Вы находитесь на странице: 1из 2

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA NISHATI NA MADINI


OFISI YA MADINI KANDA YA MASHARIKI

TANGAZO KWA UMMA


KUIBIWA KWA STAKABADHI ZA SERIKALI
(EXCHEQUER RECEIPT VOUCHER)
Ofisi ya Madini, Kanda ya Mashariki Dar es Salaam inautangazia
Umma kwamba, usiku wa Jumapili ya kuamkia tarehe 03-08-2015
wezi walivunja Ofisi ya Madini Kanda ya Mashariki iliyopo Upanga,
Dar es Salaam na kuiba vitu mbalimbali vya Ofisi vikiwemo vitabu vya
Stakabadhi za malipo ya Serikali.
Katika tukio hilo, stakabadhi namba ERV 6361601-6361800, na ERV
6361201, 6361202, 6361203, 6361204 ziliibwa.
Aidha, vitabu vipya vinane (8) vyenye Stakabadhi namba 63602016360400, 6360401-6360600, 6360601-6360800, 63608016361000, 6361001-6361200, 6361205-6361400, 63614016361600 na 6361801-6362000 viliibwa, kuharibiwa na kutupwa nje
ya ofisi ya madini.
Kwa taarifa hii, tunautangazia Umma kwamba stakabadhi zote
zilizoibwa na kuharibiwa hazitumiki na malipo yote yatakayofanyika
kupitia stakabadhi tajwa hapo juu yatakuwa ni batili.

Tunaomba yeyote mwenye taarifa sahihi zitakazoweza kusaidia


kukamatwa kwa wezi husika kutoa taarifa katika Ofisi ya Madini au
kituo chochote cha Polisi kilichopo karibu.
Imetolewa na:
Kamishna Msaidizi wa Madini
Kanda ya Mashariki Dar es Salaam

Вам также может понравиться