Вы находитесь на странице: 1из 20

www.annuurpapers.co.tz au facebook:annuurpapers@yahoo.

com

AHLU SUNNA WAL JAMAA HAJJ AND UMRA TRUST

Sauti ya Waislamu

(14) WASITIRI WAZAZI WAKO!


Mtume(saw) aliwahimiza Masahaba kuwahijia
wenzao wasioweza kwa ugonjwa au uzee na
waliokufa katika Uislamu. Waislamu wengi wanakufa
bila kuhiji wakati waliwahi kupata uwezo wa kuhiji.
Umeshawaokoa wazazi wako na MOTO? Muda
unakwisha! Gharama zote kwa Hijja ni Dola 4,500.
Umra ya Ramadhani ni Dola 2,300. Karibuni
Ahlu Sunna Wal Jamaa kwa huduma nzuri na
uongozi bora. Wasiliana nasi: Tanzania Bara:
0765462022;0782804480; 0717224437.
ISSN 0856 - 3861 Na. 1183 RAMADHAN 1436, IJUMAA , JUNI 126-JULAI 2, 2015 BEI TShs 800/=, Kshs 50/= Zanzibar:0777468018;0777458075;0777845010.

Kijana Usamah Abdullah Rahim...

Amiminiwa risasi na Polisi, afariki


Apachikwa ugaidi kwa kukutwa na kisu
'John' auwa watu 9 kwa risasi wakisali
Aambiwa labda alikosea tu. Sio gaidi

Usamah Abdullah Rahim

Hali si shwari Zanzibar


Kamishna Magereza ashikilia uhai wa Sheikh
KAMISHNA Mkuu wa Magereza Jonh Casmir Minja.

Na Bakari Mwakangwale

WA K AT I m t u h u m i w a
wa kesi ya ugaidi Said
Amour, akishindwa kufika
Mahakamani kutokana na
maradhi gerezani, juhudi za
kupata kibali kwa ajili ya
matibabu yake zimekuwa
kitendawili.
Imeelezwa kuwa tangu
kuwasilishwa kwa ombi la
kupatiwa kibali kwa ajili ya
mtuhumiwa huyo kutibiwa

Seif akataliwa kuingia Barazani


Tuhuma nzito kwa Jecha, ZEC
CUF wampa orodha ya maluki

Hajatoa uamuzi Sheikh akatibiwe au la


Bassaleh, Kilemile wataka haki itendeke

katika hospitali maalum,


ni mwezi sasa kibali hicho
hakijatolewa.
Mbali na mtuhumiwa huyo,
imedaiwa kuwa watuhumiwa
wengine wawili ambao ni
mshitakiwa namba 16 Alawi
Othman Amir na mshitakiwa
namba 18 Amiri Hamisi Juma,

pia wameshindwa kufika


Mahakama ya Kisutu, wiki
iliyopita, kutokana na kuwa
wagonjwa.
Mshitakiwa namba 12
Said Amour, ni muda sasa
hajahudhuria Mahakamani

Inaendelea Uk. 2

Mwenyekiti wa ZEC, Jecha


Salim Jecha. Soma Uk. 8.

Maalim Seif Sharif Hamad.

Tahariri/Habari

2
AN-NUUR

S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786


Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM.
www.annuurpapers.co.tz
E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk
Ofisi zetu zipo: Manzese Tip Top
Usangi House, barabara ya Morogoro, D'Salaam

Vigogo wa Serikali wafutarishe


familiazaMasheikhwaUamsho
AMESEMA kweli
Mtume (s.a.w): Laiti
watu wangeaminiwa kwa
madai yao tu, kuna watu
wangedai damu na mali
za wengine.
B a s i n a i we j u u ya
mwenye kudai, kuleta
ushahidi wa madai yake.
Kanuni hii ya Uislamu,
ndiyo inayojenga msingi
wa mwenendo wa
mashitaka na kesi katika
mahakama, katika nchi
nyingi zinazoongozwa kwa
misingi ya Utawala Bora,
Haki na Sheria.
Kuwa mtu atakuwa hana
hatia mpaka atakapotiwa
hatiani na vyombo vya
kisheria vinavyohusika na
kutambulika.
Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania,
inamtuhumu Sheikh
Msellem Ali na wenzake
kadhaa kuwa ni magaidi.
Ni mwaka wa pili
sasa, serikali haijafikisha
ushahidi
wake
mahakamani kuthibitisha
madai yake.
Hata hivyo, kwa kipindi
chote hicho, watuhumiwa
wameendelea kuteseka
gerezani huku familia zao
nazo zikiishi katika tabu
kwa kukosa wasimamizi
na watafuta Rizki wakuu
wa familia.
Hii ni dhulma ya wazi
kwa misingi ya Kiislamu,
Utawala Bora, uadilifu
na UBINADAMU kwa
ujumla.
Ndio pale mafundisho
ya Uislamu yakaagiza
kuwa, yeyote mwenye
kumtuhumu mtu, basi
haraka alete ushahidi
kuthibitisha madai yake.
Na ikatolewa sababu
k u wa k wa m a u m b i l e
yake mwanadamu, lau
ataaminiwa tu kwa kila
analosema, basi kuna watu
watadai mpaka damu ya
watu wengine kuwa ni
mali na haki yao.
Na ili kuepuka adhabu
mbele ya Mwenyezi Mungu
hiyo siku ya Hukumu,
ambayo inaanzia mara tu
baada ya kutiwa kaburini,
Uislamu ukatoa angalizo

na mwongozo muhimu
sana:
K u wa , n i b o r a m t u
ukosee umwachie huru
(usimuadhibu) mtu mkosaji
kwa kukosa ushahidi wa
madhubuti, kuliko ufanye
kosa la kumwadhibu mtu
asiye na hatia.
Na tunaambiwa Dua ya
mwenye kudhulumiwa
haina pazia baina yake na
Mungu wake.
Hivi wenye mamlaka
na hasa walio Waislamu,
ambao hivi sasa
watakuwa katika Funga ya
Ramadhani, wanajisikiaje
wakitia nia ya funga na jioni
wakifuturu huku wakijua
kuwa kuna Waislamu
wenzao wasio na hatia
wapo ndani, wanafunga
na kuftari kwa chakula
cha gerezani wakati sio
wafungwa!
Wan ako s a ta ra we h e
na Qiyamul Lail katika
misikiti yao. Wanakosa
kuendesha darsa za Quran
katika kipindi hiki cha
Shahru Ramadhaan ladhii
unzila fiihi lQuran!
Ule ukarimu na huruma
tunayotakiwa tuwe
nayo wakati wa Funga
ya Ramadhani, ipo wapi
iwapo tunafutari kwa kila
aina ya viliwa, vitafunwa
n a v i n y w e wa , l a k i n i
haitupitikii kuwa kuna
akina mama na watoto
ambao huenda hawakupata
cha kuftaria kwa sababu
waume zao wapo ndani,
sio kama wafungwa, lakini
kwa tuhuma tu!
Maadhali mwenzi wa
Ramadhani umeanza,
punde tu tutashuhudia
wanasiasa wakipigana
vikumbo kuandaa futari,
kuanzia za Ikulu, Wakuu
wa Mikoa, waliotangaza
nia za Ubunge na Urais,
mpaka za mitaani.
Ni maoni yetu kuwa
labda Masheikh wetu
wa n g e wa e l i m i s h a n a
kuwashauri viongozi wetu
hawa na wale watarajiwa,
kuwa badala ya kuandaa
futari za kisiasa zisizo na
tija mbele ya Mwenyezi

Mungu (ila kwa tija ya


hapa hapa duniani tu),
wa n g e p e l e k a h u r u m a
yao kwa akina mama,
watoto na watu wazima
wanaoteseka kwa vile
waume zao na vijana wao
wanaowategemea wapo
ndani. Wapeleke futari zao
za kisasia katika familia
hizo.
Wa l i o m a d a r a k a n i
wakionyesha mfano
huo, hapana shaka na
waliotangaza nia watafuata
nyayo. Na hiyo itakuwa
ms a a da mk u b wa k wa
familia za watuhumiwa
hao, japo haitaondoa
dhambi ya kuwafunga
watu kwa tuhuma tu.
Kidunia tunaweza
kujifariji kuwa tunafuata
sheria (ya ugaidi), lakini
kwa Mwenyezi Mungu,
huo hautakuwa utetezi.

AN-NUUR

RAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 26- Julai 2, 2015


Mwenyezi Mungu anajua
siri zilizomo katika vifua
vyetu mpaka sababu
yenyewe ya kuwatuhumu
huo ugaidi, kama ni tuhuma
za kweli au la. Anajua
pia nia ya hao wababe
waliobuni vita dhidi ya
ugaidi, wanavyopiga
propaganda na namna sisi
tulivyotoswa kuitumikia
agenda hiyo (kwa malipo
gani?)
Ni juzi tu tumemzika
Mzee wetu, Sheikh Issa
Shaaban Simba, ambaye
tunaambiwa katika moja
ya usia wake aliagiza kuwa
akifa azikwe haraka kama
Uislamu unavyoagiza.
Tu n a j u a , k wa wa t u
wema kaburi ni viwanja
katika viwanja vya Peponi.
Lakini kwa watu waovu,
waliodhulumu nafsi zao,
kaburi ni shimo katika

mashimo ya Moto wa
Jahannam.
Wakati tukiwa tumo
ndani ya Ibada hii kubwa
ya Funga ya Ramadhani,
ni vyema kila mmoja wetu
akajihesabu ni kwa namna
gani anafanya maandalizi,
ili kaburi lake lije kuwa
Bustani katika Bustani za
Peponi.
L a k i n i p i a , n i k wa
kiwango agani anajitahidi
kuepuka yale ambayo
yatahesabika kuwa
ni dhulma, iwe ni ya
kuwafanyia wengine
au kuifanyia nafsi yake
mwenyewe. Kwani hayo
ndio yatamfungulia
milango ya Jahannam mara
tu akiingia kaburini.
Tu m w o m b e A l l a h
atutakabalie Funga zetu
na Ibada zetu kwa ujumla.
Na atuepushe na kila aina
ya dhulma.

Mkuu Magereza ashikilia uhai wa Sheikh Said


Inatoka Uk. 1

kutokana na kusumbuliwa na
maradhi, ambayo mpaka sasa
hayajapatiwa tiba inayostahili
akiwa humo gerezani.
Lakini pia kuna
washitakiwa namba 16 na 18
nao hawakufika Mahakamani
kwani pia ni wagonjwa.
A m e s e m a Wa k i l i w a
watuhumiwa hao Abdulfatah Abdallah.
Akizungumzia suala la
maombi ya kupatiwa kibali
kwa ajili ya kupatiwa rufaa
mtuhumiwa namba 12 kwa
ajili ya matibabu, Katibu wa
Kamati ya Maafa ya Shura
ya Maimamu, Ustadhi Ally
Mbaruku, alisema suala hilo
limekwamia kwa Kamishna
wa Magereza.
A l i s e m a ,
k i l a
wanapofuatilia wanapewa
matumaini kwamba kibali
kinashughulikiwa kulingana
na taratibu za Magereza, hata
hivyo alistaajibu kuona suala
hilo linalohusu uhai wa mtu
kupelekwa kwa kasi ndogo.
Alisema, awali katika Ofisi
hiyo ya Kamishna Mkuu
wa Magereza, waliwasilisha
maombi ya aina mbili, kwa
nyakati tofauti likiwemo
ombi la kupatiwa kibali cha
kupeleka msaada katika
gereza hilo la Segerea,
ambapo ombi hilo lishajibiwa
na misaada imeshapelekwa.
Alisema, maombi ya kibali
cha matibabu ya Ust. Salumu,
ndiyo yalitangulia ambapo
yalipelekwa mwanzoni mwa
mwezi wa tano, mwaka huu
na maombi ya kibali cha
kupeleka misaada kilipelekwa
mwishoni mwa mwezi huo
wa tano.
Hatuelewi taratibu zao
zikoje yaani maombi ya
kibali cha matibabu ndio

kilitangulia lakini mpaka


sasa hakijatolewa na mtu
anazidi kuathirika kiafya,
lakini hiki cha kupeleka
msaada kimetoka haraka
wakati barua yake ilikwenda
mwisho. Alisema mmoja wa
wajumbe wa Kamati hiyo.
Alisema, mara ya mwisho
wa l i e l e z wa n a m a o f i s a
wa Ofisi ya Kamishna wa
Magereza, kuwa wanasubiri
ripoti kutoka kwa daktari wa
Magereza ili wafahamishwe
kuna wagonjwa wangapi,
hata hivyo alisema hadhani
kama hiyo ni hoja ya msingi,
kwani suala la Ust. Salumu,
lipo wazi na tatizo lake ni
kubwa hata Mahakama,
inalijua.
Katika barua hiyo kwa
Ofisi ya Kamishna Jenerali
wa Magereza, yenye
Kumbukumbu namba 009/
KMS/2015, imeeleza hitajio la
Kamati hiyo kupatiwa kibali
mtuhumiwa huyo apewe
rufaa, ili wampeleke katika
hospitali yoyote kubwa.
Kamati ya Maafa Shura ya
Maimamu (T) kwa heshima
kubwa kabisa tunaomba
kibali ili ndugu Saidi,
apatiwe rufaa katika hospitali
yoyote kubwa kwa ajili ya
uchunguzi na matibabu na
kamati inachukua dhamana
ya k u l i p i a g h a r a m a z a
matibabu. Imesema sehemu
ya barua hiyo.
Barua hiyo inayoonesha
kuwa ilipokelewa Mei 4, 2015,
katika Ofisi hiyo ya Kamishna
wa Magereza, imeainisha
kuwa Said Amour ni
mshitakiwa namba 12 katika
kesi namba 29/2014, aliyepo
katika gereza la Segerea,
ambaye kwa muda mrefu
anasumbuliwa na Korodani
(Scrotal Swelling).

Hali ambayo inazidi


kuwa tete siku hadi siku,
pia wanalalamika ya kuwa
hawapatiwi matibabu ya
kina.
Imesema barua hiyo ya
Mei 4, 2015, ambayo An nuur,
inayo nakala yake iliyosainiwa
na Katibu, Ally Mbaruku.
Kamati ya Maafa, ilifikia
hatua ya kuwasilisha ombi hilo
kwa Kamishina wa Magereza,
kufuatia watuhumiwa hao
kulalamika mbele ya Hakimu
wa Mahakama ya Kisutu,
J a n e t K a l u ye n d a , k u wa
hawapati matibabu.
Watuhumiwa hao mbele ya
Mahakama hiyo, walikwenda
mbali zaidi wakidai kuwa
wa n a n y i m wa m a t i b a b u
ya n a y o s t a h i l i k u t o k a n a
na Uislamu wao ambapo
wa l i wa o m b a Wa i s l a m u
kuwachangia ili wapate
matibabu.
Waislamu wapo tayari
kuwasaidia, ndio maana
tulipeleka maombi haraka
kwa Kamishna wa Magereza
ili atoe kibali cha kuruhusu
akatibiwe katika hospitali
kubwa kwa gharama za
Waislamu, lakini bado kuna
ugumu ni mwezi sasa toka
tupeleke maombi hayo kibali
hakijatoka alisema Ust.
Mbaruku.
Said Amour, ni
miongoni mwa Waislamu
wanaotuhumiwa na Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania
kwa makosa ya ugaidi, ambao
waliilalamikia Mahakama ya
Kisutu kuwa walifanyiwa
vitendo vya ukatili wakiwa
mikoni mwa Jeshi la Polisi,
huku yeye (Said Amour )
inadaiwa aliminywa sehemu
za siri na kumsababishia
uvimbe.

Inaendelea Uk. 3

Habari

AN-NUUR

RAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 26- Julai 2, 2015

Kumpachika Muislamu ukafiri ni ujinga


Na Bakari Mwakangwale
KUMPACHIKA ukafiri
Muislamu mwenzako, ni
kielelezo cha ujinga na
jambo lisilokubalika katika
Uislamu.
Aidha, Siasa kali au
msimamo mkali, ni dhana
ngeni katika Uislamu kwani
Dini hii ya haki inasema
wazi kuwa ni ya kati na kati,
wema, uadilifu na upole.
Hayo yamebainishwa
katika Kongamano
lililoandaliwa na Umoja wa
Wanazuoni wa Tanzania
(Hay-at-Ulamaa) kwa
kushirikiana na Umoja
wa Wanazuoni wa Afrika,
ambalo lilifanyika katika
ukumbi wa Karimjee jijini
Dar es Salaam.
Akizungumza katika
kongamano hilo, Sheikh
Amran Kilemile, alisema
katika Uislamu hakuna kitu
k i n a c h o i t wa Wa i s l a m u
wenye Msimamo Mkali.
Alisema, wamelazimika
kufanya Kongamano
hilo kwa kuwashirikisha
Wanazuoni wa Kiislamu
kwa lengo la kutoa elimu
kuhusu msamiati Msimamo
mkali katika Uislamu na
kwamba hakuna kitu kama
hicho katika Uislamu, kwani
Uislamu una miongozo
yake na taratibu zake katika
kuyaendea mambo yake.
Kutokana na baadhi
ya Wa i s l a m u k u wa n a
elimu ndogo, hupelekea
k u ya c h u k u a m a m b o ya
Kiislamu kwa nguvu bila ya
kuzama katika mambo hayo
na hii inatokana na ufahamu
wao kuwa ni mdogo katika
kuyaendea mambo ya
Kiislamu. Alisema Sheikh
Kilemile.
Alisema, Wanazuoni wa
Kiislamu wanawanasihi
vijana wa Kiislamu ambao
ndio wanao onekana kuingia
zaidi katika mkumbo huo
kuwa makini na mitandao
ya kijamii katika kuuendea
Uislamu wao kwani akasema,
Uislamu unahitaji ukati na
kati na kila jambo lina hatua
yake na utaratibu wake.
Alisema, mitandao ya
kijamii ipo na haiepukiki
katika Ulimwengu wa
sasa, lakini kwa jinsi
hali ilivyo sasa, inaweza
ikakuingiza katika shari ya
kuuangamiza Uislamu na
unaweza ukaitumia vizuri
na ikakupeleka katika kheri
ya kuuinua Uislamu.
We w e k i j a n a wa
Kiislamu, huzuiwi kuwa
katika mitandao ya kijamii au
kuitumia lakini itumie vizuri
ili ilete kheri na manufaa
ikusaidie wewe na uisaidie
jamii kwa ujumla. Alisema
Shkh. Kilemile.
Alisema, makundi
hayo yenye mtazamo na
dhana ya msimamo makali,

Hakuna dhana ya siasa kali katika Uislamu


Wafafanua Sheikh Kilemile, Doga, Bassaleh

Sheikh Amran Kilemile.


wamekuwa na haraka
katika kuyaendea masuala
ya dini na kufikia mahali
kuwakufurisha Waislamu
wenzao, pale wanapojaribu
kuwakosoa kwa mujibu wa
mafundiso ya Qur an.
Bila ya mizani
unamkufurishaje Muislamu
mwenzako, huu ni uchache
wa elimu na kuyafahamu
mafundisho ya Uislamu, kwa
sababu ukiufahamu Uislamu
huwezi kuwa na lugha za
kukufurishana. Alisema
Shkh. Kilemile.
Sheikh Kilemile, aliwataka
wadau na wanazuoni wa
Kiislamu nchini kushirikiana
kukemea dhana ya Msimamo
Mkali katika Uislamu kwani
ni jambo ambalo halipo katika
Uislamu na katika zama
hizi limesambaa kwa kasi
miongoni mwa Waislamu na
kuleta sintofahamu.
Shkh
Kilemile
akisherehesha mada yake
akagusia baadhi ya upotofu
unaosambazwa akisema kuwa
kuna watu wanadai kusoma
elimu ya shule ni ukafiri,
h u k u wa k i wa l a z i m i s h a
Waislamu wengine kutosoma
na kuachana na elimu hiyo
sambamba na kuwakataza
Waislamu kushiriki katika
siasa kwamba kufanya hivyo
ni ukafiri.
Akasisitiza kuwa huo ni
upotofu na ujinga walio nao
wa n a o s a m b a z a m a wa z o
hayo.
Wakati huo huo, imeelezwa
kuwa baadhi ya Waislamu
wa m e k u wa wa k i m b i l i a
aya zenye Mutashabiha na

kuacha Muhakama, hivyo


kusababisha migongano kwa
Waislamu.
H a y o ya m e b a i n i s h wa
na Sheikh Muharami Juma
Doga, wakati akiongea na
Waislamu katika kongamano
hilo ambapo alisema, lau
Waislamu wanashikamana na
muhkamat, hakuna sababu ya
kufarikiana.
A k a s i s i t i z a k u wa a ya
mutashabihat, zinahitaji ujuzi,
lakini pia ifahamike kuwa
uzito upo katika kufuata
aya zilizo wazi ambazo ndio
zimebeba roho ya Dini.
Akisherehesha aya za Qur
an na Hadithi za Mtume (s
a w), Sheikh Doga, alisema
Uislamu unafundisha kuwa
usijilazimishe kufanya jambo
lililo nje ya uwezo wako
kwani kufanya hivyo ni hatari
kubwa.
Alisema, makundi hayo
yamekuwa yanatafuta njia
zao za kuyaendea mambo
ya Uislamu katika mazingira
ambayo yanahitaji ueledi
n a i n a l e t a p i c h a k u wa
huenda wana malengo
yao waliyoyakusudia au
wanataka waonekane

wameleta kitu kipya katika


jamii ya Waislamu jambo
ambalo ni hatari.
Ukifatilia nyendo zao
utabaini wanayaendea
masuala ya Kiislamu kwa
njia zao, lakini Muhakama
( a i n a ya a ya n d a n i ya
Qur an) hawazitaki, wao
wa n a n g a n g a n a k a t i k a
Mutashabiha.
Bila shaka wana malengo
yao waliyoyakusudia ima
waonekane wameleta kitu
kipya katika jamii na hii
ni hatari kubwa kabisa.
Alisema Shkh. Doga.
Mwanazuoni huyo katika
dini ya Kiislamu, alisema
hakuna kitu kipya katika
Uislamu badala yake
wanaibuka watu (Waislamu)
wanodhani wataonyesha kitu
ambacho wote hawakijui wala
hakuna anayekifanya huku
wakitaka kuonyesha njia hiyo
ndio njia sahihi kumbe ni
kupotoka.
Alisema, kutokujua
(ujinga) kwa Waislamu,
ndio chanzo cha upotoshaji
unaotokea miongoni mwa
Waislamu hivi sasa, kwani
yanayofanyika yanaashiria ni

ukosefu wa elimu na ufahamu


wa mafundisho ya Uislamu.
Naye Dkt. Hamduni
Suleiman, akichangia katika
Kongamano hilo, alisema
yapo matatizo ya uelewa
katika kuyaendea masuala
ya Uislamu na mbaya zaidi
ni kule kijidhania kuwa wana
elimu ya Uislamu wakati
hawana zaidi ya kuleta
migongano miongoni mwa
Waislamu.
Ni vyema Waislamu hao
kama wanafahamika waitwe
katika hadhara kama hizi
zinazokutanisha Jopo la
Wanazuoni wa Kiislamu ili
wapate majibu na ufafanuzi
wa hoja na dhana zao hizo.
Alisema Dkt. Hamduni.
Akitoa maoni yake mara
baada ya Kongamano hilo,
Maalim Ally Bassaleh, alisema
mada mbalimbali zilizo
hudhurishwa na wanazuoni
kwa Waislamu zina umuhimu
mkubwa kwa wakati uliopo
,hususan suala la misimamo
mikali katika Dini.
Alisema, anaungana
na watoa mada wote na
wachangiaji juu ya kupinga
vita dhana hiyo inayokuja
kwa kasi miongoni mwa
Waislamu, sababu kubwa
ikiwa ni ujinga (kutokujua)
unaotokana na mtu kutokuwa
na elimu na jambo analo
lifanya.

Inatoka Uk. 2
Wa k i wa z u n g u m z i a
Waislamu hao walio gerezani
kiasi cha mwaka mzima sasa,
Sheikh Amran Kilemile na
Maalim Bassaleh, kwa nyakati
t o f a u t i wa m e l e z a k u wa
mamlaka husika ziwatendee
haki kwa mujibu wa sheria na
katiba ya nchi.
Maalim Bassaleh, alisema
watuhumiwa hao waliopo
magerezani ni Waislamu
wenzao ambao wapo huko
kwa muda mrefu bila sababu
za msingi kiasi kwamba
sasa wanaamua kuchukua
m a a m u z i a m b a y o s i ya
kawaida.
Maamuzi ya kugoma kula,
kugoma kuingia Mahakamani
na hata kupanda juu ya mti,
yote hiyo ni kutaka kuonyesha
hisia zao, zaidi ni kuona
hawapati haki zao na hata
kufikia kuomba waonane na
baadhi ya viongozi wa Serikali
ili wapate kuwaeleza shida
zao, lakini pia inaonekana
kama vile wanapuuzwa.
Alisema Maalim Bassale.
Alisema, wale ni
wanadamu, hata kama wana
makosa, bado wanayo haki
ya kusikilizwa lakini kwa
hali inavyokwenda hata mtu

wa kawaida mtaani anaona


kuwa kinachotendwa dhidi ya
watuhumiwa hao ni dhulma.
A l i s e m a ,
m t u
anapotuhumiwa huwa bado
a n a k u wa h a n a m a k o s a
mpaka pale Mahakama
husika itakapo thibitisha,
lakini akasema Muislamu
akituhumiwa tu ananyimwa
dhamana si ajabu mwaka
mzima au zaidi kwa tuhuma
zinazo stahili dhamana.
Lakini kuna mtu
mwingine mwenye imani
ya Kikristo naye ni kiongozi
wa dini amekamatwa na
silaha ya moto, na ikaelezwa
silaha yenyewe ina matatizo
kwamba haijulikani kuwa ni
ya halali au la.
Lakini huyu pamoja na
kukutwa na silaha yenye utata
anapata dhamana tena ya
kujidhamini mwenywe lakini
huyu Muislamu au Sheikh
hana kosa la kukamatwa
na chochote, ni tuhuma tu
lakini ananyimwa dhamana.
Alisema Maalim Bassaleh.
Akasema, mwenendo huo
ni lazima Waislamu waone
kuna uonevu kutokana na
tuhuma zao kusimamiwa
kwa misingi ya dhulma ili hali
wengine wanafatiliwa kwa

misingi ya sheria na katiba


ya nchi.
Kwa upande wake Sheikh
Kilemile, alisema Masheikh
n a Wa i s l a m u h a o k a m a
kweli wana kesi, basi ni
bora izungumzwe na tatizo
lionekane, na kwamba kama
unamtuhumu mtu, basi
tuhuma zake uziweke wazi.
Eleza tuhuma zake
ziangaliwe kwa misingi ya
haki na kama ana makosa
yaonekane, Mahakama zipo
kwa ajili hiyo, makosa yawe
wazi yafahamike, kuliko
hii hali ilivyo sasa dhidi ya
Waislamu hao. Alisema.
Sheria ya kesi ni kuwa
inafikia mahali kesi yake
inatakiwa izungumzwe kisha
Mahakama iamue kama
anatuhuma au hana, kisha
mtuhumiwa apewe haki yake
aidha kutumikia adhabu au
aachiwe huru. Aliongeza
Sheikh Kilemile.
Akasema, Waislamu hao
wanashikiliwa kwa muda
mrefu sasa lakini haieleweki
sababu za msingi zinazo
kwamisha kesi hiyo, huku
siku zinazidi kwenda na
k u p e l e k e a wa t u h u m i wa
na umma hawajui hatima
ya suala hilo na kwamba
hali hiyo haipendezi katika
misingi ya utu na haki.

Mkuu Magereza ashikilia uhai wa Sheikh Said

Habari

AN-NUUR

RAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 26- Julai 2, 2015

Amiminiwa risasi na Polisi, afariki


Na Mwandishi Wetu

KIJANA Usamah Abdullah


Rahim amepigwa risasi
na kuuliwa papo hapo na
polisi.
Baada ya kumuuwa kijana
huyo, Polisi walitoa taarifa
wakidai kuwa waliwahi
k u m u u wa k i j a n a h u y o
wa Kiislamu kwa sababu
alikuwa akipanga kuchinja
Wakristo na hata Polisi.
Kama ushahidi, Polisi hao
walionyesha kisu ambacho
walidai kuwa walimkuta
nacho Rahim na kwamba
walipotaka kumsimamisha
ili wampekue, Usamah
Abdullah Rahim, aliwatisha
kwa kisu hicho ndio
wakaamua kumpiga risasi.
Katika madai zaidi ya
P o l i s i i n a e l e z wa k u wa
miongoni mwa watu
ambao Usamah Abdullah
Rahim, alipanga kuwachinja
ni pamoja na Bi Pamela
Geller anayesifika kama
manaharakati anayeuchukia
Uislamu.
Terror suspect killed by
FBI 'planned to behead Pamela
Geller'
Usaama Rahim allegedly
planned to kill anti-Islam
activist before his death in
Boston on Tuesday.
Ndio baadhi ya vyombo
vya habari vilivyoripoti
vikijitahidi kuhalalisha
mauwaji ya Rahim
yaliyotokea Boston mapema
mwanzoni mwa mwezi huu
wa sita kwamba alikuwa
kapanga kumuuwa Pamela.
Jihadi Shot Dead in Boston
was Plotting to Behead Cops,
Another Arrest Made.
Boston Beheading Plot
Jihad in America: Enemy in
our Midst.
N d i v y o v i l i v y o k u wa
vimepambwa vyombo
vingine vya habari vya
Marekani vikielemea juu
ya madai ya kitisho cha
kuchinjwa polisi.
The man shot and killed
Tuesday by Boston police was
plotting with another suspect to
behead a cop, a law enforcement
source told Fox News.
Ndivyo FOX News
walivyoripoti wakisherejesha
kwa kudai kuwa kijana
huyo na watu wengine
wa l i k u wa wa m e p a n g a
kuchinja Wakristo na Polisi
kwa kutumia mtindo wa
magaidi wa ISIS.
Tunaamini walikuwa
na nia ya kuchinja Polisi,
alinukuliwa afisa mmoja wa
polisi akisema.
Tu l i j u a l i l i k u wa n i
tishio la kweli na ilikuwa
watekeleze mpango huo
Jumanne. Aliongeza afisa
huyo.
Akizungumzia tukio
hilo, Kamanda wa Polisi
wa B o s t o n , K a m i s h n a
William Evans alisema

Usamah Abdullah Rahim


kuwa ilikuwa ni mapema
kiasi saa moja asubuhi
ambapo maofisa wa kikosi
maalum cha kupambana
na ugaidi (Joint Terrorism
Task Force) walimsimisha
Rahim wakimhoji mambo
kuhusiana na mwenendo
wake unaotia shaka juu ya
ugaidi.
Hata hivyo akadai kuwa
Rahim alitoa kisu akitaka
kumdhuru polisi ndio
wakamuwahi kumpiga risasi.
The terrorism plot was "very
real" and "very dangerous."
Alidai Kamanda William
Evans akijitahidi kuonyesha
kuwa walikuwa hawana
namna ila kumuuwa
Usaamah Abdullah Rahim,
kwa madai kuwa ingekuwa
hatari kama wasingefanya
hivyo!
Ili kuthibitisha madai yao,
polisi walidai kuwa upo
mkanda wa video ukionyesha
tukio zima.
Hata hivyo, video iliyokuja
kutolewa haithibitishi madai
ya polisi.
U k i a c h a k u wa k i j a n a
Rahim anaonekana kwa shida
katika picha hiyo ikionyesha
kuwa ilipigwa toka mbali,
lakini kisu hakionekani
kabisa au silaha ya namna
yoyote.
Wa l a h i c h o k i t e n d o
kinachodaiwa kuwa Rahim
alitaka kuwashabulia,
hakionekani katika picha
hiyo.
Hata vile vyombo vya
habari ambavyo kwa kawaida
hushabikia taarifa za polisi
juu ya madai ya kukamata au
kuuwa magaidi, viliandika
vikisema kuwa video ya
polisi haijibu maswali juu ya
tukio la kuuliwa Rahim na
zaidi vikasema haithibitishi
kwa namna yoyote madai
kuwa Rahim alipambana na
polisi.
Ukiacha mapungufu hayo,
ndugu, jamaa na waumini wa
Msikiti anaposwali Usamah,
wanasema kuwa madai ya
polisi na kikosi chao maalum

cha kupambana na ugaidi ni


urongo mtupu.
Na kwamba hata kama
angekamatwa akiwa na kisu,
bado hiyo sio sababu ya
kumpachika jinai ya ugaidi
na kumuuwa papo hapo.
Wa n a s e m a , k a m a n i
kitisho, basi waseme ni
Uislamu wa Usamah, lakini
sio kumsingizia kuwa
anapanga kuchinja Wakristo
na Polisi kwani kukutwa
na kisu hilo ni jambo la
kawaida hasa kwa jamii ya
Wamarekani Weusi, na hasa
katika kipindi hiki ambapo
wanauliwa ovyo na polisi na
hata wananchi wa kawaida
Wazungu ambao kila uchao
wanazidi kuwa na chuki
dhidi ya Weusi (racism)
Alisema Bi Karen, mmoja
wa n d u g u wa U s a m a h
kwamba ingawa jamii ya
Wamarekani Weusi yote
ipo katika kitisho, lakini
u n a p o k u wa M u i s l a m u ,
kitisho kinakuwa kikubwa
zaidi.
Hoja nyingine ya msingi
Waislamu na ndugu wa
Usamah wanahoji, kama
Polisi na hiyo Task Force yao
ya kupambana na ugaidi
wanadai kuwa kijana huyo
alikuwa na mpango wa
kuchinja Wakristo, kwa nini
wasimkamate na kumfikisha
mahakamani watoe ushahidi
na pengine kwa kumhoji
mtuhumiwa waweze
kuutambua mtandao wake
wa kigaidi na kuuvunja.
Wakati huo huo, Kijana wa
Kizungu Dylann Roof aliingia
katika kanisa lijulikanalo
kwa jina la Emanuel African
Methodist Episcopal Church
kule Charleston, South
Carolina, na kuwafyatulia
risasi waumini ambapo
aliuwa watu 9 Wamarekani
Weusi wakisali.
Hata hivyo, tukio hilo
limechukuliwa kama uhalifu
wa kawaida nchini Marekani
na hakuna namna kijana
huyu anatuhumiwa kwa

ugaidi.
Kinyume chake, baadhi
ya taarifa zikijitahidi kumtoa
Dylann Roof katika jinai
hiyo, zimejaribu kuibua
wasiwasi kuwa huenda
kijana huyo alifanya tukio
hilo akiwa hayupo hadhiri.
Kwamba labda kuna jambo
lilimchanganya akili ndio
akaenda kanisani na kuuwa
watu hao.
Shooters of Color Are Called
'Terrorists' and 'Thugs.' Why
Are White Shooters Called
Mentally Ill'?
Anahoji mwandishi
Anthea Butler akionyesha
kutokuridhishwa na
mwenendo wa vyombo vya
habari na baadhi ya maofisa
wa vyombo vya dola.
Anasema, wakati kitendo
kilichofanyika ni ugaidi wa
dhahiri dhidi ya watu Weusi
na Makanisa yao na kwamba
sio tukio la mwanzo kwa
Marekani, vyombo hivyo,
vinakuja na kauli ambazo ni
kutaka kumfunika Dylann
Roof na kudunisha jinai
aliyofanya.
Hili sio tukio la mwanzo
katika historia ya Marekani.
Makanisa ya watu Weusi
ya m e k u wa ya k i l e n g wa
na wabaguzi wa Kizungu
(white supremacists) ambao
wamekuwa wakiyachoma
moto makanisa hayo au
kuyalipua kwa mabomu
kama namna moja wapo
ya k u wa t i s h a j a m i i ya
Weusi (terrorize the black
communities).
Anasema Anthea Butler
akitaja moja ya matukio
mabaya ya kigaidi dhidi
ya Weusi kuwa ni pamoja
na lile la kulipuliwa kanisa
la Wamarekani Weusi kule
Birmingham, Ala., mwaka
1963 ambapo wasichana
wanne (4) waliuliwa.
Wa l i o f a n ya j i n a i
hiyo walitajwa kuwa ni
wanachama wa kundi la Ku
Klux Klan (KKK), au kwa
kifupi "the Klan".
Kundi lenye rekodi na
historia chafu ya chuki,
ubaguzi uliopindukia
na mauwaji dhidi ya
Wamarekani Weusi.
Anasema Butler kuwa
katika kuripoti tukio hilo la
kuuliwa watu 9 ambalo kwa
dhahiri kabisa ni la kigaidi,
hutakuta vyombo vya habari
vikitia neno lolote kuwa huo
ni ugaidi. Kinyume chake,
pamoja na kuwa hakuna
taarifa zozote za kitabibu
wala jamaa wa Dylann Roof
hawajaleta madai/utetezi
kuwa kijana wao alikuwa
na ugonjwa wa akili, lakini
vyombo vya habari mara tu
baada ya kufanyika mauwaji
hayo vilianza kuja na
misamiati na misemo kama:
A victim of mistreatment
or inadequate mental health
resourceswe dont know his

mental condition."
Yote hii anasema, ni kutaka
kujenga hoja kumnasua
kijana Dylann Roof katika
jinai inayomkabili.
Kwa upande mwingine
kama Meya Joseph Riley
wa Charleston alivyosema,
tukio hilo linaonekana kama
jambo la bahati mbaya tu la
mtu binafsi aliye na matatizo
fulani na halina uhusiano
na kundi lolote unaloweza
kusema ni la kigaidi kama
ambavyo matukio ya watu
wenye majina ya Kiislamu
yanavyoburutwa yakatiwa
katika kapu la ISIS, Al
Shabaab na Al-Qaida. Kwa
watu kama Dylann Roof,
wao inakuwa ni kazi ya
lone wolfs au "one hateful
person".
Ni kutokana na hali kama
hizi na ubalakala kama huu,
wasomi na wachambuzi
wengi wa siasa za Marekani
na nchi za Magharibi
kwa ujumla, wanaitizama
inayoitwa Vita dhidi ya
ugaidi kama tamthilia fulani
na mzaha wa karne hii.
Ni picha na taswira ya
kubuni ambayo inakolezwa
na kuvurugwa na wanasiasa.
Kama anavyosema
mwandishi mchokozi wa
Uingereza na mchambuzi,
Adam Curtis, hili "Ni wingu
potofu la fikra ambalo
limesambaa bila kuhojiwa
m i o n g o n i m wa s e r i k a l i
duniani kote, majeshi ya
usalama na vyombo vya
habari."
Wakati nchi za Magharibi
zikitumia Vita ya Msalaba
dhidi ya magaidi kuhalalisha
uvamizi angamizi ili kupata
masilahi yao ya kibeberu, nchi
kama yetu zinazochagizwa
kushiriki katika Crusade hii
kama alivyoiita muasisi wake
George W Bush, zinajikuta
zikijitosa kibubusa matokeo
yake yakiwa ni maangamizi
kwa watu wake na nchi kwa
ujumla.
Maangamizi kwa watu
kwa sababu, kwanza
watapandikizwa magaidi
watakaoleta maafa kama
inavyotokea Nigeria,
Somalia, Yemen, Pakistan na
Kenya.
Pili, ni maangamizi
kwa nchi kwa sababu kwa
kutumia kisingizio cha
kupambana na magaidi,
mabeberu huingia kikachero
na kijeshi wakazidhibiti
nchi wazitakazo zisiweze
kufurukuta wala kuwa na
uhuru juu ya rasilimali zao
na siasa za nchi. Kila kitu
wanapangiwa na kupewa
maelekezo.
Kwa hiyo, wakati nchi
lengwa ikiangamizwa pamoja
na watu wake, mabeberu
wanavuna faida isiyo ya
kawaida kiuchumi na kisiasa
kutimia azma yao ya Global
hegemony.

China
yawazuia
Waislamu
Xinjiang
kufunga

SERIKALI ya China
imepiga marufuku
wanafunzi, walimu na
watumishi wa umma
katika eneo la Xinjiang
lenye Waislamu wengi,
kutekeleza ibada ya
Saumu katika mwezi
huu mtukufu wa

Ramadhani.
Serikali pia imezuia
watu kuhudhuria shughuli
zozote za kidini ikiwa ni
pamoja na ibada za usiku.
Ta a r i f a ya s e r i k a l i
imetaka biashara kwenye
hoteli na mikahawa
kufunguliwa nyakati za
mchana kama kawaida.
Wa n a h a r a k a t i w a
Kiislamu wamepinga agizo
hilo la serikali wakisema
linalenga kuhujumu dini
tukufu ya Kiislamu.
Ingawa serikali inasema
lengo la kuweka sheria
hiyo ni kuhakikisha
masuala ya dini
hayavurugi muundo wa
jamii, duru za kuaminika
zinasema sheria hiyo ina
malengo ya kiuchumi,
k wa n i i m e w e k wa i l i
kuhakikisha nguvu kazi
ya taifa haipungui katika
mwezi wa Ramadhani.

Chuo Kikuu cha


Kiislamu cha AlAzhar cha nchini Misri
kimepinga na kulaani
dhulma na ukandamizaji
wa kidini unaolenga haki
za msingi za Waislamu
nchini China.
Al Azhar imeitaka
jamii ya kimataifa kama
vile Umoja wa Mataifa
na asasi mbalimbali
za haki za binadamu
kulaani kitendo hicho.
Kwa miaka kadhaa
sasa, serikali ya China
imekuwa ikitekeleza
sheria hiyo ya kibaguzi
na mwaka uliopita, watu
kadhaa walifikishwa
mahakamani kwa
kufunga Ramadhani
na kukaidi sheria hiyo.
(Irib)

Habari za Kimataifa

AN-NUUR

RAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 26- Julai 2, 2015

Licha ya Ramadhani Saudia


yaendelea kuihujumu Yemen
Waharibu hospitali 62 na zahanati 115
Wanaopambana wote wapo kwenye swaumu

Saudi Arabia inaendeleza


na mashambulizi yake
ya anga katika maeneo
mbalimbali ya Yemen,
licha ya kutolewa wito
mbalimbali katika
ukanda huo na kimataifa
wa kusimamisha
mashambulizi hayo
yanayouwa wananchi
wa s i o n a h a t i a k wa
mamia ya maelfu.
Mashambulizi ya anga
ya muungano wa Saudia
katika maeneo mbalimbali
ya Yemen yaliendelea
wiki hii; huku idadi
kadhaa ya Wayemeni
wakiuawa na kujeruhiwa.
Mashambulizi hayo
yanaendelea huku
makundi husika kwenye
m g o g o r o wa Ye m e n
ya k i s h i n d wa k u f i k i a
muafaka baada ya siku
tano za mazungumzo
mjini Geneva Uswisi.
Saudi Arabia imesema
kuwa kuondoka
wapiganaji wa Mahouthi
wa Ansarullah katika
maeneo wanayoyadhibiti
ni sharti la usimamishwa
vita huko Yemen.
Ismail Ould Sheikh
Ahmad, Mjumbe
M a a l u m u wa K a t i b u
M k u u wa U m o j a wa
Mataifa katika masuala
ya Yemen, awali alijaribu
k u f a n ya j i t i h a d a z a
kufikiwa makubaliano ya
usitishaji vita huko Yemen
na baadaye makundi
ya nchi hiyo yakaweza
kuketi kwenye meza
ya mazungumzo huko
Geneva.
Sambamba na juhudi
hizo za kuupatia
ufumbuzi mgogoro wa
Yemen, lakini kutokana na
mashambulizi ya Saudia
yanayoendelea kila
uchao nchini humo, hali
ya wananchi imekuwa
mbaya zaidi hivi sasa
kwa kuzingatia uhaba
wa chakula uliopo na
kuendelea kushambuliwa
vituo vya afya na tiba
nchini humo.
Wananchi wa Yemen
hawapati huduma

RAIA wa Yemen wakiwa wamebeba mtoto aliyejeruhiwa kutokana na mashambulizi


ya majeshi ya Saudi Arabia yanayoendelea nchini humo.
muhimu za kiafya na maji m w i s h o n i m wa w i k i shaka kuwa mashambulizi
safi ya kunywa kutokana k a t i k a m a h o j i a n o n a ya anga ya Riyadh ni
na kushtadi mashambulizi televisheni ya al Mayadeen sababu kuu ya kuibuka
ya utawala wa Aal Saud, y a L e b a n o n k u w a , matatizo ya kiafya na
huku uhaba wa mafuta mashambulizi ya anga kitiba huko Yemen.
U m o j a wa M a t a i f a
pia ukiwafanya raia hao ya Saudia huko Yemen nao
umedaiwa kuhusika
wakabiliwe na hali ngumu hadi sasa yameharibu na katika kutokea maafa
ya kimaisha.
kubomoa hospitali 62 na hayo kwa hatua yake ya
Ta m i m a l S h a m i , zahanati 115.
kile kilichotafsiriwa kuwa
msemaji wa Wizara ya
T a m i m a l S h a m i ni kuikingia kifua Saudi
Afya ya Yemen alisema aliongeza kuwa, hakuna Arabia.

Uchunguzi wa mauaji ya Masheikh Uganda

Mufti aitaka serikali iwafanye uadilifu

MUFTI wa Uganda
Sheikh Shaban
Ramadhan Mubajje,
ameitaka serikali
na mashirika ya
usalama ya nchi hiyo
yanayochunguza
mauaji ya viongozi wa
Kiislamu, kufanya kazi
kwa uadilifu na kwa
viwango vya juu vya
utaalamu.
Vyombo
vya
h a b a r i v ya U g a n d a
vimemnukuu Mufti
wa nchi hiyo akiitaka
serikali, hususan wale
wanaohusika na masuala

ya usalama kutumia
utaalamu wa hali ya
juu katika kazi zao kama

kweli wanataka kupata


ufumbuzi wa kudumu
wa mlolongo wa mauaji
ya viongozi wa Kiislamu
nchini humo.
Mufti Mubajje alisema
hayo wilayani Kamuli
mwisho ni mwa wiki

wakati wa uzinduzi
wa eneo la Waislamu
lililojengwa na shirika
lisilo la kiserikali NGO
la Kamuli Good Hope
lililogharimu shilingi
milioni 75.

M a t a m s h i h a y o ya
Mufti Mubajje, yamekuja
kufuatia wimbi la mauaji
ya Masheikh katika mkoa
wa mashariki, huku
mauaji ya karibuni kabisa
yakiwa ni yale ya Sheikh
Abdul Rashid Wafula
huko Mbale.
Mufti Mubajje pia
amewataka Waislamu wa
madhehebu mbalimbali
kuungana na kuweka
pembeni tofauti zao ndogo
ndogo na kuwa mfano
b o r a k wa n i U i s l a m u
inafundisha amani na
kuishi na watu kwa wema.

Makala/Tangazo

AN-NUUR

RAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 26- Julai 2, 2015

Mafundisho ya Quran

Fethullah-Gulen

HIVI mnawaamrisha
watu kufanya wema
na hali mnaziacha
nafsi zenu na hali
ya kuwa nyinyi
mnakisoma kitabu,
hivi hamuelewi?. [AlBaqarah 44]
Pamoja na kwamba
aya hii inawasemesha
sehemu katika wana
wa Israel kwa sura
ya moja kwa moja,
lakini ni kwamba aya
hii inawasemesha
Waislamu vile vile.
K wa s u r a h i i ya
Ishara na jambo
ambalo linakusudiwa
hasa, ni kutuzinduwa
juu ya wajibu wa
kupatikana umoja na
kutovunjana kati ya yale
yanayosemwa na yale
yanayotendwa. Kwa
maana ya umoja katika
maneno na matendo.
Kwa sababu hiyo,
tunaona kwamba aya
nyingine inaelezea
maana haya kwa njia
nyingine, inasema :
Kwa nini mnasema yale
ambayo hamyatendi?
[Assaf 2]
Usiwahamashishe
wenzako kufanya
wema, wakati wewe
mwenyewe unafanya
kinyume chake.
Ndiyo hali na
maneno au kusema
na kutenda ni lugha
yenye pande mbili,
kwa ajili ya kuinusuru
haki na kuwakilisha,
itakapozungumza
hii lugha yenye sura
mbili na maonekano
mawili, kwa jina la haki
na ikapiga kelele kwa
hiyo haki taathira yake
itakuwa kubwa sana.
Kwa sababu kunapasa
juu ya binadamu
kuyatekeleza yale

ambayo anawalingania
watu wengine. Na
kusiwe na kupingana
kati ya maneno yake na
matendo yake na kati ya
hali yake inayoonekana
na maelezo yake.
Imekuja katika athari
k wa m b a M we n ye z i
Mungu mtukufu
alimwambia Mtume Issa
(a.s.):
Ionye nafsi yako
kwanza, iwapo nafsi
yako itayakubali
mawaidha, hapo wape
(wengine) mawaidha
yako. Na kama nafsi
yako haikukubali, basi
ona haya kwangu.
K wa m s i n g i h u o ,
inapasa kuishi
binadamu kufuatana na
anavyoamini na aakisi
vina vya ulimwngu wake
wa ndani miongoni mwa
fikra na hisia, itakuwa ni
kitendo cha kuitakasa
nafsi yake. Yule ambaye
hasimami usiku ni juu
yake kutoizungumzia
swala ya Tahajudi na
a o n e h a ya k u f a n ya
hivyo. Na yule ambaye
hawezi kuswali kwa
unyenyekevu wote na
kwa kujinyongesha na
wala hatendi kwa adabu
mbele za Mwenyezi
Mungu mtukufu, wala
haimtishi na kuogopa
kumuogopa Mwenyezi
Mungu, asizungumze
kuhusu sifa kamili za
swala. Na akitokuwa
n i m we n ye k u j i t o a
muhanga, kunapasa
kutozungumza tamko
moja kuhusu maudhui
ya kuishi kwa ajili ya
watu wengine.
Kwa sababu Mwenyezi
Mungu mtukufu
amefungamanisha
k wa h e k i m a f u l a n i
nguvu ya kuathiri
yale yanayosemwa, na
mfumo wa utendaji wa
msemaji.
Hapa kunapasa
ku ku mb ush a jamb o
jingine, nalo ni kuja
uwezekano wa
kuifahamu kimakosa
aya hii:
Ni kwa nini
mnasema yale ambayo
hamyatendi? [A-ssaf 2].
A y a
h i i
haifahamishi maana
ya kuwa tahadhari
kulikumbusha jambo
ambalo huishi nalo

kwa sababu kuishi ni


ibada na kufikisha ni
ibada nyingine. Yule
ambaye hakuyatekeleza
yote mawili, amebeba
dhambi mbili na amekaa
mbali na nguvu za
k u a t h i r i k wa h a t u a
mbili, na ambaye
hakulitekeleza moja la
hayo mambo mawili,
atabeba dhambi moja,
na amekuwa mbali na
k u a t h i r i k wa h a t u a
moja. Kwa sababu
nguvu ya kuathiri kama
tulivyosema inategemea
juu ya kutekelezwa yale
yanayofikishwa.
Ndiyo, kwa hakika
k u wa a m r i s h a wa t u
wengine kwa kufanya
mema na kuwakataza
na maovu na kuacha

kuyatekeleza hayo juu ya


nafsi huko, ni kuvunjana
kuliko wazi. Na mfano
wa utendaji huu wenye
makosa, unapunguza
t a a t h i r a ya m a m b o
chanya mengi, kama vile
nguvu ya balagha na
kuweka wazi na elimu.
Haya ndiyo ambayo
yanatajwa na aya hii. Ila
asije akatumbukia mtu
yeyote mwenye akili
katika mfano wa kupinga
huku na unamtaka
binadamu umakini na
kufikiri katika kuishi,
na kufikisha na yasiyo
kuwa hayo miongoni
mwa upuuzi na maneno
mengi yanayoondoa
haiba ya mwenye
kuzungumza. Na hili
lina maana kwamba

yeye ameiacha nafsi yake


kikamilifu. Kwa sababu
hiyo, imekuwa ni juu ya
mtoaji wa mawaidha, na
juu ya mtoaji wa nasaha
na mwenye kuongoza,
na mwenye kufikisha
na mwenye kuandika,
na mwenye kupanga
mambo, awe ni mkweli
katika matendo ambayo
anasimama nayo ili
yachukuliwe machukuo
ya ukweli na kwa ajili
yasipate kivuli chochote
cha shaka juu ya zile
maudhuu ambazo
anazizungumzia na
kuzitoa.
(Imenukuliwa kutoka
K i t a b u : M i ya n g a z a
y a Q u r a n k a t i k a
mbingu ya hisia, cha
Muhammad Fethullah
Gullen kilichotafsiriwa
kwa Kiswahili na
Sheikh Suleiman
Amran Kilemile)

Habari

AN-NUUR

RAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 26- Julai 2, 2015

Propaganda za udini shuleni Tanzania-8

Profesa Ibrahim Noor Shariff

TUKUMBUKE pia
kuwa katika miaka hii
tuliyonayo hapatakuwa
na kusherehekea,
kila mwaka, mauwaji
ya kimaafa kama
wanavyosherehekea
maafa ya Wazanzibari
Wa i s l a m u w e n g i
waliotolewa roho zao
bure 1964. Yakitokea, jua
kuwa washiriki wengi
watasakwa, kukamatwa
na
kupelekwa
mahakamani -- The
Hague.
Nastaajabu, lakini
sistaajabu sana kuona
Wa o m a n i wa m e k a a
kimya maana kutokana
n a u s t a a r a b u wa o ,
huwaoni kugombana
ovyo na mtu yoyote wala
huwasikii kutukanana.
N i wa t u wa k a r i m u
sana kwa vitendo na
kwa maneno mazuri.
Hivyo basi wanayasikia
yasiyokuwa ya kweli
yanayosemwa dhidi yao
na hawasemi kitu. Lakini,
kama ulivyoona wale
wenye kutapakaza siasa
kali za udini huwa kila
kukicha wanazidisha
maongope yao na
kufikia hadi ya kuonesha
picha za utumwa hata
West Indies, ambako
Waarabu hawakuweko,
na kuonesha kuwa ni
Waarabu waliokuwa na
Watumwa hata huko
katika visiwa vilioko
Amerika. Kwa ukosefu
wa bahati, ukimya wa
Waomani unaotokana
na ustaarabu wao wa
hali ya juu kabisa wa
kutokujibu uwongo wa
dhahiri unaosemwa
dhidi yao na wenye
siasa kali za udini,
kumewafanya wenye
siasa hizo kuzidisha
uwongo wao kila leo.
Propaganda dhidi ya

Waislamu si jambo geni


kwani zilianzia zaidi
ya miaka elfu iliyopita.
Propaganda dhidi ya
Waislamu wa Afrika
Mashariki zinazotokana
na wakoloni na
wamishinari wao
pia si jambo geni
kwani zilianza tokea
yalipowasili majeshi
ya Kiportugizi
mwanzoni mwa karne
ya 1 6 . P r o p a g a n d a
hizi zilizidi kutia fora
wa k a t i wa u t a wa l a
w a Wa i n g e r e z a n a
Wajarumani mwishoni
mwa karne ya 19. La
kusikitisha ni kuona
kuwa wamishinari
katika kusomesha kwao
waliwafunza wanafunzi
wao wa Kiafrika ubaya
wa Uislamu na wema
wa Ukristo na kuwa
dini ya Kiislamu ni batili
na dini yao ya Kikristo
ndiyo ya kweli na
ya haki iliyoletwa
Afrika Masharika na
Kati kumkomboa
Mwafrika na ukatili
na ubaya wa Uislamu
na Waislamu.
Wa k a t i h u o h u o
w a l i p o k u w a
wakiwasomesha haya
watoto wa Kiafrika,
wakoloni wa Kizungu
na wamishinari wao
waliziteka na kuzitia
nchi za Afrika katika
ukoloni wao ambao
mara nyingi ulisababisha
v i f o v y a Wa a f r i k a
wengi kwa mauwaji
ya kinyama kabisa na
utiwaji wa Waafrika
wengi utumwani katika
nchi zao wenyewe
Waafrika, na mamilioni
wengine ya Waafrika
waliotiwa utumwani
walipelekwa kwenye
nchi zilizotawaliwa na
Wazungu Wakristo.
Kama tulivyokwisha
kutaja pia, chini ya
utawala wa Mfalme
Leopord II (1835 1909)
wa Ubiligiji aliwatia
utumwani mamilioni
ya Wa k o n g o k a t i k a
m a s h a m b a ya m i t i
yenye utomvu wa
kutengenezea mipira;
na katika juhudi hizo
a l i wa u wa Wa a f r i k a
wasiopungua milioni
kumi, wengi walifungwa
na kuadhibiwa vikali
sana, walipigwa
mboko, wengine wengi
walikatwa viganja vya
mikono yao walipokataa

kufanya kazi bila ya


malipo. Soma vitabuni
na fungua mitandao
uangalie mwenyewe
nini wameandika
wanahistoria kukhusu
utumwa huu na
ukhabithi wake na idadi
ya Waafrika waliouliwa.
Lakini, wamishinari
wa Kizungu jana na
wamishinari wa Kiafrika
leo hawazungumzii
utumwa huu na unyama
wake, kwani kufanya
h i v y o k u t a wa w e k a
Wakristo na Ukristo
pahala pabaya sana.
Na hili ndilo jambo
wanalolipiga chenga.
Wao wamo kila leo
kushindilia katika
bongo za wanafunzi
wa Tanzania ubaya wa
Waislamu tu hata iwapo
Uislamu na Waislamu
hawakhusiki na ubaya
huo. Kufanya hili
kunayafanya masomo ya
shule ya historia kuwa si
masomo yenye kuelezea
ukweli uliotokea, bali
h u ya f a n ya m a s o m o
hayo kutiwa katika
kumbo la propaganda;
na la kusikitisha zaidi
ni kuiona Serikali ya
Ta n z a n i a a m b a y o
inajigamba kuwa haina
dini na haipendelei
wala kuichukia dini
yoyote kuwa inashiriki
kiukamilifu katika
kuwapaka uchafu
na kuwapiga vita
Waislamu na dini yao na
kuwapendelea Wakristo
wenye siasa kali za
udini kwa kuachilia
propaganda zenye
ukweli finyu na uwongo
mwingi kusomeshwa
katika shule za Tanzania
mchana kweupe bila
ya kificho na bila ya
kuona haya wala kuwa
na khofu, kunaifanya
Serikali ya Tanzania
kuwa mshiriki katika
kujenga mstakbali
mbaya kwa nchi ya
Tanzania ambayo wao
wameapa kuilinda na
kila ovu.
Wa n a p r o p a g a n d a
waliopewa fursa ya
kuandika vitabu vya
historia kwa ajili
ya kuwasomeshea
wanafunzi wa shule za
Tanzania wameitumilia
fursa hiyo vibaya sana,
k wa n i wa m e o n e s h a
waziwazi mapendeleo
ya o j u u ya U k r i s t o
na Wakristo na chuki

zao zinazotokana na
vita vyao vya msalaba
dhidi ya Uislamu na
Waislamu.
Vita hivi katika Afrika
Mashariki kwanza
vilianzishwa kwa
maneno na wamishinari
wa Kizungu na serikali
zao za kikoloni na
z i m e p o k e l e wa k wa
utiifu mkubwa sana na
wamishinari wa Kiafrika
ambao wamejibebesha
vita hivyo vya msalaba
na kuviendeleza mbele
kwa kadiri ambayo hata
waalimu wao wa kikoloni
wanaonekana leo kama
wanafunzi. Ingelikuwa
hayo wanayoyaelezea
wanapropaganda
n i ya k we l i m t u p u
tusingeligutuka,
lakini mengi zaidi
waliyoyachora
na kuyaandika si
m a t o k e o ya k w e l i ,
kama tulivyokwisha
kudhihirisha.
K w a
w e n y e
m a c h o , n a m we n ye
macho haambiwi
tazama, Tanzania
i m e s h a t u m b u k i z wa
katika vita vya udini
na hawa Watanzania
wenye siasa kali za
u d i n i . Ta n z a n i a n i
nchi yenye Waislamu
wengi na ubaya
mkubwa wanaoufanya
wanapropaganda hawa
kwa propaganda zao
d h i d i ya Wa i s l a m u
n i k u wa h a m a k i s h a
Waislamu na kupalilia
mfarakano mkubwa wa
kipumbavu kabisa baina
ya Wakristo na Waislamu
wa Watanzania. Na hili ni
jambo la khatari kubwa
sana kwa nchi nzima
ya Tanzania, na Serikali
ya Ta n z a n i a n d i y o
itakayokuja kulaumiwa
na dunia kwa kushiriki
katika propaganda
h i z i k wa k u o n e s h a
kama hawayaoni na
h a ya wa k h u s u h a y o
yanayosomeshwa
shuleni. Vita vya
maneno vimeanzishwa
zamani, jee viongozi
wenye busara Tanzania
watapigania kiungwana
na kwa haki kuviondosha
au watashika mirengo
na kuvipalilia vita hivi
na raia wa kila upande
kukutishwa maafa
kama waliyokutishwa
Waruwanda, Wabosnia,
Wa z a n z i b a r i n a
wengineo?

Jambo moja wanafaa


wenye akili zao timamu
walifikirie vizuri
n i k u wa Wa i s l a m u
Tanganyika ni wengi na
hawatakubali wachinjwe
huku wamelala chali.
Kila mwenye akili
zake timamu anaelewa
fika kuwa kukianza
chinjachinja Tanganyika,
basi watachinjwa watu
wa dini zote wa pande
zote na misiba itakuwa
Ta n g a n y i k a k o t e ,
hakuna atakayesalimika
na ukoo wake wote.
Usia wangu ni kuwa
watu wote wema
wanaoipendelea mema
Tanzania watafute kila
njia za kuungana na
kuwapinga vikali sana
wenye kutapakaza siasa
kali za chuki, za ukabila,
udini na za aina yoyote
inayokhatarisha nchi.
Kwa ajili ya
propaganda za udini
ziliomo ndani yake,
vitabu vyote vya
historia vinavyotumiwa
shuleni Tanzania leo,
v i n a t a k a v i c h o m we
moto ili kuondosha na
kuuzika mmoja katika
mizizi mikuu ya fitina
inayopaliliwa katika
bongo za wanafunzi;
mzizi wa fitina ambao
unaendelea kuila
Tanzania ndani kwa
ndani na siku moja
itakuja kuleta khatari
pevu. Inahitajia badala
yake viandikwe upya
vitabu vya historia na
mabingwa wanaoijua
historia vizuri sana
na wasiopendelea
upande wowote wala
propaganda yoyote;
mabingwa wa historia
watakaoelezea matokeo
ya historia kwa ukweli
kama utakavyowe z e k a n a n a wa n a
Adamu. Huu ndio usia
wangu wa dhati. Ukiona
nina-shambuliwa mimi
binafsi na watu fulani
k wa n i l i y o ya e l e z e a
humu na kwa usia huu
nilioutoa, jua kuwa
viumbe hao ama ni wale
waliokwisha kupikwa
na kupikika vibaya
sana na propaganda
hi z o ni l i z oz i el ez ea ,
au ni katika wale
wanaonufaika na
propaganda hizo;
viumbe ambao
hawaipendelei mema
Tanzania na watu wake.

Habari/Tangazo

8
Na Salma
Alghaithiyyah, Zanzibar
WA K AT I Wa j u m b e wa
Baraza la Wawakilishi
Zanzibar
(CCM)
wakimkataa Makamo wa
Kwanza wa Rais Maalim
Seif Sharif Hamad kuingia
katika Baraza wakati wa
kufungwa kwa Baraza, ZEC
imeshushiwa tuhuma nzito.
Tuhuma hizo ni ukiukwaji
wa sheria na taratibu za
uandikishaji wapiga kura
ambapo CUF wanadai kuwa
ZEC inatumiwa na CCM
kuandikisha mamluki wa
kukipa chama hicho tawala
ushindi.
Katika kikao chake jana,
Wawakilishi hao walikataa
uwepo wa Maalim Seif wakati
Baraza hilo litakapofungwa
leo na kuvunjwa rasmi na
Rais wa Zanzibar Dk Ali
Mohammed Shein.
Kwa mujibu wa sheria,
R a i s h u i n g i a n d a n i ya
ukumbi wa Baraza akiwa
na wageni wake ambapo
ni Jaji Mkuu wa Zanzibar
Omar Othman Makungu na
Mshauri wake Makamo wa
Kwanza wa Rais Maalim Seif
Sharif Hamad.
Kwa mujibu wa kanuni
za Baraza hilo, wageni
hao wanapoingia ndani
ya ukumbi huo, inabidi
kutenguliwa kwa baadhi
ya kanuni kwa kuwa sio
wajumbe wa Baraza.
Hivyo, Spika wa Baraza
hilo Pandu Ameir Kificho
alitoa taarifa ya kuwaarifu
wajumbe juu ya ujio wa
wa g e n i h a o n a k u t a k a
waridhie.
Tunamtegemea Rais
wa Zanzibar atakuja na
ujumbe wake maalumu,
kwa hivyo tunamtegemea
pia Jaji Mkuu, Jaji Makungu
na tunamtegemea Mshauri
Mkuu mmoja wapo wa Rais
ambaye ni Makamo wa
Kwanza wa Rais, Maalim
Seif Sharif Hamad ambaye
naye tunategemea kuingia
humu ndani.
Spika Kificho akaanza
k u wa h o j i wa j u m b e wa
baraza hilo kwa mtu mmoja
mmoja, kati ya hao wageni
watatu akianzia kwa Rais
wa Zanzibar, Jaji Mkuu na
alipofika kumtaja Maalim
Seif hali ikabadilika.
Mgeni mwengine
maalumu huyu ni mshauri
wa Rais ambaye ni Makamo
wa Kwanza wa Rais, Maalim
Seif Sharif Hamad.
Alipoanza kumtaja
jina, wajumbe wakaanza
kuongea chini kwa chini
ikaanza minongono ambapo
Spika akauliza mbona
anasikia minongono kama
hawamtaki.
Mbona nasikia
minongono kama
hamumtaki.. nataka nisikie
rasmi, aje au asiingie humu?
Alihoji Spika Kificho.
Hapo Wajumbe wakajibu
kwa sauti kwamba asije.

AN-NUUR

RAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 26- Julai 2, 2015

HalisishwariZanzibar

Hawamtaki kuingia ndani ya


ukumbi huo.
Spika akauliza tena, Ina
maana Baraza halikuridhia
Maalim Seif kuingia humu
ndani?
Wakajibu, ndio hatutaki
asije humu ndani, hatumtaki.
Huku akicheka, Spika
Kificho akasema kwa kawaida
masuala haya huwa hayana
mjadala, na akawaambia
wajumbe wa Baraza hilo
kwamba kwa kuwa yeye
ndiye aliyemuandikia
barua Makamo wa Kwanza
kumualika katika kikao hicho,
atalazimika kumuandikia
barua nyengine ya kutengua
mualiko huo kutokana na
wajumbe kumkataa asiingie
ndani ya ukumbi huo.
Kikawaida mimi ndiye
niliyemuandikia barua ya
kumualika kuja hapa, kwa
hivyo nitaandika nyengine
kwa heshima zote kwamba
usije.
Alisema Spika huku
wa j u m b e h a o wa k i p i g a
makofi na kuongea kwa
furaha.
Inavyoelekea Wawakilishi
hawa kupitia CCM,
wa m e c h u k u a h a t u a h i i
kufuatia kitendo cha wenzao
kupitia CUF kususa vikao
vya kumalizia Baraza.
Mapema wiki hii,
Wawakilishi
hao
kupitia CUF wakiwemo
mawaziri, walitoka nje ya
kikao na kusema kuwa
hawatahudhuria hata
kikao cha kuvunjwa Baraza
k i t a k a c h o h u t u b i wa n a
Mheshimiwa Rais Shein.
Walisema, wanafanya
hivyo kusajili malalamiko
yao kuwa upo ukiukwaji
mkubwa wa sheria, kanuni na
taratibu katika uandikishaji
wapiga kura.
Wa k a t i h u o h u o ,
Mwenyekiti wa Tume ya
Uchaguzi, Mheshimiwa,
Jecha Salim Jecha, ametupiwa
lawama nzito kuwa Tume
yake inafanya mambo
ambayo yanaweza kuvuruga
uchaguzi.
Moja ya tuhuma hizo ni
madai kuwa ZEC inawekewa
shinikizo iongeze siku za
uandikishaji kutoa fursa kwa
CCM kukamilisha kazi ya
kuandikisha wapiga kura
haramu.
Katika barua yao kwa
Mwenyekiti Jecha, CUF
wanadai kuwa wana taarifa
za kuaminika kwamba CCM
kwa kushirikiana na Wakuu
wa Mikoa na Wakuu wa
Wilaya pamoja na Ofisi ya
Usajili wa Vitambulisho vya
Mzanzibari Mkaazi iliandaa
wapiga kura haramu ambao
walipatiwa vitambulisho vya
ZAN ID ili kuwawezesha
kuandikishwa kuwa wapiga
kura kwa lengo la kukisaidia
CCM.

Hata hivyo wanadai kuwa,


utolewaji na usambazaji wa
vitambulisho hivyo ulikwama
na kupelekea vitambulisho
hivyo kupatikana ikiwa
uandikishaji wa wapiga
kura katika majimbo ya
Wilaya ya Magharibi A
umeshamalizika.
Ni kutokana na hali hiyo,
wanadai kuwa baada ya
kupatikana ID hizo, ndio
zinafanyika njama kuongeza
siku kutoa fursa kwa wenye
ID hizo kuandikishwa.
Jumla ya ZAN ID
zilizochapishwa kwa ajili
ya u h a r a m i a h u u k wa
Wilaya za Magharibi A na
Magharibi B ni 39,500 na
mpaka jioni ya tarehe 23 Juni,
2015 walipatiwa ZAN ID
6,525 ambazo walishindwa
k u z i t u m i a k wa k u k o s a
watu. Kati ya hizo, jumla ya
ZAN ID 1,200 zilipelekwa
zikagawiwe katika jimbo
la Bububu ambako muda
wa uandikishaji ulikwisha
malizika wakati ZAN ID
hizo zinawafikia viongozi
wa CCM.
Wanadai CUF katika barua
yao kwa Mheshimiwa Jecha
na kuongeza kudai kuwa:
Baada ya kutofanikiwa
kikamilifu, viongozi wa
CCM jioni ya siku hiyo
hiyo ya tarehe 23 Juni, 2015
walikutana katika Ofisi yao ya
Mkoa wa Mjini iliyopo Amani
na kupitisha maamuzi ya
kuitaka Tume ya Uchaguzi ya
Zanzibar iongeze siku ili kuja
kupandikiza wapiga kura
haramu kwa idadi ya mkakati
iliyokuwa imepangwa.
Na kwamba, iliamuliwa
kuwa ZAN ID hizo
zihamishiwe katika majimbo

ya Wilaya ya Magharibi B
katika uandikishaji ulioanza
tarehe 24 Juni, 2015.
Katika barua hiyo ambayo
nakala yake imesambazwa
kwa Wahariri wa Vyombo
vya Habari, CUF kupitia
kwa Naibu Katibu Mkuu
wake Nassor Ahmed
Mazrui wanadai kuwa, kazi
ya kugawa ZAN ID kwa
makundi ya watu walioletwa
kwa magari nje ya vituo vya
uandikishaji imefanyika
ambapo waliambatanisha
picha inayomuonesha
mmoja wa watu wa CCM
akigawa ZAN ID hizo katika
kituo cha Shakani, jimbo la
Dimani.
Kwa barua hii, CUF
tunaitahadharisha Tume ya
Uchaguzi ya Zanzibar kuacha
kuendelea kuitumikia CCM
k wa k u p o k e a a g i z o l a
kuongeza siku ili kusaidia
kufanikisha mikakati ya CCM
inayoshindwa. Ilihitimisha
barua hiyo ya CUF.
Katika barua yao nyingine
kwa Mwenyekiti wa ZEC,
Chama Cha Wananchi, CUF
wanadai kuwa wana taarifa
kutoka vyanzo vya habari
vilivyomo ndani ya Chama
Cha Mapinduzi (CCM)
kwamba kumeandaliwa
mpango wa kuvitumia vikosi
kusaidia katika kuipa CCM
ushindi.
Wamedai kuwa,
utumikaji huo ni pamoja na
kuandikishwa katika maeneo
ambapo sio wakazi pamoja
na kutumika kuwadhibiti
mawakala wa CUF ambao
wanahoji wanapoona

wakiletwa mamluki
au kuandikishwa watoto
wadogo.
Wanatoa mfano kuwa
wapo watu wanaokuja na ID
bandia kwa hiyo, mashine
zinakataa kuwatambua.
Hata hivyo, polisi
waliopo vituoni hutumika
k u l a z i m i s h a wa t u h a o
waandikishwe na Tume
haichukui hatua, kuonyesha
kuwa wanajua mpango huo.
Katika kituo cha
Chuini, jimbo la Mfenesini
vitambulisho 109 vilikataa
kutambuliwa na mashine,
hata hivyo nguvu kubwa
ilitumiwa na kuhakikisha
kuwa
watu
hao
wanaandikishwa. Hatua
hiyo ilipelekea mzozo baina
ya wananchi na vikosi, na
hivyo wananchi waliokataa
ukiukwaji huo wa taratibu,
uliochochewa na Tume yako,
walipigwa na kukamatwa
kwa kuwekwa katika vituo
vya Polisi na kunyimwa
dhamana.
Ilisema sehemu ya barua
kwa Mwenyekiti wa ZEC
na kuhitimisha kwa kusema
kuwa CUF itaendelea kutoa
mashirikiano kwa Tume ya
Uchaguzi ya Zanzibar kwa
mambo yote yanayofuata
misingi ya katiba na sheria
na misingi ya uchaguzi huru
na wa haki inayotambuliwa
kimataifa.
Miezi miwili iliopita
akizungumza na waandishi
wa habari ofisini kawake,
Mkurugenzi wa Tume ya
Uchaguzi Zanzibar (ZEC),
Salum Kassim Ali alieleza
kuwa tume hio haina
mafungamano na taasisi
yoyote hile katika ufanyaji
kazi wake na wamekuwa
wakifanya kazi zao kwa
ustadi mkubwa.

MASHINDANO YA TISA YA KUHIFADHI QURAN

KAMATI YA MUUNGANO YA MASHINDANO YA SHULE ZA KIISLAMU


Assalaam alaykum warahmatullahi wabarakaatuh
Umoja wa shule za msingi za Kiislamu Tanzania (TIPSO) pamoja na
kamati ya pamoja ya kuhifadhi Quran inawatangazia wazazi, walezi,
walimu, wanafunzi na Waislamu wote kufanyika mashindano ya tisa ya
kuhifadhi Quran kwa shule za misngi za Kiislamu Tanzania kama ifuatavyo:
Jumamosi 27/06/2015 katika Msikiti wa Kichangani Magomeni-Dar es
Salaam
Jumapili 28/06/2015-Fainali katika ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es
Salaam.
Muda ni kwa siku zote mbili kuanzia saa 2:00 Asubuhi 6:30 mchana.
Wote mnakaribishwa.
Holy Quran Recitation Joint Committee
Mb: Mwenyekiti 0713 334 698, Katibu 0784 211673, Mweka hazina
(Treasurer) 0717 304 353 Email:recitationquran@yahoo.com

9
Na Khalid S. Mtwangi
WAISLAMU wa Tanzania
leo hii wamepata msiba
mkubwa kutokana
na kifo cha kiongozi
mkuu Sheikh Mkuu wa
Baraza Kuu la Waislamu
Ta n z a n i a ( B A K WATA) ,
Sheikh Issa Shaaban bin
Simba. Ikubalike kwamba
Waislamu wa Tanzania
wamempoteza kiongozi wao
mashuhuri sana, na labda
haitakuwa rahisi kuziba
pengo aliloliacha. Alikuwa
katika uongozi huo kwa
muda mrefu hasa akiwa
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa
Shinyanga. Bila sababu za
msingi na vikiwa vyombo
vyenye madhumuni
tofauti, lakini Katiba ya
BAKWATA inafanana sana
n a i l e ya TA N U / C C M .
Unapata Sheikh wa wilaya
ikiwa Wilaya ya kiserekali
hata kama wilaya ile ina
Waislamu wachache sana.
Katika Uislamu, Wilaya
ni sehemu kubwa sana ya
nchi. Idadi ya Waislamu
katika Mkoa wa Shinyanga
haifahamiki vizuri, lakini
inasemekana kuwa kwa
D a a w a c h i n i y a A l Marhum Issa Bin Shaaban
Simba, idadi hiyo ilikuwa
ikiongezeka kidogo kidogo.
L a k i n i wa k a t i f u l a n i
huko nyuma, nilipata
waraka kutoka kwa
m wa n a h a r a k a t i m m o j a
Muislamu aliyewahi kuishi
Shinyanga kwa muda mrefu
tu. Waraka huu ulijaribu
kunielimisha kuhusu
mienendo ya Waislamu wa
Shinyanga katika jitihada
ya kuusimamaisha Uislamu
Mkoani humo. Kweli ama
si ya kweli, si dhamiri
kuyanukuu hayo yaliyomo
katika waraka huo. Hayo
si mada ya makala haya.
Itoshe tu kusema kuwa kwa
maoni ya huyu Muislamu
aliyeandika waraka ule, yeye
aliona kulikuwa na kasoro
kubwa katika ule mwenendo
wa kuwahudumia
Waislamu wa Shinyanga
na wa Tanzania kwa jumla.
Ningependa kusisisitiza tu
kwamba, kama kuna kasoro
alizozitoa, hazikuwahusu
viongozi wote wa Shinyanga
wa wakati ule.
Ni bahati mbaya sana
kuwa katika uongozi wa
Al Marhum Sheikh Issa Bin
Shaaban Simba, ni vigumu
sana kutaja kwa uhakika ni
wapi Waislamu wanaweza
kujivuna angalau kidogo
hapa Uislamu na Waislamu
wamepiga hatua kubwa ya
maendeleo. Wao wenyewe
katika hali ya kutaabad ama
kujivuna kuwa Uislamu
umekuwa na unaheshimika
zaidi. Yaani iwe katika
daawa ama kwa mfano
Waislamu sasa wameongeza
shule na vyuo kadhaa.
Wa i s l a m u wa Ta n z a n i a
wamshukuru kiasi gani

Makala

AN-NUUR

RAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 26- Julai 2, 2015

Bakwata leo na kesho

ALIYEKUWA Sheikh Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Al-Marhuum


Sheikh Issa Shaaban bin Simba .
Rais Mstaafu Muheshimiwa
Benjamin William Mkapa
ambaye pamoja na Ukatoliki
wake, aliwaonea huruma
Waislamu wa nchi hii na
kuwapa majengo walioweza
kusimika Chuo Kikuu hapo
Morogoro. Bahati nzuri Chuo
hicho hakimo mikononi mwa
BAKWATA. Inasemekana
kuwa kulikuwa na upinzani
mkubwa kutoka kwa baadhi
waliomo Serekali, wale
wasio Waislamu. Wakati
huo huo Kanisa Katoliki,
kwa mfano, leo hii wanaweza
kujivunia vyuo vikuu zaidi
kumi nchi humu. Labda
itakuwa si vibaya kusisitiza
kuwa BAKWATA hawana
hata Chuo Kikuu kimoja na
hii maana yake ni kwamba
Waislamu nchini kila siku
watakuwa nyuma katika
elimu.
Nadhani Waislamu wa
Tanzania hata hawajasikia
hiyo BAKWATA ina mipango
gani kuwaendeleza upande
huo. Kweli ni baada ya
ule mzozo wa viwanja vya
Changombe ndio Waislamu
waliposikia kwamba
kutakuwa kiwanja mbadala
cha kujenga chuo. Taarifa
ambayo haikuwa na msingi
wowote. Labda tosha
tu Ustadh Issa Ponda na
wenzake wameteseka kwa
kutetea mali ya Waislamu.
Hiyo ndiyo BAKWATA jana
na leo. Kesho itakuwaje?
Waislamu wasubiri uchaguzi.
Kifo cha Sheikh Bin
Shaaban Simba, Sheikh
Mkuu wa BAKWATA kitaleta
uongozi mpya pale kileleleni

ambao, ni mategemeo ya
wengi, labda nao utalazimika
kuleta mabadiliko ya
uongozi wote wa Chama
hicho nchi nzima. Ni hapo
ndipo Waislamu wa Tanzania
watakuwa wanatazamia
mabadiliko makubwa katika
musakbali wa Uislamu nchini
humu. Huko mbele kuna
nini? Watajiuliza.
Ni ukweli ambao ukubalike
kuwa imekuwa vigumu sana
huko nyuma kuleta mageuzi
katika uendeshaji na utawala
wa chombo hiki BAKWATA.
Wakati akiwa Rais wa nchi
hii Muheshimiwa Al Haj
Ali Hassan Mwinyi alijaribu
kutaka kuleta mabadiliko ya
uongozi humo BAKWATA
kwa hiyo uje utawala
mwingine; na mfumo pia
ubadilike. Mzee Rukhsa
hapa alikuta kizingiti
ambacho hakikumpa rukhsa
apite. Hakika bila shaka
k u t a k u wa n a wa s o m a j i
watakaokumbuka hotuba
ya Sheikh Mkuu wa wakati
u l e wa k a t i wa M a u l i d
iliyosomewa Shinyanga.
Sheikh Mkuu yule alisikika
akidiriki kusema huyu Rais
Mwinyi ataiweza wapi,
BAKWATA ina wenyewe.
Hakusema hapo wenyewe
ni kina nani. Kweli baadae
Rais Mwinyi hakutaka kabisa
kuigusa BAKWATA ambao
wao waliendelea kivyao na
mambo yao kama kawaida.
H u k u Wa i s l a m u
wamebaki nyuma katika
maendeleo ya nchi hii, jambo
ambalo linajulikana na kila
Muislamu na kulalamikiwa
mara kwa mara kama sio
kila siku. Naye Rais Jakaya

Kikwete alitoa malalamiko


mengi dhidi ya BAKWATA
mara baada ya kushika
hatamu za kuiendesha nchi
hii Tanzania. Bila shaka
wako watakaokumbuka
hutuba yake kule Arusha.
Alisikika akiwashauri kwa
nguvu kabisa kuwa viongozi
w a B A K WATA l a z i m a
wabadilike na mfumo wao
pia ubadilike. Takriban miaka
kumi baada ya ushauri huo
kutoka kwa Rais wa nchi hii,
BAKWATA iko pale pale.
Ni kweli kuna wakati
Al Marhum Sheikh Bin
Shaaban Simba alijaribu
kutikisa kidogo uongozi
wa Makao Makuu, kitendo
ambacho kwa muda kilileta
tumaini la maendeleo.
Wa k a t i f u l a n i a l i s i k i k a
akiwafokea wale waliokuwa
wakipita wakisema ati kuwa
BAKWATA ni chombo cha
CCM na Serekali. Huko
nyuma, takriban miaka minne
mitano hivi, nilikutana na
sheikh mmoja ambaye wakati
huo alikuwa na wadhifa hapo
makao makuu ya BAKWATA.
Kwa mbwebwe za kujiamini
kabisa, alinihakikishia kuwa
BAKWATA aliyokuwemo
yeye sio sawa na BAKWATA
ile ya zamani. Sasa inataka
kuleta mapinduzi kweli kweli
katika harakati za kuwaletea
maendeleo Waislamu wa
Ta n z a n i a . S h e i k h h u y u
anisamehe sana ataposoma
makala haya na kukuta
nikiwajulisha wasomaji
wenzangu kuwa haukupita
muda mrefu sheikh huyu
alifukuzwa katika uongozi.

Kuvuliwa kwake madaraka


lilikuwa ni jambo baya sana
k wa m a o n i ya n g u k wa
sababu huyu ni mmoja wa
wale masheikh wana elimu
na sifa stahiki. Alikuwa ana
Diploma ya Ualimu na leo ana
degree ya fani hiyo aliyoipata
kutoka Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam.
N a S h e i k h M k u u wa
wakati ule alipowaambia
Waislamu kuwa BAKWATA
ina wenyewe, hakuwataja
hao ni kina nani. Hakika
asingeweza kutaja siri hiyo
hadharani, lakini ni muhimu
hao wenyewe watambue
kuwa leo hi ni mwaka 2015
hali yake katika nyanja nyingi
sio sawa na 1968 BAKWATA
ilipozaliwa pale Iringa huku
Waislamu wakisimamiwa
wakipewa ulinzi na askari
wenye ala zao kamili. Ukumbi
mzima hapo paliposimikwa
uongozi mpya wa Waislamu
wa BAKWATA, ulizungukwa
na hawa watumishi wa
wananchi silaha zao
(bunduki) zao zikionyeshwa
wazi wazi.
N i m e wa h i k u a m b i wa
na Sheikh Khamis Mataka
kwamba katika utamaduni
wa Kiislamu kiongozi
hachaguliwi kwa kupigiwa
kura. Panapotokea kiasi
k i k u b wa c h a wa u m i n i
wakatoa hisia zao kwa sauti
kubwa kumtaja wanayemtaka
awe kiongozi wao, basi ndiye
huyo atakuwa amechaguliwa
na waumini awe kiongozi
wao. Sio hivyo alivyopatikana
Khalifa wa kwanza Sayyidna
Abubakar RA? Labda katika
hali tuliyonayo, Waislamu
nchini humu uteuzi wa
aina hiyo usiwezekane hasa
kwa vile BAKWATA kwa
mfano itatakiwa kuviridhisha
vyombo vingi vikiwemo vya
Serekali kwamba uchaguzi
wa Sheikh Mkuu mpya
wa BAKWATA umefuata
misingi ya kidemokrasia
kama inavyoeleweka na
Serekali na umeendeshwa
kama katiba ya BAKWATA
inavotaka. Lakini muhimu
ni kukumbuka kwamba wale
Waislamu wanaoongozwa
na BAKWATA watambue
kwamba wamepata nafasi
nzuri adimu sana ya kuweza
kubadili mwenendo mzima
wa utawala wa chama chao.
Mabadiliko ambayo yataweza
kuwavutia labda Waislamu
wengi, kama sio wote wa
Tanzania. Uje utawala ambao
hakika utaleta maendeleo
muhimu na makubwa kwa
Uislamu na Waislamu wa
Tanzania.
Hapo BAKWATA itaweza
kupata heshima kubwa
sana labda miongoni mwa
Waislamu wote wa Tanzania
na bila kuwaudhi wale
wanaosemekana kuwa ndio
wenyewe.

10

Makala

AN-NUUR

RAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 26- Julai 2, 2015

Darasa la Miundombinu: Ni wapi ISIS inapata bunduki zake?


Na Tony Cartalucci
Juni 10, 2015 - 'Mtandao
wa Kupashana Habari'
'NEO'

TANGU enzi za kale jeshi


lilikuwa na haja ya msaada
wa miundombinu ili
kuweza kutekeleza aina
yoyote ile ya shughuli za
kijeshi la uwanda mpana.
Katika Roma ya zamani,
mtandao mkubwa wa
barabara ulijengwa
kuwezesha siyo biashara
peke yake, bali kuruhusu
vikosi vya majeshi ya
Roma kwenda haraka
mahali walipokuwa
wanahitajiwa., na
kuwasilisha mahitaji kwa
ajili ya shighuli za kijeshi
kufuatilia uwasilishaji
huo.
Kuelekea mwisho wa
karne ya 18, jemadari
wa Ufaransa, bingwa
wa mikakati ya kijeshi
na kiongozi, Napoleon
Bonaparte akaainisha
kuwa "jeshi linatembea
kwa tumbo lake," akielezea
upana wa miundombinu
unaohitajiwa kuwezesha
jeshi kuwa na chakula cha
kutosha, na hivyo kuwa
na uwezo wa kudumisha
kiwango chake cha
kuendesha mapigano.
K w a Wa f a r a n s a ,
k u s h i n d wa k u p e l e k a
vifaa vinavyohitajiwa kwa
wakati kwa majeshi yake
yaliyokuwa yakipigana
nchini Russia, na maamuzi
ya Warussia kuchoma
ardhi yao na miundombinu
ili isitumiwe na majeshi
ya wavamizi, mwishowe
iliwezesha kushindwa
kwa Wafaransa.
Ujerumani ya ki-Nazi
ilifikia hatma hiyo hiyo
wakati ilipotanua vile
vile kupita kiasi uwezo
wake wa miundombinu
wakati wa uvamizi
wake wa Russia katika
Operation Barbarossa.
K a m a a wa l i , m a j e s h i
ya uvamizi yalikwama
ya k i wa n a u h a b a wa
vifaa kabla ya kuzingirwa
na kuteketezwa au
kulazimishwa kurudi
nyuma.
Na katika nyakati za
karibuni wakati wa Vita ya
Ghuba mapema miaka ya
1990, kuwepo kwa mkanda
mrefu wa kuwasilisha
vifaa kwa majeshi ya
Marekani ikijumlishwa
na kutazamia kukutana
na sehemu kubwa

MAMA yake Usamah (katikati) baada ya mkutano na waandishi wa habari.

MAMA Usamah (katikati) na wanawake wenzake wakiswalia jeneza la mwanae.


ya majeshi ya Saddam
Hussein, ilipunguza kasi
ya uvamizi kasi ambayo
wengi walidhani ungefika
Baghdad kama dhamira ya
kisiasa ingekuwepo. Nia
ya kumpiga ilikuwepo,
miundombinu ya kumpiga
ilikuwa hafifu.
Mafunzo kutoka
historia kwa kiasi
ambacho yanaweza
kuyakinishwa, yanaelekea
kutokuwa na undani, iwe
n i k wa m b u m b u m b u
au udanganyifu wa
kushangaza wa waweka
sera na vyombo vya habari
vya nchi za Magharibi.

Miundombinu ya ISIS
Mfarakano mkubwa
hivi sasa unaoiangamiza
Mashariki ya Kati, hasa
katika nchi za Irak na Syria
ambako kinachodaiwa
ni 'Dola ya Kiislamu\'
(ISIS) kinajiendesha na
papo hapo kupigana na
kuyashinda majeshi ya
Syria, Lebanon, Irak na Iran,
tunaambiwa, imejengwa
kwa miundombinu ya
ulanguzi na malipo ya
utekaji nyara.
Uwezo wa kupigana wa
ISIS ni wa serikali kamili.
Inashikilia eneo pana
linalosambaa kote Syria

na Irak na siyo tu inaweza


kulinda kijeshi na kupanua
eneo hili, lakini ina
raslimali za kulisimamia
eneo hilo, na hata raslimali
za kutawala makundi
ya wakazi wa maeneo
h a y o i l i y o t e k a , K wa
wachambuzi wa masuala
ya kijeshi, hasa washiriki
wa zamani wa majeshi
ya nchi za Magharibi,
p a m o j a n a wa s h i r i k i
wa vyombo vya habari
vya nchi za Magharibi
waliokuwa katika misafara
ya malori ya kijeshi ya
mizigo iliyohitajika kwa
ajili ya uvamizi wa Irak
miaka ya 1990 na halafu

m wa k a 2 0 0 3 , l a z i m a
watashangaa hayo malori
ya ISIS yako wapi leo. Kwa
hali yoyote, kama raslimali
za kuwezesha uwezo wa
kuendesha shughuli za
kijeshi ulioonyeshwa na
ISIS ulikuwa unapatikana
katika maeneo ya Syria
na Irak pekee, basi kwa
hakika majeshi ya Syria na
Irak yangekuwa na uwezo
wa kupigana kama huo
au zaidi lakini kimsingi
hawana.
Na ingekuwa njia za
kupeleka vifaa za ISIS
zipo ndani ya maeneo
hayo ya Syria na Irak, basi
kwa hakika majeshi ya
Syria na Irak yangeweza
kutumia wanachowazidi
ISIS, ndege za kivita kuvuruga uwezo wa ISIS
kutumia njia hizo.
Lakini yote hii haitokei
na kuna sababu kwanini.
Magaidi na silaha
zilizoachwa katika
uvamizi wa Libya mwaka
2011 hima zilihamishiwa
Uturuki na halafu Syria zikisimamiwa na maofisa
wa Wizara ya Mambo
ya Nje ya Marekani na
mashirika ya kijasusi huko
Benghazi - kituo cha ugaidi
kwa miongo kadhaa. Njia
za kuwasilisha vifaa za ISIS
zinatokea pale ambapo
Syria na Irak hazina uwezo
wa kupeleka vita vya anga.
Kuelekea kaskazini kwa
mashirika wa NATO,
Uturuki, na kusini
mashariki kwa washirika
wa Marekani wa Jordan
na Saudia. Nje ya mipaka
hii kuna mtandao wa
miundombinu unaoenea
ukanda mzima ikiwa ni
pamoja na Ulaya Mashariki
na Afrika Kaskazini.
Gazeti la kila siku
l a L o n d o n Te l e g r a p h
likatangaza katika
m a k a l a m wa k a 2 0 1 3
kuwa CIA inaendesha
kituo cha kupeleka silaha
hapo Benghazi wakati
ubalozi (wa Marekani)
unashambuliwa. Ilinukuu
shirika la utangazaji la
Marekani, CNN likisema
kuwa timu-kazi ya CIA
ilikuwa ikifanya kazi
zake kando ya ubalozi
huo kuandaa mradi wa
kupeleka makombora
kutoka maghala ya silaha
ya Libya kuelekea kwa
waasi nchini Syria.
Silaha pia zimetokea
Ulaya Mashariki, kwa
Inaendelea Uk. 12

11

Makala

AN-NUUR

RAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 26- Julai 2, 2015

Maswali tata yatanda kuhusu kuuawa


Boston kwa 'mkata kichwa' wa ISIS
Glenn Greenwalld na
Murtaza Hussain
HIVI karibuni katika
eneo la Boston, kijana
mweusi wa Kiislamu
mwenye umri wa miaka
26, alipigwa risasi na
kuuawa na maofisa wa
Shirika la Upelelezi la
Marekani (FBI) na Idara
ya Polisi ya Boston (BDP).
Kama ilivyoonyeshwa
siku iliyofuata, vyombo
vikubwa vya habari kwa
haraka, kwa mhemko na
bila kutafakari, vikarudia
madai ya utekelezaji
wa sheria za nchi (mara
nyingine hutumwa bila
msemaji kujitaja) kuhusu
kilichotokea: kuwa
mtu huyo aliyekufa,
Usaamah Rahim, alikuwa
anakaribia kutekeleza
mauaji yanayotokana
na ushabiki wake kwa
ISIS au kwa kuhusika
na kundi hilo la kigaidi,
kuwakata vichwa
maofisa wa polisi bila
mpangilio halisi, akiwa
anashirikiana na takriban
watu wawili wengine.
Wakati Rahim anatembea
kwenda kazini karibu
n a d u k a l a d a wa l a
CVS majira ya saa moja
asubuhi, maofisa hao wa
polisi walimfuata Rahim
kumuuliza tu kuhusu

KIJANA Usamah wakati akiwa shuleni.


mpango huo; ghafla,
akatoa 'sime' au 'kisu
cha kijeshi' ambacho
alikataa kukiangusha, na
kuwalazimisha maofisa
hao kumpiga risasi

kichwani.
Kulikuwa na kila
aina ya maswali ya
wazi yasiyoeleweka
k u h u s u m a d a i h a ya ,
na bado yaliachwa

faida isiyo ya kawaida ya


fedha ambayo hatua hizo za
uvamizi zimewezesha baadhi
ya makundi yenye nguvu
ya maslahi katika nchi za
Magharibi.
Wakati huo huo, serikali
za nchi za Magharibi na
m a k u n d i ya k i h a r a k a t i
sawia yameendelea kutumia
uzungumzaji huu kuelekea
malengo yao ya kisiasa
na kiuchumi. Usawiri wa
Vita dhidi ya Ugaidi kama
mapambano ya kimataifa
"imefanya hata mashambulizi
ya kigaidi ya ndani ya nchi
kuonekana kama sehemu ya
mapambano haya mapana."
Kinacholeta wasiwasi kwa
kiasi kikubwa pia ni kuwa
mitandao hii ya kimataifa
inaendelea kwa kasi
kubadilika kuwa jitihada ya
kuunda 'Dola ya Kiislamu
(bandia)' ya kudumu katika
ombwe lililoachwa na
uvamizi wa Marekani nchini
Irak.

Pia, inabidi iainishwe


kuwa kuuawa kwa Osama
bin Laden na kupunguzwa
kwa kiasi kikubwa nguvu
za Al Qaeda kama taaisi ya
kisiasa na kijeshi, haijaifikisha
vita hii katika tamati
yake. Badala ya kufunga
mitiririko ya fedha za vita,
sasa kuna "maadui" wapya
kama ISIS ambao lazima
wateketezwe. Vita dhidi ya
ugaidi imeondoka katika
mfumo wa sinema kubwa
ya mamilioni ya dola za
Marekani na kuwa mtiriririko
wa tenda unaolipiwa kwa
damu na dhahabu.
Mpango halisi ni kuwa
hakuna mpango kama huo.
Ni ukweli unaoonekana
kuwa nchi za Magharibi na
makundi ya washirika ni
heri waendeleze tamthiliya
kuhusu ugaidi kuliko
kuruhusu nguvu zake
za kiuchumi na kisiasa
kuingizwa mashakani kwa
kiwango kikubwa. Marekani

tu na kilichosikika ni
kiwewe kuwa 'ISIS
iko Massachusetts!' na
mihangaiko mingi
kuhusu watu kukatwa
vichwa. Hii ni moja ya
mambo yanayosumbua
sana kuhusu tukio hili:
polisi sasa wanaweza
kumsimamisha mtu
barabarani ambaye,
kwa ushahidi wowote
uliopo, hakuwa anafanya
lolote baya wakati huo,
wamwue, halafu wapaze
sauti tu "ISIS' na 'Gaidi'
n a ' k u k a t wa k i c h wa '
na kurudiarudia na
hakuna maswali yoyote
yatakayoulizwa.
Kuwashawishi
wa a n d i s h i wa h a b a r i
wakubali madai yao, FBI
na BDP walisisitiza kuwa
kulikuwa na mkanda
wa kamera ya ufuatiliaji
ambao ungeondoa shaka
kuhusu kilichotokea,
wakidai kuwa "ufuatiliaji
kwa kamera ya video
umedhihirisha kile
maofisa walichosema."
Lakini hawakutoa
mkanda huo, na badala
yake wakatumia karibu
wiki mbili kulainisha na
kuvuruga akili za watu kwa
kurudia madai kuhusu
kile ambacho video hiyo
ambayo haijaonekana
inachoonyesha.
Video hiyo mwishowe

ilitolewa. Kuiita video


hiyo kuwa ni kichekesho,
ingekuwa upendeleo.
Kamera ipo umbali wa
mita 50 kutoka tukio
l i l i p ot ok e a . K i oo cha
kamera kimefichwa na
matone ya mvua. Viwiliwili
vya watu vinatambulika
kwa taabu. Hakuna silaha
zinazoonekana, ikiwa ni
pamoja na silaha yoyote
aliyokuwa nayo Rahim.
Wa k a t i i n a o n y e s h a
kuwa Rahim hakupigwa
risasi kwa nyuma kama
kaka yake alivyosema
mwanzo (na baadaye
akakiri kuwa hakuwa
na ufahamu sahihi),
haionyeshi chochote
k i n g i n e . K wa j u m l a ,
haiwezekani kusema
nini kilitokea kutokana
na video hii iliyopigiwa
c h a p u o s a n a , n j e ya
kuwa Rahim anaonekana
alikuwa akitembea kwa
amani wakati alipofuatwa
na watu kadhaa, ambao
hawakuwa wamevaa sare
za polisi, katika mfumo wa
kutishia, kijeshi:
Vyombo vya habari
vilivyokuwa vinaikuza
video hiyo kama
uthibitisho wa kile polisi
walichosema haraka
wakaona kuwa inaonyesha
kinyume chake. "Kutoa

na washirika wake wanaamini


kuwa wanaweza kutesa,
kuvamia, kuua, kukandamiza
na kulitumia tatizo hili la
ugaidi lisionekane; kuwa
kinachohitajika tu ni kuua na
kupiga marufuku wanasiasa
kali wa kutosha na ustawi
wake (bila kuzungumzia
kuendelea kuitamalaki
dunia) utahakikishwa.
Kinachotakiwa sasa ni
habari mpya ya tumaini na
harakati - ambayo haitokani
na hadithi tupu zenye vitendo
vya kiharamia, am bako

maendeleo haya siyo taifa


la kibeberu linaloendeleza
vita ya msalaba lenye
dhamira isiyopindika
ya kufikia 'haki' yake ya
kisasi, lakini makundi
ya kidemokrasia na haki
za kijamii yakiunganika
pamoja kubadili dunia
kutoka chini hadi juu.
Bila kujali Bin Laden
alikufa kwa njia gani,
Vit a dhidi ya Ug aidi
ndiyo hasa 'tamthiliya'
inayohuzunisha.
( H i i n i s e h e m u ya
makala Fairy Tale of
the War on Terror kama
ilivyoandikwa na Peter
Bloom. Peter Bloom ni
mhadhiri katika Idara ya
Watu na Taasisi katika
Chuo Kikuu Huria.
Anaandika katika fani
za itikadi, mamlaka
na siasa za ubepari na
hivi sasa anakamilisha
tungo kuhusu 'Ubepari
wa K i i m l a Z a m a z a
Utandawazi.')

Inaendelea Uk. 17

Tamthiliya pevu ya vita dhidi ya ugaidi


Na Peter Bloom

Ugaidi kama tamthiliya


Vita dhidi ya ugaidi
inaendelea kuwa habari yenye
mashiko na ufanisi katika
kukusanya hisia za watu
pande mbili zinazohusika.
"Ugaidi wa kimataifa ni
taswira ya kubuni ambayo
imekolezwa na kuvurugwa
na wanasiasa," anaainisha
mwandishi mchokozi wa
Uingereza na mchambuzi,
Adam Curtis.
"Ni wingu potofu la fikra
ambalo limesambaa bila
kuhojiwa miongoni mwa
serikali duniani kote, majeshi
ya usalama na vyombo vya
habari."
Kisiasa, nchi za Magharibi
zimetumia vita hii ya msalaba
dhidi ya magaidi kuhalalisha
uvamizi angamizi mara
kadhaa pamoja na ukiukwaji
wa haki za binadamu ndani ya
nchi na ng'ambo. Pia inavuna

taifa lenye nguvu zaidi


ndiyo bora zaidi kimaadili,
ila ambalo badala yake
linaangalia kwa ukweli
nini kinachojificha nyuma
ya u h a r i b i f u h u u i l i
kutekeleza mabadiliko ya
kina kwa ajili ya ustawi wa
pamoja na uhuru halisi wa
kisiasa.
Tu n a c h o h i t a j i n i
mtiririko wa fikra
ambacho kinachosukuma

12

MAKALA

SWAUMU NA NDIMI ZETU

Ulimi tunu adhimu, ya MANANI kwa insani,


Ulimi tangu kadimu, kwa uneni namba 'wani',
Ulimi MWEMA mwalimu, na MUOVU kwa waneni,
NDIMI zetu TUCHUNGENI, WAFUNGAJI Ramadhani.
Ulimi johari njema, tukufu yenye thamani,
Ulimi kwa watu wema, u lulu na marijani,
Ulimi kwa taadhima, kwa kweli wakuthamini,
NDIMI zetu TUCHUNGENI, WAFUNGAJI Ramadhani.
Ulimi wainajisi, waovu yako thamani,
Ulimi wanakutusi, kwa kukupa sui nduni,
Ulimi u IBILISI, eti mkubwa SHETANI,
NDIMI zetu TUCHUNGENI, WAFUNGAJI Ramadhani.
Ulimi u sura mbili, kwa ya INSAFU mizani,
Ulimi anokujali, kwa KHERI wamuauni,
Ulimi asokujali, kwa SHARI haumukhini,
NDIMI zetu TUCHUNGENI, WAFUNGAJI Ramadhani.
Ulimi sasa kwanini, tuutie lawamani,
Ulimi mimi sioni, ulaumiwe kwanini,
Ulimi kosale nini, nijuzeni ikhiwani,
NDIMI zetu TUCHUNGENI, WAFUNGAJI Ramadhani.
Ulimi wa RAMADHANI, WAFUNGAJI uchungeni,
Ulimi kwa QUR-ANI, KUSOMA utumieni,
Ulimi za ADINANI, kwao HADITHI someni,
NDIMI zetu TUCHUNGENI, WAFUNGAJI Ramadhani.
Ulimi utumieni, kumdhukuru MANANI,
Ulimi uzuieni, kuwasengenya INSANI,
Ulimi ukalifuni, mema unene JAMANI,
NDIMI zetu TUCHUNGENI, WAFUNGAJI Ramadhani.
Ulimi nanezo beti, zimefika ukingoni,
Ulimi kwa KHAIRATI, nifanye MWENZO mwandani
Ulimi kwa SHURURATI, uwe ADUI mubini,
NDIMI zetu TUCHUNGENI, WAFUNGAJI Ramadhani
ABUU NYAMKOMOGI

MWANZA

HALALI NA HARAMU

1.Leo naja na shauri , tusikilize usia


Ni maneno ya Ghafuri, yasiyopatwa na doa
Tukajitia kiburi, mwisho wetu ni balaa
Halali halali yetu, haramu tuikimbie
2.Mola ametudhukuri, bure hakutuachia
Katufunza ya fakhari, vya halali kutumia
Haramu na vitu shari, laana vimetiliwa
Halali halali yetu, haramu tuichukie
3. Halali kitu kizuri, Allah ametuletea
Halali haina siri, kweupeni hutokea
Halali hua dhahiri, haijifichi na jua
Halali halali yetu, haramu ichukieni
4.Tuitafute halali, popote ilipokaa
Ikibidi kwenda mbali, pembe zote za dunia
Gharama tusizijali, muhimu ni manufaa
Halali halali yetu, haramu tuichukie
5. Haramu tusijadili, haifai kutumia
Haramu kwetu dajali, Mola hakuiridhia
Haramu japo ni mali, acha ndugu nakwambia
Halali halai yetu, haramu tuichukie
6. Halali iwe awali, tunapo pambaukiwa
Isijekuwa ya pili, kinyume tukachagua
Hayo nayo tuyajali, yafaa kuzingatiwa
Halali halali yetu, haramu tuichukie
7. Machumo tutafakari, kabla ya kuchukua
Tunakokwenda shubiri, na muda umewadia
Tukijifanya ayari, moto unatungojea
Halali halali yetu, haramu ichukieni
8. Yatosha nilohubiri, ndugu kuwafikishia
Yapo kwenye mstari, na hayaja expire
Si ya kale yalojiri, bado yanaendelea
Halali halali yetu, haramu tuichukie
Mtunzi ni:Zainab H. Mtima
Mbweni, Zanzibar
0717 165 602

AN-NUUR

RAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 26- Julai 2, 2015

Darasa la Miundombinu: Ni wapi ISIS


inapata bunduki zake?

Inatoka Uk. 10

mfano gazeti la New


York Times likitoa taarifa
mwaka 2013 katika makala
"Upelekaji wa silaha kwa
waasi wa Syria wapanuka,
kwa msaada wa CIA,"
kwamba:
Kutoka katika ofisi za
siri, maofisa wa kijasusi
wa Marekani wamesaidia
serikali za nchi za Kiarabu
kununua silaha, ikiwa
ni pamoja na manunuzi
makubwa kutoka Croatia,
n a wa m e wa p a k i b a l i
makamanda na vikundi
vya waasi kuamua nani
achukue silaha hizo
wakati zikiwasili, kwa
mujibu wa maofisa wa
Marekani wakizungumza
kwa sharti la kutokutajwa.
Na wakati mashirika
ya habari ya nchi za
Magharibi wakati wote
ya n a z u n g u m z i a I S I S
na makundi mengine
yanayoendesha shughuli
zao chini ya mwavuli wa
Al Qaeda kama 'waasi' au
'wenye siasa za wastani,'
ni wazi kama silaha zenye
thamani ya mabilioni
ya dola za Marekani
zinaelekezwa kwa 'wenye
siasa za wastani,'ni wao,
na siyo ISIS ambao
wangetamalaki katika
eneo hilo.
Ta a r i f a z i l i z o v u j a
siku za karibuni
zilisema kuwa kuanzia
mapema 2012 Wizara
ya Ulinzi ya Marekani
siyo tu ilianza kuweka
mkakati wa kuundwa
kwa 'eneo la kisultani
la Salafi' linaloenea nchi
za 'Syria na Irak, eneo
ambalo hasa ndiyo ISIS
iliko, ila ilikaribisha
ISIS kwa mikono miwili
na kuchangia kujenga
mazingira yaliyoiwezesha
kuzuka.
Njia za uwasilishaji vifaa
za ISIS ni pana kiasi gani?
Wakati wadadisi wengi
katika nchi za Magharibi
wanapendelea kusema
kuwa hawajui ISIS hasa
inapata mahitaji yake
kutoka wapi ili iweze
kuendeleza uwazo
wake wa kushangaza
wa kupigana, baadhi
ya waandishi wa habari
wametembelea eneo hilo
na kuchukua picha na
maelezo na kutoa taarifa

za milolongo ya magari ya
vifaa yanayofikishwa kwa
majeshi ya kigaidi. Magari
hayo yalikuwa yanatokea
katika viwanda katika
maeneo yanayoshikiliwa
na ISIS ndani kabisa ya
nchi za Syria na Irak?
Katu. Yalikuwa yanatokea
ndani kabisa ya Uturuki,
kuvuka mpaka wa Syria
bila kusumbuliwa na kitu
chochote, na kuendelea na
njia yake yakiwa na ulinzi
usio rasmi wa vikosi vya
majeshi ya Uturuki hapo
kando.
M a j a r i b i o ya S y r i a
kushambulia misafara
hii na magaidi
wanaomiminika pamoja
nayo, yamekabiliwa vikali
na ulinzi wa anga wa
Uturuki.
Shirika la Utangazaji
la Ujerumani, Deutsche
We l l e ( D W ) l i l i t o a
mkanda wa sauti wa
kwanza kutoka kianzio
muhimu cha habari nchi
za Magharibi kuonyesha
kuwa ISIS inapata vifaa
siyo kutoka 'ulanguzi
wa mafuta' au 'malipo
ya utekaji nyara', ila ni
vifaa vyenye thamani
ya mabilioni ya dola za
Marekani vinavyopelekwa
Syria kupitia mipaka ya
mwanachama wa NATO,
Uturuki, kwa njia ya
mamia ya malori kwa
siku.
Ripoti hiyo yenye
kichwa cha habari "Njia
za kupokea vifaa za
ISIS kupitia Uturuki,"
inayakinisha kile
ambacho kilishatajwa na
wachunguzi wa ramani
ya kisiasa kuanzia hata
2001 - kuwa ISIS inaishi
kwa ufadhili mkubwa wa
nchi kadhaa, ikiwemo bila
shaka, Uturuki yenyewe.
Ukiangalia ramani ya
maeneo yaliyoshikwa
na ISIS na kusoma
taarifa za mapito yake
na mashambulizi kote
katika ukanda huo na
hata mbali zaidi, mtu
anaweza kudhania
kuwa mamia ya malori
kwa siku yangehitajika
kuwezesha kiwango hiki
cha uwezo wa kupigana.
Mtu angeweza kufikiria
misafara kama hiyo
ikiingia Irak kutoka Jordan
na Saudia. Misafara kama
hiyo ingeweza kuingia
Syria kutoka Jordan.

Kwa jumla, ukizingatia


hali halisi ya miundombinu
na umuhimu wake
usioisha kwa kampeni
za kijeshi katika historia
yote ya binadamu,
hakuna maelezo mengine
ya n a y o k i d h i k u h u s u
uwezo wa ISIS kuendesha
vita ndani ya Syria na
Iraq, nje ya kiwango
kikubwa cha raslimali
kinachopelekwa kwake
kutoka ng'ambo.
Kama jeshi linatembea
k wa t u m b o l a k e , n a
tumbo la ISIS limejaa vifaa
kutoka NATO na nchi za
Ghuba, ISIS itaendelea
kutembea moto mdundo
kwa muda mrefu. Kiini
c h a k u we z a k u v u n j a
nguvu za ISIS ni kuvunja
uti wa mgongo wa njia
zake za kupokea vifaa.
Kufanya hivyo hata hivyo,
na ndiyo maana mgogoro
huu umeendelea kwa
muda mrefu, Syria, Irak,
Iran na wengine ingebidi
hatimaye wafunge mipaka
na kuwalazimisha ISIS
kupigana ndani ya mipaka
ya Uturuki, Jordan na
Saudia, mkakati mgumu
k u u f i k i a k wa n i n c h i
kama Uturuki zimeunda
maeneo ya kujihami ya
kudumu ndani ya Syria
ambayo yangehitaji
mkabiliano wa ana kwa
ana na Uturuki yenyewe
ili kuyaondoa.
Huku Iran ikiingia
katika mapambano hayo
kwa kuhamisha maelfu ya
askari kuinua operesheni
za kijeshi za Syria, kanuni
muhimu za tishio la
usalama zinaweza kuizuia
Uturuki kutumia kwa
dhamira halisi maeneo
hayo ya kujihami.
Tu l i c h o b a k i n a c h o
wakati huu, ni NATO
kimsingi ikiwa imeshikilia
eneo hilo nyara kwa
uwezekano wa vita
mbaya sana ya kikanda
katika juhudi za kulinda
na kuendeleza uharibifu
uliofanywa na ISIS
ndani ya Syria, ikiwa
imefadhiliwa kikamilifu
kwa mtandao mkubwa
wa miundombinu ikitoa
katika maeneo ya NATO.

(Tony Cartalucci,
anayeishi Bangkok, Thailand,
ni mtafiti wa ramani za
kisiasa na mwandishi, hasa
kwa jarida la mtandao, "New
Eastern Outlook.' Makala hii
imetafsiriwa Kiswahili na
Anil Kija.)

13
KUTOA ni jambo gumu
s a n a k wa m wa n a d a m u
hasa iwapo ni kitu
anachokipenda. Na vilevile
ni jambo linalopendwa sana
na Uislamu. Kwa ajili hii,
ndio tunaona kuwa Uislamu
umelitilia nguvu sana jambo
hili na kuliandalia malipo
makubwa.
Allah SW amelipangia
njia tofauti jambo hili kwa
kumfanya mtu wepesi wa
kumfanya na asiwe bakhili
na hili ni kwa kumuekea njia
ya wajibu na njia za suna.
Hakika kutoa kumeandaliwa
malipo makubwa ambayo ni
tofauti na ibada nyengine na
hili lipowazi.
Mfano wa wanao tumia
mali zao katika Njia ya
Mwenyezi Mungu, ni kama
mfano wa punje moja iliyo
chipuza mashuke saba.
Katika kila shuke zimo punje
mia. Na Mwenyezi Mungu
h u m z i d i s h i a a m t a k a ye ,
na Mwenyezi Mungu ni
Mwenye wasaa na Mwenye
kujua. (2:261.
Hili ni moja miongoni
mwa faida nyingi
zipatikanazo kwa kutoa
sadaka. Nyengine miongoni
mwa faida hizo, nikujenga
mahaba na mapenzi kati ya
wanaopeana. Ndio Mtume
SAW alivyozijenga imani za
Masahaba mpaka zikafikia
daraja ya kupendana na
kupeana bila kujali, huku
wakitarajia malipo makubwa
mbele ya Allah SW.
Jambo hili la kutoa kwa
hakika lina faida nyingi
kubwa zaidi katika hizo ni
kufunikwa na kivuli cha
Arshi ya Allah SW siku
ambayo hapatakuwa na
kivuli ila hicho. Nayo ni
siku ya Kiama ambapo
jua litawakaribia viumbe
kiasi ya shubiri moja juu ya
vichwa vyao. Kwenye hadithi
iliopokewa na Imam Bukhari
na Muslim wamelezewa watu
wa aiana 7 watakao funikwa
nna kivuli hicho, mmoja
wao ni mtu aliyetoa sadaka
akaificha mpaka ikafika
kutojua mkono wa kushoto
kilichotoa mkono wa kulia.
Jambo hili tukufu tunapata
fursa ya kujifunza katika
mwezi huu mtukufu wa
Ramadhani na inapomalizika
Ramadhani hugeuka hali
zetu tukawa wagumu wa
kutoa kama kwamba wale
waliokuwa wakitoa katika
mwezi wa Ramdhani sio
sisi bali ni watu wengine.
Inatakiwa kwa Muislamu
kuwa mwepesi wa kutoa
kwani kila unachokitoa
k wa a j i l i ya A l l a h S W
huwa hujapoteza bali
ni akiba kubwa ambayo
umejiwekea ya kukusaidia
siku ambayo hapana cha
kukusaidia isipokuwa kile
u l i c h o k i t a n g u l i z a k wa
mikono yako.
Kuwa na subira
M u i s l a m u a n a t a k i wa
kuwa mwenye kusubiri baala
zote zinazomkumba katika
maisha yake ya hapa duniani,
kwa kiasi kile ambacho
Muislamu anachokumbwa
na balaa na mitihani na
akasubiri, ndio huwa daraja
yake inapanda mbele ya
Allah SW. Ndio kwa maana
hii akasema Mtume SAW:
Allah anapowapenda
waja wake, huwajaribu kwa
kuwapatia mitihani ya kila

MAKALA/Matangazo

AN-NUUR

RAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 26- Julai 2, 2015

Ramadhani ni Darasa -Kutoa sadaka


aina.
Na hili ni moja miongoni
mwa faida nyingi zipatikazo
katika kusubiri kwa kuwa
karibu na Allah SW hii ni faida
nyengine inayopatikana kwa
kusubiri kwani Muislamu
kiasi ambacho atakuwa
ni mwenye kumkumbuka
Allah SW wakati wa raha
hailingani na kiasi atakavyo
mja kumkumbuka Allah
SW wakati atakapo kuwa
na matatizo kisha akawa
ni mwenye kusubiri huku
akifahanu wazi kuwa yote ni
yake yeye Allah SW, Hakika
Allah yuko pamoja na wale
wenye kusubiri.
Katika faida nyenginezo
miongoni mwa faida kubwa,
ni pale imani ya Muislamu
anapokumbwa na mitihani
akaweza kuvumilia na hili
lipo wazi katika jibu la
masahaba walipoulizwa na
Mtume SAW:
Je nyinyi ni waumini?
akajibu mmoja wao sisi ni
waumini wa hakika akauliza
Mtume SAW Ni upi uhakika
wa imani yenu? Akajibu,
tunashukuru wakati wa
raha na tunasubiri wakati wa
balaa na tunaridhia hukumu
ya Allah.
Katika mwezi huu wa
Ramadhani, wengi kati
yetu wanapata fursa ya
kujifunza kusubiri kwa njia
tofauti, kama vile kuvumilia
kushinnda na njaa pamoja
na kuwa nacho chakula,
kuwasamehe wanatukosea
bila kujali na kadhalika
hivyo basi litakuwa la maana
iwapo mafunzo na mazoezi
haya tunayoyapata katika
Ramadhani tutayatumia na
kuyafanyia kazi katika miezi
iliyosalia.
Kusoma Quran
Miongoni mwa ibada
zifanyazo na Muislamu
katika mwezi wa Ramadhani
ni kuyasoma maneno ya Allah
SW na ibada hii ina malipo
makubwa. Mtume SAW
kasema mwenye kusoma
herufi moja katika kitabu
cha Allah SW anaandikiwa
kafanya jema na jema moja
ni kumi mfano wake, sisemi
kuwa Alif Laam Miim kuwa
ni herufi moja bali Alif ni
herufi na Laam ni herufi na
Miim ni herufi.
Hivyo basi kulingana na
ufahamu wa tunaoupata
kutokana na hadithi hii
tukufu ni kwamba mwenye
kusoma quran analipwa
kwa kila herufi moja mema
(thawabu) kumi. Vilevile
kuna hadithi nyengine zinazo
tufahamisha tofauti za malipo
wanayolipwa wenye kusoma
Quran kwa sababu tofauti,
miongoni mwa sababu hizo ni
kama kuisoma Quran vizuri
kwani mwenye kusoma
vizuri ana malipo makubwa
zaidi kuliko yule asiyesoma
vizuri. Sababu nyengine ni
kufahamu kile anachosoma
kwani hayawezi kulingana
malipo ya anayefahamu
anachosoma na malipo ya
asiyefahamu anachokisoma.
Kadhalika kusoma pamoja
na kuzingatia maana
kunatofautisha malipo na
yule anayesoma bila ya
kuzingatia anachosoma.

Faida za kusoma Quran


ni nyingi sana yakiwemo
malipo makubwa yasiyo
kifani tuliyoyaeleza hapo juu
vilevile itakuja Quran siku
ya kiyama kuwaombea wale
waliokuwa wakiisoma katika
ulimwengu.
Katika mwezi huu wa
Ramadhani wengi wetu
hujikusanya pamoja
misikitini na majumbani
k wa a j i l i ya t e n d o h i l i
tukufu ambalo ubora wake
umeelezwa na Mtume SAW
katika hadithi maarufu
iliopokewa na Muslim:
Hawakusanyiki watu
katika nyumba miongoni
m wa n y u m b a z a A l l a h
wakawa wanakisoma kitabu
chake Allah na kukidurusi
kati yao, isipokuwa
huteremkiwa na utulivu na
wakafunikwa na rehma na
wakazungukwa na Malaika
na huwataja wao.
Isifahamike vibaya hadithi
hii kuwa Quran inafaa
kusomwa zaidi misikitini tu,
bali inafaa kusisitizwa kama
inavyosomwa misikitini
isomwe majumbani kwani
kama tunavoyajua majumba
yetu yamekosa nuru na
kutokana na kuangalia
runinga na kanda chafu
tunazo zinunua kwa gharama
kubwa, hivo basi itakua
jambo la busara iwapo badala
ya uchafu huo tukaweka
misahafu ambayo itasomwa
kwa makundi katika nyumba
zetu. Kwa kufanya hivyo,

huwenda nuru ya Uislamu


iliokosekana ikarudi kwa
barka ya maneeno hayo
matukufu Mola SW.
Inatakiwa kwa Muislamu
kila analotaka kulifanya
kabla ya kulifanya afikirie
natija ya jambo hilo iwapo
litakua na kheri alifanye
na iwapo litakuwa na shari
aliwache.
Ama faida za kuepuka
maasi kadhalika ni nyingi
sana miongoni mwa hizo ni
kuitakasa nafsi na machafu
na kuweza kuingia katika
aliowaita Allah SW walio
faulu katika neno lake tukufu
aliposema: Hakika amefaulu
yule alieitakasa nafsi yake.
Pepo
ya
Allah
wameandaliwa wale walio
safisha nafsi zao na maasi
ndipo katika itikaadi ya Ahli
suna tunaamini kuwa kila
aliyetamka shahada ataingia
peponi lakini baada ya
kuingia wenye maasi kwanza
ndani ya moto ili kusafishwa
na uchafu wa maasi walio
yachuma ulimwenguni.
Hakika katika mwezi huu
mtukufu tunapata fursa
kuuona Uislamu dhahir
shahiri katika toba kwani
wengi kati yetu ambapo tabia
hizi za kujiepusha na maasi
kama vile kusema uongo,
kusengenya, kudhulumu,
kutusi, kuzini, kuiba, kulewa
hujivisha katika mwezi wa
Ramadhani lakini mara tu
unapomalizika huyarudia
machafu. Ramadhani ni

Chuo na darasa analolipata


mja anatakiwa ashikamane
nalo katika miezi yote ya
mwaka.
M u i s l a m u a n a t a k i wa
kudumu katika kumtii Allah
SW na kufanya mazuri ya
kumridhisha kwa kiasi cha
uwezo alio ruzukiwa na
Aallah SW. Amesema Mtume
SAW Bora zaidi ya amali
(ibada), ni yenye kudumu
ijapokua itakuawa ndogo.
Mtume SAW alipopelekwa
Miraji alisikia sauti ya nyayo
za Syd Bilali katika Pepo ya
juu na aliporudi aridhini
akamuuliza Bilali kuWa ni
amali gani aliokua anadumu
nayo akasema haikua ibada
kubwa ispokua zilikua ni
rakaa mbili za udhu, kwani
hakuacha kuzisali kila
alipomaliza kutawadha.
Ama mema yanatakiwa
kufanywa kwa wingi na
vilevile Muislamu ajue kuwa
kila dakika inayo mpitia
katika uhai wake wa duniani,
ataijutia sana siku ambayo
ataijutia iwapo dakika hio
hakuitumia katika ibada.
M u i s l a m u a n a t a k i wa
mpaka wakati wa kulala
kwake, atie nia nzuri ili
usingizi wake uhesabiwe
kua ni ibada. Kwa kufanya
hivi, kutamfanya kila mmoja
wetu kupata daraja kubwa
mbele yaa Allah SW.
Haya ni baadhi tu ya
mafunzo tuyapatayo katika
mwezi huu Mtukufu wa
Ramadhani hivyo hatuna
budi kuyazingatia na
kujitahidi kuyafuata
kadri tutakavyojaaliwa na
tumuombe Allah atusaidie
kuyatekeleza kwa kadiri ya
nia zetu.

Dua Maalum Masjidi Mtambani (Leo)


Jumuiya na Taasisi za Kiislamu (T), imeandaa Dua maalumu,
itakayowashirikisha Waislamu wote leo siku ya IJUMAA, katika Msikiti
wa Mtambani, Kinondoni.
Waislamu wametakiwa kushiriki kwa wingi ili kumlilia Allah (s.w)
ndani ya Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani kwa kuzingatia uzito na
utufukufu wake, hii ni kufuatia kadhia mbalimbali walizokutana nazo
kabla ya Mwezi huu.
Pia Viongozi wa Jumuiya (Masheikh) watazungumzia: Waislamu na
uchaguzi Mkuu wa Urais na Madiwani.
Dua itaanza mara baada ya mshuko wa Ibada ya Swala ya Ijumaa,
Msikitini hapo.
Sheikh Rajab Katimba.

CHANGIA MASHINDANO YA QURAN


AL MADRASATIL FADHAKIR HONDOGO DAR
Hakuna jengo la Msikiti wala Madrasa, kuna kiwanja kilichotolewa (WAQFU)
miaka mitatu iliyopita. wanafunzi wanasomea Quran katika majani kama
wanavyoonekana katika picha.
Pamoja na kuisoma Quran katika mazingira magumu, lakini kwa kuwa huu
ni mwezi wa Quran, tumeandaa mashindano ya kuhifadhi Quran kwa vijana
wote wa eneo la Hondogo na maeneo ya jirani kuanzia Ramadhan 10-17.
Lakini hatuna mdhamini wa kutuwezesha zawadi kwa washindi
watakaopatikana katika shindano hilo.
Hivyo basi tunaomba mchango wako wa chochote ulicho nacho ili tununue
zawadi kwa ajili ya watoto hao na kuzidi kuwatia moyo na kuwa na mapenzi
na Quran yao.
kwa mawasiliano zaidi tupigie simu No. 0715 259635 au 0757 375993

14

Makala

AN-NUUR

RAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 26- Julai 2, 2015

Dunia tunayoishi ndani ya Quran-2

Na Ben Rijal
Na Ben Rijal
MOLA anatuelezea
kwa upana na kuapa
juu ya mbingu haya ni
mazingatio kwetu.
Naapa kwa mbingu
zenye njia. (51:7.)
Nani mwenye uwezo
wa k u s h i n d a n a n a
Muumba?
Na Ufalme wa
mbingu na ardhi ni wa
Mwenyezi Mungu; na
Mwenyezi Mungu ni
Mwenye uweza juu ya
kila kitu. (3: 189.)
Sifa njema zote ni
za Mwenyezi Mungu
aliye umba mbingu na
ardhi, na akafanya giza
na mwangaza. Tena
baada ya haya walio
kufuru wanawafanya
wengine sawa na Mola
wao Mlezi. (6:1.)
Nani anayeyapa
maisha kuwepo na nani
anayeyaondoa maisha
hata mwanadamu
akitumia juhudi zote
kuzuia kifo?
Yeye ndiye Mwenye
ufalme wa mbingu na
ardhi. Anahuisha na
anafisha. Na Yeye ni
Mwenye uweza wa kila
kitu. (57:2.)
Maisha yanaelezwa
k wa u p a n a k a t i k a
Quran kwa mifano
mbalimbali.
A U
N A N I
yule aliyeziumba
mbingu na ardhi, na
akakuteremshieni maji
kutoka mbinguni, na
kwa hayo tukaziotesha
bustani zenye
kupendeza? Nyinyi
hamna uwezo wa
kuiotesha miti yake. Je!
Yupo mungu pamoja
na Mwenyezi Mungu?
Bali hao ni watu walio
potoka. (27:60.)
A u n a n i y u l e
aliyeifanya ardhi mahali
pa kutua, na akajaalia
ndani yake mito, na
akaweka milima? Na
a k a w e k a b a i n a ya
bahari mbili kizuwizi?

Sayari kutoka picha ya satilaiti.

Picha iliopigwa kutoka anga za juu


Je! Yupo mungu
pamoja na Mwenyezi
Mungu? Bali wengi wao
hawajui. (27:61.)
Hapa
ndipo
panapoonekana maisha
endelevu kutokana na
maji, miti na wanyama.
J e ! H a wa o n i ya
kwamba tunayapeleka
m a j i k we n ye a r d h i
kavu, kisha kwayo
tunaitoa mimea wanayo
kula wanyama wao
na wao wenyewe? Je!
Hawaoni? (32:27.)
Wakati
ndio
unaongoza maisha na
Allah anaeleza kuwa
kuna siku ya uamuzi
kwa watu wote na kwa
wakati mmoja.
H a k i k a s i k u ya
Uamuzi ni wakati ulio
wekwa kwa wao wote.
(44:40.)
Mwenyezi Mungu
aliyeziinua mbingu
bila ya nguzo mnazo
ziona, ametawala

Fatilia kuandama kwa Mwezi

Leo Ijumaa ni tarehe 9 Ramadhani 1436


AH sawa na tarehe 26 Juni 2015.
Julai 17 mwezi wa Mfungo Mosi
utaandama. Kutokea leo hadi Mfungo
Mosi tumebakisha siku 21

kwenye Ufalme wake,


na amefanya jua na
mwezi yamt'ii, kila
kimoja kinakwenda
kwa kiwango maalumu.
Anayapanga mambo,
na anazipambanua
Ishara ili mpate kuwa
na yakini kukutana
na Mola wenu Mlezi.
(13:2.)
N a
n d i y e
aliyeitandaza ardhi
na akaweka humo
milima na mito. Na
katika kila matunda
akafanya dume na jike.
Huufunika usiku juu
ya mchana. Hakika
katika haya zimo Ishara
kwa watu wanao fikiri.
(13:3.)
Na katika ardhi
vimo vipande vilivyo
karibiana, na zipo
bustani za mizabibu,
na mimea mingine,
na mitende yenye
kuchipua kwenye shina
moja na isio chipua
kwenye shina moja,
nayo inatiliwa maji
yale yale. Na tunaifanya
baadhi yao bora kuliko
mengine katika kula.
Hakika katika hayo
zimo ishara kwa watu
wanao tia mambo
akilini. (13:4.)
Anga iliokamilika
pasi kuwa na uchafu

huonekana ndege
na wana mazingira
wanaelezea kuwa
u t a p o w a o n a
n d e g e wa m e j a z a n a
sehemu mmoja ujue
kuna mazingira
yaliokamilika.
Je! Hawawaoni
ndege walivyo wat'iifu
katika anga la mbingu?
Hapana mwenye
kuwashika isipo kuwa
M we n ye z i M u n g u .
Hakika katika haya zipo
ishara kwa watu wanao
amini. (16:79.)
Mchana na usiku
ni maana yake? Mola
anatuelezea kama
ifwatavyo:
Yeye ndiye aliye
kujaalieni usiku mpate
kutulia humo, na
mchana wa kuonea.
Hakika katika haya zipo
Ishara kwa watu wanao
sikia. (10:67.)
Ishara
zipi
tunazozipata kukuwepo
kwetu duniani?
Hakika katika
mbingu na ardhi ziko
Ishara kwa Waumini.
(45:3.)
Jee hii miezi
tulivyoipanga ipo
tangu lini? Ipo tangu
Mola alipoiumba dunia
kwa kuweza kutambua
mambo yetu mbalimbali
na kuyapanga na kujua
lipi liwe wakati upi
Hakika idadi ya
miezi kwa Mwenyezi
Mungu ni miezi kumi
na mbili katika hukumu
ya Mwenyezi Mungu
tangu alipoumba
mbingu na ardhi.
Katika hiyo iko mine
mitakatifu. Hiyo ndiyo
Dini iliyo sawa. Basi
msidhulumu nafsi zenu
humo. Na piganeni
na washirikina wote
k a m a wa o w n a v y o
pigana nanyi nyote. Na
jueni kuwa Mwenyezi
Mungu yu pamoja na
wachamngu. (9:36.)
Suala zima la duru
ya maji (Water cycle)
limechambuliwa katika
Quran.
Je! Huoni ya
k wa m b a M we n ye z i
Mungu huyasukuma
mawingu, kisha
huyaambatisha, kisha
huyafanya mirundi?
Basi utaona mvua
ikitoka kati yake. Na
huteremsha kutoka
juu kwenye milima
ya m a w i n g u m v u a
ya mawe, akamsibu
nayo amtakaye na
akamuepusha nayo
amtakaye. Hukurubia
mmetuko wa umeme
wake kupofua macho.
(24:44.)
Ya l i o m o
na
yaliofratibiwa katika
ardhi ni yepi?
Na tukazipasua
ardhi kwa chemchem,
yakakutana maji kwa
jambo lilio kadiriwa.
(54:12.)
Katika mkusanyiko
wa aya hizi juu ya dunia

Allah anasema:
N a
w a l a
hawakumhishimu
Mwenyezi Mungu
kama anavyo stahiki
kadiri yake. Na Siku
ya Kiyama ardhi yote
itakuwa mkononi
mwake, na mbingu
zitakunjwa katika
mkono wake wa
kuume. Subhanahu wa
Taa'la Ametakasika na
Ametukuka na hayo
wanayo mshirikisha
nayo. (39:67.)

Nimezikusanya
a ya k a t i k a Q u r a n
kuonyesha juu ya
mbingu, ardhi ikiwa
ndio dunia yenyewe
alioiumba Allah.
Maisha yanategemea
uhai na ndio sayari yetu
pekee yenye uhai.
Makala ijayo
nitaueleza uhai,
kisha kuyatizama
mazingira kwa upana
na majukumu ya
wanadamu.

Jee
Unajua?
1. Unazijua nchi 15 zinazoongoza kuwa

na mfumo mzuri wa elimu? Ni nchi ya Japan


ikifwatiwa na Korea ya Kusini, Singapore, Urusi,
Finland, Canada, Uholanzi, Ireland, Israel, China,
New Zealand, Norway, Belgium, Ujerumani na
Denmark.
2. Nchi zenye kuwandikisha watoto kuanza
masomo katika umri unaotakiwa Ufaransa
ikiongoza kwa kufikia asilimia 100%, Belgium 99%,
Denmark 97%, Spain 96%, Norway 96%.
3.
Wenye kufuzu na kumaliza kidato cha sita
nchi zinaongoza ni Ureno ni asilimia 99%, Slovenia
96, Ujerumani 95%, Iceland 95%, Uholanzi 94%
4. Nchi ambazo kuishi kunakuweka katika
utulivu na kujisikia inayoongoza ni Denmark
ikifwatiwa na Norway, Switzerland, Uholanzi,
Sweden, Finland, Canada, Austria, Australia,
Iceland.
5. Nchi zinazoongoza kuwa na pato kubwa
kwa watu na utajiri duniani, nchi ya kwanza ni
Qatar ikifwatiwa na Luxembourg, Singapore,
Norway, Marekani, UAE, Switzerland, Uholanzi,
Australia na Austria.
6.
Nchi zinazoongoza kwa umasikini duniani
ya kwanza ni Zambia ikifwatiwa na Ukanda wa
Ghaza, Zimbabwe, Chad, Moldova, Haiti, Liberia,
Guatamela, Suriname na Angola.
7. N c h i k u b wa k wa m a s a f a d u n i a n i
inayoongoza ni Urusi ikiwa na kilomita za mraba
17,098, 242 ikifwatiwa na Canada 9,984,670,
Marekani 9,826,675, China 9,596,961, Brazil
8,514,877, Australia 7,741,220, India 3,287,263,
Argentina 2,780,400, Kazakhsatan 2,724,900,
Algeria 2,381,741.
8. Nchi 10 duniani zenye huduma za afya
duni inayoongoza ni Siera Leone ikifwatiwa na
Mynmar, Afrika ya Kati, Congo DRC, Nigeria,
Liberia, Malawi, Msumbiji, Lesotho na Zambia.
9. Jengo lilokuwa refu zaidi duniani lipo
Taipei nchini Taiwan likiwa na ghorofa 101.
CHEMSHA BONGO NAMBA: 12
Weka duara kwenye jawabulio sawa. Jawabu kamili
wiki ijayo.
C
I
L
E
B
P
A
A
B
U

H
N
C
N
R
A
N
N
E
S

I
D
H
N
A
C
D
T
R
A

N
O
I
E
Z
I
E
I
M
S

A
N
L
T
I
F
S
G
U
S

A
E
E
L
I
T
U
D
S

S
S
J
H
Z
C
P
A
A
G

G
I
Y
P
O
I
U
Y
G
N

J
A
T
T
T
T
U
O
O
I

K
G
U
N
I
O
P
S
S
L

L
J
N
B
F
C
G
Y
U
E

1.
Mto ulio mrefu kuliko yote duniani?
2.
Nchi inayoongoza kusafirisha Sukari.
3.
Bahari iliokubwa na kina kikubwa.
4.
Mlima ulio mrefu kuliko yote duniani.
5.
Kisiwa au nchi ilio na watu wachache duniani.
6.
Nchi inayoongoza usafirishaji wa gesi asilia.
7.
Tanzania ni nchi ya ngapi katika usafirishaji
wa Tanzanite?
8.
Nchi inayoongoza usafirishaji na uzalishaji
wa Karafuu duniani ni..
9.
Nchi inayoongoza usafirishaji wa Shaba.
10. Nchi inayoongoza utengenezaji wa saa na
kuziuza duniani.

15

Makala

AN-NUUR

RAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 26- Julai 2, 2015

Matukio ya mwezi wa Ramadhani-vita vya Badr


Na Ben Rijal

V I TA v ya B a d r n i
vita vya mwanzo
vikuu katika tarehe
ya Uislamu, vikiwa
vita baina Waislamu
na Makafiri. Vita hivi
ni kielelezo kikubwa
k wa Wa i s l a m u
kuelewa kuwa hakuna
kinachoshindikana
k a m a
i m a n i
zao
zitakuwa
zimefungamana
kikweli ushindi
utapatikana tu.
Katika Suratul Anfal
Mtume SAW aliahidiwa
ushindi kama aya
zinavyofafanua.
Na Mwenyezi
Mungu alipo kuahidini
kuwa moja katika
makundi mawili ni
lenu. Nanyi mkapenda
lisilo na nguvu ndio
liwe lenu; na Mwenyezi
Mungu anapenda
ahakikishe Haki kwa
maneno yake, na aikate
mizizi ya makafiri. (8:7)
Ili ahakikishe Haki
na auvunje upotovu na
wangechukia wakosefu.
(8:8.)
Katika vita hivi kuna
matokeo mengi sana
yanayohitaji mazingatio
tokea kuanza kwake
hadi kupatikanakwa
ushindi na kadri
tutakavyoyas imulia
matokeo hayo,
hatutoyafikia ukomo.
Lakini na itoshe yale
yaliyo wazi na maarufu
tuweze kuyafahamu na
kuyazingatia.
Tarehe ya Vita
Vita vikuu vya Badr

vilitokea mwaka wa
pili tokea Mtume SAW
kuhamia Madina.
Ilikuwa katika mwezi
wa Ramadhani tarehe
17 siku ya Ijumaa na
ilikuwa ndio mwaka
wa m wa n z o t o k e a
kufaradhishwaa funga
ya Ramadhani.
Vita vya mwanzo
baina ya Waislamu
na Makafiri vilikuwa
ni vita hivi vya Badr.
Ushindi kwa Waislamu
ndio somo kubwa
la kujifunza kwani
ilikuwa ni idadi
ndogo ya Waislamu
ukilinganisha na ya
M a k a f i r i . U w i ya n o
ulikuwa 1:3. Kila
Muislamu mmoja, kuna
Makafiri watatu (1:3).
Lakini juu ya kuzidiwa
kwa idadi, Waislamu
waliweza kupambana
na maadui ikiwa ni
wachache na wenye
silaha duni.
Sababu ya Vita
Chaanzo cha vita
hivi ni kutaka kwa
Waislamu kulipiza kwa
Waislamu kwa Makafiri
wa Makka ambao
walizihodhi mali zao
walizoziwacha Makka
na ndio walizokuwa
wakizifanyia biashara.
Waislamu walipanga
k u u va m i a m s a f a r a
wa kibiashara wa
Makureshi utokao
Shamu na kuelekea
Makka. Mtume SAW
aliwataka Masahaba
zake watoke kuuvamia
msaafara huo uliokuwa
na ngamia wafikao
elu moja wakiwa

UWANJA WA VIJANA - JIONGEZEE MAARIFA

Majibu CHEMSHA BONGO namba 11


M
Z
82
90
M
M
A
A
2.5
%
B

E
C
A
M
A
I
R
S
S

S
B
S
A
F
L
I
D
P

O
N
D
D
A
I
S
F
U

P
M
C
I
N
O
T
G
I

O
L
H
N
I
N
O
H
O

T
H
I
A
K
I
T
M
J

A
M
N
A
I
1
L
N
F

M
Z
A
G
O
A
E
O
N

I
A
G
H
S
V
J
K
L

A
K
1939
2AH
1945
6AH
354
360
5%

M U

MASUALA
1.
Vita vya Badr vilipiganwa mwaka gani wa
Kiislamu? Jawabu: 2AH
2.
Khalifa wa 3 Syd Uthman bin Affan aliuwawa
akiwa na umri wa miaka mingapi? 82, 79, 90. Jawabu:
82
3.
Baada ya Msikiti wa Makka na Madinah Msikiti
gani mwengine mtukufu? Jawabu: Bayt Muqadas.
4.
Mali iliopitia mwaka Muislamu anatakiwa atoe
kima kipi kama ni Zakka? 1%, 2.5%, 5%. Jawabu: 2.5%.
5.
Katika Kalenda ya Hijra, kuna siku ngapi?
Jawabu: 354.
6.
Kilomita moja ina Milimita ngapi? Milioni 1,
Milioni 10, Milioni 25 Jawabu: Milioni 1
7.
Mto Euphrates na Tigris umehusishwa na
ustaarabu upi? Jawabu: Mesopotamia.
8.
Vita vikuu vya pili vilianza mwaka gani?
Jawabu 1939.
9.
Mtu gani aliotamka kuwa Mwanadamu ni
Mnyama wa Siasa (Political animal), Plato, Hagel,
Aristotle. Jawabu: Aristotle
10. Gazeti la mwanzo duniani lilianzishwa nchi
gani? China, USA, England. Jawabu: China.

wamebebeshwa bidhaa
za kila aina. Msafara wa
Makureshi Abu Sufyan.
Hapa itabidi tuelewe
kuwa hakukua kuvamia
msafara huu ilikuwa ni
dhulma, bali ilikuwa
ni kurejesha kati ya
mali zao zilizoporwa
na Makureshi.
Waislamu walihama
kuhamia Madina
wakiwa wapo mikono
mitupu, kuhama kwao
walihama kwa ajili ya
Allah.
Maandalizi ya Kikosi
Mtume SAW baada
ya kuwaamrisha
masahaba zake
kuuvamia msafara wa
Makureshi, hakuwa
na maana kuwa kila
Muislamu kutoka kwa
ajili ya kulitekeleza
jambo hilo, bali
aliwakhiyarisha
ndipo wakajitokeza
Waislamu wapatao 313
wakiwemo Muhajirina
82 na waliobaki ni
Waislamu wa Madina.
Aidha, walikuwa na
ngamia 70 na farasi 3
tu. Waislamu walianza
safari yao wakiongozwa
na Mtume SAW ikiwa ni
siku ya Jumatatu tarehe
8 Ramadhani. Kutokana
na uhaba wa vipando
walivyokuwa navyo
Waislamu, iliwabidi
wafanye zamu za
kupanda ngamia ikawa
kila watu watatu au
wanne wanapokezana
katika kupanda ngamia
mmoja, ikiwa mmoja
hupanda na wengine
hutembea kwa miguu.
M t u m e S AW k w a
upande wake, akawa
anapokezana na Sahaba
Ali bin Abi Talib na
Sahaba Marthad
Alghanaawy. Ikawa
kabla ya Mtume SAW
hakuwahi kushuka na
kutembea kwa miguu,
Syd Ali na mwenzake
wakamuambia
aendelee kumpanda
ngamia huyo na wao
watakwenda kwa
miguu, yote hayo ni kwa
kumfanyia heshima na
kufanya adabu kwa
kiongozi wa Umma
huu. Hebu tujiulize
nini lilikuwa jawabu la
Mtume SAW? Jibu lake
kama atalisikia yeyote
mwenye nafasi katika
jamii na kulizingatia
aliyoyazungumza
atachomwa na kuingiwa
na imani kwa walio
chini yake na kutaka
kufwata nyayo zake
Mtume SAW. Alinena
yafwatayo, Nyinyi
hamjawa na nguvu
kuliko mimi (hata
mkatembea kwa miguu
nami nishindwe), wala
mimi siwezi kuziwacha
fadhila mzitakazo
nyinyi (za kutembea
k wa m i g u u k a t i k a
mambo ya kheri.)
Waliendelea
kupokezana kumpada
ngamia huyo hadi

kufika sehemu
waliyoikusudia. Mtume
SAW alikusudia kufika
sehemu iitwayo Badri
kwani sehemu hiyo ni
nzuri na ndiyo njia kuu
ya misafara inayotokea
Shamu kuelekea Makka.
Walipokaribia sehemu
hiyo, walipiga kambi
nje kidogo na Mtume
SAW akatuma wajumbe
kuchunguza kama
msafara wa Mukureshi
kama ushawasili au
bado.
Kwa bahati huku
Abu Sufyani alikwisha
pata habari ya kuwa
Waislamu wanataka
kuuteka msafara wake,
kuweza kulifahamu hilo
Abu Sufyan akafanya
haraka kumtuma
mjumbe kwenda Makka
kuwajulisha Makureshi
wafike haraka wende
kuwapa ulinzi zisije
zikatekwa mali zao.
M j u m b e wa A b u
Sufyani alipowaeleza
Makureshi juu ya
a z m a z a Wa i s l a m u
kutaka kuwateka na
kuwanyanganya mali
zao, wakapatwa na
furaha na kuona fursa
waliokuwa wakitafuta
kuweza kupambana na
Waislamu na kuwafyeka
mara mmoja imewadia,
kwani ilikuwa tokea
Wa i s l a m u k u h a m i a
Madina imepita miaka
miwili hawajawaudhi
wala kuwatesa na
husda zao zilikuwa
zikichemka kila kukicha
kuona kuwa Waislamu
wamewakosa na sasa
wamekuwa na jeuri.
Kutokana na hali hio,
wakatiana mori kutoka
kwenye makazi yao na
kwenda kuunusuru
msafara wao.
Baadhi ya Makureshi
waliona sio busara
kupigana na Waislamu,
kwa hio baadhi yao
waliamua kurudi
Makka kutokanaa na
kukhofia mangamizo
watakayoyapata, kati ya
waliorudi alikuwemo
Abu Lahab na badala
yake akamtomeza
mwandani wake AlAas bin Hisham bin
Mughira pamoja na Ami
yake Mtume Bwana
Abass alitoka nao
lakini alifanya hivyo
kwa kuwaonea haya
M a k u r e s h i . Vi g o g o
vyote vya Makureshi
walitoka kwenda
kuulinda msafara
wao ikiwa idadi yao
ilikuwa zaidi ya watu
Elfu wakiwa na silaha
kamili za kivita na
walikuwa na vipando
v ya o v ya k u t o s h a .
Aidha, walikuwa
na vyakula vya kila
aina vya kifakhari ili
kujiburudisha wakiwa
wa n a e l e k e a B a d r i .
Wa l i wa c h u k u a p i a
wapiga ngoma kuweza
kuwastarehesha. Hayo
yote waliyafanya

kwa kutaka kuwapa


somo Waislamu na
kujifakharisha na
kuweza kuwatia woga
makabila mengine ya
Kiarabu kufahamu
kuwa Makureshi sio
watu wa mchezo.
Katika Suratul Anfal
inaelezwa:
Na mt'iini Mwenyezi
Mungu na Mtume
wake, wala msizozane
mkaingiwa woga, na
zikapotea nguvu zenu.
Na subirini. Hakika
Mwenyezi Mungu
yu pamoja na wanao
subiri. (8:46)
Wa l a m s i we
kama wale walio toka
majumbani mwao kwa
fakhari na kujionyesha
kwa watu, na
wakawazuilia watu Njia
ya Mwenyezi Mungu.
Na Mwenyezi Mungu
ameyazunguka yote
wanayo yafanya. (8:47)
Kutokana na Abu
Sufyan kufahamu kuwa
Waislamu wameshatoka
kapa kwa kuwa msafara
kishaugeuza njia na
a z m a ya Wa i s l a m u
haikufanikiwa,
akaamua kuwa hakuna
haja ya kukabiliana
n a Wa i s l a m u b o r a
warudi Makka.
Lakini Makureshi
wakamwambia hapo
itakuwa hawajafanya
la maana lililo muhimu
lazima wawaonyeshe
Wa i s l a m u w a o n i
nani na sio watu
wakuchezewa.
Kwa upande wake
Mtume SAW aliondoka
na Syd Abubakar
b i n S i d i k k u f a n ya
ujasusi kujua nguvu
ya Makureshi ikoje,
waliweza kukutana na
mzee mmoja Muarabu
akiwa sio kati ya watu
wa Makka wakamuuliza
kama ana habari gani
kuhusu Makureshi na
kuhusu Muhammad
na watu wake, Mzee
huyo akakataa katu
kusema na kuwambia
kuwa hatowambia kitu
ikiwa watashindwa
kumueleza wapi
walipotoka?
Mtume akamwambia
mzee wa Kiarabu
u k i t u a m b i a
tuliyokuuliza
tutakueleza tutokako.
Mzee akanena
hamtonielezaa kitu
hadi nikupeni mimi
habari? Mtume SAW
akamjibu ndio hivyo.
Hapo akawambia
yafwatayo:
Hakika nimesikia
kuwa Muhammad
na watu wake
wa m e t o k a M a d i n a
siku kadhaa kama
ikiwa aliyeniaambia
ni mkweli, basi leo
Muhammad atakuwepo
sehemu kadhaa, pia
kwa upande wao
Makureshi wametoka
siku kadha, kama huyo
aliyeniambia ni mkweli,

b a s i l e o wa t a k u wa
wapo sehemu kadha.
Huyu mzee alikuwa
ni mtaalamu wa safari
z a J a n g wa n i h i v y o
a l i we z a k u k i s i a n a
makisio yake yakawa
ni ya kweli. Baada ya
hapo huyo mzee Mzee
akaona naye achukue
fursa ya kuwauliza
Mtume SAW na Syd
Abubakar akaanza
masuala yake kama
ifwatavyo:
Jee nyinyi mnatokea
wapi? Mtume
akamjibu tunatokana
na maji. Mara tu
alipomaliza kutoa
kauli hio, akaondoka
na Syd Abubakar na
kumuachia kitendawili
mzee wa Kiarabu
kujiuliza ni sehemu
gani hiyo inayoitwa
maji alioambiwa.
Mtume
SAW
a l i t u m i a u j a n j a wa
mbinu za kivita kuwa
mnapofanya ujasusi
kwenye vita na
kukutana na wana vijiji
wanapowauliza, sio
kuwamwagia ukweli,
mbinu hii hadi sasa
ingali inatumika.
Mtume
SAW
aliporudi kwa
Masahaba akaona
bora aongeze kupata
taarifa za ziada kuweza
kujua nguvu za maadui
wa l i p o . H a p o t e n a
akawatoa Sahaba Ali bin
Abi Talib na wenzake
wawili wakatoka hadi
wakawakuta vijana
wawili kwenye maji
ya Badri, wakaona ni
busara kuwachukuwa
hadi kwa Mtume SAW.
Walipoulizwa kuwa
wao ni nani wakajibu
sisi ni wachotaji
maji wa Makureshi
tumetumwa tuje
kuchota maji. Mtume
akawauliza, wapo
wapi hao Makureshi?
Wa k a j i b u s e h e m u
kadha, sehemu yenye
muinuko wa ardhi
Mtume akataka kujua
idadi yao wakakiri
kuwa hawajui lakini
walikuwa ni wengi.
Wakaulizwa kwa kiasi
kila siku wanachinga
ngamia wangapi
jawabu yao ikawa ni
ngamia 9 na baadhi ya
siku hufikia hata 10.
Mtume
SAW
akafanya makisio yake
akasema kutokana
n a k u l a k wa o k wa
siku, basi idadi yao
itakuwa ni baina ya
Makureshi 900 au
1,000. Aliupotaka kujua
viongozi walikuwepo
kwenye msafara huo
wakawataja kwa majina
idadi yao ikiwa inafikia
14 ikiwa mingengwe
ya Kikuraishi. Hapo
Mtume SAW akaelewa
kuwa hakuna msafara
wa kuuvamia tena ila
lilobaki itakuwa ni
mapambano tu.
Itaendelea toleo

16
Na Mwandishi wetu

RAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 26- Julai 2, 2015

Ramadhani ni Darasa Lisilo na Kifani


ya mwezi wa Ramadhani
ikiwezekana siku kwa siku
yaani kufunga siku mmoja
na kuacha siku mmoja
funga ya Mtume Daudi AS
itakuwa bora. Isipowezekana
basi, muumini afunge siku
ya Ijumatatu na Alhamisi
pamoja na Ayamul-biidh
funga ya sitatu-shawaal,
funga ya Ashura, Arafa,
Rajab na Shaaban.

mpaka mwisho hufikia daraja


ya wale aliowasifu Allah SW
katika Quran:
Na waja wa Arrahman
Mwingi wa Rehema ni wale
wanao tembea ulimwenguni
k wa s t a h a , n a wa j i n g a
wa k i wa s e m e z a h u j i b u :
Salama! (25:63)
M i o n g o n i m wa f a i d a
kubwa zaidi ni kufaulu
kwa kuingia peponi, kama
alivyosema Mtume SAW
katika hadithi iliopokewa
na Turmidhy Enyi watu,
enezeni salamu, na mlishe
chakula na musali usiku
hali kuwa watu wamelala,
mtaingia peponi kwa amani.
Kwa hakika mna hasara
nyingi zinazopatikana kwa
mtu ambaye anayatumia
masiku yake kwa mambo ya
kipuzi, michezo, mapumbazi
ya kilimwengu au hata
kulala tu, kwani ni wakati
muhimu sana kwa Muislamu
kuupatiliza kwa kumuomba

KALENDA YA RAMADHANI
Mwaka 2015

Mola wake haja zake tofauti


kwa kuwa ni wakati wa
kukubaliwa maombi yote.
Katika kipindi hiki kama
alivyosema Mtume SAW
katika hadithi iliopokewa na
Muslim Hakika katika usiku
mna saa, haombi Muislamu
kheri yeyote iwe ya kidunia
au ya kiakhera isipokuwa
anapewa na hilo ni kila
usiku. Hasara ilioje kwa
wanaopoteza fursa hii bora?
Katika mwezi huu mtukufu
wengi wetu hupata fursa ya
kujizowezesha kujifunga
masombo na kukesha kwa
ajili ya ibada tofauti kama
vile itikaaf, kusoma Quran,
kusali, kuomba, na kadhalika,
lakini masikitiko makubwa ni
kuwa baada ya mwezi huu
kututupa mkono wa buriani
wengi wetu husahau. Tasbihi
zikatundikwa, misahafu
ikafungiwa makabatini, hadi
ikafikia kuota mavumbi juu
yake, kama kwamba yule
Mola tunayemuabudu ndani
ya mwezi wa Ramadhani siye
yule tunayemuabudu katika
miezi iliyosalia. Tumuombe
Allah atuhifadhi na hilo.
KALENDA YA RAMADHANI
Mwaka 1436H

1.

Enyi Mlioamini! Mmelazimishwa kufunga (Saumu) kama walivyolazimishwa waliokuwa kabla


yenu ili mpate kumcha Mungu. Kuran 2:183

2.
3.

Na (huku) kufunga ni bora kwenu. Ikiwa mnajua. Kuran 2:184


Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi (atimize) hisabu (ya siku alizowacha kufunga)
katika siku nyengine Mwenyezi Mungu anakutakieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo
mazito. Kuran 2:185.
Vile vile Bwana Mtume (S.A.W) kasema:Kila kitu kina Zakka, na Zakka ya mwili ni saumu.
Anaefunga Ramadhani kwa Imani na kuzingatia (basi) hufutiwa madhabi yake yote
yaliotangulia. Na kama mngelijua faida iliomo katika Ramadhani, basi mngetamani Ramadhani
iwe mwaka mzima.

4.
5.

JJ
SIKU

JUNE
JUNE
JUNE
JUNE
JUNE
JUNE
JUNE
JUNE
JUNE
JUNE
JUNE
JUNE
JUNE
JULAI
JULAI
JULAI
JULAI
JULAI
JULAI
JULAI
JULAI
JULAI
JULAI
JULAI
JULAI
JULAI
JULAI
JULAI
JULAI
JULAI

18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17

ALKHAMIS
IJUMAA
JUMAMOSI
JUMAPILI
JUMATATU
JUMANNE
JUMATANO
ALKHAMIS
IJUMAA
JUMAMOSI
JUMAPILI
JUMATATU
JUMANNE
JUMATANO
ALKHAMIS
IJUMAA
JUMAMOSI
JUMAPILI
JUMATATU
JUMANNE
JUMATANO
ALKHAMIS
IJUMAA
JUMAMOSI
JUMAPILI
JUMATATU
JUMANNE
JUMATANO
ALKHAMIS
IJUMAA

DUA YA KUSOMA UNAPOANDAMA MWEZI

MUDA
WA
MWISHO
KULA
DAKU
(IMSAK)
11:02
11:02
11:02
11:02
11:02
11:03
11:03
11:03
11:03
11:04
11:04
11:04
11:04
11:04
11:04
11:05
11:05
11:05
11:05
11:06
11:06
11:06
11:06
11:06
11:06
11:04
11:05
11:05
11:06
11:06

KUINGIA
ALFAJIRI
ADHANA

KUCHWA JUA
JIONI

ADHANA YA
MAGHARIBI
KUFUNGUA
(IFTAR)

11:17
11:17
11:17
11:17
11:17
11:18
11:18
11:18
11:18
11:19
11:19
11:19
11:19
11:19
11:19
11:20
11:20
11:20
11:20
11:21
11:21
11:21
11:21
11:21
11:21
11:19
11:20
11:20
11:21
11:21

12:17
12:17
12:17
12:17
12:18
12:18
12:18
12:18
12:18
12:19
12:19
12:19
12:19
12:19
12:19
12:20
12:20
12:20
12:20
12:21
12:21
12:21
12:21
12:21
12:21
12:21
12:22
12:22
12:23
12:23

12:22
12:22
12:22
12:22
12:23
12:23
12:23
12:23
12:23
12:24
12:24
12:24
12:24
12:24
12:24
12:25
12:25
12:25
12:25
12:26
12:26
12:26
12:26
12:26
12:26
12:26
12:27
12:27
12:28
12:28

ALLAHUMMA INNAKA AFUWWUN TUHIBBU-L-AFUA


FAAFU ANNA YAKARIMA L-AFUA

TAREHE

1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30

MWEZI

DUA YA KUSOMA UNAPOFUNGUA


ALLAHUMA LAKA SUMTU WAALA RIZKIKA AFTARTU
NIA YA KUFUNGA
"NAWAYTU SAWMA GHADIN AN ADAI FARDHI SHAHRI RAMADHAN HADHII SSANATA LILAHI TAALA IMANAN WAHTISABAN
LIWAJHI LAHIL KARIM AZAA WA JAALA"

RAMADHANI KARIM

RAMADHANI KARIM

Kukesha kwa ibada


M u i s l a m u a n a t a k i wa
asipitiwe hata na dakika
mmoja katika maisha yake
ya h a p a U l i m w e n g u n i
isipokuwa katika kumuabudu
Allah SW na hili ndilo lengo
hasa la kuumbwa kwetu,
Nami sikuwaumba
majini na watu ila waniabudu
Mimi. (51:56)
Ibada zipo za aina tofauti,
miongoni mwa hizo mna
zilizo bora kuliko nyengine
na miongoni mwa ibada zilizo
bora ni kusali, kusoma Quran,
kuomba dua n.k. Vilevile
ibada hizi zinapofanywa
wakati wa usiku, huwa na
jaza zaidi kuliko mchana
na ndio tunajifunza kuwa
Mtume SAW na Masahaba
wa k e h a wa k u p i t i wa n a
usiku pasi na kuamka na
kufanya ibada kwa muda
mrefu, hadi ilipoteremka
aya ya kuwawepesishia na
kuwataka wasikeshe kwa
muda mrefu sana.
Hakika Mola wako Mlezi
anajua ya kuwa hakika wewe
unakesha karibu na thuluthi
mbili za usiku, na nusu yake,
na thuluthi yake. Na baadhi
ya watu walio pamoja nawe
kadhaalika. Na Mwenyezi
Mungu ndiye anaye ukadiria
usiku na mchana. Anajua
kuwa hamwezi kuweka
hisabu, basi amekusameheni.
Basi someni kilicho chepesi
katika Qur'ani.
Anajua ya kuwa baadhi
yenu watakuwa wagonjwa,
na wengine wanasafiri katika
ardhi wakitafuta fadhila
ya Mwenyezi Mungu, na
wengine wanapigana katika
Njia ya Mwenyezi Mungu.
Kwa hivyo someni kilicho
chepesi humo, na mshike Sala,
na toeni Zaka, na mkopesheni
Mwenyezi Mungu mkopo
mwema. Na kheri yoyote
mnayo itanguliza kwa ajili
ya nafsi zenu mtaikuta kwa
Mwenyezi Mungu, imekuwa
bora zaidi, na ina thawabu
kubwa sana. Na mtakeni
msamaha Mwenyezi Mungu.
Hakika Mwenyezi Mungu ni
Mwenye kusamehe Mwenye
kurehemu. (73:20)
Kadhalika mna fadhila na
faida nyingi zipatikanazo
kwa mwenye kudumu
na jambo hili la kuamka
usiku kwa kufanya ibada.
Miongoni mwa mwa faida
hizo ni kuwa zinamsaidia
Muislamu kuweza

kuepukana na machafu na
makatazo yote kwa jumla,
na kumuezesha kufanya
mazuri yenye kumridhi
Mola SW katika muda
mwingi wa maisha yake,
kwani Allah SW amesema
katika hadithi Qudsi kupitia
ulimi wa mjumbe Mtume
SAW Haachi mja wangu
kujikurubisha kwangu kwa
kufanya ibada za Sunna
mpaka ninakuwa ni jicho
lake la kuonea, sikio lake la
kusikilizia, mguu wake wa
kuendea, na mkono wake
wa kushikia. Hii ikimanisha
kuwa haoni, hasikii, haendi
wala hashiki ila vyenye
kumridhisha Allah SW.
Ama faida nyegine
inayopatikana nikuwa karibu
na Allah SW kwani Muislamu
kila anavyozidisha kufanya
ibada na kuzidi kujitakasa
nafsi yake na machafu ndio
anazidi kupanda daraja na
kuwa karibu na Allah SW

RAMADHA
NI YA:

K AT I K A m w e z i w a
Ramadhani Muislamu
anapata fursa ya kujifunza
na kujizowezesha mambo
mengi yanayotakiwa na
Uislamu ambayo huwa
hayapatikani katika miezi
mengine kwa wengi katika
Waislamu na kwa wale
wachache ambao kwao
hupatikana katika miezi
mengine, katika mwezi
wa Ramadhani huwa ni
maradufu.
Katika makala hii
tutajaribu kueleza machache
miongoni mwa hayo mengi
ambayo Muislamu anajifunza
na kujizowezesha katika
mwezi huu mtukufu kwa
kiasi ambacho tumeafikiwa
na Allah SW.
Funga ni jambo ambalo
limependekezwa sana na
kuhimizwa katika Sheria
ya Kiislamu. Na hili ni kwa
hekima. Kuna faida nyingi na
tofauti zipatikanazo katika
ibada hii tukufu. Miongoni
mwa hizo ni kuwa mwenye
kufunga sana anakuwa na
afya nzuri zaidi kuliko yule
asiyefunga au anayefunga
Ramadhani hadi Ramadhani.
Na hili lipo wazi katika
maneno ya Mtume SAW
aliposema, Fungeni mtapata
afya.
Na hili vilevile
limethibitishwa na
wanasayansi wasiokuwa
Waislamu. Ama nyengine
miongoni mwa hekima na
faida nyingi ni kuwa tumbo
la binadamu linaposhiba,
viungo vyake huwa na njaa
yaani mkono hutaka kupiga,
macho hutaka kuangalia
yasiofaa, utupu hutaka
kufanya machafu n.k. Vilevile
kinyume chake ni kuwa
tumbo linapokuwa na njaa,
viungo hushiba na haviwezi
kufanya machafu. Ndipo
Mtume SAW alipowaamrisha
vijana kuowa akawaambia
kuwa asiyekuwa na uwezo
afunge, kwani funga ni kinga
ya kila baya na chafu.
F a i d a n ye n g i n e b o r a
kuliko zote ni kuwa ibada hii
tukufu haikuekewa kiwango
maalum cha malipo tofauti
na ibada nyengine zote.
Kama alivyosema Mtume
SAW hadithi iliopokewa
na Muslim Kila amali
ya b i n a d a m u i n a l i p wa
nyongeza na zaidi, jema moja
kwa kumi mpaka nyongeza
mia saba, amesema Allah
SW isipokuwa funga hakika
hiyo ni yangu na mimi ndiye
mwenye kutoa malipo yake,
kwani mfungaji anaacha
matamanio na chakula chake
kwa ajili yangu.
Kulingana na hadithi hii,
tunaona wazi ukubwa juu ya
funga hadi ikafika kutotajwa
ni kiasi gani malipo yake.
Kwa hivyo tusitosheke na
funga hii ya Ramadhani peke
yake, bali ni tujilazimieshe
hasa katika ulimwengu huu
wa sasa uliojaa machafu
kujibidisha na funga baada

AN-NUUR

MAKALA

17
Inatoka Uk. 11
video ya kupiga risasi
kwazua ubishi," kiliainisha
kichwa cha habari cha
Boston Globe, ambalo
lilieleza kuwa video hiyo
ina chenga na ilipigwa
kutoka mbali kupitia
mvua..... watu wanaoweza
kuonekana ni viwiliwili,
na hakuna silaha
zinazoonekana..... Hakuna
silaha zinazoonekana
katika mtiririko wake, na
kukutana kwa mara ya
kwanza kati ya maofisa
wa kikosi maalum na
Rahim kumefichika."
Kichwa cha habari cha
N e w Yo r k T i m e s p i a
kiliainisha: "Katika video
chenga ya kupigwa risasi
Boston, kurudi nyuma
kwa maofisa (wa polisi)
kuko wazi lakini kisu
hakionekani." Habari hiyo
ilikiri kuwa "ni vigumu
kuona kama Bw. Rahim,
26, aliyekuwa akifuatiliwa
na polisi wakati huo,
alikuwa amebeba kisu,
kama polisi walivyosema."
Video hiyo ilikuwa
inasumbua kiasi kwamba
hata CNN waliona hilo,
na kuyakinisha kuwa
wa k a t i " m a o f i s a ( wa
upelelezi) waliwaambia
waandishi wa habari kuwa
mkanda huo unajieleza
wenyewe .... bado, ulihitaji
kuhadithiwa, akilenga
mkutano na waandishi
wa habari wa FBI ambako
walitoa maelekezo tata
ya hatua kwa hatua jinsi
wa a n d i s h i wa h a b a r i
wanavyotakiwa kutafsiri
na kuelezea video hiyo
"inayojieleza yenyewe."
CNN ilisema pia kuwa
"kama haiwezekani kuona
kinagaubaga - na hakuna
sauti katika video hiyo"
na kuwa ni "chenga kwa
sababu ya umbali kutoka
k a m e r a n a wa h u s i k a
inaowarekodi."
Familia ya Rahim ilitoa
taarifa ikiainisha maswali
mengi yanayotokana na
video hiyo.
Ni bayana kuwa video
h i y o i n a z u a m a s wa l i
kuliko inavyojibu, na tukio
lenyewe limegubikwa
na kila aina ya shaka
zisizotatuliwa kuhusu nini
kilitokea hapa:
(1) Tuseme tu kwa ajili
ya kujenga hoja kuwa
walichosema polisi kuhusu
kupiga risasi ni kweli. Hivi
inashangaza kiasi hicho
- au ya kulaumu - kuwa
mtu anayesimamishwa
kwa ghafla na kwa utisho
na watu watano ambao
hawakuvaa sare angehisi
kutishiwa? Kutokutaka
kuangusha kisu chake
inawezekana pia ni
matokeo ya kupewa (kwa
makusudi au kwa uzembe)
na vitendo vya kumtishia
kwani bila hivyo mpango
wa p o l i s i u n g e k a t wa
kichwa. Kama mtu
angetaka kumchokoza

MAKALA

AN-NUUR

RAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 26- Julai 2, 2015

Maswali tata yatanda

Rahim ili hatua ya


k u p i g a r i s a s i i f i k i we
'inayohalalisha' vitendo
vya polisi, kumfuata kwa
njia hii ingekuwa muafaka
kabisa.
(2) Kuhusiana na
kilichotangulia: tukubali
kwa ajili ya kujenga hoja dai
la FBI kuwa Rahim alikuwa
akijiandaa kutekeleza
mpango wa ki-ISIS wa
kuwakata vichwa maofisa
wa polisi, na walikuwa
wanajua hilo kwa sababu
alikuwa anafuatiliwa na
polisi kwa kina kwa masaa
24, ikiwa ni pamoja na
kufuatilia mawasiliano
yake kielektroniki, ya simu
na barua pepe.
Kwanini hawakuchukua
hati ya kumkamata ili
waweze kuanza shauri
hilo, au hati ya upekuzi
kuwapata wanaodaiwa
kushirikiana naye? Kama
walikuwa na ushahidi
wa wa z i wa m p a n g o
wake, kwanini wasifanye
hivyo? Kwanini utake
kukabiliana barabarani
ambako wapita njia
wangeweza kuwa hatarini
ili "kumhoji"? Kama
hakuwa amebeba kisu,
na alikuwa amekanusha
kuwa na mpango wowote
wa kuwashambulia
maofisa wa polisi, ilikuwa
ni nia yao ya kumwacha
aendelee na shughuli
zake? Madai ya FBI na
BDP -tulikuwa na ushahidi
wa kutosha alikuwa gaidi
mfuasi wa ISIS akijiandaa
kutekeleza mpango wa
kigaidi - hayaendani kabisa
na jinsi walivyomfuata na
sababu wanayodai ndiyo
i l i y o wa t u m a k u f a n ya
hivyo.
(3) Mmoja wa wadaiwa
kushirikiana na Rahim,
binamu yake David
Wright, amekamatwa na
kufunguliwa mashtaka.
L a k i n i h a k u s h t a k i wa
kwa kusuka mpango wa
kuua maofisa wa polisi
au kufanya mashambulio
ya kigaidi, ila kwa shtaka
moja la kuzuia upelelezi,
kwamba eti alitoa rai
kuwa Rahim ateketeze
simu yake ya mkononi.
Kama Rahim alikuwa na
washirika katika mpango
huo wa kigaidi kama FBI
wakati wote inavyodai,
k wa n i n i h a t a m m o j a
kati yao hajakamatwa na
kushtakiwa?
(4) Taarifa za awali
zilidai kuwa kulikuwa na
'mpanga njama wa tatu'
nje ya Rahim na Wright.
Hati ya mashtaka ya FBI
iliyofikishwa mahakamani
dhidi ya Wright
inarudiadia kumtaja "mtu
wa tatu" ambaye alikuwa
akila njama na Rahim na
Wright na alikutana nao.

Hata hivyo hapajakuwepo


tena na kutajwa mtu huyu
'wa tatu,' na haielekei
kuwa aliwahi kukamatwa.
Kwanini? Mtu huyo wa tatu
ni mpasha habari wa FBI?
Hivi hii ni kesi nyingine
ambako mkurugenzi na
mwendeshaji wa tishio
la 'mpango wa kigaidi'
hasa ni FBI yenyewe,
kupitia kwa 'mtu wa tatu'
anayeelekezwa na FBI?
(5) Msingi gani upo
kwa madai ya kuamsha
hisia za watu kuwa Rahim
alikuwa na mahusiano,
au mfuasi ISIS? Ushahidi
pekee unaotajwa ni kuwa
alikuwa anafuatilia na
kuzipenda taarifa za aina
mbalimbali za ki-ISIS
katika mitandao. Hivi hii
sasa inatosha kutangazwa
katika vyombo vya habari
kama mshirika wa ISIS na
kushughulikiwa kwa njia
hiyo na maofisa wa polisi
wenye silaha? Angalia jinsi
Wizara ya Sheria chini
ya Rais Barack Obama
inavyojaribu kuongeza
miaka 20 kwa kifungo cha
Imamu wa jimbo la Florida
kutokana na vitabu ya
'kiharakati' alivyokuwa
navyo.
Tukiwa bado katika
mitandao, hiki ndicho
alichosema Rahim
katika ukurasa wake wa
Facebook, ikiwa ni ya
Novemba 27, 2012, huko
Boston:
Ujinga gani FBI kuita
simu yangu! Wanataka tu
nafasi yoyote ya kumvuta
Muislamu aingie katika
SAKATA fulani.... Alikuwa
anataka kukutana nami na
"Kuongea." HA! Nilisema
kuhusu NINI? Akasema,
"bwana wewe, tuna madai
kadhaa yanayokuhusu...."
Nikasema 'KWELI?'' Ni
MADAI gani? Akasema
"unaona bwana, ndicho
nilichokuwa nataka
kukutana na wewe
kuhusiana nacho. Nilipita
nyumbani kwako mara
kadhaa, lakini wakati
wote nikawa ninakukosa."
Nikasema, "Kama unataka
kuniletea hati ya shauri
mahakamani, tafuta
AMRI YA MAHAKAMA
kama madai unayoleta
kuhusu mimi ni ya kweli,
vinginevyo, POTEA"
halafu nikakata simu.....
Inashangaza, nilikuwa
namwambia ndugu
yangu kuwa nilisikia
kama sauti za kufyatua
vitu fulani katika simu
yangu. Kila Muislamu
anahitaji kuwaona hawa
mawakala wa serikali
kama nilivyofanya,
kwa sababu kama
unawaacha wakukaribie,
amini ninalokuambia,
watakufanya utoe maneno

kuhusu vitu ambavyo


vitakupatia kifungo,
kuhusu kile ulichokuwa
unahubiri KUPINGA,
yaani utumiaji nguvu
na ugaidi. Jaribuni tena,
wasuka mitego wa polisi....
Hivyo hakuwa tu na
wasiwasi wa kuundiwa
zengwe na FBI, lakini
alisema kinagaubaga
" a n a h u b i r i D H I D I ya
utumiaji nguvu na
ugaidi." Kama shirika
la habari la Associated
Press lilivyosema, katika
mtandao Rahim "aliasa
kuhusu aina ya utumiaji
n g u v u a m b a o wa n a siasa kali wa Islamic
State wanachochea kote
Mashariki ya Kati," na
"hakuweka picha zozote za
damu na hakutoa mwito
wowote wa kutwaa silaha
kama wanavyofanya
waunga mkono wengi
tu wa makundi yenye
silaha ya siasa kali, katika
mitandao." Isitoshe, "kuua
watu siyo Uislamu," Rahim
aliandika, akiainisha
kuwa kiini kimojawapo
muhimu cha imani ni
k u wa " h a t u p i g a n i n a
uovu kwa kile kinacholeta
uovu mkubwa zaidi." Hii
ni kinyume kabisa cha
picha katika mitandao
inayoonyesha mpenda
u g a idi a na ye s ha b i k i a
kundi la ISIS iliyotolewa
kwa muda wa wiki mbili
za misisimko vyombo vya
habari kutokana na madai
ya FBI.
(6) Mazungumzo ya
s i m u ya l i y o r e k o d i wa
yakatajwa na FBI kama
uyakinishaji wa njama za
Rahim, sana sana tu ni wa
kutia shaka. Wanamkuuu
Rahim akimwambia
Wright: "Ndiyo, nitakuwa
katika likizo hapa hapa
Massachusetts," jibu
ambalo hati ya FBI
inasema: "Kutokana na
masomo ya upelelezi,
uzoefu na kuhusika na
shauri hili, naamini kuwa
'kwenda likizoni,' usemi
uliotumika mara kadhaa
katika mazungumzo kati
ya WRIGHT na RAHIM,
inazungumzia kufanya
jihadi ya kutumia nguvu."
Ukweli ni kuwa
Waislamu wanakwenda
likizo kama watu wengine,
h i v y o l a b d a ' k we n d a
l i k i z o ' i n a m a a n a ya
'kwenda likizo,' na siyo
'nanuia kufanya jihadi kwa
kuwakata vichwa maofisa
wa polisi"? Tafsiri nyingine
za kinachoitwa na lugha
ya kificho - kwa mfano
'kama kufikiri na kichwa
chako kifuani mwako'
kama ishara ya 'nanuia
kukata vichwa maofisa
wa polisi' - ni vielelezo
vinavyozua tu maswali,

au angalau vinafaa kutilia


shaka kabla ya kuyakinisha
kuwa kuuawa kwa Rahim
k u l i k u wa n a u h a l a l i
wowote kwa msingi kuwa
alikuwa gaidi mla njama
kukata vichwa wa ISIS.
Hati hiyo ya mashtaka
pia ilitaja alichosema
Rahim kuwa alikuwa
anapanga 'kuwafuata'
'vijana waliovalia (mavazi
ya) buluu,' kama ushahidi
kuwa alikuwa anapanga
kuua maofisa wa polisi.
Lakini alichokuwa
akiandika katika ukurasa
wake wa mtandao, Rahim
a l i k u wa a n a l a l a m i k a
kusumbuliwa na polisi bila
sababu; wakati mmoja,
baada ya wao kumhoji
jirani yake, aliandika:
"Wanang'ang'ania lakini
wajua, hawana lolote juu
yangu. Endeleeni kuja,
wa p u m b a v u n y i e , n a
nitawafungulia mashtaka
msote kwa kunisumbua."
Ni wazi kuwa
'kuwafuata' hao
'wanaovalia buluu'
kungeweza kumaanisha
n i t a k a t a v i c h wa v ya
maofisa wa polisi, lakini pia
ingeweza kuwa na maana
rahisi tu kuwa: Nataka
kuwapeleka mahakamani.
Pia, ushahidi pikwa wa FBI
ni dhaifu na haueleweki
hata ukijitahidi. na hakuna
haja mtu yeyote kuamini
kuwa unaonyesha kuwa
R a h i m a l i k u wa g a i d i
mwenye hatia aliyestahili
kufa.
Tulicho nacho hapa
ni Muislamu mweusi
aliyeuawa akiwa
anatembea kwenda
kazini, kufuatilia ushahidi
wa mashaka na madai
shawishi yasiyo na
msingi yaliyoenezwa na
FBI na mawakala wake
wa vyombo vya habari
ambayo yamesukwa
ili kukufanya utake
kumpuuza Rahim kama
Mshirika Mwovu wa ISIS
ambaye alistahili kufa,
yote hiyo bila kujiuliza
maswali yoyote. Suala
hapa siyo kuwa hana hatia;
bado hakuna vielelezo vya
kutosha kufikia hoja isiyo
na shaka. Suala hapa ni
kuwa matukio kama haya
na madai rasmi muda wote
lazima yasikizwe kwa
maswali na kutoamini,
hasa kwa waandishi wa
habari. Hapa, 'ushahidi'
zaidi unapotolewa,
maswali mengi zaidi na
ya lazima yanaongezeka.
Ukitumia dhana iliyo
dhaifu zaidi, ni taasisi
hizo hizo za utekelezaji wa
sheria ambazo zilimwua
zilimpachika ugaidi
wa ISIS na vyombo vya
habari vikafanya wajibu
wao kufuata. Ndivyo
wanavyofanya kazi.

18

MAKALA

AN-NUUR

RAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 26- Julai 2, 2015

Dakta Shein anajijengea historia yake mwenyewe


Na Mwadini Ali

INAONEKANA viongozi
wa Chama Cha Mapinduzi
( C C M ) wa n a m t i i s a n a
kiongozi wao mkuu
upande wa Zanzibar, Dk.
Ali Mohamed Shein. Na
matokeo yake, naye Dk.
Shein, daktari bingwa wa
tiba ya magonjwa makubwa
ya mwanadamu, anawatii
sana wasaidizi wake hao
wa chama. Nazungumzia
u t i i f u u n a o wa h u s u t u
wa n a c h a m a wa C C M ,
chama kilekile ambacho
ndicho kimempandisha
chati ya kisiasa daktari
huyu, hadi kufika kuwa
mpangaji mkuu wa makao
makuu ya mamlaka ya
Zanzibar, Ikulu yaliyopo
Mnazi mmoja. Utiifu uliopo
kati ya wanachama hao wa
CCM na Dk. Shein, kumbe
hauna maana yoyote kwa
mustakbali wa Zanzibar,
na wala kwa watu wake
Wazanzibari, kutoka
Unguja na Pemba.
Sasa hii ni bahati mbaya
aliyoipata Dk. Shein katika
m i a k a ya k e m i t a n o ya
uongozi inayomalizika ndani
ya siku 120 zijazo. Bahati hii
mbaya imetokea kwa sababu
huyu Dk. Shein ndiye Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi
(BLM). Kama si kutimiza tu
matakwa ya kikatiba, urais
anaoushikilia Dk. Shein
usingekuwa na mahusiano
yoyote na chama alichopitia
kuongoza Zanzibar. Labda
hapo ndo angeutumia vizuri
wadhifa huu akawa mtiifu
zaidi kwa wananchi badala
ya kujiweka mtiifu zaidi kwa
chama chake na kusahau
kabisa maslahi ya wananchi.
Ndo ninaposema kumbe
uliopo ni utiifu uliokuja
vibaya kwa sababu kadiri
ninavopima na kutathmini
ya n a y o t o k e a n d a n i ya
Zanzibar, nchi ndogo kieneo
iliyo sehemu ya jamhuri
kubwa la Muungano,
nazidi kuthibitisha kuwa
hauzingatii chembe ya
mahitaji halisi ya wananchi
wa Zanzibar.
Chukulia suala moja
muhimu ambalo alilitolea
ahadi mara baada ya
kushikana mikono, katika
ishara ya kuridhiana, na
Maalim Seif Shariff Hamad,
ukumbi wa Salama wa
Hoteli ya Bwawani.
Ilikuwa ni siku ya kwanza
ya mwezi Novemba mwaka
2010, Dk. Shein baada ya
kutangazwa mshindi wa
urais katika uchaguzi mkuu
wa Zanzibar uliofanywa
Oktoba 31, alitoa ahadi
mbele ya ulimwengu
kuwa atayashughulikia
matatizo yaliyobainishwa
kuhusu Tume ya Uchaguzi
ya Zanzibar Zanzibar
Electoral Commission (ZEC).

RAIS wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.


Malalamiko yanayohusu
u t e n d a j i w a Tu m e y a
Uchaguzi yalitolewa kwake
na Maalim Seif, mshindani
wake katika kuwania urais,
akiwakilisha Chama cha
Wananchi (CUF). Maalim
Seif ambaye tangu pale
alikuwa Katibu Mkuu wa
chama hicho, aliyajua khasa
matatizo ya tume kwa kuwa
alikuwa akishughulikia
mwenendo mzima wa ratiba
ya uchaguzi mpaka matokeo
ya mwisho yalipokuwa
yakitangazwa.
Malalamiko yote
yaliyokuwa yakitolewa na
viongozi na wanachama wa
chama hicho, na khasa yale
yaliyohitaji hatua kubwa
zaidi katika kuyashughulikia,
yalimfikia yeye; ndipo basi
alipolazimika kuyafikisha
k wa Tu m e . L a k i n i p i a
yalimfika malalamiko kwa
sababu mwenyewe alikuwa
ndiye mgombea wa urais,
alikuwa analazimika
kufuatilia yanayokutwa na
wasaidizi wake kama shida
zinazotokana na utendaji
wa Tume.
Basi Maalim Seif, mara
tu lilipotoka tangazo la
Mwenyekiti wa Tume wakati
ule, Khatibu Mwinchande,
la kumpa ushindi Dk.
Shein, aliridhia na akaamua
matatizo aliyoyabaini
kutokea wakati wa uchaguzi,
ayafikishe kwa kiongozi
mpya kwa ajili ya kuyafanyia
kazi.
Akamwambia Dk.
Shein nakuomba sana
uyashughulikie matatizo
makubwa yanayoikabili
tume yetu ya uchaguzi.
Y a n a s a b a b i s h a
manunguniko mengi na ni
lazima yaondolewe ili tufike
wakati nchi yetu iendeshe
uchaguzi ulio huru, wa haki
na kwa njia za uwazi, ndipo
matokeo yake yatakapokuwa
yanaaminika.
Dk. Shein aliposhika

nafasi ya kuzungumza,
akiwa ameshasikia kilio cha
matatizo ya kiutendaji ya
Tume ya Uchaguzi, alitoa
ahadi palepale ya kuwa
atayafanyia kazi ipasavyo
na kwamba hiyo itakuwa
moja ya kazi zake za kwanza
akishateua serikali.
Matatizo ya Tume ya
U c h a g u z i ya Z a n z i b a r
s i m a p y a . Ya m e k u w a
yakijirudia kila wakati wa
uchaguzi. Kwa kuangalia
mjumuiko wa matatizo
yanayokabili asasi hii ya
kiserikali, ni rahisi kusema
yamekuwa yakidhoofisha
kuaminika kwa matokeo
yenyewe ya uchaguzi
yakiwemo yale ya urais. Na
ni kwa bahati mbaya sana,
katiba imefunga fursa ya
kuyahoji matokeo kwenye
chombo chochote, mara
yakishatangazwa.
Tume ya Uchaguzi ya
Zanzibar ina makamishna
saba, ikiongozwa na
mwenyekiti ambaye kwa
mujibu wa Katiba ya
Zanzibar, 1984, huteuliwa
na Rais. Sifa ya mteuliwa
ni kuwa mtu aliyekuwa
au mwenye sifa za kuwa
jaji katika Mahkama Kuu
a u M a h k a m a ya R u f a a
katika nchi yoyote iliyo
mwanachama wa Jumuiya
ya Madola, au mtu
anayeheshimika katika jamii.
Ibara ya 119 ya Katiba ya
Zanzibar ndiyo inayotoa
mamlaka ya kutambuliwa
Tu m e ya U c h a g u z i ya
Zanzibar. Uteuzi wa
mwenyekiti unatajwa
kifungu cha pili. Sasa
Dk. Shein alimteua Jecha
Salim Jecha, akijua hana
sifa ya kuwa jaji. Yeye si
mwanasheria kitaaluma.
Kwa hivyo, inachukuliwa
kuwa alimteua Jecha, katibu
mkuu wa zamani serikalini,
kwa sifa ya kuwa mtu
a n a ye h e s h i m i k a k a t i k a

jamii. Alichokifanya Dk.


Shein katika kumteua Jecha
kuongoza Tume, ni kutii zaidi
wasaidizi wake katika CCM.
Jecha anajulikana alivyo
mwanachama wa CCM. Bila
ya shaka yoyote, hakustahili
kuteuliwa kushika nafasi
hiyo. Na msimamo huu
unazingatia khasa umuhimu
wa nafasi yenyewe kushikwa
na mtu mwenye uwezo,
uzoefu na ujasiri wa kutenda
kwa kutegemea misingi ya
Katiba na siyo ushabiki wa
chama kama inavyoonekana
kutokea chini ya Jecha.
Aliahidi kutenda kazi
kwa uadilifu na kuzingatia
sheria. Ona anavyoshindwa
kuiongoza Tume katika
kurahisisha upatikanaji wa
haki za wananchi wakati
huu tume ikiwa inaandikisha
wapigakura vituoni.
Lakini, vituo vinavamiwa
na watu waliobeba silaha
za moto huku wamejivika
vitambaa usoni kuficha
kutambuliwa. Hivi kama
uandikishaji wapigakura
unahusisha watu waliobeba
bunduki huku wakijificha
wasitambuliwe kwa sura
au kwa majina yao, tena
wakipiga na kunyanyasa
watu waliofika vituoni
kujiandikisha, kusudi tu
kubeba wengine wasiokuwa
wenyeji wa maeneo husika,
tuseme masuala ya uchaguzi
yachukuliwe kuwa ni jambo
la kijeshi?
Wala Jecha hajasikika
akilalamika. Amebakia
kimya mambo yakiharibika.
Anayawachia kwa
sababu moja tu kubwa
hayamshughulishi maana
hayadhuru utashi wake wa
kusimamia uongozi kwa
misingi ya Katiba. Kwa kweli
Jecha anakosa ujasiri wa
kukemea kwa kuwa anamtii
zaidi Rais aliyemteua, rais
ambaye na mwenyewe anatii
zaidi chama alichopitia kuwa

rais.
J e c h a
k a m a
anavyoonekana aliyemteua,
kwao la muhimu ni maslahi
ya CCM wala si maslahi ya
Wazanzibari. Kwa hivyo
basi, kwa yanayoendelea
vituoni, tayari wananchi
wanaambiwa mapema
kuwa wasije kutarajia Jecha
kusimamia Tume kutangaza
matokeo yatakayowaudhi
viongozi wa CCM. Hivi
Jecha akiulizwa ni kwanini
khasa Tume haijatangaza
mpaka leo hii, majimbo
yatakayoshindaniwa katika
uchaguzi huo, atakuwa
na jibu gani? Swali hili ni
muhimu ikizingatiwa kuwa
hivi sasa ni miezi mitatu tu
kabla ya siku ya uchaguzi,
Oktoba 25, na miezi miwili
tu kabla ya siku ya uteuzi wa
wagombea,
Tu m e t a n g u J u n i
mosi ilipoingia imetuma
waandikishaji kuandikisha
wapigakura majimboni,
lakini haijaeleza kwa umma
huyo mtu anayeandikishwa
atakuwa mpigakura wa jimbo
gani. Haoni anaiongoza
tume kibubusabubusa?
Au k wa m b a ye ye n a
wenzake wanakosa dhamira
njema ya kutumia dhamana
waliyopewa kujenga historia
ya utendaji uliotukuka?
M k o s e f u wa d h a m i r a ,
haipati nia njema kwenye
hilo atendalo.
Dk. Shein alijua
k wa m b a k wa k u m t e u a
Jecha kuongoza Tume ya
Uchaguzi hakutabadilika
chochote kutoka yale
malalamiko aliyokabidhiwa
na Maalim Seif, mwanasiasa
aliyemridhia awe mmoja
wa wasaidizi wake wakuu
serikalini Makamu wa
Kwanza wa Rais. Rais huyu
alijua watendaji wa Tume,
kwa kuwa wanaongozwa
n a m t e u l e wa k e J e c h a
Salim Jecha, asiyekuwa na
dhamira ila ile ya kukibeba
chama chao, wataendesha
mambo kwa utaratibu uleule
waliouzoea miaka yote
utaratibu wa kutenda huku
wakihakikisha ni CCM tu
kushinda si zaidi ya hapo.
Halafu hapo bado
Wazanzibari na walimwengu
wadanganywe kuwa
Zanzibar itakuwa na
uchaguzi ulio huru, wa
haki na uliofanywa kwa
njia za uwazi? Jaguju. Kama
ndo hivyo, nini kimebakia?
Kwanza Dk. Shein
hakubadilisha chochote,
lakini kubwa ameigandisha
nchi isitoke tanurini kwa
moto ilipo. Alhamdulillah
ameijenga historia yake yeye
mwenyewe.

19
Na Shaban Rajab
B I L A s h a k a Wa i s l a m u
wa n a j i t a h i d i k u t e n d a
yaliyo mema kipindi hiki
ambacho wamo katika ibada
ya funga ya Ramadhani.
Tunamuomba Mwenyezi
Mungu atutakabalie saumu
na ibada zetu katika mwezi
huu mtukufu.
Jambo la kwanza ambalo
tunapaswa kufanya
kuhusiana na mwezi wa
Ramadhani, ni kufahamu
kwa usahihi kuhusu malengo
na falsafa ya mwezi huu.
Muumini anapaswa kujua
sababu ya kuwepo saumu na
ni kwa nini amefaradhishiwa
ibada hiyo. Bila shaka kwa
kufahamu sababu hizo,
atajikuta anatenda yale
ambayo humfanya awe
Mcha Mungu hata baada ya
kuondoka Ramadhani.
Mwezi mtukufu wa
Ramadhani ni ishara ya
u k a r i m u wa M we n ye z i
M u n g u k wa Wa u m i n i .
Mwezi huu ni kama maji
ya uhai ambayo hukidhi
kiu kali. Kwa muda mrefu
sasa nimebaini kuwa kila
u n a p o a n z a m f u n g o wa
Ramadhani, kuna mazingira
fulani ya utulivu hujitokeza
katika miji na mitaa yetu.
Lakini ajabu ni kwamba, hali
hiyo huanza kutoweka mara
inapoondoka Ramadhani, na
hapo hurejea hali ya kabla ya
Ramadhani.
Hivi sasa tunashuhudia
yale maeneo mengi ya starehe
za maasi na laghawi zikiwa
zimepwaya. Hakuna wateja
ama kuna wateja wachache
sana. Kwa mfano kipindi
hiki mimeshuhudia maeneo
mahiri kwa biashara ya
pombe (bar) yakiwa kimya
bila wateja waliozoeleka,
maeneo ya wasichana
wanaofanya biashara za
miili (uzinzi) nako biashara
imedorora. Hata mwandishi
wa magazeti ya burudani
(udaku) nao wameliona
hilo. Nanukuu habari
iliyoandikwa katika gazeti
la Risasi, na Waandishi Issa
Mnally na Richard Bukos:
K AT I K A h a l i y a
k u s h a n g a z a , u s i k u wa
Jumanne iliyopita, Risasi
Jumamosi (siku tano kabla ya
Ramadhani) liliwanasa akina
dada wanaojiuza ambao
walisema hawatakuwepo
katika eneo lao la biashara
kwa muda wa mwezi mmoja
kwa sababu ya mfungo
wa mwezi Mtukufu wa
Ramadhan.
Machangudoa hao
wa l i k u t wa C o r n e r B a r ,
Africana Sana- Sinza, Jijini
Dar es Salaam wakisaka
wanaume huku wakidai
wanavunja jungu.
Mmoja aliyetajwa kwa
jina la Rose, alidai yeye ni
kahaba mzoefu wa eneo
hilo na kudai kwamba mara
mfungo utakapoanza hata
wao watasitisha biashara
hiyo mpaka watu wenye
imani hiyo watakapomaliza

Makala

AN-NUUR

RAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 26- Julai 2, 2015

Utulivu mwezi wa Ramadhani

AMIR wa Baraza Kuu, Sheikh Mussa Kundecha akikhutubu katika moja ya makongamano
yaliyowahi kufanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. (Picha kutoka Maktaba Yetu)
ibada yao.
Unajua nini? Ni kweli
tunatenda dhambi, lakini sasa
si vizuri wenzetu wafunge
halafu sisi tunashughulika na
zinaa kwa kuuza mwili, hata
Mungu hapendi. Kwa hiyo
mimi nitaacha ili kuungana
na wenzetu, alinukuliwa
Rose, mwenyeji wa Mbeya.
A i d h a
w e n g i
wameshuhudia matangazo ya
wanamuziki wakiwashawishi
watu kuhudhuria katika
maonyesho yao ya mwisho
kwa ajili ya kupisha mwezi
Mtukufu wa Ramadhani.
K wa m b a wa t e j a wa o
wasipohudhuria onyesho hilo
la mwisho,(Vunja jungu), basi
itabidi wavumilie kukaa kwa
tabu bila burudani hadi hapo
Ramadhani itakapokwisha.
Na kweli maonyesho hayo ya
mwisho, iwe ni disko, dansi,
taarabu, bia nyama choma,
hufurika watu wengi, ambao
hufika kukata kiu ya mwezi
mzima.
Katika uchunguzi
nilioufanya katika kipindi hiki
cha mfungo wa Ramadhani,
umenidhihirishia kwamba
hawa waliokuwa wanajaa
katika kumbi za burudani
hizi zilizosheheni matendo
yasiyompendeza Mwenyezi
Mungu, ni watu wa jamii
zote. Yaani wapo wengi
Waislamu na wengi Wakristo.
A i d h a k u d o r o r a k wa
biashara ya vileo bar nyingi,
yaani kupungua wanywaji wa
vileo wakati huu, kupungua
wateja nyumba za wageni,
kunadhihirisha matokeo
ya uchunguzi kwamba
wateja wa machangudoa na
machangudoa wenyewe,
wa p o Wa i s l a m u n a
wasiokuwa Waislamu kwa

idadi zinazowiana.
Utafiti wangu umebaini
kuwa hivi sasa kuna
u p u n g u f u m k u b wa wa
wageni katika nyumba za
wageni. Hali hii inanipa
ujasiri wa kusema kwamba
wengi wanaoingia nyumba
hizo ni wenyeji na wengi
wanakwenda huko kwa ajili
ya kukidhi matendo yao
machafu na si kupata huduma
ya malazi au mapumziko
kama ilivyokusudiwa.
Hata hivyo kumekuwa
na maswali kuwa utulivu
unaopatikana hivi sasa je, ni
kwa sababu Waislamu ndio
waovu zaidi kuliko watu wa
jamii nyingine?
We n g i wa n a h o j i h i l o
wakiamini kuwa wasiokuwa
Waislamu, hawana sababu ya
kuacha starehe zao ovu kwa
kuwa Ramadhani sio katika
imani yao na haiwahusu.
Hivyo kama ni maovu basi,
wangeendelea nayo kwa
kuwa mahitaji ya bar, nyumba
za wageni, dansi, night club
yangeendelea kuchangamka
kwa sababu ya kuendelea
uwepo wao.
Nichukue fursa hii
kubainisha yaliyojiri katika
uchunguzi wangu wa muda
mfupi kwamba, wanaopupia
starehe hizi ovu, wapo
Waislamu na wasiokuwa
Waislamu. Lakini katika
mwezi wa Ramadhani hali
inakuwa tofauti kidogo.
Wa i s l a m u k a r i b u w o t e
wanafahamu fika maana
ya m we z i M t u k u f u wa
Ramadhani, kusudio lake,
adabu zake na mafundisho
yake na faida zake.
Lakini pia wapo Waislamu
a m b a o k wa m a k u s u d i ,
pamoja kujua maana utukufu

wa Ramadhani, lakini kwa


kibri na kwa makusudi
wanaruhusu nafsi zao zikaidi
utukufu huo na kutawaliwa
starehe na anasa zisizofaa.
Lakini wakati huo huo
wanapata hofu ya kuonyesha
uovu wao hadharani kwa
kuogopa macho ya Waislamu
walio wengi wanaoutukuza
mwezi wa Ramadhani.
Pia wapo Waislamu ambao
walibobea katika starehe
zilizojaa maovu lakini ikiingia
Ramadhani kujizuia starehe
hizo. Hawa wakati mwingine
hata hufunga na kuswali
wakati wa Ramadhani, lakini
wana chembe za woga kiasi
cha kusitisha maovu ya
starehe zao kwa muda wakati
wa mfungo.
Hawa ndio wale ambao

ni walevi lakini ndani ya


Ramadhani wanapumzika
kunywa pombe, wanapenda
dansi lakini katika Ramadhani
wanaogopa kwenda kusakata
rhumba, wazinzi lakini ndani
ya mfungo hathubutu kufika
nyumba za wageni kuzini,
Hawa ndio wale wanaovunja
jungu ili kupisha Ramadhani
na mara baada ya Ramadhani
kwisha kurejea katika
matendo yao.
Lakini pia nimebaini kuwa
wapo wasiokuwa Waislamu,
ambao hufanya hawabanwi
na Ramadhani kwa kuwa
si katika taratibu za imani
yao lakini wanadai kuwa
wanawaheshimu jamaa zao
Waislamu.
K a t i k a Wa s i o k u w a
Wa i s l a m u w a l i o k u w a
wakinywa siku nyingine
na baadhi ya rafiki zao
Waislamu, Kwa kuwa wenzao
wamefunga nao husitisha
kunywa.
Hata hawa machangudoa,
wasiokuwa Waislamu nao
huamua kupunguza shifti
wakidai kuheshimu wenzao
Waislamu, Mfano mzuri ni
Rozi, tuliyemnukuu hapo
awali.
Ni jambo la kawaida katika
mfungo huu wa Ramadhani
kumkuta asiyekuwa
Muislamu kajistiri tofauti na
anavyo kuwa siku nyingine
zisizokuwa za Ramadhani.
Vivyo hivyo hata baadhi ya
mabinti wa Kiislamu ambao
walikuwa hawana kawaida
ya kuvaa vazi la stara,
wakiwa wamekubuhu kama
mavazi ya khasara katika
miezi mingine, wakati huu
wa Ramadhani wengi wako
ndani ya vazi la stara mitaani!
Hawa wengi wao Ramadhani
ikiondoa huondoka na stara
yake.
Kwa dalili hizi chache
itoshe kubaini kwamba,
utulivu japo si kamili
unaoonekana sasa, ni
matokeo ya kusitishwa kwa
kiasi fulani huduma ovu,
ambazo wateja wake ni watu
jamii za imani tofauti.

Sheikh Zubeir aelekea kuwa Mufti


Inatoka Uk. 20
kuwa Mufti, hasa kwa

kuzingatia kwamba
Wajumbe wa Baraza la
Ulamaa la Bakwata, wote
walimkubali kwa kauli
moja kuwa Kaimu Mufti.
Sheikh Abubakar Ali
Zubeir, alizaliwa mkoani
Tanga mwaka 1953.
Alisoma masomo yake
ya dini kwa Masheikh
Mbalimbali, akiwemo
Marhum Sheikh Abdul
Rahman omar Mgaza
huko Korogwe.
Alisoma kwa Sheikh
maarufu na mwanazuoni
mkubwa mkoani Tanga,
Marhum Mohammed
Ayoub, mwasisi wa
Madrassat Tamta Tanga

ambapo aliweza kufuzu


kuwa mwalimu mzuri wa
dini.
Alianza kufanya kazi
Bakwata mwaka 1978
akiwa karibu sana na Mufti
wa wakati huo, Hemed bin
Jumaa bin Hemed.
M w a k a
1 9 9 0
a l i c h a g u l i wa k u i n g i a
katika Baraza la Ulamaa
la Bakwata.
Mwaka 2003-208 alikuwa
Naibu Mufti BAKWATA,
cheo ambacho hata hivyo
k i l i o n d o l e wa b a a d a e
k u f u a t i a k u o n d o l e wa
katiba iliyokuwepo.
Aliendelea kuwa katika
Baraza la Ulamaa hadi
alipochaguliwa na Baraza
la Ulamaa kuwa Kaimu
Mufti 2015.

AN-NUUR

20

MAKALA

20

Hivi mnawaamrisha watu kufanya wema na hali mnaziacha

Na Shaban Rajab
NIMEAMUA kugombea
kwa kuwa ni sifa stakihi.
Nitawaunganisha Waislamu
wote kuwa kitu kimoja,
nitaziondoa tofauti zilizopo
hivi sasa miongoni mwa
Waislamu.
Haya yalikuwa ni
maneno ya Sheikh Abubakar
Zubeir, aliyoyatoa baada
ya kutangaza nia yake ya
kuwania nafasi ya Umufti
ndani ya Bakwata kufuatia
kifo cha Mufti Issa Shaaban
Simba, aliyefariki dunia wiki
iliyopita na kuzikwa mkoani
S h i n ya n g a ya l i p o k u wa
makazi yake.
Baada ya kuikwaa nafasi ya
Kaimu Mufti, Sheikh Zubeir,
alitoa ahadi nyingine kuwa
iwapo akiwa Mufti, atabadili
katiba ya sasa ya BAKWATA
kwa kuwa imekuwa ndio
sababu ya migogoro kwa
Waislamu nchini na waumini
wengi kuihama taasisi hiyo na
kujiunga na taasisi nyingine
kuendeleza masuala hayo
hayo ya kidini.
Akizungumza na
waandishi wa habari
mapema wiki hii, Mjumbe
wa Baraza la Ulamaa la
Bakwata Sheikh Jongo, kwa
upande wake alisema kuwa
kunahitajika mabadiliko ya
katiba kwa kuwa iliyopo na
imesababisha mgawanyiko
baina ya Waislamu na hata
ndani ya Bakwata kwenyewe.
Sheikh Jongo alisema
katiba mbovu inasababisha
migogoro na migawanyiko
baina ya Waislamu na ndani
ya BAKWATA.
Hivyo ameipokea ahadi ya
Kaimu Mufti Zubeir ambaye
ameahidi kuwa ataibadilisha
katiba hiyo yenye udhaifu.
Akasema, ana imani kuwa
mabadiliko hayo ya katiba
yataondoa migogoro yote
iliyopo kwa sasa.
Kwa miaka mingi
Waislamu wengi nchini
wamekuwa wakilalamikia
utendaji usioridhisha wa
BAKWATA, hasa baada ya
kufariki Mufti wa zamani
Hemed bin Jumaa bin
Hemed.
Wengi wamekuwa na
imani kwamba udhaifu
wa kikatiba ndio uliokuwa
msingi wa watendaji wengi
wa Baraza hilo, hasa wa
ngazi za juu kushindwa
kutimiza wajibu wao kwa
maslahi ya Waislamu nchini
kama ilivyokusudiwa kwa
Baraza, huku wengi wao
wakitumika zaidi kisiasa kwa
maslahi binafsi huku jamii ya
Waislamu ikihujumiwa.
Waislamu walio wengi
wanaona kwamba iwapo
kweli ahadi alizozitoa Kaimu

AN-NUUR

RAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 26- Julai 2, 2015

Safari ya Hijja Hijiria 1436

Tanzania Muslim Hajj Trust, uandikishaji unaendelea,


gharama za Hijja ni US Dollar 4400, tarehe za Safari ni:
11 na 13 Septemba, kurudi 7 Oktoba, 2015.
Wahi kujiandikisha sasa
Kwa mawasiliano: +255 222 182370
0754 261910; 0717 000065
+255 222181577
0784 272723
0786 383820
website-www.hajjtrust.or.tz
0713 764636

E-mail:info@hajjtrust.or.tz

Sheikh Zubeir aelekea


kuwa Mufti wa Bakwata
Ni iwapo atasimama kwenye ahadi zake

Mkurugenzi Mtendaji Amana Banki , Dk Muhsin Salim Masoud (wa pili kulia)
akikabidhi mfano wa hundi kwa (kutoka kulia) Mkurugenzi wa Redio Sauti ya
Quran, Sheikh Jumaa Bin Hemed, Mwenyekiti wa JUWAKITA-BAKWATA, Shamim
Khan na Katibu wa JUWAKITA-BAKWATA, Mwatum Malale.

Mufti Zubeir, atakula


yaminiya kusitekeleza bila
kujali kupata kipingamizi
cha mamlaka au dola au
wanafiki miongoni mwa
wanaohudumu Bakwata,
basi zitakuwa mtaji tosha
wa Waislamu kumwezesha
kuwa Mufti wa Tanzania.
Itakumbukwa kwamba
udhaifu wa katiba katika
B a r a z a n d i o u l i o k u wa
sababu ya timua teua ya
viongozi mbalimbali wa
BARAZA kutokana na
malamaka makubwa aliyo
nayo Mufti.
Sheikh Khamis Mataka
ambaye ni Mujumbe
katika taasisi ya Baraza la
Ulamaa Tanzania, ni baadhi
ya viongozi waliowahi
k u h u d u m u B A K WATA
wa l i o i n g i a n a h o j a ya
kuleta mabadiliko ya katiba
BAKWATA na kuingiza
mfumo wa kudhibiti mapato
na matumizi, hususan katika
kitengo cha huduma za Hija
ndani ya Baraza.
Hata hivyo kwa msimamo
wao huo, hawakudumu.
Mufti aliwafukuza na kuteua
wengine na hoja na malengo
yao yakafikia mwisho.
Marhum Mufti Sheikh
Issa Shaaban Simba, alikuwa
Mufti wa BAKWATA baada
ya kutumikia nafasi ya
Kaimu Mufti kwa muda
hadi alipochaguliwa baada
ya miezi mitatu.
Sheikh Abubakar Zubeir
kadhalika, naye aliteuliwa
kuwa Kaimu Mufti Juni 22,
2015 huko Bagamoyo.
Nafasi
ambayo
inampa alama nyingi za

Inaendelea Uk. 19

Kithirisheni kufanya Ibada-Sheikh Kichwabuta


Na Abuu Nyamkomogi

WAISLAMU wametakiwa
kujizatiti kufanya ibada
mbalimbali pamoja
kukithirisha utendaji
wa mambo mema katika
kipindi hiki cha mwezi
mtukufu wa Ramadhani.
Wito huo umetolewa
wiki iliyopita katika
Ijumaa ya kwanza ya
mwezi mtukufu wa
Ramadhani na Sheikh
wa m k o a wa K a g e r a
Haruna Kichwabuta
wakati alipokuwa
akiwahutubia mamia
ya Waislamu waliokuwa
wamefurika katika msikiti
wa Bilele, uliopo mtaa wa
Uswahilini kata ya Bilele
katika manispaa ya mji wa
Bukoba.

''Ndugu zangu
Waislamu, tuchakarike
katika kukithirisha
ibada na matendo mema
katika kipindi hiki cha
mwezi mtukufu wa
Ramadhani,'' alisema
Sheikh Kichwabuta.
Akisherehesha kauli
yake hiyo, Sheikh
Kichwabuta aliwaasa
Wa i s l a m u k u o n g e z a
j i t i h a d a n a k u f a n ya
juhudi kadri ya uwezo
wao katika utekelezaji
wa ibada mbalimbali
zikiwemo ibada za swala
tano za faradhi na zile
za sunnah ikiwemo ile
ya tarawehe; usomaji wa
Qur-ani kwa mazingatio;
kuomba msamaha kwa
Allah (s.w.); kuwasaidia
wanajamii wasio na uwezo
pamoja na kusaidiana wao

kwa wao kwa hali na mali


katika msimu huu wa
mavuno na wenye ujira
mkubwa mbele ya Allah
(s.w.).
Kwa upande mwingine,
aliwanasihi Waislamu
wajiepushe na mambo
yanayoweza ama
kupunguza thamani ya
swaumu zao au hata
kuharibu funga kabisa.
"Zihifadhini swaumu
zenu kutokana na vitu
vinavyoweza kuzifisidi.
Jite n g e ni na ur o ng o ,
maneno machafu, ghushi
(udanganyifu), khiyana,
ghiba (utesi) pamoja na
namiima (uchonganishi).
A i d h a ,
aliwatanabahisha
Waislamu hasa vijana

kuwa makini na utumiaji


wa simu zao za mkononi
kwa kuwataka wajiepushe
kutazama picha chafu
na mambo mengine ya
maasia kupitia runinga
za simu zao za mkononi,
mambo
ambayo
yanaweza kuwasababisha
kubatwilika kwa swaumu
zao.
Awali akizungumzia
ubora wa mwezi mtukufu
wa Ramadhani, Sheikh
Kichwabuta aliwaeleza
Wa i s l a m u k w a m b a
mwezi mtukufu wa
Ramadhani ni mwezi
wenye baraka nyingi na
ndimo unamopatikana
usiku wenye hadhi kubwa
sana ambao ujira wa ibada

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na POA Printing Works LTD, S.L.P. 4605, Dar es Salaam.

Вам также может понравиться

  • Dini ya Fedha
    Dini ya Fedha
    От Everand
    Dini ya Fedha
    Оценок пока нет
  • Annuur 1181 PDF
    Annuur 1181 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1181 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Nyuma ya Mapazia
    Nyuma ya Mapazia
    От Everand
    Nyuma ya Mapazia
    Рейтинг: 5 из 5 звезд
    5/5 (1)
  • ANNUUR1004
    ANNUUR1004
    Документ16 страниц
    ANNUUR1004
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • Kufikirika
    Kufikirika
    От Everand
    Kufikirika
    Оценок пока нет
  • Annuur 1064
    Annuur 1064
    Документ12 страниц
    Annuur 1064
    annurtanzania
    Оценок пока нет
  • Hofu
    Hofu
    От Everand
    Hofu
    Рейтинг: 5 из 5 звезд
    5/5 (1)
  • ANNUUR 1169a PDF
    ANNUUR 1169a PDF
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1169a PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Siri ya Kifo
    Siri ya Kifo
    От Everand
    Siri ya Kifo
    Оценок пока нет
  • Annuur 1153 PDF
    Annuur 1153 PDF
    Документ16 страниц
    Annuur 1153 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Afisa Usalama Wa Taifa Ni Mtu Wa Aina Gani? Na Anafanya Nini?
    Afisa Usalama Wa Taifa Ni Mtu Wa Aina Gani? Na Anafanya Nini?
    От Everand
    Afisa Usalama Wa Taifa Ni Mtu Wa Aina Gani? Na Anafanya Nini?
    Рейтинг: 4 из 5 звезд
    4/5 (24)
  • Gazeti La Annur
    Gazeti La Annur
    Документ12 страниц
    Gazeti La Annur
    Hassan Mussa Khamis
    Оценок пока нет
  • HAYAAN, The Long Journey of the Nomad Boy
    HAYAAN, The Long Journey of the Nomad Boy
    От Everand
    HAYAAN, The Long Journey of the Nomad Boy
    Рейтинг: 5 из 5 звезд
    5/5 (2)
  • Annuur 1115
    Annuur 1115
    Документ16 страниц
    Annuur 1115
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Mafundisho ya Ndoa
    Mafundisho ya Ndoa
    От Everand
    Mafundisho ya Ndoa
    Оценок пока нет
  • Annuur 1179 PDF
    Annuur 1179 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1179 PDF
    annurtanzania
    100% (1)
  • Mtambo wa Mauti
    Mtambo wa Mauti
    От Everand
    Mtambo wa Mauti
    Рейтинг: 5 из 5 звезд
    5/5 (1)
  • Annuur 1157 PDF
    Annuur 1157 PDF
    Документ16 страниц
    Annuur 1157 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Mwana-Adam ni Nani Naye ni Nini Mungu Amkomboe: Chuo cha Kwanza, #1
    Mwana-Adam ni Nani Naye ni Nini Mungu Amkomboe: Chuo cha Kwanza, #1
    От Everand
    Mwana-Adam ni Nani Naye ni Nini Mungu Amkomboe: Chuo cha Kwanza, #1
    Оценок пока нет
  • Annuur 1158
    Annuur 1158
    Документ16 страниц
    Annuur 1158
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Fiqhi ya ‘Ibada yenye picha zilizochorwa
    Fiqhi ya ‘Ibada yenye picha zilizochorwa
    От Everand
    Fiqhi ya ‘Ibada yenye picha zilizochorwa
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1175b PDF
    ANNUUR 1175b PDF
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1175b PDF
    annurtanzania
    Оценок пока нет
  • Historia & Maisha ya Yeshua Kristo
    Historia & Maisha ya Yeshua Kristo
    От Everand
    Historia & Maisha ya Yeshua Kristo
    Оценок пока нет
  • Annuur 1056 PDF
    Annuur 1056 PDF
    Документ16 страниц
    Annuur 1056 PDF
    annurtanzania
    Оценок пока нет
  • Miaka Miwili Ya Urais Wa Magufuli: Safari Ya Matumaini Au Nyota Iliyofifia?
    Miaka Miwili Ya Urais Wa Magufuli: Safari Ya Matumaini Au Nyota Iliyofifia?
    От Everand
    Miaka Miwili Ya Urais Wa Magufuli: Safari Ya Matumaini Au Nyota Iliyofifia?
    Рейтинг: 1 из 5 звезд
    1/5 (1)
  • Annuur 1062
    Annuur 1062
    Документ16 страниц
    Annuur 1062
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • Bwana Okoa Ndoa Yangu
    Bwana Okoa Ndoa Yangu
    От Everand
    Bwana Okoa Ndoa Yangu
    Оценок пока нет
  • Annuur 1060
    Annuur 1060
    Документ16 страниц
    Annuur 1060
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • Tutarudi na Roho Zetu?
    Tutarudi na Roho Zetu?
    От Everand
    Tutarudi na Roho Zetu?
    Рейтинг: 5 из 5 звезд
    5/5 (3)
  • Annuur 1082
    Annuur 1082
    Документ16 страниц
    Annuur 1082
    MZALENDO.NET
    100% (1)
  • Nyuma Ya Pazia
    Nyuma Ya Pazia
    От Everand
    Nyuma Ya Pazia
    Оценок пока нет
  • Annuur 1091
    Annuur 1091
    Документ16 страниц
    Annuur 1091
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • Mafundisho ya Utajiri
    Mafundisho ya Utajiri
    От Everand
    Mafundisho ya Utajiri
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1176b PDF
    ANNUUR 1176b PDF
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1176b PDF
    annurtanzania
    Оценок пока нет
  • Ufufuo & Uchukuo
    Ufufuo & Uchukuo
    От Everand
    Ufufuo & Uchukuo
    Оценок пока нет
  • Annur Februari 24-Machi 1, 2012
    Annur Februari 24-Machi 1, 2012
    Документ16 страниц
    Annur Februari 24-Machi 1, 2012
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • An-Nuur 1071
    An-Nuur 1071
    Документ12 страниц
    An-Nuur 1071
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • ANNUUR1003
    ANNUUR1003
    Документ16 страниц
    ANNUUR1003
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • Annur Toleo La Ijumaa
    Annur Toleo La Ijumaa
    Документ16 страниц
    Annur Toleo La Ijumaa
    annurtanzania
    Оценок пока нет
  • Annuur 1061.
    Annuur 1061.
    Документ16 страниц
    Annuur 1061.
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • Annuur 114
    Annuur 114
    Документ12 страниц
    Annuur 114
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • Annuur 1172 PDF
    Annuur 1172 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1172 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1167a PDF
    ANNUUR 1167a PDF
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1167a PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1028
    Annuur 1028
    Документ16 страниц
    Annuur 1028
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • Annuur 1214
    Annuur 1214
    Документ20 страниц
    Annuur 1214
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1065
    Annuur 1065
    Документ12 страниц
    Annuur 1065
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • Annuur 1151
    Annuur 1151
    Документ16 страниц
    Annuur 1151
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1173 PDF
    Annuur 1173 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1173 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1055 PDF
    Annuur 1055 PDF
    Документ16 страниц
    Annuur 1055 PDF
    annurtanzania
    Оценок пока нет
  • Annuur 1078
    Annuur 1078
    Документ12 страниц
    Annuur 1078
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • Annuur 1049
    Annuur 1049
    Документ12 страниц
    Annuur 1049
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • Annuur 1111
    Annuur 1111
    Документ16 страниц
    Annuur 1111
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1036
    Annuur 1036
    Документ16 страниц
    Annuur 1036
    Hassan Mussa Khamis
    Оценок пока нет
  • Annuur 1163 PDF
    Annuur 1163 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1163 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Imaan Newspaper Issue 1
    Imaan Newspaper Issue 1
    Документ19 страниц
    Imaan Newspaper Issue 1
    Imaan Newspaper
    100% (1)
  • Annuur 1031
    Annuur 1031
    Документ16 страниц
    Annuur 1031
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • ISSN 0856 - 3861 Na. 986 DHUL-HAJJ 1432, IJUMAA NOV. 25 - DES. 1, 2011 BEI TShs 500/, Kshs 50
    ISSN 0856 - 3861 Na. 986 DHUL-HAJJ 1432, IJUMAA NOV. 25 - DES. 1, 2011 BEI TShs 500/, Kshs 50
    Документ16 страниц
    ISSN 0856 - 3861 Na. 986 DHUL-HAJJ 1432, IJUMAA NOV. 25 - DES. 1, 2011 BEI TShs 500/, Kshs 50
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • Annuur 1180 PDF
    Annuur 1180 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1180 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1046
    Annuur 1046
    Документ12 страниц
    Annuur 1046
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • Annuur 1143
    Annuur 1143
    Документ16 страниц
    Annuur 1143
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1185
    Annuur 1185
    Документ20 страниц
    Annuur 1185
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1190
    Annuur 1190
    Документ20 страниц
    Annuur 1190
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1193
    Annuur 1193
    Документ20 страниц
    Annuur 1193
    annurtanzania
    Оценок пока нет
  • Annuur 1178
    Annuur 1178
    Документ20 страниц
    Annuur 1178
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1179 PDF
    Annuur 1179 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1179 PDF
    annurtanzania
    100% (1)
  • Annuur 1182
    Annuur 1182
    Документ20 страниц
    Annuur 1182
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1112
    Annuur 1112
    Документ16 страниц
    Annuur 1112
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1180 PDF
    Annuur 1180 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1180 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1173 PDF
    Annuur 1173 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1173 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1107
    Annuur 1107
    Документ16 страниц
    Annuur 1107
    annurtanzania
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1175b PDF
    ANNUUR 1175b PDF
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1175b PDF
    annurtanzania
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1176b PDF
    ANNUUR 1176b PDF
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1176b PDF
    annurtanzania
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1110cc
    ANNUUR 1110cc
    Документ16 страниц
    ANNUUR 1110cc
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1094
    Annuur 1094
    Документ16 страниц
    Annuur 1094
    annurtanzania
    100% (1)
  • Annuur 1102
    Annuur 1102
    Документ12 страниц
    Annuur 1102
    annurtanzania
    Оценок пока нет
  • Annuur 1096
    Annuur 1096
    Документ12 страниц
    Annuur 1096
    annurtanzania
    Оценок пока нет
  • Rasimu Ya Katiba (Toleo La Pili)
    Rasimu Ya Katiba (Toleo La Pili)
    Документ0 страниц
    Rasimu Ya Katiba (Toleo La Pili)
    Muhidin Issa Michuzi
    0% (1)
  • Annuur 1091
    Annuur 1091
    Документ16 страниц
    Annuur 1091
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • Annuur 1105
    Annuur 1105
    Документ12 страниц
    Annuur 1105
    annurtanzania
    Оценок пока нет
  • Annuur 1089
    Annuur 1089
    Документ12 страниц
    Annuur 1089
    Hassan Mussa Khamis
    Оценок пока нет
  • Annuur 1093
    Annuur 1093
    Документ16 страниц
    Annuur 1093
    annurtanzania
    Оценок пока нет
  • Annuur 1088 PDF
    Annuur 1088 PDF
    Документ12 страниц
    Annuur 1088 PDF
    annurtanzania
    Оценок пока нет
  • Annuur 1090
    Annuur 1090
    Документ12 страниц
    Annuur 1090
    annurtanzania
    Оценок пока нет
  • Annuur 1090
    Annuur 1090
    Документ12 страниц
    Annuur 1090
    annurtanzania
    Оценок пока нет