Вы находитесь на странице: 1из 3

TAARIFA YA SEMINA YA URAIA KWA VIONGOZI WA TARAFA YA CHAMRIHYO NA

KENKOMBYO PAMOJA NA KATA ZAKE NA VIJIJI VYAKE WILAYANI BUNDA.

UTANGULIZI.
Semina hii ilifanyika tarehe 30/03/2012 ikiwa ni katika kukamilisha mkakati uliopangwa kwa muda
mrefu ili kurahisisha zoezi la utambuzi wa wahamiaji walowezi, pia kuwaandaa viongozi hawa katika
ushiriki wa zoezi zima la utoaji wa vitambulisho vya uraia na kuwahamasisha kushiriki kwa hali na mali
katika mapambano dhidi ya wahamiaji haramu.Semina hii iliratibiwa na ofisi ya uhamiaji wilaya kwa
msaada wa ofisi ya uhamiaji mkoa.
WASHIRIKI.
Idadi na vyeo vya washiriki katika semina hiyo ni kama inavyoonyeshwa hapa chini.

SN
1
2
3

CHEO
Makatibu Tarafa
Watendaji wa Kata
Watendaji wa Vijiji
JUMLA

IDADI
2
12
48
62

NB:Makatibu Tarafa walihudhuria wote.


Watendaji wa kata walihudhuria wote.
Watendaji wa vijiji: Hawakuhudhuria wanne(4)
WATOA MADA NA MADA ZILIZOTOLEWA.
Semina ilikuwa na watoa mada wane (4) kutoka katika taasisi mbalimbali kama ilivyoainishwa
hapa chini.
SN
1
2
3
4

MADA
Uraia
Madhara ya Rushwa
Ulinzi na Usalama wa
Nchi
Maadili ya Uongozi na
uwajibikaji

MTOA MADA
Afisa wa uhamiaji
Afisa wa TAKUKURU
OCD-Bunda

OFISI/TAASISI
ALIYOTOKA
Uhamiaji-Bunda
TAKUKURU-Musoma
Jeshi la Polisi-Bunda

Afisa kutoka ofisi ya


Mkurugenzi Mtendaji

Halmashauri ya Wilaya ya
Bunda.

MUHTASARI WA MADA ZILIZOTOLEWA.


Uraia.
Mtoa mada alielezea mambo mbalimbali ikiwemo maana ya uraia,aina za uraia na jinsi ya
kumtambua raia na asiye raia wa Tanzania kwa maana ya uthibitisho wa uraia wa mtu.Vilevile
mtoa mada alielezea masuala ya wahamiaji haramu, kwa kuwawezesha kujua mhamiaji haramu
ni nani na madhara ya kumhifadhi mhamiaji haramu, na akawaomba kutoa ushirikiano wa dhati
katika kuwafichua wahamiaji hawa.Pia alieleza kwa ufupi zoezi lililoko mbele yetu la utoaji wa
vitambulisho vya uraia.
Madhara ya Rushwa.
Mtoa mada alisisitiza zaidi madhara ya rushwa na kuwaeleza washiriki wasishawishike na
rushwa na kuwahifadhi wahamiaji haramu.
Ulinzi na Usalama wa nchi.
Mtoa mada alielezea madhara makubwa katika ulinzi na usalama wa nchi yanayosababishwa na
wahamiaji haramu wanaohifadhiwa na wenyeji hasa akitolea mifano ya ujambazi unaofanywa na
raia kutoka nchi jirani za Rwanda na Burundi katika mikoa ya Kagera na Kigoma.
Maadili ya uongozi na uwajibikaji.
Mtoa mada alitoa msisitizo katika uwekaji wa kumbukumbu za wageni hasa kwa kutumia
madaftari waliopewa na halmashauri ikiwa ni moja ya majukumu yao kisheria.Pia aliwasisitiza
viongozi hawa kutoa ushirikiano wa dhati kwa idara ya uhamiaji.
WAGENI WAALIKWA.
Katika semina hii tulikuwa na wageni waalikwa wafuatao:
1. Mkuu wa Wilaya ya Bunda-Mgeni Rasmi
2. Afisa Usalama wa Wilaya.
3. Afisa Tawala wa wilaya ya Bunda.
Muhtasari wa hotuba ya mgeni Rasmi.
Mgeni rasmi aliwaasa washiriki kuwa wazalendo katika masuala ya kitaifa, hasa ili la
kupambana na wimbi la wahamiaji haramu na kutumia semina hii kama chachu ya kuongeza
bidii katika mapambano haya.Lakini vilevile alitoa rai kwa idara ya uhamiaji kuongeza umakini
zaidi katika mipaka ya nchi kwani kumeonekana kuwa na udhaifu hivyo kuruhusu wageni
kuingia kiholela.

MICHANGO NA MAONI YA WASHIRIKI.


Washiriki walionyesha kufurahishwa sana na semina hiyo na kutoa ushirikiano wao wa dhati
kwa kuuliza maswali,kutoa maoni na ushauri pale palipohitajika kufanya hivyo.Moja ya maoni
waliotoa ni kusambaziwa sheria malimbali zitakazowasaida kaitika utendaji kazi,vilevile
waliomba wapatiwe madaftari maalum kwa ajili ya uwandikishaji wa wageni na kuwasidia
katika utunzaji wa kumbukumbu.Pia waliomba semina kama hizi zifanyike mara kwa mara
kwani zinawakumbusha majukumu yao na kuongeza ufanisi wa kazi.
CHANGAMOTO ZILIZOJITOKEZA.
Changamoto mbalimbali zilijitokeza katika semina hii, kubwa zikiwa ni:

Kutoanza semina kwa wakati uliokuwa umepangwa,hii ilijitokeza kwa sababu


washiriki waliowengi walichelewa kufika ukumbini.

Uchache wa nakala za machapisho hivyo kupelekea washiriki baadhi kukosa


nakala hizo.

Mtoa mada kutoka jeshi la polisi hakuwa na chapisho lolote kwani hakuwa
ameandaa ila aliahidi kuandaa na kuhakikisha washiriki wanapata chapisho hilo.

MATARAJIO.
Ni matarajio yetu kwamba baada ya semmina hiyo tutapata ushirikiano mkubwa kutoka kwa
viongozi hawa hivyo kurahisisha jitihada zetu za kuwatambua wahamiaji walowezi na
kupunguza kama si kukomesha kabisa wimbi la wahamiaji haramu katika wilaya yetu na mkoa
kwa ujumla.
SHUKRANI.
Tunatoa shukrani za dhati kwa kamati ya ulinzi na usalama kwa ushirikiano mkubwa walioutoa
katika kufanikisha semina hii, hasa mgeni rasmi ambaye ni mwenyekiti wa kamati hiyo kwa
kukubali kuacha shughuli zake na kuwa mgeni rasmi katika semina hiyo. Pia tunatoa shukrani
zetu za dhati kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri aliyetusaidia kutoa taarifa kwa
washiriki wote na kutupatia ukumbi mzuri na wakisasa kwa ajili ya semina hiyo.Shukrani za
pekee tunazitoa kwa ofisi ya uhamiaji mkoa kwa kuwezesha kwa kiasi kikubwa semina hii
kufanyika.
OMBI/USHAURI.
Tunaomba ufanyike utaratibu wa kufanya semina nyingine kama hii kwa tarafa zingine
zilizobaki.
Nawasilisha.

Вам также может понравиться