Вы находитесь на странице: 1из 20

Wahafidhina

munatupeleka
wapi?

www.annuurpapers.co.tz au facebook:annuurpapers@yahoo.com

Sauti ya Waislamu

ISSN 0856 - 3861 Na. 1208 RABIUL AWWAL 1437, IJUMAA , DESEMBA 18-24, 2015 BEI TShs 800/=, Kshs 50/=

Turejee katika msimamo


wa Mzee Karume

Magufuli akomeshe
uhuni katika siasa!

Uk. 17

RAIS John Magufuli.

Walioshindwa Zanzibar wakae pembeni


Vinginevyo ni aibu kwa nchi. Atakwama

PROF. Ibrahim Lipumba.

HAWA wapo katika swala ya Ijumaa. Msaada wako unahitajika. Soma Uk. 19

PROF. Kitila Mkumbo.

KKK waunda kikosi


kuchinja Waislamu
Soma Uk. 10

Mafundisho ya Qur'an/Uwanja wa Maarifa

AN-NUUR

RABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 18-24, 2015

Aal Imran: 97
Fethullah-Gulen
NA ni haki ya Mwenyezi
M u n g u j u u ya wa t u
kuikusudia nyumba
mwenye kuweza njia ya
kuiendea. [Aali-Imran
97]
K i l a
i b a d a
inayotekelezwa kwa ajili
ya M we n ye z i M u n g u
mtukufu, ibada hiyo ni
shukrani katika mkabala
wa neema nyingi ambazo
a m e z i e n e z a j u u ye t u
n a hu enda zikawa n i
mkabala wa vitendo kwa
neema hizo kwa kiwango
fulani mkabala ambao
haupatikani isipokuwa
katika njia ya Mwenyezi
Mungu, na kwa ajili yake.
Ni hivyo hivyo ibada
ya Hijja, ibada hiyo ni
shukrani katika mkabala

wa neema ya uzima wa
mwili na neema ya mali
ambayo imetolewa. Kwa
msingi huo, anasema yule
anayenuia kuhiji: Nina
hiji kwa ajili ya Mwenyezi
Mungu kwa sababu hiyo
inasema Quran tukufu
katika jambo hili: Na haki
ya Mwenyezi Mungu juu
ya watu. Na (Lam) katika
tamko ALLAH ni ya
kustahiki. Ama herufi ALA
katika ALA-NNA si herufi
hiyo ni ya kulazimisha
ama LAM ya kuarifisha
katika tamko ANNAS
hiyo ni ya Ahadi. Ni kama
hivyo ulikuwa mwanzo
kwa kuutumia msemo
ALA NNAS ni namna
ya ufasaha ya kuanza
maneno, na kuashiria yale
yatakayofuatia katika
vifungo maana: hakika,
t a m k o A L A - N N A S
linaashiria kwa baadhi
ya wa t u n i k i n a n a n i
watu hao? Hao ni wale
ambao wamekamilika
kwao gharama za njiani
na chakula na uwezo wa
kusafiri, kwa kuongezea
kupatikana mahramu kwa
upande wa wanawake.
Ni kutokana na kutaja
kwetu herufi ya Jarri

ALA katika aya ALANNAS kwa undani huu:


Hija ni ibada ngumu sana
kuliko swala na kuliko
swaumu kwa kuongezea
taabu ya safari mtalazimika
kutoa kiwango kikubwa
cha mali na mnaacha kazi
zenu, mnakuwa mbali
na nchi zenu na jamaa
zenu na kadhalika. Herufi
ya Jarri ALA ambayo
i n a t u m i wa n a Q u ra n
i n a a s h i r i a k wa m b a l i
kwenye haya mashaka
maalumu kwa sababu ya
Hijja katika ujumla wa
faradhi nyingine.
Z a i d i ya h a y o k wa
h a k i k a U we z o u n a
maana ya kuitekeleza amri
kwa radhi ya moyo na
kwa njia ya kunyenyekea
na kufuata, kwa njia iliyo
nzuri na bora sana na
hilo linafungamana na
kutaka uwezo, uwezekano,
maana ni kwamba uweza
umetumiwa hapa na hali
pa sehemu zake ambazo ni
nguvu, uwezo, uwezekano
na ulikuwa upana wa
maana ya tamko hili ndilo
chimbuko na sababu ya
kutofautiana tafsiri mbele
za Maimamu wenye
kujitahidi na sababu ya
wepesi na upana.

Kongamano lililozungumzia Athari za ugaidi, Tanga

JAWABU CHEMSHA BONGO NAMBA: 30


S

Q L

M Y

M Z

Q B

U U H

Q M S

N M A

O A

U N

H A

M O N Q R

N A

M S

Q R

H J

U R

W A

U B

M A

M A

O H A

MASUALA
1.Mtaje Shahidi wa mwanzo katika Uislamu. Jawabu: Sumaya
2.Sahaba aliokuwa na jina la Rum/Roman. Jawabu: Sohaib
3.Makabila mawili Mtume (SAW) aliwakuta Madina wakiwa kwenye
ugomvi mkubwa akawasuluhisha. Jawabu: Khazraj, Aws
4.Masahaba wawili watoto wao waliolewa na Mtume (SAW). Jawabu:
Abubakar, Umar
5.Kipando alichokipanda Mtume (SAW) alipokwenda Miraj. Jawabu:
Buraq
6.Vitabu 4 vitakatifu walivyoteremshiwa Mitume. Jawabu: Injil, Zaboor,
Tawrat, Quran
7.Aya ya kwanza kuteremshwa. Jawabu: Iqra
8.Muadhini wa mwanzo katika Uislamu. Jawabu: Bilali
9.Nyenzo ilio muhimu katika kutia Udhu. Jawabu: Maji
10.Harufu 3 za mwanzo katika Suratul Baqara. Jawabu: Alif, Lam, Mim

CHEMSHA BONGO: 31

Weka duara kwenye jawabu ilio sawa. Jawabu kamili wiki ijayo.
A

M I

40

50

60

70

80

100 200

D I

M U

W S

H A

O L

H A

H M A

576 635 632 621 767 555 622 435

570 A

M E

MASUALA
1.Mwaka aliozaliwa Mtume Muhammad (SAW).
2.Mwaka aliohama Mtume Muhammad (SAW) kwenda Madina.
3.Mwaka aliofariki Muhammad (SAW).
4.Ukoo wa Mtume Muhammad (SAW)
5.Mamake Mtume Muhammad (SAW) alimpa jina gani?
Mohammed, Adam, Abass.
6.Muhammad (SAW) alivyokwenda Syria alifwatana na nani katika
ukoo wake? Abu Talib, Abdul Mutalib, Abubakar.
7.Kwanini Bibi KHadija alitaka aolewe na Mtume Muhammad
(SAW) Uzuri, Uaminifu, Umaarufu.
8.Majina aliokuwa akijulikana Mtume Muhamad (SAW.
9.Mtume Muhammad (SAW) kabla ya kupewa Utume akijitenga
katika eneo gani?
10.Idadi ya Waislamu wa mwanzo kusilimu walikuwa wangapi?

Jee Unajua?

BAADHI ya Masheikh wakiwa katika picha ya pamoja katika Kongamano


lililozungumzia Athari za ugaidi katika jamii kongamano hilo liliandaliwa na
Kituo cha Kiislamu cha Misri cha Jijini Dar es Salaam lililofanyika katika ukumbi
wa Msikiti wa Hudhaifa Bin Al- Yamani mkoani Tanga mwishoni mwa wiki.

1.Mito 10 ilio mirefu zaidi Afrika ni Mto wa Nile ndio mto ulio
mrefu katika bara la Africa ukiwa na masafa ya urefu wa Kilomita
6,853, ukifwatiwa na mto Congo, mto Niger, White Nile, Zambezi,
mto Orange, Kasai, Luluaba, mto Senegal: http://www.afrikanfacts.
com/top-10-longest-river-in-africa/3/
2.Mlima ulio mrefu koliko yote duniani ni mlima Andes : https://
en.wikipedia.org/wiki/List_of_longest_mountain_chains_in_the_
world
3.Ziwa lilo na kina kirefu duniani ni Caspian Sea 371,000 km2
(143,000 sq mi) : http://10mosttoday.com/10-largest-lakes-in-theworld/
4.Uwanja wa ndege ulio na harakati nyingi duniani : Hartsfield
Jackson Atlanta International Airport: https://en.wikipedia.org/wiki/
List_of_the_world%27s_busiest_airports_by_passenger_traffic
5.Bandari ya mizigo inayoongoza kuwa na harakati nyingi
duniani ni badari ya Shanghai: https://en.wikipedia.org/wiki/
World%27s_busiest_port
6.Nchi ya Malta ni nchi inayoongoza kuwa na watu wavivu,
inakadiriwa asilimia 71.9 ni watu waliokua hawana harakati: http://
www.forbes.com/pictures/eihg45gjhg/swaziland-4/
7.Mji uliokuwa na usafi wa hali ya juu kabisa duniani ni
Singapore: http://ohtopten.com/top-10-cleanest-countries-world/
8.Nchi 7 ambazo zinatoa elimu ya Chuo Kikuu bure ni Brazil,
Ujerumani, Finland, Ufaransa, Norway, Slovenia na Sweden: http://
www.salon.com/2014/11/02/7_countries_where_college_is_free_
partner/
9.
Katika Afrika ya Mashariki nchi inayoongoza kuwa na
matatizo ya akili ni: http://www.rightdiagnosis.com/m/mental_
illness/stats-country.htm

AN-NUUR

Habari

RABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 18-24, 2015

Magufuli akomeshe uhuni katika siasa!


Na Mwandishi Wetu

HAKUNA mgogoro wa
kisiasa Zanzibar, bali ni
uhuni na ujanja ujanja
usio na tija kwa nchi
unafanyika.
Walioshindwa katika
uchaguzi mkuu hawataki
kuachia madaraka. Hilo
ndio tatizo.
Hayo yamesemwa na
Profesa Kitila Mkumbo
pamoja Profesa Ibrahim
Lipumba na kusisitiza
kuwa ni jukumu la Rais
Mheshimiwa John Pombe
Magufuli kukomesha
ujanja ujanja huo unao
aibisha nchi.
Wakiongea mapema
wiki hii katika kipindi
kinachorushwa na Azam
TV (TWO) wamesema
k u wa , k i l i c h o f a n y i k a
Zanzibar na kama
hakitatafutiwa utatuzi wa
haraka, ni aibu kwa taifa
na sio kwa Zanzibar pekee.
Aidha wakasema
kuwa Mheshimiwa Rais
Magufuli kama hataingilia
na kuleta ufumbuzi
unaofaa, itamkwaza hata
ye ye k u t e k e l e z a ya l e
aliyokusudia.
Hii ni kwa sababu hali
ya Zanzibar ikiachwa kwa
muda kama ilivyo hivi
sasa au kuja na ufumbuzi
ambao utazua mgogoro
zaidi, itabidi Rais atumie
muda mwingi kushugulika
na mgogoro wa kujitakia
Zanzibar.
Katika maelezo yake
Profesa Mkumbo alisajili
masikitiko yake kwamba
maamuzi ya wananchi wa
Zanzibar yanadharauliwa
huku ikijulikana wazi
kuwa nchi ipo katika
mfumo wa vyama vingi
na hairudi nyuma.
Alisisitiza kuwa
wananchi wan a akili,
wanajua wanachokitaka na
maamuzi yao ya kuchagua
viongozi wanaowataka
yaheshimiwe.
Prof. Mkumbo amesema
kuwa inachofanya CCM
ni kuleta ujanja ujanja na
kukataa kuondoka baada
ya k u wa i m e s h i n d wa
kama ambavyo hivi sasa
inafanya ujanja ujanja wa
kuleta wapiga kura kutoka
Zanzibar ili wasaidie katika
chaguzi za kupata Meya
katika Wilaya za Dar es
Salaam, ambapo imezidiwa
idadi ya Madiwani, wengi
wakiwa ni wa upinzani.
Katika kulisemea hili
Prof. Mkumbo akasema
kuwa Rais Magufuli

atajijengea imani
k wa wa n a n c h i i wa p o
atakomesha ujanja ujanja
huu wa CCM.
Kwa upande wake Prof.
Ibrahim Haruna Lipumba
amesema kuwa hakuna
s a b a b u ya k u r u d i w a
uchaguzi kwa sababu kura
zilipigwa, zikahesabiwa
na matokeo ya majimbo
mengi yakatolewa na Tume
ya Jecha.
Akasema, katika
majimbo 23 yaliyosalia
k u t a n g a z wa m a t o k e o
yake, majimbo 14
yalishahakikiwa matokeo
yake kutoka Majimboni
ikisalia kutangazwa tu
huku 9 yakiwa ndiyo
hajahakikiwa.
Akasema kuwa,
hata hayo 9 ambayo
hayajahakikiwa na Tume
ya Jecha, matokeo yake
yalishatolewa katika ngazi
za Jimbo na washindi
wa Uwakilishi kupewa
vyeti vya ushindi kama
ilivyokuwa kwa wabunge.
Ndio katika hali hiyo
Prof. Lipumba akasema
kuwa Zanzibar na
Watanzania wanaonekana
viroja na wenye kufanya
mambo ya aibu.
Kwamba wapiga kura
hao hao, wasimamizi hao
hao, vituo hivyo hivyo,
kura za Rais wa Jamhuri na
Wabunge ziwe halali, lakini
za Rais wa Zanzibar na
Wawakilishi ziwe haramu.
Maprofesa hao, wasomi
na Wahadhiri wa Vyuo
Vikuu, wakitoka vyama
tofauti vya kisiasa
wamehitimisha kwa
kusema kuwa hivi sasa
Rais Magufuli ana nguvu
ya k u p e n d wa , l a k i n i
itafika mahali (kama hata
fanya kile wanachotarajia
wananchi), nguvu hiyo
itaondoka.
Kwa hivyo wakasisitiza
kuwa kama yeye ni
msema kweli na mwamini
katika demokrasia kama
anavyotamba, basi
aikwamue Zanzibar kwa
njia ya haki.
Na hakuna haki zaidi
ya k u h a k i k i s h a k u wa
aliyeshindwa anakubali
kushindwa asiwe
kinganganizi kinyume na
kura za wananchi.
Profesa Lipumba
akakomelea kwa kusema
kuwa Rais Magufuli
anajinadi kuwa ni Msema
kweli Mpenzi wa Mungu,
basi aonyeshe kuwa si
katika wale wenye kusema
wasiyotenda.
N a a k i f a n ya h i v y o ,

PROFESA Kitila Mkumbo.


itamuimarisha na
kujijengea heshma
Zanzibar na Tanzania kwa
ujumla.

Kinyume chake,
akienda kwa msukumo
wa wahafidhina
vinganganizi wasio

h e s h i m u m a t a k wa ya
wananchi, hata agenda
nyingine za hapa kazi tu
zitakwama.

Na Mwandishi Wetu

kitaifa.
Aidha alisema Bakwata
itaanzisha kitengo cha
masuala ya uchumi
k i t a k a c h o o n g o z wa n a

wataalamu watakaokuwa
na jukumu la kuiandaa
jamii ya Kiislamu kushiriki
barabara katika kukuza
uchumi wa nchi.

Mufti Zubeir awakosoa Masheikh wa Bakwata

K I O N G O Z I WA w a
Baraza Kuu la Waislamu
Tanzania (BAKWATA)
Mufti Abubakar Zuberi,
amewakosoa baadhi
ya Masheikh ambao
wameshindwa kuwajibika
na kusema watu kama
hao wanawatia Waislamu
aibu.
Aidha Mufti Zuberi
amewataka viongozi wa
BAKWATA katika ngazi
mbalimbali nchini, kubadili
fikra na mienendo yao
katika utendaji ili taasisi
hiyo iweze kuwa dira kwa
Waislamu wote.
Mufti Zubeir alieleza
hayo jijini Dar es Salaam
hivi karibuni wakati akiwa
katika mkakati wa kuanza
safari ya kuzunguka nchi
nzima kuhamasisha umoja
na mshikamano miongoni
mwa Waislamu nchini na
kujionea hali ya utendaji ya
baraza hilo nchini.
Hata hivyo Mufti Sheikh
Abubakar Zuberi alisema
Bakwata ina sura mpya
na malengo makuu ni
kuwaunganisha Waislamu.
Alisisitiza kuwa, umoja
wa Waislamu utawasaidia
kuwa na nafasi muhimu
katika masuala mengi ya

MUFTI Sheikh Abubakar Zuberi.

Tahariri/Habari

AN-NUUR

S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786


Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM.
www.annuurpapers.co.tz
E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk
Ofisi zetu zipo: Manzese Tip Top
Usangi House, barabara ya Morogoro, D'Salaam

Nyinyi mna dini yenu


nami nina dini yangu
IJUMAA ijayo Desemba
2 5 , Wa k r i s t o k o t e
duniani, kwa mujibu wa
taratibu walizojiwekea
za kusherehekea sherehe
zao za kidini, ni siku ya
kuzaliwa Bwana wao Yesu
Kristo.
K wa Wa k r i s t u ,
umekaribia wakati
wa k u n u n u a m t i wa
Krismasi. kuupamba
k wa m a d o i d o y e n y e
kungara na kumetameta,
utasimamishwa karibu na
dirisha.
Maduka yanajazana
wanunuzi wakisaka
zawadi na watoto
wanasubiri kwa hamu
kubwa zawadi ya Baba
Krismasi Santa huku
nyimbo za Marry
Christmas zikishika kasi.
Hata hivyo yapo
maandiko ndani ya Biblia,
Mila za watu si chochote,
wanakata mti kutokana
na msitu, na mchongaji
anauchonga kwa patasi
yake, wanaupamba
kwa fedha na dhahabu,
wanaugandanisha kwa
nyundo na misumari
ili usipate kutikisika
(Jeremia 10-3,4).
Wa k a t i Wa k r i s t o
wakiwa katika hekaheka
za kusherehekea sikukuu
yao, wapo baadh i ya
Waislamu ambao kwa
namna moja au nyingine
wamepanga na kujiandaa
barabara kusherekea
sikukuu hii japo si yao.
Imepokelewa toka kwa
Abu Said Al-Khudhriy
( R a ) k wa m b a M t u m e
(Saw) amesema:
Mtafuata nyendo za
watu waliokuwa kabla
yenu, kiganja kwa kiganja,
mkono kwa mkono, hata
wakiingia kwenye shimo
la kenge mtawafuata.
Tukasema: Ee Mjumbe wa
Allah, Je, Unamaanisha
Mayahudi na Manaswara?
Akasema: Kwani nani
zaidi ya wao? [Al-Bukhari
na Muslim].
Tunakaribia kuingia
mwaka mpya wa Kikristo
(wa kalenda ya Papa
Gregory ijulikanayo kama
Gregorian Calendar),

n a k u n a Wa i s l a m u
wengi wanaosherehekea
mwaka huo mpya kama
wanavyofanya Wakristo,
jambo ambalo halimo
katika mafundisho ya
Kiislamu.
Imekuwa ni kawaida
Waislamu kujiunga na
wafanyakazi wenzao au
marafiki zao au majirani
zao na kusherehekea
sherehe hizi na kuwa
na tabia isiyoendana na
mwendo na mafundisho
ya dini yetu tukufu.
Hivyo tumeona ni
muhimu tuwatumie
Waislamu ujumbe huu
kwamba washikamane
na yaliyoruhusiwa katika
Dini yao huku wakiwaacha
wananchi wenzao
Wakristo nao wakifanya
yao yaliyoruhusiwa na
Dini yao.
Upendo, umoja na
mshikamano katika
n c h i h a u j e n g w i k wa
Mkristo kufanya la
Kiislamu au Muislamu
kufanya la Kikristo, bali
kuheshimiana, kufanyiana
insafu na kuvumiliana.
Tunafahamu kwamba
wapo majirani, marafiki
na jamaa zetu ambao
wanahusika na sherehe
hizi za Christmas na
Mwaka mp ya . Lak in i
Waislamu wana wajibu
wa kujichunga kufanya
mambo ya shirki wakati
huu.
Katika siku hiyo, basi ni
kama siku yoyote nyingine
katika maisha yetu bila
ya kuwa imehusishwa
na lolote. Kama mfano
ulivyo kwa watu wa
Vi t a b u wa s i v y o k u wa
wa k i s h e r e h e k e a wa l a
kuzifanya siku zetu za Idd
kuwa ni haswa (maalum)
kwao.
La msingi ni kuchunga
kuheshimiana na
kuvumiliana katika tofauti
za imani zetu.
Kanuni ya Uislamu ni
Nyinyi mna dini yenu
nami nina dini yangu.

AN-NUUR

RABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 18-24, 2015

NECTA yadaiwa kukwamisha wahitimu wa Al-haramain

Na Bakari Mwakangwale

WAHITIMU wa Shule ya
Kiislamu ya Al-Haramain,
kitengo cha dini, Jijini Dar
es Salaam, wamedai kuwa
Baraza la Mitihani la Taifa
(NECTA), linawakosesha
fursa ya kujiunga na vyuo
Vikuu vya ndani ya nchi.
Wa n a f u n z i h a o
wamebainisha hayo
katika mahafali yao
ya kuhitimu elimu ya
Thanaw, kwa maana ya
Upili (sekondari) kwa
mwaka 2015, yaliyofanyika
Jumapili ya wiki iliyopita
Shuleni hapo, wakielezea
baadhi ya changamoto
zinazowakabili.
Akisoma risala mbele
ya mgeni rasmi, muhitimu
Haroun Kondo Matambo,
amesema NECTA ilikuwa
ikitambua vyeti vyao lakini
hali hiyo imebadilika
k a t i k a m i a k a ya h i v i
karibuni.
Uwepo wa urasimu
katika Baraza la Mitihani
kwa baadhi ya watendaji
wake kwa kukataa kutoa
ulinganishi, bila sababu
za msingi kunawakosesha
wanafunzi kujiunga na
elimu ya juu ndani ya
nchi. Amesema Matambo.
Katika mafanikio
makubwa na ya
kihistoria ni ile hatua ya
kutambuliwa vyeti vya AlHaramain kitengo cha Dini
na kufanyiwa ulinganishi
na Baraza la Mitihani la
Tanzania (NECTA).
Kwa kuwa Shule hii
inafundisha kwa kufuata
mtaala wa Chuo Kikuu

cha Kiislamu Cha Madina,


a m b a c h o S e r i k a l i ya
Tanzania inakitambua.
Alisema.
Matambo alisema
hatua hiyo ya kukubalika
kufanyia ulinganishi vyeti
vya chuo hicho kulitoa
fursa kwa wanafunzi wake
kukubaliwa na kujiunga
na elimu ya juu ndani ya
nchi kupitia TCU.
Akifafanua alisema,
mfano kati ya mwaka
2010 na 2012, mwanafunzi
mmoja aliweza kujiunga
na Chuo Kikuu cha St.
John, na mwaka 2011,
wanafunzi wengine
waliomba kujiunga na
masomo ya elimu ya juu na
walikubaliwa katika vyuo
mbalimbali ndani ya nchi.
Alivitaja baadhi ya
Vyuo ambavyo wanafunzi
kutoka Shule hiyo ya dini
waliweza kujiunga navyo
kuwa ni Chuo Kikuu cha
Dodoma (UDOM), Chuo
Kikuu Cha Waislamu
Morogoro (MUM) pamoja
na Chuo cha Ualimu cha
Chukwani kilichopo
Zanzibar.
Mbali ya Vyuo hivyo
Vikuu, pia alisema
wanafunzi wengine
kutoka katika shule yao
wameweza kujiunga
katika vyuo vya kwa ngazi
ya Diploma na wamekuwa
wakifanya vizuri tu.
Hata hivyo akasema
N E C TA h i v i s a s a
wamebadili utaratibu.
Hawatambui vyeti vya
Alharamaini kitengo cha
Dini.
K wa u p a n d e wa k e

Sheikh Twalib Ahmed,


akiwanasihi wahitimu
hao wa Thanawi, katika
Shule hiyo ya Markazi
Al-Haramain Islamiyah,
Dar es Salaam, alisema
kwa hatua hiyo wasidhani
kuwa ndio wamemaliza
elimu bali watambue kuwa
wamepewa ufunguo ili
waanze kufungua nyumba
na waingie katika vyumba
mbalimbali vya elimu.
Msije mkadhania
hapo mlipo sasa tayari
mmeshakuwa maulamaa,
bali nyinyi mnaelekea
katika huo uulamaa,
ufunguo huo muutumie
kuingia katika mlango wa
tafsiri, hadithi, na nyanja
mbalimbali za elimu.
Alisema Shkh Twalib.
Shkh Twalib, alisema
kufikia kiwango
walichohitimu wahitimu
hao ni bahati kubwa kwa
sababu Ulimwengu wa
sasa ni kwamba, Usheikh
unapendwa sana na
unatakiwa sana.
Akawataka kutumia njia
sahihi za ufikisha ujumbe,
kwa kuzingatia kuwa wao
ni wasomi na wana elimu
ya namna ya ufikishaji
ujumbe.
Shule ya Al-Haramain
kitengo cha Dini ni Shule
inayojishughulisha
na utoaji wa elimu ya
mazingira na elimu ya dini
ya Kiislamu kwa kiwango
cha Thanaw.
Shule hiyo ilianzishwa
mwaka 1978, ikiwa na
m a l e n g o ya k u a n d a a
Walinganiaji, Makhatwib,
Maimam na Walimu.

KATIBU Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa, Dkt. Charles Msonde.

Habari za Kimataifa

AN-NUUR

RABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 18-24, 2015

Aung San Suu Kyi Misikiti 7,500 yajengwa Urusi


aiga usafi wa Magufuli
RIPOTI iliyotolewa
na kiongozi wa dini
ya Kiislamu nchini
Urusi, Sheikh Salam
Taju Diin, imeeleza
k u wa k wa k i p i n d i
chote cha utawala wa
Rais wa Jamhuri ya
Urusi Vladimir Putin,
imejengwa Misikiti
7500 nchini humo.
Hali inaonyesha
kuwa katika muda wa
utawala wa serikali
y a Vl a d i m i r P u t i n
nchini humo, wafuasi
wa d i n i t u k u f u ya
Uislamu wamefanikiwa
kujenga Misikiti mingi
nchini humo, ambapo
imefunguliwa Misikiti
7500 na kutumika rasmi
katika taifa hilo.
Katika idadi ya
Misikiti hiyo, baadhi
alianza kujengwa wakati
wa zama za utawala wa
Rais Mikhail Gorbachev
na kufunguliwa katika

Kiongozi wa upinzani wa Myanmar, Aung San Suu Kyi.

KIONGOZI wa
upinzani wa
Myanmar, Aung San
Suu Kyi, Jumapili
iliyopita alivaa
glovu na kuokota
taka katika tarafa
yake.
Majuzi Bi. Suu Kyi,
aliwaomba wabunge
wa c h a m a c h a k e
waliochaguliwa hivi
karibuni, waokote
takataka kama
sehemu ya kampeni
ya kufanya usafi
nchini humo.
Chama cha Suu Kyi
cha NLD kilishinda
viti vingi katika
uchaguzi uliofanywa
mwezi uliopita
nchini Myanmar.
Serikali ya sasa ya
kijeshi nchini humo,
imeteua kamati
kusimamia shughuli
ya kukabidhi
madaraka chama cha
Bi Suu Kyi.

Uchafu ni tatizo
la taifa nchini
M y a n m a r , Ta i f a
ambalo halina
mfumo kamili wa
kukusanya taka na
kuzitupa.
Rais wa Tanzania
Joseph Pombe
Magufuli, alitawala
vichwa vya habari
sehemu mbali
duniani pale
alipochukua jukumu
la kutangaza siku ya
uhuru kuwa ni siku
ya kufanya usafi nchi
nzima, ambapo siku
hiyo yeye, Makamu
wake Samia Suluhu
Hassan na Waziri
Mkuu Kassim
Majaliwa, walikuwa
m f a n o
k wa
kuokota na kuzoata
takataka jijini Dar
na kuwaongoza
w a t a n z a n i a
kusafisha miji
sehemu mbalimbali
nchini.

UJENZI wa Misikiti nchini Urusi.


kipindi cha Rais wa sasa.
Ripoti hiyo imetolewa
na kiongozi wa dini ya
Kiislamu nchini humo
S h e i k h I s l a m Ta j u
Din, ambaye ni katika
wanazuoni wakubwa
wa nchi hiyo.
Aidha baada ya
kubainisha ripoti hiyo

Sheikh Din alipinga


vikali kuwepo fikira ya
kigaidi katika Uislamu
na mwisho akawataka
Waislamu wa nchi hiyo
k u u n g a n a n a k u wa
kitu kimoja katika
kupambana na vikundi
vya kigaidi ikiwemo kile
cha Daesh.

Ni mara ya kwanza mwanamke kushiriki

hiyo mjini Madrakah karibu


kilometa 150 Kaskazini mwa
Makka.
Mitandao yenye uhusiano
na serikali na mashirika
ya habari ya kujitegemea
yameashiria kuwa wananchi
wa Saudi Arabia wamechagua
karibu wanawake 17.
Maafisa wa Serikali
walisema kuwa wanawake
130,000 walijiandikisha
kupiga kura, ikiwa ni sehemu
moja kwa kumi ya wapiga
kura wanaume.
Kulikuwa na wagombeaji
zaidi ya 1,000 waliokuwa
wakiwania viti mbalimbali
katika uchaguzi huo.
Imeelezwa kuwa
wanawake waliokuwa
wakigombea katika uchaguzi
huo, walikuwa wakifanya
kampeni zao huku wakiwa
wamesimama nyuma ya
pazia au wakati mwingine
wakiwa wamewakilishwa na
wanaume.
Wanawake kadhaa wa
Saudi Arabia wamepongeza
uchaguzi huo kama hatua
muhimu kwa demokrasia
nchini humo.
Hata hivyo wengine
wa l i s e m a k u wa h a u n a
u m u h i m u w o w o t e k wa
sababu bado maisha yao
yana vizuizi vingi, kama vile
kutoruhusiwa kuendesha
magari.

Wanawake washinda uchaguzi Saudi Arabia


RAIA wa Saudi Arabia
wameweka historia katika
uchaguzi uliofanyika
nchini humo Jumamosi
mwishoni mwa wiki
iliyopita, ambapo kwa mara
ya kwanza, mwanamke wa
kwanza amechaguliwa kuwa
mwakilishi katika uchaguzi
huo.
Tume ya uchaguzi ya
Saudia Arabia ilimtangaza
Salma bint Hizab al-Oteibi,
kuwa ameshinda uwakilishi
na kuwa mwanamke wa
k wa n z a m wa k i l i s h i wa
wilaya katika jimbo la Mecca.
Hii ni mara ya kwanza
kwa wanawake nchini Saudi
Arabia kushiriki kugombea

na kupiga kura katika


uchaguzi nchini humo.
Katika Uchaguzi huo wa
kihistoria katika taifa hilo
la kifalme uliofanyika siku
ya Jumamosi Desemba 12,
2015, kwa mara ya kwanza
wamechaguliwa Madiwani
wanawake.
K a r i b u wa n a wa k e 1 3
wameshinda viti katika
u c h a g u z i wa B a r a z a l a
Manispaa nchini Saudi
Arabia.
Uchaguzi huo unakuwa
wa kwanza wa wazi kwa
wapiga kura na kuwepo
wagombea wanawake.
Bi. Al-Oteibi aliwashinda
wanaume saba na wanawake
wengine wawili katika nafasi

WANAWAKE wakipiga kura, Saudi Arabia.

Hoja ya Juma Kilaghai

AN-NUUR

RABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 18-24, 2015

Nguvu ya wingi (Strength in numbers) ndiyo silaha pekee ya wanyonge!

Unamjua nyuki?

YUKI ni mdudu
mdhaifu sana.
Nyuki akiwa
peke yake unaweza
ukamnyanyasa
unavyotaka. Amebeba
mshale mmoja tu kama
silaha na akishautumia,
basi tena! Hata hivyo,
nyuki wanaujua udhaifu
wao, na hivyo ni mara
chache mno kuwakuta
wakiwa mmoja
mmoja. Mara nyingi
wanatembea na kufanya
shughuli zao katika
makundi makubwa
yanayojumuisha nyuki
malaki kadhaa au hata
mamilioni.
Wanatambua kuwa
nguvu iko kwenye
wingi na mshikamano.
Wanapokuwa kwenye
makundi yao nyuki
wanaweza kuwa
mahasimu wa kutisha
iwapo watachokozwa.
Kundi moja la nyuki
linaweza likasababisha
watu wote mtaani
kujifungia ndani!
Wanadamu tunapaswa
kuuiga mfano huu
wa nyuki. Nguvu ya
pamoja ndiyo silaha
pekee inayoweza
kumhakikishia kila
mmoja wetu maisha
bora na ya uhakika. Kwa
mfano wewe peke yako
ukiwa na shilingi mia
moja mfukoni utaifanyia
nini? Ni vigumu kusema
kwa uhakika kwa sababu,
kwa thamani ya sasa ya
shilingi yetu, shilingi
mia ni kama haina kitu
cha kununua. Je, mkiwa
watu 1,000,000 na kila
mmoja na shilingi mia
yake? Mhh, sasa hapa ni
hadithi tofauti. Mambo
yanaanza kuonyesha sura
nyingine. Yaani katika
kundi la watu 1,000,000
kila mmoja akitoa shilingi
100, tayari kuna kitita cha
shilingi milioni 100!
Tanzania inakisiwa
kuwa na watu wazima
20,680,000. Tunaambiwa
kuwa 36% ya hawa ni
masikini sana, yaani watu
7,444,800. Hili ni kundi
la watu wanaofanya kazi
za vibarua, wachuuzi wa
karanga, wachuuzi wa
maji ya chupa barabarani,
waokota chupa za
plastiki zilizotumika,
na kadhalika. Pamoja
na umasikini wao wote
hawa kila mmoja kila

Nyuki wakiwa katika sega lao.


siku anaweza akachanga
shilingi 100 kwenda
kwenye kapu la pamoja
na isimnyime usingizi.
Yaani kundi hili kila siku
linaweza kujichangia
mtaji wa pamoja wa
shilingi milioni 745! Hii
ni kwa siku! Kwa mwaka
ni shilingi milioni 745
x 365, sawa na shilingi
bilioni 272! Wow!
Sasa hebu tuchukulie
kwamba tunahitaji
kuanzisha mfuko wa
umoja ambao kazi yake
itakuwa ni kukusanya
hizi shilingi 100 za
kila mmoja kila siku.
Itachukua siku ngapi
kuwasajili hawa
watu 7,444,800 kuwa
wanachama wa huu
mfuko?
Tuchukulie kwamba
wamepatikana waasisi
100 wa huu mfuko.
Tuchukulie pia kwamba
tumekubaliana kila
mwanachama muasisi
atafute wanachama
wawili kila siku, na
wale wanachama wapya
nao kila mmoja atafute
wanachama wapya
wengine wawili kila siku.
Hii ina maana
kwamba katika siku ya
kwanza watapatikana
wanachama 100 x 2, sawa
na wanachama 200! Siku
ya pili watapatikana
wanachama 200 x 2, sawa
na wanachama 400! Siku
ya tatu wanachama 400 x
2 , sawa na wanachama
800! Siku ya tatu
wanachama 800 x 2 sawa
na wanachama 1,600!
Siku ya nne wanachama
3,200! Siku ya tano
wanachama 6,400! Siku
ya sita wanachama

12,800! Siku ya saba


wanachama 25,600! Siku
ya saba wanachama
51,200! Siku ya nane
wanachama 102,400!
Siku ya tisa wanachama
204,800! Siku ya tisa
wanachama 409,600! Siku
ya kumi wanachama
819,200! Siku ya kumi
na moja wanachama
1,638,400! Siku ya kumi
na mbili wanachama
3,276,800! Siku ya kumi
na tatu wanachama
6,553,600! Siku ya kumi
na nne, wanachama
13,107,200!
Hata hivyo kwa kuwa
lengo ni wanachama
7,444,800, ina maana
kuwa siku ya kumi na
nne kuna wanachama
wengi tu watakuwa
hawana watu wa
kuwaingiza kwenye
mfuko. Hebu fikiria
ndani ya siku 14 tu,
tayari watu 7,444,800!
Haya ni maajabu ya
kanuni moja ya hisabati
inayoitwa GEOMETRIC
PROGRESSION.
Ukweli ni kwamba
katika hali ya kawaida
ni vigumu sana kujenga
mtandao ambao
utajumuisha watu
wote. Hata hivyo kwa
kutumia kanuni hiyo ya
hisabati tuliyoitaja hapo
juu, ni rahisi kujenga
mitandao inayoweza
kuwa na wanachama
mathalani 10,000 mpaka
100,000. Watu 10,000
wanaojichangia shilingi
100 kwa siku, ni sawa
na shilingi 1,000,000.00
kila siku au shilingi
365,000,000.00 kwa
mwaka. Hebu chukulia
hawa watu 10,000 ni

jumuia inayoishi ndani


ya kata fulani humu
nchini na wanataka
kujiletea maendeleo.
Kwa mtaji wa shilingi
365,000,000 kwa mwaka,
ndani ya miaka 10, bila
shaka kata hii itakuwa
imepata maendeleo ya
kustaajabisha.
Je, tunaweza
kujipanga?!
Dhana ya matumizi ya
nguvu ya wingi katika
kuondoa udhaifu wa mtu
mmoja mmoja inaweza
pia kutumika katika
mazingira mengine.
Tuchukulie kwa mfano
tofauti iliyoko baina
ya vijana wa Kiganda
na wale wa Kitanzania
katika masuala ya
kijasiriamali.
Ukienda Kampala na
miji mingine ya Uganda,
ni jambo la kawaida
kuingia kwenye duka
na kukuta vijana watano
au sita wote wanauza.
Bila kudadisi unaweza
ukadhani kuwa vijana
hao ni waajiriwa tu,
na mwenye mali hapo
hayuko. Dhana yako
hiyo itakuwa siyo sahihi
hata kidogo. Ukweli ni
kwamba wenye mali
ndio hao walioko mbele
yako na hawana 'BOSI'
mwingine zaidi yao
wenyewe.
Kimaumbile vijana
wa Kiganda hawana
tofauti yoyote na vijana
wa Kibongo. Tofauti
pekee iko katika jinsi
makundi haya mawili
yanavyofikiri. Vijana
wa Kiganda wanaelewa
kuwa ili kuweza kufanya
biashara nzuri, ni lazima
biashara zao ziwe
katika yale maeneneo

yanayojulikana kama
ya kibiashara (business
districts). Tatizo la
maeneo haya ni kwamba
kodi za pango ziko juu
sana. Na mara nyingi
vijana hawa hawana
uwezo wa kuzimudu
wakiwa mmoja mmoja.
Ili kuondoa kadhia
hii wanakubaliana
kuungana watano au sita
na kupanga chumba cha
biashara kwa pamoja.
Wanakubaliana pia
kukata leseni moja,
na kuwa na faili moja
la kulipia kodi ya
mapato. Ambacho kila
mtu anamiliki kivyake
ni bidhaa zilizomo.
Kwa makubaliano
maalum wanakubaliana
kugawana aina ya bidhaa
za kuuza ili kusije kuwa
na mkanganyiko. Kwa
kutumia ujanja huu,
vijana hawa wanafanya
biashara kubwa huko
katika maeneo murua
kabisa ya kibiashara,
huku wakiwa kwa
pamoja wanatumia
gharama ndogo.
Tofauti na vijana
wa Kiganda, vijana wa
Kibongo ni kila mtu
kivyake. Ni mara chache
sana kutembelea maeneo
murua ya kibiashara na
kukuta vijana wa kibongo
wakiwa wamiliki wa
biashara zilizomo zaidi
ya kuwa ni waajiriwa.
Kijana wa kibongo pale
anapojijengea uwezo
kidogo biashara yake
inawekwa USWAHILINI
kwa sababu kule
anaweza kumudu
gharama za pango peke
yake na bado akabaki
na mtaji wa kununulia
bidhaa. Hata hivyo
biashara hizi mara nyingi
hazidumu (labda kama
mhusika anajihusisha pia
na kununua na kuuza
mali za wizi), kwa sababu
bei za USWAHILINI ziko
chini, na pia wateja wa
USWAHILINI hawafanyi
manunuzi makubwa.
Vijana wa kibongo
wanahitaji kubadili
jinsi wanavyofikiri.
Wanahitaji kujua kuwa ili
waweze kufanya biashara
katika maeneo ya jijini
kati na kushindana na
WAHINDI, ni lazima
wajenge tabia ya
kushirikiana. Wanahitaji
kujifunza kwa Waganda!
(Kwa maoni,
mawasiliano 0754 281
131)

MAKALA

AN-NUUR

RABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 18-24, 2015

Tuchague vya kurithi, siyo uwongo na propaganda!


T
UNAISHI katika
ulimwengu
ambao
umegubikwa na
kila aina ya mazonge.
Ulimwengu ambao
mambo mengi ya
kustaajabisha yanatokea
kila uchao. Ulimwengu
ambao propaganda,
uwongo na mfanowe
vinaonekana kama
ndio njia pekee ya
kufikia malengo mbali
mbali. Ulimwengu wa
Akhir Zaman (zama za
mwisho).
Tanzania ni moja
kati ya nchi ambazo
hazikuachwa nyuma
katika masuala ya
propaganda na uwongo.
Mtaji huu umetumika
vyema mno katika
kipindi cha uchaguzi na
wengi wanafahamu bila
shaka. Lakini ifahamike
kwamba, mambo haya
hayafanyiki kwa bahati
mbaya, bali kwa lengo
maalum. Yanafanyika
kwa bahati nzuri kabisa.
Yanapofanyika haya,
wapo wanaonufaika na
wapo wanaodhulumiwa.
Katika gazeti la Annuur toleo nambari
1205 la Novemba 27
hadi Desemba 03, 2015,
ukurasa wa mwanzo
kabisa lilisomeka:
Mtihani wa kwanza
kwa Rais Magufuli.
Yakafuata maneno; dini
sasa kufundishwa kama
taaluma, yadaiwa ibada
hazijengi mshikamano,
masheikh wasubiriwa
kupitisha muswada.
Maelezo ya kina
yanapatikana ndani ya
gazeti na natumai wengi
wamefanikiwa kuyapitia
kwa undani.
Kutokana na uzito
na ukakasi wa habari
hii, nikaamua nami
niseme kidogo kwa kuwa
tunatofautiana uwezo
wa kufikiri na kuelewa
mambo. Tuitizame
kadhia hii kupitia
makala ya mwandishi J.
Mihangwa
Katika Gazeti la Raia
Mwema toleo nambari
432 la Novemba 1824, 2015, ukurasa wa
15, kichwa cha makala
kinasomeka hivi: Rais
Magufuli, epuka viatu
vya waliokutangulia
utaharibikiwa.
Mwandishi wa makala
hii anaitwa Joseph
Mihangwa.
Mwandishi ameanza

RAIS John Magufuli.


makala yake kwa
kusema; tumejionea na
kuthibitisha wenyewe
wakati wa kampeni za
Uchaguzi Mkuu uliopita,
jinsi umma wa Kitanzania
ulivyoonesha mori ya
kutaka Mabadiliko
kwa kuondokana
na Mfumo wa sasa
unaowafukarisha, mithili
ya mfumo wa utawala wa
Mfalme Louis wa XVI wa
Ufaransa. Mwandishi pia
amegusia kwa uchache
msukumo uliopo wa
kutaka mabadiliko
kupitia Katiba mpya
ambayo itatokana na
maoni ya wananchi
wenyewe, Katiba ambayo
ipo kwenye Rasimu ya
Mapendekezo ya Jaji
Joseph Sinde Warioba.
Lakini akaendelea
kusema kwamba,
endapo serikali ya sasa
itapuuza mihemko, hii,
tuendako, amani itapata
msukosuko mkubwa
kwa kuzuka mapambano
kati ya kikundi cha
watawala wachache
wanaojitajirisha kwa
kujigawia fedha na
mali za nchi pamoja na
kutajirisha wawekezaji
kutoka nje ya nchi,
wanaovuna mali za nchi
hii kama vile ni shamba
la bibi, huku wananchi
wakiendelea kufukarika
kwa kufukarishwa na hao
wachache.

Msingi mkuu na
ambao ndio maudhui ya
makala ya mwandishi
huyu, kwamba
kukosekana uadilifu kati
ya serikali na makundi
jamii ndio chimbuko la
misukosuko, vurugu,
kukosekana amani
na mfano wa hayo.
Kupendelewa kundi moja
dhidi ya jingine ndiko
kunakopelekea yote haya
ya kukosekana amani.
Watu kutaka mabadiliko,
ni kwa sababu ya namna
serikali inavyowafanyia.
Lakini serikali iliyopo
madarakani chini ya
chama tawala CCM,
haikutaka na pengine
niseme haiko tayari
kupokea mabadiliko
haya. Nasema hivi kwa
sababu msingi mkuu
wa mabadiliko ni kwa
kupitia Katiba Mpya
ambapo CCM hawaitaki.
Wameikataa!
Turejee maudhui ya
Makala yetu, kuhusiana
na pendekezo la Taasisi
ya Elimu Tanzania
(TET) katika ufundishaji
wa somo la dini kama
taaluma, kama njia
ya kuleta upendo,
amani na mshikamano.
Wanachotaka
kutuaminisha hapa
ni kwamba, hakuna
namna yoyote ile ya
kuleta amani, utulivu,
upendo na mshikamano

ila kwa kufanya hichi


walichotuwekea mezani.
Ni kama vile umefika
nyumbani ukaambiwa
chakula kimeisha imebaki
tu ukoko, kama upo
tayari kula nikutengee!
TET sasa wametutengea
ukoko! Lakini kwetu sisi
Waislamu, bora hata huo
ukoko! Sisi Waislamu
ni kama tumetengewa
machicha ya pombe!
Serikali yetu na
watendaji wake
wanataka kujifanya
hawaelewi chanzo
cha mpasuko uliopo
nchini leo hii. Wanataka
wananchi wake waamini
kwamba, dini ndio
chimbuko la matatizo
ya uvunjifu wa amani,
kukosekana upendo
na mshikamano!!? Sasa
ndugu yangu msomaji
hebu safari na historia
fupi ya Ufaransa ya
kale uone kipi kilikuwa
chanzo cha haya ambayo
yanaogopewa na serikali
yetu ya Tanzania.
Mwandishi, J.
Mihangwa ameeleza kwa
urefu kidogo sababu
za mazonge tuliyonayo
hapa kwetu hivi leo.
Akaionya serikali ya sasa
kuachana na ulaghai wa
sasa wa kutaka kujenga
tabaka la watu wenye
mitaji na ubunifu kwa
ulaghai wa kubadilisha
mazingira ya uzalishaji
duni na kuwa uzalishaji
maridhawa. Sasa
tuangalie mfumo katili
wa Ufaransa ya kale
ulivyoendeshwa na
kuzua ghadhabu ya
wananchi wakapindua
serikali, tumithilishe na
yale tunayoyashuhudia
leo.
Wakati akichukua
madaraka mwaka 1774,
Mfalme wa Ufaransa,
Louis wa XVI, alikuta
nchi imetopea katika
lindi la uozo kijamii na
kiuchumi, kutokana
na Uongozi mbovu wa
Wafalme waliomtangulia.
Kenneth Martin, katika
kitabu chake kiitwacho,
French Liberal Thought
in the Eighteenth
Century, anaielezea
hali hiyo na hii tuliyomo
kama ifuatavyo:
Ni jamii iliyochakaa
na kulika kwa kutu ya
maovu na ufisadi; ni jamii
iliyooza na kunuka kwa
uozo, yenye migongano
ya kitabaka, rushwa na
uonevu, huku Taasisi

zikiporomoka na mawazo
kinzani yakichipuka
kama magugu kwenye
shamba lenye rutuba
lililotelekezwa.
Ingawa orodha ndefu
ya kero kwa wananchi,
maarufu kama cahiers,
ilikuwa imewasilishwa
serikalini, Mfalme Louis
hakuzifanyia kazi kero
hizo, akaziba masikio
na kundelea kula nchi
na wateule wake, hadi
hapo nguvu ya umma
ilipomshukia.
Bunge lilikuwa la
kitabaka, likiwakilisha
matakwa ya walio
nacho na matakwa
ya Mfalme mwenye
kauli isiyopingwa,
aliyejiaminisha kuwa
yeye ndiye alikuwa
Ufaransa na Ufaransa
ilikuwa ndio yeye.
Raia waligawanywa
katika matabaka
matatu yenye hadhi
tofauti kisiasa, kijamii,
kiuchumi na katika
kutendewa haki. Tabaka
la kwanza lilikuwa la
Makasisi wa Kanisa [The
Clergy], lililojumuisha
Maaskofu, Maparoko,
Mapadri na wengineo
kama ilivyo hapa
kwetu Tanzania. Wakati
wengine wakinufaika
na Memorandum
of Understanding,
wengine wametwezwa,
kudhalilishwa, licha ya
kuwa wanatozwa kodi.
Tabaka hili la kwanza
halikutozwa kodi na ndio
walikuwa wakimiliki
ardhi huku wakipumua
juu ya sheria.
Tabaka la pili lilikuwa
la watu wenye nasaba
bora [the nobility], ambao
idadi yao ilikuwa ndogo
isiyozidi watu milioni
moja. Hili lilihusisha
pia matajiri na lilihodhi
nafasi ya ushawishi
kanisani, serikalini na
jeshi na siyo msikitini.
Kila Askofu na kila Afisa
wa Jeshi isipokuwa askari
dhalili wa vikosi vya
mizinga, alitoka katika
tabaka hili. Kwa bahati
nzuri pia hapakuwa
na Sheikh, Imamu wala
Ustadh kwenye tabaka
hili la kibaguzi.
Mwandishi
akafananisha tabaka la
pili na kikundi kidogo
cha matajiri, mafisadi
walioteka mfumo wa
serikali pamoja na
uchumi wa nchi, na

Inaendelea Uk. 8

Makala

8
Na Khatibu J. Mziray
YAKOBO ajipatia mali
kwa hila (uchawi). Hicho
ni kichwa cha habari za
jinsi Yakobo alivyomlaghai
mkwewe, ambaye pia ni
mjombaye, aliyeowa binti
zake wawili, mtu na mdogo
wake. Msomaji atasema
ninamkashifu Yakobo, na
hasa akijua kuwa mimi
ni Muislamu, lakini kwa
maneno hayo ya ulozi
nasema Astaghfirullah,
Msamaha wa Allah uwe
n a m i ; k w a n i Ya k o b o
ninayemfahamu katika
Uislamu, ameepukana na sifa
zote mbaya na amekamilika
na sifa zote nzuri. Lakini
sikusema mimi, bali ni
Biblia iliyoandikwa hayo.
Inasema:
Yakobo akatwaa fito za
mlubna mbichi, na mlozi, na
mwaramoni, akazibambua
maganda, mistari myeupe
ionekane ndani ya hizo

AN-NUUR

RABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 18-24, 2015

Khabari ya Israel Taifa teule-4


Yakobo ajipatia mali kwa hila (uchawi)

fito. Akazisimamisha fito


hizo alizozibambua katika
mabirika ya kunyweshea maji,
pale walipokuja wanyama
wanywe; wakachukua
mimba walipokuja kunywa.
Wanyama wakapata mimba
mbele ya hizo fito, wakazaa
wanyama walio na milia, na
madoadoa, na marakaraka.
(Mw. 30:37-39.)
Ulozi, ni uchawi, mlozi, ni
mchawi, fimbo za mlozi, ni
fimbo za mti unaotumika kwa
kuchawia. Ndiyo maana miti
hiyo mitatu ikichanganywa
kwa pamoja ilizichawiailiziloga zile kondoo, mbuzi
na ngombe zikazaa ndama za
mabaka n.k. Hiyo inamaana
kuwa Yakobo alijua uchawi.
Hata hivyo ukisoma habari
hizo kuanzia Mw. 30:1-

43, utapata kisa kizima na


vituko vyake; na jinsi watoto
wa Labani yaani shemejie
Yakobo, walivyo lalamika
kutokana na huo ulaghai
wa kimazingaumbwe wa
Yakobo.
Lakini kwa imani ya wana
wa Israeli na Wakristo, huo ni
ufunuo, na hiyo ni sifa kwa
wana wa Israeli. Ndiyo maana
ukisoma Biblia ya Kiswahili
cha Mvita ya mwaka wa
1937, inaanza kwa kichwa cha
habari kisemacho: Werevu
wa Yakobo wa kujipatia mali
nyingi. Mw. 30:25.
Kuloga, kuroga, kuchawia,
kunasifiwa kuwa ni werevu.
Huyo ndiye Babu wa
wana wa Israeli; ambaye
sera za imani ya mila na
dini inayotokana na yeye,

kwao haramu ni halali, na


halali ni haramu, na ndio
wanaoongoza sheria za dunia
hii; na ndio washauri wakuu
wa baba la vita duniani, na
baba la ghilba na dhuluma na
mauwaji duniani (Marekani).
Maisha ya Yakobo
na majirani zake
Kama tunavyoona, jinsi
wana wa Israeli walivyo, na
wanavyokuwa mahodari
wa kutengeneza matukio
ya vita na mauaji, ndio
urithi wa Yakobo (Israeli)
mwenyewe alivyokuwa, na
alivyowarithisha. Kuna imani
iliyojengwa kwa waumini wa
Kikristo na hata wasiokuwa
wao, kuonesha ubaya wa
Wafilisti, au wenyeji wa
Kanaani, ambapo hao ndio
watu wa asili kutokana na

maandishi ya Biblia:
Wa n a wa H a mu n i
Kushi, na Misri, na Putu, na
KanaaniWakasluhi; huko
ndiko walikotoka Wafilisti
na Wakaftori. Kanaani
akamzaa Sidoni, mwanawe
wa kwanza, na Hethi, na
Myebusi, na Mwamori,
na Mgirgashi, na Mhivi,
na Mwarki, na Msini,.
Baadaye jamaa za Wakanaani
walitawanyika. Na mpaka
wa Wa k a n a a n i u l i a n z a
kutoka Sidoni kwa njia ya
Gerari hata Gaza; tena kwa
njia ya Sodoma, na Gomora,
na Adma, na Seboimu, hata
Lasha. Hao ndio wana wa
Hamu, kufuata jamaa zao,
kwa lugha zao, katika nchi
zao, kufuata mataifa yao.
(Mw.10:6-20.)
Ya k o b o a l i k u wa n a
binti yake, akiitwa Dina,
akaenda kuona michezo ya
Wakanaani, akakutana na
mwana wa mfalme, aliyeitwa
Shekemu mwana wa Hamori,
Mhivi, akamchukua akalala
Inaendelea Uk. 13

Tuchague vya kurithi, siyo uwongo na propaganda!

Inatoka Uk. 7
wameweza kupenyeza
watu wao katika sehemu
nyeti za utawala wa
nchi kama vile Jeshi,
Bunge na sehemu
nyingine muhimu za
serikali kuhakikisha
kwamba utawala wa
nchi unacheza kwa
mdundo wa muziki
wao. Mfumo huu,
tunaweza kuumithilisha
na Mfumo Kristo hapa
kwetu Tanzania, ambapo
wakristo ndio ambao
wamehodhi sehemu nyeti
serikalini.
Kama kweli Rais huyu
anataka kuwatumikia
Watanzania na asivae
viatu hivi kama
alivyosema mwandishi
J. Mihangwa, basi na
avunje mfumo kristo.
Vinginevyo itakuwa ni
kama danganya toto, kwa
kuwa aliahidi kwenye
kampeni kwamba
hatakuwa mbaguzi.
Tabaka la tatu na
la mwisho, lilikuwa
la makabwela,
lililojumuisha
wakulima wadogo
wadogo, wachuuzi,
wafanyabiashara na
wasomi wasio na
ajira serikalini. Hawa
hawakuwa na fursa ya
kuyafikia matabaka
mawili ya juu hadi kufa.
Hawa ndio walioonja
adha ya mfumo huo wa
kidikteta wa Ufaransa

ya kale. Walitozwa
kodi kubwa kwa kanisa
iliyoitwa the tithe,
kwa maana ya moja ya
kumi ya kipato chao
kiduchu. Walitozwa pia
kodi ya ardhi, kodi ya
kichwa, kodi ya mapato
kwa ujumla, chumvi,
kodi ya kusaga nafaka
na zinginezo. Wakati
haya yakifanyika, tabaka
la kwanza na la pili
halikutozwa kodi, na
inapotokea mmojawao
amefanya kosa basi
hujichagulia Hakimu au
Jaji wa kusikiliza kesi
yake.
Tabaka hili
linawafikiana zaidi
na Waislamu nchini
Tanzania kuliko hata hilo
tabaka la pili. Tabaka
la pili limechukua
sehemu ndogo sana.
Hali ya Waislamu
nchini, madhila,
udhalilishaji na mfano
wa hayo yaliyowakuta na
yanayoendelea kutokea
yako wazi hatuna sababu
ya kuyarudia. Kwa mtu
mwenye akili salama,
mwenye uwezo wa
kufikiri atabaini tatizo
la haya yanayotokea
ya kukosekana amani,
vurugu na mfano wa
hayo.
Muislamu anaweza
kukamatwa na
kubambikiziwa kesi na
kufanyiwa kila ubaya
kama tunavyoona kwa
Sheikh Ponda. Lakini

RAIS John Magufuli.


cha ajabu tukisema
tunaonekana wakorofi,
tunataka kuvunja amani!
Matokeo ya kudai haki
zetu tunapewa majina ya
siasa kali, al-shabab, alqaida n.k.
Kodi zote walizotozwa
tabaka la mwisho,
ziliishia kwenye
mifuko ya watawala na
wapambe wao; hivyo
serikali ikalazimika
kukopa kutoka nje.
Mwandishi anamshauri
Rais huyu, JPM
asijaribu kamwe kuvaa
viatu hivi walivyovaa
watangulizi wake
ataharibikiwa. Nami
namuasa atekeleze ahadi
ya kutokuwa mbaguzi.
Kama Memorandum
of Understanding
itaendelea kuwepo, basi

na Waislamu nao wapate


mgawo huo.
Wakati haya
yakiendelea kufanyika
nchini Ufaransa, kama
yanavyotokea hapa
kwetu leo, waandishi na
wanafalsafa wa tabaka la
tatu walisema, kuonya na
kuandika mengi dhidi ya
mfumo huo kandamizi
na wa kihujuma.
Francois Marie Arouet,
maarufu kama Voltaire
[1694-1778] aliandika
kushambulia Ukabaila
wa Kanisa. Ukilisema
hili kwetu Tanzania
utaambiwa unaleta
uchochezi, utakamatwa,
utawekwa ndani!
Moyo mgumu wa
Mfalme Louis katika
kuridhia maslahi mapana
ya walio wengi kwa

kuruhusu mabadiliko
haukumsaidia siku ya
kiyama ilipowadia,
Julai 1789; pale umma wa
walala hoi wa Kifaransa,
kwa kuchoshwa na sikio
la kufa, ulipofanya
mapinduzi kwa njia ya
maandamano yaliyotikisa
mitaa na Jiji la Paris,
kisha kusambaa hadi
vijijini. Magereza
yalivunjwa, na wafungwa
kufunguliwa, Ikulu [the
bastille] ikavamiwa.
Louis na mkewe
wakajaribu kutoroka,
lakini wakakamatwa
mpakani mwa nchi
kurejeshwa Paris na
kunyongwa kwa usaliti
wa Taifa.
Ni kazi ya serikali
mpya iliyopo madarakani
kuwabaini wachawi wa
amani, vurugu ambao
wanavunja umoja na
mshikamano miongoni
mwa wananchi. Rais
aliangalie hili kwa jicho
pevu ili kuvunja ukabaila
uliopo ndani ya nchi yetu
hii. Atoe semina elekezi
kwa TET katika namna ya
kuwasaidia kufikiri vema
zaidi kwa mustakbali
mwema wa nchi yetu,
na siyo kufundisha dini
kama taaluma.
(Mwandhishi wa
Makala hii ni msomaji
wa siku nyingi wa An
nuur-Juma Jumanne wa
Katesh, Manyara. 0659
789 468.)

Makala

AN-NUUR

RABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 18-24, 2015

Mauaji na majanga Mashariki ya Kati


Na Chris Martenson

KUELEWA kinachotokea
nchini Syria hivi sasa,
inabidi uelewe mbinu
na kinachowatuma
Marekani na washirika
wake wa NATO, nchi
zinazofuata malengo
sawia katika eneo la
Mashariki ya Kati na
Afrika ya Kaskazini.
Wakati watu wa nchi
za Ulaya na Marekani
wanalishwa propaganda
mbichi kuhusu
malengo ya kikanda
yanayohusika, hali halisi
ni tofauti kabisa.
Wakati propaganda
inasema madikteta hapa
na pale wameondolewa,
au kuwa demokrasia
ndiyo lengo, hakuna
mojawapo kati ya
hayo inayoendana na
kinachotokea sasa au
kilichotokea katika
ukanda huo.
Kwa wanaoanza,
tunafahamu wote
kuwa kama maeneo
ya kuchimba mafuta
yasingekuwepo, nchi
za Magharibi zisingejali
chochote kuhusu
kinachotokea katika eneo
hilo.
Lakini makundi tofauti
ya kimaslahi ya nchi za
nje yanajali. Na malengo
yao ni wazi ni pamoja
na kukamata raslimali
muhimu za nishati za
eneo hilo. Kuna wasiwasi
mkubwa kama Russia
au China wanaweza
badala yao wakaingia
na kushikilia maeneo
haya, ambayo ndiyo
akiba muhimu zaidi ya
mafuta duniani. Halafu,
tunaweza kuachana na
dhana kuwa Marekani
na washirika wa NATO
wana dhamira yoyote
ya haki za binadamu
katika suala hili.
Kama wangekuwa
wanajali, basi ingebidi
wakubali kuwa mikakati
yao na mbinu zao
zimesababisha kuteseka
kwa mamilioni ya watu,
pamoja na kuweka
mazingira ya watu
wengi wengine kuingia
katika majanga. Lakini
itakuwa ujinga kujadili
au kuelewa dhamira ya
wanachofanya katika
eneo hilo kwa darubini
ya haki za binadamu
au uhuru wa mtu
binafsi -kwani hakuna
kinachohusika hapa.

KIONGOZI wa zamani wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi.


Wagawe uwatawale
Sera zinazofuatwa
katika eneo la Mashaiki
ya Kati na Afrika
Kaskazini, zina mizizi
yake katika kugawa
eneo hilo ili kulidhibiti
kwa urahisi zaidi. Ni
mbinu kongwe; kwanza
ilitumiwa kwa kiwango
kikubwa na Waingereza
kuanzia miaka ya 1700.
Gawa na kuteka: Kuna
sababu ambayo ni
kibwagizo cha karne
nyingi.
Lakini kupata mashiko
ya unyama unaohusika,
nadhani inasaidia
kutathmini kilichotokea
Libya mwaka 2011 wakati
NATO ilipomuondoa
Muammar Gaddafi na
kuiacha nchi ni gamba
lililovunjika - kama
ilivyotakiwa.
Siwezi kukupa
sababu nzuri kwa
NATO kushiriki katika
kumwondoa Gaddafi.
Ninazo sababu mbaya tu.
Sababu rasmi ilikuwa
kwamba baada ya
harakati za Uamsho wa
kiangazi chepesi nchi
za Kiarabu mapema
mwaka 2011 (ambako
kuna ushahidi mkubwa
wa nchi za Magharibi
kuchochea miali hiyo ya
moto), mambo yaligeukia
pabaya na waandamanaji
wakapigwa risasi. Hii
iliruhusu Umoja wa
Mataifa kutangaza kuwa
inahitaji kuwalinda raia,
na Mahakama ya Jinai
ya Kimataifa kumshtaki
Gaddafi kwa jinai dhidi
ya binadamu, ikisema
anahitaji kusimamishwa

kizimbani.
Hivi ndivyo
ilivyokuwa: Hapo 27
Juni, ICC (Mahakama
ya Jinai ya Kimataifa)
ilitoa hati za kukamatwa
kwa Gaddafi, mwanae
Seif al-Islam na mkwewe
Abdullah Senussi
aliyekuwa mkuu wa
usalama wa taifa, kwa
mashitaka yanayohusu
jinai dhidi ya binadamu.
Maofisa wa serikali
ya Libya waliikataa
ICC, wakidai kuwa
"haina uhalali wowote"
na kuainisha kuwa
"shughuli zake zote
zinalenga viongozi wa
Kiafrika."
Mwezi huo, shirika
la utetezi wa wafungwa
wa kisiasa, Amnesty
International lilichapisha
taarifa ya uchunguzi
wake, ambako lilisema
tuhuma nyingi za uhalifu
dhidi ya binadamu
zilizoundwa dhidi ya
majeshi ya Gaddafi
zilikuwa hazina ushahidi
wa kuaminika, na badala
yake ni madai ya kutunga
ya majeshi ya wapinzani
ambayo yalichukuliwa na
kukubalika kwa vyombo
vya habari vya nchi za
Magharibi.
Baada ya kutolewa
hati ya mashitaka ya ICC,
ilikuwa ni mchezo wa
kuruka na kuchupa hadi
kufikia kutangazwa kwa
eneo la kutorusha ndege
chini ya amri ya NATO
juu ya Libya kuwalinda
raia.
Kutoka hapo ilikua
ni mruko wa moja
kwa moja hadi NATO
kuelekezea mtutu
chochote kinachohusiana

na serikali ya Gaddafi.
NATO ilikuwa
imechagua upande wake
na ilikuwa inasaidia uasi
moja kwa moja.
Mpangilio hapa ni ule
ule nyakati zote: matukio
yanayochaguliwa kwa
kutengenezwa kwanza
na kutumika kama
kisingizio cha kuunga
mkono upande unaotaka
kuipindua serikali iliyopo
hivyo kuacha jangwa la
mifarakano ya kidhehebu
kushamiri katika ombwe
la utawala litakalotokea
bila shaka yoyote.
Kama unafanana na
watu walio wengi nchi
za Magharibi, unajua
kidogo sana au hujui
kitu kuhusu masuala
haya. Haifuatiliwi vizuri
na vyombo vya habari.
Na Libya haiko katika
habari mara nyingi licha
ya kuwa inapitia wakati
mgumu.
Niligundua hotuba
iliyotolewa na Gaddafi
miezi michache kabla
hajauawa nikaona ina
mvuto wa kipekee na
kufichua yaliyojificha.
Nitaitoa kama ilivyo
hapa. Nanukuu:
Kwa miaka 40, au ni
kitambo zaidi, siwezi
kukumbuka, nilifanya
kila nilichoweza kuwapa
watu nyumba, hospitali,
mashile na wakati
wakiwa na njaa, niliwapa
chakula. Niliweza hata
kubadili Benghazi kutoka
jangwa hadi ukanda wa
kilimo. Nilisimama dhidi
ya mashambulio ya yule
cowboy,
Reagan, pale
alipomwua binti yangu
wa kufikia, akijaribu

kuniua mimi, badala yake


akamwua yule mtoto
mdogo asiye na hatia.
Halafu nikawasaidia
ndugu zangu na dada
zangu wa Afrika kwa
fedha kwa ajili ya Umoja
wa Afrika.
Nilifanya nilichoweza
kuwasaidia watu kuelewa
maana ya demokrasia
halisi, ambako kamati za
wananchi zinaendesha
nchi yetu. Lakini hiyo
haikuwahi kutosha,
kama walivyoniambia
baadhi, kwa vile ni
wabinafsi walitaka zaidi.
Waliiambia Wamarekani
na wageni wengine, kuwa
wanataka 'demokrasia'
na 'uhuru' bila kujua
kuwa ni mfumo wa kila
mtu na lwake, ambako
jibwa kubwa zaidi
linawala waliobaki, lakini
walikuwa wamelainishwa
na maneno hayo, katu
wasifahamu kuwa
nchini Marekani hakuna
dawa bure, hospitali
bure, nyumba ya kuishi
bure, elimu bure na
chakula bure, ila pale
watu wakipiga magoti
au kwenda kuunda
milolongo mirefu kupata
supu.
Hapana, hata
ningefanyaje, haikuwa
inatosha katu kwa baadhi
ya watu, lakini kwa
wengine, walifahamu
kuwa mimi ni mwana
wa Gamal Abdel Nasser,
kiongozi pekee wa
Kiarabu na Kiislamu
ambaye tumekuwa
naye tangu Salahuddin,
alipoutaka mfereji wa
Suez kwa watu wake,
kama nilivyoitaka Libya,
kwa watu wangu, ilikuwa
ni nyayo zake nilizojaribu
kufuata, kuwaweka
watu wangu huru na
kudhibitiwa na wakoloni
- kutoka kwa wezi ambao
wangetuibia.
Sasa nashambuliwa
na jeshi kubwa zaidi
katika historia ya vita,
mwanangu kijana wa
Afrika, Obama anataka
kuniua, kuuondoa
uhuru wa nchi yetu,
kuondoa ukazi bure
katika nyumba, tiba
bure, elimu bure, chakula
bure, kubadilisha na
kuweka wizi mtindo
wa Marekani, unaoitwa
'ubepari,' lakini sisi sote
katika nchi zinazoendelea
tunajua maana yake
Inaendelea Uk. 15

10

Makala

AN-NUUR

RABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 18-24, 2015

KKK waunda kikosi kuchinja Waislamu

U KLUX
KLAN
(KKK) kundi
ambalo
limeuwa zaidi ya
Wamarekani Weusi
2000, sasa limegeuzia
hasira zake kwa
Waislamu.
Kundi hilo katika
Jimbo la Alabama
limetoa ilani kuwa
linaandaa kikosi
cha kupambana na
Waislamu likilenga
kuzuiya Uislamu
kuenea Marekani.
Katika kutafuta
wanachama shujaa
wa kufanya kazi
hiyo, kundi hilo
limesambaza
vipeperushi vikitoa
wito kwa walio tayari
kujisajili.

Ni baada ya marufuku ya Donald


Matunda ya propaganza za chuki

KKK wakisimika Msalaba.

KKK akisoma maelekezo 'mwongozo


wao' KLOBAN.

The KKK wants


you! Help us fight the
spread of Islam in our
country. To join call
the hot line or visit our
website.

Ndivyo
unavyosomeka ujumbe
katika vipeperushi
ambavyo vimekuwa
vikisambazwa katika
mitaa na nyumba za
watu.
Chuki dhidi ya
Waislamu inaelezwa
kuwa kubwa sana
katika Marekani hasa
baada ya matukio
mawili ya hivi karibuni
yaliyodaiwa kuwa ya
kigaidi.
Matukio hayo ni
lile la Paris, Ufaransa
na San Bernardino,
California Marekani.
Katika matukio
yote mawili, ilidaiwa
kuwa kuna watu
waliuliwa na wauwaji
ni wanaodaiwa
kuwa magaidi wa IS
(Waislamu).
Sambamba na
tangazo hili la "the
Klan" anayetarajiwa
kuwa mgombea wa
urais kupitia chama cha
Republican, Donald
Trump anasema

WANACHAMA wa KKK na mavazi yao rasmi.


kuwa umefika wakati
poses, our country
Waislamu kupigwa
cannot be the victims
marufuku kuingia
of horrendous attacks
Marekani.
by people that believe
Trump anasema
only in Jihad and have
kuwa Waislamu
no sense of reason or
wamekuwa ni watu
respect for human life."
hatari wenye chuki
Anasema
isiyo na sababu dhidi
mfanyabiashara
ya Wamarekani na
billionea Donald
kwamba inakuwa
Trump akidai
vigumu kumtofautisha kuwa Marekani
haiwezi kukubali
ISIS na Muislamu wa
kuwa muhanga wa
kawaida.
"Until we are
mujahidina wenye
able to determine
chuki, wasiotumia akili
and understand this
wala kujali maisha ya
problem and the
binadamu.
dangerous threat it
Ku Klux Klan (KKK),

aka "the Klan", ni


kundi la Wazungu
wenye msimamo mkali
wanaoamini katika
ubora na utukufu
wa Wazungu (white
supremacy).
Kwa msimamo huo,
wanataka Marekani
isafishwe kutokana
na taka za Weusi,
Wahindi, Waarabu na
watu wengine wasio
kuwa Wazungu.
Mwanzo wake
ilikuwa kupinga
harakati za kupinga
utumwa na kuwapa
haki watu Weusi.

Hata hivyo, hasira


na chuki zilipelekwa
pia kwa Wayahudi
na Wakatoliki, hasa
wahamiaji wapya.
Kufikia mwaka 2012
ilikisiwa kwamba KKK
wana wanachama kati
ya 5,000 na 8,000.
Katika harakati zao
za kupinga haki sawa
pamoja na Wamarekani
Weusi, KKK walitumia
njia ya vitisho na
mauwaji, wakiuwa
viongozi wa harakati
za kupigania haki za
Weusi.
Kwa upande
mwingine, walikuwa
wakiuwa watu Weusi
tu bila ya sababu hata
kama sio kiongozi.
Walilipua mabasi
ya watoto wa shule
na kampasi za vyuo
vikuu vyenye idadi
kubwa ya watu Weusi
hasa katika Majimbo
na miji ya Pontiac,
Michigan, Louisiana,
Vanderbilt, Georgia,
Mississippi, na
Southern California.
Pamoja na mauwaji
ya kikatili ambayo
yamekuwa yakifanywa
na KKK, lakini hata
pale wanapokamatwa
watuhumiwa na
kesi kufikishwa
mahakamani, hutolewa
adhabu kidogo au hata
watuhumiwa kuachiwa
baada ya kuhukumiwa.
Mfano ni katika
Tennessee shooting
ambapo mwaka
1980, wanachama
watatu wa KKK
waliwapiga risasi na
kuwauwa wanawake
wanne, Wamarekani
Weusi Viola Ellison,
Lela Evans, Opal
Jackson na Katherine
Johnson katika mji
wa Chattanooga,
Tennessee.
Wawili katika
watuhumiwa, Bill
Church na Larry
Payne, waliachiwa
wakati Marshall Thrash

Inaendelea Uk. 11

11

Makala

AN-NUUR

RABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 18-24, 2015

KKK waunda kikosi kuchinja Waislamu


kuchoma moto msalaba
mbele ya nyumba yao
au katika eneo lenye

Inatoka Uk. 10

akitiwa hatiani na
kuhukumiwa kwenda
jela miezi 8 (kwa kosa
la kuuwa watu 4!!!).
Hata hivyo baada ya
kukaa jela kwa miezi
mitatu tu, aliachiwa
huru!
Kutokana na
malalamiko ya watu
juu ya mwenendo
huo wa kidhalimu na
mahakama kutokujali
haki za Weusi, mwaka
1982 mahakama
ilipitisha hukumu
kwamba itolewe
fidia ya Dola 535,000
kwa wale wanawake
waliouliwa.
Mwaka jana 2014
mwezi wa Aprili
mwanachama mmoja
wa KKK, Frazier Glenn

kukaa watu wasio


wataka.
Lakini inaelezwa
pia kuwa KKK wakati
mwingine wanatumia
njia mbaya ya kuuwa
kwa kuchoma moto.
Inakisiwa kwamba

WANACHAMA wapya wa KKK wakipata Darsa.


Cross, akijulikana
chuki (hate crime.)
washambuliaji na
pia kwa jila la Glenn
Inaelezwa kuwa
wauwaji hawa wa KKK
Miller alifyatua risasi
namna moja
wakipachikwa ugaidi.
katika kituo kimoja cha
wanayotumia KKK
Katika tukio hilo la
Wayahudi Kansasi City Kansasi polisi walisema kupeleka ujumbe
na kuuwa watu watatu. kuwa hilo ni kosa la
wa kitisho kwa watu
Hata hivyo, hutasikia jinai inayotokana na
wanaowalenga, ni

zaidi ya watu Weusi


400 wamechomwa
moto wakiwa hai na
KKK nchini Marekani
Sasa hawa ndio
Ku Klux Klan aka
The Klan ambao
wametangaza kuwa
sasa wanaandaa
kikosi maalum cha
kushughulika na
Uislamu na Waislamu.

(Habari na Mashirika ya
Habari ya Kimataifa)

Uhalifu wa kivita wa Israeli dhidi ya Palestina


MWAKA mmoja uliopita
waziri katika Mamlaka
ya Palestina, Ziad Abu
Ein, aliuawa na vikosi
vya Israeli, kufuatia
kipigo na kuvuta hewa
chafu iliyosababishwa
na mabomu ya machozi
wakati wa maandamano
katika eneo la Ukingo
wa Magharibi nchini
Palestina.
Abu Ein aliyekuwa
na umri wa miaka 55,
alikuwa akiongoza
kundi la Wapalestina
katika kupanda miti ya
Mizeituni, karibu na kijiji
cha Turmusayya Kaskazini
Mashariki mwa mji wa
Ramallah, alishambuliwa
na askari wa Israeli na
kupelekea kifo chake
mnamo Desemba 10, 2014.
Abdullah Aburahmah
ambae ni mwanaharakati
wa kipalestina akiwa ni
mmoja wa waandamanaji
hao, aliwaambia waandishi
wa habari kwamba Abu
Ein akaanguka baada ya
kukosa fahamu, kufuatia
afisa wa usalama wa Israeli
kumpiga kwa kofia yake
ya kujikinga ijulikanayo
kwa jina la Helmet.
" Ya l i k u wa
ni
maandamano ya amani;
askari wa Israel hawajui
jinsi ya kukabiliana na
hali kama hiyo,jambo
lililowafanya kutumia

nguvu kututisha" alisema.


Mashahidi wa tukio
hilo akiwemo mwandishi
wa habari wa Israel na
mpiga picha wa shirika
la habari la Reuters,
alisema Abu Ein alipigwa
na wanajeshi wa Israeli
wakati wa maandamano,
huku wengine wakisema
alipigwa kichwani na
kuanguka.
Wakati wote huo wa hali
tete, ulinzi uliimarishwa
zaidi nchini Israeli na katika
makazi ya walowezi wa
kiisraeli nchini Palestina,
huku maandamano
yakiendelea katika ukingo
wa Magharibi kwa wiki
kadhaa.
Aidha Abu Ein, alikuwa
ni baba wa watoto wanne
na Mwenyekiti wa Tume
ya Kupambana na ukuta
wa kibaguzi na Makazi ya
kilowezi nchini Palestina,
vilevile aliwahi kushika
wadhifa wa Naibu Waziri
wa Mambo ya wafungwa
wa kipalestina.
Alihukumiwa kifungo
cha maisha jela na Israeli
mnamo mwaka 1982,
lakini alitolewa katika
zoezi la kubadilishana
wafungwa mnamo mwaka
1985, hatimae kuwa
mwanachama wa Baraza
la Mapinduzi la chama
cha Fatah.
Wanaharakati

waliokuwa pamoja Abu


E i n wa l i s e m a k u wa .
Walikuwa wakipanda
miti ya mizeituni katika
makazi haramu ya Adey,
wakati ndipo maafisa wa
jeshi la Israeli walipotu
tushambulia kwa kiasi

kikubwa cha mabomu ya


machozi.
Rais wa Palestina
Mahmoud Abbas amelaani
vikali mauaji ya Abu Ein,
na kukiita kuwa ni "kitendo
cha kinyama ambacho
hakiwezi kuvumiliwa",

huku akiishutumu Israeli


kwa mauaji hayo ya waziri
wa k e . N a e M k u u wa
Upatanishi wa Palestina
Saeb Erekat amelaani kile
alichokiita "mauaji."
Amesema Serikali ya
Inaendelea Uk. 18

12

Safu ya Ben Rijal

AN-NUUR

RABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 18-24, 2015

Ijue Bunduki ya AK 47 na athari zake -2


Nani mbunifu wa AK-47 au tuite Kalashnikov?

BUNDUKI ya Kalashnikov
au kwa jina jengine kwa
ufupi huitwa AK-47 ni
bunduki ilio mjarab na
ndio bunduki inayotumiwa
sehemu nyingi duniani
kutokana na ubora wake.
Wengi hatujiulizi ni nani
ambaye alibuni bunduki
hii na sababu gani
zilizompelekea afanye
hivyo?
Alikuwa Mikhail
Kalashnikov mwanajeshi
wa Kirusi ambaye ndio
alioiasisi bunduki hii, na
kilichompelekea kuiunda
bunduki hii ni kule
kujeruhiwa kwake kwenye
vita na kumpitikia kuwa
aina ya bunduki ambayo
jeshi la Urusi wanazozitumia
ni dhaifu. Akiwa anauguza
jereha la bega kutokana na
risasi aliyopigwa, Mikhail
Kalashnikov alikuwa
akifikiria vipi ataweza

MIKHAIL Kalashnikov mtengenezaji na mvumbuzi wa


bunduki AK47.

kuiunda bunduki hiyo,


ilimchukuwa muda wa
miaka 6 kuweza kufikia
ukomo wa kuunda silaha hii.
Mik h ail K alash nik o v
alikuwa mwenye majuto
siku zake za mwisho wa
maisha yake ingawa mwanzo
alijilabu kuwa wakulaumiwa
ni wanasiasa lakini katika
siku zake za mwisho wa
maisha yake kabla ya kufariki
alifika kunena yafwatayo
Wakati nikitengeneza silaha
hiyo, lengo langu halikuwa
kuua mtu, bali ilikuwa
kulinda taifa langu. Kama
baadaye imeanza kutumiwa
na magaidi kuua watu, hilo

halikuwa lengo langu.


I l i k u wa k i l a s i k u ya
Mungu anaposikia habari
au anavyotizama habari
huona mauaji katika sehemu
mbalimbali za dunia ambayo
mauaji hayo yamefanyika
kutokana na matumzi ya
AK-47.
"Hata hivyo, kusema
ukweli ningefurahi zaidi
kama ningeweza kubuni
kifaa ambacho kingetumiwa
na wakulima kwa namna ile
ile ambayo AK 47 imetumika
duniani kote. pengine kwa
namna hiyo ningeisaidia
zaidi dunia. Alisema.

Kitu kimoja ambacho


kinaipa ubora bunduki
hii ni silaha unayoweza
kuisafisha kwa muda mfupi
kuliko silaha nyingi kwahio
haihitaji gharama kubwa
katika usafishaji na kuifanyia
matengenezo.
Aliwahi kusikika mara
mmoja Mikhail Kalashnikov
akisema kuwa AK 47 si
silaha bora kuliko zote
zilizowahi kutengenezwa na
kuwa ana imani ya kuwa ipo
siku, itakuja silaha nyingine
kubwa kuliko hiyo.
U n a p o ya s o m a m a n e n o
na misemo mingi ambayo
Mikhail Kalashnikov
aliokuwa akiyatamka ni
utaona alikuwa anajutia
k wa n i n i a m e t e n g e n e z a
silaha hio.
Jee Mikhail Kalashnikov
amefaidika na uvumbuzi wake?
Majaribio yake ya silaha
hii, ilimtia maradhi ya
uziwi pamoja na majirani
waliokuwa wakiishi karibu
naye. Uziwi ulimpa tabu
na hakuwa anapendelea
kutumia chombo cha
kumsaidia kusikia. Akiona
bora umsemeshe kwa
kumsogelea karibu na shikio
na kisha ukapiga makelele.
Wajuzi kama hawa ndio
huwa na mambo ya kiajabu
ajabu. Uvumbuzi wake
haukumtarajirisha zaidi ya
kupewa tunzo za juu kwa

nchi yake.
Bunduki iliyoua marais
wengi
Bunduki hii haikumwacha
wa l a k u m b a g u wa i w e
Rais au mwananchi wa
k a wa i d a k a t i k a k u l e t a
athari zake. Katika mwaka
wa 1981 Rais Anwar
Saadat akiwa anapokea
gwaride la heshima, askari
wa jeshi la Misri ambao
wakifwata misimamo
thabiti walichupa kwenye
gari yao nakufika kwenye
jukwaa na kummiminia
risasi Rais Anwar Saadat
na kufariki hapo hapo.
Mwaka wa 1972 Kapteni wa
Jeshi la Wananchi, Homoud
Barwany naye aliitumia
bunduki hii kumuua Rais
wa mwanzo wa Zanzibar
baada ya Mapinduz Abeid
Amani Karumei. Aidha
mwaka uliofwatia mwaka
wa 1973 Rais wa Cape
Verde, Amilcar Cabral naye
alikuwa ni muhanga wa
AK-47. Mwaka huo huo Rais
wa Chile, Salvador Allende
aliuwawa kwa bunduki ya
AK-47.
Msomaji wa makala hii
unamuhukumu vipi Mikhail
Kalashnikov? Unaweza
ukamwita shujaa au subiyani
aliochangia na kuendelea
kuchangia kupotea kwa roho
nyingi za watu duniani aidha
na kupatikana vilema wengi
kutokana na matumizi ya
bunduki alioiasisi?

Sheikh Abdul Aziz bin Abdul Ghany Al-Amawy na Sheikh Fadhil bin Ali Mngazija-8
SHEIKH Abdul Aziz bin
Abdul Ghany Al-Amawy
alizaliwa Barawa tarehe
15 Mfungo sita mwaka
wa 1250 (1854) akafika
Unguja akiwa kijana
mdogo kabisa. Ingawa
aliwasili visiwani
humu akiwa ni kijana
mdogo, lakini alikuwa
ameshajifunza vitabu
vingi vya dini na lugha
ya Kiarabu na kuweza
kuwa na maarifa mapana
katika uga wa dini na
lugha.
Huko alikotokea
alijifunza kwa maulamaa
wakubwa wa nyakati
hizo katika maeneo ya
Barawa akiwemo Syd
Abubakar Mihdhar,
Sheikh Haji Ali bin
Abdulrahman. Aidha
alisoma kwa Sheikh
Ahmad Al-Madhriby.
Inaelezwa kuwa Sheikh
Abdul Aziz bin Abdul
Ghany Al-Amawy
alikuwa ni kiongozi wa
dhikiri yeye na Sheikh

KATIKA makala ya mwanzo ya Masheikhe waliopita


visiwani, nilimuandika Sheikh Muhydin bin Sheikh
ambaye alikuwa mmoja kati ya wasomi wakubwa
waliopata kukuwepo Zanzibar. Katika makala hii ya
leo, nitawazungumzia wanafunzi wake wawili kati
ya wanafunzi wake wengi aliowasomesha na kufanya
kazi kubwa ya kueneza dini nao ni Sheikh Abdul Aziz
bin Abdul Ghany Al-Amawy na Sheikh Fadhil bin
Ali Mngazija.
Sahuri Al-Shirazi wa
Donge. Masheikhe hawa
wawili baada ya kuwa
na wanafunzi wengi
katika kuwafunza elimu
ya dini, waliigeukia
dhikiri na humu kwenye
dhikiri wakitumia nafasi
ya kusomesha Fiqhi.
Alioweza kumshajiisha
Sheikh Abdul Aziz bin
Abdul Ghany Al-Amawy
kuivamia dhikri na
kuzama alikuwa Syd
Ahmad Al-Madhriby.
Baada ya kuondoka
kwao Barawa na kuwasili
Unguja, alifikia mikononi
mwa Sheikh Muhydin
bin Sheikh akasoma

hapo kwa muda mrefu


na kuelimika vya
kutosha. Sheikh Abdul
Aziz bin Abdul Ghany
Al-Amawy inasemekana
kuwa katika masuala ya
Sheria na Hukumu za
Kiislamu alikuwa gwiji
na alikuwa mwenye
kujuwa lipi ndilo na lipi
alipeleke kwenye kiasi.
Alipofika umr wa
miaka 16 Abdul Aziz bin
Abdul Ghany Al-Amawy
alikuwa ameshailimika
vya kutosha na hapo
Sheikh Muhydin
alivyomuona kuwa umri
wake ni mdogo lakini
upeo wa elimu yake

ni mpan, akamchagua
katika wanafunzi wake
kumpeleka Kilwa
kuongoza masala
ya dini. Watu wa
Kilwa walimpokea
na hawakuona wala
kumjadili juu ya umri
wake lakini walimkubali
kutokana na uwezo
wa elimu yake. Sheikh
Abdul Aziz alikubalika
vya kutosha na darsa
zake zilikuwa kubwa na
zikitajika hapo Kilwa.
Sheikh Abdul Aziz
aliandika vitabu vingi
lakini bahati mbaya
vitabu vyake hivyo vyote
havijulikani vimepotelea
wapi, isipokuwa vitabu
viwili kimoja kati ya
hivyo kilikuwa na
anuwani An Nawamisis-Samadaniya kikiwa ni
kitabu cha Dua ambacho
alikiandika mwaka
wa 1280 AH (1863).
Aidha kwa watoto wake
kilipatikana kitabu cha
Tawhidi alichokimaliza

kukiandika katika
mwaka wa 1883. Kitabu
hiki alikiita Ikdul-Laali ambacho baadaye
akakifanyia sherehe
na kuita Sherehe hio
jina la Takrib Ikdi
La-ali. Inasemekana
kuwa aliandika kitabu
juu wa wafalme wa
Kibusaidi wa Zanzibar
na kilipata kuonekana na
alikiandika kwa ufundi
mkubwa kabisa nacho
kitabu hicho hakijulikani
kilipotelea wapi? Aidha
kulikuwa na mijadala
yake na Mapadri ambayo
wengi walifaidika katika
hoja zake alizokuwa
anapambana na Mapdri.
Bahati mbaya maandiko
aliyoyafanya na kuwa
kitabu nayo yamepotea.
Zanzibar ilibahatika
kuwa na Mapadri
3 ambao waliisoma
dini ya Kiislamu na
kuielewa vya kutosha
na ukitaka kupambana
Inaendelea Uk. 13

13

Safu ya Ben Rijal

AN-NUUR

RABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 18-24, 2015

Sheikh Abdul Aziz bin Abdul Ghany Al-Amawy na Sheikh Fadhil bin Ali Mngazija-8

Inatoka Uk. 12
nao ilikuwa sio rahisi.
Mapadri hao walikuwa
Bishop Tozer, Bishop
Steere na Padre Dale.
Kati ya hao wote Bishop
Tozer akiwaadhibu sana
Masheikhe ila alikuwa
hapendi kukutana na
Sheikh Abdul Aziz.
Bishop Tozer aliwahi
kusikika akisema kuwa
Wangekuwa Abdul Aziz
bin Abdul Ghany AlAmawy wachache katika
kisiwa cha Zanzibar,
kazi yetu ingekuwa
haifanyiki.
Dhikiri ilikuja ikamvaa
akawa saa zote yeye na
muridi na akiwasomesha
Muridi zaidi ya
Tasawuf na Tawhidi
na wanafunzi wake
walikuwa wakimfwata na
kuwa naye kwa karibu.
Wengine wanasema
lau kama asingegeukia
Dhikiri, basi Sheikh
Abdul Aziz angeweza
kupaa zaidi alivyopaa.
Sheikh Fadhil bin Ali
Mngazija
Sheikh Fadhil bin Ali
Mngazija ni mzaliwa
wa visiwa vya Ngazija
na alipowasili Unguja
hajasimama ila alifikia
kwa Sheikh Muhydin
bin Sheikh, na alikuwa
mmoja kati ya wanafunzi
waliokuwa wakisoma
kwa jitihada ya hali
ya juu na kutopoteza
wakati wake bure.
Alikuwa akisoma
darasa za vijana wa
hirimu yake na vilevile
alikuwa akijumuika
katika darasa za watu
wazima. Natija ya juhudi
zake zilimpelekea kwa
kipindi kifupi kuonekana
kama ni mwanachuoni
aliobobea. Alipofariki
Sheikhe wake alikuwa
na darsa kubwa ambazo
zikihudhuriwa na
wengi wa wakaazi
wa mjini Unguja na
kuonekana Sheikh
Muhydin kilichoondoka
ni kiwiliwili chake lakini
ilimu alioisomesha
ilikuwa haikupotea.
Sheikh Fadhil alikuwa
akisomesha darasa zake
katika Msikiti Gofu na
akikaa kando na Msikiti
Gofu. Kwa hio saa zote
yeye alikuwa na Msikiti
na Msikiti kuwa na
yeye kutokana na kuwa
anaishi pembezoni

mwa Msikiti Gofu.


Aliweza kuwavutia wale
wanafunzi wa Sheikhe
wake kuhamia katika
darasa zake kati ya hao
ni Syd Muhammad
bin Ahmad bin Salim,
Syd Ahmad bin Salim,
Sheikh Abdalla bin
Wazir ambaye naye
alikuwa kati ya wasomi
walioisoma Bibilia vya
kutosha na akipenda
kuendesha mijadala
na Mapadri hata watu
wakimstaajabu. Mapadri
wa Kizungu walioletwa
miaka hiyo walikuwa
wamebobea katika lugha
ya Kiarabu na mafuzo
dini ya Kiislamu kwa
jumla na walikuwa
wakipenda kuwafwata
Masheikhe kwa mijadala,
lakini kinyume chake,
Sheikh Sheikh Abdalla
bin Wazir akiwafwata
wao na ikisemekana mara
nyingi wakimkwepa
kwani alikuwa na
lugha ya kejeli nakuwa
tayari kufanya mijadala
hata kwa siku nzima.
Alipokuwa anakwenda
kufanya mijadala watu
wakipenda kumfwata
kusikiliza namna
alivyokua akijadiliana
nao. Alikuwa na ufundi
wa kucheza na lugha ya
Kiarabu na Kiengereza
ambao haikuwa rahisi
kwa masheikhe wa siku
hizo kuwa na kuzimudu
lugha mbili hizo.
Katika zama za Syd
Barghash kulitokea
ugomvi mkubwa baina
ya wakazi wenye asili
ya visiwa vya Comoro
ambao walikuwa
wakiishi Unguja na
kujigawa katika mapande
mawili nayo Inyamwatsa
Pirusa na Inya
Fuambaa. Hakuwa
Mngazija alioishi
visiwani kutokuwa
kwenye mmoja wa
mrengo huo ulioingia
katika malumbano na
kuwa na baa na belwa.
Vijana wanaotokana na
wazee waliotoka katika
visiwa vya Comoro
walikuwa na Sheikh
Fadhil na walikuwa
wanataka mabadiliko
na kuwataka wazee
wao waache kufwata
utamaduni na wafwate
misingi halisi ya dini
ilivyo. Sheikh Fadhil
alijitenga na makundi
hayo yote mawili
Kati ya wale

waliokuwa wakijiweza na
kina enhe kati ya wakazi
wa Kingazija waliokuwa
wakiishi Zanzibar
walikuwa karibu na Syd
Barghash na walikuwa
wakihudhuria majlisi
yake kwa hio wakapata
fursa ya kumchongea
Sheikh Fadhil kuwa ni
mwanaharakati anayoleta
fitna katika mji, kwa
lugha ya leo angeitwa
Muislamu mwenye
siasa kali. Sheikh
Fadhil mawazo yake na
alivyokuwa fasaha kwa
kuelezea Uislamu na
tarekhe yake uliwavutia
wengi na kuwa kama
tishio kwa watawala kwa
hivyo naye akapewa
Persona non Grata
na kuwa Prohibited
Immigrant yaani
mhamiaji asiotakiwa
na kupakiwa meli na
kurejeshwa Comoro.
Ilikuwa ni pigo kwa
wakazi wa Unguja lakini

ndio tuseme lilokuwa


liwe haliwezi kuwa
lisiwe.
Baada ya kuwasili
kwake Comoro wakaazi
wa Moroni walifarajika
na akawa anasomesha
darsa mbalimbali.
Aliuwona mji wa Moroni
upo karibu na Unguja
akajihisi fitna zitaendelea
kumwandama kwa
hio akahama Moroni
mji mkuu akaelekea
Ndzuwani ambako
alipofika tu akapewa
Ukadhi na alikuwa
kila mmoja katika mji
akihakikisha kisima
hicho kilicho na kina
kirefu na kilicho jaa maji
yasiokauka, ni vyema
kwenda kuchota maji
yaani elimu.
Sheikh Fadhil alifunga
macho mwaka wa 1302
(1885) na kuwacha pengo
kubwa lilokuja kuzibwa
baada ya miaka mingi
kupita.

Sheikh Fadhil akipenda


kuona kuwa kuna umoja
wa Waislamu na kupinga
kwa nguvu zake zote
za watu kugawanyika
na alikuwa akisimamia
vilivyo miongozo ya
Quran na Suna za
Mtume Muhammad
(SAW). Yaliomkuta
Sheikh Fadhil ni yale
kwa yale yanakwenda
na kujirejea hadi hii leo.
Fitina wanazozipika
Waislamu kutokana
na tafauti baina yao,
zinarindima na kufanya
kuwa Waislamu siku
zote wapo katika Misuko
suko.
Tumuombe Allah atupe
fahamu za masheikhe
kama Sheikh Fadhi na
atupe misimamo kama
aliyokuwa nayo ya kuona
Umoja wa Kiislamu
unasimama siku zote,
Ameen.
(Kwa mawasiliano,
maoni, maswali tumia
namba 0777436949)

Inatoka Uk. 8

hiki utakipata vizuri katika,


Mw.34:1-35.
Huyo ndiye Israeli, babu
wa wana wa Israeli. Huo ni
mfano mmoja tu wa majirani
wa Israeli (Yakobo) alivyo
ishi nao. Sasa ili tuone jinsi
Biblia ilivyo watukuza wana
wa Israeli; tuone wosia
(wasia-usia) Yakobo aliowaachia wanawe. Biblia ya
mwaka wa 1937, imeanza
kwa kichwa cha habari:
Yakobo ana wabariki wanawe
wote, Biblia ya Imprimatur,
imeanza na Mibaraka ya
Yakobo. Kulingana na urefu
wa hiyo mibaraka, nitanukuu
sehemu, na msomaji akitaka
kuiona yote nitaonesha aya
zote; Biblia ninayotumia ni
toleo la Union version.
Yakobo akawaita wanawe
, akasema, Kusanyikeni ili
niwaambie yatakayowapata
siku za mwisho. Kusanyikeni,
msikie, enyi wana wa Yakobo,
Msikilizeni Israeli, baba yenu.
Reubeni, u mzaliwa wangu
wa kwanza, Nguvu zangu,
na milimbuko ya uwezo
wangu. Umewapita wengine
kwa ukuu na kwa nguvu.
Umeruka mpaka kama maji,
basi usiwe na ukuu, Kwa
sababu ulikipanda kitanda
cha baba yako, Ukakitia
unajisi; alikipanda kitanda
changu. (Mw.49:1-4.)
Reubeni, alizini na mama
yake, mama mdogo, mke wa
nne wa Yakobo, aliyeitwa
Bilha; sasa hiyo ni mibaraka?
Ikawa Israeli, alipokuwa
akikaa nchi ile, Reubeni

akaenda akalala na Bilha,


suria wa babaye; Israeli
akasikia habari. (Mw. 35:22.)
H a t a h i v y o Ya k o b o
hakusema kitu; kusema kwake
ni huko akitoa mibaraka,
hata hivyo waandishi wa
Biblia za nyuma hata hii
ninayonukuu, hawakuwa na
hiyana; waliweka rejea hivi:
Na alaaniwe alalaye na
mke wa baba yake, kwa kuwa
amefunua mavazi ya babaye.
Na waseme, Amina. (Kumb
27:20; Nyakati 5:1.)
Sasa hiyo ndiyo mibaraka;
nilisema hapo juu kuwa,
kwa wana wa Israeli na
wale wanaowatukuza, kwao
haramu inakuwa halali na
halali inakuwa haramu.
U k i s o m a B i b l i a k wa
mtazamo huru; bila
kuegemea upande, hutaweza
kumwamini mfuasi wa dini
ya Kiyahudi na ya Kikristo
anapokwambia kuwa ana
hubiri amani katika nchi
anakoishi; au katika dunia hii.
Ukimwona anayezungumzia
amani, hiyo ni katika ulimi, si
katika imani iliyofundishwa
n a wa a s i s i wa d i n i ya
Kiyahudi. Ukitaka kujua hilo
soma Biblia, kuanzia kitabu
cha mwanzo mpaka mwisho
wa ufunuo wa Yohana, alafu
weka mizani ya amani na
vita jinsi ilivyofundishwa
na kusisitizwa, utakuta
k u wa h a ya m a c h a f u k o
tunayoyaona hapa duniani
yanatokaka na mafundisho
yaliyoasisiwa na wana wa
Israeli wakishirikiana na
watawala wa enzi hizo na
hizi.

Khabari ya Israel Taifa teule-4


naye, asubuhi akamwambia
baba yake, kuwa,
amempenda binti huyo hivyo
anapenda awe mkewe; baba
yake akamwendea Yakobo,
akamweleza habari ya binti
huyo kuolewa na kijana
wake, hata hiyo Yakobo
a k a m wa m b i a a n a s u b i r i
wa t o t o wa k e wa j e , n a
walipokuja wakamwambia
Yakobo baba yao kuwa
dada yao amefanyiwa
vibaya, wakafanya hila na
babayao, wakamwambia
yule mfalme kuwa, akitaka
kuwa mwanawe amwoe Dina
akubali kuwa raiya zake
wanaume wote watahiriwe
maana binti yake hataolewa
na mume mwenye govi
(zunga). Hamori Mhivi
akamwambia Yakobo kuwa
kuliko mwanawe akose
kumwoa Dina amekubaliana
na kutahiriwa raiya zake
nayeye mwenyewe.
Akaitisha kikao cha raiya
z a k e a k a wa e l e z e a , n a o
wakakubali, wakatahiriwa
siku moja wote; watoto wa
Yakobo wakasubiri siku tatu,
wakijua kuwa vidonda vya
tohara vimefikia upeo wa
maumivu wakawavamia
wanaume wote wakawauwa
pamoja na yule mvulana
na baba yake; na waka
wachukua wanawake na
watoto na mali zote na
kuteketeza makazi yao yote.
Na baada ya hapo mungu
wa Israeli wakawapongeza
na kuzidi kuwabariki. Kisa

14

MAKALA/MASHAIRI

TUSOMENI AN-NUUR (1)


Mhariri muadhamu, nipokee hodi hodi,
Janibu japo nikumu, ya gazetilo suudi,
Ndaniye abra nikimu, nitoe wito saidi,
Kwa habari zenye nuru, tusomeni AN-NUUR.
Naibtadi nudhumu, kwa Allah kumhimidi,
Thuma swala na salamu, kwa rasuli Muhammadi,
Kadhalika taadhimu, kwa swahaba murshidi,
Kwa habari zenye nuru, tusomeni AN-NUUR.
Baada ya taadhimu, sina budi kulinadi,
Gazeti letu adhimu, ndani lenye irishadi,
Kadhalika taalimu, na mzomzo suudi,
Kwa habari zenye nuru, tusomeni AN-NUUR.
Limesimama kawimu, pamwe na kutabaradi,
Lengole hasa ikumu, ya Ilahi Tauhidi,
Na zende zote kuzimu, za rajimu itikadi,
Kwa habari zenye nuru, tusomeni AN-NUUR.

ABUU NYAMKOMOGI,
MWANZA.

TULIDURUSU IMAAN (1)

Wito nakutoleeni, kuhusu letu IMANI,


Gazeti jipya makini, kwa ya dunia na dini,
Kwa sasa li mitaani, shime na tulisomeni,
Tulidurusu IMANI, kwa habari za yakini.
ARUSHA nakuiteni, pamwe na zenu jirani,
Wito uzingatieni, na MANYARA wajuzeni,
Na KILIMANJARO ndani, na TANGA waubaini,
Tulidurusu IMANI, kwa habari za yakini.
DAR ninakuiteni, pamwe na zenu jirani,
Wito uzingatieni, kikoa MORO na PWANI,
Muwe pamoja safuni, kwa kulisoma
IMANI,
Tulidurusu IMANI, kwa habari za yakini.
GEITA nakuiteni, pamwe na zenu jirani,
Wito uzingatieni, SIMIYU ufikisheni,
Na SHINYANGA mkoani, lipate somwa IMANI,
Tulidurusu IMANI, kwa habari za yakini.

ABUU NYAMKOMOGI,
MWANZA

AN-NUUR

RABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 18-24, 2015

Jihadi ni kwa ajili ya kukinga


uadui katika dini sio kuua
wanaokupigeni.
Akasema hii ni
aya ya mwanzo
iliyoteremshwa
k atika vit a hapo
Madina na pale
ilipoteremshwa,
alikuwa Mtume
(s.a.w) akipigana na
yule anayepigana
naye na al i kuwa
hapigani na yule
asiyepigana naye
Na Sheikh Mohamed
hadi ilipoteremshwa
al- Amiri Othmani
Surat Bakaratu.
Ta f s i r i ya A b i i
WA h a k i k a
Suudi,
na piganeni
Uislam pale
ulipoweka k a t i k a n j i a ya
sheria ya vita na Mwenyezi Mungu
jihadi imewekwa kwa maana piganeni
k w a a j i l i y a kwa ajili ya kushinda
k u k i n g a u a d u i dini yake Mwenyezi
ambao utatokea na Mungu na kutangaza
kupigana na wale neno lake, ni kwa
ambao wanaopigana k u t a n g u l i a j u u
na waislam na wala ya mtendewa wa
haikuletwa kwa ajili wazi kwa ajili ya
ya kuwaua wanao kuonyesha ukamilifu
mambo
tofautiana katika k w a
dini na maoni ya k u t a n g u l i a
au kutofautiana w a l e a m b a o
wanaokupigeni
madhehebu.
A n a s e m a nyinyi maana
Mwenyezi Mungu yake ambao wanao
m t u k u f u , N a kuchokozeni kwa
piganeni katika vita na kuweza
njia ya Mwenyezi k u s i m a m i s h a
M u n g u n a wa l e v i t a h i v y o wa t u
w a n a o k u p i g e n i wasiokuwa nyinyi
wala msipindukie miongoni mwa watu
mipaka mkawapiga wazima na vijana
w a s i o k u p i g e n i na viongozi wa dini
kwani Mwenyezi na wanawake wala
Mungu hawapendi msivuke mipaka
warukao mipaka kwa kudhihirisha
( 1 9 0 ) S u r a t u l vita au kwa kupigana
Bakarat.
A m e s e m a I b n na wanaoishi kwa
k at hir i ames ema m k a t a b a n a k wa
Abuu Jafari Razi njia ya ghafla bila
toka kwa Rabi Bin ya k u wa l i n g a n i a
A n a s i t o k a k wa au kwa kisasi na
A b i - A l - A a l i ya pia haifai kuwaua
katika kauli yake wale mliokatazwa
Mwenyezi Mungu, kuwaua miongoni
Na piganeni katika m w a w a n a w a k e
njia ya Mwenyezi na watoto na wale
M u n g u n a wa l e wanofanana na wao.

Hakika Mwenyezi
Mungu h awapendi

wavukao mipaka kwa


maana ya kwamba
hataki kwao nako ni
kutiia ila katazo na
inabainisha aya hii
kwamba lengo la vita
katika Uislam katika
mambo yafuatayo:(1) Kuzuia uadui
na kuondoa madhara
ya nafsi
(2) K u i n u s u r u
haki na uadilifu pia
kunainisha kwamba
miongoni mwa sharti
ni vidhibiti vita.
(1) K u b a i n i s h a
uzuri wa vitendea kazi
na lengo
(2) H a i r u h u s i w i
kupigana nae
isipokuwa Yule
anayepigana na wewe
na hakuna uadui kwa
wanaofanya ibada
pia inabainika kwetu
kwamba jihadi katika
uislam imekaa vizuri
mwisho wake na
vitendea kazi kwa
pamoja na tunafupisha
athari hizi katika nukta
zifuatazo:(1) K u i l e a n a f s i
katika kujitolea
(2) Kukubali uadilifu
na uhuru kwa watu wote
kwa imani zao zote
(3) K u t a n g u l i z a
hukumu kuu kuliko
maslahi maalum ya
mtu mmoja hakika yale
y anayotokea katika

ulimwengu wetu
wa kiislam ni sasa
kutokana na ufahamu
uliochanganyika juu ya

maana ya vita na jihadi


na kuteremshwa kwa
aya hizi kwa waislam
wanaotofautiana maoni
huo ni upotevu wa

wa z i h u p o r o m o k a
kwa mwenye fikra hizi
mbovu na kuteketea,
t u n a m u o m b a
M we n ye z i M u n g u
amani na ufahamu
mzuri katika dini yake.

15

MAKALA

AN-NUUR

RABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 18-24, 2015

Mauaji na majanga Mashariki ya Kati


Inatoka Uk. 9

ni nini. Ina maana


makampuni au mashirika
makubwa yanaendesha
nchi, yanaendesha dunia,
na watu wanataabika.
Hivyo hakuna mbadala
kwangu, lazima nichukue
msimamo. na Allah
akipenda, nitakufa kwa
kufuata njia Yake, njia
ambayo imefanya nchi
yetu kuwa na utajiri wa
maeneo ya kilimo, kwa
chakula na afya, na hata
kuturuhusu kuwasaidia
ndugu zetu na dada zetu
wa Afrika na Uarabuni
kufanya kazi pamoja
nasi, katika Jamahiriya ya
Libya.
Sipendelei kufa, lakini
kama itafikia hapo,
kuiokoa nchi hii, watu
wangu, wale maelfu
ambao wote ni wanangu,
basi iwe hivyo.
Agano hili liwe sauti
yangu kwa dunia,
kuwa nilisimama dhidi
ya mashambulio ya
makruseda wa NATO,
nilisimama dhidi ya
ukatili, nilisimama dhidi
ya usaliti, nilisimama
dhidi ya nchi za
Magharibi na dhamira
zake za kikoloni, na
kuwa nilisimama pamoja
na ndugu zangu wa
Kiafrika, ndugu zangu
wa kweli wa Kiarabu na
Kiislamu, kama mhimili
wa mwanga.
Wakati wengine
wakijenga majumba ya
kifahari, niliishi katika
nyumba ya kawaida, na
katika hema. Sikuwahi
kusahau ujana wangu
katika mji wa Sirte,
sikutumia hazina
ya nchi kipuuzi, na
kama Salahuddin,
kiongozi wetu shujaa
wa Kiislamu, ambaye
aliiokoa Yerusalemu kwa
Uislamu, nilichukua
kidogo sana kwa ajili
yangu mwenyewe.
Katika nchi za
Magharibi, baadhi
wameniita 'kichaa,'
'hamnazo,' lakini
wanajua ukweli na
wanaendelea kusema
uwongo, wanajua kuwa
ardhi yetu iko huru,
haiko katika makucha ya
ukoloni, kuwa taswira
yangu, njia yangu, na
imekuwa wazi na kwa
watu wangu na ambayo
nitaipigania hadi pumzi
yangu ya mwisho
kutubakiza huru, Allah
Suhanna atusaidie kubaki
na imani, na huru.
(Mwisho wa kunukuu.)
Uhalifu mkubwa wa
Gaddafi ni kuwa anatoa
sehemu kubwa mno ya

MAREHEMU Kanali Muammar Gaddafi.


utajiri wa mafuta kwa
watu wake. Alikuwa
mtu wa mabavu? Ndiyo,
ila inabidi uwe hivyo ili
utawale katika eneo lile
hivi sasa. Alikuwa ndiyo
mtu mbaya zaidi wa
mabavu? Hapana, hata
kwa udi na uvumba.
Awe mbaya
alivyokuwa, hakuua waIrak milioni moja kwa
tuhuma za kutengeneza
za silaha za maangamizi
ambazo hazikuwepo.
Wala hakuwa anakata
vichwa 50 kila wiki na
kupiga mawe hadi kufa
wanawake kwa kuzini
kama ilivyo kwa Saudia
hivi sasa.
Lakini pia, kama
aliua waandamanaji
au hapana, au alifanya
uhalifu wa kivita au
hapana, haina umuhimu
kwa wanaohodhi
mamlaka. Cha msingi ni
kuwa alikuwa amezuia
nchi za Magharibi
kupata maslahi yao, na
badala yake akatumia
utajiri wa mafuta wa
nchi yake kutoa bure au
kwa malipo kidogo sana
tiba , elimu na nyumba
kwa sehemu kubwa ya
wananchi wa Libya.
Hivyo, twende sasa
kuona mauaji yake. Hivi
ndivyo ilivyokuwa:
Majira ya saa mbili
asubuhi saa za Libya
hapo Oktoba 20,
Gaddafi na mkuu wake
wa majeshi Abubakr
Yunus Jabir, mkuu wake
wa usalama Mansour
Dhao, na kundi la askari
wanaoumuunga mkono
walijaribu kutoroka
kwa kutumia magari
75. Ndege ya kivita ya
upelelezi ya Uingereza
iliona msafara huo
ukienda kwa kasi kubwa,
baada ya majeshi ya
NATO kudaka simu ya

satellite iliyopigwa na
Gaddafi.
Ndege za NATO
zilipiga magari 11,
zikateketeza moja.
Ndege ya kivita ya
Marekani isiyo na rubani,
Predator ikiongozwa
kutoka boma la kijeshi
karibu na Las Vegas,
ilipiga makombora ya
kwanza dhidi ya msafara
huo, ikapatia takriban
kilometa tatu kutoka
Sirte. Dakika chache
baadaye, ndege za kijeshi
za Ufaransa zikaendeleza
kupiga mabomu.
Mabomu ya NATO
yalikwamisha msafara
huo na kuua dazeni
kadhaa za wapiganaji
watiifu kwa Gaddafi.
Baada ya shambulio la
kwanza, magari takriban
20 yalitoka katika kundi
kubwa na kuendelea
kwenda kusini. Pigo
lingine la mabomu ya
NATO liliharibu au
kuteketeza magari 10
kati ya hayo. Kwa mujibu
wa gazeti la Uingereza
la Financial Times,
vikosi vya wapiganaji
wanaompinga Gaddafi
vya Free Libya vikiwa
katika eneo hilo pia
viliupiga msafara huo.
Kwa mujibu wa taarifa
yake, NATO ilikuwa
haina habari wakati wa
shambulio hilo kuwa
Gaddafi alikuwa katika
msafara. NATO ilisema
kwa mujibu wa azimio
la Baraza la Usalama
la Umoja wa Mataifa la
mwaka 1973, hailengi
watu ila vitu vinavyoleta
hatari katika uwanja
wa vita. NATO baadaye
ilisikia "kutoka vyanzo
huru na taarisa za kijasusi
za washirika" kuwa
Gaddafi alikuwa katika

msafara huo na kuwa


shambulio hilo ni wazi
lilichangia kukamatwa
kwake.
Kuiamini NATO,
ilikuwa haina habari
kuwa Gaddafi alikuwa
katika msafara huo,
lakini bado ikawa ina
ndege isiyo na rubani
inangoja hapo kando
pamoja na ndege kadhaa
za kivita za kulenga
vitu vilivyoko ardhini
(na siyo makombora ya
kutungua ndege kama
ambavyo ungetazamia
kwa vikosi vinayodhibiti
anga ndege zisiruke).
Ilipita tu magari hayo
mara kadhaa katika
juhudi ya kuua kila
aliyekuwa humo kwa
sababu walikuwa "vifaa
vya kijeshi vinavyoleta
hatari."
Kwa sababu unaishi
katika ulimwengu halisi,
unajua kuwa NATO
ilikuwa inafahamu ni
wapi hasa alipo Gaddafi
wakati wote na kuwa
alikuwa katika msafara
huo akijaribu kukimbia
mashambulizi ya
NATO. Zaidi, unaweza
kushangaza kidogo
kufahamu kuwa mengi
kati ya magari hayo
yalikuwa ni aina ya pick
up ambayo hayawezi
kuleta hatari yoyote
ile kwa vikosi vya
NATO. Suala lilikuwa
ni kumwua Gaddafi,
na vifaa mbalimbali
vilikusanywa kwa lengo
hilo.
Kuuawa kwa Gaddafi
kulikuwa ni kupangwa
kifo cha kiongozi wa nchi
nyingine na washikadau
wa nchi za Magharibi.
Kwa hali hiyo, Gaddafi
alikuwa ni mlengwa
tu mwingine katika
mlolongo wa viongozi
waliouawa wakijaribu

kuzuia washikadau hao


hao wasifikie malengo
yao.
Baada ya NATO
kumaliza uharibifu nchini
Libya kwa kumwondoa
Gaddafi na kuacha bonge
la ombwe katika dola
ya nchi hiyo, iliondoka
papo hapo, kuiacha nchi
hiyo ijitegemee iwezavyo.
Libya ilitumbukia, bila
shaka, katika vita ya
wenyewe kwa wenyewe
na imebakia hapo tangu
wakati wimbi la utumiaji
nguvu kuleta serikali
ya kidini lilipoanza na
kuongeza uwepo na
udhibiti wa ISIS (Dola ya
Kiislamu Irak na Shamu).
Kama NATO/
Marekani wangefuata
kanuni ya kwanza
ya Pier "ukikivunja,
unakinunua," bado
wangekuwa nchini
Libya wakitoa fedha na
misaada wakati nchi hiyo
ikirudi katika utulivu na
kuanza safari ndefu ya
kujijenga upya.
Lakini hapakuwa
na bahati kama hiyo.
Siyo hata kidogo jinsi
wanavyojiendesha.
Ni ubepari maafa
unaofuatwa. Dhana
elekezi ni kubomoa nchi
na kutengeneza pesa kwa
kutumia vipande vyake.
Siyo kuwasaidia watu.
Vinginevyo, unawezaje
kuelezea uharibifu
unaoendelea katika nchi
kama Irak, Libya, Yemen
na Syria?
Licha ya kuwa na
mapungufu ya kiutawala
kwa viwango vya nchi
za Magharibi, nchi zote
hizo zilikuwa zimetulia
na kuwa na maendeleo
mazuri tu kabla maslahi
ya nje hayajaingia
na kuzigeuza kuwa
majinamizi halisia.
Ni hali hii ambayo
inaelezea kwanini
makundi ya kiharamia
na kupinga maendeleo
kama ISIS yalizuika. Ni
jibu la kiasili tu la watu
walioingiliwa wakihitaji
kurudisha udhibiti juu ya
maisha yao ambayo bila
hivyo hayana matumaini
na hata maana. Sitaki
kuihalalisha, ila kueleza
mazingira ambayo
yamefikia kuzuka
kiwake.
(Hii ni sehemu ya
kwanza ya Makala
Murder And Mayhem
In The Middle East
iliyoandikwa na
Chris Martenson
na kutafsiriwa kwa
Kiswahili na Anil Kija.)

16

MAKALA

AN-NUUR

RABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 18-24, 2015

Magufuli afikishiwe madai ya Waislamu


Na Bakari Mwakangwale

BAADA ya kupatikana kwa


Serikali mpya ya John Pombe
Magufuli, ambayo ni awamu
ya Tano ya uongozi katika
Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, chini ya Chama
Cha Mapinduzi (CCM),
siku zinasonga mbele na
maisha yanaendelea baada
ya uchaguzi.
Kwa ujumla kila raia
katika makundi ya kijamii
yanatafakari mustakabali
wao chini ya uongozi huu
mpya, ni vipi watakuwa
katika faraja ya matarajio
ya kuweza kutoka pale
walipoachwa na utawala
uliopita. Miongoni mwa
makundi hayo ya kijamii lipo
kundi la Waislamu, kundi
ambalo naweza kusema kuwa
ni wahanga wa awamu zote
chini ya Chama Cha CCM,
na kutokana na madhila
wayapatayo, inaonesha kama
vile kundi hilo limekata
tamaa na utawala wa CCM,
chini ya kiongozi yoyote
anayetoka katika Chama
hicho.
Lakini kundi hili sina
shaka kuwa linafahamu
kuwa kisiasa, Rais atakaye
shinda anakuwa ni Rais
w a Wa t a n z a n i a w o t e
waliompigia kura na wasio
mpigia kura, kinachofata
ni kuangalia ni namna gani
wanaweza kwenda naye
sawa. Ni vyema kujipa moyo
kuwa anaweza kuwatendea
h a k i , k wa n i M u i s l a m u
hapaswi kutaka tamaa.
Katika hili, ipo mifano mingi
ni kwa namna gani Mitume
wa Mwenyezi Mungu na
Maswahaba wao waliweza
kuishi katika tawala za
mbalimbali na wakaweza
kupata yao.
Rais Magufuli ameingia
madarakani na kauli mbiu ya
Hapa Kazi tu kauli ambayo
mara baada ya kuapishwa
imeanza kujionyesha
k i v i t e n d o k wa k u f a n ya
maamuzi ambayo katika
tawala zilizopita ilikuwa ni
nadra kufanywa.
Lakini Rais Magufuli,
katika kampeni zake wakati
akiomba ridhaa ya kuongoza
nchi, alikuwa akijinadi
kuwa yeye ni mwadilifu,
mtu wa watu, mchapa kazi
na mfuatiliaji wa mambo.
Mh. Magufuli ameingia
madarakani na kudhihirisha
yale aliyokuwa akijinadi
nayo, hivi sasa kwa watumishi
wa Serikali, hususani kwa
wasio waadilifu hakuna asiye
na hofu juu ya mustakabali
wake, na kasi hiyo sasa
imekuwa ni faraja kubwa kwa
wananchi wanyonge. Rais
Magufuli amekuwa kivutio
kwa makundi mbalimbali

Lakini kwa kauli iliyo laini huenda


Akaona haki Sheikh Msellem wakasalimika

RAIS John Magufuli.

SHEIKH Msellem.

SHEIKH Farid Hadd.

ya Watanzania, hususani
wanyonge miongoni mwao
ni wale ambao walikuwa
upande wa pili ambao ndio
wapiga kura, ndani ya kipindi
hiki kifupi tokea kuapishgwa
kwake, kutokana na utendaji
wake wa kazi.
Katika moja ya hotuba zake
Rais Magufuli, amesikika
akiorozesha kero sugu
mbalimbali zinazowasumbua
wananchi, miongoni mwa
kero hizo ni kubambikiwa
kesi, na kuahidi akisema,
Kero hizi ni lazima
tutazishughulikia kwa nguvu
zote. Katika kudhihirisha
msimamo wa Rais Magufuli,
Waziri Mkuu Mh. Kassim
Majaliwa, Novemba 29, 2015,
akifungua maadhimisho ya
miaka 20 ya Dayosisi ya
Pwani ya Kanisa la African
Inland Church Tanzania
(AICT), Jijini Dar es Salaam,
a l i w a t a k a Wa t a n z a n i a
waiombee Serikali ya awamu
ya Tano, ili iweze kuongoza
kwa haki na uadilifu
kwa lengo la kuwaletea
Watanzania maendeleo.
Kutokana na hali hiyo,
napenda kulizungumzia
kundi la moja katika jamii la
Waislamu, ambalo linaamini
kwa mifano iliyo hai kuwa ni
wahanga na ni wadhulumiwa
katika mambo mbalimbali
ya kijamii chini ya tawala
zilizopita.
Kwa kawaida binadamu
unapoandamwa na mitihani,
na katika kuikabili mitihani
hiyo ukawa unamlilia
M we n ye z i M u n g u k wa
njia ya kukata tamaa, si
rahisi ukapata ujasiri wa
kukabiliana na mitihani
zaidi na zaidi. Ni bora kundi
hili likajipanga, kwenda

kumkabili Rais Magufuli,


na kumueleza madai yao.
Rais Magufuli amekuwa
akinadi kuwa Hii ni Serikali
ya Magufuli na hata katika
kampeni mara kwa mara
alikuwa akisema Chagua
Magufuli mara chache
alikuwa akisema chagua
CCM, hizi kauli huenda
mwenyewe aligundua kitu.
Katika Qu ran: 20:24.
Mwenyezi Mungu
anamwambia Nabii Mussa,
Nenda kwa Firauni, bila
shaka yeye amepindukia
mipaka.
Nabii Mussa, alihofu baada
ya amri hiyo akasema, Ewe
Mola wangu nipambanulie
(nikunjulie) kifua changu
(niweze kustahimili balaa
zitakazonifika). Quran 20:25.
Na katika Quran 20:46, Allah
anajiubu, (Mungu) akasema:
msiogope bila shaka mimi
ni pamoja nanyi, nasikia na
naona.
Baada ya hapo Mwenyezi
Mungu alitoa mwongozo kwa
Nabii Mussa, ambapo katika
Qur an, 20:44, Allah (s.w)
anasema Kamwambieni
maneno laini huenda atashika
mawaidha au ataogopa.
Aya hii inatufundisha siasa
nzuri ya kuwafikishia watu
mawaidha, nayo ni kutumia
lugha nzuri na katika hali
ya upole . Upole na maneno
laini humvuta asiyetaka
kusikiliza akasikiliza, lakini
pia hata asiye Minkum
naye anastahili kufikishiwa
nasaha, ikiwa ni mtawala basi
atawale kwa misingi ya haki
na uadilifu.
Lilokubwa na linalowatesa
na kuwaumiza zaidi
Waislamu kwa sasa, ni kadhia
ya uwepo wa Waislamu na

Masheikh ndani (Mahabusu)


ambao wamedhalilishwa
kwa kufanyiwa vitendo
vichafu. Rais afikishiwe hili.
Aelezwe kuwa yeye sasa
ndiye Amiri Jeshi Mkuu,
aliangalie hili kwa misingi ya
haki na sheria.
Ni kweli anaweza akawa
anajua, lakini kujua kwake ni
kule kwa misingi ya dhulma
zilizopelekea kuwepo wao
ndani lakini zipo hoja nyingi
za kumdhihirishia kuwa
Waislamu na Masheikh hao
ni wahanga tu kwa tuhuma
zisizo na ushahidi wowote.
Mbali na hilo, Rais huyu
mfatiliaji (Mh. Magufuli)
aelezwe kwamba Waislamu
hawataki kupendelewa, bali
wanataka haki na usawa siku
zote, kama hawa Masheikh
na Waislamu wana hatia,
basi sheria ifuate mkondo
wake na ieleweke kama wana
makosa wahukumiwe kwa
mujibu wa sheria na kama
hawana, basi waachiliwe
warudi uraiani washiriki
katika kazi ya ujenzi wa Taifa
lao.
Rais Magufuli, aelezwe
kwamba kama kuna raia
wanaoongoza katika
kubambikiwa kesi, hakuna
k a t i k a r a i a wa k e k a m a
Waislamu. Na kwa sababu
ameahidi kuifanyia kazi
kero hii, basi ni vyema
akashajihishwa kulifanyika
kazi kwa haraka.
Bila shaka akilivalia njuga
suala hili la kubambikiwa
kesi atabaini madudu mengi
kuliko anavyofikiria na
atabaini kuwa waathirika
wakubwa ni Waislamu.
Nimalize kwa kuweka
orodha ya Waislamu katika
magreza mbalimbali kufatia

utafiti usio rasmi ambao


gazeti la An nuur, umebaini
kuwa Waislamu hao ni wale
ambao wanatuhumiwa kwa
tuhuma za ugaidi, uvamizi
wa kutumia silaha.
Ndani ya gereza la Segerea
kuna Waislamu wapatao
130, wanaohusishwa na kesi
za Ugaidi katika idadi hiyo
wapo katika mafungu ya
kezi zipotazi 13, ikiwemo ile
maarufu ya Sheikh Mselem
Ally na Farid Had. Kesi
hizo kwa ujumla zimekuwa
zikiahirishwa siku baada ya
siku yapata mwaka wa pili
sasa.
Katika gereza la
Morogoro, wapo Waislamu
wenye tuhuma kama hizo.
Waislamu hawa wapo katika
makundi mawili, kwanza
ni wale wenye kesi namba
17 ya mwaka 2015 na kesi
namba 16 ya mwaka 2015.
Hawa wanahusishwa na lile
sakata la Msikiti wa Kidatu
Wilayani Kilombero, jumla
wapo Waislamu 26 na kesi
zao zimekuwa zikipigwa
danadana tu, hakuna
kinachoendelea na mpaka
sasa wanasota mahabusu.
Jijini Mwanza kuna kesi
ya Waislamu nane, ambao
wanatuhumiwa kwa tuhuma
za Ugaidi, ambao wapo
mahabusu katika Gereza la
Butimba, hao ni kama hawa
wafuatao, Amini Msharaba,
Nassoro Muhammad, Sensei
Kioka, Omari Awadhi, Abdi
Shariif, Mohammad Ibrahiim
na wenzao wawili, hawa
wapo gerezani yapata miezi
si t a t a n g u wa k a ma t we .
Lakini kuna kesi ya Imam
Hamza, ambayo inaendelea
kuunguruma kwa muda
mrefu sasa.
Jijini Arusha, kuna
kesi ya tuhuma za ugaidi
inayomkabili Imam Hambali
na Waislamu wengine zaidi ya
61, ambao pia wamewekwa
kwa makundi nao hakuna
kinachoendelea zaidi ya
kufikishwa Mahakamani na
kusomewa mashitaka kisha
kupigwa tarehe. Ama mkoani
Kagera, katika Wilaya ya
Muleba, yupo Ustadhi
Yusuph na Abdul-Hamiid,
(Wakazi wa Buseresere,
Wilaya ya Chato, Mkoani
Geita).
Kwa ujumla hiyo ndio hali
halisi ilivyo. Ni wakati sasa wa
Serikali kuangalia inaweza
kuiondoa vipi dhulma hii
si katika kupendelewa, bali
kupewa haki si kuachiwa
tu. bali hata kuzipeleka kesi
hizo kwa misingi ya sheria na
endapo wakakutwa na hatia
wakihukumiwa pia ni haki
yao vile vile.

17

MAKALA

AN-NUUR

RABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 18-24, 2015

Wahafidhina munatupeleka wapi?


Na Rashid Al-Ghafri

JENGA
nchi ni
mwananchi
mwenyewe
na mvunja nchi
ni mwananchi
mwenyewe pia.
Ninavyoona ni kweli
kabisa mjenga nchi
ni mwananchi, lakini
kwangu mvunja
nchi anaweza pia
kuwa mlowezi na
mvamizi au adui
yoyote kutoka nje,
hasa wenye masilahi
ya kukomba mali
kama walivyokuwa
Waingereza, Wafaransa
na Wajerumani na sasa
Wamarekani.
Raisi wa kwanza
wa Zanzibar licha
ya ukereketwa wake
wa kimapinduzi,
hakuwa na uzembe
wa kuwakumbatia
wale ambao
walionekana hawana
uchungu na nchi kwa
kuwambia"Huwezi
kuwa mwananchi kama
huna machungu ya
nchi".
Maneno haya
kwa lugha ya kisasa
tunaweza kusema
kuwa ni maneno
msumari kabisa na
muda huu tuliwonawo
Wazanzibar tunaweza
kuyatafakari maneno
haya na tukifanya
hivyo tutawaelewa
wale ambao sio
wananchi kwani
wapo ambao hawana
uchungu na nchi.
Wahafidhina wa
Zanzibar wengi wao
hawana uchungu na
nchi au wanajaribu
kuupiga chenga
kuzidi kufanikisha
walichokusudia.
Kutokuwa na
uchungu wa nchi ndio
kutapelekea kuvunja
nchi kutokana na
tamaa zao na uchu
walionao wa madaraka
huku wakijua
wanachokifanya lakini
zaidi wakilinda maslahi
ya tumbo.
Kulichumia tumbo
kwa kuwaangamiza
wananchi na nchi,

Turejee katika msimamo wa Mzee Karume

RAIS wa kwanza wa Zanzibar, Marehemu Mzee


Abeid Amani Karume.

ni dhulma hivyo
inawapasa muelewe
kuwa dhuluma
munazowafanyia
Wazanzibar hazitokufa
na badala yake
mutalipwa uovu wa
dhuluma hizo kesho
mbele ya hukumu.
Wahafidhina kutokana
na tabia yenu hii ya
kuipindisha haki kuona
batili na batili kwenu
kuiona haki kwa
maslahi tu ya matumbo
yenu, itafika siku
mchana muone usiku
na kutamani usiku uwe
mchana.
Wahafidhina nini
hasa mulichokikusudia
kwa wananchi
wa visiwa hivi
vilivobarikiwa kila
aina ya neema kuanzia
bahari hadi ardhi, au
ndio tuwaelewe kuwa
munatupeleka kule
ambako Mwalimu
Nyerere alikusudia
na nyinyi ndio
munatekeleza hilo au
kuna wasia aliwaachia.
Kwa makusudi
kabisa mumethubutu
kuivunja na kuisigina
katiba ya Zanzibar
ili muwakomoe
Wazanzibar kwa
kile walichoamua

kukifanya kwa mujibu


wa katiba hiyo.
Kuivunja katiba
hamjui kwamba
munaiingiza nchi
kwenye giza.
Hebu tuwekeeni
wazi, ni wapi hasa
mnatupeleka?
Ni mwezi na siku
kadhaa sasa tokea
kujiongezea muda wa
kuwepo madarakani
kwa kisingizio cha
ufutwaji wa uchaguzi
mumekuwa mukikalia
nafasi hizo bila ridhaa
nyengine ya wananchi
huku hali zao
zikiendelea kudidimia.
Kila huduma kwa sasa
ni shida kupatikana
sio tu kwa taasisi za
serikali pekee ambazo
zimezorota kwa
kutokuwepo usimamizi
wa kweli, bali hata
wenye kuendesha
huduma binafsi wengi
wao wamejipa likizo
bila kutarajia lakini
likizo hilo ambalo
hatujui litamalizika
lini limewalazimi
kulingana na hali
tuliyonayo sasa.
Bidhaa nyingi
zimekumbwa na
mfumko mkubwa wa
bei hivyo wananchi

wanyonge wakizidi
kuelemewa na mzigo
wa maisha. Mzigo
huu walitarajia kupata
nafuu baada ya
uchaguzi lakini wapi.
Bado tunapelekwa kule
ambako wao wanaona
tukishiba sisi hakuna
mwingine mwenye
njaa.
Tafakarini kuwa
dhima kubwa ya
Wazanzibar ipo
mikononi mwenu
popote mutakapo
waingiza ni nyinyi
mutakao beba lawama
na kama kuna nguvu
nyuma yenu inawatia
mkazo kuendeleza
dhamira zenu,
mjue kuwa mwisho
watakugeukeni na
kujirusha mbali kabisa
na hilo.
Uchumi wa nchi
yetu ya Zanzibar
kwa uhalisia kabisa
umekufa na hii yote ni
mipango ya zamani ya
wahafidhina ambayo
wanaiendeleza kwa
matakwa yao. Vijana
wengi hawana ajira
na wenye kujiajiri
wenyewe vikwazo kila
kukicha. Tuangalie
eneo la darajani
wote walokuwa
wakijishughulisha
walitimuliwa kwa
kisingizio kuwa ni eneo
la kujenga bustani,
iko wapi hiyo bustani
ilojengwa na miaka
kadhaa imepita sasa.
Licha ya rasilimali
za mafuta na gesi
zilizogunduliwa katika
visiwa hivi, ninaamini
hata kama uchimbaji
wake utafanyika chini
ya usimamizi wa hawa
wahafidhina, hakuna la
maana litakalopatikana
kwa nchi.
Ninayasema
haya kwa ushahidi
unaojidhihirisha
wenyewe katika zao
maarufu la karafuu
hususani kisiwani
Pemba kwani siku za
msimu kila unapopita
barabarani kuna
vizuizi vimeekwa ili

rasilimali ya karafuu
ambayo wakubwa
wameitumbulia macho
kwa kuiweka kwenye
udhibiti wao. Zao hili
bado halijawanufaisha
wakulima licha ya kazi
kubwa wanayopata
na wengine ulemavu
wa maisha au hata
kupoteza maisha
kabisa wakati
wa harakati za
uokowaji wa zao
hili walilotegemea
kuwainua kiuchumi
lakini wapi yao kazi
faida ya wakubwa.
Harakati zote za
upatikanaji wa zao
hili ni za wakulima
wenyewe lakini zao
likiwa tayari ni la
wakubwa na ndio
vizuizi vikawekwa
mabarabarani kila
baada ya kilomita
kadhaa na hili ni
sawa na ule usemi
wa Kishihiri "Mbuzi
wa Salimini lakini
maziwa ya bwana
wake Salimini". Na
ndio ukaona wakubwa
wanajipangia bei
watakayo wenyewe na
kama wewe mkulima
hutaki bei hiyo, basi
huna pengine pakuuza.
Bei wanayopewa
wakulima bado hayo
hayajawa malipo halisi
ya zao hilo badala
yake wanachopewa ni
kifuta jasho tu cha kazi
ngumu wanayoifanya
kwani malipo halisi
ni kuboreshewa hali
nzuri ya nchi yenye
miundombinu imara
kwa kila nyanja
na hapo itakuwa
kweli rasilimali hiyo
imewafaidisha.
Tuangalie hali
ilivo katika barabara
zinazopita maeneo
yanayozalisha zao hili
zikoje ukilinganisha na
thamani ya zao husika
katika soko la dunia.
Mfano barabara ya
Mkoani Chake Chake
ni mbovu na ya hatari
kabisa haimithiliki
kuambiwa ni barabara
inayounganisha
bandari na sehemu ya
kuu ya biashara katika
Inaendelea Uk. 19

18

MAKALA/HABARI

AN-NUUR

RABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 18-24, 2015

Uhalifu wa kivita wa Israeli dhidi ya Palestina


Inatoka Uk. 11
Israeli ni lazima ibebe
jukumu kwa mauaji
ya Waziri Abu Ein na
uhalifu wake unaofanya
dhidi ya wananchi wa
Palestina wasio na hatia,
huku mauaji hayo mapya
yakitarajiwa kuwa na
madhara makubwa.
M a u a j i ya A b u E i n
ya l i k u wa n i t u k i o l a
kipekee, Kwa kweli ni
miongoni mwa hatua za
ukandamizaji na uhalifu
wa kivita, unaofanywa
na Israel wanaomiliki
vikosi wakati wote dhidi
ya Palestina inayokaliwa
kimabavu.
Mwaka mmoja tangu
mauaji ya Abu Ein, ni
hasara kubwa ikiongezeka
k wa Wa p a l e s t i n a
waliochukua hatua mpya
tangu mwanzoni mwa
Oktoba mwaka huu.
Hiyo ndio hali tete
iliyopo mjini Jerusalemu
ya Mashariki na maeneo
mengine yanayokaliwa
kimabavu nchini
Palestina,kufuatia uvamizi
dhalimu na vitendo vya
k i n ya m a v ya I s r a e l i ,
pamoja na msimamo mkali
wa walowezi wake dhidi
ya wapalestina.
Matokeo yake ni
mvutano unaoendelea na
mateso ya kila siku kwa
wapalestina wakiwemo
watoto, kutokana
na ukandamizaji na
uchokozi wa Israeli,hali
inayopelekea mauaji ya
kila siku kwa wapalestina
wasio na hatia.
Tu n a c h o k i o n a h a s a
upinzani usio na vurugu,
kwa kuwashirikisha
maelfu ya Wapalestina
kwenye maandamano ,
kuelekea kwenye vituo
vya ukaguzi vya Israeli,
kwa lengo la kudai uhuru
na haki zao.
Mara kwa mara
maandamano hayo
yanakumbana na
mashambulizi ya jeshi
la Israeli,ambalo
hutumia risasi za
moto ili kuwatawanya
waandamanaji hao wa
kipalestina. Hatua
iliyopelekea kupoteza
maisha ya wapalestina
wasiopungua 108 tokea
mwanzoni mwa mwezi
Oktoba mwaka huu.
Israeli inafanya
ukiukwaji mkubwa wa
haki za binaadamu kwa
wapalestina,hasa pale
wanapowawekea vikwazo
hata kuingia Msikiti wa
Aqswa,huku jeshi hilo
likijikita zaidi kimakazi
m j i n i J e r u s a l e m u ya
mashariki na kufunga
kamera kadhaa ili
kufuatilia ibada za

wapalestina msikitini
humo na eneo zima husika.
Hivyo tatizo ni
kwamba asilimia 95 ya
Wapalestina ni marufuku
kufika Jerusalemu, Daktari
mmoja alizaliwa huko na
akafanya kazi ya udaktari
kwa miaka 15, hata hivyo,
tangu mwaka 2005, Israel
inakataa kumruhusu
a e n d e h u k o , i n g a wa
yeye ni mwanachama wa
kuchaguliwa wa bunge
Palestina.
Wakati huo huo kuna
ongezeko kubwa la vurugu
zinazofanywa na walowezi
wa Israeli dhidi ya
Wapalestina,zilizopelekea
mauaji ya Mohammed
Abu Khudeir akiwa na
umri wa miaka 16, ambapo
tukio hilo lilifanyika
mnamo mwezi Julai 2014;
baada ya kutekwa nyara
na kuchomwa moto akiwa
hai na walowezi wa Israeli.
K wa m f a n o h u u n i
dhahiri kwamba,ukatili
wa Israeli hauheshimu
kabisa uhai wa
wapalestina wasio na
hatia,wakitekwa,kupigwa
na hata kuuwawa katika
maeneo mbalimbali hasa
Jerusalemu ya mashariki.
Mauaji mengine ni
yale ya Dawabshy akiwa
na umri wa miezi 18,
yaliyofanywa na walowezi
wa kiyahudi kijijini
Duma,mnamo tarehe
31 Julai 2015. Ambapo
wa l i r u s h a m a f u t a ya
petroli ndani ya nyumba
ya familia yao usiku, hatua
iliyopelekea kuchomwa
mota hadi kufa,huku
wazazi wake wakijeruhiwa
vibaya na baadae baba
yake kufariki dunia.
Mauaji haya mawili
ni ujumbe tosha kwa
jumuiya ya kimataifa
na kwamba wananchi
wa Palestina wanadai
haki yao ili kujiokoa na
ukandamizaji huu na
mateso haya,yaliyopelekea
kuuwawa wapalestina
zaidi ya 108,wakiwemo
wa t o t o 2 4 , wa n a wa k e
5,tangu mwanzo mwa
mwezi Oktoba mwaka huu
wa 2015.
Aidha, katika kipindi
hiki zaidi raia wa Palestina
12,000 wameuwawa na
we n g i n e k u j e r u h i wa ,
kufuatia matumizi ya
nguvu ya Israeli, ambapo
silaha mbalimbali
hutumika zikiwemo risasi
za moto, mabomu na
kadhalika.
Mtu anaweza kuuliza:
Kwa nini hii inatokea?
Baada ya miaka 22
ya mazungumzo,
Wapalestina waligundua
kuwa barabara ya amani
imefungwa na Israeli,
inayotumia mwanya huo

katika kupanua makazi


yake ya kilowezi, huku
uvamizi huo wa Israeli
ukidumu kwa zaidi ya
miaka 48.
W a p a l e s t i n a
walilazimishwa
kukubali yaliyojiri
katika makubaliano ya
O s l o m n a m o m wa k a
1993 chini ya usimamizi
wa Umoja wa Mataifa,
lakini kwa bahati mbaya
hakuna kilichowanufaisha
wa p a l e s t i n a z a i d i ya
maonevu, ukandamizaji
na kuvunjiwa utu wao,
kunakofanywa na Israeli
ikisaidiana na walowezi
wa k e wa i s h i o n c h i n i
Palestina.
Kwa upande mwingine
idadi ya walowezi hao wa
Israeli waliopo katika ardhi
ya Palestina imeongezeka
s a n a n d a n i ya m u d a
wa m i a k a 2 2 , a m b a p o
wamefikia kutoka 115,000
hadi 650,000.
Wa z i r i M k u u w a
Israeli Netanyahu anadai

kwamba,mapigano
yanayoendelea hivi sasa
ni matokeo ya uchokozi
kutoka upande wa
Palestina,hivi ndivyo
walivyo madikteta na
viongozi wa kimabavu
daima hufanya hivyo
badala ya kutafuta mizizi
na chanzo cha mgogoro.
Chanzo cha mgogoro
ni Israeli kujitangazia
umiliki wa sehemu ya
ardhi ya Palestina kuwa ni
yake,hasa Jerusalemu ya
Mashariki tokea miaka 48
iliyopita,hali iliyopelekea
kuweka viziwizi ili
kutenganisha mji huo na
Ukingo wa magharibi ili
kuhodhi ardhi yote ya
Palestina.
Dola ya Palestina tayari
imekabidhi ushahidi
wa k e wa u h a l i f u wa
kivita, unaofanywa na
Israeli dhidi ya Palestina
na wananchi wake kwa
Mahakama ya Uhalifu
ya Kimataifa (ICC),
i l i k u o n g e z a k a s i ya

uchunguzi wa ukiukwaji
wa haki za binaadamu
unaofanywa na Israeli.
Waziri wa Mambo ya Nje
wa Palestina Mheshimiwa
Riad Maliki alisema:
"Suala la Palestina ni
mtihani kimataifa ...
mtihani huo dunia
ikiushindwa itakuwa ni
hasara si kwa Palestina
tu bali kwa Ulimwengu
mzima, kwani Palestina
imeamua kutafuta haki, si
kisasi."
Kama hayati Nelson
Mandela wa Afrika Kusini
aliyepambana na ubaguzi
wa rangi alisema, suala la
Palestina ni ukweli na haki
kuliko suala tulilonalo ".
Contact us: P.O Box
20307, 612 UN Road
Upanga West, Dar es
Sa la am Tel: 2152813,
2150643 Fax: 2153257
Email: pict@pal-tz.
orgWebsite: www.pal-tz.
org

Chuki dhidi ya Waislamu inakolea Marekani


Inatoka Uk. 20

zaidi ya asilimia 57 ya
wananchi wa Marekani
wa n a p i n g a m a t a m s h i
hayo ya chuki za kidini ya
Donald Trump.
Mamia ya wanaharakati
wa kijamii na haki
za binadamu nchini
Marekani, walikusanyika
Alhamisi iliyopita mbele
ya hoteli moja kubwa
inayomilikiwa na Trump,
ili kuonesha hasira zao
dhidi ya mwanasiasa huyo
mwenye chuki za kidini.
Kuna uwezekano
Donald Trump akateuliwa
na chama cha Republican
kugombea urais wa
Marekani.
Waliojumuika mbele
ya hoteli hiyo kulaani
matamshi ya chuki za
kidini ya Trump ni pamoja
na kutoka Jumuiya ya
Waislamu wa Marekani,
Taasisi ya Kulinda Haki ya
Uhuru na Katiba, Kanisa la
Marekani na Maveterani
wa Vita wa Marekani.
Wa c h a m b u z i wa
mambo wanaamini kuwa,
mashambulio ya kigaidi
yaliyotokea hivi karibuni
mjini Paris Ufaransa,
yametoa fursa kwa maadui
wa Uislamu kupata
kisingizio cha kuzidi
kuonesha chuki zao dhidi
ya Waislamu.
Lakini bado duniani
wapo watu wenye fikra

DONALD Trump.
huru, ambao wanaelewa
vyema kuwa vitendo vya
kigaidi vinavyofanywa
kwa jina la Uislamu, havina
mfungamano wowote na
dini hiyo tukufu.
Wakati ubaguzi dhidi
ya Waislamu ukikolea,
Mwanafalsafa maarufu
nchini humo Noam
Chomsky, ameilaumu
Marekani kwa kukithiri
hali hiyo.
Mchambuzi huyo
mashuhuri wa masuala ya
kisiasa nchini Marekani,
a m e s e m a s e r i k a l i ya
Washington na washirika
wake wanafaa kulaumiwa
kutokana na mashambulio
ya k i g a i d i ya m we z i
uliopita yaliyoitikisa Paris,
mji mkuu wa Ufaransa.
Chomsky, ambaye
pia ni mwanafilosofia
alisema hatua ya

Marekani kuzivamia Iraq


na Afghanistan imekuwa
chanzo na chimbuko la
harakati za ugaidi duniani.
Katika mahojiano na
televisheni ya PressTV
ya Iran, msomi huyo
wa Marekani alisema
serikali ya Washington
na washirika wake wana
chaguo la kuutokomeza
ugaidi duniani iwapo
watakuwa na irada ya
kisiasa.
Ameongeza kuwa,
ugaidi na hususan
kama unaoendelezwa
na kundi la Daesh,
hauwezi kumalizwa kwa
mashambulizi ya kijeshi
tu.
Katika tukio la kigaidi
la Novemba 13 mjini Paris,
Ufaransa watu zaidi ya
130 kuuawa na mamia ya
wengine kujeruhiwa.

19
KAMA kuna sehemu
ambayo Kanisa
limefanikiwa kubatiza
Wa i s l a m u , b a s i n i
Wilaya ya Same.
Majina kama Marry
Omari, Eliewaha
K a t h i m u , N a t u j wa
Emanuel Mohammed,
Yohane Mathayo Saidi,
Nthembia Kathibeti
Rajabu, ni ya kawaida
kabisa kuonyesha kuwa
awali baba na babu wa
vijana wa sasa walikuwa
Waislamu, lakini watoto
na wajukuu, wameishia
kubatizwa.
Unapofanya utafiti
kidogo unachogundua
ni kuwa japo Uislamu
ulikuwa wa mwanzo
kuingia, lakini baada
ya watu kuingia katika
Uislamu kupitia
Maulidi na Muridi wa
Twa r i k a , h a p a k u wa
n a m we n d e l e z o wa
k u wa s o m e s h a . K wa
hiyo wengi wakabaki
Waislamu wa majina.
Na hata baadae
i l i p o k u j a B a k wa t a ,
haikushughulika
na kuwaelimisha
Waislamu,
ila
kudumisha ukiritimba
wa umiliki wa Misikiti
na kuhakikisha hakuna
anayeingia kusomesha
bila kibali chao
wakati wao wenyewe
hawakuwa tayari
kupeleka mwalimu.
Kinyume chake,
walipoingia Wakristo
walikuja kama watu
wenye misheni maalum
ya k u f u t a U i s l a m u
wakianzia milimani na
kumalizia tambarare.
Pa m o j a n a k u j e n g a
makanisa, walijenga
shule na hospitali, lakini
pia kila aliyebatizwa
walihakikisha kuwa
anausoma Ukristo na
kukomazwa kiimani
kupitia taratibu zao za
Kikanisa.
Same Milimani wakati
awali katika miaka ya
1940s mpaka 1960s,
i l i k u wa M k r i s t o n i
wa kutafuta, hivi sasa
imekuwa kinyume
chake. Kuna baadhi ya
vijiji kama utauguwa
uambiwe kwamba dawa
ni kumpata Muislamu
wa eneo hilo, akushike
kichwani, basi itabidi
ufe tu.
Ukiingia katika milima
ya Vudee unakutana na

MAKALA

AN-NUUR

RABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 18-24, 2015

Hali ya Uislamu Vudee

HUU ni msikiti wa Ndolwa /Mjingo kama unavyo


onekana katika picha juu. Hapa ni waumini wakisikiliza
hotuba ya Ijumaa. Imam ni Mwalimu wa shule
aliyehamia kijijini hapo karibuni. Anajaribu kuokoa
jahazi kwa anachokijua.

ngumu ya kiuchumi
ambapo Kanisa hutumia
fursa hivyo kugawa
chakula cha msaada na
msaada wa masomo kwa
watoto, basi ndio kabisa
masalia ya Waislamu,
yanazidi kukombwa.
Msikiti wa Ndolwa
amejenga Mzee Omari
Danieli na familia yake,
lakini ndio uwezo wake
umefikia mwisho.
Wa m e p i g a m a t o f a l i
lakini hawajayachoma.
Waumini wanaosali
hapo Ijumaa kwa
Ijumaa, ni familia yake
na majirani na Waislamu
wa Kijiji cha Mjingo.
Msikiti wa pili Imamu
wake anasema kuwa
Waislamu wa eneo hilo
ni kiasi cha hamsini.
Kuhusu kuritadishwa,
an asema ku wa hi l o
l i m e k u wa n i j a m b o
la kawaida na ni kwa
s a b a b u Wa i s l a m u
hawana elimu ya msingi
ya dini yao. Na hata yeye
mwenyewe anasema
hana elimu ya kutosha,
lakini imebidi awe ndio
kuiongozi.
Ombi la Waislamu wa
Vudee na Same milimani
kwa ujumla, ni kuwa
wasaidiwe kusomesha

vijana wa pale pale


wanaume na wanawake
angalau elimu ya msingi
ya dini ya Kiislamu ili
waje kuwa walimu.
Jingine ni kusaidiwa
kujenga hiyo misikiti
iwe na hadhi ya Msikiti
pamoja na udogo wake.
Kwa vile ibada na
Uislamu pekee katika
maeneo hayo ni swala
ya Ijumaa na Eid, watu
wakishamaliza kuswali,
virago (madathi), au
tuseme miswala
hukunjwa na kuwekwa
juu ya dari ili isiliwe na
mchwa.
Mwenye kutaka
kupeleka msaada huko,
akiwa ana gari barabara
ni nzuri ila gari iwe na
uwezo wa kupanda
milima na dereva awe
mzoefu wa kupanda
milima. Hata gari za
Noah zinapanda huko.
Wanaweza kupeleka
misaada moja kwa moja
kwa Mwenyekiti wa
Msikiti Mzee Omari
Danieli, Kwa namba
0674 045 986/0787 134
554.
Au kama unatuma
vifaa tuma Kwa
Amiri wa Kamati ya
Kuendeleza Uislamu
(W), Same, Khatibu
Juma Mziray Juhudi
Studio, Box 62, simu,
0757 013 344. Same.

Wahafidhina mnatupeleka wapi?


Inatoka Uk. 17

vimsikiti viwili, chakavu


vilivyoachana
kwa
masafa
yasiyopungua kilomita
40. Msikiti mmoja
ukiitwa Breni ambao uko
njiani na ulinyanyuliwa
mwaka 1998 baada ya
kuachwa kwa muda
mrefu na kuanguka.
Idadi ya waumini wake
ni 50 chini ya Imamu
Salim.
Msikiti mwingine
ni ule wa Ndolwa /
Mjingo ukiwa chini
ya Mwenyekiti Omari
Danieli na Imamu akiwa

Mwalimu Ali Hamad


Ali. Waumini katika
msikiti huu ni 36. Pamoja
n a k u p i g i wa m b i u
kwamba kungekuwa
na ugeni, siku tuliyofika
msikitini hapo waumini
walioswali siku hiyo ni
wanaume 9 wanawake
4 watoto wa kike 3 na
wavulana 3.
Kama nilivyotangulia
kusema, t at izo kuu
katika eneo hili ni Elimu.
I d a d i ya Wa i s l a m u
inapungua siku hadi
siku kwa kubatizwa.
Ikichangiwa na hali

kisiwa hicho.
Barabara ya Chake
Chake- Wete maarufu
njia kongwe, licha
ya kuwa nayo ipo
katika maeneo
yanayotoa utajiri huo,
ni barabara yenye
mashimo matupu
utafikiri ni shamba
ambalo mkulima
amelitayarisha kwa ajili
ya kupanda migomba.
Katika hali ya
barabara hizi mgonjwa
anaweza kufika
akiwa huko hali gani,
kwenye yale majengo
ambayo yanayoitwa
spitali kama sio hoi
bin taabani licha ya
maradhi aliyonayo na
hivo ukifika huko ni
majengo yasiyokuwa

na hata panadoli
licha ya fedha nyingi
zinazoingia kwa zao
hili.
Zitoweni faida za
rasilimali za visiwa
vyetu kwani hii ni haki
ya wote tunahitaji jasho
letu liimarishe huduma
za afya, elimu maji na
huduma nyinginezo
na sio kujinufaisha
matumbo yenu pekee.
Kwa hali inavoelekea
ni mbaya isiyopigika
mfano au kufikirika
kabisa hasa kwa visiwa
vyenye ustaarabu
wa hali ya juu, yaani
visiwa vyetu vya
Zanzibar na hapo
ndio ninapowauliza
wahafidhina ni wapi
hasa mnakotupeleka?

AN-NUUR

20

MAKALA

20

RABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 18-24, 2015

JAE JAE JAE

AN-NUUR

RABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 18-24, 2015

Changia damu okoa maisha kwani sote ni


wagonjwa watarajiwa.
Tunaomba watu wote kuchangia damu
kwa hiari siku ya Jumamosi tarehe 19/12/2015
katika Hospitali za Temeke na Mbagala
Rangi tatu iliyopo Zakheem kuanzia saa 1:00
asubuhi.
Nyote mnakaribishwa
Limetolewa na Jumuiya ya JAE-Temeke.

Chuki
dhidi
ya
Waislamu
inakolea
Marekani
Misikiti inachomwa moto
VITENDO vya chuki
d h i d i y a Wa i s l a m u
vimeongezeka nchini
Marekani.
Wat u wen ye c h uk i
za kidini wameuchoma
moto Msikiti mwingine
huko California.
Wakuu wa Jumuiya ya
Waislamu wa Marekani
walisema Ijumaa iliyopita
kuwa, watu wenye chuki
za kidini walitupa bomu
la chupa ndani ya Msikiti
wa Coachella, California
na kusababisha msikitini
humo kuwaka moto.
Polisi wa Marekani
wameanza uchunguzi
kubaini sababu za
kuchomwa Msikiti huo na
kuchunguza kama jinai
hiyo inatokana na chuki
za kidini au la.
Chuki za kidini
zimeongezeka nchini
Marekani baada ya
mkwasi wa mali Donald
T r u m p , a n a y e wa n i a
kuteuliwa na chama cha

Republican kugombea
urais nchini humo, kutoa
matamshi ya chuki dhidi
ya Waislamu.
Siku moja baada ya
kutoa matamchi yake ya
kutotakiwa Waislamu
kuingia Marekani,
yaani siku ya Alhamisi,
m a a d u i wa U i s l a m u
waliuvamia na kuuvunjia
heshima Msikiti wa mji
wa Philadelphia huko
Marekani.
Vile vile Ijumaa hii
iliyopita, ofisi za Baraza
la Uhusiano wa Marekani
na Uislamu la mjini
Washington, zilifungwa
baada ya kuenea habari
k wa m b a m a a d u i wa
Uislamu walitaka
k u z i l i p u a k wa b o m u
baada ya kupatikana
kifurushi cha kutatanisha
katika ofisi hizo.
Awali Maafisa wengi
wa usalama wa Marekani
walionya kuwa, matamshi
ya kichochezi ya Donald

Trump, yataongeza chuki


na mashambulizi dhidi ya
Waislamu nchini humo.
Trump ameitaka
s e r i k a l i ya M a r e k a n i
ipige marufuku kuingia
Waislamu nchini humo
bila ya kujali wanatokea
wapi.
M a t a m s h i h a y o ya

kichochezi yanaendelea
kulaaniwa kote
ulimwenguni.
Umoja wa Mataifa,
Umoja wa Ulaya, Ikulu
ya Marekani White House
na Mashirika mbalimbali
kutoka pembe zote za
dunia wameendelea
kulaani matamshi hayo

ya chuki za kidini ya
mwanasiasa huyo wa
chama cha Republican
cha Marekani.
Hata hivyo uchunguzi
wa maoni uliofanywa
na taasisi ya NBC News
na gazeti la Wall Street
Journal unaonesha kuwa,
Inaendelea Uk. 18

HAIIBA TIMAMU TEA

CHAI YA AJABU KWA AJILI YA KUKABILIANA NA

UVIMBE KWENYE MATITI WAYEYUKA NDANI YA SIKU 3!


Na. Rahma Rashidi
Miezi michache iliyopita niligundua kuwa matiti yangu yalikuwa yameota
mauvimbe kadhaa ndani. Niliogopa sana. Nilimweza mume wangu na
kumwambia apapase ili aweze kujihakikishia. Alipofanya hivyo alitoa macho
kwa woga. Aliniambia nifanye subra atafakari ni nini kifanyike. Jioni aliporudi
alikuja na kibokisi kimoja kilichokuwa kimeandikwa Haiiba Timamu Tea.
Aliniambia kuwa niitumie hiyo chai kwa sababu alikuwa ameambiwa kuwa
inaweza kunisaidia. Niliitumia hiyo chai kwa siku tatu na ghafla nikakuta yale
mauvimbe yametoweka! Imepita miezi kadhaa sasa sijaona mauvimbe yale
yakirudi. Hata hivyo kama tahadhari nimeamua niwe natumia hii chai mara
kwa mara.
https://www.facebook.com/Herbal-Impact-157972014402705/

SHINIKIZO LA DAMU (HYPERTENSION/HIGH


BLOOD PRESSURE)
UGONJWA WA MOYO
KIHARUSI
JONGO (GOUT)
MAUMIVU YA VIUNGO (RHEUMATISM)
MAUMIVU SUGU YA KICHWA
BAWASIR (PILES/HEMORRHOIDS)
MAGONJWA YA INI
SARATANI MBALIMBALI
UOTO/UVIMBE MBALIMBALI KATIKA VIUNGO
VYA UZAZI VYA MWANAMKE (FIBROIDS,
POLYPS NA CYSTS)
KUSHINDWA KUZUIA MKOJO (URINARY
INCONTINENCE)
ATHARI ZA KISUKARI CHA UKUBWANI
PUMU
UPUNGUFU WA KINGA ZA MWILI
KASI YA KUZEEKA
MATATIZO YA MFUMO WA MZUNGUKO WA
DAMU
MKAKAMO WA NGOZI;
UDHAIFU WA MACHO
KUPOTEZA KUMBUKUMBU
KASI NDOGO YA KUPONA MAJERAHA
MAKOVU KWENYE MAPAFU
UGONJWA WA NGOZI KUCHUJA RANGI,
YAANI, VITILIGO

HAIIBA TIMAMU TEA


INAPATIKANA
HERBAL IMPACT
MOSQUE STREET, NO. 1574/144
(MKABALA NA MSIKITI WA
SUNNI), KITUMBINI, DAR ES
SALAAM
TUTEMBELEE AU TUPIGIE SIMU
NAMBA:
0754281131/0655281131/06862
81131/0779281131

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Ltd, Dar es Salaam.

Вам также может понравиться

  • Annuur 1214
    Annuur 1214
    Документ20 страниц
    Annuur 1214
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1216d
    ANNUUR 1216d
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1216d
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1209aaa
    ANNUUR 1209aaa
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1209aaa
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1231 PDF
    Annuur 1231 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1231 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1219
    Annuur 1219
    Документ20 страниц
    Annuur 1219
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Fiqhi ya ‘Ibada yenye picha zilizochorwa
    Fiqhi ya ‘Ibada yenye picha zilizochorwa
    От Everand
    Fiqhi ya ‘Ibada yenye picha zilizochorwa
    Оценок пока нет
  • Annuur 1213 PDF
    Annuur 1213 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1213 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1232 PDF
    Annuur 1232 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1232 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1262
    Annuur 1262
    Документ20 страниц
    Annuur 1262
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru!
    Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru!
    Документ485 страниц
    Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru!
    MZALENDO.NET
    100% (3)
  • Annuur 1204
    Annuur 1204
    Документ20 страниц
    Annuur 1204
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1226 PDF
    Annuur 1226 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1226 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1230 PDF
    Annuur 1230 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1230 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1176b PDF
    ANNUUR 1176b PDF
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1176b PDF
    annurtanzania
    Оценок пока нет
  • Annuur 1220
    Annuur 1220
    Документ20 страниц
    Annuur 1220
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1223
    Annuur 1223
    Документ20 страниц
    Annuur 1223
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1218 PDF
    Annuur 1218 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1218 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1229 PDF
    Annuur 1229 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1229 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1144
    Annuur 1144
    Документ16 страниц
    Annuur 1144
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • download
    download
    Документ53 страницы
    download
    Prence Hussein
    Оценок пока нет
  • Tishio la Ukombozi: Ubeberu na Mapinduzi Zanzibar
    Tishio la Ukombozi: Ubeberu na Mapinduzi Zanzibar
    От Everand
    Tishio la Ukombozi: Ubeberu na Mapinduzi Zanzibar
    Оценок пока нет
  • Annuur 1076
    Annuur 1076
    Документ12 страниц
    Annuur 1076
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • Kufikirika
    Kufikirika
    От Everand
    Kufikirika
    Оценок пока нет
  • Annuur 1143
    Annuur 1143
    Документ16 страниц
    Annuur 1143
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1153 PDF
    Annuur 1153 PDF
    Документ16 страниц
    Annuur 1153 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1082
    Annuur 1082
    Документ16 страниц
    Annuur 1082
    MZALENDO.NET
    100% (1)
  • Annuur 1091
    Annuur 1091
    Документ16 страниц
    Annuur 1091
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • Dawa Za Jadii
    Dawa Za Jadii
    Документ27 страниц
    Dawa Za Jadii
    Ibrahim Mussa
    Оценок пока нет
  • Annuur 1264
    Annuur 1264
    Документ20 страниц
    Annuur 1264
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1138
    Annuur 1138
    Документ16 страниц
    Annuur 1138
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1173 PDF
    Annuur 1173 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1173 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1228d
    ANNUUR 1228d
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1228d
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1210a
    Annuur 1210a
    Документ20 страниц
    Annuur 1210a
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1124
    Annuur 1124
    Документ16 страниц
    Annuur 1124
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1202
    Annuur 1202
    Документ20 страниц
    Annuur 1202
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1182
    Annuur 1182
    Документ20 страниц
    Annuur 1182
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • TAWASSUL
    TAWASSUL
    Документ2 страницы
    TAWASSUL
    Yadie Aria
    Оценок пока нет
  • Bacaan Ziarah Singkat
    Bacaan Ziarah Singkat
    Документ2 страницы
    Bacaan Ziarah Singkat
    saputra artha pratama
    Оценок пока нет
  • An Nuur 1128
    An Nuur 1128
    Документ16 страниц
    An Nuur 1128
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • HAYAAN, The Long Journey of the Nomad Boy
    HAYAAN, The Long Journey of the Nomad Boy
    От Everand
    HAYAAN, The Long Journey of the Nomad Boy
    Рейтинг: 5 из 5 звезд
    5/5 (2)
  • Matsayin Karatun Boko Da Aikin Gwamnati A Musulunci
    Matsayin Karatun Boko Da Aikin Gwamnati A Musulunci
    Документ17 страниц
    Matsayin Karatun Boko Da Aikin Gwamnati A Musulunci
    Islamcall4all
    100% (1)
  • TAWASSUL
    TAWASSUL
    Документ3 страницы
    TAWASSUL
    Wisang Geni
    100% (1)
  • Annuur 1090
    Annuur 1090
    Документ12 страниц
    Annuur 1090
    annurtanzania
    Оценок пока нет
  • Annuur 1172 PDF
    Annuur 1172 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1172 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1217
    Annuur 1217
    Документ20 страниц
    Annuur 1217
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Yasinan
    Yasinan
    Документ6 страниц
    Yasinan
    Ulis Cmr
    Оценок пока нет
  • RM Linguas 04
    RM Linguas 04
    Документ3 страницы
    RM Linguas 04
    Paiva Magaio
    Оценок пока нет
  • Hadithi 40
    Hadithi 40
    Документ16 страниц
    Hadithi 40
    Abdul Karim Mohamed
    Оценок пока нет
  • Maulidi - Si Bida, Si Haramu
    Maulidi - Si Bida, Si Haramu
    Документ39 страниц
    Maulidi - Si Bida, Si Haramu
    Stambuli Abdillahi Nassir
    Оценок пока нет
  • Annuur 1049
    Annuur 1049
    Документ12 страниц
    Annuur 1049
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • Annuur 1183 PDF
    Annuur 1183 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1183 PDF
    annurtanzania
    100% (2)
  • Swahili 05
    Swahili 05
    Документ17 страниц
    Swahili 05
    samweliman2
    Оценок пока нет
  • Mfalme - Nilipumzika: Mashairi Ya Kisasa - Modern Swahili Poetry
    Mfalme - Nilipumzika: Mashairi Ya Kisasa - Modern Swahili Poetry
    От Everand
    Mfalme - Nilipumzika: Mashairi Ya Kisasa - Modern Swahili Poetry
    Оценок пока нет
  • Kale ya Washairi wa Pemba: Kamange na Sarahani
    Kale ya Washairi wa Pemba: Kamange na Sarahani
    От Everand
    Kale ya Washairi wa Pemba: Kamange na Sarahani
    Оценок пока нет
  • Nyuma ya Mapazia
    Nyuma ya Mapazia
    От Everand
    Nyuma ya Mapazia
    Рейтинг: 5 из 5 звезд
    5/5 (1)
  • Hofu
    Hofu
    От Everand
    Hofu
    Рейтинг: 5 из 5 звезд
    5/5 (1)
  • Nyayo Za Obama
    Nyayo Za Obama
    От Everand
    Nyayo Za Obama
    Оценок пока нет
  • Nchi ya Kanaani, Itiririkayo Maziwa na Asali(Swahili Edition)
    Nchi ya Kanaani, Itiririkayo Maziwa na Asali(Swahili Edition)
    От Everand
    Nchi ya Kanaani, Itiririkayo Maziwa na Asali(Swahili Edition)
    Оценок пока нет
  • Mapepo Na Namna ya Kuya shug hulikia
    Mapepo Na Namna ya Kuya shug hulikia
    От Everand
    Mapepo Na Namna ya Kuya shug hulikia
    Рейтинг: 1 из 5 звезд
    1/5 (1)
  • Sanaa ya Kufuata
    Sanaa ya Kufuata
    От Everand
    Sanaa ya Kufuata
    Оценок пока нет
  • Annuur 1230 PDF
    Annuur 1230 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1230 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1262
    Annuur 1262
    Документ20 страниц
    Annuur 1262
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1232 PDF
    Annuur 1232 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1232 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1264
    Annuur 1264
    Документ20 страниц
    Annuur 1264
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Press Realse 28
    Press Realse 28
    Документ4 страницы
    Press Realse 28
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1229 PDF
    Annuur 1229 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1229 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • HOTUBA YA BAJETI OFISI YA RAIS Final
    HOTUBA YA BAJETI OFISI YA RAIS Final
    Документ15 страниц
    HOTUBA YA BAJETI OFISI YA RAIS Final
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • HOTUBA YA BAJETI OFISI YA RAIS Final
    HOTUBA YA BAJETI OFISI YA RAIS Final
    Документ15 страниц
    HOTUBA YA BAJETI OFISI YA RAIS Final
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Press Release - Muungano Na Mazingira
    Press Release - Muungano Na Mazingira
    Документ4 страницы
    Press Release - Muungano Na Mazingira
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1228d
    ANNUUR 1228d
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1228d
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1228d
    ANNUUR 1228d
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1228d
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1227 PDF
    Annuur 1227 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1227 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1226 PDF
    Annuur 1226 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1226 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1224
    Annuur 1224
    Документ20 страниц
    Annuur 1224
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1225
    Annuur 1225
    Документ20 страниц
    Annuur 1225
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1223
    Annuur 1223
    Документ20 страниц
    Annuur 1223
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1213 PDF
    Annuur 1213 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1213 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1220
    Annuur 1220
    Документ20 страниц
    Annuur 1220
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1217
    Annuur 1217
    Документ20 страниц
    Annuur 1217
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1218 PDF
    Annuur 1218 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1218 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Karume Shujaa
    Karume Shujaa
    Документ11 страниц
    Karume Shujaa
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1212
    Annuur 1212
    Документ20 страниц
    Annuur 1212
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1215 PDF
    Annuur 1215 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1215 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    100% (1)
  • Hotuba Ya Maalim Seif - January 9 2016
    Hotuba Ya Maalim Seif - January 9 2016
    Документ27 страниц
    Hotuba Ya Maalim Seif - January 9 2016
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1210a
    Annuur 1210a
    Документ20 страниц
    Annuur 1210a
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет