Вы находитесь на странице: 1из 20

www.annuurpapers.co.tz au facebook:annuurpapers@yahoo.

com

AHLU SUNNA WAL JAMAA HAJJ AND UMRA TRUST

Sauti ya Waislamu

(16) TUSHIRIKIANE KUPELEKANA HIJJA!


Wajibu wa kuisimamisha nguzo ya Hijja unatuhusu
mmoja mmoja na sote kwa pamoja. (Aal Imran:97).
Inawezekana, kwa kuchanga, tukapelekana Hijja
mmoja mmoja kila mwaka katika familia, mtaa
au msikiti. Huo ndio Uislamu. Muda unakwisha!
Gharama zote kwa Hijja ni Dola 4,500. Umra ya
Ramadhani ni Dola 2,300. Karibuni Ahlu Sunna wal
Jamaa kwa hudumanzuri na uongozi bora.Wasiliana
nasi: Tanzania Bara: 0765462022; 0782804480;
0717224437. Zanzibar: 0777468018; 0777458075;
ISSN 0856 - 3861 Na. 1185 RAMADHAN 1436, IJUMAA , JULAI 10-16, 2015 BEI TShs 800/=, Kshs 50/= 0777845010.

'Mfungwa' asimulia mateso rumande


Shukrani zikufikie Afande Dada mmoja
Amnusuru mtuhumiwa kuoza mkono
Mtuhumiwa wa ugaidi amsilimisha

Makundi haya mithili ya


Anti-Balaka Vs Seleka
Gifti Kaiya Robert.

SALUM Ali Salum.

Tunataka kuipeleka wapi Zanzibar?


Kampeni bado, watu wanapigwa risasi
Kutakalika au Bububu waanze kuhajiri?

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu.

Mauwaji ya Al-Shabaab tena Kenya


Tujifunze kutoka Shambulio la Kimeta
Akitujia fasiki na habari, tuchunguze
Huu ndio uadilifu na ndio salama ya nchi

Soma Uk. 10-11

Hivi ni Vikosi vya SMZ,


ni Wazanzibari au nani?
Nauliza tu.
Muonekano wao,
wanafanana na Anti-Balaka

na Seleka. Makundi mawili


yaliyoitia Afrika ya Kati
katika mauaji ya kinyama
na kutisha.
Uk. 2

Tahariri/Makala

2
AN-NUUR

S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786


Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM.
www.annuurpapers.co.tz
E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk
Ofisi zetu zipo: Manzese Tip Top
Usangi House, barabara ya Morogoro, D'Salaam

Ramadhani inaondoka
Tukumbuke kutoa Zakatul-Fitri
RAMADHANI inaondoka.
La kukumbushana hapa
ni kuwatunatakiwakutoa
Zakatul Fitri.
Zaka hii hutolewa kabla
ya kusaliwa swala ya Idd na
inamwajibikia kila Muislamu
mwanaume au mwanamke,
kijana, mtoto au mzee..
Zaka ni ile haki
aliyoifaradhisha Mwenyezi
M u n g u k wa M u i s l a m u
katika mali yake anayotakiwa
kuwapa wanaostahiki. Neno
zaka, katika lugha (katika
kamusi ya lugha ya Kiarabu)
maana yake ni Kujitakasa,
kwa sababu anayetoa zaka
anataraji kuitakasa mali yake,
nafsi yake na kupata baraka
kutoka kwa Mola wake.
Mwenyezi Mungu
Anasema: Chukua Sadaka
katika mali zao, uwasafishe na
kuwatakasa kwa ajili ya hizo
(sadaka zao). (Tawba 103).
Kwa hiyo katika zakatul
Fitri, Maulamaa wanatueleza
kuwa lengo lake ni kwa ajili ya
kuitakasa funga ya mfungaji.
Na hutolewa kwa ajili ya
kuwapa wale wasio na uwezo
waweze kusherehekea vizuri
sikukuu ya Idd, kama walivyo
wale wenye uwezo.
Kwa mtumwa (katika zama
za nyuma) au mtumishi, ni
tajiri yake anayewajibika
kumtolea zaka hii.
K i o n g o z i wa f a m i l i a ,
Baba, ndiye anayewajibika
kutoa zakat fitri kwa niaba
ya mkewe, watoto wake,
mtumishi wake na wale
wote walio chini ya ulezi au
uangalizi wake.
Hiyo inatokana na vile
ilivyosimuliwa na Ibn Abbas,
k wa m b a , I n a p o k w i s h a
Ramadhani, toeni sadaka
inayohusiana na funga
zenu. Mtume wa Mwenyezi
Mungu kakokoteza sadaka
hii kuwa ni kibaba kimoja
cha tende kavu au shayiri au
ngano inayotolewa na kila
muungwana au mtumwa,
mwanaume au mwanamke,
kijana au mzee.. kibaba ni
sawa na kilo mbili na nusu.
Na ikumbukwe kwamba
fitri hii hutolewa kabla ya
mtoaji kwenda kuswali,
ili kumpa fursa mpokeaji
kuondoa mawazo ya wapi pa
kupata mlo wa kusherehekea
Idd yeye na familia yake.
Kwa kuwa pesa siku hizi
ndiyo inayokidhi mahitaji

mengi zaidi, kama vile


chakula, mboga, mafuta ya
kupikia, mkaa na hata nguo
za sikukuu za watoto na
mambo mengine, inajuzu
Zakat Fitri kutolewa kwa
pesa tasilimu. Pesa yaweza
kuthaminishwa na bei ya kilo
zilizotajwa lakini ni hiyari ya
mtoaji kuzidisha.
Lengo la kukokoteza zaka
hii ni kuwasaidia wenye
kuhitaji na kuhakikisha
kuwa kila familia inapata
inachohitaji siku ya Idd ili
familia zote ziwe pamoja
katika furaha ya Idd, hii
ikiwa ni ishara ya ushirikiano
na umoja miongoni mwa
Waislamu.
Tukumbushane tu kwamba
kutoa zaka ni nguzo ya tatu
ya Uislamu. Mtume (saw)
amesema:
Nguzo za Uislamu ni
tano. Kutamka shahada kuwa
hapana Mola anayestahiki
kuabudiwa isipokuwa Allah,
na kwamba Muhammad ni
Mtume wa Mwenyezi Mungu
na kusimamisha swala na
kutoa zaka na kufunga mwezi
wa Ramadhan na ya mwisho
ikiwa ni kuhiji Makka kwa
mwenye uwezo wa kufika
huko.
Falsafa ya kutoa zaka ni
kuwasaidia wanaohitajia
msaada kutokana na hali
zao duni. Katika kutoa zaka,
uhusiano mzuri unajengeka
baina ya Waislamu matajiri
na Waislamu masikini. Na
hii ni kwa sababu, siku zote
moyo wa mtu huelekea na
kumpenda yule anayemfanyia
wema na ihsani.
Zaka inasaidia pia katika
kuzisafisha na kuzitakasa
nyoyo. Mwenyezi Mungu
anasema: Chukua sadaka
katika mali zao, uwasafishe na
kuwatakasa kwa ajili ya hizo
(sadaka zao). At Tawba 103.
Katika kutoa zaka au
sadaka kunaizoesha nafsi
kuwapendelea heri watu
wenye haja na katika
kuwaonea huruma na pia
kunaipatia nafsi baraka
nyingi kutoka kwa Mwenyezi
Mungu (sw).
Mwenyezi Mungu
Anasema: Na chochote
m t a k a c h o t o a , b a s i ye ye
atakilipa; naye ni Mbora wa
wanaoruzuku. (Saba-a 39).
Na Mtume (Saw)
amesema:Mwenyezi Mungu

anasema: Ewe mwanadamu,


toa na sisi tutakupa.
Mwenyezi Mungu
amewafaradhishia matajiri
wa Kiislamu katika mali
zao kiasi cha kuwatosha
masikini wao. Na kama
matajiri wakitekeleza wajibu
huu, masikini wasingepata
taabu ya njaa na mavazi. Ila
wajibu huu unawapitia mbali
matajiri wengi kutokana na
ubahili. Hili ni funzo pia
linalopatikana katika kutoa

AN-NUUR

RAMADHAN 1436, IJUMAA JULAI 10-16, 2015


zakatul Fitr.
I t o s h e k wa Wa i s l a m u
kufahamu na kuzingatia kuwa
kutoa zaka yeyote ni ibada.
Na kwa ajili hiyo, kutia nia ni
jambo muhimu kama ilivyo
katika ibada yoyote ile. Nia
ni kitu cha moyoni na hakina
uhusiano na ulimi na kusudi
lake ni kuwa, mtu anapotoa
zaka akusudie kuitoa kwa ajili
ya Mwenyezi Mungu.
Mtume (saw) amesema:
Hakika ya amali yoyote

ni kutokana na nia, na mtu


hulipwa kutokana na nia
yake.
Tu n a w a j i b i k a k u i t o a
z a k a p a l e wa k a t i wa k e
unapowadia, na haijuzu
kuichelewesha isipokuwa
kwa dharura inayokubalika.
Tu n a w a t a k i a h a t m a
njema ya mwezi Mtukufu
wa Ramadhani. Toeni
Zakatul Fitri kwa kiwango
kinachotakiwa, kwa
wakati wake na kuwapa
wanaostahiki.

vitendo hivyo. Haiwezekani


wala haikubaliki.
Lakini wakati huo huo,
anayepanda jukwaani kudai
vitendo hivyo ni haramu
na viovu, ndiye ahojiwe na
ashutumiwe kwa uchochezi
ilhali mfanyaji wa matendo
ya kutisha watu wanaotaka
kupiga kura na kupeleka
watu kwa nguvu katika vituo
wasivyohusika hata haulizwi
kitu!
Wiki kadhaa zilizopita
m wa n z o n i k a b i s a m wa
mfungo, wakati nilipokuwa
Morogoro, jioni moja
nilikwenda kumtembelea
jamaa yangu mmoja wa
Kizanzibari. Nilipofika kwa
bahati mbya alikuwa bado
hajarudi kazini. Nikakutana
na mke wake, akanaikaribisha
na tukazungumza mengi
mno.
Nikamuuliza vipi kuhusu
hali ya mkwe wake, yaani
m a m a wa m u m e wa k e ,
anaishi Bububu Unguja,
mimi nimezoea kumuita Bibi.
Niliuliza hali yake kusudi
kwani umri umemtupa. Ni
Bibi mkongwe. Nilipouliza
nikajibiwa kuwa hajambo
vizuri na alilolisema ni kuwa
anataka kuja Morogoro
kwani Zanzibar hawezi kukaa
hasa kipindi cha uchaguzi.
Nilipouliza anaogopa nini,
nikaelezwa kuwa anaogopa
machafuko yanayotokea
kipindi cha uchaguzi, kwani
uchaguzi wa miaka ile ya
vurugu askari walikwenda
hadi nyumbani kwake
wakitafuta watu ili wawapige.
Hilo ndilo linalomfanya atake
kuondoka Zanzibar kipindi
cha uchaguzi, hataki yamkute
kama yaliyomkuta chaguzi
zilizopita.
Haifurahishi hata kidogo
na inaumiza sana, kuwa
kwetu sisi uchaguzi si jambo
la amani na furaha watu
wa n a f u r a h i a k u m t a f u t a
kiongozi wa nchi yao. Siku
zote imekuwa tafrani, zogo,
kelele, virungu, risasi,
na mambo mengine hata
yasiyosemeka.
Mbona ni tofauti na
we n z e t u ? S e r e k a l i ye t u
haipati funzo lolote ikisikia
nchi fulani imefanya uchaguzi
wa haki salama, hakuna
fujo hakuna mauaji, hakuna
virungu wala Janjaweed?
Kila mtu kaenda katika kituo
cha kupigia kura na kurudi

salama usalimini. Hakuna


hata chembe ya funzo SMZ
inapata?
Bado hatujaingia katika
kampeni, lakini kuna viashiria
vibaya kuwa hali haitakuwa
shwari. Uzoefu wa hali ya
mambo yalivyokuwa huko
nyuma, inaonyesha kabisa
kuwa huenda mambo yakawa
mabaya mwaka huu. Mungu
atulinde.
Inashangaza kuona nchi
imekuwa na makundi ya
watu wenye silaha na magari
kutoka serekalini wakipita
mitaani na nyuso wamefunika,
tena wameshaanza kupiga
na kujeruhi watu, huku
wameshika silaha za kisasa na
kijadi, ni Zanzibar au Congo?
Sura, mavazi yao
hazitofautiani na Seleka, Anti
Balaka wa kule Afrika ya
Kati, na makundi ya waasi
wa Congo ambao wanazitia
nchi zao katika moto kila
siku na mauaji ya kutisha
kisha wanaoumia ni watoto,
wanawake, na wasiojiweza
na hata wanaojiweza. Sisi
tunakuwa na makundi haya
yanayopiga watu mitaani ili
iwe nini? Tunatafuta nini?
Kama hatutaki uchaguzi
isemwe tu, waliopo waendelee
kuliko kuumiza watu ili watu
na chama fulani kiendelee
kuwa madarakani.
Mimi naipenda nchi yangu
sina kumbukumbu nzuri juu
ya kilichotokea nyuma, kwani
mwaka 2001 ndio kwanza
nilikuwa naanza darasa na
kwanza. Lakini ukisoma na
kuwasikiliza watu waliopitia
dhiki ya mwaka huo, utajua
wazi kuwa kuna unyama
mkubwa ulitendeka. Sasa
na hii si dalili njema hata
kidogo. Ni kama tunarudi
kule tulikotoka. Tunarudi
katika hali ambazo watu
wameshaanza kuzisahau.
Lakusikitisha ni kuwa, hata
muda wa kampeni bado,
lakini tayari vikundi vya watu
na nyuso wameficha wanapita
wakipiga na kujeruhi.
Tunaelekea wapi? Kama
mwanzo umekuwa ndio
huu, vipi kuhusu katikati
na mwisho? Tutamaliza
salama kweli? Kwa vijana
hawa walioandaliwa kwa
SMG, mapanga, mikuki, sime,
mindu, magongo na silaha
nyengine, tunataka kuipeleka
wapi Zanzibar?

Makundi haya mithili ya Anti-Balaka Vs Seleka


Na Rashid Abdallah

HIVI ni Vikosi vya SMZ,


ni Wazanzibari au nani?
Nauliza tu.
Muonekano wao,
wanafanana na Anti-Balaka
na Seleka. Makundi mawili
yaliyoitia Afrika ya Kati katika
mauaji ya kinyama na kutisha.
Lakini hawa ni kundi la
watu na wengine huwaita
Janjaweed.
Mara nyingi hujitokeza
wakati Zanzibar inakaribia
uchaguzi na kuanza kufanya
fujo la kupiga, kutesa,
kuharibu mali na hata wakati
mwengine kuua.
Hivi ninavyoandika
m a k a l a h i i , wa p o wa t u
wanauguza majeraha ya
risasi na wengine ya marungu
na magongo. Walipigwa na
watu ambao wamekuwa
wakivamia watu mitaani, na
hasa kulikokuwa na vituo vya
uandikaji wa wapiga kura.
Kwa sababu zisizoeleweka au
wanazozielewa wao wenyewe
na hao waliowatuma, wakifika
hupiga watu, utadhani mtu
anauwa nyoka, kisha hao
wanatokomea.
Watu hawa mithili ya wale
ambao katika chaguzi za huko
nyuma walipachikwa jina la
Janjaweed, itakuwa si sahihi
kusema kuwa haijulikani
wana mkono wa nani. Hawa
ni watu ambao wanabeba
silaha za moto hadharani
na kuzitumia hadharani.
Ufupi wa kiswahili ni kuwa
mamlaka za nchi zinajua ni
nani hawa na kwa nini wapo.
Aliwahi kuandika Ali
Salehe akisema kuwa hataki
awe katika ambao watakuwa
na moyo wa kujidanganya
wakati makundi ya vijana
yakiwa na silaha, yakijiziba
nyuso na huku bila sare
rasmi za Polisi, Jeshi wala
Vikosi vya Zanzibar yakifanya
vitendo visivyokubalika
kidemokrasia na huku
mamlaka zikinyamaza kimya
halafu tuseme, SMZ haijui au
tujidanganye kuwa kutakuwa
na uchaguzi huru na haki.
(Janjaweed hao) wakifanya
hivyo, wakikiuka taratibu zote
za kikatiba na kisheria kwa
ajili ya kujaliza mapandikizi
kwa njia za nguvu katika
Daftari la Kuduma la Wapiga
Kura (DKWK), mamlaka
z i m e n ya m a z a k i m ya n a
kujidai hazijui wala hazioni

Habari

AN-NUUR

RAMADHAN 1436, IJUMAA JULAI 10-16, 2015

'Mfungwa' asimulia mateso rumande


Na Bakari Mwakangwale

MTU mmoja kwa jina la


Gifti Kaiya Robert, ametoa
s h u k r a n i z a d h a t i k wa
wale waliofanikisha kupata
m a t i b a b u ya l i y o n u s u r u
mkono wake kukatwa.
Aidha, shukrani hizo
amezipeleka kwa Masheikh
wa t u h u m i wa wa u g a i d i
walioko Segerea, na hasa
Sheikh Salum Ally, ambaye
alifanikisha kusilimu kwake
na sasa anaitwa Issa.
Kijana Issa (20) anasema,
anahisi ana deni kubwa
kwa askari mmoja wa kike
katika Kituo cha Kawe, kwani
ndiye angalau aliona huruma
akampa huduma ya kwanza
ya kidonda chake ambacho
kilikuwa kina hali mbaya
kiganja cha mkono kikielekea
kuoza.
Akisimulia mkasa huo
baada ya kutoka rumande,
anasema hali hiyo ilitokana
na kuwekwa rumande huku
akiwa na jeraha la ajali ya gari
bila ya matibabu.
Anasema, alikaa
rumande Polisi na jeraha
lake na kusababisha mkono
kuharibika.
Uchungu wa mwana aujua
mzazi, ndipo akatokea askari
mmoja wa kike akanunua
bendeji na spiriti na kumpatia
maji ya moto kwa ajili ya
kujisafisha.
H a l i i l i k u wa m b a ya ,
sikutegemea kama hii leo
kiganja changu kingekuwa
hivi, nilijua nitakatwa, maana
siku hiyo nilipofungua
kusafisha wadudu (funza)
walikuwa wakitoka.
Yule dada (askari)
alipouangalia mkono,
alitokwa na machozi, askari
wengine walienda mbali na
mimi maana nilikuwa natoka
harufu mbaya na kali sana.
Alisema Kaiya.
Awali akisimulia mkasa
uliompeleka rumande,
alisema alikuwa akifanya kazi
tokea mwezi Novemba, 2014,
kwa mama mmoja aliyemtaja
kwa jina moja la Mama Mary
maeneo ya Salala, Tegeta Jijini
Dar es Salaam.
Alisema, baada ya muda
aliomba kuodoka kwenda
kwao Kyela kusalimia wazazi
wake, lakini mwajiri wake
huyo hakuafiki na akaamua
kuondoka kwa nguvu.
Alisema, katika safari yake
hiyo mwezi April 9, 2015,
wakiwa maeneo ya Mikumi,
basi alilopanda lilipata ajali na
kupinduka ambapo walikufa
baadhi ya watu na wengine
kujeruhiwa vibaya akiwemo
yeye aliyepasuka kiganja cha
mkono.
B a a d a ya a j a l i h i y o
nililazwa katika hospitali
ya Mikumi, kwa ajili ya
matibabu, hata hivyo
nililazimika kuwasiliana na
bosi wangu (mama Mery)
kumfahamisha matatizo
n i l i y o ya p a t a n a a l i k u j a

kunichukua, akashauriwa
anipeleke Mwananyamala au
Muhimbili. Alisema Kaiya.
Alisema, katika hali
iliyomshangaza, mwajiri
wake huyo alimfikishia kituo
cha Polisi, Kawe, na kutoa
maelezo kuwa amemwibia
ambapo hata askari
walishangaa kumuona akiwa
na jeraha kubwa mkononi.
Lakini walimuuliza kuwa
huyu kijana ameiba nini,
alishindwa kutoa maelezo
z a i d i ya k u s e m a k u wa
kaniibia nyumbani kwangu,
nilishangaa nikawaeleza
Polisi mimi sijaiba bali ni
mfanyakazi wake nimepata
ajali Mikumi, nilikuwa naenda
nyumbani Kyela labda tatizo
sikumuaga. Alisema Kaiya.
Alisema, pamoja na
maelezo yake, Polisi
walimsikiliza mwajiri wake na
kuamuru awekwe rumande.
Alisema, alikaa hapo Polisi
na jeraha lake na kusababisha
mkono kuharibika, pasi na
bosi wake kutokea na wala
polisi hawakujali kumpeleka
hospitali ilihali walikuwa
wakiona kidonda kikiharibika
siku hadi siku.
Akasema, Mungu ni
Mkubwa, alimpa huruma
askari mmoja wa kike ambaye
alianza kumpa huduma
ya kwanza angalau apate
kukisafisha kidonda.
Alisema, alikaa kituoni
hapo (Polisi) kwa muda wa
siku tano akiwa na jeraha lake
la mkono, pasi na bosi wake
kutokea, hivyo akasema Polisi
walikubaliana apelekwe
gerezani kama mahabusu
kisha apelekwe Mahakamani.
Kaiya alisema, alipelekwa
Segerea, na April 14, 2015
alianza kwenda Mahakama
ya mwanzo Kawe, hata hivyo
bosi wake hakuweza kutokea
Mahakamani, hata siku moja
mpaka pale Mh. Hakimu
Anthony, alipoamua kuifuta
kesi hiyo Mei 27,2015.
Kaiya
anasema,
anawashukuru Waislamu
kuanzia wale waliopo
gerezani Segerea kwa
kumuonyesha njia ya imani
ya kweli lakini pia shukrani
kwa Waislamu kwa ujumla
chini ya Kamati ya Maafa
ya Shura ya Maimamu, kwa
kumsaidia kupata matibabu
hadi kiganja chake, kurudi
katika hali ya kawaida.
KIUKWELI nimejifunza
mengi, kwa jinsi wanavyo
zungumzwa na uhalisia wao ni
vitu viwili tofauti, ukiwa nao
karibu utagundua huruma
na wema wa Waislamu na
Uislamu.
Gifti Kaiya Robart
ameyasema hayo akieleza jinsi
alivyopokewa na Waislamu
gerezani, kupewa maneno
ya faraja, hadi alipoamua
kusilimu.
, aliyekuwa katika gereza la
Segerea, Jijini Dare s Salaam,
ambaye kwa sasa yupo uraiani
chini ya Kamati ya Maafa ya

Shura ya Maimamu baada ya


kutoka akiwa kasilimu Mei
2, 2015.
Kaiya, anaeleza kuwa
baada ya kuanza maisha
mapya Segerea, kwa mara
ya kwanza alipoingia
gerezani humo April 14,
2015, alikutana na Masheikh
na Waislamu ambao awali
alikuwa akisikia taarifa zao
kupitia vyombo vya habari
kuwa wanatuhumiwa kwa
Ugaidi.
Yaani mtu ukiingia humo,
kwanza unakuwa na hofu
kuwa nao kutokana na picha
unayokuwa nayo kichwani
kuwa wao ni Magaidi, lakini
ukiwafuatilia utagundua
wema wa Masheikh hao na
uzuri wa Uislamu. Alisema
Kaiya.
Kaiya ambaye anaongeza
namba ya watuhumiwa na
wafungwa wanaoingia katika
gereza la Segerea wakiwa
Wakristo na kutoka wakiwa
Waislamu, anawataja na
kuwashukuru Abubakar
Mngodo, Said Qassim na
Hassan (Mzungu), ambao
wamefanikisha yeye kuingia
katika dini ya haki (Uislamu).
Yule Ustadhi aliyepanda
juu ya mti (Salum Ally
Salum), ndiye aliyenisilimisha
lakini pia nawashukuru na
kuwakumbuka Abubakar,
Said na Hassan, jina
maarufu Mzungu, ndiyo
walioniwezesha kusilimu.
Alisema Kaiya.
Kaiya, aliyeingia gerezani
humo akiwa na jeraha lake
kubwa mkononi, akitokea
kituo cha Polisi cha Kawe,
Jijini Dar es Salaam, alisema
baada ya kusilimu Waislamu
hao walianza kumfundisha
Uislam na kusoma Qur an.
Wamenifundisha baadhi
ya mambo, lakini pia
wameniusia kuwa baada ya
kusilimu nijifunze na niufate
Uislamu sio watu, sasa mie
nataka niusome Uislamu
ili niufate Uislamu, ndivyo
walivyoniambia Masheish
wa n g u k u l e g e r e z a n i .
Alisema Kaiya.
Alisema, aliingia katika
gereza hilo akiwa mnyonge
na kujikatia tamaa kufuatia

kitendo alichofanyiwa na
bosi wake, mama Mery, lakini
akasema siku chache baada
ya kukutana na Waislamu
gerezani, alijikuta yupo katika
faraja.
Nilipoingia humo
gerezani siku za mwanzo
nikiwa katika hali ya unyonge,
akanijia Sheikh mmoja
anaitwa Salumu, (Salum Ally
Salum) na kuniuliza matatizo
yangu, baada ya kumtajia jina
langu.
A k a a n z a k u n i e l e z a
mambo ya kiimani na
kunifariji, baada ya
kunisikiliza akaniuliza kama
nina ndugu nikamwambia
kwa hapa Jijini sina ndugu.
Wema wao ulinivutia sana
nikasahau tuhuma zao za
ugaidi. Nimejifunza kuwa
ukiwa na imani ya dini, maisha
ya gerezani yanakuwa yenye
faraja na ukitoka unakuwa
ni mtu mwenye utu zaidi.
Alisema Kaiya.
Kaiya aliye mwenyeji wa
Kyela Mkoani Mbeya, alisema
akiwa gerezani sambamba na
watuhumiwa hao wa ugaidi,
walimueleza kuwa akitoka
awasiliane na Kamti ya Maafa
ya Waislamu kwa ajili ya
kupatiwa mafunzo zaidi
ya Uislamu na kutafutiwa
madaktari watakaoweza
kushughulikia jeraha la
kidonda katika kiganja chake.
Alisema, Mei 27, 2015,
aliachiwa huru na Mahakama
ya Mwanzo Kawe, kufuatia
bosi wake aliyemshitaki
kutofika hata siku moja
Mahakamani.
Kamati ilinipokea
na sasa nipo kwa Katibu
Ally Mbaruku, na haraka
walinipekeka hospitali kwa
ajili ya matibabu na baada ya
kupigwa X-ray, ikaonekana
hakukuwa na mawasiliano
kati ya vidole na kiganja.
Alisema Kaiya ambaye hapa
Jijini hana ndugu.
Kwa upande wake Katibu
Ally Mbaruku, alisema
wamempokea kijana huyo
kutoka mikononi mwa
M a s h e i k h n a Wa i s l a m u
walioko gerezani.
Katibu Mbaruku amesema,
katika mahitaji yake tayari

mambo mawili yamesha


fanyika ikiwa ni matibabu ya
kiganja cha mkono ambapo
hivi sasa vidole vimerudisha
mawasiliano yaliyopotea
baina ya vidole na kiganja na
la pili ni Tohara.
Akasema, hatua inayofuata
kwa sasa kwa Kaiya (Issa)
ni kupelekwa chuoni
k u j i f u n z a U i s l a m u k wa
ujumla na kwamba tayari
chuo kimeshapatika Visiwani
Zanzibar na ataungana na
mmoja kati ya waliosilimu
(Nassoro), akiwa gerezani
Segerea.
Ataungana na mwenzie
aliyesilimu gerezani
(Nassoro) kwenda Zanzibar,
k a t i k a m a s o m o ya d i n i
mara baada ya mfungo wa
Ramadhani, ila misaada zaidi
kwa ajili ya ndugu zetu hawa
wakiwa masomoni inahitajika
kwani ndugu zao ni sisi na
si vinginevyo. Alisema Ust.
Mbaruku.
Watu waliosikiliza kisa
hiki cha Robert wamekuwa
wakihoji, inakuwaje polisi
wetu kuwa na roho ngumu
au hiyo ndio kuonyesha kuwa
wanafuata na kutekeleza
sheria.
Mtu mmemuona
ana jeraha kubwa la ajali,
kesi yenyewe wala hata
haieleweki, kwa nini wasimpe
dhamana akajitibie kama
wao hawawezi kumpeleka
hospitali?
Alihoji muumini mmoja
baada ya kusikiliza kisa cha
Robert kuachwa siku kadhaa
akiwa mikononi mwa polisi
na jera lake la ajali bila ya
matibabu.
Hata kama ni kutekeleza
sheria kuwa wasimwachie
mtuhumiwa, lakini hawana
ubinadamu? Kwani sheria
ni kwa ajili ya nani? Sio
watu? Sasa kama kutekeleza
sheria kwenyewe itakuwa ni
kuangamiza maisha ya watu,
nini maana ya sheria hiyo.
Aliongeza muumini huyo
aliyejitaja kwa jina moja la
Shakir akisisitiza kuwa polisi
hawawezi kutoka katika
lawama kufuatia kitendo
hicho.

Na Mwandishi Wetu

Mhe. Maalim Seif Sharif


Hamad.
Sheikh Alawy ambaye
amezikwa hapo hapo Ole
Kanambe, alifariki jumamosi
usiku akiwa na umri wa
miaka 81 baada ya kuugua
kwa muda mrefu.
Mmoja kati ya watoto
wa marehemu Sheikh
Alawy, Sheikh Mussa bin
Alawy amesema, mbali na
marehemu huyo kuwa na
darsa kubwa kutoka maeneo
jirani, wanadarsa wengine
walikuwa wakitoka maeneo

ya mbali kisiwani Pemba


yakiwemo Tumbe, Fundo,
Kengeja na Mkoani kufuatilia
darsa zake.
Sheikh Alawy aliyezaliwa
mwaka 1934 akiwa Sheikh
maarufu katika eneo la Ole
Kanambe kisiwani Pemba
na Zanzibar kwa ujumla,
ameacha kizuka mmoja na
watoto 12.
Mwenyezi Mungu ailaze
roho yake mahala Pema
Peponi (Ammiin)

Sheikh maarufu afariki Pemba


SHEIKH maarufu wa
Ole Kanambe, Pemba na
Z a n z i b a r k wa u j u m l a ,
Sheikh Alawy bin Omar bin
Salim Baalawy, amefariki
dunia na kuzikwa Jumapili
wiki iliyopita.
M a z i s h i
y a k e
yalihudhuriwa na maelfu ya
Waislamu kutoka maeneo
mbali mbali kisiwani Pemba
wakiongozwa na Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar

4
Na Azza Ally Ahmed
MAKAMU wa Rais ya
Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Dk. Ghalib
Bilali, ameishukuru
taasisi ya Istiqama kwa
kufanya dua maalumu
ndani ya mwezi mtukufu
wa Ramadhani kuliombea
Taifa amani.
Dk. Bilali ametoa
shukrani hizo alipokuwa
akiongea na Waislamu
katika sherehe ya
kuwapongeza washindi wa
mashindano ya kuhifadhi
Quran zilizofanyika katika
ukumbi wa Istiqama, Ilala
jijini Dar es Salaam hivi
karibuni.
Dk. Bilali alisema
kuwa lazima Watanzania
wafahamu kuwa
wamezungukwa na nchi
nyingi jirani, ambazo
sehemu kubwa ya nchi
hizo wamepatwa na
misukosuko mikubwa ya
ukosefu wa amani, hivyo
akasisitiza umuhimu wa
kuitunza amani ya nchi.
Nawashukuru
Watanzania kwa kuitunza
amani ya nchi yao na
kuendelea kuidumisha,
kwani kufanya hivyo
ni kuthamini amani
tuliojaaliwa na Mungu,
takriban miaka 50
sasa tumeishi katika
amani Alhamdulillah
hatujapata matatizo
yanayosababishwa na
ukosefu wa amani,
hatujapata matatizo ya
kutibua nchi yetu, zaidi
pamekuwa kimbilio la
nchi za jirani. Alifafanua
Dk. Bilali.
Aidha Makamu huyo
wa R a i s a l i i p o n g e z a
Istiqama kwa kazi
k u b wa wa n a y o i f a n ya
ya kuwaandaa vijana
wa taifa la kesho, vijana
watakaokuwa wanaijua
dini na dunia yao na pia
kuwa na maadili mema
hivyo kuisaidia jamii
nzima.
Kwa upande wa
Waziri wa Ulinzi Mhe.
Hussein Mwinyi, ambaye
naye alihudhuria katika
m a s h i n d a n o h a y o ya
Quran, aliwashukuru
Jumuiya ya Istiqama kwa
kazi wanayoifanya ya
kuwafunza vijana kitabu
kitakatifu cha Mwenyezi
Mungu.
Alisema dunia
tuliyonayo hivi sasa,
wazazi wengi wamekuwa
wakishughulishwa zaidi
na shughuli za kidunia
na kupoteza fursa ya
kuwasimamia watoto wao.
Hivyo aliipongeza
Jumuiya ya Istiqama kwa

Makala

AN-NUUR

RAMADHAN 1436, IJUMAA JULAI 10-16, 2015

Dk. Bilali ashukuru Waislamu


kwa kuombea Taifa amani
Mwinyi awashutua wanaopalilia farka

kuchukua jukumu hilo la


kuwasimamia watoto na
kuelimisha juu ya dini yao.
Alisema
kama
taasisi kama Istiqama
zisingekuwepo, ni wazi
kuwa sehemu kubwa ya
vijana ingekuwa katika
wakati mgumu kimaadili,
kwa kuwa wazazi wengi
hawana muda wa kuwalea
na kuwafunza watoto
wao masuala ya imani na
maadili.
Naye
Makamu
Mwenyekiti wa Istiqama,
Sheikh Nassoro Ally,
alimshukuru Dk. Ghalib
Bilal na Mhe. Hussein
Mwinyi kwa kuwa bega
kwa bega na taasisi hiyo
k i l a wa n a p o k u wa n a
shughuli za kidini.
Aidha aliwashukuru
waumini
wote
waliohudhuria katika
hafla hiyo kwa kuwa
pamoja nao.
K a t i k a ma sh i n da n o
hayo mshindi wa kwanza
wa Juzuu 30 alikuwa ni
Said Nassor Said ambaye
a l i z a wa d i wa S h i l i n g i
milioni tatu kutoka Benki
ya Kiislamu ya Amana.
Mashindano mengine
ya Quran yaliandaliwa
na taasisi ya al Hikma
Education Centre chini ya
Mwenyekiti Sheikh Nurdin
Kishki na kufanyika katika
uwanja wa Taifa jijini Dar

es Salaam mwishoni mwa


wiki.
K a t i k a ma sh i n da n o
hayo ya 16 ya Afrika
Mashariki, mshindi wa
k wa n z a wa J u z u u 3 0
alikuwa ni Mohammed
Moge Aden (20) kutoka
Kenya, ambaye alizawadia
gari aina ya Toyota Noah.
H a ta h iv y o , k u bwa
lililowagusa Waislamu
waliohudhuria katika
mashindano hayo ni
tahadhari aliyoitoa mgeni
rasmi katika mashindano
hayo Alhaj Ali Hassan
Mwinyi.
Mzee mwinyi alitumia
fursa hiyo kuwaasa
Waislamu kuwa makini
na kuchukua tahadhari
kutokana na kukithiri
mgawanyiko
na
kuhasimiana Waislamu
kwa kigezo cha tofauti za
mitazamo na misimamo
miongoni mwao.
Ndugu zangu
Waislamu, tuna mtihani
mkubwa, na hili
l i n a t u f a n ya t u w e n a
wajibu na kazi kubwa ya
kufanya. Moja ya kazi hizo
ni kushirikiana na kuwa
wamoja. Leo dunia kama
tunavyoiona inatumbukia
katika mtihani mkubwa
kwa
Waislamu
kutofautiana. Hivi leo
Wa i s l a m u wa n a wa u a
Waislamu wenzao kama

kule Nigeria, kuna haja


kubwa ya kutumia
akili zetu na miili yetu
kuepuka mtihani huu.

Mzee Mwinyi aliwaasa


Waislamu.
K wa u p a n d e wa k e
Sheikh Nurdin Kishki,
alisema kuwa mashindano
hayo yameonyesha uwezo
mkubwa walio nao vijana
wa Kiislamu katika
kuihifadhi na kuisoma
Quran.
Sheikh Kishki alisema
malengo makuu ya
kuandaa mashindanio
hayo ni kuwasaida watoto
na vijana wa kitanzania,
kuwatoa katika hatua moja
na kuwapeleka katika
hatua nyingine.
Vijana
wetu
wanaweza, wana uwezo
wa k u s o m a t u m e o n a
vijana wamehifadhi
juzuu 30, msahafu mzima.
Hii inaonyesha kuwa
vijana wakiwezeshwa
wanaweza. Alibainisha
Sheikh Kishki.
Sheikh huyo alisema
vijana hao wakifuatiliwa
na wakatunzwa, baadae
wanaweza kuwa viongozi
wazuri sana kwa Taifa hili.
Aidha alitoa wito
k wa wa z a z i k u wa p a
kipaumbele viaja wao
kwa kuwatimizia yale ya
wajibu kwao.
Alisema wazazi
wengi wamejisahau na
wameacha kuwekeza kwa
vijana ambao ndio taifa la
baadae.

Nafasi za masomo ya kozi ya ualimu

Coast Teachers Training Collage (CTTC)


kina watangazia kozi ya ualimu ifuatayo:
Diploma ya ualimu wa shule ya msingi
kwa mwaka 2015/2016.
Kozi ya miaka mitatu (3) kwa waliomaliza
kidato cha nne.
Kozi ya miaka miwili (2) kwa mwenye
cheti cha ualimu daraja la III A
Sifa za kujiunga na kozi hii.
(i) Aliyemaliza kidato cha Nne (4) awe
na ufaulu wa daraja la III, au
(ii) GPA 1.6 kwa wale waliomaliza
mwaka 2014, au
(iii) Cheti cha ualimu daraja la III A.
Tembelea website ya NACTE:
www.nacte.go.tz, au piga simu namba:
0655573011/0789887799/0762904904.
Usajili No. Reg/tlf/093
Pia tunatoa kozi ya ualimu wa chekechea.
Masomo ya chekechea, msingi (English
Medium), Sekondari wa Sichana na
Wavulana. Chuo kipo Kibaha Mpakani.
Nafasi ya kutwa na bweni.

5
Na Shaban Rajab
HIVI karibu tumeshuhudia
habari kwamba Taifa la
Marekani limeridhia
kuanza kutumika sheria
inayoruhusu ndoa za
j i n s i a m o j a , b a a d a ya
Mahakama Kuu ya nchi
hiyo kuhalalisha ndoa hizo.
"Today is a big step in our
march toward equality. Gay
and lesbian couples now have
the right to marry, just like
anyone else".
Alinukuliwa akisema Rais
Barack Obama baada ya
kupitishwa sheria hiyo.
Hii ina mana kwamba
kuanzia sasa, sheria ya ndoa
ya Marekani inamruhusu
mwaume kumposa
mwanaume mwezake,
au mwanamke kumposa
m wa n a m k e m we n z a k e .
Kwa Marekani sasa hivi
hilo ni jambo la kawaida,
sahihi, halali na la heshima
kama ambavyo mwanamme
anavyomposa mwanamke.
N d i o m a a n a b a a d a ya
Marekani kutangaza rasmi
kuridhia sheria hiyo ya
ushoga na usagaji, Rais Robert
M u g a b e wa Z i m b a b we
alimkejeli Rais Barack
Obama, pale aliponukuliwa
akisema kuwa yuko mbioni
kumtumia posa Rais Obama
siku za hivi karibuni. Bila
shaka Mugabe alikusudia
kuueleza ulimwengu
kuwa hata akitokea mtu
akimtumia mwanaume posa,
iweni mtu zima au kiongozi,
si kosa wala kukosa adabu
au kumvunjia mtu heshima,
kwasababu katika nchi
zinazoruhusu ndoa za
kishoga na kisagaji sheria
inaruhusu hayo. Kwa maana
nyingine ni kwamba, Mugabe
kumposa Obama kwa sheria
ya ndoa ya Marekani, sio
tusi wala kumkosea Rais
huyo heshma. Bali ndiyo
demokrasia na haki za
b i n a d a m u wa n a y o t a k a
Wamarekani.
Nchini Marekani hivi sasa,
katika familia ya baba na
mama na watoto mabinti
kwa wavulana, inapokuja
posa kwa ajili ya wanandugu
au familia kubainisha na
kuijadili, wakati dhana
ya kawaida iliyozoeleka
ni kwamba posa ni kwa
mabinti, haitakuwa jambo
la ajabu tena kwa baba
kufungua posa mbele ya
familia na kukuta kumbe
kaposwa yeye baba.
Awali sheria zinazoruhusu
ushoga na usagaji
n c h i n i h u m o , z i l i k u wa
zinatofautiana kati ya jimbo
na jimbo. Yaani baadhi ya
majimbo yalisharidhia ndoa
hizi lakini mengine yalizuia
uchafu huo. Lakini sasa nchi
nzima watu wanaruhusiwa
kufunga ndoa za jinsia moja
wakipenda. Lakini jambo
jingine ambalo litakuwa ni
la dhahiri nchini Marekani,
kwa namna moja au nyingine
Kanisa litaathirika sana na
sheria hii. Tunafahamu kuwa
tangu awali kabla ya sheria
hii kupitishwa, katika baadhi
ya majimbo ya Marekani
ndoa za jinsia moja zilikuwa
zinafungwa katika baadhi
ya Makanisa. Pamoja na
kuendelea kufungwa ndoa
hizo makanisani, hakukuwa
na nguvu yeyote ya waumini
au ya kikanisa ambayo
ilionekana kupinga vikali na
kuzuia kitendo hiki. Kanisa

Habari za Kimataifa

AN-NUUR

RAMADHAN 1436, IJUMAA JULAI 10-16, 2015

Laana yenu huko huko

Mugabe amwambia Obama asubiri kuposwa


Ni baada ya kuhalalishwa ndoa za mashoga
Kanisa hatarini kuporomka Ulaya, Marekani

ASKOFU wa Toronto , Brent Hawkes, akifungisha ndoa ya mashoga katika kanisa


la Toronto's Metropolitan Community mwaka 2001.
Katoliki ambalo ndilo Kanisa
Kubwa zaidi duniani, kwa
namna moja au nyingine
lilionekana kutokukubaliana
na ndoa za namna hii. Lakini
kwa bahati mbaya, watumishi
wake wengi ndio wamekuwa
vinara wa vitendo hivi vya
ushoga na ulawiti wa watoto
nk. Ilifika wakati hata Umoja
wa Mataifa kulishutumu
Kanisa hilo kwa kushindwa
kuwachukulia hatua
watumishi wake hao, japo
Kanisa lina kila kithibitisho
cha watumishi husika
kujihusiaha na vitendo hivyo.
Lawama hii ya UN ilileta
mvutano mkubwa kati ya
Kanisa na UN, Kanisa likidai
kuwa UN inalidhalilisha
Kanisa hilo licha ya kanisa
lenyewe kutoa ushirikiano
juu ya kadhia hiyo.
K wa j i n s i n d o a h i z i
zinavyochukuliwa na
baadhi ya makanisa, ni wazi
kwamba kwa nchi kama
Marekani, ambako tayari
sheria imesharuhusu na
kuna shinikizo kubwa la
wanaharakati na mashoga
wenywewe, ndoa za jinsia
moja zitakuwa zinafungwa
makanisani na litakuwa ni
jambo la kawaida katika
taasisi hizo za kidini. Aidha,
ni wazi kwamba ndoa za
k i s h o g a s a s a z i t a k u wa
z i k i f u n g wa n a s e r i k a l i
iwapo wanaofunga ndoa
hiyo watataka hivyo. Sheria
iliyoruhusu ndoa za kishoga
ni ya serikali, basi lazima pia
serikali ihusike kufunga ndoa
hizo kwa watu wake.
Kwa upande wa Uislamu,
haidhaniwi kwamba
utatokea Msikiti, Imamu au
Sheikh akahusika na kufunga
ndoa hizi chafu. Hili lipo
wazi kwa kuwa Uislamu

na Waislamu ulimwenguni
pote, wanatambua na
wanatambuliwa kuwa tendo
hilo kwao ni haramu kubwa.
Hakuna dhehebu, Sheikh,
I m a m wa l a U l a m a a wa
Kiislamu aliyewahi kujaribu
kufanya hilo.
Hata hivyo, hatari
iliyopo ni kwamba, iwapo
atatokea shoga au msagaji
anayejinasibisha na Uislamu
akataka kuhalalisha uchafu
wake na mwenziwe, basi
huyo itamlazimu aritadi
akafunge ndoa ya Kanisa au
ya serikali.
Tu n a k u m b u k a P a p a
Francis alipokuwa akijibu
maswali ya wanahabari
wakati akirejea kutoka Brazil.
Ilikuwa ni siku moja mara
baada ya kurejea kutoka
katika kuadhimisha siku
ya vijana duniani, tamasha
la asili ya Kanisa katoliki
ambalo lilifanyika mwaka
2013 nchini Brazil. Mara
baada ya kurejea Ulaya, Papa
Francis alizungumza na
waandishi wa habari katika
mkutano na kunukuliwa
akizungumzia kuhusu
watumishi mashoga. Katika
mkutano na waandishi wa
habari ambao ulichukua
takriban dakika 82 wakiwa
angani, Papa Francis alisema
kuwa hana shida na mtu
ambaye ni shoga na ambaye
anamtumikia Mungu
kikamilifu.
"If someone is gay and he
searches for the Lord and has
good will, who am I to judge?
We shouldn't marginalize people
for this. They must be integrated
into society." Alinukuliwa
akisema Papa Francis.
Yaani anasema, "Kama
mtu ni shoga na anamtafuta
Bwana na ana nia njema, mimi

ni nani hata nihukumu?"


Papa Francis anasema na
kuongeza, "Hatupaswi
kutenga watu kutokana na
hili suala. Inabidi wakubalike
na kuchukuliwa ndani ya
jamii."
Kauli ya Papa Francis
inaonekana kukinzana na
ile ya mtangulizi wake,
Papa Benedick XVI,
ambaye mnamo mwaka
2005 , alisaini waraka wa
kueleza kuwa wanaume
wanaojihusisha na masuala
ya ushoga, hawatakiwi kuwa
makuhani. Kwa mtazamo
wa Papa Francis, ni kwamba
watumishi mashoga
wasamehewe na dhambi
zao zisahauliwe. Hata hivyo
licha ya mtazamo huo wa
Papa, bado sera ya Kanisa
katoliki hairuhusu masuala
kama hayo, ila kutokana na
kauli ya kiongozi huyo Mkuu
wa Kanisa Katoliki, huenda
k u k a wa n a m a b a d i l i k o
kwenye mtazamo wa Kanisa
kuhusu jambo hilo.
C h a m a k i k u b wa c h a
kupigania haki za mashoga
nchini Marekani, Human
Rights Campaign walionekana kufurahishwa
na kauli ya Papa.
Rais wa chama hicho
Chad Griffin, alisema kwa
miaka kadhaa sasa walikuwa
wakiwaona mashoga na
wasagaji wanaotokea Vatican
wakikandamizwa, lakini
kauli ya Papa angalau inaleta
matumaini.
A i d h a Pa p a F r a n c i s
alizungumzia kuhusu
wanawake kuwa na jukumu
zaidi katika Kanisa, lakini
alisisitiza kuwa bado
hawawezi kuwa wachungaji
au makuhani.
Katika Uislamu, tunaamini

kuwa Mwenyezi Mungu


kamuumba binadamu mume
na mke ili wamwabudu.
Hata hivyo, ili wapatikane
hao wanaadamu wa
kumwabudu Mola wao,
lazima yawepo maisha na
uzazi. Ndipo Mwenyezi
M u n g u a k a s e m a k u wa
amemuumba mwanadamu
Mume na mke ili wakaijaze
dunia. Kimantiki na hata
kibaiolojia, Mwenyezi Mungu
kamuumba mwanadamu
mwanamke na mwanamme
ili upatikane uzao kati yao.
Na uzao ni lazima uwepo
muuganiko wa mbegu za
uzazi za kike na kiume. Hapo
itapatikana familia, jamii na
mataifa kwa ujumla. Lakini
pia mke na mume huleta
muungano na umoja katika
kijamii. Na zaidi, mume na
mke hupata utulivu wa nafsi
na faraja. Haya yote hayawezi
kupatikana kwa kuingia
katika tamaa za kimwili na za
uasi kwa Mwenyezi Mungu,
kwa kukosoa utaratibu sahihi
wa mahusiano ya mume na
mke aliouweka Muumba.
Kuna shinikizo la nchi
hizi za kishoga za Ulaya
na Marekani kuzibana
nchi za Kiafrika kuzitaka
kuingia katika mkumbo
huu wa kikhabithi. Hoja
kubwa ya kuzibana nchi
za Kiafrika ni kupitia kile
kinachoitwa misaada
ya kifedha na kiuchumi
kutoka serikali hizo. Hata
hivyo, baadhi ya viongozi
wa Kiafrika wamesimama
kidete na kupinga hadharani,
bila woga upumbavu huu.
Lakini pia wapo viongiozi
wachache wa Kiafrika kwa
u d h a i f u n a w o g a wa o ,
wamezitumbukiza nchi zao
katika uozo huo na kuridhia
sheria chafu kwa watu wao.
Nchini Msumbiji tangu
mwaka 1,886 ilikuwa ni
marufuku kujihusisha na
uhusiano wa jinsia moja.
Lakini June 29, 2015 Msumbiji
ilitangaza kuhalalisha na
kukubali kuzitambua ndoa
za jinsia moja. Rais wa
zamani Armando Guebuza,
aliweka saini sheria inayotoa
kibali cha liwati nchini
h u m o D e s e m b a m wa k a
jana. Hawakuishia hapo,
lakini pia serikali ilihalalisha
wanawake kutoa ujauzito.
Hata hivyo pamoja
na kwamba mataifa
makubwa yameonyesha
k i l e wa o wa n a c h o k i i t a
kuwa ni demokrasia,
huku zikizishawishi nchi
nyingine hasa hizi changa
za Kiafrika kutunga sheria
zinazohalalisha ndoa za jinsia
moja, bado kuna nchi ambazo
zimeonyesha misimamo
ya dhahiri na ya wazi ya
kupinga ushenzi huo. Nchi
hizo watu wao na serikali
zao hawataki kabisa kusikia
biashara ya kuhalalisha ndoa
hizo. Zimbabwe, Gambia,
Nigeria, Uganda, Mauritania,
Sudan ni baadhi tu ya nchi
ambazo zimetangaza wazi
kuwa hazitaki mchezo katika
uchafu huu.
Kwa muda mrefu sasa,
Rais Robert Mugabe wa
Zimbabwe, ndiye ambaye
amekuwa kinara wa
kudhihirisha wazi kupinga
k wa k e u p u m b a v u h u o
hadharani na kwa nguvu
zake zote. Kwa mfano tangu
miaka ya 1990, aliweka
msimamo wa nchi yake wazi
Inaendelea Uk. 19

Makala/Tangazo

AN-NUUR

RAMADHAN 1436, IJUMAA JULAI 10-16, 2015

Mafundisho ya Quran: Al Baqara 65

Fethullah-Gulen
KWA hakika mliwajuwa
wale ambao walivuka
mpaka katika nyinyi
katika siku ya Jumamosi,
tukawaambia kuweni
manyani hali ya kuwa
wadhalili. [Al-Baqarah
65]
Ugeuzwaji ambao
umekuja katika aya hii
t u k u f u n a M we n ye z i
Mungu ndiye mjuzi sana
ugeuzwaji huo ni kama
alivyosema Mujahidi, ni

ugeuzwaji katika tabia na


mwenendo zaidi kuliko
kuwa ni ugeuzwaji wa sura
maana walipambazukiwa
kwa tabia na mienendo na
ndani ni kama manyani.
Na ugeuzwaji wa kitabia
unafungua mlango wa
kuhama huu ugeuzwaji,
kwenda kwa vizazi vingi
sana. Na kunawezekana
kushuhudia huu
ugeuzwaji wa tabia katika
baadhi ya jamii za wakati
huu.
Na kama ambavyo
linawezekana kuwa
t a m k o A - S s a b t i Jumamosi kwa maana
ya siku inayojulikana
katika wiki, vivyo hivyo
kunawezekana likawa
tamko hilo limepasuka
kutoka katika chanzo
cha siku ya mapumziko
a m b a y o wa n a i t u k u z a
Mayahudi, na ambayo
wanaitumia katika
kufanya ibada. Na tafsiri
ya mwisho ndiyo yenye
nguvu sana.

Kwa msingi huo, kwa


hakika maana ya aya,
kufuatana na tafsiri ya
mwisho ni haya:
Hakika hawa Mayahudi
a m b a o wa l i b e b e s h wa
jukumu jepesi na dogo,
nalo ni kuichagua siku
m o j a t u k wa a j i l i ya
kumwabudu Mwenyezi
M u n g u , wa l i l i k i m b i a

jukumu hilo na wakaivunja


ahadi ambayo waliikataa
juu ya nafsi zao mbele za
Muumba wao. Ahadi hii
ambayo ilikuwa ni jambo
la kawaida kwa sababu
ya kuumbwa kwao hali
ya kuwa ni binadamu,
na ni jambo la lazima
kwa sababu ya kuwa
kwao ni watu ambao

wamechaguliwa kutoka
kwa Mwenyezi Mungu.
Na wao kwa sababu ya
kutenda kwao mfano
wa kosa na madhambi
haya, wameporomoka
mpaka wamekuwa chini
katika walio chini katika
hadhi ya binadamu. Na
wamekanusha fadhila
ya kuchaguliwa kwao
juu ya watu na juu ya
mataifa mengine.
Akaubadilisha Mwenyezi
Mungu ubinadamu wao
na hisia zao na fikra
zao. Na amewabadilisha
nafsi zao za manyani
katika kufikri na hekma
ya maisha yakaonekana
yote hayo juu ya sura ya
nje. Wakaonekana katika
hali ambayo wakiwa na
unyonge mkubwa sana.
(Imenukuliwa kutoka
Kitabu: Miyangaza ya
Quran katika mbingu ya
hisia, cha Muhammad
Fethullah Gullen
kilichotafsiriwa kwa
K i s wa h i l i n a S h e i k h
Suleiman Amran Kilemile)

KIRINJIKO ISLAMIC ENGLISH MEDIUM PRIMARY SCHOOL


P.O. Box 62, SAME Tel: 027 2758180, 0784 296424 TANZANIA

OMBI LA UJENZI WA MSIKITI

Na simamisheni Sala na toeni Zaka; na kheri mtakazozitanguliza, kwa ajili ya Nafsi zenu, mtazikuta kwa Mwenyezi Mungu.
Hakika Mwenyezi Mungu anayaona (yote) mnayoyafanya.
Kwa muda mrefu sasa watoto wa Shule ya Msingi ya Kiislamu, Kirinjiko, wamekuwa wakiswali katika msikiti wa
jirani zao Kirinjiko Islamic Secondary School kwa swala za Ijumaa. Ama kwa swala tano za kila siku, wamekuwa
wakiswali katika jengo la maktaba.
Kutokana na kukuwa shule na kuhitajika jengo hilo kwa shughuli tu
za kimaktaba pekee, Shule sasa inahitaji kuwa na Msikiti wake. Zaidi
ni kwamba, hata katika swala za Ijumaa, inawabidi watoto kutembea
masafa kiasi kufika msikiti wa sekondari.
Ni kwa sababu hiyo, uongozi wa Shule ya msingi ya Kiislamu Kirinjiko
unawaomba Waislamu kutoa sadaka zao kufanikisha ujenzi wa Msikiti
huo.
Kwa wale ambao watapenda kuwasilisha sadaka zao kupitia Benk,
akaunti ya shule ni Kirinjiko Islamic English Medium Primary School
ac. No 40510004846 (NMB Bank) au 005120109700001 (Amana Bank).
Pay in Slip ikionesha kuwa ni mchango kwa ajili ya msikiti, itumwe
kwa Mwalimu Mkuu SLB 62 SAME.
Kwa mawasiliano zaidi, tumia simu namba 0655 697 075, 0767 697
075 na 0758 989 477.

Jengo la utawala la Shule ya msingi ya


Kiislamu Kirinjiko

7
Na Juma Jumanne

KUJITAMBUA
ni kiini na msingi
wa mafanikio
yoyote katika kila
n u k t a ya m a i s h a
ya mwanadamu.
Kufanikiwa kwa
maana ya kufanikiwa
unakokufahamu
wewe, kunatokana
na kujitambua
katika eneo husika.
Bila kujali kama ni
taasisi, makampuni,
mashirika na au
mtu binafsi, suala
la kujitambua
limekuwa mchango
mkubwa sana katika
kuleta mabadiliko
chanya. Mathalani,
kiongozi wa nchi
anapojitambua
anakuwa ni chachu
ya kupeleka mbele
maendeleo ya nchi
yake katika nyanja
zote za kimaendeleo.
Pengine mtu
anaweza kuhoji
kwamba, kwani
k u j i t a m b u a
kunasaidiaje mambo
yote haya? Na
kujitambua maana
yake nini?
A m a i l i k u we z a
kumfahamu mtu
anayejitambua
nimejaribu kudondoa
sifa za watu wenye
kujitambua ambazo
ni pamoja na: Mwenye
kujitambua anakuwa
hadhiri muda wote
katika kutekeleza
wajibu na majukumu
yake ya kila siku.
Mwenye kujitambua
anafahamu vema
nafasi yake yeye
binafsi bila kujali wingi
wa wenye majukumu
yanayofanana na
yake. Hili huepusha
kutegeana na hivyo
kupelekea kufanya
kazi kwa ufanisi zaidi.
Mtu anayejitambua
h a n a k a wa i d a ya
kulalamika kutokana
na matokeo, bali yeye
hutafuta suluhisho
sahihi na kuliingiza
katika utendaji.
Mwenye kujitambua
anatumia vema muda
wake katika shughuli
zenye manufaa.
Huwezi kumkuta mtu
wa aina hii akipiga
porojo vijiweni, bali
akichoka hupumzisha

Makala

AN-NUUR

RAMADHAN 1436, IJUMAA JULAI 10-16, 2015

Kujitambua-1

Mohammed Moge Aden (20) kutoka Kenya mshindi wa kwanza wa shindano


la kuhifadhi Qur'an Juzuu 30 lililoandaliwa na Taasisi ya Al-Hikma na
alizawadiwa gari aina ya Toyota Noah. Mashindano hayo ya Afrika Mashariki
yalifanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam wiki iliyopita.

akili yake ili kukipa


ki ch wa u we z o wa
kufikiria zaidi.
Mwenye kujitambua
h u f a n ya m a a m u z i
sahihi bila kutegemea
msemo wa waswahili
k w a m b a , We n g i
Wape. Mtu mwenye
kujitambua hana
kawaida ya kuogopa
kufanya maamuzi,
na huyafanya kwa
kujiamini. Ana
shauku ya kujifunza
na kukua kiakili,
kifikra na kiroho. Siyo
sisi leo tunafikiria
starehe mbali mbali
na kuziacha imani
zetu zikiporomoka.
Mtu anayejitambua
anakuwa imara muda
wote katika kila hali.
Jamii yetu ya sasa, mtu
akipatwa na tatizo,
basi atataka kila mtu
ajue. Ni wepesi mno
kutetereka hata kwa
mambo madogo tu.
Ni mwenye kuidhibiti
vilivyo tabia yake
binafsi. Haendeshwi
na matamanio ya nafsi,
bali yeye huyaelekeza
anavyotaka yeye.
Huwathamini
wengine kwa uadilifu,

k wa u s a wa , h a n a
upendeleo.
Anayejitambua
ukweli wa kujitambua,
akiwa ni Muislamu,
huumiza kichwa
chake kwamba, ni
lini na kipi afanye ili
mwisho wa siku, Quran na Sunnah vitumike
kama hukmu na
sheria katika miamala
yote. Kinyume na
leo kwamba, Qur-an
na Sunnah vinaishia
ndani ya misikiti tu.
Ukitoka nje kila mmoja
anaishi anavyoona
mwenyewe na akili
zake. Wengi wetu
wala hatuoni kama
ni tatizo kuishi katika
mazingira haya
tuliyonayo leo. Ndio
m a a n a u t a wa k u t a
watu wakitamka kwa
vinywa vipana kabisa
kwamba kusoma
elimu ya mazingira ni
ukafiri. Wamesahau
kwamba elimu hiyo
wanayoipinga ndiyo
inayowatengenezea
mazingira mazuri ya
wao kumuabudu Allah
(Subhanahu Wa-tala).
Kuna tofauti gani na
mtu anayeogopa kula
nyama ya nguruwe

i l h a l i a n a k u n y wa
mchuzi wake!?
Wa k e z e t u n a
wao wanajifungulia
hospitalini na wala
h a k u n a a n a ye h o j i
aliyemsaidia
k u j i f u n g u a
Muislamu au kafiri.
Tu n a c h o t i z a m a
usalama wa mama na
mtoto.
Mwenye kujitambua
ni mchache wa
kukosea na mwingi
wa kufanya vizuri na
kwa ufanisi mkubwa.
Hii inatokana na
ukweli kwamba mtu
wa namna hii muda
wote anafahamu yuko
wa p i , k i p i a f a n ye
na kipi asifanye.
Anakuwa makini kwa
kila jambo lake. Akiwa
msikitini anafanya kile
kinachoendana na
mazingira ya msikitini.
Akisimama kuswali,
akimaliza kuswali
m p a k a wa k a t i wa
kutoka. Siyo mtu mtu
mwingine unakuta
anapiga porojo
msikitini, anavuta
sigara chooni msikitini
na kila jambo kwake
ni sawa tu. Na ukitaka
kujipima katika hili,

fanya tathmini kabla


h u j a l a l a , k wa m b a
kuanzia asubuhi
ulivyoamka umeomba
dua, umeingia kwa
mguu gani chooni,
umetokaje chooni,
umetokaje nyumbani
na umerudije hadi
ukaingia nyumbani
kwako?
K i m s i n g i ,
k u j i t a m b u a
kunatamalaki katika
maeneo mengi
lakini kwa uchache
nimegusia nukta hizi
ambazo zitaibua fikra
nyingi zilizokuwa
zimelala. Jamii leo
imekuwa ikiishi
katika madhila mbali
mbali, sababu kubwa
ikiwa ni kukosekana
kwa viongozi
wanaojitambua.
Kibaya zaidi ni kwamba
viongozi pamoja na
wanaoongozwa, wote
wanaogelea katika
jahazi moja la
kutojitambua. Hali hii
ipo mpaka misikitini
ambapo unakuta
Imamu yupo yupo
tu. Amekaa anasubiri
aletewe taarifa njema
au mbaya, kama ndoa,
msiba na kadhalika.
Hajishughulishi
kutafuta taarifa
muhimu na kungamua
c h a n g a m o t o
zilizopo katika jamii
inayomzunguka.
Mchango wetu
katika hali tuliyonayo
ni mkubwa mno,
ambao msingi wake
mkuu ni uelewa na
uwezo wa kupima
mambo unaotokana
na kutojitambua.
Maimamu wetu
wamekuwa kama
watu waliokosa kazi.
Hawathaminiwi,
wanadharauliwa lakini
inapotokea kwamba
mtu amefiwa, anataka
kusoma khitma, au
kufunga ndoa, hapo
ndipo nafasi ya Imamu
huonekana.
(Makala hii
imeandikwa na Juma
Jumanne,
Simu: +255 659 789
468/ +255 752 527 833
au
Barua Pepe:
jumannej3@gmail.
com.)

Makala

AN-NUUR

RAMADHAN 1436, IJUMAA JULAI 10-16, 2015

Nasaha kwa Waislamu mintarafu Uchaguzi Mkuu

Kila sifa njema


zinamstahiki Mwenyezi
Mungu. Swala na
Amani zimfikiye Mtume
M u h a m m a d ( S wa l l a
A l l a a h u a l a y h i wa
sallam) na jamaa zake.
Kwa mujibu wa Katiba
ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Ibara ya 28
(1): Kila Mtu ana wajibu
wa kutii na kufuata katiba
hii na sheria za Jamhuri ya
Muungano.
H i v y o Wa i s l a m u
ambao ni rai katika
Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, maamuzi
yote yanayofanywa
katika Bunge, Baraza
l a Wa w a k i l i s h i n a
Madiwani, wanatakiwa
kuyatekeleza bila ya hiyari
kwani yanawagusa wao
kama raia. Ni mtizamo
wa makosa na jambo la
hatari, iwapo Waislamu
wenye kujitambua juu ya
dhima, lengo na jukumu
lao la kuwepo hapa
ulimwenguni, wataamua
kutoshiriki kwenye
mchakato wa kisiasa kwa
namna yoyote wakati huu
wa kuelekea Uchaguzi
Mkuu wa Rais, wabunge,
madiwani na wawakilishi.
Kosa kama hili hatuoni
likifanywa na watu wa
upande wa pili.
Mfano hai ni kutolewa
TAMKO LA JUKWAA LA
WAKRISTO TANZANIA
K U H U S U K AT I B A
INAYOPENDEKEZWA,
MAHAKAMA YA KADHI
NA HALI YA USALAMA
NA AMANI YA NCHI.
Mfano wa pili ni pale
Chama cha Wanataaluma
wa Kikristo (CPT) na
Tume ya Haki na Amani
ya B a r a z a M a a s k o f u
(TEC) kwa pamoja,
waliposambaza waraka
u n a o t o a d o k e z o k wa
waumini wao namna ya
kushiriki Uchaguzi wa
2010 kama Wakristo.
Kwa mujibu wa waraka
huo ambao mara ya kwanza
ulichapishwa na gazeti la
Sunday Citizen, Jumapili
Aprili 3, 2010, mradi huu
wenyewe uliyokuwa na
awamu 15 ulianza Januari
2009, ukiwa na lengo
la kuelekeza Wakristo
Wakatoliki kupiga kura
kwa kuangalia maslahi
yao.
Vifungu vichache
vilivyonukuliwa kutoka
katika waraka huo,
vinaeleza madhumuni ya
Wakristo katika Uchaguzi
Mkuu wa mwaka 2 010.
Katika uk. 6 na 7.
Katika uwanja wa siasa
tunapaswa kuangalia
namna wagombea
wanavyoteuliwa na
vyama vyao. Kwahiyo
ni muhimu kuandaa
viongozi kushirikiana

nao na kushikana nao na


kudhibiti kwa lengo la
kuwasaidia kuwa jasiri
waliyo waaminifu katika
kazi zao. Tu wa s a id ie
tangu ngazi ya serikali za
kijiji, mitaa hadi ngazi ya
halmashauri ya Wilaya
k u t a f u t a t a a r i f a k wa
pamoja na kama jumuiya ya
kanisa, ni lazima tujifunze
kuhimiza mahitajio yetu
yazingatiwe na wenye
maamuzi. Maoni yetu
yasikilizwe na kufanyiwa
kazi tunu za Kikristo
tunazozisimia zionekene
katika mgawanyo wa
bajeti ya Serikali.
K wa u p a n d e wa k e ,
Shura ya Maimamu
Ta n z a n i a , K a m a t i
Kuu ya Siasa, angalau
ilijitoa kimasomaso kwa
kutoa Muongozo kwa
Wa i s l a m u k u e l e k e a
Uchaguzi Mkuu wa
mwaka 2010. Na baadhi ya
Waislamu wakiongozwa
n a B A K WATA , n d i o
waliokuwa wa kwanza,
kukejeli, kukatisha tamaa
na kuupinga muongozo
huo.
Ni masikitiko makubwa
sana kama ilivyokuwa
kwenye chaguzi zilizopita
kwenye mchakato wa
Uchaguzi Mkuu, kwa
Waislamu kuingia kwenye
mchakato huo kwa
ushabiki uliotokana na
kuathiriwa na Propaganda
za wan as ia s a k u p itia
vyama vyao vya kisiasa na
kuchagua mtu kwa chama
kile anachokipenda, bila
kuzingatia nini watapata
kama Waislamu. Yaani
kuwa kama mashabiki wa
timu za mipira, mtu hata
timu ya ifungwe, bado
ataipenda na kushabikia.
Hivyo mtu kujali zaidi
kukinisuru chama bila
kujali mustakabali wake
wa kijamii na kidini.
Matokeo ya hali hii ni
kwa vyama vya kisiasa
kuwa n a u h a k ik a wa
kupata kura za Waislamu,
bila wao kuwekeza lolote
la kuwasaidia Waislamu
na dini yao.
Hiki ni kipindi cha
kipekee na fursa kwa
Waislamu wa Tanzania
kutumia akili zao na
k u z i f a n ya z i we h u r u
na utumwa wa akili za
kufikirishwa na kutumika
kama turufu ya wana siasa
kufikia malengo yao.
Kupiga kura kwa
ajili ya kuchagua mtu
atakaye kuwa kiongozi
wa kuwatawalia mambo
yao kwenye jamii husika
ni suala nyeti ambalo
linahitaji umakini
mkubwa. Linahitajia watu
kupewa elimu ya siasa
juu ya namna gani ya
kuwatathimini wagombea
ili kujiridhisha kwamba

BAADHI ya viongozi wa dini waliohudhuria mashindano ya Kuhifadhi Qur'an


yaliyoshirikisha nchi za Afrika Mashariki yaliyoandaliwa na Taasisi ya Al-Hikma
mwishoni mwa wiki.
wanafaa. Kufanya
makosa katika uchaguzi
wa kiongozi wa kisiasa,
akachaguliwa asiye stahiki
ni kujiingiza katika janga
kubwa mno.
Ufisadi umedhihiri
bara na baharini kwa iliyo
yafanya mikono ya watu,
i l i M we n ye z i M u n g u
awaonyeshe baadhi ya
waliyo yatenda. Huenda
wakarejea kwa kutubu.
(Suratul Al-Rum 30:41).
Kutokana na unyeti wa
kazi ya kuiongoza jamii,
ndio Allah (s.w.) ameandaa
walimu (Mitume wake) wa
kufundisha kinadharia na
kimatendo. Kwani kazi ya
kuiongoza jamii, ni kazi
ya kuiokoa kutokana na
matatizo ya kila namna
na kuiongoza kwenye
njia ya maisha ya utulivu,
furaha na amani. Bila jamii
kuifahamu njia hii na
kuifuata vilivyo, maisha ya
furaha na amani ya hapa
ulimwenguni na Akhera
ni ndoto.
Kwa hiyo, dhana ya
siasa kuachiwa pekee yao
watu ambao ni Majahili
na mafisadi, kuwaachia
watu ambao hawastahiki
kuiongoza jamii,
Mufisiduna fil-ardhi, ni
maangamizi.
Amesema Allah (s.w.):
Na wanapo ambiwa:
Msifanye uharibifu
ulimwenguni. Husema:
Bali sisi ni watengenezaji.
H a k i k a wa o n d i o
waharibifu, lakini
hawatambui. (Baqara
2:11-12).
I k i wa Wa i s l a m u
wataingia kwenye
mchakato wa vyama vya
kisiasa kuelekea Uchaguzi

Mkuu wa Taifa wa mwezi


wa Oktoba mwaka huu,
kwa watakao afikishwa
na Allah (s.w.) kufika huko,
kwa dhana ya kufuata
mkumbo au ushabiki
wa vyama vya kisiasa
usiokuwa na malengo
ya mustakabali wao wa
kidini na kijamii, na
ikiwa wao ni wapiga kura
au wapigiwa kura kwa
maslahi ya Kula na sio
kujijenga kwa kistratejia
kwa mustakabali wao wa
kidini na kijamii, itakuwa
ni kujiingiza kwenye
nakama na matatizo ya
kujitakia kwa mustakabali
wao wa kidini na kijamii.
Kuingia kwa Waislamu
k we n ye u c h a g u z i wa
kisiasa ni miongoni mwa
nyenzo tu ya kuwawezesha
kumkamata na kuwazui
madhalimu na mafisadi
wasipate nafasi ya kufanya
ufisadi wao katika ardhi.
Madaiyah (walinganizi
wa Dini ya Uislamu) ndio
a m b a o wa n a j u k u m u
kubwa la kuielimisha jamii
juu ya dhana ya siasa. Kwa
hivyo endapo watawaachia
watu ambao ni majahili
na wachumia tumbo na
vitu (Materialists) kuingia
k we n ye v y o m b o v ya
maamuzi, ni kwamba wao
binafsi na jamii itakuwa
taabuni.
Waislamu wa Tanzania
hawaingii katika Uchaguzi
wa Mkuu ujao kwa lengo
la kusimamisha dola ya
Kiislamu, bali kama raia
na wanajaii wenye wajibu
kuona jamii wanamoishi
inatengemaa. Kwa msingi
huo, tumedharurika
kuingia kwenye Uchaguzi
wa Kidemokrasia

k wa k u j i p i m a i wa p o
kutoshiriki au kushiriki
ni vipi kutapelekea kuzidi
madhara au nafuu kwa
mustakabali wao wa kidini
na kijamii kama raia wa
Tanzania.
Kuna kanuni ya kisheria
katika Uislamu ya UsulFiqh ambayo inasema
A d h a r u r a t Tu b i h u
M a d h u r a t ( D h a r u r a
Ya h a l a l i s h a Ya l i y o
Haramishwa). Kwa mujibu
kanuni hiyo ya kiusuli, ki
dharura mbili yaangaliwa
ile dharura yenye nafuu
na kuifanya au kuitekeleza
na kuiacha nyingine yeye
madhara makubwa zaidi
kwenye Dini na Waislamu
binafsi.
Mathalani, katika fatwa
ya Sheikh Muhammad Ibn
Swaalih Al-Uthaymiyn,
katika kujibu swali la
15 muulizaji anauliza je
mmeshatoa Fatwa juu
ya kujuzu Uchaguzi (wa
kisiasa)? Na ipi hukumu
yake?
Jawabu la 15: Naam
tumeshafutu juu ya hili, na
hapana budi kufanya hivyo.
Kwasababu iwapo sauti ya
Waislamu itakosekana,
Bunge litatawaliwa na
watu wa shari watupu.
N a p i n d i Wa i s l a m u
wakishiriki katika
chaguzi, watachagua wale
wanaoona wanastahiki
kwa hilo na itapatikana
kheri na Baraka.
Wabbilah Tawfiq.
(Makala hii imeandikwa
na Abu Saumu, Kombo
Hassani Kidumbu wa
Mikanjuni Tanga. E-mail:
hassanikombo@yahoo.
com.)

Makala

AN-NUUR

RAMADHAN 1436, IJUMAA JULAI 10-16, 2015

Shinikizo la juu la damu na namna ya kulikabili

Na Mujahidi Mwinyimvua

MOJA ya magonjwa
yanayongezeka
kwa kasi kubwa
kusababisha vifo,
vikiwemo vile vya
ghafla ni shinikizo la
juu la damu.
Ugonjwa huu ni
m u u a j i wa k i m ya
kimya na ukibaini
dalili zake, jua kuwa
mambo yanakaribia
kuharibika.
Katika Uislamu
tumefundishwa
k u c h u n g a
tunavyoingiza
katika tumbo letu.
Tusipokuwa makini,
basi shinikizo
kubwa la damu
halitatuacha salama.
Rejea mafundisho
haya kupitia Mtume
Mhammed (s.a.w):
Mwanadamu
hajapata kujaza
chombo shari
kuliko tumbo
lakevinamtosha
mwanadamu vijitonge
vitakavyousimamisha
uti wa mgongo wake.
Ikiwa hapana budi,
basi theluthi moja iwe
ni ya chakula, theluthi
nyingine ya maji na
theluthi nyingine
ya pumzi yake.
(Tirmidhiy).
Shinikizo la juu la
damu (hypertension)
ni ile hali ambapo
damu inapita katika
kuta za mishipa ya
damu ya ateri kwa
nguvu kubwa.
Shinikizo la juu la
damu linaathiri zaidi
viungo takribani
vinne, ambavyo ni
ubongo, moyo, figo na
macho.
Damu ikiwa inapita
kwa nguvu kubwa
katika mishipa ya
damu, inaweza
kupasua mishipa
iliyomo katika ubongo
na hivyo kupelekea
mtu kupata kiharusi
au kupoteza maisha.
Pia, mtu akiwa na

shinikizo la juu la
d a m u m o y o wa k e
unafanya kazi kupita
kiasi ya kupampu
damu ili iende
sehemu nyingine
mwilini. Kwahiyo,
moyo huo unaweza
kupata shambulio au
kushindwa kufanya
kazi kabisa na hivyo
mtu kufa ghafla.
Vilevile, damu
ikisafiri kwa nguvu
katika mishipa ya
damu, inaharibu
m i s h i p a ya d a m u
inayokwenda katika
figo. Hivyo, figo
litashindwa kufanya
kazi na kupelekea
uchafu ujae katika
damu badala ya
kuchujwa na kutoka
nje kama mkojo au
jasho.
Zaidi ya hayo,
shinikizo la juu la
damu linapelekea
m i s h i p a ya d a m u
inayokwenda katika
macho kupasuka na
kivyo damu kuingia
katika macho na
kudhoofisha macho au
kuleta upofu kabisa.
Kwa mtu mwenye
presha ya kawaida
anatakiwa awe na
presha kiasi cha 120/80
mmHg. Baadhi ya
tafiti mpya zinashauri
mtu awe na presha
kiasi cha 119/79 au
chini kidogo.
T a k r i b a n i
watu asilimia 90
mpaka 95, hakuna
chanzo maalumu
kinachosababisha
shinikizo la juu la damu.
Ila kuna vichocheo
vinavyoongeza kasi
ya tatizo hilo. Hitoria
ya ukoo au kurithi.
Kama katika familia
wazazi walikuwa na
tatizo hilo, watoto au
wajukuu wanaweza
kupata shinikizo la juu
la damu.
Ulaji usiofaa
ukiwemo ule wenye
vyakula vyenye
chumvi nyingi ni

kichocheo kingine.
Unene kupita kiasi nao
unaongeza shinikizo
la juu la damu.
Maisha yasiokuwa
na mazowezi au
kazi za kutoka jasho
nayo ni kichocheo.
Msongo wa mawazo
ni kichocheo kikubwa
cha shinikizo la juu
la damu. Mawazo
zaidi yanapandisha
presha na hivyo
kuhatarisha uhai
wa mtu. Msongo wa
mawazo hauepukiki,
vema watu wajitahidi
kupata elimu ya
namna ya kudhibiti
msongo wa mawazo

ili kupunguza athari


yake. Kufanya kazi
bila ya kupata muda
wa kupumzika nako
kuna chochea kupanda
kwa presha. Kunywa
pombe kupita kiasi
na kuvuta sigara ni
vichocheo vya tatizo
hili. Kuna baadhi ya
kina mama wenye
mimba, presha zao
zinapanda.
Shinikizo la juu la
damu pia linaweza
kusababishwa na
magonjwa kama vile
kisukari na magonjwa
ya figo.
Presha inaweza
kudhibitiwa kwa

kutumia dawa, lakini


bora zaidi ni kutumia
njia za asili. Dawa
zinaweza kuleta
madhara mengine
kama kutetemeka na
kukosa usingizi. Njia
za asili ni pamoja na
ulaji unaofaa wenye
matunda, mboga za
majani, mafuta kidogo,
na wanga kidogo. Pia,
kufanya kazi za kutoka
jasho au mazowezi,
kuwa na uzito unaofaa
kiafya, kupunguza
unywaji wa pombe na
kuacha kuvuta sigara.
Vilevile, kupima afya
mara kwa mara.

10
Na Omar Msangi
TAARIFA za vyombo
v ya h a b a r i m a p e m a
wiki hii zimedai kuwa
Kenya imepigwa tena
na Al-Shabaab ambapo
inadaiwa kuwa watu 14
waliuliwa. Shambulio
hilo linalodaiwa
kufanyika Mandera,
ambapo hukaliwa na
Waislamu wengi wa asili
ya Somalia, linadaiwa
k u wa l e n g a j a m i i ya
wageni wa eneo hilo walio
Wakristo. Ikadaiwa kuwa
Al-Shabab walivamia
eneo hilo watu wakiwa
wamelala usiku na
kuanza kuvurumisha
mabomu katika nyumba
zao.
"These were Al-Shebab
from the nature of the attack.
They used explosives and
guns."
Hii ni moja ya kauli za
magazeti katika kuonyesha
kuwa wahusika ni AlShabaab. Taarifa inasema
ikinukuu anayedaiwa
kuwa
shuhuda
kwamba ni Al-Shabab.
Sio kuwa walikamatwa
na ikathibitika kuwa
ni Al-Shabaab. Laa, ila
ni kutokana na aina ya
shambulio (the nature
of attack.) Nature gani.
Wa n a j i b u - t h e y u s e d
e x p l o s i ve s a n d g u n s .
Kwamba walitumia
milipuko na bunduki!
Mtu unauliza, hivi kila
anayetumia milipuko na
bunduki ni Al-Shabaab?
Polisi hawatumii bunduki?
Wanajeshi hawatumii
milipuko?
Sikiza kauli nuingineA pro-Shebab website,
Somalimemo, said the AlQaeda-affiliated rebels had
confirmed they carried out
the attack against "Christian
Kenyans".
Kwamba
kuna
mtandao wenye
kuwapenda Al-Shabaab
unaoitwa Somalimemo,
umesema kuwa magaidi
wanaohusiana na AlQaida wamekiri kufanya
shambulio hilo.
Kitu kinaitwa mtandao,
website, facebook n.k,
m t u ye y o t e a n a we z a
kutengeneza mtandao
wake na akaupa jina lolote
akatupa huko chochote
anachotaka kwa kutumia
jina na utambulisho
wowote anaotaka. Kwa
hiyo ni kwa watu wajinga
tu wa IT na mitandao ndio
wanaoweza kuchukulia
kuwa hapo kimesemwa
kitu na wakakipa uzito.
L a k i n i
k u n a
kitu muhimu zaidi
kimesemwa hapo.

Makala

AN-NUUR

RAMADHAN 1436, IJUMAA JULAI 10-16, 2015

Mauwaji ya Al-Shabaab tena Kenya


Tujifunze kutoka Shambulio la Kimeta
Akitujia fasiki na habari, tuchunguze
Huu ndio uadilifu na ndio salama ya nchi

Admiral Thomas H.
Moorer.
Kama tulivyotangulia
kusema, Mandera ni mji
wa Waislamu Wasomali.
Sasa inadaiwa walilenga
Christian Kenyas.
A l S h a b a a b m o u n t s
another attack on nonMuslims. Al Shabaab
Islamists again attack nonMuslims.
Ndivyo vilivyoripoti
vyombo mbalimbali
vikubwa na vya kimataifa.
Kwamba, Al-Shabaab,
Waislamu (Islamists),
wameuwa tena Wakristo
Kenya.
Kwa ajili ya mjadala,
tuchukulie kwamba ni

General Raymond G.
Davis.
kweli kuna watu waliuliwa
na kama tunavyoambiwa,
waliouliwa ni Wakristo.
Swali la msingi hapa ni je,
nani wamefanya mauwaji
hayo? Vyombo vya dola
vya Kenya na vyombo vya
habari, vinatuambia kuwa
wahusika ni Al-Shabaab,
ambao ama wana kambi
zao ndani ya Mandera
(cells) au walifanya
kuingia wakashambulia
na kuondoka.
Tukijaaliya kuwa Al
Shabaab ni Waislamu
wanaodai kupigania
nchi yao itawaliwe kwa
Sheria za Kiislamu, hilo

linaondoa uwezekano
wa wao tena kufanya
mauwaji hayo maana
ni kinyume na Uislamu
wanaodai kuupigania
na kuutawalisha katika
maisha yao na katika nchi
yao. Lakini hoja hiyo,
inaweza isitusaidie sana
katika kujadili jambo hili,
hasa kwa vile limegubikwa
na ulaghai mwingi kuliko
ukweli.
Oktoba 22, 2003 Tume
iliyoteuliwa kuchunguza
kushambuliwa kwa meli
ya kivita ya Marekani
USS Liberty mwaka 1967
ambapo wanajeshi 34
waliuliwa, ilitoa taarifa
yake. Katika taarifa hiyo
i l i e l e z wa k u wa m e l i
hiyo ilishambuliwa kwa
makusudi na wanajeshi
wa Israel, huku wakijua
kuwa wanayoipiga ni meli
ya Marekani, na kama ni
kuuwa, watakao uliwa ni
askari wa Marekani.
Hiyo haikuwa ni Tume,
wasiwasi au ya Ukawa
fulani hivi. Ilikuwa ni
Tume iliyojumuisha wazito
katika Jeshi na Serikali
ya Marekani. Waliotajwa
ni pamoja na Admiral
Thomas H. Moorer,
Mstaafu kutoka Jeshi la
Wanamaji (United States
Navy), General Raymond
G. Davis, aliyewahi kuwa

Mnadhimu Mkuu wa Jeshi


(Chairman, Joint Chiefs
of Staff) , Mstaafu Rear
Admiral Merlin Staring
(Former Judge Advocate
General Of The Navy) na
aliyewahi kuwa Balozi wa
Marekani nchini Saudi
Arabia Ambassador James
Akins.
Tu m e i l i n u k u u n a
kuonyesha ushahidi
mwingi wa matokeo ya
uchunguzi wao ambao
ulitengua madai ya
mwanzo kuwa shambulio
hilo lilifanyika kimakosa.
(Tazama: Findings of the
Independent Commission of
Inquiry into the Israeli Attack
on USS Liberty, the Recall
of Military Rescue Support
Aircraft while the Ship
was Under Attack, and the
Subsequent Cover-up by the
United States Government.)
Mbali na taarifa ya
Tume hiyo, wapo watu na
taasisi binafsi zilichonguza
jambo hilo na kuja na
matokeo kama hayo hayo
ya Tume rasmi ya serikali.
Lakini swali muhimu
hapa ni je, kwa nini Israel
ilifanya hivyo? Swali
hili linatupeleka katika
kitu kinaitwa Operation
Cyanide.
Kama anavyosema
mwandishi Peter
Hounam (aliyekuwa Chief
Investigative Journalist
for The Sunday Times of
London), mwaka 1966
kulikuwa na mpango wa
siri (covert operations)
wa p a m o j a b a i n a ya
Israel na Marekani wa
k u m wa n g a m i z a R a i s
Gamal Abdel Nasser.
Operation hiyo kijeshi
ndio iliitwa, Operation
Cyanide. Mpango
wenyewe ulikuwa
kwamba meli ya kijeshi
ya Marekani ipigwe
na kuzamishwa kabisa
halafu lipigwe debe kuwa
waliofanya uhalifu, ukatili
na uchokozi huo ni Misri.
Hapo tena Marekani iingie
kwa nguvu zote kijeshi
kumwangamiza Gamal
Abdel Nasser na Cairo
yake ili asiwe tishio kwa
Israel. (Tazama: Operation
Cyanide: Why bombing the
USS Liberty nearly caused
World War III na Operation
Cyanide The Attack on
USS Liberty was a Failed
Provocateur Action and
Pretext for US Invasion of
Egypt for Israel.)
Lakini tukiacha hilo,
kuna lile tukio la shambulio
l a ug a i d i wa k i m e t a .
Ilikuwa tarehe 8 Oktoba,
2001 wajumbe muhimu
wa Bunge la Seneti
walipokea barua zenye
Inaendelea Uk. 11

11
Inatoka Uk. 10
viiniyoga au vijimbegu vya
kimeta (anthrax spores).
Wabunge hao walikuwa
ni Mwenyekiti wa Kamati
ya Seneti ya mambo ya
Sheria (Senate Judiciary
Committee Chairman)
Patrick Leahy, na Tom
Daschle (Senate Majority
Leader ). Wabunge hao
wawili walikuwa mstari wa
mbele kupinga muswada
wa sheria ya kupambana
na ugaidi, maarufu, USA
PATRIOT Act.
Hoja ya Wabunge hao
na wegine ilikuwa kuwa
sheria hiyo inakiuka haki
za binadamu na kuwapora
wa n a n c h i u h u r u . N a
kubwa zaidi ni kuwa ni
katika sheria za kidhalimu
ambayo ilikuwa ikiipeleka
Marekani kuwa taifa la
kipolisi.
Mtiririko wa matukio
unaonyesha kuwa
barua hizo zenye kimeta
zilitumwa pia kwa vyombo
vya habari vikiwemo ABC
News, CBS News, NBC
News, the New York Post,
na American Media IncAMI (publisher of the
National Enquirer).
Katika shambulio hilo
lililokuja kujulikana kama
Anthrax Terror Attacks,
m a a r u f u k wa k i f u p i
Amerithrax, watu watano
walikufa, huku wengine 17
wakiambukizwa ugonjwa
wa kimeta lakini wakawahi
kutibiwa.
Mara tu baada
ya s h a m b u l i o h i l o ,
harakaharaka ikadaiwa
kuwa wahusika ni AlQaida, Saddam Husein
na Osama Bin Laden.
Tarifa zilianzia Ikulu,
White House, ambapo
Rais George W Bush
na makamo wake Dick
C h e n e y , wa l i j i t o k e z a
waziwazi wakisema
kuwa muhusika ni Osama
Bin Laden na Al-Qaida.
Mwingine aliyeleta madai
hayo ni John McCain.
Katika kukoleza
madai hayo, aliyekuwa
kachero mkuu wa FBI
Robert Mueller akatakiwa
haraka atoe vielelezo na
uthibitisho kuwa wahusika
ni Al-Qaida. (Tazama: FBI
was told to blame Anthrax
scare on Al Qaeda by White
House officials BY JAMES
GORDON MEEK , DAILY
NEWS WASHINGTON
BUREAU, Saturday, August
2, 2008, 6:32 PM)
Na kweli. Debe
likapigwa kisawasawa
kwamba kimeta hicho
n a wa l i o t u m a b a r u a
hizo ni Al-Qaida. Barua
zenyewe, zote zilikuwa

Makala

AN-NUUR

RAMADHAN 1436, IJUMAA JULAI 10-16, 2015

Mauwaji ya Al-Shabaab tena Kenya

Patrick Leahy

Tom Daschle

BARUA zenye kimeta zilizodaiwa kutumwa na


Alqaidah.

na ujumbe unaofanana
zikiwa na maneno ambayo
mtu yeyote akisoma
atahitimisha kuwa
zimetoka kwa Muislamu.
Maneno yalikuwa Allah
is great, Death to America,
Death to Israel.
Ndio haya tunayoona
huku kwetu leo, kila
wakikamatwa watu
wa n a o t u h u m i wa k wa
ugaidi tunaambiwa kuwa
walikuwa na bendera
yenye maandishi ya
Kiarabu, wakivaa kanzu na
baraghashia! Ukizingatia
kuwa baadhi ya barua hizo
zilitumwa katika vyombo
v ya h a b a r i , u n a we z a
kufikiria ni kwa kiwango

gani magazeti, redio


na televisheni zilipiga
zumari kusherehesha
kuwa Osama, Saddam
Hussein na Al Qaidah
yao, wameishambulia
Marekani kwa kimeta.
Ilikuwa ni katika
mazingira hayo,
h a r a k a h a r a k a Pa t r i o t
Act ilipitishwa ikielezwa
k u wa n i m u h i m u i l i
kupambana na magaidi
wa Al-Qaidah, ambao
sasa wanashambulia kwa
kimeta. Pili, tukio hilo la
kumuhusisha Saddam
Hussein na kimeta, ndio
pia lilitumika kujenga
hoja kuwa ana silaha za
maangamizi (Weapon of

Mass Destruction-WMD).
Kwa kisingizio hicho, Iraq
ikavamiwa mwaka 2003 na
kuuwa mamilioni ya watu
wasio na hatia wakiwemo
askari wa Marekani zaidi
ya 4000 waliokwenda
vitani kupigana vita
batili. Labda tuseme
vita ya kuwafaidisha
m a b e b e r u wa n a o t a k a
kudhibiti mafuta. Mpaka
leo Iraq inateketea na
watu kuteseka. Lakini nani
anajali?
Kwa mujibu wa gazeti
la The New York Times la
Novemba 29, 2011, serikali
ya Marekani imekubali
kulipa fidia ya Dola milioni
2.5 (zaidi ya shilingi bilioni
5) kwa mjane na watoto
wa Robert Steven. Huyu
Robert Steven, ambaye
alikuwa mwandishi wa
habari, ni mmoja wa wale
watu watano waliokufa
katika shambulio la ugaidi
wa k i m e t a u l i o d a i wa
kuwa umefanywa na AlQaida. Baada ya kuanza
kuibuka habari kuwa
ilikuwa uwongo, kimeta
kile hakikutoka Iraq kwa
Saddam Husein wala kwa
Osama bin Laden, bali
kilikuwa cha ndani ya
Marekani, Bi Maureen
ambaye ni mkewe Steven
alifungua kesi mwaka
2003 akiishitaki serikali
kwamba ndiyo iliyohusika
na kifo cha mumewe. Kesi
ilinguruma kwa muda
mrefu, baadae akashinda.
FBI wenyewe ilipofika
2 0 0 8 wa l i s e m a k u wa
kimeta kile kilitoka katika
maabara ya kijeshi (Armys
biodefense laboratory at
Fort Detrick, in Frederick,
Md.) kule Maryland. Na
wakamtuhumu Dr. Bruce
Edwards Ivins kuwa ndiye
aliyesambaza kimeta hicho
kupitia barua. Hata hivyo,
muda mfupi baada ya
tuhuma hizo, Dr. Ivins
alikutwa amekufa katika
mazingira ya kutatanisha
ikidaiwa kuwa alikunywa
sumu ikitajwa kwa jina
la Tylenol with codeine.
(Tazama: U.S. Settles Suit
Over Anthrax Attacks.)
Yapo mambo kadhaa ya
kuzingatia hapa. Moja ni
kuwa sheria ya kupambana
na ugaidi ya Marekani-US
Patriot Act, ilipitishwa
kwa shinikizo baada ya
kutengenezwa mazingiria
ya uwongo (hoax, false
flag terror attack) ya
kitisho cha ugaidi wa
Al-Qaida (psychological
fear, psychological

manipulation).
Pili, awali sheria hiyo
ilipingwa, wabunge
wa k i d a i k u wa n i ya
kidhalimu yenye
kutengeneza mazingira
na visingizio vya kuonea
watu, kuvunja haki za
binadamu na kuwapora
watu uhuru wao kwa
kutengeneza taifa la
kipolisi.
Tatu, Patriot Act hiyo
ambapo ilipingwa kwa
hoja hizo na kupitishwa
baada ya kufanyika
usanii wa psychological
manipulation, ndiyo nasi
tuliletewa huku tukatakiwa
kutengeneza mfano
wake na kushinikizwa
kuipitisha.
Sheria hiyo, ndiyo
ambayo sasa inatumika
kuwakamata akina Sheikh
Msellem na kuwaweka
ndani bila ya dhamana
kwa hoja kuwa wanafuata
sheria ya kuzuiya ugaidi.
Jambo moja tukubaliane:
kwamba, maadhali
ilibidi kuandaa usanii
w a A n t h r a x Te r r o r
Attacks ambapo watu
watano wasio na hatia
waliuliwa, hapana shaka
kuwa hapakuwa na kitisho
cha kweli na halisi wala
m a z i n g i r a y o y o t e ya
kutaka kuwa na Patriot
Act. Kwa hiyo, kufanyika
usanii huo uliogharimu
maisha ya watu huku
wakisingiziwa watu
wengine wasio husika,
bila shaka waliotengeneza
usanii huo, walikuwa na
malengo yao ambayo bado
wanayapigania ndani ya
nje ya nchi yao-katika
nchi mbalimbali duniani
ambazo tayari zimeweka
mfano wa sheria hiyo.
Sasa labda na sisi
tujiulize, tunapowakamata
Masheikh na watu
wengine, kwa tuhuma
za ugaidi, lengo letu nini?
Tu n a y o a g e n d a ye t u ,
kama taifa na kama nchi,
tunayoifanyia kazi au ndio
tunatumikia agenda ile ile
ya wale waliosema kimeta
a l i c ho t um i wa Pa t r i c k
L e a h y k i m e t o k a k wa
Osama Bin Laden. Lakini
kama ni hivyo, tujue kuwa
hao hao leo wanashikana
uchawi wenyewe kuwa
kilitoka katika maabara
zao wenyewe?
Hoja hapa sio kuwa
kama wapo watuhumiwa
wa k we l i wa u g a i d i ,
wasichukuliwe hatua za
kisheria. Ila ni tahadhari
tu tusijeingizwa katika
agenda ambazo hatimaye
zitaivuruga nchi yetu.
Bi Maureen, mjane wa
Mr. Stevens amelipwa
Inaendelea Uk. 14

12

MAKALA

KUMI LA KUACHWA HURU...!

Kumi la kuachwa huru, sikilizeni anama,


Kumi la kuachwa huru, si kumi la lelemama,
Kumi la kuachwa huru, twapaswa kufanya hima,
TUHUISHE KUMI HILI, KWA KHERI KUKITHIRISHA.

Kumi la kuachwa huru, si la kudumu dawama,


Kumi la kuachwa huru, tuzizidishe kwa MEMA,
Kumi la kuachwa huru, si kwa fila na athama,
TUHUISHE KUMI HILI, KWA KHERI KUKITHIRISHA.

Kumi la kuachwa huru, LAILI twapaswa KAMA,


Kumi la kuachwa huru, kwa TAUBA na NADAMA,
Kumi la kuachwa huru, SI kwa NAUMU kunama,
TUHUISHE KUMI HILI, KWA KHERI KUKITHIRISHA.
Kumi la kuachwa huru, ni KUMI la KUUNGAMA,
Kumi la kuachwa huru, DHUNUBU zetu ADHIMA,
Kumi la kuachwa huru, mbele ya ALLAH KARIMA,
TUHUISHE KUMI HILI, KWA KHERI KUKITHIRISHA.
Kumi la kuachwa huru, TUTASWADAKI tamama,
Kumi la kuachwa huru, kwa kutoa DARAHIMA,
Kumi la kuachwa huru, ziwe KINGA kwa JAHIMA,
TUHUISHE KUMI HILI, KWA KHERI KUKITHIRISHA.
Kumi la kuachwa huru, ndilo kumi akrama,
Kumi la kuachwa huru, lenye tumbi taadhima,
Kumi la kuachwa huru, TULISHARIFU kwa WEMA,
TUHUISHE KUMI HILI, KWA KHERI KUKITHIRISHA.
ABUU NYAMKOMOGI-MWANZA.

WAJIBU WA WAFUNGAJI !

Ramadhani i ukingoni, pamwe na zetu swaumu,


Adhimu letu mbeleni, wahitaji kuwakimu,
Kwa ZAKATU kuthamini, FITIRI sote muhimu,
FITIRI tuandaeni, kuwakimu wahitaji.
Kwa ada si ZAKA ngeni, kwa wafungaji swaumu,
Si bidaa kwa mizani, bali sunna muadhamu,
Muakada tambueni, kwa za sunna akisamu,
FITIRI tuandaeni, kuwakimu wahitaji.
Rasuli ashabaini, si leo tangu kadimu,
Jambo hili hadithini, waulizeni alimu,
Kiwango mkibaini, na jinsi ya kukasimu,
FITIRI tuandaeni, kuwakimu wahitaji.
Kwa dokezo shairini, mafakiri ni muhimu,
Kadhalika maskini, tunopaswa kuwakimu,
Wawe nao furahani, SIKU YA IDD adhimu,
FITIRI tuandaeni, kuwakimu wahitaji.
Ewe kaka Ramadhani, nawe ukhti Swaumu,
Mwawajibika safuni, wahitaji kuwakimu,
Nyote ZAKATU toeni, FITIRI msihujumu,
FITIRI tuandaeni, kuwakimu wahitaji.
Haya shime ikhiwani, wahitaji tuwakimu,
Mijini na vijijini, sawia tuwakasimu,
Wajibu tusiukhini, kwa ubakhili kukimu,
FITIRI tuandaeni, kuwakimu wahitaji.
Beti saba shairini, za kumbusho zimetimu,
Kazi kwenu waumini, wafungaji wa swaumu,
Mwisho nakutakieni, njema nyote swaumu,
Wahitaji kuwakimu, ni letu sote jukumu.
ABUU NYAMKOMOGI
MWANZA.

RAMADHAN 1436, IJUMAA JULAI 10-16, 2015

Uzalendo kuipenda nchi ni haki na wajibu

Kumi la kuachwa huru, kumi la kazi na dhima,


Kumi la kuachwa huru, ni la kufunga dhamama,
Kumi la kuachwa huru, si la ajizi la hima,
TUHUISHE KUMI HILI, KWA KHERI KUKITHIRISHA.

Kumi la kuachwa huru, si shahari ni ayama,


Kumi la kuachwa huru, si tumbi kumi ayama,
Kumi la kuachwa huru, ndilo hili layoyoma!
TUHUISHE KUMI HILI, KWA KHERI KUKITHIRISHA.

AN-NUUR

Sheikh Mohamed
Obaidillahi Mohamed
Ally
SHUKURANI zote
anastahiki Mwenyezi
Mungu na rehema na
amani zimfikie Mtume wetu
Muhamad (S.A.W).
S h e r i a ya K i i s l a m u
inatazama haki na wajibu
kwamba ndio inasimamia
u t u k u f u wa b i n a d a m u
nayo ni mwanga wa siha na
msimamo katika kutekeleza
haki na wajibu kufuatana
na matakwa ya Mwenyezi
Mungu na ridhaa zake kama
ilivyokuwa ndio unyororo
wa maslahi ya kundi la watu
wengi na bila ya madhara
k wa w e n g i n e , n a k wa
watu ni wajibu kujuana na
kukubaliana katika haki na
wajibu katika vitu vinavyo
tokea miongoni mwa mambo
ya kimaisha kwa namna ya
kutovunja amri ya mwenyezi
mungu na matakwa yake
na sheria zake na kwa vile
inadhamini utukufu wa
binadamu na maslahi yake
na kuhakikisha kudumu kwa
uadilifu baina ya watu.
Haki za mzalendo katika
uislamu. Haki akushi kwa
hakika maisha ya binadamu
na kuhifadhi haki hiyo.
Uislamu una kariri juu ya
uadilifu kwa viumbe vyote
((Yeyote mwenye kuua nafsi
bila ya nafsi au ufisadi katika
ardhi ni kama kwamba
ameua watu wote)) (32)
maidah.
Pia una kataza uislamu
juu ya kuua mtu na pia
mtu kujiua mwenyewe na
inachukiza na ina madhambi
makubwa (na musijisikie
wenyewe kwa hakika
Mwenyezi Mungu hakuacha
kuwa kwenu ni mpole na
yeyote atakayefanya hayo
kwa uadui na dhuluma
tutamchoma moto, na
hakuacha kuwa juu ya hayo
ni mepesi) (30) Nisai na
anasema mtume (S.A.W)
((yeyote mwenye kujiua
mwenyewe kwa chuma
basi chuma chake kitakua
mkononi mwake anajichoma
nacho tumboni katika moto
wa jahanamu milele ya
milele na mwenye kujirusha
toka juu kwa makusudi iwe
mlimani au juu ya ghorofa
au juu ya mti na akajiua yeye
mwenywe basi ataangukia
moto wa jahanamu milele.
Ameipokea imamu
Muslim haki ya heshima : kwa
hakika uislamu kama vile
ulivyotoa haki ya kuishi kwa
binadamu, mnarudia vilevile

umeipa haki ya heshiima.


Binadamu kwa uislamu
ni mwenye kuheshimika
dhati yake achilia mbali
kupendwa na watu au utaifa
au rangi au dini kwa hakika
tumemtukuza binadamu: ))
(70) Israi na mara nyingine
alikuwa mtume (S.A.W)
amekaa na baadhi ya
masahiba wake likapitishwa
jeneza , akalisimamia
mtume (S.A.W) kutukuza
na kuheshimu, akaambiwa
lile ni jeneza la myahudi,
mtume akasema ((kwani
hiyo sio nafsi)) ameipokea
Imamu Bukhari.
Haki ya uhuru: kwa
hakika uislamu unakiri
kuwa sote ni watumwa wa
Mwenyezi Mungu peke yake
pasi na mwingine miongoni
m wa v i u m b e a u m a we
au vitu vingine hayo yote
yamekaririwa kwa umbali
na kwa daraja la juu. Juu ya
uhuru wa binadamu.
Haki ya usawa: unakiri
uislamu kuwa binadamu
wote ni sawa mbele ya
sheria ya uislamu (hakuna
ubora wa mwarabu kwa
asiye mwarabu wala asiye
mwarabu kwa mwarabu
wala mwekundu kwa
mweusi wala mweusi kwa
mwekundu isipokuwa kwa
ucha mungu tu)).
Ameipokea Imamu
Mulsim. Haki ya imani: kwa
hakika umekiri uislamu
vyanzo vikuu katika uhuru
wa kuamini ni kufikiri
((nyinyi mnadini yenu na
mimi nina dini yangu)) (6) Al
Kafiruun na kisha umekiri
uislamu mukabili wa hilo
juu ya kutolazimisha imani
au dini katika kuamini au
maoni ((hakuna kulazimisha
katika dini)) Al-Bakara (256).
Haki ya elimu: umekiri
uislamu kuwa elimu ni haki
ya kila mmoja , na aya ya
kwanza iliyoteremshwa
katika Qur-ani kwa mtume
(S.A.W) ((soma kwa jina
l a m o l a wa k o a m b a ye
amekuumba ) (1) Al-alaki.
Haki ya kuheshimu
wadhifa: unakiri uislamu
kutokuchunguzana
katika ujuzi maalum (na
wala msichunguzane)
(12) Hujurat anakataza
m t u m e ( S . A . W ) j u u ya
kuchunguzana aibu (na
wala msiwaudhi waislamu
wa l a m s i wa f e d h e h e s h e
na msiwachunguze aibu
zao, kwani mwenye
kufuatilia aibu ya nduguye
muislamu Mwenyezi
Mungu atamfedhehesha
aibu yake, na yeyote
mwenye kufedheheshwa
na Mwenyezi Mungu
ataaibishwa hata ndani ya
msafara wake)) ameipokea
Imamu Muslim.
Haki ya uongozi:
uislam unakiri miongoni
mwa wajibu wa kiongozi
kuchunga maslahi ya
watu na kuhakikisha
amani ya ulazima juu ya
uhai wao na utukufu wao
((hakika Mwenyezi Mungu
anakuamrisheni kutekeleza
amana kwa wenyewe)) na
anasema mtume ((nyote ni
wachunga na kila mchunga

a t a u l i z wa j u u ya k i l e
alichokichunga . Hadi
mwisho)
Ameipokea imamu
bukhari.
Wajibu wa mwananchi
katika uislamu: wajibu wa
mwananchi kwa upande
wa mola wake na muumba
wake. Miongoni mwa
mifano ya haki ambazo
tulizozitaja hivi punde kwa
hakika hiyo ni zawadi ya
Mwenyezi Mungu kwa waja
wake ina wajibika kumsifu
na kumshukuru na wajibu
wa mwanzo wa kushukuru
ni kutakasa matendo yake
yote kwa ajili ya Mwenyezi
Mungu na kutomshirikisha
katika uungu wake.
( ( s e m a h a k i k a s wa l a
yangu na suna zangu na
uhai wangu na ufaji wangu
ni kwa ajili ya Mwenyezi
Mungu hana mshirika na
kwa hivyo nimeamrishwa
na mimi ni wa kwanza juu
ya kunyenyekea)) 162 163
An-ami
Wa j i b u wa m t u k wa
upande wa wazazi wake: kwa
hakika umetukuza uislamu
kwa upande wa kuwatii
wazazi wawili na kuwatii
na kuunganisha na ibada
yake ((ameshahukumu mola
wako usiabudu isipokuwa
yeye na kwa wazazi wawili
uwafanyie ihsani)) (23)
Israil
Uzalendo wa kiislamu
na kujihisi juu ya uzalendo:
ilikuwa kwa Othman (R.A)
alikuwa na uzalendo wa hali
ya juu tena ni ule wa uislamu
kwa upande wa ndugu zake
juu ya uzalendo siku aliyo
nunua nusu kisima cha
Roma toka kwa myahudi
ambaye alikuwa ni kiongozi
wa kuuza maji pale madina
yenye nuru kwa bei ya juu.
Pindi ilikuwa siku hizo
kulikuwa madina wakinywa
akalipa Othmani kwa yule
myahudi na kutaka amuuzie
akakataa, akaomba amuuzie
hapo nusu ya kisima na
wagawane kwa masiku ya
kuuza maji yale siku ya
Othmani na siku ya myahudi
. Akakubali myahudi na
akamlipa Othmani kwa
nusu hiyo 12,000 Dirham
na akafanya siku ya kuuza
maji yake ni kwa ajili ya
Mwenyezi Mungu wanywe
watu wote bure wakawa
watu wakichota maji mengi
zaidi siku ya Othmani kwa
ajili ya siku mbili zaidi kiasi
alichohitaji ilikifika siku
ya myahudi ilifika siku ya
myahudi hakuna hata mtu wa
kununua . Akauza myahudi
fungu lake kwa Othman na
akafanya Othmani baada
ya hapo kumiliki kisima
chote kwa ajili ya Mwenyezi
Mungu bure bila hesabu
kwa yote yaliyoitangulia
yanatubainishia kwamba
uzalendo sio kudai haki peke
yake bali pia ni kuipenda
nchi na kutekeleza wajibu .
Atekeleze kwa upande wake
mwenyewe na familia yake
na nchi yake.

13
Na Khalid S Mtwangi
UCHAGUZI Mkuu unakuja.
Hivi sasa uko takriban
miezi minne kutoka sasa.
Wale waliojitolea kuwania
nafasi na vyeo katika zile
sehemu zinazojazwa kwa
kupigiwa kura, hivi saa
t a ya r i m a t u m b o m o t o .
Wanaonekana wakihaha
kuzitafuta hizo kura kwa
wananchi kwa sababu ni hizo
kura ndizo zitawawezesha
kuingia katika nafasi zile
wanaoziwania. Joto hilo
tayari linawasumbua sana
wale waliojitokeza kutaka
kujaza nafasi ya juu kabisa
ya URAIS wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
Hawa wako thelethini na
nane, idadi ambayo ni
kubwa na haijatokea katika
historia fupi ya Tanzania,
labda na Afrika kote.
Ingawa hawa wote,
wakiwa wananchi na raia
wa nchi hii, wanatumia
haki yao ya kiKatiba, lakini
kwa kuangalia vizuri na
kwa makini, ile orodha yao
inaweza kutoa maoni aina
mbili ambayo yanaweza
kusumbua fikra za watu.
Kwanza ni kuwa kweli nchi
hii imepiga hatua kiasi cha
kuweza kuwa na wananchi
wengi waliokomaa kisiasa
na kiutawala kiasi hicho.
Lakini wazo la pili linaweza
kuashiria pia wasi wasi
kidogo. Hivi kweli hadhi
ya nafasi kubwa ya URAIS
inaweza kuonekana rahisi
kiasi cha kuweza kuwavutia
wananchi wengi kiasi hicho
n a wa k i l a a i n a ? H a s a
i k i k u m b u k wa k wa m b a
baadhi ya hao waliojitokeza
kuwania nafasi hiyo hata
hawajulikani kisiasa. Hakuna
walichokifanya nchini humu
ambacho kinaweza kumvutia
mpiga kura ambaye anaweza
kukubali kweli huyu
anaweza kuleta makubwa
kuliko aliyoyakamilisha
huko nyuma.
Kama ilivyokwishaelezwa
idadi ya wale wanaoutafuta
URAIS ni kubwa na haijatokea
popote pale katika nchi za
Afrika, hivyo basi humo
wamo watu wa kila aina.
Kweli wengi wao ni wasomi
wenye shahada za Vyuo
Vikuu na pengine uzoefu wa
siku nyingi katika utawala na
mengineyo. Lakini kuibeba
nchi nzima hii Tanzania na
umasikini wake wa kutupwa,
sio mchezo wa pata potea.
Pamoja na kuwa kiongozi
mwenye elimu ya juu sana
kuna sifa zingine nyingi
ambazo pia ni muhimu zaidi
kuliko huko kusoma mpaka
kupata shahada nyingi. Sir
Winston Churchill alikuwa
Waziri Mkuu wa Uingereza
wakati hata elimu ya

MAKALA

AN-NUUR

RAMADHAN 1436, IJUMAA JULAI 10-16, 2015

Kura yangu nimpe nani?

Mhe. Samuel Sitta

Mhe. Edward Lowassa.

secondary ilikuwa ngumu


sana kwake. Mwanzoni
mwa miaka ya themanini,
Denmark ilimpata Waziri
Mkuu ambaye utaalam wake
ulikuwa ni fundi mchundo.
Ni wakati huo ambao nchi
hiyo ilikuwa ikitoa misaada
mingi ya maendeleo kwa
nchi kama Tanzania. Mfano
mwingine labda usiofaa
lakini tukumbuke kuwa
Jemedari Idd Amin Dadda
alikuwa rais wa Uganda.
Muheshimiwa huyu
elimu yake iliomwezesha
tu kupanda cheo jeshini
kufika kuwa EFFENDI; cheo
ambacho kilipikwa na utwala
wa Kingereza kwa ajili ya
WaAfrika wa KAR (Kings
Afrcan Rifles) huko Afrika
ya Mashariki. Kwa hiyo kile
kigezo cha kuwa na elimu ya
juu, ingawa katiba inatamka
hivyo, ni sifa ambayo sio
muhimu kila siku.
L a k i n i y o t e h a ya n i
kitendawili kwa Mwananchi
mpiga kura. Anapotafakari
haya na mengi mengine sasa
kura yake ampigie nani?
Idadi kubwa ya wagomba
URAIS, kwa mfano, ama
hata wanaogombea ubunge
inazidi kupasua kichwa
c h a M wa n a n c h i m p i g a
kura. Hivyo ni sawa kabisa
kujiuliza kura yangu ni
mpigie nani? Pamoja na hayo
yalitajwa mpaka sasa kuna
kigezo kingine kinachoweza
kumsumbua mpiga kura.
Nchi hii inajulikana kuwa
ni utawala wa kisekula, yaani
dini haina nafasi katika siasa
wala katika utawala. Kila
siku inanadiwa kuwa ingawa
wananchi na viongozi wana
dini zao, Serekali haina dini.
Itikadi hii ikisisitizwa kwa
wananchi wote. Wasomaji
watamkumbuka aliyekuwa
Mkuu wa Mkowa wa Dar
es Salaam na baadae akawa
Katibu Mkuu wa CCM,
Muheshimiwa Ustazi Luteni
Yusuf Rajab Makamba.

Kiongozi huyu kweli aliishika


itikadi hii ya kutochanganya
dini na siasa kiasi kwamba
Wa i s l a m u h a wa k u we z a
kufurukuta. Lakini ilikuwa
ni ajabu kwamba kasi yake
hiyo ilikuwa inawalenga
Waislam tu, huku mara
mara kwa mara alionekana
kufajirika anaponukuu Biblia
alipokuwa akizungumza
na Wananchi. Ilionekana
kuwa mbele yake wafuasi
wa Biblia walikuwa na hadhi
ya kipekee. Haikutokea au
labda mara chache sana
alisikika akiwakoromea
wanaofuata dini isiyokuwa
Uislam hata pale
wanapoonekana wamevuka
mipaka ya usekula. Kadhia
ya M we m b e C h a i n d i y o
legacy yake aliyowaachia
Waislamu wa Dar es Salaam
na wa Tanzania kwa jumla.
Hawataisahau kamwe!
Turudie kusema
tena kuwa nchi hii ni ya
kisekula wananchi wana
dini zao. Huyu Mwananchi
anayewania URAIS ama
ubunge naye ana dini
yake. Inawezekana kweli
awe akiweza kutenga hisia
za dini yake pembeni kila
pale anapotakikana kutoa
maamuzi, kwa mfano
katika kutafuta maendeleo
ya wananchi wa nchi hii?
Kufuatana na matukio ya kila
siku na uzoefu unaopatikana
kwa kutafakari mazoea hayo
hakika ni mara nyingi hutokea
kiongozi, awe wa siasa ama
utawala, anapata ugumu
kuitenga dini yake pembeni
anapokuwa kazini. Ukweli
h u u h a s a u n a wa k u m b a
viongozi na watawala wasio
Waislamu. Kwa kutia mkazo
ukweli huu ilikuwa hata
ni tabia Hayati Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere.
Naye ametokea kukiri hivyo.
Tazama ukurasa 335 kitabu
DEVELOPMENT AND
RELIGION IN TANZANIA
alichokitunga JAN P van

BERGEN. Kama hayo


hayatoshi, Kanisa Katoliki
k i l a s i k u l i n a wa s h a u r i
waumini wake kuwapigia
k u r a wa u m i n i we n z a o .
Soma Ilani ya Uchaguzi
iliyotolewa na Makanisa
wakati wa uchaguzi Mkuu
uliopita. Makanisa wazi wazi
yalisisitiza kwa waumini
wao kufuata mafundisho
ya Yesu ya udugu. Hakika
katika nchi kama Tanzania
halitakuwa jambo la busara
kama udini uwe mwongozo
hata katika kupiga kura.
Lakini hapo hapo utakuwa
upungufu wa fikra kama
mpiga kura atasahau kabisa
k u wa wa g o m b e a wa n a
dini zao. Kwa vile katika
wale wanaogombea wasio
Waislamu ndio wengi, mara
zote itakuwa jambo la busara
kama mpiga kura Muislamu
atakumbuka hayo.
K wa k u wa k u m b u s h a
tu, hebu Muislamu mpiga
kura akumbuke jinsi gani
Bunge lilitupilia mbali ule
m s wa d a wa k u r u d i s h a
nchini zile Mahakama ya
Kadhi. Msomaji atakumbuka
kuwa waliopiga kura kuuwa
mswada ule na kwa nguvu
zao zote bila ya kuwa na
nguvu ya hoja hawakuwa
Wabunge Waislamu. Bahati
mbya zaidi ni kuwa idadi ya
hao wasiokuwa Waislamu ni
kubwa kiasi kwamba kabisa
kulikuwa hakuna tamaa ya
kupitishwa mswada ule.
Wasingeweza kupingana
na mahubiri ya mapadri na
wachungaji ambao wao siku
zote wanapinga maendeleo
kama hayo ya Waislamu
hata kama hayatoathiri
hata kidogo maendeleo ya
Kanisa. Baba Papa Leo XIII
aliyelitawala Kanisa Katoliki
kutoka 1878 mpaka 1903
alitamka kuwa:
Freedom and truth are
incompatible. Truth must be
enforced by the State (Vatican?)
by the Churchs command
whenever possible.
Yaani uhuru na ukweli
haviowani. Ukweli ni lazima
utiwe nguvu na utawala pia
amri ya Kanisa kila inapobidi
(kurasa 146-150, VICARS
OF CHRIST, The Dark Side
of Papacy by Peter de Rosa,
zamani akiwa Padre na
muhadhiri wa chuo Vatican).
Hii maana yake ni kuwa
Mbunge asiye Muislamu
atatekeleza yale aliyoambiwa
na kiongozi wake wa Kanisa.
Muhasham Mukombe
Polycarp Cardinal Pengo
amewahi kumwambia kama
hayo Muheshimiwa Rais
Jakaya Kikwete hadharani.
A g h l a b k u p i n g wa ya l e
anayohubiri padre ama
mchungaji.
Hapo hapo kabla
ya kupiga kura yake
itafaa Mwananchi huyu

kuchunguza mwenendo wa
huyo anayeisaka kura yake ili
awe Rais ama Mbunge. Wengi
wa wale wanaotafuta vyeo
vya kuchaguliwa wamekuwa
wanasiasa kwa muda mrefu
hivyo yale waliyoyafanya
ama waliyoyatetea kwa faida
ya wananachi yanajulikana.
Kwa hiyo itakuwa vizuri
kama mpiga kura atajiuliza
kweli huyo atakae kura
yangu atanisaidia huko
mbele hasa katika kuboresha
maisha yangu? Hayo maisha
yangu pia ya kiroho hasa
kama anavyotaka padre.
Kwa mfano wale wanapotaka
kupeperusha bendera ya
CCM katika kinyanganyiro
cha URAIS yumo Wairi
Mkuu aliyejiuzulu
Muheshimiwa Edward
L o wa s s a . M wa n a s i a s a
huyu anakwenda kwa kasi
sana, labda kwa sababu
alijitayarisha mapema sana
na kwa muda mrefu. Harakati
zake zilianza tu baada ya
kujiuzulu na iliashiria kuwa
alikuwa akitafuta makubwa
zaidi. Afrika yetu hii ni ya
ajabu. Mwanasiasa anaweza
kujiuzulu kutokana na kashfa
inayoendana na wadhifa
wake katika siasa za nchini
mwake, na bado akawa
na sifa za kutafuta kura
za wananchi akigombania
wadhifa mwingine wa siasa
pengine mkubwa zaidi ya ule
aliojiuzulu. Wengine wana
maoni kwamba aliyepata
doa kama hilo hastahili
kuingia tena katika ulingo
wa siasa. Kuna uhakika gani
kama hatarudia makosa
aliyoyafanya hapo nyuma
mpaka akajiuzulu.
Hata hivyo Muislamu
itabidi ajiukumbushe utendaji
k a z i wa M u h e s h i m i wa
Edward Lowasa huko nyuma.
Ni Muheshimiwa Lowassa
n d i ye ye ye a l i ye t i l i a n a
mkataba na Makanisa kuwa
Serekali itakuwa inatoa
ruzuku kubwa kwa Makanisa
wanapoendesha hule na
z a h a n a t i z a o . K wa m b a
Serekali kamwe haita ingilia
kati katika uendeshaji
huo hasa pale Makanisa
yatakuwa yanapata misaada
ya kifedha kutoka nje ya nchi.
Hiyo MEMORANDUM OF
UNDERSTANDING ilieleza
masharti hayo na kusisitiza
kuwa Serekali haitaingilia
kamwe katika utekelezaji
wake.
Huko nyuma Waislamu
wamekuwa wakiulalamikia
kwa sauti kali hiyo
MEMORANDUM OF
UNDERSTANDING
lakini hakuna aliyewajali,
hawajapata maelezo yeyote
kutoka Serekalini hadi leo.
Litakuwa si kosa kutabiri
kuwa akiufuma huo URAIS,
Muheshimiwa EDWARD
N G O N YA I L O WA S S A
atatekeleza kwa marefu na
mapana vipengele vyote
vya mkataba huo. Lakini
katika watakaompigia kura,
wamo walio Waislamu, nao si
wachache!! Sasa kura yangu
nimpigie nani?

14

Makala

RAMADHAN 1436, IJUMAA JULAI 10-16, 2015

Mauwaji ya Al-Shabaab tena Kenya


Inatoka Uk. 11

fidia ya Dola milioni


2. 5 (Us$ 2,500,000)
kama fidia ya
kuuliwa mumewe
katika usanii na
mzaha (hoax) huu
wa anthrax terror
attack. Fedha hizi
si sawa na uhai wa
mumewe. Lakini
imekuwa kama ishara
ya wahusika kukiri
kosa na kumuonea
huruma mjane huyo.
Labda tujiulize,
iwapo utakosekana
ushahidi madhubuti
wa kuwatia hatiani
Masheikh na
Wa i s l a m u a m b a o
wanashikiliwa kwa
zaidi ya miaka
miwili sasa, fidia
gani tutawalipa
Watanzania wenzetu
hao ambao ni kama
wapo kifungoni japo
hawajahukumiwa?
Lipo jambo moja
ambalo tunatakiwa
kulizingatia. Wiki
iliyopita tulielezea
kwa kirefu juu
ya mchezo wa
kutega watu ili
kuwakamatisha
ugaidi. Lakini
ifahamikie pia kuwa
katika kukoleza
jambo hili, hutokea
wakapatikana
vichaa ama kwa
kulipwa au kwa
akili zao mbovu,
wakafanya matukio
ya kweli. Na hivyo
wakikamatwa
w a n a k u w a
wamefanya kosa
la kweli. Na hawa
ndio mara nyingi
katika nchi kama
hii yetu, hutumika
kuleta chuki, fitna
na farka baina ya
jamii-Waislamu na
Wakristo ili mchezo
upate kunoga maana
hauwezi kwenda
tu kwa Sting
Operations, kama
ambavyo katika nchi
za Kiislamu au za
Waarabu hutumika
Sunni Vs Shia.
Katika mazingira

Dr. Bruce Edwards Ivins

Robert Steven.
h a y a , n c h i y e t u wanaotuhumiwa bila
h a i t a s a l i m i k a kujijua au kwa ujinga
k a m a t u t a i s h i a wao. Katika toleo
k u s h u g h u l i k a lililopita tulisema,
tu
na
h a w a tuwatizame akina
Mahmoud Omar na
hao wenye uwezo
wa kuandaa mizaha
ya kuchezea akili za
Leo Ijumaa ni tarehe 23 Ramadhani watu (psychological
1436 AH sawa na tarehe 10 Julai 2015.
Julai 17 mwezi wa Mfungo Mosi manipulation).
T u m a l i z i e
utaandama. Kutokea leo hadi kufikia
tulikoanzia.
Kenya
Mfungo Mosi tumebakisha siku 7
hivi sasa imeingizwa

Fatilia kuandama kwa Mwezi

AN-NUUR

katika mchezo wa
kifimbo cheza wa
kupigwa na magaidi.
Na kila likitokea
shambulio na watu
kuuliwa, haraka
haraka hudaiwa
kuwa ni Al Shabaab!
Kwa mifano hiyo
miwili ya Shambulio
la ugaidi wa kimeta
(Amerithrax) na
ile Operation
Cyanide, kuna
haja yanapotokea
mashambulizi
kama haya, kuweka
propaganda kando
na kulitizama
j a m b o k wa k i n a .
Kama alivyosema
Tony Cartalucci,
hii inayoitwa Vita
D h i d i ya U g a i d i
imegubikwa na
ulaghai mwingi
(The War on Terror
is a Fraud) ikilenga
kupepea masilahi
ya ubeberu na hasa
k i l e k i n a c h o i t wa
udhibiti wa duaniahegemony.
Katika ugaidi wa
Amerithrax, kachero
mmoja mstaafu
katika FBI aliwahi
kunukuliwa akisema:
They really wanted
to blame somebody in
the Middle East."
Kwamba katika
shambulio hilo la
ugaidi wa kimeta,
viongozie wa serikali
walikuwa wakitafuta
mtu wa Mashariki
ya Kati (Muarabu)
wa kumbambika
l a wa m a . ( Ta z a m a :
FBI was told to blame
Anthrax scare on Al
Qaeda by White House
officials-BY JAMES
GORDON MEEK
, D A I LY N E W S
WA S H I N G T O N
BUREAU, Saturday,
August 2, 2008)
Sasa
tuwe
makini isije haya
tunayoambiwa ya
Al Shabaab kuipiga
Kenya, na hii mizaha
inayoanza kujitokeza
mara kwa mara katika
nchi yetu, ikawa ni
yale yale, wanatafuta
Wa i s l a m u wa
kuwabambika ugaidi
kutimiza malengo
yao katika nchi zetu.

Jee Unajua?

1. W a a f r i k a
waliojipatia umaarufu duniani
ni: Nelson Mandela, Kwame
Nkrumah, Robert Mugabe,
Julius Nyerere, Marcus Garvey,
Patrice Lumumba, Martin
Luther King, Thabo Mbeki,
Malcolm X, Kofi Annan,
Muhammad Ali, Steve Biko,
Muammar Gaddafi, Winnie
Mandela, Shaka Zulu, Chinua
Achebe, W. E. B. Du Bois, Haile
Selassie , Thomas Sankara,
Pele, Bob Marley, Olusegun
Obasanjo, George Weah.
2.Nchi ziliomo katika
ukanda wa Sahel ni: Senegal,
K u s i n i m wa M a u r i t a n i a ,
Mali ya kati, Kaskazini mwa
Bu r k i n a F aso, Ku si n i ya
Algeria, Niger, Kaskazini ya
Nigeria, Sehemu ya kati ya
Chad, Kusini na kati ya Sudan
pamojana Kaskazini mwa
Eriteria. Sahel inaonekana
kuanzia Magharibi ya Afrika
hadi Mashariki ya Afrika.
3.Wanachama wa SADC
ni nchi zifwatazo : Angola,
Botswana, Democratic
Republic of Congo, Lesotho,
Madagascar , Malawi,
Mauritius , Mozambique,
Namibia, Seychelles, South
Africa, Swaziland, United
Republic of Tanzania , Zambia
na Zimbabwe.
4.Nchi za visiwa vidgo
duniani (Small Island
Developing State): AIMS
(Atlantic, Indian Ocean and
South China Sea):Cape Verde,
Comoros, Guinea-Bissau,
Maldives, Mauritius, So
Tom and Principe, Seychelles,
Singapore. Caribbean region:
Antigua and Barbuda,
Bahamas, Barbados, Belize,
Cuba, Dominica, Dominican
Republic, Grenada, Guyana,
Haiti, Jamaica, Saint Kitts
and Nevis, Saint Lucia, Saint
Vincent and the Grenadines,
Suriname, Trinidad and
T o b a g o . Pa c i f i c r e g i o n :

Cook Islands, Fiji, Kiribati,


Marshall Islands, Federated
States of Micronesia, Nauru,
Niue, Palau, Papua New
Guinea, Samoa, Solomon
Islands, Timor-Leste, Tonga,
Tuvalu, Vanuatu.
5.Visiwa vikubwa
duniani: Greenland, New
Guinea, Borneo, Madagascar,
Baffin, Sumatra, Great
Britain, Honshu, Victoria,
Ellesmere.
6 . M i t o ya T i g r i s n a
Euphrates inapakana na nchi
zifwatazo: Uturuki, Syria,
Iraq, Iran na Kuwait.
7.Urusi ndio nchi pekee
duniani iliopakana na nchi
nyingi zikiwemo: Azerbaijan,
Belarus, China (S), China (SE),
Estonia, Finland, Georgia,
Japan, Kazakhstan, Latvia,
Lithuania, Mongolia, North
Korea, Norway, Poland,
Ukraine, USA inapakana
nayo kwenye sehemu ya
maji.
8.Nchi
ambazo
zinapakana na nchi mmoja tu
katika mpaka wao Gambia na
Senegal, Haiti na Dominican
Republic, Ireland na United
Kingdom na Lesotho na
Afrika ya Kusini, Cyprus
naAkrotiri and Dhekelia
(UK), Dominican Republic
na Haiti, Denmark na
Ujerumani, Monaco na
Ufaransa, Papua New Guinea
na Indonesia, Qatar na Saudi
Arabia, Ureno na Uspani, San
Marino na Utaliana, Korea ya
Kusini na Kaskazini, TimorLeste na Indonesia, Vatican
City na Utaliano.
9.Nchi za Kiafrika
zisopakana na bahari
(landlocked countries)
Burkina Faso, Burundi,
Central African Republic,
Chad, Mali, Niger, Rwanda,
Uganda, Ethiopia, South
Sudan. Botswana, Malawi,
Zambia, Zimbabwe.

MAJIBU YA CHEMSHA BONGO NAMBA: 13


D

22

10

CHEMSHA BONGO NAMBA: 14


Weka duara kwenye jawabulio sawa. Jawabu kamili
wiki ijayo.
C
A
N
A
D
A
B
S
F
V
B

M
U
A
M
I
N
I
F
U
A
U

25
45
70
R
G
N
M
Y
E
W
Q

40
G
U
I
N
E
A
P
A
L
M

50
A
U
S
T
R
A
L
I
A
A

A
B
Y
S
S
I
N
I
A
S
L

N
A
J
A
S
H
K
V
T
S
I

T
A
N
Z
A
N
I
A
K
E
N

N
G
A
M
I
A

K
A
Z
A
K
H
A
S
T
A
N

A
N

C
H

T
I
C
P
A
A

I
N
D
A
A
J

Masuala
1.
Ilikuwa sifa gani kubwa ya Mtume SAW kwa
Makureshi? Muaminifu
2.
Mtume SAW alipomuoa Bibi Khadijah umri wake
ulikuwa ni miaka mingapi?
3.
Mtume SAW alipopewa Wahyi kwa mara ya
kwanza alikuwa na umri wa miaka mingapi?
4.
Hijra ya kwanza Waislamu walikwenda wapi?
5.
Mfalme wa Abyssinia ambaye Waislamu
walikutana naye akiitwa nani?
6.
Watu wa Mtume Saleh walimuua mnyama gani?
7.
Nchi gani iliokuwa na masafa ya kilomita za mraba
2,724,900(km2) na idadi ya wakaazi 16,372,000 ndio nchi
iliokubwa kuliko zote kutokuwa na bahari?
8.
Jangwa (Desert) 10 yaliokuwa na ukubwa kabisa
duniani ni : Antarctic Desert.
9.
Nchi yenye wakazi wengi duniani ni.
10.
Nchi ipi ina bajeti kubwa ya kijeshi duniani?

15

TANGAZO

AN-NUUR

RAMADHAN 1436, IJUMAA JULAI 10-16, 2015

BISMILLAHI RAHMANI RAHIIM

ISLAMIC PROPAGATION CENTRE

KIRINJIKO ISLAMIC TEACHERS COLLEGE


(NA.YA USAJILI WA NACTE-REG/TLF/078

P.O. Box 62, Same Kilimanjaro, Mob: 0657 705 878

NAFASI ZA DIPLOMA YA UALIMU WA SHULE ZA MSINGI


2015/2016

Waislamu Kote NchiniWaislamu


Mnatangaziwa
Nafasi za
Mafunzo ya Diploma
na NACTE
au VETA
ufaulu
Kote Nchini
Mnatangaziwa
Nafasi zakinachotambulika
Mafunzo ya Diploma
ya Ualimu
wana
Shule
zawa D nne katika mtihani
ya Ualimu wa Shule za Msingi katika Chuo cha Ualimu Kirinjiko Islamic
wa kidato cha nne (CSEE).
kilichopo Same Mkoani Kilimanjaro.
B: NAMNA
YA KUOMBA:
Msingi katika Chuo cha Ualimu Kirinjiko Islamic kilichopo
Same
Mkoani Kilimanjaro.
Chuo kimepata usajili kamili wa NACTE na kinaendeshwa kwa misingi
1. Mwombaji anatakiwa kujaza fomu ya maombi AU
na maadili
ya Kiislamu.
na maadili ya Kiislamu. Chuo kimepata usajili kamili wa NACTE na kinaendeshwa
2. Kuombakwa
kwamisingi
njia ya mtandao
(Online
Application) kupitia Tovuti ya
NACTE(www.nacte.go.tz).
A: SIFA ZA MWOMBAJI:
TANBIHI: Atakayeomba kwa njia ya fomu, hatatakiwa kuomba kupitia
1. Awe Muislamu na; A: SIFA ZA MWOMBAJI:
njia ya mtandao wa NACTE.
2. Amehitimu kidato cha nne (CSEE) na kufaulu kwa kiwango cha Division
1. Awe Muislamu na;
I-III au GPA.1.6, AU
D: ADA YA MAOMBI:
3. Mwenye cheti cha Grade IIIA, AU
Ada ya maombi ya NACTE ni shilingi elfu ishirini (20,000/=) tu.
2. level
Amehitimu
cha nne
(CSEE)
na chuo
kufaulu kwa
kiwango
Division
I-III au GPA.1.6,
4. Mwenye cheti (NVA
4) cha kidato
kozi yoyote
kutoka
katika
C: MWISHO
WAcha
KURUDISHA
FOMU:
Mwisho wa kurudisha fomu za maombi ni tarehe 15/08/2015.

AU

Fomu za Maombi zinapatikana chuoni Kirinjiko Islamic Teachers college na katika vituo vilivyoorodheshwa hapa chini.
3. Mwenye cheti cha Grade IIIA, AU
705627.
Karume,Nyumba Na. 05 :
Arusha: Ofisi ya Islamic
4. Mwenye
cheti
(NVA
level
4)
cha
kozi
yoyote
kutoka
katika
chuo
kinachotambulika
NACTE
Mtwara:
Amana Islamic S.S:na
0715
0765024623
Education Panel, Jambo
465158/
231007.
Msikiti mtihani
wa Majengo
Plastic,au Ghorofa
2 waShinyanga
VETA naya
ufaulu
D nne katika
wa kidato cha
nne0787
(CSEE).
Songea: Kwa Kawanga Karibu na
karibu na Manispaa ya
mkabala na msikiti Mkuu
B: NAMNA
Shinyanga
Mjini
Bondeni YA KUOMBA::
Msikiti
wa
NURU
:
:0752180426
Kahama
ofisi
ya
0783552414/0762817640
0713249264/0683670772.
1. Mwombaji anatakiwa kujaza fomu ya maombi AU
AN NUUR Karibu na msikiti
Kilimanjaro: Moshi: Msikiti wa
Mkuzo Islamic High School
2. Kuomba
kwa njia
ya mtandao (Online
Application)
kupitia Tovuti
ya 348375.
wa
Ibadhi
: 0753
Riadha :712
216490Same
:0717
993930/0688794040
Juhudi Studio mkabala na
Mbeya: Ofisi za Islamic Education
NACTE(www.nacte.go.tz).
Dar es Salaam: Ubungo Islamic
Benki ya NMB Same: 0757
Panel
Uhindini

High ya
School
: hatatakiwa kuomba kupitia
013344. Atakayeomba kwa njia
0785425319.
Rexona Video
TANBIHI:
fomu,
njia ya mtandao
wa
0756584625/ 0657350172
Same: Kirinjiko Islamic Secondry
mkabala na Mbeya RETICO:
NACTE.
School: 0784 296424/0655 Ofisi ya Islamic Ed. Panel
0713 200209/0785425319.
697 075, Usangi- Falhum Temeke -Msikiti wa Nurul Ya
Rukwa :Sumbawanga:Jengo la
kin :
Kibakaya : 0787 142054.
Haji Said Shule ya Msingi
D: ADA
YA MAOMBI:
Ugweno
Kifula Shopping 0655144474/0787119531
Kizwike 0717082 072.
Morogoro
Wasiliana
na
Centre- Yusuph Shanga :
Tabora: Kituo cha Kiislamu
Ramadhani
Chale
:
078458776.
Isevya:
0784
0715704380.
Tanga: Twalut Islamic Centre
944566/0787237342
Dodoma Hijra Islamic Primary
Mabovu Darajani : 0715
Nzega:
Dk
Mbaga-0754
School : 0716 544757/071
894111 Uongofu Bookshop:
576922/0784576922.
Singida: Ofisi ya Islamic
0784 982525, Korogwe:
Iringa: Madrastun Najah: 0714
Education. Panel karibu na
SHEMEA SHOP : 0754
522 122.
Nuru snack Hotel : 0786
690007/071569008. Mandia
Pemba: Wete: Wete Islamic
425838/0784 928039.
Shop - Lushoto: 0782257533.
School
:
0777
Manyara: Ofisi ya Islamic Ed.
Handeni Mafiga -0782
432331/0712772326.
Panel Masjid Rahma:
105735/0657093983
Unguja : Madrasatul Fallah:
0784491196
Mwanza
Nyasaka
Islamic
0777125074.
PANDU
Kigoma: Msikiti wa Mwandiga:
Secondary School : 0717
BOOKSHOP
0777462056
0714717727 Kibondo
417685/0786 417685.Ofisi ya
karibu na uwanja wa
Islamic Nursery School:
Islamic Education Panel
Lumumba
0766406669.
Kasulu:
Mtaa wa Rufiji mkabala na
Mafia: Ofisi ya Ust. Yusufu Ally
Murubona
Isl.SS:
Msikiti Al-Amin 0785 086
jirani na msikiti mkuu :
0714710802.
770/0714097362
0773580703.
Lindi Wapemba Store: 0784
Musoma Ofisi ya Islamic Ed
974041/0783 488444/0653
Panel
-Mtaa
wa
Kwa maelezo zaidi piga simu: 0787 188964, 0784 267762 na 0654 613080

16

AN-NUUR

MAKALA/RATIBA YA MFUNGO
Na Ben Rijal

Matukio ya Mwezi wa Ramadhani-Vita vya Badr-3


hata kama hakuuliza yeye basi
angalie kama kuna maslahi,
hana budi kuliwafiki. Na
Mtume SAW sio alikubali rai
ya Masahaba kwenye vita
hivi tu, bali ilikuwa ndio
khulka yake kushauriana na
anaowaongoza. Alizijali rai za
masahaba wake. Kuchukua
rai za mtu anawaongoza ni
kufata nyao za Mtume SAW.
Funzo jengine ni
k u s i m a m i s h a d i n i k wa
kujitolea. Haya tunayaona
namna
Waislamu
walivyokuwa imara
kutomuacha kiongozi wao
peke yake, bali walikuwa nae
bega kwa bega kuhakikisha
wanainusuru dini ya Mola
wao mbali ya uchache wao
n a k u t o k u wa n a s i l a h a
z a k u t o s h a . Yo t e h a ya
waliyasahau na kuangalia

moja tu, la kumnusuru


Mtume SAW na makafiri.
Waislamu wa wakati huu
hatunae Mtume SAW, lakini
moja ya njia ya kuinusuru dini
hii na kumnusuru Mtume
SAW na maadui ni kufuata
maarisho yake na miongozo
yake katika harakati zetu
zote.
Funzo jengine ni kuwa
ushindi unatokana na imani,
ndio ilivyokuwa katika
vita hivi. Imani thabiti ya
Masahaba ilikuwa kubwa
kwa Mola wao kuwa
atawanusuru pia kuwa kwao
tayari kutii amri za Mtume
SAW. Kwa kufanya hivyo
ndio nusura ikawafika. Laiti
wangelikuwa waasi, basi
wasingeliupata ushindi kama
huu kwani siri ya ushindi
ni kutakasa nyoyo na kila

KALENDA YA RAMADHANI
Mwaka 2015

machafu na kuwa na imani


thabiti.
Aidha, kuna funzo ambalo
Mtume SAW alilolifanya
ambalo kwa miaka ya sasa
lipo kinyume kabisa. Katika
vita vya mmoja mmoja,
Mtume SAW aliwatoa wale
ambao wa ukoo wake na
kuhakikisha ndio watakao
anza mapambano. Leo kila
alio wako utamtaka awe
nyuma na kuwasukuma
mbele wale waliokuwa sio
wako.
Vita vya Badr ni chuo
ambacho kimejaa mafunzo
pomoni. Ilivyokuwa
vimepiganwa katika mwezi
hu wa Ramadhani, tujitahidi
kujifunza na kuelewa falsafa
ya k e n a k u t o o n a k u wa
Waislamu katika dunia hii
tunaonewa, wakati idadi
yetu ipo kubwa kinyume
waliopigana vita vya Badr
walikuwa wachache wa idadi
na wingi wa imani. Tuliopo
sasa ni wengi wa idadi na
wachache wa imani.
KALENDA YA RAMADHANI
Mwaka 1436H

1.

Enyi Mlioamini! Mmelazimishwa kufunga (Saumu) kama walivyolazimishwa waliokuwa kabla


yenu ili mpate kumcha Mungu. Kuran 2:183

2.
3.

Na (huku) kufunga ni bora kwenu. Ikiwa mnajua. Kuran 2:184


Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi (atimize) hisabu (ya siku alizowacha kufunga)
katika siku nyengine Mwenyezi Mungu anakutakieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo
mazito. Kuran 2:185.
Vile vile Bwana Mtume (S.A.W) kasema:Kila kitu kina Zakka, na Zakka ya mwili ni saumu.
Anaefunga Ramadhani kwa Imani na kuzingatia (basi) hufutiwa madhabi yake yote
yaliotangulia. Na kama mngelijua faida iliomo katika Ramadhani, basi mngetamani Ramadhani
iwe mwaka mzima.

4.
5.

JJ
SIKU

JUNE
JUNE
JUNE
JUNE
JUNE
JUNE
JUNE
JUNE
JUNE
JUNE
JUNE
JUNE
JUNE
JULAI
JULAI
JULAI
JULAI
JULAI
JULAI
JULAI
JULAI
JULAI
JULAI
JULAI
JULAI
JULAI
JULAI
JULAI
JULAI
JULAI

18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17

ALKHAMIS
IJUMAA
JUMAMOSI
JUMAPILI
JUMATATU
JUMANNE
JUMATANO
ALKHAMIS
IJUMAA
JUMAMOSI
JUMAPILI
JUMATATU
JUMANNE
JUMATANO
ALKHAMIS
IJUMAA
JUMAMOSI
JUMAPILI
JUMATATU
JUMANNE
JUMATANO
ALKHAMIS
IJUMAA
JUMAMOSI
JUMAPILI
JUMATATU
JUMANNE
JUMATANO
ALKHAMIS
IJUMAA

DUA YA KUSOMA UNAPOANDAMA MWEZI

MUDA
WA
MWISHO
KULA
DAKU
(IMSAK)
11:02
11:02
11:02
11:02
11:02
11:03
11:03
11:03
11:03
11:04
11:04
11:04
11:04
11:04
11:04
11:05
11:05
11:05
11:05
11:06
11:06
11:06
11:06
11:06
11:06
11:04
11:05
11:05
11:06
11:06

KUINGIA
ALFAJIRI
ADHANA

KUCHWA JUA
JIONI

ADHANA YA
MAGHARIBI
KUFUNGUA
(IFTAR)

11:17
11:17
11:17
11:17
11:17
11:18
11:18
11:18
11:18
11:19
11:19
11:19
11:19
11:19
11:19
11:20
11:20
11:20
11:20
11:21
11:21
11:21
11:21
11:21
11:21
11:19
11:20
11:20
11:21
11:21

12:17
12:17
12:17
12:17
12:18
12:18
12:18
12:18
12:18
12:19
12:19
12:19
12:19
12:19
12:19
12:20
12:20
12:20
12:20
12:21
12:21
12:21
12:21
12:21
12:21
12:21
12:22
12:22
12:23
12:23

12:22
12:22
12:22
12:22
12:23
12:23
12:23
12:23
12:23
12:24
12:24
12:24
12:24
12:24
12:24
12:25
12:25
12:25
12:25
12:26
12:26
12:26
12:26
12:26
12:26
12:26
12:27
12:27
12:28
12:28

ALLAHUMMA INNAKA AFUWWUN TUHIBBU-L-AFUA


FAAFU ANNA YAKARIMA L-AFUA

TAREHE

1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30

MWEZI

DUA YA KUSOMA UNAPOFUNGUA


ALLAHUMA LAKA SUMTU WAALA RIZKIKA AFTARTU
NIA YA KUFUNGA
"NAWAYTU SAWMA GHADIN AN ADAI FARDHI SHAHRI RAMADHAN HADHII SSANATA LILAHI TAALA IMANAN WAHTISABAN
LIWAJHI LAHIL KARIM AZAA WA JAALA"

RAMADHANI KARIM

RAMADHANI KARIM

na ikaweza kuleta ushindi


wa haraka.
Matokeo Bada ya Vita
Vita hivi waliuliwa
viongozi wengi wa makafiri
ikawa idadi ya waliouliwa
katika makafiri ni 70 na
mateka wakawa 70, upande
wa Waislamu waliuliwa
14 kati ya hao 6 wakiwa
Muhajirina na 4 wakiwa
katika Maansari.
Kwisha kwa vita Mtume
SAW akamtuma mjumbe
kwenda kupeleka Madina
habari za ushindi, kisha
akawakusanya mateka na
akawauliza Masahaba zake
nini awafanye kwa kuwa
Wa h y i h a u k u t e r e m k a
wakati huo. Syd Abubakar
akatoa rai kuchukuliwe fidia
kisha waachwe huru kwani
huwenda siku za mbele
wakasilimu, Syd Umar kwa
upande wake alipendekeza
wa k a t w e v i c h w a w o t e
a s i b a k i m t u k a a t i ya o .
Mtume SAW akachukua
rai ya Syd Abubakar na
a k a wa t a k a wa l e we n ye
uwezo wajikomboe na wale
wasio kuwa na fedha wenye
kujuwa kusoma na kuandika
wawasomeshe Waislamu
mpaka watapohitumu
kusoma na kuandika ndio
kitakuwa kikombozi chao
chakuwa huru.
Baada ya muda ikaja aya
ambayo iliwafiki rai ya Syd
Umar. Hata hivyo, rai ya
Umar ndiyo ilikuwa sahihi
iliteremka baadae badae aya
kufahamisha Mtume kuwa
ikuwa asichukuwe fidia bali
alikuwa awauwe.
Haimfalii Nabii yeyote
kuwa na mateka mpaka awe
ameshinda barabara katika
nchi. Mnataka vitu vya dunia,
na Mwenyezi Mungu anataka
Akhera. Na Mwenyezi
Mungu ni Mtukufu Mwenye
nguvu Mwenye hikima.
(8:67)
Lau isingeli kuwa
hukumu iliyo kwisha
tangulia kutoka kwa
Mwenyezi Mungu, ingeli
kupateni adhabu kubwa kwa
vile mlivyo chukua. (8:68)
Basi kuleni katika mlivyo
teka, ni halali na vizuri, na
mcheni Mwenyezi Mungu.
Hakika Mwenyezi Mungu
ni Mwenye kusamehe na
Mwenye kurehemu. (8:69)
Mafunzo Yanayopatikana
Mafunzo ynayopatikana
katika vita hivi ni mengi
mno baadhi yao ni kama
ifwatavyo: Kiongozi
kutojiamulia tu kujiona kuwa
ni kiongozi, lakini kiongozi
hutakiwa kuchukua ushauri
kwa anawaongoza na kama
atapewa ushauri wa jambo

RAMADHA
NI YA:

KATIKA sehemu ya kwanza


ya makala hii, tulifafanua
juu ya Vita vya Badr kuwa
ni vita vya mwanzo vikuu
katika tarehe ya Uislamu,
vikiwa vita baina Waislamu
na Makafiri. Vita hivi ni
kielelezo kikubwa kwa
Waislamu kuelewa kuwa
hakuna kinachoshindikana
kama imani zao zitakuwa
zimefungamana kikweli
ushindi utapatikana tu.
Katika sehemu hii ya
mwisho, tunaelezea hali
ilivyokuwa vitani hadi
Waislamu kupata ushindi.
Kuanza kwa Vita
Kabla ya kuanza vita,
Mtume SAW akalipanga
jeshi lake kisha akawasomea
h o t u b a n a k u wa k a t a z a
kuwauwa badhi ya makafiri
na akawataja kwa majina
akiwemo bwana Abbas
ami yake Mtume SAW na
hii inatokana na kujuwa
kwake Mtume kuwa hao
wa m e t o k a n a k u f wa t a
rubaa kwa kuwaonea haya
makafiri lakini hawakuwa
tayari kwenda kupigana na
Waislamu.
Mtume akawambia
m w e n y e k u u l i wa l e o
katika vita hivi hali yakuwa
amepigana kwa kutaraji
thawabu, basi ataingiaa
peponi.
M a n e n o
h a y o
yaliwashajiisha Waislamu
hapo tena vita vikaanza
kama kawaida ya Warabu
k a t i k a m a p a m b a n o ya
siku hizo, vita huanza kwa
kupambana mmoja mmoja
kutoka kila upande kisha
ndio vita hupamba moto.
U p a n d e wa M a k a f i r i
walitoka wapiganaji 3 akiwa
Utbah bin Rabiah na ndugu
yake aitwaye Shaaiba bin
Rabiah na mwanawe aitwae
Walid bin Utbah bin Rabiaah.
Kwa upande wa Waislamu
Mtume SAW akawachagua
Hamza bin Abdul Muttalib
ami yake Mtume SAW,
kisha Syd Ali bin Abi Talib
mtoto wa ami yake Mtume
na wa mwisho alikuwa ni
Ubaidah bin Harith ikiwa
wote hao watu wa Makka na
wanakutana kiukoo.
Mtume aliwachaguwa
hawa baada ya kuwarejesha
Maansari waliojitokeza ili
mapambano yaanze kwa
ndugu kwa ndugu. Hamza
akamuuwa Shaibaah wakati
Syd Ali akamuua Waliyd
ama Ubaaydah alipambana
na Harith mapambano yao
yalikuwa makali na Ubaydah
alijeruhiwa vibaya ndipo Syd
Hamza akamaliza Harith
na kumchukuwa Ubaydah
h a d i k w a Wa i s l a m u .
Makafiri baada ya kuona
wa m e s h i n d wa n j i a h i i ,
wakaamua kuanza vita kwa
pamoja na Mtume alikuwa
ashawaandaa watu wake
namna ya kupambana akiwa
amewaweka wapiganaji kwa
safu, wapiganaji wa mishale
wa mikuki, mbinu hii ilifana

RAMADHAN 1436, IJUMAA JULAI 10-16, 2015

17
Na Bakari Mwakangwale

ALHAMDULILLAH,
kila sifa njema anastahili
Mola wa Ulimwengu,
bila shaka kila
aliyejaaliwa afya njema
sasa anahesabu kuwa
yupo katika kumi la pili
la Ibada ya Mwezi wa
Ramadhani.
Ama wale ambao
hawakujaliwa kuudiriki
Mwezi huu au kumi hili,
kutokana na dharura
zinazokubalika, Allah
(s.w) awape subra na
a f ya n j e m a , n a wa l e
waliotangulia mbele ya
haki Mwenyezi Mungu
awarehem.
Na mwenye kuwa
mgonjwa au safarini, basi
(atimize hesabu) katika
siku nyingine 2: 185.
Qur an, inasema,
kila mwenye kumcha
Mwenyezi Mungu,
a t a k u wa n i m w e n y e
kufuzu, hii ni amri
ambayo ipo siku zote na
ni wajibu kuifuata katika
mwenendo wa maisha
yetu ya kila siku.
Pamoja na kwamba
amri hiyo ipo siku zote,
lakini uchaji Mungu,
umekithirishwa zaidi
ndani ya Mwezi huu
Mtukufu wa Ramadhani.
Na sasa tupo katika
Mwenyezi wa Ramadhani.
Ibada ambayo imechukua
nafasi ya nguzo ya nne
katika jumla ya nguzo
tano za Uisalamu.
Wenye kudarasisha na
wenye kutoa mawaidha
sehemu mbalimbali
hivi sasa, wengi wao
wanauelezea mwezi huu
kuwa ni kama Chuo kwa
Waislamu, na kwamba
malipo na matarajio yake
baada ya hapo, ni kupata
cheti cha kuwa Mcha
Mungu.
Swali la kujiuliza ni
kwa nini lengo la funga
halifikiwi kwa wafungaji
walio wengi, mara baada
ya kumalizika au kutoka
katika Chuo funga ya
Ramadhani.
Uhalisia na mwenendo
wa Wa i s l a m u w e n g i
kuonyesha kwamba
h a wa j a f i k i a l e n g o l a
f u nga ( Ucha-Mun g u)
hujipambanua kutokana
na matendo yao, unaweza
ukajiuliza hivi kweli huyu
ndiye yule aliyekuwa
katika ibada ya Swaumu,
kwa muda wa siku 29
mpaka 30.
Binafsi, naona lipo
tatizo la jumla ambalo
linahitajika kufanyiwa

MAKALA

AN-NUUR

RAMADHAN 1436, IJUMAA JULAI 10-16, 2015

Kwa nini lengo la swaumu halifikiwa?

AMIR wa Baraza Kuu, Sheikh Mussa Kundecha akizungumza na waumini katika


moja ya makongamano ya kuelimishana juu ya kuujua Uislamu.
kazi na viongozi wetu wa
Dini, kwamba ipo haja ya
kuwaelimisha Waislamu
malengo ya ibada,
(hususani nguzo tano za
Uislamu) ili tuweze kufikia
malengo yaliyokusudiwa
na Mwenyezi Mungu kwa
Waislamu (kupitia nguzo
hizo).
Na hili ni tatizo la
viongozi wetu Masheikh,
Maimamu, Maustadhi
pamoja na wanazuoni,
kwamba wameacha
jukumu lao la kuwaelimishi
maamuma juu ya swala
zima la ibada hii, mapema
kabla ya kuingia kwake
kwamba wakiwa ndani
ya Swaumu ni yepi
hawatakiwi kuyafanya na
wajipambe kwa yepi ili
waweze kufikia lengo la
funga, na si hivyo tu, bali
waelimishe juu ya alengo
la ibada kwa ujumla, hasa
katika zile Nguzo Tano za
Uislamu.
Kama nivyotangulia
kueleza hapo juu kuwa
tatizo la msingi ni
Wa i s l a m u k u t o k u w a
na elimu ya Swaumu
kwa kuwa Masheikh,
wameacha jukumu lao
la kuelimisha Waislamu,
hivyo lengo haliwezi
kufikiwa kwa sababu
miongoni mwa Waislamu
hudiriki kuupokea mwezi
kwa maaswi bila kujua
kuwa hilo ni tatizo kwa
mustakabali wa funga
yake.
Maaswi hayo hubebwa

na kitu kinachoitwa vunja


jungu, ambapo baadhi ya
Waislamu wanaotarajia
kufunga huyapupia
maovu kuanzia mwezi 25
- 30 Shaaba, hili ni tatizo
ni ngumu kufikia lengo
lililokusudiwa. Na sioni
juhudi zozote za dhati za
kuliondoa tatizo hili na
njia rahisi ya kuliondoa ni
elimu kwa Waislamu.
Lakini Waislamu hao
hao baada ya kuingia
katika funga ya Ramadhani
hawazingatii yale
yanayobatilisha funga,
kwani hujihusisha na
mambo ya laghwi (Upuuzi)
kama vile kucheza karata,
bao, kupiga porojo kwa
dhana kuwa wanakazia
swaumu.
Labda wewe uliye
jaaliwa kuwa na elimu
sahihi ya Swaumu, jaribu
kufanya utafiti mdogo tu
kwa Waislamu wasiozidi
kumi ama Msikitini au
katika mtaa wako utabaini
kile ninacho kielezea hapa.
Wa i s l a m u w e n g i ,
wanazingatia kuwa
Swaumu ni kutia nia na
kujizuilia na kula (kuanzia
alfajiri mpaka magharibi).
Alhamdulillah, kwa hili
linalofahamika kwa kila
Muislamu.
Lakini Muislamu huyu
hana elimu ya kufahamu
ni yepi yanayoharibu au
yanayopunguza thamani
ya funga yake, ukiachilia
mbali yale ya msingi

yanahusiana na kula na
kunywa mchana, jimai
nakadhalika.
Yanayoharibu funga
au thamani yake, yapo
mengi ambayo wengi
wanayachukulia ni
mambo ya kawaida tu,
kama vile kusema uongo,
kusengenya (kupo kwa
aina nyingi), unaweza
ukafanya matendo haya
na ukajiona bado upo
katika swaumu kwa kuwa
mfungaji anakuwa hajala
wa hajanywa.
Abuu Hurairah (r.a)
ameeleza kuwa Mtume
wa Allah (s.w) amesema:
Yoyote yule ambaye
hataacha mazungumzo
mabaya na vitendo viovu,
Allah (s.w) hana haja na
kuacha kwake chakula
chake na kinywaji chake
(Allah (s.w) hatopokea
funga yake)-Bukhari.
Ni vigumu kujua
matendo ya ndani
ya mtu na hakuna
m t u a t a k a ye k u a m b i a
umefungua kwa kufanya
vitendo viovu, lakini wewe
mwenyewe unatakiwa
kujihesabu kuwa
hukupata kitu kutokana
na funga yako, na hii
inahitaji elimu ya imani
zaidi, ambayo Waislamu
wengi hawatuna.
Mtume (s a w)
anatufahamisha katika
hadithi: Abuu Huraira
ameeleza kuwa Mtume wa
Allah amesema: Ni watu

wangapi wanaofunga,
lakini hawana funga ila
huambulia kiu tu.
(Darimi).
Lakini hata ugomvi pia
au kuhitarafiana na kuingia
katika mzozo, jambo
ambalo linaonekana ni la
kawaida sana linapelekea
mtu kuharibu swaumu
yake au kuitia dosari, kwa
mwenye kujua hili basi
hujiepusha na kuilinda
funga yake kwa kusema,
Nimefunga, nimefunga
Kama ambavyo
hadithi ya Mtume (s a
w) inavyofafanua suala
hilo: Abuu Hurairah (r.a)
ameeleza kuwa Mtume (s a
w) amesema:Wakati mmoja
wetu atakapo amka akiwa

amefunga, asitumie
au asitoe lugha chafu
na asifanye matendo
maovu, na kama yeyote
yule anamchokoza
au anagombana
naye, hana budi
kusema: Nimefunga,
nimefunga.
Sasa ni wazi kuwa
k a m a i t a k u wa u m o
katika swaumu na vitu
kama hivi mfungaji
hujiepushi navyo,
kamwe kulifikia lengo la
swaumu, kwa maana ya
kukuacha katika kufuzu
kuwa Mcha Mungu ni
ndoto.
Jambo ambalo hutoa
picha kuwa lengo la
f u n g a h a l i j a f i k i wa ,
a n g a l i a i l e s i k u ya
Sikuku ya Idd-Fitrti,
Wa i s l a m u w e n g i
huingia kwa fujo katika
maovu mbalimbali kwa
dhana kuwa sasa wapo
huru kufanya yale yote
ambayo walijizuilia kwa
muda wa mwezi mzima.
Hivyo basi ni jukumu
la wadau wa Dini ya
Kiislamu kulitambua hili
kuwa swaumu haifikiwi
lengo lake kutokana na
Waislamu kutokuwa na
elimu ya ibada hii.
Wa i s l a m u w e n g i
wanaingia katika ibada
mbalimbali kama
mazoe, mfano Muislamu
anafunga kutokana na
mazoea kwa kuwa yeye
ni Muislamu ili apate
swawabu, ama anaswali
ili apate swawabu, na
anakwenda kuhiji Makka
ili aitwe Alhaji, fulani.
Waislamu tubadilike,
t u z i f a n ye i b a d a k wa
ikhlasi na kwa kuzingatia
malengo yaliyokusudiwa.

18
Na Abuu Nyamkomogi
NI kwa nini lengo
la funga halifikiwi?
Hili ni swali ambalo
linapaswa tujiulize. Na
katika makala yangu
iliyotangulia, nilijaribu
kuelezea dhana ya vunja
jungu kuwa hii yaweza
kuwa moja ya sababu.
Hata hivyo, tukiangalia,
hata wale ambao
h a wa i n g i i n a k u t o k a
katika Ramadhani kwa
Vunja Jungu, bado
hatuoni funga zao kuwa
na athari na matokeo
yaliyotarajiwa. Kwanini?
Kwa walioshikamana na
'vunjajungu', zipo sababu
kadhaa zinazowafanya
wasiweze kufikia lengo la
funga ya mwezi mtukufu
wa Ramadhani, miongoni
mwazo ni pamoja na
zifuatazo:
Mosi, kutofahamika
kwa fasili au maana halisi
ya dhana ya swaumu
au funga kwa baadhi ya
wafungaji. Ebu jaribu
kuutalii mfano huu halisi
wa dereva wa daladala
na kondakta wake kwa
makini ili uweze kumaizi
ninachokimaanisha katika
nukta hii.
Kulipata kutokea katika
mojawapo ya Ramadhani
ya mwaka fulani huko
n y u m a k o n d a k t a wa
daladala fulani, iliyokuwa
ikifanya safari zake kati ya
Mwanza mjini na Kiwanja
cha Ndege (Airport)
cha jijini humo, kutoa
mfululizo wa maneno
machafu dhidi ya abiria
wake mmoja katika
majibizano naye kiasi
kilichomfanya dereva
wake ashindwe kuvumilia
h a l i i l e n a h a t i m a ye
kudiriki kumkumbusha
k o n d a k t a wa k e k wa
kumuuliza swali hili
la kitashtiti (rhetorical
question):
Lakini si umefunga
wewe? Kondakta yule
naye akamjibu dereva
wake kwa kumuuliza
swali
la kitashtiti. Kwani
nimekula?
Naam, ukiudurusu
mfano huo kwa makini
utabaini kuwa mafuhumu
ya kondakta huyo na
dereva wake juu ya dhana
ya swaumu yanatofautiana
kwa kiwango kikubwa
sana.
Kwa mujibu wa
ufahamu wa kondakta
yule, kwake swaumu ni
kujizuia kunako kula na
kunywa wakati ambapo
kwa mafuhumu ya dereva
wake swaumu ni zaidi ya
hapo. Mafuhumu ambayo

MAKALA

AN-NUUR

RAMADHAN 1436, IJUMAA JULAI 10-16, 2015

Hatma ya Funga zetu

BAADHI ya viongozi wa Jumuiya ya Istiqama ya jijiji Dar es Salaam wakifuatilia


makabidhiano ya zawadi kwa mshindi wa kwanza wa kuhifadhi Qur'an juzuu 30
yaliyofanyika katika ukumbi wa Jumuiya hiyo hivi karibuni.
ndio sahihi.
Ni katika mwelekeo wa
mafuhumu kama haya
ya dereva ndipo Mtume
(s.a.w.) akatutanabahisha
kwalo kupitia sehemu ya
hadithi iliyosimuliwa na
Abu Hurairah (r.a.) na
kupokelewa na Imamu
Darmi isemayo:
''Ni wangapi katika
wafungaji hawana
wanachostafidi kutokana
na funga zao ila kuambulia
k us h in da n a n ja a n a
kiu tu''. Kwa mantiki ya
sehemu hii ya hadithi
swaumu au kufunga ni
zaidi ya kula na kunywa.
Kwa ufupi wa maneno,
wafungaji Ramadhani
wenye mtazamo mithili ya
wa yule kondakta kuhusu
dhana ya swaumu wapo
katika jamii tuliomo na
yumkini ni wengi zaidi
ukilinganisha na wenye
mtazamo wa yule dereva
juu ya ufahamu wa fasili
ya dhana hiyo kutokana
na ukweli kwamba
mwenendo wa wafungaji
wengi unaashiria hali hiyo.
Jaribu kuchunguza hali
hiyo katika kipindi hiki
cha Ramadhani, naamini
utasadiki kinachoelezwa
katika makala haya.
Pili, kutolifahamu au/
na kutolizingatia lengo
la funga ni mojawapo
inayosababisha baadhi ya
wafungaji kutolifikia lengo
la swaumu ijapokuwa
hawakujihusisha na suala
la 'vunjajungu' kabla ya
kuanza kwao utekelezaji
wa ibada ya funga.

Ni vyema ieleweke
wazi, kabla ya kuendelea
na mjadala wa nukta
hii, kwamba lengo
la funga ya mwezi
mtukufu wa Ramadhani
limewekwa bayana
na aliyetufaradhishia
ibada hiyo ya swaumu
mwenyewe ambaye
si mwingine, bali ni
Allah (s.w.) kama
atubainishiavyo lengo la
ibada hiyo pale aliposema:
''Enyi mlioamini!
Mmelazimishwa
kufunga (Swaumu) kama
walivyolazimishwa
waliokuwa kabla yenu
ili mpate kumcha Mungu
(kuwa wachaji Mungu)''
(2:183).
Kwa mujibu wa
uchambuzi na upembuzi
wa hali halisi ya mazingira
ya wafungaji Ramadhani
katika nukta ya ufahamu
wao kuhusu suala hili yaani
lengo la funga, wafungaji
wamegawanyika katika
makundi manne.
Kundi la kwanza ni lile
la wafungaji wasio na
ufahamu wowote kuhusu
lengo la funga. Kundi la
pili ni lile la wafungaji
walio na ufahamu usio
sahihi kuhusu lengo la
funga. Kundi la tatu ni
lile la wafungaji wenye
ufahamu sahihi kuhusu
lengo la funga, lakini
wasiojua namna ya
kulifikia na kundi la nne
na la mwisho kwa mujibu
wa uchambuzi wa makala
haya ni lile la wafungaji
wenye ufahamu sahihi

kuhusu lengo la funga na


namna ya kulifikia.
Kwa kuanza na
ufafanuzi wa kundi la
kwanza la wale wafungaji
wasio na ufahamu
wowote kuhusu lengo la
funga, hawa ni wafungaji
ambao hawajui kusudio
la wao kufunga, na hata
wanapoulizwa na watu
wengine kuhusu lengo
la kufunga kwao hakuna
wa n a c h o we z a k u j i b u
zaidi ya kuwa wanafunga
kwa mazoeya tu kwa vile
wanajihisi wanawajibika
wakiwa ni Waislamu.
Kwa upande wa kundi
la pili la wale wafungaji
walio na ufahamu usio
sahihi kuhusu lengo
la funga. Hawa ni aina
ya wa f u n g a j i a m b a o
wa m e l i f a h a m u l e n g o
la funga ndivyo sivyo.
B a d a l a ya l i l e l e n g o
alilotubainishia Allah
(s.w.) katika aya ya mia
themanini na tatu ya
Suratul-Baqara kama
i l i v y o d o k e z wa h u k o
nyuma, wao wameelewa
kuwa lengo la funga
ni kupata thawabu.
Na endapo ukiwauliza
wafungaji walio katika
kundi hili kusudio la
kufunga kwao, watakujibu
pasi na shaka tena kwa
kinywa kipana kwamba
wao hufunga ili kupata
thawabu. Ni ukweli usio
na tone la shaka kwamba
anayeitekeleza ibada hii
ya swaumu itakikanavyo
hupata thawabu au jazaa
yake, lakini hilo si lengo.

Wafungaji katika kundi


la kwanza ni sawa na
wasafiri wasiojua kule
waendako au watakiwako
kufika. Wasafiri wa aina
hii ni vigumu kama si
muhali kufika mahali
wanakotarajiwa au
kunakotarajiwa kwa kuwa
hawajui wanakopaswa
kwenda.
Wafungaji katika kundi
la pili ni sawa na wasafiri
wa l i o a m u a k u e l e k e a
kituo 'B' badala ya 'A'
kama ilivyokusudiwa na
kubainishwa tangu awali
na Mratibu wa safari yao
kwamba wasafiri wote
wanapaswa kufika kituo
hicho na si vinginevyo.
Wasafiri wa aina hii
nao ni ni vigumu kama
si muhali kufika mahali
wanakotarajiwa au
kunakotarajiwa kwa kuwa
wamekengeusha lengo
la asili waliloratibiwa na
Mratibu wa safari yao
kabla hata hawajaanza
safari husika.
Wafungaji katika kundi
la tatu ni sawa na wasafiri
wajuao kule waendako
au watakiwako kufika
lakini hawajui watafikaje.
Wasafiri wa kundi hili
wana nafuu kidogo
ukilinganisha na wale wa
hayo makundi mawili ya
mwanzo japo nao kufika
wanakotakiwa bado ni
mashaka makubwa kwa
kuwa hawafahamu nyenzo
zitakazowawezesha
kufika panapostahili kwa
mujibu wa kusudio la
safari husika.
Na wafungaji katika
kundi la nne ni sawa
na wasafiri wa wajuao
kule waendako na jinsi
ya kufika huko. Wasafiri
wa aina hii ni sahali sana
kufika wanakotarajiwa au
kunakotarajiwa kwa kuwa
wanafahamu fika lengo
halisi la safari yao pamoja
na nyenzo za kuwafikisha
kituo cha mwisho (last
destination)cha safari yao.
Nihitimishe kwa
kukiri kwamba kuwa na
ufahamu kuhusu suala
fulani ni jambo moja na
kulitekeleza suala hilo
ni jambo jingine. Hata
hivyo, ni vyema hapa
i k u m b u k we k wa m b a
kutekeleza jambo fulani
sahihi pasi na kuwa na
ufahamu sahihi kuhusu
jambo husika aghalabu
husababisha ama kuwako
nakisi ya ufanisi katika
utekelezaji huo au
kufisidika kabisa kwa
jambo husika.
(Mwandishi wa makala
haya ni msomaji wa muda
mrefu wa gazeti la ANNUUR anayeishi jijini
Mwanza).

19

Makala

AN-NUUR

RAMADHAN 1436, IJUMAA JULAI 10-16, 2015

Zanzibar haiwezi kuendelea kuwa Ghetto


Tunahitaji mabadiliko. Maendeleo lazima

Na Rashid Abdallah
NYUKI anayeshika maua
mazuri yanayopendeza,
mwisho wa siku
anatengeneza asali tamu.
Asali ambayo ina kila sifa,
utamu, dawa, biashara na
mambo mengine mengi.
Lakini nzi anayeshika shika
shika uchafu, hana la maana
kwa binadamu ila kuleta
maradhi.
Natamani mwaka huu
tuungane sote tubadilishe
uongozi wa nchi hii,
kwani uongozi uliopo sasa
umekuwa ukienda kuelekea
Inatoka Uk. 5
juu ya ushoga na usagaji. Hata
alipozuru Uingereza wakati
fulani kabla ya nchi yake
kuwekewa vikwazo, watu wa
Uingereza walimpiga mayai
viza kutokana na msimamo
wake wa kupinga ushoga
na usagaji. Lakini pamoja na
hayo, aliwaeleza wazi kuwa
upuuzi wao uishie London,
wakikanyaga Zimbabwe,
washike adabu zao.
Nchini Mauritania
ukikamatwa kwa kosa la
ushoga au usagaji hukumu
yake ni kifo. Mwaka jana
nchi za Nigeria, Uganda na
Gambia zilipitisha sheria
ambayo zinatoa adhabu
kali kwa usagaji na ushoga.
Nchini Uganda ilifikia
wafadhili wengi ikiwemo
Marekani kutangaza
kufuta baadhi ya misaada
waliyokuwa wakiitoa kwa
serikali ya nchi hiyo baada
ya kupitishwa kwa sheria
hiyo na Rais Yoweri Museven
kusaini rasmi.
Hata hivyo Mahakama
ya kikatiba nchini Uganda
ilifuta sheria hiyo kali dhidi
ya mapenzi ya jinsia moja,
iliyotiliwa saini na Rais
Yoweri Kaguta Museveni
mwezi Februari mwaka
huu, ikisema kuwa wabunge
walioidhinisha sheria
hiyo hawakutimiza idadi
iliyokuwa inahitajika.
Jaji Steven Kavuma,

maendeleo kama hatua


za mlevi. Wanagangania
mambo ambayo ndio kwanza
yanaipeleka Zanzibar
shimoni na kuwasababishia
wananchi matatizo lukuki.
Ukisikia ugonjwa wa
kipindupindu, basi nzi
wakati mwengine huwa
wameshaicheza nafasi
yake kiukamilifu. Ukiona
vibada vingi, umasikini na
matatizo mengi, ndani ya
Zanzibar, basi sera za CCM
zinazoiyongoza nchi hii ni
sababu ya matatizo yote.
Tutakuwaje masikini na
rasilimali zipo za kutosha.
Ni uzembe, sera mbovu na
kungangania mambo yasiyo
na faida. Miaka 50 na zaidi
ya uhuru, hali haibadiliki
kuwa bora, bali mbaya zaidi.
Wenzetu tuliopata uhuru
miaka sawa muda huu wako
mbali. Vichochoro vya miji
yao kwa uzuri havifanani
hata na barabara zetu kuu na
mitaa maarufu ya miji yetu.
Zanzibar imegeuzwa kuwa
ghetto.
Ghetto (geto), sisemi ghetto
kwa maana ya vile vyumba
ambavyo vijana wanaishi,
na mara nyingi vyumba vile
huwa vichafu, na kila kikiwa
kichafu ndio linakuwa ghetto
lina sihi kabisa, tumezoea

vyumba vichafu vya mabaro


baro ndio tunaita maghetto,
kwa matumizi tuko sahihi,
kwa vile tumeshazoea na
linafsirika hivyo kwa kila
mmoja wetu.
Lakini ghetto hasa ni eneo
katika mji lililo-duni ambalo
watu wanaishi kwa sababu
ya matatizo mbali mbali,
yakiwemo ya kiuchumi,
shida, mashinikizo, uonevu.
Pia ghetto linatafsiriwa
kuwa ni maeneo katika
miji ya Magharibi ambayo
Mayahudi walitakiwa kuishi.
Tafsiri nyengine ya Ghetto
ni kundi au tabaka la watu
ambao wametengwa.
Lakini katika jamii kama
yetu tunalitafsiri tofauti, kuwa
ni chumba cha barobaro, pia
zipo jamii zimelitafsir tofauti,
hata historia ya neno lilikuwa
zaidi ni kwa Mayahudi.
Mayahudi katika nchi za
Ulaya walikuwa ni wachache
pia walikuwa na dini tofauti.
Hivyo walitengewa maeneo
yao yakiitwa Maghetto.
Si lengo kuchambua
sana kuhusu ghetto, kwani
b a a d a ya h a p o p i a i p o
maana ya kihistoria ya neno
hilo. Tukiingia ndani zaidi,
tutawakuta Mayahudi kuwa
ndio walengwa wa neno hilo
huko katika nchi za Magharibi

katika karne zilizopita, na


hasa Italia. Lakini kwa sasa
Ghetto linatafsirika kuwa ni
eneo ambalo duni, umasikini
mwingi, eneo la watu wa
tabaka la chini. Kwa ufupi ni
katika mazingira magumu
ambayo watu wanaishi.
Leo tusifungue vitabu
vya tarekhe, lakini ambacho
nataka kukionesha ni kuwa
Zanzibar imegeuka kuwa
Ghetto. Ni eneo la vibanda
vingi, duni, umasikini.
Ni kama watu ambao
wametengwa. Yote kwa
maoni yangu ni kwa sababu
ya sera za CCM na kila kilicho
cha CCM, ikiwemo serikali
yake na viongozi wake.
Vikwazo kutoka katika
m u u n d o wa m u u n g a n o
wa serikali mbili, Zanzibar
umeifanya kuwa ni ghetto.
Muungano huu unaibinya
Z a n z i b a r . U m e k u wa n i
kikwazo cha Wazanzibari
kuendelea. Nchi imekaa
sivyo ndivyo, hali ni ngumu.
Ndio maana wananchi na
wote wanaoitakia mema
Zanzibar, wakataka itumike
fursa hii ya kuandika Katiba,
mfumo ubadilike uwe wa
Serikali Mbili. Lakini wapi,
CCM imeweka guu.
Linalosikitisha zaidi ni
kuwa kuna watu ndani ya

Laana yenu huko huko

aliiambia mahakama kuwa


Sheria hiyo ni batili kwa kuwa
mchakato wake ulikiuka
katiba, kwa kupitishwa bila
kiwango stahili cha watunga
sheria.
Ajabu ni kwamba, Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa
Ban Ki-Moon, alifurahia
uamuzi huo na kuuita kama
ushindi kwa utawala wa
sheria, na kutuma salamu
za pongezi kwa wale wote
waliochangia kufutwa kwa
sheria hiyo, hasa watetezi
wa haki za binadamu nchini
Uganda ambao waliongoza
kupinga sheria hiyo.
Awali sheria hiyo ilikuwa
imepiga marufuku mapenzi
ya watu wa jinsia moja na
kuwataka raia wa Uganda
k u wa f i c h u a wa t u w o t e
wanaojihusisha na vitendo
vya ushoga, ambapo
waliobainika kujihusisha
walikabiliwa na adhabu ya
kifungo cha maisha jela.
Nchini Nigeria Rais wake
aliyemaliza muda wake
Goodluck Jonathan, alitia
saini muswada wa sheria
ambayo iliweka adhabu ya
kifungo cha hadi miaka 14 jela,
kwa watu watakaopatikana
na hatia ya ushoga.
Sheria hiyo hiyo

inamuadhibu kwa kifungo


cha miaka kadhaa, mtu yeyote
atakayejisajili, kushiriki
au kuendesha kikundi
cha mashoga, au kushiriki
kwa njia yoyote katika
uhusiano wa kimapenzi
unaowashirikisha watu wa
jinsia moja.
Aliyekuwa msemaji
wa Rais, Bw. Reuben
Abati, alisema sheria hiyo
imewekwa kwa ajili ya umma
wa nchi hiyo, kwa sababu
zaidi ya asilimia 90 ya raia
wa Nigeria wanapinga ndoa
za watu wa jinsia moja.
M a r e k a n i i l i k u wa ya
kwanza kuikosoa Nigeria
kwa kupitisha sheria hiyo,
ikidai kuwa ni kikwazo
kikubwa kwa uhuru wa watu.
Vuta nikuvute ilitokea
katika Bunge la senate nchini
Ufaransa, ambapo mwisho
wa siku iliamuliwa kupitisha
kwa muswada wa sheria
ya kuruhusu ndoa za jinsia
moja nchini humo, licha ya
upinzani mkali kutoka kwa
wabunge wenye msimamo
mkali, wakiwamo viongozi
wa dini.
Uamuzi huo ulipitishwa
Aprili 12, 2013 na taifa hilo
lenye asili ya katoliki, kama
ambavyo Rais Francois
Hollande alivyoahidi kwenye

uchaguzi mkuu mnamo


Aprili mwaka 2012, sera
ambayo ilimfanya avune
kura nyingi za wafuasi wa
ndoa hizo.
Aliyekuwa mtetezi
mkubwa wa muswada
huo, Waziri wa Haki nchini
huko, Bi. Christian Taubira,
alisema kuwa muswada
huo ulikuja kutokana na
umuhimu wake, hasa kwa
watoto wanaoishi na wazazi
wa jinsia moja, ili nao wapate
haki zao sawa na watoto wa
wazazi wa kawaida (watoto
wanaotokana na baba na
mama).
Kwa mujibu wa muswada
huo, wenye ndoa za jinsia
moja, watarushusiwa kuasili
watoto kwa ajili ya kuwalea.
Yote haya ni kwa kuwa wao
hawana uwezo wa kuzaa.
Mpaka sasa ufaransa
imegawanyika kuhusiana na
ndoa za jinsia moja. Januari
mwaka huu, takriban watu
3 4 0 , 0 0 0 wa l i a n d a m a n a
kupinga ndoa za aina hii,
wakisisitiza uwepo wa baba
na mama katika familia.
Ambapo wiki mbili
b a a d a e , k u n d i l a wa t u
takriban 125,000 walijitokeza
mtaani kuunga mkono ndoa
za jinsi moja.
Ulaya ni bara ambalo kuna

Zanzibar bado wao wanataka


t u e n d e l e e k u wa k a t i k a
mbinyo huo huo. Wanataka
tuendelee kuishi katika
maghetto.
M a ya h u d i wa l i p o i s h i
ghetto, hawakuishi kwa hiari
yao. Walilazimishwa. Na sisi
hatuishi kwa hiari, lakini
CCM ndio inatulazimisha
tuishi hivyo. Ndio maana
n a t a m a n i u c h a g u z i wa
mwaka huu utabadilishe
hali ya mambo.
Maendeleo ya nchi yetu
yanahitajika, na sio hiari.
Maendeleo yetu ni wajibu.
Ni lazima yapatikane. Ila
ni muhali kupatikana CCM
ingalipo madarakani. Huu ni
ukweli ambao kila mwenye
akili na asiye mbinafsi
anauona na kuukiri. Na si
Zanzibar tu, bali hata Bara.
Watu wamekaa madarakani
kwa zaidi ya miaka 50, leo
hawaoni vibaya wakidai
kuwa wakipata Urais
watajenga misingi ya uchumi
wa kati! Mbinu ipi mtakuja
nayo katika uzee kama
ujanani mlishindwa!
Umasikini uliokithiri,
lazima uwondoshwe
na si kweli kuwa Mungu
katuumba ili tuwe masikini.
Mambo mengine ni kujitakia.
Hilo wananchi tulijuwe.

nchi kadhaa zimeruhusu


ndoa za namna hii. Watu
ambao watu ambao nchi
zao haziruhusu, wamekuwa
wakikimbilia huko ili kuoana
na kuishi kwa sheria za huko.
K wa m f a n o m a s h o g a
wawili Waganda, walikimbia
nchi yao na kuelekea Sweden
ili kuoana huko kwa kuwa
nchi yao inakataza vitendo
vya ushoga na usagaji.
Serikali ya Uingereza
ilipitisha sheria inayoruhusu
ndoa za jinsia moja Julai 2013,
lakini zilianza kufungwa
rasmi katikati ya mwaka
2014 kwa kuwa serikali
ilitaka muda kidogo kwa
ajili ya marekebisho ya sheria
nyingine kama zile za haki
yakurithi na masuala ya
mafao.
Baadhi ya nchi ambazo
zimekuwa vinara wa
kuruhusu ndoa za jinsia
moja ni pamoja na Canada,
Australia, Sweden, Iceland,
Ureno, Argentina, New
Zealand na Hispania.
Pamoja na kwamba bado
kuna baadhi ya nchi chache za
Magharibi ambazo zinapinga
biashara hii ya ndoa za
kisodoma na nchi nyingi
za Kiafrika na bara Asia
zinapinga, lakini kwa jinsi
mambo yanavyokwenda,
siku za mbele wokovu pekee
na wa uhakika wa kuepuka
kasi hii ya kusambaa
usodoma kwa mgongo wa
demokrasia ulimwenguni ni
Uislamu.

AN-NUUR

20

MAKALA

20

Na Bakari Mwakangwale
WA I S L A M U k u p i t i a
Kamati ya Maafa ya Shura
ya Maimamu, wametoa
sadaka ya vyakula kwa
Wa i s l a m u w a l i o p o
gerezani Segerea Jijini
Dar es Salaam, kwa ajili
ya matumizi ya daku na
futari.
Vyakula hivyo
vimepatikana kupitia
michango ya Waislamu
kutoka sehemu mbalimbali
na kuwasilishwa na
Kamati hiyo.
Katibu wa kamati hiyo
Ustadhi Ally Mbaruku,
alisema sadaka hiyo
ambayo ni ya awamu
ya pili, imewasilishwa
Jumanne wiki hii ikiwa
ni mfululizo wa misaada
hiyo katika Mwezi huu
Mtukufu wa Ramadhani.
Tu m e wa p e l e k e a
Wa i s l a m u w e n z e t u
waliopo katika gereza
la Segerea vyakula
mbalimbali, lengo
vitumike kwa matumizi
ya futari na daku, hii ni
amwamu ya pili, awamu
ya kwanza ya msaada
kama huo tulipeleka Juni
28, 2015. Alisema Ust.
Mbaruku.
Alisema vyakula hivyo
vinapatika kutokana na
michango ya Waislamu
kutoka
sehemu
mbalimbali, ambao
wa n a c h a n g i a n a wa o
huwasilisha gerezani kwa
utaratibu maalum.
Alisema, wameelekeza
misaada hiyo katika gereza
hilo kwa sababu maalumu,

RAMADHAN 1436, IJUMAA JULAI 10-16, 2015

AN-NUUR

RAMADHAN 1436, IJUMAA JULAI 10-16, 2015

Safari ya Hijja Hijiria 1436

Tanzania Muslim Hajj Trust, uandikishaji unaendelea,


gharama za Hijja ni US Dollar 4400, tarehe za Safari ni:
11 na 13 Septemba, kurudi 7 Oktoba, 2015.
Wahi kujiandikisha sasa
Kwa mawasiliano: +255 222 182370
0754 261910; 0717 000065
+255 222181577
0784 272723
0786 383820
website-www.hajjtrust.or.tz
0713 764636

E-mail:info@hajjtrust.or.tz

Futari, daku Segerea

ikizingatiwa uwepo wa
magereza mengi ndani na
nje ya Jiji la Dar es Salaam,
ambako kote humo kuna
Waislamu.

Ust. Mbaruku, alisema


wametoa kipaumbele
katika gereza hilo
kutokana na kuwapo kwa
Waislamu wengi, ambao

wamekuwa wakikamatwa
na kufikishwa katika
gereza hilo kwa tuhuma
za ugaidi.
Karibia Waislamu wote

wanao tuhumiwa kwa kesi


za ugaidi wanafikishiwa
katika gereza hilo, wawe
wa m e k a m a t wa h a p a
Jijini (Dar ) au kutoka
mikoani au raia wa nchi
jirani hupelekwa huko.
Alisema Ust. Mbaruku.
Ust. Mabaruku, alisema
wangependa kupeleka
misaada kama hiyo katika
magereza yote ndani na
nje ya Jiji la Dar es Salaam,
lakini uwezo umekuwa
mdogo.
Hata hivyo alisema,
u w e z o n a n g u v u ya
kufanya hivyo inategemea
na Waislamu kujitolea
kwa wingi zaidi.
Alivitaja aina ya vyakula
walivyopeleka kuwa ni
mchele kilo 200, tambi
kilo 35, unga (sembe) kilo
25, viazi mviringo gunia
moja, mafuta ya kupikia
lita 20.
Vyakula vingine
alivitaja kuwa ni magimbi
kiroba kimoja, maharagwe
kilo 110, mihogo viroba
viwili, sukari kilo 31
pamoja na tende kilo 100.
Alisema sadaka
hiyo kwa upande wa
uongozi wa magereza,
imepokelewa na Sajenti
Mwazani kwa niaba ya
Mkuu wa Gereza hilo,
ambapo kwa upande
wa Waislamu gerezani
humo waliwakilishwa na
Sheikh Mkuu wa gereza,
Abuswadu Samata,
Katibu wake Saidi Hassan,
pamoja na Ustadhi Saidi
Kasim Ally, mtuhumiwa
wa ugaidi.

falsafa ya dini (Theology)


katika chuo cha Al-Azhar
Shariff Misri, alisema Jumuia
ya o ya Wa n a f u n z i wa
Kitanzania Chuoni Al Azhar,
imekuwa ikifanya kazi ya
k u wa h a m a s i s h a v i j a n a
wa Kiislamu kuzitumia
ipasavyo nafasi za udhamini
wa masomo zanazotolewa
na Chuo Kikuu cha Al Azhar.
Alisema hivi sasa kuna
wanafunzi wa kitanzania
zaidi ya 131 wanaosoma
fani mbalimbali nchini
Misri zikiwemo shahada
za fani za Dini ya Kiislamu
(Islamic Theology), Sheria
za Kiislamu, Sheria za dini
na za kawaida, Lugha ya
kiarabu na dini ya Kiislamu,
Tafsiri (Tarjamaa), huduma
za kijamii, Ualimu, biashara
na uandishi wa habari,
ambao wengi wao ni kutoka

matawi ya Al Azhar Sharif


nchini.
Aidha alisema miongoni
mwao, wapo wanafunzi
wachache wa kitanzania
wanaosoma uhandisi katika
Chuo Kikuu cha Cairo lakini
kwa udhamini wa serikali.
Bw. Mbarazi amewataka
vijana wa Kiislamu Tanzania
kuchangamkia mafunzo
yanayotolewa na matawi
ya chuo cha Al Azhari
Sharif nchini kama lile
la Changombe jijini Dar
na Arusha, kwani kupitia
mafunzo katika matawi
hayo, ndipo ambapo
wanafunzi kupata fursa
ya kudhaminiwa na Chuo
Kikuu cha al Azhar Sharif
kwa ajili ya elimu ya juu
nchini Misri.
Aidha vijana wa Kiislamu
wanaosoma katika chuo

hicho, kwa kupitia


umoja wao wanapokuwa
likizo nchini wamekuwa
wakitoa taaluma za kidini
k wa Wa i s l a m u k u p i t i a
mihadhara, semina, warsha
na makongamano huku
wanafunzi wa sekondari na
shule ya msingi wa kitanzani
wakipata elimu kupitia
muda wa mafunzo ya ziada
(tuitions).
Mbarazi ambaye pia ni
kiongozi wa Chama cha
Wanafunzi wa Kitanzania
wanaosoma nchini Misri,
yaani Tanzaia Students
Union in Egypt (TSU),
alisema umoja wao umekuwa
ukifanya kazi ya kuleta
umoja kwa wanafunzi wote
wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania wanaosoma
Misri na kushirikiki kamilifu
katika ujenzi wa Taifa lao.

Aidha alisema umoja wa


huo imekuwa ukiwasaidia
wanafunzi wa kitanzaia
nchini Misri, katika
masomo yao ili kuhakikisha
kila mmoja anamaliza
na kuondoka na elimu
inayostahili.
Bw. Mbarazi kuwa
muda sasa umekuwepo
Umoja wa Waliomaliza
Chuo cha Al Azhari
Duniani, lakini kulikuwa
hakuna mawasiliano kati
ya wanafunzi wa Tanzania
wanaomaliza Azhar na
Umoja huo.
Alisema kutokana na
juhudi za Umoja huo wa
wa n a f u n z i wa n a o s o m a
Azhar, wamefanikiwa
kuunganisha mawasiliano
kati ya pande hizo mbili.

Mashindano ya Qur'an Istiqama

MAKAMU wa Rais Dkt. Gharib Bilal (wa pili kulia) akimkabidhi Said Nassor
Said hundi ya shilingi milioni tatu baada ya kuibuka mshindi wa kwanza wa
shindano la kuhifadhi Qur'an juzuu 30. Katikati ni Dkt. Muhsin Masoud ambaye
ni Mkurugenzi wa Benki ya Kiislamu ya Amana. Hafla ya kukabidhi zawadi kwa
washindi iliyofanyika katika ukumbi wa Istiqama ulioko Ilala, jijini Dar es Salaam
hivi karibuni.

Wanafunzi Al Azhar waitaka serikali kuitambua Thanawi


Na Shaban Rajab

JUMUIYA ya Wanafunzi
wa Kitanzania wanaosoma
Chuo Kikuu cha Kiislamu
cha Al Azhar Sharif nchini
Misri, wameitaka serikali
ya Tanzania kuvitambua
viwango vya ufaulu vya
elimu ya sekondari
(Thanawi) vinavyotolewa
na matawi yaliyo chini ya
chuo hicho nchini.
Tayari Umoja huo kwa
msaada wa Balozi wa
Tanzania nchini Misri, tayari
wamefikisha madai yao
serikalini na kuahidiwa kuwa
yanafanyiwa kazi.
Akizungumza na Annuur Jumanne wiki hii,
Hassan Daud Mbarazi,
mmoja wa wanafunzi wa
Kitanzania anayesomea

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na POA Printing Works LTD, S.L.P. 4605, Dar es Salaam.

Вам также может понравиться

  • Dini ya Fedha
    Dini ya Fedha
    От Everand
    Dini ya Fedha
    Оценок пока нет
  • Kufikirika
    Kufikirika
    От Everand
    Kufikirika
    Оценок пока нет
  • Annuur 1082
    Annuur 1082
    Документ16 страниц
    Annuur 1082
    MZALENDO.NET
    100% (1)
  • ANNUUR 1176b PDF
    ANNUUR 1176b PDF
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1176b PDF
    annurtanzania
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1145e
    ANNUUR 1145e
    Документ16 страниц
    ANNUUR 1145e
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru!
    Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru!
    Документ485 страниц
    Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru!
    MZALENDO.NET
    100% (3)
  • Annuur 1262
    Annuur 1262
    Документ20 страниц
    Annuur 1262
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • الصارم البتار في التصدي للسحرة الأشرار - TAFSIRI YA as-Sârimul-Battâr Fit-Tasaddî Lis-Saharatil-Ashrâr
    الصارم البتار في التصدي للسحرة الأشرار - TAFSIRI YA as-Sârimul-Battâr Fit-Tasaddî Lis-Saharatil-Ashrâr
    Документ168 страниц
    الصارم البتار في التصدي للسحرة الأشرار - TAFSIRI YA as-Sârimul-Battâr Fit-Tasaddî Lis-Saharatil-Ashrâr
    mohammad ngatenda
    100% (1)
  • Annuur 1140
    Annuur 1140
    Документ16 страниц
    Annuur 1140
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1091
    Annuur 1091
    Документ16 страниц
    Annuur 1091
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • Annuur 1078
    Annuur 1078
    Документ12 страниц
    Annuur 1078
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • An Nuur 1128
    An Nuur 1128
    Документ16 страниц
    An Nuur 1128
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1144
    Annuur 1144
    Документ16 страниц
    Annuur 1144
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1183 PDF
    Annuur 1183 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1183 PDF
    annurtanzania
    100% (2)
  • Annuur 1143
    Annuur 1143
    Документ16 страниц
    Annuur 1143
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1182
    Annuur 1182
    Документ20 страниц
    Annuur 1182
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1181 PDF
    Annuur 1181 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1181 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1158
    Annuur 1158
    Документ16 страниц
    Annuur 1158
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Download
    Download
    Документ53 страницы
    Download
    Prence Hussein
    Оценок пока нет
  • Annuur 1173 PDF
    Annuur 1173 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1173 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1167a PDF
    ANNUUR 1167a PDF
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1167a PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1153 PDF
    Annuur 1153 PDF
    Документ16 страниц
    Annuur 1153 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • ANNUUR1004
    ANNUUR1004
    Документ16 страниц
    ANNUUR1004
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • Annuur 1231 PDF
    Annuur 1231 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1231 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1112
    Annuur 1112
    Документ16 страниц
    Annuur 1112
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1195
    Annuur 1195
    Документ20 страниц
    Annuur 1195
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1028
    Annuur 1028
    Документ16 страниц
    Annuur 1028
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • Annuur 1060
    Annuur 1060
    Документ16 страниц
    Annuur 1060
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • Annuur 1213 PDF
    Annuur 1213 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1213 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1039
    Annuur 1039
    Документ16 страниц
    Annuur 1039
    Hassan Mussa Khamis
    Оценок пока нет
  • Annuur 1229 PDF
    Annuur 1229 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1229 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annur:Toleo La Ijumaa Tarehe 13-01-2012
    Annur:Toleo La Ijumaa Tarehe 13-01-2012
    Документ16 страниц
    Annur:Toleo La Ijumaa Tarehe 13-01-2012
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • Annuur 1180 PDF
    Annuur 1180 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1180 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1217
    Annuur 1217
    Документ20 страниц
    Annuur 1217
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1115
    Annuur 1115
    Документ16 страниц
    Annuur 1115
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Wazanaki Na Vitungo
    Wazanaki Na Vitungo
    Документ10 страниц
    Wazanaki Na Vitungo
    Amossy Itozya
    Оценок пока нет
  • Zanzibar Daima Online
    Zanzibar Daima Online
    Документ33 страницы
    Zanzibar Daima Online
    Hassan Mussa Khamis
    Оценок пока нет
  • Annuur 1230 PDF
    Annuur 1230 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1230 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Ukweli Ni Huu, (Kuusuta Uwongo) - Aman Thani Fairooz
    Ukweli Ni Huu, (Kuusuta Uwongo) - Aman Thani Fairooz
    Документ76 страниц
    Ukweli Ni Huu, (Kuusuta Uwongo) - Aman Thani Fairooz
    MZALENDO.NET
    67% (6)
  • Annuur 1172 PDF
    Annuur 1172 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1172 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Ebook - Tanzania - TANZANIAN - Islam - Imân Na Uislam PDF
    Ebook - Tanzania - TANZANIAN - Islam - Imân Na Uislam PDF
    Документ112 страниц
    Ebook - Tanzania - TANZANIAN - Islam - Imân Na Uislam PDF
    bookdistributor
    Оценок пока нет
  • Annuur 1124
    Annuur 1124
    Документ16 страниц
    Annuur 1124
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1202
    Annuur 1202
    Документ20 страниц
    Annuur 1202
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annur Toleo La Ijumaa
    Annur Toleo La Ijumaa
    Документ16 страниц
    Annur Toleo La Ijumaa
    annurtanzania
    Оценок пока нет
  • Annuur 1062
    Annuur 1062
    Документ16 страниц
    Annuur 1062
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • Nyuma Ya Pazia
    Nyuma Ya Pazia
    От Everand
    Nyuma Ya Pazia
    Оценок пока нет
  • Tishio la Ukombozi: Ubeberu na Mapinduzi Zanzibar
    Tishio la Ukombozi: Ubeberu na Mapinduzi Zanzibar
    От Everand
    Tishio la Ukombozi: Ubeberu na Mapinduzi Zanzibar
    Оценок пока нет
  • Hofu
    Hofu
    От Everand
    Hofu
    Рейтинг: 5 из 5 звезд
    5/5 (1)
  • Mguso Mzuri Wa Upako
    Mguso Mzuri Wa Upako
    От Everand
    Mguso Mzuri Wa Upako
    Оценок пока нет
  • Wale Wanaojifanyisha
    Wale Wanaojifanyisha
    От Everand
    Wale Wanaojifanyisha
    Оценок пока нет
  • Wale wanaokushitaki
    Wale wanaokushitaki
    От Everand
    Wale wanaokushitaki
    Рейтинг: 5 из 5 звезд
    5/5 (2)
  • Siri ya Kifo
    Siri ya Kifo
    От Everand
    Siri ya Kifo
    Оценок пока нет
  • Nyuma ya Mapazia
    Nyuma ya Mapazia
    От Everand
    Nyuma ya Mapazia
    Рейтинг: 5 из 5 звезд
    5/5 (1)
  • Eneza Huduma Yako Kwa Miujiza na Udhihirishaji wa Roho Mtakatifu
    Eneza Huduma Yako Kwa Miujiza na Udhihirishaji wa Roho Mtakatifu
    От Everand
    Eneza Huduma Yako Kwa Miujiza na Udhihirishaji wa Roho Mtakatifu
    Рейтинг: 3.5 из 5 звезд
    3.5/5 (2)
  • Penzi la Damu
    Penzi la Damu
    От Everand
    Penzi la Damu
    Оценок пока нет
  • Wale ambao ni Wajinga
    Wale ambao ni Wajinga
    От Everand
    Wale ambao ni Wajinga
    Оценок пока нет
  • Namna Unavyoweza Kuwa Mkristo Aliyehodari
    Namna Unavyoweza Kuwa Mkristo Aliyehodari
    От Everand
    Namna Unavyoweza Kuwa Mkristo Aliyehodari
    Рейтинг: 3 из 5 звезд
    3/5 (1)
  • Mfalme - Nilipumzika: Mashairi Ya Kisasa - Modern Swahili Poetry
    Mfalme - Nilipumzika: Mashairi Ya Kisasa - Modern Swahili Poetry
    От Everand
    Mfalme - Nilipumzika: Mashairi Ya Kisasa - Modern Swahili Poetry
    Оценок пока нет
  • Muhammad Mustafa
    Muhammad Mustafa
    От Everand
    Muhammad Mustafa
    Оценок пока нет
  • Anagkazo (Nguvu ya kushurutisha!)
    Anagkazo (Nguvu ya kushurutisha!)
    От Everand
    Anagkazo (Nguvu ya kushurutisha!)
    Оценок пока нет
  • Annuur 1230 PDF
    Annuur 1230 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1230 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1228d
    ANNUUR 1228d
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1228d
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1232 PDF
    Annuur 1232 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1232 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1264
    Annuur 1264
    Документ20 страниц
    Annuur 1264
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1231 PDF
    Annuur 1231 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1231 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1228d
    ANNUUR 1228d
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1228d
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1227 PDF
    Annuur 1227 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1227 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1226 PDF
    Annuur 1226 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1226 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1229 PDF
    Annuur 1229 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1229 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1223
    Annuur 1223
    Документ20 страниц
    Annuur 1223
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1213 PDF
    Annuur 1213 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1213 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1220
    Annuur 1220
    Документ20 страниц
    Annuur 1220
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1219
    Annuur 1219
    Документ20 страниц
    Annuur 1219
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1217
    Annuur 1217
    Документ20 страниц
    Annuur 1217
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1224
    Annuur 1224
    Документ20 страниц
    Annuur 1224
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1225
    Annuur 1225
    Документ20 страниц
    Annuur 1225
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1216d
    ANNUUR 1216d
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1216d
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1218 PDF
    Annuur 1218 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1218 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1209aaa
    ANNUUR 1209aaa
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1209aaa
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1210a
    Annuur 1210a
    Документ20 страниц
    Annuur 1210a
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1214
    Annuur 1214
    Документ20 страниц
    Annuur 1214
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1207...
    Annuur 1207...
    Документ20 страниц
    Annuur 1207...
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1208
    Annuur 1208
    Документ20 страниц
    Annuur 1208
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1202
    Annuur 1202
    Документ20 страниц
    Annuur 1202
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1204
    Annuur 1204
    Документ20 страниц
    Annuur 1204
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1195
    Annuur 1195
    Документ20 страниц
    Annuur 1195
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1200
    Annuur 1200
    Документ20 страниц
    Annuur 1200
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1201
    Annuur 1201
    Документ20 страниц
    Annuur 1201
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет