Академический Документы
Профессиональный Документы
Культура Документы
com
Sauti ya Waislamu
ISSN 0856 - 3861 Na. 1220 JAMADUL AWWAL 1437, IJUMAA , MACHI 11-17, 2016 BEI TShs 800/=, Kshs 50/=
Msekwa, Mwalimu
Nyerere siye
muanzilishi
wa harakati
za siasa Tanganyika
Soma Uk.10
Sheikh Muhammad
Burhan hatunaye
ANNUUR NEW.indd 1
3/9/2016 2:36:21 PM
AN-NUUR
Sura Al-Maidah 54
Fethullah-Gulen
ENYI wale ambao
mmeamini, atakayeacha
miongoni mwenu dini yake
basi pande hizi atawaleta
Mwenyezi Mungu watu
ambao anawapenda
na wao wanampenda,
wanyenyekevu kwa
waumini, wana nguvu juu
ya makafiri, wataipigania
dini ya Mwenyezi Mungu
hawataogopa lawama ya
mwenye kulaumu, hiyo
ndiyo fadhila ya Mwenyezi
Mungu anampa anayemtaka
na Mwenyezi Mungu ni
mkunjufu wa fadhila
mwenye kujua. [Al-Midah
54]
Kwa hakika aya hii
imekusanya juu ya mambo
muhimu sana ya kuongozwa
na uzindushi juu ya
uwezekano ni kutoka kwa
uwezekano wa kuacha dini
kati ya waumini na kwamba
huenda wakashindwa
baadhi ya watu ambao
wanausimamia Uislamu
kuonyesha kutilia manani
na kuguswa ambako
kunahukumiwa na
uchunguzi wa amana hii
huko mbele. Kwa sababu
hii wakati waliposhindwa
Banu-Umayya kuichukua
amana ambayo
walijitokeza kwa kuchukua
muda katika muda fulani na
wakadhoofika na uchukuzi
wa amana hiyo, amana
ilihama na kwenda kwa
Abbasiyyin kisha ikaenda
kwa Saifouziyyin na kutoka
kwa hao ikaendelea kwa
Othmaniyyin. Na watu
ambao Mwenyezi Mungu
atawaleta ameyaleta maelezo
yao kwa tamko la Nakra
lisilo wahusu watu au mtu
MWEZI MWANDAMO
Leo ni Tarehe 1 Jumada-at-Thania (Mfungo
9) mwaka 1437 AH, sawa na tarehe 11 March,
2016.
Tarehe 6 June tunategemea kuangalia mwezi
kwa Ramadhan na Tarehe 7 June 2016 tukijaaliwa
tutaanza Ramadhan Rasmi. Kutokea hii leo
Ijumaa ya tarehe 11 Machi 2016 hadi kufika
kuanza mfungo wa Ramadhani tunebakisha siku
87.
ANNUUR NEW.indd 2
anayemtaka na Mwenyezi
Mungu ni mkunjufu wa
fadhila mwenye kujuwa.
Na inasema aya nyingine
kwamba si haki kwa mtu
yoyote kupinga juu ya
yale ambayo ameyagawa
Mwenyezi Mungu.
Na kama alivyomchagua
Mwenyezi Mungu mtukufu
Mtume wetu na maswahaba
wake katika wakati muhimu
ule wa historia ya kuja
Mtume Muhammad (s.a.w),
atafanya uchaguzi wa watu
wengine kwa ajili ya kuipa
nguvu dini yake katika hizi
zama ambazo kumeachwa
ndani yake kuitumikia
dini na ngome za Uislamu
zimezingirwa katika pande
zake zote.
Ni kweli kwamba
uchaguzi huu huenda
ukafanyika katika maana
yoyote katika maana ya
ulimwengu wa roho. Na kwa
hali yoyote ile kwa hakika
Mwenyezi Mungu mtukufu
ataliweka juu tamko la dini
hii mara nyingine kupitia
watu ambao anawapenda
na wanampenda kwa
sbabu hii sifa za watu hawa
zimekuwa muhimu sana.
Na mwendelezo wa aya
unaweka wazi umuhimu wa
maudhui haya.
Watu hawa ni kundi
lililo safika lililotwaharika
mpaka kiwango cha kuwa
katika mkabala wa kwamba
Mwenyezi Mungu mtukufu
wakati alipowapenda na
akawachagua kama kundi
wao nao wanampenda
Mwenyezi Mungu mtukufu
kutoka katika vina vya
nafsi zao na aya nyingine
inayaelezea mapenzi haya
kwa kusema: Kwamba wao
hawatakuwa katika safu
ya maadui wa Mwenyezi
Mungu hata kama
watakuwa maadui hao ni
baba zao, au mababu zao au
ndugu zao au watoto wao
au jamaa zao. Mapenzi yao
yamefungwa kwa ajili ya
Mwenyezi Mungu mtukufu
peke yake, wanapenda kwa
ajili ya Mwenyezi Mungu
na wanachukia kwa ajili ya
Mwenyezi Mungu, wanatoa
kwa ajili ya Mwenyezi
Mungu na wanapokea kwa
ajili ya Mwenyezi Mungu,
hakizishughulishi nyoyo
zao wala miamala yao kitu
chochote isipokuwa mapenzi
ya Mwenyezi Mungu
hapana kitu chochote
kinachoyatangulia mapenzi
hayo au kinachokaa mahali
pake. Hii ndiyo sifa ya
kwanza na sifa muhimu
sana katika kundi ambalo
litakuja utakapofika wakati
wa kuja kwake na ambalo
liko nyuma ya chuo cha
maswahaba watukufu,
maana sifa ya kumpenda
Mwenyezi Mungu mtukufu
na kutaka radhi zake wakati
wote na kuyapata nguvu
mapenzi haya na radhi hii
juu ya yote yasiyokuwa
hayo.
MASUALA
1.Nani Alikuwa Shahidi wa mwanzo katika Uislamu? Jawabu :
Sumaya
2.Waislamu wa mwanzo wakikutana kujifunza dini kwenye nyumba
ya nani? Jawabu : Aqram
3.Waislamu wa mwanzo kukamatwa na kuteswa vibaya na makafiri
aliuwa Yassir na mke wake Summaya na mwanawao akiitwa? Jawabu :
Amar
4.Sahaba wa mwanzo kusoma Quran kwa sauti kubwa ndani ya
Alqaba ni Jawabu : Abdalla bin Masud
5.Kamanda wa mwanzo wa Kijeshi Waislamu alikuwa ni.. Jawabu
: Hamza
6.Watoto wa Syd Ali aliozaa na Bibi Fatma ni nani na nani? Jawabu :
Hassan, Huseein, Umm Kulthum, Zainab
7.Nani Shahidi wa mwanzo wa kiume katika Uislamu? Jawabu : Yassir
8.Mama wa Musaib bin Umair akitwa kwa jina gani? Jawabu : Khunas
Maalik
9.Sahaba aliokuwa tajiri wakati wa Mtume (SAW) mmoja wao alikuwa
ni nani? Jawabu : Abdulrahman
10.Sahaba yupi Wakfu wake unatumika hadi hii leo? Jawabu : Syd
Uthman
CHEMSHA BONGO: 42
Weka duara kwenye jawabu ilio sawa. Jawabu kamili wiki ijayo.
H
ibn
ibn
ibn
675
650
MASUALA
1.Taja jina la Quraish aliokuwa adui mkubwa wa Waislamu na kuwapa
mateso
2.Sahaba yupi alioongoza kukusanywa na kuandikwa kwa kitabu kitakatifu
cha Quran.
3.Mtume Muhammad (SAW) alimtuma sahaba yupi kama Gavana wake
katika nchi ya Yemen?
4.Taja jina la Sahaba aliomtaka Syd Uthman kuharakisha ukusanywaji wa
Quran..
5.Jina la mama wa Mtume Ismail ni..
6.Kukamilika kuandikwa na kukusanywa Quran chini ya usimamizi wa Syd
Uthman ulikuwa ni mwaka gani?
7.Alikuwa na umri wa miaka 13 na ni bin amu yake Mtume (SAW) na
alipofariki Mtume (SAW) inakisiwa umri wake ulikuwa ni miaka 13, jina
lake ni
8.Kutafsiriwa kwa Quran na kupewa maelezo kwa Quran maneno hayo
yanaitwaje?
9.Sehemu aliosimama Mtume Ebrahim kujenga Alqaba inaitwaje?
10.Jamii Iliomzunguka Mtume Muhammad (SAW) ikimjua kwa jina lipi?
Jee Unajua?
3/9/2016 2:36:25 PM
Habari
AN-NUUR
WAKINIONA, wanakuwa
na hofu ya kutisha, huwezi
kuamini kuwa ndio
wale majabali wa kutesa
wanapokuwa katika himaya
yao.
Nadhani hofu yao ni kuwa
huenda nikaita Waislamu
wawashughulikie, lakini
mimi atanilipia Allah. Wao
hofu hiyo watafakari siku
watakapoingia kaburini na
kukutana na Mola wao.
MUHANGA wa tuhuma za
Ugaidi, Ustadhi Jamali Yasin,
amesema amekuwa akiwaona
watesaji wake alipokuwa
mikononi mwa Jeshi la Polisi.
Anasema, mara kadhaa
amekutana na watesaji hao
Masjid Mtambani ila hajui
kama wanakuja kuswali au
ndio wapo kazini.
Ust. Yasini, amesema
hayo, akiongea na Waislamu
akielezea juu ya mkasa wake
wa kukamatwa na Polisi, Jijini
Dar es Salaam, ambapo alidai
akiwa mikononi mwa Jeshi la
Polisi, alipata mateso na baada
ya kuachiwa amekuwa dhaifu
kiafya.
Nimebahatika kuwaona
mara mbili watesaji wangu,
kwanza niliwaona katika
Msikiti wa Mtambani,
Kinondoni mara ya pili
nikakutana nao Masjid Haq,
tulitazamana uso kwa uso na
walijua kuwa nimewabaini.
Amesema Ust. Jamali.
Alisema, katika mazingira
hayo anamokutana nao
anaweza kupiga kelele
na kusema hawa ndio
watesaji wake na Waislamu
wanaotuhumiwa kwa ugaidi,
lakini akasema Allah (SW)
humpa moyo wa subra na
kuzishinda ghadhabu zake
juu yao, huku akimuomba
Mungu amjaalie hivyo kila
atakapowaona.
Ust. Jamali, alisema
anamuomba Mungu ampe
busara na subra juu ya watu
hao na kwamba si rahisi
kuamini kuwa Askari hao
ni Waislamu na wanaingia
Misikitini kwa nia haswa ya
kufanya ibada, kwani wamejaa
unyama kuliko ubinadamu na
hadhani kama wana chembe
ya imani na inawezekana
wasiwe Waislamu lakini
wanalazimika kujichanganya
Misikitini ili kutekeleza wajibu
wao.
ANNUUR NEW.indd 3
3/9/2016 2:36:29 PM
Tahariri
AN-NUUR
ANNUUR NEW.indd 4
AN-NUUR
Na Bakari
Mwakangwale
3/9/2016 2:36:30 PM
5
Bomba la gesi
sababu ya
kuvamiwa Syria
MPWA wa Rais wa zamani wa
Marekani, John F. Kennedy,
ambaye ni mwanasheria
amesema kuwa sababu
iliyoifanya Marekani ishiriki
katika kampeni za kumpindua
Rais wa Syria ni mradi wa gesi
wa Qatar.
Mwanasheria huyo, Robert
F. Kennedy Jr, ameandika
makala iliyochapishwa jana na
gazeti la Politico akisema kuwa,
Marekani ilichukua uamuzi wa
kumpindua Rais Bashar al Assad
wa Syria baada ya Rais huyo
kukataa kuunga mkono mradi
wa gesi wa serikali ya Qatar.
Mradi huo ulikusudia
HABARI ZA KIMATAIFA
AN-NUUR
Ukata wanukia
vikosi vya kulinda
amani Somalia
ANNUUR NEW.indd 5
3/9/2016 2:36:31 PM
6
NCHI sita wanachama wa
Baraza la Ushirikiano la Ghuba
ya Uajemi (PGCC) zimekiweka
Chama cha Wanaharakati wa
Lebanon, Hizbullah, ambayo
inaendesha mapambano dhidi
ya utawala wa Kizayuni na
magaidi huko Syria katika
orodha ya magaidi.
Baraza la Ushirikiano la
Ghuba ya Uajemi Jumatano
ya wiki iliyopita liliwaweka
wanaharakati wa Hizbullah
na makundi yote yenye
mfungamano na wanaharakati
hao kwenye orodha waliyoiita
ya waungaji mkono ugaidi,
kwa lengo la kuishinikiza zaidi
wanaharakati hao, ambao wana
nafasi kubwa katika matukio
ya ndani ya Lebanon na ambao
wanaendesha mapambano
dhidi ya utawala ghasibu wa
Kizayuni na pia wakiwa na
nafasi muhimu katika kutatua
mgogoro wa Syria.
Nchi za Kusini mwa Ghuba
ya Uajemi mwaka 2013 pia
ziliwawekea vikwazo baadhi
ya wanachama wa Hizbullah
kufuatia kuweko kijeshi
Hizbullah katika mgogoro wa
Syria.
Aidha mwaka huo huo baadhi
ya nchi wanachama wa Baraza la
Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi
ikiwemo Saudi Arabia, Emirates
na Bahrain ziliwataja Hizbullah
kuwa ni kundi la kigaidi.
Hata hivyo Katibu Mkuu
wa Hizbullah Sayyid Hassan
Nasrullah, amesema kuwa
lau kama wangelikaa kusubiri
mipango na mikakati ya Umoja
wa Waarabu, basi leo hii Israel
ingelikuwa iko nchini Lebanon.
Sayyid Nasrullah alisema
hayo mwishoni mwa wiki
na kubainisha kuwa, lau
wasingelikuwepo Hezbullah
basi leo hii Lebanon ingelikuwa
inatawaliwa na Israel,
kungelikuwa na makoloni
huko Lebanon na vijana wa
Kilebanoni wangelikuwa
wamejaa kwenye jela za
Wazayuni hivi sasa.
Alisisitiza kuwa, chaguo lao
kwa ajili ya kukomboa ardhi ya
Waislamu lilikuwa ni lazima na
litaendelea kuwa la lazima na
lau wangelikaa kimya, basi ardhi
yote ya Lebanon ingelikuwa
sawa na ya mashamba ya
Shaba'a yanayoendelea kukaliwa
kwa mabavu na Israel.
Alisema hapo ndipo
inapoonekana faida na
umuhimu wa kuiunga mkono
Syria kwa maslahi ya wananchi
wa Lebanon.
Wale wanaotutuhumu
kuwa muqawama wetu ni wa
kimadhehebu, wanapaswa
kujiuliza, tulipowaunga
mkono Waislamu wa Bosnia,
tuliwaunga mkono kwa kuwa
ni Mashia? Waislamu wa
Palestina, Waislamu wa Bosnia
ni Ahlusunna Waljamaa, lakini
tuliwaunga mkono.
ANNUUR NEW.indd 6
Makala
AN-NUUR
Aidha imeonekana
kuwatangaza Hizbullah kuwa
ni kundi la kigaidi, ni zawadi
bora ya kuutunukia utawala wa
Kizayuni.
Mrengo wa Hizbullah ndani
ya Bunge la Lebanon umetoa
taarifa na kueleza kwamba hatua
hiyo ya nchi wanachama wa (P)
GCC ni huduma kubwa, ambayo
nchi hizo imetoa kwa utawala
wa Kizayuni baada ya miongo
saba ya kuvamiwa na kukaliwa
kwa mabavu Palestina.
Mbegu za awali za
wanaharakati wa Hizbullah
wa Lebanon zilichipua katika
muongo wa 1980 baada ya nchi
hiyo kuvamiwa na kukaliwa kwa
mabavu na jeshi la utawala wa
Kizayuni. Mnamo mwaka 1982,
jeshi la Israel lilivuka mpaka wa
Lebanon hadi ndani ya ardhi ya
nchi hiyo na kusonga mbele hadi
mji mkuu Beirut.
Kutokana na kutawanywa
vifaru vya Israel kuanzia Kusini
mwa Lebanon hadi Beirut
na kuingia askari wa jeshi la
wanamaji la Marekani na wa
nchi za Magharibi ndani ya
ardhi ya Lebanon na kuanzisha
vituo vyao mjini Beirut, hapo
ndipo Hizbullah ilipojitosa
kwenye ulingo wa kukabiliana
na hujuma za wavamizi wa
Kizayuni na waungaji mkono
wao ili kuikomboa ardhi ya
Lebanon na uvamizi huo.
Matokeo na matunda ya
miongo miwili ya mapambano
ya vikosi vya Hizbullah dhidi
ya jeshi la utawala wa Kizayuni
lililojizatiti kwa silaha za kisasa
kutoka Marekani, yalikuwa ni
kuulazimisha utawala huo urudi
nyuma kwa kuondoka mjini
Beirut na kwenda kupiga kambi
Kusini mwa Lebanon.
Hatimaye mwezi Mei
mwaka 2000, katika kipindi cha
Uwaziri Mkuu wa Ehud Barak,
jeshi la utawala wa Kizayuni
lilifungasha virago na kukimbia
kutoka Kusini mwa Lebanon
huku likikiri kuwa limeshindwa
kukabiliana na wanamapambano
wa Hizbullah. Majeshi ya Israel
yalilazimika kuondoka Lebanon
baada ya miaka 22 ya kulifunga
faili la uvamizi na kuikalia kwa
mabavu.
Mwaka 2006, Israel ilijaribu
kuvamia tena Lebanon lakini
ilikutana kwa mara nyengine
tena na upinzani wa Hizbullah
katika vita vya siku 33, ambapo
baada ya mwezi mmoja wa
kuishambulia Lebanon kwa
makombora ya angani, nchi
kavu na baharini, hatimaye
jeshi la utawala huo likatangaza
usitishaji vita wa upande
mmoja na kuacha uhasama
wa mapigano, na hivyo
kuhuisha tena kumbukumbu
ya kukombolewa Kusini
mwa Lebanon na waharakati
Hizbullah katika vita hivyo.
Hadi sasa Hizbullah ndio
imekuwa ngome ya Lebanon
hususana katika eneo la Kusini
na pia wanachama wake ni
sehemu ya Bunge la Lebanon.
3/9/2016 2:36:32 PM
AN-NUUR
ANNUUR NEW.indd 7
Utumbo.
unachokula halitazimuliwa
kwa utaratibu unaotakiwa,
na mwili wako utaishia
kuelemewa na tindikali
kiasi cha kushindwa
kufanya kazi.
Madini makuu
yanayotengeneza akiba ya
alkali mwilini ni sodium,
calcium, potassium, na
magnesium. Tunayapata
madini haya kutoka
katika mboga za majani
na matunda pekee, kwa
sababu mwili unahitaji
madini haya yakiwa katika
mfumo wa ki-organic, na
si vinginevyo. Madini haya
yakiwa katika mfumo wa
ki-inorganic hayawezi
kutumiwa na mwili. Maana
ya mfumo wa ki-organic
ni kuwa viunganishi
(chemical bond) vya viasili
(elements) mbalimbali
ikiwa ni pamoja na madini,
ni dhaifu na ni rahisi
kuvunjika na kuviacha
viasili hivyo vikiwa
huru. Maana ya mfumo
wa ki-inorganic ni kuwa
viunganishi (chemical
bond) vya viasili (elements)
mbalimbali ikiwa ni pamoja
na madini, ni imara sana
na siyo rahisi kuvunjika
na kuviacha viasili hivyo
vikiwa huru.
Viasili ambavyo
havijaachwa huru
haviwezi kutumiwa na
mwili kwa mahitaji yake
mbalimbali, na badala
yake vitausababishia mwili
msongo (stress) usio na
sababu katika harakati
za kujaribu kuvitoa nje
ya mwili. Mfano rahisi ni
chumvi ya mezani ambayo
tunaitumia kama kiungo
cha kuongeza ladha
kwenye chakula. Chumvi
ya mezani huundwa na
viasili viwili ambavyo ni
madini ya sodium na yale
ya chlorine. Kiunganishi
kati ya viasili hivi ni imara
Inaendelea Uk. 8
3/9/2016 2:36:34 PM
Makala
AN-NUUR
ANNUUR NEW.indd 8
ya dharura italazimika
kufanya kazi bila kikomo,
basi utaanza kupata dalili
za magonjwa mbalimbali.
Dalili hizi ni ujumbe
unaotumwa na mwili
wako kuwa umegeuza
tairi la akiba kuwa ndiyo
gurudumu lako la kufanyia
safari zako za kila siku.
Iwapo sodium ya ki-organic
imeisha kutoka katika akiba
yako, hutadondoka na kufa
mara moja!
CALCIUM: Kuna madini
mbadala ya kuzimulia
tindikali inayolundikana
mwilini, mathalani madini
ya calcium. Mwili wako
ni chanzo kizuri sana cha
madini ya calcium kwa
sababu sehemu kubwa ya
mifupa yako inaundwa na
madini haya. Hata hivyo
tatizo la kutegemea madini
ya calcium kama kizimuo
cha tindikali mwilini ni
ukweli kwamba madini
haya yana kazi yake
maalum na tofauti kabisa
ndani ya mwili. Madini ya
calcium yanapochukuliwa
kwa ajili ya kwenda
kuzimulia tindikali
husababisha mifupa
kudhoofika. Magonjwa
mengi ya mifupa ikiwa ni
pamoja na yale ya kuwa na
meno mabovu chimbuko
lake ni hii hali. Hali hii
pia hupelekea calcium
kulundikana kwenye
damu, kitendo ambacho
husababisha damu kuwa
nzito na kuta za mishipa
ya damu kukakamaa.
Kinachofuata hapo ni
ugonjwa wa shinikizo la
damu, ugonjwa wa moyo
na hatimaye ugonjwa wa
kiharusi.
Ili kuepukana na
madhara ya tindikali ndani
ya mwili ni vizuri kula
lishe sahihi, lakini pia kuna
umuhimu wa kuachana na
tabia zinazochochea mwili
kuzalisha tindikali. Tabia
hizi ni zile zote zinazozaa
fikra na hisia hasi kama
kinyongo, hasira, gere, na
sononi.
3/9/2016 2:36:35 PM
9
MAKAMU Chancelor
wa Ujerumani Sigmar
Gabriel, amesema tajiri
Donald Trump, anayesaka
kugombea wa kiti cha rais
wa Marekani kwa tiketi ya
chama cha Republican ni
hatari kwa amani ya dunia
na maendeleo.
Katika mahojiano
na gazeti la Welt Am
Sonntag, Sigmar Gabriel,
ambaye pia ni Waziri wa
Uchumi wa Ujerumani
amemfananisha Trump
na Marine le Pen, Mkuu
wa chama cha mrengo wa
kulia cha Ufaransa FN na
Geert Wilders, kiongozi
wa chama kingine cha
mrengo wa kulia cha
Uholanzi, ambao amesema
wana misimamo mikali na
hatari kwa usalama, amani,
maelewano ya kijamii na
maendeleo ya dunia.
Matamshi ya Makamu
Chancelor huyo wa
Ujerumani ni mwendelezo
wa kauli za viongozi
wa bara Ulaya, ambao
wameeleza wasiwasi
wao kuhusu uwezekano
wa kuteuliwa Trump
kuwa mgombea urais wa
Marekani kupitia chama
cha Republican.
Hivi karibuni,
Waingereza nusu milioni
walisaini waraka unaoitaka
serikali ya nchi hiyo
kumzuia Donald Trump
kuingia nchini humo
baada ya kutoa wito wa
kuzuiwa Waislamu kuingia
Marekani.
Vilevile mwanasiasa
huyo ambaye
ameudhihirishia
ulimwengu dhamira yake
ya kibaguzi, aliwahi kutoa
mwito wa kutumiwa
mbinu za Manazi wa
Ujerumani chini ya uongozi
wa Adolph Hitler, dhidi
ya wafuasi wa dini hiyo ya
Mwenyezi Mungu nchini
Marekani.
Wiki iliyopita, Mgombea
huyo wa kiti cha rais wa
Marekani kwa tiketi ya
chama cha Republican,
alimfukuza mwanamke
mmoja mweusi wa nchi
ANNUUR NEW.indd 9
Makala
Donald Trump
AN-NUUR
3/9/2016 2:36:36 PM
10
AN-NUUR
Na Mohamed Said
MWALIMU Nyerere alikuwa
na uwezo mkubwa sana
wa kuridhisha watu kwa
nguvu ya hoja zake (power of
persuasion). Uwezo huo ndio
uliomsaidia kupata mafanikio
makubwa katika malengo
yake ya kisiasa. Uwezo huo
unajidhihirisha katika matukio
yafuatayo:
Kwanza, ni pale alipofanikiwa
kuwaridhisha kwa nguvu ya
hoja zake, wanachama wa Asasi
ya Kijamii ya kupigania maslahi
ya wafanyakazi wa Kiafrika
katika serikali ya Kikoloni,
iliyokuwa inaitwa Tanganyika
African Association (TAA);
kuvunja chama chao hicho na
badala yake kuunda chama
kipya cha siasa cha Tanganyika
African National Union (TANU),
mwezi Julai 1954, ili kiwe ni
chombo cha kupigania uhuru wa
Tanganyika.(Pius Msekwa Raia
Mwema toleo la 446 24 Februari
2016 Siku Nyerere Alipokataa
Viatu New York)
Nimeona nianze na nukuu
hii ili msomaji aelewe nini
Mzee Msekwa amesema pale
nitakapoeleza historia ya
uhuru wa Tanganyika kama
nilivyoelezwa na wazee wangu
ambao walikuwa bega kwa bega
na Mwalimu Nyerere wakati wa
kudai uhuru wa Tanganyika.
Imekuwa sasa jambo la kawaida
sana kwa wale waliokuja kuingia
TANU baadae sana kuonyesha
dharau kwa chama cha TAA
ambacho ndicho TANU ilitokea.
Wakati mwingine dharau hii
inaweza ikampita mtu ikiwa
hana ujuzi wa kusoma katikati
ANNUUR NEW.indd 10
ya mistari.
Angalia jinsi Mzee Msekwa
alivyoileta TAA kwa wasomaji
wake. Mzee Msekwa ameiita
TAA, Asasi ya Kijamii
ya kupigania maslahi ya
wafanyakazi wa Kiafrika katika
serikali ya Kioloni, iliyokuwa
inaitwa Tanganyika African
Association (TAA) Mzee
Msekwa anaogopa kuipa TAA
haki yake kuwa kilikuwa
chama cha siasa chinichini
kwa sababu akifanya hivyo
atashindwa hapo baadae
kumvisha Mwalimu Nyerere
joho analotaka kumvisha kuwa
hapakuwapo harakati za kudai
uhuru wa Tanganyika hadi
pale alipotokea Nyerere mwaka
wa 1952. Huu msimamo wa
Mzee Msekwa ndiyo historia
iliyozoeleka na ndiyo historia
rasmi ya uhuru wa Tanganyika.
Kabla sijaieleza historia ya
TANU ningependa kusema kitu
kuhusu kauli ya Mzee Msekwa
kuwa TAA kuwa kilikuwa
chama cha, kupigania maslahi
ya wafanyakazi wa Kiafrika
katika serikali ya kikoloni.
Hii pia si kweli. Chama
cha kupigania maslahi ya
wafanyakazi wa Kiafrika
kilikuwa Tanganyika
Government Servant Association
(TAGSA) na viongozi wake
ndiyo hao hao pia walikuwa
katika TAA wengine kwa dhahir
na wengine kwa kificho. Baadhi
ya viongozi hawa ni Thomas
Marealle, Ally Sykes, Dr. Wilbert
Mwanjisi, Rashid Kawawa
kuwataja wachache. Hawa
ndiyo walikuwa wanasiasa wa
nyakazti zile.
Chama cha TAA kilikuwa
kikifanya mambo mtambuka,
kikishughulika na kila ovu
lililomgusa Mwafrika wa
Tanganyika awe mkulima
wa Meru au mfanyakazi wa
serikalini.
Vuguvugu la siasa Tanganyika
lilikuja na sura na mwelekeo
mpya mwaka wa 1950 palitokea
mapinduzi Makao Makuu
ya TAA New Street baada
ya kuona kuwa viongozi
waliokuwapo madarakani wengi
wao wakiwa watu wazima
hawakuwa wanakwenda na kazi
ya mabadiliko ya siasa kama
ilivyokuwa dunia nzima kwa
makoloni yote ya Muingereza
wananchi kuanzisha vuguvugu
la kutaka kujitawala. Waingereza
walikuwa wanashughulishwa
na wazalendo India na Gahana
kudai nchi zao. Hapa ndipo
3/9/2016 2:36:36 PM
11
Makala
Na Omar Msangi
ANNUUR NEW.indd 11
AN-NUUR
Itiqaf ya AK-47!
Jela maisha ongeza miaka 30
Somo kutoka Duka Brothers
3/9/2016 2:36:39 PM
12
BIN RIJAL
ANNUUR NEW.indd 12
Mpunga ulioshamiri
AN-NUUR
asumini?
Kila lugha huita mpunga
kwa jina lake, hebu
tuangalie lugha mbalimbali
waitavyo, Waswahili
huita mpunga, urzu kwa
Kiarabu, Kicomoro maele,
Wajarumani huita reis,
Wataliani riso, Wajapani
ine au sakih, Wamalay
huita bras au padi, Wareno
arroz, Waviatnam huita lua
nep au lua, Wahaiti diri,
Afrikana rys, Chichewa
mpunga, Hausa huitwa
shinkafe, Waigbo huita
osikapa, Sesotho raease,
Wasomali barris, Wazulu
irayisi, Wafarsi barnj,
Waturuki pirinc, Wafaransa
riz n.k.
Mpunga asili yake ni
bara la Asia na unamea
vizuri katika sehemu za
Kusini na Kusini Mashariki
ya bara hilo la Asia. Ndio
utaona kuwa wakazi wa
bara hilo wanapendelea
kula wali kuliko chakula
chengine chochote
kile. Mfano wakazi wa
Indonesia milo yao mitatu
yote ile hula wali, kuanzia
chai ya asubuhi, chakula
cha mchana na chakula cha
usiku.
Wataalamu wa mambo
ya kale wanatufahamisha
kuwa mpunga ulianza
kuonekana katika mto
Yangtze Kusini mwa nchi
3/9/2016 2:36:40 PM
13
Habari/Tangazo
AN-NUUR
WANAFUNZI wametakiwa
kutumia vizuri na kwa usahihi
mitandao ya kijamii ukiwemo
ule wa`Internet` katika
kujisomea ili waweze kupata
faida chanya kupitia mitandao
hiyo.
Wito huo umetolewa na Bw.
Ismal, ambaye ni mwalimu wa
shule ya Sekondari ya Kiislamu
Kiblatain, iliyoko eneo la Kawe
jijini Dar es salaam wiki hii.
Mwalimu huyo alisema kuwa
utandawazi umeisogeza dunia
kuwa kama jiji na kurahisisha
mawasiliano na ukusanyaji wa
data na ufundishaji wa masomo
kuwa mwepesi.
Alisema kuwa teknolojia hiyo
ya elimu kwa njia ya mtandao
pia inaweza kutumiwa na
wanafunzi kupata faida kubwa
katika kuitafuta elimu kwa njia
rahisi, salama na kwa gharama
nafuu.
Hata hivyo mwalimu huyo
alisema kuwa ili kukabiliana na
tatizo la wanafunzi kupoteza
muda na fedha zao kutumia
vibaya mitandao hiyo, kuna haja
ya kutoa elimu ya matumizi
sahihi ya mitandao pamoja na
kubainisha athari au madhara ya
matumizi mabaya katika maisha
yao.
Wanafunzi wengi nchini
wamekuwa wakitumia vibaya
huduma ya `internet`, kiasi
cha kuwafanya waathirike
kimaadili na kifikra, jambo
ambalo limekuwa linagharimu
mustakabali wa maisha yao na
familia zao kwa ujumla.
Mwalimu huyo alisema
kuwa yeye ni mfano wa watu
waliofaidika sana na nyenzo za
mawasiliano za mitandao, hasa
katika ukusanyaji wa nyaraka
mbalimbali za rejea za masomo
na maelekezo ya namna ya
kufundisha kwa mbinu mpya za
kisasa.
Naye mwanafunzi wa shule
hiyo Ahmed Sabri, amewataka
wanafunzi wenzake kuitumia
fursa ya matumizi ya mitandao
vizuri, ili iweze kuleta faida
katika suala zima la elimu.
Mwanafunzi huyo amewataka
wanafunzi wenzake wenye
tabia za kutumia mitandao
hiyo kwa matumizi ambayo
sio sahihi, kubadili fikra na
kutumia nyenzo hiyo huria ya
mawasiliano katika masuala ya
kielimu na kuacha mara moja
kudurusu mitandao kwa ajili
na kuangalia picha za
mapenzi, kutumiana maoni
ya juu ya wasanii nk. Mambo
ambayo hayana maadili na
yanayowasababishia wanafunzi
kutokufuatilia masomo yao
inavyotakiwa alisema Ahmed
Sabri.
ANNUUR NEW.indd 13
3/9/2016 2:36:42 PM
14
MAKALA/MASHAIRI
UADILIFU WA DPP !
AN-NUUR
Itiqaf ya AK-47!
Shura ya Maimamu
Kamati ya Maafa
Kamati ya Maafa ya Shura ya
Maimamu, inatoa wito kwa Waislamu
kuchangia huduma za malazi kwa
Masheikh Farid Had, Mselem Ally
na Waislamu wengine waliopo katika
gereza la Segerea Jijini Dar es
Salaam, kwa tuhuma za Ugaidi.
Hakika kwa kila atakae toa atakuwa
amejiwekea akiba isiyo oza, mbele
ya Mwenyezi Mungu.
Unaweza kuchangia kupitia Namba
zifuatazo:0655, 0767, 0789, 0774/ 74 52 88.
Katibu Ustadhi Ally Mbaruku.
ANNUUR NEW.indd 14
Inatoka Uk. 11
mwenzao. Akina
Mahmoud walikuwa
Waislamu kutoka Misri.
Wakati polisi
na Task Force zao
wakiendelea kukamata
vijana wa Kiislamu
mitaani kwa tuhuma
za ugaidi, huku
waliokamatwa awali,
ni miaka sasa hali zao
ikiwa hazijulikani,
utashangaa kwamba
bado wapo watu wenye
ujasiri wa kupita huku
na kule kulani njia,
wanazodai kuwa ni
za kutuchelewesha.
Wanataka na kuhimiza
qitali cha IS na akina
Jihad John. Sasa iwapo
utaona kuwa labda
hiyo ni kutokana na
Imani yao thabiti.
Kwamba hao ndio
akina Abu Bakr alBaghdadi Al Quraishiy,
wewe itabidi ujilaumu
mwenyewe kwa ujinga
wako. Na hiyo ni iwe
kwa kutumia vigezo
vya Aya na Hadithi
(Uislamu) au akili tu ya
kawaida.
Yupo Wakili mmoja
katika mawakili walio
wahi kuchukua kesi
za Waislamu anasema
wakati akiwa katika
kituo kimoja cha polisi
walifika watu wakitaka
msaada kwa jamaa
yao mmoja ambaye ni
polisi kituoni hapo.
Katika mazungumzo
yao, wakili yule
akiwasikia kwa
mbali bila kuonyesha
kuwa anasikiliza
kinachozungumzwa,
Polisi aliwauliza, hao
watu ni Waislamu
au. Jamaa wakajibu
hapana sio Waislamu.
Ingekuwa Waislamu
tungewapachika kesi ya
ugaidi. Alisema Polisi
yule.
wanaharakati, wasio
taka kucheleweshwa,
wanaojidai kuwa
wanaharaka ya
kusimamisha Dola,
kumbe wanatumiwa
na FBI, wakawatosa
kupitia Itiqaf za
Majambia.
Kama mtu mwenye
sifa fulani ametajwa
katika Quran kuwa
huyo mahali pake ni
katika tabaka la chini
kabisa la Jahannam,
hapana shaka huyo
ni katika maadui
wakubwa wa Uislamu
na Waislamu. Ila
tu la kufahamu ni
kuwa Mtume (s.a.w)
hakuwahi kushika
silaha kupambana
na wanafiki.
Kinachotakiwa ni
kuwafahamu na kujua
namna ya kuwaepuka,
muepuko mwema.
Ila tusiache kutafuta
namna ya kuwanasihi
kwa sababu kuna
wengi wao wanafanya
kazi hiyo, bila kulipwa
hata senti moja.
Bali hutumiwa au
kujifanyia mambo kwa
ujinga wao tu wenyewe
wa Dini na Dawah
yake pamoja na ujinga
wa kuijua dunia ya leo.
Katika hili tujue
kuwa, makafiri
wanapanga ugaidi feki
na kuunda magaidi
feki kama hao IS, Boko
Haram, Al Qaida, ili
ipatikane sababu ya
kuhujumu Waislamu.
Lakini ili njama zao
zifanikiwe vizuri,
ni lazima wawepo
watu wa kuonyesha
kuwa kitisho cha
ugaidi ni cha kweli.
Ndio unawaona
wakihangaika
kuwatumia wenzetu
kuandaa itiqaf za
majambia na program
kama zile za Ijumaa
na darsa za Firdous
kuwanasa vijana wa
Kiislamu.
3/9/2016 2:36:43 PM
15
Makala
AN-NUUR
Kutoka Mimbarini
WAISLAMU nchini
wametakiwa kuwa
mstari wa mbele
katika kuziimarisha
nyumba za Allah
(S.W.) kiibada na
kimazingira.
Wito huo umetolewa
Ijumaa iliyopita na
Sheikh Anas Ismail
Feruzi alipokuwa
akiwahutubia
mamia ya Waislamu
waliokuwa
wamefurika kwa ajili
ya kutekeleza ibada
ya swala ya Ijumaa
katika msikiti mkuu
wa Ijumaa wilayani
Ukerewe mkoani
Mwanza.
Mara baada ya
utangulizi wa khutba
yake, iliyokuwa na
anwani 'Kuimarisha
Nyumba za
Mwenyezi Mungu',
aliwatanabahisha
Waumini waliokuwa
wamefurika msikitini
hapo kwamba dhima
ya kuziimarisha
nyumba za Allah
(S.W.), ambazo
ni misikiti, ni yao
waumini.
Kwa uthibitisho
zaidi wa hilo,
aliwakumbusha
waumini hao
kauli yake Allah
(S.W.) isemayo
''Wanaoamirisha
misikiti ya Mwenyezi
Mungu ni wale
waliomuamini
Mwenyezi Mungu
na siku ya mwisho,
na kusimamisha
swala na kutoa zaka
na hawamwogopi
yeyote ila Mwenyezi
Mungu; basi hao
ndio wanaotarajiwa
kuwa miongoni mwa
walioongoka'' (9:18).
Akitoa ufafanuzi
kuhusiana na
maana ya dhana
ya uimarishaji wa
misikiti, Sheikh Anas
aliainisha maana mbili
ambazo wanazuoni,
miongoni mwao ni
Sheikh Abdurrahman
bin Assaad, wamezitoa
kuhusiana na
ANNUUR NEW.indd 15
Inatoka Uk. 10
3/9/2016 2:36:45 PM
16
Makala
AN-NUUR
ANNUUR NEW.indd 16
anawaadhibu wanaodhulumu
hata kama dhuluma kutoka
kwa Muislamu kwenda kwa
kafiri.
Kauli ya QUR-ANI kwa
upande wa wazazi wawili
ambao ni mushirikina,
ambao wanajaribu kumtoa
mtoto wao katika imani ya
Uislam na kumpeleka katika
ushirikina.
Na tumemuusia
mwanadamu kuwafanyia
ihsani wazazi wake, mama
yake ameichukua mimba
yake kwa udhaifu juu ya
udhaifu na kumnyonyesha
na kuja kumuachisha
katika miaka miwili,
kwamba unishukuru mimi
na wazazi wako, marejeo
yenu ni kwangu na wazazi
wako wakikushurutisha
kunishirikisha na yale
ambayo huna ilimu nayo,
usiwatii lakini kaa nao
kwa wema hapa duniani
madam ni wazee wako, ila
usiwafuate tu mwendo wao
mbaya kisha marejeo yenu ni
kwangu, hapo nitakuambieni
mliyokuwa mkiyatenda
Luquman (14/15).
Na katika himizo la Qurani
tukufu na hadithi za Mtume
(s.a.w) juu ya wema na
ihsani kwa wasio Waislam,
ambao hawapigani vita
katika dini yenu, Mtume
(s.a.w) akateremshiwa na
Mwenyezi Mungu Mtukufu,
hakukatazeni kuwafanyia
ihsan na uadilifu wale ambao
hawakupigana nanyi katika
nchi zenu, hakika Mwenyezi
Mungu anawapenda
wafanyao uadilifu, Mwenyezi
Mungu anakukatazeni kwa
wale ambao wanapigana
nanyi katika dini na
kukufukuzeni kuwafanya
marafiki na wawafanyao
marafiki, basi hao ndio
madhalimu Al-mumtahina
(8-9). Basi ameamrisha
Mtume kukubali zawadi zao
na kuwakaribisha nyumbani
na kuishi nao kwa wema.
Watu hao ni hawa
wanaotimiza wajibu wao na
wanaoiogopa siku ambayo
shari yake itaenea sana na
huwalisha chakula masikini
na mayatima na wafungwa
na hali ya kuwa wenyewe
wanakipenda chakula hicho,
husema wenyewe katika
nyoyo zao wanapowapa
chakula hicho tunakulisheni
kwa ajili ya kutaka radhi
ya Mwenyezi Mungu tu
hatutaki kwenu malipo wala
shukurani (789
3/9/2016 2:36:50 PM
17
Na Musa Ame
SHUKRANI zote zinamstahiki
Allah (sw) na sala na salamu
zimfikie Mtume (saw) na
Masahaba zake na wanaofuata
muongozo wake mpaka siku ya
mwisho.
Nimeonelea bora tuelimishane
kuhusu mada hii ya aqida kwa
vile somo la aqida ni somo
la msingi katika kumfahamu
Muumba, na katika kutengeneza
itikadi ya Muislamu. Elimu
ya aqida ni fighi kubwa zaidi
kuliko fiqhi ya sala. Kwa
sababu isipotengenea aqida ya
Muislamu, huenda sala yake na
ibada zake nyengine zote zikawa
batili.
Somo hili linakuwa nyeti kwa
sababu kukosekana aqida sahihi
kunapelekea kosa la shirki,
ambalo hubatilisha ibada zote
za mja na kumpeleka motoni.
Maulamaa wanaliona somo la
aqida kuwa ni somo bora kuliko
masomo yote.
Katika mfululizo wa mada
hizi za aqida tutatumia kitabu
kiitwacho Aqidat Tahawiyya
tumechagua kitabu hicho kwa
vile ni kitabu kinachokubalika
na Maulamaa wote wa aqida na
kimesifiwa na jopo la Maulamaa
na si vibaya kunukuu baadhi ya
maoni yao juu ya kitabu hichi.
Ibn Kathyr anasema Alikuwa
yeye (Imam Tahawy) ni
mpokezi mzuri na muaminifu
wa hadith (Bidaya Wanihaya).
Hapa Ibn Kathyr anamuelezea
mtunzi wa kitabu hichi kuwa ni
mwanachuoni muaminifu wa
hadithi na mpokezi mzuri wa
hadithi za Mtume (saw).
Ibn Hajar Asqalany anasema
kuwa Alikuwa mwanachuoni
mkubwa na maarufu alikuwa
na ujuzi kuhusu khitilafu za
Maulamaa na alikuwa na uoni
mzuri. ( Lisan al Mizan).
Imam Dhahaby anasema
kuwa Alikuwa Muhadithyna na
Ulamaa wa Misri mwenye ujuzi
wa hadithi na fiqhi. (Tarikh al
Kabyr).
Kwa ujumla Maulamaa
wakubwa wanakubaliana
kuhusu kitabu hichi na hakuna
hitilafu katika kukitumia
kama ni kitabu cha elimu ya
Aqida, kwa wakati huu kitabu
hichi pamoja na sherhe zake
hutumiwa katika mitaala ya
vyuo vikuu katika kusomesha
somo la aqida.
Kuhusu mtunzi wa kitabu
jina lake ni Abuu Jaafar Ahmad
Ibn Muhammad Ibn Salamah
Tahawy aliyezaliwa Egypt
mwaka 239 , na kufariki mwaka
321 Hijria. Baba yake alikuwa ni
Mtaalamu wa hadithi . Alisoma
pia kwa Imam Ismail Ibn Yahya
Muzany Ulamaa wa Kishafi na
alisoma kitabu cha Mukhtasry
Muzani , kitabu maarufu cha
elimu ya fiqhi katika Madhehebu
ya Shafy. Baada ya hapo alisafiri
maeneo kadhaa kutafuta elimu
ANNUUR NEW.indd 17
MAKALA
AN-NUUR
Aqida-1
3/9/2016 2:36:53 PM
18
TANGAZO
AN-NUUR
ANNUUR NEW.indd 18
3/9/2016 2:36:54 PM
19
Ukurasa wa Watoto
AN-NUUR
3/9/2016 2:37:00 PM
AN-NUUR
20
MAKALA
20
Soma gazeti la
AN-NUUR
KWA TSH 800/=
kila Ijumaa
AN-NUUR
ya kusajili Wadhamnini au
kubadilisha Wadhamnini,
tatizo ambalo linaisumbua
Misikiti mingi nchini hivi
sasa. Amesema Wakili
Nassoro.
Wakili Nassoro, ambaye
amekuwa karibu zaidi na
jamii ya Kiislamu katika
maswala mbalimbali
akiwasaidia Waislamu katika
masuala ya kisheria, alisema
anashauri zaidi kuacha
kufanya kazi kwa mazoea,
kwani hivi sasa hali ya
kimazingira imebadilika.
Alisema, kila inapobidi
katika maswala mabalimbali
katika jamii ya Waislamu
iombe na kupata ushauri wa
wataalamu katika kuyaendea
masuala mbalimbali kwani
dunia imebadilika ili waweze
kwende vyema kwa lengo
la kuongeza ufanisi katika
Misikiti na Taasisi zao.
Wakili Nassoro, alisema
kwa maana hiyo sasa, imefika
wakati Taasisi, Mabaraza,
Jumuiya na Misikiti zote
zirekebishe Katiba zao
ili kuweka vipengele au
vifungu maalum vilivyo wazi
vya namna ya utatuzi wa
migogoro kwa kutaja taratibu
za utatuzi wa migogoro.
Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Ltd, Dar es Salaam.
ANNUUR NEW.indd 20
3/9/2016 2:37:01 PM