika Khasais, na Sulaiman Balkhi Hanafi katika Yanabiul-Mawadda kutoka kwenye Mishkat wote wamesimulia kutoka kwa Jash Bin Junada as-Saluni kwamba wakati wa hijja ya muago, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kule Arafa: Ali anatokana na mimi, na mimi natokana na Ali. Hakuna mtu anayenifidia mimi (yaani, hakuna awezaye kufanya kazi ya ujumbe wangu) isipokuwa mimi na Ali. Sulaimani Balkhi Hanafi katika Yanabiul-Mawaddat, sura ya 7, anasimulia kutoka Zawaid-e-Musnad cha Abdullah Bin Ahmad Bin Hanbal kutoka kwa Ibn Abbas kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kumuambia Ummul-Muminin Salma: Ali anatokana na mimi na mimi natokana na Ali. Nyama yake na damu yake inatokana na nyama yangu na damu yangu. Yuko kwangu mimi kama alivyokuwa Harun kwa Musa. Ewe Umm Salma! Sikiliza, na uwe shahidi kwamba huyu Ali ni bwana na mkuu wa Waislamu. Hamidi katika kitabu chake JamBainus-Sahihain na Ibn Abil-Hadid katika SharheNahjul-Balagha wanasimulia kwamba, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: Ali anatokana na mimi na mimi natokana na Ali. Ali kwangu mimi ni kama kichwa kilivyo kwa mwili; mtu anayemtii yeye, ananitii mimi; na mtu anayenitii mimi, anamtii Allah. Muhammad Bin Jarir Tabari katika Tafsir yake na Mir Sayyid Ali Hamdani, mwanachuoni wa ki-Shafii, katika Muwadda ya 8 cha Muwaddatul-Qurba, wanasimulia kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambaye alisema: Hakika Allah (swt) aliisaidia imani hii ya kiIslamu kupitia Ali, kwa vile yeye anatokana na mimi, na mimi natokana na yeye, na aya hii tukufu imeteremshwa kwa ajili yake. Basi je, yeye ni kama mtu ambaye ana dalili

179

Mikesha ya Peshawar
za wazi kutoka kwa Mola wake na kufuata ushahidi kutoka Kwake? (11:17) Sheikh Sulaimani Balkhi Hanafi ameainisha katika sura ya 17 ya kitabu chake YanbiulMawdda kuhusu suala hili hili chini ya maelezo mafupi: Kuhusu Ali kuwa kama nafsi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na hadithi kwamba Ali anatokana na mimi, na mimi natokana na Ali. Katika sura hii amesimulia hadithi 24 katika njia tofauti na kwa maneno tofauti kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ambaye alisema Ali alikuwa kama nafsi yake mwenyewe. Kuelekea mwishoni mwa sura hii, alisimulia hadithi kutoka kwenye Manaqib kama ilivyosimuliwa na Jabir, ambaye alisema kwamba, alimsikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema kwamba, Hadhrat Ali anazo sifa ambazo kwamba kama mtu anakuwa na moja kati ya hizo, ingelitosha kuthibitisha murwa wa mtu huyo na ubora wake. Na kwa sifa hizo ilimaanishwa hadithi za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuhusiana na yeye kama vile: Yeyote yule ambaye mimi ni mwenye kumtawalia mambo yake basi huyu Ali ni mwenye kutawalia mambo yake, au Ali yuko kwangu mimi kama alivyokuwa Harun kwa Musa, au Ali anatokana na mimi na mimi natokana na Ali au Ali yuko kwangu mimi kama nafsi yangu ilivyokuwa kwangu, utii kwake ni utii kwangu, au Kupigana dhidi ya Ali ni kupigana dhidi ya Allah, na kufanya amani na Ali ni kufanya amani Allah, au Rafiki wa Ali ni rafiki wa Allah, na adui wa Ali ni adui wa Allah, au Ali ni Hujjat (udhihirisho) wa Allah juu ya viumbe Wake, au Mapenzi kwa Ali ni imani, na uadui dhidi yake ni ukafiri, au Kundi la Ali ni kundi la Allah, nakundi la maadui wa Ali ni kundi la Shetani; au Ali yuko pamoja na haki, na haki pamoja naye, (na hivyo) havitengani, au Ali ndiye mgawaji wa Pepo na Moto, au Mtu anayejitenga na Ali, amejitenga na mimi, na anayejitenga na mimi, anajitenga na Allah, au Wafuasi wa Ali wataokolewa Siku ya Hukumu. Mwishowe, alinukuu hadithi nyingine yenye maelezo marefu kutoka kwenye Manaqib ambayo mwishoni mwake Mtume anasema: Naapa kwa jina la Allah ambaye ameweka utume juu yangu, na kunifanya mimi mbora wa viumbe Wake: Ewe Ali! Hakika wewe ni Hujjat (udhihirisho) wa Allah kwa ajili ya watu, mdhamini Wake, mjuzi wa siri Zake, na Khalifa juu ya waja Wake. Kuna hadithi nyingi kama hizo kwenye vitabu vyenu. Maneno nafsi zetu kwa uwazi huonesha ushirikiano wa karibu kati ya Mtume na Ali katika masuala yote ya ubora. Nafikiri kwamba aya hii ni ushahidi tosha wa msimamo wangu. Aidha, swali lako la pili linajibiwa na aya hiyo hiyo. Tumethibisha kwamba, ukiondoa utume na Wahyi, ambavyo vinamhusu Mtume tu peke yake, Ali alishirikishwa pamoja naye katika masuala yote ya ubora. Vile vile ina maana kwamba katika sifa za hali ya juu za ubora Ali alikuwa mbora zaidi ya Masahaba na kwa mtu yeyote katika umma huu. Kwa hakika aya hii inathibitisha kwamba anawapita Mitume wote wengine waliopita, kama vile ambavyo Mtume anawapita Mitume wote wengine.

180

Mikesha ya Peshawar

KWA VILE MTUKUFU MTUME ALIKUWA MBORA KWA MITUME WOTE WENGINE NA ALI PIA ALIKUWA MBORA KWAO
Katika Ihyaul-Ulum ya Imam Ghazali, Sharhe Nahjul-Balaghah ya Ibn Abil-Hadid Mutazil, Tafsir ya Imam Fakhrud-Din Razi, na Tafsir za Jarullah Zamakhshari, Baidhawi, Nishapuri na kadhalika, utaikuta hadith hii ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): Wanachuoni wa umma wangu ni kama mitume wa Bani-Israili. Katika hadith nyingine amesema: Ulamaa wa umma wa Mtukufu Mtume walikuwa sawa au bora kuliko mitume wa Bani-Israil kwa sababu tu kwamba chanzo chao cha elimu kilikuwa ndio kiini hasa cha elimu, Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.). Kwa hiyo, Ali ibn Abi Talib bila shaka alikuwa mbora kwa mitume, kwa vile Mtukufu Mtume amesema: Mimi ni Jiji la elimu na Ali ni lango lake. Vile vile amesema: Mimi ni nyumba ya hekima na Ali ni lango lake. Wakati Ali mwenyewe alipoulizwa kuhusu jambo hili, yeye alieleza baadhi ya vipengele vya ubora wake kwa mitume wa Bani-Israil. Mnamo mwezi 20 ya Ramadhan, wakati Ali alipokuwa katika kitanda chake cha umauti kufuatia lile shambulizi la Abdul-Rahman Ibn Muljim Muradi, alimtuma Imam Hasan kuwaita wale Mashia waliokuwa wamejikusanya kwenye mlango wa nyumba yake. Walipoingia ndani, walikuzunguka kitanda chake huku wakilia kimya kimya. Ali akasema: Mnaweza kuuliza swali lolote mnalolitaka kabla sijakuacheni, lakini maswali yenu yawe mafupi. Mmoja wa wale waliokuwepo pale alikuwa ni Sasaa bin Suwhan. Wanachuoni wenu maarufu kabisa kama Ibn Abdul-Birr na Ibn Saad, wameandika kuhusu maisha na tabia yake, wamemtegemea yeye Sasaa, wakithibitisha kwamba yeye alikuwa ni mtu mwenye elimu kubwa. Sasaa alimwambia Ali: Naomba unifahamishe ni nani mbora, ni wewe au Adam. Imam Mtukufu akasema: Haifai kwa mtu kujisifia mwenyewe, lakini kulingana na kauli adilifu: Na neema za Mola Wako alizokujaalia zisimulie, ninakwambia kwamba mimi ni bora kuliko Adam. Alipoulizwa ni kwa nini imekuwa hivyo, Ali alieleza kwamba Adam alikuwa na kila namna ya huruma, starehe na neema kwa ajili yake ndani ya Pepo. Alitakiwa tu kujizuia kutokana na chakula kile kilichokatazwa. Lakini hakuweza kujizuia na akala kutoka kwenye mti ule. Matokeo yake yeye alifukuzwa kutoka peponi. Mwenyezi Mungu hakumkataza yeye Ali kutokana na kula ngano (ambayo, kwa mujibu wa imani ya Kiislam ndio mti uliokatazwa). Lakini kwa kuwa yeye hakuwa na mwelekeo kwenye dunia ya mpito, yeye alijizuia kwa hiari yake mwenyewe kula ngano. (Hoja ya kauli hii ya Ali ilikuwa kwamba ubora wa mtu mbele ya Mwenyezi Mungu ulitegemea kwenye uchamungu na utii, na kwamba kilele cha uchamungu kinaegemea katika kujizuia hata kwa kile ambacho kinaruhusiwa kihalali).

181

Mikesha ya Peshawar
Sasaa akauliza: Ni nani mbora, wewe ama Nuh? Ali akajibu: Mimi ndiye mbora. Nuh aliwalingania watu wake kumuabudu Mwenyezi Mungu lakini hawakutii. Kitendo chao cha aibu kilikuwa ni kumtesa yeye. Yeye aliwalaani na akamuomba Mwenyezi Mungu: Ewe Mola Wangu! usiabakishe hata mtu mmoja juu ya ardhi miongoni mwa madhalimu hawa. Baada ya kifo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ingawaje watu walinisababishia matatizo makubwa, mimi sikuwalaani kamwe. niliyabeba mateso yao kwa subira kubwa. Sasaa akauliza: Ni nani aliye mbora, wewe ama Ibrahim? Ali alijibu: Mimi na mbora, kwani Ibrahim alisema: Mola Wangu! nionyeshe jinsi unavyofufua wafu. (Mungu) Akasema: Kwani huamini? Akasema: Hasha! bali ili moyo wangu utue ..... (2:260) Imani yangu ilikuwa kiasi kwamba nilisema: Hata kama pazia la yale yaliyo ghaibu lingefunuliwa, imani yangu isingeongezeka. Sasaa akauliza: Ni nani mbora, wewe au Musa? Imam Mtukufu akajibu: Mimi ndiye mbora, kwani wakati Mwenyezi Mungu Mtukufu alipomtuma Musa kwenda Misri kumlingania Firauni kwenye haki, Musa alisema: Mola Wangu! Kwa hakika niliuwa mmoja wao, kwa hiyo naogopa wataniuwa. Na ndugu yangu Harun ni fasihi zaidi ulimi wake kuliko mimi. Basi mtume aende pamoja nami kunisaidia, ili anisadikishe. Hakika mimi na hofu watanikadhibisha. (28: 33-34) Mtukufu Mtume aliniagiza mimi, kwa amri ya Allah kwenda Makka kuzisoma aya za Sura ya Al-Baraa kutoka juu ya Kaaba kwa makafiri wa Quraishia. Mimi sikuwa na hofu, ingawaje kulikuwa na watu wachache ambao walikuwa hawajapoteza ndugu yao wa karibu kwa upanga wangu. Kwa kuitii amri yake, niliitekeleza kazi hiyo peke yangu. Nilizisoma aya za al-Baraat na nikarejea. Sasaa akauliza tena: Ni nani mbora, wewe au Isa (ibn Mariam)? Ali akasema: Mimi ni mbora, kwani wakati Mariam alipokuwa mjamzito kwa Rehma za Mwenyezi Mungu, na wakati wake wa kujifungua ukakaribia, ulishushwa wahyi kwake: Ondoka katika Nyumba hii tukufu, kwani Nyumba hii ni nyumba ya ibada, sio mahali pa kuzalia watoto. Matokeo yake aliondoka kwenye Nyumba tukufu hiyo na akaenda kwenya kichaka ambako alijifungua mtoto Isa. Lakini wakati mama yangu mimi, Fatima binti al-Asad, alipojisikia uchungu wa uzazi ndani ya eneo la Kaaba tukufu, alingangania kwenye ukuta na akamuomba Mwenyezi Mungu kwa jina la Nyumba ile na mjenzi wa Nyumba ile, ili apunguziwe maumivu yake. Mara ufa ukajitokeza katika ukuta huo, na mama yangu akasikia sauti ya kimuujiza ikimwambia, Ewe Fatima! Ingia kwenye Nyumba ya Kaaba. Yeye akaingia ndani na mimi nikazaliwa ndani ya Kaaba tukufu.

182

Mikesha ya Peshawar

KIOO CHA MITUME YOTE KAMA ILIVYOONYESHWA NA HADITH YA UFANANISHO


Imesimuliwa vilevile katika vitabu vya ulamaa wenu kwamba Ali alikuwa ni kioo cha sifa za hali ya juu za mitume wote waliotangulia. Ibn Abil-Hadid Mutazili ndani ya Sharhe Nahjul-Balaghah yake, Jz. 11, uk. 449, Hafidh Abu Bakr Faqih Shafii, Ahmad bin Husein Baihaqi katika Manaqib, Imam Ahmad bin Hanbal ndani ya Musnad, Imam Fakhrud-Din Razi katika Tafsir al-Kabir kuhusiana na aya ya Mubahila, Muhuid-Din Ibn Arabi ndani ya Yawaqit al-Jawhir, suala la 32, uk. 172; Sheikh Suleyman Balkhi Hanafi katika Yanabiul-Mawadda, mwanzoni mwa Sura ya 40 kwa idhini ya Musnad ya Ahmad bin Hanbal, Sahih ya Baihaqi, na Sharhil-Mawaqif wat-Tariqatil-Muhammadiyya, NurudDin Maliki katika Fusulul-Muhimma, uk. 120; kutoka kwa Baihaqi; Muhammad bin Talha Shafii ndani ya Matalibus-Suul uk. 22; na Muhammad bin Yusuf Ganji Shafii katika Kifayatut-Talib, Sura ya 23, wamesimulia kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) pamoja na tofauti kidogo ya maneno, hapa na pale, akisema kwamba: Yeyote anayetaka kuiona elimu ya Adam, uchamungu wa Nuh, unyenyekevu wa Ibrahim, utukufu wa Musa, au ule utiifu wa Isa (Yesu), anaweza kumuangalia Ali ibn Abi Talib. Mir Seyyed Ali Hamadani amesimulia hadith hiyohiyo pamoja na nyongeza kidogo katika Mawaddatul-Qurba yake, Mawadda 8. Anasimulia kutoka kwa Jabir kwamba Mtume (s.a.w.w.) amesema. Kwa hakika Mwenyezi Mungu amekusanya sifa tisini za mitume kwa Ali, ambazo hakumpa mtu mwingine yeyote. Yule Hafidh mkubwa Muhammad bin Yusuf Ganji Shafii, baada ya kunukuu hadith hii, anatoa maelezo haya: Ali alikuwa sawa na Adam katika elimu kwa vile Mwenyezi Mungu amemfundisha Adam kila kitu, kama anavyosema ndani ya Qurani Tukufu, Na akamfundisha Adam majina .....(2:31). Hali kadhalika, Ali alikuwa na elimu ya mambo yote. Kwa sababu ya elimu iliyoshuka moja kwa moja kutoka kwa Allah swt., Adam alipewa ukhalifa wa Allah, kama Qurani tukufu inavyosema: ..... Nitajaalia khalifa juu ya ardhi..... (2:30). Kwa kuwa elimu ya Adam iliongozea kwenye ubora wake, hivyo kwamba hata Malaika walisujudu kwa heshima juu yake, Ali pia alikuwa mtukufu sana wa viumbe wote na khalifa baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Elimu ya Ali ni sawa na ya Nuh kwa vile Ali alikuwa mkali dhidi ya makafiri na mpole kwa waumini. Allah amemsifia ndani ya Qurani: Na wale walio pamoja naye wana nyoyo imara dhidi ya makafiri, na wapole miongoni mwao wenyewe. (48: 29). Huu ni ushahidi mwingine kwamba aya hii ilishuka kwa kumsifia Ali, kama nilivyosema mapema. Nuh alikuwa mkali sana kwa makafiri, kama Qurani tukufu anavyosema: Na Nuh akasema: Mola Wangu! usibakishe hata mkazi mmoja juu ya ardhi miongoni mwa makafiri. (71:26). Ali alikuwa sawa na Ibrahim katika utulivu wa moyo. Qurani tukufu inasema: Kwa hakika, Ibrahim alikuwa mpole sana wa moyo. (9:114).

183

Mikesha ya Peshawar
Ali alikuwa na sifa zote ambazo Mitume wengine walikuwa nazo mmoja mmoja. Hadithi hii inayokubaliwa na wote huthibitisha kwamba Ali alikuwa na fadhail za hali ya juu sana, ambazo kila moja ya hizo ilikuwa sawa na sifa za juu sana za Mitume. Ni wazi kwamba, mtu ambaye alikuwa na fadhaila za juu sana za mitume wote, basi aliwapita wote kwa cheo. Sheikh Sulayman Balkhi Hanafi katika Yanabiul-Mawadda, Sura ya 40, ananukuu kutoka kwenye Manaqib ya Khawarizmi kutoka kwa Muhammad Bin Mansur, ambaye alisema kwamba alimsikia Ahmad Ibn Hanbal akisema: Kulikuwa hakuna sifa kama hizo kwa Sahaba yeyote wa Mtume, kama zilivyokuwa kwa Ali Bin Abu Talib. Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafii vile vile anasimulia maneno yenye maana hiyo hiyo. Ibn Abil-Hadid Mutazali katika Sharhe-Nahjul-Balagha, juzuu ya 1, uk. 46, anasema: Ali alikuwa ndiye mtu mwenye kufaa sana katika nafasi ya Wilaya (Ulinzi) kwa fadhaili za ubora wake. Ukimuondoa tu Mtume wa Allah, alikuwa ni mtu mwenye kustahiki sana kwa cheo cha Khalifa. Ali kwa hakika alikuwa mwenye kustahiki zaidi kwa Ukhalifa, lakini aliwekwa kando kwa mbinu za kisiasa za watu duni. Angalau wangelimjulisha Ali kwamba walikuwa wakifanya mkutano huko Saqifa Bani Sada kuangalia juu ya suala muhimu la kumchangua Khalifa. Hawakufanya hivyo ili kumnyima haki yake ya urithi.

KUKUBALIWA KWA ABU BAKR NA WATU WOTE


Hafidh: Je, sisi ni madhalimu au ni wewe? Unasema kwamba masahaba waliwachagua wale ambao wamepora Ukhalifa. Kwa hakika unafikiri kwamba sisi ni wajinga ambao kibubusa tunawafuata wazee wetu. Lakini kuna uthibitisho gani wenye nguvu kama Ijma makubaliano ya wote kwa ujumla? Masahaba wote na Umma, pamoja na Ali, walimchagua Abu Bakr na wakala kiapo cha utii kwake. Kwa hakika makubaliano ya pamoja ya watu ni ya mwisho na kukubaliana nayo ni lazima. Mtume alisema: Watu wangu hawakubaliani katika (jambo lenye) kosa; watu wangu hawakubaliani katika upotofu wa kutoka kwenye njia iliyonyooka. Hivyo hatukuafuata wazee wetu kibubusa. Ukweli ni kwamba katika siku ya kwanza baada ya kifo cha Mtume, Umma kwa pamoja uliamua katika mkutano kumsimamisha Abu Bakr kama Khalifa. Kwa sababu ilikuwa ni ukweli uliokubaliwa, lazima na sisi tuukubali. Mumbezi: Tafadhali tujulishe Ukhalifa umeegemezwa katika misingi ipi? Hafidh: Iko wazi. Uthibitisho mzuri wa kuwepo ukhalifa baada ya Mtume ni Ijma (makubaliano ya wote kwa ujmla) ya Umma ambayo kwayo ukhalifa umekuja kupatikana. Mbali na haya, sifa bora sana kwa Abu Bakr na Umar kwa ajili ya ukhalifa ilikuwa ni kukomaa kwao kiumri. Ali, pamoja na fadhaili zote na ukaribu kwa Mtume, ilikuwa arukwe kwa sababu ya ujana wake. Na, ili kuwa waadilifu na wenye haki, haikuwa sawa kwa

184

Mikesha ya Peshawar
kijana kuyaweka pembeni madai ya masahaba watu wazima. Na hatuchukilii kuachwa huku kwa Ali kama ni kushindwa kwake, kwani ubora wake kwa upande mwingine hukubaliwa na wote. Vile vile kuna hadithi iliyosimuliwa na Khalifa Umar kutoka kwa Mtume, ambaye alisema: Utume na uongozi haviwekwi pamoja katika familia moja. Kwa hiyo, Ali alinyimwa ukhalifa kwa sababu anatokana na familia ya Mtume. Alikuwa hafai kwa ajili ya cheo hicho.

HOJA DHIDI YA UHALALI WA IJMAI


Muombezi: Nimeshangaa kwamba unaweza kuleta hoja za kijinga kama hizi. Kwanza, unasema kwamba Ijmai, makubaliano ya Umma, ndio hoja yenye nguvu zaidi, na kwa kuunga mkono nukta yako umesimulia hadithi. Neno ummai maana yake umma wangu, hivyo hadithi hiyo (tujaalie kuwa ni ya kweli) inamaniisha kwamba wakati umma wote unapokubaliana kwenye jambo fulani, uamuzi wao hauwezi kuwa na makosa. Siwezi kukubaliana na hili. Allah aliutofautisha ummah huu kwa sababu ya ukweli kwamba miongoni mwao kutakuwepo na kundi lililoongoka. Mwakilishi wa Allah atakuwa miongoni mwao. Wakati umma unapokusanyika pamoja, kundi lile lililoongoka litakuwa miongoni mwao. Lakini hadithi hii (hata kama ni ya kweli) haioneshi ushahidi wowote kwamba Mtume aliitoa haki yake mwenyewe na kuruhusu ummah kuchagua Khalifa. Na hata kama Mtume alikuwa ameuchia ummah kuchagua Khalifa, haki hii itakuwa inaachiwa ummah wote. Kwa vile Waislamu wote hunufaika kutokana na Ukhalifa, lazima wangelikuwa na haki ya kuelezea maoni yao katika kumchagua Khalifa. Kwa hiyo, kukusanyika kwa ummah wote baada ya Mtume kufariki kungelikuwa muhimu ili kwamba kwa idhini yao ya pamoja, mtu mkamilifu angeweza kuchaguliwa kuwa Khalifa. Je, kulikuwapo na mkusanyika kama huo wa Waislamu? Je, hii ndiyo njia ambayo Abu Bakr aliyofikia kuwa ukhalifa? Hafidh: Abu Bakr alibakia kwenye ukhalifa kwa zaidi kidogo ya miaka miwili. Wakati wa kipindi hiki Waislamu kwa jumla walikula kiapo cha utii kwake. Hii yenyewe ina maana ya maoni ya pamoja miongoni mwao, ambayo ni uthibitisho wa uhalali wa Ukhalifa wake. Muombezi: Unajaribu kuliepuka suala lenyewe. Swali langu halikuwa kuhusu kipindi chote cha Abu Bakr. Nilikuwa nauliza kuhusu uamuzi uliochukuliwa katika Saqifa ya Bani Sada. Je, mkusanyiko ule pale ulikusanya ummah wote, au kulikuwa na watu wachache tu ambao walikula kiapo cha utii? Hafidh: Ni dhahiri kwamba kulikuwa na masahaba wachache mashuhuri wa Mtume, lakini baadae Ijmai ilipita.

185

Mikesha ya Peshawar
Muombezi: Je, Mtume, mtu anayefaa zaidi kuongoza ummah, aliitoa haki yake kwa upande wa ummah wake? Je, alitoa haki yake ili kwamba watu wa ukoo wa Aus, ambao walikuwa maadui kwa ukoo wa Khazraj, wale kiapo cha utii kwa ajili ya hofu ya maadui wao kushika madaraka? Je, aliacha haki yake ili kwamba watu wake waunde serikali kwa misingi ya hofu na ulafi? Je, unaweza kuita kikundi hiki kidogo cha watu kuwa ndio ummah? Je, Waislamu wa Makka, Yemen, Jeddah na miji mingine hawakuwa sehemu ya ummah? Je, hawakuwa na haki ya kutoa maoni yao kuhusiana na ukhalifa? Kama kulikuwa hakuna hila, kwa nini wasingojee na kupata msimamo wa Waislamu wote katika suala muhimu kama hili la Ukhalifa? Katika njia hii, Ijmai kwa maana yake halisi ingewza kupatikana. Hata leo, ili kusimamisha serikali ya kidemokrasi au kuchagua kiongozi wa taifa, hufanyika uchaguzi mkuu. Wananchi wanapiga kura zao, na kiongozi anachaguliwa kwa wingi wa kura. Viongozi wa nchi zilizostaarabika na watu wote wastaarabu wataucheka utaratibu wenu huu wa Ijmai usio na mpangilio mzuri. Hafidh: Kwa nini unajiigiza katika mazungumzo yasiyopendeza? Ijmai ina maana kwamba kulikuwa na mkusanyiko wa watu wenye akili na masahaba wakubwa ambao walikutana ndani ya Saqifa. Muombezi: Unasema kwamba Ijmai ilimaanisha kwamba kulikuwa na mkusanyiko wa watu wenye akili na masahaba wakubwa wa Mtume, lakini huna msingi wowote kwa maelezo haya isipokuwa hadithi uliyoitaja. Ni wapi hadithi imetaja watu wenye akili au masahaba wakubwa? Narudia kwamba neno umma maana yake ni umma wote, sio idadi ndogo ya Masahaba, hata kama wakiwa wana elimu. Hata kama unayosema yakiwa ni kweli, kwamba Ijmai maana yake mkusanyiko wa watu wenye akili na masahaba wakubwa, je, watu wenye akili na masahaba wakubwa wa Mtume walikomea kuwa ni hao watu wachache tu ambao walikusanyika chini ya paa dogo la Saqifa siku hiyo? Je, kulikuwa hakuna watu wengine wenye akili na masahaba wakubwa katika ulimwengu wa ki-Islamu? Na je, wote kwa pamoja walipiga kura kwa ajili ya Khalifa? Hafidh: Kwa vile suala la Khalifa lilikuwa ni jambo nyeti, watu walikuwa wanahofia kwamba huenda kukatokea machafuko. Ilikuwa haiwezekani kuwaarifu Waislamu katika sehumu nyingine. Wakati Abu Bakr na Umar waliposikia kwamba baadhi ya Ansar wamekusanyika kule, na wao vile vile walikwenda kule kuzungumza. Kwa sababu Umar alikuwa mwanasiasa mweledi, aliona kwamba inafaa kwa ummah kula kiapo cha utii kwa Abu Bakr. Wengine walimfuata na kula kiapo cha utii kwa Abu Bakr, lakini kikundi cha Ansar na watu wa ukoo wa Khazraj wanaomuunga mkono Sad Bin Ubaida, hawakula kiapo cha utii na wakaondoka Saqifa. Hiyo ndio ilikuwa sababuya kwa nini walifanya haraka. Muombezi: Hivyo na wewe unakubali, kama wanahistoria na maulamaa wenu walivyokubali, kwamba katika siku ya Saqifa, wakati mashauri ya msingi yalipokuwa

186

Mikesha ya Peshawar
yanafanyika kulikuwa hakuna Ijmai. Kwa ajili ya maslahi ya kisiasa, Abu Bakr alimpendekeza Umar na Abu Ubaida Bin Jarra, na wao pia, kwa kulirudisha pendekezo hilo, walitaja jina la Abu Bakr, wakimuambia kwamba yeye anastahiki zaidi kwa nafasi hiyo. Wao mara moja tu wakala kiapo cha utii kwake. Baadhi ya watu wa ukoo wa Aus waliokuwa pale vile vile walikula kiapo cha utii kwa Abu Bakr kwa msimamo wao wa uadui dhidi ya ukoo wa Khazraj, na vile vile walihofia kwamba Sad bin Ubaida angeweza vinginevyo kuwa Amir. Kwa njia hii uungaji mkono ulipanuka na kuwa mkubwa. Hata hivyo, kama Ijmai ingekuwa ni hoja yenye nguvu kuweza kutegemewa, wangelisubiri mpaka umma wote au, kama ulivyosema: watu wenye akili wakusanyike pale kupata idhini ya umma wote. Hafidh: Nimekuambia kwamba hofu ya machafuko ililazimisha kundi hili kutenda kama walivyofanya. Watu wa ukoo wa Aus na Khazraj wamekusanyika katika Saqifa na walikuwa wakigombana wenyewe kwa wenyewe. Kila mmoja wao anataka kuamua uhuru wa dola ya ki-Islamu kwa ajili yao wenyewe. Muombezi: Nakubaliana na unayoyasema. Muhammad Bin Jarir Tabari (tazama Tarikh yake, Jz. 2, uk. 457) na wengine wameandika kwamba, Waislamu hawakukusanyika chini ya Saqifa kumchagua Khalifa wao. Koo za Aus na Khazraj zilitaka kujichagulia Amir wao wenyewe. Abu Bakr na Umar wakanufaika kutokana na tofauti zao. Kama kweli walikusanyika kujadili Ukhalifa, kwa kweli wangeliwaita Waislamu wote kutoa maoni yao juu ya suala hilo. Kama ulivyosema: Hawakuwa katika hali ya kuweza kuwajulisha Waislamu wote, na muda ulikuwa unakimbia. Ilikuwa kweli kwamba walikuwa hawana mawasiliano ya mara moja na Makka, Yemen, Taif, au miji mingine ya mbali ya Waislamu. Lakini je, walikuwa hawana hata njia ya kuwasiliana hata na Jeshi la Usama Bin Zaid, ambalo lilikuwa limepiga kambi nje kidogo ya Madina? Hivi wasingeweza kuwaarifu masahaba wakubwa wa Mtume ambao walikuwa kule? Mmoja wao alikuwa mtu maarufu, Kamanda wa jeshi la Waislamu, aliyechguliwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe. Abu Bakr na Umar walikuwa chini yake. Wakati Usama aliposikia kwamba, kwa hila watu watatu wamemchagua Khalifa bila kuwashauri watu wengine, au hata kuwajulisha, na kwamba walikuwa wamekula kiapo cha utii kwa mtu moja, alipanda farasi wake mpaka kwenye mlango wa Msikiti na akesema kwa sauti kubwa: Vurugu yote hii ni ya nini? Kwa amri ya nani mmemchagua Khalifa? Kulikuwa na umuhimu gani, wa watu wachache ambao bila kuwashauri masahaba, wamemchagua Khalifa? Umar akajitokeza mbele kumtuliza na kusema: Usama! Kazi hiyo imekwisha. Kiapo cha utii kimekwishatolewa. Usisababishe vurugu sasa miongoni mwa watu. Na wewe mwenyewe pia ule kiapo cha utii. Usama akakasirika, na kusema: Mtume amenifanya mimi Amir wenu, akasema. Inawezekana vipi Amir aliyeteuliwa na Mtume atoe heshima ya utii kwa watu wa chini ambao waliwekwa chini ya amri yake? Ingawa mengi zaidi yalitokea, kiasi hiki kidogo kinatosha kuthibitisha hoja yangu.

187

Mikesha ya Peshawar

ALI ALIKOSA KUARIFIWA KWA MAKUSUDI KUHUSU MKUTANO WA SAQIFA


Kama unasema kwamba Jeshi la Usama vile vile lilikuwa mbali na mji wa Madina na kwamba muda ulikuwa unakimbia, je, utadai kwamba umbali kutoka Saqifa na Msikitini na kwenye makazi ya Mtume vile vile ulikuwa mkubwa? Kwa nini hawakumuarifu Ali, au Abbas ami yake Mtume mwenye kuheshimiwa? Kwa nini hawakuwashauri Bani Hashim, kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)? Hafidh: Katika namna zote hali wakati ule ilikuwa ngumu kiasi kwamba hawakuthubutu kuwa wazembe na kuondoka Saqifa. Muombezi: Samahani, walikuwa nao muda wa kutosha. Waliacha makusudi kumuarifu Ali, Bani Hashim, na masahaba wakubwa. Hafidh: Unasemaje kwamba walifanya makusudi kuacha kuwaarifu? Muombezi: Dalili moja ya wazi ni kwamba Umar alifika kwenye mlango wa nyumba ya Mtume lakini hakuingia ndani. Hafidhi: Kwa hakika kisa hiki kimebuniwa na Marafidhi. Muombezi: Angalia ukurasa wa 456 Tarikh, ya Muhammad Bin Jarir Tabari, Jz. 2, mmoja wa Maulamaa wenu wakubwa. Anaandika kwamba Umar alifika mlangoni kwa nyumba ya Mtume lakini hakuingia ndani. Alituma ujumbe kwa Abu Bakr: Njoo haraka; nina shughuli muhimu na wewe. Abu Bakr akamtumia jibu kwamba hakuwa na muda. Umar akutuma ujumbe mwingine: Tunakabiliwa na mgogoro. Kuwepo kwako ni muhimu. Abu Bakr akatoka nje na Umar akamueleza kwa siri kuhusu kukusanyika kwa Ansar ndani ya Saqifa na akasema kwamba walipaswa kwenda huko mara moja. Wote wakaondoka, na njiani wakakutana na Abu Ubaida wakamchukuwa na kuongozana naye. Kwa ajili ya Allah hebu jaribu kuwa muadilifu. Kama walikuwa hawakupanga njama, kwa nini Umar aende mpaka kwenye mlango wa nyumba ya Mtume na kisha asiingie ndani? Wangeliweza kuomba msaada. Je, katika Umma wote alikuwepo Abu Bakr tu, ambaye alikuwa na hakima zote, na kwamba masahaba wengine na kizazi cha Mtume walikuwa ni wageni ambao hawakustahiki kujulishwa kuhusu suala hili?

188

Mikesha ya Peshawar
Je, Ijma yenu hii kwa haki inaundwa na watu watatu? Ni wapi katika sehemu yoyote ya ulimwengu ambako utaratibu kama huu unakubalika? Tuchukulie kwamba watu watatu au kikundi chochote cha watu, wakakusanyika katika mji na wakaunda Ijma na kisha wakamchagua kiongozi wa nchi. Je, ni wajibu juu ya Maulamaa na wasomi wa miji mingine yote kuwatii? Au hata kama baadhi ya watu wenye ujuzi na wasomi ambao hawakuchaguliwa na wengine kutoa mawazo, je, ni lazima kwamba wasomi na maulamaa wote waliobakia wawafuate wao? Je, ni sahihi kukandamiza hisia za umma wote kwa tabia ya vitisho vya kundi moja la watu? Kama kwa upande mwingine, katika mijadala ya kielimu, kundi la watu wakafichua kwamba Ukhalifa haukithibitshwa na sheri za dini au za asili, ni haki kuwaita Rafidhi? Unasema kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliliacha suala la Ukhalifa juu ya umma au kwa wasomi wa Umma, kama unavyoita. Je, wasomi wa Umma wanaundwa na Abu Bakr, Umar na Abu Ubaida Jarra? Kila mmoja akipendekeza jina la mwingine, na kisha wawili kati yao wakamkubali wa tatu. Na hiyo ikawa mwisho. Je, ni wajibu kwa Waislamu wote kuwafuata wao? Wachache, wengi, na Ijma humaanisha vitu tofauti kabisa. Kama mkutano wa kushauriana unafanywa kwa ajili ya kuangalia tatizo fulani, na idadi ndogo ya watu ikatoa wazo moja, ambapo ile idadi kubwa ya watu ikatoa wazo jingine, kisha inasemwa kwamba, moja ni maoni ya wachache. Maoni ya idadi kubwa ya watu yanaitwa maoni ya wengi, na kama wote (bila tofauti yoyote) wakatoa kauli moja, inaitwa Ijmai. Je Ijmai ilifikiwa ndani ya Saqifa au baadae Msikitini, au baada ya hapo katika mji wa Madina? Kama, hata hivyo, kwa kustahi matakwa yako, tukiondolea mbali haki za umma wote na kusema kwamba maoni ya wasomi na masahaba wa Mtume yalikuwa yanatosha kwa ajili ya Ijmai, nauliza je! Kulikuwa na Ijmai amabayo kwamba wasomi wote na masahaba mashuhuri wa Mtume walishiriki? Je, kikundi kidogo kile kule Saqifa kilikubaliana wote katika maoni yao? Jawabu lake lazima litakuwa ni hapana. Mwandishi wa Mawaqif mwenyewe amekiri kwamba kulikuwa hakuna Ijmai wakati wa Ukhalifa wa Abu Bakr, na kwa yakini vile vile kulikuwa hakuna maoni ya wote miongoni mwa wanachuoni wa Madina. Sad Bin Ubaida Ansari, kizazi chake, masahaba mashuhuri wa Mtume, Bani Hashim wote, rafiki zao, na Ali Bin Abu Talib, - wote walimpinga Abu Bakr kwa muda wa miezi sita. Watu hawa katu hawakula kiapo cha utii kwake. Mjini Madina, makazi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), hakuna Ijmai iliyofikiwa ambayo kwayo wasomi na masahaba walimuunga mkono Abu Bakr kama Khalifa. Wanahistoria wenu mashuhuri wenyewe, kama Imamu Fakhrud-Din Razi, Jalalud-Din Suyuti, Ibn Abil-Hadid Mutazali. Tabari, Bukhari na Muslim, wameandika kwamba Ijma kamwe haikutokea hapo Madina. Bani Hashim, Bani Umayya, na masahaba kwa ujumla isipokuwa hao watu watatu waliotaja hapo juu hawakuwepo Saqifa ili kupiga kura zao. Aidha, wengi waliupinga uamuzi huo kwa nguvu sana. Kusema kweli, baadhi ya masahaba wakubwa ambao walikataa kula kiapo cha utii kule Saqifa, walikwenda msikitini na kulalamika kwa Abu Bakr. Miongoni

189

Mikesha ya Peshawar
mwa muhajirina walikuwa ni; Salman Farsi, Abu Dharr Ghifari, Mikidadi bin Aswad Kindi, Ammar-e-Yasir, Buraida Aslami, na Khalid Bin Said Bin Aas Amawi. Miongoni mwa Ansari walikuwa; Abul-Hathama bin Tihan, Khuzaima Bin Thabit DhushShahadatain, Abu Ayyub Ansari, Ubai bin Kab, Sahl Bin Hunaif, Uthman Bin Hunaif, ambao walipingana na Abu Bakr ndani ya Msikiti. Nimetoa tu kwa mukhtasari mfupi juu ya matukio haya. Hakuna Ijmai ya aina yoyote iliyofikiwa. Ijma inayosemwa ya wasomi na masahaba mashuhuri wa Madina ni uwongo mtupu. Kwa kutegemea juu ya vyanzo vyenu wenyewe, nitakupa ordha ya majina ya wale ambao walipinga Ukhalifa. Ibn Hajar Asqalani na Baladhuri, kila mmoja katika Tarikh yake, Muhammad Bin Khawind Shah katika kitabu Rauzatus-Safa, Ibn Abdul-Birr katika Istiab na wengine wanasema kwamba , Sad Bin Ubaida na sehemu ya Makhawarij na kikundi cha Makuraishi hawakula kiapo cha utii kwa Abu Bakr. Aidha, watu kumi na nane ambao walikuwa Masahaba wakubwa na mashuhuri wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hawakula kiapo cha utii kwa Abu Bakr. Walikuwa ni Mashia wa Ali Bin Abu Talib. Majina ya watu hao kumi na nane ni haya yafuatayo: 1. Salman Farsi 2. Abu Dharr Ghifari 3. Mikidadi Bin Aswad-e-Kindi 4. Ammar Yasir 5. Khalid Bin Saidbin al-Aas 6. Buraida Aslami 7. Ubaid Bin Kab 8. Khuzaima Bin Thabit Dhush-Shahadatain 9. Abul-Hathama Bin Tihan 10. Sahl Bin Hunaif 11. Uthmani Bin Hunaif Dhush-Shahadatain 12. Abu Ayyub Ansari 13. Jabir Ibn Abdullah Ansari 14. Hudhaifa bin Yaman 15. Sad Bin Ubaida 16. Qais Bin Sad 17. Abdullah Bin Abbas 18. Zaid Bin Arkam Na Yakubi anaandika katika Tarikh yake: Kikundi cha Muhajirina na Ansari kilijitenga bila kula kiapo cha utii kwa Abu Bakr, na walikuwa ni wafuasi wa Hadhrat Ali. Miongoni mwao walikuwa ni Abbas Bin Abul-Muttalib, Fazl Bin Abbas, Zubair Ibnul-Awwam Bin As, Khalid Bin Said, Miqdadi Bin Umar, Salman Farsi, Abu Dharr Ghifari, Ammar Yasir, Baraa Bin Azib, na Ubai Bin Kab.

190

Mikesha ya Peshawar
Je, watu hawa hawakuwa wasomi wa Umma? Ali, Abbas, ami yake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na watu wengine mashuhuri wa ukoo wa Bani Hashim je, watu hawa hawakuwa ni wenye busara na waaminifu? Ilikuwa Ijma ya aina gani hiyo, ambayo ilifanyika bila ushauri wa watu hawa? Wakati Abu Bakr anachaguliwa kwa siri siri, na Masahaba wengine mashuhuri hawakujulishwa, je, hii inakuwa ni Ijma? Au ni njama za kisiasa?

HADITH THAQALAIN NA HADITH SAFINA


Aidha, Bani Hashim, familia ya Mtume, hawakuwepo pale Saqifa. Uamuzi wao wa thamani hauwezi kukataliwa kwa mtazamo wa hadithi iliyosimuliwa katika mikesha iliyopita, na inayokubaliwa na madhehebu zote. Mtukufu Mtume alisema: Ninakuachieni kati yenu vitu viwili vizito: Kitabu cha Allah (Qurani Tukufu) na Ahlul Bayt wangu (watu wafamilia tukufu: Ali, Fatimah, na kizazi chao). Kama mkishikama na viwili hivi, kamwe, kamwe hamtapotea baada yangu. Watu hawa hawakuunga mkono Ukhalifa wa Abu Bakr. Kwa nyongeza, kuna hadithi nyingine mashuhuri ijulikanayo kama Hadith-e-Safina, ambayo niliitaja katika mikesha iliyopita. Mtume alisema: Ahlul Bayt wangu ni kama safina ya Nuh. Yeyote anayeipanda ameokolewa, na anayeipa mgongo ameangamia. Hadithi hii inaonesha kwamba, kama ambavyo watu wa Nuh waliokolewa kutokana na mafuriko makubwa kwa Safina yake, watu wa Mtume wetu wataokolewa kutokana na mabalaa kwa kushikamana na watu wa familia ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Ibn Hajar katika kitabu chake Sawaiq-e-Muhriqa, Sura ya 50, akifafanua juu ya aya ya 4, (kati ya aya tano anazofafanua), ananukuu hadithi mbili kutoka kwa Ibn Sad kuhusu wajibu wa kuwafuata Ahlul Bayt watukufu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Katika moja ya hadithi hizo Mtume alisema: Mimi na Ahlul Bayt wangu ni mti wa Peponi ambao matawi yake yako katika ardhi; hivyo mwenye kutafuta njia ya kuelekea kwa Allah lazima ajiambatanishe nao. Katika hadithi ya pili Mtume alisema: Miongoni mwa Umma wangu katika kila zama kuna watu waadilifu kutoka kwenye Ahlul Bayt wangu ambao huondoa uchafu unaoletwa kwenye dini na watenda maovu na ambao hufutilia mbali madai ya uwongo ya wenye kuchupa mipaka na tafsir za watu wasio elimika. Naifahamike kwenu kwamba Maimamu wenu kwa hakika ndio wale ambao wataokuelekezeni kwa Allah. Hiyvo lazima muwe waangalifu kuhusu wale mnaowachukuwa kuwa viongozi wenu. Kiini cha hadithi za aina hii ni kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa anauambia Umma wake: Mpaka muwafuate Ahlul Bayt wangu, vinginevyo maadui watakupotezeni. Watu ambao wangeweza kushawishi Ijmai, kiapo cha utii, na uteuzi wa Khalifa, walipinga utaratibu ulioulezea.

191

Mikesha ya Peshawar
Sasa hiyo ilikuwa ni Ijmai ya aina ngani? Masahaba wakubwa, wasomi, na kizazi cha Mtume walikuwepo hapo Madina wakati wa Saqifa. Hivyo hakuna shaka kwamba suala hili halikuamuliwa kwa wingi wa kura, wachilia mbali Ijma. Ibn Abdul-Birr Qartabi, mwanacuoni mkubwa wa madhehebu yenu, katika kitabu chake Istiab, Ibn Hajar katika Isaba, na Maulamaa wengine wanaandika kwamba, Sad Bin Ubaida, ambaye alikuwa ni mgombea wa Ukhalifa, kwa msimamo mkali kabisa alikataa kula kiapo cha utii kwa Abu Bakr na Umar. Hakutaka kusababisha vurugu, hivyo aliondoka na kwenda Syria. Kwa mujibu wa riwaya katika Rauzatus-Safa, kwa uchochezi wa mtu maarufu, yeye aliuawa. Kwa mujibu wa wanahistoria, mtu ambaye alitenda jinai hiyo ni Khalid Bin Walid. Baada ya kumuua Malik Bin Buwaira na kumuoa mke wake, wakati wa mwanzo wa Ukhalifa wa Abu Bakr, Umar akawa ni mwenye kumchukia sana, wakati Umar alipokuwa khalifa, Khalid akamuua Sad Bin Ubaida kwa ajili ya kutaka kupata upendeleo wa Umar. Hafidh: Kwa vile kulikuwa na hatari ya vurugu, na hawakuweza kupata mawasiliano kwa umma wote, walilazimika kutegemea juu ya hao watu wachache waliokuwepo Saqifa ambako kiapo cha utii kilichukuliwa. Baadaye Umma waliuridhia (Ukhalifa huo). Muombezi: Kama kulikuwa hakuna njia za kuwasiliana na Masahaba mashuhuri wa Mtume (saw), na wasomi wa Umma ambao walikuwa nje ya Madina, tafadhali tuambie kwa ikhlasi: Kama kulikuwa hakuna njama katika suala hili, kwa nini wasiwaite wale walio kuwepo mjini Madina kwenye mkutano wa Saqifa? Je, haikuwa ni muhimu kwao kupata ushauri wa Abbas, Ali ibn Abu Talib, na Bani Hashim? Je, maoni ya Umar na Abu Ubaida Bin Jarra yalitosha kwa ulimwengu wote wa ki-Islam? Hoja yako iliyotegemea juu ya Ijma, iwe ya jumla au makhususi, haikubaliki. Wasomi na Masahaba wakubwa hawakushiriki kwayo, badala yake waliipinga. Kama nilivyosema: Ijmai maana yake ni kwamba asiwepo hata na mtu mmoja ambaye hakubaliani na wengine. Katika Ijma hii umekiri kwamba wasomi kwa ujumla hawakushiriki. Imamu Fakhrud-Din Razi katika Nihayatul-Usul anasema kwamba, kulikuwa hakuna Ijmai ya makubaliano katika Ukhalifa wa Abu Bakr na Umar, mpaka baada ya kuuawa kwa Sad Bin Ubaida. Nashindwa kuelewa vipi unaiita Ijmai hii ya kuwazika kuwa ni uthibitisho kwa ajili ya uhalali wa Ukhalifa. Dai lako la pili, kwamba Abu Bakr alikuwa mtu mzima kuliko Ali na kwa hiyo alikuwa anafaa zaidi kwa ajili ya Ukhalifa ni dhaifu kuliko hoja ya kwanza. Kama umri ulikuwa sharti juu ya Ukhalifa, basi walikuwepo watu wazima wengi kuliko Abu Bakr na Umar. Kwa hakika Abu Qahafa, baba yake Abu Bakr alikuwa mkubwa kuliko mtoto wake, na alikuwa yu hai wakati ule. Kwa nini asichaguliwe kuwa Khalifa? Hafidh: Umri wa Abu Bakr ukiungana na uwezo wake, ulimfanya kuwa chaguo la sawa sawa. Wakati kulikuwa kuna mzee, mwenye ujuzi, mtu anayependwa na Mtume katika Umma, kijana mdogo asiye na uzoefu hawezi kupewa amana ya uongozi.

192

Mikesha ya Peshawar
Muombezi: Kama hiyo ingekuwa ni kweli, basi shabaha ya upinzani wako ni Mtume mwenyewe. Wakati alipoondoka kwenda kwenye vita vya Tabuk,wanafiki kwa siri walipanga kufanya maasi mjini Madina wakati akiwa hayupo. Kwa hiyo aliteua mtu mzoefu kushika nafasi yake ili aweze kudhibiti hali mjini Madina na kuivunja ile mipango ya wanafiki. Nakuomba utueleze, Mtume alimuacha nani katika nafasi yake mjini Madina kama mrithi na Khalifa wake? Hafidh: Inajulikana sana kwamba alimfanya Ali khalifa na mrithi wake. Muombezi: Je, Abu Bakr, Umar na masahaba wengine wazee zaidi hawakuwepo Madina wakati huo? Ndio. Na bado Mtume akamfanya kijana mdogo, Ali, kuwa Khalifa na mrithi wake. Kwa ajili ya kusoma baadhi ya aya za Sura ya Al-Baraa, ya Qurani Tukufu kwa watu Makka, mtu pengine angefikiri kwamba, mtu mzoefu lazima angekuwa anafaa kwa kazi hiyo. Lakini Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimurudisha mzee Abu Bakr kutoka kwenye nusu ya safari yake, na akamuamuru yule kijana mdogo, Ali kutekeleza jukumu hili muhimu. Mtukufu Mtume akasema kwamba Allah amemwambia kwamba mtu wa kuwasilisha hiyo Qurani tukufu lazima awe ni yeye mwenyewe Mtume au mtu ambaye anatokana naye. Halikadhalika, kwa ajili ya kuwaongoza watu wa Yemen, kwa nini Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimtuma Kiongozi wa Waumini Ali badala ya mzoefu zaidi Abu Bakr, Umar, au wengine waliokuwepo pale? Na katika matukio mengi kama haya, wakati wakiwepo Abu Bakr, Umar na wengine, alimteua Ali kutekeleza majukumu makubwa. Hivyo ina maana kwamba ukhalifa unaousisitiza ni ustahili. Imenijia hivi punde tu kwamba uthibitisho wa nguvu wa kukataliwa kwa ukhalifa wa watu hawa ni upinzani wa ile inayoitwa ijmai kwa Ali, ambaye kwa mujibu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), alikuwa ni mwenye kubainisha kati ya haki na batili. Maulamaa wenu mashuhuri wamesimulia hadithi nyingi kuhusiana na suala hili. Sheikh Suleimani Balhki Hanafi katika kitabu chake Yanabiul-Mawadda, Sura ya 16 akinukuu kutoka Kitabus-Sabiin-Fi-Fadhail-e-Amirul-Muminin, Imamul-Haram Abu Jafar Ahmad bin Abdullah Shafii, katika hadithi ya 12 iliyosimuliwa kutoka Firdaus ya Dailami ya hadithi ya sabini, Mir Sayyid Ali Hamadani Shafii katika Mawaddatul-Qurba, Mawadda ya 6, Hafidh katika kitabu chake Amali, Muhammad bin Yusuf Ganji Shafii katika kitabu chake Kifayatut-Talib, Sura 44 anasimulia pamoja na hitilafu ndogo katika maneno, kutoka kwa Ibn Abbas, Abi Laila Ghifari, na Abu Dharr Ghifari kwamba, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema (kifungu cha mwisho kikiwa sawa katika kila hadithi): Punde tu baada ya kuondoka kwangu kwenye ulimwengu huu, yatatokea machafuko. Wakati yakitokea, lazima mumfuate Ali Bin Abi Talib kwa vile atakuwa mtu wa kwanza kukutana na mimi na kupeana mikono na mimi katika Siku ya Hukumu. Yeye ametukuka kwa daraja na ni mwenye kubainisha kati ya haki na batili. Wakati Mtume alipofariki, machafuko makubwa yalitokea. Muhajirina na Ansar walitaka

193

Mikesha ya Peshawar
kupata Khalifa kutoka upande wao. Kwa mujibu wa maelekezo ya Mtume, Umma ulipaswa kumleta Ali ili kwamba aweze kubainisha kati ya haki na batili. Hafidh: Hadith hii ina simulizi pekee (Hadith Ahad) na kwa hiyo si ya kutegemewa. Muombezi: Nilikwisha jibu pingamizi lako kuhusu hadithi pekee. Maulamaa wa ki-Sunni huchukulia hadithi kama hiyo kama hoja ya msingi, hivyo huwezi kuikataa katika misingi hiyo. Mbali na hilo, sio hadithi hiyo pekee katika jambo hili. Kuna riwaya nyingi kama hizo zilizosimuliwa na Maulamaa wenu wenyewe ambazo zinaelekeza kwenye maana hiyo hiyo, ambzo baadhi yake nimezitaja katika mikesha iliyopita. Kwa kuzingatia kikwazo cha muda wetu kuwa mfupi, nitakomea katika kutaja tu hapa baadhi ya majina ya waandishi. Moja ya riwaya hizi inasimuliwa na Muhammad Bin Talha Shafii katika kitabu chake Matalibus-Suul, Tabari katika Tafsir Kabir, Baihaqi katika Sunan yake, Nurd-Din Maliki katika kitabu chake Fusull-Muhima, Hakim katika kitabu chake Mustadrak, Hafidh Abu Naim katika kitabu chake Hilya, Ibn Asakir katika kitabu chake Tarikh Ibn Asakir, Ibn Abil-Hadid katika Sharhe yake ya Nahjul-Balagha, Tabrani katika kitabu chake Ausat, Muhibud-Din katika kitabu chake Riyaz Hamwaini katika kitabu chake Faraid, Suyuti katika kitabu chake Durr-e-Mansur, kutoka kwa Ibn Abbas, Salman, Abu Dharr na Hudhifa wote wanasimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), akinyoosha mkono wake kuelekea kwa Ali Bin Abi Talib, alisema: Hakika huyu Ali ndiye mtu wa kwanza ambaye alitangaza imani yake kwangu na wa kwanza ambaye atakayepeana mikono na mimi katika Siku ya Hukumu. Yeye ni Siddiq-e-Akbar (mkweli mkubwa) na Faruq wa Umma huu (mtambuzi wa Umma huu). Atabainisha kati ya haki na batili.

HADITH ALI YUKO PAMOJA NA HAKI NA HAKI IKO PAMOJA NA ALI


Muhammad Bin Yusuf Ganji katika Sura ya 44 ya kitabu chake Kifayatut-Talib anasimulia hadithi hiyo hiyo pamoja na nyongeza ya maneno: Na ni mtawala juu ya waumini na ni mlango wangu kwa ajili ya kupitia waumini; na ni Khalifa (mrithi) wangu baada yangu. Ganji Shafii anasema kwamba Muhadith-e-Sham (mwanahadithi wa Syria) anazo hadithi mia tatu zenye kumsifia Ali. Vile vile imeandikwa na Muhammad Bin Talha Shafii katika kitabu chake Matalibus-Suul, Khatib Khawazimi katika Manaqib, Samani katika Fadhailus-Sahaba, Ibn Sabbagh Malik katika Fusulul-Muhimma, Khatib Baghdadi katika Tarikh-e-Baghdad, Jz. 14, uk. 21, Hafidh Mardawaih katika Manaqib, Dailami katika Firdaus, Ibn Qutayba katika Imama was-Siyasa, Jz. 1, uk.111, Ganji Shafii katika Kifayatut-Talib, Imamu Ahmad Hanbal katika Musnad, na maulamaa wenu wengi wamesimulia kwamba, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: Ali yuko pamoja na haki na haki iko pamoja na Ali popote ageukiapo. Katika vitabu hivyo

194

Mikesha ya Peshawar
hivyo vile vile kuna hadith nyingine iliyosimuliwa na Sheikh Sulemani Qunduzi Hanafi, katika Sura ya 20 ya Yanabiul-Mawadda, kutoka kwa Hamwaini kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: Ali yuko pamoja na haki na haki iko pamoja na Ali. Hafidh Abi Naiim Ahmad ibn Abdullah Ispahani katika kitabu chake Hiyatul-Auliya Jz. 1, uk. 63, anasimulia kwamba, Mtume alisema: Enyi kundi la Ansar! Je, nikuelekezeni kwa mtu ambaye kama mkishikamana naye kamwe hamtapotea? Wote wakasema: Ndio, Ewe Mtume wa Allah. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: Mtu huyo ni Ali. Mpendeni kama mnavyonipenda mimi, na mheshimuni kama mnavyoniheshimu mimi, yale niliyokuambieni yalikuwa ni amri ya Allah iliyosimuliwa kwangu na Jibril. Lengo la ujumla la hadithi hizi ni kuonyesha dalili za upendeleo wa Mtume kuhusiana na mrithi wake. Mtume aliamrisha Umma wake kugeukia kwa Ali baada yake na kumfuata yeye. Kwa mwanga wa hadithi kama hizi, tueleze upinzani wa Ali kwa Abu Bakr una maanisha nini kwako. Kwa hakika inasikitisha sana na kushangaza kwamba haraka kubwa mno ilifanywa katika siku ya Saqifa. Kila mtu mwenye akili ambaye anajua yaliyotokea katika siku hiyo amefadhaika mno. Kama kulikuwa hakuna njama, kwa nini wasingoje (angalau kwa saa chache) ili kwamba Ali Bin Abi Talib, Bani Hashim, na Abbas waweze kuelezea maoni yao juu ya Ukhalifa? Hafidh: Kulikuwa hakuna njama. Kwa vile walihofia vurugu, walifanya haraka kuamua suala la Ukhalifa kwa ajili ya usalama wa Uislamu. Muombezi: Una maana kwamba Abu Ubaida Jarra, mchimba kaburi wa zamani wa Makka, na wengine walikuwa na wasiwasi zaidi na usalama wa Uislamu kuliko Abbas, ami yake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anayeheshimiwa, na Ali Bin Abi Talib? Una maana kwamba kama wangelingojea kwa muda kidogo, au kama Abu Bakr na Umar, wakiwashughulisha watu, wangemtuma Abu Ubaida kumjulisha Abbas na Ali juu ya hali hii mbaya, hilo lingefanya Uislamu uangamie? Tafadhali jaribu kuwa mkweli. Kama wangewakaribisha watu wanaostahili huko Saqifa, nafasi yao ingelikuwa salama zaidi. Kusingelikuwa na hitilafu katika Uislamu kama ilivyo leo. Baada ya miaka 1335, sisi ndugu wa ki-Islamu tusingezozana wenyewe kwa wenyewe kama tulivyo usiku huu, bali tungekuwa tumeungana katika kumpinga adui yetu wa pamoja. Sehemu kubwa ya msingi wa jengo hili lenye kasoro la Uislamu uliwekwa siku hiyo. Ilikuwa ni kwa ajili ya haraka za watu wale watatu za kutaka kukamilisha mipango yao ya siri. Nawab: Bwana mheshimiwa, tafadhali tueleze kwa nini walifanya haraka. Kwa nini wasiwajulishe hata watu waliokuwa Msikitini au katika nyumba ya Mtume? Muombezi: Sababu sio za kutafuta mbali. Walifanya haraka kwa sababu walijua kwamba kama wakingojea Waislamu wote waje, au angalau hata watu mashuhuri wa jeshi la Usama Bin Zaid, masahaba mashuhuri wa Mtume waliokuwepo mjini Madina, au Bani Hashim, jina la Ali, miongoni mwa mwa mengine, lingependekezwa. Uwezekano wa kisiasa wa

195

Mikesha ya Peshawar
Abu Bakr na Umar ungelipunguzwa sana. Hivyo basi waliharakisha mipango yao ili kwamba, wakati ambapo Bani Hashim na masahaba mashuhuri wakiwa wanajishughulisha na taratibu za mazishi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), wao walifanikiwa katika kumteua Abu Bakr kuwa Khalifa juu ya msingi wa kura za watu wawili! Waliucheza mchezo huo, na usiku huu hapa ninyi watu wazuri mnaupa jina la ijmai! Hata ulamaa wenu wakubwa, kama Tabari, Ibn Abil-Hadid na wengine wameandika kwamba Umar alisema: Ukhalifa wa Abu Bakr ulisimamishwa kwa haraka sana. Allah atusaidie! Amma kwa madai yenu mengine, ambayo mnayatoa kutoka kwa khalifa Umar, kwamba utume na utawala haviwezi kuchanganywa kwenye familia moja, vile vile yanakataliwa kwa mujibu wa Qurani Tukufu:

Au wanawahusudu watu kwa yale aliyowapa Allah kutokana fadhila Zake? Basi tuliwapa ukoo wa Ibrahim Kitabu na hikma na tukawapa mamlaka makubwa. (4:54) Hadithi hii ambayo inahusishwa na Khalifa Umar, ni ya kubuniwa. Mtume kamwe hajasema neno lenye kukinzana na amri ya Qurani Tukufu. Aidha, ukhalifa hauwezi kutenganishwa na utume kwa sababu Khalifa wa kweli ni mfano wa sheria ya Mungu inayofanya kazi ulimwenguni. Kuuchukulia ukhalifa kama kazi ya kisiasa tu iliyotenganishwa na utume ndio kosa lenyewe hasa lililofanywa na Abu Bakr na Umar. Kama Harun, ndugu yake Mtume Musa, angeweza kuondolewa kwenye ukhalifa wa Musa, Ali vile vile angeweza kunyimwa ukhalifa wa Mtume. Na kwa vile utume na ukhalifa, kwa mujibu wa Qurani, vilichanganywa juu ya Musa na Harun, hapana shaka ulichanganywa juu ya Muhmmad na Ali. Hadithi yenu hii ilibuniwa na Bani Umayya. Kama utume na ukhalifa usingeweza kuchanganywa katika familia moja, basi kwa nini katika Majilis-eShura (Kamati ya ushauri) Khalifa Umar alimpendekeza Ali kwenye ukhalifa? Hata hivyo, ninyi vile vile mnamkubali kuwa ni Khalifa wenu wa nne! Ni ukinzano wenye kushangaza kwamba kwa kumetegemea juu ya hadithi ya Umar, mnakataa kuchanganywa utume na ukhalifa, lakini wakati Umar mwenyewe alipoidhinisha hali hii miaka michache baadae, mkaiunga mkono! Je, mnaweza kupinga na kuunga mkono pendekezo lile lile moja? Mnasema kwamba utume na utawala havichanganywi katika familia moja, ingawa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amefanya kuwa ni wajibu kwa Umma wake kufuata kizazi chake. Alisema kwamba kuwa na uadui nao ni kupotea njia. Amesema katika mara nyingi, Ninakuachieni vitu viwili vizito: Kitabu cha Allah (Qurani Tukufu) na Ahulul-Bayt wangu. Kama mkifungamana na viwili hivi, kamwe hatapotea baada yangu. Hadithi hii sahihi imekubaliwa na madhehebu zote. Nimeitaja katika mikesha iliyopita pamoja na vyanzo vyake.

196

Mikesha ya Peshawar

HADITHI YA SAFINA HADITHI YA SAQIFA


Wakati wa mafuriko makubwa yeyote yule ambaye alichukuwa hifadhi katika safina ya Huh aliokolewa. Yeyote yule ambaye aliipa mgongo akaacha kuipanda aligharikishwa, ikiwa ni pamoja na mtoto wa Nuh. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) vile vile aliwatambulisha kizazi chake kama Safina ya Nuh, akimaanisha kwamba watu wa umma wake katika wakati wa mitihani lazima wajiambatanishe na kizazi chake. Kwa hiyo, kwa mujibu wa maamrisho haya ya wazi, umma katika hitilafu zao zote, wanapaswa kutafuta manufaa ya Ahlul-Bayt wa Mtume. Ali Bin Abu Talib, kwa mujibu wa Mtume alikuwa ndiye msomi zaidi na mtu bora zaidi miongoni mwao. Kwa nini hawakumjulisha wakapata kushauriana naye? Lakini wapi! Hawakufanya hivyo. Wanasiasa walinyakuwa mamlaka na wakamnyima Ali haki yake ya kudumu. Sheikh: Ni kwa misingi ipi unasema kwamba wangelimfuata Ali na kwamba maoni na ijmai ya masahaba ingelipaswa kuachwa? Muombezi: Sijasema kwamba maoni ya Masahaba na ijma yao haipaswi kuheshimiwa. Tofauti moja kati yenu na mimi ni kwamba mara tu mnaposikia jina la sahaba, hata kama akiwa ni mnafiki, kama Abu Huraira, ambaye Khalifa Umar alimpiga na kumuita mwongo, mnamuinamia kwa heshima. Nawaheshimu mashaba wale tu ambao wanachukuana na masharti ya uswahiba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Aidha nimeonesha kwamba kulikuwa hakuna ijma ndani Saqifa. Kama mnaweza kupinga hoja yangu, sasa ni wakati wa kufanya hivyo. Nitakubaliana na muafaka wa hadhara hii. Kama mnaweza kuonyosha kutoka kwenye vitabu nyenu kwamba ndani ya Saqifa, umma wote au watu wasomi wenye akili wa umma walikusanyika pamoja na kukubaliana kwamba Abu Bakr awe Khalifa, tutakuwa tayari kulibali hilo. Na kama ukiondoa watu wawili (Umar na Abu Ubaida) na watu wachache wa kabila la Aus, hakuna mtu mwingine aliyekula kiapo cha utii, lazima mkubali kwamba sisi Mashia tumeongozwa sawasawa. Tunaliacha kwenye maoni ya kisomi kuamua iwapo masahaba watatu walikuwa na haki ya kushikilia hatamu za umma wote. Wawili walikula kiapo kwa wa tatu, na baadae wakawatishia wengine kwa panga, moto, na fadheha, kuwalazimisha kukubali utashi wao.

197

Mikesha ya Peshawar

JE, IJMAI INAPASWA KUKUBALIWA KWA SABABU YA KIGEZO CHA YALIYOPITA?


Sheikh: Hatujui kama kulikuwa na uzembe kwa upande wao kwa sababu hatukuwepo kule siku hiyo. Katika muda huu mrefu hatuwezi kutambua walikuwa katika shinikizo la aina gani. Leo pamoja na hali hiyo kuwa ni ukweli uliothibiti, sio neno iwapo kama ijma ilikamilishwa katika hatua za pole pole. Hatupaswi kupinga. Lazima tukubaliane na watu wale na tufuate njia waliyotuonyesha. Muombezi: Uzuri ulioje wa hoja hiyo! Unatutaka sisi tufikirie kwamba Uislamu hauna misingi? Kama watu wawili au watatu wakiunda mpango na wakaungwa mkono na watu wengine, je, ni jukumu la Waislamu kuwafuata wao? Je, hiyo ndio maana ya dini ya Mtume wa Uislamu? Qurani Tukufu inasema: Basi wabashirie waja wangu, wale ambao husikiliza maneno, wakafuata lililo bora lao (39:17-18) Uislamu umesimama juu ya misingi ya kweli na hoja, sio juu ya kufuata kibubusa, naam kwa hakika si kwa kumfuata Abu Ubaida, mchimba kaburi. Mtume alituonesha njia. Alisema kwamba wakati umma ukiwa umegawanyika, lazima tumfuate mtu ambaye ameongozwa. Unatuuliza ni kwa nini ni wajibu juu yetu kumfuata Ali. Tunajibu kwamba wajubu huo umetegemea juu ya aya za Qurani na hadithi zilizoandikwa katika vitabu vyenu wenyewe.

HADITHI ZA MTUKUFU MTUME (S.A.W.W.) ZINAZOWAHIMIZA WAUMINI KUMFUATA ALI


Kuna hadithi nyingi ambazo hufanya wajibu juu ya umma kumfuata Ali. Mojawapo ya hizo imesimuliwa na Ammar-e-Yasr, ambayo imeandikwa na maulamaa wenu wafuatao katika vitabu vyao: Hafidh Abi Nuaim Ispahani katika Hilya; Muhammad Bin Talha Shafii katika Matalibus-Suul; Baladhuri katika Tarikh; Sheikh Sulaiman Balkhi Hanafi katika Yanabiul-Mawadda, Sura ya 43, kutoka kwa Hamwaini; Mir Sayyid Ali Hamadani Shafii katika Mawaddatul-Qubra, Mawadda ya 5; Dalami katika Firdaus. Wanasimulia hadithi ndefu yenye maelezo kinaganaga ambayo haiwezi kusimuliwa hapa kwa ukamilifu. Inaweza kuelezewa kwa ufupi tu kwamba, wakati walipomuuliza Abu Ayyub kwa nini alikwenda kwa Ali na hakuchukua kiapo cha utii kwa Abu Bakr, yeye alijibu kwamba siku moja alikuwa amekaa na Mtume wakati Ammar-e-Yasir alipokuja na kumuuliza Mtume swali. Katika kuendelea na mazungumzi yao, Mtume akasema: Ewe Ammar! Kama watu wote watakwenda njia mmoja, na Ali peke yake akaenda njia

198

Mikesha ya Peshawar
nyingine, itakupasa kumfuata Ali. Ewe Ammar! Ali hatakuruhusu wewe kupotea kutoka kwenye njia ya mwongozo na hatakuongoza kwenye upotovu; Ewe Ammar! Utii kwa Ali ni utii kwangu, na utii kwangu ni utii kwa Allah. Katika mwanga wa Maamrisho haya, na katika mwanga wa upinzani wa Ali kwa Abu Bakr, je, watu siwangemfuata Ali? Hata kama Bani Hashim, Bani Umayya, Masahaba mashuhuri, watu wajuzi wenye elimu wa umma, Muhajirina, na Ansari wasingekuwepo pamoja naye (na walikuwa pamoja naye) watu wangelimfuata Ali. Hafidh: Wakati wa mjadala wetu, umesema vitu viwili vya ajabu. Kwanza, umerudia rudia kumuita Abu Ubaida mchimba kaburi. Unaweza kuthibitisha kwamba hii ilikuwa taaluma ya bwana mkubwa huyu? Pili, umesema kwamba Ali, Bani Hashim, na masahaba hawakula kiapo cha utii kwa Abu Bakr, walimpinga. Lakini wanahistoria na wanahadithiwote wameandika kwamba Ali, Bani Hashim na masahaba wa Mtume walikula kiapo cha utii kwa Abu Bakr. Muombezi: Sio sisi peke yetu tunaodai kwamba Abu Ubaida alikuwa mchimba kaburi. Imo katika vitabu vyenu wenyewe. Unawza kurejea kwenye Al-Bidayya wan-Nihaya, Jz. 5, uk. 266-267 (kitabu) kilichokusanywa na Ibn Kathir Shami, ambaye anasema kwamba, kwa vile Abu Ubaida amezoea kuchimba kaburi za watu Makka, Abbas alimtuma mtu kumtafuta Abu Talha, mchimba kaburi wa Madina, na mtu mwingine kumtafuta Abu Ubaida, ili kwamba wote wawili waweze kuchimba kaburi la Mtume.

KULAZIMISHWA KWA ALI NA BANI HASHIM KULA KIAPO BAADA YA MIEZI SITA
Unasema kwamba Ali, Bani Hashim, na masahaba wa Mtume walikula kiapo cha utii kwa Abu Bakr. Umesoma maneno walikula kiapo cha utii, lakini hukuelewa ni kwa nani na vipi walivyokula kiapo. Wanachuoni wenu wote wa hadithi na wanahistoria wakubwa wameandika kwamba Ali na Bani Hashim walikula kiapo cha utii (kwa nje), lakini hilo limefanywa baada ya miezi sita, na hata hivyo chini ya vitisho vikubwa. Hafidh: Sio vyema kwa mtu mtukufu kama wewe kutumia maneno ambayo hutumiwa na Mashia wa kawaida kwamba, Ali aliburuzwa kutoka kwenye nyumba yake na alitishiwa kuuawa kama asingekula kiapo cha utii. Ukweli ni kwamba katika siku chache za mwanzo za ukhalifa kwa utashi na kwa furaha alikubali ukhalifa wa Abu Bakr. Muombezi: Ali na Bani Hashim hawakula kiapo cha utii kwa mara moja. Wanahistoria wenu wameandika kwamba Ali alikula kiapo cha utiibaada ya kifo cha Hadhrat Fatima. Bukhari katika katika Sahih yake, Jz. 3, Sura ya Ghazawa Khaibar, uk. 37, na Muslim Bin Hujjaj, katika Sahih yake, Jz. 5, uk. 154, wameandika kwamba Ali alikula kiapo cha utii

199

Mikesha ya Peshawar
baada ya kifo cha Fatima. Baadhi ya maulamaa wenu wanaamini kwamba Fatima alikufa siku 75 baada ya kifo cha Mtume. Ibn Qutayba vile vile anashikilia maoni hayo hayo, lakini wanahistoria wenu wengi wanadai kwamba alikufa miezi sita baada ya kufariki kwa Mtume. Kwa hiyo ina maana kwamba kiapo cha Ali kilikuja wakati fulani baada ya miezi 3 au 6 baada ya kufariki kwa Mtume. Masudi katika kitabu chake Murujus-Sahab, Jz. 1, uk. 414, anasema: Hakuna mtu kutoka Bani Hashim aliyekula kiapo cha utii kwa Abu Bakr mpaka baada ya kifo cha Bibi Fatima. Ibrahim Bin Saqafi anasimulia kutoka kwa Zuhri kwamba Ali hakula kiapo cha utii kwa Abu Bakr mpaka miezi sita baada ya alipofariki Mtume, na watu hawakuwa na ujasiri wa kumshawishi isipokuwa baada ya kifo cha Bibi Fatima. Ibn Abil-Hadid katika Sharhe Nahjul-Balagha anasimulia jambo hilo hilo. Kwa hali yoyote, maulamaa wenu wenyewe wanasisitiza kwamba kiapo cha Ali hakikuwa cha haraka bali kilikuja tu baada ya muda fulani kupita na hata hivyo ni wakati mazingira yalipomlazimisha kufanya hivyo. Ibn Abil-Hadid, katika Sharhe Nahjul-Balagha, Jz. 2, uk. 18, anasimulia kutoka kwa Zuhri, kutoka kwa Aisha, ambaye amesema: Ali hakula kiapo cha utii kwa Abu Bakr kwa muda wa miezi sita, na hakuna mtu kutoka Bani Hashim aliyekula kiapo mpaka Ali alipofanya hivyo. Ahmad Bin Asam-e-Kufi Shafii katika Futuh na Abu Nasr Hamidi, katika Jama Bainus-Sahihain anasimulia kutoka kwa Nafiy, akinukuu kutoka Zuhri, ambaye alisema: Ali hakula kiapo cha utii mpaka baada ya miezi ya kufariki kwa Mtume (s.a.w.w.).

ALI ALIBURUZWA KUTOKA NYUMBANI KWAKE NA NYUMBA YAKE IKACHOMWA MOTO


Hafidh: Ni wapi maulamaa wetu waliposema kwamba Ali aliburuzwa kutoka kwenye nyumba yake na nyumba ikachomwa moto, kama kwa kawaida inavyoaminiwa na Mashia? wanalisimlia hili kwa mhemuko mkubwa katika majlis zao za kidini. Vile vile huchochea hisia za watu kwa kusema kwamba Fatima aliteswa na hatimaye akaharibu mimba yake. Muombezi: Waheshimiwa mliohudhuria mnawashutumu Mashia, mkijaribu kuficha makosa ya viongozi wenu waliotangulia. Mnasema kwamba hadithi hizi zimebuniwa na Mashia. Ukweli ni kwamba kwa amri ya Abu Bakr, Umar na wenzake walikwenda nyumbani kwa Ali, wakamtisha kwa upanga, wakamburuza mpaka Msikitini na wakamlazimisha kula kiapo cha utii kwa Abu Bakr. Ukweli huu umeandikwa na maulamaa wenu wenyewe. Kama mnataka, nitakusimulieni. Hatusemi kitu chochote kutoka kwenye vitabu vyetu. Tunasema kile mnachosema ninyi. Hafidh: Ndio, tafadhali endelea. Tuko tayari kusikiliza.

200

Mikesha ya Peshawar

HOJA KUMI NA MBILI ZINAZOUNGA MKONO UKWELI KWAMBA ALI ALICHUKULIWA KUPELEKWA MSIKITINI KWA NCHA YA UPANGA
Muombezi: (1) Abu Jafar Baladhuri Ahmad Bin Yahya Bin Jabir Baghdadi, mmoja wa wanahadithi na wanahistoria wenu wa kutengemewa, anaandika katika kitabu chake cha Tarikh - Historia kwamba, wakati Abu Bakr alipomuita Ali ili kula kiapo cha utii, Ali alikataa. Abu Bakr alimtuma Umar akiwa na kijinga kwenda kuchoma moto nyumba ya Ali. Fatima akaja mlangoni na kusema: Ewe mtoto wa Khattab! Umekuja kuichoma nyumba yangu? Akasaema: Ndio, hili lina athari zaidi kuliko kitu chochote alichokifanya baba yako. (2) Izzud-Din Ibn Abil-Hadid Mutazili, na Muhammad Bin Jarir Tabari, wanasimulia kwamba Umar alikwenda kwenye mlango wa nyumba ya Ali pamoja na Usay Bin Khuzai, Salama Bin Aslam na kikundi cha watu. Kisha Umar akaita, Tokeni nje! Vinginevyo nitaichoma nyumba yenu! (3) Ibn Khaziba anataarifu katika kitabu chake Kitab-e-Gharrar kutoka kwa Zaid Bin Aslam, ambaye alisema: Nilikuwa mmoja wa wale waliokwenda pamoja na Umar tukiwa na vijinga vya moto mpaka kwenye mlango wa nyumba ya Fatima. Wakati Ali na watu wake alipokataa kula kiapo cha utii, Umar alimuambia Fatima: Yeyote yule aliyeko ndani ya nyumba atoke nje. Vinginevyo nitaichoma nyumba na yeyote aliyemo ndani.Ali, Hasani, Husein, Fatima, na kikundi cha Masahaba wa Mtume, na Bani Hashim walikuwemo ndani. Fatima akasema: Utaichoma nyumba yangu moto pamoja na mimi mwenyewe na watoto wangu? Akasema: Ndio, Wallahi, kama hawatoki nje na kula kiapo cha utii kwa Khalifa wa Mtume. (4) Ibn Abd Rabbih, mmoja wa maulamaa wenu mashuhuri, anaandika katika kitabu chake Iqdul-Farid, Jz. 3, uk. 63, kwamba Ali na Abbas walikuwa wamekaa nyumbani kwa Fatima. Abu Bakr akamuambia Umar: Nenda ukawalete watu hawa. Kama wakikataa kuja, pigana nao. Hivyo Umar akaenda nyumbani kwa Fatima na vijinga vya moto. Fatuma akaja mlangoni na akasema: Umekuja kuchoma nyumba yetu? Akasema: Ndio na kadhalika. (5) Ibn Abil-Hadid Mutazili katika sharhe yake ya Nahjul-Balagha, Jz. 1, uk. 134, akinukuu kutoka kitabu cha Jauhari, Kitab-e-Saqifa ameandika kwa kinaganaga

201

Mikesha ya Peshawar
kuhusu suala la Saqifa-e-Bani Saad: Bani hashim na Ali walikuwa wamekusanyika nyumbani kwa Ali. Zubair pia alikuwemo kwa vile naye alijiona kama ni mmoja wa Bani Hashim. Ali alizoea kusema, Zubair alikuwa siku zote pamoja nasi mpaka watoto wake walipokuwa wakubwa. Wao wakamgeuza dhidi yetu. Umar akaenda nyumbani kwa Fatima na kikundi cha watu. Usayd na Salma vile vile walikuwa pamoja naye. Umar akawataka watoke nje wachukue kiapo cha utii. Wao wakakataa. Zubair akachomoa upanga wake na akatoka nje. Umar akasema: Mkamateni mbwa huyu. Salma Bin Aslam akamnyanganya upanga huo na akautupa kiambazani. Kisha wakambururuza Ali kumpeleka kwa Abu Bakr. Bani Hashim wengine wakamfuata na walikuwa wanangojea kuona Ali atafanya nini. Ali alikuwa akisema kwamba yeye ni mtumishi wa Allah na ndugu yake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Hakuna aliyemsikiliza. Walimpeleka kwa Abu Bakr, ambaye alimtaka kula kiapo cha utii kwake. Ali akasema: Mimi ndiye ninayestashiki zaidi katika nafasi hii, na sitakula kiapo cha utii kwako. Ni wajibu juu yako kula kiapo cha utii kwangu. Umeichukuwa haki hii kutoka kwa Ansar kwa kutegemea uhusiano wako na Mtume (s.a.w.w.). Na mimi vile vile, kwa msingi huo huo, nalalamika dhidi yako. Hivyo kuwa muadilifu. Kama unamuogopa Allah, kubali haki yangu, kama Ansar walivyofanya kwa yako. Vinginevyo, itakupasa ukubali kwamba unanidhulumu kwa makusudi. Umar akasema: Hatutakuacha mpaka ule kiapo cha utii. Ali akasema: Mmekula njama wote vizuri sana. Leo unamuunga mkono, ili kwamba kesho aweze kuurudsha ukhalifa kwako. Naapa Wallahi kwamba sitakubaliana na maombi yenu na sitakula kiapo cha utii (kwa Abu Bakr). Yeye anapaswa atoe kiapo cha utii kwangu. Kisha aliwageukia watu na akasema: Enyi Muhajirina! Muogopeni Allah. Msipore haki ya mamlaka ya familia ya Muhammad. Haki hiyo imeamriwa na Allah. Msimuondoe mtu anayestahiki kutoka katika nafasi yake. Kwa jina la Allah sisi Ahlul-Bayt tuna mamlaka makubwa katika suala hili kuliko mlivyo ninyi. Kuna mtu miongoni mwenu ambaye ana ujuzi juu ya Kitabu cha Allah (Qurani), Sunna ya Mtume, na sheria za dini yenu. Ninaapa Wallahi sisi tunavyo vitu vyote hivi. Hivyo msifuate nafsi zenu mkaja mkapotea kutoka kwenye ukweli. Ali alirudi nyumbani bila kula kiapo cha utii na akajitawisha mwenyewe nyumbani kwake mpaka Fatima alipofariki. Hapo tena, alilazimishwa kula kiapo cha utii. (6) Abu Muhammad Abudullah Bin Muslim bin Qutayba Bin Umar Al-Bahili Dinawari, ambaye alikuwa mmoja wa maulamaa na Kadhi rasmi wa mji wa Dinawari, anaandika katika kitabu chake mashuhuri Tarikhul-Khulafati Raghibin wa Daulati Bani Umayya, kijulikanacho kama Al-Imama was-Siyasa, Jz. 1, uk. 13: Wakati Abu Bakr alipofahamu kwamba kundi la watu walio na uadui kwake wamekusanyika katika nyumba ya Ali, alimtuma Umar kwao. Wakati Umar alipompigia kelele Ali atoke nje na kula kiapo cha utii kwa Abu Bakr, wote walikataa kutoka nje. Umar alikusanya kuni na kusema Naapa kwa jina la Allah, ambaye ana uhai wangu katika miliki Yake,

202

Mikesha ya Peshawar
amma mtatoka nje, au nitaichoma nyumba pamoja na wote waliomo ndani. Watu wakasema: Ewe Abu Hafsa! Fatima vile vile yumo ndani. Akasema: Hata akiwemo, nyumba nitaichoma moto tu. Hivyo wote wakatoka nje na kula kiapo cha utii, isipokuwa Ali, ambaye alisema: Nimeweka nadhiri kwamba, mpaka nitakapomaliza kuikusanya Qurani, sitatoka nje ya nyumba wala kuvaa nguo kiukamilifu. Umar hakulikubali hili, lakini malalamiko ya huzuni ya Fatima na kubezwa na wengine, kulimlazimisha kurudi kwa Abu Bakr. Umar alimhimiza kumlazimisha Ali atoe kiapo cha utii. Abu Bakr alimtuma Qanfaz mara kadhaa kumuita Ali, lakini safari zote alikatishwa tamaa. Mwishowe Umar, na kundi la watu walikwenda kwenye mlango wa nyumba ya Fatima. Wakati Fatima aliposikia sauti zao, alipiga kelele: Ewe baba yangu, Mtume wa Allah! Ni mateso gani haya tunayopata kutoka kwa mtoto wa Khattab na mtoto wa Abi Quhafa! Wakati watu hao walipoyasikia malalamiko ya Fatima, baadhi yao walirudi nyuma mioyo yao ikiwa imevunjika, lakini Umar alibaki pale na baadhi ya watu wengine mpaka mwishowe wakamburuza Ali kutoka nje ya nyumba. Walimchukuwa Ali na kumpeleka kwa Abu Bakr, na akamuambia achukue kiapo cha utii kwake. Ali alisema: Kama sikula kiapo cha utii kwako utanifanya nini? Wakasema: Tuna apa kwa jina la Allah kwamba tutaivunja shingo yako.Ali akasema: Mtamuuwa mtumishi wa Allah na ndugu wa Mtume? Umar akasema: Wewe sio ndugu wa Mtume wa Allah. Wakati haya yakijiri, Abu Bakr alinyamaza kimya. Kisha Umar akamuuliza Abu Bakr iwapo yeye (Umar) alikuwa hafuati amri yake katika suala hili. Abu Bakr akasema kwamba muda Fatima yuko hai hatamlazimisha Ali kula kiapo cha utii kwake. Kisha Ali aliweza kufikia kaburi la Mtume, ambako akiomboleza na kulia, alimueleza Mtume kile ambacho Harun alimueleza ndugu yake (Mtume Musa), kama ilivyoandikwa katika Qurani Tukufu:

..Ewe mtoto wa mama yangu! Hakika watu hawa wamenidharau, na wakakaribia kuniuwa( 7:150)

FATIMA ALIWAAMBIA ABU BAKR NA UMAR KWAMBA ANAWALAANI HAO WOTE KATIKA KILA SALA
Baada ya kuelezea Suala hili kwa urefu, Abu Muhammad Abdullah Bin Qutayba anasema kwamba Ali hakula kiapo cha utii na akarudi nyumbani. Baadae Abu Bakr na Umar walikwenda nyumbani kwa Fatima kumbembeleza na kuomba msamaha wake. Fatima akasema: Allah awe ni shahidi wangu kwamba ninyi wawili mmenikosea. Ninawalaani katika kila Salat, na nitaendelea kuwalaani mpaka nitakapomuona baba yangu na kumlalamikia dhidi yenu.

203

Mikesha ya Peshawar

(7) Ahmad Bin Abdul-Aziz ni mmoja wa maulamaa wenu. Ibn Abil-Hadid anaandika kuhusu yeye katika maneno yafuatayo: Alikuwa mtu msomi, mwanahadithi na mwandishi mkubwa. Yeye anaandika katika kitabu chake, Kitab-e-Saqifa, na Ibn AbilHadid Mutazili vile vile anamnukuu katika Sharhe Nahjul-Balagha, Jz. 1, uk. 9, kutoka kwa Abil-Aswad, ambaye amesema: Kundi la Masahaba na Muhajirina mashuhuri walielezea kuhusu kuudhiwa kwao na ukhalifa wa Abu Bakr na wakauliza ni kwa nini wao hawakushauriwa. Vile vile Ali na Zubair walionyesha hasira zao, wakakataa kula kiapo cha utii na wakarudi nyumbani kwa Fatima. Fatima alilia kwa nguvu na akawasihi kwa taadhima sana, lakini bila mafanikio yoyote. Walichukuwa upanga wa Ali na wa Zubair wakazirusha kwenye ukuta na kuzivunjilia mbali. Kisha wakawaburuza mpaka Msikitini na kuwalazimisha kula kiapo cha utii. (8) Jauhari anasimulia kutoka kwa Salma bin Abdur-Rahman kwamba wakati Abu Bakr aliposikia kwamba Ali, Zubair, na kundi la Bani Hashim walikuwa wamekusanyika nyumbani kwa Fatima, alimtuma Umar kwao. Umar alikwenda mpaka mlangoni mwa nyumba ya Fatima na akaita kwa sauti kubwa: Tokeni nje, vinginevyo, naapa nitaichoma nyumba yenu! (9) Jauhari, kwa mujibu wa Ibn Abil-Hadid katika sharhe ya Nahajul-Balagha, Jz. 2, uk. 19, anasimulia kutoka kwa Shabi: Wakati Abu Bakr aliposikia kuhusu mkusanyiko wa Bani Hashim katika nyumba ya Ali, alimuambia Umar: Wewe na Khalid nendeni mkamlete Ali na Zubair waje wale kiapo cha utii. Hivyo Umar aliingia nyumbani kwa Fatima na Khalid akabakia nje. Umar akamuambia Zubair Upanga huu ni wa nini? Akajibu, Nimeupata kwa ajili ya kula kiapo kwa Ali. Umar akaunyakua upanga ule na kuutupa kwenye jiwe ndani ya nyumba na kuuvunja. Kisha akamtoa nje kwa Khalid. Alirudi tena ndani ya nyumba ambako kulikuwa na watu wengi, akiwemo Miqdadi, na Bani Hashim wote. Akimsemesha Ali, alisema: Nyanyuka! Ninakupeleka kwa Abu Bakr. Lazima ule kiapo cha utii kwake. Ali akakataa. Umar akamburuza mpaka kwa Khalid. Khalid na Umar wakamlazimisha katika barabara ambayo ilikuwa imejaa watu ambao walishuhudia kitendo hiki. Wakati Fatima alipoona tabia hii ya Umar, yeye pamoja na wanawake wengi wa Bani Hashim (ambao walikuja kumliwaza), walitoka nje. Walikuwa wakiomboleza na kulia kwa vilio vya sauti ya juu. Fatima alikwenda msikitini ambako alimuambia Abu Bakr: Mapema ilioje umewafukuza Ahlul Bayt wa Mtume wa Allah. Naapa kwa jina la Allah, sitazungumza na Umar mpaka nitakapomuona Allah (yaani Siku ya Hukumu). Fatima alionesha kuchukizwa kwake mno na Abu Bakr na hakuzungumza naye kwa muda wote uliokuwa umebakia wa maisha yake. (Tazama Sahih Bukhari, sehemu ya 5 na 7). (10) Abu Walid Muhibud-Din Muhammad bin Muhammad Bin Ash-Shahna Al-Hanafi (amekufa 815 A.H.), mmoja wa maulamaa wenu wakubwa anaandika katika katika kitabu chake, Raudhatul-Manazir Fi Khabarul-Awail wal-Awakhir kuhusiana na

204

Mikesha ya Peshawar
suala la Saqifa: Umar alikwenda nyumbani kwa Ali akiwa amejiandaa kuichoma nyumba moto pamoja na wote waliokuwemo ndani yake. Umar alisema: Ingieni kwenye kile ambacho umma umeingia. Tabari, katika kitabu chake Tarikh Jz. 2, uk. 443, anasimulia kutoka kwa Ziyad Bin Kalbi kwamba, Talha, Zubair, na baadhi ya Muhajirin walikuwa nyumbani kwa Ali. Umar bin Khattab alikwenda huko na kuwataka watoke nje. Kama hawakutoka, alisema, angeichoma nyumba moto. (12) Ibn Shahna, katika Hashiyya-e-Kamil ya Ibn Kathir, Jz. 11, uk. 112, anaandika kuhusiana na suala la Saqifa kwamba: Baadhi ya Masahaba wa Mtume, na Bani Hashim, Zubair, Atba Bin Abi Lahab, Khalid Bin Said Bin As, Mikidadi Bin Aswad Kindi, Salman Farsi, Abu Dharr Ghifari, Ammar Bin Yasir, Baraa Bin Azib, na Ubai Bin Kab walikataa kula kiapo cha utii kwa Abu Bakr. Walijikusanya katika nyumba ya Ali. Umar Bin Khattab alikwenda kule kwa nia ya kuichoma nyumba. Fatima akamlalamika. Umar akasema: Ingia kule ambako wengine wameingia. Hizi ni sampuli tu za ukweli mwingi wa kihistoria ulioandikwa na wanahistoria wenu. Suala hili lilikuwa linajulikana sana kiasi kwamba washairi wa zamani wamelitaja. Mmoja wa washairi wenu, Hafidh Ibrahim wa Misr, anasema katika shairi la kumsifu Umar: Hakuna mtu mwingine bali Abu Hafsa (Umar) ambaye angelikuwa na ujasiri wa kumuambia mkuu wa ukoo wa Adnan (Ali) na jamaa zake, akisema: Kama mkishindwa kula kiapo cha utii, nitaichoma nyumba yenu, hata Fatima mwenyewe. Hafidhi: Hadithi hizi zinaonyesha tu kwamba walichukuwa vijinga vya moto kuwatisha na kuwatawanyisha wapinzani wa ukhalifa. Kusema kwamba nyumba ya Ali ilichomwa moto na matokeo yake Fatima kuharibu mimba yake, ni maneno yaliyobuniwa na Mashia.

RIWAYA KUHUSU KUHARIBIKA MIMBA YA FATIMA


Muombezi: Ungesoma Kitab-e-Isbatul-Wasiyya, kilichokusanywa na Abil-Hasan Ali Bin Husain Masudi, mwaandishi wa Murujudh-Dhahab. Aliandika kwa urefu sana kuhusu tukio la siku hiyo: Walimzingira Ali na kuchoma mlango wa nyumba yake. Walimburuza kumtoa nje ya nyumba na wakambana mbora wa wanawake, Fatima, kati ya mlango na ukuta kwa nguvu sana kiasi kwamba Muhsin, mtoto wake ambaye alikuwa hajazaliwa, akafa kwa mimba yake kuharibika. Mashia hawakuyabuni mambo haya. Kilichotokea kimehifadhiwa katika kurasa za historia. Kuharibika kwa mimba ni habari za kweli. Vile vile unaweza kurejea kwenye Sharhe Nahjul-Balagha, Jz, 3, uk. 351. Ibn Abil-Hadid anaandika kwamba alimuambia mwalimu wake, Abu Jafar Naqib, kwamba wakati Mtume

205

Mikesha ya Peshawar
alipoelezwa kwamba Hubbar Bin Aswad amevipiga vitoto vya binti yake (vikiwa tumboni bado) kwa mkuki, ambapo kwa sababu hiyo Zainab akaharibu mimba yake, Mtume aliruhusu yeye auwawe. Abu Jafar akasema: Lau Mtume wa Allah angelikuwa hai bado, kwa hakika angeamuru adhabu ya kifo vile vile kwa yule ambaye amemtisha Fatima kiasi kwamba mtoto wake Muhsin, alikufa kwa mimba yake kuharibika. Hafidhi: Sielewi inasaidia lengo gani la manufaa kwa kusimulia visa hivi. Mambo ya aina hii husababisha kutokuelewana kwa pande hizi mbili. Muombezi: Unakataa kusimulia kwangu mambo haya. Lakini ninafanya hivi kukana shutuma za waandishi waovu wanaowapoteza ndungu zetu ambao hawana ujuzi, na kuwaita Mashia makafir na kusema kwamba mambo haya yalikuwa ni ubunifu wa Mashia. Hatusemi kitu chochote kuhusu Ali mbali na kile ambacho Mtume amesema kuhusu yeye. Tuliwaeleza katika mikesha iliyopita kwamba tunamchukulia Ali kama mja mtiifu wa Allah, makamu na mrithi wa Mtume aliyeteuliwa kwa utaratibu wa Mungu. Unadai kwamba hakuna maana ya kusimulia mambo haya. Kama msingezileta nukta hizi, tusingezijadili. Kama msingesema usiku huu kwamba hizi ni imani za Shia bila hoja ya msingi kwazo, nisingelazimika kuiambia hadhara hii kwamba hizi ni imani za maulamaa wa ki-Sunni wasio na upendeleo. Nawab: Mheshimiwa, tunaamini kwamba Husein, ash-Shahid, alikuwa ameongoka sawasawa na kwamba aliuawa kwa dhulma na maofisa wa Bani Umayya. Lakini kuna baadhi ya watu, hususan miongoni mwa vijana wetu, ambao wanasema kwamba vita vya Karbala vilikuwa ni vya kijeshi (kisiasa), na sio kadhia ya kidini. Inasemekana kwamba Husein Bin Ali alielekea Kufa kutafuta mamlaka, na ni jukumu la kila serikali kuzima hatari kama hizo. Kwa hiyo, Yazid alizuia tishio hili. Walimtaka Mtukufu Imamu kula kiapo cha utii bila masharti kwa Khalifa Yazid, ambaye kwamba utii kwake ilikuwa ni wajibu. Walimtaka aende Syria akaishi kule na Khalifa kwa heshima au arudi mjini kwake (Madina). Lakini hakufuata ushauri wao, na hatimaye aliuawa. Wanahitimisha kwamba maombolezo yoyote kwa ajili ya mtu wa kidunia kama huyu, ambaye aliuawa kwa ajili ya mapenzi yake ya mamlaka, sio tu hayana maana, bali pia ni bida. Je, una jibu kwenye nukta hii? Unakanusha vipi wazo la kwamba vita vya Karbala havikuwa kilele cha harakati za kisiasa?

IMAMU HUSEIN KAMWE HAKUTAMANI NGUVU ZA KISIASA


Muombezi: Kila tendo zuri au baya linategemea elimu yetu juu ya Allah. Wapinzani lazima kwanza wamtambue Allah, na kisha lazima wakubali Kitabu cha Mungu, Qurani. Kutokana na kukubali huko, ina maana kwamba tunatambua kwamba chochote kile kilichoko ndani ya Kitabu ni sahihi. Mtu yeyote anayeamini kwamba Husein Bin Ali alishawishiwa na malengo ya kidunia anakataa ukweli wa Qurani Tukufu. Allah (swt) ametoa

206

Mikesha ya Peshawar
ushahidi wa usafi wa Husein katika Qurani Tukufu. Anasema: Allah anapenda kuwaondoleeni uchafu, Enyi watu wa nyumba (Ahlul-Bayt)! Na kuwatakaseni kwa utakaso ulio safi kabisa (Qurani; 33:33). Maulamaa wenu wengi, kama Muslim, Tirmidhi, Thalabi, Sijistani, Abu Nuaim Isfahani, Abu Bakr Shirazi, Suyuti, Hamwani, Ahmad Bin Hanbal, Zamakhshari, Baidhawi, Ibn Athir, na wengine wameshikilia kwamba aya hii iliteremshwa kwa kuwatukuza wale watukufu watano, Ahlul-Bayt (watu wa Nyumba): Muhammad, Ali, Fatima, Hasan na Husein. Aya hii ndio uthibitisho mkubwa wa kutokukosea (Masum) na usafi wa watu hawa watukufu. Uchafu mkubwa sana ni mapenzi ya mamlaka ya kidunia. Kuna hadithi nyingi kutoka kwa Mtume na Maimamu zinazolaumu hamu ya mamalaka ya kidunia na utekelezaji wa matamanio yetu maovu. Mtume alisema: Mapenzi na urafiki na dunia ni mzizi wa maovu yote. Abu Abdillah Husein hakuwa na mapenzi na mamlaka ya kidunia. Kwa kweli hakuhatarisha maisha yake na maisha ya familia yake kwa ajili ya kupata utawala wa mpito katika dunia hii. Kama kusimama kwa Husein dhidi ya Yazid kulikuwa kwa ajili ya mamlaka ya kilimwengu tu, Mtume asingeamuru watu kumsaidia. Maulamaa wenu wenyewe wanathibitisha nukta hii. Sheikh Suleimani Balkhi Hanafi katika Yanabiul-Mawadda kutoka katika vitabu vya historia vya Bukhari, Baghawi, na Ibnus-Sikkin kutoka Dhakhairul-Uqba ya Imamul-Haram Shafii, na Sirat-e-Mulla wanasimulia kutoka kwa Anas Bin Harith Bin Bayya, ambaye amesema kwamba alimsikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema: Hakika, mtoto wangu Husein atauawa katika ardhi ya Karbala. Kila mtu kati yenu ambaye atakuwepo wakati huo lazima amsaidie. Taarifa inaendelea: Anas Bin Harith alifika Karbala na kwa kutii amri ya Mtume, aliuawa shahidi pamoja na Imamu Husein. Kwa hiyo ina maana kwamba kule Karbala Imamu Husein alisimama kwa ajili ya haki na sio kwa mapenzi ya dunia hii. Kuandaa safari kwa Imamu Husein akiwa na kundi dogo, wakiwemo wanawake na watoto wadogo, ni ishara nyingine kuonesha kwamba alitoka nyumbani kwake sio kwa madhumuni ya kupata mamlaka. Kama hiyo ingekuwa ndio nia yake, angelikwenda Yemen, ambako anaungwa mkono na wengi. Yemen ingelikuwa ni kituo cha kimantiki cha kuanzishia shughuli za kijeshi. Kwa hakika rafiki zake mara nyingi wamemshawishi kwenda Yemen, lakini walikuwa hawatambui madhumuni yake. Lakini Imamu Husein alijua kwamba hakuna njia ya kupata mafanikio ya dhahiri. Safari yake ilianza na watu 84, wakiwemo wanawake na watoto, akilenga kwenye msingi mzuri. Ule mti mtukufu la ilaha illallah (hakuna mungu isipokuwa Allah) ulipandwa na babu yake, ukarutubishwa na damu yake na damu ya mashahidi wa Badir, Uhud, na Hunain. Mti huo uliaminishwa kwa mtunza bustani mzuri, Ali Bin Abu Talib, ambaye alizuiwa kwa vitisho vya mauaji na uchomaji moto mali wa makusudi. Matokeo yake ilikuwa kwamba ile chemchem ya Tawhid (upweke wa Mungu) na utume ukakumbwa na mbadiliko ya kipupwe. Taratibu utawala wa bustani ukaangukia

207

Mikesha ya Peshawar
mikononi mwa Bani Umayya waovu. Kuanzia ukhalifa wa Uthman Bin Affan, Bani Umayya wakahodhi utawala wa dola. Abu Sufyan, mzee na kipofu, lakini daima hamu yake ya mamlaka ilikuwa kali, alipiga kelele kwenye baraza ya Bani Umayya: Enyi Bani Umayya! Uzuieni ukhalifa kwenye familia yenu wenyewe. Pepo na moto ni ngano za watu wa kale. Enyi Bani Umayya! Ukamateni ukhalifa kama mpira. Naapa kwa kile ambacho nakiapia, kwamba kila siku nimetamani utawala huu kwa ajili yenu. Uchungeni ili kwamba uwe ni urithi wa vizazi vyenu. Makafiri hawa waliwaondoa watunza bustani sahihi kutoka kwenye bustani. Maji ya uhai yalisimamishwa na mti mtukufu ulisinyaa mpaka wakati wa utawala wa Yazid, wakati ulipoonekana kuelekea kufa. Imamu Huseini akasafiri kwenda Karbala kuinyweshea ile bustani ya utume na kuimarisha ule mti mtukufu wa la ilha illAllah. Baadhi ya watu wanahoji kwa nini Imamu Husein asipandishe bendera ya upinzani mjini Madina. Hawajui kwamba angebakia Madina malengo yake yangelibakia bila kueleweka. Imamu Husein alikwenda Makka katika mwezi wa Rajabu alihutubia maelfu ya watu, akiwambia kwamba Yazid alikuwa anaungoa mti wa Tawhid. Alisema kwamba Yazid ambaye alidai kuwa Khalifa wa Waslamu, alikuwa anauharibu msngi wa Uislamu. Akiwa ametawaliwa na ulevi wa pombe na kamari, Yazid alijiburudisha kwa kucheza na mbwa na manyani. Imamu Husein aliona kutoa mhanga maisha yake ni muhimu kwa ajili ya kuuhifadhi Uislamu.

IMAMU HUSEIN ALIKATAA USHAURI WA KUUACHA UJUMBE WAKE


Marafiki wa Imamu Husein na jamaa zake wamshawishi asiende Kufa, wakisema kwamba watu wa Kufa waliomtaka aende kule wana sifa mbaya wasioaminika. Watu wengi walikusanyika kwa Bani Umayya na kupokea pesa na upendeleo wa kisiasa kwa malipo ya kuwaunga mkono kwao. Kwa hiyo, kwa mujibu wa wengi wa wafuasi wake, Imamu Husein hakuwa na nafasi ya kuweza kuwashinda. Walimuomba aache safari yake hiyo. Walimhimiza aende Yemen ambako alikuwa na wafuasi wengi, na ambako angeweza kuishi kwa amani. Lakini Huseini hakuweza kuelezea ukweli wa hali yake. Hata hivyo, alimtosheleza kila mmoja kwa jibu fupi. Aliwaambia marafiki wa karibu na jamaa zake, kama ndugu yake, Muhammad Bin Hanafiyya: Unasema jambo sahihi. Mimi vile vile najua kwamba sitapata umiliki wa dhahiri, lakini siendi kwa ajili ya ushindi wa kidunia. Ninakwenda ili nikauawe. Natamani kwamba kwa kupitia nguvu yangu ya kuteseka kwa uonevu, ningeweza kuungoa msingi wa udhalimu na ukatili. Nimemuona babu yangu, Mtume, katika ndoto akiniambia: Fanya safari ya kwenda Iraq. Allah (swt) anataka kukuona wewe ukiuliwa. Muhammad Bin Hanafiyya na Ibn Abbas wakasema: Kama hivyo ndivyo, kwa nini unakwenda na wanawake? Akajibu: Babu yangu amesema kwamba Allah anataka

208

Mikesha ya Peshawar
kuwaona wao wakiwa mateka. Hivyo, kutokana na amri ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ninawachukuwa na kwenda nao. Kutekwa kwa wanawake kutakuwa ndio sehemu ya maamuzi ya kuuliwa kwake shahidi. Watauonesha ulimwengu ukatili wa Bani Umayya kwa kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Bibi Zainabu binti wa Ali na Fatima, alitoa hotuba fasaha ya malalamiko katika baraza ya Yazid iliyojaa watu, ambapo mamia ya watu, wakiwemo watu maarufu, watu wakubwa kutoka Bani Umayya, na mabalozi wa nje, walisheherekea ushindi wao. Imamu wa nne, Zainul-Abidin Ali Ibn Husein, naye vile vile alitoa hotuba ya madai fasaha juu ya haki na uadilifu katika mimbari ya Msikiti wa Bani Umayya, mbele ya Yazid. Baada ya kumtukuza Allah (swt) Zainul-Abidin alisema: Enye watu! Sisi kizazi cha Mtume Muhammad, tumejaaliwa na Allah sifa sita na tumefanywa wabora kwa viumbe wote kwa kupewa fadhila saba. Tumepewa elimu, uvumilivu, ujasiri, haiba yenye kupendeza, ufasaha, ushujaa, na tunapendwa na waumini. Sisi ni bora juu ya kila mtu kwa sababu Mtume Muhammad anatokana na sisi; Siddiq Ali Bin Abu Talib anatoka kwetu; Jafar-eTayyar anatoka kwetu; Hamza anatoka kwetu, wajukuu wawili wa Mtume, Hasan na Husein, wanatoka kwetu; na Mahdi wa uma huu (Imam-e-Hujjat Bin Hasan) anatokana na sisi. Mtu ambaye hanijui mimi anapaswa ajue kuhusu familia yangu na hadhi yake; mimi ni mtoto wa Mtume wa Allah aliyetukuka mno na mbora, Muhammad Mustafa! Kisha kutoka kwenye mimbari ileile ambayo Muawiya na Yazid waliitumia kumtukana Ali, Imamu alimtukuza babu yake mashuhuri wa kupigiwa mfano, Ali Bin Abu Talib, mbele ya Yazid na wakuu wa Bani Umayya. Watu wengi wa Syria hawajawahi kusikia sifa za Ali na fadhila zake. Imamu akasema: Mimi ni mtoto wa mtu yule ambaye alipigana mbele ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.); ambaye awalipiga makafiri kule Badir na Hunain; ambaye katu hakupoteza imani yake kwa Allah japo kwa sekunde. Mimi ni mtoto wa mtu mchamungu mno zaidi wa waumini wote, mrithi wa mitume, muuaji wa makafir, mtawala wa Waislamu, rehema ya waabuduo, mfalme wa wale ambao wanalia kwa hofu juu ya Allah, mvumilivu mno wa wavumilivu, mbora wa wanaotekeleza Salat. Mimi ni mtoto wa mtu ambaye alisaidiwa na Jibril na Mikail. Mimi ni mtoto wa mtu yule ambaye alikuwa mlinzi wa heshima ya Waislamu na mkataji vichwa vya makafir. Ni mtoto wa mtu yule ambaye alipigana vita takatifu dhidi ya maadui, ayelikuwa fahari ya Makuraishi, mtangulizi wa wale walioukubali ujumbe wa Allah na Mtume Wake, wa kwanza kati ya wale walioukubali Uislamu, ulimi wa hekima ya Allah, msaidizi wa dini ya Allah, mlinzi wa amri za Allah, bustani ya hekima ya Allah, hazina ya elimu Yake. Mimi ni mtoto wa mkuu wa wenye subira, mvunjaji wa vizuizi, ambaye moyo wake ulikuwa imara zaidi, ambaye maamuzi yake yalikuwa imara zaidi, ambaye tabia yake ilikuwa imara sana kuliko mtu yeyote. Alikuwa simba mkali kwenye uwanja wa vita, ambaye aliwakata maadui na kuwaangusha chini kwa upanga wake na kuwatawanya kama upepo mkali unavyotawanya majani makavu. Alikuwa ndiye shujaa zaidi miongoni mwa watu wa Hijaz, jasiri zaidi miongoni mwa watu wa Iraq, Mwislamu safi zaidi, yeye ambaye

209

Mikesha ya Peshawar
alikula kiapo cha utii kule Aqaba, shujaa wa Badir na Hunain, mtu jasiri zaidi wakati wa kiapo cha utii chini ya mti, mtoa kafara wa aina yake, ya kipekee wakati wa kuhama kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), mkuu wa ulimwengu wa ki-Arabu, mlinzi wa Kaba Tukufu, baba wa wajukuu wawili wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Hizi ni sifa za babu yangu, Ali Bin Abu Talib. Mimi vile vile ni mtoto wa Khadijatul-Kubra; mimi ni mtoto wa Fatima Zahra; mimi ni mtoto wa yule ambaye ameuawa kwa dharuba nyuma ya shingo; mimi ni mtoto wa yule ambaye aliutoka ulimwengu huu akiwa na kiu; mimi ni mtoto wa yule ambaye alinyimwa maji wakati ambapo maji yaliruhusiwa kwa viumbe waliobakia. Mimi ni mtoto wa yule ambaye mwili wake haukuoshwa wala kuvishwa sanda; mimi ni mtoto wa yule ambaye kichwa chake kitukufu kilinyanyuliwa katika ncha ya upanga; mimi ni mtoto wa yule ambaye wanawake wake walikashifiwa na kunyanyaswa waziwazi katika ardhi ya Karbala na kuchukuliwa mateka. Mimi ni mtoto wa yule ambaye wanawake wake waliletwa Syria kama mateka. Kisha Imamu alilia kwa sauti kubwa, na kuendelea: Mimi niMimi ni yaani, aliendelea kueleza fadhila za wahenga zake waliomtangulia na mateso ya mtukufu baba yake na Ahlul-Bayt. Kama matokeo ya hotuba yake hii, watu walilia sana. Baada ya kuliwa shahidi kwa Imamu Husein, majlis ya kwanza (kikao cha maombolezo) kwa ajili ya mateso ya kikatili aliyoyapata Imamu Husein ilifanyika katika Msikiti huu mkuu wa Bani Umayya. Imamu Zainul-Abidin, baada ya kusimulia sifa za Ali mbele ya maadui, alitoa maelezo yenye kugusa nyoyo juu ya mateso aliyopata mtukufu baba yake ambayo yalisababisha kilio kikubwa cha kuumiza kutoka kwa watu wa Syria mbele ya Yazid. Alitishika sana na kuondoka Msikitini pale. Ilikuwa ni kutoka Msikitini hapa, kutokana na hotuba ya Imamu, ndipo watu wakasimama dhidi ya Yazid. Kwa sababu ya kelele za upinzani mkubwa wa watu, Yazid alilazimika kumlaani Ubaidullah Bin Marjana kwa kitendo chake kiovu. Hatimaye, ngome ya dhulma ya Bani Umayya iliteketezwa. Leo hatuoni katika Syria yote kaburi hata moja la Bani Umayya. Tukirudi kwenye swali lako, Imamu Husein mara kwa mara alitabiri kuuawa kwake shahidi. Wakati mmoja aliwahi kusimulia mjini Makka, mnamo siku ya Tarwia (siku ya 8 ya Dhul-Hijja 60 A.H.), akisema: Kifo kimeambatanishwa kwa kila mmoja wa kizazi cha Adamu kama mkufu ulivyoambatanishwa kwenye shingo ya msichana. Nina shauku ya kukutana na wahenga wangu kama vile Yaqub alivyokuwa kwa ajili ya kukutana na Yusuf. Sehemu ambayo nitafia imekwishateuliwa kwa ajili yangu, na lazima niende kwenye sehemu hiyo. Ninawaona chui mwitu wakiniuwa, wakichana vipande vipande mwili wangu kati ya Nawawis na Karbala. Imamu Husein alijua kwamba hatafika Kufa, makao makuu ya Iraqi (zama hizo). Alijua

210

Mikesha ya Peshawar
kwamba atauawa na watu ambao walikuwa kama wanyama wakali, wakikata mwili wake vipande vipande. Alifanya safari hiyo kwa madhumuni ya kufa shahidi na sio kwa sababu za kisiasa. Njiani humo aliwambia watu juu ya kifo chake kinachomngojea. Aliwaeleza marafiki zake na jamaa zake kwamba mfano mmoja ulikuwa unatosha kuthibitihsa jinsi ulimwengu huu usivyokuwa na thamani. Alisema kwamba baada ya Nabii Yahya kukatwa kichwa chake, kichwa hicho kiliwasishwa kwa mzinifu. Alisema kwamba kichwa chake yeye hivi punde kitachukuliwa kupelekwa kwa mlevi, Yazid. Fikiria suala hili kwa muda. Hur Bin Riyahi pamoja na kikosi cha farasi cha askari 1000 waliizuia njia ya Husein. Kufa ilikuwa umbali wa maili thalathini tu. Hurr alikuwa ameteuliwa na Ubaidullah Ibn Ziyad kumzuia Imamu Husein. Hurr alikuwa asimuachie andelee kwenda Kufa wala kuachana naye bila kupata maelekezo zaidi. Kwa nini Imamu alijisalimisha kwa Hurr? Kama Husein alikuwa akitafuta mamlaka ya kisiasa, kwa hakika asingeweza kuzuiwa na Hurr, ambaye alikuwa hana zaidi ya askari 1000. Imamu alikuwa na askari 1300. Hali ya kuwa angewashinda, Imamu angelifika Kufa, ambako ana watu wengi wanaomuunga mkono. Kutoka huko hali ya kuwa jeshi limeongezeka nguvu, angeweza kukabiliana na adui na kupata umiliki. Lakini alikubali amri ya Hurr, alisimama pale katika jangwa akizunguukwa na adui. Baada ya siku nne majeshi ya nyongeza ya adui yaliwasili pale, na mtoto wa Mtume akalazimika kustahamili mateso ya ukatili. Ushahidi mzuri katika kuunga mkono maoni yangu ni hotuba ya Imamu katika usiku wa kuamkia Siku ya Ashura. Mpaka usiku ule askari 1300 walikuwa wako tayari kupigana kwa ajili yake. Husein aliwakusanya watu hao pamoja na akawaambia: Wale ambao wamekuja kwa ajili ya kupata faida ya kidunia, basi wajue kwamba yeyote atakayebakia hapa kesho katika ardhi hii atauawa. Adui ana haja na mimi peke yangu; naondoa nguvu ya kifungo cha utii kutoka katika shingo zenu. Huu sasa ni usiku, na mnaweza kuondoka katika giza hili la usiku. Wengi walikubali pendekezo lake na wakaondoka. Watu 42 tu walibakia, 18 Bani Hashim na 24 Masahaba. Baada ya usiku wa manane, askari 30 wa adui walielekea kwenye kambi ya Imamu kwa ajili ya mashambulizi ya usiku, lakini walipomsikia Husein akisoma Qurani Tukufu, walijawa na jazba na wakaungana na Imamu. Hawa ndio wale watu 72 waliojitolea mhanga maisha yao Siku ya Ashura. Wengi wao walikuwa wachamungu, na wengi walikuwa ni wasomaji wa Qurani Tukufu. Leo mhanga mtukufu wa Husein unakubaliwa na marafiki na maadui kwa pamoja. Hata wale ambao ni wageni katika dini yetu wamevutia na ushujaa wake. Katika DairatulMarif ya Kifaransa, kuna makala ndefu yenye anwani ya Mashahidi watatu iliyoandikwa na mwanachuo mwanamke wa Kiingereza. Dhamira yake ni kwamba katika historia yote kumekuwa na mashahidi watatu, ambao kwa kujitolea kwao mhanga maisha yao, wamekuwa kivutio kikubwa katika kuendeleza njia ya haki. Wa kwanza alikuwa ni Socrates, na wa pili alikuwa ni Yesu - Isa Masihi (mwandishi alikuwa ni Mkristo). Sisi Waislamu, kwa hakika tunaamini kwamba Isa hakusulubiwa. Qurani Tukufu kwa uwazi inasema:

211

Mikesha ya Peshawar

Na hawakumuuwa wala hawakumsulubisha, bali walifananishwa kwao (mtu mwingine, kama Isa), na kwa hakika wale ambao wanatofautiana kwalo wana shaka juu ya hilo. Hawana elimu kuhusiana nalo, bali hufuata dhana tu. Kwa yakini hawakumuuawa. Hasha! Allah alimchukuwa juu Kwake. (Qurani 4:157-158) Shahidi wa tatu, anaandika mwanamke huyu, alikuwa ni Husein, mjukuu wa Muhammad. Anaandika: Wakati tunapokusanya matukio ya kihistoria na kuyaangalia yale mazingira ambamo watu hawa watatu walitoa maisha yao, tunakubali kwamba mhanga wa Husein uliipita ile mingine miwili. Ukweli ulikuwa kwamba, Socrates na Yesu walitoa tu maisha yao wenyewe kwa kafara katika njia ya Mungu, lakini Husein alitoka nyumbani kwake kwenda nchi ya mbali ya jangwa kwenda kuzunguukwa na adui. Yeye na familia yake yote waliuawa mashahidi kwa ajili ya kutetea njia ya haki. Aliwapeleka rafiki na jamaa zake kumkabili adui na kutoa mhanga maisha yao kwa ajili ya dini ya Allah. Hii kwa hakika ilikuwa ni ngumu mno kuliko kutoa maisha yake mwenyewe. Mfano wa dhahiri zaidi wa mateso ya udhalimu aliyopata Husein ulikuwa ni yale mauaji ya kikatili ya mtoto wake mdogo wa miezi sita. Alimbeba mtoto mikononi mwake akiomba maji kwa ajili yake (ambayo yalikuwa mengi), lakini maadui wakatili wale, badala ya kumpa maji, walimuuwa mtoto yule kwa mshale. Ushenzi huu wa maadui unathibitisha kwamba Imamu Husein alikuwa ni muathiriwa wa udhalimu. Uvumilivu wake wa kushangaza ulivunjilia mbali kabisa nguvu za Bani Umayya na uliwashutumumbele ya ulimwengu. Ilikuwa ni kwa ajili ya mihanga yake na Ahlul-Bayt wake watukufu ambapo dini ya Muhammad ilipata uhai mpya. Nawab: Kwa hakika tunawiwa mno na wewe. Tumevutiwa sana na maelezo yako ya mambo yanayomhusu Imamu Husein. Mpaka sasa tulikuwa tunafuata watu wengine na tulikuwa tunazikosa fadhila za ziarat (kuzuru kaburi tukufu la Imamu). Tumeambiwa kwamba kuzuru kaburi la Imamu Husein ni bidaa uzushi. Ama kwa hakika ni bidaa nzuri iliyoje hiyo, kwa vile humfanya mtu awe na ari na kumsaidia aelewe ukweli kuhusu kizazi cha Mtume.

MAANA HALISI YA BIDAA (UZUSHI)


Muombezi: Neno bidat, lina asili yake katika madhehebu ya maulamaa wa ki-Sunni na ya Nasib na Khawarij, ambao walikuwa ni maadui waliothibitika wa Ali. Wameiita ziarat bidaa bila kufikiria ukweli kwamba bidaa inahusian na jambo linalohusu Mtume au

212

Mikesha ya Peshawar
AhlulBayt wake, ambalo halikuamriwa na Allah. Hata hivyo, kuhusu suala la kuzuru kaburi la Husein, kuna hadithi nyingi katika vitabu vya maulamaa wenu wenyewe. Nitakomea kwenye hadithi moja mashuhuri iliyoandikwa katika vitabu vyote vya maqatil na hadith mukhtar. Siku moja Mtume alikuwa nyumbani kwa Aisha wakati Husein alipoingia ndani. Mtume alimchukuwa mikononi mwake, akambusu na kumnusa. Aisha akasema: Maisha ya baba yangu na mama yangu yawe mhanga kwa ajili yako! Kiasi gani unampenda Husein! Mtume akasema: Hujui kwamba mtoto huyu ni sehemu ya ini langu na ua langu? Baada ya hapo Mtume akaanza kulia. Aisha akauliza sababu ya kulia kwake. Mtume akajibu kwamba alibusu mahali ambako Bani Umayya watakuja kumjeruhi Husein. Aisha akauliza kama watamuuwa. Akasema, Ndio atauawa. Hawatapata usaidizi wangu (kesho akhera). Aliyebarikiwa ni yule anayekwenda kuzuru kaburi lake baada ya shahada yake.Aisha akamuuliza Mtume, ni malipo gani yatakuwa kwa ajili ya ziarat hiyo. Mtume akasema: Itakuwa ni sawa na hijja yangu moja. Aisha akasema, Hijja moja ya kwako! Akasema, Hapana, mbili, Aisha alipoonesha mshangao tena, akasema, Hapana, Hijja nne. Jinsi alivyozidi kuonesha mshangao ndivyo malipo yalivyozidi kuongezeka, mpaka mwishowe akasema, Aisha! Kama mtu atakwenda kuzuru kabutri la Husein, Allah atampa malipo sawa na Hijja 90 na Umra 90 zilizofanywa na mimi. Kisha Aisha akanyamaza. Sasa nakuulizeni, Ziarat kama hiyo ni uzushi (bidaa)?

FAIDA ZA KUZURU MAKABURI YA MAIMAMU WATUKUFU


Kuna faida nyingine ambazo hupatikana kwa kuzuru makuburi ya Maimamu. Sehemu za ndani kabisa za eneo la kaburi, zinazoitwa haram, hubakia wazi kwa ajili ya wangeni usiku na mchana. Haram hizo na misikiti karibu yake kwa kawaida huwa zinakutwa zimejaa mahujaji na wafanyao ibada. Wale ambao wamezoea kusali si zaidi ya Salat za wajibu mara nyingi hufanya jitihada maalumu za kiibada wakati wa kuzuru makaburi matukufu. Wanamuomba Allah kwa unyofu na kusoma Qurani. Je, ibada kama hiyo ni bidaa? Nawab: Kwa hakika hatuna wa kumlaumu isipokuwa sisi wenyewe kama hatukuyaangalia mambo haya kwa ukaribu zaidi. Miaka michache iliyopita nilikwenda Baghdad kuzuru kaburi la Imam ADham Abu Hanifa na Abdul-Qadir Jilani. Siku moja nilikwenda kutembea karibu ya Kadhmain (sehemu aliyozikwa Imamu wa saba, Musa Ibn Jafar Al-Kadhim na Imamu wa tisa, Muhammad Ibn Ali at-Taqi). Wakati niliporudi, wenzangu walinilaumu vikali sana. Nashangaa kwamba kuzuru makuburi ya Imam Adham huko Mudham, Sheikh Abdul-Qadir huko Baghdad, la Khwaja Nidhamud-Din huko India, la Sheikh Akbar Muhyi-d-Din Ibn Arabi huko Misr kunaweza kuchukuliwa kwamba kunastahili

213

Mikesha ya Peshawar
malipo ya thawabu. Kila mwaka watu wengi miongoni mwa madhehebu ya Sunni huzuru sehemu hizi ingawa Mtume kamwe hajalipendekeza hilo. Inawezekana vipi kwamba ziarat kwenye kaburi la Shahidi mkuu, mjukuu wa Mtume, ambayo Mtume ameipendekeza, iambiwe kuwa ni bidaa? Naamua kwa dhati kabisa kwamba, Allah akipenda, mwaka huu nitakwenda kuzuru kaburi la mjukuu kipenzi cha Mtume, Husein. Nitamuomba Allah anisamehe makosa yangu yaliyopita.

MKUTANO WA NANE; ALKHAMISI USIKU ( 1 SHABAN, 1345 A.H.)


Sayyid Abdul-Hayy: Mheshimiwa, usiku uliopita ulichangia katika kutokuelewana miongoni mwa Waislamu. Muombezi: Nieleze jinsi nilivyofanya hivyo. Sayyid: Wakati unaelezea sisi wenyewe, uliwagawanya Waislamu kwenye makundi mawili: Waislamu na waumini. Lakini waislamu wote ni kitu kimoja na wako sawa. Wale wanaosema maneno Hakuna mungu isipokuwa Allah na Muhammad ni Mjumbe Wake, hao ni ndugu. Hawapasi kutenganishwa katika makundi mawili kwa sababu hili lina madhara kwa Uislamu. Mashia wanajiita wenyewe waumini, na wanatuita sisi Waislamu. Lazima utakuwa umeona kwamba kule India Mashia wanaitwa waumini na Masunni wanaitwa Waislamu. Ukweli ni kwamba Uislamu na Iman ni maneno yanayofanana kwa sababu Uislamu maana yake kukubali amri za dini. Utambuzi huu ndio ukweli wa Iman. Umma wote umekubali kwamba Uislamu ni Iman halisi. Umekwenda kinyume na maoni ya wengi.

TOFAUTI KATI YA UISLAMU NA IMANI


Muombezi: Kwanza, rejea yako juu ya watu wa kawaida haina maana ya watu wa umma wote kwa ujumla. Inarudi kwa watu wa kawaida wa kundi la Masunni. Pili, maelezo yako kuhusu Uislamu na Imani sio sahihi. Sio Mashia tu wanaohitalifiana na Masunni bali hata ma-Ashari, Mutazali, Mahanafi, na Mashafii vile vile wana maoni tofauti kuhusu hilo. Tatu, mimi kwa kweli sielewi ni kwa nini mwanachuoni kama wewe unakimbilia pingamizi zisizo na maana. Mgawanyo huu katika makundi mawili umefanywa na Allah katika Qurani Tukufu. Pengine umesahau lile suala linalohusiana na Masahaba wa kuliani na Masahaba wa kushotoni waliotaja katika Qurani Tukufu ambayo inasema:

Wakaaji wa jangwani wanasema: tumeamini. Sema: Hamjaamini bali semeni,

214

Mikesha ya Peshawar
tumenyenyekea (tumesilimu); lakini imani bado haijaingia nyoyoni mwenu. (Qurani; 49:14) Kwa hakika lazima uelewe kwamba aya hii iliteremshwa katika kuwalaumu lile kabila la jangwani la Bani Asad, ambao walikuwa Waislamu kwa majina tu. Wakati wa mwaka wa ukame, walijazana mjini Madina, na ili kupata msaada walidai kwamba wao ni waumini. Lakin nyoyoni mwao walikuwa si waumini kwa Allah na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Aya hii inathibitisha kwamba kuna makundi mawili ya Waislamu. Waislamu waaminifu, ambao wamekubali uhalisi wa Imani, na wale ambao wanatamka imani maneno kwa mdomo tu. Katika nyanja yetu ya kijamii kundi la mwisho wanapasika na usalama na manufaa ya sheria zilizokusudiwa kwa Waislamu wote. Lakini, kwa mujibu wa amri za Qurani Tukufu, hawapasiki na malipo yoyote katika akhera. Kutamka kwao kwamba hakuna mungu ispokuwa Allah na Muhammad ni Mjumbe Wake, na kujionyesha kwao katika jambo la kwamba wao ni Waislamu, hakuna maana ya kweli. Sayyid: Umesema sawa, lakini Uislamu bila Imani hauna maana, kama vile ambavyo Imani bila Uislamu haina ubora. Allah anasema katika Qurani Tukufu: Na msimwambie anayekutoleeni salamu: Wewe sio muumini...... (Qurani; 4:94). Aya hii inathibitisha kwamba lazima tumtendee mtu kwa mujibu wa mtu anavyoonekana kwa nje. Kama mtu yeyote atasema, Hakuna mungu isipokuwa Allah na Muhammad ni Mjumbe wa Allah, lazima tukubali imani yake. Hii yenyewe ni ushahidi mzuri kwamba Uislamu na Imani ni maneno yanayofanana. Muombezi: Aya hii iliteremshwa kuhusiana na mtu mahususi, imma Usama Bin Zaid au Muhallam Bin Jasama-e-Laisi, ambaye inasemekana aliuwa mtu katika vita, mtu ambaye ametamka, Hakuna mungu isipokuwa Allah. Aliuawa kwa dhana kwamba alitamka maneno haya kwa woga. Lakini kwa vile unafikiri kwamba iko katika hali ya ujumla, sisi vile vile tunawaona Waislamu wote kuwa ni safi. Labda kwa kweli pale tunapowaona wakikiuka ile misingi ya dini. Lakini kuna tofauti kati ya Uislamu na Imani kwa sababu kuna daraja mbali mbali za Imani. Imam Jafar Bin Muhammad As-Sadiq anasema katika hadithi ya Umar na Zubair: Amma kuhusu Imani kuna masharti, daraja, na hatua. Baadhi ya hizo ni dhaifu na udhaifu wao uko wazi; baadhi ni nzuri zenye uzito; baadhi zimetimia na zimefikia ukamilifu. Imani dhaifu ni hatua ya kwanza kabisa ambayo kwamba mtu hupita kuingia katika Uislamu kutoka kwenye ukafiri. Daraja za juu za Imani zinawezekana. Rejea zake zimetajwa katika baadhi ya hadithi. Miongoni mwao ni hadithi katika Usul Kafi na NahjulBalagha kutoka kwa Amir wa Waumini (Ali) na Jafar Bin Muhammad As-Sadiq ambaye amesema: Allah ameigawanya Imani katika daraja saba ambazo ni wema, ukweli, kusadikisha kwa moyo, kujisalimisha kwenye utashi wa Allah, utii, elimu, na uvumilivu.

215

Mikesha ya Peshawar
Sifa hizi saba zimegawanywa bila ulingano miongoni mwa wanadamu. Mtu ambaye anazo sifa zote hizi ni muumini kamili. Kwa hiyo, Uislamu uko katika kundi la kwanza la Imani, ambamo kuna tamko la mdomo la imani katika utume wa Muhammad na Upweke wa Allah. Imani haijaingia katika moyo wa mtu kama huyo. Mtume wa Allah alikiambia kikundi cha watu: Enyi watu! Ninyi ni miongoni mwa wale ambao mmekubali Uislamu kwa ndimi zenu, lakini bado kwa nyoyo zenu. Ni dhahiri kwamba Uislamu na Imani viko tofauti. Lakini hatutakiwi kupekuwa nyoyo za watu wengine. Nilisema usiku uliopita kwamba dalili ya muumini ni vitendo vyake. Lakini hatuna haki ya kuchunguza kuhusu vitendo vya Waislamu. Hata hivyo tunalazimika kuonyesha tabia za Imani, ili kwamba wale ambao wamezama katika usingizi waweze kutiwa moyo wa kutekeleza wajibu wao. Hivyo wataelewa ukweli wa Imani na watajua kwamba wokovu katika akhera utakuja tu kwa kufanya matendo mema, kama hadithi inavyosema: Imani maana yake kukiri kwa ulimi, kusadikisha katika moyo, na kutenda kwa viungo vyetu. Kukiri kwa ulimi na kusadikisha moyoni ni vitangulizi vya vitendo. Naam tunajua kwamba ulimwengu huu mbaya ni utangulizi tu wa ulimwengu ujao. Njia ya wokovu kwa ajili ya mtu huyo imefungwa katika akhera mpaka awe ni mtu mwenye kufanya matendo mema hapa duniani. Allah (swt) anasema katika Qurani Tukufu:

Naapa kwa Zama! Hakika mwanadamu yumo katika hasara, isipokuwa wale walioamini na wakatenda matendo mema (103:1-3) Kwa ufupi, kwa mujibu wa Qurani Tukufu, uchamungu ndio msingi wa Imani. Na kama mtu hana matendo mema katika sifa yake, kukubali kwake kwa mdomo au kusadikisha kwenye moyo bado kutamuacha mbali na Imani. Kama ni kweli kwamba inatupasa kumchukulia kila mtu kuwa ni Mwislamu, yule ambaye anasema , Hakuna mungu isipokuwa Allah na Muhammad ni Mjumbe wa Allah, kwa nini mnawachukilia Mashia kama makafiri? Hakika Mashia wanaamini katika upweke wa Allah, utume wa Muhammad, Kibla moja, Kitabu kimoja. Wanatekeleza matendo yote ya wajibu, wanatekeleza saumu kama ilivyoelekezwa, wanakwenda kuhiji, wanatoa khums na zakat (kodi za kidini), wanaamini kufufuliwa katika mwili, na Siku ya Hukumu. Je, ninyi sio ndio mnaosababisha utengano miongoni mwa Waislamu? Mnawatenga mamilioni ya Waislamu na kuwaita makafiri ingawa hamna hata chembe ya ushahidi kuunga mkono madai yenu. Hamtambui kwamba hizi ni mbinu za maadui ambao wanataka kusababisha migogoro miongoni mwa Waislamu kwa njia za uwongo kama huu. Ukweli ni

216

Mikesha ya Peshawar
kwamba hatuna tofauti katika misingi ya imani isipokuwa katika Uimamu na ukhalifa. Na vipi ingekuwa kama kungekuwa na tofauti katika matendo ya imani? Hitilafu kama hizo zipo miongoni mwa madhehebu zenu nne, nazo ni mbaya zaidi kuliko zile zilizoko kati yetu na ninyi. (haitakuwa sahihi sasa kuonyesha tofauti kati ya madhehebu za Hanafia na Maliki au kati ya Shafii na Hanbal.). Kwa maoni yangu mimi, ninyi hamna hata chembe ya ushahidi kuthibitisha ushirikina au ukafiri wa Mashia. Kosa pekee la Mashia lisilosameheka, kwa mujibu wa kile walichoeneza Khawariji na Manasibi, kwa njia ya Bani Umayyah ni kwamba Shia hawapotoshi katika kutafsir hadithi. Hawawapi nafasi watu kama Abu Huraira, Anas, na Samura kuwa kati ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na sisi. Hata maulamaa wenu wenyewe na makhalifa wenu wakubwa waliwashutumu kama waongo. Kosa kubwa wanalohusihswa nalo Mashia ni kwamba wanafuata kizazi cha Mtume, Ali na Maimamu kumi na mbili, na sio hao Maimamu wanne. Lakini ninyi hamna ushahidi kutoka kwa Mtume unaoonyesha kwamba ni lazima Waislamu wawafuate Ashari, au Mutazali katika misingi ya imani na Maliki, Hanafi, Hanbal nau Shafii katika matendo ya ibada. Kwa upande mwingine kuna maelekezo mengi kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) yanayotuambia kwamba kizazi na Ahlull-Bayt wa Mtume wanalingana na Qurani Tukufu, na kwamba umma lazima ushikamane nao. Miongoni mwa hadithi hizo ni Hadith Thaqalain, Hadth-e-Safina, Hadith-e-Bab-e-Hitta. Je, unaweza kunukuu hadthi moja tu ambayo kwayo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema kwmba baada yake yeye watu wake lazima wamfuate Abul-Hasan Ashari na Wasil Bin Ata, na kadhalika, katika misingi ya imani na mmojawapo wa Maimamu wanne Malik Bin Anas, Ahmad Bin Hanbal, Abu Hanifa, au Muhammad Bin Idris Shafii katika matendo ya ibada? Sheikh Suleiman Balkhi Hanafi katika kitabu chake Yanabiul-Mawadda, Sura ya 4, anasimulia kutoka kwa Faraid Hamwaini akinukuu kutoka kwa Ibn Abbas kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuambia Amirul-Muminin (Ali): Ewe Ali! Mimi ni Jiji la elimu na wewe ni Lango lake. Hakuna mtu awezaye kuingia katika jiji bila kwanza kuingia katika lango. Ni mwongo yule anayedai kunipenda mimi ambapo akiwa ni adui yako, kwa sababu wewe watokana na mimi na mimi natokana na wewe. Nyama yako ni nyama yangu, damu yako ni damu yangu, nafsi yako ni nafsi yangu, haiba yako ndio haiba yangu mimi. Amebarikiwa yule mtu ambaye anakutii wewe, ole wake yule ambaye anakuasi wewe. Rafiki yako ni mwenye kunufaika, na adui yako yuko kwenye hasara. Mtu ambaye yuko pamoja na wewe amefuzu, na mtu ambaye yuko mbali na wewe amepotea. Baada yangu mimi, wewe na Maimamu wote katika kizazi chako ni kama Safina ya Nuh: ambaye atapanda humo ataokolewa, na yeyote yule ambaye atakataa kupanda humo ataangamia. Mfano wao (Maimamu) ni kama nyota: wakati nyota moja inapozama, nyingine hutokeza. Mpangilio huu utaendelea mpaka Siku ya Kiyama.

217

Mikesha ya Peshawar
Imeelezewa wazi kabisa katika Hadith-e-Thaqalain (inayokubaliwa na madhehebu zote) kwamba Kama mtashikamana na Ahlul-Bayt, kamwe hamtapotea. Hata shupavu Ibn Hajar Makki anaandika katika matokeo ya utafiti wake katika Sawaiq Muhriqa, Sura ya 2 sura ndogo,1, uk. 92, kuhusiana na aya ya Qurani Tukufu:

Na wasimamisheni hakika hao wataulizwa. (37:24) Na Sheikh Suleiman Balkhi Hanafi vie vile amenukuu kutoka kwenye Sawaiq katika kitabu chake Yanabiul-Mawadda, Sura ya 95, uk. 296, (kilichochapishwa Istanbul) akisema kwamba hadithi hii imesimuliwa katika njia tofauti. Ibn Hajar anasema: Hakika, hadithi ya kushikamana na Vitu Viwili Vizito (Thaqalain) imesimuliwa katika njia tofauti, imesimuliwa na Masahaba zaidi ya 25 wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Ibn Hajar anasema kuhusiana na aya hiyo hapo juu ya Qurani kwamba Siku ya Hukumu, watu watauliza kuhusu Wilayat ya Ali na kizazi cha Mtume. Anaandika kwamba kwa mujibu wa baadhi ya vyanzo, hadithi hii ilisimuliwa katika siku ya Arafa, na baadhi wanasema ilisimuliwa wakati Mtume yuko katika kitanda cha mauti na nyumba yake ikiwa imejaa Masahaba wake. Wengine wanasema ilikuwemo ndani ya hotuba yake ya mwisho baada ya Hija ya muago. Ibn Hajar anatoa maoni yake kuhusiana na sehemu mbalimbali ilikosimuliwa hadithi hii: Hakuna kutokulingana katika uwezekano kwamba Mtume katika kupenda kwake kuonesha Utukufu wa Qurani na kizazi chake kitukufu, alirudia rudia hadithi hii katika sehemu hizi na nyingine tofauti. Imesimuliwa kwa usahihi kabisa kwamba Mtume alisema: Ninakuachieni miongoni mwenu vitu viwili vizito: kama mkivifuata, kamwe hamtapotea. Na viwili hivyo ni Kitabu cha Allah (Qurani) na Ahlul-Bayt wangu. Tabrani ameisimulia hadithi hii na nyongeza hii: Angalieni jinsi mtakavyojihusisha na viwili hivi: Qurani na Ahlull-Bayt, hivyo msijaribu kuwatangulia, vinginevyo mtaangamia. Msiwapuuze, vinginevyo mtaharibikiwa. Msijaribu kuwafundisha, kwani wao wanajua zaidi kuliko ninyi. Hata Ibn Hajar mshupavu, baada ya kunukuu kutoka kwa Tabrani na wengine, anaandika: Mtume aliita Qurani na kizazi chake, Vizito Viwili kwa sababu viwili hivi ni vizito mno na vitukufu katika kila kipengele. Mtume vile vile alisema: Namshukuru Allah ambaye ameijaza mioyo ya Ahlull-Bayt wangu kwa hekima. Na Mtume vile vile alisema katika hadithi iliyotajwa huko mwanzoni: .....Na kamwe msijaribu kuwafundisha (kizazi changu) kitu chochote kwa vile ni wenye elimu zaidi ya ninyi wote. Muwaone ni bora kwa maulamaa wenu wote kwa sababu Allah amewaumba safi (watoharifu) na amewatambul-

218

Mikesha ya Peshawar
isha kwenye umma kuwa na uwezo za kimiujiza na sifa nyingi nyingine zisizo na idadi. Kuna nukta moja katika hadithi hii ambayo inasisitiza kushikamana kwa Ahlull-Bayt: yaani, kwamba mfuatano wa vizazi vya Ahlull-Bayt, hautakatika mpaka Siku ya Hukumu. Inashangaza kwamba baadhi ya watu wanakiri kwamba watu wa Ahlull-Bayt wana elimu kubwa lakini wanakiuka amri za Mtume na kuwafanya kama viongozi wao; wale watu wengine ambao hawana haki ya kutangulizwa. Je, mnaweza ninyi au sisi kubadisha Qurani Tukufu? Je, tunaweza kuchangua kitabu kingine chochote? Sayyid: Hapana, haiwezekani kamwe. Hii ni amana ya Mtukufu Mtume, ujumbe mtukufu, na chanzo kikuu kabisa cha mwongozo. Muombezi: Mwenyezi Mungu akubariki! Umezungumza kweli kabisa. Wakati tukiwa hatuwezi kuibadili Qurani tukufu na kuiwekea kitabu kingine badala yake, kanuni hiyo hiyo ni lazima ifuatwe kuhusiana na wale ambao wanalingana na hiyo Qurani tukufu. Hivyo, ni kwa mujibu wa kanuni gani ambayo kwamba wale ambao hawatokani na kizazi cha Mtume walikubaliwa kuwapita wale wa kizazi chake? Nataka jibu rahisi kwa swali hili ili tuweze kujua iwapo kwamba wale makhalifa watatu - Abu Bakr, Umar, na Uthman walitokana na Ahlul-Bayt wa Mtume (s.a.w.w.), na kwamba walijumuishwa katika hadith zile tulizozitaja (ya Thaqalain, Safina na Bab-e-Hitta). Kama wameingizwa, basi lazima tuwafuate, kwa mujibu wa maagizo ya Mtume. Seyyed: Hakuna anayeamini kwamba yeyote kati ya makhalifa hao, mbali na Ali, walikuwa wameingizwa kwenye Ahlul-Bayt wa Mtume. Kama ilivyo, makhalifa hao watatu waliotajwa walikuwa ni masahaba wazuri wa Mtume (s.a.w.w.) Muombezi: Je, Mtume alituambia tufuate mtu maalum au kikundi cha watu? Ikiwa kundi moja linasema kwamba ni jambo lenye manufaa kufuata watu wengine, hivi tumtii Mtume ama tufuate uangalifu kama ulivyoamuliwa na umma? Seyyed: Ni dhahiri kwamba utiifu kwa Mtume ni wajibu wa lazima. Muombezi: Baada ya kwamba Mtume ametuelekeza tufuate Qurani tukufu na kizazi chake, kwa nini wamependelewa kufuatwa wengineo? Je, Abul-Hasan Ali bin Ismail Ashari, Wasil bin Ata, Malik bin Anas, Abu Hanifa, Muhammad Idris Shafii na Ahmad Hanbal walitokana na kizazi cha Mtume au Amirul-Muminin Ali na wale kumi na moja toka kwenye kizazi chake? Seyyed: Ni wazi kabisa, hakuna ambaye amewahi kamwe kusema kwamba watu hawa wanatokana na kizazi cha Mtume, lakini walikuwa mafaqihi maarufu na watu wachamungu wa umma.

219

Mikesha ya Peshawar
Muombezi: Lakini kwa mujibu wa makubaliano ya pamoja ya umma, maimamu hawa kumi na mbili ni kizazi cha moja kwa moja cha Mtukufu Mtume. Ulamaa wenu wenyewe wanakubali kwamba wao wanalingana na Qurani tukufu, na kwamba utii kwao unaongoza kwenye uongofu. Zaidi ya hayo, Mtukufu Mtume alisema kwamba wao ndio wenye elimu zaidi kati ya watu. Kwa kuzingatia kanuni hizi mbili zenye nguvu, ni majibu gani watakayotoa wakati Mtume atakapowauliza ni kwa nini walikiuka miongozo yake yeye, na wakawaachia watu wengine kukitangulia kizazi chake? Kuna maagizo yoyote kutoka kwa Mtume kwamba hawa Ashari na Mutazila wawafuate viongozi wao au kwamba Maliki, Hanbali, Hanafi na Shafii wawafuate viongozi wao katika matendo ya ibada? Hakuna yoyote kiasi kwamba aliyataja majina yao kwa miaka 300 baada ya kifo cha Mtume. Ni baada ya hapo tu, kwa sababu za kisiasa au nyinginezo ambazo mimi sizitambui, wao ndipo wakatokea uwanjani. Lakini hawa Maimam na kizazi cha Mtukufu Mtume walikuwa wakijulikana vema wakati wa uhai wa Mtume mwenyewe. Ali, Hasan, Husein na Fatima walikuwa wakijulikana kama Ahlul-Kisaa, yaani watu wa chini ya shuka. Walikuwa ni wao ambao kwa sifa zao ile Aya ya Utakaso - Ayat-Tathiira - ilishuka kwa ajili yao. Hivi inafaa kweli, kuwaita wale wanaowafuata Ali, Hasan, Husein na wale Maimam wengine kuwa ni makafiri? Mmewafadhilisha wale ambao hawatokani na kizazi cha Mtume juu ya wale ambao walikuwa mafaqihi wakamilifu, wa kupigiwa mfano. Ni majibu gani mtakayotoa kwenye mahakama tukufu ya haki mtakapoulizwa ni kwa nini mliwapotosha watu, kwa nini mliwaita wafuasi wa Ahlul-Bayt makafiri na wazushi? Mnatutia makosani kwa sababu sisi sio wafuasi wa kanuni za kiimani za wa-Hanafi, Maliki, Hanbali au Shafii. Na bado hamumfuati Ali, licha ya maagizo ya wazi na ya dhahiri kabisa kutoka kwa Allah na Mtume wake kwamba mnapaswa kufanya hivyo. Bila ya sababu nzuri za maana, mnafuata moja ya madhehebu nne hizi na mmeifunga milango elimu ya sharia - fiqh. Sayyed: Tunategemea juu ya Maimam hawa wanne kwa namna ileile kama ninyi mnavyotegemea kwa Maimam kumi na mbili. Muombezi: Vizuri sana! ni jambo zuri kiasi gani hilo ulilosema! Idadi ya Maimam kumi na mbili haikuainishwa na Mashia au ulamaa wao karne nyingi baada ya kifo cha Mtume. Hadithi nyingi zilizosimuliwa na kutoka kwenye vyanzo vya wote, Shia na Sunni, zinathibitisha kwamba Mtume mwenyewe aliiainisha idadi hiyo ya Maimam kuwa ni kumi na mbili. Miongoni mwa ulamaa wenu ambao wamesimulia jambo hili ni Sheikh Sulayman Qanduzi Hanafi, ambaye anaandika katika Yanabiul-Mawadda yake, Sura ya 77, kuhusiana na tamko hili: Watakuwepo makhalifa kumi na mbili baada yangu.

220

Mikesha ya Peshawar
Yahya bin Hasan katika Kitabul-Umma amesimulia kwa njia ishirini kwamba Mtukufu Mtume amesema kwamba warithi wake watakuwa ni kumi na mbili kwa idadi, na wote watatokana na Quraishi. Imesimuliwa kwa njia tatu ndani ya Sahih Bukhari, katika njia tisa ndani ya Sahih Muslim, kwa njia tatu ndani ya Sunnan Abu Dawuud, kwa nji moja ndani ya Sunnan-Tirmidhi, na kwa njia tatu ndani ya Jam-e-Bainas-Sahihain ya Hamidi. Wako ulamaa wenu wengi, kama vile Hamwaini katika Faraid, Khawarizmi na ibn Maghazili kila mmoja katika Manaqib yake, Imam Thalabi katika Tafsiir yake na ibn Abil-Hadid ndani ya Sharh Nahajul-Balaghah, na Sayyid Ali Hamadani Shafii katika Mawaddatul-Qubra, Mawadda 10. Wote wamesimulia hadithi kumi na mbili zilizosimuliwa na Abdullah ibn Abbas, Ubaya bin Rabii, Zaid bin Haritha, Abu Huraira na AmirulMuminin Ali. Wote hawa wanasimulia kwa njia tofauti, lakini maneno yale yale kwamba Mtume amesema kwamba idadi ya warithi wake na Maimam watakuwa w12 na kwamba wote watatokana na Maquraishi. Baadhi ya hadith zinasema kwamba wao watatokana na Bani Hashim. Katika baadhi ya riwaya yale majina mahususi ya warithi kumi na mbili hao pia yametajwa. Wengine wao wanatoa idadi tu. Nimetoa kati ya hadith nyingi za ulamaa wenu. Sasa je, mnaweza kutaja hadith moja tu ambayo inaashiria kwamba idadi ya warithi wake watakuwa wanne tu? Hata kama ingekuwepo hadith moja tu kama hiyo, sisi tutaikubali kuliko ile ya kwetu wenyewe. Bila kuzingatia ukweli kwamba hamuwezi kunukuu hadith hata moja kuhusu maimam wenu wanne, kuna tofauti kubwa sana kati ya Maimam wa Shia na hao Maimam wenu. Maimam wetu kumi na mbili ni warithi walioteuliwa ki-mbinguni. Kuhusu maimam wenu, ni kiasi hiki tu kinachoweza kukubalika: walikuwa na elimu ya fiqhi (sharia za kiislam) na waliweza kutafsiri Qurani tukufu na hadith. Baadhi yao, kama Abu Hanifa, kulingana na kukiri kwa ulamaa wenu wenyewe, walikuwa hawakujuishwa miongoni mwa wasimuliaji wa hadith, mafaqih, au mujtahidi, bali walikuwa ni watu waliotegemea juu ya rai zao wenyewe. Hii peke yake ni ushahidi wa kukosa kwao kuwa na elimu. Kwa upande mwingine, Maimam wa Shia ni waongozaji walioteuliwa ki-mbinguni, warithi walioagizwa, wa Mtukufu Mtume. Kwa kweli katika kila zama wanakuwepo baadhi ya mafaqihi wenye elimu ya hali ya juu na wanachuoni miongoni mwa Mashia ambao wanazitafsiri amri za Allah, wakizingatia Qurani tukufu, hadith na makubaliano ya maoni. Tunafuata fatwa za ulamaa kama hao. Ingawa mafaqihi wenu walikuwa wanafunzi wa, na walipata nyingi ya elimu yao, kutoka kwa Maimam wa Shia, ninyi mnawafuata wahenga wenu ki-kichwakicha tu, wale kati ya wanafunzi wao, ambao walikengeuka kutoka kwenye misingi ya elimu na wakategemea kukisia kwao. Sayyed: Unawezaji kudai kwamba Maimam wetu walipata manufaa ya elimu yao kutoka kwa Maimam wenu? Muombezi: Ni ukweli wa kihistoria kwamba Imam Jafar as-Sadiq aliwazidi wengine

221

Mikesha ya Peshawar
wote katika elimu. Yule Aalim mashuhuri, Nurud-Din bin Sabbagh Maliki anakiri ndani ya kitabu chake, Fusulul-Muhimma kwamba Mtukufu Imam alikuwa akijulikana na kuonekana wazi kwa elimu yake. Yeye anaandika: Watu walipata elimu ya nyanja mbali mbali kutoka kwake. Watu walikuja kutoka nchi za mbali kupata maelekezo. Akajulikana sana katika nchi zote na ulamaa walisimulia hadith nyingi kutoka kwake kuliko kwa mtu mwingine wa Ahlul-Bayt ..... Kundi kubwa la watu mashuhuri wa umma, kama Yahya bin Said ibn Jarih, Malik bin Anas, Sufyan Thawri, Abu Ainiyya, Abu Ayyub Sijistani, Abu Hanifa, na Saba - wote wamesimulia hadith zake. Kamalud-Din Abi Talha pia anaandika katika Manaqib yake kwamba maulamaa maarufu na viongozi wa kidini wamenukuu hadith kutoka kwa mtukufu Imam na wamepata elimu kutoka kwake. Miongoni mwao anataja majina ya wale waliotajwa kwenye FusululMuhimma. Hata maadui walikiri fadhaili za mtukufu Imam. Kwa mfano, Maliki katika Fusulul-Muhimma na hususan Sheikh Abu Abdur-Rahman Salmi katika TabaqatulMashaikh yake anaandika: Hakika, Imam Jafar as-Sadiq aliwapita wenzie wote wa wakati wake. Alikuwa na elimu ya kisilika na ujuzi katika dini, uchamungu kamilifu katika ulimwengu, kujizuia kutokana na matamanio yote ya kidunia, na hekima ya kina kikubwa. Na Muhammad bin Talha Shafii ameziandika sifa hizi zote za mtukufu Imam katika Matalibus-Suul yake, Sura ya 6, uk. 81: Mtu huyu mwenye elimu kubwa alitokana na viongozi mashuhuri wa Ahlul-Bayt. Alijaaliwa na elimu nzito na alikuwa wakati wote katika hali ya kumkumbuka Allah. Alisoma Qurani tukufu mara kwa mara na alitoa tafsiri yake. Wafuasi wake walijikusanyia lulu kutoka kwenye bahari ya elimu yake. Aligawanya muda wake wakati wa mchana na usiku katika miundo mbalimbali ya ibada. Kumtembelea yeye kulikuwa kama ukumbusho wa akhera. Kuisikiliza hotuba yake kulimuongoza mtu kupata uchamungu, na kufuata maelekezo kulimuongozea mtu kwenye kupata pepo. Uso wake mngaavu ulijulisha kwamba alitokana na familia ya Mtukufu Mtume. Usafi wa vitendo vyake pia ulionyesha kwamba anatokana na Ahlul-Bayt wa Mtume. Wengi wa ulamaa wamepokea hadith na kupata elimu kutoka kwake. Miongoni mwao walikuwa ni Yahya bin Said Ansari, ibn Jarih, Malik bin Anas, Sufyan Thawri, Ibn Ainiyya, Shaba na Ayyub Sijistani. Wote walishukuru kwa bahati njema na fursa ya kusoma kutoka kwake.

222

Mikesha ya Peshawar

KUHUSISHWA KWA USHIA NA IMAM JAFAR AS-SADIQ


Nawab: Mashia wanaamini katika Maimamu kumi na mbili. Kwa nini Ushia unahusishwa na jina la Imam Jafar Sadiq na kuitwa madhehebu ya Jafar? Muombezi: Kila Mtume, kwa mujibu wa amri ya Mungu, huteua mrithi wake. Muhammad alimtangaza Ali kuwa mrithi wake na akaamuru umma kumtii yeye. Lakini baada ya kifo cha Mtume, Ukhalifa ulichukuliwa na Abu Bakr, Umar na Uthman. Wakati wa ukhalifa wao, isipokuwa wakati wa siku za mwanzo, Abu Bakr na Umar walimtaka ushauri Ali juu ya masuala yote mazito na kutenda kwa kufuata ushauri wake. Aidha, maulamaa wakubwa na wanachuoni maarufu wa dini nyingine ambao walikuja Madina kwa ajili ya kutafuta elimu ya dini walikinaishwa kabisa na majadiliano yao na Ali. Katika maisha yake yote, Ali aliendelea kuuhudumia Uislamu katika njia nyingi. Baada ya kuuliwa kwake shahidi, wakati Bani Umayya walipokuwa watawala, uimamu kwa ukatili mkubwa ukakandamizwa. Imam Hasan Mujtaba, Imam Husein, Imam Zainul-Abidin, na Imam Muhammad Baqir walikuwa waathirika wa ukatili mkubwa wa Bani Umayya. Njia zote za kuwafikia wao zilifungwa isipokuwa kwa wafuasi wao wachache, wengine hawakuweza kunufaika kutokana na elimu yao. Kila mmoja wao aliuawa. Hata hivyo, wakati wa mwanzo wa karne ya pili baada ya Hijra, chini ya shinikizo kubwa la ukatili wa Bani Umayya, watu waliasi dhidi ya yao. Mapigano makali ya umwagaji damu yalifuatilia kati ya Bani Abbas na Bani Ummaya. Wakati ambapo Bani Umayya walikuwa wamejishughulisha katika kuulinda utawala wao, hawakuweza kuendeleza unovu wao kwa Ahlull-Bayt. Kwa hiyo, Imam Jafar akajitokeza kutoka kwenye kule kutengwa alikokuwa amefanyiwa na Bani Umayya. Aliwaelekeza watu kuhusiana na sheria za dini. Wapenda elimu 4000 walijikusanya kuizunguka mimbar yake na kuzima kiu yao kutoka kwenye bahari ya elimu isiyo na kikomo ya mtukufu Imam. Baadhi ya masahaba zake wameandika kanuni mia nne ambazo zinajulikana kama Usul-e-Arba Mia yaani hukumu mia nne. Yafiiy Yamani anaandika kwamba Imam Jafar aliwapita wote katika elimu yake. Jabir Ibn Hayyan Sufi, aliandika mkusanyo wa kurasa elfu moja, akiorodhesha takriban vijitabu 500 juu ya mafundisho ya Imamu Jafar. Baadhi ya mafaqihi wakubwa wa ki-Sunni vile vile walikuwa ni wanafunzi wake. Abu Hanifa, Malik Bin Anas, Yahya Bin Said Ansari, Ibn Jarih, Muhammad Bin Ishaq, Yahya Bin Satid Qattan, Sufyan Bin Uyayna, Sufyan Thawri wote hawa walinufaika kutoka kwenye elimu yake kubwa mno. Ukubwa huu wa uchanuaji wa elimu ulitokea wakati huu kwa sababu Bani Umayya walizuiya mwenendo wa wazazi wake, na kwa bahati mbaya Bani Abbas wangeliwazuiya kizazi chake kuzungumza kwa uhuru. Ukweli wa wa Ushia

223

Mikesha ya Peshawar
uliwekwa wazi na sifa za Ahlull-Bayt wa Muhammad zilitangazwa na Imamu Jafar Sadiq. Kwa hiyo, madhehebu hii ikaja kujulikana kama Jafaria, lakini hakuna tofauti kati ya Imamu Jafar na yeyote katika Maimamu wanne miongoni mwa wahenga zake waliomtangulia au Maimamu sita waliokuja baada yake. Wote walikuwa viongozi wa kiroho waliowekwa na Mungu. Ingawa marafiki na maadui wote kwa pamoja walitambua ubora wake katika elimu na ukamilifu wake katika sifa zote, viongozi wenu waliopita walikataa kumfanya kama mwanachuoni mkubwa wa dini na mtu mkamilifu wa zama zake. Walikataa kutambua madhehebu yake sambamba na madhehebu nyingine nne ingawa yeye alishikilia daraja la juu zaidi katika elimu uchaji kama ilivyokubaliwa na maulamaa wenu wenyewe. Kwa vile alitokana na Ahlull-Bayt wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), alikuwa na haki ya kupata kipaumbele juu ya wengine. Pamoja na mambo yote haya, maulamaa wenu washupavu wameonesha dharau sugu kama hii kwa kizazi cha Mtume wao kiasi kwamba wanachuoni wenu wa daraja za juu kama Bukhari na Muslim, hawakuweza kuandika hata hadithi moja kutoka kwa faqih huyu au Ahlul-Bayt. Aidha, hawakunukuu hadithi yoyote kutoka kwa Imam yoyote au Sadat (mabibi) wa kizazi kitukufu: Alawi, Husaini, Abidi, Musawi, Ridhawi, au kutoka kwa maulamaa kama hawa na mafuqahaa kama, Zaid Bin Ali Bin Husein, yule Shahid, Yahaya Bin Zaid, Muhammad Bin Abdullah, Husein Bin Ali, Yahya Bin Abdullah bin Hasan na kaka yake Idris, Muhammad Bin Jafar Sadiq, Muhmmad Bin Ibrahim, Muhammad Bin Zaid, Abdullah Bin Hasan, Ali Bin Jafar (Arizi) na wengine, wote hao ambao walikuwa maulamaa na mafaqih wakubwa na ambao walitokana na familia ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kwa upande mwingine, wamenukuu hadithi kutoka kwa watu kama Abu Huraira, ambaye tabia yake mnaijua ninyi wote, na kutoka kwa yule mwongo mkubwa na mzushi, Akrama, yule Khawariji. Maulamaa wenu wenyewe wamethibitisha kwamba watu hawa walikuwa waongo na bado wanakubali hadithi zao kwa mioyo yao yote. Ibn Bayyit anaandika kwamba Bukhari amenukuu hadithi nyingi kufikia kiasi cha hadithi 12,000 kutoka kwa Khawariji na Nasibiyya, kama Imamu bin Hattan, mwenye kuvutiwa na Ibn Muljim, muuwaji wa Amir wa Waumini. Wafuasi wa Imam-e-Adhma (Abu Hanifa), Imamu Malik, Imamu Shafii na Imamu Hanbal huwaona hawa kama Waislamu safi ingawa hakuna hata mmoja aliyetokana na Ahlul-Bayt wa Mtume, na kila mmoja wa madhehebu zile iko huru kuchukuwa njia zake mwenyewe ingawa kuna tofauti kubwa katika misingi na halikadhalika katika matendo ya ibada miongoni mwao. Ni masikitiko makubwa kiasi gani kwamba wanawaita wafuasi wa Jafar Bin Muhammad As-Sadiq makafiri! Na katika sehemum zote zinazotawaliwa na Masunni, ikiwemo Makka, ambayo kwa kuihusu Allah anasema: Yeyote anaingia humo yuko huru, hawako huru kuelezea imani yao au kutekeleza Sala zao. Hivyo ninyi watu

224

Mikesha ya Peshawar
wema mnapaswa muelewe kwamba sisi Shia sio chanzo cha hitilafu zilizoko katika Uislamu; hatukuleta mtengano miongoni mwa Waislamu. Kusema kweli, migogano mingi hutokea upande wenu. Ni niyni mnaowaita Waislamu milioni 100 makafiri, ingawa ni waumini waaminifu sambamba na ninyi. Hafidh: Ni kweli, kama ulivyosema, kwamba mimi sio mtu dhalimu. Nakubali kwamba kumekuwepo na vitendo viovu kwa sababu ya ushupavu. Ningependa kusema bila kujidai au kumpendeza yeyote kwamba nimenufaika sana kutokana na mazungumzo yako na nimejifundisha vya kutosha. Lakini kwa idhini yako, niruhusu niseme kitu kimoja, ambacho ni malalamiko, na halikadhalika ni utetezi wa madhehebu stahiki ya Sunni. Unaweza kuniambia ni kwa nini wahubiri na maulamaa wa ki-Shia kama wewe hamchungi watu wenu wa kawaida kutokana na kutoa maneno ambayo hupelekea kwenye ukafiri? Matokeo yake ni kwamba wengine hupata nafasi ya kutumia neno kafiri dhidi yao. Mtu anaweza kuwa shabaha ya mashambulizi kwa sababu ametoa maelezo yasiyo sahihi. Hivyo ninyi watu vile vile msiwafanye Masunni kuwa shabaha ya mashambulizi yenu. Mashia husema mambo ambayo huathiri nyoyo za Masunni, ambao kwa kulipiza huhusisha ukafiri kwa Mashia. Muombezi: Naomba unieleze ni maelezo gani au vitendo gani hupelekea kwenye ukafiri vinavyofanywa na Mashia? Hafidh: Mashia kuwakosoa Masahaba wakubwa na baadhi ya wake safi wa Mtume, ni dhahiri hicho ni kitendo cha ukafiri. Kwa vile Masahaba wamepigana kwa miaka mingi pamoja na Mtume dhidi ya makafiri, ni wazi kwamba huduma yao ilikuwa safi kabisa kutokana na maadili yasiyokamilika. Kwa hakika wanastahiki Pepo, hususan wale ambao walipata baraka za Mungu. Kwa muijibu wa Qurani Tukufu : Hakika Allah aliridhishwa sana na waumini wakati walipokula kiapo cha utii kwako chini ya mti (Qurani 48;18) Hakuna shaka kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwaheshimu. Mtu ambaye anakataa ubora wao hakika amepotea. Qurani inasema: Wala hazungumzi kwa matamanio yake. Hayakuwa haya ila ni ufunuo uliofunuliwa. (Qurani; 53:3-4) Mtu kama huyo anamkataa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Qurani Tukufu, na mtu ambaye anamkataa Mtume na Qurani Tukufu hapana shaka yoyote ni kafiri. Muombezi: Nilitegemea kwamba nukta kama hizo zisingeletwa katika mkutano huu wa hadhara. Majibu yangu yanaweza kuwafikia watu wasio na elimu na wanaweza wakaeneza propaganda potovu. Ingekuwa vizuri kama tungejadili masuala haya kwa faragha. Nitakuja kwako siku moja na tutalitatua tatizo hili kwa faragha. Hafidh: Nasikitika, lakini watu wetu wengi katika mikesha kadhaa iliyopita wamesisitiza kwamba nukta hii ijadiliwe. Majadiliano yako siku zote ni yenye busara. Kama utatoa majibu mazuri yenye mvuto, hakutakuwa na matokeo mabaya. Vinginevyo ukubali kushindwa na hoja yetu.

225

Mikesha ya Peshawar
Nawab: Ni sawa sawa. Wote tunataka suala hili litatuliwe hapa hapa na sasa hivi. Muombezi: Nakubaliana tu matakwa yenu. Si kutarajia mtu mwenye uwezo kama wewe, baada ya maelezo kamili ambayo nimeyatoa katika usiku wa masiku yaliyopita juu ya suala la ukafiri ungeihusisha madhehebu ya Shia na ukafiri. Tayari nimewasilisha kwa ukamilifu uthibitisho kwamba Shia Ithna Ashari ni wafuasi wa Muhammad na kizazi chake kitukufu. Umeleta masuala mbalimbali. Nitajibu kila moja ya hayo kwa kuyatenganisha.

KUWALAUMU MASAHABA HAINA MAANA YA UKAFIRI


Kwanza umesema kwamba ukosoaji wa Mashia juu ya Masahaba na baadhi ya wake wa Mtume hupelekea kwenye ukafiri. Sielewi msingi wa maelezo haya. Kama ukosoaji unaungwa mkono na ushahidi, unaweza kukubaliwa. Na hata kama mtu akitoa madai ya uwongo, hii haimfanyi kuwa kafiri. Ataitwa mwenye dhambi, kama mtu anayekunywa pombe au anayefanya zinaa. Na hakika kila kosa dhidi ya sheria ya Mungu linasameheka. Ibn Hazm Zahiri Andalusi (amezaliwa 456 A.H.) anasema katika kitabu chake Al-Fasl filmilal wan-Nihal sehemu ya 3, uk. 227: Kama mtu anamtukana Sahaba wa Mtume kwa ujinga, si wa kulaumiwa. Kama akifanya hivyo hali ya kuwa ana elimu juu ya hilo, ni mwenye dhambi kama wenye dhambi wengine ambao hufanya zinaa, wizi, nk. Naam kama akiwalaani kwa makusudi, kwa vile walikuwa Masahaba wa Mtume, atakuwa kafiri kwa sababu tabia kama hiyo ni sawa na uadui dhidi ya Allah na Mtume Wake. Vinginevyo, kuwatukana tu Masahaba hakuwezi kuwa sawa na ukafiri. Kwa hiyo, Khalifa Umar alimuomba Mtume amruhusu kumkata kichwa Hatib, aliyekuwa mnafiki, ingawa alikuwa ni mmoja wa Masahaba wakubwa, muhajir, na mbaye alishiriki katika vita ya Badir. Kwa kule kumtukana na kumhusisha na unafiki, Umar hakuitwa kafiri. Basi vipi inawezekana kwamba Mashia waitwe makafiri kwa kuwatukana baadhi ya Masahaba, tukichukulia kwa muda huu kwamba unayosema ni sahihi. Aidha, maulamaa wakubwa wa madhehebu yenu wameikataa nukta yenu hii. Miongoni mwao ni Kadhi Abdur-Rahman Shafii, ambaye katika kitabu chake Muwafiq amekataa hoja ya maulamaa wenu washupavu kuhusu ukafiri wa Mashia. na Muhammad Ghazali anaandika kwamba kwalaani na kuwatukana Masahaba kamwe sio ukafiri; hata kuwalaani Masheikh wawili (Bukhari na Muslim) hakuwezi kuwa sawa na ukafiri.

226

Mikesha ya Peshawar
Mulla Sad Taftazani anaandika katika Sharhe Aqaid-e-Nasi kwamba, baadhi ya watu wasio na uvumilivu wanasema kwamba wale ambao wanawatukana Masahaba ni makafiri. Ni vigumu kukubali mtazamo huo. Ukafiri wao hauthibitishwi kwa sababu baadhi ya maulamaa wamewapendelea, wakapuuza matendo yao maovu, na kutoa utetezi wa kipumbavu katika kuwaunga mkono. Wamesema kwamba Masahaba wa Mtume walikuwa hawana dhambi yoyote, ingawa maelezo haya yalikuwa kinyume na ukweli wa mambo. Wakati mwingine walipigana wenyewe kwa wenyewe. Husda na kupenda madaraka mara kwa mara kuliwasababishia kufanya matendo maovu. Hata baadhi ya Masahaba wakubwa hawakuwa huru kutokana na vitedno viovu. Hivyo, kama kwa msingi wa ushahidi fulani mtu akawakosoa, hapaswi kulaumiwa kwa hilo. Baadhi ya watu, kwa sababu waliwapendelea Masahaba walificha maovu yao, lakini baadhi wameandika matendo yao maovu na kuwalaumu. Mbali na hili, Ibn Athir Jazari, mwandishi wa Jamul-Usul, amewajumuisha Mashia katika madhehebu ya ki-Islamu, basi mnawezaje kuwaita makafiri? Wakati wa kipindi cha Makhalifa wa kwanza, baadhi ya watu waliwalaani Masahaba kwa ajili ya matendo yao maovu. Hata hivyo, Makhalifa hawakuamuru wauawe kwa ukafiri wao. Kwa hiyo, Hakim Nishapuri katika kitabu chake Mustadrak, sehemu ya 4, uk. 335, 354, Imamu Ahmad Hanbal katika Musnad, sehemu ya 1, uk. 9, Dhahabi katika Talkhise Mustadrak, Kadhi Ayaz katika Kitab-e-Shifa, sehemu ya 4, sura ya 1, na Imamu Ghazali katika IhyaulUlum, Jz. 2, anataarifu kwamba wakati wa Ukhalifa wa Abu Bakr, mtu mmoja alikuja kwake na akatoa lugha chafu na laana dhidi yake kiasi kwamba wale waliokuwepo pale walishikwa na hasira. Abu Barza Salmi alimuomba Khalifa kama angemruhusu ili amuuwe yule mtu kwa sababu amekuwa kafiri. Abu Bakr alisema kwamba haiwezekani kufanya hivyo kwa vile hakuna mtu yeyote isipokuwa Mtume anayeweza kupitisha hukumu kama hiyo.

MAKHALIFA WENYEWE HAWAKUCHUKULIA KULANIWA WAO KUWA NI UKAFIRI


Kwa kweli, mabwana wakubwa wa ki-Sunni huwakiuka hata wale ambao wanawaunga mkono. Makhalifa wenyewe walisikia matusi lakini hawakuwalaumu watu kwa ukafiri au kuamuru wauawe. Aidha, kama kumlaani Sahaba ni sababu ya ukafiri, kwa nini msimuite Muawiya na wafuasi wake makafiri? Walimlaani na kumtukana mkamilifu zaidi wa Masahaba, Ali Bin Abu Talib. Kuwa na uchaguzi wa upendeleo katika suala hili huonesha tu kwamba lengo lako ni kitu kingine. Unataka kupigana dhidi ya Ahlul-Bayt na wafuasi wao! Kama kuwalaani Masahaba ni ukafiri, kwa nini msimlaumu Ummul-Muminin Aisha kwa ukafiri? Wanahistoria wenu wote wamesema kwamba alikuwa mara kwa mara

227

Mikesha ya Peshawar
akimtukana Khalifa Uthman na kwa uwazi akatangaza: Muuwenu mzee huyu mpumbavu, kwani hakika amekuwa kafiri. Hata hivyo, kama Shia atasema kwamba ilikuwa vema kwamba Uthman aliuawa kwa sababu alikuwa kafiri, mara moja mtasimama dhidi yake. Lakini wakati Aisha alipomuambia Uthman mbele yake kwamba yeye ni Nathal na kafiri, Khalifa hakumkataza kufanya hivyo wala Masahaba hawakumkemea. Wala ninyi hamuoni kwamba alifanya kosa. Nawab: Mheshimiwa, unamaanisha nini kwa neno Nathal? Muombezi: Firuzabadi, ambaye ni mmoja wa maulamaa wenu mwenye daraja ya juu, anatoa maana yake katika Qamusul-Lughat kama mzee mjinga. Vile vile kulikuwa Myahudi aliyekuwa na ndevu ndefu mjini Madina aliyekuwa akiitwa kwa jina hilo, ambaye alifananishwa na Uthman. Mfafanuzi juu ya Qamus, Allama Qazwini, vile vile anatoa maana hiyo hiyo, anasema kwamba Ibn Hajar katika kitabu chake Tabsiratul-Muntaha, anaandika, Nathal Myahudi mwenye ndevu ndefu aliyeishi Madina; alifanana sana na Uthman.

KHALIFA ABU BAKR ALIMTUKANA ALI


Mwisho, kama mtu anayemtukana Sahaba ni kafiri, kwa nini Khalifa Abu Bakr, mbele ya Masahaba na mkusanyiko wa Waislamu, alimtukana Sahaba bora zaidi, Ali Bin Abi Talib? Mnatukuza sifa za Abu Bakr ingawa mlipaswa kumlaumu. Hafidh: Kwa nini unamsingizia lawama hii ya uwongo? Ni lini Khalifa Abu Bakr alimtukana Khalifa Ali? Muombezi: Samahani! Sisi hatusemi kitu chochote mpaka tuwe tumefanya utafiti wa kutosha. Pengine ungetazama Sharhe Nahjul-Balagha, Jz. 4, uk. 80, ambapo imeandikwa kwamba Abu Bakr, akimdhihaki Ali kutoka kwenye mimbari ya Msikiti, alisema: Yeye (Ali) ni mbwa mwitu, ushahidi wake ambao ni mkia wake. Anasababisha matatizo, anapuuza umuhimu wa matatizo makubwa, na kuchochea watu kufanya vurugu. Anaomba msaada kutoka kwa wanyonge na kukubali usaidizi kutoka kwa wanawake. Yeye ni kama Ummit-Tahal (kahaba mmoja wa siku za ujahilia, kama alivyoelezwa na Ibn Abil-Hadid) ambaye kwamba wanaume wa familia yake walikuwa wanapenda kufanya naye zinaa. Sasa mnaweza kulinganisha matusi ya Abu Bakr kwa Ali na ukosoaji unaofanywa na Mashia dhidi ya Masahaba. Kama kumtukana Sahaba yeyote ni sawa na ukafiri, basi Abu Bakr, binti yake Aisha, Muawiya na wafuasi wake wanapaswa kuitwa makafiri. Kama hakumfanyi mtu kuwa kafiri, basi huwezi kuwaita Mashia makafiri kwa jambo hilo.

228

Mikesha ya Peshawar

KHALIFA UMAR ALISHIKILIA KWAMBA KUMLAANI MWISLAMU SIO UKAFIRI


Aidha, kwa mujibu wa hukumu za wanachuoni wenu wakubwa na Makhalifa, wale ambao wanawatukana Makhalifa sio makafiri. Imam Ahmad Hanbal katika Musnad yake, Jz. 3, Ibn Sad Katib katika Kitab-e-Tabaqat, Kadhi Ayaz katika kitabu chake Shifa, sehemu ya 4 ya sura ya 1, wanasimulia kwamba, gavana wa Khalifa Umar, Ibn Abdul-Aziz, aliandika kutoka Kufa kwamba mtu mmoja amemtweza na kumtukana Umar Ibn Khattab, Khalifa wa pili. Gavana huyo alitaka ruhusa ya kumuuwa huyo mtu. Umar Ibn Khattab akajibu kwamba hairuhusiwi kumuua Mwislamu kwa kutukana au kumlaani Mwislamu yeyote isipokuwa mtu ambaye anamtukana Mtume.

KWA MUJIBU WA ABUL-HASAN ASHARI HATA KUMUITA ALLAH AU MTUKUFU MTUME (S.A.W.W.) KWA MAJINA MABAYA SIO UKAFIRI
Baadhi ya maulamaa wenu wakubwa, kama, Abul-Hasan Ashari na wafuasi wake, wanaamini kwamba kama mtu ana imani katika moyo wake na bado akaonyesha ukafiri (km. Kwa kuabudu kiyahudi au kikristo, kwa mfano) au akasimama na kupigana dhidi ya Mtume, au akamuita Allah au Mtume kwa majina mabaya, hata hivyo sio kafiri. Imani maana yake kuamini ndani ya moyo na kwa vile hakuna mtu anayeweza kuujua moyo wa mtu mwingine, haiwezi kusemwa iwapo ule ukafiri wa dhahiri unatoka moyoni au la. Maulamaa wa ki-Ashari vile vile wamejadili masuala haya katika vitabu vyao. Ibn Hazm Andalusi ameandika kwa urefu kuhusu nukta hizi katika kitabu chake Kitabul-Fazl (sehemu ya 4, uk. 204, 206). Kwa kuzingatia ukweli huu, ninyi mna haki gani ya kuwashutumu Mashia kwa ukafiri?

MASAHABA WENGI WALITUKANANA WENYEWE KWA WENYEWE LAKINI HAWAKUCHUKULIWA KAMA MAKAFIRI
Katika vitabu vyenu sahihi, kama Musnad cha Imamu Ahmad Bin Hanbal, Jz. 2, uk. 236; Siratul-Halabiyya, Jz. 2, uk. 107, Sahih Bukhari, Jz. 2, uk. 74, Sahih Muslim, Kitab-e-Jihad wa Asbabun-Nuzul Wahid, uk. 118, kuna hadithi nyingi zinzoonesha kwamba Masahaba wengi walitukanana wenyewe kwa wenyewe mbele ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Lakini Mtume hakuwaita watu hawa makafiri. Aliwaonya. (hadithi za kuhusu mizozo hii na uadui

229

Mikesha ya Peshawar
wa wao kwa wao zimeandikwa katika vitabu vya Sunni tu, sio katika vitabu vya Shia). kwa mtazamo wa maneno haya, natumaini kwamba mmetosheka kwamba kulaani au kumtukana Sahaba yeyote hakumfanyi mtu kuwa kafiri. Kama tunamlaani mtu fulani bila sababu, tutakuwa ni watenda dhambi, sio makafiri. Na kila dhambi inaweza kusamehewa.

MTUKUFU MTUME (S.A.W.W.) ALIYAJUA MATENDO YOTE MABAYA NA MAZURI YA MASAHABA


Pili, umesema kwamba Mtume aliwaheshimu na kuwastahi Masahaba wake. Hii ni sahihi. Kwa nyongeza, Waislamu wote na wasomi wanakubali kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alijua matendo mema na mabaya ya watu. Aliyaridhia matendo yao mema. Kwa hiyo, aliheshimu uadilifu wa Nushirwan na ukarimu wa Hatim Tai. Kama alimheshemu mtu fulani, ilikuwa ni kwa sababu ya matendo yake mazuri. Lakini kule kuridhiwa anakooneshwa mtu kwa kufanya tendo jema, hakuthibitishi kwamba mwisho wake utakuwa wa mafanikio. Pengine atafanya matendo mabaya siku za baadae. Kama akifanya, kumkemea kabla ya kufanya, sio uadilifu, hata kama ingejulikana kwamba atafanya uovu katika siku zijazo. Ali alijua uovu na mwisho wa ushenzi wa mlaaniwa Abdur-Rahman Ibn Muljim Muradi na kwa kurudia rudia alimuambia kwamba yeye ndiye muuaji wake. Wakati mmoja kwa uwazi alisema: Napenda aishi, lakini amedhamiria kuniua mimi, na rafiki huyu muovu anatokana na ukoo wa Murad. Maelezo haya yameandikwa na Ibn Hajar Makki kuelekea mwisho wa sehemu ya 1 ya Sawiq, uk. 72. Bado Ali hakukusudia kumuadhibu. Hivyo, hadithi ambayo inaonesha kwamba stahili ya kitendo makhususi au maelezo sio lazima iwe yenye athari wakati wote unaokuja.

SIFA YA KUWA MMOJAWAPO KWENYE BAIAT-E-RIDHWAN


Tatu, umesema kwamba kwa vile Masahaba walikuwa katika Baiat-e-Ridhwan na wakachukua kiapo chao cha utii kwa Mtume, hawakustahili lawama, bali walistahiki kusifiwa kwa sababu wao ndio wanaorejewa kwenye aya tukufu uliyoisoma (48:18). Wanachuoni watafiti na maulamaa wametoa maoni kwa mapana sana juu ya suala hili, wakisema kwamba ridhaa ya Mungu ya aya hii inahusika tu kwenye kitendo kile makhususi, Baiat (kiapo cha utii), na kwamba haiendelei bila kikomo. Ninyi wenyewe mnaelewa kwamba wakati wa tukio la Baiat kule Hudabiyya, walikuwepo watu 1500, ambao kati yao baadae idadi ya watu walijumuishwa katika aya za unafiki. Allah aliwaahidi moto wa milele. Je, inawezekana kwambwa Allah na Mtume wameweza kuridhia baadhi ya watu na kwamba baadhi yao (ya watu hao hao) waje

230

Mikesha ya Peshawar
wabakia motoni milele? Kwa hiyo ina maana kwamba ile ridhaa ya Mungu hakuwa kwa ajili ya Baiat-e-Shajara (kiapo cha utii chini ya mti) peke yake, bali ilitegemea juu ya imani nyofu na matendo mema. Wale ambao wameamini katika upweke wa Mungu (Tawhid) na Utumme (Nubwat) na wakala kiapo cha utii walistahiki radhi za Mungu. Walitangazwa kuwa watu wa Peponi. Lakini wale waliokula kiapo cha utii bila imani, au ambao hawakula kiapo, wanastahili ghadhabu Yake. Hakika, Masahaba walifanya matendo mazuri, na kwa ajili ya matendo yao mazuri (kama kula kiapo chini ya mti) lazima wasifiwe. Na hata kama muumini, awe yeye ni Sahaba au la, akifanya kosa, anaweza kukosolewa.

MASHIA WANAKUBALI UBORA WA MASAHABA


Madhehebu ya Shia siku zote imeelezea matendo mema ya Masahaba. Aidha, hukubali matendo mema hata ya wale ambao wamekuwa ni shabaha ya ukosoaji mkali. Kwa mfano, inatambua kile kiapo chao cha utii cha chini ya mti, kuhama kwao pamoja na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kushiriki kwao katika vita, lakini vile vile hulaumu na kushutumu matendo yao mabaya. Hafidh: Ninashangazwa kukusikia wewe ukisema kwamba, Masahaba wa Mtume walifanya matendo maovu. Mtume alitangaza kila mmoja wao ni mlezi na kiongozi wa jumuiya. Alisema katika hadithi mashuhuri kwamba: Hakika masahaba wangu ni kama nyota; kama mnafuta yeyote kati yao, mtakuwa mmeongoka. Imani yenu kwa dhahri sio ya kawaida, na hatukubali imani isiyo ya kawaida.

HADITHI YA KUWAFUATA MASAHABA YACHUNGUZWA


Muombezi: Ninalazimika kujadili baadhi ya vipengele vya hadithi hii kabla sijaendelea kujibu. Kwa kweli, hakika hatuwezi kuzungumza kuhusu chanzo, usahihi, au udhaifu wa hadthi kwa njia ya kukosoa, kwani tutatoka kwenye mada kuu. Majadiliano yetu yataangalia kwenye maana yake. Wale amabao wamebarikiwa heshima ya kumuona Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), au ambao wamesimulia hadithi kutoka kwake, wanaitwa Sahaba, iwe walikuwa ni wahamiaji (Muhajir) kutoka Makka au wale waliowasaidia (Ansar) kule Madina au wengine. Kutokuelewana kukubwa mwiongoni mwenu ni kwamba, kwa sababu ya nia zenu nzuri juu ya Masahaba, mnawachukuliya wote kuwa wameepukana na makosa yote ingawa ukweli ni kinyume chake. Miongoni mwa Masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), walikuwepo wema na wabaya, ambao Allah na Mtume Wake walikuwa

231

Mikesha ya Peshawar
wanawafahamu vizuri sana. Hili linaweza kuthibitishwa vizuri na ile Sura ya Munafiqun (wanafiki) na aya za sura nyingine, kama Tawba ambayo vile vile inajulikana kama AlBaraa (Kinga) na Ahzab (koo), ambazo ziliteremshwa kwa ajili ya kuwalaumu Masahaba ambao walikuwa wanafiki na waovu. Maulamaa wenu mashuhuri wenyewe wameandika katika baadhi ya makosa na matendo mabaya ya Masahaba katika vitabu vyao sahihi. Hisham Bin Muhammad Sayib Kalbi, mmoja wa ulamaa mashuhuri wa madhehebu yenu ameandika kitabu juu ya makosa na kasoro za Masahaba. Wanafiki ambao wamelaumiwa na Allah (swt) na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) walikuwa ndumila kuwili, ambao walikuwa Waislamu kwa nje tu. Nyoyo zao zilikuwa imechafuliwa na dhulma na upotofu; na wote hao walijumuishwa katikakundi la Masahaba. Hivyo tutawezaje kuwa na nia njema kwa Masahaba wote? Na vipi tutakuwa na hakika kwamba kumfuata yeyote kati yao kutahakikisha uwongofu? Je, sio ukweli kwamba katika suala la Aqaba kulikuwa na Masahaba ambao walionekana kuwa waaminifu lakini walikusudia kumuua Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)?

SUALA LA AQABA NA MPANGO WA KUMUUA MTUKUFU MTUME (S.A.W.W.)


Hafidh: Baadhi ya maulamaa wanalichukilia suala la Aqaba kuwa ni ubunifu wa Mashia. Muombezi: Ni vibaya sana kwako wewe kutegemea juu ya imani za baadhi ya watu ambao wana mawazo ya ki-Khawariji na Manasibi. Suala hili kwa uwazi kabisa linajulikana kwa wote kiasi kwamba maulamaa wenu wenyewe wamelikubali. Tafadhali hebu rejea kwenye Dalailun-Nubuwat kilichoandikwa na Hafidh Abu Bakr Ahmad Bin Husain Baihaqi Shafii, ambaye ni mmoja wa wanachuoni na mafaqihi wenu maarufu. Ameandika kisa cha Batn-e-Aqaba kwa nyororo (sanad) sahihi ya wasimuliaji; na vile vile Imamu Ahmad Bin Hanbal, kuelekea mwisho wa Jz. 5 ya Musnad yake, anataarifu kutoka kwa Abu Tufail, na Ibn Abil-Hadid anaandika katika Sharhe yake ya Nahjul-Balagha, na inajulikana kwa maulama wote kwamba, Mtukufu katika usiku huo alilaani kikundi cha Masahaba. Nawab: Lilikuwa ni jambo gani, na ni nani hao ambao walitaka kumuua Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)? Muombezi: Maulamaa wakubwa wa madhehebu zote wameandika kwamba njiani wakati Muhammad anarudi kutoka vita ya Tabuk, wanafiki kumi na wanne walikula njama ya kumuua. Mpango ulikuwa ni kumsukuma kutoka kwenye ngamia wake angukie kwenye mporomoko wakati akipita Aqaba wakati wa usiku, uchochoro mwembamba ambao mtu mmoja tu anaweza kupita. Wakati walipojaribu kutekeleza mpango wao Malaika Jibril alimjulisha Mtume juu ya mpango huo. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamtuma Hudhaifa NakhaI kujificha nyuma ya mlima. Wakati wale wahaini walipowasili na kuzungumza

232

Mikesha ya Peshawar
wenyewe pamoja, aliwatambua wote. Saba miongoni mwao wanatokana na Bani Umayya. Hudhaifa alirudi kwa Mtume na kuwataja wote. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamuamuru kuiweka siri njama hiyo, na akasema Allah ndiye mlizi wao. Katika sehemu ya kwanza ya usiku Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alianza safari, akifuatiwa na jeshi lake. Ammar-e-Yasr alimwongoza ngamia kwa mbele na Hudhaifa alikuwa akimswaga kwa nyuma. Wakati walipofikia kile kichochoro chembamba, wale wanafiki walimtupia ngamia mifuko yao ya ngozi iliyojaa mchanga (au makopo ya mafuta), ikatoa sauti kubwa, wakidhania kwamba mnyama yule aliyetishika atamtupa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) chini ya ule mporomoko mkali. Lakini Allah (swt) alimkinga na wahaini wakakimbia na kutokomea katika kundi. Je, watu hawa hawakuwemo mwiongoni mwa Masahaba? Je, ni kweli kwamba kuwafuata wao maana yake ni njia ya wokovu? Wakati tunapozungumza kuhusu Masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wa Allah kwa nini tufumbie macho makosa yao?

MTUME KAMWE HAKUTUAMRISHA TUWAFUATE WAONGO


Mikesha iliyopita nilitaja tabia ya Abu Huraira, nikiwaeleza kwamba Khalifa Umar alimtandika viboko kwa sababu alizoea kusimulia hadithi za uwongo kutoka kwa Mtume. Je, hakuwa miongoni mwa Masahaba? Je, hakusimulia idadi kubwa ya hadithi kwa uongo? Halikadhalika, hawakuwa Masahaba wengine kama Sumra Bin Junda wamejumuishwa miongoni mwao? Je, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wa Allah anaweza kuamuru jumuiya kufuata waongo na waghushaji? Kama hadithi hii ni sahihi, yaani, kwamba kama tukimfuata yeyote katika masahaba, tutaongoka, basi tafadhali tujulishe ni yupi tumfuate, kama masahaba wawili wanakwenda njia mbili tofauti. Au kama kuna makundi mawili kila moja linapigana dhidi ya jingine, au kila moja kinyume na jingine, ni yupi ambaye itatupasa sisi kumuunga mkono? Hafidh: Kwanza, masahaba watukufu wa Mtume wa Allah hakuwa maadui wenyewe kwa wenyewe. Na hata kama mmoja alimpinga mwingine, lazima tuupime ukweli huo vizuri. Yule ambaye ni safi na ambaye maelezo yake yana mantiki zaidi anapaswa kufuatwa. Muombezi: Kama, kwa mujibu wa maelezo yako, tunafanya uchunguzi makini na kuona kwamba mmoja wao ni ni safi na yuko katika upande wa haki, basi kundi la upande mwingine la masahaba lazima liwe chafu na kwenye upande wa makosa. Basi hadithi hii kimsingi inapoteza sifa kwa sababu haiwezikani kwamba masahaba wasiokubaliana wanaweza wote kuwa vyanzo vya uongofu.

233

Mikesha ya Peshawar

UPINZANI WA MASAHABA HUKO SAQIFA


Kama hadithi hii ni sahihi kwa nini mnaleta upinzani dhidi ya Mashia, kwa sababu wao wamefuata kundi la Masahaba kama Salman, Abu Dharr, Mikidadi, Ammar-e-Yasir, Abu Ayyub Ansar, Hudhaifa Nakhai na Khuzaima Dhush-Shahadatain, nk., ambao nimewataja katika mikesha iliyopita? Kwa hakika watu hawa hawakula kiapo cha utii kwa Abu Bakr. Kwa hiyo, kati ya Masahaba waliopingana wenyewe kwa wenyewe, ni nani waliokuwa upande wa haki? Kwa vyovyote vile kundi moja lilikuwa upande wa makosa ingawa hadithi uliyonukuu hutuambia kwamba tunaweza kufuata yeyote kati ya Masahaba na kuongoka.

UPINZANI WA SAD BIN UBAIDA KWA ABU BAKAR NA UMAR


Je, Sad Bin Ubaid hakuwa mmoja wa Masahaba ambao hawakula kiapo kwa Abu Bakr na Umar? Wanahistoria wote wa Shia na Sunni kwa pamoja wanashikilia kwamba yeye alikwenda Syria na akaishi kule mpaka katikati ya kipindi cha Ukhalifa wa Umar, ndipo aliuawa. Kwa hiyo kumfuata yeye na kumpinga Abu Bakr na Umar, kwa mujibu wa hadithi hii, ni njia ya wokovu.

TALHA NA ZUBAIR WALIMKABILI ALI HUKO BASRA


Je, Talha na Zubair sio miongoni mwa Masahaba waliokula kiapo cha utii chini ya mti? Je, hawakumpinga mrithi wa haki Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Khalifa wa nne anayekubaliwa kwa mujibu wa imani yenu? Je, hawakuwa Masahaba hawa ni wenye kuhusika na umwagaji wa damu ya Waislamu wasio idadi? Sasa, tafadhali tujulishe ni lipi katika makundi haya mawili ya Masahaba ambao walipigana wenyewe kwa wenyewe ambalo kweli limeongoka. Kama utasema kwamba, kwa vile makundi yote yalikuwa na utii yalikuwa katika upande wa haki, utakuwa umekosea. Haiwezikani kudai kwamba makundi yanayopingana yote yawe yameongoka. Kwa hiyo ina maana kwamba Masahaba ambao walikuwa upande wa Ali walikuwa kwa hakika wao ndio walioongoka. Kundi lililokuwa ule upande mwingine lilichukuwa njia ya makosa; na huu ni uthibitisho mwingine wa kukataa maelezo yako kwamba Masahba wale wote ambao walikuwepo katika Baiat-e-Ridhwan, chini ya mti, walikuwa wameongoka. Miongoni mwa wale ambao walikula kiapo cha utii walikuwa hawa wawili, Talha na

234

Mikesha ya Peshawar
Zubair, ambao vile vile walipigana dhidi ya khalifa wa haki. Kwa hakika wamepigana dhidi ya mtu ambaye kuhusu yeye Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: Ewe Ali, kupigana dhidi yako ni kupigana dhidi yangu. Je, hii si sawa na kupingana dhidi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)? Basi vipi unasema kwamba neno Ashab au kuwepo chini ya mti wa kiapo ni uthibitisho wa wokovu?

MUAWIYA NA AMR IBN AL-AS WALIZOEA KUMLAANI NA KUMTUKANA ALI


Muawiya na Amr al-As walikuwa Masahaba lakini bado walipigana dhidi ya mrithi wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kumlaani na kumtukana Ali katika mikutano ya hadhara na hata katika hutuba zinazotolewa baada ya Sala ya Ijumaa. Walifanya hivyo licha ya ukweli, kama ilivyoandikwa na maulamaa wakubwa wa madhehebu yenu katika vitabu vyao sahihi, kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alirudia rudia kusema: Yule ambaye anamtukana au kumlaani Ali, ananitukana mimi. Yule ambaye ananitukana mimi anamtukana Allah. Mwanachuoni Taftazani kwa kinaganaga alishughulikia suala hili katika Sharhe Maqasid. Yeye anaandika kwamba kwa vile Masahaba walikuwa maadui wenyewe kwa wenyewe, baadhi yao walikuwa wamepotea kutoka kwenye njia ya haki. Baadhi yao kwa ajili ya husda na matamanio ya kidunia, walifanya aina zote za makosa ya kiukatili. Ni wazi kwamba Masahaba wengi, ambao hawakuwa masum (wasiokosea) walifanya matendo maovu. Lakini baadhi ya maulamaa kwa sababu wanawapendelea, walijaribu kuficha makosa yao. Kuna hoja nyingi za kukataa hadithi hii iliyoko kwenye mjadala. Hakuna shaka kwamba hadithi hii ni ya kughushi. Maulamaa wenu wengi wameonyesha wasiwasi wao kuhusu usahihi wa vyanzo vyake.

VYANZO VYA HADITHI MASAHABA WANGU NI KAMA NYOTA NI DHAIFU


Baada ya kunukuu hadithi hii katika kitabu chake Sharhush-Shifa, Jz. 2. uk. 91, Kadhi Ayaz anasema kwamba Darqutni katika kitabu chake Fazail na Ibn Abdul-Birr wasema kwamba hadithi hii sio sahihi. Vile vile imesimuliwa kutoka kwa Abd Bin Hamid katika Musnad yake ambaye ananukuu kutoka kwa Abdullah Ibn Umar kwamba Bazar alikataa kukubali usahihi wa hadithi hii. Vile vile alisema kwamba Ibn Adi ananukuu katika kitabu chake Kamil pamoja na rejea zake mwenyewe kutoka kwa Nafi, na yeye kutoka Abdullah Ibn Umar, kwamba vyanzo vya hadithi hii ni dhaifu sana. Baihaqi vile vile ameelezwa kwamba aliandika kuwa habari ya hadithi hii inajulikana sana lakini vyanzo vyake ni dhaifu.

235

Mikesha ya Peshawar
Miongoni mwa vyanzo vya hadithi hii ni Harith Bin Ghazin, ambaye tabia yake inajulikana, na Hamza Ibn Abi Hamza Nussairi, ambaye alishutumiwa kwa kuongopa. Udhaifu wa hadithi hii uko wazi. Ibn Hazm vile vile anasema kwamba hadthi hii ni ya kubuni na ni yenye kukataliwa. Hivyo katika majadiliano yetu hatuwezi kutengemea juu ya hadithi kama hii yenye nyororo (asnad) dhaifu ya vyanzo. Hata tukichukulia kwamba hadithi hii ilikuwa sahihi, isingeweza kutumika katika maana ya ujumla; ingeashiria tu kwa wale Masahaba watiifu na wachamungu ambao kwa mujibu wa amri ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wamefuata Kitabu cha Allah na kizazi kitukufu cha Mtume.

MASAHABA HAWAKUWA MASUM (WASIO KOSEA)


Nikiwa nimeyasema haya, kama nitawakosoa baadhi ya Masahaba, msinichukulie mimi kama si mwadilifu. Hata hivyo wao walikuwa ni wanadamu, na iliwezekana wao kukosea. Hafidh: Sisi pia tunaamini kwamba Masahaba hawakuwa masum, lakini wakati huo huo ni ukweli unaokubalika kwamba wote kwa pamoja walikuwa ni watu wema. Hawakufanya makosa yoyote. Muombezi: Madai yako ni mno, kama ukisisitiza kwamba wote walikuwa waadilifu na walioepukana na makosa, kwa vile katika vitabu sahihi vilivyoandikwa na maulamaa wenu wanahoji dhidi ya hilo. Wanatuambia kwamba hata baadhi ya Masahaba wakubwa wakati mwingine walifanya makosa. Hafidh: Hatuzitambui taarifa kama hizo. Tafadhali tueleze kuhusu taarifa hizo kama unaweza. Muombezi: Tukiyaacha yale waliyoyafanya wakati wa zama za ujinga (yaani, kabla ya kuja kwa Uislamu), wamefanya maovu mengi baada ya kusilimu. Inatosha kutaja tukio moja tu kwa njia ya mfano. Maulamaa wenu wakubwa wanaandika katika vitabu vyao sahihi kwamba katika ule mwaka wa kuiteka Makka (8 A.H.) baadhi ya wale Masahaba wakubwa walijiingiza katika burudani ya sherehe na shamra shamra na kwa siri wakanywa pombe. Hafidh: Hiki kwa hakika ni kisa cha kubuni. Wakati pombe ilikuwa imetangazwa kuwa ni haramu, Masahaba wa kuheshimika hawakuhudhuria japo hafla kama hizo, sembuse kutaja unywaji wa tembo. Muombezi: Haikubuniwa kamwe na wapinzani. Kama itakuwa imebuniwa kwa hali yoyote ile, basi ilifanywa hivyo na ulamaa wenu wenyewe.

236

Mikesha ya Peshawar
Nawab: Kama kulikuwa na hafla kama hiyo, majina ya huyo mwenyeji na wageni vilevile yatakuwa yametajwa. Unaweza kuelezea nukta hiyo? Muombezi: Ndio, maulamaa wenu wenyewe wameielezea hiyo.

KUNYWA POMBE KWA MASAHABA KUMI KATIKA MKUTANO WA SIRI


Ibn Hajar katika kitabu chake Fathul-Bari, Jz. 10, uk. 30, anaandika kwamba Abu Talha Zaid Bin Sahl alitayarisha hafla ya pombe katika nyumba yake na akakaribisha watu kumi. Wote walikunywa pombe na Abu Bakr alisoma baadhi ya mashairi kuwasifia baadhi ya makafiri ambao waliuliwa katika vita ya Badr. Nawab: Je, majina ya wageni yametajwa vile vile? Kama ndivyo, tafadhali tujulishe. Muombezi: (1) Abu Bakr Bin Abi Kuhafa, (2) Umar Ibn Khattab, (3) Abu Ubaida Garra, (4) Ubai Bin Kab, (5) Sahl Bin Baiza, (6) Abu Ayyub Ansari, (7) Abu Talha (mwandaaji), (8) Abu Dajjana Samak Bin Kharsa, (9) Abu Bakr Bin Shaghuls, (10) Anas Bin Malik, ambaye alikuwa na umri wa miaka 18 wakati ule na ambaye alikuwa ndiye mgawaji wa pombe hiyo. Baihaqi katika Sunan yake, Jz. 8, uk. 29 vile vile amesimulia kutoka kwa Anas mwenyewe kwamba yeye alikuwa ndiye mdogo kuliko wote wakati huo na alikuwa akiwapimia pombe. (Kufikia hapa kukawa na vurumai kubwa ndani ya mkutano huo.) Sheikh: Naapa kwa jina la Allah kwamba kisa hiki kimebuniwa na maadui! Muombezi: Umehamaki sana na umetoa kiapo cha kufuru! Lakini hauko katika makosa ya moja kwa moja kabisa. Masomo yako yana kikomo. Kama ungesoma kwa mapana zaidi, ungejua kwamba maulamaa wako mwenyewe wameandika yote haya. Sasa yakubidi uombe msamaha wa Allah. Sasa ninalazimika kuelezea mambo kwa mujibu wa maelezo ya maulamaa wenu wenyewe. Muhammad Bin Ismail Bukhari katika Sahih yake (akifafanua juu ya Ayat-e-Khamr, aya inayohusu pombe, katika sura ya Maida ya Qurani Tukufu); Muslim Ibn Hajar katika Sahih yake (Kitab-e-Ashraba Bab-e-Tahrimul-Khamr); Imamu Ahmad Bi Hanbal katika Musnad yake, Jz. 30, uk. 181 na 227; Ibn Kathir katika Tafsir yake, Jz. 11, uk. 93; JalaludDin Suyut katika Durrl-Mansur, Jz. 2, uk. 321; Tabari katika Tafsir yake, J. 7, uk. 24; Ibn Hajar Asqalani katika Isaba, Jz. 4, uk. 22 na Fathul-Bari, Jz. 10, uk. 30; Badru-d-Din Hanafi katika Umdatul-Qari, Jz. 10, uk. 84; Baihaqi katika Sunan yake, uk. 286 na 290; na wengine wameandika ukweli huu pamoja na maelezo marefu.

237

Mikesha ya Peshawar
Sheikh: Pengine mambo haya yalitokea kabla pombe haijafanywa haramu. Muombezi: Tunayoyapata kutoka kwenye vitabu vya Tafsir na historia yanaonesha kwamba hata baada ya aya za kuharamisha pombe baadhi ya Waislamu na Masahaba waliendelea kunywa pombe iliyokatazwa. Muhammad Bin Jarir Tabari anasimulia katika Tafsir-e-Kabir, Jz. 2, uk. 203, kutoka kwa Abil Qamus Zaid Bin Ali, ambaye alisema Allah ameteremsha mara tatu aya zinazokataza pombe. Katika aya ya kwanza anasema:

Wanakuuliza kuhusu ulevi na kamari. Sema: katika hivyo mna dhambi kubwa na manufaa kwa watu, lakini dhambi zake ni kubwa kuliko manufaa yake (2:219) Lakini Waislamu hawakuacha pombe mara moja. Wakati mmoja watu wawili, wakiwa wamelewa, walisali Swala zao na kuzungumza mambo yasio kuwa na maana, aya nyingine iliteremshwa, isemayo:

Enyi ambao mmeamini! msikaribie Sala hali mmelewa, mpaka myajue mnayo yasema (4:43) Hata baada ya aya hii, unywaji wa pombe uliendelea, lakini watu hawakusali wakiwa wamelewa. Siku moja mtu mmoja alikunywa pombe (kwa mujibu wa taarifa ya Bazar, Ibn Hajar na Ibn Mardawiyya mtu huyo alikuwa ni Abu Bakr) na akatunga shairi kwa ajili ya makafiri ambao waliuawa katika vita ya Badir. Wakati Mtume aliposikia hili alikasirika sana. Alikwenda kule inakofanyika hafla hiyo na akataka kumpiga. Yule mtu akasema, Naomba kinga ya Allah kutokana na ghadhabu ya Allah na Mtume Wake. Allah awe shahidi yangu, sitakunywa pombe tena. Kisha aya ifuatayo ikateremshwa:

Enyi ambao mmeamini! Bila shaka ulevi, na kamari na kuabudu masanamu na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya shetani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa. (5:90).

238

Mikesha ya Peshawar
Miongoni mwa Masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) walikuwepo wazuri na wabaya kama ambavyo wapo miongoni mwa Waumini na Waislamu wengine. Wale miongoni mwao ambao walijaribu kumtii Allah na Mtume Wake walifikia daraja ya juu. Wale ambao walifuata tamaa za kidunia walikuwa wakidharauliwa na wengine. Hivyo wale ambao wanakosoa Masahaba wa kidunia, wanafanya hivyo kwa sababu fulani. Yale matendo maovu ya baadhi ya masahaba, ambayo yameandikwa katika vitabu sahihi vya maulamaa wenu wenyewe, vile vile yanafaa kulaumiwa kwa mujibu wa ushahidi wa Qurani Tukufu. Mashia wanawalaumu katika misingi hiyo. Kama kuna majibu ya mantiki kwenye hoja hii, tuko tayari kuikubali.

UVUNJAJI KIAPO WA MASAHABA


Inashangaza kwamba hata baada ya kusikia sifa zao za kulaumika (nimetaja chache tu kati ya nyingi) bado mnaendelea kuniuliza kuhusu maovu yao! Sasa ningependa kuwasilisha mfano mwingine wa matendo yao ya kuchikiza, ambayo yameandikwa katika vitabu vyote vya madhehebu zote: Uvunjaji wa kiapo. Allah amelifanya ni wajibu suala la mtu kutekeleza ahadi. Anasema: Na timizeni ahadi ya Allah mnapo ahidi, wala msivunje viapo baada ya kuvithibitisha (16:91) Na tena Allah amewaita wale ambao wanaovunja kiapo walaaniwa. Anasema: Na wale ambao wanavunja ahadi ya Allah baada ya kuzifunga, na wanayakata yale ambayo Allah ameamrisha yaungwe, na wanafanya ufisadi katika nchi; hao ndio watakaopata laana, na watapata nyumba mbaya. (13:25) Hivyo ni wazi kutoka kwenye aya za Qurani Tukufu na kutoka katika idadi kubwa ya hadithi kwamba kuvunja kiapo ni dhambi kubwa, hususan kiapo kilichofanywa kwa Allah na Mtume wake. Uzito wa kosa hili ulikuwa mkubwa sana kwa Masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Hafidh: Ni kiapo gani cha utii ambacho Masahaba walifanya na Mtume na wakakivunja? Itawezaje kuwa chini ya mashambulizi ya aya za Qurani? Nadhani kwamba kama utaliangalia suala hili kwa makini utakubali kwamba mambo yote haya ni ubunifi mtupu wa Mashia. Masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) walikuwa wameepukana na makosa yote haya.

239

Mikesha ya Peshawar

KATIKA QURANI TUKUFU WAKWELI HUMAANISHA MUHAMMAD NA ALI


Muombezi: Nimekuambieni mara kwa mara kwamba Mashia wamejifunga kuwafuata viongozi wao. Vinginevyo hawawezi kuwa Mashia. Qurani Tukufu imetoa ushahidi wa ukweli wa viongozi wao. Maulamaa wenu mashuhuri kwa mfano, Imamu Thalabi na Jalalud-Din Suyut katika vitabu vyao vya Tafsir, Hafiz Abu Nuaim Ispahani katika kitabu chake Ma Nazal minal-Qurani fi Ali, Khatib Khawarizmi katika Manaqib, Sheikh Sulayman Balkhi Hanafi katika Yanabiul-Mawadda, sura ya 39, akisimulia kutoka kwa Khawarizmi, Hafiz Abu Nuaim na Hamwaini na Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafii katika Kifayatut-Talib, sura ya 62, wote wamenukuu kutoka kwenye kitabu cha historia cha mwanachuoni mkubwa Muhaddith-e-Sham kwamba katika aya Tukufu,

Enyi mlioamini! Mcheni Allah na kuweni pamoja na wakweli.

(9:119)

Wakweli maana yake Muhammad na Ali. Hivyo wafuasi wa familia hii tukufu hawawezi kuwa waongo au waghushaji kwa sababu ni yule mtu tu ambaye hana sababu za kweli na na zenye nguvu ndiye anaweza kusema uwongo au kughushi visa vya uwongo na kupata kitu cha kutegemea juu ya njia hii. Wanachosema Mashia kimeandikwa na maulamaa wenu wenyewe. Kwanza mnapaswa kuwakataa maulamaa wenu, ambao wameandika mambo haya. Lau maulamaa wenu wasingeandika kuhusu uvunjaji wa kiapo wa Masahaba katika vitabu vyao sahihi, nisingelitaja hilo katika mkutano huu. Hafidh: Ni nani katika maulamaa wa ki-Sunni ambaye ameandika kwamba Masahaba walivunja kiapo cha utii. Maneno matupu hayawezi kusaidia. Muombezi: Mimi sio ninazungumza tu. Hoja yangu ni yenye mantiki kamili. Masahaba walivunja kiapo chao cha utii mara nyingi. Walivunja kiapo cha utii ambacho kwacho Mtume wa Allah aliwaamuru wao, cha muhimu zaidi ni kiapo cha utii kule Ghadir-eKhum.

240

Mikesha ya Peshawar

HADITHI YA GHADIR NA ASILI YAKE


Maulamaa wote, wa Shia na Sunni wanakubali kwamba, katika mwaka wa 10 wa Hijra, Mtume wa Allah akiwa anarudi kutoka kwenye hija yake ya mwisho, aliwakusanya pamoja Masahaba wote pale Ghadir-e-Khum siku ya 18 Dhil-Hijja. Baadhi ya wale ambao walikuwa wametangulia waliitwa warudi kwa amri ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na wale ambao walikuwa nyuma walingojewa. Maulamaa wenu wengi wanahistoria na vyanzo vya Shia wanaioa idadi ya watu 70000, na baadhi ya maulamaa wenu wengine, kwa mfano, Thalabi katika kitabu chake cha Tafsir, Sibt Ibn Jauzi katika Tadhkiratu-KhasaisilUmma fi Marifatil-Aimma na wengine wameandika kwamba walikuwepo watu 120,000 waliokusanyika pale. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliamuru itengenezwe mimbari. Alipanda katika mimbari na akatoa hotuba ndefu, ambayo sehemu yake kubwa ikiwa imejaa sifa na tabia za Amirl-Muminin. Alisoma takribani aya zote zilizoshuka kwa ajili ya kumsifu Ali na akawakumbusha watu cheo kitukufu cha umakamu wa Amirul-Muminin. Kisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: Enyi watu! Je, mimi sina mamlaka zaidi juu ya nafsi zenu kuliko ninyi wenyewe? Rejea hii ni kwenye aya tukufu, Mtume ni bora zaidi kwa waumini kuliko nafsi zao (33:6) Mkusanyiko ule ukajibu kwa sauti moja Hakika, Ewe Mjumbe wa Allah! Kisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akatangaza: Yule ambaye mimi ni (maula kwake) mwenye kumtawalia mambo yake, huyu Ali ni (maula kwake) mwenye kumtawalia mambo yake. Baada yakusema hivi alinyoosha mikono yake na akaomba kwa Allah. Ewe Allah, kuwa rafiki kwa yule ambaye ni rafiki kwake (yaani Ali) na kuwa adui kwa yule ambaye ni adui kwake (yaani Ali) msaidie yule ambaye anamsaidia yeye na mtelekeze yule ambaye anamtelekeza yeye. Kisha hema lilikitwa kwa amri ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambaye alimuamuru Kiongozi wa waumini Ali kukaa ndani ya hema. Umma wote uliamriwa kutoa kiapo cha utii kwa Ali. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema kwamba ametoa maelekezo haya kulingana na amri ya Allah. Mtu wa kwanza kutoa kiapo ni siku hiyo alikuwa ni Umar. Kisha Abu Bakr, Uthmani, Talha, na Zubair walifuatia, na watu wote hawa waliendelea kutoa kiapo cha utii kwa muda wa siku tatu (yaani wakati ambapo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alibakia pale). Hafidh: Unaweza kuamini kwamba tukio la umuhimu kama wa namna hiyo limetokea kama inavyodaiwa na wewe na kwamba hakuna hata mmoja katika maulamaa maarufu aliyelisimulia hilo? Muombezi: Sikutazamia maelezo kama haya kutoka kwako. Habari ya Ghadir Khum iko wazi kama mwanga wa mchana na hakuna yeyote ila shupavu na mtu mkaidi ndiye awezaye kuleta fedheha kwa kukataa tukio kama hili. Suala hili muhimu limeandikwa kwenye

241

Mikesha ya Peshawar
kumbukumbu na maulamaa wenu wote wachamungu katika vitabu vyao sahihi. Ningependa kutaja hapa baadhi ya majina ya waandishi na vitabu vyao ili uelewe kwamba maulamaa wenu wote maarufu walitegemea hadithi hii. 1. Imam Fakhrud-Din Razi Tafsir-e-Kabir Mafatihul-Ghaib. 2. Imam Ahmad Thaalabi Tafsir-e-Kashful-Bayan. 3. Jalalud-Din Suyuti Tafsir-e-Durrul-Manthur. 4. Abul-Hasan Ali Bin Ahmad Wahidi Nishapuri Asbabun-Nuzul. 5. Muhammad Bin Jarir Tabari Tafsirul-Kabir. 6. Hafidh Abu Nuaim Ispahani Ma Nazal Minal-Qurani fi Ali na Hilyatul-Auliya. 7. Muhammad Bin Ismail Bukhari Tarikh, Jz. 1, uk. 375. 8. Muslim Bin Hajjaj Nishapuri Sahih, Jz. 2, uk. 325. 9. Abu Dawud Sijistani Sunan. 10. Hafidh Ibnul-Iqda Kitabul-Wilaya. 11. Ibn Kathir Shafii Damishqi Tarikh. 12. Imam Ahmad Ibn Hanbal Musnad Jz. 4, uk. 281&371. 13. Abu Hamid Muhammad Bin Muhammad Al-Ghazali Sirrul-Alamin. 14. Ibn Abdul-Birr Istiab. 15. Muhammad Bin Talha Shafii Matalibus-Suul, uk. 16. 16. Ibn Maghazili Faqih Shafii Manaqib. 17. Nurud-Din Bin Sabbagh Maliki Fusulul-Muhimma. 18. Husain Bin Masud Baghawi Masabihus-Sunna. 19. Abul-Muayyid Muwafiq Bin Ahmad Khatib Khawarizmi Manaqib. 20. Majdud-Din Bin Athir Muhammad Bin Muhammad Shaibani Amul-Usul. 21. Hafidh Abu Abdur-Rahman Ahmad Bin Ali Nisai Khasaisul-Alawi na Sunan. 22. Sulaiman Balkhi Hanafi Yanabiul-Mawadda, Sura ya 4. 23. Shahabud-Din Ahmad Bin Hajar Makki Sawaiq Muhriqa na Kitabul-ManhulMalakiyya, hususan Sawaiq, sehemu ya 1, uk. 25. pamoja na ushupavu wake mkubwa, anasema: Hii ni hadithi ya kweli; ukweli wake hauwezi kutiliwa shaka. Hakika imesimuliwa na Tirmidhi, Nisai na Ahmad, na kama ikichunguzwa, vyanzo vyake ni vizuri vya kutosha. 24. Muhammad Bin Yazid Hafiz Ibn Maja Qazwini Sunan. 25. Hafidh Abu Abdullah Muhammad Bin Abdullah Hakim Nishapuri Mustadrak. 26. Hafidh Sulaiman Ibn Ahmad Tabrani Aust. 27. Ibn Athir Jazari Usudul-Ghaiba. 28. Yusuf Sibt Ibn Jauzi Tadhkiratul-Khasaisul-Umma, uk. 17. 29. Abu Umar Ahmad Bin Abi Abd Rabbih Iqdul-Farid. 30Allama Samhudi Jawahirul-Iqdain. 31. Ibn Taimiyya Ahmad Bin Abdul-Halim Minhajus-Sunna. 32. Ibn Hajar Asqalani Fathul-Bari na Tahdhibut-Tahdhib. 33. Abdul-Qasim Muhammad Bin Umar Jarrullah Zamakhshari Rabiul-Abrar.

242

Mikesha ya Peshawar
34. Abu Said Sijistani Kitabud-Darayab Fi Hadithil-Wilaya. 35. Ubaidullah Bin Abdullah Haskani Duatul-Huda ila Ada Haqqil-Muwala. 36. Razin Bin Muawiya Al-Abdari Jam Bainus-Sahihis-Sitta. 37. Imam Fakhrud-Din Razi anasema katika Ktabul-Arbain kwamba jumuiya yote kwa pamoja wanathibitisha hadithi hii. 38. Muqibili hadithul-Mutawatira. 39. Suyut Tarikhul-Khulafa. 40. Mir Sayyid Ali Hamadani Mawaddatul-Qurba. 41. Abu Fath Nazari Khasaisul-Alawi 42. Khwaja Parsa Bukhari Faslul-Khitab. 43. Jamaluddin Shirazi Kitabul-Arbain. 44. Abdul Rauful-Manawi Faizul-Qadir fi Sharh-i-Jamius-Saghir. 45. Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafii Kifayatut-Talib, sehemu ya 1. 46. Yahya Bin Sharf-Nauwi Tahzibul-Asma wal-Lughat. 47. Ibrahim Bin Muhammad Hamwaini Faraidus-Simtain. 48. Kadhi Fadhlullah Bin Ruzhahan Ibtalul-Batil. 49. Shamsuddin Muhammad Bin Ahmad Sharbini Sirajul-Munir. 50. Abul Fath Shahristani Shafii Milal wan-Nihal. 51. Hafidh Abu Bakr Khatib Baghdadi Tarikh. 52. Hafidh Ibn Asakir Abul-Qasim Damishqi Tarikh-i-Kabir. 53. Ibn Abil-Hadid Mutazali Sharhe Nahjul-Balagha 56. Alauddin Samnani Urwatul-Wuthqah. 57. Ibn Khaldun Muqaddima. 58. Mawlana Ali Muttaqi Hindi Kanzul-Ummal. 59. Shamsuddin Abul Khair Damishiqi Asanu Matalib. 60. Sayyid Sharif Hanafi Jurjani Sharh-i-Mawaqit 61. Nizamuddin Nishapuri Tafsir-I-Gharaibul-Qurani.

HADITHI YA GHADIR IMESIMULIWA NA TABARI, IBN IQDA NA HADDAD


Nimesimulia vyanzo nilivyoweza kukumbuka. Lakini zaidi ya Maulamaa wenu wakubwa mia tatu wameisimulia hadithi ya Ghadir, aya za baligh (kuhubiri), kamalud-Din (ukamilifu wa dini), na mazungumzo katika eneo la Msikiti, kutoka kwa Masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) zaidi ya mia moja. Kama tungetakiwa kueleza majina ya wasimuliaji wote hawa, yangetengeneza kitabu kamili. Hata hivyo, kiasi hiki, kinatosha kuthibitisha kwamba hadithi hii inakubaliwa na wote kama hadithi ya kweli.

243

Mikesha ya Peshawar
Baadhi ya Maulamaa wenu wakubwa wameandika vitabu juu ya suala hili. Kwa mfano, mufasir mashuhuri na mwanahistoria wa karne ya nne hijiriya, Abu Jafar Muhammad Bin Jarir Tabari (amekufa 310 A.H.), anatoa maelezo kamili ya hadithi ya Ghadir katika kitabu chake Kitabul-Wilaya na ameisimulia kupitia sanad sabini na tano za wapokezi. Hafidh Abul-Abbas Ahmad Bin Said Abdur-Rahman Al-Kufi, mashuhuri kwa jina la Ibn Iqda (amekufa 333 A.H.), amesimulia hadithi hii sharif katika kitabu chake KitabulWilaya kupitia sanad 125 za wapokezi kutoka kwa Masahaba 125 wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Ibn Haddad Hafidh Abu l-Qasim Haskani (amekufa 492 A.H.), katika kitabu chake Kitabul-Wilaya, amesimulia kwa urefu hadithi ya Ghadir sambamba na kushuka kwa aya za Qurani. Kwa ufupi, wanachuoni wenu wote wateule na maulamaa wa daraja za juu (isipokuwa idadi ndogo ya wapinzani washupavu - wakaidi), wamenukuu asili ya hadithi hii kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.),ambaye alimtangaza Ali kama makamu wake siku ya mwezi 18 Dhul-Hijja katika mwaka wa hija yake ya mwisho. Vile vili ni ukweli kwamba Khalifa Umar alikuwa wa kwanza miongoni mwa Masahaba kuonesha furaha yake juu ya tukio hili. Huku akiwa ameushika mkono wa Ali, alisema: Hongera ewe Ali! Asubuhi hii imeleta neema kubwa kwako. Umekuwa maula wangu na maula wa waumini wote wanaume na waumini wanawake.

USHAURI WA JIBRIL KWA UMAR


Mwanafiqh wa ki-Shafii, Mir Sayyid Ali Hamadani wa karne ya nane hijiriyya, mmoja wa wanachuoni wa kutengemewa wa madhehebu yenu, anaandika katika kitabu chake Mawaddatul-Qurba, Mawadda ya 5, kwamba idadi kubwa ya Masahaba wamemnukuu Khalifa Umar katika sehemu tofauti akisema: Mtume wa Allah alimfanya Ali Maula, mkuu na kiongozi wa taifa (la ki-Islamu). Alitangaza katika mkutano wa hadhara kwamba yeye (Ali) ni maula wetu. Baada ya kuomba kwa ajili ya rafiki zake na kuwalaani adui zake, alisema: Ewe Allah! Wewe ni shahidi wangu. (yaani, Nimekamilisha jukumu langu la utume.). Katika tukio hili kijana wa kupendeza mwenye kunukia uzuri alikuwa amekaa kando yangu. Aliniambia, Hakika Mtume wa Allah amefungamana na agano ambalo hakuna yeyote wa kulivunja isipokuwa mnafiki. Hivyo Umar! Jiepushe kutokana na kulivunja. Nilimueleza Mtume wa Allah kwamba wakati anaongea na mkusanyiko ule wa watu, kijana wa kupendeza, mwenye kunukia uzuri alikuwa amekaa kando yangu na kwamba aliniambia kitu kama hicho. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema, hakuwa wa kizazi cha Adam, bali alikuwa Jibril, (ambaye alitokea katika umbo hilo). Alitaka kusisitiza kuhusu nukta ambayo nimeitangaza kuhusu Ali.

244

Mikesha ya Peshawar
Sasa nataka kutafuta haki kutoka kwenu, je, ilikuwa sahihi kwa wao kuvunja angano imara na Mtume wa Allah ndani ya miezi miwili, kuenda kinyume na kiapo chao kitakatifu cha utii kwa Ali, kuchoma moto nyumba yake, kuchomoa panga dhidi yake, kumfedhehesha, kumburuza mpaka msikitini kumlazimisha kula kiapo cha utii? Hafidhi: Sikutengemea kwamba mwanachuoni wa kuheshimiwa na Sayyid mstaarabu kama wewe ungelihusisha mambo ya kidunia kwa Masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwatangaza wao kwamba ni chanzo cha uongofu kwa ajili ya umma wakati aliposema: Masahaba wangu ni kama nyota; kama mkimfuata yeyote kati yao, mtaongoka.

HADITHI YA KUWAFUATA MASAHABA SIO SAHIHI


Muombezi: Kwanza ningekuomba usirudie kitu kile kile kila mara. Punde tu ulihoji kutoka kwenye hadithi hii hii na nimekupa majibu yake. Masahaba kama watu wengine walikuwa ni wenye kufanya makosa. Hivyo wakati wanathibishwa kwamba wao sio masum (wasiokosea), kwa nini mtu ashangae, kama pamoja na ushahidi sahihi, mambo ya kidunia yanahusishwa kwao? Pili ili kuisafisha akili yako, nitakupa majibu tena, ili kwamba usije ukategemea juu ya hadithi hiyo baadae. Kwa mujibu wa utafiti wa maulamaa wenu wakubwa, hadithi hii si ya kutegemewa, kama nilivyoelezea mapema. Kadhi Ayaz Maliki ananukuu kutoka kwa maulamaa wenu wakubwa kwamba kwa vile wasimuliaji wa hadithi hii hujumuisha majina ya watu wajinga na wasio na elimu, Harith Bin Qazwin na Hamza Bin Abi Hamza Nasibi, ambao wameonekana kuwa ni waongo, hadithi hii haifai kusimuliwa. Vile vile, Kadhi Ayaz, katika Sharh-e-Shifa na Baihaki katika kitabu chake Kitab, wametamka kwamba hadithi hii ni ya kughushi na wamekichukulia chanzo chake kama kisichoaminika.

BAADHI YA MASAHABA WALIKUWA NI WATUMWA WA TAMAA ZAO NA WALIGEUKA DHIDI YA HAKI


Tatu, kamwe sijasema kitu chochote cha ukorofi, ninasema tu kile ambacho maulamaa wenu wamekiandika. Nakushauri usome Sharh-e-Maqasid ya Fazil Taftazani, ambamo ndani yake anaelezea kwa uwazi kwamba kuna mifano mingi ya uadui miongoni mwa Masahaba, ambayo huoneshsa kwamba baadhi yao walikuwa wamegeuka kuwa watenda dhambi na madhalimu. Hivyo tunaona kwamba watu si wakuheshimiwa tu kwa sababu eti walikuwa Masahaba wa Mtume. Heshima ya kweli iko kwenye matendo yao na tabia zao. Kama hawatokani na wanafiki, bali walikuwa watii na waaminifu kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakika lazima watukuzwe na waheshimiwe. Tutaweka mavumbi ya miguu yao

245

Mikesha ya Peshawar
kwenye macho yetu. Hivyo, enyi wapenda haki, je, mnathibitisha kwamba hadithi nyingi kwenye vitabu vyenu sahihi zinazohusu kupigana dhidi ya Amirul-Muminin Ali, kama vile asemavyo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): Kupigana dhidi ya Ali ni kupigana dhidi yangu, zote hizi ni za uwongo? Au mnakiri kwamba hadithi hizi ni za kweli kikamilifu hasa? Je, hazikuandikwa pamoja na vyanzo vya kuaminika katika vitabu vyenu vya maulamaa wenu wenyewe wa mashuhuri? Hatuhitaji kutaja kwamba hadithi hizi zimeandikwa na maulamaa wa ki-Shia pamoja na maoni kamili ya wote pamoja katika vitabu vyao vyote. Kama mnakubali hadithi hizi, lazima mkubali kwamba Masahaba wengi walikuwa wachupa mipaka na wenye dhambi kama Muawiya. Umar Ibn As, Abu Huraira, Samra Bin Jundab, Talha, Zubair wote hawa ambao waliasi na wakipigana dhidi ya Ali, kwa kweli waliasi dhidi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe. Na kwa vile wamepigana dhidi ya Mtume, kwa hakika walipotea kutoka kwenye njia iliyo nyooka. Hivyo, kama tunasema kwamba baadhi ya Masahaba walikuwa watumwa wa tamaa zao, hatukuwa tumekosea, kwa sababu tulichokisema kilikuwa ni kweli. Mbali na hili, hatuko wenyewe tu katika kushikilia kwamba baadhi ya Masahaba walikuwa wenye dhambi, madhalimu na wachupa mipaka. Tunategemeza msimsmo wetu juu ya vitabu vya maulamaa wenu wenyewe wakubwa.

MAONI YA IMAMU GHAZALI KUHUSU MASAHABA KUVUNJA KIAPO KILICHOCHUKULIWA SIKU YA GHADIR-E-KHUM.
Kama utachunguza kitabu cha Sirrul-Alamin kilichokusanywa na Abu Hamid Bin Muhammad Ghazali Tusi, kamwe hutapinga kile ambacho ninasema. Hata hivyo, ninalazimika kunukuu sehemu ya tansifu yake ya nne kwa kuunga mkono maelezo yangu. Anasema: Ushahidi na mantiki vikawa na mwanga, na kuna makubaliano ya wote pamoja miongoni mwa Waislamu kuhusiana na matini (maandiko) ya hotuba ya katika siku ya Ghadir-e-Khum kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: Yule ambaye ni maula kwake (ambaye namtawalia mambo yake), Ali ni maula wake (mwenye kumtawalia mambo yake). Kisha Umar mara moja akasema, Hongera, hongera, Ewe Abul-Hasani! Wewe ni maula wangu na vile vile maula wa waumini wote wanaume na wanawake. Aina hii ya pongezi kwa uwazi inaonesha kukubaliwa kwa amri ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na kukubaliwa kwa uongozi na ukhalifa wa Ali. Lakini baadae walizidiwa na tamaa zao za kidunia. Kupenda utawala na mamlaka kuliwanyima huruma. Walijichukulia

246

Mikesha ya Peshawar
wenyewe kumchagua Khalifa kule Saqifq-e-Bani Sadat. Walitaka kupandisha bendera ya kizazi chao wenyewe na kuteka nchi ili kwamba majina yao yaweze kuhifadhiwa katika historia. Walilewa tamaa ya madaraka. Walipuuza maamrisho ya Qurani, na maagizo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Waliuza dini yao kwa ajili ya dunia hii. Biashara mbaya iliyoje waliyofanya na Allah! Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa katika kitanda chake alichofia aliomba apewe kalamu na wino ili kwamba aweze kufafanua suala mrithi. (Allah anisamehe kwa kulisema hili), Lakini Umar alisema: Muacheni mtu huyu. Anaweweseka. Hivyo wakati ambapo Qurani Tukufu na hadithi hazikuweza kuwasaidia, walitegemea juu ya Ijma (makubaliano ya wote pamoja). Lakini hii vile vile ni batili kwa sababu Abbas, kizazi chake, Ali, mke wake na watoto wao hawakujihusisha na wale ambao wamekula kiapo cha utii kwa Abu Bakr. Halikadhalika, watu wa Saqifa vile vile walikataa kula kiapo kwa Khazraji, na Ansar vile vile waliwakataa wao. Enyi watu mnaoheshimiwa! Tafadhali kumbukeni, Mashia hawadai chochote isipokuwa kile ambacho maulamaa wenu wa haki wanacho kidai. Lakini kwa vile mnatuchukia sisi, mnaona makosa katika yale tunayo yasema, hata yawe ya mantiki kiasi gani. Lakini kamwe hamuwalaumu maulamaa wenu ni kwa nini wameandika mambo kama haya ingawa kwa kweli wameufichua ukweli na wakachapisha ukweli huu kwenye kurasa za historia. Sheikh: Sirrul-Alamin haikuandikwa na Imamu Ghazali. Cheo chake kilikuwa cha juu sana kwa yeye kuweza kuandika kitabu kama hicho, na maulamaa wakubwa hawaamini kwamba kitabu hiki kiliandikwa na yeye.

SIRRUL-ALAMIN NI KITABU CHA IMAMU GHAZALI


Muombezi: Maulamaa wenu wengi wamekiri kwamba kitabu hiki kiliandikwa na Imamu Ghazali. Yusufu Sibt Ibn Jauzi alikuwa muangalifu sana katika rejea zake kwa wanachuoni wengine (na vile vile alikuwa mshabiki wa dini yake). Katika kitabu chake Tadhkira Khawasul-Umma, uk. 36, anajadili kutoka kwenye maelezo hayo hayo ya Imamu Ghazali katika kitabu chake Sirrul-Alamin na ananukuu dondoo hiyohiyo ambayo nimeinukuu. Kwa vile hakuna maoni yaliyofanywa kuhusu maelezo hayo, inaonesha kwanza, kwamba anakubali kitabu hiki kimeandikwa na Imamu Ghazali. Pili, vile vile anakubaliana na maoni yake, ambayo kwa ufupi nimeyaelezea, ingawa yeye mwenyewe ameyaelezea kwa urefu. Kama asingekubaliana nayo angeyatolea ufafanuzi. Lakini hakika maulamaa wenu mashabiki wanapokutana na maelezo kama haya ya manachuoni wakubwa na wakashindwa kuyakataa kimantiki, amma husema kwamba kitabu hicho

247

Mikesha ya Peshawar
hakikuandikwa na mwandishi huyo, au kwamba ni ubunifu wa Mashia. Au hata wakati mwingine wanakwenda mbali zaidi kufikia kusema kwamba watu hawa waadilifu wote walikuwa wenye dhambi na makafiri.

REJEA KWENYE CHEO CHA IBN IQDA


Kuna ushahidi kwamba maulamaa wenu wengi waliteswa kwa sababu tu walisema ukweli. Maulamaa mashabiki na watu wasio wasomi wa madhehebu yenu huchukulia kuwa ni haramu kusoma vitabu visivyofuata desturi na kanuni. Wandishi wa vitabu kama hivyo waliweza hata kuuawa kama ilivyokuwa kwa Hafidh Ibn Iqda Abul-Abbas Ahmad bin Muhammad Bin Said Hamadani ambaye alikufa 303 A.H. Alikuwa mmoja wa maulamaa wenu wakubwa. Wanachuoni mashuhuri wa madhehebu yenu, kama Dhahabi na Yafii, wamemkubali na wakasema kwmba amejifunza hadithi 300,000 pamoja na vyanzo vyao, na kwamba alikuwa mchamungu mkubwa. Katika mkusanyiko wa hadhara katika mji wa Kufa na Baghdad katika karne ya tatu A.H., alisimulia kwa uwazi makosa ya Masheikh wawili (Abu Bakr na Umar). Kwa sababu hiyo watu wakamuita Rafizi na wakajizuia kunukuu hadithi kutoka kwake. Ibn Kathir Dhahabi na Yafii wanaandika kuhusu yeye: Sheikh Ibn Iqda alikaa katika Msikiti wa Basra (Msikiti maarufu ulioko kati ya Baghdad na Kadhmain) na akasimulia kasoro na makosa ya Masheikh wawili (Abu Bakr na Umar) kwa watu. Kwa ajili hii hadithi zilizosimuliwa na yeye zimekataliwa. Vinginevyo hakuna shaka ya yeye kwamba ni mtu mkweli na mchamungu. Al-Khatib Baghdad vile vile alimsifia katika Tarikh yake lakini mwishoni akasema: Kwa vile alielezea kasoro na makosa ya Masheikh wawili (Abu Bakr na Umar) yeye alikuwa ni Rafizi. Hivyo watu nyie msiwe katika mawazo kwamba ni Mashia tu ambao wanafichua ukweli wa masuala haya. Maulamaa wenu wakubwa kama Imamu Ghazali na Ibn Iqda walizoea kuonyesha kasoro katika Masahaba wakubwa.

REJEA KUHUSU KIFO CHA TABARI


Katika kila zama ya historia kumekuwa na mifano ya maulamaa ambao wameteswa au kusumbuliwa kwa sababu ya kuongea au kuandika kwao ukweli. Kwa mfano yule mfasiri na mwanahistoria maarufu, Muhammad Ibn Jarir Tabari, ambaye alikuwa ni fahari ya maulamaa wenu, alikufa katika mwaka wa 310 A.H. mjini Baghdad. Lakini kwa sababu utawala uliogopa machafuko ya raia, walikataa jeneza lake kutolewa mchana. Alizikwa kwa lazima wakati wa usiku ndani ya nyumba yake mwenyewe.

248

Mikesha ya Peshawar

KUUWAWA KWA NASAI


Mfano mwingine wa mateso ulikuwa ni kuuawa kwa Imamu Abdur-Rahman Ahmad Ibn Ali Nasai. Alikwa ni mtu wa heshima na anachukuliwa kama mmoja wa Maimamu wa Sahih Sitta (vitabu sahihi sita). Anatokana na maulamaa wenye vyeo vikubwa wa madhehebu yenu katika karne ya tatu A.H. Wakati alipofika Damascus katika mwaka wa 303 A.H., aliona kwamba, kwa sababu ya Bani Umayya, wakazi wa sehemu ile walikuwa wakilikashifu jina la Amirul-Muminin Ali Bin Talib kwa uwazi kabisa baada ya kila salat ya faradhi, hususan katika hotuba za salat za jamaa. Alisikitishwa sana kwa kuiona hali hii na aliamua kukusanya hadithi zote za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) zenye kumsifia AmirrulMuminin pamoja na nyororo za vyanzo vyao, zote zile ambazo alizikumbuka. Kutokana nazo hizo, aliandika kitabu, Khasaisul-Alawi, katika kutetea cheo kitukufu na sifa bora za Ali. Alikuwa kila mara akiwasomea watu kutoka juu ya mimbari, hadith kutoka kwenye kitabu chake, zenye sifa za Mtukufu Imam Ali. Siku moja wakati alipokuwa anasimulia sifa za hali ya juu za Ali, kundi la wafanya vurugu lilimburuza kutoka kwenye mimbari na kumpiga sana. Walimpiga mateke kwenye korodani zake na kukamata kwa nguvu uume wake, wakamburuza nje ya Msikiti na wakamtupa mtaani kwenye barabara. Kwa matokeo ya majereha haya alikufa baada ya siku chache. Mwili wake ulichukuliwa ukapelekwa Makka ambako alizikwa. Matukio haya ni matokeo ya uadui na ujinga. Sasa naomba msamaha kwamba nimesukumwa nje mbali kidogo kutoka kwenye nukta yangu. Nilichomaanisha ni kwamba nafasi ya Wilayat (Umakamu) wa Amirul-Muminin haikuandikwa na maulamaa wa ki-Shia peke yao tu. Maulamaa wenu mashuhuri vile vile wamesimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mbele ya watu 70,000 au 120,000, alinyanyua mkono wa Ali na akamtambulisha kama Imamu (Kiongozi na mlezi) wa watu.

MASHAKA YA SUNNI KUHUSU MAANA YA MAULA


Hafidh: Hakika hukuna shaka kuhusu tukio hili na matini ya hadithi hii, lakini wakati huo huo haina umuhimu ambao ufasaha wako wa hisia unaonesha. Mbali na hili, kuna baadhi ya mashaka kuhusiana na matini ya hadithi hii. Kwa mfano neno maula, umetuambia kwamba lina maana: Mtu ambaye ana mamlaka makubwa juu ya wengine, ingawa inajulikana kwamba katika hadithi hii maula maana yake mpenzi, msaidizi na rafiki. Mtume alijua kwamba Ali alikuwa na maadui wengi na hivyo alitaka kuwashauri watu kwamba yeyeyote yule ambaye alimpenda au alikuwa rafiki au msaidizi wake, Ali vile vile alimpenda na alikuwa rafiki yake na msaidizi wake. Sababu iliyomfanya atake kiapo cha utii kwa watu ilikuwa kwamba hakutaka wao wamsabibishie Ali matatizo.

249

Mikesha ya Peshawar
Muombezi: Nafikiri wakati mwingine bila sababu unachukuwa tabia ya viongozi wako waliokutangulia. Kama utaufikiria ukweli huu kwa makini, ukweli wa suala hili utakuwa wazi. Hafidhi: Ni mambo gani yanayothibitisha maoni yako? Tafadhali tujulishe.

MAANA YA MAULA KAMA KIONGOZI BWANA KUTOKANA NA AYA YA - YA AYYUHAR-RASUL BALIGH.


Muombezi: Ushahidi wa kwanza ni Qurani Tukufu na uteremshwaji wa aya: Ewe Mtume! Fikisha uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wako. Na ikiwa hukufanya hayo basi hukufikisha ujumbe wake. Na Allah atakulinda na watu (5:67) Hafidh: Utadai vipi kwamba aya hii iliteremshwa siku hiyo na kwa madhumuni haya? Muombezi: Maulamaa wenu wote wanaoheshimika wameikubali: Jalalud-Din Suyuti: Durrul-Mansur; Jz. 2, uk. 298; Hafidh Ibn Abi Hatim Razi: Tafsir-e-Ghadir; Hafidh Abu Jafar Tabari: Kitabul-Wilaya; Hafidh Abu Abu Abdullah Mahamili: Amali; Hafidh Abu Bakr Shirazi: Ma Nazala minal-Quran Fi Amiril-Muminin; Hafidh Abu Said Sijistani: Kitabul-Wilaya; Hafidh Ibn Mardawiyya: Tafsir-e-Ayah; Hafidh AbulQasim Haskani: Shawahidut-Tanzil; Abul-Fatha Nazari: Khasaisul-Alawi; Muinud-Din Meibudi: Sharh-e-Diwan; Kadhi Shekani: Fathul-Ghadir; Jz. 3, uk. 57; Sayyid Jamalud-Din Shirazi: Arbain; Badrud-Din Hanafi: Umdatul-Qari Fi Sharh-e-Sahih Bukhari, Jz. 8, uk. 584; Ahmad Thalabi: Tafsir Kashful-Bayan; Imamu Fakhrud-Din Razi: Tafsir-e-Kabir, Jz. 3, uk. 636; Hafidh Abu Nuaim Ispahani: Ma nazala minal-Qurani Fi Ali; Ibrahim bin Muhammad Hamwaini: Faraidus-Simtain; Nizamud-Din Nishapuri, Tafsir, Jz. 6, uk. 170; Sayyid Shahabud-Din Alusi Baghdadi: Ruhul-Maani, Jz. 2, uk. 348; Nurud-Din Bin Sabbagh Maliki: Fusulul-Muhimma, uk. 27; Ali Bin Ahmad Wahidi: Asbabun-Nuzul, uk. 150; Muhammad Bin Talha Shafii: Matalibus-Suul, uk. 16; Mir Sayyid Ali Hamadani Shafii: Mawadda ya 5 kutoka Mawaddatul-Qurba; Sheikh Sulaiman Balkhi Hanafi: Yanabiul-Mawadda, sura ya 39. Kwa ufupi, kwa kadiri ninavyojua mimi, maulamaa wenu mashuhuri thalathini wameandika katika vitabu vyao sahihi na katika sharhe zao kwamba aya hii tukufu iliteremshwa siku ya Ghadir-e-Khum kumhusu Amirul-Muminin Ali. Hata Kadhi Fazl Bin Ruzbahan, pamoja na uadui wake na ushabiki, anaandika: Hakika imethibitishwa katika vitabu vyetu sahihi kwamba wakati aya hii ilipoteremshwa, Mtume wa Allah akiwa ameushika mkono wa Ali alisema: Kwa yeyote yule ambaye mimi ni

250

Mikesha ya Peshawar
maula (bwana) wake, huyu Ali vile vile ni maula wake. Hata hivyo, inashangaza kwamba Kadhi huyu huyu mpotofu katika Kashf Ghumma anatoa taarifa ya ajabu kutoka kwa Razi Bin Abdullah: Wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) tulizoea kusoma aya hii hivi: Ewe Mtume wetu (Muhammad) fikisha yale uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wako, yaani kwamba Ali ni bwana wa waumini. Kama hutafanya, basi utakuwa hukufikisha ujumbe wake. Vile vile Suyuti katika Durrul-Mansur kutoka kwa Ibn Mardawiyya, Ibn Asakir na Ibn Abi Hatim kutoka kwa Abu Said Khudiri, Abdullah Ibn Masud (mmoja wa waandishi wa Wahyi) na Kadhi Shukani katika Tafsir-e-Fathul-Ghadir wanasimulia kwamba wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wao vile vile walisoma aya hiyo katika njia hiyo hiyo. Kwa ufupi hili onyo lililomo katika aya hii linasema: Kama hukufanya basi utakuwa hukufikisha ujumbe (kabisa) huonesha kwamba ujumbe ambao Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliamriwa kuutoa ulikuwa wa umuhimu mkubwa sana. Kwa hakika ulikuwa ni muhimu kwa ukamilifu wa utume wenyewe. Kwa hiyo, kwa hakika suala katika mjadala lilikuwa habari ya uimamu, utunukiaji wa mamlaka juu ya mtu ambaye angewaongoza watu kwa mujibu wa mafundisho ya Uislamu baada ya kifo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

KUSHUKA KWA AYA SIKU YA LEO NIMEKUKAMILISHIENI DINI YENU PALE GHADIR-E- KHUM
Mazingira ya pili ambayo yanathibitisha nukta yangu ni kule kushuka kwa aya:

Siku ya leo nimekukamilishieni dini yenu na kukutimizieni neema yangu kwenu na kuwachagulieni Uislamu kuwa ndio dini yenu. (5:3) Hafidh: Lakini ni jambo linalokubalika kwamba aya hii iliteremshwa siku ya Arafa, na hakuna hata mmoja katika maulamaa aliyedai kwamba aya hii iliteremshwa siku ya Ghadir. Muombezi: Nakuomba usifanye haraka isiyo na maana katika kuukataa ukweli huu. Kama mambo yalivyo, nakubali kwamba baadhi ya maulamaa wenu wamesema kwamba aya hii iliteremshwa siku ya Arafa, lakini idadi kubwa ya ulamaa wenu waheshimika vile vile wamesema kwamba iliteremshwa siku ya Ghadir. Vile vile baadhi ya ulamaa wenu wana maoni ya kwamba pengine aya hii iliteremshwa mara mbili, mara ya kwanza pale

251

Mikesha ya Peshawar
mwishoni mwa siku ya Arafa na tena siku ya Ghadir. Kwa hiyo, Sibt Ibn Jauzi anasema katika Khawasul-Umma, uk. 18: Inawezekana kwamba aya hii iliteremshwa mara mbili, mara ya kwanza katika siku ya Arafa na mara nyingine katika siku ya Ghadir-e-Khum, kama vile aya ya: Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu, ilivyoteremshwa mara mbili, mara ya kwanza mjini Makka na mara nyingine tena mjini Madina. Wanachuoni wenu wakuaminika, kama Jalalud-Din Suyuti katika Durrul-Mansur, Jz. 2, uk. 256 na Itqan, Jz. 1, uk. 31; Imamu l-Mufassirin Thalabi katika Kashful-Bayan; Hafidh Abu Nuaim Ispahani katika Ma Nuzala Minal-Qurani Fi Ali; Abul-Fatha Nazari katika Khasaisul-Alawi; Ibn Kathir Shami katika Tafsir Jz. 2, uk. 41 akimfuata Hafidh Ibn Mardawiyya: Muhammad Bin Jarir Tabari, Mwanachuo, mfasiri na mwanahistoria wa karne ya tatu A.H. katika Tafsir-e-Kitabul-Wilaya; Hafidh AbullQasim Haskani katika Shawahid-ut-Tanzil; Sibt Ibn Jauzi katika Tadhkira-e-KhawasulUmma uk. 18; Abu Ishaq Hamwaini katika Faraidus-Simtain sura ya 12; Abu Said Sijistani katika Kitabul-Wilaya; Al-Khatib-e-Baghdadi katika Tarikh-e-Baghdad, Jz. 8, uk. 290; Ibn Maghazili Faqih Shafii katika Manaqib, sura ya 14 na Maqtalul-Husain, sura ya 4, wote wameandika kwamba katika siku ya Ghadir-e-Khum Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimteuwa Ali kwa amri ya Mungu kwenye cheo cha Wilaya (Makamu). Aliwaeleza watu kila kile ambacho aliamriwa kukisema kuhusu Ali na akainua mikono yake juu kiasi kwamba weupe wa makwapa yake ulionekana. Aliwahutubia watu hivi: Mpongezeni Ali kwa sababu ni Amir wa waumini. Jumuiya yote ilitekeleza amri hii. Walikuwa hawajaachana kila mmoja kuchukua njia yake wakati aya iliyotajwa hapo juu iliposhuka. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alifurahishwa mno kwa kuteremshwa aya hii. Hivyo, wakati akiwahutubia watu alisema: Allah ni Mkubwa, Ambaye ameikamilisha dini kwa ajili yao na amekamilisha neema Zake kwao na ameridhishwa na Utume wangu na umakamu wa Ali baada yangu. Imamu Haskani na Imamu Ahmad Bin Hanbal wametoa maelezo kamili ya tukio hili. Kama ninyi, waheshimiwa, mngeacha mawazo yenu yaliyojipandikiza juu ya suala hili, mtaweza kuzielewa aya tukufu na hadith, ambazo huonesha kwamba neno Maula maana yake walii (bwana) yaani, mtu aliye na mamlaka juu ya wengine wote. Kama maula au wali haikumaanisha mtu ambaye ana mamlaka makubwa juu ya wengine, neno liliofuatia baada yangu lingekuwa halina maana. Na maneno haya ambayo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliyarudia rudia kuyasema kutoka kwenye ulimi wake mtukufu, yanathibitisha kwamba maula na wali humaanisha mtu ambaye ana mamlaka makub-

252

Mikesha ya Peshawar
wa juu ya wengine wote, kwa sababu alisema kwamba cheo kile haswa kilitolewa kwa Ali baada yake. Tatu, unaweza kuyaangalia yale mazingira. Katika jangwa lile lenye joto, ambako kulikuwa hakuna hifadhi kwa ajili ya wasafiri, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akakusanya umma wote. Watu walikaa kwenye vivuli vya ngamia, miguu yao ikiwa imefunikwa, katika joto kali linalochoma la jua. Katika hali hii Mtume alitoa hotuba ndefu, ambayo Khawarizmi na Ibn Mardawiyya katika Manaqib zao na Tabari katika Kitabul-Wilaya na wengine wameisimulia. Je, inaleta maana kufikiria kwamba Mtume angetaka maelfu ya wafuasi wake kukaa siku tatu katika jangwa linalochoma kwa ajili ya kula kiapo kwa Ali kuonesha tu kwamba Ali alikuwa rafiki yao? Kwa hakika hakukuwa na mtu hata mmoja katika jumuiya yote ambaye alikuwa bado haujui ule uhusiano wa karibu kati ya Mtume na Ali au hajasikia kuhusu habari zake (kama nilivyokwishaeleza mapema). Kuteremshwa kwa aya ya Qurani iliyoko kwenye mjadala kwa mara ya pili, hususan katika mazingara tofauti pamoja na maelekezo hayo makali kwamba watu wangeweza kuwekwa kwenye takilifu kubwa na mashaka, isingeweza kuwa na maana tu kwamba lazima wao wawe marafiki wa Ali. Itakuwa utekelezaji huu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ama ulikusudiwa kuonesha umuhimu mkubwa sana, au ulikuwa ni upuuzi. Na hakika Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) yuko mbali na matendo yote ya kipuuzi. Kwa hiyo ni jambo la busara kuhitimisha kwamba, matayarisho haya hayakufanywa hivi hivi kwa ajili ya kuelekeza tu kwamba watu lazima wafanye urafiki na Ali. Kwa hakika tukio hili linaashiria kukamilika kwa ujumbe wa Mtume: kuthibitishwa kwa Uimamu, chanzo cha mwongozo wa umma baada ya kifo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

MAONI YA SIBT IBN JAUZI KUHUSU MAANA YA NENO MAULA


Baadhi ya ulamaa wenu mashuhuri wasifika wamikiri kwamba maana ya msingi ya neno Maula ni bwana. Miongoni mwao ni Sibt ibn Jauzi, ambaye baada ya kutoa maana kumi za neno hilo katika kitabu chake Tadhkiratul-Khawas, Sura ya 2, uk. 20, anasema kwamba kati ya zote hizo, ile maana ya kumi ndio inayoendana na kile alichokimaanisha Mtukufu Mtume kukisema. Yeye anasema: Hadithi hii inamaanisha haswa utii; hivyo hii maana ya kumi ndio iliyo sahihi, na yenyewe ina maana ya bwana mwenye mamlaka juu ya wengine. Kwa hiyo hadithi hii ina maana ya yeyote yule ambaye mimi ni bwana (maula) kwake, Ali pia ni bwana (maula) kwake. Katika kitabu cha Marajul-Bahrein Hafidh Abul-Faraj Yahya bin Said Saqafi anaitafsiri kwa maana kama hiyo hiyo. Yeye anasimulia hadithi hii kwa vyanzo vyake kutoka kwa viongozi wake, ambao wamesema kwamba, Mtukufu Mtume, akiwa amemshika Ali

253

Mikesha ya Peshawar
mkononi alisema: Yeyote yule ambaye mimi ni bwana (Maula) juu ya nafsi yake, Ali naye pia ni bwana (Maula) juu ya nafsi yake. Sibt ibn Jauzi anasema, Hadith ya Mtukufu Mtume inayosema kwamba Ali anayo mamlaka au ni bwana juu ya nafsi za waumini wengine inathibitisha wazi Uimam au Umakamu wa Ali na kwamba utiifu kwake yeye ni wajibu.

MAONI YA IBN TALHA SHAFII KUHUSU MAANA YA NENO MAULA


Muhammad Bin Talha Shafii katika Matalibus-Suul katikati ya sehemu ya 5, sura ya 1, uk. 16, anasema kwamba neno maula lina maana nyingi, kwa mfano: bwana, msaidizi, mrithi, muaminifu, na kiongozi. Kisha anasema kwamba hadithi hii tukufu inaitolea tafsri ya ndani aya ya Mubahila, (3:61). Ndani yake Allah (swt) amemuita Ali nafsi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kulikuwa hakuna utenganisho kati ya nafsi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na nafsi ya Ali kwa vile amezichanganya mbili hizi kwa kijina kiashiriacho kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Muhammad Bin Talha anaongeza: Katika hadithi hii Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anaonesha kwamba wajibu wowote walionao waumini kumhusu yeye, wanao wajibu huo vile vile kumhusu Ali. Kwa vile Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni hakika alikuwa bwana wa waumini katika mambo yao yote, msaidizi wao, kiongozi, na mtawala yote haya yakiwa vidokezo vya neno maula basi ina maana kwamba alimaanisha kitu hicho hicho kwa Ali (as). Na hii kwa hakika ni nafasi ya juu sana, cheo kitukufu mno, ambacho kilitolewa maalumu kwa Ali. Ni kwa sababu hii kwamba Siku ya Ghadir Khum ilikuwa ni siku ya idd (siku kuu) shangwe kwa ajili ya wapenzi na marafiki wa Ali. Hafidh: Kwa mujibu wa maelezo yako, kwa vile neno maula lina maana nyingi, itakuwa ni makosa kuamua kwamba lilitumika katika suala hili kuonesha maana moja bwana, na kuziweka kando hizo maana nyingine. Muombezi: Unatambua vema kanuni za msingi za wanachuoni kwamba wakati ambapo neno linaweza kuwa na maana nyingi tofauti, linakuwa na maana moja tu ya msingi na kwamba maana nyingine zinakuwa ni vinyambulika. Kwa mfano, walii wa nikah (ndoa) maana yake mtu anayesimama kama wakili, au mdhamini. Walii wa mwanamke ni mume wake, walii wa mtoto ni baba yake ambaye ana mamlaka kamili juu yake. Wali ahd (mrithi mstahiki) wa mfalme maana yake mtu ambaye haki yake ya kutawala haiwezi kukataliwa kama ataishi baada ya baba yake. Mbali na hili pingamizi lako linakurudia wewe, juu ya ni kwa nini umeweka mpaka kwenye maana yake rafiki na msaidizi wakati lina maana nyingine nyingi. Hivyo hili

254

Mikesha ya Peshawar
uainishaji huu bila ya lengo maalumu ni batili. Pingamizi ulilofanya linakurudia wewe mwenyewe na sio kwetu kwa sababu maana ambazo tumezibainisha hazikukosa kuwa na lengo maalum lililoainishwa. Aya za Qurani Tukufu, hadith, na maoni ya wanachuoni, vyote vinathibitisha maana hiyo hiyo tuliyoitoa. Miongoni mwa hizi ni zile sababu ambazo maulamaa wenu wakubwa, kama Sibt Ibn Jauzi, Muhammad Ibn Abi Talha Shafii wamezitoa kuhusiana na maana yake. Aidha, imesimuliwa kwa idadi kubwa ya hadithi kutoka kwenye vyanzo vyenu na vyangu kwamba aya hii tukufu ilikuwa inasomwa hivi kimaana: Ewe Mtume wa Allah! Fikisha kile ambacho kimeteremshwa kwako kutoka kwa Mola wako kuhusu wilaya ya Ali (umakamu) na kuwa kwake bwana wa waumini. Jalalud-Din Suyuti, ambaye ni mmoja wa maulamaa wenu mashuhuri amekusanya hadithi hizi kwenye kitabu chake, Durrul-Mansur.

HOJA ALIYOITOA ALI NDANI YA MSIKITI WA KUFA ILIYOKO JUU YA MSINGI WA HADITH YA GHADIR
Kama hadith hii na neno maula havikuwa uthibitisho wa Ali kama Imamu na Khalifa, Amirul-Muminin asingerudia mara kwa mara kuhoji kutokana nayo. Kwa hakika katika mikutano ya kamati za washauri alizirejea kama ushahidi wa Uimamu wake, kama walivyoandika: Khatib Khawarizmi katika Manaqib yake uk. 217; Ibrahim Ibn Muhammad Hamwaini katika Faraid sura ya 58; Hafidh Ibn Iqda katika KitabulWilaya; Ibn Hatim Damishqi katika Durrun-Nazim, na Ibn Abil-Hadid katika Sharhe-e-Nahjul-Balagha, Jz. 2, uk. 61. Cha umuhimu haswa ni ule ushahidi uliotolewa na masahaba thelathini kule Rahba. Maulamaa wenu mashuhuri wamesimulia majadiliano aliyoyafanya Ali pamoja na Waislamu kule Rahba-e-Kufa (yaani, katika uwanja wa msikiti wa Kufa). Ifuatayo ni sehemu ya orodha ya wale ambao wameandika tukio hili: Imam Ahmad Hanbal katika Musnad yake sehmu ya 1, uk. 129; Ibn Athir Jazari katika Asadul-Ghiba, Jz. 3, na Jz. 5, uk. 206 na 276; Ibn Qutayba katika Maarif uk. 194; Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafii katika Kifayatul-Talib; Ibn Abil-Hadid katika Sharh-e-Nahjul-Balagha, Jz. 1, uk. 362; Hafidh Abu Nuaim Isfahani katika HilyatulAuliya, Jz. 5, uk. 26; Ibn Hajar Asqalani katika Isaba, Jz. 2, uk. 408; Muhbud-Din Tabari katika Dhakhir-e-Uqba, uk. 67; Imamu Abdur-Rahman Nisai katika Khasaisul-Alawi, uk. 26; Allama Samhudi Katika Jawahirul-Iqdain; Shamsud-Din Jazari katika Asnul-Matalib, uk, 3; Sulaimani Balkhi Hanafi katika YanabiulMawadda, sura 4; Hafidh Ibn Iqda katika Kitabul-Wilaya. Ali alisimama mbele ya watu na akawataka kutoa ushahidi kuhusu kile walichosikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema kuhusu yeye pale Ghadir-e-Khum. Mashaba thelathini, pamoja na watu wa Badir kumi na

255

Mikesha ya Peshawar
mbili (wale ambao wamepigana katika vita ya Badr), walisimama na wakasema kwamba waliona katika Siku ya Ghadir-e-Khum Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akiushika mkono wa Ali akiwaambia watu: Je, mnajua kwamba ninayo mamlaka makubwa juu ya waumini kuliko waliyonayo katika nasi zao wenyewe? wote wakasema: Ndio. Kisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: Kwa yeyote yule ambaye mimi ni maula wake (mwenye kumtawalia mambo yake), basi huyu Ali ni maula wake (mwenye kumtawalia mambo yake).

HALI YA HUZUNI KWA WALE AMBAO HAWAKUTHIBITISHA HADITH YA GHADIR


Watu watatu kutoka katika mkusanyiko huu hawakutoa ushahidi wa tukio hili. Mmoja wao alikuwa Anas Bin Malik, ambaye alisema kwamba amedhoofika kwa uzee amesahau mambo yote kuhusu tukio hilo. Ali aliwalaani watu wale watatu. Alisema: Kama mnasema uwongo, Allah akupeni ukoma, ambao hata vilemba vyenu havitaweza kuuficha. Haukupita muda Anas aliposimama kutoka sehemu aliyokuwa amekaa ukoma ukatokea mwilini mwake. (kwa mujibu wa baadhi ya taarifa alipatwa na upofu na ukoma pamoja).

HOJA YA NNE: JE, MIMI SINA MAMLKA MAKUBWA JUU YENU KULIKO MLIYO NAYO KWENU WENYEWE?
Muombezi: Nne, njia ambayo hadithi hii imesimuliwa yenyewe inaonesha kwamba neno maula maana yake ni bwana. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika hotuba yake kule Ghadir, aliwauliza watu: Je mimi sina mamlaka makubwa juu yenu kuliko mliyonayo kwenu wenyewe? Hii inarejea kwenye yale maneno ya Qurani Tukufu: Mtume ana mamlaka makubwa juu ya waumini kuliko waliyo nayo juu yao wenyewe. (33:6) Aidha, kuna hadithi ya kutengemewa katika vitabu vya madhehebu zote ambayo inansmulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: Hakuna muumini ambaye kwamba sina mamlaka makubwa juu yake katika ulimwengu huu na katika Akhera, kuliko aliyonayo mwenyewe. Wote wakajibu kwa sauti moja kwamba ana mamlaka makubwa juu yao kuliko waliyonayo wao wenyewe. Baada ya hapo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: Yule ambaye mimi ni mawla (namtawalia mambo yake) huyu Ali ni mawla wake (mwenye kumtawalia mambo yake). Hivyo kutokana na muktadha wa hadithi hii hufuatia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimaanisha mamlaka au ubwana juu ya wengine wakati alipotumia neno maula. Hafidh: Katika vitabu vingi hakuna kumbukumbu kama hiyo ya Mtume kuwa amewahi kusema maneno haya: Je, mimi sina mamlaka juu yenu kuliko mliyonayo juu yenu wenyewe?

256

Mikesha ya Peshawar
Muombezi: Katika kusimulia hadithi ya Ghadir, wasimuliaji wametumia maneno tofauti kidogo, lakini kadiri ya hadithi za Shia zinavyohusika, maulamaa wote wa ki-Shia wanasema kwamba matini na muktadha wa hadithi ya Ghadir ni kama ilivyosimuliwa hapo juu. Na katika vitabu sahihi vingi vya Sunni, vilivyoandikwa na maulamaa wenu wakubwa, kama Sibt Ibn Jauzi katika Tadhkira-e-Khawasul-Umma uk. 18; Imamu Ahmad bin Hanbal katika Musnad yake; Nurud-Din Sabagh Maliki katika Fusulul-Muhimma; na kundi la wengi wengine ambao wamesimulia hadithi ya Ghadir, maneno Je, mimi sina mamlaka makubwa juu yenu kuliko mliyonayo wenyewe hupatikana humo. Sasa kwa ajili ya baraka nawasilisha hapa Tarjuma ya hadihti hii ambayo imesimuliwa na Imamu Ahmad Bin Hanbal katika Musnad yake, Jz. 4, uk. 281, kutoka kwa Baraa Bin Azib. Yeye alisema: Nilikuwa nasafiri na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Tulifika Ghadir. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akatangaza: Kusanyikeni kwa ajili ya Sala. Ilikuwa ni kawaida kama kulikuwa na kitu muhimu ambacho kilikuwa kitokee punde, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwaamuru watu kukusanyika kwa ajili ya Sala. Wakati watu wakiwa wamekwishakutanika na Sala imekwisha kutekelezwa, Mtume alizoea kutoa hotuba. Sehemu maalumu ilitayarishwa kwa ajili ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kati kati ya miti miwili. Baada ya kumalizika kwa Sala Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akiwa amenyanyua mkono wa Ali juu kupita kichwa chake, alizungumza na watu waliokusanyika pale: Je, mnajua kwamba mimi ni bwana wa waumini na nina haki zaidi juu ya kuliko waliyo nayo wao wenyewe juu ya nafsi zao. Wote wakasema, Ndio, tunajua hivyo. Alisema tena, Je, mnajua kwamba nina haki zaidi juu ya klia muumini kuliko aliyo kuwa nayo yeye mwenyewe? Wote wakajibu, Ndio tunalijua hilo. Baada ya hapo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema, Yeyote yule ambaye mimi ni maula wake (mwenye kumtawalia mambo yake) huyu Ali ni maula wake (mwenye kumtawalia mambo yake). Kisha akamuomba Allah: Ewe Allah! Kuwa rafiki kwa yule ambaye ni rafiki kwake (yaani, Ali) na kuwa adui kwa yule ambaye ni adui kwake. Mara tu kufuatia hili, Umar Bin Khattab alikutana na Ali na akasema, Hongera, Ewe mwana wa Abu Talib! Sasa umekuwa maula wa waumini wote wanaume na wanawake. Vile vile Mir Sayyid Ali Hamadani Shafii katika Mawaddatul-Qurba Mawadda ya 5; Sulaimani Balkhi katika Yanabiul-Mawadda na Hafidhi Abu Nuaim katika kitabu chake Hilya wameandika hadithi hii pamoja na tofauti kidogo katika maneno. Hafidhi Abul-Fatha, ambaye kutoka kwake Ibn Sabbagh vile vile amenukuu katika kitabu chake Fusulul-Muhimma, amesimulia hadithi hii katika maneno haya: Enyi watu! Allah Swt ni Maula wangu, nami ninayo mamlaka makubwa juu yenu kuliko mliyonayo juu yenu wenyewe. Inakupaseni mfahamu kwamba yeyote yule ambaye mimi ni maula kwake na huyu Ali vile vile ni maula wake. Ibn Maja Qazwini kaika Sunan yake na Imamu Abu

257

Mikesha ya Peshawar
Abdur-Rahman Nisai katika kitabu chake Ahadith (uk. 81, 83, 93, 24) wameisimulia hadithi hii kwa namna hiyo hiyo. Na Zaid Ibn Arqam anaandika katika hadithi yake Na. 84 kwamba Mtume wa Allah alisema katika hotuba yake: Je, mnajua kwamba ninayo mamlaka makubwa juu ya waumini wote, wanaume na wanawake, kuliko waliyonayo wao wenyewe? Wote wakasema: Tunashuhudia kwamba unayo mamlaka makuu juu ya kila muumini kuliko aliyonayo yeye mwenyewe. Katika wakati huo Mtume akasema: Kwa yeyote yule ambaye mimi ni maula (bwana) kwake huyu Ali vile vile ni maula (bwana) wake. Kisha akaunyoosha mkono wa Ali. Kwa nyongeza Abu Bakr Ahmad Bin Al-Khatib Baghdadi (amekufa 462 A.H.), katika kitabu chake Tarikh-e-Baghdad, Jz,. 8, uk. 289, 290, amesimulia hadithi ndefu kutoka kwa Abu Huraira kwamba kama mtu yeyote atafunga siku ya mwezi 8 Dhul-Hijja (Siku ya Ghadir), atalipwa malipo ya funga ya miezi sita. Kisha hapo akaindika hadithi hiyo hapo juu katika njia hiyo hiyo.

MASHAIRI YA HASAN MBELE YA MTUKUFU MTUME


Mazingira ya tano kuthibitisha wilaya (umakamu) ya Ali ni usomaji wa mashairi ambayo Hasan Bin Thabit aliyasoma kwa ruhusa ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), katika mkusanyiko wa watu ambapo cheo cha Ali cha umakamu kilitajwa. Sibt Ibn Jauzi na wengine wameandika kwamba wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliposikia beti hizo, alisema: Ewe Hasan! Kadiri unavyoendelea kutusaidia au kutusifia sisi kwa ulimi wako, basi ruhul-quds yule roho tukufu naye vile vile atakuwa anakusaidia wewe. Mfasiri mashuhuri na msimuliaji wa hadithi wa karne ya nne A.H., Hafidh Ibn Mardawiyya (amekufa 352 A.H.), katika manaqib yake; mkuu wa Mimamu, Muwaffaq Bin Ahmad Khawarizmi katika Manaqib yake na Maqtalul-Husain, sehemu ya 4; Jalalud-Din Suyuti katika Risalatul-Azhar fi ma Aqdahush-Shuara na wengi katika wanachuoni wenu, wasimuliaji wa hadithi, na wanahistoria wanasimulia kutoka kwa Abu Said Khudri kwamba katika Siku ya Ghadir-e-Khum, baada ya hotuba ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na uteuzi wa Ali kama mrithi wake, Hasan Bin Thabit alisema: Je, unaniruhusu nisome mashairi juu ya tukio hili? Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: Ndio, soma pamoja na baraka za Allah. Hivyo alisimama sehemu iliyonyanyuka kidogo na akasoma kwa mfululizo beti zilizotungwa.maana ya beti hizo ni kama ifuatavyo: Katika Siku ya Ghadir-e-Khum Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwakusanya watu pamoja, na niliisikia sauti yake ikiwaita. Mtume akawambia, Ni nani maula wenu na walii? Watu wakasema kwa uwazi, Allah ni Maula wetu na wewe ni walii (mlinzi) wetu na hakuna anayekataa ukweli huu. Hivyo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamuambia Ali: Simama! Ninaridhika na wewe kuwa imamu (makamu) na hadi (mlezi) baada yangu. Hivyo yeyote yule ambaye mimi ni maula wake huyu Ali vile vile ni maula wake. Kwa hiyo, ninyi watu

258

Mikesha ya Peshawar
wote lazima muwe watiifu na waminifu katika kumsaidia yeye. Kisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akaomba kwa Allah: Ewe Allah! Kuwa rafiki kwa yule ambaye ni rafiki kwake (Ali) na kuwa adui kwa yule ambaye ni adui kwake. Mashairi haya ni ushahidi wa wazi kwamba siku ile masahaba wa Mtume hawakulitafsiri neno maula katika njia nyingine yoyote isipokuwa ya Imamu na kwamba Ali atakuwa Khalifa baada ya Mtume kufariki. Kama neno maula halikuwa na maana ya Imamu au bwana juu ya wengine, basi Mtume mara moja angelimkatiza Hasan wakati anasoma ubeti, Ninaridhika na wewe kuwa Imamu na mlezi baada yangu, na angemuambia kwamba amekosea na kwamba hakuwa na maana kwamba Ali atakuwa Imamu na mrithi baada yangu, na kwamba kwa neno maula alimaanisha rafiki au msadizi. Lakini kwa kweli Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuunga mkona kwa kusema, Ruhul-Qudus naye vile vile atakusaidia. Mbali na hili, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa uwazi alielezea nafasi ya uimamu au wilaya (umakamu) wa Ali katika hotuba yake. Inakubidi uichunguze hotuba ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliyoitoa kaita Siku ya Ghadir-e-Khum na ambayo imeandikwa kwa ukamilifu na Abu Jafar Muhammad Ibn Jarir Tabari (amekufa 310 A.H.) katika kitabu chake Kitabul-Wilaya. Anaandika kwamba Mtume alisema: Sikilizeni na mtii. Hakika, Allah swt ni Maula wenu na Ali ni imamu wenu. Mpaka Siku ya Hukumu uimamu utabakia kwenye familia yangu, kizazi cha Ali.

MASAHABA WAVUNJA AHADI YAO WALIYOWEKA SIKU YA GHADIR


Maana yoyote mtakayoitoa kwa neno maula, ni ukweli unaokubalika kwamba Masahaba waliweka ahadi kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika siku ile. Kuna kupatana kabisa kati ya madhehebu hizi mbili juu ya nukta hii. Basi kwa nini walivunja ahadi hiyo? Hata tukichukulia tu kwa muda huu kwamba kwa kusema maula Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimaanisha rafiki au msaidizi tu, kwa kumuogopa Allah hebu tuambieni kama mnafikiri kwamba urafiki ule ulimaanisha kwamba waje wachome moto nyumba ya Ali, kuitishia familia yake, na na kumtishia yeye kwa panga zilizochomolewa! Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitoa maelekezo ya wazi kwamba Masahaba lazima wale kiapo cha utii kwa Ali. Unafikiria kwamba alikusudia kwamba wao kwa hiyo waje wamtese mkwe wake mwenyewe? Baada ya kifo cha Mtume, hawakuvunja kiapo chao? Je, wale waliovunja kiapo, kwa maoni yenu ninyi, hivi walitimiza masharti ya urafiki? Je, waliisoma aya 25 sura ya 13, Al-Rad (Radi) ya Qurani Tukufu? Na wale wanaovunja ahadi za Allah baada ya kuzifunga, na wanakata yale ambayo kwamba Allah ameamrihsa yaungwe, na wanafanya ufisadi katika nchi; hao ndio watakaopata laana, na watapata makazi mabaya. (13:25)

259

Mikesha ya Peshawar

MASAHABA WAVUNJA AHADI KULE UHUD, HUNAIN, NA HUDAIBIYYA


Katika vita ya Uhud na Hunain, wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipowafanya Masahaba wote waahidi kwamba siku hiyo hawatakimbia, je, sio hakika kwamba walikimbia? Walikimbia kutoka kwenye uwanja wa vita na wakamuacha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kukabiliana na adui. Hili limeandikwa na wanahistoria wenu wenyewe, kama Tabari, Ibn Abil-Hadid, na Ibn Asame Kufi. Je, huku sio kuvunja kiapo chenye uzito mkubwa? Naapa kwa Allah kwamba mnawatoa makosa bure Mashia wakati tunaposema yale tu ambayo wanahistoria wenu mashuhuri wameyasema.

MASHIA WANAWALAUMU MASAHABA WALE TU AMBAO VITENDO VYAO HAVIKUWA VYA HAKI
Sielewi ni kwa nini ninyi watu mmekuwa mkitushambulia kwa karne nyingi. Mnachoandika chochote ninyi kinakubaliwa, lakini kama tukiandika yale ambayo maulamaa wakubwa wa Sunni waliyo andika, tunaitwa makafiri kwa sababu tu tunakosoa dhulma za baadhi ya Masahaba. Hata hivyo, kama ukosoaji wa Masahaba humaanisha Urafidha, basi kwa dhahiri Msahaba wote walikuwa Marafidhi, kwa sababu wote kila mmoja alikosoa vitendo vibaya vya mwenziye. Hata Abu Bakr na Umar walifanya hivyo. Baadhi ya Masahaba wa Mtume walikuwa waumini wachamungu na walikuwa wakiheshimiwa sana. Wengine waliendekeza matamanio yao machafu na walilaumiwa. Kama unataka ushahidi wa kihistoria wa ukweli huu, nashauri kwamba usome Sharh-e-NahjulBalagha ya Abil-Hadid, Jz. 4, uk. 454, 462, na usome majibu ya marefu ya Zaid kwa ukinzani wa Abul-Maali Juwaini, ambayo Abu Jafar Naqib ameyaandika. Hapo ndipo utakapojua ni kiasi cha migogoro ilyokuwepo miongoni mwa Masahaba, ambao kwa hakika walilaaniana wenyewe kwa wenyewe kama waovu na makafiri.

KUKIMBIA KWA MASAHABA KULE HUDAIBIYYA


Katika maelezo yake ya suala la Hudaibiyya, Ibn Abil-Hadid, katika Sharh-e-NahjulBalagha, na wengine miongoni mwa wanahistoria wenu vile vile wameandika kwamba, baada ya kukamilika kwa mkataba ule wa amani, Masahaba wengi akiwemo Umar Bin

260

Mikesha ya Peshawar
Khattab, walionesha kuchukia kwao kuhusiana na masharti ya mkataba. Walimueleza Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwamba walikuwa hawakuridhika na mkataba wa amani na walitaka kupigana. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akawaambia kama walitaka kupigana walikuwa wako huru kufanya hivyo. Hivyo walishambulia. Lakini Masahaba wakashindwa vibaya na wakakimbia milimani na hawa hata hawakurudi kumlinda Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Ndipo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuambia Ali achomoe upanga na kuwafukuza Makuraishi. Walipomuona Ali mbele yao, Makuraishi walirudi nyuma. Baadae Masahaba waliokimbia walirudi na kuomba msamaha kwa Mtume. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akawaambia: Kwani mimi sikujueni ninyi! Nyie sio watu wale wale ambao walitetemeka kwa hofu katika vita vya Badir mpaka Allah swt akatuma malaika kwa ajili ya kutusaidia! Ninyi sio Masahaba wangu wale wale ambao katika Siku ya Uhud mlikimbia milimani na mkaniacha bila ulinzi? Ingawa niliendelea kuwaita, lakini ninyi hamkurudi. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akawahesabia udhaifu wao wote, na waliendelea kuelezea masikitiko yao kwa ajili ya vitendo vyao. Ibn Abil-Hadid anasema mwishoni mwa kazi yake ya kuandika kwamba karipio hili lilielekezwa haswa dhidi ya Umar, ambaye hakuamini ahadi zozote zilizowekwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kisha anaandika kwamba, kwa mwanga wa maelezo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Khalifa Umar lazima alikimbia kutoka kwenye vita ya Uhud kwa sababu katika mazungumzo yake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alilitaja hilo pia. Sasa mnaweza mkaona wenyewe kwamba kama tukielezea ukweli huu, ambao umeandikwa na maulamaa wenu wakubwa kama Abil-Hadid na wengine, mara moja tunalengwa kushambuliwa (eti) kwa sababu tumemtukana Khalifa, lakini hakuna kikwazo kwa AbilHadid. Kwa kweli hatuna nia ya kumtukana mtu yeyote. Sisi tunasimulia mambo ya kihistoria tu, na mnatuangalia kwa macho ya dharau. Mnayapuuza mambo hayo.

MASHIA WATATAFUTA FIDIA YA HALI YA MAMBO SIKU YA HUKUMU


Mashia watakuwa na malalamiko mengi Siku ya Hukumu dhidi ya Ulamaa wenu. Ulimwengu utatoweka, lakini lazima msimame mbele ya Mahakama Adilifu ya Allah kwa ajili ya kujibu uonevu wenu. Hafidh: Tafadhali niambie ni kwa uonevu upi ambao mtatafuta haki Siku ya Hukumu? Muombezi: Kuna mifano ambayo naweza kuionesha. Wakati Siku ya Hukumu Tukufu itakapowadia, kwa hakika nitaitafuta haki. Hafidh: Nakuomba usichochee mihemuko ya (watu) wengine. Tuambie ni uonevu gani uliokupata.

261

Mikesha ya Peshawar
Muombezi: Uonevu na dhulma sio jambo geni leo kwetu sisi. Lakini msingi wake ulijengwa mara tu baada ya kufariki kwa babu yetu, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Haki ya bibi yetu mdhulumiwa, Fatima Zahra ambayo aliachiwa na baba yake, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kwa ajili ya kuwalea watoto wake, iliporwa. Hakuna kujali kokote kulikofanywa kwa ajili ya malalamiko na upingaji wake wa dhati. Hatimaye alifariki katika ujana wake akiwa amevunjika moyo. Hafidh: Tafadhali, unawachochea watu bila sababu yoyote. Tuambie ni haki gani ya Fatima iliyoporwa? Tafadhali kumbuka kwamba kama utashindwa kuthibitisha dai lako, kwa kiasi fulani utashindwa katika Mahakama Tukufu ya Haki. Jione uko katika Mahakama ya Mungu ya Uadilifu na utetee kesi yako. Muombezi: Siku moja tutakuwa mbele ya Mahakama Tukufu. Tunategemea kupata haki. Kama wewe pia unayo hisia ya uadilifu, basi yakupasa kama hakimu muadilifu kusikiliza hoja yangu bila chuki. Naamini utakubali uhalali wa dai letu. Hafidh: Naapa kwamba sina chuki au ukaidi. Hakika umeona katika mikesha hii kwamba sihoji kipumbavu. Wakati niliposikia hoja zenye mantiki nilizikubali. Kunyamaza kwangu kwenyewe kulikuwa kunaonesha kwamba nimekubaliana na mwenendo huu wa haki. Kwa asili mimi sio mtu wa kupenda mizozo. Nakiri kwamba kabla sijakutana na wewe hapa, nilitaka nikushinde. Lakini nimevutiwa mno na usafi wako, upole wako, tabia nzuri, wepesi na hisia ya kweli, kiasi kwamba nimeweka nadhiri mbele ya Allah kwamba nasalimu amri kukubali ukweli wote wenye mantiki ingawa msimamo huu utavunja mioyo juu ya matarajio ya wengine. Niamini mimi, sioyule mtu wa ule usiku wa kwanza. Nakueleza kwa ukweli na uwazi kabisa kwamba hajo zako zimeacha athari ya ndani mno katika moyo wangu. Kwa dhati kabisa natumaini kwamba nitaweza kufa pamoja na mapenzi na upendo kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kizazi chake, ili kwamba niweze kusimama kwa furaha na kuridhia mbele ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Muombezi: Naam, hakika msimamo kama huo ulikuwa unategemewa kwa mwanachuoni kama wewe. Hakika mimi pia nimevutiwa sana na maelezo yako, na imejengeka kwangu hisia ya urafiki kwa upande wako. Sasa ningependa kuleta ombi kwako. Natumaini utalikubali. Hafidh: Ndio, tafadhali. Muombezi: Usiku huu ningetaka niwe hakimu na wengine wawe mashahidi, ili kwamba uweze kuamua bila chuki yoyote iwapo dai langu ni haki. Baadhi ya waumini wasio na ujuzi wanasema kwamba hakuna maana kujadili suala ambalo limetokea miaka 1,300 iliyopita. Hawajui kwamba masula yanayohusiana na elimu yanajadiliwa katika kila zama. Majadiliano ya haki hufichua ukweli na madai ya urithi yanaweza kufanywa kisheria na

262

Mikesha ya Peshawar
mwenye kurithi, kwa wakati wowote ule. Kwa vile mimi ni mmoja wa warithi, nataka kukuuliza swali. Tafadhali nakuomba unipe jibu la haki. Hafidh: Ndio, nitapendezewa sana kusikia maelezo yako. Muombezi: Kama kwa amri ya Mungu baba anampa mtoto wake mali, na, baada ya kifo cha baba, kama mali ile inachukuliwa kutoka kwa mtoto ambaye anamiliki mali ile, je, itakuwa ni aina gani ya madai? Hafidh: Kitendo cha mnyanganyi kitakuwa sio cha haki kabisa. Lakini unamkusudia nani wakati unaposema muonevu na muonewa?

FADAK NA UPORWAJI WAKE


Wakati ngome ya Khaibar iliposhindwa na kutekwa, malodi, makabaila na watu mashuhuri wa Fadak walikuja kwa Mtume. Fadak ilikuwa ni eneo katika bonde la milima ya Madina. Lilikuwa na vijiji saba ambavyo vimeenea mpaka kwenye mwambao wa bahari. Vingi vilikuwa na rutuba sana na kulikuwepo na chemchem nyingi zenye miti (oasisi). Kulikuwepo na mkataba wa amani na watu unaosema kwamba nusu yote ya Fadak itakuwa chini ya miliki yao na nusu nyingine itakuwa mali ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Ukweli huu umesimuliwa na Yaqut Hamawi, mwaandishi wa Majimul-Buldan, katika kitabu chake Futuhul-Buldan, Jz. 6, uk. 343; Ahmad Bin Yahya Baladhuri Baghdadi (alikufa 279 A.H.) katika kitabu chake Tarikh; Ibn Abil-Hadid Mutazali katika Sharhe yake ya Sharh-e-Nhjul-Balagha, (iliyochapishwa Misir), Jz. 4, uk. 78, akinukuu kutoka kwa Abu Bakr Ahmad Bin Abdul-Aziz Jauhari; Muhammad Bin Jarir Tabari katika kitabu chake Tarikh-e-Kabir na wengine wengi katika muhadithina na wanahistoria wenu.

KUTEREMSHWA KWA AYA YA MPE HAKI YAKE JAMAA WA KARIBU


Wakati Mtume aliporudi Madina, Jibril aliteremsha aya ifuatayo: Na mpe jamaa yako wa karibu haki yake, na masikini, na msafiri; wala usitumie ovyo kwa fujo. (7: 26) Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitafakari juu ya umuhimu wa wahayi huu. Jibril alitokea tena na akamjulisha kwamba Allah ameamuru kwamba: Fadak itolewe kwa Fatimah. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamuita Fatima na akasema: Allah emeniamuru kuitoa Fadak kama zawadi kwako. Hivyo mara moja alimpa Fatima umiliki wa Fadak.

263

Mikesha ya Peshawar
Hafidh: Tafadhali fafanua unachosema kuhusu tukio ambalo aya hii tukufu imeteremshwa. Je, imeandikwa kwenye vitabu vya historia na tafsir vya Shia, au vile vile umeiona (habari hii) katika vitabu vyetu vya kutegemewa? Muombezi: Mkuu wa wafasir, Ahmad Thalabi katika kitabu chake Kashful-Bayan; Jalalud-Din Suyuti katika Tafsir yake, Jz. 4, akisimulia kutoka kwa Hafidh Ibn Mardawiyya; yule mufasir mashuhuri Ahmad Bin Musa (aliyekufa 352 A.H.) Akisimulia kutoka kwa Abu Said Khadiri na Hakim Abu l-Qasim Haskani; Ibn Kathir; Imadud-Din Ismail; Ibn Umar Damishqi; Faqih-e-Shafii katika kitabu chake cha Tarikh, na Sheikh Sulaimani Balkhi Hanafi katika Yanabiul-Mawadda, sura ya 39, akisimulia kutoka Tafsir-e-Thalabi, Jamul-Fawaid na Uynul-Akhbar wote wanasimulia kwamba wakati aya, Na mpe jamaa yako wa karibu haki yake, ilipoteremshwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wa Allah alimuita Fatima na akampa Fatima Fadak kubwa kama zawadi kwake. Kwa hiyo, kadiri Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alivyoishi, Fadak ilibakia katika miliki ya Fatima. Bibi yule mtukufu aliikodisha ardhi ile; mapato yake yalikusanywa katika awamu tatu. Kutoka katika hesabu hii alichukuwa pesa ya kutosha kwa ajili ya chakula chake na cha watoto wake na akagawanya alubaki kwa watu masikini wa Bani Hashim. Baada ya kifo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), maofisa wa Khalifa anayetawala walinyakua mali hii kutoka kwa Fatima. Nakuulizeni enyi waheshimiwa, mnieleze katika jina la uadilifu mtakiitaje kitendo hiki? Hafidh: Hii ndio mara ya kwanza nimesikia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimpa Fatima Fadak kwa amri (ya Allah). Muombezi: Inawezekana kwamba hukuweza kusikia kuhusu (suala) hili. Lakini kama ambavyo nimekuambia, wengi wa maulamaa wenu wakubwa wameandika kuhusu suala hili katika vitabu vyao vya kutegemewa. Ili kuthibitisha nukta hii kwa uwazi nakurejeshea kwa Hafidh Ibn Mardawiyya, Waqid na Hakim (Angalia Tafsir na Tarikh zao); JalaludDin Suyut Durrul-Mansur, Jz. 4, uk. 177; Kanzul-Umma ya Mullah Ali Muttaqi na maelezo mafupi ambayo ameandika juu ya Kitabul-Akhlak ya Musnad ya Ahmad Bin Hanbal kuhusu tatizo la Sila-e-rahm; na Sharh-e-Nahjul-Balagha ya Ibn Hadid, Jz. 4. Maulamaa wote hawa wamesimulia katika njia tofauti, isipokuwa maelezo kutoka kwa Abu Said Khudr, kwamba aya hiyo hapo juu ilipoteremshwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliitoa Fadaka na kumpa Fatima Zahra.

HOJA KUTOKA HADITH YA LA NURITH HATUACHI URIHTI


Hafidh: Ni ukweli unaokubalika kwamba Mahalifa waliinyanganya Fadak juu ya msingi wa hadithi inayojulikana sana iliyosimuliwa na Abu Bakr, ambaye alitamka kwamba yeye mwenyewe amemsikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema: Sisi Mitume hatuachi

264

Mikesha ya Peshawar
urithi wowote nyuma yetu; chochote tunachoacha kama urithi ni sadaka (yaani, ni mali ya umma).

FADAKA ILIKUWA ZAWADI SIO URITHI


Muombezi: Kwanza, sio mali ya urithi bali ni zawadi. Pili, hiyo hadithi inayodaiwa kuwa ni ya Mtume haikubaliki. Hafidh: Utatoa hoja gani ya kuikataa hadithi hii? Muombezi: Kuna sababu nyingi za kuikataa hadithi hii.

HADITHI LA NURITH NI YA KUBUNIWA


Kwanza kabisa, yeyote yule aliyeiandaa hadithi hii, aliitamka bila kufikiria kuhusu yale maneno aliyotumia. Kama angekuwa muangalifu kuhusu hadithi hii, kamwe asingelisema: Sisi Mitume hatuachi urithi wowowte, kwa sababu angelijua kwamba uwongo wake ungefichuliwa na maneno haya haya ya hadithi hii ya kubuni. Kama angetumia maneno Sikuacha urithi wowote nyuma, hadithi yake ya majaribio ingekuwa yenye kuelekea kuwa ya kweli zaidi.

Lakini wakati ametumia wingi Sisi Mitume tunawajibika kuchunguza ukweli wa hadithi hii. Sasa kwa msingi wa maelezo yako mwenyewe tunarejea kwenye Qurani Tukufu kwa ajili ya mwongozo. Tunaona kwamba kuna idadi ya aya ambazo zinatueleza kwamba kwa kweli mitume waliacha urithi. Hii inathibisha kwamba hadithi hii ni ya kutupwa moja kwa moja.

FATIMA ALITETEA MADAI YAKE


Katika kitabu chake Kitab-e-Saqifa mwanachuoni mkubwa na muhadithina, Abu Bakr Ahmad Bin Abdul-Aziz Jauhari, ambaye kuhusu yeye Abil-Hadid anasema katika kitabu chake Sharh-e-Nahjul-Balaghah kwamba alikuwa ni mmoja wa maulamaa wakubwa na muhadithina wa Masunni; Ibn Al-Athir katika kitabu chake Nihaya; Masud katika Akhbaruz-Zaman na katika Ausat; Ibn Abil-Hadid katika Sharh-e-NahjulBalaghah Jz. 4, uk. 78, akinukuu kutoka kitabu cha Abu Bakr Ahmad Jauhari Saqifa na Fadak katika njia tofauti na kutoka kwenye idadi ya vyanzo, baadhi ambavyo hurejea kwa Imamu wa tano Muhammad Baqir kupitia kwa Siddiq Sughra Zainab-e-Kubra na baadhi ambavyo hurejea kwa Abdullah Ibn Hasan kutoka kwa Siddiq Kubra Fatima Zahra na kutoka kwa Ummul-Muminin Aisha na vile vile kutoka kwa Muhammad Bin Imran

265

Mikesha ya Peshawar
Marzabani, yeye kutoka kwa Zaid bin Ali bin Husein; yeye kutoka kwa baba yake, na yeye kutoka kwa baba yake, Imam Husein; na yeye kutoka kwa mama yake maarufu, Fatima Zahra; na maulamaa wengine wengi wa madhehebu yenu wamesimulia hotuba ya Fatima mbele ya mkusanyiko mkubwa wa Waislamu. Wapinzani walifadhaishwa wakati waliposikia hoja zake na hawakuweza kujibu. Kwa vile walikuwa hawana majibu ya kutoa walianzisha ghasia.

HOJA YA FATIMA YA KUKATAA HADITH LA NURITH


Moja ya hoja za Fatima za kukataa hadithi hii ilikuwa kwamba, kama hadithi hii ingekuwa ni ya kweli, basi kwa nini kulikuwa na aya nyingi mno kuhusu urathi wa mitume. Alisema: Katika sehemu moja Qurani inasema: Na Suleimani alikuwa mrithi wa Daudi. (27:16) Kuhusu Mtume Zakariya Qurani Tukufu inasema:

Basi nipe mrithi kutoka kwako, ambaye atarithi kutoka kwangu na mrithi (vile vile) wa nyumba ya Yaaqub (19:5-6) Kuhusu maombi ya Zakariya Qurani Tukufu inasema:

Na Zakariya alipomuomba Mola Wake: Mola Wangu, usiniache peke yangu (bila mtoto), na Wewe ndiye Mbora wa wanaorithi. Basi tukamkubalia na tukampa Yahya (21:89-90) Baada ya haya akasema: Ewe mtoto wa Abu Qahafa! Je, imo ndani ya Kitabu cha Allah kwamba wewe ni mrithi wa baba yako na mimi ninanyimwa urithi wa baba yangu? Umefanya kashfa kubwa mno. Enyi watu! Je, mmekiacha kwa mkusudi Kitabu cha Allah (Qurani Tukufu) na kukipuuza moja kwa moja? Je, mimi sio mtoto wa Mtukufu Mtume? Kwa nini unaninyima mimi haki yangu? Kwa nini aya zote hizi za urithi, ambazo zimekusudiwa kwa watu wote kwa ujumla na hususan kwa Mitume zimejumuishwa katika Qurani Tukufu? Je, si kweli kwamba aya za Qurani zitabakia bila kubadilishwa mpaka

266

Mikesha ya Peshawar
Siku ya Hukumu? Je, Qurani haisemi: .....na ndugu wa nasaba wana haki zaidi wao kwa wao katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu..... (8:75) na: Allah anakuusieni juu ya watoto wenu! Mtoto mwanaume atapata vigawanyo viwili vya mwanamke (4:11) na: Mmelazimishwa, mmoja wenu anapofikiwa na umauti, kama ameacha mali, kuwausia wazazi wake wawili na jamaa wa karibu kwa uadilifu. (Huu) ni wajibu kwa wamchao Mwenyezi Mungu (2:180). Basi kwa nini mimi hasa hasa niwe nimenyimwa urithi wa baba yangu? Je Allah ameteremsha aya maalumu kwako, ambazo zinamuondoa baba yangu (kutoka kwenye haki yake hii). Je, wewe unajua maana ya nje na ya ndani ya Qurani Tukufu kuliko baba yangu Muhammad na binamu yake Ali?

UTETEZI WA FATIMAH HAUNA MAFANIKIO


Wakati waliponyamazishwa na hoja hizi na ukweli wa mambo, wakawa hawana majibu. Walikimbilia kwenye hila na lugha ya matusi. Alilia huku akisema: Leo mumeuvunja moyo wangu. Siku ya Hukumu nitafungua mashitaka dhidi yenu katika Mahakama Tukufu ya Haki na Allah Mwenye nguvu zote ataamua kesi hiyo kwa uadilifu. Allah ndiye Hakimu bora zaidi. Muhammad ndiye mkuu na bwana; muda wa ahadi, wetu na wenu ni Siku ya Ufufuo. Siku hiyo muonevu atakuwa mwenye hasara, na toba yenu haitawasaidia kitu. Kwani kwa kila kitu kuna muda maalumu uliopangwa na mtajua muda mfupi tu ujao nani atapatwa na adhabu ya dharau.

KHALIFA ALITUMIA LUGHA CHAFU


Hafidh: Nani atathubutu kukashifu kipande cha mwili wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Fatima Zahra? Hili siliamini. Hila na udanganyifu inawezekana, lakini kutumia lugha ya matusi haiwezikani. Tafadhali usiseme vitu kama hivyo. Muombezi: Hakuna mtu aliyekuwa na ujasiri wa kusema vitu kama hivyo isipokuwa Khalifa wako, Abu Bakr. Akiwa ameshindwa kujibu hoja nzito za Bibi huyo muonewa, mara moja alipanda kwenye mimbari na kumtukana Fatimah na mume wake na binamu yake Mtume, kipenzi cha Allah na cha Mtume Wake, Amirul-Muminin Ali. Hafidh: Nadhani riwaya hizi za kizushi zimeenezwa na mashabiki wa kidini. Muombezi: umekosea. Riwaya hizi hazikuenezwa na mashabiki wa ki-Shia. Maulamaa wakubwa wa Sunni ndio waliozisambaza. Kwa kiasi chochote cha kukosa uvumilivu wanachoweza kuwa nacho watu wetu wa kawaida, kamwe huwa hawabuni hadithi. Kama utachunguza vitabu vyenu vya sahihi, utakiri kwamba maulamaa wenu wakubwa

267

Mikesha ya Peshawar
wameyakubali mambo haya. Ibn Abil-Hadid Mutazali katika Sharh-e-Nahjul-Balagha Jz. 4, uk. 80, iliyochapishwa Misri, akisimulia kutoka kwa Abu Bakr Ahmad Bin AbdulAziz Jauhari, ameandika kwa urefu kuhusu Abu Bakr kupanda juu ya mimbari baada ya malalamiko ya upinzani wa Ali na Fatimah.

KUPINGANA KWA ALI NA ABU BAKR


Wanachuoni wengi wamesimulia kwamba, wakati Fatimah alipomaliza kutetea hoja yake, Ali akaanza upingaji wake katika mkusanyiko wa hadhara wa Waislamu katika Msikiti wa Madina, akielekea upande alikokuwa Abu Bakr, alisema: Kwa nini unamnyima Fatimah urithi wa baba yake, ingawa alikuwa ndiye mmliki wake na alikuwa anaimiliki mali hiyo wakati wa kipindi cha uhai wa baba yake? Abu Bakr akajibu: Fadak ni ngawira ya Waislamu. Kama Fatimah atatoa ushahidi kamili kwamba ni mali yake, kwa hakika nitampa; vinginevyo, nitamnyima mali hiyo. Mtukufu Imamu akasema: Je, sio ukweli kwamba wakati unatamka hukumu kuhusu Waislamu, kwa ujumla, unapitisha hukumu inayokinzana mno kuhusiana na sisi.? Je, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakusema kwamba dhima ya kuthibitisha inakuwa juu ya mdai na ile ya utetezi juu ya mdaiwa? Umepuuza hukumu ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kinyume na sheria ya dini, unataka mashahidi kutoka kwa Fatimah ambaye alikuwa katika umiliki wa mali hiyo tangu wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Aidha, je, maneno ya Fatimah, ambaye ni mmoja wa Ashab-e-Kisa (Watu wa Shuka) na ambaye amejumuishwa katika aya ya utakaso, sio ya kweli? Kama watu wawili wangetoa ushahidi kwamba Fatimah amefanya makosa fulani, hebu niambie ungemshughilikia vipi? Abu Bakr akasema: Ningetoa adhabu juu yake kama ambavyo ningefanya kwa mwanamke yeyote. Mtukufu Imamu akasema: Kama ungefanya hivyo, ungekuwa kafiri mbele ya Allah, kwa sababu ungekuwa umekataa ushahidi wa Allah kuhusu usafi wa Fatimah. Allah anasema: Hakika, hakika, Allah anataka kukuondoleeni kila aina ya uchafu, Enyi Watu wa Nyumba na kuwatakaseni kwa utakaso halisi. Je, aya hii haikuteremshwa katika kutukuza sisi? Abu Bakr akasema: Kwanini isiwe hivyo? Imamu akasema: Je, inawezekana kwamba Fatimah, ambaye usafi wake umethibitishwa na Allah, angeweza kutoa madai ya uwongo kwenye mali ndogo kama hii? Unakataa ushahidi wa mtu aliyetakaswa na unakubali ushahidi wa Bedui ambaye anakojoa juu ya kisigino cha mguu wake mwenyewe! Baada ya kusema haya, Imam akarudi nyumbani kwake akiwa amekasirika. Malalamiko yake yaliamsha hisia za watu. Kila mtu alisema: Ukweli uko pamoja na Ali na Fatimah.

268

Mikesha ya Peshawar
Wallahi Ali anasema kweli. Kwa nini binti ya Mtume afanyiwe fedheha kiasi hicho?

UFIDHULI WA ABU BAKR


Ibn Abil-Hadid anasimulia kwamba watu walivutiwa sana upingaji wa Ali na Fatimah na wakaanza kuleta fujo. Abu Bakr ambaye aliona kwamba wale watu wawili watukufu tayari wameondoka pale Msikitini alipanda mimbari na akasema: Enyi watu! Kwa nini mnachanganyikiwa hivi. Kwa nini mumsikilize kila mtu? Kwa vile tu nimekataa ushahidi wao, wanazungumza upumbavu. Ukweli ni kwamba yeye ni mbweha ambaye amesalitiwa na mkia wake mwenyewe. Anasababisha kila aina ya vurugu. Anapuuzia uzito wa vvurugu na kuchochea watu kufanya fujo na ghasia. Anatafuta msaada kutoka kwa wanyonge. Anatafuta msaada kutoka kwa wanawake. Yeye ni sawa na Ummut-Tihal ambaye watu wa nyumbani kwake mwenyewe walipendelea kuzini naye. Je, maneno haya si matusi ya kufedhehesha? Je, yanakubaliana na sifa, heshima, mapenzi na huruma ambavyo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema vinawastahikia familia yake? Mpaka lini mtabakia na imani hii potofu na ushabiki? Mpaka lini mtawapinga Mashia na kuwaita Marafidhi na makafiri kwa sababu tu wanakosoa maneno na vitendo vya watu ambavyo vimeandikwa katika vitabu vyenu?

HISTORIA INAHUKUMU MTU


Lifikirieni suala hili kwa uadilifu. Je, ufedhuli ule wa sahaba mzee wa Mtume ulikuwa ni wa haki? Lugha mbovu na ya matusi ya Muawiya, Marwan na Khalid hazikuwa za kuhuzunisha hivyo kama ile ambayo inakuja kutoka kwenye mdomo wa mtu ambaye anaitwa sahaba wa kwenye pango. Watukufu Waislamu! Hatukuwepo katika wakati ule. Tunasikia majina ya Ali, Abu Bakr, Umar, Uthman, Talha, Zubair, Muawiya, Marwan, Khalid, Abu Huraira, nk. Hatuna urafiki wala uadui na yeyote kati yao. Tunaona mambo mawili: kwanza, wale ambao walipendwa na Allah na Mtume Wake na ambao kwao heshima na utii vimeamriwa juu yao. Pili, tunapima matendo na kauli zao. Kisha tunaamua bila upendeleo. Tunajizuia kuruhusu upendeleo wetu kwa mtu fulani kupotosha uamuzi wetu.

MSHANGAO WA HADID JUU YA ABU BAKR KUWAKASHIFU ALI NA FATIMAH


Sio sisi peke yetu ambao tumeshitushwa na tabia kama hii. Hata maulama wenu waadilifu wanashangazwa kuyaona haya. Ibn Abil-Hadid anaandika katika Sharh-e-NahjulBalagha yake, Jz. 4, uk. 80, kwamba maneno ya Khalifa yalimjaza na mshangao. Alimuuliza mwalimu wake Abu Yahya Naqib Jafar Bin Yahya Bin Abi Zaidul-Basari, maneno haya ya Khalifa yalikuwa yanamhusu nani. Yeye alisema kwamba kauli hizo

269

Mikesha ya Peshawar
hazikuwa za kupitia. Uhusikaji wake ulikuwa wa wazi. Ibn Hadid akasema: Kama ungekuwa wa wazi, nisingeuliza. Hapo alicheka na akasema: Mambo haya yalisemwa dhidi ya Ali. Ibn Hadid akayarudia maneno haya kwa mshangao: Maneno yote haya yalisemwa dhidi ya Ali? Mwalimu wake akasema: Ndio, Ewe mwanangu! Hivi ndivyo utawala unavyomaanisha.

KUMUUDHI ALI NI KUMUUDHI MTUKUFU MTUME


Kuhusu wote wawili Ali na Fatimah, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kwamba shida zao ni shida zake yeye pia. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: Yule ambaye anatawasumbua hawa wawili ananisumbua mimi, na mtu anayenisumbua mimi anamsumbua Allah. Vile vile imeandikwa katika vitabu vyenu sahihi kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: Yeyote yule ambaye anamtukana Ali ananitukana mimi, ambaye ananitukana mimi anamtukana Allah. Muhammad bin Yusuf Ganji Shafii, katika kitabu chake Kifayatut-Talib Sura ya 10, anasimulia hadithi ndefu kutoka kwa Ibn Abbas, ambaye alikiambia kikundi cha Wasiria ambao walikuwa wakimlaani Ali kwamba yeye alimsikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema kumhusu Ali: Yeyote yule anayekutuka wewe amenitukana mimi, na yeyote anaye nitukana mimi amemtukana Allah, na ambaye anamtukana Allah atatupwa moja kwa moja Motoni. Baada ya hadithi hii alinukuu hadithi nyingine nyingi kutoka kwenye vyanzo sahihi ambazo zote zinathibitisha kwamba wale ambao wanamtukana Ali ni makafiri. Sura ya 10 ya kitabu hiki inaitwa: Kuhusu ukafiri wa mtu ambaye anamtukana Ali. Vile vile Hakim katika kitabu chake, Mustadrak, Jz. 3, uk. 121, ameinukuu hadithi hii hii. Hivyo kwa mujibu wa hadithi zote hizi, wale ambao wanamlaani Ali, wanamlaani Allah na Mtume Wake. Wote hao (kama Muawiya, Bani Umayyah, Manasibi, Khawariji) wenyewe wamelaaniwa. Basi, sasa kiasi hiki kinatosha. Hakika Siku ya Hukumu kwa hakika itafika. Kwa vile wahenga wetu walioonewa walichukuwa njia ya ukimya na kuacha uamuzi juu ya Siku hiyo, sisi vile vile tutabakia kimya. Kuna nukta ya pili ambayo inakataa hadithi hii ya kudhaniwa Sisi hatuachi urithi Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: Mimi ni jiji la elimu na Ali ni lango lake; na mimi ni nyumba ya hekima na Ali ni mlango wake. Madhehebu zote zimelikubali hili. Hakika mtu ambaye alikuwa ni lango la elimu ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alielewa hadithi zote na maelekezo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), hususan zile zinahusiana na matatizo ya mirathi. Kwani ustawi wa taifa zima hutengemea juu ya hadithi hizi. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) vile vile alisema: Mtu ambaye anataka kupata elimu lazima aje kwenye mlango wa Ali. Kama elimu yake ingelikuwa sio kamili, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) asingese-

270

Mikesha ya Peshawar
ma kwamba Ali alikuwa hakimu bora katika Umma mzima. Alisema: Ali ni mbora miongoni mwenu wote katika kuzitafsiri sheria. Hadithi hii imeandikwa katika vitabu vyenu vyote vya sahihi. Hivi Mtukufu Mtume angeweza kutangaza ubora wa ubingwa wa mtu wa sheria kama mtu huyo alikuwa hayaelewi matatizo ya mirathi na haki za watu? Sehemu ya lengo la Mtukufu Mtume lilikuwa ni kuleta mageuzi ya kijamii kwa ajili ya watu katika dunia hii na amani na starehe kwa ajili yao katika akhera. Angeweza vipi basi kumfanya yeye Ali kuwa Amirul-Muminin na kisha bado asimfikishie desturi kama hii ambayo inaathiri utaratibu wote wa kijamii? Sheikh: Hakuna kati ya vitu hivi viwili kilichothibitishwa kwa mujibu wetu. Hadithi ya Jiji la elimu haikubaliwi na maulamaa wetu mashuhuri na masala ya umakamu na urithi (wa nafasi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)) pia vile vile yamekataliwa na wale maulamaa wakubwa. Bukhari na Muslim katika kukusanya kwao hadithi na wengine miongoni mwa maulamaa wakubwa, wanasimulia kutoka kwa Ummul-Muminin Aisha kwamba, kichwa cha Mtume wakati wa kifo chake kilikuwa kimelala kifuani mwake mpaka alipokata roho. Alieleza kwamba hakutengeneza wosia. Lau angelitengeneza wosia Ummul-Muminin angesimulia na suala la wosia lingeliweza kutatuliwa.

HADITHI MIMI NI JIJI LA ELIMU NA ALI NI LANGO LAKE


Muombezi: Kuhusu hadithi hii umekuwa sio mkweli hata kidogo. Nilikwishakuambia tayari kwamba madhehebu zote kwa pamoja zinakubaliana kwamba hii imesimuliwa takiriban kwa mwendelezo kamili. Maulamaa wenu wafuatao wamethibitisha usahihi wa hadithi hii: Imam Thalabi, Firuzabadi, Hakim Nishapuri, Muhammad Jazari, Muhammad Bin Jarir Tabari, Suyuti, Sakhawi, Muttaqi Hindi, Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafii, Muhammad Bin Talha Shafii, Kadhi Fadhl Bin Ruzbahan, Munawi, Ibn Hajar Makki, Khatib Khawarizmi, Sulaiman Qanduzi Hanafi, Ibn Maghazil Faqih Shafii, Dailami, Ibn Talha Shafii, Mir Sayyid Ali Hamadani, Hafidh Abu Nuaim Ispahani, Sheikhul-Islam Hamwaini, Ibn Abil-Hadid Mutazali, Tibrani, Sibt Ibn Jauzi na Imam Abdur-Rahman Nisai.

UMAKAMU ULITUNUKIWA JUU YA ALI


Kuhusu masala ya umakamu, kuna kauli nyingi za kuaminika zinayothibitisha kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitengeneza wosia wake. Hakuna mtu mwenye ujuzi anayekataa jambo hili.

271

Mikesha ya Peshawar
Nawab: Khalifa wa Mtume pia ni makamu wake, mtu ambaye aliendesha mambo yake ya ndani. Kwa mfano, walilipa posho kwa wake za Mtume. Kwa nini unasema kwamba Ali aliteuliwa kuwa makamu? Muombezi: Unasema kweli. Ni wazi kwamba Khalifa wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa pia ni makamu wake. Wakati wa mikesha iliyopita nimewasilisha hoja zangu na kauli za kuaminika kuhusiana na ukhalifa. Kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimteua Ali kuwa Khalifa wake na makamu wake ilikuwa ni sahihi kabisa. Ambapo wengine walikuwa wanajishughisha na mambo yao na njama za kisiasa, huyo makamu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alishughulika na taratibu za mazishi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Baadaye alijishughulisha katika kurudisha fedha za amana na vitu vingine vya thamani na kuangalia masuala mengine ambayo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa ameyakabidhi kwake. Hili liko wazi mno kiasi kwamba hakuhitajiki uthibitisho wowote. Maulamaa wetu wote wanakubalina kuhusiana na jambo hili.

HADITHI KUHUSU USHIKA UMAKAMU


Ili kuthibitisha hoja yangu ngoja nirejee kwenye baadhi ya hadithi: (1) Kuunda udugu Imam Thalabi katika kitabu chake Manaqib na Tafsir, Ibn Maghazili Faqih Shafii katika Manaqib yake na Mir Sayyid Ali Hamadani katika kitabu chake Mawaddatul-Qurba (Mawadda ya 6) anasimulia kutoka kwa khalifa wa pili, Umar bin Khattab, ambaye anasema kwamba wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa anaanzisha undugu kati ya masahaba, alisema: Huyu Ali ni ndugu yangu katika ulimwengu huu na kesho akhera. Miongoni mwa kizazi changu yeye ni khalifa wangu; ni mrithi wangu (makamu) katika Umma wangu. Yeye ndiye mrithi wa elimu yangu; ndiye mlipaji wa deni langu. Kilicho chake ni changu pia; kilicho changu ni chake pia; manufaa yake ni manufaa yangu na hasara yake ni hasara yangu. Yule ambaye ni rafiki yake kwa hakika ni rafiki kwangu na ambaye ni adui kwake kwa hakika ni adui kwangu. (2) Kuuliza kwa Salman: Sheikh Suleiman Balkhi Hanafi katika sura ya 15 ya Yanabiul-Mawadda amesimulia hadithi ishirini katika kuunga mkono umakamu wa Ali kutoka kwa Imam Thalabi, Hamwaini, Hafidh Abu Nuam, Ahmad Bin Hanbal, Ibn Maghazili, Khawarizmi na Dailami. Nawasilisha baadhi ya hizo kwa ajili ya mwongozo wenu. Anasimulia kutoka kwenye Musnad ya Ahmad Bin Hanbal (na Sibt Ibn Jauz katika Tadhkirat-e-Khawasul-Umma, uk. 26, na Ibn Maghazili Shafii katika Manaqib yake vile vile wamesimulia hadithi hizi) kwamba Anas Ibn Malik amesema: Nilimuomba Salman amuulize Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni nani mrithi wake (wasii). Salman akamuuliza Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Ewe Mtume wa Allah! Ni nani makamu wako? Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema, Ewe Salman! Ni nani

272

Mikesha ya Peshawar
mrithi wa Salman? Akasema, Yusha Bin Nun. Kisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema, Makamu wangu na mrithi wangu, ambaye atalipa madeni yangu na atakayekamilisha ahadi zangu, ni Ali Bin Abi Talib. (3) Kila Mtume alikuwa na Mrithi wake, Ali ni Mrithi wangu. Imesimuliwa kutoka kwa Muwaffaq Bin Ahmad, ambaye ananukuu kutoka kwa Buraida kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: Kila Mtume alikuwa na makamu na mrithi, na kwa hakika, makamu na mrithi wangu ni Ali. Muhammad Bin Yusuf Ganji Shaii katika kitabu chake Kifayatut-Talib, sura ya 62, uk. 131 ananukuu hadithi hiyo hiyo ambayo vile vile imesimuliwa na Muhadith wa Syria katika kitabu chake Tarikh. (4) Ali ni mwisho wa Mawasii. Sheikhul-Islam Hamwaini anasimulia kutoka kwa Abu Dharr Ghifari, ambaye amesema, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema, mimi ni mwisho wa Mitume na wewe, Ewe Ali, ni mwisho wa mawasii mpaka Siku ya Hukumu. (5) Ali ni makamu wangu kutoka kwenye kizazi changu: Imesimuliwa kutoka kwa Khatib Khawarizmi, ambaye anasimulia kutoka kwa Ummul-Muminin Ummi Salama, ambaye amesema; Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: Allah amechagua mrithi kwa ajili ya kila Mtume na baada yangu mimi makamu wangu kutoka kwenye kizazi changu na Umma wangu ni Ali. (6) Ali alitetea cheo chake katika hotuba. Imesimuliwa kutoka Maghazili Faqih Shafii, ambaye anasimulia kutoka kwa Asbagh Bin Nabuta, mmoja wa Masahaba wakubwa wa Amirul-Muminin, na Muslim na Bukhari vile vile wamenukuu kutoka kwake kwamba bwana wake Amirul-Muminin amesema katika moja ya hotuba zake: Enyi watu! Mimi ni Imam (kiongozi) wa viumbe wote. Ni mrithi wa (makamu) wa mbora mno wa viumbe; mimi ndio baba wa kizazi kilicho takasika kabisa na chenye kuongoza; mimi ni ndugu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.); mrithi wake, rafiki yake muaminifu na mwenza wake wa karibu. Mimi ni bwana wa waumini; ni kiongozi wa wale ambao wana nyuso angavu, mikono angavu na miguu angavu; mimi ni mkuu wa Mawasii wote. Kupigana dhidi yangu ni kupigana dhidi ya Allah. Kufanya amani na mimi ni kufanya amani na Allah. Utii kwangu ni utii kwa Allah; urafiki na mimi ni urafiki na Allah; wafuasi wangu ni marafiki wa Allah; na wasaidizi wangu ni wasidizi wa Allah. (7) Allah alinifanya mimi Mtume na Ali makamu wangu. Vile vile Ibn Maghazili Shafii katika Manaqib yake anamnukuu Abdullah Bin Masud kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: Ujumbe wa utume uliishilizwa kwangu mimi na Ali; katu hakuna kati yetu sisi aliyewahi kusujudu mbele ya sanamu; hivyo Allah alinifanya mimi Mtume na Ali kuwa makamu.

273

Mikesha ya Peshawar
(8) Umakamu wa Ali ni sehemu ya kanuni ya kiapo cha utii kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Mir Sayyid Ali Hamadani Shafii anaandika katika kitabu chake Mawaddatul-Qurba Mawadda ya 4, kutoka kwa Atba Bin Amir Jahni, ambaye amesema: Tunatoa kiapo cha utii kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), tukukiri ukweli kwamba hakuna mungu isipokuwa Allah. Ni Mmoja na mshirika na hakika Muhammad ni Mtume Wake na Ali ni makamu Wake. Hivyo kama tunaacha chochote kati ya mambo haya matatu tutakuwa makafiri. (9) Ninawaita watu kwenye haki na Ali anaitia nuru. Katika Mawaddatul-Qurba hiyo hiyo, vile vile imeandikwa kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: Hakika Allah ameteua makamu kwa kwa ajili ya kila Mtume: Seth, makamu wa Adamu; Joshua, makamu wa Musa; Simon Petro makamu wa Yesu; na Ali ni makamu wangu; na makamu wangu ni mbora wa makamu wote. Nawaita watu kwenye haki na Ali anaitia nuru.

ALLAH ALIMTEUA ALI KUTOKA MIONGONI MWA WATU WOTE KUWA MAKAMU WANGU
Mwandishi wa Yanabi ananukuu kutoka kwenye Manaqib ya Muwaffaq Bin Ahmad Khawarizmi, ambaye alisimulia kutoka kwa Abu Ayyub Ansari, ambaye amesema kwamba wakati Mtume wa Allah alipokuwa yu mgonjwa kitandani, Fatimah alikuja na kuanza kulia. Kisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: Ewe Fatimah, wewe umebarikiwa makhususi na Allah ambaye amekupa mume ambaye Uislamu wake ni wa mbele zaidi, ambaye elimu yake ni bora kuliko ya mtu yeyote yule, na ambaye uvumilivu wake unapita uvumilivu watu mengine wote. Kwa hakika Allah swt. Amewapa upendeleo maalumu watu wa ulimwengu huu. Kutoka miongoni mwao Alichagua na kuniteua mimi kama Mtume na Mjumbe Wake. Kisha akawapa baraka nyingine maalumu na kutoka miongoni mwa watu akamchagua mume wako. Na amenifunulia kwamba nikuoze wewe kwake na nimfanye makamu wangu.

AHLUL-BAYT WAMEJAALIWA SIFA SABA ZISIZO NA USHINDANI


Baada ya kuandika hadithi hii katika Manaqib yake, Ibn Maghazili Faqih Shfii anaandika maneno haya ya nyongeza, ya Mtukufu Mtume: Ewe Fatimah! Sisi Ahlul-Bayt tumejaaliwa sifa saba, ambazo hakuna katika vizazi vya wanadamu kilichokuwa nazo, na hakuna miongoni mwa vizazi vyao kitakachokuwa nazo. Mtume mtukufu mno miongoni mwa Mitume anatokana na sisi, na ni baba yako. Makamu wangu ni mbora mno kwa makamu

274

Mikesha ya Peshawar
wengine wote, na ni mume wako. Shahidi (aliyejitolea mhanga) anayewapita mashahidi wengine wote, na ni ami yako, Hamza. Kutoka miongoni mwetu sisi (Ahlul-Bayt) kuna mtu ambaye ana mbawa mbili ambazo kwazo anaruka kwenda popote anapopenda, huko Peponi, na ni binamu yako, Jafar. Kutokana na sisi kuna wajukuu wawili ambao ni mabwana wa vijana wa Peponi, na ni watoto wako. Na ninakuambia, kwa jina la Allah ambaye anamiliki uhai wangu, kwamba Mahdi wa Umma huu, ambaye kwamba Isa Bin Mariamu atasali Salat nyuma yake, atakuwa ni katika kizazi chako.

MAHDI ATAIJAZA ARDHI NA UADILIFU


Ibrahim Bin Muhammad Hamwaini, baada ya kusimulia hadithi hii alinukuu maneno haya ya nyongeza: Baada ya kumtaja Mahdi Mtume alisema: Ataujaza ulimwengu huu na uadilifu wakati utakapokuwa umejaa ukatili na dhulma. Ewe Fatima! Usihuzunike na usilie. Kwa sababu ya mapenzi na heshima yangu kwako, Allah swt., ni mpole zaidi kwako kuliko mimi. Amekupa wewe mume mwenye mafanikio ya hali ya juu mno ya kiroho, na aliye tukuka mno katika hadhi ya kifamilia, mwenye huruma sana kwa watu, muadilifu mno katika kushughulikia mambo ya watu, na msahihi mno katika maamuzi yake. Nafikiri kiasi hiki kinatosha kuridhisha udadisi wa Nawab Sahib na kuondoa kuelewa vibaya kwa Sheikh Sahib.

WAKATI WA KIFO CHAKE, KICHWA CHA MTUKUFU MTUME (S.A.W.W.) KILIKUWA JUU YA KIFUA CHA AMIRUL-MUMININ (A.S.)
Amma kwa madai ya kwamba wakati wa kifo cha Mtume, kichwa chake kilikuwa juu ya kifua cha Ummul-Muminin Aisha, sio kweli. Maulamaa wenu wenyewe wameonesha kwamba wakati wa kifo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kichwa chake kilikuwa kimeegamia juu ya kifua cha Amirul-Muminin. Sheikh: Ni katika kitabu kipi ambacho ma