Вы находитесь на странице: 1из 20

Safari ni nzito!

www.annuurpapers.co.tz au facebook:annuurpapers@yahoo.com

Sauti ya Waislamu

Aungana na Salmin Barzakh

ISSN 0856 - 3861 Na. 1214 RABBIUTH THAN 1437, IJUMAA , JAN 29-FEB. 4, 2016 BEI TShs 800/=, Kshs 50/=

Karume Shujaa
Aliepusha balaa la Aus na Khazraj
Dua zetu, Shein atuvushe salama
Yale ya Micheweni 2001 yasirejee

Soma Uk. 13

DK. Aman Abeid Karume

Naamini maandishi yangu


yatawaathiri wengi pamoja na mimi
mwenyewe kwa kila hali kiafya, na
hata kisaikolojia.
Lakini ni tafakari isiyofikirika
kutokea katika nchi ambayo
inajivunia kuwa na asilimia 99% ya
Waislamu ambao ni ndugu.

CUF haitashiriki
Uchaguzi Machi
DK. Ali Mohamed Shein.

MAALIM Seif Sharif Hamad.

Kwako Dk. Ndalichako

Tatizo ni majipu ya
Kamati ya Kutunuku

CHAMA cha
Wananchi,
CUF, kimesema
hakitashiriki
uchaguzi
wa marudio
uliopangwa
kufanyika Machi
20, 2016.
CUF imesema,
haitashiriki
kwa sababu
uchaguzi huo sio
halali kwa vile
uchaguzi halali
ulishafanyika.
CUF inatoa

wito kwa
Wazanzibari
wote
wanaoipenda
nchi yao
na ambao
wanaamini
katika utawala
wa sheria,
demokrasia
na kuheshimu
Katiba na Sheria
za nchi yetu
kutoshiriki
katika uchaguzi
huo usio halali.
(Soma Tamko la
CUF uk.5)

An nisaa: 29

Fethullah-Gulen
ENYI wale ambao
mmeamini msile mali
zenu kati yenu kwa batili,
isipokuwa zitakapokuwa
ni biashara yenye kutokana
na maridhiano kati yenu
na msiziuwe nafsi zenu
hakika Mwenyezi Mungu
hakuacha kuwa kwenu ni
mwenye huruma sana.
[AN-NISAA 29]
Wakati Quran inaposema:
Msile mali zenu kati yenu
kwa batili inatumia msemo
wenye kukusanya. Quran
inayaelekeza macho kwenye
uharamu wa kula mali
za umma ubavuni mwa
mali za jamaa na wenye
udugu au kutumia vitu
vyao, pasi na radhi yao,
kama unavyoingia katika
maelezo hayo, uporaji, na
wizi na matumizi mabaya
na ujinga katika kutumia
mali na kupata mali kwa njia

AN-NUUR

Mafundisho ya Qur'an/Uwanja wa Maarifa

zisizokubaliwa na sheria.
Ama faida yenye
kupatikana kutokana
na kubadilishana mali
kutokana na kuridhiana
pande zote zinazohusika,
na faida yenye kutokana
na biashara (hiyo sio kosa)
na Ndiyo iliyotajwa hapa,
kwa sababu biashara ni
njia muhimu na nyenzo ya
kupata faida. Hiyo ni faida
inayotosha kwa ajili ya
maisha, hakuna haja wala
ulazima wa kutumbukia
katika njia za haramu, wala
kwenye njia ambazo uhalali
wake na uharamu wake
hauko bayana.
Kunawezekana
kulifahamu angalizo la
maneno haya na msiziue
nafsi zenu angalizo ambalo
limekuja katika aya hii juu
ya maana mbili:
1. Hakika yule ambaye
anatenda madhambi ya
kuteleza katika riba au
kamari au rushwa na
kadhalika katika njia za
haramu, hakika mtu huyo
kwa kufanya hivyo, atakuwa
ameiua nafsi yake kihali na
ameimaliza.
2. Hakika watu
watakapoingia katika
muamala wowote katika
miamala iliyoharamishwa na
iliyobatili na yenye dhulma
katika kuchuma mali na
kuzitoa, na kila matumizi
yoyote yaliyo katika namna
hii, na kuukubali msingi
wowote wenye kutegemea
kwenye utaratibu huo

kama ubepari au uhuru


wenye kuvuka mpaka
na kadhalika, kufanya
hivyo kutapelekea kwenye
kudhihiri mifumo mingine,
kama majibu ya kitendo
hicho kama vile, ukomonisti.
Na ehee ni kama hivyo
mtaufungua mlango mbele
ya wauaji na wamwagaji
damu na kwenye matendo
ya kuwakimbiza watu na
kuwatoa katika maeneo yao.
Ndiyo, mtakapoingia
tokea mwanzo katika mfano
wa mifumo hii matokeo ni
kwamba nyinyi mtaingia
katika kuwaua baadhi
yenu baadhi. Kwa sababu
hiyo, msiuache Uislamu na
mkaupuuza, matokeo yake
mtaingia katika njia zenye
kupotea zenye kutofautiana.
Yatakuwa matokeo yake
ni kwamba baadhi yenu
watawaua baadhi nyingine.
Ndiyo kwa hakika hali ya
dunia ambayo unafanyika
ndani yake utekelezaji
wa mifumo hii hali ya
kuonekana mbele ya macho
yetu hali hiyo inaunga
mkono na inaisadikisha aya
hii.
3. Uwazi wa aya hii
unakubaliana kikamilifu
pamoja na maana ya
kukataza kujiua, maana,
kusimama mtu na kujiua
yeye mwenyewe, isipokuwa
ni kwamba, zinapatikana
baadhi ya sehemu nyingine
za aya hii. Kwa mfano,
kuharibu uwiano uliopo
kati ya matabaka na
makundi linaivuta jamii
hiyo kwenye matatizo
misuguano ya ndani, kama
ambavyo kusimama baadhi
ya wajinga ukichimbuka
kutokana kuelewa kwao
kwa makosa kuhusu
Zuhdi kwa kuacha njia
zilizo kubaliwa na sheria,
kwa ajili ya kuchuma na
kuchagua ufukara na uduni
wa maisha, hilo linapelekea
kwenye unyonge wa umma
na kuangamia, kama
ambavyo kutawalia mmoja
wao juu ya mali za watu
wengine kwa njia ambazo
hazikubaliani na sheria au
kuwashakiza watu wengine
juu ya unyanganyi huu
na kutawalia kusikokuwa
kwa kisheria kunamfanya
mtu huyo astahili kuuliwa
na hizi ni baadhi ya nukta
zenye kufahamika kutokana
na aya.
Na inadhihirika rehma ya
Mwenyezi Mungu iliyo pana
na yenye kuenea, kusimama
kwake kwa kuongoza
kwenye njia ya salama
zaidi na hili ndilo jambo
linalongojewa kutoka kwa
Mwenyezi Mungu mwenye
kuneemesha neema kubwa
kubwa na neema ndogo
ndogo.

RABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JAN 29-FEB 4, 2016

JAWABU CHEMSHA BONGO NAMBA: 36


B

384,400 Km

980,00Km

111,111,000Km

788

88,888

12,345,679

4.5

4.57 bilioni

888,999 Km

25

75

35

MASUALA
1.Sayari ipi ilio na baridki kali kabisa? Jawabu: Neptune
2.Sayari ipi ilio na uzito mkubwa kuliko zote? Jawabu: Jupiter
3.Jua lina asilimia ngapi ya Hydrogen na Helium? Jawabu: 25, 35
4.Umri wa Jua miaka mingapi? Jawabu: 4.57 bilioni
5.Masafa ya kutoka duniani hadi mwezini. Jawabu: 384,400km
6.Kwenye Mwezi kuna maisha? Ndio, Sio. Jawabu: Sio
7.Mwezi wa Kiislamu hufwata mzunguko wa
Jawabu: Mwezi
8.Mwezi wa Kizungu hufwata mzunguko wa
Jawabu: Jua
9.Matumaini ya maji kupatikana yapo katika Sayari ipi? Jawabu: Mars
10.Jua likitoka Magharibi itakuwa nini? Jawabu: Mwisho wa dunia.

CHEMSHA BONGO: 37

Weka duara kwenye jawabu ilio sawa. Jawabu kamili wiki ijayo.

M L

B T U

A A T

D I

M G

O J

A Z

G A

D A U

M A

M B N K

O S

D O U I

H R

M X

M U

D M U E

U E

K N A

M A

W I

A Y

O M E

N U

A S

T K O A

W D

A I

M R

MASUALA
1.Asili ya mto Amazon unatokea wapi? Peru, Brazil Kenya.
2.Mto gani unaigawa Urusi na China? Amur, Missisipi.
3.Azerbhajan mji mkuu wake ni Baku ipo katika sehemu ya ziwa gani? Lake
Balghash, Caspian Sea, Zambezi
4.Ziwa gani kubwa nchini Ulaya?
5.Nchi gani ya Afrika ina jina la ziwa na ndio jina la nchi? Zambia, Tanzania,
Malawi
6.Muislamu yupi nchini Marekani akijinasibisha na Utume?
7.Muislamu gani nchini Marekani aliopinga watu kujinasibisha rangi yao
na Uislamu?
8.Jina la asili la mwanzo la Msumbiji lilikuwa ni :
9.Nchi ya Ureno ikijulikana awali kama :
10.Kisiwa cha Comoro kinajulikana kwa jina gani kwa Kiarabu?:

Jee Unajua?

1.Ujerumani ndio nchi yenye watu wake wenye kuzaa kwa idadi ndogo,
katika kila watu 1,000 huzaliwa watoto 8.2: http://www.bbc.com/news/
world-europe-32929962
2.Nchi za Kiafrika zinaongoza kwa uzazi nchi ya Niger katika kila watu 1,000
huzaliwa watoto 45, Mali 44, Uganda 43, Zambia 42, Burundi na Malawi
42, Somali 40: https://www.cia.gov/library/publications/the-world-factbook/
rankorder/2054rank.html
3.Nchi ya Lesotho inaongoza kwa watu kufariki kwa idadi kubwa, katika
kila watu 1,000 hufariki watu 14: https://www.cia.gov/library/publications/
the-world-factbook/rankorder/2066rank.html
4.Kati ya nchi zenye wanawake wengi kuliko wanaume ni Estonia, Latvia,
Russia, Ukraine, Belarus, Armania, Lithuania: http://www.aneki.com/
women_men.html
5.Nchi zinaongoza miji yake kuwa na usafi wa hali ya juu ni Finland
ikifwatiwa na Norway, Sweden, Iceland, Canada, Switzerland: http://
www.aneki.com/cleanest.html?&order=desc&orderby=table_cleanest.
value&number=10&cntdn=asc
6.Kati ya nchi zinazozalisha nishati mbadala kwa wingi ni Zambia, Nepal,
Congo DRC, Albania, Tajiksatn, Norway: http://www.aneki.com/highest_
renewable_electricity.html
7.Miji ilio na maisha magumu na matumizi ya chini ni: Brazzaville iliopo
Congo, Bangui Afrika ya Kati, Baghdad huko Iraq : http://www.aneki.com/
worst_cities.html
8.Kati ya nchi ambayo Matetemeko ya ardhi ndio kwao ni Afghanistan,
Algeria: http://www.aneki.com/list_countries.php?t=Earthquake_Prone_
Countries&slide=3
9.Nchi zinaongoza viogozi wao kula rushwa ni Indonesia, Philippines,
Congo DRC, Nigeria, Serbia na Montenegro, Haiti, Peru, Ukraine: http://
www.aneki.com/corruption_leaders.html
10.Nchi ya Sweden inaongoza katika usawa wa jinsia ikifwatiwa na Norway,
Iceland, Denmark, Finland, New Zealand, Denmark: http://www.aneki.com/
best_gender_equality.html

Habari

RABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JAN 29-FEB 4, 2016

Karume Shujaa
Salma Said, Zanzibar
Bismillahir Rahmanir Rahim.
NA KUMBUKENI neema ya
Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu.
(Zamani) mlikuwa maadui, Naye
akaziunganisha nyoyo zenu,
hivyo, kwa neema yake mkawa
ndugu. Na mlikuwa ukingoni mwa
shimo la moto (wa Jahannam),
Naye akakuokoeni nalo.
Namna hivi Mwenyezi Mungu
anakubainishieni aya zake ili
mpate kuongoka. (3:103)
Nimeanza na kumtanguliza
Mwenyeenzi Mungu kwa kuwa
ninachokiandika ni kitu kizito na
hakijawahi kuandikwa popote kwa
ukamilifu wake zaidi ya kwenye
kitabu kile kilichotayarishwa na
Chama Cha Wananchi (CUF) na
kwenye ripoti za Shirika la Human
Rights Watch ya mwaka 2012.
Ni mambo ambayo yanahitaji
mazingatio makubwa kwetu sote
kama wananchi kwa kila mmoja na
nafsi yake kuwa ana dhima kubwa
ya kuhakikisha usalama wake na
usalama wa mwenzake. Lakini pia
kwa viongozi ambao nao wamebeba
dhima na jukumu kubwa zaidi
mbele ya Mwenyeenzi Mungu na
wanaowaongoza.
Naamini maandishi yangu
yatawaathiri wengi pamoja na mimi
mwenyewe kwa kila hali kiusalama,
kiafya, na hata kisaikolojia. Ni
kwa sababu najaribu kuvuta hisia
za miaka 15 iliyopita ambapo
makubwa yalitokea katika nchi yetu
ya majonzi na huzuni ya unyama
uliokithiri. Ni maumivu yasiopona.
Ni uonevu usiosahaulika. Na ukatili
usiosameheka. Lakini tafakari
isiyofikirika kutokea katika nchi
ambayo inajivunia kuwa na asilimia
99% ya Waislamu ambao ni ndugu.
Nimekuwa nikitumia mfano
mmoja kila mara panapotokea
masuala ya kuzungumzia umuhimu
wa kudumisha amani na maelezo
haya ninayoyandika leo ni kama
hadithi au simulizi lakini ni simulizi
ya ukweli ambao imetokea Januari
27 mwaka 2001 wakati ambao nchi
iligubikwa na harufu ya damu
ya Wazanzibari iliyomwagika.
Maumivu makali yaliokosa tiba.
Majonzi na masikitiko makubwa
yaliojaa ndani ya nyoyo za wengi.
Nchi iligubikwa kiza kinene
ambayo yaliokuwa hayajawahi
kushuhudiwa yakashuhudiwa.
Yaliokuwa hayajaonekana na
kusikika, yakaonekana na kusikika
katika aridhi hii ya Tanzania
kwenye Visiwa vya Zanzibar.

Yalianza Januari 26 ambapo


Imamu wa Msikiti wa Mbuyuni
Sheikh Juma Mohammed akiwa juu
ya vespa yake akielekea nyumbani
kwake maeneo ya Mtendeni,
alipigwa risasi na kufariki hapo
hapo wakati akitokea kusali sala
ya Ijumaa. Na siku ya Januari 27
ndio watu wapatao 62 walifariki
na wengine kadhaa kujeruhiwa na
kuacha vilema, wajane na mayatima.
Wengine wakaingia kuishi porini
na kwa mara ya kwanza, Tanzania
ikatoa wakimbizi waliokimbilia eneo
la Shimoni, Mombasa Nchini Kenya
na wengine Somalia.
Sababu ya kutokea hayo ilikuwa
ni maandamano yalioandaliwa
na Chama Cha Wananchi (CUF)
yaliokuwa yakipinga matokeo ya
uchaguzi yaliomuweka madarakani
Rais Amani Abeid Karume katika
kipindi cha Awamu ya Kwanza ya
utawala wake, huku Amiri Jeshi
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na
Usalama akiwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Benjamin
William Mkapa.
Sio mambo ya kukumbushwa
kila wakati kwa sababu sio mambo
mazuri na sio mambo ya kuigwa
wala ya kutolewa mifano kwa kuwa
ni mambo ambayo yameshapita,
lakini hayawezi kuondoka katika
nyoyo za watu kwa sababu
waliotenda na waliotendewa bado
wapo katika nchi hii ambao wengi
wao wahai na wanatembea kama
kawaida. Lakini kubwa na la kutisha
na kusikitisha pia, viashiria vya
kurejea haya vinaonekana waziwazi.
Ni hisia zilizo kali unazipata
unapoyakumbuka madhila
yaliowafika ndugu na jamaa ambao
waliathirika na matukio yale,
ingawa sikuwepo nchini siku ya
tukio lenyewe, lakini mwaka 2002
nilibahatika kuwa miongoni mwa
wanaharakati wachache kutoka
Chama Cha Waandishi wa Habari
Wanawake Tanzania (TAMWA) na
Chama Cha Wanasheria Wanawake
Tanzania (TAWLA) waliokwenda
kufanya tafiti za tukio lile kwa
kuangalia athari walizopata akina
mama na watoto wakati wa matukio
hayo. Mbali ya kufanya tafiti, pia
tulitumia fursa hiyo kuwatoa khofu
wanawake hao wajitokeze kwa
wingi kwenye Tume iliyoundwa
na Serikali iliyokuwa chini ya
Mwenyekiti wake, Hashim Mbita
kwa ajili ya kukusanya maoni
na ushuhuda wa yaliowafika
waathirika wa matukio hayo ya
Januari 27, 2001.
Shirika moja la kimataifa
liitwalo Urgent Action Fund ndilo
lililotupeleka Kisiwani Pemba
kufanya utafiti huo ambao katika
utafiti ule kuna mambo mengi
tuliyaona, sio ya kujifunza tu,
bali tuligundua kuna watu bado
wameathiriwa vibaya sana na
matukio yale kiafya na kisaikolojia,
na ndio maana khofu na woga
ulitawala zaidi miongoni mwa
wanawake wengi ambao tulifanya
nao mazungumzo.
Wanaharakati hao wote
wakitokea Tanzania Bara isipokuwa
kwa upande wa Zanzibar nilikuwa
mimi na Ally Saleh na kwa hakika

AN-NUUR

RAIS Mstaafu, Mhe. Benjamin


Mkapa.
sisi ndio tuliandika mapendekezo
hayo na kuwashauri wanaharakati
wenzetu kuja kufanya kazi pamoja
ambapo katika kazi hiyo kulikuwa
na wanaume wawili tu, Ally Saleh
(BBC) wakati huo na Khamis
Suleiman (Chanel Ten).
Nimetoa picha hiyo ili muone
namna mazingira ambayo
tuliofanyia kazi wakati huo ni
sisi wanawake ambao tulikuwa
tukiwakabili na kuwauliza masuali
wale waathirika waliokumbwa na
matatizo wakati huo lakini licha ya
kuwa wanaharakati waliokwenda
kufanya utafiti walikuwa ni
wanawake pekee, lakini haikuwa
kazi nyepesi kuwadadisi na kuweza
kupata maelezo yao.
Mambo mengi tulijifunza
kutojiamini, woga, khofu, aibu na
haya ndio vilivyokuwa vikitawala
katika mahojiano yetu. Wanawake
wakituogopa wakiona kama
kwamba tumekwenda kuhoji
ili tuwazamishe zaidi badala ya
kuwasaidia na kuwapa faraja.
Pamoja na kuwa tulipofika
tulifuatana na wenyeji na tulijigawa
kwa makundi katika kufanya usaili
huo, lakini baadhi ya waathirika
wakiogopa sana kuongea na sisi
baadhi yao wakisogea upande
wangu wakionesha kuniamini zaidi
kuliko wale wenzangu, wakati
huo mimi ni mgeni sana Kisiwani
Pemba. Kumbe wameona peke
yangu niliyevaa Hijaab.
Nikajiuliza ni kitu gani
kilichowapa imani wanifuate mimi
zaidi? Lakini baadae nikagundua
kuwa kumbe ni khofu tu walikuwa
wakiamini wale waliokuja ni
watu waliotumwa kutoka Bara
kufuatilia mambo yao. Baadhi ya
watu wakinifuata nje na kuniuliza
Eti wale wenzako ulokuja nao sio
usalama wa taifa, maana isije kuwa
tunatoa maelezo yetu baadaye
tukajiwa usiku kufuatwa majumbani
kupigwa tena? Masikini walikuwa
wakionesha khofu zao.
Kwa kuona hisia waliokuwa nazo,

ikabidi nitumie taaluma yangu na


kuwaeleza kuwa hapana sote tupo
sawa na sote tunafanya kazi pamoja
na lengo letu sio kuwaongezea
matatizo waliyopata, bali kuja
kuwasaidia namna gani ya kuweza
kujiondoa katika mawazo mazito
waliyonayo. Baada ya hapo jioni
tunapomaliza kazi hujumuika
nikawaeleza wenzangu suala hilo
kwamba kuna baadhi ya watu
wanaogopa na hawatuamini kwa
hivyo tukatumia mbinu mpya
ya kuweza kuwavuta wengi na
kuwahoji.
Tulijigawa mafungu na tukaitisha
mkutano lakini katika kuuliza
masuali ilikuwa tunaita mtu mmoja
mmoja na anaeleza masuali yake
hadi mwisho ingawa hatukupenda
mtu kumlazimisha kusema kila
kitu lakini wengi wao wakiongea
wakilia sana na kutuonesha
makovu yao. Wenye majeraha ya
risasi, kuna waliopigwa mikwaju,
kuna waliobakwa na kuna ambao
wameathirika kisaikolojia kutokana
na vitendo walivyofanyiwa.
Najua machungu na athari za
ubakaji, najua namna gani mtu
ambaye anakuwa ameathirika
kimwili na kisaikolojia katika jambo
hilo, na pia nafahamu maumivu ya
mtu ambaye anahadithia madhila
yaliompata anapohadithia anaona
kama kitendo kile anafanyia tena,
hivyo maumivu yake yanakuwa
makali zaidi kuliko mara ya kwanza
kwa maana anapohadithia anakuwa
na hisia kali (deep feeling).
Nikayakumbuka maelezo ya
rafiki yangu mmoja wa kike kutoka
Congo niliekuwa nikiishi naye
bweni moja wakati nasoma nchini
Kenya, aliwahi kubakwa namna
ambavyo akinieleza madhila
waliofanyiwa kabla ya ubakaji
nikayafananisha na yale ambayo
nilikuwa nikiyasikia kwa msichana
mmoja wa Wete. Nililia sana na
nilishindwa kuzuwia hisia zangu.
Nilijisikia naumia sana. Niliporudi
baada ya kazi nikamwambia Ally
Saleh siamini nilichokisikia. Siamini
kama haya yamewahi kutokea
Zanzibar. Ally Saleh akanambia,
Naam! Yametokea.
Siku ya pili nikakutana na
mwanamke ambaye anaelezea
namna ambavyo amebakwa
au ameingiliwa kwa nguvu na
wanaume wawili mbele ya mume
wake ambaye alifungwa ukumbini
kwake akiona huyu mkewe
akibakwa. Alilia sana wakati
ananielezea ingawa yeye baadae
alijikaza, lakini mimi nilishindwa
kumuangalia usoni. Uso wangu
niliuinamisha chini nikifuta machozi
mpaka anamaliza nilikuwa na
masuali ya kumuuliza, lakini kila
nikitaka kunyanyua uso nimuulize,
nilishindwa.
Mwanamke mmoja ameanza
na kuuliza suali, jee mimi ndoa
yangu ipo wakati nimeingiliwa
na wanaume ambao sio waume
zangu? Anasema ameshindwa
kumuelezea mumewe kama
ameingiliwa kwa sababu mume
wake alikuwa miongoni mwa
wanaume waliokimbilia maporini
kuishi huko.
Nitaanza vipi au nitamtazama
vipi mume wangu akijua kama
nimevuliwa nguo na mtu asiyekuwa
yeye. Siwezi hilo, siwezi kabisa.
Namuomba Mwenyeenzi Mungu
anisamehe makosa ambayo

Inaendelea Uk. 6

Tahariri/Makala

AN-NUUR

S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786


Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM.
www.annuurpapers.co.tz
E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk
Ofisi zetu zipo: Manzese Tip Top
Usangi House, barabara ya Morogoro, D'Salaam

Zanzibar inahitaji muafaka


na maridhiano
Kura si njia ya uhakika

TAYARI Mwenyekiti
wa Tume ya Uchaguzi
ya Zanzibar Bw. Jecha
Salum Jecha, ametangaza
tarehe ya uchaguzi wa
marudio Zanzibar kuwa
ni 20 machi 2016 siku ya
Jumapili.
Bw. Jecha alisema
watakaopigiwa kura hizo
za marudio watakuwa
ni wagombea walewale
waliogombea nafasi
ya Urais wa Zanzibar,
Wawakilishi na
Madiwani na kwamba
hakutakuwa na kampeni
za uchaguzi.
Tangazo hilo la Jecha
limekuja baada ya awali
kufuta uchaguzi wa
Zanzibar Oktoba 28,
2015 na hatma ya kisiasa
Zanzibar kubakia katika
sintofahamu.
Kwa kipindi chote
cha karibu miezi mitatu
cha kufutwa uchaguzi
huo, hakuna suluhu
iliyopatikana kati ya
pande mbili zilizokuwa
zinachuana katika
uchaguzi huo, yaani
vyama vya CCM na
CUF licha ya kufanyika
mazungumzo pogo ya
kusaka suluhu.
Mpaka Jecha
analitangazia Taifa
kuhusu tarehe ya
marudio ya uchaguzi,
msimamo wa CUF na
mgombea wake Maalim
Seif Sharif Hamad ni
kutokubali kushiriki
uchaguzi wa marudio.
Ila Tume kumtangaza
mshindi halali wa
uchaguzi uliofutwa.
CCM na mgombea
wake Dk. Ali Mohammed
Shein, wamesimamia
kurudiwa uchaguzi kama
ilivyotangazwa na Tume
huku wakiwashadidia
wafuasi wao kuwa
wawape ushindi wa
kishindo!
Hata hivyo, pamoja
na Bw. Jecha kutangaza
tarehe ya kurejewa
uchaguzi Zanzibar ili
kutanzua mkwamo
uliopo na kumaliza

hitilafu iliyotokea, lakini


tunachokiona ni kwamba,
Zanzibar haina mazoea
ya kutatua mizozo yake
ya kisiasa kwa njia ya
uchaguzi.
Zanzibar ilipofikia
ina historia nzuri ya
kumaliza mivutano yake
ya kisiasa kwa njia ya
muafaka na maridhiano,
iwe ni masuala ya
uchaguzi, ya kidola au
kivyama.
Kwa sasa, ili kunusuru
hali ya Zanzibar,
kunahitajika muafaka
wa namna yake kuliko
wakati mwingine
wowote, ili kupata
suluhu ya kweli. Kutafuta
suluhu na kuondoa
mkwamo wa kisiasa
kwa shuruti ya kurudia
kupiga, tunaona kuna
kila ishara ya kuongeza
zaidi ombwe la mzozo
wa kisiasa visiwani
humo. Maana kwanza
tujiulize, kwa nini ule wa
awali ulifutwa? Mjadala
wa kisheria, kikatiba na
kisiasa ukionyesha kuwa
kulikuwa na sababu za
kufutwa kwa mujibu
wa sheria ya uchaguzi,
sheria za nchi na katiba
yake, hapo sasa unaweza
kuletwa ufumbuzi
wa kurejea uchaguzi.
Lakini kama umefutwa
tu kihuni, kurudia
uchaguzi haiwezi kuwa
ufumbuzi.
Tangu kuanza kwa
mfumo wa vyama vingi
nchini 1992, hakujawahi
kutokea kufanyika
uchaguizi mkuu
Zanzibar, ukafanyika
ukaisha na pasiwepo
matatizo ya kisiasa.
Tangu uchaguzi wa
mwaka 1995, 2000, 2005.
Chaguzi zote hizo
zimefanyika lakini
hazikuweza kuondoa
matatizo ya kisiasa
Zanzibar. Hazikuisaidia
Zanzibar kuwa na
utulivu wa kisiasa
unaostahiki. Tena
unaweza kusema kuwa
uchaguzi wa mwaka

uliopita ndio umefanyika


kwa Amani na kwa
kufuata taratibu zote
zinazotakiwa kuliko
miaka yote na bila
malalamiko. Lakini ndio
huo umefutwa! Sasa
mwingine wa nini, kama
sio kutaka kulazimisha
jambo ambalo wananchi
walishalikataa kwa kura
zao?
Ni imani yetu
kwamba pamoja na

AN-NUUR

RABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JAN 29-FEB 4, 2016


kutangazwa tarehe ya
kurejewa uchaguzi,
bado tunaamini suluhu
ya kweli na ya haki
ya kisiasa Zanzibar
haiwezi kuwa nje ya
maridhiano ya pande
husika. Kwa jinsi hali
ilivyo sasa ambapo CCM
wameshaweka msimamo
wa kurejewa uchaguzi
na CUF msimamo wa
kutoshiriki uchaguzi wa
marejeo, ni dalili tosha

kwamba hakuna suluhu


kamili itakayopatikana
kwa kura ya marudio.
Zaidi utashuhudiwa
uchaguzi wa upande
mmoja wenye mabavu,
huku upande mwingine
ukisusia. Na hapo tuna
shaka ya kuhitimishwa
ile serikali ya Umoja
wa Kitaifa iliyoonyesha
njia ya kutuliza shari za
kisiasa na kuleta nuru
Zanzibar.

hivi sasa serikali kama


inawatafutia sababu
tu, hivyo jambo lolote
lisemwe na wahusika
wenyewe kama Katibu
Mkuu na Naibu Waziri.
Bakari ni mmoja wa
watu ambao walikuwa
ni waandishi wa maneno
makali ya ubao huo wa
Kisonge ambao zaidi
huwa unawalenga
wapinzani.
Moja ya maandishi
yake aliyoandika wakati
wa uhai wake ni kuwa
hata tukifa sote hatutoi
nchi, ambapo maandishi
hayo huandikwa mara
kwa mara tokea kufariki
kwa mmoja wa wana
CCM wahafidhina
ambaye alikuwa mstari
wa mbele katika kutaka

kuvunja serikai ya umoja


wa kitaifa Salmin Awadh
Salmin ambaye naye
alikufa ghafla muda
mfupi baada ya kumaliza
kikao cha ndani cha ofisi
Kuu ya CCM Kisiwandui.
Salmin aliwahi
kusema mara kadhaa
kwamba atapeleka hoja
binafsi ndani ya Baraza
la Wawakilishi kutaka
kuivunja serikali ya
Umoja wa Kitaifa.
Bao la Kisonge
limekuwa likipata
umaarufu kila siku
kufuatia kuandika
ujumbe ambao
unawalenga wapinzani
na kuwatupia vijembe
jambo ambalo limekuwa
likipigiwa kelele
Inaendelea Uk. 7

Msiba mara mbili Kisonge


Na Mwandishi Wetu

NI msiba mara mbili


Kisonge. Kuondokewa
na kijana wao na kukosa
kumzika.
Ilikuwa wakitaka maiti
ipelekwe Fuoni, wanaKisonge wapate fursa
kushiriki, lakini ndugu
wakamuwahisha Barzakh
kama zilivyo taratibu za
Kiislamu.
Huo ni msiba wa
Salum Bakari, kijana
anayeishi Fuoni
anayedaiwa kuwa
ni miongoni mwa
waandishi wa Ubao
unaomilikiwa na
Chama Cha Mapinduzi,
maarufu Bao la Kisonge,
aliyefariki juzi ghafla.
Bakari aliumwa
na tumbo ghafla
na kukimbizwa
hospitali Kuu ya
Mnazi Mmoja ambapo
wakati madaktari
wakijitayarisha
kumfanyia matibabu
alifariki dunia.
Kwa mujibu wa daktari
wa Mnazi Mmoja ambaye
hakutaka kutajwa jina
lake alikiri kumpokea
kijana huyo mchana
na akasema alitakiwa
kufanyiwa upasuaji,
lakini kabla ya kufanyiwa
alifariki dunia.
Ni kweli aliletwa
hapa hospitali na
tukampokea akiumwa
na tumbo na aliletwa
mchana, lakini ilibidi
afanyiwe operesheni
kutokana na maumivu
alokuwa akiyapata,
bahati mbaya akafariki,
alisema daktari huyo
ambaye alikataa kutajwa
jina gazetini kwa madai
ya kuwa yeye sio
msemaji.
Pia daktari huyo
alisema kutokana na hali
ya nchi ilivyo anaogopa
kuongea zaidi kwa kuwa

MAKALA YA MTANGAZAJI

AN-NUUR

RABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JAN 29-FEB 4, 2016

AZIMIO LA BARAZA KUU LA UONGOZI LA TAIFA KUHUSU TANGAZO LA MWENYEKITI WA


TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR LA KUITISHA UCHAGUZI WA MARUDIO ZANZIBAR
BARAZA Kuu la Uongozi la
Taifa la THE CIVIC UNITED
FRONT (CUF Chama Cha
Wa n a n c h i ) , l i k i wa n d i y o
chombo cha juu cha maamuzi
k a t i k a C h a m a b a a d a ya
Mkutano Mkuu wa Taifa,
limefanya kikao cha dharura
leo, tarehe 28 Januari, 2016,
katika Ofisi Kuu ya CUF, mjini
Dar es Salaam.
Kikao hicho kilikuwa na
ajenda moja tu, ambayo ni
kufanya maamuzi kuhusiana
na tangazo la Mwenyekiti
wa Tume ya Uchaguzi ya
Zanzibar la kuitisha uchaguzi
wa marudio.
Baada ya kujadili kwa kina
tamko hilo la Mwenyekiti wa
Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar,
Jecha Salum Jecha, la kuitisha
uchaguzi wa marudio tarehe
20 Machi, 2016 na mwenendo
mzima wa hali ya kisiasa
Zanzibar tokea alipotoa tamko
lake batili la tarehe 28 Oktoba,
2015 kudai kwamba amefuta
uchaguzi mkuu wa Zanzibar
wa tarehe 25 Oktoba, 2015 na
matokeo yake, Baraza Kuu
la Uongozi la Taifa limefikia
maazimio yafuatayo:
1. KWAMBA Uchaguzi
Mkuu wa Zanzibar
umeshafanyika tarehe 25
Oktoba, 2015, ambapo
kwa upande wa uchaguzi
wa Wajumbe wa Baraza la
Wawakilishi na Madiwani
ulikwisha kamilika na washindi
wote kupewa shahada za
kuwathibitisha na kuwatambua
kama washindi halali.
Kwa upande wa uchaguzi
wa Rais wa Zanzibar, matokeo
yalikwisha bandikwa nje ya
vituo vya majumuisho vya
majimbo yote 54. Kilichokuwa
kinaendelea baada ya hapo
ni kuhakiki matokeo hayo
kutoka majimboni na kazi hiyo
ilikwishakamilika kwa majimbo
40 na katika hayo, matokeo ya
uchaguzi wa Rais kwa majimbo
31 yalikwishatangazwa kabla
ya Mwenyekiti wa Tume ya
Uchaguzi, Jecha Salum Jecha,
kutangaza isivyo halali kwamba
ameufuta uchaguzi huo.
2. KWAMBA Chama Cha
Wananchi (CUF) hakitoshiriki
katika uchaguzi wa marudio
uliopangwa kufanyika tarehe
20 Machi, 2016 kwa sababu
uchaguzi huo si halali kwani
uchaguzi halali ulishafanyika.

3. KWAMBA linatoa wito


k w a Wa z a n z i b a r i w o t e
wanaoipenda nchi yao na
ambao wanaamini katika
utawala wa sheria, demokrasia
na kuheshimu Katiba na Sheria
za nchi yetu kutoshiriki katika
uchaguzi huo usio halali wa
marudio.
4. KWAMBA sababu kuu ya
Baraza Kuu kufikia maamuzi
haya ni kutokana na matamko
yote mawili ya Mwenyekiti wa
Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar,
Jecha Salum Jecha, kutokuwa
halali na kwenda kinyume na
Katiba ya Zanzibar na Sheria
ya Uchaguzi ya Zanzibar Nam.
11 ya 1984.
Hakuna kifungu chochote
cha Katiba ya Zanzibar au
Sheria ya Uchaguzi ya
Zanzibar kinachotoa uwezo
kwa Mwenyekiti wa Tume ya
Uchaguzi ya Zanzibar na hata
kwa Tume yenyewe kufuta
uchaguzi au kuitisha uchaguzi
wa marudio.
5. KWAMBA linazipongeza
na limetiwa moyo sana na
taasisi na jumuiya zote za
kimataifa na kikanda zikiwa ni
pamoja na Jumuiya ya Madola
(The Commonwealth), Umoja
wa Ulaya (European Union),
Umoja wa Afrika (African
Union), Jumuiya ya Maendeleo
ya Nchi za Kusini mwa Afrika
(SADC) na Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EAC) pamoja na nchi
za Marekani na Uingereza kwa
msimamo wao wa kuungana
na Wazanzibari na kutetea
haki yao ya kidemokrasia na
maamuzi halali waliyoyafanya
katika uchaguzi mkuu wa
tarehe 25 Oktoba, 2015 na
kutaka mchakato wa uchaguzi
huo ukamilishwe na matokeo
yake kutangazwa.
6. KWAMBA linazipongeza
na kutiwa moyo pia na taasisi
za hapa nchini zikiwemo
taasisi na jumuiya za kidini,
taasisi za haki za binadamu,
vyombo huru vya habari,
vyama vyengine vya siasa na
Wazanzibari na Watanzania
wote wanaopenda amani na
demokrasia kwa msimamo
wao wa kutetea maamuzi ya
Wazanzibari waliyoyafanya
katika uchaguzi mkuu wa
tarehe 25 Oktoba, 2015 na
kuendelea kusisitiza haja ya
kuheshimu na kufuata Katiba
na Sheria za nchi yetu na pia
haja na umuhimu wa kutunza
amani ya nchi yetu kwa kutaka

haki itendeke.
Baraza Kuu linazihakikishia
t a a s i s i n a j u m u i ya h i z o
zote na pia kuwahakikishia
Wazanzibari na Watanzania
wote kwamba CUF itaendelea
kusimama kidete katika
kulinda na kutetea Katiba
na Sheria za nchi yetu na
p i a k u t e t e a m a a m u z i ya
Wazanzibari waliyoyafanya
tarehe 25 Oktoba, 2015.
7. KWAMBA limesikitishwa
na kushangazwa na kitendo
cha Msajili wa Vyama vya
Siasa, Jaji Francis Mutungi,
kuandika barua na kutoa
t a a r i f a k wa v y o m b o v ya
habari kutaka vyama vya siasa
vishiriki uchaguzi wa marudio
uliopangwa kufanyika tarehe
20 Machi, 2016 bila ya kujali
kwamba uchaguzi huo ni
haramu na unakiuka matakwa
ya Katiba ya Zanzibar na Sheria
ya Uchaguzi ya Zanzibar Nam.
11 ya 1984.
Baraza Kuu halikutarajia mtu
mwenye hadhi ya Ujaji kufanya
kazi ya kutumikia maslahi ya
watawala ambao wameamua
kuvunja Katiba na Sheria za
nchi yetu na kukanyanga
misingi ya haki na demokrasia
huku akishindwa kukemea
uhuni mkubwa uliofanywa wa
kubaka demokrasia na haki za
watu.
8. KWAMBA limesikitishwa
na kitendo cha Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Dk. John Pombe
Magufuli, kukwepa dhamana
na wajibu wake kama Mkuu wa
Nchi na Amiri Jeshi Mkuu kwa
kuiacha njiani kazi aliyoianza
ya kutafuta ufumbuzi
wa mkwamo wa uchaguzi
Zanzibar.
Baraza Kuu linamtaka
Rais Magufuli kujitathmini
na kujiuliza anajiweka vipi
na kutoa taswira gani mbele
ya macho ya Watanzania na
jumuiya ya kimataifa kutokana
na kutosimamia ahadi yake
aliyoitoa mbele ya Watanzania
wakati akilizindua Bunge
jipya kwamba atafanya kazi
na vyama vya CUF na CCM ili
kuupatia ufumbuzi mkwamo
huu.
9 . K WA M B A l i n a l a a n i
matumizi ya nguvu kubwa ya
vyombo vya ulinzi na usalama
vya Jamhuri ya Muungano
na Vikosi vya SMZ dhidi ya
wananchi wasio na hatia na
ambao wamekuwa watulivu
licha ya vitendo vingi vya

uchokozi wa makusudi na hata


mashambulizi ya hujuma dhidi
yao yanayofanywa na makundi
ya vijana wa CCM waliowekwa
katika makambi kadhaa kisiwani
Unguja.
1 0 . K WA M B A l i n a i t a k a
jumuiya ya kimataifa na hasa
taasisi zinazosimamia haki za
binadamu na zinazopambana
na makosa ya jinai kimataifa
ikiwemo Mwendesha Mashitaka
wa Mahakama ya Kimataifa ya
Makosa ya Jinai (International
Criminal Court ICC) kufanya
uchunguzi wa kauli na matendo
ya uhalifu, uvunjwaji mkubwa
wa haki za binadamu na ubaguzi
ambao umekuwa ukifanywa
dhidi ya wananchi wa Zanzibar
na kuchukua hatua dhidi ya watu
walio nyuma ya maamuzi na
utekelezaji wa matukio hayo.
11. KWAMBA linawapongeza
wananchi wa Zanzibar kwa
kuonesha ukomavu wa hali
ya j u u n a k u wa wa t u l i v u
licha ya machungu makubwa
waliyoyapitia na wanayoendelea
kuyapitia tokea pale maamuzi yao
yalipopinduliwa na CCM kwa
kumtumia Mwenyekiti wa Tume
ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jecha
Salum Jecha. Baraza Kuu linatoa
wito kwa Wazanzibari wote
kuungana pamoja chini ya chama
chao cha CUF walichokipa ridhaa
halali kupitia uchaguzi mkuu wa
tarehe 25 Oktoba, 2015 kutetea
maamuzi yao waliyoyafanya
kupitia sanduku la kura kwa njia
za amani.
Baraza Kuu linawasisitiza tena
Wazanzibari kwamba waendelee
kutunza amani ya nchi yetu na
kutambua kwamba kutunza amani
si udhaifu bali ni jambo linaloipa
nguvu jumuiya ya kimataifa
kufuatilia haki za kidemokrasia
za wananchi wa Zanzibar.
12. Baraza Kuu la Uongozi
la Taifa linawatahadharisha
CCM na watawala wasiowajali
na kuwaheshimu wananchi
kwamba zama za utawala wa
mabavu usioheshimu Katiba
na Sheria za nchi hazina nafasi
tena katika dunia ya leo. Baraza
Kuu lina imani kwamba HAKI
ITASHINDA.
LIMETOLEWA NA:
BARAZA KUU LA UONGOZI
LA TAIFA
THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF Chama Cha Wananchi)
DAR ES SALAAM
28 JANUARI, 2016

Hoja ya Juma Kilaghai

AN-NUUR

RABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JAN 29-FEB 4, 2016

UCHANGANYAJI USIO SAHIHI WA VYAKULA


BUFFET! Vyakula vya kila
aina unajichagulia tu. Nyama
za kila aina ngombe,
mbuzi, kuku, samaki, kamba,
nakadhalika. Maandalizi:
Ziko za kuchemsha, za kuoka,
za kurost, za kuchoma,
nakadhalika. Huo ni upande
mmoja. Upande wa kitoweo!
Protini tupu. Upande wa
pili kuna vyakula kama
wali mweupe, biriani, pilau,
viazi vya kusongwa (mushed
potatoes), ndizi zilizopikwa
rojo, chips za viazi, tambi,
makaroni, chapati za kukanda,
chapati za maji, nakadhalika.
Huu ni upande wa chakula!
Wanga mtupu.
Upande wa tatu ni ule wa
vitu ambavyo siyo muhimu
sana. Hapa unaweza kukutana
na mboga mbili tatu za majani;
na matunda kama ndizi mbivu,
tikiti, nakadhalika. Katika
taaluma ya lishe, vyakula katika
kundi hili ndivyo ambavyo ni
muhimu sana kwa maana ya
kuboresha afya. Ukichukulia
gramu kwa gramu, vyakula
hivi vimebeba virutubisho vingi
sana (madini lishe, vitamini,
ufumwele [fibers], vizuia
vioksidishaji [anti oxidants],
nakadhalika), ukilinganisha na
vyakula vya protini na wanga.
Hata hivyo, kimazoea vyakula
hivi tunavipa umuhimu mdogo
sana!
Haya ni mazingira ya buffet.
Mara nyingi tunakutana
na mazingira haya pale
tunapokuwa wageni kwenye
mahoteli makubwa, au
tunapohudhuria sherehe
Inatoka uk. 3
nimefanyiwa bila ya ridhaa yangu.
Alisema mama huyo ambaye yeye
ni kutokea maeneo ya Mkoani.
Yupo Bibi mmoja ambaye ni mtu
mzima sana yeye nilimsifu kwa
kujikaza, lakini akionesha uchungu
namna alivyokuwa akieleza namna
wajukuu zake walivyoingiliwa
wakati yeye amefungwa kamba
ukumbini, watoto walipelekwa
chumbani na kuingiliwa.
Nilikuwa nikisikia makelele ya
wajukuu zangu ni watoto wadogo
wale, nina hakika wamewabikiri
kwa sababu wakipiga makelele sana
sana.
Inawezekana mambo hayo ya
kuwabiriki watoto wadogo hasa
wale waliokuwa wamemaliza
sekondari yamefanyika kweli kwa
makusudi kwa sababu baada ya
miaka kadhaa tulipokwenda Pemba,
baadhi ya waandishi wenzetu
wa habari wakitwambia hadithi
walizokuwa wakihadithiwa na
wanajeshi wasio na maadili ambao
wakijisifia kwamba waliwabikiri
watoto wengi sana kipindi cha
Januari 27, 2001 walipopelekwa
Kisiwani Pemba. Na wakiomba hali

zilizoandaliwa kwa bajeti


kubwa, au tunapokuwa wageni
kwenye makaazi ya matajiri.
Katika mazingira yetu ya
kawaida, iwe ni majumbani
au ni kwenye migahawa, japo
suala la mchanganyiko wa
vyakula vingi halipo, lakini
dhana ile ile ya kitoweo na
chakula inaendelea kutawala.
Mlo hukamilishwa kwa
kuunganishwa kitoweo na
chakula!
Kitoweo hapa ni nyama, kuku,
samaki, dagaa na vitu vingine
vyenye asili ya protini, wakati
chakula ni ugali, ubwabwa,
viazi, chapati, mihogo, magimbi,
nakadhalika vyote vikiwa na
asili ya wanga.
Watu wengi sana tuna tatizo
la kujaa gesi tumboni na
kutopata haja kubwa vizuri.
Ni tatizo ambalo tumeishi
nalo kwa muda mrefu mno
kiasi cha kuzoeleka na kuwa
sehemu ya maisha. Kimsingi
hili ni tatizo linalotokana na
uchakataji (processing) mbovu
kabisa wa chakula unaotokana
na kuchanganya vyakula vya
protini na wanga kwenye mlo
mmoja.
Hali hii inatokana na ukweli
kwamba watu wengi sana
hatujui kuwa vyakula vya wanga
na vile vya protini havitakiwi
vichanganywe kabisa! Kama
kuna haja ya kuchanganya
vyakula vinavyotoka katika
makundi haya na vyakula
vingine, basi vyakula sahihi
vinavyofaa kwa ajili ya
kuchanganyia ni mboga za
majani. Kwa maneno mengine,

wanga unaliwa kwa mboga za


majani, na protini inaliwa na
mboga za majani.
Kwa nini usahihi ni kula
protini au wanga kwa mboga
za majani pekee, na siyo
vinginevyo? Kuna sababu
mbili. Sababu ya kwanza ni
kuwa vimeng'enya (enzymes)
vinavyotakiwa kuchakata
wanga ni tofauti kabisa na
vile vinavyotakiwa kuchakata
protini. Vimeng'enya hivi
vimeundwa kwa namna ambayo
hufanya kazi katika pH tofauti
(vile vya wanga ni katika
mazingira ya alkali, na vile vya
protini ni katika mazingira ya
tindikali). Sasa unapochanganya
vyakula vinavyotoka katika
makundi haya kwenye mlo
mmoja, mwili unashindwa
kuelewa kuwa ni vimeng'enya
gani vitolewe ili kufanya
Uchakataji.
Matokeo? Uchakataji
wa chakula unakuwa ni
mbovu kabisa na vyakula
vilivyochanganywa kwenye
mlo husika huishia kuoza
na kuchachuka matumboni.
Kuoza na kuchachuka huku
kunazalisha gesi nyingi ya
ajabu. Sababu ya pili ni kwamba
vyakula vya protini vinatumia
nishati nyingi sana kuchakatwa
ukilinganisha na vile vya wanga.
Kwenye mfuko wa tumbo kile
chakula kinachohitaji nishati
nyingi kuchakata ndicho
ambacho kitaanza kuchakatwa.
Hii ina maana kuwa kama mlo
unajumuisha mchanganyiko
wa wanga na protini, wanga
utakaa kusubiri mzunguko wa

Karume Shujaa
kama hiyo itokee ili wawapate tena.
(Allah atuepushie mbali kwa fadhila
zake na huruma yake).
Kwa kweli sitawacha
kuyakumbuka yaliomkuta Mama
mmoja wa Micheweni akielezea
habari zake huku nikiwa mkono
wangu ukishikilia shavu langu
na kuona michirizi ya machozi
ikichuruzika. Mama anasema
alifukuzwa na majeshi na kuanguka
chini na kisha kuingilia kinyume
na maumbile kwa kuwa alikuwa
na mtoto mchanga na aliwaeleza
kwamba yeye ndio kwanza
amejifungua yupo kwenye nifasi,
lakini wakamwambia hivyo hivyo
tukutie adabu.
Baada ya kumfanyia kitendo
hicho akawa hawezi kutembea
kwa maumivu aliokuwa akiyapata
akaanza kukimbia kidogo kidogo
na kupita kwenye bonde bahati
mbaya huku akipepesuka akaja
akakanyaga kama utelezi mtoto
wake akadondoka kwenye matope.

Mama yule huku na khofu ya


kunusuru roho yake kwa kuwa
alisikia sauti za wanajeshi wengine
wakiwatafuta watu waliojificha
misituni, huku mtoto anazama
katika tope. Uchungu wa mama
ukachukua nafasi yake. Akaamua
kuhangaika kumtoa mtoto
katika tope hata kama wanajeshi
watamkuta. Anainama anamtoa
mwanawe kwenye matope
anamuona mtoto wake hawezi
kupumua na punzi za mbali
kumbe anavuta pumzi za mwisho.
Mtoto ameshakabwa na matope
aloyameza. Mama akaanza kulia
peke yake akaishiwa nguvu akakaa
chini anaogopa kupiga kelele
wanajeshi wasimsikie na huku
anajaribu kumvuta yale matope
kwa mdomoni lakini wapi. Kitoto
kile kikafariki mikononi mwake!
Hiyo ni mifano michache tu
kati ya watu ambao tumefanya
nao mahojiano ambao wakati ule
ambao ni kutoka katika maeneo

kuchakata protini ukamilike.


Kwa kawaida uchakataji wa
protini huchukua kati ya masaa
4 hadi 6. Kutokana na kuwa na
asili ya sukari, wanga hauwezi
kukaa kwa muda wote huo bila
kuanza kuchachuka (ferment).
Matokeo ya kuchachuka
kwa wanga wakati wa kusubiri
uchakataji wa protini ukamilike
ni gesi ya ajabu kuzalishwa!
Kimsingi sababu hii ndiyo pia
inayopelekea ishauriwe kuwa
matunda yote matamu yaliwe
walau nusu saa kabla ya kula
chakula kingine. Hii ni kwa
ajili ya kutoa nafasi kwa sukari
yote iliyoko kwenye matunda
hayo kuchakatwa na kufyonzwa
mwilini kabla ya kukutana na
vile vyakula vinavyochukua
muda mrefu kuchakata.
Ukiondoa tatizo la kuzaliwa
gesi nyingi tumboni pale mlo
unapojumuisha protini na
wanga, tatizo kubwa zaidi
ni mwili kushindwa kupata
virutubisho vya kutosha kutoka
katika huo mlo mchanganyiko.
Ili mwili uweze kufyonza
virutubisho vilivyomo
kwenye chakula kwa ufanisi,
ni sharti chakula hicho kiwe
kimesagwa vizuri, kitu ambacho
hakipatikani pale mlo husika
unapokuwa umejumuisha
wanga na protini. Kwa bahati
nzuri tatizo la uchanganyaji
wa vyakula ni jepesi kutatua.
Utatuzi wake hauhitaji gharama
yoyote ya kifedha, bali ni suala
la kubadilika zaidi kimtazamo.
(Kwa mawasiliano zaidi piga
0754281131/0655281131)
ya Wete, Chakechake, Micheweni
na Mikoani kwa njia za mikutano
na kuwauliza kwa kukaa nao
kwa faragha kujua yaliowasibu
ingawa baadhi yao walishindwa
kueleza. Hawakupenda
kuyaeleza wala kuandikwa yale
mambo yaliowasibu wakisema
yameshapita na yameshatendewa.
Na ni mengi yanayofanana na
hayo tuliohadithiwa na wengine
wakianza kutueleza kwa kula viapo
wakithibitisha maelezo yao.
Ni mambo mengi sana yalitokea,
yanaumiza na yanatia uchungu
sana. Lakini suali ni moja tu, jee
tunataka haya yatufike tena? Na
kama hatutaki, mbona dalili za
kutokea haya zipo wazi? Mbona
tunatafuta sababu za makusudi za
kuturejesha huko tulipotoka?
Sio dhamira yangu kurejesha
machungu kwa waathirika wala
sio lengo langu kuwaumiza wale
walioumia, lakini lengo langu
ni kukumbusha kwamba huko
tulishatoka na sasa tupo kwengine
kabisa. Tumshukuru Mwenyezi
Mungu kwamba aliwamiminia
busara Rais Mstaafu Amani

Inaendelea Uk. 14

Habari

AN-NUUR

RABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JAN 29-FEB 4, 2016

Tatizo ni majipu ya Kamati ya Kutunuku


Na Bakari Mwakangwale

BARAZA la Wakuu wa
Shule za Kiislamu Tanzania,
limeonyesha hofu katika
uharaka wa mabadiliko ya
kurejesha viwango vya ufaulu
vya zamani uliofanywa na
Waziri wa Elimu, Dk. Joyce
Ndalichako.
Baraza hilo limesema kuwa,
tatizo sio mfumo wa GPA wala
Divisheni, bali utaratibu wa
kutunuku usio na vigezo vilivyo
wazi uliokuwepo wakati wa Dr.
Joyce Ndalichako akiwa Katibu
Mtendaji Baraza la Mitihani.
Wamesema, wakati huo
kulikuwa na kitu kinaitwa
Kamati ya Kutunuku, ambao
ndio walikuwa na mamlaka ya
kutoa viwango vya ufauli kwa
vigezo ambavyo walivijua wao
wenyewe.
Wakafafanua kuwa alama za
ufaulu zilikuwa ni siri kubwa
ya Baraza la Mitihani na zenye
kubadilikabadilika somo hadi
somo na mwaka hadi mwaka.
Wasiwasi huo wa Wakuu wa
Shule za Kiislamu, umekuja
kufuatia hatua ya hivi karibuni
ya Waziri Ndalichako kutangaza
kurejesha mfumo wa zamani wa
kukokotoa matokeo ya Mitihani
ya Taifa chini ya Baraza la
Mitihani la Taifa, na kuachana na
mfumo mpya wa GPA.
Katika barua yao kwenda
kwa Waziri Mkuu, Mh.
Kassim Majaliwa, Baraza hilo
(BAWAKITA), limeonyesha
wasiwasi wao huo baada ya
Waziri wa Elimu, kusikiliza
madai ya Chama cha Wamiliki
na Mameneja wa Shule na Vyuo
Visivyo vya Serikali (Tangmosco)
wakidai kuwa mabadiliko hayo
kwenda katika mfumo wa GPA
yameingia pasi ya kushirikishwa.
Barua hiyo iliyosainiwa na
Mwenyekiti wake Mwalim
Hamisi Togwa, imesema hatua
ya Waziri Ndalichako, kumtaka
Katibu Mtendaji wa sasa Dr.
Charles Msonde, aeleze kuhusu
matumizi ya mfumo wa GPA
kunaifanya jamii ione na
kuelewa kwamba mfumo huo
kaunzisha yeye.
BAWAKITA, imebainisha
kuwa mfumo wa GPA,
ulianza kutumika katika
kutangaza matokeo kabla ya
Katibu Mtendaji wa sasa, kwa
watahiniwa wa Ualimu ngazi ya
cheti na Diploma.
Kwa maana hiyo, Baraza
hilo limemweleza Waziri Mkuu
kwamba wana wasiwasi na
uharaka wa Waziri wa Elimu,
Mheshimiwa Dk. Ndalichako
kurejesha mfumo wa zamani
ambao ulibadilishwa baada ya
kubainika kuwa na matatizo
makubwa.

WAZIRI wa Elimu, Dk. Joyce


Ndalichako.

KATIBU Mtendaji wa NECTA,


Dr. Charles Msonde.

Ikifafanua hoja ya
ushirikishwaji wa Tamongsco,
katika maamuzi ya kutumia
mfumo huo wa GPA, Baraza hilo
limesema, walishirikishwa katika
Tume iliyoongozwa na Profesa
Sifuni Mchome, ambayo ilitoa
ripoti yake Juni 15, 2015.
Imeeleza kuwa Tume hiyo
ilikuwa na ushiriki mkubwa
wa wadau mbalimbali wa
Elimu ambapo mambo mengi
yaliibuliwa na kuwa chachu
ya mabadiliko katika sekta ya
Elimu, ukilinganisha na tume
tatu zilizo tangulia kati ya
mwaka 2011 na 2013.
Ikifafanua zaidi barua
hiyo, imesema kuwa kabala
ya mabadiliko hayo kwa
muda mrefu wadau wa elimu
walikuwa hawafahamu mfumo
sahihi wa ukokotoaji wa matokeo
ya mitihani ya Taifa katika
ngazi mbalimbali kama ilivyo
bainishwa na ripoti ya Prof.
Sifuni Mchome.
Mh. Waziri Mkuu, ni Tume
hiyo ndiyo iliyopendekeza
ushirikishwaji wa wadau wa
elimu katika kuboresha mfumo
wa ukokotoaji wa matokeo,
ambapo ilisambaza dodoso juu
ya mapendekezo ya alama na
madaraja ya ufaulu katika shule
za Sekondari. Imesema sehemu
ya barua hiyo.
Ikaeleza kwamba kuuatia
hatua hiyo, Baraza lilimuandikia
barua Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Ufundi, aliyepita
wakiipongeza Serikali kwa
hatua iliyochukua katika
kuwashirikisha wadau katika
kuboresha mfumo wa ukokotoaji
na kuondoa mfumo wa usiri
chini ya Kamati ya Kutunuku,
ambapo sasa kila mwalimu
anajua wazi madaraja ya ufaulu
na namna yanavyopatikana.
Baraza hilo, limeweka wazi
kuwa kabla ya kuanza kutumika

kwa alama za ufaulu zilizopo,


hakuna mdau yeyote anaweza
kusema kwamba alama hizi ni
ndogo na anataka zirejeshwe za
zamani ambazo ni kubwa.
Wameeleza kuwa hiyo ni
kutokana na kuwa alama za
ufaulu zilikuwa ni siri kubwa
ya Baraza la Mitihani na zenye
kubadilikabadilika somo hadi
somo na mwaka hadi mwaka.
Barua hiyo imebainisha
kwamba, katika zama hizo
ambapo vigezo vya ufaulu
vilikuwa siri kubwa ya Kamati
ya Kutunuku, ilikuwa pia zama
ambapo shule za baadhi ya
mashirika ya kidini zilidaiwa

kutesa kila mwaka.


Baraza hilo limesema ni wazi
kuwa mchakato wa uboreshaji
wa Elimu katika nchi yeyote
unahitaji muda na mikakati
mbali mbali, kwani uwazi na
ushirikishwaji katika elimu
unaotekelezwa na Baraza la
Mitihani hivi sasa ni kigezo na
mkakati muhimu katika kutoa
elimu bora.
Barua hiyo yenye
Kumbukumbu namba
BAWAKITA/OWT/
ELIMU/2016/01/3, imemueleza
Waziri Mkuu, kwamba
wanapinga juhudi zozote
zinazoweza kuwarudisha
kule ambako wadau wa Elimu
hawakujua mchango wa CA
(Continuous Assessment) katika
ufaulu wala alama za ufaulu.
Kurudi huko, imebainisha
barua hiyo kuwa kunaweza
kurudisha mfumo ambao
unaweza kutoa mwanya kwa
Kamati ya Kutunuku kuamua ni
shule gani iongoze kwa kucheza
na alama ya ufaulu kutoka somo
hadi somo.
Sisi hatupingi uboreshaji
wowote wa majina ya madaraja
iwe GPA au Division na hata
kupandisha alama za ufaulu.
Cha msingi (Serikali)
izingatie kanuni ilizojiwekea za
utawala bora ambazo pamoja
na mambo mengine, zinahitaji
ushirikishwaji wa kina wa wadau
wote na uwazi katika kufikia
maamuzi. Imeeleza barua hiyo
ya Januari 21, 2016.

Inatoka Uk. 4
sana na watu mbali mbali,
viongozi wa dini na wanasiasa
ambao wana khofu ya kuzuka
machafuko kutokana na maneno
yanayoandikwa katika ubao
huo.
Wakati wa kampeni, jeshi la
polisi lilipiga marufuku ubao
huo kuandika ujumbe wowote
ambao utachochea hamasa na
kusababisha uvunjifu wa amani
nchini.
Juzi Kamanda wa polisi wa
Mkoa wa Mjini Magharibi,
Mkadam Khamis Mkadam
alisema kuwa ujumbe
unaoandikwa pale Kisonge ni
mkali lakini hilo ni jukumu la
vyama vya siasa na sio jeshi la
polisi.
Kamanda Mkadam aliwataka
wanasiasa kuwakataza vijana
wao ili kuibakisha nchi katika
hali ya amani kwani maneno
yanaweza kuamsha hisia kali na
hatimae kuzusha mapigano ya
wenyewe kwa wenyewe.
Bakari amezikwa juzi katika

makaburi ya Uwanja wa Ndege


Kiembe samaki na amesaliwa
katika Msikiti wa Nassor Bachu
Kikwajuni.
Kabla ya kuzikwa kulitokea
mvutano kati ya wanafamilia na
wafuasi wa CCM wa Kisonge
wakati familia ikitaka azikwe
haraka wakereketwa wenzake
wakitaka apelekwe Fuoni kwa
ajili ya kuzikwa siku ya pili ili
wanachama wenzake wapate
kuwahi maziko.
Hatutaki azikwe na Kisonge,
tutamzika sisi wenyewe,
ndio wazee wake, ya Kisonge
alipokuwa hai, sasa ameshafariki
mwili wa marehemu upo
mikononi mwa familia na
familia ndio yenye jukumu
la kumzika, tunaharakisha
tukamsitiri haraka na ndio
maana hatukutana kumpeleka
Fuoni maana huenda yakaja
maamuzi mengine, tukitoka
hapa tunakwenda makaburini
leo leo, alisema Ustadh mmoja
ambaye ni miongoni mwa
wanafamilia.

Msiba mara mbili Kisonge

Makala

AN-NUUR

RABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JAN 29-FEB 4, 2016

Kwanini mabeberu wanachangamkia sana Burundi?

Na Nizar Visram
HABARI za hivi majuzi
zinasema suala la Burundi
litajadiliwa na kamati
maalum ya Bunge la
Afrika Mashariki (EALA)
linaloshughulikia utatuzi
wa migogoro. Mwenyekiti
wa kamati hiyo, Abdullah
Mwinyi amesema ujumbe
wa Rais Pierre Nkurunziza
umekubali kuhudhuria
mkutano huo utakaofanyika
mjini Arusha wiki hii.
Kamati hiyo pia itatoa
fursa kwa raia na asasi
za kiraia kutoa maoni
yao kuhusu mgogoro wa
Burundi ambao umepelekea
mamia ya watu kupoteza
maisha yao. Moja ya asasi
iliyosambaza risala yake
ni jumuiya ya wanasheria
wa Afrika (PALU) ambao
wamependekeza kuwa
Nkurunziza asiruhusiwe
kushika uwenyekiti wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki
(EAC) mpaka akubali
kushiriki mikutano ya
usuluhishi.
Kwa mujibu wa katiba ya
EAC, uwenyekiti unatakiwa
ushikwe na Nkurunziza
baada ya Rais Magufuli
kumaliza muda wake.
Wengine wamediriki hata
kusema kuwa Burundi
ifukuzwe kutoka EAC
Wakati kamati ya EALA
inapanga mkutano wa
usuluhishi, tarehe 6 mwezi
huu mawaziri wa mambo
ya nje wa Tanzania, Uganda,
na Angola walihitimisha
kikao cha faragha kuhusu
Burundi uliofanyika mjini
Arusha. Hii ni baada ya
mazungumzo ya amani
yaliyopangwa kufanyika
Arusha kuahirishwa kwa
vile ujumbe wa Nkurunziza
ulikataa kuhudhuria
wakisema hawatakaa meza
moja na wale wanaochochea
vurugu nchini Burundi.
Wakati huo huo, Rais
Museveni ameteuliwa na
marais wenzake wa EAC
kuwa msuluhishi katika
mgogoro wa Burundi. Yeye

MWENYEKITI wa kamati
maalum ya Bunge la Afrika
Mashariki (EALA) , Abdullah
Mwinyi.
aliahidi kungatuka baada
ya mihula miwili lakini sasa
anaendelea na muhula wa
tano akiwa ametawala nchi
kwa muda wa miaka 30.
Sasa anatarajia kugombea
urais mwezi ujao baada ya
kubadili katiba iliyoweka
kikomo. Alifanya mabadiliko
hayo mnamo 2005 na tangu
wakati huo amekuwa
akisema shamba ambalo
nimelisafisha, kulipalilia
na kulilima mwenywe sasa
iweje niwaachie wengine
walivune? Kwa maneno
mengine nchi imegeuzwa
shamba lake.
Hata hivyo EAC imemteua
kuwa msuluhishi wa Burundi
, jambo ambalo limekubaliwa
na AU, UN na wafadhili.
Kwa muda huu Rais
Magufuli ni mwenyekiti wa
EAC na ndio maana huwa
anamtumia waziri wake wa
mambo ya nje, Augustine
Mahiga kushughulikia
mgogoro wa Burundi.
Mpaka sasa hajasafiri nje ya
nchi na haieleweki iwapo
atahudhuria mkutano mkuu
wa EAC au wa Umoja wa
Afrika (AU) unaotarajiwa
kufanyika mjini Addis Ababa
ili kuzungumzia mgogoro
wa Burundi. Tanzania ina
nafasi nzuri kwa vile Burundi
imekuwa na uhusiano wa
karibu na Tanzania. Wengi
tutakumbuka wakati ule
marais wa EAC walipokuwa
wakikutana Tanzania na
Burundi zilitengwa kwa
sababu ilionekana sisi
hatukuwa tayari kujiunga
na miradi ya EAC. Wenzetu
walijihesabu kama nchi
zilizokuwa zinakubaliana
(Coalition of the Willing CoW).
Mgogoro wa Burundi
ulianza pale mahakama

RAIS Museveni ameteuliwa na


marais wenzake wa EAC kuwa
msuluhishi katika mgogoro wa
Burundi.

ya katiba ilipoamua kuwa


Nkurunziza alikuwa na haki
ya kugombea urais kwa
muhula wa tatu, ingawa
katiba iliyosainiwa na pande
zote mjini Arusha iliweka
kikomo cha mihula miwili.
Ni kwa sababu muhula
wa kwanza Nkurunziza
alikuwa amechaguliwa na
wabunge na sio kwa kura za
wananchi. Hivyo muhula huo
haukupaswa kuhesabiwa,
ilisema mahakama. Katika
jopo la majaji watano,
mmoja alitofautiana kwa
kusema kuwa hao wabunge
waliwawakilisha wananchi
kwa hiyo awamu ya kwanza
ilipata ridhaa ya wananchi.
Huyo jaji alilazimika
kuikimbia nchi, baada ya
kudai kuwa majaji wenzake
walikuwa wamelazimishwa
kumuunga mkono
Nkurunziza.
Wapinzani wakadai kuwa
hata hivyo mahakama hiyo
ya katiba haiwezi kuwa huru
kwa sababu majaji wake
wameteuliwa na Nkurunziza.
Kuna wanaosema kuwa hoja
hii haina mashiko, kwani
hata katika nchi za magharibi
kama Ufaransa majaji
wa mahakama ya katiba
huteuliwa na rais. Hata
Obama anawateua majaji wa
mahakama ya juu. Hivyo,
baada ya mahakama ya katiba
kumruhusu, Nkurunziza
aligombea urais mwezi
Julai 2015 na akachaguliwa
kuongoza muhula wa tatu
kwa kupata asilimia 70 ya
kura. Uchaguzi huo ulisusiwa
na wapinzani. Marekani
na EU wakakataa kutuma
waangalizi wa uchaguzi.
Wakati Nkurunziza
analaumiwa kwa kugombea
urais muhula wa tatu,
hatusikii lawama kutoka nchi

za magharibi zikielekezwa
kwa marais wa Rwanda,
Uganda na DRC (Congo)
ambao pia wameongeza
mihula yao. Kagame
na Kabila nao, sawa na
Nkurunziza, waliteuliwa
kushika muhula wa kwanza
na kwa hiyo wanadai
hauhesabiki.
Kagame aliteuliwa
kuwa rais mwaka 2000,
kisha akachaguliwa kwa
kishindo mwaka 2003 na
2010. Sasa awamu yake
ijayo itakuwa ya nne lakini
yeye anasema ni ya tatu. Pia
anakusudia kuondoa kikomo
ili aendelee kuchaguliwa
bila kikomo. Kama ni kosa
kwa Nkurunziza, kwanini
isiwe kosa kwa Kagame na
wengine?
Baraza la Usalama la
Umoja wa Mataifa (UN)
lilipiga kura tarehe 12
Novemba mwaka jana na
kupitisha azimio likilaani kile
ilichokiita mauaji, utesaji
na ukandamizaji wa haki za
binadamu nchini Burundi.
Ufaransa ndio ilitayarisha
muswada wa azimio hilo
na kuzihimiza nchi 15
wanachama wa baraza hilo
kuunga mkono. Hapa inabidi
tujiulize iweje azimio kuhusu
nchi ya Kiafrika lipigiwe debe
na nchi ya Ulaya badala ya
Waafrika wenyewe?
Hata hivyo nchi za Kiafrika
zikisaidiwa na Urusi zilipinga
kipengele kinachotaka
Burundi iwekewe vikwazo.
Mwishowe azimio
likapitishwa bila ya kipengele
cha kikwazo. Sasa baada
ya kupitishwa kwa azimio
hilo, ikatangazwa kuwa
UN itafanya mipango ya
kuhamisha baadhi ya askari
wake kutoka DRC (Monusco)
hadi Burundi. Wazo mbadala
likatolewa kuwa badala ya
UN kutuma majeshi yake,
ni vizuri Umoja wa Afrika
(AU) ikafanya kazi hiyo.
Ikapendekezwa kuwa majeshi
ya Monusco yanaweza
yakaunganishwa na majeshi
ya AU. Rais Obama wa
Marekani akampigia simu
Rais Jacob Zuma wa Afrika
Kusini na wakazungumzia
hali ya Burundi.
AU ina sera ya kuwa na
vikosi kila kanda barani
Afrika. Hivyo, kwa upande
wa Afrika Mashariki kuna
kile kinachoitwa kikosi cha
akiba cha Afrika Mashariki
(East African Standby Force).
Ni kikosi hiki ndicho
kinachofikiriwa kupelekwa
Burundi. Uamuzi wa
Inaendelea Uk. 18

Makala
Na Omar Msangi

JOSEPH "Jihad Jack"


Terrence Thomas ni
kijana ambaye aliwahi
kuhukumiwa kifungo
cha miaka mitano jela na
Mahakama Kuu ya Australia
tarehe 31 Machi, 2006 kwa
tuhuma za ugaidi. Ilidaiwa
kuwa Joseph Thomas
aliwahi kupewa pesa na
magaidi wa Al Qaida na
kwamba pesa hizo ilikuwa
ni mtaji wa kuanzisha kundi
la Al Qaida Australia. Joseph
Terrence Thomas anatajwa
kuwa raia wa kwanza wa
Australia kushitakiwa na
kuhukumiwa kwa sheria
yenye utata ya kupambana
na ugaidi (anti-terrorism
laws) iliyowekwa baada ya
mashambulizi ya Septemba
11, 2001 Marekani.
Ukitizama kwa undani
na kuchambua tuhuma na
baadae hukumu, unaweza
kusema kuwa kama ni kosa,
basi ilikuwa ni Thomas
kusilimu na kuoa mke kutoka
Pakistan.
Baada kusilimu na
kuoa Mpakistan, Thomas
aliondoka Australia Machi
2001 kwenda kwa wakweze,

AN-NUUR

RABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JAN 29-FEB 4, 2016

Joseph "Jihad Jack"


Sheikh Msellem Ali
Mhanga kama Herero, Lumumba
Uhuru anasema ana lengo muhimu
Lipi zaidi ya kutumikia mabeberu?

JIHAD Jack akiwa na mkewe.

kabla hata ya shambulio la


Septemba 11. Kwa kutumia
makachero na jeshi la
Pakistan, Thomas alikamatwa
huko huko akawekwa
ndani ambapo aliteswa na
kuandikishwa maelezo ya
kukiri kuwa yeye ni Al Qaida
na alikuwa akipokea pesa
kutoka Al Qaida. Hata hivyo,
baadae Mahakama ya Rufaa
ilifutilia kwa mbali adhabu
hiyo na kumuona hana hatia
kwa sababu kilichodaiwa
kuwa ni ushahidi kilipatikana
baada ya Thomas kuteswa
sana. Kwa maana nyingine
ni kuwa kama ni kukiri, Mr
Thomas alikiri kujinusuru
kutokana na mateso makali
aliyopewa akiwa rumande,
mikononi mwa vyombo vya
usalama.
Katika kufuatilia kesi ya
mdogo wake, Les Terrence
Thomas (kaka yake Joseph)
anasema kuwa amekumbana
na visa vya watu kuteswa bila
ya kuwa na hatia au bila ya
kuhukumiwa kwa tuhuma
zinazowakabili. Amesema,
kuna watuhumiwa wengi
wa makosa ya ugaidi katika
rumande za Melbourne na
Sydney ambapo wanapewa
Inaendelea Uk. 10

Jinsi nchi za Magharibi zinavyotengeneza ugaidi

Na Andre Vitchek
Januari 22, 2016 'Mtandao
wa Kupashana Habari,' na
'Counterpunch'
UGAIDI una mifumo tofauti
na sura nyingi, lakini baya
zaidi kati yake ni ukatili.
Tunaambiwa tuamini
kuwa magaidi ni wehu na
wakora, wanaozunguka na
mabomu, bunduki nzito
na mikanda ya milipuko.
Ndiyo tunavyoambiwa
tuwafikirie. Wengi wao

wana madevu; takriban wote


wanaonekana 'kutokea nchi
za nje, siyo 'Wazungu, siyo
wa Magharibi. Kimsingi ni
wapiga wake, wabaka watoto
na wateketezaji sanamu za
Kiyunani na Kirumi. (Hii
ndiyo picha tunayopewa
tuwaone kwayo kila
anayetajwa kuwa ni gaidi. Ni
jitu katili la kutisha.)
Hali halisi ni kuwa, wakati
wa Vita Baridi (ushindani
wa kiitikadi na tishio la
vita kati ya Marekani na
Urusi ya kikomunisti)
kulikuwa na 'magaidi' wenye
muonekano wa Kizungu.
Walikuwa ni wanaharakati
wakijumuika katika vikundi
vya kimapinduzi, nchini
Italia na kwingineko Ulaya.
Ila ni wakati huu tu ambako
tunajifunza kuwa matukio
ya kigaidi walioyafanya,
kumbe yalibuniwa na
kutekelezwa na taasisi za
himaya ya Marekani, serikali
kadhaa za kupinga mageuzi
barani Ulaya na mashirika ya
kijasusi. Unakumbuka, nchi
za NATO zilikuwa zinalipua

treni katika njia za mahandaki


(chini ya ardhi), au kulipua
vituo vizima vya treni (kisha
kusingizia kuwa ni kazi ya
magaidi.)
"Ilibidi ifanyike,"
ili kuharibu sifa ya
wanaharakati, kuhakikisha
tu kuwa watu hawapoteza
mwelekeo na kupitia kura
vyama vya Kikomunisti au
vya Ujamaa wa dhati.
Pia kulikuwa na makundi
kadhaa ya kigaidi Amerika
ya Kusini - makundi ya
uamsho wa kimapinduzi
yakipigania uhuru na dhidi ya
ukandamizaji, zaidi kupinga
ukoloni wa Magharibi. Ilibidi
wazungukwe, walainishwe,
na kama walikuwa
madarakani, wapinduliwe.
Lakini magaidi walianza
tu kufahamika kwa kiwango
kikubwa nchi za Magharibi
baada ya kuteketea kwa
Urusi na nchi za kikomunisti
kwa jumla kupitia maelfu ya
njia za kiuchumi, kijeshi na
propaganda, na kufumba na
kufumbua nchi za Magharibi

zikajikuta ziko kweupe,


wako pekee yao bila mtu
wa kupigana naye. Kwa
njia moja au nyingine ilihisi
kuwa zinahitaji kuhalalisha
matendo yao ya kutisha
barani Afrika, Mashariki ya
Kati, Amerika ya Kusini na
Asia.
Ilikuwa inahitaji adui
mwingine mkubwa mwenye
nguvu kuhalalisha bajeti
zao kubwa sana za kijeshi
na kijasusi. Ilikuwa haitoshi
kupambana na vigaidi
uchwara mia kadhaa katika
mapori ya Colombia (FARC),
Ireland ya Kaskazini (IRA)
au Corsica (harakati ya
kujitenga na Ufaransa). Ilibidi
kuwa na kitu kikubwa, kitu
kinacholingana na 'himaya
ya uovu' inayotisha, kama ya
Urusi.
Ni kwa kiasi kikubwa,
kukosekana kwa tishio hili
kulikuwa kunawakosesha
usingizi (Wazungu mabeberu
wa Ulaya na Marekani).
Walitaka tishio pekee, siyo

Inaendelea Uk. 10

10
Inatoka Uk. 9
mateso ya kutisha wakati
hawajahukumiwa kwa
kosa lolote. Na wote hao ni
Waislamu au watu kutoka
Mashariki ya Kati na Asia.
Wiki iliyopita gazeti
hili lilichapisha kisa cha
kijana Saidi Michael Danieli
alivyoteswa akiwa mikononi
mwa vyombo vya dola, yote
kutaka akiri kuwa yeye ni
gaidi/mshiriki wa jinai ya
Sitakishari. Hata baada ya
kuthibitisha kuwa hana hatia,
bado polisi wakambambika
tuhuma ya kukutwa na
sare walizodai ni za Al
Shabaab. Katika kusimulia
yaliyomsibu, Saidi Michael
Danieli aligusia pia majaaliwa
ya mwezake, marehemu sasa,
aliyemtaja kwa jina moja la
Khalfan ambaye aliteswa na
kufariki.
Aliponiona tu, alieleza
kuwa amenitaja ili nifike
nimuone katika hali
aliyokuwa nayo, hata akifa
ifahamike kuwa amekufa
akiwa mikononi mwa Polisi.
Kweli jamaa alifariki usiku
wa saa nane, siku ile ile
niliyoingia mimi.
Anaelezea Saidi Michael

Makala

RABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JAN 29-FEB 4, 2016

Joseph "Jihad Jack"


Sheikh Msellem Ali

Sheikh Msellem Ali Msellem

AN-NUUR

Danieli, akisimulia
yaliyomkuta kijana Khalfan
hadi mauti kumfika akiwa
mikononi mwa polisi.
Haya anayosimulia Saidi,
yaliyomkuta Khalfan na
yale ya Joseph "Jihad Jack"
Terrence Thomas, ndiyo
majaaliwa ya Waislamu dunia
nzima hivi sasa.
Andre Vltchek ameandika
Makala aliyoipa jina
How the West Creates
Terrorism. Humo anaeleza
na kuchambua jinsi nchi
za Marekani na Ulaya
zilivyounda zimwi hili ugaidi,
zinavyotengeneza magaidi
kila uchao na kuwatumia
katika kufanikisha agenda
zao za kibeberu. Andre
Vltchek anasema, mabeberu
wa Marekani na Ulaya,
ndio magaidi wa kweli na
wabaya wasio na mfanowe.
Ni waharibifu, wanyonyaji,

waporaji na wauwaji. Sasa


ili wasizomewe katika
kuvamia, kuuwa na
kupora, wametengeneza
ugaidi bandia wakaupigia
propaganda ukakubalika
huku wao wakijitangaza
kuwa ni wasamaria wema
wanaoitakia mema dunia kwa
kupambana na magaidi (walio
waunda wenyewe). Kwa hiyo,
wanapovamia Iraq na kuuwa
watu kinyama Fallujah,
inaonekana wanapambana na
magaidi sio wananchi wasio
na hatia wa Fallujah. Hivyo
hivyo wakifanya unyama
wao Libya, Syria, Somalia
na kila mahali wanapotaka
mali kama walivyoshiriki
kumuuwa Patrice Lumumba.
Hii ndiyo kawaida yao toka
wakipambana na walichodai
kuwa ni evil Soviet threat,
walipokuwa wakipambana
na Fidel Castro na mikakati
yao kwa ujumla katika
uporaji Amerika ya Kusini
kupitia Operation Mongoose
na Operation Northwoods
ambapo waliunda Latin
American terror groups.
Ili kuufanya Uislamu uwe
adui mwenye hadhi, Himaya
Inaendelea Uk. 11

Jinsi nchi za Magharibi zinavyotengeneza ugaidi

Inatoka Uk. 9
ushindani wa malengo ya
usawa na maadili kimataifa.
Hivyo nchi za
Magharibi (zikabuni na)
zikaambatanisha ugaidi na
Uislamu. Uislamu ambao
ni moja ya tamaduni kubwa
zaidi duniani, kwa lengo
la kuwatisha mama wa
nyumbani wa matabaka
ya wenye fedha mitaa ya
miji mikubwa ya nchi za
Magharibi! Na zaidi ya hapo
ilibidi Uislamu uzungukwe
udhibitiwe kwani Uislamu
ulikuwa na mwelekeo wa
wazi mno wa Ujamaa na
ulikuwa na amani kupita
kiasi (kwa hiyo uvurugwe
kuondoa Amani katika nchi
za Waislamu na badala yake
kupandikiza machafuko na
mauwaji).
Wakati huo katika historia,
viongozi wote muhimu wa
mwelekeo wa siasa usio
wa kidini na wa Kijamaa
katika nchi za Kiislamu,
kama Iran, Indonesia na
Misri, walipinduliwa na
nchi za Magharibi, urithi

usiopingika kitamaduni na
kimaadili. (Kwa maana kuwa
ukishaupaka matope Uislamu
kuwa ni dini ya kigaidi na
magaidi, unaacha Umagharibi
(Ukristo?) kuwa ndio
utamaduni bora na ustaarabu
wenye maadili yanayofaa.)
Hivi ndivyo inavyofanya kazi

WANAJESHI wa Kenya wakiwa wamebeba majeneza yenye miili


ya wenzao waliuawa nchini Somalia hivi karibuni.

wao kutemewa mate, au


walipigwa tu marufuku.
Lakini hiyo haikutosha kwa
nchi za Magharibi!
Ili kuufanya Uislamu uwe
adui mwenye hadhi, Himaya
(ya Marekani) ilibidi kwanza
ielekeze hisia katika siasa kali
na kuharibu asasi na taasisi
za Kiislamu zisizohesabika.
Halafu kuunda hizo mpya,
hivyo kuzipatia mafunzo,
kutoa silaha na fedha, ili

ziweze kuonekana zinatisha


vya kutosha.
Bila shaka kuna sababu
moja zaidi muhimu kwa
'ugaidi,' hasa 'ugaidi;
(unaodaiwa kuwa) wa
Kiislamu, kuwa ni wa
lazima kwa kuhakikisha
uendelevu wa fikra za nchi
za Magharibi, utofauti wake
na udhibiti wa dunia nzima:
Inahalalisha dhana ya nchi
za Magharibi ya ubora wake

Kwa karne nyingi, nchi


za Magharibi zimekuwa
zikijitifua katika uwanda wa
dunia kama dubu lenye kiu ya
damu. Licha ya propaganda
inayowafaa inayotolewa na
vyombo vya habari vya nchi
za Magharibi vyenye njia
za kuonekana kote duniani,
ilikuwa inaanza kueleweka
kuwa Himaya inabaka,
kuua na kusomba mali kila
sehemu duniani. Miongo
michache mingine na dunia
ingeziona nchi za Magharibi
kama ugonjwa mbaya wenye
simu. Hali kama hiyo ilibidi
izuiliwe kwa njia zozote zile!
Hivyo wanaitikadi na
wapropaganda wa Himaya
wakaja na wazo jipya tena
Inaendelea Uk. 11

11
Inatoka Uk. 10
(ya Marekani) ilibidi kwanza
ielekeze hisia katika siasa kali
na kuharibu asasi na taasisi
za Kiislamu zisizohesabika.
Halafu kuunda hizo mpya,
hivyo kuzipatia mafunzo,
kutoa silaha na fedha, ili
ziweze kuonekana zinatisha
vya kutosha.
Kuna mambo kadhaa ya
kuchanganua hapa kutokana
na maneno haya ya Andre
Vltchek. Moja ni kuwa
magaidi na ugaidi kama
ulivyo katika sura yake ya
sasa, ni jambo lililobuniwa
na mabeberu. Ni mkakati
na program inayoratibiwa
na mabeberu wa Ulaya na
Marekani katika kufanikisha
malengo yao. Nitafafanua
zaidi mbele. Pili, serikali yetu
na serikali zote duniani, kadiri
zitakavyojitahidi kutumia
nguvu na mbinu mbalimbali
kupambana na magaidi,
magaidi wataendelea
kuwepo na kunona zaidi.
Ugaidi utakoma pale tu
ambapo waliouanzisha
watakapoutema kama
walivyoacha ukoloni wa
kuvamia na kukalia nchi

Makala

AN-NUUR

RABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JAN 29-FEB 4, 2016

Joseph 'Jihad Jack' Sheikh Msellem Ali

MAUAJI ya kutisha yaliyofanywa na Wajerumani nchini Namibia wakati wa ukoloni.


wakaja na ukoloni mambo
leo.
Tatu, wengi wa
wanaokamatwa kwa
tuhuma za ugaidi, ni watu

waliotumbukizwa kwa ujinga


wakidhani wanatumikia
agenda njema kumbe
wanamtumikia beberu kafiri.
Na vijana wengi wa Kiislamu

wanaingia katika kundi


hili. Hivi sasa kuna vijana
wengi wa Kiislamu hufanya
mijadala kuhusu habari za
Inaendelea Uk. 12

Jinsi nchi za Magharibi zinavyotengeneza ugaidi

Inatoka Uk. 10

la kufana: Na tuunde kitu


ambacho kinaonekana na
hata kusemwa vibaya zaidi
yetu sisi, hivyo tunaweza
kuitangazia dunia kuwa
sisi bado ndiyo watulivu na
wasikivu zaidi kitamaduni
duniani kote!
Na tutengeze mlengwa
halisi: na tupigane na kitu
tunachokitengeneza wenyewe
(ugaidi) - tupigane nacho
katika jina la uhuru na
demokrasia!
Ndivyo jinsi kizazi
kipya, kizazi kipya cha
'ugaidi' kilivyozaliwa. Na
kinaishi! Kinadunda vyema!
Kinazaliana kama salamanda
za Capek.
Ugaidi wa nchi za Magharibi
Ugaidi wa nchi
za Magharibi huwa
hauzungumziwi, licha ya
kuwa katika hali yake mbaya
zaidi inapiga dunia bila
kuvuta pumzi na kwa muda
mrefu, maiti kwa mamia ya
mamilioni zikijazana kila
mahali.

Hata vikosi vya nje na vya


Von Wissman, hivyo akawa
sana. Lakini ni nani mwalimu
kukodiwa vya Himaya, kama
mwangalifu zaidi asifikishwe
wao? Kwa karne nyingi,
Mujahiddin, Al Qaida au
mahakama ya kijeshi akivuka
himaya za Ulaya zilikuwa
ISIS. haviwezi kufikia ukatili
mpaka).
zinaua, kutesa, kubaka na
ambao umefikiwa mara kwa
Hivyo ugaudi halisi ni
kukata viungo watu katika
mara na wakubwa wao wa
upi, na ni kwa vipi ambako
mabara yote duniani. Ambao
Uingereza, Ufaransa, Ubelgiji, ISIS na wengine wangefuata
hawakufanya hivyo moja
Ujerumani au Marekani.
uongozi wake? Wanasema
kwa moja 'waliwekeza' katika
Ni kweli wanajitahidi sasa
kuwa ISIS inakata vichwa
kuunda vikundi vya misafara
kuwafikia wakufunzi wao na
vya mateka wao. Ni vibaya
Inaendelea Uk. 12
wafadhili wao, lakini kimsingi
ni kuwa hawana uwezo wa
kufikia viwango vyao vya
ukaliti na uuaji.
Inahitaji "utamaduni
wa Magharibi" kuua watu
takriban milioni 10 katika
eneo moja tu la kijiografia,
kwa muda mfupi tu vile!
(Inaashiria kwa mfano
Namibia, wakati ukoloni
wa Ujerumani ulipozima
uasi dhidi ya uvamizi wa
kikoloni, ukateketeza kabila
kubwa la wa-Herero ukawaua
karibu wote. Kule Namibia
alipelekwa jemadari wa cheo
cha jenerali ndiyo maana
alitenda atakavyo, hapa
Tanganyika (Ujerumani ya
Afrika Mashariki, Deutsch
WAKOLONI wa Kijerumani wakiwanyonga wananchi wa
Ostafrika) aliletwa kamanda
kabila laHerero nchini Namibia.
wa cheo cha Meja, yaani

12

Makala

AN-NUUR

RABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JAN 29-FEB 4, 2016

Jinsi nchi za Magharibi zinavyotengeneza ugaidi

Inatoka Uk. 11
ya wakoloni, au kupeleka
watu kujiunga na vikosi vya
maangamizi.
Mfalme Leopold II na
mawakala wake waliua
takriban watu milioni 10
katika eneo la Afrika ya
Kati na Magharibi, ambayo
sasa inajulikana kama
Congo. Alikuwa akiwinda
watu kama wanyama,
akiwalazimisha kufanya
kazi katika mashamba yake
ya mpira. Kama alidhani
hawajazi mapipa yake
kwa haraka inavyotakiwa,
hakusita kuwakata mikono,
au kuwachoma moto wakazi
wote wa vijiji katika vibanda
vyao, wakiwa hai.
Wahanga milioni 10
walipotea. Milioni 10! Na
hiyo haikutokea katika
wakati wa mbali uliopita,
katika "zama za giza," lakini
katika karne ya 20 chini
ya utawala unaoitwa ni
ufalme wa kikatiba, na pia
hujitangaza kuwa ni wa
kidemokrasia. Inafananaje
na ugaidi ambao unatawala
katika maeneo yanayokaliwa
na ISIS? Tulinganishe idadi
na kiwango cha ukatili!
Na Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo tangu
1995 imepoteza tena kiasi
cha watu milioni 10 katika
mzunguko wa kikatili wa
vita na mauaji, ulioanzishwa

Inatoka Uk. 11
Jihad, Al Shabaab, Makafiri
Vs Waislamu, na mambo
kama hayo, kupitia Wasapu,
Facebook na vitu kama hivyo,
na wengine kufikia hatua ya
kuhamasishana kufanya jinai
kwa hoja ya kupambana na
makafiri. Ukitafuta mzizi wa
yote haya ni kutumbukizwa
kijinga katika kile alichosema
Andre Vltchek kwamba:
In order to make Islam a
worthy enemy, the Empire had
to first radicalize and pervert
countless Muslim movements
and organizations, then create
the new ones, consequently
training, arming and financing
them, so they could really look
frightening enough.
Anachotufahamisha Andre
Vltchek ni baada ya mabeberu
kumaliza vita baridi na Mrusi
na baada ya kufanikisha
mikakati ya Mongoose na

WANAWAKE wa kabila la Herero nchini Namibia.

na mawakala wa nchi za
Magharibi, Rwanda na
Uganda (ona kiongezeo cha
filamu ya mwandishi huyu ya
Kamari ya Rwanda).
Wajerumani walifanya
mauaji ya kimbari katika eneo
la kusini magharibi ya Afrika,
iitwayo sasa Namibia. Kabila
la wa-Herero liliteketezwa, au
kufikia kiasi cha asilimia 90

ya kabila lote. Watu kwanza


walitolewa kwenye ardhi
yao na kwenye nyumba zao
na kutupwa katika jangwa.
Kama walinusurika, vikundi
vya wauaji waliowatangulia
wa-Nazi vilifuata, vikitumia
risasi na njia nyingine za
mauaji ya halaiki. Majaribio
ya kitiba juu ya binadamu
yalifanywa, kuthibitisha

Joseph "Jihad Jack"


Sheikh Msellem Ali

WANANCHI wa kabila la Herero nchini Namibia.

ubora wa taifa la Ujerumani


na Wazungu kwa jumla.
Hawa walikuwa ni raia wa
kawaida, watu ambao kosa
pekee walilokuwa nalo ni
kuwa hawakuwa Wazungu,
na walikuwa wamekalia
ardhi ambayo inavamiwa na
kutwaliwa na Wazungu hao.
Wapiganaji wa Taliban na
hata ISIS hawajawahi kufikia
hapo!
Hadi sasa, serikali ya
Namibia inadai kurudishwa
kwa vichwa visivyohesabika
vya watu wa nchi hiyo,
vichwa ambavyo vilikatwa
na kupelekwa Chuo Kikuu
cha Freiburg na mahospitali
kadhaa jijini Berlin, kwa
majaribio ya kitiba.
Hebu fikiria, ISIS ikate
vichwa vya maelfu ya
Wazungu, ili kufanya
majaribio ya kitiba
kuthibitisha kuwa Waarabu
ni bora kuliko Wazungu.
Ni jambo ambalo haliwezi
kufikirika! (Ila jambo moja
usisahau ISIS ni mtoto wa
Wazungu hao hao anayekula
na kupumua kwa pesa na
silaha za Wazungu hao.)
(Makala hii: How the
West Creates Terrorism,
imeandikwa na Andre
Vltchek na kutafsiriwa kwa
Kiswahili na Anil Kija)

Northwoods, hivi sasa wapo


kwa Waislamu. Wanaunda
vikundi vya kigaidi katika
nchi za Kiislamu kupitia
mitaala ya kuwatia katika
siasa kali na imani kali,
kisha huwapa mafunzo
ya kigaidi, silaha na
kuwawezesha kipesa na
kuwatumia kwa mambo yao.
Kijana akiona Al Shabaab net
au Jihad.com anaamini kuwa
huu ni mtandao wa wanaJihad na akisoma mjadala
unaoendelea pale, huona
hawa ndio Waislamu, ndio
Mujahidina naye hujimwaga.
Wengine wakishajuana
huanzisha Darsa Duara lao
katika Wasapu, wanajipa
majina kama AK-47 na vitu
kama hivyo. Sasa hawa
unaweza kusikia mmoja
kadakwa na vyombo vya
Inaendelea Uk. 15

13
Na Mwandishi Maalum,
Zanzibar
ANAYEMFUATIA kwa ujasiri
na msimamo alikuwa Salmin
Awadh Salmini.
Kwa hakika CCM
imeondokewa na majemadari,
ambao kama kuna kuonana,
hivi sasa wanaulizana ya
mitaa ya Barzakh, sio tena ya
Kisiwandui!
Na hapo ndipo yalipo
mazingatio kwa kila Muislamu.
Kwamba, tunaweza kukataa
kutoa serikali kwa staili ya
Jecha Salim Jecha, lakini hatuna
ubavu wa kukataa kutolewa
roho zetu na kuchukuliwa uhai
wetu muda unapofika.
Ni majira ya saa 11 Alfajiri
nafungua simu yangu napata
ujumbe ulioanza na:
Innaa Lillahi Wainnaa Ilayhi
Rajiuun. Asha Bakari hatunaye
tena. Ameshatangulia mbele
ya haki. Waarifu na wengine.
Ujumbe huo ukitokea Dubai.
Naam Alhamdulillah
Mwenyeenzi Mungu ampokee
na amsamehe mja wake huyo.
Amin.
Asubuhi ilipofika
kila unapopita, taarifa
zimeshasambaa na kauli
unayoisikia katika vinywa vya
watu ni hii Nakwambieni nchi
hii haipatikani kwa karatasi
sisi tumepindua labda na nyie
mpindue.hatutoi hatutoi
hatutoi, wenye madaraka ni sie.
Ni kauli ya Bi Asha Bakari
wakati wa uhai wake ni kauli
iliyompa umaarufu mkubwa
katika siasa za Zanzibar ambayo
imemalizia maisha yake.
Sisi ndio wenye madaraka.
Nawaambia tena jamaa
zangu, wallaahi, wallaahi,
wameshindwa kutawala
1995 hawatawali tena maisha
yao yote na narudia tena
na siogopi kusema. Serikali
hii ni ya kimapinduzi si ya
mchezo, hawawezi, hawawezi
kutupinduahatuwezi
kukabidhi serikali kwa njia ya
vikaratasi (kura).
Nchi haitolewi kwa kura,
haya kuitisha uchaguzi
kusumbua watu na kupoteza
gharama zote hizo ya nini?
Hata hivyo, mtu unaweza
kusema, hiyo ni kauli ya Asha
Bakari si ya CCM wala Serikali
ya Mapinduzi Zanziar. Lakini
ukweli ulio wazi ni kwamba
aliyofanya Jecha ni kutafsiri
kivitendo aliyosema Asha
Bakari! Lakini maadhali CCM
imemuunga mkono Jecha, ina
maana kuwa huo ndio msimamo
wa CCM na SMZ yake. Na kwa
maana hiyo, hata tangazo la
kurudia uchaguzi halina maana
yoyote.
Vyovyote iwavyo, hayo ndiyo
matamshi yaliompa umaarufu
mkubwa Asha Bakari Makame
na kuonekana jasiri hapa
Zanzibar akijulikana zaidi kwa
jina la Mtama ambalo alipewa

Makala

RABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JAN 29-FEB 4, 2016

Safari ni nzito!
Tumkumbuke Asha kwa Dua
Aungana na Awadh Barzakh
Jecha anakazia tu kauli zao

MAREHEMU Asha Bakari Makame.

MAREHEMU Salmin Awadh Salmin


na Baba yake Mzazi Bwana
Bakari Makame. Anayemfuatia
kwa ujasiri na msimamo wa
namna hiyo alikuwa Salmin
Awadh Salmini ambaye, naye
alishatangulia mbele za haki.
Kwa hakika CCM imeondokewa
na majemadari, ambao kama
kuna kuonana na kujuliana
hali, hivi sasa wanaulizana ya
mitaa ya Barzakh, sio tena ya
Mapinduziii! Salmin Awadh
alifikia mahali pa kuona kuwa
hata kuwa na Serikali ya Umoja
wa Kitaifa, ni kama wanasogelea
katika kutaka kutoa nchi kwa
vikaratasi akataka kupeleka
hoja binafsi Barazani, serikali
hiyo ivunjiliwe kwa mbali.
Bahati mbaya jambo halikuwa
mpaka akaondoka yeye.
Na hapo ndipo yalipo
mazingatio kwa kila Muislamu
na kwa hakika kwa kila
binadamu. Kwamba, tunaweza
kukataa kutoa serikali kwa

AN-NUUR

staili ya Jecha Salim Jecha,


lakini hatuna ubavu wa
kukataa kutolewa roho zetu na
kuchukuliwa uhai wetu muda
unapofika!
Asha Bakari (Allah
amrehemu) alikuwa ni
Mwanamke aliyekuwa mstari
wa mbele katika kukihami
na kukitetea Chama Cha
Mapinduzi (CCM) katika uhai
wake wote. Lakini kwa bahati
mbaya, Chama iwe CCM, CUF
au chochote, hakina uwezo wa
kutetea uhai wa wanachama
wake! Amekitumikia chama
kwa muda mrefu na kukamata
nyadhifa mbali mbali ndani ya
chama hicho huku akiamini
dhana ya uhafidhina ambayo
ni viongozi wachache
waliobaki ndani ya Chama Cha
Mapinduzi waliobakia kutetea
msimamo huo wa uhafidhina.
Hao ni wale ambao hawataki
demokrasia kufuata mkondo

wake na kungangania dhana ya


mapinduzi daima zaidi kuliko
uhalisia au lengo la Mapinduzi
yenyewe ambalo limeasisiwa
na aliyekuwa Rais wa Kwanza
Zanzibar, Marehemu Mzee
Abeid Amani Karume.
Lengo la Mapinduzi ni
kukataa ubaguzi wa aina yeyote
na kuwepo usawa kwa wananchi
wote katika kupata huduma
za kijamii kama elimu, afya na
huduma nyenginezo zitolewazo
na serikali.
Bi Asha pamoja na kuwa
akipingwa na wengi kutokana
na msimamo wake, lakini
hakuvunjika moyo hata
kidogo. Licha ya kukabiliwa na
changamoto mbali mbali, hasa
kwa kuwa akitokea katika Kijiji
Cha Mtambwe kijiji ambacho pia
alichozaliwa Katibu Mkuu wa
Chama Cha Wananchi (CUF),
Maalim Seif Sharif Hamad.
Mimi mwanangu Mtama,
amejiunga na CCM muda
mrefu tokea wakati wa ASP
na anakipenda chama na
anamaliza uhai wake akiwa
ndani ya Chama Cha Mapinduzi
CCM lakini sio lazima na mimi
nimfuate yeye, mimi CUF na
yeye ni CCM na hilo alilitambua
awali, alisema Mzee Bakari
ambaye ni Baba yake Bi Asha.
Ujasiri wa Bi Asha na
msimamo wake thabiti ndio
uliompa umaarufu mkubwa
ndani ya siasa za Zanzibar
ambapo alionekana kama
ni turufu muhimu mbele ya
wapinzani wao wa CUF kwa
kuwa anatokea Kisiwani Pemba.
Lakini jengine kutoka kijiji
kimoja na Maalim pia ilionekana
kama ni nguvu kubwa ambayo
ikitumika wazi wazi katika
kumdhoofisha Maalim Seif
kutokana na kutoka ndani
ya kijiji na familia zilizo na
mahusiano ya karibu.
Asha Bakari alizaliwa
Disemba 25, 949 na kupata elimu
yake ya msingi katika Shule
ya Utaani mwaka 1957 hadi
1964 na kujiunga na Sekondari
katika shule ya Fidel Castro
mwaka 1965 hadi mwaka 1968.
Baadae alijiunga na Chuo cha
Uhazili mwaka 1970 kwa mwaka
mmoja akisomea masomo ya
sekretari katika ngazi ya cheti
na kuongeza na miaka mengine
miwili katika chuo hicho kwa
kuendelea na kozi hiyo hiyo kwa
ngazi ya Advence mwaka 1978
hadi 1979 na baadae kujiunga
na kozi ya Diploma ya Political
Science and Management
mwaka 1984 hadi mwaka 1985
nchini Bulgeria.
Katika nafasi ambayo
ameshikilia ndani ya serikali
ni pamoja na uwalimu kuanzia
mwaka 1969 hadi mwaka
1970, sekretari wa Wizara ya
Elimu kuanzia mwaka 1970
hadi mwaka 1974, Sekretari wa
Wizara ya Habari mwaka 1974
hadi mwaka 1980, na kisha

Inaendelea Uk. 14

14

MAKALA/MASHAIRI

Karume Shujaa

DKT. Ali Mohamed Shein. Maalim Seif Sharif Hamad.


Inatoka Uk. 6

Abeid Karume na Maalim


Seif Shariff Hamad,
wakishauriwa na wazee wa
CCM na CUF, wakatutoa
huko katika shimo la moto
kama walivyokuwa Aus
na Khazraj. Lakini mbona
tunataka kurejea tena
kule tulipotoka ambapo
tulikubaliana kutoka huko
kabisa kwa Kusameheana,
Kusahau yaliopita na
Kusonga mbele na kuunda
Serikali ya Umoja wa
Kitaifa? Tukazika tofauti
za kisiasa na kusahau yale
yaliotangulia. Inakuwaje
leo hali ya Zanzibar
inaendelezwa kubaki katika
khofu, woga na kiza kizito?
Ni wajibu wa viongozi
kuyasoma haya na
kuyafikiri huku wakijua
wana dhima kubwa mbele
ya Mwenyezi Mungu. Wana
dhamana kubwa mbele
ya jamii na wale watu
waliowapa dhamana ya
kuongoza. Ni jukumu lao,
wasilikimbie. Waikumbuke
siku ambayo wataitwa na
kuulizwa na Mola wao
juu ya uchunga wao. Kila
mmoja ni mchunga na
kila mchunga ataulizwa.
Waliyasimamia vipi haya
yasitokee? Wataulizwa
ilikuwaje wakaamua na
kutoa fursa kwa baadhi
ya watu kuyatenda
haya? Viongozi waliopo
madarakani wana wajibu
wa kuhakikisha usalama
wa nchi na watu wake.
Na njia ya kuleta usalama
sio kuruhusu au kuweka
mazingira yanayopelekea
wananchi kufanyiwa yale
waliyofanyiwa wanawake
wa Wete, Mkoani na
Micheweni.
Ningependa nisisitize
kuwa, muhimu hapa sio
kukumbushana machungu,
lakini kutanabahishana
kwamba kuna makosa
tukifanya, yanaleta balaa,
maafa na athari mbaya
kwa wananchi. Katika Aya
nilizozinukuu mwanzo,
Waislamu wanatakiwa
kurejea historia juu ya
hali mbaya ya uhasama
iliyokuwa baina ya Aus na
Khazraj. Lakini Uislamu
ukawaletea neema ya
udugu na upendo wa dhati
wakaepukana na balaa la

chuki, visasi na kuuwana.


Tunaposoma aya hizi
Wazanzibari, tukiwa katika
vyama vyetu vya siasa vya
CUF na CCM na tukiwa
katika visiwa vyetu vya
Unguja na Pemba, tujihisi
kama walivyokuwa Aus na
Khazraji. Allah (SWT) kwa
huruma yake na Rehma
zake akatuletea Serikali
ya Umoja wa Kitaifa kwa
kusimama kwa ubinadamu
wetu na Uzanzibari wetu.
Sasa hofu yangu ni kuwa,
tusipojali na kuenzi neema
hii, tunachotafuta ni balaa
kuliko niliyoigusia kwa
kifupi sana. Je, tunalitaka
hilo?
Tukisimama na
kutambua na kuheshimiana,
awali ya yote, kama
binadamu, pili kama
Waislamu na Wakristo na
tatu kama Wazanzibari
na Watanzania, hatuwezi
kuthubutu kufanyiana yale
aliyofanyiwa yule mama
wa Micheweni na kichanga
chake!
Rafiki yangu mmoja
alinambia Rais Mstaafu
wa Zanzibar Dk Amani
Karume siku moja alisema
ameingilia mlango mbaya
lakini amejua kutafuta
mlango mazuri wa kutokea.
Kwa maana alipoingia tu
madarakani, yakafanyika
mauaji hayo ya Januari
26/27, 2001. Lakini ameiaga
Ikulu kwa kuunda serikali
ya Umoja wa Kitaifa na
kumaliza chuki na uhasama
wa kisiasa.
Ni matarajio yangu, na
kwa hakika ya wengi kuwa,
maadhali Rais wa Zanzibar,
Dk Ali Mohammed Shein
ameingia Ikulu na mguu
wa kulia, kwa kukabidhiwa
nchi ikiwa salama,
atatuepusha na balaa
linalotunyemelea.
Hii ndiyo dua yetu,
na tunamuombea kwa
Mwenyezi Mungu ampe
ujasiri atuvushe salama,
yasije kutokea tena yale
yaliyowakuta akina mama
na mabinti wa Pemba
ambayo yakisimuliwa, hata
ukiwa na roho ngumu kama
jiwe au chuma, utajikuta
ukitokwa na machozi.

AN-NUUR

RABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JAN 29-FEB 4, 2016

Safari ni nzito!

Inatoka Uk. 7
kuwa sekretari wa Baraza
la Wawakilishi ambapo
aliitumikia mwaka 1983
hadi 1985.
Baadae akateuliwa
kuwa mjumbe wa Baraza
la Wawakilishi kuanzia
mwaka 1985 hadi mwaka
1990 wakati huo akiwa
Naibu Waziri wa Usafiri
na Mawasiliano mnamo
mwaka 1990 hadi mwaka
1995 na baadae kuwa
Naibu Waziri wa Habari,
Utamaduni, Utalii, Vijana
na Wanawake, mnamo
mwaka 1995 hadi mwaka
2000 alikuwa Waziri wa
Wanawake na Watoto
na Mjumbe wa Baraza
la Wawakilishi akitokea
kwenye jumuiya za
wanawake wa CCM
Zanzibar.
Mbali na nafasi hizo
za serikali, lakini Bi Asha
alikuwa mstari wa mbele
katika kukiendeleza Chama
ambapo mnamo mwaka
1964 alikuwa ni Mjumbe wa
Vijana wa Paunia kupitia
Chama Cha ASP na baadae
mwaka 1972 alijiunga na
Afro Shirazi Youth League
hadi hapo mwaka 1977
vyama vya TANU na ASP
vilipoungana na kuzaliwa
Chama Cha Mapinduzi
(CCM) yeye akawa
miongoni mwa wajumbe wa
mwanzo wa chama hicho.
Tokea hapo mwaka
1978 kwenye jumuiya ya
wanawake wa CCM kisha
kuwa mjumbe wa JUWATA
na baadae kuwa mjumbe
wa Wazazi wa chama hicho
cha CCM mwaka 1980 na
akaanza kukamata nyadhifa
nyengine mbali mbali ndani
ya chama ikiwemo Mjumbe
wa Kamati Kuu ya CCM na
1992 hadi 2010 Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya CCM
(NEC) mwaka 2007 hadi
anamaliza uhai wake yeye
ni Makamo Mwenyekiti
wa Umoja wa Wanawake
Tanzania (UWT).
Katika uhai wake Bi
Asha amaekabiliwa na
changamoto mbali mbali
lakini zaidi kwa wapinzani
wake wa Chama Cha
Wananchi (CUF) ambao
alikuwa ni mpinzani wao
mkubwa katika siasa. Bi
Asha ambaye maarufu
anajulikana kwa msimamo
wake wa maneno alitokuwa
akiyatoa mara kadhaa
kuhusiana na Maalim
Seif kushika dola yeye ni
miongoni mwa wahafidhina
wachache waliokuwa
wakipinga na kusema
kwamba Hii ni nchi ya
kimapinduzi na haitoki kwa
karatasi.
Matamshi yake hayo
yakimaanisha hata mkipiga
kura hamuwezi kushinda

Labda na nyie mfanye


Mapinduzi mpindue
kama tulivyopindua lakini
hatutoi..hatutoihatutoi.
Hizo ndo kauli zake ndani
ya Baraza la Wawakilishi na
hata katika Bunge Maalumu
la Katiba.
Mbali ya ujasiri wake huo
wa kusimamia uhafidhina,
lakini Bi Asha pia alikuwa
ni mtetezi mzuri wa maslahi
ya Zanzibar kwa muda
mrefu amekuwa akisimamia
na kutetea suala la Zanzibar
katika Muungano lakini
kilichokuwa kikimponza na
kuitwa msaliti ni kushikilia
uhafidhina na umapinduzi
tu.
Inawezekana wengi
wakamuona Bi Asha ni
mtu aliyekuwa anasimamia
dhana isiyokubalika na
wengi katika ulimwengu
huu wa sasa, lakini ni
miongoni mwa wanawake
wachache ambao
wameweza kusimama
imara na kutetea kile
wanachokiamini katika
maisha yao.
Bi Asha kwenye
Umapinduzi hajawahi
kukengeuka hata siku
moja. Ni miongoni mwa
wengine walioipigia debe
serikali ya umoja wa kitaifa
kwa wakati ule ingawa
kwa baadae akaungana
na wenzake na kutaka
kura ya maoni ya kuivunja
kutokana na dhana ile ya
uhafidhina na umapinduzi

kuwa mbele. Badhi ya


wakati alikuwa na uzalendo
na kuipenda nchi yake
na linapokuja suala la
kuitetea Zanzibar kwenye
Muungano yeye ilikuwa
kama anajifunga kibwebwe
na kuanza kucharura
khasa akipaza sauti yake
akisema na kutetea haki
za Zanzibar na wakati
mwengine aliungana na
back benchers kwa kuikosoa
serikali na kutaka kamati
teule ziundwe katika
kuwafichua wenye kufanya
ubadhirifu ndani ya serikali.
Ukiacha ya kwenye siasa
pia alikuwa ni mcheshi,
mtu mwenye kupenda watu
hodari na ni mzungumzaji
mzuri na daima akipenda
kutania muda wote.
Binafsi nimejuana naye
kwa muda mrefu akiniita
Mwanangu na kunitaka
nimwite Mama kutokana
na mahusiano na urafiki
wake na Baba yangu tokea
wakiwa wadogo ambapo
walicheza pamoja.
Kama ilivyo kwa
binaadamu wengine
hawakosi kuwa na makosa
na kasoro katika maisha
yake lakini tusahau
yale mabaya yake na
tumkumbuke kwa mema
yake. Ni binaadamu
kinachotakiwa sasa ni
kumuombea katika safari
yake hiyo nzito ya kurejea
kwa Mola wake akielekea
maisha ya Barzakh.

Tanzania Islamic Centre


Manispaa ya Kinondoni

P.O. Box 90042, +255 713 586 186 au 713 455 255
Dar es Salaam, Tanzania

NAFASI YA MAFUNZO YA USHONAJI


Chuo cha ushonaji Tanzania Islamic
Centre kinawatangazia wanawake wote
kuwa kinatoa mafunzo ya ushonaji
(tailoring) na kudarizi (Embroidering) kwa
ada nafuu sana.
Chuo kina maadili na mazingira
mazuri ya kujifunzia. Kipo Msikiti wa
Kichangani, Magomeni Mapipa.
Fomu zinapatikana hapa chuoni.
Wanawake wote mnakaribishwa katika
mafunzo.
Wasiliana kwa simu No 0713586186 na
0713 455 255
Wabillah Tawfiq

15
Inatoka Uk. 11
dola na kisha kufuatia
msururu wa kukamatwa
kwa kila aliyekuwa katika
mtandao huo. Hao ndio
tunasema kuwa wamenaswa
kwa ujinga kwa sababu,
kwanza wanayojadili
ukiyaweka katika mizani,
yanakwenda kinyume
kabisa na mafundisho
yenyewe ya Uislamu. Pili,
hayawezi kutatua matatizo
ya Waisamu yaliyopo na
tatu ni kuwa wanajadili
mambo ya hatari bila hata ya
kujua kuwa kwa utaalamu
uliopo, wanayoandika si
siri, kila wanachoandika
kinasomwa na wengine bila
wao kujua, wakiwepo polisi,
wanausalama wa ndani na
nje.
Ugaidi unavyowasaidia
mbeberu
Mfalme Leopold II na
wenzake, waliangamiza
takribani Waafrika milioni
10 wa Congo hivi sasa, watu
wakisakwa kama wanyama
wa porini ili wakafanye kazi
katika mashamba ya mpira
(rubber plantations) ya
mabeberu. Ndiyo yaliyojiri
pia Namibia ambapo
Wajerumani waliangamiza
kabila la Herero kwa
mauwaji ya halaiki (mass
killing) ambapo manusura
walitimuliwa katika majumba
yao na mashamba yao
wakakimbilia jangwani
kuwapisha Wazungu.
Mpaka leo mashamba yao
yanatumiwa na Wazungu.
Hawa walikuwa raia
wasio na hatia ambao kama
ni kosa, basi kosa lao lilikuwa
kutokuwa Wazungu, halafu
wakazaliwa katika ardhi safi
kwa kilimo na yenye madini.
Watu wa makabila ya
Herero na Namaqua,
Namibia, wakati huo
German South-West Africa,
walipinga ukoloni na ubeberu
wa Ujerumani katika nchi
yao. Kutokana na hilo
wakatangaziwa ugaidi na
uasi. Adhabu yao ikawa
kuteswa na kuuliwa kwa
kunyongwa, kupigwa risasi,
kufanywa panya wa majaribio
na kufukuzwa katika miji
na vijiji vyao, wengi wakafa
jangwani kwa kiu na njaa.
Zaidi ya kuwafanyisha
kazi kitumwa, huku
wakiwa wamewafunga
minyororo, serikali ya
Wazungu wa Ujerumani,
haikutosheka, lakini ikawa
inaleta wataalamu wake
wa vyuo vikuu na hospitali

Makala

AN-NUUR

RABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JAN 29-FEB 4, 2016

Joseph 'Jihad Jack' Sheikh Msellem Ali

WANANCHI wa kabila la Herero waliokimbia makazi yao.


wakitaka kufanya utafiti,
vinachukuliwa viungo vya
watu wa Namibia. Ripoti ya
Umoja wa Mataifa (United
Nations' Whitaker Report) ya
mwaka 1985, inataja mauwaji
ya watu wa makabila ya
Herero na Nama uliofanywa
na Ujerumani, kwamba
ndio mauwaji mabaya na
ya mwanzo ya Kimbari
katika karne ya 20. Hivi leo
serikali ya Namibia inajaribu
kuibana serikali ya Ujerumani
irudishiwe mafuvu ya watu
wake (Waafrika) waliokatwa
vichwa na Wazungu
vikapelekwa katika maabara
ya Chuo Kikuu cha Freiburg
na hospitali mbalimbali za
Berlin kufanyia majaribio ya
kisayansi!
Waliyofanya Wajerumani,
ndiyo hayo hayo waliyofanya
Uingereza, Ufaransa na
Marekani katika ubeberu
wao duniani. Leo mabeberu
hao hao wanatuundia
ISIS na akina Jihad John,
ili kufunika unyama wao
wanaoendelea kufanya
katika nchi mbalimbali.
(Tafuta: Exposing Lies of the
Empire.)

Katika zama zile Ujerumani


inaangamiza watu wa
Namibia, inawezekana
mji wa pili kutoka mahali
wanapouliwa watu, wasijue
kinachowapata wenzao. Leo
ukifanya jambo dogo tu,
dakika hiyo hiyo ulimwengu
utajua na kupiga kelele. Sasa
mabeberu hawawezi tena
kufanya unyama kama ule wa
Namibia bila ya kuzomewa.
Walichofanya ni kuunda
jinamizi la ugaidi. Ukitizama
historia, yaliyowakuta watu
makabila ya Herero na
Namaqua, Namibia (German
South-West Africa), ndiyo
yaliyowakuta wananchi wa
Fallujah, Iraq wakipinga
uvamizi na uporaji wa
Marekani. Lakini ulimwengu
haukuwalilia wananchi
wa Fallujah kwa sababu
mabeberu walikwishatangaza
kuwa wanapambana na
magaidi. Katika Fallujah
askari wa Marekani
walilipua na kuuwa mpaka
wagonjwa hospitalini na watu
waliokuwa misikitini kisha
wakazuiya chakula kuingia.
Lakini nani wa kuisema

Marekani wakati inapambana


na magaidi!!! Ugaidi kwa
hakika limekuwa blanketi zito
kabisa la kufunika mauwaji
na uporaji wa mabeberu wa
Kizungu ambao umekuwa
ukifanyika toka wakati
wa Mfalme Leopold II na
wenzake.
Hivi karibuni Kenya
ilitumbukia katika msiba
mzito. Idadi kubwa ya askari
wake walio Somalia waliuliwa
na wapiganaji wa Al Shabaab.
Akitoa salamu zake za rambi
rambi, Rais Uhuru Kenyatta
alisema kuwa jeshi la Kenya
litaendelea kuwepo Somalia
mpaka lengo lao la kwenda
kule litimie.
Mtu utajiuliza, kwa lengo
lipi Kenya ilikwenda Somalia
zaidi ya kutumikia lengo la
mabeberu? Kama ni uadui,
Wasomali/Al Shabaab
haikuwahi kuwa na uadui na
Kenya. Ilikuwa na uadui na
Marekani iliyopindua serikali
yao ya Umoja wa Mahakama
za Kiislamu na kuweka
vibaraka.
Kama katika miaka ya
1800s mpaka mwanzoni
mwa miaka ya 1990s wapo
baadhi yetu walitumiwa
na mabeberu wa Kizungu
kuhilikisha kabila la Herero
kule Namibia, wakatumiwa
kukata vichwa vya wenzetu
kuvipleka katika maabara
za Ujerumani, wakatumiwa
kuwauwa wazalendo
kama Patrice Lumumba,
leo tutakuwa na tofauti
gani iwapo tunatumiwa na
mabeberu wale wale wa
Kizungu kutesa watu wetu
na wengine kuwapeleka kufa
Somalia kutumikia agenda ya
Mmarekani?

WAJERUMANI waliwafunga minyororo kabila la Herero nchini Namibia kipindi cha ukoloni.

16

Safu ya Ben Rijal

AN-NUUR

RABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JAN 29-FEB 4, 2016

Sheikh Said Abdalla Lindy Mmakonde-12

naye Sheikh Said bin Abdalla Lindy


alifaidika na kusoma kwa gwiji
huyo.
Sheikh Said alitokea kuwa
na hima ya kusoma na hakuwa
mwenye kupoteza wakati wake
zaidi ya kusoma na mlezi wake
alipokabidhiwa, hakumfanya
mtoto wa kumlea awe kazi yake
kutumika na kumtuma, bali alitokea
kumpenda zaidi hata ya wanawe
na kwa hio hakuwa anampa kazi
yoyote ile, iwe ya kuteka maji,
kuchanja kuni au kazi zozote zile
za nyumbani zaidi ya kumtaka
kumuona kuwa ameelimika vya
kutosha.
Sheikh Said Abdalla Lindy
Mmakonde aliichukua fursa hiyo
vilivyo kwani alichukua ahadi
alivyotoka nyumbani kuwa
atasoma mwisho wa kipawa chake
ahakikishe kuwa atalipata lengo
alilolikusudia. Alikuwa akifwatana
na mlezi wake katika kudarasisha.
Sheikh Said Abdalla Lindy
Mmakonde alikuwa na fani ya
kuzungumza na kusomesha na
akipenda kupita njia za mkato
na kufanya ufupisho na hayo
yakiwavutia vijana wenye
kunyanyukia kupenda kuhudhuria

darsa zake. Alikuwa akisomesha


Msikiti uliopo Vuga wa Maalim
Murad ambapo vijana wa mji ndio
maeneo waliokuwa wakiishi.
Sheikh Said Abdalla Lindy
Mmakonde katika mwaka wa
1372 AH (1953) aliomba ruksa ya
kurudi Tanganyika nako huko ni
kwao akasomeshe. Wajue wale
ambao hawakumuona kama kweli
alielimika. Hapo akawataka ruksa
waliompokea kuwa wakati wa
kurudi nyumbani umefika na Mtu
ni kwao na walimpa ruksa hiyo
kwa kuelewa lisilo budi hutendwa.
Ni wakati wake umefika kurudi
nyumbani.
Wengine husema Mtu ni kwao
ugeni sio kitu chema, lakini Sheikh
Said Abdalla Lindy Mmakonde
hakuyatamka hayo, ila alihisi ni
vyema kurudi Tanganyika kwenda
kuifanya kazi inayohitajika. Kwa
hiyo katika mwaka huo wa 1372
AH (1953) alihamia Tabora na
kupokewa na wenyeji wa hapo na
kufanya kazi kubwa iliyostahiki
kwa kusomesha watu wa rika
mbalimbali.
Alipokuwa anadarasisha
Tabora, wale ambao wakisema
Kiarabu kama asili ya lugha
yao, walikuja kufahamu kuwa
wanahitajia kwenda kusoma kwake,
chembelecho maneno ya vijana,
kwani Sheikhe alikuwa akikisema
Kiarabu kimbele kinyuma,
ikimaanisha akikizungumza
kwa njia za kisomi sio cha mtu
aliozaliwa na lugha yake.
Kuhamia kwake Tabora
kulimchukua miaka 4 kabla ya
kufariki. Alifariki tarehe 19 Mfungo
Tisa 1376 AH (January 1957) na
kuwacha pengo kwani hapo Tabora
wenyeji walifaidika naye vya
kutosha. Tunamuomba Mola atupe
juhudi kama alizokuwa nazo Sheikh
Said Abdalla Lindy Mmakonde,
Ameen.

MHE. Bernad Membe.

Dk. Salim Ahmed Salim.

KATIKA safu yetu hii ya Masheikhe waliopita, wasomaji


wamekuwa na kiu kutaka kujuwa juu ya Masheikhe waliopita
wa Tanganyika, kwani watakuwa wa Tanganyika kwa wakati
ambao ninawazungumza Masheikhe waliopita huko nyuma.
Bahati mbaya kwa upande wa Tanganyika hakuna juhudi
zilizofanyika kuwafanyia utafiti Msheikhe waliopita hata
nilipowasiliana na Sheikhe wangu wa Tanga tarehe za Mwa
hapo Tanga, alionambia kuwa hakuna maandishi ya kutosha
ya Masheikhe hata wa karibuni kina Hemed bin Juma. Makala
hii itamgusia kwa ufupi Sheikh Said Abdalla Lindy Mmakonde
aliotokea Lindi kusoma Unguja na kumalizikia na kusomesha
KAMA nilivyowahi kueleza huko
nyuma kuwa Zanzibar ilikuwa ni
kituo muhimu cha kueneza dini ya
Kiislamu na wanafunzi waliokuwa
wanaenda kusoma visiwani
Zanzibar wakitoka katika maeneo
ya Afrika ya Mashariki na wengine
wakitokea katika maeneo ya Afrika
ya Kati na Kusini mwa Afrika
na walimu wao wengi walikuwa
wenyeji ambao walielimika vya
kutosha. Aidha, katika nyakati
mbalimbali walitokea walimu
kutoka Yemen, Misri, na Saudi
Arabia.
Baadhi ya wasomi wa visiwani
waliona kiu chao bado hakijakatika
kwa maji walioyapata visiwani,
kwa hio wakafunga safari kwenda
Misri na Saudi Arabia kusoma kisha
wakarudi kusomesha visiwani.
Jina litakustaajabisha, lakini
hivyo Sheikhe ndivyo alivyokuwa
akijinasibisha kwa jina lake. Sheikhe
huyu alijinasibisha kuwa ni mkazi
wa kutoka Lindi, asili ya kabila
lake ni Mmakonde na ndivyo
alivyokuwa akijulikana.
Sheikh Said Abdalla Lindy
Mmakonde alizaliwa katika mwaka
wa 1307 AH (1890) akasoma kwao
Lindi kwa Masheikhe wa huko
kisha akapelekwa visiwani Zanzibar

katika mji mkuu wake Unguja kwa


Sheikh Issa bin Ahmad Msunjini.
Hapa utaona kapelekwa kwa
mtu mwenye asili ya visiwa vya
Comoro.
Lindi na Msumbiji sio mbali na
Wamakonde wengi wanatokea
Msumbiji na watu wa visiwa vya
Comoro katika nyakati tafauti
kutokana na misukosuko ya maisha
ya kuingia ukame na mabalaa
mengine ya kimaumbile, walihama
visiwa hivyo na kuhamia Msumbiji,
Durban Afrika ya Kusini na visiwa
vya Zanzibar. Watu wa maeneo
ya Lindi, Mtawara, visiwa vya
Comoro na Zanzibar walikuwa na
maingiliano makubwa.
Sheikh Said Abdalla Lindy
Mmakonde alipelekwa kwa Sheikh
Issa bin Ahmad Msunjini ambaye
Sheikhe huyu ndio alioujenga
Msikiti ujulikanao Msikiti Mabati
uliopo katika mtaa wa Kisiwandui
katika mwaka wa 1326 (1908).
Sheikh Issa alimlea Sheikh Said
Abdalla Lindy Mmakonde na
kumsomesha na kumpeleka kwa
kila mwalimu ambaye atafaidika.
Kwa hiyo ilivyokuwa yeye Sheikh
Issa akisoma kwa gwiji wa elimu wa
siku hizo Sheikh Abdalla Bakathir

Zanzibar isipuuze ushauri wa wakongwe


Dk. Salim, Membe, Butiku, wana funzo
Tuache ubinafsi kwa maslahi ya wengi

WAZIRI Mkuu mstaafu, Dk.


Salim Ahmed Salim, ameungana
na Mkurugenzi wa Taasisi ya
Mwalimu Nyerere Joseph Butiku
na Bernad Membe, kueleza
kushangazwa kwake na uamuzi
wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar
(ZEC), kufuta uchaguzi visiwani
humo.
Dkt. Salim amesema, hata
Jumuiya za kimatifa nazo
zilishtushwa na uamuzi huo.
Mwanadiplomasia huyo wa
kimataifa ametoa kauli hiyo, baada
ya Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim
Jecha, kutangaza kufuta matokeo
ya uchaguzi huo Oktoba 28, mwaka
jana, ambapo siku chache zilizopita,
Jecha ametangaza kuwa uchaguzi
huo utarudiwa Machi 20 mwaka
huu.
Dk. Salim amesema, kutokana na
hali hiyo, kinachotakiwa hivi sasa ni

haki itendeke kwa kila kila upande


kwa kukaa pamoja na kutafuta
suluhisho la kudumu kwani
Tanzania haijazoea migogoro ya
siasa ambayo si jambo jema katika
sura ya kimataifa.
Dk. Salim alitoa kauli yake wakati
alipozungumza na MTANZANIA
nyumbani kwake, Msasani, jijini
Dar es Salaam hivi karibuni.
Dk. Salim ambaye ana sifa ya
kuwa msuluhishi wa kimataifa na
ambaye amewahi kuwa Katibu wa
uliokuwa Umoja wa Nchi Huru za
Afrika OAU, (sasa AU), alisema
kitendo cha kufutwa uchaguzi wa
Zanzibar ni jambo lililowashangaza
wengi kwa kuwa uchaguzi
ulifanyika kwa amani na utulivu,
huku waangalizi wa ndani na nje
wakiwa wametoa ripoti za kuusifia.
Alisema, kufutwa na sasa tarehe
Inaendelea Uk. 17

17

MAKALA/TANGAZ0

AN-NUUR

RABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JAN 29-FEB 4, 2016

Zanzibar isipuuze ushauri wa wakongwe

Inatoka Uk. 16
ya kurejewa ikiwa imeshatangazwa,
kumeibua sintofahamu kubwa
katika nchi kwa sababu uchaguzi
uliopita Tanzania ilipata sifa, kwa
uchaguzi kufanyika kwa amani na
utulivu. Lakini sasa bado suala hili
halieleweki.
Hata hivyo Dk. Salim, alisema
hadhani suala la kufutwa uchaguzi
lilikuwa ni la mtu mmoja, kwamba
hadhani ni la Jecha peke yake na
kusema huo sio mustakabali mzuri
visiwani humo.
Alisema, Zanzibar ni nchi ndogo
lakini ina historia kubwa kisiasa,
hivyo juhudi za pamoja zinahitajika
kufanyika kutatua mgogoro uliopo
kwa maslahi ya Watanzania kwa
ujumla.
Aliwataka Viongozi katika suala
la Zanzibar haki itendeke na waache
ushabiki wa vyama na kwamba,
wote waweke ushabiki pembeni
na watatue mgogoro huo kwa
mustakabali wa Wazanzibari na
Watanzania kwa ujumla.
Alishauri pande zote ziendelee
kukutana hadi suluhu ya pamoja
ipatikane, japo viongozi kadhaa
wameshakutana na kufanya
mazungumzo bila kupata suluhu.
Dk. Salim alitoa tahadhari
kwamba nchi ipo katika hali
mbaya na Watanzania hatujazoea
na kwamba, suala la Zanzibar
likiendelea linaweza kuzaa matatizo
makubwa katika Taifa.
Akizungumzia kuhusu vitendo
vya ubaguzi yakiwamo mabango
yaliyokuwa yameandikwa ujumbe
wa kibaguzi kwa maandishi
makubwa katika sherehe za miaka
52 ya Mapinduzi ya Zanzibar,
zilizoadhimishwa Januari 12, Dk.
Salim alisema ameshangazwa na
hali hiyo.
Alisema kitendo cha baadhi ya
wanachama wa CCM kubeba bango
hilo hadharani kimeitia doa na ni
aibu kwa Zanzibar na Tanzania
wakati inafahamika kuwa suala la
ubaguzi lilimalizika tangu mwaka
1964.
Aliongeza kuwa, kitendo kile ni
jambo la kufedhehesha na halistahili
kupewa nafasi hata kidogo.
Alisema wakianza kubagua,
watakaoathirika wengi ni watoto wa
viongozi na kwamba, ubaguzi huo
ni ujinga na unaudhi.
Alisema kitendo cha wana-CCM
kubeba bango hilo kinaonyesha
wazi kuwa wameishiwa hoja kwa
sababu suala la Hizbu lilikufa tangu
mwaka 1964.
Hata hivyo, Dk. Salim alihoji
kuwa iweje wanachama wabebe
mabango yanayochochea ubaguzi
katika sherehe za Mapinduzi na
waliachwaje kufanya hivyo, hali
ya kuwa viongozi walikuwapo na
waliona.
Alisema, kama kuna mtu yeyote
anaona hilo ni sawa, basi huyo ni
sawa na kusema kafilisika kabisa.
Itakumbukwa kuwa mwaka 2005
katika harakati za kuwania nafasi
ya Urais ndani ya CCM kuelekea
Uchaguzi Mkuu, Dk. Salim alidaiwa
waziwazi na baadhi ya wana kambi
wa CCM kuwa hakustahili kuwania
kiti hicho kwa kuwa yeye alikuwa
ni mwanachama wa Hizbu, chama

kilichokuwa kinaongoza serikali ya


Zanzibar kabla ya Mapinduzi na
kwamba ana asili ya Uarabu.
Kauli hizo za kibaguzi
zilimuumiza sana Dk. Salim,
ambaye wakati huo alikuwa
akikubalika.
Mapema kabisa baada ya
kufutwa uchaguzi wa Zanzibar,
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi
ya Mwalimu Nyerere, Mzee Joseph
Butiku, aliitaka Tume ya Uchaguzi
ya Zanzibar (ZEC) kufanya kazi
kwa kuzingatia katiba na sheria za
nchi na kuacha kutanguliza mbele
maslahi binafsi ya kisiasa.
Akizungumza na vyombo
vya habari, Mzee Butiku,
alisema amekerwa na tabia ya
Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar
kusitisha uchaguzi na kushindwa
kuwatangazia wananchi kiongozi
wao waliomchagua, huku
ikishindwa pia kuheshimu matakwa
ya wananchi waliopiga kura katika
visiwa vya Zanzibar.
Mzee Butiku bila kumungunya
maneno, aliitaka Tume ya Uchaguzi
ya Zanzibar kufanya kazi kwa
weledi na kuheshimu maamuzi ya
wananchi, badala ya kutanguliza
mbele maslahi binafsi ya kisiasa,
jambo ambalo inaweza kusababisha
machafuko na umwagaji wa damu
visiwani humo.
Pia aliwataka wananchi wa
Zanzibar kutokubali kurudia
tena upigaji wa kura, hadi
hapo yatakapotolewa maelezo
ya kuridhisha na wahusika
waliosababisha uchaguzi huo
kufutwa na watakaobainika
kuharibu waweze kuchukuliwa
hatua kali za kisheria.
Aidha Mzee Butiku aliwataka
viongozi kuheshimu sheria na
katiba ya nchi na kwamba, chama
ambacho kinadhani kimeshindwa
katika uchaguzi huo kikubali
matokeo badala ya kuifanya
Zanzibar ni mali ya chama fulani.
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Bernard Membe, kadhalika
alinukuliwa na vyombo vya habari
akitoa maelezo ya kupinga uamuzi
wa kufutwa kwa matokeo yote
ya uchaguzi visiwani Zanzibar,
akisema dunia inashangaa, na
akaitaka CCM na Serikali isiwaachie
watu wawili tu, kutafuta njia za
kutatua mgogoro huo.
Membe alionyesha waziwazi
kutoridhishwa na uamuzi wa kufuta
uchaguzi huo wa Rais wa Zanzibar,
Wawakilishi na Madiwani.
Alisema, kinachoishangaza
dunia si kuahirisha uchaguzi, bali
ni kufuta matokeo ya majimbo yote
badala ya yale yaliyobainika kuwa
na matatizo.
Katika hatua za kujaribu kutatua
mgogoro huo, inasemekana
kuwa Rais wa Zanzibar Dk Ali
Mohamed Shein na Maalim Seif
tayari wameshakaa vikao tisa Ikulu
Zanzibar, pamoja na marais wa
zamani wa visiwa hivyo, Mzee
Ali Hassan Mwinyi, Dk. Salmin
Amour na Dk. Amani Karume
lakini bila kupatikana mafanikio,
wala maelezo ya kina juu ya
mazungumzo hayo.
Aidha, Rais John Magufuli naye
ameshakutana na pande hizo
mbili kwa nyakati tofauti, ambapo
Maalim Seif alimtaka kuwa kinara
wa kusuluhisha mzozo uliopo,
lakini tangu wakati huo haonekani

kutilia mkazo.
Tayari Katibu huyo Mkuu wa
CUF ameshatangaza kujitoa kwenye
mazungumzo hayo.
Membe alifafanua zaidi
kwamba, kilichotokea Zanzibar
kimeihuzunisha dunia na kwamba,
kilichoishitua dunia ni kule kufuta
matokeo kwa ujumla wake.
Kwamba imeshangaza katika
majimbo yote, hakuna hata moja
lililofanya vizuri na hapo ndipo
wengi wanapopata wasiwasi.
Aidha alisema haridhishwi
na jinsi mgogoro huo wa kisiasa
unavyotafutiwa ufumbuzi kutokana
na kuwahusisha zaidi Dk. Shein na
Maalim Seif.
Alisema kama kuna mwanasiasa
wanaodhani tatizo la Zanzibar
litamalizwa na sehemu moja ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
wanafanya makosa makubwa kwani
umoja uliopo Bara na Zanzibar ni
umoja wa kusaidiana wakati wa
raha na matatizo.
Kwamba tatizo ambalo linaweza
kuhatarisha usalama Zanzibar,

linaweza kusababisha matatizo


katika Muungano hivyo wahusika
wasikae kimya na kuangalia
kitakachotokea.
Wakati ZEC imetangaza Machi 20
kuwa tarehe ya kurudia uchaguzi,
CUF imesema haitashiriki uchaguzi
huo.
Wakati matokeo ya uchaguzi
yakiwa yametangazwa katika
majimbo 32 na baadhi ya wagombea
kukabidhiwa vyeti vya ushindi
na matokeo kubandikwa vituoni
huku matokeo hayo yakiendelea
kutangazwa kwenye kituo kikuu
cha kutangazia matokeo katika
Hoteli ya Bwawani, ghafla zoezi hilo
likasitishwa Mwenyekiti wa Tume
ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha
Salum Jecha, pale alipojitokeza
kwenye kituo cha televisheni cha
Taifa na kutangaza kufutwa kabisa
uchaguzi Oktoba 28 mwaka jana.
Hatua hiyo ilipingwa vikali
na CUF, vyama mbalimbali vya
wanasheria na kushangaza Jumuia
za kimataifa na waangalizi wa
uchaguzi wa ndani na nje ya nchi.

Ahlu Daawa Hajj and Travel Agency


Inawatanganzia Waislam wote kuwa imeandaa safari ya Hijja mwaka 2016
sawa na mwaka 1437 Hijria kwa Dola US$ 3,555
Kutakuwa na punguzo la asilimia 16% kuanzia muda huu mpaka Feb
29/2016. Itakuwa Dola $2986 tu.
Kuanzia mwezi Machi 01-2016 mpaka Juni 12-2016 kutakuwa na punguzo
la asilimia 6% sawa na Dola $3,341 tu.
MAMBO YATAKAYOGHARAMIWA
1. Semina za Hija, 2. Huduma za afya na kuchinja 3.Airport Charge na
ticket za Ndege 4.Nyumba Makkah na Madina 5.Irham na Kuchinja
kwa ajili ya Tama-tuu 6.Chakula wakati wote 7.Usafiri na ziara
Makkah na Madina 8.Mahema Mina na Arafa.
UMRA MWEZI WA RAMADHANI ITAKUWA NI DOLA US $1995
Fomu zinapatikana sehemu zifuatazo:1.Ofisi ya Ahlul Daawa Dar es Salaam Mtaa wa Dosi na Mkadini
nyumba Namba 26 mkabala na Showroom ya magari Tell. 0713
730 444, 0773 804 101 ,0785 930 444 au 0773 930 444.
2. Ofisi ya Ahlu Daawa Zanzibar Rahaleo Tel: 0777 484 982, 0777
413 987.
3. Abubakr Maulana wa Markaz Kiwalani Dar es Salaam, Tel:
0784 453 838
4. Abdallah Salehe Mazrui (Hoko) Dar es Salaam, Tel: 0715 724
444
5. Abdallah Hafidh Mazrui, Wete Pemba Tel: 0777 482 665
6. Mohammed Hafidh Mazrui Mkoani Pemba 0777 456 911
7. Sheikh Daud Khamis Shekha Tel: 0777 679 692
8. Maalim Seif Humoud Hamed (Kijichi Zanzibar) 0777 417 736
WAHI KULIPIA
1. Ofisi ya Ahlul Daawa Dar es salaam Tel: 0713 730444, 0773
804101,0785 930444.
2. Ofisi ya Ahlul Daawa Zanzibar Rahaleo Tel: 0777 484982,
0777 413 987.
Maalim Seif Humoud Hamed (Kijichi Zanzibar) Tel: 0777 417 736
TANBIH
(a) Atakaemaliza
taratibu
zote
mwanzo
ndie
atakayeshughulikiwa mwanzo
(b) Ili uwemo katika fungu la kwanza unatakiwa umalize
taratibu zote kabla ya punguzo
(c) Kumbuka kikundi cha Ahlul Daawa kwa bei nafuu kuliko
wote na huduma kuliko wengi.
Wabillah Tawfiq

18

MAKALA

AN-NUUR

RABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JAN 29-FEB 4, 2016

Kwanini mabeberu wanachangamkia sana Burundi?

Inatoka Uk. 8
kupeleka wanajeshi 5,000
huko Burundi ulichukuliwa
mnamo Disemba 2015 na
Baraza la Amani na Usalama
la AU. Nkurunziza alipewa
muda wa kukubaliana na
uamuzi huu, lakini akaupinga
na kusema majeshi yake
yatapambana na kikosi cha
uvamizi cha AU.
Aghlabu tunapoongelea
majeshi ya UN au ya AU,
kisichotajwa ni kuwa majeshi
hayo huwa yanafadhiliwa
na mataifa makubwa kama
Marekani. Bendera ni ya UN
au AU na askari ni Waafrika,
lakini Marekani na Ulaya
wanatoa kila kitu kuanzia
silaha hadi sare na posho.
Wakati AU imechachamaa
kupeleka majeshi ya kulinda
amani ili kuzuia mauaji
nchini Burundi, wachunguzi
wanahoji iweje AU hiyo hiyo
ilikaa kimya wakati majeshi
ya Ufaransa yalipoishambulia
Ivory Coast mwaka 2010.
Halafu kuna uvamizi wa
Libya (2011), Mali (2012) na
CAR (2013) uliofanywa na
majeshi ya kigeni. Je yalikuwa
wapi hayo majeshi ya AU ya

RAIS Piere Nkurunzinza


kulinda amani?
Tanzania ilikuwa nchi
ya kwanza katika jumuiya
ya EAC kuunga mkono
upelekwaji wa majeshi
ya kulinda amani nchini
Burundi (Maprobu). Ingawa
Nkurunzinza amesema hii
itakuwa ni sawa na uvamizi
wa nchi yake na majeshi

TBC ni kuingilia uhuru wa habari

Inatoka Uk. 20

zaidi.
Hata hivyo wakazi
wengi wa jiji la Dar es
Salaam wamesikitishwa na
kutofurahishwa na hatua hiyo
tofauti na alivyodai Nape, kwani
walisema kitendo cha serikali
kuingilia chombo cha habari
na kuweka maamuzi yake ni
kuingilia uhuru wa vyombo vya
habari kwa mujibu wa sheria
na vile vile kuzuia uhuru wa
wananchi kupata habari.
Kurwa mkazi wa Mbagala
alisema kutorushwa mijada ya
Bunge moja kwa moja, kunatoa
fursa kwa watendaji wa TBC
kuhariri sehemu kubwa ya
mijadala hiyo, hasa sehemu
ambazo haiifurahishi serikali
na kuruhusu ile ambayo kwao
wanaona inawafaa, jambo
ambalo ni sawa na kuwakatili
wananchi.
Maide Omar, mkazi wa
Manzese yeye alikwenda mbali
zaidi na kuhoji kama TBC ni
mali ya viongozi, ni mali ya
serikali au mali ni ya umma wa
Watanzania?.
Alihoji inakuwaje televisheni
ya Taifa iwe na wasaa mrefu wa
kurusha moja kwa moja hewani
harusi ya mtu kwa maslahi ya
familia Fulani, lakini ikose muda

wa kurushwa moja kwa moja


vikao vya Bunge, jambo ambalo
lina maslahi kwa umma.
Hemed Diwani mkazi wa
Kimara, alisema kuwa kwa
jinsi TBC inavyendesha vipindi
vyake, haifahamiki kama ni
mali ya walipa kodi Watanzania
na kama inaendeshwa kwa
ruzuku inayotokana na kodi za
wananchi wote.
Kwa jinsi inavyoendeshwa na
aina ya vipindi inavyovirusha,
imekuwa kama ni mali ya
watendaji wa serikali na chama
tawala, wao wanaonekana kama
vile ndio wahariri na waamuzi
wa kipi kitangazwe na kipi
kisitangazwe.
Alisema kwa jinsi inavyofanya
kazi, haionekani kama watendaji
wake wana uhuru wa kufanya
maamuzi yao kwa kuzingatia
uhuru wa weledi wa kitaaluma
kwa mujibu wa sheria za habari
na utangazaji.
Alitolea mfano wa kauli
aliyoitoa Nape, na serikali
kuwa, wao wanaonekana kuwa
mamlaka na uwezo wa kuamua
ni kipi kirushwe hewani na
kipi kiachwe, bila kujali kuwa
waathirika ni wananchi na
walipa kodi wanaowafanya TBC
wawepo hewani.

Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini

ya kigeni, Waziri Mahiga


amesema lengo litakuwa ni
kuwalinda raia na wala si
kupambana na jeshi la nchi
au na serikali yake. Suala hili
lilizungumzwa na Mahiga
alipokutana na mwenyekiti
wa AU, Bi Nkosazana
Dlamini-Zuma mjini Durban
na mjini Addis Ababa. Baadae
likatolewa tamko rasmi
likimuomba Nkurunzinza
kushirikiana na Maprobu.
Mpaka sasa haieleweki ni
nchi zipi zitatoa majeshi
yake kuchangia hii Maprobu.
Burundi yenyewe imetuma
majeshi yake kulinda amani
huko Somalia na DR Congo.
Sasa nayo inatakiwa ilindwe
amani yake.
Ni vizuri tukajiuliza,
kwanini mataifa makubwa
yanachangamkia sana
utumiaji wa majeshi ya
usalama nchini Burundi?
Suali hili linagusiwa
na Charles Kambanda,
mwanasheria kutoka Rwanda
anayeishi Marekani. Aliwahi
kuwa profesa katika Chuo
Kikuu cha Rwanda. Hivi
karibuni akihojiwa na Idhaa
ya Redio KPFA alisema
mgogoro wa Burundi ni
wa kisiasa na kiini chake
ni maliasili ya nchi hiyo
inayogombaniwa na mataifa
makuu ulimwenguni.
Kambanda amesema,
nchi za kibeberu zimenuia
kuudhoofisha utawala
wa Burundi ili iweze
kuudhibiti. Kwa njia hii nchi
hizi zitakuwa na nafasi ya
kunyonya utajiri na maliasili
za Burundi.
Anasema kinachofanyika
nchini Burundi si tofauti
na DRC, kwa vile kuna
makampuni ya kimataifa
yanayogombania maliasili

katika maeneo haya. Mbinu


wanazotumia ni kutengeneza
mazingira ili kurahisisha
uporaji wa maliasili
unaofanywa na makampuni
ya kimataifa kupitia madalali
wao wa kienyeji. Hii ndio hali
ilivyo katika maeneo ya DRC
Mashariki ambayo inapakana
na Burundi. Na Burundi
nayo inazalisha asilimia sita
ya madini ya nikeli (nickel)
duniani. Tayari makampuni
ya kigeni yamewarubuni
baadhi ya viongozi wa
upinzani ambao ndio
watakaokuwa madalali.
Kambanda anasema
hii ndio sababu ya
kimsingi inayozifanya
nchi za Marekani na Ulaya
kuhimiza na kuwezesha
kile wanachokiita kikosi
cha kulinda amani huko
Burundi. Wamefaulu kuuza
wazo hilo kwa AU ingawa
EAC na SADC haziko tayari
kuunga mkono. Badala
yake zinataka yafanyike
mazungumzo ili kufikia
maridhiano.
Naye mwandishi Gearid
Colmin anasema Marekani
na wenzake wa Ulaya wana
mkakati wa kuidhibiti
Burundi kwa kumuondoa
Nkurunziza na kuuweka
utawala utakaolinda maslahi
yao. Hivi ndivyo ubeberu
umekuwa ukifanya katika
nchi nyingi za Afrika, Asia,
Amerika Kusini na Mashariki
ya Kati. Anasema mkakati
huu umekuwa ukiendeshwa
kupitia vyombo vya habari
tangu 2005. Lengo lao ni
kuchora upya mipaka ya
nchi za Maziwa Makuu
kama wanavyofanya katika
nchi za Kiarabu. Katika nchi
hizo mataifa ya kibeberu
yalichora upya mipaka ya
nchi na kuwatawaza wafalme
vibaraka chini ya kile
kinachoitwa makubaliano ya
Simon-Picot. Hii ilifanyika
baada ya Vita Kuu ya Kwanza
na ingali inaendelea hadi leo.
Si ajabu, kwani hivi
karibuni ilitangazwa kuwa
mjumbe wa serikali ya
Marekani anayeshughulikia
Kanda ya Maziwa Makuu
anatembelea Burundi.
Kisha atafika Dar es Salaam,
Rwanda, DRC na Addis
Ababa. Akiwa mjini Addis
atahudhuria mkutano wa
kilele wa AU pamoja na
wajumbe wenzake kutoka
Marekani. Wanachokitafuta ni
nini?
(0713-562181 nizar11941@
gmail.com)

19

MAKALA

AN-NUUR

RABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JAN 29-FEB 4, 2016

Afande Kova nyuma ya Pazia la Ugaidi


Inatoka Uk. 20

wa Ugaidi bandia nchini jambo


lililopelekea kukabiliana na mateso
kutokana na uzito wa tuhuma,
pasi ya kupelekwa Mahakamani.
Ama kwa wale waliopelekwa
Mahakamani kesi zao zimekuwa
zikipigwa danadana kwa maelezo
kuwa upelelezi hauja kamilika
huku wakiendelea kusota rumande
kutokana na dhamana zao
kuzuiliwa.
Wapo walio kamatwa kwa
tuhuma hizo wakaishia kuteswa
kisha wakaachiwa wakiwa
wameathirika na wengine
wakifariki muda mfupi baada
ya kutoka rumande na wengine
kupoteza wazazi wao kwa mstuko.
Amesema Uts. Awadhi.
Naye Ustadhi Abuu, alisema ipo
haja ya kumwandikia Afande Kova,
barua ya kumkaribisha uraiani
na kumkumbusha kuwa cheo ni
dhamana, na kwamba kila wakati
mtu anatakiwa kuwa mwangalifu
ili kupitia mikono yake na mamlaka
yake asije kudhuru watu wasio na
hatia.
Tumkumbushe matukio yote ya
kuwabambikia kesi Waislamu na
alivyoyashadidia, lakini kwaTawfiq
ya Allah (s.w) Waislamu tunashinda
kesi na tuhuma hizo hizo bandia
kila kukicha kwa kukosa ushahidi
na kuamua kuzifuta au kuwaachia
baada ya kuwatesa, bila kujua hiyo
ni dhulma na ana dhima kubwa
kwa Mwenyezi Mungu. Alisema
Ust. Abuu.
Alisema, ni vyema Waislamu
wakifanya mchakato wa
kumuandikia kitabu maalum ili
vizazi vijavyo vimfahamu huku
akipendekeza kuwa kitabu hicho
kiitwe, Afande Kova dhidi ya

Waislamu nyuma ya Pazia la


Ugaidi.
Alisema, pamoja na kufahamu
kuwa Waislamu wanakamatwa
na kudhaniwa kuwa ni magaidi,
lakini wengi hawafahamu madhila
yanayowapata na yanayoendelea
kuwapata katika vituo vya Polisi,
na zoezi hili lote lilikithiri chini ya
ukamanda wa Afande Kova.
Kwa upande wake Sheikh Ally
Yaqub amesema wakati Kamanda
mstaafu Kova, akisema yapo
mambo ambayo hatayasahau
katika utumishi wake aelewe pia
kuwa wapo Waislamu ambao
hawatomsahau. Sasa inagekuwa
nyema ikawa wanamkumbuka kwa
Kheri.
Naye Ustadhi Hussein
Mchomolo, aliye mkazi wa Masasi,
ambaye ni muhanga aliyewahi
kukamatwa, kuhojiwa kisha
kuteswa, anasema yeye ni katika
ambao jina la Kova litabaki katika
kumbukumbu katika maisha yake
yote. Alisema, awali baada ya
kukamatwa akiwa kwao Masasi
na kufikishwa Makao Makuu ya
Jeshi la Polisi (Central Police) Jijini
Dar es Salaam, bila kufahamu kosa
lake akiwa na wenzake alihusiswa
na tukio la ujambazi lililotokea
Ikwiriri.
Ust. Mchomolo, alisema awali
wakiwa hapo Polisi, ilitolewa amri
kwa watuhumiwa hao wa ujambazi
kutoka Mkoani Mtwara, kuwa
wasipatiwe chakula kinachotoka
kwa ndugu zao.
Wakiwa humo mahabusu,
alisema ulifika ugeni wa maafisa wa
Jeshi la Polisi akiwemo IGP, Ernest
Mangu, walilazimika kuukabili
ugeni huo na kulazimisha kuongea
nao.
Mmeelezwa kuwa sisi ni watu

wa Ikwiriri, wakati mnafahamu


kuwa tumetoka Mtwara, hivyo tuna
matatizo tunataka tuwafikishieni na
mtupatie majibu.
Hapo ndipo Afande Kova,
akaniuliza mnataka majibu sasa
hivi au hata kesho? Nikamjibu
kuwa yale yatakayo wezekana
kujibuwa sasa mtatujibu na yale
yatakayo hitaji hadi mkae shura
mtajua ni wakati gani mtatujibu.?
Alisema Ust. Mchomolo,
akirejea maongezi yake baada ya
kulazimisha kusikilizwa na IGP,
mbele ya mwenyeji wake Afande
Kova.
Alisema, hatua hiyo ilitoa fursa
kwao kuruhusiwa kuongea na
Afande Kova, ambapo alimchukua
hadi katika ofisi ya RCO na kufanya
mahojiano naye kwa ufasaha.
Baada ya maongezi yetu
alimwita Mkuu wa Kituo hicho
na kumpa oda kuwa sasa chakula
kinacholetwa na ndugu zetu
kipokelewe na katika faili letu
libadilishwe tuhuma, badala ya
kuandikwa kuwawauwaji wa
Ikwiriri sasa liandikwe kuwa
ni watuhumi wa Ugaidi toka
Mtwara. Alisema Ust. Mchomolo,
na kuongeza kuwa huyo ndiye
Afande Kova na tuhuma zinazo
wakabilia Waislamu, wakati wa
uongozi wake, akidai kwamba
alikuwa anaamua tu ni tuhuma ya
aina gani apewe Muislamu.
Kufuatia hali hiyo, Ust.
Mchomolo, alisema hiyo inatoa
fundisho kuwa Waislamu wanao
kamatwa na wengine kufikishwa
Mahakamani kwa tuhuma za ugaidi
ama uvamizi wa vituo vya Polisi,
si kweli kuwa wamefanya makosa
hayo.
Mfano hai ni huo, kama
ilivyokuwa kwetu, tumekamatwa

kwa tuhuma ya tukio la Ikwiriri,


ulipokosekana ushahidi,
tukazushiwa ya ugaidi, ina maana
yeye ndiye alikuwa anaamua
huyu au hawa wapewe tuhuma
gani, sisi tulishangaa sana kwa
hatua aliyoifanya Afande Kova,
fikiria kwanza tulipewa tuhuma
za mauaji ya Polisi wa kituo cha
Polisi Ikwiriri, lakini akaja akaamua
tupewe tuhuma za Ugaidi, huyo
ndiye Afande Kova, hakika
hatuwezi kumsahau. Alieleza.
Kwa upande wake Maalim Yasin
Khamis, alisema Afande Kova,
ni binadamu na huu ni wakati
muafaka wa kuelezwa wazi mabaya
yake huenda ikamsaidia katika
kipindi hiki ambacho yupo nje ya
madaraka akatanabahi na kumrejea
Muumba wake.
Alisema, pamoja na kuwa yapo
matukio mengi, lakini anakumbuka
kadhia ya uwanja wa Waislamu
Changombe, kuwa hatolisahau
kutokana na kipigo kilichowakuta
wanawake wa Kiislamu kutoka kwa
Polisi, bila huruma wakiwa ndani
ya Msikiti wa Markazi Changombe.
Uzuri wa bahati ni kwamba
AfandeKova, yupo hai ni wakati
muafaka kuelezwa madhila aliyo
wasababishia Waislamu, angekuwa
amefariki ingekuwa si sahihi
kuyaeleza mabaya yake, lakini sasa
aelezwe huenda akatanabahi na
Mwenyezi Mungu ni mwingi wa
kusamehe.
Alisema Maalim Khamisi na
kumalizia kwa kumkaribisha
Afande Mstaafu Suleiman Kova
katika maisha ya uraiani, waungane
katika swala za jamaa Misikitini.

Inatoka Uk. 20

zinazopasa na kwa kuwajibika."


Hata hivyo, hakuna taarifa
inayoashiria kuwepo na
msingi wa kuwa na wasiwasi
imetolewa.
Akiwa amepata mshtuko
mkubwa, mtoto huyo hathubutu
tena kuandika tangu mkasa huo
utokee, kwa mujibu wa familia
hiyo.
Binamu yake aliema katika
mahojiano na Shirika la
Utangazaji la Uingereza (BBC)
kuwa 'kama mwalimu angekuwa
na wasiwasi wa kufuatilia, ni
kuhusu uwezo wa kuandika" wa
mtoto huyo.
Tangu mwezi Julai mwaka
jana, walimu nchini Uingereza
wamepewa maelekeo ya kuarifu
taasisi husika chochote ambacho
kinaashiria siasa kali, kama
inavyoainishwa katika sheria ya
kupambana na ugaidi.
Matukio kadhaa ya aina
hiyo yamefikishwa Baraza
Kuu la Waislamu Uingereza
ambalo limetoa taarifa kueleza
"wasiwasi mkubwa" kuhusu
matukio ya aina hiyo.
(Imetafsiriwa kutoka lugha
ya Kifaransa na Anil Kija)

Hofu ya ugaidi inapopunguza uwezo wa kutumia akili Uingereza


familia hiyo.
Kila kitu kilianzia katika
zoezi la lugha darasani,
mnamo Desemba 7 2015 katika
shule moja ya msingi eneo la
Lancashire, Kaskazini Mashariki
ya Uingereza. Mvulana hiyo
aliandika "naishi katika nyumba
ya kigaidi" (I live in a terrorist
house) badala ya "naishi katika
nyumba yenye ngazi" (I live
in a terraced house). Bila
kuhangaika kuzungumza na
mtoto huyo, uongozi wa shule
hiyo haraka ukaitahadharisha
polisi ambao waliingilia, asubuhi
iliyofuata wakafika kwake
kumhoji, ilisikika Paris Jumatano
Januari 21.
Katika taarifa kwa
vyombo vya habari, polisi na
Halmashauri ya wilaya hiyo
wanakiri kuwa ilikuwa ni
"kosa kudhania kuwa mzozo
huo unatokana na kosa tu la
kuandika neno moja."
Taarifa hiyo inasema "shule
hiyo na polisi walichukua hatua

AN-NUUR

20

MAKALA

20

Soma gazeti la
AN-NUUR
KWA TSH 800/=
kila Ijumaa

AN-NUUR

RABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JAN 29-FEB 4, 2016

RABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JANUARI 29 - FEBRUARI 4, 2016

Afande Kova nyuma ya pazia la ugaidi


Wakati wewe hutosahau Sitakishari,
Waislamu nao hawatakusahau pia
Karibu uraiani, karibu Masjid mtaani

Na BakariMwakangwale
WAKATI Kamanda
Suleiman Kova akitangaza
kustaafu utumishi
katika Jeshi la Polisi,
ametajwa kuingia katika
kumbukumbu mbaya
dhidi ya umma wa
Kiislamu nchini wakati
wa utumishi wake.
Imeelezwa kuwa, hiyo
ni kutokana na miaka ya
hivi karibuni Waislamu
kuwa wahanga wa tuhuma
za ugaidi. Afande Kova
amestaafu baada ya
kufikia ukomo wa umri
wa utumishi wa umma
Serikalini, akiwa katika
nafasi ya Kamanda wa
Kanda Maalum Jijini Dar
es Salaam tangu mwezi
Juni 2008.
Kabla ya hapo amekuwa
katika nyadhifa mbalimbali
katika Jeshi la Polisi nchini.

Akitangaza kustaafu
kwake, mapema hivi
karibuni katika viwanja
vya Chuo Cha Maafisa wa
Polisi Kurasini, Jijini Dar
es Salaam, na kutambulisha
Kamanda Simon Siro,
kukaimu nafasi yake,
aliyataja baadhi ya matukio
kuwa kwake yatabaki kuwa
ni kumbukumbu kichwani
mwake. Kufuatia kauli hiyo
ikawasukuma Waislamu
nao kutoa maoni yao juu
ya utumishi wake hususan
kwa umma wa Kiislamu,
kwamba ameondoka huku
akiacha maumivu makali
katika familia za Kiislamu
na hawezi kusahaulika
kutokana na madhila aliyo
wasababishia.
Ustadhi Said Awadhi,
alisema chini ya Kamanda
Kova, baadhi ya Waislamu
wamekuwa ni wahanga

Inaendelea Uk. 19

Kamanda mstaafu Suleiman Kova.

Hofu ya ugaidi inapopunguza


uwezo wa kutumia akili Uingereza
Na Mwandishi Maalum,
SaphirNews, Paris

KWA kukosea kuandika


neno moja kisarufi,
mwanafuzi wa umri wa

miaka 10 ameshuhudia
polisi wakitinga
nyumbani kwake
kumhoji na kuangalia
kompyuta inayotumiwa

na familia hiyo ili


kufuatilia walichodai ni
mahusiano na vikundi
vya kigaidi katika

Inaendelea Uk. 19

Kuondoa matangazo ya Bunge:

TBC ni kuingilia uhuru wa habari


Na Shaban Rajab

SERIKALI imeondoa
sehemu ya vipindi vya
matangazo ya moja
kwa moja ya vikao vya
Bunge vilivyokuwa
vikirushwa na
Televisheniya Taifa
TBC kutoka Dodoma.
Uamuzi huo wa
serikali umetangazwa
na Waziri wa Habari,
Utamaduni na Michezo
Nape Nnauye katika
kikao cha pili cha
mkutano wa 11 wa
Bunge la Jamhuri
ya Muungano mjini
Dodoma Jumatano wiki

hii.
Kufuatia kauli hiyo
ya serikali, TBC sasa
itakuwa ikirusha baadhi
tu ya matangazo ya
moja kwa moja ya
vikao na mijadala ya
Bunge, huku sehemu
nyingine ya mijadala
hiyo ikirekodiwa na
kurushwa hewani
katika kipindi maalum,
ambacho Nape alikitaja
kuwa kinaitwa Leo
katika Bunge.
Baadhi ya wananchi
wameonyesha
kuridhishwa na
utaratibu huo na
wameipongeza serikali.

Lengo la kuondoa baadhi


ya vipindi vya moja
kwa moja bungeni ni
kupunguza gharama za
uendeshaji kwa shirika.
Alisema Nape.
Wakati Nape akitoa
kauli hiyo ya serikali,
wabunge wengi, hasa
wale wa vyama vya
upinzani walikerwa na
kupinga hatua hiyo na
kudai hakutajadiliwa
chochote bungeni hapo
kabla ya kuwekwa sawa
suala hilo la kuzuiwa
TBC kurusha matangazo
ya moja kwa moja ya
Bunge.
Hata hivyo Spika Job

Ndugai, alisema pamoja


na kuonekana wabunge
hao kutoridhishwa na
hatua hiyo, kwa mujibu
wa kanuni hawana
uwezo wa kuzuia kauli
iliyotolewa na serikali.
Bw. Nape alisifu
hatua hiyo ya serikali
na kusema kuwa
kwa kurekodiwa na
kutayarishwa matangazo
ya vipindi vya mijadala
ya Bunge na kurushwa
majira ya saa nne usiku,
kutatoa fursa kwa watu
wengi kupata fursa ya
kulitizama Bunge kwa
kuwa muda mwingi
wa mchana ambao TBC

ilikuwa ikirusha moja


kwa moja matangazo
ya vikao hivyo, watu
wanakua maofisini na
katika shughuli zao za
uzalishaji hivyo kukosa
kuona kinachoendelea
Bungeni.
Watanzania sasa
watapata fursa zaidi,
hasa wale ambao muda
wa kurushwa moja
kwa moja vipindi vya
mijadala ya Bunge
katika muda wa kawaida
wanakuwa maofisini
kazini au katika shughuli
nyingine. Alieleza Nape
Bungeni na kuzua tafrani
Inaendelea Uk. 18

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Ltd, Dar es Salaam.

Вам также может понравиться

  • Annuur 1208
    Annuur 1208
    Документ20 страниц
    Annuur 1208
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1219
    Annuur 1219
    Документ20 страниц
    Annuur 1219
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1228d
    ANNUUR 1228d
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1228d
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1153 PDF
    Annuur 1153 PDF
    Документ16 страниц
    Annuur 1153 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1115
    Annuur 1115
    Документ16 страниц
    Annuur 1115
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Gazeti La Annur
    Gazeti La Annur
    Документ12 страниц
    Gazeti La Annur
    Hassan Mussa Khamis
    Оценок пока нет
  • Annuur 1231 PDF
    Annuur 1231 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1231 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1181 PDF
    Annuur 1181 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1181 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1183 PDF
    Annuur 1183 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1183 PDF
    annurtanzania
    100% (2)
  • Annur:Toleo La Ijumaa Tarehe 13-01-2012
    Annur:Toleo La Ijumaa Tarehe 13-01-2012
    Документ16 страниц
    Annur:Toleo La Ijumaa Tarehe 13-01-2012
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1169a PDF
    ANNUUR 1169a PDF
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1169a PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
    Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
    Документ2 страницы
    Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
    Hassan Mussa Khamis
    Оценок пока нет
  • Annuur 1082
    Annuur 1082
    Документ16 страниц
    Annuur 1082
    MZALENDO.NET
    100% (1)
  • Annuur 1049
    Annuur 1049
    Документ12 страниц
    Annuur 1049
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1209aaa
    ANNUUR 1209aaa
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1209aaa
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1077
    Annuur 1077
    Документ12 страниц
    Annuur 1077
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1216d
    ANNUUR 1216d
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1216d
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Mabaraza Ya Usuluhishi
    Mabaraza Ya Usuluhishi
    Документ20 страниц
    Mabaraza Ya Usuluhishi
    Chris John
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1175b PDF
    ANNUUR 1175b PDF
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1175b PDF
    annurtanzania
    Оценок пока нет
  • Annuur 1262
    Annuur 1262
    Документ20 страниц
    Annuur 1262
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1204
    Annuur 1204
    Документ20 страниц
    Annuur 1204
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1179 PDF
    Annuur 1179 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1179 PDF
    annurtanzania
    100% (1)
  • Annuur 1218 PDF
    Annuur 1218 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1218 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1122
    Annuur 1122
    Документ16 страниц
    Annuur 1122
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annur Toleo La Ijumaa
    Annur Toleo La Ijumaa
    Документ16 страниц
    Annur Toleo La Ijumaa
    annurtanzania
    Оценок пока нет
  • Annuur 1144
    Annuur 1144
    Документ16 страниц
    Annuur 1144
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1064
    Annuur 1064
    Документ12 страниц
    Annuur 1064
    annurtanzania
    Оценок пока нет
  • Annuur 1173 PDF
    Annuur 1173 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1173 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1213 PDF
    Annuur 1213 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1213 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1062
    Annuur 1062
    Документ16 страниц
    Annuur 1062
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • D Hamana
    D Hamana
    Документ36 страниц
    D Hamana
    Iddy Uwesu
    Оценок пока нет
  • Annuur 1143
    Annuur 1143
    Документ16 страниц
    Annuur 1143
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1056 PDF
    Annuur 1056 PDF
    Документ16 страниц
    Annuur 1056 PDF
    annurtanzania
    Оценок пока нет
  • An Nuur 1128
    An Nuur 1128
    Документ16 страниц
    An Nuur 1128
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • ANNUUR1004
    ANNUUR1004
    Документ16 страниц
    ANNUUR1004
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • Annuur 114
    Annuur 114
    Документ12 страниц
    Annuur 114
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • Annuur 1217
    Annuur 1217
    Документ20 страниц
    Annuur 1217
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1028
    Annuur 1028
    Документ16 страниц
    Annuur 1028
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • Annuur 1230 PDF
    Annuur 1230 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1230 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1176b PDF
    ANNUUR 1176b PDF
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1176b PDF
    annurtanzania
    Оценок пока нет
  • Dini ya Fedha
    Dini ya Fedha
    От Everand
    Dini ya Fedha
    Оценок пока нет
  • Annuur 1055 PDF
    Annuur 1055 PDF
    Документ16 страниц
    Annuur 1055 PDF
    annurtanzania
    Оценок пока нет
  • Annuur 1264
    Annuur 1264
    Документ20 страниц
    Annuur 1264
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1232 PDF
    Annuur 1232 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1232 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1112
    Annuur 1112
    Документ16 страниц
    Annuur 1112
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Hotuba Ya January Makamba
    Hotuba Ya January Makamba
    Документ27 страниц
    Hotuba Ya January Makamba
    Audra Love
    Оценок пока нет
  • Annuur 1172 PDF
    Annuur 1172 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1172 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1151
    Annuur 1151
    Документ16 страниц
    Annuur 1151
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Bwana Okoa Ndoa Yangu
    Bwana Okoa Ndoa Yangu
    От Everand
    Bwana Okoa Ndoa Yangu
    Оценок пока нет
  • Fiqhi ya ‘Ibada yenye picha zilizochorwa
    Fiqhi ya ‘Ibada yenye picha zilizochorwa
    От Everand
    Fiqhi ya ‘Ibada yenye picha zilizochorwa
    Оценок пока нет
  • Mfalme - Nilipumzika: Mashairi Ya Kisasa - Modern Swahili Poetry
    Mfalme - Nilipumzika: Mashairi Ya Kisasa - Modern Swahili Poetry
    От Everand
    Mfalme - Nilipumzika: Mashairi Ya Kisasa - Modern Swahili Poetry
    Оценок пока нет
  • HAYAAN, The Long Journey of the Nomad Boy
    HAYAAN, The Long Journey of the Nomad Boy
    От Everand
    HAYAAN, The Long Journey of the Nomad Boy
    Рейтинг: 5 из 5 звезд
    5/5 (2)
  • Mwongozo wa Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyinginge
    Mwongozo wa Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyinginge
    От Everand
    Mwongozo wa Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyinginge
    Рейтинг: 4.5 из 5 звезд
    4.5/5 (3)
  • Afisa Usalama Wa Taifa Ni Mtu Wa Aina Gani? Na Anafanya Nini?
    Afisa Usalama Wa Taifa Ni Mtu Wa Aina Gani? Na Anafanya Nini?
    От Everand
    Afisa Usalama Wa Taifa Ni Mtu Wa Aina Gani? Na Anafanya Nini?
    Рейтинг: 4 из 5 звезд
    4/5 (24)
  • Kufikirika
    Kufikirika
    От Everand
    Kufikirika
    Оценок пока нет
  • Hofu
    Hofu
    От Everand
    Hofu
    Рейтинг: 5 из 5 звезд
    5/5 (1)
  • Tutarudi na Roho Zetu?
    Tutarudi na Roho Zetu?
    От Everand
    Tutarudi na Roho Zetu?
    Рейтинг: 5 из 5 звезд
    5/5 (3)
  • Tishio la Ukombozi: Ubeberu na Mapinduzi Zanzibar
    Tishio la Ukombozi: Ubeberu na Mapinduzi Zanzibar
    От Everand
    Tishio la Ukombozi: Ubeberu na Mapinduzi Zanzibar
    Оценок пока нет
  • Nyuma Ya Pazia
    Nyuma Ya Pazia
    От Everand
    Nyuma Ya Pazia
    Оценок пока нет
  • Hawara
    Hawara
    От Everand
    Hawara
    Оценок пока нет
  • Annuur 1262
    Annuur 1262
    Документ20 страниц
    Annuur 1262
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1231 PDF
    Annuur 1231 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1231 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1264
    Annuur 1264
    Документ20 страниц
    Annuur 1264
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1229 PDF
    Annuur 1229 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1229 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1232 PDF
    Annuur 1232 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1232 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1227 PDF
    Annuur 1227 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1227 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1225
    Annuur 1225
    Документ20 страниц
    Annuur 1225
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1226 PDF
    Annuur 1226 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1226 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1230 PDF
    Annuur 1230 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1230 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1223
    Annuur 1223
    Документ20 страниц
    Annuur 1223
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1207...
    Annuur 1207...
    Документ20 страниц
    Annuur 1207...
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1216d
    ANNUUR 1216d
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1216d
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1220
    Annuur 1220
    Документ20 страниц
    Annuur 1220
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1224
    Annuur 1224
    Документ20 страниц
    Annuur 1224
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1217
    Annuur 1217
    Документ20 страниц
    Annuur 1217
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1218 PDF
    Annuur 1218 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1218 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1213 PDF
    Annuur 1213 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1213 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1210a
    Annuur 1210a
    Документ20 страниц
    Annuur 1210a
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1209aaa
    ANNUUR 1209aaa
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1209aaa
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1195
    Annuur 1195
    Документ20 страниц
    Annuur 1195
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1204
    Annuur 1204
    Документ20 страниц
    Annuur 1204
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1201
    Annuur 1201
    Документ20 страниц
    Annuur 1201
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1202
    Annuur 1202
    Документ20 страниц
    Annuur 1202
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1200
    Annuur 1200
    Документ20 страниц
    Annuur 1200
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет