Вы находитесь на странице: 1из 20

www.annuurpapers.co.tz au facebook:annuurpapers@yahoo.

com

AHLU SUNNA WAL JAMAA HAJJ AND UMRA TRUST


(6) SIRI YA KULIPA MAPEMA

Sauti ya Waislamu

ISSN 0856 - 3861 Na. 1227 RAJAB 1437, IJUMAA , APRILI 29-MEI 5, 2016 BEI TShs 800/=, Kshs 50/=

Asilimu akibatiza

Aliwaelezea vipi Yesu alivyowapenda


Lakini akajikuta akitamka Shahada mbili
Baba akamshikia bastola, naye akasilimu

Mtume(SAW) amemueleza anayetawadha


na kukaa Msikitini akingojea Sala kuwa
anapata thawabu kama yumo ndani ya Sala.
Kadhalika mwenye kulipa mapema kwa Hijja
anaanza kuneemeka mapema. Gharama
zote kwa Hijja 2016/1437 ni Dola 4,600.
Umra ya Ramadhani ni Dola 2,700. Karibuni
Ahlu Sunna wal Jamaa kwa huduma nzuri na
uongozi bora. Wasiliana nasi: Tanzania Bara:
0679895770/ 0688895777; 0765462022;
0712735363. Zanzibar: 0777468018;
0777458075; 0777845010; 0777497300.

Katimba hatunaye
IDDI Katimba ni katika
wanaharakati walioshiriki
semina ya kuratibu harakati
za maendeleo ya Waislamu
nchini iliyoandaliwa na
Islamic Propagation Centre
(IPC) Januari 12-18, 1991,
jijini Dar es Salaam.
Hiyo ilikuwa ndiyo
semina iliyozalisha chachu
ya kuratibu harakati
zilizochangia kuanzishwa
shule za Kiislaamu nchini.
Ni semina hiyo pia
iliyopitisha azimio la
kuanzishwa gazeti hili la
Kiislaamu la AN-NUUR.
Kwa taufiki ya Allah
(S.W), gazeti lilifanikiwa
kusajiliwa na kuanza kutoka
rasmi mnamo mwezi Agosti,
1991 pamoja na shule ya

sekondari ya Kiislaamu ya
Ubungo ambayo ilianza
rasmi mnamo Januari, 1992.
(Soma Uk. 9)

MARHUUM Iddi Katimba

Vituko vya Muungano


Tumetoa sadaka kila kitu

Aminah Assilmi (Janice Huff).

Mafia Style:

Baada ya urafiki
msiba juu ya msiba

Soma Uk. 10

ANNUUR NEW.indd 1

MZEE Aboud Jumbe.


KANUNI inayouendesha
Muungano (wetu),
imekuwa ni moja tu:
Kadiri Tanzania
inavyozidi kupanda,
Zanzibar izidi kuanguka.
Gharama za kuimarika
kwa Muungano,
zimekuwa ni kudhoofika
kwa Zanzibar.
(Wakati) gharama
kubwa ya Tanganyika
katika Muungano huu ni
kupoteza jina lake la asili,
faida kubwa ya Zanzibar,

Dkt. Salmin Amour.


ni kubakia na jina lake.
(Lakini) Zanzibar kama
nchi, dola na taifa huru
haipo.
Na viongozi
waliothubutu kufanya
jambo kuitutumua
Zanzibar, basi kifimbo
cha Mwalimu Nyerere
kiliwachapa.
Hicho ndicho kifimbo
kilichowachapa Mzee
Aboud Jumbe, Maalim
Seif Sharif na Salmin
Amour. Soma Uk. 8

4/27/2016 12:27:41 PM

Surat Araaf 189-190

Fethullah-Gulen
(ALIPOWAPA mtoto
mwema walimfanyia
washirika katika kile
alichowapa ametukuka
Mwenyezi Mungu na yale
wanayomshirikisha nayo.
[AL-AARAAF 189-190]
Kuna hakika ambayo
imethibiti nayo ni
kwamba baadhi ya
waumini wanaingia mara
nyingi katika duara ya
kumshirikisha Mwenyezi
Mungu. Je, kutokuwa
kurejea huko ni kwa mkato
wa watu wa Shirki. Na
kama inavyoweka wazi
aya hii tukufu, kwa hakika
mapenzi ambayo yamevuka
mpaka kwa watoto, ni njia
katika njia za kumshirikisha
Mwenyezi Mungu kwani
badala ya kuwaangalia
watoto wetu na wajukuu
wetu kwamba wao ni neema
na msaada na amana kutoka
kwa Mwenyezi Mungu
iliyowekwa katika shingo
zetu; tunawaangalia kana
kwamba sisi tunawamiliki.
Bali baadhi ya watu
wanaacha swala na ibada
kwa sababu yao kana
kwamba mapenzi yao kwa
watoto, ni zaidi kuliko
mapenzi yao kwa Mwenyezi
Mungu mtukufu. Badala ya
kuwapenda kwetu watoto
kwa ajili ya Mwenyezi
Mungu, tunawapenda
watoto pasi na kumfikiria
Mwenyezi Mungu
Iwapo msemo huu
unafaa, na tunahisi
kiwango cha mahusiano na
hisia na mapenzi ambayo
yanapelekea kwenye daraja
la shirki ya ujumla pasi na
kukusudia; kwa sababu
hiyo kunapasa kutenda
kufuatana na kanuni hii:
Moyo mmoja haukunjuki
mapenzi mawili na tuwe
juu ya maandalizi wakati
wote dhidi ya kushirikisha
kitabia. Hakika jambo hili
ni jepesi sana kwa upande
wa kusema na kwa upande
wa kiasi cha kusema tu,
isipokuwa utekelezaji wake
katika maisha ni mgumu
sana kuliko inavyoonekana.
Pamoja na hayo, kunapasa
kufanya yale yote yaliyo
katika uwezo wetu, ili

ANNUUR NEW.indd 2

AN-NUUR

Mafundisho ya Qur'an/Uwanja wa Maarifa

kujisafisha na kushirkisha
na kutoa kila juhudi kwa
ajili ya kutokaribia katika
sehemu ambazo inanuswa
kwa umbali kutoka sehemu
hizo harufu ya kushirikisha.
Tutakapofanya hivi,
yanakuja maombi ya Mtume
(s.a.w.) kama kielelezo
muhimu na cha lazima:
Ee Mola wangu wa haki,
hakika mimi ninajikinga
kwako na kushirikisha na
wewe kitu chochote na hali
ya kuwa mimi ninajuwa na
ninaomba msamaha kwako
kwa lile ambalo silijuwi.
Kunawezekana
kuyaangalia maudhui ya
kuwapenda watoto kwa
mitizamo tofauti: Huenda
mtu asipatilizwe katika
masuala ya hisia. Isipokuwa
yeye analazimishwa
kwa upande wa dini,
kuzirekebisha (kuzidhibiti)
hisia zake za kimaumbile
kwa mfano huenda akawa
mmoja wao ni mroho katika
kula na katika kunywa
na huenda akatamani
kuishi maisha ya juu, na
anaonyesha matakwa na
pupa kubwa katika jambo
hili, kwa hiyo anafanya
mambo pasi na kufanya
hesabu yoyote ya mwisho
wa mwenendo huu. Kwa
sababu binadamu kwa
maumbile yake ameumbwa
hali yakuwa ni dhaifu mbele
ya matakwa yake na bakhili
na mwenye haraka. Mambo
haya yanapatikana katika
maumbile yake. Kama
ambavyo yeye anabeba
katika mbavu zake pamoja
na hisia za mfundo na
chuki na uadui, anabeba
pia hisia za kibinadamu.
Hii kumekuwa ni juu yake
kusimama na kuyaziba
madirisha na milango
iliyo na mambo haya
katika nafasi ya njia mbili,
inazopelekea kwenye shari
na kwenye kheri. Kwa
sababu hiyo, kumekuwa
ni juu yake kusimama na
kuyaziba madirisha na
milango iliyofunguliwa
katika uhakika wake juu
ya shari na kukiunda
juu ya hisia zake na kwa
fikra za hisia zake zaidi.
Kufanya hivi, ndiko
tunakokuita kwa msemo
wa kidini, Kuchuma
maumbile ya pili ili afikie
kwenye ukamilifu ambao
umekadiriwa kwake.
Maana kwamba afanye
kutokana na maumbile
yake ambayo anayafungulia
mlango juu ya kila kitu
ayafanyie mlango mmoja
tu wenye kupelekea kwa
Mwenyezi Mungu mtukufu
na kuimarisha uhusiano
wake na Mwenyezi Mungu
mtukufu.
Kuwapenda watoto kwa
namna hii, huko ndiko

kuliko katika maumbile ya


binadamu na lau si kuwepo
kwa mapenzi haya, watoto
wasingepata matunzo
yoyote na asingewapa
umuhimu mtu yeyote, kwa
kuwalea na kuwafundisha
na pasingekuwa na
maendeleo si kwa nchi
wala kwa binadamu.
Tunawaona pambizoni
mwetu watoto wengi walio
katika hali mbaya na wenye
kuasi na pamoja na hayo,
wanabaki katika maangalizi
ya baba zao na mama
zao. Na lau si mapenzi
ya binadamu upande wa
watoto, barabara zingejaa
watoto wenye kufukuzwa
kutoka majumbani mwao.
Isipokuwa marekebisho
ya nyoyo kwa upande wa
hisia hii kama zilivyohisia
nyingine, kwa hisia ya
kumpenda Mwenyezi
Mungu mtukufu, ili
kupatikane kufika kwenye
unyoofu wenye kutakiwa.
Kwa sababu kufungamana
na Mwenyezi Mungu,
kutakuwa ndiyo msingi
wa maisha. Hapana
namna ya kuepukana na
kupotoka. Kwa sababu
hiyo kunapaswa kustawi
mapenzi ya Mwenyezi
Mungu mtukufu na
kuimarika katika kila
moyo. Hili linafungamana
na riyadha na mazoezi
maalumu, maana iwapo
atasema mtu yeyote ambaye
hajajuwa katika maisha yake
mazoezi yoyote ya kiroho,
Hakika mimi ninaitoa
mali yangu na watoto
wangu katika njia yake
pekee Bwana wangu, huwa
mavuno haya wakati fulani
ni kujionyesha na wakati
mwingine ni kuonyesha.
Sababu ni jambo la lazima
kabla ya kusema maneno
haya kuyaandikisha mambo
mabaya katika roho na
kuotesha mambo mema.
Jambo baada ya jambo,
mahali pa mambo maovu
ili vina vya nafsi zetu
vichanganyike na Uislamu
na uwe Uislamu ni sehemu
ya tabia yetu, tuna maumbile
yetu; kwa hiyo yatakuwa
matendo yetu mema na ya
kitabia wakati huo. Kama
haikuwa hivyo, tusingekuwa
na kujiepusha na sura mbili
katika kufikiri na sura mbili
katika maisha na utendaji.
Aya inahama kutoka kwa
Adam (a.s.) kuelekea kwa
binadamu mmoja mmoja
na kundi kwa kundi na
inaendelea kama mnyororo
mrefu kwa sifa ya kuwa
unaonekana katika ujumla
wa umoja wake mkuu na
katika ujumla wa namna
yake kwa kupambanuka
na kwa kutofautiana
na kujitosheleza katika
mkusanyiko wake.

RAJAB 1437, IJUMAA APRILI 29 - MEI 5, 2016

UWANJA WA VIJANA-JIONGEZEE MAARIFA


CHEMSHA BONGO: 49

Weka duara kwenye jawabu ilio sawa. Jawabu kamili wiki ijayo.
M

3:154

40

41

42

na Q

43

na S

na N

44

45

na W I

JK B

46

47

H na

48

94:5-6 U

W W 25

55

AN R

W Z

40:68

MASUALA
1.
Sura ipi na aya ya ngapi isemayo Kisha baada ya dhiki
alikuteremshieni utulivu - usingizi ambao ulifunika kundi moja
kati yenu. Na kundi jengine nafsi zao ziliwashughulisha hata
wakamdhania Mwenyezi Mungu dhana isiyo kuwa ya haki,
dhana ya kijinga. Wakisema: Hivyo tuna lolote sisi katika jambo
hili? Sema: Mambo yote ni ya Mwenyezi Mungu. Wanaficha
katika nafsi zao wasiyo kubainishia. Wanasema: Lau ingelikuwa
tuna lolote katika jambo hili tusinge uliwa hapa. Sema: Hata
mngeli kuwa majumbani mwenu, basi wangelitoka walio
andikiwa kufa, wakenda mahali pao pa kuangukia wafe.(Haya ni
hivyo) ili Mwenyezi Mungu ayajaribu yaliyomo vifuani mwenu,
na asafishe yaliyomo nyoyoni mwenu. Na Mwenyezi Mungu
anayajua yaliyomo vifuani.
2. Sura ipi aya hii imerejewa mara 34 Basi ni ipi katika neema
za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha.
3. Zitaje Sura neno Hamim ndio inaanzia.
4. Mitume mingapi wametajwa kwa majina yao katika Quran?
5. Mti gani ambao ni mchungu wenye miiba watu wa motoni
ndio kitakuwa chakula chao?
6. Mtume yupi alikuwa na wajihi wa kupendeza na kuwatia
kiwewe wanawake?
7. Mtume yupi aliiona Nuru ya Mwenye-enz-Mungu?
8. Taja Baba na watoto wakiwa ni Mitume?
9. Allah akitaka jambo liwe huwa? Itaje Sura na Aya.
10. Sura ipi na aya ya ngapi Mwenye-enzi-Mungu
anamhakikishia Mtume (SAW) baada ya dhiki ni faraji?
(Tunaomba radhi kwa makosa yaliotokea wiki iliopita katika
kupangilia kazi hii ya Chemsha Bongo)

Jee Unajua?

1. Nchi ya Kazakhsatan ni mmoja ya nchi yenye eneo kubwa la ardhi


iliokuwa na rutba yenye kufaa kwa kilimo: http://data.worldbank.
org/indicator/AG.LND.AGRI.ZS
2. Idadi ya watu wenye ulemavu duniani kote wanafikia watu milioni
650: http://www.rollingrains.com/readings/2010/03/the-number-ofpeople-with-disabilities-worldwide.html
3. Inakisiwa kuwa kuna watu kama bilioni 3.2 wapo mashakani
kuugua homa ya Malaria. Kunakuwa na idadi ya wogonjwa milioni
214 kwa mwaka na kati ya hao hutokea vifo vya watu 438,000 kila
mwaka vinavyotokana na homa ya malaria: http://www.who.int/
features/factfiles/malaria/en/
4. Asilimia 90 ya vifo vya ugonjwa wa malaria hutokea katika nchi
za kusini mwa jangwa la Sahara: http://www.worldmalariaday.org/
about/key-facts
5. Nchi ya Marekani ndio nchi yenye ufanisi mkubwa wa masuala
ya mtandao wa Internet na kufikia nukta ya kuunganisha kila kitu
chao cha maisha na Teknolojia iwe madawa, mambo ya kijeshi,
miundo mbinu, makazi n.k.: http://www.thetoptens.com/hightech-countries/
6. Kahawa ni mmoja ya kinywaji kinachonywewa kwa wingi duniani,
nchi ya Brazil ndio msafirishaji mkubwa wa kahawa duniani,
ikifwatiwa na nchi ya Viatnam na Indonesia, katika orodha hio nchi
ya Ethiopia ni nchi ya 5: http://www.mapsofworld.com/world-maps/
top-coffee-exporting-countries.html
7. Nchi ya Marekani, China, Brazil ni kati ya nchi zinaongoza
kwa ukulima duniani: http://www.investopedia.com/financialedge/0712/top-agricultural-producing-countries.aspx
8. Nchi ya Canada ni nchi yenye kutoza bei ndogo ya umeme duniani
ikifwatiwa na nchi ya China na Marekani: https://www.ovoenergy.
com/guides/energy-guides/average-electricity-prices-kwh.html
9. Katika mwaka wa 1952 nchi ya Uiengereza ilishuhudia vifo vya
watu 12,000 kutokana na watu kuwasha mkaa wa mawe kwa wingi
majumbani mwao ili kuweza kupata joto katika majira ya baridi:
http://www.disasterium.com/10-worst-man-made-disasters-of-alltime/
10. Nchi ya Austria ni nchi inayoongoza duniani kuzirejeza taka
(recyclying) kiasi cha asilimia 63 ya taka zake huzirejeza: http://
files.www.planetaid.org/blog/recycling-rates-around-the-world/
recycling_rates_around_the_world_Full_Size.jpg na http://shop.
ecology.com/?art=recycling_infographics
(Kwa wasomaji wa Uwanja wa Maarifa tumeazimia kuuboresha
ukumbi huu tunaomba maoni yenu juu ya ukumbi huu, tuma
kwa barua pepe zuwarde@gmail.com au ujumbe mfupi kupitia
simu 0777436949)

4/27/2016 12:27:43 PM

Habari
Na Shabani Kihara

JANICE Huff, akiwa muumini na


muhubiri wa kanisa la Baptisti,
alijikuta akisilimu akiwa katika
jitihada za kuwabatiza wanafunzi
wenzake Waislamu.
Baba yake aliposikia kuwa binti
yake kasilimu, alichukua bunduki
yake akaikoki akitaka kumuuwa.
Hata hivyo, naye badala ya kuuwa,
akasilimu akifuatiwa na mkewe na
bibi.
Janice Huff, aliyezaliwa
Oklahoma, si mtu aliyekuwa
akijulikana sana kabla ya kusilimu
Mei 21, 1977 akiwa Colorado.
Kuhusu elimu, Janice Huff, ana
Shahada (degrees) za Ualimu,
Utangazaji (broadcasting) na
Mawasiliano (communications).
Baada ya kusilimu na kujipa jina
la Aminah Assilmi, Janice Huff,
alikuja kuwa mwanaharaki mkubwa
wa Kiislamu ambapo katika uhai
wake alipata kuwa Mwenyekiti
wa Umoja wa Kimataifa wa akina
mama wa Kiislamu- International
Union of Muslim Women. Mwaka
2009 alitajwa na Royal Islamic
Strategic Studies Centre (Amman,
Jordan) kuwa mmoja wa Waislamu
500 mashuhuri zaidi duniani.
Kisa chake cha kuvutia kilianza
pale kompyuta ya Chuo Kikuu
ilipokosea na kumsajili kuwa katika
darasa linalohusika na masuala
ya tamthilia na maigizo. Kule
alikutana na wanafunzi Waislamu.
Alipowaona tu wanafunzi hao na
kutambua kuwa ni Waislamu, aliona
kama wanaishi katika kiza kinene
cha kufikia ufalme wa mbinguni.
Mara moja alijihisi kuwa ana
jukumu la kutimiza.
Katika jitihada zake za kujaribu
kuwabatiza wale wanafunzi
Waarabu wa Kiislamu, aliwahubiria
sana kwa kuwaeleza:
Mtaungua motoni, tena milele
kama mkikataa kumkubali Yesu
kama mwokozi wenu.
Alitumia ushawishi mkubwa
kujaribu kuiteka mioyo yao.
Niliwaelezea vipi Yesu
alivyowapenda na alikufa katika
msalaba kwa ajili ya dhambi zao
na walichotakiwa kufanya ni
kumkubali tu moyoni mwao.
Alisimulia Assilmi.
Pamoja na jitihada zake, bado
aliona mahubiri yake yanagonga
mwamba, hayaleti tija yoyote na
akajiuliza ni kwanini ameshindwa
kuwashawishi wenzake katika neno
jema la Mungu. Hapo akaamua
kuisoma Quran ili apate mwangaza
kidogo wa Kiislamu, ambao
ungemsaidia kuwaelewa vizuri
Waislamu ili awashawishi kirahisi
na kuingia katika Ukristo.
Assilmi alisema baada ya
kuyaona na kuyaelewa yaliyokuwa
katika Quran, alipatwa na mshtuko
mkubwa, akimaanisha aliyoyaona
kutoka katika Quran kiasi cha
hata zile ndoto za kuwabadili
wenzake, ziliishia kwa kubadilika
yeye mwenyewe. Assilmi aliusoma
Uislamu vizuri na kwa kipindi cha
miaka miwili, alisoma kwa kina na
alimudu kusoma Quran yote vizuri,
Sahih Muslim na vitabu vyengine 15
vya Kiislamu.
Katika kusoma kwake Quran,
Assilmi akakutana na maswali
ambayo yalijibiwa na rafiki yake wa
Chuo Abdul-Aziz Al-Sheikh. Baada
ya kuugundua ukweli kutoka katika
Uislamu, Assilmi hakuwa na jingine

ANNUUR NEW.indd 3

RAJAB 1437, IJUMAA APRILI 29 - MEI 5, 2016

Asilimu akibatiza

Aminah Assilmi (Janice Huff).


isipokuwa ni kukubali kwa ulimi
na kukiri kwa moyo kuwa Hapana
Mola apasaye kuabudiwa kwa haki
ila Mwenyezi Mungu (Allah) na
Muhammad ni Mtume wake na
alichagua jina la Amina Assilmi. Hii
ilikuwa tarehe 21 Mei 1977.
Mwanzoni aliahidi hatofunika
nywele zake na kama mumewe
akioa mke mwengine, basi atamhasi.
Hata hivyo baada ya kuzama kwa
kina katika dimbwi la maarifa ya
Uislamu akajikuta akivaa hijab, hata
akawa mtetezi wa ndoa za mitala.
Nilijua kwamba kama Allah
karuhusu jambo hilo, ni lazima
kutakuwa na faida kubwa ndani
yake, niliona mantiki yake.
Hata hivyo baada ya kusilimu,
Amina alikimbiwa na marafiki wake
wengi kwani hakuwa mtu mzuri
tena kwao. Dada yake ambaye ni
mtaalamu wa afya ya ubongo na
akili, alifikiri amechanganyikiwa
hivyo alijaribu kumpeleka katika
vituo vya kupima akili. Baba mzazi
wa Amina aliposikia kusilimu
kwake, alighadhibika na kujaza
bunduki yake risasi kwa hasira
kumtafuta amuue. Ni bora afe.
Baba alisema na kujiapiza.
Siku alipoanza kuvaa hijab,
dada huyu ambaye alishatunukiwa
zawadi ya uandishi wa habari,
alifukuzwa kazi. Na baada ya
kujitangaza wazi kuwa yeye sasa ni
Muislamu, alipewa talaka na mume
wake. Baada ya talaka, alikataliwa
kukaa na watoto zake wawili
wadogo, ambao aliwapenda sana.
Hata katika kesi hakimu wa serikali
hakumpa chaguo kabla ya kutoa
hukumu. Alitakiwa kuchagua, ama
akatae Uislamu na apewe watoto
au aendelee na Uislamu wake huku
akiwakosa watoto.
Kama tujuavyo, mapenzi ya mtoto
na mama yalivyo, Masharti hayo
yalikuwa magumu na kumuumiza
zaidi Amina hasa akikumbuka
ushauri wa daktari wake kuwa
hataweza kupata mtoto mwengine
kutokana na matatizo aliyokuwa
nayo. Hata hivyo katika hali ya
kushangaza, bado aliamua kubaki
na Uislamu. Watoto wake wadogo,
mmoja mvulana na mwingine wa
kike, wote walipelekwa kwa mume
wake wa mwanzo.

AN-NUUR

Alisema maumivu yalizidi


moyoni. Nimepigwa na wakati
sijawahi kunyanyua mkono wangu
kumpiga yeyote. Alisema amina.
Mabadiliko katika maisha yake
yalizidi kuonekana pale alipojaribu
kufikisha hawala katika benki
yake huku akiwa amevaa niqaab
(akifunika uso kasoro macho).
Mlinzi wa benki alimuoneshea
bastola yake akimtayarisha
kumshughulikia iwapo atasogea
hata hatua moja kuingia benki.
Japokuwa familia yake
ilimkasirikia, aliendelea kuwasiliana
nao na kuwaitikia kwa heshima,
taadhima na uvumilivu. Maisha
yake mapya yakambadili na kuwa
mtu mwema, mpole na muadilifu,
kitu kilichovutia hadi familia yake
na kuanza kumkubali na kumpenda.
Ile taswira ya uzuri wa Uislamu
iliyokuwa haionekani, ikajitokeza
kwa Amina na ikaivuta familia yake
kuingia Uislamu.
Wa kwanza katika waliosilimu

alikuwa ni bibi yake, ambaye


alikuwa na zaidi ya miaka 100.
Aliyefuatia ni yule aliyetaka
kumuua aliposikia mwanawe kawa
Muislamu. Baba alisilimu na baada
ya miaka kadhaa mama yake naye
akaungana nao katika Uislamu.
Dada yake Amina ,ambaye
alifanya juhudi ili nduguye
akachunguzwe katika hospitali za
vichaa naye akasilimu. Mwanawe
mkubwa Whittney, baada ya kufika
miaka 21 naye aliukubali Uislamu.
Miaka 16 baada ya kuachana na
mume wake wa mwanzo, naye
akawa Muislamu.
Amina Assilmi baadae aliolewa
na mtu mwengine, japokuwa
matabibu walimueleza kuwa
hataweza kupata mtoto, Mwenyezi
Mungu alimbariki na akapata mtoto
mwingine wa kiume.
Aliachishwa kazi kutokana na
kuvaa hijab, lakini sasa yeye ni Rais
wa Baraza la Kimataifa la Wanawake
wa Kiislamu (International Union
of Muslim Women). Mara nyingi
amekuwa akihitajika sana katika
nchi mbalimbali duniani kufanya
mihadhara.
Nina furaha sana kuwa
Muislamu. Uislamu ndio maisha
yangu. Uislamu ndio mapigo
yangu ya moyo. Uislamu ndio
damu inayosafiri katika mirija
yangu ya damu. Uislamu ndio
nguvu zangu. Uislamu ndio kila
kitu changu. Pasi na Uislamu,
mimi si chochote si lolote. Na kama
Allah asingeniangalia kwa jicho
la huruma, nisingeweza kuishi.
Alisema Amina Assilmi.
Katika uhai wake, Assilmi
alifanikiwa kuhiji mara mbili,
ambapo katika hija moja alikuwa
mgeni wa Mfalme wa Saudi Arabia
na alikaa katika moja ya Ikulu
(ndogo) iliyo jirani na Kaba.
Aminah Assilmi alifariki katika
ajali ya gari iliyotokea Newport,
Tennessee, Ijumaa ya tarehe 5 Machi,
2010 na kuzikwa Machi 6 katika
makaburi ya Kituo cha Kiislamu,
Knoxville, Tennessee. Aliacha watoto
watatu, Amber (Binti), Whittney na
Mohammed.

BAADHI ya watoa mada katika semina ya walimu wa madrasa,


wakizungumzia namna ya kuwa na tabia njema katika masuala
ya kibinadamu na kupambana na uasi. Semina hiyo iliandaliwa na
kituo cha Kiislamu cha Kimisri, iliyofanyika mwishoni mwa wiki
iliyopita katika ukumbi wa mikutano Markaz Chang`ombe jijini
Dar es salaam.

4/27/2016 12:27:47 PM

Tahariri/Makala

AN-NUUR

S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786


Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM.
www.annuurpapers.co.tz
E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk
Ofisi zetu zipo: Manzese Tip Top
Usangi House, barabara ya Morogoro, D'Salaam

Rais Magufuli autizame upya


Mfumo OPRAS utatusaidia
PAMOJA na kwamba hivi
sasa kuna vikao vya Bunge
la Bajeti linaloendelea
mjini Dodoma,
kukiwa tayari serikali
imeshawasilisha katika
Bunge hilo mwelekeo
wa bajeti ya serikali
2016-2017, huku ripoti
ya ukaguzi ya Mkaguzi
na Mdhibiti Mkuu wa
Serikali (CAG) nayo
ikiwa imeshakabidhiwa
serikalini na bila shaka
bungeni, masikio ya
Watanzania yameelekezwa
Dodoma kusikia
kitakachojiri.
Ingekuwa kipindi kile
ambapo vikao vya Bunge
vilikuwa vinarushwa
moja kwa moja kupitia
televisheni, Wananchi
wangepata fursa si ya
kusikia tu, bali na kuona
pia kile kinachojiri. Kiu
ya wananchi ni kuona
serikali inachukua hatua
kuondoa vikwazo vyote
vinavyosababisha huduma
za serikali zisiwafikie au
kuwa hafifu.
Tuchukue fursa hii
kukumbusha japo kwa
uchache tu kwamba Julai
2004, serikali ilianzisha
matumizi ya mfumo
wa wazi wa mapitio na
tathmini ya utendaji kazi
(OPRAS), kupitia Waraka
wa Utumishi Na. 2 wa
mwaka 2004.
Kuanzishwa kwa mfumo
huo kulimaanisha kuwa
serikali imefuta mfumo
wa zamani wa kupima
utendaji kazi wa watumishi
wa umma kwa siri, mfumo
ambao ulionekana kuwa
hauboreshi utendaji kazi na
uwajibikaji wa watumishi
katika utumishi wa umma.
Mabadiliko hayo ya
kutathmini utendaji kazi
wa watumishi wa umma
yalikwenda sambamba
na sera ya Menejimenti
na Ajira katika Utumishi
wa Umma ya mwaka 1998
na Sheria ya Utumishi
wa Umma Na. 8 ya
mwaka 2002, ambazo zote
zilisisitiza uwekaji wa
mifumo ya menejimenti
ya utendaji bora wa
kazi inayojali matokeo
ya kazi na kwamba,
masuala ya ajira, uteuzi
na kupandishwa ngazi
katika utumishi wa umma
yangekuwa kwa ushindani,
uwazi na unaozingatia sifa,
ujuzi na uadilifu wa hali
ya juu.
Uanzishwaji wa OPRAS
ilikuwa ni hatua muhimu
kwa serikali katika
kuboresha utendaji kazi na
utoaji huduma kwa umma.
Ni chombo muhimu
cha uwajibikaji kwa
kila mtumishi ambacho
kinasisitiza umuhimu wa
ushirikishwaji, umiliki na

ANNUUR NEW.indd 4

uwazi ambapo watumishi


walikusudiwa kuhusisha
katika kupanga malengo,
utekelezaji, kufanya
ufuatiliaji wa utekelezaji
wa malengo na mchakato
wa kufanya mapitio ya
utendaji.
Matokeo ya mfumo
huo yalitarajiwa kuwa ni
mawasiliano ya mara kwa
mara kati ya wasimamizi
wa kazi na watumishi,
na kuwepo uelewa wa
pamoja wa mahusiano
yaliyokuwapo kati ya
malengo ya taasisi na yale
ya watumishi binafsi.
Ili kuhakikisha kuwa
utekelezaji wa OPRAS
unaeleweka kwa pande
zote za mwajiri na
mwajiriwa, serikali iliamua
kutoa mwongozo huo wa
utekelezaji wa OPRAS
katika Utumishi wa
Umma.
Mwongozo huo
ulitarajiwa kuwezesha
kutoa maelezo ya jinsi ya
kujaza fomu ya OPRAS na
jinsi ya kufanya mapitio na
jinsi ya kutumia matokeo
ya mapitio na tathmini ya
utendaji kwa mfano utoaji
wa zawadi, adhabu na
hatua za maendeleo kwa
nia ya kuboresha utendaji
wa watumishi.
Hata hivyo tunasikitika
kwamba mfumo huu
haukuweza kuleta
matunda yaliyokusudiwa
tangu wakati huo, na
kushindwa kwake kutoa
matunda yaliyokusudiwa
kumekuwa moja sababu
za utendaji mbovu kwa
watumishi wa umma na
kuendelea kuwepo ufujaji
na matumizi mabaya ya
nyadhifa serikalini.
Ndio maana leo
tunashuhudia Rais
akifanya kazi kubwa
ya kutumbua majipu,
yakiwepo watumishi hewa
waliyoigharimu serikali
mabilioni ya fedha.
Tuchukue fursa hii
kumkumbusha Rais
Magufuli na serikali
yake kuwa mfumo huo
wa OPRAS, unaweza
kusaidia sana kudhibiti
uwajibikaji serikalini kama
utasimamiwa vizuri na
kutekelezwa kwa vitendo.
Ni mategemeo yetu
kwamba mwongozo
huo wa OPRAS,
ambao tunaona
haukufanyiwa kazi
kama ulivyokusudiwa,
ukitumika kama
ulivyokusudiwa na
kusimamiwa vizuri,
utaiondolea serikali mzigo
wa watumishi wabovu
katika taasisi za umma
na kubakia na watendaji
wanaojali zaidi matokeo
bora katika utoaji wa
huduma kwa umma.

AN-NUUR

RAJAB 1437, IJUMAA APRILI 29 - MEI 5, 2016

Kutafsiri maneno ya Allah (s.w.) bila elimu ni dhambi

Na Dk. Mahmud
Hassan Mahmud

SHUKURANI
zote anastahiki
Mwenyezi Mungu
na ninashuhudia
kwamba, hakuna
apasaye kuabudiwa
kwa haki isipokuwa
Mwenyezi Mungu, na
ninashuhudia kwamba
Mtume Muhamad ni
Mjumbe wake.
Mwenyezi Mungu
amekataza kutoa
maana ya maneno
yake bila ya ujuzi wala
elimu. Atakayelifanya
hilo, huyo ana
dhambi kubwa bali
amemuweka kwenye
daraja la juu amesema
Mwenyezi Mungu
mtukufu sema kwa
hakika amekataza
Mola wangu mlezi
mambo machafu,
yale ya wazi na yale
ya siri na madhambi
na ujeuri bila ya haki
na kumshirikisha
Mwenyezi Mungu.
Yule asiyeteremsha
dalili na aya ya
Mwenyezi Mungu
katika mambo
ambayo hamyajui,
akapangilia vitu vya
haram, daraja nne
zinamsubiri. Atalianza
lililo jepesi, nalo ni
mambo machafu,
kisha likafuata lililo
kubwa kwa lile jepesi,
nalo ni la madhambi
na dhulma, kisha la
tatu ni zito kuliko
hayo mawili, nalo
ni kumshirikisha
Mwenyezi Mungu,
la nne ambalo ni zito
zaidi ya yote hayo, nalo
ni kuyasema mambo
ya Mwenyezi Mungu
bila ya elimu. Nako
ni kumsemea mambo
yake Mwenyezi Mungu
bila ya elimu katika
majina yake.
Amesema Allah
(S.w) Wala msiseme
kwa yale yanayosifu

ndimi zenu uongo,


kwamba hayo ni halali
na hali ya kuwa ni
haram ili mumzulie
halali na yaliyo
haram ili mumzulie
Mwenyezi Mungu
uongo hali ya kuwa
ni halali. Kwa hakika
wale wanaomzulia
Mwenyezi Mungu
uongo hawatafaulu,
starehe yao ni ndogo
na watapata adhabu
yenye kuumiza.
Hapo
Mwenyezi Mungu
amewatangulizia
makemeo juu ya
kumuongopea kuhusu
hukumu zake, kwa
kauli zao juu ya
asiyoyakataza kuwa
ni haramu na yale
asiyoyahalalisha
kuwa ni halali. Huu
ni ubainifu toka kwa
Mwenyezi Mungu
kwamba haifai kwa
mtu kusema kwa utashi
wake tu, kuwa hiki ni
halali na hiki ni haram
isipokuwa mpaka
ajue na awe na hakika
kuwa anachokisema
amehalalisha
Mwenyezi Mungu au
ameharamisha.
Na amesema Ibnu
Wahbi, nilimsikia
Maliki akisema
Haikuwa miongoni
mwa amri za watu
wala kwa wale
waliopita miongoni
mwa waliotutangulia,
wala kumuwahi hata
mmoja wa kumfuata,
akasema juu ya jambo
kuwa hiki ni halali
na hiki ni haram,
na wala hawakuwa
wenye kufanya jeuri
juu hilo. Bali walikuwa
wakisema tu, nachukia
hiki na tunaona hili ni
zuri, inatakikana hii na
wala hatuoni hili.
Ameipokea hii
Atiqi Bin Yakubu na
akazidisha, Na wala
hawasemi hii ni halali
na hii ni haram, hivi
hukusikia neno la
Mwenyezi Mungu
Mtukufu. Mumeyaona
aliyoyateremsha
Mwenyezi Mungu
miongoni mwa riziki,
nanyi mkazifanya ni
haram na halali. Hivi
Mwenyezi Mungu
ameharamisha au

mnamzulia. Basi
vya halali ni vile
alivyovihalalisha
Mwenyezi Mungu
na Mtume wake na
vya haram ni vile
alivyoharamisha
Mwenyezi Mungu na
Mtume wake.
Toka kwa Amr Bin
Shuaib, toka kwa
baba yake, toka kwa
babu yake amesema,
amesikia Mtume (saw)
watu wakibishana kwa
Quran, akasema Kwa
hakika wameangamia
wale waliopita
kabla yenu kwa hili,
wakipigana kwa
kitabu cha Mwenyezi
Mungu wao kwa wao.
Bali kimeteremshwa
kitabu cha Mwenyezi
Mungu, ili wasadikishe
baadhi yao na
baadhi, na wala sio
wakanushane baadhi
yao na baadhi, basi yale
muyajuayo yasemeni
na yale msiyoyajua
basi yapelekeni kwa
wanaoyajua.
Basi amri kwa
wasiojua jambo katika
kitabu cha Mwenyezi
Mungu, yampasa
apeleke kwa anayejua
kwa kuyaegemeza
kwa wanazuoni na
wala usilazimishe
neno usilolijua, ni
bora ukalipeleka kwa
anayejua.
Amesema Mtume
(s.a.w) ni mbingu
gani itakayonifunika
mimi na ardhi gani
inanihifadhi mimi,
ikiwa nitasema kwa lile
nisilolijua.
Na amepokea Ayubu
toka kwa Ubaya
Malikat, amesema
Ni ardhi gani
itanihifadhi na mbingu
gani itanifunika na
nitakwenda wapi na
nitafanya nini, pale
nitakaposema katika
kitabu cha Mwenyezi
Mungu kwa mambo
ambayo hayakutakiwa
na Mwenyezi Mungu.
Na imesihi toka
kwa Bin Masudi na
Ibnu Abbas, Yeyote
mwenye kufutu
(kujibu) katika kila
wanayo muuliza, huyo
ni mwendazimu.
Email : eg_islamic_
center39@yahoo.com

4/27/2016 12:27:49 PM

5
Banki ya Kiislamu ya Dubai
kufunguliwa Kenya
BENKI kubwa ya Kiislamu nchini
Falme za Kiarabu imetangaza
kufungua tawi lake nchini Kenya
kabla ya mwisho wa mwaka 2016.
Benki hiyo ya Dubai itakuwa
benki ya tatu ya Kiislamu
kuendesha huduma kwa mujibu wa
Shariah nchini Kenya.
Licha ya mamlaka ya benki za
Kenya kutoa leseni mpya kwa
benki na kusababisha kufungwa
kwa baadhi ya benki muhimu
nchini humo, Benki ya Kiislamu ya
Dubai inasubiri uamuzi wa mwisho
kutoka Benki Kuu ya Kenya ili
kuanzisha rasmi utoaji wa huduma
zake nchini humo.
Hivi karibuni Mwanasheria
Mkuu wa serikali ya Kenya,
Profesa Githu Muigai, alisema
serikali ya Kenya itaweka sheria
itakayosimamia taasisi za fedha
za Kiislamu kabla ya mwisho wa
mwaka huu.
Profesa Muigai aliliambia
Baraza la Kiislamu la Kenya
mjini Nairobi, kuwa serikali
inawasiliana na wadau mbalimbali
ili kuandaa rasimu ya sheria hiyo.
Alisema rasimu hiyo inatarajiwa
kuwasilishwa bungeni katika miezi
michache ijayo ili iweze kuwa sheria
mwishoni mwa mwaka huu.
Bw Muigai alisema pamoja na
kuwa mwaka 2008 Kenya iliweka
msingi wa kisheria kuruhusu
benki za Kiislamu kufanya kazi,
bado mabadiliko zaidi yanatakiwa
kufanyika ili benki hizo ziweze
kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
Tangu wakati huo benki kadha
za Kiislamu zilianza kutoa huduma
nchini Kenya na benki nyingine za
kawaida zilianza kutoa huduma
zinazotolewa na Benki za Kiislam.
Kuingia katika soko mabenki
ya Gulf African Bank na First
Community Bank kunatarajiwa
kuanzishwa kwa mara ya kwanza
mfumo kamili wa kibenki wa Sheria
kwa silimia 100.
Kuanzishwa kwa mfumo kamili
wa kibenki kwa mujibu wa sharia
kulikuwa kunasubiriwa kwa hamu
kubwa na jamii ya Kiislamu, hasa
ikizingatiwa kuwa miaka miwili
iliyopita kulizinduliwa madirisha
ya huduma za kibenki kwa taratibu
za Kiislamu katika benki kadhaa za
kawaida.
Benki za Barclays Bank (Kenya)
Limited na Kenya Commercial Bank
Limited zimekuwa zikitoa huduma
hizo za kibenki kwa mujibu wa
sheria kupitia dirisha hilo, huduma
ikiitwa, "LARIBA Banking".
Kumekuwa na ongezeko la benki
za Kiislamu katika nchi mbalimbali
duniani, hususani katika
ulimwengu wa Waislamu.
Mtaalamu wa masuala ya
fedha katika mfumo wa fedha
wa Kiislamu Bw. Mohaimin
Chowdhury anaifafanua kuwa
Waislamu husema kuwa Uislamu ni
mfumo kamili wa maisha, na si dini
ya imani tu ya kiroho.
Kwa hali hiyo, vipengele vyote
vya maisha ya mwanadamu
lazima viendane ni misingi ya
Uislamu. Hii ina maana kuwa,
mbali ya kufuata faradhi za ibada
zilizoagizwa kama vile kuswali
Swala tano, kutoa Zaka, kufunga
Mwezi wa Ramadhani na kwenda
Hija, Muislamu pia hana budi
kufuata misingi ambayo Uislamu
umeiweka, kuhusiana na mambo
mengine katika maisha ya kijamii
kwa mfano, mahusiano yake na
wengine kifamilia na kijamii, na
masuala ya kifedha.

ANNUUR NEW.indd 5

HABARI ZA KIMATAIFA

AN-NUUR

RAJAB 1437, IJUMAA APRILI 29 - MEI 5, 2016

Baada ya kujutia ya Libya

Askofu alalamikia
Obama ageuka sasa anapinga mapinduzi Syria maudhi ya ngono
kwa watoto

Rais Barack Obama (kulia). Kushoto marhuum Gaddafi.


RAIS Barack Obama amesema
itakuwa ni makosa makubwa
Jumuia za Kimataifa kuwatuma
wanajeshi wa nchi kavu
nchini Syria kumpindua Rais
Assad, kwa sababu hilo pekee
halitasuluhusiha matatizo ya
kisiasa ya Syria.
Rais Obama amesema kuwa
haina maana kwa makundi ya waasi
kama vile Islamic State ndani ya
Syria, kuendelea na makabiliano
huku akisema kuwa jeshi la taifa
hilo pekee linafaa kukomesha
mapigano nchini humo.
Hata hivyo Rais Obama
amesema kuwa itakuwa vigumu
sana kudhani kwamba suluhu
ni kumuondoa Rais Assad na
kuongeza kuwa ni muhimu
kuendelea kushambulia ngome za
Islamic State ndani ya Syria kwa
pamoja na kuzidisha juhudi za
kumaliza mapigano ya wenyewe
kwa wenyewe ya muda mrefu
nchini humo.
Aidha Bw. Obama
ametanabahisha kuwa kwa muda
wake uliosaliam madarakani,
hadhani kwamba ataweza kumaliza
tatizo la Syria.
Alisema kuwa itakuwa
vigumu kwa majeshi yake ama
hata muungano unaongozwa na
Marekani kuitokomeza kabisa
Islamic State katika kipindi cha
miezi 9 za uongozi wake.
Kwa mujibu wa taarifa ya shirika
la habari la REUTERS, Rais Obama
alisema mashambulizi yatalenga
haswa kukatiza msururu wa
wapiganaji wanaoenda Ulaya na
kusababisha maafa makubwa.
Hata hivyo kauli ya Rais Obama
imeonyesha kuwashtua wengi kwa
kuonyesha kuikubali serikali ya
Rais Assad, ambapo awali lengo la
kuibuliwa machafuko nchini humo
kupitia waasi wa IS, yanayoaminiwa
kuwa yamechochewa na Marekani
na Mataifa kadhaa ya Magharibi,
lilikuwa ni kuondoa madarakani
serikali ya Assad.
Akinukuliwa na BBC hivi
karibuni, Rais Obama alieleza
hadharani kwamba nchi yake na
washirika wake walikosea kuivamia

Libya na kumuondoa madarakani


aliyekuwa kiongozi wan chi hiyo
Mammar Gaddafi.
Rais Obama alikiri kwa mara
ya kwanza kwamba serikali yake
ilishindwa katika kutatua mzozo wa
Libya.
Alikiri kuwa kuivamia Libya
huenda ndilo kosa kubwa zaidi
alilolitenda wakati wa utawala
wake.
Akielezea majuto yake dhidi
ya Libya, Rais Obama alisema
kuwa, Marekani haikua na
mpango mahususi wa jinsi taifa
hilo litakavyotawaliwa baada ya
kuondolewa madarakani kwa
Kanali Muammar Gaddafi.
Alizungumza hayo katika
mahojiano na televisheni ya Fox
News, akibainisha mafanikio na
mapungufu ya utawala wake.
Marekani na Muungano wa
NATO zilitekeleza mashambulio ya
anga nchini Libya kwa kisingizio
cha kuwalinda raia baada ya
kuzuka maasi dhidi ya Muammar
Gaddafi mwaka 2011.
Lakini baada ya kufanikisha
mauaji ya kiongozi huyo, tangu
wakati huo hadi sasa Libya
imetumbukia katika vita vya
wenyewe kwa wenyewe kati ya
makundi ya waasi huku makundi
mawili yakiunda serikali na
Mabunge tofauti.
Katika hatua za kurejesha utulivu
serikali ya muungano wa kitaifa
inayoungwa mkono na Umoja wa
Mataifa, imewasili katika mji mkuu
Tripoli ili kuanza mipango ya
kuongoza nchi ya kurejesha hali ya
kawaida.
Rais Obama amebakisa muda wa
miezi tisa tu kumaliza muda wake
madarakani ambapo Uchaguzi
Mkuu nchini humo umepangwa
kutafanyika Novemba na Rais
Obama atakabidhi madaraka kwa
mrithi wake Januari mwakani baada
ya kuongoza kwa mihula miwili.
Wakati Obama akieleza hayo,
baada ya kusitishwa mapigano
kwa kipindi cha wiki nane, Serikali
ya Syria na waasi wameingia tena
katika mapambano makali.

ASKOFU Mkuu wa mji wa


Lyon nchini Ufaransa, amesema
kuwa kuteuliwa Makasisi
wasiofaa ndiyo sababu
inayosababisha kuongezeka
kwa vitendo vya ufisadi na
maudhi ya ngono dhidi ya
watoto nchini humo.
Kwa mujibu wa gazeti
linalochapishwa nchini humo
la Le Figaro, Kadinali Philippe
Barbarin, Askofu Mkuu wa
mjini Lyon, alitoa taarifa
Jumatatu wiki hii akitangaza
kuwa kuna makosa makubwa
yanayofanyika wakati wa
kuteuliwa Makasisi.
Taarifa hiyo imetolewa
baada ya kufanyika kikao cha
faragha kilichowajumuisha
Makasisi wapatao 200, kwa
lengo la kuchunguza kesi
zinazowahusisha baadhi ya
Makasisi wanaofanya uhalifu
wa kuwabaka watoto wadogo
nchini humo.
Taarifa hiyo ilisema kuwa
Makasisi wamefanya makosa
na uzembe mkubwa katika
utekelezaji wa majukumu
yao. Baadhi ya Makasisi
wanakubaliana na hatua ya
Kadinali Philippe Barbarin,
kutaka kujiuzulu wakati
wengine wanasisitiza juu ya
kufuatiliwa kisheria kesi za
ubakaji wa watoto kwenye
mahakama za Ufaransa.
Mahakama moja ya mjini
Lyon ilipokea malalamiko ya
familia mbili zilizoathirika na
uhalifu huo wa Makasisi dhidi
ya watoto wao na kuanzisha
uchunguzi kuhusiana na suala
hilo.
MAhakama pia imewakosoa
vikali viongozi wa Kanisa
Katoliki la Lyon, akiwemo
Kadinali Philippe Barbarin,
kwa kutotoa habari mapema
kuhusiana na uhalifu huo kwa
Mahakama.irib.

KADINALI Philippe Barbarin,


Askofu Mkuu wa mjini Lyon.

4/27/2016 12:27:51 PM

Hoja ya Juma Kilaghai

AN-NUUR

RAJAB 1437, IJUMAA APRILI 29 - MEI 5, 2016

Harufu mbaya kutoka kwenye mapafu

WIKI iliyopita tuliangalia


maeneo ambapo hutokea
harufu mbaya katika miili
yetu na sababu zake. Leo
tunamalizia mada hiyo kwa
kuangalia kundi lingine la
harufu mbaya zinazotokea
kwenye kinywa na au
pua. Hili ni lile la harufu
zinazotokea kwenye mapafu.
Harufu zinazotoka kwenye
mapafu zina vyanzo viwili.
Chanzo kimoja ni aina fulani
ya maradhi au maambukizi
yanayoweza kuwa kwenye
mapafu au kwenye viungo
vingine vya ndani ya mwili.
Chanzo cha pili ni baadhi ya
vyakula ulivyokula au vinywaji
ulivyokunywa, ambavyo
baada ya kuchakatwa huachia
gesi yenye harufu kwenye
damu. Damu iliyobeba gesi
hizi inapokwenda kwenye
mapufu huachia gesi hizi ili
zipumuliwe na kutolewa nje ya
mwili.
Magonjwa kwenye mapafu
yanayoweza kuzalisha harufu
fulani ni mengi. Miongoni mwa
haya ni saratani ya mapafu,
pumu na ugonjwa unaoitwa
cystic fibrosis kwa kitaalamu.
Ugonjwa huu ambao hutokana
na uharibifu wa geni fulani
kwenye vinasaba, husababisha
maambukizi ya mara kwa mara
kwenye mapafu. Maambukizi
haya husababisha mlundikano
wa kamasi zito linaloziba
matundu kwenye mapafu na
kumfanya mgonjwa apumue
kwa shida. Kwa kawaida harufu
inayotokana na pumu au cystic
fibrosis ina harufu ya tindikali.
Aidha, magonjwa ya viungo
vingine ndani ya mwili
yanaweza pia kuzalisha harufu
ambazo zitabebwa na damu na
kutolewa nje kwa njia ya mapafu
wakati wa kupumua. Mara
nyingi harufu hizi hutumiwa
kama dalili ya kuwepo kwa
ugonjwa fulani ndani ya mwili.
Kwa mfano mgonjwa wa
kisukari anaweza kutoa harufu
inayofanana na ya matunda
yaliyoiva sana na kuelekea
kwenye kuoza. Magonjwa ya
figo na ini pia yanaweza kutoa
harufu maalum zinazowezesha
kuyatambua kwa wepesi. Kwa
mfano, magonjwa mengi ya figo
yanaweza kumfanya mgonjwa
apumue pumzi yenye harufu ya
samaki.
Kwa bahati mbaya harufu
zinazotokana na magonjwa
yaliyomo kwenye viungo
mbalimbali siyo rahisi
kudhibitika mpaka pale
ugonjwa husika utakapobainika
na kutibiwa. Kabla hilo
halijafanyika mgonjwa inabidi
akubali tu adha ya kutumia njia
za dharura kupunguza uzito wa
hizo harufu. Njia hizo ni pamoja

ANNUUR NEW.indd 6

na kutafuna ubani (chewing


gum) na kutumia viosha kinywa
vyenye mint.
Kwa upande mwingine
harufu mbaya inayotokea
kwenye mapafu kwa sababu ya
vitu tulivyokula, kunywa au
kuvuta inadhibitika. Ni dhahiri
kabisa kuwa kuvuta sigara
kutayasababisha mapafu yako
yatoe harufu. Kiasi chochote cha
mswaki utakachopiga hakiwezi
kufika kwenye mapafu na
kuondoa harufu husika. Njia
pekee ya kuondokana na harufu
ya mapafu inayotokana na
kuvuta sigara ni kuacha kuvuta.
Harufu nyingine inayotokea
kwenye mapafu kutokana na
vitu tulivyotumia ni ile ya kilevi
(alcohol). Ni dhahiri unapotaka
kuachana na harufu hiyo ni
kuachana na matumizi ya
pombe.
Baadhi ya vyakula, mfano
vitunguu maji na vitunguu
saumu, pia huachia gesi zenye
harufu ambazo hubebwa na
damu hadi kwenye mapafu.
Wakati wa kupumua harufu
hizi hutoka nje ya mwili kupitia
kinywani na au kwenye pua.
Njia pekee ya kuachana na
harufu hizi ni kuachana na
matumizi ya vyakula hivi, na

hususan pale vinapokuwa


vibichi.
Harufu mbaya kutokea tumboni
Katika harufu zote
zinazochafua haiba ya mtu
kupitia kwenye kinywa chake
au pua yake, hakuna iliyo
mbaya kama ile ambayo chanzo
chake ni tumboni. Kwa bahati
nzuri harufu mbaya ambazo
chanzo chake ni tumbo hutokea
mara chache. Inaaminika kuwa
huenda sababu ni yale mazoea
tuliyojijengea ya kuharakisha
kuwaona wataalamu wa tiba
pale tunapohisi matatizo
yoyote tumboni. Hoja ni kuwa
tatizo ulilonalo linapopatiwa
ufumbuzi, basi harufu mbaya
ambayo ilikuwa isababishwe na
tatizo hilo nayo huondoka.
Sababu mbalimbali
zinazoweza kusababisha
harufu mbaya kutokea tumboni
ni pamoja na saratani ya
tumbo, vidonda vya tumbo,
machakato unaozaa kiungulia
((Gastroesophageal Reflux Disease),
gesi, kuziba kwa utumbo (Bowel
Obstruction), gesi, na magonjwa
yanayotokana na mfuro
(inflammation) kwenye kuta
za ndani za utumbo, kutokana
na baadhi ya vyakula na au
maambukizi ya bakteria, hasa

aina ya Clostridium difficile (C.


difficile, or C. diff).
Baadhi ya watu miili yao
haina uwezo wa kuvumilia
gluten kutoka katika ngano (na
nafaka nyingine za jamii hiyo),
pamoja na sukari aina ya lactose
kutoka katika maziwa. Matumizi
ya vyakula hivi huibua mfuro
endelevu kwenye utumbo hali
ambayo huzaa matatizo mengi
ya kiafya ikiwa ni pamoja na
hayo ya harufu mbaya. Watu
wenye harufu mbaya kinywani
au puani ambayo inaaminika
kuwa inatokea tumboni
wanaweza wakaondokana na
hali hiyo kwa kuacha kutumia
vyakula hivyo, haswa iwapo
kwa kupitia vipimo itakuwa
imebainika kuwa hawana
maambukizi ya C.dff.
Kwa bahati mbaya kama
chanzo cha tatizo lako ni
C.diff., basi ujue kuwa una
vita kubwa iko mbele yako.
Sababu ya kusema hivyo ni
kwamba C.dff. ni miongoni
mwa bakteria wagumu sana
kutibu. Viuavijasumu vingi
havina uwezo wa kuua aina
hii ya bakteria na inaaminika
kuwa badala ya kuwaua
vinawachochea kujiimarisha
zaidi na kujenga usugu.
Baadhi ya matabibu
hupendekeza kuwa badala ya
kupambana na bakteria hawa
kwa njia ya viuavijasumu ni
bora zaidi kuchukua hatua za
kuimarisha kinga za mwili na
kuuacha mwili ufanye kazi
yake ya kuwadhibiti. Njia
mojawapo ni kuongeza idadi
ya bakteria wazuri tumboni
kupitia matumizi ya vyakula
vilivyochachuliwa kama
mtindi na baadhi ya achari, au
kumeza vivunge vya bakteria
hao vilivyoandaliwa kitaalamu
(probiotics) na vinavyopatikana
kwenye maduka makubwa ya
dawa (pharmacies). Njia nyingine
ni pamoja na kuachana na
matumizi ya sukari na wanga
uliochakatwa, kunywa maji
ya kutosha, kugeuza sehemu
kubwa ya chakula chako kuwa
mbogamboga na matunda,
kuongeza matumizi ya vitamin
C kwa siku, kutumia tembe tano
hadi kumi za kitunguu saumu
kila siku, kufanya mazoezi ya
wastani walau mara nne kwa
juma, kujizuia kula hadi kushiba
sana, au bila kuwa na njaa na
kulala kiasi cha saa sita hadi
nane kwa siku.
(Juma Killaghai ni mtaalam
wa lishe, ni mtaalam wa stadi za
tiba, na pia ni mkemia mtafiti
wa bidhaa zinazotokana na
viumbe hai (Organic Natural
Products Research Chemist).
Kwa mawasiliano unaweza
kumpata kwa namba 0754281
131;0655281131;0686281131; na
0779281131)

4/27/2016 12:27:59 PM

Hoja ya Visram

AN-NUUR

RAJAB 1437, IJUMAA APRILI 29 - MEI 5, 2016

Rais Zuma afikishwa mahakamani kwa ubadhirifu

Na Nizar Visram
TAREHE 5 Aprili mwaka
huu bunge la Afrika Kusini
(AK) lilijadili na kuipigia
kura hoja ya kutokuwa na
imani na Rais Jacob Zuma
wa nchi hiyo. Kwa vile
wabunge wengi ni kutoka
chama tawala cha ANC,
matokeo yake wabunge
233 waliipinga hoja na
143 waliunga mkono.
Matokeo yake ni kuwa
hoja ilishindwa na Zuma
akasalimika. Kwa mujibu
wa katiba ya AK hoja hiyo
ilihitaji theluthi mbili ya
kura ili kumfanya Zuma
ajiuzulu.
Wakati wa kuwasilisha
hoja bungeni, kiongozi wa
upinzani, Mmusi Maimane
kutoka chama cha Democratic
Alliance (DP) alisema Zuma
anakiaibisha chama chake
cha ANC kilichoongoza
vita vya ukombozi chini
ya viongozi mashuhuri
kama Oliver Tambo, Albert
Luthuli, Walter Sisulu,
Nelson Mandela na Ahmed
Mohammed Kathrada.
Maimane akasema kati ya
vigogo hao ni Kathrada
peke yake aliyebaki, naye
amemtaka Zuma ajiuzulu.
Hii peke yake ingemfanya
Zuma aone aibu na aachie
madaraka, alisema Maimane.
Zuma amebaki madarakani,
lakini utawala wake
umeathirika sana kutokana
na kashfa iliyopelekea bunge
lijadili hoja ya kumtimua
(impeachment).
Hoja hii iliwasilishwa
bungeni baada ya mahakama
ya katiba ya AK kutoa
hukumu kuwa Zuma ana
hatia ya kukiuka katiba kwa
kutumia vibaya fedha za
umma katika kujenga makazi
yake binafsi yaliyo katika
kijiji cha Nkandla. Mahakama
hiyo pia imemuona amevunja
katiba kwa kukataa kurejesha
fedha hizo, akidai kuwa
ujenzi huo ulikuwa ni kwa
lengo la kuimarisha usalama
wake kama rais.

ANNUUR NEW.indd 7

Hapo awali tume ya


uchunguzi (Ombudsman)
ilitoa hukumu kuwa Zuma
anapaswa kulipa dola milioni
16 alizotumia kujenga makazi
yake ya Nkandla. Ndipo
Zuma akadai kuwa ujenzi
huo ulikuwa ni kwa ajili ya
usalama wake akiwa rais.
Wananchi wakashangaa iweje
bwawa la kuogelea, viwanja
viwili vya mpira, chumba
cha mazoezi ya mwili (gym)
na zizi la ngombe viwe kwa
ajili ya usalama wake? Ndipo
vyama vya upinzani vikaenda
katika mahakama ya katiba
ambayo ikakubaliana na
uamuzi wa Ombudsman.
Tarehe 31 Machi mwaka
huu mahakama hiyo ikasema
kuwa Zuma amehalifu katiba
katika matumizi ya mamilioni
ya dola yaliyotumiwa
kujenga nyumba yake
binafsi. Mazingira ya siasa
yakachafuka pale Zuma
alipokataa kulipa. Wananchi
wakapatwa na hasira mpaka
mwishowe Zuma akalazimika
kuungama na akakubali
kulipa.
Zuma (umri miaka 73),
akaonekana katika runinga
akiomba radhi na kusema
kuwa hakuwa na nia ya
kuhalifu katiba. Kisha
akakubali kulipa sehemu
ya fedha hizo. Tayari rais
huyo akaonekana mwenye
kigeugeu na ndipo upinzani
ukawasilisha bungeni hoja ya
kutokuwa na imani naye
Kati ya watu waliomtaka
ajiuzuli ni mwanaharakati
mashuhuri na mkongwe wa
ANC , Bw Ahmed Kathrada
mwenye umri wa miaka 87.
Yeye akajumuika na watu
waliotoa wito kwa Zuma
ajiuzulu. Mwanaharakati
huyo alijitokeza baada kuona
wito wa kujiuzulu kwa Zuma
umeongezeka, siyo tu kutoka
vyama vya upinzani bali
hata ndani ya ANC. Tarehe 2
Aprili Kathrada alimuandikia
Zuma barua wazi. Alianza
kwa kusema yeye hana
cheo au wadhifa bali ni
mwanachama mwaminifu wa
ANC, akiwa mwanaharakati
wa chama hicho tangu utotoni
mwake miaka ya 1940. Kisha
anaongeza kuwa wakati wa
vita vya ukombozi alijihusisha
na jeshi la ukombozi la
ANC Umkhonto we Sizwe.
Kutokana na harakati zake za
kupinga ukaburu mwaka 1952
alihukumiwa na wenzake 20
kifungo cha nje cha miaka
miwili. Kisha makaburu
wakamfunga gerezani mwaka
1956 hadi 1961. Halafu
mwaka 1964 yeye na wenzake
wakafungwa kifungo cha

maisha katika kisiwa cha


Robben. Gerezani alikuwa
na wenzake kina Walter
Sisulu na Nelson Mandela.
Walifunguliwa mwaka
1989 baada ya makaburu
kulazimishwa kuondoka
madarakani.
Hii ndio sifa ya Kathrada
aliyoelezea katika barua
aliyomuandikia Rais Zuma.
Anasema sababu ya kuandika
barua hiyo ni kuwa Zuma,
kwa kubaki madarakani,
anasababisha wananchi
kukosa imani na chama
cha ukombozi cha ANC na
serikali yake.
Akamwambia:
Komredi Zuma, ingawa
maishani mwako umechangia
katika harakati za ukombozi
wa nchi yetu, lakini
mchango huo utaingia doa
iwapo utaendelea kubaki
madarakani licha ya kashfa
kadha zinazokuandama.
Moja ya kashfa hizo ni
kuwa Zuma anashirikiana
mno na matajiri na
wawekezaji, kiasi kwamba
ndio wanaomuamulia mambo
ya kiserikali. Anawaamini
wao kuliko watu wake.
Kwa mfano, hivi karibuni
ripoti imekuwa ikienea
kote kuwa Zuma alikuwa
na uhusiano wa karibu na
tajiri aitwae Gupta. Mnasaba
wao ulifikia mahali ambapo
inasemekana hata uteuzi
wa mawaziri ukifanywa na
Gupta.
Hii ilidhihirika baada
ya naibu waziri wa fedha
alipodai kuwa Gupta
alimuahidi cheo cha uwaziri
kamili. Naibu huyo hakuweza
kuamini kuwa anapandishwa
cheo si na rais wake aliyemteua
bali na mwekezaji!
Gupta alihamia Afrika Kusini
kutoka India mnamo 1993
alipoona kuna fursa nzuri ya
kutajirika baada ya nchi hiyo
kujikomboa kutoka makucha
ya makaburu. Leo anamiliki
kampuni kadha zikiwemo
za migodi, mawasiliano na

vyombo vya habari.


Mfano mmoja wa uhusiano
wa Gupta na Zuma ni
kuwa mtoto wa Zuma ni
mkurugenzi wa bodi katika
kampuni zaidi ya sita za
Gupta. Maisha yao ni ya
anasa kiasi kwamba familia ya
Gupta ilikuwa na sherehe ya
harusi na wageni wakaalikwa
kutoka India. Ndege maalum
ikakodiwa kuwaleta na ikatua
uwanja wa jeshi la anga la
Afrika Kusini badala ya
uwanja wa kawaida. Yaani
jeshi la anga linalinda ndege
ya Gupta.
Wananchi wakaona kuwa

serikali ya Zuma ilikuwa


imebinafsishwa. Ndio maana
aliyekuwa waziri wa fedha,
Bw Pravin Gordhan akadiriki
kusema Ni lazima tuamke
na kuzuia nchi yetu isije
ikaporwa.
Wakati hoja ilipokuwa
ikijadiliwa bungeni, kambi
ya chama tawala cha
ANC ilimtumia Mwalimu
Nyerere ili kumlinda Zuma.
Walimnukuu Mwalimu
akiwaambia mabalozi wa
magharibi jijini Dar es Salaam
mnamo 1978 kuwa waache
kuzichukulia nchi za Kiafrika
kama makoloni yao.
Kambi ya upinzani
ikajibu kuwa aliyosema
Mwalimu ni sawa lakini yeye
hakuwalinda wabadhirifu
na mafisadi. Walisema kama
Mwalimu angekuwa hai hii
leo angeungana na Kathrada
kumtaka Zuma ajiuzulu, kwa
sababu wananchi wa Afrika
Kusini hawakutoa mhanga
roho zao ili rais wao atumie
fedha zao kwa manufaa yake
binafsi.
Ni vizuri tukajiuliza, je
tunajifunza nini kutoka
sakata hili la Zuma? Kwa
maoni yangu, ni muhimu
kujua kuwa Zuma si peke
yake katika bara letu.
Nchi zetu zina watawala
wanaofuja mali ya umma
au wanaopora utajiri wetu.
Aghlabu katiba inawalinda
wasifikishwe mahakamani
wanapokuwa madarakani au
hata wanapostaafu. Katiba
ya Afrika Kusini inaruhusu
rais wa nchi afunguliwe
mashitaka na mahakama ya
huko inaweza ikatoa hukumu
dhidi ya rais bila ya woga.
Kama inawezekana huko
Kusini, kwanini isiwezekane
kwengineko?
Mwandishi na
mwanaharakati mashuhuri,
Frantz Fanon, katika kitabu
chake cha The Wretched
of the Earth (mafukara wa
ulimwengu) alisema viongozi
wa Kiafrika wanapaswa
kuwaeleza wananchi ukweli,
kujifunza kutoka kwao, na
kuwa pamoja nao. Na si
Afrika tu, bali ulimwenguni
kote. Kumekuweko na wito
wa kuwafikisha mahakamani
watu kama Bush, Blair na
Netanyahu kwa makosa
ya uhalifu wa kivita na
jinai dhidi ya binadamu.
Bahati mbaya mahakama ya
kimataifa (ICC) ni wepesi
sana kuwahukumu watu
kama rais Kenyatta lakini
haiwagusi watawala wa
Magharibi.
(nizar1941@gmail.com0713-562181)

4/27/2016 12:28:02 PM

Kalamu ya Ghassani

AN-NUUR

RAJAB 1437, IJUMAA APRILI 29 - MEI 5, 2016

Hatujaila keki yetu wala hatunayo!

Na Mohammed Ghassani
NIMETUMIWA ujumbe katika
simu ya mkononi usemao: you
can not eat your cake and have
it, soma e-mail. Nilipofungua
akaunti yangu ya barua-pepe,
nikakuta ufafanuzi wa ujumbe
huo. Kumbe nilikuwa nasutwa
kwa kuandika makala iliyopita
katika safu hii.
Nikumbushe kuwa katika
makala hiyo, nilikuwa nimempa
heshima yake mkereketwa wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM)
hapa Zanzibar, Mohammed Raza
Dharamsi, kwa uthubutu wake
wa kuitetea Zanzibar dhidi ya
ukandamizwaji inayofanyiwa
kwa jina la Muungano.
Nimesutwa kwamba nilikwenda
mbali mno katika kuipa maana
hatua ile ya Raza. Kwamba
aidha nilikuwa ninamkuza sana
asivyostahili au nimepotosha
kile hasa alichokikusudia.
Nimehojiwa pia kwamba
nahalalisha bendera ya Zanzibar
hali nikijuwa vyema kwamba
kuwepo kwake ni hatari kwa
Muungano.
Nikaambiwa kuwa mimi na
Raza hatuwezi kuizungumzia
Zanzibar kama nchi baki, huku
tukijuwa kuwa ilijiingiza kwa
hiari yake kwenye Muungano.
Kwamba hatuwezi kuzungumzia
Zanzibar yenye nguvu zaidi au
kwa maneno yake Zanzibar
iliyo Zanzibar zaidi ya hivi
ilivyo sasa halafu wakati
huo huo tukasema tu waumini
wa Muungano. Huko, mbali ya
kuwa ni kwenda kinyume na
katiba, bali pia ni utoto wa kuila
keki yetu, kisha tukataka tubakie
nayo!
Ukweli ni kuwa makala hiyo
inayozungumziwa haikuwa
imejikita hasa katika bendera
ya Zanzibar wala kuonesha
upinzani kwa Muungano.
Nilichojaribu kufanya ni
kuonesha mshikamano wangu
na Mzanzibari mwenzangu
kwa ajili ya Watani wetu,
Mama yetu Zanzibar. Lakini
nachukulia ujumbe ule kama
njia ya kunifanya niseme zaidi
kuhusu kizungumkuti hiki cha
uhusiano wa Tanganyika na
Zanzibar kupitia Muungano
tulionao. Nami hakuna jambo
nisilolionea haya kulisema kama
hilo. Sijawahi kujihisi vibaya
kujitambulisha kwa Uzanzibari
wangu popote pale na, kwa
hivyo, sioni tabu kuutetea dhidi
ya chochote na yeyote. Basi,
ikiwa aliyenitumia ujumbe

ANNUUR NEW.indd 8

anasema kuwa mtu hawezi kuila


keki yake na akabakia nayo,
mimi nakusudia kuhoji kuwa
Muungano wetu umeonesha
uwezekano wa mtu mmoja kuila
keki yake na kuendelea kuwa
nayo, huku mwengine kutokuila
kabisa lakini pia asiwe nayo!
Uwezekano huo, kwa
mfano, ndio ulioipa uthubutu
Tanganyika, kwa jina la
Muungano, kuyaendea kinyume
au kuyavunja Makubaliano ya
Muungano (Articles of Union)
kwa kisingizio cha kuimarisha
Muungano huo. Makubaliano
haya ya Muungano ndiyo
msingi na sehemu muhimu ya
katiba ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania. Kuyavunja
haimaanishi tu kuvunja katiba,
bali pia ni kuwatovukia adabu
Watanganyika na Wazanzibari
wote.
Mkataba wa makubaliano
hayo ulisainiwa na waasisi wake
ukiwa na vipengele kumi na
moja tu, leo hii vipengele vya
Muungano ni zaidi ya ishirini na
mbili. Maana yake ni kwamba
vimeongezeka kwa zaidi ya
asilimia mia moja, na bahati
mbaya ni kwamba vingi ya
hivyo, kwa makusudi kabisa,
vimewekwa kupoteza nguvu na
hadhi ya Zanzibar.
Siandiki kama mtaalamu
wa masuala ya sheria, maana
mimi siye. Wala siandiki
kama mwanasiasa anayetetea
maslahi yake, maana sinayo.
Lakini mimi, kama walivyo
Wazanzibari wengi, ni
mtu ninayeziangalia siasa
zilizouzunguka Muungano
huu kwa mashaka. Nazishuku,
na nitathibitisha shaka yangu,
kwamba ni siasa zinazoitukuza
Tanganyika kwa kuidhalilisha
Zanzibar.
Naitaja Tanganyika kwa
kuwa Tanganyika haikufa, bali
ambayo imekuwa ikiendelea
kuuliwa katika Muungano huu
ni Zanzibar. Ni Zanzibar ndiyo
ambayo imeendelea kupoteza
na kupoteza, kadiri Muungano
huu unavyoimarika. Lakini
hatupotezi kwa kuridhia.
Nasisitiza tena kwamba
hatujapata kuridhishwa hata
kidogo na namna ambavyo
Tanganyika imekuwa ikiutumia
Muungano huu dhidi yetu,
kama nchi na kama mshirika
muhimu katika Muungano
wenyewe. Tunalazimishwa tu.
Na, kwa hakika, mtu wa
mwanzo kutufanya hayo,
alikuwa ni Mwalimu Julius
Nyerere mwenyewe, ambaye
anachukuliwa kuwa ni mwasisi
wa Muungano na, hivyo,
kimsingi angelitarajiwa kuwa
mtu wa mwanzo kuyaheshimu
makubaliano baina yetu na sio
kuyakengeuka. Nitatoa mifano.
Kuna kitu kinaitwa Misingi
Mikuu ya Muungano, kama
ilivyoorodheshwa na Kamati
Maalum iliyoteuliwa na Rais
wa Zanzibar wa Awamu ya
Tano kupendekeza Muundo
Muafaka wa Muungano.

PICHA maarufu inayoitwa ya utiaji saini Hati za Muungano


baina ya Rais Abeid Karume (kulia) na Mwalimu Julius Nyerere
(kushoto). Ni kweli Karume alisaini Makubaliano ya Muungano
kama yanavyotekelezwa leo na Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania?
Kwanza ni kuwepo kwa
washirika wanaoonekana wazi
katika utekelezaji wa shughuli
za Muungano na, pili, washirika
hao kuwa na uwezo sawa katika
maamuzi.
Uwepo na uwezo huo
hudhihirika kwa washirika
hawa kuwa na kauli sawa
wakati wa kufanya maamuzi,
katika kutafuta suluhisho la
matatizo na pia kuwa na fursa
sawa ya kuzijadili, kuzitunga na
kuzipitisha sheria zinazohusu
mambo ya Muungano kitaifa
na kimataifa. Nini alikifanya
Mwalimu Nyerere? Chini ya
mwezi mmoja tu, baada ya
kutiwa saini kwa Makubaliano
ya Muungano, alianza
kuipopotowa Zanzibar kwa
kutunga sheria ya kuzibatiza
jina la Muungano shughuli
zote za Tanganyika ambazo
hazikuwa katika yale mambo 11
ya Muungano. Kati ya sheria hizi
ni ile iliyoitwa The Transitional
Provision Decree (N0. 1) ya
mwaka 1964, ambayo iliwapa
uhamisho wafanyakazi wote wa
serikali ya Tangayika na kuwa
wa serikali ya Muungano. Kwa
sheria hii, ndio Mahkama kuu
ya Tanganyika ikafanywa kuwa
Mahkama Kuu ya Tanzania.
Sheria hiyo ilichapishwa katika
Gazeti la Serikali la tarehe
01.05.1964. Bado Muungano
mbichi!
Wiki mbili baada ya hapo,
yaani tarehe 15.05.1964,
akachapisha sheria nyengine
iliyoitwa The Transitional
Provision Decree (No. 2) ambayo
ilielekeza kuwa kila pale
penye neno au kumbukumbu
inayosomeka Tanganyika sasa
pasomeke Serikali ya Muungano
wa Tanzania.
Ni vipi sheria hizi mbili
ziliikosea Zanzibar? Ni kwamba
yule mshirika wa Zanzibar
katika Muungano (Tanganyika)
sasa alikuwa ametoweka na
hivyo Zanzibar haikuwa na
upande wa kujadiliana nao

panapohusika mambo ya
Muungano. Kwa hivyo, hata lile
agizo lililokuwemo katika Katiba
ya Muda kwamba Tanganyika and
Zanzibar are one United Sovereign
State likabadilika na sasa ikawa
Tanzania is one State and is a
Sovereign United Republic,
ambayo ndiyo iliyomo hadi
sasa, na ndiyo inayotajwa na
hao wanaodai kuwa Zanzibar
kuwa na bendera yake ni
kuvunja katiba. Kumbe tamko
hili lenyewe liko kinyume na
misingi ya Muungano, ambayo
ni sehemu muhimu ya katiba
yenyewe.
Kuanza hapo haikuwa tena
ajabu wala aibu kwa vikao
vya chama na serikali kukaa
Chimwaga kwa jina la Tanzania,
kupitisha maamuzi yoyote
wanayoyapendelea wakubwa wa
Tanganyika, bila ya kuzingatia
upande wa pili wa Muungano.
Lakini ikawa ni dhambi kubwa
kwa Wazanzibari kukaa na
kuizungumzia khatima ya
nchi yao ndani ya Muungano.
Hata viongozi waliowekwa
au kutumwa na Wazanzibari
wenyewe walipothubutu
kufanya jambo ambalo
lingelimaanisha kuitutumua
Zanzibar, basi kifimbo cha
Mwalimu Nyerere kiliwachapa.
Hicho ndicho kifimbo
kilichowachapa akina Aboud
Jumbe, Maalim Seif Sharif na
Salmin Amour.
Hizi ndizo siasa za Muungano
huu, za mkubwa kummeza
mdogo, za mbinu na hila na
vituko na vitimbi. Mambo
haya, bila ya shaka, ndiyo
ambayo yamekuwa yakiwatia
khofu Wazanzibari kuhusiana
na khatima ya nchi yao katika
Muungano. Kuna kauli maarufu
sana ya kumezwa kwa Zanzibar
na kufutwa kabisa. Inasemwa
kuwa hii ndiyo sera ya siri
ya CCM, ingawa wenyewe
wanalikanusha hilo. Lakini
mtiririko kama huo wa matukio
Inaendelea Uk. 14

4/27/2016 12:28:04 PM

9
Na Abuu Nyamkomogi
JUMAMOSI ya tarehe
16.04.2016 nikiwa mkoani
Kagera nilipokea katika simu
yangu ya mkononi ujumbe
mfupi wa maandishi mara
baada ya swala ya alfajiri,
kutoka kwa aliyewahi kuwa
Mudiir wa muda mrefu katika
Kituo cha Kiislamu cha Kulelea
Mayatima (IYF) kilichopo
wilayani Ilemela jijini Mwanza,
Sheikh Nasib Issa, uliosomeka
hivi:
Innaalillaah wainnaa ilayh
rajiuun. IDD MUSSA KATIMBA
amefariki dunia usiku huu
mazishi ni kesho Mabatini,
Mwanza.''
Huo ulikuwa ni ujumbe wa
kwanza kabisa, kati ya jumbe
kadhaa nilizotumiwa kwa
siku hiyo, kunitaarifu kuhusu
msiba wa mmojawapo wa
wanaharakati wa Kiislaamu
wa muda mrefu katika jiji
la Mwanza. Mara baada ya
kupokea ujumbe huo na
kuuhakiki, sikuwa na namna ya
kufanya kwa muda huo zaidi ya
kusema:
Innaa lillaahi wainnaa
ilayhi raajiuun. Kisha nami
nikaanza kuwataarifu, baadhi
ya Waislamu wanaomfahamu
marehemu, kwa kadri
nilivyojaliwa. Hata hivyo,
sikujaaliwa kushiriki si mazishi
wala maziko yake kwa kuwa
katika kipindi hicho sikuwako
jijini Mwanza.
Taazia ya mwanaharakati
huyu ilinifanya niyakumbuke
majina ya wanaharakati
wengine wanne wa jijini humo
ambao aliungana nao mnamo
1991 kuelekea jijini Dar es
Salaam kuhudhuria semina
ya kutathmini maendeleo
ya Uislamu nchini pamoja
na kuratibu harakati za
maendeleo ya Waislamu
nchini iliyoandaliwa na
kuratibiwa na Kituo cha
Kueneza Uislamu nchini-Islamic
Propagation Centre (IPC).
Majina ya wanaharakati hao,
alioshirikiana nao marehemu
Katimba, waliokuwa wajumbe
au wawakilishi wa Waislamu
wa mkoa wa Mwanza katika
semina ile ni pamoja na Mzee
Miraji Mbwana, Ustadh Hussein
Yasin, Ustadh Haruna Cheyo
pamoja na Bw. Abdallah Amin
ambaye ni mtoto wa aliyewahi
kuwa Sheikh wa kwanza wa
mkoa wa Mwanza aliyefahamika
kwa majina ya Sheikh Amin
Abdallah.
Semina hiyo iliyofanyika
kwa juma moja kuanzia Januari
12-18, 1991 na kuhudhuriwa
na marehemu Katimba pamoja
na wanaharakati hao wengine
niliowataja. Kwa wasiofahamu,
hiyo ilikuwa ndiyo semina
iliyozalisha chachu ya kuratibu,
pamoja na mambo mengine,
harakati za maendeleo ya
kielimu ya Waislamu nchini
na ndio iliyochangia kwa kiasi
kikubwa kuibuka kwa baadhi ya
shule za zamani na hata za sasa
za Kiislaamu nchini ikiwemo,
pamoja na shule nyingine,
shule ya msingi ya Kiislaamu ya
Thaqibu na shule ya sekondari

ANNUUR NEW.indd 9

Makala

AN-NUUR

RAJAB 1437, IJUMAA APRILI 29 - MEI 5, 2016

Buriani Idd Katimba

MARHUUM Idd Mussa Katimba (wa pili kulia).


ya Kiislaamu ya Nyasaka, zote
za jijini Mwanza. Kadhalika
semina hii, ndio iliyopitisha
azimio la kuanzishwa gazeti
hili la Kiislaamu la AN-NUUR
ambalo kwa taufiki ya Allah
(S.W.) lilifanikiwa kusajiliwa na
kuanza kutoka rasmi mnamo
mwezi Agosti, 1991 pamoja na
shule ya sekondari ya Kiislaamu
ya Ubungo ambayo ilianza rasmi
mnamo Januari, 1992.
Tunamuomba Allah (S.W.),
kwa jitihada zake hizi za
kushiriki, kwa niaba ya
Waislamu wa mkoa wa Mwanza,
katika semina ile adhimu na ya
kihistoria ya 1991 ya kutathmini
maendeleo ya Uislamu nchini
pamoja na kuratibu harakati
za maendeleo ya kielimu ya
Waislamu nchini, amghufirie
dhambi zake na amjazie
penye upungufu katika amali
zake. Allaahumma ghfirlahu
warhamahu waskanahu fil
Jannat. Allaahumma inkaana
muhsinan fazid fii hasanaatihi.
Wainkaana musiian, fatajaawaz
anhu.
Wakati wa uhai wake,
marehemu Katimba alishiriki
katika harakati mbalimbali za
Kiislaamu ikiwa ni pamoja na
semina za uongozi kwa viongozi
wa Kiislaamu pamoja na ujenzi
wa vituo mbalimbali vya elimu
vya Kiislaamu vya ndani na
nje ya jiji la Mwanza. Miongoni
mwa vituo hivyo ni pamoja na
shule za sekondari Ubungo,
Thaqaafa, Kirinjiko pamoja na
Nyasaka. Mojawapo ya semina
za kiuongozi inayoelezwa
kuhudhuriwa na marehemu
Katimba ni ile iliyofanyika
mnamo Desemba, 2013 katika
kituo cha elimu cha Kiislaamu
Kirinjiko na iliwajumuisha
viongozi kadhaa wa baadhi ya
taasisi za Kiislaamu ambapo
uongozi wa shule ya sekondari
na madrasat Thaqaafa
uliwakilishwa na marehemu
Katimba katika semina ile.
''Nakumbuka 2013 mimi na
maustadh wenzangu wawili

kutoka Thaqaafa tulikwenda


na mzee Katimba kuhudhuria
semina kule Kirinjiko'', anaeleza
mmoja wa maustadh aliyewahi
kuwa Mudiir katika madrasa
hiyo, ambaye yeye na maustadh
wenzake walishiriki katika
semina ya ufundishaji wa
masomo ya lugha Kiarabu na
Maarifa ya Uislamu wakati
ambapo marehemu Katimba
alishiriki katika semina ya
viongozi wa taasisi za Kiislaamu.
Aidha, marehemu Katimba
alifanya jitihada za kila
namna kuhakikisha vijana
mbalimbali wa Kiislaamu
wanapata elimu katika vituo
vyao hivi, hilo linathibitishwa
na Bw.Hamad Khamis (38)
ambaye ni mmojawapo kati ya
wanafunzi wawili wa mwanzo
kabisa kutoka jijini Mwanza
waliopata fursa ya kujiunga na
shule ya Kiislaamu ya Ubungo
mnamo 1992, ambapo alimtaja
mwenzake waliyejiunga naye
katika shule hiyo kwa jina moja
la Abdallah, kupitia mikononi
mwa Idd Katimba.
''Sikiliza ndugu yangu, mzee
huyu (Marehemu Katimba)
ndiye aliyefanya jitihada za kila
namna kwa kushirikiana na
baadhi ya Waislamu kunipeleka
mimi na Abdallah (mwanafunzi
mwenzake waliojiunga naye
shule ya Kiislaamu ya Ubungo)
Ubungo Islamic 1992 kwa ajili
ya masomo ya sekondari, kwa
kweli nitamkumbuka daima kwa
hilo.
Anaeleza kijana huyo
anayeishi wilayani Kahama
kwa sasa ambaye mwandishi
wa makala haya alikutana naye
siku ya tatu baada ya maziko
nyumbani kwa marehemu eneo
la mabatini jijini Mwanza.
Aidha, inaelezwa kwamba
marehemu Katimba alikuwa ni
mtu mwenye kujali na kuguswa
sana na matatizo mbalimbali
yanayowakabili Waislamu
wenzake na kuyatafutia
ufumbuzi; ama kwa jitihada
zake binafsi au kwa kushirikiana

na Waislamu wenzake; kwa


kadri ya uwezo wake. Ithibati
ya jambo hili inatolewa na
kijana yatima Amri Idd Katimba
ambaye kwa sasa ni mhitimu
wa Shahada ya Sheria katika
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
aliyelelewa na marehemu
Katimba kwa muda wa miaka
ishirini na ambaye bado alikuwa
chini ya ulezi na usimamizi
wake hadi umauti ulipomkuta
katikati ya mwezi huu. Kijana
huyu ambaye kitaaluma ni
mwanasheria, ana umri wa
miaka ishirini na minne (24) kwa
sasa alimsimulia mwandishi wa
makala haya namna marehemu
Katimba alivyomchukua akiwa
yatima baada ya wazazi wake
kufariki dunia na kuanza
kumlea yeye mwenyewe tangu
akiwa na umri wa miaka minne
hadi sasa.
Kijana huyu baada ya kufiwa
na wazazi wake akiwa na umri
wa miaka minne. Marehemu
Idd Katimba alibeba jukumu la
kumchukua kijana huyu ambaye
baba yake mzazi alifahamika
kwa jina la Ali Idd, na kwenda
kuishi naye nyumbani kwake.
Alikuwa akimpatia malezi ya
kimwili, kiakili na kiroho. Kwa
lugha nyingine Marehemu
Katimba alikuwa akisimamia
lishe, taaluma na maadili
ya kijana huyu hadi kipindi
alipoaga dunia majuma
mawili yaliyopita. Kijana huyu
alipofikia umri wa kwenda
shule aliandikishwa kwa ubini
wa marehemu ambao ndio
anautumia hadi sasa, na ndiyo
sababu ya yeye kuitwa Amri
Idd Katimba badala ya Amri Ali
Idd. Hata hivyo, sikumuuliza
zaidi juu ya suala hili kwa kuwa
halikuwa lengo la msingi la
makala haya.
Chini ya ulezi na usimamizi
wa marehemu Katimba, kijana
huyu alifanikiwa kupata elimu
ya mazingira na ile ya muongozo
kupitia vituo kadhaa vya
elimu. Kijana huyu alichukulia
masomo yake ya elimu ya
msingi katika shule ya msingi
Lake iliyopo eneo la Isamilo
jijini Mwanza; masomo yake
ya elimu ya sekondari katika
shule ya sekondari Thaqaafa
iliyopo mtaa wa Unguja jijini
Mwanza; na masomo yake ya
elimu ya juu katika Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam kilichopo
wilaya ya Kinondoni jijini
humo. Aidha, wakati kijana
huyu akiendelea na masomo
yake ya elimu ya mazingira
alikuwa pia akichukua masomo
yake ya elimu ya muongozo
katika madrasa mbalimbali
zikiwemo madrasat Arafa
iliyoko katika msikiti wa Arafa
mabatini walikokuwa wakiishi
pamoja na madrasat Thaqaafa
sehemu ambayo ndiko alikokuja
kuchukulia masomo yake
ya elimu ya sekondari hapo
baadae. Kwa upande wa elimu
ya muongozo kijana huyu kwa
sasa ana kiwango cha elimu ya
mutawassitu.
Wakati kijana huyu alipokuwa
akisoma, Matokeo yake
kitaaluma yalikuwa mazuri na
yenye kuridhisha kiasi ambacho
Inaendelea Uk. 15

4/27/2016 12:28:09 PM

10

MAKALA
Na Omar Msangi

HIVI karibuni baadhi


ya vyombo vya habari
vimekariri maneno ya
aliyekuwa Waziri wa Mambo
ya Nje wa Marekani (U.S.
Secretary of State) Madeleine
Albright, akisema kuwa Rais
wa Urusi Vladimir Putin,
ni mtu muovu. Aliyasema
maneno hayo mwaka 2000
muda mfupi baada ya Putin
kuchukua madaraka kutoka
kwa Boris Yeltsin. Kubwa
zaidi akionyesha kuwa uovu
wa Putin ni kuwa ana uwezo
wa kuhatarisha maslahi ya
Marekani kupitia EU na
NATO katika Ulaya.
Hivi karibuni kigogo
mmoja wa siasa za Urusi
Alexey Pushkov akihojiwa
juu ya kauli hiyo ya Albright
akasema kuwa, Urusi
haishughulishwi nini kasema
Albright, muhimu ni kuwa
kwa lolote itakalotaka
kufanya Marekani, haiwezi
kujifanyia tu kwa kujifanya
mwamba wa dunia, lazima
izingatie kuwa kuna Urusi.
La kuzingatia hapa ni
kuwa wakati Madeleine
Albright anamwambia Putin
ni muovu, ni muda mfupi tu
uliopita alitoa kauli akisema
kuwa watoto nusu milioni
wa Iraq waliokufa, ilikuwa
ni kafara halali kwa ajili ya
hicho walichotaka Marekani.
Itakumbukwa kuwa kutokana
na vikwazo ilivyowekewa
Iraq Agosti 6, 1990 hadi
Mei 2003, mamilioni ya
watu walikufa kutokana na
njaa na kukosa matibabu.
Alipohojiwa na waandishi
wa habari juu ya ubaya wa
vikwazo hivyo kutokana na
madhara yake kwa wananchi
wa Iraq, Madeleine Jana
Korbel Albright alijibu kwa
sentensi fupi tu: we think the
price is worth it.
Swali kutoka kwa
mwandishi Lesley Stahl
lilikuwa kwamba vikwazo
ilivyowekewa Iraq vimeuwa
watoto nusu milioni, idadi
ambayo ni kubwa kuliko
watoto waliokufa kutokana na
bomu la atomiki Hiroshima.
Is the price worth it?"
Aliulizwa.
Kufa watu nusu milioni!
Kwa Madame Madeleine Jana
Korbel Albright, ni gharama
halali ya kupata masilahi ya
Marekani pale Iraq! Sasa huyu
ndiye anamwita Putin real
evil man!
Ila kama alivyosema
Pushkov, kosa la Putin na

ANNUUR NEW.indd 10

AN-NUUR

RAJAB 1437, IJUMAA APRILI 29 - MEI 5, 2016

Mafia Style:

Baada ya urafiki
msiba juu ya msiba

RAIS Vladmir Putin wa Russia (kulia) na Bi. Madeleine Albright.

Urusi kwa ujumla, ni kuwa


wanataka kujifanya nao
miamba wa dunia kama
wanavyofanya sasa hivi

upya kurasa 28 za siri za


ripoti ya Septemba 11 kama
familia za wahanga na jamii
ya Wamarekani kwa ujumla

kuizuiya Marekani/NATO na
mpango wake na ISIS katika
Syria.
Tukiachana na siasa hizo
za kutunishiana misuli za
wababe, zipo zile za Marekani
na Saudi Arabia. Siasa za
mkubwa kumfanya mdogo
tambara, kichaka, kibaraka
na mtumwa. Mapema wiki
iliyopita Rais Barack Obama
amesema kuwa hivi sasa
maofisa wa ngazi za juu wa
Idara za Usalama, wanapitia

MFALME Salman
inavyotaka. Kinachotakiwa
ni kuwa kurasa hizo ziwekwe
hadharani (declassification).
28 pages ni kurasa
ambazo zinadaiwa
kunyofolewa kutoka ripoti
maalum juu ya Septemba 11,
na inadaiwa kuwa kurasa
hizo zimeondolewa na
kufanywa siri kubwa kwa
sababu zinaihusisha Saudia
Arabia. Kwamba zinafichua
kuwa Saudi Arabia, kama
Serikali, na baadhi ya watu

wa nyumba ya kifalme
(royal family), walihusika
katika shambulio la kigaidi
lililoporomosha majengo
pacha ya-WTC na kuuwa
watu wanaokadiriwa kufikia
4000.
Mbunge wa zamani,
Seneta Robert Graham, ,
ambaye alishiriki uandishi
wa ripoti ya serikali juu ya
Septemba 11, akihojiwa na
CBS (CBS This Morning/CBS
Evening News) hivi karibuni,
anasema kuwa kurasa hizo 28
ambazo zimefichwa zinaweza
kufichua uhusika wa Saudia
katika kuwasaidia magaidi
walioteka ndege wakapiga
World Trade Center, New
York na nyingine kugonga
Pentagon, huku ndege ya tatu
ikianguka kule Pennsylvania
tarehe 11, Septemba 2001.
How US Covered Up Saudi
Role in 9/11, ni Makala na
uchambuzi uliofanywa na
Paul Sperry juu ya hizi kurasa
28. Katika Makala hiyo
mwandishi ananukuu taarifa
za vyombo vya usalama
juu ya uhusika wa Saudi
Arabia kupitia ubalozi wake
Washington na jinsi serikali
ya Marekani ilivyowaziba
mdomo na kuwashika mikono
FBI na CIA kuchunguza
suala hilo. Mwandishi Sperry
anasema kwamba alifanya
mahojiano na kachero wa
kikosi cha kupambana na
ugaidi- Joint Terrorism Task
Forces (JTTF), Washington
na San Diego, ambaye
alimwambia kuwa kulikuwa
na mawasiliano ya karibu
baina ya magaidi waliokuwa
wamepiga kambi San Diego
na Ubalozi wa Saudia,
Washington na kwamba ni
Prince Bandar bin Sultan bin
Abdulaziz Al Saud, ambaye
wakati huo alikuwa Balozi wa
Saudia Arabia, Washington,
ambaye alimpelekea mmoja
wa magaidi aliyekuweko
San Diego kiasi cha Dola
130,000. Na kwa sababu hiyo,
kama alivyosema kachero
wa FBI John Guandolo,
ilikuwa Bandar awe gaidi
mtuhumiwa namba moja wa
9/11. Hata hivyo, kinyume
chake, wakati Wamarekani
bado wakiwa hawajaanua
tanga la msiba wa Septemba
11, Bandar akaonekana
akiwa na Rais Bush tarehe 13
mwezi huo huo wa Septemba
wakivuta cigar pale Truman
Balcony na baada yapo
baadhi ya wanafamilia wa
Bandar na Osama bin Laden,
wakasaidiwa na idara za
Inaendelea Uk. 11

4/27/2016 12:28:14 PM

11
Inatoka Uk. 10
usalama kurejea Saudi Arabia.
Anasema kachero wa FBI
Mark Rossini, kwamba ni
Ikulu ya Marekani iliyozuiya
kukamatwa watuhumiwa
wakuu wa familia ya kifamle,
akiwemo Prince Bandar
Sultan bin Abdulaziz Al Saud.
FBI waliziba kabisa
masikio kila walivyotajwa
Wasaudia. Ilikuwa kaa la
moto kuwagusa. Alisema
Afisa mmoja wa Polisi (Fairfax
County) Lt. Roger Kelly.
Akizungumzia jambo hilo,
mmoja wa makamishna wa
Tume ya 9/11, John Lehman,
anasema kuwa ilikuwa
ni jambo la kushangaza
kwamba magaidi walikuwa
na uhusiano wa karibu
na Balozi Bandar, mkewe
Bandar halikadhalika ofisi
inayohusika na mambo ya
Kiislamu (Islamic affairs office)
katika ubalozi wa Saudia
ndani ya Washington. Hata
hivyo, la kushangaza na
kutisha zaidi ni kuwa serikali
ya Marekani haitaki kurasa
za uchunguzi zinazoihusisha
Saudia, ziwekwe hadharani.
(Soma pia: 9/11, The 28 Pages,
The CIA & The Art of the
Hangout).
Katika ujumla wake,
kinachoelezwa ni kuwa
Saudi Arabia ni mtuhumiwa
namba moja wa shambulio la
kigaidi Septemba 11, lakini
Saudia imekuwa na msuli wa
kuizuiya Marekani kufunua
mdomo!
Gazeti la New York Times
likizungumzia jambo hili
likasema: Saudis Tell U.S. To
Back Off Bill On 9/11 Lawsuits.
Swali hapa ni je, tangu
lini Marekani ikapokea amri
kutoka Saudi Arabia? Au
kama anavyouliza Kristen
Breitweiser, katika Makala
yake, Saudi Arabia Coerces US
Over 9/11:
When did the U.S.
government start taking orders
from foreign nations? Have we
become a foreign territory of the
Kingdom of Saudi Arabia? Did
Saudi Arabia somehow become a
branch of the U.S. government
with sway over the President,
Congress, and the Judiciary?
Ukizungumzia Putin
au Xi Jinping kuitunishia
msuli, Washington, ni jambo
linaloeleweka, lakini sio
Mfalme Salman bin Abdulaziz
Al Saud. Sasa ukilizingatia
hilo, utaona kwamba hapa
kuna mchezo wa namna
mbili na Marekani inanufaika
kwa namna zote. Moja ni
kuwa tafiti na uchambuzi wa

ANNUUR NEW.indd 11

Makala

RAJAB 1437, IJUMAA APRILI 29 - MEI 5, 2016

Baada ya urafiki
msiba juu ya msiba

PRINCE Bandar Sultan bin Abdulaziz Al Saud.


kisayansi, kisomi, kitaalamu
na kimazingira, unazidi
kufichua kwamba tukio lile
haiwezi likawa limefanywa
na magaidi kutoka Saudia au
Afghanistan. Kulikuwa na
mchezo mchafu. Sasa katika
hali kama hiyo, maelezo
kwamba serikali ya Saudi
Arabia ilihusika lakini White
House, inailinda familia ya
kifalme, inakuwa ni kichaka
cha kujificha. Kwamba sasa
itakuwa inashutumiwa kwa
kuwahami watuhumiwa
wakuu wa Septemba
11. Itakuwa inaepuka
kunyoshewa kidole kwamba
ilihusika kwa namna yoyote
kupanga au japo kujua
kilichotokea. Wazungu
wanaita Damage Control.
Mchezo wa pili ni kuwa
Saudi Arabia inasokotewa
kitanzi, ama ipate kupigwa
kama Afghanistan au itiwe
kitanzi na kuamriwa kufanya
lolote inalotaka Marekani. Na
hilo limeanza kujitokeza wazi.
Hivi sasa sheria inayozuiya
Saudi Arabia isitiwe kitanzi
kama mtuhumiwa namba
moja wa ugaidi wa Septemba
11, 2001 ni ile inayojulikana
kama Foreign Sovereign
Immunities Act (FSIA). Hii
ni sheria ya kinga kwa dola
za nchi nyingine, kama
hapa tulivyo na sheria ya
kinga kwa Rais asifikishwe
mahakamani. Lakini hivi sasa
baada ya kuibuliwa madai
ya Kurasa 28, umeanza
mchakato wa kutunga
sheria nyingine inayoitwa
Justice Against Sponsors of

AN-NUUR

Terrorism (JASTA), na ilivyo


ni kuwa sheria hii inakuja
maalum ili kuondoa kinga
kwa Saudi Arabia iliyokuwa
nayo chini ya FSIA. Kwa
mujibu wa wanaharakati
wanaoshughulikia kupitishwa
kwa sheria hiyo, ikishapita ni
kuwa itawezesha kukamatwa
kwa wanafamilia ya kifalme
na vigogo wengine wa
serikali ya Saudia ambao
wanatuhumiwa hivi sasa
kuhusika na Septemba 11.
Kwa hakika ni wazi
kuwa Wasaudia hivi sasa
tumbo joto, maana JASTA
itapelekea kuwekwa
hadharani unaodaiwa kuwa
ushahidi (hata ukiwa wa
uongo) wa kuwatia hatiani
wakihusishwa na ugaidi
wa 9/11, miaka 15 baada
ya shambulio lenyewe.
Anasema Kristen Breitweise.
Na kwa hakika
inasemekana kuwa Barack
Obama alitumia fimbo hiyo
ya JASTA katika mkutano wa
Doha Jumapili wiki iliyopita
wa kujadili bei ya mafuta
(GCC petrodollar summit),
ambapo ilibidi Waziri wa
Mafuta wa Saudia, Ali AlNaimi (mtoto wa mfalme
Salman) kutupilia kwa mbali
hoja na msimamo wake
na kufuata ilichoamriwa
na Washington ikitumiwa
kama fimbo ya kuipiga Iran
na Urusi. (Angalia: Fear and
Loathing in the Arabian NightsBy Pepe Escobar.) Kwa mujibu
wa uchambuzi wa Pepe
Escobar, pamoja na JASTA,
kitanzi kingine kinachoikabili

Saudia ni kuzuiwa mali zake


ilizolimbikiza Marekani na
Ulaya zinazokadiriwa kufikia
dola bilioni 281 ($281 billion).
Kwa mtindo wa
Kimafia, Mafia-style offer
you cant refuse, Saudi
Arabia inatakiwa izalishe
mafuta mengi kuliko soko
linavyoruhusu, ili kuibana
Iran ikose soko la mafuta
yake. Na hiyo inaharibu
uchumi wa Saudia yenyewe.
Kwa hakika ni msiba juu
ya msiba. Beberu hana rafiki,
anachotizama ni masilahi
yake tu. Saudia ilionekana
na inaonekana mpaka sasa ni
kipenzi cha Marekani. Ufalme
wenyewe umejiridhisha kuwa
upo katika mikono salama
ya akina Bush na CIA yao.
Na ili kulinda usalama huo,
ilikubali kutumiwa kuipiga
Iraq, Afghanistan, Libya,
na sasa inatumiwa kuuwa
Waislamu Syria na Yemen.
Ikifanya hivyo, kumbe na
yenyewe inasukiwa mkakati
wa kitanzi cha kurasa 28 za
Siri. Hoja hapa sio kwamba
Saudia na akina Bandar
walihusika na ugaidi wa
Septemba 11 au la, maana
hata Saddam Hussein
alipigwa kwa sababu za
uwongo kwamba alikuwa na
silaha za maangamizi (WMD).
Kama anavyosema
Pepe Escobar, mabeberu
(wanaharakati watasema
makafiri), wanajua sana
kucheza karata zao za
kuunenepesha ukafiri na
ubeberu wao. Ngoma na
debe la Kurasa 28, lilipigwa
sana katika vyombo vya
habari vya Ulaya, wiki
mbili kabla ya mkutano wa
OPEC, Doha. Kazi ikawa
nyepesi kabisa katika kikao.
Mfalme anapokea simu,
Vipi umesikia habari
ya kurasa 28. Nadhani
unakumbuka habari ya
Operation Enduring Freedom
(OEF)-vita ya Afghanstan
2001 halikadhalika ile
Operation Iraqi Freedom
iliyomngoa Saddam Hussein.
Sasa, hatudhani kwamba
ungependa tufikishane huko.
Kuna hili suala la mafuta,
tushirikiane.
Japo Ufalme unajitahidi
kujitutumua katika hali ya
kuweweseka,-Tazama: Saudi
Arabia Warns of Economic
Fallout if Congress Passes 9/11
Bill, lakini hii ndiyo Mafiastyle.
Unapewa ofa ambayo
huwezi kuikataa- offer you
cant refuse. Hapo ndipo
ilipofikishwa Saudi Arabia.

4/27/2016 12:28:15 PM

12

Safu ya Ben Rijal

AN-NUUR

RAJAB 1437, IJUMAA APRILI 29 - MEI 5, 2016

Wanyama waliotajwa katika Quran-Ndege - 2


KATIKA makala haya yatamzungumzia ndege Hudhud kama
aliyoelezwa kwenye Quran na kisha tutamuangalia katika taaluma
ya elimu ya uhai. Mtume Suleiman ni kati ya Mitume ambao
walikuwa Mitume na walikuwa wafalme. Alikuwa na nguvu na
alikuwa akifahamu lugha za wanyama.

HIVI sasa kuna taaluma


ya tabia za wanyama
(Animal behavior) katika
taaluma hii wataalamu
wanajaribu kuelewa
vitendo vya wanayama
na kelele wazipigazo na
kuweza kufahamu nini
wanachokimaanisha. Ndege
mara nyingi wanapoimba
au wanapotoa sauti zao
huwa na maana nyingi, mara
nyingi ndege dume huimba
pale tunaposikia sauti
anazozitoa ni huwa anaimba
na kutoa taarifa za mahaba
kumvutia ndege jike, hilo
wataalamu wameweza
kuligundua hilo.
Mwenyezi Mungu SWT
ametutajia mambo mengi
katika Qur-ani Tukufu

ambayo yalikuwa makhsusi


kwa ajili ya Nabii Wake
Suleiman AS kati ya hayo
ni kama ifwatavyo: Nabii
Suleiman AS alimuomba
Mwenyezi Mungu amjaalie
ufalme ambao hakumjaalia
yeyote kabla yake au baada
yake. Na Mola akapokea
maombi yake akampa kama
alivyotaka. Kama ilivyokuja
katika Surat Saad aya ya 35, "
Mola wake alimdhalilishia
upepo umpeleke popote pale
apendapo au atakapo. Kama
alivyosema katika Suratil

Saad aya ya 36:


"Basi tukaufanya upepo
umtumikie, ukenda kwa
amri yake, popote alipo taka
kufika."
Mola wake alimfunza
usemi wa ndege na kufahamu
maneno anayosema. Mfano
ulio hai ni kisa cha ndege
Hud-hud wakati aliporejea
kutoka nchi ya Yemen
alimweleza mambo ya ajabu
aliyoyaona huko. Kama
alivyotufahamisha katika
Suratin Naml aya ya 16:

"Enyi watu! Tumefunzwa


usemi wa ndege..."
Mola wake alimfunza
usemi wa mdudu chungu.
Mfano uliohai alimsikia
wakati anaposema mdudu
chungu mmoja:
Enyi wadudu chungu!
Ingieni majumbani mwenu,
asikupondeni Sulaiman
na majeshi yake bila ya
wao kutambua. Mola
katufahamisha haya katika
Suratin Naml aya ya 18.
"Mpaka walipo fika
kwenye bonde la wadudu
chungu, alisema mdudu
chungu mmoja: Enyi wadudu
chungu! Ingieni majumbani
mwenu, asikupondeni
Sulaiman na majeshi yake
bila ya wao kutambua."
Mola wake alimpa ujuzi wa
kutumia farasi wa asli ambao
hutulia wanapo simama,
na huenda mbio wanapo
kwenda. "Alipo pelekewa
jioni farasi wasimamao
kidete, tayari kutoka shoti.
Mola wake alimyayushia
maadeni ya shaba ikawa
inatiririka kwa wingi moja
kwa moja kwa muda wa
siku 3 mfululizo kama
yanavyotiririka maji, na
ilikuwa katika nchi ya Yemen.
Kama alivyosema katika

Inaendelea Uk. 13

Masheikhe wetu: Sheikh Abdulshakur bin Muhammad bin Abdul-Razak


MAKALA tulioimalizia ilikuwa
ni ya Sheikh Abdalla Bakathir
ikiwa haikukamilika, na
haiwezi kukamilika pasi na
kuwakamilisha wale waliosoma
kwake kisha ndio kuweza
kumuelezea kwa kina kutokana
na hayo. Katika makala haya
nitamzungumzia Sheikh
Abdulshakur bin Muhammad bin
Abdul-Razak.
Kiasili Sheikh Abdulshakur bin
Muhammad bin Abdul-Razak ni
Bohora wa Surat ambaye wazee
wake walikuja kustakimu visiwani
Zanzibar kabla ya zama za Seyyid
Said (katika makala zitazofwata
zitawazungumzia hao wafalme wa
Zanzibar).
Wazee wake walikuwa ni
mashuhuri kwa biashara na
walikuja kuwa wanamiliki mali
nyingi na ikafika kuwa sehemu
takriban kubwa ya eneo la
Mkunazini likiwa ni miliki yao.
Ingawa kiasili alikuwa ni wa
madhehebu ya Bohora, lakini yeye
alikuja kufwata madhehebu ya
Imam Shafi na alipoanza kusoma
alianza kusoma kwa Sheikh

ANNUUR NEW.indd 12

Suleyman Hayat mpaka kufa


kwake. Baada ya hapo alisafiri
na kwenda Mombasa akakaa
muda mrefu huko Mombasa
akiwa anasoma na alisoma zaidi
kwa Sheikh Ali bin Abdalla al
Mazrui. Baada ya hapo akaelekea
Hadhramout na huko alikaa kwa
muda mrefu sana na kusoma
katika Ribat mbalimbali. Aidha
inasemekana alifika India na Iran
na huko kote alikwenda kwa
kusoma wala sio kuendeleza
biashara za familia yake.
Sheikh Abdulshakur bin
Muhammad bin Abdul-Razak
alitokea kuwa mwana chuwoni
mkubwa wa lugha. Mbali ya lugha
ya sili yake ambacho ni Kihindi,
alikuwa akikielewa Kiajemi vilivyo
na alikuwa akikifahamu kilivyo
lugha ya Kiarabu na Nahwi yake
na akikisarifu vilivyo. Inasemekana
kuwa katika nyakati zake alikuwa
akikubalika na uelewa wa hali
ya juu ya Nahwi ya Kiarabu na
alikuwa akijiamini kuwa hakuna
aliokuwa akiweza kumpiku zaidi
ya Sayyid Ahmad bin Sumeyt na
Sheikh Abdalla Bakathir. Akiamini
kuwa hao tu ndio waliomzidi lakini

hakuna mwengine yoyote yule.


Akimfikia makamu yake, aidha
alikuwa kikwaruzana na masheikhe
wengine mara kwa mara.
Sheikh Abdulshakur bin
Muhammad bin Abdul-Razak
alikuwa mtu wa manambar na
alikuwa heshi kuhamaki na akthar
ya mambo yalikuwa yakimuudhi
na akipwayuka katika kuyakataza
na kuyatolea maelezo, kutokana
na tabia hii watu wengi walikuwa
hawaendi kusoma kwake.
Kati ya mambo yake ya kiajabu
alikuwa akitokea mwanafunzi
yoyote yule ametia buluu kanzi
yake alikuwa hamsomeshi. Hapo
zamani bluu ikitiwa katika kanzu
wakati wa kufua ili kuifanya kanzu
ingare. Aidha mtu akivaa kanzu
yenye vifungo vya chaza au mvutaji
sigereti alikuwa hamsomeshi.
Kati wa wanafunzi wake
maarufu ni Sheikh Muhsin bin
Ali al Barwany sheikhe ambaye
alikuja kupigiwa mfano kwa elimu
aliokuwa naye na ndio kupewa
wasia wa kuendeleza kitovu
cha elimu ya dini ya Kiislamu
hapo Ukutani na Sheikh Abdalla
Bakathir, Sheikh Muhsin alimsifu

sana Sheikh Abdulshakur bin


Muhammad bin Abdul-Razak kwa
ubingwa aliokuwa nao wa Nahwi
na Fiqhi aidha na mbinu alizokuwa
nazo za kusomesha.
Sheikh Muhsin alikuwa
anahudhuria darasa za Sheikh
Abdulshakur bin Muhammad bin
Abdul-Razak pale Sheikh Abdalla
Bakathir alivyokuwa Hadharmout.
Sheikh Sheikh Abdulshakur bin
Muhammad bin Abdul-Razak
akisomesha darasa zake Msikiti
Jibril na nyumbani kwake.
Sheikh Abdulshakur bin
Muhammad bin Abdul-Razak
alibarikiwa kuishi umri mrefu na
alikuja kupinda kutokana na uzee
na akipenda kukariri aya ya 68 ya
Suratul Yasin isemayo Na tunaye
mzeesha tunamrudisha nyuma
katika umbo. Basi je! hawazingatii?

Sheikh Abdulshakur bin


Muhammad bin Abdul-Razak
alifariki mwezi wa 8 Mfungo Mosi
mwaka 1839 AH(15 June 1921)
akiwa anakaribia kuwa na umri wa
miaka 90.
Mola atupe nasi ujuzi wa
kuelewa lugha na kufahamu
fahamu kama za Sheikhe huyu,
Ameen.

4/27/2016 12:28:15 PM

13

Safu ya Ben Rijal

AN-NUUR

RAJAB 1437, IJUMAA APRILI 29 - MEI 5, 2016

Wanyama waliotajwa katika Quran-Ndege - 2

Inatoka Uk. 12

Surat Sabaa aya ya 12, "...Na


tukamyayushia chemchem ya
shaba."
Mwenyezi Mungu
alimsahilishia Majini na
Mashetani akawafanya hao
Majini na Mashetani wawe
wakimtumikia Nabii Suleima
A.S. mbele yake kwa amri
ya Mola wake. Na yeyote
katika Majini aliyewacha
kutii amri ya Suleiman, basi
alimwonjesha adhabu ya
Moto unao waka kwa nguvu.
Na katika Majini walikuwako
walio kuwa wakifanya kazi
mbele yake kwa idhini ya
Mola wake. Na kila anaye
jitenga na amri yetu katika
wao, tunamwonjesha adhabu
ya Moto unao waka."Pia
katika Surat Sabaa aya ya
13, "Walikuwa wakimfanyia
alipendalo, kama mihrabu,
na masanamu, na madeste
makubwa kama mahodhi, na
masufuria makubwa yasiyo
ondolewa mahala pake."
Katika Surat Saad aya ya 37,
"Na tukayafanya Mashetani
yamtumikie, wote wajenzi na
wapiga mbizi."
Suratul Naml na Kisa cha
Mtume Suleiman na Hudhud
Tunaposoma Suratul Naml
tunakipata kisa kizima cha
Mtume Suleiman AS na ndege
Hudhud na alifanya kitu
gani? Kisa kimeanza pale
Allah SWT alipoeleza kisa
cha Nabii Suleiman na ndege
Hud-hud. Hakika Mtume
Suleiman alitoa majukumu
kwa ndege wote na kila
mmoja wao alikuwa na
jukumu lake na kupewa kazi
maalum, na walikuwa mara
zote ndege hao na viumbe
vyengine hufika kabla ya
Mfalme kufika kama kawaida
ya majeshi wanavyofanya
kwa wafalme wao.
Ibn Abbas RA amefafanua
juu ya kazi ya ndege Hudhud,
ambayo ilikuwa ni kutafuta
maji katika jangwa na ardhi
ya ukame, kwa uwezo
wa Mwenyeenzi Mungu
Hudhud alikuwa na uwezo
wa kujua sehemu zenye
maji yaliyojificha. Kwa hiyo
Hud-hud walipewa kazi
ya kutafuta maji na baadae
kuongoza jeshi kuyapata
maji hayo, huchimba mpaka

ANNUUR NEW.indd 13

kupata maji na kuyatumia


kawa matumizi yao na haja
zao nyenginezo.
Siku moja Mtume Suleiman
AS alimtafuta Hud-hud,
alimkosa na hakumuona
katika sehemu yake
aliyopangiwa. Akasema
Nabii Sulayman kama Quran inavyotupa habari katika
Suratul Namli (27:20-44).
Tuziangalie aya za Quran
zinavyoelezea kisa hichi.
Na akawakagua ndege,
na akasema: Imekuwaje,
mbona simwoni Hud-hud,
au amekuwa miongoni mwa
walio ghibu?(27: 20), Kwa
yakini nitamuadhibu kwa
adhabu kali, au nitamchinja,
au aniletee hoja ya kutosha. (
27: 21).
Basi (Hud-hud) akakaa
si mbali na akasema:
Nimegundua usilo gundua
wewe, na ninakujia hivi
kutoka nchi ya Sabai, na
nakuletea khabari za yakini.
(27: 22)
Hakika mimi nimemkuta
mwanamke anawatawala,
naye amepewa kila
kitu, na anacho kiti cha
enzi kikubwa. (27:23),
Nimemkuta yeye na watu
wake wanalisujudia jua
badala ya Mwenyezi Mungu;
na Shet'ani amewapambia
vitendo vyao na akawazuilia
Njia. Kwa hivyo
hawakuongoka, (27:24 ).
Na hawamsujudii
Mwenyezi Mungu ambaye
huyatoa yaliyo fichikana
katika mbingu na ardhi, na
anayajua mnayo yaficha na
mnayo yatangaza. (2725 )
Mwenyezi Mungu hapana mungu ila Yeye,
Mola Mlezi wa A'rshi
tukufu. (27:26 ), Akasema
(Sulaiman): Tutatazama
umesema kweli au wewe ni
miongoni mwa waongo. (27:
27).
Nenda na barua yangu hii
na uwafikishie, kisha waache
na utazame watarejesha
nini. (27: )28, (Malkia)
akasema: Enyi wahishimiwa!
Hakika nimeletewa barua
tukufu. (27: 29), Imetoka
kwa Sulaiman nayo ni: Kwa
jina la Mwenyezi Mungu,
Mwingi wa rehema, Mwenye
kurehemu. (27:30 ),
Msinifanyie jeuri, na fikeni
kwangu nanyi mmekwisha
kuwa wenye kusalimu amri.

(27: 31).
Akasema: Enyi
wahishimiwa! Nipeni shauri
katika jambo langu hili, kwani
mimi sikati shauri yoyote
mpaka mhudhurie. (27:32
),
Wakasema: Sisi ni
wenye nguvu na wakali kwa
vita; na amri iko kwako, basi
tazama ni nini unaamrisha.
(27: 33), Akasema: Hakika
wafalme wanapo uingia
mji wanauharibu, na
wanawafanya wale watukufu
wake kuwa wanyonge. Na
hivyo ndivyo watendavyo.
(27:34), Lakini mimi
nitawapelekea zawadi, nami
nitangoja watakayo rudi nayo
wajumbe. (27: 35).
Basi alipo fika (mjumbe)
kwa Sulaiman, alisema
(Sulaiman): Hivyo ndio
nyinyi mnanisaidia kwa
mali? Aliyo nipa Mwenyezi
Mungu ni bora zaidi kuliko
aliyo kupeni nyinyi. Lakini
nyinyi mnafurahia hii zawadi
yenu. (27:36 ),
Rejea
kwao! Kwa yakini sisi
tutawajia kwa majeshi wasio
yaweza kuyakabili. Na hakika
tutawatoa humo na hali wao
wamekuwa madhalili na
wanyonge. (27:37 ),

Akasema: Enyi wahishimiwa!


Ni nani kati yenu atakaye
niletea kiti chake cha enzi
kabla hawajanijia nao
wamekwisha salimu amri.
(27:38)
Akasema: Afriti, katika
majini: Mimi nitakuletea kabla
hujainuka pahala pako hapo.
Na mimi kwa hakika nina
nguvu na muaminifu. (27:
39), Akasema mwenye ilimu
ya Kitabu: Mimi nitakuletea
kabla ya kupepesa jicho lako.
Basi alipokiona kimewekwa
mbele yake, akasema: Haya

ni katika fadhila zake Mola


wangu Mlezi, ili anijaribu
nitashukuru au nitakufuru.
Na mwenye kushukuru,
kwa hakika, anashukuru
kwa manufaa ya nafsi
yake; na anaye kufuru, kwa
hakika Mola wangu Mlezi ni
Mkwasi na Karimu. (27:40
), Akasema: Mgeuzieni kiti
chake cha enzi hiki, tuone
ataongoka, au atakuwa
miongoni mwa wasio
ongoka. (27:41 ).
Basi (Malkia) alipo fika
akaambiwa: Je! Kiti chako
cha enzi ni kama hiki?
Akasema: Kama kwamba
ndicho hichi. (Sulaiman na
watu wake wakasema): Na
sisi tumepewa ilimu kabla
yake (Malkia), na tukawa
Waislamu. (27: 42), Na
yale aliyo kuwa akiyaabudu
badala ya Mwenyezi Mungu
yalimzuilia. Hakika yeye
(Malkia) alikuwa katika
kaumu ya makafiri. (27:43 )
Akaambiwa: Liingie
behewa la hili jumba. Alipo
liona alidhani ni maji, na
akapandisha nguo mpaka
kwenye miundi yake.
(Sulaiman) akasema: Hakika
hilo ni behewa lilio sakafiwa
kwa viyoo! Akasema (Malkia):
Mola wangu Mlezi! Mimi
nimejidhulumu nafsi yangu,
na sasa nanyenyekea pamoja
na Sulaiman kwa Mwenyezi
Mungu, Mola Mlezi wa
walimwengu wote. (27: 44)
Tunapozisoma aya hizi
tunakuja kufahamu uwezo
mkubwa wa kufahamu
na nguvu alizokuwa nazo
Mtume Suleiman AS.
Makala itakayofwata wiki
ijayo tutamuangalia Hudhud
aliotajwa katika Quran na
ufahamu wetu wa kileo katika
sayansi.

4/27/2016 12:28:16 PM

14

MAKALA/MASHAIRI

UFU KWETU MTIHANI!

Namhimidi Qahari, kifo alotuumbiya,


Kwa kheri na si kwa shari, japo tunakichukiya,
Thineni aya nambari, MULKU ebu rejeya,
Ufu kwetu mtihani, na mizani ya mwenendo!
Kwa mwenye njema nadhari, kwayo atazingatiya,
Mauti kwetu indhari, na mtihani sawiya,
Lengo mwendo tughairi, wetu katika duniya,
Ufu kwetu mtihani, na mizani ya mwenendo!
Kwa ya shari kuhajiri, kwa ya kheri kuhamiya,
Yaso dini idamiri, kwa ya dunia daniya,
Au yenye kutughuri, ya hawaa za duniya,
Ufu kwetu mtihani, na mizani ya mwenendo!
ABUU NYAMKOMOGI

HATUNAYE, IDD KATIMBA!

Abtadi kumsifu, Khaliku na Mfishaji,


Kwa wake uadilifu, wa hayati uumbaji,
Kadhalika na kwa ufu, uso na ubaguaji,
Hatunaye buriani, akhana IDD KATIMBA.
Mauti hayaarifu, katika wake ujaji,
Pweke yunouarifu, ujiowe Muumbaji,
Baghtata hukhatafu, roho zetu waumbwaji,
Hatunaye buriani, akhana IDD KATIMBA. .
Sote kwa huo wasifu, kutufika twataraji,
Pasi kujali dhaifu, na mwenye nguvu kwa taji,
Tujiadidi kwa ufu, kwa wa Ilahi uchaji,
Hatunaye buriani, akhana IDD KATIMBA.
Barzakhi tutatufu, baada ya ufishwaji,
Malaika watukufu, ndanimwe watatuhoji,
Faridi na si sufufu, kwa wa kwetu utendaji,
Hatunaye buriani, akhana IDD KATIMBA.
Thuma sote tutakifu, kwa kupulizwa buruji,
Mahashari ashirafu, mbele ya Wahidi JAJI,
Kwa mizani mukawafu, tutalipwa afuwaji,
Hatunaye buriani, akhana IDD KATIMBA.
Tushike ya uongofu, njia iso aawaji,
Ya Qur-an tukufu, na Sunna za muonyaji,
Kwa matendo matukufu, yaso na ubanangaji,
Hatunaye buriani, IDD MUSSA wa KATIMBA.
ABUU NYAMKOMOGI

KARIBU MGENI WETU

Tahamidi kwa Manani, Bwana wa ukamilifu,


Mtukufu mwenye shani, asiye na upungufu,
Japo moja nuksani, kwa mambo yake sufufu,
Karibu wetu mgeni, RAJABU MTAKATIFU.
Yu Yeye alobaini, mieziye iso zidifu,
Ashara wa ithnani, idadiye kamiIifu,
I ndani ya QURAANI, TAUBA nenda kashufu,
Karibu wetu mgeni, RAJABU MTAKATIFU.
Thathna sita ayani, arba mitakatifu,
Ndipo utaibaini, yote kwa ukamilifu,
Rajabu wa pili ndani, ya minne ile safu,
Karibu wetu mgeni, RAJABU MTAKATIFU.
Adhimu yake thamani, zaidi ya maradufu,
Aula tuuthamini, dhuluma si yake kufu,
Ya ndanimwe tusikhini, tuyaenzi kwa insafu,
Karibu wetu mgeni, RAJABU MTAKATIFU.
Maovu tuyaacheni, kwa ya Ilahi hawafu,
Na mema tuzidisheni, katu yasije tukifu,
Kesho yaje tuauni, baada ya wetu ufu,
Karibu wetu mgeni, RAJABU MTAKATIFU.
Nimefika ukingoni, siwezi kujikalifu,
Lengo kukumbusheni, mzidishe matukufu,
Yatakayokufaeni, kesho mbele ya RAUFU,
Karibu wetu mgeni, RAJABU MTAKATIFU.
ABUU NYAMKOMOGI

ANNUUR NEW.indd 14

AN-NUUR

RAJAB 1437, IJUMAA APRILI 29 - MEI 5, 2016

Hatujaila keki yetu wala hatunayo!


Inatoka Uk. 8
unaonesha kuwa muna
angalau nusu ukweli
katika kauli hii, kama
si ukweli mtupu.
Maana kila tukienda
mbele, ndivyo Zanzibar
inavyozidi kupoteza
kwa kuutononesha
Muungano. Kwa miaka
yote 40 ya Muungano,
kanuni inayouendesha
Muungano huu imekuwa
ni moja tu: kadiri
Tanzania inavyozidi
kupanda, Zanzibar izidi
kuanguka. Gharama
za kuimarika kwa
Muungano zimekuwa
ni kudhoofika kwa
Zanzibar.
Huu ni ukweli
wa kusikitisha na
kuogofya na ndio
unaotayarisha mazingira
ya Wazanzibari kutaka
bendera yao (na huko
mbele kuja kudai
mengine). Maana
unapofikia pahala
ukajikuta umeshapoteza
mambo mengi kati
ya yale uliyokuwa
umeyamiliki na
yaliyokufanya wewe
kuwa wewe, huwa
huna hakika tena kuwa
hata hicho kilichomo
mikononi mwako
kitabakia. Huna uhakika
wa utambulisho wako
kuwa utaendelea
kuwapo. Ikiwa kumi
vimekwenda, kwa nini
kimoja kibakie?
Miaka yote hiyo 40
ya Muungano huu
imekuwa ikiishuhudia
Zanzibar ikipoteza kila
chake kinachoifanya
kuwa Zanzibar. Wakati
huo huo, kwa jina la
Tanzania, Tanganyika
imekuwa ikiingiza kila
kinachoifanya kuwa
Tanganyika, isipokuwa
jina lake tu. Kwa maana
nyengine ni kwamba
gharama kubwa ya
Tanganyika katika
Muungano huu ni huko
kupoteza jina lake la
asili na faida kubwa ya
Zanzibar ni huko kubakia
na jina lake. Zanzibar
kama nchi, dola na taifa
huru haipo.
Nadhani walio nihoji
wanaamini kuwa
haya ndiyo matokeo
ya kawaida kwa nchi
inapoingia katika
muungano na nchi
nyengine. Ndio maana
ya kutumia huo msemo
kwamba you can not
eat your cake and have
it. Ukitaka ubakie na
keki yako, ili uufaidi ule
uzuri wake kwa macho
yako, basi usiile. Kama

unataka uifaidi ile ladha


yake katika kinywa chako
na ulishibishe tumbo
lako, basi ile. Lakini
ukiila, ujuwe kuwa
hutoiona tena milele.
Hivyo ni kutuambia
kuwa Zanzibar ilipoingia
katika Muungano ilikuwa
imechagua kuila keki
yake na kwamba sasa
haiwezi kuwa nayo
tena milele na milele,
vyenginevyo Muungano
huu uvunjike. Haiwezi
kutaka ibakie na uhuru,
u-nchi, u-taifa na
u-dola wake, kwa ufupi
Uzanzibari wake, halafu
wakati huo huo ikataka
iwe katika Muungano.
Maana kuwamo
katika Muungano
kunamaanisha kuyatoa
muhanga mambo hayo.
Muhanga ulioje huo (ama
kwa maneno ya Raza:
Tumetoa sadaka kila
kitu)
Lakini namna mambo
yanavyokwenda,
yanakiuka busara za
msemo huu. Zanzibar
ni upande mmoja tu wa
Muungano huu, upande
wa pili ni Tanganyika.
Kama ni kuila keki yake
na kutokuwa nayo,
Tanganyika nayo pia
ingetakiwa isiwe nayo.
Nakusudia kusema
kuwa zile nguvu, ule
uwezo, yale madaraka,
yanayotafsiriwa kwa
uhuru, utaifa na udola,
nayo pia yasingelikuwa
mikononi mwake (hapa
usiniambie Tanganyika
nayo imepoteza kila kitu,
maana nimeshaonesha
kuwa ilichokipoteza ni
jina tu). Sasa kwa nini
Tanganyika iendelee
kuwa na keki yake hata
baada ya kuila? Yumkini
haikuila kabisa au kama
iliila, basi ilimega kidogo
tu! Kwa Zanzibar hali
ni tafauti. Nakusudia
kusema kwamba ingawa
ni kweli kuwa Zanzibar
hainayo tena keki yake
(imeshapoteza uhuru,
utaifa na utambulisho
wake) lakini haijapata
kuila keki hiyo. Kwa
nini? Kwamba busara
ya msemo huo ni
kwamba hata kama sasa
utakuwa umeshaikosa
keki yako, basi utakuwa
umefaidika na mengine.
Kwa mfano, tumbo
litakuwa limeshiba na
kiwiliwili kitakuwa
kimepata virutubisho.
Si tunajuwa kuwa keki
hutengenezwa kwa
mayai, unga wa ngano
na siagi? Tunaambiwa
kuwa kipande kimoja cha

keki kina faida kubwa


katika kiwiliwili kuliko
hata sahani nzima ya
wali! Basi ikiwa kweli
Wazanzibari tumeila
keki yetu, angalao si
tungelikuwa tumejengeka
kimwili?
Ninachokusudia
kukihoji hapa ni
kwamba kama kweli
Zanzibar ilikubali kuutoa
muhanga Uzanzibari
wake na kuutumia
muhanga huo, basi
ingelikuwa imeshafaidika
angalau kimaada. Yaani
ingelikuwa hatuna
Uzanzibari wetu, lakini
angalau tungelikuwa na
uchumi imara na mfumo
madhubuti wa huduma
za kijamii. Huko ndiko
kujengeka kimwili kwa
kuila keki yetu wenyewe.
Lakini Zanzibar ya leo,
ya miaka 40 baada ya
Muungano, ni dhalilifu
na kosefu zaidi katika
uchumi na huduma za
kijamii. Hili linamaanisha
kuwa Wazanzibari
hatukuila keki yetu.
Tungeliila tungelikuwa
na misuli imara.
Tungelikuwa na uchumi
madhubuti na hali nzuri
za maisha.
Hapa swali ni kwamba
kama hatukuila, keki
hiyo iko wapi? Uko wapi
uhuru wetu? Uko wapi
utaifa wetu? Uko wapi
utambulisho wetu? Ziko
wapi nguvu na madaraka
yetu? Jibu ni kwamba
vyote hivyo havipo. Na
kama ni hivyo, ni wazi
kuwa keki imeliwa,
ingawa walaji hatukuwa
sisi. Ni Muungano ulioila
keki yetu. Huo ndio
uwezekano wa kutokuila
keki yako bali pia usiwe
nayo!
Basi jitihada hizi za
kutaka kuwa na bendera,
kujiunga na mashirika
ya kimataifa na nyengine
zozote za mfano wake,
ni matokeo ya kuvizwa
kwa Zanzibar katika
Muungano. Ni radda
ya siasa zilizouzunguka
Muungano huu. Siasa
ambazo zinamfanya
mmoja aile keki yake
na abakie nayo na
mwengine asiile na asiwe
nayo. Ni mchakato wa
mabadiliko, ambapo
Zanzibar inaitafuta
keki yake. Hivi sasa,
hata kama Mwalimu
Nyerere angelikuwa hai,
asingelilizuia hilo!
(Kwa mara ya mwanzo
makala hii ilichapishwa
katika gazeti la Hali
Halisi, Na. 8 la Juni
2005.)

4/27/2016 12:28:17 PM

15
Inatoka Uk. 9
alifanikiwa kupata daraja la
kwanza la pointi/alama kumi na
tano (15) katika matokeo yake ya
masomo yake ya kidato cha nne
na kupata daraja la kwanza la
pointi/alama (6) katika matokeo
ya masomo yake ya kidato
cha sita, halikadhalika ndiye
mwanafunzi aliyeongoza kwa
kanda ya ziwa nzima katika
ufaulu wa somo la lugha ya
Kiarabu kwa matokeo ya kidato
cha sita kwa mwaka 2011. Baada
ya ufaulu wake wa kidato cha
nne alifanikiwa kuchaguliwa
kujiunga na shule ya sekondari
Umbwe ya mkoani Kilimanjaro,
lakini hakwenda kutokana
na mchepuo, wa masomo ya
Historia, Kiswahili na Kiingereza
(HKL) kutokuwepo shuleni
hapo, ambao yeye aliupendelea
zaidi kutokana na utashi pamoja
na utayari wake wa kujikita
zaidi katika masomo ya lugha
hapo baadae kuliko mengineyo.
Kwa mazingira haya na baada
ya kushauriana na baba yake
mlezi, alijiunga na shule ya
sekondari Thaqaafa ambako
mbali na kuchukua mchepuo wa
masomo ya Historia, Kiswahili
na Kiingereza (HKL) aliongeza
pia na somo la lugha ya Kiarabu.
Katika matokeo yake ya masomo
ya kidato cha sita alifanikiwa
kupata alama (B) katika masomo
yote ya Lugha yaani Kiswahili,
Kiingereza na Kiarabu wakati
ambapo alipata ufaulu wa alama
(D) katika somo la Historia
jambo ambalo lilidhihirisha
dhamira yake ya tangu awali
ya kupendelea zaidi masomo
ya lugha kuliko vinginevyo.
Hata hivyo, ndoto zake za
kuendelea zaidi na masomo ya
lugha zilififia baada ya kujikuta
amechaguliwa kujiunga katika
kitivo cha sheria katika Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam
ambako alifanikiwa kuhitimu na
kupata Shahada yake ya Sheria
mnamo 2015.
Kutokana na malezi
aliyoyapata na makuzi
aliyoyapitia chini ya marehemu
Katimba, kijana huyu amejifunza
mengi ambayo alisema ni
vigumu kuyaeleza yote ila alitaja
machache ikiwa ni pamoja na
subira na uvumilivu, upendo,
ukarimu, insafu, hekima na
busara pamoja na uchamungu.
Kwa upande wa wasifu wa
marehemu, kijana huyu anaeleza
kwamba:
''Pamoja na sifa mbalimbali
zinazoweza kuelezwa na kila
mmoja wetu kutokana na jinsi
alivyomfahamu mzee (Idd
Katimba), mimi kwa upande
wangu ninaona kwamba mzee
huyu alikuwa ni mzazi, mlezi na
kiongozi.''
Akaongeza kwa kusema,
''Kwa kweli kwangu mimi
alikuwa ni mtu wa kupigiwa
mfano.'' Akahitimisha kwa
kumwombea dua,''Allah
amsamehe pale alipoteleza kama
mwanadamu''.
Aidha, marehemu Katimba
aliwahi kushika nyadhifa

ANNUUR NEW.indd 15

Makala/Tangazo

AN-NUUR

RAJAB 1437, IJUMAA APRILI 29 - MEI 5, 2016

Buriani Idd Katimba

MARHUUM Idd Mussa Katimba katika harakati kuhuisha Uislamu.


mbalimbali katika baadhi ya
vituo vya Kiislaamu ikiwa ni
pamoja na nafasi ya Mwenyekiti
wa msikiti wa Arafa pamoja
na nafasi ya Mkurugenzi wa
kitengo cha dini pamoja na
Mjumbe wa bodi ya shule ya
sekondari ya Thaqaafa.
''Sheikh Katimba amekuwa
Mwenyekiti wa msikiti huu
(Arafa-mabatini) kwa muda
mrefu sana na kwa kweli
alijitahidi kufanya mengi mazuri
katika uongozi wake'', alinieleza
muumini mmoja msikitini hapo
ambaye hakupenda kutajwa jina
lake gazetini'.
Kadhalika marehemu
Katimba aliwahi kuwa ripota
wa gazeti hili, kwa nyakati
tofauti tofauti, ambaye alikuwa
akifanya jitihada ya kufuatilia
na kuyaripoti matukio
yaliyowahusu Waislamu katika
maeneo mbalimbali hapa nchini.
Mifano ya baadhi ya habari
zilizoripotiwa/zilizoandikwa na
yeye kupitia gazeti hili ni pamoja
na ile iliyomo katika toleo namba
198 la gazeti hili iliyohusiana
na tanbihi iliyotolewa kwa
Waislamu na aliyekuwa Rais
mstaafu wa awamu ya pili
Mzee Ali Hassan Mwinyi
wakati akiwa ziarani mjini
Tabora. Pamoja na ile habari
iliyomo katika toleo namba 165
ya gazeti hili iliyohusiana na
shule ya Waislamu ya sekondari
Sengerema (Sengerema Muslim).
Mbali na kushika nyadhifa
hizo pamoja na kujitolea
kwake kwa hali na mali katika
kufanikisha harakati mbalimbali
za maendeleo ya Uislamu na
Waislamu, marehemu Katimba
alijishughulisha na biashara ya
uuzaji wa matairi ya magari
kama njia ya kujipatia kipato
kwa ajili ya kujikimu kimaisha.
Marehemu Idd Mussa
Katimba ni mtoto wa kwanza
kati ya watoto zaidi ya kumi
wa marehemu mzee Mussa
Katimba. Baadhi ya wadogo

zake ni pamoja na Sheikh Rajabu


Katimba, Khamis Katimba,

Ally Katimba, Sheila Katimba,


Hawa Katimba, Salima Katimba
pamoja na Ramadhani Katimba
na Safia Katimba ambao wote
wawili kwa sasa ni marehemu.
Marehemu Katimba ameacha
mke mmoja ambaye ni Bi. Hajjat
Titi Juma pamoja na watoto
wanne wa kike ambao ni Zena,
Rukia, Mwangaza pamoja na
Hafsa.
Marehemu Katimba alikuwa
akisumbuliwa na ugonjwa wa
kisukari kwa muda mrefu.
Alifariki dunia usiku wa 15.
04. 2016 kuamkia kumi na
sita akiwa na umri wa miaka
takriban sitini na mitatu (63),
kwa kuwa alitarajia kutimiza
umri huo mnamo 17. 04. 2016;
na kuzikwa mnamo 16. 04.
2016 baada ya swala ya alasiri
katika makaburi yaliyopo katika
barabara ya Nyerere jirani na
soko kuu la mavazi ya mitumba
la Mlango Mmoja la jijini
Mwanza.
Tunamuomba Allah (S.W.)
amlaze ndugu yetu marehemu
Idd Mussa Katimba mahala
pema peponi. Amiin.

AFRICA MUSLIMS
AGENCY, KUWAIT
TANZANIA OFFICE,

VACANCIES ANNOUNCEMENT

Direct Aid (Africa Muslims Agency Tanzania


office) invites qualified Tanzanians to fill 1(One)
post as Media Co-ordinator.
General Conditions
i. All applicants must be citizens of Tanzania and
not above 45 years old
ii. Applicants must attach an up to date Current
Curriculum Vitae (CV) having reliable contact,
postal address, e-mail and telephone numbers.
iii. Applicants should apply on the strength of the
information given in this advertisement.
iv. Applicants must attach their detailed relevant
certified copies of academic certificates:

Institution and arrangements the necessary press


conference, television and radio
5 To verify the information materials and determine
their suitability for publication and to make sure
safety of the language.
6 To make follow up what is published in the media
all news related to the Institution and to prepare
appropriate responses
7 To ensure that the information materials is free
of any abuses to the peoples, groups, organs or
prejudice states
8 Oversee large projects undertaken by the
Organization in particular and in massive, then
sending reports instantaneous
-Application letters should be written in Swahili 9 To visit the Institutions centers and to cover
or English
their activities
-All applications should be addressed to; Africa 10 To prepare periodic reports on his work precisely
Muslims Agency by using the following address; on time by aims of work developments
Tanzania@direct-aid.org or Postal address;
Director,
1.1.3 QUALIFICATIONS AND EXPERIENCE
Africa Muslims Agency,
I) Bachelor of Marketing ii) Bachelor of Mass
P.O. Box 9211,
communication iii) Bachelor of Bussiness
Dar es Salaam
administration or equivalent qualification from a
Important; Remember to attach your application recognized Institution
letter.
Must have a working experience of at least three
1.0 MEDIA CO-ORDINATOR
five years in the relevant field.
1.1.1 JOB PURPOSE
Covering important and large projects done by 1.1.4 OTHER SKILLS
the organization in the country and raising level of -Public relations
projects Institution covering to the state.
-Marketing
-Press skills
1.1.2 DUTIES AND RESPONSIBILITIES -Communications skills
1 To implement policies and procedures of -Photograph and video skills
association to achieve goals of Media admistration -Computer skills
and Public Relations Department.
-Photo editing and video programs
2 Supervising of all trade dealing with the National -Language ability
press, broadcasting and National television.
-Knowledge of Media ethics, regulations and
3 To communicate with the Media institutions, to Laws of country
appear on television and radio programs, and news
papers to highlight the role of the Organization in Deadline for submissions/uploading
of applications with all the required
charity activities and work
4 To attend social events, that organized by the supporting documents is 6 /May, 2016

4/27/2016 12:28:21 PM

Makala

16
Na Khatib J Mziray
ENYI mlioamini!
Mmelazimishwa
kufunga (Sumu) kama
walivyolazimishwa waliokuwa
kabla yenu ili mpate kumcha
Mungu. (Quran 2:183.)
Kulingana na aya
hiyo, tunafahamu kuwa,
Mitume waliomtangulia
Nabii Muhammad S.A.W.
Walilazimishwa kufunga; na
kuwa, katika funga ndipo
panapapotikana tija ya Ucha
Mungu.
Lakini kwa wasiokuwa
Waislamu, wanasema kuwa,
Muhammad S.A.W. Ndiye
aliyeleta ibada ya funga, na
wameandika poropoganda
nyingi kuhusu funga.
Moja katika nguzo za imani
katika Uislamu, ni kuamini
mitume wa Mwenyezi Mungu
na vitabu walivyoteremshiwa
(Ufunuo-Wahayi) kutoka kwa
Mwenyezi Mungu.
Vitabu hivyo ni Torati,
aliyopewa Nabii Mussa A.S.
Zaburi, aliyopewa Nabii Daudi
A.S. Injili, aliyopewa Nabii
Isa (Yesu) A.S. Na Quran
Aliyopewa Nabii Muhammad
S.A.W. Kwa maana hiyo,
inatulazimu kuviangalia vitabu
vitatu vilivyoitangulia Quran,
kuwa vinaizungumziaje funga
(saumu)?
Nabii Musa A.S. ndiye
aliyeteremshiwa Torati (Sheria).
Nabii Mussa A.S.
Alikabidhiwa Torati akiwa
amefunga; kwa kuwa funga
ilishamfikisha katika Ucha
Mungu:BWANA akamwambia
Musa, Andika maneno haya;
kwa kuwa mimi nimefanya
agano nawe, na pamoja
na Israeli, kwa mujibu wa
maneno haya. Naye alikuwa
huko pamoja na BWANA
siku arobaini na masiku yake;
hakula, wala kunywa maji. Naye
akaandika katika hizo mbao,
hayo maneno ya maagizo, hizo
amri kumi. (Biblia 34:27-28.)
Kwa bahati mbaya waandishi
hawakueleza hapo kuwa, Nabii
Musa A.S. Alikuwa amefunga,
bali wamesema kuwa hakula
wala kunywa maji, lakini
tutaona baadae. Kwa kuwa
andiko limesema kuwa, Nabii
Mussa A.S. aliandika amri
hizo za Mwenyezi Mungu,
tunahakika kuwa Manabii
waliofuata baada yake
watakuwa wakitekeleza amri
hizo ikiwemo hiyo ya kufunga:Habari za Nehemia,
mwana wa Hakalia.Hata
ikawa niliposikia maneno
hayo, nikalia nikaomboleza
siku kadha wa kadha; kisha
nikafunga, nikaomba mbele za
Mungu wa mbinguni; nikasema,
Nakusihi, Ee BWANA, Mungu
wa mbinguni, Mungu mkuu,
mwenye kuogofya, mwenye

ANNUUR NEW.indd 16

RAJAB 1437, IJUMAA APRILI 29 - MEI 5, 2016

Funga ya Ramadhani

kutimiza agano lake na rehema


zake kwa hao wampendao na
kuzishika amri zake. (Biblia
Nehemia 1:1-5.)
Nehemia alikuwa ni Mtume;
mambo hayo yalimtokea,
hakukuwa na wakati muafaka
wa kumwomba Mungu Mkuu
(Allahu Akbar) wa mbinguni, ila
wakati wa funga; na Mwenyezi
Mungu ambaye anatimiza agano
lake na rehema zake kwa wale
wanaompenda na kuzishika
amri zake ikiwemo funga:Piga kelele, usiache.
Paza sauti kama tarumbeta;
Uwahubiri watu wangu, Na
nyumba ya Yakobo dhambi
zao... Husema, Mbona
tumefunga, lakini huoni?
Mbona tumejitaabisha nafsi
zetu, lakini huangalii? Siku ya
kufunga kwenu mnatafuta anasa
zenu, wenyewe, na kuwalemea
wote watendao kazi kwenu.
Tazama, ninyi mwafunga mpate
kushindana na kugombana
na kupiga ngumi ya uovu.
Hamfungi suku hii ya leo hata
kuisikizisha sautu yenu juu.
(Biblia Isaya 58:1-4.)
Kwa wale wanaoamini
kuwa wana wa Israeli (Yakobo),
kuwa ni taifa takatifu; kama
ni waumini wa Biblia, basi,
hawayaelewi maandiko; au
wametiwa shemere kichwani
iliyoviza vile vipaji vya kuelewa
jambo:Nabii Isaya akiwa na umri
wa miaka 25 aliitwa na Mungu
Hekaluni kwenye mwaka wa
740 K.K. Atangaze maangamizi
ya taifa la Israeli kwa sababu
halikumtii Mungu. (Utangulizi
wa Isaya, uk 651 Biblia ya
Imprimatur).
Na moja ya makosa yao ni
hilo analo waambia hapo juu;
kuwa wamebadilisha sheria za
funga wakaweka za kwao; kuwa
hawafungi kwa ajili ya kutii amri
ya Mungu:Je! Kufunga namna hii ni
saumu niliyoichagua mimi? Je!
ni siku ya mtu kujitaabisha nafsi

AN-NUUR

yake? Ni kuinama kichwa kama


unyasi, na kutanda nguo za
magunia na majivu chini yake?
Je! utasema ni siku ya kufunga
na ya kukubaliwa na BWANA.
(Isaya 59:5.)
Mungu alimwambia Nabii
Isaya, awaambie hivyo kuwa;
hivyo wanavyo funga hawana
Saumu, maana kuacha kula, na
Saumu ni vitu viwili tofauti;
maana saumu hupatikana pale
unapofunga kwa kutekeleza zile
kanuni na sheria za funga:Je! saumu niliyoichagua,
siyo ya namna hii? Kufunga
vifungo vya uovu, kuzilegeza
kamba za nira, kuwaacha huru
walioonewa, na kwamba mvunje
kila nira? (Biblia Isaya 58:6.)
Hapo, Mwenyezi Mungu
anamwanbia Nabii Isaya, kuwa
awafundishe wana wa Israeli
namna ya saumu aliyoiamrisha
na anayoiridhia kwa mwenye
kufunga:Je! siyo kuwagawia wenye
njaa chakula chako, na kuwaleta
masikini waliotupwa nje
nyumbani kwako? Umuonapo
mtu aliye uchi, umvike nguo;
wala usijifiche na mtu mwenye
damu moja nawe? (Biblia Isaya
58:7.)
Hayo ni matendo
anayotakiwa mfungaji ayafanye;
kuwakaribisha masikini,
mayatima wafuturu kwako;
na wale wasio na nguo ukiwa
na uwezo uwasaidie nguo; na
usiwafanyie hivyo wale tu ulio
na nasaba nao. Funga na saumu
inayokidhi matakwa hayo ya
Mwenyezi Mungu ina malipo
yafuatayo:Ndipo nuru yako
itakapopambazuka kama
asubuhi, na afya yako
itatokea mara; na haki yako
itakutangulia; utukufu wa
BWANA utakufuata nyuma
ukulinde. Ndipo utaita, na
BWANA ataitika; naye atasema
Mimi hapa. (Biblia Isaya 58:8-9.
)
Tukiendelea na funga na
Manabii waliomtangulia Nabii
Muhammad:-

(Nabii) Yeremia amezaliwa


kadiri ya mwaka 645 K.K. katika
ujirani wa Yerusalemu. Ukoo
wake ni wa makuhani. Tunajua
habari zake hasa kutokana na
kitabu chake. Kwenye mwaka
626 K.K. aliitwa na Mungu
alipokuwa bado kijana
Utangulizi wa Yeremia uk. 698,
Biblia ya Imrimatur:Ikawa katika mwaka wanne
wa Yehoyakimu, mwana wa
Yosia, mfalme wa Yuda neno hili
likamjia Yeremia, kutoka kwa
BWANA, kusema, Twaa gombo
la chuo, ukaandike ndani yake
maneno yote niliyokuambia juu
ya Israeli Basi , ikawa katika
mwaka wa tano wa Yehoyakimu,
mwana wa Yosia, mfalme wa
Yuda, katika mwezi wa kenda,
watu wote waliokuwa katika
Yerusalemu, na watu wote
waliokuja Yerusalemu kutoka
miji yote ya Yuda, wakapiga
mbiu ya kufunga mbele za
BWANA, (Biblia Yeremia 36:19.)
Nabii Yeremia, anatwambia
kuwa, kufunga ni mwezi wa
tisa; sio septemba, au Januari,
au Februari; ni mwezi huu
unaoandama mbinguni.
Waislamu wanatii sheria ya
Mwenyezi Mungu, ya kupiga
mbiu dunia nzima, kuwa
mwezi wa tisa (Ramadhani)
umeandamaaa; na watu
wanafunga dunia nzima.
Watu wa Ninawi
walipotangaziwa kufunga na
Nabii Yona (Yunus), walihalifu
wakafunga kwa kuvaa magunia,
na kufungisha wanyama wao;
jambo lililokatazwa kama
tulivoona hapo juu kwa Nabii
Isaya. Soma Yona 7:1-7. Nabii Isa
(Yesu) alifunga:Kisha Yesu alipandishwa na
Roho nyikani, ili ajaribiwe na
Ibilisi. Akafunga siku arobaini
mchana na usiku, mwisho
akaona njaa. (Bibli Mathayo 4:1)
Neno Roho likiandikwa
kwa kuanza na herufi kubwa;
inamaanisha kuwa ni Roho
Mtakatifu, au Nguvu ya utendaji
kazi ya Mwenyezi Mungu.
Kwa maana hiyo ni sawa
na kusema kuwa Mungu
alimpandisha Yesu nyikani
na kumwacha ajaribiwe na
Ibilisi; kwa maana ingine ni
kuwa Mungu alikaa pembeni
akisikiliza mahojiano ya Yesu
na Ibilisi; kwa maana hiyo ni
kuwa, baada ya Mwenyezi
Mungu kumtawadha Yesu kuwa
Mtume, alitaka apewe mtihani
na Ibilisi, ili aone kuwa atafaulu
kumkiri Mwenyezi Mungu
kuwa ndiye wakuabudiwa au
atafeli kwa kumkubali Ibilisi
na kumwabudu. Ndiyo maana
Ibilisi alimwambia Yesu:Kisha Ibilisi akamchukua
mpaka mlima mrefu mno,
akamwonyesha milki zote
za ulimwengu, na fahari
yake, akamwambia Haya
yote nitakupa, ukianguka
kunisujudia, Ndipo Yesu
alipomwambia, Nenda
zako Shetani; kwa maana
imeandikwa, Msujudie Bwana
Mungu wako, umwabudu yeye
peke yake. (Mathayo 4:8-10.)

4/27/2016 12:28:23 PM

17

MAKALA

Udini-1
Na H. Hashim

KWA muda mrefu Watanzania


tumekuwa tukiaminishwa kuwa
Tanzania hakuna udini. Hata
kwa wachache wanaoamini kuwa
kuna udini, wengi miongoni
mwao hawana ujasiri wa kukiri
hadharani ukweli huo kwa
kuhofia athari za kutofautiana
na imani ya wengi ya kwamba
hakuna udini. Kwa kupumbazika
huku kuwa Tanzania hakuna
udini, tunaacha udini usambae na
kuimarika bila kudhibitiwa.
Miongoni mwa wachache
wanaokiri hadharani uwepo wa
udini, wengi wao husukumia
lawama zote za udini kwa watu
wa dini zisizo zao. Wapo pia
wanaojinasibisha na upambanaji
dhidi ya udini, lakini kwa siri
hupiga vita dini zisizo zao pamoja
na waumini wake. Hali hiyo nayo
husababisha udini usambae na
kuimarika bila kuthibitiwa.
Udini ni moja kati ya vyanzo
vikubwa vya vita na machafuko
ya kisiasa na kijamii. Pamoja na
ukweli huo, Watanzania wengi
hatushituki tunaposikia na kuona
nchi nyingine wakipigana wenyewe
kwa wenyewe kwa sababu za kidini
au kikabila tukidhani hilo haliwezi
kutokea kwetu. Hatushituki
kwa sababu tumeaminishwa na
kuamini kuwa tuko kwenye kile
tunachokiita kisiwa cha Amani.
Kama tutakavyoona huko mbele,
kupiga vita dini na waumini wake,
kwa kisingizio cha kupiga vita
udini, sio tu kuwaingiza wengine
kwenye hatari, bali pia kujiingiza
mwenyewe hatarini. Ni sawa na
kumpiga mawe jirani yako huku
mwenyewe ukiwa unaishi kwenye
nyumba ya vioo.
Ingawa kwa muda mrefu
tumekuwa tukiaminishwa, na
wengi miongoni mwetu tukaamini,
kuwa Tanzania hakuna udini,
ukweli ni kwamba kuna mivutano
mingi ya kidini ambayo haiko wazi
sana kiasi cha kuonekana kwa kila
mtu. Kwa sababu hiyo, jitihada
zinahitajika kubaini mivutano hiyo
hasa tukizingatia ukweli kwamba
walioko vitani sasa, walianzia
kwenye mivutano na migongano
kama tuliyonayo ambayo
walishindwa kuisuluhisha mapema
kwa njia za amani.
Harakati za kivita huanza muda
mrefu kabla risasi ya kwanza
kupigwa. Harakati za udini
zisipothibitiwa mapema zinaweza
kugawanya jeshi la kupiga vita
udini na kuwafanya askari wake
wapigane wenyewe kwa wenyewe
kwa misingi ya dini zao. Kadiri
harakati za udini zinavyoendelea,
ndivyo zinavyotupunguzia uwezo
wa kutofautisha dini na udini, na
muumini wa dini na mdini. Hali
hiyo ikiendelea, itatufikisha kwenye
vita kati ya dini na dini, badala ya
wapinga udini na wapigania udini.
Nchini Kenya kwa mfano,
hakuna aliyetarajia kuwa tukio
moja tu la uchaguzi lingesababisha
mapigano ya wenyewe kwa
wenyewe kwa misingi ya kikabila
kama ilivyotokea mara tu baada
ya uchaguzi wa mwaka 2007

ANNUUR NEW.indd 17

nchini humo. Vita vya wenyewe


kwa wenyewe havikutarajiwa
kutokea nchini humo kwa sababu
kabla ya hapo nchi hiyo ilikuwa na
amani, na mara kwa mara ilikuwa
ikijishughulisha na kutafuta amani
katika nchi nyingine zilizokuwa
hazina amani. Kama hali hiyo
iliweza kutokea Kenya, inaweza
kutokea pia Tanzania iwapo
hatutakuwa waangalifu na makini
Aidha hakuna aliyetarajia mtu
kuuwawa katika ardhi ya Tanzania
kuhusiana na mzozo wa kidini.
Lakini kuna tukio lililowahi kutokea
huko Buserere mkoani Geita,
ambapo mtu mmoja aliuwawa na
wengine saba kujeruhiwa katika
mzozo uliohusisha dini zao katika
suala moja tu na dogo la kuchinja.
Hiyo ilikuwa cheche katika mbuga
yenye majani makavu. Hatujui
cheche hiyo ingeathiri mbuga kwa
kiasi gani endapo isingezimwa au
kuzimika mapema.
Tanzania kuna Udini
Ingawa wengi hatupendi kusikia
kuwa Tanzania kuna udini, ukweli
ni kwamba udini upo. Ni rahisi
kuwagombanisha Watanzania kwa
sababu za kidini kuliko za kikabila
au kitu kingine. Kuna sababu
kadhaa zifuatazo zinazonifanya
niamini hivyo. Kwanza: Yeyote
anayefuatilia mijadala Bungeni,
atakubaliana na mimi kuwa kila
linapojadiliwa suala linalogusa dini
(hata kama sio la kidini), mjadala
wake huwa mkali na kutawaliwa na
jazba kubwa kuliko jambo lingine
lolote lisilohusiana na dini. Katika
masuala mengine yote, wabunge
hugawanyika kwa misingi mingine
tofauti kabisa na dini zao kama vile
ya vyama vya siasa na mitazamo
yao. Linapokuja suala la dini,
huweka kando tofauti zao zote
na kugawanyika kwa misingi ya
dini zao (Waislamu na Wakristo)
kila upande ukiwa na msimamo
usioyumba wala kutetereka.
Hakujatokea mgawanyiko wowote
kwa misingi ya makabila yao, ikiwa
ni ishara kuwa ukabila haupo au
upo kwa kiwango cha chini sana.
Pili; Kama tutakavyoona huko
mbele hiki, wapo wengi miongoni
mwetu, wakiwemo viongozi
wakubwa wa dini na serikali, na
wenye ushawishi mkubwa katika
jamii, ambao hufuatilia masuala
ya dini nyingine na kutoa kauli
zisizokubalika kuhusu dini hizo
kuliko wanavyofuatilia tofauti
nyingine kama vile za vyama vya
siasa, kikabila na kiitikadi. Tofauti
ndogo ya kidini hukuzwa na kutiwa
chumvi mno na kuonekana kubwa,
lakini tofauti nyingine huweza
kuvumiliwa, kupuuzwa na hata
kutoonekana kabisa.
Katika uchaguzi wa mwaka 2005
kwa mfano, kulikuwa na wagombea
kumi wa Uraisi. Miongoni mwa
hao kumi, sita walikuwa kutoka
mkoa mmoja tu miongoni mwa
mikoa zaidi ya 25 iliyokuwapo
nchini. Wanne miongoni mwa hao
sita walitoka kabila moja na wawili
waliobaki kabila lingine moja la
mkoa huo. Ingawa hao ni miongoni
mwa wagombea kumi tu katika
nchi yenye makabila zaidi ya 120,
lakini hilo halikuwa tatizo kwa
Watanzania. Hata sasa, miongoni
mwa wenyeviti wa vyama vya siasa
nchini, watatu miongoni mwao ni
wa kabila moja lakini hilo halijawa
tatizo kwa Watanzania; wala
halielekei kuwa tatizo; na tunaomba
isitokee likawa tatizo.
Kinyume na hali hiyo, imekuwa
rahisi chama cha siasa kuhusishwa
na udini kwa sababu tu viongozi
wake wa juu wapatao wanne ni
wa dini moja, hata kama ni wa

AN-NUUR

RAJAB 1437, IJUMAA APRILI 29 - MEI 5, 2016

madhehebu tofauti, kati ya dini kuu


mbili tu zilizopo nchini. Kwenye
matamko ya viongozi wa dini
kuhusu dini nyingine, inashangaza
watu wenye heshima na dhamana
katika jamii kama viongozi wa dini
kujiuliza kwa mfano ni kwa nini
katika viongozi wanne wa juu wa
serikali, watatu miongoni mwao ni
wa dini moja bila hata kujali wanne
wanaowafuatia ni wa dini gani.
Mfano mwingine wa kushangaza
ni kusikia watu wenye heshima na
dhamana katika jamii wakiwemo
viongozi wa dini, kuhoji wingi wa
wajumbe wa dini moja kati ya dini
mbili katika Tume ya Mabadiliko ya
Katiba bila hata kuzingatia ukweli
halisi unaotakiwa katika muundo
wa tume hiyo wala nyadhifa za
wajumbe hao katika tume hiyo.
Ni dhahiri sharti la kila upande
wa muungano kutoa nusu ya
wajumbe, huku upande mmoja
ukiwa na zaidi ya 98% ya watu
wa dini moja, kunaifanya idadi ya
wajumbe wa dini moja kuwa wengi
kuliko wa dini nyingine. Lakini
baadhi ya watu walihoji ukweli huo
wakijifanya hawauoni.
Tatu; Ingawa, haiwezekani
kukakosekana kwa wenye udini
katika dini yoyote ile, kila suala la
udini linapozungumziwa, hakuna
upande unaokubali kuhusika na
udini huo. Kila upande wa dini
moja huelekeza lawama zote kwa
dini nyingine na kujivua lawama
zote. Katika kitabu chake cha
Sumu ya Udini, kwa mfano
Mwalimu Daniel Mwankemwa
anakiri kuwa suala la udini linazidi
kushika kasi miongoni mwa
jamii yetu, lakini lawama zote
anazielekeza kwa wale aliowaita
wanaharakati wa Kiislamu bila
hata kuthibitisha Uislamu wao
wala uhusiano wa harakati zao na
Uislamu. Aidha, amefanya hivyo
bila kuzingatia ukweli kuwa kuna
wanaharakati wa dini nyingine ya
Kikristo, akiwemo yeye mwenyewe,
hata kama hawajajinasibisha au
kunasibishwa na uanaharakati.
Nne; Mara kwa mara kauli za
wanaojinasibisha na wapambanaji
dhidi ya udini, huchochea udini
huo badala ya kuupunguza. Kauli
zao hutolewa zikiwa na maneno
yanayoonekana kupinga udini,
lakini yakichunguzwa kwa undani,
yanaonekana kubeba agenda
zilizofichika za kuimarisha udini
huo.
Katika toleo namba 463 la
gazeti la Msemakweli kwa mfano,

kuna mtu anayejiita Msomaji


Msemakweli aliyeandika yafuatayo:
Waislamu wana usongo sana
na Wakristo na wanataka Wakristo
tufutike katika uso wa dunia kwa
mujibu wa imani yao. Dini hiyo
kwao kuua ni jadi na wakiua mtu
ambaye sio Muislamu, wanadai
kupokea thawabu kubwa kutoka
kwa Mungu wao na adhabu zao
nyingi zinalenga kwenye mauaji.
Ni dhahiri kauli kama hizo
huchochea udini badala ya
kupambana nao. Mtu mwenye
mtazamo kama huu akipewa
mamlaka itakuwaje?
Tano; Wanaojinasibisha na
wapambanaji dhidi ya udini
ama hawamjui adui yao halisi au
wanajifanya hawamjui ili kuficha
malengo yao mengine. Badala
ya wapambanaji hao kumlenga
adui, hulenga kundi alilomo (au
wanalodhani yumo) adui huyo
ambalo halihusiki kabisa na
matendo yake. Mara kwa mara
hutokea kushutumiana baina
ya waumini wa dini tofauti kwa
kuhusisha dini zao ingawa katika
hali halisi shutuma hizo zinahusu
mtu mmoja au kundi dogo tu la
watu ambazo hazihusiani na imani
yao ya dini.
Sita; Ingawa upendo husisitizwa
katika dini zote, katika kile
kinachoonekana kuwa ni vita
dhidi ya udini, hakuna hata haki
licha ya upendo. Kuna unafiki
mwingi ambapo baadhi ya watu
hupiga vita dini badala ya udini.
Upendo ni zaidi ya kutoa haki kwa
maana ya kukubali kupoteza kwa
ajili ya yule umpendaye. Katika
kile kinachoonekana kuwa ni vita
dhidi ya udini, kuna kusingiziana
na kushutumiana kupita kiasi
(kutotendeana haki) na kutokubali
kupoteza kwa ajili ya wengine
(kutopendana). Kwa kiasi kikubwa,
kuna jitihada za kupata kuliko
wengine na kupata zaidi kuliko
inavyostahili (kudhulumiana).
Ishara hizi zinatuthibitishia
kuwa Tanzania kuna udini, na
kwamba huenda hatujamjua mdini
ni nani hivyo tunapambana na
adui tusiyemjua. Ni dhahiri hakuna
atakayefanikiwa kupambana na
udini ikiwa hawezi kutofautisha
matendo ya mtu binafsi na ya
dini yake, au na ya watu wengine
katika dini yake, hata kama yeye
mwenyewe atanasibisha matendo
hayo na dini hiyo.

4/27/2016 12:28:27 PM

18

Makala

RAJAB 1437, IJUMAA APRILI 29 - MEI 5, 2016

Tawhiid -8
Na Mussa Ame

SHUKRANI zote zinamstahikia


Allah (sw). Sala na salamu
zimfiie Mtume Muhammad
(saw), mtukufu wa daraja,
Masahaba wake na wote
wanaofuata mwenendo wake
mpaka siku ya malipo.
Somo la nane katika masomo
haya ya tawhiid, ni kipengele
cha sabiini na saba katika kitabu
cha Aqidatu Tahawy.
Tunaamini kuwa sala
inasaliwa nyuma ya kila mtu
katika watu wa Qibla yaani
wafuasi wa Mtume (saw),
kama ni mwema au muovu,
na tunaamini kuwasalia
wanapokufa.
Itikadi hii inafafanua kuwa
ni wajibu wa Waislamu kuwatii
viongozi, na kusali nyuma
yao hata kama viongozi hao ni
waovu au madhalimu.
Imesimuliwa kuwa Abdillahi
Bn Umar (ra) alisali nyuma
ya Hajaj Bn Yussuf Thaqafy
kiongozi dhalimu muuaji na
muovu. Salaf wanakubaliana
kusali nyuma ya kiongozi
Muislamu hata akiwa ni dhalimu
au muovu, anafanya dhambi
kubwa. Masahaba akiwemo
Abdalla Bn Masood (ra) walisali
nyuma ya Walid Bin Uqba Bn
Abi Muayt aliyejulikana kwa sifa
ya kuwa mlevi. Hii inatokezea
pale tu ambapo hakuna
uwezekano wa kusali nyuma ya
Imamu mwengine, ikiwa yeye
kiongozi muovu ndiye Imamu
pekee, basi hakuna kosa kusali
nyuma yake.
Kipengele cha tisini na tisiini
na moja katika kaitabu cha Ibnu
Qudama cha Luumatul Itiqad
kinasema kuwa:
Ni suna kumsikiliza Khalifa
wa Waislamu hata kama
atakuwa muovu muda kwamba
haamrishi maovu. Ni lazima
kumtii Kiongozi wa Kiislamu
ikiwa watu wanampenda
au wanamchukia, kwani
inakatazwa kuwapinga viongozi
na kuwafanyia uasi.
Ibn Abil Izz amefafanua
sababu ya kukatazwa kuwaasi
viongozi, ni yale madhara
yanayopatikana kutokana na
kuwaasi na kuwakamatia silaha
kuwaondosha kwa nguvu. Ibn
Taymiya anasema kuwa sababu
ya kuamrishwa kuvumiliwa
viongozi madhalimu ni kuwa
kuwaondosha kwa nguvu
madhara yake ni makubwa zaidi
kuliko faida yake. Kunakuwa na
umwagaji damu na hilo ni jambo
baya kabisa.
Kipengele hichi kimeeleweka
vibaya na baaadhi ya watu
kuwa hakuna haja ya kufanya
daawa wala kumkosoa kiongozi.
Wao wameona kuwa Uislamu

ANNUUR NEW.indd 18

unawakubali madikteta wote


na lazima wavumiliwe. Hii si
sahihi kwa sababu viongozi
wote wa Salaf walifanya
juhudi kubwa ya kuelimisha
watu ili kuleta mabadiliko ya
kifikra na walikosoa viongozi.
Maimamu wengi katika historia
ya Uislamu, walifungwa jela
au waliadhibiwa na watawala
jeuri wa wakati wao kutokana
na kuwakosoa katika udhalimu
wao. Ukisoma baadhi ya vitabu
vya Maulamaa wa Saudi Arabia,
utaona wametumia kipengele
hichi kuwalaumu Maulamaa
wanaokosoa utawala huo,
kuwa ni Khawarij na wanataka
kuiangusha Dola ya kitauhidi ya
Saudia. Lakini ukweli ni kuwa
Maulamaa hawa wanakosoa
tu mwenendo wa Dola hiyo ya
Kiislamu, kwa kushirikiana na
Wazayuni kumwaga damu ya
Waislamu huko Yemen, Iraq ,
Syria na kwengineko na kuaacha
kuwasaidia Waislamu wa
Palestina.
Kutokana na aqida hii,
msimamo unaodaiwa
kuwa wa ISIS wa kutaka
kuwaondoa madarakani kwa
nguvu watawala wa Syria na
kusababisha kumwagika damu
ya Waislamu na kuwafanya
wawe wakimbizi ni makosa ya
kiaqida. Kwa maana ni haramu
kuwakamatia silaha viongozi, na
kuongoza uasi utakaosababisha
vita baina ya Waislamu
wenyewe kwa wenyewe na
kumwaga damu ya maelfu ya
watu wasio na hatia.
Kuna hadithi nyingi sahihi
zilizokataza mambo yote
mawili, la kwanza kushirikiana
na viongozi madhalimu katika
kuwasaidia udhalimuwao,

AN-NUUR

pia imekatazwa kuwapinga


kwa kutumia nguvu, uasi
na mapigano, jambo ambalo
linaweza kusababisha hasara
kubwa ya kumwagika damu
isiyo na hatia ya Waislamu, na
faida yake kama iko ni ndogo
sana.
Amesimulia Nuuman Ibn
Bashir (ra) kwamba alitoka
kwetu Mtume (saw) alisema:
Eleweni watatokea
baada yangu viongozi
wanaodhulumu, na kusema
uongo, atakayewasadiki kwa
uongo wao, na akawasaidia
katika dhuluma zao , si katika
mimi, na mimi si katika yeye,
na asiyemsadiki kwa uongo
wake, na asiyemsaidia katika
dhuluma yake, yeye ni katika
mimi na mimi ni katika yeye.
(Ameipokea Ahmad ST2244).
Katika riwaya ya Jabir, wala
hawataingia kwenye hodhi
langu, na wasiowasadikisha
katika uongo wao, na
wasiowasaidia katika dhuluma
zao, mimi ni katika wao
na wao ni katika mimi na
wataingia katika hodhi langu.
(Ameipokea Ahmad ST2241).
Amesimulia Nafii bn Umar
(ra) kwamba Mtume (saw)
amesema:
Ni wajibu wa mja Muislamu
kusikiliza na kutii katika
mambo anayoyapenda na
anayoyachukia isipokuwa
anapoamrishwa katika maasi,
hapo hakuna kusikiliza wala
kutii. (SB 7144 SM 1839).
Amesema Imam Nawawy
kwamba, maana ya hadithi ni
kwamba msitoke katika utiifu
wa viongozi ila matakapoona
maovu ya wazi yanayokatazwa
kwenye Uislamu, mkiona

mambo hayo yakatazeni na


mseme haki popote mtapokuwa.
Ama kutoka katika utiifu moja
kwa moja na kupambana nao,
ni haramu kwa makubaliano ya
Wanazuoni wa Kiislamu hata
kama watakuwa mafasiki na
madhalimu. (Sherhe ya Sahihi l
Muslim kitabu la imara hadithi
ya 1709.)
Kwa hivyo suala la kuamrisha
mema na kukataza maovu
haliondoki mbele ya viongozi
madhalimu, bali ni wajibu,
lakini katika utaratibu mzuri si
kuwatukana.
Ama makatazo ya kuwapiga
vita na kukamata silaha dhidi
yao pia yameelezwa katika
hadithi sahihi.
Ummi Salamah(ra),
amesema Mtume (saw):
Hakika mtatawaliwa na
viongozi ambao baadhi ya
matendo yao yatawafikiana na
sheria na mtachukia matendo
yao mengine (yasiyowafiki
sheria), atakayechukia
ameepukana na adhabu, na
atakayewakataza amesalimika,
lakini atakayewaridhia na
akwafuata (ataangamia)
wakasema ewe Mtume (SAW)
hatupigani nao?, akasema laa
(msiwapige) muda wa kwamba
wanakusimamishieni sala.(SM
1854 T2265).
Amesimulia Awfi bn Malik
(RA) kutoka kwa Mtume (SAW)
amesema:
Wabora katika viongozi
wenu ni wale mnaowapenda
na wao wanakupendeni,
na mnawaombea na wao
wanakuombeeni, na viongozi
wabaya ni wale ambao
wanakuchukieni na wao
mnawachukia na wanakulaanini
na nyinyi mnawalaani.
Pakasemwa ewe mjumbe wa
Allah (SW) hatuwaondoshi
kwa upanga? Akasema laa!
Sivyo muda wa kwamba
wanakusimamaishieni sala,
katika riwaya nyengine eleweni
anayetawaliwa na kiongozi
akaona mambo ya maasi,
naachukie yale maasi tu lakini
asijivue katika kuwatii.(SM
1855).
Amesimulia Hudhayfa bn
Yamani (RA) kutoka kwa Mtume
(SAW) amesema Watakuja
baada yangu viongozi ambao
hawaongozi kwa uongozi wangu
wala hawafuati sunna yangu,
mtaongozwa na watu nyoyo zao,
nyoyo za shetani katika miili ya
wanaadamu. Pakasemwa ewe
Mjumbe wa Allah(SW), nifanyeje
nikikutana nao, akasema
Msikilize na mtii amiri wako,
japo atakupiga mgongo wako,
na ataipora mali yako msikilize
na mtii. (SM1847).
Hadithi zimeeleza wazi
kuhusu makatazo ya kuwapiga
vita kwa silaha, wakati huo huo
haja, ya kuwanasihi kwa lugha
nzuri.
Wabillahi tawfiiq.

4/27/2016 12:28:27 PM

19
M

Ukurasa wa Watoto

AN-NUUR

RAJAB 1437, IJUMAA APRILI 29 - MEI 5, 2016

Nguzo za Uislamu

Jenny (kushoto) na mwenzake wakitamka shahada ya kusilimu.

Wiki iliyopita
tujifunza kuwa
Uislamu ni Dini ya
Allah (SW).
Uislamu ni Dini ya
kumtii Allah (SW)
kwa unyenyekevu.
Uislamu ni Dini
inayofuatwa na
maumbile.
Uislamu ni Dini
iliyofundishwa na
Mitume wote.
Uislamu ni Dini ya
walimwengu wote.
Uislamu ni
Dini ya haki na
inayosimamia haki
katika jamii.
Leo tutajifunza juu
ya nguzo za Uislamu.
Uislamu umejengwa
juu ya nguzo tano:
1. Kutoa shahada
mbili.
2. Kusimamisha
Swala tano.
3. Kutoa Zakat.
4. Kufunga mwezi
wa Ramadhani.
ANNUUR NEW.indd 19

5. Kuhiji katika
nyumba takatifu (AlKaabah) kwa kila
mwenye uwezo.
Nini maana ya
Shahada mbili?
Shahada ya
kwanza ni kusema:
Nashuhudia kuwa
hapana mungu
apasaye kuabudiwa
kwa haki ila Allah.
Shahada ya pili
ni kusema: Na
ninashuhudia kuwa
Muhammad ni
Mtume wa Allah.
Muislamu wa kweli
anashahadia kila
akiswali.
Waislamu
walioshahadia
kikweli, hufuata yale
yote aliyowaamrisha
Allah (SW) na
Mtume wake.
Pia hijiepusha
na vitu vyote
alivyokataza Allah
(SW) na Mtume
wake.
4/27/2016 12:28:33 PM

AN-NUUR

20

MAKALA

20

RAJAB 1437, IJUMAA APRILI 29 - MEI 5, 2016

Soma gazeti la
AN-NUUR
KWA TSH 800/=
kila Ijumaa

AN-NUUR

RAJAB 1437, IJUMAA APRILI 29 - MEI 5, 2016

Jumuiya kongwe ya Kiislamu Dodoma yafufuka


Na Bakari Mwakangwale

JUMUIYA ya Waislamu Mjini


Dodoma, imejipanga kuwatumikia
Waislam kwa kuinua maendeleo
yao katika nyanja za kiuchumi
kwa kuzingatia kuwa watu ndiyo
mtaji wa mafanikio katika jamii
husika.
Hayo yamebainishwa katika
taarifa ya Bodi ya Jumuiya hiyo
(THE DODOMA GENERAL
MUSLIM ASSOCIATION) ikitoa
taarifa yake kwa Waislamu mapema
hivi karibuni Mjini Dodoma, kwa
kipindi cha mwaka 2003-2016.
Taarifa hiyo imesema, Taasisi
hiyo ipo kwa lengo la kuwaweka
pamoja Waislamu wa Dodoma
sambamba na kuwatumikia pamoja
na kuinua maendeleo ya Uislamu
kwa ujumla.
Uislamu kama dini, hauna
rangi wala ubaguzi wa aina yeyote
ile, hivyo Taasisi hii ipo kwa lengo
la kuwaweka pamoja Waislamu
hapa mkoani Dodoma, pamoja
na kuwatumikia kwa kuinua
maendeleo ya kidini, ustawi wa
Jamii ya Kiislamu katika nyanja za
Kijamii na Kiuchumi. Imesema
taarifa hiyo.
Taarifa hiyo imepambanua
kwamba Bodi inayo ongoza ndiyo
itakayo kuwa na jukumu la kubeba
na kuhakikisha huduma za Kiimani
(kiroho) zinafanyika pia kuweka
uwiano sawa wa huduma za
ustawi wa Kijamii na maendeleo ya
kiuchumi kwa Taasisi, kwani Taasisi
ni watu, bila watu Taasisi haipo na
kwamba watu ndiyo mtaji ambao
unaweza kuwatoa hapo walipo na

kusonga mbele.
Taarifa hiyo imesema, maandalizi
mengine yanaweza kufanyika
kwa kuwahimiza Waislamu
kuchangamkia fursa mbalimbali
zinazoanzishwa miongoni mwa
jamii wanamoishi.
Mathalani taarifa hiyo
ikasema fursa za elimu zilizopo
sasa, zitumike kwa Waislamu
kuwapeleka watoto wao Shuleni
sambamba na kuwahimiza elimu
ya dini, kwa kufanya hivyo ikasema
taarifa hiyo wataweza kuwapata
vijana wenye elimu nzuri hapo
baadae ikiwa watasimamiwa vizuri.
Taarifa hiyo ikaeleza lengo la
kuwakusanya Waislamu katika
mkutano wake huo kuwa ni
kuwahamasisha Waislam wa
Dodoma pamoja na Wilaya zake
kujiunga katika Taasisi hiyo
(DGMA).
Tumefanya hivi kuwaita kwa
misingi ya kuleta mapenzi, upendo
na umoja miongoni mwetu ili
tuweze kufaidika kupitia Taasisi
hii. Imesema taarifa hiyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti
wa Taasisi hiyo, Sheikh Mohammed
Thabiti, akiongea katika mkutano
huo, alisema kila Muislamu ana
wajibu wa kuwaeleza Waislamu
wenye nia njema na Taasisi hiyo
ili waweze kujiunga kwa lengo la
kuunganisha nguvu.
Maimamu na Viongozi wa
Taasisi nyingine ni Mabalozi wa
kuitangaza kwa waumini Taasisi
hii, pia kuwaeleza au kuwaelekeza
waweze kufika ofisini na kupata
taratibu za namna ya kujiunga.
Amesema Shkh Thabiti.
Alisema, huduma za Kiroho au

Dini huwezi kuzitenganisha na


masuala ya ustawi wa maendeleo ya
Kiuchumi na Kijamii kama nguvu
za kiuchumi, Elimu, Afya pamoja
na kutengeneza uwiano sawa kwa
mambo ya kijamii na mazingira
wezeshi.
Nasaha zangu, kwenu
tunatakiwa kujitahidi kwa kadri
tuwezavyo kuepuka migogoro
miongoni mwetu kwani hilo
linaweza kuturudisha nyuma
kimaendeleo, mfano halisi angalieni
mgogoro wa Taasisi hii umedumu
kwa muda mrefu sana na kuififisha
Taasisi ambayo ina malengo mazuri
kwa umma wa Kiislamu, hata hivyo
migogoro tumeimaliza sasa tuchape
kazi. Amesema M wenyekiti huyo.
Historia fupi ya Taasisi hiyo
inajieleza kwamba chimbuko la
(DGMA), ni mwaka 1958, kupitia
kwa Waislamu walioishi Dodoma
na ilisajiliwa na kupata usajili
wake mwaka 1959, kutoka Ofisi ya
Kabidhi Wasii.
Tokea wakati huo ilikuwa na
malengo ya kusimamia maendeleo
ya Jamii ya Kiislamu, mathalani
kusaidia waumini wanaohusika
kisheria katika dini, kama vile
Wasiojiweza, Vilema, Yatima,
Wajane, Wazee Vikongwe pamoja
na Ajuza.
Hata hivyo harakati za Taasisi
hiyo zilififia miaka kumi baadaye
yaani mwaka 1968, baada ya
kuundwa kwa BAKWATA kwa
amri ya Serikali (GN. No. 168
ya 1968) na kuifuta Taasisi ya
THE EAST AFRICAN MUSLIM
WELFARE SOCIETY.
Hata hivyo amri hiyo
haikuhusu Taasisi ya THE

DODOMA GENERAL MUSLIM


ASSOCIATION hivyo iliendelea
kuwepo, lakini baadhi ya Waasisi
wa Bodi ya Wadhamini wa
Taasisi walihama Dodoma, kwani
walitaharuki na amri hiyo ya
Serikali ya kuifuta EAMWS.
Kwa kutofahamu waliamini
kwamba Taasisi yao nayo imefutwa
na kukabidhi nyaraka za Taasisi
na mali kimakosa kwa BAKWATA,
kwa kuwa hawakupata taarifa
nyingine rasmi kuwa Taasisi na
Jumuiya nyingine za Kiislamu
hazikuhusika na amri hiyo.
Katika miaka ya hivi karibuni,
baadhi ya wadau wa Taasisi
walifanya harakati za kuirejesha
Taasisi hiyo mikononi mwa
Waislamu baada ya kubaini kuwa
baadhi ya mali zake kuanza kuuzwa
kinyemela.
Ambapo, iliundwa kamati
maalum iliyojulikana kama
Kamati Maalum ya kushughulikia
Mustakabali waTaasisi ya THE
DODOMA GENERAL MUSLIM
ASSOCIATION, ambapo kamati
imekuwa ikisimamia Taasisi na
kufanya juhudi za kurudisha mali
za Taasisi hiyo, ikiwemo Shule ya
Sekondari ya Jamhuri pamoja na
viwanja vilivyopo katika maeneo
mablimbali katika Mjini wa
Dodoma.
Ukweli ni kwamba tokea
mwaka 1968, uhai wa Taasisi hii
ulikumbwa na misukosuko mingi,
hali iliyofanya tujifinze, kwani
kama hujapata tatizo ni vigumu
kujua ufumbuzi sasa tumefungua
ukurasa mpya, kwani tusingeweza
kuufungua bila yakujifunza kupitia
misukosuko ya nyuma. Imesema
taarifa ya Bodi ya Taasisi hiyo.

HAIIBA TIMAMU TEA

CHAI YA AJABU KWA AJILI YA KUKABILIANA NA

TATIZO LANGU LA KUHISI KAMA SINDANO ZINACHOMA KWENYE NYAYO


NA GANZI LIMEONDOKA BAADA YA KUTUMIA HAIIBA TIMAMU TEA
Na. Seif Abdallah
Kwa muda mrefu nilikuwa nakabiliwa na tatizo la hisia za kuchomwa
chomwa na sindano kwenye nyayo pamoja na ganzi. Pamoja na kujaribu
matibabu ya aina tofauti tofauti kwa muda mrefu hali hii iliendelea. Siku
moja jamaa yangu mmoja alinipa namba za simu na kunishauri niwasiliane
na wahusika huenda wangeweza kunisaidia. Niliwapigia wahusika simu
wakaniambia nitembelee ofisi zao zilizoko mtaa wa Mosque, kitumbini jijini
Dar es Salaam. Nilipofika waliniambia tatizo langu lilikuwa linahusu zaidi
mishipa ya fahamu na mzunguko wa damu. Walinipatia chai ya Timam na
kunipa ushauri wa lishe. Nilishangaa sana kuwa ndani ya siku tatu zile
sindano na ganzi vilitoweka na hadi leo ile hali sijaisikia tena!

SHINIKIZO LA DAMU (HYPERTENSION/HIGH


BLOOD PRESSURE)
UGONJWA WA MOYO
KIHARUSI
JONGO (GOUT)
MAUMIVU YA VIUNGO (RHEUMATISM)
MAUMIVU SUGU YA KICHWA
BAWASIR (PILES/HEMORRHOIDS)
MAGONJWA YA INI
SARATANI MBALIMBALI
UOTO/UVIMBE MBALIMBALI KATIKA VIUNGO
VYA UZAZI VYA MWANAMKE (FIBROIDS,
POLYPS NA CYSTS)
KUSHINDWA KUZUIA MKOJO (URINARY
INCONTINENCE)
ATHARI ZA KISUKARI CHA UKUBWANI
PUMU
UPUNGUFU WA KINGA ZA MWILI
KASI YA KUZEEKA
MATATIZO YA MFUMO WA MZUNGUKO WA
DAMU
MKAKAMO WA NGOZI;
UDHAIFU WA MACHO
KUPOTEZA KUMBUKUMBU
KASI NDOGO YA KUPONA MAJERAHA
MAKOVU KWENYE MAPAFU
UGONJWA WA NGOZI KUCHUJA RANGI,
YAANI, VITILIGO

HAIIBA TIMAMU TEA


INAPATIKANA
HERBAL IMPACT
MOSQUE STREET, NO. 1574/144
(MKABALA NA MSIKITI WA
SUNNI), KITUMBINI, DAR ES
SALAAM
TUTEMBELEE AU TUPIGIE SIMU
NAMBA:
0754281131/0655281131/06862
81131/0779281131

https://www.facebook.com/Herbal-Impact-157972014402705/

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Ltd, Dar es Salaam.
ANNUUR NEW.indd 20

4/27/2016 12:28:35 PM

Вам также может понравиться