Вы находитесь на странице: 1из 16

ISSN 0856 - 3861 Na.

1139 SHAWWAL, IJUMAA , AGOSTI 22-28, 2014 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=
Sauti ya Waislamu
www.annuurpapers.co.tz
Muhongo awarushia
Waislamu makombo
Na hiyo kwa shingo upande baada ya kulalamika
Udini huu kama wa polisi Ferguson utaleta balaa
Itabidi kulazimisha Sospeter wajue Waislam wapo
NECTA watuhumiwa kuleta
Utanganyika katika mitihani
Wabagua Zanzibar katika kanuni zake
Ni kinyume na matakwa ya muungano
Waislamu walalamika kwa Kawambwa
Wataka matokeo kidato cha 6 yatenguliwe
Dkt. Charles
Msonde,
Katibu
Mtendaji
Baraza la
Mitihani
Tanzania.
WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
Trayvon Martin. Michael Brown.
Mansour afungulia mlango
wanyonge juu ya dhamana
Kumbe hakuna kosa lisilo na dhamana
Hata Uamsho ingetumika kanuni hii pia
Mtume(saw) amesema, Kutoa katika
Hijja ni sawa na kutoa katika Jihadi, .
Uwezo wa baadhi yetu ni uwezo wetu.
Waislamu ni kama jengo au kiwiliwili
kimoja. Tupelekane Hijja na tusaidiane
kuisimamisha nguzo ya Hijja! Kadiri
tutavyokwenda wengi Hijja, ndivyo na
Allah Atavyotupa utukufu na nguvu
nchini mwetu. Karibuni Ahlu Sunna wal
Jamaa kwa mipango mizuri na huduma
bora. Gharama zote ni Dola 4,500.
Tafadhali wasiliana nasi: Tanzania Bara:
0655/0765/0682/0777 - 462022; Zanzibar: 07
77468018/0685366141/0657606708.
(15) MATAJIRI WA KIISLAMU!
2
AN-NUUR
SHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 22-28, 2014
AN-NUUR
S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786
Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM.
www.annuurpapers.co.t E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk
Ofsi zetu zipo: Manzese Tip Top
Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam
Tahariri/Habari
I L I k u o n y e s h a
mshikamano na familia ya
Brown, kijana aliyepigwa
risasi na kuuwawa na
polisi kule Fegurson,
Missouri, Sybrina D.
Fulton, mama Trayvon
Martin, kijana mwingine
aliyeuliwa kwa mtindo
huo mwaka juzi, aliandika
barua ya mkono wa pole
na katika kuhitimisha
akasema:
If They Refuse to Hear Us,
We Will Make Them Feel Us.
Hapana shaka ujumbe
huu umeelekezwa kwa
serikali ya Marekani na
vyombo vyake vya Dola
na Sheria.
Katika kutoa ujumbe
huo Sybr i na al i sema
kuwa asidhaniwe kuwa
analeta uchochezi, lakini
anachotaka ni mamlaka
husika zizingatie kuwa
masaibu yanayowakuta
Wa ma r e k a n i We u s i
ya kubaguliwa na uhai
wao kut ot hami ni wa,
hayakubaliki na hakuna
bi nadamu anayeweza
kuyavumilia.
Kwamba wadhulumiwa
na wenye kubagul i wa
ha wa we z i kuka a t u
wakaridhia kuona vitendo
vya kuwahuj umu na
kuwanyanyasa vikijirejea
mara kwa mara. Akawataka
hao wanaoona raha kuuwa
watoto wa wenzao halafu
wasichukuliwe hatua za
kisheria, wafikirie lau
ingekuwa ni watoto wao
wangejisikiaje.
Ni katika hali kama hiyo,
tunamuuliza Waziri wetu
wa Nishati na Madini,
kama ingekuwa vijana wote
waliochaguliwa kwenda
kusoma China wangekuwa
Wa i s l a mu wa t u p u ,
angejisikiaje. Kama nafsi
na dhamira yake kama
Mkristo inamwonyesha
kuwa jambo hilo halifai
kufanyiwa Wakristo, kwa
nini yeye aliona ni sawa
kuchagua vijana wote 10
Wakristo kwenda kusomea
utaalamu wa mafuta na
Watu wasilazimishwe
kuonyesha kuwa wapo
Pasipo haki, uadilifu amani haidumu
gesi!
Na kwa maana hiyo
hiyo, kila aliyepo katika
madaraka fulani ya kufanya
maamuzi serikalini na
katika taasisi za umma,
ajiulize, kama inatokea
mtu mwingine akatumia
madaraka yake kuchagua
watu wa dini yake na
kuacha wengine kabisa,
yeye angejisikiaje.
J apo yaweza kuwa
vi gumu kuj enga hi si a
hiyo sasa kwa sababu hali
halisi imekuwa ya upande
mmoja kufaidi kwa muda
mrefu, lakini ukweli ni
kuwa hakuna anayeridhia
hal i kama hi yo. Ndi o
maana Mzee Mtei alikuja
j uu sana i l i pot eul i wa
Tume ya Jaj i Warioba,
ambapo wajumbe wa Bara
wakijumuishwa na wale
wa Zanzibar, ilionekana
kuwa Waislamu ni wengi.
Ile kuwa Mwenyekiti na
Makamo wake walikuwa
Wakri sto, hai kuwa na
uzito kwa Mzee Mtei. La
muhimu aliangalia idadi
ya watu wote.
Hoja ya Mtei ilikuwa
k wa mb a j a p o n c h i
hi i t una s e ma kuwa
haiongozwi kwa misingi
ya dini, lakini huwezi
kukwepa ukweli kwamba
dini ina mchango mkubwa
katika kuelekeza maamuzi
na utendaji wa watu.
Na wanapokuwa wa dini
moja mahali, hapana shaka
kile kinachowaunganisha,
dini, kitafanya kazi kuliko
kabi l a zao na mambo
mengine. Ndio haya ya
Wizarani kwa Waziri wetu
Muhongo.
K a m a a l i v y o
tahadharisha Bi Sybrina,
hebu watu wasilazimishwe
kuonyesha kuwa wapo.
S o t e t una t a k a na
tunapigania nchi hii idumu
katika amani. Na amani
haiwezi kudumu pasipo
haki.
LEO ni harambee ya
kukusanya vi faa vya
ukarabati wa Shule ya
Kiislamu ya Mivumoni
iliyoteketea kwa moto
mapema wiki iliyopita.
K i l a M u i s l a m u
ametakiwa kufika siku
ya Ijumaa (leo) kuswali
Msikitini hapo akiwa na
kifaa chochote cha ujenzi
kulingana na uwezi wake.
H a r a m b e e h i y o
imetangazwa na Imamu
wa Msikiti huo Sheikh
Sul e i ma n Abda l l a h,
akiongea na Waislamu
waliofka Msikiti hapo kwa
ajili ya ibada ya swala ya
Ijumaa na kujionea athari
ya moto uliowaka Msikitini
Harambee Mtambani leo
Na Bakari Mwakangwale
hapo.
Tunawaita Waislamu
siku ya Ijumaa (leo) katika
kheri unahitajika masaada
wa hali na mali, ikiwa una
vitabu, Kompyuta, smenti,
Nondo, Mbao, Misumari,
waya za umeme, swichi
au pesa wewe lete, toa kwa
ajili ya Mwenyezi Mungu,
kwa ajili ya kurudisha
huduma haraka kwa vijana
ili waendelee kusoma,
hat ut ar aj i i kus i t i s ha
masomo wakati Waislamu
mpo. Alisema Imamu
Suleiman.
I mamu Sul e i mani ,
alisema gharama za vifaa
zinakadiriwa kuwa ni kiasi
cha 6m/-, kwa ajili ya vifaa
kutokana na athari ya moto
huo ulioteketeza sehemu
yote ya Shule, iliyopo
ghorofaya pili.
Mpaka sasa uongozi
wa Msikiti huo umesema,
tayari walianza kupokea
misaada siku ya pili tu
baada ya janga la moto,
kutoka kwa Waislamu,
Mi si ki ti , vi ongozi wa
Kisiasa na watu binafsi
kutoka Serikalini.
Miongoni mwa Misikiti
hiyo ni Masjidi Veteran-
Ihsan, wametoa 1.32m/-,
Msikiti wa Kigogo (Shia),
1m/-, kwa upande wa
vyama wamepokea kiasi
cha Tsh. 5,000,000/- kutoka
Chadema, ACD wao
wametoa mifuko 20, ya
saruji pia Katibu Mkuu wa
Baraza la Mitihani (NECTA)
Dkt. Charl es Msonde,
amechangia 5,000,000/-,
pamoja na kiongozi mmoja
kutoka TAMISEMI, katoa
5,000, 000/-.
KI TUO cha Ki t uo cha
Kiislamu cha kimisri cha Dar
es salaam kwa kushirikiana
na umoja wa wanazuoni
wa Ki i sl amu Tanzani a
kimefanya kongamano la
kidini llilofanyika chuoni
hapo mwishoni mwa wiki
iliyopita.
Mashei kh mbal i mbal i
waliwasilisha mada katika
kongamano hilo lililokuwa
na anuani uharamu wa kuua
katika sheria ya Kiislamu
ambapo mgeni rasmi alikuwa
ni Rais mstaafu Alhaj Mzee
Ali Hassan Mwinyi.
Ka b l a y a k u a n z a
uwasilishwaji wa mada za
Masheikh katika kongamano
h i l o , muo n g o z a j i wa
kongamano Sheikh Mohamed
al-Amiri Athumani, ambaye
ni mwalimu wa Markaz,
aliwakaribisha Masheikh wa
kimisri na wa kitanzania
kuwasilisha mada zao ambapo
kongamano lilifunguliwa kwa
kusomwa Qurani na Sheikh
Elysayed Awadh, ambaye ni
mwalimu wa Markaz.
Miongoni mwa Masheikh
waliokaribishwa kuwasilisha
mada zao katika kongamano
hi l o ni Shei kh Khami s
Mataka, Katibu Mkuu wa
taasisi ya Wanazuoni na
Masheikh Tanzania, ambaye
alitoa mada kuhusu namna
roho ilivyo na thamani kubwa
katika Uislamu, ambapo
aliwakumbusha watu juu
ya uharamu wa kuua katika
Qurani na hadithi.
Ai dha al i zungumzi a
suala hilo kwa mujibu wa
Qurani Surat Nisai, ambapo
aliegemea katika neno la
mwenyezi Mungu Na yeyote
atakayemuua muumini kwa
makusudi basi malipo yake
ni moto wa Jahanam atakaa
Kongamano lafanyika Markaz Changombe
Na Mwandishi Wetu humo milele na hasira za
mwenyezi Mungu ni zake
na atamuandalia adhabu
kubwa.
Likafuatiwa na neno la
makaribisho lililotolewa na
Mudir wa Markaz, Sheikh
Salah Sayed Hussein Miftah,
a mba ye a l i a nz a kwa
kumkaribisha mgeni rasmi
Rais mstaafu wa awamu ya
pili ya serikali ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania
al-Haj i Mzee Ali Hassan
Mwinyi, ambaye alilipamba
kongamano kwa kuf i ka
kwake kwa mara ya kwanza
baada ya miaka mingi kupita.
Akiwasilisha mada yake,
Sheikh Mataka alijikita pia
katika hadithi ya Mtume
(saw) Kila Muislamu kwa
Muislamu ni haramu roho
yake na mali yake na heshima
yake .
Na ye Dk. Abda l l a h
Dar uwes hi , ambaye ni
mwalimu wa Markaz hiyo
ya ki mi sri al i wasi l i sha
mada iliyokuwa na anuani
kuhifadhi nafsi ya binadamu
ni makusudio makubwa ya
sheria, ambapo alifafanua
kwamba kusudio la sheria
ni kuhakikisha maslahi ya
binadamu (waja).
Aidha alibainisha kuwa
hayo ndio makusudio ambayo
Ui s l amu umeyahi f adhi
n a k u b a i n i k a k a t i k a
mambo makuu matano na
akaichukulia dalili juu ya
kuhifadhi nafsi ya binadamu
na baadae Sheikh Yahya Mkali
kutafsiri mada yake.
Kwa upande wake Sheikh
Suleiman Kilemile, ambaye
ni Mwenyekiti wa Umoja
wa Wanazuoni wa Kiislamu
Tanzania, alizungumzia juu
ya uharamu wa kuwaua
wale wanaoishi kwa mkataba
na ahadi katika sheria ya
Kiislamu.
Sheikh Kilemile alitumia
fursa hiyo kufafanua mada
yake juu kuhusu ukubwa wa
kosa la kumwaga damu au
kuua wale wanaoishi kwa
mikabata ya amani katika miji
ya Kiislamu kwa njia ya vibali
(visa na permit).
Al i sema kuwa huo ni
mkataba wa amani hivyo
hai f ai kwa mt u yeyot e
kuuvunja mkataba huo kwa
njia ya kumwaga damu au
kwa kufanya uadui wowote.
Al i f a f a n u a h a d i t h i
ya Mtume (saw) isemayo
yeyote atakayemuua mtu
anayeishi kwa mkataba wa
amani, huyo hatoisikia harufu
ya pepo, kwani harufu yake
hupati kana mwendo wa
miaka arobaini.
Ul i f i k a wa k a t i wa
k u z u n g u mz a S h e i k h
Mohamed Iddi Mohamed
(Abuu Iddi), ambaye ni Naibu
Katibu Mkuu wa Umoja wa
Wanazuoni wa Masheikh wa
Kiislamu Tanzania na Imamu
Mkuu Masjid Mnyamani.
Ma da ya ke i l i kuwa
ni thamani ya uhai katika
Uislamu. Alibainisha kwamba
uhai ni zawadi toka kwa
mwenyezi Mungu mtukufu,
hivyo haifai kuifanyia uadui
neema hii isipokuwa kwa
haki zake au hukumu za
mwenyezi Mungu.
Kongamano hilo lilifikia
tamati kwa maneno al-Haji
Hassan Mwinyi, ambaya
alitilia mkazo juu ya neema
ya amani.
Mwisho alisimama Sheikh
Swalah Miftah, Mudir wa
Markaz na kuwashukuru wote
waliohudhuria kongamano
na kumshukuru Rais mstaafu
kwa kushajiisha Markazi
katika kongamano hilo.

3
AN-NUUR
SHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 22-28, 2014
Habari
Muhongo awarushia Waislamu makombo
TAARIFA za uchunguzi
zinaonyesha kuwa Waziri
wa Nishati na Madini,
Profesa Sospeter Muhongo
kaongeza watu watano
katika orodha ya kwenda
kusomea ut alamu wa
mafuta na gesi, China.
P r o f . M u h o n g o
amechukua hatua hiyo siku
kadhaa baada ya hapo awali
kuchagua kwa asilimia
100 Wakri st o wat upu
watakaolipiwa na serikali
ya China kusoma katika
vyuo vikuu vya nchi hiyo
katika ngazi ya Shahada
ya Uzamili (Masters) na ile
ya Uzamivu (Ph.D) katika
utaalamu wa mafuta na
gesi.
Hatua hiyo ya kuwapa
Wai sl amu si furi (0%),
i l i zua mal al ami ko na
maswali mengi na joto
lake lilivyozidi kupanda,
Waziri akaona alipoze kwa
maelezo kuwa kaongeza
watu watano katika wale
kumi aliowateuwa awali
wakiwa Wakristo watupu.
Waliotajwa kuongezwa
watakwenda kusomea
Shahada ya Uzalimili (MSc)
katika mafuta na gesi.
Hat a hi vyo t aar i f a
ndani ya Wi zara hi yo
zi naf ahami s ha kuwa
wakati wal e kumi wa
awali watasomeshwa na
serikali ya China, hawa
alioongeza Mheshimiwa
Waziri Muhongo katika
kupoza mambo, itabidi
Wizara itafute namna ya
kuwalipia jambo ambalo
hal i j af ahami ka kuwa
Muhongo atapata wapi
baj et i yake, kwa vi l e
haikuwepo toka awali.
Wengi wanaonyesha
wasiwasi kuwa isije kauli
hi yo i met oka kat i ka
kupoza joto hali ikawa
ngumu baadae kwa hao
waliotupiwa makombo
wakakwama njiani hata
masomo wasimalize.
Awali katika orodha
iliyotolewa kufaidi msaada
huo wa kusomeshwa na
serikali ya China walitajwa
kuwa ni Erasma Rutachura
(PhD), Abel Masanja (MSc),
Beatrice Tubuke (MSc),
Faustine Matiku (MSc) na
Alvin Mulashani (MSc).
Wengine ni Kunugula
Lwakutubi (MSc), Nigel
Kimaro (MSc), Ansila Kiusa
(MSc. ), Hebert Msangi
(MSc.) na Victor Mugarula
(MSc).
Hawa wanasomeshwa ili
kuja kuwa wataalamu katika
mafuta na gesi, rasilimali
ambazo zinaonekana kuwa
Na Mwandishi Wetu
zitachukua nafasi kubwa
sana ya uchumi wa nchi hii
kwa siku za hivi karibuni.
Ni kutokana na uteuzi
huu wa awali ambao wengi
walioona orodha hiyo
walisema wazi kuwa huo
ni udini, walihoji kuwa
iwapo hivi sasa siasa,
sera, mweleko na wito ni
kumshirikisha kila mtu,
kila mwananchi, mbona
inapokuja suala la dini
mwelekeo huo unapigwa
chenga?
Au inapozungumzwa
kila mwananchi kushiriki
katika uchumi wa nchi,
Muislamu yeye hayumo?
Wa t a a l a mu ha wa
wanaoandal i wa, ndi o
wat akuj a kus i mami a
sekta hii muhimu kwa
uchumi wa nchi , sasa
unapoandaa watu wa dini
moja tu, maana yake ni
kuwa unataka wakirudi na
kushika nafasi mbalimbali,
nao wateuwe na kuajiri wa
chini yao walio katika wao,
hii maana yake nini? Si ndio
udini wanaouzungumzia
na kuuupi gi a kel el e
Waislamu?
Alihoji mtumishi mmoja
katika sekta binafsi ambaye
hat a hi vyo hakut aka
kutajwa jina lake gazetini.
Lakini mtu anapofanya
kitu kama hichi, kutumia
nafasi ya Uwaziri wake
na kutumia dhamana ya
uongozi aliyopewa na taifa
kufanya ubaguzi na udini
kama huu ulio wazi kabisa,
lengo lake nini, kama si
kutaka kuleta machafuko
katika nchi. Aliongeza.
Ka t i k a k uf a f a n ua
a l i s e ma k u wa k wa
takriban wiki mbili sasa,
kumekuwa na machafuko
kul e Ferguson, Ji mbo
la Missouri, Marekani
kutokana na kuuliwa kwa
kupigwa risasi kijana wa
Kimarekani mwenye asili
ya Afrika.
Anasema, hasira ya watu
inakuja baada ya kuwa
yametokezea matuki o
kama hayo mengi ambapo
wat u weus i huul i wa
na polisi kwa kupigwa
ri sasi bi l a ya sababu
za msingi, kinyume na
sheria na hakuna hatua
wanazochukuliwa polisi
wanaofanya jinai hiyo.
Akasema kuwa, vurugu
za sasa kule Ferguson,
ni kuwa watu wamefkia
mahali wamechoka.
Wanaona kuwa wao
hawat hami ni wi kama
binadamu, damu yao na
uhai wao unaonekana
hauna thamani kwa hiyo
unaweza kutolewa ovyo tu
na isiwe lolote.
Sasa isidhaniwe na
Waislamu wa Tanzania
wataendelea kushuhudia
ubaguzi na udini kama huu
halafu wakae kimya tu,
watameza itafika mahali
wat ashi ba, yat akuwa
hayamezeki t ena, na
ikifka hapo wasilaumiwe,
wa c ha wi wa t a k uwa
ni hawa wanaot umi a
madaraka yao kuendeleza
udini na ubaguzi katika
nchi hii. Alimaliza.
Huyu Trayvon Martin
a l i p i g wa r i s a s i n a
kuuliwa na Polisi, George
Zimmerman, usiku wa
Februari 26, 2012, kule
Sanford, Florida.
Wakat i huo Mart i n
alikuwa bado kijana mdogo
wa umri wa miaka 17 na
mwanafunzi wa sekondari.
Japo kij ana Trayvon
h a k u wa n a s i l a h a ,
maml aka za ki sheri a
zilimwachia huru George
Zimmerman, kwa madai
kuwa alimuuwa Trayvon
aki wa kati ka harakati
za kuj ihami/kuj ilinda,
utadhani kulikuwa na
mapambano kati ya kijana
huyo na askari mweye
silaha.
Hat ua hi yo i l i i bua
hasira ambapo yalifanyika
maandamano nchi nzima
na kupelekea kukamatwa
tena George Zimmerman
akishitakiwa kwa mauwaji.
Hata hivyo, ilipofika
Julai 13, 2013 aliachiwa
tena mahakama ikikariri
hoja za awali kuwa hana
hatia kwa sababu alikuwa
akijihami.
Hatua hiyo iliibua tena
hasira na maandamano
makubwa na kuwapa
moyo Wamarekani Weusi
wakiungwa mkono na raia
wenzao Weupe kuwa kuna
haja ya kuchukua hatua
kuhakikisha kuwa mfumo
huo usio rasmi wa kibaguzi
unangoka.
Katika salamu zake za
rambirambi na kuwafariji
wafwa, Sybrina D. Fulton,
ambaye ni mama wa
Trayvon Martin, baada
ya maelezo marefu ya
kuonyesha masi ki ti ko
yake, al i mal i zi a kwa
kusema kuwa iwapo wenye
mamlaka katika serikali
ya Marekani hawatataka
kuwasilikiza, basi jamii
inayobaguliwa itawafaya
wahisi na watambue kuwa
nao Weusi wapo.
Alisema, If they refuse
to hear us, we will make them
feel us.
Na akaongeza kuwa
wal a hi i i si chukul i we
k uwa ni uc ho c he z i
kwani kinacholengwa ni
kuwafanya wabaguzi na
wanaouwa ovyo watoto
wa wenzao, wafkie mahali
wafkirie, lau ingekuwa ni
watoto wao wanaouliwa
wangejisikiaje.
Waki fi ki shwa hapo,
anasema, hapana shaka
haraka watachukua hatua
za kurekebisha hali iliyopo.
Polisi, George Zimmerman Baba yake Michael Brown
Mama yake Trayvon Martin
MAANDAMANO nchini Marekani kupinga mauaji yanayofanywa na polisi dhidi
ya watu weusi.
Mama yake Michael Brown.
4
AN-NUUR
SHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 22-28, 2014
Habari
NECTA watuhumiwa kuleta Utanganyika katika mitihani
BARAZA l a Mi t i hani nchi ni
(NECTA) limeshutumiwa kuleta
ubaguzi kati ya Bara na Visiwani
katika utendaji wake.
Ubaguzi huo umetajwa kuwa
ni ule wa kuona kuwa wenye haki
kutendewa haki katika mitihani ya
Lugha ya Kiarabu na Maarifa ya
Uislamu, ni Wazanzibari tu, lakini
kwa Bara hawana haki hiyo.
Ni katika muktadha huo huo,
ikakumbushwa kuwa Baraza hilo
lilikuwa likiweka utaratibu wa
kuwafelisha watoto wa Kiislamu,
wakati likiwarahisishia kufaulu wale
wa Kikristo.
Ikafafanuliwa kwa kusema kuwa
somo la Islamic Knowledge, lilikuwa
likiwekewa alama za juu za ufaulu,
wakati lile la Bible, likiwekewa alama
za chini.
Hayo yameelezwa na Baraza
la Wakuu wa Shule za Kiislamu,
likimtaka Wizari ya Elimu na Mafunzo
ya Ufudi, kutengua matokeo ya
wanafunzi wa Kiislamu wa kidato
cha sita kufuatia kuenguliwa masomo
ya Dini katika kupanga madaraja ya
ufaulu.
Katika Barua yao kwenda kwa
Waziri wa Elimu, Mh. Shukuru
Kawambwa, Baraza hilo limesema,
zipo sababu za kutosha zenye maslahi
na Taifa za kubadilisha matokeo hayo
ya wanafunzi ambao wameathirika
kwa kuenguliwa kwa masomo hayo.
Baraza la Wakuu wa Shule za
Kiislamu linapinga mabadiliko haya
na kuomba yatenguliwe. Baraza
linaamini kwamba ziko sababu
za kutosha na zenye maslahi na
Taifa letu za kubadilisha matokeo
ya wanafunzi walio athirika na
mabadiliko hayo yaliyofanywa na
NECTA. Imesema Barua hiyo.
Barua hiyo imeyatafsiri mabadiliko
hayo yaliyofanyika kuwa ni ya
kibaguzi kwa sababu yanawabagua
watahiniwa wa masomo ya Arabic
na Islamic Knowledge kwa misingi
ya Zanzibar na Tanganyika, hivyo
wakaitaka NECTA iwatendee haki
watahiniwa hao kupitia masomo
hayo ya Dini.
Wakuu hao wa Shule za Kiislamu
nchini wakasema kinacho wasikitisha
zaidi ni kuona kwamba kila mara
Baraza l a Mi t i hani ( NECTA)
wanaf anya maamuzi ambayo
yanapelekea kusababisha mgogoro
na wadau wake wa dini ya Kiislamu.
Baraza hilo limemweleza Waziri
Kawambwa, sababu za kutaka
kutenguliwa kwa matokeo hayo
kuwa ni kinyume na sheria za nchi na
haioneshi utawala bora pia utaratibu
huo utaleta sintofahamu isiyokuwa
na msingi kwa wadau wa Baraza la
Mitihani hasa wale wa Vyuo Vikuu
vya ndani na nje ya nchi.
Hii ni kwa sababu wanafunzi
wawili, mmoja kutoka Tanganyika
na mwingine kutoka Zanzibar
ambao watakuwa wamesoma KLA
na kila mmoja akafaulu sawa na
mwingine, yule wa Zanzibar atapewa
cheti chenye ufaulu wa juu zaidi,
kuliko huyu wa Tanganyika hali
hii italishushia Baraza la Mitihani
la Tanzania hadhi yake. Imesema
Barua hiyo.
Walimu hao wamesema, Baraza
la Wakuu wa Shule za Kiislamu,
Na Bakari Mwakangwale
l i nashi ndwa kuel ewa mant i ki
inayotumiwa na wataalamu wa
Wizara ya Elimu kuamua lugha gani
ya kigeni ina umuhimu katika nchi
hii.
Kwa uelewa wao, wamesema
somo la Kifaransa lina watahiniwa
wachache kuliko somo la Kiarabu
humu nchini, lakini wataalamu
wa Wizara ya Elimu wanaendelea
kulihesabu somo la Kifaransa katika
kupanga madaraj a ya matokeo
ya mtihani wa kidato cha sita na
kuliondoa somo la Kiarabu.
Somo la Kifaransa lina watahiniwa
wachache kuliko somo la Kiarabu
humu nchini, lakini wataalamu
wako wanaendelea kulihesabu somo
hilo katika kupanga madaraja ya
matokeo ya mtihani wa kidato cha
sita, tunashindwa kuelewa maamuzi
haya yanafanywa ili kumfurahisha
nani na kumridhisha nani? Imesema
na kuhoji barua hiyo.
B a r a z a h i l o l i me s e ma ,
lmesikitishwa na hatua ya Baraza la
Mitihani kwa kuyaengua masomo ya
Arabic na Islamic Knowledge katika
mchakato wa kutoa madaraja ya
wanafunzi katika mtihani wa kidato
cha sita.
Baraza hilo limeeleza kwamba ni
kawaida kwa Wizara ya Elimu au
hata Baraza la Mitihani kuwasiliana
na wadau wanapotaka kufanya
mabadiliko ili kupata maoni yao au
hata kuwapa taarifa tu ili wajiandae
pia kufanya maamuzi bora kwa
wakati muafaka, lakini kwa hili
imekuwa tofauti.
Waki zungumzi a waraka wa
Kamishna wa Elimu wa mwaka 2006
na Tahasusi zenye somo la Kiarabu,
wamesema waraka huo haujabadilika
bado na Baraza la Mitihani limekuwa
likitunuku kama somo moja wapo.
Mheshi mi wa, waraka wa
Kamishna wa Elimu wa April 1,
2006, haujabadilika mpaka hivi
sasa, Baraza la Mitihani limekuwa
likitunuku somo la Kiarabu kama
somo mojawapo la Lugha katika
Shule mbalimbali na miaka tofauti.
Imeainisha barua hiyo, iliyotiwa saini
na Mwekiti wa Baraza hilo, Mwl.
Hamisi Togwa.
Wakuu hao wa Shule za Kiislamu,
kati ka barua hi yo kwa Wazi ri
Kawambwa, wameai ni sha na
kuchanganua mifano ya watahiniwa
wa wakidato cha sita kwa mwaka 2014
kutoka Tanzania Bara walioathiriwa
na uamuzi wa kuyaengua masomo
hayo.
Aidha, Baraza hilo la Wakuu wa
Shule za Kiislamu, wamemkumbusha
Waziri Kawambwa, kuwa huko
nyuma kumekuwa na malalamiko
kutoka kwa Waislamu, kwamba
Baraza l a Mi t i hani wal i kuwa
wakipuuza kwa makusudi kuajiri
waratibu wa somo la Arabic na Elimu
ya Dini ya Kiislam.
Pia Baraza la Mitihani, wamekuwa
wakiweka alama za ufaulu kwa somo
la Islamic Knowledge kuwa za juu
zaidi ikilinganishwa na somo la Bible
Knowledge, ili kuwafelisha Waislamu
na kuwarahishia kufaulu Wakristo.
Ama, mgogoro wa matokeo ya
somo la Islamic Knowledge kwa
mwaka 2012, pia ni miongoni mwa
mambo yaliyo liweka Baraza la
Mitihani (NECTA) na Waislamu kuwa
katika sintofahamu kubwa.
Awali, akiongea na An nuur,
Ofsini kwake kufuatia kuenguliwa
huko kwa masomo ya Dini, Kaimu
Katibu Mtendaji wa NECTA, Dkt.
Charl es Msonde, al i sema kazi
yao ni kutekeleza miongozo ya
Serikali (Wizara ya Elimu) pasi ya
kukengeuka.
Pamoj a na hi vyo, al i s ema
changamoto anayoiona na kusikia
kwa wadau mbalimbali, ni kufahamu
ni ipi michepuo (Combinition)
inayotambulika na hususani kwa
Waislamu baada ya kuona masomo
yao hayajahesabiwa kama sehemu
ya ufaulu.
Hoj a i nakuj a kwamba, j e
masomo hayo yapo katika michepuo
inayotambulika na Wizara ya Elimu?
Mtoto alipokwenda kujiunga na
kidato cha Tano, alisoma kombi yenye
masomo hayo? Alihoji Dkt. Msonde,
akijenga hoja yake.
Alisema, Wakuu wa Shule za
Sekondari wameainishiwa masomo
ya michepuo yanayotambulika na
Wizara ya Elimu ya kitado cha Tano
(A-Level), kuwa ni HGE, HGL, HGK,
HKL, mengine ni KLF, EGM, PCM,
PCB, CBG, pamoja na PGM, ECA,
CBA, CBN.
Hata hivyo alisema, mwanafunzi
hakatazwi kusoma masomo ya ziada
anayoyapenda kama ni Maarifa ya
Uislamu, Arabic, au Divinity na hata
kama ni kompyuta Sayansi, na Baraza
litayasahihisha na kuyapa madaraja
na yatatambulika popote ndani na
nje ya nchi.
Dkt. Msonde, alibainisha kwamba
katika usahihishaji changamoto
huwa ni katika ukokotoaji kwani
hufanywa na mfumo wa Kompyuta
ambao tayari upo katika programu
(programmed) ya kombinisheni
zinazotambulika na Wizara ya Elimu.
Lakini, alisema pamoja na hali hiyo
bado Waislamu na wadau wengine
wanayo nafsi ya kushauri kwa
sababu wao ni wadau wa elimu na
wanahaki ya kusikilizwa.
Kwa mfano, alisema hoja ya msingi
ambayo inaweza kutumika katika
hilo ni kutumia idadi ya wanafunzi
wanaosoma na kufanyia mtihani
masomo hayo na hakutakuwa na
sababu ya kuwazuia ikiwa itabainika
ipo haja kwani wao ndio wanaohitaji.
Hi i mi chepuo i l i yopo na
i nayot ambul i ka na Wi zar a,
imewekwa na wanaadamu na haina
maana kwamba itakaa milele, hapana
imewekwa kwa mahitaji ya watu na
kwa wakati husika hivyo inaweza
kubadilishwa au kuongezwa mingine.
Kwa mfano kombinisheni hizi
zilitolewa mwaka 2006, lakini hayo
yalikuwa ni mahitaj ya watu kwa
wakati huo inawezekana sasa watu
wanamahi taj i mengi ne zai di .
Alisema Dkt. Msonde.
Al i s ema, kwa s as a wadau
wanaweza kusema hivi kuna HKL,
KLF, lakini kulingana na mahitaji kwa
kipindi hiki inaonekana ongezeko la
wasomaji wa somo hilo kuwa kubwa
hivyo kuna haja ya somo la Arabic
kuwa katika mchepua wa Lugha,
hivyo pakawa na KLA, LFA au hata
HGA kwa kuwa tayari kuna HGK.
Sasa hoja hii unaijenga wapi,
unaweza ukaandika kwa Kamishna
wa Elimu katika Wizara ya Elimu,
kwa sababu yeye ndiye anayetoa
hiyo miongozo na sisi tunatekeleza
au kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya
Elimu, lakini hoja hiyo isiwe katika
malalamiko, bali iwe katika ushauri
kama wadau wa elimu. Alishauri
Dkt. Msonde.
Aidha, Dkt. Msonde, alieleza
kwamba hata kama masomo hayo
kwa sasa hayapo katika michepuo,
lakini Baraza la Mitihani linayagredi
kama kawaida na kuyapa maksi kama
kawaida na yatakuwa na manufaa
kulingana na malengo ya mtahiniwa.
Akifafanua alisema, Vyuo Vikuu
wanapopokea maombi ya kujiunga
wao huanza kupitia pasi alizoombea
mtahiniwa katika masomo husika,
kwani alidai hawafati pointi kutoka
Baraza.
Vyuo Vi kuu ha vi c ha gui
mtahiniwa kwa sababu ya idadi
ya poini za Baraza, wao huchagua
mtu kujiunga na Chuo Kikuu kwa
kutegemea na kozi aliyoiomba na
masomo yanayohusiana na kozi
aliyoiomba.
Katika cheti cha Baraza la mitihani
masomo yote aliyofanyia mtihani
mtahiniwa yanatolewa ambayo
yatakuwa na nguvu ya kuombea
kujiunga na Chuo chochote duniani
au taasisi yoyote ya elimu. Alidai
Dkt. Msonde.
Ama kuhusu Zanzibar, kuwa wao
masomo hayo ya dini yametumika
Inaendelea Uk. 5
WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa.
5
AN-NUUR
SHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 22-28, 2014
Habari
TANGU alipotoweka kijana
wake Juni 28 mwaka huu,
Bw. Mahat Elmi Hassan,
mwenye umri wa miaka 51
hakai mbali na simu yake ya
mkononi, akitumaini kupata
habari mpya kuhusu mahali
alipo kijana wake mkubwa
mwenye umri wa miaka 17,
Abdi Mahat Elmi.
Ki j ana wangu Abdi
alikuwa akifanya kazi kama
mwal i mu wa madrassa
katika eneo la Koreni, katika
Kaunti ya Lamu miezi miwili
kabla ya kupotea kwake,
Hassan aliuambia mtandao
wa Sabahi.
Aliongeza kuwa kupotea
kijana wake kulitokea wakati
wa msako wa watu wa vikosi
vya usalama vya Kenya
dhidi ya watuhumiwa wa
mashambulio katika Kaunti
ya Lamu.
Katika miezi hiyo miwili,
ni mara chache sana siku
ilipita bila yeye kupiga simu
na kusema anavyoendelea
na kuuliza juu ya sisi kurudi
nyumbani, alisema Hassan,
mkazi wa Garissa.
Alisema kabla ya kupotea
kwake, aliwaambia kwamba
maofsa wa polisi walikuwa
wakikamata watu pasipo
sababu maalumu.
Walielezea wasiwasi wao
kwamba kijana wao anaweza
kuwa mwathirika wa ufagiaji
wa polisi.
Bw. Hassan alisema Elmi,
alikwenda Kaunti ya Lamu
kufanya kazi kama mwalimu
wa madrassa kusaidia familia
yake maskini.
Baada ya kupotea kwake,
familia hiyo ilikwenda Lamu
kumtafuta na kuuliza yeyote
anayejua mahali alipo, lakini
pasipo mafanikio.
Kwa sasa nabeba simu
hata ninapokwenda kuoga
ni ki wa na mat umai ni
kwamba yeye au mtu yeyote
atapiga simu kunipa habari
nzuri, alisema.
Elmi siyo kijana pekee
ambaye haj ulikani alipo
katika wiki za hivi karibuni.
Viongozi wa kisiasa wa
ndani na vikundi vya haki
za binadamu wanalaumu
polisi kwa kupotea watu
wasiopungua 21 wakati wa
operesheni ya usalama katika
mkoa wa Pwani.
Bw. Hussei n Khal i d,
Mkuregenzi Mtendaji wa
asasi ya haki za binadamu
ya Haki Afrika, alisema wana
hofu kwamba vikosi vya
usalama vinaweza kuwa
viliwakamata watu ambao
hawakurekodi wa kati ka
vitabu au hata kuishia katika
mauwaji yanayotokana na
Familia zataka majibu kuhusu
watu 21 wasiojulikana walipo
Ni baada ya fagiafagia ya usalama Pwani
katika viwango vya ufaulu,
alisema ni kanuni ndio
zinazo ruhusu hivyo kwa
kuwa tayari wao masomo
hayo yanatambulika.
Alisema, kifungu cha
23 cha Baraza la Mitihani
ki meani s ha kwamba
Kami shana wa El i mu
anaweza akatoa miongozo
na yeye au Baraza l a
Mi t i hani wanat aki wa
waifuate.
La ki ni kumbuka
Zanzi ba ni nchi , i na
Waziri wake wa Elimu,
ina Katibu Mkuu wake na
ina Kamishna wake pia,
lakini Baraza la Mitihani
(NECTA) sio la Tanzania
Bara pekee, ni Taasisi ya
Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Kwa hiyo, mimi naweza
kupokea maelekezo ya
Kamishana wa Bara na
bado pia naweza kupata
maelekezo na miongozo
kutoka kwa Kamishina wa
Zanzibar. Alisema Dkt.
Msonde.
Hivyo, alisema kwa
upande wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar,
Kamishna wake wa Elimu
katika muongozo uliopo
NECTA hadi sasa wa
mwaka 2012, ambao
Bar aza unaout umi a,
umetoa ufafanuzi wa
michepuo ya masomo
husika kwa Zanzibar.
Mu o n g o z o h u o
umeniambia kwamba,
kat i ka yal e mas omo
a m b a y o z a m a n i
waliyokuwa wakiyaona
ni ya hiyari kwa Zanzibar,
sasa yamekuwa ni ya lazima
na kunitaka yatambulike
kwa hatua zinazofaa kwa
muunganisho maaluma.
Alisema Dkt. Msonde.
Alisema, waraka huo
wa Kamishana wa Elimu
Zanzi bar, umeai ni sha
michepuo ya masomo hayo
kuwa ni Arabic Kiswahili
Islamic Knowledge, Arabic
Kiswahili English, Arabic
History Kiswahili, Arabic
History Geography na
Arabic Kiswahili French.
Akasema, yeye binafsi
anaona umefika wakati
yakat ambul i ka i ki wa
data zitaonyesha kuna
ongezeko la watahiniwa
wa Masomo hayo na
anaweza kushirikiana na
wadau wengine kujenga
hoja kwa Kamishana na
Kat i bu Mkuu Wi zara
ya Elimu kwa manufaa
ya Tai fa i l i kuepusha
migongano na wadaui
wake.
NECTA watuhumiwa
kuleta Utanganyika
Inatoka Uk. 4
Na Bosire Boniface, Garissa kut umi a nguvu nyi ngi
katika vita vinavyoendelea
kuhusiana na ugaidi.
T u m e t h i b i t i s h a
kwa hati watu 21 ambao
hawajulikani walipo. Sita
kati yao hawaonekani huko
Lamu tangu kuzinduliwa
operesheni ya usal ama
baada ya mashambulio ya
Mpeketoni. Alisema Bw.
Khalid.
Alisema watu wengine
ambao hawajulikani walipo
waliripotiwa kuonekana kwa
mara ya mwisho mwezi Mei
katika kaunti za Mombasa,
Taveta na Kwale wakati
wa operesheni nyingine za
usalama.
Bw. Khalid aliongeza kuwa
mashuhuda na wanafamilia
wa watu ambao hawajulikani
walipo, walisema ndugu zao
walionekana kwa mara ya
mwisho wakichukuliwa na
maofsa wa polisi na kwamba,
ndugu wamewasilisha ripoti
za watu wasiojulikana waliko
kwa mamlaka za eneo na
katika taasisi yake.
F a mi l i a z i n a h o f i a
k wa mb a n d u g u z a o
wasiojulikana walipo, ama
wameuawa au wanashikiliwa
kinyume cha sheria. Serikali
inatakiwa kuchukua hatua
na kueleza watu hao wako
wapi kwa kuwa polisi ni
watu wa mwisho kuonekana
na watu hao. alibainisha
Mkurugenzi huyo.
Mwakilishi wa Wanawake
wa Kaunti ya Lamu, Shakila
Abdal l a, al i sema pol i si
wanawakamata watu bila ya
sababu.
Ni haki ya katiba na haki
ya mtu yeyote kuarifiwa
makosa yake anapokamatwa
na kubainishiwa mahali
anapopelekwa, lakini polisi
hawataki hata kuwaruhusu
waliokamatwa kuwajulisha
ndugu zao. Mwakilishi
huyo aliuambia mtandao wa
Sabahi.
Alisema kuwa wamefanya
mikutano na viongozi wa
usal ama kut aka kuj ua
wal i po baadhi ya watu
waliokamatwa na polisi kwani
ukamataji huo wa kiholela na
kutoweka watu hakutaleta
matokeo yanayotakiwa ya
operesheni ya usalama na
badala yake, kutaleta hofu na
watu wanaweza kushindwa
kushirikiana na polisi.
Kwa upa nde wa ke ,
Ka mi s hna wa Ka unt i
ya Lamu, Mi i ri Nj enga,
alisema mamlaka zilikuwa
zinachunguza madai ya
kutoweka watu hao.
Ni t u h u ma n z i t o
dhidi ya vikosi vyetu vya
usalama ambavyo viko hapa
kuwatafuta wahusika wa
vurugu zinazotokea katika
Kaunti, alisema Bw. Njega
Alidai kuwa wanahitaji
ushahidi ambao kwa hakika
utabainisha polisi ambao
wanahusika na kutoweka
kwao.
Aidha alisema kwamba
hawawezi kut hi bi t i sha
kwamba baadhi ya tuhuma
za wat u wasi oj ul i kana
walipo, wanaweza kuhusika
katika vurugu na kuamua
kukimbia operesheni ya
usalama kwenda kaunti au
nchi nyingine.
Kaimu Kamanda wa Polisi
wa kaunti ya Mombasa,
Sevelino Kubai, alinukuliwa
akikanusha kuwepo kwa
ufanyaji makosa wowote
kwa upande wa pol i si
na kus ema, wal i kuwa
wanachunguza kesi zote za
watu wasiojulikana walipo.
Kamanda Kubai alisema
Mb u n g e wa Mv i t a ,
Abdul s wamad Shar i f f
Na s s i r na Se ne t a wa
Mombasa, Hassan Omar,
wamewasilisha ripoti kuhusu
watu wasiojulikana walipo.
Kamanda huyo alisema
kuwa viongozi wanasema
watakwenda mahakamani
kuwashitaki polisi, wakitaka
waelezwe walipo kuhusu
watu wasiojulikana walipo,
aliiambia Sabahi.
Tul i kuwa t unaf anya
uchunguzi kuhusu ripoti za
madai ya watu wasioonekana.
Wakati huohuo, tunawataka
viongozi kutoshikilia madai
ya uongo kuhusu polisi
bila kuwa na ushahidi wa
kutosha.
Madai kwamba polisi
wanaweza kuwa wamewaua
watu hao wasioj ulikana
walipo ni ya kufedhehesha.
Taari fa za ki na za mtu
yeyot e t ul i yemkamat a
zimerekodiwa katika kitabu
cha kumbukumbu cha polisi.
Kama uchunguzi wet u
ut agundua mmoj awapo
ha hus i ki na uha l i f u,
ataachiwa huru. alisema
Kubai.
Alisema ukosoaji wa kikosi
cha polisi kushughulikia
operesheni ya usal ama
ulikuwa ni jaribio la kuzuia
mchakat o na kwamba,
hawawezi kuzui wa na
madai ambayo lengo lake ni
kuharibu au kuchelewesha
vita dhidi ya uhalifu.
Wa k a t i h u o h u o ,
Wafuatiliaj i wa Haki za
Binadamu (HRW) Jumatatu
wiki hii walisema Kitengo
cha Polisi cha Kuzuia Ugaidi
Kenya (ATPU), kilihusika
kwa kufanya matukio ya
mauaji kinyume cha sheria
na kitendo cha kufanya watu
wasijulikane walipo.
Disko marufuku Kiwengwa
WAZI RI wa Ha ba r i ,
Ut amaduni , Ut al i i na
Michezo Zanzibar, Saidi
Al i Mbaruok, amepi ga
marufuku shughuli zote za
kupiga disko katika eneo
la Kiwengwa hadi pale
Serikali ya Wilaya itapotoa
maelekezo maalumu ya
kupigwa disko hilo kwa
utaratibu unaofaa.
Agizo hilo amelitoa hivi
karibuni huko Kiwengwa,
Mkoa wa Kaskazi ni A
Wilaya ya Kaskazini B
Unguj a, kati ka Ofi si ya
Umoj a wa Maendel eo
wa Kij ij i cha Kiwengwa,
wakati alipokuwa akifanya
mazungumzo na wamiliki wa
mabaa, mikahawa, kumbi za
starehe juu ya kukithiri wa
upigwaji wa magoma kucha.
Waziri Mbaruok alisema,
amel azi mi ka kuzi f unga
shughuli zote za upigaji
madisko usiku kutokana
na kutokuwa na utaratibu
mzuri wa upigaji ngoma
hizo usiku, hali ambayo
imesababisha wageni wa
kitalii na wenyeji kuchukia
hali hiyo kwa kukosa usingizi
na kusumbuliwa wagonjwa.
Ames ema, hal i hi yo
hai wezekani kuonekana
inaendelea kwani inapoteza
muelekeo na mstakabali
mwema wa nchi na raia kwa
ujumla.
Ni mepokea uj umbe
kwamba watalii wamefika
kusema wanaondoka na
kutafutiwa sehemu nyengine
wakapunzike kutokana na
zogo kuwa jingi la madisko,
hili haliwezekani liendelee,
alinukuliwa akisema Waziri
huyo.
A i d h a a l i s e m a
h a i we z e k a n i k u o n a
utamaduni wa burudani
unavurugwa, jambo ambalo
ni kosa kufanya hivyo na
kwenda kinyume na taratibu
na silka zao.
Kuanzi a l eo napi ga
marufuku mpaka Sheha wa
Shehia hii aridhie, hata kama
kuna kibali kwani Sheha
ndiye anayejua hali za raia
wake, kuna wagonj a na
wenye maradhi ya kuhitaji
kupumzika au la, hatutaki
kuona masuala yasio na
utaratibu.
Mi mi kazi yangu ni
kuutangaza utalii sio utalii
uharibiwe, tufahamu kuwa
utalii Zanzibar ndio uchumi
unaotegemewa kwa sasa kwa
hivyo tuulinde, aliongeza
Waziri Said.
Hata hivyo Waziri huyo
alichukizwa na vitendo vya
uwasharati vilivyotapakaa
katika kijiji hicho, kujengwa
mabaa karibu na nyumba
za ibada hivyo kumwagiza
M k u u w a Wi l a y a
kulishughulikia.
Nao wakazi wa Kiwengwa,
Ot humani Mnyanj a na
Mt umwa Rashi di , ki l a
mmoj a kwa maoni yake
walisema Kiwengwa hivi
sasa imepoteza muelekeo
kwani watoto wao wanaishia
katika madisko na kukosa
masomo, jambo ambalo ni
hatari kwao.
6
AN-NUUR
SHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 22-28, 2014
Habari
Mansour afungulia mlango
wanyonge juu ya dhamana
KUMBE hakuna kosa lisilo na
dhamana. Kanuni au sheria
hiyo ndiyo iliyomtoa rumande
Mansour Himid.
Kwa muj i bu wa mael ezo
yal i yot ol ewa mahakamani ,
hata kama kuna kosa linatajwa
kuwa halina dhamana, lakini
Mahakama Kuu imepewa uwezo
wa kutengua kifungu hicho kwa
jinsi itakavyolitathmini kosa na
mtuhumiwa.
Hayo yalibainishwa katika
maelezo ya Jaji Mwampashe kabla
ya dhamana kutolewa kwa Bwana
Mansour Himid.
Katika Mahakama ya Mkoa,
Vuga, aliyekuwa Waziri wa
zamani wa serikali ya Mapinduzi
(SMZ), Mansour Yussuf Himid,
al i pewa dhamana ambapo
kesi yake imeahirishwa mpaka
Agosti 28 mwaka huu baada ya
kuahirishwa na Hakimu Khamis
Ramadhani.
Awal i kesi i l i pof i ki shwa
mahakamani, Mansour alinyimwa
dhamana kwa maelezo kuwa
moja ya kosa analotuhumiwa
halina dhamana.
Ombi l a Mansour kutaka
kupatiwa dhamana linatokana na
kushitakiwa kwa makosa matatu,
la kwanza likiwa ni kumiliki
silaha, kinyume cha sheria.
Mwendesha Mashitaka Raya
akisaidiwa na Maulid Ali litaja
tuhuma nyingine zinazomkabili
Mansoor kuwa ni kupatikana na
risasi 295 kinyume cha kifungu
cha 6 (3) na 34 (1) (2) sheria namba
7 ya Zanzibar ya mwaka 1964,
na kosa la tatu ni kupatikana na
marisau (risasi za shotgun) 112
kinyume cha kifungu cha 34 (1)(2)
sheria ya risasi na silaha namba 2
ya mwaka 1991.
Raya alipinga ombi la dhamana
la mshitakiwa Mansour kutokana
na tuhuma ya kumiliki risasi
nyi ngi ki nyume cha sheri a
ya Zanzibar kwamba, halina
dhamana.
Hata hivyo, katika hatua hii
ya pili, ilielezwa mahakamani
hapo kuwa Mansour anapatiwa
dhamana kutokana na maelekezo
kutoka Mahakama Kuu.
Hakimu Khamis Ramadhani
alitoa dhamana hiyo baada ya
kutakiwa kusimamia maamuzi ya
kupatiwa dhamana yaliyotolewa
na Mahakama Kuu chini ya Jaji
Abraham Mwampashe.
Hatua hiyo ilifuatia kusikilizwa
k wa o mb i l a d h a ma n a
lililowasilishwa Mahakamani
hapo na mawakili wanaomtetea
Mansour.
Jaji Abraham Mwampashe,
akitoa dhamana hiyo, alisema
kuwa Mahakama imeangalia
hoja za kisheria zilizotolewa na
pande zote mbili na kisha kufkia
uamuzi wa kutoa dhamana.
Alisema, kutokana na kifungu
cha sheria cha (150) kifungu
kidogo cha nne(4) sheria No
(7 ) ya mwaka (2004) sheria ya
Zanzibar, kinaipa Mahakama
Na Mwandishi Wetu
Bwana Mansour Himid.
Kuu uwezo wa kutoa dhamana
kwa mtuhumiwa ikiwa itaridhika
na hoja zilizowasilishwa.
Hakuna kosa lolote lisilokuwa
na dhamana, kifungu kidogo
cha nne (4) kiko wazi kimeeleza
Mahakama Kuu ina uwezo wa
kutengua makosa yote yaliokuwa
hayana dhamana ikiwa itajiridhisha
kama yalivyoorodheshwa katika
kifungu kidogo cha kwanza.
Alisema Mwampashe.
Kwa kuzingatia matakwa hayo
ya kisheria alisema kuwa alitizama
faida na hasara za mtuhumiwa
kuwepo rumande na kuwa nje,
akaona kuwa bora awe nje.
Na hiyo ni kwa kuzingatia
gaharama kwa upande wa serikali
halikadhalika hasara na usumbufu
kwa mshitakiwa.
Aki fafanua zai di al i sema
kuwa mtuhumiwa hana historia
ya uhalifu, na kwamba ana
majukumu ya kuendesha biashara
zake ambazo kuna faida ya ajira
kwa vijana walioajiriwa hapo
katika vitega uchumi vyake.
Akaongeza kuwa Mahakama
haiwezi kumyima mtu dhamana
bila ya kuambiwa sababu ya
msingi kwamba kuwepo kwake nje
kunawezaje kuathiri mwenendo
mzima wa kesi yake.
Wakati huo huo Jaji Mwampashe
amesema kuwa kumnyi ma
mtu dhamana itakuwa dhulma
hasa itakapotokea kuwa baadae
anashinda kesi au kesi kufutwa.
Al i ye kuwa r uma nde
atakuwa amedhulumiwa
na waliokuwa wakimtegemea
watakuwa pia wamedhulumiwa
na kut i wa kat i ka has ar a
ikiwemo kukosa huduma
muhimu kutoka kwa ndugu
wanayemtegemea.
Ni kutokana na maelezo haya ya
Jaji Mwampashe watu mbalimbali
wamet oa maoni yao kuwa
Mahakama Kuu ikifanya kazi zake
vyema na kwa kuzingatia maslahi
ya nchi na watu wake, huenda
mlango huu uliofunguliwa katika
kesi hii ya Mansour, ukawasaidia
wengi.
Kwamba si wote wanaojua
kama kuna uzingatiaji hata wa
kibinadamu tu, jambo ambalo
kama likifanyika huenda hata
kesi kama zile za Masheikh wa
Uamsho zisingechukua muda
mrefu kwa watuhumiwa wake
kukaa ndani kwa zaidi ya miaka
miwili, ambapo baadhi ya kesi zao
zimefutwa.
Awali Jeshi la Polisi lilimkamata
na kumshikilia Mansour kwa
tuhuma za kukutwa na silaha.
Silaha hizo zilitajwa kuwa ni
bunduki moja aina shotgun yenye
risasi 112 pamoja na bastola aina
ya bereta aliokuwa na risasi 295.
Polisi ilidai kuwa licha ya
silaha hizo kumilikiwa kihalali
na Mansour, lakini kisheria
hazikutakiwa ziwe na risasi nyingi
kiasi hicho kama zilivyokutwa
nyumbani kwa Mansour.
Ilielezwa kuwa kwa mujibu wa
sheria ya Zanzibar, silaha aina ya
bastola ilitakiwa isizidi risasi 25 na
bunduki aina ya shotgun isizidi
risasi 20.
MAHAFALI ya wanafunzi wa
Kiislamu wa shule za msingi
jijini Dar es Salaam, yamefanyika
katika shule Kinondoni Muslim
Secondary School mwishoni
mwa wiki iliyopita.
Mahafali hayo yalifanyika chini
ya usimamizi wa Jumuiya ya
Walimu wa Somo la Maarifa ya
Uislam Mashuleni ambapo mgeni
rasmi alikuwa ni Mbunge wa
Temeke Bw. Abbas Mtemvu.
Akisoma risala ya walimu
katika mahafali hayo mbele ya
mgeni rasmi, Mwenyekiti wa
Jumuiya hiyo, Saidi Makongoro,
alisema Jumuiya yao inayojulikana
kama Muslim Education Teachers
Association (MUETA) ilianzishwa
mwaka 2006.
Katika nasaha zake Bw. Abasi
Zuberi Mt emvu, al i wat aka
wanafunzi hao kusonga mbele
katika safari ya kujielimisha kwani
elimu haina mwisho.
Mimi mwenyewe hapa nasoma
shahada yangu huko Marekani,
una t a ki wa uwe ke dhi ma
mwenyewe kwamba, Mwenyezi
Mtemvu awataka wahitimu kusonga mbele safari ya elimu
Na Abdulkarim Msengakamba
Mungu anijalie nifkie elimu ya
juu na Mungu atawajalia mtafka
hadi vyuo vikuu. Mbunge huyo
aliwatia moyo wahitimu.
Aidha aliwahimiza wazazi
kuwapenda watoto wao, kwa
kuhakikisha wanasoma kwa bidii
na wawafuatilie kuhakikisha
wanapata elimu iliyo bora na sio
bora elimu.
Na kwamba katika kutafuta
el i mu, pasi we na kubagua,
zisomwe elimu nzote, hakuna ya
dunia na Akhera.
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Walimu wa somo la Maarifa ya
Uislamu mashuleni, Saidi Makongoro, akimkabidhi risala mgeni
rasmi Mbunge wa Temeke, Mh. Abbas Mtemvu.
7
AN-NUUR
SHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 22-28, 2014 Makala
ALIYEKUWA Rais wa tatu wa
Marekani, Thomas Jefferson,
aliwahi kusema: He who knows
nothing is closer to the truth than he
whose mind is flled with falsehoods
and errors.
Ufupi wa maneno msemo huu
una maana kuwa bora mtu ubaki
hulijui jambo kwa sababu utafanya
j uhudi kul i j ua, au hata kama
hukufanya juhudi, lakini ikitokea
ukafahamishwa, utajua ukweli.
Lakini kama ulikuwa umejazwa
taarifa za uwongo na potofu, halafu
ukafanya ndiyo elimu yako juu ya
jambo hilo, itakuwa vigumu sana
kutoa uwongo huo na kujaza mahali
pake taarifa sahihi.
Yupo msomaji mmoja katuma
ujumbe ambao pengine ingekuwa
vyema kuwashirikisha wasomaji
wengi ne kat i ka kuut af akar i .
Anasema:
An nuur taarifa zenu zinasikitisha.
Mnashangaa ISIS kuuwa watu
kwa kukata vichwa makafri. Kuna
hadithi Mtume Muhammad (s.a.w)
alichinja Wayahudi mia saba mpaka
akachimba mitaro ya damu kama
mvua. Sasa naye Mtume wetu
Muhammad s.a.w unataka useme
alikuwa hana huruma? (0713 033
978)
Huyu labda aseme ni Adolf Alois
Hitler. Sio Mtume (s.a.w). Ifikirie
Madina ya wakati ule na idadi ya
Wayahudi waliokuwepo, halafu
linganisha na madai haya ya mito ya
damu kama mvua!
Inawezekana anachozungumzia
hapa ni tukio la Banu Qurayzah.
Lakini hata kama ni kisa hicho cha
Banu Qurayzah, bado huu utakuwa ni
uwongo na upotoshaji mkubwa kwa
sababu Mtume (s.a.w) na Maswahaba
zake hawakuwahi kuuwa Myahudi si
kutoka Banu Qurayzah, Banu Nadhr,
wala Banu Qaynuqa, kwa sababu ya
Uyahudi (ukafri) wao.
Mambo manne ya kuzingatia
hapa. Moja ni kuwa hata kama
unazungumzia Banu Qurayzah,
lakini bila kueleza muktadha wake
(context), ambao ni vita ya Ahzab, na
walichofanya makabila mbalimbali ya
Kiyahud, kabla na mara baada ya vita
hiyo, unajenga picha kuwa Waislamu
waliwakamata na kuwauwa kwa
sababu ya Uyahudi au ukafri wao
kama wanavyofanya ISIS.
Laki ni pi l i ni kuwa kama
ilivyo katika suala la holocost ya
Wayahudi, zipo simulizi nyingi za
tukio la Banu Quraizah zimeandikwa
kwa kunukuliwa kutoka katika
simulizi za Kiyahudi lengo likiwa
kujenga huruma kwa Wayahudi na
wakati huo huo kuupaka matope
Uislamu.
Tatu, tuzingatie kuwa katika
zama hizi za kuwatumia Waislamu
kupigana kwa niaba ya mabeberu,
l i naweza kupenyezwa j ambo.
Inasemwa tu kuna hadithi inasema.
Na kwa bahati mbaya watu wetu sio
wasomaji. Elimu yao kwenye CD.
Anaibuka mtu na CD/DVD, hiyo
ndiyo elimu yake ndiyo fatwa yake.
Kisa kama hicho cha Banu Quraizah,
kinaweza kunyumbulishwa kikatiwa
nakishi nje ya muktadha wake,
ki karembwa na kut umi wa na
mawakala waliopewa tenda na
makafri ya kutengeneza fanatiki
wa Kiislamu wa kuwatumia katika
Kasema kweli Clinton:
Tunao Fanatics wachafuzi wa dini
Elimu yao CDs za wakala wa proxy war
BI Hilary Clinton.
Na Omar Msangi proxy war yao na vita dhidi ya ugaidi
(crusade).
Nne, kwa vile watu sio wasomaji,
hata hawana habari kuwa kuna
taarifa nyingi za uwongo zikiwemo
zi nazoi t wa hadi t hi ambazo
zimeingizwa katika vitabu vya
Kiislamu. Sasa ni mpaka usome uwe
na mafum ya ujumla ya Uislamu na
misingi ya kufahamu hadithi sahihi
na bandia, ndio unaweza kutambua
hadithi potofu.
Lakini nadhani pia kuwa ipo
haja kwa Masheikh wetu kuboresha
hata mitaala yao. Watoe elimu
ya kuwasaidia watu kujitambua
na kutambua itikadi na dhana
mbalimbali zilizopenyezwa katika
dini. Wakati nasoma Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam palikuwa na
somo la DS. Hapo utasomeshwa
siasa za kikomunisiti na kibeberu
na uchambuzi wake juu ya faida na
madhara ya kila moja wapo. Kwa
vile nchi yetu ilikuwa ya kijamaa,
ukomunisti ndio ulikuwa ukipewa
maelezo mazuri zaidi.
Sasa katika hali hii ya mchafukoge,
confusion na ujinga ndani yake,
nadhani kuna haya kwa Masheikh
wetu kusomesha itikadi na siasa za
makundi mbalimbali wakiwemo
wanaoitwa Salaf-Takfri.
Quran inasema: Mwenyezi
Mungu hakukukatazeni kuwafanyia
ihsani na uadilifu wale ambao
hawakupigana nanyi kwa ajili ya
dini wala hawakukufukuzeni katika
nchi zenu. Hakika Mwenyezi Mungu
anawapenda wafanyao uadilifu.
(60:8)
Lakini hata katika uwanja wa
vita kwa wale ambao imelazimu
Waislamu kupigana nao, bado
Mtume s.a.w anaweka kanuni za
vita ikiwa ni pamoja na kutozifanyia
ufedhuli maiti au kuuwa wanawake
na watoto na yeyote ambaye hajashika
silaha na kuingia katika uwanja wa
vita. Na pia ifahamike hapa kuwa
hutawajumuisha makafri wote katika
kapu moja. Kwa hiyo hakuna hoja
kuwa Mayahudi/makafri, huko Gaza
au Somalia, wanauwa Waislamu, kwa
hiyo na wewe unatafuta kafiri wa
Tanzania, unamuuwa!
Sasa Mwenyezi Mungu hawezi
kuagiza haya katika Quran tukufu,
halafu Mtume wake awe anachinja
watu ovyo kwa vile tu ni Mayahudi-
kama ISIS wanavyowachinja Yazid
na Waislamu (Shia na Suni wasio
wakubali) wanaowakuta katika miji
wanayoteka.
Kipo kile kisa mashuhuri kati
ya Muislamu na Yahud ambapo
Mui sl amu mmoj a na Yahudi
walidhulumiana. Kesi ikafika kwa
Mtume s.a.w. Baada ya Mtume
kusikiliza pande zote mbili, akaona
haki ipo kwa Yahudi. Akampa haki
Yahud. Kama ushahidi wa kafiri
haukubaliki, hapana shaka Mtume
(s.a.w) asingemsikiliza Yahud na
kumpa haki yake, kama huyu
msomaji anavyosema katika meseji
nyingine kuwa:
Katika Uislamu kafri hafai kuwa
shahidi kutoa tu ushahidi haruhusiwi
wewe unatoa taarifa kutoka kwa
makafri mtu anaitwa Michael sijui
nani huko sisi Waislamu ushahidi
wetu unatoka kwenye Quran na
Sunnah. (O713 033 978)
Hydrogen cyanide (HCN), wakati
mwingine ikiitwa prussic acid, ni
katika sumu kali zinazojulikana
duniani. HCN ikiwa hewani katika
kiwango cha (concentration) 300 mg/
m3 inamuuwa binadamu ndani ya
dakika 10. Ikifkia concentration ya
3500 ppm (3200 mg/m3), inamuuwa
mtu ndani ya dakika moj a tu.
Hii ni kwa sababu cyanide ion
hukwamisha upumuaji ndani ya cell
(cellular respiration) kwa kitendo
chake cha kuzuiya ufanyaji kazi wa
kimengenya (enzyme) cytochrome c
oxidase ndani ya mitochondria.
Historia ya kuvumbuliwa sumu hii
na matumizi yake katika uchimbaji
wa madini ya dhahabu na silver
ikiwa kama sodium cyanide na
pot assi um cyani de, i nawat aj a
wanasayansi Pierre Macquer (1752),
Carl Wilhelm Scheele (1782), Claude
Louis Berthollet (1787), Joseph Louis
Gay-Lussac (1811) na Gay-Lussac
(18150).
Sasa ukiona chupa imeandikwa
cynide na tahadhari kuwa ni sumu
kali, wewe tizama katika Quran
na Sunnah, kama haijaandikwa na
kwa vile maelezo hayo yametolewa
na akina Joseph Louis, we usijali,
kunywa au jipake, maana ushahidi
na maelezo ya kafri hayakubaliki!!!
Wi ki i l i yopi t a kuna t aari f a
zilinikera sana kwa jinsi zilivyokuwa
zinawatukana Waafrika, lakini pia
zikawa zinapewa nafasi kubwa
na kukaririwa sana, kutwa kucha
katika Aljazeera. Nadhani na katika
CNN, BBC na wengine. Habari
zenyewe ilikuwa juu ya kuingia
kwa ugonjwa wa ebola Nigeria.
Wataalamu na mamlaka husika
wakatoa taarifa za tahadhari kuwa
watu wasile nyama za porini, na
hasa nyani kwani inaaminika kuwa
kirusi kinachosambaza ugonjwa huo
kinatokana na wanyama wa porini.
Katika taarifa hiyo, mpasha habari wa
Aljazeera, anaonekana akitembelea
vilabu vya pombe za kienyeji na
mama lishe wanaouza supu na
mishikaki ya nyama pori na kuhoji
watu juu ya ushauri huo wa kitaalamu
kuwa wajiepushe kula nyama pori
katika kipindi hiki cha mlipuko wa
ebola. Watu hao katika mama ntilie
wakiwa na minofu yao ya wanyama
pori wakiwemo nyani, tumbili na
swala, wakaja juu. Wanasema kuwa
wao hawatasikiliza ushauri huo kwa
sababu nyama pori imekuwa ikiliwa
katika eneo lao toka zama za mababu
zao. Hawawezi kuacha urithi wa
wakale wao. Mtu mmoja anaonekana
akitoa hoja hiyo huku kashikilia
fuvu la nyani lililokwishachomwa
ananyofoa minofu akila.
Hapana shaka kurejewa sana
kwa taarifa ile ni kama kusema,
watizameni hawa na ujinga wao,
watizameni Waafrika walivyo
wajinga.
Hoja kama hii ya wa-Nigeria wala
nyani, ni sawa na ile ya huyu ndugu
yangu wa Chuo Kikuu Dar es Salaam
na mhandisi mtarajiwa. Ile kwamba
babu zao walikuwa wakila nyani
haitazuiya kupata maambukizi ya
ebola iwapo watakutana na tumbili
mwenye virusi vya ugonjwa huo.
Jaaliya kuwa utafiti huo juu ya
ebola na namna unavyoambukizwa
umefanywa na John. Hoja kuwa
utaalamu huo umetokana na utafti
wa John (kafri) na hoja kuwa maelezo
ya John hayapo katika Quran
na Sunnah, haitakuzuiya wewe
ukimkumbatia na kushika damu
au majimaji kutoka mwili wa mtu
mwenye ebola kuambukizwa.
Morogoro ni katika mikoa ambayo
tatizo la homa ya matumbo (typhod)
ni kubwa sana. Katika baadhi ya hoteli
ukiingia wameweka tangazo kuwa
hata kupiga mswaki na kusukutua
utumie maji yaliyochemshwa au
wanakuwekea maji ya chupa bafuni
kwa ajili ya kupigia mswaki.
Inawezekana aliyefanya utafti wa
taifodi na jinsi inavyoambukizwa
ni Alexander na maelezo anayotoa
yasiwemo kabisa kwenye Quran na
Hadithi, maana Qurna ni Kitabu cha
Mwongozo, sio kitabu cha sayansi
au taal uma nyi ngi ne muhi mu
katika maisha. Mengine katika
maisha unasoma na kufanya utafti
mwenyewe au unauliza wajuzi ikiwa
hujui. Sasa wewe kachote maji mtoni
Morogoro unywe bila ya kuchemsha,
maana tahadhari inayotolewa na
kafri juu ya taifodi na kipindupindu
haikubaliki katika Uislamu!!!
We Funded The Wahhabis We
Are Fighting Today- Hilary Clinton
Confesses .
Hiyo ni taarifa ambayo ilisambaa
sana wiki iliyopita ambapo sehemu
ya mazungumzo ya Hilary Clinton,
Wazi ri wa Mambo ya Nj e wa
Marekani wakati wa awamu ya
kwanza ya urais wa Barack Obama
iliwekwa katika mtandao. Ukifungua:
We Funded The Wahhabis We Are
Fighting Today, bado utaikuta
ambapo Clinton anasema kuwa wao
ndio walio waandaa Mujahidina
wakapigane na Mrusi kwa niaba yao
kwa sababu walijua hiyo itakuwa
vita ya muda mrefu na ya gharama
kubwa kwa maana ya kuuliwa askari
wengi. Wakaone Waislamu wakafe
kwa niaba ya askari wa Marekani na
kwa malengo ya Marekani. Lakini
ili ionekane ni agenda ya Waislamu,
waakamua misaada na mafunzo
yapitie Pakistan na Saudi Arabia.
Muislamu akiona ni makachero na
Masheikh wa Pakistan na Saudia,
wanao wakusanya na kuwapiga
dawah juu ya Jihad Afghanistan,
wataamini kuwa hiyo ni Jihad ya
kweli. Na ndio hivyo hivyo Saudia
na Qatar zinavyotumika katika suala
la ISIS hivi leo.
Akihojiwa hivi karibuni na Fox
News Hilary Clinton, anasema:
We have brilliant idea. We created
these mujahideen. We said, lets go
to Pakistan create these mujahideen,
equip them, we send them missiles and
everything. And we were successful. The
Soviet left Afghanistan. We said, great,
good bye, leaving these trained people
who are fanatical in Afghanistan and
PakistanSo the people we are fghting
today (ISIS), we created them.
Sasa leo wewe ukisema kuwa
huyaamini haya anayosema Clinton
kwa sababu hayapo katika Quran
na Sunnah na Clinton mwenyewe ni
kafri, haitaondoa ukweli huo.
Sana sana utakuwa tu unathibitisha
yale aliyosema Bi Clinton kuwa
miongoni mwetu Waislamu wapo
fanatics (mashabiki, walokole
wachemkaji wasiotumia akili) na
ndio hao wanaotumiwa katika proxy
war.
8
AN-NUUR
SHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 22-28, 2014
Makala
Na Omar Msangi
Inaendelea Uk. 9
KATIKA miaka ya 1980s wakati
nipo Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam, niliwahi kuhudhuria
semina Kuala Lumpur, Malaysia,
iliyokuwa imeandaliwa na The
International Islamic Federation
of St udent Organi zat i ons
(IIFSO), kwa pamoja na The
International Institute of Islamic
Thought (IIIT) wakishirikiana na
Vijana wa Harakati za Kiislamu,
waki j ul i kana kwa j i na l a
Angkatan Belia Islam Malaysia
(ABIM) au Malaysian Islamic
Youth Movement.
Pale Bombay (sasa Mumbai), mji
mkuu wa Jimbo la Maharashtra,
nilikaa zaidi ya masaa 24 kusubiri
kuunganisha ndege, kwa hiyo
ikabidi nipelekwe hotelini. Baada
ya kupata chakula katika hoteli
niliyoshukia, nilitoka kutembea
kuangalia mji. Sikufika mbali.
Ilibidi nirudi. Sikuweza kuhimili
kero ya kuzongwa na ombaomba,
akina mama, watoto, wazee
mpaka watu wazima wanaume
na wazee. Waliowahi kufka India,
watanielewa.
Kwa wakati ule mimi haikunijia
akilini kuwa nchi za ughaibuni,
nje ya Afrika, nazo zaweza kuwa
na kundi la masikini wa kutupwa
na ombaomba wa kiwango kile.
Wakati huo nilikuwa sij aj ua
kuwa katika India kuna watu
wanawekwa kati ka kapu l a
untouchable Dalits.
Pamoja na mambo mengine,
katika semina ile, palijadiliwa
mat at i zo yanayowakabi l i
Waislamu katika elimu na ikatajwa
kuwa tatizo kubwa ni, mtizamo
potofu katika elimu na dunia.
Kwamba mtizamo kuwa kuna
elimu ya dunia na elimu ya akhera,
au elimu ya kikafri na elimu ya
dini (ya Kiislamu), limekuwa ni
tatizo kubwa na lau Waislamu
hawatafanya j uhudi kubwa
kulitatua, litawaangamiza. Ni
katika zama hizo ambapo, tatizo la
mgawanyo katika elimu (Crisis of
Duality in Education Systems and
Disciplines of Knowledge), kwa
maana hii ya kuwa na elimu ya
madrasa na elimu ya shule kama
vitu viwili tofauti, lilizungumzwa
sana. Ukiacha kuwa mtizamo
huo, unazaa makundi mawili
ya Waislamu wanaokinzana,
lakini pia huzalisha wasomi
Waislamu waliochanganyikiwa
na hivyo wanakuwa hawana
msaada wowote wa maaana
katika jamii ya Wauslamu wala
nchi kwa ujumla. Makundi mawili
yanayokizana ni lile linaloitakidi
kuwa elimu ya manufaa ni ya
madrasa (dini) pekee, na kundi
la pili, ni lile linalokwenda shule
na kuona kuwa hawa wanaobaki
katika madrasa na vyuo vya
Kiislamu, wakisoma dini, hawana
kitu.
Ilikuwa ni katika kutatua tatizo
hilo, wasomi wa Kiislamu walikuja
na kitu kilichoitwa Islamization
of Knowl edge. Hata hi vyo,
msamiati huu nao ulionekana
kuwa una matatizo. Unaposema
Msiba! MSAUD imefa wapi?
Hakuna historia, Civics ya kikafri
Vidato bila kuelimika ni balaa tupu
Islamization of knowledge,
unachosema bila kutamka ni
kuwa elimu ni ya kikafiri sasa
unataka kuisilimisha. Lakini
hakuna elimu ya kikafri, bali kuna
mawazo ya kikafri na mtizamo
wa kikafiri. Unapozungumzia
civics au sosholojia kwa mfano,
hii ni taaluma ya namna jamii
zinavyoishi na kuhusiana katika
mambo mbalimbali ya kijamii,
kisiasa, kisheria, kiuchumi,
uongozi na mambo kama hayo.
Sasa hayo ni mambo ambayo
yapo katika jamii yoyote, iwe
ya Ki i sl amu au ya ki kafi ri .
Kitakachotofautisha ni itikadi
na mtizamo. Kama ni Kiislamu,
civics (elimu ya uraia) itayatizama
mahusiano hayo kwa misingi ya
Kiislamu. Kama ni ya kishirikina
hivyo hivyo. Kwa hiyo, civics
ya Wahindu, itaitizama jamii
ya India katika mtizamo wake
wa kuwa na ubaguzi- The caste
system ambapo utawakuta
varnas, Brahmins, Kshatriyas,
Vaishyas na Shudras. Wapo pia
wale untouchable Dalits.
Muislamu wa India hawezi
kusema kuwa kusoma historia
iliyozaa untouchable Dalits
au ci vi cs na s os hol i oj i a
ya I ndi a i navyoel eza j i nsi
makundi ya varnas, Brahmins,
Kshatriyas, Vaishyas na Shudras,
yanavyowiana katika jamii ni
ukafiri. Ukafiri ni mfumo huo
wa kibaguzi na itikadi iliyouzaa.
Na kama hukusoma ukajua hayo
matatizo yaliyo katika jamii,
na chanzo chake, utaisaidiaje
jamii kuepukana na mfumo huo
mbaya? Suala ni kuondoa itikadi
iliyojenga ushirikina, sio kuacha
kusoma kwa hoja kuwa historia
ya India ni ukafri.
I n a w e z e k a n a c i v i c s
inayofundishwa katika shule za
Tanzania ikasema kuwa hakuna
kuoa mke zaidi ya mmoja. Kuzini
sio haramu ilimuradi usipate
ukimwi au kumtia mimba mtoto
wa shule. Civics hiyo hiyo inaweza
kukuambi a kuwa mtoto wa
zinaa ana haki ya kurithi, jambo
ambalo ni kinyume na Uislamu.
Civics hii inatofautiana vipi na
ile tunayosoma katika darsa zetu
Misikitini na katika vyuo vya
Kiislamu kuwa Maquraishi wa
Makkah walikuwa wakiwazika
watoto wao wa kike wakiwa
hai, mpaka Quran inasema:
Waidhaal mauudatu suilat. Bi
ayyidh dhanbin qutilat! Au civics
hii inayofundisha kuwa Waarabu
wa Makka waliwazika watoto
wao wa kike wakiwa hai ni ya
Kiislamu? Au ni ukafri nayo pia
haifai kufundishwa itolewe ndani
ya Quran na vitabu vya Kiislamu?
Ni hivyo hivyo tunasoma
katika Maarifa ya Uislamu, jinsi
ukafri na ushirikina ulivyokuwa
umetawala Makkah na Madina
watu wakiitakidi kuwa kuna
miungu wengi-Mungu wa jua,
mungu wa mvua, mpaka tende
zilitengenezwa miungu watu
wakishikwa na njaa wananyofoa
mkono wa Mungu wanakula.
Katika Quran, Allah anatueleza
kuwa Makuraishi walidai kuwa
malaika ni watoto wakike wa
Mungu. Kisha tunaelezwa kisa
cha Qaumu Lut na ubaradhuli
wao mpaka wakagharikishwa.
Swali ni je, kusoma historia hii
iliyoelezwa katika Uislamu na
ndani ya Quran (kwa maana ya
elimu), ni ukafri? Au historia hii
ni Uislamu?
Sasa kama leo kuna watu
wanasema kuwa bi nadamu
katokana na nyani, hawana tofauti
na wale waliochonga masanamu
wakayaabudu na historia yao
ikaelezwa katika Quran. Hili ni
somo. Hii ni rekodi na historia ya
maisha ya watu na mambo yao.
Suala hapa ni kuwajua na kutafuta
namna ya kuuokoa ulimwengu na
dhana potofu juu ya kuumbwa
kwa ulimwengu na vilivyomo.
Kama nilivyosema, katika
Quran tunaelezwa visa vya akina
Ad, Thamud, watu wa Nuhu,
Qaumu Lut, n.k. Hiyo ni historia.
Halikadhalika leo tunajifunza juu
ya kuja wakoloni Afrika, Wareno,
Wajerumani, Waingereza, na
jinsi wazee wetu akina Suleiman
Mamba, Bushi ri , Mkwawa,
Mirambo n.k, walivyopambana
nao. Hiyo ni historia, sio ukafri.
Lakini ambalo ni la ukweli ni
kuwa historia inategemea nani
anaandika. Kama kwa mfano
Watanganyika hatutaandika
hi st ori a yet u, t ukat egemea
historia iliyoandikwa na Wazungu
waliotutawala, wao hawataandika
kuwa walikuja kututawala na
kupora mali, watasema walikuja
kutuletea ustaarabu. Sasa tatizo
hapa sio Mzungu wala historia
kuwa ni ukafri. Tatizo ni wewe
ul i yekuwa mvi vu na l abda
mjinga usiyejitambua kiasi cha
kushindwa kuandika historia
yako mwenyewe ukangoja watu
wengine ndio wakuandikie.
9
AN-NUUR
SHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 22-28, 2014
Makala
Inatoka Uk. 8
Msiba! MSAUD imefa wapi?
Mohamed Said (Historian),
amezungumzi a sana j ambo
hili akionyesha jinsi historia ya
Tanganyika ilivyopotoshwa.
Kwamba ul e mchango wa
wazee wa Ki i sl amu kat i ka
kupigania uhuru wa nchi hii,
umetupwa kabisa wala wazee
hao kama Sheikh Ramia, Dossa
Aziz, Mshume Kiate, Suleiman
Takadiri na wengineo, hawatajwi
kabisa. Historia ya kupigania
uhuru Tanganyika imefanywa
ni simulizi za kumsifu Nyerere.
Hata wale wazee waliompokea
Nyerere Dar es Salaam wakamvua
kaptura aliyokuja nayo kutoka
Musoma wakamshonea suruali ili
awe muungwana kama Waislamu
wa Pwani , hakuna mahal i
popote wanapotajwa. Sasa hapa
Waislamu hawawezi kulaumu
historia, wakasema historia hii
ni ya kikafiri. Wajilaumu kwa
nini mpaka sasa hawajaandika
historia sahihi ya nchi hii na
kuwafundi sha watoto wao.
Kwa nini wameruhusu historia
ikapotoshwa na wanachukua
hatua gani. Kudai kuwa historia
ni ukafri, ni kutangaza ujinga wa
kutokujua hata maana ya historia.
Hakuna fzikia wala
uhandisi wa kikafri
J amaa yangu Sai d Omar
Nsigarila aliniambia siku moja
kuwa wakati wapo Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam, mwalimu wao
wa fzikia baada ya kusomesha
mada juu ya maumbile ya maji
na kanuni zake ikiwemo ile
kwamba maji yakiganda huwa
mepesi na hivyo huelea juu jambo
linalosababisha kuwa katika nchi
za baridi wakati wa kipupwe
(winter) theluji huelea juu ya
bahari na yasiyo ganda hubaki
chini jambo linalowezesha samaki
na viumbe wengine baharini
kuendelea kupata uhai. Mhadhri
huyo alipomaliza kusomesha
akawa anasema kuwa akina
Nsigarila wao hawana tabu katika
hili, akimaanisha kuwa Nsigarila
(na Waislamu wanaoamini juu
ya kuwepo kwa Mungu), wao
wataona na kusema kuwa hayo
ni kwa ajili ya uwezo wa Mungu
Muumba. Na ndio pale Quran
inaposema kuwa hakika katika
kuumbwa kwa mbingu na ardhi,
zipo alama za kuonyesha kuwepo
kwa Mungu Muumba na uwezo
wake.
Sasa iwapo Waislamu wataacha
fzikia, kemia na elimu zingine
zifundishwe kwa mtizamo wa
kikafiri, badala ya kusema huo
ni uwezo wa Allah mhadhiri
akasema, nature is so kind,
kama yul e muhadhi r i wa
Nsigarila, tatizo hapa sio la fzikia.
Fizikia itabaki kuwa fzikia wala
hakutakuwa na fzikia ya Kiislamu
au ya Kikristo.
Ka ma we we una s o me a
uhandisi, kanuni za uhandisi
katika ujenzi iwe ni wa majengo,
madaraja, au barabara, zitabaki
zilezile duniani kote, iwe ni
katika nchi ya Kiislamu au ya
kikafri. Ila msomeshaji anaweza
kutia maneno yake ya kikafiri
na kishirikina lakini sio kubadili
kanuni za kiuhandishi za ujenzi.
Unajua kwa nini? Kwa sababu
katika uhandisi unacheza na
udongo (soil analysis), vyuma,
kokoto (mawe), saruji, miti na
vyote hivyo vimeumbwa na Allah
na vikawekewa kanuni fulani
ambazo kwa elimu ya fizikia,
kemia na hesabu, binadamu
anavitia katika matumizi. Kanuni
hizi, hazitegemei mtumiaji kuwa
ni kafri au Muislamu. Zitafanya
kazi Makkah kama ambavyo
zitafanya Vatican. Na wewe
ukizikosea hata kama ulikuwa
unazitumia kujenga (kukarabati)
Msikiti wa Makkah au wa Mtume
Madinah, utaporomoka.
Ukafi ri hauwezi kubadi l i
fomula ya photosythesis au
kubadili vitu vilivyoko ndani
ya cell-mitochondria, ribosome,
cytoplasm, centriole, lysosome,
nucleus, nucleolus, .nk. Hivi ni
vitu kaviumba Allah, na elimu
ni kuvisoma na kujua namna
ya kuvi ti a kati ka matumi zi
ya binadamu. Allah anasema,
akitaka jambo kuwa ni kusema
kun fayakun. Lakini kajaaliya
kupatikana kwa chakula chetu na
kuzalishwa kwa oxygen, carbon
dioxide na mzunguko wake, upitie
mfumo fulani ambao tunausoma
shuleni. Kama photosynthesis
imeumbwa na Allah kuisoma sio
ukafiri. Kama law of floatation
inategemea Allah alivyoumba vitu
akavipa density tofauti tofauti na
akaweka kanuni za mahusiano
baina yao katika hali tofauti
tofauti (mpaka tunaweza kuunda
meli na ndege), kusoma hayo, si
ukafri. Ila msomeshaji anaweza
kusomesha kwa mtizamo wake
wa kikafri au wa Kiislamu.
Il i kutatua tati zo l a nani
anasomesha na anasomesha katika
mtizamo gani, ndio IIIT, wakaja na
dhana ya Islamization of Knowledge,
ambayo kama nilivyosema, baadae
ikaonekana kuwa inapeleka ujumbe
potofu kwa sababu inajenga dhana
kuwa kuna elimu ya kikafri. Msamiati
ukabadilika sasa unaotumika ni
Integration of knowledge. Na
watu wapo kazi ni waki andi ka
vitabu na kutengeneza mitaala.
Semina iliyomalizika katika Chuo
Kikuu cha Waislamu, Morogoro
wiki iliyopita, ilikuwa ni katika
kutizama jambo hili na namna ya
kulifanikisha katika Tanzania na
kanda ya Afrika. Kwengine kama
ilivyotolewa mfano wa Indonesia,
Waislamu wamepiga hatua kubwa
sana ambapo hivi sasa vyuo vikuu
wanasomesha fani mbalimbali,
wakiwa wametengeneza mitaala na
vitabu vya taaluma mbalimbali kwa
kuzingatia epistemolojia ya Kiislamu.
Kwa nini nimesema yote haya
na kwa urefu kiasi hiki? Kama
ambavyo sikujua kuwa kuna dalits,
ombaomba kule India, tunao watu
wenye visomo, lakini wanahitaji
kuelimishwa.
Wakati tunasoma Chuo Kikuu
Dar es Salaam, ilikuwa ummah
wa Kiislamu Tanzania, likitokea
jambo, hukaa wakisikiliza Wanafunzi
wa Kiislamu Chuo Kikuu-Muslim
Students Association of UDMS
(MSAUD) wanasemaje juu ya jambo
hilo. Na ilikuwa watu wakitoka mjini
kuja kuswali Ijumaa katika msikiti
wa Chuo Kikuu ili kusikia wasomi
wanasemaje katika jambo lililotokea,
kwa maana kuwa wat al i t ol ea
ufafanuzi na kutoa mwelekeo sahihi
kwa Waislamu.
Jumamosi ya wi ki i l i yopi ta,
ni l i pokea uj umbe wa maneno
(sms) ambao ningependa wasomaji
wengine nao wapate faida kutokana
na yaliyomo. Unasema:
Unakataa elimu ya circular
(sekula) sio ya kikafiri unatolea
mfano biology, physics, chemistry,
mbona umeacha civics au hujui
kwenye civics kuna masuala ya
kupinga ndoa zaidi ya (mke) mmoja,
kumuozesha binti akiwa mdogo,
yaani early marriage, kuna mambo
chungu mzima ya kupinga Uislamu.
Kuna history, kuna Kiswahili, kuna
geography, hata hiyo physics na
biology na chemistry ina mifumo ya
ukafri hata kuiendea elimu yenyewe
mfumo wake siyo wa Kiislamu. Ni
kweli mimi nakubali ni ukafri na siyo
tu kwa kusikia. Nimesoma kuanzia
form one nikaenda form fve na six
PCM sasa niko civil engineering
mwaka wa tatu Mlimani COET
(Chuo Kikuu cha Dar es Salaam).
Na hata kama nimesoma nikafika
huko, haki lazima izungumzwe
watu wafahamu kwamba elimu ya
circular ni ukafri kuna mambo mengi
yanapinga Kitabu cha Allah lazima
watu waelezwe waelewe. (0713 033
978).
Sina hakika kwamba huyu ni
katika viongozi na wanakamati wa
MSAUD au ni mwanajumuiya tu ya
MSAUD!
Nimetaja uwepo wa taasisi ya
The International Institute of Islamic
Thought (IIIT), ambayo inatizama
namna ya kuondoa tatizo la duality
katika elimu. Na kwa hakika mpaka
sasa wamefanya kazi kubwa sana.
Waswahili wana msemo wao,
mkono husafishwa ukichafuliwa
na mtoto, haukatwi. Waislamu
wameacha makafiri wanachafua
el i mu, waondoe uchaf u, s i o
kuharamisha elimu na kuikimbia.
PICHA juu ni kielelezo cha umasikini wa untouchable Dalits, India.
10
AN-NUUR
SHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 22-28, 2014
Makala
Na Michael Albert
"NYUMA ya kila gaidi wanasimama
dazeni kadhaa za wanaume na
wanawake, ambao bi l a wao
asingeingia katika ugaidi. Wote ni
wapiganaji wa maadui, na damu yao
itakuwa juu ya vichwa vyao. Sasa hao
ni pamoja na mama wa mashahidi,
ambao waliwapeleka jehanam kwa
maua na mabusu. Watawafuata
wana wao, hakuna haki zaidi ya
hiyo. Waende, kama zilivyo nyumba
zao ambazo ziliwalea hao nyoka.
Vinginevyo, vijoka vingine vidogo
vitalelewa humo."
-Ayelet Shaked, mbunge wa Israel
Mi mi ni Mya hudi l a k i ni
utambulisho huo haunielezi nilivyo.
Nilikuwa Bar Mitvah-ed, lakini siku
hiyo ilimaliza uhusiano wangu wa
kidini. Nilibwabwaja aya kadhaa
za kukariri za Kiyahudi ambazo
kwa yaki ni si kuwa nazi el ewa.
Nilisherehekea (ibada) kwa sababu
tu ilinibidi kufanya hivyo. Familia, na
mengine yote.
Zaidi, mara nyingine, mara moja
tu tangu au kuanzia hapo, ambako
nimekuwa, binafsi nimekutana na
chuki dhidi ya Wayahudi, ana kwa
ana. Mzazi wa binti mmoja niliyekuwa
natoka naye aliongea kitu cha kuudhi
kuhusu Wayahudi kushikilia dunia na
karibu ningemzaba vibao. Sina subira
nyingi kwa ubaguzi katika hali yoyote,
lakini nilishangaa kuwa upuuzi
aliokuwa anaongea ulinivuruga
akili kwa kiasi ulichofkia. Haikuwa
suala la uhusiano wa damu, na kwa
hakika halikuwa suala la imani za
dini ambazo zilisababisha nilichohisi.
Hivyo labda kuyasema 'maswali
manne' mara kadhaa kama mtoto
kumekuwa na athari ya kitamaduni.
Hivi mabaki ya utoto wangu ya
ushiriki kwa namna fulani katika
Uyahudi, kwa mfano kumpenda
Rabbi Schankman wa Hekalu Israel
hadi nikafikia umri wa miaka 13,
kunanifanya mimi, sasa, kuhisi kwa
nguvu kuudhiwa na kuchoshwa
na matukio ya sasa ya Gaza tofauti
na kama nisingefka katika Hekalu
mara kadhaa? Sijui, ila sidhani kama
suala hilo linabadilisha chochote.
Kinacholeta maana ni umwagaji
damu wa kut i sha unaot okea
Gaza. Hata hivyo kina matukio
mengi ya umwagaji damu. Hivi
maneno yanaweza kufanya hiki
kinachoendelea kuingia katika orodha
ya wenye mataji ya uovu?
Maiti? Ndiyo. Maiti zimejazana.
Maj engo yaliyovunj wa? Ndiyo.
Mirundiko ya mawe na vumbi imejaa
na inaongezeka.
Nilipokuwa ninafkia ukubwani,
utumiaji nguvu ulikuwa ni Vietnam.
Katikati ya hilo, nilijiuliza jinsi
binadamu ambao wamefurahia
hata uhuru binafsi kidogo tu na
maendeleo, tofauti, kwa mfano, na
kupigwa na kufungiwa wakiwa
watoto, na kukataliwa elimu na
maendeleo ya fahamu zao, wanaweza
kuwa hata chembe wasiojali na
kujidanganya kama serikali ya nchi
yangu ilivyokuwa.
Ila wakati "kuuangamiza mji ili
kuuokoa" kuliweka kiwango cha
juu sana cha udhihirishaji wa uovu
- siwezi kukwepa kuona hitilafu ya
Kuua 'nyoka' na nafsi
kina ya kipengere cha 'kuuokoa.'
Wakati huo, na zaidi tangu harakati
za wakati huo na athari zake, hata
bila kuongeza kingine, kuendeleza
vitendo vya kidhalimu kwa sababu za
ki-dola au za kutafuta faida kulihitaji
madai ya nguvu ya kimaadili. Ila, kwa
wa-Israeli, hilo halielekei kuwa kweli.
Ndiyo, kwa ajili ya utumiaji wa
kimataifa wanatengeneza uhalalishaji
wa kipuuzi - kimsingi wanasema huu
ni ulinzi wetu dhidi ya wao kujilinda
wenyewe, Na, ili kuwa wazi, kwa
wale wanaosema kuwa Israel ina
haki ya kujilindaa, kuna jibu moja tu
sahihi. Ndiyo. Inayo.
Na ki nachomaani shwa hapo
ni kukwepa kushambul i wa na
wanaokaliwa kwa mabavu. Israel
inaweza kuondoka Gaza, kuondoa
ukaliaji, kuondoa ubaguzi. Hiyo
ndiyo njia pekee ya jeshi la ukaliaji
- kokote, wakati wowote - kujilinda
dhidi ya waliokaliwa kikoloni. Acha
kuendeleza uhalifu. Suluhisho ni
kuondoka. Kama huelewi hilo, lifkirie
kwa njia hii. Fikiria Waingereza
waliokuwa Marekani wakipigana
na waliochukua ardhi kule kuifanya
kuwa kol oni l ao wawambi e,
'hamjui, tuna haki ya kujilinda.' Jibu
hapo lingekuwa" ndiyo, mnayo,
na haki yenu ya kufanya hivyo
inahalalisha kuondoka kwenu, ila
siyo kutuelekezea risasi sisi.
Au ingekuwa vipi kwa ma-Nazi
nchini Ufaransa, au labda mfano
bora zaidi ni ma-Nazi nchini Poland
- jijini Warsaw. Fikiria wangesema,
lo! Tuna haki ya kujilinda. Pia jibu
lingehitaji kuwa, ndiyo, mnayo, na
haki hiyo inahalalisha kuondoka
kwenu, na siyo kuangamiza maisha
yetu, utamaduni na majengo.
Ni hivyo pia kwa Marekani katika
maeneo ya kingo za kusini mashariki
ya Asia (Vietnam, Laos na Cambodia).
Na pia kwa Israeli eneo la Gaza.
Jilindeni, kwa hali yoyote, kweli,
na ili kufanya hivyo, tokeni. Ila hiki
sicho ninachotaka kusema katika
kihadithi hiki. Ila nataka kuainisha
kitu kipya kuhusu matukio hayo,
labda yanayohitaji maneno machache.
Ni kuwa wa-Israeli wanaonekana
kuridhika, hasa kwa matumizi ya
ndani, na kwa kiwango fulani hata
kimataifa, kutokubabaisha ni nini
wanachokifanya.
Bisha hodi - kinachoropoka kifaa
cha kurusha kombora darini. Mlio
mkubwa, na hospitali iliyo chini yake
imeteketea. Usiwe na wasiwasi. Ni
'nyoka wafu' waliokuwa wanatibiwa
na nyoka wa f u wa l i okuwa
wanawatibu.
Simu inalia. Badala ya nyumba
kuna lundo la matofali na vumbi.
Usiwe na wasiwasi. Ni vitoto vya
nyoka vilivyokufa na nyoka wafu
mama zao. Ni maskani mengine ya
nyoka yamegeuzwa jivu. Huree!
Ni wazi kuwa huu ni uharamia.
Kama huoni hilo, sijui ni kwa njia
gani naweza kukuwezesha kuelewa
hilo. Lakini suala ni kuwa 'tahadhari'
hizi unaweza kuziona ni wazimu.
Ni mzaha wa kutokujali kuwaambia
watu watoke wakati wanapoweza
kwenda ni mahali ambapo panafuata
katika orodha ya kupigwa. Tahadhari
hizo pia zinaonyesha kwa ushahidi
wa wazi, usioweza kabisa kupingika,
ambao nchi nyingi zinajaribu kufcha,
au kutokuwa na hatia ya hilo katika
mazingira bora zaidi.
Ni kuwa, kubi sha ml angoni
kut angaza ki l e ki nac hokuj a
kunaonyesha kuwa wa-Israel i
hawapigi majumba na mahospitali
na mengineyo katika maisha ya
Gaza na kufaulu kwa kukisia, lakini
kwa dhamira. Kugonga mlango ni
kusema, tunaweza kupiga popote
tunapotaka, hadi kufikia vijumba
vidogo, kokote tunapoteka, hadi
kichembe cha mwisho. Ni kama
wanasema, angalia tulichofanya.
Mnaona vitoto vimelipuliwa na
kuchakazwa? Mnaona hospitali
imegeuzwa jivu? Mnaona kituo cha
umeme kinatoa tu miali ya moto
kukizunguka? Mnaona shule ile,
msikiti ule, bustani, ufukwe, vituo
vya kujaza maji vyote vimegeuka
milundiko ya vumbi na binadamu
waliochakazwa? Hiki mnachoona
ndicho hasa tulichotaka kufanya.
Hakuna uharibifu usiotarajiwa.
Kuna uharibifu uliolengwa. Sisi
wa-Israeli kimsingi tunataka kuua
chochot e ki nachot embea. Na
tunataka kuwaambia wale ambao
bado wanatembea wakati tukiwa
tumekamilisha kazi kuwa tulifanya
hivyo, kwa makusudi. Tunajua jinsi
ya kushawishi hisia!
Nilipokuwa nasoma sekondari
nilikuwa nakaa hadi usiku wa
manane, mara kadhaa, kujaribu
kufkiria jinsi mtu anavyoweza kuwa
Mjerumani mwema. Ni kwa jinsi gani
ambako watu wanaweza kuendelea
na shughuli zao za kila siku wakati
nchi yao ikiwa inaendesha jehanamu
ya kutisha ya ukiukwaji wa haki -
kwa jambo hilo, mitambo ya kuulia
(hasa Wayahudi). Ila nilielewa baada
ya muda. Msukumo wa kutaka
kumudu, wa kutaka kustahili nafasi
fulani na kutokufikiri kuna njia
nyingine, na, kwa watu wengi zaidi,
utulivu unaoletwa na kutokujua
(kunakolindwa kwa kuuliza maswali
machache kama mt u at aul i za
chochote), na, kwa watu wengi
zaidi, woga wa kijinga na hamu ya
kiasi iliyokuzwa kwa makusudi,
ndiyo yaliyofanikisha. Na nikaona
hayo pia katika vita ya Marekani
kusini mashariki ya Asia, na kuhusu
ushindi wa ubaguzi, na sasa pia,
kama tunavyoteketeza mazingira.
Hivyo ninalipata hilo.
Il a kuna makundi ya askari
wanaovamia na kutenda hayo.
Ni 'brownshirts,' wanaovaa kaki
za kahawia. Hii ni ngumu zaidi
kueleza. Nilikuwa nadhani labda
kulikuwa na hitilafu fulani katika
lugha ya Kijerumani - nilokuwa najua
hawana vinasaba tofauti na wengine
walikuwa, hata hivyo, wakiongea
kwa njia tofauti. Halafu nikajifunza
kuwa mafunzo yanayozalisha askari,
na kwa upungufu kidogo zaidi
yale yanayozalisha watu wazima,
kimsingi yanalenga kuondoa uwezo
wa kufkiri kibinadamu na hisia hiyo.
Na kuwa wengi wanaanguka. Hivyo
sasa tunao wa-Israeli. Na uwezo
wa kujidanganya na ukosa mantiki
wa kukataa kilicho wazi, na hata
dhamira ya kudhuru ya kifashisti,
miongoni mwa watu kwa jumla - hata
kama wasingedai kila wakati kuwa
na uelewa wa ndani na maalum wa
uovu wa ubaguzi - ni wa kushangaza.
Inasikitisha kweli. Inachukiza.
Hata nikiwa nalilia uchungu
wa Palestina na kutumainia kuwa
watashinda, sehemu yangu pia
inajiuliza, wakati vumbi likitulia, hivi
wa-Israeli wanaohimiza kufumuliwa
kwa miali ya moto Wapalestina na
Wapalestina watasema nini miongoni
mwao ili waweze kuishi na nafsi zao?
Maiti ambazo zinaonekana kabisa
kama watu zilikuwa kweli ni nyoka?
Au labda nilikuwa, kwa muda mfupi
angalau, zimwi? Na wanawaambia
nini watoto wao? Ili waweze kuishi
na watoto wao. Na ili watoto wao
wasiwe mazimwi - mtu unatazamia.
Na kwa kina zaidi, vipi kwa wa-
Marekani wenye historia inayonuka
ya kuunga mkono uuaj i huu
watajieleza? Na kuwaambia watoto
wao? Na nahofa jibu litakuwa hapana
kabisa. Kwani kopo la jivu la historia
- ambalo ni CNN na New York
Times - yataziba hisia ya ukosaji na
ukweli kwa njia ya majitaka ambayo
wanaripoti.
(Makala hii Killing Snakes and
Self kama ilivyoandikwa na Michael
Albert,
imefasiriwa kwa Kiswahili na
Anil Kija)
11
AN-NUUR
SHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 22-28, 2014
Makala
TUKITUPIA jicho yale yanayofanywa
na makundi haya itafahamika wazi
malengo hasa ya makundi hayo.
Kwa mfano, mambo yanayofanywa
na Boko Haram Nigeria kama mauaji
kuwateka nyara wasichana wa shule
na mengine mfano wa hayo, ni
matukio ambayo humfanya mtu kwa
uchache kutilia shaka kama kweli
kundi hilo linapigania Uislamu na
haki za Waislamu. Sasa limeibuka
kundi Dola la Kiislamu la Iraq na
Sham kwa kifupi DAESH. Imekuwa ni
jambo la kawaida kusoma au kusikia
katika vyombo vya habari juu ya jinai
na mauaji ya kutisha yanayofanywa
na kundi hili. Kwa hakika kundi
hili la kigaidi ambalo licha ya kudai
kuwa linafuata mienendo ya jihadi ya
kisalaf, lakini kwa hakika ni mfuasi
wa fkra potofu za Kiwahabi ambazo
ni fikra mgando na zilizopitwa
na wakati. Kwa maana kwamba,
mitazamo na fkra kama hizi hazina
nafasi kabisa katika ulimwengu wa
Kiislamu.
Kundi la Daesh hutumia ukatili,
utesaji namauaji ya kutisha ambapo
mfano wa jinai hizo ni mauaji ya
umati ya raia wasio na hatia nchini
Syria, mauaji ambayo hutekelezwa
hadharani na kuwajumuisha watoto
wadogo, wanawake na vizee. La
kusikitisha zaidi ni kwamba, kundi
hili la kigaidi linafanya mauaji haya
kwa jina la Uislamu na utawasikia
wakisoma dua ndefu na kumsabihi
Mwenyezi Mungu kabla ya kumchinja
mtu au kumpiga risasi.
Uislamu upi na Mungu yupi
anayeruhusu kuuawa nafsi isiyo
na hatia yoyote? Je hii ni jihadi ya
kutaka kuasisi dola la Kiislamu au ni
ugaidi na jinai dhidi ya binadamu?
Harakati za kundi la Daesh kwa
hakika ni fitna kubwa ya karne.
Msiba mkubwa zaidi ni kuwepo
watu wanaoshabikia mauaji ya kundi
hilo na kuwamiminia sifa lukuki
wapiganaji hao wakiwaita kuwa ni
mujahidina. Historia ya kundi hilo
inarejea nyuma mwaka 2004, yaani
wakati Abu Mus'ab Zarqawi alipoasisi
mtandao uliokuja kujulikana kwa jina
la Jama'at Tawhid wa Jihad huku
akiwa kiongozi wake. Baada ya
Zarqawi kutangaza utiifu wake kwa
Osama bin Laden, mkuu wa zamani
wa mtandao wa al-Qaida, kundi hilo
liligeuzwa na kuwa tawi la taasisi
ya al-Qaida nchini Iraq. Baada ya
Marekani kuivamia Iraq, kundi hilo
taratibu lilijionyesha kuwa lililokuwa
likiendesha jihadi dhidi ya vikosi vya
Marekani nchini humo. Ni kutokana
na hali hiyo ndio maana vijana wengi
waliokuwa wakitaka kupambana na
vikosi hivyo
vamizi, wakajiunga nalo ambapo
haraka likageuka na kuwa kundi
lenye nguvu la wanamgambo nchini
Iraq.
Mwaka 2006 Zarqawi aliuawa na
uongozi wa kundi hilo ukachukuliwa
na Abi Hamzah al-Muhajir ambaye
alikuwa kiongozi wa mtandao wa
al-Qaida nchini humo na mrithi wa
Zarqawi mwenyewe. Mwishoni
mwa mwaka 2006 kuliundwa kundi
la wanamgambo kupitia makundi
kadhaa ya Iraq ambalo lilikuj a
kujulikana kwa jina la 'Daulatul-Islam
fl-Iraq huku kiongozi wake mkuu
Kundi la Daesh; Mujahidina au Magaidi?
Na Salum Bendera
SWAHIBA wangu mmoja siku zote hupenda kusisitiza
kwamba, katika ulimwengu wa leo asiye na elimu au weledi
na ufahamu wa mambo ya dunia yake basi ataishi kwa taabu
na atakuwa mfano wa bendera ambayo hufuata upepo.
Tukiachana na ya sahiba wangu hayo, waswahili wana msemo
wao mashuhuri usemao: Usilolijua ni sawa na usiku wa giza.
Hivi ndivyo hali ilivyo hii leo katika ulimwengu tunaoishi.
Vyombo vya habari vya Magharibi vimehodhi kila kitu; lakini
kwani ukweli unaweza kuufcha siku zote? Ghiliba na hadaa
za Wamagharibi zimefahamika sasa. Kwa hakika njama za
Wamagharibi dhidi ya Uislamu hazikuanza leo wala jana;
lakini bila shaka katika siku za hivi karibuni zimeshadidi mno.
akiwa ni Abu Omar al-Baghdadi.
Mwezi April mwaka 2010 vikosi
vya Marekani vilimuua Abu Omar
al-Baghdadi na Abu Hamzah al-
Muhajir katika operesheni ya kijeshi.
Ni baada ya hapo ndipo Abu Bakar
al-Baghdadi alichukua uongozi wa
kundi hilo akimrithi Abu Omar al-
Baghdadi. Mwanzoni mwa mwaka
2011 sambamba na kuanza kwa
mgogoro na vita nchini Syria, kundi
linalojulikana kwa jina la 'Jab'hatu
Nusra kwa ajili ya Watu wa Sham'
ambalo ni tawi la Dola la Kiislamu
la Iraq liliundwa nchini humo humo
na haraka likageuka kuwa moja ya
makundi yanayoendesha vita dhidi
ya serikali ya Rais Bashar al-Assad.
Hatimaye mwaka 2013 Abubakar al-
Baghdadi alitangaza kuyaunganisha
pamoja makundi ya, Jab'hatu Nusra
na Dola la Kiislamu la Iraq na kuzaliwa
kundi la 'Daulatul-Islam fl-Iraq wa
Sham ' kwa kifupi Daesh (ISIS). Hata
hivyo upinzani wa al-Qaeda dhidi
ya hatua ya kuyaunganisha pamoja
makundi hayo na uungaji mkono
kwa Jab'hatu Nusra, uliibua vita
kati ya Daesh na kundi la Jab'hatu
Nusra nchini Syria, vita ambavyo
hadi sasa vimeshapelekea zaidi ya
wanamgambo 1000 wa makundi hayo
kuuawa.
Mbali na j inai na mauaj i ya
kinyama ya DAESH, kundi hili
limekuja na mambo ya ajabu ajabu
kama Jihad Nikah. Wachambuzi wa
mambo wanasema huu ni uzinzi na
ukandamizaji kwa jina la jihadi ya
ndoa. Magaidi hao wa Kitakfri hivi
karibuni waliamua kufungua ofsi za
ndoa kwa shabaha ya kuwarubuni
wanawake ili waelekee Syria na
Iraq kwa shabaha ya kuwahudumia
wanamgambo wa kitakfri wa kundi
la Daesh wanaopigana na serikali za
Syria na Iraq. Shirika kutetea haki za
binadamu la Human Right Watch
(HRW) lilitangaza kuwa, magaidi wa
kitakfri wamefungua ofsi hizo katika
mji wa al Bab ulioko katika jimbo la
Halab nchini Syria. Wanamgambo wa
Daesh wamekuwa wakiwashawishi
na kuwarubuni wanawake na
waj ane kuorodhesha maj ina na
anwani za makazi yao kwa lengo
la kwenda kutoa huduma ya ngono
kwa wanamgambo wa Daesh. Sasa
hawa wanaweza kuitwa mujahidina
au ni magaidi wanaotenda jinai
kwa jina la Uislamu? Hivi kweli
kundi hili limeufahamu Uislamu
unavyoapaswa?
Waislamu tuwe macho na njama
za makundi kama haya ambayo si ya
Kiislamu, au yameufahamu vibaya
Uislamu au pengine yanatumiwa na
maadui wa Uislamu kuharibu sura
nzuri ya dini hii tukufu.
Mchezo sasa unaanza kunoga na
kuwa hatari zaidi kwa Waislamu
Kama Osama, ISIS wageuziwa kibao
Ila bado wanalindwa wakamilishe kazi
al-Malik amengoka. Zamu ya Bashar
Hivi sasa ndege za kivita za Marekani
zinafanya mashambulizi yasiyosita
ikiwaangamzia wapiganaji wengi
wa ISIS.
Hayo yakijiri, Rais Barack Obama
ametangaza kuruhusu kikosi maalum
kui ngi a I raq/ Syri a kuwal i nda
Wamarekani.
Hat ua hi yo i naf uat i a t uki o
lililopigiwa sana zumari la kuuliwa
mwandishi wa habari James Foley.
American fighter jets and drones
continued to pound Islamic State
militants in Iraq on Wednesday, and
military planners weighed the possibility
of sending a small number of additional
U.S. troops to Baghdad.
Ndivyo vilivyoripoti vyombo vya
habari jana huku zikifuatiwa na picha
za video zikionyesha jinsi ndege
za Marekani zinavyovurumisha
makombora katika maeneo walipo
ISIS.
Hata hivyo, picha inayojitokeza
ni kuwa bado Marekani haijaridhika
kuwa ISIS wamemaliza kazi, kwani
hata hayo mashambulizi, yanakuwa
ya kiwango fulani, ikiacha kitisho cha
ISIS kuonekana kuendelea kuwepo.
Mashambul i zi haya mapya,
yalianza baada ya kusambazwa
video iliyodaiwa kuwa ilitengenezwa
na ISIS wakati wakimkata shingo na
kumuuwa James Foley.
James Foley, mwenye umri wa
miaka 40, ni mwandishi wa habari
wa Kimarekani akitokea Rochester,
New Hampshire.
Alitoweka akiwa Syria, akiwa
anafanya kazi na Shirika la Habari
la Agence France-Presse (APF),
halikadhalika kampuni ya GlobalPost
(Boston).
Akizungumzia suala hilo, Rais
Barack Obama aliapa akisema kuwa
Marekani itakabiliana na ISIS mpaka
iwatokomeze.
Alisema, hakuna Mungu ambaye
anaweza kuvumilia kuona haya
yanayofanywa na ISIS.
The (ISIS) fighters had rampaged
across cities and villages, abducted
women and children and subjected them
Inaendelea Uk. 12
12
AN-NUUR
SHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 22-28, 2014
12
MAKALA/Mashairi
Tumefunga wetu babu, kwa swaumu kutimiza,
Twamshukuru WAHABU, kwa hilo sisi kuweza,
Kilosalia hesabu, kiama na yetu jaza,
MWENI kumsindikiza, ni wetu sote wajibu.
Thelathini bila tabu, zote tumezitimiza,
Kulikoni! ni ajabu, kwa SITA kutoziweza,
Thakili kwa la thawabu, MchaMungu kulibeza,
MWENI kumsindikiza, ni wetu sote wajibu.
Kwanini ! li juu jibu, la SITA wengi kubeza,
Wallahi hakujaribu, MUHAMMAD nadokeza,
SITA shawali ajibu, kuacha kutekeleza.
MWENI kumsindikiza, ni wetu sote wajibu.
Mizaniye kithawabu, mithili ya mwaka jaza,
Alotujuza HABIBU, si kwamba ninachombeza,
Kwa hadithi mujarabu, swahihi katuhimiza,
MWENI kumsindikiza, ni wetu sote wajibu.
Mabanati, mashababu, kwalo alotuhimiza,
Kadhalika mashaibu, pamoja na maajuza,
Twapaswa kujiratibu, thuma kulitekeleza,
MWENI kumsindikiza, ni wetu sote wajibu.
Shime japo taratibu, SITA twanze dunduiza,
Shawali isijeghibu, bila SITA kutimiza,
Kwa sita beti wajibu, wangu nimeutimiza,
Kwa SITA asindikizwe, Mgenetu RAMADHANI.
ABUU NYAMKOMOGI-
MWANZA
ELIMU
Elimu tunu adhimu, aali iso kifani,
Elimu tunu adhimu, kwa insi si hayawani,
Elimu tunu adhimu, kutoka kwa RAHMANI,
Elimu tunu adhimu, taadhima kwa insani,
Shime tuisharifuni, kikoa tunu adhimu.
Elimu bora johari, yenye aali thamani,
Elimu bora johari, kwayo kufuye sioni,
Elimu bora johari, si lulu si marijani,
Elimu bora johari, kwayo havioni ndani,
Shime tuithaminini, kikoa bora johari.
Elimu angavu nuru, kwa uoni wa yakini,
Elimu angavu nuru, kwa ya akhera yakini,
Elimu angavu nuru, kwa ya dunia yakini,
Elimu angavu nuru, akhera na duniani,
Shime tuitafuteni, kikoa angavu nuru.
ABUU NYAMKOMOGI-
MWANZA.
MGENI ASINDIKIZWE !
to torture and rape and killed
Muslims, both Sunni and Shia,
by the thousands.
Vyombo vya habar i
vilimnukuu Obama akisema
na kuhitimisha kwa kusema
kuwa:
"No just God would stand
for what they did yesterday and
what they do every single day.
Their ideology is bankrupt."
A l i s e m a O b a m a
akimaanisha kuwa mauwaji
n a uk a t i l i ul i o k uwa
ukifanywa na ISIS ukifuatiwa
na hi l i l a kumc hi nj a
mwandishi, Foley, hakuna
Mungu wa haki anayeweza
kulikubali.
Pi gi a mst ari maneno
their ideology is bankrupt.
Ideology, inayokusudiwa
hapa ni Uislamu kwa vile
hawa ISIS wanadai kuwa
ni Waislamu wanaopigania
kus i mami s ha dol a ya
Kiislamu.
Ambayo tafsiri yake ni
kuwa maadui wa Uislamu
wametengeneza Waislamu-
I S I S , n a k u wa t u mi a
kuutangaza Uislamu kuwa
ni itikadi iliyoflisika!!!
Hayo yakasemwa pia na
Waziri wa Mambo ya Nje,
John Kerry, akisema:
Islamic State group is an
"Ugly, savage, inexplicable,
nihilistic, and valueless evil."
"ISIL is the face of that evil, a
threat to people who want to live
in peace, and an ugly insult to
the peaceful religion they violate
every day with their barbarity."
Kuweka kibwagizo hiki
cha Mungu kinakuja kwa
sababu hawa ISIS wanadai
kuf anya hi vyo kat i ka
harakati zao za kusimamisha
ukhalifah.
Hili ndilo kwa upande
mmoja makafri na maadui
wa Uislamu wamefanikiwa
katika vita yao dhidi ya
Uislamu kwa kuwatumia
Waislamu wenyewe.
Viongozi wa Marekani
na kat i ka NATO, Hi vi
sasa wameungana wakiwa
n a ms i ma mo mmo j a
wakitangaza kuwa dola ya
Kiislamu inasimamia ushenzi
na ukati l i usi okubal i ka
katika ulimwengu wa watu
wastaarabu.
I s l ami c Cal i phat e a
"cal i phate of barbari sm",
al i nukul i wa Wazi ri wa
Mambo ya Nje wa Ufaransa,
Laurent Fabius, akisema
huku akishajiisha jumuiya
ya ki matai fa kuungana
kuwapiga vita ISIS na mradi
wao wa Khilafah.
Ya p o ma d a i k u wa
huenda mkanda uliotolewa
akionekana Foley akichinjwa
ni wa kughushi , l aki ni
i we kwel i au l a, bado
Mchezo sasa unaanza kunoga na
kuwa hatari zaidi kwa Waislamu
ukweli unabaki kuwa ISIS
imetumiwa na maadui wa
Uislamu kuupaka Uislamu
matope na kuwa sababu ya
majeshi ya Marekani kurejea
Iraq na kufanya ufisadi
mwingine Iraq, Syria na nchi
za Kiislamu.
Katika Iraq, tayari ISIS
wamewezesha kungolewa
madarakani al i yekuwa
Wazi ri Mkuu wa I raq,
Nour al - Mal i k ambaye
japo alikuwa akitumiwa na
Marekani, lakini kuna baadhi
ya mambo yal i mshi nda
kuyakubali.
ISIS wakapewa uwezo na
kuachiwa kukaribia kuingia
Baghdad. Hapakuwa na
namna, Malik akaondoka.
Sasa ameingia mtu ambaye
tayari ashaongea na wakuu
wa Marekani na kuridhiana
cha kufanya na hapo ndipo
mabomu kutoka angani
yakaanza kuwaanguki a
ISIS, wakiambiwa komeni,
hakuna ruhsa kui ngi a
Baghdad.
Kwa upande mwingine,
ISIS wamewezesha Jimbo la
Kurdistan kuwa na nguvu ya
kupigania kujitawala na sasa
wanadhibiti visima vyao vya
mafuta nje ya udhibiti wa
Baghdad na tayari inaelezwa
kuwa wanauza maf ut a
Marekani na Israel.
Baadhi ya wachambuzi
wa mambo wanasema kuwa
tukio hili la kuuliwa James
Foley, limetumiwa kufikia
malengo mawili.
Moja ni kufunika ukweli
kuwa ISIS ni mtoto wa
kuzaa na kul el ewa na
Marekani/NATO. Kwamba
kwa jinsi Mmarekani huyo
alivyochinjwa kikatili, na
hasira inayooneka kuibuka
kut oka Washi ngt on na
NATO, inafuta dhana yoyote
kuwa kuna mahusiano na
maelewano kati ya wawili
hao.
Jambo la pili linatajwa
k u wa k wa h a s i r a
iliyoonyeshwa na Marekani,
hiyo imekuwa sababu na
kisingizio cha Marekani
kurej esha maj eshi yake
Iraq, lakini pia kisingizio
hicho hicho kitatumiwa pia
kupeleka askari wa Marekani
kule Syria ambapo Marekani
na NATO wana mradi wa
kumngoa Bashr Assad.
Na hi l i l i naj engewa
hoja kutokana na maelezo
kuwa James Foley, alitekwa
akiwa Syria na kwamba
kuna mwandishi mwengine
wa Marekani Steven Sotlof
aliyetekwa huko Syria na
ISIS wametishia kuwa naye
watamchinja.
Lakini pia katika taarifa
zilizotawala vyombo vya
habari vya Marekani jana,
ilipigiwa sana ngoma kuwa
Marekani iliwahi kupeleka
kikosi kujaribu kuwaokoa
waandi s hi hao l aki ni
kimekwama. Hiyo ikaelezwa
kuwa ni namna ya kujenga
mazingira ya kuingia kijeshi
Syria.
Lakini pia ile kauli ya
Obama inayoelekeza kuwa
Marekani i t afanya ki l a
iwezalo ikibidi kuwafuata
I SI S popot e wal i po i l i
kuwangoa na kuwanyima
safe haven within Syria
Foley had been killed.
Inavyoelezwa ni kuwa hivi
sasa waliokuwa wapinzani
wa Bashar, wanael ekea
kuzi di wa nguvu kwa
hiyo kabla ya kumalizwa
na kuonekana kuwa vita
i memal i zi ka, mabeberu
wanataka kuwapa uhai kwa
kuwa na askari wake ndani
ya Syria.
Inatoka Uk. 11
MPIGANAJI wa ISIS kabla ya kumchinja mwandishi Foley.
13
AN-NUUR
SHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 22-28, 2014
MAKALA
Agosti 15, 2014 (Mtandao wa
Kupashana Habari)
UTAWAL A wa Ob a ma
unashinikiza mabadiliko ya
utawala nchini Irak kwa msingi
kuwa waziri mkuu wa sasa,
Nouri al-Maliki amejiweka
mno katika kundi la kidini.
Hali halisi, hata hivyo ni kuwa
uonevu wa Maliki dhidi ya
wa-Sunni haukuwa sehemu ya
sababu za Marekani kuamua
kuwa aondolewe. Iwe ni kweli
amekuwa 'mdini' kupita kiasi
au hapana siyo suala muhimu.
Sababu ya kushambul i wa
kwake ni kuwa alikataa kutia
saini makubaliano ya hatma
ya majeshi ya Marekani nchini
humo, mwaka 2011. Alikataa
kutoa ilani ya kutoshitakiwa
kwa maelfu ya askari ambao
utawala huo ulitaka wabakie
Irak kufuatia kuondoka rasmi
kwa majeshi ya Marekani nchini
humo. Ndicho kilichokasirisha
Marekani, Ndiyo sababu utawala
huu unataka Maliki aondolewe.
Hakikisha hii taarifa ya Ikulu
ya Marekani ya kumuunga
mkono waziri mkuu mteule
Haider al-Ibadi (mshindani wa
Maliki) na Makamu wa Rais
Joe Biden masaa kadhaa baada
ya mabadiliko (kupinduliwa?)
yalipotangazwa. Taarifa hiyo ina
kichwa cha habari: "Kilichojiri
katika mazungumzo ya simu ya
Makamu wa Rais na Waziri Mkuu
mteule wa Irak Haider al-Abadi."
" Ma ka mu wa Ra i s J oe
Biden alimpigia simu Waziri
Mkuu mteule Haider al-Abadi
kumpongeza kwa kuteuliwa
kwake kuunda serikali mpya
na kuunda programu ya kitaifa
i nayoendana na mkakat i
unaoendelea wa kupatikana
Katiba Mpya nchini Irak. Waziri
Mkuu mteule ameeleza nia
yake ya kufanya haraka kuunda
serikali pana, yenye kushirikisha
makundi tofauti na kuweza
kukabiliana na hatari ya Dola ya
Kiislamu ya Irak na Syria (ISIl,
pamoja na Lebanon), na kujenga
hali nzuri ya baadaye kwa wa-
Iraki wa jumula zote.
Makamu wa Rais alimpelekea
pongezi za Rai s Obama na
kuelezea msimamo wake wa
kuunga mkono kwa nguvu
serikali mpya na shirikishi ya
Irak, hasa kwa ajili ya kukabiliana
na ISIL.
Vi ongozi hao wawi l i pi a
walijadili hatua za kuchukuliwa
ili kuanza kutumia kikamilifu
makubaliano ya mkakati wa jumla
wa katika nyanja zake zote, ikiwa
ni pamoja na masuala ya uchumi,
diplomasia, na ushirikiano wa
kiusalama. Waziri Mkuu mteule
Kuzuia mipango ya Marekani: Sababu za Obama kutaka Maliki aondolewe
Na Mike Whitney Abadi alimshukuru Makamu
wa Rais Biden kwa kumpigia
simu hiyo, na wakakubaliana
kuendelea kuwasiliana wakati
mwenendo wa kuunda serikali
unaendelea. (Kutoka Ikulu ya
Marekani)
Ulipata chembe hiyo kuhusu
"makubaliano ya pande mbili ya
mkakati wa jumla katika nyanja
zake zote"?
Ndiyo hasa kinachogomba hapa.
Ndiyo hasa kinachosababisha
sokomoko yote hii. Hapa kuna
sehemu ndogo tu ya taarifa ya
makubaliano hayo chini ya kichwa
"Ulinzi na Usalama:"
"Kamati ya kijeshi ya pamoja
ya Irak (JMC) ................ilijadili
masual a kama usal ama wa
mipakani, mikakati ya kijeshi ya
Irak, ,na kushiriki kwa majeshi
ya usal ama ya I rak kat i ka
mazoezi ya kikanda ya mafunzo.
Mkutano mwingine wa kamati
hiyo unatazamiwa kufanyika
Washington kabla ya mwisho
wa mwaka. Kaimu Waziri wa
Ulinzi al-Dlimi alitia saini hati
ya makubaliano (MoU) kuhusu
ushirikiano katika usalama na
Wizara ya Ulinzi ya Marekani.
Makubaliano hayo yanalenga
ushirikiano wa nguvu kati ya
majeshi ya Marekani na Irak, na
kuweka mifumo ya kuongeza
ushirikiano katika maeneo kadhaa
kwa mfano mipango ya ulinzi,
ushirikiano dhidi ya ugaidi, na
mazoezi ya pamoja.
Programu ya FMS (ushirikiano
wa kijeshi na usalama) ya Irak
ni moja ya zilizo kubwa zaidi
duniani na ni alama muhimu ya
ushirikiano wa muda mrefu wa
usalama unaotazamiwa na nchi
hizo mbili. Tunaendelea kuwa na
nia ya kufkia mahitaji ya vifaa ya
Irak kwa haraka iwezekanavyo."
(Makubaliano ya Mkakati wa
Ushirikiano, Wizara ya Mambo
ya Nje ya Marekani)
Hii sana sana ndiyo pua ya
ngamia chini ya hema. Hakuna
shaka kuwa lengo kamili la
utawala huu ni kuweka "mabuti ya
Marekani ardhini" ambayo, hata
hivyo, ndiyo sababu ya Obama
kuruhusu wanamgambo magaidi
(ISIS) kutwaa asilimia 30 ya ardhi
ya Irak, kukamata mji mkuu wa
pili wa nchi hiyo, na kusonga
mbele hadi kufikia viunga vya
jiji la Baghdad kwa maili 50
(kilomita 100) bila kunyoosha
kidole kusaidia. Ni kwa sababu
Obama anataka kisingizio cha
kuongeza idadi ya askari waliopo
nchini humo.
Kuna njia gani bora zaidi ya
kuweka maelfu ya askari wa
jeshi la Marekani nchini Irak, ila
kwa kuwatisha watunga sera wa
Irak kukubaliana na Marekani,
pale wakiangalia chinjachinja
magaidi wa ISIS wakikata vichwa
na kutoboa shingo kokote pale
RAIS Barack Obama wa Marekani.
wanakopata nafasi.
(Angalizo: Ni rahisi kuona kuwa
wakati ISIS haisimamiwi moja kwa
moja na Marekani, kuwepo kwake
Irak kwa hakika kunaendana na
malengo ya jumla ya kimkakati ya
Marekani). Mtafti wa kujitegemea
na mwandishi wa habari Soraya
Sepahpour-Ulrich, analekea
kuwa mmoja wa wachambuzi
wachache wanaoelekea kuelewa
ki na c hoe nde l e a . Anga l i a
kibwagizo hiki kutoka televisheni
ya Iran kutokana na mahojiano na
Ulrich:
"Marekani ina mipango ya
muda mrefu ya kuwepo bila
kikomo nchini Irak, na katika
Ghuba ya Uajemi kwa jumla,"
alisema Ulrich. "Kudhibiti eneo
la Ghuba ya Uajemi ndiyo kiini
cha mkakati wa Marekani........
kuwepo kwa ISIL kunawasaidia
katika lengo hili."
Baada ya Waziri Mkuu Nouri
al-Maliki wa Irak kuwaondoa
majeshi ya Marekani kutoka
Irak kwa kukataa kutia saini
makubaliano ya hatima ya majeshi
unaowaruhusu kukaa bila kikomo,
Marekani imepata njia ya kurudi
huko, alisema.
Serikali ya Maliki ilikataa kutoa
kinga kwa maelfu ya askari wa
Marekani, ambao walikuwa
wabaki nchini Irak baada ya 2011
chini ya kisingizio cha kutoa
mafunzo kwa askari wa nchi hiyo.
Serikali ilikuwa imekubali
baadhi ya majeshi ya Marekani
kubakia kwa kirefu zaidi kwa
ajili ya "mafunzo," lakini ikakataa
kuwaki nga na kushi taki wa.
Matokeo yake ni kuwa majeshi
hayo ya mpito hayakuwekwa.
Chini ya mkataba wa pamoja wa
usalama wa mwaka 2008, unaoitwa
Status of Forces Agreement
(SOFA - makubaliano ya nafasi
kisheria ya majeshi), askari wote
wa Marekani waliondoka hadi
kufikia Desemba 2011. Ulrich
alisema "inatatiza kuona kuwa
ISIL (ISIS) imekamata miji na
majimbo ambayo ni muhimu kwa
sera za Marekani katika ukanda
huo - jimbo moja lina mafuta
mengi, utoaji wa mafunzo na
fedha wa wa-Kurdi unaofanywa
na Marekani, na Israel ilianza
kutoa mafunzo kwa wa-Kurdi
mwaka 2005, na dhana kuwa
mafuta ya Irak yatakwenda Israel,
na inatokea sasa."
"Siamini kwa sekunde moja
kuwa Marekani imeacha wazo
la kuweka Irak na Syria chini ya
udhibiti wake kamili," mtafiti
huyo bi nafsi na mwandishi
alisema. (Marekani yainua hatari
ya ISIL kubaki Irak." televisheni ya
Iran. (Mwisho wa makala)
Baada ya kusoma sehemu
hi i ya uchambuzi huu wa
mwandishi, Mike Whitney kama
ulivyotafsiriwa kwa Kiswahili na
Anil Kija, hebu rejea maneno ya
kijana huyu. Anasema:
Uislamu unapigwa vita lakini
Allah ametuahidi Waislamu
tutashinda hata kama makafiri
wa t a c huki a na wa na f i ki
watachukia. Haya yanayotokea
Waislamu kuuliwa na makafiri
tunafurahi kwa sababu ni nusra
inakuja. Hata masheikh wetu
wakikamatwa sisi tunafurahi zaidi
maana Allah amewapenda zaidi
kawapa mitihani na tunawaombea
washinde na sisi tumepewa
mtihani juu ya nafsi zao kwetu sisi
Inaendelea Uk. 14
14
AN-NUUR
SHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 22-28, 2014
MAKALA
ILIKUWA Agosti 6, mwaka 1945
Marekani ilitumia bomu la atomiki
kuiangamiza miji ya Japan na
watu wake. Kitendo ambacho
hakikuwahi kutokea kabla yake na
hata zama hizi. Kwa kutumia ndege
ya kivita aina ya B-29 bomber, siku
ya Jumatatu tarehe 6, Agosti 1945,
Marekani iliiangamiza kabisa mji
wa Hiroshima Japan kwa bomu
lenye urefu wa futi 10, ambalo
lilitapika tani 20,000 za mionzi
ya TNT na kwa mkupuo mmoja
ilitosha kuiyeyusha Hiroshima,
takriban kwa pamoja robo tatu
ya majengo 90,000, watu 350,000
na kila kilichokuwepo wakati ule
kiliangamia.
Ndani ya dakika tatu, Hiroshima
ikawa imevurugika. Kama tukio hilo
halitoshi, siku tatu baadae Marekani
ikatupa bomu jengine la aina hiyo
hiyo katika mj i mwengine wa
Nagasaki na kusababisha madhara
yale yale.
Leo dunia imesheheni malimbikizo
na shehena kubwa ya silaha za
maangamizi na maelfu ya vituo
vya nishati vyenye kutumia nishati
ya nuklia, itapotokea ajali au vita
na mmoja akatumia mabomu haya
au ajali itakayolipua mabomu ya
nishati hii au kulipuka vituo vingi
kwa wakati mmoja, dunia itakuwa
vipi? Itakuwa kama lile shairi la
mwandishi Jane Franklin, nani
amcheke nani .
Dunia isisahau milipuko midogo
tu ya vituo vya nishati za nuklia vya
Chernyobyl, Ukraine mwaka 1986 na
ule wa Fukushima Japan mwaka 2011
jinsi ulivyoleta madhara makubwa
kwa mali na maisha ya wanadamu.
Hata hivyo, Marekani ndiyo yenye
shehena kubwa zaidi ya nishati za
maangamizi kwa sasa duniani na
ndiyo iliyowahi kutumia silaha za
aina hii za maangamizi. Pamoja na
hayo inatumia uwezo wa kiuchumi
kuongeza shehena hizi na kuzitisha
na kuzibana itakavyo dola nyengine
dhaifu ili zisimiliki silaha za aina hii.
Na kama dola hizo tayari wanazo
waangamizwe.
Kwa upande wa pili Marekani,
gaidi namba moja na Washirika
wake pamoja na mfumo waliobeba ni
wajibu wanyangnywe usimamizi wa
dunia ili wasije wakawadhuru watu
zaidi kama wanavyoendelea sasa.
Na hilo ni kwa dola ya Kiislamu
ya Khilafah yenye misingi ya haki
na uadilifu kuchukuwa uongozi wa
kilimwengu.
Katika j uhudi zetu dhidi ya
kuuondoa mfumo wa kibepari/
kidemokrasia na wanaoungangania
tusitishike na silaha na nguvu
walizonazo. Sisi tuna Mwenye nguvu
zisizoshindwa ambaye ni Allah.
Kamnusuru Mtume wake SAAW
katika vita vigumu vya makundi(
Al-Ahzab) , katu hatoshindwa
kutunusuru sisi kwa zama hizi .
Allah Anasema:
Allah Aliwarudisha nyuma
makafiri juu ya ghadhabu zao na
hawakupata kheri yoyote. Allah
Amewatosheleza waumini katika
vita . Na Allah ni mwenye nguvu na
uweza (Masoud Msellem, Kumb:
18 / 1435 AH Ijumaa, 12th Shawwal
1435 08/08/2014.)
JANGA LA HIROSHIMA NA NAGASAKI
Marekani gaidi nambari moja
Kuzuia mipango ya Marekani: Sababu za Obama kutaka Maliki aondolewe
Inatoka Uk. 13
ni nusra tutashinda Inshaallah.
Msingi wa utetezi wa bwana
huyu ni kitendo cha Marekani
kuwashambaulia ISIS ambao
yeye anawakubal i kuwa ni
muj ahi di na wanaopi gana
kusimamisha Khilafah Iraq na
Syria. Utetezi huo pia anauleta
kufuatia kamatakamata hapa
nchini ya watu wanaotuhumiwa
kushiriki kuhamasisha watu
kwenda kupigana Syria/Somalia
au kufanya vitendo vinavyodaiwa
kuwa vya kigaidi.
Plato anasema: "We can easily
forgive a child who is afraid of
the dark. The real tragedy of life is
when men are afraid of the light."
Huyu ni katika wale wanaodai
kuwa maelezo ya akina Mike
Whi tney, hayakubal i ki kwa
sababu ni makafiri na hayapo
katika Quran, lakini anayosema
Whitney, ndio ukweli wenyewe.
Hebu fkiria kiroja hiki: kwamba
hali halisi ya ISIS ndiyo hiyo
inayoelezwa na Mike Whitney.
Na kama ilivyoelezwa na Hilary
Clinton-kwamba hawa ISIS ni
mamluki wao wanaowatumia
kufkia malengo yao ya kibeberu
katika nchi za Waislamu, halafu
nyinyi Waislamu Tanzania, na
kwingineko, mnanyanyua mikono
mnaomba, Allahumma nsuru l
mujahidina (ISIS) fi Iraq, wafi
Suria!!!
Katika Afghanistan, mahesabu
yake yalikuwa magumu kidogo na
kwa hakika pengine isingekuwa
rahisi sana kwa Waislamu wa
kawaida kugundua japo kwa
wale wa serikali ya Pakistan
na Saudi Arabia walij ua ila
wakahiyari kuwauza Waislamu
wenzao. Lakini Allah (SWT)
kajaaliya ukweli wa kilichotokea
umefahamika na Allah anaendelea
kutujaaliya kujua yaliyojificha
chi ni ya ISIS na US-NATO,
MOSSAD; katika mradi wao wa
Khilafah Iraq/Syria.
Hivi itakuwa ni akili kujitosa
kat i ka mr adi huu, hal af u
i ki wa s ababu ya kuul i wa
na kuangami zwa kwa mi j i
ya Wai sl amu, tuseme kuwa
tunafurahi kwa sababu ni nusra
au Allah ameahidi kutunusuri!
Jaal i ya watokee fanati ki
aliosema Clinton kuwa ndio
wanaowatumia katika j ihad
bandia, waanze kufanya vitendo
ambavyo hatima yake ni kuita
hasira za wakala wa kupambana
na ugaidi nchini. Nini litakuwa
j ukumu l a Wai sl amu? Upi
utakuwa uamuzi wa busara na
wenye kuendana na mafundisho
ya Uislamu? Je, tutawanasihi
waachane na jambo hilo la hatari
kwao, kwa Waislamu na nchi, au
tutawaacha wajitose katika mradi
huo wa akina Clinton na ISIS yao
halafu hatimaye tuseme kuwa
tunafurahi wao kukamatwa kwa
sababu Allah amewapenda kwa
kuwapa mtihani huo?!!!
Zinapotokea operesheni kama
hizi kama ilivyokuwa katika
kadhia ya mabucha ya nguruwe
mwaka 1993, ni dhahiri watu
wenye chuki na wenye nia mbaya
wanaweza kutumia fursa hizo
kuwahujumu Waislamu wasio na
hatia. Kwa hawa tunamwomba
Allah awape subra na awanusuru
na vitimvi, hila na shari za watu
wabaya. Lakini kwa upande
mwi ngi ne, t uf anye j uhudi
kubwa kuielimisha jamii yetu ya
Waislamu, tusiwe sisi wenyewe
ndio sababau ya kujiangamiza kwa
mikono na kauli zetu wenyewe.
Tukilifanya hili, hata tukiomba
nusra ya Allah, itakuwa na maana
sana na kwa hakika itakuwa na
matokeo bora kabisa, maana
tutakuwa tumetekeleza wajibu
wetu, sasa palipotuzidi uwezo,
tunamwachia Allah.
(Mhariri-An nuur)
MARUBANI waliohusika na uangushaji wa bomu la Atomi katika miji ya Hiroshima na Nagasaki, Japan.
15
AN-NUUR
SHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 22-28, 2014
Barua/Habari/Tangazo
KWA jina la Allah, Mwingi wa
rehma, Mwenye kurehemu.
Ndugu mhariri wa gazeti tukufu
la Kiislamu la Annuur, naomba
unipe fursa ili niweze kutoa maoni
yangu machache kuhusiana
na fatuwa za hivi karibuni za
masheikh wa Saudi Arabia za
kuharamisha maandamano ya
kuwaunga mkono wananchi wa
Palestina.
Hivi karibuni Sheikh Abdul
Aziz Al Sheikh, Mufti wa Saudi
Arabia na Mkuu wa Kamati ya
Maulama wa nchi hiyo alisema
kuwa, kufanya maandamano ya
kuwaunga mkono Wapalestina wa
Gaza ni hatua ya kuleta vurugu
na isiyo na faida. Naye Sheikh
Swaleh al-Haidan, Mwenyekiti
wa Baraza Kuu la Mahakama
la Saudia ametoa fatuwa ya
kuharamisha maandamano ya
kuwaunga mkono Wapalestina.
Al-Haidan alikwenda mbali zaidi
na kusema katika fatuwa yake hiyo
kwamba, kufanya maandamano
ya kuwaunga mkono Wapalestina
ni sawa na kufanya uharibifu
katika ardhi.
Bila shaka wote au akhthari
ya Waislamu walishangazwa
na kushtushwa na fatuwa ya
hivi karibuni ya mamfuti hao
wawili wa Saudi Arabia. Fatuwa
hizo zilitolewa katika kipindi
ambacho Wapalestina wa Gaza
wanakabiliwa na mabomu na
mashambulio ya kinyama ya
Israel ambapo watoto wadogo wa
Kipalestina walikuwa wakiuawa
kinyama bila hata chembe ya
huruma.
Fatuwa hizo zilitolewa katika
kipindi ambacho ulimwengu
mzima ulikuwa ukishuhudia
maandamano ya kuwaunga
mkono Wapalestina; maandamano
ambayo yamepiga hodi hata katika
nchi za Ulaya. Hata wasiokuwa
Wai s l amu wameandamana
Marekani, Ufaransa, Uingereza
na kwingineko katika Ulaya na
hata Latin America kama Bolivia
na Venezuela ili kuwaunga mkono
wananchi wa Palestina huko Gaza
na kulaani mauaji ya kinyama
ya Israel dhidi ya wananchi hao
wasio na ulinzi.
Fatuwa hi zo za mashei kh
wa Saudia zimetolewa katika
kipindi ambacho ulimwengu
mzima umekumbwa na huzuni
kutokana na kushuhudia damu
ya Wapalestina ikimwagwa bure
bilashi.
Fatuwa hizo zimetolewa katika
kipindi ambacho walimwengu
kupi t i a r uni nga wal i kuwa
wakishuhudia vipande vipande
na viungo na miili iliyotapakaa
damu ya Wapalestina hasa watoto
wadogo ambao La haula lahum
wala quwa; watoto ambao fkra
zao ni lini patakucha wakacheze
nje.
Fatuwa hizo za mamufti wa
Saudia za kupinga na kuharamisha
maandamano ya kuwaunga
mkono Wapalestina zilitokewa
katika kipindi ambacho kila
kona ya ulimwengu kulikuwa
kukisikika sauti ya kuwaunga
Fatwah hizi za Mufti Saudia
ni aibu kwa Waislamu wote
Kama haramu kuwaunga mkono Wapalestina
Halali kumuunga mkono Binyamin Netanyahu?
mkono Wapalestina.
Kwa hakika fatuwa kama hizi
zinatia simanzi na huzuni na kwa
mtazamo wangu, ni aibu kubwa
kwa Waislamu na ulimwengu
wa Kiislamu. Fatuwa kama hizi
zinategemea mafundisho gani
ya Uislamu. Kama kuandamana
kuwaunga mkono Wapalestina ni
haramu, basi ni halali kuwaunga
mkono Wazayuni wanaowaua
kila leo Wapalestina na kufyonza
damu zao?
Je, hatuiambiwi katika Uislamu
kwenye hadithi mashuhuri ya
Bwana Mtume SAW kwamba:
Mwenye kuamka (asubuhi) bila
ya kutilia maanani masuala ya
Waislamu, basi sio Mwislamu?
Sasa la kujiuliza ni kwamba,
f a t uwa z a k uh a r a mi s h a
maandamano ya kuwaunga
mkono wananchi wa Palestina
zimetegemea kigezo gani. Ala
kulli haal, hakuna asiyetambua
katika ulimwengu wa leo jinai na
unyama unaofanywa na utawala
wa Israel dhidi ya wananchi wa
Palestina. Na ndio maana hata
wasiokuwa Waislamu wamekuwa
wakipaza sauti zao na kutaka
wananchi wa Palestina wasaidiwe
kwa hali na mali.
Baytul Muqaddas kibla cha
kwanza cha Wai sl amu ki ko
Pal esti na na ki l a l eo Israel
inawakandamiza Wapalestina
na hata kibla hicho kiko hatarini
kubomoka kutokana na njia za
chini kwa chini zilizochimbwa na
utawala huo wa Israel kuelekea
katika kibla hicho.
Nadhani umewadia wakati kwa
Waislamu kuwa macho na fatuwa
kama hizi ambazo zinahudumia
maadui na kimsingi zinapingana
wazi na mafundisho ya Kiislamu.
Wabillah Tawfq
Salum Bendera.
KINGDOM OF SAUDI ARABIA
COMMITTEE OF DA-AWAH IN AFRICA
MAJINA YA WASHINDI WA MASHINDANO YA FAMILIA YA MTUME
(S.A.W.) NA SWAHABA 1435H/2014M.
Yafuatayo ni majina ya washindi wa mashindano ya Familia ya Mtume na Swahaba
yaliyo fanyika kati ya mwezi tano na wasita 2014.:
ZAWADI ALIYOPATA NAMBA YA SIMU JINA LA MSHINDI
SAFARI YA HIJA 715020753 255+ ALLIY ABDALLAH 1
SAFARI YA HIJA 767200788 255+ OMARI JUMA MASOUD 2
SAFARI YA HIJA 777859106 255+ MUSSA HAMAD ALLY 3
SAFARI YA HIJA 773222546 255+ KHAMISI JUMA KOMBO 4
KOMPYUTA (LAPTOP)) 654203339 255+ SUAD ABDUL AZIZ 5
KOMPYUTA (LAPTOP)) 714831498 255+ HANIFA ALLY ISA 6
KOMPYUTA (LAPTOP)) 777933828 255+ MWANAHARUSI ISSA HAJI 7
KOMPYUTA (LAPTOP)) 774145574 255+ KAZIJA HAJI AME 8
KIFAA CHA KUFUNDISHIA QURANI 713836311 255+ NASIR MOHAMED NASIR 9
KIFAA CHA KUFUNDISHIA QURANI 784235412 255+ ADAM BAKARI KAMA 10
KIFAA CHA KUFUNDISHIA QURANI 754987813 255+ DAUD NOORDIN SAID 11
KIFAA CHA KUFUNDISHIA QURANI 776012081 255+ AMINA KHAMISI 12
KIFAA CHA KUFUNDISHIA QURANI 779445166 255+ SHIFAA KHAMISI 13
KIFAA CHA KUFUNDISHIA QURANI 778426723 255+ RAHMA ALLY HAJI 14
SIMU YA MKONONI 654219192 255+ ALLY A. BAGHRAMESHI 15
SIMU YA MKONONI 769207412 255+ HASSAN HUSSEIN 16
SIMU YA MKONONI 789529142 255+ ATHUMAN BASHIRU HASAN 17
SIMU YA MKONONI 777756631 255+ YUSUF ALLY RASHID 18
SIMU YA MKONONI 774225257 255+ REHANI ABUBAKARI 19
SIMU YA MKONONI 779896080 255+ ZAWADI SAID KHAMISI 20
WASHINDI WATAFAHAMISHWA KUPITIA NAMBA ZAO ZA SIMU NAMNA
WATAKAVYO KABIDHIWA ZAWADI ZAO.
16
AN-NUUR
SHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 22-28, 2014
16
MAKALA
Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na POA Printing Works Limited, S.L.P. 4605 Dar es Salaam.

AN-NUUR
16
SHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 22-28, 2014
Tanzania Muslim Hajj Trust. Uandikishaji
unaendelea, gharama za Safari ni $ 4400
Tarehe za safari ni 22 na 24 Septemba na Kurudi
16 na 19 Oktoba, 2014.Tunasafri na Shirika la
Ndege
Umoja wa Falme za Kiarabu EMIRATES.
Wahi kujiandikisha sasa.
Kwa Mawasiliano:
+255222181577 +255222182370
0786 383820 0717 000065
info@hajjtrusttz.org or Website: wwwhajjtrusttz.org
Safari ya Hijja Hijiria 1435/2014
WAISLAMU wametakiwa
kuitumia Qur an ili kuweza
kukabilina na misukosuko
inayowakabili hivi sasa
ambayo uf umbuzi na
utatuzi wake unapatikana
ndani ya kitabu hicho.
Wito huo umetolewa na
Ustadhi Shaaban Omari,
akiwahutubia Waislamu
katika ibada ya Swala ya
Ijumaa ya wiki iliyopita
katika Msikiti wa Mtambani,
Kinondoni Jij ini Dar es
salaam.
Al i s e ma , k u p i t i a
mafundi sho ya Qur an
na sunnah kwa pamoj a
Wa i s l a mu wa na we z a
kuj i nusur u na kadhi a
mbalimbali zinazowakumba
ambapo ndani yake msaada
wa Allah (sw) utafatia baada
ya wao kuonyesha juhudi
zao.
Waislamu tunashindwa
kuitumia Qur an kama
m w o n g o z o w e t u
katika kutatua matatizo
yanayotukabili hivi sasa,
badala yake tunajifanyia
mambo nje ya utaratibu
wa kitabu hicho, matokeo
yake hatufkii lengo letu.
Alisema Ust. Omari.
Al i sema, hat a wal i o
nj e ya Uislamu, ambao
wanai f uat i l i a Qur an,
wamebaini hilo na kuwaona
Wai sl amu bado wapo
katika usingizi mzito na
kuwashangaa kutokana na
kuisoma kila siku Qur an,
lakini bado hawajui njia ya
ufumbuzi wa masuala yao
kupitia Qur an.
Ust . Omari , al i sema
al i bai ni hi l o kupi t i a
maongezi yake na Mkristo
mmo j a wa Ki z u n g u
katika nchi fulani jirani na
Tanzania, aliyemweleza
kwamba si ku ambayo
Waislamu wataamka na
kuyafanyia kazi maneno
yaliyomo katika Qur an
yao, watapiga hatua kubwa
katika maendeleo.
Alisema, Mzungu huyo
a l i mwe l e z a k wa mb a
Waislamu wanaonekana
kubeba Qur an yao na
kut embea nayo l aki ni
hawaelewi kuwa wamebeba
nyenzo yenye uzito wa kiasi
gani.
Ust . Omari al i sema,
badala ya kufanyia kazi
aya za Qur an, Waislamu
wamekuwa walalamikaji
badala ya kuwa watendaji.
SHIRIKA la Under The
Same Sun kwa kushirikiana
na chama cha watu wenye
ulemavu wa ngozi nchini
(TAS) kimeiomba Serikali
kuangalia uwezekano wa
kushirikiana na Jumuiya
za Kimataifa ili kuunda
kikosi kazi kitachosaidia
shughuli za upelelezi ili
kubaini chanzo cha mauaji
kwa watu wenye ulemavu
wa ngozi (Albino).
Aidha Taasisi hizo pia
zimeitaka Serikali kuchukua
h a t u a z i n a z o s t a h i l i
z a k uk o me s ha wa t u
wanaojihusisha na vitendo
vya ukatili ikiwemo mauaji
na ukataji wa viungo vya
mwili kwa watu wa jamii
hizo ili waweze kuishi kwa
Ishikeni Quran kwa vitendo
Na Bakari Mwakangwale
Kilio cha walemavu wa ngozi
Na Rose Masaka,
MAELEZO, Dar es
Salaam
amani kwani ni haki yao ya
msingi.
A k i z u n g u mz a n a
waandishi wa habari Ijumaa
iliyopita Jijini Dar es Salaam,
Katibu Mkuu wa Chama
hicho Bi. Ziada Nsembo
amesema TAS imesikitishwa
na vitendo hivyo vya kikatili
kwa kuwa mauaji ya watu hao
vinavyochochewa na imani
za kishirikina miongoni wa
wanajamii.
B i . Zi a d a a l i s e ma
kuishi ni haki ya kimsingi
iliyoanishwa katika Katiba
ya Nchi, hivyo wanashangaa
ba a dhi ya wa na j a mi i
wanachukulia Albino kama
ni watu wasiostahili kuishi
na viungo vyao ni moja ya
njia ya kujipatia utajiri, imani
ambayo ni potofu.
Tumekuwa na msi ba
kutokana na kilio cha muda
mrefu tunachotendewa,
b a a d h i y a we n z e t u
wamepoteza viungo vyao
vya mwili ikiwemo mikono
pamoj a na vi ungo vya
sehemu za siri kutokana
na imani za kishirikina
zilizojengeka katika jamii,
alisema Bi Nsembo.
Kwa upande wake ,
Afisa Habari wa TAS Bw.
Joseph Torner amesema
kuwa kitendo cha kinyama
alichofanyiwa mtoto wa
miaka 15 Upendo Sengerema
wiki iliyopita cha kukatwa
mkono wake wa kulia chini
ya kiwiko na watu watatu
kijiji cha Usinge mkoani
Tabora ni cha kinyama na
kusikitisha.
Torner aliongeza kuwa hili
ni tukio la pili kutokea ndani
ya miezi mitatu na waganga
wa ki enyej i wamekuwa
wakihusika katika matukio
haya, ambayo katika kipindi
cha karibuni matukio ya aina
hii yalisimama kutokana na
wahusika kuogopa vyombo
vya dola.
Torner al i sema kuwa
Serikali haina budi kufuta
vibali kwa waganga wa
kienyej i ili watu wenye
u l e ma v u wa n g o z i
waweze kuishi bila hofu,
kwani wengi wao tayari
wameathirika kisaikolojia
na l i narudi sha nyuma
maendeleo kwani watoto
wanaogopa kwenda shule na
watu wazima wanashindwa
kujishughulisha na shughuli
mbalimbali za maendeleo
ikiwemo kilimo.
Chama cha albino TAS
na UTSS na wadau wengine
wa taasisi zisizo za kiserikali
wanakus udi a kuf anya
maandamano ya amani
nchi nzima katika muda
utaopangwa ili kuijulisha
serikali iweze kuwasaidia
kikamilifu.
MSIKITI wa Mtambani uliopo jijini Dar es Salaam ulipoungua moto wiki iliyopita.

Вам также может понравиться