Вы находитесь на странице: 1из 20

Majipu Mahakamani,

Polisi
yanacheleweshwa

www.annuurpapers.co.tz au facebook:annuurpapers@yahoo.com

Sauti ya Waislamu

ISSN 0856 - 3861 Na. 1218 JAMADUL AWWAL 1437, IJUMAA , FEB. 26-MACHI 3, 2016 BEI TShs 800/=, Kshs 50/=

Soma Uk.4

Bora kufa kuliko mateso haya


Wagoma kula, kwenda Mahakamani
Ni Waislamu watuhumiwa wa ugaidi

Gogu wa
Magogu!
Tatizo Makahaba wa habari
Kosa la Sheikh Msellem nini?

RAIS John Magufuli

SHEIKH Ali Msellem.

SHEIKH Farid Hadd

USTADH Salum

MWANASHERIA Mkuu wa serikali, George Mcheche Masaju


(kushoto). Mkurugenzi wa mashtaka Bw. Biswalo Eutropius Mganga

Juhudi za Polisi kumkamata


Askofu Mpemba zimeishia wapi?

Mafundisho ya Qur'an/Uwanja wa Maarifa

An nisaa: 118

Fethullah-Gulen

SHETANI ambaye
amemlaani yeye
Mwenyezi Mungu
alisema: kwa
hakika nitafanya
katika waja wako,
fungu maalumu.
[An-Nisaa 118]
Maneno haya
yaliyotuka ambayo
aliyazungumza
shetani pamoja na
Mwenyezi Mungu
mtukufu, na
ambayo yamekuja
katika aya hii na
katika aya nyingine
nyingi. Ama ni
kwamba Mwenyezi
Mungu mtukufu
aliyasikia na

akamruhusu, kwa
kusema maneno
haya. Na ama ni
kwamba kufuatana
na maelezo ya
wafasiri wengi,
haya ni maneno
yaliyopita katika
fikra na mawazo
yake na yale
yaliyohukumiliwa
na maumbile
yake, na kwamba
Mwenyezi Mungu
mtukufu ametueleza
maneno hayo.
Ni sawa sawa
haya yalikuwa ni
maelezo ya ulimi
wa hali ya shetani,
au ni ghadhabu
ya maumbile yake
kwani yeye anaweka
wazi azma yake ya
kuwatesa waja wa
Mwenyezi Mungu
ambao hawakufikia
kwenye ngazi ya
Ikhlasi. Na kwa
hakika mchezo wa
shetani wa kwanza
ambao ulipita
pamoja naye juu
ya mgongo wa
ardhi hii, mchezo

huo unaendelea
leo. Kutoka
upande wake na
kutoka upande
wa wafuasi wake
wao wanaendelea
katika mbinu za
kuwafitini watu na
kuwahadaa kwa
matumaini ya batili
na kufanya mbinu
za kumsukuma
binadamu ili
kubadilisha
maumbile yake
na maumbile ya
viumbe wengine na
kuharibu uwiano.
Waliomfuata, kwa
hakika wamo
katika hasara
iliyowazi na ni
katika watu wenye
bahati mbaya.
Ama wale ambao
wamewezeshwa
kukaa mbali na
shetani na njia yake,
hao ndiyo wenye
bahati nzuri na hao
ni kwa ajili ya kukaa
kwao karibu na
Mwenyezi Mungu
mtukufu.

BAADHI ya Masheikh na watoa mada katika Semina kwa


Maimamu na viongozi wa Dini iliyofanyika katika ukumbi
wa CCM jijini Arusha hivi karibuni. Semina hiyo ilikuwa
ikiwataka viongozi wa dini kutotoa fat`wa pasipo na elimu ya
jambo husika na kuwataka viongozi hao wa Dini kusoma ili
wanapotoa daawa wawe fasaha.

AN-NUUR

JAMADUL AWWAL 1437, IJUMAA FEB 26-MACHI 3, 2016

JAWABU CHEMSHA BONGO NAMBA: 39


D

11

365

128

357

65

30

354

29 na 31

20 na 30

25

10 na 30

43

45

31

55

50

30

80

1965

29 na 30

33

1969

1437

42

MASUALA
1.Kabla ya mwezi wa Ramadhani, huwa ni mwezi gani? Shaaban
2.Huu ni mwaka gani wa Kiislamu? 1437
3.Mwezi wa Kiislamu una siku ngapi? 29 na 30
4.Idadi ya siku katika mwaka wa Kiislamu ni siku ngapi? 354
5.Kuna siku ngapi pungufu baina ya mwezi wa Kiislamu na mwezi wa
Kizungu?11
6.Msikiti wa mwanzo nchini Marekani ulijengwa katika mji gani? Detroit
TMI
7.Mwaka wa 1964 alisilimu bingwa wa masumbwi Mohammed Ali ilikuwa
mwezi gani? Aidha mwaka huo huo alisilimu mwana harakati wa kudai
haki za watu Weusi Marekani, ilikuwa mwezi gani? Februari na April
8.Malcolm X aliuwawa mwaka gani? 1965
9.Yarrow Mamount baada ya kuachiwa huru kuwa mtumwa alifika kuwa
ni mbia (Sahareholder) wa Bank ya Colombia, Jee unajua aliishi miaka
mingapi? 128
10. Quran ndio imemfanya mtu Mweusi kujivua katika minyororo ya
utumwa na kujihisi huru, hakuna dini yoyote ile iliowatetea watu huru
kuondokana na ubeberu wa watu wa Ulaya na Marekani . Maneno haya
yalisemwa katika mwaka wa 1889 na Edward Blyden.

CHEMSHA BONGO: 40

Weka duara kwenye jawabu ilio sawa. Jawabu kamili wiki ijayo.
J

22

23

24

25

23

629AD

628 AD

630AD

MASUALA
1.Asiokula, kunywa, kulala ni nani?
2.Unapokwenda Chafya unatakiwa useme kalima gani?
3.Jina jengine la Mfalme wa Abysynia (thiopia) ambae aliwapokea Waislamu
akiitwa nani?
4.Sahaba gani alisoma ujumbe wa Mtume (SAW) mbele ya Mfalme Najash?
5.Khutba ya mwisho alioitoa Mtume (SAW) ikiwa ni wasia mkubwa kwa
Waislamu ilikuwa tarehe ngapi katika mfungo tatu?
6.Mkataba wa Hudaybiyah Mtume Mohammed (SAW) aliwekeana mwaka
gani na Makafiri?
7.Utume wa Mtume Mohammed (SAW) umedumu kwa miaka mingapi?
8.Mtoto yupi wa kike wa Mtume Muhamad (SAW) alikuwa ndio mkubwa
wao?
9.Mtoto yupi wa kike wa Mtume Mohammed (SAW) aliye wa mwanzo
kufariki?
10.Nani alikuwa Mhandisi wa Firauni?

Jee Unajua?

1.Phd ni shahada ya tatu aipatayo mtu kutoka Chuo Kikuuu na huitwa Doctor
anapoipata, kuna wengine huwa na Shahada zaidi ya 3, kwa kujikusanyia
Shahada kutoka vyuo vikuu mbalimbali. Anayeongoza duniani kuwa na
Shada nyingi kutoka vyuo vikuu vilivyokuwa ni vingi ni mzee wa miaka 72
Michael Nicholson wa Kalamazoo huko Marekani akiwa na Shahada kwa
ujumla 29 kuelekea 30 : http://abcnews.go.com/US/michigan-man-29-collegedegrees-stopping/story?id=16597200
2.Rais wa Zimbabwe ndio Rais mwenye Shahada nyingi za vyuo vikuu
Barani-Afrika akiwa na Shahada 7. Shahada zake mbili alizipata akiwa jela na
moja ya Master aliipata akiwa kishakuwa Rais wa Zimbabwe : http://www.
universityworldnews.com/article.php?story=20101029224442993
3.Aliyekuwa kiongozi mkuu wa kampuni ya Armament ya Afrika ya Kusini,
Shamim chippy Shaik alipokonywa Shahada yake ya Phd kutoka Chuo
Kikuu cha Natal ambacho kwasasa kinajulikana kwa jina la KwaZulu Natal
mwaka wa 2008 baada ya kugundulika kuwa katika risala yake zaidi ya
asilimia 75 alidokoa maandishi yake : http://www.usnews.com/education/
best-global-universities/articles/2012/05/02/10-high-profile-people-whosedegrees-were-revoked
4.Ikiwa muamko wa kusoma Vyuo Vikuu unaongezeka Barani Afrika na
kuwa na wafanyakazi wengi waliopitia vyuo vikuu, kinyume chake nchi
ya Uiengereza ina watu kwa idadi ya wastani wasiopita vyuo vikuu wala
kutegemewa kufana hivyo : http://www.theguardian.com/higher-educationnetwork/blog/2013/jun/04/higher-education-participation-data-analysis
5.Inakisiwa kuwa duniani kuna watu wenye Sahahada ya vyuo vikuuu
wafikao asilimia 6.7 tu : http://www.huffingtonpost.com/2010/05/19/percentof-world-with-col_n_581807.html
6.Vyuo vikuu vilio bora duniani vimewekwa na ubora wake Chuo Kikongwe
Tanzania, Chuo cha Dar es Salaam (University of Dar es Salaam) kimewekwa
daraja ya +701 : http://www.huffingtonpost.com/2010/05/19/percent-of-worldwith-col_n_581807.html
7.Chuo Kikuu cha Massachusetts Institute of Technology ndio Chuo Kikuu
namba mmoja duniani : http://www.topuniversities.com/university-rankings/
world-university-rankings/2013#sorting=rank+region=+country=+faculty=+s
tars=false+search=
8.Vijue vyuo Vikuu 10 vinavyoongoza duniani, Chuo cha Stamford
kinashikilia nafasi ya 3, Havard namba 2, Oxford namba 6 n.k.: http://www.
topuniversities.com/student-info/videos/top-10-universities-world-201516
9.Kuna vyuo vikuu visiopungua 23,729 duniani: http://www.webometrics.
info/en/node/54
10.Donald Trump ni mgombea wa Rais wa kupitia chama cha Republican
nchini Marekani aliozusha tafrani za Waislamu wasiruhusiwe kuingia nchi ya
Marekani, katika mmoja ya hotuba zake amesema kuwa wale waliokwenda
Skuli na Rais Obama hawajapata kumuona : http://www.politifact.com/
truth-o-meter/statements/2011/feb/14/donald-trump/donald-trump-sayspeople-who-went-school-obama-nev/

Habari

AN-NUUR

JAMADUL AWWAL 1437, IJUMAA FEB 26-MACHI 3, 2016

Bora kufa kuliko mateso haya


Na Bakari Mwakangwale

WAISLAMU wenye tuhuma


za Ugaidi Mjini Morogoro,
wameingia katika mgomo wa
kula wakidai ni bora wafe
kuliko kuendelea na mateso
wakiwa hawajahukumiwa.
Watuhumia hao Jumanne
wiki hii, wakiwa Mahakamani
Mjini Morogoro, wameieleza
Mahakama nia yao ya kugoma
kula kuanzia siku hiyo.
Wanasema, wamechoshwa
na mwenendo wa kesi
uliotawaliwa na danadana
upande wa mashitaka ukidai
kuwa upelelezi haujakamilika,
kila wanapofika Mahakamani
hapo.
Akiongea na An nuur, kwa
njia ya simu kutoka Mjini
Morogoro, muda mfupi
baada ya tukio hilo, Ustadh
Juma Kitunga, alisema
Waislamu hao wamekusudia
kuingia katika mgomo,
wakitaka Serikali ikamilishe
upelelezi wake na kesi ianze
kusikilizwa.
Wale Waislamu
wanaotuhumiwa kwa Ugaidi,
leo (Jumanne wiki hii)
wameiambia Mahakama ya
Morogoro Mjini, kwamba
wanaingia katika mgomo wa
kula kutokana na ile hali ya
kila siku kesi kuahirishwa.
Amesema Ust. Kitunga.
Alisema, Waislamu hao
wamepaza sauti hiyo baada
ya Hakimu anayesikiliza
kesi hiyo kuiambia
Mahakama kuwa kesi
imeahirishwa mpaka Machi
8, 2016, kutokana na upelelezi
kutokamilika, ambapo
mmoja wa watuhumiwa hao
alinyoosha mkono, akiashiria
ana jambo la kuieleza
Mahakama.
Ust. Kitunga, alieleza
kwamba, baada ya kupewa
nafasi, mtuhumiwa huyo
alisema:
Mheshimiwa Hakimu,
kutokana na kesi kutosikilizwa
kwa muda mrefu sasa, kila
siku danadana, tunapenda
kuiarifu Mahakama yako
kuwa kuanzia leo (Jumanne
wiki hii) sisi watuhumiwa
wote 29 wa Ugaidi, tunaanza
mgomo wa kula kama shauri
letu halijapatiwa ufumbuzi,
tupo tayari kufa njaa kuliko
kuendelea kuwa katika
dhulma hii. Alisema Ust.
Kitunga, akinukuu maelezo ya
mtuhumiwa huyo.

Baada ya kauli hiyo,


Hakimu alibaki kaduwaa
pale Mahakamani pengine
hakutarajia Waislamu hao
kutoa kauli na msimamo huo
na hakuwa na la kufanya zaidi
ya kuonekana akiandika kitu
katika faili lake.
Imeelezwa kuwa Waislamu
hao wapo mahabusu kwa
muda wa miezi kumi sasa
na hakuna dalili zozote za
kuanza kusikilizwa kwa kesi
yao zaidi ya kupigwa kalenda
kwa muda wote huo.
Watuhumiwa hao 29,

wamegawanywa katika
makundi mawili tofauti
moja linatuhumiwa kwamba
lilikutwa Msikitini, wakidaiwa
kukutwa na milipuko na
kundi la pili ni lile lilohusu
kamatakamata ya Polisi,
akiwemo mwanafunzi Juma
Ismail (13), aliyekamatwa
akiwa Msikitini Kilombero.
Ust. Kitunga, alisema
katika hati zao za mashitaka
zinaonyesha kuainishiwa vitu
walivyo kutwa navyo ikiwa ni
milipuko, sare za Jeshi pamoja
na kuhusishwa na mauaji.

Hata hivyo, kila


wakipelekwa Mahakamani,
upande wa mashitaka
(Serikali) wanadai uchunguzi
haujakamilika.
Awali, imeripotiwa kuwa,
mahabusu hao walianza
kugoma kutoka wakiwa
gerezani kwa ajili ya kwenda
Mahakamani na baada
ya juhudi za Polisi, ndipo
walipotoka, hali iliyopelekea
kuingia Mahakamani majira
ya saa nne, badala ya saa
mbili asubuhi kwa muda wa
kawaida.

Juhudi za Polisi kumkamata


Askofu Mpemba zimeishia wapi?
utawala wa sheria, haki,
uadilifu na weledi wa
BAADA ya kushinda kesi
utendaji kazi wa Jeshi la
ya uchochezi dhidi ya
Polisi, wangeueleza umma
Serikali, Imamu Hamza
kama bado wanamtafuta
Omari, amehoji juhudi
na kama walimkamata kesi
za Jeshi la Polisi Jijini
yake ilifunguliwa katika
Mwanza, kumkamata
Mahakama gani na kesi
Askofu Mpemba, zimeishi yake iliishaje.
wapi.
An nuur, ilipotaka
Imam Hamza ameuliza
kujua kwa nini anahoji
swali hilo akiongea na
hayo, Imam Hamza,
mwandishi wa habari hizi,
alisema katika kadhia hiyo
akitoa shukran zake kwa
Kamanda wa Polisi wa Jijini
Waislamu kupitia gazeti la
Mwanza, wakati huo, Ernest
An nuur, waliokuwa nae
Mangu (Kwa sasa ni IGP)
pamoja katika kadhia hiyo
alitoa oda kupitia vyombo
tokea alipokamatwa mwaka vya habari ya kuwatafuta
2012, mpaka kwisha baada
watu watatu.
ya Mahakama ya Wilaya
Kwa kinywa chake
ya Nyamagana, Mwanza,
Kamanda Mangu, kupitia
kumwachia huru, wiki
vyombo vya habari
iliyopita kwa maelezo kuwa zikiwemo Televisheni,
hana hatia.
alionekana akiutangazia
Imam Hamza alisema
umma nchini akisema
katika kadhia hiyo, Jeshi la
kwamba watu watatu
Polisi liliwataja viongozi
lazima wapatikane kwa
watatu wa kiimani
udi na uvumba, ambao
akiwemo Askofu Mpemba, aliwataja kuwa ni mimi
lakini ni Masheikh
(Hamza Omari), Ilunga
wawili waliokamatwa na
Hassan Kapungu pamoja na
kufikishwa Mahakamani.
Askofu Mpemba. Alisema
Hivyo akasema ni
Imam Hamza.
vyema pia ikafahamika pia
Imam Hamza, alisema
wamefikia wapi kumtia
kufatia tangazo hilo, katika
mbaroni mtuhumiwa
msako wao, Jeshi la Polisi,
mwenzao huyo kama
lilianza kumkamata yeye
lilivyotangaza, mwaka 2012. (Imam Hamza) na baada
Alisema, kwa kuzingatia
ya kupelekwa Polisi,
Na Bakari Mwakangwale

moja kwa moja dhamana


yake ilizuiliwa na kukaa
rumande kwa muda wa
miezi mine.
Alisema, baada ya
yeye, umma utakumbuka
kwamba Jeshi la Polisi,
lilitangaza kumkamata
Almarhum Sheikh Ilunga
Kapungu, muda mfupi
baada ya kutoka katika
matibabu nchini India,
ambapo maelezo yake
yalifikishwa Mahakamani,
kwa maana hiyo mpaka
anafariki, inafahamika
alikamatwa na alikuwa ana
kesi.
Alisema, kwa upande
mwingine Waislamu
wamekuwa wakijiuliza ni
vipi mpaka sasa Askofu
Mpemba, hajakamatwa
pamoja na kutajwa na Jeshi
la Polisi kuwa ni miongoni
mwa viongozi watatu wa
Dini wanaotafutwa kwa
udi na uvumba, lakini
waliokamatwa ni Imam
Hamza Omari na Sheikh
Ilunga Kapungu.
Alisema, hali hiyo inatoa
tafsiri kuwa vyombo vya
dola vinafanya kazi kwa
upendeleo, akahoji ni vipi
wengine wakamatwe na
mwingine achwe ikiwa
umma ulitangaziwa
kuwa ni miongoni mwa
watuhumiwa wanaotafutwa
na Jeshi la Polisi.

Tahariri

AN-NUUR

S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786


Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM.
www.annuurpapers.co.tz
E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk
Ofisi zetu zipo: Manzese Tip Top
Usangi House, barabara ya Morogoro, D'Salaam

Majipu Mahakamani,
Polisi yanacheleweshwa

TANGU Rais wa
awamu ya tano ya
serikali ya Jamhuri
ya Muungano
Rais John Pombe
Magufuli, iingie
madarakani, kazi yake
ya kwanza kabisa
ambayo imeifanya na
inaendelea kuifanya
ni kuboresha utendaji
na uwajibikaji wa
watumishi wa umma,
kupambana na rushwa
na ubadhirifu wa mali
ya umma, kusimamia
na kufuatilia
kukusanya kodi na
kubana matumizi ya
serikali.
Rais Magufuli
na safu yake ya
uongozi wa juu
serikalini wamekuwa
wakiendesha
operesheni hii ya
kudhibiti utendaji kwa
watumishi wa umma
na kuwawajibisha
wale wanaobainika
kwenda kinyume na
maadili ya kazi, kwa
mtindo unaoitwa wa
kutumbua majibu.
Kama uadilifu
unachukua nafasi yake
katika utumbuaji huo
wa majibu, bila shaka
huo utakuwa mwanzo
mzuri kwa Rais
Magufuli na wenzake
kutengeneza serikali
inayowajibika barabara
kwa wananchi, tofauti
na serikali za Marais
wa awamu zilizopita.
Hata hivyo, kuna
Idara mbili muhimu
sana, ambazo kwa
hakika bado Rais
Magufuli hajasikika
kuchukua hatua za
kutumbua majipu,
licha ukweli kwamba
yapo na yanaonekana
dhahiri.
Sote tunatambua
kwamba amani na
usalama wa nchi
ndio kigezo kikubwa
na muhimu katika

kujenga msingi imara


wa maendelao na
ustawi wa maisha ya
raia katika Taifa lolote
lile. Lakini pia amani
na usalama katika
jamii msingi wake ni
wananchi kupata haki
kwa nayestahili haki,
watu kujenga hofu ya
kutenda makosa na
kuheshimiana.
Jeshi la Polisi na
Mahakama ni Idara
zinazohusika moja
kwa moja katika
kusimamia haki na
usalama wa raia hapa
nchini. Ni vyombo
ambavyo wananchi
wanavitegemea katika
kusimamia haki, amani
na usalama wa maisha
yao ya kila siku.
Pamoja na umuhimu
wake huo na kustahiki
kufanya kazi kwa
uadilifu mkubwa,
lakini katika mazingira
ya hapa kwetu tunaona
vyombo hivyo vikiwa
vinara wa utendaji
mbovu uliojaa kila aina
ya uonevu na uovu.
Rushwa, dhulma,
uonevu, zimekuwa
ndio sifa za watendaji
wengi katika vyombo
hivi kwa muda mrefu
sasa.
Pamoja na unyeti
wake katika kusimamia
haki na usalama wa
maisha ya Mtanzania,
tunashangaa kuona
tangu akingie
madarakani Rais
Magufuli, mpaka sasa
bado hajatumbua
majipu na kuleta
mabadiliko kiutendaji
katika Idara hizo. Kwa
kipindi kirefu taasisi
hizi mbili zimekuwa
zikifanya kazi bila
woga wa kuchukua
rushwa, kuonea au
kudhulumu watu,
jambo ambalo sasa
limekuwa la mazoea.
Tunakumba mwaka

2013 mwezi wa tano,


wakati akichangia
hotuba ya makadirio ya
mapato na matumizi
ya Wizara ya Mambo
ya Ndani Bungeni
Dodoma, Mbunge
wa Mbozi Magharibi
David Silinde,
alililaumu jeshi la Polisi
kwa kushindwa kuzuia
vitendo vya uhalifu
vinavyohusishwa na
mambo ya udini.
Wabunge wa
Kambi ya Upinzani
walicharuka na kuitaka
Serikali kulivunja Jeshi
la Polisi na kulifanya
kuwa kitengo ndani
ya Jeshi la Wananchi
Tanzania (JWTZ), kwa
kile walichodai kuwa
limeoza na limekithiri
vitendo vya dhuluma
na rushwa.
Sambamba na
hilo, wapinzani hao
walimtaka Waziri
wa Mambo ya Ndani
wakati huo, Dk.
Emmanuel Nchimbi
pamoja na Mkuu wa
Jeshi a Polisi nchini
wakati huo, Said
Mwema, wajiuzulu na
endapo wakishindwa
kufanya hivyo basi
Serikali iwafukuze
mara moja.
Silinde alisema kila
mtu anajua taifa lipo
katika udini, lakini
Serikali inadanganya,
inaingiza siasa katika
mambo serious
(makini). Alisema ana
hakika Jeshi la Polisi
linamdanganya Waziri
wa Mambo ya Ndani
na Rais kutokana na
udhaifu wake, hivyo
wananchi wanahitaji
ukweli ili tutatua
tatizo na udini kupata
suluhisho.
Jeshi la Polisi
limeoza, enough is
enough (imetosha)
tuchukue hatua,
hakuna wakati wa
kusubiri tena, alisema
Silinde.
Tunakumbuka pia
katika ripoti ya Taasisi
ya Afro Barometer
iliyofanywa kwa
kushirikiana na
Taasisi ya Kupunguza
Umasikini (Repoa),
ilionyesha katika ripoti
hiyo kuwa, Polisi
bado wanaongoza
kwa kupokea rushwa
wakifuatiwa na
TRA, Mahakama na
Takukuru inashika
nafasi ya nne.
Ripoti hiyo
ilionyesha kuwa
miongoni mwa

AN-NUUR

JAMADUL AWWAL 1437, IJUMAA FEB 26-MACHI 3, 2016

walihojiwa, asilimia
50 waliitaja polisi
kukithiri kwa rushwa,
TRA (asilimia 37),
Mahakama asilimia
36, Takukuru asilimia
29 wakati maofisa wa
Serikali za mitaa ni
asilimia 25.
Utafiti huo ulibaini
kuwa miongoni mwa
watu watatu ambao
wanaenda kupata
huduma Polisi na
mahakamani, mmoja
kati ya watu hao
anadaiwa rushwa.
Watu wanane
kati ya 10 ambao
walihojiwa ambao
tayari walishatoa
rushwa, walikiri kuwa
hawakutoa taarifa
mahali popote licha ya
kutoa rushwa.
Pia utafiti huo
ulibaini kuwa asilimia
34 ya wahojiwa,
walitoa rushwa
wakati wanatafuta
haki mahakamani na
wengine asilimia 34
walitoa rushwa kwa
kuepuka usumbufu wa
Polisi.
Ni tafiti nyingi
zimethibisha kuoza
kimaadili katika
taasisi zetu hizi nyeti
za kusimamia haki na
usalama wa raia.
Rais JPM na serikali
yake wana kazi
kubwa kumaliza

uonevu uliopo ndani


ya jeshi la Polisi na
katika Mahakama.
Huko mwenye haki
ni mwenye fedha,
huko yamejengeka
mazoea kuwa mwenye
kanzu, akafuga ndevu
na akavaa kilemba
ni tuhumiwa wa
ugaidi, huyo atasota
rumande na na kiona
cha mtema kuni. Hata
itakapothibitika hana
hatia ameshalemazwa
viungo au ashatiwa
maradhi.
Katika mahamaka
zetu nyingi, vijana
wengi huenda Segerea
kwa kushindwa
kuweka mambo yao
sawa kwa hakimu
kabla ya kesi. Ukiwa
na pesa utanusurika.
Hivyo basi, kwa
mazoea haya ya muda
mrefu, tunaamini
wengi waliopo
magereza walifungwa
kwa sababu hawakuwa
na pesa za kuwahonga
polisi wa upelelezi au
hakimu.
Ni vyema Rais
Magufuli akafanya
haraka kutumbua
majipu yaliyojikita
ndani ya Idara hizi,
maana kwa miaka
mingi zimekuwa
mzigo na mateso kwa
raia badala ya kuwa
mkombozi wa haki.

Tanzania Islamic Centre


Manispaa ya Kinondoni

P.O. Box 90042, +255 713 586 186 au 713 455 255
Dar es Salaam, Tanzania

NAFASI YA MAFUNZO YA USHONAJI


Chuo cha ushonaji Tanzania Islamic
Centre kinawatangazia wanawake wote
kuwa kinatoa mafunzo ya ushonaji
(tailoring) na kudarizi (Embroidering) kwa
ada nafuu sana.
Chuo kina maadili na mazingira
mazuri ya kujifunzia. Kipo Msikiti wa
Kichangani, Magomeni Mapipa.
Fomu zinapatikana hapa chuoni.
Wanawake wote mnakaribishwa katika
mafunzo.
Wasiliana kwa simu No 0713586186 na
0713 455 255
Wabillah Tawfiq

AN-NUUR

HABARI ZA KIMATAIFAJAMADUL AWWAL 1437, IJUMAA FEB 26-MACHI 3, 2016

Marekani yadaiwa kuipa ISIS silaha za kemikali


AFISA wa zamani wa Jeshi
la Marekani Scott Bennett,
amesema kuwa silaha za
kemikali zinazomilikiwa
na kundi la Daesh zimetoka
Marekani.
Hayo yamefichuliwa na
Bw. Scott Bennett katika
mahojiano yake na IRIB hivi
karibuni.
Bennett, ambaye aliwahi
kuwa afisa wa jeshi la
Marekani, amelaani jinai
zinazoendelea kufanywa na
wapiganaji wa kundi la Daesh
katika nchi za Iraq na Syria na
kusema, kundi hilo linamiliki
silaha za kemikali kutoka
Marekani na kwamba lilipata
silaha hizo hatari kupitia
Saudi Arabia na Uturuki.
Bennett alisema kuwa
Serikali na Congress ya
Marekani zimelipa kundi
hilo la kigaidi silaha hizo
za kemikali kwa makusudi,
ili litimize malengo ya
Washington katika eneo la
Mashariki ya Kati.
Afisa huyo wa zamani wa
jeshi la Marekani ameongeza
kuwa, Washington
imeshindwa kufikia malengo
yake nchini Syria, kwani licha
ya miaka kadhaa ya mgogoro
wa ndani nchini humo,
Wasyria bado wana imani na
serikali ya Rais Bashar Assad
na wanashiriki katika vita
dhidi ya kundi la Daesh kwa
lengo la kurejesha amani na
utulivu katika nchi yao.
Imeelezwa kuwa mgogoro
ndani ya Syria ulianza
mwaka 2011 kufuatia
hujuma na mashambulizi
makubwa ya makundi ya
kigaidi yanayoungwa mkono
na Marekani na washirika
wake wakubwa ikiwemo
Saudi Arabia, kwa lengo la
kuiondoa madarakani serikali
ya Rais Bashar Assad.
Hivi karibuni Shirika la
Kijasusi la Marekani CIA,
limesema kuwa kundi la
Daesh linatumia silaha za
kemikali katika mashambulizi
yake.
John Brennan, Mkurugenzi
wa CIA amenukuliwa na
shirika la habari la CBS News
akisema kuwa, wana ushahidi
unaoonyesha kuwa Daesh
wanatumia silaha hizo hatari
dhidi ya binadamu.
Brennan amefichua
kuwa kundi hilo lina ujuzi
wa kutengeneza silaha za
kemikali kwa kutumia gesi ya

klorini na haradali (mustard),


kama iliyotumika katika vita
vya kwanza vya dunia.
Kadhalika Mkurugenzi
huyo wa CIA
ametahadharisha kuwa, kuna
uwezekano wa Daesh kuwauzia

Wamagharibi silaha hizo za


kemikali, ili kupata fedha za
kuendeshea harakati zao za
kigaidi.
Kauli hii inakuja siku mbili
baada ya Mkurugenzi wa Idara
ya Kiintelijensia ya Marekani,
James Clapper kuiambia Kamati
ya Bunge la Congress ya nchini
humo kuwa Daesh wanatumia
silaha za kemikali nchini Iraq na
Syria.
Marekani imetoa madai hayo,
huku ikiliunga mkono kundi
hilo ikishirikiana na washirika
wake wa zikiwemo nchi za Saudi
Arabia, Qatar na Uturuki, tangu
kuanzishwa kile kinachoitwa
hujuma dhidi ya Syria Machi
mwaka 2011.
Hayo yote yanajiri wakati
shirika la Ujasusi la Urusi
likitangaza kuwa limeona
shehena za silaha za sumu
zikitoka Uturuki, zikipelekewa
kundi la Daesh na silaha hizo pia
zilitumia dhidi ya wananchi wa
Syria. abna.ir

John Brennan, Mkurugenzi wa CIA.

SILAHA za maangamizi za Marekani.

Mtoto wa miaka minne jela maisha kwa mauaji

MAHAKAMA moja nchini


Misri imemhukumu kifungo
cha maisha jela mtoto
mmoja wa miaka minne kwa
tuhuma za kufanya mauaji
akiwa na umri wa baina ya
mwaka mmoja na miwili.
Kwa mujibu wa toleo la
mtandaoni la gazeti la New
Vision la nchini Uganda,
Ahmed Mansour Karmi,
amedaiwa kupatikana na
hatia ya mashitaka manne
ya mauaji, manane ya jaribio
la mauaji, shitaka moja la
wizi wa kutumia mabavu na
jingine la kuwatishia maisha
askari na maafisa wa polisi wa
nchi hiyo, yote hayo akidaiwa
kufanya kabla ya kutimiza
umri wa miaka miwili.
Ahmed ambaye hakuwa
kortini wakati wa hukumu
hiyo, ni mmoja kati ya
watuhumiwa 115 ambao
wamehukumiwa kifungo
cha maisha jela kwa tuhuma
za kuhusika na jinai
zilizofanywa nchini Misri

Ahmed Mansour Karmi

mapema mwaka 2014.


Faisal al-Sayd, wakili
wa mtoto huyo amesema
kuwa jina la mtoto huyo
liliongezwa kwenye orodha
ya watuhumiwa kimakosa
na kwamba, mahakama
haikumkabidhi Jaji aliyetoa
hukumu hiyo cheti cha
kuzaliwa cha mtoto huyo, ili
kuhakikisha kuwa alizaliwa
Septemba mwaka 2012 au la.
Wakili huyo alisema licha
ya kukabidhi cheti hicho,
lakini Mahakama hiyo
iliipeleka kesi hiyo katika
Mahakama ya kijeshi, ambapo
mtoto huyo alihukumiwa

pamoja na watuhumiwa
wengine 114.
Mwanasheria huyo
aliyenukuliwa akizungumza
kwa hasira alisema, Hii
inadhihirisha kuwa Jaji
hakuisoma wala kuitafakari
kesi iliyokuwa mbele yake
na huu ni ushahidi kwamba,
hakuna haki nchini Misri.
Inaelezwa kuwa zaidi
ya wanachama 40,000 wa
upinzani wakiwemo wafuasi
wa Ikhwanul Muslimin,
wanazuiliwa katika
mazingira ya kutisha katika
korokoroni za nchini Misri
bila kuthibitika kufanya kosa
lolote.
Maelfu ya watu
wamewekwa kizuizini nchini
Misri baada ya jeshi la Misri
likiongozwa na Jenerali Abdul
Fattah al-Sisi, Julai mwaka
2013 kuiondoa madarakani
serikali ya Muhammad Morsi,
Rais wa kwanza kuwahi
kuchaguliwa kidemokrasia
katika nchi hiyo ya Kaskazini
mwa Afrika.irib

Makala

AN-NUUR

JAMADUL AWWAL 1437, IJUMAA FEB 26-MACHI 3, 2016

Erbil: Propaganda ya nchi za Magharibi na halisia mbili sambamba


Na Andre Vitchek
Februari 18, 'Mtandao wa
kupashana habari'

NILIFIKIRIA kuandika insha hii


nilipokuwa nafanya kazi katika
Kurdistan ya Irak, siyo mbali na
jiji la Mosul, moja ya maeneo
yaliyotekwa na ISIS. Tangu
nifike hapo kwa mara ya mwisho
mwishoni mwa 2014, eneo lote
hilo la 'Kurdistan' limekuwa
likianguka. Kukosekana kazi
kumekuwa kunaongezeka, kwa
duru za kukisia ni kiasi cha
asilimia 50. Umaskini unapanuka,
na takwimu halisi zinapigwa
msasa. Mishahara haijalipwa
kwa miezi kadhaa na wakimbizi
wanaofika kutoka Mosul wako
katika hali ya kufa kwa njaa,
wakiwategemea tu jamaa zao na
marafiki kwa misaada.
Lakini nchi za Magharibi
zimekuwa zikiimba sifa za eneo
tiifu la Irak, Ni kwa sababu - kama
ilivyo katika nchi kadhaa za Afrika
au Indonesia - eneo la Kurdistan
limekuwa tayari kutoa sadaka watu
wake yenyewe. Mradi makampuni
ya nchi za Magharibi na ya Uturuki
yanaweza kujaza mifuko yao
na mradi wanaridhika, kwanini
wawajali watu wa eneo hilo na
taabu zao?
Kuna uhalisi mmoja tu ambao unaweza kuonekana na
kuyakinishwa, ambao unaelezwa
na watu wa eneo hilo, endapo mtu
atataka kusikiliza. Uhalisia wa pili
ni ule ulioundea na propaganda
ya nchi za Magharibi. Hapa, eneo
la Kurdistan limeonyeshwa kama
lenye usalama, la demokrasia na
rafiki kwa nchi za Magharibi.
Wakati wa usiku huko Erbil,
nilijaribu kuangalia taarifa za
habari. Sikuweza kupata vituo
vyovyote nilivyozoea - RT, Press TV
au TeleSUR.
Jeshi la Syria mwishowe lilikuwa
linakomboa jiji la Aleppo. Russia
ilikuwa inatoa msaada wa ndege
za kijeshi. Matumaini yalikuwa
yanarudi kidogo kidogo kwa nchi
ambayo ilikuwa imeharibiwa kabisa
na maslahi ya nchi za Magharibi,
Uturuki na Saudia na makundi
kadhaa, yaliyotengenezwa moja
kwa moja na NATO (umoja wa
kujihami wa nchi za Magharibi), ya
kigaidi.
Kutokana na ushirikiano wa
Syria na Russia, zaidi ya watu
milioni moja walioondolewa
kwenye makazi yao ndani ya nchi,
wameweza kurudi nyumbani.
Nilipata habari hizi mwenyewe,
kwa sababu nakaa Lebanon na
kufanya kazi kote katika Mashariki
ya Kati. Na naweza kushuhudia
kuwa ufuatiliaji habari unaotolewa
na vianzio bora zaidi kati ya vianzio
mbadala. kwa mfano RT (Radio
Television ya Syria) imekuwa ikitoa
maelezo ya kina bila ushabiki
wakati wote.
Sasa, nikiwa katika eneo hili
lisilojua chochote ila kushabikia
nchi za Magharibi, nilikuwa nahitaji
kupata habari za hivi sasa kuhusu
hali inavyoendelea. Lakini hoteli
yangu ilikubali tu vianzio (vituo)
rasmi vya propaganda ya Himaya
(ya Marekani) kama CNN, Fox
News na BBC - vituo vinavyotoa
propaganda hasi masaa 24, siku
saba kwa wiki.
CNN na BBC walikuwa wote
wanatoa vielelezo vya picha kutoka
mpaka wa Syria na Uturuki.
Maelezo yalikuwa yanafanana:

Dr. Bashal Al-Asad Rais wa Syria

RAIS Vladmir Putin wa Urusi.

watu wanakimbia Aleppo, kutaka


kuvuka kuingia Uturuki kuokoa
maisha yao. Uturuki "inafanya kila
inachoweza kusaidia."
Mafanikio ya kivita ya Syria
na Russia yalionyeshwa kuwa ni
mkasa, balaa halisi. Vituo hivi
viwili vya televisheni vinatoa
mwelekeo kwa mabilioni ya watu
kote duniani, kuainisha kiimla ni
matukio gani muhimu yaonekani
katika mabara yote. Wanatengeneza
mtiririko mmoja rasmi wa habari,
mfumo mmoja wa mapokeo. Wakati
nikiangalia luninga, nikashangaa
kuona kuwa dunia ina uhalisia
wa aina mbili: mmoja wa kweli,
ambao umeundwa na habari za
watu na shuhuda zao, na mwingine
"uhalisia bandia," uliofinyangwa
na kukarabatiwa, lakini ndiyo
unatawala hisia. Hakuna tendo
jema, hakuna tukio halisi jema
lingeweza kuleta matumaini
na furaha kwa watu wa sayari
yetu. Inapingana na maslahi ya
Himaya. Vyombo vya propaganda
vingeutumbukiza katika uchafu na
uharibifu tu, na mzaha wa kutisha.
Picha za makundi ya wakimbizi
mpakani mwa Syria na Uturuki
zikiwa na maelezo ya kina ya
propaganda, yakirudiwa tena
na tena na mtangazaji wa BBC,
zimeshonwa kuiaiminisha dunia
kuwa juhudi za Syria na Russia
hazikuwa zinaiokoa Aleppo, mji
wa Syria wenye watu wengi Zaidi,
ila kinyume chake, wamekuwa
wanauteketeza! Baada ya dakika
mbili za kuangalia "habari" katika
BBC, nilianza kujisikia vibaya.
Tofauti kati ya Uhalisia
nilivyouona na nilivyoona kwa
macho yangu mwenyewe, na huu
wa kubuni, ulikuwa mkubwa mno.
Nilishangaa, jinsi hao waandishi
waandamizi wa habari na
washiriki wao wanaotumikia
Himaya wanaweza kujitathmini
wakijiangalia katika kioo, asubuhi.
Nilizima sanduku hilo na kufungua
ukurasa wa RT kwenye kompyuta
yangu. Ilikuwa rahisi kabisa bado!
Angalau kwangu na wengine
ambao bado hawajaathirika!
Unakuja Ecuador, nchi
inayoinuka, yenye maeneo ya
kupendeza ya kupumzika, vituo
vya tiba na taasisi za kitamaduni
zisizoisha, lakini punde unaambiwa
kuwa taifa limezongwa na rushwa
na halina hali njema. Unajibu
kuwa ulikuwa unaifahamu
kabla, miongo kadhaa iliyopita,
ambako ilikuwa kama Peru, ya
kibaguzi, ya kukatisha tamaa,
chafu na inayokinzana na watu
wake yenyewe! Bado wanasisitiza:
imeshindwa, mabadiliko ya haraka

yanahaitajiwa!
Unakwenda Brazil, huko
Amazonia. Unazungumza na
watu katika mapori na katika
maeneo yaliyokuwa makazi
duni ya kujazana mijini. Watu
wanakwambia kuwa hali sasa ni
nzuri kuliko mwanzoni, ikiwepo
serikali ya kijamaa kwa miaka
mingi sasa. Halafu unafungulia
televisheni ya O'Globo usiku; na ni
uharo tu mara nyingine tena.
Upo Zimbabwe, ambako
ulishaambiwa utazamie uchafu
umezagaa na shida nyingi.
Unatokea Nairobi inayofuata nyayo
za nchi za Magharibi ambako
zaidi ya asilimia 50 ya wananchi
wanaishi katika makazi mjazano
ya kutisha. Jijini Harare, mji mkuu
wa Zimbabwe, ni nadra kuona
makazi duni, ila kuna utamaduni na
ujenzi wa miundombinu, pamoja na
kiwango kikubwa zaidi cha kusoma
na kuandika katika Bara lote la
Afrika. Jiji liko safi. Lakini unasoma
jarida la The Economist na takriban
machapisho mengine makubwa
yote ya Uingereza na unaambiwa
kuwa nchi hiyo inachungulia
kaburi.
Unakwenda China... Kila kitu
kimepinduka ukilinganisha na kile
ulichokuwa unatazamia, ukisoma
magazeti ya nchi za Magharibi.
Katika Jamhuri ya Watu wa China
unaona taifa la Kikomunisti
lenye malengo halisi ya baadaye,
likiwa na uhuru zaidi wa sanaa na
fikra kuliko unavyoweza kukuta
kokote barani Ulaya, na pia nafasi
nyingi zaidi. Lakini unaporudi
Paris au London na kuzungumza
ulichokiona, unachekwa.
Uhalisia bandia umeshinda. Hasa
katika nchi za Magharibi, takriban
kila mmoja amenaswa hapo,
amepigwa na bumbuazi.
Uhalisia rahisi na wa kweli
unatemewa mate, unanyanyaswa,
unabezwa na siyo tu na vyombo vya
habari na vianzio vya propaganda,
kama zamani. Wengi zaidi kati ya
watu wa kawaida nchi za Magharibi
kwa unyenyekevu na kujiamini
katika haki ya wanachofanya
wanajitolea: wanahisi kuwa
inawapasa kudhihirisha utiifu wao
kwa kile serikali zao zinachosema.
Wanafanya hivyo huku wakijisifu
kwa nguvu kuhusu demokrasia,
uhuru binafsi na uhuru wa kisiasa
katika sehemu yao ya dunia.
Cha kushangaza ni kuwa jinsi
wanavyozidi kunyonywa bongo,

wawe watiifu kupindukia, ndiyo


wanavyozidi kujisifu jinsi walivyo
huru, wanavyozidi kujinadi kuwa
wabeba bendera pekee wa kweli wa
demokrasia.
Inaleta hisia ya ufashisti na
kukata tamaa!
Halisia mbili: moja ya kweli
lakini iliyopigwa ikanyamaza. Ya
pili inapiga kelele, inasukumana,
ikiungwa mkono na mabilioni ya
dola za Marekani, lakini iliyojengwa
juu ya uwongo, urekebishwaji wa
habari na malengo ya ki-Machiaveli,
ya kutawala kwa mbinu zozote zile.
Kutumia maneno ya rafiki yangu
mpendwa Eduardo Galeano (sasa
marehemu, kitabu chake muhimu
zaidi ni 'Open Veins of Latin
America' - Mishipa inayobubujika
damu ya Amerika ya Kusini).
Alisema "hivi hawa ambao bado
wana heshima iliyobaki, wafikiriaji,
waandishi habari, waandika insha
na watengeza filamu wenye hamasa
kwa yule mwanamke anayependeza
anayeitwa Halisia wanafanya nini?
Wanaweza, wanahitaji kufanya
hivyo na inawapasa, kurudia tena
na tena kile ambacho kiko wazi,
hata bila kuwa na kifaa chochote
machoni. Inawabidi waseme ukweli,
hata kama wananchi waliovishwa
itikadi tawala watakuwa
wanawatemea mate muda wote.
Si vigumu kiasi hicho na
inakuwa kama hivi:
Kurdistan ya Irak imesaliti
nchi za Mashariki ya Kati na sasa
inaanguka, ikiwa imetelekezwa
na wasimamizi wake wa nchi za
Magharibi.
Majeshi ya Syria na Russia hivi
sasa yanakomboa jiji muhimu la
Kiarabu, Aleppo.
Mapinduzi katika nchi za
Amerika ya Kusini yanahujumiwa
zaidi kutoka nje, na pia mawakala
wao ndani ya nchi hizi. Lakini
mengi kati ya mapinduzi hayo
bado yamesimama, yako imara.
Tutapigana na kuyalinda hadi
pumzi zetu za mwisho. Na
tutazungumza na kuandika
kuhusu nchi hizo, kwa hamasa, bila
kuchoka.
Jaroslav Seifert, mshairi wa
Czech, mshindi wa nishani ya Nobel
na mtunzi wa baadhi ya mashairi
mazuri yaliyowahi kuandikwa
katika karne ya 20, wakati mmoja
aliwarukia waandishi wenzie:
"Mwandishi ni mdhihirishaji hisia
za taifa lake... Kama mtu akiuruka
ukweli, inaweza kuonekana kama
hatua yenye malengo halisi. Endapo
mwandishi anauruka ukweli, ni
mwongo!"
Waandishi insha na wafikiriaji
wa kweli wana jukumu la kulinda
uhalisia: ule wa uhakika, ule wenye
soni na wa kweli.
Na ukweli ni kwamba, kuna
uhalisia mmoja tu! Ambacho
Himaya ya Marekani na vyombo
vyake vya propaganda wameweza
kufanya kutengeneza uhalisia 'wa
pili' au 'sambamba' siyo kingine
ile ni uwasilishaji potofu wa hali
halisi, kitu ambacho hakiwazuii
watu kufikiri, kuelewa, na zaidi
ya yote, kuota kuhusu dunia bora
zaidi yenye msingi wake katika
ubinadamu, ukweli na haki.
(Makala hii Erbil: Western
Propaganda and Two Parallel
Realities kama ilivyoandikwa na
Andre Vitchek imetafsiriwa kwa
Kiswahili na Anil Kija.)

Makala
Na Rashid Mtagaluka

WAKATI wa kampeni za Uchaguzi


Mkuu wa Rais, Wabunge na
Madiwani zilizokuwa zimeanza
Agost 22 na kumalizika Oktoba
24 mwaka 2015, Rais John
Pombe Joseph Magufuli pamoja
na mambo mengine, aliahidi
kuongoza Taifa letu kwa kufuata
Sheria, Kanuni na Taratibu.
Mheshimiwa Magufuli ambaye
kwa kifupi alikuja kufahamika
kwa kifupi cha JPM alitoa ahadi
hiyo alipokuwa kwenye mikutano
mbalimbali ya kampeni ambayo
iliandaliwa na Chama chake
Cha Mapinduzi (CCM). Kati
ya mambo ambayo Watanzania
yaliwashawishi hadi kuamua
kumpa kura zilizotosha kumpeleka
Ikulu ya Magogoni Waziri huyo
wa zamani wa Ujenzi ni msimamo
wake wa kutangaza kuongoza nchi
bila ya ubaguzi wa kabila, itikadi
za vyama vya siasa wala dini ya
mtu!
Na kweli Novemba 5, 2015 Rais
Dk Magufuli aliapishwa rasmi
kuchukua nafasi ya Dk Jakaya
Mrisho Kikwete, na baadaye kwa
kushauriana na Makamu wa Rais
Mheshimiwa Samiya Suluhu
Hassan, alimteua George Masaju
kuwa Mwanasheria Mkuu wa
Serikali ya awamu ya tano, na
baadaye Majaliwa Kassim Majaliwa
(MB) akateuliwa kuwa Waziri
Mkuu.
Baada ya sherehe za kuapishwa
kwa Waziri Mkuu, wabunge
walirejea bungeni ambako rais
DK Magufuli aliwahutubia, ikiwa
ni mara yake ya kwanza kufanya
hivyo toka alipochaguliwa baada
ya uchaguzi wa Oktober 25 mwaka
jana. Kwenye hotuba yake rais
Magufuli mbali ya kuwashukuru
wananchi kwa kumuamini na
kumchagua, aliahidi kuwa kiongozi
atakayewatumikia watu wote bila
ubaguzi, na kwamba lengo lake
ni kuhakikisha Tanzania inasonga
mbele kimaendeleo. Aidha, Rais
kwenye hotuba yake hiyo akaeleza
malalamiko aliyoyapokea kwa
wananchi ambayo anaona ni kero
kwao, maeneo ambayo anasema ni
lazima yashughulikiwe ipasavyo ili
kuleta uaminifu kwa wananchi.
Binafsi naamini kwamba,
mojawapo ya kero alizozizungumza
Rais katika hutuba yake hiyo
pale Bungeni mjini Dodoma ni
pamoja na uonevu, unyimwaji
haki na udhalilishaji wa dhahiri
na wa kitaathira wanaofanyiwa
baadhi ya viongozi wa Dini tukufu
ya Kiislamu na vyombo vyenye
dhamana ya masuala ya ulinzi na
usalama hapa nchini kwa kisingizio
cha kusaka wahalifu wa makosa
mbalimbali ya kijinai. Ukiachilia
mbali suala la masheikh wa Jumuiya
ya Uhamsho wa Mihadhara ya
Kiislamu Visiwani Zanzibar ambalo
mpaka sasa linaendelea kupigwa
danadana huko mahakamani kwa
zaidi ya miaka mitatu sasa, yapo
yanayowahusu mamia ya Waislamu
ambao kwa mujibu wa mashuhuda,
sio tu hali zao ni taabani, lakini pia
bado hawajafikishwa mahakamani.
Kutokana na Waislamu hao
kukosa watu wa kusaidia kupaza
sauti zao na kuzifikisha kwa
wakubwa ambao kwa vyovyote
vile, huwenda hawana taarifa
na vitendo vinavyodaiwa ni vya
udhalilishaji wanavyofanyiwa

AN-NUUR

JAMADUL AWWAL 1437, IJUMAA FEB 26-MACHI 3, 2016

Kilio cha Waislamu kwa Rais Magufuli

MHE. GEORGE Masaju kuwa


Mwanasheria Mkuu wa Serikali

WAZIRI Mkuu, Mhe.


Majaliwa Kassim Majaliwa

Watanzania wenzetu hao,


nachukuwa fursa hii kukibeba kilio
hicho hadi kwa Alhaj Abubakar
Zuber Bin Ally, Sheikh Mkuu na
Mufti wa Tanzania. Uwamuzi
wangu wa kumuomba Mheshimiwa
Mufti Sheikh Zuber afikishe kilio
hiki kwa Mheshimiwa Rais JPM
unatokana na Dhima aliyonayo kwa
Waislamu wa Tanzania mbele ya
Mwenyezi Mungu Muumba pamoja
na mtazamo wake chanya juu ya
jamii.
Nina imani kubwa na Alhaji
Abubakar Zuber kwasababu ni
kiongozi wa DINI aliyewekwa
na waumini wa DINI kwa ajili
ya kuelekeza na kusimamia
maslahi mapana ya DINI, tofauti
na baadhi ya viongozi wenzake
wanaougeuza uongozi wa DINI
kuwa DILI la kujaza matumbo
yao! Hii haimaanishi Mheshimiwa
Mufti akifikisha ujumbe huu kwa
Rais Magufuli ni lazima ufanyiwe
kazi papo kwa papo la!, kwani
inajulikana tangu zama za Manabii
kwamba, kazi ya mjumbe siku zote
ni kupeleka tu kile alichotumwa,
lakini suala la utekelezaji si jukumu
lake! Hata hivyo nimefarijika
kupata taarifa ya kusikitishwa
kwake mara Ustaadh Jamal Yassin
mhanga wa mateso ya vyombo
vya dola anayetokwa damu katika
sehemu zake zote za siri kufika
ofisini kwake mapema mwezi huu
na kumsimulia mkasa uliomkuta
yeye binafsi kwa upande wa
kwanza, na Waislamu wengine
kwa ujumla wake. Ustaadhi Yassin
alilazimika kupiga hodi ofisi za
Mufti zilizoko Makao Makuu
Kinondoni kwa lengo la kuhitaji
msaada wa matibabu akiamini
kuwa, uadilifu wa kiongozi huyo
mpya anayetimiza siku 168 Ijumaa
hii tokea achaguliwe, ungepelekea
kupata ufumbuzi wa afya yake
inayoendelea kuzorota siku hadi
siku!
Yassin ni mfano mdogo tu wa
mamia ya Waislamu wanaoendelea
kukamatwa na jeshi la Polisi kila
kukicha hapa nchini kutokana
na mavazi yao ya kanzu, kilemba
pamoja na ndevu wakituhumiwa
kuwa ni magaidi! Mufti Ibni Ally,
najua Ustaadh Yassin amekusimulia
mengi kama ambavyo nami pia
amenisimulia kuhusu vitendo vya
kishenzi visivyojali japo chembe
ya utu, huruma, heshima na

ustaarabu vinavyofanywa na polisi


wanaojulikana kama Task Force
katika vituo mbalimbali.
UstaadhYassin (38) ambaye ni
mzaliwa wa Pemba, Ole Kiyanga
Visiwani Zanzibar alianza
kunieleza siku nilipokutana naye
mjini Morogoro hivi karibuni
kuwa shughuli zake kubwa za
kujiendeshea maisha yake zilikuwa
ni uchuuzi wa dagaa anaowatoa
Pemba na kuwapeleka Dar es
Salaam kwa usafiri wa majahazi.
Anasema mwanzoni mwa mwezi
Julai mwaka jana akiwa anatoka
kuwatembelea wateja wake akirejea
nyumbani kwake Kigamboni,
alipanda daladala linalofanya
safari zake kati ya Mbagala Rangi
Tatu-Posta na kulazimika kushuka
BP Kurasini karibu na daraja
na mzunguko wa barabara ya
kuelekea Kariakoo na nyingine
Posta kutokana na dereva wa basi
hilo kuamua bila sababu iliyo wazi
kukatisha ruti.
Nilikuwa na abiria wenzangu
wawili wote akina mama.
Tulipokaribia ule mzunguko
tukakuta gari ya polisi Landrover
Defender imeegeshwa pale. Mara
wakatokea askari wawili wakiwa
na silaha na kutuambia kuwa tuko
chini ya ulinzi. Anasimulia na
kuongeza.
Tukakalishwa chini na palepale
askari akanikanyaga begani na
buti za polisi alizovaa. Nilikuwa
nimevaa kanzu na kichwani
nimepiga kilemba. Haya ndiyo
mavazi yangu ya kawaida siku
zote.
Hapo tukaanza kuulizwa dini
zetu, wale akina mama mmoja
akasema yeye ni Msabato na
akaachiwa aendelee na safari
yake. Mwenzake akasema yeye
ni Muanglikana na yeye pia
akaachiwa, anabainisha Yassin na
kuendelea.
Mimi nikasema ni Muislamu
na kwa hakika hapakuwa na
haja ya kujitambulisha hivyo
muonekano wangu pekee ulitosha
kunitambulisha mimi dini gani.
Jibu lililotoka kwa askari ni kuwa.
Huyo mwenye ndevu ndiye
tunayemtaka.
Hapo hapo nikaanza kurushwa
kichurachura kuvuka barabara
huku nikipigwa. Baada ya kuvuka
barabara nikafungwa pingu. Hapo
nikaingizwa ndani ya gari ile ya
polisi hadi Central Police.
Nikiwa nje ya jengo la Polisi
nikavuliwa nguo zote nikabaki na
chupi tu. Nikalazwa kifudifudi
pembeni ya barabara huku
wakinipekua kuangalia kama

nina mabomu. Wakati wakifanya


upekuzi wakawa wanakoki silaha
na kuulizana kama wanimalize au
vipi.
Hapo hapo nikamuelekea Allah
na kutoa shahada kumpwekesha
Mola wangu na kushuhudia kuwa
Mtume Muhammad ni Mjumbe
Wake. Wale askari wakawa
wanaambizana wenyewe kwa
wenyewe kuwa, Hawa Waislamu
ni magaidi tu tummalize huyu.
Akatokea afande mmoja anaitwa
Mohamed. Huyu akauliza mbona
wale wengine mmewaachia?
Mwingine akajibu akasema, Hawa
wenye ndevu si wakuachia hawa
wanavunja vituo vya polisi.
Ni kweli Watanzania tumefikia
mahala pa watumishi waliopewa
dhamana ya ulinzi wa raia na
mali zao huku mishahara yao
ikitegemea kodi za wananchi hao
kuwatuhumu, kisha mashahidi
wakawa wenyewe na hatimaye
wanajigeuza mahakimu
kuwahukumu na kufanya kazi ya
askari jela na mnyongaji juu kwa
juu ilihali mahakama zetu zipo?
Akiendelea kusimulia anasema
kuwa wakati huo ilikuwa mida
kama saa mbili za usiku hivi
kiza kilikuwa kimeshaingia nami
nikaingizwa ndani ya jengo la
Central Police. Wakati nilipokuwa
nasulubiwa pale nje wapita njia
wote walikimbia sehemu ile pakawa
patupu huoni mtu, anaendelea
kuhadithia Ustaadh Yassin kwa
taabu na kuendelea.
Sasa nikafungwa pingu
kwa nyuma na nilipofika ndani
nikafungwa mnyororo kiunoni na
miguuni. Askari mmoja akaleta
tape measure akawa anapima
kanzu yangu hadi ilipoishia na
akapima pale ilipoishia kanzu hadi
unyayoni.
Nikaulizwa kwanini navaa
kilemba na kuweka ndevu.
Mimi nikajibu kuwa hayo ni
mafundisho ya dini ya Kiislamu
kama alivyofundisha kiongozi wetu
Muhammad (SAW) yeye katunasihi
tujifananishe na yeye.
Baada ya hapo anasema
wakaleta kiti wakamweka kisha
wakamuamrisha kunyanyuka na
akaingizwa kwenye kijichumba
kidogo wakafungua maji wakaanza
kummwagia.
Kwa mujibu wa Ustaadh Yassin,
maji yale yalikuwa yakitoka
katika pressure kali na ya
baridi na yalikuwa yanawasha
vibaya kiasi yalimuumia sana.
Ngozi yake ikaanza kuvimba, na
haukupita muda akawa hoi, nguvu
zikamwishia na akili yake anasema
akaihisi inapotea. Anasimulia kuwa,
walipoacha kumtesa wakaanza
kumhoji na wakamwambia kuwa
akikubali yale wanayotaka kuwa
yeye ni mshirika wa Alshabab wa
Somalia wangemjengea nyumba
pamoja na kumpa gari kwa madai
kuwa alishakuwa rafiki yao.
Kwa ufupi walimuuliza masuala
mengi yahusuyo tukio la Sitaki
shari na wakataka aeleze nani
alishirikiana nao katika shambulio
lile jambo ambalo alisisitiza kuwa
halijui kwa namna yoyote ile. Hapo
wakaanza kumtwanga makofi,
mateke, ngumi na shoti za umeme
hali iliyosababisha apoteze fahamu.
Nilipozinduka ndipo
wakanipekeka shimoni. Panaitwa
shimoni kwa sababu hizo selo
zipo chini ya jengo hilo na hata
magari yanapopita nje barabarani
unayasikia kwa juu. Hapo shimoni
nilikuta Waislamu wengi na baadhi
yao nikawafahamu. (anawataja
baadhi yao).
Nilikakaa shimoni nikiuguza
majeraha niliyopata mgongoni,
Inaendelea Uk. 7

8
BILA shaka wengi tunakumbuka
sakata la sensa ya watu na makazi
mwaka 2012. Baadhi ya Waislamu
waligoma kuhesabiwa kwa sharti
la kuwekwa kipengele cha dini ili
kuondoa utata uliojitokeza kuhusu
idadi ya watu kwa munasaba wa
dini zao. Serikali yetu ilipinga
sharti hilo.
Mgomo wa baadhi ya Waislamu
HAO ulitokana na taarifa zisizo
rasmi zilizopeperushwa hewani
na TBC. Tulipinga kauli za
madai kwamba, Waislamu tuwachache kwa kurejea takwimu
mbalimbali za sensa zilizotangulia.
Tulikuwa na haki hiyo kwa kuwa
hatujawahi kupewa taarifa za
kutokea maafa yaliyopelekea
Waislamu kupungua. Lakini pia,
hata idadi ya Waislamu kuingia
dini zingine haioneshi kuwa na
athari ya kutosha kufanya idadi ya
Waislamu ipungue. Tulichonyimwa
hapa ni VIGEZO vilivyotumika
kusema kwamba huyu ni Muislam
na yule siye! Na hapa ndipo lilipo
tatizo na utata ambao ulipelekea
Waislamu wengi kuingia matatizoni
kwa kupigwa, kudhalilishwa na
kushitakiwa.
Kila mmoja amepewa akili
na uwezo wa kufikiri tofauti na
mwenzake. Ndiyo maana Allah
Mtukufu amewasifu wale wenye
kufanya mambo yao kwa shura,
kwa kuwa yeye anatufahamu
zaidi kuliko tunavyojifahamu sisi.
Anasema Mwenyezi Mungu.
Katika dodoso la sensa, mtu
huulizwa mambo mengi ambayo
ndiyo msingi wa kupatikana taarifa
itakayokuwa na mchanganuo wa

Makala

JAMADUL AWWAL 1437, IJUMAA FEB 26-MACHI 3, 2016

Hoja si wingi

SHEIKH Ponda Issa Ponda.


idadi ya watu kwa mujibu wa
dini zao, umri na mfano wa hayo.
Nukta yangu ya msingi ni dini. Mtu
anapoulizwa kuhusu dini yake ni
rahisi sana kusema kwamba yeye
ni dini fulani. Halikadhalika, umri
na mengineyo ni katika mambo
hayampi tabu muulizwaji. Lakini

AN-NUUR

hebu tujiulize kwamba, hivi ni kweli


kila jibu ndiyo jibu sahihi!?
Allah anasema; Mabedui
wamesema: Tumeamini. Sema:
Hamjaamini, lakini semeni:
Tumesilimu. [Qur-an 49:14]. Hebu
na hapa pia tujiulize swali moja
tu la msingi, kwamba; aliyeamini
ni nani na aliyesilimu ni nani? Sisi
tuna kawaida ya kuitana waumini,
lakini ni kweli sote ni waumini!?
Ninachokusudia hapa ni kutaka
kuwatanabahisha ndugu zangu
Waislamu kwamba, kila sifa ina
vigezo vyake! Ili mtu awe muumini
hana budi kushabihiana na sifa za
wanazotakiwa kuwa nazo waumini.
Ili tuwe wanaharakati hatuna budi
kuwa na sifa za wanaharakati,
vinginevyo tutakuwa tumesilimu!
Mgomo wetu kwenye zoezi la
sensa ulikuwa sahihi mno lakini
nadhani kuna mahali tulitofautiana
katika uelewa. Pengine siyo uelewa,
lakini serikali yetu haikutuweka
wazi kuhusu vigezo wanavyotumia
kujua kuwa huyu ni Muislamu na
huyu siye hata kama anajinasibisha
na Uislamu. Kuitwa Suleiman, na
kadhalika haimaanishi kwamba ni
Muislam. Majina ya watu hayana
mchango wowote wa kumfanya
mtu ashabihiane na kundi fulani
kwa sifa, mwenendo, nidhamu yake
n.k.
Kumbukeni kwamba, zoezi

la sensa huwachukua mpaka


usalama wa taifa, wanajeshi, askari
polisi na makundi mengine. Hata
viongozi wa serikali pia huhesabiwa
japokuwa hudai kwamba serikali
haina dini! Kumbe hata serikali
ina dini lakini ambayo hudhirika
kwa matukio, misimu na au kwa
dharura! Sehemu kubwa ya watu
hawa, siyo ahlul-bayit! Nadiriki
kusema hivi kwa sababu ya matukio
mbali mbali ambayo wamekuwa
wakifanyiwa Waislamu na watu
wenye mamlaka, tena wenye majina
ya Kiislamu.
Maulamaa nitaomba mnisaidie,
anawezaje mtu kuwa Muislamu
naye haswali swala tano!?
Anawezaje mtu kuwa Muislamu
ikiwa anaongoza katika kupinga
Uislamu, kuuhujumu Uislamu,
anadumu na kuogelea katika
madhambi makubwa kama
ushirikina, zinaa, wizi, ujambazi
n.k.!? Ndiyo maana serikali haina
tabu hata kama ikatangazwa
redioni, televisheni kwamba
Waislamu ni wachache.
Ikiwa kweli sisi Waislamu ni
wengi, ni ipi athari yetu katika
jamii? Leo Uislamu unatafsiriwa
kimadhehebu, kimitazamo,
kimanhaj! Mtume Muhammad
(swallalahu alayh wa sallam)
alikuwa dhehebu gani? Tofauti zetu
hizi ndizo ambazo zimetufanya
tukagawanywa katika makundi
mawili ya bad muslim and good
muslim! Ni wakati gani na kwa
nani Muislamu anakuwa mbaya au
mzuri!? Hatujiulizi haya!?
Wabillah Tawfiiq!
Juma Jumanne [0659789468].
KATESH, MANYARA.

Kilio cha Waislamu kwa Rais Magufuli

Inatoka Uk. 7
ubavuni, miguuni na kifuani
kutokana na vipigo nilivyopata.
Sikuweza kulala kwa masiku.
Baadae nikapelekwa kituo cha
polisi cha Shitakishari, Buguruni
na Msimbazi pamoja na wenzangu
niliowakuta shimoni tukiwa
tukihamishwa siku baada ya siku.
Baadae tukarudishwa
shimoni pale tulipotoka Central
Police. Kutoka hapo sasa ndipo
tukapelekwa Oyster Bay kwa
mahojiano na Task Force ambacho
ni kitengo maalum kwa ajili ya
ugaidi.
Walionihoji hapo Task
Force waliniambia kuwa
mateso niliyokwishapata huko
nilikotoka ni madogo, hapo
nitapata mateso makubwa zaidi.
Wakanitahadharisha kuwa itabidi
nionyeshe silaha ziko wapi kabla
hawajanishughulikia zaidi anazidi
kuweka wazi Ustaadh Yassin.
Maswali yakawa ni yale yale na
akaanza kupigwa safari hii miguuni
baada ya kufungwa katika kitu
kama pipa ambacho kinashikilia
miguu. Anasema alipigwa hadi
akawa hawezi kusimama. Kutoka
hapo sasa akapelekwa Mikese,
Morogoro. Wakati anapelekwa
huko alikuwa amefungwa kitambaa
cheusi usoni.
Hapo Mikese ni sehemu ya
wazi hatukuwa ndani ya majengo.
Hapo panaitwa gereji, kwa
kuwa hapo ni sehemu makhsusi ya
kuwashughulikia Waislamu.

Hapo nilioneshwa kaburi na


nikaambiwa kuwa katika kaburi
lile amezikwa mvaa kanzu fupi,
kilemba na mfuga ndevu kama
mimi.
Nilivuliwa nguo na kuanza
kupigwa bakora nyingi sana
huku mahojiano yakiendelea na
mimi nikiwa uchi. Waliniambia
nikiri kuwa mimi ni gaidi. Mimi
nilikataa, anasema na kuendelea.
Kuna mwenzetu alivunjwa
mkono katika mahojiano na baada
ya kuvunjwa mkono kwa ajili ya
maumivu yale alikiri kuwa yeye ni
gaidi. Alinieleza kuwa yeye hakuwa
anahusika na yaliyotokea Sitakishari
lakini aliambiwa kuwa asipokiri
atavunjwa mkono wa pili na baba
na mama yake watakamatwa na
kuteswa kama alivyoteswa yeye.
Kwa ajili ya kuwanusuru
waazazi wake aliona bora
awakubalie wanalolitaka. Hapa
tulikuwa kama watu 18 kisha
wakaletwa wanawake watatu.
Siwezi kueleza yaliyowafika hawa
wanawake.
Nilipigwa sindano ambayo kwa
kweli sijui ya nini na kuanzia hapo
nilipoteza fahamu. Nilipozinduka
niliambiwa na walioniokota kuwa
walinikuta Mbezi Barabara ya
Morogoro na walidhani ni maiti.
Hivi sasa mimi ni mgonjwa kwa ajili
ya kipigo kile. Natokwa na damu
katika sehemu zangu mbili za siri.
Mufti naomba ukenda kwa Mkuu
wa nchi, kama hutojali, ongozana
naye huyu Ustaadh ili asidhani

labda umekwenda kuwachongea


hao vijana wake Task Force.
Sheikh Mkuu nimeona kibali
kilichoandikwa kwa niaba ya Katibu
Mkuu wa BAKWATA ambacho
naamini ni katika juhudi zako za
kunusuru maisha ya kijana yule ili
Waislamu na Watanzania popote
walipo waweze kumchangia pesa
za kujitibu. Lakini Muft kwanini
serikali isilazimishwe kama sio
kuombwa imgharamie Yassin na
kijana mwingine matibabu yao
kwakuwa inaonesha wazi wao
ndiyo chanzo cha matatizo yao?
Sheikh Mkuu tafadhali
namuomba akifika kwa Mtumbua
majipu amuulize sababu za
vyombo vya dola hususan askari
polisi kuwatendea watuhumiwa wa
ugaidi vitendo vya kinyama kama
alivyotusimulia Ustaadh Yassin
kabla hawajathibitisha ugaidi wao
ndiyo utawala bora wenyewe huu?
Kama vitendo hivyo havisawiri
na misingi ya utawala Bora
unaohubiriwa na viongozi wetu wa
serikali wawapo majukwaani, basi
wahusika wanayafanya hayo kwa
maagizo ya kiongozi gani?
Mheshimiwa Mufti, Watanzania
ambao ni waumini wa dini
mbalimbali wanajiuliza nini hatima
ya Taifa letu huko twendako ikiwa
hata kwenda kumjulia hali tu
ndugu yako Central Polisi nawe
unakamatwa na kujumuishwa na
watuhumiwa wa ugaidi?
Ukiachana na Ustaadh Yassin pia
yuko Said Michael Daniel, kijana

wa Kiislamu aliyesilimu miaka


minne iliyopita mkoani Mwanza
aliposukumizwa maabusu na
kubambikiwa kesi ya uvamizi wa
kituo cha Sitaki shari Ukonga jijini
Dar es Salaam baada ya Agost 17,
2015 kwenda kumuona ndugu yake
aliyemtaja kama miongoni mwa
ndugu zake wa karibu.
Muathirika huyo wa mateso hivi
sasa naye kama ilivyo kwa Yassin,
yupo uraiani akitokea gereza
la Segerea baada ya mahakama
kumwachia huru Desemba 31, 2015
kutokana na afya yake kuzorota
baada ya kipigo cha mfululizo.
Ikumbukwe kuwa, yanafanywa
haya yote huku viongozi wetu
tuliowapa dhamana ya kutuongoza
wakijinasibu kwenye luninga na
majukwaa ya kisiasa kwamba, nchi
yetu inaongozwa kwa mujibu wa
sheria, kanuni na taratibu.
Kwa ujumla Mufti hali siyo
nzuri kabisa iwapo haya ndiyo
yanayofanywa kwa ndugu zetu
katika imaan kabla ya kufikishwa
mahakamani, wakati Katiba ya
nchi Ibara ya 13 (b) inabainisha
wazi kuwa, ni marufuku kwa mtu
aliyeshitakiwa kwa kosa la jinai
kutendewa kama mtu mwenye kosa
hilo mpaka itakapothibitika anayo
hatia ya kutenda kosa hilo.
Nimalizie kwa kusema kuwa
nimemfikishia hiki kilio cha
Waislamu.
(Mwandishi anapatikana kwa
simu 0718 406242 Chuo Kikuu cha
Waislamu cha Morogoro.)

Makala

AN-NUUR

JAMADUL AWWAL 1437, IJUMAA FEB 26-MACHI 3, 2016

Kikwete atafanikiwa kusuluhisha mgogoro wa Libya?

Na Nizar Visram
TAREHE 1 Februari mwaka
huu tulitangaziwa kuwa
Rais mstaafu Jakaya Kikwete
ameteuliwa na Umoja wa
Afrika (AU) kuwa mwakilishi
wake katika mchakato wa
kusuluhisha mgogoro wa Libya.
Uteuzi huo ulifanywa mjini
Addis Ababa katika kikao
cha wakuu wa nchi za Afrika,
naye Kikwete amewashukuru
wakuu wa nchi za AU kwa
imani kubwa waliyoonyesha
kwake na pia amewashukuru
wadau wa siasa nchini Libya
kwa kuridhia uteuzi wake. AU
imemueleza Kikwete kuwa
inayo matarajio makubwa juu
yake na iko nyuma yake.
Katika jukumu hili, Kikwete
atakuwa anaongoza jopo la
marais watano walioteuliwa na
AU. Kazi yao kubwa itakuwa
ni kusuluhisha makundi
yanayounda serikali mbili
tofauti nchini Libya moja iliyo
mashariki ambayo inatambuliwa
na Umoja wa Mataifa (UN) na
ya pili iliyo katika mji mkuu wa
Tripoli ambayo inatawala kwa
kutumia majeshi.
Ni vizuri tukajiuliza kama
imani hii ya AU inatosha, kwani
bila shaka Kikwete atakumbwa
na matatizo yanayotokana na
mapigano yanayoendelea tangu
Libya kuvamiwa na majeshi
ya NATO, ikapelekea kuuliwa
kikatili kwa mtawala wa nchi
hiyo Muammar Gaddafi miaka
mitano iliyopita. Kikwete siyo
tu atakumbana na matatizo ya
ndani, bali pia na mataifa ya
NATO ambayo yana nia tofauti
na ile ya AU. Wakati AU inataka
ushuluhishi kwa njia ya amani,
NATO kama kawaida yake
inajiandaa kutumia nguvu zake
za kijeshi. Ili kulielewa hili ni
vizuri tukaangalia chimbuko la
mgogoro huu.
Mnamo mwaka 2011 Gadhafi
alipinduliwa na akauliwa
baada ya uvamizi wa majeshi
ya NATO. Walifanya hivyo
kinyume na azimio la Umoja wa
Mataifa (UN) ambalo halikutoa
idhini ya kuishambulia Libya.
Sasa imetimia karibu miaka
mitano na Marekani na wenzake
wa NATO wanapanga uvamizi
mwengine katika nchi hii
inayoongoza kwa utajiri wa
mafuta barani Afrika. Haya
yamesemwa na Marekani
wenyewe.

RAIS mstaafu Jakaya Kikwete

AL-Marhuum Muammar Gaddafi

Tarehe 27 Januari msemaji wa


makao makuu ya kijeshi nchini
Marekani (Pentagon), Bw Peter
Cook alikaririwa akisema kuwa
majeshi yake yanajitayarisha
kwa mashambulizi ya Libya.
Kazi inayofanywa sasa ni
kuchunguza ni kikundi kipi
wataweza kushirikiana nacho.
Pia kuna Jenerali Joseph F.
Dunford Jr. ambaye ni mkuu
wa majeshi ya Marekani. Tarehe
23 Januari mwaka huu alisema
nchi hiyo na washirika wake wa
NATO wanafanya maandalizi
ya uvamizi mwengine nchini
Libya ili kudhibiti ukuaji wa
majeshi ya ISIL (Daesh) nchini
humo. Hawa wengi wao ni
askari na wafuasi wa Gaddafi
ambao wamejichimbia katika
mji wake wa Sirte. Akaongeza
kuwa uvamizi huu wa kijeshi
utafanyika kwa kushirikiana na
serikali mpya ya Libya. Hii ni
serikali iliyochongwa na mataifa
ya NATO kupitia mwakilishi
wa UN Bw Martin Kobler.
Alipoulizwa ni lini wanatarajia
kuanza mashambulizi Dunford
alijibu itachukua wiki chache.
Licha ya Marekani nchi
zingine zilizo msitari wa
mbele katika uvamizi huu ni
Uingereza, Ufaransa na Italy.
Ndio maana tarehe 2 Februari
mwaka huu wawakilishi kutoka
nchi 23 walikutana mjini Rome
kuzungumzia uvamizi huu
wa pili nchini Libya. Hizi ni
nchi zilizoshirikiana na NATO
katika uvamizi wa 2011.
Walijadili mkakati wa kuwazuia
mujahidina wasidhibiti mafuta.
Kwa maneno mengine, wakati
AU inamteua Kikwete kwenda
kusuluhisha mgogoro miongoni
mwa makundi ya Libya, mataifa
ya kibeberu ya NATO yanafikiria
kutumia majeshi yao ili kudhibiti
mafuta.
Lakini jaribio hili halitakuwa
rahisi hata kidogo. Mnamo
2011 walitumia kisingizio
cha kuwaokoa raia kutoka
udikteta wa Gaddafy. Safari hii
wanasema adui ni mujahidina
wa ISIS (Daesh). Hii si rahisi
kukubalika kwani raia wengi wa

Libya wanapinga kuingiliwa na


majeshi ya kigeni.
Mnamo Disemba mwaka jana
makomando 20 kutoka Marekani
waliovalia kiraia walijipenyeza
nchini Libya wakiwa na
silaha. Mara moja wapiganaji
wa Libya waliwakamata,
wakawanyanganya silaha na
kuwafurusha kutoka nchini
mwao. Idhaa ya NBC nchini
Marekani ilipowauliza maofisa
wa Pentagon kuhusu tukio hili,
walikubali kuwa ni kweli, tena
wakaongeza kuwa makomandoo
wao wamekuwa wakiingia Libya
mara kwa mara.
Mataifa ya NATO
yakiongozwa na Marekani
yaliivamia Iraq na sasa yako
Syria. Matokeo yake katika
nchi hizi kimezuka kikundi cha
Daesh. Hata hivyo kikundi hiki
kinaonekana kupungua nguvu
katika nchi hizi. Daesh huko
Syria inaonekana inarudi nyuma
hasa baada ya majeshi ya Urusi
kuingia na kutumia ndege zake
za kivita ili kufagilia majeshi
ya rais Assad. Kwa hivyo
kuna uwezekano wa kutafuta
mahali pa kuhamia, na mahali
penyewe yumkini ni Libya.
Ni kwa sababu Libya kwanza
imegawanyika na haina serikali
moja ya kitaifa. Pili nchini
Libya tayari kuna mujahidina
wapatao 5,000 katika maeneo
ya mwambao nao wanaunga
mkono ISIS. Idadi hii inazidi
kukua pamoja na kudhibiti
uzalishaji na uuzaji wa mafuta.
Kwa hiyo wenzao wa Iraq na
Syria wanaweza wakakimbilia
Libya na kuanzisha kambi ya
mafunzo huko.
Katika hali kama hii Libya
inaweza kuwa makao makuu
mapya ya ISIS. Kutoka
hapa mujahidina wanaweza
wakasambazwa kuelekea
nchi za Kiarabu, Afrika ya
Kaskazini, ya Kati, Magharibi
na hata Mashariki. Wanaweza
kuendeleza harakati yao katika
nchi kama Nigeria, Niger, Chad,
Mali, Mauritania na Sudan. Pia
Libya imepakana na Tunisia
na Algeria ambako tayari kuna

mujahidina wenzao
Wanaweza wakaelekea hadi
nchi za Ulaya. Ikumbukwe
kuwa kisiwa cha Italy kiitwacho
Lampedusa ni maili 200 tu
kutoka Libya. Hili ni tishio
kubwa kwa nchi za magharibi.
Hivyo kinachotia hofu na
wasiwasi zaidi kwa mataifa
ya NATO ni kuwa hawa
mujahidina wa Daesh wanaweza
kutumia Libya ili kuvuka bahari
ya Mediterania na kuingia Ulaya
ambako tayari kuna vijana
watakaosaidiana na wenzao
kutoka Libya. Ikumbukwe kuwa
Daesh ni kikosi cha kimataifa
na wala si Waarabu peke yao.
Inasemekana wametoka nchi 60
duniani.
Nchini Libya majeshi
yanadhibiti sehemu kubwa
mashariki mwa nchi, wakati
makundi kadha ya mujahidina
yako magharibi ambako
wameunda Baraza la Vijana wa
Kiislamu (Majlis Shura Shabab
Al Islam - MSSI)
Ni mwezi uliopita tu Daesh
wamefanikiwa kudhibiti
machimbo mawili ya mafuta
maeneo ya mashariki ambayo
yanazalisha asilimia 80 ya
mafuta yote ya Libya. Inakisiwa
kuwa Daesh ina wapiganaji
takriban 3,000 na wanadhibiti
kilometa 300 za mwambao.
Wengi wao ni kutoka nje ya
Libya na wamekuwa wakipigana
nchini Iraq na Syria. Mnamo
Novemba walipouchukua mji
wa Darna walianza kubomoa
maduka ya manukato na
mapambo ya kina mama,
pamoja na saluni. Wengi wao
ni wafuasi wa Gaddafi ambao
waliingia mitini baada ya rais
wao kuuawa mnamo Oktoba
2011. Ni sawa na wafuasi wa
Saddam Hussein (Iraq) ambao
walijiunga na Daesh baada ya
rais wao kukamatwa mnamo
2003 na kunyongwa.
Leo wakati NATO
inajitayarisha kuivamia
Libya kwa mara ya pili, AU
nayo inamteua Kikwete
kusuluhisha kwa njia ya amani.
Inatukumbusha mwaka 2011
wakati AU pia ilijaribu kuzuia
mashambulizi ya NATO lakini
ikashindwa. Tarehe 23 Februari
2011 wakati vurugu zipoanza
nchini Libya, Baraza la Amani
na Usalama la AU (PSC)
lililaani utumiaji wa nguvu
kukandamiza maandamano ya
wananchi dhidi ya utawala wa
Gaddafi. Hata hivyo Baraza hilo
halikukubaliana na msimamo
wa NATO wa kuivamia kijeshi
Libya.
Tarehe 10 Machi 2011 PSC
ikaandaa mpango wa kuzuia
vurugu kwa njia ya maridhiano.
Pande zote zilitakiwa ziache
kutumia silaha na badala yake
zianzishe mazungumzo ya
amani. Kamati ya AU ikateuliwa
ili kufuatilia jambo hili kwa
kuonana na wahasimu.
Kamati hiyo ikaandaa safari

Inaendelea Uk. 16

10

Makala
Na Omar Msangi

MWAKA 2003 wakati


George W Bush anatafuta
kuungwa mkono na Rais
wa Ufaransa, wakati huo
Jacques Ren Chirac
katika azima yake ya
kuivamia Iraq, alitumia
vifungu vya Biblia
kuonyesha kuwa Saddam
Hussein alikuwa mtu
muovu na kwamba,
ilikuwa agizo la Biblia na
agizo la Mungu kwamba
Saddam apigwe. Bush
alinukuu kutoka Kitabu
cha Ezekiel juu ya habari
ya Gogu wa Magogu.
Neno la Bwana likanijia,
kusema, mwanadamu
kaza uso wako umwelekee
Gogu wa nchi ya Magogu,
mkuu wa Roshi, Mesheki,
na Tubali, ukatabiri juu
yake useme, Bwana Mungu
asema hivi, Tazama mimi ni
juu yako ewe Gogu mkuu
wa Roshi na Mesheki na
Tubai nami nitakugeuza na
kutia kulabu katika mataya
yako, nami nitakutoa
pamoja na jeshi lako lote,
.(hiyo ni Ezekiel 38).
Ukienda mbele katika
Ezekiel 39 unasoma:
Na wewe mwanadamu
tabiri juu ya Gogu useme
Bwana Mungu asema
hivi, Tazama mimi ni juu
yako ewe Gogu mkuu
wa Roshi, Mesheki na
Tubali nami nitakugeuza
na kukuongoza, nami
nitakupandisha toka
pande za mwisho za
Kaskazini nami nitakuleta
juu ya milima ya Israel na
nitaupiga upinde wako
utoke katika mkono wako
wa kushoto na mishale
yako nitaiangusha itoke
katika mkono wako wa
kulia. Utaanguka juu ya
milima ya Israel, wewe
na vikosi vyako vyote na
watu wa kabila nyingi
walio pamoja nawe,
nami nitakutoa na
kuwapa ndege wa kila
namna walao nyama na
wanyama wa nchi, uliwe
na wao. Utaanguka katika
uwanda kwa maana
mimi nimenena neno hili
asema Bwana Mungu.
Nami nitapeleka moto
juu ya MagoguNa jina
langu takatifu nitalifanya

AN-NUUR

JAMADUL AWWAL 1437, IJUMAA FEB 26-MACHI 3, 2016

Gogu wa Magogu!

Tatizo Makahaba wa habari


Kosa la Sheikh Msellem nini?

Rais wa zamani wa Ufaransa Jacques Ren Chirac (kushoto) akiwa


na Rais mwenzie wa zamani wa Marekani, George Bush.

KOMANDOO Erik Dean Prince


kuwa limejulikana kati
hivi leo umekuwa wa
ya watu wangu Israel
propaganda. Uwongo
wala sitaliacha jina langu
umefanywa uonekane
takatifu kutiwa unajisi tena, ndio kweli, huku uovu
nao mataifa watajua ya
ukifanywa ndio wema
kuwa mimi ndimi Bwana
na waovu na wauwaji,
na Aliye Mtakatifu katika
wakijifanya na kulazimisha
Israel.-Hiyo ni Ezekiel 39: waonekane na kukubalika
1-7.
kuwa ndio wasamaria
Katika kusoma utabiri
wema. Wanaodhulumiwa
na ujumbe huu kutoka
na kuuliwa kwa jeuri na
Ezekiel, Bush alikuwa
ukatili, wanaonekana ndio
amekusudia kumshawishi
wabaya na magaidi wa
Chirack kuona kuwa Gogu
kimataifa.
ni Saddam Hussein na
Mwandishi na
nchi ya Magogu, ndiyo
mchambuzi Justin King
Iraq. Na kwa maana hiyo,
ameandika Makala yake
wana wajibu wa Kikristo,
aliyoipa kichwa cha
kwa maelekezo ya Biblia,
habari, 10 Secret Armies
kwenda kumpiga Saddam
of the Central Intelligence
Hussein.
Agency. Humo anaeleza
Ulimwengu tunaoishi
na kuchambua vikundi

vya kigaidi vilivyoundwa


katika nchi mbalimbali
ili kulinda masilahi ya
mabeberu. Akielezea ile
Bay of Pigs anaonyesha
jinsi magaidi waliopewa
mafunzo na mabeberu
walivyoleta maafa
makubwa Cuba. Ukija El
Salvador unakutana na
death squads, wakiuwa
wanavijiji na wanaharakati
walioonyesha upinzani
dhidi ya serikali iliyokuwa
kibaraka wa mabeberu.
Anakuchambulia pia ile
Operation Cyclone ambayo
ndiyo iliyozaa Mujaheddin
wa Afghanistan, Al-Qaida
na ISIS.
Kwa upande mwingine,
mwandishi Finian
Cunningham katika Makala
yake Russia Lances the
Poison in Syria, anaeleza
jinsi Urusi ilivyowavuruga
mabeberu katika Syria kwa
ile hatua yake ya kuingia na
kuwapiga kikweli magaidi
wa IS.
Wiki iliyopita jarida la
Kikristo likiitwa LifeZette
lilichapisha Makala
likikumbushia tukio (la
uwongo) la IS kuchinja
Wakristo 20 kutoka Misri.
Executed Because They
Are Christians, ndivyo
lilivyoweka kichwa gazeti
hilo ikimaanisha kuwa
waliuliwa si kwa sababu
nyingine ila kwa vile ni
Wakristo. Katika Makala
hiyo iliyoandikwa na Fr.
Benedict Kiely, inaelezwa
jinsi IS walivyo katili na
kwamba hao IS, ni wafuasi
wa (Mtume) Muhammad.
Habari hii ambayo
imekaririwa na kupigiwa
sana debe na Fox News,
inachosema ni mambo
matatu. Moja ni kuonyesha
kuwa Wafuasi wa Mtume
Muhammad (s.a.w) ni watu
waovu. Pili, kwa uovu
wao huo, wanawachinja
Wakristo kikatili kwa vile
wanamfuata Yesu. Tatu,
Wakristo wanatolewa wito
kuungana na walimwengu
wote walio wema
kuunganisha nguvu zao
kupambana na magaidi
hao.
Yanayoelezwa hapa na
Fr. Benedict pamoja na
Inaendelea Uk. 11

11
Inatoka Uk. 10

Fox News, ndio yale yale


aliyosema Bush, kumwita
Saddam Hussein kuwa
ni Gogu wa Magogu.
Tofauti hapa ni kwamba
toka Saddam, wakati
ule ikiwa Al-Qaida, sasa
inapofikia IS, Gogu huyu ni
Waislamu wote na Uislamu
kwa ujumla na ndio haya
yanayowakuta akina Sheikh
Msellem Ali Msellem.
Ipo hivi, ili mkakati wa
mabeberu wa kutengeneza
jinamizi la kufunika maovu
yao wakati wanauwa watu,
kuvamia nchi mbalimbli
na kusambaza utando
wa kijeshi dunia nzima
ufanikiwe, ni lazima
watengeneze uwongo
unaonyesha kuwa hili
zimwi ni tishio la dunia
nzima. Kwa hiyo, kila
mahali lazima ionyeshwe
kuwa kuna magaidi na ni
hatari. Kama walivyounda
IS na Al-Qaida hapo awali,
wanaunda vikundi vya
kigaidi halisi na hewa
katika nchi mbalimbali na
kupitia propaganda, watu
wanaimbishwa wimbo wa
ugaidi.
Wimbo huo unapoletwa
huku kwetu tukaanza
kuimba na kukamata
watu wetu, tunachofanya
ni kutumiwa kuupalilia,
kumwagilia maji na
kuwekea mbolea
mkakati wa mabeberu
upate kustawi. Kustawi
kwenyewe kunaanza na
kumwandama Gogu wa
uwongo tukimwacha
muuwaji na fisadi wa kweli
pembeni. Baada ya hapo,
Gogu wa kweli anapata
nguvu ya kuvamia, kuuwa
na kupora kila mahali kama
anavyofanya hivi sasa Syria
huku akijifanya anampiga
Gogu wa Syria. Kama
Gogu Bush alivyompiga
Gogu bandia Saddam
Hussein, akimsingizia
kuwa ana Silaha za
Maangamizi (WMD).
Msomi na mchambuzi
Stephen Kinzer kutoka
Watson Institute for
International Studies,
Brown University,
anasema kuwa imekuwa
ni aibu ya Karne kwa
wandishi wa Marekani (na

Makala

JAMADUL AWWAL 1437, IJUMAA FEB 26-MACHI 3, 2016

Gogu wa Magogu!

ulimwengu) kutokana na
jinsi walivyoripoti suala la
IS katika Syria. Ufupi wa
maneno anachosema katika
Makala yake; The Media
are Misleading the Public
on Syria, ni kwamba wale
magaidi IS na wenzao
wengine wanaoungwa
mkono na Marekani na
NATO, ndio wanaoonekana
wakombozi wa Syria,
huku Urusi inayowapiga
kikweli magaidi IS,
inaonekana kuwa ndio
muuwaji. Katika lugha ya
Bush, anachosema Stephen
Kinzer ni kuwa wakati
Marekani na washirika
wake waliowatengeneza
IS na kuwatuma kazi
Syria, wanapaswa
kuonekana kuwa ndio
Gogu na kupigwa vita na

AN-NUUR

walimwengu wote, vyombo


vya habari vinafanya kazi
ya kuwaaminisha watu
kuwa Gogu huyo ndiye
mtu mwema, na kwamba
kila anayepinga uovu,
uvamizi na uporaji wa
Ma-Gogu wa kweli, ndio
Gogu. Hili ndilo analosema
Stephen kwamba ni aibu
ya Karne kwa wandishi wa
habari.
Makahaba wa habari
"Asubuhi hii nilijikuta
nimeganda mbele ya
'taarifa ya habari; ya shirika
la Fox News kwa muda
mfupi na baadaye taarifa
nyingine ya National Public
Radio (NPR). Ilitosha
kunihakikishia kuwa
propaganda ya kifashisti
wakati wa utawala wa
wafuasi wa Adolf Hitler

nchini Ujerumani (wakati


wa Vita Kuu ya Pili
Duniani), ilikiwa laini
sana ukilinganisha na
kufyatuliwa wakati wote
wa mtiririko hatari wa
uwongo na vyombo vya
habari vya Marekani.
Haya ni maelezo ya
mwandishi Paul Craig
Roberts katika Makala
yake Presstitutes At Work,
akieleza na kuchambua
uwongo unaosambazwa
na Magazeti ya New York
Times, Washington Post
na vyombo vingine vya
habari vya Magharibi juu
ya kinachoitwa vita dhidi
ya ugaidi na akizungumzia
zaidi hali ilivyo Syria na
magaidi wa IS. Anasema,
vyombo hivyo vya
habari, alivyoviita watoa
propaganda ya kuzoa tu
isiyochujwa na bila kuhoji
taarifa yoyote inayotolewa
na serikali ya Marekani,
kwamba vinawalisha watu
uwongo vikidai kuwa
tatizo lote nchini 'Syria
linatokana na Warusia na
Rais Bashir al-Assad wa
nchi hiyo. Kwa upande
mwingine vinawatia watu
ujinga kwa kuwaaminisha
kuwa Marekani haina
cha kulaumiwa kabisa.
Kwamba, eti, Marekani
inachofanya ni kupambana
na ISIS, wakati ni nchi
hiyo iliyounda IS na
inayoendelea kuwalea,
kuwapa nguvu IS na
kuwatumia kuleta maafa
Syria kwa lengo la
kumngoa Bashar Assad.
Watoa propaganda na
kusambaza uwongo huu,
ndio wale wale waliokuwa
wameiongopea dunia
kuwa Saddam Hussein
alikuwa na "silaha za
maangamizi. Wakadai
kuwa huyo ni Gogu wa
Magogu, wakaivamia Iraq
na kuiharibu na mpaka sasa
wanafanya ufisadi nchini
humo.
Kama alivyosema Paul
Craig Roberts, kwa hakika
wanaotumiwa kupika na
kusambaza uwongo na
propaganda hizi chafu,
hawastahiki kuitwa
wandishi wa habari, bali
makahaba wa habari.
Kwa bahati mbaya hawa
Inaendelea Uk. 14

12

Safu ya Ben Rijal JAMADUL AWWAL 1437, IJUMAA FEB 26-MACHIAN-NUUR


3, 2016

Miti na maisha yetu-5

WASANII hupenda kuzungumzia


viumbe mbalimbali na hata
kuweza kuvishabihisha na
wanadamu. Utasikia midomo
mekundu useme zuwarde, miguvu
yake useme tembo, anasema sana
useme chiriku, ananuka useme
Fungo, anameremeta useme mbwa
la mwezi n.k.
Hebu tumuangalie mshairi na
ubeit wake juu ya Chungwa.
Chungwa
Ladha ya chungwa si sawa, hata
liwe susu moja
Utamu wa kila chungwa,
walionja moja moja
Wala sijaota mbawa, nisemayo
yana hoja.
Hapo tunamuona mshairi huyu
na chungwa kaja na kitendawili
lakini hicho nakuachia wewe
msomaji ukifasili, na ilivyokuwa
tutakuwa na kusara ziada hivi
karibuni za wasomaji, nategemea
kupata tafasili kutoka kwako wewe
msomaji.
Jina la kitaalamu la Chungwa ni
Citrus sinensis katika Familia ya
Rutaceae.
Watakayoisoma makala
haya labda asilimia 1 au 2 ndio
wataokuwa hawajapatapo katika
maisha yao kula chungwa.
Kuna Chungwa, Danzi, Chenza,
Limau, Kangaja, hizi zote ni
katika mkumbo wa machungwa.
Chungwa aghlabu huwa tamu
lakini hupatikana matamu na
yaliokuwa sio matamu. Danzi asili
yake ni chungu na nadra watu
kula madanzi ila mara nyingi
hutengenezewa siki ya madanzi.
Chenza nazo huwa zilizo tamu na
kinyume chake. Limau chungu
hutengenezewa zaidi kutia chapuo
mchuzi, Kangaja mara nyingi huwa
kali.
Katika kumbukumbu za
tarehe tunasoma kuwa Wachina
walilielezea chungwa kwa dahari
kwani katika mwaka wa 314 kabla
ya kuzaliwa Mtume Issa AS (BC)
Wachina walikuwa wanalieleza
chungwa lilivyo na utamu wake,
kwa hio asili ya machungwa
yalitokea bara la Asia na kuenea
India kisha wavumbuzi wa Ulaya
kuyaeneza dunia nzima.
Machungwa yalifikia Ulaya
kupitia mlango wa Ureno
na walikuwa Waislamu ndio
walioyafikisha katika nchi ya
Ureno na ya kashamiri.
Kiarabu chungwa ni Burtukal,
Waarabu wakaita nchi ya Ureno
Baladi Burtugal yaani nchi ya
Machungwa na wenyeji ikawa
tabu kusema Burtugal wakisema
Portugal na ndio likapatikana jina

MACHUNGWA ni kati ya matunda muhimu kwa maisha yetu.


Aidha muhimu kwa kuendeleza chumi zetu. Katika Afrika
machungwa huwa ni zao tu, hata mtu saa nyengine huona apande
mchungwa nayeye ahesabiwe ana michungwa lakini sio kwa
kujenga dhana ya kujiendeleza na ukulima wa michungwa.
Nchi ya Afrika ya Kusini, Misri na Morocco ndio katika nchi
za Kiafrika waliojizatiti na kilimo cha machungwa na kuuza
Ulimwenguni, juu ya hayo bado kazi pevu inahitajika.
Duniani leo kila ifikapo asubuhi katika nchi za Ulaya
na Marekani katika kila nyumba 5 utakuta nyumba mbili
wanaburudika na sharubati ya machungwa, huku kwetu walaji
machungwa husubiri msimu.

Machungwa yakiwa yapo sokoni


la nchi ya Ureno.
Machungwa hunawiri
katika maeneo ya tropiki na
yanayokaribiana na tropiki. Katika
fruti ambayo inaliwa kwa wingi
duniani ni chungwa na ingawa
yanazalishwa zaidi katika nchi za
joto-tropiki lakini walaji wengi
wapo nje ya nchi za tropiki.
Hebu tuyaangalie majina ya
machungwa kutokana na lugha
mbalimbali, Kiengereza hujulikana
kwa jina la Orange, Kijarumani
Apfelsine, Kitaliana Arancia,
Kispeni Naranja, Kiarabu Burtukal,

Kiafrikana Lemoen, Waalbania


huita Portokall, watu wa Bosnia
hulita Naranda, huko Brazili
huitwa Laranja, huko Czech
hujulikana kwa jina la Pomeran,
Wadenmark hulita Appelsin,
Estonia Apelsin, Finland huitwa
Appelsiini, huko Hungary hulita
Narancs, Iceland Appelsna.
Watu wa Indonesia
huitachungwa kwa majina ya Jeruk
; Limau Manis, Kilingala husema
Lilala, Wabuki huita Voasary,
Malay Limau manis, Norway
huitwa Bokml appelsin, Wapolish

MAITI alizokumbana nazo Christopher Columbus zikiwa ni


wahanga wa Scurvy.

hulita Pomaracza, Wareno


Laranja, Washona hulita Ranjisi,
Waslovak Pomaranc, Wasomali Liin
xaali, Watgirinya huita Burtukhan,
Waturuki husema Portakal,
Wavitnam huita Qu cam, watu
wa Welesh huita Oren., wenyeji wa
Wolof huita Sorance.
Faida za Chungwa : Chungwa
lina faida mbalimbali hebu tujaribu
kuziangalia faida zitokanazo na
chungwa. Chungwa lina Vitamini
zifwatazo C, A, B2, B1. Hii vitamini
A husaidia kuondokana na kutoona
usiku (Night blindness), kuna
watu hupatwa na maradhi ambayo
huwa afikapo usiku kile ambacho
akiweza kukiona nyakati za
mchana kwenye nuru, ifikapo usiku
huwa hawezi kuona, matokeo hayo
huwa mtu huyo ana mapungufu
ya vitamini A kwa hio hushauriwa
kula machungwa. Aidha ugonjwa
utokanao na kutokwa na damu
kwenye ufizi husababishwa na
ukosefu wa Vitamini A na mgonjwa
huelezwa atumie machungwa.
Mvumbuzi wa mabara,
Christopher Columbus aliathiriwa
na abiria wake kutokwa na
damu kwenye fizi zao, ingawa
inazungumzwa juu juu maradhi
hayo na Christopher Columbus
alivyosafiri na kuvuka bahari ya
Atlantic wengi wa mabaharia wake
waliathirika na kotokwa na damu
kwenye fizi kwa kukosa matunda.
Mvumbuzi huyu alipofika
La Isabela ambayo ni Puerto
ilioko Dominica alikuta mji huo
ni mahame kutokana na watu
wake kusumbuliwa na Malaria,
Fluu, Kifua kikuu na Kaswende,
lakini uchunguzi mkubwa wa
kitaalamu wa mambo ya kale
imekuja kuelezwa kuwa kutokwa
na damu kwenye fizi (Scurvy) ndio
iliokuwa sababu kuu ya kuchukua
maisha ya watu wengi wa kisiwa
hicho na kufanya kisiwa hicho
alipopita kuwa mahame (Rejea :
http://www.ancient-origins.net/
news-general/first-colonists-ledchristopher-columbus-hit-severescurvy-001572)
Katika faida za chungwa
Sharbati ya chungwa huwa
na protini nyingi. Maganda
yake hutengenezewa sabuni na
huongezwa vionjo vya utengenezaji
wa jamu. Baadhi ya mafuta
ya kupikia hutumia mbegu za
machungwa. Chungwa ni mjarab
kukuweka mbali na maradhi ya
ngozi, kupata mtoto wa jicho, na
kusumbuliwa na tumbo. Sharbati
ambayo hutengenezwa kutokana
na machungwa yalio matamu sio
danzi wala limau husaidia sana
kudhibiti maradhi ya vidonda vya
tumbo. Bilauri mmoja ya sharubati
ya machungwa ni bora koliko kula
kidonge cha Vitamini C.
Nchi zinazozalisha machungwa
kwa wingi duniani: namba moja ni
nchi ya Brazil ambayo huzalisha
tani milioni 35.735, Marekani15.864,
China14.507, India 10.936, nchi ya
Mexico 8351, Spain 3.563, Misri
3.174, Uturuki, Utaliano 1.938 na
nchi ya Afrika ya Kusini huzalisha
tani milioni 1.725 (Rejea: http://
worldknowing.com/top-10-largestorange-producing-country-in-theworld/)
Nchi zinazosafirisha machungwa
kwa wingi duniani inayoongoza
ni nchi ya Brazil husafirisha
machungwa yafikao tani 1, 298,
Inaendelea Uk. 15

13

Safu ya Ben Rijal

AN-NUUR

JAMADUL AWWAL 1437, IJUMAA FEB 26-MACHI 3, 2016

Masheikhe wetu: Sayyid Omar Abdalla (Mwinyi Baraka)-3


KATIKA makala iliopita nilijaribu
kuonyesha kusoma kwake na
tumeona kuwa Sayyid Omar
Abdalla kwanza alikwenda
kusoma Chuo cha SOAS na
kupata shahada ya Diploma
ambayo ndio aliokuja nayo na
kuwa sasa kishakuwa msomi
anayotakiwa kuwa anaongoza
Chuo cha Kiislamu Muslim
Academy ingawa mwenyewe
alikuwa akiona kuwepo na pengo
na kuwa hajaelimika atakavyo.
Baada ya kurudi masomoni na
kuwa anashirikiana na watawala
katika kuweza kukiendeleza Chuo
cha Muslim Academy, Sayyid
Omar alihudhuria mikutano
mingi na hata ikajiri afike Nigeria
kwenda kuweza kuangalia namna
wao wanavyoendesha masomo
ya Kiislamu katika nchi ambayo
Kiengereza kinatawala na kipo juu.
Unapopitia nyaraka mbalimbali
saa nyengine unahangaishwa
kufahamu mtawala Muiengereza
katika utawala wake namna
ambavyo alivokuwa anaziangalia
dini kuu mbili na kuhakikisha
kuwa hazipishani na wakati huo
huo anakuja na upendeleo kwa
upande mmoja halafu upendeleo
huo unakuja unafichwa na
kuonyeshwa juhudi za kuwaweka
waumini wa dini kuu mbili
Afrika ukiwa Uislamu na Ukiristo
kuwa upo sawa. Muiengereza
alikuwa amejaribu katika nchi ya
India, Sudan na Nigeria kuweka
mtaala wa elimu ya dini ya
Kiislamu ambao unafahamika na
utaweza kutumika unavyostahiki,
aidha alifanya katika nchi hizo
kuwa na Makadhi pamoja na
Mahakama zake ambazo Waislamu
hawatakuwa na shida na ili
kuweza kuyatolea ithibati hayo,
utayaona katika kumbukumbu
za kuanzishwa kwa Muslim
School. Mkoloni alijaribu kukaa na
viongozi mbalimbali wa dini na
wasomi wa kuiweka Ofisi ya Kadhi
na Mahkama yake, na akahakikisha
kuwa wale wasomi wanaofahamika
na wenye ujuzi ndio wakupewa
nafasi ya kuongoza kuanzia Kadhi
na watendaji wake. India na Sudan
walifanya vizuri sana katika
kujipanga kwa mitaala ya dini ya
Kiislamu. Utaona hadi leo Sudan
wana taratibu nzuri ya kuwanisha
baina ya uongozi wa dunia na
akhera.
Sayyid Omar bin Abdalla
alipata fursa ya kwenda Nigeria
na alivutiwa kuona mpangilio
wa mitaala ya Madrasa namna
ilivyopangiliwa namna walimu
walivyofunzwa namna ya
kumsomesha mtoto kujua kusoma
Quran na Sheria na hapo hapo
kufunzwa msingi wa mwanzo
wa lugha ya Kiarabu, kujua vitu
mbalimbali vinaitwaje kwa Kiarabu
hasa vile vilivyomzunguka. Haya
yalimvutia sana Sayyid Omar
Abdalla na safari yake hio ya
Nigeria ilikuwa akipenda kuielezea
katika mihadhara yake na kuanza
kuandaa mipango ya utekelezaji
kwa Zanzibar na Afrika ya
Mashariki kwa jumla.
Sayyid Omar aliporudi Ulaya
akawa anasoemsha dini katika

MAKALA Haya nitamalizia juu ya kusoma kwake, kufanya


kazi kwake na misukosuko ya hapa na pale aliokumbana nayo.
Tunaona katika nyakati mbalimbali wasomi wa Kiislamu hupata
misukosuko ya kila aina hasa kwa kufanyiwa fitna na wengi
wao humalizikia kuwekwa korokoroni na kuonekana kama ndio
shahada ya kuwa mlinganiaji wa dini ya Kiislamu. Wengi wao
huwekwa korokoroni na Waislamu wenzao. Kuna maandiko
yanaonyesha kuwa Sayyid Omar Abdalla kafungwa mara mbili
kwa misimamo yake, lakini unapopitia kumbukumbu mbalimbali
na kufanya mahojiano na mtu ambaye alibahatika kuwa naye
Zanzibar, Uiengereza na kufungwa pamoja naye anathibitisha
kuwa kafungwa mara mmoja tu.

Sayyid Omar Abdalla na Maalim Zubeir Rijal katika ujenzi wa taifa


Skuli ya Teacher Training na akaja
kuwa Mwalimu Mkuu wa Skuli
ya Muslim Academy kwa hakika
alikuwa anaposemesha dini mara
zote akipenda kuingiza na taaluma
yake alioipata Chuo cha Makerere
College ikiwa elimu ya viumbe
(Biology).
Ilipofika mwanzo wa miaka ya 60
Sayyid Omar Abdalla alifanikiwa
kupata Scholarship nyengine
kwenda Uiengereza. Wakati huo
akiwa Muiengereza akijua makoloni
yanamtoka lakini alianza kujisafisha
na kuweka nidhamu ambayo kila
mwaka akijaribu kuhakikisha
wanafunzi wangapi wanakwenda
nje kusoma masomo ya juu na
Zanzibar kwa wakati wake ikiwa
na idadi ya watu 300,000 ukichukua
na asilimia na uwastani wake
ilikuwa na wanafunzi wasiopungua
400 wakiwa wapo nchi za kigeni
wanasoma, wengi wao walikuwepo
Misri kwa program ya Gamal
Abdulnasir na wengine wakiwepo
Uiengereza, Iraq, Marekani, India
na kwengineko.
Sayyid Omar Abdalla alijiunga
na Chuo Kikuu cha Oriel College,
Oxford na safari hii akafanya
shahada ya Masters ambayo somo
lake lilikuwa juu ya Falsafa na hapa
ndipo mkanganyiko nitajaribu
kuweka sawa na haya ninayosema
nasema kwa kupitia Faili lake na
mazungumzo nna murid wake
Sheikh Ahmed ambaye kawa
naye hapa Zanzibar kama katika
wanaohudhuria mihadahara

yake na kuwa naye kwenye rubaa


za kheri na wakawa pamoja
Uiengereza na wakafungwa jela
pamoja.
Katika Chuo cha Oxford Sayyid
Omar Abdalla alisoma somo la
Falsafa (Philosophy) alipokuwa
anajifunza somo hili alionyesha
maajabu mengi namna alivyokuwa
akiweza kuona wana Falsafa
watangulizi wa Kiyunani kina
Aristotle na wengineo walivyokuja
kuwa athiri wasomi wa Kiislamu
kama Ibn Sinna (Avicenna) na
kuweza kuwafahamu wana falsafa
wa Kiislamu ambao wengine hata
roho walikua wakielezea katika
kitu chengine ambacho kitabaki
na kuondoka na kurejea kwa njia
nyengine.
Sayyid Omar alivutiwa na
Mwanafalsafa Ibn Bajja na Imam
Ghazali na unaposoma Risala
yake ya mwisho Chuwomi Oxford
(Thesis) alioipa jina Some Felicity
in Medieval, Islamic Philosophy
ndio utapofahamu kwanini
alishikana na Ibn Bajja akawa tafauti
na Ibn Rushd, hawa kina Ibn Rushd
na Ibn Sinna waliuweka pembeni
Uungu na wakenda katika nadharia
ambayo mwanadamu ameiasisi.
Sayyid Omar alivutiwa zaidi na
Imam Ghazali ambaye akiweza yeye
kumfahamu zaidi, Imam Ghazali
alianza kuzama na nadharia za kina
Aristotle, kisha akazama kuona
Uungu na umoja yaani si umoja
huu lakini upweke wa Allah kuwa
hakuna mwengine wa kuabudiwa

ila ni yeye tu katika mamlaka yake


na uongozi wake.
Leo katika elimu ya Ikolojia
(Ecology) kunazungumzwa juu ya
mwindaji na mwindwaji na haya
Imam Ghazali katika kitabu chake
cha Ihya Ulumu Deen anagusia
na utafahamu utapomsikia Sayyid
Omar Abdalla alivomfahamu Imam
Ghazali, naye kuwa na uelewa wa
somo la ilimu ya viumbe. Imam
Ghazali akifahamisha namna
ya ndege Allah alivyomjaalia
kuwa kila saa awe anakula kisha
anakitoa chakula kama kinyesi,
anakula tena na kurudia kula,
Imam Ghazali anaeleza kuwa
kuumbwa kwa ndege kuwa na
umbo dogo ni kwasababu awe yupo
natunaendelea kuwaona kwa dahar,
lakini kuweza kubakia kwake ndege
kuepukana na maadui awe kila
akila akikaa awe hashibi baAda ya
muda mdogo anataka kula tena na
hio inamfanya kuwa kwa udogo
wake angekuwa anakula na kushiba
basi maadui wake kina nyoka na
wengine wangewamaliza kirahisi,
hapa ndipo kuna kazi kufahamu na
inataka malinganisho ya ilimu ya
dunia na akhera.
Katika somo la Ikolojia haya
maingiliaano wanayaita Predator
prey relation) na Sayyid Omar
Abdalla nilimsikia anamuelezea
Imam Ghazali kwa wigo wa Ikolojia
na namna wanyama wanavyopotea
kutoonekana tena (Extinct) ni
namna Allah alivyopanga vipi
viumbe viweze kupambana na
wengine na kujihami na kuendelea
kukuwepo, Falsafa ya Imam Ghazali
ilimvaa vya kutosha na Sayyid
Omar Abdalla alifika hadi hawezi
kutoa mhadhara baada ya kutoa aya
chache na kuja na hadithi za Mtume
Muhammad (SAW) asimgusie
Imam Ghazali. Bahati nzuri hii
risala yake ya Oxford imechapishwa
na vyema ukaipata ukaisoma.
Sayyid Omar Abdalla alirejea
Zanzibar mwaka wa 1963 baada
ya kumaliza masomo yake hapo
Oxford na alifika kuwa na kasi
kubwa ya kutoa mihadhara na
akipata nafasi iwe kwenye hitima,
majlisi, radio au popote pale
akichukua nafasi hio kuweza kutoa
mawaidha mazito ambayo ni zaidi
yalikuwa ulinganisho wa dini ya
Kiislamu na Kikiristo.
Yalipotokea Mapinduzi ya
1964 alikuwa ni mwalimu bado
hakuyapa kisogo aliendelea kufanya
kazi na kwenda sambamba na
mabadiliko yaliotokea, ithibati ya
hio ni hio picha ya ujenzi wa uwanja
wa Amani, akiwa yumo katika
ujenzi wa taifa na huku ana shoka
anachanja mnazi.
Matokeo machache juu ya
Sheikhe huyu: Sayyid Omar
Abdalla ilikuwa kila siku ya
Ijumaa akipenda kuwa na rubaa
na wenzake ya kumuomba Mungu
katika zile taratibu ambazo Mola
anasema Niombeni nikujibuni
yeye na wenzake waliweka taratibu
ya kuleta maombi au tuite Nyiradi
siku za Alkhamisi na Ijumaa,
katika mwaka wa 1968 alikamatwa
na wenzake kama 25 kwa
Inaendelea Uk. 15

14

MAKALA/MASHAIRI

Laata na Ng'uza

Mmengia Lata na N'guza, Wakidai wao Mungu


Nasi bila kuchunguza, tukavaa zao pingu
Sasa wanatutiza, Kwa idhara na virungu
Miujiza walisema, tutaiona haraka
Wagonjwa wangesimama, na Wafu wangefufuka
Nyati hangekuwa kima, na Simba akawa paka
Edai neema Lata, majumbani zitajaa
Shida tutaitafuta, na raha zitatuvaa
Yote hatukuyapata, labda nyingi balaa
Simba amekuwa paka, na paka hajulikani
Nyati kageuka nyoka, atambaa majanini
Kima juu anashuka, ataka kazi za Ndani
Bata amekuwa chui, na ng'ombe kawa pelele
Kuku hawafi kwa ndui, wamalizwa na uzile
Na mdudu buibui, ala shina na viale
N'guza ataka tutii, Kwa Kadiri apendavyo
Lakini hayajutii, mambo yetu Kenda ovyo
Wanyonge hasaidii, wanabaki hivyo hivyo
Kwa nguvu Lata, adai tumpe sijida zetu
Anasema hamjui, Mtume na mola wetu
Lakini hayaondoi, Mabaya yalofurutu
N'guza yeye atunyima, tusile ashibe yeye
Atesa hata wanyama, hajali hata nduguye
Kimhoji utamkoma, kusema ukujutiye
Lata adai na nguvu, ahuuwisha akifisha
Kisema anaubavu, makubwa kuyadogosha
Atia Watu makovu, wanyone aadabisha
N'guza atwaa ya kwake, na yaliyomzunguka
Vyote wiwe chini yake, Tumuombe tukitaka
Ni Bahari tumbo lake, Lazibeba hata taka
Jichole lina mtoto, Lata haoni vizuri
Japo mwembamba Kya fito, vazi lake ni Kiburi
Kwa maneno ya mkato, Lata yeye ni Tajiri
N'guza japo anaona, rangi zote hazijui
Kwake zote za fanana, nyeupe na baibui
KAZI yake kutubana, vyetu Vimo havikui
Ng'uza Atisha wavyele, Kwa visu na hizirani
Ataka wote Walale, ahodhi vlivyondani
Wabakie vile vile, na KAZI Yao ya mwani
Wadai tuwahamidi, hata Kama zumbukuku
Kubwa wafanya juhudi, tutii zao shauku
Kuwakana sina budi, Si Mungu ni makhaluku
Wote hawana Amana, wakisema hawatendi
Ya ukweli wayakana, uungwana hawapendi
Wa baya wao ni Wana, wakusanya Kwa makundi
Wao siwakamilifu ndo, mana nawabeza
Na wala singii hofu, wito wao kupuuza
Katwaani siwasifu, japo kwenu tachukiza
Kasoro zao ziwazi, kila Mtu azijua
Ni vimbe wa Azizi, na hili walitambua
Mungu hawi na kizazi, na sifa ya kupungua

AN-NUUR

JAMADUL AWWAL 1437, IJUMAA FEB 26-MACHI 3, 2016

Gogu wa Magogu!
Inatoka Uk. 11

wanaotenda aibu
hii ya Karne, BBC,
Fox News, New
York Times, CNN,
na wengine, ndio
walimu wetu na
tumekuwa kama
vipaza sauti vyao.
Kwa hiyo tunaingia
katika ukahaba
huu, tena kwa
namna mbaya kabisa
inayotudhuru sisi
wenyewe.
Wanasiasa wetu na
watendaji serikalini
na katika vyombo
vya dola nao ni
hivyo hivyo. Bush,
Obama na Cameroon,
wakisema yule ni
Gogu wa nchi ya
Magogu, mkuu wa
Roshi, Mesheki na
Tubai, apigwe, nasi
tunaimba wimbo huo
huo. Bila kujua kuwa
tukiwapata akina
Gogu wetu bandia,
ndio tunamfungulia
milango Gogu wa
kweli aweke kambi
zake za kijeshi
apate kutudhibiti
kisawasawa na
kupora atakacho na
atakavyo. Agenda
yake ya Hegemony
inatimia.
Dhul-Qarnayn
Katika Quran
Gogu ametajwa
kama Yaajuju na
Maajuju ambapo
ilibidi apatikane Dhul
Qarnayn wa kujenga
ukuta mkubwa na
madhubuti kumzuiya
Yaajuju kuingia
katika miji ya watu
kufanya ufisadi. Ili
kuepuka ufisadi,
uovu na agenda
chafu zilizobebwa
na vita hii feki
dhidi ya ugaidi,
Dhul-Qarnayn

tunayemuhitajia ni
vyombo vya habari
na wanasiasa walio
tayari kusema ukweli
na kufichua uwongo.
Na kwa maana hiyo,
ule ukuta aliojenga
Dhul-Qarnayn,
kama ilivyokuja
katika Surat Kahfi, ni
kusema ukweli.
Mwandishi
Finian Cunningham
amefanya utafiti
na kuandika
alichokiita Pentagon
Mercenaries:
Blackwater, AlQaeda whats in
a name? Humo
anaeleza jinsi
makampuni binafsi
yanavyotumiwa
kutengeneza magaidi
wa kuwafanyia kazi
mabeberu. Anatoa
mfano wa Komandoo
Erik Dean Prince
ambaye zamani
alikuwa katika
kikosi maalum cha
makomandoo wa
jeshi la Marekani
(US Special Forces
commando) ambaye
sasa hivi ameanzisha
kampuni iitwayo
Blackwater (baadae
Xe Services and
Academi), ambayo
imekuwa wakala
mkuu wa Pentagon
katika kuunda
na kutengeneza
wapiganaji binafsi
(rebels). Kampuni
hii imefungua tawi

Mashariki ya Kati
likijulikana kwa jina
la Reflex Responses au
R2. Na kwa mujibu
wa taarifa moja ya
The New York Times,
R2, ndiyo inafanya
kazi ya kutoa
mafunzo na kuunda
vikosi vya magaidi na
wapiganaji waliopo
Yemen na Syria.
Sasa kama
wapo vijana wetu
wa Kitanzania/
Afrika, walionasa
katika chambo
cha makachero
na majasusi wa
mabeberu, tusiwaone
kuwa hao ni Gogu.
Tujue kuwa ni
waathirika tu wa
mbinu chafu za
Gogu na mikakati
ya akina Erik Prince
na R2 zao. Kwa hiyo
tutafute namna ya
kuwatibu. Sio kupigia
zumari u-Gogu wao
bandia. Tutakuwa
tunawafanyia kazi
akina Bush.
Kama tuna
matatizo na Sheikh
Msellem juu ya
msimamo wake
katika siasa zetu,
tuseme lililo la kweli.
Tusiparamie agenda
ya akina Bush ya
kutumia vipengele
vya Biblia kumwita
Saddam Hussein
kuwa ni Gogu wa
Magogu.

15

Habari/Makala

Nasaha
Umuhimu wa kuchunga wakati
KILA sekunde moja
inapoondoka, hairudi na
wakati wako wa maisha
unazidi kupungua. Saa,
siku, wiki, mwezi, mwaka,
muongo na hata karne,
ni vipindi vya muda na
nyakati, ambavyo vikipita
havirudi tena. Kadiri
wakati unavyopita na umri
nao unasogea kuelekea
ukingoni mwa maisha.
Kwa kuwa muda
au nyakati zinapita na
kupunguza umri, basi
kuna haja ya wanadamu
kutafakari juu wa wakati
walinao. Anafanya nini na
kwa maslahi gani.
Wakati ndio unaotoa
fursa ya kupanga ratiba
ya kutenda na kuwa na
mpangilio wa maisha ya
kila siku. Kwa mantiki hiyo,
haliwezi kuwa jambo zuri
kwa wanadamu kupoteza
wakati. Tusipoteze muda
kwa kufanya mambo ya
kipuuzi hali ya kuwa kuna
mambo mengi, ambayo
yanaweza kutushughulisha
na yenye faida hapa
Duniani na huko akhera.
Kwa msingi huo, ni
vyema Waislamu wakawa
mfano wa kutumia wakati
vizuri. Kupanga matumizi
mazuri ya muda kwa kuwa
walishabainishiwa katika
Quran kwamba, kila jambo
la kheri ni ibada.
Mwenyezi Mungu
anasema katika Quran,
Nami sikuwaumba majini
na watu ila waniabudu
Mimi.
Hapa linabainishwa
wazi kuwa lengo kuu la
Mwenyezi Mungu (sw)
kuwaumba wanadamu ni
kumuabudu Yeye pekee.
Wanachuoni wa Kiislamu
wanafafanua zaidi kwamba
maana ya ibada kwa ujumla
wake ni kila anachokipenda
Mwenyezi Mungu na
kukiridhia, hiyo ni ibada
bila shaka.
Kwa maana hiyo
wanadamu wajifunze
kuacha kuishi kwa mazoea
kwa kuwa wanakula,
wanalala na wanapumua.
Kwamba wanaweza
kufanya vyovyote bila
kuathiri muda wao wa
maisha hapa duniani. Inafaa
tuzingatie sana kutumia
muda katika mambo
mema na mazuri, ambayo
yatawakurubisha zaidi kwa
Mola.
Tumia muda kwa
kufanya kazi halali
unayoweza kukupa kipato
cha kusaidia kuendesha
maisha. Tumia muda
kumuabudu na kumuomba
Mwenyezi Mungu, tumia
muda kusoma Quran ili
kujifunza moja au mawili

ambayo yatakusogeza
zaidi kwa Allah (Sw) na
kumjua Mola wako na yale
aliyotuamrisha kutafuata
hapa duniani katika maisha
yako. Furahi na familia
yako, tumia muda wako
kupumzika na kustarehe
katika starehe za halali,
tumia muda katika kutenda
mema katika jamii nk.
Kwa kujali muda, ni
rahisi kuepuka kufanya
mambo ya kipuuzi,
ambayo hayatokusaidia
hapa duniani wala Akhera.
Ni muhimu sana kuacha
kuishi na kutenda kwa
mazoea, kwa kuwa wakati
hautabiriki na kwa kuwa
watu hawajui muda wala
saa ya kuondoka hapa
duniani.
Tukumbashane tu
kwamba, kila Muislamu
hawezi kufika ngazi yeyote
siku ya Kyama hadi pale
atakapojibu maswali manne
ya Allah (sw). Miongoni
mwa maswali hayo ni
lile litakalohoji namna
ulivyotumia muda wako
katika maisha ya duniani.
Yaani muda wako uliutumia
katika kufanya mambo gani.
Uliutumia katika mambo ya
heri au ya shari.
Mwenyezi Mungu
kaumba usiku na mchana
kwa makusudio maalum.
Akashauri wanadamu
watafute riziki mchana
na usiku mpumzike.
Ndio maana usingizi wa
usiku haukwepeki. Hata
ukilazimika kutolala usiku,
mwisho wake ni kupatwa
na maradhi na hutamudu
kuukosa.
Hata vipindi vya swala
vimewekewa wakati wake
maalum. Hii ni ishara tu
kwamba Mwenyezi Mungu
ametaka kutudhihirishia
umuhimu na utukufu wa
wakati. Nakumbusha tu
kwamba, kuna haja ya
kupangilia shughuli zetu
kwa kujali sana wakati.
Ishini kwa kufanya
ibada kwa wakati na hapo
mtakuwa mmeoinyesha
jamii tabia sahihi ya
Kiislamu, nanyi mtakuwa
kiigizo chema kwa
walimwengu.
Inshaallah Mwenyezi
Mungu awajaalie muwe
miongoni mwa wale
wenye kusikia machache
na kuyazingatia. Na
awawezeshe katika umri
wenu uliobaki, muweze
kuutumia muda wenu
vizuri kwa kutenda
yale anayoyapenda na
kuyaridhia.
Na Shaban Rajab

AN-NUUR

JAMADUL AWWAL 1437, IJUMAA FEB 26-MACHI 3, 2016

Miti na maisha yetu-5

Inatoka Uk. 12
170 m/t (metric tones)
ikifwatiwa na Afrika
ya Kusini 970,795 m/t,
Marekani 585, 788 m/t. Misri
454,407 m/t na Morocco 294,
572.
Jambo ambalo ni
tatizo kubwa kwa nchi
zinazoendelea hasa nchi
za Kiafrika nikuwa kilimo
kimekuwa kama wenyewe
tusemavyo ni kazi ya jadi
wala sio kama tumekiweka
kitupeleke mbela na kuja
na mbinu za kila aina juu
ya ukulima. Machungwa
kwetu huwa ni fruti ya
msimu, msimu ukisha
machungwa hayaonekani
na yakipatikana bei yake
hapo utasema unataka
chungwa kwa dawa lazima
ulipate kwahio utajitaarisha

ulinunue kwa bei kubwa.


Machungwa kwa
wenzetu hupandwa kwa
nidhamu ya kikulima kisha
huchumwa kwa kutumia
mbinu za kisasa sio zile za
uwende na kingoiko au
upande mchungwa ukutane
na nyoka juu ya mchungwa
uchupe utoke mbio. Hayo
kwa wenzeu hayapo na hata
sisi tukitaka kufwata mbinu
hizo, tunaweza. Lakini
namna tunavyoipanda miti
yetu huwa mchafu koge
kwahio huwa ni vigumu
kuweza kutaka kutumia
mbinu hizo.
Watu wa Ulaya mlo
wa kila siku asubuhi hula
siagi, chizi na jamu na
kati ya jamu ipendwayo
huitwa Marmalade
hutokana na machungwa.

Inatoka Uk. 13

anayokwenda Ulaya,
aliyotumwa akamjibu
yupo pahali sawa, binti
akasema haiwezi kuwa,
akawa anajipanga sasa
kwenda kumtoa yeye
mwenyewe kilichomudhi
hakifahamiki, lkawa
anamuhudumia msafiri
wa Kifaransa ambaye
hajui Kiengereza, ikawa
vuta ni kuvute na wakati
unakwenda Sayyid Omar
akamsogelea yule bibi wa
Kifaransa na kumuamikia
kwa Kifaransa na kutaka
kujua nini shida yake,
akawa Sayyid Omar
sasa anatafsiri kutoka
Kifaransa anapeleka
kwa Kiengereza kwa
mratibu wa Tiketi, binti
wa Kikenya hakuamini,

Sasa chakuulizwa iweje


machungwa mwisho
hufika kutupwa au kuuzwa
kwa bei ya kutupwa
kitu ambacho kinaweza
kutengenezwa jamu au
sharbati ya machungwa vitu
ambavyo hutumika kila
siku?
Kilimo kwanza, kilimo
uti wa mgongo, kilimo kazi
ya jadi, kilimo ndio roho ya
uchumi wetu, hizi huitwa
ni kashkashi tu wala sio
yaliyo katika programu za
kwelikweli. Chumi zetu
tunaweza kuzikuza kwa
hali ya juu kutokana na
matunda tunayoyalima
ikiwa tutajipanga.
Suala jee twaenda
wapi? Twaenda waendako
wengine au sisi tuna njia
yetu ya domo kaya tu?

Masheikhe wetu: Sayyid Omar Abdalla (Mwinyi Baraka)-3

kuambiwa wanapanga
njama ya kupindua
Serikali, akawekwa
korokoroni kwa mwezi
mmoja badaye ilikuja
kuelekweka kuwa
ilikuwa ni fitna tu,
tena hapo Mzee Abeid
Amani Karume akaamua
kuwachia, afya yake
iliathirika sana kwani
akisumbuliwa na kisukari
na akawa hapati dawa
ya kupiga shindano ya
Insulin. Sayyid Omar
baada ya kutolewa jela
alikuwa akiishi na khofu
akaona asije akafungwa
tena akaamua kuhama
Zanzibar huku tayari
kapatiwa nafasi ya
kurudi Uiengereza lakini
aliona vyema kwenda
kuishi katika visiwa vya
Comoro ambavyo ana
nasaba navyo.
Safari mmoja akiwa
anasafiri kutokea
Kenya anaelekea Ulaya,
amesimama kwenye
foleni, binti wa Kikenya
alio katika kupima
mizigo na kutoa namba
ya viti kwenye ndege
kumuona mzee na
majuba na kashika
bakora akamshika
kumwambia eeh muzee
nenda kwenye foleni
ile ya kwenu Mombasa,
ndege itakukimbia.
Sayyid Omar alikaa
kimya lakini jeuri ya
kitoto ikazidi kwa
kumtaka mmoja ya
wafanyakazi kumtoa
kwenye Foleni, Sayyid
Omar akatoa Pasi ya
kusafiria ikiwa na hadhi
ya kidiplomasia na
mrundo wa tiketi, mpaka
akaiona tiketi yake

alivyoyasuluhisha
binti akataka kujua
wapi aliposoma kujua
Kiengereza na Kifaransa,

Sayyid Omar Abdalla


akamwambia You better

asked Kibaki, he knows me


better, we were together at
Makerere College Binti wa
Kikenya alitahayari bali
aliogopa asije kushitakiwa
kwa wakubwa wake na
Sayyid Omar alipomuona
anatetemeka huku hana
raha akamwabia Jitahidi
kuwaona watu wote ni
sawa.
Alifika Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam akatoa
uwaidh juu ya umuhimu
wa kujiendeleza kiroho
kwa kuwa na dini, wakati
wa masuala kijana

akaona aaah, huyu


mzee ndio watu wa
kizamani Wakoloni
waliwafundisha lugha
ndio katuhutubia kwa
Kiengereza, akamvaa
akamwambia unajua
nini Karl Marx kasema?
Religion is the opium of

the mass kwa maana ya


kuwa Dini ni kasumba
kwa umma. Sayyid
Omar Abdalla kwa
mshangao wa wengi
aliusoma ukurasa mzima
wa Das Capital juu ya
maneno hayo na kusema
ukurasa gani upo wenye
manerno hayo ambayo
aliyasoma kwa ghibu,
na akamtaka kijana
huyo amsome Maurice
Bucaile katika kitabu
What is the Origin of
man na The Quran, The
Science and the Bible.
Kijana badala ya kutaka
kumshushua Sheikhe
alijikuta kajishusha
hadhi na kujuta aliyotaka
kuyafanya.
Sayyid Omar Abdalla
akipenda kuurejea na
kurejea msemo wa
mwana sayansi wa
Fizikia maarufu kwa
jina la Albert Einstein
usemayo Science
without religion is lame,
religion without science
is blind. Somo la sayansi
pasi kujuwa dini ni sawa
na kilema na sayansi pasi
kujuwa dini ni mithili ya
kipofu. Sheikhe huyu
alikuwa na elimu zote
mbili hizo na akiweza
kufahamisha na kutowa
ujumbe kwa watu wa rika
zote wakiwa wasomi na
wale wasiokuwa wasomi.
Yapo mengi
ambayo ningeweza
kumzungumza Sheikhe
huyu, nategemea haya
machache yanatosha.
Fatwana na mie wiki
ijayo kumjua Sheikh
Abubakar Bakathir.
Tumuombe Allah nasi
tufwate nyayo za Sayyid
Omar Abdalla (Mwinyi
Baraka), Ameen.

16

Makala

AN-NUUR

JAMADUL AWWAL 1437, IJUMAA FEB 26-MACHI 3, 2016

Uislamu ni Dini ya haki hakuna kulazimishana


Na Sheikh Abdusalaam
Mohmed Abdusalami
SHUKURANI zote anastahiki
Mwenyezi Mungu na rehema
na amani zimfikie yule ambaye
hakuna Nabii baada yake.
Kwa anayefuatilia aya za
Qurani takatifu atakuta kuwa,
haikumlazimisha mtu yeyote
anayekwenda kinyume na dini
ya Kiislamu katika imani juu ya
kuingia Uislamu.
Uislamu unakataza kulazimisha
mtu katika dini, amesema
Mwenyezi Mungu (hakuna
kulazimisha mtu kuingia katika
dini, uongofu umeshapambanuka
na upotofu (256 Al-Bakarat).
Aya hii ni miongoni mwa hoja
kubwa ambazo zinabainisha
ukubwa wa Uislamu, kwani hii
ni dalili ya wazi kwamba vyanzo
vya Uislamu ni uhuru wa imani
na katika chanzo hiki, inadhihiri
takrima ya Mwenyezi Mungu kwa
binadamu na kuheshimu matakwa
yake na mapendekezo yake na
ukaachwa uchaguzi uwe katika
nafsi yake mtu mweyewe katika
yanayohusu uongofu au upotevu
katika imani.
Lakini Uislamu uko wazi na
umebainisha kila jambo kwa
wenye akili. Uislamu ni dini

pekee ambayo inalingania kuwa


hakuna kulazimisha mtu katika
kuingia katika dini na ndiyo
inayowabainisha watu wake
kabla ya wengine kwamba, wao
hawaruhusiwi kulazimisha wengine
kuingia katika dini hii.
Ameipokea Imamu Twabarani
toka kwa Bin Abbas, kwamba mtu
mmoja katika watu wa Madina
anayeitwa Huswainiy, alikuwa
na watoto wawili Wakristo na
alikuwa yeye ni Muislamu, akasema
kumwambia Mtume (S.A.W) Je,
niwalazimishe juu ya Uislamu?.
Ndipo alipoteremsha Mwenyezi
Mungu aya hii.
Ama wale ambao wanaosema
kwamba Uislamu umeenea kwa
ncha ya upanga, hao ni wenye
kumzushia uongo Mwenyezi
Mungu.
Kwa hakika uhuru wa kuabudu
hiyo ni haki ya mwanzo kabisa ya
binadamu, ambayo inamsifu mtu
kuwa mtu, na kile kinachoweza
kumvua mtu utu wake ni uhuru wa
kuabudu kwani humvua utu wake
mwanzo kabisa.
Pamoja na uhuru wa kuabudu,
kuna uhuru wa kulingania na
amani ya maudhi na fitina na
kama si hivyo, basi huo utakuwa
ni uhuru wa jina tu, ambao hauna
dalili katika maisha ya Kiislamu
yanayoendelea.
Na hii ni sura nzuri ya kuwepo
dini na maisha na ni msimamo
mkubwa kwa jamii ya kibinadamu
bila ya kujionyesha, nayo ni
dini ambayo inalingania kuwa
hakuna kulazimishwa mtu kuingia
katika dini, nayo ndiyo dini
inayowaamrisha wafuasi wake
kabla ya watu wengine kwamba,
hawaruhusiwi kulazimisha watu
kuingia katika dini hii.
Basi wangeingia watu wote hapa
duniani katika dini ya Uislam,
lakini Mwenyezi Mungu ana

hekima zake katika kuwapa watu


uhuru kwa yale wanayoyachagua
na wanayoyaendea kwa njia
mbalimbali.
Pale aliposema, Na
kama angalitaka Mola wako
kuwalazimisha kwa nguvu
kuamini, bila shaka wangeamini
wote waliopo katika ardhi asibaki
hata mmoja, lakini ni Mwenyezi
Mungu hataki kuwalazimisha
watu kwa nguvu, basi wewe je,
utawashurutisha watu hata wawe
waumini? (99 Yunus)
Hapana shaka kuwa binadamu
kwa yale aliyompa Mwenyezi
Mungu miongoni mwa akili, kusikia
na kuona, yeye ni muweza wa
kupambanua kati ya haki na batili
ili aweze kuchagua njia sahihi.
Amesema Mwenyezi Mungu,
Kwa hakika tumemuumba
mtu kutokana na mbegu ya uhai
iliyochanganyika ya mwanamume
na mwanamke ili tumfanyie mtihani
kwa amri zetu na makatazo yetu
kwa hiyo tukamfanya mwenye
kusikia na mwenye kuona.
Hakika sisi tumemuongoa,
tumembainishia njia zote mbili hizi,
kuwa hii ndiyo ya kheri na hii ni ya
shari, basi mwenyewe tena atakuwa
mwenye shukurani au awe mwenye
kukufuru (kukanusha) (23 Insani).
Na zikazidi kuteremshwa aya
za Qur-ani Tukufu zaidi ya sura
moja, juu ya uhuru wa kuabudu na
kutolazimisha mtu kuingia katika
dini hii.
Hapo anasema Mwenyezi
Mungu kwa Mtume wake (S.A.W)
kwa kumwambia Nasema huu
ni ukweli uliotoka kwa Mola
wenu, basi anayetaka na aamini
na anayetaka na akufuru) (29 al
Khafi).
Na amesema tena, Bila
shaka angependa Mwenyezi
Mungu angewajengea nguvu
hata wasingeshirikiana na sisi

hatukukufanya kuwa mlinzi juu


yao, wala wewe si wakili juu yao)
107 Al-An-aam.
Pia amesema, Na wakipuuza
atalipa Mwenyezi Mungu nasi
hatukukupeleka uwe mlinzi, wewe
kazi yako ni kuwafundisha tu si juu
yako) ila kufikisha tu (48)
Na amesema tena, Basi
kumbusha hakika wewe ni
mkumbushaji tu, wewe si mwenye
kuwateza nguvu (21-22) Alghashia.
Na amesema tena, Mwenye
kumtii amemtii Mwenyezi
Mungu kwani anayoyaamrisha
Mtume yametoka kwa Mungu
na anayekengeuka anajidhuru
mwenyewe, hatukukupeleka wewe
kuwa mlinzi juu yao, wakipotea
ulaumiwe wewe la, hatukukufanya
hivyo (80 Anisaa).
Na dini hii ya Uislam iliyo
nyepesi, sio dini ya kumlazimisha
mtu bali ni dini rahisi inayosimamia
vyanzo vya kukinaisha, na
kushikamana nayo juu ya akili iliyo
makini kwa upande wa mwongozo
wa mazungumzo ya kujenga, na
mazingatio ya uhuru na kujadili na
mambo ya kielimu na mahojiano
na kwa uhodari na kuondoa fitina
na sheria ya Kiislamu inahimiza
na kutia nguvu juu ya utukufu wa
mwenendo huu.
Hivyo tunakuta Mwenyezi
Mungu anamwamrisha Mtume
wake (S.A.W) kuwa awaite watu
katika dini ya Kiislamu kwa
heshima na anamsemesha kwa
kusema (wala msibishane na watu
walipewa kitabu kabla yenu, ila
kwa yale majadiliano yaliyo mazuri
isipokuwa wale waliodhulumu
miongoni mwao, na semeni
tunaamini yaliyo teremshwa kwetu
na yaliyotereshwa kwenu na
Mungu wetu na Mungu wenu ni
mmoja nasi ni wenye kunyenyekea
kwake) (46 Ankabuut.)

Benghazi ambako waasi nao


wakakubali kuacha mapigano
ili kupisha uundwaji wa serikali
ya mpito itakayosimamia
uchaguzi ulio wazi na huru. Pia
wafanyakazi na wageni kutoka
nchi za Kiafrika walitakiwa
wahakikishiwe usalama wao.
Baada ya hapo kamati
ikatembelea Ufaransa,
Uingereza, Ubelgiji, Italy na
Marekani ili kueleza mkakati wa
AU na kuomba ushirikiano wa
mataifa hayo ya NATO.
Wakati mchakato huu wa
AU unaendelea ghafla tarehe
21 Agosti waasi wa Benghazi
wakaingia Tripoli. Kambi za
kijeshi zikaingiliwa na silaha
zikaanza kutapakaa nchini kote.
Yaliyofuata ni historia.
Miaka mitano baada ya
uvamizi wa 2011 takriban
wananchi milioni mbili wa Libya
wamelazimika kukimbilia nchi
za jirani za Tunisia na Misri.
Hii ni theluthi ya wakazi wote.
Waliobaki wanaishi maisha
ya tabu, wakiwa wamepoteza
makazi yao kutokana na vita
baina ya makundi yenye

silaha, baina ya Mashariki na


Magharibi.
Uvamizi wa 2011 uliofanywa
na NATO uliungwa mkono na
asasi ya kimataifa kuhusu haki
za binadamu (Human Rights
Watch HRW). Sasa asasi hiyo
hiyo inaripoti kuwa makundi
yenye silaha nchini Libya
yamekuwa yakiteketeza nyumba
za raia. Wanawapora raia,
wanawakamata, wanawatesa.
Halhasili wanachokifanya ni
uharamia wa kivita.
HRW inasema maelfu ya
raia, wakiwemo wageni,
wamefungwa gerezani bila ya
kuhukumiwa, huku wakiteswa
kila siku. Hivi sasa kuna kile
wanachokiita serikali ya
umoja wa kitaifa ambayo
inatambuliwa na Umoja wa
Mataifa (UN). Lakini ndani
ya nchi hakuna anayeisikiliza.
Katika ukingo wa baharini
ambako kuna mafuta, makundi
ya mujahidina yameshika
hatamu.
Nchi kwa hivyo
imegawanyika katika sehemu
mbili, kutokana na makundi

ya waasi ambao walisaidiwa


na majeshi ya uvamizi ya
Marekani na Ubelgiji yalipoingia
mwaka 2011. Kundi moja ni la
mujahidina ambao walipewa
misaada ya hali na mali kutoka
Marekani na Uingereza. Nchi
hizo za kibeberu ziliwapa
mafunzo, silaha na fedha ili
kumpindua Gaddafi.
Sasa Uingereza inafikiria
kutuma wanajeshi 1,000 ili
kuendesha mafunzo kwa
jeshi jipya la Libya. Pia Italy
inakusudia kutuma majeshi
6000. Haiyumkiniki kuwa
mujahidina (au Daesh)
watakubali kufuata amri ya
mabeberu hao. Hapo ndipo
mpasuko utaongezeka na
huo utakuwa uvamizi wa pili
wa Libya. Katika hali kama
hii ndipo rais mstaafu Jakaya
Kikwete na jopo lake linatarajiwa
kuwasuluhisha wananchi wa
Libya. Labda atafanikiwa.
Lakini je, atafanikiwa
kuwashawishi na wavamizi wa
NATO?
(0713-562181- nizar1941@
gmail.com)

Kikwete atafanikiwa kusuluhisha mgogoro wa Libya?


Inatoka Uk. 9

ya kwenda Libya, lakini nchi


za NATO zikawasilisha Azimio
katika Baraza la Usalama la UN.
Azimio namba 1973 likapitishwa
na majeshi ya NATO yakaandaa
majeshi yake kwenda Libya
kuweka kile walichokiita
marufuku ya ndege kurushwa
ndani ya nchi hiyo (no-fly
zone). Nchi tatu za Kiafrika
zilikuwemo katika Baraza hilo
nazo ni Afrika Kusini, Nigeria
na Gabon. Licha ya azimio la
AU nchi hizo zilikubaliana na
azimio hilo bila kujali kuwa AU
ilikuwa na mpango mwengine
wa maridhiano.
Hata hivyo kamati ya AU
ikakutana mjini Nouakchott
tarehe 19 Machi na wakapanga
safari ya kwenda Libya siku
inayofuata. Ikawa inasubiri
kupata kibali cha ndege yao
kuruhusiwa kuingia Libya
kwa mujibu wa azimio la UN.
Ndipo tarehe 10 na 11 Aprili
kamati ikazuru Libya. Katika mji
mkuu wa Tripoli wakakutana
na Gadaffi ambaye akakubali
mkakati wa AU. Kisha wakaenda

17
Na Shaban Rajab
NABII Muhammad (saw)
alipotumwa na Mwenyezi
Mungu Mtukufu kuja
ulimwenguni kuuhusisha
Uislamu ulioasisiwa na
Mitume waliomtangulia,
alimkuta mwanamke
akiishi chini ya
mazingira na kivuli cha
ukandamizaji.
Katika ulimwengu
ule, mwanamke hakuwa
na haki yeyote katika
jamii zaidi ya kuonekana
kama bidhaa inayoweza
kuuzwa wakati wowote.
Mwanamke alichukuliwa
kama ni chombo cha
kumstarehesha na kukidhi
matamanio ya kimwili ya
mwanamume. Mwanamke
alihesabika kuwa ni chombo
cha uzalishaji, hakuwa
na uhuru wa kupanga na
kuamua. Kwa ufupi haya
ni sehemu ya mazingira
ambayo Uislamu ulimkuta
mwanamke akiishi hapa
duniani.
Kwa rehema za
Mwenyezi Mungu, Uislamu
kupitia kupitia kwa
Mtume Muhammad (saw),
ukamuondolea mwanamke
unyonge, udhalili, dhulma,
uonevu na unyanyasaji
uliokuwepo. Uislamu
ukamjengea mwanamke
mazingira bora, kanuni na
sheria ambazo zilihakikishia
uhuru, usalama, amani,
haki na usawa katika jamii
yake. Kupitia mafundisho
ya Mtume Muhammad
katika Uislamu, mwanamke
aliwekewa mazingira ya
kujiona kuwa ni binadamu
kamili, mwenye haki
sawa kama mwanamume
na ukamhakikishia
kupata haki zote kama
binadamu, bila ya kuhitaji
upendeleo maalum kama
inavyofanyika sasa.
"Wanawake ni ndugu
baba mmoja, mama
mmoja na wanamume,
wanayo haki kwa sheria
(kufanyiwa na wanamume)
kama ile haki iliyo juu yao
kuwafanyia wanamume"
Abu Dawoud.
Kwa jicho la mfumo
kamili huu wa maisha
(Uislamu) wanamume na
wanawake kiasili ni sawa
sawa bila tofauti yeyote
mbele ya Mola wao.
Ila tofauti na ubora
utajitokeza katika amali
njema anazozifanya kila
mmoja wao. Ni dhahiri
kuwa mzuri na mwingi
wa amali njema hawezi
kulingana sawa na mchache
wa amali njema bila ya
kuangalia ni mwanamume
au mwanamke. Hii ndio
mojawapo wa misingi na
kanuni za Uislamu.
Pamoja na kwamba
wengi hawajui, iwe ni kwa
makusudi au kwa kutotaka
kujifunza, mwanamke ni
kiumbe aliyetoa mchango
mkubwa sana katika kuenea
kwa Uislamu tangu enzi za
Mtume wetu Muhammad
(saw). Mtume Muhammad
alipata msaada mkubwa
sana kwa wanawake katika
kueneza ustaarabu wa
Kiislamu.
Leo nitamzungumzia Bi.
Khadija bint Khuwaylid,
mke wa kwanza wa Mtume
(saw). Yeye aliolewa

MAKALA/TANGAZO

AN-NUUR

JAMADUL AWWAL 1437, IJUMAA FEB 26-MACHI 3, 2016

Khadijah Bint Khuwaylid


Ummul Muuminin

akiwa na miaka 40 na
Mtume Muhammad (saw)
akiwa na miaka 25. Kwa
kifupi ni kwamba Mtume
Muhammad alimuoa
Bi. Khadija hata kabla
ya kupewa Utume na
Mwenyezi Mungu.
Bi. Hadija alizaliwa
katika mji wa Makkah
katika familia yenye
heshima. Baba yake alifariki
katika vita. Mama yake ni
Fatima bint Zaidah.
Hata hivyo katika
mtandao wa al-islam.org,
inaelezwa kuwa kabla ya
kuolewa na Mtume (saw),
Bi. Khadija aliwahi kuolewa
mara mbili na Abu Halah
bin Zaraarah na Atiq bin
Aaid. Alijaaliwa watoto
katika ndoa hizi, nao ni
Hind na Haalah (alizaa
na Abu Haalah) na Hind
aliyezaa na Atiq.
"Mwana Khadija kabla ya
kuolewa na Mtume (s.a.w.)
alikwisha olewa na waume
wawili kabla ya Mtume
Muhammad (s.a.w.) na
amepata watoto wawili.
Zimetaja kidogo baadhi
ya hoja zinazosemwa juu
ya Bi. Khadija kuhusu
watoto aliopata kwa waume
wengine kabla ya Mtume
Muhammad (s.a.w.) kama
ifuatavyo:
Wanasema shahidi wa
kwanza katika Uislamu ni
mtoto wa Mwana Khadija
aitwae Harithi bin Abi
Hala, alipata shahada pale
Mtume (s.a.w.) alipotangaza
Uislamu hadharani. Al'
Isaba J. 1 Uk. 293, Al'Awaail
J. 1 Uk. 311-312.
Hata hivyo katika riwaya
ya Qatada inasema kuwa,
shahidi wa kwanza katika
Uislamu ni Sumaiya, mama
yake Ammar bin Yasir. Al'
Isaba J. 4 Uk. 335.
Pia imepokewa kuwa
Bi. Khadija (a.s) alikuwa
na nduguye akiitwa
Hala, aliolewa na mtu
mmoja katika koo ya Al
Makhzumi, akazaa mtoto
wa kike aliyeitwa Hala,
kisha aliachika akaolewa na
mtu mmoja katika koo ya
Tamim aitwaye Abu Hindi,
akamzalia mtoto jina lake
Hind.
Huyo Abu Hindi,
alikuwa na mke mwingine
ambaye alimzalia watoto
wawili Zaynab na Ruqayya.
Hatimaye Abu Hindi na
mkewe wa pili walikufa,
akabakia Bi. Hala ndugu
ya Bi. Khadija, pamoja na
watoto wawili Zaynab
na Ruqayya. Yule mtoto
wake wa kuzaa, Hind,
alikwenda kwa jamaa
za mumewe. Ndipo Bi.
Khadija alipowakusanya
wote akawa nao, Bi. Hala na
watoto wawili walioachwa
na mama yao Zaynab na
Ruqayya.
Bi. Khadija alipoolewa
na Mtume (s.a.w.) Bi. Hala
alifariki, wakabaki Zainab
na Ruqaya wakilelewa na
Mtume (s.a.w.). Katika
mila za Kiarabu, walikuwa
wakiamini kuwa mtoto

wa kufikia ni mtoto wako


halisi, kwa hiyo watoto
hawa wakapewa ubinti wa
Mtume (s.a.w.) (Zainab binti
Muhammad na Ruqaya
binti Muhammad). Sahihu
Minsiiratin Nabi J. I Uk. 123.
Bi. Khadija alibahatika
kuwa mfanyabiashara
hodari na tajiri kutoka
katika familia yenye
heshima. Misafara yake
ya biashara ilikuwa ya
kudumu na alikuwa
miongoni mwa matajiri
wachache katika mji wa
Makkah. Muhammad
ibn Abdillahi wakati huo
akiwa kijana, naye aliingia
katika shughuli za misafara
ya biashara na kuwa
mfanyabiashara. Lakini
kilichomfanya Muhammad
kuwa na jina na miongoni
mwa vijana wanaosifika ni
kutokana na sifa zake za
uaminifu, sifa zilizoweza
kuenea katika mji mzima
wa Makkah.
Sifa hizi za Muhammad
ndizo zilizomvutia na
kumshawishi Bi. Khadijah
akamuomba Muhammad
afanye naye biashara kwa
kumpa bidhaa kwenda nazo

Sham - Syria. Pia alimpa


mmoja katika wafanyakazi
wake Maysarah afuatane
naye. Waliporudi Maysarah
alimsifia sana Muhammad
ibn Abdillahi kwa tabia
yake ya uaminifu, ukweli na
uadilifu.
Vitabu vya historia ya
Kiislamu vinabainisha
kwamba mara tu baada
ya Mtume kurudi kutoka
Shamu aliiwasilisha
mara moja faida kubwa
iliyopatikana kutokana na
biashara kwa Bi. Khadija.
Bi. Khadija aliifurahia
sana kuona hata faida
aliyoipata, hakuwahi
kuipata kutoka kwa watu
wengine aliowaajiri kabla ya
Mtume Muhammad.
Kwa kigezo hicho Bi.
Khadija akazidi kuthibitisha
habari zilizomfikia juu ya
uaminifu na ukweli wa
Muhammad, ukiachilia
mbali yale aliyoelezwa na
mtumishi wake Maysarah
ambaye alikuwa msaidizi
wa Mtume katika safari
yao ya Shamu. Sifa hizi
zilikuwa na mvuto wa aina
yake kwa Bi. Khadija hadi
akahiari kutaka kuolewa
naye. Sifa hizo njema
zikamteka Bi. Khadija na
kujikuta akimpenda Mtume

na kutamani awe na mume


mwenye sifa njema kama
Nabii Muhammad.
Akamtuma mshenga kwa
Mtume amuelezee nia yake
ya kutaka kuolewa naye.
Ni vema ikakumbukwa
kwamba wakati huo Bi.
Khadija alikuwa ana umri
wa miaka arobaini na
Bwana Mtume alikuwa
amefikia umri wa miaka
ishirini na tano. Bwana
Mtume kwa kuzingatia
utukufu, heshima na tabia
njema za Bi. Khadija bila ya
kusita akakubali kumuoa
bibi huyu.
Posa zilipelekwa na Ami
yake Hamzah bin Abdul
Muttalib. Ndipo mipango
na taratibu za harusi
zikaanza na hatimaye
wawili hao wakawa ni mke
na mume. Ndoa ilifungwa
miezi miwili tangu Mtume
kurejea kutoka Shamu.
Ndoa ilifanyika baada ya
kupata baraka za Ami yake
Abu Taalib, aliyekuwa
akimlea Mtume (saw).
Walijaaliwa kupata
watoto sita Kassim,
Abdullah, Zainab,
Ruqayyah, Ummu Kulthum
na Faatimah. Kassim
na Abdullah walifariki
wakiwa wadogo. Khadija
alipendana sana na
Mtume (saw) kwa muda
wote na sifa za Mtume za
uaminifu zilimfanya apewe
jina Assadiq Al Amiin.
(mwenye kusema ukweli na
muaminifu). (Itaendelea)

NAFASI ZA MASOMO SUDAN 2016/2017


Ofisi ya Munazzamat Al- Daawa Al- Islamiyya (MDI) iliyopo
Mikocheni kwa Mwalimu Nyerere mkabala na Regency Park
Hotel jijini Dar es Salaam, inapenda kuwatangazia nafasi za
masomo kwa wale wote wanaotaka kujiunga na chuo kikuu cha
INTERNATIONAL UNIVERSITY OF AFRICA, Khartoum Sudan.
KOZI ZINAZOTOLEWA
1. Shahada ya kwanza katika Medicine, Pharmacy, Dentist,
Nursing, Laboratory Sciences, Petroleum and Minerals,
Engineering, Electronics & Electrical Engineering, Computer
Science, Pure Science, Applied Chemistry, Microbiology,
Geology and Physics, Agricultural Production and Processing.
2. Shahada ya kwanza katika law & Sharia, Islamic studies,
Economics, Administration, Political Science, Education,
Administration and technology, Curriculum & Methods
of Teaching, Media, Arts (Arabic, Geography, History and
General Psychology)
Fomu za maombi zinapatikana kwa TSH 10,000=/ tu kuanzia
tarehe 20 Februari mpaka tarehe 05 Machi 2016, saa 3:00
asubuhi mpaka saa 7:00 mchana, kila siku isipokuwa Ijumaa na
jumapili, katika vituo vifuatavyo:
DSALAAM: Ofisi ya MDI iliyopo Mikocheni kwa Mwalimu Nyerere
mkabala na Regency Park Hotel.
ZANZIBAR: Katika ofisi ya MDI (Kituo cha kusaidia mayatima)
kilichopo eneo la Mpendae kwa mchina mwisho, mkabala na skuli
ya kijangwani.
MWANZA: Msikiti wa SHEIKH AMINI uliopo Mtaa wa Rufiji
IRINGA: Shule ya Ummu Salama iliyopo old Dodoma road
Gangiloga.
SIFA ZA MUOMBAJI:Awe amemaliza kidato cha nne na sita au Thanawiya kwa kupata
daraja la kwanza, la pili au la tatu. Pia mwombaji lazima alete Vyeti
halisi (Original academic certificates) Siku ya kurudisha fomu.
Kwa maelezo zaidi piga simu:Makao Makuu, DAR ES SALAAM:
0713/785 779 234 au 0652/786 806 662
ZANZIBAR: 0777 415 835 au 0715 415 835
MWANZA: 0782 621 802 au 0688 304 852
IRINGA: 0784/ 0715 448 484

18

TANGAZO

AN-NUUR

JAMADUL AWWAL 1437, IJUMAA FEB 26-MACHI 3, 2016

ISLAMIC PROPAGATION CENTRE


P.O Box 55105,Phone: 0222450069, 0784 267762, 0755 260087 & Fax 022 2450822, Dar es Salaam website :www.ipctz.org

NAFASI ZA KIDATO CHA TANO KWA MWAKA 2016/2017


Waislamu kote nchini mnatangaziwa nafasi za kidato cha Tano kwa shule zifuatazo:

KIRINJIKO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL

SAME KILIMANJARO

NYASAKA ISLAMIC SECONDARY SCHOOL

MWANZA

UBUNGO ISLAMIC HIGH SCHOOL

DAR ES SALAAM
1. Shule hizi ni za Kiislamu zenye lengo la kuwapa wanafunzi taaluma ya hali ya juu na malezi bora ya Kiislamu.
2. Shule hizi ni za bweni za mchanganyiko wa wavulana na wasichana .
3. Zipo Combination za masomo YOTE yaani SAYANSI, ARTS na BIASHARA.
4. SIFA:
Muombaji anatakiwa awe na ufaulu wa :
(i) Credit tatu (yaani A,B na C),
(ii) Daraja la tatu (division three) au zaidi,
(iii) Angalau Gredi D kwenye masomo ya combination.
5. Fomu za Maombi zinapatikana kwa gharama ya shilingi 10,000/= katika vituo vilivyoorodheshwa hapa chini.
Arusha
- Ofisi ya Islamic Education Panel, Jambo Plastic, Ghorofa ya 2 mkabala na msikiti Mkuu Bondeni : 0783
438676/0715 438676.
Kilimanjaro - Moshi: Msikiti wa Riadha:0767345367/0686938077 - Same Juhudi Studio mkabala na Benki ya NMB Same: 0757
013344.
- Same: Kirinjiko Islamic Secondry School: 0784 296424/0713 115041 - Usangi- Falhum Kibakaya : 0787 142054. - Ugweno Simbomu
centre Mwl. Hidaya A.
Mussa: 0784 655614
Tanga - Twalut Islamic Centre Mabovu Darajani : 0715 894111/0713 01446 - Uongofu Bookshop: 0784 982525
- Korogwe: SHEMEA SHOP : 0754 690007/071569008. - Mandia Shop - Lushoto: 0782257533. - Handeni Mafiga -0782
105735/0657093983
Mwanza
- Nyasaka Islamic Secondary School : 0717 417685/0786 417685. - Ofisi ya Islamic Education Panel Mtaa wa
Rufiji mkabala na Msikiti Al-Amin
0785 086 770/0714097362.
Bukoba
- Ofisi ya Kutaiba Saccos: 0765 748056
Musoma
- Ofisi ya Islamic Ed Panel -Mtaa wa Karume,Nyumba Na. 05 : 0765024623/0787868611
Shinyanga
- Msikiti wa Majengo karibu na Manispaa ya Shinyanga Mjini :0655608139/0768895484
Kahama
- Ofisi ya Kamati ipo karibu na zahanati ya Doctor Dalali: 0754 994738/0782 994738
Dar es Salaam - Ubungo Islamic High School : 0756584625/0657350172/0712 033556
- Ofisi ya Islamic Ed. Panel Temeke -Msikiti wa Nurul Yakin : 0655144474/0787119531
Morogoro
- Wasiliana na Ramadhani Chale : 0715704380. - Ifakara wasiliana na Mwl. Sharifu: 0659 158958
Geita
- Ofisi ya Kamati karibu na mashine ya kukobolea mpunga shilabera: 0765 748056
Dodoma
- Hijra Islamic Primary School : 0716 544757/0718661992
Singida
- Ofisi ya Islamic Education. Panel karibu na Nuru snack Hotel : 0786 425838/0784 928039.
Manyara
- Ofisi ya Islamic Ed. Panel Masjid Rahma: 0784491196
Kigoma
- Msikiti wa Mwandiga: 0714717727 - Kibondo Islamic Nursery School: 0766406669. - Kasulu: Murubona Isl.SS:
0714710802/0763 298440
Lindi
- Wapemba Store: 0784 974041/0783 488444/0653 705627.
Mtwara
- Amana Islamic S.S: 0715 465158/0787 231007.
Songea
- Kwa Kawanga Karibu na Msikiti wa NURU : 0713249264.
- Mkuzo Islamic High School :0654 876317
Mbeya - Ofisi za Islamic Education Panel Uhindini 0785425319. - Rexona Video mkabala na Mbeya RETICO: 0713

200209/0785425319.
Rukwa
- Sumbawanga:Jengo la Haji Said Shule ya Msingi Kizwike: 0757090228/0786 313830
Tabora
- Kituo cha Kiislamu Isevya: 0784 944566/0718 556355 Nzega - Dk. Mbaga-0754 576922/0784576922.
Iringa
- Madrastun Najah: 0714 522 122.
Pemba
- Wete: Wete Islamic School : 0777 432331/0712772326.
Unguja
- Madrasatul Fallah: 0777125074. - PANDU BOOKSHOP 0777462056 karibu na uwanja wa Lumumba
Mafia
- Ofisi ya Ust. Yusufu Ally jirani na msikiti mkuu : 0773580703.
USIKOSE NAFASI HII ADHIMU WAHI KUCHUKUA FOMU SASA!
MKURUGENZI
WABILLAH TAWFIIQ

19

TANGAZO

AN-NUUR

JAMADUL AWWAL 1437, IJUMAA FEB 26-MACHI 3, 2016

AN-NUUR

20

20

MAKALA

JAMADUL AWWAL 1437, IJUMAA FEB 26-MACHI 3, 2016

Uchaguzi wa Bunge
Syria kufanyika Aprili
RAIS Bashar al-Assad wa Syria
ametangaza kuwa Aprili 13
mwaka huu wa 2016, kuwa siku
ya uchaguzi wa Bunge nchini
humo.
Taarifa ya Rais Assad,
imetolewa muda mfupi baada
ya Urusi na Marekani kutangaza
kuwa Februari 27 ndiyo tarehe
ya usitishaji vita katika nchi hiyo
ya Kiarabu.
Rais Bashar al-Assad
amebainisha kwamba, Damascus
mara kadhaa imekuwa ikieleza
kuwa, kutangaza tu mpango
wa usitishaji vita hakutoshi,
bali kuna haja ya jambo hilo
kutekelezwa kwa vitendo.
Hata hivyo mpango huo wa
usitishaji vita haujayajumuisha
makundi ya kigaidi na ISIS
na al-Nusra. Hii ni katika hali
ambayo, Rais Bashar al-Assad
ameiomba Jamhuri ya Kiislamu
ya Iran iendeleze misaada yake
kwa serikali ya Damascus katika
njia ya kupambana na magaidi.
Rais Bashar amebainisha
kwamba misaada ya Urusi
na Iran imekuwa na nafasi
muhimu katika kulifanya jeshi
la Syria lisonge mbele na kupata
mafanikio katika vita dhidi ya
waasi.
Hayo yanajiri siku chache
baada ya watu zaidi ya 80
kuuawa katika milipuko ya
mabomu katika mji mkuu
Damascus na mkoa wa Homs
siku ya Jumapili.
Mlipuko mmoja katika siku
hiyo ya Jumapili ulitokea katika
wilaya ya Sayeda Zeinab,
Damascus, karibu na Haram ya
Bibi Zeinab (SA), mjukuu wa
Mtume Mtukufu SAW.

Soma gazeti la
AN-NUUR
KWA TSH 800/=
kila Ijumaa

AN-NUUR

JAMADUL AWWAL 1437, IJUMAA FEB 26-MACHI 3, 2016

Tumieni ujana wenu vizuri


Na Bakari Mwakangwale

VIJANA wa Kiislamu
wametakiwa kutambua
kuwa wana dhima juu ya
kuisimamia dini yao kwa
kutumia neema ya ujana
wao.
Wito huo umetolewa na
Ustadhi Maulid Haruna
Nkumilwa, akiwahutubia
Waislamu katika ibada
ya Swala ya Ijumaa, wiki
iliyopita katika Msikiti wa
MSAUD, Jijini Dar es Salaam.
Ust. Nkumilwa, alisema

umri wa ujana unadhima


kubwa katika kusimamisha
Uislamu na ndio wakati wa
kujifunza na kuijua zaidi dini.
Lazima kijana wa
Kiislamu ajitambue na ajue
kwamba ana umuhimu
katika kuisimamia dini
yake, na katika umri huo pia
ajue anapaswa kuitambua
(kujifunza) dini yake ili
aweze kusimamia mambo
yanayohusu Uislamu kwa
ujumla akiwa na elimu
sahihi. Alisema Ust.
Nkumilwa.

Alisema, kijana wa
Kiislamu anapoona kuna
matatizo katika dini yake,
hana budi kutumia fursa
ya ujana na elimu yake kwa
kuyatatua kwa kuzingatia
mafundisho ya Uislamu,
kupitia Qur an na Sunna na si
vinginevyo.
Alisema, katika usia wake,
Mtume (s a w) anasema,
tumia ujana wako, kabla ya
kufikiwa na utu uzima, na
kwamba hakuna kipindi
ambacho mtu anatakikana
kutafuta elimu kwa nguvu
kama mahala pa ujana.

MAKOMBORA kutoka Marekani.

Marekani yaongoza kuuza silaha Mashariki ya Kati


RIPOTI inaonesha Marekani
inaongoza katika biashara ya
silaha Mashariki ya Kati, ambapo
asilimia kubwa ya silaha hizo
wamekuwa wakiuziwa magaidi na
nchi za kiarabu.
Uchunguzi uliofanywa na taasisi
ya Stockholm International Peace
Research Institute (SIPRI) yenye
maskani yake nchini Sewden,
ambao ripoti yake imesambazwa
Jumatatu ya wiki hii, inaonesha
kuwa kiwango cha usafirishaji nje
silaha kimeongezeka kwa asilimia
14 katika kipindi cha miaka mitano
iliyopita, huku Marekani na Urusi
zikiongoza kwa kusafirisha nje

silaha.
Uuzaji wa silaha duniani
umeongezeka kufuatia ongezeko la
vita na machafuko hususan katika
maeneo ya Mashariki ya Kati na
katika baadhi ya nchi za Afrika
katika miaka ya hivi karibuni.
Ripoti hiyo ya Februari 22,
2016 inaonesha kuwa Marekani
inaongoza katika biashara hiyo,
ambapo asilimia kubwa ya silaha
hizo wamekuwa wakiuziwa
makundi ya magaidi na baadhi ya
nchi za kiarabu.
Afisa mmoja mwandamizi
wa taasisi hiyo, Pieter Wezeman
alisema, muungano wa nchi za

Kiarabu unaofanya mashambulizi


nchini Yemen, unatumia silaha
za kisasa kabisa zinazonunuliwa
kutoka Marekani na nchi za Ulaya.
Kwa mujibu wa uchunguzi huo,
Saudi Arabia inashika nafasi ya
kwanza kwa kununua silaha katika
eneo la Mashariki ya Kati huku
wanunuaji wakubwa wa silaha
duniani wakiwa ni India, Saudi
Arabia, China na Umoja wa Falme
za Kiarabu.
Ripoti hiyo imeongeza kuwa,
uvamizi wa kijeshi unaoongozwa
na Saudia nchini Yemen, umeifanya
Saudi Arabia kuwa mnunuzi
mkubwa wa silaha katika eneo hilo.

Ripoti imebainisha kuwa


kiwango cha silaha zilizosafirishwa
barani Afrika, Asia na Mashariki ya
Kati zimeongezeka.
Zaidi ya nusu ya silaha
zilizouzwa Afrika zililetwa na nchi
mbili tu, yaani Morocco na Algeria,
ambazo zinaelezwa kuwa zimeingia
katika mashindano makali ya uuzaji
silaha kati yao.
Licha ya mizozo inayozikabili
nchi za Kusini mwa jangwa la
Sahara, lakini si soko kubwa sana la
silaha nzito kwa sababu ya uchumi
unaosuasua. Inaelezwa kwamba
hali ya umasikini unazuia nchi za
Afrika kununua silaha kwa wingi.
abna.ir

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Ltd, Dar es Salaam.

Вам также может понравиться

  • HAYAAN, The Long Journey of the Nomad Boy
    HAYAAN, The Long Journey of the Nomad Boy
    От Everand
    HAYAAN, The Long Journey of the Nomad Boy
    Рейтинг: 5 из 5 звезд
    5/5 (2)
  • Tishio la Ukombozi: Ubeberu na Mapinduzi Zanzibar
    Tishio la Ukombozi: Ubeberu na Mapinduzi Zanzibar
    От Everand
    Tishio la Ukombozi: Ubeberu na Mapinduzi Zanzibar
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1209aaa
    ANNUUR 1209aaa
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1209aaa
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1217
    Annuur 1217
    Документ20 страниц
    Annuur 1217
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1216d
    ANNUUR 1216d
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1216d
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1214
    Annuur 1214
    Документ20 страниц
    Annuur 1214
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1213 PDF
    Annuur 1213 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1213 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1207...
    Annuur 1207...
    Документ20 страниц
    Annuur 1207...
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1208
    Annuur 1208
    Документ20 страниц
    Annuur 1208
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1077
    Annuur 1077
    Документ12 страниц
    Annuur 1077
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1169a PDF
    ANNUUR 1169a PDF
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1169a PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1232 PDF
    Annuur 1232 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1232 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1228d
    ANNUUR 1228d
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1228d
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 112
    Annuur 112
    Документ16 страниц
    Annuur 112
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • Annuur 1172 PDF
    Annuur 1172 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1172 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1204
    Annuur 1204
    Документ20 страниц
    Annuur 1204
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1059
    Annuur 1059
    Документ16 страниц
    Annuur 1059
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • Annuur 1262
    Annuur 1262
    Документ20 страниц
    Annuur 1262
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1153 PDF
    Annuur 1153 PDF
    Документ16 страниц
    Annuur 1153 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Imaan Newspaper Issue 4
    Imaan Newspaper Issue 4
    Документ15 страниц
    Imaan Newspaper Issue 4
    Imaan Newspaper
    Оценок пока нет
  • Annuur 1231 PDF
    Annuur 1231 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1231 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1176b PDF
    ANNUUR 1176b PDF
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1176b PDF
    annurtanzania
    Оценок пока нет
  • Annuur 1219
    Annuur 1219
    Документ20 страниц
    Annuur 1219
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Kuvunjwa Kwa Msikiti Na Uhamisho Wa Wahadhiri 11 Waislamu UDOM
    Kuvunjwa Kwa Msikiti Na Uhamisho Wa Wahadhiri 11 Waislamu UDOM
    Документ5 страниц
    Kuvunjwa Kwa Msikiti Na Uhamisho Wa Wahadhiri 11 Waislamu UDOM
    Evarist Chahali
    Оценок пока нет
  • Annuur 1144
    Annuur 1144
    Документ16 страниц
    Annuur 1144
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annur Toleo La Ijumaa
    Annur Toleo La Ijumaa
    Документ16 страниц
    Annur Toleo La Ijumaa
    annurtanzania
    Оценок пока нет
  • Annuur 1179 PDF
    Annuur 1179 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1179 PDF
    annurtanzania
    100% (1)
  • Kuitwa Kwenye Usaili Mzumbe University May 2013 PDF
    Kuitwa Kwenye Usaili Mzumbe University May 2013 PDF
    Документ6 страниц
    Kuitwa Kwenye Usaili Mzumbe University May 2013 PDF
    yuvambena
    Оценок пока нет
  • Annuur 1138
    Annuur 1138
    Документ16 страниц
    Annuur 1138
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Gazeti La Annur
    Gazeti La Annur
    Документ12 страниц
    Gazeti La Annur
    Hassan Mussa Khamis
    Оценок пока нет
  • Annuur 1170
    Annuur 1170
    Документ20 страниц
    Annuur 1170
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Majina Ya Madaktari Na Vituo Walivyo Pangiwa
    Majina Ya Madaktari Na Vituo Walivyo Pangiwa
    Документ13 страниц
    Majina Ya Madaktari Na Vituo Walivyo Pangiwa
    kabange1
    Оценок пока нет
  • Annuur 1168 PDF
    Annuur 1168 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1168 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1115
    Annuur 1115
    Документ16 страниц
    Annuur 1115
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1035
    Annuur 1035
    Документ16 страниц
    Annuur 1035
    Hassan Mussa Khamis
    Оценок пока нет
  • Annuur 1226 PDF
    Annuur 1226 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1226 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1090
    Annuur 1090
    Документ12 страниц
    Annuur 1090
    annurtanzania
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1188a
    ANNUUR 1188a
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1188a
    Anonymous x8QGwFF
    100% (1)
  • ANNUUR1004
    ANNUUR1004
    Документ16 страниц
    ANNUUR1004
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • Annuur 1173 PDF
    Annuur 1173 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1173 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1096
    Annuur 1096
    Документ12 страниц
    Annuur 1096
    annurtanzania
    Оценок пока нет
  • Annuur 1041
    Annuur 1041
    Документ12 страниц
    Annuur 1041
    Hassan Mussa Khamis
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1167a PDF
    ANNUUR 1167a PDF
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1167a PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1111
    Annuur 1111
    Документ16 страниц
    Annuur 1111
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • ANNUUR1003
    ANNUUR1003
    Документ16 страниц
    ANNUUR1003
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • Annuur 1076
    Annuur 1076
    Документ12 страниц
    Annuur 1076
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • Annuur 1064
    Annuur 1064
    Документ12 страниц
    Annuur 1064
    annurtanzania
    Оценок пока нет
  • Annuur 1063
    Annuur 1063
    Документ16 страниц
    Annuur 1063
    Hassan Mussa Khamis
    Оценок пока нет
  • Annuur 1158
    Annuur 1158
    Документ16 страниц
    Annuur 1158
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Afisa Usalama Wa Taifa Ni Mtu Wa Aina Gani? Na Anafanya Nini?
    Afisa Usalama Wa Taifa Ni Mtu Wa Aina Gani? Na Anafanya Nini?
    От Everand
    Afisa Usalama Wa Taifa Ni Mtu Wa Aina Gani? Na Anafanya Nini?
    Рейтинг: 4 из 5 звезд
    4/5 (24)
  • Mtambo wa Mauti
    Mtambo wa Mauti
    От Everand
    Mtambo wa Mauti
    Рейтинг: 5 из 5 звезд
    5/5 (1)
  • Dini ya Fedha
    Dini ya Fedha
    От Everand
    Dini ya Fedha
    Оценок пока нет
  • Annuur 1264
    Annuur 1264
    Документ20 страниц
    Annuur 1264
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1227 PDF
    Annuur 1227 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1227 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1232 PDF
    Annuur 1232 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1232 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1231 PDF
    Annuur 1231 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1231 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1262
    Annuur 1262
    Документ20 страниц
    Annuur 1262
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1225
    Annuur 1225
    Документ20 страниц
    Annuur 1225
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1228d
    ANNUUR 1228d
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1228d
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1230 PDF
    Annuur 1230 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1230 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1228d
    ANNUUR 1228d
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1228d
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1229 PDF
    Annuur 1229 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1229 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1210a
    Annuur 1210a
    Документ20 страниц
    Annuur 1210a
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1226 PDF
    Annuur 1226 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1226 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1224
    Annuur 1224
    Документ20 страниц
    Annuur 1224
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1219
    Annuur 1219
    Документ20 страниц
    Annuur 1219
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1220
    Annuur 1220
    Документ20 страниц
    Annuur 1220
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1223
    Annuur 1223
    Документ20 страниц
    Annuur 1223
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1208
    Annuur 1208
    Документ20 страниц
    Annuur 1208
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1201
    Annuur 1201
    Документ20 страниц
    Annuur 1201
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1207...
    Annuur 1207...
    Документ20 страниц
    Annuur 1207...
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1200
    Annuur 1200
    Документ20 страниц
    Annuur 1200
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1202
    Annuur 1202
    Документ20 страниц
    Annuur 1202
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1195
    Annuur 1195
    Документ20 страниц
    Annuur 1195
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1204
    Annuur 1204
    Документ20 страниц
    Annuur 1204
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет