Вы находитесь на странице: 1из 1

CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM

MRADI WA LUGHA ZA TANZANIA

KONGAMANO KUHUSU HALI YA LUGHA ZA TANZANIA


31 OKTOBA 1 NOVEMBA 2013
Usuli
Sera ya Utamaduni inatamka kwamba lugha za jamii ni hazina kuu ya historia, mila, desturi, teknolojia na utamaduni wetu kwa jumla. Sera inahimiza watu na mashirika mbalimbali: (i) kutafiti, kuhifadhi, na kutafsiri lugha za jamii; (ii) kuandika kamusi na sarufi za lugha za jamii; (iii) kuchapisha na kusambaza maandiko mbalimbali katika lugha za jamii. Mradi wa Lugha za Tanzania ulianzishwa mwaka 2001 kwa kuitikia changamoto iliyomo katika Sera ya Utamaduni. Mpaka sasa mradi huu umefanya utafiti katika sehemu mbalimbali za Tanzania na kuchapisha vitabu na makala mbalimbali kuhusu lugha za jamii na kuhamasisha watu mbalimbali kutafiti na kuandikia lugha hizi. Mwaka 2009 mradi ulitoa ATLASI (ya kwanza) YA LUGHA ZA TANZANIA. Mradi pia umeanzisha kamusi ya kwanza ya mtandaoni ya Lugha ya Alama ya Tanzania (http://tz.signwiki.org).
Orodha ya Vitabu vilivyochapishwa na Mradi wa Lugha za Tanzania Kamusi: Kinyambo, Kimashami, Kisumbwa, Kikahe, Lugha ya Alama ya Tanzania, Kizinza, Kiasu, Kibondei, Kiruuri, Kisimbiti, Kimeru, Kizigula, Kihangaza, Kiikizo, Kigweno, Kigogo, Kihaya, Kijita, Kimochi, Kimakonde. Sarufi: Kinyambo, Kinyiha, Kimashami, Kimwela; Hadithi: Kividunda, Kikwere. Kamusi zinazoandaliwa: Kimasai Kiyao,

Fursa za Kukuza Uchumi na Demokrasia kwa Kutumia Lugha za Jamii Kuandika au kurekodi masimulizi ya hadithi za jadi na maarifa ya jamii; Redio za jamii na magazeti ya kata na vijiji kuhusu maisha ya jamii husika, changamoto na mbinu za mafanikio; Mabango na vipeperushi vya kampeni kuhusu magonjwa kama malaria, ukimwi, kifua kikuu, matende, na uzazi salama; Matangazo ya biashara, sera na sheria; Vitabu vya kamusi na sarufi na vitabu vya kufundishia lugha. Nakala za machapisho ya Mradi yanapatikana kwenye Ofisi za Mradi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, CASS, Idara ya Lugha za Kigeni na Isimu, na zitaonyeshwa wakati wa Kongamano litakalofanyika Ukumbi wa Nkrumah, Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam. Mnakaribishwa
Ramani ya Lugha za Tanzania
(Ni sehemu ya Atlasi ya Lugha za Tanzania)

Waratibu wa Mradi wa Lugha za Tanzania (2001-2013)

Prof. J.M. Rugemalira


jmruge@uccmail.co.tz josephatr@hotmail.com
+255 713 212161

Dkt. H.R.T. Muzale


hmuzale@udsm.ac.tz hmuzale@hotmail.com

+255 755 007005

Simu ya Ofisini: +255 22 2410031

Вам также может понравиться