Вы находитесь на странице: 1из 12

www.annuurpapers.co.

tz

Sauti ya Waislamu

Sheikh Azzan hoi Hospitalini Mnazi Mmoja Uk. 11

Waislamu wahoji mapingu yote ya nini

Katiba Mpya ifafanue nini maana ya kukashifu dini


Andha Kanoon, SMZ na yale ya UAMSHO
Uk.6

ISSN 0856 - 3861 Na. 1090 DHULQADAH 1434, IJUMAA , SEPT. 13-19, 2013 BEI TShs 500/=, Kshs

GNU- Zanzibar yawindwa


Na Waandishi wetu, Zanzibar
IMEBAINIKA kuwepo hujuma mbali mbali za kuiandama na kuihujumu Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar (GNU), tangu kuasisiwa kwake baada ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010. Wataalamu na wapembuzi wa mambo ya kisiasa wamekaririwa wakisema mtiririko wa matukio mbali mbali Nchini, unaashiria kuwepo kundi lisiloitakia mema Serikali hiyo iliyozaliwa baada ya Maridhiano ya Kisiasa ya Zanzibar ya Mwaka 2009. Wameainisha hujuma hizo kuwa ni pamoja na uchokozi wa makusudi uliokuwa ukitekelezwa

Maalim Ally Basaleh (kushoto).

Amitabh Bachchan

Vijay Singh.

Umma waapa kuilinda

na baadhi ya makada na vijana wahalifu kwa visingizio mbali mbali dhidi ya harakati ikiwemo ya Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu (JUMIKI) ili kuwachochea wananchi hatimaye wafarikiane, warejeshe hisia za chuki na ugomvi,

Inaendelea Uk. 9

SHEIKH Azzan Hamdan

SHEIKH Farid Hadd

2
S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786 Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM. www.annuurpapers.co.tz E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk Ofisi zetu zipo: Manzese Tip Top Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

AN-NUUR

KWA mujibu wa taarifa za BBC Swahili (9 Septemba, 2013 - Saa 14:11 GMT), suala la siasa kali Somalia, limekuwa likijadiliwa mjini Mogadishu. Wanaojadili suala hili ni pamoja na wasomi wa Kisomali, walimu wa dini na Masheikh ambao wanakutana katika kikao maalum kilichokuwa kikiendelea katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu. Kama ilivyoripotiwa na BBC, lengo la kikao na mjadala huo, ni kujaribu kutanzua tatizo la wanaodaiwa kuwa Waislamu wenye msimamo mkali wa kidini. Cha mno, BBC ikasema, n i u e l e wa wa u f a s i r i unaotumika na makundi ya Kiislamu yenye msimamo mkali wa kidini kama vile lile la Al-Shabab. Kwamba wajumbe wa kikao hicho wapatao 160 watakuwa wakitafsri na kutathmini tafsiri mwafaka kwa nia ya kuhamasisha jamii kuhusiana na tofauti ya tafsiri ya kidini na tofauti nyinginezo. Ufupi wa maneno, dhana na hoja inayojengwa hapa na kuongoza kikao hicho ni kuwa tatizo la Somalia ni msimamo mkali wa kidini wa baadhi ya makundi ya Kiislamu. Na hivyo, ili kutatua mgogoro wa Somalia, ndio inatafutwa tafsiri sahihi ya dini (Uislamu) na hivyo kuitofautisha na ile potofu wanayodaiwa kuwa nayo Al Shabab. Kwa mujibu wa makala moja iliyochapishwa katika gazeti hili, ni kutokana na dhana hiyo, mtangazaji wa BBC alitaka kupata maoni ya Sheikh Mohammed Issa juu ya mambo mawaili: Kwanza msimamo wa U i s l a m u j u u ya a m a n i ikilinganishwa na Waislamu siasa kali wanaodaiwa kufanya mashambulizi ya kigaidi yanayouwa watu wasio na hatia wakiwemo wanawake na watoto. Pili, iwapo Sheikh a n a d h a n i m k u t a n o wa wasomi hao wa Kisomali utasaidia kuleta ufumbuzi wa mgogoro wa Somalia. Kwa mujibu wa maelezo ya nakala hyo, majibu ya Sheikh Mohammed Issa, katika sura ya dhahiri ya maswali, yalikuwa sahihi kabisa. Alipatia kabisa. Lakini kwa muktadha wa habari na dhana inayobebwa

Tatizo la msingi Somalia, sio Siasa Kali za Kiislam

na mkutano wa Mogadishu, kwa maana katika mazingira ambapo maswali yaliulizwa, ilihitaji maelezo na majibu tofauti. Yalihitajika majibu na maelezo ambayo yataonesha upotofu wa dhana kuwa mgogoro wa Somalia unatokana na zinazodaiwa kuwa siasa kali za kidini. Kwa upande wa pili, majibu yaonyeshe chanzo cha mgogoro ni nini na kumdhirisha adui halisi wa wananchi wa Somalia. Majibu yaonyeshe wazi kuwa mikutano kama hiyo ni kupoteza muda na haiwezi k u s a i d i a c h o c h o t e k wa sababu kinachojadiliwa kwa kudhaniwa ndio tatizo, sio. Makala inasema, Sheikh yeye alichosema ni kuwa hadhani kuwa itasaidia kwa sababu Masheikh wenyewe hawapo pamoja kifikra, hawana msimamo mmoja. Yaweza kuwa ni kweli alivyosema. Lakini kwa muktadha wa swali, hata kama wangekuwa n a m a wa z o p a m o j a n a msimamo mmoja, na ulio sahihi kabisa; wasingeweza kuleta ufumbuzi wa tatizo la Somalia kwa sababu wao sio waliousababisha na wao sio waliomtuma Marekani na Ethiopia kufanya vurugu Somalia. K u b wa wa n a c h o we z a k u f a n ya n i k u mwa mb i a Marekani wewe ndio tatizo. Acha. Waache Wasomali na mambo yao. Lakini ile kwamba Masheikh hao walikutana wa k i d h a n i k u wa t a t i z o la msingi la Somalia ni al Shabab, ni dhahiri kuwa hawana ubavu wa kumtaja anayeikoroga Somalia, hata wakionyeshwa. Tu m e ya e l e z a h a ya n a kutoa ufafanuzi huu kwa nia jema, kwa maana ya kutaka suala hili lieleweke vizuri kwa sababu licha ya kuwa linaonekana kuwa ni la Wasomali, lakini linatuhusu Waislamu (na wananchi) wa Tanzania na ulimwengu kwa ujumla. Kama tulivyotangulia kusema, majibu wa Sheikh Mohammed Issa, kwa kutizama sura ya nje ya swali, yalikuwa sahihi kabisa. Lakini kama ilivyoelezwa katika makala, walikolenga BBC ni kwingine kabisa. Na kutokana na muktadha wenyewe wa habari na swali, majibu yalitakiwa kurejea kwenye muktadha (context) huo huo

LONDON JINA la Mtume Muhammad (s.a.w), limeongoza kwa kupewa i d a d i k u b wa z a i d i ya watoto wa kiume waliozaliwa katika mji mkuu wa Uingereza, London katika mwaka 2012. Jina hilo tukufu limeshika nafasi ya pili kwa kupewa watoto wa kiume waliozaliwa

Jina Muhammad laongoza London


nchini kote Uingereza baada ya jina la Harry. Idara ya Takwimu ya Taifa ya Uingereza i m e s e m a k u wa j i n a la Muhammad, ndilo lililoongoza kwa kupewa watoto wengi zaidi wa kiume waliozaliwa jijini London katika mwaka uliopita wa 2012. Taarifa ya idara hiyo imesema jina tukufu la Muhammad limetolewa na wazazi kwa watoto elfu saba na mia moja thelathini na tisa wa kiume waliozaliwa mwaka jana. Muhammad pia lilisajiliwa kati ya majina mia moja yaliyoongoza mwaka jana katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris na lilipendelewa zaidi na watu katika mji wa Marselle Vilevile na Oslo nchini Norway.

Tahariri/Habari

DHULQADAH 1434, IJUMAA SEPT.13-19, 2013

AN-NUUR

Zanzibar yaanza harakati kuchimba mafuta na gesi


SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar na Kampuni ya Mafuta ya Shell ya Uholanzi, zimetia saini makubaliano ya ushirikiano katika kuendeleza sekta ya mafuta na gesi. Makubaliano hayo yametiwa saini Agosti 28, 2013 mjini The Hague, ambapo Waziri wa Ardhi, Makazi, Maji na Nishati Ramadhani Abdalla Shaaban, alitia saini makubaliano hayo kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwakilishi wa Kampuni Shell Tanzania Axel Knospe, alitia saini kwa niaba ya Kampuni hiyo. Makubaliano hayo yamefikiwa mjini The Hague wakati wa ziara ya Rais wa Zanzibar na

Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed aliyoifanya nchini humo. Kabla ya kusainiwa kwa makubaliano hayo D k . S h e i n , a l i f a n ya mazungumzo na uongozi wa juu wa kampuni ya Shell, yaliyojielekeza katika kuimarisha u s h i r i k i a n o k a t i ya
Inaendelea Uk. 3

Ubungo Islamic high School


P.o. Box 55105 Tel: 2450069, 0712 974428, fax: 2450822 Dar es salaam. E-mail: ipcubungoislamic@gmail.com

MAANDALIZI YA KUJIUNGA KIDATO CHA I, 2014 (PRE- FORM ONE ORIENTATION COURSE)
UBUNGO ISLAMIC HIGH SCHOOL inatangaza program maalum ya maandalizi ya kujiunga na kidato cha kwanza 2014. Program hii itaanza tarehe 16/09/2013 hadi tarehe 16/12/2013. Jumatatu hadi ijumaa kuanzia saa 2:00 kamili asubuhi hadi saa 9:00 Alasir. Masomo yatakayofundishwa ni:Elimu ya dini ya Kiislamu, English language, Lugha ya kiarabu, basic Mathematics na Computer. ADA: Ni Tshs 60,000/= (Elfu sitini) tu. Inalipwa yote kabla ya kuanza programu. Fomu za Kujiunga zinapatikana shuleni BURE baada ya kulipa ada. Mlete mwanao apate Elimu yenye tija itakayomweze kujiunga na kidato cha kwanza. Kwa mawasiliano zaidi piga simu namba: 0714 888 557/0712 974428 Wabllah tawfiq Mkuu wa Shule

Katiba Mpya ifafanue nini maana ya kukashifu dini


Na Bakari Mwakangwale
msingi mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Katiba hii. Alisema, katika kifungu hicho Waislamu walitaka p a f a n y i we m a r e k e b i s h o pasomeke baina ya wananchi wa Tanganyika na Zanzibar, ili kubainisha wahusika wa Muungano huo ni watu gani. P e n d e k e z o lililopendekezwa na Waislamu ni kwamba Hati ya makubaliano ya Muungano iliyorejewa katika Ibara ndogo ya kwanza pamoja na makubaliano baina ya wananchi wa Tanganyika na Zanzibar (hili lilikuwa halipo) ndiyo msingi mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Katiba hii. Alisema, na sehemu hiyo ya kwanza ibara ya pili ambayo inasomeka, Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara ikijumuisha sehemu yake ya Bahari na eneo lote la Zanzibar ikijumuisha sehemu yake ya Bahari. Ambapo juu ya kipengele hicho Waislamu wamependekeza Jina Tanzania Bara liondoke na badala yake lije jina Tanganyika, ni kwa sabau, alifafanua kuwa zilizo ungana ni nchi mbili, tena zenye uhuru na mamlaka kamili, ambapo nchi moja inaitwa Tanaganyika na nchi ya pili inaitwa Zanzibra. Ama kuhusu Ibara ya tatu ambayo inazungumzia alama na sikuku za Taifa katika kifungu cha kwanza, ambacho kinasomeka, Alama za Taifa (a) Bendera ya Taifa (b) Wimbo wa Taifa (c) Nembo ya Taifa, kama zitakavyo ainishwa katika sheria itakayotungwa na Bunge. Na kifungu cha pili kinaeleza sikuku za kitaifa zitakuwa ni (a) Siku ya U h u r u w a Ta n g a n y i k a itakayoadhimishwa 9, Desemba (b) Siku ya M a p i n d u z i ya Z a n z i b a r itakayo adhimishwa Januari 12 (c) Siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar itakayo adhimishwa April 26 (d) Sikuku nyengine zitakazoainishwa na sheria ya nchi. Maalim Basaleh, akafafanua kwamba sikuku nyingine zitakazo anishwa na sheria ya nchi ni kama vile sikuku za kidini. Sasa Waislamu wamependekeza kifungu hicho kisomeke (kiwe) pamoja na Ibara ya 31, ya kifungu kidogo cha tatu cha rasimu ya Katiba, ambacho kinaeleza kwamba, Shughuli ya uendeshaji wa Jumuiya za dini itakuwa ni mamlaka ya Serikali. Akielezea sababu za Waislamu kutaka kifungu hicho kijumuishwe pamoja na kipengele cha (d), alisema, lengo ni kutaka kupunguza matumizi ya fedha za Serikali katika kugharamia sherehe za kidini. Maana alisema, imekuwa ni mtindo usio rasimi au imekuwa ni kama kawaida wakati wa sikuku za Kiislamu hukuti ofisi yoyote ya Serikali ikipambwa, lakini akadi sikuku ya Krisimasi ambapo hutoa taswira kuwa ndiyo sikuku rasmi ya Serikali. Kwa hiyo kile kifungu kwamba shughuli za uendeshaji wa Jumuiya za dini, itakuwa nje ya mamalaka ya Serikali, kifungu hiki kiko tayari lakini kiunganishwe na hiki cha suala la sikuku za Serikali au zinazo kubalika na Serikali. Alisema. Kuhusiana na masuala ya utumishi wa umma katika Sura ya 11, kifungu cha 176, ambacho kimeeleza juu ya misingi mikuu ya utumishi wa umma, ambacho kifungu kidigo cha (1) kimeeleza. U t u m i s h i wa U m m a katika Jamhuri ya Muungano utazingatia misingi na kanuni zifuatazo, katika kifungu kidogo ( J) kuhakikisha kwamba watu watateuliwa

Habari

DHULQADAH 1434, IJUMAA SEPT.13-19, 2013

AN-NUUR

WA I S L A M U n c h i n i wa m e t a k a K a t i b a i j a y o ifafanue kukashifu dini nyingine maana yake nini, kupitia kifungu kilichopo katika mapendekezo ya Rasimu ya Katiba kinachoelezea uhuru wa kutangaza Dini. Maalim Ally Basaleh ameyasema hayo akiongea na Waislamu mara baada ya Ibada ya swala ya Ijumaa wiki iliyopita, katika Msikiti wa Idrisa, Jijini Dar es Salaam. Basaleh amesema, Waislamu walikutana katika viwanja vya Sabasaba na kukaa kitako kwa makini kupitia rasimu hiyo na kurekebisha vifungu ambavyo endapo vitaachwa bila kurekebishwa, vinaweza kuleta matatizo. Alisema, Waislamu bado wanakumbukumbu ya Muislamu kuhubiri Yesu si Mungu hadaharani likawa ni kosa la jinai akakamatwa, akashitakiwa na akapatikana na hatia kisha Mahakama ikamuhukumu kwenda jela. Sasa, hivi vifungu vilivyoingizwa kijanjajanja bila ufafanuzi havitakiwi, ukiangali Wakristo wanaamini Yesu alisulubiwa, aliuwawa na ni mwana wa Mungu kwa Waislamu hiyo ni kufru hawaamini hivyo. Sisi Waislamu tunaamini k u w a Ye s u s i M u n g u , hajasulubiwa wala hajauwawa na wao (Wakristo) huona hiyo ni kashfa, sasa nani hapa kakashifiwa? Alisema na kuhoji Maalim Basaleh. Akifafanua alisema, katika sura ya nne kifungu cha 31, kifungu kidigo cha 3, kinasema. Ni marufuku kwa mtu kikundi au Taasisi ya Dini kutumia uhuru wa kutangaza Dini kwa kukashifu imani na Dini nyingine, kujenga chuki au kuchochea vurugu na ghasia kwa madai ya kutetea imani au dini. Alisema, baada ya kupitia na kuona kuwa kifungu hicho kina matatizo endapo k i k i a c h wa h i v y o h i v y o , Waislamu wamependekeza k wa m b a , i e l e z w e h u k o kukashifu dini nyingine maana yake nini. Maana kifungu kinasema mtu akikashifu dini ya mtu mwingine atakuwa amekosa, sasa huku kukashifu dini ya mtu mwingine maana yake haswa ni nini? Hapa lazima Katiba ifafanue kashfa ni nini katika kutangaza imani ya mtu. Alisema na kuhoji Maalim Basaleh. Ama kuhusu susla la Muungano, Maalim Basaleh alisema, Ibara ya kwanza kifungu namba mbili ya rasimu hiyo inayosomek,a Hati ya makubaliano ya Muungano, iliyorejewa katika Ibara ndogo ya kwanza ndiyo

Zanzibar yaanza harakati kuchimba mafuta na gesi


Inatoka Uk. 2

katika nafasi mbalimbali kwa kuzingatia uwezo wa kitaaluma, weledi, maalifa na uzoefu wa kitaaluma katika eneo husika. Alisema, Waislamu katika pendekezio waliyoyatoa, wameona yaongezwe maneno yafuatayo, Na Uwiano wa Kiimani. Akasema, bila ya kuwa na uwiano huo ndiyo kunatokea ubaguzi katika ajira, ukaona Wakristo ni wengi Waislamu wachache hata kama wapo wenye sifa.

Serikali ya Zanzibar na Kampuni hiyo. Kwa mujibu wa makubaliano hayo Kampuni ya Shell, itaisaidia Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kujenga uwezo wa kitaalamu katika hatua za awali za uendelezaji wa sekta hiyo. Sambamba na hatua hiyo, kampuni hiyo itasaidia pia shughuli za maendeleo ya vijana katika kuwajengea uwezo kwa kuwapatia elimu na mafunzo mbalimbali, yakiwemo stadi za ujasiriamali. Akizungumza mara baada ya kutia saini makubaliano hayo, Wa z i r i w a A r d h i , Makazi, Maji na Nishati Ramadhani Abdalla Shaaban, alisema kutiwa saini kwa makubaliano hayo ni hatua moja kubwa na mwelekeo sahihi katika jitihada za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuendeleza sekta ya nishati Zanzibar. Kwa upande wake, mwakilishi wa kampuni ya Shell Tanzania, Bwana Axel Knospe, alieleza kuwa wakati mashauriano ya k i e n d e l e a k a t i ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania juu ya kuliondoa suala la mafuta na gesi katika mambo ya muungano, Kampuni hiyo itaendelea na dhamira yake ya ushirikiano na Zanzibar,

hadi hapo muda utakapokuwa tayari kuanza kazi ya shughuli za uchimbaji mafuta na gesi ambapo itaifanya kazi hiyo kwa kuzingatia uwajibikaji kiuchumi, kijamii, kimazingira na kuifanya sekta hiyo kuwa endelevu Wakati Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zikishughulikia kwa pamoja suala la kisheria na kisera kuipatia Zanzibar haki pekee ya kuendeleza sekta ya mafuta na gesi Zanzibar, Kampuni ya Shell itaendelea na dhamira yake ya kushirikiana na Zanzibar hadi hapo muda muafaka utakapofika kuanza shughuli za uchimbaji wa mafuta na gesi, alinukuliwa Bw. Axel Knospe. Wakati akizungumza na Rais wa Zanzibar huko Hague, Waziri wa Bia shar a ya N je na Ushirikiano wa Kimataifa wa Uholanzi Bibi Lilianne Ploumen, alimueleza Rais kuwa Serikali ya nchi hiyo iko tayari kutumia utaalamu na uzoefu wake katika sekta ya mafuta na gesi kuisaidia Zanzibar kuendeleza sekta hiyo. Bibi Ploumen, alieleza kuwa Serikali ya nchi hiyo iko tayari kutoa fursa za mafunzo kwa watumishi wa Serikali ya Zanzibar katika sekta ya

nishati, ili kuhakikisha kuwa wanakuwa na uzoefu katika kusimamia rasilimali hizo, utunzaji wa mazingira na ushiriki wa wananchi k a t i k a m a t u m i z i ya rasilimali hiyo kuepusha migogoro. Alisema kuwa Mambo ya msingi ya kupewa kipaumbele ni pamoja na namna ya uendeshaji, usimamizi na matumizi bora ya rasilimali hizo, ushirikishwaji wananchi na utunzaji mazingira. Aidha Waziri huyo alisisitiza haja ya Zanzibar kujifunza kutoka nchi nyingine, kuepuka makosa yaliyofanywa na baadhi ya nchi ikiwemo Uholanzi yenyewe. Dr. Shein alimaliza ziara yake ya siku tano nchini Uholanzi hivi karibuni. Katika ziara hiyo Dk Shein amefuatana na Waziri wa Ardhi, Makazi, Maji na Nishati wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Ramadhani Abdalla Shaaban, Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Rashid Seif Suleiman, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mahadhi Juma Maalim na Mshauri wa Rais Ushirikiano wa Kimataifa, Uwekezaji na Uchumi, Balozi Mohamed Ramia. (Habari hizi ni kwa mujibu wa Zanzibar islamic new.world press.com)

4
WA Z A N Z I B A R I n a Wa t a n g a n y i k a wa n a malezi tafauti kuhusiana na sura ya Muungano. Ambapo Watanganyika wanauangalia huu kuwa ni Muungano wa Serikali M o j a , Wa z a n z i b a r i wanauangalia kuwa n i wa S h i r i k i s h o l a S e r i k a l i Ta t u . H a t a kama si Serikali Moja wala Tatu iliyoandikwa popote katika sheria kuu zinazoongoza nchi hizi mbili, bado tabia, matendo na maono ya wa t u wa p a n d e h i z i yanasomeka hivyo. Ndiyo maana, si rahisi kwa Mtanganyika kumkuta anajiita kwa jina hilo, maana kwa wengi wao Tanganyika imeshapotea, lakini kila mara utamkuta Mzanzibari akijiita na akijinasibisha kwa Uzanzibari wake. Huu ni uamuzi wa kimapinduzi kwa pande zote mbili za Muungano. Kwa Tanganyika ni wa kimapinduzi kwa kuwa umeweza kupindua fikra za takriban vichwa milioni 40 na kuvifanya viamini kitu kimoja. Kwa Zanzibar ni wa kimapinduzi kwa kuwa vichwa milioni moja tu, ambavyo ni chini ya asilimia 3 tu ya Watanzania wote na vinavyokaa katika chini ya asilimia moja tu ya ardhi yote ya Tanzania, vimeweza kuhimili hisia za kutokuridhika kwa miaka 50 ya Muungano huu. Lazima tukiri kwamba ni ujasiri tu ndio unaomwezesha m wa n a d a m u k u we z a kukaa na fundo la moyo kwa miaka mingi kama hii. Kubwa zaidi kwetu ni kukiri kwamba kuna kutokuridhika huko kwa upande wa Zanzibar, ndipo tuweze kusaidiana kuyageuza mateso yetu kuwa faraja. Kukubali huko kutayaendeleza Mapinduzi ya kweli ya Zanzibar kwa kuyapa maana katika maisha ya kila siku na ya kila mmoja wetu. Mapinduzi hasa ni matokeo ya kutokuridhika, ambako husababishwa na mgogoro kati ya njia ambazo watu wanaouona ukweli na njia ambazo wangelipenda ukweli huo Zanzibar inauona ukweli kuwa Muungano huu, katika hali uliyo, ni tatizo kwake na, sasa, ingelitaka kuuona kuwa ni sehemu ya utatuzi wa tatizo hilo. Huko hakuwezekani ila kwa Mapinduzi; na hayo si

Makala

DHULQADAH 1434, IJUMAA SEPT.13-19, 2013


mkubwa unapoanguka, husababisha maafa kwa pale unapongokea (panaweza kuchimbika shimo kubwa) na kule unakoangukia (unaweza kuelemea nyumba au wapiti njia na kuwajeruhi kama si kuwatoa roho zao). Lakini mara tu kipindi hiki kinapoanza, hutanguliwa haraka sana na kipindi cha ujenzi wa mahusiano mapya. Huu ni mfano wa ujenzi wa nyumba mpya juu ya kongwe, ambapo mwenye nyumba huendelea kujenga nyumba mpya, huku yeye akiwemo ndani. Huvunja kiambaza kimoja kwanza na kusimamisha kipya mahala pa kilichovunjwa, kabla hajakwenda katika kiambaza chengine. Ingawa huweza kuchukua muda mrefu kwa nyumba kukamilika, kutegemea na uwezo wa kifedha, kiufundi na mazingira ya ujenzi. Lakini ni staili yenye faida m o j a k u b wa : h a k u n a wakati ambapo mwenye nyumba analazimika kulala nje, hata kama katika kipindi cha ujenzi huwa hakai katika makazi mazuri sana. Hapo ndipo, kwa maoni yangu, nchi hii inapoelekea. Muungano huu utaanza kuvunjika na mpya kuundika kwa wakati mmoja. Ninachoeleza ni kwamba tunakwenda katika kipindi ambacho hatutasema kuwa hatuna Muungano moja kwa moja, lakini pia hatutakuwa na Muungano huu. Mwisho tutaingia kwenye kuimarisha mahusiano mapya tutakayoyajenga. U k we l i n i k wa m b a Zanzibar na Tanganyika, bali pamoja na mataifa mengine yaliyo jirani, yataendelea kuwa na mahusiano dumu daima. Lakini tafauti na sasa, mahusiano yajayo kwa sababu ya Mapinduzi haya, yatakuwa na sura nyengine na matakwa mengine. Hata hivyo, tuzinduke Wazanzibari, kwamba jambo pekee linaloweza kutufikisha hapo ni moja tu. Nalo ni mkono mmoja kuyashikilia Mapinduzi yetu na mwengine kuishikilia Zanzibar yetu. Yaani isiwe tu Mapinduzi Daima, lakini iwe pia Zanzibar Daima; maana Mapinduzi Daima hayana m a a n a i k i wa h a t u n a Zanzibar. (Makala kwa hisani ya Mohammed Ghassani/ Zanzibar Daima Online no.3)

AN-NUUR

Bila Zanzibar yetu, Mapinduzi Daima hayana maana yoyote

Noti ya Rupia 10 ya mwaka 1928 iliyokuwa ikitumika katika serikali ya Zanzibar. mapinduzi ya mapanga na marungu, wala bunduki na mizinga, bali ya fikra na mkakati. Haya ni Mapinduzi ambayo yanatakiwa yapitie hatua tano za matayarisho kwa ajili ya mapinduzi ya kuporomoka kwa mfumo mkongwe, ya kuharibika kwa mahusiano makongwe, ya kujenga mahusiano mapya; na ya kuuimarisha mfumo mpya. Ama kwa kujijua au kutojijua, tayari tumeshapita kipindi cha kwanza cha matayarisho kwa ajili ya Mapinduzi, kipindi ambacho kilitawaliwa na woga wa wananchi na mateso ya watawala. Kilikuwa ni kipindi ambacho, i n g a wa p a l i k u wa n a kiwango kikubwa cha kutokuridhika na jinsi Muungano huu unavyoikandamiza Zanzibar, si Wazanzibari wengi waliothubutu kueleza kutokuridhika h u k o . B a l i h a t a wa l e wachache waliothubutu, walisemea vibuyuni a m b a k o a m a walichokisema kilimalizwa huko huko au wenyewe walimalizwa kwa njia zao za kumalizana. Sasa tulipo, kwa maoni yangu, ni katika hatua ya pili ya Mapinduzi, ambapo mfumo mkongwe wa Muungano usio na maslahi kwa Zanzibar unaelekea kuporomoka. Kawaida kipindi hichi ni matokeo ya kupotea kwa uongozi ndani ya kundi la watawala, ambapo mgawanyiko wa makundi humfanya kila mmoja kutenda vyake. Mara nyingi hatua hii haifikiwi mpaka ajitokeze kiongozi anayejiona kuwa mwanamageuzi kutaka kuunusuru mfumo mkongwe; na akafeli. Mwanasiasa wa Kifaransa na mtaalam wa uchumi AnneRobert-Jacques Turgot na mwanasiasa na waziri mwenzake Jacques Necker walijaribu kuunusuru ufalme wa Ufaransa kabla ya mwaka 1798 na Waziri Mkuu wa zamani wa Urusi Pyotr Arkadyevich Stolpyin alifanya jaribio kama hilo nchini Urusi kabla ya Vita vya Kwanza vya Dunia, lakini wote walishindwa. Huo huwa ni wakati ambapo, kutokana na mtikisiko wake, mfumo mkongwe huwa kama tayari umeshakufa kitambo, lakini kwa kuwa watu wanaothubutu k u ya t h i b i t i s h a m a u t i yake hawajatokea, basi huendelea kuwepo tu ukiendea upepo na kudura ya Mungu. Nabii Suleiman (A.S) alikuwa amefariki siku nyingi, lakini watumishi wake waliendelea k u t u m i k a wa k i d h a n i bosi wao amekaa kitini akiwasimamia, hadi mchwa alipokuja kuila fimbo yake. Kuna watu waliojua kuwa Awamu ya Tatu ya Serikali ya Ufaransa imeshakufa tangu mwaka 1934, lakini maziko yake yalifanywa mwaka 1940. Wa z o n i n a l o j a r i b u kuliwasilisha hapa ni kwamba, sasa umefika wa k a t i wa ya l e ya l e matakwa ya Wazanzibari, kama yalivyoelezwa kupitia Ripoti za Tume za Jaji Nyalali, Jaji Kisanga na sasa kupitia Tume ya Jaji Warioba ndiyo yatakayouongoza Muungano wa Tanzania na wala sio Katiba hii ya Serikali Mbili ambayo Chama cha Mapinduzi inadhani kwamba itabakia milele. Na viashiria vya utabiri huo vimeanza kujengeka sasa. Changamoto iliyo mbele yetu kwa sasa ni ukweli kwamba hatua za tatu, nne na tano zinakuja kwa kasi na, yumkini, hatuna matayarisho mazuri kuzikabili. Kwa mfano, hatua ya tatu, ambayo ni ya kuharibika kwa mahusiano makongwe, kwa mintarafu ya kuharibika kwa muundo wa sasa wa Muungano, ina matatizo yake. Mojawapo ni kwamba, wenye maslahi na mahusiano haya hivi sasa, wameanza kutumia nguvu zao za ziada kuzuia yasiharibike. Na ingawa, kutokana na matakwa ya kiwakati hawatafanikiwa, lakini kama ilivyo kawaida ya mti

Habari za Kimataifa

DHULQADAH 1434, IJUMAA SEPT.13-19, 2013

AN-NUUR

Marekani, Israel watumiaji Iran katika kumi bora wakubwa silaha za kemikali ulinzi wa angani duniani
Mtaalamu mmoja wa masuala ya kisiasa amesema kuwa, Marekani na utawala haramu wa Kizayuni ndio watumiaji wakubwa wa silaha za kemikali duniani. Mark Glenn, ameyasema hayo katika mahojiano na televisheni ya Press TV na kufafanua kuwa, tuhuma zinazotolewa dhidi ya serikali ya Syria kuhusiana na matumizi ya silaha za kemikali, hazina ukweli wowote. Amesisitiza kuwa, kwa miaka mingi tawala za Marekani na Israel kwa pamoja zimekuwa zikitumia silaha za kemikali katika pembe mbalimbali za dunia. Alisema kuwa wakati utawala wa Kizayuni ulipotumia silaha za k e m i k a l i z i l i z o p i g wa marufuku dhidi ya watoto katika Ukanda wa Gaza, viongozi wa Washington hawakutoa onyo wala karipio lolote kwa waliotenda jinai hiyo. Leo hii viongozi hao t e n a b i l a ya k u we p o ushahidi wowote ule, wanaituhumu Syria na kutishia kuishambulia kijeshi nchi hiyo. Mtaalam huyo ameongeza kuwa, hatua hizo za Washington hazina lengo jingine zaidi ya kutaka kusafisha jina baya la Marekani katika uso wa dunia. Hata hivyo Bw. Mark Glenn, ameelezea kuwepo uwezekano wa kutoshambuliwa kijeshi Syria na kwamba, kuna dalili Rais Barack Obama akawa amesitisha hatua ya kutaka kuishambulia Syria.

ZANA za ulinzi w a a n g a n i zilizotengenezwa Iran

hayo katika sekta ya ulinzi yametokana na juhudi za wataalamu

Urusi itaisaidia Syria ikivamiwa kijeshi


ST. PETERSBURG RAIS Vladimir Putin wa Urusi amesema nchi yake itaisaidia Syria iwapo nchi hiyo itavamiwa kijeshi. Akizungumza Ijumaa iliyopita baada ya kumalizika kikao cha viongozi wa nchi za G20 katika mji wa Saint Petersburg nchini Urusi, Putin alisema nchi yake imekuwa ikiisaidia Syria kwa silaha, kiuchumi na kibinadamu na itaendelea kufanya hivyo. Aidha alisema madai kuwa serikali ya Syria imetumia silaha za kemikali ni uzushi. Alisema magaidi ndio waliotumia silaha hizo za kemikali ili kuchochea hujuma ya kijeshi dhidi ya Syria. Matamshi hayo ya Putin yamekuja baada ya Marekani na washirika wake hususan Ufaransa na Uingereza wakizidisha wimbo wa kutaka kuingia katika vita dhidi ya Syria, kwa madai kuwa eti jeshi la Syria limetumia silaha za kemikali katika mapambano dhidi ya waasi. Serikali ya Syria imekanusha vikali madai hayo na kusema kuwa waasi wanaopata himaya ya Marekani, Qatar, Saudi Arabia, Israel na Uturuki, ndio ambao wametekeleza hujuma kwa kutumia silaha za kemikali dhidi ya raia. Rais Putin Jumanne wiki iliyopita alionya kuwa nchi yake ina mipango yake ya siri ya kukabiliana na shambulio la kijeshi la Marekani dhidi ya Syria. Akizungumza katika mahojiano na televisheni One ya Urusi, Putin alisema bado ni mapema kubainisha wazi mipango ya nchi yake katika kukabiliana na uvamizi wa kijeshi unaotarajiwa nchini Syria. Siku za nyuma Rais Putin alisema kuwa, tuhuma za matumizi ya silaha za kemikali zinazoelekezwa kwa serikali ya Syria, ni upuuzi mtupu. Aidha Rais huyo alimtanabahisha Rais wa Marekani Barack Obama kwa kusema kuwa, ametunukiwa tuzo ya amani

RAIS wa Iran Hassan Rohan


RAIS Vladimir Putin Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kati ya nchi kumi bora duniani katika uga wa utengenezaji zana za kujihami angani. Hayo yamedokezwa na Brigedia Jenerali Farzad Esmaili Kamanda, wa Kitengo cha Jeshi la Iran cha Kujihami Angani cha Khatamul Anbiya ( S AW ) , wa k a t i akizungumza Jumanne iliyopita katika hafla ya kuzindua mafanikio ya jeshi katika uga wa mawasiliano. A m e o n g e z a k u wa baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu mwaka 1979, Iran imeweza kupiga hatua kubwa katika sekta ya kujihami angani na sasa ni kati ya nchi kumi bora duniani katika kutengeneza zana na vifaa vya jeshi la anga. Amesema mafanikio nchini humo. Brigedia Jenerali Esmaili, ameongeza kuwa vikwazo na vitisho vya maadui vimegeuka na kuwa fursa nzuri ambayo imesababisha Iran ijitosheleze katika sekta ya ulinzi. Katika hafla hiyo ya Jumanne, umezinduliwa mfumo wa mawasiliano unaojulikana kama Troposcatter, ambao unaweza kutuma mawimbi ya mawasiliano kwa masafa marefu. Aidha kumezinduliwa pia mfumo wa mawasiliano wa Observer 32, ambao una uwezo mkubwa wa kutoa maelezo kuhusu ndege zilizoko angani bila kutumia mifumo ya kawaida ya mawasiliano.

ya Nobeli, hivyo anatakiwa kufikiria mara mbili juu ya vita vitakayowalenga raia wasio na hatia huko Syria, ikiwa uvamizi huo utatimia Mkuu wa Kamati ya Siasa za Nje ya Bunge la Urusi Bw. Alexei Pushkov, amesema Marekani inataka kusambaratisha nguvu za kijeshi za Syria kama ilivyofanya huko Libya ili kuyaandalia njia makundi ya kigaidi huko Syria. Mbali na kutaka kuangamiza nguvu za kijeshi za Syria, Marekani inataka pia kuipindua pia serikali ya Rais Bashar Assad wa nchi hiyo. (irib.ir)

6
Na Omar Msangi ANAONEKANA mama na binti yake mdogo wanamchungulia kwa uchungu mtu aliye korokoroni. Mtu yule anayeonekana kuchoka akiwa na huzuni kubwa kwa masaibu ya kuwa jela, anawafuata taratibu na kuongea nao wakitizamana kupitia lango la chuma. Baina ya vyuma vya mlango (iron bars) pana uwazi ambapo wanaweza kuonana na kupitisha mkono kushikana. Hawa ni mke na mume na binti yao Neelo. Mke analia na mume machozi yanatiririka akijaribu kumfariji mkewe. Sisikiti na kuhuzunika kuwa jela, huzuni na uchungu wangu ni juu ye n u . M t a i s h i j e m k e wa n g u n a b i n t i ye t u mpenzi Neelo. Anapomwona baba anatoa machozi, Neelo, binti mdogo wa kiasi miaka 5 anaimba wimbo wa kumtoa huzuni baba yake: Learn to laugh while crying. Learn to cry while laughing. As much life as God Has given us, we will live that much.. We are two and we have a little girl. That is our small world. With happiness is filled every corner of our home. There are big joys in small things. Like shining stars in long nights. Huo ni wimbo ambao, Jan Nissar Akhtar Khan, ali penda kumwimbia mwanawe huku akicheza naye anaporejea kutoka kazini. Ufupi wa maneno akionyesha jinsi wawili yeye na mkewe pamoja na mtoto wao, walivyokuwa wakiishi maisha ya furaha. Katika wimbo huu baba anampa nasaha binti yake akimwambia awe na furaha muda wote asipende kuwa mtu wa majonzi na kulia bila mpango. Acheke hata anapokuwa na jambo la kumtoa machozi. Leo ni zamu ya binti kumfariji baba yake aliyeko jela anapolia kwa uchungu wa namna mbili: K wa n z a k u f u n g wa jela kwa kosa ambalo hakutenda. Pili, kuona familia yake ikiteseka kwa kukosa huduma, huruma na mapenzi ya mume na baba. Wakiwa bado wana hamu ya kuongea, anakuja askari na kuwaambia

Makala

DHULQADAH 1434, IJUMAA SEPT.13-19, 2013


ile iliyokuwa ikivuna magogo kinyume cha sheria akamwambia kuwa a l i k u wa a m e m w e k e a d a u a f i s a m we n z a k e aliyekuwepo kabla yake. Kila mwezi akimpa Rupia 1,000. Sasa yeye atampa Rupia 1,500 mpaka 2,000 kwa mwezi. Hata hivyo kijana mchapakazi akiwa na hamu ya kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na kama mzalendo mtetea masilahi ya nchi, akakataa. Siku moja akiwa n y u m b a n i n a m k e we akajiwa na kikosi cha a s k a r i wa l i o m k a ma t a wakimwabia kuwa anatuhumiwa kwa mauwaji-kwamba alimuuwa mtu mmoja a k i i t wa R a m G u p t a . Huyu ni mmoja wa watu aliopambana nao wakivuna magogo kinyume cha sheria. Kesi ikanguruma mahakamani. Mashahidi na vidhibiti (vywa uwongo) vikaletwa. Jan Nissar Akhtar Khan akahukumiwa kutumikia kifungo miaka 20 jela. Mwishowe alitoka kwa msamaha wa Rais katika sherehe za kila mwaka za Mahtma Gadhi. Hata hivyo, hiyo ni baada ya kukaa jela kwa miaka 11 na miesi 6. Siku moja akipita mitaani, akamwona Ram Gupta akihutubia mkutano wa hadhara wa kampeni za uchaguzi. Akagundua kuwa kumbe mtu aliyedaiwa kumuuwa yupo hai. Lakini alishagundua pia kuwa mkewe hakuwa amejiuwa, bali yeye na binti yao waliuliwa na huyu huyu Ram Gupta. Alipomwona tu akaanza kumfukuza. Ram akakimbia mwishowe akajikuta anaingia ndani ya mahakama ile ile ambapo Jan Nissar Akhtar Khan alihukumiwa kifungo na Jaji alikuwa yule yule. Khan akaingia na kumuuwa mbele ya Jaji yule yule akieleza alivyohukumiwa kwa dhulma na jinsi mkewe na binti yake walivyouliwa na Ram halafu ikasingiziwa kuwa wamejiuwa. Je, unanikumbuka, Mheshimiwa Jaji? Mi ni yule yule Jaan-E-Nissar ambaye miaka kumi na moja na nusu iliyopita katika koti kama hii hii, ulinihukumu kwenda jela miaka 20 kwa kosa la kumuuwa mtu huyu, au niseme mnyama huyu (maana hastahiki kuitwa binadamu) Ram! Inaendelea Uk.8

AN-NUUR

Andha Kanoon, SMZ na yale ya UAMSHO

Kweli ni Serikali ya Umoja wa Kitaifa DPP Unguja, msikilize Amitabh Bachchan

RAIS wa SMZ, Dkt. Shein muda umekwisha wa kuongea na mfungwa. Inabidi mke aondoke huku wakitizamana kwa huzuni na mumewe. Wakati akiondoka binti anabubujikwa na machozi huku akiimba rote rote., anageuka nyuma na kumtizama baba yake, mtoto analia kwa kwikwi hali inayomfanya baba naye kushindwa kuhimili na kuelemewa na uchungu, anashindwa kabisa kumtizama Neelo. Haikupita siku nyingi baada ya kutembelewa n a m k e we , m f u n g wa Jan Nissar Akhtar Khan (Amitabh Bachchan) anapokea barua kutoka kwa mkewe ikimfahamisha kuwa ameamua kujiuwa yeye na kumuuwa binti yao kwa sababu hataweza kuhimili tabu ya maisha bila mume wake mpenzi aliyeko jela. Anasema amebakwa na watu wanne. Na hivyo haoni sababu ya kuishi tena katika maisha hayo ya fedheha. Anasema: Akijiuwa, Nini itakuwa hatma

MAKAMU wa Rais, Seif. ya Neelo ambaye baba yake yupo jela na ambaye mama yake anakaribia kujiuwa?. Neelo atabakia peke yake Awe nani akiwa hana elimu kwa sababu hana baba wala mama wa kumsomesha? Kibaka, mwizi, ombaomba au malaya changudoa? Mimi ni mama, siwezi kukubali kuona mtoto wangu akiwa katika hali hiyo. That is why I am taking her along with me. May God forgive me. Kwa maana hiyo, nimeamua kuondoka naye. Namnyonga kisha namimi najiuwa. Wako mkeo mpenzi Zakhiya. Mungu wangu nisamehe. Mfungwa Khan anatolewa jela na kwenda k u s h i r i k i m a z i s h i ya mkewe na mwanawe. Anapowalaza katika mwanandani, inamjia picha walivyokuwa wakiishi kwa furaha huku sauti ya kuimba rote rote We are two and we have a little girl. That is our small

SHEIKH Azzan world. With happiness, is filled every corner of our home. Kwa vile alikuwa kazoea kumletea binti yake zawadi ya chokleti, anaonekana akiweka chokleti ndani ya sanda ya binti yake azikwe nayo. Hiki ni kisa ambacho kipo katika filamu ya Kihindi (Bollywood film) ya mwaka 1983 iitwayo Andha Kanoon (Blind Law) Katika filamu hii kijana Pankaj Sonker (Jan Nissar Akhtar Khan ) anaajiriwa kama afisa misitu baada ya kumaliza masomo yake. Anaonekana akiishi kwa furaha na mkewe Zakhiya pamoja na binti yao Neelo. Siku moja akiwa kazini, Sonker anakutana na majangili wa mbao wakiwa wamevuna na kuchukua magogo kutoka katika moja ya misitu anayoisimamia bila ya kibali. Anaonekana akiwakabili na kadiri walivyotaka kumhonga akagoma akisimama katika sheria. Mwenye kampuni

7
Na Abu Nassir
KATIKA kipindi cha BBC (Kiswahili) matangazo ya jioni Jumatatu Septemba 9, kulikuwa na habari juu ya kukutana Masheikh mjini Mogadishu kujadili uhalali wa misimamo ya baadhi ya vikundi vya Kiislamu. Madai ni kuwa kuna baadhi ya makundi ya Kiislamu (kama Al Shabab) hutumia dini kufanya mashambulizi ya kigaidi ambapo katika mashambulizi hayo huuliwa watu wasio na hatia wakiwemo wanawake na watoto. Na hivyo kuonekana k u wa n d i o m s i n g i wa tatizo la Somalia. Kwa hiyo kukutana Masheikh hao, ni katika namna ya kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa Somalia kwa maana kuwa wakitoa fatwa kuwa misimamo mikali ya kidini na mashambulizi ya kigaidi hayafai katika Uislamu, ndio utapatikana ufumbuzi wa mgogoro wa Somalia. Ni kwa muktadha huo, mtangazaji akataka maoni ya Sheikh Mohammed Issa kama mmoja wa viongozi wa Kiislamu Tanzania. Maswali ya msingi yalikuwa mawili: Kwanza mtangazaji akataka maoni ya Sheikh juu ya vikundi vya Kiislamu vinavyotumia dini kufanya mashambulizi (ya kigaidi). Kwa usahihi kabisa Sheikh Mohammed Issa akajibu kuwa hiyo haikubaliki kwani hata jina lenyewe la Uislaamual-Islamu, maana yake ni amani. Hata hivyo la kuzingatia hapa ni kuwa walichokuwa wakitaka BBC, sio kuelimishwa juu ya Uislamu na amani. Bali kuwatumia Wa i s l a m u w e n y e w e (Masheikh), kuhamisha lawama na agenda. Waislamu waonekane ndio tatizo, na hivyo kuhalalisha uharamia wanaofanyiwa katika Crusade iliyoasisiwa na George Walker Bush. Kutokana na msingi wa swali, jibu la Mohammed Issa limefanya kazi kubwa tatu na za manufaa kwa madhalimu. Kwanza kukubali kuwa ni kweli kuna Waislamu wanatumia Uislamu vibaya kufanya ugaidi. Na hii ndiyo hoja ya Bush na wote wanaowapiga v i t a Wa i s l a m u ( h a t a hapa nchini). Wanasema, hawapambani na Waislamu, ila watu wanaotumia dini vibaya. Hata katika mauwaji ya Mwembechai, Serikali kupitia kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Yusuf Rajab Makamba, ilisema ilikuwa ikipambana n a wa h u n i wa l i o k u wa wameficha silaha Msikitini. Pili, jibu la Sheikh linakubali kuwa ni kweli kuna magaidi Waislamu na kwamba hawa ndio tatizo la dunia hivi sasa. Na kwa hiyo, (Tatu), jibu linahalalisha

Makala

DHULQADAH 1434, IJUMAA SEPT.13-19, 2013


Na labda kuboresha zaidi kwa vile maudhui ni Somalia, unaweza kuja na mlengo huu. KwambaVurugu inayoendelea Somalia, chanzo chake ni uvamizi wa kibeberu na vibaraka wao. Kama kuna watu wanapigana Somalia, wanapigana kupambana na vibaraka wa mabeberu wanaoikalia Somalia kwa kisingizio cha kulinda amani. Kisha unamrudishia swali mtangazaji: Pengine kabla ya kutizama haya ya Masheikh, tuwaulize hawa mabeberu, kwanini hawataki Somalia kuwe na amani? Kwa nini kila Wasomalia wanapojitafutia ufumbuzi wa matatizo yao wanawavuruga? Kama huyo BBC atataka kujua ni kwanini unasema mabeberu wanawavuruga, unamrejesha nyuma wakati Umoja wa Mahakama za Kiislamu ulipoanza kusimamisha amani na kukubalika na Wasomali wote. Ni mabeberu (Marekani) iliyokuwa inatoa silaha na fedha kwa wababe wa kivita (magaidi) ili kupambana na kuvuruga amani. Magaidi hao waliposhindwa, ndio wakaivamia kwa kumtumia Meles Zenawi wa Ethiopia. Kumshibisha zaidi, Sheikh angemrejesha mtangazaji wa BBC Tanzania. Kwamba kumekuwa kukipigwa sana propaganda za al Shabab, siasa kali, mara Boko Haram na majina kama hayo. Likatokea la kutokea. Bomu likalipuka Kanisani Arusha. Watu wakafa na wengine kujeruhiwa vibaya. Propaganda zikaanza k u wa a l i ye l i p u a a l i va a kanzu na kibandiko. Lakini aliyekamatwa katika eneo la tukio ni Victor. Pamoja na viapo na hasira za mamlaka mbalimbali za Dola na ahadi za kufanya uchunguzi, hadi kieleweke. Leo kimyaa!!! Haijulikani kesi ya Victor imeishia wapi. Victor aliyekamatwa kwa kutuhumiwa kulipua bomu (tuhuma za ugaidi), huenda yupo nje ama kwa dhamana au kwa kuachiwa huru, huku Masheikh wanaotuhumiwa kwa kutamka kauli zinazodaiwa kuwa ni uchochezi (UAMSHO), wanasota rumande kwa mwaka sasa wakinyimwa dhamana na wakipelekwa mahakamani kwa ulinzi mkali wa polisi! Huku wengine wanafikia kupelekwa mahakamani kwa helkopta. Swali kwa mtangazaji: Yote haya yanafanywa k wa s a b a b u g a n i ? H i i ndiyo namna ya kujenga na kudumisha amani ya nchi au kuvuruga? Je, huu ndio utawala bora, utawala wa sheria unaowatendea haki wananchi wake bila kujali dini zao, makabila yao, jinsia na hadhi zao katika jamii? Swali la pili: BBC walitaka

AN-NUUR

Sheikh Mohammed Issa umetutosa Waislam


Ulivyojibu ni sawa kabisa, lakini BBC walilenga kwingine kabisa!!!

Crusade na mashambulizi wanayofanyiwa Waislamu sehemu mbalimbali duniani yakiwemo yale ya ndege zisizo na rubani (drone). Labda nitoe maelezo kidogo. Msingi wa swali ni kuwa Masheikh wanakutana Mogadishu kujadili ufumbuzi wa mgogoro wa Somalia. Lakini tunaambiwa kuwa mtizamo wa Masheikh hao ni kuwa wao wanaona kuwa asili ya tatizo ni vikundi vya Kiislamu kama al Shabab vinavyofanya mashambulizi ya kigaidi. Hii sio sahihi. Kwa hiyo kosa linaanzi hapa. Ukiacha historia ya nyuma, mgogoro wa sasa hivi wa Somalia chanzo chake ni uharamia na ubeberu wa Marekani kwa kuitumia E t h i o p i a k u va m i a n c h i hiyo na kuondoa Serikali ya Umoja wa Mahakama za Kiislamu ambayo ilishaleta amani, usalama na utengamano katika nchi baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vya muda mrefu. Vinavyoitwa vikundi vya Kiislamu vinavyodaiwa kuwa na msimamo mkali na kufanywa kuwa ndio tatizo (Al Shabab), viliibuka kama wapigania uhuru na wapinga u va m i z i wa M a r e k a n i / Ethiopia, kama inavyoweza kutokea kwa nchi yoyote

Sheikh Mohammed Issa. ikivamiwa. Baada ya Ethiopia kuondoa, vikundi hivyo vimeendelea kupambana na majeshi ya nje yaliyoingizwa Somalia kwa kisingizio cha kulinda amani, kulinda Serikali kibaraka iliyowekwa baada ya kupinduliwa ile ya wananchi wenyewe. Kama hii ndiyo habari, ndio ukweli, kikao cha Masheikh hao na swali la BBC, tatizo la msingi limeachwa na kutaka kuwafanya wengine ndio tatizo. Katika hali hii, majibu sahihi ya swali hapa ilikuwa kufanya mjadala wa viziwi. BBC wanataka kujua msimamo wa Sheikh juu ya al Shabab na harakati za kufanya mashambuli ya kigaidi, majibu sahihi yanakuwa hivi (huu ni mfano tu). Kuna watu katika nchi zao walishawahi kuuwa watu wao kwa kimeta (anthrax) wakiwaambukiza kupitia barua zinazotumwa kupitia masanduku ya posta. Na ndani ya barua hizo wakaandika neno Allahu A k b a r i l i i d h a n i we n a kuaminika kuwa barua hizo zimetoka kwa Waislamu. Wakapiga sana propaganda kuwa waliotuma barua hizo ni al Qaida (Waislamu). L a k i n i b a a d a e wa k a wa wanaparurana wenyewe kwa

wenyewe ilipobainika kuwa kimeta hicho kilitoka katika maabara zao wenyewe za kijeshi. Baada ya maelezo hayo, sasa unamuuliza mtangazaji wa BBC: Labda tungewauliza kwanza hawa watu, kwa nini hawaoni vibaya kuuwa hata watu wao wenyewe ili muradi tu wapate sababu ya k u wa s i n g i z i a u b a ya Wa i s l a m u ? N a n d u g u Mtangazaji usisahau k u wa n d i o h a wa h a wa waliosababisha kuuliwa askari wao katika lile tukio maarufu la Pearl Harbor na katika Operation Cyanide, ili tu ipatikane sababu ya kuingia vitani. Hawa ni watu gani wasioona vibaya hata kuuwa watu wao wenyewe, kama walivyopeleka askari wao kufa Iraq kwa sababu z a u r o n g o ? Au k a m a walivyokuwa wameweka mikakati katika ile Operation Northwoods walipue meli na ndege zao wenyewe wamsingizie Fidel Castro ili tu wapate sababu ya kumpiga? Inakuwaje watu hawa hawaoni vibaya kusema urongo, kama ule wa Gulf of Tonkin (the USS Madox Incident) na kuuwa watu wasio na hatia ili muradi tu kupata masilahi ya kidunia?

Inaendelea Uk, 10

8
Inatoka Uk. 6 Unanikumbuka sasa? Unakumbuka sasa i l e h u k u m u ya k o ya kifungo cha miaka 20 jela ambapo Sheria yako kipofu haikuweza kuona kuwa sikuwa na hatia na mtu aliyedaiwa kuuliwa alikuwa hai? Nimemuuwa leo mbele ya macho yako baada ya kutumikia kifungo. Sasa huwezi kunihukumu tena maana h u we z i k u m wa d h i b u mtu mara mbili kwa kosa moja. Na kama utataka kuniadhibu, basi nilipe. Nirejeshee miaka yangu 11 na miezi 6 niliyokaa jela nikiwa sina hatia. Nirudishie mke wangu Zakhiya na mwanangu N e e l o wa l i o u l i wa n a Ram (ambapo Sheria yako kipofu haikumuona muuwaji) mkasingizia kuwa mke wangu kajiuwa mwenyewe. Mheshimiwa Jaji, acha sarakasi na usanii huu wa Sheria kipofu. Kitie moto kiti chako cha mamlaka ambacho ukikikalia unawahukumu na kuwaadhibu watu wasio na hatia. Vunja na itupilie kwa mbali kalamu yako iliyoandika hukumu ya dhulma dhidi yangu. Kabla ya hapo, Jan Nissar Akhtar Khan anaonekana akipita mitaani akiimba Andhaa Kanoon. Sheria Kipofu. Inaweza kukusaliti muda wowote. Inaweza kuadhibu watu wasio na hatia. Haisaidii wanyonge. Ni rafiki wa wezi. Ni mchezo wa hoja na sarakasi za maneno na misamiati ya wanasheria. Haitoi haki. Inachukia kusamehe. Kama watu wa n g e i o g o p a s h e r i a , uhalifu ungekoma (lakini h a w a i o g o p i ) . Wa t u wanauliwa na kuteswa, lakini Sheria inachapa usingizi. Sheria inaweza kuwa na mkono mrefu, inaweza kuwa na nguvu, lakini kipofu, haioni! Inaandika bila ya kuona. Kwa sababu hiyo, wengi wanaozea jela wakiwa h a wa n a h a t i a . We n g i wameumia na kuteseka mikononi mwa sheria (ambayo) ni rafiki wa majambazi, watoa rushwa na mafisadi. Pamoja na kisa hiki, filamu inaeleza pia kisa cha Vijay Singh, ambaye akiwa mtoto mdogo alishuhudia baba yake na dada yake wakiuliwa huku dada yake mwingine akinajisiwa na maharamia watatu. Hata hivyo, wauwaji hao hawakufanywa chochote

Makala

DHULQADAH 1434, IJUMAA SEPT.13-19, 2013


n d a n i wa k a s o t a s a n a rumande dhamana zao zikiwa zimezuiwa kwa sababu kosa walilokuwa wakituhumiwa la Uhaini (kutaka kupindua Serikali), lilikuwa halina dhamana. Baadae waliachiwa baada ya Jaji kuhukumu kuwa hawakuwa na hatia kwa sababu Zanzibar sio Dola na hakuna uhaini unaoweza kufanyika mahali ambapo hakuna Dola. Kwa msemo wa Amitabh Bachchan, Sheria Kipofu (ya Zanzibar ), haikuwa imeona kuwa watu hao ambao baadhi yao ni watu wakubwa sana katika Serikali ya sasa, hawakuwa na hatia kwa sababu isingewezekana kufanya uhaini mahali ambapo hakuna Dola. Hoja na wasiwasi wangu ni kuwa isijekuwa kinachowaweka ndani Sheikh Mselem, Sheikh Azzan, Sheikh Farid na wenzao kwa mwaka sasa ni yale yale ya Andha Kanoon Na kama ni hivyo, nadhani itakuwa vyema kwa wanasiasa, viongozi wa SMZ, Mwanasheria Mkuu, DPP, Polisi na Majaji, kuitizama upya filamu hii na kuzingatia maudhui yake. Khan alilipa kisasi kwa kumuuwa Ram Gupter wakati Vijay naye a l i wa u wa wa l e w o t e ambao walimuuwa baba yake wakawa wanatamba kwa sababu wanakula na wakubwa wa kusimamia sheria. Na kwa kuwa sheria ni kipofu, haikuwaona na kuwaadhibu. Ila kwa sisi, kwa vile kwa bahati nzuri sana, wa h u s i k a w o t e wa n a i m a n i j u u ya M u n g u Mfalme wa Siku ya Malipo na Hakimu wa Mahakimu, basi tuizingatie siku hii: Siku hiyo mtu atamkimbia nduguye. Na mamaye na babaye. Na mkewe na wanawe. Kila mtu miongoni mwao Siku hiyo atakuwa na hali itakayomtosha mwenyewe. Hiyo ndiyo Siku ya Kiama ambayo tunaambiwa kuwa kwa hakika Mtetemeko wake ni kubwa mno. Inna zalzata ssaati shaiun adhiim. Na kwamba Siku mtakapokiona hicho Kiama, kila mwanamke anyonyeshaye atamsahau amnyonyeshaye na kila mwenye mimba ataizaa mimba yake kabla ya wakati kufika. N a u t a wa o n a wa t u wamelewa, kumbe hawakulewa. Lakini ni adhabu ya Mwenyezi Mungu iliyo kali. Kwa hiyo, Tumche Mola wetu -Ittaquu r-Rabbakum inna zalzata Ssaati shaiun adhiim.

AN-NUUR

Andha Kanoon, SMZ na yale ya UAMSHO

Amitabh Bachchan kwa sababu walikuwa na fedha za kuwahonga polisi na mahakimu. Vijay Singh, akachukua ahadi ya kulipa kisasi. I had lost my trust in the law since I was child. Why dont you get a good doctor to check the eyes of your so called Law. Nilipoteza imani na Sheria toka nikiwa mtoto. Kwanini hamtafuti dakitari mzuri wa macho kutibu macho ya hicho mnachokiita Sheria? Ni kauli aliyokuwa akiisema Vijay Singh kuwaambia watu waliokuwa wakimtaka asichukue sheria mkononi. Ni kutokana na visa kama hivi, Vijay Singh na Jan Nissar Akhtar Khan, wa l i c h u k i a s h e r i a n a kuibeza kwamba yenyewe ni kipofu hata ikiletewa ushahidi wa uwongo, haiwezi kutambua. Kwa sababu hiyo inafunga watu wasio na hatia. Inaachia majambazi, wahujumu uchumi na mafisadi bila kuwaadhibu. Na maudhui haya ndio likawa jina la filamu-Andhaa Kanoon (Sheria Kipofu). Siku ya Jumamosi iliyopita kulikuwa na ujumbe ukisambazwa kupitia simu za mkononi. Ujumbe huo wa maneno ulikuwa ukisema: Jumuiya ya UAMSHO: Taarifa maalum, Sheikh Azzan alizimia jela usiku mkubwa siku Jumamosi 31/8 akazinduka asubuhi kisha akazimia tena

Vijay Singh saa 2 asubuhi Jumapili akachukuliwa kwa machela akiwa amezimia na kupelekwa hospitali Mnazi Mmoja. Siku ya pili baada ya kufikishwa alizimia tena kwa mara ya tatu juzi tarehe tarehe 5 hali yake ilikuwa mbaya sana usiku wa manane. Leo ni ya 8 hajapata matibabu yoyote zaidi ya Drip. Anayezungumzwa hapa ni Sheikh Azzan Khalid Hamdan ambaye, pamoja na Masheikh wenzake wapo ndani kwa takriban mwaka sasa. Hawa sio kwamba wamehukumiwa kifungo, kama Jan Nissar Akhtar Khan (Amitabh Bachchan), lakini wapo rumande tu na kesi yao wala haijawahi kuzungumzwa. Wapo ndani kwa sababu wasimamia sheria wamezuiya dhamana. Wanasema kwa makosa wanayotuhumiwa kwayo, hawastahiki kupata dhamana. Jan Nissar alitolewa jela kwenda kumzika mkewe na mwanawe. Zipo taarifa kuwa akiwa ndani Sheikh Mselem alifiwa na mwanawe tarehe 13 Machi, 2013. Hakuwahi kumzika mwanawe k i p e n z i . K wa s a b a b u alitakiwa kupelekwa kwa mikiki mikiki, mbwembwe na vitisho vya FFU (eti chini ya ulinzi mkali, utadhani jambazi, gaidi au mhaini). Yeye na familia wakaona kama ni hivyo, FFU na mitutu, mabomu na marungu mpaka makaburini, basi. Faradhi hiyo kifaya watafanya

wengine. Sheikh Mselem kaingia ndani kamuacha mwanawe, Mungu akimjaaliya Sheria Kipofu ikimtoa salama, anakuta mwanawe HAYUPO. Jan Nissar Akhtar Khan alitumikia kifungo jela baada ya kuhukumiwa k u wa k a u wa . L a k i n i hakuuwa. Aliyedaiwa k u u l i wa a l i k u wa h a i akila na kunywa, wakati Khan akiteseka jela. Sheria ilikuwa kipofu. Haikuweza kuona kuwa mashahidi na vielelezo vilivyowasilishwa mahakamani, vilikuwa urongo mtupu. Haikuweza kuona kuwa anayedaiwa kufa, yupo hai. Wala haikumuona kuwa ndiye aliyemuuwa Zakhiya na Neelo. Leo tunaambiwa kuwa Masheikh wa Uamsho wametenda kosa ambalo inabidi dhamana zao zizuiwe. Tujaaliye kuwa sheria kama hiyo ipo. Kwa hiyo DPP anaweza kuitumia bila ya kulaumiwa kuwaweka Masheikh hao mwaka mzima bila ya dhamana na asilaumiwe kwa sababu hoja itakuwa kuwa si yeye ni sheria. Lakini swali ni je, hayo makosa wanayodaiwa k u f a n ya ya m e t h i b i t i ? Kama upo ushahidi wazi kuwa wametenda makosa hayo, kitu gani kinaleta kigugumizi hata kesi zao zisisikilizwe? Kama Sheikh Azzan na Masheikh wenzake wa UAMSHO watakuwa wamewekwa ndani kwa dhulma, kwa maana kuwa ni yale yale ya Andhaa Kanoon (Blind Law), Sheria Kipofu, nani atalipa dhulma hii? Filamu hii Andhaa Kanoon, ilikuwa maarufu sana Unguja miaka ya 1980/90s, enzi hizo za Malindi (Cine Afrique), Majestic na Empire. Hata hivyo sidhani kuwa kuna ambaye wakati huo aliyekuwa akizingatia sana ujumbe wa filamu. Zaidi ilikuwa watu wakifurahia ufundi na usanii wa hali ya juu wa Amitabh Bachchan na Rajnikant (Vijay Singh). Inasifiwa kuwa hivi sasa kuna Serikali ya Maridhiano na Umoja wa K i t a i f a b a a d a ya kumalizika kipindi cha siasa za chuki na uhasama. Hizo zilikuwa zama ambapo baadhi ya watu waliwekwa

Makala/Habari

DHULQADAH 1434, IJUMAA SEPT.13-19, 2013

AN-NUUR

Kituo cha Habari cha Palestina (Tanzania)


SIKU ya Ijumaa tarehe 6 Septemba 2013 majeshi ya I s r a e l ya l i u va m i a msikiti mtakatifu wa Al Aqsa nchini Palestina, kwa madhumuni ya kuwaruhusu walowezi wa Kiyahudi kuingia na kuswali katika msikiti huo unaopewa hadhi ya tatu na Waislamu bilioni moja na nusu duniani Kitendo hiki cha majeshi ya Israel kiliwakasirisha s a n a Wa i s l a m u w a Palestina na ulimwenguni kote. Kwani kimekuwa kikifanywa mara kwa mara siyo tu na Wayahudi wenye msimamo mkali, bali na watawala na raia wote wa Israel. Hii ndiyo Israel ambayo inadai eti ni nchi pekee katika Mashariki ya Kati inayofuata misingi ya kidemokrasia na utawala bora. Ukweli ni kuwa wanachokifanya Waisraeli, ni kulazimisha mawazo yao yaliyopitwa na wakati kwa kisingizio cha imani yao, kwa lengo la kubadili historia ya Palestina. Inatoka Uk. 1 na pia kukosa imani na Serikali yao waliyoichagua. Tu n a a m i n i h i v y o kwa sababu hata Maafisa wa Balozi za Kimataifa wamebaini hujuma zinazotendeka halafu wakashingiziwa Uamsho sasa nini hii kama si kuiwinda na kuihujumu Serikali ya Umoja wa Kitaifa, alisema na kuhoji Maalim Abdul Ahme mmoja wa Watafiti katika Taasisi ya Demokrasia ya Nchi za Ulaya alipoongea na wanahabari hivi karibuni mjini hapa katika kudadisi na kutafakari hali ya kisiasa Nchini. Mwanaharakati huyo alisema hakuna ubishi juu ya uhalisi wa kuwepo kundi lisiloitakia mema GNU kupitia viashiria mbali mbali tangu ilipoasisiwa Serikali hiyo. Alitaja viashiria hivyo kuwa pamoja na Wastani wa Asilimia 33 waliopinga dhidi ya walioikubali ambao ni Asilimia 66.4. M s o m i n a m wa n a h a r a k a t i h u y o wa mambo ya siasa aliyeambatana na M a a f i s a wa K i b a l o z i

Msikiti Mtakatifu wa Al Aqsa Unavyonajisiwa na Wayahudi


Ndio maana, hivi karibuni Israel iliendelea kuushambulia msikiti mtakatifu wa Al Aqsa. Wakalazimisha milango ifunguliwe ili kuwaruhusu Mayahudi wenye mawazo mgando waingie humo msikitini na kuunajisi Watawala wa Israeli katika mji wa Al Quds ( Jerusalem) kila wiki huwa wanabuni sheria na kanuni mpya kwa lengo la kuwazuia Waislamu walio chini ya miaka 35 au 40 kuswali katika msikiti huo. Wa k a t i h u o h u o watawala wa Israel wanachimba ardhi iliyo chini ya msikiti wa Al Aqsa, wakidai kuwa wanatafuta mabaki ya hekalu lao lililokuwepo hapo zamani. Wamekuwa wakifanya hivyo kwa miaka mingi, zaidi ya miengo mine, bila ya mafanikio. Lengo la uchimbuaji huo ni kupata sababu ya kuuvamia na kuukalia mji Al Quds kwa kisingizio kuwa Wayahudi wamekuwa na historia ndefu hapo. Matokeo yake ni kuupa mji huo mtakatifu kwa Waislamu taswira ya Kiyahudi (Judaization). Wanataka kufanya hivyo kwa kufuta alama zote za Kiislamu kama vile misikiti, makaburi na majengo ya kale. Haya yanafanyika siyo tu katika mji wa Al Quds, bali katika maeneo yote ya Palestina. Hivi karibuni watawala wa Israel walibuni kanuni mpya ili kuugawa msikiti mtakatifu baina ya Waislamu na Wayahudi, sawa na walivyofanya katika msikiti wa Ibrahim katika mji wa Hebron. Kwa kufanya hivyo wameweka vikwazo vya kila aina ili kuwadhalilisha Waislamu wa Kipalestina wanaokwenda kuswali katika Msikiti wa Al Aqsa. Mara kadhaa Waisraeli wamekuwa wakiingia kwa nguvu katika msikiti huo wakiwa wanalindwa na majeshi na polisi wa Israel. Wakati huo huo huwa wanafanya vitendo vya kuwadhalilisha na kuwabughudhi waumini wa Kiislamu kwa kuvua nguo au hata kwa kunywa pombe. Wiki iliyopita wakati wa siku ya mwaka mpya wa Wayahudi, polisi wa Israel waliongozana na m a m i a ya Wa ya h u d i wakaingia msikitini ambako walikumbana n a Wa a i s l a m u we nye hasira ambao walitumia mawe ili kuwazuia. Ya k a t o k e a m a p i g a n o baina ya Waislamu wa Kipalestina na Walowezi wa Kiyahudi ambao walikuwa wakisaidiwa na polisi wa Israel. Matokeo yake Wapalestina kadha walijeruhiwa na wakakamatwa. Wakati wa malumbano hayo katika uwanja wa msikiti, wanajeshi wa Israel walitumia mabomu ya machozi na risasi ili kuwadhibiti Waislamu. Ta k r i b a n 6 0 k a t i ya o walijeruhiwa, 25 wakiwa wamepigwa risasi. Waumini 15 ambao ni watoto walikamatwa. Sheikh Raed Salah ambaye ni kiongozi wa

asasi ya Kiislamu iitwayo Um el Fahem, naye a m e p i g wa m a r u f u k u kuingia katika msikiti huo kwa muda wa miezi sita. Kutokana na udhalilishaji na uchochezi h u u k w a Wa i s l a m u , tunapaswa tujiulize kama kweli Waisraeli wana nia ya kuzungumzia amani na Wapalestina kama inavyofanyika hivi sasa chini ya uangalizi wa Marekani. Kwani Israel imekuwa siku zote ikihalifu sheria ya kimataifa bila ya kukhofu. Nayo mataifa ya Magharibi ya n a t u m i a u n d u m i l a kuwili na unafiki, kitu ambacho kinawafanya Waisraeli kuwagandamiza Wapalestina na kuzuia kuundwa kwa Taifa la Palestina lenye mipaka inayotambulika kimataifa. Contact us: P.O Box 20307, 612 UN Road Upanga West, Dar es Salaam Tel: 2152813, 2150643 Fax: 2153257 Email: pict@pal-tz.org Website: www.pal-tz.org inashangaza hawa jamaa wanakerwa na hii hali lakini piga ua hawatutoi katika mstari twataka Nchi yetu bwana, aliibuka kijana Katika Maskani y a C o m m o n We a l t h iliyopo Michenzani baada ya kusikiliza Hotuba ya Makamo Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM, Zanzibar, Bwana Shaka, dhidi ya Viongozi Wakuu wa Serikali ya Zanzibar, ambayo ikirushwa moja kwa moja na kituo kimoja cha Redio, cha Mjini hapa. Uchunguzi unabaini juhudi za hatua za kisheria na za kinidhamu dhidi ya matusi na baadhi ya hujuma hizo, ikibidi kuwashitaki watukanifu na wahujumu ingawa wapembuzi bado wanashikilia kwamba yote hayo yanakuja ili kuwaparaganya Wazanzibari juu ya azma yao iliyowaweka pamoja ya kudai Mamlaka Kamili ya N c h i ya o k u p i t i a Mabadiliko ya Katiba ambayo mchakato wake unaendelea.

GNU- Zanzibar yawindwa


katika Kongamano la hivi karibuni la Utafiti wa Kisiasa, Nchini Norway, alisema pamoja na kundi hilo lililotumia haki yao ya demokrasia kupinga ujio wa GNU, wapo pia ambao dhahiri hawaipendi Serikali hii zikiwemo za wao kuwachukia Viongozi Wakuu wa SErikali ya sasa ya Zanzibar, au sababu za ubinafsi wa kukosa vyeo na madaraka serikalini. Wa s i j i s a h a u t u Viongozi na wananchi kwani serikali hii iliyopendekezwa na Wa z a n z i b a r i w e n g i haitowacha kuwindwa katika hali zote, alishauri usoni mwa wanahabari mmoja wa Maafisa wa Balozi za Nje aliyewahi kuhudumu Tanzania kwa muda mrefu. Miongoni mwa hujuma dhidi ya GNU na Viongozi wake Wakuu, ni matusi ya siri na ya dhahiri ya hivi karibuni ambapo umma umeshuhudia hali hiyo kupitia vikao na hata majukwaa ya kisiasa yakiwemo ya mikutano ya hadhara. Anatukanwa matusi ya nguoni Maalim Seif na Dokta Shein na Mhe. Karume hii siyo bure ja ma n i n i ip o n a mn a hawa jamaa hawaitaki hii serikali wala hawayataki haya maridhiano, alisema kijana aliyejitambulisha kwa jina la Kassim, Mkaazi wa Mwembeladu Zanzibar, ambaye alikuwapo Pembezoni mwa Mkutano wa Hadhara wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa maeneo ya Kombawapya h i v i k a r i b u n i wa k a t i ambao wahadhiri wa hafla hiyo wakimimina matusi ya kufa mtu dhidi ya Viongozi hao wa Serikali. Hata hivyo akina Kassim na baadhi na vijana wengine waliokuwepo hapo wakijieleza kuwa wafuasi wa CCM, kama

ilivyokuwa kwa wengine waliopiga mayowe katika mikutano mingine iliyofanyika hivi karibuni, walisikika wakila kiapo kwa maneno na kuahidi kwamba nafsi zao haziko tayari kuyatosa maridhiano ya kisiasa ya Zanzibar na Serikali iliyopo yenye muundo wa Umoja wa Kitaifa. Taarifa za uchunguzi na za uhakika, katika hali isiyotarajiwa miongoni mwa Viongozi na Wa b u n g e wa C h a m a Ta wa l a , wa l i k a r i r i wa wakimpasha Rais Dr. Shein kwa matusi makubwa katika miongoni mwa vikao vya faragha. Inashangaza CCM mwenziwe anamwambia Dr. Shein amechoshwa na Wapemba kama vile yeye Rais si Mpemba au jamaa huyu tunamjua ameoa na kuzaa na Mpemba wala hajawatupa watoto.

10
Bismilahi Karima, kumcha Mungu gharama Kumcha Mungu gharama, QUR-AN imesema Kikisogea kiyama, na Mtume akasema Kumcha Mungu gharama, dunia inakusonga.

Mashairi/Makala

DHULQADAH 1434, IJUMAA SEPT.13-19, 2013

AN-NUUR

Kumcha Mungu gharama

Sheikh Mohammed Issa umetutosa Waislam


Inatoka Uk.7
kujua maoni ya Sheikh Mohammed Issa iwapo anadhani kuwa mkutano wa Masheikh hao wanaokutana Mogadishu unaweza kuleta ufumbuzi. Hapa ndipo Sheikh alituzamisha kabisa na kutugaragaza katika tope. Jibu lake lilikuwa kama kuhamisha lawama kutoka kwa madhalimu na kuwabebesha l a wa m a M a s h e i k h / Waislamu. Alisema kwamba hadhani kwamba itasaidia kwa sababu Masheikh wenyewe hawajakaa sawa. Kwa maana ya kuwa na misimamo tofauti na pengine miongoni mwao ndio wanaopandikiza fikra potofu kwa vijana. Jibu kama hili, kutokana na maudhui ya habari iliyokuwa i k i j a d i l i wa n a k wa muktadha wa siasa za kidunia hivi sasa, kama atakuwa amelisikia B u s h / O b a m a , atakunywa wiski yake kwa furaha. Jibu la mwanzo limemsaidia kutia nguvu hoja potofu na kisingizio kuwa kuna Waislamu wanatumia dini vibaya kufanya ugaidi na hivyo ni sawa sawa kuwapiga vita. Na katika jibu la Mohammed Issa, akisisitiza kuwa Waislamu hao wamepotoka, alieleza mafundisho ya Mtume kuwa kakataza katika vita wasiguswe wanawake na watoto na hata mimea isikatwe. Swadakta. Maelezo sahihi kabisa. Lakini kwa msingi wa swali na muktadha wake (context), kwa kujibu na kutoa maelezo haya, unakiri kuwa kuna Waislamu waliopotoka wanaofanya ugaidi. K wa u p a n d e wa pili Bush atakenua meno kwa sababu jibu la Sheikh linazidi kuwashindilia Waislamu kuwa ndio wenye matatizo. Linamuacha dhalimu pembeni. Muktadha wa swali ni mgogoro wa Somalia. Sasa unapoulizwa kuwa Je, unadhani mkutano wa Masheikh utaleta ufumbuzi? Jibu muafaka/ munasibu, sio kutoa maelezo ya kuonyesha misimamo na matatizo ya Masheikh miongoni mwao (kwamba kwa mfano kuna Bakwata, Baraza Kuu, Shura ya Maimamu, Hayat Ulamaa na ile ya Sheikh Mohammed Idd na mwenzake Sheikh Khamis Mattaka). Jibu hapa lazima lirejee kwenye context ya habari. Kwamba k a m a m g o g o r o wa Somalia ni uvamizi wa mabeberu na vibaraka wa k e , u t a k o m a t u iwapo mabeberu hao itawajia huruma na kuwa na ubinadamu japo kidogo tu kwa b i n a d a m u we n z a o . Wakakoma kutumia neema aliyowapa Allah ya maguvu na mali kuwadhulumu, kuwatesa na kuwauwa binadamu wenzao wasio na hatia. Pengine ili kufafanua zaidi Sheikh angegusia ya hapa kwetu Ta n z a n i a . K wa m b a Waislamu wamekuwa wakilalamika kuwa wanadhulumiwa na anayelalamikiwa ni Serikali. Sasa malalamiko kama haya hayawezi kuisha kwa kuita vikao vya Masheikh na Maaskofu, au kwa kuwasakama baadhi ya Masheikh kuwa ni wachochezi, kama Serikali inavyofanya. Hatua sahihi ni kwa Serikali kuwasikiliza Waislamu na kuyapatia ufumbuzi madai yao. Au kama madai ya Waislamu s i o ya k w e l i , b a s i Serikali itoe ufafanuzi. Ikae na kujadiliana na wanaolalamika na kufanya uchambuzi, yepi madai ni ya kweli yashughulikiwe na yepi si kweli. Kama anavyosema mwandishi Paul Craig Roberts, hawa BBC, CNN, Sky News na wengine kama hao, ndio washenga na wapambe wa kupiga propaganda za wapenda vita ambao ni Mazayuni na wale wanaowachukia W a i s l a m u (neoconservative agents). Hawa hivi sasa ndio walioshikilia bango la kutaka Syria ipigwe na kuvurugwa kabisa kama ilivyofanywa Iraq na Libya. Kisingizo kinachotumiwa ni kuwa Rais Bashar Assad anatumia silaha z a s u m u d h i d i ya wapinzani wake. Kwa mnasaba wa swali la BBC, labda Sheikh angemtaka mtangazaji asisahau kuwa wakati White House na Seneti yake ikipiga baragumu la silaha za sumu, hivi sasa wapo madaktari wa Uingereza (London Surgeons) ambao wanafanya kazi kwa kujitolea kusaidia kutibu (kuwafanyia upasuaji) watoto waliozaliwa wakiwa na vilema kutokana na athari ya kemikali iliyotumiwa na Marekani katika vita ya Vietnam.' Kwa mujibu wa taarifa ya BBC wenyewe ya hivi karibuni, japo vita ya Vietnam ilimalizika takriban miaka 40 iliyopita, lakini bado madhara ya vita hivyo yanaendelea kwa kuzaliwa watoto we n ye m a u m b o ya ajabu (horrific facial deformities, birth defects). Na hii ni kutokana na mamilioni ya galoni za sumu, maarufu, Agent Orange au Herbicide Orange (HO), iliyotumiwa na Marekani katika vita hiyo. Katika operesheni iliyojulikana kama Operation Ranch Hand, inakisiwa kuwa zaidi ya ekari milioni 25 (hekta milioni 10) za mashamba yenye vyakula, ziliharibiwa kabisa. Nchi kwanza ikakumbwa na njaa ya kutisha. Watu waliokufa kutokana na kemikali hiyo, inatajwa idadi yao kuwa ni 400,000, huku Msalaba Mwekundu (Red Cross) wakisema kuwa zaidi ya watoto milioni moja walizaliwa na ulemavu, kwa maana ya miili ya ajabu kutoka na sumu hiyo. Da Nang iliyopo katikati ya Vietnam, inaaminika kuwa n d i y o ye n ye i d a d i kubwa zaidi ya watoto wanaozaliwa na miili ya ajabu duniani na watoto hao wamekuwa wakipewa jina la jumla wa t o t o wa A g e n t Orange au Kizazi cha Agent Orange. (Picha zao hazifai kuweka katika gazeti kwa jinsi zinavyotisha ila mtu binafsi anaweza kuzitizama katika mtandao). Hao ndio watu ambao hivi sasa wanataka Syria ipigwe kwa kisingizio cha kuwa na silaha za sumu. Labda swali la Sheikh Mohammed Issa kwa BBC, lingekuwa: Unafiki huu wa mabeberu wanaojifanya k u wa o n e a h u r u m a Wasomali na wananchi wa Syria, mpaka lini? Kama kuna silaha za

Kukaribia kiyama, kumcha Mungu gharama Kaa la moto nasema, viganja unguzwa nyama Utashindwa kusimama, kukaa wala kuhema Kumcha Mungu gharama, dunia inakusonga. Usingizi utakoma, paa ukilitazama Kula chakula ni wima, na maji yakikukwama Watu wanakusakama, ni chizi wakuandama Kumcha Mungu gharama, dunia inakusonga. Mume kama sio mwema, mke wake atakoma Au mke sio mwema, kutwa ndani ni lawama Ndoa inakuwa wima, kila mtu kulalama Kumcha Mungu gharama, dunia inakusonga. Jirani wakusakama, ndugu wakupa shutuma Wazazi watakuhama, na radhi kuisukuma Watoto wananguruma, kama wameona kima Kumcha Mungu gharama, dunia inakusonga. Kumbuka Ibrahima, Mtume wake Karima Babaye kumuandama, motoni akamtuma Kisa mawaidha mema, ushirikina kasema Kumcha Mungu gharama, dunia inakusonga. Makundini ukisema, majibu utayakoma Hasa unaposimama, aya za Mungu kusoma Ndipo watakuandama, macho yakiwaparama Kumcha Mungu gharama, dunia inakusonga. Watajenga uhasama, ukizuia dhuluma Ya ALLAH yanawakwama, sura zao kukunjama Kampeni kama za vyama, huku na huko lawama Kumcha Mungu gharama, dunia inakusonga. Jingine lisilo jema, ni dola kuunguruma Jela watakusukuma, mateso kufuata nyuma Kupigwa cha moto chuma, wakutoe na bandama Kumcha Mungu gharama, dunia inakusonga. Wala siyo hizi zama, tukumbukeni na nyuma Ni Mitume wetu wema, Mussa na Haruna jama Firauni kuwakwama, kila siku ni tuhuma Kumcha Mungu gharama, dunia inakusonga. Wenye raha na salama, wafichao ya kiyama Kanzu ni zao alama, na kula wali kwa nyama Duniani wamezama, wakasahau kiyama Kumcha Mungu gharama, dunia inakusonga.

Siku katika masiku, babu kanipa hadithi Yamhusu dada Shuku, Kila siku yu hadathi Akiliye kama kuku, Chakubimbi na habithi Dunia izumbukuku, nasaha wako urithi Urithi wa baba yangu, katika hadithi yake Kaniasa mambo chungu, ya kheri na shari zake Kufunzwa na ulimwengu, laana yakini yake, Chunga mjukuu wangu, maadili usivuke Shukurani msafiri, hilo ndilo jina lake Kajaaliwa kigori, sura pia umbo lake Nidhamu yake sanjari, upole haiba yake Kutwa alijisitiri, dini maadili yake Kaponzwa na walimwengu, dunia ikamshika Ulimwengu na mizungu, akaanza badilika Rafikize ni machangu, Jiji lote wasifika Kasahau mdudu chungu, hawi panya wala nyoka Dini kaweka pembeni, hijabu hazina mana Haramu msikitini, disko kwake ndo sana Swala za rakaataini!, bora aende kwa bwana Wazazi kumthamini, wakaonya wao mwana Shuku mwanetu kipenzi, tabia nzuri ni kito Ugeberi ni ushenzi, sitiri wako mvuto Mekufunza tangu enzi, haya mambo ya mpito Dini ikakupa nyenzi, kipi mekosa mtoto? Shuku kaharibikiwa, majanga yakamfika Himila akapatiwa, na magonjwa kadhalika Ahadi alotajiwa, mefanya kababaika Kaishia kutumiwa, dunia mehadaika Hadithi lipomaliza, nami nakoma nudumu Lengo toe muangaza, mabatili Islamu Mboni mzitoe kiza, mumngamue dhalimu Nilosema mkibeza, Mola atawahukumu Nasri Kione nasriibrahimu@yahoo.com No: 0759202192

Dunia hadaa

Ngonda Z. Mwanza.

kemikali zimetumika Syria, iwe zimetumiwa na Serikali ya Bashar au na waasi, bado ukweli unabaki kuwa silaha hizo zisingetumika kama Marekani isingewachochea na kuwapa silaha na kuwawezesha waasi, kwa kila namna, kuanzisha vita ya kumngoa Bashar. Kama Somalia kuna al Shabab, bado ukweli unabakia kuwa kundi hilo lisingeibuka kama si Marekani na Ethiopia kuiongoa madarakani S e r i k a l i ya U m o j a wa Mahakama za Kiislamu iliyofanikiwa k u wa d h i b i t i a k i n a Mohamed Farah Aidid, Osman Ali Atto, Musa Sudi Yalahaw, Abdi Hassan Awale Qeybdiid na wababe wengine wa kivita, hata amani ikarejea. Mogadishu ikakalika t e n a . Wa l i o k i m b i a wakaanza kurejea. John Pilger katika makala yake, From Hiroshima to Syria, the enemy whose n a m e we d a r e n o t speak, anasema kuwa ameshuhudia watoto waliozaliwa na maumbo ya kutisha Iraq kutokana na silaha za sumu (depleted uranium) zilizotumiwa na Marekani katika uvamizi wake 2003. Depleted uranium hiyo imetumiwa pia na Israel kule Gaza (2008), tena kwa kupiga watoto wa shule na wagonjwa hospitalini (UN schools and hospitals). Haya mbona BBC hawasemi wakati yapo wa z i ? Wa t a t u m i wa mpaka lini kama Vipaza Sauti na Wizara ya P r o p a g a n d a ya wapenda vita? Je, haikutosha walivyotumiwa kupigia debe habari za vita na Crusade iliyosababisha kuuliwa mamilioni ya watu wasio na hatia Afghanistan, Iraq, Libya, Somalia, Pakistan, Yemen, na Misri? BBC na wenzao wanataka wauliwe watu wangapi ndio waweze kuona vibaya kutumiwa katika propaganda hizi chafu zinazosababisha umwagikaji wa damu na kuharibiwa nchi? Au n i k w a v i l e wanaouliwa ni Wasomali, Wahindi, Waarabu, sio wananchi wa London, Washington

11

Habari

DHULQADAH 1434, IJUMAA SEPT.13-19, 2013

AN-NUUR

Sheikh Azzan hoi Hospitalini Mnazi Mmoja


Na Waandishi wetu, Zanzibar

Waislamu wahoji mapingu yote ya nini


hiyo wakiendelea na mjadala juu kuishauri serikali kutoa kibali cha kutibiwa nje ya nchi, k i n a c h o wa s h a n g a z a wananchi na Waislamu kwa ujumla, hasa waliowahi kumtembelea Sheikh Azzan katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja mjini hapa, ni hali inayomkabili Naibu Amiri wa (JUMIKI). Siyo tu kwa na maradhi yanayomkabili, la hasha, bali ni pingu nzito aliyofungwa nayo kitandani alikolazwa, katika chumba maalumu katika mahabusu ya Hospitali hiyo ya Rufaa. Ni kweli yuko kizuizini na ni taabu kumuona kutokana na vikwazo alivyowekewa, lakini nashangaa yale mapingu aliyofungwa maskini, huyu ni muhalifu wa aina gani, alihoji Ust. Ali, mmoja wa Masheikh na Maimamu wa hapa waliofika kumjulia hali Sheikh huyo. Kiongozi huyo alilazwa hapo akitokea mahabusu wanakoshikiliwa yeye na Viongozi wengine wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, yapata mwaka mmoja sasa. Uchunguzi umebaini kuendelea mashauriano ya madaktari bingwa, we n ye m a m l a k a ya kuishauri Serikali juu ya ridhaa ya kumpeleka kiongozi huyo nje ya nchi kwa ajili ya matibabu ya dharura.

Mbunge Matatani kwa Uchochezi


Na Waandishi wetu, Zanzibar JESHI la Polisi, Zanzibar limelazimika kumuita katika vyumba vya selo, Mbunge wa Jimbo la Donge, Bw. Sadifa Haji Khamis, kutokana na vitendo vya uchochezi na uvunjifu wa amani. Mashahidi pamoja na taarifa ya Jeshi la Polisi, wamethibitisha kumuona na kumnasa kinara huyo aliyevinjari kwa matusi katika mikutano ya hivi karibuni akirandiarandia ndani ya Kituo cha Polisi cha Mahonda, Wilaya ya Kaskazini B, Unguja. Kinara huyo alifika Kituoni hapo kwa wito maalumu wa Jeshi la Polisi kupitia RB No. 3/2013 ya Tarehe 1 Septemba Mwaka huu, kupitia malalamiko ya Wananchi wa Jimbo la Donge. Ilidaiwa Kituoni hapo kwamba mnamo Tarehe 1/9/2013, Sadifa n a Wa f u a s i w a k e walifika na kuishusha Bendera halali ya Chama c h a Wa n a n c h i ( C U F ) iliyokuwa ikipepea katika Tawi la Mwanakombo, Jimbo la Donge, Wilaya ya Kaskazini B, Unguja hali ambayo kwa kiasi kikubwa ilisababisha uchochezi na uvunjifu wa amani. Hiki ni kiburi na kitendo cha uhuni na ukosefu wa nidhamu na pia kitendo cha kutishia amani kinachopinga na kuvunja kwa makusudi Sheria halali za Nchi hii, alisema Bw. Masoud kaazi wa maeneo hayo na msomi wa Mambo ya Sheria akiwasilisha malalamiko hayo usoni mwa makamanda wa P o l i s i wa l i o k u wa wakiitegea sikio kadhia hiyo ambayo haijawahi kushuhudiwa kwa miaka ya karibuni tangu kuja kwa Maridhiano ya Kisiasa ya Zanzibar. Taarifa kutoka Mahonda zimebainisha kuwa Jeshi la Polisi limeahidi kukamilisha upelezi hadi ifikapo Tarehe 16 Septemba, 2013 ambapo tayari mashuhuda wa tukio hilo wameshatinga Kituoni hapo kueleza kisa na mkasa wa kadhia hiyo. M a s h a h i d i wamewaarifu baadhi ya Viongozi waliofika eneo la tukio kwenda kuwatuliza wananchi, kwamba mara tu Sadifa na wafuasi wake walipokwisha kuipachua Bendera hiyo kwa jeuri kubwa waliichukua na kwenda nayo moja kwa moja katika Mkutano wake wa hadhara wa C C M u l i o f a n y i k a Kombawapya siku hiyo, akaianika bendera hiyo kadamnasi, katika mkutano uliobebeshwa lawama kubwa za kuwatusi Viongozi Wakuu wa Serikali ya Zanzibar. Tunataka Serikali ichukue hatua dhidi ya uhuni huu na pia Sheria ichukue mkondo wake kwani huu ni uchochezi na uvunjifu wa amani na uchokozi wa makusudi uliolenga kuwagombanisha wananchi na pia ni kinyume kabisa na Maridhiano ya Kisiasa ya Zanzibar sasa nchi yetu imetulia haya nini tena, alisema na kuhoji Mkurugenzi wa Haki za Binaadamu, Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma wa CUF, Bw.Salim Bimani. Kinachobainika ni shauku kubwa waliyonayo Wa n a n c h i wa D o n g e na Mwanakombo, waliokaririwa wakisema wanaisubiri kwa hamu siku

NAIBU Amiri wa JUMIKI), Sheikh Azzan Khalid Hamdan

NAIBU Amiri wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu ( JUMIKI), Sheikh Azzan Khalid Hamdan, yuko hoi katika hospitali ya rufaa ya Mnazi Mmoja Zanzibar. Kwa mujibu wa taarifa ya uchunguzi wa madaktari, Sheikh Azzan amelazwa hospitalini hapo kutokana na maradhi ya figo, akiendelea na matibabu. Licha ya kuwa taaban kitandani kwa maradhi hayo, huku akiendelea kusubiri madaktari bingwa wa hospitali

hiyo ambayo wametakiwa wafike Kituoni kwa hatua zaidi. Kwa mujibu wa Sheria kosa la aina hiyo linaweza kumgharimu muhusika Kifungo cha jela kinachoweza kutimia mwaka mmoja, faini, au yote mawili kwa pamoja.

SHURA YA MAIMAMU (T)


Inawatangazia Waislamu wote kuwa kutakuwa na Ibada ya Itikaf itakayofanyika Masjid Irshaad Chihota Tandika. Siku ya Jumamosi tarehe 14/9/2013 itakayoanza saa tatu usiku baada ya swalat Ishaai Amir

Itikaf

12

AN-NUUR
MAKALA

DHULQADAH 1434, IJUMAA SEPT.13-19, 2013

AN-NUUR

12

SHAWWAL 1434, IJUMAA

SEPT. 6-12, 2013

Mfadhili asaidia wanawake 300 mafunzo Ujasiriamali

Tanzania Muslim Hajj Trust Safari ya Hijja 2013 Uandikishaji unaendelea gharama za Hijja ni dola za Kimarekani $ 4200. Safari ni tarehe 5 na 7 Octoba, na Kurudi Tarehe 27 na 28 Octoba, 2013. Wahi kujiandikisha Sasa. Uandikishaji wa Hijja Zijazo 2014, 2015 kwa Kulipia kidogo kidogo, unaendelea. Simu: 0717 000 065, 0784 222 911, 0754 304 518, 0754 498 888 Au kupitia Tovuti yetu. www.hajjtrusttz.org. na kuuza batiki, mafuta ya mgando, sabuni ya maji.nk. Wa j a s i r i a m a l i h a o walimshukuru mfadhili wao kwa kuwawezesha kupata elimu hiyo na kuahidi kuitumia kikamilifu elimu waliyoipata kuinua maisha yao. Hata hivyo Bw. Mukaddamu alisema kuwa kukamilika kwa mafunzo hayo kwa upande wa kina mama, kunampa fursa ya kuanzisha mafunzo mengine kwa upande wa vijana na kundi jingine linalohitaji. Akisoma risala kwa niaba ya akina mama wenzake, Bi. Siraji Juma Ditopile, alisema Mukaddam kwao ni mkombozi na kwamba ni jukumu la akina mama kuifanyia kazi elimu waliyoipata na kutobweteka katika kuitumia, ili dhamira iliyokusudiwa iweze kufikiwa. Naye Bi. Angela Shayo, alisema amefaidika sana na semina hiyo kwani sasa ataweza kutengeneza batiki pamoja na mafuta ya mgando kwa msaada wa elimu hiyo, na kwamba ana matumaini kuwa watajikwamua na umaskini unaowakabili. Katika tukio jingine Bw. Kamaldeen Mukaddam, alitoa msaada wa vifaa vya ofisini ambavyo ni Meza kumi pamoja na viti kumi kwa shule ya Msingi Msimbazi Mchanganyiko, kufuatia walimu wa shule hiyo kukosa vitendea kazi hivyo shuleni hapo, jambo lililopunguza kasi ya kujituma na moyo wa kujitolea kwa walimu hao. Akikabidhi vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi milioni nne za Kitanzania, Bw. Mukaddam alisema ana imani kuwa vifaa hivyo vitakuwa ni kichocheo cha walimu hao kufanya kazi zao kwa bidii na kwa nafasi. Aliwataka walimu hao kufanya jitihada za makusudi, kwani anaamini kuwa shuleni hapo wanaweza kutoka viongozi wa baadae na kushika nafasi za ubunge na uwaziri. Aidha amewataka wazazi kuwahimiza watoto wao kusoma kwa bidii, kwani walimu sasa watajitahidi kufanya kazi kwa bidii tofauti na siku za nyuma ambapo walikuwa wakitumia madawati kwa muda mrefu kufanya kazi zao za kila siku. Akipokea msaada huo, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Reuben Gadi, alisema n i m u h i m u s a n a k wa o kwani meza hizo za kisasa, wamekuwa wakiziona zikitumika katika ofisi za serikali na mashirika na kwamba, wao wamezoea kukalia madawati kwa muda mlefu. Mwalimu Mkuu huyo alisema ana imani kuwa, walimu wake watazitumia meza hizo kwa lengo lililokusudiwa katika kuendeleza sekta ya elimu shuleni hapo. Aidha Bw. Mukaddam aliahidi kuendelea kuisaidia shule hiyo ambayo inakabiliwa na uhaba mkubwa wa vyoo, ambapo hivi sasa choo kilichopo shuleni hapo ni kimoja na kinatumiwa na walimu arobaini, hali ambayo inadhalilisha ikizingatiwa kwamba shule yenyewe ipo mjini.

Akabidhi samani shule ya msingi Msimbazi

BAADHI ya wananchi waliohudhuria mafunzo ya ujasiriamali. Msimbazi Mchanganyiko aliyosomea na kuhitimu Na Abdulkarim S. wilayani humo. katika masuala ya kijamii. Msengakamba Akizungumza katika Bw. Mukaddam alisema sherehe za ufungaji wa mafunzo hayo yatawasaidia mafunzo ya ujasiriamali akina mama hao kupata M D A U wa m a e n d e l e o yaliyofanyika kwa muda elimu sahihi ya kujikwamua jimbo la Ilala jijini Dar es wa siku tano katika shule kimaisha pamoja na familia Salaam, Bw. Kamaldeen ya msingi Msimbazi zao. Hossein Mukaddam, Mchanganyiko Jumapili Mafunzo hayo a m e f a d h i l i s e m i n a ya iliyopita, Bw. Mukaddam ya ujasiriamali mafunzo ya ujasiliamali alisema dhamira yake ya yaliyowashirikisha akina kwa akina mama wa jimbo kujitolea ni kuikwamua jamii mama wapatao 300, katika umasikini uliokithiri, yatawasaidia kuboresha la Ilala na kutoa msaada wa kwani hiyo ni taaluma biashara zao za kutengeneza samani kwa shule ya msingi

CAIRO WA N A S I A S A waliokuwa karibu na Rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak, wamemtaka kiongozi wa j e s h i l a M i s r i , Jenerali Abdulfatah al-Sisi, kugombea urais kwenye uchaguzi mkuu ujao. Aliyekuwa Waziri Mkuu katika siku za

Washenga wa Mubarak wamtaka al-Sisi agombee urais


mwisho za utawala wa Hosni Mubarak, Bw. Mohammad Shafiq, amesema hatogombea tena urais iwapo alSisi atakubali kujitosa uwanjani. Shafiq aliwania urais kwenye uchaguzi mkuu mwaka jana, ambapo a l i s h i n d wa n a D k . Muhammad Mursi, aliyepinduliwa Julai 3 mwaka huu na jeshi la nchi hiyo likiongozwa na Jenerali al-Sisi. A i d h a wa z i r i wa z a m a n i wa m a m b o ya nje katika utawala wa Mubarak, Bw. Amr Musa, amesema iwapo al-Sisi ataamua kugombea urais, basi atashinda kwa kura nyingi. Musa ambaye aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa zamani wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, amesema Misri inahitaji kiongozi mwenye misimamo thabiti kuhusiana na suala la ugaidi na kudai kwamba Jenerali Abdulfattah al-Sisi, ndiye mtu anayeweza kuchukua maamuzi magumu katika kupambana na tatizo hilo.

Jenerali Abdulfatah al-Sisi.

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.

Вам также может понравиться

  • Annur:Toleo La Ijumaa Tarehe 13-01-2012
    Annur:Toleo La Ijumaa Tarehe 13-01-2012
    Документ16 страниц
    Annur:Toleo La Ijumaa Tarehe 13-01-2012
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • Annuur 1082
    Annuur 1082
    Документ16 страниц
    Annuur 1082
    MZALENDO.NET
    100% (1)
  • Annuur 1262
    Annuur 1262
    Документ20 страниц
    Annuur 1262
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1122
    Annuur 1122
    Документ16 страниц
    Annuur 1122
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1158
    Annuur 1158
    Документ16 страниц
    Annuur 1158
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1062
    Annuur 1062
    Документ16 страниц
    Annuur 1062
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • Annuur 111
    Annuur 111
    Документ16 страниц
    Annuur 111
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • Annuur 1170
    Annuur 1170
    Документ20 страниц
    Annuur 1170
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1119
    Annuur 1119
    Документ16 страниц
    Annuur 1119
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1109
    Annuur 1109
    Документ16 страниц
    Annuur 1109
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1041
    Annuur 1041
    Документ12 страниц
    Annuur 1041
    Hassan Mussa Khamis
    Оценок пока нет
  • ANNUUR1003
    ANNUUR1003
    Документ16 страниц
    ANNUUR1003
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • Annuur 115
    Annuur 115
    Документ16 страниц
    Annuur 115
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • Annuur 1028
    Annuur 1028
    Документ16 страниц
    Annuur 1028
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • Annuur 1111
    Annuur 1111
    Документ16 страниц
    Annuur 1111
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 114
    Annuur 114
    Документ12 страниц
    Annuur 114
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • Annuur 1056 PDF
    Annuur 1056 PDF
    Документ16 страниц
    Annuur 1056 PDF
    annurtanzania
    Оценок пока нет
  • Annuur 1077
    Annuur 1077
    Документ12 страниц
    Annuur 1077
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • Annuur 1115
    Annuur 1115
    Документ16 страниц
    Annuur 1115
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1176b PDF
    ANNUUR 1176b PDF
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1176b PDF
    annurtanzania
    Оценок пока нет
  • Annuur 1064
    Annuur 1064
    Документ12 страниц
    Annuur 1064
    annurtanzania
    Оценок пока нет
  • Annuur 1217
    Annuur 1217
    Документ20 страниц
    Annuur 1217
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1169a PDF
    ANNUUR 1169a PDF
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1169a PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Gazeti La Annur
    Gazeti La Annur
    Документ12 страниц
    Gazeti La Annur
    Hassan Mussa Khamis
    Оценок пока нет
  • Annuur 1173 PDF
    Annuur 1173 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1173 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1172 PDF
    Annuur 1172 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1172 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1179 PDF
    Annuur 1179 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1179 PDF
    annurtanzania
    100% (1)
  • Annuur 1102
    Annuur 1102
    Документ12 страниц
    Annuur 1102
    annurtanzania
    Оценок пока нет
  • Annuur 1157 PDF
    Annuur 1157 PDF
    Документ16 страниц
    Annuur 1157 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1049
    Annuur 1049
    Документ12 страниц
    Annuur 1049
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • Annuur 1155
    Annuur 1155
    Документ16 страниц
    Annuur 1155
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1144
    Annuur 1144
    Документ16 страниц
    Annuur 1144
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1060
    Annuur 1060
    Документ16 страниц
    Annuur 1060
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • Annuur 1027
    Annuur 1027
    Документ16 страниц
    Annuur 1027
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • Annuur 1180 PDF
    Annuur 1180 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1180 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1035
    Annuur 1035
    Документ16 страниц
    Annuur 1035
    Hassan Mussa Khamis
    Оценок пока нет
  • Gazeti La Annur Toleo La Disemba 16-2011
    Gazeti La Annur Toleo La Disemba 16-2011
    Документ16 страниц
    Gazeti La Annur Toleo La Disemba 16-2011
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • An-Nuur 1071
    An-Nuur 1071
    Документ12 страниц
    An-Nuur 1071
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1209aaa
    ANNUUR 1209aaa
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1209aaa
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Imaan Newspaper Issue 1
    Imaan Newspaper Issue 1
    Документ19 страниц
    Imaan Newspaper Issue 1
    Imaan Newspaper
    100% (1)
  • Annuur 1219
    Annuur 1219
    Документ20 страниц
    Annuur 1219
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1029
    Annuur 1029
    Документ20 страниц
    Annuur 1029
    annurtanzania
    100% (1)
  • Maulidi - Si Bida, Si Haramu
    Maulidi - Si Bida, Si Haramu
    Документ39 страниц
    Maulidi - Si Bida, Si Haramu
    Stambuli Abdillahi Nassir
    Оценок пока нет
  • Annuur 1078
    Annuur 1078
    Документ12 страниц
    Annuur 1078
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • Annuur 1007
    Annuur 1007
    Документ16 страниц
    Annuur 1007
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • Fiqhi ya ‘Ibada yenye picha zilizochorwa
    Fiqhi ya ‘Ibada yenye picha zilizochorwa
    От Everand
    Fiqhi ya ‘Ibada yenye picha zilizochorwa
    Оценок пока нет
  • Tishio la Ukombozi: Ubeberu na Mapinduzi Zanzibar
    Tishio la Ukombozi: Ubeberu na Mapinduzi Zanzibar
    От Everand
    Tishio la Ukombozi: Ubeberu na Mapinduzi Zanzibar
    Оценок пока нет
  • Nyayo Za Obama
    Nyayo Za Obama
    От Everand
    Nyayo Za Obama
    Оценок пока нет
  • Afisa Usalama Wa Taifa Ni Mtu Wa Aina Gani? Na Anafanya Nini?
    Afisa Usalama Wa Taifa Ni Mtu Wa Aina Gani? Na Anafanya Nini?
    От Everand
    Afisa Usalama Wa Taifa Ni Mtu Wa Aina Gani? Na Anafanya Nini?
    Рейтинг: 4 из 5 звезд
    4/5 (24)
  • Mwana-Adam ni Nani Naye ni Nini Mungu Amkomboe: Chuo cha Kwanza, #1
    Mwana-Adam ni Nani Naye ni Nini Mungu Amkomboe: Chuo cha Kwanza, #1
    От Everand
    Mwana-Adam ni Nani Naye ni Nini Mungu Amkomboe: Chuo cha Kwanza, #1
    Оценок пока нет
  • Miaka Hamsini ya Kiswahili Nchini Kenya
    Miaka Hamsini ya Kiswahili Nchini Kenya
    От Everand
    Miaka Hamsini ya Kiswahili Nchini Kenya
    Оценок пока нет
  • Dini ya Fedha
    Dini ya Fedha
    От Everand
    Dini ya Fedha
    Оценок пока нет
  • Mafundisho ya Ndoa
    Mafundisho ya Ndoa
    От Everand
    Mafundisho ya Ndoa
    Оценок пока нет
  • Hofu
    Hofu
    От Everand
    Hofu
    Рейтинг: 5 из 5 звезд
    5/5 (1)
  • HAYAAN, The Long Journey of the Nomad Boy
    HAYAAN, The Long Journey of the Nomad Boy
    От Everand
    HAYAAN, The Long Journey of the Nomad Boy
    Рейтинг: 5 из 5 звезд
    5/5 (2)
  • Mafundisho ya Utajiri
    Mafundisho ya Utajiri
    От Everand
    Mafundisho ya Utajiri
    Оценок пока нет
  • Ufufuo & Uchukuo
    Ufufuo & Uchukuo
    От Everand
    Ufufuo & Uchukuo
    Оценок пока нет
  • Milenia ya Kristo
    Milenia ya Kristo
    От Everand
    Milenia ya Kristo
    Оценок пока нет
  • Ujasusi Ni Nini? Na Je Majasusi Wanafanya Kazi Gani Hasa?
    Ujasusi Ni Nini? Na Je Majasusi Wanafanya Kazi Gani Hasa?
    От Everand
    Ujasusi Ni Nini? Na Je Majasusi Wanafanya Kazi Gani Hasa?
    Оценок пока нет
  • Yisrael
    Yisrael
    От Everand
    Yisrael
    Оценок пока нет
  • Annuur 1190
    Annuur 1190
    Документ20 страниц
    Annuur 1190
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1183 PDF
    Annuur 1183 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1183 PDF
    annurtanzania
    100% (2)
  • Annuur 1182
    Annuur 1182
    Документ20 страниц
    Annuur 1182
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1193
    Annuur 1193
    Документ20 страниц
    Annuur 1193
    annurtanzania
    Оценок пока нет
  • Annuur 1185
    Annuur 1185
    Документ20 страниц
    Annuur 1185
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1181 PDF
    Annuur 1181 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1181 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1179 PDF
    Annuur 1179 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1179 PDF
    annurtanzania
    100% (1)
  • Annuur 1173 PDF
    Annuur 1173 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1173 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1175b PDF
    ANNUUR 1175b PDF
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1175b PDF
    annurtanzania
    Оценок пока нет
  • Annuur 1178
    Annuur 1178
    Документ20 страниц
    Annuur 1178
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1094
    Annuur 1094
    Документ16 страниц
    Annuur 1094
    annurtanzania
    100% (1)
  • Annuur 1180 PDF
    Annuur 1180 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1180 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1176b PDF
    ANNUUR 1176b PDF
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1176b PDF
    annurtanzania
    Оценок пока нет
  • Annuur 1107
    Annuur 1107
    Документ16 страниц
    Annuur 1107
    annurtanzania
    Оценок пока нет
  • Annuur 1112
    Annuur 1112
    Документ16 страниц
    Annuur 1112
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1102
    Annuur 1102
    Документ12 страниц
    Annuur 1102
    annurtanzania
    Оценок пока нет
  • Annuur 1105
    Annuur 1105
    Документ12 страниц
    Annuur 1105
    annurtanzania
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1110cc
    ANNUUR 1110cc
    Документ16 страниц
    ANNUUR 1110cc
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Rasimu Ya Katiba (Toleo La Pili)
    Rasimu Ya Katiba (Toleo La Pili)
    Документ0 страниц
    Rasimu Ya Katiba (Toleo La Pili)
    Muhidin Issa Michuzi
    0% (1)
  • Annuur 1091
    Annuur 1091
    Документ16 страниц
    Annuur 1091
    MZALENDO.NET
    Оценок пока нет
  • Annuur 1093
    Annuur 1093
    Документ16 страниц
    Annuur 1093
    annurtanzania
    Оценок пока нет
  • Annuur 1096
    Annuur 1096
    Документ12 страниц
    Annuur 1096
    annurtanzania
    Оценок пока нет
  • Annuur 1088 PDF
    Annuur 1088 PDF
    Документ12 страниц
    Annuur 1088 PDF
    annurtanzania
    Оценок пока нет
  • Annuur 1090
    Annuur 1090
    Документ12 страниц
    Annuur 1090
    annurtanzania
    Оценок пока нет
  • Annuur 1089
    Annuur 1089
    Документ12 страниц
    Annuur 1089
    Hassan Mussa Khamis
    Оценок пока нет