Вы находитесь на странице: 1из 6

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI


IDARA YA UHAMIAJI
Anuani ya Simu:
NUKUSHI:

UHAMIAJI

OFISI YA UHAMIAJI WILAYA


S.L.P 417

BUNDA

OFISI
YA UHAMIAJI
+255 282622426
S.L.P 369
KUMB
.NA.BND/INV/VOL111/21/33
MUSOMA
SIMU:

Monday, 16 February 2015

TAARIFA YA UTENDAJI KAZI WILAYA YA BUNDA KWA KAMISHNA MKUU


WA UHAMIAJI
1.0

Utangulizo
Afande kamishna mkuu
Nichukuwe fursa hii kukupongeza kuteuliwa kwako kuongoza Idara ya
Uhamiaji
Ofisi ya uhamiaji wilaya ya Bunda ilifunguliwa rasmi mwaka 2004 ikiwa
na maafisa uhamiaji wawili (2). Wakati huo tulipata chumba kimoja
katika jengo la moja ya majengo ya Halmashauri ya Wilaya. Baada ya
maaafisa hao kuanza kazi na kuelimisha jamii juu ya shughuli za
uhamiaji, wananchi walianza kujitokeza kupata huduma za uhamiaji
hapa hapa wilayani Bunda na kusababisha ofisi hiyo kuwa ndogo na
ambayo haikuwa na hadhi. Baada ya hapo ofisi imekuwa inahamia
katika majengo tofauti tofauti hadi mwezi februari 2011 tulipopanga
katika jengo hili. Ofisi ya uhamiaji Wilaya ya Bunda inahudumia jumla
ya Tarafa nne (4), Kata thelathini na moja(31) na vijijimia moja na nne
Kati ya hivyo baadhi ya vijiji ni visiwa ndani ya ziwa victria ambavyo
inatuwia vigumu kufika kutokana na kutokuwa na boti. Ofisi hii pia
inahudumia mahoteli yaliyoko katika eneo la magharibi la hifadhi ya
Taifa ya mbuga ya Serengeti (Serengeti National Park Western zone).
Pamoja na hayo kuna shule za binafsi (English Medium Primary
Schools). Viwanda vya mafuta, mashamba ya kilimo na wahamiaji
haramu ambao huingia kinyemela na kuishi vijijini kwa uficho. Yote
hayo yanahitaji huduma ya ofisi ya Wilaya tu kwani hatuna kituo cha
kuingilia na kutoka nchini kutokana na jiografia ya Wilaya ya Bunda
kutokuwa kwenye mpaka na nchi yoyote.

2.0

Watumishi
Kwa sasa ofisi ya uhamiaji Wilaya ya Bunda ina jumla ya watumishi
tisa (9) kati ya hao nane (8) ni maaskari wa uhamiaji na mmoja ni
askari wa magereza ambaye tulimuomba atusaidie kuendesha gari la
ofisi. Miongoni mwetu wako maaskari wawili (2) ambao wako shule
katika vyuo vya SAUT Mwanza na chuo cha uhamiaji Arusha. Kwa
kulinganisha na ukubwa wa Wilaya na kazi zilizomo bado tunamahiaji
wa askari wa uhamiaji na zaidi sana askari wa kike kwani hapa tuko
askari wa kiume tu.
Inatuwia vigumu kumsindikiza mtuhumiwa wa kike. Mafisa waliopo na
vyeo vyao ni kama ifuatavyo:1.
2.
3.
4.
5.
6.
7.
8.
9.

3.0

DCIS. Elizeus Mushongi Afisa uhamiaji Wilaya


SSM Oswald Nswima
Msaidizi wa AUW
SGT. Juma Suleiman Juma
SGT. Nuru P. Mwasulama
SGT. Balele David Balele
SGT. Mhando R. Mwajasho yuko shule SAUT
CONST.Benedict N. Sanga
CONST.Walter Lema
yuko shule Arusha
A5810 S/SGT
Adam Mgeta
Dreve

Hali ya Uhamiaji haramu Wilayani


Wialaya hii kama ziliovyo Wilaya nyingine inakabiliwa na wahamiaji
haramu wengi takwimu za mwaka 2013 zinavyoonyesha Wilaya ilikuwa
na wahamiaji haramu waliohisiwa ni zaidi ya elfu mbili 2000. Maafisa
uhamiaji kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama
tunaendelea na zoezi la kuwasaka wahamiaji haramu katika maeneo
mbalimbali kama vile nyumba za kulala wageni, Mhotelini, Viwandani,
shule za binafsi, Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, migodini na vijijini. Kwa
mwaka 2013 katika hili naomba nimshukuru Afisa Uhamiaji mkoa wa
Mara Afande Ally Dadi na uongozi wa mkoa kwa misaada ya hali na
mali wanapotupa ili kufanikisha shughuli hii nzito. Kwa sasa
tunakabiliwa na wimbi kumbwa la wahabeshi (Ethiopians) wanaopita
hapa walielekea Dar es salaam ili waweze kwenda Afrika ya kusini. Siku
hizi wamebuni mbinu mbali mbali ikiwa ni pamoja na kutumia pikipiki
za abiria (bodaboda) na wakati mwigine wanatembea kwa miguu.
Pikipiki inaweza kwenda sehemu ambapo gari halipiti hivyo kuhitaji
zaidi pikipiki iliyo nzima. Ili tuwate tunalazimika kukaa muda mrefu
katika kuzuizi cha mto Rubana kwani walio wengi wanapitia hapo. Pia
2

kutokana na watu wa mkoa kuwa na asili ya ufugaji wanaanza kuleta


raia wa Rwanda na Burundi ili waweze kuwafanyia kazi kwa bei nafuu.
(cheap Labour).

4.0

Makosa mbalimbali ya kiuhamiaji na hatua zilizofikiwa


Majukumu ya kusimamia mashauri yote mahakamani yanafanywa na
wanasheria toka mkoani kwani hapa Wilayani hakuna mwanasheria.
Kwa ujumla ofisi ya uhamiaji Wilaya kuanzia mwezi Jan- Desemba 2013
imepeleka mahakamani mashauri 2 mashauri hayo yote yako katika
hatua ya kusikilizwa kwa hatua za awali
(Preliminary hearing)
wahusika ni raia wa Ethiopia na Kenya waliofukuzwa nchini ni 7 wote
wakiwa raia wa Ethiopia hawa walirudishwa kwao kwa kutokuwa na
hati za kusafiria pia ilishindikana kuwafikisha mahakamani kwa kukosa
mkalimani kwani wao wanaongea kihabeshi. Katika kipindi hicho jumla
ya waethiopia 11 walikamatwa na kufikishwa katika ofisi ya uhamiaji
mkoa kwa hatua zaidi vilevile katika kipindi hicho hicho raia 9 wa Afrika
mashariki waliondoshwa nchini na kurejeshwa kwao hao ni pamoja na
Kenya 6, Burundi 1, Rwanda 1, na Uganda 1.Kutokana na kutokuwa na
kituo cha kuingia na kutoka nchini hakuna watu waliozuiliwa kuingia
nchini. Pia hakuna mtanzania aliyeshtakiwa katika kipindi tajwa.

5.0

Majengo ya ofisi
5.1 Afande,jengo linalotumiwa na ofisi ni la kukodi mali ya mtu
binafsi ambalo limekuwa linachukua gharama kubwa mpaka
januari 2014 gharama ya kukodi ilikuwa shilingi 2,000,000/= kwa
mwaka, lakini tuliletewa taarifa ya kupanda kwa gharama ya
kukodi jengo hilo kufikia shs 2,700,000/=. Jengo hili halina maji
inabidi yachotwe nje ya ofisi. Kwa idadi yetu jengo halitoshi
kwani lina vyumba vichache ukilinganisha na idadi yetu na
shughuli zetu. Hakuna sehemu ya faragha kwa ajili ya mahojiano
na watuhumiwa.
5.2

Kiwanja cha Ofisi


Afande Ofisi ya Uhamiaji Wilaya iliomba na kupewa kiwanja
namba 269 Block F toka Halmashauri ya Wilaya kilichoko karibu
na ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Bunda. Kiwanja hicho tayari
kimesafishwa na trip 2 za mawe zimewekwa na wahisani
wanaopenda maendeleo. Pia msaada mkubwa umetoka kwa
Afisa Uhamiaji mkoa ambaye tayari amelipia huduma ya maji ili
ujenzi utakapoanza wajenzi wasipate taabu. Kwa namna ya
pekee nimshukuru mkuu wa Wilaya ya Bunda ambaye amekubali
kubeba mzigo wa kutafuta wafadhili na kusimamia ujenzi huo
3

kwa kushirikiana na ofisi yetu. Naomba kwako Afande kamishna


mkuu wa Uhamiaji msaada wa hali na mali katika azma yetu ya
kujenga ofisi.

6.0

5.3

Kiwanja cha Ujenzi wa nyumba za Watumishi


Pia tulipeleka maombi yetu ya kupatiwa kiwanja cha ujenzi wa
nyumba za watumishi kwa maelekezo yako kwenye barua na
JB.217/257/01/35 ya 11/9/2012. Mpaka sasa hatujapewa kiwanja
hicho mara tukipata tutakufahamisha. Ili watumishi nao waweze
kupata nyumba za kuishi kwani maisha tunayoishi nayo si
mazuri.

5.4

Makusanyo ya Maduhuli ya Serikali


Kwa mwaka 2013 ofisi ya Wilaya ya Bunda imekusanya jumla ya
shilingi za Tanzania 5,200,000/= tu kutokana vyanzo vya ETD na
RPA (Peasant) na dola za kimarekani 600

5.5

Vitenda Kazi
Nichukue fursa hii kuipongeza Idara ya Uhamiaji kwa jitihada
kubwa zinazofanywa kuhakikisha vitendea kazi hasa vyombo vya
usafiri vinapatikana sehemu nyingi za kazi zina vyombo vya
uhakika. Ofisi ya Uhamiaji Wilaya ya Bunda ina pikipiki moja STK
8560 na gari moja landrover Defender STK 2559. Kwa bahati
mbaya gari hili liliwahi kupata ajali lilipopelekwa gereji
halikutengenezwa ipasavyo kwa vile aliyepatwa ajali hilo
aliagizwa kulitengeneza mwenyewe. Kwa sasa gari hili linahitaji
matengenezo makubwa (major repair) kwa vile bodi yake inavuja
hasa mvua inaponyesha huwa tunalazimika kusimama hadi
mvua itakapoisha. Kama kuna uwezekano tunaomba gari ambalo
ni zima lisilohitaji matengenezo ya mara kwa mara ili tuweze
kufanya kazi vizuri na kwa wakati wote.

5.6

Mafuta
Kwa upande wa mafuata nichukue fursa hii kumshukuru pia RIO
kwa jitihada anazofanya kutupatia mafuta. Tatizo linalotupata ni
kutotosha mahitaji yetu kutokana na ukubwa wa Wilaya. Safari
moja ya kwenda kisorya au Mekomaliro vijiji vilivyo mipakani na
Wilaya za Ukerewe au Serengeti inachukua lita 50 na kuendelea
kutegemea na shughuli zinazofanyaika. Kwa uchache tunahitajia
ujio wako katika Wilaya ya Bunda utatuwekea mazingira mazuri
ya kufanyia kazi kwa kutuongezea mafuta

Changamoto tunazokabiliana nazo


4

Afande kamishna mkuu wa Uhamiaji changamoto ni nyingi lakini kwa


kifupi tuna changamoto zifuatazo:6.1

Wananchi hawako tayari kutoa taarifa za wahamiaji haramu kwa


kuwa wengine ndio wanaowatunza lakini wanataka fedha ili
watoe taarifa.
6.2 Elimu zaidi inatakiwa kwa wananchi kuhusu athari za Uhamiaji
haramu kwani wananchi wengi hawaelewi.
6.3 Wilaya haina bajeti ya kufanya kazi tunapokuwa na watu wa
kusindikiza ni lazima kufanya mawasiliano mkoani na kama hela
haipo tunawajibika kukaa na mtuhumiwa na wakati tunatoa hela
zetu mfukoni ingawaje baadae tunarudishiwa ila kuna maelekezo
ya kutofanya hivyo.
6.4 Upungufu wa mafuta ya kufanyia kazi.
6.5 Uchakavu wa gari la ofisi ambalo linatakiwa kurekebishwa mara
mkwa mara.
6.6 Ofisi haina samani za kutosha hata zilizopo ni chakavu. Pia kuna
kelele nyingi za kupakia na kupakua soda.
6.7 Watumishi hawana nyuma za kuishi wanapanga kitu ambacho
hata utendaji wetu wa kazi unakuwa wa mashaka kwa vile
wageni wengine tunaishi nao akikamatwa anadai wewe jirani
ndiye uliyemtaja.
6.8 Ofisi haina photocopy machine tunapotaka kutoa kopi lazima
twende mitaani kitu ambacho hatuna imani kama kopi hazibaki
kwenye mashini zao.
6.9 Uhaba wa watumishi nao ni tatizo hasa wa kike tunalazimika
kuvunja sheria wakati wa kusindikiza watumiwa wa kike. Hii
inasababisha kutoanzishwa kwa uhamiaji kata ambayo ndiyo
ingetusaidia zaidi kuwatambua wahamiaji walio katani.
6.10 Katika eneo hilio hakuna radio za jamii (comunify radio) kwa ajili
ya kusaidia kurusha vipindi vya uhamiaji.
6.11 Watumishi wengi wamekaa hapa Wilayani na Mkoa wa Mara kwa
muda mrefu.
6.12 Tunaomba ufanyike mpango Afisa Uhamiaji awe na silaha ya kazi
hasa kwenye maeneo nyeti kama mkoa wa mara.
7.0

Mipango yetu ya mbele (Way forward)


7.1 Kuimarisha utendaji kazi kwa kiwango cha hali ya juu kwa
watumishi wa huduma zetu.
7.2 Kuongeza nguvu katika kufanya doria ili kukabiliana na wahamiaji
haramu katika mahoteli nyumba za kulala wageni, stand za
magari, mto Rubana, viwandani, mashuleni n.k nap engine pote
ambapo ni maficho ya wahamiaji haramu
7.3 Kuendelea kutoa Elimu kwa wananchi juu ya athari za Uhamiaji
haramu, sheria za uhamiaji na uraia kupitia uhamiaji shirikishi.
5

7.4

7.5
7.6

7.7
7.8

8.0

Endapo tutapata uwezeshwaji na maofisa wa kutosha tunatarajia


kuanzisha uhamiaji kata ili kuwa karibu na wananchi waweze
kutoa taarifa za wahamiaji.
Kuendelea kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya
katika kutkeleza majukumu yake.
Kumfanya mwana Bunda kuwa askari namba moja wa uhamiaji
kwa kuwa tayari kushiriki katika kuwafichua wahamiaji haramu
na wale wote wanaovunja sheria za uhamiaji.
Kumjenga mwana Bunda kuona uhamiaji ni mali yake.
Kuwezesha mawasiliano kati ya jamii na uhamiaji.

HITIMISHO
Ofisi ya uhamiaji wilaya inaahidi kwa dhati mbele yako kuwa licha ya
changamoto tulizotaja tutaendelea kuchapa kazi kwa ari na kasi
kubwa. Tunatarajia kuwa katika uongozi wako utafanya mabadiliko
mengi ya maendeleo tuachane na kufanya kwa mazoea bali kwa
ubunifu wa hali ya juu. Afande, tuna imani sana na wewe na uongozi
wa idara kwa ujumla tunaomba kuwepo na mabadiliko makubwa ya
utendaji kati ya watumishi walioko Dar es salaam na Mikoani. Kwa wale
walioko Mikoani hasa wa chini na kati wanapata maneno ya kukatisha
tamaa toka kwa wale walioko Makao Makuu. Pia barua zinazotumiwa
huko huwa hazijibiwi kwa haraka. Nichukue fursa hii kwa mara nyingine
katika wilaya ya Bunda na mkoa wa mara kuwakaribisha.
Tunatarajia ujio wako utaongeza nguvu katika utendaji kazi wetu na
maelekezo utakayotoa tuko tayari kuyapokea, kutekeleza maelekezo
utakayotoa kwenye ziara yako ambayo tumeifurahia. Tunakutakia
wewe binafsi, viongozi uliofuatana nao kiongozi wa mkoa afya njema.
Asanteni kwa kunisikiliza na naomba kuwasilisha.

Imeandaliwa na

DCIS, Elizeus Mushongi,


Afisa Uhamiaji Wilaya,
BUNDA.
6