Академический Документы
Профессиональный Документы
Культура Документы
tz
Sauti ya Waislamu
Tuambiwe ukweli FFU wamsindikiza nani kalipua bomu Wapo wapi Uamsho waliotua Dar kuchoma Makanisa
ISSN 0856 - 3861 Na. 1070 JAMADUL THAN 1434, IJUMAA - MEI 10-16, 2013 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=
Ponda Mtambani
Kivumo cha Takbiira chatikisa Kisutu Yathibitishwa kiwanja kimeporwa Ponda akitetee Mahakama ya Ardhi
Wabunge wasicharuke tu, wahoji mambo ya msingi Kasema kweli Samia Suluhu, tuwe na yakini kwanza
Uk. 6
CHUO Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), kinatarajiwa kuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa Kimataifa
wa Umoja wa Nchi za Kiislamu (OIC). Mkutano huo kwa mwaka huu unatarajiwa kufanyika Septemba 2 kwa mashirikiano ya nchi ya Oman, Umoja wa OIC na
Inaendelea Uk. 2
2
www.annuurpapers.co.tz
Tahariri/Makala
Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM. E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk Osi zetu zipo: Manzese Tip Top Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam
JAMADUL THAN 1434, IJUMAA MEI 10-16, 2013 Kumekuwa na mlolongo wa kukamatwa Waislamu wanaokutwa na kanda zenye mawaidha ambapo ndani yake kuna ujumbe wa Quran kuwa Yesu si Mungu. Lakini kwa upande mwingine, hatujawahi kuona wauza kanda za kutukuza uungu wa Yesu, wakibughudhiwa. Sasa hapa ni lazima isemwe wazi, je kinachokusudiwa hapa ni kupiga marufuku Waislamu kusema kuwa Yesu sio Mungu? Kusema Yesu si Mungu, ni jambo lisilokubalika kwa Mkristo kwa sababu ni sawa na kupinga uungu wa mungu wake Yesu. Lakini pia ni kufru kubwa kwa Muislamu akisikia mtu akisema kuwa Yesu ni mungu. Katika hali hii, ufumbuzi ni nini? Je, ni kuwapiga marufuku Waislamu wasihubiri kuwa Mungu si Yesu ambayo ni sawa na kuwazuiya wasisome baadhi ya aya za Quran? Je, wakatazwe w o t e , Wa i s l a m u n a Wa k r i s t o ? M u i s l a m u asiseme kuwa Yesu si Mungu na Mkristo asiseme kuwa Yesu ni Mungu? Yo t e h a y a i n a p a s a yafafanuliwe, vingine itabaki kuwa ni utata mtupu na katika utata huu ndio tunaona Serikali inaungana na Wakristo kuwashambulia Waislamu kuwa ndio wanaotukana na kuwakashifu Wakristo. Wale wanaopiga vijembe vya kuwaombea wenye majini na mapepo hawaonekani. Imekuwa sawa na ile agenda ya ugaidi. Haisemwi kwamba ni kuwapiga vita Waislamu, lakini kila tukio, anayekamatwa ni Muislamu/Muarabu. Ndio maana hata Arusha tumekimbilia kuwakamata Waarabu wakati Arusha wapo raia wengi wa kigeni. Kwa mtindo huu wasiwasi wetu ni kuwa tutazidi kuivuruga amani ya nchi badala ya kuitengeneza.
AN-NUUR
bungeni. Akichangia tarehe 6 Mei katika kikao kinachoendelea Dodoma, Mheshimiwa Zitto Kabwe alitaka Watanzania wasome kutoka yaliyowakuta Ivory Coast na Liberia. Katika uchambuzi wake akasema kuwa kuna lawama ya muda mrefu sana ya Waislamu kuhusu BAKWATA. Kwamba Waislamu miaka mingi toka mwaka 1969 wakati Serikali imeunda BAKWATA wanalalamika. Wanalalamika kuwa wakati Serikali imewapa Wakristo uhuru wa kuwa na taasisi zao huru na haiziingilii, inapokuwa kwa Waislamu, inataka kuwadhibiti Waislamu wote chini ya Bakwata ambayo haina uhalali wowote (legitimacy) ya kuwasemea Waislamu. Mtizamo huu, msimamo na mkakati huu wa kuwanyima u h u r u Wa i s l a m u , n d i o uliomfanya Anna Abdallah atoe mfano wa wapinga Bakwata. Anachotaka kuona ni kuwa Waislamu wanarejeshwa katika ile miaka ya Mwalimu Nyerere ambapo Muislamu hakuruhusiwa kufanya jambo lolote la Kiislamu mpaka apate kibali cha Bakwata, na ukienda Bakwata hupati kwa sababu ilishapewa maelekezo. Hivi tunavyoandika maoni haya kuna Waislamu wanakabiliwa na kesi ya kuchoma makanisa, wengine wapo nje kwa dhamana na wengine kwa zaidi ya miezi sita sasa dhamana zao zimezuiliwa. Makanisa haya ni yale yaliyodaiwa kuchomwa siku ya vurugu za maandamano kupinga hatua ya Polisi kusita kumchukulia hatua kijana aliyekojokolea Quran. Mara nyingi panapotokea matukio kama haya, ndipo hupatikana fursa kwa wahalifu nao kufanya yao kama tunavyoona wakivamia na kupora maduka. Lakini wakati Waislamu wakisubiri hukumu kufuatia kesi hiyo, watu waliochochea waumni wa Kikristo Tunduma wakaandamana na kufanya fujo na kuchoma moto msikiti, taarifa tulizo nazo ni kuwa hakuna mashitaka yoyote waliyokwisha somewa. Labda
swali ni je, ujumbe gani wanapewa Waislamu? Kama mtu anaweza kungoa dirisha la msikiti na asichukuliwe hatua yoyote na vyombo vya dola, salamu gani anapewa mtu huyu? Je, kesho na keshokutwa kwa ujumbe huu aliopewa kuwa yeye haguswi, atashindwa kufanya jingine kubwa? Lakini kwa upande, mwingine, katika hali hii, Waislamu waliovunjiwa msikiti wao ambao wanategenea kuwa kuna Serikali yenye kujali usalama wa wnaanchi wote, wanapewa ujumbe gani? Wa k a t i Wa z i r i w a Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Dkt. Emannuel Nchimbi akifunga mkutano wa viongozi wa kidini, jijini Dar es Salaam alisisitiza kauli ya Serikali ya kukataza mihadhra ya kashfa na kauli za kujenga chuki. Ambalo tungependa lifafanuliwe zaidi, ni hili la mihadhara ya kashfa. Je, kinachokusudiwa nini?
SUZA. Taarifa hiyo imekuja kufuatia ziara ya siku nne ya maafisa wa nchi ya Oman walioambatana na maafisa wa OIC iliyonza mapema wiki hii mjini Zanzibar. Mwenyekiti wa Mamlaka ya kumbumbuku na nyaraka ya nchi ya Oman Dkt. Hamed Mohammed al Dhawiyaniy amesema Zanzibar imepata nafasi hiyo kutokana na kuwa na mahusiano mema na nchi nyingi ulimwenguni na hasa katika nchi za Kiarabu. Amesema, historia na utamaduni wa Kiislamu wa Zanzibar na namna ulivyotumika katika kusambaza Uislamu nchi nyingine, umekuwa kigezo muhimu cha Zanzibar kupata nafasi hiyo. Kwa vile Zanzibar ina historia nzuri katika kusambaza Uislamu nchi nyingine, tunaimani kuwa hata malengo ya mkutano wetu huo yatakiwa kwa kiasi kikubwa , alisema Dkt. al Dhawiyaniy ambaye pia ni mkuu wa msafara huo. Kwa upende wake Mkurugenzi Mkuu wa OIC
katika kitengo cha utati na utamaduni Dkt. Halit Eren amesema mkutano huo utakuwa fursa adhimu kwa Zanzibar kujitangaza katika mataifa mbalimbali na kuendelea kujiongezea umaarufu kimataifa. Amesema, kwa vile watakuja washiriki kutoka mataifa mbalimbali kutoka nchi wanachama wa OIC, Zanzibar itakuwa ni nafasi yake muhimu kufahamika kimataifa na kujipatia nafasi za masomo duniani. Amefahamisha kuwa watoa mada 164 kutoka nchi mbalimbali tayari wameshapeleka maombi yao ili kuwasilisha katika mkutano huo na kuwataka Wazanzibari nao kupeleka maombi yao. Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo cha SUZA Dkt. Haji Mwevura Haji amesema vyuo mbalimbali kutoka nchi tofauti viliomba kuwa mwenyeji wa mkutano huo, lakini SUZA kimeamuliwa kuwa mwenyeji kutokana na historia ya Zanzibar. Amefahamisha kuwa licha ya Zanzibar kutokuwa mwanachama wa jumuiya ya OIC, lakini kigezo hicho hakiizuii Zanzibar kuwa mwenyeji wa mkutano huo
wa kimataifa. Amegusia kuwa mkutano huo unaweza kuwa fursa adhimu kwa Zanzibar kunufaika kupitia jumuiya hiyo kama ambavyo nchi ya Uganda ilifaidika kwa kujengewa Chuo Kikuu cha Mbale. We n z e t u U g a n d a walifaidika na OIC kwa kujengewa Mbale University, nasi pia tuna matarajio mengi ilikwemo kuitangaza SUZA na kupata scholarships duniani, alisema Dkt. Haji D k t . H a j i amewahakikishia maosa hao ushirikiano wa kutosha ili mkutano huo uweze kutimiza malengo yaliyopangwa. Umoja wa Nchi za Kiislam Duniani, OIC, unajishughulisha na mambo mbalimbali ya kimaendeleo ikiwemo kusaidia nchi wanachama wa umoja huo katika huduma za kijamii ikiwemo ujenzi wa taasisi za kielimu, afya na miundombinu. Mkutano Mkuu ndio unaojadili na kupitisha miradi na misaada mbalimbali ambapo mkutano uliopita ulifanyika nchini Omani.
3
Na Bakari Mwakangwale WANAODAIWA kuwa ni vinara wa vurugu za kuchinja zilizoibuka hivi karibuni katika mji wa Tunduru na kusababisha kuvunjwa na kuchomwa moto Msikiti, wahawajafikishwa katika vyombo vya sheria. Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari kutoka katika mji huo mdogo wa Tunduma, watu hao wametajwa kuwa ni Diwani wa Chadema na Mchungaji mmoja, ambao kabla ya tukio walikuwa ni chachu ya kuibuka kwa vurugu hizo. Sambamba na watuhumiwa hao, chanzo hicho kimedai pia kuwa watuhumiwa wa vurugu hizo na kusabisha kuchomwa moto na kuvunjwa Msikiti, mpaka sasa hawajafunguliwa mashitaka yoyote. Walikishwa mahakamani na kuambiwa warudi nyumbani bila ya kusomewa mashitaka. Watuhumiwa karibia wote wapo nje kwa dhamana, lakini hawajasomewa shitaka lolote, walipelekwa Mahakamani kisha walitajwa majina yao
Habari
AN-NUUR
Waislamu. Hata hivyo alisema mashitaka yaliyowasilishwa mahakamani ni ya jinai na kwamba, Mahakama haizungumzii tarataibu za Bakwata kubadilishana ardhi na Agritanza. Hata hivyo alisema Sheikh Ponda ana haki ya kutetea mali za Waislamu, hivyo alishauri angefungua kesi hiyo katika mahakama ya Ardhi. Baada ya kutoa maelezo yote juu ya kesi hiyo, Hakim Nongwa alimtaka Sheikh Ponda kutoa utetezi wake kabla ya kuhumu kutolewa. Wakili wake, Bw. Yahya Njama, alisimama na kutoa utetezi kwa mteja wake ambapo alieleza kuwa Sheikh tayari ameshakaa rumande kwa muda mrefu, pia aliieleza mahakama kuwa Sheikh Ponda hajawahi kutenda kosa lolote na ikizingatiwa kwamba yeye ni kiongozi anayetegemewa na watu anaowaongoza. Baada ya hapo Hakim Victoria Nongwa alitoa hukumu ya kesi ambapo watuhumiwa wote 49 waliachiwa huru na Sheikh Ponda kupewa kifungo cha nje cha masharti ya kutotenda kosa kwa mujibu wa kifungu cha 25 (g) cha sheria ya adhabu za makosa ya jinai. Mara baada ya kutolea hukumu hiyo, mara moja vivumo vya takbir vilisikika nje ya mahakama hiyo kutoka kwa umati mkubwa wa Waislamu waliokuja kushuhudia hukumu hiyo.
4
Na Ibn e Abdul Haq
April 30, 2013 Mtandao wa kupashana habari PTV - Baada ya miaka 12 na vifo vya watu milioni baadaye, Marekani na washirika wake wa NATO wameelezea wazi nia yao ya kuondoa majeshi kutoka Afghanistan mwakani. Vita ya Afghanistan imekuwa mkwamo mtupu, mkiwa kijeshi na katika mahusiano ya kiraia, wakati uharibifu wa maisha, mali na miundombinu ikiwa kubwa sana. Muhimu zaidi, tofauti na madai ya awali, vita ya duniani kote dhidi ya ugaidi haijafanya dunia iwe mahali salama zaidi. Matukio ya ugaidi yamekuwa yakiongezeka, yakizingira nchi moja baada ya nyingine zinazoizunguka Afghanistan. Ili tusisahau, takriban vita vyote vilivyotokea baadaye vinavyopiganwa na Marekani na NATO vimeanzia katika vita iliyoingizwa Afghanistan baada ya 9/11. Sehemu kubwa ya siasa ya nje ya Marekani kuanzia 9/11 imewekwa katika mtazamo kuwa ilishambuliwa na Waislamu siku ile. Mtazamo huu ulitumika, zaidi ya kwingine, kuhalalisha vita nchini Afghanistan na Irak. Ni wazi kuwa kila vita iliyopiganwa na Marekani na washirika wake katika muongo wa kwanza wa karne mpya imejikika katika dhana iliyofuatia 9/11 ya kushambulia kujihami kwanza. Inakubalika kwa kiwango kikubwa sasa kuwa kutumia 9/11 kama msingi wa kushambulia Irak ilikuwa si halali; wateka nyara ndege hakuna aliyekuwa raia wa Irak, hapakuwa na uhusiano wowote wa kikazi kati ya Saddam Hussein na Osama bin Laden, na Irak haikuhusika na mashambulio ya vimelea vya anthrax (kimeta). Lakini bado inaaminika kwa kiasi kikubwa kuwa shambulio la Marekani kwa Irak lilikuwa sawa. Kwa zaidi ya muongo mmoja sasa, mashirika hodhi ya habari duniani yamekuwa yakichomekea riwaya hii ya kutunga kama tukio lisilo na ubishi. Inaelekea kuwa itikadi hii itaingia katika ngazi za juu zaidi wakati warembeshaji wa wanasiasa Marekani wakijaribu kuhalalisha mpango wa kujiondoa Afghanistan na kudhihirisha kuwa vita dhidi ya ugaidi imekuwa ni mafanikio makubwa yasiyo na mfano wake katika historia ya binadamu. Jukwaa limeshaandaliwa kwa mpambano mkali wa kisaikolojia na vyombo vya habari utakaofumuliwa katika hisia za watu wasiojua linaloendelea. Kwa mfano, majuzi tu mwaka 2011, gazeti la New York Times likizungumzia mashambulio ya Marekani dhidi ya Irak kama vita ya kujiamulia, iliita mapambano ya Afghanistan vita ya lazima. Jarida la Time liliviita vita sahihi. Na mwaka 2009, Barack Obama aliripotiwa kusema moja ya sababu za kumaliza ushiriki wetu nchini Irak ni kuwa na askari na raslimali za kuwafuata watu
Makala
AN-NUUR
Hamid Gul, mkuu wa zamani wa shirika la ujasusi la majeshi ya Pakistan (ISI) alisema nadhani kuna mfananisho na Osama bin Laden. Kusema kweli, mtu huyo katika mkanda wa video hata si mfananisho halisi, kwani ni mzito zaidi na maji ya kunde zaidi ya bin Laden, ana pua pana zaidi, amevaa vito vya thamani, na anaandikia mkono wa kulia. Shirika la upelelezi la FBI, hata hivyo, kwa hali yoyote haliuoni mkanda huu wa video kuwa ushahidi kwa nguvu wa uhusika wa bin Laden kwa 9/11. Hivyo, Ikulu ya Marekani, serikali ya Uingereza, FBI au Ripoti ya Tume ya 9/11 hawajatoa ushahidi kamili kuwa Osama bin Laden alihusika na 9/11. 3. Kulikuwa na ushahidi wa wateka nyara Waislamu kutokana na simu kwenye ndege? Wasomaji wengi wanadhani hapawezi kuwa na shaka kuwa ndege zote zilitekwa na wafuasi wa Al Qaeda, kwa sababu kuwepo kwao na yaliyotokea kwenye denge ziliripotiwa katika simu za abiria na wahudumu wa ndege, na simu za mkononi zikiwa na nafasi muhimu. Simu iliyopata sifa sana ilikuwa ni ya mchambuzi wa habari wa CNN, Barbara Olson kwa mumewe, mwanasheria mkuu Ted Olson. Kwa mujibu wa CNN, aliripoti kuwa mkewe alimwita mara mbili kwenye simu ya mkononi kutoka ndege ya American Airlines safari ya 77 akisema kuwa abiria wote na wahudumu wa ndege walikuwa wamekusanywa nyuma ya ndege na ...wateka nyara wenye visu
SHINDANO LA KIELIMU
Kwa kusherehekea kumbukumbu ya kutimiza miaka kumi na tatu tangu kuanzishwa kwa Darasa la Hadithi za Bwana Mtume (s.a.w.) katika msikiti wa Kipata. Wadhamini wa Darasa hilo wameandaa shindano la kielimu katika somo la Hadithi. Mwanafunzi/msomi yeyote nchini anakaribishwa kushiriki. Zawadi nzuri imetayariishwa kwa mshindi, Inshallah. MAMBO MUHIMU YANAYO MUHUSU MSHIRIKI: 1. Vitabu vya rejea ni; Nukhbah, Bulughul-Maraam na Sunan Abi Daawoud. 2. Waraka wa maswali unapatikana Msikiti wa Kipata kwa Ustaadh Maneno; Naibu wa Imamu. Aidha dukani kwa Ibnu Hazm (jirani ya Msikiti wa Mtoro) kwa Ustaadh Jamali. 3. Waraka huo unatakikana kurejeshwa mapema kabla ya tarehe 8, JUNI, 2013. 4. Washindi wote watatangazwa siku ya Jumamosi ya tarehe 29, JUNI, 2013 katika haa maalumu itakayo fanyika katika Msikiti wa Kipata, Inshallah. Wabillah Tauq
Makala
AN-NUUR
upande mwingine, vyombo mbalimbali vya habari hasa vya Ulaya, vilitabiri kuwa tukio hilo ilikuwa ndio mwanzo wa vita ya wenyewe kwa wenyewe Iraq. Kiongozi na Ulamaa mashuhuri wa Shia Ali alHusayn Al-Sistani katika jambo lisilo la kawaida kwake, alitokea katika Televisheni akiwataka waumini na wafuasi wake kutulia. Naye Sheikh Muqtada Al-Sadri, alikatiza ziara yake Lebanon na kurejea Iraq ambapo aliwataka wafuasi wake, na hasa kikosi chenye silaha cha Washia kuhakikisha kuwa kinalinda Misikiti ya Wasuni isije ikashambuliwa na mtu yeyote (Washia wenye hasira). Kwa upande mwingine, Masheikh wa Kisuni baada ya kulani shambulio hilo, waliendesha kampeni kubwa ya kutuliza hali ikiwa ni pamoja na kufanya mazungumzo ya mara kwa mara na Masheikh wa Kishia. Kwa hakika vitabu vya historia vimeweka kumbukumbu hii wazi kabisa kwamba viongozi wa kidini wa Iraqi walifanikiwa kuwaongoza wananchi wa Iraq wakafanikiwa kuzuiya kulipuka kwa matendo ya kulipizana visasi ambayo yangeleta vita ya wenyewe kwa wenyewe. Lakini swali ni, je, baada ya Masheikh kufanikiwa kutuliza waumini wao na wananchi kwa ujumla katika tukio hilo la kulipuliwa Msikiti wa al-Askari, Iraq ilitulia? Jibu ni kuwa haikutulia. Ingawa Masheikh walifanikiwa kutuliza waumini wao katika tukio hilo, lakini masiku yaliyofuatia yalishuhudia umwagaji damu wa kutisha ambapo Misikiti ilikuwa ikilipuliwa, waumini wa pande zote mbili wakiuliwa, ikawa hasa ni umwagaji damu baina ya Washia na Wasuni. Ingekuwa Tanzania ingekuwa ni ulipuaji Misikiti na Makanisa huku damu ikimwagika na roho zikiangamia kwa maelfu. Taarifa mbalimbali zinaonyesha kuwa watu waliouliwa katika mashambulizi haya yaliyoacha Iraq ikiwa nchi iliyogawika mapande mawili, zinasema kuwa watu zaidi ya 3,000 walikuwa wakiuliwa kila mwezi. Documentary moja iliyotolewa hivi karibuni, imefichua jinsi wavamizi wa Iraq walivyochochea mgogoro baina ya Washia na Wasuni, baada ya kuona kuwa wananchi wameshika silaha wamekuja juu kupinga uvamizi. Vilianzishwa vikosi vya Washia vya kufanya mashambulizi na mauwaji dhidi ya Wasuni. Vikosi na makundi ya kihalifu yakapewa silaha, mafunzo na fedha. Matokeo yake ni janga kwa wananchi
Polycap Kadinali Pengo vifanye kazi yao kwa umakini mkubwa na viseme kweli bila kujali nani anahusika. Katika kitabu A Plan to Divide and Destroy the Theology cha Dr. Michael Brant anaelezwa jinsi mabeberu walivyopatana kuweka mradi kabambe wa kuwagawa Waislamu na kupandikiza chuki miongoni mwao (Sunni na Shia) katika zile nchi zenye Waislamu wengi kama Pakistan. Baada ya kikao cha makachero wa nchi za kibeberu kilichofanyika mwaka 1983, Uingereza ikiwa kinara kwa sababu ina uozefu kwa sababu ilitawala nchi nyingi za Kiislamu, Dr. Brant anasema kuwa ulianzishwa mradi wa kuwashughulikia Waislamu katika nchi za Kiislamu uliotengewa kiasi cha Dola milioni 4 kila mwaka. Inaelezwa kuwa lengo ni kuhakikisha kuwa Waislamu hawawi kipingamizi mahali popote ambapo mabeberu watataka kuingia kuvuna rasilimali na masilahi yake mengine. It was calculated that by 2010 the situation between Shias and Sunnis would be so bad that USA would be able to capitalize upon it to its maximum benet. Also, with its stooges in already in place at the top theocratic positions in Sunni factions and the new breed of Shia scholars reaching the top positions (nurtured by the CIA from the start), US wouldnt have to sacrice a lot. Huo ni muhutasari wa yaliyotarajiwa kuwa manufaa watakayopata mabeberu kutokana na mradi huo. Hapana shaka hali tunayoiona na kuisikia Pakistan, Iraq na kwingineko, ni matokeo ya mkakati huu uliowekwa mwaka 1983. La kuzingatia hapa ni kuwa kama kutakuwa na watu wa nje ambao wanadhani watanufaika kwa namna yoyote iwapo Watanzania watachukiana na kupambana wenyewe kwa wenyewe, hawataingia kwa gia ya Wasuni na Washia wala Wasukuma na Wachaga. Uchochoro mwepesi ni wa Waislamu Vs Wakristo. Kwa hiyo, tunapochunguza suala hili, ni lazima tuzame kwa mapana na marefu. Kama ni mtu kawehuka tu tujue, lakini tujue kwa uhakika. Kama ni mtu mwenye masilahi ya kisiasa au aliyetumiwa na watu wengine wa ndani kwa masilahi Fulani, tujue na tujue pia kwa uhakika. Lakini pia kama kuna uhusiano na watu wa nje tujue na tujue kwa uhakika pia.
6
Na Omar Msangi
NI lazima wawe Waarabu. Isingekuwa jambo la kueleweka iw a p o w a t u wa nje waliokamatwa wakituhumiwa kuhusika na shambulio la bomu Kanisani Arusha, ingesemwa kuwa ni Wajerumani, Wataliano au Wamarekani! Akitoa taarifa fupi ya awali Bungeni Jumanne wiki hii, Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda alisema kuwa Waarabu wanaoshikiliwa walikamatwa tu katika utaratibu wa kawaida wa kutaka kujiridhisha kuwa hawahusiki kwa namna yoyote. Akifafanua akasema kuwa Wa a r a b u h a o w a l i k u w a wakisafiri kwenda Nairobi kwa njia ya barabara, lakini kwa vile mipaka ilikuwa imefungwa, haikuwa rahisi kwao kupita. Walikamatwa ili wahojiwe. Labda swali hapa laweza kuwa, kama mipaka ilikuwa imefungwa ili kuwachunguza watu wote wanaopita, Jumapili siku ya tukio hilo hawakuwahi kupita Wazungu? Kwa nini wakamatwe Waarabu peke yao? Kabla ya kutokea vurugu wilayani Geita zilizosababisha kuuliwa kiongozi mmoja wa kidini, palifanyika mhadhara mkubwa wa Kikristo ambapo Wakristo walihamasishwa juu ya suala la kuchinja. Mhadhara ule ndio uliozua balaa kwa sababu Wakristo walipotoka pale walikwenda kutekeleza waliyoambiwa jambo lililoleta vurugu. Iliwahi kuarifiwa katika baadhi ya vyombo vya habari kuwa katika mhadhara ule palikuwa na Wazungu, watu kutoka nje. Serikali mpaka leo haikuwahi kusema lolote juu ya uwezekano wa Wazungu wale kuhusika kuwachochea Wakristo wa Geita. Swali ni je, mhadhara ule ungekuwa ni wa Waislamu na wangekuwepo Waarabu, hali ingekuwaje? Je, Serikali ingekuwa kimya mpaka leo? Isingesema lolote kuhusiana na wageni wale? Mwezi Februari mwaka huu 2013 kundi kubwa la Wazungu lilikuwa limesambaa katika Wilaya ya Same. Wa k i w a k a t i k a v i k u n d i vidogo vidogo walikuwa na Kamera za Video wakipiga picha maeneo mbalimbali kuanzia kule Kiwanja, Stesheni, Kavambughu, Majevu, Mwembe, Same mjini na maeneo mengine. Japo wananchi walikuwa wakijiuliza, Wazungu wale walikuwa na lengo gani, hasa walivyokuwa wakichukua tahadhari wakigundua kuwa kuna mtu anawafuatilia, lakini hapakuwa na namna yoyote ilionekana Serikali ikishughulishwa na Wazungu hao. Inawezekana walikuwa washajieleza kwa mamlaka husika na serikali ilishajua nini wanafanya na iliridhika. Hatujui. Lakini ni mara nyingi tumeona Masheikh wa
MAKALA
AN-NUUR
Makala
AN-NUUR
8
Na Omar Msangi
NCHI yetu inapita katika kipindi tete na lau hatutakuwa makini, tutatumbukia katika janga ambalo huenda tukaona tu mlango wa kuingilia, lakini itakuwa tabu kuona wa kutokea hata kama tutataka kutoka. Lakini kabla ya kwenda mbele niungane kwanza na Watanzania wote kulani tukio lililotokea Arusha ambapo inatuhumiwa kuwa mtu mmoja alirusha bomu kanisani lililoua mpaka sasa watu watatu na wengine wengi kujeruhiwa. Shambulio hilo lilifanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti, jijini Arusha. Taarifa za awali ambazo zishatolewa na Serikali zinafahamisha kuwa kijana mmoja anayejulikana kwa jina la Victor Ambrose anashikiliwa na Polisi akituhumiwa kurusha bomu hilo. Vijana wengine wa Kitanzania waliotajwa (kwa jina moja tu) kukamatwa ni Joseph na David. Aidha wanashikiliwa pia raia wanne kutoka nchi za Kiarabu. Tunaambiwa kuwa watu hao wa Kiarabu waliingia nchini Jumamosi usiku kwa ndege kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), na kwamba walitaka kuondoka Jumapili kwa gari kuelekea Kenya kwa njia ya barabara kupitia Namanga. Hadi sasa taarifa ya Polisi haijafafanua ni kwa nini Waarabu hao wamekamatwa kwa maana kuwa ni sababu gani zilizopelekea watuhumiwe kuhusika na tukio hilo. Hata hivyo taarifa ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulugo inasema kuwa, Victor Ambrose ndiye aliyewataja watuhumiwa hao Waarabu na kuelekeza walipo. Mulugo alisema raia hao wa Saudi Arabia waliingia nchini kupitia kiwanja cha Kimataifa cha Kilimanjaro (KIA) Mei 4, na Mei 6, walikuwa wakitoroka nchini kupitia mpaka wa Namanga wakielekea nchini Kenya. Liliripoti gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Mei 7, 2013. Pengine swali la kuuliza hapa ni je, Waarabu hao walikuwa WAKITOROKA au wakienda Kenya (Nairobi) kwa njia ya barabara? Na kama Victor Ambrose ndiye aliyewataja, huyu Victor ni nani na nini uhusiano wake na Waarabu hao? Awali gazeti la Mwananchi likiripoti habari hizi, likimnukuu msemaji wa wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Arusha, Padri Festus Mangwangi, lilisema kuwa mtu aliyerusha bomu hilo alikuwa amevaa Kanzu. Hiyo ilikuwa Jumatatu, Mei 6, 2013. Katika kuripoti taarifa ya Serikali juu ya watuhumiwa likasema, Wasaudia wanne mbaroni, FBI watua. Likimnukuu Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mwananchi likasema kuwa Waarabu hao waliingia nchini Jumamosi na siku iliyofuata ndipo kukatokea ulipuaji huo. Na kwamba lengo la shambulizi hilo lilikuwa kumdhuru Askofu Padilla. Lilisema Mwananchi na kumnukuu Mkuu huyo wa Mkoa akisema kuwa Victor Calisti Ambrose ndie aliyesaidia kuwapata watu hao wa Saudi Arabia.
Makala
AN-NUUR
Wapo wapi Uamsho waliotua Dar kuchoma Makanisa Wabunge wasicharuke tu, wahoji mambo ya msingi Kasema kweli Samia Suluhu, tuwe na yakini kwanza
Serikali ambapo katika baadhi ya matukio zilikuwa zikiachwa alama na vidhibiti ambavyo kwa namna yoyote vitaonyesha kuwa wahusika ni waasi wa kundi la Farabundo Mart National Liberation Front (FMLN). Hata hivyo uchunguzi uliokuja kufanywa kiasi miaka 31 baadae ulikuja kubaini kuwa waliohusika na mauwaji hayo walikuwa maosa wa Jeshi la Serikali na kwamba walitumiwa na mataifa ya nje ambao walikuwa wakitaka kuzima sauti za wananchi wazalendo ambao walikuwa wakipinga ubeberu wa mataifa hayo. Mataifa hayo ya kibeberu yanatajwa pia kwamba pamoja na kuwatumia wanajeshi wa Serikali kuzima harakati za wananchi wazalendo, walikuwa pia wakitumia vikundi vya kigaidi (armed rebels) kuuwa viongozi wa dini na wa Serikali. Kwa upande mwingine taarifa hiyo inataja pia jinsi Mahakama Kuu (Supreme Court) ya El Salvador ilivyotumiwa kuhakikisha kuwa watuhumniwa wakuu, ambao walikuwa makamanda wa jeshi, waliokimbilia nchi za nje, hawakamatwi na kurejeshwa nchini El Salvador kushitakiwa. Learn from History, 31st Anniversary of the Assassination of Archbishop Oscar Romero, ni taarifa iliyochapishwa kutokana na yaliyonukuliwa kutoka National Security Archive Electronic Briefing Book No. 339. Taarifa hiyo kama ilivyoandikwa na kuwekwa katika mtandao na Kate Doyle na Emily Willard (March 23, 2011), inafafanua jinsi maosa kadhaa wa kijeshi (Captains) Alvaro Rafael Saravia, Eduardo Avila, na Fernando (El Negro) Sagrera, walivyohusika katika kumuuwa Askofu Mkuu Romero. H o w We K i l l e d t h e Archbishop, ni taarifa ndefu iliyonukuliwa ikinukuu mahojiano ya Alvaro Saravia akielezea walivyohusika kumuuwa Askofu Mkuu huyo. Mauwaji ambayo ni kama yalitia Petroli katika mgogoro wa El Salvador. Watu wakazidi kuuwana. Lakini muhimu kufahamu hapa ni kuwa waliohusika kumuuwa Askofu Mkuu Romero ni maofisa katika jeshi na walitumiwa na mabeberu waliotaka kulinda masilahi yao katika Amerika ya Kusini. Kama alivyosema Mheshimiwa Mnyaa (MB), katika suala hili tusiangalie tu Waislamu na Wakristo, kwa maana kuwa tusitizame ndani tu. Akasema kuwa tutizame isije ikawa kuna chokochoko za kutoka nje. Tukumbuke kuwa kuna Balozi mmoja aliwahi kusimama katika jukwaa la kidini na kuwataka Wakristo wawe macho na Waislamu. Kwa maana nyingine alikuwa akiwaambia Wakristo wa Tanzania wawatizame Waislamu kama maadui zao. Yupo Bwana mmoja karejea
hivi majuzi kutoka safari yake ya kikazi Kilwa. Nilipokuwa nazungumza naye Jumatatu wiki hii akasema kuwa alikutana na mama mmoja akiwa anahadithia jinsi walivyotahadharishwa na Padiri wao Kanisani kuwa (eti) wawe macho maana wale watu wanaochoma Makanisa wameingia Kilwa. Hapa lazima tujiulize, hizi taarifa kuwa kuna kikosi cha Waislamu waliodhamiria kuchoma makanisa zimetoka wapi? Je, nini lengo la viongozi wa makanisa kusambaza habari hizi? Je, vyombo vya usalama vina taarifa hizi na hatua gani zimechukuliwa? Ukiacha taarifa za mama huyu wa Kilwa, lakini upo waraka maalum wa Makanisa ambapo ilidaiwa kuwa kuna kikosi cha Waislamu kimeingia Mbeya kwa ajili ya kuchoma makanisa. Akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari Desemba mwaka jana, Katibu Mkuu wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (PCT), Askofu David Mwasota aliwataka Wakristo kujitayarisha kupambana na Waislamu aliodai kuwa wameunda vikosi vya kuchoma makanisa. Akawataka kujihami kwa visu, mikuki na mishale. Likielekea mitamboni, bado uchomaji moto makanisa jijini Dar es Salaam ulikuwa ukiendelea ambapo Kanisa la Kipentekoste la Faraja International Yombo Dovya lilikuwa likiteketea huku jingine la KKKT Yombo Dovya nalo likinusurika kuteketezwa na watu wanaojiita wanaharakati wa Kiislamu. Mlinzi wa Kanisa hilo aliripotiwa kujeruhiwa. Hivi ndivyo lilivyoripoti gazeti la Msema Kweli likisherehesha taarifa ya Katibu Mkuu wa PCT, Askofu David Mwasota. Lililo la uhakika ni kuwa vyombo vya usalama vina habari na barua hiyo ya wachungaji. Swali ni je, madai hayo kuwa kuna kikosi cha Waislamu wachoma makanisa kilichoingia Mbeya zilikuwa za kweli? Kama jibu ni ndio, serikali ilichukua hatua gani dhidi ya watu hao? Mbona mpaka sasa hatujasikia kuwa kuna watu walikamatwa wakienda Mbeya kuchoma makanisa? Kama taarifa hazikuwa sahihi, serikali ilichukua hatua gani dhidi ya wanaosambaza uzushi na taarifa hizo za kichochezi? Makanisa yaliyodaiwa kuchomwa Yombo, ulikuwa ni uzushi mtupu. Hakukuwa na Kanisa lililochomwa moto. Swali ni je, hatua gani zilichukuliwa kwa waliosambaza habari hizo za uwongo? Je, hatudhani kuwa kwa kutokukemea taarifa kama hizo na kuwachukulia hatua wahusika, tunasababisha ziaminike na hivyo kuwafanya Wakristo kuwachukia Waislamu? Inaonyesha kuwa kuna watu wamekamia kuona kuwa Waislamu wanasajiliwa kama wahalifu wachoma makanisa na Serikali inakuwa upande wao kwa huruma. Je, katika mazingira haya, watu hawa wakipata fursa
9
kwenye madrasa juu ya heshima na adabu yako pale pale. Hayo ni matakwa ya Quran na Hadith. Ingawa kweli Waislamu wa leo wameamua kuwa w amechoka kuonewa, ile khulka yao ya adabu bado imo na hujitokeza hata pale ambapo wao wameamua kuchukua hatua za kujaribu kukomesha kuonewa huko. Itakumbukwa kwamba katika kadhia ile ya kuvunja mabucha ya nyama ya nguruwe Waislamu hawakuzuka tu kuanza kuyavunja na kubomoa, maduka yale. Kwa heshima kubw a kabisa walipeleka malalamiko yao kwa viongozi wanaohusika ili wachukue hatua zinazostahili. Sheria za nchi mpaka leo haziruhusu uuzaji wa nyama ya nguruwe katika makazi ya watu mijini. Hilo walikuwa wakilifahamu ndipo kwa heshima waliyofundishwa madrasa na nyumbani walipeleka malalamiko yao panapostahili. Ushahidi unaofahamika ni kuwa ilikuwa ni baada ya kuonyesha heshima hiyo, walilopewa ni dharau na kubezwa tu. Inasemekana kuwa hata dini yao ilidharauliwa. Bahati mbaya Sheikh Jongo hakuzungumzia huyu Muislamu anayedharauliwa na dini yake pia kubezwa afanyeje kuhifadhi heshima yake, ya Waislamu wenziwe na dini ile ya Uislamu, dini ya Allah. Nilibahatika kuhudhuria Swalat-il-Jumaa ya tarehe 3 May, 2013 kule msikiti maarufu wa Wa-Manyema Khutba akiwa Sheikh Hamid Masoud Jongo. AlhamduliLlahi huyu Sheikh amekuwa Imam kiongozi wa msikiti huo kwa takriban miaka
TANGAZO
AN-NUUR
Na Khalid S Mtwangi IMEKUWA inafahamika kwa muda mrefu sana kuwa ile elimu inayotolewa katika madrasa za Kiislamu sifa kubwa ni ile ya kuwafundisha wanafunzi umuhimu wa kuwa na heshima na adabu kwa kila mtu. Waliopata elimu yao huko wana sifa hiyo sana kila wanapokuwepo. Lakini pia ni khulka hiyo ndiyo imetumiwa na maadui wa Uislamu kuwakandamiza Waislamu kwa sababu ya kuwaheshimu wakubwa kazini na katika maisha ya kawaida. Tukumbukle ule msemo unaofahamika miongoni mwa Waislamu kuwa HEWALLAH SI UTUMWA. Kweli hivi sasa mambo yamebadilika kidogo kuhusu msemo huo na hapo ndipo pameanza matatizo na kuleta yale yasio na maana yeyote ya kuitwa ati kuna Waislamu wenye msimamo mkali . Hawa vijana wameamua tu kwamba sasa kuonewa kwa sababu ya itikadi yao basi. Lakini kwa kiasi kikubwa yale wanayofundishwa nyumbani na Inatoka Uk. 8 (Wakristo) kwa kuwathibitishia kuwa nyendo na njama za mashabiki wa makundi hayo zinajulikana na wanafuatiliwa tangu unyayo hadi kivuli kabla hawajaleta madhara. Habari kama hii inathibitisha jambo moja tu: kuwa kuna jitihada za makusudi za kuchochea chuki na uhasama baina ya Waislamu na Wakristo. Kabla ya viongozi wetu, na hasa Wabunge kucharuka, labda waulize vyombo vyetu vya usalama: Je, walikuwa na taarifa ya boti tatu za kukodiwa zilizoleta Waislamu 150 kutoka Zanzibar kwa lengo la kuchoma makanisa? Je, waliwaona walipotua Mbweni na kuchukua daladala hadi Tandika ambapo inaelezwa kuwa haikuwa tabu kuwagundua kwani inasemwa kuwa walikuwa na alama za kuwatambulisha kuwa ni Uamsho (Waislamu)? Je, vyombo vya usalama vilichukua hatua gani, maana tumeambiwa kuwa waliwatoa wasiwasi Wakristo kuwa watulie na wawe na amani kwa sababu Polisi wanafuatilia nyendo za Waislamu hao wachoma makanisa tangu unyayo hadi kivuli. Kama taarifa zote hizi zilizoelezwa katika gazeti tulilolinukuu hazikuwa sahihi, maana yake ni kuwa lilikuwa linapandikiza chuki, uhasama na uchochezi. Je, vyombo vya dola vilichukua hatua gani? Kwa Serikali kukaa kimya, maana
wasifanye hivyo kwa kuwa na wao watakuwa kama vile wameungana na Iblis ambaye ndiye aliyekuwa akimpoteza hivyo yule Swahaba. Mtume alipendekeza tu nasaha ziendelee. Kufuatana na mfano huu kama alivyonasihi Rasu-ul-Llah ni wazi kuwa kweli mtoto hana haki ya kuweza kumlaani ama hata kumkemea mzazi wake kwa matendo mabaya anayoyatenda huyu mzazi wake. Hiyo si heshima kabisa kufuatana na maadali ya Kiislamu, alisisitiza Sheikh Hamid Masoud Jongo. Alisistiza kwa mkazo kabisa kuwa ni muhimu kwa wazazi wa Kiislamu kuwafundisha watoto wao heshima na adabu kufuatana na mafundisho ya Quran na Hadith. Hapo alipendekeza kuwa Madrasa ziwe ndio kitovu cha mafundisho hayo. Hakika kwa muda mrefu sana Madrasa hata kama ni yale ya pembeni, mwa nyuumba yamekuwa ndio kiini cha maadili ya Kiislamu na msingi wa utekelezaji wa yale Muislamu anatakikana ayatekeleze iwe FARDHI ama SUNNA. Kwa siku hizi pia ni muhimu kuisisitiza kwa hawa vijana kuwa ni lazima waihami dini ya Sub-hana Wa Taala. Kwa muda mrefu Waislamu wamekuwa wakinyanyaswa kwa vile wamefundishwa heshima na adabu ya hali ya juu kabisa. Kumekuwa wale adui wa Uislamu wamekiona hicho kama Waislamu wanyonge wanaoweza kusukumwa huku na kule. Ingawa kweli Sheikh Hamid Masoud Jongo hakulitaja hili, lakini bila shaka atakubaliana na hoja ya kuwataka Waislamu
Mbatia kwamba katika kufanya kazi zake, vyombo vya dola viwe na uadilifu wa hali ya juu.
Omar Bakar Almas Video Production wanakutangazia kuwa katika maduka yao ya mtaa wa Livingstone na Mahiwa mkabala na Kariakoo Bazar na lile la mtaa wa Mafia jirani na Msikiti wa Manyema Kariakoo jijini Dar es Salaam zinapatikana DVD, CD Original na mawaidha ya Kiislamu kutoka kwa Masheikh wetu maarufu. Pia CD mpya za Sheikh Nurdin Kishki za kila wiki zinapatikana pamoja na Hija ya mwaka 2012 aliyeiongoza yeye, Njoo ujipatie DVD bora zenye kiwango cha kimataifa. Kwa mawasiliano zaidi piga simu kwa namba zifuatazo: 0754 805 528, 0785 793 395 au 0716 888 358 NYOTE MNAKARIBISHWA
Tangazo
Visiegemee upande wa dini yoyote. Na kama alivyosema pia Muadhama Polycap Kadinali Pengo, katika kuchunguza tukio hili, ni lazima ukweli uanikwe hadharani bila kujali unamgusa nani.
10
Na Said Rajab JUMATATU ya April 15 mwaka huu, jiji la Boston, Massachusetts nchini Marekani, lilishambuliwa kwa mabomu mazito mawili wakati wa mashindano ya mbio za Marathon za Boston. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, watu watatu walipoteza maisha na wengine 171 kujeruhiwa vibaya. Kwa takriban wiki yote ile, tulishuhudia vyombo vya habari vya nchi za Magharibi vikiripoti tukio lile kama habari ya kwanza yenye uzito mkubwa. Licha ya hatari ya kuhukumu kabla ya uchunguzi kufanyika, hisia za watu wote duniani zikaelekezwa na vyombo hivyo kwamba waliolipua mabomu yale ni Waislamu. Wakati mtuhumiwa mmoja alipouawa kwa risasi, na msako wa mwingine ulipoanza, ambao wote ni ndugu, na raia wa Marekani wenye asili ya Chechnya, tulishuhudia maneno ya chuki dhidi ya Uislamu yakihusishwa na tukio hilo. Walikuwa wakijaribu kuhusisha uhalifu ule na Uislamu wa Watuhumiwa. Gazeti la An nuur liliandika kwa kirefu sana kuhusu habari ile na miye siyo lengo langu hasa kuwachosha wasomaji. Bali ningependa tu kuchambua kidogo baadhi ya mambo, ili iwe changamoto ya kra kwa wasomaji wanaofuatilia masuala ya dunia. Matukio kama hayo yanapotokea, basi fursa pia hupatikana ya kuwekana sawa kimtazamo. Kwa masikitiko makubwa, kelele hizi za vyombo vya habari, zikiungwa mkono na maoni ya wanasiasa wenye chuki dhidi ya Uislamu, zikajenga mtazamo kwamba, ingawa Waislamu wote siyo magaidi, lakini magaidi wengi hakika ni Waislamu. Hata hivyo, mtazamo kama huo unakosa mashiko, pale unapoulinganisha na idadi halisi ya mashambulizi ya kigaidi. Gazeti la Europol lilichapisha tak w imu zin azo o n y es h a kwamba kati ya mwaka 2006 mpaka 2008, asilimia 99.6 ya shughuli zote za kigaidi barani Ulaya, zilifanywa na wasio Waislamu. Na rekodi rasmi za FBI zinaonyesha kwamba asilimia 94 ya mashambulizi ya kigaidi katika ardhi ya Marekani kuanzia mwaka 1980 mpaka 2005 yalifanywa na wasio Waislamu. Kinachokera zaidi ni kwamba taarifa potofu za vyombo vya habari ndizo zinazoaminika na kujenga mitazamo hasi dhidi ya Waislamu, lakini zile halisi hazipewi nafasi, kwa hiyo hazijulikani kwa watu wengi. Tatizo lingine kubwa la vyombo vya habari ni kutoa tuhuma za jumla jumla. Yaani Muislamu mmoja akituhumiwa kufanya uhalifu, basi jamii nzima ya Waislamu inalaumiwa kwa hilo. Kimsingi, Uislamu unakataza vitendo vya ukatili na kumwaga damu za watu wasio na hatia, kama tulivyoona katika mabomu ya Boston. Lakini kwanini Waislamu wote wanaoishi Marekani walaumiwe, wasumbuliwe na watishiwe kwa sababu ya mabomu ya Boston? S i y o Wa k a t o l i k i w o t e wanaohusishwa na kashfa ya kulawiti watoto, kwa sababu tu baadhi ya mapadri wamekuwa wakifanya uchafu huo! Siyo
Makala
AN-NUUR
na simanzi zetu? Lazima tuumizwe na kukasirishwa na vitendo vyote vya ukiukaji haki na mauaji ya binadamu wasio na hatia duniani kote. Tunaona upendeleo waziwazi. Vifo vinavyotokea ulimwengu wa Magharibi vinaripotiwa kwa kina na kugeuzwa ajenda ya dunia, lakini vifo na madhila yanayotokea katika ulimwengu wa Waislamu vinaripotiwa kidogo sana! Mbaya zaidi madhila hayo huletwa na Serikali za Magharibi, hususan Marekani. Ukichimba zaidi, utaona ulimwengu wa Magharibi umetumia shambulio la Boston kukamilisha ajenda zake za kisiasa. Jinsi vyombo vya habari vilivyoripoti kwa kina tukio hilo, msukosuko waliopata Waislamu kabla ya kutambuliwa mtuhumiwa, kukamatwa kwa mwanafunzi mmoja wa Saudi Arabia, aliyekuwepo kwenye eneo la tukio na jitihada kubwa za kuwatupia lawama Waislamu, kabla ya ukweli kufahamika ni sehemu tu ya picha pana zaidi. Inafahamika vizuri kwamba shambulio hili la Boston litageuzwa geuzwa ili kukamilisha malengo fulani ya sera ya nje ya Marekani, ikiwa ni pamoja na kuhalalisha matumizi ya kijeshi, na kuhuisha propaganda inayovia kwamba Marekani inakabiliwa na tishio la magaidi. Makaburi ya wale waliokufa kwenye
Inatoka Uk. 12 waliosalimika kuishi maisha ya hofu, serikali imeshindwa kukomesha hali hiyo. Wakati akitoa taarifa Bungeni baada ya kuzuru eneo la tukio huko Arusha kufuatia tukio hilo, Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mizengo Pinda, alisema kuwa watu nane wameshakamatwa, wanne wakiwa ni wa asili ya Uarabuni, wanne Watanzania ambao aliwataja kuwa ni Victor Ambrose, mwenzake ni Joseph na mwingine ambaye hakutajwa. Naye kama ilivyokuwa kwa wabunge wengine, hakusita kuonya kwamba katika tukio la safari hii siasa, dini na kauli za kichochezi zisihusishwe na tukio hili, na badala yake vyombo vya dola viachwe vifanye kazi yake na kutoa majibu. Hata hivyo, baadhi ya vyombo vya habari na baadhi ya wasemaji wa Polisi, bado hawajaona kama kuna haja ya kuacha kutoa habari za matukio ya jinai huku wakidhihirisha chuki zao za kidini. Baada tu ya kutokea mlipuko katika kanisa hilo, gazeti moja la kila siku liliripoti siku ya Jumatatu, kwamba aliyerusha bomu hilo alikuwa amevaa kanzu nyeupe na koti la mvua. Na alikimbia baada ya kurusha bomu hilo na kwamba tukio hilo lilishuhudiwa na mtoto mdogo. Hiyo ni kauli aliyonukuliwa akizungumza msemaji wa kanisa Katoliki Jimbo la Arusha Padri Festus Mangwangi. Iliendelea kuwa aliyerusha bomu huyo wakati wanakimbia huku akiwachanganya watu
6, Msemaji wa Kanisa Katoliki Jimbo la Arusha Bw. Padri Festus Mangwangi amenukuliwa akieleza kwamba, aliyerusha bomu kanisani ni mtu aliyekuwa kavaa kanzu. Kwamba hata baada ya kulirusha, alikimbia huku akipiga kelele za mwizi na kutokomea huku watu wakiwa wamezubaa. Katika gazeti la Mtanzania la Jumanne, lilitaarifu kuwa anayetuhumiwa kurusha bomu ni dereva wa bodaboda Victor Ambrose, ambaye inaonekana alirusha bomu na kutoweka na pikipiki. Hapa tunahabarishwa juu ya watu wawili wanaosadikiwa kurusha bomu. Kuna aliyevaa kanzu nyeupe na koti la mvua na Victor Ambrose, dereva wa bodaboda! Je, wananchi washike lipi? Kwa upande mwingine, yapo magazeti kama NIPASHE ambayo yaliripoti kuwa Waarabu walikamatwa WAKITOROKA baada ya shambulizi. Anachosema mwandishi hapa ni kuwa Waarabu hao ndio waliolipua bomu maana kama si wao hawakuwa na sababu ya kutoroka. Swali ni je, walikuwa wakitoroka au wakienda Nairobi? Katika mazingira haya, kuna haja ya vyombo vya habari navyo kuacha kuripoti matukio haya yanayogusa imani za watu, kwa kuegemea hisia za mwandishi au Mhariri, au kwa msukumo wa udini na chuki ili kupoteza uhalisia wa tukio lenyewe.
11
Na Sheikh Abou Bakar Soliman SHUKRANI zote anastihiki Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe wote na Rehema na Amani zimfikie yule aliye tumwa kuwa ni Rehema kwa viumbe vyote ambae ni mtume wetu Muhamad. Ama baada ya utangulizi huu umefikia Uislamu msamaha wake ukomo wa ukubwa ambao haujapata kukia hapo kale wale hautokiwa baadae katika sheria. Maisha ya Amani yemeletwa na Uislamu kwa watu wote. Basi mazungumzo yetu ya leo ni juu ya vyanzo vya kra na nadharia juu ya msamaha huu. Sisi waislamu tunaamini tupo katika haki na wengine wapo katika batili. Sisi tupo katika uongofu na wengine wapo katika Upotevu sisi ni waumini na wengine ni makafiri katika mtazamo wetu na vipi tuishi nao makafiri kwa mshamaha huu ambao Uislamu umeuleta. Msamaha huu una shina na msingi wa kikra muhimu.
Mwanzo wa shina hilo ni imani yetu kuwa kutofautiana na watu ni kwa uwezo wa mwenyezi Mungu na yeye ndiye anayetaka haya yote yatokee na hakuna wa kuzuia anayoyataka Mungu na uwezo wa Mwenyezi Mungu umeambatana na hekima zake kwani yeye halifanyi jambo isipokuwa lina hekima. Anaijua atakaejua na ataekosa kuijua na hivyo sio kwa tama za Muislamu hii ni kinyume cha matakwa ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Amesema mwanyezi Mungu Mtukufu. (Lau angetaka Mola wako wangeamini watu wote duniani hivi wewe unawachukia watu hadi wawe waumini Na shina la pili ni kwamba kari na muumini hisabu zao sio hapa duniani na hazitolewi ni kiumbe bali hesabu zao juu ya ukari au Imani inakua ni huko akhera na inatoka kwa mwenyezi Mungu Mtukufu anasema Allah Na wakikujia wambie Mwenyezi mungu anayajua ninayoyafanya. Mwenyezi Mungu atahukumu kazi yenu siku ya kiama kwa yale mnayotofautiana hadi 68 69 hukumu siku ya kiama inatoka kwa Mwenyezi Mungu na sio kutoka kwako wewe. Na pia anasema Mola Mtukufu Mwenyezi Mungu ni Mola wetu na Mola wenu sisi tunamatendo
Makala/Tangazo
AN-NUUR
Uislamu unaamrisha uadilifu (usawa) kwa watu wote na usawa sio kwa Waislamu peke yao. Akasema Allah Na mnapo hukumiwa kati ya watu hukumianeni kwa usawa (Uadilifu Nisai 58) Basi uadilifu wa mwenyezi Mungu ni kwa viumbe wake wote kwani zimeteremshwa aya tisa katika Surat nisai 105113 kwa kumtetea myahudi ambaye alituhumiwa wizi na ilikuwa walio iba ni ni Waislamu au katika walio tuhumiwa juu ya unafiki. Walijaribu kumbandikizia hizi tuhuma huyu myahudi na alikusudia mtume kutaka kuwatetea wezi hawa na i k a t e r e m k a Q u r- a n i i l i kumtakasa huyu Myahudi na
kumtetea. Na kuwaonyesha hawa ambao walijaribu kumpa tuhuma asiyehusika basi usawa haugawanyiki na wala haupimiki kwa mizani bali ni kwa uadilifu na usawa na mwenyezi Mungu anasema:Enyi mlioamini kuweni na msimamo kwa ajili ya mwenyezi Mungu mashahidi wa Usawa (uadilifu) na wala zisikudanganyeni uadui wa watu hadi mkaacha uadilifu (USAWA) fanyeni uadilifu huko ndio karibu na ucha Mungu na mcheni Mwenyezi Mungu Su-rat Maidah. Uadui maana yake sawa ikiwa uadui huo na dharau hizo ni kwenu nyinyi kwao au bughudha yao kwenu isikuchukulieni vitu hivyo mkaacha kufanya uadilifu (usawa) na katika hadithi (Dua ya aliyedhulumiwa hata kama ni kari haina pazia kati yake na mwenyezi Mungu Tunamuomba Mw enyezi
na tatizo kwa sababu nyingine. Mshirika wa CIA wa zamani Milt Bearden, aliyesaidia kutoa mafunzo kwa wapiganaji wa Mujahidina nchini Afghanistan, amekumbushia kuwa ingekuwa jambo la ajabu kuwa wanachama wa Al Qaeda walivaa vibanio kichwa vya aina hiyo. Kibanio kichwa chekundu ni kielelezo maalum cha mavazi ya wafuasi wa madhehebu ya Shia. Kinatokea wakati wa kuanzishwa kwa dhehebu hilo ...Kinawakilisha utayari wa mvaaji wa kibanio kichwa chekundu kutoa maisha yake, kujiua kwa ajili ya harakati. Wa-Sunni, ambao kwa wingi zaidi ndiyo wafuasi wa Osama bin Laden hawafanyi hivi. Tukisikia muda mfupi baada ya kuvamiwa Irak kuwa baadhi ya watu katika serikali ya Marekani hawakuwa wanajua tofauti kati ya Waislamu wa Sunni na Shia. Hivi ni watu kama hawa walioamua kuwa wateka nyara waelezewe kuwa walikuwa wamevaa vibanio kichwa vyekundu? 6. Habari kuhusu mizigo ya Atta kwenye ndege inaonyesha kuhusika kwa washiriki wa Al Qaeda? Ushahidi ambao unasemekana kutoa uthibitisho wa nguvu zaidi kuwa ndege hizo zilitekwa na Mohamed Atta na wanachama wengine wa Al Qaeda ni kuwepo kwa mabegi mawili ya Atta yaliyogunduliwa uwanja wa ndege wa Boston baada
ya mashambulio. Mabegi yalikuwapo, tulielezwa, kwa sababu licha ya Atta kuwepo Boston hapo Septemba 10, yeye na mshirika mwingine wa Al Qaeda, Abdul al-Omari, walikodisha Nissan ya buluu na kuendesha hadi Portland, jimbo la Maine, na kulala huko. Waliingia ndege ya safari fupi kurudi Boston mapema kesho yake tayari kupanda ndege ya Safari ya 11, lakini mabegi ya Atta yalibaki nyuma. Mabegi hayo yanasemekana yalikuwa na ushahidi mwingi wa kuonyesha kuhusika na utekaji nyara, ikiwa ni pamoja na kompyuta ya uendeshaji ndege ya kushika mkononi, mtaala wa kuonyesha jinsi ya kuruka, mikanda miwili ya video kuhusu ndege za Boeing, rula ya hesabu za mruko angani, nakala ya Qurani, na hati ya maelekezo kuhusu akifa nini kifanyike. Vifaa hivi vilichukuliwa kote kama ushahidi kuwa Al Qaeda na hivyo Osama bin Laden walihusika na mashambulio ya 9/11. Yakiangaliwa kwa karibu, hata hivyo, habari hizi za Atta kwenda Portland zinapoteza uthabiti wowote. Tatizo moja ni wazo kuwa Atta alikuwa amepanga kupeleka vitu hivi katika sanduku ambalo lingepelekwa ndege ya Safari ya 11. Nini ambacho kompyuta ya uendeshaji ndege na vifaa vingine vya kuruka angani ndani ya begi katika sehemu ya mizigo ingemsaidia kwa shughuli ya utekaji? Angetaka vipi kuchukua hati yake ya nini kifanyike baada ya kifo chake ndani ya
ndege aliyopanga kuibamiza katika Kituo cha Biashara cha Kimataifa? Tatizo kubwa zaidi la habari hiyo hata hivyo haikutokea hadi Septemba 16, siku tano baada ya 9/11, baada ya kuporomoka kwa habari nyingine ya awali. Kwa mujibu wa taarifa za habari mara baada ya 9/11, vifaa hivyo vinavyoonyesha kuhusika, badala ya kukutwa katika mabegi ya Atta ndani ya uwanja wa ndege, vilikuwa katika Mitsubishi nyeupe, ambayo Atta aliiacha katika uwanja wa ndege wa Boston kunakoegeshwa m a g a r i . Wa t e k a j i w a w i l i waliendesha Nissan ya buluu hadi Portland halafu wakapanda ndege ya safari fupi kurudi Boston asubuji yake, lakini majina yao ni Adnan na Ameer Bukhari. Habari hii iliporomoka mchana wa Septemba 13 wakati ilipogunduliwa kuwa kina Bukhari hao wawili, ambao maosa wa serikali waliripotiwa kuwashuku kutokana na vifaa vilivyokuwa katika Nissan pale uwanja wa ndege ndogo wa Portland, hawakufa katika tukio la 9/11. Adnan alikuwa bado hai na Ameer alikufa mwaka uliotangulia. Ukichukulia habari hii ya Atta kwenda Portland, ni vipi unaweza kukwepa hitimisho kuwa ilikuwa imetungwa? (Makala hii imefasiriwa kutoka Kiingereza na Anil Kija kutoka makalakama ilivyoandikwa na Ibn e Abdul Haq)
12
AN-NUUR
MAKALA
12
Na Bakari Mwakangwale WATU waliodai kuwa ni maasa Uhamiaji na mmoja mkemia wametoka kapa, baada ya Mama Ponda, na wanae kugoma kuchukuliwa damu, mate na nywele, kwa ajili ya kujiridhisha na Uraia wa Sheikh Ponda. Watu hao inadaiwa kwamba walifika nyumbani kwa Bi. Mariamu Ally Kassa (Mama Ponda) mtaa wa Ngamiani, Ujiji Kigoma, mapema wiki hii na kumtaka Mama huyo pamoja na wanae wakubali kuchukuliwa vitu hivyo. Akiongea na An nuur, kwa simu kutoka Kigoma, Bw. Maabadi Issa Ponda, alisema alifuatwa na watu watatu ambapo wawili walidai kuwa ni Maafisa Uhamiaji kutoka Kigoma na mmoja alikuwa amejitambulisha kuwa ni mkemia kutoka Dar es Salaam, akiwa na vifaa vyake kwa ajili ya kuchukua walivyohitaji, kutoka kwao. Wale jamaa walikuja haja yao kubwa walitaka wachukue damu ya mama, mate au nywele pamoja na vitu kama hivyo kutoka kwa ndugu wa kuzaliwa na Sheikh Ponda. Baada ya mjadala mrefu tuligoma kutoa vitu hivyo. Alisema Bw. Maabadi. B w. M a a b a d i , a l i s e m a kwanza walitaka kujua kwamba huyo anayetakiwa kuchunguzwa damu, kwa maana ya Sheikh Ponda Issa Ponda, kama anafahamu suala hili. Alisema, watu hao hawakuwa na majibu yaliyonyooka kwa familia hiyo kwa ujumla kwani alidai walihoji zaidi kutaka kujua uhalali wa majibu ikiwa watachukua hivyo wanavyo hitajia, ikiwa hicho wanachodai kuwa uchunguzi watafanya wao wenyewe. Bw. Maabadi alisema, katika majibu yao jamaa hao walidai, kuwa Sheikh Ponda hana tatizo kwa kuwa yupo chini ya himaya ya Serikali, hivyo hatokuwa na hiyari ya kukataa kuchukuliwa damu kwa ajili ya vipimo. K w a m u j i b u w a B w. Maabadi, alimnukuu mama yao akisema kwamba yeye kama mama Ponda, hatochukuliwa damu, wala nywele kwa ajili wa hayo wanayokusudia kwenda kuyafanya dhidi ya mwanaye. Alisema, Mama Ponda aliwaeleza watu hao kuwa kama yupo mtu ambaye anasema Ponda Issa siyo mtoto wake, ajitokeze na ushahidi lakini siyo kusikia maneno ya uzushi na kusababisha usumbufu. Kwa kifupi mjadala ulikuwa mrefu sana mama na sisi wote tukibaki na msimamo wetu kuwa hatuchukuliwi damu, mate wala nywele, huku wao wakitusihi tukubaliane nao, mwisho waliamua kuondoka. Alisema Bw. Maabadi. Akiongea kufuatia tukio hilo, Bi. Mariamu Kassa (Mama wa Ponda), alitihibitisha kufuatwa na watu hao nyumbani kwake, wakimtaka yeye na mwanae mmoja wachukuliwe damu,
Wote watahadharisha kunyoshea mtu kidole Waandishi bado wanatuchanganya Mrusha bomu ni Ambrose au mwenye kanzu nyeupe
wa mzozo wa kuchinja, ambapo alisema inafahamika wazi kwamba kuna sheria kamili juu ya suala hilo, ambayo aliitaja kuwa ni sheria ya mwaka iliyopitishwa mwaka Desemba 6, 2008 ya Animal Welfare. Alihoji inakuwaje watu wanavunja sheria hiyo kwa kuanzisha uchochezi wa kuchinja na kusababisha vurugu na serikali kuwafumbia macho huku ikitambua fika uwepo wa sheria hiyo na kwamba walioleta hoja ya kuchinja wameikiuka sheria hiyo? Kwa upande wake Bw. Barwani yeye alisisitiza haja ya kuwepo mjadala wa kitaifa juu ya tatizo la udini nchini. Hata hivyo alishangazwa na juhudi za serikali kukia hatua ya kuazima vikosi vya FBI kutoka Marekani kuchunguza matukio ya mauaji ya Padri na mlipuko wa Olasiti, wakati miaka nenda rudi makumi ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) wamekuwa wakiuliwa, wengine kujeruhiwa vibaya na Inaendelea Uk. 10
Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.