Вы находитесь на странице: 1из 8

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA


KATIKA KAMATI YA MAUDHUI YA MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA
DAR ES SALAAM

SHAURI LA UKIUKAJI WA KANUNI ZA UTANGAZAJI
NAMBA 4/2014
DHIDI YA CLOUDS ENTERTAINMENT FM RADIO
UAMUZI
UAMUZI WA KAMATI YA MAUDHUI KUHUSU LALAMIKO LA UKIUKAJI WA KANUNI ZA UTANGAZAJI,
MWAKA 2005

1.0 Utangulizi:

Tarehe 15/06/2014, kituo cha Clouds Entertainment FM Radio cha Dar es Salaam kilikiuka Kanuni za
Utangazaji (Maudhui) za mwaka 2005, kupitia kipindi chake cha Njia Panda kilichorushwa hewani kati ya
saa 8.00 mchana na saa 10.00 jioni. Kipindi hiki kilikuwa na mada iliyohusu Safari ya Kuzimu. Maudhui ya
kipindi hiki yalijaa simulizi za kufikirika, za kishirikina na kichawi.

2.0 Maelezo ya kosa

2.1 Kurusha kipindi chenye simulizi za kishirikina na kichawi
Kituo cha Clouds Entertainment FM kilitangaza kipindi ambacho kimejaa simulizi za kufikirika, kishirikina
na kichawi ambazo zinaweza kujenga Imani potofu za kichawi kwa wananchi na jamii iliyokuwa inasikiliza
kipindi hiki.

2.2 Kutokuwasilisha ratiba za vipindi kwa mujibu wa Sheria
DJ SEK BLOG
Kituo cha Clouds Entertainment FM hakikufuata Kanuni za Utangazaji (Maudhui) za mwaka 2005
zinazowataka kuwasilisha ratiba ya vipindi vyao kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ili viidhinishwe
na vilevile kuvichapisha katika gazeti kabla ya kurushwa hewani. Kipindi cha Njia Panda hakikuwasilishwa
kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kwa ajili ya kuidhinishwa. Hii ni kinyume na Kanuni Na.
22(1),(3),(a),(b).

3.0 Kanuni zilizokiukwa
3.1 Kosa la Kwanza
Kituo cha Clouds Entertainment FM Radio kimekiuka Kanuni zifuatazo za Huduma ya Utangazaji
(Maudhui) 2005: Na. 5(a), (b), (c), (d), (f), (g), (h), 14(1) na 15(b)

5. Every licensee shall ensure that the programme and its presentation:-
(a) upholds national sovereignty, national unity, national interest, national security and Tanzanians
economic interests;

(b) projects Tanzanian national values and national points of view;

(c) observes good taste and decency;

(d) upholds public morality;

(f) does not injure the reputation of individuals;

(g) protects children from negative influences;

(h) does not incite or perpetuate harted against or vilify, any group or persons .............
DJ SEK BLOG
Tafsiri ya Kanuni hizi kwa mujibu wa Kamati katika shauri hili ni kama ifuatavyo:-

5. Kila mwenye leseni ya utoaji huduma za utangazaji lazima ahakikishe kuwa vipindi vyake vinazingatia:-

(a) mshikamano wa kitaifa, umoja na maslahi ya Taifa, usalama wa Taifa, na kulinda manufaa ya uchumi
wa Tanzania;

(b) kulinda maadili ya Mtanzania na Taifa;

(c ) ubora wa kipindi pamoja na staha;

(d) kuzingatia maadili ya umma;

(f) kutoharibu /kuchafua sifa za watu;

(g) kuwalinda na kuwaepusha watoto kuiga tabia hasi;

(h) havileti uchochezi wala kujenga chuki kwa mtu au kundi la watu

14(1) Every licensee shall have particular regard to the need to protect children from unsuitable
programme material;
DJ SEK BLOG
15(b) Every free-to air licensee shall refrain from using language meant to mislead or unnecessarily
cause alarm and despondency;

Tafsiri ya Kanuni hizi kwa mujibu wa Kamati katika shauri hili ni kama ifuatavyo:-

14(1) Kila mwenye leseni anatakiwa azingatie umuhimu wa kuwalinda watoto na vipindi visivyofaa;

15(b) Kila mwenye leseni ya utangazaji wa vipindi vya Radio na Televisheni vinavyosikilizwa au
kutazamwa bila malipo anatakiwa kutotumia lugha ya upotoshaji au inayoweza kusababisha hofu na
kukatisha tamaa.

3.2 Kosa la Pili
Kituo cha Clouds Entertainment FM Radio kimekiuka Kanuni zifuatazo za Huduma ya Utangazaji
(Maudhui) 2005: Na. 22(1),(3),(a),(b):-

22(1) A licensee shall publish programme schedule in a daily newspaper circulating widely in Tanzania at
least one month in advance.
(3) a licensee shall submit to the Authority:
(a) advance quarterly programme schedule fourteen days before each quarter;
(b) transmission reports detailing programmes actually broadcast within seven days after the end of
each calendar month.

Tafsiri ya Kanuni hizi kwa mujibu wa Kamati katika shauri hili ni kama ifuatavyo:-

22(1) Mwenye leseni anapaswa kuchapisha ratiba ya vipindi vyake katika gazeti linalochapishwa kila siku
na kusomwa na sehemu kubwa ya nchi ya Tanzania angalau mwezi mmoja kabla ya vipindi kusikika
hewani.
(3) Mwenye leseni anapaswa kuwasilisha kwa Mamlaka :-
(a) ratiba ya vipindi vyake vya robo mwaka siku kumi na nne kabla ya robo mwaka inayotarajia kuanza;
(b) kutoa taarifa za kina za vipindi halisi vinavyotangazwa ndani ya siku saba kabla ya mwisho wa kalenda
kila mwezi.

4.0 Ushahidi wa Makosa
4.1 Kusikiliza CD ya kipindi cha Njia Panda

Ili kujiridhisha kama maudhui ya kipindi cha Njia Panda na uwasilishaji wake ulikiuka Kanuni za
Utangazaji, Kamati na uongozi wa Clouds Entertainment FM Radio walisikiliza sehemu ya kipindi hicho.
Maudhui ya kipindi hicho yalionyesha wazi ukiukwaji wa Kanuni za Utangazaji.

5.0 Maelezo ya utetezi
5.1 Maelezo ya Dkt. Isaac Maro
Mtangazaji wa kipindi cha Njia Panda DKt. Isaac Maro, alianza kutoa utetezi wake kwamba kipindi cha
Njia Panda kina miaka kumi na tatu tokea kuanzishwa na hapo mwanzo kilikuwa kinajulikana kama APEX
na kilianzishwa kwa lengo la kuangalia mambo yanayohusiana na HIV. Kilipoanzishwa, kilikuwa
kinazungumzia mambo matatu ya kufanya ili kujikinga na HIV ambayo ni Kuacha, Kuwa mwaminifu na
Kutumia Kondomu.

Dkt. Isaac Maro aliendelea kutoa utetezi wake kwamba baadae tafiti zilionesha kuwa ukizungumzia
Ukimwi kwa kuangalia hayo mambo matatu tu ni sawa na kuangalia tatizo kutoka kwenye matawi na
hivyo badala ya kuangalia kiini cha tatizo na kikaanzishwa kipengele kinachoitwa Nini Chanzo yaani
Root Causes.

Kipindi kilipanuka na kuanza kuangalia changamoto ambazo kijana anapitia na kuzungumzia umasikini,
elimu, imani potofu, dini na maisha ya kawaida ya Mtanzania. Kwa bahati mbaya sana waandaaji wa
kipindi ni madaktari na jinsi walivyokuwa wanaenda kwenye chanzo walikuwa wanakutana na watu
ambao walikuwa wanasema walipata ukimwi kwa sababu ya kulogwa na moja ya maeneo yenye
changamoto ni imani potofu. Hivyo walianza kutumia watu kuelezea imani potofu, na jinsi gani
zinasaidia kuchochea maambukizi.

Dkt. Maro alisistiza kwamba haya ni matukio ambayo yalitokea miaka mingi iliyopita na waliangalia
kutafuta stori ambayo itapelekea watu kuamini kwamba mambo yale yaliyotokea ambayo watu
walikuwa wakiyaamini yalikuwa siyo ya kweli na hayapo. Mila hizi potofu mwisho wa siku zitasababisha
mgonjwa asiende hospitali.

5.2 Maelezo ya Bwana Ruge Mutahaba

Mkurugenzi wa vipindi wa Clouds Entertainment FM Bwana Ruge Mutahaba alitoa utetezi wake kwa
kusema changamoto kubwa inayokikabili kituo chake ni kutafuta ubunifu wa kuwafikia walengwa ambao
ni vijana. Bwana Ruge alisema maneno yafuatayo:-
..ukisikiliza kipindi cha Njia Panda siku zote kimekuwa kinazungumza kuhusu. an individual person.
na story yake na namna alivyokutana na jambo lililogeuza maisha yake na jambo hilo mwisho wa siku
lilivyo muathiri kuelekea kupata maambukizi.

Bwana Ruge aliendelea kusema kwamba kituo chake kilianzisha kampeni ya Vunja Ukimya ambayo
ilikuwa na lengo la kuzungumzia HIV kwa uwazi na kuleta vijana wengi ambao walijitangaza kuathirika na
ugonjwa wa Ukimwi ilikuisaidia jamii. Alisema kipindi kilicholalamikiwa kilihitimishwa kwa kuelezea
mambo yanayohusu uchawi na ushirikina hayana msaada wowote.

Bwana Ruge alisisitiza kwamba kipindi kiliruka kwa wiki tatu. Mhusika alianza kuzungumzia maisha yake
ya kawaida, akaenda kwenye sehemu ya pili ya kuingia kwenye misukule na akaenda kwenye sehemu ya
tatu akazungumza kwamba hata ile ajali na matukio yaliyotokea ilikuwa ni ajali ya kawaida kama
nyingine zinavyotokea na kwamba yeye hana nguvu hiyo na hayo mambo siyo ya kweli.

Bwana Ruge alisema huyu aliyekuwa anasimulia ni mtu mpumbavu yaani Stupid na aliyoyasema
yalikuwa siyo ya kweli. Alisema maneno yafuatayo:

hakuna aliyesema wale walikufa kwa kulogwa.tunachozungumza ni kwamba there is a stupid guy
alikuja kusema amehusika na hii kitu.this guy is a stupid guy lakini mwisho wa siku inakuja kujulikana ni
uongo

Bwana Ruge alisema waliamua kuweka masimulizi hayo kwa sababu watu wanaamini vitu ambavyo
havipo kwenye jamii.

6.0 Kukiri Kosa

Mkurugenzi wa Clouds Entertainment FM Bwana Ruge Mutahaba alisema kwamba hawakufanya kosa
lolote na hitimisho la kipindi katika wiki ya tatu lilieleza kwamba mambo yaliyosemwa ni ya uongo na
hakuna kitu kama hicho.

7.0 Tathmini ya Kamati

Kamati iliridhika na kusisitiza kwamba, kituo cha Clouds Entertainment FM Radio katika kipindi cha Njia
Panda kilikiuka Kanuni za Utangazaji kwa kutangaza maudhui yenye simulizi za kishirikina na kichawi
jambo ambalo ni kinyume na taratibu na Sheria za nchi.

Habari na simulizi za Safari ya Kuzimu zinaweza kupelekea kuipotosha jamii na ni kinyume na utamaduni
wa Taifa. Jambo hili linaweza kumomonyoa utaifa wa Watanzania, vilevile linaweza kuumiza hisia za
wananchi wa Tanzania na kusababisha mvurugano miongoni mwa wananchi, pamoja na kuhatarisha
usalama wa taifa. Kitendo hiki ni kinyume na Kanuni za Utangazaji (Maudhui).
DJ SEK BLOG
Vilevile, lugha iliyotumika kuendesha kipindi hicho ilikuwa ni ya moja kwa moja isiyopunguza ukali wa
maneno badala ya kutumia tafsida. Lugha iliyotumika ni lugha inayoweza kuwajengea hofu wasikilizaji,
na inaweza kuwajengea watoto tabia mbaya na kuwapotosha kutokana na kusikia mambo yasiyofaa.
Jambo hili ni kinyume na Kanuni za Utangazaji (Maudhui),2005,

8.0 Uamuzi wa Kamati

Kamati iliridhika kuwa kipindi cha Njia Panda kilichorushwa hewani na kituo cha Clouds Entertainment
FM Radio tarehe 15/06/2014 kilikiuka Kanuni za Utangazaji, 2005 Na. Na. 5(a), (b), (c), (d), (f), (g), (h),
14(1), 15(b) na 22(1),(3),(a),(b):- kama ilivyonukuliwa hapo juu.

Baada ya kusikiliza na kutafakari kwa kina maelezo ya utetezi kutoka kwa Mkurugenzi wa Vipindi wa
Clouds Entertainment FM Radio na Mtangazaji wa kipindi cha Njia Panda, Kamati ya Maudhui inaamua
yafuatayo:-

1.1 Clouds Entertainment FM Radio inapewa onyo kali; na,
1.2 Clouds Entertainment FM Radio inatozwa faini ya shilingi milioni nne za Kitanzania ambazo inapaswa
kuzilipa kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ndani ya mwezi mmoja toka siku ya uamuzi huu.

Endapo Clouds Entertainment FM Radio itakiuka tena Kanuni za Utangazaji, hatua kali zaidi za Kisheria
zitachukuliwa dhidi yao.
Uamuzi huu umetolewa na kusomwa Dar es Salaam siku hii ya ., Mwezi wa Agosti Mwaka 2014.

Haki ya kukata rufaa dhidi ya uamuzi huu iko wazi ndani ya siku 30 tangu uamuzi unapotolewa

Uamuzi Umesainiwa na:
Eng. Margaret T. Munyagi

......
(Sahihi)
Mwenyekiti

WAJUMBE WA KAMATI YA MAUDHUI

1. Bwana Walter Bgoya (Sahihi).......................................
2. Bwana Joseph Mapunda (Sahihi).................................
3. Bwana Abdul Ramadhani Ngarawa (Sahihi)

Вам также может понравиться