Вы находитесь на странице: 1из 2

SAMSUNG ELECTRONICS TANZANIA YAENDELEZA VITA DIDHI YA BIDHAA BANDIA.

Kusamba kwa bidhaa bandia kumetapakaa dunia nzima katika miaka ya nyuma karibuni. Kwa mujibu wa Counterfeiting Intelligence Bureau (CIB) of the International Chamber of Commerce (ICC), bidhaa bandia zinachukua asilimia 5 hadi 7 ya mauzo ya dunia. Mwaka 2005 ripoti iliyofanywa na Organization for economic Co operation and Development (OECD) inasema kwamba karibu dola za kimarekani bilioni 200 ya mauzo ya dunia yanaweza kuwa yalikuwa ya bidhaa zilizo bandia au za magendo, na kufikia mwaka 2007 mauzo hayo yalifikia bilioni 250 za dola za kimerekani. Imekadiriwa kwamba ongezeko la bidhaa zilizobandia kwa upande wa vifaa vya umeme umekuwa zaidi ya mara mbili kati ya 2005 na 2008. Sababu za ukuaji huu ni nyingi ikiwa ni pamoja na Ukuaji wa mtandao wa mauzo kidigitali, watumiaji wenyewe kutafuta bidhaa za bei rahisi bila kujali ubora pamoja na nyinginezo nyingi. Bidhaa bandia ni suala zito katika inchi zilishozaendelea na zinazoendelea/zenye maendeleo duni. Mapema mwaka 2012, shirikisho la viwanda Tanzania lilisema kwamba bidhaa bandia zimeletea serikali hasara kati ya asilimia 15 - 25 ya jumla ya mapato ya nyumbani kwa mwaka, na kati ya shilingi 540 bilion na shilingi 900 billion ($343 million and $566 million) kwa mwaka katika ukwepaji wa kodi inayohusiana na bidhaa za bandia na zisizokuwa za kiwango. Serikali ya Tanzania, asasi tofauti zisizokuwa za serikali na makampuni binafsi wanafanya kazi kupiga vita dhidi ya bidhaa bandia. Samsung Electronics Tanzania, moja ya kampuni inayoongoza na kufanya vizuri kwa upande wa simu za mkononi inaendeleza vita yake dhidi ya bidhaa bandia, zinavyogushiwa, zilizoibiwa na zisizokuwa na dhamana. Karibuni, Samsung Electronics Tanzania imehimiza wateja wake na wananchi wote watumiaji wa simu za mkononi za Samsung ambao hawajasajiliwa simu zao kwa e warrant, wafanye hivyo ili kufaidika na dhamana ya miezi 24 na huduma nyingine za kufurahisha. The e-warranty platform of Samsung Electronic Tanzania, inatoa fursa ya kipekee kwa wateja wake kuangalia uhalisi wa bidhaa yoyote ya Samsung Samsung Electronic Tanzania katika vita yake dhidi ya bidhaa zisizoeleweka, imeenda maili zaidi kwa kuzindua kituo cha huduma kwa wateja katikati ya jiji la Dar es Salaam Kariakoo. Mwenendo huu ni moja ya tamaduni za Samsung ambapo wateja wa Samsung waliosajili simu zao za mkononi katika e-warranty platform watapata huduma nzuri na za bure kabisa za matengenezo. Kituo cha huduma cha wateja wa Samsung kinatumia mbinu za kuweza kutoa huduma bora kabla, wakati na baada ya mauzo kwa kuwa na mafundi pamoja na washauri

waliobobea wanaotoa huduma kwa haraka bila malipo kwa bidhaa yeyote ya Samsung iliyo ndani ya dhamana. Bw. Mubarak Mikidad (Meneja wa Huduma wa Samsung Tanzania) alisisitiza jinsi ya usajili katika e-warranty platform ya Samsung ilivokua rahisi. Kwasasa wateja wanaweza kusajili simu zao za mkononi bila kujali uko mtandao gani wa utoaji huduma za simu. Wateja wanasisitizwa kuendelea kusajili simu zao katika e-warranty platform ya Samsung kwa kutuma tarakimu 15 za IMEI namba kwa short code/ namba fupi 15685 katika mitandao yote ya simu. Namba za IMEI zinapatikana kwenye kabrasha la simu au kwa kupiga*#06# pia inaonekana katika sehemu yenye uwazi kwenye betri kwenye kipande cheupe kilichoandikwa IMEI.

Вам также может понравиться