Вы находитесь на странице: 1из 20

www.annuurpapers.co.tz au facebook:annuurpapers@yahoo.

com

AHLU SUNNA WAL JAMAA HAJJ AND UMRA TRUST


(7) TAJIRIKA KWA KUHIJJI!

Sauti ya Waislamu

ISSN 0856 - 3861 Na. 1228 SHAABAN 1437, IJUMAA , MEI 6 - 12, 2016 BEI TShs 800/=, Kshs 50/=

Mtume(saw) amesema, Mahujaji wanalipwa


kwa kila walichokitumia katika Hijja, shilingi
moja kwa milioni moja. Mali ya Muislamu
huongezeka anapohiji! Unapata duniani na
unafanikiwa Akhera. Wahi sasa kuja kulipa
uitakase mali yako. Gharama zote kwa Hijja
2016/1437 ni Dola 4,600. Umra ya Ramadhani
ni Dola 2,700. Karibuni Ahlu Sunna wal
Jamaa kwa huduma nzuri na uongozi bora.
Wasiliana nasi: Tanzania Bara: 0679895770/
0688895777; 0765462022; 0712735363.
Zanzibar: 0777468018; 0777458075;
0777845010; 0777497300.

Tunajichimbia shimo-Shahari
Mh. Riziki Shahari.

Tusiwafikishe watu wakaona


Hawana cha kupoteza ila roho
Tusiwagawe watu kwa dini, kabila

Usione vyaelea

Watu wamekaa rumande!

Ukandamizaji utavunja
Muungano- Ally Saleh
Aibua hoja ya muundo wa Shirikisho

Mhe. ALLY Saleh, Mbunge wa Mji Mkongwe (CUF).

Sio Ugaidi ni ubunifu

Haikuwa kazi rahisi kufikia hapa tulipo hivi sasa. Tupo tuliokaa rumande
kwa kushitakiwa kuwa tumeleta vurugu Msikitini. Kesi zimeunguruma katika
Mahakama za mwanzo hadi kufika Mahakama Kuu. Soma Uk. 20

ANNUUR NEW.indd 1

Abdul Nadir Mumin.

5/4/2016 3:26:46 PM

Suratu An-faal

Kwa hakika uadui


wa ukafiri ambao
umejijenga dhidi ya
imani, unausukuma
upande wa ukafiri

Fethullah-Gulen

ISIPOKUWA, ili
atimize Mwenyezi
Mungu jambo ambalo
lilikuwa ni lenye
kutendwa ili aangamie
yule atakayeangamia
kutokana na hoja
na asalimike
atakayesalimika
kutokana na hoja. Na
kwa hakika Mwenyezi
Mungu ni mwenye
kusikia mjuzi. [ALANFAAL 42]
Uhakika kufuatana
na aya hii (Na lau
angetaka Bwana wako
wangeamini walio
katika ardhi wote
kabisa) [Younusu
99] kulikuwa
kunawezekana kuwa
na utaratibu maalumu
mwingine katika dunia.
Isipokuwa ni kwamba
matakwa ya Mwenyezi
Mungu yamehukumilia
kuwapo kwa
mapambano ya tangu,
kati ya imani na kati ya
ukafiri kipindi chote
cha maisha ya dunia.
Na kunawezekana
kuishuhudia hakika
hii ambayo iko wazi
wakati wa kuichunguza
historia ya binadamu
tokea Adam (a.s.)
mpaka leo. Kwa msingi
huo, muda wa kuwa
tunataka kuishi katika
dunia ya imani, ni
juu yetu tusisahamu
kitambo chochote
kwamba sisi tutapatwa
na kero za ukafiri na
mabavu yake na nguvu
zake, na khiyana yake
na uadui wake.

mapambano haya ni
ya lazima. Umefanyika
mpango wa jambo
hili upangaji ambao
umevuka uelewa wa
kwenye kutekeleza uadui kibinadamu mpaka
juu ya waumini kwa
kunapatikana kufikia
sura yenye kuendelea.
kwenye hatua ya
Kunapasa kutopatikana
mapambano uso kwa
mbele zao hisia kwamba
uso. Ikadhihirika kwa
wao wanakwenda kati
uwazi wote uhai wa
ya watu ambao hawahisi
yule ambaye anastahiki
na hawatambui kitu
kuishi, kutokana na
chochote ili aangamie
haja na yule ambaye
atakayeangamia
anastahiki kufa
kutokana na hoja na
kutokana na ushahidi
awe hai atakayekuwa
na hoja, wakaporomoka
hai kutokana na hoja.
wanyonge na yale yote
Kusipatikane kwa mtu
ambayo wameyabeba
yeyote udhuru mbele
katika mfundo na
ya Mwenyezi Mungu
kutopenda na chuki na
mtukufu na hali ya kuwa
kuwa mbali na unyoofu
hawezi kusema: Ni
na kushiriki katika
kwanini na kwa sababu
sharia. Haukubaliki
gani?
mbele zao udhuru
Na huenda kukazuka
wowote katika jambo
kinyume cha haya
hili.
tuliyoyaelezea punde
Ama wale ambao
hivi, maana watakuwa
hawakutenda kosa
waumini wenye
lolote au uhalifu
kushindwa juu ya mambo wowote, bali
yao na inakuwa dunia
wamesimama tu kwa
ya ukafiri ndiyo yenye
kuwatia adabu wale
kushinda. Isipokuwa
ambao wanastahiki
matokeo hayabadili
kutiwa adabu katika
pamoja na hali hiyo.
Badr na mahali
Na haumiliki upande
pengine, kuna hakika
walio katika pande mbili
wamegusa upeo wa
hizi udhuru wowote
uhakika wa maisha
ambao watautoa mbele
kwa utulivu wote wa
za Bwana wao, kwa
moyo, wa kiroho na wa
sababu usumbufu na
kihisia.
mapambano maalumu
Kwa ufupi kwa
kumeshapatikana.
hakika mambo
Kuishi nayo na
yaliyopita katika Badri
kuyatenda na katika
na katika mapambano
hayo ameangamia
yote ya mfano wa Badr,
aliyeangamia na
hapakubakia jambo
amekuwa hai aliyekuwa ambalo tunawezekana
hai.
kulizungumzia nje
Kwa ajili ya kuliweka ya kipimo sahihi cha
wazi zaidi jambo
chombo hiki. Si mbele
hili tunasema: Kwa
za wale ambao wa
hakika Mwenyezi
kuuliwa mbele za
Mungu mtukufu
wale ambao wameishi,
ameyafanya makundi
si mbele za wale
mawili yanakutana
ambao wamefuzu
mahali ambapo
wala wale ambao
lau yangeahidiana
wamepata hasara.
yangetofautiana katika
Hapo hapakubakia
ahadi, na ameyaandaa
jambo lolote kwa
mazingira ya
sababu mambo yalipita
mapambano, na uwanja kufuatana na vile
wake na masharti
alivyopanga Mwenyezi
ambayo yameyafanya
Mungu msikivu mjuzi.

Mwandamo wa mwezi

Leo ni Tarehe 28 Rajab mwaka 1437 AH, sawa na tarehe 6 May, 2016.
Tarehe 6 June tunategemea kuangalia mwezi kwa Ramadhan na
Tarehe 7 June 2016 tukijaaliwa tutaanza Ramadhan Rasmi. Kutokea
hii leo Ijumaa ya tarehe 6 May 2016 hadi kufika kuanza mfungo wa
Ramadhani tumebakisha siku 30.

ANNUUR NEW.indd 2

AN-NUUR

Mafundisho ya Qur'an/Uwanja wa Maarifa

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 6 - 12, 2016

UWANJA WA VIJANA-JIONGEZEE MAARIFA


JAWABU CHEMSHA BONGO NAMBA:49
M

3:154

40

41

42

na

43

na

na

44

45

na

JK

46

47

na

48

94:5-6

25

55

AN

40:68

CHEMSHA BONGO: 50

Weka duara kwenye jawabu ilio sawa. Jawabu kamili wiki ijayo.
W

12:25

7:30

8:9

7:22

50:34

914

114

22

49:6

MASUALA
1. Itaje Sura ipi na aya ya ngapi? Na wote wawili wakakimbilia
mlangoni, na mwanamke akairarua kanzu yake Yusuf kwa nyuma. Na
wakamkuta bwana wake mlangoni. Mwanamke akasema: Hapana malipo ya
mwenye kutaka kumfanyia maovu mkeo isipo kuwa kufungwa au kupewa
adhabu chungu.
2. Itaje Sura ipi na Aya ya ngapi? Enyi mlio amini! Akikujieni mpotovu
na khabari yoyote, ichunguzeni, msije mkawasibu watu kwa kuto jua, na
mkawa tena wenye kujuta kwa mliyo yatenda.
3. Itaje Sura na Aya ya ngapi (Ataambiwa) ingieni kwa salama. Hiyo
ndiyo siku ya daima dawamu
4. Zipo Sura ngapi katika Quran?
5. Zeynab, Rukaya, Ummul Kulthum, Fatma hawa ni akina nani?
6. Kipando cha mnyama aliompanda Mtume Muhammad (SAW) katika
safari ya Miraj anaitwaje?
7. Vitabu vitukufu waliopewa Mitume ni Taurat, Zaboor, Injeel na ..
8. Surat Al Faatiha ina aya ngapi?
9. Unaposhukuru unatakiwa useme kalima gani?
10. Kitabu cha Injeel kateremshiwa Mtume yupi?

Jee Unajua?

1. Katika vita vikuu vya Pili Duniani inakisiwa kuwa watu wapatao
milioni 25 waliouwawa kwa nchi ya Urusi pekee: http://www.
secondworldwarhistory.com/world-war-2-statistics.asp
2. Bangladesh ni nchi yenye mito mingi duniani ikiwa ina mito zaidi ya 800:
https://answers.yahoo.com/question/index?qid=20120825102745AAE9akK
3. Nchi ya Canada ina maziwa yafikayo idadi ya maziwa 31,752: http://
www.zmescience.com/other/great-pics/geographical-facts-youre-not-goingto-believe-22022010/
4. Mlima Everest unaopakana baina ya nchi ya Nepal na Tibeti ndio
Mlima mrefu kuliko yote: http://www.answers.com/Q/What_country_in_
the_world_has_the_most_mountains?#slide=1
5. Nchi ya Nepal ndio nchi ilio na milima mingi duniani: http://10mosttoday.
com/10-highest-mountains-in-the-world/ na https://answers.yahoo.com/
question/index?qid=20100525024502AAtXTMk
6. Nchi ya Guyana ndio nchi inayoongoz kwa watu kujiua, kati ya watu
100,000 watu 44 hujiua : http://list25.com/25-countries-with-the-highestsuicide-rates-in-the-world/5/
7. Nchi za Ulaya ya Mashariki ndio nchi zinazoongoza kuwa na walevi
wengi, nchi ya Belarus ndio inayoongoza kwa wastani mtu mmoja hunywa
Lita 17.5 kwa mwaka na ulevi ndio unaochukua maisha ya watu wengi, kati
ya vifo vyote vinavyotokea katika nchi hio asilimia 34 hutokana na ulevi :
http://www.marketwatch.com/story/10-countries-where-people-drink-themost-2014-05-30?page=5
8. Nchi ambazo Pombe zimepiga marufuku kati ya hizo ni Falme za
nchi za KiarabuUAE, Iran, Iraq, Libya, Saudi Arabia, Bangladesh, Brunei
: http://www.thedailymeal.com/drink/10-countries-where-alcohol-illegalslideshow/slide-4
9. Nchi 10 zinazopendwa kufanya uchawi ni Nigeria, Zambia, Malawi,
Kenya, Congo DRC, Ghana, Uganda, Papua New Guinea, Gambia na
Tanzania : http://kkdaniels.blogspot.com/2015/08/top-10-african-countriesat-practicing.html
10. Mexico ndio nchi inayoongoza kuwa na wizi mwingi duniani : http://
www.insidermonkey.com/blog/11-countries-with-the-highest-rates-ofidentity-theft-in-the-world-351940/
(Kutokana na kutokuwa na wasomaji wengi katika Ukumbi wa
Uwanja wa Maarifa na kutopata majibu ya kuuboresha huu wa Uwanja
wa Maarifa, tunafikiria kuanzisha ukumbi mwengine. Tuma barua pepe
zuwarde@gmail.com au ujumbe mfupi kupitia simu 0777436949 unahisi
ninii uwe mbadala wake?)

5/4/2016 3:26:50 PM

Habari

AN-NUUR

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 6 - 12, 2016

Tunajichimbia shimo-Shahari
Na Bakari Mwakangwale

UMEPIGWA mfano kwamba


viongozi wa serikali
wamekuwa kama wale
waliotajwa katika vitabu vya
dini kwamba mioyo wanayo,
lakini hawataki kufahamu
kwayo, macho wanayo, lakini
hawataki kuona kwayo kama
ambavyo wana masikio,
lakini hawasikii kwayo.
Hiyo ni kutokana na
kuyafumbia macho madai ya
Waislamu bila ya kuyatafutia
ufumbuzi halikadhalika
kwenda kinyume na kanuni
za haki, uadilifu na utawala
bora kwa ujumla.
Yakatajwa baadhi ya
madai ya Waislamu kuwa
ni pamoja na MoU, utendaji
wa baadhi ya watumishi wa
NECTA, pamoja na suala la
Masheikh wanaoshikiliwa
kwa miaka mitatu sasa bila
kesi zao kuzungumzwa
wala kujulikana hatma yao.
Kwamba kosa lao nini?
Tahadhari hiyo imetolewa
Bungeni mjini Dodoma na
Mbunge wa Viti Maalum wa
Mafia, kupitia Chama Cha
Wananchi CUF, Bi. Riziki
Shahari akichangia hotuba
ya Ofisi ya Rais, Tamisemi na
Utawala Bora, katika Bunge la
Bajeti linaloendea hivi sasa.
Mh. Riziki, akichangia
hotuba hiyo, alipinga uwepo
wa Utawala Bora nchini,
akihoji ni utawala bora gani
ambao haujali watu wake na
hauzingatii misingi ya haki za
binadamu na hata kupuuza
watu wake.
Akasema, ni jambo la
kusikitisha kuwa viongozi wa
serikali wanaojigamba kuwa
waadilifu na wanaofuata
haki na utawala bora, lakini
inapokuja suala la Waislamu
wanakwenda kinyume kabisa.
Kwa hali hii mnataka
Waislamu wasimame wapi na
waielewe vipi Serikali hii, hivi
hawa Waislamu si sehemu ya
jamii ya wanchi wa nchi hii?
Utawala bora gani
usiofanyia kazi madai ya watu
wake. Kwa mwenendo huu
tuelewe kuwa tunajichimbia
shimo wenyewe na
tutaangamia. Amesema Mh.
Riziki na kutahadharisha.
Mh. Riziki, akahoji na
kuweka wazi zaidi kwamba
ni jambo la kushangaza iwapo
wanazungumzia Utawala

ANNUUR NEW.indd 3

Bora, huku utawala wenyewe


ukiwa na watumishi ambao
wanawagawa wananchi wao
katika makundi ya kiitikadi na
kidini jambo ambalo ni hatari.
Aidha, Bi. Riziki,
akalieleza Bunge hilo la
Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, kwamba Bunge
hilo lilishaambiwa muda
mrefu kuwa Waislamu
wanalalamikia suala
la Memorandum of
Understanding (MoU)
kwamba kuna pesa zinatolewa
na Serikali kwa upande
mmoja wa dini vipi kuhusu
wao, lakini akasema hakuna
majibu wanayopewa zaidi ya
kuambulia kejeli.

Si hayo tu, lakini pia


akasema, Waislamu hao
hao walilalamikia Baraza la
Mitihani la Taifa (NECTA)
juu ya (aliyekuwa) Mtendaji
Mkuu na Serikali iliunda
kamati ya uchunguzi, lakini
hawakueleza chochote mpaka
sasa badala yake mtu huyo
huyo amewekwa juu na
mbaya zaidi katika eneo lilelile
la elimu, alilolalamikiwa na
jamii ya Waislamu.
Ifahamike kwamba
binadaamu akifikishwa
mahala ambapo anaona
hana cha kupoteza ila roho
yake, haoni thamani hata
ya hiyo roho yenyewe, roho
ina thamani kama maisha

yake yatakuwa na thamani


pia lakini kama ataishi kwa
mashaka na uonevu ni hatari.
Amesema Bi. Riziki.
Awali, kabla ya kuanza
kuchangia hutoba hiyo, alitoa
nasaha zake kwa wabunge
wenzake waliotangulia
kuchangia hotuba hiyo
akisema, inaonekana
Wabunge wengi wanaonekana
kukata tamaa kufuatia
kuzungumza maswala
hayo hayo kila awamu bila
kufanyiwa kazi.
Akasema, hakuna sababu ya

kwetu tunaendelea kujivika


kilemba cha ukoka kwamba;
sisi ni kisiwa cha amani wakati
kilichopo ni utawala wa kibabe.
Alisema Ally Saleh na
kuongeza kuwa Serikali ya
Tanganyika (Tanzania) inayojidai
kwamba ndiyo ya Muungano,
imesimamia kuvunjwa kwa
Katiba ya Zanzibar kwa
kuiweka kwa nguvu Serikali
huko Zanzibar kinyume
na matakwa ya Wazanzibari
waliyoyadhihirisha Oktoba 20,
2015.
Akasisitiza kuwa kulikuwa
hakuna msingi wowote wa
kikatiba wala kisheria wa
kufuta uchaguzi wa Zanzibar
ambao ulifanyika kwa amani na
washindi kutangazwa na kupewa
shahada za ushindi.
Katika kuonyesha kuwa kuna
mambo mengi ya kujadiliwa
ili kuweka mazingira mazuri
kuhakikisha kuwa muungano
unadumu, Ally Saleh alisema
kuwa serikali ya Tanganyika,
iliyojivika koti la Muungano,
inaonekana kama mkoloni
anayeinyonya Zanzibar.
Akasema, ni kutokana na sura
hiyo inayojitokeza, Muungano
unakosa ridhaa ya wananchi
na hivyo serikali kulazimika
kutumia jeshi kuulazimisha.
Kambi Rasmi ya Upinzani
Bungeni inatoa rai kwa Serikali
hii ya awamu ya tano kwamba;
kama kweli ina nia ya kuuenzi
na kuudumisha Muungano, basi
izingatie maoni ya wananchi
waliyoyatoa kwenye Tume ya
Mabadiliko ya Katiba kuhusu
muundo wa Muungano ili kuwa
na Muungano unaoridhiwa na
wananchi wa pande zote mbili za
Muungano. Alisema.
Kwa upande mwingine Ally
Saleh akahoji juu ya vitendo
vinavyofanywa na vikosi pamoja
na wanaoitwa Mazombie vya

kupiga watu na kuharibu mali.


Hayo yote yakionekana
kuwa yana baraka za serikali
kwa vile hakuna hatua zozote
zinazochukuliwa dhidi ya jinai
zinazofanywa na makundi hayo.
Akahoji, inakuwaje mambo
hayo kufanywa hadharani
lakini, Jeshi la Polisi chombo cha
Muungano, limekuwa likisema
halijui kama kuna makundi hayo
na wala vitendo vyao.
Naibu Waziri wa Mambo ya
Ndani (Mh.) Hamad Masauni
na Waziri wa Ulinzi na Jeshi
la Kujenga Taifa, Dk. Hussein
Mwinyi wamesema eti hawajui
chochote kuhusu matendo hayo
ya dhulma ya wale wanaoitwa
Mazombie.
Lakini wakati Panya Road
ilipotikisa Dar es Salaam
ilichukua muda mchache tu
kufyagiwa wote, hata manyoya
yao hayakuonekana.
Akahoji, vipi la mazombie
lishindikane, hali ambayo
inajenga dhana kuwamba
huenda vitendo vyao vya
kihalifu na jinai, vinainufaisha
CCM Zanzibar, na ndio
maana Serikali ya Muungano
imelinyamazia kimya.
Kwa upande mwingine, Ally
Saleh akaonyesha wasiwasi
wake juu ya uwepo wa kesi za
kubambikiwa ambapo akadai
kuwa, jeshi la polisi limekuwa
likiwakamata raia wema alimradi
ni wanachama au wapenzi wa
CUF na kuwabambika kesi za
uongo.
Akatoa mfano kuwa katika
kipindi cha uchaguzi Zanzibar,
takriban watu 250 walikamatwa
na polisi wakiwemo viongozi
wakuu wa CUF.
Akasema, ni katika mkumbo
huo, walikumbwa Naibu
Katibu Mkuu wa CUF Nassor

kukata tamaa, bali washikamane


na amri ya kutoa nasaha na
kukumbusha kama vitabu vya

Dini vinavyoagiza.

Ukandamizaji utavunja Muungano-Ally Saleh


Na Mwandishi Wetu

IMEELEZWA kuwa kama


gharama ya muungano ni
kukandamiza demokrasia
Zanzibar, basi hiyo itakuwa
pia ndio sababu ya uhakika ya
kuuvunja Muungano wenyewe.
Hayo yamesemwa na Waziri
Kivuli na Msemaji Mkuu wa
Kambi Rasmi ya Upinzani
Bungeni katika Ofisi ya
Makamu wa Rais-Muungano,
Mheshimiwa Ally Saleh (MB).
Ally Saleh, ambaye pia
ni Mbunge wa Jimbo la Mji
Mkongwe, amesema hayo
mapema wiki hii akichangia
hotuba ya bajeti ya Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano
na Mazingira.
Mheshimiwa Saleh katika
hotuba yake amedai kuwa,
Serikali ya Tanzania imekuwa
msemaji hodari wa demokrasia
za wengine, huku ikiendesha
ukandamizaji wa demokrasia
Zanzibar kwa lengo la kukilinda
chama tawala, CCM na serikali
yake.
Akatoa mfano wa uchaguzi
uliopita ambapo alidai kuwa
ilitumika hadaa na njia haramu
kupindua matakwa ya wananchi,
ukaletwa uchaguzi kiini macho
na matokeo ya kuupika.
Ally Saleh akasema, ulikuwa
ni uvunjaji wa wazi wa katiba
na sheria ya uchaguzi, lakini
badala ya serikali ya muungano
kusimamia haki, ikaja na
visingizio kwamba haina
mamlaka ya kuingilia Tume ya
Uchaguzi Zanzibar.
Hata hivyo akasema kuwa,
wakati ikileta madai hayo,
ikatumia jeshi kuzima matakwa
ya wananchi na kusimamia batili
kutendeka.
Tumekuwa hodari kusemea
ukandamizaji wa demokrasia
katika nchi nyingine, lakini

Inaendelea Uk. 4

5/4/2016 3:26:50 PM

Tahariri/Makala

AN-NUUR

S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786


Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM.
www.annuurpapers.co.tz
E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk
Ofisi zetu zipo: Manzese Tip Top
Usangi House, barabara ya Morogoro, D'Salaam

Tuache kibri tujenge


umoja kwa Waislamu

TUNACHUKUA
fursa hii kukumbusha
Waislamu kwa ufupi
kuhusiana na kupoteza
maadili (kupotea
mwelekeo tulioachiwa
na Mtume (s.a.w.) kama
alivyoamrishwa na
Allah (s.w.) atufikishie.
Na yeye amefufikishia.
Ni dhahiri
kwamba Waislamu
wameupoteza ule
Uislamu tuliofundishwa
na Mtume (s.a.w.) iwe
ni kwa kujua au kwa
kutokujua.
Waislamu hawana
umoja, wamejigawa
makundi kwa makundi
na kujengeana uadui wao
kwa wao, hali yakuwa
wameisahau kauli ya
Allah (s.w.):
Na shikamaneni
katika kamba ya Allah
(s.w.) wala msiachane.
(Qur. 3:103).
Kwa mtazamo wa
mafundosho ya Quran,
kujigawa makundi
hakutaiepuka adhabu
(kwa Allah (s.w.) kama
alivyosema Allah (s.w.).
"Tumeiteremsha
adhabu kwa wale
waliojigawa makundi".
(Qur. 15:90).
Hatudhani kuwa jamii
ya Waislamu hususan
viongozi wa taasisi na
mashirika mbalimbali ya
Waislamu hawajui aya
hazi na makusudio yake.
Lakini matokeo ya kibri,
jeuri, hasad na tamaa
zimewafikisha Waislamu
hapa walipo.
Tujiulize katika maisha
ya Mtume (s.a.w.)
yalikuwepo makundi
kama haya tuliyojiundia
sisi? Kama yalikuwepo,
juhudi gani zilifanyika
kuyamaliza na Waislamu
wakabaki kitu kimoja?
Tunaona katika
mazingira tuliyo nayo
sasa, ni dhahiri kwamba
tumepoteza mwelekeo
wa Uislamu na maadili
yake, sheria na Tawhiid,
na kukubali kuchezewa
kama mwanasesere
(toy) na makafiri kupitia
udhaifu huu.
Amewahi kusema
Mtume (s.a.w.),
"Atakayeishi muda mrefu
(Maswahaba) ataona
mambo mengi ya uzushi
na jiuepusheni nayo."
Kauli hii ya Mtume
(s.a.w.) imetimia maana

ANNUUR NEW.indd 4

umma wa Kiislamu
umetopea katika
uovu na uzushi kama
tunavyoshuhudia
Waislamu wakijigawa
katika makundi na
kujengeana uhasama na
kupoteza umoja wao wa
Kiislamu.
Huu si Uislamu
aliotuletea Allah (s.w.)
kupitia kwa Mjumbe
wake. Tunajiuliza, kwa
jinsi hali ilivyo hapa
nchini ni nani ataunusuru
Uislamu (dini hii ya
Mwenyezi Mungu) kama
inavyosema Quran, "Ni
nani atakayeinusuru dini
hii". (Qur. 61:14).
Wako wapi wanazuoni
wa Kiislamu, viongozi
wa Kiislamu, Masheikh,
Maulamaa, Maimam,
ambao kimsingi ndio
dira katika kusimamia
miongozo ya dini, ndio
wanaotegemewa kujenga
umoja wa jamii ya
Kiislamu nchini.
Tukumbuke kuwa
Uislamu ni dhamana
tuliyoyopewa na
Muumba na kuamuru
watu waishi katika
ustaarabu wake.
Ameeleza Mwenyezi
Mungu: "Tumekuridhieni
Uislamu kuwa dini
yenu." (Qur. 5:3).
Ni vipi tumeuacha
ustaarabu wa Uislamu
ambao Allah (s.w.)
ameturidhia, kiasi cha
kubaki katika Uislamu
wa vipande vipande hali
ya kuwa viongozi wapo?
Umoja katika Uislamu
hapa nchini umepigiwa
kelele sana. Zimeelezwa
athari walizopata
na wanazoendelea
kupata Waislamu kwa
kuwekwa kwao katika
mafungu mafungu, tena
yanayohasimiana.
Lakini pamoja na
kudhihiri athari na
kufahamika kiini cha
tatizo, bado hadi sasa
hakuna hatua zozote za
uhakika zilizochukuliwa
kunusuru hali.
Tunaona wakati
umefika wa hatua za
makusudi na za haraka
kuchukuliwa. BARAZA
KUU, BAKWATA,
MABARAZA ya
WANAZUONI na Taasisi
nyingine za Kiislamu
nchini, pamoja na tofauti
zao za kifalsafa. Kuna
haja ya kuketi na kuweka
mkakati wa pamoja wa

kutengeneza jamii moja


ya Waislamu nchini.
Tukiacha kibri na jeuri,
tamaa za maslahi binafsi,
chuki na husda, hili
litawezekana na utakuwa
mwanzo mzuri kuitimiza
aya ya Quran:
Na shikamaneni
katika kamba ya Allah
(s.w.) wala msiachane.
(Msifarikiane). (Qur.
3:103).
Kama ni tofauti zenu

AN-NUUR

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 6 - 12, 2016


za kifalsafa katika
taasisi zenu bakini
nazo, vumilianeni na
heshimianeni kwazo,
lakini hakuna haja ya
tofauti zenu hizo ziwe
sababu ya kuendelea
kuwagawa Waislamu.
Ikiwa mtabaini
mapema na kutahayari
na kuchukua hatua,
mtaunusuru Uislamu
kwa kuweka kipaumbele
cha umoja wao kwanza,

maslahi ya taasisi baadae.


Tunaamini ikikosekana
jamii ya Kiislamu
iliyojengwa katika
misingi madhubuti ya
umoja, hakuna taasisi
madhubuti ya Kiislamu
itakayoweza kufaulu
katika malengo yake
kama ilivyokusudiwa.
Kama taasisi zenu ni
kwa ajili ya Waislamu,
basi ni vyema mkajenga
udugu wao kwanza.

Ukandamizaji utavunja Muungano-Ally Saleh


Inatoka Uk. 3
Mazrui na wajumbe
wa Kampeni Mansour
Himid na Muhammed
Riamy, ambapo wapo
waliobambikiziwa kesi za
kuchoma moto nyumba,
na matukio ya ulipuaji
wa mabomu.
Kuhusu kero za
Muungano, Ally Saleh
alisema kuwa kero hizo
zimeendelea kuwepo
kwa sababu ya kukosa
dhamira ya kweli ya
kisiasa, na muundo
usiokidhi haja.
Kwa sababu hiyo,
Muungano umekuwa
na matatizo mengi na
mengine yakidumu kadri
ya umri wa Muungano
wenyewe.
Muungano huu
umekosa taratibu za
kikatiba na kisheria za
kutatua migongano,
mivutano au uchukuaji
wa madaraka (Usurp of
Power) unaofanywa na
Serikali ya Muungano
dhidi ya Zanzibar na
kadhalika Zanzibar
inapojitutumua kudai
haki na stahiki zake
katika Muungano
ambazo hazitimizwi,
alisema.
Akadai kuwa fursa
adhimu ya kutengeneza
mfumo mzuri wa
Muungano ilipatikana
kupitia Mapendekezo ya
Tume ya Warioba, lakini
CCM wakaipiga teke nia
hiyo kupitia Bunge la
Katiba na kuleta mambo
ambayo yataendeleza
kero kama zilivyokuwa
na kuzidi.
Mheshimiwa Spika,
Wengi tunaamini hizo
zinazoitwa KERO za
Muungano zinatumika
kama mtaji wa kisiasa
na kila zinapobakia au
kuzuka nyingine na
zisipatiwe suluhu, ndipo
mtaji huo unapokuwa
mkubwa zaidi. Mtaji huu
unatumika kuwazuga
watu, yaani Watanzania
kuwa kero ni sehemu
ya Muungano na kuwa
zote zimetatuliwa
isipokuwa chache tu,

yaani kuwaaminisha
Watanzania kuwa
Muungano ni wa usawa
na wa haki ilhali hakuna

nia kabisa ya kumaliza


kero za Muungano.
Alisema Waziri huyo
Kivuli.

Mheshimiwa Spika,
aliyekuwa Msemaji
Mkuu wa Kambi Rasmi
ya Upinzani Bungeni
katika Bunge la kumi,
Mheshimiwa Tundu
Lissu alizungumzia
kwa kina juu ya suala la
Mgawano wa Mapato ya
Muungano na jinsi Zanzibar
inavyopunjika na jinsi
mfumo huo ulivyogeuza
Zanzibar kuwa koloni. Hilo
ni katika suala la fedha
ambazo zinatokana na
wafadhili yaani mgao wa
asilimia 4.5.
Mheshimiwa Spika,
pamoja na takwimu
kuonyesha kuwa kiasi
fulani cha fedha hupelekwa
Zanzibar, lakini bado
kiwango hakijafikia asilimia
ambayo imekubalika na
pande hizo mbili ambapo
kiwango hicho hakijawahi
kuvuka asilimia 2.8. Tatizo
hili limekuwa la nenda rudi
miaka mingi bila suluhu ya
kweli na ya kudumu.
Mheshimiwa Spika,
Kwa mujibu wa hotuba
ya Mheshimiwa Lissu,
fedha hizo hujumuisha pia
makandokando mengine
kadhaa ila hutajwa na
kutiwa katika kapu
moja ambalo huonekana
limenona.
Alisema kwa mwaka
juzi Zanzibar iliyopaswa
kupokea shs billion
71.23 ilipewa asilimia
kumi tu ya fedha hizo.
Inasikitisha kwamba;
Ripoti ya Utekelezaji ya
Ofisi ya Makamu wa
Rais iliyopelekwa katika
Kamati ya Katiba na Sheria,
haikugusia chochote juu
ya eneo hili muhimu
la masuala ya fedha za
Muungano na mgawanyo
wake.
Mheshimiwa Spika, Kitu
kingine kinachohusu fedha
ambacho kwa kukosekana
nia ya kisiasa hakijapatiwa
ufumbuzi pamoja na
kuundwa kwa Tume ya
Pamoja ya Fedha ya Jamhuri
ya Muungano ya 1984 ni
suala la sehemu ya Zanzibar
katika mtaji uliounda Benki

Kuu ya Tanzania ikiwa ni


fedha za Zanzibar kutokana
na iliyokuwa Bodi ya Sarafu
ya Afrika Mashariki. Leo
miaka 50 tangu kuundwa
kwa Benki Kuu, hakuna
suluhu ya suala hilo.
Suala hilo maarufu kama
Hisa za Zanzibar, lilitolewa
agizo na Bunge kwa Serikali
kuleta Bungeni taarifa
yake, lakini limepuuzwa na
Zanzibar haijapata fedha
zake halali. Kisingizio ni
kutopata taarifa jambo
ambalo linatia khofu kuwa
taarifa hizo hazitapatikana
tena.
Mheshimiwa Spika,
kimsingi kuna utata
mkubwa juu ya mgawanyo
na matumizi ya fedha
za Muungano. Ripoti ya
Tume ya Pamoja ya Fedha
imesema wazi kuwa
kiasi kikubwa cha fedha
za Muungano hutumika
kwa mambo yasio ya
Muungano, lakini Serikali
ya Muungano imekuwa
ikikalia mapendekezo ya
kutenganisha matumizi ya
fedha za Muungano, ikijua
inaidhulumu Zanzibar.
Mheshimiwa Spika,
kero za Muungano
zinazidi kuongezeka
kutokana na uzembe
wa viongozi waliopewa
dhamana ya kuusimamia
muungano. Maamuzi
kuhusu masuala muhimu
ya muungano kama vile
ajira za Wazanzibari
katika Muungano au
ushirikiano wa Zanzibar
na taasisi za kimataifa, au
utozaji kodi mara mbili
kwa wafanyabiashara wa
Zanzibar yanachukua
muda mrefu mno kiasi cha
kuongeza kero juu ya zile
zilizokuwepo toka mwanzo.
Ndio maana, kutokana
na kero hizi zisizo na
utatuzi Wazanzibari,
katika maoni ya Tume ya
Warioba wakataka tuwe na
Serikali ya Mkataba jambo
ambalo liliungwa mkono
na Tume hiyo kwa kuja na
pendekezo la muundo wa
shirikisho katika Jamhuri ya
Tanzania.

Nukuu ya Ally Saleh juu ya Mgawo wa Mapato.

5/4/2016 3:26:51 PM

HABARI ZA KIMATAIFA

AN-NUUR

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 6 - 12, 2016

Saudia kufungua ubalozi Israel


Mahusiano ya siri yaimarika

SAUDI Arabia imesema


huenda ikafungua ubalozi
wake mjini Tel Aviv
Israel, iwapo utawala wa
Israel utakubali kusitisha
mgogoro katika eneo la
Mashariki ya Kati.
Jenerali Anwar Eshki,
kamanda mwandamizi wa
zamani wa jeshi la Al-Saud,
ameiambia televisheni ya
al-Jazeera ya Qatar kuwa,
iwapo Waziri Mkuu wa
Israel Benjamin Netanyahu,
atakubali mpango huo
wa kusitisha mgogoro na
kuwapa Wapalestina haki
zao zote, basi Saudi Arabia
itafungua ubalozi Tel Aviv.
Jenerali Eshki, ambaye
kwa sasa ni Mwenyekiti
wa Kituo cha Mafunzo ya
Kiistratejia na Sheria cha
Mashariki ya Kati kilichoko
Jeddah, ameongeza kuwa
utawala wa Al-Saud
hauna haja ya kushinikiza
kutengwa utawala wa
Israel katika eneo hili la
Mashariki ya Kati.
Itakumbukwa kuwa
mwaka 2002, Saudia
kwa mara ya kwanza
ilipendekeza kuwa
iwapo utawala wa Israel
utawaagiza walowezi wa
Kizayuni kuondoke katika
Ukingo wa Magharibi wa
Mto Jordan na Ukanda wa
Gaza, basi utazishawishi
nchi nyingine za Kiarabu
kuutambua utawala huo
dhalimu.
Hata hivyo kamanda
huyo wa zamani wa jeshi la
Al-Saud na ambaye aliwahi
kuwa mshauri wa Mwana
Mfalme wa Al-Saud na
aliyekuwa balozi wa Saudia
nchini Marekani, Bandar
Bin Sultan, alikwepa
kujibu swali alipotakiwa
kufafanua ni kwa nini
utawala wa Saudia
umetuma vikosi nchini
Yemen na umeshindwa
kutuma vikosi katika
Ukanda wa Gaza ili
kuwalinda Wapalestina.
Zaidi ya watu 8,280
wameuawa wakiwemo
watoto 2,236 tangu Saudia

ANNUUR NEW.indd 5

na washirika wake
waanzishe mashambulizi
ya anga dhidi ya Yemen
Machi mwaka jana, kwa
lengo la kumrejesha
madarakani Rais wa nchi
hiyo aliyekimbia Abd
Rabbu Mansur Hadi.
Wakati kukiwa na
wasiwasi kuhusu ukaribu
wa Saudia na Israel, kuna
taarifa kwamba utawala
haramu wa Israel unatoa
mafunzo ya kijeshi kwa
askari wa Saudi Arabia
katika mpango wa siri wa
uhusiano wa tawala hizo
mbili.
Naibu Katibu Mkuu
wa Hizbullah ya Lebanon
Sheikh Naim Qassem,
amefichua kuwa maafisa
wa Saudi wanapata
mafunzo kufuatia uhusiano
wa siri wa Israel na Saudia,
ambao sasa umeimarika
na kuwa ushirikiano wa
kijeshi.
Imeelezwa kuwa Israel
imeamua kuwapa mafunzo
askari wa Saudia baada
ya utawala wa Saudia
kushinikiza Jumuiya
ya Nchi za Kiarabu na
Barazala la Ushirikiano
la Ghuba ya Uajemi
kuitangaza harakati ya
Hizbullah kuwa kundi la
kigaidi.
Wakati ushirika huo
ukionekana kuimarika kwa
sasa, kwa miaka mingi
Saudia imejizuia kutoa
mafunzo na misaada yake
kwa wanaharakati wa
kupigania ukombozi wa
Palestina.
Siku ya Jumapili, gazeti la
Kizayuni la Jerusalem Post
liliripoti kuwa, si tu kuwa
Israel haijatengwa bali pia
sasa imeingizwa katika
duara la Saudi Arabia.
Sehemu ya mpango huo
ni Israel kufungua ofisi ya
kidiplomasia Abu Dhabi na
kuimarisha maingiliano na
nchi za Ghuba ya Uajemi."
Kwa mujibu wa tovuti
ya Bloomberg, mikutano
kadhaa ya siri imekuwa
ikifanyika kati ya maafisa

WAZIRI Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu (kushoto) na Mfalme


Salman wa Saudi Arabia.

wa Saudia na Israel.
Imeelezwa kuwa pande
hizo mbili zimekutana
mara tano katika kipindi
cha miezi 17 mwaka 20141015, ambapo maafisa hao
wa Saudia na wa utawala
wa Israel walikutana kwa
nyakati tofauti nchini India,
Italia na Jamhuri ya Czech.
Aidha mapema mwezi
Juni mwaka jana, maafisa
mashuhuri wa zamani wa

Saudia na Israel walikutana


katika taasisi ya Council
on Foreign Relations huko
Washington. Kikao hicho
kilihudhuriwa na Anwar
Majed Eshki, mshauri
wa zamani wa serikali ya
Saudia, na Dore Gold balozi
wa zamani wa Israel aliye
karibu na Waziri Mkuu
wa Utawala wa Kizayuni
Benjamin Netanyahu.

Ujerumani waandamana
kupinga wapinga adhana
Chama cha siasa nchini
Ujerumani kinachopinga
Uislamu nchini Ujerumani,
wiki hii kimepata upinzani
mkubwa kutoka kwa
mamia ya waandamanaji
wanaopinga sera za chuki za
chama hicho.
Polisi nchini Ujerumani
wamewazuia mamia ya
waandamanaji wanaopinga
chama cha mrengo wa kulia
cha AFD, chenye sera za
kupiga vita Uislamu.
Polisi wametumia maji
wa kuwasha kuwatawanya
waandamanaji waliobeba
mabango na kuchoma
moto matairi katika eneo la
kuingilia kwenye mkutano
wa chama hicho, ili kuwazuia
wanachamana wake.
Hali hiyo ililazimu maafisa
zaidi ya 1000 kutumwa katika
eneo la mkutano katika mji
wa Stuttgart kutoa ulinzi.
AFD kinatarajiwa kuzindua

KIONGOZI wa AFD-FraukePetry.
upya kampeni zake na
kutangaza wazi kuwa
kinapinga dini ya Kiislamu.
Chama hicho kimekuwa
kikipiga marufuku mwito wa
Waislamu katika swala yaani
adhana, vazi la burga, uwepo
wa minara ya Misikiti.irib.

5/4/2016 3:26:52 PM

Makala

AN-NUUR

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 6 - 12, 2016

Tusikubali kutekwa na starehe za dunia


Starehe kamili ipo akhera

Na Shaban Rajab

STAREHE inapozidi akili


ya mwanadamu, basi hata
lile linalodhuru hulifumbia
macho au hulifunika
pazia ili lisimshughulishe
au kumrudisha nyuma
au kuzuwia azma yake.
Starehe pia ina kawaida ya
kumsahaulisha mwanadamu
kutenda yaliyo ya heri na
ya msingi kwa maisha yake
na kwa kukosa ya hofu
Mwenyezi Mungu pia.
Starehe ikikolea, humfanya
mwanadamu kuishi kwa
kujipangia atakavyo kama
vile hakuna anayedhibiti
maisha na uhai wake. Ile
hali ya mtu kustarehe hadi
kukinai, akalala na akaamka
salama, humpa kibri na jeuri
na kujihakikishia salama ya
kuiona kesho na kesho kutwa
na kujiamini kuwa uhai
utaendelea kuwepo maisha
ya starehe yataendela kama
kawaida.
Katika hali ya kawaida,
starehe humfumba macho
mwanadamu hata pale
umri wake utakapopea,
humfanya asigundue udhaifu
wa kizee hata pale maungo
yatakapokataa kunyambuka
vyema na nywele kubadilika
rangi na uzee kuingia.
Mara nyingi starehe
hunogeshwa zaidi na hulka
za kivivu na kupenda urahisi.
Inapokolea humfanya mtu
asahau anakotoka, aliko
na anakoelekea na zaidi
anasahau aliyemneemesha
pia. Na hata kama
ameruzukiwa, ni vigumu
kwake kukumbuka kuwa
wako wenye kudhikishwa,
ambao ujira wao ni sehemu
ya ruzuku yake.
Mara nyingi starehe
ikimkolea mtu, Ibilisi
anakuwa ndiye rafiki wa
karibu kwake. Wakati
mwingine humfanya mtu
akajitafsiria mambo kinyume,
ili kukidhi matamanio yake.
Kawaida hujenga mazoea.
Starehe ukiizoea, hujenga
pumbazo kifikra na hali hii
humfanya mtu kuchagua
kile tu anachoona kitakidhi
matamanio yake.
Hata Firauni katika utawala
wake wa kiovu kule Misri,
aliponzwa na kibri, jeuri na

ANNUUR NEW.indd 6

starehe kiasi kwamba hakuwa


tayari kuona kuna mtawala
zaidi yake yeye. Alilewa
starehe za madaraka, alipata
utii wa shuruti, kila alichotaka
alipatiwa, akalemaa kiasi
cha kumfanyia kibri hata
Mwenyezi Mungu Muumba
na yeye akajiita mungu.
Alilewa starehe na kulemaa,
lakini Anayemiliki uhai wa
viumbe alimtafuna mithili
ya gogo linalomungunywa
na mchwa ndani kwa
ndani hata linapotanabahi,
mambo yalishaharibika.
Alimeangamia.
Tufahamu kwamba
kustarehe si dhambi wala
kosa. Lakini starehe sharti
ziwe za halali, kwa wakati
na kwa kiasi. Tatizo ni
pale zinapozidi na kukosa
mipaka kiasi cha kufanya
maasi. Tatizo ni pale starehe
inapogeuzwa kuwa ndio
mfumo wa maisha kiasi cha
mtu kuhadaika kwazo na
kuwa pumbao na kuadhiri
mfumo sahihi wa maisha
aliouridhia Mwenyezi
Mungu.
Wale ambao wamehadaika
na kutopea katika starehe, ni
vyema kurudi katika misingi
ya maisha kwa kuzoea maisha
ya uwastani na ya kiasi huku
wakiwa na hakika kwamba,
Mwenyezi Mungu ndiye
mkadiriaji wa kila jambo.
Ifahamike kwamba maisha
ya hapa duniani ni mchezo
wa muda tu na pumbao.
Kuonyeshana ufahari kwa
lengo la kupata sifa na kutaka
kuheshimiwa, kushindana
kukithiri katika mali na
watoto ni kama mfano wa
mvua inayowafurahisha
wakulima kwa mimea yao,
kisha inasita. Furaha ya
mkulima wakati wa kunyesha
mvua ni kustawi mimea yake.
Lakini hugeuka kilio pale
mvua ikatikapo na mimea
(mazao) kuwa na rangi ya
njano, kisha inajisokota na
hatimaye hukauka.
Vile vile kwa kuendekeza
starehe kupitiliza katika
kipindi kifupi cha uhai,
kunawafanya watu kusahau
kuwa akhera (kuna)
adhabu kali. Ni vyema
wale waliozoea starehe na
kuonyesha fahari wakatia
yakini akilini kwamba, kila

jambo linatendeka kwa kiasi


na lina wakati wake, nafasi
yake na malipo yake.
Ni vyema wale
walioathiriwa na mazoea
haya wakajitambua mapema
na kubadilika kwani
anayetubu na kubadilika
kwa dhati, Mola huleta radhi
zake. Maisha ya dunia si
chochote isipokuwa ni sterehe
danganyifu.
Kujamiinana (katika
mahusiano ya ndoa halali)
ni aina pia ya starehe. Nje
ya ndoa ni starehe ya kiovu.
Ulevi pia ni starehe ovu,
maonyesho ya urembo,
kamari, night clubs nk.
Michezo ni mazoezi na aina
ya starehe kwa watu wengine.
Kulala kunaweza kuwa aina
ya starehe kwa baadhi ya
watu, japo kila mtu ni lazima
alale. Maana ya starehe ni
kitu au jambo ambalo mtu
kwa hiari yake hupenda
kulifanya, ili kuiburudisha na
kuiridhisha nafsi yake.
Namna ya kuiridhisha nafsi
kunatofutiana baina ya mtu
na mtu na hapo ndipo kila
mtu anapokuwa na starehe
yake. Hata hivyo kupenda
wanawake, watoto na mali
si vibaya na wala Mwenyezi
Mungu hajaharamisha.
Tahadhari ni mapenzi
hayo yasije kuwa sababu
ya kukufuru, kuendekeza
laghawi na israaf nk.
Starehe mara nyingi huenda
sambamba na matamanio.
Matamanio ni hisia za kupata
vile unavyovipendelea na
kuhisi raha (kustarehe)

unapovipata. Hulka ya
mwenye kutamani mara
nyingi hatosheki. Akipata
mia anatamani kupata na
mia nyingine. Kadhalika
aliyetopea kwa starehe
hakinahi. Akistarehe leo na
kesho atataka aendelee na
starehe nyingine.
Binadamu anaweza kuwa
na raha kama atabarikiwa
kuwa na vitu vinavyoonekana
kuwa ni vya msingi hapa
duniani kama afya, mali, mke,
watoto, hadhi (heshima).
Lakini raha hii kwa binadamu
ni kwa wakati au kipindi
fulani tu, si kwa muda
wote. Hali hii inajitokeza
kwasababu ni vigumu
binadamu kufurahi muda
wote wa maisha yake, kwa
kuwa hana pa kuziweka
hisia za matatizo ya kidunia
kama vile hofu na wasiwasi
na hali ya kutotosheka au
kuridhika, matatizo ya uzao,
ya nyumbani nk.
Kwa maana hiyo, raha
kamili katika maisha ya
binadamu hapa duniani
kamwe haiwezi kupatikana.
Labda katika maisha mengine
baada ya yale ya dunia. Raha
au starehe wanazoweza
kuambulia wanadamu katika
maisha ya duniani ni raha
kwa wakati fulani tu.
Mwenyezi Mungu
tunakuomba uilinde jamii
yetu na starehe potofu,
ijaalie kufuata njia ya haki na
kuionyesha popote ilipo batil
ili waikimbie na uiwezeshe
kuifuata haki ilipo ili
utunusuru (Amiin).

5/4/2016 3:26:52 PM

Hoja ya Visram

AN-NUUR

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 6 - 12, 2016

Obama aungama makosa aliyofanya nchini Libya

Na Nizar Visram
RAIS wa Marekani Barack
Obama amekiri kwa mara
ya kwanza kwamba serikali
yake ilishindwa katika
uvamizi wa Libya mwaka
2011. Amesema hilo huenda
ndilo kosa kubwa zaidi
alilolitenda wakati wa utawala
wake. Bw Obama amesema
Marekani haikua na mpango
mahususi wa jinsi Libya
itakavyotawaliwa baada ya
kuuliwa kwa mtawala wake
Kanali Muammar Gaddafi
tarehe 20 Oktoba 2011.
Obama alisema haya katika
mahojiano ya hivi majuzi na
runinga nchini Marekani.
Matokeo yake ni kuwa Libya
imetumbukia katika dimbwi
la matatizo baada ya nchi hiyo
kusambaratika.
Mwanzoni NATO walidai
kuwa lengo lao lilikuwa ni
kuwalinda raia wa Libya ili
wasishambuliwe na majeshi ya
Gaddafi. Lakini baada ya muda
wakaamua wampindue Gaddafi
na kuikabidhi nchi kwa waasi.
Siku za nyuma Obama amewahi
kuwalaumu wenzake wa NATO.
Amesema waziri mkuu wa
Uingereza, Bw David Cameron
hakufanya matayarisho ya
kutosha walipoanza uvamizi wa
Libya. Pia Obama alimlaumu
rais wa wakati huo wa Ufaransa,
Bw Nicolas Sarkozy.
Matokeo ya makosa yote
haya ni kuwa Libya ambayo ni
nchi iliyo na utajiri mkubwa
wa mafuta, sasa imemeguka
vipande vinavyotawaliwa na
makundi ya waasi waliopewa
silaha, mafunzo na fedha
na NATO. Baada ya majeshi
ya NATO na waasi kumuua
Gaddafi na kupindua serikali
yake, waasi wakaanza
kugombania ngawira. Kila
kikundi chenye silaha kikadai
maeneo yake na ndipo
wakaanza kushambuliana na
kuwashambulia raia.
Wakati wa mauaji ya Gaddafi
benki kuu ya Libya ilikuwa
na akiba ya dola bilioni 85.
Waasi wakaanza kupora
hazina hii ya wananchi na
ndipo vita vipya vikaanza

ANNUUR NEW.indd 7

huku NATO wakishangilia.


Kikundi kilichojiita Dola ya
Uislamu (ISIS) kikawazidi
nguvu wengine. Dola bilioni
1.1 za walipa kodi wa Marekani
zikatumika. kuisambaratisha
Libya na kusababisha kukua
kwa ISIS siyo tu Libya bali katika
bara la Afrika na kwengineko.
Kikundi cha mujahidina
kilichosaidiwa na NATO
ndio baadae wakaja kumuua
Balozi Christopher Stevens wa
Marekani na wasaidizi wake
watatu mjini Benghazi tarehe 11
Septemba 2012. Marekani ikabidi
wafunge ubalozi wake huko
Tripoli na kuikimbia Libya.
Kosa walilofanya Marekani
huko Libya walifanya pia
Afghanistan na Iraq. Ukiachia
raia wa nchi hizo waliouawa
na nchi kusambaratishwa,
Marekani nayo ikapoteza askari
wake 7,000 na wengine wengi
kujeruhiwa vibaya. Wakati
Obama anajutia alichokifanya
huko Libya, anayofanya huko
Syria ni baya zaidi. Katika nchi
hiyo, licha ya maelfu ya raia
waliouawa, milioni 12 hawana
mahali pa kuishi na milioni nne
wameikimbia nchi yao, wengi
wao wakielekea Ulaya ambako
wanapigwa mabomu na polisi.
Mwaka jana tu wamekufa raia
1,500
Shirika la ujasusi la Marekani
(CIA) linasema nchini Libya
wameibuka mujahidina wapatao
6,000 wa kikundi cha ISIS.
Wanasema nchini Syria wako
kati ya 20,000 na 30,000 ingawa
wengine wanakisia ni 50,000
ukichanganya na walioko Iraq.
Wote hawa wanaeneza harakati
zao hadi Ulaya ambako wana
mawakala wao. Si ajabu kuwa
washambuliaji wa mjini Paris na
Brussels walipata mafunzo yao
huko Syria. Huu ndio uongozi
wa kina Bush, Blair, Obama na
Cameron.
Wakati Obama anazungumzia
makosa yaliyofanyika, Bi
Hillary Clinton anaonekana
akichukua msimamo tofauti.
Yeye wakati anagombea urais
nchini Marekani amekuwa
akisifu utumiaji wa majeshi
huko Libya na kusema Marekani
imetumia vilivyo nguvu zake za
kijeshi.
Mwaka 2011 Bi Clinton
alikuwa waziri wa mambo ya nje
wa Obama. Wakati huo baada
ya Gaddafi kuuliwa kikatili na
waasi wakisaidiwa na majeshi
ya NATO, Clinton alionekana
katika TV akisherehekea na
kufurahia mauaji hayo. Bi Hilary
Clinton ndiye aliyemshauri
Obama kuidhibiti anga ya Libya
ili Gaddafy asiweze kusafirisha
askari wake au kuwashambulia
waasi. Matokeo yake waasi
waliweza kujiimarisha kwa
kupokea misaada ya silaha na

mafunzo.
Kwa mujibu wa gazeti la
The Washington Post Clinton
alishauriwa na wanasheria wa
wizara yake kuwa kuivamia
Libya ni uhalifu wa sheria ya
kimataifa. Makamo wa rais
Bw Joe Biden na mshauri wa
Obama wa mambo ya usalama
wa taifa, Bw Tom Donilon nao
walipinga mpango wa kuivamia
Libya. Clinton alipuuza ushauri
wao na akafaulu kumfanya
Obama atoe misaada ya kijeshi
na kifedha kwa waasi. Mabilioni
ya dola yaliyokamatwa kutoka
akaunti za serikali ya Gaddafi
yalikabidhiwa kwa waasi.
Katika mkutano nchini
Uturuki, Clinton pia
alizishawishi serikali 30 za Ulaya
na Uarabuni kuwasaidia waasi.
Mara nyingi vyombo vya
propaganda vya magharibi
vimekuwa vikitulisha uwongo
kuwa uvamizi wa Marekani
na NATO katika nchi kama
Iraq, Libya na Syria ni kwa
madhumuni ya kuondoa
udikteta na kuleta demokrasia.
Ukweli ni kuwa mashambulizi
haya ni matokeo ya mikakati
iliyopangwa kwa muda mrefu
ili kutimiza lengo lao la kisiasa
na kiuchumi. Ushahidi mmoja
ulitolewa na Jenerali Wesley
Clark wa Marekani, aliyeongoza
majeshi ya NATO akiwa
kamanda mkuu wakati wa
uvamizi wa Yugoslavia mnamo
1999. Yeye alitamka kuwa
Marekani siku zote ilikuwa na
mpango wa kuzivamia nchi saba
katika muda wa miaka mitano.
Nchi zenyewe alizozitaja ni Iraq,
Syria, Lebanon, Libya, Somalia,
Sudan na mwishowe Iran.
Mwaka 2004 Jenerali (mstaafu)
Clark alijaribu kugombea urais
wa Marekani kwa niaba ya
chama cha Democratic lakini
hakuteuliwa na chama hicho
Mnamo 2007 mtangazaji
Amy Goodman wa runinga ya
Democracy Now alimuuliza
Clark kuhusu mkakati huu.
Clark akasema alipokuwa jeshini
alitembelea makao makuu
ya wizara ya majeshi jijini
Washington na huko akauona
waraka wa siri ulioelezea
mkakati huo. Jenerali Clark
alisema ni jambo la kawaida kwa
marais wa Marekani kuanza
kugundua makosa yao baada
ya kuachia madaraka. Kwa
mfano rais George W Bush
katika kitabu chake cha 2010
anazungumzia uvamizi wa
Iraq akisema alifanya makosa.
Halafu naye rais Clinton mnamo
2008 alisema alifanya makosa
makubwa wakati wa mauaji ya
halaiki nchini Rwanda mnamo
1994.
Kuhusu uvamizi wa Iraq hata
waziri mkuu wa Uingereza,
Bw Blair aliomba radhi kwa

kutoandaa mipango baada ya


kumuondoa Saddam Hussein.
Obama anaungama makosa yake
ya Libya lakini kosa lake kubwa
(tena kosa la jinai) ni kuungana
na rais Sarkozy wa Ufaransa
na waziri mkuu Cameron wa
Uingereza katika kuivamia Libya
kinyume cha sheria ya kimataifa
na kinyume cha azimio la baraza
la usalama la Umoja wa Mataifa.
Uvamizi wa Iraq wa mwaka
2003 umepelekea raia milioni
moja kupoteza maisha yao.
Kabla ya hapo vikwazo vya
NATO vilipelekea raia milioni
moja wa Iraq kufa. Ndio maana
kuna shinikizo kuwa kina Bush
(mkubwa na mdogo) na Tony
Blair wa Uingereza wafikishwe
mahakama ya kimataifa. Na
kuhusu Libya kinachofichwa ni
kuwa sababu halisi ya kumuua
Gaddafi siyo udikteta, bali
ni kwa sababu yeye alikuwa
anaanzisha mawasiliano ya
satelaiti kwa Afrika nzima ili
tuache kutegemea makampuni
ya magharibi. Halafu pia kwa
sababu ya kosa la kuuza mafuta
yake kwa China pamoja na
kukataa kuruhusu vituo vya
kijeshi vya Marekani nchini
mwake.
Gaddafi pia alikuwa
akianzisha benki kwa bara zima
la Afrika ili tuache kutegemea
wafadhili wa magharibi.
Yote haya yaliwakwanza
sana watawala wa NATO.
Baada ya Marekani na NATO
kuisambaratisha Libya, sasa
wanakabidhi kazi ya kuikarabati
nchiyo kwa Rais Mstaafu Jakaya
Kikwete, akiwa mwakilishi
maalum wa Umoja wa Afrika
(AU).
Wakati NATO walipoivamia
Libya ni AU ndiyo iliyopaza
sauti yake ikipinga. Ilikuwa
tayari kuingilia kati na
kuzungumza na Gaddafi ili
yamalizwe bila ya vita. Ujumbe
ulitumwa hadi Libya ukaonana
na Gaddafi. NATO waliipuuza
AU. Leo wanaifadhili AU
eti waikarabati nchi hiyo
waliyoibomoa.
Tusidanganyike na radhi
wanazoomba. Hatua za kisheria
lazima zichukuliwe kama
zinavyochukuliwa dhidi ya
watawala wa Kiafrika. Swali
ni je, nani wa kumfunga paka
kengele? Tungeanza na kukataa
hivi vilemba vya ukoka vya
kupewa usuluhishi wa Libya.
Ukweli wa mambo ni kuwa
waliolikoroga, ndio wanaoweza
kulimaliza maana ndio hao
hao wanaoendelea kununua
mafuta kutoka kwa makundi
yanayouwana halikadhalika
kuwapa silaha. Ufupi wa
maneno, ni vijana wao. Na ndio
hao hao wanaowatumia huko
Syria.
(0713-562181
nizar1941@gmail.com)

5/4/2016 3:26:54 PM

8
NILIPATWA na ugumu kweli
kuamini kuwa Yesu hakufa
msalabani
Hayo yalikuwa ni maneno
ya Balqis Chepkwony (awali
akiitwa Caroline Chelangat
Chepkwony) baada ya kusoma
kitabu cha Mhadhiri maarufu wa
Kiislamu wa Afrika Kusini na
mzaliwa wa Pakistan, marehemu
Ahmed Deedat, kiitwacho
Crucifixion or Cruci-fiction (Ni
kweli Yesu kasulubiwa au ni
ubunifu tu!)
Caroline Chelangat
Chepkwony, alikuwa
mwanafunzi mwenye juhudi
sana na siku zote alikuwa
akishika nafasi ya juu katika
maisha yake ya masomo ya shule
ya msingi. Baba yake alitaka awe
daktari wa binadamu, lakini
Mzungu mmoja rafiki wa baba
yake alishauri Caroline awe
mtakwimu bima (Actuary) na
wakafuata ushauri ule.
Kama ilivyo kawaida katika
mataifa mengi ya Kiafrika, ni
wanafunzi wafanyao vizuri
zaidi tu kitaifa, ndio wanaoweza
kupata nafasi katika shule
chache za serikali. Nchini
Kenya Caroline Chelangat,
alikuwa mmoja wa wanafunzi
walioteuliwa kuendelea na
elimu ya sekondari katika
shule ya serikali. Alichagua
katika shule ya sekondari ya
Alliance (Alliance Girls High
School), shule inayotambulika
kwa kutoa elimu nzuri na
kufaulisha watoto sana, sifa zake
zikitawala katika vyombo vya
habari vya redio, televisheni
na magazeti kinapofika kipindi
cha kutangazwa matokeo.
Wanafunzi wa hapo wakipenda
kuiita shule yao bush
(kichaka) na wanafunzi wakiitwa
busherians (wanakichaka). Jina
hilo lisilo rasmi limetokana na
msitu mkubwa uliozunguka
shule hiyo. Shule hiyo mara
kwa mara imekuwa ikifanya
vyema katika mitihani ya taifa
kidato cha nne, ikiwa ni kawaida
kuingia kumi bora katika shule
za Kenya.
Baada ya kufanya vizuri
katika mitihani hiyo ya elimu ya
sekondari, alifaulu kwa kupata
wastani wa alama A katika wa
masomo yote Alipata daraja
la juu la (A) katika masomo
ya sayansi ya Hesabu, Fizikia,
Kemia, Komyuta na Jiografia.
Moja kwa moja Caroline
alinyakuliwa na Chuo Kikuu cha
Nairobi (UoN), Chuo kikubwa
zaidi nchini Kenya, ambacho
kilimchukua kwa kitivo cha
somo la Hesabu, akisomea
Utakwimu Bima (Actuarial
Science).
Wakati huo kilikuwa ni Chuo
Kikuu hicho cha Nairobi pekee
nchini Kenya kilichokuwa
kinatoa shahada ya Utakwimu
Bima. Mwaka huo 2002, Chuo
cha Nairobi kilikuwa kikichukua
wanafunzi 16 tu, Kenya nzima
waliochaguliwa na serikali na

ANNUUR NEW.indd 8

Makala

AN-NUUR

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 6 - 12, 2016

Zana za mapigano zamuokoa


Balqis Chelangat Chepkwony
Kufufuka au kurudishiwa fahamu?
Ipi ilikuwa miujiza ya Nabii Yona?
Suluhisho thabiti la ubishani wa Utatu

Balqis Chepkwony (awali akiitwa Caroline Chelangat Chepkwony)


Chelangat alikuwa mmoja wa
waliostahili.
Akiwa mwaka wa pili wa
masomo, Caroline alikutana
na Salim, mwanafunzi katika
hicho aliyekuwa akichukua
masomo yake katika Kitivo
cha Sanaa (Faculty of Arts).
Moja ya vipaumbele vya Salim
katika maongezi ilikuwa
ni mazungumzo ya dini.
Alimchokoza Chelangat
kuhusu imani yake ya dini.
Salim alimuomba Chelangat
afanye ufatiliaji mzuri kuhusu
dini na yeye akamsikiliza.
Bila kupoteza muda, Salim
alimkabidhi Chelangat
baadhi ya vitabu na makala
yanayoongelea linganishi ya dini
mbalimbali na kumtajia orodha
ya tovuti ambazo zinachambua
masuala ya dini vyema, tena
kwa kutumia akili ya kawaida.
Baadhi ya vitabu ambavyo
Caroline alivisoma ni pamoja na
vya Marhuum Sheikh Ahmed
Deedat kuanzia kile cha Is the
Bible Word of God? (Je, Biblia ni
Neno la Mungu?). Crucifixion or

Cruci-fiction! (Kusulubiwa kweli


au kusulubiwa kwa kubuniwa?),
Resurrection or Resuscitation?,
(Kufufuka au kurudishiwa
fahamu?)
Vingine ni What Was the Sign
of Jonah? (Ipi ilikuwa muujiza
wa Yunus?), Who Moved
the Stone? (Nani aliyesogeza
jiwe?), Quran Miracle of
Miracles (Quran ni muujiza wa
miujiza), What the Bible Says
About Muhammad (pbuh)?
(Biblia inasema nini kuhusu
Muhammad?) Christ in Islam
(Kristo ndani ya Uislamu) na
Combat Kit (Zana za mapigano).
Vitabu vyingine alivyosoma
kabla ya kusilimu ni pamoja
na kile cha Let the Bible Speak
(Wacha Biblia izungumze) cha
Abdul Rahman Dimishkiah,
Oneness of God: The Ultimate
Solution to the Trinitarian
Controversy (Umoja wa Mungu:
Suluhisho thabiti la ubishani wa
utatu) cha Marmarinta Umar
P. Mababaya na Pillars of Faith
(Nguzo za Imani) cha Jaafar
Shaikh Idris.

Vitabu hivyo na venginevyo


vya Ahmed Deedat, vilivunja
kabisa imani ya Kikristo ya
Caroline na hatimaye akabakiwa
na moja tu la kufanya: kuamua
kuingia katika Uislamu. Hivyo
ilipotimu tarehe 14 Aprili 2005,
akiwa na umri wa miaka 22
ndipo Caroline alipoamua rasmi
kuwa Muislamu na kuliacha
jinale la Kikristo na kuchukua
la Kiislamu, akibakisha majina
yake ya Kikalenjin (Kalenjin
ni moja ya kabila za Kenya).
Sasa amekuwa akiitwa Balqis
Chelangat Chepkwony.
Kabla ya kusilimu, akili yake
ilijaa mawazo mgando na hasi
kuhusu Uislamu na Waislamu.
Nilikuwa nikiwachukulia
Waislamu kama watu wa ajabu
na waliopotea kweli, kwani
walikuwa wakimuamini Mtume
ambaye amekufa. Alisema.
Baada ya kusilimu, Balqis
aliweza kuangalia kwa
wasaa video za Ahmed
Deedat, akifanya midahalo na
wanatheolojia mashuhuri wa
Kikristo. Ilimchukua mwezi
mmoja na nusu tu kuhifadhi
Juzuu Amma, Juzuu ya mwisho
katika Quran iliyo kwa lugha
ya Kiarabu (Quran ina juzuu
30, Juzuu moja ikiwa na kurasa
20 na Quran nzima ina kurasa
604). Japo alibanwa sana na
ratiba za masomo shuleni na
projects (miradi ya majaribio),
bado alithubutu kuhifadhi Juzuu
nzima ya mwisho ya Quran. Hii
inaweza kuwa sawa na kuiweka
kichwani injili ya Mathayo, neno
kwa neno!
Jamia Mosque, Msikiti
mkubwa zaidi nchini Kenya
uliopo jijini Nairobi, una
kitengo maalumu kwa ajili ya
wanaosilimu, mahususi kwa
ajili ya kuandaa madarasa ya
kuwasaidia walioingia katika
Uislamu ili kuijua dini yao. Naye
Balqis baada tu ya kusilimu,
aliweza kufika hapo, alisoma na
kuhitimu masomo hapo katika
Taasisi hiyo ya Jamia.
Balqis alifatilia masomo ya
Kiislamu kwa dhati, akiendana
na aya, Kishike kitabu [yaani
dini] kwa nguvu! [Q 19:12].
Baada ya kupata shahada
yake ya kwanza kutoka Chuo
Kikuu cha Nairobi mwaka
2006, na kama ilivyo ada kwa
mhitimu yeyote, Balqis naye
aliingia katika michakato ya
kutafuta kazi. Familia na rafiki
zake walimsaidia pia katika
hilo. Mzazi wake wa kiume,
ambaye alikuwa ni mhasibu
mkuu (Chief Accountant) wa
Chuo Kikuu cha Moi (Moi
University), bila shaka alikuwa
anajuana na wafanyabiashara
wengi au makampuni mengi.
Hii ingetosha kumpatia kazi
nzuri yenye hadhi Balqis.
Tena kwa shahada aliyokuwa
nayo, alikuwa na asilimia 100
ya kuchukuliwa na mabenki
Inaendelea Uk. 15

5/4/2016 3:26:54 PM

Makala/Tangazo

AN-NUUR

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 6 - 12, 2016

Tabia njema sababu ya kudumisha mapenzi kwa Waislamu

Na Shekih Mohamed Al-amir


Osman.

KWA hakika jamii yeyote


miongoni mwa wanajamii
katika wanadamu, hawezi
kuishi peke yake kwa furaha
bila ya kuungana na mtu
mwingine kwa tabia nzuri.
Tabia nzuri ni dalili
kutoka katika Qurani na
Hadithi alizotuteremshia
Allah (sw) juu ya umuhimu

ANNUUR NEW.indd 9

wa tabia nzuri, kwani ndizo


zinazohakikisha maisha
bora hapa duniani na kesho
akhera. - Hii ni moja ya amri
za Mwenyezi Mungu.
Amesema Allah (sw)
Samehe na amrisha mema
wapuuzeni wajinga) (199 AlAaraf).
Kumtii Mtume (S.A.W)
toka kwa Abii Dhari (R.A)
amesema, amesema Mtume
(S.A.W), Muogopeni
Mwenyezi Mungu popote
mlipo na fanya jema haraka
pale utapofanya baya kwani
jema hufuta baya, ishi na
watu kwa tabia nzuri.
Ameipokea Tirmithi.
Pia ni sababu ya kupata
mapenzi ya Mwenyezi
Mungu mtukufu. Amesema
Mwenyezi Mungu Mtukufu,
Na fanyeni mema
kwani Mwenyezi Mungu
anawapenda wafanyao

mema (195 Al-Bakarat).


Na amesema Mwenyezi
Mungu, Allah anawapenda
wafanyao uadilifu, usawa
(42 Al-Maidah). Na toka
kwa Usama Bin Shariki
(R.A) amesema, Tulikua
tumekaa mbele ya Mtume
(S.A.W) tukiwa tumetulia
kama vichwani mwetu
wametua ndege, hakuna hata
mmoja anayezungumza kati
yetu, mara wakataka watu
kujua, wakasema ni mja
gani wa Mwenyezi Mungu
anayependeza sana kwa
Mwenyezi Mungu? Akasema
ni Yule mwenye tabia nzuri
zaidi. Ameipokea AlHakim na Twabaraa.
Sababu ya mapenzi ya
Mtume (S.A.W) toka kwa
Jabiri bin Abdillahi (R.A),
amesema Mtume (S.A.W),
Kwa hakika inayempenda
sana mimi na atakayekuwa

karibu sana na mimi siku ya


kiama ni yule mwenye tabia
nzuri. Ameipokea Imam
Tirmidhi.
Na tabia nzuri huongeza
uzito katika mizani. Toka kwa
Abii Dardai, toka kwa Mtume
(S.A.W) amesema, Hakuna
kitu chochote kilicho kizito
zaidi katika mizani kuliko
tabia nzuri. Ameitoa Abuu
Daudi.
Toka kwa Abii Hurairata
(R.A) amesema aliulizwa
Mtume (S.A.W) juu ya mambo
mengi yanayowaingiza watu
wengi peponi? Akasema
Ni kumuogopa Mwenyezi
Mungu na tabia nzuri.
Hivyo Muislamu anatakiwa
kuishi kwa tabia nzuri kwa
watu ili apate maisha bora
hapa duniani hadi huko
akhera.
Email : eg_islamic_
center39@yahoo.com

5/4/2016 3:26:59 PM

10

MAKALA
Na Omar Msangi

HIVI majuzi Rais Barack


Obama amemteua Marine
Corps Lt. Gen. Thomas David
"Tom" Waldhauser kuwa
kamanda mpya wa Kamandi
ya Kijeshi ya Marekani katika
Afrika-U.S. Africa Command
(Africom). Waldhauser
akithibitishwa na Bunge la
Congress, atachukua nafasi
ya Army Gen. David M.
Rodriguez. Kamanda wa
kwanza alikuwa Generali
William E. "Kip" Ward (20072011) akifuatiwa na Genrali
Carter F. Ham (2011-2013.)
Kwa Wamarekani, kupitia
Congress, pengine taarifa
muhimu kwao, itakuwa ni kujua
sifa za Lt. Gen. Waldhauser
katika Operation Desert Storm
(Gulf War) na Operation Enduring
Freedom (OEF) ili wapate
kuamua iwapo atamudu nafasi
hiyo mpya au la. Ila kwetu sisi
Afrika, nadhani muhimu kwetu
ni kujua, hii Africom ya nini?
Kwa nini Africom? Inatufaa kwa
lipi? Nini agenda na malengo ya
wenye Africom yao?
Katika yale yanayoelezwa
na wenyewe, malengo ya
Africom kwa sasa ni kusaidia
kupambana na ugaidi, makundi
yenye msimamo mkali (violent
extremists) na kuzisaidia nchi za
Afrika kuwa na Amani.
Ushirikiano katika masuala
ya ulinzi ni katika malengo
yetu makubwa katika Africom
(core missions at U.S. Africa
Command) kwani kwa
ushirikiano huo tutawaimarisha
washirika wetu katika
kukabiliana na changamoto za
usalama.
Alisema Kamanda Rodriguez
alipotembelea Djibouti,
Somalia, Ethiopia, Kenya na
Uganda mwaka jana akielezea
umuhimu wa Africom kwa
Afrika. Akaongeza kuwa
Afrika hivi sasa imekuwa na
itaendelea kuwa eneo muhimu
la kinyanganyiro cha rasilimali
na mambo ya kiuchumi kwa
ujumla, hivyo suala la usalama
linakuwa na umuhimu mkubwa.
Kama taifa kubwa duniani,
Marekani inajaribu kuidhibiti
dunia nzima kupitia uwezo
wake wa kijeshi. Ukitoka
Pentagon, utakutana na
European Command, Central
Command, Pacific Command,
Southern Command na Northern
Command.
Kabla ya kuundwa Africom,
Afrika ilikuwa chini ya
European Command ukiacha
nchi za Misri, Seychelles,
Djibouti, Eritrea, Ethiopia,
Kenya, Somalia (Horn of Africa
states) na Sudan, ambazo
zilikuwa chini ya Central
Command huku Comoros,
Madagascar, Mauritius na
Reunion, zikiwa chini ya
Kamandi ya Pacific (Pacific

ANNUUR NEW.indd 10

AN-NUUR

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 6 - 12, 2016

Sio Ugaidi ni ubunifu


Mshenga mpya wa ajali anakuja
Ukoloni unarudi kwa ruhusa yetu

Lt. Gen. Thomas David "Tom"


Waldhauser.

Gen. David M. Rodriguez.

Generali William E. "Kip" Ward

Command.)
Ilikuwa ni mwaka 2007
ambapo Africom iliundwa,
lakini makao makuu yake
yakiwa Stuttgart, Ujerumani
huku ikielezwa kuwa Kamandi
hiyo itaigawa Afrika katika
makundi matano yote yakilenga
kuhudumia jumuiya na umoja
wa kikanda wa kiuchumi ndani
ya Afrika (Africas main Regional
Economic Communities). Timu
moja itashughulika na nchi za
Algeria, Libya, Mauritania,
Morocco na Tunisia (Arab
Maghreb Union). Kanda yetu ya
Afrika Mashariki-East African
Community (EAC) ikiwa
na nchi za Burundi, Kenya,
Rwanda, Tanzania na Uganda,
nayo itakuwa na watu wake
mahsusi ndani ya Africom wa
kuishughulikia.
Kanda nyingine ni ile ya
Economic Community of West
African States (ECOWAS), ikiwa
na nchi za Benin, Burkina Faso,
Cape Verde, Cote dIvoire,
Gambia, Ghana, Guinea-Bissau,
Liberia, Mali, Nigeria, Senegal,
Sierra Leone na Togo.
Kuna pia zile nchi za Jumuiya
ijulikanayo kama Economic
Community of Central African
States (ECCAS). Hizi ni Angola,
Burundi, Cameroon, Central
African Republic, Chad,
Republic of Congo (Brazzaville),
Democratic Republic of Congo
(Kinshasa), Equatorial Guinea,
Rwanda na Sao Tome na
Principe. Hizi nazo zitakuwa
na deski lake ndani ya Africom.
Ukitoka hapo unakutana na

Jumuiya ya Southern Africa


Development Community (SADC),
ambapo unazikuta nchi za
Angola, Botswana, Democratic
Republic of Congo, Lesotho,
Madagascar, Malawi, Mauritius,
Mozambique, Namibia,
Seychelles, South Africa,
Swaziland, Tanzania, Zambia
na Zimbabwe. Na yenyewe
hii, imewekewa watu maalum,
kuishughulikia.
Kipo pia kikosi maalum cha
wataalamu, kuzishughulikia
nchi za Kanda inayoitwa
Horn of Africa. Humo
zinatumbukizwa nchi za
Djibouti, Ethiopia, Eritrea,
Kenya, Seychelles, Somalia,
Sudan, Tanzania na Uganda.
Yemen inatumbukizwa humo
pia. Zote hizo zinahudumiwa
na kikosi kinachoitwa Combined
Joint Task Force Horn of Africa
(CJTF-HOA) chenye makao
yake Djibouti ambapo Pentagon
imeweka askari wake wapatao
2000.
Ukiacha CJTF-HOA,
Marekani ina kambi kamili za
kijeshi (military base) Djibouti,
Camp Lemonnier. Lakini
pia inazitumia Seychelles,
Kenya, Ethiopia, Morocco,
Mali, Rwanda na baadhi ya
nchi nyingine za Kiafrika
kufanya harakati zake za kijeshi
ipendavyo.
Japo makao makuu ya
AFRICOM, bado yapo Stuttgart,
Ujerumani, lakini utaona
kuwa kupitia utaratibu huo wa
kuishika Afrika kijeshi kupitia
kanda hizo, ni kana kwamba

Bara lote hivi sasa limedhibitiwa.


Upo utaratibu na mikakati ya
kuandaa vikosi vinavyoitwa
The African Standby Force (ASF)
ambayo, kinadharia ipo chini ya
Umoja wa Afrika (AU), lakini
makamanda watoa mafunzo na
wapanga na waongoza mipango
ni Pentagon (U.S. Special Forces)
na NATO (NATO Strike Force/
NATO Response Force (NRF)).
Ukiacha zile kanda za
kiuchumia-EAC, AMU,
ECOWAS, ECCAS na SADC,
ambazo zina madeski yake
maalum ndani ya Africom,
vimeundwa pia vikosi maalum
vya kipolisi na kijeshi kwa kile
kilichoitwa kusaidia kupambana
na magaidi. Hapa unakutana
na Pentagons Trans-Sahara
Counter-Terrorism Initiative
(TSCTI), ikizihudumia nchi za
Algeria, Chad, Mali, Mauritania,
Niger, Senegal, Morocco,
Nigeria na Tunisia. Washirika
wa Washington katika nchi za
NATO ambao ni Uingereza,
Ufaransa, Ujerumani, Hispania
na Uholanzi, nao wanaingia
katika Trans-Sahara CounterTerrorism Initiative.
Kupitia mpango huu,
vinaundwa vikosi maalum
(Special Forces) vikipewa
mafunzo na kusimamiwa na U.S.
Africa Command (USAFRICOM)
pamoja na Special Operations
Command (SOCAFRICA).
Taarifa zinaonyesha kuwa
katika eneo letu hili la Afrika
Mashariki, kumeundwa kikosi

Inaendelea Uk. 11

5/4/2016 3:27:02 PM

11
Inatoka Uk. 10
kikijulikana kwa jina la East
African Standby Brigade
(EASBRIG) ambayo makao
makuu yake yapo katika Chuo
cha Maofisa wa Kijeshi (Defence
Staff College) Karen, Nairobi.
Humo kukiwa na wataalamu
wa kijeshi kutoka Marekani
na nchi za Ulaya. EASBRIG
ina wanajeshi kutoka Burundi,
Comoros, Djibouti, Eritrea,
Ethiopia, Kenya, Madagascar,
Mauritius, Rwanda, Seychelles,
Somalia, Sudan, Tanzania na
Uganda. Gazeti la The Nation,
la Oktoba 29, 2009, lilimnukuu
mmoja wa makamanda wa
kijeshi wa Kenya Julius Karangi,
akieleza uwepo wa EASBRIG
katika Kenya halikadhalika
uwepo wa makamanda wa
kijeshi wa kigeni ambao
alisema kuwa watasaidia
sana kuimarisha kikosi hicho
maalum.
Aidha, inaelezwa kuwa U.S.
Africa Command (Africom)
itafanya kazi bega kwa bega na
EASBRIG katika kupambana na
magaidi eneo hili la Afrika chini
ya ule mkakati wa ujumla wa
Vita dhidi ya ugaidi (Global War
on Terrorism).
Kwa hiyo katika mazungumzo
rasmi ya kiserikali yanayowekwa
hadharani, Africom ni sadaka
kwa Waafrika. Ni msaada
unaokuja kwa hisani ya watu
wa Marekani kutokana na roho
nzuri na huruma ya Wamarekani
kutaka kutuimarisha kiulinzi
na usalama. Ndio maana
ukaona hivi sasa kuna
harakati na program nyingi za
mafunzo, misaada ya kijeshi
na yanayoitwa mazoezi ya
pamoja. Na ili kuhakikisha
kuwa program hizo zinakwenda
vizuri, tayari jeshi la Marekani
lina kambi za kijeshi (military
bases) katika nchi kadhaa za
Kiafrika.
Katika mlango huo wa
kusaidia kutujengea uwezo wa
kiusalama, imepatikana sababu
ya Marekani kuwa na kambi
zake za kijeshi katika nchi zetu
kwa ridhaa yetu wenyewe!
Swali ni je, utando huu wa
kijeshi ukishalikamata Bara
zima, nchi za Kiafrika na Bara la
Afrika litabakia tena kuwa huru?
Hivi ndani ya nchi yako
kukiwa na kambi ya Marines
na ghasia zake zote za vifaa vya
kisasa vya kijeshi, jeshi la nchi
yako litakuwa tena na kauli?
Wenye Marines katika ardhi
yako, wakitaka jambo kutoka
kwako, unaweza kuwakatalia?
Ukiwa na jeshi ambapo
makamanda wake wanapokea
maelekezo na kupewa mafunzo
na U.S. Africa Command
(USAFRICOM) pamoja na
Special Operations Command
(SOCAFRICA), bado utasema
kuwa hilo ni jeshi lako?

ANNUUR NEW.indd 11

Makala

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 6 - 12, 2016

Sio Ugaidi ni ubunifu

MMOJA wa Makamanda kutoka Afrika akiyatembelea Makao


Makuu ya AFCOM.
Maswali kama haya ndiyo
yanayopelekea wachambuzi wa
mambo kusema kuwa ujio wa
Africom ni ukoloni mpya.
New Colonialism: Pentagon
Carves Africa Into Military
Zones, ni Makala iliyoandikwa
na mwandishi Rick Rozoff
(Global Research, May 05, 2010).
Katika Makala hiyo anasema
kuwa kwa utaratibu kama huu,
utaona kwamba ni kana kwamba
Marekani inajitengenezea
majeshi ya kuifanyia kazi
(Surrogate Armies) kuidhibiti
Afrika
Hayo yanaelezwa pia katika
ule uchambuzi uliopewa
anuwani ya AFRICOM and the
USAs Hidden Battle for Africa
uliochapishwa Machi 30, 2010.
Humo inaelezwa juu ya kikao
kilichofanyika Januari 2, 2002,
kule Washington DC agenda
ikiwa mafuta ya Afrika (African
Oil: A Priority for US National
Security and African Development).
Katika kikao hicho ambacho

AN-NUUR

kilihudhuriwa na wazito wa
makampuni ya mafuta, maofisa
wa serikali na mtaalamu wa
kijeshi katika Afrika Lt-Col.
Karen Kwiatkowski pamoja na
Waziri Mdogo wa Mambo ya Nje
anayeshughulikia Afrika (wakati
ule wa Bush) Water Kansteiner,
ndiko kulikoibuka program hizi
tunazozishuhudia leo katika
Africom.
Likiripoti juu ya habari hizi,
gazeti la The Christian Science
Monitor linasema kuwa ilikuwa
ni katika kikao cha Januari
2002 kule Houston, Texas,
kilichoandaliwa na kundi
linalojiita African Oil Policy
Initiative Group (AOPIG),
ambapo yaliibuka mambo mengi
yaliyoongoza sera za Marekani
kwa Afrika, hasa katika masuala
ya raslimali, na hasa mafuta.
Katika uchambuzi waAFRICOM and the USAs
Hidden Battle for Africa, vita
dhidi ya ugaidi inatumiwa kama
kisingizio kuficha lengo halisi la

Africom la ujumla ambalo ni US


Hegemony, lakini pia ukoloni
mpya wa kudhibiti rasilimali
ya mafuta na madini katika
bara hili. Na kwa maana hiyo,
ugaidi si jambo la kuondoka
kwa sababu sio adui halisi bali
mkakati wa kufikia malengo
fulani ya kibeberu na maadhali
malengo hayo yanaendelea
kutekelezwa, basi ugaidi
utaendelea kuwepo ili kisingizio
cha kuwa na Special Forces na
kambi za kijeshi katika Bara hili,
kiendelee kuwepo.
Nimalizie kwa kusema kuwa,
hakuna jipya linalofanyika.
Ni Ukoloni, unyanganyi na
ubeberu ule ule wa tangu
zama. Ila hivi sasa watu
wamestaarabika kidogo. Kama
alivyojisema JB katika moja ya
filamu zake akionekana kutapeli
watu. Alisema mimi sio tapeli.
Mimi ni mbunifu.
Kwa kuja Vita Dhidi ya
Ugaidi, unaletewa mpango
wa kukusaidia kupambana na
Al-Shabaab, unawakaribisha
mwenyewe, unawakabidhi
polisi wako na wanajeshi wako
wakuundie Special Forces huku
mahali pengine wakipewa fursa
ya kuweka kabisa kambi zao za
kijeshi.
Kwa hiyo, Vita Dhidi ya
Ugaidi, nayo ni ubunifu wa
aina yake katika uvamizi,
uporaji na ukoloni. Hivi sasa
wanatuambia eti gaidi Abdul
Nadir Mumin ameikimbia Al
Shabaab akiwa na mipango ya
kuanzisha kundi la ISIS Afrika
Mashariki. Kwamba eti, Afrika
Mashariki ni region that is ripe
for the groups expansion but
has yet to be exploited.
Kwamba, hii Afrika Mashariki
yetu, ni eneo lenye fursa nzuri
za kusitawi magaidi wa ISIS
lakini fursa hizo hazijatumiwa
ipasanyo. (Tazama: The Orangebearded Jihadi general spreading
ISIS brand in Somalia-By Jack
Moore.)
Kama kawaida
wanatengeneza video za
propaganda, wanazirusha
kwenye Sky News zao.
Mtu unajiuliza, kama kuna
AMISOM na wameshatuletea
East African Standby Brigade
(EASBRIG) na Combined Joint
Task Force Horn of Africa
(CJTF-HOA), hayo mazingira
tena mazuri ya kusitawi magaidi
wa ISIS, yanatoka wapi?
Alijisemea mtaalamu mmoja
kwamba ubeberu wa zama
hizi, unatumia sophisticated
techniques consciously designed to
confuse the human mind.
(Soma zaidi: AFRICOM and
the Recolonisation of Africa.)

5/4/2016 3:27:07 PM

12

AN-NUUR

TANGAZO

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 6 - 12, 2016

Bismillahir Rahmaanir Rahiim

ISLAMIC PROPAGATION CENTRE

NAFASI ZA KIDATO CHA TANO - 2016/2017

KIRINJIKO ISLAMIC HIGH SCHOOL

UBUNGO ISLAMIC HIGH SCHOOL

NYASAKA ISLAMIC HIGH SCHOOL

Waislamu kote nchini mnatangaziwa nafasi za Kidato cha Tano kwa shule zifuatazo:

Ubungo Islamic High School


Kirinjiko Islamic High School
Nyasaka Isamic High School

Dar es Salaam : 0687 820895/0657 350172


Same, Kilimanjaro: 0784 296424/0756 676441
Mwanza: 0786 417685/0713 749020

Shule hizi ni za Kiislamu zenye lengo la kuwapa wanafunzi taaluma ya hali ya juu na malezi
bora ya Kiislamu. Shule hizi ni za BWENI za mchanganyiko wa wavulana na wasichana.
Zipo Combinations zote za SAYANSI, ARTS na BIASHARA.
Muombaji awe na ufaulu wa masomo matatu (3) kwa kiwango cha Credit (yaani A, B na C)
Daraja la III (Division three) au zaidi na Grade D kwenye masomo ya Combination.

Mwisho
nini
tarehe
30/05/2016
Mwishowa
wakurudisha
kurudishafomu
fomu
tarehe
02/05/2016.

Fomu za maombi zinapatikana kwa gharama ya Shilingi 10,000= katika Tovuti:www.ipcorg.tz na katika vituo vifuatavyo:

ARUSHA: Ofisi ya Islamic Education Panel, Jambo


Plastic, Ghorofa ya 2 mkabala na Msikiti Mkuu
Bondeni : 0783 438676/0715 438676.
KILIMANJARO: Moshi: Msikiti wa Riadha:07673453

67/0686938077. Same Juhudi Studio mkabala na


Benki ya NMB Same: 0757 013344. Same: Kirinjiko
Islamic Secondry School: 0784 296424/0713
115041. Usangi- Falhum Kibakaya : 0787 142054.
Ugweno Simbomu centre Mwl. Hidaya A. Mussa:
0784 656514
TANGA: Twalut Islamic Centre Mabovu
Darajani : 0715 894111/0713 014469. Uongofu
Bookshop: 0784 982525. Korogwe: SHEMEA
SHOP : 0754 690007/071569008. Mandia Shop
- Lushoto: 0782257533. Handeni Mafiga -0782
105735/0657093983
MWANZA: Nyasaka Islamic Secondary School : 0717
417685/0786 417685. Ofisi ya Islamic Education
Panel Mtaa wa Rufiji mkabala na Msikiti AlAmin 0785 086 770/0714097362.
BUKOBA: Ofisi ya Kutaiba Saccos: 0765 748056
MUSOMA: Ofisi ya Islamic Ed Panel -Mtaa wa
Karume,Nyumba Na. 05 : 0765024623/0787868611
SHINYANGA: Msikiti wa Majengo karibu na Manispaa
ya Shinyanga Mjini :0655608139/0768895484

KAHAMA: Ofisi ya Kamati ipo karibu na zahanati ya

Doctor Dalali: 0754 994738/0782 994738

Dar es Salaam: Ubungo Islamic High School : 07


56584625/0657350172/0712 033556. Ofisi ya
Islamic Ed. Panel Temeke -Msikiti wa Nurul Yakin
: 0655144474/0787119531
MOROGORO: Wasiliana na
Ramadhani Chale :

0715704380. Ifakara wasiliana na Mwl. Sharifu:


0659 158958
GEITA: Ofisi ya Kamati karibu na mashine ya
kukobolea mpunga shilabera: 0765 748056
DODOMA: Hijra Islamic Primary School

: 0716

488444/0653 705627.
MTWARA: Ofisi ya Islamic Education Panel,
Mtaa wa Magomeni A mkabala njia panda ya
uwanja wa ndege: 0715 465158/0787 231007.
SONGEA: Kwa Kawanga Karibu na Msikiti wa
NURU : 0713249264. Mkuzo Islamic High
School :0654 876317
MBEYA: Ofisi za Islamic Education Panel Uhindini
0785425319. Rexona Video mkabala na
Mbeya RETICO: 0713 200209/0785425319.
Rukwa: Sumbawanga:Jengo la Haji Said
Shule ya Msingi Kizwike: 0757090228/0786
313830
TABORA: Kituo cha Kiislamu Isevya:
0784
944566/0718 556355. Nzega - Dk. Mbaga-0754
576922/0784576922.
IRINGA: Madrastun Najah: 0714 522 122.
PEMBA: Wete: Wete Islamic School : 0777
432331/0712772326.
UNGUJA: Madrasatul Fallah: 0777125074.
PANDU BOOKSHOP 0777462056 karibu na
uwanja wa Lumumba

544757/0718661992
SINGIDA: Ofisi ya Islamic Education. Panel
karibu na Nuru snack Hotel : 0786
425838/0784 928039.
MANYARA: Ofisi ya Islamic Ed. Panel Masjid
Rahma: 0784491196
KIGOMA: Msikiti wa Mwandiga: 0714717727.
Kibondo Islamic Nursery School:
0766406669. Kasulu: Murubona Isl.SS:
0714710802/0763 298440
MAFIA: Ofisi ya Ust. Yusufu Ally jirani na
LINDI: Wapemba Store: 0784 974041/0783
msikiti mkuu : 0773580703.

WAHI KURUDISHA FOMU ILI UJIHAKIKISHIE NAFASI


FORM V TANGAZO.indd 1

ANNUUR NEW.indd 12

4/18/2016 5:23:55 AM

5/4/2016 3:27:08 PM

13

Safu ya Ben Rijal

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 6 - 12, 2016

Wanyama waliotajwa katika Quran: Ndege - 3


Mchoro wa Hudhud aliochorwa
na Zhao Mangfu ukionekana
katika Makumbusho ya Shanghai.
Na Ben Rijal
KATIKA makala iliopita
tulichambua aya mbalimbali
zinazomuelezea ndege Hudhud
ambaye ni ndege mwenye
kupendeza na kuelezewa
juu yake katika Quran jinsi
alivyokosekana wakati Mtume
Suleiman AS alipokuwa akikagua
vikosi vyake.
Tumeweza kufahamu kuwa
Mtume Suleiman AS, alikuwa
akijua na kuzifahamu lugha za
wanyama na majini wote walikuwa
chini yake. Mtume Suleiman AS
baba yake ni Mtume Daud AS
akiwa ni kati ya Mitume ambao
baba alikuwa ni Mtume na mtoto.
Orodha hio ya Mitume ikiwa baba
ni Mtume na mwana ni Mtume, ni
kama ifwatavyo, Mtume Ebrahim,
watoto Ismael na Ishaq na wote
walikuwa ni Mitume, Mtume
Zakariyah na mwana Yahya, Ishaq
na Yakoob, Mtume Yakoob na
mwana Yusuf.
Ndege Hudhud ni ndege
mwenye kupendeza na wataalamu
wa Sayansi baada ya kumsoma
kupitia Quran na Baibilia,
walifanya utafiti kuona kama ndege
huyu bado yupo au ametoweka?
Wamekuja kuelewa kuwa bado
yupo na anaonekana katika sehemu
za mabara ya Ulaya, Afrika na
bara la Asia. Katika bara la Afrika
huonekana zaidi katika maeneo
ya Afrika ya Kaskazini, Afrika
ya Kusini na kwenye kisiwa cha
Madagascar.
Kabla hatujamuelezea kwa kina
hebu tuangalie anavyojulikana
katika Ulimwengu tunaoishi:
Wayahudi huko Israel
wamemtukuza na kumfanya
ni ndege wa taifa hilo. Wamisri
wa kale katika maandishi yao
yameonyesha kuwa Hudhud ni
ndege adhimu, kizungu anaitwa
kwa jina la Hoope kwani anavyolia
hulia Ooop Ooop, kama alivyo
jogoo na yeye ana upanga juu
ya kichwa chake kitu ambacho
kinakuwezesha kumuelewa mara
mmoja unapomuona. Mabawa
yake yana rangi ya mdalasini na
kwenye mabawa yake akiwa na
rangi nyeusi na nyeupe pamoja
na kwenye mkia ambazo ni rangi
zenye kuleta haiba. Malaji yake
makubwa ni kukamata wadudu
wadogo wadogo, hula vyura,
mbegu mbalimbali, na mdomo
wake huuweka wazi mara nyingi
kwa kuwa tayari kwa mawido.
Hudhud ana tabia ya
kuvutia pale anapoota jua
huwa anagaragara huku akiwa

ANNUUR NEW.indd 13

ametanua mbawa zake na mkia


wake kuweka juu. Katika moja ya
jambo lake lilokuwa sio la kawadia
kumlinganisha na ndege wengine,
ni pale anaporuka na kuanza safari
zake hufanana na kipepeo.
Hudhud ana hikma za kujiweka
kuwa katika maisha endelevu kwani
kwenye nyumba yake huweka
harufu ya uvundo ya kuwafanya
maadui wake kutomkaribia, lakini

wastani wanaishi umri wa miaka


mingapi inategemea wanapoishi
kwa mfano nchi tajiri kutokana
na maisha yao kutononoka huishi
maisha ya miaka mingi kufikia
mfano 70 kwa wastani na nchi za
kimaskini watu huishi watani wa
miaka ya 40na 50.
Tumeweza kuona Hudhud
wanafikisha maisha yao
kufikia umri wa miaka 10, kwa
walivyokuwa sio waharibifu, kwa
hio Hudhud mwanadamu sio adui
wake mkubwa. Viumbe ambao
huwa ni maadui kwa binadamu
idadi yao hupungua kutokana na
vita baina ya mwanadamu na hao
viumbe.
Chambuzi za Huduhud kitaalamu
Wataalamu wanamhesabu
Hudhud kama ni mnyama na
kumuweka katika ukoo Upupidae
na jina la kitaalamu anajulikana
kama Upupa epops.
Hudhud ni katika ndege wa kale
wanaofahamika katika Historia.
Yupo duniani kwa zaidi ya miaka
alfu na Zaidi. Umbo lake ni la kati
lisozidi centimeter 25 na uzito wake
hauzidi baina ya gramu 46 na 89.
Unapokuwa kwenye msitu katika
maeneo wanapopatikana, ni rahisi
sana kujua aliaye kama ni Hudhud

Yaonekanavyo mayai ya
Hudhud.

wakati huo huo kuwavutia wadudu


kuingia katika tundu lake na
kuweza kupata chajio chake kwa
urahisi kabisa.
Wanyama wengi hujenga
mamlaka ambayo huwa hataki
mwengine kumuingilia. Kwa
mfano Simba kwenye mamlaka
yake hunyunyiza mkojo sehemu
yote anayoimiliki. Kwa hio, huwa
tayari kupambana na Simba yoyote
atakayejiingiza katika mamlaka
yake kutaka kumvunjia, hapa ni
kuzungumzia kutaka kufanya
mapenzi na jike lake.
Upande wa Hudhud, dume
hujenga mamlaka yake katika
jumba lake na kubembea na
mwandani wake wakiwa peke yao.
Hapo atakayetaka kuja kumharibia
hupambana naye na mapambano
mara nyingi huwa makubwa
hata kupelekea kutofoana macho
au kujeruhiyana na mwengine
kufariki. Wachunguzi wa maisha
ya wanyama wamegundua kuwa
maisha yao hayazidi miaka 10.
Kujua umri ambao viumbe
mbalimbali huishi ni muhimu
kwani inasaidia kujua namna ya
kukabiliana, kwa mfano jamii ya
nzi hawazidishi maisha yao zaidi
ya siku 30, wakati mbu maisha yake
yote hayapindukii zaidi ya miezi 2
na ni mbu jike ndio anayomuuma
mwanadamu kutafuta protini na
mbu dume yeye hutumia zaidi
juisi ya maua. Kuweza kujua umri
wa maisha ya viumbe mbalimbali
husaidia katika kupambana nao
kuweza kuwaangamiza.
Wanadamu nao kujulikana kwa

AN-NUUR

Surat Al-Naml 27:20-22 katika


Baibilia katajwa kwenye Taurat,
Leviticus 11:13-19 na kwenye
Deuteronomy 14:18.
Wamisri wa kale wakimtukuza
na wakimuona kuwa ni mtakatifu
na hata kuchorwa kwenye makaburi
yao. Huko Uajemi huonekana kama
alama ya thamani na kumuweka
kama ni kiongozi wa ndege wote.
Katika kitabu Mantiq al-Tayr
na Attar, kitabu chenye maana
Mkutano wa Ndege utaona namna
Hudhud alivyotukuzwa kuwa yupo
juu kuliko ndege wa aina yoyote
yule.
Baadhi ya nchi za Ulaya
humuona Hudhud ni mwizi
na katika zile nchi za Kaskazini
za Ulaya zijulikanazo kama
Scandanivia, Hudhud ni uchuro
akilia huwa kila mtu anatetetemeka
kuona kama anabashiria vita. Watu
wa Estonia wakimsikia Analia,
hujua kuna vifo vitatokea na
hubashiri kuwa anapolia hutokea
vifo vingi vya ngombe.
Wayunani wa kale wakimwita
mfalme wa ndege. Wayahudi katika
mwaka wa 2008 walimtukuz na
kumfanya alama ya nchi yao. Huko
Afrika Kusini katika Chuo Kikuu
cha Johannesburg, nembo ya Chuo
hicho ina picha ya Hudhud. Huko
Ujerumani kwenye Manispaa
ya Armstedt, wao katika makoti
yao wameweka beji ya Hudhud
wakati nchini Morocco huuzwa
sokoni ikiwa ni dawa kwa maradhi
mbalimbali, ingawa Serikali inapiga
marufuku lakini ukenda katika
maduka ya Morocco utamkuta
Hudhud anauzwa akiwa mzima
au mabaki yatokanayo na ndege
huyu huuzwa na kutokosekana
wanunuaji.
Hudhud tumuenzi au

Hudhud akiwa anatafuta chajio


kwa mlio wa kufwatana Oop Oop
Oop ingawa kina Jogoo mwitu nao
hufanana kimlio, lakini Hudhud
anapolia hufwatanisha kiasi mara
tatu akapumzika kisha kaendeleza
kulia Oop Oop Oop.
Uonekanaji wake
Kama huko kabla tulivyoelezea
kuonekana kwake zaidi huonekana
katika mabara matatu ikiwa bara la
Ulaya, Asia na Afrika ya Kaskazini.
Hudhud waliopo Ulaya, huhama
nyakati za baridi na kuhamia barani
Afrika wakati wa bara la Afrika
wao hubakia nyakati za kiangazi na
kipupwe pasi kuhama. Uhamaji wa
Hudhud kwenda masafa marefu
kutoka Ulaya hadi kufika Afrika
kwa utaaalmu wa Sayansi kuweza
kugundua hivi sasa ni kielelezo
kinachotufahamisha pale Mtume
Suleiman alipokagua majeshi yake
akiwa Hudhud haonekani. Hudhud
alikuwa sehemu za Saba huko ni
Yemen na Mtume Suleiman alikuwa
Jerusalem. Hii ni ithibati ya yale
yaliolezwa kwenye Quran na Bibilia
hayana towa.
Mahusiano yake na Mwanadamu
Huyu ni ndege wa kale kwa hio
mwanadamu yupo karibu naye,
kwenye Quran kaelezewa kwenye

WAENGEREZA wameweza
kumtambua na kumpa hifadhi
Hudhud katika karne ya 18
tumuangamize? Jawabu unayo
wewe. Fawtana na mie katika
makala hizi wanyama waliotajwa
katika Quran. Atakayofwatia ni
mbwa.

5/4/2016 3:27:11 PM

14

MAKALA/MASHAIRI

TUFUNGENI SHAABAN
Rajabu i ukingoni, aula kukujuzeni,
Na Shabani i njiani, kesho kutwa si mwakani,
Mbeleye ni Ramadhani, si baidi kwa mizani,
Shabani imewadia, tujiandae kufunga.
Muhammad adinani, alikifunga Shabani,
Pima wake uthamani, ujisaili kwanini,
Thuma ujitathimini, kwa RAHMANI unani,
Shabani imewadia, tujiandae kufunga.
Hakuacha asilani, kuifunga maishani,
Siku moja 'sijedhani, bali wote karibuni,
Mimi nawe kulikoni, kutoifunga Shabani,
Shabani imewadia, tujiandae kufunga.
Twaridhika tuna nini, nijuzeni ikhiwani,
Kulikoni na kwanini, tusiifunge Shabani,
Tumgeze adinani, kwa kuifunga Shabani,
Shabani imewadia, tujiandae kufunga.
Haya shime waumini, wa Bara na Visiwani,
Tutie nia moyoni, ya kuifunga Shabani,
Ya ILAHI tuauni, tujeifunga Shabani,
Shabani imewadia, tujiandae kufunga.
ABUU NYAMKOMOGI

SWADAKTA, MBUNGE WA MAFIA!


(MH.RIZIKI BINT SHAHARI)
Riziki nakupongeza, kwa uloinena kweli,
Kadhia ulodokeza, si ya puya ni ya kweli,
Hukutaka kuchagiza, kwa kuipamba kwa kweli,
RIZIKI 'menena KWELI, MASHEKHE kosalo nini?
Ni haki uloeleza, kwa kila mpenda kweli,
Kwa hilo anokubeza, si mwingine mcha kweli,
Aso na njema ruwaza, ila ya kupinga kweli,
RIZIKI 'menena KWELI, MASHEKHE kosalo nini?
Hukutaka kwendekeza, habari ziso za kweli,
Au umma kuukwaza, kwa kuipindua kweli,
Ama dira kupoteza, kwa kuikiuka kweli,
RIZIKI 'menena KWELI, MASHEKHE kosalo nini?
Hukutaka kwao 'izza', kwa kukengeusha kweli,
Wala kujipendekeza, kwa wapinzani wa kweli,
Ukweli ukawajuza, lengo isimame kweli,
RIZIKI 'menena KWELI, MASHEKHE kosalo nini?
Kuna wataokubeza, kwa kuitongoa kweli,
Pamwe na kwa kuuliza, Bungeni jambo la kweli,
Mengi watahanikiza, dhidiyo yaso ya kweli,
RIZIKI 'menena KWELI, MASHEKHE kosalo nini?
MDINI nakueleza, watakuita kwa kweli,
Mambo uloyauliza, wajibu kama si kweli,
Wasanze kuhanikiza, dhidi yako yaso kweli,
RIZIKI 'menena KWELI, MASHEKHE kosalo nini?
Ninotaka kukujuza, kwa kuitongoa kweli,
Maadui 'meongeza, kosalo kulonga kweli!
Kwa ulimwengu wa giza, adui msema kweli!
RIZIKI 'menena KWELI, MASHEKHE kosalo nini?
Adharusi endeleza, dhidi ya wakana kweli,
Wasaka tonge na 'feza', na vyeo viso vya kweli,
Hata wakikupuuza, ALLAH shahidi wa kweli,
RIZIKI 'menena KWELI, MASHEKHE kosalo nini?
Akudumishe MUWEZA, katika kunena kweli,
Pamwe na kuwahimiza, wengine kunena kweli,
Mwisho ninakupongeza, kwa kuitangaza kweli,
RIZIKI 'menena KWELI, MASHEKHE kosalo nini?
ABUU NYAMKOMOGI

ANNUUR NEW.indd 14

AN-NUUR

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 6 - 12, 2016

Kutoka kibanda cha miti


hadi Kituo cha elimu Sinza
Inatoka Uk. 20

ambao walifanya
juhudi zao kwa
kujitolea mali nguvu
zao na kufanikisha
uwepo wa Masjid Nur
na kuendelezwa mpaka
sasa.
Hata kama Msikiti
huo wa matope ulihitaji
fundi, lakini wao
wenyewe waliweza
kujitoa na kuweza
kuujenga kwa ajili
ya kupata sehemu
ya kufanyia ibada na
kusomeshea watoto
wao kwani Madrasa
pia ilikuwepo tokea
awali. Anaeleza Imam
Malange.
Mbali ya kusajili,
timu hiyo ya uongozi
pia ilifatilia namna
ya umilikishwaji wa
ardhi hiyo kisheria
kwa ajili ya shuhughuli
mbalimbali za kidini,
hali ilikwenda hivyo
kidogo dogo mpaka
miaka ya 1990s.
Hapakuwa na
utaratibu ulio bora
katika mikakati
ya uongozo lakini
tunaweza kusema
kwamba kwa wakati
huo ndio ilikuwa
kiwango chao kwa
kadri walivyo jaaliwa
na kuweza kusimamia
hatua hizo na kuweka
msingi imara wa kituo
na mpaka sasa kufikia
hivi kilivyo. Anaeleza
Imam Malange.
Mwaka 1993,
upana wa shughuli za
kiharakati Msikitini
hapo katika sekta ya
elimu ziliongezeka
zaidi kutoka Madrasa
mpaka Shule ya Awali
(Nursery School), na
ilipofika mwaka 2002,
kituo kilipiga hatua
zaidi kwa kuanzisha
Shule ya Msingi
(Primary School).
Kwa ujumla vituo
vyote vinne vya
elimu chimbuko lake
ni Madrast Ikhlasi,
iliyoanza miaka hiyo
sambamba na Masjid

Nur, lakini baadae


zilikuja kuungana
na Madrasat Islahi
ya Sheikh Mituro,
ambayo aliihamishia
Msikitini kutoka
nyumbani kwake
ilipokuwa awali
baada ya kuongea na
uongozi wa Msikiti, ili
kuunganisha Madrasa
hizo.
Imamu Malange,
anasema kwa maeneo
haya ya Sinza kwa
miaka hiyo ya 1980s,
Madrsa hiyo ya AlMarhum Shkh Hamisi
Saidi Mituro, ilikuwa
maarufu zaidi na vijana
wengi wa Kiislamu wa
hapo Sinza, wamepitia
katika Madrasa hiyo.
Nakumbuka wakati
Shule ya Msingi
ipo darasa la nne,
tukapiga hatua zaidi
ya kuanzisha Shule ya
Sekondari, hiyo ilikuwa
ni mwaka 2005, na
Shule zote hizo mpaka
sasa zinaendelea
kutoa elimu kwa
vijana wa Kiislamu na
zikiwa katika usajili
kamili wa Serikali.
Amethibitisha Imam
Malange.
Mbali na kuendesha
Shule hizo, lakini
Masjid Nur, chini
ya Jumuiya hiyo ya
Waislamu Sinza,
tayari ina Chuo cha
Ualimu, na uongozi
upo katika hatua za
mwisho kukamilisha
usajili kupitia NACTE,
baada ya kukamilisha
maelekezo muhimu
waliyopewa.
Ni matumaini yetu
ndani ya mwezi wa
tano, mwaka huu, kozi
ndogo ndogo zitakuwa
zimeanza kama vile
mafunzo ya Kompyuta,
Ualimu ngazi ya
Shule za awali, na
ifikapo mwezi wa tisa
mwaka huu, tutakuwa
tumeanza kutoa elimu
ya Ualimu ngazi ya
Diploma kwa ngazi ya
Shule ya Msingi.

Hata hivyo Imamu


Malange, anauelezea
mgogoro wa mwaka
1997, wa kiuongozi
uliyoukumba Msikitini
huo kama ilivyokuwa
ada kwa miaka hiyo
kwa suala la mivutano
ya kiuongozi katika
Misikiti mbalimbali
hususani Jijini Dar es
Salaam, ilikuwa ni la
kawaida.
Anasema hali hiyo
ilisababishwa zaidi na
toauti za kimtazamo na
fikra hususani katika
suala zima la utawala
na matumizi ya Misikiti
jambo ambalo lilikuwa
likisababisha kuibuka
kwa mivutano hiyo.
Hata hivyo anaeleza
kuwa mgogoro huo
katika Msikiti wao
umebaki kama historia
ya kufikia mafanikio.
Kupitia mgogoro
wetu hapa Msikitini,
ambao mvutano
mkubwa ulikuwa
baiana ya Wazee na
Vijana, nimeweza
kujifunza kwamba
vijana peke yao bila
kupata fikra za wazee
wenye busara inaweza
ikawa tabu kidogo
kufikia mafanikio
kwani wakati
mwingine vijana jazba
zinatawala mmno,
lakini uwepo wa wazee
huwa wanapoza presha
hivyo mwisho wa
siku manasikilizana.
Anasema Imamu
Malange.
Kwa kuwathamini
Wazee, liliundwa
Baraza maalum la
wazee wa Msikiti,
wakiwemo waasisi
wa Msikiti wa awali
kabisa, ambao
wanatupa fikra zao na
sisi vijana tunasimamia
na kufatilia malengo na
mikakati ya Jumuiya na
Masjid. Anabaianisha
Imamu Malange.

5/4/2016 3:27:13 PM

15
Inatoka Uk. 8

makubwa makubwa au
mashirika ya bima.
Hii ilidhihirika ukweli wake
pale makampuni mbalimbali
yalipoanza kumgombania,
wakianzia na kima cha chini
cha mshahara cha Kshs 40 000
(takriban 482 $ au Tshs 748,300)
kwa mwezi wakati huo.
Ingawa alikuwa hayupo
sawa kifedha wakati huo, Balqis
alikataa kazi zote hizo kwa
sababu aliamini kufanya kazi
katika makampuni ya bima na
mabenki hayo ya kibiashara,
ilikuwa ni haram kwa sheria za
Kiislamu.
Kha! Atakuwa kashaanza
kuwa mwehu!, Hivyo
ndivyo walivyosema rafiki na
ndugu. Lakini kwa upande
wake, ilikuwa ni makosa
na kinyume cha maadili
(unethical) kufanya kazi katika
mashirika yanayoendekeza
riba yakipingana na maneno ya
Mwenyezi Mungu: Mwenyezi
Mungu ameihalalisha biashara
na ameiharimisha riba.[Q
2:275].
Alikuwa na yakini kuwa
akijitenga na kitu kwa ajili ya
Allah (sw), basi Mwenyezi
Mungu atamfidia na kitu kingine
bora kuliko alichokiacha. Alifata
maneno ya Mtume Muhammad
kwa nguvu zote.
Huwezi kuacha chochote
kwa ajili ya Allah, aliyetukuka,
ila atakupa kingine bora badala
yake.
Balqis alipozwa moyo
na mafundisho ya Uislamu
yaliyompa faraja, tumaini na
nguvu: Enyi watu, muogopeni
Mola wenu, na muwe na kiasi
katika kutafuta maisha ya
dunia, kwani hakuna roho
itakayoondoka bila kupokea
vyote ilivyokadiriwa, hata kama
vinachelewa. Hivyo muogopeni
Allah na mumche, muwe na
kiasi katika kutafuta rizki;
chukua lile lililoruhusiwa na
uwache lililokatazwa.
Badala yake, Balqis akaamua
kufanya kazi katika kampuni
ya ukaguzi wa mahesabu
iliyoko huko Nairobi, karibu
na barabara iitwayo Mombasa
Road. Hapo alikuwa akilipwa
Kshs 10,000 (takriban 120 $
au Tshs 187,000) kwa mwezi.
Kutoka katika mshahara huo,
alitenga Kshs 2500 (takriban 30 $
au Tshs 46,760) kulipia chumba
huko Eastleigh, sehemu iliyopo
kiunga cha jiji la Nairobi.
Ukiachilia mbali gharama
nyengine kama matibabu,
mshahara wa Balqis haukuwa
ukimtosha ila yeye aliendelea
kuvumilia.
Baada ya mwezi, akapata
kazi nyengine kama msarifu
(bursar) wa Shule ya Sekondari
ya WAMY (WAMY High School)
akipokea kiasi cha shilingi za
Kenya 20 000 (takriban 241 $ au
Tshs 374,000).

ANNUUR NEW.indd 15

Makala/Tangazo

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 6 - 12, 2016

Zana za mapigano zamuokoa


Balqis Chelangat Chepkwony

Balqis Chelangat Chepkwony


Alifanya kazi hapo kwa miezi
miwili kabla ya ahadi ya Mungu
kutimia kwake. Alipokea simu
asiyoitegemea. Naongea na
Chelengat?, Mpigaji alihoji.
Je, unaweza kujipanga kwa
ajili ya usaili (interview) wa kazi
ofisini kwetu.
Akapata kazi nzuri hapo
akiwa mhasibu wa kampuni ya
mafuta ya Hass (Hass Petroleum
Company) hapo Nairobi.
Kampuni hiyo imestawi Afrika
Mashariki nzima na maeneno
ya maziwa makuu na inazidi
kupanua huduma zake sehemu
nyenginezo.
Balqis aliita kampuni hii kama
baraka kutoka kwa Allah, kwani
ndio kampuni pekee Kenya
inayotenganisha wafanyakazi
wake wa kiume na wa kike na
inaruhusu wanawake kuvaa
mavazi yao ya kidini, ikiwemo
niqab (kuziba uso). Kampuni
pia, imetenga nafasi kwa ajili
ya swala na katika nyakati hizo
wafanyakazi wanaruhusiwa
kusimamisha kazi zao ili waende
kuswali.
Mshahara wa kuanzia ulikuwa
mara dufu ya alichokuwa
akipokea katika shule ya
WAMY. Sanjari na hilo, kampuni
imempa mkopo usio na riba
ambao amenuia kuutumia kwa
ajili ya kununua mahali pa
kuishi Nairobi.
Kwa sasa, mshahara wake wa
kila mwezi si chini ya Kshs 130
000 (takriban 1,546 $ au Tshs 2,
431, 510). Sasa anaelewa vizuri

AN-NUUR

zaidi ule usemi wa Mtume


kuwa:
Huwezi kuacha jambo kwa
ajili ya Allah, aliyetukuka ila
yeye atakupa lengine bora
badala yake.
Alikataa kufanya kazi katika
mashirika yanayoenda kwa riba,
kwa ajili ya khofu kwa Allah
na sasa anafanya kazi katika
kampuni inayoruhusu mazingira
ya Kiislamu.
Kulingana na msomi mkubwa
aitwae Sheikh Muhammad
Swaleh al-Uthaymeen, anatoa
taarifa ya Ucha Mungu.
Al-Muttaqun (Wachaji
Mungu) ni wale ambao
wanajilinda na adhabu ya Allah
kwa kufanya yale aliyoamrisha
Mwenyezi Mungu na kujiepusha
na yale aliyoyakataza.
Wenye bidii watapata njia
ya kufanikisha ndoto zao kwa
uwepesi kama wakimtegemea
Mungu (sio kumtegea). Vitu
unavyotaka kuwa navyo kama
kazi nzuri, nyumba nzuri,
gari zuri, mke mwema, utajiri
na mengineyo yanapatakana
kiurahisi iwapo utajiegemeza
kwenye uchaMungu.
Quran haikuacha hilo: Na
anayemwogopa [anayemcha]
Mwenyezi Mungu, (Mwenyezi
Mungu) humfanyia mambo yake
kuwa mepesi.[Q 65:4].
Hata njia yako kuelekea
peponi itafanywa rahisi na huu
ndio ufanisi mkubwa na wa
kweli.
Mafanikio kwa hivyo
yanafikiwa kwa daraja ya

kumtambua Mwenyezi Mungu


na kufuata maamrisho yake.
Ndoto zako zote zitatimia kama
unamtumaini yeye kupitia
ucha Mungu wako, na Yeye
atakusahilishia njia yako na hofu
na mashaka yote yatakuondoka
kichwani mwako.
Ili kujenga daraja kati ya
mafanikio na wewe, ucha
Mungu lazima uzingatiwe.
Kuwa mcha Mungu
kunamaanisha kuitafuta dini ya
haki, kujua maamrisho (halal na
ya haram) ya Mungu yaliyopo
katika maandiko matakatifu ya
hiyo dini ya kweli, na kuyafanyia
kazi. Kuna ambao wamepata
mafanikio bila ya kuwa wacha
Mungu. Haya mafanikio ya
kidunia hayatamsaidia akhera.
Je, kuna faida gani mtu
kuupata ulimwengu wote na
kuyapoteza maisha yake?
[Marko 8:36].
Balqis sasa ameolewa, na
amejaaliwa kupata watoto
wawili wa kiume. Wanandoa
hao walifurahi kumpa mtoto
wao wa kwanza jina la
Muhammad. Tarehe 30 Januari
2010, Nairobi, alizaliwa mtoto
mwingine. Balqis alibarikiwa
kuwa na mtoto wa pili, na siku
7 baada ya kujifungua, mtoto
akaitwa rasmi jina la Ahmad.
Balqis sio mpenzi pekee wa
Mtume Muhammad. Gazeti
la The Times linaripoti kuwa
Muhammad kwa sasa ni jina
la pili maarufu baada ya Jack
kwa kupewa watoto wa kiume
Uingereza na linatazamiwa
kushika namba moja ifikapo
mwanzoni mwa mwaka kesho,
uchunguzi wa The Times
umegundua.
Na Januari 2005, makala ya
The Guardian ilisema kwamba:
Huko Brussels, Mohammed
limekuwa jina maarufu zaidi
kwa watoto wote wanaozaliwa
kwa miaka minne iliyopita.
Pamoja na hilo, katika kitabu
Religion on the Rise, Hofmann
anasema: kwa miaka kadhaa
sasa, Muhammad limekuwa
jina linalopewa kwa watoto
wengi Ufaransa.
Bi. Balqis pamoja na kuwa
mwanataaluma, lakini pia
amesomea Kifaransa, Alliance
Francaise hapo Nairobi.
Alisoma Kifaransa kupitia
Alliance Franaise, Nairobi.
Vile vile, anayo shahada ya
CPA (K), ambayo inapatikana
kwa kufaulu sehemu sita zote
za mitihani hiyo ya wahasibu
wataalamu iliyo chini ya
usimamizi wa Bodi ya Wahasibu
Wataalamu wa Kenya na
Sekretarieti za Mitihani ya
Taifa (Kenya Accountants and
Secretaries National Examination
Board, KASNEB).
Makala kwa msaada wa
wordpress.
Barua pepe:
balqischepkwony@yahoo.
com. Makala inachapishwa
kwa mara ya pili kutokana na
maombi ya wasomaji wetu,
waliotuomba itolewe upya na
kwa ukamilifu baada ya kuwa
ya awali ilikatika.)

5/4/2016 3:27:17 PM

Makala

16
Na Bakari Mwakangwale

JUMANNE wiki iliyopita,


Watanzania walisherehekea
miaka 52 ya Muungano
baina ya mataifa mawili
Tanganyika na Zanzbar,
Muungano uliozaa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania,
mnamo April 26, 1964.
Kufuatia maadhimisho
hayo, wananchi wengi
walijadili hususani kupitia
mitandao mbalimbali ya
kijamii, wakiangalia zaidi
changamoto zinazoukabili
Muungano huo, utata wa
muungano huo pamoja na
uhalali wake huku wakihofia
mustakabali wake.
Mijadala hiyo ilitumia
zaidi maoni au hotuba za
aliyekuwa Mbunge wa Bunge
Maalum la Katiba, Mh. Tundu
Lisu, aliyeongea akichangia
juu ya suala la Muungano
katika Bunge hilo, mwaka
jana.
Suala la aina gani ya
Muungano, lilichukua
nafasi na mvutano mkubwa
katika Bunge la kutunga
Katiba mpya ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania,
ambapo mvutano mkubwa
ulikuwa ni aina gani ya
Muungano unaofaa kwa
pande zote mbili, Tanganyika
na Zanzibar, ili kuepusha
manunguniko.
Katika mitandao hiyo,
zinaonekana picha za video
(Clip) Mbuge huyo wa
Bunge maalum Mh. Lissu,
akiongelea suala hilo kwa
kina huku akirejea vitabu
mbalimbali na kuwanukuu
walio kuwa viongozi
waandamizi wa Serikali ya
Zanzibar na Tanganyika,
wakiulalamikia fumo wa
Muungano uliopo sasa.
Baadhi ya wachangiaji hao
wamesema, wakati umma
wa Tanzania ukisherekea
Muungano huo, kuna
maswali muhimu yaliulizwa
na Mh. Tundu Lissu,
ambayo ni ya msingi kwa
Watanganyika na Wazanzibar
kuyajua lakini mpaka Serikali
ya jakaya Kiwete, inaondoka
madarakani hayajajibiwa.
Walinukuu maswali
hayo ambayo wameyaita
kuwa ni ya msingi ni juu ya
Muungano kwamba, hati ya
Muungano ipo? , na kama
hati hiyo ipo, je ni halali?
Wamesema, Muungano
huo umekuwa ukikingiwa
kifua na Seriakli ya Tanzania
Bara, kila watu wanapoibuka
kuuhoji na hata kuwajibishwa
bila kujali nafasi ya mhusika

ANNUUR NEW.indd 16

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 6 - 12, 2016

Muungano

Mh. Tundu Lisu.

na kurejea na kutolea mfano


kwa aliyekuwa Rais wa
Zanzibar wakati huo Mzee
Alhaji Aboud Jumbe, ambaye
baada ya kuhoji alivuliwa
Urais.
Ni Mwalim Nyerere huyo
huyo ndiye alimwajibisha
Mzee Jumbe, kule Dodoma,
alipohoji kuhusu Muungano
na Nyerere huyo huyo
alinukuliwa akisema kuwa
ikiwa Wazanzibar wataona
kuwa Muungano hauwafai
bila ushawishi kutoka nje na
kuona Muungano unahasara
kwao hatowalazimisha.
Ameeleza mmoja wa
wachangiaji.
Katika mitandao hiyo
anaonekana Mh. Tundu Lissu,
akimnukuu aliyekuwa Rais
wa Zanzibar, Mzee Aboud
Jumbe, akilalamikia uhalali
wa Muungano huo akisema
kwamba yeye (Alhaj Jumbe)
alikuwa mjumbe wa Baraza la
Mapinduzi tokea kuanzishwa
kwake mwaka 1964,
mpaka mwaka 1984, lakini
ameshindwa kupata ushahidi
katika kumbukumbu zake
kukumbuka kama kulifanyika
kikao cha Baraza la
Mapinduzi ama Zanzibar au
Dar es Salaam, ili kuthibitisha
mkataba wa Muungano.
Mh. Mwenyekiti, hati za
makubaliano ya Muungano

AN-NUUR

hazikuthibitishwa na
Zanzibar, na kama hati hizo
zipo kweli, si halali kwa
sababu hazikuweza kupata
ridhaa ya wananchi wa
Zanzibar.
Lakini pia hizo siku
za kwanza za Muungano
ni kipindi muhimu kwa
wajumbe (wa Bunge la
Katiba) mkakielewa kwa
sababu mambo makubwa
yalitokea katika miezi
miwili ya kwanza baada ya
Muungano. Amesema Mh.
Lissu, akiwa Bungeni.
Mh. Lissu, akizunguzmia
zaidi Muungano huo,
katika Bunge la Katiba,
aliomba kuzungumzia zaidi
kile ambacho watu wengi
wamekiita Tanganyika
kuvaa joho la Tanzania na
Tanganyika kujigeuza kuwa
Jamhuri ya Muungano.
Mh. Lisu, alithibisha hilo
kwa kurejea kitabu cha Mzee
Pius Msekwa, aliyekuwa
Makamu Mwenyekiti wa
CCM na Spika wa Bunge la
Jamhuri la Muungano.
Alileza kuwa Mzee
Msekwa, ameandika kuwa
siku hiyo ya Muungano,
Apri 26, 1964, Mwl. Nyerere,
alitunga amri mbili siku hiyo
hiyo ya Muungano.
Alisema, amri ya kwanza
iliitwa Amri ya masharti ya

mpito ya mwaka 1964 kwa


amri hiyo iliwabadilisha
watumishi wote wa Serikali
ya Tanganyika na kuwafanya
kuwa watumishi wa Jamhuri
ya Muungano, kwenye
mambo ya Muungano
na kwenye mambo ya
Tanganyika.
Pili, alisema akinukuu
kwamba, amri hiyo
iliigeuza Mahakama Kuu ya
Tanganyika kuwa Mahakamu
Kuu ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania na sheria hiyo
iliigeuza nembo ya Taifa ya
Jamhuri ya Tanganyika (Bibi
na Bwana) iligeuzwa na kuwa
nembo ya Taifa ya Jamhuri ya
Muungano.
Siku hiyo hiyo pia
Mwalimu Nyerere, alitunga
amri nyingine inaitwa
Amri ya Katiba ya muda
amri hiyo ilisema kwamba,
Katiba ya Tanganyika ndio
itakuwa Katiba ya Jamhuri ya
Muungano.
Hii maana yake ni kwamba
Mwl. Nyerere na Serikali
ya Tanganyika, ilijiingiza
katika masuala ya Zanzibar
kwa kuifanya Katiba ya
Tanganyika kuwa katiba ya
Zanziba vile vile. Ameeleza
Mh. Lissu, akinukuu kitabu
hicho.
Kwa maana hiyo, Mh.
Lissu, alisema uhai wa
Tanganyika, ulitolewa
kwa njia hiyo ya amri, na
kwamba athari za jumla za
amri hizo ni kwamba eneo la
kisiasa ambalo ndio ilikuwa
Tanganyika, lilitolewa uhai
wake moja kwa moja kwa
amri hizo, na kwamba hiyo
ndio sababu pia hata jina
la kijiografia, lililojulikana
zamani kama Tanganyika,
ilibidi libadilishwe na kuwa
Tanzania Bara.
Zaidi Mh. Lissu, aliendelea
kurejea akisema kwamba
Mwaka 1968, Mwl. Nyerere,
alinukuliwa na gazeti moja
akizungumzia Muungano na
kusema maneno yafuatayo:
Iwapo umma wa Zanzibar,
bila ya ushawishi kutoka nje
kwa sababu zao wenyewe,
wakiona kuwa Muungano
una hasara kwa uhai
wao, sitowapiga mabomu
kulazimisha, Muungano
hautakuwa tena na sababu ya
kuendelea iwapo washiriki
wake wataamua kuukana.
Lakini cha ajabu pamoja
na maneno hayo, Mwaka
1984, Wazanzibar walipohoji
Muungano, kupitia kwa Rais
wao Alhaji Aboud Jumbe,
akafukuzwa kazi na kuwekwa
Mji Mwema, Kigamboni Jijini
Dar es Salaam, mpaka leo.

5/4/2016 3:27:18 PM

17

MAKALA

Udini-2
Na H. Hashim

NCHINI Tanzania kuna


wasioamini kuwa kuna
udini. Kuna wanaoamini
kuwa upo lakini, kwa
sababu mbali mbali,
hujifanya kutoamini. Kuna
wanaojitahidi kuaminisha
wengine kuwa hakuna
udini huku wenyewe
wakiwa wanauendekeza
na kuuendeleza. Baadhi
hujifanya wako mstari wa
mbele katika kupiga vita
udini, kumbe wako mbele
kuupigania. Aidha, katika
kuustawisha udini, baadhi
ya watu hutumia mbinu ya
kuwatuhumu, kuwashutumu
na kuwalaumu wengine kwa
udini. Pamoja na ukweli
huo, hakuna anayekubali
kuwa yeye ni mdini.
Kutoamini kwetu, au
kujifanya hatuamini, kuwa
Tanzania kuna udini ni
kikwazo katika mapambano
dhidi ya udini. Kama
alivyowahi kusema jemadari
mmoja, vita ni hadaa. Ukiwa
mbali unamfanya adui
aamini kuwa uko karibu na
ukiwa karibu unamfanya
aamini kuwa uko mbali.
Ukiwa na nguvu unamfanya
aamini kuwa wewe ni
dhaifu na ukiwa dhaifu
unamfanya aamini kuwa
una nguvu. Ukiwa tayari
kushambulia unamfanya
aamini kuwa huna hata wazo
la kumshambuli, na ukiwa
hujajiandaa unamfanya
aamini kuwa umejiandaa
vya kutosha kukabiliana
naye endapo atathubutu
kukushambulia.
Katika hali kama hiyo,
inawezekana kabisa
wapigania udini wakatufanya
tuamini kuwa wanapigana
dhidi ya udini, au kutufanya
tuendelee kuamini kuwa
Tanzania hakuna udini. Ili
kupambana na udini, ni
muhimu kutambua ukweli
kwamba udini upo licha
ya jitihada za baadhi ya
watu kutuamiisha kuwa
haupo. Aidha ni muhimu
kutofautisha dini na udini, na
muumini wa dini na mdini.
Katika kile kinachoitwa
mapambano dhidi ya
udini, kuna wengi ambao
kwa makusudi au kwa
bahati mbaya wamekuwa
wakipambana na dini badala
ya udini, na kupambana na
waumini wa dini badala ya
wadini. Wapo wengi ambao,
katika kile wanachokiita vita
dhidi ya udini, hawazingatii
ukweli kwamba hakuna
kundi kubwa la watu, kama

ANNUUR NEW.indd 17

AN-NUUR

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 6 - 12, 2016

Adui udini hajafahamika vizuri


ilivyo kwenye dini linalokosa
wahalifu, na ukweli kwamba
mhalifu ana kabila, dini,
chama cha siasa, eneo
anakotokoka na kadhalika.
Kwa kutozingatia ukweli huo,
wengi wanapomshughulikia
mhalifu hawamweki katika
kundi lake halisi la wahalifu
na badala yake humweka
katika makundi yake mengine
yenye watu tofauti na yeye
wasiohusiana na matendo
yake ya uhalifu.
Binafsi nimewahi
kulaumiwa vikali nikiitwa
mdini nikihusishwa na dini
ya Kiislamu inayodhaniwa
kuwa ni dini yangu kwa
sababu tu ya jina langu
la Halifa. Kilichofanya
nilaumiwe ni makala
niliyowahi kuandika nikihoji
sababu zinazowafanya
watu wanapomsifu
Marehemu Mwalimu
Nyerere kuwashutumu
Maraisi waliomfuatia hata
kama hakuna umuhimu wa
kufanya hivyo. Mtu mmoja
anayeheshimika katika
fani ya uandishi, Yusufu
Halimoja, aliandika makala
yalichapishwa katika gazeti la
Rai toleo namba 960 la tarehe
23.02.2012 yenye kichwa
cha habari Tutajuta kwa
kuukumbatia udini akijibu
makala yangu hayo.
Licha ya kujinasibisha kuwa
yeye ni mpiganaji dhidi ya
udini, katika makala yake
hayo alijidhihirisha kuwa
ni mdini. Alinilenga mimi
binafsi akinishutumu kwa
udini, uzushi na mwenye
chuki binafsi na baba wa
Taifa Mwalimu Julius
Nyerere na Raisi mstaafu
wa awamu ya tatu Benjamin
William Mkapa. Licha ya
kuwaaminisha watu kuwa
nawachukia Nyerere na
Mkapa, aliwaaminisha
pia kuwa kinachonifanya
niwachukie sio kingine
isipokuwa imani yao ya dini
yaani Ukristo. Kwa kufanya
hivyo, anawaaminisha pia
kuwa nawachukia Wakristo
na kuuchukia Ukristo
wenyewe.
Bila shaka hizo ni shutuma
nzito zinazohitaji uthibitisho
usio na chembe ya mashaka
kabla ya kuzitoa ili kuepuka
kuchochea udini badala ya
kuupiga vita. Kwa sababu
tu ya jina langu la Halifa,
ambalo kwa kawaida huitwa
Waislamu, anaelekeza kwa
Waislamu wote shutuma
ambazo licha ya kwamba sio
za kweli zinanihusu mimi
binafsi.
Binafsi simfahamu
Halimoja isipokuwa kupitia

maandishi yake na yeye


hanifahamu isipokuwa
kupitia maandishi yangu,
hivyo hakuwa na sababu
ya kunishutumu isipokuwa
kuhusisha maandishi yangu
na dini anayodhania kuwa
mimi ni muumini wake.
Naamini kuwa kikubwa
kilichomfanya aamini kuwa
mimi ni Muislamu ni jina
langu akiwa amesahau
kuwa hata yeye anaweza
kudhaniwa kuwa ni
Muislamu kwa sababu ya
jina lake la Yusufu ambalo
limezoeleka kwa Waislamu
zaidi kuliko kwa Wakristo
waliozoea kuliita Joseph.
Nikimnukuu,
ananishutumu kwa kusema:
Nilichogundua katika
makala yake (Halifa) ni udini.
Inamuumiza sana (Halifa)
kusikia huyu Raisi aliyekuwa
Mkristo analundikiwa sifa.
Sipendi udini, lakini naweza
kusema kwamba Waislamu
wengi humuandika Mwalimu
Nyerere kwa ubaya. Karibu
wote wanamwona kuwa
alikuwa mbaya wao.
Aliendelea kusema:
Niseme tu kwamba,
hata kama watu wengine
hawakubali kwamba udini
umeota mizizi Tanzania,
umeota mizizi. Na
wanaoendekeza udini ni
Waislamu.
Hizo nazo ni shutuma nzito
sana ambazo licha ya kuhitaji
uthibitisho usio na chembe ya
mashaka, zinahitaji pia busara
katika kuzieleza vinginevyo
ni shutuma zinazochochea
udini badala ya kupambana
nao.

Tufikirie kauli yake


hii: Waislamu wengi
humuandika Nyerere
kwa ubaya. Karibu wote
wanamwona kuwa alikuwa
mbaya wao.
Bila shaka anazungumzia
Waislamu wa Tanzania
ambao ni karibu nusu ya
Watanzania wote. Je, ni
wangapi miongoni mwao
ni waandishi? Ni wangapi
miongoni mwa hao waandishi
wamewahi kuandika habari
za Nyerere angalao mara
moja? Ni wangapi miongoni
mwa walioandika habari za
Nyerere wamemuandika kwa
ubaya? Je, hao waliomuandika
kwa ubaya miongoni
mwa waliomuandika ndio
wengi anaodai ni karibu
Waislamu wote? Mtu mmoja
anayedhaniwa kuwa ni
Muislamu akifanya baya
huhusishwa na Waislamu
wote bila hata kuthibitisha
kuwa ni Muislamu?
Ni muhimu pia kujiuliza.
Je, wanaomuandika Nyerere
kwa ubaya wamefanya hivyo
kwa sababu ya Uislamu
wao? Wamefanya hivyo
kwa kuwakilisha Waislamu
au Uislamu? Kumuandika
Nyerere kwa ubaya ni
udini? Hakuna Waislamu
wanaomuandika Nyerere
kwa uzuri? Hakuna Wakristo
wanaomuandika Nyerere
kwa ubaya? Wakristo
wanaomuandika kwa ubaya
hufanya hivyo kwa udini
upi? Nyerere ana nafasi gani
katika Ukristo kiasi ambacho,
kumsema yeye vibaya ni sawa
na kuusema Ukristo vibaya?

5/4/2016 3:27:22 PM

18

Makala

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 6 - 12, 2016

Tawhiid -9
Na Mussa Ame

Shukrani zote zinamstahikia


Allah (sw) na sala na salamu
zimfiie Mtume Muhammad
(saw), mtukufu wa daraja,
Masahaba wake na wote
wanaofuata mwenendo wake
mpaka siku ya malipo.
Somo la tisa katika mfululizo
wa masomo ya tawhiid ni
kuhusu nani aamrishe mema
na nani akataze maovu.
Kama tulivyoona katika somo
la nane, kuna haja kubwa
sana kuwalingania watu
wote hasa viongozi , kwani
wakitengenea viongozi, basi
umma utatengenea pia, na
wakiharibika wao basi umma
nao utaharibika. Huko akhera
tutakapokutana na Mola wetu,
viongozi watawalaumu sana
Mashekhe kwa kutowaonya, na
kuwaacha bila ya kuwalingania.
Kwa sababu hii Mtume (saw)
amesema:
Amesimulia Tamim bn
Aws(ra) amesema Mtume (saw)
Dini ni nasaha tukauliza kwa
nani? Akasema kwa Allah (sw)
na kitabu chake na Mtume (saw)
na viongozi wa Waislamu na
watu wote.( Sahihi Muslim55).
Amesimulia Abi Saidi Khudry
(ra) Amesimulia Mtume (saw)
Jihadi bora ni kusema neno
la uadilifu mbele ya mtawala
jeuri. (Sahihi Jamiu 1100).
Kuna jambo linajitokeza
katika nyakati hizi, watu kusoma
dini kwa malengo ya kubishana,
na kujionesha na kutumia
elimu vibaya kwa kuwatukana
Maulamaa na kuwafarakanisha
Waislamu pasipo na sababu za
msingi. Elimu yao ni kuchochea
farka na ugomvi. Elimu hii
haitomsaidia mtu duniani wala
akhera.
Amesimulia Jabir (ra) kutoka
kwa Mtume (saw) amesema:
Usijifundishe elimu ili
ushindane na wasomi, wala
kujionesha kwa wajinga.
Anayefanya hivyo atapata moto,
atapata moto.(Ibn Majah 256
ameisahihisha Ibn Hibaan 1/278).
Lengo la kusoma dini isiwe
kubishana na kutukana wasomi
wenzako. Jitahidi uelimishe kwa
kuwastahi Maulamaa wote, eleza
tofauti zao na makubaliano yao
na waache watu wachaguwe
hoja inayowafaa.
Wenye elimu ya dini
wamebeba dhima kubwa ya
kufikisha elimu waliyonayo.
Jamii iko katika kiza cha ujahili,
kwa hivyo wenye elimu watumie
elimu zao kusomesha darsa na
kuzitumia fursa zote za daawa
zilizopo. Wanafunzi katika
mashule walinganiane, usiche
kuwalingania majirani, ndugu
na walio karibu yako wote.

ANNUUR NEW.indd 18

MAHUJAJI wakiwa Makkah, Saudi Arabia.


Allah (sw) anasema:
Wamelaaniwa wale
waliokufuru katika wana wa
Israeli kwa ulimi wa Daud na
Issa mwana wa Maryam hayo
ni (sababu ya) uasi wao na
walikuwa wakichupa mipaka.
Walikuwa hawakatazani maovu
waliyokuwa wakiyafanya. Uovu
ulioje wa jambo hili walilokuwa
wakilifanya. (Maidah 78-79).
Amesimulia Abuu Bakar (ra),
hakika mimi nimemsikia Mtume
(saw) akisema:
Watu watapomuona
dhalimu wala wasimkanye,
basi yakaribia Allah (sw)
awaletea kutoka kwake adhabu
itakayowakumba wote. (Sahihi
Jamiu 1973 Sahihi IbnMajah
3236).
Amesimulia Hudhayfa
(ra) kutoka kwa Mtume(saw)
amesema:
Naapa kwa Yule ambaye
nafsi yangu iko katika mikono
yake, mtaamrisha mema
na mtakataza maovu, laa
sivyo, inakaribia Allah (sw)
atawaletea adhabu kutoka
kwake, kisha mumuombe
asiwajibu.(Ameisimulia
Tirmidhy na Albany
ameisahihisha Albani Sahihi
Targhyb2313).
Amesimulia Jaryr bn Abdillahi
(ra) nimemsikia Mtume (saw)
akisema:
Hakuna mtu atakayekuwa
katika kaumu ya watu
wanaofanya maasi, na anao
uwezo wa kuyaondosha maovu
hayo, na asiyaondoshe ila
atapatwa na adhabu kutoka
kwa Allah (sw) kabla hajafa.
(Ameipokea Ibn Hibaan ana
akaisahihisha Albani Sahihi
Targhyb 2316).
Hadithi hizo ni makemeo
kwa watu walio na elimu
lakini hawaelimishi umma.
Kwa hivyo wanaficha elimu
yao. Wako watu wanaona aibu
kujitangaza kuwa ni Muislamu
kwa kuogopa kukosa vyeo,
na kutiliwa mashaka. Wako
Waislamu wakiwa makazini
hawasali wanaogopa kuitwa
siasa kali. Waislamu wa aina hii
siyo tu kuwa hawana uwezo wa
kuwalingania watu wa imani

AN-NUUR

nyengine, lakini wao wenyewe


wanahitaji kupigwa msasa wa
daawa ili angalau wajiamini
nakutembea kifua mbele kwani
dini sahihi mbele ya Allah (sw)
ni Uislamu. Kila Muislamu
anayekutana na Mkiristo au na
mtu asiye na dini, ni jukumu
lake kumlingania kwa njia
nzuri ili aufahamu Uislamu,
ukiacha kuwalingania makafiri
watakulingania wao, huna
salama, lingania dini yako au
utalinganiwa wewe.
Kuna sehemu za mikoani
wako watu hata hawajui
kuwa kuna Uislamu, na
hawajatembelewa na mtu, mara
nyingi Mashekhe wako mjini,
hii si mbaya. Lakini kwa nini
hatupangi ratiba ya kutembelea
mashamba, tukaihubiri imani.
Kuna maeneo Waislamu hawajui
hata kutia udhu, hawajui sala
wala funga, lakini hata msikiti
hawana wanasali kwenye
mabanda, msahafu hawajauona,
mimi nahisi tunayo dhima kwa
watu hawa, watakuja kutudai
kesho akhera, kwa kutowafanyia
uadilifu.
Kuna vikundi ambavyo
wanawazuia watu wasitoe
mawaidha wala wasijiunge
na kamati za daawa pia
wanawakataza kujiunga na
taasisi za kidini. Hoja yao
kubwa ni kwamba haitakiwi
kutoa daawa mpaka uwe
Mwanachuoni.
Amesema Ibn Uthymin
Kuamrisha mema na kukataza
maovu ni katika sadaka bora
kama alivyosema Allah (sw)
katika suratul Aaali Imran -110
lakini hakuna budi katika suala
hili kuwe na sharti. Sharti ni
kuwa anayeamrisha mema na
kukataza maovu ni lazima awe
na elimu ya sheria, kama hana
elimu hiyo basi kwake si lazima
kwani Allah (sw) ameharamisha
kusema neno usilolijua (Aaarf
:33). Katika jambo baya ni
kusema mtu hili ni jambo jema
naye hajui kama jema au kusema
hili linakatazwa na hajui kuwa
linakatazwa(nukuu katika
hadithi ya Sahihi Muslim 720)
Wako waliofahamu kuwa
si ruhusa kulingania mpaka

uwe Mwanachuoni, maana


ya maneno haya ni kuwa ujue
kile unacholingania kuwa
ni haramu au halali, mfano
usije ukahalalisha haramu na
ukaharamisha halali, lakini
ikiwa unawaamrisha watu sala,
funga, hija unaamrisha mambo
mema na unakataza maovu ya
wazi hapo unahitaji kujua lile
unalosema tu, si lazima kujua
elimu nyengine. Allah (sw)
amelazimisha mtu kumlingania
mkewe na wanawe kwanza.
Mume si lazima awe Shekhe
ni kuwahimiza yale mema
na kuwakataza yale mambo
maovu ya dhahiri yasohitaji
elimu kubwa. Haina maana
kuwa mume asimkataze mkewe
kwenda uchi wala asimhimize
sala kwa sababu hajui aya na
hadithi. Inatosha tu kusema
Allah (sw) amekataza kwenda
uchi, jisitirini, Allah (sw)
ameamrisha sala twendeni
tukasalini.
Mtume (saw) amewaambia
Masahaba wafikishe japo aya
moja, maana yake ikiwa unaijua
aya moja tu, basi ifikishe hiyo
hiyo usisubiri kuwa Ulamaa.
Ukiwa shule jiunge katika
kikundi cha daawa na uamrishe
sala funga hija, na uwakataze
zinaa, kulewa, kuiba kuua, hayo
mambo yako wazi hayahitaji
elimu ya nahau wala balagha.
Ama kutoa fatwa, kutafsiri
msahafu, mambo hayo
tuwaachie Maulamaa.
Wanakubaliana Maulamaa
kuwa kuamrisha mema na
kukataza mabaya kuna daraja
mbali mbali. Daraja ya juu ni
kutoa fatwa, hii inawahusu
Maulamaa wakubwa,
kufundisha vitabu vya dini
inawahusu Mashekhe, ama
kuamrisha mema na kukataza
maovu ya wazi kazi hii
inamhusu kila Muislamu, kwani
ni ile aya moja aliyosema Mtume
(saw), mfano zina haramu
ulevi umekatazwa sala ni
fardhi wanawake jistirini
kiwango hichi kila Muislamu
anaweza.
Amesimulia Abii Saidi (ra)
amesema nilimsikia Mtume
(saw) akisema:
Atakayeona katika nyinyi
uovu, na auondoe kwa mkono
wake, kama hawezi aondoe kwa
mdomo wake, kama hawezi
achukie moyoni na huo ni
udhaifu wa imani. (Sahihi
Muslim 49).
Suala la kutumia mkono ni
wajibu wa Dola au mtu kwa
mkewe, lakini mdomo kila mtu
anao. Tuondoeni maovu kwa
midomo yetu, tusiwasubiri
Mashekhe.
Wabillahi tawfiiq.

5/4/2016 3:27:29 PM

19
M

Ukurasa wa Watoto

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 6 - 12, 2016

Uislamu ni usafi

Wiki iliyopita tulijifunza


juu ya Nguzo za
Uislamu. Tukamalizia
kwa kusema kuwa:
Maana ya Shahada
mbili ni kusema:
Nashuhudia kuwa
hapana mungu apasaye
kuabudiwa kwa haki ila
Allah.
Na ninashuhudia kuwa
Muhammad ni Mtume
wa Allah.
Na kwamba, Waislamu
walioshahadia kikweli,
hufuata yale yote
aliyowaamrisha Allah
(SW) na Mtume wake.
Pia hujiepusha na vitu
vyote alivyokataza
Allah (SW) na Mtume
wake.
Leo tutajifunza somo
jipya, nalo ni Akhlaq.
Akhlaq ni mwenendo
au tabia nzuri. Na
tutanza na usafi.
Uislamu ni Dini ya
usafi. Kila Muislamu
yampasa awe msafi.
Uislamu wa mtu
haukamiliki mpaka awe
msafi wa mwili, nguo,
mazingira na kubwa
zaidi msafi wa tabia.
ANNUUR NEW.indd 19

AN-NUUR

RAIS John Magufuli akiongoza kampeni ya usafi


Waislamu tunatakiwa
jijini Dar es Salaam.
tumuige Mtume wetu
Muhammad (s.a.w)
kwani alikuwa msafi wa
tabia, mwili na nguo.
Allah (s.w) akamsifu
katika Quran kwa
kusema:
Na bila shaka (ewe
Muhammad) una tabia
njema kabisa. (68:4)
Muislamu hawi
mchafu.
Muislamu hakai katika
nyumba chafu.
Muislamu husafisha
Ni muhimu kunawa mikono
nyumba yake
kwa maji safi na sabuni.
na mazingira
yanayoizunguka.
Muda wote, vyombo
vya nyumbani kwa
Waislamu ni visafi.
Vyombo vyao vya kulia
chakula huwa visafi.
Muislamu havai nguo
chafu.
Muislamu wa kweli ni
yule anayeiga tabia ya
Mtume (s.a.w).
Mtume alikuwa msafi.
Akatuambia kuwa
hataingia Peponi ila
yule aliye msafi.
Na usafi ni wa tabia,
mwili, nguo, mazingira
na kauli.
Wananchi wakisafisha mazingira yao.

5/4/2016 3:27:31 PM

AN-NUUR

20

MAKALA

20

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 6 - 12, 2016

Soma
gazeti
la 6 - 12, 2016
SHAABAN 1437,
IJUMAA MEI
AN-NUUR
KWA TSH 800/=
kila Ijumaa
AN-NUUR

Kutoka kibanda cha miti hadi Kituo Cha Elimu Sinza


Na Bakari Mwakangwale

HAIKUWA kazi rahisi


mpaka kufikia mafaniko
na muonekano wa Masjid
Nur Sinza, Palestina ya
Jijini Dar es Salaam, ambao
msingi wake ni Jumuiya ya
Waislamu wa Sinza, (The
Muslim Community Of
Sinza). Anasimulia Imamu
msaidizi wa Masjid Nur
Sinza Palestina, Msikiti
ulipo jirani na Hospitali
maarufu ya Sinza Palestina,
Sheikh Abdillah Omari
Malange, akielezea historia
ya Msikiti huo, ambao kwa
sasa ni kitovu cha Elimu kwa
jamii ya Waislamu.
Haikuwa kazi rahisi
kufikia hapa tulipo hivi sasa.
Tupo tuliokaa rumande
kwa kushitakiwa kuwa
tumeleta vurugu Msikitini.
Kesi zimeunguruma katika
Mahakama za mwanzo hadi
kufika Mahakama Kuu, yote
hayo yalijiri kutokana na
kutofautiana kifikra baina ya
Wazee na vijana wa Msikiti
huu (Nur). Anaeleza Imam
Malange.
Gharama nyingi za
kuwalipa mawakili na muda
mwingi wamepoteza kwa
kushughulikia migogoro
ya Msikiti na hatimae
kwa Tawfiq ya Allah (s.w)
anasema Imam Malange,
kwamba wameweza kuihimili
hali hiyo na kuondoka
katika wimbi la migogoro na
kuwa katika mafanikio kwa
Waislamu kupitia Msikiti wao
(Masjid Nur).
Masjid Nuru, sasa imekuwa
NURU kwa jamii na umma
wa Kiislamu ndani ya Jiji
la Dar es Salaam na nje pia,
hali hiyo unaweza kusema
ni matunda ya maamuzi
magumu kupitia mgogoro wa
kihistoria uliowahi kuibuka
Msikitini hapo na kupelekea

Waislamu katika kundi la


vijana (Wanaharakati) kulala
rumande kwa kuupigania
Msikiti huo kuwa kituo
cha Elimu kwa misingi ya
Uislamu.
Imam Malange, anasema
utakuwa haujautendea haki
Msikiti huo utakapouelezea
historia yake kama hujagusia
mgogoro huo ambao ulibuka
mwaka 2002, na kuzua
taharuki Sinza na Jiji kwa
ujumla, kwani Waislamu
waliamua kushughulika,
wenyewe baada ya kuona
hawatendewi haki.
Kwa mujibu wa Imamu
Malange, anasema katika
mgogoro wa muda mrefu
wa pande mbili zilizokuwa
zinakinzana kifikra, walijikuta
wametumiwa kikosi maalum
cha wahuni waliofika
Msikitini hapo majira ya
saa mbili usiku wakiwa
na mapanga, marungu na
nondo wakidai kwamba
wametumwa kuwaadabisha
vijana wa Msikiti wa Sinza, na
kusababisha virugu kubwa na
kuharibu Msikiti.
Anakumbuka kuwa wakati
huo, Shkh Juma Mbukuzi,
akiwa Amir wa Shura ya
Maimam, alitinga Msikitini
hapo, mapema siku iliyofuatia
kushuhudia uharibifu
uliofanywa na wahuni hao,
akiwa na Waislamu katika
gari (Kosta) nne zilizo jaa
Waislamu (Wanaharakati)
lakini mpaka muda huo
hapakuwa na Polisi waliofika
au kukamatwa mtu yoyote
kuhusika katika vurugu na
uharibifu huo.
Kwa Amir Mbukuzi,
alitoa masikitiko yake kwa
Serikali kwa kulifumbia
macho tukio hilo lililokuwa
limetokea usiku, na kuhoji
inakuwaje hakuna mtu
yeyote aliyekamatwa wala
Polisi kufika katika tukio na
kuwashughulikia wahuni

MASJID Nuur Sinza Palestina, Dar es Salaam.


hao waliofanya uharibifu
Msikitini hapo na kujeruhi
baadhi ya Waislamu.
Baada ya hotuba fupi ya
Amir Mbukuzi, Waislamu
waliokusanyika Msikitini
hapo, walishindwa kuvumilia
dhulma hiyo hivyo
waligawana mitaa, na kuingia
mtaa kwa mtaa kuwasaka
wahuni hao waliotumwa
kufanya vurugu Msikitini.
Sinza yote siku hiyo
ilijulikana kuwa kuna
Waislamu wanashughulika
hapakuwa na maneno mengi
zaidi ya vitendo mpaka
Serikali nayo ilijua kuwa
Sinza hakukaliki, Waislamu
wanalipa kisasi. Hata hivyo
baada ya operesheni hiyo
usiku wake tulikamatwa
viongozi wanane na kuwekwa
rumande katika Gereza la
Keko, Jijini Dar es Salaam,
baada ya dhamana yetu
kuzuiwa. Anasema Imam
Malange.
Tukio hilo na hali ilivyo
sasa kwa ujumla ndani
ya ardhi ya Masjid Nur,
yanabeba historia nzima ya
Jumuiya ya Waislamu Sinza
Palestina inayo kumbukwa
kuanzia Julai 8, 1983, japo

uhai wa eneo hilo ulikuwepo


nyuma ya hapo, lakini kwa
mwaka huo ndio ilitambuliwa
rasmi kisheria kwa kupata
usajili wake.
Jumuiya hiyo ilipata usajili
huo ikiwa chini ya uongozi
wa kuteuwana miongoni
mwa viongozi hao ni AlMaruhum Sheikh Said Hamisi
Mituro aliyefari mwaka 2012,
Shekh Yusuph Mwinyihindi,
pamoja na Abdallah
Mohammed Hamisi.
Katika ardhi hiyo ya
Jumuiya ya Waislamu wa
Sinza, palikuwa na Msikiti,
mdogo wa matope, ambao
Imam Malenge, aliukuta
katika miaka hiyo ya 1980s,
akiwa kama mwanafuzi wa
Madrasa, ilikuwa nyumbani
kwa Sheikh Said Hamisi
Mituro, jirani na Msikiti huo.
Sina kumbukumbu nzuri
juu ya Msikiti huo nyuma
ya miaka hiyo ya 1980,
isipokuwa inaelezwa kuwa
ni Waislamu wa kipindi
hicho wa maeneo hayo,
waliokuwepo nyuma ya
miaka hiyo kama vile AlMaruhum Mzee Diwani,
Mzee Duchi, na wengineo,
Inaendelea Uk. 14

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Ltd, Dar es Salaam.
ANNUUR NEW.indd 20

5/4/2016 3:27:36 PM

Вам также может понравиться

  • Bwana Okoa Ndoa Yangu
    Bwana Okoa Ndoa Yangu
    От Everand
    Bwana Okoa Ndoa Yangu
    Оценок пока нет
  • Annuur 1232 PDF
    Annuur 1232 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1232 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Dini ya Fedha
    Dini ya Fedha
    От Everand
    Dini ya Fedha
    Оценок пока нет
  • Annuur 1214
    Annuur 1214
    Документ20 страниц
    Annuur 1214
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Fiqhi ya ‘Ibada yenye picha zilizochorwa
    Fiqhi ya ‘Ibada yenye picha zilizochorwa
    От Everand
    Fiqhi ya ‘Ibada yenye picha zilizochorwa
    Оценок пока нет
  • Annuur 1230 PDF
    Annuur 1230 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1230 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Imani Ya Mtu Wingine
    Imani Ya Mtu Wingine
    От Everand
    Imani Ya Mtu Wingine
    Оценок пока нет
  • Annuur 1231 PDF
    Annuur 1231 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1231 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • A BOOK OF DIVINE BLESSINGS - Entering into the Best Things God has ordained for you in this life - SWAHILI EDITION: School of the Holy Spirit Series 3 of 12, Stage 1 of 3
    A BOOK OF DIVINE BLESSINGS - Entering into the Best Things God has ordained for you in this life - SWAHILI EDITION: School of the Holy Spirit Series 3 of 12, Stage 1 of 3
    От Everand
    A BOOK OF DIVINE BLESSINGS - Entering into the Best Things God has ordained for you in this life - SWAHILI EDITION: School of the Holy Spirit Series 3 of 12, Stage 1 of 3
    Оценок пока нет
  • Annuur 1144
    Annuur 1144
    Документ16 страниц
    Annuur 1144
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Eneza Huduma Yako Kwa Miujiza na Udhihirishaji wa Roho Mtakatifu
    Eneza Huduma Yako Kwa Miujiza na Udhihirishaji wa Roho Mtakatifu
    От Everand
    Eneza Huduma Yako Kwa Miujiza na Udhihirishaji wa Roho Mtakatifu
    Рейтинг: 3.5 из 5 звезд
    3.5/5 (2)
  • Annuur 1219
    Annuur 1219
    Документ20 страниц
    Annuur 1219
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Mti Na Huduma Yako
    Mti Na Huduma Yako
    От Everand
    Mti Na Huduma Yako
    Рейтинг: 2.5 из 5 звезд
    2.5/5 (2)
  • ANNUUR 1209aaa
    ANNUUR 1209aaa
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1209aaa
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Historia & Maisha ya Yeshua Kristo
    Historia & Maisha ya Yeshua Kristo
    От Everand
    Historia & Maisha ya Yeshua Kristo
    Оценок пока нет
  • Annuur 1213 PDF
    Annuur 1213 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1213 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Sayansi ya Kupata utajiri
    Sayansi ya Kupata utajiri
    От Everand
    Sayansi ya Kupata utajiri
    Рейтинг: 5 из 5 звезд
    5/5 (1)
  • Annuur 1182
    Annuur 1182
    Документ20 страниц
    Annuur 1182
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • HAYAAN, The Long Journey of the Nomad Boy
    HAYAAN, The Long Journey of the Nomad Boy
    От Everand
    HAYAAN, The Long Journey of the Nomad Boy
    Рейтинг: 5 из 5 звезд
    5/5 (2)
  • Annuur 1227 PDF
    Annuur 1227 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1227 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Laikos: Watenda Kazi wa Kawaida na Huduma
    Laikos: Watenda Kazi wa Kawaida na Huduma
    От Everand
    Laikos: Watenda Kazi wa Kawaida na Huduma
    Оценок пока нет
  • Annuur 1262
    Annuur 1262
    Документ20 страниц
    Annuur 1262
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Kufikirika
    Kufikirika
    От Everand
    Kufikirika
    Оценок пока нет
  • Annuur 1226 PDF
    Annuur 1226 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1226 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1181 PDF
    Annuur 1181 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1181 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1076
    Annuur 1076
    Документ12 страниц
    Annuur 1076
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • Annuur 1082
    Annuur 1082
    Документ16 страниц
    Annuur 1082
    MZALENDO.NET
    100% (1)
  • Annuur 1218 PDF
    Annuur 1218 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1218 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1208
    Annuur 1208
    Документ20 страниц
    Annuur 1208
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1217
    Annuur 1217
    Документ20 страниц
    Annuur 1217
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1223
    Annuur 1223
    Документ20 страниц
    Annuur 1223
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1195
    Annuur 1195
    Документ20 страниц
    Annuur 1195
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1112
    Annuur 1112
    Документ16 страниц
    Annuur 1112
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1210a
    Annuur 1210a
    Документ20 страниц
    Annuur 1210a
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • An Nuur 1132xx
    An Nuur 1132xx
    Документ16 страниц
    An Nuur 1132xx
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1204
    Annuur 1204
    Документ20 страниц
    Annuur 1204
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • ANNUUR1004
    ANNUUR1004
    Документ16 страниц
    ANNUUR1004
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1176b PDF
    ANNUUR 1176b PDF
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1176b PDF
    annurtanzania
    Оценок пока нет
  • An Nuur 1128
    An Nuur 1128
    Документ16 страниц
    An Nuur 1128
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1183 PDF
    Annuur 1183 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1183 PDF
    annurtanzania
    100% (2)
  • Hotuba Idd Fitr 2018 Final
    Hotuba Idd Fitr 2018 Final
    Документ22 страницы
    Hotuba Idd Fitr 2018 Final
    Mohammed Said
    Оценок пока нет
  • Annuur 1201
    Annuur 1201
    Документ20 страниц
    Annuur 1201
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1115
    Annuur 1115
    Документ16 страниц
    Annuur 1115
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annur Februari 24-Machi 1, 2012
    Annur Februari 24-Machi 1, 2012
    Документ16 страниц
    Annur Februari 24-Machi 1, 2012
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • Gazeti La Annur
    Gazeti La Annur
    Документ12 страниц
    Gazeti La Annur
    Hassan Mussa Khamis
    Оценок пока нет
  • Annuur 1220
    Annuur 1220
    Документ20 страниц
    Annuur 1220
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1180 PDF
    Annuur 1180 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1180 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1178
    Annuur 1178
    Документ20 страниц
    Annuur 1178
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Hotuba Ya Mapinduzi Miaka 54
    Hotuba Ya Mapinduzi Miaka 54
    Документ20 страниц
    Hotuba Ya Mapinduzi Miaka 54
    khalfan said
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1167a PDF
    ANNUUR 1167a PDF
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1167a PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1078
    Annuur 1078
    Документ12 страниц
    Annuur 1078
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • Annuur 1030
    Annuur 1030
    Документ16 страниц
    Annuur 1030
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • Annuur 1207...
    Annuur 1207...
    Документ20 страниц
    Annuur 1207...
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1229 PDF
    Annuur 1229 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1229 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1063
    Annuur 1063
    Документ16 страниц
    Annuur 1063
    Hassan Mussa Khamis
    Оценок пока нет
  • Hotuba Ya January Makamba
    Hotuba Ya January Makamba
    Документ27 страниц
    Hotuba Ya January Makamba
    Audra Love
    Оценок пока нет
  • Annuur 1262
    Annuur 1262
    Документ20 страниц
    Annuur 1262
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1264
    Annuur 1264
    Документ20 страниц
    Annuur 1264
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1229 PDF
    Annuur 1229 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1229 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1226 PDF
    Annuur 1226 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1226 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1228d
    ANNUUR 1228d
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1228d
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1224
    Annuur 1224
    Документ20 страниц
    Annuur 1224
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1225
    Annuur 1225
    Документ20 страниц
    Annuur 1225
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1227 PDF
    Annuur 1227 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1227 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1220
    Annuur 1220
    Документ20 страниц
    Annuur 1220
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1207...
    Annuur 1207...
    Документ20 страниц
    Annuur 1207...
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1219
    Annuur 1219
    Документ20 страниц
    Annuur 1219
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1223
    Annuur 1223
    Документ20 страниц
    Annuur 1223
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1218 PDF
    Annuur 1218 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1218 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1216d
    ANNUUR 1216d
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1216d
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1217
    Annuur 1217
    Документ20 страниц
    Annuur 1217
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1213 PDF
    Annuur 1213 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1213 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1210a
    Annuur 1210a
    Документ20 страниц
    Annuur 1210a
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1209aaa
    ANNUUR 1209aaa
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1209aaa
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1208
    Annuur 1208
    Документ20 страниц
    Annuur 1208
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1195
    Annuur 1195
    Документ20 страниц
    Annuur 1195
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1204
    Annuur 1204
    Документ20 страниц
    Annuur 1204
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1201
    Annuur 1201
    Документ20 страниц
    Annuur 1201
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1202
    Annuur 1202
    Документ20 страниц
    Annuur 1202
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1200
    Annuur 1200
    Документ20 страниц
    Annuur 1200
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет