Академический Документы
Профессиональный Документы
Культура Документы
HABARIZA
ZA
NISHATI
NISHATI&MADINI
&MADINI
NewsBulletin
http://www.mem.go.tz
Ni
Rasmi
Wabunge
Toleo
No.117
51
Toleo No.
Limesambazwa
kwa Taasisi
naTaasisi
Idarana
zote
MEM
Limesambazwa
kwa
Idara
zote MEM Tarehe - 23-29 Januari , 2015
Aprili 28 - Mei 4, 2016
Bomba la Mafuta n
kupita Tanzania
>>SOMA UK. 2
Somahabari Uk.2
HABARI ZA NISHATI/MADINI
NewsBulletin
http://www.mem.go.tz
Bomba la Mafuta
kupita Tanzania
Na Asteria Muhozya, DSM
aziri wa Nishati na
Madini, Profesa
Sospeter Muhongo
amesema kuwa,
bomba la kusafirisha
mafuta ghafi kutoka Hoima Ziwa
Albert nchini Uganda litapita nchini
baada ya hoja za Tanzania kupitisha
bomba hilo nchini kukubaliwa na
Uganda.
Profesa Muhongo aliyasema hayo
mwishoni mwa wiki, mara tu baada
ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Mwalimu Julius
Nyerere (JNIA), akitokea nchini
Uganda, ambapo pia aliambatana na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati
na Madini, Profesa Justin Ntalikwa
na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika
la Maendeleo ya Petroli Tanzania
(TPDC), Dkt. James Mataragio.
Kauli ya Profesa Muhongo inakuja
baada ya Rais wa Uganda Yoweri
Museveni kutangaza hivi karibuni
wakati wa Mkutano wa 13 wa
Ushoroba wa Kaskazini kuwa, bomba
hilo la mafuta ghafi kutoka Hoima,
Ziwa Albert nchini Uganda litapita
katika ardhi ya Tanzania kwenda
Bandari ya Tanga.
Akieleza kuhusu siri ya ushindi
wa Tanzania, Prof. Muhongo
alisema kuwa, zipo sababu kadhaa
zilizochangia ushindi huo ikiwemo
kina kirefu cha maji katika bandari
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati), akiwaonesha waandishi wa habari ramani
ya mahali litakapopita bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini.
NewsBulletin
HABARI ZA NISHATI/MADINI
http://www.mem.go.tz
TAHARIRI
Makamishna wa Madini
kukutana Morogoro
Na Greyson Mwase,
Dar es Salaam
akamishna Wasaidizi wa
Madini kutoka Makao
Makuu ya Wizara ya
Nishati na Madini pamoja
na Kanda zake, na Maafisa
Madini Wakaazi nchini wanatarajia kufanya
kikao kazi chenye lengo la kujadili shughuli
zinazotekelezwa na Mradi wa Usimamizi
Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP)
pamoja na Sekta ya Madini kwa ujumla.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Wizara
ya Nishati na Madini iliyotolewa hivi
karibuni jijini Dar es Salaam imeeleza kuwa
kikao hicho cha siku mbili kitakutanisha
Makamishna wasaidizi wa Madini walioko
Makao Makuu ya Wizara, Makamishna
Wasaidizi wa Madini wa Kanda, Maafisa
Madini Wakaazi na Katibu Mkuu wa
Wizara Prof. Justin Ntalikwa lengo likiwa ni
kujadili maendeleo ya utekelezaji wa miradi
inayosimamiwa na SMMRP na Sekta ya
TEL-2110490
FAX-2110389
MOB-0732999263
BODI YA UHARIRI
MSANIFU: Lucas Gordon
WAANDISHI: Veronica Simba, Asteria Muhozya, Greyson
Mwase, Teresia Mhagama, Mohamed Saif, Rhoda James ,
Nuru Mwasampeta na Zuena Msuya
FIVE
PILLARS OF
REFORMS
INCREASE EFFICIENCY
QUALITY DELIVERY
OF GOODS/SERVICE
SATISFACTION OF
THE CLIENT
SATISFACTION OF
BUSINESS PARTNERS
SATISFACTION OF
SHAREHOLDERS
HABARI ZA NISHATI/MADINI
NewsBulletin
http://www.mem.go.tz
NewsBulletin
http://www.mem.go.tz
Na Teresia Mhagama,
Arusha
HABARI ZA NISHATI/MADINI
Meneja wa Maabara ya Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), Mhandisi Mvunilwa Mwarabu
akionesha mashine ya kupima kiwango cha madini inayoitwa Atomic Absorption Spectroscopy (AAS).
ya Wakala huo, Barabara ya Chole jijini
Dar es Salaam, Capripoint Mwanza,
Mafao House Arusha na Uhindini
Mbeya.
Alisema kuwa Maabara ya Wakala
wa Ukaguzi wa Madini Tanzania ina
ubora wa kimataifa yaani ISO 17025,
ikimaanisha kuwa huduma zake
zinatambulika na kukubalika ndani na
nje ya nchi.
Kwa upande wa Madini ya
HABARI ZA NISHATI/MADINI
NewsBulletin
http://www.mem.go.tz
NewsBulletin
HABARI ZA NISHATI/MADINI
http://www.mem.go.tz
W
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, (katikati)
akiwa na ujumbe kutoka Ubalozi wa China ukiongozwa na Kansela
Gou Haodong (kulia kwa Waziri) pamoja na watendaji wa Wizara
wakiwa katika kikao cha pamoja kabla ya kusainiwa kwa kibali cha
kuhamisha leseni ya uchimbaji wa kati wa madini kutoka Kampuni
ya uchimbaji wa madini ya China ya Henan AfroAsia GeoEngeneering (Tanzania) kwenda Kampuni ya uchimbaji wa Dhahabu
EM Tanzania Limited.
aziri wa Nishati
na Madini Profesa
Sospeter Muhongo
amesaini kibali cha
kuhamisha leseni ya
uchimbaji wa kati wa madini kutoka
ampuni ya uchimbaji wa madini ya
China ya Henan AfroAsia GeoEngeneering (Tanzania) kwenda
Kampuni ya uchimbaji wa Dhahabu
ZEM Tanzania Limited.
Akizungumza mara baada ya
kusaini kibali hicho hivi karibuni,
jijini Dar es salaam,Profesa Muhongo
alisema kampuni hiyo itaanza
shughuli za uchimbaji mwanzoni
mwa mwezi Desemba mwaka huu,
katika kijiji cha Nyasirori wilayani
Butiama Mkoani Mara.
Alifafanua kuwa kusaini kibali
hicho kunatoa fursa kwa kampuni
ya China ya uchimbaji wa madini ya
ZEM, ambayo iliingia makubalianao
ya kufanya kazi na kampuni ya
Henan AfroAsia Geo- Engeneering
(Tanzania) mwezi Desemba mwaka
2015. Gharama za mradi huo
zinakadiriwa kufikia kiasi cha dola za
Marekani mlioni43.3.
Aidha Profesa Muhongo alisema
kuwa kampuni za China kuendelea
kuwekeza katika miradi mikubwa ya
maendeleo ni kuendelea kuimarisha
ushirikiano kati ya nchi hizo mbili
Tanzania na china ulioanzishwa na
Mwasisi Baba wa Taifa Mwalimu
Julius Nyerere.
Kwa upande wake Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na
Madini anayeshughulikia Madini
Profesa James Mdoe aliisisitiza
kampuni hiyo kutekeleza masharti
katika leseni za uchimbaji wa madini
ili kuweza kufanya kazi kwa ufanisi
mkubwa.
Vilevile aliwataka wawekezaji hao
kutekeleza mradi huo katika muda
walioahidi ili kuondoa usumbufu
na dhana ya kutokuwa na imani na
Kampuni hiyo.
Aliongeza kuwa, mradi huo
umepokelewa vyema na wakazi
pamoja na wachimbaji wadogo wa
eneo hilo kwani hakuna malalamiko
yoyote yaliyojitokeza hadi kufikia
hatua ya kuanza uchimbaji. Naye
Kansela wa ubalozi wa China nchini
Tanzania, Gou Haodong aliwataka
wawekezaji hao kujenga mahusiano
mazuri kati yao na wakazi wa vijiji
vinavyozunguka mgodi huo kwa
kuwawekea huduma za kijamii.
Haodong alitaja miradi hiyo kuwa
ni pamoja na kujenga visima vya
maji safi na salama karibu na makazi
ya watu kwani wanavijiji wengi
wamekuwa wakitembea umbali
mrefu kwenda kufuata huduma ya
maji. Sambamba na hilo alieleza kuwa
kampuni hiyo ya uchimbaji inatakiwa
kutoa huduma ya afya kwa wananchi
wa maeneo hayo kwa kuwajengea
zahanati na kuwezesha upatikani wa
huduma za dawa na madaktari.
Kansela huyo wa Ubalozi wa
China nchini, alisisita kuhusu suala la
elimu ambalo alisema kuwa ni vyema
kampuni za uchimbaji wa madini
zikaweka mazingira mazuri ya elimu
bora kwa jamii zinazowazunguka ili
kuunga mkono Serikali ya Tanzania
ya kutoa elimu bora kwa kila
mtanzania.
HABARI ZA NISHATI/MADINI
NewsBulletin
http://www.mem.go.tz
NewsBulletin
http://www.mem.go.tz
HABARI ZA NISHATI/MADINI
Vijana wa Kitanzania
wakiwa wamevaa
madini ya aina
mbalimbali ya Vito
yaliyokatwa na
kunakshiwa nchini
Tanzania.
Madini hayo ya Vito
vilivyonakshiwa
pamoja na ghafi
ikiwemo Tanzanite
yanayopatikana nchini
Tanzania yalikuwa
yakiuzwa wakati wa
Maonesho ya Tano
ya Kimataifa ya Vito
yaliyofanyika Jijini
Arusha kuanzia tarehe
19-21 Aprili, 2016.
10
HABARI ZA NISHATI/MADINI
NewsBulletin
http://www.mem.go.tz
MAKALA
Na Veronica Simba
Madini
ya
Graphite
yanatumika kwenye betri za
simu zote ambazo ni smart
phones; kwenye betri za
magari yanayotumia umeme
na pia kutengeneza Penseli ambazo
zamani waliziita za risasi. Ukweli hiyo
siyo risasi bali ni Graphite.
Hivyo ndivyo Kamishna Msaidizi
wa Madini Kanda ya Kusini, Mhandisi
Benjamin Mchwampaka alivyoanza
kunieleza kuhusu maendeleo ya
shughuli za Mradi wa Nachu wa
kuchimba madini ya Graphite, huko
wilayani Ruangwa, Mkoani Lindi.
Mhandisi Mchwampaka anaeleza
kuwa, Mradi huo unaendelezwa
na Kampuni ya Uranex Tanzania
Manufaa yanayotarajiwa
Manufaa kadhaa yanatajwa
kuwa yatapatikana na kuwanufaisha
wananchi wa Wilaya ya Ruangwa na
Taifa zima kwa ujumla, kutokana na
Mradi wa Nachu wa kuchimba madini
ya Graphite. Baadhi ya manufaa
yanayoelezwa kuwa yataletwa na
Mradi huo ni ajira kwa Watanzania,
malipo ya kodi na manufaa mengine
yanayotokana na kuongezeka kwa
shughuli za kiuchumi.
Kwa mujibu wa taarifa ya Uranex,
Kampuni hiyo imeandaa mpango wa
Ajira na Mafunzo kwa Watanzania
ambapo kipaumbele kitakuwa ni ajira
kwa Watanzania wenye sifa kwanza
kabla ya kuajiri wataalam kutoka
nje. Watanzania wengi zaidi ya 800
wataajiriwa wakati wa ujenzi wa
mgodi, lakini idadi itapungua hadi
kufikia wastani wa 360 wakati wa
uzalishaji.
Aidha, inatarajiwa kuwa mradi
wa kuchimba Graphite utakapoanza,
utakuwa ndiyo Mgodi mkubwa wa
kuzalisha madini hayo duniani. Kwa
sasa Mgodi mkubwa wa Graphite uko
China na unazalisha tani 150,000 za
Graphite kwa mwaka.
Vilevile,
imeelezwa
kuwa,
Kampuni haijaweka msamaha wa
kodi wa aina yoyote, hivyo kodi
zote zinazostahili kulipwa zitalipwa.
Uzalishaji unatarajiwa kufikia kiwango
cha tani 250,000 baada ya mwaka wa
pili wa kuanza uzalishaji.
Pia, imeelezwa kuwa Mgodi
umepanga
kununua
bidhaa
zipatikanazo hapa nchini na kama
zitakosekana ndipo zitaagizwa nje.
Aidha, huduma nyingi zitakazohitajika
mgodini zitatolewa na Kampuni za
hapa nchini.
Fidia kwa watakaopitiwa na Mradi
Kwa mujibu wa Kamishna
Mchwampaka, hatua iliyofikiwa
kwa sasa ni uthamini wa mali za
watu ambao wanatakiwa kupisha
eneo ambapo mgodi utafunguliwa
na tayari kazi ya uthamini kwa mali
yaani mazao, nyumba na ardhi tupu
lilikamilika mwishoni mwa mwezi
Februari, 2016 na hatua itakayofuata
ni kuanza kuwalipa wahusika kwa
mujibu wa taratibu za nchi.
Ni jambo la fahari kwa Watanzania
kuwa na wingi wa rasilimali za madini
ya aina mbalimbali. Ili madini ya
Graphite yalinufaishe Taifa ipasavyo,
wananchi wa Ruangwa hawana budi
kutoa ushirikiano pale inapotakiwa
pamoja na kuchangamkia fursa
mbalimbali zinakuja sambamba na
uwekezaji huo.
NewsBulletin
http://www.mem.go.tz
HABARI ZA NISHATI/MADINI
11
pango wa Uhamasishaji
Uwazi katika mapato
ya madini, gesi asilia
na mafuta( TEITI)
umezindua ripoti ya 5
na 6 ya Mapato ya Serikali kwa mwaka
2012/2013 na 2013/2014 kutoka katika
uchimbaji wa madini,mafuta na gesi
asilia.
Akizindua Ripoti hiyo jijini Dar
es salaam, aliyekuwa Mkaguzi Mkuu
na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali,
Ludovock Utouh pamoja na mambo
mengine alisema ripoti ya TEITI
imeongeza uwazi wa mapato ya Serikali
yatokanayo na Madini, Mafuta pamoja
na Gesi Asilia.
Alisema Ripoti hiyo itawarahisishia
wananchi kufahamu matumizi na
mapato yatokanayo na rasilimali hizo na
kuondoa dhana iliyojengeka kwa jamii
juu ya upotevu wa mapato yatokanayo
na madini, mafuta na gesi asilia katika
shughuli za utafutaji na uchimbaji wa
madini,mafuta na gesi asilia nchini.
Alifafanua kuwa, matokeo ya Ripoti
ya Tano ya TEITI mwaka 2012/2013
imeonesha kuwa Serikali ilipata mapato
ya shilingi bilioni 956 kutokana na
kampuni 46 za madini na kampuni 19
za mafuta na gesi asilia.
Aidha, matokeo ya ripoti ya ya Sita
TEITI ya mwaka 2013/2014 imeonesha
kuwa Serikali imepata mapato ya shilingi
bilioni 1,221 kutokana na kampuni 38 za
madini na kampuni 21 za mafuta na gesi
asilia katika shughuli za uchimbaji na
utafutaji wa mafuta na gesi asilia nchini.
Alisisitiza kuwa baada ya kuundwa
12
HABARI ZA NISHATI/MADINI
NewsBulletin
http://www.mem.go.tz