Вы находитесь на странице: 1из 20

Kesi ya Sheikh Msellem

danadana zaendelea

www.annuurpapers.co.tz au facebook:annuurpapers@yahoo.com

Sauti ya Waislamu

ISSN 0856 - 3861 Na. 1211 RABIUL AWWAL 1437, IJUMAA , JANUARI 8 - 14, 2016 BEI TShs 800/=, Kshs 50/=

Mh. Magufuli anaturudisha


kule kwa Sheikh Takadiri

Soma Uk. 20

Kamkaribisha Mufti Ikulu, lakini


Tuna ya kujifunza kwa Mwinyi, Mtei
JK yalimkuta. Prof. Chachage akajibu

MUFT Sheikh Abubakar Zubeir

MZEE Edwin Mtei. (Uk. 9)

Maimamu wataka Dk. Shein


aheshimu
kura
za
wananchi
Wasema hakuna Shura baada ya Shura

RAIS John Pombe Magufuli.

Kweli, hofu ya ugaidi huwafanya


watu kuwa wajinga kupindukia
Putin kidume. Awaumbua wenye IS

Soma Uk. 10

ANNUUR NEW.indd 1

Mapinduzi si kupindua Uchaguzi-Karume


Huo ni usaliti kwa Mapinduzi yenyewe

Dkt. Ali Mohamed Shein

MAALIM Seif Sharif Hamad

1/7/2016 3:17:00 PM

2
HAKIKA shukrani zote
zinamstahikia Allah.
Tunamhimidi,
tunaomba msaada Kwake,
na tunaomba maghfira.
Tunaomba hifadhi kwake
Allah
kutokana
na
maovu ya nafsi zetu,
na makosa ya matendo
yetu.
Yeyote Allah
Anayemuongoza, hakuna
wa kumpotosha, na yeyote
Allah Anayempotosha,
hakuna wa kumuongoa.
Ninashuhudia
pia
kwamba hakuna yeyote
anayestahiki kuabudiwa
isipokuwa Allah, na
ninashuhudia kwamba
Muhammad (Swalla
Allaahu alayhi wa aalihi
wa sallam) ni mjumbe na
Mtume Wake.
Amesema Allah (SWT):
Enyi
mlioamini!
Mcheni Allaah kama
ipasavyo
kumcha;
wala msife isipokuwa
mmekwishakuwa
Wa i s l a m u
kamili.
(Suratul Al-Imraan: 102).
Enyi watu! Mcheni
Mola wenu Ambaye
amekuumbeni katika
nafsi (asli) moja. Na
Akamuumba
mkewe
katika nafsi ile ile.
Na Akaeneza wanaume
wengi na wanawake
kutoka katika wawili hao.
Na mcheni Allaah ambaye
kwaye mnaombana. Na
(mwatazame) jamaa.
Hakika ni Mlinzi
juu yenu (anayaona kila
mnayoyafanya). (Suratul
An-Nisaa: 1)
Enyi mlioamini!
Muogopeni Allaah
na semeni maneno ya
haki. Atakutengenezeeni
vizuri vitendo vyenu na
Atakusameheni madhambi
yenu; na anayemtii
Allaah na Mtume Wake,
bila shaka amefanikiwa
mafanikio makubwa.
(suratul Al-Ahzaab: 70-71).
Amesema Allah (s.w):
Na uwe kutokana na
nyinyi umma unao
lingania kheri na unao
amrisha
mema
na
unakataza maovu. Na
hao ndio walio fanikiwa.
(Suurat Al 'Imran 3: 104).
Na amesema Allah (s.w):
Na saidianeni katika
wema na uchamungu. Wala
msisaidiane katika dhambi
na uadui. Na mcheni
Mwenyezi
Mungu.
Hakika Mwenyezi Mungu
ni Mkali wa kuadhibu.
(Suurat Al- Maida 5: 2).
Muislamu kama yeye
binafsi hawezi kuibadili
jamii bila kusubiana na
watu wengine wenye lengo
kama lake.
Kazi ya harakati ya

ANNUUR NEW.indd 2

Mafundisho ya Qur'an/Uwanja wa Maarifa

Darsa Duara-1

Daawah (Ulinganizi) ili


kuweza kuubadili Umma
ni kazi tukufu ya kuweza
kuuongoza Umma kwa
kuokoa kutoka kwenye
minyororo ya utumwa
wa mfumo wa maisha ya
Kitwaaghuut ambao ni
giza la dhuluma, ufisadi,
utapeli, hadaa, Shirki, nk.
Na kupelekea kuweza
kuishi maisha ya uadilifu,
haki, insafu, utulivu na
amani ya kweli ya hapa
ulimwenguni na kesho
Akhera.
Hali hiyo itaufanya
Umma wa Kiislamu
kuweza kufikia lengo,
Dhima
na
Jukumu
lakuletwa kwao hapa
ulimwenguni na Allah
(s.w.).
Dalili: Amesema Allah
(s.w.): Mwenyezi Mungu
ni Mlinzi wa wale
wa l i o a m i n i . H u wa t o a
gizani na kuwaingiza
katika mwangaza. Lakini
walio kufuru, walinzi wao
ni Mashet'ani. Huwatoa
kwenye mwangaza na
kuwaingiza gizani. Hao
ndio watu wa Motoni, na
humo watadumu. (Surat
Al- Baqara 2: 257).
Amesema Allah (s.w.):
Na pale Mola wako
Mlezi alipo waambia
Malaika: Mimi nitamweka
katika ardhi Khalifa
(mfwatizi), wakasema:
Utaweka humo atakaye
fanya uharibifu humo
na kumwaga damu, hali
sisi tunakutakasa kwa
sifa zako na tunakutaja
kwa utakatifu wako?
Akasema:
Hakika Mimi nayajua
msiyo yajua. (Surat AlBaqara 2: 30).
Yeye ndiye aliye
mtuma Mtume wake
kwa uwongofu na Dini ya
Haki, ili aitukuze juu yadini
zote. Na Mwenyezi
Mungu anatosha kuwa
Shahidi. (Suratul Al Fath'I 48: 28).
Amesema Allah
(s.w.):Sikuwaumba
majini
na watu ila
waniabudu Mimi. (Surat
Adh-dhaariyaat 51: 56).
Na amesema Allah
(s.w.):Na kwa hakika
kwa
kila
umma
tuliutumia Mtume
kwamba: Muabuduni
Mwenyezi Mungu, na
muepukeni Shetani. Basi

kati yao wapo alio waongoa


MwenyeziMungu.
Na kati yao
wapo
ambao ulio wathibitikia
upotovu. Basi tembeeni
katika ardhi, muangalie
ulikuwaje mwisho wa
wanao kanusha. (Suurat
An Nahl 16: 36).
Kwa hivyo, kazi ya
Harakati za kutaka
kuubalidi Umma ili uweza
kuishi Kiislamu ni kazi
Tukufu. Ni kwamba
ina kanuni, miiko, sheria,
tararibu na muongozo
wake. Endapo kitu
kimoja kati ya hivyo
kitakosewa, kuvunjwa,
na au kukeukwa itakuwa
Harakati pasipo na tija.
Moja
ya
kanuni
hizo ni kufanya kazi
kamaummah. Si kazi
ya kila mtu kivyake. Na
katika silka aliyoumbwa
nayo mwanadamu ni
kwamba hawezi kufanya
Harakati zake zozote iwe
ni za kimaisha au za
kijamii bila kufungamana
na watu wengine; kwani
watu hao wanakuwa ni
msaada kwake wa kuweza
kufikia malengo yake
kwa Tawfiq ya Allah
(s.w.).
Dalili: Amesema Allah
(s.w.): Hakika rafiki yenu
mlinzi ni Mwenyezi
Mungu na Mtume wake
na walio amini, ambao
hushika Sala na hutoa Zaka
nao wananyenyekea.
Na atakaye fanya
urafiki na Mwenyezi
Mungu na Mtume wake
na walio amini, basi hakika
kundi la Mwenyezi Mungu
ndilo lenye kushinda.
(Suurat Al-Maida 5: 55-6).
Swali la msingi sasa
hapa linakuwa hao
walioamini na ambao
wapo tayari kufanya kazi
ya Allah kwa ikhlas,
wanapatikanaje?
Ukiwa wewe mtu
binafsi wa kufanya
kazi ya kupigania Dini,
unawapataje wenzako
ambao nao watakuwa
na ikhlas, wa kufanya
nao kazi?
(Abu Saumu, Kombo
Hassani Kidumbu- E-Mail:
hassanikombo@yahoo.
com, 0714 720 965 Mahali:
Mikanjuni,Tanga.)

AN-NUUR

RABIUL AWWAL 1437, IJUMAA JANUARI 8 - 14, 2016

JAWABU CHEMSHA BONGO NAMBA: 33


A

Q A R

M U H A

M A

D R

U R

U L

A L

M U H A

M A

A D U M A

O O D

H A

O N S

H A

O O D

A B A

W A

H H I

H T

A I

N U

H A

H A

M U S

MASUALA
1.Itaje Sura inayotaja juu ya matunda mawili? Jawabu : Attin.
2.Jina kamili la Imam Shafi. Jawabu : Muhama Idrissa.
3.Sura ipi ya Quran inayomalizia kwa majina ya Mitume wawili? Jawabu :
Suratul Al Alaa.
4.Alipohama Mtume Muhammad (SAW) Makka kwenda Madina alimtaka
sahaba yupi alale kwenye kitanda chake? Jawabu : Ali Abi Talib.
5.Suratul Faatiha ina aya ngapi? Jawabu : 7.
6.Ashuraa ipo katika mwezi gani wa Kiislamu? Jawabu : Muharam.
7.Mtume Hud (AS) alitumwa kwa Umma upi? Jawabu : Ad.
8.Mtume Saleh alitumwa kwa Umma upi? Jawabu : Thamood.
9.Mtume Mussa alifwatana na Mtume gani kwenda kukabiliana na Firauni?
Jawabu : Haroon.
10.Jina la ngamia Mtume Muhammad (SAW) alimpanda alipoingia Madina?
Jawabu : Kaswah

CHEMSHA BONGO: 34

Weka duara kwenye jawabu ilio sawa. Jawabu kamili wiki ijayo.

N S

O A

H U A

W A

U L

T U

D A

K D

H S

H I

U M A

M Z

A U

W I

Y D

M H E

D T

H M A

53 A

54 I

M Y

10 E

U
A

H I

H M

M A

H M I

H T

H A

N E

MASUALA
1.Jina la kitabu cha Hadithi kilichokusanywa na Imam Malik kinaitwa:
Muwatta, Bukhari, Riyadh Salihina.
2.Sahaba yupi aliotajwa kwa jina katika Quran?
3.Taja jina la mava ambalo wamezikwa Masahaba na ambalo hadi sasa
wanazikwa watu.
4.Taja jina kati ya wake wa Mtume Muhammad (SAW) aliokuwa na umri
mdogo na alikuwa sio mjane.
5.Mtume Muhammad (SAW) alipohajiri kwenda Madina alikuwa na umri
gani?
6.Mtume Muhammad (SAW) alipohajiri kwenda Madina aliishi Madina
kwa miaka mingapi kabla ya kufariki?
7. Shahidi wa mwanzo kuuwawa katika Uislamu alikuwa ni: Syd Hamza,
Bibi Sumayah au Bilali (RA).
8.Mtumwa wa mwazno kusilimu?
9. Taurat aliteremshiwa Mtume gani?
10.Nimrood aliishi katika zama za Mtume yupi?

Jee Unajua?

1.Uwanja wa ndege wa Paro uliopo Bhutan ni mmoja kati ya viwanja vya


ndege vilivyo hatari duniani, pale inapotaka kutuwa ndege abiria hupewa
dawa ya kutopata kushtuka. Marubani 8 tu ambao huruhusiwa kuendesha
ndege katika kiwanja hicho, hairuhusiwi ndege kutuwa katika kiwanja
hicho nyakati za usiku. Uwanja wa ndege huu upo baina ya nyumba na
milima: http://www.curiosityaroused.com/world/12-most-dangerousairports-to-avoid/
2.Nchini Canada pesa ijuliknayo Penny imekuwa haitumiwi tena pesa
iliyodumu kutumiwa kwa miaka 154, maamuzi hayo yamekuja kutokana
na gharama kubwa inayopatikana katika utengenezwaji wake: http://www.
curiosityaroused.com/culture/what-are-pennies-made-of/
3.Inakadiriwa kuwa watu wengi duniani wana simu za mkononi kuliko
kuwa na vyoo majumbani mwao, aidha inasadikiwa thuluthi ya skuli zote
ziliopo duniani huwa hazina vyoo: http://water.org/water-crisis/watersanitation-facts/
4.Kila siku hufa watoto 500 duniani kote kwa kukosa maji safi na salama:
http://waterfortheworld.net/index.php?id=12
5.Makadirio yanaonyesha kuwa dunia hii tuliopo asilimia 72 imezungukwa
na maji na kati ya asimia hio ya maji ni asilimia 97 ni maji ya chumvi. http://
www.livescience.com/29673-how-much-water-on-earth.html
6.Watu Bilioni moja maji safi na salama kwao ni ndoto: http://thewaterproject.
org/water_scarcity
7.Maji hayana mipaka, inakisiwa kuwa kuna nchi 148 zinagawanya maji
na nchi nyengine : http://www.unwater.org/water-cooperation-2013/watercooperation/facts-and-figures/en/
8.Ziwa Victoria lina kilomita za mraba 69,485 km2 ni ziwa la 3 kwa ukubwa
duniani : http://10mosttoday.com/10-largest-lakes-in-the-world/
9.Yajuwe maziwa yalio makubwa duniani ikiwa Afrika imo kwenye listi
hio kuwa na maziwa mengi makubwa : http://www.factmonster.com/ipka/
A0001777.html
Mto Nile ndio ulio na masafa marefu ukiwa na kilomita 6,695 ukianzia
kutokea Afrika Mashariki : http://www.primaryhomeworkhelp.co.uk/
rivers/longest.htm

1/7/2016 3:17:01 PM

Habari

AN-NUUR

RABIUL AWWAL 1437, IJUMAA JANUARI 8 - 14, 2016

Maimamu wataka Dk. Shein aheshimu kura za wananchi


Na Mwandishi Wetu

HAKUNA Shura baada


ya Shura, bali kutekeleza
yaliyoamuliwa katika
Shura.
Huo ndio msimamo wa
Jumuiya ya Maimamu
( JUMAZA) na Taasisi
nyingine za Kiislamu
Zanzibar.
Kwa mtizamo huo
wa Kifiqihi ya Kiislamu
katika uongozi, JUMAZA
wanasema kuwa hakuna
uchaguzi baada ya
uchaguzi kwa sababu
wananchi walishafanya
maamuzi.
Wa k a s e m a k u wa
kinachotakiwa ni
kukamilisha utekelezaji
wa maamuzi ya wananchi,
na sio kuwapuuza na
kuyatupilia kwa mbali na
kuja na uchaguzi mpya.
Kwa upande mwingine,
imeelezwa kuwa
madhumini ya Mapinduzi
haikuwa kuiweka CCM
madarakani milele bali
kurejesha madaraka kwa
wananchi.
Wa n a o r e j e a k a t i k a
madhumuni ya mapinduzi
Na Mwandishi Maalum
UCHAGUZI wa nini
wakati kilichosababisha
Jecha kutangaza kufuta
uchaguzi, ni msimamo wa
wahafidhina wa CCM
kwamba maadhali SMZ
ilipatikana kwa mapinduzi,
h a i we z i k u t o l e wa k wa
vikaratasi vya kura.
Hayo ni maoni ya baadhi
ya Wazanzibari kufuatia
kauli ya Makamo wa Pili
wa Rais wa Serikali ya
Mapinduzi, Zanzibar, Balozi
Seif Idi, na CCM Zanzibar
wakiwatangazia wana-CCM
na wananchi wa Zanzibar
kuwa wajiandae kwa marudio
ya uchaguzi.
Hivi karibuni uongozi
wa CCM Zanzibar umetoa
kauli ukishadidia kuwa
lazima kuwepo uchaguzi wa
marudio na kwamba chama
hicho kipo tayari na hivyo
kuwataka wanachama wake
kujiandaa ili kupata ushindi
wa kishindo.
Hata hivyo, hoja za
Wazanzibari walio katika
vyama vya upinzani ni kuwa
unaodaiwa kuwa mkwamo
wa kisiasa haupo, na kama
upo unatokana na CCM
kugoma kukubali matokeo
ya uchaguzi ambapo dhahiri
kilishindwa.
Na hiyo ni kutokana na
msimamo wao wa kihafidhina
kwamba hawawezi kutoa
nchi kwa vikaratasi.
Kama huo ndio msimamo,
yanini kupoteza pesa kurejea

ANNUUR NEW.indd 3

kuwa ndio sababu ya


Jecha kufuta uchaguzi,
walisema kwamba kama
kweli hoja ni dosari hizo,
basi utumike utaratibu
wa kisheria ambao ni
kurudiwa uchaguzi kwa
majimbo tu yenye dosari.
J U M A Z A
inashangazwa sana na
hatua ya kufuta Uchaguzi
huu iliyochukuliwa na
Mwenyekiti wa Tume ya
Uchaguzi, Jecha Salim
Jecha. JUMAZA inauliza
kwanini wakati tulipokuwa
na kasoro kubwa zaidi
katika chaguzi za mwaka
1995, 2000, 2005 na 2010
Uchaguzi haukufutwa na
kutakiwa kurejewa tena iwe
Uchaguzi wa mwaka 2015
DKT. Ali Mohamed Shein (kulia), Maalim Seif Sharif Hamad (kushoto) akisalimiana tu? Na jee, kama uchaguzi
utakaorejewa nao ukawa na
na Balozi Seif Idd. Katikati yao ni Mhe. Pandu Amiri Kificho.
kasoro zitakazolalamikiwa,
na kutaka yaheshimiwe lao la tarehe 6 Januari machafuko na hata kufa utafutwa tena? Tutafanya
wanasema kuwa, ni jambo mwaka huu wamesema watu.
chaguzi ngapi kwa mtindo
la kusikitisha na ambalo kuwa hawaoni kuwa
Walitoa pia mifano ya huu?
halikuwa linategemewa ni busara kurejewa kwa nchi kadhaa za Kiafrika
Hoja hii ya JUMAZA
kuwa CCM watatumia Uchaguzi uliofanyika kwa a m b a p o d e m o k r a s i a ndiyo pia inayotolewa
nguvu kutaka kub ak i ufanisi na kukamilika.
ya kuheshimu kura wa na Mwanasheria Fatma
madarakani kwa mtindo
Aidha walirejea historia wananchi ilivurugwa.
Karume akisema kuwa
wa kuvuruga katiba na ya nyuma na kuonyesha
Wakitoa maoni yao juu k a m a k u n a m a h a l i
kuendeleza ubaguzi.
jinsi ghilba za marudio ya zilizodaiwa kuwa dosari
JUMAZA katika tamko ya uchaguzi zilivyoleta ambazo ndio zinatajwa
Inaendelea Uk. 8

Uchaguzi wa nini wakati serikali


haitolewi kwa karatasi za kura?
Moja kwa Sita bado kitendawili tata
Huenda kikawafumbua macho wengi
Jussa hajasema kweli. Anapiga siasa

Alhaji Ali Hassan Mwinyi

Mhe. Ismail Jusa Ludu

uchaguzi ambapo matokeo


yanajulikana kwamba lazima
CCM itangazwe mshindi
na isipotangazwa, uchaguzi
unaharibiwa? Alisema na
kuuliza bwana mmoja wa
maskani iliyo jirani na ofisi za
CUF Mtendeni.

Kama ulivyofanyika
ubabe kufuta uchaguzi chini
ya mtutu wa bunduki kwa
staili ya umafia, wafanye
hivyo hivyo kumtangaza mtu
wao wa CCM wanayemtaka,
wasiharibu kodi za wananchi
na muda wao kuendesha

kiini macho cha uchaguzi.


Aliongeza.
Wakati hayo yakijiri, Rais
Mstaafu, Alhaji Ali Hassan
Mwinyi, aliye katika jopo la
wazee na Marais wastaafu
wanaodaiwa kuwa na
mazungumzo na Katibu
Mkuu wa CUF, Maalim
Seif Shariff Hamad katika
j i t i h a d a z a k u i k wa m u a
Zanzibar katika unaodaiwa
kuwa mkwamo wa kisiasa,
amejikuta akikabiliwa na
t u h u m a a k i d a i wa k u wa
haitakii mema Zanzibar, bali
kuangalia masilahi binafsi na
ya CCM.
Hiyo ni kutokana na kauli
zake za hivi karibuni ambazo
zinadaiwa kuwa zinayaweka
masilahi ya Zanzibar na
Wazanzibari mbali kabisa.
Hiyo ni pamoja na ile kauli
yake akihutubia hadhara ya
sherehe za Maulid ya Mtume
Muhammad (SAW) akisema

Zanzibar ni raha tupu, huku


wakiwataka Wazanzibari
wasitafute mambo mengine,
b a d a l a ya k e wa i t a z a m e
Syria inavyovurugwa kwa
vurugu.
Kauli hiyo imetafsiriwa na
wengi kwamba ni kushadidia
watu kubaki na CCM na
Serikali yake na kwamba
kujali kura za wananchi
walizopiga katika uchaguzi
uliopita, ndio kutafuta ya
Syria.
Wengi wanashangaa, kwa
Mzee Mwinyi kuona kuwa
suala la kupuuza kura za
wananchi na kufuta uchaguzi
uliogharimu mabilioni ya
kodi za wananchi ni matatizo
madogo madogo ambayo
hayazuii Zanzibar kuwa raha
tupu!
Kama uzee ni dawa, basi
uzee wa mwenzetu huyu,
umekuwa sumu inayouwa
Wazanzibari na Zanzibar
kama nchi, alisema mzee
mmoja.
Wa k a t i h u o h u o , k i l e
kitendawili cha Moja
kwa Sita, bado kimekuwa
kikiwatatiza wengi.
Hoja inayotolewa ni kuwa
inakuwaje jambo la chama
likawa la mtu mmoja.
Pekee anakwenda katika
mazungumzo utadhani
anawakilisha kampuni
binafsi.
Kadiri ninavyowatizama
hawa CUF, wananitia
wasiwasi. Suala la matokeo
ya uchaguzi sio la mtu, sio
Inaendelea Uk. 8

1/7/2016 3:17:09 PM

Tahariri/Habari

AN-NUUR

S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786


Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM.
www.annuurpapers.co.tz
E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk
Ofisi zetu zipo: Manzese Tip Top
Usangi House, barabara ya Morogoro, D'Salaam

Misamaha ya kodi taasisi za Dini:

Lengolakenininananianafaidika?

MISAMAHA ya
kodi isiyoleta tija
inayotolewa na
serikali kwa taasisi,
makampuni na
wafanyabiashara
wakubwa kwa
ujumla, ni jambo
ambalo limekuwa
likilalamikiwa kwa
muda mrefu na
wananchi, wabunge
na wanahatakati wa
kijamii hapa nchini.
Kila
mwaka
wabunge wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano
Ta n z a n i a h u p i t i a
na kuchanganua
kwa makini bajeti
ya Serikali. Lakini
misamaha ya kodi kwa
upande mwingine,
haipati nafasi sawia
ya kupitiwa vizuri
Bungeni, hivyo kuwa
vigumu kufahamika
bayana ni kiwango
gani cha misamaha
k i n a c h o t o l e wa n a
imesababisha hasara
kiasi gani kwa serikali,
au imewasaida vipi
wananchi.
Hata hivyo mwaka
2009/10 peke yake,
ilibainika kuwa
asilimia 2.3 ya pato
la taifa au TZS 695
b i l i o n i z i l i t o l e wa
kama misamaha ya
k o d i . U k u b wa wa
kiwango cha fedha
kinachohusishwa na
misamaha kiliibua
maswali kuhusu
makusudi ya motisha
hizi na iwapo kiwango
kinachotumika kinafaa
kutolewa.
Kwa kuwa misamaha
ya kodi ilionekana
kuwa mikubwa
mno kwa nchi
ambayo inakabiliwa
na changamoto ya
kukusanya fedha za

ANNUUR NEW.indd 4

kutosha kugharamia
bajeti yake, mwaka
2009 Serikali ya
awamu ya nne ya Rais
mstaafu Jakaya Mrisho
Kikwete, ilieleza
Bungeni kwamba
imefuta misamaha ya
kodi kwa mashirika
na taasisi za dini hapa
nchini kama moja ya
hatua ya kuongeza
mapato.
Serikali ilieleza
kwamba hatua yake
hiyo, ilitokana na
kubaini kukithiri kwa
matumizi mabaya ya
misamaha ya kodi
inayotolewa katika
taasisi hizo za kidini.
Tulishuhudia hoja
hiyo ikiibua mvutano
mkubwa kati ya
serikali na viongozi
wa dini ambao ndio
wanaosimamia
mashirika na
taasisi hizo za dini
zinazosamehewa kodi.
Viongozi mbalimbali
wa dini hasa wa
Kikristo, walijitokeza
kupinga kwa nguvu
hatua hiyo ya serikali
ambapo tulishuhudia
wakilazimika kuweka
kambi Dodoma, ili
kushinikiza kuzuiwa
hoja hiyo ya kufutwa
misamaha Bungeni.
Kweli, shinikizo lao
lilifaulu na hatimaye
hoja ile ilikwama.
Serikali ikarejesha
misamaha kwa sharti
la kuwataka viongozi
hao kuwa waadilifu
kwa misamaha
wanayopewa na
serikali.
Tunafamu kwamba
lengo la serikali
kuweka misamaha
ya kodi kwa taasisi
na mashirika ya
dini, lilikuwa ni

kuyawezesha
mashirika na taasisi
hizo kuisaidia serikali
kutoa huduma
nafuu za kijamii kwa
wananchi kama vile
kutumika kugharimia
afya, maji na elimu nk.
Lakini pamoja
na kuwepo kwa
misamaha hiyo, bado
huduma za kijamii
katika taasisi hizo
zimeendelea kuwa
za ghali kama ilivyo
katika taasisi za binafsi.
Hakuna nafuu yeyote
inayopatakina hadi
sasa. Ada katika shule
zao ni sawa au zaidi
ya shule za binafsi na
serikali. Gharama za
huduma za matibabu
katika hospitali zao
hazina tofauti na zile
za binafsi. Ndipo
linapokuja swali, nini
sababu ya misamaha
hii na ni nani anafaidika
na misamaha hii?
Tunaamini kabisa
kwamba, fursa hii
ya s e r i k a l i k u t o a
misamaha ya kodi kwa
taasisi na mashirika ya
dini, ilikuwa ni kwa
lengo la kuisaidia
serikali kufikisha
huduma nafuu kwa
Mtanzania. Kwamba
mashirika hayo
yaweze kupata uwezo
wa kutoa huduma
kwa wananchi kwa
gharama nafuu. Lakini
hali imekuwa sivyo.
Kimsingi, kwa jinsi
hali ilivyo sasa ya
huduma za kijamii
zinazotolewa katika
taasisi hizi za dini,
hakuna tena sababu
ya kuwepo misamaha
ya kodi, maana lengo
limekiukwa.
Wanaofaidika na
misamaha hii bila
shaka ni hao hao
v i o n g o z i wa d i n i
na marafiki zao,
lakini sio waumini
wala wananchi
wanaozunguka taasisi
husika.
Kwa
maana
nyingine, tuna imani
kwamba serikali
inatambua kuwa
fursa waliyoitoa,

AN-NUUR

RABIUL AWWAL 1437, IJUMAA JANUARI 8 - 14, 2016

inawanufaisha
wachache, tena
wenye uwezo badala
ya kunufaisha wengi
ambao ni makabwela.
Ndio maana
walipochunguza,
wakangundua
udhaifu, wakafuta
msamaha huo kwa
kuwa kihalisia ulikuwa
hauna maana kwa
mwananchi na kwa
hivyo hauna madhara
ukiondolewa.
Tukiacha suala la
misamaha ya kodi,
bado kuna nafuuu
nyingine wanayopata
mashirika na taasisi
za kidini hasa katika
sekta ya Afya. Kwa
muda mrefu serikali
imekuwa ikitoa
ruzuku katika vituo
vya afya na hospitali
za taasisi za kidini,
ili kuweza kutoa
huduma ya afya kwa
wananchi.
Pamoja na kutolewa
ruzuku hizo, bado
tunaona hospitali
hizo zikiendeshwa
kibiashara zaidi
huku huduma zake
z i k i e n d e l e a k u wa
za gharama kubwa
i k i l i n g a n i s h wa n a
hospitali za serikali,
ambazo
nazo
huendeshwa kwa
fedha za serikali.
Tunaona kuna haja
ya serikali kufikiri upya
kuhusu misamaha ya
kodi kwa taasisi zetu
za dini.
Tunaona siku hizi
v i o n g o z i wa d i n i
wakiiba sadaka za
waumini. Wakitajirika,
wakijenga mahekalu
yao binafsi kwa
sadaka, wakinunua
magari ya thamani
kwa matumizi yao
binafsi kwa sadaka
na kwa kutumia
fursa za misamaha
ya kodi waliyo
nayo. Wanajenga na
kuendesha shule zao
binafsi kwa mgongo
wa taasisi za kidini,
wakipata misamaha
ya kodi lakini huduma
zikiwa juu zaidi kwa
Mtanzania.
W e
n
g
i

wameshindwa kuwa
waadilifu kiasi cha
kuaminiwa kutumia
fursa ya misamaha wa
kodi kutoka serikalini
ili kuihudumia jamii.
Tunaona hata serikali
inapogusa eneo hilo
la kuondoa misamaha,
viongozi hawa
hungaka na kuwa
wakali kama mbogo,
lakini wanakiri
kwamba kuna udhaifu
j a p o wa o n a d a wa
sio serikali kufuta
misamaha hiyo.
Wengi wanaficha
uhalisia wao,
wakihadaa kwamba
inachotakiwa
kufanya serikali ni
kuwatafuta wakosaji
na kuwachukulia
hatua, lakini si kufuta
misamaha ya kodi!.
L e o t u k i a m b i wa
taasisi za dini ni
miongoni mwa zile
kampuni zinazotakiwa
kuwasilisha nyaraka
kwa ajili ya kuhakiki
kama zinalipa
ushuru wa Bandari
uliosababisha serikali
kupoteza kiasi cha
shilingi bilioni 48
haishangazi.
Ta y a r i t u m e o n a
katika orodha
iliyotolewa na TPA
Jumatano ya Desemba
30, 2015 ambapo taasisi
na mashirika haya ya
dini, tena makubwa
na yanayoaminiwa
yakiwemo.
Dalili kama
hii inadhihirisha
wazi kwamba hata
hiyo misamaha ya
kodi haiwezi kuwa
inatumika vizuri hata
baada ya kutolewa
onyo na serikali 2009.
Ni ushauri wetu kwa
serikali kwamba, kwa
hali tuliyofikia ambapo
mashirik a ya d ini
yamekuwa yakifanya
biashara kama taasisi
au kampuni nyingine
za kibiashara, iangalie
upya kipengele hiki
cha misamaha ya kodi.
Vinginevyo kuwe na
utaratibu madhubuti
wa kuhakikisha kuwa
malengo ya misamaha
hiyo yanafikiwa.

1/7/2016 3:17:09 PM

5
MWIGIZAJI
maarufu wa filamu
za Hollywood nchini
Marekani Samuel
Jackson, amesema
hivi sasa waumini
wa dini ya Kiislamu
nchini humo
wanabaguliwa kama
wanavyobaguliwa
watu Weusi.
Samuel Jackson
aliyasema hayo hivi
karibuni kwamba
waumini wa dini
ya Kiislamu nchini
Marekani kwa sasa
wamekuwa kama watu
Weusi kwa kubaguliwa
na wanaonekana
hivi sasa kuwa ni
Weusi wapya wa
Kimarekani, ambapo
hufanyiwa dhulma
na kudharauliwa na
daima hawapewi haki
zao za msingi.
Aidha mwigizaji
huyo aliashiria
matukio ya kigaidi
ya hivi karibuni
yaliyotokea Paris

Habari za Kimataifa

AN-NUUR

RABIUL AWWAL 1437, IJUMAA JANUARI 8 - 14, 2016

Waislamu wanabaguliwa
kama watu weusi Marekani
na California, kuwa
matukio hayo yalikuwa
ndio ufunguo wa
kushadidia hali
hiyo ya ubaguzi na
kuwanyanyapaa
Waislamu.
Alimalizia maelezo
yake kwa kusema
kuwa baada ya
matukio hayo nchini
Marekani na Ufaransa,
siku hadi siku
kumekuwa kukitokea
suala la kuvamiwa
Misikiti na kuichoma
moto, kuwanyanyapaa
Waislamu katika
mataifa hayo na
mataifa mengine katika
bara la Amerika na
Ulaya. ABNA.

SAMUEL Jackson

Bunge Marekani laishtukia NSA kwa kudukuwa mawasiliano yake

KAMATI ya
Uchunguzi ya Baraza
la Wawakilishi la
Marekani imelitaka
Shirika la Usalama
wa Taifa NSA, kutoa
taarifa kuhusu ripoti
kwamba shirika hilo
lilinasa mawasiliano
kati ya maafisa wa
Waisrael na wabunge
wa Marekani.
Katika barua
iliyotumwa kwa
Mkurugenzi wa NSA
Michael Rogers,
Mwenyekiti wa Kamati
ya Usimamizi Jason
Chaffetz na Mwenyekiti
wa Kamati Ndogo Ron
DeSantis, walisema
habari iliyotokea katika
toleo la Jumanne la
jarida la Wall Street,
iliibua maswali kuhusu
utaratibu unaofuatwa
na wafanyakazi wa
NSA katika kuanisha
iwapo mawasiliano
yaliyonaswa
yanawahusisha
wabunge wa Bunge la
Marekani Congress.
Jarida hilo
likiwanukuu maafisa
wa sasa na wa
zamani wa serikali
ya Marekani, lilisema
NSA ilikuwa ikimlenga
Waziri Mkuu wa
Israel Benjamin

ANNUUR NEW.indd 5

MKURUGENZI wa NSA
Michael Rogers.

Netanyahu na maafisa
wengine wa Israel,
baada ya kuanzisha
kampeni yao katika
Bunge la Marekani
kujaribu kukwamisha
makubaliano ya
nyuklia ya Iran.
Sambamba na kunasa
mawasiliano ya maafisa
wa serikali ya Israel,
uchunguzi huo ulinasa
pia taarifa za ndani
kuhusu juhudi zao
za uraghibishi, ikiwa
ni pamoja na baadhi
ya mazungumzo
yao na wabunge wa
Congress na makundi
ya Wayahudi wa
Marekani, liliripoti

jarida hilo.
Barua kutoka kwa
Chaffetz na DeSantis,
wote kutoka chama cha
Republicans, ilimtaka
Rogers kuwapatia
taarifa juu ya utaratibu
wa shirika hilo kuamua
iwapo mawasiliano ya
wabunge yamenaswa
katika udukuzi wa
NSA, na kwa kiasi
gani wafanyakazi wa
shirika hilo wamekuwa
wakitoa taarifa
hizo kwa mashirika
mengine ya Marekani
pamoja na Ikulu (White
House).
Kamati hiyo pia
iliitaka NSA iipe
maelezo mafupi
kuhusu wafanyakazi
wake. Jarida la Wall
Street liliripoti kuwa
NSA ilifuata muongozo
unaozitaka ripoti
zake za uchunguzi
kuondoa majina
yoyote ya Wamarekani,
wakiwemo wabunge
waliotajwa katika
mawasiliano ya
Waisrael yalionaswa.
Ripoti ya Jarida hilo
ilisema hata baada ya
Rais Barack Obama
kutangaza miaka
miwili iliyopita kuwa
angeweka ukomo
kwenye kuyachunguza

mataifa washirika,
NSA iliendelea
kumchunguza Waziri
Mkuu wa Israel
Banjamini Netanyahu,
pamoja na maafisa wa
ngazi za juu nchini
humo.
White House ilikataa
kuzungumzia shughuli
zozote mahususi za
kijasusi zilizofanywa
na Marekani. Lakini
maafisa wa White
House walisema
Marekani haifanyi
uchunguzi nje ya nchi,
mpaka pawepo na
sababu ya usalama wa
taifa inayoisukuma
kufanya hivyo na
kusisitiza kuwa, kanuni
hiyo inatumika kwa
viongozi wa dunia na
raia wa kawaida.
Na katika juhudi
za kuonyesha kuwa
uhusiano wa kiulinzi
kati ya Marekani na
Israel haujaathiriwa
na ripoti hizo, maafisa
walibainisha kuwa
maafisa wa Marekani
walisafiri kwenda Israel
mwezi huu kuanzisha
tena mazungumzo ya
makubaliano mapya
ya miaka 10 kuhusu
msaada wa kijeshi wa
Marekani. DW.

Nkurunziza kurejesha
mchezo wa hatari
Burundi
WAKATI mzozo nchini
Burundi ukiendela
kupanuka zaidi,
tayari kuna harufu ya
kuibuka mzozo mbaya
wa ukabila huku Rais
Pierre Nkurunziza
akiwa ameshatishia
kukabiliana na wanajeshi
wa kusimamia amani wa
Umoja wa Afrika.
Rais Nkurunziza
amesema kikosi cha kulinda
amani cha Umoja wa Afrika
ambacho kimependekezwa
kwenda kulinda amani
nchini humo, kitakiuka
katiba ya Burundi ambayo
inapinga uingiliaji wowote
iwapo kuna serikali
inayofanya kazi na hakuna
vita kati ya pande mbili.
Rais huyo amesema
Burundi itachukulia hatua
hiyo ya kupelekewa vikosi
vuya Afrika nchini kwake
kuwa ya uvamizi na ikiwa
wanajeshi wa kigeni
wataingia nchini humo,
atawakabili.
Tayari kuna taarifa
kwamba Rais Nkurunziza,
ambaye anatoka kabila
la Hutu anaonekana
kuwatenga maafisa kijeshi
wa Kitutsi, ambao utiifu
wao unatiliwa shaka.
Baadhi ya Watusti
wamedaiwa kuanza pia
kuliasi jeshi na tayari Kanali
mmoja ametangaza kuunda
kundi jipya la waasi wiki
iliyopita.
Kuasi kwa Luteni Kanali
Edouard Nshimirima,
kumeeneza uvumi kuwa
wanajeshi wengine Watusti
watamfuata na kusababisha
kuzidi kwa mzozo huo na
umwagikaji mkubwa wa
damu.
Serikali ya Burundi
imeilaumu Rwanda ambayo
ina makabila sawa na
Burundi na inayoongozwa
na Rais Mtutsi Paul
Kagame kwa kusajili na
kutoa mafunzo kwa waasi
wanaompinga Nkurunziza,
madai ambayo serikali ya
Rwanda imeyakanusha.
Bado ulimwengu
unakumbuka kwamba
zaidi ya watu 800,000
kutoka kabila la Watsusi na
Wahutu wenye msimamo
wa wastani waliuawawa
nchini Rwanda wakati wa
mauwaji wa halaiki 1994.

RAIS Pierre Nkurunziza.

1/7/2016 3:17:11 PM

Hoja ya Juma Kilaghai

AN-NUUR

RABIUL AWWAL 1437, IJUMAA JANUARI 8 - 14, 2016

Ulimwengu wa kemikali na madhara yake


KAMA una tabia ya
kufuatilia mambo
unaweza ukawa
umegundua kuwa
hivi sasa watu wengi
hawana kumbukumbu
vizuri. Kinachotisha
zaidi ni kwamba kundi
kubwa la hawa watu
ni vijana chini ya umri
wa miaka thelathini.
Nasema hali hii inatisha
zaidi kwa sababu
kimazoea inaaminika
kuwa kupungukiwa na
kumbukumbu ni zao
la uharibifu wa seli za
ubongo na mishipa ya
fahamu unaosababishwa
na umri kusonga mbele.
Kwa hiyo ni kitu gani
kinaendelea? Ni kitu
gani kinasababisha vijana
ambao kinadharia bado
bongo zao na mishipa
ya fahamu ni safi nao
wakumbwe na tatizo
ambalo chimbuko lake
ni uchakavu? Kuna tafiti
zimebainisha kuwa moja
ya sababu kubwa sana
za hali hii ni maisha
ya kisasa ambayo
yamesababisha kundi
kubwa la kemikali hatari
kutumika katika maisha
ya kila siku. Kemikali
hizi zinatajwa kama
ni sumu kwa seli za
ubongo pamoja na zile
za mishipa ya fahamu.
Baadhi ya kemikali hizi
ni madini ya alminium;
madini ya fluorine; na
dawa za kupunguza
lehemu (cholesterol)
mwilini zinazoitwa
statins.
Maisha ya kisasa
yameongeza wingi wa
madini ya alminium
tunayoingiza kwenye
miili yetu kwa kiasi
kikubwa sana. Ongezeko
hili ni kupitia maji ya
kunywa, hususan yale
yanayosambazwa na
mamlaka za maji na
yale ya chupa; dawa
mbalimbali, hususan
kundi kubwa ya zile
za kuzimua tindikali
tumboni (antiacids);
vipodozi vya kuzuia
jasho kwenye makwapa
na kuzuia harufu ya
kikwapa (antiperspirants
and deodorants); na
mabaki yanayoingia
kwenye chakula
kilichopikwa na
kuhifadhiwa na vyombo
vilivyotengenezwa kwa
madini alminium.
Tafiti zingine
zimebainisha kuwa

ANNUUR NEW.indd 6

Ni kitu gani kinaendelea? Kumbukumbu inazidi kuwa bidhaa adimu!

moja ya sababu nyingine


kubwa za watu kupoteza
kumbukumbu ni
madini ya fluoride.
Mara nyingi madini
ya fluoride huingia
kwenye miili yetu kupitia
matumizi ya chai; dawa
za mswaki; maji ya
kunywa; na baadhi ya
madawa ya kifamasia,

(rosuvastatin); Zocor
(simvastatin) and Vytorin
(simvastatin/ezetimibe).
Kufuatia tafiti kadhaa
zilizohusisha makundi
makubwa ya watumiaji,
hatimaye mnamo mwezi
wa 2, mwaka 2012 taasisi
ya chakula na dawa ya
Marekani, FDA, ilitoa
orodha yenye maonyo

ghrelin kuwepo. Hii ina


maana kuwa unapokuwa
muda wote katika hali
ya kushiba seli zako za
ubongo zinazochakaa
hazifanyiwi ukarabati.
Upotevu wa seli nyingi
za ubongo kutokana na
kutofanyika ukarabati
inaweza pia kuwa chanzo
kimojawapo cha upotevu

hususan viua vijasumu


vikali vya kundi la
fluoroquinolones.
Kutokana na ubaya
wa fluoride, baadhi ya
serikali za nchi za Ulaya
kama Sweden, Norway,
Denmark, Ujerumani,
Italia, Ubelgiji, Austria,
Ufaransa, and Uholanzi
zimepiga marufuku
bidhaa zenye madini
hayo katika nchi zao.
Kumekuwa na
mvutano wa muda
mrefu kuhusu dawa
za kupunguza lehemu
(cholesterol) mwilini
zinazoitwa statins. Baadhi
ya watafiti wamekuwa
wakizihusisha dawa hizi
na madhara mengi ya
kiafya ikiwa ni pamoja
na watumiaji kupoteza
kumbukumbu. Baadhi
ya dawa hizi ni Lipitor
(atorvastatin); Crestor

mapya kwa watumiaji


wa dawa hizi kwamba
zilikuwa zinaongeza
uwezekano wa mtumiaji
kupata kisukari cha
ukubwani na kuugua
ugonjwa wa kupoteza
kumbukumbu.
Shibe iliyopindukia
nayo inaweza kuwa
tatizo jingine. Shibe
iliyopindukia ni ile
inayohusisha kifungua
kinywa cha kutosha,
chakula cha mchana cha
kutosha na chakula cha
usiku cha kutosha siku
saba kwa juma. Tafiti
zimebaini kuwa kuna
homoni inazalishwa
na mwili pale mtu
anapokuwa na njaa
inayoitwa ghrelin.
Tafiti hizi zimebaini pia
kuwa ukarabati wa seli
za ubongo haufanyiki
bila ya hii homoni ya

wa kumbukumbu.
Kutopata muda wa
kutosha wa kupumzika,
hususan wakati wa
usiku, ni chanzo
kingine kikubwa cha
kumbukumbu dhaifu.
Kwa baadhi ya viumbe,
mwanadamu akiwemo,
usiku (kwa maana ya
kuingia giza) ni muda
mahsusi kwa ajili ya
kupumzika. Viumbe
hawa ni wale ambao
hawaoni gizani. Ni
dhahiri kuwa tofauti na
mababu zetu, hivi sasa
tumepunguza sana muda
wa kupumzika usiku
kutokana na msaada
wa mataa, hususan yale
yanayotumia umeme.
Kwa viumbe ambao
hawakuumbwa
kuhangaika usiku,
lakini wanafanya
hivyo kwa msaada wa

mwanga wa taa, bila


ya shaka wanadhuru
afya zao kwa kiwango
kikubwa. Sababu
kubwa ni kwamba kuna
homoni zinafanya kazi
gizani tu, na pale giza
linapokosekana, homoni
hizi hazizalishwi na
kwa maana hiyo faida
zinazooanishwa na hizo
homoni hazipatikani.
Moja ya homoni hizi ni
ile inayojulikana kama
Human Growth Hormon
(HGH). Homoni hii
huhusika na uwezeshaji
wa seli za mwili - ikiwa
ni pamoja na ubongo
- kukua, pamoja na
ukarabati wake. Bila
homoni hii mwili
hauwezi kuwa na misuli
iliyojengeka na mifupa
iliyojaza vizuri. Aidha
homoni hii hutusaidia
kupunguza kiwango cha
mafuta kinachohifadhiwa
mwilini, huimarisha
uwezo na hamu yetu ya
kufanya tendo la ndoa, na
huufanya mwili kuwa na
nguvu kwa ujumla. Hata
hivyo tafiti zimebaini
kuwa njia nyingine
zinazoweza kutusaidia
kuvuna homoni hii ni
kwa kufunga (kuacha
kula) na kufanya
mazoezi.
Msongo ni tatizo
lingine kubwa sana
linaloweza kuchangia
ongezeko la tatizo la
kumbukumbu hafifu.
Msongo pamoja na athari
zingine hupelekea mtu
akakosa usingizi. Kama
tulivyoona bila usingizi
mwili wako hauwezi
kuzalisha HGH, na bila
hii homoni uwezekano
wa seli zako za ubongo
kuzalishwa kwa kiwango
kinachotakiwa na kukua
inavyotakiwa unakuwa
mdogo.
Ubongo wako ni
raslimali muhimu sana
ambayo inatakiwa
ilindwe kwa kila hali.
Chukua hatua muafaka
kuhakikisha unalifikia
lengo hilo. Moja ya
hatua hizi ni kuondosha
au kupunguza
matumizi ya vitu vyote
vinavyotuhumiwa
kuharibu ubongo pamoja
na mishipa ya fahamu.

1/7/2016 3:17:13 PM

7
SHUKRAN zote
njema ni zake Allah
Taala, Mola Mlezi
wa ulimwengu
wote. Rehema na
amani zimwendee
mtume Muhammad
(Swallalahu Alayh
Wassalam), sahaba
zake, aali zake na wote
waliofuata sunnah
yake mpaka siku ya
Qiyaamah.
Ni takriban miaka
thelathini na sita sasa
tangu kutokea kwa
vita ya Tanzania na
Uganda, almaarufu
vita vya Kagera.
Ni vita ambavyo
vilipiganwa kati ya
mwaka 1978-1979.
Kutokana na utata
uliopatikana kufuatia
vita hivyo na ambao
mpaka leo wengi wetu
hawajui vema ni nani
aliyeanzisha vita ile,
nimeamua nieleze
kwa uchache kuhusu
vita hivyo. Tusafiri
pamoja na makala
ya Inocent Kasyate,
ya Julai 26, 2009,
ambayo nimeifanyia
marekebisho kidogo ya
lugha, kwa kuongeza
na kupunguza bila
kuharibu maudhui
yenyewe.
Nani Aliyeanzisha Vita Hivyo?
Je, ni Iddi Amini au Tanzania?
Kila mwaka nchi yetu
imekuwa ikisherehekea
kumbukumbu ya
mashujaa wa vita
ya Kagera. Ni tukio
linalokumbushia juu
ya ushiriki wa nchi
ya Tanzania katika
vita pekee kubwa
iliyoigharimu nchi yetu
kwa kiwango kikubwa
kabisa. Hebu kwanza
tuangalie mtizamo wa
nje ya Tanzania juu ya
chanzo cha vita ile:
Miaka thelathini na
sita iliyopita, serikali
ya kijeshi ya Uganda
ikiongozwa na Iddi
Amin ilipinduliwa
na muungano wa
majeshi ya wakombozi
ambao walikuwa ni
waasi waliokuwa
wakiishi nchini Kenya
na Tanzania katika
miaka ya sabini

ANNUUR NEW.indd 7

Makala

AN-NUUR

RABIUL AWWAL 1437, IJUMAA JANUARI 8 - 14, 2016

Vita vya Kagera

RAIS wa zamani wa Uganda Iddi Amin.


wakisaidiwa na jeshi la
Uganda. Kupinduliwa
kwa serikali ya
Iddi Amini kulileta
hatima ya uongozi
wa mtu ambaye
ni miongoni mwa
madikteta waliowahi
kutokea katika
historia ya Afrika.
Makala hii inataka
kuchokonoa kutoka
kwa wanaokumbuka
kama kweli vita hii
ilisababishwa na Iddi
Amini ama kuna
sababu zingine za
msingi zilizojificha
nyuma ya pazia?
Swali la kujiuliza juu
ya vita ya Kagera ya
mwaka 1978 79 ama
Tanzania na Uganda ni
je vita hii ilisababishwa
na nini? Hisia na imani
za watu wengi kuanzia
kwenye vitabu,
majarida na magazeti,
na hata wavuti
mbalimbali duniani
ni kuwa Iddi Amini
ndiye alikuwa mtu
mbaya ambaye aliamua
kutuma majeshi yake
kuivamia Tanzania
bila sababu yeyote,
na ndipo Tanzania
ikajibiza mashambulizi.
Kuna imani nyingine
kuwa hapo tarehe
19/04/1978 ilitokea
ajali ya gari ambayo

ilimuua Makamu wa
Rais wa Amini, ndugu
Mustapha Adrisi;
kutokana na ajali hiyo
watu waliamini kuwa
ajali hiyo ilipangwa na
ilileta hali ya wasiwasi
mkubwa katika jeshi
la Uganda. Hali hii
ilimfanya Amini aamue
kuivamia Tanzania ili
kuhamisha mawazo
ya maafisa wa jeshi
na hata akili za
wananchi wa Uganda.
Hili linathibitishwa
na taarifa iliyowahi
kutolewa na Rais
Milton Obote ambaye
alipinduliwa na Iddi
Amin ambaye alisema
kuwa: Kuna ushahidi
wa kutosha kuwa
uvamizi wa Amini
dhidi ya Tanzania
ulikuwa ni hatua za
makusudi za Amini
kujinasua kutokana na
kushindwa kwa Amini
kulidhibiti jeshi lake.
Tatizo moja kubwa
ambalo limejitokeza
kila tunapojaribu
kuelezea kuhusu
historia ya Uganda
wakati wa utawala
wa Iddi Amini, ni
ile kukosekana kwa
mtizamo wenye
usawa na kuachana
na mitizamo iliyojaa
uzandiki (stereotyping)

juu ya Iddi Amini.


Ni wazi kizazi cha
leo kinamjua Iddi
Amini kama mtawala
dhalimu kabisa na hili
limeachiwa likaenea
dunia nzima bila utafiti
wa kina. Na ili tuweze
kujua nini hasa ni
ukweli wa hali halisi
wa vita ya Kagera, ni
lazima tuitizame hali
ya Uganda kati ya
mwaka 1977 na 1978
kabla ya vita kutokea.
Kwa mujibu wa
Compton Encyclopedia
Yearbook, 1979,
inasema kuwa mwaka
1977 Uganda ilipata
mafanikio makubwa
kiuchumi hasa
kutokana na bei kubwa
ya zao la kahawa
kwenye soko la Dunia.
Ukiacha mafanikio
hayo, kitabu hicho
kinaendelea kusema
kuwa mafanikio hayo
kiuchumi yaliambatana
na kuundwa kwa
vikundi vya waasi
nje na ndani ya
nchi vyote vikitaka
kumpindua Iddi
Amini ambaye naye
aliponea chupuchupu
kuuawa mara nne.
Kuponea huku kuuawa
kulisababishwa na
uimara ulioambatana
na unyama wa

wanausalama wa
Iddi Amini na pia
heshima kwa amiri
jeshi mkuu. Kutokana
na uongozi wa Amini
kuwa wa kibabe hasa
ikizingatiwa alikuwa
tayari ana maadui
wengi, vyombo vya
habari vya magharibi
vilikuwa havina
uhusiano mzuri na
Iddi Amini hasa
ikizingatiwa ugonjwa
wa kutu ya kahawa
(frost) kule Brazili
uliwezesha mauzo ya
kahawa ya Uganda
kuleta mafanikio katika
uchumi hivyo hakujali
sana nchi za magharibi.
Tarehe 28/07/2006,
kupitia kituo cha
redio cha STAR FM,
mtangazaji Semwanga
Kisolo alikumbusha
wasikilizaji kuwa
kipindi cha Iddi Amini
alihakikisha mishahara
ya wafanyakazi
wa umma ilikuwa
inalipwa si zaidi ya
tarehe ishirini na tano
na kama ingelichelewa
Iddi Amini mwenyewe
alikuwa akitoa karipio
kali kwa wanaohusika.
Anaeleza kuwa Amini
alikuwa mtu anayejali
muda kuwahi kazini
na katika matukio
muhimu ya kitaifa na
alisisitiza wafanyakazi
pia wajaliwe ili waweze
kuwahi na kutimiza
majukumu yao.
Anasema kuwa wakati
wa serikali ya Iddi
Amini, majeshi yote,
polisi, magereza, jeshi
la anga, na usalama wa
Taifa na hata maafisa
wa kati katika utumishi
wa umma, waliishi
maisha ya kujitosheleza
(comfortable): kama
kumudu kusomesha
watoto katika shule
nzuri, kuendesha
magari mapya katika
idara mbalimbali za
serikali. Magari hayo
yalikuwa kama Fiat
Mirafiori, Honda Civic,
na Honda Accord.
Kwa ufupi kipindi cha
utawala wa Iddi Amini
sarafu ya Uganda
Inaendelea Uk. 16

1/7/2016 3:17:13 PM

Habari

AN-NUUR

RABIUL AWWAL 1437, IJUMAA JANUARI 8 - 14, 2016

Maimamu wataka Dk. Shein aheshimu kura za wananchi

Inatoka Uk. 3

palikuwa na dosari, basi


hapo ndipo pafanyike
marudio na hayo ndiyo
matakwa ya sheria ya
uchaguzi.
Nini kimetokea
mwaka huu? Kama dosari
zilijitokeza Pemba kama
wanavyodai kwa nini
urudiwe Unguja? Kwa
nini hawataki kutumia
uamuzi wa mwaka 2000
wa kurudia maeneo yenye
dosari tu?
Alisema Fatma Karume
a k i h o j i wa n a b a a d h i
ya vyombo vya habari
ambapo alinukuu kauli
ya Rais Mstaafu Benjamin
Mkapa akisisitiza kuwa
matakwa ya sheria ni
kurudia uchaguzi maeneo
yenye dosari, sio kufuta
uchaguzi.
Katika mahojiano hayo
Fatma Karume alisema
kuwa anajihisi kusalitiwa
kwani CCM wamegeuza
mapinduzi kuwa ni
wao kupora madaraka

Inatoka Uk. 3
la Katibu Mkuu wa Chama
au mgombea pekee, ni la
chama. Lakini kila nikitizama
kinachoitwa mazungumzo,
ni mtu mmoja Vs Sita wa
upande wa pili, ambao
tafsiri yake ni kuwa hao CUF
wenyewe kamwe hawatajua
kinachozungumzwa!
Alisema Mzee mmoja na
kusisitiza kuwa hajawahi
kuona wala kusikia
mahali popote duniani
ambapo mgogoro wa
kisiasa unatatuliwa kwa
kufanywa mazungumzo
ya sura ya jambo binafsi
na bila kuzingatia uwiano
wa ushiriki wa pande mbili
husika katika mgogoro.
Hadi sasa, zaidi ya
habari za kuambiwa, CUF,
hawajui kwa uhakika nini
Maalim aliongea na Rais
M s t a a f u K i k w e t e wa l a
alichoongea na Rais JPM au
anachozungumza na wazee
Marais wastaafu.
CCM ikitangaza kujiandaa
na uchaguzi wa marudio,
kuna wasiwasi kuwa hilo
ndilo ambalo Maalim
amekubaliana na Rais
Magufuli walipokutana Ikulu
jijini Dar es Salaam.
Ukiangalia mfuatano
wa matukio baina ya kikao
cha Rais na Kamati ya CCM,
Zanzibar na kutolewa tamko
la kurudiwa uchaguzi, lakini
pia ukisikiliza msisitizo wa
CCM, Zanzibar kwamba eti
nao hawamkubali Jecha na
Tume yake, kuna wasiwasi
kwamba hapa kuna mchezo.
Alisema mchambuzi

ANNUUR NEW.indd 8

ya wananchi na kuleta
ukoloni wa watu Weusi
dhidi ya watu Weusi jambo
linalowapora Wazanzibari
haki yao ya msingi ya
kumchagua kiongozi
wanayemtaka.
W a k a t i
h u o
huo,
Maimamu
Zanzibar wameelezea
kutokuridhishwa
kwao na yanayodaiwa
kuwa mazungumzo
ya n a y o f a n y i k a I k u l u
Zanzibar kutafuta
muafaka.
Wamesema, kwanza
mazungumzo hayo
yametawaliwa na usiri
m k u b wa n a k wa m b a
mpaka sasa hakijulikani
kinachozungumzwa.
Lakini pia wakasema
kwamba mazungumzo
yamechukua muda mrefu
huku hao hao wa upande
wa CCM wanaoshiriki
mazungumzo hayo,
wakitoka wanatoa kauli
za chuki, uchochezi
na kuwakatisha tamaa

RAIS Mstaafu, Benjamin


William Mkapa.
wananchi.
Wananchi wa Zanzibar
tulipata matumaini
tulipoona kuwa viongozi
wakuu wa kisiasa
wanakutana kuzungumzia
hali ya kisiasa nchini,
tuliamini kuwa katika
vikao hivyo Viongozi
hawa wenye kuheshimika

wakitawaliwa na busara,
hekima, uadilifu na
wakiweka mbele maslahi
ya taifa badala ya vyama
vyao, basi muda si mrefu
tungepata ufumbuzi wa
mgogoro huu.
Ilisema taarifa ya
J U M A Z A i l i y o s o m wa
na Katibu wake Sheikh
Muhiddin Zuber na
kuongeza kuwa, bahati
mbaya ni vikao 8 sasa
vimeshafanyika tokea
kikao cha mwanzo cha
tarehe 9 Novemba, 2015
(lakini) hakuonekani kuwa
matumaini yale wananchi
waliyoyajenga kwao kuwa
yatatimia.
Lakini zaidi anasema
kuwa pamoja na vikao
hivo kuchukua muda
mrefu sana na kufanyika
kwa siri kubwa, baadhi
ya wajumbe wanaoshiriki
mazungumzo hayo
wamekuwa wakitoa kauli
zinazoshabikia msimamo
wa upande mmoja
hali inayowatoa imani

Uchaguzi wa nini wakati serikali


haitolewi kwa karatasi za kura?

Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Magdalena Sakaya


mmoja akisisitiza kuwa
haoni ni kwa namna gani
CCM wangekuwa na ujasiri
wa kutangaza marudio ya
Uchaguzi Mkuu bila ya
kupata ushirikiano na
viongozi wa CUF.
Sioni namna ambavyo
CCM wanaweza kuibuka na
kutangaza habari za marudio
ya uchaguzi iwapo katika
vikao vyao na CUF wanauona
msimamo thabiti usio yumba

MZEE Hassan Nassor Moyo

wa aliyekuwa mgombea
urais kupitia CUF kupinga
jambo hilo. Alisema.
Katika hali kama hiyo
amesema kuwa hata ile kauli
ya Jussa kwamba CUF ipo
imara na itasimamia kura
za wananchi, inaonekana ni
kupiga porojo tu na danganya
toto.
Taarifa ya chama hicho
iliyotolewa na Ismail Jussa
kufuatia kauli ya viongozi wa

CCM juu ya uchaguzi mkuu


imesema kwamba, CUF
inawahakikishia Wazanzibari
kwamba haitotetereka
na itasimamia kwa dhati
maamuzi yao waliyoyafanya
kwa njia za kidemokrasia
kupitia Uchaguzi Mkuu wa
tarehe 25 Oktoba, 2015 na
italinda chaguo lao la Rais
wa Zanzibar, Wawakilishi na
Madiwani wao.
Hata hivyo, imeelezwa

wananchi juu ya kuwepo


kwa nia njema katika
mazungumzo hayo.
Na kwa maana hiyo
JUMAZA wanasema kuwa,
wananchi wana wasiwasi
iwapo mazungumzo
hayo yanaweza kuivusha
Zanzibar salama katika
mkwamo huu wa kisiasa.
Awali JUMAZA
walieleza kuwa hali inazidi
kuwa mbaya Zanzibar
hasa kiuchumi huku watu
wa k i wa h a wa j u i n i n i
mustakbali wa maisha yao
na nchi kwa ujumla.
Wa m e s e m a , w a o
walikuwa ni katika
waangalizi wa uchaguzi, na
kama zilivyosema taarifa
za waangalizi wengine
wa ndani na wale wa nje,
hakukuwa na dosari za
kiwango cha kuhalalisha
kufutwa uchaguzi.
Na ndio maana tangazo
la Jecha la kufuta uchaguzi
limezua balaa ambalo
haijukani litaishia wapi.
kuwa kitendawili cha Moja
kwa Sita na nguvu mpya
ya C C M k a t i k a h a l i ya
kujiamini kutangaza uwepo
wa uchaguzi, inatoa picha
tofauti.
Ni ishara kuwa Moja
imemezwa na Sita, huku
CUF na UKAWA wakiwa
kizani juu ya kinachojadiliwa
baina ya Maalim, Dr. Shein,
Balozi Seif na wazee watatu
walio makada wa CCM.
Pengine ni kutokana na
utata na wasiwasi uliopo
juu ya kinachoendelea baina
ya Maalim Seif na makada
hao wa CCM, Mzee Hassan
Nassor Moyo amesema kuwa
kamwe hatamuunga mkono
K a t i b u M k u u wa C U F ,
Maalim Seif Sharif Hamad,
ikiwa ataridhia kurudiwa
Uchaguzi Mkuu Zanzibar.
Mzee Moyo amesema hayo
akijenga hoja kuwa dunia
nzima inajua kuwa Uchaguzi
ulifanyika vizuri na kwamba
mshindi anajulikana.
Alisema, kuitisha
Uchaguzi Mkuu mwingine,
ni dhulma, dhambi na
kutowatendea haki wananchi
waliopiga kura zao.
Akiungana na Mzee Moyo,
Naibu Katibu Mkuu wa CUF,
Magdalena Sakaya amesema
kuwa msimamo wa CUF
ni kwamba hawatakubali
uchaguzi urudiwe.
Alisema Baraza Kuu la
Uongozi Taifa, ambalo ndio
chombo cha mwisho kutoa
uamuzi, limeshatoa uamuzi
na msimamo kwamba hakuna
kurudiwa uchaguzi, bali
kilichopo ni kukamilishwa
utangazaji wa matokeo.

1/7/2016 3:17:14 PM

9
R A I S
J o h n
Pombe Magufuli
( JPM) amejitahidi
kutengeneza mazingira
ya kuaminiwa na
ameaminika.
Kila kona ni slogan za
Rais Magufuli. Kila mtu
anamuunga mkono Mh.
Rais Magufuli.
Kamualika Mufti
Zuber wa BAKWATA
akamsifia sana.
Kipi tena mnataka
Wa i s l a m u z a i d i ya
heshma aliyopewa Mufti
kukaribishwa Ikulu?
AWA L I y a y o t e
naomba nitangulie
kusema na mapema
kuwa yawezekana
wakatokea watakao
tofautiana nami
na pengine hata
kunishambulia. Hii ni
kwasababu kila mmoja
ana haki ya kuwa na
mtazamo wake na hata
ujasiri wa kufumbia
macho dhulma
pale inapofanywa
kwasababu dhulma
hiyo haimgusi yeye
wala familia yake.
Wakati tunaelekea
kupata uhuru mwishoni
mwa miaka ya 1960,
wengi tunakumbuka
k u l i k u wa
n a
mgawanyiko miongoni
mwa wapigania uhuru.
Mgawanyiko huu
ulipelekea kuwa na
vyama viwili, TANU
na AMNUT. Japo
AMNUT haikuwa na
nguvu sana kiasi cha
kuitikisa TANU, bado
ukweli unabaki kuwa
yalikuwepo makundi
mawili tofauti. Moja
katika mtazamo wa
AMNUT ilikuwa
kwamba, ilikuwa
ni mapema kwa
Tanganyika kupewa
uhuru, kwakuwa kwa
hali ilivyokuwa kwa
w a k a t i u l e , TA N U
kupewa uhuru ilikuwa
kuwapa nafasi Wakristo
wanufaike na kufaidika
na uhuru peke yao huku
Waislamu wapigania
uhuru wakiishia kuwa
raia wa daraja la tatu.
Kwa maoni yao, ilikuwa
n i b o r a k u c h e l e wa
kupata uhuru ili kupata
muda wa kusawazisha
tofauti zilizokuwepo,
hasa za kielimu, baina
ya wananchi wa dini
kuu mbili, Uislamu na
Ukristo.

ANNUUR NEW.indd 9

Makala

AN-NUUR

RABIUL AWWAL 1437, IJUMAA JANUARI 8 - 14, 2016

Mh. Magufuli anaturudisha


kule kwa Sheikh Takadiri

RAIS Dk. John Magufuli (kulia) akiwa na Muft wa BAKWATA Sheikh Abubakar Zuberi.

Katika kujibu hoja


h i y o , m s i m a m o wa
Mwalimu Nyerere
ulikuwa kwamba,
mkoloni yule yule
aliyewakandamiza
Waislamu wakabaki
nyuma, hawezi kutatua
tatizo hilo. Badala yake,
ni jukumu la Viongozi
katika Tanganyika huru
kushughulikia tatizo
hilo. Kisiasa, ni wazi hoja
ya Mwalimu Nyerere
i l i k u wa n a m a a n a ,
na hi vyo Waislamu
wengi wakamuunga
mkono. Kutokana na
jinsi Mwalimu Nyerere
alivocheza karata zake za
kisiasa katika kupigania
uhuru na hata baada
ya kupatikana uhuru,
ilimjengea imani kwa
Waislamu na wananchi
kwa ujumla.
Kutokana na Imani
hiyo, na hasa Waislamu,
ilikuwa ni vigumu kwa
mtu kumnyooshea
kidole kuwa hatendi
haki. Na akithubutu,
atashambuliwa na
k u t e n g wa . N i k wa
namna hii Sheikh
Suleiman Takadir alipata
misukosuko na hata
kutengwa na Waislamu
wenzake. Matokeo yake,
malalamiko na madai ya
ubaguzi na hujuma dhidi
ya Waislamu wakati wa

serikali ya Awamu ya
Kwanza, imebakia kuwa
historia chungu kwa
Umma wa Kiislamu
nchini Tanzania. Kama
alivyojisemea Remmy
Ongala, imekuwa
ni kilio cha samaki,
machozi yamekwenda
na maji. Hakuna hata
anayesikia na kujali kilio
cha Waislamu katika
walioshikilia mpini.
Wakati wa kamapeni,
Mh. John Pombe
Magufuli mara kadhaa
alisisitiza kuwa
hatowabagua watu kwa
rangi zao, kwa makabila
yao wala kwa dini zao.
Hii ilileta faraja kuwa Mh.
Magufuli ataleta usawa
na haki katika serikali
yake. Hata hivyo, Rais
John Pombe Magufuli
(JPM) nae ameingia kwa
gia ileile. Amejitahidi
kutengeneza mazingira
ya kuaminiwa na
ameaminika. Kila
kona ni slogan za Rais
Magufuli. Kila mtu
anamuunga mkono
Mh. Rais Magufuli. Sasa
katika mazingira haya
na katika kuzingatia
historia na uzoefu wa
mambo wakati wa
Mwalimu Nyerere, kuna
haja ya kuwa makini.
Katika mazingira
haya yanayoendelea

kujiumba, iwapo
atatokea wa kulalamika
kwamba kuna hujuma
dhidi ya kundi fulani,
iwe la kidini au kikabila,
watu watamshangaa.
Na ni hivi majuzi tu
kakutana na Mufti Zuber
wa BAKWATA naye
akamsifia sana. Kipi tena
cha kuthibitisha kuwa
Rais ni mtenda haki,
asiye bagua watu zaidi
ya heshma aliyopewa
Mufti kukaribishwa
Ikulu?
Mara baada ya
kuapishwa kuwa
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania,
Mh. Magufuli alianza
kwa hotuba kali sana
wa k a t i a k i l i z i n d u a
Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
Hotuba ile ilileta hamasa
ya hali ya juu sana na
hata kuamsha ari ya
uungwaji mkono kutoka
kwa Watanzania wa
ngazi ya kati na chini.
Kilichofuatia ni kuanza
na operation aliyoiita
operation ya kutumbua
majipu! Operation hii
ilifanyika kwa kuanzia
bandari na Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA).
Msisimko na shangwe
za uungwaji mkono
zilisikika kila kona ya
Tanzania. Haikuchukua

muda, akaanza
kuonekana kama mtu
aliyekuja kulikomboa
taifa letu Naam,
mazingira yakawa
wazi kufanya atakalo
n a h a k u n a m t u wa
kulalama wala kudadisi.
Kwanini? Kwasababu
ameaminiwa kuwa yeye
anafanya kwa maslahi
ya taifa. Yeyote atakaye
nyoosha kidole kudadisi
au kuhoji, anaonekana
m t u wa a j a b u t e n a
anataka kukwamisha
harakati za kizalendo.
Ubaya wa mazingira
kama haya ni kuwa
huenda watu wakawa
wazito kumsaidia
Mheshimiwa Rais pale
wanapohisi kwamba
mambo hayaendi sawa.
Wingu la umaarufu
na kuungwa mkono
litawazuiya watu
k u wa wa k we l i k wa
Rais kwa kuhofia
yasije yakawakuta
yaliyomkuta Sheikh
S u l e i m a n Ta k a d i r i .
Lakini kwa Mheshimiwa
Rais naye, kwa kusikia
nyimbo na ngonjera za
sifa tu na kuungwa
mkono, anaweza
asipate fursa ya
kutizama pale penye
dosari ndogo ndogo
ambapo pangehitaji
marekebisho.
Binafsi naamini
kwamba, haitakuwa
t u n a m s a i d i a
Mheshimiwa Rais JPM
iwapo hatutasema pale
tunapoona kuwa mambo
hayaendi sawa kama
ilivyo dhamira njema
ya Rais. Mheshimiwa
Rais JPM ni binadamu
na katika ari na hamasa
ya kulitumikia taifa
anaweza kujikwaa
hapa na pale. Na
hivyo ni wajibu wetu
kumsaidia Rais wetu
kipenzi. Na hapa mimi
nitazungumzia yale
ambayo nadhani hata
katika mazungumzo
yake na Mufti Zuberi
hawakuyagusa.
Uteuzi wa Baraza la
Mawaziri
Uteuzi wa Baraza
la Mawaziri, kwangu
mimi, umeacha maswali
mengi kuliko majibu.
Japo inashangaza
Wa i s l a m u k u p i g wa
Inaendelea Uk. 15

1/7/2016 3:17:18 PM

10
Na Omar Msangi
UKIENDA Zanzibar
ukifika pale bandarini
Dar es Salaam, utakutana
na kijana kashika kipaza
sauti akiwahimiza abiria
kwamba saa zao, simu,
m i k a n d a ya s u r u a l i ,
sarafu na vitu vya chuma,
waweke ndani ya mabegi
yao, tayari kwa ukaguzi.
Kwa nini wanafanya
hivyo? Hofu ya ugaidi
ndiyo imetufikisha
hapo. Baada ya hofu,
watu hawana tena muda
wa kujiuliza, zoezi lile
linamzuiya vipi gaidi?
Kiasi wiki tatu zilizopita
zilisambaa habari katika
vyombo vya habari vya
Kenya na vya kimataifa
juu kilichodaiwa ushujaa
na uzalendo wa akina
mama wa Kiislamu
ambao walichukua
hatua za kuwanusuru
abiria wenzao Wakristo.
Kinachoelezwa ni kuwa
basi lililokuwa likisafiri
kutoka Nairobi kwenda
Mandera, lilivamiwa na
magaidi wa Al-Shabaab
wapatao 15. Wakaingia
ndani ya basi wakiwa
na bunduki nzito AK4 7 . Wa k a a n z a z o e z i
la kuwatenganisha
Waislamu na Wakristo
ili wawauwe Wakristo.
Hata hivyo, akina mama
Waislamu wakavua hijabu
zao na kuwapa Wakristo
wavae, kwa hiyo zoezi la
kuwatambua Wakristo
likakwama Al-Shabaab
wakakimbia.
Ni katika taarifa ya
habari, katika televisheni
zetu, unamkuta mtangazaji
anatangaza habari hizo
kwa mkazo akiwaaminisha
wasikilizaji na watazamaji
kuwa hizo ni habari za
kweli kabisa! Ile akili
ndogo tu ya mtu kujiuliza,
hivi hao akinamama
wakivua hijabu na
kuwapa Wakristo wavae,
Al-Shabaab walikuwa
hawaoni? Kitisho cha
ugaidi kimewaondolea
hata kile kiwango cha
chini kabisa cha kufikiri
na kutumia akili.
Kuna lile tukio la
Paris ambapo ilidaiwa
kuwa magaidi walilipua
mabomu katika uwanja wa
mpira. Unatizama taarifa
ya habari au unasoma
gazeti, imewekwa picha ya
mashabiki wapo uwanjani,
wengine wanaongea na
simu wakicheka, wengine
wamekaa wanasogoa.
Ilimuradi hakuna ishara
yoyote ya taharuki. Lakini
mwandishi anakuambia
kuwa hawa ni mashabiki
wanaosubiri kuokolewa

ANNUUR NEW.indd 10

Makala

AN-NUUR

RABIUL AWWAL 1437, IJUMAA JANUARI 8 - 14, 2016

Kweli, hofu ya ugaidi huwafanya


watu kuwa wajinga kupindukia
Putin kidume. Awaumbua wenye IS
Waanza kukimbia. Agenda kukwama

RAIS Barack Obama wa Marekani (kushoto) akiwa na Rais Vladimir Putin wa Urusi.
na polisi wa uokozi baada
ya magaidi kupiga bomu!
Hivi kweli pale uwanja
wa taifa wakati wa mechi
liripuke bomu, yupo
mtu atasubiri waje polisi
kumuokoa? Lakini yote
hayo, wala watu hawana
tena muda wa kufikiri.
Ngoma ya kitisho cha
ugaidi iliyopigwa kwa
muda mrefu, ishawatia
ujinga uliokusudiwa.
N a m k u m b u k a
m wa l i m u wa n g u wa
inorganic chemistry Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam
m wa k a 1 9 8 4 , P r o f e s a
Saxena akisema kuwa
yeye alikuwa hatoi mtihani
mgumu maana akitaka
wanafunzi wake wote
wafaulu. Kwa hiyo mtihani
wake anaokupa unahitajia
kutumia asilimia 10 tu ya
akili yako, kufaulu. Sasa,
ukifeli ujue kuwa sio kosa
lake. Jilaumu mwenyewe
kwa kushindwa kutumia
japo sehemu moja tu
ya kumi ya akili yako.
Inavyoonekana katika
hili la kitisho cha ugaidi,
t u m e f i k i s h wa m b a l i .
Vichwa havifanyi kazi
tena.
Aliwahi kusema Josef
Stalin kuwa-The easiest way
to gain control of a population
is to carry out acts of terror."Akimaanisha kwamba njia
nyepesi ya kuwadhibiti

watu na kuwapelekesha
unavyotaka, ni kuwapa
kipigo cha ugaidi,
kuwaundia ugaidi. Kwa
nini? Kwa sababu, Fear
of Terror Makes People
Stupid ikiwa na maana
kuwa kitisho cha ugaidi
huwatia watu ujinga.
Kinawaondolea kufikiri
na kutumia akili zao. Na
ndio maana Rais Franklin
Roosevelt katika hotuba
ya k e ya k wa n z a k wa
wananchi wa Marekani
alisema kuwa kama kuna
jambo la kuogopa, basi ni
hofu yenyewe.
Kwa bahati mbaya katika
ulimwengu tunaokwenda
nao wa utandawazi na
ubeberu wa ma-neocons,
wanaotengeneza hofu
na kitisho cha ugaidi
ni vyombo vya dola ili
k u k i d h i m a t a k wa n a
agenda za mabeberu.
K a t i k a v i wa n g o v y a
kimataifa, wametegeneza
kitisho cha ugaidi wa
Saddam Hussein na
Al-Qaida wakapata
sababu ya kuzipiga na
kuzisambaratisha Iraq na
Afghanistan. Wakaunda
kitisho cha Gadhafi kuwa
anauwa watu wake, na
sasa cha Bashar Assad.
Libya ishasambaratishwa,
Syria ipo chumba cha
wagonjwa mahututi (ICU).
Ili uone kitisho cha

ugaidi kinavyotia
watu ujinga, tizama IS
wanavyopambwa kwamba
wana nguvu za kutisha
na jeshi lisilowezekana.
Kwa zaidi ya miaka miwili
Marekani na washirika
wake wanajitahidi
kuwaangamiza, lakini
wapi! Bado wana nguvu
na uwezo wa kupenya
h a d i Pa r i s wa k a p i g a
n a wa k a o n d o k a b i l a
kukamatwa! Na watu
wanaamini. Wala mtu
hajiulizi, kama ni kweli
hao IS wana nguvu
kiasi hicho, hizo silaha
wanapata wapi?
Marekani, Uingereza
na washirika wao,
wanadai kupeleka ndege
za kivita kuwapiga IS
kwa miaka miwili sasa,
IS wanadunda tu. Na
watu wanaamini kuwa
Marekani na washirika
wake wamewashindwa
IS. Ukiwaambia kuwa
Marekani inafanya usanii,
haiwapigi IS kwa sababu
ni vijana wake, wanaona
kama unafanya masikhara.
Lakini sasa imefika
mahali, Vladimir Putin
kafanya kweli. Alianza
kwa kutoa kauli kwamba
ule mtindo wa mtu mmoja
(Marekani) kuwaburuza
walimwengu wote na
kuwafanya wengine
wajinga, ufikie mwisho.

Kisha akaingia Syria akawa


anawapiga kikweli IS. Hivi
sasa IS wanasambaratika.
Wanakimbia wanatoka
nje ya Syria na Iraq. Miji
inakombolewa. Kitendo
cha IS kukimbilia nje ya
Syria maana yake ni kuwa
wengi wao walikuwa
sio waasi wananchi wa
Syria. Walikuwa mamluki
waliopenyezwa nchini
humo.
Russia Vindicated by
Terrorist Surrenders in Syria,
ndivyo anavyochambua
mwandishi Finian
C u n n i n g h a m ,
akimaanisha kuwa
i l e k wa m b a m a g a i d i
hivi sasa wanabwaga
manyanga, kunaisafisha
U r u s i . L a k i n i wa k a t i
huo huo, inawaanika
mabeberu wa Marekani
n a U l a ya k wa m b a n i
w a o n g o . Wa l i k u w a
hawapigi IS kwa sababu
ni mamluki wao. Wao ndio
waliwatengeneza na wao
ndio walikuwa wakiwapa
silaha kupitia Uturuki
huku wakiwamiminia
mapesa, tena baadae
kupitia uuzaji wa mafuta
yaliyokuwa yakichimbwa
katika maeneo yaliyokuwa
yakishikiliwa na vijana
wao IS.
Ilichofanya Urusi ni
kukata mzizi wa fitna.
Kwanza ni kushambulia
na kuangamiza malori
ya mafuta kutoka kwa
magaidi kwenda nchi za
NATO. Pili, kushambulia
magari yaliyokuwa
yakiwapelekea silaha
IS. Baada ya kuona
wamezidiwa, hivi sasa IS
wanaomba waruhusiwe
kuondoka chini ya mpango
utakaosimamiwa na Umoja
wa Mataifa na Kamati
ya Kimataifa ya Msalaba
Mwekundu (United
Nations and International
Committee for the Red Cross.)
BBC wakiripoti juu ya
kubadilika kwa hali katika
uwanja wa mapambano
wanasema, Syria fighters
evacuation from Zabadani
under way. Hata hivyo
hawakomi kupiga
p r o p a g a n d a . K wa n z a
wanakwepa kutaja
kwamba hali hiyo imekuja
kutokana na kipigo kutoka
Urusi. Pili hawataji kuwa
wanaobwaga manyanga
ni magaidi wa IS, alNusra Front na Jaish alIslam wakiongozwa na
kamanda Zahran Alloush,
aliyeuliwa na majeshi ya
Urusi. Huyu anatajwa
kuwa ndiye akipokea
silaha na vifaa vingine
kupitia Saudi Arabia
Inaendelea Uk. 10

1/7/2016 3:17:19 PM

11
Inatoka Uk. 10
na Qatar. Mwandishi
Finian Cunningham,
akizichambua Saudi
Arabia na Qatar katika
mchezo huu wa ugaidi
anasema: Saudi Arabia and
Qatar, serves as a conduit
for American CIA weapons
to the more known terrorist
outlets.
Hili BBC wamekwepa
kulisema badala yake
wanaeleza kana kwamba,
wanaokimbia ni wapinzani
wa kawaida wa Bashar,
Voice of America (VOA)
wakimpa Zahran Alloush,
cheo cha rebel leader.
Ukija katika nchi
zetu, ujinga ni ule ule,
tena wenye maangamizi
makubwa kwa nchi. Hivi
sasa Kenya, vipo vikosi
maalum ambavyo hupokea
amri na maelekezo kutoka
makachero wa nchi za
Ulaya, Marekani na
Israel (Western Security
Agencies), sio kutoka kwa
Amiri Jeshi Mkuu wa
nchi wala kwa wakuu wa
vyombo vya usalama vya
nchi hiyo. (Tazama: Inside
Kenyas Death Squads).
Kwa ujumla kutokana na
propaganda ya kitisho
cha ugaidi, serikali zetu
z i m e f i k i s h wa m a h a l i
p a k u a m i n i k wa m b a
hatupo salama mpaka
tupate ulinzi kutoka kwa
mabeberu. Na kwa sababu
hiyo, tunawaruhusu
kuweka kambi zao za
kijeshi (military bases)
na kuwa na kauli juu
ya majeshi yetu. Zipo
nchi hivi sasa wanajeshi
wao wamekuwa kama
mgambo wa kuwabebea
mikoba makamanda
wa jeshi la Marekani.
Kupitia kitisho cha
ugaidi, tunapumbazwa,
tunapumbazika,
tunafanikisha agenda
ya beberu kusambaza
makucha yake ya kijeshi
duniani (Network of Military
Bases) kufikia lengo lake la
World Hegemony.
Tunachopata nini? Nchi
huru inafikishwa mahali
inakuwa koloni kasorobo.
Haina sauti hata juu ya
rasilimali zake. Haiwezi
kuamua ifanye biashara
na nani katika madini
yake na mafuta/gesi yake.
Na wenyewe hawafichi.
Wanasema wazi kwamba
wa n a c h o l e n g a k a t i k a
kusambaza makucha yao
ya kijeshi ni namna mbili.
Kwanza kudhibiti uchumi
wa dunia na masoko yake
ya fedha. Pili, kudhibiti
na kukomba rasilimali
zote muhimu. Lakini kwa
ujinga tuliokwishatiwa
kutokana na kitisho cha

ANNUUR NEW.indd 11

Makala

AN-NUUR

RABIUL AWWAL 1437, IJUMAA JANUARI 8 - 14, 2016

Kweli, hofu ya ugaidi huwafanya


watu kuwa wajinga kupindukia

MWANDISHI Finian Cunningham

ugaidi, tunawakaribisha
kwa mikono miwili kwa
hoja kuwa wanatusaidia
kupambana na ugaidi.
Ndio wataalamu wetu
wa kutufundisha na
kutuelekeza namna ya
kukabiliana na Al-Qaida
na Al-Shabaab!
Lakini baya zaidi,
ili ugaidi ukolee,
m t a l e t e wa u g a i d i
ambao utaporomosha
na kuondoa Amani
mliyokuwa nayo.
Matukio kama ya
Westgate, Garrisa na
Mandera, lazima yaje
m a r a k wa m a r a i l i
kukumbushwa kuwa
m a g a i d i wa p o . N a
k wa b a h a t i m b a ya ,
wala hamtajua
n a n i a n a wa p i g a a u

anawachezea akili kwa


s a b a b u k wa u j i n g a
mliokwishatiwa, kazi
yenu itakuwa kuimba
Al-Shabaab, Al-Qaida,
Boko Harm na majina
kama hayo. Lakini pia
utawala bora, wa sheria
na haki, utaondoka.
Watu watahujumiwa,
watateswa, watauliwa
bila kujali sheria na
haki za binadamu.
Maana katika harakati
za kupambana na
ugaidi, afisa wa polisi
amepewa kibali cha
kupiga risasi kwanza,
mengine baadae.
Anaripoti yule Afisa wa
GSU Recce Company
(Kenya) akisema kuwa
wanawakamata watu
katika bar (kilabu

ya pombe, hotelini,
mtaani au majumbani)
wanawafikisha polisi,
lakini hawawasajili,
bali huwapeleka porini
n a k u wa p i g a r i s a s i
(Elimination Programme).
Ndio maana katika
ile documentary ya
Aljazeera wakapewa
jina la Death Squad.
N i n a a n d i k a h a ya
nikizingatia kuwa kuna
Watanzania wenzetu
wamo mikononi mwa
vyombo vya dola
kwa muda mrefu sasa
wakikabiliwa na tuhuma
za ugaidi. Watuhumiwa
hawa unaweza
kuwagawa katika
makundi mawili. Wapo
ambao inawezekana
hawana hatia kabisa.
Ni wahanga ama wa
njama za makusudi
au wameangukia
katika bahati mbaya
ya mtego wa panya.
L a k i n i ya we z e k a n a
wapo ambao kulikuwa
na sababu za msingi
za kuwatilia shaka na
pengine walishafanya
au walikuwa mbioni
k u f a n ya m a m b o ya
hatari. Hawa nao ni
wahanga tu wa mpango
mzima wa maadui.
Wametumbukia kwa

WANANCHI wa Nigeria wakiandamana kushinikiza serikali ya nchi yao iharakishe


kurejeshwa kwa mabinti zao wanaodaiwa kutekwa na kundi la Boko Haram.

ujinga, hata kama


walikuwa wakilipwa au
walighilibika kiimani,
bado ni katika ujinga tu.
Ili twende vizuri na
tuwe salama kinchi,
nadhani la muhimu na
kuzingatia hapa ni kuwa
katika kuwashughulikia
wa t u h u m i wa h a wa ,
tusije tukajikuta
tukiongozwa na ujinga

ule ule uliopandikizwa na


kitisho cha ugaidi.
Wiki iliyopita kulikuwa
na mjadala mzuri sana
katika Azam TWO,
u k a t o l e wa m f a n o wa
Nigeria: Kwamba polisi
wanasema wamegundua
mahali Boko Haram
wanapotengeneza
mabomu (kiwanda cha
silaha). Sasa mtu unajiuliza,
nchi gani hiyo duniani
ambapo watatokea waasi/
magaidi, wajenge kiwanda
cha silaha katikati ya mji
(au hata ikiwa pembezoni),
waingize mali ghafi za
kutengeneza mabomu,
m p a k a wa n a ya t u m i a
mabomu hayo kuuwa
watu, serikali na vyombo
vyake vya usalama havina
habari?
Sasa huu ndio ujinga
ninao zungumzia. Kwamba
kama tutajiaminisha (kwa
ujinga) kwamba kuna watu
wanaweza kumiliki AK-47
na mabomu, wanazunguka
nayo mitaani, huku
serikali haina habari,
basi kwa usalama wa
nchi, sisi tutakuwa ndio
magaidi wabaya zaidi
kuliko tunaowatuhumu
kwa ugaidi.
Kamanda Suleiman
Kova akitangaza kustaafu
amesema kuwa katika
matukio ambayo
hatayasahau, ni pamoja na
la Sitakishari. Na kweli, lile
sio la kusahaulika mpaka
kiteguliwe kile kitendawili
cha maburungutu ya noti
zinazomeremeta (ndio
kwanza zinatoka Benki
Kuu) zikiwa hazijaguswa
kabisa kutumika, lakini
Afande Kova akatuambia
zimechimbuliwa chini
aridhini! Zilikuwa
zimefukiwa shimoni na
magaidi/majambazi!
Lazima ifike mahali
tujiulize, mabeberu
wanapiga ngoma ya kitisho
cha ugaidi watutie ujinga
ili wafanikishe ya kwao.
Sisi tunapoitikia, tukapiga
zumari na kucheza ngoma
hii, tunatarajia kupata nini
kama nchi?

1/7/2016 3:17:20 PM

12

Safu ya Ben Rijal

AN-NUUR

RABIUL AWWAL 1437, IJUMAA JANUARI 8 - 14, 2016

Masheikhe wetu: Sheikh Abdalla Saleh Farsy-10 Sehemu ya Pili


KAMA tilivyosoma katika makala iliopita kuwa Sheikh
Abdalla Saleh Farsy alikuwa ni alim, alikuwa hakusita
kujisomea ili kuweza kupanua mawazo na kujiongezea
elimu. Katika makala hii ya pili itamuangalia zaidi Sheikh
Abdalla Saleh Farsy katika kazi zake alizozifanya na
namna alivyopokewa katika jamii kazi zake ikiwa pamoja
na tafsiri ya Quran na vitabu mbalimbali alivyoviandika.
Nyingi ya kazi zake hazikuwa na haki miliki na wengine
wamezigeuza kuzifanya kuwa ni kazi zao. Kuna juhudi
hivi sasa inayofanywa na Jumuia moja ya Kiislamu
kuweza kuzikusanya kazi zake zote alizozifanya kati ya zile
alizozichapisha na zile ambazo hakuzichapisha.

KATIKA makala za
nyuma niliandika
juu ya wahubiri wa
Kikristo waliokuwa
wanaletwa katika
ukanda wa Afrika
ya Mashariki ikiwa
wengi wao walikuwa
wajuzi wa kuielewa
Quran na walikuwa
wanakizungumza
Kiarabu kwahio
walikuwa wanaifanya
kazi yao ya uhubiri
kwa kuelewa vipi
kukabiliana na
Waislamu wengi hasa
wale ambao walikuwa
wakazi wa mwambao.
Quran ya mwanzo
kwa lugha ya Kiswahili
iliandikiwa mwaka
wa 1923 na Padri
Dale ambaye alifanya
kazi nzito ya kutafsiri
Quran kwa Kiswahili
ambayo Kiswahili
chake kilikuwa cha
watu wa Pwani.
Tafsiri hiyo ilikuwa na
kurasa 542 na kurasa
zisopungua 142 ikiwa
ni Sharhi (maelezo
ya ufafanuzi) Quran
hii hasa ililengwa
kwa wahubiri wa
Kikiristo walioajiriwa
na University
Mission to Central
Africa (UMCA),
iliyoanzishwa mwaka
1873. Wahubiri
hao wakiitumia na
kuwashtua Masheikhe
namna walivyokuwa
wanaielezea, hio ikawa
ndio Quran iliopo kwa
Kiswahili.
Tafsiri hii ya Padre
Dale ililenga zaidi
kuikingia kifua
Ukiristo na sherhe
yake ilikuwa imezama
sana kuwa nje ya
ukweli wa Kiislamu.
Kutokana na hayo,
ikaonekana kuwa kuna
haja haraka kabisa
kupatikana kwa tafsiri

ANNUUR NEW.indd 12

SHEIKH Abdalla Saleh Farsy.

ya Kiswahili ambayo
imeandikwa na
Waislamu wenyewe.
Hapo ndipo Sheikh
Mubarak bin Ahmed
akiwa kiongozi mkuu
wa Makadiani wa
Afrika ya Mashariki
akaanza kuandaa
matayarisho ya
uandikaji wa Tafsiri
ya Quran kwa
Kiswahili na katika
mwaka wa 1942.
Tafsiri hio ikapelekwa
kwa mchapishaji na
kuhakikiwa katika
kamati ya lugha ya
Kiswahili iliokuwa
ikijulikana kwa jina
la Inter-Territorial
Swahili Language ili
iweze kukubalika na
kusomeka kirahisi na
Waswahili. Kamati
hiyo ilithibitisha kuwa
lugha iliotumika ni
lugha ya Kiswahili
bulbul na inakubalika
kisha tafsiri hiyo
ikapelekwa kwa
viongozi mbalimbali
wa Makadiani wa
Afrika ya Mashariki
na kukubaliwa kuwa
lugha iliyotumika
inakidhi haja.
Sheikh Amri
Abeid malenga wa
lugha ya Kiswahili
maarufu wakati huo
katika Tanganyika na
ukanda wa Afrika ya
Mashariki, aliokuja
kuheshimika na
kupewa jina uwanja

wa mpira wa Arusha
kwa jina lake Sheikh
Amri Abeid Stadium.
Sheikh Amri Abeid
akiwa muumini
wa madhehebu ya
Makadiani alipewa
mafunzo ya dehehebu
hilo ambalo liliasiwa
nchini India,
alifanyiwa mpango
wa kwenda kupata
taaluma ya ndani
ya madhehebu
hio na alikwenda
nchini Pakistan kati
ya mwaka wa 1954
hadi 1956 huko
alipikwa vya kutosha.
Wakati Sheikh Amri
Abeid anakwenda
Pakistan, Makadiyani
walikuwa tayari
wameshatoa nakala ya
Quran ya Kiswahili
ambayo inakingana
na mwenendo
wa kuwa Mtume
Muhammad (SAW)
ndio Khatim yaani
mwisho wa Mitume
wote. Sheikh Amri
Abeid alikuja kuwa
mtetezi mkubwa wa
tafsiri hii na wafuasi
wa madhehebu ya
Suni kuemewa na
kuonekana kuwa kuna
haja ya kutengenezwa
tafsiri ambayo itakidhi
haja ya watu wa
madhehehbu hio ikiwa
idadi yao ni wengi
katika ukanda wa
Afrika Mashariki kama
yalivyokuwa madhebu

ya Malik kuwa na
wafuasi wengi katika
Afrika ya Kaskazini.
Nchini Kenya tafsiri
ya Quran iliyoegemea
madhehebu ya Sunni
ilikuwa inatafsiriwa
kwa khatua na Sheikh
Al-Amin Ali Mazrui,
lakini haikuwa kamili
na ndipo Sheikhe
Abdalla Saleh Farsy
akaanza kuitafsiri
Quran kwa Kiswahili
katika mwaka wa 1956
kwa kuirejeza tafsiri
ya Makadiyani. Mmoja
kati ya wanafunzi
wake Sheikh Abdalla
Saleh Farsy, marehemu
Shariff Abdulwahab
Alawy ambaye nilipata
fursa ya kujadiliyana
naye katika nyakati
mbalimbali, alinambia
kuwa Sheikh Abdalla
Saleh aliwateua
wanafunzi wake
watano akiwa yeye
mmoja kati ya hao
na kuwapa kazi
ya kila baada ya
darsa kutalii nao na
kutafsiri baadhi ya aya
kuzitafsiri naye Sheikh
Abdalla alikuwa kila
aendapo alikuwa
na kitabu chake
maalumu ambacho
alikuwa ananukulu
na kufanya tafsiri.
Alikuwa na mkoba
wake maalumu ambao
humo ulikuwa mfano
wa maktaba, kwani
wakati wote alikuwa
na rejea (references)
mbalimbali
zilizoshikamana na
Uislamu na tarekhe
yake. Kwahivyo
alianza kazi hii kwa
juhudi kubwa sana na
alikuwa akiwasiliana
na watu mbalimbali
ikiwa Kenya,
Pakistan na maeneo
mengineo. Kazi yake
iliweza kukamilika
ilipofika mwaka wa
1961 alikuwa tayari
kishakamilisha
juzuu 12 na kuweza
kuchapishwa. Sheikh
Abdalla alipata moyo
kuona kazi yake kuwa
sasa imo kwenye
mikono ya Waislamu
na kueleweka maelezo
ya kina ya Quran
na kuonyesha yale
mapunguku ya

Makadiyani. Sheikhe
alikuwa na upungufu
wa kifedha lakini
juu ya kuwa na
upungufu wa kifedha
wa kumwezesha
kuichapisha kopi
yake ya kwanza lakini
hayo hayakumsitisha
kuiendeleza kazi yake
hio na ilipofika mwaka
wa 1969 chini ya
udhamini wa Islamic
Foundation ya Kenya
ilitoka tafsiri hio
kwa mara ya kwanza
maarufu ambayo
Sultan wa Qatar
alisaidia pakubwa
kifedha kuweza
kuchapishwa nakala ya
mwanzo (first edition)
na kutolewa nakala
4,000 kugaiwa bure na
nakala 3,000 zikawa
zinauzwa kwa shilling
3,000.
Islamic Foundation
ya Nairobi yenye
kuunga mkono Jamaat
al Islam ya Pakistan,
ndiyo iliyosimamia
upigwaji wa chapa
kwa mara ya mwanzo
Tafsiri ya Sheikh
Abdullah Saleh
Farsy, na kumpatia
tafsiri hiyo gwiji
mwanaharakati wa
Pakistan Sayyid Abdul
Ala Maududi ambaye
baada ya kufanyiwa
tafsiri na kufahamu
yalioandikwa,
akaikubali tafsiri ya
Qurani Takatifu ya
Sheikh Abdalla na kwa
upande wake Sheikh
Abdullah Saleh Farsy
akaitegemea tafsiri ya
Maududi inayoitwa
'Qur'an Fahmi Ke
Bunyadi Usul' (Msingi
wa kuifahamu Quraan), na Syd Maududi
akaombwa utangulizi
wa tafsiri yake hio
Tafhim Al-Qur-aan
itumike kwenye
utangulizi wa Qurani
Takatifu ya Sheikh
Abdalla hapo ikawa
Waswahili wamepata
tafsiri iliokamilika.
Sambamba na tafsiri
hii ipo tafsiri ya
Kiswahili ilioandkiwa
na Mzanzibari
mwengine Sheikh Ali
Muhsin Barwany kwa
jina la Al Muntakhab
Qurani Takatifu
(quranitukufu.net).

1/7/2016 3:17:21 PM

13
SAFARI hii makala hii
itajaribu kuangaza utupwaji
wa taka na mbinu za
kutumika. Taka zinakuwa
mazonge kwetu kutokana na
kushindwa kujuwa namna
ya kuzitupa. Tuzitupe vipi
na tuzitupe wapi?
Jiulize wewe unaosoma
makala hii unazitupaje taka
ulizonazo ikiwa kutoka
unapoishi, kiwandani kazini
au popote pale. Jee, unazitupa
popote pale utapoona kuna
upenyu utakuwezesha
kutupa taka, au unazitupa
katika msingi (mtaro) wa
maji, au unazitupa katika
maeneo ya skuli ambapo
baada ya masomo huwa
hakuna usimamizi au
unazitupa pembeni mwa
jirani yako au unazitupa
palipotengwa taka tuzitupe,
au unazifukia au unazichoma
moto?
Kama ningeweza kupata
watu 100 wakawa wakweli
kunambia wanavyozitupa
taka, naamini jawabu
nitayoipata zaidi ya asilimia
90 watanipa jawabu
isioridhisha. Ukijiuliza
kwanini ikawa hivyo? Moja
kati ya jawabu nikuwa ni
dharau na watu kuona mji,
nchi, makazi yao sio lolote lile
na wao kutokuwa na wajibu
wa usafi kwa kuwa wapo
wahusika wanaowajibika
kusafisha wakiwa wanalipwa
na serikali. Fikra hizi ni
potofu zinahitajika kupatiwa
ufumbuzi kwa haraka kabisa
ili dhana nzima ile ya yale
Yawe Endelevu ipatikane.
Wa t u wa n a f i k r a
mbalimbali fikra walizonazo
zinatafautiana na fikra za
b i n a d a m u k u n a wa k a t i
zinahitajika kutafautiana
na kuna wakati zinahitajika
ziwe za aina mmoja. Kwenye
uvumbuzi hapa ndipo fikra za
mwanadamu zinatafautiana
n a k u t a f a u t i a n a k wa k e
kunapelekea binadamu
kufanya tafiti na kuweza kuja
na mambo yenye manufaa.
Lakini kuna sehemu fikra
za wanadamu hazitakiwi
kutafautiana na ukitaka
kutafautiana na fikra za
pamoja huwa ni majanga.
Kwa mfano kupiga chanjo
ya Polio, jambo hili ni lazima
wala hakuna kutafautiana
na utapo jifanya hutaki ni
janga litakalo kukabili kwa
mtoto atakaye kuja kuzaliwa,
tumeyaona haya Nigeria.
Sasa sisi tukiwa kama ni
wananchi tumo katika taifa
letu kuna haja kabisa fikra
zetu ziwe zenye kukubaliana
kwa yale yalio lazima tuwe
tunakwenda sambamba kwa
uslama na maendeleo yetu.
Tunatupa taka kila kukicha
na tunazlizalisha kila siku
ikiwa kitu hicho kila siku
unakizalisha kisha inabidi
ukitupe itakulazimu uwe na
mbinu yakinifu zilizokuwa
mujarab kufanya hivyo.
Huko nyuma tushasema
namna ya kuzigawa hizo
taka na kuzitupa, sasa
lakujiuliza wahusika

ANNUUR NEW.indd 13

Safu ya Ben Rijal

Yawe endelevu-3

Aina ya Tanuri ya kuchomea taka

Tanuri la kileo la kuchomea taka

Gari la kukusanya taka.


wametutengea mwahali
muwafaka pakutupia taka
zetu? Wapanga Miji na
Vijiji ni sehemu muhimu
kwetu kutupangia maeneo
makhsusi ambayo tutakuwa
tunatupa taka zetu kisha
Manispaa zetu kuwa na
mipango madhubuti ya
ukusanyaji na kuzipeleka
katika jaa kubwa la utupwaji
wa taka.
Mara nyengine huwa
tunashindwa kuwalaumu
wananchi kwa kuwa mtu
anapoishi hajui akazitupe
wapi taka ndio anapoona
popote pale pametupwa
taka nayeye ataona ni sawa
kufanya hivyo. Jee hio ni
sababu ya kujihalalisha hayo
tunayoyafanya kuwa ni
sawa? Inaweza ikawa ndio
lakini nitasema sio, muhimu
kupatafuta pale palipotengwa
na kutakiwa mtu kuzitupa

taka anazozizalisha.
Ninapoishi mie kulikuwa
na jaa kubwa ambalo taka
zote za Manispaa zikitupwa
hapo, lakini mji ulipotanuka
na kukua imebidi jaa hilo
liondoshwe lisogezwe nje
ya mji kidogo na huko
liliposogezwa kutokana
na kutotumika utaalamu
wa kuzitupa taka, matokeo
yake katika kipindi kifupi
eneo hilo lilijaa kwa kuwa
gari la Manispaa linachukua
hizo taka na kisha kuzitupa
kwenye shimo ambalo lilipata
kuchimbwa mawe, gari la
Manispaa linabeba taka
kisha huja gari la kuzifukia
na kumwagwa mchanga
na nyengine huchomwa
moto. Hapo utajiuliza dunia
ndivyo inavyozidhibiti taka
kwa mtindo huo? Haya
nayazungumzia eneo la
kisiwa cha Unguja lakini

AN-NUUR

RABIUL AWWAL 1437, IJUMAA JANUARI 8 - 14, 2016

utapotembea katika maeneo


mengi ya Afrika Mashariki
mambo ndio hayo kwa hayo
hayatafautiani.
Utupwaji wa Taka
Katika kutupa taka kuna
njia tatu kuu zinatakiwa
zizingatiwe nazo ni:
Kuzikwa kwa taka (Landfill),
Kuzichoma taka kwenye
tanuri (Incineration) na njia
nyengine ni Kurejezwa kwa
taka (Recycling).
Utupaji wa taka kwa
kufukia kunahitajia kutengwa
eneo maalumu na kisha
kuhakikishwe kuwa taka
zinazokwenda kumwagwa
na kutupwa ni kuwa tayari
zimeshabaguliwa. Kisha
kuandaliwe mtindo wa jaa
la kimambo leo (sanitary
landfill).
Nivipi jaa hilo
linavyokuwa? Katika mwaka
wa 1935 mtido huo uliasisiwa
nchini Marekani katika mji
wa Fresno, California na hadi
sasa asilimia 58 ya taka zote za
Marekani zinatumia mtindo
huo, ikiwa taka zinafukiwa
kwa kiwango kikubwa lakini
sio kwa njia ya kupopoa lakini
kwa taratibu maalumu ikiwa
zinafukiwa kisha wataalamu
wanaangalia na kufwatilia
kinachoendelea.
Kinachofanyika ni
huchimbwa shimo kubwa au
kati ya mashimo yalioachwa
kisha huchimbiwa na Plastiki
kubwa ikiwa na upana wa
kiasi centimeter 120, baada
ya taka kuingizwa humo
kisha udongo huekewa juu,
na kuhakikishwa kuwa maji
hayaingii wala hayapenyi
kutoka kwenye hilo shimo
na kupenya kwenye ardhi
(Leacheates). Ufukiaji huu
unapokuwa tayari huwa
kila tabaka hujazwa taka
na udongo na kazi hii
i k a wa i n a e n d e l e a k i l a
siku zikipinduka na huku
taka zinaoza, shimo hilo
linapokuwa limejaa hujazwa
juu udongo bila ya kuongeza
chochote. Sasa eneo hilo
ambalo lilifanyiwa kazi hio
linakuja mwisho kugeuzwa
kuwa sehemu ya bustani na
kuwa eneo la burdani, na
maeneo hayo tunayo mengi
ima yalichimbwa mawe,
kifusi, jasi ambayo tunaweza
kuja kuyageuza kuwa
maeneo ya thamani baada
ya kuwa maeneo yaliotupwa
yasio na faida.
Mpango huu wa majaa
ya kileo unagharama kwa
kiasi fulani lakini unajiuliza
washauri na wataalamu
wanashauri nini katika
utupwaji wa hizi taka kwa
jaa hili la kimambo leo?
Vijana wanasoma somo la
Environmental Engineering
wamefuzu vizuri masomo
yao wameajiriwa na wapo
na hamu kuja mbele na
k u o n ye s h a u we z o wa o
katika elimu walioisoma ila
balaa iliopo ni kuwa kuna
vinganganizi wazee kama
mie kiumri lakini sio mie
wasiotaka fikra za vijana na
kubakia na fikra mgando
(Stagnant) na vijana hao
huvunjwa moyo kisha huja
wakafunga miko na kusema

potelea mbali wacha twende


tutafika. Nchi kama Japan
m f a n ya k a z i a n a y o b u n i
chochote kile iwe uvumbuzi
au jambo litaleta faida kwa
nchi sio hupandishwa cheo
tu, bali hutunzwa fedha
tele. Ndipo unapoona Japan
kila kukicha ipo inapiga
maendeleo wakati maeneo
ya kwetu kila kijana akija
na kuleta mageuzi, huwa
ndio adui katika kazi, mjuaji,
anataka kuja kuharibu
mambo, hayo yaliotengenea
ndio yepi tukiuliza hayana
jawabu.
Kuna njia ya uchomaji wa
taka (Incineration) inagawa
njia hii kwa miaka hii kwenye
mabadiliko ya tabia nchi na
kuongezeka kwa joto duniani
imekuwa haishauriwi sana,
lakini bado inahitajika hasa
kwa sisi nchi zanaozendelea
kwani taka kama zinazotoka
katika mahospitali yetu
zinahitajiwa kuchomwa
kitaalamu kwenye matanuri.
Nchi inahitajia aidha iwe
na matanuri maalumu
ya kuchomea taka katika
kupunguza mzigo wa taka, na
yasiiwe yamezagaa. Kwenye
mshadhari wa mahoteli
(Chains of hotel) kunahitajia
kuwe na Tanuri moja la
kuchomea taka kwa hoteli
zote zilizokuwepo hapo aidha
na taka kutoka majumbani
nazo zikapelekwa hapo kwa
kuchomwa. Kwanini, kwanini
tunabaki kama hivi ikawa
taka kwetu mzigo? Kwanini,
kwanini? Jawabu sote tunazo
kuwa tunashindwa kuvipa
vipaombele yalio takiwa
k u p e wa u m u h i m u . S a a
nyengine gari za Prado 4 hayo
yanayoitwa Mashangingi
zinajenga Tanuri safi kabisa
la kileo. Lakini wapangaji
wapo kufikiria manunuzi ya
magari ya fakhari kwa taifa
kisha watanue, watatanua
mpaka lini?
Kuzirejeza taka (recycle)
hii nayo ni njia ya kupunguza
m z i g o wa t a k a , u t a o n a
kwa hapa Zanzibar hamna
mtambo hata mmoja wa
hakika wa kuzirejeza taka
na kwa Tanzania bara ipo
kwa mikoa michache ambaye
inahesabika yenye taratibu ya
mashine za kuzirejeza taka
tupo duniani au tupo kwenye
Kusadikika nchi alioielezea
Shaabni Robert?
Awamu ya 5 ya Serikali
ya Muungano inachanga
moto kubwa ya kufanya
na moja ni hili la taka na
lazima lipewe umuhimu
kwa kiwamngo cha juu, hasa
ukizingatia nchi inataka
kuelekea kwenye kipato cha
kati, na kufikia huko taka
tujuwe zitazidi kuzalishwa
na kukiwa hakuna taratibu
za kuzidhibiti ifahamike ni
kuelekea kuchangia uchafu
n a m a r a d h i k u e n e z wa
yanayotokana na uchafu.
Hivi miji yetu mingi ipo
na usalama duni wa afya
kwa watu na kupunguza
hata wanaotamani kuja
kutembelea nchi yetu na nchi
zetu za Kiafrika kwa jumla
kuingia na khofu.
Namalizia makala hii kwa
kusema Jee taka zimekuwa
kitanzi kwetu?

1/7/2016 3:17:22 PM

14
Na Shaban Rajab
SIKU hizi matukio ya
watumishi wa majumbani
(yaya) kuwatesa watoto
yameonekana kuwa ni
m e n g i n a k u wa g u s a
watu wengi. Yawezekana
matukio na namna
hii yamekuwepo kwa
kipindi kirefu siku
za nyuma lakini
yalikuwa hayafamiki au
kugundulika. Na hata
yakigundulika taarifa
zake ziliishia eneo
lilipotokea tukio husika.
Lakini kutokana na
kasi ya kukua sayansi na
teknolojia ya mawasiliano,
wingi wa vyombo vya
habari vya kielekroniki
kama mitandao ya kijamii
na televisheni na internet,
siku hizi matukio haya
yamekuwa yakigundulika
mapema na kufahamika
kwa haraka sana. Matukio
haya ya utesaji watoto
mbali na kuzua hisia za
hofu na hasira miongoni
mwa jamii, lakini
yamewafanya wazazi,
hasa kina mama kufikiria
upya ni nani wa kumuajiri
kuwa yaya.
K wa k u wa f a m i l i a
nyingi wazazi hawashindi
nyumbani, yameripotiwa
matukio ya yaya
kuwatwesa watoto katika
madimbwi ya maji, yaya
kumweka mtoto kwenye
jokofu na yeye kutoweka,
wakati mwingine yaya
kumweka mtoto mchanga
hata kwenye jiko la oven.
Ai dha yames h uh udia
matukio mengi ya watoto
kunyimwa chakula,
kupigwa, kutelekezwa
nyumbani bila uangalizi
huku yaya akikata
mitaa. Matukio ya wizi
ndio hayaelezeki. Hayo
ni baadhi tu ya madhila
ambayo hufanywa na
watumishi wa majumbani
kwa watoto wakati wazazi
wao hawapo nyumbani.
Zipo sababu nyingi
ambazo zinaweza kuwa
chanzo cha kuwepo
kwa ufedhuli huu kwa
watoto. Pande zote mbili,
mwajiri na mwajiriwa
z i m e k u wa n a k a s o r o
katika mahusiano yao.
Upande mmoja unaweza
kuwa sahihi na upande
wa pili ukawa na matatizo
kulingana na mazingira ya
pande husika.
Kwa mfano kwa upande
wa Mayaya, mojawapo
ya kasoro au udhaifu
unaoweza kuwa sababu ya
malezo mabaya ya watoto
inaweza kuwa historia ya
maisha pamoja na malezi
aliyopitia yaya katika
makuzi yake.
Yaya wengine wametoka
katika familia zenye malezi
yasiyokuwa na madili.

ANNUUR NEW.indd 14

MAKALA/MASHAIRI

AN-NUUR

RABIUL AWWAL 1437, IJUMAA JANUARI 8 - 14, 2016

Uhusiano wa mwajiri na Yaya


Hupunguza matukio ya kuteswa watoto

MMOJA wa wasichana wanaofanya kazi za ndani. (Picha kwa hisani ya Mtandao)


Wengine wapitia malezi ya
uteswaji na unyanyaswaji
kiasi cha kuathirika
kisaikolojia kiasi kwamba,
hawaoni shida kutumia
mazoea waliyolelewa,
kulelea watoto wa waajiri
wao kwa style waliyokulia
wao. Na hata wanapopata
ajira, aliyempa ajira hiyo
ya uyaya naye asihangaike
kujua kama aliyemwajiri
ana ufahamu wa mambo
yote ya msingi ya ulezi
wa watoto na kutunza
nyumba.
Hata hivyo kulingana
na washauari wa masuala
ya kifamilia, kwa kiasi
kikubwa madhila
haya kwa watoto mara
n y i n g i h u s a b a b i s h wa
na uhusiano mbaya kati
mayaya na waajiri wao,
kuanzia kitabia na kiutu. Baadhi ya familia
(baba na mama) hasa
akina mama, wamejenga
mazoea kwamba, yaya
ni binadamu asiye na
thamani muhimu ndani
ya familia. Hakuna fikra
ya utambuzi kwamba yaya
ndiye mlezi wa watoto,
mtunza nyumba na wakati
mwingine ni mtunza siri
za ndani. Waajiri wengi
hawawapi Mayaya muda
wa kupumzika hata kidogo,
kauli kwao mara zote, ni
ya kufoka na kukemea
badala ya kufundisha
na kuelekeza. Nyumba
nyingi waajiri hawako
tayari kukaa meza moja ya
chakula na Yaya, wakala
pamoja kama familia.
H a wa we z i k u a n g a l i a
televisheni pamoja na
Yaya wala kuzungumza
mazungumzo ya kawaida
na yaya.
Katika familia za namna

hii, utu kwa yaya ni kitu


adimu sana. Kuna hisia za
ubwana na utwana. Yaya
hana nafasi ya kuwa huru
kushauri kutoa maoni
a u k u s h ita k ia ja mbo .
Anakula jikoni, anakaa
jikoni, kukaa sebuleni kwa
bwana iwe ni wito au
shughuli maalum.
Katika familia hizi, yaya
akivunja kikombe au glasi
ni kama amenunua kesi
ya mauaji. Atakaripiwa,
atatukanwa matusi ya kila
namna, kejeli, dharau na
wakati mwingine kipigo
kitakuwa juu yake. Lakini
hatma ya yote lazima
a t a k a t wa u j i r a wa k e
kiduchu, kufidia uharibifu
uliotokea.
Katika familia nyingi,
siku za sikukuu wazazi
watawanunulia watoto
wao zawadi mbalimbali,
ikiwani pamoja na nguo,
viatu, kutembezwa
sehemu za burudani
nk. Katika hesabu hii,
yaya hayupo wala hana
sikukuu. Kisa analipwa
mshahara hivyo ajipe raha
mwenyewe asitegemee
hisani ya familia.
Wapo baadhi ya Mayaya
hata wakiuguliwa, kufiwa
au kuumwa, wakiomba
mapumziko au kusafiri
kujumuika na familia zao
kwenye matatizo, asilani
ruhusa haitatoka la, akizidi
kukera ataondoka na ndio
kujifukuzisha utwana
wake.
Kwa kifupi tunaweza
k u s e m a k u wa , wa n a
familia wengi wanawaona
watumishi wa kazi za
ndani kama watu wenye
dhiki kali na hata ajira
wanayopewa na mabwana
ni kama kupewa ihsani tu

wasiyostahili.
Watoto anaweza kuwa
wa t u n d u s a n a , k i a s i
k wa m b a a n a y e wa l e a
anaweza kuwa na kipimo
cha adhabu ya kiungwana
mradi asiwaumize
au kuwadhuru, ili
kuwajengea hofu
wasirudie makosa. Lakini
wengi hawawezi kufanya
hivyo hata kama watoto
watamkosea. Atanyamaza
hadi afikishe ujumbe kwa
mama mwenye nyumba.
Lakini alishuhudia mtoto
a n a ye m l e a a m e f a n ya
kosa na kweli linahitaji
kumchapa kidogo au
kumfinya kama mwana
familia na hata wazazi
wakirudi akawaeleza kisa
chote. Katika mahusiano
mabovu ya namna hii,
ndio maana tunashuhudia
kuna matukio mengi ya
kuteswa watoto, ambao
hawana makosa. Watoto
wanadhulumiwa na
k u k o s a m s a a d a k wa
s a b a b u ya u m r i wa o
mdogo.
I m e f i k a b a a d h i ya
wazazi hasa wale wenye
uwezo, kuanza kutumia
teknolojia ili kuhakikisha
usalama wa watoto wao
wanapokuwa nje ya
nyumba, badala ya kujenga
magusiano ya kiutu baina
ya pande mbili hizo.
" N i k i wa n a u w e z o
nitaweka kamera kwa
n y u m b a ya n g u . K wa
sababu kama umeweka
k a m e r a uk i wa k a z i ni
hautakuwa na wasiwasi.
Anazungumza mzazi
mmoja wa huko Uganda.
L a k i n i m s h a u r i wa
mambo ya jamii Bi. Anne
Nafula anaona kwamba
k u w e k a m i t a m b o ya
kamera sio suluhu la
kutosha kwa masuala

kama haya.
"Lazima mwajiri aelewe
k wa m b a m f a n ya k a z i
nyumbani sio mfanyakazi
tu, anafaa amuweke karibu
kama mmoja wa ukoo au
jamii ili ajione ni sehemuya
familia na amwangalilie
mtoto kwa njia nzuri,
lakini ukimchukulia
kwamba hana thamani
katika nyumba yako, basi
atafanya vile anavyopenda"
Alibainishamtaalam huyo.
Aidha kulingana na
ripoti za vyombo vya
habari ni wazi matukio ya
yaya kuolewa au kupata
watoto na waajiri wao
yameongezeka.
Haya ni matokeo ya
wazazi kuthamini zaidi
kazi na kutumia muda
wote kazini kuliko
mahusiano ya kifamilia. Bi.
Nafula analaumu baadhi
ya wanawake walioolewa
kwa kutelekeza majukumu
yao na kumwaachia yaya
kufanya shughuli zote
za nyumba hata zile
zinazochochea mahusiano
ya mume na mke.
M a j u k u m u
yanayostahili kufanywa
n a m k e wa n y u m b a ,
yanapatiwa msichana
w a k a z i . Wa n a w a k e
we n g i wa m e s h i n d wa
na majukumu yao hata
ya kulea watoto, hata
kuangalia waume zao. Na
wengi kwa kuzoe huduma
z a Ya ya , wa m e k u wa
wavivu kupita kiasi.
Na baadhi ya wanaume
wenye husuda ya mapenzi
na wakayakosa kwa wake
zao, hawaangali sana
urembo linapofika swala
la mapenzi, wanaangalia
yule anayemletea huduma,
kumpelekea maji ya kuoga,
maji ya kunywa nk.
Sote tunakiri kwamba
kitendo cha kumfanyia
mtoto mateso, ni uhalifu na
unyama mkubwa. Adhabu
yake ni jela kisheria iwapo
mtuhumiwa atapatikana
na hatia. Nchi9ni Uganda
mtuhumiwa huadhibiwa
kwa kufungwa hadi miaka
15 gerezani wakati nchini
Kenya adhabu ya kosa hilo
ni zaidi ya miaka kumi.
Lakini ifahamike kuwa
kukinga ni bora kuliko
kuponya. Ni vyema wenye
nyumba kujenga urafiki na
watumishi wao. Hapo hata
wakitokea wale ambao
hawavumiliki, basi ni haki
ya mwajiri kumfukuza
au kumchukulia hatua za
kisheria mtumishi wake.
Kwa kufanya hivyo,
kwa kweli kutapunguza
kwa kiwango kikubwa sio
tu kuteswa kwa watoto,
bali pia kuwa na familia
imara.

1/7/2016 3:17:23 PM

15
Inatoka Uk. 9

ganzi na kushindwa
kupaza sauti, pengine ni
kutokana na mazingira
ya kizalendo
yaliyokwishajijenga.
Ukiangalia Baraza la
Mawaziri alilotangaza
Mh. Magufuli, utaona
kuwa Waislamu katika
Baraza hilo (Japo kwa
majina yao tu) ni 9
(8?) kati ya 34 sawa na
24%! tu. Hii ina maana
Wakristo katika Baraza
la Mawaziri ni 76%!
Tu n a j u a h i i n i
Awamu ya Hapa Kazi
tu, na kigezo cha mtu
kuingia katika Timu
ya Kumsaidia Rais, ni
uchapa kazi. Swali ni
je, hakuna Waislamu
wachapa kazi wenye
sifa za kuwa mawaziri
wa kumudu kasi ya
Mheshimiwa Rais JPM?
Tunajua pia kuwa
Imani ya mtu, haitafsiri
utendaji kazi wake au
uvivu wake au hata
ufisadi wake na hivyo
katika Hapa Kazi Tu,
hoja ya Imani wakati
wa u t e u z i , ya we z a
kuwa haikuzingatiwa.
Lakini pengine tujiulize,
itakuwa halali na sawa
kisiasa, watu wa dini
moja kufanya maamuzi
na kuamua mustakabali
wa nchi hii peke yao? Je,
hii inasaidia vipi kujenga
umoja na mshikamano
w a Wa t a n z a n i a n a
kuondoa ubaguzi? Je,
hii ndiyo tafsiri stahiki
(kivitendo) ya kauli na
ahadi ya Mheshimiwa
Rais Magufuli kwamba
ataongoza kwa haki
bila ya kubagua dini za
watu?
Wa p o M a w a z i r i
waliotolewa kutoka
s e h e mu mb al i mb al i
na hawajawahi kuwa
viongozi wa kisiasa,
haiingii akilini kwangu
k u wa Wa i s l a m u
hawapo!
Ikiwa inadhaniwa
kuwa suala la imani
sio muhimu katika
uteuzi, hii ina maana
inahalalisha watu wengi
wa dini moja kufanya
maamuzi ya nchi peke
yao. Labda tusaidiane
kwa pamoja, tunajua
katika nchi hii zipo Dini
Kuu mbili, Uislamu na
Ukristo. Je, iwapo haya
ya 20 kwa 80 yaliyo kwa
Waislamu yatageuziwa

ANNUUR NEW.indd 15

Makala

AN-NUUR

RABIUL AWWAL 1437, IJUMAA JANUARI 8 - 14, 2016

Mh. Magufuli anaturudisha


kule kwa Sheikh Takadiri

MZEE Edwin Mtei


kwa upande wa pili,
wenzetu wataridhia
tukitumia hoja ile ile
serikali haina dini na
hat u a n g alii din i ya
mtu?
Aliwahi kulalamika
Mzee Mtei ilipoteuliwa
Tume ya Mzee Warioba
juu ya Katiba akisema
k u wa k u l i k u wa n a
Waislamu wengi na
akasisitiza kuwa hoja
kwamba nchi haina
dini na haiongozwi
kwa misingi ya dini,
haistahiki kutolewa.
A k a s e m a , h a t u we z i
kupinga ukweli kwamba
mtizamo na maamuzi
ya watu yanaathiriwa
na Imani za dini zao.
Lakini tutakumbuka
pia kwamba wakati
wa Mzee Ally Hassan
Mwinyi ilitokea katika
Baraza lake la Mawaziri,
yakaongezeka majina
ya Waislamu kinyume
na ilivyokuwa ada.
Japo idadi yenyewe
wala haikufikia robo ya
Mawaziri wote, lakini
zikapigwa sana kelele na
kudaiwa kuwa Mwinyi
anataka kuisilimisha
Tanzania. Hayo yaliwahi
kutokea pia kwa Rais
Mstaafu JK alipoteuwa
idadi fulani ya Mabalozi
ikaonekana kuwa
kulikuwa na majina
mengi ya Waislamu.
Nakumbuka marehemu
Profesa Seithy Chachage
aliwahi kutupiwa
swali kwamba haoni
kuwepo kwa majina
mengi ya Kiislamu ni
dalili kuwa Kikwete
anapendelea Waislamu?
Jibu la Profesa Chachage

PROF. Chachage
lilikuwa kwamba inabidi
kwanza ufanyike utafiti
tujue serikalini katika
nafasi zote muhimu,
kuna Waislamu wangapi
na Wakristo wangapi,
ndio tuseme.
Kama huu ndio ukweli
kama alivyoubainisha
Mzee Mtei, na kama hii
ndiyo hali unapogeuza
mambo kwa upande wa
pili, kwa nini idhaniwe
kuwa Waislamu wao
wataridhia kuona Baraza
la Mawaziri na Timu
ya Watendaji Wakuu
Serikalini katika Uwiano
huu wa 20 kwa 80?
Kama Mh. Rais
anaamini kuwa kuna
Waislamu walimpigia
kura na hata kumpigania
hata akashinda, siamini
kuwa walikuwepo tu
Waislamu wa kupiga
kura, lakini wa kushika
nafasi za Mawaziri na
Makatibu Wakuu, tabu
kuwapata.
Katika mambo ambayo
Waislamu wamebaki na
butwaa, ni uteuzi wa
Mh. Ndalichako kuwa
Waziri wa Elimu. Mtu
ambae alisababisha
mpaka maandamano
dhidi yake kutokana
na tuhuma za hujuma
i l i y o k u wa i k i d a i wa
k u f a n y wa d h i d i ya
Waislamu akiwa Katibu
Mtendaji wa Baraza la
Mitihani la Taifa. Mh.
Ndalichako alidiriki
kubadilisha matokeo
ya mtihani yaliyokuwa
tayari yametangazwa
b a a d a ya k u p i g i wa
kelele! Wakati akiwa

DKT. Jakaya Kikwete


Katibu Mtendaji wa
Baraza la Mitihani la
Ta n z a n i a . L e o n d i o
kapewa nafasi ya kuwa
Waziri wa Elimu!
Uteuzi wa Makatibu
Wakuu
Uteuzi wa Makatibu
Wakuu haukuwa na
nafuu kwa Waislamu
hata kidogo. Kwani kati
ya Makatibu Wakuu
na Manaibu wao
walioteuliwa wapatao
50, kati yao Waislamu
japo kwa majina ni 10
(11?) tu sawa na 20%,
huku waliosalia sawa
na 80% ni Wakristo.
Hawa ndio watendaji
wa serikali. Hawa ndio
wanaopanga na kuratibu
mipango ya maendeleo
ya nchi. Bado hoja ni zile
zile, inawezekana ikawa
ni kweli kuwa hakuna
Waislamu wachapakazi
na wenye sifa za kuwa
M a k a t i b u Wa k u u
wanaoweza kumudu
kasi ya Mheshimiwa Rais
JPM? Kama ilivyokuwa
kwa Mawaziri, wapo
pia Makatibu Wakuu
walioteuliwa wakitokea
katika taasisi za elimu ya
juu na taasisi nyingine. Je,
huko hakuna Waislamu
wenye sifa na uwezo
wa kushika nyadhifa
h i z o ? I n a we z e k a n a
wakawa wapo, lakini
Mh. Rais hakuona haja
ya kuzingatia uwiano
wa dini mbalimbali
katika uteuzi. Lakini
mtu anaweza kuhoji,
kama ingekuwa si
kuzingatia imani, basi

ingetokea bahati mbaya


Waislamu nao wakawa
wengi katika orodha
ya Makatibu Wakuu
kama ilivyokuwa kwa
Wakristo katika Baraza
la Mawaziri. Lakini
bahati mbaya imekuwa
ya kuwaangukia
Waislamu kwa nyanja
zote! Sijui Sayansi ya
Bahati Nasibu-sio jambo
la kupanga (Science of
Coincidence), inasemaje
hapa.
Ikumbukwe kuwa
Mh. Rais aliahidi
wakati wa kampeni
kuwa, katika utawala
wa k e h a t o wa b a g u a
watu kwa rangi zao,
makabila yao wala dini
zao. Kauli sahihi kabisa.
Lakini labda tujiulize,
kipi cha kuthibitisha
ahadi hii? Kama
nilivyotangulia kusema,
ya w e z e k a n a k a t i k a
kuongozwa na ahadi
hiyo ya kutokubagua,
Mheshimiwa Rais
hakutizama kabisa suala
la dini katika uteuzi
wa k e . L a k i n i l a b d a
pengine tuligeuze jambo
hili liwe kwa upande
mwingine. Asilimia 10
ya Mawaziri Wakristo,
90 Waislamu, asilimia
80 ya Makatibu Wakuu,
Waislamu, waliosalia
dini nyingine!
Huu ni mwanzo wa
safari ndefu mbele
ye t u . Tu n a m u o m b a
Mh. Magufuli atembee
juu ya maneno yake,
atende haki. Hoja za
kisiasa kwamba katika
uteuzi hatujali dini bali
sifa, haitatusaidia sana
na wala haifanyi kazi.
Labda atokee mtu aje
na utafiti wa kisayansi
kuthibitisha mambo
mawili. Moja, kwamba
kadiri alivyochambua,
hao asilimia 20 tu,
ndio Waislamu pekee
aliopata katika seti ya
Waislamu nchini wenye
sifa za kuwa Mawaziri
na Makatibu Wakuu.
Lakini pia katika utafiti
huo, atuonyeshe sifa
zilizozingatiwa katika
hao waliowateua ili
kuweza kuona kwamba
kweli katika seti ya
Waislamu wenye sifa,
hakuna mwenye sifa
hizo.
Abdallah Juma
P.O.BOX 7201
Dar es Salaam

1/7/2016 3:17:23 PM

16
Inatoka Uk. 7
ilibadilishwa kwa kati
ya shilingi 7 na 7.50
kuanzia mwaka 1971
1979. Mfumuko wa
bei ulikuwa ni chini
kwa kipindi chote cha
utawala wa Iddi Amini.
Hadi Iddi Amini
anapinduliwa mwaka
1979, hospitali kuu
ya Mulago pamoja
na hospitali zote
za serikali Uganda
zilikuwa na magodoro,
mashuka na mito na
mablanketi na hakuna
mgonjwa aliyelala
chini kama ilivyo leo
hii. Pia kila chumba
cha binafsi hospitalini
hapo kilikuwa na
televisioni ya rangi.
Matibabu yote kwa
Waganda yalikuwa
ni bure. Kwa ujumla
kiuchumi Uganda
ilikuwa haijafikia hali
mbaya hata kidogo na
ndio maana baada ya
Iddi Amini kuingia
madarakani jumuiya
ya kimataifa iliiwekea
vikwazo vya kiuchumi
Uganda, lakini Uganda
iliweza kumudu hali
hiyo bila matatizo.
Baada ya kuvunjika
kwa Jumuiya ya Afrika
Mashariki mwaka 1977,
Uganda iliunda Shirika
la Ndege (Uganda
Airlines) na shirika
la reli kutokana na
masalia ya Jumuiya ya
Afrika Mashariki. Hii
yote ilikuwa ni katika
kuimarisha Hadhi ya
Taifa- National Pride.
Tatizo kubwa kwa
Iddi Amini lilikuwa
ni vikundi vya waasi
waliokuwa katika
nchi za jirani wakipata
misaada mbalimbali
kutoka nchi za
magharibi wakijipanga
kuivamia Uganda
na kumngoa Iddi
Amini wakati wowote.
Ikumbukwe tu kuwa
vikundi vya waasi
vilikuwa vikiongozwa
na watu kama Yoweri
Museveni ambaye
kwa sasa ni raisi wa
Uganda.
Hadi hapa ni wazi
kuwa Iddi Amini

ANNUUR NEW.indd 16

Makala

AN-NUUR

RABIUL AWWAL 1437, IJUMAA JANUARI 8 - 14, 2016

Vita vya Kagera

RAIS wa zamani wa Uganda, Dkt. Milton Obote.


ambaye anaelezwa
chanzo cha vita hii?
kama mtu katili na
Tuanze na harakati za
aliyechukiwa sana
awali katika eneo la
nchini Uganda
mpakani Mtukula
anaonekana kama
- kati ya Tanzania
alikuwa ni kiongozi
na Uganda mwaka
mwenye mafanikio ya
1978. Kwa mujibu
kiuchumi. Je ni kwa
wa Generali Yusuf
nini alichukiwa; ama
Himidi akinukuliwa na
ni kwanini utawala
gazeti la Standard la
wake usababishe watu
Tanzania toleo la tarehe
kuunda vikundi vya
3/07/1978, Generali
waasi? Ni wazi watu
Himidi aliyekuwa
kama Milton Obote,
ni kamanda wa
ambaye alikuwa
Brigadi ya Magharibi,
rafiki mkubwa wa
alisema kuwa Uganda
Julius Nyerere ndiye
inajihusisha na
aliyehusika sana
matendo ambayo
kumpaka matope
yanaweza kusababisha
mapambano ya kijeshi
Iddi Amini akieleza
kati ya nchi hizo mbili.
kuwa vita ya mwaka
Matendo yaliyokuwa
1978 -79 ilisababishwa
yanalalamikiwa na
na Iddi Amini. Ni
Generali Himidi
wazi kunahitajika
uchambuzi zaidi
inasemekana yalikuwa
wa kina na usio na
yametokea na
upendeleo wa aina
kuelekezwa kwa raia
yoyote (objective) na
wa Tanzania kutoka
si hizi hekaya za akina
kwa watu ambao
Obote na Museveni
kiasili walikuwa
kwani hazina uzani
Waganda ambao
sawasawa.
inaaminika walitokea
Swali la msingi:
upande wa Tanzania.
Ni je, ni nini hasa
Hii inaonesha kuwa

uchokozi wa mwanzo
kabisa ulitokea
Tanzania, kwani
Iddi Amini aliwahi
kulalamika kuwa
Tanzania inatumia
eneo la Mtukula
kuwapenyeza waasi
wa Uganda ambapo
aliweka kikosi
maalumu kujaribu
kuzuia shambulizi
lolote ambalo
alilitarajia.
Je, waganda ambao
walitokea Tanzania ni
akina nani? Na kama
walikuwepo, ni wazi
Iddi Amin alikuwa
sahihi ama alikuwa
anaongopa? Ingawa
hakuna uhakika sana,
lakini kama mtu
atarejea katika kitabu
kiitwacho: Sowing
the Mustard Seed: The
Struggle for Freedom and
Democracy in Uganda
ambacho kimeandikwa
na mwanamapinduzi
wa Uganda, Yoweri
Kaguta Museveni,
tunaweza kuona
uhalali wa madai
ya Amin. Katika
ukurasa wa 62, ni
kuwa katika kipindi
hicho, yeye alikuwa ni
mpigananji wa msituni
akiongoza kikundi
cha wakombozi wa
Uganda waliokuwa
wakiendesha harakati
zao katika eneo la
Kagera, sehemu
iitwayo Kagera
Salient. Kikundi
cha akina Museveni
kilijulikana kama
FRONASA. Je,
si inawezekana
ndio waliokuwa
wakiendesha mauaji
dhidi ya raia wa
Uganda mpakani
Mtukula mwaka 1978
ambapo waliwaua
wakazi wanne wa
Kiganda waliokuwa
wakinywa pombe ya
kienyeji MALWA
mpakani? Mauaji hayo
ndiyo yaliyomchagiza
Amin kuamua
kuiona Tanzania

kama mchokozi. Na
inawezekana kabisa,
FRONASA ilikuwa
inagombanisha nchi
mbili hizi ziingie
vitani huku wakijua
watafaidika na vita
hiyo.
Kwa mfano,
inasemekana Iddi
Amini aliunda kikosi
maalum kuweka
usalama eneo la
Mtukula Malire
Troops baada ya
mauaji ya raia wa
Uganda na watu
wenye asili ya Uganda
ambao waliingia
kutokea Tanzania
na baada ya mauaji,
walikimbilia nchini
Tanzania. Chanzo cha
uvamizi wa Tanzania
inasemekana ilikuwa
katika kujibu mapigo
baada ya jeshi la
Uganda, kupitia
kikosi cha Malire
Troops kuingia Kagera
kuwasaka wauaji

wa raia mmoja wa
Uganda aliyeuawa.
Raia huyo alikuwa ni
shemeji wa Kamanda
Mkuu wa Malire
Troops, Luteni Kanali
Juma Ali. Malire
Troops waliingia
Kagera hadi kilomita
80 ndani ya Kagera.
Kwa mujibu wa
gazeti la Weekly
News, toleo la tarehe
5/11/1978. Majeshi ya
Tanzania yaliivamia
Uganda kuanzia
tarehe 10 31, 1978
na kuteka maili 400
za mraba sehemu
ya Uganda ambapo
mapambano makali
yalifanyika katika
kilima cha Minziro.
Mpaka nukta hii,
bila shaka umepata
picha kwa kiasi
fulani, chanzo cha
vita hii ambayo ilitia
nchi yetu kwenye
lindi kubwa la
umaskini. Kimsingi
zipo sababu zaidi
ya hizi na tutaziona
zaidi Inshaallah.
(Juma Jumanne,
Katesh, Manyara, 0659
789 468.)

1/7/2016 3:17:24 PM

17

MAKALA/TANGAZO

AN-NUUR

RABIUL AWWAL 1437, IJUMAA JANUARI 8 - 14, 2016

Uislamu ni dini ya msamaha na kuhurumiana

Na Dk. Akili Mohamed Akili

SHUKURANI zote
anastahiki Mwenyezi
Mungu, Mola mlezi
wa dunia na rehema na
amani zimfikie mbora wa
Manabii na Mitume wote,
Sayyid na Muhammad
(S.A.W) .
U i sl amu n i din i ya
msamaha na huruma
n a m u o n g o z o , k wa n i
ameamrisha Mwenyezi
Mungu mtukufu kwa waja

wake juu ya msamamo na


uadilifu katika kutelekeza
ibada na amekataza
kuvuka mipaka.
Aidha Allah (s.w)
amekataza
kuvuka
mipaka na kwa
hakika dini ya Kiislam
inakataza mtu kijitenga
na kungangania rai aina
moja tu na imeharamishwa
pia kuamini Mungu asiye
Mwenyezi Mungu mmoja.
Kiutamaduni au kidini
na kimaendeleo sio vizuri
kuvuka mipaka na ni
vyema kufanya jambo
la kati na kati na pia
kuhimiza kufanya mambo
yaliyo mema.
Uislam ni dini ya
rehema na msamaha na
umependelewa umma
huu na umma nyingine
miongoni mwa umati,
kwa kuwa ni ummah
bora kama alivyosema
Mwenyezi Mungu
mtukufu, Na hivyo hivyo
tumekufanyeni umma

Wekeni Mfumo wa Zakkah

Inatoka Uk. 20

Zanzibar (JUZASA) Sheikh


Talib ametolea mfano wa nchi
kama Denmark ambako licha
ya kuwepo asilimia ndogo
ya Waislamu kama 3% lakini
imeweka utaratibu mzuri
wa ukusanyaji wa Sadaka na
Zaka jambo ambalo husaidia
kwa kiasi kikubwa kuondoa
dhiki kwa wenye shida ndani
ya nchi hiyo na hata nje ya
nchi hiyo.
Zanzibar ambayo ina
Wasilamu asilimia 99%
ilipaswa kuwa ni mfano
wa nchi nyengine, lakini
amesema bado elimu
ya kutekeleza ibada hiyo
muhimu haijawafikia watu
wengi na bado wenye
uwezo hawajaamua kufuata
utaratibu ambao umewekwa
katika mafundisho ya Bwana
Mtume Muhammada (s.a.w)
wa kuwasaidia watu wasio na
uwezo katika jamii.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa Jumuiya
hiyo, Sheikh Said Masoud
(Gwiji), amesema, bado

muamko wa watu wenye


uwezo kutoa Sadaka na Zaka,
ni mdogo kabisa.
Bado muamko ni mdogo
sana hasa kwa ndugu zetu
Wafanyabiashara kutoa zaka
na sadaka wanaona tabu sana
lakini hili jambo ni ibada na
linatakiwa litiliwe nguvu
kwani, (wakati mwingine)
fedha na vitu vinavyotolewa
zaka vinapelekwa kwa wale
wenye uwezo na kuwaacha
wahitaji. Alisema Sheikh
Masoud.
Lakini hata misaada
ikipelekwa kwa wahitaji, sio
katika utaratibu wa kuleta tija
iliyokusudiwa.
Kwa upande wake Katibu
wa Jumuiya hiyo ya JUZASA,
Sheikh Omar Abubakar
Mohamed amesema jumuiya
hiyo imeshatoa zaka kwa
watu 46 zikiwemo fedha
taslim, na vitu vyengine kama
Vyarahani, Friza na baadhi ya
watu tayari wameshajengewa
nyumba za kuishi na familia
zao.

Kesi ya Sheikh Msellem danadana zaendelea


Inatoka Uk. 20

ukisha kamilika hupelekwa


Mahakama Kuu kwa ajili ya
kuanza kusikilizwa.
Hivi karibuni Mahakama
ya Hakim Kisutu Jijini Dar
es Salaam, iliutaka upande
wa mashitaka (Serikali)
kukamilisha upelelezi
katika kipindi hiki kabla
shauri hilo halijapelekwa
Mahakama Kuu.
Kwa mara nyingine tena

ANNUUR NEW.indd 17

kesi hiyo imeahirishwa


kufuatia Hakimu,
anayesikiliza kesi hiyo
kutokuwepo Mahakamani
kufuatia kufiwa na mzazi
wake hivyo kulazimika
kwenda katika maziko.
Yule Hakimu
anayesikiliza kesi
hii hayupo kwa hiyo
imeahirishwa na Hakumu
mwingine aliyefahamika
kwa jina moja la Mchauru.
Ameeleza Wakili Hamidu.

wa kati na kati ili muwe


mashahidi kwa watu na
awe Mtume kwenu ni
shahidi kwenu (143)
Albakarat.
K wa m a a n a u m m a
b o r a we n ye u a d i l i f u
kwa utukufu na ubora.
Dalili za mapatano ya
wanazuoni juu ya ukati
na kati yamekusudia juu
ya mizani na usawa na
kutukuka na ni umma wa
watu ambao upo katikati
ya kuvuka mipaka.
I m e p e n d e l e wa d i n i
yetu hii kwa msamaha
na uwepesi na kuondoa
m a t a t i z o n a wa f u a s i
wake. Hizi zote ni sifa
kwa umma huu na dini
hii, isipokuwa wapo watu
wanaokwenda kinyume
na mafundisho ya Allah
(s.w) na hatimae kutoka
kabisa katika alama za
umma huu na kutengana
na njia iliyonyooka na
kwenda na miongozo
sahihi ya dini yetu.
Muonekano huu wa
kwenda kinyume na
mafundisho ya Allah

huwapa nafasi maadui wa


Uislam kuubebesha mzigo
wa dhulma miongoni mwa
mizigo hiyo ni kuuzushia
na madai ya uongo ambayo
wanaupambanisha nao
Uislam kama tuhuma za
ubabe na ugaidi.
Kutokuwa na msamaha
na mengineyo juu ya
madai ambayo hayana
msingi wowote katika
Uislam na wala hayana
muegemeo wake katika
elimu wala juu ya matukio
ya kihistoria ya Uislamu.
Hufanya hivyo kwa
kukusudia au bila ya
kukusudia kutokana
na fikra mbaya
iliyopandikizwa juu ya
vichwa vya watu. Huo
ni msaada mkubwa kwa
maadui wa Uislam na
katika kuhakikisha mradi
wao katika kuwapata
Waislam na dini yao.
Sheria imekemea
kuvuka mipaka na pia
kujitenga katika dini.
Amesema Mwenyezi
Mungu mtukufu, Sema
eti watu wa kitabu

msivuke mipaka katika


dini yenu kwa yasiyo ya
haki 77 Al-Maidah.
Anasema Bin Khathir
(R.W) anawakataza
Mwenyezi Mungu watu
wa kitabu juu ya kuvuka
mipaka na kujitenga na
amesema Mtume (s.a.w),
Wameangamia wale
wanaovuka mipaka na
akafafanua Imamu
Nawawi katika Sahihi
Muslim (220/16). Amesema
Imamu Nawawiyi, Ni
wale waliozama katika
upotevu wa wanaovuka
mipaka katika kauli zao na
vitendo vyao.
Na akasema Mtume
(s.a.w) Jitahadharisheni
na kuvuka mipaka kwani
wameangamia watu
waliopita kabla yenu kwa
kuvuka mipaka katika
dini. Ameipokea Imamu
Ahmad na hivi ndivyo
ilivyo mpenzi msomaji,
tunaiona sheria ya Kiislam
inahimiza juu ya kufanya
mambo kwa kiasi.

Ahlu Daawa Hajj and Travel Agency

Inawatanganzia Waislam wote kuwa imeandaa safari ya Hijja mwaka 2016 sawa
na mwaka 1437 Hijria kwa Dola US$ 3,555
Kutakuwa na punguzo la asilimia 16% kuanzia muda huu mpaka Feb 29/2016.
Itakuwa Dola $2986 tu.
Kuanzia mwezi Machi 01-2016 mpaka Juni 12-2016 kutakuwa na punguzo la
asilimia 6% sawa na Dola $3,341 tu.
MAMBO YATAKAYOGHARAMIWA
1. Semina za Hija, 2. Huduma za afya na kuchinja 3.Airport Charge na ticket
za Ndege 4.Nyumba Makkah na Madina 5.Irham na Kuchinja kwa ajili ya
Tama-tuu 6.Chakula wakati wote 7.Usafiri na ziara Makkah na Madina
8.Mahema Mina na Arafa.
UMRA MWEZI WA RAMADHANI ITAKUWA NI DOLA US $1995
Fomu zinapatikana sehemu zifuatazo:1.Ofisi ya Ahlul Daawa Dar es Salaam Mtaa wa Dosi na Mkadini nyumba
Namba 26 mkabala na Showroom ya magari Tell. 0713 730 444, 0773
804 101 ,0785 930 444 au 0773 930 444.
2. Ofisi ya Ahlu Daawa Zanzibar Rahaleo Tel: 0777 484 982, 0777 413
987.
3. Abubakr Maulana wa Markaz Kiwalani Dar es Salaam, Tel: 0784 453
838
4. Abdallah Salehe Mazrui (Hoko) Dar es Salaam, Tel: 0715 724 444
5. Abdallah Hafidh Mazrui, Wete Pemba Tel: 0777 482 665
6. Mohammed Hafidh Mazrui Mkoani Pemba 0777 456 911
7. Sheikh Daud Khamis Shekha Tel: 0777 679 692
8. Maalim Seif Humoud Hamed (Kijichi Zanzibar) 0777 417 736
WAHI KULIPIA
1. Ofisi ya Ahlul Daawa Dar es salaam Tel: 0713 730444, 0773
804101,0785 930444.
2. Ofisi ya Ahlul Daawa Zanzibar Rahaleo Tel: 0777 484982, 0777 413
987.
Maalim Seif Humoud Hamed (Kijichi Zanzibar) Tel: 0777 417 736
TANBIH
(a) Atakaemaliza taratibu zote mwanzo ndie atakayeshughulikiwa
mwanzo
(b) Ili uwemo katika fungu la kwanza unatakiwa umalize taratibu
zote kabla ya punguzo
(c) Kumbuka kikundi cha Ahlul Daawa kwa bei nafuu kuliko wote
na huduma kuliko wengi.
Wabillah Tawfiq

1/7/2016 3:17:24 PM

18

MAKALA/TANGAZO

UONGOZI wa gazeti la An-Nuur


unatoa shukurani kwa Wasomaji
wa gazeti hili kukushukuruni
kwa dhati kutuitikia na kuwa
An-Nuur ni Sauti ya Waislamu.
Gazeti hili linataka kuboresha
matoleo yake kwenu wasomaji
na ikiwezekana kuongeza kurasa
na hayo hayawezekani pasi na
kupata mashirikiano yenu kwa
kutoa maoni yenu juu ya matoleo
yetu mbalimbali. Kipi mnakiona
ni vyema kuongezwa na kipi
mnaona kipunguzwe na kipi
kiondolewe kabisa.
Survey hii tutaifanya kwa njia
tatu nazo ni: (i) Kutumia njia ya
Posta, (ii) Barua pepe (e-mail)
na (iii) Ujumbe mfupi (SMS).
Watakaotuma kwa njia ya Barua
pepe na Posta, wajaribu kukopi
Jadweli hapo chini.
Majibu kwa ujumbe mfupi
Kwa wale watakaotuma kwa
kutumia ujumbe mfupi (SMS,)
tutaomba wachukue wakati wao,
kwenye Makala tulizoorodhesha
aziandikie, kisha afanye hivi:
1.Ukarasa wa mwanzo aupe
point tuseme (4) 2. Tahariri (4)
3.Uchambuzi wa Msangi (4) 4.

AN-NUUR

RABIUL AWWAL 1437, IJUMAA JANUARI 8 - 14, 2016

SURVEY KWA WASOMAJI


Habari za Kimataifa (2), mpaka
mwisho.
Wasomaji watoe maoni yao
wanafikiri kipi kiongezwe na kipi

Jadweli ya Survey

Makala
1.Ukarasa wa mwanzo na wa mwisho (Habari)
2. Tahariri.
3. Uchambuzi wa Omar Msangi.
4. Habari za Kimataifa.
5.Hoja za Juma Kilaghai.
6. Makala kwa Jumla.
7. Safu ya Ben Rijal
8. Masheikhe waliopita.
9. Mashairi.
10. Waandishi
Msangi
Juma Kilaghai
Ben Rijal
Khatib J Mziray na Waalikwa wengine

kiondolewe, tumeweka mfano


hapo chini.
Chakuongezwa: Barua za

Mashindano kila mwezi na


kutolewa zawadi n.k. (huu ni
mfano tu)
Chakuondolewa: Chemsha
Bongo, Mashairi n.k. (ni mfano)

wasomaji, Malezi ya watoto,


Ubora (Points)

Chakuongezwa

Chakuondolewa

Points: 1. Afadhali, 2. Inatosheleza 3. Nzuri 4. Nzuri sana.


Simu kwa ajili ya ujumbe mfupi: 0654 00 15 45, 0777 43 69 49, 0714 111 669, 0655 91 06 23
Barua pepe: annuurpapers@yahoo.co.uk
Barua za kawaida: P. O. Box 55105 Dar es Salaam

ABDULRAHAMAN AL SUMAIT MEMORIAL UNIVERSITY- ZANZIBAR

(SUMAIT University)
(FORMERLY UNIVERSITY COLLEGE OF EDUCATION-ZANZIBAR)

15TH GRADUATION
The Vice Chancellor of SUMAIT University invites all Granduands of the academic year
2013/2014 to the 15th Graduation, which will be held on Tuesday 19th January 2016 at
the SUMAIT University premises- Chukwani.
All Graduands are required to confirm their participation to the Academic Office not later
than Thursday 14th January 2016. Graduands are reminded to pay TZS 10,000/=
(nonrefundable) before Friday 15th January 2016 for graduation gowns.
Please note that travel, meals and boarding expenses will be met by the Graduands
themselves. All Graduands are requested to report at the University by 3.00 pm on
Monday 18th January 2016 for rehearsal and logistical briefings. Graduands who will
not participate in the rehearsal will not be allowed to take part in the event.
For more information please contact SUMAIT University at the following address:
The Academic Office,
SUMAIT University,
P.O.BOX 1933, Zanzibar,
E- mail: info@zitec.org/amacez@zitec.org
Website: www.sumait.ac.tz
Mobile: 0776-463405/ 0773-181786

ANNUUR NEW.indd 18

1/7/2016 3:17:25 PM

19
KUNA imani kuwa
Msalaba ni nembo
ya Ukristo, lakini
inawezekana kuwa watu
hawajui kuwa nini maana
ya neno msalaba. Neno
msalaba linatokana na
neno sulubu, kwa maana
ya tabu, mateso, shida
n.k. Hivyo kama ni kazi,
ni kazi ya mateso, kama
ni maisha, ni maisha ya
mateso, kama ni kipigo,
ni kipigo cha mateso na
kama ni kifo, au kuuawa,
ni kifo au kuuawa kwa
mateso mabaya.
Kuunganishwa kile
kinachoaminika kuwa
Ye s u a l i s u l u b i s h wa
k wa m a a n a ya k u wa
alipigiliwa msalabani,
na kuunganishwa kuwa
msalaba ni nembo ya
ukombozi kwa dini ya
Kikristo, inawezekana
kuwa si sahihi, kwa kuwa,
k u wa s u l u b i s h a wa t u
kulikuwepo hata kabla ya
Yesu kuzaliwa. Na ilikuwa
ni sheria ya ukatili ulio
tendwa na serikali ya
Kirumi kwa enzi hizo.
Ndiyo maana walikuwa
na mahali maalumu
pa kusulubishia watu
palipoitwa Goligotha.
Ya a n i m a h a l i p e n y e
mafuvu ya watu walio
teswa na kufia hapo na
kuozea hapo.
Ndiyo maana sheria
ya Taurati ikatofautisha
unyongwaji wa mtu
aliyestahili kunyongwa na
ile sheria ya Kirumi, pale
ilipoandikwa hivi:
Akiwa mtu ametenda
dhambi ipasayo kufa,
akauwawa, nawe
ukamtundika juu ya mti,
mzoga wake usikae usiku
kucha juu ya mti, lazima
utamzika siku hiyo hiyo,
k wa n i a l i ye t u n d i k wa
amelaaniwa na Mungu,
usije ukatia unajisi katika
nchi yako akupayo Bwana
Mungu wako iwe urithi
wako. (Kumb. 21: 22-23)
Alama ya pande nne,
au jumlisha sio msalaba.
Neno hilo la msalaba,
limeingizwa na mfalme
wa Rumi ili kuchochea
jazba na hasira kwa askari
wake wakati wakipigana
vita kwa kuvamia mataifa
mengine, ili wahakikishe
kuwa wanawasulubu
bila huruma
wale
wote waliowaita
kuwa ni maadui zao.
Kilichozungumziwa hapo
juu, ni kutundikwa mtini

ANNUUR NEW.indd 19

MAKALA/TANGAZO

Vita ya Msalaba

au kunyongwa, iwe ni
kwa kamba au nduano
(ndwana).
Mwaka A.D. 312
Constantine alikwenda
kupigana vita na Maximian
aliyekuwa amejitwalia
kwa hila ufalme wa Italy
na wa Afrika. Constantine
alipokuwa akisafiri
kwenda vitani alisema
kwamba aliona maono ya
ajabu: maana mbinguni
ilitokea dalili au ishara
k a m a ya m s a l a b a wa
mwanga ukizungukwa
n a m a n e n o ya m o t o
ya l i y o n g a a : m a n e n o
yenyewe ni haya: Kwa
ms alaba h u u u ta p a ta
ushindi. Basi Constantine
akaamuru kwamba mfano
wa msalaba ushonwe
katika bendera zote za
majeshi yake. Akaenda
akamshinda Maxsentius
kisha aliporudi Rumi
akasimamisha sanamu
humo mjini mfano wake
yeye mwenyewe, sanamu
aliyechorwa katika jiwe
kuu. Na sanamu huyo
alikuwa na msalaba
mkononi, nao umeandikwa
chini ya anuwani yake ya
kusema kwamba msalaba
huo ulishindia vitani.
(Historia ya Kanisa uk.55,
cha Canon H.J.E. Butcher.)
Ndiyo maana, Peter
the Hermit, alipozusha
poropoganda, za kuwa,
Waislamu wanawauwa
Wakristo kule Yerusalemu,
na akaomba kibali kwa
Pope Urban II; alifanya
kazi hii hii inayofanywa
na Marekani, na mataifa ya
Ulaya; ya kuzunguka nchi
za Ulaya, na kukusanya
mataifa kusulubu
Waislamu.
Wa f u n d i s h a j i
wa
Ukristo, wanatwambia
kuwa, msalaba ni alama
ya ukombozi, na askari
wa Crusades walivaa
m a va z i ya l i y o c h o r wa
misalaba kama alama
ya ukombozi, lakini
kazi waliyofanya ni ya
kuwaokoa Waislamu
kwa kuwakata vichwa
kwa upanga!Sasa katika
vita vinavyoitwa vya
magaidi, wanavyofanyiwa
Wa i s l a m u , n i h a y o
h a y o . K a t i k a v i t a ya
Iraq, Mchungaji Teghua
aliandika kwamba:
mipango ilishapangwa,

na mashirika ya Makanisa
ya dunia yalikuwa
yanasubiri tu Rais George
Bush, awaokoe wa Iraq
na Waislamu kwa risasi
na makombora. Naye
mwandishi wa gazeti
la Kanisa liitwalo
Msemakweli, toleo na.
266 la Jumapili ya April
6-12, 200, aliandika
kuwa: Bustani ya Edeni
kukarabatiwa upya nchini
Iraki baada ya vita, Eneo
h i l o l i m e h a r i b i wa n a
utawala wa Sadam.
Kwa maelezo
ya
mwandishi, ni kuwa vita na
mauwaji waliyofanyiwa,
n a wa n a v y o e n d e l e a
kufanyiwa watu wa Iraq,
ambao ni Waislamu, lengo
kuu ni kuwa Rais Sadam
Husseni alipaharibu kwa
kuwa hakuna misalaba
na anatajwa Allah s.w.
badala ya Kristo.
Zamani miaka ya
sitini kulikuwa na vitabu
wanafundishiwa watoto
wa darasa la pili; vilikuwa
na hadithi zikiwavutia
watoto, kulingana na picha
na maudhui zake. Moja ni
ile iliyochorwa shamba
la mtama, na mtoto aliye
kuwa analinda mtama, na
ndege wanaokula mtama.
Kijana anaye linda
amelala chali, na ndege
wanakula mtama; alafu
maandishi yanasomeka
Baba aliniambia nilinde
mtama,
nimekalia
kichalichali, mtama waliwa
na ndege, mvivu wee.
Sasa tusemeje? Mwenyezi
Mungu ametujaalia mali
asili na akatujaalia kupata
Uhuru. Akatujaalia
kupata viongozi (walinzi
wanchi) na wana nchi,
hivi tuna tofauti gani na
yule mtoto aliyekuwa
akilinda mtama?
Uroho na Ufisadi kwa
maana halisi ya ufisadi, wa
watu wa vita ya msalaba
wa n a t a k a k u i c h u k u a
Edeni, alipoumbiwa
Nabii Adamu, kama
walivyoeleza; ili
waibadilishe Historia
yake, iwe nchi ya Biblia;
lakini wanasingizia
silaha za maangamizi.
Wanataka waichukue Iraq
litengenezwe sanamu
la Adamu na mkewe,
na mungu aliyeshika
upanga akiwa pekupeku

AN-NUUR

RABIUL AWWAL 1437, IJUMAA JANUARI 8 - 14, 2016


a k i s a i d i wa n a m b wa
kumfukuza Adamu wa
Biblia na mkewe, kama
picha inavyonesha (picha
y a A d a m u n a H a wa
wakifukuzwa na mungu
akiwa ameshika upanga
akisaidiwa na mbwa akiwa
pekupeku- Astaghfirullah)
iliyokuwa katika Biblia za
nyuma za 1937.
Ukisoma Biblia,
kwanza utakuta jinsi Iraq
(Uru wa Wakalidayo)
ilivyotukuzwa na wana wa
Israeli. Hiyo ni kutokana
na kuwa ndiko atokako
Nabii Ibrahimu. Hata
hivyo kutokana na
kupatikana kwa kizazi
kinachoitwa wana wa
Israeli, yaani Waisraeli,
(Wayahudi), na kutokana
na kujinasibisha kwao
n a wa I r a q , B i b l i a
inatwambia
kuwa
Ibrahimu aliwaambia
kuwa wasije wakaoa
mabinti wa Kanaani, bali
waende Iraq (Uru wa wa
Kalidayo) wakaoe huko
katika ukoo wa Ibrahimu
na Sara. Isaka akaoa
huko, na Yakobo pia.
Sasa unaweza kujiuliza
kuwa ni kwa nini Uyahudi,
Ukristo na Umagharibi,
wamekuwa na uhasama
wa kiasi hiki tunachokiona
kinachosababisha
umwagikaji wa damu
m k u b wa h i v i ? J i b u
linakuwa moja tu ni kuwa,
wa Iraq ni Waislamu na
cha pili ni uroho na ulafi
wa mafuta.
Biblia inasema:
Ninyi ni wa baba yenu,
Ibilisi na tamaa za baba
yenu ndizo mpendazo
kuzitenda. Yeye alikuwa
mwuaji tangu mwanzo;
wala hakusimama katika
kweli kwa kuwa hamna
hiyo kweli ndani yake.
Asemapo uongo, husema
yaliyo yake mwenyewe;
k wa sab ab u yeye ni
mwongo, na baba wa
huo. (Yohana Mtakatifu
8:44.)
Kwa mujibu wa
historia ya Biblia. Yohana
alipelekwa na serikali ya
Rumi kufungwa katika
kisiwa cha Patmo, na huko
ndiko alipoandikia hii Injili
yake pamoja na kitabu
cha Ufunuo wa Yohana
Mtakatifu. Kwa maana
hiyo, ni kuwa, aya hiyo
hapo juu, anawaambia
wale waliomfunga
n a wa l e w o t e we n ye
matendo yanayofanana
naya hao waliomfunga,
kuwa wanafanya hivyo
kutokana na urithi wa

baba yao ambaye ni Ibilisi.


Hata hivyo Yohana
ametusaidia hiyo kazi ya
nyumbani katika kitabu
cha Ufunuo:
Kisha nikaona mnyama
akitoka baharini, mwenye
pembe kumi, na vichwa
saba, na juu ya pembe zake
ana vilemba kumi, na juu
ya vichwa vyake majina
ya makufuru. Na Yule
mnyama niliyemwona
alikuwa mfano wa chui,
na miguu yake ilikuwa
kama miguu ya dubu,
na kinywa chake kama
kinywa cha simba; yule
joka akampa nguvu zake
na kiti chake cha enzi na
uwezo mwingi. (Ufunuo
13:1-2.)
S he r he , ( uf a f a nuz i )
13:1 Mnyama baharini
ni utawala wa Waroma
(17:10, 12-14). Bahari hiyo
ni Bahari ya kati. 13:2
Mnyama huyo hupata
nguvu yake kwa shetani..
Maelezo hayo utayapata
katika Biblia toleo la
Imprimatur; za Wakatoliki.
Crusades hizo zilileta
mambo matatu yaliyo
makuu juu ya Kanisa la
Kiristo: Mapadre wa
Rumi walijipatia mali
nyingi mno kwa neno hilo,
kwa sababu matajiri wengi
mno walitoa mali yao yote
ili kulipa gharama za
Crusades. Kisha mapope
waliwatoza kodi Wakristo
wote pia wa pande za
magharibi kwa ajili hiyo,
na kodi hiyo iliendelea
k u t o l e wa k wa m i a k a
mingi baada ya Crusade
ya mwisho. Nguvu na
utajiri wa Kanisa la Rumi
ulizidi sana kwa ajili hiyo.
Pili, Uovu mwingi mno
ukaingia kanisani kwa
ajili ya Indulgences,
zilizouzwa kuwasamehe
madhambi wote
waliokwenda vitani. Hii
ndiyo asili, na mwanzo,
wa jambo hilo la kuuza
misamaha; au, kwamba si
mwanzo wake, ni jambo
lililozidisha sana sana
jambo hilo la Indulgences.
Ta t u , P a m o j a n a
hayo, hizo Crusades
zilifaa sana kwa njia
moja, maana, nguvu za
Wa i s l a m u z i l i k w i s h a
katika mashindano hayo.
(Maelezo hayo ni kwa
mujibu wa kitabu-Historia
ya Kanisa, cha Bw. Canon.
H.J.E. Butcher, uk. 87.)
Vuta fikra, tazama
yanayoendelea katika nchi
za Waislamu na Uislamu.
Wabillah Tawfiiq.
(Khatibu J . Mziray
0757 013344. Same.
Januari 2016.)

1/7/2016 3:17:25 PM

AN-NUUR

20

MAKALA

20

RABIUL AWWAL 1437, IJUMAA JANUARI 8-14, 2016

Soma gazeti la
AN-NUUR
KWA TSH 800/=
kila Ijumaa

AN-NUUR

RABIUL AWWAL 1437, IJUMAA JANUARI 8 - 14, 2016

Kesi ya Sheikh Msellem


Danadana zaendelea

Na Bakari Mwakangwale
SERIKALI ndiyo yenye
dhima ya kukamilisha
upelelezi wa tuhuma za
Ugaidi iliyowapa Sheikh
Mselem Ally na wenzake
23, waliopo mahabusu
katika Gereza la Segerea
Jijini Dar es Salaam.
Hayo yamebainishwa
na Wakili wa upande
wa utetezi akizungumza
na An nuur, Mh. Ubaid
Hamidu, kufuatia
kuendelea kuahirishwa
kwa kesi hiyo, huku wateja
wake wakiendelea kusota
mahabusu kwa miaka
miwili sasa.
Kwa mujibu wa Hakimu
aliyesikiliza kesi hiyo,
Alihamisi ya wiki iliyopita
katika Mahakama ya
Kisutu Jijini Dar es Salaam,
ni kwamba kesi hiyo
imeahirishwa hadi Januari
15, 2016.
Alisema, umma wa
Kiislamu na wapenda
amani unapaswa
kufahamu kuwa katika

kadhia hii tatizo lipo


upande wa Jamhuri ya
Muungano, ambayo ndiyo
iliyowafungulia kesi ya
ugaidi na kuwajumuisha na
Waislamu wengine.
Kama ni danadana
basi inapigwa na upande
wa Jamhuri (Serikali) na
wala sio Mahakama ya
Kisutu, kwani yenyewe
inasaidia watuhumiwa
hao wasikae Mahabusu
moja kwa moja wakisubiri
upelelezi wa tuhuma zao
ukamilike ndio sababu
wanaletwa Mahakamani
kufahamu jinsi upepelezi
unavyokwenda kama
sheria inavyotaka.
Amefafanua Wakili
Hamidu.
Alisema, Serikali ambao
ndio mshitaki, imekuwa
na mwendelezo wa kutoa
maelezo yao Mahakamani
kwamba upelelezi
haujakamilika na mbaya
zaidi hakuna sheria inayo
walazimisha kufunga
upelelezi kwa kesi hizo
ambazo zinapaswa
kusikilizwa na Mahakama

Kuu.
Akifafanua zaidi,
Wakili Hamidu, alisema
Mahakama ya Kisutu,
haina uwezo wa kusikiliza
kesi zinazowatuhumu
watu na masuala ya ugaidi
badala yake kesi hiyo
inapaswa kusikilizwa
katika Mahakama Kuu.
Mahakama hii ya
Kisutu, huwa haisikilizi
hizi kesi za Ugaidi, badala
yake huwa inasimamia
mpaka pale upelelezi
utakapo kamilika na

Inaendelea Uk. 17

SHEIKH Mselem Ally.

Wekeni mfumo wa Zakkah


Utoaji ovyo ovyo hauleti tija

Na Salma Said

TAASISI za Kiislamu nchini


zimeshauriwa kushawishi
kuwepo kwa mfumo wa
pamoja wa ukusanyaji wa
Zaka na Sadaka ili ziweze

kuleta tija iliyokusudiwa.


K a t i b u M t e n d a j i wa
Kamisheni ya Wakfu na Mali
ya Amana Zanzibar, Sheikh
Abdalla Talib amesema
moja ya malengo ya amri
ya Zakkah na Sadaka, ni
kupunguza na kuondoa

umasikini katika jamii.


Hata hivyo alisema lengo
hilo haliwezi kufikiwa iwapo
hakutakuwa na mfumo
unaoratibiwa kitaalamu
kama ilivyokuwa wakati wa
Mtume (s.a.w)
Akifungua mkutano wa
Jumuiya ya Zaka na Sadaka

Inaendelea Uk. 18

HAIIBA TIMAMU TEA

CHAI YA AJABU KWA AJILI YA KUKABILIANA NA

HAIIBA TIMAMU TEA IMENIREJESHEA MAISHA YANGU!


Na. Salim Kajenge
Miaka michache iliyopita nilikumbwa na ugonjwa mbaya sana wa
kushindwa kuzuia mkojo. Ilikuwa nikijisikia tu haja ya kukojoa na mkojo
huo unafuata! Hali hii ilinilazimisha kuacha kabisa kuondoka na kwenda
mbali na maeneo ya nyumbani. Ukweli wa mambo ni kwamba nilikwazika
sana. Jitihada zote za kutafuta tiba hazikuzaa matunda. Mwezi wa
Desemba 2014 nilisoma kwenye gazeti la Annur kuhusu dawa moja
iliyokuwa inaitwa chai ya ajabu. Niliamua niijaribu japo sikuwa na
matumaini sana. He! Nilishangaa kuwa baada ya kuitumia kwa siku chache
hali yangu ilianza kubadilika. Niliitumia hii chai kwa majuma matano na
baada ya hapo nikasitisha baada ya kuona kuwa nimepona kabisa!
https://www.facebook.com/Herbal-Impact-157972014402705/

SHINIKIZO LA DAMU (HYPERTENSION/HIGH


BLOOD PRESSURE)
UGONJWA WA MOYO
KIHARUSI
JONGO (GOUT)
MAUMIVU YA VIUNGO (RHEUMATISM)
MAUMIVU SUGU YA KICHWA
BAWASIR (PILES/HEMORRHOIDS)
MAGONJWA YA INI
SARATANI MBALIMBALI
UOTO/UVIMBE MBALIMBALI KATIKA VIUNGO
VYA UZAZI VYA MWANAMKE (FIBROIDS,
POLYPS NA CYSTS)
KUSHINDWA KUZUIA MKOJO (URINARY
INCONTINENCE)
ATHARI ZA KISUKARI CHA UKUBWANI
PUMU
UPUNGUFU WA KINGA ZA MWILI
KASI YA KUZEEKA
MATATIZO YA MFUMO WA MZUNGUKO WA
DAMU
MKAKAMO WA NGOZI;
UDHAIFU WA MACHO
KUPOTEZA KUMBUKUMBU
KASI NDOGO YA KUPONA MAJERAHA
MAKOVU KWENYE MAPAFU
UGONJWA WA NGOZI KUCHUJA RANGI,
YAANI, VITILIGO

HAIIBA TIMAMU TEA


INAPATIKANA
HERBAL IMPACT
MOSQUE STREET, NO. 1574/144
(MKABALA NA MSIKITI WA
SUNNI), KITUMBINI, DAR ES
SALAAM
TUTEMBELEE AU TUPIGIE SIMU
NAMBA:
0754281131/0655281131/06862
81131/0779281131

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Ltd, Dar es Salaam.
ANNUUR NEW.indd 20

1/7/2016 3:17:27 PM

Вам также может понравиться