Вы находитесь на странице: 1из 28

TANZANIA EDUCATION DEVELOPMENT RESEARCH

ORGANIZATION

MTAZAMO WA WANANCHI
KUHUSU USHIRIKI VIJANA KATIKA
SIASA NA
MATARAJIO KUELEKEA UCHAGUZI
MKUU 2015

Mwigulu
(27%)

Nchemba

Zitto Kabwe (19%)

January Makamba
(14%)

James
(11%)

Mbatia

UTAFITI HUU UMEFANYWA NA:


Tanzania Education Development Research Organization TEDRO
Dar es Salaam TANZANIA
Email: tedroeducation@yahoo.com
Website: www.tedro.info
1

DAR ES SALAAM - FEBRUARI 2015

Utangulizi
Nimeshuhudia miaka ya 1985 hadi 1995 ambapo mimi mtafiti 1 wa kazi hii;
nikiwa na uelewa kwa kiasi fulani, kuona watu waliokuja kugombea nyadhifa
mbali mbali za kisiasa, hususani ubunge walikuwa watumishi wa umma au
waajiriwa wenye umri wa miaka isiyopungua 50 na kuendelea, wakitumia
wasifu wa kazi zao kujitangaza na hata yale waliokwishafanyia wananchi
kupitia nyadhifa zao ili kupata kura na kuwatumikia wananchi. Wakati
mwingine, wagombea walikuwa wamekwisha kustaafu ndipo wakagombea
nyadhifa za kisiasa. Ilikuwa nadra sana, kukuta kijana ametoka shuleni au
chuo ama kuacha ajira yake na kuingia katika siasa kama mgombea.
Yawezekana hapakuwa na muamko, maslahi, ama hofu ya kushindwa, ama
wananchi kwa wakati ule hawakuwa na imani sana na kijana, na mambo
mengine kama hayo. Hii ilitokana na ukweli kwamba kila mwanasiasa
aliyetaka kugombea alikuja kumuona baba yangu 2 na kumuomba ushauri
kabla ya kujitangaza kijijini na hata katika kata yetu kwa ujumla. Japokuwa
sikuona kijana wa wa miaka 25 hadi 35 akitokea kugombea nyadhifa hizi,
inakuwa jambo la kushangaza ambalo ni suala la kumbukumbu tu ya
kihistoria kwamba Hayati Baba wa Taifa alikuwa Waziri Mkuu wa Tanganyika
mwaka 1961 baada ya uhuru na Rais wa Tanganyika mwaka 1962. Hivyo,
akiwa na miaka 39 alikuwa waziri Mkuu na akiwa na miaka 40 alikuwa Rais
wa kwanza wa Tanganyika. Katika muonekano na uhalisia wa zama
tulizonazo, tunasema mwalimu ndiye mtu pekee aliyekuwa Rais akiwa
mdogo kuliko marais wote wane hadi kufikia sasa. Swali la msingi la
kujiuliza, je nini maoni ya wananchi kuhusu utendaji wa wanasiasa vijana na
Matarajio yao kwa vijana kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015 yakoje?

1.1

Kuhusu Tanzania

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Muungano wa nchi mbili za Tanganyika


na Zanzibar, zilizokuwa nchi moja tangu tarehe 26 Aprili, 1964. Nchi hizi
mbili zilipata uhuru wake kwa nyakati tofauti Tanganyika ikiwa imepata uhuru
mwaka 1961 kutoka kwa Waingereza na Zanzibar ikipata uhuru wake mwaka
1

Jacob Daniel Kateri, born in 1978 witnessed politicians contesting coming to see my
father for an entry strategy, but I never saw youth in 1985 to 1995 as it is today.
2
Late Daniel S. Kateri (1932-2007) in his life-time having worked to his retirement as
civil servant was such a sage who with his wisdom made our home a landing hub for most
politicians who intended to contest for various political posts in Same district, ward and even
village.

1963 kwa njia ya mapinduzi kutoka katika utawala wa Kisultani. Kufuatia


Muungano wa Tanganyika iliyokuwa inaongozwa na Chama cha Siasa cha
TANU na Zanzibar iliyokuwa inaongozwa na Chama cha Siasa cha ASP,
vyama hivi vilikuja kuungana tarehe 05 Februari, 1977 na kuwa chama
kimoja ambacho ni Chama cha Mapinduzi (CCM) ambacho ndicho chama
tawala hadi sasa nchini Tanzania, na moja ya vyama vya siasa vikongwe
barani Afrika.
Kwa kuzingatia wimbi la demokrasia duniani, Tanzania iliingia katika siasa za
vyama vingi tangu mwaka 1992; mfumo uliopokelewa kama chachu ya
kupanua fursa za kuendesha nchi kwa misingi ya utawala bora, uwajibikaji na
uwazi ili kuongeza tija katika nyanja mbalimbali za kiutawala, siasa na hata
uchumi. Kwa msukumo huo, siasa za vyama vingi ziliendeshwa kupitia
chaguzi kuu nchini kuanzia mwaka 1995, 2000, 2005 na 2010; na hadi utafiti
huu unafanyika, ni sehemu ya kutathmini utendaji wa kundi muhimu la
kijamii, yaani kundi la vijana linalosongwa na pamoja na mambo mengine,
ukosefu wa ajira. Hivyo basi, siasa inachukuliwa kama sehemu ya vijana
kuonyesha uwezo na umahiri wao kiuongozi lakini pia ufumbuzi wa tatizo la
ajira.
Katika kipindi chote cha siasa za vyama vingi hapa nchini, wagombea
wamekuwa wakitumia fursa ya kikatiba kugombea nafasi mbalimbali bila ya
kujali jinsia, itikadi, dini na hata kabila. Wanawake kwa namna ya pekee
wamekuwa wakipewa nafasi za viti maalumu3 ili kuhakikisha wanapata
uwakilishi katika nyadhifa muhimu kwa viti vya udiwani na ubunge. Nafasi
hizi za viti maalumu hazijatokea kupendekezwa ama kutolewa kwa vijana
kama kundi muhimu linalopaswa kupewa nafasi, na hivyo wengi wao katika
zama hizi wanafanya jitihada kugombea nafasi mbalimbali za uchaguzi mkuu
kama vile udiwani na ubunge.
Ni wazi kwamba Tanzania ni moja ya nchi duniani ambazo katika ngazi za
vyama vya siasa i.e. Chama tawala na hata vyama vya upinzani, vijana
wamekuwa wakipewa nafasi kubwa katika uongozi wa juu. Nafasi
walizokwisha shika vijana ni pamoja na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Naibu
Makatibu Wakuu Taifa, Wajumbe wa Mkutano Mkuu katika vyama vyao (WaNEC), Wasemaji wa vyama, n.k. Kupitia nafasi za kuchaguliwa kupitia
Uchaguzi Mkuu, Taifa letu limeshuhudia vijana wanasiasa na hasa wabunge
wa Chama Tawala wakipewa nyadhifa kubwa za Uwaziri, Naibu Waziri,
Wenyeviti wa Kamati muhimu za Bunge, na wengine kwa jitihada zao na
3

Viti Maalumu Wanawake refers to special seats reserved for women in decision
making bodies.

uzalendo kwa Taifa wakiibua mambo makubwa ya kimaslahi kwa Taifa kwa
ujasiri mkubwa na umahiri.
Pia katika kipindi kifupi, tumeshuhudia vijana katika nyadhifa mbalimbali za
kisiasa, wakiwajibika pale ambapo wanahusika aidha moja kwa moja au hata
sio moja kwa moja, na hivyo kuachia nyadhifa zao kama sehemu ya
uwajibikaji. Katika hali hiyo, tumeona misimamo ya vijana hao na uaminifu
wao kwa vyama, serikali na hata kwa wananchi, huku wakipokea anguko za
kisiasa kwa ukomavu wa kisiasa kama sehemu ya uawjibikaji.

1.2

Kuhusu TEDRO

Asasi isiyo ya kiserikali ijulikanayo kwa jina la TEDRO i.e. Tanzania


Education Development Research Organization ilianzishwa Machi 2011
kwa lengo la kuendesha utafiti katika Sekta ya Elimu nchini. Hadi sasa asasi
ya TEDRO inaendesha utafiti wa Mitandao ya kijamii inavyoathiri wanafunzi
wa sekondari na kutazama njia rafiki katika kutumia mitandao hiyo kama njia
ya kujifunzia na kuendeleza sekta nzima ya elimu. 4 Pia kwa kutambua kuwa
demokrasia ni suala mtambuka na vijana ni chachu katika jamii, TEDRO
imeamua kuendesha pia utafiti huu wa Ushiriki wa Vijana katika
Siasa kama wagombea. Utafiti tunaouendesha ni muendelezo wa
uchambuzi wa changamoto za elimu, ndani ya dira ya TEDRO na program ya
mchango wa elimu katika kufungua fursa za ajira, siasa ikiwa mojawapo ya
fursa zenye kimbilio la vijana leo hii. Ni dhahiri kwamba, uwezo wa wahitimu
wa ngazi yoyote kupata ajira hutokana na elimu waliyoipata, hutoa taswira
ya ubora wa elimu yenyewe.
Kama inavyojieleza, maendeleo ya elimu yanaweza kujulikana katika utendaji
wa wataalamu waliopatiwa elimu na ufanisi wao. TEDRO kwa kupitia
programu ya Tanzania Education System and Competence in the
Career inayotazama kwa kina jinsi gani elimu itolewayo inakidhi hitaji la
soko na uwezo wa wahitimu katika soko; kwa awamu ya kwanza kabisa,
shirika letu limetumia fursa na kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu
4

ICT & Media in Tanzania Education System: An Exploratory Study towards understanding
ICT & Media Threats among Urban Students in Tanzania (The study underway was granted
research permit from COSTECH on 28th April, 2014.

kukusanya maoni toka kwa wananchi ili kutathmini vijana walioingia katika
siasa kupitia uchaguzi Mkuu tangu mwaka 2000 hadi sasa.
TEDRO yenye makao yake Makuu Dar es Salaam, kwa kupitia utafiti huu
inawapa vijana walioko katika siasa fursa ya kujitathmini kupitia maoni ya
wananchi yaliyotolewa katika ripoti hii na hivyo kuweza kujiaandaa kwa
ufanisi zaidi wanapoelekea uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Utafiti huu
unaojulikana kama Vijana katika Siasa Kuelekea Uchaguzi Mkuu
2015 ni kichocheo muhimu katika kuwafanya vijana na hata wanasiasa
wengine kuwa makini katika siasa na kuelewa kuwa, katika utendaji mzuri
wenye kuwatumikia watu, siasa yaweza kuwa nyenzo muhimu katika kutatua
changamoto za kimaendeleo katika Taifa letu.
Ni wazi kwamba vijana wamekuwa na msukumo mdogo sana kushiriki katika
kupiga kura, na hata kuomba kupigiwa kura kama wagombea, jambo
linaloweza kuwa na ushawishi hasi kwa jamii nzima. Likiwa ni kundi
linalopenda mabadiliko kama ilivyo popote duniani, vijana wanakuwa na
mwamko mkubwa pale wanapoona kijana mwenzao, wa rika lao, wa
mazingira yao, ajuaye shida zao anagombea kwa nafasi ya kuchaguliwa. Kwa
tathmini ya muonekano kupitia uchaguzi wa serikali za Mtaa, maeneo mengi
vijana wamejitokeza kwa wingi kupiga kura na hata kugombea. Yawezekana,
vijana wamejitokeza aidha kwa sababu wagombea waliokuwepo ni vijana pia,
au vijana wamegombea zaidi kwa sababu wapiga kura vijana
wameongezeka, au elimu ya uraia imetolewa vya kutosha.

1.3

Malengo ya utafiti huu

Ni dhahiri kwamba huu ni utafiti wa kwanza na wa pekee kufanywa na asasi


ya TEDRO. Lengo kuu likiwa ni kutathmini ushiriki wa vijana katika siasa
kama wagombea, namna vijana wanavyopokelewa na wanachi katika siasa
na matarajio tunapoelekea uchaguzi mkuu wa 2015. Lengo hili kuu,
limepelekea utafiti huu kuchambua malengo mahususi manne yafuatayo:
(i)
(ii)
(iii)
(iv)

Ushiriki wa vijana katika siasa kama wagombea


Mchango wa wanasiasa vijana katika kufuata misingi ya utawala
bora na uwajibikaji
Utekelezaji wa ahadi za wagombea kwa wapiga kura
Matarajio ya wananchi kwa vijana tunapoelekea uchaguzi Mkuu wa
2015.

1.4
i.

Maswali ya msingi katika utafiti huu

iv.

Kuna mwenendo gani wanasiasa vijana katika uchaguzi mkuu kama


wagombea?
Ni kwa kiasi gani vijana wanasiasa huongoza kwa kufuata misingi ya
utawala bora?
Ni kwa kiasi gani vijana wanasiasa wa kuchaguliwa wametekeleza
ahadi na matarajio ya wapiga kura?
Nini matarajio ya wananchi kwa vijana?

1.5

Matarajio ya utafiti huu

ii.
iii.

i.

ii.

iii.

iv.

Kwa matokeo ya utafiti huu, ni matarajio ya asasi yetu ya TEDRO kuwa


wasomaji wetu na watanzania kwa ujumla, hususani wananchi na
vijana wenye nia za kujihusisha na siasa, watatambua kuwa kundi la
vijana lina wajibu mahususi katika kukuza demokrasia na utawala bora.
N hivyo, kuongeza ushiriki wa vijana katika kutatua changamoto za
maendeleo katika Taifa letu.
Pia utafiti huu umetoa nafasi ya wananchi kutoa maoni yao kuhusu
namna vijana wanavyotumikia nafasi zao za kisiasa kama viongozi wa
watu kwa kufuata misingi ya utawala bora; hivyo basi wananchi
wamezingatia mambo yaliyoulizwa kama ushirikishwaji katika
maamuzi, kupiga vita rushwa na uwazi katika mambo yanayohusu
maslahi ya taifa kwani ndio dhana zilizoweza kufafanua maana ya
utawala bora.
Kwa kuelewa usemi wa wahenga kuwa ahadi ni deni utafiti huu
unatoa changamoto kwa vijana walioko madarakani na wanaotarajia
kugombea nyadhifa mbalimbali kutambua kuwa kutekeleza ahadi ni
moja ya vitu vinavyopelekea kijana na hata mgombea mwingine
kupata ushawishishi, kukubalika na hata kuaminika katika jamii.
Kutoa mtazamo wa jumla toka kwa wananchi kuhusiana na wanasiasa
vijana Taifa linapoelekea Uchaguzi Mkuu wa 2015.

2.

Mapitio ya maandiko na tafiti zilizopita

2.1

Tafsiri ya kina kuhusu dhana ya Vijana

Utafiti huu unaohusisha vijana katika nyanja ya siasa, unaanza kwa


kuchambua dhana ya kijana. Tafsiri mahususi ni ile ya umri kati ya miaka 18
hadi 25, na wakati mwingine kati ya miaka 18 hadi 35. Zaidi ya maana za
7

kidemographia, katiba inatambua kijana kwa misingi ya kupiga kura kwamba


inaanzia miaka 18 na kuendelea, wakati kugombea nafasi za uongozi katika
siasa umri wa kuanzia in miaka 25 na kuendelea kwa nafasi ya udiwani na
ubunge, wakati nafasi ya uraisi huanzia miaka 40 na kuendelea.
Licha ya kwamba maana ya kidemographia, kijana ni miaka 18 hadi 35, ni
dhahiri kwamba kwa maana ya kijana ileambapo tunaenda zaidi kwa kuweka
bayana kwamba umri halisi wa kikatiba wa kugombea nafasi za kisiasa za
udiwani na ubunge huanzia miaka 25 hadi 35 na kwa nafasi ya uraisi huanzia
miaka 40 na kuendelea. Tafsiri hii pana ya kijana imeweza hata
kuzishawishi fikra za wananchi na umma wa ulimwengu huu kwamba endapo
mtu akiwa raisi katika umri wa hadi kufikia miaka 55 bado anachukuliwa ni
raisi kijana.
Ni wazi kwamba hata Mheshimiwa Raisi Jakaya Mrisho Kikwete aliyeanza
kutumikia Wadhifa wa Uraisi akiwa na miaka 55 watu walimpokea kama Rais
kijana, japo katika maana halisi ya kijana sio sahihi ila katika mtazamo
mpana na ulinganishi na watanglizi wake, alitambulikana kama kijana. Ni
wazi kwamba historia inabaki kuwa aliyebeba madaraka haya makubwa ya
Urais akiwa kijana zaidi ni Hayati Baba wa Taifa Julius Kambarage Nyerere
akiwa na miaka 39 alikuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Tanganyika na akiwa
na miaka 40 akawa Raisi wa kwanza wa Tanganyika.
Kuondoa utata wa tafsiri ya neno kijana kutoka uhalisia wa miaka 18 hadi
35, utafiti huu unawajumuisha vijana wanasiasa wote waliokuwa na miaka
isiyozidi 35 kuanzia mwaka 2000 ili kuweza kukidhi tafsiri pana ya mtazamo
wa walio wengi kuhusu neno kijana katika nyanja ya siasa na utawala kwa
utamaduni wa Afrika.
Ikiwa vijana ni kundi lenye watu wengi nchini ukilinganisha na makundi
mengine, faida ya uwingi wa kundi hili, ni pale tu litakapotumika kama nyezo
ya kujenga demokrasia na ushawishi; na ili kuwafanya wawe chachu ya
mabadiliko katika siasa.5
Kuna ushahidi hadi likitoka andiko la Ellis (2007) kuwa ushiriki wa vijana
katika siasa ulikuwa mdogo ukilinganisha na watu wa rika zingine popote
duniani. Upigaji kura kama moja ya misingi ya ushiriki katika siasa na
demokrasia ni mfano halisi uliokwisha kuwa na ushiriki mdogo wa vijana. Hii
inaenda hata katika ushiriki wa vijana katika uanachama na uongoi katika
siasa na hata mabunge. Hali hii imetafsiriwa na Ellis (2007) kuwa inatokana
na mifumo ya kiutawala nje ya serikali, mfano utawala wa kimila ambao
5

www.fes-tanzania.orgnational-activitiesyoung-leaders-training-programme.html translated.

hufuata umri katika uongozi na kutotoa fursa kwa vijana kuwa viongozi (Ellis,
2007).
Vikwazo katika ushiriki wa kijana ni pamoja na umri wa kikatiba katika kupiga
kura au kugombea nafasi za kisiasa. Umri wa kupiga kura kwa nchi ya
Tanzania huanzia miaka 18, wakati nchi a Amerika ya kusini ni miaka 16,
wakati Indonesia na Korea ni miaka 17, Cameroon na Japan miaka 20, Cote
DVore, Gabon, Singapore, UAE na Pakistan ni miaka 21. Ila umri wa kupiga
kura kwa Africa ni kama Tanzania ambao wastani wake pote ni miaka 18.
Hakuna tafiti zilizotoa angalizo au pingamizi la umri endapo, kuwaacha vijana
hadi miaka 18 ndio waanze kushiriki kupiga kura ni chanzo cha wao hata pale
umri unapofika huacha kushiriki ama vinginevyo (UNICEF & United Nations
Programme on Youth, 2011).
Imethibitika kwamba demokrasia ya zama hizi zenye kuwahusisha kwa kiasi
kikubwa vijana katika mchakato wa siasa ni jambo la msingi. Ushiriki wa
kundi la vijana hufanya zile tunu msingi za kidemokrasia zionyeshe uhai
wake na hivyo kuzuia utawala usio na kikomo kudumu katika siasa za leo na
hata baadae.
Andiko lililofanywa na shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP
(2011) limeweka wazi dhamira ya dhati iliyo nayo jumuiya ya kimataifa
katika kutambua umuhimu wa vijana katika siasa, kwa kuzingatia kwamba
vijana ni chachu ya mabadiliko, kama ilivyo katika kanuni za Umoja wa
Mataifa.6
Katika andiko la mwanazuoni nguli wa zama za leo, hayati Chachage (2005),
amejadili mtazamo wa tafsiri ya wanasayansi ya jamii kuhusu kuibuka na
kushamiri kwa muamko wa vijana katika siasa ikiwa ni pamoja na mapungufu
ya watangulizi katika kutimiza mahitaji ya jamii husika. Wengine wakienda
mbali zaidi na kusema ni ishara ya vijana kutoridhika na hali iliyopo au ilivyo
kwa wakati husika; na hivyo shauku na muamko wa vijana ni tamaa ya
kutaka kufanya vizuri zaidi ama tofauti kwa maslahi na matakwa ya kizazi
cha vijana. Iwe iwavyo, tafsiri inabaki kuwa msukumo wa vijana hautokani na
kingine chochote, bali shauku ya mabadiliko, yote yakiwa ni msukumo
utokanao na mabadiliko yatokeayo kwinginepo duniani (Chachage, 2005).
Pia upo mtazamo kuwa, msukumo wa vijana unatokana na mfumo wa
kidesturi kushindwa kutimiza matakwa ya kizazi na jamii ya sasa; ikiwa ni
pamoja na ongezeko la uelewa wa haki na wajibu wa kiraia alionao kijana
6

The UN has long recognized that Youth are major human resources for development and
key agents for social change, economic growth and technological innovation.

katika jamii; huku wakijiona kuwa wanaweza kuwa na njia mbadala na


madhubuti za kutatua matatizo yaliyopo (Ibid).
Chachage (2005) anaweka bayana mtazamo kinzani 7 na msukumo wa vijana
katika zama za leo. Japokuwa imezoeleka kwamba vijana ni taifa la kesho,
fikra hizi zilipata upinzani mkubwa nchini Tanzania miaka ya 1980, vijana
walipaza sauti zao wakisema, vijana ni taifa la leo 8. Pia utafiti huu
umemnukuu mwanafalsafa na mwanahistoria nguli wa Ufaransa Frantz Fanon
aliyesema (Nukuu niliyoitafsiri):
Kila kizazi ni lazima kuyatambue malengo yake, kiyatekeleze au
kuyasaliti9
Usemi huu umetafsiriwa kuwa wajibu wa vijana kwa siku zijazo hutegemeana
na jinsi wanavyotumia fursa walizonazo wakati huu, rasilimali walizonazo
wakati huu, na hivyo, kuacha jukumu la kuiandaa kesho waitamaniyo kwa
kizazi kingine ni usaliti.
Katika hotuba yake ya kuhitimisha siku ya Viongozi vijana duniani kupitia, USAfrica Leaders Summit, Rais wa Marekani Barack Obama alisema mataifa ya
Africa hayana budi kuwekeza kwa viongozi vijana kwani kundi hili linaweza
kupaza sauti na kusikika (huenda ni kwa sababu ni wapenda mabadiliko,
wana nguvu na pia ni wengi). Kundi hili laweza kuwa chachu ya kuleta
mabadiliko katika kilimo, kupiga vita maradhi na hata kuleta amani katika
bara la Afrika (Washington D.C, Agusti 6, 2014).10
Ushawishi katika kuwahusisha vijana katika siasa na uongozi pia
umesisitizwa na watu maarufu duniani akiwepo Dr. Koffi Annan, aliyekuwa
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, katika nukuu inayotafsirika kama
ifuatavyo:
Hakuna aliyezaliwa raia mwema, hakuna taifa lililoanza likiwa la
kidemokrasia. Bali, yote ni michakato inayokuja katika kipindi fulani
cha kihistoria wa uhai wa mtu au taifa husika. Hivyo, vijana
wanatakiwa kuhusishwa kutoka wanapozaliwa, kwa kuwa taifa
7

Traditional thinking that Vijana ni taifa la kesho translated to Youth are the nation of
tomorrow
8
After 1980s youth contests led to rethinking that Vijana ni taifa la leo translated to Youth
are the nation of today
9
Frantz Fanon once contended, each generation must out of necessity, discover its mission,
fulfill it, or betray it.
10
American President Barack Obama remarks at the US-Africn Leaders Summit that focused
on, Investing in Africas Future

10

llinalowatenga vijana linajilaani a kujichimbia kaburi la kifo 11 (Koffi


Annan, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa).
Katibu Mkuu wa UN aliyeko madarakani Ban Ki Moon ameendelea kuiagiza
taasisi ya Umoja wa Mataifa ya United Nations Inter-Agency Network on
Youth and Development kutoa hamasa kwa vijana ulimwenguni pote kushiriki
katika siasa, uongozi na kukuza demokrasia na utawala bora. 12 Andiko la
ripoti ya UNDP (2012) limetoa msisitizo, 13 kama ilivyowekwa katika tafsiri ya
Kiswahili ya utafiti huu:
Ni lazima vijana wapewe nafasi katika kufanya maamuzi kuanzia ngazi
za chini, ngazi ya taifa and hata kimataifa (Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja
wa Mataifa, Ban Ki-moon).

3.

Maelezo Kuhusu Mbinu ya Utafiti

3.1

Utangulizi

Utafiti huu umeandaliwa na kufanyika Tanzania Bara (Tanzania Visiwani


haikuhusishwa katika awamu hii) na ni utafiti wa kwanza kufanywa
unaousiana na ushiriki wa vijana katika siasa. Maeneo yaliyohusishwa katika
utafiti huu ni kanda za kijiographia hapa nchini ili kuwezesha uhusishwaji
mpana wa Watanzania. Katika kila kanda, utafiti huu umehusisha wilaya 1
hadi 3, na katika kila wilaya, wamehojiwa wananchi wa vijiji vitatu, ambavyo
vingine vipo katika kata moja ama kata tofauti kwa kuzingatia siasa za eneo
husika. Katika kila kijiji, wamehojiwa watu 15. Vijiji hivi vimechaguliwa
makusudi katika kila wilaya kwa kuzingatia vuguvugu za kisiasa zama hizi za
vyama vingi, ili mitazamo isiathiriwe na mwelekeo wa wananchi wa vijiji
vilivyo chini ya ushawishi wa chama kimoja.

3.2

Mgawanyo wa maeneo yaliyohusishwa

11

Koffi Annan, once said that No one is born a good citizen, no nation is born democratic.
Rather both are processes that continue to evolve over a lifetime. Young people must be
included, since the society that custs itself off from its youth servers, is condemned to bleed
to death
12
UNDP (2012), Enhancing Youth Political Participation throughout Electoral Circle, A Good
Practice Guide.
13
Youth should be given a chance to take an active part in the decision making at local
national and global levels said, Ban Ki-moon.

11

Awali ya yote, watafiti wa TEDRO kwa kutambua ukumbwa wa nchi yetu ya


Tanzania, hususani Tanzania bara ambapo utafiti huu umefanyika kwa
awamu ya kwanza waliweza kutafuta tafsiri ya migawanyo kikanda, wilaya,
majimbo ya uchaguzi na vijiji. Mambo mengine ni pamoja na tofauti ya itikadi
za kisiasa, upatikanaji wa habari muhimu kuhusiana na siasa na uhalisia wa
wananchi waishio mijini na vijijini. Mgawanyo huu ulikuwa kama jedwali
linavyoonyesha:

Kanda

Wilaya/
majimbo
Uchaguzi

Mashariki na Pwani

Morogoro, Kinondoni & Kisarawe

Vijiji 3 kila Wilaya

Kusini

Kilwa, Lindi Mjini & Mtwara Mjini

Vijiji 3 kila Wilaya

Nyanda za Juu Kusini

Njombe, Mbeya Mjini na Ludewa

Vijiji 3 kila Wilaya

Kanda ya Kati & Kaskazini


Magharibi

Singida Mjini, Kasulu & Kigoma

Vijiji 3 kila Wilaya

Kanda ya Kaskazini

Tanga Mjini,
Arumeru

Kanda ya Ziwa

Bukoba Vijijini,
Nyamagana

Jumla

Wilaya 18 Tanzania

IDADI
YA
WALIOHOJIWA

3.3

Moshi

ya Vijiji

Vijijini

&

Vijiji 3 kila Wilaya

Biharamulo

&

Vijiji 3 kila Wilaya

WAANCHI

Vijiji 54 Tanzania
WANANCHI 910

Hatua zilizofuatwa katika kuufanya utafiti huu

Wataalamu wa TEDRO walitoa mafunzo kwa ajili ya kukusanya taarifa za


utafiti huu, ambapo watafiti wasaidizi 25 walipatiwa mafunzo. Watafiti
wasaidizi hao ni wahitimu vyuo ambao walichukuliwa kwa kazi hii kwa
kuzingata uzoefu na uadilifu wao katika kufanya kazi ya aina hii. Watafiti
hawa walishiriki mafunzo na kisha kufanya majaribio (Pilot) ambapo pamoja
na mambo mengine, majaribio yalipima endapo dodoso linaeleweka kwa
wananchi na muda ambao watafiti wasaidizi watatumia ili kukamilisha kazi

12

hii. Marekebisho ya muhimu yalifanyika ili kuwezesha walengwa kuelewa na


hivyo kutoa taarifa sahihi kwa kazi hii.

3.4

Mambo ya kiitifaki, ruhusa na maadili

Kama ilivyo kwa tafiti zinginezo, utafiti huu uliandaliwa na andiko lake
limekabidhiwa kwa Tume ya Sayansi na Teknolojia, ambayo ndio mamlaka
yenye dhamana ya kutoa ruhusa ili utafiti kufanyika. Pia utafiti huu
umehusisha kujitambulisha kwa watafiti wa TEDRO katika mamlaka za
kiutawala mikoani na wilayani. Mara nyingi, watafiti walipeleka barua ya
utambulisho kwa Ofisi ya Mkurugenzi wa kila wilaya iliyohusika, na wakati
mwingine barua ya utambulisho ilianzia kwa Katibu Tawala wa Mkoa (RAS),
Wilaya (DAS) nas kwa Mkurugenzi (DED).
Baadhi ya Wilaya watafiti walipatiwa barua za ruhusa na baadhi ya wilaya
ambapo walichelewa kutoa ruhusa, watafiti waliendelea kukusanya taarifa,
hasa pale ilipotokea kuwa wanagharamika wilayani kwa siku zaidi ya mbili
bila kufanya kazi tangu wafikishe barua wilayani, na kulazimika kutumia
nakala ya barua ya Utambulisho kutoka TEDRO kukusanya taarifa; na pale
ilipotokea kuwa ruhusa haikutolewa ofisi ilishauri waende wilaya walizotoa
ruhusa kufanikisha zoezi la utafiti kwa wakati na kwa gharama iliyokuwa
katika uwezo wa ofisi yetu. Kwa sababu za kiitifaki na urasimu katika
kufuatilia ruhusa, utafiti huu uliotarajiwa kuhusisha wilaya 24 hapo awali kwa
sampuli ya vijiji 72 na wahojiwa 1,080, hatimaye ni asilimia 84.2% maeneo
yaliyotarajiwa yaliweza kufikiwa.
Kila watafiti walipoenda kukusanya taarifa walijitambulisha kwa mhojiwa
ambaye alikuwa mwananchi mwenye umri wa miaka 18 na zaidi,
waliyemkuta katika kaya, maeneo ya kazi na hata katika biashara na kuomba
kufanya mazungumzo naye yanayohusu vijana na ajira, hususani wale
walioko katika siasa tayari ama wagombea watarajiwa.
Kaya ilitambulika pale ambapo kijiji au mtaa husika uliweza kufahamika
sehemu ya huduma muhimu kwa umma kama hospitali, shule ama kitua cha
magari au soko, wakati mwingine njia panda na hata makutano ya barabara
yalitumika ili kupata sehemu ya kuanzia. Mtafiti wa TEDRO alitumia eneo hili
kama sehemu ya kuanzia huku akihesabu nyumba tano kwenda pande kuu
tatu kufuatia mahali alipofikia palivyo. Kila kaya alipohoji, aliruka kaya tatu
na kuchukua kaya ya nne kwa kila upande hadi kukamilisha idadi ya
wahojiwa. Mambo yaliyozingatiwa ni jinsia ya mhojiwa na umri kwa maana
13

pana ya motto wa kike ama wa kiume kwenye miaka 18 katika kaya, mzazi
wa kiume au mzazi wa kike. Makundi yalizingatiwa kila mtafiti alipotoka kaya
moja kwenda nyingine.
Watafiti waliaswa na kusimamiwa ili kuhakikisha wanakusanya taarifa za
kweli ili kufanya utafiti huu uakisi ukweli wa kimtazamo wa wananchi
waliohojiwa na kuufanya kuwa andiko lenye kuweza kufanyiwa rejea wakati
wa kufanya tathmini za kisiasa na hata kuwezesha kundi la vijana wanasiasa
kutumia utafiti huu kujifunza na kujitathmini wanapojiandaa kushiriki
uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Angalizo lingine kwa watafiti lilikuwa ni
kuhakikisha wanakwepa makundi yenye ushawishi wa ghasia na ushabiki wa
kisiasa ili kuwaepusha na vurugu pale ambapo hakuna uvumilivu wa kisiasa
ama maeneo yenye migogoro yenye kutafsiriwa kuwa ya kisiasa. Haya yote
yalizingatiwa hadi hatua ya ukusanyaji taarifa ikakamilika bila kupokea
taarifa za uvunjifu wa amani maeneo taarifa zilipokusanywa.

3.5

Kuingiza taarifa na kuandaa ripoti

Taarifa zimeingizwa kwa kutumia SPSS 14 i.e. ambao ni mfumo wa uingizaji


data na kuziweka katika namna ziwezavyo kuhusianishwa kirahisi. Waingiza
taarifa walipatiwa mafunzo maalumu na wakisimamiwa na Msimamizi wa
uingizaji taarifa aliyeandaa mfumo mzima wa kuingizia taarifa. Wataalamu
katika utafiti waliohusishwa katika uandaaji wa andiko la utafiti huu
walishirikishwa katika kutumia taarifa zilizokusanywa na kuingizwa katika
mfumo wa data wa komputa.

14

SPSS statistical Package for Social Science Studies

14

4.

Matokeo ya Utafiti

4.1

Taarifa binafsi za kidemografia

Utafiti huu uliotarajiwa kuhusisha wilaya 24 Tanzania Bara, umeendeshwa katika


wilaya 18, kila wilaya ikiwa imewakilishwa na wahojiwa 45 waliochaguliwa 15
kutoka kila kijiji; hivyo utafiti huu kuhusisha vijiji 54 kwa ujumla. Wilaya ambapo
utafiti umefanyika ni Njombe Mjini, Ludewa, Mbeya Mjini, Kilwa, Lindi Mjini, Mtwara
Mjini, Morogoro Mjini, Kisarawe, Kinondoni, Tanga Mjini, Vunjo, Arumeru, Singida,
Kasulu, Kigoma Mjini, Bukoba Vijijini, Biharamulo na Mwanza Mjini (Nyamagana).
Katika utafiti huu, taarifa binafsi za wahojiwa zilizokusanywa ni pamoja na zile
zinazohusu umri wa wahojiwa, jinsia, hali ya ndoa, kazi, kiwango cha elimu na
vyama vya siasa vinanvyoongoza majimbo sehemu uchaguzi ulipofanyika.
Taarifa binafsi za Wahojiwa

(i)

Wahojiwa walikuwa wa makundi ya umri mbalimbali, na taarifa zinaonyesha


wahojiwa wa umri kati ya miaka hadi 20 ni 8%, miaka 21 hadi 30 ni 32%,
miaka 31 40 ni 32%, miaka 41 50 ni 13%, miaka 51 hadi 60 ni 13% na
Zaidi ya miaka 60 ni 2%.

15

(ii)

Kuhusiana na jinsia ya waliohojiwa, taarifa zinaonyesha kuwa wanaume ni


58% na wanawake ni 42%. Uwiano huu katika jinsia unatoa fursa ya kwamba
hakuna kundi lililozidi kwa kiasi kikubwa kinachoweza kuathiri matokeo ya
utafiti kwa sababu tu kundi moja limetawala zaidi. Isitoshe, wanaume wana
ujasiri kuliko wanawake katika kukubali kuhojiwa, na hivyo hii huenda
imesababisha uwiano huu wa wanaume kuwa wengi zaidi kuliko wanawake.

(iii)

Hali ya ndoa nayo imepewa uzito katika kukusanya taarifa binafsi maana
ushiriki katika siasa na mambo ya kijamii kuna uhusiano wa karibu sana na
hali ya ndoa ya mhojiwa. Katika utafiti huu, wahojiwa ambao hawajaoa au
kuolewa ni 37% na waliooa/olewa ni 51% huku makundi mengine yakiwa ni
12% ambayo ni yale ya mzazi mmoja, watalaka na wajane.

(iv)

Taarifa nyingine muhimu kwa wahojiwa ilikuwa ya kiwango cha elimu,


inayoonyesha kuwa wahojiwa waliohitimu elimu ya msingi ni (40%),
sekondari (33%), chuo (23%) na wasiosoma wakiwa (4%).

(v)

Wahojiwa wamejitambulisha na kutaja itikadi zao ambapo, kwa ujumla wapo


wasio na vyama, na wapo wafuasi wa CCM, CHADEMA, CUF, TLP na NCCR
Mageuzi. Pia mahojiano yalihusisha majimbo ya uchaguzi ya vyama vya siasa
vyote vilivyoorodhoshwa hapa, isipokuwa UNDP na vyama visivyo na
uwakilishi bungeni.

4.2 Ushiriki wa Vijana katika nafasi za Uchaguzi Mkuu


4.2.1 Kugombea na Matokeo ya Uchaguzi
Utafiti huu umeandaliwa kwanza kutazama mwenendo wa ushiriki wa vijana katika
nafasi za uchaguzi mkuu kama wagombea, hususani udiwani na ubunge. Matokeo
yanaonyesha kuwa 65% ya wananchi waliohojiwa wanakiri kuwa vijana
wameshiriki katika kugombea nafasi za udiwani, huku 35% wakisema vijana
hawajashiriki kugombea nafasi hizo katika maeneo utafiti ulipofanyika. Kwa
upande wa vijana kugombea ubunge, 63% wanakiri kuwa vijana wamekuwa
wakigombea nafasi za ubunge na 37% wakisema hapana, hakujawa na ushiriki wa
vijana kugombea nafasi hizo katika maeneo yao.
Pia utafiti ulienda zaidi kutaka kujua endapo pale vijana walipoonyesha nia ya
kugombea, waliweza kushinda au walishindwa. Matokeo ya utafiti huonyesha kuwa
20% wanasema kijana alishinda udiwani tu, 32% wanasema kijana alishinda
ubunge tu, 30% wanasema vijana waliogombea walishinda maeneo yao katika
udiwani na ubunge pamoja, huku 18% wakisema vijana waliogombea
hawakushinda udiwani wala ubunge.
16

4.2.2 Sababu za kushinda Vijana


Utafiti huu umepelekea majibu mbalimbali ya sababu zilizofanya vijana washinde
katika nafasi walizogombea za uchaguzi mkuu, hususani udiwani na ubunge.
Sababu hizo ni kama zifuatazo na asilimia za waliozipendekeza:
Na
.

Sababu

Asilimia

1.

Kiwango cha elimu na uwezo wa kuelezea sera za vyama vyao

16%

2.

Kutaka mabadiliko, hivyo kuondoa waliokaa sana na kuweka


vijana

48%

3.

Kutoa ahadi zinazotekelezeka, ikiwepo ajira kwa vijana

6%

4.

Kuungwa mkono na vijana katika kampeni hadi siku ya kura

17%

5.

Kada mahiri wa chama chake, hivyo kaungwa mkono na chama

8%

17

chake
6.

Kugombea kupitia chama cha upinzani kupelekea vijana


kushinda

13%

9.

Ni chagua na kipenzi cha watu, kila kigombea kijana huleta


ushawishi

7%

10
.

Kulinda kura zisiibiwe, na hivyo kufanya vijana wakashinda

10%

11
.

Kupendelewa na kura kuibiwa

2%

12
.

Udhaifu wa watangulizi kushindwa kutekeleza ahadi walizotoa

6%

13
.

Amekuwa na jamii kwa karibu akitoa misaada mbalimbali

16%

4.2.3 Sababu za vijana kushindwa katika uchaguzi


Matokeo ya utafiti yanaonyesha kuwa, sio vijana wote walioshinda wakati wa
uchaguzi mkuu. Katika kutafuta sababu za kushindwa, zimejitokeza sababu nyingi
kama ifuatavyo:
Na
.

Sababu

Asilimia

1.

Rushwa ilitumika kuhakikisha kijana hapiti naye hakuwa na hela

23%

2.

Vijijini hawajaamua kuwapa vijana, bado wanataka wazee

3%

3.

Vijana wamekuja kwa kupitia Upinzani ambayo bado haikubaliki


maneo mengi ya vijijini

32%

4.

Aliyekuwepo
mwenyewe

aachie

6%

5.

Vijana hawaombi ushauri kwa wazee, wanakuja tu na kutukana


majukwaani

7%

6.

Kijana hakuwa amejipanga, na hivyo kushindwa kutetea kiti,


hakuwa na hela

24%

9.

Alikubali hongo ili matokeo yabadilishwe na hivyo kupoteza

26%

ni

mzee

na

anakubalika

18

sana

hadi

nafasi yake
10
.

Kuibiwa kura

4%

11
.

Kazi nzuri iliyofanywa na Mbunge aliyekuwepo haikuwapa


vijana nafasi tena

13%

12
.

Matusi na karaha za vijana waliotaka nafasi mbalimbali zilikera


wapiga kura, hasa wazee

6%

13
.

Hawana uzoefu na kazi hiyo

11%

4.2.4 Kuhusu ongezeko la Vijana katika siasa


Utafiti huu umetoa fursa kwa wananchi kutoa maoni kuhusiana na mtazamo kuwa
kumekuwa na ongezeko la vijana kuingia katika siasa kama wagombea wa nafasi
mbalimbali za uchaguzi mkuu. Mtazamo huu umetolewa majibu kama ifuatavyo:
83% wamesema ndio wanakubali kuwa kuna ongezekola vijana kuingia katika siasa;
4% wamesema kuwa hawakubaliani na mtazamo kuwa kuna ongezeko la vijana
kuingia katika siasa kama wagombea; na 13% hawajui. Mtazamo huo,
umewakilishwa katika mchoro unaofuata hapa chini.

19

4.2.5 Sababu za Vijana kuingia katika siasa kwa nafasi za Uchaguzi Mkuu
Utafiti huu uliweka sababu mbalimbali zinazoweza kuwa kichocheo cha vijana
kuingia katika siasa. Sababu kadhaa zimechukua uzito, hasa pale ambapo wananchi
aliohojiwa kuzikubali kuwa zimechangia vijana kuingia katika siasa. Sababu
zilizopewa nafasi kubwa na asilimia zake ni uzalendo 67%, kimbilio baada ya kukosa
ajira 57%, uwezo mdogo wa watangulizi wao katika nafasi husika 60%, mafanikio ya
wanasiasa vijana walio mahiri 72%, vyma vya siasa kuwapa vijana nafasi katika
vyama vyao 59%, kukubalika kwa vijana tu sababu ni vijana 63%. Matokeo haya
yameonyeshwa katika jedwali linalofuata chini:
Na
.

Sababu

Asilimia
Ndio

Hapan
a

Uzalendo

67%

33%

Uchu wa madaraka

37%

63%

Kimbilio baada ya kukosa ajira

43%

57%

Kushauriwa kugombea sababu ya umahiri wa vijana katika


siasa za zama hizi

50%

50%

Uwezo mdogo wa watangulizi wao

60%

40%

Mafanikio ya wanasiasa mahiri

72%

28%

Vyama vya siasa kuwapa nafasi vijana

59%

41%

Uwezo wa kielimu, hasa wanapohitimu shule na vyuo

47%

53%

Kukubalika kwa vijana

63%

37%

10

Kutumiwa na wanasiasa wakongwe wanaotaka kuwa na


watetezi wa maslahi yao

33%

67%

4.3 Wanasiasa vijana na misingi ya Utawala Bora


Utafiti huu ulitaja mambo ya kuzingatiwa katika hali ya kawaida ili kutambua
endapo misingi ya utawala bora imepewa nafasi katika utafiti huu. Mambo ya
msingi yalikuwa kujua ni kwa kiasi gani wanasiasa vijana wanafuata misingi ya
utawala bora wakiwa katika nyadhifa za kisiasa. Kwa vigezo vya utafiti wetu,
mambo yaliyopewa kipaumbele ni endapo hawajihusishi na vitendo vya rushwa
(23%), wanapinga na kukemea wala rushwa (67%), wanatumia mbinu shirikishi
20

katika utawala (42%), wanaweza kutengeneza mfumo wa kiuwajibikaji (31%), uwazi


(45%) na kufuata misingi ya utawala wa sheria (17%).

4.5

Matarajio ya Wananchi kwa Wanasiasa Vijana

4.5.1 Uwezekano wa Wanasiasa vijana kuendelea kushikilia nafasi zao


uchaguzi Mkuu 2015
Wananchi walipata fursa kupitia utafiti huu, kutoa mtazamo wao na maoni
kuhusiana na Matarajio yao kwa wanasiasa vijana katika nafasi ya udiwani. Katika
sehemu ya kwanza ya dhana hii, wananchi wametoa maoni yao kuhusiana na
wanasiasa hawa kuendelea kushikilia nafasi walizo nazo katika uchaguzi Mkuu wa
mwaka 2015. Mtazamo wa wananchi kwa kufuata vigezo vya utafiti wetu ni kwamba
waliosema watarejea wote (21%), Sio wote lakini zaidi ya nusu (23%), nusu yao
(11%), robo yao watarejea (6%), hawatarejea katika nafasi zao hata kidogo (33%)
na sijui (5%).
Upande wa Ubunge, wananchi walikuwa na maoni tofauti na yale ya udiwani.
Matokeo huonyesha kuwa 63% wanasema wabunge vijana wote watarejea katika
nafasi zao za kuchaguliwa; 20% wansema watarejea zaidi ya nusu, 4% wanasema
nusu yao watarejea, 2% watarejea robo, 4% hakuna atakayerejea tena katika nafasi
yake na 7% hawajui. Maoni haya yamewekwa katika kielelezo cha mchoro kama
ifuatavyo:

Sababu mbalimbali zimetolewa kutokana na maoni ya wananchi kwa upande wa


ubunge na upande wa udiwani, kila upande kwa nafasi yake. Jedwali lifuatalo
21

linaelezea sababu za kurejea na kutorejea kwa wanasiasa vijana katika nafasi zao.
Kwa upande wa udiwani sababu kuu zilizopelekea 21% kupendekeza kuwa
watarejea katika nafasi zao hutokana na kujituma, kutekeleza ahadi zao na kuwa na
uongozi shirikishi katika kutoa taarifa za maendeleo kwa wananchi. Kwa upande wa
ubunge, 62% waliosema watarejea katika nafasi zao uchaguzi mkuu ujao wametoa
sababu kuwa wanapigania wananchi, maslahi ya taifa na harakati zao zinaonekana
bungeni katika sakata za ufisadi ikiwamo Richmond na Escrow.
Pale ambapo 33% ya wananchi wamesema kuwa viongozi vijana wanasiasa
hawatarejea katika nafasi ya udiwani tena wametoa sababu kuwa ni
kutowashirikisha wananchi taarifa za maendeleo, kuwepo wagombea wanaokubalika
zaidi watakaogombea uchaguzi mkuu wa 2015 na pia hali ngumu ya maisha walio
nayo madiwani kwa kuishi kwa posho na sio mishahara yenye tija ukilinganisha na
wabunge. Kwa upande wa maoni toka kwa 4% ya wananchi kuwa wabunge vijana
hawatorejea nafasi zao, sababu ni kwamba hawajatimiza ahadi zao kwa wananchi
walizozitaja kuwa ni barabara za vijijini, huduma za maji afya na ajira kwa vijana.

4.5.2 Mtazamo wa Wananchi kukubali Rais kijana


Matokeo yanaonyesha kuwa wananchi wapo tayari kukubaliana na Rais kijana
endapo vyama vya siasa vitapendekeza mmoja wa wanasiasa vijana katika nafasi
hiyo. Kukubalika huko kumepokelewa kwa viwango tofauti, ambapo 82% wamesema
atakubalika, 11% wamesema hatakubalika, 7% wamesema hawajui. Maoni haya
yamewekwa katika kielelezo chini.

22

4.5.3 Wanasiasa Vijana wanaopewa nafasi kubwa endapo watasimamishwa


na chama tawala
Katika utafiti huu, tumetoa nafasi za kila mhojiwa kupendekeza wanasiasa vijana
watatu kwa nafasi ya Urais anaodhani kuwa wakisimamishwa na chama tawala
wana uwezo wa kutetea ilani ya chama, wana uwezo wa kutetea sera za chama na
kuhimili ushindani wa wapinzani na kukipelekea chama tawala kushinda katika
uchaguzi Mkuu wa 2015. Kati ya wote waliohusishwa katika kutoa maoni, ni 78% tu
waliotaja wanasiasa vijana, huku 13% wakitaja wasio vijana na 9% wakisema
hawaoni kijana anayefaa kwa nafasi hiyo.

Kwa kutumia mapendekezo yaliyotolewa na 78% ya wananchi waliohusishwa katika


utafiti huu, wanasiasa vijana 8 wamependekezwa na kila mmoja kupata asilimia
kadhaa ya waliotoa maoni. Wanasiasa vijana hao ni Mwigulu Nchemba 38%,
Emmanuel Nchimbi 24%, William Ngeleja 11%, Lazaro Nyalandu 10%, Hamisi
Kigwangala 7%, Deo Filikunjombe 5%, Esther Bulaya 2%, Wengine Wasio vijana 13,
Hakuna anayefaa 9%. Matokeo haya yamewakilishwa katikakielelezo kinachofuata
kama ifuatavyo:

23

4.5.4 Wanasiasa Vijana wanaopewa nafasi kubwa endapo watasimamishwa


na vyama vya Upinzani na ukiwamo umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa)

Kwa upande wa wanasiasa vijana kutoka chama cha upinzani na kupitia


vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), utafiti huu ulitoa
nafasi tatu za kupendekezwa majina ambayo kila mhojiwa alipendekeza
majina ya Wanasiasa vijana akifahamu kuwa wana uwezo wa kutetea sera za
vyama vyao na ambao wakitokea kupendekezwa na vyama vyao kugombea
nafasi ya Uraisi, wanangekubalika zaidi kwa wananchi.
Matokeo yanaonyesha kuwa ni 77% tu yawahojiwa walipendekeza majina ya
vijana hao, huku 16% wakisema hawaoni kijana kutoka upinzani na hata
katika umoja wa vyama vinavounda umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA),
24

na 7% wakisema hawajui. Wanasiasa waliopendekezwa na wananchi katika


utafiti huu ni James Mbatia (15%), Zitto Kabwe (18%), Tundu Lissu (11%),
Halima Mdee (6%), David Kafulila (9%), Julius Mtatiro (7%), John Mnyika
(11%), Joshua Nassari (3%) na Moses Machali 6% na waliosema hawajui
wakiwa 7%. Matokeo haya yamewakilishwa katika kielelezo kinachofuata.

Katika sehemu hii ya ripoti, uchambuzi wa waliopendekezwa unaweza uwe


umeathiriwa na mambo mengi ikiwa ni pamoja na mazingira na mwenendo
wa kisiasa wa kila aliyependekezwa.
Awali ya yote, waliopata nafasi za juu katika mapendekezo haya,
walishaonyesha dalili za kutangaza nia ya kuwania Urais, na hivyo
yawezekana kuwa wamejenga ushawishi kwa kiwango fulani, kiasi
kinachoweza kuathiri maoni yaliyopendekezwa.
Pili, historia a siasa nchini imekuwa ikipita katika hatua mbalimbali kufuatia
matukio kadhaa yahusuyo maslahi ya taifa, rasilimali za nchi, ufisadi na hata
uwajibishwaji kisiasa. Vijana wanasiasa vijana wamehusika aidha katika
kuibua hoja, au kuwajibishwa dhidi ya hoja zenye maslahi kwa taifa na wakati
25

mwingine wakiwa mstari wa mbele kupiga vita ufisadi. Matukio haya


yanweza kuwa sababu za nafasi za wanasiasa mbalimbali katika utafiti huu.
Tatu, kwa wanasiasa wa chama tawala wenye nyadhifa za uwaziri au naibu
waziri, wamekuwa katika nafasi za juu, ikiwa ni sababu inayoweza kuwafanya
wajulikane sana, na hata shughuli zao za kiuwaziri ama naibu waziri zikiwapa
nafasi kubwa ukilinganisha na wasio mawaziri na manaibu waziri. Sababu hii
inawapa nafasi Mh. Lazaro Nyalandu (Waziri wa Maliasili na utalii), Januari
Makamba (Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia), Mwigulu Nchemba (Naibu
Waziri wa Fedha), Emmanuel Nchimbi (aliyewahi kuwa Naibu Waziri na
Waziri), William Ngeleja (aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini).
Nne, nafasi za waliopendekezwa katika vyama vyao, mfano kwa kupitia
chama cha tawala, wabunge, manaibu mawaziri na mawaziri ni wajumbe wa
Halmashauri kuu ya chama, ni wajumbe wa Sekretarieti ya chama, na hata
kwa wanasiasa vijana wa vyama vya upinzani. Utendaji wao katika chama,
ushiriki wao katika kampeni zinazohusisha vyama vyao hadi kuwapelekea
ushindi ni sehemu ya mambo yayowashawishi wapiga kura na wanachama
walioshiriki katika kutoa maoni haya kadiri ya uchambuzi.
Pia, harakati za shughuli za kibunge ikiwa ni pamoja na umahiri wa wabunge
vijana kutoa hoja na hata kutetea hoja zao kupitia vyombo vya habari
ambapo wananchi huweza kuwajua na kuwatathmini. Fursa hii inawapa
nafasi kubwa wabunge wa upinzania wengi hawajatangaza nia na
hawategemei ila harakati zao bungeni zimekuwa kichocheo kwa wananchi
kwa kiasi kikubwa. Ni dhahiri kwamba licha ya Mbunge Zitto Kabwe kuwa nje
ya uongozi wa Chama, amepata nafasi kubwa katika mapendekezo ikiwa ni
pamoja na nafasi aliyonayo katika kuongoza kamati ya Kudumu ya Hesabu za
Serikali.
Kutumiwa na chama katika kampeni za chaguzi ndogo nayo inaweza kuwa
uwanja wa kisiasa kwa wanasiasa vijana kweza kufahamika, hasa pale
baadhi yao walipotokea kuwa mstari wa mbele kuendesha kampeni zilizovipa
vyama vyao ushindi.
Pamoja na mapendekezo ya wananchi, ni dhahiri kwamba wao kwa
kutofahamu au kwa kuridhishwa na utendaji wa wanasiasa vijana kadiri ya
mapendekezo, hawakuweza kuzingatia umri wa mgombea Urais kadiri
inavyopendekeza Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa sababu
hiyo, wapo wanasiasa vijana wasiofikisha umri wa kuwania Urais, lakini kwa
kuwa mapendekezo haya ndio yanayojenga kila mwanasiasa, utafiti huu
umeyawakilisha kadiri ya mapendekezo.
26

4.5.5 Wakishindanishwa vijana wote bila kujali itikadi za vyama


Matokeo ya utafiti huu unaonyesha kuwa endapo watashindanishwa vijana
wote bila kujali itikadi zao za vyama, matokeo yakaonyesha kuwa Mwigulu
Nchemba 27%, Zitto Kabwe 19%, Januari Makamba 16%, James Mbatia 11%,
Emmanuel Nchimbi 10%, Tundu Lissu 5%, Lazaro Nyalandu 4 wakati 8%
hawajui. Matokeo haya yameonyeshwa katika kielelezo kinachofuata.

4.5.6 Ungefanyika Uchaguzi leo vyama vyote vikiwa vimesimamisha


wanasiasa vijana
Sehemu hii ya utafiti, imejumuisha vyama vyote bila nchini, na maoni ya
wananchi yakionyesha kuwa 53.4% ya wananchi wangepigia kura Chama cha
Mapinduzi (CCM), 27.3% ya wananchi wangepigia kura Chama cha
Demokrasia na Mandeleo (CHADEMA), 7.3% wangepigia chama cha
Wananchi CUF, 4.4% wangepigia NCCR-Mageuzi, 0.6% TLP na 7% wakisema
hawajui. Matokeo ya sehemu hii yapo katika kielelezo kinachofuata.
27

28

Вам также может понравиться