Вы находитесь на странице: 1из 1

Eneo la kijiografia (Mipaka): Mkoa wa Shinyanga uko Kaskazini Magharibi mwa Tanzania , Kusini mwa Ziwa Victoria kati

i ya latitudo 2 o 15' Kaskszini na 4 o 30' Kusini na longitudo 31 o 14' Magharibi na 35 o 11' Mashariki. Mkoa unapakana na mikoa ya Mwanza, Kagera na Mara upande wa Kaskazini, Arusha na Singida upande wa Mashariki, Kigoma upande wa Magharibi na Tabora upande wa Kusini.

Eneo: Mkoa una eneo la kilometa za mraba 50,781, kati yake kilometa za mraba 18,300 ni misitu na hifadhi za wanyamapori, na kilometa za mraba 31,400 ni ardhi inayofaa kwa kilimo na ufugaji. Eneo linalobaki lenye ukubwa wa kilometa za mraba 1,081 ni milima, miamba, makorongo na mawe.

Utawala:

Mkoa umegawanyika katika wilaya saba za Bariadi, Bukombe, Kahama, Kishapu, Maswa, Meatu na Shinyanga, kila moja ikiwa na Halmashauri ya wilaya isipokuwa Shinyanga ambayo ina Halmashauri ya wilaya na Manispaa. Idadi ya wilaya, Tarafa, Kata na vijiji imeonyeshwa katika jedwali lifuatalo:Mgawanyo wa Mkoa Kiutawala

WILAYA Bariadi Bukombe Kahama Maswa Meatu Kishapu Shinyanga (R) Shinyanga (U) JUMLA

ENEO KM2 9,777 10,842 9,461 2,736 8,871 4,334 4,212 548 50,781

TARAFA 4 3 5 3 3 3 3 3 27

KATA 26 14 34 18 19 20 16 13 160

VIJIJI 124 125 221 99 71 103 107 19 869

Вам также может понравиться