Академический Документы
Профессиональный Документы
Культура Документы
Baraza la Mawaziri
www.annuurpapers.co.tz au facebook:annuurpapers@yahoo.com
Sauti ya Waislamu
Uk. 2
ISSN 0856 - 3861 Na. 1207 SAFAR 1437, IJUMAA , DESEMBA 11-17, 2015 BEI TShs 800/=, Kshs 50/=
Kamilisheni kutangaza
Matokeo ya Uchaguzi
Tunarejea Ulaya ila tutarudi-EU EOM
Wakutana na Othman, Jaji Makungu
Kinana apiga chenga ya mazungumzo
Othman Masoud.
Aal Imran: 86
Fethullah-Gulen
VIPI atawaongoza
Mwenyezi Mungu watu
ambao wamekufuru
baada ya kuamini
kwao na wakashuhudia
kwamba Mtume ni
kweli na zikawajia hofu
zilizo wazi na Mwenyezi
Mungu hawaongozi watu
waliyo madhalimu. [Aali
Imraan 86]
Hakika wale ambao
wanasimama ubavuni
mwa madhalimu, wenye
kuunga mkono ukafiri na
batili pamoja na kuwa wao
wameshuhudia uzuri wa
ukweli na wanauona ubaya
Baraza la Mawaziri
R a i s wa J a m h u r i ya
Muungano wa Tanzania
Dkt. John Joseph Pombe
Magufuli jana ametangaza
Baraza lake la Mawaziri
akiunganisha baadhi ya
wizara na kufuta cheo
cha Naibu Waziri katika
wizara nyingi.
Katika Baraza hilo
Mawaziri waliorejea
kutoka serikali iliyopita
ya Jakaya Mrisho Kikwete
ni George Simbachawene
na Angela Jasmini Kairuki
ambao wameteuliwa kuwa
Mawaziri katika Ofisi ya
Rais TAMISEMI, Utawala
Bora na Utumishi wa
Umma.
Sura ngeni ni Suleiman
Jafo, ambaye anakuwa
N a i b u Wa z i r i k a t i k a
Wizara hiyo.
Januari Yusuph
Makamba amerejeshwa
na kuwa Waziri katika
Ofisi ya Makamu wa Rais
Muungano na Mazingira
na Naibu wake ni Luhaga
Mpina akiwa ameingia
kwa mara ya kwanza
katika Baraza.
Jenista Mhagama
amerejea na kuwa Waziri
wa Katika Ofisi ya Waziri
AN-NUUR
H F
M A
Q A
D A
Q R
H A
Y
O Q
U A
H M A
N A
N I
M S
M H A
M K
H A
M A
M A
L
I
M A
K
H A
U B
U M M U
D L
M A
10 19 3
32
MASUALA
1.Wataje watu wane wa mwanzo Kusilimu. Jawabu: Khadija, Zaid ibn
Harith, Ali bin Abi Talib, Abubakar
2.Wataje wanawake wa mwanzo kusilimu. Jawabu: Ummul Fadl, Asma
Umais, Fatma Khatab.
3.Mke wa mwanzo wa Syd Uthman bin Afan (RA). Jawabu: Ruqayyah
4.Nani alimnunua Zaid bin Harith? Jawabu: Hakim Hazim,
5.Syd Ali (RA) alisilimu akiwa na umri gani? Jawabu : Miaka 10
6.Sahaba Sad Abi Waqas alisilimu akiwa na umri wa miaka mingapi?
Jawabu: Miaka 19
7.Kipindi cha muda gani adhana iliadhiniwa kwa siri? Jawabu : Miaka 3
8.Taja jina la mwanadamu wa mwanzo kuuwa? Jawabu : Qabil
9.Waislamu walikuwa wakikutana kwa siri na kujifunza dini katika
nyumba ya nani? Jawabu : Aqram
10.Mtume Mussa (AS) akikutana na Mola wake kwenye Mlima? Jawabu:
Sinai
CHEMSHA BONGO: 30
Weka duara kwenye jawabu ilio sawa. Jawabu kamili wiki ijayo.
Q L
M Y
M Z
Q B
U U H
Q M S
N M A
O A
U N
H A
M O N Q R
N A
M S
Q R
H J
U R
W A
U B
M A
M A
O H A
MASUALA
1. Mtaje Shahidi wa mwanzo katika Uislamu.
2. Sahaba aliokuwa na jina la Rum/Roman.
3. Makabila mawili Mtume (SAW) aliwakuta Madina wakiwa
kwenye ugomvi mkubwa akawasuluhisha.
4. Masahaba wawili watoto wao waliolewa na Mtume (SAW).
5. Kipando alichokipanda Mtume (SAW) alipokwenda Miraj.
6. Vitabu 4 vitakatifu walivyoteremshiwa Mitume.
7. Aya ya kwanza kuteremshwa.
8. Muadhini wa mwanzo katika Uislamu.
9. Nyenzo ilio muhimu katika kutia Udhu.
10. Harufu 3 za mwanzo katika Suratul Baqara.
Jee Unajua?
3
Na Bakari Mwakangwale
SHEIKH Ponda Issa Ponda
amewashukuru Waislamu
wa Morogoro kwa msaada
wao na ushirikiano mkubwa
walioonyesha baada ya yeye
kupigwa risasi.
Sheikh Ponda ametoa
shukrani hizo alipokuwa
akiongea na Waislamu katika
Msikiti wa Mtambani Jijini
Dar es Salaam, Ijumaa ya
wiki iliyopita, akizungumzia
mkasa wake wa kupigwa
risasi kisha kuwekwa
mahabusu zaidi ya miaka
miwili.
Ilipotokea ile kadhia
mimi kupigwa risasi, kwa
kweli Waislamu wa Morogoro
walionyesha mshikamano wa
hali ya juu kabisa.
Kwani katika gari
n i l i y o k u we m o l i l i k u wa
limezingirwa na gari tatu za
askari, lakini hawakushuka
katika gari zao, ila baada
ya k u p i g wa i l e r i s a s i ,
nilisikia sauti ya Askari
Polisi, ikiamuru Yule pale
muokoteni. Alisema Shkh
Ponda, akisimulia hali ya
tukio hilo.
Kufuatia amri hiyo, Shkh
Ponda, alisema hapo ndipo
aliona Askari wale wakichupa
kutoka katika magari yao
na kushuka chini wakiwa
mbio wakimfuata katika eneo
alipoangukia ili wamchukue.
Katika purukushani
hizo alisema, kilichotokea
katika mazingira hayo ni
mvutano baina ya Askari
na Waislamu kwa haraka
waliweza kushikana mikono
na kutengeneza kitu kama
ukuta, ambao kutokana na
wingi wao walisaidia Askari
Polisi kuweza kumfikia kwa
haraka.
Waislamu hao wakawa
wanasema wakiwaambia
Polisi, hatutoka hapa, labda
mtuue wote wale askari
walipowakaribia wakiwa na
silaha zao nikadhani Umma
ule utatawanyika uniache,
lakini haikuwa hivyo.
Hali ile iliwakwamisha
Polisi kwani ilikuwa kwanza
wawasambaratishe kisha
wanifikie, na wangefanya
hivyo yangetokea mauaji
mengine ya Waislamu.
Alisema.
Wa k a t i m a b i s h a n o
hayo yakiendelea, alisema
umma ule wa Kiislamu
baadhi yao, kwa haraka
wa l i s o g e z a p i k i p i k i n a
kumpakia kisha waliondoka
bila askari kufahamu kama
nimeondoka kutokana na
wingi na msongamano wa
Waislamu.
Alisema, mpaka Polisi
wanaanza kupiga mabomu
ya machozi kuwatawanya,
tayari Waislamu walikuwa
wamewazidi Polisi maarifa
na kuondoka nae katika
eneo hilo na kumuwahisha
hospitalini.
Shkh Ponda, alisema
kitendo kile kilikuwa si tu cha
kishujaa, bali katika mtazamo
wa kibinadamu kilikuwa na
Habari
AN-NUUR
kumpeleka hospitali na
kutokana na kutokwa na
damu nyingi hali ambayo
ingesababisha matatizo zaidi
na lolote lingeweza kumtokea.
Kwa maana hiyo utaona
kwamba lile tukio la kuwazuia
Askari wasinichukue badala
yake Waislamu kufanikiwa
kunichukua lilikuwa na
mchango mkubwa sana katika
Na Mwandishi Wetu
kukutana na Mwenyekiti
wa ZEC Jecha Salim Jecha,
ambaye ndiye aliyeleta
sintofahamu hiyo, hata
hivyo hawakuweza
kumpata.
Badala yake EU EOM
ilikutana na wadau wakuu
Visiwani, vikiwemo vyama
vya siasa, Mwana Sheria
Mkuu wa Serikali wa
zamani na wa sasa, wadau
wa sharia na mahakama,
asasi za kiraia na maafisa
uchaguzi.
Hapana shaka msimamo
wa Mwanasheria Mkuu wa
sasa Jaji Omari Makungu
utakuwa ule wa SMZ na
C C M wa k u d a i k u wa
uamuzi wa Jecha ni halali
na Dr Shein anastahiki
kuendelea kuwa Rais,
kikatiba na kisheria na
kwamba kinachotakiwa ni
kurudiwa uchaguzi.
Kwa upande wa
Mwanasheria Mkuu wa
zamani Bwana Othman
Masoud, ameweka wazi
msimamo wake hadharani
mapema kwamba kitendo
kilichofanyika ni cha
kihuni na kisichotarajiwa.
Tahariri/Habari
AN-NUUR
Usafi ni muhimu
kwa kila binadamu
WASWAHILI tuna
msemo usemao mtu
ni afya. Na moja ya
vigezo vikubwa vya
mtu kuwa na afya
njema ni usafi.
Usafi unaanzia
kwa mtu mwenyewe,
kuanzia mwili wake,
mavazi yake, makazi
na mazingira yote
yanayotuzunguka.
Mazingira hayo
ni pamoja na yale
tunayofanyia shughuli
ze t u za k u t up a t i a
vipato vya kuendesha
maisha ya kila siku,
mazingira ya angani,
majini na ardhini.
Usafi ndio kinga kuu
ya maradhi mbalimbali
yanayomwandama
mwanadamu. Kwa
ujumla tunaweza
kusema kuwa usafi ni
nuru ya maisha ya kila
mwanadamu.
Wa i s l a m u w a n a
usemi wao al
Islam nadhiif
wakimaanisha kuwa
Uislamu ni dini ya
usafi na Muislamu
sharti uwe msafi. Kwa
maana ya ujumla ni
kwamba binadamu ni
usafi nafsi na mwili.
Kwa mwanadamu
yeyote anayejitambua
na anayejali uhai wake,
haitarajiwi kwamba
l a z i m a a s u k u m we
au akumbushwe
na serikali au Rais
kutimiza wajibu wake
huo wa kimaisha kwa
maslahi yake.
Rais Magufuli
katumia tu busara
zake kuwashtua
wa t a n z i a k wa m b a
AN-NUUR
na hatimae kuwafikisha
Mahakamani watu wote
waliohusika kumshinikiza
Mwenyekiti wa Tume Jecha
Salim Jecha kutoa tamko la
kufuta uchaguzi na matokeo
yake.
Mbali ya hayo chama hicho
kilitoa wito kwa Viongozi
wote wa vyama vya siasa
kujitathmini wajibu wao
katika kuheshimu maamuzi
ya wananchi yanayofanywa
kwa njia ya demokrasia ili
kujenga misingi mizuri ya
utawala bora.
Chama cha Wanasheria
Zanzibar tunaamini
k wa m b a R a i s we t u wa
Z a n z i b a r a t a n g a m u a
mtego huu unaokusudia
kumuweka katika Historia
ya Rais wa Zanzibar aliewahi
kuvunja Katiba ya Nchi na
kumuondolea rekodi nzuri
aliyonayo ya kuheshimu
sheria na Katiba ya Nchi
na Utawala Bora alisema
mmoja wa wanasheria
Bwana Shaaban.
Kwa upande wake Rais
wa chama hicho Awadh
Ali Said alisema Chama
Cha Wanasheria Zanzibar
kimefadhaishwa na
uamuzi huo hasa kwa
kuzingatia mamlaka
aliyonayo Mwenyekiti
huyo kisheria katika
kufikia Uamuzi kama huo.
Kwa Mujibu wa Sheria,
Tume haina uwezo wala
Mamlaka ya kufuta
matokeo yaliyokwisha
tangazwa na ambapo
mgombea ameshapewa
shahada ya kuchaguliwa.
Alisema akizingatia
kuwa wapo wagombea
wa Uwakilishi ambao
kama wale wa Ubunge
walishapewa vyeti vya
ushindi na maofisa wa
Tume.
Rais huyo ambae ni
wakili anasema wajibu
wa Tume ni kuchapisha
matokeo hayo kwenye
gazeti la serikali kama
kanuni ya 59 (4) na kifungu
cha 88 (c) cha Sheria ya
Uchaguzi vinavyoeleza
na kama kuna Mgombea
ambae hajaridhika na
matokeo au maamuzi ya
Msimamizi wa Uchaguzi,
basi anachotakiwa kufanya
ni kwenda Mahakama
K u u k wa m u j i b u wa
kifungu cha 86 cha Sheria
ya Uchaguzi na Ibara ya 72
(1) ya Katiba ya Zanzibar
ya 1984 ambayo ndio
yenye Mamlaka ya kufuta
uchaguzi na matokeo yake.
Akitaja athari ya tamko
la Mwenyekiti wa Tume
ya U c h a g u z i Z a n z i b a r
yanaweza kuiingiza Nchi
katika mgogoro wa Mkubwa
wa Kikatiba katika maeneo
kadhaa kadhaa ambapo
aliyataja kuwa ni muda wa
tu na sio kuendelea
kukaa madarakani
bila ya kufanyika kwa
Uchaguzi au kwa sababu
ya Uchaguzi kufutwa.
Akaongeza kuwa, ni
wazi Nchi itaendeshwa
m u d a m r e f u b i l a ya
kuwepo kwa Baraza la
Wawakilishi ambalo ni
mhimili muhimu katika
uendeshaji wa Serikali.
A l i s e m a K a t i b a ya
Zanzibar imeruhusu hali
ya kuendesha Nchi bila ya
Baraza la Wawakilishi kwa
muda usiozidi siku tisini
(90) tu kuanzia siku Baraza
lilipovunjwa.
Akionesha khofu juu ya
suala hilo alisema hatari
ya kuwa na Rais ambaye
yuko juu ya Sheria na
Katiba ya Nchi, Ibara ya
37 ya Katiba ya Zanzibar
ya 1984 inaipa Mamlaka
Baraza la Wawakilishi
kuondoa kinga ya Rais
kutoshitakiwa anapokuwa
madarakani kama
inavyotolewa na Ibara ya
36 ya Katiba.
Alisema katika
mazingira yaliyopo hivi
sasa, Baraza la Wawakilishi
halitakuwepo na haliwezi
kuitishwa kikatiba.
Na kwa hivyo, ni wazi
kuwa ikiwa Rais atafanya
matendo yoyote yenye
kuvunja katiba ya Nchi
na kukiuka Kiapo chake,
hakutakuwa na Mamlaka
nyengine yoyote yenye
uwezo wa kuhoji matendo
ya Rais.
Alisema hii inatoa fursa
na inatengeneza hatari
ya k u wa n a S e r i k a l i
inayoongozwa na Dikteta.
Habari za Kimataifa
AN-NUUR
DONALD Trump
WANA DAMU
amezungukwa
na neema
nyingi sana. Neema
zote hizi tumepewa
bila kuzifanyia kazi
yoyote. Hii ina maana
kuwa tunapaswa
kumshukuru sana
yule aliyetupa neema
hizo, yaani Mwenyezi
Mungu. Neema kubwa
kabisa na ya kwanza ni
uhai. Wengi wetu hili
hatulizingatii hadi pale
yanapozuka mazingira
fulani yanayoonyesha
kuwa neema hii inataka
kutuondoka.
Haijalishi umri,
haijalishi ukamilifu wa
viungo, haijalishi hali
ya siha, na haijalishi hali
ya kiuchumi. Watoto,
vijana, wazee; viwete,
vipofu, mabubu, viziwi,
na taahira; wadhaifu,
wenye nguvu, wazima na
wagonjwa; masikini na
matajiri wote tutafanya
kila linalowezekana
kungangania neema
ya uhai, pale neema
hiyo itakapoonekana
kutishiwa!
Je, kuna siku
umekumbuka
kumuelekea Mwenyezi
Mungu na kumwambia,
nakushukuru ewe Mola
wangu kwa kunijaalia
neema hii ya uhai?
Baada ya uhai neema
nyingine kubwa ni siha
njema. Siha njema ndiyo
raslimali muhimu kuliko
zote katika raslimali
ulizonazo. Raslimali hii
ndiyo inayokuwezesha
kupata na kuendelea
kuwa na raslimali
zako nyingine. Wenye
matatizo ya kiafya hili
wanalijua vizuri sana.
Fursa za kiuchumi na
maendeleo zinazopotea
kutokana na afya
kutokuwa sawa ni nyingi
mno.
Je, kuna siku
umekumbuka
kumuelekea Mwenyezi
Mungu na kumwambia,
nakushukuru ewe Mola
wangu kwa kunijaalia
neema hii ya siha njema?
Baada ya siha njema,
neema nyingine kubwa
sana ni muda. Baada ya
siha njema, muda ndiyo
raslimali inayofuata kwa
ubora miongoni mwa
raslimali ulizonazo.
Mara nyingi matumizi
ya raslimali hii ndiyo
yanayomtofautisha mtu
mwenye elimu na mtu
mjinga, mtu mwenye
kipato kizuri na mtu
mwenye kipato duni, na
mtu mwenye mafanikio
katika nyanja mbalimbali
na mtu anayekabiliwa na
mkwamo. Huwezi kuwa
na ufanisi na tija kwenye
shughuli zako kama una
tatizo la matumizi ya
muda.
Je, kuna siku
AN-NUUR
ambayo huimarisha
urijali na kumfanya
mwanamme ajisikie ni
mwanamme wa ukweli.
Kuongezeka kwa homoni
ya oxytocin, ambayo
humfanya mhusika awe
na uwezo wa kujenga
mahusiano mazuri na
watu wengine kwenye
jamii. Kuongezeka kwa
homoni ya dopamine,
ambayo inahusishwa
na uwezo wa utambuzi
na kumfanya mhusika
kijisikia raha. Kupungua
katika mzunguko wa
damu kwa homoni
ya cortisol na homoni
nyingine zinazohusishwa
na kuwepo kwa
msongo. Kupungua
kwenye mzunguko wa
damu kwa kemikali
zinazoitwa cytokines
ambazo zinahusishwa
na ongezeko la mfuro
(inflammation) katika seli
za mwili; na Kupungua
kwa sukari ya damu.
(Kwa mawasiliano
zaidi piga namba 0754
281 131/0655 281 131)
7
Na Khatibu J. Mziray
IVI karibuni
t u l i i s h i a
mahali ambapo
inaonekana kana kwamba
k u n a k u b a r i k i wa n a
mungu hata katika
kufanya mambo ya hovyo
na kwa ulaghai. Lakini
Mwenye Enzi Mungu
hana udhaifu huo wa
kubariki dhambi. Hata
hivyo tuone kuwa ndani
ya Biblia mzazi ana hadhi
gani:
Wa h e s h i m u b a b a
yako na mama yako; siku
zako zipate kuwa nyingi
katika nchi upewayo na
BWANA, Mungu wako.
Usimshuhudie jirani
yako uongoUsiitamani
nyumba ya jirani yako,
u s i m t a m a n i m k e wa
jirani yako; wala mtumwa
wake, wala mjakazi wake,
wala ngombe wake, wala
punda wake, wala cho
chote alicho nacho jirani
yako. (Kutoka 20:12-17.)
Swali ni hili: Ni vipi
mtume wa Mwenyezi
Mungu (Yakobo) alivyoasi
sheria hiyo ya Mwenyezi
Mungu kwa kutamani
u k u b wa wa E s a u n a
pia kumdanganya baba
Habari
AN-NUUR
Z AY U N I
au
Zionism ni
miongoni mwa
i t i k a d i m b a ya i l i y o
kinyume na mafundisho
ya Biblia. Inatokana na
mlima Sayuni ulioko
nchini Israeli. Baadhi ya
wanazuoni waliifananisha
Zionism na Apertheid
ya Makaburu wa Afrika
y a k u s i n i . We n g i n e
wakaitetea kwamba
usayuni hauna cha
kufanya na rangi au utaifa
wa mtu.
Kimsingi maneno ya
Mungu hayana tatizo,
tatizo liko kwa wanadamu
kuyatafsiri sawa na
matakwa yao, nao ukomo
wa akili au limitation
umechangia kuupotosha
ukweli wa Mungu. Ndiyo
maana mitume na manabii
hawakutumainia akili
zao za kuzaliwa, bali
walitumainia ufunuo wa
Mungu wahyi. Musa
aliandika mambo ya
sirini ni ya Bwana Mungu
wetu lakini mambo
yaliyofunuliwa ni yetu sisi
na watoto wetu milele ili
tuyafanye maneno yote ya
yote niliyowafundisha na
tazama mimi niko pamoja
nanyi hadi ukamilifu wa
dahari.
Dhana ya usayuni
ambapo
Mungu
anaonekana ni Mungu wa
Waisraeli tu ilitokana na
maneno ya msisitizo ya
manabii ambao Mungu
alikuwa akiwainua ili
kusema na taifa la Israeli
lililopotoka. Jambo la
kukumbuka ni kwamba
kutokana na mfumo
aliokuwa ameuasisi Nabii
na mtume Musa, Waisraeli
ilibidi waongozwe na
wa o n a j i wa a n d i s h i
wengine wamewaita
waamuzi au majaji.
B a a d a y e Wa i s r a e l i
wakaukataa mfumo wa
wa a m u z i wa k a wa n a
mfumo wa Wafalme, ni
wakati huo wa kuongozwa
na wafalme ndipo baadhi
yao yaani wafalme
wasiomcha Mungu,
washirikina walioabudu
uchawi wakitumainia
nguvu
zingine
zisizotokana na Mungu,
n d i p o wa l i p o i n u l i wa
manabii kuonya.
Chini ya mazingira hayo
ya Waisraeli kupotoka
Inaendelea Uk. 8
8
Inatoka Uk. 7
waumini wanaziita kuwa
ni mibaraka. Sina haja
ya kufafanua aya hizo
hapo juu, labda tu niseme,
kuwa, huo ndio mtaala
(manhaji) uliojengea
Ukristo toka Antiokia,
miaka 14 baada ya Yesu
kuondoka- (Matendo
11:26.)
Sasa angalia huo wajibu
wa mama mzazi tena mke
wa mteule wa Mwenyezi
Mungu!
Esau akamchukia
Ya k o b o k wa a j i l i ya
ule mbaraka babaye
aliombarikia. Esau
akasema moyoni mwake,
Siku za kumlilia baba
yangu zinakaribia, ndipo
nitakapomwua ndugu
yangu Yakobo. Rebeka
akaarifiwa maneno ya
Esau, mwanawe mkubwa.
Akapeleka mtu kumwita
Yakobo, mwanawe mdogo,
akamwambia, Tazama
katika habari za Esau,
ndugu yako, anajifariji
Makala
AN-NUUR
Mungu mwingi wa
huruma, mwenye fadhila,
si mwepesi wa hasira,
mwingi wa rehema na
kweli; mwenye kuwaonea
huruma watu elfu elfu,
mwenye kusamehe
uovu na ,makosa na
dhambi; wala si mwenye
kumhesabia mtu mwovu
kuwa hana hatia kamwe;
mwenye kuwapatiliza
watoto uovu wa baba zao,
na wana wa wana wao pia,
hata kizazi cha tatu na cha
nne. (Kutoka 34:5-7.)
Kuna watu hawaamini
kuwa wana wa Israeli
walipatilizwa, na
wanaendelea kupatilizwa
kutokana na matendo
ya imani zao; na hasa
kwa kuwa wanaonekana
kuwa wameshikilia
mambo mengi ya
mifumo inayoaminiwa
kuwa ni ya kiuchumi na
aliyetakaswa isipokuwa
Naaman mtu wa Shamu,
tena walikuwako wajane
wengi katika nchi ya Israeli
zamani za Nabii Ealiya
lakini Eliya hakutumwa
kwa Mwisraeli yeyote
isipokuwa huko Sarepta
nchi ya Sidoni. Wote
waliposikia maneno
hayo wakajaa ghadhabu
wa k a m r u k i a k wa n i a
moja ya kutaka kumuua
lakini wakasita kwasababu
kulikuwa na kifungu cha
sheria kwenye torati yao
kilichowataka kufanya
kitakatifu siku ya sabato.
Wa k a a m u a k w e n d a
kumsukumiza shimoni,
lakini Yesu akapuruchuka
na kuwatoka.
Kilichowaudhi kutokana
na maneno hayo ya Yesu ni
kwasababu alifundisha
kinyume na itikadi yao ya
Usayuni. Aliwaonyesha
na kuwathibitishia
k wa m b a M u n g u wa o
anawaheshimu hata watu
wa mataifa mengine, akatoa
ushahidi wa Nabii Eliya
alivyotumwa kwa mjane
wa Serepta nchi ya Sidoni
kwa watu wasiokuwa
Waisraeli, akawatolea
mfano mwingine kwamba
Mungu alimtakasa
Naamani asiye Mwisraeli
kwahiyo akahitimisha
k wa m b a M u n g u wa o
anawaheshimu na
kuwathamini watu wa
mataifa mengine. Hilo
ikawaudhi wakaamua
kumuua.
9
Na Omar Msangi
ENYA imeingia na
kuzama katika tope
la mzaha wa ugaidi
sasa nayo ikifanya kile
kinachoitwa Anti-terror
drills. Haya ni mazoezi
ya p o l i s i , wa n a j e s h i
na watoa huduma
ya mwanzo ambapo
wanaigiza lau ingekuwa
kuna tukio la ugaidi
wangefanyaje. Katika
mazoezi hayo, hupatikana
washambuliaji bandia
katika polisi, majeruhi na
hata maiti bandia. Kisha
waokoaji yakiwemo
m a g a r i ya wa g o n j wa
(ambulances) ambayo
Makala
AN-NUUR
WANAFUNZI wa Chuo
Kikuu cha Strathmore
wakiwa madirishani
kutaka kuruka kutoka
ghorofa za juu. Kushoto
mmoja wa wanafunzi
aliyejeruhiwa akisaidiwa
na wenzake.
Na Mwandishi Wetu
ALI ni ya
wasiwasi na
kuogofya kwa
Waislamu wa Kenya,
Uganda na Afrika
Mashariki kwa ujumla.
Wakati kule Uganda
pamekuwa na msururu
wa kuuliwa Masheikh,
Kenya nako hali imekuwa
hivyo hivyo.
Hadi sasa Masheikh
12 wameshauliwa nchini
Uganda katika kipindi
cha miaka mitatu.
La kusikitisha ni kuwa,
unaodaiwa uchunguzi
wa polisi, mpaka
sasa haujabaini nani
wanahusika na mauwaji
hayo.
Hali ikiwa hivyo
Uganda, baada ya
mfululizo wa mauwaji
ya Masheikh Kenya,
wakiwemo Sheikh
Aboud Roggo na Sheikh
Abubakar Shariff aka
Makaburi, Jumapili
ya wiki iliyopita
limegundulika kaburi
10
Inatoka Uk. 9
ya msemaji wa Chuo
Kikuu hicho Betty Ngala,
aliyefariki ni mfanyakazi
wa Chuo Bi Esther
Kidambi, mwenye umri
wa miaka 33. Bi Ester
Kindambi aliruka kutoka
gorofa ya 3 katika jitihada
za kuokoa maisha yake
baada ya polisi waliokuwa
wakiigiza shambulio la
kigaidi kutumia risasi za
moto jumuiya ya Chuo
Kikuu ikiwa haina habari.
Taarifa zaidi zinasema
kuwa kishindo cha risasi
kutoka bunduki nzito
kilisababisha wanafunzi
kukimbia ovyo na kuruka
kutoka ghorofa za juu
j a mbo l i l i l os ababis h a
baadhi kuvunjika miguu,
wengine wakilazwa
hospitali katika vitengo vya
wagonjwa mahututi (ICU).
Makamo Mkuu wa chuo
(vice chancellor ), Prof.
John Odhiambo amesema
kuwa chuo kitawalipia
gharama za matibabu
walioumia ambapo
alisema kuwa hadi sasa
20 bado wapo hospitali
wawili hali zao zikiwa
mbaya. Katika taarifa yake,
Makamo Mkuu Msaidizi
wa Chuo hicho George
Njenga, amekiri kulazwa
wanafunzi ICU akisema
kuwa katika majeruhi
yupo Profesa mmoja wa
Chuo ambaye aliruka
Inatoka Uk. 9
Kiislamu hakuonekana
tena hadi Jumapili
alipogundulika kuwa
moja ya maiti 12
zilizofukiwa katika shimo
moja.
Maiti ya mama huyo
ilikutwa imevunjwa
vunjwa mifupa na
kungolewa meno, jambo
linaloonyesha kuwa
aliteswa sana kabla ya
kuuliwa na kufukiwa
akiwa uchi kabisa.
Taarifa kutoka
Mandera zinafahamisha
kuwa maiti za watu hao
12 waliokutwa katika
shimo moja, ni katika
jumla ya Waislamu 59
walikuwa wametoweka
kwa siku za karibuni
katika mazingira ya
kutatanisha huku
taarifa zikisambaa kuwa
walikuwa wamenaswa
na Polisi wa kupambana
na ugaidi. Hadi sasa
maiti 25 za watu hao
waliokuwa wamepotea
zimeshagundulika.
Pamoja na serikali ya
Kenya kukanusha mara
kwa mara kuwa haihusiki
na kuuliwa Masheikh
wala kupotea kwa baadhi
ya Waislamu katika
mazingira ya kutatanisha,
Makala
AN-NUUR
madirishani na kukatwa na
vioo. Wengine walijikuta
wakitumbukia katika
mto Mbagathi uliofurika
wakiongea na waandishi
wa habari wamesema
kuwa ni siri iliyo wazi
kuwa wanaohusika
na vitendo vya kuteka
wananchi wasio na hatia
na kisha kuwauwa ni
jeshi na vyombo vya
11
Inatoka Uk. 10
na kushambulia wanachuo
wa chuo cha afya cha San
Bernardino, California,
Marekani. Polisi katika
California wamethibitisha
k u f a n y i k a wa l i c h o i t a
Active Shooter Drill hapo
San Bernardino. (Tazama:
Police Confirm Active
Shooter Drill During San
Bernardino Terror Attack.
Tazama pia: Breaking: San
Bernardino Mass Shooting
False Flag with Active
Shooter Drills. Au VVC
Alerts Public to Upcoming
Active Shooter Training.)
Wafuatiliaji wa mambo
wanasema kuwa baada
ya zoezi la Active Shooter
Drill ambapo picha za
v i d e o z i l i c h u k u l i wa ,
ndio ghafla Polisi hao
wakaibuka na taarifa kuwa
kuna magaidi wakavamia
nyumba za baadhi ya watu
na kuanza kupekua na
kupiga picha. Mlolongo
ukawa mrefu ikiwa ni
pamoja na kuibua visa
kwamba huyu alipata
k u s o m a s e m i n a r i ya
Kiislamu Pakistan, aliwahi
kwenda Saudi Arabia na
mambo kama hayo ili
kukoleza habari zao za
magaidi wa IS.
Na katika tukio la hivi
karibuni la Paris ambapo
tuliambiwa kuwa magaidi
wa IS waliuwa takribani
watu 130, mchezo kama
huo ulifanyika masaa
machache tu kabla ya tukio.
Na baadhi ya wachambuzi
wanasema kuwa baadhi
ya picha zilizochukuliwa
katika Drill ile wauguzi
wakisaidia majeruhi, ndio
nyingine zimeonyeshwa
kuwa ni za shambulio
(Tazama: Hours Before
the Terror Attacks, Paris
Practiced for a Mass
Shooting.)
Itakumbukwa pia
kwamba kiasi miaka 10
iliyopita, July 7, 2005,
l i l i f a n y i k a l i l i l o i t wa
shambulio la kigaidi
London, maarufu the
London 7/7 bombings.
Taarifa zinaonyesha kuwa
wakati shambulio hilo
likifanyika, wakati huo huo
lilikuwa likifanyika zoezi
la kuigiza The London
7/7 Mock Terror Drill
ambapo polisi walifyatua
mabomu na wakawepo
wauguzi na magari ya
wagonjwa (ambulances)
kubeba majeruhi na
maiti bandia. Taarifa za
kuwepo zoezi hilo la
kuigiza zilifichuliwa na
Mkurugenzi wa Kampuni
ya Visor Consultants, iliyo
wakala wa Polisi katika
jiji la London (London
Metropolitan Police),
wakati akihojiwa na BBC.
Peter Power aliwahi kuwa
kachero wa ngazi za juu
wa Scotland Yard. Lakini
inaelezwa pia kwamba hilo
halikuwa zoezi la kwanza.
Mock terror drill ya 7/7
iliyoandaliwa na Visor
Makala
AN-NUUR
JUU mmoja wa watu anayedaiwa kupoteza miguu miwili katika shambulio la Boston
akitajwa kwa jina la "Jeff Bauman" akisaidiwa na muongoza filamu Steven Allan Spielberg
mwenye heti. Chini vikopo vya damu bandia na waigizaji majeruhi wa ugaidi.
Consultants, ilitanguliwa
na zoezi kama hilo mwezi
Aprili mwaka huo huo
lililopewa jina la Atlantic
Blue, miezi mitatu kabla
ya s h a m b u l i o . K a b l a
ya hapo mwaka 2003,
lilifanyika pia likipewa
jina la OSIRIS 2.
Ukiacha habari
ya Atlantic Blue ni
kupatikana kwa taarifa
kuwa baadhi ya watu
walikuwa wakijua
kitakachotokea kabla
ya shambulio lenyewe.
Mmoja wao akiwa Waziri
wa Fedha wa Israel wakati
huo Benjamin Netanyahu.
Wakati huu Netanyahu ni
Waziri Mkuu. Kwa mujibu
wa taarifa za Shirika la
Habari la Associated Press
(Jerusalem), Netanyahu
akiwa Londion alizuiwa
kutoka hotelini kwake
k we n d a k a t i k a k i k a o
ambacho kilikuwa
kikifanyika katika hoteli
iliyo jirani kabisa na
mahali ambapo lilitokea
shambulio.
The London 7/7
Mock Terror Drill: What
Relationship to the Real
Time Terror Attacks?
Anauliza Prof Michel
Chossudovsky ambapo
anasema ni jambo la
kushangaza kidogo
kwamba wakati wananchi
wanatangaziwa kuwa kuna
magaidi wanashambulia,
wakati huo huo polisi
wanaigiza kufanya ugaidi
(fictional scenario of
multiple bomb attacks)
huku mamlaka za uokozi
zikihudumia majeruhi wa
kuigiza.
Ukitoka London 7/7
bombings na kwenda
9/11, inaelezwa kuwa
muda mfupi kabla ya
shambulio la Septemba
11 2001, katika majengo
pacha, World Trade
Center na Pentagon, CIA
walikuwa wakiendesha
a pre-planned simulation
to explore the emergency
response issues that would
be created if a plane were
to strike a building. Zoezi
lililofanyika katika ofisi
za CIA (CIA Chantilly
Virginia Reconnaissance
Office.) Serikali ya Rais
wa M a r e k a n i wa k a t i
huo George W Bush
akizungumzia zoezi hilo
lililofuatana na shambulio
la Septemba 11 alisema kwa
kifupi kuwa hiyo ilikuwa
bizarre coincidence kwa
maana kwamba kilikuwa
kiroja na jambo lisilo la
kawaida.
Ukija katika lile tukio
maarufu la Boston
Marathon Bombing
mwaka 2013, mambo ni
yale yale. Polisi (wasanii)
na wasanii wengine wa
uigizaji wa majeruhi, maiti,
waandishi wa habari,
wauguzi na waokoaji,
wa l i k u wa wa k i f a n ya
zoezi la shambulio la
Inaendelea Uk. 12
12
Inatoka Uk. 11
bomu ndio mara, ghafla
watu wanatangaziwa
kuwa kuna shambulio
l a k i g a i d i . ( Ta z a m a :
Eyewitness: Authorities
Announced Drill Before
Boston Explosions.)
Ukisoma taarifa
za Boston Marathon
Bombing, unachogundua
ni kuwa kwanza
palikuwa na bomu
feki ambapo kulikuwa
na wasanii waliokuwa
wakiigiza kwamba
wameumia kutokana na
bomu huku askari na
waokoaji wakihangaika
kuwanusuru majeruhi.
Mmoja wa waigizaji hao
a m e g u n d u l i k a k u wa
askari Lt. Nick Vogt,
katika igizo hili akicheza
kama "Jeff Bauman". Nick
alipoteza miguu yake yote
miwili wakati akipigana
Kandahar, Afghanistan
mwaka 2011. Huyu
katika hii iliyodaiwa
kama shambulio la
kigaidi Boston, aliigiza
kuwa miguu yake yote
miwili imelipuliwa
n a k u s a m b a r a t i s h wa
na magaidi na ndiye
anayetajwa kama shahidi
kwamba aliwaona
walipuaji. Kilichofanyika
ni kuwa alibandikwa kitu
kama miguu ya bandia,
iliyoungiwa pale miguu
yake halisi ilipokatikia.
Ikafanyiwa make-up,
na kuonekana kana
kwamba imekatika sasa
hivi inavuja damu, kumbe
damu yenyewe bandia
Makala
AN-NUUR
ASKARI Lt. Nick Vogt (kushoto) akiwa na askari mwenzake baada ya kukatika
miguu akiwa Afghanistan. Katika Boston alitajwa kama "Jeff Bauman".
13
AN-NUUR
HAKUNA asioijua
bunduki. Siku zote
bunduki inajulikana
kuwa ni silaha ya kuuwa
wala sio ya kupapasa.
Kuwa na bunduki ni
ushujaa wala hakumtii
khofu mwanadamu
pale atapokuwa
anamiliki bunduki
kwa kuamini kuwa
anaweza kukabiliana na
majambazi hata wanyama
wakali.
U n a we z a k u wa n a
mkuki, mshale, panga
na kujiamini kuwa una
silaha kali na nzito, lakini
ukitokewa na mwenye
bunduki utajitambua
kuwa huyo aliokutokea
ana silaha kali kuliko
ulionayo wewe. Bunduki
HEIKH Hassan
alielekea bara
kwa kustakimu
na kufanya kazi
kubwa ya tabligh, kuna
we n g i n e wa n a o s e m a
kuwa kule bara aliitwa
kwenda kuokoa jahazi.
Kuna wengine wanasema
alikwenda kwa hiari
yake. Kuna kauli nzito
inayoelezea kuwa
kuhama kwake Zanzibar
na kuelekea Tanganyika
ni kutokana kuombwa na
Al-Habib Syd Umar bin
Sumeit kufanya hivyo.
Alipokuwa Tanganyika
a l i f a n ya k a z i k u b wa
sana ya kusomesha na
ilipoundwa Jumuia ya
Wa i s l a m u wa A f r i k a
ya Mashariki The East
African Muslim Welfare
Society (EAMWS)
iliyokuwa chini ya ulezi
wa kiongozi Mohammed
El Husaini Aga Khan
iliyoasisiwa katika mwaka
wa 1945, Sheikh Hassan
bin Ameir alikuwa katika
wa s h a u r i wa k u u wa
jumuia hii na kusimama
14
MAKALA/MASHAIRI
ABUU NYAMKOMOGI-MWANZA.
AN-NUUR
Na Sheikh Mohamed
Ubaidillah Mohamed Ally
HUKURANI zote
anastahiki Mwenyezi
Mungu, Mola mlezi
wa ulimwengu rehema na
amani zimfikie mbora wa
Manabii na Mitume, Mtume
wetu Muhamad na jamaa
zake.
Miongoni mwa uhuru
ambao umeudhamini
Uislamu kwa wasiokuwa
Wa i s l a m u n i u h u r u wa
kuamini na ibada. Uislamu
haukulazimisha watu na
wala kuwateza nguvu juu ya
kuingia katika dini hii, bali
ameachiwa mtu mwenyewe
achague dini na Imani
anayoipenda yeye ndani ya
nafsi yake.
Amesema Mwenyezi
Mungu mtukufu, hakuna
kulazimishana katika dini
k wa n i a m e s h a b a i n i s h a
uongofu juu ya upotevu
(256) Al-Bakarat. Na kwa
kuitekeleza aya hii tukufu
wamefuata Waislamu kwa
kuwalingania watu juu ya
Uislamu na kuwaonyesha
usahihi wake bila ya
kuwalazimisha watu au
kuwateza nguvu.
Hebu tumtazame kiongozi
wa waumini, Omari bin
Khatwab (r.a). Anapita kwa
kizee cha kike cha Kiyahudi
na kumtangazia Uislamu na
anamlingania kwa kusema
(silimu ewe kizee utasalimika,
hakika Mwenyezi Mungu
amemleta Muhamad kwa
haki. Akasema yule Bibi
(mimi ni mzee na umauti
kwangu ni karibu). Akasema
Omari (r.a) (Ewe Mwenyezi
Mungu shuhudia na akasoma
kauli ya Mwenyezi Mungu
(Hakuna kulazimisha katika
kuingia katika dini, kwa
hakika ameshabainisha
uongofu katika upotovu)
(256 Al-Bakarat). Kwa yakini
uhuru wa kuabudu na imani
ndio uhuru wa kwanza
katika haki za binadamu,
ambayo inathibiti kwa kila
yule aliye binadamu. Na yule
anayenyang`anywa uhuru
wa imani hiyo, amevuliwa na
kuporwa ubinadamu wake
mwanzoni kabisa. Pamoja na
uhuru wa kuabudu ni uhuru
wa kulingania imani na
amani isiyokuwa na maudhi
yeyote, wala fitina. Na kama
si hivyo, basi huo utakuwa
uhuru wa jina tu na hauna
wa n d i o m wa n z o wa
dola ya Kiislamu, hadi pale
ilipokuwa na nguvu na
umma wenye uwezo. Na
laiti ungetaka kuwalazimisha
watu juu ya imani kwa nguvu
na kulazimisha, yangetokea
h a y o k wa u we z o wa k e
lakini Uislamu haukufanya
hivyo na hivyo kuyahami
majumba yao ya ibada na
mahekalu yao, na kuifanya
hii kuwa dalili na sababu ya
kupewa ruhusa Waislamu
(Wameruhusiwa wale ambao
wanapigwa kwamba wao
wamedhulumiwa na hakika
Mwenyezi Mungu juu yao
kuwanusuru ni muweza).
Katika miji yao bila ya haki
isipokuwa kule kusema tu,
Mola wetu mlezi ni Mwenyezi
Mungu. Na laiti kama si
kuwatenganisha Mwenyezi
Mungu watu baadhi yao, basi
yangevunjwa Masinagogi na
majumba ya ibada na Misikiti,
ambayo yanatajwa sana
majina na Mwenyezi Mungu
kwa wingi na atamnusuru
M we n ye z i M u n g u y u l e
anayeinusuru dini yake, kwa
hakika Mwenyezi Mungu ni
mshindi mwenye nguvu (3940) al-Haji.
Hakika Uislamu
haukusimama kwa kuwateza
nguvu wale wanaoupinga
kwa kutumia nguvu na
kuwatoa katika imani zao
na kuchukua kwa ujeuri
mali zao na vyanzo vyao
vya uchumi na kuwavunjia
heshima zao na kumwaga
damu zao na historia ya
Uislamu katika sehemu hii.
Hapa duniani yapo yale
yaliyokubaliwa na wanazuoni
wa sheria (Fikhi) kwamba laiti
akilizamishwa kuingia katika
dini ya Uislamu huyo haufai
Uislamu wake. anasema
katika kitabu cha Mughani
(Laiti akilazimishwa mtu
kuingia katika Uislamu
ambaye haifai kulazimishwa
kwake kama vile anayeishi
kwa makubaliano na
yule anayeishi kwa kibali
maalumu, naye akasilimu
huyo hauthibiti Uislamu wake
kwa hukumu ya Uislamu
hadi pale itakapopatikana
na dalili za kutolazimishwa
kwake).
Mughni Ibnu KudamaUislamu umempa uhuru
yule asiye Muislamu wa
kufanya ibada zake ambazo
zinaendana na imani zake,
kisha unamuarmisha
juu ya kuhifadhi nyumba
anazofanyia ibada hizo na
ni haramu kwa Muislamu
kuzifanyia uadui nyumba
za ibada au kuzivunja au
kuziharibu au kuwafanyia
uadui wahudumu wake,
sawa sawa uwe wakati wa
amani au wa vita kwani
wakati wa Mtume, wageni
wa majirani ilifikia hatua
ya kuhudumiana na kuishi
vizuri katika dola ya
Kiislamu na wale wasiokuwa
Waislamu hadi kufikia dalili
15
Inatoka Uk. 13
MAKALA
AN-NUUR
alipokuwa anasomesha
Dar es Salaam katika
miaka ya 1950 akiwa na
mtafiti wa Kimarekani
James Brenan
Sheikh Hassan bin
Ameir alifanya kazi ya
Daawa kwa upana kabisa
pamoja na kuwahamasisha
watu kujiunga na TANU.
Sheikh Hassan alikuwa ni
msomi aliokuwa na imani
kuwa watu wote ni sawa
na alikuwa hakubaliani
kabisa watu kujigawa kwa
misingi ya kidini.
Viatabu alivyoviandika
Sheikh Hassan
alibarikiwa kupata fursa
ya kuandika vitabu na kati
ya vitabu alivyoviandika
ni:
Wa s i a l a t u l R r a j a
(Shrerehe ya Safinatul
Najaa)
Fathul Kabir (Sherehe ya
Mukhtasarul Kabir)
Idhanil Maani FiAsamail Husana (Sherehe
ya Taibatil Asmai)
Musliku Karib Fi
mughnil Muhtaj (Sherehe
ya Maslaqul Qarib)
Madarijul Ulaa (Sherehe
ya Tabaraka Dhul Ulaa).
Kuna
baadhi ya
vitabu alivyoviandika na
kutochapishwa ni pamoja
na:
Tuhfatul Zinjibariya(
Sherehe ya Robol Ibada).
Maulidi Barzanji
(Sherehe ya Maulidi ya
Barzanji).
Anwaru Saniyyat
(Sherehe ya Addurarul
Bahiya).
Sheikh hassan bin Ameir
alifunga macho tarehe 8
Oktoba mwaka wa 1979
katika mtaa wa Michenzani
na kuzikwa kijijini mwao
Mtegani Makunduchi.
Maziko yake yalikuwa
makubwa mno kwa wale
wanaoyakumbuka, kwani
m b a l i ya wa k a z i wa
Zanzibar, watu wengine
walitoka nje ya mipaka
ya Zanzibar kwa kuja
kumlaza kigogo hichi.
Nuru yake ipo na
inangara hadi leo, lakini
bado kazi nzito inahitajika
kufanyika kuanzia
Makunduchi hadi mjini
Unguja na Pemba, Mrima
mpaka Kongo.
Mola atupe kila yalio
mema, na utupe satwa
ya kufwata nyayo za
watangulizi wetu hawa
Ameen.
(Baadhi ya maelezo haya
mafupi nimeyapata kwa
Sheikh Salmin Bin Hafidh
ambaye naye amepokea
kwa Sheikh Ameir Tajo,
Haji Bin Hafidh, Hamid
Bin Hafidh. Aidha rejea
za kitabu cha Conflict
and Haromy in Zanzibar
na Ali Muhsin Barwany
na Maisha na Nyakati za
Abdulwahid Sykes na
Moahammed Said).
16
Inatoka Uk. 15
Matokeo mbalimbali ya
matumizi
mabaya ya bunduki ya
Ak 47
Seattle, Washington,
kijana wa umri wa miaka
2 6 , K yl e A a r o n H u f f
aliwafetulia risasi katika
eneo jirani na Seattle's
Capitol Hill na kuuwa
wasio na hatia 6 na kujeruhi
watu 2. Katika mwezi wa
April 2007 Seung-Hui Cho
aliua watu 32 kwa kutumia
bunduki katika mji wa
Virginia na kujeruhi watu
wengi kabla ya kujiuwa
mwenyewe. April 30, 2009
katika mji wa Apeldoorn,
nchini Uholanzi kijana wa
Kiholanzi mwenye umri
wa miaka 38 aliendesha
g a r i k wa k a s i k a t i k a
sehemu ambayo kulikuwa
kukifanyika gwaride huku
wana ukoo wa kifalme
wakiwa wamehudhuria
aliuwa watu 7 na kujiua
mwenyewe mwishowe.
Katika mji mkuu wa
Guinea, Conakry askari
aliokuwa amevalia sare
ya kijeshi alifyetua risasi
katika maandamano ya
kampeni ya uchaguzi
na kuuwa watu wengi
na wengine kujeruhiwa
hayo yalitokea tarehe 28
September mwaka wa
2009. Jazba zilimpanda
Malik Nadal Hassan pale
alipoambiwa anapelekwa
kwenye mapambano
nchini Iraq, alichukua
mtutu wa bunduki na
kuwashambulia wana jeshi
wenzake na kuwauwa 12
na kuwajeruhi kiasi cha
wanajeshi 30 katika mji wa
Ft. Hood, Rexas.
M we z i wa J u l a i 2 2
mwaka wa 2011 Anders
Behring Breivik aliovaa
nguo za jeshi alivamia
kempu ya vijana nchini
Norway wakiwa kwenye
kisiwa cha Utya nakuuwa
vijana 69. Katika mwezi
wa March 11, mwaka
wa 2012 mwanajeshi wa
Kimarekani ajulikanaye
kwa jina la Robert Bales,
aliwafetulia risasi raia 17
wa Kiafghani huko mjini
Kandahar. Mwezi wa
Okotober tarehe 5 mwaka
wa 2011 meli mbili za
mizigo zikiwa zinasafiri
katika mto Mekong nchini
T h a i l a n d z i l i va m i wa
na wabeba bunduki na
kuuliwa mabaharia 13
na miili yao kutupwa
kwenye mto. April 2, 2015
katika mji wa Garissa
nchini Kenya, waliodaiwa
kuwa ni wapiganaji wa AlShaabab walivamia chuo
cha Garissa kijulikancho
kwa jina la Garissa
University College na
kuwauwa watu 147 na
kujeruhi wengine wapatao
watu 79. (Rejea: https://
en.wikipedia.org/wiki/
MAKALA
AN-NUUR
Bunduki ya AK 47
Mikhail Kalashnikov
List_of_events_named_
massacres.)
Dondoo juu ya AK
47-Kalashnikov
Kamanda wa kijeshi wa
Kirusi katika vita vikuuu
vya pili vya Dunia Mikhail
Kalashnikov ndio muasisi
wa bunduki ya AK 47
b a a d a ya k u j e r u h i wa
kwa risasi kwenye bega
katika vita vya Bryansk,
a l i p o k u wa a n a t i b i wa
bunduki ya Kalashnikov
kuitumia kupambana na
vikosi vya Warusi nchini
Afghanistan.
Katika vita vya Vietnam,
wanajeshi Wamarekani
wakionelea bora kutumia
bunduki ya Kalashnikov
kwa ubora wake, hata
hivi sasa wanajeshi wa
Marine wa Kimerekani
huitumia zaidi bunduki
ya Kalashnikov. Bendera
ya Msumbiji ina alama ya
bunduki ya Kalashnikov.
Aidha sare za jeshi la
Zimbabwe na Burkina Faso
zina alama ya Kalashnikov
pamoja na jeshi la Timo ya
Mashariki.
Bendera ya vugu
vugu la wanaharakati wa
Hezbollah nchini Lebanon
ina picha ya Kalashnikov.
Baadhi ya wazazi wa
nchi za Kiafrika hupenda
kuwapa majina watoto wao
jina la Klash ikiwa jina
jengine linalotumika kwa
bunduki ya Kalashnikov,
AK-47.
Mji wa Izhesk nchini
Urusi ndipo pahali
palipoasisiwa bunduki
ya Kalashnikov na ndipo
a l i p o z a l i wa m c h e z a j i
wa mchezo wa kikapu
maarufu nchini Urusi
Andrey Kirilenko na sare
yake ya mchezo huko
Marekani katika ligi
ya NBA ina namba 47.
Katika sehemu ya Sinai
kuna jukwaa lenye alama
ya AK-47 limechongwa
kuonyesha kama alama ya
kishujaa. Bunduki ya AK47 ikiwa imepakwa rojo ya
dhahabu iligundulikana
nchini Iraq katika kasri la
Saddam Hussein baada ya
kuondolewa madarakani.
Kwa kumkumbuka
Mikhail Kalashnikov na
mchango wake, nchi ya
Urusi imetengeneza pesa
ya gwaru na hata nchi
ya New Zealand kwa
kuadhimisha miaka 60
tangu kuasisiwa bunduki
ya AK-47 walitengeneza
pesa ya Dolari 2 kama ni
kumbukumbu.
Gazeti la Liberation la
Kifaransa limeipa daraja
ya juu kabisa bunduki ya
Ak-47 kuwa ni uvumbuzi
wa kipawa cha juu
kushinda bomu la atomiki
au roketi zilizokwenda
mwezini. Mwana Sanaa
wa nchi ya Colombia
alizibadilisha bunduki
zilizokusanywa baada ya
vita na mapambano jeshii
la serikali na wanaouza
dawa za kulevya.
Alizichukua binduki hizo
na kutengeneza chombo
cha mziki cha gita (guitar),
katika mwaka wa 2007
alimzawadia aliokuwa
Katibu Mkuu wa Umoja
wa Mataifa, Kofi Annan
gita la aina hio.
Itaendelea toleo lijalo
17
Inatoka Uk. 20
kwamba shuleni hapo,
kila taaluma na kila jambo
lenye manufaa kwa jamii
linasomeshwa au angalau
kutolewa taarifa kulingana
na umri wa watoto.
Katika hali hiyo,
mtoto anakuwa akiwa na
mtazamo sahihi wa Maisha
ya Dunia na Akhera na
kwamba Uislamu ni
mfumo kamili wa maisha
na sio dini ya kuwafungia
watu Misikitini na ndani
ya wigo wa ibada maalum
tu.
I l i k u wa n i s h u g u l i
ambayo, iliwaridhisha
wazazi kwamba, katika
Chalinze Elimu ya Dini
ya Kiislamu inapatikana
kama neno Islamic,
linavyomaanisha lakini
pia Elimu ya Msingi
ya Mazingira inapatikana
kama neno Modern
Primary School,
linavyomaanisha.
Ni kutokana na ukweli
huo uliodhihiri katika
maonyesho ya watoto,
mgeni rasmi katika hafla
hiyo Bwana Abdul Bukhety
aliwahimiza wazazi
kusaidia maendeleo ya
shule hiyo kwa hali na
mali ili iweze kufanya
vizuri zaidi.
Bwana Bukhety ambaye
ni Afisa Elimu (Shule
za Msingi) Wilaya ya
Bagamoyo, alitilia mkazo
suala la kuwekeza katika
elimu huku akiwataka
wazazi waepuke
kuwarusha watoto
wao madarasa k wan i
ni kinyume cha sheria,
halikadhalika kukiuka
kanuni za makuzi ya
mtoto.
Katika nukta hiyo
alisema kuwa kumekuwa
na kawaida ya baadhi ya
wazazi kuwarusha watoto
wao wanapokuwa darasa
la sita au la tano, kwenda
kidato cha kwanza.
Akasema, hata kama
mtoto atakuwa na uwezo,
lakini kitaalamu ni
muhimu amalize muda
uliopangwa kitaalamu
kuwa ndio wa kumaliza
elimu ya msingi.
Kwa upande mwingine,
Afisa huyo aliwataka
Waislamu kuwa mbali na
dhana potofu za baadhi
ya watu wanaoharamisha
kufanya kazi serikalini.
Akasema, hoja
zinazotolewa na watu hao,
mbali ya kuwa hazina
mashiko ya kidini, lakini
pia ni kujitia dhiki na
ugumu wakati kanuni ya
Uislamu ipo wazi kwamba
Dini hii Mwenyezi Mungu
ameifanya nyepesi.
Akitoa mfano wa
ugumu anaoweza kujipa
mtu kwa fikra potofu
kama hizo akasema kuwa
unaposema kufanya kazi
serikalini ni ukafiri kwa
sababu utalipwa mshahara
MAKALA
Amir Lulu
AN-NUUR
unaotokana na fedha za
pombe na riba, itabidi pia
na wewe ukiwa na gari au
baisikeli, basi upite porini
maana hata hiyo barabara
inatengenezwa kwa pesa
hizo hizo.
Ni hivyo hivyo ukienda
hospitalini, huduma za
maji, umeme na mambo
kama hayo.
Akasema, unachotakiwa
kuzingatia ni kuwa
u m e f a n ya k a z i ya k o
(halali) vizuri na unastahiki
kulipwa mshahara
kwa kazi uliyofanya au
huduma uliyotoa.
Katika mazingira kama
yetu Tanzania, akasema
haisaidii hata kidogo
kususa, zaidi ya kuwa
utapata hasara kubwa
zaidi.
Wa k a t i h u o h u o ,
wa z a z i n a wa s h i r i k i
wa kongamano hilo
wamechanga jumla ya
shilingi 10, 252, 500, zikiwa
ni fedha taslim na ahadi
i l i k u wa u n g a m k o n o
Chalinze Islamic Modern
Islamic Seminary katika
kuboresha zaidi shule
hiyo.
Fedha hizo zitaelekezwa
katika kumalizia jengo
la msikiti na nyumba za
walimu.
Akiendesha harambee
ya kuchangia, Amir Lulu
pamoja na kuwakumbusha
wa z a z i u m u h i m u wa
kutoa zakka na sadaka,
akamtaka kila mzazi
aguswe na mambo mazuri
yaliyooneshwa na watoto
n a a f a h a m u k wa m b a
inahitajika juhudi ikiwa
ni pamoja na fedha.
Akirejea maonyesho ya
watoto walioigiza kama
m a d a k t a r i , wa u g u z i ,
waandishi wa habari,
masheikh, na waliosoma
Quran kwa kuhifadhi
halikadhalika kutoa
tafsiri na ufahamu wa aya
walizosoma, Amir Lulu
akasema kuwa hakuna
uwekezaji ulio bora kama
huo wa kutoa pesa, ili
kuzalisha watoto wenye
k u i j u a D u n i a ya o n a
Akhera yao.
Katika kutoa wito
wa ujumla, uongozi wa
shule hiyo umewataka
Waislamu kutembelea
shule hiyo iliyo kiasi cha
nusu kilometa Chalinze
Mzee, barabara ya Tanga
na kwamba muda wowote
wanakaribishwa kutoa
michango yao.
Aidha kama wapo
watakaotaka kuleta vifaa
vya ujenzi, yakiwemo
mabati, saruji, mbao n.k,
pia wanakaribishwa.
Habari na maelezo zaidi
yanaweza kupatikana
kutoka kwa Mkurugenzi
wa Kituo kupitia namba
0652 055 556.
18
HABARI
AN-NUUR
A I S L A M U
wametakiwa
kuviunga mkono
vituo vidogo vya elimu
(Madrasa) kutokana na
juhudi zao binafsi katika
kuwaandaa watoto wa
Kiislamu katika maadili
n a m af unzo bo ra ya
Kiislamu.
Wito huo umetolewa
m w i s h o n i m wa w i k i
iliyopita na Ustadh
Othman Ntalaruka,
a k i o n g e a n a Wa z a z i
n a Wa i s l a m u k a t i k a
Maonyesho ya tano ya
Madrasa na Shule ya awali
ya Firdaus, iliyopo Tabata,
Jijini Dar es Salaam.
Ust. Ntalaruka, ambaye
ni Mkurugenzi wa Chuo
cha TEHAMA, kinachotoa
e l i m u n a m a a r i f a ya
Kompyuta (TEHAMA
Tarin Collage) kilichopo
Tandika Jijini Dar es
Salaam, alisema ni wajibu
wa kila Muislamu na
wadau wa elimu kuunga
mkono juhudi za vituo
vidogo vya elimu ili vipate
nguvu ya kuandaa umma
wa Kiislamu ulio bora.
Alisema, vituo kama
vya elimu mfano wa
Madrasa na Nasari ya
Firdaus, Tabata, ndivyo
vinavyowajengea watoto
msingi bora wa elimu na
malezi bora kwa vijana
wa Kiislamu na hatimaye
kupatikana viongozi
waadilifu katika jamii.
A l i s e m a , e l i m u ya
mtoto sawa iwe ni wa
nasari, Msingi au
Sekondari, mafanikio
yake yanachangiwa na
pande kuu tatu, ambazo
ni Wazazi (Waislamu)
mwalimu pamoja na shule
husika (wadau).
Kwa maana hiyo,
alisema katika pande kuu
hizo tatu panapo legalega
katika moja ya sehemu
hizo tatu, basi mara nyingi
k i l e a l i c h o k u s u d i wa
kukipata mtoto hakipati
kwa ukamirifu wake.
Kwa hiyo, niwausie
wazazi na walezi ili tuweze
kufanikiwa katika kuwapa
taaluma sahihi watoto
wetu na kuweza kufikia
malengo yaliyokusudiwa
katika pande hizi tatu,
tunalazimika kujitolea
kuvipa nguvu vituo hivi
kwani tukizembea siku
ya hukumu tutaulizwa
k u wa h a k u n a n a m n a
katika maisha ya sasa
kiulimwengu katika jamii
yoyote inayohitaji kupiga
hatua kiuchumi bila
kuwekeza katika taaluma
hii ya Kompyuta.
Aidha, Mwenyekiti wa
Madrasa hiyo ya Firdausi,
Ustadhi Ismail Kapona,
akiongea katika hafla
hiyo alisema pamoja na
mafanikio waliyonayo
lakini kituo kinakabiliwa
na changamoto kadha wa
kadha.
Alisema, moja ya
changamoto kwa upande
wa Madrasa ni uwepo
kwa utaratibu wa baadhi
ya shule za msingi
unaolazimisha watoto
kubaki katika shule
zao baada ya muda wa
masomo kwa maelezo
k wa m b a wa n a t a k i wa
kusoma masomo ya jioni
(Tuition), jambo ambalo
linanyima vijana wengi wa
kiislamu fursa ya kusoma
dini yao.
H a t a
h i v y o
tumejitahihidi kuweka
mazingira mazuri
kukabiliana na changamoto
hiyo ili kuhakikisha
wanafunzi wetu wanapata
kile ambacho Madrasa
imekusudia kukitoa
kwa vijana wa Kiislamu,
lakini tukihakikisha pia
19
Inatoka Uk. 10
mahakamani, bali
kuwaangamiza
(elimination).
Na zaidi wakasema
kuwa hupokea amri
na maelekezo kutoka
makachero wa Israel.
Kwamba wanapewa
orodha ya watu
wanaotakiwa kuuliwa,
na wao hutekeleza na
kurejesha taarifa za
utekelezaji. (Tazama:
Inside Kenyas Death
Squads.)
Katika kile
kinachodaiwa kuwa ni
harakati za kupambana
na ugaidi, vikosi maalum
kama ATPU na Idara
ya Usalama, vimepewa
mamlaka yaliyo nje
ya katiba na sheria
ambapo hufanya kazi ya
kutuhumu, kuamua kesi
na kuadhibu (kuuwa).
Wengi wa Masheikh
waliouliwa au kupotea na
kuteswa, wameangukia
mikononi mwa vikosi
hivi ambapo mara
kadhaa huuwa watu
wakiwa majumbani
mwao halafu husingizia
kuwa ni magaidi
waliouliwa wakipambana
na polisi.
Katika mauwaji ya
Sheikh Abubakar Shariff
Ahmed aka Makaburi,
polisi mmoja katika
kikosi cha kupambana
na ugaidi alikiri wazi
kwamba amri ya kuuliwa
Sheikh huyo ilifanywa
na watu wa ngazi za juu
katika serikali na polisi
waliopo Nairobi.
Kwa upande
mwingine, kuna
wanaouliwa kimya
kimya kama hao
waliofukiwa katika
shimo moja ambapo
polisi mmoja akihojiwa
na Aljazeera alisema
kuwa kinachofanyika ni
kukamatwa walengwa,
lakini wanapofikishwa
kituo cha polisi huwa
hawaandikishwi,
bali huchukuliwa na
kupelekwa porini
kuuliwa.
Kwa hiyo hata
ukifuatilia habari zao
polisi hutazipata maana
hakuna mahali utakuta
kwamba alirekodiwa
kuingizwa rumande au
japo kufikishwa polisi
kuhojiwa.
Hayo yakijiri Kenya,
bado imekuwa ni
kitendawili, nani
amekuwa akiuwa
Masheikh Uganda.
Taarifa zinasema kuwa
katika Masheikh 12
waliouliwa, wote staili
ya kuuliwa kwao ni ya
MAKALA
AN-NUUR
ugaidi ukiwemo
mauwaji ya Masheikh
hao, lakini hakuna hata
mmoja anayefikishwa
mahakamani.
Wakati mauwaji ya
Masheikh yakiendelea,
imepatikana orodha
inayodaiwa kuwa na
majina ya Masheikh
wanaotakiwa kuuliwa.
Katika orodha hiyo
wapo ambao tayari
washauliwa huku
ikiwaweka katika
wasiwasi wale ambao
wamo katika orodha hiyo
wasijue zamu yao lini.
Hayo yakijiri huko
Kenya na Uganda, hali si
shwari pia Tanzania.
Hivi sasa kuna
Masheikh na makumi ya
Waislamu wanashikiliwa
na vyombo vya dola
kwa zaidi ya miaka
miwili sasa, huku
hatma ya kesi zao ikiwa
haijulikani. Wakati huo
huo tunasikia habari
za mateso ya Shimoni
na Guantanamo,
sio Guantanamo
Bay detention camp
(Guantnamo, G-bay),
Marekani, lakini ndani
ya Dar es Salaam hii hii
aliyorithi Hapa Kazi tu,
Rais Dr. JPM kutoka kwa
Kasi Mpya JK.
Kutokana na kukwama
kuzungumzwa kesi
hizo na kufikia hatma,
inakuwa vigumu
kufahamu ni nani hasa
alikamatwa kwa tuhuma
za kweli au la.
Lakini wakati huo
huo, kumekuwa na
matukio ya hapa na
pale ambapo vijana na
hata akina mama wa
Kiislamu wamekuwa
wakikamatwa na
kutupiwa madai ya
ugaidi, wakaishia
kuteswa na kisha
kuachiwa bila ya
kufikishwa mahakamani.
Kama tulivyotangulia
kusema, Afisa mmoja wa
kikosi maalum cha polisi
wa Kenya-GSU Radiation
Unit aliwahi kukiri
kwamba wao hupewa
maelekezo na makachero
kutoka Israel juu ya
namna ya kuwamaliza
watuhumiwa wa ugaidi.
Hatujui haya
yanayofanyika hapa
kwetu, ni yetu wenyewe
au na yenyewe kuna
namna tunapata
maelekezo kutoka kwa
watu fulani nje ya nchi!
AN-NUUR
20
MAKALA
20
Soma gazeti la
AN-NUUR
KWA TSH 800/=
kila Ijumaa
AN-NUUR
Na Mwandishi Wetu
Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Ltd, Dar es Salaam.