Вы находитесь на странице: 1из 20

www.annuurpapers.co.tz au facebook:annuurpapers@yahoo.

com

Sauti ya Waislamu

AHLU SUNNA WAL JAMAA HAJJ AND UMRA TRUST

(3) HIJJI UDHAMINIWE NA ALLAH!

Mtume(saw) amesema kuwa Mwenye kuhiji


amedhaminiwa na Allah na ni mgeni wake.
Tuyaweke maisha yetu katika udhamini wa
Allah. Tulishaitwa sote tangu zama za Nabii
Ibrahim(as) tukawe wageni wa Allah, na
hakuna wito mwengine Gharama zote kwa Hijja
2016/1437 ni Dola 4,600. Umra ya Ramadhani
ni Dola 2,700. Karibuni Ahlu Sunna wal
Jamaa kwa huduma nzuri na uongozi bora.
Wasiliana nasi: Tanzania Bara: 0679895770/
0688895777; 0765462022; 0712735363.
Zanzibar: 0777468018; 0777458075;
BEI TShs 800/=, Kshs 50/= 0777845010; 0777497300.

Maalim Bassaleh awe kigezo


ISSN 0856 - 3861 Na. 1223 JAMADUL AAKHER 1437, IJUMAA , APRILI 1-7, 2016

Waislamu, Wakristo
wamkosa Idrisa
Mimbar zitumike
vyema kutoa ujumbe

Kwa pamoja tukatae

Tukumbuke, wema hushinda uovu


Mwishowe, batili ni yenye kuondoka

Hapa inahitajika Fatwa

Wazanzibari tulichagua maridhiano


na kukataa mfarakano. Tulichagua
umoja na kukataa mgawanyiko.
Tulichagua upendo na kukataa chuki.
Tulichagua matumaini na kukataa
khofu. Tulichagua amani na kukataa
fujo. - Uk. 4.

MUFTI Abubakar Zubery (wa pili kushoto), akimuombea dua Mkuu wa


Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (katikati), hivi karibuni. Kutoka
kulia ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum,
Mshauri Mkuu wa Mufti, Sheikh Abubakar Khalid na Msaidizi wa Sheikh
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Othman Mkambaku.

ISMAIL Jussa Ladhu.

MAALIM Ally Bassaleh.

Mufti kamwombea Dua RC Makonda!


Kamfikishia yanayowasibu Waislamu?

ANNUUR NEW.indd 1

3/30/2016 1:12:21 PM

Suratul An-aam 124

Fethullah-Gulen
MWENYEZI Mungu
ndiye mjuzi zaidi wa
mahali atakapouweka
ujumbe wake. [Al AnAam 124]
Kuzaliwa kwa Uislamu
na ujumbe wake, katika
mji wa Makkah kisha
kuenea kwake katika
pande mbalimbali za
ulimwengu, baada ya
hapo kumejengwa juu
ya hekma nyingi sana
na kama ambavyo
kunawezekana
kuifanyia tathmini aya
tukufu:Mwenyezi
Mungu ndiye mjuzi zaidi
wa kupajuwa mahali pa
kuuweka ujumbe wake.
Katika mtizamo na
uelewa huu vile vile
kunawezekana kufanyia
tathmini kwa upande
wa elimu inayotafiti
asili ya binadamu na
maendeleo yake na
mazoea yake na itikadi
zake . Anthropology na
jiografia na Historian
na Ubinadamu na kwa
upande wa lugha na
mahali na baki ya vipeo
vyengine vya masuala
haya. Ndiyo hakika
Mwenyezi Mungu
mtukufu yeye ndiye mjuzi
sana wa yule ambaye
anamchagua kwa ajili ya
utume wake na kwa ajili
ya ujumbe wake na katika
jamii gani utadhihirika
ujumbe wake, na katika
ujumla wa mazingira
gani ya mapambano ya
kimataifa, na ya kidini
na kibinadamu na baada
ya kufikia mapambano
haya, kiwango gani ndipo
humpeleka Mwenyezi
Mungu mjumbe mpya
na dini mpya. Na sasa
tutayapekua mambo
hayo:
1. Upeo wa
ubinadamu kwa ajili
ya ujumbe: Aya hii
inaashiria kwenye
kwamba Mwenyezi
Mungu mtukufu
ndiye anayemjuwa
sana mjumbe ambaye
anamchagua na ataweka
kwake amana ya
kuufikisha ujumbe huu

ANNUUR NEW.indd 2

AN-NUUR

Mafundisho ya Qur'an/Uwanja wa Maarifa

wa Mwenyezi Mungu na
yule ambaye kunafanyika
kuuelekeza ujumbe
huu. Na katika zama za
Mtume kulikuwa kuna
watu ambao wanadhani
kwamba Walid bin
Mughera na Urwa bin
Masoud A-Thaafi, ni
wabora sana kwa kupewa
ujumbe na wanafaa mno.
Na kwa hakika Quran
imetaja rai ya watu hawa
kwa hawa watu wawili
katika aya nyingine kwa
kusema: Na wamesema:
Kwanini isingeteremshwa
hii Quran juu ya mtu
kutoka miji miwili
ambayo ni mtukufu.
[A-Zukhruf 31] Quran
ikawa jibu kwa kusema:
Sisi tumegawa kati yao
maisha yao katika uhai
wa dunia. [Al-Zukhruf
32]. Na hapana shaka
kwamba masuala yote, na
jambo kubwa mno mfano
wa jambo la utume,
hakuwezekani kuliacha
kwa maoni ya huyu au
yule. Akiwa Mwenyezi
Mungu mtukufu anajuwa
na yeye anajuwa hapana
shaka yoyote siri za
binadamu ambazo
zimo katika raha ya
binadamu na moyo wake
na analenga kwenye
kuzihusisha siri hizo, kwa
huyo binadamu, yeye
ndiye anayejuwa sana
pasi na shaka yoyote, mtu
ambaye anafaa sana kwa
kusimama na jukumu
hili. Kwa msingi huu,
mtu ambaye anamtukuza
yeye Mwenyezi Mungu
mtukufu kwa ujumbe,
ndiye mtu anayefaa sana.
Kwa hakika kusimama
kwa Al-Walid Bin AlMughira na wengine
kwa kumdogosha
Mtume wetu (S.A.W.)
na kumwangalia kwa
kumzingatia kuwa hafai
kwa utume kitendo
hicho kinahesabiwa
kuwa ni kuchuma
madhambi makubwa na
wao kwa mtazamo huu
wameporomoka katika
mtazamo wa Mwenyezi
Mungu mtukufu.
Wameshuka kwenye
daraja la chini sana na
kwenye cheo duni sana.
Na Mwenyezi Mungu
mtukufu anatueleza
unyonge na uduni
ambao utawapata watu
hawa katika mtiririko
wa aya hiyo hiyo
(Utawapata wale ambao

wamefanya maovu
uduni kutoka mbele
za Mwenyezi Mungu,
adhabu ngumu kwa
sababu ya yaliyokuwa
wanayatenda [Al-Annam
124].
Na Mwenyezi Mungu
mtukufu anasema:
Mwenyezi Mungu
anawateuwa kutokana
na malaika wajumbe na
kutokana na watu. [AlHajj 75]. Hapana juu yetu,
isipokuwa kumheshimu
na kumtukuza Yule
ambaye ameteuliwa
na Mwenyezi Mungu
mtukufu. Na kama
haikuwa hivyo, kuonesha
kutoridhika kwa namna
yoyote ile dhidi ya yule
ambaye ameteuliwa
na Mwenyezi Mungu,
kuna kiporomosha
cheo cha mtu huyo na
kunamfanya awe duni
mwenye kudhalilishwa
na anakuwa ni mwenye
kunyimwa msaada
na Baraka ambazo
wanafaidika nazo Mitume
na Mawalii na wateule na
wenye kukurubishwa.
Ndiyo mfano wa
mtu huyu vyovyote
kitakavyo kuwa cheo
chake, atafungamanishwa
na unyonge na uduni na
atanyimwa misaada yote
ya Mwenyezi Mungu.
Kisha kwa hakika
utukufu wa Mtume wetu
(s.a.w.) na kufaa kwake
na kukubalika kwake
hayo yanajulikana na
yanakubaliwa katika
zama zote na nyakati
zote na kwa watu wote.
Na umoja na kuwa
vitabu vya mbinguni vya
zamani vimepotoshwa
kwa hakika wanawazuia
watukufu mifano ya
mjuzi sana Rahmatullah
Al-Hindi na mjuzi sana
Al-Jisri wamekuta katika
vitabu hivi bishara mia
moja na kumi na nne
na misemo kuhusu
kuja kwa Mtume huyu
mtukufu. Ndiyo kwa
hakika wamekubaliana
Manabii wote kwa
kuzingatia tokea Dawoud
na Sulayman na Mussa
(a.s.) na kukomelea kwa
Yahya na Zakaria na Issa
(a.s) juu ya bishara ya
kuja kwa mjumbe huyu
mtukufu na waliwaeleza
watu wao kwamba
Mtume huyo atakuwa
ni mwenye kukusanya
ubora wote wa Mitume
(a.s.). Na kwa mazingatio
haya, Mtume (s.a.w.)
ndiyo mwenye daraja kwa
wote. (Itaendelea)

JAMADUL AAKHER 1437, IJUMAA APRILI 1-7, 2016

JAWABU CHEMSHA BONGO NAMBA: 44

al

211 :30

7 :19

20 :12

8 :9

6:6

20 :7

3 :15

4 :1

MASUALA
1.Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi aliye kuumbeni kutokana
na nafsi moja, na akamuumba mkewe kutoka nafsi ile ile. Na akaeneza
kutokana na wawili hao wanaume na wanawake wengi. Na tahadharini
na Mwenyezi Mungu ambaye kwaye mnaombana, na jamaa zenu. Hakika
Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaangalieni Suara ipi na aya gani?
Jawabu: 4:1 (An-Nisaa)
2.Kibla cha mwanzo kilikuwa wapi? Jawabu Bayt al Maqdis
3.Kuba lijulikanalo kwa Kiengereza Dome of the rock liliopo Jerusalem
linaitwaje kwa Kiarabu? Jawabu Qubatt as Sakhrah
4.Siku gani inakaririwa sana katika Quran? Jawabu Qiyama
5.Sehemu gani katika Quran imetajwa kuwa maji ndio chimbuko la
maisha? Jawabu 21 :30
6.Mwanamke gani wa pekee jina lake linasomeka kwenye Quran?
Jawabu Maryam
7.Kushuka kwa wahyi wakawanza na wapili kilipita kipindi cha muda
gani? Jawabu Miaka 2 miezi 6
8.Sura ipi inaanza bila Bismillahi? Jawabu Tawba
9.Sura ipi Bismillahi inajitokeza mara mbili? Jawabu Suratul Naml
10.T'alaka ni mara mbili. Kisha ni kukaa kwa wema au kuachana kwa
vizuri. Wala si halali kwenu kuchukua chochote mlicho wapa wake zenu,
ila ikiwa wote wawili wakiogopa ya kwamba hawataweza kushikamana
na mipaka ya Mwenyezi Mungu. Basi mkiogopa kuwa hawataweza
kushikamana na mipaka ya Mwenyezi Mungu hapo itakuwa hapana
lawama ikiwa mwanamke atajikomboa. Hii ndiyo mipaka ya Mwenyezi
Mungu; basi msiikiuke. Na watakao ikiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu,
hao ndio madhaalimu. Aya hii ni yangapi katika Sura ipi? Jawabu 2:229

CHEMSHA BONGO: 45

Weka duara kwenye jawabu ilio sawa. Jawabu kamili wiki ijayo.
A

77 :19

KJ

57 :26

14

86

49 :7

ER

28

47 :1

45 :5

MASUALA
1.Sura gani na aya ya ngapi? Na kupishana usiku na mchana, na riziki anayo iteremsha
Mwenyezi Mungu kutoka mbinguni, na kwayo akaifufua ardhi baada ya kufa kwake,
na mabadiliko ya upepo, ni Ishara kwa watu wenye akili.
2.Sura gani na aya ya ngapi? Walio kufuru na wakazuilia njia ya Mwenyezi Mungu,
Yeye atavipotoa vitendo vyao.
3.Sura gani na aya ya ngapi?Na jueni kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu yuko nanyi.
Lau angeli kut'iini katika mambo mengi, bila ya shaka mngeli taabika. Lakini Mwenyezi
Mungu amekupendezeeni Imani, na akaipamba katika nyoyo zenu, na amekufanyeni
muuchukie ukafiri, na upotovu, na uasi. Hao ndio walio ongoka
4.Sura gani na aya ya ngapi? Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
5.Sura gani na aya ya ngapi? Na bila ya shaka tulimtuma Nuhu na Ibrahim, na
tukaweka katika dhuriya zao Unabii na Kitabu. Basi wapo miongoni mwao walio
ongoka, na wengi katika wao ni wapotovu.
6.Kuna aya ngapi za Sajda katika Quran?
7.Jamaa yupi wa Mtume aliotajwa katika Quran?
8.Sura za Makka ni ngapi?
9.Sura za Madina ni ngapi?
10.Siku ya Qiyama hali ya watu itakuwaje?

Jee Unajua?

1.Katika karne ya 6 ikiwa ni mwaka 700 na Waislamu walikuwa tayari wanazo


hospitali kama zilivyo leo na madaktari na kufanya shughuli zote za kitibabu
: https://www.nlm.nih.gov/exhibition/islamic_medical/islamic_12.html
2.Katika karne ya 7 kulikuwa na madaktari bingwa wa Kiisalamu na
walianzisha fani mbalimbali ikiwa kati ya hao ni Ibn Zuhur, Ibn Sina,
Al-Kindi, Al-Razi, Ibn Haytham : https://en.wikipedia.org/wiki/List_of_
Muslim_doctors
3.Ingawa kwa kuwa ni Muislamu hatajwi lakini ndio muasisi wa kutumia
zana za kupasulia mgonjwa anapoumwa Ab al-Qsim Khalaf ibn al-Abbs
az-Zahrw (9361013), inasemekana kuwa alitengeneza aina zisopungua 200
ya zana za kupasulia wagonjwa : https://en.wikipedia.org/wiki/Al-Zahrawi
4.Alikuwa Bibi wa Kiengereza Mary Wortley Montagu (1689-1762) ndio
aliotoa utaalamu wa Chanjo ya Ndui kutoka kwa magwiji wa Kiislamu huko
Uturuki nakuipeleka Uiengereza, kufanya hayo alikabiliana na upinzani
mkubwa lakini wapinzani wake walikuja kunyanyua mikono baada ya
ukweli kudhihiri : http://www.muslimheritage.com/article/lady-montaguand-introduction-smallpox-inoculation-england
5.Fahamu kuwa huu Ulimwengu wetu unefanyiwa kazi kubwa na wataalamu
wa Kiislamu katika maendeleo ikiwa kina Al-Farabi, Ibn Rushd, AlKhawarizim, pitia mtandao huu uwaone katia ya wengi majina 15 yaliofanya
kazi nzito : http://www.famousscientists.org/famous-muslim-arab-persianscientists-and-their-inventions/
6.Abu Abdallah Mohammad ibn Jabir ibn Sinan al-Raqqi al-Harrani al-Sabi
al-Battani maarufu Al-Battani na Wazungu humwita Albategnius, Albategni
au Albatenius alikuwa mjuzi wa mambo ya nyota na aliweza kutengeneza
darubuni yake ya kuangalia sayari aliishi katika miaka ya 858-929 : http://
www.famousscientists.org/al-battani/
7.Wajue wanataaluma ya Sayansi ambao walikuwa ni sio wenye kujikita
moja kwa moja katika Sayansi (part-timers) kati ya hao ni Eratosthens 276
BC, Nicholas Copernicus 1473-1543, Johannes Kopler 1571-1630http://www.
famousscientists.org/part-time-scientists/

3/30/2016 1:12:26 PM

3
Na Bakari Mwakangwale
SHEIKH mpya wa BAKWATA
Mkoa wa Morogoro
Abdallah Salim Mkangambe
amesema kazi yake ya
kwanza atakayoanza nayo
ni kuhakikisha vijana wa
Kiislamu wanaosoma katika
shule za sekondari mkoani
humo wanapata elimu ya dini.
Hayo ameyasema mwishoni
mwa juma lililopita mjini
Morogoro muda mfupi mara
baada ya kumalizika kwa
uchaguzi Mkuu uliomweka
madarakani kwa kura 34 dhidi
ya kura mbili za mshindani wake
Sheikh Idd Hussein Nyagongo.
Akifafanua zaidi kuhusu azma
yake hiyo, sheikh Mkangambe
alisema hadhani kama kwa
kushirikiana na Waumini wa
dini ya Kiislamu mkoani humo
watashindwa kusambaza vitabu
vya Elimu ya Dini ya Kiislamu
walau 20 kwa kila shule iliyopo
mkoani humo.

Habari

JAMADUL AAKHER 1437, IJUMAA APRILI 1-7, 2016

Bakwata Moro wapata


Sheikh mpya wa mkoa
Nina vipaumbele vyangu
vitatu vya kwanza ambavyo
naamini tukishirikiana na
wenzangu tutaweza kufikia
matarajio ya Waislamu walio
wengi ambayo ni kuona Baraza
haliwi katika sura hii iliyopo,
bali linabadilika, alisema
Mkangambe.
Kuhusu vipaumbele vingine,
sheikh huyo mpya wa Mkoa
alivitaja kuwa ni Uchumi na
Ardhi ambavyo kwa pomoja
amesema ni lazima jamii ya
Waislamu iamke na kuwekeza
katika Ardhi ikiwa itahitaji
kujikwamua Kiuchumi na

AN-NUUR

Kielimu.
Uchumi, Ardhi na Elimu
ni vitu muhimu sana kwetu
Waislamu na hasa katika
ulimwengu huu wa Sayansi na
Teknolojia ambao maendeleo
yoyote yanategemea iwapo una
Elimu, Ardhi ama Uchumi kwa
kiasi gani, aliongeza.
Mbali na hayo Sheikh
Mkangambe ameahidi kutatua
changamoto mbalimbali mkoani
humo ikiwemo hitilafu za
makundi ya kidini na kijamii
ili kurejesha heshima na
ustawi mzuri wa maendeleo ya
Waislamu mkoani Morogoro.

Kwa upande wa wajumbe


wa mkutano huo wa mkoa
wamesema sheikh huyo
pamoja na mambo mengine,
analo jukumu la kuhakikisha
anarejesha mali za Waislamu
ambazo wamedai Baraza
limekuwa likikosa pesa za
kujiendesha ilihali mali zake ziko
mikononi mwa watu binafsi.
Katika uchaguzi huo uliokuwa
umesimamiwa na Naibu
Katibu Mkuu Dini Sheikh
Mohammed Khamisi, Bakwata
Mkoa ilifanikiwa kuwapata
masheikh watano watakaounda
jopo la maulamaa ambalo
kwa mujibu wa katiba yao
ndilo litakalomsaidia sheikh
Mkangambe kufanya maamuzi
mbalimbali yenye maslahi ya
kidini na kijamii mkoani humo.
Wengine ni wajumbe 10
wa Halmashauri Kuu ya
Bakwata mkoa watakaomsaidia
Mwenyekiti mpya wa
Halmashauri hiyo sheikh
Mwisheh Ismail Mwisheh katika
kazi za kila siku za Baraza hilo.

Wakaribishwa kuswali kanisani

KATIKA kuonyesha moyo


wa mapenzi kwa wakimbizi,
mapadiri Massimo Biancalani
na Alessandro Carmignani,
wamewakaribisha Waislamu
kufanya ibada yao ya swala
tano katika kanisa.
Mapadiri hao walikuwa
tayari kuondosha kila kitu
ndani ya kanisa lao ambacho
kingekwaza ibada ya
swala kwa Waislamu, kila
wanapokuja kuswali.
Hata hivyo, Askofu Mkuu
Fausto Tardelli wa Kanisa
la Vicofaro, Pistoia, Toscana
nchini Italia, amepiga ruhusa
hiyo.
Askofu Mkuu huyo, ametoa
kauli kali ya kuwakemea
Mapadri hao wawili akisema
kuwa ukarimu katika
kuwahudumia wakimbizi,
haihusishi kuchanganya
ibada.
Massimo Biancalani na
Alessandro Carmignani
walitangaza wiki iliyopita
kuwaruhusu Waislamu
kuswali ndani ya Kanisa
baada ya Parokia yao
kuwakaribisha wakimbizi 18
Waislamu.
Massimo Biancalani alisema
waliondoa vikalio katika altari
ili kuwasaidia wakimbizi hao
wa Kiislamu kujihisi wapo
nyumbani.
Sioni kuna tatizo gani,
tunaweza kuwatia ugumu

ANNUUR NEW.indd 3

Askofu Mkuu Fausto Tardelli apinga

kufanya ibada zao, Mtu yeyote


akitaka kuja kuswali Kanisani
anakaribishwa na hata kama
wanataka kwenda sehemu
nyingine wanaruhusiwa
kufanya hivyo. Alisema Padri
huyo.
Lakini Askofu Mkuu Fausto
Tardelli, alisema mpango huo
ni hatua ya mbali ambayo
inaweza kuhatarisha na
kuharibu kuwaunganisha
wakimbizi hao katika jamii.
Alisema kuwapa misaada
na kuwakaribisha haina
maana kuwapatia nafasi
Kanisa kufanya ibada zao na
kwamba kuna maeneo bora na
sahihi zaidi yanapatikana.
Pamoja na kupinga Askofu
Mkuu wa Kanisa hilo,
Makuhani wa Kanisa hilo
nao walipinga vikali kauli ya
Askofu na kutaka wakimbizi
hao waendelee kufanya ibada
zao kanisani hapo na kutaka
Parokia nyingine ziige mfano
wao.
Ukimbizi ni dharura,
kutetea uhai lakini je, Uislamu
unasemaje juu ya kuswali
ndani ya Kanisa?
Italia ni katika moja ya nchi
za Ulaya zenye idadi ndogo
sana ya Waislamu. Kwa
mujibu wa makisio ya mwaka
2011, idadi ya Waislamu
katika nchi hiyo ni kiasi cha

asilimia 2 tu.
Hata hivyo, Msikiti mkuu
wa nchi hiyo, maarufu, The
Mosque of Rome (Kitaliano:

Moschea di Roma), ulio


Parioli, ndio msikiti
mkubwa kuliko misikiti
yote, katika Ulaya na nje ya
nchi za Kiislamu, Urusi na
India.
Msikiti huo una ukubwa
wa mita za eneo 30,000
(30,000 m2) ukiweza
kuchukua watu 12,000 kwa
wakati mmoja.
Walioshiriki uanzilishi
na ufadhili wa ujenzi wa

msikiti huo ni aliyekuwa


mwanasa Sultan wa
Afghanistan Prince
Muhammad Hasan na
mkewe Princess Razia,
huku kiasi kikubwa cha
fedha za ujenzi kikitolewa
na Mfalme Faisal wa Saudi
Arabia.
Mafundi walioandaa
michoro ya msikiti
walikuwa Paolo Portoghesi,
Vittorio Gigliotti na Sami
Mousawi.
Aliyekuwa Rais wa Italia
Sandro Pertini, alishiriki
kuweka jiwe la msingi
mwaka 1985 pamoja na
kuufungua rasmi msikiti
huo tarehe 21 Juni, 1995.

BAADHI ya Masheikh watoa mada wakiwa katika Semina ya walimu


wa Madrasa iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Chuo cha
Markaz Chang`ombe, jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

3/30/2016 1:12:28 PM

Tahariri/Makala

AN-NUUR

S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786


Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM.
www.annuurpapers.co.tz
E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk
Ofisi zetu zipo: Manzese Tip Top
Usangi House, barabara ya Morogoro, D'Salaam

Maalim Bassaleh awe kigezo

Waislamu, Wakristo wamkosa Idrisa


Mimbar zitumike vyema kutoa ujumbe

MAALIM Ali Bassaleh, ni


mfano mzuri wa kiongozi
wa Kiislamu, ambaye
anatumia vyemba mimbar
katika siku za Ijumaa
kufikisha ujumbe mahsusi
kwa Waislamu kulingana
na wakati na matukio.
Toka zama, alikuwa
na kawaida ya kuandaa
mada ya hutba ya Ijumaa
mapema kabla ya siku ya
swala. Akipenda kufuatilia
taarifa za vyombo vya
habari vya ndani na nje
ya nchi, akipenda kusoma
magazeti mbalimbali ili
kupata na kujua matukio
mbalimbali yanayokuwa
yanajiri katika jamii. Zaidi

akipenda kusoma vitabu


mbalimbali.
Wakati huo akiwa
Masjid Idrisa, alikuwa
akiandaa hutba yake
kwa kuzingatia matukio
yaliyojiri nchini kwa
kunasibisha na nafasi
ya Waislamu, iwe ni
kwa kuzingatia maslahi
au madhara au kutoa
tahadhari, kuonya,
kukemea au kuchukua
hatua.
Baada ya kuandaa
hutba yake kulingana
na matukio, pamoja
na kwamba ataitoa
kwa waumini kupitia
kipaza sauti cha Msikiti
(Masjid Idrisa, Kariakoo),
Maalim Bassaleh alikuwa
amezoea kuichapa
hutba yake na nakala
zake kusambazwa kwa
Waislamu.
Jambo hilo liliwasaidia
waumini kuweka
kumbukumbu na kupata
rejea ya somo la hutba
lililotolewa kila walipohitaji
kufanya hivyo. Mwenendo
wake huo wa kupenda
kutoa waadhi au hutba kwa
uhakika na kwa kunukuu
machapisho na vitabu
mbalimbali, watu wa Dar
es Salaam wakampachika
jina la utani, Mzee wa
kunukuu.
Kwa kifupi tunaweza
kusema kuwa, Maalim
Bassaleh alikuwa anajua
kujiandaa na kuiandaa
hutba yenyewe. Hata
anaposimama mimbarini,
Msikiti ulikuwa ukijaa
hadi nje kiasi kwamba,
hata wasiokuwa Waislamu

ANNUUR NEW.indd 4

siku za Ijumaa walikuwa


wakipenda kusikiliza
hutba zake nje ya Msikiti,
wakitaka kujua Maalim
anakuja na somo gani
Ijumaa hiyo.
Tuchukue fursa hii
kuwakumbusha Maimam,
Masheikh na Makhatibu
wetu kwamba, hutba ya
Ijumaa, hutba za sikukuu za
Eid ni somo zito linalohitaji
maandalizi makubwa
kabla ya kuwasilisha kwa
waumini.
Hutba inahitaji iandaliwe
kiasi cha kuwafanya
watu wahamasike na
kushawishika kujifunza
kwayo. Somo la hutba
linahitaji utaalam
wa muwasilishaji na
uwasilishwaji, somo la
hutba liendane na maisha
ya Waislamu kwa wakati
husika.
Tuweke tu wazi kwamba
katika misikiti mingi,
hutba za Ijumaa zimekuwa
zinafanywa mithili ya zima
moto. Yaani zinatolewa
kwa ajili ya kutimiza tu
wajibu Swala ya Ijumaa
ipite. Hakuna maandalizi
ya kutosha, somo linakinahi
mapema, haliwavutii
wasikilizaji, wala halitoi
ujumbe wa wiki kwa
waumini.
Tufahamu kwamba swala
ya Ijumaa ndio mkutano
wa ibada unawakusanya
Waislamu wengi zaidi kwa
pamoja kila wiki kuliko
swala nyingine.
Swala ya Ijumaa ni nafasi
muhimu ya kuwafikishia
Waislamu ujumbe mahsusi
kutokana na wingi wao
katika swala. Hutba nzuri
ni kichocheo cha kuwafanya
Waislamu kufurika zaidi
Misikitini, wakiwa na
hakika ya kupata elimu
na ufahamu wa dini yao,
maisha yao, maadili yao
kupitia hutba.
Hutba ni darasa kwa
wasiojua, ni ukumbusho
kwa walio sahau, hutba
huweza kuongoa watu
na kuhamasika kufanya
ibada na kumkurubia zaidi
Mwenyezi Mungu.
Kulipua kuhutubu,
kunapunguza ushawishi wa
kujifunza waumini. Lakini
pia tunaidhalilisha dini
yetu na hata Masheikh na
Maimam wetu kiufahamu.

AN-NUUR

JAMADUL AAKHER 1437, IJUMAA APRILI 1-7, 2016

Kwa pamoja tukatae


Tukumbuke, wema hushinda uovu
Mwishowe, batili ni yenye kuondoka

WAZANZIBARI
tulichagua maridhiano
na kukataa mfarakano.
Tulichagua umoja na
kukataa mgawanyiko.
Tulichagua upendo
na kukataa chuki.
Tulichagua matumaini
na kukataa khofu.
Tulichagua amani na
kukataa fujo.
Tarehe 5 Novemba
2009 daima itakumbukwa
kuwa ni siku ambayo
nchi yetu iliandika
historia mpya pale
viongozi wawili
wazalendo na mashujaa,
Dk. Amani Abeid
Karume na Maalim
Seif Sharif Hamad,
walipowaongoza
Wazanzibari kufikia
MARIDHIANO.
Haikuwa kazi rahisi
lakini kwa kuongozwa
na hisia za uzalendo na
mapenzi kwa nchi yao
na wananchi wenzao,
Dk. Karume na Maalim
Seif waliamua kujitolea
kuongoza enzi mpya za
siasa. Walijua kwamba
katika vyama vyao viwili,
CUF na CCM, wapo watu
ambao wasingewaunga
mkono na pengine
wangeyatumia
MARIDHIANO yale
kutaka kuwahujumu
kisiasa. Na kweli,
walikuwapo watu wa
aina hiyo na wapo hadi
leo.
Kwa kutambua
kuwa watu waovu
wasiopendelea umoja na
masikilizano miongoni
mwa Wazanzibari
watakuja kusema kuwa
MARIDHIANO hayo
yalikuwa ni maamuzi
ya watu wawili tu, na
hayawakilishi matakwa
ya watu, Dk. Karume
alipendekeza kwa
Maalim Seif kukubali rai
ya kufanya kura ya maoni
ili kupata ridhaa ya
Wazanzibari kuhusiana
na mwelekeo huo mpya
wa siasa na hasa kuhusu
haja ya kuanzisha
muundo wa Serikali ya
Umoja wa Kitaifa.
Tarehe 31 Julai 2010
ikafanyika kura ya maoni
ya kwanza katika historia
ya Zanzibar. Asilimia
66.4 ya Wazanzibari
wakapiga kura ya
NDIYO kuchagua
MARIDHIANO na
muundo wa Serikali
ya Umoja wa Kitaifa.
Baada ya maamuzi hayo
ya Wazanzibari, ndipo
Baraza la Wawakilishi

RAIS Mstaafu wa Zanzibar, Dkt. Aman Abeid Karume


(kushoto) akisalimiana na Maalim Seif. Kulia ni
Ismail Jussa (kulia).
likafanya Marekebisho ya
10 ya Katiba ya Zanzibar
na kuingiza muundo huo
ndani ya Katiba.
Maamuzi hayo ya
Wazanzibari yalikuwa
na maana kubwa sana
kwa nchi yetu na watu
wake. Kwa kupiga kura
ya NDIYO, Wazanzibari
tulichagua maridhiano
na kukataa mfarakano,
tulichagua umoja na
kukataa mgawanyiko,
tulichagua upendo na
kukataa chuki, tulichagua
matumaini na kukataa
khofu, tulichagua amani
na kukataa fujo.
Inasikitisha kwamba
miaka sita baadaye wale
waovu miongoni mwetu
ambao hawakutaka
MARIDHIANO
(wakiwemo wale
ambao kwa dhahiri
walijionesha kuyaunga
mkono kwa sababu tu
walitaka kulinda ulwa
wao kwa kumridhisha
Rais aliyekuwa
madarakani lakini
kwa siri wakiyapinga),
wameturudisha kule
kule kwenye mfarakano,
mgawanyiko, chuki,
khofu na fujo.
Lakini pamoja na
juhudi hizo ovu za
kuturudisha tulikotoka,
ukweli mmoja unabaki
kwamba Wazanzibari
wengi hawako tayari
kurudishwa huko.
Wazanzibari wameona
faida ya siasa za
MARIDHIANO, UMOJA,
UPENDO, MATUMAINI
NA AMANI.
Binafsi, bado naamini
kwamba MARIDHIANO,
UMOJA, UPENDO,
MATUMAINI NA
AMANI vitashinda.
Wazanzibari ni watu
wema. Kutokana na

wema wao, watachagua


WEMA dhidi ya UOVU.
Kwa sababu
hizo basi, NATOA
NASAHA ZANGU
KWA WAZANZIBARI
WENZANGU kwamba
tukatae njama zote za
kuturudisha tulikotoka.
Katika siku za hivi
karibuni kumekuwa na

watu WAOVU ambao


wamekuwa wakiandika
maneno ya ovyo na matusi
katika mitandao ya kijamii.
Wengine ni watu wazima
ambao ungetegemea kwa
umri wao wangeonesha
mfano mwema kwa kizazi
cha leo. Bahati mbaya,
baadhi ya vijana wameingia
kwenye mtego wa WAOVU
hao na kujibizana nao
kwa matusi na lugha
zinazoturudisha kwenye
mfarakano, mgawanyiko,
chuki na ubaguzi, mambo

ambayo tukiyakataa
kupitia kura ya maoni ya
tarehe 31 Julai, 2010.
Nawapa NASAHA
ndugu zangu tukatae
kuingia katika mtego
huo. Tuoneshe kama SISI
NI TOFAUTI NA WAO.
Tusijibu lugha zao za
matusi, chuki na ubaguzi
na sisi tukaandika lugha
za matusi, chuki na
ubaguzi. Haitoonekana
tofauti kati yetu.
Tuithamini na kuilinda
kazi kubwa iliyofanywa
na Dk. Amani Karume
na Maalim Seif Sharif
Hamad.
TUNAYOPITIA
SASA NI MAJARIBU
TU. TUSIKUBALI
KUSHINDWA
TUKARUDISHWA
TULIKOTOKA.
TUWAONESHE
WAOVU KWAMBA
SISI NI WEMA. NA
WEMA SIKU ZOTE
HUUSHINDA UOVU.

3/30/2016 1:12:29 PM

HABARI ZA KIMATAIFA

AN-NUUR

JAMADUL AAKHER 1437, IJUMAA APRILI 1-7, 2016

Matamshi ya Trump kuhusu Waislamu yanakera


MGOMBEA uteuzi kwa tiketi
ya chama cha Democratic
kwa ajili ya kinyang'anyiro
cha uchaguzi wa rais nchini
Marekani, Bernie Sanders,
amekosoa vikali matamshi
yanayotolewa na mgombea
chama cha Republican, Donald
Trump dhidi ya Waislamu,
akisema mashambulizi dhidi
ya Waislamu kwa kutumia
kisingizio cha matukio kama
yale ya hivi majuzi yaliyotokea
mjini Brussels yanakasirisha
na yanapingana na katiba ya
Marekani.
Bernie Sanders amesema
Donald Trump anayemiliki
vilabu vya kamari na bilionea
anayezusha mjadala mkubwa,
anafanya mchezo wa kuigiza
wa televisheni na kwamba,
anatumia matukio ya Brussels
kama kisingizio cha kuchochea
chuki dhidi ya Waislamu.
Sanders amesisitiza kuwa,
matamshi na mwenendo huo
unaeneza hofu na woga katika
jamii ya Marekani.

Mashindano
kuhifadhi Quran
kufanyika
Singapore
MASHINDANO ya kitaifa
ya kuhifadhi Quran nchini
Singapore yanatarajiwa
kufanyika wiki ijayo siku ya
Jumamosi na Jumapili Aprili
2-3.
Makundi matatu yanatarajiwa
kushiriki ambayo ni ni ya umri
wa miaka 7 mpaka 12, miaka 13
mpaka 18 na miaka 19 mpaka 25.
Washiriki hao
watashindanishwa
kwa kuzingatia namna
walivyohifadhi (hifz).
Matamshi,(Tajweed) na ufasaha
(fasahah).
Imeelezwa kuwa lengo la
mashindano hayo ni kuibua
vipaji vipya katika uwanja
wa usomaji wa Quran na
kuhamasisha kuhifadhi Quran.
Lengo jingine ni kuifanya
jamii kuwa na utamaduni wa
kuhifadhi Quran na pia kupata
vijana watakaoiwakilisha
Singapore katika mashindano ya
Kimataifa.
Mashindano hayo yatafanyika
katika Msikiti wa Darul Aman
na washindi watapata vyeti na
pesa taslim. Ahbaabur.blogspot.

ANNUUR NEW.indd 5

Kampeni za urais zadaiwa zinaiaibisha Marekani

BERNIE Sanders, Mgombea uteuzi kwa tiketi ya chama cha Democratic


kwa ajili ya kinyang'anyiro cha uchaguzi wa rais nchini Marekani.
Mgombea huyo wa tiketi ya
chama cha Domocratic alisema
kuwa, kundi la kigaidi la Daesh
ni genge ovu lililofanya uhalifu
na jinai dhidi ya binadamu huko
Ufaransa, Marekani na Ubelgiji
lakini mapambano dhidi ya
kundi hilo hayapasi kukiuka
katiba ya Marekani.
Bw. Sanders alisema haipasi
kuwapa watu kama Trump fusra
ya kutumia matukio kama ya
Ubelgiji kwa ajili ya kutumia
vibaya matukio ya kusikitisha
kama yale ya Brussels kuhujumu
Waislamu wote duniani.
Wakati Bw. Sanders
akimlaumu Trump kwa kauli
zake za chuki na ubaguzi dhidi
ya Waislamu, hivi karibuni
mgombea wa kiti cha rais
kupitia chama cha Republican,
Ted Cruz, amefuata nyayo za
Trump baada ya kupendekeza
kufanyika msako mkali dhidi
ya wafuasi wa dini ya Kiislamu,
kwa kile alichokiita kuwa msako
huo una lengo la kuwazuia

wasiingie kwenye kundi la


wenye misimamo iliyofurutu
ada.
Cruz aliyasema hayo saa
chache baada ya kutokea
mashambulizi ya kigaidi katika
jiji la Brussels Ubelgiji, matamshi
ambayo yamewaghadhabisha
viongozi wa kidini na watetezi
wa haki za binadamu nchini
Marekani.
Kadhalika mwanasiasa huyo
ambaye anaonekana kufuata
nyayo za mgombea mwenzake
wa chama cha Republican,
Donald Trump, alisema kuna
haja ya kuimarisha usalama
katika mipaka ya nchi hiyo ili
kuzia wale aliyowataja kuwa
watu wenye misimamo mikali.
Baraza la Mahusiano
ya Kiislamu la Marekani
limeelezea kusikitishwa kwake
na matamshi ya chuki ya
mwanasiasa huyo wa chama
Republican na kusema kuwa,
kauli za aina hiyo hazitakuwa
na matokeo mengine zaidi ya

Ombi kutaka Uislamu usiwe


dini ya taifa Bangladesh lafutwa
MAHAKAMA Kuu nchini
Bangladesh imelikataa
na kulifutilia mbali
ombi lililowasilishwa na
wanaharakati wasio egemea
dini la kutaka Uislamu isiwe
dini ya kitaifa
Jopo maalum la Majaji watatu
wa Mahakama hiyo limetupilia
mbali ombi hilo muda mfupi
baada ya kesi hiyo kufunguliwa
na bila ya kuruhusu kutolewa
ushahidi wowote.
Ombi hilo ambalo kwa

mara ya kwanza liliwasilishwa


miaka 28 iliyopita, limezusha
maandamano nchi nzima ya
makundi ya Kiislamu katika nchi
hiyo masikini.
Bangladesh ilitangazwa rasmi
kuwa nchi isiyoendeshwa kidini
baada ya vita vya kudai uhuru
kutoka Pakistan mwaka 1971.
Wasioegemea dini wamekuwa
wakidai kwamba kutumika kwa
Uislamu kama dini ya kitaifa
kunakwenda kinyume na sheria
ya nchi isiyotambua dini.ABNA

kuzidisha ubaguzi wa kidini


na chuki dhidi ya Waislamu na
Uislamu duniani.
Nihad Awad, Mkurugenzi
Mkuu wa Baraza hilo alisema
matamshi ya Cruz ni sawa na
yale yanayotolewa na Trump na
kwamba, yanakanyaga uhuru
wa kuabudu na kuhatarisha
maisha ya jamii ya Waislamu
nchini Marekani.
Viongozi wa Kiislamu
nchini Marekani wamesema
kuwa maneno ya chuki dhidi
ya Uislamu yanayotolewa
na wanasiasa wa chama cha
Republican, ndiyo sababu
ya kuongezeka hujuma
na mashambulizi dhidi ya
Waislamu nchini humo.
Taarifa iliyotolewa hivi
karibuni na viongozi wa
jumuiya za Waislamu nchini
Marekani mjini Washington
ilimtaka Trump, kuwaomba
radhi Waislamu kutokana na
matamshi yake ya hivi karibuni
yaliyojaa chuki dhidi yao.
Hivi karibuni Waziri wa
Mambo ya Nje wa Marekani
John Kerry amekiri kuwepo
utovu wa nidhamu katika
kampeni za uchaguzi wa rais
nchini humo na kusema jambo
hilo linasababisha Marekani
kuaibika kimataifa.
Katika mahojiano na
televisheni ya CBS, Kerry
alinukuliwa akisema, "Kila
mahala ninapoenda, kila
kiongozi ninayekutana
naye, wananiuliza ni nini
kinachoanedelea Marekani.
Hawawezi kuamini
yanayojiri na naweza kusema
wameshangazwa."
irib.

Benki ya kwanza ya Kiislamu


kufunguliwa Urusi
TAASISI ya kwanza ya kibenki
inayofuata kanuni za Kiislamu
inatarajiwa kuanza kufanya kazi
mwishoni mwa mwezi huu katika
mji wa Kazan nchini Urusi.
Mmoja wa waanzilishi wa taasisi
hiyo alisema kuwa taasisi hiyo
inayoitwa The partinership Banking
Centre, itafanya kazi kama kampuni
tanzu ya Tatagroprombank.
Taasisi hiyo inayofanya kazi
na watu binafsi na makampuni
mbalimbali, itakuwa na lengo la
kupitishia uwekezaji wa Kiislamu
katika nchi ya Urusi na pia kusaini
makubaliano ya kikazi na Benki ya
Maendeleo ya Kiislamu ya Islamic
Development Bank.
Fursa hii imeingia nchini Urusi
baada ya kupitishwa sheria mpya
katika Bunge la Duma Januari
mwaka huu, inayoruhusu mfumo
wa kibenki unaoweza kuzingatia
taratibu za kidini.ABNA.

3/30/2016 1:12:30 PM

Hoja ya Juma Kilaghai

AN-NUUR

JAMADUL AAKHER 1437, IJUMAA APRILI 1-7, 2016

Inawezekana lishe yako ndiyo inayokuua!

UNA namna nyingi


sana chakula
unachokula kinaweza
kukugeuka na
kuwa ndiye adui yako
anayekumaliza. Kwa mfano,
vyakula vilivyochakatwa,
na hasa nafaka ikiwa ni
pamoja na sukari, huchochea
mfuro, au inflammation kwa
Kiingereza, ndani ya mwili.
Tafiti zinaonyesha kuwa
magonjwa mengi sana ya
kimfumo chimbuko lake ni
mfuro. Mfano wa mfuro ni
ule uvimbe unaoupata pale
unapojigonga kwenye paji la
uso au unapojikwaa kwenye
dole gumba la mguu huku
ukiwa hujavaa viatu. Aina hii ya
uvimbe unajitokeza hata katika
seli ndani ya mwili. Aghalabu
hali hii hutokea pale kinga za
mwili zinapoamka kupambana
kwa kuhisi kuwa kuna kitisho
kimeingia ndani ya mwili.
Mfuro unaotokea pale kinga
za mwili zinapopambana
na vimelea mbali mbali vya
maradhi siyo tatizo sana kwa
sababu unakuwa ni wa muda.
Tatizo ni pale mfuro unapokuwa
endelevu. Kwa bahati mbaya hali
ya mfuro endelevu inatukabili
karibu watu wote kutokana na
ulaji wetu. Sehemu kubwa ya
lishe yetu inatokana na vyakula
vilivyochakatwa, na sehemu
kubwa ya hivyo vyakula ni vile
vya nafaka na mafuta ya mbegu.
Vyakula hivi vinapoingia
mwilini mfumo wa kinga za
mwili hudhani kwamba kuna
adui kaingia na unajikusanya
kufanya mashambulizi.
Kwa sababu wanga
uliochakatwa na mafuta ya
kupikia ya mbegu vimekuwa
ndiyo vyakula vyetu vikuu,
tofauti ikiwa ni mapishi tu, ina
maana kuwa asubuhi, mchana
na usiku, mifumo ya kinga
zetu za mwili iko katika hali ya
vita; na muda wote huo mwili
unakabiliwa na mfuro.
Mfuro endelevu
unasababishaje maradhi? Ili uwe
na siha njema, vitu mbalimbali
vilivyomo ndani ya seli za mwili
wako na vile vilivyoko nje ya seli
hizo vinatakiwa viwe katika hali
ya uwiano fulani muda wote.
Kitaalamu uwiano huu huitwa
homeostatis. Mambo yanaanza
kuharibika pale uwiano huu
unapoanza kuvurugika.
Seli zako za mwili ni kama
visiwa vinavyoelea baharini.
Kila seli kwa nje imezungukwa
na majimaji ambayo ndani
yake kuna vitu vingi muhimu
kwa utendaji kazi muruwa
wa mwili, ikiwa ni pamoja na
viini-lishe vingi vinavyosubiri
kuingia ndani ya seli kwa ajili
ya kuwezesha shughuli za

ANNUUR NEW.indd 6

Mafuta ya mbegu
seli kwenda inavyotakiwa.
Aidha kila seli ndani ni kama
bahari yenye visiwa vingi. Vitu
vinavyoitwa organele, ambavyo
ni maumbile kadhaa wa kadhaa
yenye majukumu tofauti
huelea kama visiwa kwenye
majimaji yaliyomo ndani ya
seli. Majimaji yaliyomo ndani
ya seli yana vitu vingi ndani
yake, ikiwa ni pamoja na viini
lishe vilivyoingizwa humo
kwa minajili ya kuchakatwa
ili kuzalisha nishati, kufanya
ukarabati, kuzimua mazao hatari
ya pembeni ya mchakato wa
kuzalisha nishati; na kuunda
maumbo mengine ambayo ni
muhimu kwa utendaji sawa
wa mwili. Majimaji haya pia
hupokea kwa ajili ya kutoa nje
ya seli, na hatimaye nje ya mwili,
uchafu au taka zinazozalishwa
na organele katika michakato
mbalimbali.
Katika ngozi ya kila seli
(cell membrane) kuna vipokezi
(receptors) ambavyo hufanya
kazi ya kuingiza ndani ya seli
vile vilivyomo kwenye majimaji
ya nje ya seli vinavyotakiwa
kungia ndani, na kutoa nje ya
seli vile vilivyomo kwenye
majimaji ya ndani ya seli
vinavyotakiwa kutolewa nje.
Mwili unapokumbwa na mfuro
utendaji kazi wa hivi vipokezi
kwenye ngozi ya seli huathirika.
Hii ina maana kuwa kazi ya
kuingiza na kutoa nje ya seli
vitu mbalimbali haifanyiki kwa
wepesi na ufanisi unaotakiwa,
jambo ambalo huvuruga uwiano
wa vitu hivyo.
Hali ikiwa hivyo ni rahisi

sana kupata magonjwa ya


kimfumo ikiwa ni pamoja na
kisukari, shinikizo la damu na
magonjwa yanayotokana na
mlundikano wa uchafu ndani
ya seli. Ni rahisi kupata kisukari
kwa sababu glukosi ambayo
inatakiwa itoke kwenye majimaji
yaliyoko nje ya seli na kuingia
ndani ya seli ili ichakatwe
kuzalisha nishati haitaingia
kwa kasi na ufanisi unaotakiwa.
Kwa sababu hii sukari
italundikana kwenye damu na
kukusababishia mkusanyiko wa
dalili zote ambazo kwa pamoja
ni kielelezo cha ugonjwa wa
kisukari. Aidha ni rahisi kupata
shinikizo la damu la juu la
damu kwa sababu kunapokuwa
na mlundikano wa vitu
vinavyotakiwa viingie ndani ya
seli lakini vimeshindwa, mwili
huongeza shinikizo la damu
kama njia ya kulazimisha vitu
husika vipenye katika ngozi ya
seli.
Baadhi ya magonjwa ya
moyo, magonjwa yanayoathiri
seli zilizoko nyuma ya jicho,
magonjwa ya mishipa ya fahamu
katika maeneo mbalimbali
ya mwili, na magonjwa ya
viungo mbalimbali vya mwili
yanaweza pia kusababishwa na
mlundikano wa uchafu ndani ya
seli.
Ukiondoa kusababisha
mfuro, vyakula vya wanga
uliochakatwa pia husababisha
magonjwa kwa njia nyingine.
Kwa mujibu wa tafiti,
uchakataji wa glucose (sukari

kuu inayopatikana baada ya


kuchakata wanga) huzalisha
kemikali inayoitwa malonylcoA. Malonyl-coA hupunguza
kwa kiasi kikubwa uwezo wa
mitochondria (viwanda vya
kuzalisha nishati vilivyomo
ndani ya seli) kudhibiti chembe
chembe zilizobeba umeme
hasi (high energy electrons)
zinazotumika wakati wa
uzalishaji wa nishati inayotwa
Adenosine Tri-phosphate (ATP),
ambayo ni kwa ajili ya matumizi
ya baadaye mwilini. Hizi high
energy electrons husababisha
kuzaliwa kwa kiwango kikubwa
cha chembe zilizobeba umeme
chanya zinazoitwa free radicals.
Chembe hizi zina uwezo wa
kubadilisha umbo na utendaji
kazi wa vinasaba kwenye seli
(DNA mutations) na kuharibu
vimengenya mbalimbali ndani
ya mwili!
Aidha glucose inaweza kuleta
shida kwenye ini (husababisha
ugonjwa wa ini bonge, yaani
fatty liver disease), inaweza
ikasababisha unene uliopea,
inaweza kuchochea kisukari cha
ukubwani, na pia ni chakula
kikuu cha seli za saratani.
Tafiti zimebaini kuwa baadhi
yetu miili yetu huchakata wanga
bila madhara ukilinganisha
na wengine. Watu wa aina hii
husemekana wana mifumo
ya ujenzi na uvunjifu wa
kemikali ambayo inaendana na
vyakula vya wanga/nafaka au
CARBOHYDRATE TYPE kwa
kitaalamu. Njia pekee ya kujua
kama wewe ni miongoni mwa
waliomo katika kundi hili au
siyo ni kwa njia ya kipimo cha
kutambua mfumo wako wa
ujenzi na uvunjifu wa kemikali
mwilini (metabolic typing test).
Hata hivyo kabla hujabaini
aina ya mfumo ulio nao, njia
bora kabisa ya kujilinda ni
kuchukua hatua za kupunguza
ulaji wa wanga, hasa
uliochakatwa, na matumizi ya
mafuta ya mbegu kwa ajili ya
kupikia.
(Juma Killaghai ni mtaalam
wa lishe, ni mtaalam wa stadi
za tiba na ni Mkemia Mtafiti
wa bidhaa zinazotokana na
viumbe hai (Organic Natural
Products Research Chemist).
Kwa mawasiliano piga:
0754281131/0655281131
Juma Killaghai ana kibali cha
Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii kwa ajili ya kutoa elimu
inayohusu masuala ya siha; na
pia ana leseni ya Baraza la Tiba
Mbadala na Tiba Asilia kwa
ajili ya kutoa tiba asilia.)

3/30/2016 1:12:30 PM

Makala

AN-NUUR

JAMADUL AAKHER 1437, IJUMAA APRILI 1-7, 2016

Dkt. Shein na safari ya miaka mitano


Na Mwandishi Maalum

WIKI iliyomalizia 20
Machi 2016 Ulimwengu
umeshuhudia chaguzi siku
hiyo katika bara la Afrika.
Macho na masikio ya
ulimwengu yaliangaza zaidi
Zanzibar si kwa uangalizi
bali kuhabarisha kile
kitakacho tokea.
Kwa nini Zanzibar?
Uchaguzi wa marejeo
umevuta hisia na mvuto wa
waandishi na wachambuzi
mbalimbali kwa vile
kususiwa na waangalizi wote
wa ndani na nje, uliosusiwa
na vyama takriban 10 kati ya
14,umegubikwa na mzozo
wa kisheria juu ya ufutwaji
na ufanyikaji wa Uchaguzi
mpya ni miongoni mwa
maswali mengi na ambayo
huwa kama kitendawili
kisicho na mteguzi.
Mazingira na mtiririko wa
matukio tokea Oktoba 28
ulipofutwa uchaguzi wa
Oktoba 25 uliupa uchaguzi
wa Machi 20 picha ya aina
yake kutizamwa kiuandishi
(Reporter) zaidi kuliko
kiuangalizi (Observer).
Kuelekea siku ya Uchaguzi
Wiki moja kuelekea Machi
20 tulishuhudia matukio
kadhaa ya Miripuko katika
maskani ya CCM Kisonge
na nyumba ya Kamishna
wa Polisi, Uchomwaji moto
wa Nyumba za wananchi,
Uchomwaji moto wa Maskani
za CUF, pia tumeshuhudia
ukamatwaji wa wafuasi
na viongozi wa CUF
kuhusishwa kwao na matukio
kadhaa yaliyotokea. Kubwa
zaidi lililoibua mjadala
mkubwa ni kutekwa kwa
Mwandishi mahiri wa Radio
DW na Mwananchi Bi. Salma
Said. Mtiririko wa hayo yote
pamoja na Uimarishwaji
mkubwa wa Ulinzi kwenye
viunga vya Zanzibar kulizidi
kuleta taswira ya kipekee
kwa Uchaguzi wa Machi 20.
Siku ya Uchaguzi
Machi 20 iliwadia
siku ya upigaji kura kwa
Uchaguzi ambao uliokuwa
hauna Kampeni na ambao
ulifuatiwa na mtiririko
kadhaa wa kadhaa. Vyombo
takriban vingi vilijikita
kuhabarisha hasa upande
wa Pemba kutokana na
kuwa na wafuasi wengi wa
CUF. Taarifa za awali kabisa
zilianza kutoka kujulisha

ANNUUR NEW.indd 7

DKT. Ali Mohamed Shein (kushoto) akimbatiana na Maalim


Seif Sharif Hamad. (Picha kutoka Maktaba yetu).
mahudhurio na muitikio
wa wananchi katika vituo
kadhaa vya wapiga na
kuonesha muitikio mdogo
wa wapiga kura kiasi ya
wapiga kura chini ya 10 kwa
saa 1 kwa upande wa Unguja
na wapiga kura 6 kwa saa
moja kwa upande wa Pemba.
Hii ilikuwa inajidhihirisha
wazi katika maeneo mengi
kote Unguja na Pemba
kwa waandishi mbalimbali
waliokuwa wanataarifu
Uchaguzi huo. Hali ya
Utulivu na na woga ilitawala
sana siku ya Uchaguzi na
baadhi ya maeneo ya vituo
vya kura askari walizidi idadi
ya wapiga kura. Muitikio
mdogo wa wapiga kura na
hali ya utulivu na ukimya
ilizidi kutanda viunga vingi
vya mitaa yote ya Zanzibar.
Utoaji wa Matokeo
Matokeo yalianza kutoka na
mara hii tulishuhudia wepesi
na uharaka wa kuhesabu
kura kuliko chaguzi zote
Zanzibar. Kura Laki tano kwa
chaguzi zote zilopita Zanzibar
huwa ni kama kaa la moto
na huchukua zaidi ya masaa
48 kuweza kuhisabiwa na

kuhitimishwa kutangazwa.
Mara hii iliichukua Tume
masaa 16 tu kuja na matokeo
ya mwisho na kumtangaza
Dkt Ali Mohammed Shein
ndie mshindi wa kiti cha
Rais wa Zanzibar kwa miaka
mitano mpaka Machi 2021.
Hapana shaka palitarajiwa
nderemo na vifiji kuanzia
Bwawani na kwenye
viunga vyake tokea hapo
alipotangazwa majira ya saa
4 asubuhi kuwa mshindi.
Ila hali ilikuwa tofauti mji
uliendelea kuwa kimya
kizito na kuanzia jioni jioni
ndipo palipoanza kuonekana
makundi machache ya
wafuasi wa CCM wakielekea
Kachorora na Kisonge na
ambao wengi wao ni vijana
na kutumbuizwa na muziki
uliokuwepo hapo. Hali katika
mitaa mingi ilibaki kimya na
yenye simanzi kubwa. Hii
ilizidi kuleta taswira ya safari
refu sana ya miaka mitano
ya Dkt Shein kuongoza
Zanzibar. Naam wingu la
kwanza zito limetanduka
lakini, Je safari ya miaka
mitano na muonekano wa
wananchi wengi kutokupiga

kura kunampa Dkt Shien


utashi wa kisiasa kuongoza
jamii inayoonekana imempiga
pande?.
Safari ya Kiza Kuelekea 2021
Baadhi ya wachambuzi na
waandishi wengi wanaitizama
Zanzibar na Tanzania kwa
ujumla baada ya Machi 20.
Hili halihitaji uwe mkwasi
sana kujua mazingira ya
Uendeshaji wa Serikali zetu
zenye Bajeti tegemezi kwa
zaidi ya 50%. Hii haihitaji
uweledi kujua ni kiasi gani
Dkt Shein ataongoza jamii
iliyogawanyika kwa miaka
mitano na kuweza kuleta
maendeleo na kuifanya
Zanzibar kuwa Dubai
ya Afrika. Hii haihitaji
Uchambuzi mpana sana kwa
jamii iliyotengwa na Jumuiya
za Kimataifa na Ulimwengu
inawezaje kufikia malengo
yake na hapa ikumbukwe
kuwa Zanzibar asilimia
kubwa ya mahitaji yake
yanatoka nje. Hii haihitaji
uchambuzi mkubwa kwa nchi
inayotegemea zao moja ghafi
tu na isiyo na viwanda vya
uzalishaji inaweza kuwa na
hali gani baada ya miaka 5.
HITIMISHO
Kwa maono ya suala
la Zanzibar kila upande
unaohusika uweze kuchukua
majukumu yake na kuchukua
dhamana ya uongozi. Maslahi
mapana ya Zanzibar na
ustawi wake yazingatiwe na
tuache kuweka maslahi ya
vyama vyetu mbele. Tujadili
kwa hoja na kuzingatia kuwa
huwezi kuuwa au kutesa
fikra. Kiwiliwili ndicho
kinachokufa lakini fikra na
mitazamo itaendelea kuwepo.
Na pia tusibadili ukweli kuwa
Uadui maana Mungu aliumba
ukweli na uongo daima
haikai juu ya ukweli ni sawa
vyenye mikangamo tofauti.
Ukweli mkangamo wake ni
mzito daima utakaa juu na
kudhihirika. Jamii zinahitaji
maendeleo kuliko siasa.
Ukishinda uchaguzi kwa hali
ya Majeshi kuwa katika hali
ya dharura (Standby) huwezi
kukaa na kuongoza kwa
dharura na majeshi yakakaa
kwa dahrura kwa muda wote
wa miaka mitano. Utakuwa
umetawala viwiliwili na sio
nyoyo za wananchi wako
na ambao ni nguvu kazi
unayotegemea kujenga nchi
yako.

3/30/2016 1:12:31 PM

Makala

AN-NUUR

JAMADUL AAKHER 1437, IJUMAA APRILI 1-7, 2016

Jitahidini kutenda haki japo ngumu!


Na Juma Jumanne

AWALI ya yote hatuna budi


kumshukuru Muumba kwa
neema zisizokuwa na hesabu
tunazoendelea kunufaika nazo.
Rahma na amani zimwendee
mtume Muhammad, sahaba zake,
aali zake na wote waliofuata,
wanaofuata na watakaofuata
sunnah yake mpaka siku ya
kiyama.
Naam! Wanasema mwenye
macho haambiwi tazama, tuongeze
katika msemo huu kwamba hata
mwenye masikio pia haambiwi
sikia. Lakini yapo mazingira
ambayo hupelekea mtu kuambiwa
tazama hata kama ana macho na au
anaweza kuambiwa kwa kuulizwa
kwamba, umesikia hiyo!?
Kwa wenye akili safi na salama
zilizochujwa bila shaka wameona na
kwa hakika wengi wao wamebaki
na maswali yasiyojibika. Ni kuhusu
sakata la marudio ya uchaguzi
visiwani Zanzibar yaliyofanyika
siku ya Jumapili ya Machi 20,
2016. Uchaguzi ambao umerudiwa
ili yapatikane yaliyokuwa
yanatakikana, yaliyojificha nyuma
ya pazia. Yakawa yamefanyika
yaliyokusudiwa.
Watu sasa wanaweza kuulizana
maswali na wasipate majibu. Nukta
kubwa ambayo inaweza kuzua
utata zaidi ni pale atakapojiuliza
raia tu wa kawaida, kwamba
imewezekanaje mwanafunzi
asiyejua kusoma wala kuandika
akafaulu tena kwa daraja A? Nani

DKT. Ali Mohamed Shein.

mwalimu wa huyu mwanafunzi


ambaye siku zote anashika mkia!?
Watu hudai kwamba ngombe
hanenepi siku ya mnada, lakini hii
ya leo ni kali.
Labda tujaalie kweli kafaulu
mtihani tumwambie awaelekeza
waliofeli, ataweza kutoka mbele
ya darasa aelekeze namna
alivyopasua mtihani. Kwa
wale walipota bahati ya kusoma
elimu ya msingi na sekondari,
nadhani watanielewa nikitumia
neno mkondo. Wingi wa
mikondo hutegemeana na idadi ya
wanafunzi, lengo likiwa ni kuleta
ufanisi katika ufundishaji.
Inapokuja suala la kufanya

mtihani, kila mkondo huwa


na kinara wake kwa maana ya
mwanafunzi bora kuliko wote
kwa ufaulu na siyo kwa umri,
utanashati, ubabe na mfano wa
hayo. Pamoja na kuwepo kinara
katika kila mkondo, pia anakuwepo
kinara wa darasa zima. Inaweza
kutokea kwamba, mwanafunzi
anayesoma mkondo A akashika
nafasi ya kwanza kwenye mkondo
wake lakini yakitolewa matokeo ya
jumla hayupo hata kwenye kumi
bora. Na ikitokea wanafunzi wa
mkondo mwingine hawakufanya
mtihani ambao ndio wako vizuri
kitaaluma, hawa washika mkia ndio
watakaokuwa vinara.
Kwa picha hii, unaweza
kuwauliza waliopata daraja A
kwenye uchaguzi wa marudio,
kwamba kinachowafanya
washangilie ushindi ni kitu gani
hasa!? Lazima tukubali kwamba,
yapo baadhi ya mambo hata nafsi
inakataa kuchangamka kwa sababu
ya kujua ukweli wake.
Haya ndiyo maeneo ambayo
mtu unajifunza jambo kwamba,
kweli tunatofautiana. Binafsi siwezi
jamani kupata ujasiri nisimame,
nitangazwe kwamba nimefaulu
kwa namna ninavyojifahamu
uwezo wangu. Huu wote ni utamu
wa dunia. Huku kote huku, ni
kutojiamini. Watu wenye ujasiri
kama huu wa kusimamia dhulma
ifanyike, hawana yakini na kifo
hata chembe. Mbona wameondoka
wenzao mfululizo, hawashtuki tu!?
Ufisadi upi mkubwa kuliko huu?
Kwa speed hii ya kufaulisha

Taazia: Sheikh Twahir Haydar Mwinyimvua


MWAKA wa 2012 TV Imaan
iliniomba niendeshe kipindi
cha historia ya Waislam
Tanzania. Hii ilitokana na
mahojiano ambayo nilifanya
katika kipindi kilichoitwa,
Ulimwengu wa Kiislam
kipindi ambacho kilipendwa na
watazamaji wengi sana.
Tulitengeneza vipindi kadhaa
Tanga, Zanzibar na Dar es
Salaam kwa kufanya mahojiano
na watu maarufu na kipindi
changu nilikiita Walioacha
Alama katika Historia ya
Tanzania.
Katika mmoja wa watu
niliofanyanao mahojiano
alikuwa Sheikh Twahir Haydar
Mwinyimvua. Sheikh Haydar
huenda si wengi katika watu
wa leo walimjua lakini yeye ni
mtu maarufu kwa wenyeji wa
Dar es Salaam kama alivyokuwa
maarufu baba yake Sheikh
Haydar Mwinyimvua, mmoja
wa watu waliokuwa mstari wa
mbele katika TANU na mkono
wa kulia wa Nyerere wakati wa
kupigania uhuru wa Tanganyika.
Sheikh Twahir Haydar
amefariki tarehe 21 Machi
2016 nyumbani kwake

ANNUUR NEW.indd 8

Mwananyamala B. Sheikh
Haydar umri wake wote
amefanyakazi Kabidhi Wasii
hadi alipostaafu kazi miaka
michache iliyopita.
Msaada wake katika
ofisi hii ndiyo Waislamu
watamkumbuka daima. Kusajili
taasisi yoyote ya Kiislamu
nchini petu, ni kitu kigumu
sana kuanzia mwaka wa 1968
pale BAKWATA ilipoundwa na
kufanywa ndiyo kila kitu kwa
Waislamu. Sheikh Twahir juu
ya matatizo yote yaliyokuwapo,
alijitahidi sana kuwaelekeza
Waislamu nini wafanye ili
waweze kusajili taasisi zao. Hii
haikuwa kazi nyepesi kwake
kwani juu yake walikuwapo
wakubwa zake kimadaraka
ambao walifanya kila juhudi
kuhakikisha kuwa taasisi za
Kiislamu hazipati tasjila.
Mfano wa karibu sana ni
pale mwaka wa 1992 Waislamu
walipotaka kusajili Baraza Kuu.
Ala kuli hali wakati wa Rais Ali
Hassan Mwinyi angalau mambo
yalikuwa mepesi kidogo na
kipindi hiki Waislamu wengi
watamkumbuka Sheikh Twahir
alivyowasaidia kusajili taasisi

zao.
Nilipofanya mazungumzo
naye mwezi Septemba 2012 kwa
ajili ya kipindi cha televisheni
nilimuomba tutoke katika
kazi yake anieleze historia ya
East African Muslim Welfare
Society (EAMWS) baada ya
kupigwa marufuku na serikali
ya Nyerere mwaka wa 1968
na Sheikh Hassan bin Amir
aliyekuwa Mufti wa Tanganyika
kufukuzwa nchini.
Sheikh Twahir alinieleza
mengi kuanzia maisha yao
Kisutu Dar es Salaam yeye
akiwa kijana mdogo akisoma
Al Jamiatul Islamiyya Muslim
School katika miaka ya 1950
na baba yake akiwa mmoja wa
wanachama shupavu wa TANU.
Alinieleza usuhuba mkubwa
uliokuwapo baina ya baba yake
Sheikh Haydar Mwinyimvua,
Sheikh Suleiman Takadir na
Mwalimu Nyerere. Alinieleza
kazi na mafanikio yaliyofikiwa
na EAMWS na pigo Uislamu
uliopata baada ya kupigwa
marufuku.
Picha alonipa Sheikh Twahir

wasiojua kusoma wala kuandika


hatutoki. Tatizo hapa siyo
mwanafunzi kufaulu hali ya
kuwa hajui chochote, bali tatizo
ni yule aliyemuwezesha kufaulu.
Mwalimu wa aina hii anautakia nini
mustakbali wa elimu kwa kizazi
cha kesho? Tujaalie kwamba ndiyo
kapata ajira kabisa, ataelekeza nini
katika jamii!? Hebu tujiongeze.
Allah Mtukufu anasema;
Hapana kulazimisha katika Dini.
Kwani Uwongofu umekwisha
pambanuka na upotofu. Basi anaye
mkataa Shet'ani na akamuamini
Mwenyezi Mungu bila ya shaka
amekamata kishikio madhubuti,
kisicho vunjika. Na Mwenyezi
Mungu ni Mwenye kusikia,
Mwenye kujua [2:256].
Vipi tulazimishane kwenye siasa
ambazo zimejaa uwongo, hadaa,
ulaghai, udhalimu, ufisadi, ubabe
na kila aina ya maovu?
Inauma sana licha ya kuwa
tulijua fika kwamba hili jambo
haliwezekani kwa kunukuu vifungu
vya sheria. Sheria zenyewe za
kutungwa na mwanadamu, ambazo
kwa asilimia kubwa huongozwa
na hawaa na utashi binafsi. Kama
ilivyokuwa kwa masheikh wa
Zanzibar kuletwa bara, na hili
vile vile limekwenda kwa mtindo
huo huo. Hakuna taratibu zozote
zilizofuatwa.
Hongereni kwa ushindi mnono,
ila tendeni haki japo ngumu
kutokana na mlango mlioingilia,
lakini jitahidini hivyo hivyo.
Assalaam Alaykum
Warahmatullah Wabarakatuh!
Juma Jumanne (MANYARA).

Haydar ya viongozi wa EAMWS


waliokuwa wakiratibu shule za
Kiislamu wakiwa na Waziri wa
Elimu Nesmo Eliufoo ubavuni
kwa Tewa Said Tewa aliyekuwa
Mwenyekiti wa EAMWS. Kulia
wa pili aliyesimama ni Muft
Sheikh Hassan bin Amir
Sheikh Twahir siku ile alinitia
chuoni kunisomesha na nilitoka
na mengi. Hakika Sheikh Twahir
ukimtoa Mzee Waikela, hakuna
aliyekuwa kamzidi katika
kuifahamu historia ya EAMWS
na shida zilizokuwakuta
Waislamu katika miaka ile.
Bahati mbaya hadi leo vipindi
vile vyote nilivyofanya TV
Imaan haijavirusha kwa sababu
kadhaa kubwa ni kufuatia
kufungiwa Radio na TV Imaan
kwa kipindi cha miezi sita
kwa kile kilichojulikana kama
kukiuka taratibu.
Mpaka pale siku TV
Imaan itakaporusha kipindi
nilichofanya na marehemu
Sheikh Twahir Haydar
Mwinyimvua, Waislamu
tutosheke na haya machache
niliyoeleza hapa.
Tunamuomba Allah
amsamehe madhambi yake na
amuweke mahali pema peponi.
Amin
Mohamedsaid.com

3/30/2016 1:12:31 PM

Tangazo

AN-NUUR

JAMADUL AAKHER 1437, IJUMAA APRILI 1-7, 2016

Bismillahir Rahmaanir Rahiim

ISLAMIC PROPAGATION CENTRE

NAFASI ZA KIDATO CHA TANO - 2016/2017

UBUNGO ISLAMIC HIGH SCHOOL

KIRINJIKO ISLAMIC HIGH SCHOOL

NYASAKA ISLAMIC HIGH SCHOOL

Waislamu kote nchini mnatangaziwa nafasi za Kidato cha Tano kwa shule zifuatazo:

Ubungo Islamic High School


Kirinjiko Islamic High School
Nyasaka Isamic High School

Dar es Salaam : 0687 820895/0657 350172


Same, Kilimanjaro: 0784 296424/0756 676441
Mwanza: 0786 417685/0713 749020

Shule hizi ni za Kiislamu zenye lengo la kuwapa wanafunzi taaluma ya hali ya juu na malezi
bora ya Kiislamu. Shule hizi ni za BWENI za mchanganyiko wa wavulana na wasichana.
Zipo Combinations zote za SAYANSI, ARTS na BIASHARA.
Muombaji awe na ufaulu wa masomo matatu (3) kwa kiwango cha Credit (yaani A, B na C)
Daraja la III (Division three) au zaidi na Grade D kwenye masomo ya Combination.
Mwisho wa kurudisha fomu ni tarehe 02/05/2016.

Fomu za maombi zinapatikana kwa gharama ya Shilingi 10,000= katika Tovuti:www.ipcorg.tz na katika vituo vifuatavyo:
ARUSHA: Ofisi ya Islamic Education Panel, Jambo
Plastic, Ghorofa ya 2 mkabala na Msikiti Mkuu
Bondeni : 0783 438676/0715 438676.
KILIMANJARO: Moshi: Msikiti wa Riadha:07673453

67/0686938077. Same Juhudi Studio mkabala na


Benki ya NMB Same: 0757 013344. Same: Kirinjiko
Islamic Secondry School: 0784 296424/0713
115041. Usangi- Falhum Kibakaya : 0787 142054.
Ugweno Simbomu centre Mwl. Hidaya A. Mussa:
0784 655614
TANGA: Twalut Islamic Centre Mabovu
Darajani : 0715 894111/0713 014469. Uongofu
Bookshop: 0784 982525. Korogwe: SHEMEA
SHOP : 0754 690007/071569008. Mandia Shop
- Lushoto: 0782257533. Handeni Mafiga -0782
105735/0657093983
MWANZA: Nyasaka Islamic Secondary School : 0717
417685/0786 417685. Ofisi ya Islamic Education
Panel Mtaa wa Rufiji mkabala na Msikiti AlAmin 0785 086 770/0714097362.
BUKOBA: Ofisi ya Kutaiba Saccos: 0765 748056
MUSOMA: Ofisi ya Islamic Ed Panel -Mtaa wa
Karume,Nyumba Na. 05 : 0765024623/0787868611
SHINYANGA: Msikiti wa Majengo karibu na Manispaa
ya Shinyanga Mjini :0655608139/0768895484

KAHAMA: Ofisi ya Kamati ipo karibu na zahanati ya

Doctor Dalali: 0754 994738/0782 994738

Dar es Salaam: Ubungo Islamic High School :


0756584625/0657350172/0712 033556. Ofisi ya
Islamic Ed. Panel Temeke -Msikiti wa Nurul Yakin
: 0655144474/0787119531
MOROGORO: Wasiliana na
Ramadhani Chale :

0715704380. Ifakara wasiliana na Mwl. Sharifu:


0659 158958
GEITA: Ofisi ya Kamati karibu na mashine ya
kukobolea mpunga shilabera: 0765 748056
DODOMA: Hijra Islamic Primary School

: 0716
544757/0718661992
SINGIDA: Ofisi ya Islamic Education. Panel
karibu na Nuru snack Hotel : 0786
425838/0784 928039.
MANYARA: Ofisi ya Islamic Ed. Panel Masjid
Rahma: 0784491196
KIGOMA: Msikiti wa Mwandiga: 0714717727.
Kibondo Islamic Nursery School:
0766406669. Kasulu: Murubona Isl.SS:
0714710802/0763 298440
LINDI: Wapemba Store: 0784 974041/0783

488444/0653 705627.
MTWARA: Amana Islamic S.S: 0715
465158/0787 231007.
SONGEA: Kwa Kawanga Karibu na Msikiti
wa NURU : 0713249264. Mkuzo Islamic
High School :0654 876317
MBEYA: Ofisi za Islamic Education Panel
Uhindini 0785425319. Rexona Video
mkabala na Mbeya RETICO: 0713
200209/0785425319.
Rukwa: Sumbawanga:Jengo la Haji
Said Shule ya Msingi
Kizwike:
0757090228/0786 313830
TABORA: Kituo cha Kiislamu Isevya: 0784
944566/0718 556355. Nzega - Dk. Mbaga0754 576922/0784576922.
IRINGA: Madrastun Najah: 0714 522 122.
PEMBA: Wete: Wete Islamic School : 0777
432331/0712772326.
UNGUJA: Madrasatul Fallah: 0777125074.
PANDU BOOKSHOP 0777462056 karibu
na uwanja wa Lumumba
MAFIA: Ofisi ya Ust. Yusufu Ally jirani na
msikiti mkuu : 0773580703.

WAHI KURUDISHA FOMU ILI UJIHAKIKISHIE NAFASI


FORM V TANGAZO.indd 1

ANNUUR NEW.indd 9

3/21/2016 3:58:37 AM

3/30/2016 1:12:32 PM

10

Makala

JAMADUL AAKHER 1437, IJUMAA APRILI 1-7, 2016

Uchaguzi wa Marekani ni demokrasia ya kiini macho

Na Nizar Visram
KWA muda wa miezi kadha
sasa habari kutoka Marekani
zimekuwa zikitawaliwa na
kinyanganyiro cha urais.
Wagombea wanaowania
tiketi za chama wamekuwa
wakipambana na kulumbana
huku washabiki wao wakitiana
ngumi na kushikana mashati.
Mgombea mmoja anasema
ukinichafulia mkutano wangu
nami ntamwaga mboga katika
mkutano wako. Alimradi
watazamaji wengi wamekuwa
wakichukulia mchakato mzima
kama burudani ya aina yake.
Kinachofanyika kwa sasa ni
uchaguzi wa awali (primaries)
utakaopelekea kufanyika
kwa uchaguzi wa urais nchini
Marekani tarehe 8 Novemba
2016. Wao hufanya uchaguzi
wa rais kila baada ya miaka
minne. Katiba yao imeweka
kikomo cha mihula miwili,
hivyo Rais Obama analazimika
kungatuka na kumpisha
mwengine atakayechaguliwa
Hivyo, huu uchaguzi wa awali ni
mchakato wa kumteua mgombea
wa urais kutoka kila chama.
Vyama vikuu vinavyojulikana
zaidi ni Democratic na
Republican. Utaratibu wao wa
kuteua wagombea na hata wa
kumchagua rais ni tofauti na
wa hapa Tanzania. Kwa kweli si
wote wanaoelewa utaratibu huu.
Sitashangaa hata Wamarekani
wenyewe wasipoelewa. Wao
wanadai kuwa wanaongoza
dunia katika demokrasi. Lakini
cha ajabu ni kuwa mgombea wa
chama hateuliwi na wanachama,
na rais hachaguliwi na wananchi
moja kwa moja kama tufanyavyo
sisi hapa kwetu. Ndio maana
wanapofanya uchaguzi basi
ubalozi wao hapa jijini huwaita
waandishi ili kuwaelimisha na
wengine hata hupewa fursa ya
kwenda Marekani ili waandike
makala za kuusifu mfumo wao.
Huko Marekani wananchi
watawachagua watu
watakaomchagua rais kwa niaba
yao. Watachagua kikundi cha
wapiga kura (electoral college)
ambao ndio watakaopiga kura
ya kumchagua rais. Hivi sasa
kinachofanyika ni mchakato
wa kuwateua wagombea urais
ulioanza tarehe 1 Februari

ANNUUR NEW.indd 10

na utakaomalizikia tarehe
14 Juni mwaka huu. Uteuzi
huu unahusu majimbo 50
nchini kote. Watu watapiga
kura kuwachagua wajumbe
watakaohudhuria mkutano
mkuu wa chama (nominating
convention) ambao ndio
utamchagua mgombea wa urais
atakayepeperusha bendera
ya chama. Katika hatua hii ya
kichama hata Wamarekani walio
ughaibuni nao wanashirikishwa.
Kwa mfano, chama cha
Republican kitawachagua
wajumbe 2,472 watakaohudhuria
mkutano mkuu (convention)
ambako mgombea urais wa
chama atateuliwa. Chama hiki
kilianza na wanachama 17
waliotangaza nia ya kugombea
tangu Machi mwaka jana. Hii ni
idadi kubwa ya watia nia ambao
haijapata kutokea huko. Wengi
wao ni watu wenye nyadhifa
wakiwa magavana wa mikoa au
maseneta (wabunge). Ila mmoja
ni tofauti. Huyu ni Donald
Trump ambaye si gavana wala
seneta bali ni bilionea kutoka
New York ambaye amewekeza
hata katika Mashariki ya Kati.
Hiyo ndio sifa yake ambayo
imewavutia Wamarekani wengi.
Trump si mwanasiasa
kama wagombea wengine.
Yeye ni bilionea anayefanya
biashara ya kujenga na kuuza
majengo, pamoja na kuendesha
mahoteli na vituo vya kamari
(casino). Anadai kuwa kwa
vile amefanikiwa kutajirika,
basi akiwa rais atahakikisha
wananchi nao wanatajirika.
Lakini kisichosemwa ni kuwa
kampuni zake zimewahi
kufilisika mara nne. Huo si
mfano mzuri wa kuigwa. Wengi
wanamuona kama ndumila
kuwili, kwa vile aliwahi
kujiunga na Democrat. Aliwahi
hata kumuwezesha kifedha Bi
Hillary Clinton katika kampeni
zake mnamo 2008. Trump pia
amewahi kuwaunga mkono
wanawake waliokuwa wakidai
haki ya kutoa mimba. Sasa
anapinga jambo hilo na hata
kuishambulia serikali kwa
kuziwezesha asasi za uzazi wa
mpango (family planning).
Mwaka 2000 alikuwa akiunga
mkono mfumo wa bima ya
matibabu kwa wananchi wote
ukisimamiwa na serikali. Leo
anadai eti huko ni kuingilia
uhuru wa raia kujichagulia
bima. Yaani anataka makampuni
ya bima yaruhusiwe kushindana
katika soko huria na kila
mmoja ajiamulie kujiunga au
kutojiunga bila ya kuingiliwa
na serikali. Aidha, Trump
amekuwa akichochea chuki
na ubaguzi wa kidini dhidi ya
Waislamu wanaoishi Marekani
kwa kuwaita wakuja wasio
na haki ya kuishi nchini.
Anasahau kuwa Waislamu
walianza kuingia Marekani
kabla ya babu yake kuhamia
huko kutoka Ujerumani. Halafu
anasema akiwa rais, Waislamu

AN-NUUR

hawataruhusiwa kuingia
Marekani.
Anazishambulia pia
China, Mexico na Japan kwa
kuyalaumu makampuni
yanayowekeza huko badala ya
kuwekeza nyumbani. Hawa
anawaita wasaliti waliokosa
uzalendo. Anasahau kuwa
kufanya biashara na nchi hizo na
kuwekeza huko ni muendelezo
wa sera ya utandawazi, sera ya
kibeberu ambayo ina manufaa
kwa mabepari wa kimataifa.
Trump anasema akiwa rais
atawaua watuhumiwa wa
ugaidi bila ya kuwafikisha
mahakamani. Anasema ataua
hata familia zao. Huyu ndie rais
mtarajiwa wa Marekani na sera
zake za kifashisti.
Mpinzani mkuu wa Trump
katika chama cha Republican
ni seneta Ted Cruz. Huyu
huwa anaelezwa kuwa ni
mwenye siasa za wastani.
Kinachosahauliwa ni kuwa
Cruz naye anaunga mkono
mashambulizi zaidi katika
Mashariki ya Kati, pamoja
na upunguzaji wa kodi kwa
matajiri.
Kwa upande wa Democrat
mgombea seneta Bernie Sanders
amewavutia watu wengi,
hasa vijana, kutokana na sera
yake anayoiita usoshalisti
wa kidemocrasia. Yeye
anazungumzia mapinduzi
ya kisiasa lakini tukiangalia
zaidi tunaona kuwa msimamo
kama huo hauwezi kukubaliwa
asilani na chama cha Democratic
ambacho siku zote kimekuwa
kikitumikia maslahi ya
kibepari kikishrikiana na
Republican, kwa muda wa
miaka 150. Ni kweli vyama
hivyo vinatofautiana, lakini si
kimsingi. Democratic ni cha
mrengo wa kulia na Republican
ni cha mrengo wa kulia zaidi.
Ndio maana hata Sanders
akishinda urais itamuwia
vigumu kutekeleza ahadi zake.
Ni sawa na rais Obama ambaye
kabla ya kuchaguliwa aliahidi
kufunga gereza la Guantanamo,
lakini jitihada zake zimegonga
ukuta. Hivi sasa tunaambiwa
Obama anashindwa kutekeleza
ahadi zake kwa sababu bunge
(Congress) linatawaliwa na
chama cha Republican. Lakini
ukweli ni kuwa mwaka 2009 na
2010 bunge lilikuwa na wingi
wa Democratic, kina Sanders
na wenzake pamoja na rais
wao katika ikulu ya White
House. Hata hivyo hakuna
hatua walizochukua tofauti na
Republican. Wakati huo uvamizi
wa kijeshi katika Mashariki ya
Kati uliongezeka.
Kuhusu gharama za kampeni,
michango mingi ya Hillary ni
kutoka makampuni makubwa
wakati Sanders anategemea
wachangiaji wadogo. Wakati
mmoja Hillary alikuwa
amekusanya dola milioni 29.4
na Sandera dola milioni 26.2.
Fedha za Hillary zilitoka kwa

wachangiaji matajiri wachache


waliotoa kima kikubwa, wakati
Sanders alisaidiwa na watu
wengi waliotoa kima cha chini.
Hawa ni walalahoi 650,000
waliochanga wastani wa dola
30 kila mmoja. Sanders pia
amechangiwa na vyama vya
wafanyakazi na vijana wengi
wamejitolea kumsaidia katika
kampeni zake. Ndio maana
Sanders huwa anajisifu kuwa
yeye anawasemea watu wadogo
na kumshambulia Hillary
kuwa anawakilisha maslahi
ya makampuni makubwa
Yeye anadai kuwa huwa
anazungumza na wananchi
wengi ambao hulalamika
kuwa uchumi wa Marekani
umepogoka. Ndio maana
unakuta Marekani ambayo
ni nchi tajiri pekee duniani
isiyokuwa na mfumo wa
matibabu bure kwa wote.
Sanders anasema hii ni aibu na
chini ya utawala wake ataondoa
aibu hii ya kuwaachia watu
wakifa kwa sababu hawana pesa
za kulipia matibabu.
Wakati huohuo Sanders
anakusudia kuongeza mshahara
kima cha chini kianzie dola
15 kwa saa. Ameahidi pia
elimu bure mpaka ngazi ya
chuo kikuu. Lakini ni Sanders
huyu huyu ambaye akiwa
katika bunge aliunga mkono
mashambulizi ya kijeshi nchini
Iraq na Afghanistan. Katika
miaka yake yote alipokuwa
mbunge amekuwa akiunga
mkono mashambulizi ya
Marekani katika nchi kama
Somalia, Haiti, Bosnia,
Liberia, Zaire, Albania, Sudan,
Yugoslavia, Yemen na kadhalika.
Hivi karibuni aliitaka serikali
ikamate mali zote za Urusi
na akaishauri Saudi Arabia
iendeleze vita katika nchi za
Kiarabu.
Mnamo 2006 alipiga kura
kuunga mkono azimio dhidi ya
Iran. Pia aliunga mkono uvamizi
wa Israel nchini Lebanon.
Akaunga mkono kuuwekea
vikwazo utawala wa Palestina
kwa sababu tu wananchi
wake walichagua chama cha
Hamas katika uchaguzi wa
kidemokrasia. Mwaka 2014
akaunga mkono uvamizi na
mauaji ya Israel huko Gaza.
Akaunga mkono mpango wa
Obama wa kuuwa raia wa Syria
na Iraq kwa kutumia ndege
zisizo na rubani. Alipoulizwa
akasema akiwa rais atajaribu
asiue raia wengi!
Kuhusu huu uchaguzi, ni
vizuri tukaelewa kuwa hakuna
mgombea wa urais yeyote
wa Marekani anayetarajia
kuchaguliwa au aliyechaguliwa,
ambaye anaweza kuthubutu
kuikosoa Israel. Wana asasi ya
kizayuni iitwayo AIPAC ambayo
ndio inahakikisha kuwa kila rais
au rais mtarajiwa anatangaza
utii wake kwa Israel
Ndio maana kabla ya Obama
kuchaguliwa kwa muhula wa
pili aliiangukia AIPAC. Na
ndivyo kina Trump, Hillary
na Sanders nao wanatarajiwa
kuiangukia AIPAC ili
waruhusiwe kugombea urais.
(0713-562181 nizar1941@
gmail.com)

3/30/2016 1:12:33 PM

11

Makala

AN-NUUR

JAMADUL AAKHER 1437, IJUMAA APRILI 1-7, 2016

Profesa Sheikh Mohammed Abubakar


ni rafiki yake wa karibu na
Maruhum, wanaitaja misiba
ya Masheikh Hemed Albuhur,
na ule wa Sheikh Mohammed
Bin Ayoub, ambayo ndiyo
iliyofananishwa na msiba wa
Sheikh Mohammed Abubakar,
kwa wingi wa watu.
Hata hivyo, Sharif Muhdhar,
anasema kwa zama za hivi
karibuni baada ya Misiba ya
Masheikh hao kwa vijana
wa kuanzia miaka ya 1980,
unaweza kusema kwamba
hawajawahi kuona mkusanyiko
wa msiba wenye watu wengi
kwa Jiji la Tanga, kama wa
Sheikh Mohammed Abubakar
Alburhan.
Ustadhi Samir Sadiq, ambaye
kwa sasa ndiye ameshika nafasi
ya Mudir wa Shamsi Maarif,
anafafanua kwa nini maziko ya
Mudir wake yamehudhuriwa na
maelfu ya watu wengi pengine
zaidi ya Masheikh wake.
Kwa kweli mimi msiba
niliowahi kuuona sijapata kuona
kama huu kwa umri wangu
wa akili timamu nikiwa humu

Na Bakari Mwakangwale

KATIKA elimu ya Sekula, upo


utaratibu wa kutunukiana
falsafa za taaluma kama
Udaktari (PhD) au Uprofesa,
kutegemea ukaribu wa
muhusika na Chuo Kikuu
husika. Wanaweza kumtunuku
mtu katika tasnia ya Siasa,
Utamaduni na masuaka ya
kijamii.
Kumbe, hilo pia lipo kwa
upande wa elimu ya Maarifa
ya Uislamu ambayo huitwa
Ijaza. Hii ni tunu katika Ilimu
au zawadi, ambayo inazingatia
uelewa na ufahamu (Weledi)
wa muhusika katika mambo
mbalimbali kadiri alivyojaaliwa
na Allah (sw).
Anaeleza Sharif Muhdhar
bin Abdulrahman Khitami
(59), ambaye ni Mkenya,
akimuelezea Almaruhum
Sheikh Mohammed Abubakar
Albukhur, aliyekuwa Mudir
wa Chuo maarufu cha Dini,
Maahd Shamsil Maarif, Duga
Jijini Tanga. Anamtaja Sheikh
Mohammed, kuwa alikuwa
ni mtu wa aina yake katika
kuhifadhi masala ya kielimu
ya Dini kwa ujumla, anasema
kwa ujumla katika elimu ya
Kisekula, hufahamika katika
taaluma ya fani mbalimbali
ambapo mtu akibobea humo,
ndipo huitwa Profesa au
Dokta. Anasema, Almaruhum
Mohammed Abubakar, katika
fani hizi za Ilimu ya Dini, kama
vile Nahau, Swarifa, Balagha,
Sirah, Tafsiri, elimu ya Mirathi
na mengine mengi ambapo kwa
ujumla wake yapo takribani
16, yeye kwa ujumla alikuwa
amebobea kwa upande wa pili
wa elimu angeweza kuwa ni
Profesa au Dokta. Na kwamba
ilikuwa hakuna unaeweza
kumlinganisha naye katika ilimu
hizo.
Tena Sheikh alikuwa ni mtu
wa ajabu, pamoja na bahari
ya ilimu aliyokuwa nayo
ilikuwa ukimwambia wewe
katika swala fulani sioni mfano
wake, anasema hapana yupo
Sharif Muhammad wa Kenya,
(Marhum kwa sasa) ndiye
alikuwa akimtaja kuwa ni zaidi.
Lakini na huyo wa Kenya,
alikuwa akiulizwa naye anasema
yupo Muhammed Abubakar
wa Tanga (Tanzania) kuwa yeye
ni zaidi. Kwa kweli hakuwa
mjivuni. Anasema Sharif
Muhdhar.
Ni kwa maana hiyo basi,

ANNUUR NEW.indd 11

ALMARUHUM Sheikh Mohammed Abubakar Albukhur.


Sharif Muhdhar, anasema
kwamba Baba yake ilimlazimu
kumtunuku daraja ya elimu
maarufu kama Ijaza, Sheikh
Mohammed Abubakar, na
kumvika kilemba maalum
ambacho asili yake kilirithiwa
kutoka kwa Mtume Muhammda
(s a w).
Sharif Muhdhar, anafafanua
kwa kueleza kwamba
alimfahamu Almarhumu Sheikh
Mohammed Abubakar, kupitia
kwa Baba yake ambaye alikuwa
ni Sharif Abdulrahman Khitami,
ambaye alikuwa ni mwanafunzi
wake.
Anahadithia tukio la
Almaruhum Sheikh Mohammed
Abubakar kutunukiwa kilemba
hicho kwamba ilikuwa Mei
2, 2004, ambapo Mzee wake
Abdulrahman Khitami, alifika
Jijini Tanga akiwa mmoja wa
wageni waalikwa katika hafla ya
uzinduzi wa Msikiti wa chuo cha
Maahd Shamsil Maarif, Duga.
Katika hafla hiyo, Mzee wake
ambaye alikuwa ni Sharif na
Sheikh kutokea nchi ya jirani
ya Kenya, ndiye aliyepewa
heshima ya kufungua Msikiti
huo na ndipo alipofanya tukio la
kihistoria kwa kumtunukia kwa
kumvisha kilemba Almaruhum
Shkh. Mohammed Abubakari.

Kwa mujibu wa Sharif


Muhdhar, alisema kwamba
Mzee wake alitoa maelezo
ya uzito wa Kilemba hicho
kwamba asili yake kimetoka
kwa Mtume Muhammad (S a
w), na kufafanua kuwa hata
yeye (Sharif Abdulrahman
Khitami) alivishwa na Masharifu
wenzake na hao nao walivishwa
na masharif wenzao, ambao
mtiririko wake kilitokea kwa
Mtume Muhammad (s a w)
yaani ni kitendo cha kiasili.
Sharif Abdulrahman Khitami,
alifariki mwaka 2006, na
kuzikwa kwao Kenya, ambapo
Sheikh Mohammed Abibakari,
alisafiri mpaka nchini Kenya
na kushirika katika mazishi
ya Sheikh wake yaliyofanyika
katika Mji wa Lamu.
Ama kuhusu, maziko ya
Sheikh Mohammed Abubakar,
anasema yamekuwa ni ya
kihistoria, kwani wenyeji wa
Jiji hilo, wanasema umekuwa
ni miongoni mwa misiba
michache iliyopata kutokea na
kuhudhuliwa na watu wengi.
Baadhi ya wazee wa Jiji la Tanga,
kama Sharif Hussen Hashim,
ambaye ni mwenzake na Sheikh
Mohammed Abubakar, katika
maswala ya kielimu, na Sheikh
Saidi Abdallah Makata, ambaye

Jijini Tanga, msiba niliouona


kujaa umma kabla ya huu wa
Sheikh Abibakar, ulikuwa
ni wa Sheikh Mohammed
Ayoub.
Lakini huu wa Sheikh
Mohammed Abibakar,
ulikuwa ni umma mkubwa
zaidi ya Sheikh Ayoub,
nadhani labda msiba wa
Sheikh Ayoub, ulikuwa
jirani sana na maziko yake
ukilinganisha na huu wa
Sheikh Abibakar.
Hii ni kutokana na kwamba
Sheikh Abibakar, kasomesha
wanafunzi wengi, sasa
ukichanganya na wanafunzi
wa Sheikh Mohammed
Ayoub.
Sheikh Ayoub, alifariki
usiku wa Jumanne, na

kuzikwa Alasiri, siku iliyofatia,


hiyo inamaana watu wengi
walichelewa kuzika na wengine
hawakuweza kusafiri kuwahi
mazishi.
Hatua ya kuweka mazishi ya
Sheikh Abibakar, siku moja zaidi
baada ya kifo chake, ilitoa fursa
ya kila anaemfahamu, popote
alipo alitia nia ya kufika msibani
kulingana na nafasi yake kwani
alikuwa ni mtu wa watu.
Hali hii imepelekea kwamba
kila aliyepata taafia popote alipo
alipata wasaa wa kizika, kuna
watu wamekuja karibia kila kona
ya Tanzania na mijini ya Lamu,
Nairobi na Mombasa katika nchi
ya jirani ya Kenya.

3/30/2016 1:12:34 PM

12

Tangazo

AN-NUUR

JAMADUL AAKHER 1437, IJUMAA APRILI 1-7, 2016

Bismillahir Rahmaanir Rahiim

ISLAMIC PROPAGATION CENTRE


KIRINJIKO ISLAMIC TEACHERS COLLEGE - SAME, KILIMANJARO

KOZI YA UALIMU WA LUGHA YA KIARABU, KIINGEREZA,


KISWAHILI NA ELIMU YA DINI YA KIISLAMU NGAZI YA CHETI 2016/2017

Muda wa Kozi ni miaka miwili


SIFA ZA MUOMBAJI:

(a) Awe Muislamu.


(b) Awe amefaulu masomo matatu (3) au zaidi kwa kiwango cha D au zaidi katika Mtihani wa Kidato cha 4.
(c) Atakayekuwa na ufaulu wa kiwango cha D au zaidi katika masomo ya Lugha ya Kiarabu, Kiingereza,
Kiswahili na Elimu ya Dini ya Kiislamu atapewa kipaumbele zaidi.
Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni tarehe 15 JULAI, 2016.
Fomu za maombi zinapatikana kwa gharama ya Shilingi 5,000/= (elfu tano) katika Tovuti:www.ipcorg.tz na katika vituo vifuatavyo:
ARUSHA: Ofisi ya Islamic Education Panel, Jambo
Plastic, Ghorofa ya 2 mkabala na Msikiti Mkuu
Bondeni : 0783 438676/0715 438676.
KILIMANJARO: Moshi: Msikiti wa Riadha:07673453

67/0686938077. Same Juhudi Studio mkabala na


Benki ya NMB Same: 0757 013344. Same: Kirinjiko
Islamic Secondry School: 0784 296424/0713
115041. Usangi- Falhum Kibakaya : 0787 142054.
Ugweno Simbomu centre Mwl. Hidaya A. Mussa:
0784 655614
TANGA: Twalut Islamic Centre Mabovu
Darajani : 0715 894111/0713 014469. Uongofu
Bookshop: 0784 982525. Korogwe: SHEMEA
SHOP : 0754 690007/071569008. Mandia Shop
- Lushoto: 0782257533. Handeni Mafiga -0782
105735/0657093983
MWANZA: Nyasaka Islamic Secondary School : 0717
417685/0786 417685. Ofisi ya Islamic Education
Panel Mtaa wa Rufiji mkabala na Msikiti AlAmin 0785 086 770/0714097362.
BUKOBA: Ofisi ya Kutaiba Saccos: 0765 748056
MUSOMA: Ofisi ya Islamic Ed Panel -Mtaa wa
Karume,Nyumba Na. 05 : 0765024623/0787868611
SHINYANGA: Msikiti wa Majengo karibu na Manispaa

ya Shinyanga Mjini :0655608139/0768895484

KAHAMA: Ofisi ya Kamati ipo karibu na zahanati


ya Doctor Dalali: 0754 994738/0782 994738
Dar es Salaam: Ubungo Islamic High School
: 0756584625/0657350172/0712 033556.
Ofisi ya Islamic Ed. Panel Temeke -Msikiti
wa Nurul Yakin : 0655144474/0787119531
MOROGORO: Wasiliana na Ramadhani Chale :
0715704380. Ifakara wasiliana na Mwl. Sharifu:
0659 158958
GEITA: Ofisi ya Kamati karibu na mashine ya
kukobolea mpunga shilabera: 0765 748056
DODOMA: Hijra Islamic Primary School : 0716
544757/0718661992
SINGIDA: Ofisi ya Islamic Education. Panel
karibu na Nuru snack Hotel : 0786 425838/0784
928039.
MANYARA: Ofisi ya Islamic Ed. Panel Masjid
Rahma: 0784491196
KIGOMA: Msikiti wa Mwandiga: 0714717727.
Kibondo Islamic Nursery School: 0766406669.
Kasulu: Murubona Isl.SS: 0714710802/0763

298440
LINDI: Wapemba Store: 0784 974041/0783
488444/0653 705627.
MTWARA: Amana Islamic S.S: 0715 465158/0787
231007.
SONGEA: Kwa Kawanga Karibu na Msikiti wa NURU
: 0713249264. Mkuzo Islamic High School :0654
876317
MBEYA: Ofisi za Islamic Education Panel Uhindini
0785425319. Rexona Video mkabala na Mbeya
RETICO: 0713 200209/0785425319.
Rukwa: Sumbawanga:Jengo la Haji Said
Shule ya Msingi Kizwike: 0757090228/0786
313830
TABORA: Kituo cha Kiislamu Isevya:
0784
944566/0718 556355. Nzega - Dk. Mbaga-0754
576922/0784576922.
IRINGA: Madrastun Najah: 0714 522 122.
PEMBA: Wete: Wete Islamic School : 0777
432331/0712772326.
UNGUJA: Madrasatul Fallah: 0777125074.
PANDU BOOKSHOP 0777462056 karibu na
uwanja wa Lumumba
MAFIA: Ofisi ya Ust. Yusufu Ally jirani na msikiti
mkuu : 0773580703.

Kwa maelezo zaidi piga simu: 0787 188964, 0784 267762 na 0654 613080

USIKOSE NAFASI HII ADHIMU - WAHI KUCHUKUA FOMU SASA!

ARABIC CHETI.indd 1

ANNUUR NEW.indd 12

3/21/2016 3:59:12 AM

3/30/2016 1:12:35 PM

13

Safu ya Ben Rijal

AN-NUUR

JAMADUL AAKHER 1437, IJUMAA APRILI 1-7, 2016

Miti Duniyani na maisha yetu Msufi

KATIKA makala zetu ya


Miti duniani na maisha yetu
hadi wiki iliopoita ilikuwa
tunaizungumzia miti ya
vyakula zaidi pasina kugusia
miti ya biashara. Katika
makala ya safari hii tutagusia
msufi ambao hutoa sufi na
kutengenezewa nguo.
Kitaalamu Msufi huitwa
Ceiba pentandra ukiwa umo
katika jamii ya Malvacea, mti
huu kila mmoja huita kwa
majina yake. Hebu tuangalie
majina ya Msufi kutokana
na lugha mbalimbali :
Kiengereza White Silk-Cotton
Tree, Kispeni Ceiba, Kifaransa
Fromager, Wasurinam huita
Kankantrie, Kihindi Safed
semal, Kitamil Ilavam,
Bengali Shwet Simul, Ashante
Twi and Fanteen - Ony,
au Onyina na Mandigo wao
huita ban, bnda (Dioula),
bant (Malink), banti.
Maelezo ya kivazi cha nguo
ya sufi ikielezewa namna
ya thamani yake ilivyo
apani ilipigana vita vingi
vya wenyewe kwa wenyewe
kuanzia mwishoni mwa
nusu ya karne ya 15 hadi
karne ya 17. Wapiganaji wa
kipindi hicho walishindana
miongoni mwao kuvaa
bidhaa zilizokuwa za kipekee
ambazo zingewafanya
kuonekana kwamba ni wa
kipekee. Hususan, viongozi
wa vita hivyo, walivaa
jinbaori makoti yaliyovaliwa
juu ya ngao wakati wa vita
ili kutambulika. Koti la rangi
nyekundu lililovaliwa wakati
wa vita ambalo tumeliangazia
katika kipindi hiki, lina
muundo unaoonekana wazi
wa mundu upande wa nyuma
huku kwa mbele, likionekana
kama muundo wa lango la
kuingia kenye hekalu ambalo
linaashiria matakwa binafsi

ANNUUR NEW.indd 13

ya wapiganaji ya kutaka
ulinzi kutoka kwa miungu.
Kitambaa kilichotengenezwa
kwa sufi kilichotoka Ulaya,
kilitiwa rangi ambayo ilikuwa
ghali na huenda kiliwasili
nchini Japani kupitia ufanyaji
biashara na Wareno. Utumiaji
wa vitambaa vyenye thamani
kama hivyo pia ulikuwa
ishara ya kuonyesha nguvu.
Pia utagundua hisia ya kutaka
kutambulika ya wapiganaji
wanapokuwa vitani katika
enzi za vita vikali. Hakika
nguo za sufi ndio nguo
ambazo zimetawala duniani
na wazalishaji wa sufi wengi
wao hawafaidi mapato
yatokanayo na sufi.
Msufi hutoa pamba na ni
mmoja kati ya mti maarufu
duniani katika mti ambao sio
wa chakula. Msufi ni maarufu
tunaweza kusema kuliko
ya aina yoyote ile ya miti
mengineo. Nusu ya viwanda
vilivyo vya kutengenezea
nguo duniani hutumia
pamba katika matengenezaji
wa nguo. Aidha pamba
hutumiwa katika utengenezaji
wa miripuko, mafuta, chakula
kwa ngombe na dawa za
kupigia meno.
Misufi ya kutengenezwa
viwandani imeanzishwa
duniani lakini juu ya hayo
bado sufi itokanayo katika
miti ya asili huwa na thamni
kubwa inagwa mara nyingi
huhujumiwa na wadudu
na kutumiwa kwa dawa
za kupambana na hao
wadudu. Pamba ina pambana
kujiweka katika soko na
matumizi ya nailoni, na aina
nyenginezo. Biashara ya
Pamba imekuwa ni moja ya
kutumiwa Watumwa katika
kazi ya kuuhisha Misufi,
katika nchi ya Marekani
Watumwa waliotokea Afrika
walikuwa kwenye mashamba
ya miti iliopandwa Misufi
wakiimarisha na Mapinduzi
ya viwanda yalitokana na
kushamiri kutokana na
kukuwepo kwa Pamba.
Katika karne ya 18 na 19
Waengereza walikuwa ndio
wenye viwanda vingi vya
kutengeneza nguo zitokanazo
na Pamba. Mwana taaluma
wa Kimerekani Ely Whitney
katika mwaka wa 1793 ndio
alioasisi mashine ya kwanza
ya kukamulia mbegu za
Pamba na kupunguza kazi ya
mwanadamu kufanya hayo

na waliokuwa wakifanya kazi


kubwa walikuwa sio wengine
ila ni watumwa. Ili kuifanya
Misufi iendelee kuzalisha
madawa ya kunyunyuzia
hutumiwa kwa wingi na
kuleta madhara, katika ardhi
ya kilimo duniani kote Misufi
huchukua eneo la asilimia
3 tu lakini hutumia robo
ya dawa zinanyunyuziwa
kuuwa wadudu na hayo
huchangia vifo vya watu
20,000 kila mwaka katika nchi
zinazoendelea.
Miaka kama 7,000 iliopita
Misufi ilianza kupandwa
katika bonde ua Indus
sehemu ijulikanayo kama nchi
ya Pakistan hivi sasa. Baada
ya hapo ikaanza kupandwa
katika nchi za Mexico na
Peru. Juu ya hayo wataalamu
wameweza kugundua nyuzi
za Pamba zikiwa ni mabaki
yaliotumiwa katika nchi za
Pakistan na Mexico kama
miaka 5,000 kabla ya kuzaliwa
kwa Mtume Issa AS. Misufi
kutoka Pakistan ilianza
kuenea na kushamiri katika
nchi za Mashariki ikiwa
China, Korea na Japan na
kuingia katika bara la Ulaya
katika mwaka wa 900.
Sufi ni muhimu sana
kwani mbali ya nguo kuna
mengi hutenegenezwa
kutokana na Sufi, Pamba na
mbegu zake kati ya hayo ni
taulo za kufutia maji baada
ya kugoea hutengenezwa
kutokana na pamba. Tukae
kufikiria umemaliza kukoga
na unaharaka unataka
kutoka huna taulo ingebidi
ufanye nini? Aidha bidhaa
kama karatasi, noti za
fedha tutumiazo, nyavu za
kuvulia, mabendegi, baadhi
ya pamba za kutumiwa
katika upasuaji, kamba
hutengenezwa kutokana
na Pamba. Aidha nyuzi za
Pamba hutumika katika
utengenezaji wa miripuko,
walaji sosej (Sausage) ile
sehemu ya juu ya sosheji
hutokana na nyuzi za pamba.
Filamu zinazotengenezwa
na kutoa picha ni kutokana
Msufi na nishati itumiwayo
na roketi hutumia mafuta
yanayokamuliwa kutokana
na mbegu za Msufi. Hata
wala Isikrimu (ice cream) na
watafunao ubani ni kati ya
vitu vinavyotegemea Msufi
katika matengenezo yake.
Nchi zinazoongoza

kusafrisha Pamba kwa wingi


duniani kwa maalfu ya Metric
tani namba mmoja ni China
6,532, India 6,423, Marekani
3,553, Pakistan 2, 308, Brazil
1,524, Uzbekistan 849,
Uturuki 697.
Nchi ya China inaongoza
kwa uzalishaji wa Pamba
duniani lakini nayo ndio
inayoongoza ununuwaji
wa pamba kwa thamani
kubwa, kwa mwaka wa
2014 walinunua Pamba
yenye thamni ya Bilioni 12.8
pesa za Kimarekani akiwa
nikama anayeongoza kwa
asilimia 21.8 nchi inayonunua
Pamba kwa wingi duniani,
ikifwatiwa na nchi ya
Bngladesh Dolari bilioni
5.3, Vietnam bilioni dolari
4.3, Uturuki Dolari bilioni 3,
Hon Kong Dolari bilioni 2.5,
Indonesia Dolari bilioni 1.6,
Utaliano Dolari bilioni b1.6,
Ujerumani Dolari bilioni 1.3,
nchi ya Mexico Dolari bilioni
1.1.
Katika orodha niliyoiweka
hapo juu nchi ya Vietnam
imekuwa ni nchi yenye
mahitaji makubwa ya pamba
na yenye kununua kwa wingi
ukilinganisha kitakwimu,
ikifwatiwa na India, China,
Japan na Indonesia. Nchi
ambazo manunuzi yao
yanapungua ni Hon Kong,
Korea ya Kusini, Thailand,
Utaliano, Pakistan, Uturuki,
Ujerumani na nchi ya
Marekani.
Nchi ya Bangladesh ina
viwanda vingi vya nguo na
wanatumia vijana, watoto
na wanawake kuwalipa
mishahara midogo, lakini
kutokana na umasikini
wanakuwa hawana budi
jamii ya watu hao kutoingia
katika kazi za viwandani.
Jambo la kusikitisha kuwa
nguo hizo nyingi huuzwa
katika nchi za Magharibi
ambazo zinapinga utumiwaji
wa watoto kufanyishwa kazi
kabla ya kuwa watu wazima.
Aidha nchi hizo ndio mstari
wa mbele kupinga malipo
madogo ya wafanyakazi
duniani. Tujiulize hizi nchi
za Magharibi ni waokozi
wa dunia hii au wacheza
watu shere? Jawabu unayo,
fwatana na mie wiki ijayo.

3/30/2016 1:12:35 PM

14

MAKALA/MASHAIRI

SIKU YA WAJINGA AU WAZUSHI ?


Nabtadi kualifu, si tungo kuzibananga,
Jambo moja kuarifu, si mengi kutangatanga,
Si jingine mintarafu, hiyo siku ya wajinga,
Sio siku ya wajinga, ya wazushi na warongo!
Tarehe mosi tengefu, Aprili naipinga,
Si siku inosadifu, urongo wanoulonga,
Lengolo udanganyifu, kwa kaumu kuikenga,
Sio siku ya wajinga, ya wazushi na warongo !

Kumu katika insafu, kwa puya kutozienga,


Usimuasi Raufu, kwa longolongo kutunga,
Daima kweli sanifu, kukomesha hili janga,
Sio siku ya wajinga, ya wazushi na warongo !
Kwa urongo kurudufu, Jahanamu utatinga,
Hamna ndanimwe ufu, wala uhai wa anga,
Ikabu zake lufufu, shadidi zitakusonga,
Sio siku ya wajinga, ya wazushi na warongo !
Haya shime kaka Sefu, nawe dada Mwanamanga,
Leo sote kwa insafu, tujitanibu kukenga,
Tujenge usadikifu, kwa kweli kutwa kulonga,
Sio siku ya wajinga, ya wazushi na warongo!
Tuache ukengeufu, wa puya kutwa kulonga,
Ukweli tuusharifu, akhera kwetu ni kinga,
Kaditama kualifu, Abuu natia nanga,
Sio siku ya wajinga, ya wazushi na warongo!
ABUU NYAMKOMOGI

SIKU YA USHAIRI DUNIANI


(Maskini Ushairi!)

Tama nimejishikia, insi nawaajabia,


Fani yazidi fifia, wao washerehekea,
Dhamira nafikiria, yao sijaing'amua,
Maskini ushairi, fani inayojifia!
Sifahamu kwa dunia, wengine watatongoa,
Nilonge kwa Tanzania, Bara nilikokulia,
Kwa lengo la kuzindua, wala si la kubeua,
Maskini ushairi, fani inayojifia!
Hali ninojionea, kwa ya kwangu mizania,
Katu si ya kuridhia, wala kutafakharia,
Kipi cha kujivunia, Ushairi Tanzania?
Maskini ushairi, fani inayojifia!
Weledi umepungua, wa nudhumu Tanzania,
Utunzi umekomea, kurasa za nadharia,
Si kama ilivyokua, zile zama azalia,
Maskini ushairi, fani inayojifia!
UKUTA naulizia, i hai imejifia?
Kama hai kaulia, basi mfu fiilia!
Nani wa kusimamia, washairi Tanzania?
Maskini ushairi, fani inayojifia!
Wito ninawatolea, wote walosherekea,
Haya kuyazingatia, pasipo kuyabeua,
Mwisho beti nakomea, sita sitaendelea,
Maskini ushairi, fani inayojifia!
ABUU NYAMKOMOGI

ANNUUR NEW.indd 14

JAMADUL AAKHER 1437, IJUMAA APRILI 1-7, 2016

Athari ya mawaidha mazuri katika


kubadilisha mwenendo wa jamii

Wameivika wasifu, eti siku ya wajinga,


Wallahi si yake kufu, kwalo mimi nawapinga,
U mwingi udanganyifu, katu wala si ujinga,
Sio siku ya wajinga, ya wazushi na warongo !
Kwa tumbi udanganyifu, ndanimwe 'sijejiunga,
Ebu basi jikalifu, kutogeuka mshenga,
Kwa kupamba upotofu, kadhalika na ujinga,
Sio siku ya wajinga, ya wazushi na warongo !

AN-NUUR

Na Sheikh Kamal
Ahmed Hassan
AMESEMA Mwenyezi
Mungu mtukufu Ita
watu katika dini ya
Mola wako mlezi kwa
hekima na mawaidha
mazuri na jadiliana
nao kwa yale yaliyo
mema Zaidi.
Amesema Imamu
Kurtubi katika
tafsiri Mawaidha
na maneno mazuri
ambayo ameyaweka
Mwenyezi Mungu
kuwa ni hoja kwao
katika kitabu chake.
Na amesema Ibnu
Kayim /mawaidha
mazuri ni kuamrisha
mema na kukataza
mabaya kwa matumaini
na kwa utisho na
kwa umuhimu wa
mawaidha mazuri .
Ameweka mlango
mzima Imamu Bukhari
katika sahihi yake
akasema, hakua Mtume
(s.a.w) akiwavamia
watu au kuwarefushia
mawaidha ili
wasikimbie na
kuondoka.
Juu ya mawaidha
ya Mtume (s.a.w)
kwa masahaba ili
kubadilisha mwenendo,
imeelezwa kutoka kwa
Abdilahi Bin Masud
amesema, amesema
mtu mmoja ewe
Mtume wa Mwenyezi
Mungu mimi siachi,
kuwa ninaiwahi
swala kwa namna
anavyorefusha fulani
sijapatapo kumuona
Mtume (s.a.w) akitoa
mawaidha makali kwa
hasira kuliko siku hiyo,
na akasema enyi Watu

hakika mnakimbiza
watu misikitini, basi
anayeswalisha watu,
basi na afifishe kwani
wapo miongoni mwao
wagonjwa na madhaifu
na wenye haja.
Hekima, mjadala
kwa njia nzuri ni
miongoni mwa
vitu vya lazima. Ni
lazima pia kuwa
mpole, kutumia kauli
laini na kuwapenda
watu. Hebu tazama
mfano huu ulio hai
katika kubadilishwa
mwenendo. Kuna
kijana mmoja alikuja
kwa Mtume (s.a.w)
akasema ewe Mtume
wa Mwenyezi Mungu
niruhusu mimi
kuzini, watu wakapiga
mayoe.
Mtume (s.a.w)
akasema nisogezeeni
kwangu, wakamsogeza

hadi akakaa mbele


ya Mtume (s.a.w)
akasema, jee
unapenda kuziniwa
mama yako akasema
hapana. akasema
na watu hawapendi
kuziniwa mama zao,
akasema jee unapenda
kuziniwa binti yako?
Akasema hapana, vile
vile watu hawapendi
kuziniwa mabinti zao.
Akasema je unapenda
kuziniwa dada yako
? Akasema hapana.
Akasema na watu
hawapendi kuziniwa
dada zao. akaweka
Mtume (s.a.w) juu ya
kifua chake akasema:
ewe Mwenyezi Mungu
mfutie madhambi
yake na usafishe moyo
wake, na uhifadhi uchi
wake.
wabilah tawfiq
email : eg_islamic_
center39@yahoo.com

TAASISI YA UKUMBUSHO WA ZAKKA


MOROGORO (TAUZAMO)
NI TAASISI YA KIDINI ILIYOANZISHWA NA
KUSAJILIWA KISHERIA MWAKA 2014 MKOANI
MOROGORO KWA LENGO LA KUIHAMASISHA
JAMII YA WAISLAMU KUIKUMBUKA NA
KUITEKELEZA NGUZO YA TATU YA ZAKKA.
PAMOJA NA HAYO TAUZAMO KUPITIA
UTOAJI ZAKKA INALENGA KUIUNGANISHA
JAMII KUWA KITU KIMOJA, KUFUFUA UCHUMI
WA KIISLAMU ULIOKUFA NA KUIFANYA
QURAN NDIYO MUONGOZO SAHIHI KWA
UMMA.
TAYARI TAUZAMO IMEFANIKIWA KUWA
NA BAYTUL MALL ILIYOKO MTAA WA SIMU
KATIKA KATA YA MJI MPYA MANISPAA
YA MOROGORO PAMOJA NA KUFUNGUA
AKAUNTI KATIKA BANK YA KCB TAWI LA
MOROGORO NAMBA 3301064116.
ILI KUWEZA KUFIKIA MALENGO HAYO
NA MENGINE, TAASISI INAHITAJI UUNGAJI
MKONO KWA HALI NA MALI KUTOKA
KWENYE TAASISI NA VIKUNDI MBALIMBALI.
UNAWEZA KUFIKA OFISINI MAKAO
MAKUU MTAA WA SIMU KATA YA MJI MPYA
MANISPAA YA MOROGORO AU WASILIANA
NASI KWA SIMU NAMBARI 0686240494 AU
0717337919
TANGAZO HILI NI KWA HISANI YA MWENYEKITI WA
TAUZAMO SHEIKH SALEH HUSSEIN SANGA (BWAWANI).

3/30/2016 1:12:37 PM

15
SHUKRANI zote zinamstahikia
Allah (sw). Sala na salamu
zimfikie mtukufu wa daraja,
Masahaba wake na wote
wanaofuata mwenendo wake
mpaka siku ya malipo.
Somo la nne katika mfululizo
wa masomo haya ya Tawhiid,
ni taratibu za kukufurishana,
yaani ni wakati gani Muislamu
ataitikadiwa kuwa ni kafiri.
Somo hili ni muhimu sana kwani
makundi yote yaliyochupa
mipaka na kuanza kugeuka
kuwa ni makundi ya kihalifu
kupitia jina la Kiislamu, yalianza
kupotea katika suala la kumjua
ni nani kafiri na inakuwaje
mpaka unamuitakidi mtu kuwa
ni kafiri.
Kipengele nambari sitini
na saba katika kitabu cha
Imam Tahawy kinasema
hatumuitakidi yeyote katika
watu wa kibla,(yaani wafuasi
wa Muhammad (saw)) kuwa ni
kafiri kwa kufanya madhambi
makubwa, mpaka aitakidi kuwa
hiyo dhambi kubwa ni halali,
pia hatusemi kuwa dhambi
haimdhuru mtu madhali
ameamini.
Huu ndio mtizamo sahihi
wa Kiislamu tofauti na ile ya
makundi mawili, moja likiitwa
Khawarij ambalo lilikuwa na
itikadi kuwa kila Muislamu
anayefanya dhambi kubwa ni
kafiri. Ametoka kabisa katika
Uislamu, na akhera atakaa
milele motoni . Hilo ni Kundi
lililochupa mipaka katika
suala la kukufurishana, wao
waliitakidi kuwa Ali (ra) na
Muawiyya(ra ) na wafuasi wao
wote ni makafiri na waliamini
kila mtu ambaye si Khawarij ni
kafiri. Waliwakataza wafuasi
wao kusema na watu ambao
si Khawarij, kutowaozesha na
kutoolewa na wasio Khawarij.
Baya Zaidi, walihalalisha
kumwaga damu ya kila
asiyekuwa Khawarij kwa vile
waliwaona ni makafiri (lakini
tambua pia kuwa katika
Uislamu hakuna amri wala
hukumu ya kuua makafiri. Mtu
atauliwa kutokana na hukumu
ya kimahakama kutokana na
kosa kulingana na shera ya
Kiislamu.).
Kundi la Muutazila wao
waliamini kuwa dhambi
kubwa inamuweka mfanyaji
baina ya Uislamu na Ukafiri,
haimfanyi awe kafiri kikamilifu
lakini akhera atadumu motoni
milele. Muutazila na Khawarij
walihitilafiana kuhusu mwenye
kufanya dhambi kubwa, duniani
namna yake iko vipi, lakini
walikubaliana kuwa akhera
watadumu milele motoni.
Kundi la Murjia liliamini
kuwa Muislamu hata afanye
dhambi kubwa kiasi gani,
haitomdhuru madhali
ameamini yaani kule kuamini
tu kunamtosha, na imani
haidhuriwi na madhambi hata

ANNUUR NEW.indd 15

Makala

JAMADUL AAKHER 1437, IJUMAA APRILI 1-7, 2016

Tawhiid -4

yawe kiasi gani. Hili ni Kundi


lililochupa mipaka katika suala
hili, kwa kuamini kuwa dhambi
haiathiri imani ya mtu .
Msimamo wa sahihi wa
Uislamu ni kuwa dhambi
inapunguza imani ya mtu na
imani inakuwa kwa kufanya
mambo mema. Huu ndiyo
msimamo wa Uislamu.
Lakini Imam Abuu Hanifa
yeye ana msimamo kuwa
imani haiongezeki, na huu
ni msimamo dhaifu, kwani
aya na hadithi zinaonesha
dhahiri kuwa imani inapungua
kwa madhambi na inakuwa
kwa kufanya mema kama
tutakavyoona mbele inshaallah.
Ama Ulamma aliyetoa fatwa
ya aqida na akijitahidi lakini
akakosea katika fatwa yake,
basi hahesabiwi kuwa ni kafiri
hata kama atakosea. Hii ni kwa
sababu ya hadithi sahihi kuwa
Ulamaa mchamungu akijitahidi
na akakosea, basi atapata jema
moja na akajitahidi na akapatia
basi atapata mema mawili.
Mtu akiwa na itikadi za kikafiri
kwa mfano akawa na itikadi
za makundi ya Muutazila au
Kwawarij lakini hana elimu
na kile anachokiamini, na
inawezekana akawa ndiyo
elimu pekee aliyonayo ,
labda amejitahidi sana lakini
amesomeshwa hivyo, akakulia
hakupata mtu wa kumuelimisha,
basi hawi kafiri, lakini atakuwa
amepotea, ni jukumu la wenye
elimu kumuelimisha na hukumu
yake iko kwa Allah (sw), kwani
wanaadamu hatuwezi kujua
kilicho katika moyo wake.
Jukumu la mlinganiaji ni
kufikisha ujumbe kwa lugha
nzuri, na kushawishi watu
waache ushirikina, lakini
si jukumu lake kuhukumu
watendao maovu na akawatia
motoni, kwa kuwaambia, wewe
utaingia motoni au hutaingia
peponi. Anachotakiwa kusema
ni jambo la ujumla, mfano wenye

AN-NUUR

kumshirikisha Mungu wataingia


motoni, asiseme wewe Juma,
nimekukataza kumshirikisha
Mungu hutaki, utaingia motoni,
au wewe Bakari hutaingia
peponi . Hilo ni kosa kwani
anayejua kwa uhakika nani
ataingia motoni na nani ataingia
peponi ni Allah (sw) peke yake.
Kuna baadhi ya vikundi
hutumia muda mwingi ,
kuwahukumia Waislamu
wenzao moto na wengine
wanaowasema ni watu wa
motoni ni Maulamaa, labda kwa
makosa madogo wanayoyafanya
au kwa kuhitilafiana katika
jambo Fulani. Hiyo ni itikadi
mbaya kinyume na mafundisho
ya Uislamu. Katika hadithi
inayopatikana katika Sahihi
Bukhari 7506 na Sahihi Muslim
2756 iliyosimuliwa na Abuu
Hurayra (ra) ,huyu Bwana
( inasemekana katika bani
Israiyl) aliwaamrisha wanawe
kuwa atakapokufa wamchome
moto , walitupe nusu ya jivu
baharini na nusu yake barani,
ili asijekuadhibiwa. Alifapokufa
na kufufuliwa aliulizwa kwa
nini ukaamrisha hayo akajibu,
kwa sababu ya kukuogopa
Wewe (Allah sw) na Allah (sw)
alimsamehe, kwa sababu ya
khofu yake, pamoja na kwamba
aliamrisha jambo la kikafiri.
Ila hapa tuzingatie kuwa
wapo wale watu ambao Qurani
imewataja wazi kwa majina
kuwa ni makafiri. Mfano
Firauni, Hamana Qaruun Abuu
Jahl Abuu Lahb na wengineo.
Na wale ambao Mtume (saw)
amewataja wazi kuwa ni
watu wa motoni, kwa hadithi
sahihi ambazo Maulamaa
wanakubalina nazo kama Abuu
Talib Ami yake Mtume (saw).
Hata hivyo tufahamu kuwa, hata
huyo Firaun aliyejiita Mungu
Mkuu, mpaka dakika za mwisho
Nabii Mussa anaamrishwa na
Mola wake akampe dawah, tena
amwendee kwa lugha laini. Sio

kumshambulia kuwa wewe


kafiri wa motoni.
Ama kwa yale madhambi
ya jumla yaliyoahidiwa moto
ukiacha shirki, kama zinaa ,
ulevi wizi, dhulma, riba nk
waliyoyafanya haya hukmu
yao anaijua Allah (sw), nani
amuadhibu na nani amsamehe,
watu wasijiingize katika kazi
ya kuhukumu wenzao, kazi hii
aachiwe Allah (sw) mwenyewe
ambaye anajua mambo ya
ghaibu Elimu zetu sisi haziwezi
kujua watu wa motoni wala wa
peponi ila wale ambao Qurani
na sunna imewataja kuwa watu
wa motoni, na wale waliotajwa
wazi na kubashiriwa pepo
kwenye hadithi sahihi.
Ni katika madhambi
makubwa sana kumuambia
Muislamu kuwa ni mtu wa
motoni au kuapa kuwa hatoingia
peponi, au kumwita kafiri wa
kiimani. Amesimulia Abuu
Dhari(ra) kutoka kwa Mtume
(saw) amesema Asimzulie
mtu kumzulia mwenzake
ufasiki, wala asimzulie ukafiri
ila atarejeshewa nao ikiwa yule
aliyemsingizia hanao(SB 6045
SM61).
Imesimuliwa na Jundub
bn Abdillah (ra), amesema
Mtume (saw) Alisema mtu
naapa kwamba Allah (sw)
hamsamehe Fulani, Allah (sw)
akasema nani anayeniapia
kwamba simsamehe Fulani?,
basi mimi nimemsamehe yeye,
na amali zako nimezibatilisha.
(Sahihi Targyb ya Albani 2961).
Amesimulia Abi Dhari (ra)
kwamba amemsikia Mtume
(saw), akisema Anayemwita
mtu kafiri au akasema adui wa
Allah (sw), na yule mtu hayuko
hivyo ila (lile jina) humrejea
mwenyewe.(Malik ST2772).
Sasa hapa watu wanaweza
kuwa na masuali mengi ambayo
yanahitaji kujibiwa, kwanza
jee ni hukumu gani ya aya
zinazowaita wale wasihukumu
kwa kitabu kuwa ni makafiri?.
Hoja hii mara nyingi hutolewa
na wale ambao wanaitwa
Khilafa, kuwa hawa Waislamu
ambao hawahukumu kwa kitabu
wao ni makafiri. Inshaallah
tutaeleza hoja hiyo kwa kirefu
lakini kuna ukafiri aina mbili
unapotajwa kwenye Qurani
na sunna . Ukafiri wa kiimani
yaani kutoka kwenye Uislamu
na ukafiri wa vitendo yaani mtu
kuwa na vitendo vya kikafiri,
ukafiri huu haumtoi Muislamu
katika imani ila anakuwa
muovu ,hapa amepewa jina
la kafiri kwa sababu kitendo
hicho alichikifanya hufanywa na
makafiri.
Hapa pia tunatoa jawabu
kwa wale wanaozitumia hadithi
zilizotaja ukafiri, kuwa ukafiri
unaokusudiwa ni wa vitendo
si wa imani. Na kila hadithi
iliyotajwa ina maelezo yake
na makubaliano ya Maulamaa
kuhusu matumizi ya hadithi
hiyo na aya pia.
Wabbillahi tawfiiq.

3/30/2016 1:12:37 PM

16

Makala

AN-NUUR

JAMADUL AAKHER 1437, IJUMAA APRILI 1-7, 2016

Kitendawili cha uhuru na madaraka 2

Na Mwinjilisti Kamara Kusupa


(0786 311 422).

KUNA msomaji mmoja


aliyenitumia SMS hii hukumtaja
Nyerere wala sijaona uwiano kati
ya yaliyoandikwa akimaanisha
contents na kichwa cha makala.
Kusupa inakuuma nini Mohamed
Said anaposema Waislamu
ndio waliopigania uhuru wa
Tanganyika?
Nimeinukuu SMS hiyo kwa nia
njema, bado naikumbuka kauli ya
Mohamed Said aliposema, tatizo
la historia ya Tanzania inaanza na
Nyerere na inaishia na Nyerere.
Hatari ninayoona Mohamed Said
anaweza kuendeleza tatizo lilelile,
naye akaanza na Nyerere, akaishia
na Nyerere ila kwa namna nyingine
ya kukanusha. Kwa nyaraka za
zamani alizo nazo atathibitisha
Nyerere siyo mwanzilishi wa
harakati za uhuru, Nyerere
aliikuta TAA, Nyerere hakuijenga
TANU ila TANU ilijengwa na
Waislamu. Atahitimisha kuwa
Nyerere hakumngoa mkoloni bali
mkoloni alingoka kwa juhudi za
Waislamu ambao mwisho Nyerere
kama mtawala hakuwatendea haki
Waislamu waliomsaidia.
Historia hiyo itakuwa na pengo,
kizazi kipya kikiaminishwa katika
historia yenye pengo hakitanufaika
ipasavyo, kwasababu uzuri na
faida ya historia katika maisha
ya binaadamu unaeleweka,
kwamba historia inamfunulia
mtu ukweli unaomwezesha
kujitambua alikotoka hadi alipo
na jinsi alivyofika. Mtu anayejua
alikotoka na jinsi alivyofika alipo,
atakuwa jasiri kupanga/kuamua
aelekee wapi kwa manufaa ya
hao watakaoishi baada yake. Mtu
asiyejua atokako hawezi kujua
amefikaje hapo alipo, hatakuwa na
uhakika wa kule aendako.
Waafrika wamefanya kosa
kukubali kuandikiwa historia
yao na Mzungu, wamefanya
kosa zaidi kuikubali historia
hiyo ya kuandikiwa kwamba
ndiyo iwafundishe. Kuna mazuri
mengi ya Waafrika yaliyofichwa
kwa makusudi na Wazungu pia
kuna mabaya mengi ya Wazungu
yasiyoelezwa, Mzungu amefanya
hivyo kwa manufaa yake.
Waafrika wakipuuza historia yao
watabaki watumwa wa kudumu
kwasababu hata kesho yao au
hatima yao itabidi iamuliwe na hao
wanaowajua wametoka wapi, wako
wapi, na wamefikaje hapo walipo.
Wanaowajua ndio watawapangia
Waafrika wasiojua waelekee wapi,
kwasababu wenyewe Waafrika
hawajui wamefikaje hapo walipo
wala hawajui watokeje.
Kwanini nasema kalamu ya
Mohamed Said inachora nusu
ya ukweli na kuacha pengo?
Kwanza haelezi kwanini Waislamu
waliikataa AMNUT yaani
All Muslims National Union of
Tanganyika. Pili haelezi ni kitu gani
kilichotokea ama kilichofanyika
hadi waliopigania uhuru wasipewe
uhuru kinyume chake waishie

ANNUUR NEW.indd 16

kunyimwa haki zao!


Mimi naamini katika uhalisia
nawashawishi walio makini
tuukubali uhalisia ili uwe mwanzo
wa safari mpya kuielekea na
baadaye kuifikia Tanzania
tunayoitaka.
Haiwezekani waliopigania uhuru
wasiwe huru lazima liibuke swali
litakalomfuata msemaji sawa na
kivuli kinavyomfuata anayethubutu
kukikimbia kivuli chake. Uhuru
alipewa nani? Je, watoaji waliamini
kuwa wanatoa uhuru?
Tukiifikia nukta hii, tukubali
kwamba ilifanyika biashara ya
kuuziana mbuzi kwenye gunia,
mchinjaji akikuta gunia lina nyoka
bado walioamini watamdai nyama
ya mbuzi hasa ikitokea wawe
hawakufika machinjioni.
Bado nasisitiza kilichotolewa siyo
uhuru, maana uhuru una sifa zake,
mpigania uhuru wa Kenya Jaramogi
Oginga Odinga kwa ujasiri mkuu
akaandika kitabu not yet uhuru
akimaanisha huu siyo uhuru
tulioupigania.
Nakiita kitendawili cha
uhuru na madaraka lakini
kadri tutakavyozama tutajikuta
tunajadili kiini macho cha uhuru,
kitendawili ni fumbo linaloweza
kupatiwa jawabu kitateguliwa
lakini kiini macho kama yalivyo
mazingaombwe, hakina jibu
hadi hapo mtu atakapoukubali
uhalisia. Kwamba anachoona
ni udanganyifu, mkweli hawezi
kuburudishwa na wafanya
mazingaombwe.
Turudi nyuma hadi usiku wa
tarehe 09 Desemba mwaka 1961
unaoaminika Tanganyika ilipata
uhuru, mzee mmoja aliyekuwako
(naamini wengi walikuwako na
bado wangali hai ingawaje hawataki
kusema). Mzee anasema siku hiyo
kwenye High table walikaa watu
sita The Dwarf of Edinburg Gavana
Richard Turnball, Chief Minister
Julius Nyerere, Kadinali Laurean
Lugambwa na Mashehe wawili
asiowakumbuka majina yao.
Gavana alitoa hotuba akizionya
nchi za Kiafrika zinazopata uhuru
kwamba zisiitegemee Marekani
kutatua matatizo yao kiuchumi,
baadaye askari akaenda kuteremsha
bendera ya Union Jack na
kupandisha bendera ya TANU.
Gavana akakabidhiwa
bendera yake naye akamkabidhi
Nyerere kitabu yaani katiba ya
Tanganyika ambayo haikuandikwa
(haikutungwa) na Watanganyika,
katiba ilitungwa/iliandikwa na
wenyewe wakoloni, hapo shughuli
ya makabidhiano ikakamilika.
Je, hapo uhuru uko wapi?
Kiuhalisia Nyerere alikabidhiwa
madaraka ya kuitawala Tanganyika
badala ya Gavana yaani atawale
kwa kutumia katiba yao wakoloni.
Wakoloni waliondoka kimwili lakini
masalia waliyoyaacha yalitosha
kuulinda to maintain the colonial
status qo. Katiba ya kikoloni, sheria
za kikoloni, watendaji wa kikoloni,
vyombo vya dola yaani Jeshi
kuu au Tanganyika Rifles Police,
Magereza, Mahakama na Civil
Services vyote vilikuwa vya kikoloni.
Lugha iliyotumika kufundishia

HAYATI Julius Kambarage Nyerere


mashuleni na vyuoni ilikuwa ya
mkoloni. Masomo yaliyofundishwa
au syllabus ilikuwa ya kikoloni
na ilitimiza malengo ya kikoloni,
utendaji na utumishi viliendelea
kutimiza malengo yale yale
aliyoasisi mkoloni. Je, uhuru
ungeonekana kwa sura ipi katika
uendeshaji wa dola?
Tuchukulie mfano tu
kwamba chini ya mazingira
niliyoyaorodhesha juu, Wazungu
wangekuwa wamekabidhi
madaraka kwa Chief Minister
Sykes na watendaji wote
wangekuwa waumini wa dini
ya Kiislamu, kama ilivyokuwa
kwa nchi jirani ya Zanzibar na
nchi za Nigeria na Somalia. Je,
Waislamu hao ambao wangekuwa
wamechukua nafasi za wakoloni
wangeiendesha Tanganyika tofauti
na nchi zingine zilizokuwa kwenye
Jumuia ya madola?
Jibu lake ni la kufikirika, hata
hivyo tukiziangalia nchi mbili
Zanzibar na hiyo iliyoitwa British
Somaliland iliyojumuisha Eritrea,
Djibout na Ogaden haitupi ugumu
kubashiri, maana Zanzibar yalitokea
manunguniko ya kudhulumiana
hadi kusababisha mauaji ya kutisha
1959, hadi leo manunguniko
kuhusu dhuluma yangalipo.
Somalia iligawanyika vipande
hadi leo haijatulia, hali inayoacha
swali na changamoto kubwa
inakuwaje Mwislamu kuendesha
dhuluma dhidi ya Mwislamu
mwenzake? Ndiyo maana kwenye
kitabu changu cha Peace and
Conflicts in Africa namaliza na
mada ya a way out. Hayo ni
mapendekezo jinsi gani dola za
Kiafrika zinaweza kujinasua kwa
kutoka kwenye hali ya machafuko
hadi kwenye amani.
Ni vizuri uandishi ukatoa
hitimisho chanya kuwashauri
wahanga wafanye nini ili kutoka
kwenye hali mbaya waliyo nayo
kuelekea kwenye neema.
Nirudi kwenye uhuru wa
bendera, hili lilikuwa suala gumu
kwa kila aliyekalia kiti cha Urais,
katika kitabu cha HII NDIYO
TANZANIA TUNAYOITAKA

nimeujadili Urais kiundani


kwenye somo la Urais kiti cha
moto. Ugumu uliletwa na mengi
mojawapo likiwa jukumu la Urais
kulinda status quo waliyoiacha
wakoloni.
Hiyo status qo haikueleweka
kwa Waafrika waliokuwa na
matarajio makubwa na uhuru kama
ambavyo bendera haikueleweka
kwa Mutwa Mkwawa, nitadokeza
kifupi mwishoni mwa makala
kisa cha Mkwawa na bendera ya
Wadachi.
Nchi jirani ya Kenya baada
ya kuondoka mkoloni baadhi
ya Wakenya waliona kama
wametoka Waingereza na badaye
Wakikuyu wanawatawala Wakenya
wengine katika jina la uhuru
wakanungunika. Hapa kwetu
Tanganyika baadhi wakaona
kama wametoka Waingereza
wamewaachia madaraka ndugu
zao Wakristo kwakuwa ndio
waliosomeshwa na kuandaliwa
kutawala, wakanungunika. Kwa
Nyerere ukabila haukuonekana
wala kunungunikiwa kwasababu
alitoka kwenye kabila dogo la
Wazanaki, ambalo halikuwa na
wasomi wengi kama Wachaga,
Wahaya na Wanyakyusa,
lisingeweza kuwa dominant tribe.
Lakini kama ingetokea
Tanganyika kutawaliwa na Rais
Mchaga, usomi wa Wachaga na bidii
yao ya kutafuta mali vingefunikwa
na kabila lao, angeonekana Rais
Mchaga ndiye anayewawezesha
kiuchumi Wachaga wenzake
na pia anawapendelea kushika
nafasi nyingi za ajira. Kwahiyo
manunguniko yasingekuwa udini
bali ukabila kama ilivyo kwenye
nchi jirani za Kenya, Burundi na
Rwanda.
Hii inatokana na kwamba
enzi za ukoloni waliotawaliwa
waliaminishwa kitu hewa kwamba
wao ni Waafrika wakati hakuna
kabila linaloitwa Waafrika. Mkoloni
alipotawala wakati anatukana
au kumnyanyasa mtu Mweusi
hakumwita wee Mkikuyu! wee
Mjaluo! Mtutsi, Mhutu, Mhaya,
Msukuma, au Mngoni, alimuita wee
Mwafrika!
Aliwafanya wahanga waungane
kama Waafrika ili kutetea haki zao
ama kudai uhuru wao, ndio maana
mikusanyiko yao katika vyama
ilibeba neno African TAA, TANU,
KANU, ANC, PAC n.k
Baada ya Mzungu kurudi
Ulaya ndipo Waafrika walipoanza
kutazamana katika uhalisia wao na
kujingamua kwamba kumbe wao
siyo Waafrika bali ni mkusanyiko
wa makabila tofauti na dini
tofauti wakaanza kunyoosheana
vidole, vazi la ukoloni lililokuwa
limewafunika walikuwa wamelivua
na kubaki watupu.
Kuhusu madaraka na mamlaka
(power and authority) ukweli
ni kwamba mkoloni ndiye
aliyezianzisha dola za Kiafrika
Inaendelea Uk. 18

3/30/2016 1:12:38 PM

17
Na Abuu Nyamkomogi
HAWAKUNIPIGA kisu wala
fimbo. Walinipiga kwa mabuti,
mateke. Wakanipiga sana
vibao (makofi), kwa hiyo uso
wangu ulikuwa umevimba.
Walinipiga ngumi, mateke,
popote pale wananipiga. Tarehe
18 Machi, Ijumaa mwaka 2016,
ni miongoni mwa siku ambazo
sitazisahau za mateso kutokana
na uandishi wa habari na
utetezi wa haki za binadamu.
Maneno hayo, yaliyotamkwa
na mwandishi wa habari na
ripota jasiri na mahiri Bi.
Salma Said wakati akihojiwa
na Idhaa ya Kiswahili ya
Sauti ya Ujerumani-DW kama
yalivyonukuliwa katika toleo
la gazeti hili la juma lililopita
chini ya habari kuu iliyobeba
anwani 'Sitaisahau tarehe
18-Salma', ndio yaliyonisukuma
kuteua anuwani ya makala
haya kama isomekavyo hapo
juu. Nitafafanua sababu ya
msukumo wa uteuzi huo kadri
tunavyoendelea na upembuzi
wetu katika makala haya huko
mbele inshaallah.
Nimetumia ibara ya 'Pole
na Hongera' katika anuwani
ya makala yangu haya kwa
wakati mmoja, si kwa bahati
mbaya bali kwa makusudi, kwa
malengo makuu mawili. Mosi,
nimetumia neno 'Pole' kwa
lengo la kumfariji mwandishi
husika kutokana na mazonge
au masaibu yaliyomsibu baada
ya kutekwa nyara kwa siku
mbili mtawalia, kadhia ambayo
ilijiri katika majuma mawili
yaliyopita. Pili, nimetumia neno
'Hongera' kwa madhumuni ya
kumshajiisha au kumtia moyo
mwandishi asikate tamaa na
badala yake aendelee na harakati
zake za mapambano ya kutetea
haki na uadilifu pamoja na
kupinga dhulma na uonevu,
vinavyoonekana kukithiri na
kuzidi kukita mizizi katika jamii,
kwa kutumia kalamu yake isiyo
na woga wala hofu dhidi ya
madhalimu wasiopenda kuona
haki na uadilifu vikitamalaki
katika jamii.
Aidha, sababu zilizonisukuma
kuteua anwani ya makala
haya ni mbili. Mosi, ni kipigo
kikali, alichokumbana nacho
mwandishi husika kipindi
alipokuwa ametekwa nyara
kama alivyosimulia katika
mahojiano yake na Idhaa ya
Kiswahili ya Sauti ya Ujerumani;
kipigo ambacho kiliziathiri
baadhi ya sehemu za viungo
vyake vya mwili ikiwemo uso
ambao ulivimba kutokana na
kipigo hicho, na hapa ndipo
nalazimika kusema ''Pole dada
Salma''.
Pili, ni utambuzi wa
mwandishi husika juu sababu
inayoonekana kupelekea hali
hiyo ambayo, si nyingine
isipokuwa, ni uandishi wake wa

ANNUUR NEW.indd 17

MAKALA

AN-NUUR

JAMADUL AAKHER 1437, IJUMAA APRILI 1-7, 2016

Pole na hongera Salma Said!


habari na utetezi wake wa haki
za binadamu. Kwa muktadha
huu, nalazimika kutoa kongole
kwa mwandishi huyu kwa
kusema ''Hongera dada Salma''.
Sababu aliyoidokeza, japo
si moja kwa moja, katika
mahojiano yake na Idhaa ya
Kiswahili ya Sauti ya Ujerumani
yumkini ikawa kweli kutokana
na ushahidi wa baadhi ya
maandishi yake yaliyojikita
katika ufichuzi wa dhulma na
uonevu kwa upande mmoja
pamoja na utetezi wa haki
za binadamu kwa upande
mwingine. Nakumbuka katika
mojawapo ya makala yake yenye
anwani 'Karume Shujaa' katika
toleo nambari 1214 la gazeti hili
la Ijumaa ya tarehe 29.01.2016
alitanabahisha kuhusiana na
yanayoweza kumsibu kutokana
na maudhui ya makala yale,
na akanena hivi na hapa
namnukuu:
''Naamini maandishi yangu
yatawaathiri wengi pamoja
na mimi mwenyewe kwa
kila hali kiusalama, kiafya,
na hata kisaikolojia. Ni kwa
sababu najaribu kuvuta hisia
za miaka 15 iliyopita ambapo
makubwa yalitokea katika nchi
yetu ya majonzi na huzuni
ya unyama uliokithiri. Ni
maumivu yasiopona. Ni uonevu
usiosahaulika. Na ukatili
usiosameheka.''
Kwa kifupi, maudhui ya
makala yale yalikuwa yakijaribu
kuitanabahisha jamii ya
Wazanzibar na viongozi wake
juu ya kadhia ya kusikitisha
iliyojiri visiwani Zanzibar
kutokana na harakati za kisiasa
mnamo 2001 na kubaini madhila
kadhaa yaliyowasibu baadhi ya
wananchi wa visiwani humo
na athari zake kwao na kwa
taifa na hivyo kutoa indhari
kwa wahusika ili yaliyojiri
kipindi hicho yasije kujirudia
katika uchaguzi wa marudio
uliofanyika visiwani humo hivi
karibuni.
Baadhi ya maelezo katika ile
nukuu niliyoirejelea hapo juu
kutoka katika makala yale ya Bi.
Salma yanatoa ishara kwamba
kazi ya kufichua maovu na
hasa yanayozihusu tawala za
kidhalimu ina gharama zake.
Miongoni mwazo ni pamoja
na athari za kiusalama na
kiafya zinazoweza kumfika
au kumkabili mtu aliyeamua
kubeba jukumu la kutetea haki
na kupinga dhulma katika jamii
japo kwa kutumia kalamu tu,
achilia mbali silaha!
Ukweli huo unaweza
kuakisiwa na mazonge
yaliyomkabili mwandishi huyo
hivi karibuni na kumfanya
achukue tahadhari kwa kuelekea

jijini Dar es Salaam akitokea


Zanzibar baada ya kupokea
vitisho kadha wa kadha na
baadae kutekwa nyara katika
mazingira ya kutatanisha
alipowasili jijini Dar es Salaam
na hatimaye kupata mateso
kama alivyosimulia katika
mahojiano yake na Idhaa ya
Kiswahili ya Sauti ya Ujerumani.
Usalama wake ulionekana
kuwa hatarini kwa kuendelea
kwake kuwa visiwani Zanzibar
kutokana na vitisho vya
mara kwa mara vilivyokuwa
vikimkabili, hususan katika
kipindi cha kuelekea uchaguzi
mkuu tata wa marudio
uliofanyika hivi karibuni
visiwani humo, kutokana na
kazi yake ya uandishi wa habari.
Kwa muktadha huo, Bi. Salma
akaamua kuelekea jijini Dar es
Salaam ambako nako usalama
wake ukagubikwa na hatari
zaidi baada ya kutekwa na watu
wasiojulikana na kuzuiliwa
kusikojulikana hali ambayo
ilisababisha kwa namna moja
au nyingine kuibua taharuki ya
kiusalama si tu miongoni mwa
wanahabari wenzie, bali pia
miongoni mwa watetezi wa haki
za binadamu juu ya hatma ya
usalama wa maisha yake jambo
ambalo likapelekea viongozi wa
asasi hizo kushirikiana pamoja
baada ya kuguswa na kadhia
iliyomsibu Bi. Salma na kutoa
tamko la kulaani hali hiyo na
hatimaye kutoa siku mbili
kwa Jeshi la Polisi kuhakikisha
mwandishi huyo anapatikana
kwa kuwa jeshi hilo ndilo lenye
dhima kisheria ya kusimamia,
kuhifadhi pamoja na kulinda
usalama wa ndani wa raia na
mali zao.
Aidha, mwandishi huyu
anaelekea kuathiriwa afya yake
kutokana na kipigo alichopokea
na mateso aliyoyapata kutoka
kwa watekaji wake kutokana
na mashambulizi ya ngumi,
makofi pamoja mateke
aliyokuwa akipigwa sehemu
mbalimbali za mwili wake kiasi
cha kumsababishia kuvimba
uso kama alivyoeleza katika
mahojiano yake na Idhaa ya
Kiswahili ya Sauti ya Ujerumani.
Kwa muhtasari, hizo ndizo
baadhi ya athari za kiusalama na
kiafya zilizomsibu mwandishi
jasiri na ripota mahiri wa
Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya
Ujerumani Bi. Salma Saidi wa
visiwani Zanzibar kutokana na
kazi yake ya uandishi wa habari
na utetezi wake wa haki za
binadamu. Kwa muktadha huu,
nikariri tena hapa kauli yangu ya
faraja kwa mwandishi na ripota
huyu ''Pole dada Salma kwa yote
yaliyokusibu''.
Pamoja na kutoa pole na

Bi. Salma Said


hongera kwa Bi. Salma, kama
nilivyodokeza mwanzoni mwa
makala haya, kuna funzo moja
kubwa tunalolipata, kutokana
na mazonge yaliyomkuta tangu
alipokuwa Zanzibar na hata
alipofika Dar es Salaam, nalo
ni kuwa mapambano dhidi ya
dhulma yana gharama zake
ambazo watetezi na wapigania
haki na wapinga dhulma pamoja
na wafichua maovu katika jamii
yetu wanapaswa kuzitambua,
katika utekelezaji wa kazi hii
nzito na yenye kuhitaji ujasiri
na subira ya hali ya juu, ili
wasitamauke/wasikate tamaa
na wawe na msimamo thabiti
hadi dakika ya mwisho ya
mapambano yao. Baadhi ya
gharama tunazoweza kuzibaini
kupitia kadhia ya dada Salma
ni pamoja na vitisho na vipigo,
kutoka kwa maadui wa haki
na ukweli, ambavyo vinaweza
kumkabili mhusika kama
sehemu ya kutaka kupunguza
kasi yake katika kufichua maovu
na kutetea haki na uadilifu
katika jamii.
Kwa mhusika kutotambua
uwapo wa suala hilo la
gharama, katika uendeshaji
wa harakati na utekelezaji
wa kazi hii ya mapambano
baina ya haki na dhulma, ni
rahisi sana kwa mpambanaji
wa aina hiyo kuweza kukata
tamaa na kuvunjika moyo na
hatimaye kujiondoa katika
medani ya mapambano pindi
akumbanapo na changamoto
mithili ya zilizomkabili Bi.
Salma Said wakati wa mchakato
wa kutekeleza jukumu lake la
kiuanahabari la kuihabarisha
jamii kuhusiana na mambo
chanya na/au hasi yanayojiri
katika jamii, lakini maamuzi
ya kuona haki inatamalaki na
dhulma inatoweka katika jamii
husika yanabaki mikononi
mwa jamii yenyewe/wanajamii
wenyewe.

3/30/2016 1:12:40 PM

18

Makala

AN-NUUR

JAMADUL AAKHER 1437, IJUMAA APRILI 1-7, 2016

Kwa nini tufe njaa na walituahidi Dubai?

Na Makame wa Makame Silima

NAAAM Uchaguzi wa
marejeo wa Zanzibar Machi
20 umemaliza kwa amani
na woga. Mungu ni mwema
sana kwa kuwapa watu wake
Wazanzibari moyo wa subra
wa kuelewa kuwa Zanzibar
na amani yao ni jambo la
kwanza kuliko chochote.
Wazanzibari walioshiriki
Uchaguzi wametimiza haki
yao ya Kidemokrasia na wale
waliokuwa hawakushiriki,
pia wametimiza haki yao ya
Kidemokrasia pia.
Kwa mujibu wa sheria ya
sasa ya Zanzibar, masuala
ya kupiga au kutopiga kura
yanabaki ni hiari na maamuzi
ya mtu binafsi. Nawapongeza
wote wale ambao walibaki
majumbani kwao kwa Amani
na Utulivu mkubwa na wale
waliokwenda kupiga kura
kwa Amani na Woga mkubwa.
Nasema woga kwa mazingira
yaliyotokea kuelekea uchaguzi
wenyewe wa visa kadhaa
vyenye sura ya uvunjifu wa
amani yetu adhimu. Waliotoka
kupiga kura wamechukua
ujasiri mkubwa zaidi kuliko
wale ambao hawakwenda na
wale ambao hawakwenda
wamechukua busara kubwa
kubaki majumbani kwa usalama
na hivyo kupelekea kutokuwa
na tukio lolote la uvunjifu wa
amani siku ya Uchaguzi Machi
20.
Makundi haya yote imani na
matarajio yao kubwa ni kutimia
matakwa yao na kuondokana
na hali duni ya maisha katika
Nyanja zote Elimu, Afya,
Uchumi, na Michezo. Dkt
Shein ametangazwa mshindi
na kuapishwa Machi 24 kuwa
Rasi wa Zanzibar kwa miaka
mitano ijayo. Ingawa Uchaguzi
haukuwa na Kampeni lakini
kwa vile ni merejeo, basi
wananchi waliopiga kura
na kumchagua Dkt Shein
walikuwa wanaingia vituo
vya kupigia kura na mwangwi
wa sauti ya ahadi zake za
kuboresha maisha na kubwa
haswa kugeuza Zanzibar
kuwa Dubai ya Afrika na
wale waliobaki majumbani
waliitamani Zanzibar kuwa
Singapore.
Yupo alieshinda na kubeba
dhamana ya kuongoza nchi
nae si mwengine ni Dkt Shein.
Mantiki ya kuwa Zanzibar
kuwa Dubai ya Afrika
wananchi wanaikimbuka na
wanahitaji iwekwe kwenye
vitendo na ionekane.
Baada ya kutangazwa kwa
matokeo na kumpa Dkt Shein
dhamana ya uongozi kwa mara

ANNUUR NEW.indd 18

MJI wa Dubai
ya pili tumeshuhudia na kusikia
Marekani na washirika wote wa
Jumuiya ya Ulaya wakitoa tamko
ambalo linaashiria kutokuwa
tayari kutoa ushirikiano na
Serikali mpya ya awamu ya
pili ya Dkt Shein. Na wao
kuhimiza tena majadiliano baina
ya pande zote katika kuleta
demokrasia inayoshirikisha
pande zote. Kilichonishtusha
ni kusikia kauli mbili kutoka
kwa mawaziri waandamizi wa
serikali na ambao kwa kiasi
kikubwa wanatarajiwa kurudi
tena kwenye uongozi. Mh
Mohammed Aboud Zanzibar
ni nchi huru na itaendelea kuwa
huru. Tuko tayari kupokea
misaada inayozingatia utu
na heshima kwa Zanzibar na
wananchi wake kinyume cha
hivyo tuko tayari kufa njaa .
Na Mh Omar Yussuf kwa
upande wake amesema Zanzibar
inategemea 20% mpaka 28%
kama msaada wa kibajeti na pia
mikopo kutoka Mabenki ya Nje
na ya kimataifa ili kuikamilisha
kila mwaka katika utekelezaji
wa miradi mbalimbali ya
maendeleo. Mh Omar Yusuf
ambae aliwahi kuwa Naibu
Waziri wa Fedha amesema
wanategemea kuongezeka
watalii kwa mwaka unaofuata
na pia kuweza kupunguza safari
za nje kama afanyavyo Rais
Magufuli na pia wagonjwa wote
kutibiwa hapa kwa kuweka
program maalum ya kuleta
madaktari.
Kwa kauli hizi za kuwa tuko
tayari kufa njaa nimeshtushwa
sana na kuanza kuhisi
Serikali hii mpya ya Dkt Shein
imeanza kuwasaliti wananchi
wake na hususan wafuasi
wake waliotegemea Dubai
ya Afrika. Matumaini yao
yameanza kwenda harijojo.
Kwani mipango ya kutengeneza
Zanzibar kuwa Dubai ya
Afrika ilitegemea mfadhili
gani?. Kwa kiwango gani na Je
Dubai yetu tulotaka kuijenga

ina uhusiano gani na maneno


ya Marekani au Ulaya mpaka
sisi tushindwe kuitengeneza
wenyewe? Je, Dubai ipi yenye
njaa ni hiyo ya UAE ama hii ya
Jangombe na Kiboje?
Kwa mbali zaidi najiuliza, hii
njaa hakuifafanua vizuri itaanzia
wapi huko juu kwa viongozi
kwa maana ya mawaziri au kwa
Vuai wa Umbuji, Makame wa
Tumbatu, Silima wa Nungwi au
Kombo wa Micheweni?.Ikiwa
hiyo aliyosema itachukua dhana
ya sharti za Ubaharia kuwa
Awe wa mwisho au Haokoki

yeye mpaka abiria wote kwenye


chombo wameokoka, basi tuko
tayari kufa nayo. Kwa maana
itaanzia kwao na wafe wao
kwanza kabla ya mwananchi
yeyote wa kawaida kufa .
Napenda kuwasihi viongozi
wetu wa Zanzibar kuwa uongozi
ni dhamana na kila kiongozi
ni mchunga na ataulizwa kwa
kile alichokuwa anachunga.
Wasimamie ahadi na kauli
zao kwa vitendo ili Dubai ya
Afrika tuikute imetia nanga
2021.
Kuna nchi nyingi kwa mifano
duniani za mfano wetu Kama
Cuba na Vitnam zimepiga
hatua zenyewe na ndani ya
vikwazo vizito na vita vya ndani
kutoka Marekani na Ulaya na
wamefanikiwa kusimama na
sasa ni miongoni mwa nchi
zenye uchumi wa kati. Tusitafute
visingizio vya kukosa misaada
ndio tufe njaa hapana ,Serikali
ilopewa dhamana ni wajibu
wake na si wajibu wa wafadhili
ama wahisani kuleta maendeleo.
Huu ni mwaka wa zaidi ya 50
tuko huru na tunaamua mambo
yetu ilipaswa Maji, Elimu, Afya
na Umeme ni vitu ambavyo
mwananchi haaamki akawaza.
Seuze hii njaa ambayo mshaanza
kututajia.

Kitendawili cha uhuru na madaraka 2


Inatoka Uk. 16

yaani Afrika iliyokoloniwa tofauti


na Afrika ya akina Mutwa Mkwawa,
Mangi Meli na wengineo.
Waingereza, Wafaransa na
Wabeligi wasingeacha mamlaka na
madaraka waliyoyaasisi kwa watu
wasiowaamini, bali walikabidhi kwa
mawakala wao na walihakikisha

kila wakala anatawala ili kwanza


kutimiza malengo yao na pili
kulinda (kuhami) maslahi
yao, mtawala aliyethubutu
kwenda kinyume aliuawa ama
alipinduliwa kabla hajawaletea
madhara.
Wanaodhani walipigania
uhuru wa Tanganyika
watafakari mara mbili ni uhuru
gani huo uliotolewa kama
zawadi? Ni uhuru gani huo
wa kubadilishana bendera na
katiba?
Mtu pekee aliyeistukia
bendera ni Mutwa Mkwawa,
Wadachi walipoona kila
wakimsomesha Mkwawa
kuhusu dhana ya ukoloni
haelewi, waliamua kumtuma
mjumbe wao akiwa na ujumbe
wa mwisho kwa Mkwawa.
Mjumbe huyo alikuja na
vitu viwili risasi na bendera,
akamwambia Mkwawa
unatakiwa uchague kimojawapo.
Ukichagua bendera maana yake
umechagua amani utaitundika

hapa kwenye Lipuli yako


(makao makuu ya serikali
yake), kuashiria kwamba nchi
yako inachukuliwa kiulaini
na wewe utaitika kwa Kaisari
wa Udachi. Ukiikataa bendera
ukachagua risasi, maana yake
risasi hizi zitaingia mwilini
mwako na askari zako na nchi
yako itachukuliwa kinguvu,
unachagua kipi? Mkwawa
akachagua risasi lakini
akawaagiza makomandoo
wake wamkate mkono wa kulia
ulioleta bendera. Mkwawa
akamjibu nenda kamwambie
aliyekutuma nimechagua
hizi aliyasema hayo huku
akizichekecha risasi za Wadachi
mfano wa mtu anayechekecha
mahindi. Tangu hapo Mkwawa
akajiandaa kwa vita. Alipigana
na Wadachi mikupuo mitatu,
mara ya kwanza Wadachi
walivamia wakiwa na Askari
300, Mkwawa akawaua wengi,
mara ya pili wakavamia na
Askari 600 akawashinda ila
Wahehe wengi waliteketezwa
na mabomu. Safari ya tatu
Wadachi wakatumia mbinu kali
za ushushushu wakamshinda
lakini Mkwawa akafanikiwa
kuwatoroka. Uhuru hautolewi
kwenye sahani kama pilau.
(Itaendelea toleo lijaloInshaallah)

3/30/2016 1:12:41 PM

19

Ukurasa wa Watoto

AN-NUUR

JAMADUL AAKHER 1437, IJUMAA APRILI 1-7, 2016

Somo la Kwanza: Tawhiid -5

Kuku

WIKI iliyopita
tulimalizia darasa
letu kwa kusema
kuwa:
1. Aliyeumba ardhi
na kuitandaza ni Allah
(SW)
2. Aliyeumba
milima na kuikalisha
juu ya ardhi ni Allah
(SW)
3. Anayeshusha
mvua kutoka
mawinguni ni Allah
(SW).
4. Aliyeotesha
mimea ya aina
mbalimbali katika
ardhi ni Allah (SW).
5. Allah (SW)
ametukuka kweli
kweli.
6. Allah (SW)
ni fundi, muweza
mwenye ujuzi kuliko
wajuzi wote.
Katika darsa la leo,
tutaangalia, ni nani
fundi wa watu na
wanyama.
Hebu tujaribu kujibu
maswali yafuatayo:
Kuku ametoka wapi?
Kuku ametokana na
yai.
ANNUUR NEW.indd 19

Yai limetoka wapi?


Yai limetagwa na kuku.
Kuku wa kwanza
aliyetaga yai la kwanza
ametoka wapi?
Bila shaka hakuna
mwisho wa maswali na
majibu haya.
Labda tuulize swali la
mwisho.
Nani aliyemuumba
kuku wa kwanza?
Ngombe ni mnyama
anayefugwa.
Tunakula nyama ya
ngombe.
Nyama ya ngombe ni
tamu sana.
Pia tunakunywa
maziwa ya ngombe.
Maziwa ya ngombe ni
mazuri sana.
Ngombe ametoka
wapi?

Ngombe amezaliwa
na mama yake.
Mama yake ngombe
ametoka wapi?
Mama yake ngombe
amezaliwa na mama
yake.
Ngombe wa kwanza
ametoka wapi?
Nani aliyemuumba
ngombe wa kwanza?

Yai

Ng'ombe

Maziwa
3/30/2016 1:12:43 PM

AN-NUUR

20

MAKALA

20

JAMADUL AAKHER 1437, IJUMAA APRILI 1-7, 2016

Soma gazeti la
AN-NUUR
KWA TSH 800/=
kila Ijumaa

AN-NUUR

JAMADUL AAKHER 1437, IJUMAA APRILI 1-7, 2016

Bweni Ilala Islamic laungua


Na Bakari Mwakangwale

BWENI la Shule ya
Kiislamu ya Ilala, Jijini
Dar es Salaam, limeteketea
kwa moto na kusababisha
hasara ya zaidi ya Shilingi
Milioni 45.
Moto huo uliozuka
majira ya saa saba usiku
wa Ijumaa kuamkia
Jumamosi ya wiki iliyopita,
umeunguza bweni lote la
wavulana la shule hiyo na
hakuna mali iliyookolewa.
Akielezea tukio hilo,
Meneja msaidizi wa
Shule hiyo (Ilala Islamic)
Mwalim Ramadhan Fadhil
Shaaban, alisema katika
ajali hiyo wanafunzi wote
wamenusurika na kwamba
hakuna mwanafunzi aliye
pata madhara pamoja
na wafanyakazi wengine
waliokuwepo wakati huo.
Hata hivyo, Mwl.

Ramadhani, alisema
pamoja na kusalimika
huko lakini hawakuweza
kunusuru mali ya aina yoyote
na kupelekea moto huo
kuteketeza karibia magodoro

140, masanduku (Tranka)


ya wanafunzi ya kuhifadhi
nguo, madaftari pamoja na
vitau vyao.
Mwl. Ramadhan, alisema
kwa sasa ni mapema
kuweza kuzungumzia
chanzo cha moto huo zaidi
ya kukubali kuwa hiyo
ni Kadari ya Mwenyezi
Mungu, ambayo imeweza
kuwakuta.
Lakini, kwa upande
mwingine alisema,
kutokana na tukio lenyewe
lilivyo kaa kwa kufuata
taratibu za kisheria ni
kwamba uchunguzi
utafanyika ili kuweza
kubaini chanzo cha moto ni
nini ndipo taarifa inaweza
kutolewa.

BWENI la Shule ya Sekondari ya Kiislamu ya Ilala


ya Jijini Dar es Salaam baada ya kuteketea kwa
moto.

HAIIBA TIMAMU TEA

CHAI YA AJABU KWA AJILI YA KUKABILIANA NA

TATIZO LANGU LA PUMU LIMEPUNGUA SANA BAADA YA KUTUMIA HAIIBA


TIMAMU TEA
Na. Mwalimu Said
Mwanzoni mwa mwaka jana (2015) nilipata ugonjwa wa kichwa wa kutisha.
Muda wote bila kujali kuwa ni mchana au ni usiku kichwa kiliniuma bila kikomo.
Baada ya kuhangaika kwa muda mrefu bila mafanikio kazini nikapewa likizo ya
ugonjwa. Ilinitisha sana kwa sababu sikujua mwisho wa huu ugonjwa ingekuwa
nini.Kwa bahati siku moja rafiki yangu mmoja alinishauri nitumie chai fulani
inayoitwa HAIIBA TIMAM TEA. Ilikuwa ni muda wa usiku lakini baada ya
kuwasiliana na wahusika nikabaini kuwa nyumbani kwangu na kwao hakukuwa
mbali sana. Usiku huo huo nilifanya jitihada nikapata pakiti moja ya hiyo chai.
Mambo ya ajabu sana! Baada ya kuchemsha usiku ule na kutumia asubuhi
niliamka bila maumivu yoyote! Hadi hivi leo miezi kadhaa imeshapita na yale
maumivu hayajarudi tena.
https://www.facebook.com/Herbal-Impact-157972014402705/

SHINIKIZO LA DAMU
(HYPERTENSION/HIGH BLOOD PRESSURE)
UGONJWA WA MOYO
KIHARUSI
JONGO (GOUT)
MAUMIVU YA VIUNGO (RHEUMATISM)
MAUMIVU SUGU YA KICHWA
BAWASIR (PILES/HEMORRHOIDS)
MAGONJWA YA INI
SARATANI MBALIMBALI
UOTO/UVIMBE MBALIMBALI KATIKA
VIUNGO VYA UZAZI VYA MWANAMKE
(FIBROIDS, POLYPS NA CYSTS)
KUSHINDWA KUZUIA MKOJO (URINARY
INCONTINENCE)
ATHARI ZA KISUKARI CHA UKUBWANI
PUMU
UPUNGUFU WA KINGA ZA MWILI
KASI YA KUZEEKA
MATATIZO YA MFUMO WA MZUNGUKO
WA DAMU
MKAKAMO WA NGOZI;
UDHAIFU WA MACHO
KUPOTEZA KUMBUKUMBU
KASI NDOGO YA KUPONA MAJERAHA
MAKOVU KWENYE MAPAFU
UGONJWA WA NGOZI KUCHUJA RANGI,
YAANI, VITILIGO

HAIIBA TIMAMU TEA


INAPATIKANA
HERBAL IMPACT
MOSQUE STREET, NO. 1574/144
(MKABALA NA MSIKITI WA
SUNNI), KITUMBINI, DAR ES
SALAAM
TUTEMBELEE AU TUPIGIE SIMU
NAMBA:
0754281131/0655281131/06862
81131/0779281131

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Ltd, Dar es Salaam.
ANNUUR NEW.indd 20

3/30/2016 1:12:45 PM

Вам также может понравиться