Вы находитесь на странице: 1из 20

www.annuurpapers.co.tz au facebook:annuurpapers@yahoo.

com

AHLU SUNNA WAL JAMAA HAJJ AND UMRA TRUST


(9) HIJJA NI FURSA YA KIPEKEE!

Sauti ya Waislamu

ISSN 0856 - 3861 Na. 1230 SHAABAN 1437, IJUMAA , MEI 20-26, 2016 BEI TShs 800/=, Kshs 50/=

Mtume(saw) amesema, "Husamehewa


mwenye kuhiji na anaowaombea". Hakuna
katika ibada nyengine yoyote uhakika huu
wa Muislamu kukubaliwa maombi yake na
kupata fursa ya kuwaombea wengine, kisha
kukubaliwa, ila katika Hijja! Gharama zote
kwa Hijja 2016/1437 ni Dola 4,600. Umra
ya Ramadhani ni Dola 2,700. Karibuni Ahlu
Sunna wal Jamaa kwa huduma nzuri na
uongozi bora. Wasiliana nasi: Tanzania Bara:
0679895770/ 0688895777; 0765462022;
0712735363. Zanzibar: 0777468018;
0777458075; 0777845010; 0777497300.

Masheikh wapata watetezi


Maftaha ahoji ugaidi wao nini!
Zitto, Riziki, Mbowe wataka Tume

Fanyeni kazi kabla hamjalazwa hapa


Ilunga miaka miwili, Msenguzi kafuatia

Bi. Mkubwa
mahakamani
SHEIKH Msellem Ali.

Tuhuma ugaidi wa kimeta


Masheikh wawili watoweka
Huenda wameuliwa na ATPU

PICHA juu wanafunzi wa Ubungo Islamic High School wakiwa katika somo la
kuswalia maiti. Chini Maiti ya Ustadh Juma Mustapha Msenguzi ikipelekwa
makaburini kwa maziko. Soma Uk. 10

BI. Nuseiba Mohammed Haji akiwa kizimbani katika


mahakama ya Milimani (Milimani Law Courts),
Nairobi, Jumanne (Mei 10, 2016) wiki iliyopita. Uk.4

AN-NUUR

Mafundisho ya Qur'an/Uwanja wa Maarifa

Suratu An-faal:45

Allah. Ukelele huu ni


muhimu kwa sababu
waathiri taathira hasi
juu ya morali wa
maadui na unaongeza
morali wa upande wa
Waislamu. Hii ni kwa
sababu anatia kwao
waumini shauku na
hamasa. Pindi kukiwa
kule kusema kwetu leo
Allah, Allah kwa ncha
ya ulimi kunachemsha
kwetu hamasa na hofu
Fethullah-Gulen
katika safu za maadui
zetu, ni jambo
la dhana mambo ya
ENYI wale ambao
kwa hivyo lile ambalo
mmeamini, pindi
mnapokutana na kundi unaliweza utazowenye
kuvuma kutoka katika
la maadui, kuweni
imara na mkumbukeni vina vya nyoyo na ni
jambo ambalo anaweza
mwenyezi mungu
kulichuma binadamu.
kwa msingi ili mpate
Pindi
kufaulu [al-anfaal 45]
tutakapokwenda
Kunawezekana
kwenye maudhui
kuyafahamu mambo
ya kwamba ushindi
yafuatayo katika
unafungamana na
kumtaja Mwenyezi
kumtaja Mwenyezi
Mungu.
Mungu na kwa
Panaashiriwa katika
aya hii kwamba kwenye kuthibiti hayo, ni
maudhui muhimu.
moyo kunapasa
Kunapasa kusimama
kusivuke mpaka
mbele zake kwa juhudi
juu yake kughalika
zote. Kwa msingi huo,
milele katika maisha
kuna mambo ya maisha
ya kawaida na ya kila
ambayo yanatuka juu
siku na hapana mfano
ya mabega ya waumini,
wakati ya kuingia
wenye kukutana na
katika mambano na
maadui nayo ni haya:
maadui. Kunapasa
Katika hali ya kuingia
kuwazindua wenye
katika
makabiliano
nyoyo zilizoghalika,
yoyote
ya kivita
kwenye jambo hili kati
ya muda na mwingine, vyovyote vitakavyo
kuwa, kunapata
kwa hiyo muumini,
atazindukana kwenye
kuinyanyua hali ya
kumtaja Bwana wake
kimorali ya kundi
ambaye anapigana
letu kwa kudhihirisha
njia yake kwa moyo
subira, na ujasiri na
wake na alimi wake na
kuthibiti azma. Kisha
panageuka pale mahali kudhihirisha ujasiri
ambapo wanakufa
na ukakamavu ndani
ndani yake watu na
ya uwezo wa akili ili
wanauliwa kuwa
kuzusha mtikisiko wa
mahali patakatifu na
nafsi na kuyumba na
mahali pa kufanyia
kutawanyika katika
ibada.
upande wa maadui.
Kumtajia Mwenyezi
Kumtaja Mwenyezi
Mungu wakati huu,
Mungu
kwa wingi sana
ni ukelele wenye
ili
kuimarisha
hali yetu
kurudiwa rudiwa
ya
kiroho
na
kimorali
katika vita Allah, Allah,

na kuupa nguvu na
kuutikisa upande
wa pili kwa sura ya
kutojali ambayo iko
kwetu wakati wa kufa
na kuzifunga harakati
na utulivu wetu kwa
mapigo ya nyoyo zetu
zenye kuungana na
Mwenyezi Mungu.
La kuzingatiwa
hapa ni kuwa mambo
yote hayo ni funguo
muhimu za ushindi.
Kutokuwa hivyo, na
kukosekana subira
na umadhubuti,
hakuwezekani kukia
kwenye mafanikio
(kufuatana na kanuni
za Mwenyezi Mungu)
kama ambavyo
hakuwezekani
kupata ushindi katika
vita katika hali ya
kughalika na kumtaja
Mwenyezi Mungu.
Hata kama linapatikana
hilo, hakutapatikana
kupata malipo, maana
hakuna kufuzu katika
akhera na kwenye
kupatikana haki ya
mifano ya watu kama
hawa.
Kwa msingi huu
ni juu ya wale ambao
wanapigana na
wanafanya jihadi katika
dini ya Mwenyezi
Mungu kuthibiti kwa
azma yote kwa upande
na kuelekea kwenye
kumtaja Mwenyezi
Mungu. Kwa upande
mwingine wajiepushe
kutegemea nguvu
na uwezo mwingine.
Hata pale ambapo
wanakuwa na uwezo
na nguvu nyingi, bado
wamtaje Mwenyezi
Mungu na wategemee
uwezo na nguvu zake
na warudie rudie dua
ifuatayo:
Ee Mola wa haki
tumejiepusha na uwezo
wetu na nguvu zetu na
tumetegemea kwenye
uwezo wako na nguvu
zako.

Mwandamo wa mwezi
Leo ni Tarehe 13 Shaaban mwaka 1437 AH, sawa na tarehe 20 May,
2016. Tarehe 6 June tunategemea kuangalia mwezi kwa Ramadhan na
Tarehe 7 June 2016 tukijaaliwa tutaanza Ramadhan Rasmi. Kutokea
hii leo Ijumaa ya tarehe 20 May 2016 hadi kuka kuanza mfungo wa
Ramadhani tumebakisha siku 17.

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 20 - 26, 2016

UWANJA WA VIJANA-JIONGEZEE MAARIFA


JAWABU CHEMSHA BONGO NAMBA:50
D

14:

2
H

42

555

224

85:

9
Q

47:
1

3:2

6:5

14:

2
L

MASAUALA
1. Sura ipi na aya ya ngapi isemayo Ambaye anao ufalme wa mbingu na ardhi; na
Mwenyezi Mungu ni shaahidi wa kila kitu. Jawabu: 85:9
2. Sura ipi na aya ya ngapi isemayo Walio kufuru na wakazuilia njia ya Mwenyezi
Mungu, Yeye atavipotoa vitendo vyao. Jawabu: 47:1
3. Sura ipi na aya ya ngapi isemayo Na Shet'ani atasema itapo katwa hukumu:
Hakika Mwenyezi Mungu alikuahidini ahadi ya kweli. Nami nalikuahidini; lakini
sikukutimizieni. Na sikuwa na mamlaka juu yenu, isipo kuwa nilikuiteni, nanyi
mkaniitikia. Basi msinilaumu mimi, bali jilaumuni wenyewe. Mimi siwezi kuwa
mtetezi wenu, wala nyinyi hamwezi kuwa watetezi wangu. Hakika mimi nilikataa
tangu zamani kunishirikisha na Mwenyezi Mungu. Hakika madhaalimu watakuwa na
adhabu chungu. Jawabu: 14:2
4. Mtume yupi aliotumwa kuwa Rehma kwa Ulimwengu, Issa, Mussa Muhammad
(SAW)? Jawabu: Muhamas (SAW)
5. Taja jina la Mtume aliozaliwa kimiujiza pale mama yake hakukutana na
mwanamume? Mussa, Issa, Nuh. Jawabu: Issa
6. Ashabul Kahf-Watu wa pangoni walifwatana na mnyama gani? Jawabu: Mbwa
7. Lini Uislamu ulianza? Wakati wa Mtume Nuh, Adam, Ebrahim? Jawabu: Adam
8. Kalenda ya Kiislamu huitwa kwa jina gani? Jawabu: Hijrah
9. Mwezi upi ulio katikati baina ya Rajab na Ramadhani? Jawabu: Shaaban
10. Itaje Miezi 4 Mitukufu iliotajwa katika Quran. Jawabu: Dhul Qada, Dhul Hijja,
Muharram, Rajab

CHEMSHA BONGO: 51

Weka duara kwenye jawabu ilio sawa. Jawabu kamili wiki ijayo.
U

38:30

185

12

8:26

7:7

114:5

76:14

MASAUALA
1. Itaje suara na Aya ya ngapi Na Daudi tukamtunukia Suleiman. Alikuwa mja
mwema. Na hakika alikuwa mwingi wa kutubia.
2. Itaje Sura na Aya ya ngapi? Na vivuli vyake vitakuwa karibu yao, na mashada
ya matunda yataning'inia mpaka chini.
3. Itaje Sura na Aya ya ngapi? Na vivuli vyake vitakuwa karibu yao, na mashada
ya matunda yataning'inia mpaka chini.
4. Malaika yupi akitumwa Wahyi kwa Mitume?
5. Malaika anayotoa roho?
6. Malaika yupi atakayowauliza waliokufa kwenye Makaburi yao?
7. Hawali, hawanywi wala hawamuasi Mwenye-enzi-Mungu ni wenye kufwata
amri tu na kutekeleza nani hao?
8. Ipi nyumba ya Mungu?
9. Mitume wakitumiwa kitu gani?
10. Kuhani yupi katika nchi ya Syria alipomuwana Mtume (SAW) alimtambua kuwa
ndio aliotajwa katika vitabu vilivyopita kuwa ndio Mtume aliobashiriwa?

Jee Unajua?

1. Nchi ya Indonesia ndio nchi ya Kisiwa yenye watu wengi, ina watu wakao
239,259,710: http://www.mapsofworld.com/world-top-ten/world-top-ten-mostpopulated-island-countries-map.html
2. Wakazi wa nchi ya Libya ndio ambao wenye kutoa talaka kwa kiwango cha chini
kabisa wakifwatiwa na Georgia, Mongolia, Armenia: http://www.mapsofworld.com//
world-top-ten/countries-with-lowest-divorce-rate.html
3. Nchi ya Sri Lanka inaongoza kuwa na Sheria zilizo mchafukoge: http://www.
thetoptens.com/countries-with-worst-laws/
4. Nchi ya Eretria ni moja kati ya nchi zenye kuongoza kwa rushwa duniani: http://
www.cheatsheet.com/business/7-most-corrupt-countries.html/?a=viewall
5. Nchi ya Sierra Leon ndio nchi inaongoza kuwa na huduma duni za kifaya duniani:
http://www.therichest.com/rich-list/poorest-list/the-10-worst-health-care-systems-inthe-world/?view=all
6. Kati ya nchi Tajiri duniani nchi ya Ireland ndio yenye Wauguzi (Manasi)i wengi:
http://www.theguardian.com/society/2016/feb/09/which-country-has-worlds-besthealthcare-system-this-is-the-nhs
7. Nchi ya Uholanzi inaongoza kwa watu wake kuwa na Baskeli nyingi watu kama
16, 625,800 wanaendesha Baskeli na zikikuweko kama Baskeli milioni 16 na ushweya
na waendeshaji baskeli ni wengi sana: http://top10hell.com/top-10-countries-withmost-bicycles-per-capita/
8. Nchi ya Poland inasemekana kuwa na watembea kwa miguu wengi wanaopata
ajali: http://top10hell.com/top-10-countries-with-most-bicycles-per-capita/
9. Katika kila watu laki mmoja watu 31 hujiuwa katika nchi ya Lithuania: http://
www.therichest.com/rich-list/the-biggest/10-countries-with-the-highest-suicide-ratesin-the-world/?view=all
10. Kati ya nchi zinazoongoza kwa watu wasiojua kuandika na kusoma ni Sudan ya
Kusini, Bukina Fasso: http://www.countryranker.com/top-10-countries-with-highestilliteracy-rate-in-the-world/
(Kutokana na kutokuwa na wasomaji wengi katika Ukumbi wa Uwanja wa
Maarifa na kutopata majibu ya kuuboresha huu wa Uwanja wa Maarifa, tunakiria
kuanzisha ukumbi mwengine, tuma barua pepe zuwarde@gmail.com au ujumbe
mfupi kupitia simu 0777436949 unahisi kipi kiwe mbadala wake?)

Habari

AN-NUUR

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 20 - 26, 2016

Masheikh wapata watetezi


Na Bakari Mwakangwale

MBUNGE wa Kigoma Mjini,


Mh. Zitto Kabwe, ametaka
iundwe Tume huru itakayo
baini ukweli wa madai ya
kudhalilishwa Masheikh
waliopo katika Gereza la
Segerea Jijini Dar es Salaam.
Mh. Zitto ametoa hoja hiyo
mapema wiki hii Bungeni Mjini
Dodoma, kufuatia Naibu Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi
Mh. Masauni, kutoa taarifa
inayodai kwamba Masheikh
hao hawakufanyiwa vitendo
vyovyote vya udhalilishaji.
Mh. Zitto alisema ni vyema
iundwe tume, ambayo sio
Commission ya Bunge bali iwe
ni Commission ya experts, kama
watu wa Haki za Binadam,
ili ukweli uweze kufahamika

na kwamba endapo jambo


hilo likiachwa bila kutolewa
ufafanuzi ukweli ni kwamba nchi
hii haitobaki salama.
Kwa hiyo nilikuwa naomba
utumie busara zako uagize
iundwe Independent Commission
(Tume Huru) kwa ajili ya
kufanya verication ya ripoti ya
madaktari kwa ajili ya kwenda
Gerezani (Segerea) na kuwahoji
Masheikh hao waliolalamika
na ripoti hiyo iweze kuletwa
Bungeni ukweli ubainike.
Alisema Mh. Kabwe.
Awali Mh. Kabwe, aliliomba
Bunge liruhusu uchunguzi huru
(Independent Verication) juu
ya ripoti ya Madaktari, ambayo
Serikali kupitia Waziri wake
wa Mambo ya Ndani ya Nchi
iliwasilishwa katika Bunge hilo.
Alisema, jambo hilo si dogo,

Ujumbe wa Ramadhan Quiz


Na Bakari Mwakangwale

WANAFUNZI wa Kiislamu
wametakiwa kujijengea
utamaduni wa kujisomea
vitabu mbalimbali ili
kujiongezea ufahamu, maarifa
na ubunifu kwani Uislamu ni
Dini ya kusoma.
Wito huo umetolewa na
Ustadhi Yassir Masoud,
akiongea na wanafunzi wa
Kiislamu katika ufunguzi wa
mashindano ya Ramadhani Quiz
Compitation 2016, uliofanyika
Jumapili ya wiki iliyopita
katika Msikiti wa Kichangani
Magomeni, Jijini Dar es Salaam.
Ust. Yassir, alisema kwa
ujumla Dini ya Kiislamu
imebeba amri na mafundisho
mengi kuhusu kusoma,
miongoni mwa mahimizo
katika Qur an ni pale Allah (sw)
aliposema hawafanani wale
waliosoma na wale wasiosoma.
Na ndio maana amri ya
kwanza aliyoshushiwa Mtume
(s a.w) ni kusoma na utamaduni
wa kusoma upo katika jamii ya
Kiislamu. Kwa maana hiyo ni
vyema mkajenga utamaduni wa
kusoma vitabu mbalimbali ili
kujiongezea maarifa na ufahamu
na kuweza kujifunza kutoka
kwa watu wengine, ni vyema
mkafahamu Uislamu ni Dini ya
kusoma. Alisema Ust. Yassir.
Alisema, Ust. Yassir kwamba
cha kusikitisha ukifatilia kwa
undani utabaini kuwa Umma wa
Kiislamu umeacha utamaduni
wake wa kusoma, kama historia
inavyojieleza kuwa Uislamu
unahistoria ndefu katika nyanja

ya elimu na kusoma.
Alisema, hali hiyo
inathibitishwa na uwepo wa
Vyuo Vikuu vya Waislamu
katika miji mbalimbali Duniani
kuliko dini yoyote zaidi ya miaka
1000 iliyopita, ambapo vyuo
hivyo vipo mpaka sasa katika
miji ya Tunis, Aljeria, Egypt na
kwingineko.
Tujitahidi kudumu katika
kusoma na hayo tukayo yasoma
tuyaingize katika matendo,
Mwenyezi Mungu anaposema
hawawi sawa walio soma na
wasio soma si kitu cha kusoma tu
na kuacha inapaswa kuingizwa
katika matendo. Alisema Ust.
Yassir.
Ramadhani Quiz Competition,
ni zoezi linalo andaliwa na
Taasisi ya Kiislamu ya An Nahl
Trust, na kushirikisha wanafunzi
wa Kiislamu waliopo katika
Mashule ya Sekondari Jijini Dar
es Salaam, ambapo wanafuzi
wanatakiwa kujibu maswali
yanayohusu mambo mbalimbali
ya kimasomo na ya kijamii.
Kwa mujibu wa Ust. Yassir,
alisema lengo kuu la mashindano
hayo ni kuwajenga vijana wa
Kiislamu katika utamaduni wa
kusoma na kujisomea mambo
mabalimbali, uwezo wa kujieleza
kulingana na kile walichokisoma
na ufahamu wa mambo kwa
upana.
Mashindano hayo hufanyika
kila mwaka, ambapo hufanyika
mwezi mmoja kabla ya Mwezi
Mtukufu wa Ramadhani, na
kilele chake hukia katika mwezi
wa Ramadhani wenyewe na
washindi hupewa zawadi za aina
mbalimbali.

bali ni suala nyeti na kwamba


zimesha sikika hoja za Wabunge,
na endapo litachaachwa hivi hivi
linaweza kuligawa Taifa, na wao
kama Wabunge ambao wanatoka
katika imani tofauti tofauti.
Miaka mitatu iliyopita baadhi
ya Masheikh kutoka Zanzibar
waliilalamikia Mahakama ya
Kisutu, Jijini Dar es Salaam,
kuwa wakiwa mikono mwa Jeshi
la polisi na Usalama wa Taifa,
walifanyiwa vitendo vichafu na
vya udhalilishaji.
Hata hivyo, suala hilo
limekuwa likiibuka mara kwa
mara Bungeni Dodoma, ambapo
katika Bunge la mwaka jana
Serikali iliahidi kuunda Tume
ya kuchunguza tuhuma hizo,
lakini mpaka sasa hakuna
kilichofanyika.
Aidha, siku chache baada
ya kuteuliwa kuwa Mawaziri
katika Serikali hii ya awamu
ya tano kwa pamoja Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi Mh.
Charles Kitwangi na Waziri wa
Sheria na Katiba Mh. Harison
Mwakyembe, walifanya ziara
katika gereza la Segerea, ambapo
ilielezwa kuwa Masheikh hao pia
walikisha malalamiko yao.
Wakati huo huo, Kwa upande
wake Mh. Riziki Shahari,
akichangia suala hilo alisema,
Kamati ya Bunge ya Kudumu ya
Bunge inayohusika na Wizara
husika, ilikwenda Gerezani
Segerea na kuongea na Masheikh
hao mbele ya Maosa wa
Magereza, ambapo walilalamika
hali zao na walieleza kwamba
hawajaenda kuulizwa.
Leo Mh. Waziri, mnaleta
karatasi na kuongea hayo,
karatasi yenyewe imezeeka na
haikuwa suala la Daktari aandike
kisha ampe Naibu Waziri, bali
kinachotakiwa ni watu waende
wakawaulize kilicho wasibu.
Amesema Mh. Shahari.
Alisema, ifahamike kuwa
Masheikh hao wana wafuasi wao
nyuma yao na wanawapenda, ni
wazi wanaumia, wana wazazi,
wana watoto, wana ndugu zao,
hao wote na wengine wanaumia.
Wote hao wameshuhudia
kilio chao wameshuhudia
wakijieleza kupitia Mahakamani
kuwa jamaa zao hao
wamedhalilishwa na Vyombo
vya Usalama, wameeleza wazi
kuwa wamefanyiwa visivyo.
Amesema Mh. Riziki.
Alisema, baada ya kuelezwa
vipimo vya Masheikh hao na
vyeti kukishwa Bungeni hapo
na kuelezwa ni majibu ya vipimo
vya Masheikh hao alilazimika
kuwasiliana na Mawakili wao ili
kujua ni nani alikuwa nao katika
zoezi hilo la kuchukuliwa vipimo

na Madaktari hao, lakini alidai


inaonekana haifahamiki.
Suala hapa sio kupimwa
afya, bali kinachotakiwa
uchunguzi juu ya tuhuma
walizotoa na Waziri wa wakati
huo Mh. Mathias Chikawe,
pamoja na istazai alizotoa humu
Bungeni, alisema atapeleka
jopo likawaulize na kufanya
uchunguzi lakini haifahamiki
aliishi wapi. Alisema Mh. Riziki.
Kwa upande wake Msemaji
Mkuu wa Kambi ya Upinzani
Bungeni, Mh. Freeman Mbowe,
alisema, suala hilo ni wazi
linawahusu viongozi wa kiimani
na wanapoanza kuwachangaya
viongozi hao na tuhuma ambazo
zinashindwa kuthibitishwa
kwa zaidi ya miaka mitatu,
haifahamiki ni Taifa la namna
gani linataka kujengwa.
Mh. Mbowe alisema
uhalali wowote wa Mashitaka
unaowahusu viongozi hao wa
Kiimani (Masheikh) lazima
ulindwe kwa umakini zaidi
lakini cha kushangaza Waziri
anazungumza na kuona kama ni
jambo jepesi tu, jambo ambalo si
sahihi.
Alisema, inashangaza kuona
Serikali inawarundika ndani
viongozi wa kiroho kwa mwaka
wa nne sasa huku uchunguzi
haukamiliki, na wengine
wanapigwa risasi na hakuna
taarifa yoyote ya Serikali au
kuonyesha kujali badala yake
wanaona ni mambo mepesi tu.
Mh. Mbowe alisema jambo
linalotia machungu zaidi kwa
viongozi hao wa kiroho ni pale
zinapojengwa hisia kwamba,
wanasimamia ama kuunga
mkono mlengo fulani wa kisiasa
na kuwa ndio msingi wa kujenga
chuki na kuwapandikiza kesi na
makosa yasiyo na ushahidi.
Kwa upande wake Mh.
Maftah, akiunga mkono hoja
ya Mh. Riziki Shahar, alisema
tokea anakuwa katika nchi hii
amekuwa akiona na kusikia
jinsi viongozi wa Kiislamu
wanavyodhalilishwa.
Alitoa mfano wa mauwaji ya
Mwembechai ambapo Waislamu
walipigwa risasi msikitini.
Akaongeza kwamba hivi sasa
kuna Masheikh wapo Mahabusu,
takribani kwa miaka mitatu
wakipachikwa tuhuma za ugaidi
na hakuna kinachoendelea katika
kesi zao.
Naomba kuuliza Mh.
Mwenyekiti, hivi magaidi ni
Waislamu nchi hii? Inasikitisha
sana kwamba Masheikh
wanawekwa ndani bila sababu za
msingi. Alisema Mh. Maftah.

Tahariri/Habari

AN-NUUR

S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786


Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM.
www.annuurpapers.co.tz
E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk
Osi zetu zipo: Manzese Tip Top
Usangi House, barabara ya Morogoro, D'Salaam

Waislamu wanahitaji mageuzi

MMOJA wa Maimamu
Jijini Dar-es-Salaam alipata
kusema kuwa, ili uweze
kuwa mwanachama wa
Baraza la Waislamu nchini
(BAKWATA) ni kuwa
Muislamu. Ikitizamwa
kwa kina kidogo, kauli ya
Imamu huyu ni sahihi kwa
sababu maana halisi ya
BAKWATA ni Baraza Kuu
la Waislamu Tanzania.
Hivyo Muislamu
yeyote nchini anaweza
kunasibishwa na chombo
hiki.
Aliyewahi kuwa Mufti,
Marhum Sheikh Hemed
bin Jumaa bin Hemed,
pamoja na kuwepo
matatizo ya kimfumo
katika kuzungumza au
kutaariana mambo ya
Waislamu kati ya uongozi
wa Baraza na Waislamu,
lakini alijaribu angalau
kuzungumza katika
vyombo vya habari kwa
kutoa hotuba kadhaa,
akijaribu kufanya ziara za
mikoani kuangalia hali ya
maendeleo ya Waislamu.
Tangu hapo, hali
mawasiliano ya Kitaasisi
kati ya Waislamu na
uongozi ilidorora kabisa.
Kumsiki Mufti akiongeana
Waislamu ni aidha katika
sherehe za Maulidi, sikukuu
za Eid au kusikika katika
tukio maalum, tena lenye
kushabihiana na maslahi ya
serikali basi.
Hatuna kumbukumbu
kusikia wala kufahamu
utaratibu ambao Mufti
amejiwekea, kuzungumza
na Waislamu ili apate japo
michango na mawazo yao.
Wala kusikia Mufti au
kiongozi wa ngazi ya juu
wa Baraza akitoa taarifa ya
maendeleo ya Waislamu na
taasisi kwa ujumla.
Hatuna hakika kama
Mufti Abubakar anafuatilia
kwa karibu hali ya
mambo ya Waislamu
yanavyokwenda huko
mikoani, wilayani, ukiacha
huko makao makuu.
Mikutano ya kila mwaka au
inayofanyika anapojisikia
kiongozi au kungoja
kugongana na tukio fulani
la kitaifa, kama vile Maulid
au Baraza la Iddi haiwezi
kuleta tija kwa Waislamu.
Waislamu wana hamu
kubwa ya kujua, kwa
mfano, ni kwa kiasi gani
Baraza limepiga hatua za
maendeleo, linamiliki kiasi
gani cha mali za wakfu
na wanazitumia vipi kwa
mujibu wa malengo ya
wakfu. Waislamu wana
hamu ya kujua bajeti ya

kila mwaka ya Baraza


(kama ipo) ya mipango ya
maendeleo ya Waislamu
katika elimu, afya, huduma
za kijamii, habari na
mawasiliano na kwa hakika
kila nyanja.
Kuna vyuo vingapi
vinatoa elimu bora, kuna
maktaba ya Kiislamu
ambayo ndiyo kitivo cha
rejea katika elimu ya dini,
kiongozi wa Waislamu
Kiislamu hapa nchini
anahoa kupotea kwa elimu
hiyo?
Yote haya yanahitajia
uongozi madhubuti wenye
uoni (vision) na makini.
Vinginevyo inakuwa
ada tu kuwa na Mufti,
Mwenyeiti, Sheikh na
Katibu wa mkoa, lakini
hata hao wanaojinasibu
kuwa Bakwata damu
damu hakuna faida
katika Uislamu wao na
maendeleo ya Uislamu
katika maeneo yao zaidi ya
wale wanaopata masilahi ya
mshahara na posho.
Hivi leo Muislamu
akiulizwa kama kuna mfuko
wa maendeleo ya Waislamu
BAKWATA ni wangapi
watakuwa na taarifa juu ya
mfuko huo, wangapi wana
taarifa za mafanikio au
hasara ya kuwepo Bakwata?
Isipokuwepo Bakwata,
Waislamu wanapungukiwa
nini zaidi ya kuwa kuna
watu watakosa vyeo vya
usheikh wa mkoa/wilaya na
posho zinazoandamana na
vyeo hivyo?
Kuna wakati Marehemu
Mufti Issa Shaaban Simba,
alisema BAKWATA
wapo katika mchakato
wa kuanzisha Benki ya
Kiislamu nchini. Leo
wangapi wana taarifa kama
mchakato huo ulifanyika
au umekia wapi, nani
aliyepewa jukumu la
kuusimamia n.k?
Ndio maana tunasema
kuna haja Mufti Abubakar,
kuleta mageuzi ndani ya
Baraza ili kuondoa hitilafu
hizi na kuweka utaratibu
mpya wa kiutendaji
unaopimika.
Waislamu wanahitaji
kuunganishwa na uongozi
bora walio ukosa tangu
uhuru. Hawawezi kupiga
hatua bila kutatua kasoro
hii.
Ni zamu ya Mufti
Abubakar kuamua kuleta
mageuzi ndani ya Baraza
kwa maslahi ya Waislamu.
Vinginevyo ni kujibebesha
mzigo wa cheo cha
masuuliya mbele ya Allah
(SW).

AN-NUUR

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 20 - 26, 2016

Bi Mkubwa mahakamani
Tuhuma ugaidi wa kimeta
Masheikh wawili watoweka
Huenda wameuliwa na ATPU

BI Nuseiba Mohammed
Haji, amekishwa rasmi
mahakamani akidaiwa
kula njama za kuandaa
shambulio la kigaidi la
kimeta (anthrax).
Akisimama kizimbani
katika mahakama ya
Milimani (Milimani Law
Courts), Nairobi, Jumanne
(Mei 10, 2016) wiki
iliyopita, muda mwingi
Bi Nuseiba alikuwa
akitabasamu na hata
kucheka.
Vyombo vya habari
kwa upande wao
vilikuwa na karamu
ya habari vikishadidia
habari hiyo na kuonyesha
kama Kenya inakabiliwa
na kitisho kikubwa kwa
kuwepo kile walichoita
cell of extremist medics.
Kwamba kutoka ugaidi
wa AK-47 za Al-Shabaab,
hivi sasa ugaidi wa
Kenya umepanda daraja
kwa kuanzisha vitengo
vya ugaidi wa kimeta
vinavyoendeshwa na
madakitari, akina Bi
Nuseiba Mohammed Haji
na mumewe Mohammed
Ali Abdi.
Shirika la Habari la AP
(Associated Press-American
multinational nonprot
news agency) lenye makao
makuu yake New York
City, likiandika juu
ya tukio hilo lilisema
kwamba Bi Nuseiba, ni
mshitakiwa namba mbili
akituhumiwa kumsaidia
mumewe kuandaa
shambulio la kimeta.
Anashitakiwa pia
kumsaidia mumewe
Mohammed Ali Abdi
kuendesha mafunzo
ya kigaidi ili kuanzisha
kundi la Islamic State.
Nuseiba alikamatiwa
Uganda na kusarishwa
hadi Kenya kuungana na
mumewe ambaye yeye
alikamatwa Kenya akiwa
katika mafunzo yake
ya vitendo ya udakitari
katika hospitali moja
nchini humo.
Nuseiba Mohammed
Haji, naye pia ni
mwanafunzi wa kozi ya
udakitari katika Chuo
Kikuu cha Kampala
International University,

BI. Nuseiba Mohammed Haji akiwa kizimbani katika


mahakama ya Milimani (Milimani Law Courts),
Nairobi, Jumanne (Mei 10, 2016) wiki iliyopita.
Uganda.
AP wakifafanua juu
ya shitaka linalomkabili
Nuseiba wanasema:
(She) is alleged to have
been an accomplice in a
foiled plan to launch an
anthrax attack in Kenya by
a cell of extremist medics
linked to the Islamic State
group.
Kwamba mama
huyo wa Kiislamu na
mwanafunzi wa kozi ya
udakitari anashitakiwa
kwa kuwa mshirika
katika mpango wa
kuishambulia Kenya
kwa kimeta, shambulio
ambalo liliteguliwa na
polisi.
Waandaaji wa mpango
huo wakitajwa kuwa ni
madaktari (wanafunzi)
walio wanachama wa IS.
Baada ya kusomewa
shitaka hilo, polisi
waliomba mahakama
kwamba Bi Mkubwa
huyo akae rumande kwa
siku 30 zaidi ili kuruhusu
uchunguzi kufanyika.
Mtuhumiwa
alitarajiwa kukishwa
tena mahakamani Mei
16 ambapo ungetolewa
uamuzi juu ya ombi
la polisi kuendelea
kumshikilia mtuhumiwa.
Wakati huo huo
imeripotiwa kuwa
watuhumiwa wengine
wawili, Ahmed Hish na
Farah Dagane, ambao
pia ni wanafunzi wa
Shahada ya udakitari,
wametoweka katika

mazingira ya kutatanisha.
Hata hivyo, taasisi
za kupigania haki
za binadamu katika
Kenya zinatuhumu
kuwa huenda watu hao
wameuliwa katika kile
walichoita:
Extra-judicial
executions and forced
disappearances carried out
by the police on suspects
they are unable to prosecute
because insucient
evidence.
Kwamba kutoweka
kwa watu hao kuna kila
dalili kuwa kunaangukia
katika mauwaji na
kutoweka watu
kunakofanywa na Polisi
dhidi ya watuhumiwa wa
ugaidi.
Na kwamba Polisi
wa Kenya wanafanya
hivyo kwa kuwa hawana
ushahidi wa kukisha
mahakamani dhidi ya
watuhumiwa. Kwa hiyo
huamua kuwauwa kimya
kimya tu!
Polisi wa Kenya
wamekuwa wakikabiliwa
na shutuma kali kwamba
wameuwa mamia ya
watuhumiwa kinyume
cha sheria (extra-judicial
executions) huku wengie
wakitoweka tu bila hata
maiti zao kuonekana.
Imesema moja ya
taarifa za watetezi wa
haki za binadamu.
AP ya New York City,
ikikoleza propaganda juu
ya ugaidi Kenya ikasema
Inaendelea Uk.5

5
Inatoka Uk. 4
kwamba Kenya inakabiliwa na
changamoto ya kupambana na
magaidi wa IS ambapo kwa sasa
kuna kambi za kuwapa mafunzo
vijana wa Kenya kujiunga na
kundi hilo. Na kwamba wapo
vijana takribani 20 wa Kenya
ambao wamekwenda Libya
kujiunga na IS.
Wakati huo huo, hayo yakijiri
Nairobi, mmoja wa wasichana
wanaodaiwa kutoroka katika ule
usanii wa Bring Back Our Girls,
amepewa fursa ya kuhutubia
Kamati ya Bunge la Marekani
juu ya Mambo ya Nje (House
Foreign Aairs Subcommittee on
Africa) kuelezea hatari Boko
Haram.
Akipewa jina la bandia "Sa'a",
msichana huyo kutoka Nigeria
alisimama mbele ya Kamati
hiyo Mei 11, 2016 akiongozana
na Frank Wolf, ambaye ndiye
alimchukua kule Nigeria na
kumpeleka Marekani. Wolf
alikuwa Mbunge (1981-2015)
akiwakilisha Wilaya ya Virginia.
Hivi sasa ni Mlei katika Chuo
Kikuu cha Baylor.
Wolf anasema kuwa
alikwenda Nigeria kuchunguza
na kupata habari za ndani juu
ya uharamia na ugaidi wa Boko
Haram.
Na katika kufanya utati huo
anasema kuwa ameshuhudia
jinsi Boko Haram wanavyoua
watu, wanashambulia na
kuuwa wanavijiji, wanawateka
wasichana na kuwageuza
mabomu ya kujitoa muhanga
(suicide bombers) huku wengine
wakiwafanya watumwa wa
ngono.
Na kwamba amekuja na
msichana huyo ili apate
kutoa ushahidi wa kile yeye
binafsi kilichomka, asaa
huenda serikali ya Marekani
na Wamarekani watapata
kuelewa vizuri hatari ya ugaidi
uliopo Kaskazini mwa Nigeria
(wanakoishi Waislamu wengi).
Kwa upande wake Saa
akishadidia nukta hiyo akasema
kuwa Nigeria ya Kaskazini si
mahali salama pa kuishi mtu
yoyote, lakini ana matarajio
kwamba kwa ushuhuda
aliotoa, huenda walimwengu
watazinduka na kuchukua
hatua.
Amedai kuwa yeye alikuwa
miongoni mwa wasichana wa
Chibok waliotekwa na Boko
Haram miaka mitatu iliyopita,
lakini aliruka wakiwa katika lori
walilopakiwa likipita msituni.
Anasema, aliona bora kufa
kuliko kukosa uhuru wake
akiwa mikononi mwa BK.
Akanogesha kwa kudai kuwa
amesoma Katiba ya Marekani
na kukuta kwamba inajali sana
uhuru wa binadamu na mtu
akikunyima uhuru, ni bora ufe.
Na kwa maana hiyo akasema
kuwa alikuwa amefanya uamuzi
sahihi wa kuruka katika lori lile
la BH hata kama angekufa.

Habari za Kimataifa

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 20 - 26, 2016

Bi Mkubwa mahakamani

MSICHANA kutoka Nigeria akipewa jina la bandia "Sa'a,"


alipokuwa akitoa ushuhuda wake juu ya ugaidi wa Boko Haram
mbele ya Kamati ya Mambo ya Nje, kule Marekani inayohusika na
mambo ya Afrika (House Foreign Aairs Subcommittee on Africa.).
Hiyo ilikuwa Mei 11, 2016.

MWAKILISHI wa Jimbo la Florida


Bi Frederica Smith Wilson (D-Fla.).
Akasema, anaamini kwamba
kwa kuka kwake Marekani na
kutoa ushuhuda, sasa ana tamaa
hatua zitachukuliwa kuwatia
adabu magaidi na kuifanya
Nigeria nchi salama ya kuishi.
Baada ya maelezo hayo mbele
ya kamera za waandishi wa

AN-NUUR

CHRISTOPHER Henry
"Chris" Smith.
habari, Mwakilishi wa Jimbo
la Florida Bi Frederica Smith
Wilson (D-Fla.), akapigilia
msumari akisema kuwa
inavyoonekana kinachotokea
Nigeria ni Mauwaji ya Kimbari
(genocide) yakiacha kizazi
cha watoto wasio kwenda

shule kwa sababu shule zote


zimeangamizwa na magaidi wa
Boko Haram, huku walimwengu
wakiwa hawana habari kabisa.
Kwa maneno yake mwenyewe
alisema:
"It appears as if genocide is
taking place" leaving a "whole
generation of children who are not
being educated because schools
are being destroyed. I wonder in
my heart and soul, what should
we be doing, what can we do as
a country?" the congresswoman
added. "We can't just pretend it's
not happening. Do we need to start
a revolution? Do we need to march
to the White House? Do we need to
march to Nigeria? What can we do,
all of us as a Congress?"
Maswali haya ya Mbunge
Frederica Wilson, ni namna ya
kuichagiza serikali ya Marekani
kuchukua hatua haraka juu ya
ugaidi unaofanyika Nigeria.
Jambo ambalo lilidakiwa na
Mwenyekiti wa Kamati hiyo
Christopher Henry "Chris" Smith
(R-N.J.) akitumia neno "gross
indierence" kusisitiza kuwa ni
jambo lisilokubalika kufumbia
macho ugaidi unaofanyika
Nigeria.
Katika kuzidi kuchochea,
Mnigeria Emmanuel Ogebe
akasema kuwa Boko Haram
wamewahi kushambulia raia
wa Marekani, lakini anashangaa
State Department imekaa
kimyaa.
Ukisikiliza maneno ya Saa,
hayana tofauti na yale ya yule
binti wa Balozi wa Kuwait katika
Washington ambaye alipewa jina
la Nayirah akatumiwa kupiga
propaganda juu ya kilichodaiwa
kuwa ni ukatili wa Saddam
Hussein.
Binti huyo alipelekwa mbele
ya Bunge la Marekani kutoa
ushaidi ikidaiwa kuwa ni
muuguzi katika hospitali moja
nchini Kuwait na kwamba
alishuhudia askari wa Saddam
wakichukua watoto wachanga
na kuwatupa katika sakafu
yenye baridi kali na kuwaacha
wafe. (Tazama: 1. False Flag Actor
- Nayirah al-aba - Kuwaiti
Royal Family. (2) Deception on
Capitol Hill-New York TimesJanuary 15, 1992)

Amina Abdallah Vs Nuseiba Mohamed


Na Omar Msangi

JINA Amina Abdallah Arraf


al Omari lilivuma sana wakati
unaanza mgogoro wa Syria. Amina
alijitokeza kama mwanamke
mpigania haki za wananchi wa
Syria akijitokeza katika vyombo
vya habari na hasa mitandao ya
kijamii kama mtu anayechua
maovu ya Rais wa Syria Bashar
al-Assad. Amina Abdallah
alijitangaza kama mwanamke
khabithi (lesbian) na hivyo

akaupa mtandao wake (Blog)


jina la A Gay Girl In Damascus.
Aliufungua rasmi mtandao huo
Februari 19, 2011, akawa anatoa
ujumbe kuwa akiondolewa Bashar,
pamoja na kupatikana uhuru wa
kisiasa na demokrasia, hata watu
kama yeye ambao ni mabaradhuli
wa kike (lesbians), watakuwa
huru kufanya mambo yao. Lakini
pamoja na kuwa shoga wa
kike, akawa anajitapa kuwa ni
Muislamu sa, anavaa hijabu,
anaswali, anafunga na kwamba

anajivunia kuwa Muislamu na


anaamini kuwa Mungu hakukosea
kumuumba shoga wa kike.
Tarehe 27 Mei, 2011 CNN
wakarusha kipindi wakimsifu
Amina kuwa, ni mwanamapinduzi na kwamba mapinduzi
anayopigania Syria yatafanya hali
kuwa nzuri hata kwa mashoga.
(Davies, Catriona (27 May 2011).
"Will gays be 'sacricial lambs' in
Arab Spring?". CNN.)

Inaendelea Uk. 12

Hoja ya Juma Kilaghai

AN-NUUR

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 20 - 26, 2016

Hakuna ugonjwa usio na dawa! (2)


TAFITI zinaonyesha
kwamba kuna wakati
saratani ni matokeo ya
mchakato wa ukarabati
wa seli zilizoharibika
ndani ya mwili. Tati hizi
zinaonyesha kwamba
mimba inapotungwa, seli
katika mimba hiyo changa
hugawanyika haraka
sana na kutengeneza
makundi mawili ya seli
zenye maumbile na kazi
tofauti. Kundi la kwanza
la seli hizo (Kiini tete,
au embryo kwa lugha ya
kitaalamu) huendelea
kugawanyika na kubadilika
likiwa safari kutengeneza
kiumbe ambacho hatimaye
kitazaliwa kama mtoto. Hali
kadhalika kundi la pili nalo
huendelea kugawanyika
na kubadilika na hatimaye
kutengeneza kondo la uzazi
(placenta) ambalo kazi yake
ni kulizingira lile kundi la
kwanza.
Kila moja ya seli katika
kundi hili la seli ambalo
sasa limetengeneza kondo
la uzazi, ina gamba ambalo
limebeba umeme hasi.
Seli hizi kitaalamu huitwa
Trophoblasts. Kazi ya hizi
Trophoblasts ni kutoa ulinzi
kwa kiini tete kisiweze
kushambuliwa na mfumo
wa kinga za mwili za mama!
Bila seli hizi chembechembe
nyeupe za damu katika
mwili wa mama ambazo
huunda sehemu kubwa ya
jeshi la kinga katika mwili wa
mwanadamu zingeshambulia
kiini tete hicho na kukiharibu
kwa dhana kwamba ni
adui ailiyeingia mwilini!
Kinachotokea ni kwamba
kwa kuwa chembechembe
hizi nyeupe za damu nazo
zimebeba umeme hasi
kama zilivyo Trophoblasts,
zinapokaribia eneo kiliko
kiini tete umeme hasi wa
Trophoblasts na ule wa
chembechembe cheupe
husukumana (repels each
other) na hivyo kusababisha
chembechembe hizo nyeupe
kusogezwa mbali na kiini
tete. Tati zinaonyesha kuwa
ulinzi huu wa Trophoblasts
hukoma ghaa katika juma la
nane la ujauzito.
Tati zinaonyesha kuwa
sababu ya hatua hii ni
kwamba katika kipindi hiki
kiumbe kinachoendelea
kukua na kubadilika tayari

Tiba za saratani Sehemu ya kwanza

kina kongosho linalofanya


kazi na kongosho hili
huzalisha kiasi kikubwa
cha vimenganyo (pancreatic
enzymes) ambavyo
haviruhusu trophoblasts au
chembechembe nyeupe za
damu kutoka kwa mama
kusogea katika eneo hilo.
Vimengenya hivi vina
uwezo wa kuchakata na
kuyeyusha protini (digest)
hivyo basi chembechembe
yoyote nyeupe katika eneo
hilo, au seli ya trophoblast
itaharibiwa kwa protini
yake kuchakatuliwa na
kuyeyushwa na vimengenya
hivyo.
Tati zinaonyesha kuwa
mwili unapositisha uzalishaji
wa trophoblasts, chache ya
hizi seli hubakia zikiogelea
kwenye damu katika kipindi
chote cha maisha ya kiumbe.
Kazi ya hizi trophoblasts ni
kusaidia katika ukarabati wa
seli za mwili zinazoharibika
kwa sababu mbalimbali.
Katika eneo ambalo seli
zimeharibika na zinahitaji
kukarabatiwa seli chache
za trophoblasts huenda
katika eneo hilo na kuanza
kugawanyika kwa kasi
inayozifanya kuongezeka
kwa wingi ndani ya muda
mfupi, huku zikifanya
kazi ya kusaidia ukarabati.
Tatizo linakuja pale ambapo
uharibifu wa seli husika ni
kitendo endelevu na pengine
cha kudumu. Kwa mfano,
kwa wavutaji wa sigara
wa muda mrefu ambapo
uharibifu wa seli za mapafu
yao ni endelevu. Hii ina
maana kwamba katika eneo

husika trophoblasts zitakuwa


zinajigawanya kwa kasi na
zitaongezeka kupindukia
mipaka (out of control growth).
Uchunguzi wa kimaabara
unaonyesha kuwa seli za
trophoblasts zinazojikuta
katika mazingira ya aina
hii hufanana kwa kila
hali na seli za saratani!
Hii imepelekea baadhi ya
wanasayansi kuamini kuwa
saratani chanzo chake ni nia
nzuri na jitihada ya mwili
kutaka kurekebisha kasoro
zinazojitokeza katika seli za
mwili. Jitihada zinapokwenda
mrama kutokana na uharibifu
katika seli husika kuwa
endelevu, basi saratani
hujitokeza.
Imethibitika kuwa
vimengenyo vinavyozalishwa
na kongosho (pancreatic
enzymes) ni msaada mkubwa
wa kuzuia trophoblasts
kutengeneza saratani mwilini.
Ugunduzi huu ulifuatia
jitihada kubwa za Dr. William
D. Kelly wa kule nchini
Marekani ambaye aliamini
kuwa saratani ni zao la mwili
kushindwa kuchakata vizuri
vyakula vya jamii ya protini
kutokana na upungufu wa
vimengenya vinavyozalishwa
na kongosho, hususan
vile ambavyo kazi yake ni
kuchakata na kuyeyusha
protini (proteolitic enzymes).
Ili kuusadia mwili kufanya
kazi hiyo kwa ufanisi Dr.
Kelly alipendekeza mfumo
wa tiba kwa wagonjwa

wake ambao ulijumuisha


marekebisho katika lishe,
matumizi ya tiba-lishe
(nutritional suppliments), na
uondoshaji wa sumu mwilini.
Dr. Kelly ambaye alipingwa
sana na madaktari wa mfumo
(conventional cancer doctors)
alisashwa na Dr. Nicholas
Gonzales wa New York
ambaye alifanya kazi kubwa
ya kutati kesi moja moja
ya wagonjwa wa Dr. Kelly
kwa udhamini wa taasisi ya
Memorial Sloan - Kettering
Cancer Center.
Ripoti ya kazi ya Dr.
Gonzales, iliyokuwa na
kurasa 500, ilithibitisha kuwa
tiba ya Dr. Kelly ilikuwa kweli
inafanya kazi katika saratani
za aina nyingi mwilini.
Utati wa ziada
uliofanywa katika kazi
ya Dr. Kelly na wengine
waliomfuata umethibitisha
bila shaka kuwa uchache wa
vimengenya vya kongosho ni
sababu ya msingi ya kuibuka
kwa saratani mwilini; na
kuwa wagonjwa wa ugonjwa
wa kisukari ambao kimsingi
kongosho zao zinazalisha
kiwango kidogo cha hivi
vimengenya, wako katika
hatari mara tatu zaidi ya
kupata ugonjwa wa saratani.
Hii ina maana kuwa
mgonjwa wa kisukari
anatakiwa achukue tahadhari
mara tatu zaidi kuliko mtu
wa kawaida katika kulinda
seli zake za mwili zisiharibike
na kujenga mazingira ya
trophoblasts kuzaliana kwa
wingi. Uharibifu huu ni
ule unaoweza kufanywa
na uvutaji wa sigara, ulaji
wa vyakula vilivyotunzwa
kwa kemikali, matumizi ya
vipodozi bandia (synthetic
cosmetics), matumizi ya
nyama zilizochakatuliwa na
kuhifadhiwa kwa kemikali,
matumizi ya nyama za
kuchoma zilizoungulia na
kufanya mkaa, nakadhalika.
Aidha mgonjwa wa sukari
anahitaji kutumia nyongeza/
tiba- lishe (nutritional
supplements) za vimengenya,
hususan vile ambavyo kazi
yake kubwa ni kuchakata na
kuyeyusha protini.

7
Na Abuu Nyamkomogi
NILIWAHI kuandika katika
toleo namba 1224 la gazeti
hili zaidi ya mwezi mmoja
uliopita makala yenye anwani
'Makhatibu Wanapaswa
Kubadilika. Katika makala
yale, pamoja na mambo kadhaa
niliyoyaandika, niligusia
pia suala la umuhimu wa
maandalizi kabla ya utekelezaji
wa jambo fulani na sehemu ya
maelezo ya ufafanuzi wangu
kuhusu suala hili ilisomeka
hivi:
''Maandalizi ni jambo la
msingi katika kuleta ufanisi
katika utekelezaji wa jambo
lolote. Ni ukweli kwamba kuna
tofauti kubwa ya kiathari na
kimatokeo kati ya shughuli
au kazi inayofanywa kwa
kutanguliwa na maandalizi
na ile inayofanywa pasi na
kutanguliwa na maandalizi''.
Nimelazimika kurejelea
nukuu hiyo kutoka katika
makala yale kutokana na
maudhui yake kuwa na
mafungamano, kwa kiasi
fulani, na jambo ninalokusudia
kulidurusu katika makala haya
ya leo, nalo si jingine bali ni
kuwakumbusha ndugu zangu
Waislamu kuhusiana na kufanya
maandalizi ya Ramadhan
wakati huu wa kuelekea katika
mwezi huo mtukufu ambao
tumewajibishiwa na Allah (S.W.)
kutekeleza ibada ya swaumu
ndanimwe (2:185).
Nimeonelea kulingana na
uchambuzi wa mada ya makala
haya, niyagawe maandalizi
ninayokusudia kuyajadili
katika makala yetu ya leo
katika matapo mawili. Tapo la
kwanza nimeamua kuliita tapo
la maandalizi ya kinadharia
na la pili nimeliita tapo la
maandalizi ya kivitendo. Kwa
maelezo ya ufafanuzi kuhusu
matapo haya ni kwamba
maandalizi ya kinadharia ni yale
yanayohusiana na kuwa na ujuzi
au maarifa, au kupata elimu
sahihi juu ya jambo fulani kabla
ya kulitekeleza wakati ambapo
maandalizi ya kivitendo ni yale
yanayohusiana na utekelezaji wa
jambo fulani baada ya kupata
ujuzi au maarifa kuhusiana
nalo kama sehemu ya mafunzo
kwa njia ya vitendo au mazoezi
kwa lengo la kupata tajiriba ya
kukuwezesha kulitenda kwa
ufanisi zaidi jambo hilo katika
siku za usoni.
Nitafafanua zaidi maelezo
hayo kuhusiana na aina
zote mbili za maandalizi
nilizozidokeza katika aya
iliyotangulia hapo juu; kwanza
kwa kutumia mifano ya
jumla inayotuzunguka katika
mazingira yetu tunamoishi
na kisha nitaangazia mifano
mahsusi inayowiana/
inayoendana na mada ya
mjadala husika wa makala
haya. Kabla ya kutoa ufafanuzi

Makala

AN-NUUR

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 20 - 26, 2016

Tujiandae kwa Ramadhani

MABANGO ya kuukaribisha mwezi wa Ramadhani katika mabasi


ya umma London, Uingereza.
huo na kabla ya kuingia katika
uchambuzi wa kiini cha mada ya
makala haya, ni vyema nikatoa
utangulizi japo mfupi kuhusiana
na mwezi wa Ramadhan
kwa kuwa ndio mwezi
ambao tunaokusudia kujadili
maandalizi ya funga ambayo
hufanyika ndanimwe kama
tutakavyoona katika uchambuzi
wa makala haya huko mbele
inshaallaah.
Ramadhan ni mmojawapo
kati ya miezi kumi na
miwili inayopatikana katika
mzunguko wa mwaka kama
inavyobainishwa na Allah (S.W.)
katika Qur-ani kwamba:
''Idadi ya miezi (ya mwaka
mmoja) mbele ya Mwenyezi
Mungu ni kumi na miwili
katika elimu ya Mwenyezi
Mungu (Mwenyewe) tangu siku
alipoumba mbingu na ardhi.....
(9:36).
Naam, ni dhahiri kwamba
hadi muda huu ninaoandika
makala haya tayari mwezi wa
Shaaban umeshaingia; kwa
muktadha huo, hapana shaka
kwamba zimesalia siku chache
kabla ya kuingia/kuanza kwa
mwezi wa tisa kwa mujibu wa
kalenda ya Kiislaamu. Mwezi
huu wa tisa hujulikana kwa jina
la Ramadhan ambao tunatarajia,
panapo majaliwa ya Allah (S.W.),
kuudiriki na kutekeleza ibada ya
funga yake ambayo ni mojawapo
kati ya nguzo tano za Uislamu,
ndani ya hizo wiki tatu zijazo
inshaallaah.
Hata hivyo, kuudiriki au
kutoudiriki mwezi huo ni
jambo lililo nje ya uwezo wetu
bali liko ndani ya uweza wa
Allah (S.W.) lakini jambo lililo
ndani ya uwezo wetu ni suala
la kufanya maandalizi kwa
ajili ya kuitendea swaumu ya
Ramadhan haki yake kama
ipasavyo/kwa ufanisi iwapo
tukijaliwa kuweza kuudiriki
mwezi huo.
Kwa kuanza na mfano

wa jumla unaohusiana na
maandalizi ya kinadharia
ni kwamba kwa kawaida
maandalizi ya namna hii
huhusiana na utoaji wa elimu
au mafunzo ya fani mbalimbali
yanayoendeshwa katika taasisi
anuwai za kielimu na hususan
vyuo vya kati na vya elimu ya
juu hutanguliwa na ukishaji
au utoaji wa ujuzi au maarifa
ya kinadharia kwa walengwa
kuhusiana na fani husika
wanazochukua/wanazosomea
mathalani ualimu, udaktari,
uhandisi, uandishi wa habari
na utangazaji, kwa kutaja
chache. Hii ni baadhi tu ya
mifano ya fani chache kati ya
nyingi zinazoweza kurejelewa
katika kusherehesha dhana ya
maandalizi ya kinadharia.
Ama kwa upande wa mfano
wa jumla wa maandalizi
ya kivitendo ni kwamba
ujuzi au maarifa yatolewayo
kinadharia hutafsiriwa kwa
utendaji na walengwa katika
fani mbalimbali mithili ya hizo
tulizozitaja katika mfano wa
maandalizi ya kinadharia katika
aya iliyotangulia hapo juu;
hujikita katika mafunzo kwa njia
ya vitendo, kwa mfano walimu,
madaktari, wahandisi, waandishi
wa habari na watangazaji
huelekea au hupelekwa katika
maeneo au vituo mbalimbali
vya kufanyia mafunzo kwa
vitendo kwa ajili ya kutekeleza
au kutafsiri kivitendo, kwa
kipindi fulani, yale mambo
waliojifunza kinadharia wakati
wakiwa vyuoni na ambayo
wanatarajia kuyatekeleza kwa
ufanisi zaidi, watakapopata
ajira au watakapokuwa katika
vituo vyao vya kazi, kupitia fani
walizosomea baada ya kuhitimu
masomo au kukamilisha
mafunzo yao.
Baada ya maelezo ya
ufafanuzi na mifano hiyo
michache, inayoakisi mazingira
yanayotuzunguka, kuhusu aina

hizo mbili za maandalizi katika


kukia ufanisi au tija maridhawa
ya jambo fulani; nirejelee sasa
katika uchambuzi wa mada
ya mjadala wetu ili tuweze
kukumbushana kunako suala la
kujiandaa kwa ajili ya ibada ya
swaumu ya mwezi mtukufu wa
Ramadhani katika kipindi hiki
cha kuelekea mwezi huo.
Mara nyingi wengi wetu
wanaposikia suala la kufanya
maandalizi kwa ajili ya funga ya
Ramadhani, kra zao huelekea
zaidi katika kukiria futari na
daku au kwa lugha nyingine
yaweza kusemwa kwamba kra
zao humli zaidi katika maakuli
na si vinginevyo. Ninasema
hivyo kwa sababu nilipokuwa
katika kufanya maandalizi
ya kuandika makala haya
nilijaribu kuwauliza Waislamu
kadhaa kunako maandalizi yao
kuhusu swaumu ya Ramadhan,
yaani namna walivyojiandaa
au wanavyotarajia kujiandaa
kwa ajili ya funga hiyo,
majibu ya wengi kati ya
wale niliozungumza nao
yalinithibitishia ukweli wa
ninachokieleza hapa kwamba
kra kuhusu maandalizi ya
Ramadhani kwa wengi wetu
yamemili katika maakuli.
Jambo hili linabeba ujumbe
mmoja mkubwa nao ni kwamba
lengo la ibada ya swaumu ya
Ramadhani halifahamiki na ndio
maana hata maandalizi ya ibada
hii kwa wengi wetu hayajielekezi
kwenye kuliendea lengo halisi
la funga ambalo ni TAQWA
kama lilivyobainishwa na Allah
(S.W.) katika suratul-baqara
aya ya mia moja na themanini
na tatu (2:183). Pamoja na Allah
(S.W.) kutubainishia lengo la
ibada hiyo kupitia aya hiyo,
bado wengi wetu tunaonekana
kutolizingatia kabisa lengo
hili na kibaya zaidi yaelekea
tumeamua kubuni lengo
lingine kabisa nalo ni MLO/
KULA ambalo ni kinyume na
lile tuliloelekezwa na Allah
(S.W.) ndani ya Qur-an na ndio
maana unakuta hata maandalizi
yanayotushughulisha zaidi
ni yale ya kimaakuli na si
vinginevyo.
Naomba nieleweke vizuri
hapa kwamba simaanishi ya
kuwa maakuli ni jambo lisilo na
umuhimu au pengine ni jambo
lisilopaswa kutiliwa maanani,
la hasha! Bali ninachomaanisha
hapa ni kwamba tunapaswa
kuyachukulia maakuli kuwa
wasila wa kutusaidia kuka kule
tunakokusudia kuka (lengo) na
si kuyageuza yenyewe (maakuli)
kuwa ndio kusudio kuu la
utekelezaji wa ibada ya funga ya
Ramadhani.
Kwa mantiki hii, nguvu
kubwa ingepaswa kuwekezwa
katika lengo na si wasila; na
yumkini ama kwa kutozingatiwa
hili au kwa kupewa wasila
uzito usiostahili badala ya
Inaendelea Uk. 16

Makala

AN-NUUR

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 20 - 26, 2016

Udini-5

Kilichosababisha niitwe mdini


KATIKA jitihada za kumpamba
Nyerere kwa lengo la kuwachafua
maraisi wengine waliomfuatia,
mwandishi mwingine Stephano
Mango katika gazeti la Dira
toleo namba 144 la 29.12.2011
ameandika yafuatayo katika
makala yake yenye kichwa cha
habari Watanzania hawana nguvu
ya kiuchumi, kisiasa:
Kwa busara ya Mwalimu
Nyerere, aliona na kuamini kuwa
siasa ya chama kimoja ingewaleta
watu pamoja katika kukia
malengo stahiki ya kuendeleza
nchi kijamii, kiuchumi na
kiutamaduni. Yafaa tujiulize: Je,
raisi wa sasa akifanya hivyo ataitwa
mwenye busara? Wangapi leo
wanakubaliana na hiyo inayoitwa
busara ya Mwalimu Nyerere ya
kuwa na chama kimoja tu cha siasa?
Anaendelea kuandika akisema:
Mwalimu alijikita katika Azimio la
Arusha ambalo lilikuwa ni uamuzi
mwingine wa kuboresha uhuru kwa
maendeleo ya wananchi, ambapo
ndani ya azimio hilo viongozi wa
nchi walifungwa na vipengele
kadhaa kuhusu maadili stahiki ya
uongozi wa umma. Anaendelea
kuandika akisema: Jambo hilo
lilisaidia kuthibiti wafanya biashara
walanguzi au chembechembe
zozote za kibepari kuingia katika
siasa na uongozi wa wananchi
ambapo kwa dhati iliamuliwa siasa
ya ujamaa na kujitegemea kuwa
ndiyo dira ya nchi na uongozi wake.
Hali ya Tanzania ilikuwa nafuu
kuliko sasa.
Ingawa hali haikuwa nafuu kama
mwandishi huyu anavyodai, hata
kama ingekuwa nafuu, hiyo sio hoja
kwa sababu unafuu huo unaweza
kuwa umechangiwa na mambo
mengi na sio Nyerere na serikali
yake tu. Mara nyingi, hali kuwa
nzuri au mbaya husababishwa na
mchanganyiko wa mambo mengi
na sio serikali iliyopo madarakani.
Aidha, kila mtu ni sehemu ya
serikali, hivyo kabla ya kuilaumu
serikali ni muhimu ajiulize yeye ana
mchango gani katika lawama hizo.
Kwa ambao hawakuuona
uongozi wa awamu ya kwanza
wanaweza kuamini kuwa Tanzania
ilikuwa kama peponi wakati huo,
lakini hata mtoto aliyekuwa na umri
wa chekechea wakati huo anaweza
kukumbuka baadhi ya matatizo
yaliyokuwapo.
Kinyume na mwandishi
anavyotaka watu waamini, hayo
anayoita maadili ya Azimio la
Arusha hayakufanikiwa kuwafunga
watu katika uadilifu, na ushahidi ni
kulisika kwa mashirika ya umma,
kushamiri kwa wahujumu uchumi
na uhaba wa karibu kila bidhaa
muhimu nchini. Kuna kipindi
serikali ilitawaliwa kwa nguvu
ya ushawishi wa matajiri kiasi
ambacho hata aliyekuwa Waziri
Mkuu wa wakati huo, Edward
Sokoine aliwahi kusema, serikali
ilikuwa likizo.
Mwandishi huyo anaendelea
kuwadanganya watu kuwa baada

HAYATI Mwalimu J.K. Nyerere

ALHAJI Ali Hassan Mwinyi.

ya mwalimu Nyerere kumaliza


ngwe yake ya uongozi na kumpasia
mzee wa ruksa, Ali Hassan
Mwinyi, kijiti ili aendeleze kuijenga
Tanzania, ndipo mambo yalipoanza
kuharibika.
Kinyume na mwandishi
anavyotaka watu waamini, hakuna
Mtanzania wa kawaida ambaye
hakufurahia mabadiliko aliyofanya
raisi wa awamu ya pili, maarufu
kama Mzee Ruksa ya kufungua
milango ya biashara.
Kitendo chake hicho kiliifanya
nchi ijae bidhaa ambazo tulizoea
kuziita adimu na ambazo ama
Mtanzania wa kawaida kabla ya
hapo alizoea kuzikosa, kuzipata
kwa foleni yenye adha na karaha,
au kwa bei ya juu sana iliyoitwa
mwendo wa kuruka. Hata jina la
Mzee Ruksa alilipewa na wananchi
kwa upendo waliokuwa nao kwake
na kumuunga mkono katika uamuzi
wake huo.
Mwandishi anadai kuwa
viongozi wa CCM chini ya uenyekiti
wa Raisi Mwinyi walifanya
mabadiliko makubwa katika
Azimio la Arusha na kuleta Azimio
la Zanzibar ambalo linatutafuna
hadi leo. Anaendelea kudai kuwa
kansa inayoendelea kuitafuna nchi
ni ukosefu wa uzalendo miongoni
mwa viongozi wetu ambao kimsingi
wanatokana na kufaidika kwa
kuvunjwa kwa Azimio la Arusha na
kujilimbikizia mali na kulisi bila
huruma rasilimali za nchi hii.
Kama nilivyokwishasema,
Nyerere alikuwa mwepesi na
hodari wa kuingilia kati lolote
lililokwenda kinyume na matakwa
yake, na shupavu kutetea kile
anachoamini. Amewahi kuingilia
kati suala la Zanzibar kujiunga na
OIC akafanikiwa. Amewahi pia
kuzima jaribia la kundi la wabunge
waliojiita G55 la kutaka serikali
ya Tanganyika. Alikataa masharti
ya IMF hata pale nchi ilipokuwa
ikihitaji sana msaada wake.
Ukilinganisha na hayo, naamini
kuwa Azimio la Zanzibar lilikuwa

rahisi kwake kuliingilia iwapo


angetaka kufanya hivyo.
Azimio la Arusha likiwa
limeshavunjwa, Nyerere mwenyewe
aliwahi kusema kulizungumzia
kunahitaji akili ya mwendawazimu,
bila shaka akimaanisha kuwa
halikubaliki. Aidha, uzalendo
hauletwi na maazimio wala kanuni
na sheria zilizoorodheshwa katika
karatasi. Uzalendo ni tabia ya mtu
binafsi. Ukosefu wa uzalendo
na kulisi nchi vilikuwepo hata
wakati wa Azimio la Arusha. Kama
tulivyokwishaona, mashirika ya
umma yalitafunwa na kulisika
wakati huo. Walanguzi na
wahujumu uchumi walikuwepo
kwa kiwango cha juu hata wakati
huo.
Mwandishi analalamika
kuwa leo kiongozi anachosema
ni kingine na anachotenda ni
kingine. Anashangaa na kutoa
mfano wa serikali kutangaza bei
ya sukari kuwa sh. 1700, lakini
kuikuta dukani ikiuzwa sh. 2500
hadi 3000. Kwake hilo analiona
kuwa ni walanguzi kupindisha na
kuvunja sheria, kudharau nguvu
na mamlaka ya serikali na dola
kwa ujumla wake, jambo ambalo
anataka kuwaaminisha watu
kuwa lisingeweza kutokea enzi za
Nyerere.
Hata hivyo, tofauti na wakati
wa Nyerere, serikali ya sasa haina
kawaida ya kutangaza bei. Hata
kama ilitangaza bei ya sukari
wakati fulani, haikutangaza
kuwa bei hiyo ni ya kudumu na
haitabadilika hivyo hakuna la ajabu
sana ikibadilika. Pamoja na hayo,
wahalifu hawawezi kukosekana
hivyo kukiuka bei iliyotangazwa
na serikali sio jambo la kushangaza
sana. Kama hilo linamshangaza
mwandishi, basi wakati wa Nyerere
angeshangaa zaidi.
Wakati wa Nyerere kulikuwa na
Tume ya Bei iliyokuwa na jukumu
la kupanga bei karibu kwa kila
bidhaa na kusimamia utekelezaji
wake. Hata hivyo, ilika wakati

wananchi wakaibatiza tume hiyo na


kuiita Timua Bei badala ya Tume
ya Bei.
Ilibatizwa jina hilo kwa sababu
licha ya kuwepo kwake, bidhaa
nyingi zilikuwa zikiuzwa kwa
mwendo wa kuruka yaani bei
kubwa kuliko ambavyo leo mtu
anaweza kukiria. Mfano: Kuna
wakati bei iliyopangwa na serikali,
kupitia Tume ya Bei, ya mafuta ya
taa ilikuwa sh. 4.20 kwa lita lakini
ilikuwa kawaida kuona mafuta
hayo yakiuzwa sh. 20.00 kwa chupa
moja ya cocacola yenye ujazo wa
mililita 300 yaani sawa na sh. 66.00
kwa lita au zaidi ya mara 15 ya bei
halali.
Kwa mujibu wa maoni ya
mwandishi, mfumo wa uongozi
uliopo sasa hauwezi kuakisi
matakwa ya watu wengi kwa
misingi imara ya kidemokrasia
kwani itikadi za vyama na siasa
katika uchaguzi ndiyo zinachukua
sura ya utawala nchini. Ingawa
kwa kiasi kikubwa nakubaliana
na maoni yake, lakini ni muhimu
tukumbuke kuwa kwa sasa
demokrasia imeimarika sana kuliko
wakati wa awamu ya kwanza.
Hata hayo mwandishi aliyoandika,
asingeweza kuyaandika katika
awamu ya kwanza akawa na hakika
ya usalama wake.
Wakati wa awamu ya kwanza na
ya pili raisi hakuwa na mpinzani
na mfumo uliokuwapo ulikuwa
unamhakikishia kupata zaidi ya
90% za kura. Nakumbuka wakati
mmoja waalimu wa shule ambayo
ilikuwa mojawapo ya vituo vya
kupigia kura walilazimishwa,
na watu waliosadikiwa kuwa
ni Usalama wa Taifa, kuandika
maelezo chini ya usimamizi mkali,
kama vile wako kwenye mtihani,
kuhusu sababu za raisi kupata kura
za hapana 10% ya kura zilizokuwa
zimepigwa katika kituo hicho.
Kiwango hicho kilionekana
kikubwa mno kiasi cha
kuishughulisha serikali na vyombo
vyake. Maelezo waalimu hao
waliyotakiwa kutoa yalilenga
kuwajua wenye mawazo
yanayopingana na ya raisi, chama
na serikali, jambo ambalo kwa
wakati huo lilikuwa karibu sawa
na uhaini. Baada ya maelezo,
karatasi zilikusanywa na hadi leo
miongoni mwao hakuna anayejua
kilichofuatia.
Kwa upande wa wabunge na
madiwani, wananchi walikuwa
wanapewa fursa ya kuchagua
mtu mmoja kati ya wawili tu
walioteuliwa na chama. Hadi
hapo, hata mwenye akili za
kawaida anaweza kuona kuwa
tayari sehemu kubwa ya uchaguzi
inakuwa imeshafanyika na matokeo
kutabirika hata kwa 80%.
Kitendo tu cha kumwekea
mgombea mpinzani dhaifu kwa
makusudi na alama inayopendwa
zaidi, kati ya jembe na nyumba
kwa wabunge, au kuku na yai kwa
madiwani, kilimpa nafasi kubwa ya
ushindi. Utati unaonyesha kuwa
75% ya waliokuwa wakishinda
katika uchaguzi wa wabunge ni
wale waliokuwa wakitumia alama
ya jembe. Kwa ujumla, chaguzi
za sasa zinaakisi matakwa ya
watu kuliko za enzi za Nyerere
mwandishi anazotamani au
kujifanya anazitamani.
Katika gazeti la Dira toleo namba

Inaendelea Uk. 16

Tangazo

AN-NUUR

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 20 - 26, 2016

Bismillahir Rahmaanir Rahiim

ISLAMIC PROPAGATION CENTRE

NAFASI ZA KIDATO CHA TANO - 2016/2017

KIRINJIKO ISLAMIC HIGH SCHOOL

UBUNGO ISLAMIC HIGH SCHOOL

NYASAKA ISLAMIC HIGH SCHOOL

Waislamu kote nchini mnatangaziwa nafasi za Kidato cha Tano kwa shule zifuatazo:

Ubungo Islamic High School


Kirinjiko Islamic High School
Nyasaka Isamic High School

Dar es Salaam : 0687 820895/0657 350172


Same, Kilimanjaro: 0784 296424/0756 676441
Mwanza: 0786 417685/0713 749020

Shule hizi ni za Kiislamu zenye lengo la kuwapa wanafunzi taaluma ya hali ya juu na malezi
bora ya Kiislamu. Shule hizi ni za BWENI za mchanganyiko wa wavulana na wasichana.
Zipo Combinations zote za SAYANSI, ARTS na BIASHARA.
Muombaji awe na ufaulu wa masomo matatu (3) kwa kiwango cha Credit (yaani A, B na C)
Daraja la III (Division three) au zaidi na Grade D kwenye masomo ya Combination.

Mwisho
nini
tarehe
30/05/2016
Mwishowa
wakurudisha
kurudishafomu
fomu
tarehe
02/05/2016.

Fomu za maombi zinapatikana kwa gharama ya Shilingi 10,000= katika Tovuti:www.ipcorg.tz na katika vituo vifuatavyo:

ARUSHA: Ofisi ya Islamic Education Panel, Jambo


Plastic, Ghorofa ya 2 mkabala na Msikiti Mkuu
Bondeni : 0783 438676/0715 438676.
KILIMANJARO: Moshi: Msikiti wa Riadha:07673453

67/0686938077. Same Juhudi Studio mkabala na


Benki ya NMB Same: 0757 013344. Same: Kirinjiko
Islamic Secondry School: 0784 296424/0713
115041. Usangi- Falhum Kibakaya : 0787 142054.
Ugweno Simbomu centre Mwl. Hidaya A. Mussa:
0784 656514
TANGA: Twalut Islamic Centre Mabovu
Darajani : 0715 894111/0713 014469. Uongofu
Bookshop: 0784 982525. Korogwe: SHEMEA
SHOP : 0754 690007/071569008. Mandia Shop
- Lushoto: 0782257533. Handeni Mafiga -0782
105735/0657093983
MWANZA: Nyasaka Islamic Secondary School : 0717
417685/0786 417685. Ofisi ya Islamic Education
Panel Mtaa wa Rufiji mkabala na Msikiti AlAmin 0785 086 770/0714097362.
BUKOBA: Ofisi ya Kutaiba Saccos: 0765 748056
MUSOMA: Ofisi ya Islamic Ed Panel -Mtaa wa
Karume,Nyumba Na. 05 : 0765024623/0787868611
SHINYANGA: Msikiti wa Majengo karibu na Manispaa
ya Shinyanga Mjini :0655608139/0768895484

KAHAMA: Ofisi ya Kamati ipo karibu na zahanati ya

Doctor Dalali: 0754 994738/0782 994738

Dar es Salaam: Ubungo Islamic High School : 07


56584625/0657350172/0712 033556. Ofisi ya
Islamic Ed. Panel Temeke -Msikiti wa Nurul Yakin
: 0655144474/0787119531
MOROGORO: Wasiliana na
Ramadhani Chale :

0715704380. Ifakara wasiliana na Mwl. Sharifu:


0659 158958
GEITA: Ofisi ya Kamati karibu na mashine ya
kukobolea mpunga shilabera: 0765 748056
DODOMA: Hijra Islamic Primary School

488444/0653 705627.
MTWARA: Ofisi ya Islamic Education Panel,
Mtaa wa Magomeni A mkabala njia panda ya
uwanja wa ndege: 0715 465158/0787 231007.
SONGEA: Kwa Kawanga Karibu na Msikiti wa
NURU : 0713249264. Mkuzo Islamic High
School :0654 876317
MBEYA: Ofisi za Islamic Education Panel Uhindini
0785425319. Rexona Video mkabala na
Mbeya RETICO: 0713 200209/0785425319.
Rukwa: Sumbawanga:Jengo la Haji Said
Shule ya Msingi Kizwike: 0757090228/0786
313830
TABORA: Kituo cha Kiislamu Isevya:
0784
944566/0718 556355. Nzega - Dk. Mbaga-0754
576922/0784576922.
IRINGA: Madrastun Najah: 0714 522 122.
PEMBA: Wete: Wete Islamic School : 0777
432331/0712772326.
UNGUJA: Madrasatul Fallah: 0777125074.
PANDU BOOKSHOP 0777462056 karibu na
uwanja wa Lumumba

: 0716
544757/0718661992
SINGIDA: Ofisi ya Islamic Education. Panel
karibu na Nuru snack Hotel : 0786
425838/0784 928039.
MANYARA: Ofisi ya Islamic Ed. Panel Masjid
Rahma: 0784491196
KIGOMA: Msikiti wa Mwandiga: 0714717727.
Kibondo Islamic Nursery School:
0766406669. Kasulu: Murubona Isl.SS:
0714710802/0763 298440
MAFIA: Ofisi ya Ust. Yusufu Ally jirani na
LINDI: Wapemba Store: 0784 974041/0783
msikiti mkuu : 0773580703.

WAHI KURUDISHA FOMU ILI UJIHAKIKISHIE NAFASI


FORM V TANGAZO.indd 1

4/18/2016 5:23:55 AM

10

Makala

AN-NUUR

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 20 - 26, 2016

Kikata utamu hakina hodi

Fanyeni kazi kabla hamjalazwa hapa


Nendeni mkafanye
kazi kabla hamjaja kulala
hapa.
Ilikuwa ni nasaha na
kauli ya mwisho ya Juma
Mustapha Msenguzi kwa
watu waliokuwa karibu
naye.
Aliitoa kauli hiyo
akiwaambia Suleiman
Daudi na Dr. Swalehe
Juma Nyumba.
Ilikuwa ni saa 3 usiku
Ijumaa, Mei 6, 2016
ambapo wawili hao
walimpitia hospitali
Msenguzi kumjulia hali
na kumuaga kuwa kesho
yake wangesari kwenda
Iringa kufanya semina ya
Kamati ya Wataalamu wa
Afya.
Dr. Swalehe Juma
Nyumba ni Amri wa
Kamati ya Wataalamu
wa Afya (Taifa) chini ya
Kamati ya Kuendeleza
Uislamu.
Nendeni mkafanye
kazi kabla hamjaja kulala
hapa.
Ilikuwa ni kauli fupi
ya Juma Mustapha
Msenguzi akiwatizama
Suleiman Daudi na Dr.
Swalehe Juma Nyumba,
kwa jicho la kuagana nao
lakini pia kuwahimiza
kutumia vyema neema ya
uhai na afya.
Na kweli ilikuwa ni
usia na kauli ya kuagana
kwani kilichofuatia ni
wasari hao kushiriki
kumuosha na kumkani
Msenguzi kabla ya
mazishi yaliyofanyika
Magugu, Babati Alhamisi
Mei 12, 2016 saa 3
asubuhi.
Ilibidi warejee kutoka
Iringa baada ya kuwakia
habari kwamba Juma
Mustapha Msenguzi
amefariki usiku wa
Jumanne Mei 10.
Siku moja kabla ya
kukutana na kutoa

JUMA Mustapha Msenguzi (kushoto) wakati wa uhai wake.

PICHA juu ni mwili wa marhuum Juma Mustapha Msenguzi


ukipelekwa mazikoni na waumini. Chini baada ya mwili huo baada
ya kuzikwa.

usia kwa Dr. Jumba


na Suleiman Daudi,
Msenguzi aliwaita
viongozi wenzake wa
Kamati ya Kuendeleza
Uislamu Singida waje
hospitali Dodoma

waongee.
Hiyo ilikuwa tarehe
5 Mei, 2016 na katika
mambo aliyotaka kujua
ni namna kila mmoja
wao anavyotekeleza
majukumu yake katika

yale waliyokubaliana
kufanya.
Na kubwa ilikuwa
kupatikana fedha na
kuhakikisha kuwa maji
yanapatikana katika
kituo chao cha mkoa
walichokuwa wakijenga.
Mpango ilikuwa
wapate maji ya uhakika
ndio wapate kuitisha
tamasha la kitaifa kama
inavyofanyika katika
mikoa mingine.
Kwa bahati mbaya
katika kikao kile
ilionekana kwamba
hakuna hatua iliyokuwa
imepigwa katika
kutekeleza jambo lile hali
iliyomfanya Msenguzi
kulia sana.
Mimi siwaambii
mnichangie pesa za
matibabu yangu,
nazungumzia pesa
kwa ajili ya Kituo cha
Kiislamu, ilikuwa
kauli yake kwa viongozi
wenzake.
Lakini alikuwa pia
ameongea na wakeze
wakiwa Singida ambapo
aliwahimiza kufanya kazi
za jamii (Uislamu) badala
ya kuja kumtizama
kwani Dodoma yupo na
Waislamu.
Hata hivyo, aliona haki
ya wakeze kuja kumuona
na akawapa maelekezo
ya kuja kwa zamu, hata
hivyo akafariki kabla
hawajaja kumuona.
Juma Mustapha
Msenguzi alizaliwa
mwaka 1976 Magugu,
Babati mkoa wa Manyara
na kupata elimu yake ya
Msingi huko huko (19871994).
Kati ya mwaka 1996
hadi 2003 alikuwa
mwanafunzi katika Chuo
cha Kiislamu, maarufu
Markaz Changombe,
jijini Dar es Salaam,
Inaendelea Uk. 11

11

MAKALA

AN-NUUR

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 20 - 26, 2016

Fanyeni kazi kabla hamjalazwa hapa


Inatoka Uk. 10

ambapo alihitimu katika


kiwango cha Thanawi
(sekondari).
Kutokea hapo akawa
anafanya shuguli za
kidini ikiwa ni pamoja
na kuendesha madrasa
Babati na Singida.
Hadi anafariki
alikuwa Amri wa
Kamati ya Kuendeleza
Uislamu mkoa wa
Singida, halikadhalika
Amir wa Kanda ya Kati
inayojumuisha mikoa
ya Singida, Manyara na
Dodoma.
Katika jumla ya
miradi mikubwa
aliyoacha katika hatua
za kukamilika ni ujenzi
wa Kituo cha Kiislamu
cha Mkoa ambacho ndio
kilimtoa machozi baada
ya kuona sipidi inakuwa
ndogo na kuingia dalili
ya uzembe na uvivu.
Alianza kuugua kiasi
miezi mitatu iliyopita
na wiki kadhaa kabla
ya kifo chake alikwenda
Dodoma kufanyiwa
vipimo zaidi ambapo
iligundulika kuwa
alikuwa na tatizo la go
(zilikuwa zimefeli).
Alilazwa katika
hospitali ya Chuo Kikuu
Dodoma (UDOM)
kitengo cha go na
mauti yakamkuta akiwa
hospitalini hapo.
Juma Mustapha
Msenguzi, zaidi ya
kazi kubwa alizofanya
akiwa Amir wa Mkoa
na Kanda, alikuwa
akishiriki matamasha
na semina mbalimbali
zilizokuwa zikihusisha
mikoa yote nchini na
hapo akitoa mchango
wake kwa kuwa mmoja
wa watoa mada na
kuendesha Darsa Duara.
Mazishi yake

MARHUUM Juma Mustapha Msenguzi (kushoto) akiwa na Amiri


Taifa Ustadh Mohammed R. Kassim.

WAUMINI mbalimbali wakiwa katika maziko ya Ustadh Msenguzi

WAUMINI mbalimbali wakiwa katika maziko ya Ustadh Msenguzi

yalihudhuriwa na umati
wa watu ambapo kutoka
Singida yalikuja mabasi
matatu huku wengine
wakija na magari binafsi.
Mikoa mingine
iliyoleta wawakilishi
katika mazishi ni Pemba
(Sheikh Salum Juma),

Unguja Amir Hamis


Hamad Omar huku
Mwanza wakija watu 20
wakiongozwa na Amir
wa Mkoa Ustadh Ninga.
Tabora walikuja watu
7 wakiongozwa na
Amir Adam Kusega,
Arusha watu 10, Iringa

aliwakilisha Amir
Dhulkii, Dar es Salaam
watu 5 wakiongozwa
na Amiri Taifa Ustadh
Mohammed R. Kassim,
Dodoma watu 6 na
Tanga ikawakilishwa na
Amir Khatibu Idd.
Juma Mustapha
Msenguzi ametangulia
mbele ya haki akiacha
wajane 2 na watoto
5-Innaalillaahi wainnaa
ilayhir rajiuun.
Hili suala ni la
kawaida, lakini
halizoeleki. Tupo
hapa duniani kwa
kazi maalum, nayo
ni kumtumikia Allah
(swt). Tupo kwa ajili
ya kuhakikisha kuwa
dunia inakuwa mahali
pa amani na furaha ya
kweli.
Hizo zilikuwa nasaha
za Amri Taifa Ustadh
Mohammed Ramadhani
Kassim katika maziko.
Wakati
tunamuuguza
marehemu, alisema
fanyeni kabla
hamjaka hapa kwa
sababu ukika hapa
(ukiwa mgonjwa)
huwezi kufanya tena.
Marehemu alisema
hayo akisisitiza tufanye
kazi hii ya Allah bado
tukiwa na neema ya
afya.
Aliongeza Amir,
ambapo kila mwakilishi
wakiwemo Msheikh
waliohudhuria
walikazia nasaha hizo
kwa kuwataka waumini
kushikamana na kazi
njema alizokuwa
akifanya marehemu.
Waongeze juhudi
na kufanya yote
watakayofanya kwa
Ikhlas wakitegemea
malipo kutoka kwa
Allah (SW).

12

MAKALA

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 20 - 26, 2016

Amina Abdallah Vs Nuseiba Mohamed


Inatoka Uk. 5

Katika kipindi hicho cha kuanza


ghasia Syria, mtandao wa Amina
ukawa ni moja ya vyanzo muhimu
vya habari vya kutegemewa na
vyombo vya habari vya Ulaya na
Marekani, na hata katika nchi za
Kiarabu. Mwandishi Katherine
Marsh wa gazeti la The Guardian,
la Uingereza akimsia Amina na
mtandao wake akasema kuwa huyo
ni mwanamke wa shoka, shujaa
aliyethubutu kukata minyororo
ya mila potofu za Kiarabu.
Mwanamke mkweli aliyejitokeza
kupigania haki za raia wa Syria
bila kuhoa kujitangaza kwamba
yeye ni shoga wa kike. Kwa
hiyo anastahiki kuungwa mkono.
(Tazama: Marsh, Katherine (6 May
2011). "A Gay Girl in Damascus
becomes a heroine of the Syrian revolt".
The Guardian (London).)
Magazeti makubwa ya
kuheshimika kama The New York
Times, yakamsifu Amina Abdallah
Arraf kwamba ni mwanamama
mwenye uraia wa nchi mbili,
Syria na Marekani kwa sababu
Mama yake ni Mmarekani huku
baba yake akiwa Msyria. Katika
kumsifu zaidi The New York
Times wakasema kuwa Amina
ana mizizi mirefu ("very deep"
American roots) ya Kimarekani kwa
sababu yeye alizaliwa Staunton,
Virginia, Oktoba 1975 baba akiwa
ni Abdallah Ismail Arraf na mama
Bi Caroline McClure Arraf. Na
kwamba huyu babu McClures
alihamia Virginia kutoka Ulster
mwaka 1742. Katika kukamilisha
utambulisho wa Amina ikaandikwa
kwamba mababu wa Amina wa
upande huu wa kikeni, walipigana
vita ya mapinduzi ya Marekani
(American Revolution at Yorktown)
na hivyo huyu Amina ana haki ya
kujiita kuwa ni Binti wa Mapinduzi
ya Kimarekani-DAR [A Daughter of
the American Revolution]. (Mackey,
Robert; Liam Stack. "After Report
of Disappearance, Questions About
Syrian-American Blogger", The New
York Times, 7 June 2011)
Maelezo zaidi yakasema kuwa
familia yake ilihamia Syria wakati
Aisha akiwa na umri wa miezi sita
tu na kuishi huko kwa muda japo
baadae Aisha alirejea tena Marekani
mwaka 1982 na kukulia huko.
Vyombo vya habari vikimnukuu
Amina vinasema kuwa alijitambua
kuwa ni shoga wa kike akiwa
na umri wa miaka 15, lakini hiyo
haikumzuiya kuwa Muislamu.
Blog ilizidi kupata umaarufu
baada ya kuchapisha habari
kwamba Amina alivamiwa na
makachero wawili wakitaka
kumteka akiwa nyumbani kwao,
lakini baba yake akapambana nao
akawatimua. Amina akiandika
habari hiyo Aprili 26, 2011 katika
Blog yake aliipa kichwa cha habari:
"My Father the Hero."
Kutekwa nyara
Tarehe 6 Juni, 2011 vyombo
vya habari viliripoti kuwa Amina
Arraf alikuwa ametekwa na
makachero wa serikali ya Syria.
Katika kusherehesha tukio hilo
lililovyotokea, ikaandikwa kwamba
alitekwa saa 12 jioni wakati Amina

Tom MacMaster (kulia).


akiwa eneo la kituo cha mabasi
Abbasid (Abbasid bus station), mtaa
wa Fares al Khouri, katika jiji la
Damascus akienda kukutana na
baadhi ya wenzake ambao kwa
pamoja walikuwa wakiandaa
maandamano dhidi Bashar Assad.
Akiwa anatembea walitokea
askari watatu waliokuwa na silaha
wakamkamata na kuondoka
naye. Ikadaiwa kuwa tukio hilo
liliripotiwa na mtu aliyeitwa Rania
Ismail, ambaye ni katika ndugu wa
damu wa Amina. (Tazama: "Syrian
Lesbian Blogger Amina Abdallah
Missing In Damascus". Lez Get
Real. 2011-04-27.)
Baada ya habari hizo kusambaa,
zikawasha moto nyikani mchana
wa jua kali wakati wa kiangazi.
Vyombo vya habari vikaja juu,
wakitaka serikali ya Bashar
imwachie Amina. Zikatengenezwa
websites na Facebook pages
maalum kwa ajili ya watu kutoa
maoni yao na shinikizo kwa
Bashar halikadhalika kwa serikali
ya Marekani kuchukua hatua.
Watu zaidi ya 10,000 wakasaini
waraka uliotumwa katika mtandao.
Almuhimu kwa ujumla wake,
vyombo vya habari vikawa
vinapaza sauti kila kona vikimsifu
Amina na kuhimiza aachiwe
haraka. (Nassar, Angie (7 June 2011).
"A Gay Girl in Damascus blogger
kidnapped". NOW Lebanon.)
Kwa upande wake mwandsihi
Andrew Belonsky akiandikia
jarida linaloitwa-Death and
Taxes" akasema ni lazima serikali
ya Marekani itumie nguvu zake
kuhakikisha kuwa Amina Arraf
anaachiwa. Tarehe 7 Juni, 2011
White House kupitia U.S. State

AN-NUUR

Department (Wizara ya Mambo


ya Nje) ikatoa kauli ikisema
kuwa inalitizama jambo hilo na
kutafakari hatua za kuchukua.
(Tazama: 1. "Gay Girl in Damascus"
Kidnapped: How Should U.S.
Respond?". International Business
Times. (2) "'A Gay Girl in Damascus'
Blogger Kidnapped at Gun point in
Syria". FoxNews.)
Mpaka hapo mambo
bambam. Sasa subiri!
Amina Arraf al Omari hakuwa
mtu wa kweli. Habari zote
zilizosimuliwa hapa zilikuwa
za kutunga tu. Ulikuwa urongo
mtupu. Ilikuwaje?
Mtandao A Gay Girl In
Damascus, ulianzishwa na Tom
MacMaster na mkewe Britta
Froelicher. Wakajifanya ndio
Amina na kuingiza taarifa zote
hizo ambazo vyombo vya habari
navyo vilikuwa vinaziokota na
kuzisambaza.
Picha walizokuwa wakitumia
kuwa ni za Amina zilikuwa
za Jelena Lei, msichana wa
ki- Croatia, aliyekuwa akifanya
kazi Uingereza. (Tazama: Chuck,
Elizabeth (8 June 2011). "Londoner
says missing Syrian blogger stole her
identity". MSNBC. Addley, Esther;
Hassan, Nidaa (8 June 2011). "Syria:
Mystery surrounds 'Gay Girl in
Damascus' blogger abduction". The
Guardian (London). (30) Steger,
Isabella (8 June 2011). "Photos of
Syrian-American Blogger Called into
Question". Wall Street Journal.
Rudia kusoma makala hii
ukitizama jinsi habari ya Amina
ilivyokuwa ikipewa uzito katika

vyombo vya habari mpaka kuka


katika Bunge la Marekani na White
House. Kumbe yote hewa. Mambo
ya kutunga. Uwongo mtupu.
Lakini usisahau kuwa ni kwa
kutumia uwongo kama huo, Bashar
anapigwa, Syria imesambaratishwa.
Wapo watu leo hii, wakiwemo
Masheikh wa kuaminika na
wenye elimu zao, wanatoa
fatwa wakisema kuwa japo
IS wanapigania kusimamisha
Dola ya Kiislamu, lakini mambo
wanayofanya ni kinyume cha
Uislamu. Watatoa Aya na Hadithi.
Masikini ambacho hawafahamu
ni kuwa hoja ya msingi hapa
ni kuwa IS ni nani? Je, wapo
IS kama tunavyoambiwa na
wanavyowasilishwa kwetu kupitia
vyombo vya habari?
Wasichojua watoa fatwa hawa
na wanaodaiwa kuwa wachambuzi
wa BBC n.k. ni kuwa ISIS au
yeyote anayenasibishwa na wao
ni hao hao akina Tom MacMaster
na Britta Froelicher katika koti la
Amina Abdallah Arraf al Omari
na mtandao wao wa A Gay Girl In
Damascus.
Wasichana wa Nigeria wakipewa
majina ya bandia kama akina "Sa'a"
wanapelekwa Marekani kutoa
ushuhuda juu ya ukatili wa Boko
Haram (Waislamu wa Nigeria
Kaskazini) kwamba wanauwa
Wakristo, kuteka wasichana na
kuwafanya watumwa wa ngono
huku wengine wakiwavisha
mabomu wajilipue. Kutokana
na ushuhuda wa kina Saa, Bi
Frederica Smith Wilson (D-Fla.),
anasema:
"It appears as if genocide is
taking place" leaving a "whole
generation of children who are not
being educated because schools are
being destroyed.
Je, habari hizo ni za kweli? Je,
Abubakar Shekau (kiongozi wa
Boko Haram), ni mtu halisi au ndio
wale wale akina Amina Abdallah
Arraf al Omari aka A Gay Girl In
Damascus?
Ukisikia Al-Shabaab wameuwa
watu Garissa, hoja ya msingi ya
kuhangaika nayo sio kwamba
walilofanya linakubalika au
halikubaliki. Ni wazi halikubaliki
kwa vigezo vyote, iwe ni kidini,
kisiasa au vyovyote vile. Swali
ni je, nani Al-Shabaab? Je, ni
wale waliotokana na Umoja wa
Mahakama za Kiislamu au ni
wengine wa kutengenezwa na
akina Tom MacMaster?
Sasa ni hivyo hivyo, watasema
kuwa kina Aisha na Saleh
wana uwezo kutengeneza na
kushambulia kwa kimeta na
itapigwa propaganda mpaka
mtaamini. Hata maprofesa wa vyuo
vikuu walio wataalamu wa elimu
ya virusi-virolojia (virologists),
watapumbazika kwa propaganda,
kuamini na kutishika kuwa Bi
Nuseiba Mohammed Haji na
mumewe Mohammed Ali Abdi
wana uwezo wa kutengeneza bomu
la anthrax!
Huku kwetu ndio hayo hayo.
Sheikh Msellem Ali na wenzake
wapo ndani mwaka wa tatu sasa.
Hakuna kesi hakuna chochote. Kila
siku habari ni ileile uchunguzi
haujakamilika.

13

MAKALA

AN-NUUR

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 20 - 26, 2016

Chuki kamwe haitakuwa na maslahi kwenu


Na Shaban Rajab

CHUKI kusababisha hasidi


na uadui. Chuki wakati
mwingine humfanya mtu
kuwa mpumbavu. Chuki
humfanya mtu kuwa na kibri,
dharau, hasira, mbinafsi na
mwenye choyo. Mwenye
chuki, kila litakalomkia
kuhusu anayemchukia au
anachokichukia, liwe ni jambo
au kitu sahihi au chenye
kweli ndani yake, hata kama
kunadhihiri matiki na usahihi,
kwa msukumo wa chuki,
kwa mwenye nafsi ya chuki
jambo hilo litakuwa batili na
lisilokubalika kwake.
Kwa kifupi niseme tu
kwamba chuki ni maradhi
mabaya, ambayo hatma yake
ni mwenye nayo kupata hasara
na fadhaa. Chuki ya kijamii
inaonyeshwa kwa viwango
tofauti. Inaweza kuonyeshwa
kwa matusi au maneno yenye
kuumiza hisia au kwa jitihada
za kitaifa za kuangamiza jamii
nzima. Wale wanaokandamizwa
hawana mtu wa kuwafariji
huku wakandamizaji wakiwa ni
wenye nguvu.
Pamoja na kwamba viongozi
wa dini wamekuwa wakitajwa
kuwa ndio msingi wa kujenga
maadili, kutetea haki na
kulaani dhuluma katika jamii
na kwamba jamii pia ina utii
mkubwa kwa viongozi hawa,
lakini Dini na viongozi wake
wanaonekana hawajasaidia sana
kupinga chuki katika kijamii.
Ingawa baadhi ya viongozi
hao na baadhi ya wanaharakati
wa haki za kibinadamu
wanaelezwa kwamba
wamekuwa mashuhuri
kwa sababu ya kupinga
ukandamizaji, lakini kwa ujumla
viongozi wa dini wanaonekana
kuuunga mkono wakandamizaji.
Huko Marekani ambako
ubaguzi kwa watu weusi
uliungwa mkono kisheria
na kupigwa marufuku ndoa
kati ya weusi na weupe
kukiendelea hadi mwaka 1967,
lakini pamoja na sheria hizo
kuondolewa bado hata leo
kuna masalia ya vitendo vya
kibaguzi na unyanyapaa dhidi
ya watu weusi, wahamiaji na
watu wa jamii ya Kiislamu
vinavyoendelea kufanyika
kwasababu ya mazoea ya kuwa
na chuki tu.
Huko Afrika Kusini wakati
wa ubaguzi wa rangi, watu
wachache walipokuwa
wakidumisha mamlaka yao
kwa kutumia sheria ambazo pia
zilipiga marufuku ndoa kati ya
watu wa rangi tofauti, lakini
ajabu ni kwamba baadhi ya watu
waliounga mkono ubaguzi huo

Hanufaiki mwenye nayo


Wala anayechukiwa

walikuwa watu wanaoshikilia


sana dini.
Inashngaza kwa nini jamii
fulani zinakandamiza jamii
nyinginezo kwa chuki za
kiimani, huku wakiwa ni watu
wenye dini zinazohubiri upendo.
Yeye ambaye hapendi
hajamjua Mungu, kwa sababu
Mungu ni upendo. Yeyote
akisema: Mimi nampenda
Mungu, na bado anamchukia
ndugu yake, yeye ni mwongo.
Kwa maana yeye ambaye
hampendi ndugu yake, ambaye
amemwona, hawezi kuwa
anampenda Mungu, ambaye
hajamwona. (1 Yohana 4:8, 20).
Mistari hiyo katika Biblia
inaonyesha chanzo cha chuki
katika kijamii, kwamba
wanadini na watu wasio
wanadini, wanaonyesha chuki ya
kijamii kwa sababu hawajamjua
Mungu na hawampendi.
Tunajiuliza, inakuwaje na
viongozi wa dini wawe vinara
wa kueneza chuki kupitia
mafundisho yao, kiasi cha
kusababisha watu wa imani
nyingine kudhulumiwa,
kudharauliwa, waonewa na
wasipate kusikilizwa shida zao.
Viongozi wa namna hii inatia
shaka kama kweli wanampenda
na wanamjua kiasi cha wao
kuwa chanzo cha upendo kwa
wanajamii.
Leo hii kila kona duniani,
hususan katika mataifa ya bara
Ulaya na Marekani, jamii ya
Kiislamu inaonekana kama
wahalifu na wasiostahili kuwepo
duniani.
Kisa cha chuki yote hiyo ni
matokeo ya propaganda ya
uhalifu unaotokana na ugaidi,
ambao unanasibishwqa na
Uislamu na Waislamu.
Dhana hiyo hiyo imekuwa
kichocheo kikubwa cha
kuchukiwa jamii ya Waislamu
kila kona. Badala ya nguvu

kuelekezwa kupambana na
magaidi wawe ni Waislamu au
wasiokuwa Waislamu, nguvu
zinaelekezwa kupambana na
Waislamu kwasababu tu, imani
yao inanasibishwa na ugaidi.
Chuki ya kijamii inaonyeshwa
kwa viwango tofauti. Inaweza
kuonyeshwa kwa matusi au
maneno yenye kuumiza hisia
au kwa jitihada za kitaifa za
kuangamiza jamii nzima.
Chuki imekuwa sababu
kubwa ya jamii ya kushindwa
kuishi pamoja kwa amani na
upendo na kwa kuaminiana.
Leo watu wa jamii moja, wa
hadhi moja, wa imani moja
wanafurahia kuwakandamiza
wengine. Wanaokandamizwa
hawana wa kuwafariji huku
wakandamizaji wakiwa na
nguvu zao kama jamii na
wakitegemea pia ukimya wa
mamlaka kutokemea matendo
yanayotokana na chuki hizo.
Wakati hali ikiwa hivyo Dini
ambazo tunaamini ndizo msingi
wa haki, upendo, umoja na
ustawi wa maadili, hazionekani
kusaidia kupinga chuki hiyo ya
kijamii ambayo ni hatari kwa
usalama wa watu katika Mataifa
yao.
Pamoja na kwamba baadhi
ya watu wamekuwa mashuhuri
kwa sababu ya kupinga
ukandamizaji, lakini watu hao
wamekosa mchango unaostahiki
kutoka kwa viongozi wa dini.
Badala yake katika nchi nyingi
viongozi wa dini kwa kicho
cha ukereketwa wa dini zao
wamekuwa wakiwaunga mkono
wakandamizaji, huku wengi wao
wakilindwa na mamlaka.
Huko Marekani ambako
ubaguzi kuelekea watu weusi
uliungwa mkono kisheria. Watu
waliteketezwa kwa sababu ya
ubaguzi. Hata hivyo sheria
mbovu za mamlaka zilizokuwa
zinapiga marufuku ndoa kati

ya weusi na weupe, ubaguzi


wa rangi, jinsia, ziliendelea
kufuatwa hadi mwaka 1967.
Lakini kwa kuwa ubaguzi
ulishakolea na kuwa jambo la
mazoea, hadi leo kuna vimelea
vya kibaguzi nchini humo, hasa
dhidi ya weusi na watu wa jamii
ya Kiislamu na wahamiaji kwa
ujumla.
Huko Afrika Kusini wakati
wa ubaguzi wa rangi hadi
miaka ya 1990s, watu wachache
walipokuwa wakidumisha
mamlaka yao kwa kutumia
sheria mbovu ambazo zilipiga
marufuku ndoa kati ya watu wa
rangi tofauti na weusi kushiriki
siasa.
Hadi leo nako kuna mazoea
ya kibaguzi licha ya kwamba
tunaelezwa kuwa sera za
kibaguzi zilishaondolewa tangu
awamu ya kwanza ya uongozi
wa Hayati Nelson Mandela.
Lakini tumeshuhudia hivi
karibuni tu, wahamiaji nchini
humo wakiuliwa, wakichomewa
makazi yao nk, tena na weusi
wenzao. Yote hayo ni matokeo
ya wenyeji kuishi kwa miaka
mingi katika zama za chuki
na ubinafsi wa makaburu. Leo
miaka 35 Imepita lakini nafsi
ile ile ya chuki waliyokolezwa
na Makaburu bado wanayo na
wanaitumia dhidi ya wageni,
wenyeji wakijiona wao ndio
wenye mamlaka na haki dhidi ya
wengine.
Kila binadamu mwenye
nafsi na moyo, hakosi kuwa ni
mwenye kuchukia. Ni mojawapo
ya sifa za mwanadamu. Ni kama
ilivyo nafsi ya ubinafsi, kila
mtu ana sifa ya ubinafsi lakini
tofauti ni viwango vya ubinafsi
wenyewe.
Wapo wenye ubinafsi
uliopitiliza (excessive
individualism) kwa mfano
masadi. Watu wa namna hii
wapo tayari kutumia nafasi
zao katika jamii, kukomba na
kuhodhi kila kitu (kisichokuwa
chao) kwa kiwango wasichoweza
kukitumia kwa maslahi yao
tu na watu wenye haki na
walichohodhi wakateseka na
kuathirika.
Kadhalika hata kwenye sifa ya
chuki, mtu anaweza kuchukia
kwa heri, kwa maana kuchukua
uovu, dhuylma maasi nk. Lakini
wapo wenye chuki zilizopitiliza
za uadui na ubinafsi.
Mwenye chuki ya namna
hii yupo tayari kutumia
nafasi au mamlaka, mali,
nguvu au umashuhuri alio
nao kukandamiza, kupora na
kudhulumu haki za wengine
kwa sababu ya chuki yake tu
dhidi ya anaowachukia.
Kwa mfano kiongozi
Inaendelea Uk. 14

14

AN-NUUR

MAKALA/MASHAIRI

INNAA LILLAAHI WAINNAA ILAYHI RAAJIUUN


(HATUNAYE, AMIR MSENGUZI)
Kalamu i mkononi, taarifa kukupeni,
Si wengine Waumini, wa Bara na Visiwani,
Japokuwa ya huzuni, qadari ipokeeni,
MSENGUZI hatunaye, akhera katanguliya.

MSENGUZI kwa yakini, hatunaye duniani,


''Inna lillahi semeni, ''wainna'' kamilisheni,
Aula kwa Waumini, kunenavyo msibani,
MSENGUZI hatunaye, akhera katanguliya.
Tumewa kwa yakini, ndugu zangu Waumini,
Na Mwanakati makini, kwa harakati za dini,
Amir wa Waumini, kanda ya kati nchini,
MSENGUZI hatunaye, akhera katanguliya.
ABUU NYAMKOMOGI

UFU KWETU MTIHANI!


Namhimidi Qahari, kifo alotuumbiya,
Kwa kheri na si kwa shari, japo tunakichukiya,
Thineni aya nambari, MULKU ebu rejeya,
Ufu kwetu mtihani, na mizani ya mwenendo!
Kwa mwenye njema nadhari, kwayo atazingatiya,
Mauti kwetu indhari, na mtihani sawiya,
Lengo mwendo tughairi, wetu katika duniya,
Ufu kwetu mtihani, na mizani ya mwenendo!
Kwa ya shari kuhajiri, kwa ya kheri kuhamiya,
Yaso dini idamiri, kwa ya dunia daniya,
Au yenye kutughuri, ya hawaa za duniya,
Ufu kwetu mtihani, na mizani ya mwenendo!
ABUU NYAMKOMOGI

SWADAKTA, MBUNGE WA MAFIA!


(MH.RIZIKI BINT SHAHARI)

Riziki nakupongeza, kwa uloinena kweli,


Kadhia ulodokeza, si ya puya ni ya kweli,
Hukutaka kuchagiza, kwa kuipamba kwa kweli,
RIZIKI 'menena KWELI, MASHEKHE kosalo nini?
Ni haki uloeleza, kwa kila mpenda kweli,
Kwa hilo anokubeza, si mwingine mcha kweli,
Aso na njema ruwaza, ila ya kupinga kweli,
RIZIKI 'menena KWELI, MASHEKHE kosalo nini?
Hukutaka kwendekeza, habari ziso za kweli,
Au umma kuukwaza, kwa kuipindua kweli,
Ama dira kupoteza, kwa kuikiuka kweli,
RIZIKI 'menena KWELI, MASHEKHE kosalo nini?
Hukutaka kwao 'izza', kwa kukengeusha kweli,
Wala kujipendekeza, kwa wapinzani wa kweli,
Ukweli ukawajuza, lengo isimame kweli,
RIZIKI 'menena KWELI, MASHEKHE kosalo nini?
Kuna wataokubeza, kwa kuitongoa kweli,
Pamwe na kwa kuuliza, Bungeni jambo la kweli,
Mengi watahanikiza, dhidiyo yaso ya kweli,
RIZIKI 'menena KWELI, MASHEKHE kosalo nini?
MDINI nakueleza, watakuita kwa kweli,
Mambo uloyauliza, wajibu kama si kweli,
Wasanze kuhanikiza, dhidi yako yaso kweli,
RIZIKI 'menena KWELI, MASHEKHE kosalo nini?
Ninotaka kukujuza, kwa kuitongoa kweli,
Maadui 'meongeza, kosalo kulonga kweli!
Kwa ulimwengu wa giza, adui msema kweli!
RIZIKI 'menena KWELI, MASHEKHE kosalo nini?
Adharusi endeleza, dhidi ya wakana kweli,
Wasaka tonge na 'feza', na vyeo viso vya kweli,
Hata wakikupuuza, ALLAH shahidi wa kweli,
RIZIKI 'menena KWELI, MASHEKHE kosalo nini?
Akudumishe MUWEZA, katika kunena kweli,
Pamwe na kuwahimiza, wengine kunena kweli,
Mwisho ninakupongeza, kwa kuikashifu kweli,
RIZIKI 'menena KWELI, MASHEKHE kosalo nini?
ABUU NYAMKOMOGI

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 20 - 26, 2016

Chuki kamwe haitakuwa na maslahi kwenu

Inatoka Uk. 13
wa serikali, chama,
taasisi, shirika au
Jumuia akimchukua
mwanachama au mjumbe
au mfanyakazi, au hata
kiongozi mwenzake, kwa
chuki yake yupo tayari
kutafuta mbinu yeyote
ovu ya kumtia adabu
anayemchukia.
Na mara nyingi
mwenye chuki katika
maeneo haya hutumia
zaidi tna na majungu
kama njia ya kicho
inayoweza kuitumika
kumdhoosha

unayemchukia.
Hatma yake
anayechukiwa, bila
sababu za msingi
anaweza kufutwa kazi,
kusimamishwa kazi,
kupunguzwa cheo,
kunyanganywa mali
zake au kulisiwa
na wakati mwingine
hata mauaji yanaweza
kufanyika.
Polisi akimchukia
mtuhumiwa, atamtia
mateke, virungu na
kumtesa kwa kila kila
namna ili kukidhi kiu
yake ya chuki kwa

Ilunga miaka miwili


Msenguzi kafuatia
Bismilahi awali, kwa jinalo naanzia,
Allah asiye mithili, mamboye kujifanyia,
Katumiliki jalali, ya akhera na dunia,
Ilunga miaka miwili, Msenguzi kafuatia.
Ilunga miaka miwili, kwa Rabuka kurejea,
Aliifunga kauli, mauti kumkia,
Ametinga ziraili, na Juma kumchukua,
Ilunga miaka miwili, Msenguzi kafuatia.
Wito huu ni muhali, kiumbe kuukataa,
Hata uwe na vibali, vya wote wanasheria,
Vyovyote hii ajali, hakuna wa kuzuia,
Ilunga miaka miwili, Msenguzi kafuatia,.
Ni mwezi mei ya kweli, mwenzenu
nakumbukia,
Tarehe tano kamili, Ilunga alipotea,
Juma kafunga kauli, na yeye katangulia,
Ilunga miaka miwili, Msenguzi kafuatia.
Juma kijana jamili, dini alishikilia,
Akenda kila mahali, ya Allah kutuambia,
Vijana hawa ni ghali, wengi wapo na dunia,
Ilunga miaka miwili, Msenguzi kafuatia.
Awasamehe jalali, pale walipokosea,
Na azidishe amali, yale waliopatia,
Aikinge yao miili, na moto wa kubabua,
Ilunga miaka miwili, Msenguzi kafuatia.
Nausia tafadhali, wale wapenda dunia,
Vya haramu vya halali, vyote wanafakamia,
Hawatoweka kufuli, roho zao kuzuia,
Ilunga miaka miwili, Msenguzi kafuatia.
Wengine ni madhalili, wa nafsi nawambia,
Wafanya mbaya amali, huku wakichekelea,
Wanaleta ufedhuli, wenzao wakijia,
Ilunga miaka miwili, Msenguzi kafuatia.
Yailahi yaqahhari, mikono ninainua,
Ewe ajuaye siri, nakukishia dua,
Dunia ina ghururi, tukinahishe sawia,
Ilunga miaka miwili, Msenguzi kafuatia.
Mwl. Zabibu I. Ngonda
Mwanza.

anayemkamata.
Kwa nafasi yake,
atafanya ghiliba za kila
namna kumtia mtu ndani
na kuzuia dhamana,
atambambikia kesi
isiyomhusu mtuhumiwa.
Ataandika maelezo ya
uongo kwa mtuhumiwa
na kwa nafasi yake
ya kuwa mtendaji
wa chombo cha dola,
hakuna wa kumhoji wala
kumkosoa. Yote hayo
atayafanya hata kama
anakiuka sheria.
Kwa kuwa mwenye
chuki mara zote
hufanya uovu wake kwa
kicho ili isifahamike
dhahiri kwasababu
uovu anaofanya hauna
mashiko ya haki, yupo
tayari kumdhuru
mwenzake na kutimiza
matakwa yake hata
kwa kutumia njia za
kishirikina. Hawa kwa
chuki tu, wapo tayari
hata kuua.
Hata hivyo chuki
mbaya zaidi kwa
wanadamu ni ya kidini.
Kwa bahati mbaya
chanzo cha chuki hii
kwa watu a imani tofauti
ni viongozi wa dini na
viongozi wa serikali.
Hawa ndio wamekuwa
wachochezi na walezi
wakubwa wa chuki hii
miongoni mwa wananchi
ambao wanaamini katika
imani tofauti.
Mafundisho potofu ya
viongozi wa imani moja
dhidi ya imani nyingine
yamechangia sana
kuongezeka viwango
vya chuki kwa watu.
Upendelao wa viongozi
na watendaji wengi wa
serikali kwa wananchi
kwa misingi ya imani
zao, nako kumechochea
muendelezo huu wa
chuki na sasa imekuwa
ni ugonjwa sugu nchini.
Chuki imetokea
kuwa adui mkubwa
kabisa ambaye tunaishi
naye, tunatembea naye
na tunalala naye na
kushauriana naye kila
kukicha. Chuki hii ni
nafsi iliyojaa uadui
uwovu na majivuno,
yakiambatana na kiburi
na kutafuta kukomoana,
pasipo sababu za maana.
Nafsi ya chuki
ikichukua nafasi kubwa
katika tabia ya mtu,
ikakita mizizi yake
kwenye nafsi zetu basi
huondoa mfungamano
wa kiraki na kindugu
na hata majadiliano baina
ya watu hukosa busara
na hekma, kiasi cha
kusababisha utengano na
uhasama.
Itaendelea toleo lijalo

15

MAKALA

AN-NUUR

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 20 - 26, 2016

Uislamu kiumbe hai cha ajabu


Na Juma Jumanne

KWA muda mrefu sasa


kumekuwa na mkwamo wa
kiakili miongoni mwa baadhi
ya Waislamu na wasiokuwa
Waislamu juu ya ukongwe wa
kiumbe Uislamu. Kiumbe huyu
wa ajabu na mkongwe kabisa,
amekuwa akishughulisha akili
za watu wanaodai kumkubali
(Waislamu) na wasiokuwa
Waislamu. Pamoja na Waislamu
kudiriki kutamka ukongwe
wa kiumbe huyu, wengi wao
bado wanaamini kwamba,
Uislamu amekuja nao mtume
Muhammad (swalallahu alayh
waalihi wassalam). Wasiokuwa
Waislamu wao wanapinga na
kukataa moja kwa moja kuhusu
ukweli huu wa ukongwe wa
uislamu.
Makala hii haikusudii kuleta
mjadala katika nukta hii lakini
si vibaya tukapeana japo kwa
uchache kwa kuwa leo tupo,
kesho hatupo. Nikupeni mfano
mdogo tu ambao utaondoa
ule mgando wa ubongo katika
kulitazama jambo hili. Kwa kila
aliyejaaliwa kuwa na macho
salama yanayofanya kazi yake
ya kuona, na akapewa akili ya
kuweza kutofautisha baina ya
viwili; usiku na mchana bila
shaka anafahamu ni wakati
gani nyota hujidhihirisha
(huonekana). Wote
mtakubaliana nami kwamba,
nyota huonekana wakati wa
usiku.
Pamoja na ukweli huu,
haimaanishi kuwa mchana
hakuna nyota, la hasha! Nyota
zipo muda wote masaa ishirini
na nne (24) lakini huonekana
usiku. Kwa maana hiyo, nyota
zinaonekana kwa muda wa
takriban masaa 12 na hujicha
(hazionekani) kwa masaa 12
mengine. Hebu tujaalie kwamba,
kipindi cha kuchomoza jua
mpaka kuzama kwake na
kufanya nyota zionekane,
inatosha umri wa mtu mzima.
Mtu mzima ambaye ana akili
zake timamu na mwenye uwezo
wa kuoa/kuolewa.
Mtu mzima huyu aliyezaliwa
punde tu baada ya kuchomoza
jua, itakapoka jioni (jua
likizama) ataona nyota. Toka
azaliwe mtu mzima huyu
hajawahi kuona nyota, ndio
kwanza anaziona tena nyingi
kabisa angani. Swali langu la
msingi ni je, mtu huyu akisema
kwamba yeye ndio wa kwanza
kuona nyota atakuwa sahihi? Na
je, akisema kwamba hapajawahi
kuwepo nyota hapo kabla
atakuwa sahihi?
Mtume Muhammad
(swalallahu alayh waalihi
wassalam) amesema; tafakari
juu ya viumbe (maumbile)
aliyoumba Allah (subhanahu
wa taala), wala usitafakari juu
ya Allah. Kupitia maumbile
aliyoumba Allah aliyetukuka
tunapata kujifunza mambo
mbalimbali. Nyota ni katika

maumbile hayo. Tumia vema


akili yako!
Kimsingi zipo sababu
nyingi na ni za kihistoria za
kutokubalika Uislamu na wengi
miongoni mwa wanadamu. Ni
za kihistoria kwa sababu kiumbe
Uislamu kama tulivyotangulia
kusema, ni mkongwe, hivyo
hata sababu za kupingwa kwake
ni kongwe. Hakuna jambo
jipya ambalo labda kuna zama
halikusemwa na kusemwa katika
zama zingine. Ustaarabu wa
kiumbe huyu ni wa kihistoria.
Ipo sababu moja kubwa
ambayo inamfanya kiumbe huyu
kuonekana tatizo. Si kwa jingine
bali ni kwa ule uwezo na ujasiri
wake wa kutumia vema neema
alizopewa. Milango mitano ya
fahamu tuliyoitaja ni miongoni
mwa neema hizo. Uwezo wake
wa kuzungumza, akili yake ni
katika neema pia alizokuwa
nazo. Kwa ustaarabu aliokuwa
nao kiumbe Uislamu, hana
kawaida ya kuvumilia kuona
mambo yakifanywa ndivyo
sivyo akanyamaza asiseme.
Ni lazima aseme. Anaposema
ukweli, kama waswahili
wasemavyo kwamba ukweli
unauma, ndipo anapoonekana
analeta vurugu. Anaonekana
kuingilia taratibu za watu.
Lakini kwa kuwa kiumbe
huyu siyo bubu, ana macho
yenye siha njema hawezi
kukaa kimya asiseme. Ujasiri
huo wa kusema anao. Kiumbe
huyu, huridhika kuona kila
kitu kikipewa hadhi au sifa
stahiki. Hawezi kukaa kimya
kwenye sehemu inayotoa harufu
mbaya wakati anayo pua na
anafahamu kazi ya pua. Hawezi
kutulia akinywa, kupigwa au
kuumizwa kwa namna yoyote
ile hali ya kuwa ana ngozi
ambayo humuwezesha kuhisi.
Anatambua kazi ya ngozi ni nini
na wapi itumike.
Kiumbe huyu hana kawaida
ya kujifananisha. Leo hii, watu
kwa kujifanya wanakwenda
na wakati na kwa kuogopa
kuonekana washamba, hujidai
wakijua kila jambo. Akika
hotelini anaweza akaagiza
chakula chochote bila ya
kuomba msaada wa maelekezo
ili ajue ni kitu gani hicho.
Anaweza akaagiza pilipili kwa
kumuiga raki yake wa kichina,
ambapo Wachina pilipili kwao ni
kitu cha kawaida. Atajilazimisha
kula ilimradi tu, asijulikane
mshamba. Ushamba upi
mkubwa kuliko huo!! Uislamu
hauna ushamba huo.
Uislamu upo wazi na
unamtaka kila mtu kuwa muwazi. Uislamu una akili, una
mdomo, ulimi na ngozi pia.
Kwa akili hiyo hiyo, Uislamu

MAHUJAJI wakiwa katika vilima vya Safa na Marwa.


utatumia mdomo kuuliza
jambo ambalo ni geni kwake.
Kwa kuwa una ulimi na ngozi,
huwezi kuvumilia kuumia kwa
kuchelea kuonekana mshamba.
Uislamu unatambua kwamba,
kutokuuliza kwa kuogopa
kuonekana mshamba ndio
ushamba wenyewe. Haya ni
katika mambo yanayofanya
Uislamu uonekane ni tatizo
katika jamii.
Kiumbe Uislamu hawezi
kukaa kwa amani kwenye
maeneo yanapozungumzwa
maovu. Kwa kuwa anasikia,
hawezi akakaa maeneo hayo
labda kwa kuondosha hizo
kelele au kujaribu kuziondosha.
Atakapojaribu kuzuia starehe
hizo za watu kufanya maovu,
kiumbe huyu huonekana ni
tatizo. Anaharibia watu mambo
yao.
Kiumbe huyu hawezi
kunyamaza kuona mtu
akipigwa, akidhalilishwa na
kuuliwa tena bila ya hatia
yoyote.
Kama ilivyo kwa pombe
(kilevi), ambapo wingi na
uchache wake ni haramu.
Wingi na uchache wa kitu
huwezi kubadilisha asili ya
kitu ama jambo husika. Ukweli
huu unapowekwa wazi,
kinachofuatia ni masaibu kwa
kiumbe huyu. Ndio tunaona leo
kiumbe huyu anazidi kupigwa
vita kila kona ya dunia. Lakini
hili wala siyo jambo la ajabu
kwa kuwa, historia inaonesha
kwamba kila zama kulikuwa
na wapotofu wengi kuliko
waliomkubali kiumbe huyu.
Nabii Yunus (alayh salaam)
ndiye aliyepata bahati ya watu
wake kumkubali japo ni baada
ya misukosuko mingi.
Haya madhila anayofanyiwa
kiumbe huyu, ni katika namna
ya kujaribu kumziba milango
yake ya fahamu isifanye kazi.
Walichosahau maadui wa
kiumbe huyu ni kwamba,

hawawezi kuzuia akili ya


kiumbe Uislamu isifanye kazi.
Namna nzuri na ya kipekee
ya kumpiga vita kiumbe huyu
ni kuondoa mzoga na uvundo
uliowekwa chumbani ili aingie
ndani alale. Ukimlazimisha
kuingia ndani na kumfungia
mlango asitoke anaweza
akavunja mlango wako, dirisha
lako na au akachimba chini
kwa chini akatoka. Utamuita
mkoro kwa jambo ambalo
umesababisha wewe. Pua yake
inafanya kazi vema.
Ukimshika mikono
ukamfunga kamba na
kumlazimisha aangalie uovu
unaoendelea mahali popote
pale utachoka mwenyewe.
Utachoka kwa sababu hatatulia.
Atafurukuta na huenda akaikata
kamba yako ukamuona mkoro
na ni tatizo. Macho yake ni sa,
hivyo hayuko tayari kuangalia
uchafu na uozo.
Masikio ya kiumbe huyu, siyo
antenna au ungo, bali ni kwa ajili
ya kusikiliza sauti nzuri. Hayapo
kwa ajili ya kusikiliza porojo,
muziki, ngoma na mfano wa
hayo. Ili asikusumbue yakupasa
uyajue yanayomchukiza ili
uweze kuyaepuka kiwepesi na
siyo kugombana.
Nimalizie tu kwa kusema
kwamba, hebu yafanyieni kazi
yale anayohitajia kiumbe huyu
muone kama atakuwa mkoro.
Muwekeeni mazingira mazuri
muone kama ataendelea kuwa
tatizo kama mnavyodai. Na wale
tunaojiita Waislamu tutambue
kwamba hatupendwi kwa
sababu nilizoeleza. Namna nzuri
zaidi ni kuzidi kushikamana
na sababu hizi ambazo kwao
ni kero na siyo kuziepuka.
Leo tupo, kesho hatupo!
Tunaondokaje kwa mfano!???
(Juma Jumanne, (0789 151059,
0659 789468)
KATESH, MANYARA.)

16

Makala

AN-NUUR

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 20 - 26, 2016

Kilichosababisha niitwe mdini


Inatoka Uk. 7

106 la tarehe 18.08.2011, mwandishi


mwingine aliandika makala
yenye kichwa cha habari, HII
NDIYO TOFAUTI YA NYERERE
NA KIKWETE. Kwa ujumla
aliyoandika hayatofautiani sana na
ambayo nimekwisha eleza.
Yeyote akisoma makala hayo,
atagundua kuwa, mwandishi
hakuwa na sababu ya msingi
ya kuwalinganisha watu
hao isipokuwa kwa lengo la
kuonyesha mapungufu ya Kikwete
na kumvunjia heshima kwa
kumtukuza Nyerere. Hata hivyo,
kwa kuwa watu wana maoni tofauti,
wakati mwingine kinachokusudiwa
kumtukuza Nyerere, ndiyo
hicho hicho ambacho huonyesha
mapungufu yake pia. Aidha wakati
mwingine kinachokusudiwa
kuwakashifu waliomfuatia Nyerere,
ndicho kinachowapa sifa pia.
Kama wenzake waliotangulia,
anajaribu kupamba kila
lililofanywa na Nyerere na
kuchafua yaliyofanywa na maraisi
waliofuatia. Katika kufanya
hivyo, yeye na wengine kama
yeye hujikuta wakisifu chochote
alichofanya Nyerere ingawa hicho
hicho kingefanywa na mwingine
wangemlaumu, na pengine
ameshakifanya na kulaumiwa.

Inatoka Uk. 7
lengo, na ndio maana mara
kwa mara kila ukapo msimu
wa funga imekuwa ikisikika
mashekhe, maustadh, pamoja
na wadarsishaji mbalimbali,
katika madarsa ya mwezi wa
Ramadhan, wakiulizwa maswali
yanayohusiana na maakuli
yahojiyo iwapo mfungaji
kama hana futari na/au daku
analazimika kufunga au la! Kwa
kweli huwa nashindwa kuelewa
mantiki ya maswali kama haya
kwa kuwa kinachoonekana
kuuliziwa zaidi ni kuhusu
suala la ukosefu wa futari na
daku tu na si kuhusu ukosefu
wa kifungua kinywa, chakula
cha mchana wala chakula cha
usiku. Hivi kwanini sasa mtu
huyu asitumie kile atarajiacho
kunywa/kula asubuhi na/au
mchana kama futari yake na
kile atarajiacho kula usiku kama
daku yake?
Kadhalika si ajabu leo hii
kuwakuta akina mama wa
Kiislaamu na mabinti zao
wakitumia muda wao mwingi
katika mwezi wa Ramadhan
katika kufanya maandalizi ya
futari na daku ilhali wakitumia
muda mdogo au wakikosa muda
kabisa wa kutekeleza ibada
mbalimbali za kuwaelekeza
katika lengo la funga ya
mwezi mtukufu wa Ramadhan
mathalani kujisomea Qur-an
pamoja na kuhudhuria halaqa
na/au darsa mbalimbali za tafsiri
ya Qur-an na Hadith za Mtume
(S.A.W.) na pia kukosa kushiriki
katika ibada nyingine ambazo
hazipatikani katika mwezi
mwingine wowote isipokuwa

Nyerere alitumia nguvu za dola


kuzima wapinzani wake na hata
wanaotofautiana naye tu kimawazo.
Watu waliwekwa kizuizini kwa
miaka mingi bila kukishwa
mahakamani. Maandamano
hayakuruhusiwa isipokuwa yale tu
yaliyokubaliwa na kuandaliwa na
Chama (CCM) au Serikali. Ajabu ni
kwamba, wapo wanaomsifu kwa
hayo, lakini kwa sasa hujiweka
msitari wa mbele kupinga uingiliaji
kati wa polisi hata pale ishara za
uvunjifu wa amani zinapoonekana
wazi katika maandamano au
mikusanyiko ya watu ambayo mara
nyingi huandaliwa na vyama vya
siasa.
Kama tulivyoona, Nyerere
kukumbatia siasa ya chama
kimoja ilikuwa busara kwa mujibu
wa maoni ya baadhi ya watu
akiwemo mwandishi wa kwanza,
lakini waliomfuatia Nyerere
hushutumiwa na watu hao hao
kwa kile wanachodai kugandamiza
mfumo wa siasa ya vyama vingi
kwa kuingilia kati tu vitendo
vinavyoashiria uvunjifu wa amani
vinavyofanywa na baadhi ya
viongozi na wanachama wa vyama
vya upinzani.
Wakati wa Nyerere,
tulifundishwa kuwachukia
wapinzani wake kisiasa bila

wao kupewa fursa ya kujieleza.


Kupinga mawazo yake ilikuwa
sawa na uhaini. Tuliwaimba akina
Kambona vibaya kwenye mchaka
mchaka na kuwaita wahaini kwa
sababu tu walikuwa wakitofautiana
na Nyerere kimawazo. Kwa
Nyerere, wapambe wake wanataka
tuamini kuwa kufanya hivyo
ilikuwa ni kudumisha nidhamu
na mshikamano, lakini kwa sasa
kumtukana na kumdhalilisha
raisi hadharani ni kudumisha
demokrasia na haki ya kujieleza.
Wapo wanaojifanya wanatamani
Azimio la Arusha huku wakiwa
wanamiliki majumba ya
kupangisha, wana mishahara zaidi
ya mmoja na wakiwa na hisa katika
makampuni ya kibepari, mambo
ambayo yalikatazwa katika azimio
la Arusha.
Wapo ambao hufurahia uhuru
wa vyombo vya habari ambao
wakati mwingine huutumia
vibaya hata kumtukana rais na
kuikashifu serikali, lakini ni hao
hao kwa kutumia uhuru huo
huo huishutumu serikali kwa
kuwa lege lege. Wanasahau kuwa
wakati wa Nyerere wanaojifanya
kuutamani wasingekuwa na fursa
hiyo, na pengine wangewekwa
kizuizini mahali pasipojulikana bila
kushitakiwa bila ndugu zao kujua
wala kuwasiliana nao.

Tujiandae kwa Ramadhani


katika mwezi wa Ramadhani tu,
mathalani swala ya tarawehe.
Kwa muktadha huu,
tunapaswa kubadilika katika
maandalizi yetu kwa kutoishia
katika kujali zaidi maandalizi
ya kimaakuli pekee, kama
ifanywavyo na wengi wetu, bali
tunatakiwa kupiga hatua moja
mbele zaidi katika kujiandaa
na funga ya mwezi mtukufu
wa Ramadhani kwa kufanya
maandalizi yenye kuzalisha
tija na yatakayochangia kuleta
ufanisi katika funga zetu na
kutukisha katika kilele chake.
Na maandalizi yenyewe ni yale
yenye kuhusisha nadharia na
utendaji katika kuiendea ibada
adhimu ya funga ya Ramadhani.
Kwa kuanza na maandalizi
ya kinadharia katika kuiendea
funga ya Ramadhani ni kwamba
kila muislamu anayetarajia
kutekeleza ibada ya funga
ya Ramadhani hana budi
kujitahidi na kujibidiisha, kwa
kadri ya uwezo wake, katika
kuhakikisha anapata maarifa
au ujuzi kuhusiana na masuala
mbalimbali yanayohusiana
na q-hi ya swaumu/funga ya
Ramadhani kama vile kupata
maarifa juu ya maana ya funga,
lengo la funga, umuhimu wa
funga, nguzo za funga, sunna
za funga, vitenguzi vya funga,
sababu za kutokiwa lengo la
funga kwa kutaja machache.
Maarifa ya mambo haya
na zaidi ya haya, kwa zama

tulizomo, yanaweza kupatikana


kwa njia mbalimbali ikiwemo
mtandao wa intaneti. Kwa hiyo
muislamu, pamoja na kwamba
anaweza kutumia njia zingine
kujipatia maarifa haya, anaweza
pia kwa hatua za mwanzo;
kabla hajafanikiwa kupata
maarifa hayo kupitia njia hizo
zingine; kutumia njia ya simu
yake ya kiganjani yenye intaneti
kutafuta na kujipatia maarifa ya
mambo kadha wa kadha (kupitia
tovuti na wavuti mbalimbali za
Kiislaamu) yanayohusiana na
funga ya Ramadhani kwa urahisi
na kwa gharama nafuu kabisa.
Kwa upande wa maandalizi
ya kivitendo katika kuiendea
funga ya mwezi mtukufu wa
Ramadhani, suala hili linaweza
kumithilishwa na ile dhana
ya mafunzo kwa vitendo
niliyoidokeza katika ule mfano,
kutoka katika mazingira yetu
tunamoishi, niliyoutoa huko
nyuma. Kwa mantiki hii, ni
vizuri kwa muislamu kutumia
fursa hii adhimu kushiriki katika
mafunzo haya yahusikayo,
kwa namna moja au nyingine,
na kutafsiri yale maarifa ya
kinadharia kuhusiana na
swaumu katika vitendo kwa
kufunga swaumu za sunna
za mwezi wa Shaaban, kadri
atakavyojaliwa, katika kipindi
hiki cha kuelekea mwezi
mtukufu wa Ramadhan.
Imethibiti kwamba ni katika
mwezi huu Mtume (S.A.W.)

DKT. Jakaya Mrisho Kikwete


Namheshimu sana Hayati
Mwalimu Nyerere kwa kazi zake
nzuri alizofanya kwa nchi yake,
kwa Afrika na Dunia nzima. Hata
hivyo, kama binadamu alikuwa
na mapungufu ambayo hatupaswi
kuyashabikia na kuyafumbia
macho. Aidha ninakerwa sana na
watu wanaomtumia Nyerere kwa
malengo yao binafsi wakijifanya
wanamuenzi. Ninakerwa zaidi na
wale wanaoamua kumlundikia
sifa hata asizostahili kwa lengo la
kuwakashifu maraisi waliomfuatia.
Hakuna sababu ya kumsifu mtu
kwa kumkashifu mwingine, wala
kumkashifu mtu kwa kumsifu
mwingine. MWISHO WA
MAKALA.

alifunga mara nyingi (siku


nyingi) zaidi kuliko miezi
mingine ukiondosha mwezi
wa Ramadhan, ambao kwa
mujibu wa Qur-an na Hadith
ndio ambao tumewajibishiwa
kuufunga wote, hata hivyo
hakuwahi hata mara moja
kuufunga mwezi mzima wa
Shabaan kama inavyobainishwa
katika hadith iliyosimuliwa na
mama wa Waumini Bi.Aisha
(R.A.) ''Mtume (S.A.W.) alikuwa
akifunga hadi tukadhani
kuwa hatofungua kamwe, na
alikuwa akiacha kufunga hadi
tukadhani hatofunga tena.
Sijamuona Mtume (S.A.W.)
akifunga mwezi mzima kama
alivyokuwa akifunga Ramadhan,
na sijamuona akifunga mara
nyingi kama alivyofunga katika
Shaaban'' (Bukhari na Muslimu).
Nihitimishe makala haya kwa
kurejelea sehemu ya nukuu,
kuhusu suala la maandalizi,
niliyoanza nayo mwanzoni
kabisa mwa makala haya
iliyosomeka hivi ''Maandalizi
ni jambo la msingi katika kuleta
ufanisi katika utekelezaji wa
jambo lolote''. Hivyo basi, ni
vyema kwa kila muislamu
anayetarajia kufunga swaumu
ya Ramadhan kujitahidi kadri
ya uwezo wake kufanya
maandalizi ya kinadharia
na ya kivitendo ili kuweza
kutekeleza ibada ya swaumu
ya mwezi wa Ramadhan kwa
ufanisi unaoweza kumwezesha
mfungaji kukia lengo la
ibada hiyo adhimu ambayo
kwa kawaida hufanyika ndani
ya mwezi mmoja katika kila
mwaka.

17

SAFU YA BEN RIJAL

AN-NUUR

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 20 - 26, 2016

Jee tuwe kunguru au tafrani za panya? -2


Na Ben Rijal

Tutaendelea na tulipo wacha


juu ya uvazi wa suruali wenye
kukirihisha. Uvazi huu ambao
vijana huvaa suruali chini ya
kiuno na kuonyesha suruali zao
za ndani, hakika uvazi huu haumo
kamwe katika mila na dasturi za
Kiislamu na watu wa pwani kwa
jumla lakini hivi sasa uvazi huu
umeshamiri.
Nilikuwa natafuta jina la
uvazi huu kwa Kiswahili, bahati
nilikutana na kijana ambaye
nasoma makala hizi za gazeti la
An-Nuur akanipa jina linalotumika.
Aidha nilibahatika kuangalia
kwenye Channel mmoja ya
Televisheni ya Kiswahili (Runinga)
ambapo nilimuona mwanamama
fulani akifahamisha jina la
Kiswahili la uvazi huu nalo linaitwa
kata K. Sijajua kwanini ikaitwa
hivyo lakini inanijia dhana kuwa
kukata ni kupasua au kuchinja
na Kata K inaweza kuwa
imekata hio suruali chini ya kiuno.
Bibi ambaye alikuwa akielezea
alikuwa naye akipinga uvazi
huo ingawa na yeye nafsi yake
na uvazi wake aliouvaa na nyusi
kuchongwa alitaka marekebisho.
Hali ya wanawake kama hao
nitawazungumzia siku nyengine.
Katika maelezo ya mwanamama
huyo ambayo naye uvazi huu wa
Kata K unamkirihisha, akaka
mbali na kusema hao wanaovaa
uvazi huu hizo suruali za ndani
ni Boksa (Boxer) akaja na maelezo
hayo ya Boksa kuwa hizo suruali
za ndani wazionyeshazo vijana ni
zenye kukirishisha kwani chafu
zimejaa nongo, akauliza haya
kinachoonyeshwa ni kitu gani?
Panda shuka za Marekani na watu
Weusi
Sio kila suala hupata jawabu,
lakini mara nyingi suala hupata
jawabu. Hivi sasa nchi ya Marekani
ndio imekuwa ni kioo cha jamii
mbalimbali kujitizama, iwe kivazi,
mijendo, ulaji, ujenzi wa nyumba,
kusema na huku unatafuna
lugha, uvaaji wa koa za kip

Na Khatib Juma Mziray


KULINGANA na wale tunaoamini
Qadar, ni kuwa, kila jambo
lililotokea na linalotokea na
litakalotokea; limekadiriwa na
Mwenyezi Mungu Muumba
wa mbingu na nchi na vyote
vilivyomo. Kwa lugha rahisi, ni
kuwa; Mwenyezi Mungu anayajua
yote kabla hayajatokea; na sababu
za kutokea kwake, na hatima yake.
Kumekuwa na janga la
wakimbizi kutokea Asia, Mashariki
ya Kati, Afrika Kaskazini na
Magharibi mwa Aka. Nchi za
Ulaya na Marekani zinawasingizia
kuwa wanakimbizwa na hali mbaya
ya uchumi wanchi za Afrika na
Asia.

Vijana katika mji wa Detroit


na uvazi wa Kata K
kape, uchorwaji katika mwili na
kadhalika.
Vijana wengi hujiona
kifanywacho na Wamerekani ni
sawa na ukiiga ndio umepatia, iwe
ni utamaduni isiwe utamaduni,
hadhi hii ya nchi ya Marekani
kuvutia hisia za watu duniani sio
huku kwetu imekuja baada ya Vita
vikuu vya Pili Duniani, kutokana
na Marekani kutoa mchango
mkubwa katika kungolewa Hitler
na anazungumza Kiengereza
lugha ambayo mwenyewe ni
Muiengereza. Wao Wamarekani
ndipo walipopata nafasi ya
kujitutumua na kuwa ni taifa lenye
nguvu duniani na kuwa na mvuto
wa kila aina.
Ili kuweza kuikoleza hii mada, ni
vyema tukaangalia Ugozi wa nchi
ya Marekani, nchi hii ni bingwa
wa kile kinachoitwa demokrasia
na utetezi wa haki za binadamu
lakini ukizama na kuutafuta ukweli
utakuja kukuta ni mmoja ya nchi ya
ukandamizaji wa haki za binadamu
hasa za watu Weusi na wale
Waletino.
Katika nchi ya marekani watu
Weusi hupambana na madhila
ya kila aina na wengine hujikuta
kuuwawa na Polisi kwa sababu
zisizokuwa na misingi na mwisho
wake hao askari wanaotenda
matendo hayo ya jinai huachiwa
na kupewa heko kwa kuvuliwa
koa. Katika mwaka wa 2015
kutokana na gazeti la The Guardian
kumeoyeshwa kuwa Wamarekani
Weusi 1,134 katika mwaka jana
waliuwawa na askari Polisi ya
Marekani na wote hao wameuliwa

kwa madhila ya Ugozi wa rangi


ambao unanuka nchini humo ikiwa
kwetu Afrika unayayuka hata huko
Afrika Kusini makombo yake ni
machache. (http://www.theguardian.
com/us-news/2015/dec/31/the-countedpolice-killings-2015-young-black-men).
Mauaji haya hayajaanza leo wala
jana na ndipo wanaharakati wawili
katika miaka ya 60 walinyanyua
sauti zao kuyapinga haya, mmoja
wao ni Martin Luther King Junior
na wa pili ni Malcolm X au kwa
jina lake la Kiislamu anajulikana
kwa jina la Al-Hajj Malik Alshabaz.
Wanaharakati hawa wawili kila
mmoja alitoa hotuba ambayo ni
kioo kwa vijana wa Kimarekani
Weusi wakitaka kujijua na hata
vijana wasomi wa nchi za Kiafrika
nao huzizungumzia kwa kuona na
wao hayo yalioko huko yasiwe hata
watawala wakiyataka.
Martin Luther King Jnr katika
sehemu ya Hotuba yake aliyasema
haya:
But one hundred years later, the
Negro still is not free. One hundred
years later, the life of the Negro is
still sadly crippled by the manacles
of segregation and the chains of
discrimination. One hundred years
later, the Negro lives on a lonely island
of poverty in the midst of a vast ocean
of material prosperity. One hundred
years later, the Negro is still languished
in the corners of American society
and nds himself an exile in his own
land. And so we've come here today to
dramatize a shameful condition.
Hichi ni kisehemu cha hotuba
yake maneno haya yanakuvutia
na yana utamu, lakini ni mazito na
yenye kusikitisha ingawa miongo
4 imepita tangu kuuwawa kwake
kwani aliuwawa tarehe 4 April 1968.
Maneno yake hayo kwa tafsiri ya
juu juu anasema:
Miaka 100 badaye, bado mtu
Mweusi hayupo huru, miaka
mia imeghibu, bado maisha ya
Mweusi yanatia huzuni kwa kuwa
anatengwa na yumo kwenye pingu
za watawala, miaka mia imepita
mtu Mweusi anaishi katika dimbwi
la ufukara, bado mtu Mweusi
huyu yumo katika maisha yasio
na matumaini na kujiona bado yu
mgeni katika nchi yake mwenyewe,
kilichotuleta hapa ni kuzitoa hisia
zetu katika aibu hii. Maneno
mazito mno ikiwa bado yaliomfanya
ayaseme ndio yalivyo hivi leo.
Malcolm X kwa upande wake
yeye alikuwa anaamini lugha
ya ubabe ni ubabe ukitumiliwa
nguvu kuonewa na wewe ufanye
hivyo hivyo kinyume na Martin
Luther King ambaye imani yake
ikimwambia akufanyie ubabe

Wakimbizi Ulaya

Swali ni je, kabla ya nchi za Ulaya


na Marekani kuzivuruga nchi hizo
kwa njia hii au ile, kulikuwa na tabu
ya maisha Mashariki ya Kati, Afrika
Kaskazini n ahata Somalia? Tazama
mfano wa Libya, Syria na Yemen.
Wananchi wa Afghanistan na
Pakistani kabila Marekani haija
peleka majeshi yake na kuzivamia
na kuziharibu; mbona hatukusikia
watu hao wakikimbilia Ulaya?
Iraq, mbona hatukusikia wananchi
wa Iraq wakikimbilia Ulaya
kabla Marekani na washirika

wake (mataifa 32) hawajaivamia,


kuiharibu na kumwua Rais
Saddam Husseni? Mbona kabla
Marekani hajaingiza tina Somalia
hatukusikia wakimbizi Wasomali
waliokuwa wanakimbilia Ulaya
kwa ukata wa maisha? Mbona
hatukusikia Wanigeria wakikimbilia
Ulaya kabla ya kuanzishiwa kikundi
cha Boko Haram?
Nchi ya Nigeria baada ya kupata
Uhuru, Waziri Mkuu alikuwa Sir.
Abubakari Tafawa Balewa; tina
zilizushwa ikapinduliwa serikali

muonyeshe wema.
Malcolm X naye ndio aliuwawa
mwanzo kabla ya Martin Lther King
kwa kuzitetea haki za watu Weusi.
Aliuwawa na Mweusi mwenzake
katika mwezi wa Februari tarehe 5,
1965. Kipande cha hotuba yake naye
ananena haya:
We have a common enemy. We have
this in common: We have a common
oppressor, a common exploiter, and a
common discriminator. But once we
all realize that we have this common
enemy, then we unite on the basis of
what we have in common. And what we
have foremost in common is that enemy
the white man. Hes an enemy to all
of us. I know some of you all think that
some of them arent enemies. Time will
tell.
Tarjuma ya maneno hayo ni
Adui wetu ni mmoja na ndio
huyo huyo mwenye kutubagua
na kututenga, ikiwa tukiyaelewa
hayo kuwa adui yetu ni mmoja
ambye ni mwenye kutukandamiza,
kutunyanyasa na kutubagua,
tutapoyajua hayo basi tuungane
kwa kuwa tuna jambo moja
linalotuleta kwa pamoja. Adui yetu
ni mtu Mweupe ambaye ni adui
wetu sote, najua wengine kati yenu
mtaona kuna baadhi yao hawamo
katika huo mkumbo lakini wakati
utakuelezeni.
Wana harakati hawa wawili
wote katika mahubiri yao, Ugozi
na tina za Wamerekani Weusi
hazijawabagua ila walifanya maisha
yao yamalizike wakiwa bado vijana
wanahitajika wauwawe kwa mtutu
wa bunduki.
Kata K (Sagging paits)
Jee nini hasa uvaaji huu na
umetokea wapi na kwanini uvaaji
huu ukatokea huko Marekani na
kutuvamia kwa vijana wetu wa leo
humu Afrika? Uendapo ukipishana
na vijana uvazi ndio huo. Baada ya
kukuonyesha sura ndogo ya nchi
ya Marekani na walivyo, wiki ijayo
nitaimalizia makala haya juu ya
Kata K na sababu kuwa uvazi huu
tuite uvazi ulio sio wa kukumbatiwa
katika utamaduni wetu.
Fwatana na mie katika
makala ijayo ambayo itakuwa ya
mwisho juu ya suala hili ambalo
linatupelekea tuwe Kunguru
na kumalizikia kukosa kujuwa
utamaduni wetu halisi. Aidha kuja
na tafrani za panya.
KUMRADHI
Naomba radhi wasomaji wangu
wapendwa kwa kukosekana makala
ya wanyama. InshaAllah wiki ijayo
itakuwepo. - Ben Rijal
yake; waasi wakamshika wakamtesa
mateso ambayo usingedhania
mwanadamu anaweza kumfanyia
hata mnyama. Baada, miaka
hiyo, nilipata gazeti lililoelezea
kifochake, kuwa ulikuwa ni mwezi
wa Ramadhani na Sir. Abakari
alikuwa amefunga; watesaji
walimkata kiungo kimoja baada
ya kimoja, wakamtoboa macho,
wakamkata sehemu zake za
siri bado akiwa hai; aliwaambia
kuwa: Ni heri mungeniua moja
kwa moja kuliko kunitesa hivi;
lakini kuna siku mutamkumbuka
Abakari Tafawa Balewa. Baada ya
hapo ndipo Nigeria ikagawanyika
makundi mawili Generali Ojuku

Inaendelea Uk. 18

18
Inatoka Uk. 17

akaitenga Kusini akidai kuwa wao


ni Wakristo; hawawezi kutawaliwa
na viongozi wa Kaskazini ambao
ni Waislamu. Akaanzisha vita
vilivyoua watu zaidi ya milioni
moja. Cha kusikitisha, ni kuwa,
kisirani hicho kililetwa hapa
Tanzania tukachangishwa michango
ya kusaidia vita vya Biafra; hiyo
ni awamu ya kwanza ya utawala
wetu. Katika Diary (kitabu cha
kumbukumbu) zangu kuna maneno
haya:Tarehe 1/7/2002, B.B.C. na sauti
ya radio ya Ujerumani zimetangaza
kuwa, Wasomali wa asili ya
Kibantu, wapatao mia nne (400)
wamepelekwa kuishi Marekani,
baada ya kubaguliwa Somalia,
walikuwa huko kutokana na vizuizi
vya watumwa.
Swali ni hili:- Hatujasikia Umoja
wa nchi za Afrika wakipelekewa
malalamiko kuwa, kuna Wasomali
wa asili ya kibantu wanaobaguliwa
huko Somalia.
Hata hivyo kuna Wazigua
Wasomali, au Wasomali Wazigua
wa Handeni, wanajulikana na
wanatambua ndugu zao wakati
mwingine wanawatembelea,
hatujasikia wakilalamika kuwa
wanabaguliwa huko Somalia.
Hata hivyo taarifa hiyo
inamaanisha kuwa utumwa
ulipopigwa marufuku hao wabantu
walikuwa safarini wakisarishwa
ikabidi waachwe huko Somalia.
Hata hivyo tujiulize, utumwa
umepigwa marufuku karne ya
17/18; mpaka karne ya 21, ni miaka

MAKALA

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 20 - 26, 2016

Wakimbizi Ulaya

zaidi ya 400. Serikali ya Marekani


iliyokuwa ndiyo mnunuaji
wa watumwa nambari moja;
inayowanyanyasa Wamarekani
Weusi; karne ya 21 anawahurumia
Wabantu wa Kisomali inawapeleka
kuishi Marekani! Kuna siri gani?
Ikumbukwe kuwa wakati huo
Marekani ilisha pata kipigo cha
askari wake kuuawa na kuburuzwa
nyuma ya gari na kuzungushwa
mjini Somalia.
Huo ulikuwa ni ule wakati wa
utawala wa wababe wa kivita,
walioitawala Somalia kimakabila;
ndipo Wasomali ambao karibu
asilimia miamoja 100% ni Waislamu,
wakaamua kuanzisha utawala
wa Mahakama ya Kadhi. Utawala
ambao uliwaadabisha wababe wote
wa kivita, na Somalia kwa muda wa
mwaka mmoja ikawa na amani na
kuanza kushamiri maendeleo yake.
Marekani na washirika wake
hawakufurahi kuona Somalia
inatawaliwa Kiislamu; kwani
itaonekana kuwa Waislamu
wanaweza kile walichoshindwa
Wamarekani na washirika wake.
Wakati wote huo hatukusikia
makundi ya Wasomali
wanaokimbilia Ulaya. Uongozi
wa Marekani ukaushauri utawala
wa Ethiopia, ukawapa silaha
asakari wa Ethiopia wakaivamia

AN-NUUR

Somalia wakaupindua utawala


wa Mahakama ya Kadhi. Ndipo
vijana wa Kisomali wakaunda jeshi
la vijana (Al-shabab) kuitetea nchi
yao. Vijana hao wameendeleza
mapambano baadae wakapachikwa
ugaidi.
Swali la kujiuliza ni hili:- Wale
vijana waliopelekwa Marekani,
wakiitwa kuwa ni Wabantu wa
Somalia, wameishia wapi?
Isijekuwa ndio waliofunzwa
namna ya kufanya mauaji
wakarudishwa Somalia wakajipa
jina la Al-shabab ili kuharibu
maana halisi na malengo ya wale
Al-shabab (vijana) wa asili! Kwa
sababu wakati kulikuwa na utekaji
wa meli bahari ya hindi; wakubwa
wa poropoganda walisema kuwa,
watekani ni vijana wa Kisomali
ambao hawakwenda shule; lakini
ikakia wanateka meli ndani ya
bahari kilometa elfu moja 1,000,
karibu na kisiwa cha Madagaska; na
wana mwongoza nahodha mpaka
Somalia.
Ungetegemea miujiza ya namna
gani kwa mtu asiyeenda shule
kuijua jograa ya bahari kwa kiasi
hicho?
Isije kuwa ni wale walioitwa
kuwa ni Wabatu wa Somalia
waliopelekwa Marekani ndio
waliopewa elimu hiyo na

kurudishwa Somalia, kuteka meli!


Wakati Marekani na washirika
wake walipokamilisha kuingiza
kikundi cha upinzani Libiya, nchi za
kwanza kuwasaidia kuishambulia
Libiya, ni Ufaranza na Italy; na
wakimbizi waliokuwa wanakimbilia
nchi za Ulaya kutoke Afrika
Kaskazini, walikuwa wakiingilia
Italy. Unaweza kujiuliza kuwa,
nchi hizo si ndizo zilizo furahia
kuishambulia Libiya na kumwua
Rais Gada?
Sasa zinalalamika nini waathirika
hao wakikimbilia kwao kutokana na
matendo ya mikono yao?
Nchi hizo za Ulaya ni za wacha
Mungu, ndiko mahali dini yao
(Ukristo) ulipoanzia, Matendo 11:26.
Usingetegemea wacha Mungu
hao ndio wanaofanya uharibifu
hapa duniani kwa kiasi hiki; na
baadhi yao hawataki Waislamu
waruhusiwe kuingia Ulaya.
Kuna msomaji amesoma makala
ya Ugaidi ni nini nani gaidi?
Aliniandikia ujumbe mreefu,
akilaumu kuwa, tumekuwa
tukishusha hadhi ya gazeti letu
kwa kuandika makala za kusimama
upande mmoja wa imani ya dini;
na kushambulia upande wa pili wa
dini ya wasiokuwa Waislamu.
Anasema kuwa, pamoja na kuwa
naye ni Muislamu, lakini haaki
mwenendo wa makala zangu.
Nilitafuta jina lake katika
mtandao nikakuta anaitwa
Kalindula Huseni.
Itaendelea toleo lijalo

Hitilafu za kimadhehebu zisitutoe katika Uislamu

Na: Sheikh Muhsin Asayid


Mohamed
KWA jina la Mwenyezi Mungu
na shukurani zote anastahiki
Mwenyezi Mungu na rehema
na amani zimkie mjumbe wa
Mwenyezi Mungu, Bwana wetu
Muhammad na jamaa.
Amesema Allah S.W
(shikamaneni katika dini ya
Mwenyezi Mungu nyote na wala
msifarikiane) (103 Al- Amran) na
hapana shaka kwamba kuhitilaana
katika mtazamo na kukadiria vitu
na kuhukumu juu yake, ni jambo la
kimaumbile na kitabia.
Amesema Mwenyezi Mungu
Mtukufu; (Na mtiini Mwenyezi
Mungu na Mtume wake na wala
msigombane mtaharibikiwa na
zitaondoka nguvu zenu). (46 Anfaal.)
Katika mahusiano, kuna
kufarakana kati ya mtu kwa namna
mbalimbali kiasi cha kutowezekana
kujenga maisha na kusimamisha
mahusiano ya kijamii kati ya watu,

wakiwa watu hao wanatofautiana


katika mitazamo. Hekima ya
Mwenyezi Mungu Mtukufu
imepelekea kuwa baina ya watu
kuna kutofautiana kati yao sawa
sawa, tofauti ya kimaumbile au
ulewa tunatafuta mwenyewe.
Kila mmoja analo
alilowepesishiwa nalo kwa
maumbile yake, hivyo watu
wapo tofauti na waumini wana
daraja. Wapo wale ambao
wanadhulumu nafsi zao, wapo
wengine wanajihifadhi. Hivyo
basi kutofautiana kimadhehebu
isitufanye kutoka katika dini
ya Allah, pia wapo wengine
wanashindania katika mambo ya
kheri.
Amesema Mwenyezi Mungu
Mtukufu na laiti angetaka Mola
wako mlezi, angewafanya watu
wote umma mmoja na hawaachi
kutofautiana isipokuwa wale
aliowarehemu Mola wako mlezi,
hivyo ndivyo alivyowaumba (118
Surat Huud).
Ni nini maana ya kutofautiana?
Nini sababu zake na ni zipi adabu
zake?
Kutofautiana na kuhitilaana ni
kule kupita kila mtu na njia yake,
inayosigana na ya mwengine. Na
kutofautiana ni neno kuu zaidi
kuliko kinyume chake, kwani kila
vinyume viwili vinatofautiana na
sio kila linalotofautiana ni kinyume.
Na pale walipokuwa wakitofautiana
watu katika maneno, huenda
yakapelekea katika ugomvi.
Amesema Mwenyezi Mungu
(Yakatofautiana makundi kati yao)
(37 Surat Mariam) Na amesema,
(Na laiti angetaka Mola wako

mlezi, angewafanya watu wote


umma mmoja na wala hawaachi
kuhitilaana isipokuwa wale
aliowarehemu Mola wako mlezi na
hivyo ndivyo alivyowaumba ) (118
Surat Huud).
Kisha amesema (Hakika yenu
mpo katika kauli tofauti) (18
Surat Dhariati). Na kutofautiana
kumegawanyika katika sehemu
mbili. Tofuati mbaya na tofuati
nzuri na tofauti huchukuwa nafasi
ya uvumilivu, nayo ni mazoezi ya
kiakili na kutoa maoni ya kufungua
upande wa kra na kugawanyika
kwa ufumbuzi.

Sababu za kutofautiana.
Kufuata anasa kwa kukadiria
kra au madhehebu maalumu.
Amesema Mwenyezi Mungu
Mtukufu (Na wala msifuate
anasa itakupoteza katika njia
ya Mwenyezi Mungu) (26 Surat
Swadi).
Kuipenda nafsi ambayo huota
ndani yake makosa na utukufu
na kujitenga na haki. Amesema
Mwenyezi Mungu Mtukufu,
(Na wala msiwe miongoni mwa
washirikina na miongoni mwa wale
waliotofautiana na kuisambaratisha
dini yao na wakawa makundi, kila
kundi kwa lile lililonalo hulifurahia)
(32 Surat Ruum).
Sababu nyingine ni tofauti ya
mjinga kwa mwanazuoni, au kwa
ujumla tofauti ya mtu ambaye
hamiliki chochote juu ya jitihada.
Amesema Mwenyezi Mungu
Mtukufu (Basi waulizeni wenye
kujua kwa kuwa nyinyi hamjui) (7
Surat Al-Anbiyai).
Sababu nyingine ni kungangania

rai moja kuliko kubaya, ambako


humtoa mtu katika kutoa haki. Kwa
hakika amesema Mtume (SAW)
(Si mwenzetu mwenye kulingania
unganganiaji wa rai moja).

Adabu za kutofautiana.
Kuna adabu za kuhitilaana
ambazo inatakikana kuzichunga
kwake kutoka kwa wanazuoni na
watu wengine kwa namna sawa
sawa miongoni mwa hizo.
Dhana nzuri kwa Mashekhe ni
bora kwani wao ni wenye kujitahidi
na Mtume (S.A.W) amesema,
(atakapo jitahidi hakimu na
akakosea, ana ujira na atakapopatia
ana ujira mara mbili) Ameipokea
Bukharin na Muslim.
Isije ikapelekea tofauti hii ikaleta
tna kati ya wanaotofautiana na
kutengana. Kufanya juhudi za
kuondoa tofauti kwa vyombo
vya kisheria, na inatakikana kwa
Waislamu kuondoa tofauti kwa
ajili ya kuitaka haki na kuhifadhi
pia umoja wa Waislamu. Na
mtakapogombana kwa jambo
lolote, basi rudini katika kitabu cha
Mwenyezi Mungu na Mtume ikiwa
mnamuamini Mwenyezi Mungu
na siku ya mwisho, hivyo ni bora
kwenu na ni uzuri zaidi wa uogofu)
(59 Surat Al Bakarat).
Unyenyekevu kwa Waislamu
na kushikamana na kutafuta
haki kwa mazungumzo kama
alivyotufundisha Mwenyezi Mungu
(Na waambie watu maneno mazuri)
(83 Surat Al-bakarati).
Email : eg_islamic_center39@
yahoo.com

19
M

Ukurasa wa Watoto

AN-NUUR

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 20 - 26, 2016

Uislamu ni usa - 3

huchana nywele zake


vizuri.
Sauda ni dada yake Ali.
Sauda ni mtoto msa
kama Ali.
Hupiga mswaki na
kukoga vizuri mara kwa
mara.
Sauda hukata kucha zake
kila zikiwa ndefu.
Sauda husuka nywele
zake vizuri.
Kweli Ali na Sauda ni
watoto wasa.
Kila siku ya Ijumaa
asubuhi Ali hukata kucha
zake za mikono na miguu.
Hufanya hivyo
kwa sababu ndivyo
alivyotufundisha Mtume
(s.a.w)
Watoto wote wanatakiwa
wawe kama Ali na Sauda.
Wawe wasa.
Allah huwapenda watoto
wasa.
Allah anawataka
Waislamu wavae nguo sa
na nzuri.
Wavae nguo nzuri zaidi
wakati wa swala.
Allah anatuhimiza katika
Quran akisema:
Enyi mlioamini,
chukueni mapambo yenu
katika kila Sala. (7:31)

WIKI iliyopita tulijifunza


juu ya Usa wa kinywa na
meno.
Tukasema kuwa ni
muhimu na lazima kupiga
mswaki kila unapoamka
asubuhi.
Ni muhimu kupiga
mswaki kila baada ya kula.
Unahimizwa kupiga
mswaki kila unapotawadha.
Hiyo ni katika sunna za
kuchukua udhu.
Ni jambo Alilohimiza
Mtume (s.a.w).
Tukiendelea na darsa
letu la usa, leo tutaangalia
usa wa mwili.
Tuendelea na simulizi juu
ya mtoto Ali.
Ali anapoamka asubuhi
hupiga mswaki.
Kisha hukoga vizuri kwa
sabuni na maji sa.
Ali hukoga kila
anapotoka shuleni.
Ali hukoga kila
anapomaliza kufanya kazi.
Ali hukoga kila
anapotoka kucheza.
Ali hukoga kabla ya
kulala.
Baada ya kukoga Ali

HAIIBA TIMAMU TEA

CHAI YA AJABU KWA AJILI YA KUKABILIANA NA

PRESHA YANGU IMEKUWA YA KAWAIDA KWA MARA YA KWANZA KATIKA


KIPINDI CHA MIAKA 13!
Na. William Ichumo
Sku moja nilipewa taarifa kuwa mdogo wangu mwenye miaka 55 alikuwa
anaumwa na kuwa hali ilikuwa mbaya. Niipofuatilia nilibani kuwa maelezo yale
yalikuwa ni kweli.
Nilkuwa nahitaji nimtoe Morogoro aje Dar es Saaam kuwaona wataalam lakini
kikwazo changu kikubwa ilikuwa fedha. Niimweleza Bwana Juma Killaghai
ambaye ni rafiki yangu kuhusu hilo tatizo naye akanipa paeeti mbili za Timam Tea
na kuniambia nijaribu kwanza kumpa mgonjwa hizo. Huwezi ukaamini! Ndugu
yangu sasa amenyanyuka anaendelea na shughuli zae za kilimo na wala hakuna
dawa nyingine yoyote aliyotumia!
https://www.facebook.com/Herbal-Impact-157972014402705/

SHINIKIZO LA DAMU
(HYPERTENSION/HIGH BLOOD
PRESSURE)
UGONJWA WA MOYO
KIHARUSI
JONGO (GOUT)
MAUMIVU YA VIUNGO (RHEUMATISM)
MAUMIVU SUGU YA KICHWA
BAWASIR (PILES/HEMORRHOIDS)
MAGONJWA YA INI
SARATANI MBALIMBALI
UOTO/UVIMBE MBALIMBALI KATIKA
VIUNGO VYA UZAZI VYA MWANAMKE
(FIBROIDS, POLYPS NA CYSTS)
KUSHINDWA KUZUIA MKOJO (URINARY
INCONTINENCE)
ATHARI ZA KISUKARI CHA UKUBWANI
PUMU
UPUNGUFU WA KINGA ZA MWILI
KASI YA KUZEEKA
MATATIZO YA MFUMO WA MZUNGUKO
WA DAMU
MKAKAMO WA NGOZI;
UDHAIFU WA MACHO
KUPOTEZA KUMBUKUMBU
KASI NDOGO YA KUPONA MAJERAHA
MAKOVU KWENYE MAPAFU
UGONJWA WA NGOZI KUCHUJA RANGI,
YAANI, VITILIGO

HAIIBA TIMAMU TEA


INAPATIKANA
HERBAL IMPACT
MOSQUE STREET, NO. 1574/144
(MKABALA NA MSIKITI WA
SUNNI), KITUMBINI, DAR ES
SALAAM
TUTEMBELEE AU TUPIGIE SIMU
NAMBA:
0754281131/0655281131/06862
81131/0779281131

AN-NUUR

20

MAKALA

20

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 20 - 26, 2016

Soma gazeti la
AN-NUUR
KWA TSH 800/=
kila Ijumaa

AN-NUUR

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 20 - 26, 2016

Tunahitaji wasichana wanamitindo Waislam


Na Mwandishi Wetu

UMETOLEWA wito kuwa


wanahitajika wanamitindo
Waislamu ambao watabuni na
kushona nguo za kike zenye
kukidhi sheria za Kiislamu.
Wito huo umetolewa katika
maonyesho ya mitindo ya kimataifa
(International Modest Fashion Week)
yaliyofunguliwa Istanbul, Uturuki,
Ijumaa iliyopita, Mei, 13, 2016.
Wanamitindo waliohudhuria
maonyesho hayo wamesema
kuwa, pamoja na kuvaa Kiislamu,
lakini wasichana na wanawake wa
Kiislamu wanatakiwa kupendeza.
Kwa hiyo kunahitajika kuwa
na wanamitindo kwa ajili ya watu
wenye heshma zao wanaotaka
kujisitiri.
Ikaelezwa kuwa, ukiacha
mwamko uliopo miongoni mwa
Waislamu ambapo kila uchao,
mahitajio ya hijabu yanaongezeka,
lakini wapo hata ambo sio
Waislamu ambao wangependa
kuvaa kistaarabu.
Jumla ya wanamitindo na
wabunifu wa mishono mbalimbali
ya nguo (designers) wapatao 70
walishiriki maonyesho hayo
wakitafuta soko la bidhaa zao.
"(We want) to create mainstream
fashion out of modest fashion and

to energize Islamic communities to


produce (clothing) for Muslim women.
They want to have their rules but they
also want to look chic."
Alisema Kerim Ture ambaye ni
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni
ya Modanisa ambayo ndiyo
iliyoandaa maonyesho hayo.
Ikaelezwa kuwa, soko la nguo
za heshma linazidi kupanuka na
kwamba linatarajiwa kukua na
kukia Dola bilioni 327 ($327 billion)
ikapo mwaka 2020.
Hiyo ni kwa mujibu wa utati
rasmi uliochapishwa katika taarifa
ya hivi karibuni juu ya uchumi
wa Kiislamu katika uwanja wa
kimataifa (Global Islamic Economy
report).
Kinachosisitizwa ni kuwa kuvaa
Kiislamu sio kuvaa hovyo.
Lazima kuwe na hijabu nzuri za
mitindo ya kuwafanya wasichana
na wanawake wa Kiislamu, kwanza
wasipate tabu kuzipata nguo za
Kiislamu lakini pia ziwe nzuri za
kupendeza.
Kauli mbiu ni kuwa kupendeza
mwanamke sio kuvaa ovyo. Sio
kuvaa nusu uchi. Sio kuacha
baadhi ya maungo nyeti wazi kuwa
maonyesho kwa kila mpita njia.

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Ltd, Dar es Salaam.

Вам также может понравиться