Вы находитесь на странице: 1из 3

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI


IDARA YA UHAMIAJI
ANUANI YA SIMU: UHAMIAJI
TELEFAX:
SIMU: +255 282622426

OFISI YA UHAMIAJI(W)

Unapojibu tafadhali taja:

S.L.P 417
BUNDA.
02 Machi 2012

KUMB Na. BND/IMM/MOA/08/132


________________________________________________________________________________________________________

AFISA UHAMIAJI(M)
S.L.P 369
MUSOMA.
YAH: TAARIFA YA UTENDAJI KAZI MWEZI MACHI 2012 WILAYA YA BUNDA.
A: UTANGULIZI
Katika kipindi cha Mwezi Machi 2012 shughuli za utoaji huduma kwa wananchi na wageni
ziliendelea kama kawaida. Ofisi ilishirikiana na vyombo vingine vya ulizi na usalama katika
kutatua masuala mbalimbali yahusuyo usalama kwa ujumla.
B: WATUMISHI
Ofisi ina jumla ya watumishi sita(wote wakiwa ni askari) ambao ni;
1. T.W NYANGASA-DCIS-DIO
2. MOSES J. MUTASH-INSP-MSAIDIZI WA DIO
3. MHANDO MWAJASHO-SGT
4. NURU P. MWASULAMA-SGT
5. BEN N. SANGA-CONST
6. WALTER E. LEMA-CONST

C: MASOMO
Kati ya watumishi hao,watumishi wawili wako masomoni;
1. NURU P. MWASULAMA-CHUO CHA UHASIBU ARUSHA
2. MHANDO MWAJASHO-SAUT MWANZA
D: HATI ZA DHARURA ZA KUSAFIRIA (ETD) ZILIZOTOLEWA
Jumla ya ETD arobaini na mbili (54) zilitolewa katika kipindi hiki kama inavyoonyeshwa katika
jedwali hapa chini kwa kuzingatia umri na jinsia za watu waliopatiwa hati hizo.
UMRI(MIAKA) WANAUME

WANAWAKE

0-15

JUMLA KUU

16-40

27

35

40+

10

18

JUMLA

37

17

54

E: UPELELEZI NA DORIA.
Katika kipindi hiki upelelezi na doria vimefanyika kama kawaida.Pia ofisi ilikabidhiwa raia
watatu (3) wa Ethiopia kutoka jeshi la polisi,tuliwafanyia mahojiano na kuwakabidhi katika ofisi
ya uhamiaji mkoa kwa hatua zaidi.Majina yao yameorodheshwa hapa chini.
1. ALISO AMAN
2. ABERA WALBO
3. TAMIRAT TUMERO GUNTE
F: KESI ZILIZOPELEKWA MAHAKAMANI
Katika kipindi hiki hakuna kesi yoyote iliyopelekwa mahakamani.
G: WATU WALIOFUKUZWA NCHINI.
Hakuna mtu yoyote aliyefukuzwa nchini katika kipindi hiki.

H: VITA DHIDI YA WAHAMIAJI HARAMU.


Katika kupambana na wimbi la wahamiaji haramu, ofisi kwa msaada wa ofisi ya uhamiaji mkoa
imefanya semina kwa viongozi wa Tarafa mbili za Chamrihyo na Kenkombyo pamoja na Kata
na vijiji vyake.Jumla ya washiriki 63 walipata semina hiyo.Pia ofisi ilialika wawezeshaji kutoka

TAKUKURU,HALMASHAURI YA WILAYA na JESHI LA POLISI(Taarifa kamili ya semina


hiyo utaipata baada ya taarifa hii).
I:CHANGAMOTO.
Katika kipindi hiki tumepata changamoto kubwa ya kutokuwa na gari hivyo kupelekea
kushindwa kuyafikia maeneo ya mbali katika doria zetu.
J:SHUKRANI.
Ofisi inatoa shukrani za dhati kwa vyombo vyote vya ulinzi na usalama vya wilaya kwa msaada
na ushirikiano tunaoupata kutoka katika vyombo hivyo.

Naomba kuwasilisha

T.W Nyangasa
AFISA UHAMIAJI(W)
BUNDA.