Академический Документы
Профессиональный Документы
Культура Документы
Sauti ya Waislamu
ISSN 0856 - 3861 Na. 1188 SHAWWAL 1436, IJUMAA , JULAI 31-AGOSTI 6, 2015 BEI TShs 800/=, Kshs 50/=
Mchezo wenu
ni mauti kwetu!
Siri ya Sitakishari haijasemwa bado
Tuambiwe mamluki wanatoka wapi
Kawaingiza nani nchini na kuwalinda
Hofu yatanda,
ni huzuni tupu!
MGOMBEA Urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Magufuli (kushoto),
kulia ni mgombea mwenza Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Tahariri/Makala
2
AN-NUUR
S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786
Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM.
E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk
Ofisi zetu zipo: Manzese Tip Top
Usangi House, barabara ya Morogoro, D'Salaam
www.annuurpapers.co.tz
Tujiulize, maisha
yetu yana thamani?
Do Black Lives Matter
in Africa? Ndivyo
anavyouliza David
Swanson baada ya
kusoma yaliyo katika
kitabu: Tomorrow's
Battlefield: U.S. Proxy
Wars and Secret Ops
in Africa.
Kinachoelezwa
katika kitabu hicho na
uchambuzi wa David
kama ulivyotumwa katika
mtandao Aprili 29, 2015,
ni jinsi mabeberu katika
mikakati yao ya kutimiza
haja na malengo yao
wanavyosababisha
maafa makubwa ikiwa
ni pamoja na mauwaji
ya kikatili kwa Waafrika
(na nchi yoyote lengwa).
Kinachojitokeza ni kuwa
ule ukoloni uliofanywa
n a Wa j e r u m a n i n a
Wa i n g e r e z a k a t i k a
karne ya 18, 19 na 20,
sio fasheni tena. Huu
ni wakati wa Ukoloni
Mambo Leo, ambao kilele
chake ni Utandawazi
na Udhibiti wa Dunia
ukiwa na mbabe mmoja
(hegemony). Na njia
maar ufu ya kupita,
ni kuendesha vita na
mauwaji lakini huku
ukionekana kuwa
wewe ndio msamaria
mwema wa dunia. Ndio
kinachofanyika katika
proxy war na vita dhidi
ya ugaidi.
Ni katika kutizama
j i n s i Wa a f r i k a s i s i
tunavyobamizwa na
kuuliwa kinyama katika
hizi proxy war na vita
dhidi ya ugaidi, watu
wanauliza, maisha ya
Muafrika yana thamani
kweli?
La kusikitisha ni
j i n s i Wa a f r i k a s i s i ,
tunavyogeuzwa kuwa
vibaraka na wasaliti wa
kujisaliti sisi wenyewe,
watu wetu na nchi zetu,
ama kwa ujinga tu au kwa
kugeuka Judas Iscariot
mwana wa Simon.
Wiki iliyopita,
tulisherehekea siku ya
mashujaa. Hii ni siku
adhimu ya kuwakumbuka
wazee wetu waliojitoa
muhang a kupig ania
na kutetea hadhi yetu
na nchi yetu mbele ya
wakoloni. Katika kipindi
kimoja cha televisheni
ikichambuliwa namna
wazee hawa walivyojitoa
muhanga, kilielezwa
kisa cha Mkwawa
alivyopambana na
Wajer umani na hata
alipoona anazidiwa
nguvu, akaona itakuwa
ni fedheha kubwa
kukamatwa na wavamizi
hao akiwa hai, akaamua
kujiua mwenyewe.
Labda tujiulize, kuna
lolote tunalojifunza
kutoka kwa wazee hawa?
Je, tunawaenzi kikweli au
tunawadhihaki? Ikiwa
wao walimwaga damu
kuwazuiya wakoloni
kutawala na kupora
mali zetu, tutasemaje
tunawaenzi ikiwa leo
wa ko l o n i wa l e wa l e
tunawakaribisha kupitia
mlango wa nyuma?
K a ma alivyo sema
aliyekuwa Waziri wa
M a m b o y a N j e wa
U i n g e r e z a , Ro b e r t
F i n l a y s o n " Ro b i n "
Cook, kwamba hakuna
afisa yeyote wa Idara
ya Usalama duniani,
a s i y e j u a k u wa h i k i
kinachoitwa ugaidi na
magaidi wa Al Qaidah
(na wenye majina
mengine) ni pseudo
gangs wanaotumiwa
na mabeberu. Leo
tunavyopigia debe
ugaidi na kukaribisha
propaganda za magaidi
waliojificha katika misitu
ya Pwani badala ya
kulikamata kambaku
kwa mapembe yake,
huu sio usaliti na dhihaka
kwa mashujaa wetu
tunaojidai kuwaenzi?
Do Black Lives Matter
in Africa? Ukitizama
dhihaka ya Westgate,
dhihaka ya Garissa na
matukio kama hayo,
pamoja na msururu wa
watu ambao wamekuwa
wakiuliwa kwa tuhuma za
ugaidi Kenya; ukitizama
dhihaka ya Boko Haram
na mamia ya maelfu
ya watu waliouliwa
kinyama na jinsi vyombo
vyetu vya habari
vinavyoshabikia habari
hizo, lakini zaidi jinsi
serikali zetu na vyombo
vyake zinavyolipeleka
jambo hili, pengine
badala ya watu wengine
kuuliza Do Black Lives
Matter in Africa?,
tujiulize sisi wenyewe:
Je, tunathamini maisha
yetu? Tunajithamini
kuwa sisi ni binadamu
wenye damu, akili
na utu sawa na hao
wanaotuletea proxy war
na fraud zao za War on
Terror?
To ka tuan ze ser a
ya kubinafsisha na
kugenisha rasilimali
zetu, na hasa katika
madini, kumekuwa na
kilio kwamba tumekuwa
tukipunjwa na kwamba
tumezidiwa ujanja
katika kuweka mikataba.
Kilio kipo mitaani
kwa watu wa kawaida
mpaka ndani ya Bunge
hadi kufikia mahali
serikali kusema kuwa
inarekebisha mikataba
hiyo na kuja na sera
AN-NUUR
Si tunasema ni marafiki
zetu? Sasa watakuwa
marafiki gani wasiotusikiliza
hata tukitoa maoni juu ya
namna bora ya kutuchinja?
Kwamba wanoe kisu kiwe
kikali ili wasitutese?
Kwetu, hilo wanalolitaka,
kama ibebidi, ni bora
walipate kupitia mikataba ya
sisi kupoteza wapate wao,
kuliko kupitia njia hizi za
kutuundia pseudo gangs na
kutuchagiza kuingia katika
mchezo wa kifimbocheza
wa kupambana na magaidi
wanaofadhiliwa na
kulindwa na mabeberu
hao hao kupitia mlango
wa nyuma.
Taz ama ha l i i l iv yo
Congo DRC, Afrika ya
Kati, Somalia, Nigeria,
Mali na sasa Kenya. Tubaki
na swali hili: Do Black
Lives Matter in Africa?
Je, tunathamini maisha
yetu? Tunajithamini kuwa
sisi ni binadamu wenye
damu, akili na utu sawa na
hao wanaotuletea proxy
war na fraud zao za War
on Terror?
Inatoka Uk. 1
Nyerere.
Mwalimu aliwahi
kuonya kuwa, chama
kitakachodharau maoni
ya watu, kinaweza kupata
kipigo, kikakosa hata mtu
wa kukisaidia kuomboleza
na kukifuta machozi.
Hali hiyo imejitokeza
kufuatia aliyekuwa kada
maarufu wa chama hicho na
Waziri Mkuu mstaafu, Mhe.
Edward Ngoyayi Lowassa
kukihama chama hicho na
kujiunga na UKAWA kupitia
Chama cha CHADEMA na
hatimaye jana (Alhamisi)
kuchukua fomu ya kuwania
Urais kupitia chama hicho.
Bila shaka Mheshimiwa
huyu kuna dalili ya kuwa
mgombea Urais kupitia
Muungano wa vyama vya
upinzani (UKAWA).
Tukio hili linaashiria
kusadiki onyo alilolitoa
Mwalimu Nyerere wakati wa
uhai wake. kuhusu muelekeo
usioridhisha wananchi wa
CCM na serikali yake.
Hilo tuwaachie wenyewe
CCM, lakini mimi kama
mwananchi, katika hali hii
ya kisiasa iliyopo ya UKAWA
Makala
AN-NUUR
Walimu na wanafunzi wa
Aboud Jumbe Mwinyi.
wa visiwani wakiwasiliana kwa
kuandika barua kwa kutumia
harufu za kiarabu.
Wa i s l a m u w a l i o g o p a
k u wa p e l e k a wa t o t o wa o
Makala
AN-NUUR
Inatoka Uk. 3
miaka mingi katika visiwa vya
Zanzibar, hapa nitaziorodhesha
skuli za Serikali visiwani
Zanzibar.
Skuli ya mwanzo ya
Serikali ilianzishwa mwaka
1905, mwanzilishi wake
akiwa Sultani Sayyid Ali bin
Hamoud, aliyepata elimu ya
kizungu Afrika Kusini na
Harrow huko Uiengereza.
Skuli hii ilikuwa ndani ya kasri
ya kifalme na kuwekwa hapo,
ilikuwa kutoa agizo kuwa elimu
ya kizungu sio ukafiri. Walimu
waliokuwa wakisomesha hapo
walikuwa kutoka nje, wengi
wao wakiwa wazungu. Mbali ya
walimu hao wazungu, aliletwa
mwalimu kutoka Oman,
Sheikh Abdurahman Al-Kindi,
aliyekuwa akisomesha dini na
kizungu.
Aidha akaletwa mwalimu
mwingine akijulikana kwa jina
la Sheikh Abdyul Barri AlAjizy na mwalimu mwengine
kutoka Uingereza akiitwa Mr.
Rivers- Smith. Mwalimu huyu
alikuwa akisomesha lugha ya
Kingereza na kufanywa kuwa
mwalimu mkuu kutokana na
ujuzi wake aliokuwa nao katika
utawala.
Baada ya kipindi kifupi, skuli
hii ikapata wanafunzi wengi
baada ya kupatikana mwamko
na wazee walikuwa wakipigana
vikumbo kupeleka watoto wao
katika skuli hii. Kutokana na
wingi wa wanafunzi, skuli hii
ikahamishwa kutoka kwenye
kasri ya mfalme na kuhamia
karibu na Msikiti wa Ijumaa
wa Forodhani. Baadaye katika
mwaka wa 1925 ikahamia
katika eneo la Mnazi Mmoja na
kuitwa kwa jina la Government
Central School.
S k u l i y a G ove r n m e n t
School ilitoa wanafunzi wengi
waliokuja kushika nafasi
katika Serikali. Skuli nyengine
iliyokuwa na sifa ilikuwa ni
Darajani Primary School,
iliyoanzishwa katika maeneo
ya Darajani. Mwandishi wa
makala hii alisoma skuli hiyo.
Serikali ya kikoloni ilibidisha
kufunguliwa skuli mbalimbali
kwa Unguja na Pemba.
Wakati huo hakukuwa na
mchanganyiko wa watoto wa
kiume na wa kike, kwa hiyo
jengo lililohamwa la Forodhani,
liligeuzwa na kuwa skuli ya
msingi ya watoto wa kike katika
mwaka wa 1925, mwiko wa
kuzitenga skuli za kike mbali
Katika juhudi za
kuendelezwa elimu visiwani,
ilifunguliwa Skuli ya Biashara
(Commercial School) baina ya
mwaka wa 1923-1924. Skuli
hii ilitoa wanafunzi ambao
hawakuwa wanafanya kazi za
ukarani visiwani Zanzibar, bali
wengine walifika kufanya kazi
sehemu nyengine za Afrika
Mashariki na kukubalika. Aidha
kulifunguliwa Skuli ya ufundi
ikijulikana kama Industrial
School baina ya mwaka wa
1924-1932, ikiwa inafundisha
ufundi wa mekanika wa magari,
useremala. Nako kwenye
kijiji cha Dole ikaanzishwa
skuli kwa jina la Rural Middle
School katika mwaka wa
1935. Skuli hii ilichukua zaidi
wanafunzi waliokuwa wakikaa
mashambani.
Katika mwaka wa 1935
ikaanzishwa skuli ya mwanzo
ya Sekondari chini ya mwalimu
mahiri Hollingsworth, ambaye
AN-NUUR
LICHA ya serikali ya
K e nya n a M a r e k a n i
kutiliana saini katika
mi k atab a k a d h a a ya
maelewano na kuafikiana
kuimarisha uhusiano wa
nchi hizo mbili katika
sekta za kibiashara na
kidiplomasia na katika
mapambano dhidi
ya ugaidi, agenda ya
ushoga aliyokuja nayo
Rais Barack Obama
imekwama.
Pamoja na kwamba Rais
Obama aliingia nchini
Kenya Julai 24 usiku na
kupata mapokezi ya
kihistoria katika nchi hiyo
inayomchukulia kama mtoto
wa nyumbani, aliyerudi na
taji la ukuu wa nchi kubwa
n a yenye nguvu z a i di
duniani, alipogusia suala la
haki za mashoga alielezwa
uso kwa uso kuwa suala hilo
halina nafasi Kenya na wala
haliwezi kuwa mipango ya
Wakenya na haliko katika
fikra za Wakenya.
Akiongea mbele ya
waandishi wa habari katika
Ikulu ya Kenya, Rais Obama
alipinga kwa nguvu ubaguzi
dhidi ya watu wanaojihusisha
na mapenzi ya jinsia moja na
kueleza hadharani kuhusu
haki za mashoga ambapo
aliyataka mataifa ya Afrika
6
Na Juma Jumanne
TUKIWA tunaelekea
kwenye uchaguzi mkuu
mwezi Oktoba, mengi
yanasemwa kila kona za
mitaa, vitongoji, vijiji,
ilimradi kila mtu anaonesha
hisia na shauku yake juu ya
jambo hili. Kwenye vijiwe
vya kahawa ndio usiseme.
Wakati watu wanaendelea
na pilika za hapa na pale
za porojo na mengineyo,
serikali nayo katika
kuliendea hilo inafanya
uratibu kwa lengo lile lile la
kufanikisha uchaguzi. Moja
ya mambo ambayo serikali
inayasimamia kidete
ni suala la uandikishaji
wapiga kura ili kuwapata
washiriki halali wa zoezi
hili kwa mujibu wa vigezo
vilivyowekwa vya wapiga
kura.
Kama tunavyojua, nchi yetu
inaendeshwa kwa mfumo wa
kidemokrasia unaotokana
na uwepo wa vyama vingi
vya siasa. Hili hutoa fursa
kwa mpiga kura kumpigia
mg ombea amtakaye kwa
mujibu wa vigezo anavyojua
yeye, kwamba nikimchagua
fulani atafanya hiki na kile
kwa manufaa ya ummah.
Na sisi kama Waislamu, pia
hatukuachwa nyuma kwani
hatuishi hewani, tupo katika
nchi hii hii tukikamuliwa kodi
na TRA.
Mfumo huu wa
k i d e m o k r a s i a u l iv yo n i
kwamba, tunawapigia kura
watu ambao wanaonekana
wana sifa kwa mujibu wa vyama
vyao wanavyoviwakilisha.
Hata kama kuna mtu ambaye
kwa uelewa na ufahamu
wetu tunaona anafaa kuliko
hawa tulioletewa, hakuna
fursa ya kumchagua. Ni
lazima tuwapigie hao hao
walioonekana wanafaa
zaidi kwenye vyama vyao.
Lakini ifahamike kuwa, hawa
wagombea wa nafasi mbali
mbali ni watu ambao kila
mmoja amejipima mwenyewe
na kuona kuwa anafaa na
anaweza kuongoza nchi.
Makala/Tangazo
AN-NUUR
Dkt. John Magufuli (kushoto), kulia ni mgombea mwenza Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Kwa kuwa kuna mfumo kingine kisichokuwa Chama maeneo yanayofikika kufanya
wa vyama vingi, ilitegemewa Cha Mapinduzi. Kwa haraka kampeni. Lengo la kampeni ni
k w a m b a k u t a k u w a n a haraka unaweza kusema pamoja na kukitangaza chama
kupokezana vijiti. Awamu kwamba, pengine kinafanya husika, sera yake na ilani yake.
hii chama hiki kinashinda vizuri sana ndiyo maana kila Dhana yangu ni kwamba,
na awamu nyingine chama awamu kinashinda.
ahadi ambazo chama hutoa
kingine kinashinda. Jambo
Nasema hivyo kwa sababu kwa wananchi ndizo ambazo
la kushangaza ni kwamba, kila chama kina ilani yake, humfanya mwananchi aungane
tangu kuanzishwa mfumo sera na kanuni yake. Inapofika na hicho chama na hatimaye
wa vyama vingi hapa nchini wakati wa uchaguzi, kila chama kukipigia kura inapofika wakati
m wa k a 1 9 9 2 , h a i j awa h i hupata fursa ya kuzunguka wa uchaguzi.
kutokea kushinda kwa chama kila mahali kote nchini kwa
Nchi hii ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, ni
zao la nchi mbili ambazo
ni Tanganyika na Zanzibar.
Kwa upande wa Tanganyika
kuna mchanganyiko wa dini
mbali mbali, kuu zikiwa
Uislamu na Ukristo. Visiwani
n a o n i h iv yo h iv yo, i l a
tofauti na Bara, Waislamu
wamewazidi Wakristo kwa
mbali. Tunaambiwa ni takriban
asilimia zaidi ya 99% wakati
huku Bara Waislamu na
Wakristo hawakuachana sana
kwa idadi (%).
Ikiwa ukweli ndio huo,
m a a n a y a ke n i k wa m b a
Wa i s l a m u n d i o w e n y e
Inaendelea Uk. 9
TANGAZO
AN-NUUR
AU
Fomu za Maombi zinapatikana chuoni Kirinjiko Islamic Teachers college na katika vituo vilivyoorodheshwa hapa chini.
3. Mwenye cheti cha Grade IIIA, AU
705627.
Karume,Nyumba Na. 05 :
Arusha: Ofisi ya Islamic
4. Mwenye
(NVAJambo
level 4) cha 0765024623
kozi yoyote kutoka katika chuo
kinachotambulika
NACTE
Mtwara:
Amana Islamic S.S:na
0715
Educationcheti
Panel,
465158/
231007.
Msikiti mtihani
wa Majengo
Plastic,au Ghorofa
2 waShinyanga
VETA naya
ufaulu
D nne katika
wa kidato cha
nne0787
(CSEE).
Songea: Kwa Kawanga Karibu na
karibu na Manispaa ya
mkabala na msikiti Mkuu
B: NAMNA
Shinyanga
Mjini
Bondeni YA KUOMBA::
Msikiti
wa
NURU
:
:0752180426
Kahama
ofisi
ya
0783552414/0762817640
0713249264/0683670772.
1. Mwombaji anatakiwa kujaza fomu ya maombi AU
AN NUUR Karibu na msikiti
Kilimanjaro: Moshi: Msikiti wa
Mkuzo Islamic High School
2. Kuomba
kwa njia
ya mtandao (Online
Application)
kupitia Tovuti
ya 348375.
wa
Ibadhi
: 0753
Riadha :712
216490Same
:0717
993930/0688794040
Juhudi Studio mkabala na
Mbeya: Ofisi za Islamic Education
NACTE(www.nacte.go.tz).
Dar es Salaam: Ubungo Islamic
Benki ya NMB Same: 0757
Panel
Uhindini
High
School
:
013344.
0785425319.
Rexona
Video
TANBIHI: Atakayeomba kwa njia ya fomu, hatatakiwa kuomba kupitia njia ya mtandao wa
0756584625/ 0657350172
Same: Kirinjiko Islamic Secondry
mkabala na Mbeya RETICO:
NACTE.
School: 0784 296424/0655 Ofisi ya Islamic Ed. Panel
0713 200209/0785425319.
697 075, Usangi- Falhum Temeke -Msikiti wa Nurul Ya
Rukwa :Sumbawanga:Jengo la
kin :
Kibakaya : 0787 142054.
Haji Said Shule ya Msingi
D: ADA
YA MAOMBI:
Ugweno
Kifula Shopping 0655144474/0787119531
Kizwike 0717082 072.
Morogoro
Wasiliana
na
Centre- Yusuph Shanga :
Tabora: Kituo cha Kiislamu
Ramadhani
Chale
:
078458776.
Isevya:
0784
0715704380.
Tanga: Twalut Islamic Centre
944566/0787237342
Dodoma Hijra Islamic Primary
Mabovu Darajani : 0715
Nzega:
Dk
Mbaga-0754
School
:
0716
544757/071
894111 Uongofu Bookshop:
576922/0784576922.
Singida: Ofisi ya Islamic
0784 982525, Korogwe:
Iringa: Madrastun Najah: 0714
Education. Panel karibu na
SHEMEA SHOP : 0754
522 122.
Nuru snack Hotel : 0786
690007/071569008. Mandia
Pemba: Wete: Wete Islamic
425838/0784 928039.
Shop - Lushoto: 0782257533.
School
:
0777
Manyara:
Ofisi ya Islamic Ed.
Handeni Mafiga -0782
432331/0712772326.
Panel Masjid Rahma:
105735/0657093983
Unguja : Madrasatul Fallah:
0784491196
Mwanza
Nyasaka
Islamic
0777125074.
PANDU
Kigoma: Msikiti wa Mwandiga:
Secondary School : 0717
BOOKSHOP
0777462056
0714717727 Kibondo
417685/0786 417685.Ofisi ya
karibu na uwanja wa
Islamic Nursery School:
Islamic Education Panel
Lumumba
0766406669.
Kasulu:
Mtaa wa Rufiji mkabala na
Mafia: Ofisi ya Ust. Yusufu Ally
Murubona
Isl.SS:
Msikiti Al-Amin 0785 086
jirani na msikiti mkuu :
0714710802.
770/0714097362
0773580703.
Lindi Wapemba Store: 0784
Musoma Ofisi ya Islamic Ed
974041/0783 488444/0653
Panel
-Mtaa
wa
Kwa maelezo zaidi piga simu: 0787 188964, 0784 267762 na 0654 613080
Makala
8
Na Shaba Rajab
SUALA la kuanzishwa
Mahakama ya Kadhi kwa
Waislamu nchini, ni suala
ambalo kamwe haliwezi
kutoka katika fikra za
Waislamu. Waislamu
kuwa na Mahakama
ya Kadhi, ni muhimu
kwa kuwa kungewapa
uhakika wa kusimamia
kwa usahihi wa mambo
yao ya kiibada na kiimani.
Suala hili lilishika kasi
zaidi, hasa pale Chama
cha Mapinduzi (CCM)
kilipoamua kuliingiza suala
hilo katika Ilani yake ya
uchaguzi ya mwaka 2005.
Hapo Waislamu wakawa
na matumaini kwamba,
sasa umefika wakati wa
kuwahudumia Waislamu
kwa haki na kwa yakini
katika Sheria za Ndoa,
Talaka, Mirathi na Wakfu.
Hata hivyo baada ya suala
hilo kuonekana kuridhiwa
na serikali na mchakato
wa k u l i we k a k i s h e r i a
kuanza, kuliibuka shinikizo
kali kutoka kwa Wakristo
wakiitaka serikali kuachana
na suala hilo.
Licha ya serikali
kuunda timu kuchunguza
uendeshaji wa mahakama
hiyo katika nchi nyingine
zenye Mahakam hiyo ili
kujiridhisha na hatimaye
kukiri kuwa haikuwa na
tatizo, bado wasiopenda
uwepo wake walishinikilia
kuikataa. Hata pale ofisi
ya Waziri Mkuu ilipounda
kamati ya kufanikisha
mchakato huo, bado jambo
hilo lilisuasua huku muda
nao ukizidi kuyoyoma.
Shinikizo la Wakristo
kuikataa Mahakama hiyo
lilikolea na wao ndio
walisikilizwa, hoja za
Waislamu zikatupiliwa kwa
mbali.
Hata katika Bunge la
katiba, Tume ya Katiba nayo
haikutaka kusikia haja hiyo
ya Waislamu. Walitupilia
mbali maoni yao ya kuhitaji
chombo chao hicho.
Serikali ilisitisha
uwasilishwaji wa muswada
wa Mahakama ya Kadhi
katika Mkutano wa 19 wa
Bunge uliohitimishwa mjini
Dodoma April mwaka huu
na ukawa ndio mwisho wa
matumaini ya kuanzishwa
mahakama hiyo kwa
Waislamu.
K atibu wa Bunge,
Dk. Thomas K ashilila
AN-NUUR
9
Inatoka Uk. 6
K i n a c h o z i d i
kunichanganya zaidi
ni kwamba, kila mmoja
anasema vizuri kuhusu
msimamo wa chama
chake, kwamba wakiingia
watadhibiti maovu yote.
Lakini pamoja na ushawishi
huo, binafsi nimeshindwa
kushawishika kwa nukta
moja tu, ambayo ni
uaminifu. Nafsi inashindwa
kukubali kuwaamini watu
ambao hawana elimu ya
muongozo, watu ambao
wako mbali na mafundisho
ya dini, watu ambao wako
mbali na Mungu!!
M g o m b e a U r a i s wa
CCM, kwa awamu hii ni
Dk. John Pombe Magufuli.
Ni katika viongozi ambao
wanadaiwa kufanya vyema
katika nyadhifa mbali mbali
alizowahi kushika, na hasa
aliposhiriki zoezi la kuuza
nyumba za serikali.
Ni muhimu sana
kufahamishana juu ya
mambo nyeti kama haya kwa
kuwa, aghalabu tumekuwa
tukishiriki uchaguzi lakini
mp a ka leo hii hatuna
lolote la kujivunia kwamba
limetekelezwa na serikali
Makala
AN-NUUR
SHEIKH Msellem.
tuliyoichagua.
Kumbuka uchaguzi
haupo mbali. Kura yangu
nimpe nani ambaye
atanihakikishia usalama wa
dini yangu, wazazi wangu,
m a s h e i k h z a n g u, m ke
wangu, wanangu, ndugu
zangu, rasilimali za taifa na
mengineyo?
Ila kuna mambo mawili,
matatu inafaa tuyafahamu
uzuri tusije jichanganya.
Kuna matatizo yetu ya
msingi kama Waislamu,
ambayo hayawezi kutatuliwa
na yeyote atakayeingia
madarakani kama sisi
wenyewe hatujakuwa na
mtaji wa kutosha. Mtaji
utakaomfanya yeyote
anaiyeingia madarakani
kututizama kama Mwalimu
Nyerere alivyowatizama
wazee wetu wakati wa
kupigania uhuru na miaka
ya mwanzo ya Uhuru hata
akawa anavaa kofia na
kufunga swaumu ya sunna
akiwa na Sheikh Ramia na
wazee wa Kiislamu. Pili,
yapo mambo yanatuhusu
kama Watanzania, tunaoishi
na wenzetu wa dini nyingine
katika nchi hii Tanzania,
ambao tunalazimika kuwa
chini ya serikali yoyote
itakayokuwa madarakani
kwa mujibu wa Katiba na
Sheria za nchi. Hapa ndipo
ninapojadili mimi, kura
yangu nimpe nani Oktoba.
Tatu, kipo kisa cha Wayahudi
kupewa manna na salwa
wao wakasema wamechoka
chakula kimoja miaka
nenda miaka rudi, wakataka
wa b a d i l i s h i we wa p a t e
mchicha, kabichi, matango,
vitunguu, ngano, kunde na
kama hayo. Wakakemewa
kuwa wanataka kubadili
vizuri kwa vilivyo vibaya.
Quran inasema:
Na (kumbukeni habari
hii kadhalika) Mliposema:
Ewe Mussa! Hatuwezi
kusubiri kwa chakula cha
namna moja tu (Manna
na Salwa), basi tuombee
kwa Mola wako atutolee
vile vinavyooteshwa na
ardhi, kama mboga zake na
matango yake na ngano yake
na adesi zake na vitunguu
vyake. Akasema (Mwenyezi
Mungu), mnabadili vitu
d u n i k wa v i l e v i l iv yo
bora?.(2:61)
Katika agenda yetu hii
ya Uchaguzi Mkuu na
wagombea wake, katika
kupima Sera, Ilani na ahadi
za vyama vilivyoingia
katika kinyanganyiro hiki,
ka tika ku wa tiza m a n a
kuwapima wagombea, la
kuzingatia hapa ni kwamba
hatuzungumzii habari ya
Manna na Salwa.
Jamani nisaidieni; Kura
Yangu Nimpe Nani Mwezi
Oktoba Mwaka 2015?
Mkamilifu ni Allah pekee.
Wabillah Tawfiiq!
(Juma Jumanne-Simu:
+255 659 789 468/ +255
752 527 833, Kateshi,
Manyara)
Wahitimu kuelekea
Makerere College
Mara tu Chuo cha
Makerere kilipoanza kuchukua
wanafunzi kutoka nchi za
Afrika Mashariki, Zanzibar
ilipeleka wanafunzi na wengi
wa wanafunzi wa mwanzo wa
Makerere College walikuwa ni
watu muhimu katika sehemu
ya serikali na utawala.
Wanafunzi wa mwanzo
waliopelekwa walikuwa
Othman Shariff, aliyekuja kuwa
mwanaharakati wa kutetea
Zanzibar kupata Uhuru na
bingwa wa kutibu wanyama,
Ali Khamis bingwa wa kilimo
akaja kuwa Spika wa mwanzo
wa Baraza la Wakilishi, Ahmed
Rashid alikuwa ni kati ya
wataalamu wa mwanzo katika
Afrika Mashariki katika fani ya
mifugo, Ali Muhsin Barwany
kiongozi wa ZNP mpiganiaji
wa Uhuru wa Zanzibar, alikuwa
kati ya mawaziri wa Serikali ya
mwanzo ya Zanzibar kabla ya
Mapinduzi.
Wanafunzi hao wanne
waliokwenda Makerere
College wakafwatiwa baada
ya miaka miwili na Sheikh
Mohd Nassor Habsi, Sheikh
Omar Abdalla ndio aliyekuwa
mwanafunzi wa kwanza kwa
Zanzibar kufuzu kwa somo la
Uhai (Biology) na kufwatiwa
na Maalim Zubeir Rijal ambaye
yeye akatakhasusi juu ya somo
la wanyama (Zoology) kisha
kuwa ni mwanafunzi wa
mwanzo kuchukua shahada
ya kwanza (BSc Honours)
ya Zoolog y katika chuo
cha Queen Marry College
cha Uingereza, Abdulrasul
10
Na Omar Msangi
JUMAMOSI ya wiki
iliyopita Julai 25, 2015 gazeti
la JamboLeo lilitufahamisha
k u wa wa t u h u m i wa wa
uvamizi wa kituo cha Polisi
Sitakishari wametoa siri
nzito. Siri yenyewe ni kuwa
watuhumiwa hao wamesema
kuwa wanakusanya silaha
kwa ajili ya kusimika dola ya
itikadi ya imani yao.
Habari zilizopatikana
kutoka ndani ya askari
waliopo kwenye operesheni
inayofanywa katika kijiji
cha Mandikongo, Bupe na
Chamanzi Wilaya ya Mkuranga
mkoani Pwani zinaeleza
kuwa baadhi ya watuhumiwa
wamesema kwamba wanavamia
vituo vya polisi ili kukusanya
silaha ambazo zitawapa nguvu
ya kugeuza utawala nchini ili
uwe wa itikadi ya dini yao.
Limeandika gazeti hilo.
Gazeti hilo limedai kuwa kwa
mujibu wa taarifa zilizotolewa
na vijana hao wa Afande
Mangu, pamoja na kuteka vituo
ili kupata silaha, watuhumiwa
hao huwa wanapewa mafunzo
(ya kijeshi?) na wakufunzi wa
ndani na nje.
Tu n a p a t a wa k u f u n z i
kutoka ndani na nje, lakini
suala kubwa linalotukwamisha
ni jinsi ya kuingiza silaha, hivyo
kutokana na kuwezeshwa na
wahisani wetu ndio maana
tunakusanya bunduki za
ndani.
Anadaiwa kusema
a s k a r i m m o j a a k i nu k u u
maneno ya mtuhumiwa
wa tukio la Sitakishari na
kuongeza akisisitiza kuwa
polisi watapambana vikali
kuhakikisha kuwa vikundi
kama hivyo vinachakazwa
kokote viliko ndani ya nchi.
Kule Upareni, ukisikia
m s e m o, N d a m a y a e t e
mikono, maana yake ni kuwa
kama kuna jambo mlikuwa
mkilisubiri kwa hamu, basi
muda wake umetimia.
Kama lilivyosema gazeti
tunalolisherehesha hapa,
Sitakishari kuna siri nzito.
Haihitaji kuwa mtaalamu
bingwa wa masuala ya uhalifu
(criminolog y), kugundua
mashimo katika taarifa hizi
tunazopewa juu ya suala la
Sitakishari na hata yale
matukio yanayodaiwa kutokea
Morogoro watu wakikamatwa
na bendera zenye maandishi
ya Kiarabu!
Gazeti linatuambia kuwa
waliokamatwa wamesema
kuwa wanateka vituo vya polisi
ili kupata silaha za kusimamisha
dola inayoongozwa na dini yao.
Tuanze kusema kuwa kama ni
siri, haya maneno sio mara ya
kwanza kusemwa. Bila shaka
tutakumbuka kuwa baada ya
lile tukio la Songea la mtu
Makala
AN-NUUR
Wandishi wa Habari.
Na Shaban Rajab
Inaendelea Uk. 11
Inaendelea Uk. 11
11
Inatoka Uk. 10
Makala
AN-NUUR
Haram.
Yapo mambo matatu hapa
ya kuzingatia. Kwa muda sasa
kumekuwa kukiendeshwa
harakati za kuwakamata watu
ikidaiwa kuwa ni operasheni
ya kuwasaka magaidi. Hili
likichanganywa na haya ya
Sitakishari, inapandikizwa
Inatoka Uk. 10
a k i o n g e a n a m wa n d i s h i
mapema wiki hii jijini Dar es
Salaam.
Alisema kuwa hivi sasa wapo
katika mawasiliano na familia
na ndugu za watuhumiwa,
ili kukamilisha mipango ya
kupata mawakili.
Alisema ujumbe wa
Waislamu wa Morog oro
wamelazimika kuja jijini
Dar es Salaam kukutana
na K amati ya Kutetea
Waislamu, inayowahudhumia
watuhumiwa wa ugaidi na
uchochezi katika Gereza la
Segerea, wakiwemo Sheikh
waliposhitakiwa, baadhi ya
Waislamu wanaofuatilia kesi
za wenzoa hao, wamelalamikia
kitendo cha kuzuiwa na polisi
kuingia mahakamani kila
zinapotajwa kesi za wenzao
hao.
Wakati huo huo, wakati
sakata la ug aidi likizidi
kuwaandamana baadhi ya
Waislamu na viongozi wao nchini,
Waislamu mkoani Morogoro
wameutaka umma wa Kiislamu
nchini kuwaunga mkono katika
wa Kilombero, wakidaiwa
kukutwa na maguruneti mawili
ya kutupa kwa mkono na sare
zisizoruhusiwa.
Walidaiwa kuwa walikutwa
na viatu jozi mbili, kofia, koti
ambavyo vinafanana na sare za
jeshi la wananchi.
Baadhi yao walifunguliwa
mashitaka ya kukutwa na vitu
vya milipuko na mafuta ya
mlipuko (water jelly Explosives
Vol IV.)
12
MAKALA
UTUNZI U MASHANI
AN-NUUR
HUKURANI
zote anastahiki
mwenyezi
mungu mola mlezi
wa ulimwengu na
rehema na amani
zimfikie mbora wa
viumbe bwana wetu
muhamad na jamaa
zake na sahaba zake
wote: ama baada
ya utangulizi huu
mfupi:Kwa hakika
dini ya kiislamu
ambayo ni nyepesi
inaling ania umoja
daima na kuzoeana
kati ya watu wote na
inakataza kutengana
na kusambaratika
kwani miongoni mwa
msiba mkubwa ambao
umeukumba umma
huu ni kuonjwa kwa
kudhoofika kwa nguvu
yake ni kutokana
na kutengena na
na kusambaratika.
amesema mwenyezi
mungu "enyi mlioamini
mnapokutana na
kundi la maadui basi
liangamizeni na mumtaje
mwenyezi mungu kwa
wingi ili mpate kkufaulu
na mumtii mwenyez i
mungu na mtume wake
na wala msigombane
mtagawanyika na
kuharibikiwa na
kuondoka nguvu zenu na
subirini hakika mwenyezi
mungu yupo pamoja na
wenye kusubiri. hanfali
miongoi mwa upendeleo
pekee wa umma huu ni
uma mmoja. amesema
mwenyezi mungu ((na
13
MAKALA
RAIS Jakaya Kikwete (katikati), kulia kwake ni Kaimu Muft Sheikh Zuber na
Mhe. Bernard Membe.
Inatoka Uk. 8
hilo kutokana na manufaa
yao binafsi. Kitendo cha
Rais Kikwete kupenda
kuzungumzia suala la
Waislamu Makanisani,
kilidhihirisha kwamba hofu
aliyo nayo kuwa mkwamo
m k u u wa k u a n z i s h wa
mahakama hiyo ulikuwa
Kanisa.
Kama
Kanisa
wangeridhia, basi moja
kwa moja na serikali nayo
ingeliharakisha suala hili la
Waislamu bila mizwengwe
yeyote.
Lakini Rais Kikwete
alisema pia kuwa kiini cha
mjadala kuhusu Mahakama
ya Kadhi ni wanasiasa na
akajivua kuhusika. Balala
yake akatupa mzigo kwa
awamu ya Rais Mstaafu
Benjamin Mkapa, Philip
Mangula na Mzee Kingunge
Ngombale Mwiru.
Chimbuko
la
kinachosemwa sasa kuhusu
Mahakama ya Kadhi ni
bungeni, na muasisi wa
hoja hii ni Mheshimiwa
Augustino Lyatonga Mrema
alipokuwa Mbunge wa
Temeke.
Bwana Mrema alikuja
na hoja binafsi bungeni
ya kutaka kuundwa kwa
Mahakama ya Kadhi
n ch i n i , a l i s e m a R a i s
Kikwete na kubainisha kuwa
hoja hiyo iliungwa mkono
na aliyekuwa Mbunge wa
Bagamoyo wakati huo,
marehemu Baruti Rajabu.
Alisema kuwa baadaye
ikafuatiwa kwa nguvu na
hoja binafsi ya aliyekuwa
Mbunge wa Moshi Vijijini
k u p i t i a T L P, T h o m a s
Ngawaiya.
Aliongeza Rais Kikwete
kusema kuwa kwa busara za
Spika wa kipindi hicho, Mzee
Pius Msekwa, akisaidiwa
na kiongozi wa shughuli
za serikali bungeni wakati
huo, Waziri Mkuu mstaafu
Frederick Sumaye, alikataa
hoja hiyo kujadiliwa bungeni
moja kwa moja kutokana
na kile alichokitaja kuwa
ni unyeti wake, na kuamua
kuipeleka katika Kamati
ya Bunge ya Katiba na
Sheria, ambako kamati hiyo
iliyoongozwa na wenyeviti
wawili tofauti, Arcado
Ntagazwa. Alipoteuliwa
kuwa waziri, nafasi hiyo
ilishikwa na Athumani
Janguo.
Alisema baada ya kamati
hiyo kukamilisha utafiti na
kukabidhi ripoti kwa Spika,
aliikabidhi serikalini ambako
AN-NUUR
ya Muungano na suala la
Mahakama ya Kadhi si la
Muungano, hivyo lisubiri
wakati wa kuandaa Katiba
ya Tanganyika.
Lakini Bunge Maalum la
Katiba likaikataa Katiba ya
Warioba na kutunga Katiba
Mpya Pendekezwa yenye
mambo yote ya Muungano
na yasiyo ya Muungano bila
ya kuingiza Mahakama ya
Is ita r a jiwe a h a d i ya
kuondoa dhulma ndani
ya mfumo ulioasisi
dhulma kwamba itakuja
kutekelezwa. Uchaguzi
mkuu ujao Waislamu wakae
kitako na kutafakari kwa
kina. Nini hatma yao katika
nchi hii.
14
MAKALA
AN-NUUR
Na Ben Rijal
ATIKA makala
ya wiki iliopita
niliweza kuelezea
matokeo mawili ambayo
yalitokea katika mwezi
wa S h awa l wa k a t i wa
Mtume (SAW), nayo ni
tokeo la Banu Kaynukaa
na vita vya Uhud. Katika
muendelezo huo katika wiki
hii nitazungumzia ju ya vita
vya Uhud
Vita hivi vilikuwa katika
mwezi wa Shawal, ilikuwa
mwaka wa tano tokea Mtume
(SAW) kuhamia Madina.
K atika mwezi kama huu
kwenye kalenda ya Kiislamu
kulitokea nusra kubwa kwa
Waislamu juu ya makafiri wa
Kikuraishi wa Makka ,vilitokea
vita vikubwa vilivyoitwa vita
vya Khandaq au kwa jina
jengine vita vya Ahzaab.
Kuitwa kwa vita vya vita
vya khandaq ni kutokana na
kuchimbwa khandaki kubwa
na Waislamu kutokana na fikra
ya Sahaba Suleimna bin Farsy .
M a t o ke o y a k i l a k i t u
hutokea kutokana na sababu
i n ayo s a b a b i s h a k u t o ke a
tokeo na sababu ya vita vya
Uhud ni pale Mayahudi
wa kabila la Bani Nadhiri,
walivyotaka kumkengeuka
Mtume Muhammad (S.A.W)
kwa kumuendea kinyume na
kutaka kumtoa katika mji wa
Madina kwa dhana zao kuwa,
Mtume Muhammad (SAW)
kafika Madina kuwatawala na
kuwawekea sheria kali.
Kutokana na hayo likatoka
kundi la Bani Nadhiri,
walikwenda Makka kwa
Makuraishi na baadhi ya
makabila mengine ya Kiarabu
yakiwemo makabila ya Atfaan,
Bani Fuzara na Murrah kwa
kuwataka msaada wa kumpiga
vita Mtume (SAW) kwa
kuwaeleza yafuatayo, Sisi
tuko pamoja na nyie kwa
kumtoa Muhammad, na dini
yenu ni bora kuliko dini ya
Muhammad. Mayahudi ni
watu wa mbinu na siku zote
huwa na hila na kuhakikisha
kuwa utulivu unakosekana.
Zilipomfika habari hizo
Mtume (SAW) za Mayahudi
na makafiri wa Makka kuwa
114
260
103
Masuala:
1.Wataje wanawake 4 ambao watakuwa ni wanawake wa Peponi
waliojulikana wakiwa bado wahai. Jawabu: Maryam, Asya, Khadija,
Fatma
2.Majina mengine ya Quran. Jawabu: Furqan, Kitaab, Noor, Huda
3.Sura ngapi katika Quran. Jawabu: 114
4.Mtume yupi katajwa sana katika Quran? Jawabu: Mussa
5.Sahaba yupi aliomshauri Khalifa Syd Abubakar aikusanye Quran,
iwe katika kitabu kimoja? Jawabu: Umar
6.Sahaba yupi alikusanya Quraan katika mfumo huu tuliokuwa nao
Sasa? Jawabu: Uthman
7.Ukifunga mwezi wa Ramadhani na ukafwatisha siku sita za Shawal
utakuwa sawa umefunga? Jawabu: Mwaka.
8.Msikiti ulikokuwa mkongwe kuliko yote. Jawabu: Alqaaba
9.Ameangamia pamoja na mikono yake miwili, ni nani huyo? Jawabu:
Abulahab
10. Tafsiri zinazojulikana za Quran kwa lugha kutoka Kiarabu
kwenda lugha mbalimbali ni ngapi? 103, 250, 1,000 Jawabu: 103
15
MAKALA
AKALA ya
wiki iliopita
ilielezea juu
ya mawingu katika
kitabu kitukufu cha
Quran na makala ya
wiki hii yatamurika
mawingu na faida
zake.
Tu n a p o a n g a l i a
angani huona mawingu,
lakini mawingu
huwa yanatembea na
kusogea na kutoweka
saa nyengine mawingu
huja kwa maumbile
tafauti, nikujuliza
haya mawingu ni kitu
gani? Akiniuliza mtoto
wa skuli ya msingi
nitamwambia kama
ifwatavyo, Mawingu ni
mkusanyiko wa matone
ya maji yaliojikusanya
juu ya anga, mawingu
hufanyika pale maji
yanapoyayuka ardhini
na kuwa mvuke na
kwenda ang ani na
kukamuliwa na
kupozwa kisha ndio
huona mawingu.
Kuna tabaka ya anga
yetu ijulikanayo:
troposphere ikiwa
sehemu ya chini ya
mawingu na kuna
tabaka nyengine
mbili zijulikanazo
kama stratosphere
au mesosphere. Haya
mawingu tunayaona
hubeba tani milioni
za matone ya maji,
huyaona mawingu
kuwa ni meupe
kutokana na jua kupika
na mwanga unaporudi
huyafanya tuyaone
mawingu kuwa ni
meupe.
Stratus, Cumulus
na Cirus ni aina ya
mawingu na maumbo
yake, Stratus huwa
na umbo la bapa na
husaidia kuifanya
sayari yetu hii ya dunia
kupozwa na kuweza
kukalika.
Maisha ya viumbe
hutegemea maji na maji
ndio maisha na pale
maji yatapomalizika
duniani ni kusema
uhai utasita kukuweko,
mvua zinaponyesha
kwa kukuza kilimo ni
kutokana kwa kuweko
kwa mawingu na ile
duru itwayo duru ya
maji kufanyika mvua
inategemea zaidi
mawingu.
Mvua inavyokuwa
Mzunguko wa maji
katika dunia ni safari
ambayo hatuihisi lakini
ni safari muhimu sana
katika maisha yetu
ya kila siku. Dunia
yetu imezungukwa na
bahari, mito, maziwa,
chemchemu n.k.
Kwahio safari huanzia
duniani yaani nchi kavu
nakuelekea mawinguni
mvua zinaponyesha
kisha maji yakarudi
ardhini, baadhi yakawa
AN-NUUR
D
N
I
K
A
H
I
70
A
A
Y
U
S
U
F
F
S
25
K
M
E
T
I
C
A
L
R
Z
K
A
M
P
R
I
H
R
A
A
A
S
A
A
E
N
O
E
M
T
C
L
P
D
D
L
C
L
B
A
U
A
U
S
I
A
H
P
I
N
S
W
A
E
A
N
I
P
A
Z
Y
I
G
A
N
D
N
O
T
A
K
B
I
A
L
M
A
K
U
N
P
A
C
I
F
I
C
U
G
C
Jee Unajua?
16
AN-NUUR
MAKALA
Inatoka Uk. 14
njaa Waislamu, mbinu hiyo
haikufaulu na wala hakujatokea
vita, Allah akapitisha nusra
yake kuyatawanya makundi
hayo kwa njia mbili kuu, njia
ya kwanza kwa kumtumia
mtu mmoja ambaye alisilimu
kipindi si kirefu, naye ni
Naaim bin Masoud na kuanza
kuwagongesha makafiri na
Mayahudi kwa kutoka mpaka
kwa Mayahudi wa kabila la
Banii Kuraidha, hali ya kuwa
wanadhani kuwa bado Naaim
bin Masoud hajasilimu kwa
kuwambia msikubali kushiriki
katika vita na Makuraish
mpaka wakupeni rehani ya
watu wao, tena katika viongozi
ili wasiweze kuondoka mpaka
mkubaliane, pindi hamkufanya
hivyo, watakuwacheni peke
y e nu m k awa h a m n a wa
kukunusuruni Madina.
Mayahudi wakawafik fikra
yake hiyo, akatoka tena Sahaba
Naaim bin Masoud mpaka
kwa Makuraishi wakiwa pia
wana dhana kuwa bado yupo
katika ukafiri nao, akawapa
ushauri kwa kuwambia kuwa
Bani Nadhiri wanajilaumu
kwa walioyoyafanya
kwa Muahammad na
wamekubaliana kuwa waje
wachukuwe watukufu
miongoni mwenu na
wawasalimishe kwa
Muhammad, ili awauwe na
watakuja tu Mayahudi kutaka
hilo na ole wenu mkiwapa watu
wenu.
Baada ya kumwaga
propaganda hiyo kali, kisha
akatoka mpaka katika kabila
la Atfaan, akawambia kama
alivyowambia Makurashi, hapo
ndipo kila mmoja alipotoa
uaminifu juu ya mweziwe na
wakaamini waliyoambiwa na
Naaim bin Masoud na hikma
na propaganda ya Sahaba
ikiwafan ya kug awa n yika
kutokana na hikma kubwa
iliyotumiwa na Sahaba Naaim
bin Masoud.
Ama njia ya pili ni pale
Allah alipowaletea upepo mkali
wenye kutisha katika usiku wa
giza lenye baridi ndani yake,
kila mmja hamjuwi alokuwepo
pembeni yake kutokana na
tayari wameshachukua
uamuzi kwamba njia yoyote
ya kidiplomasia kuhusu
miradi ya nyuklia ya Iran
zinapaswa kufungwa.
Kundi hilo la wanasiasa
b a d o l i n a a m i n i k u wa ,
linaweza kuilazimisha Iran
kulegeza misimamo yake
kwa kuzidisha mashinikizo
ya kiuchumi.
Hata hivyo katika kipindi
cha miaka 10 iliyopita ya
vikwazo vikubwa dhidi
ya Iran, uwezo wake wa
nyuklia ulipanda kiasi cha
kuweza kuzalisha nishati
iliyorutubishwa kwa asilimia
20 kwa ajili ya kuzalisha
nishati ya kituo cha utafiti
Inatoka Uk. 20
Yafuatayo ni majina ya washindi wa mashindano ya Familia ya Mtume na Swahaba yaliyo fanyika kati ya mwezi wa tano na
wasita 2015.:( TANZANIA BARA NA VISIWANI)
N
a.
JINA LA MSHINDI
ZAWADI ALIYOPATA
SAFARI YA HIJA
Na.
JINA LA MSHINDI
SAFARI YA HIJA
SAFARI YA HIJA
11
12
SAFARI YA HIJA
)KOMPYUTA (LAPTOP)
13
)KOMPYUTA (LAPTOP)
)KOMPYUTA (LAPTOP)
14
RASHIDI A. KIBIRITI
)KOMPYUTA (LAPTOP)
15
LATIFA SEBASTIAN
16
17
SHAKILAABDULMALIK MOHAMED
SIMU YA MKONONI
18
SIMU YA MKONONI
SIMU YA MKONONI
19
SIMU YA MKONONI
1
0
SIMU YA MKONONI
20
MWANAHAMISI KHATIBU
MKOMBOLAGUHA
SIMU YA MKONONI
WASHINDI WATAFAHAMISHWA KUPITIA NAMBA ZAO ZA SIMU NAMNA WATAKAVYO KABIDHIWA ZAWADI ZAO.
1
cha Tehran.
Hivi sasa baada ya juhudi
za miaka 35 na mazungumzo
ya miaka miwili kuhusu
kadhia ya nyuklia ya Iran,
serikali ya Marekani imekiri
kuwa vikwazo na vitisho vya
kijeshi dhidi ya nchi hiyo
havikuwa na faida yoyote.
Hata hivyo inaonekana
kuwa, wanachama wengi wa
Congress ya Marekani ama
hawajaelewa uhakika huo
au kutokana na kuathiriwa
na mashindano ya kisiasa
baina ya vyama hasimu na
mifungamano yao na lobi za
Wazayuni, wanataka kukariri
njia ile ile iliyoshindwa. Hii
ni pamoja na kuwa kukataa
makubaliano yaliyoungwa
mkono na wanachama
watano wa kudumu wa
Baraza la Usalama la Umoja
wa Mataifa, nchi 28 za Umoja
wa Ulaya na nchi karibu zote
za dunia hakutakuwa na tija
nyingine zaidi ya kuifanya
Marekani itengwe katika uga
wa kimataifa.
Hii ni pamoja na kuwa,
ukiukaji wowote wa
Marekani azimio nambari
2231 la Baraza la Usalama
lililoidhinisha makubaliano
hayo ya nyuklia, utaizuia nchi
hiyo kuiweka tena vikwazo
Jamhuri ya Kiislamu.
17
MAKALA
AN-NUUR
A I B U Wa z i r i
wa zamani wa
Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa
nchini, Balozi Dk. Shareef
A b d u l k a d e e r, a m e t o a
thadhari kwa Waislamu
kufuatia kuripotiwa habari
ya kugundulika sehemu
ya nakala ya Quran
inayoelezwa kuwa inaweza
kuwa ndiyo ya kale zaidi
huko Uingereza.
Dk. Abdulkadeer aliandika
katika ukurasa wake wa
face book kuwa, pamoja na
kutolewa habari za ugunduzi
huo na kusambaa katika
mitandao ya kijamii na vyombo
vya habari sehemu mbalimbali
duniani, kwamba yawezekana
kipande hicho cha kale ndio
Qurna ya kale zaidi duniani,
bado kuna haja ya Waislamu
kuipokea habari hiyo kwa
tahadhari.
Alisema kugundulika
kwa Quran hiyo ya kale,
inawezekana kuna matayarisho
ya kugunduliwa vipande
vingine kutoka katika
makusanyo makubwa ya
maandiko (collection) yaliyopo
katika hazina ya Chuo Kikuu
cha Birmingham Uingereza.
Akitoa ufafanuzi, Dk.
Abdulkadeer alisema nakala
ya Quran, tena kamilifu na
ambayo ndiyo ya kale kabisa
duniani ni nakala iliyopo
nchini Uturuki, ambayo ni
Msahafu kamili uliokusanywa
na Sayydna Othman bin
Affan, aliokuwa akiusoma
nyumbani kwake hadi pale
alipouliwa ndani ya nyumba
hiyo akiwa anasoma Msahafu
huo na matone ya damu yake
bado yapo kwenye kurasa za
Msahafu huo.
Alisema kuwa Sayydna
Othman aliposhika ukhalifa
miaka sabab baada ya kifo cha
Mtume Muhammad (saw) na
kukuta watu wanajiandikia au
kuandikwa sehemu mbalimbali
za Quran kwa ajili ya matumizi
18
Na Mwinijisti Kamara
Kusupa
WALI ya yote
namshukuru
M h a r i r i
aliyenipa tena fursa
ya kuwasiliana na
wa s o m a j i wa A n n
u u r, n i k i r i u k we l i
wa moyoni kwamba
huko nyuma magazeti
mawili ya Kiislamu
Nasaha na An uur
yalikubali kuchapisha
mada zangu licha ya
kunielewa fika kwamba
mimi ni Mkristo tena
mwinjilisti, nami
sikuona kikwazo
chochote katika
kushirikiana na
Waislamu.
Hata baada ya mimi
kukutwa na zahama ya
kufungwa, mag azeti
hayo mawili yalinisaidia
kwa namna ya kipekee
ambayo hata ndugu
z a n g u wa d a mu n a
ndugu zangu katika imani
(Wakristo wenzangu)
hawakunisaidia kama
walivyonisaidia waandishi
wa Nasaha na Ann uur.
Nimeyaeleza kwa kirefu
ndani ya kitabu changu
cha MAISHA YANGU
GEREZANI SIMULIZI
LA SIKU 1888 ZA
MATESO.
Baada ya kutoka
gerezani kama ilivyo
ada kwa yeyote
anayetoka kifung oni
huwa mgeni ndani ya
nchi yake. Mawasiliano
na waliokuwa karibu
hupotea, hata hivyo
niliendelea kununua
na kusoma An nuur na
A LH U DA kwa kuwa
NASAHA sikuiona tena
mitaani wala sikujua
nimuulize nani.
Kuna jambo la pili
lililoongeza ufa kati
y a n g u n a Wa i s l a mu
waliokuwa karibu nami
hapo awali, baada ya
kumaliza kifungo nilikuta
wanaendesha harakati
tofauti za kuutokomeza
Mfumo Kristo ambao
siuelewi na kwa hiyo
sikuwaelewa. Nikiwa
mwenye kuikubali imani
ya Kikristo, singeweza
kujumuika nao na kukiri
kwa kinywa changu
kwamba Mfumo
Kristo utokomezwe.
Zamani tulipokuwa
karibu tuliimba wimbo
mmoja wa haki sawa
MAKALA
AN-NUUR
kuvichukua vyombo
vyake.
Hilo chukizo la
uharibifu limefichwa
yawezekana sehemu ya
maandiko ya unabii wa
Danieli yalifichwa kwa
makusudi ili kuulinda
uovu.
B a a d a
y a
kutahadharisha hilo, Yesu
akasema maneno yenye
changamoto walakini
hapo atakapokuja tena
mwana wa Adamu,
ataikuta imani duniani?
Naye Yuda mdog o
wake tumbo moja
n a Ye s u a l i a n d i k a
walakini katika kutafuta
mambo yote nimeona
niwaandikie juu ya jambo
m o j a t u k u wa o n y a
kwamba muishindanie
imani waliyokabidhiwa
watakatifu mara moja
tu. Maana ya maneno
hayo ni moja kwamba
mwanadamu anapaswa
kuipigania imani awapo
d u n i a n i , k wa s a b a b u
hatapata wasaa mwingine
wa kuitetea ama
kuipigania imani yake
baada ya kufa kwake.
Mtu akiisha kufa hana
tena nafasi ya kuamini
wala kuikiri imani yake,
k wa k u wa m a z i n g i r a
hayaruhusu.
19
Inatoka Uk. 18
kulikumbatia chukizo
linaloharibu na hatimaye
kuliweka patakatifu?
Nilitarajia Watanzania
kushikamana na kuutetea
ukweli kwamba kama
tulivyoupinga na kuukataa
ubaguzi wa rangi, sasa
tunaupinga na kuukataa
ushog a kwa vitendo.
N i l i t a r a j i a t u t awe k a
wazi misimamo ya
Taifa hili kwamba ikiwa
Uingereza iliyo kinara
wa Commonwealthy
inasema hivyo na inaamini
hivyo, basi Tanzania si
kwamba tunaikataa tu
misaada iliyoambatana
na shinikizo la kuukubali
ushoga, bali kuonyesha
tumechukizwa na
msimamo wa Uingereza,
Tanzania inajitoa kwenye
Jumuia ya madola.
Kwa s a b a b u n i a s a s i
isiyotusaidia chochote
kimaisha na sasa
imeangia hatua nyingine
ya kupig ana kufa na
kupona ili kutuondoa
kwenye maadili ya utu
na kutupeleka kwenye
ushetani. Maana ushoga
haustahili hata kuitwa
unyama kwani mbwa
pamoja na uumbwa wake,
bado dume la mbwa
halimwingilii kingono
dume mwenzake.
Jambo linalopaswa
kuhojiwa na watu makini
ni hili kwamba ni kitu
g ani kinachowafanya
watu wakubwa kama
Cameroon na Baraka
O b a m a k u wa p i g a n i a
mashoga kwa nguvu zote?
Je, wana huruma sana na
mashoga wa Afrika hadi
wawapiganie kiasi hicho?
Kama wana huruma ni
kwanini wasiwahurumie
watoto wafao kwa utapia
mlo katika nchi maskini
za Kiafrika? Kwanini
wasiwahurumie watoto
wa Iraq, Libya na Yemen
walikovamia bila sababu
za msingi?
Hapa
ndipo
inapojidhirisha wazi
kwamba hawawapiganii
mashoga kama wanadamu,
bali wanapigania
utamaduni wao unaoua
uhuru wa kweli na kuachia
u h u r u wa k i s h e t a n i
binaadamu kuwa mbaya
kwa kiwango chochote
anachotaka yaani uhuru
ambao kimsingi unaasi
maagizo ya Mwenyezi
HABARI
AN-NUUR
VACANCIES
AN-NUUR
20
MAKALA
20
AN-NUUR
(19)
HIJJA
INAZAA
UMOJA
NA
NGUVU.
SHAWWAL 1436, IJUMAA
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa katika
picha ya pamoja na ujumbe wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Dawa za
Kulevya na Uhalifu (UNODC) Afrika Mashariki, pamoja na baadhi ya watendaji wa Tume
ya Udhibiti wa Dawa za Kulevya Zanzibar. (Picha na Salmin Said, OMKR)
hayo, Makamu wa Kwanza
wa Rais wa Zanzibar Mhe.
Maalim Seif Sharif Hamad,
alisema Serikali inachukua
hatua mbalimbali kuiepusha
Zanzibar kuwa kituo cha
kuingizwa na kusafirishiwa
dawa za kulevya.
Aliongeza kuwa juhudi hizo
pia zinajumuisha kuwasaidia
wananchi wasijiingize
katika vitendo vya kutumia
kilichohudhuriwa na
Mawaziri watatu wa serikali
ya Rais Barack Obama
a m b a p o Jo h n K e r r y,
Ernest Moniz na Jacob
Lew, Mawaziri wa Mambo
ya Nje, Nishati na Fedha
wa Marekani walifanya
jitihada za kuwashawishi
wenzao katika Bunge hilo,
wakijaribu kusisitiza faida
za makubaliano ya nyuklia
ya kundi la 5+1 na Iran
na kujaribu kujibu hoja
za upinzani kutoka kwa
baadhi ya Maseneta dhidi
ya makubaliano hayo.
Matamshi ya muda mrefu
ya mawaziri hao wa serikali
ya Marekani, yalijikita zaidi
katika suala la kushindwa
Washington kuipigisha
Viongozi waandamizi
wa serikali ya Marekani
wanaona kuwa, iwapo
makubaliano yaliyofikiwa
kati ya Iran na kundi la 5+1
yatapingwa na Congress,
Iran itaingia katika mkondo
wa kurutubisha madini ya
urani kwa kiwango kikubwa
bila ya kuwa chini ya udhibiti
wa Wakala wa Kimataifa wa
Nishati ya Atomiki.
Kerry alisisitzia kuwa,
Inaendelea Uk. 16
Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na POA Printing Works LTD, S.L.P. 4605, Dar es Salaam.