Академический Документы
Профессиональный Документы
Культура Документы
tz
Sauti ya Waislamu
Age of Deception
ISSN 0856 - 3861 Na. 1094 DHUL-HIJJA 1434, IJUMAA , OKTOBA 11-17, 2013 BEI TShs 500/=, Kshs
Uk. 6
Sheikh Ibrahim Omari, maarufu Ibrahim Rogo , ameuliwa kama alivyouliwa Sheikh Aboud Mohammed Rogo.
Ni baada ya taarifa za ugaidi wa magazeti Sheikh atoa tahadhari, nasaha kwa Wahariri
2
AN-NUUR S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786
www.annuurpapers.co.tz
Tahariri/Makala/Tangazo
Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM. E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk Ofisi zetu zipo: Manzese Tip Top Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam
AN-NUUR
ZIPO taarifa kuwa kuna kamatakamata ya chini kwa chini inaendelea hasa maeneo ya Ilala na Buguruni ambapo watu kadhaa wamekamatwa na wanashikiliwa na Polisi. Inadaiwa kuwa watu hao, baadhi walikamatwa Misikitini na wengine nyumbani na wote inadaiwa kuwa walikuwa wakiangalia kanda za Al Shabaab. Kwa ambaye amewahi kuona CD hizo kama zilivyozagaa katika mitandao na akawahi kuangalia taarifa ya habari ya TBC1 Jumanne saa mbili usiku, ataridhika kuwa documentary hizo zimeandaliwa na watu maalum kwa lengo la kupiga propaganda ya k u wa t i a k a t i k a h a t i a Waislamu na kuupaka matope Uislamu. Kitu wanachotakiwa k u f a h a m u Wa i s l a m u ni kuwa hizi ni zama za udanganyifu (Age of Deception) kama anavyosema Mohamed Elbaradei. Documentary kama hizo zimetengenezwa nyingi na kuingizwa katika mtandao kwa malengo mawili. Moja ndio hizo vyombo vya habari kama TBC hutumia katika taarifa zao za habari katika jitihada za kuhusisha Waislamu na ugaidi. Pili, kuwatia hatiani Waislamu na kuleta kama kidhibiti kuwa wanajifunza ugaidi. Wanajua wakiziweka katika mtandao au CD Kuna watu watazifanyia biashara na wapo Wa i s l a m u w a t a t a k a kuzitizama. Lakini wanajua pia wapo Polisi waliokwisha andaliwa, wanajua nini cha kumfanya mtu watakayemkuta na CD hizo. Watamtia katika ugaidi. Sasa kuna haja kwa vijana wa Kiislamu na Waislamu kwa ujumla kuwa makini. Tutambue kuwa kwa muda mrefu kumekuwa na jitihada kubwa sana za kujiaminisha sisi wenyewe kuwa hapa Tanzania kuna kitisho cha kweli cha magaidi. Toka tulikuwa tukiambiwa kuwa magaidi hao ni wa kutoka nje
mpaka sasa tumefikia mahali pa kufanya juhudi mpya kwamba sasa magaidi hao wapo ndani ya nchi na wana kambi za kutoa mafunzo hayo kwa Watanzania wenzetu. Juhudi jingine ambayo tumekuwa tukiifanya kwa juhudi kubwa sana ni kuwatambulisha magaidi hao ni akina nani. B a a d a ya k a z i h i y o kubwa na ya muda mrefu ambayo imefanywa kwa juhudi kubwa na vyombo vya habari, mambo makubwa manne sasa yanajidhihirisha kama kielelezo cha mafanikio yaliyofikiwa. Moja, ni kukubalika kuwa nchi inakabiliwa na kitisho cha magaidi. Pili, kuwatambua magaidi hao kuwa ni al Qaida na Al Shabaab walio nje na ndani ya nchi. Tatu, Al Qaida na Al Shabaab hao ni wananchi wenzetu Waislamu. Nne, t u m e j i a m i n i s h a k u wa magaidi hao wana uwezo mkubwa sana usio wa kawaida, hata nchi ikitaka haiwezi kuwazuiya. Tunalotakiwa kutambua hapa ni kuwa kwa yote tuliyokuwa tukifanya, (Mwenyezi Mungu aepushilie mbali), yanaweza kutuletea balaa kubwa na hili likitokea itabidi tujilaumu wenyewe. Nitafafanua. Ifikirie nchi kama Marekani na maguvu yake ki-intelijinsia, kijeshi, kipolisi, Sheria za uhamiaji, u d h i b i t i wa wa s a f i r i kuingia kupitia viwanja vya ndege na bandarini, tekinolojia na umakini wa vyombo vya kusimamia sheria, lakini tunaambiwa kuwa magaidi kutoka nchi duni kwa kila kitu, Afghanistan wameingia na kushambilia sehemu nyeti kama Pentagon na WTC! Haikuishia hapo bado tunaambiwa kuwa kumekuwa na mashambulizi mengine madogo nadogo kama hili la juzi la Boston Marathon Bombing! Kwa waliowahi kufika Marekani baada ya Septemba 11, 2001 wanajua kiwango cha upekuzi na harakati za kiusalama zinazofanyika. Lakini bado tunaambiwa kuwa Al Qaida wameweza kufanya
shambulizi la Boston na kuuwa watu! Mambo mawili hapo yanajitokeza: Moja ni kuwa lazima tukubali kuwa magaidi hao ni hatari sana na uwezo wao ni mkubwa sana na kwamba kama hata baada ya kuuliwa Osama Bin Laden, bado wana uwezo wa kupiga Marekani, basi sisi huku uwezo wa kukabiliana nao utakuwa ni mdogo sana. Pili, kama hilo la kwanza sio sahihi, basi tukubali kuwa tumetiwa upumbafu wa kutisha kuwa likitokea jambo hatuna muda wa kuhoji hakika yake. Tunakwenda tu na ujinga tuliokwishalishwa kuwa hao ni Al Qaida. Hatari iliyopo ni kuwa ukishaaminishwa kuwa wapo Al Qaida wenye uwezo wa kiwango hicho na ukifikishwa mahali kuwa akili yako ishaliwa na virusi vya kulemaza kufikiri na kuhoji, kinachoweza kutokea ni kuwa usiyemdhania kabisa anaweza kutumia fursa hiyo kufanya shambulio akijua wazi kuwa wala hutahangaika kuchunguza nini kimetokea na nani kahusika. Anajua kabla hata Tw i t t e r h a i j a s e m a waliohusika ni Al Qaida/Al Shabaab, tawi la Tanzania, wewe tayari ushajiaminisha kuwa hakuna wa kufanya hilo ila magaidi wa Al Shabaab/Al Qaida. Katika zama hizi za elektroniki na dijitali, ambapo mtu anaweza kuanzisha blog/page, katika mtandao na akaipa jina na anuwani anayotaka, nini na nani mweye Twitter ipi? Lakini anajua kwa upumbafu waliokwishatiwa watu kupitia vyombo vya habari, ikitokea tu Al Jazeera ikasema, Twitter ya Al Qaida/Al Shabaab,
imesema wanahusika, hutakuwa na muda wala akili ya kuhoji na kutafakari. Utaimba hilo hilo la Twitter. Huu ni upumbafu wa kutisha na kwa hakika unaochefua na ndio utakaotuangamiza. Na kwa hali hii ambapo Al Qaida wana nasibishwa na wanaorukuu na kusujudu, basi watakaofanya shambulio ambao wewe wala hutawafikiria, wanajua wazi kuwa watu wa upande mwingine watataka kulipa kisasi. Na hiyo itakuwa njia ya uhakika ya kuitia nchi katika machafuko. Hivi sasa kuna ukaguzi mkubwa unaofanyika kwa watu wanaoingia katika maduka makubwa kama Mlimani City na Quality Plaza. Lakini tujiulize, hivi pale Westgate hapa kuwa na walinzi? Hapa kuwa na camera za security. Awali ikasemwa gaidi mwanamke kaingia na kikosi cha watu 30 na lundo la AK-47. Sasa tunaambiwa ni kama watu saba/nane tu wanaoshikiliwa na kuhojiwa. 23 hawajulikani wameyeyukia wapi. Ndio hii mara wadau wakuu katika kututia ujinga ( wa h a r i r i / wa a n d i s h i ) wa n a s e m a h a o 2 3 n a Kamanda Mkuu Samantha wametoroka kupitia mtaro wa maji machafu. Hebu ichukulie Westgate kama Mlimani City au Quality Plaza. Ndani kuna askari na makachero kwa mamia wanaopambana na magaidi. Nje jengo limezungukwa na mamia ya Polisi na wanajeshi wakiwa na silaha nzito. Mtaro upi wa maji machafu magaidi 23 na kamanda wao watatumia kutoroka? Kama si mtaro huo wa maji machafu, Samantha alipitaje ngome hii ya askari? Labda askari h a o wa t u a m b i e n d i o wa l i o m r u h u s u k u p i t a
na kwa maana hiyo wao watakuwa ndio wa mwanzo kuhojiwa watuambie nini kilitokea. Kama tunaamini kuwa magaidi waliweza kuingiza silaha za kutosha p a l e We s t g a t e M a l l , Nairobi, bila kugundulika na vyombo vya usalama, wakashambulia na kuondoka, hapana shaka magaidi hao kama w a t a i n g i a Ta n z a n i a , itakuwa vigumu kuwadhibiti. Kwa mtindo huu wa kuwa na Boston Marathon Bombing baada ya harakati zote za kiusalama baada ya Septeba 11, pamoja na kumuuwa Osama Bin Laden, ni wazi kuwa hakuna Usalama wa Taifa, Polisi, Mgambo, Polisi Jamii au Jeshi wanaoweza kuzuiya magaidi hawa. We unapekuwa watu Mlimani City, wao watapiga sokoni Kariakoo. Ukizidisha upekuzi Kariakoo watapiga soko la Tandale! Unazidisha ulinzi Dar na Arusha, wanashambulia Kibondo na Kirando! Sisi tunadhani kuwa kubwa la kufanyika hapa ni kufanya utafiti wa kisomi kukitambua kwanza kwa uhakika hiki kirusi Al Qaida/Al Shabaab na ugaidi wake kwa sababu kinavyoonekana kasi yake ya kujibadili (mutation) ni kubwa mno ambao unampa uwezo wa kushambulia usipotarajia, akapita mahali bila wewe kumtambua kama tunavyoaminishwa kuwa walifanya WTC, Pentagon, Boston, Westgate Kenya na kwingineko. H i i m a a n a ya k e n i kuwa dawa ya kupekuwa watu, kutumia mbinu za kipolisi na usalama wa taifa, zinaweza kuishia kuuwa na kutesa tu watu wasio na hatia, lakini bado hatutakuwa salama.
P.o. Box 55105 Tel: 2450069, 0712 974428, fax: 2450822 Dar es salaam. E-mail: ipcubungoislamic@gmail.com
UBUNGO ISLAMIC HIGH SCHOOL inatangaza program maalum ya maandalizi ya kujiunga na kidato cha kwanza 2014. Program hii itaanza tarehe 16/09/2013 hadi tarehe 16/12/2013. Jumatatu hadi ijumaa kuanzia saa 2:00 kamili asubuhi hadi saa 9:00 Alasir. Masomo yatakayofundishwa ni:Elimu ya dini ya Kiislamu, English language, Lugha ya kiarabu, basic Mathematics na Computer. ADA: Ni Tshs 60,000/= (Elfu sitini) tu. Inalipwa yote kabla ya kuanza programu. Fomu za Kujiunga zinapatikana shuleni BURE baada ya kulipa ada. Mlete mwanao apate Elimu yenye tija itakayomweze kujiunga na kidato cha kwanza. Kwa mawasiliano zaidi piga simu namba: 0714 888 557/0712 974428 Wabllah tawfiq MKUU WA SHULE
3
MOMBASA J A M I I ya Wa i s l a m u Mombasa nchini Kenya, wamedai kuwa Maofisa wa Kupambana na Ugaidi Kenya ndio waliomuua Sheikh Ibrahim Omar na wenzake watatu. Aidha wamedai kuwa maofisa hao wanaandaa m i p a n g o ya k u m u u a Sheikh mwingine aliyetajwa kwa jina la Abu Bakar Makaburi. Habari kutoka Mombasa Kenya, zimeeleza kuwa Sheikh Ibrahim Omari, maarufu Ibrahim Rogo na wenzake watatu walipigwa risasi na kuuliwa wakiwa ndani ya gari lao katika barabara ya Bamburi mjini Mombasa. Mashuhuda wamedai kuwa Sheikh Ibrahim Omar na wenzake hao walipigwa risasi zaidi ya arobaini, hali iliyoonyesha kuwa maadui hawakutaka kumbakisha hata mtu mmoja kwenye msafara huo, uliokuwa unatoka katika msikiti ambao marhuum Sheikh Aboud Mohammed Rogo, kaka wa marehemu ambaye naye anadaiwa kuuliwa na polisi mwaka jana, na wahusika hajakamatwa hadi sasa. Ta a r i f a z i n a e l e z a kwamba Abu Makaburi na Sheikh Ibrahim Omar, kabla ya kukutwa na mauti walikuwa wakipata v i t i s h o v ya k u u l i wa , ikidaiwa kuwa vitisho hivyo vililenga kuzima vuguvugu la Da'awah ya haki. Kufuatia kushambuliwa Jengo la kibiashara la Westagte ambapo watu zaidi ya 67 waliuliwa, imedaiwa kuwa maofisa wa serikali wamekuwa wakipanga mkakati wa kuwapoteza vijana na Masheikh ambapo katika orodha yao, imebainika kuwemo majina ya Sheikh Ibrahim na Abu Bakar Makaburi. Imeelezwa kwamba siku mbili kabla ya Sheikh Rogo na wenzake kufikwa n a m a u t i , u l i e n e z wa uvumi katika mji wa Mombasa kuwa Abu Bakar M a k a b u r i a m e u l i wa , jambo lililowatia hofu Waislamu wa eneo hilo. Pamoja na kuuliwa Sheikh Ibrahim Rogo na wenzake watatu, habari zinaarifu kwamba mtu a n a y e c h u n g u z wa n a kufuatiliwa kwa karibu zaidi na maofisa hao wa kupambana na Ugaidi, ni Abu Bakar Makaburi na kwamba, mpango uko mezani na utatekelezwa wakati wowote.
Habari
AN-NUUR
Kwa upande wao, Waislam wa Mombasa wameeleza kuwa Serikali ya Kenya imeamua kuwaua baada ya kushindwa vita vyao na Somalia. A wa l i P o l i s i K e n ya ilitangaza kuwa, watu wanne akiwemo Sheikh Ibrahim Ismail Rogo, wa m e u a wa u s i k u wa Alhamisi Octoba 3, baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana wakiwa ndani ya gari dogo mjini Mombasa. Taarifa ya Polisi ya Kenya imeeleza kuwa, Sheikh Ibrahim Rogo alikuwa mrithi wa Sheikh Aboud Rogo, ambaye naye aliuawa pamoja na familia yake kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana mwezi Agosti 2012. Mauaji ya Sheikh Ibrahim Rogo ambayo yameutikisa mji wa Mombasa, ya m e t o k e a b a a d a ya kupita takriban wiki mbili tangu kutokea uvamizi wa maduka ya Westgate jijini Nairobi, uliodaiwa kufanywa al Shabab au al Qaeda ambapo watu wasiopungua 63 waliuliwa na wengine kujeruhiwa. Polisi wamesema k u wa m u h u b i r i h u y o alikuwa amehubiri katika m s i k i t i u l i o h u s i s h wa na wanamgambo wa Kiisilamu wa Al Shabaab. Baadhi ya wananchi wa Mombasa wanakituhumu kikosi maalumu cha kupambana na ugaidi kuwa ndicho kilichotekeleza mauaji hayo. Sheikh Ibrahim Rogo, ambaye alikuwa akitoa mihadhara kwenye Msikiti wa Musa mjini Mombasa, alituhumiwa na jeshi la polisi kuwa anawachochea vijana wa Kiislamu kujitumbukiza kwenye makundi ya kigaidi. Polisi ya Kenya imesema kuwa, Gaddafi Mohammad, Issa Abdallah na Omar Abu Rumeisa ni miongoni mwa waliouawa, huku Salim Aboud akinusurika katika shambulio hilo. Sheikh Ibrahim Rogo, alikuwa muhubiri katika msikiti aliokuwa akihubiri k a k a ya k e m a r e h e m u Sheikh Aboud Rogo, ambaye pia aliuawa kwa kupigwa risasi mwaka jana. Vyombo vya usalama Kenya vimekuwa vikimshutumu Sheikh Rogo kuwa anatoa mafunzo yanayodaiwa kuwa ni yenye itikadi kali, ambayo yanadaiwa k u wa s h a w i s h i v i j a n a kujiunga na makundi ya kigaidi kama Al Shabaab.
mbalimbali vya habari, S h e i k h R o g o a l i k u wa ameliarifu jeshi la polisi nchini Kenya, Julai 24, 2 0 0 2 k wa m b a m a i s h a yake yalikuwa hatarini na kwamba alihitaji ulinzi. Ripoti hiyo aliiwasilisha pia kwenye Kamisheni ya Haki za Binaadamu ya Kenya na pia mahakama ya nchi hiyo. Kwenye taasisi hizo zote, Sheikh Rogo aliripoti kwamba, watu waliojidai kuwa polisi walikuwa wa m e j a r i b u k u m t e k a nyara yeye na mwenzake, Abubakar Sharif Ahmed. Hata hivyo kilisababisha mauaji ya Sheikh Aboud Rogo, hakijajulikana hadi leo wala wahusika kukamatwa. Lakini mashirika ya haki za binadamu ya ndani na nje ya Kenya yaliinyoshea vidole mamlaka za Kenya, kwamba hata kama hazihusiki moja kwa moja, bado zina wajibu wa moja kwa moja wa kuwalinda raia wake, na katika hili kufanya uchunguzi wa kina. Wa z i r i M k u u w a wakati huo, Raila Odinga alilitolea maelezo jambo hilo, akisema kwamba waliofanya mauaji hayo ni maadui wa Kenya ambao wanataka kuiingiza nchi hiyo kwenye mapambano ya kidini. Kufuatia mauaji hayo, Al-Amin Kimathi, Mwenyekiti wa Jukwaa la Waislamu la Haki za Binaadamu nchini Kenya, alisema hana sababu ya kuiamini serikali kwani si mara moja wala mbili mauaji kama haya kutokea na wala hakukuwa na hatua zilizochukuliwa. Kenya ilipeleka wanajeshi wake nchini S o m a l i a m wa k a j a n a , kwa lengo la kupambana na wanamgambo wa alShabaab, ambao Kenya inawatuhumu kwa kufanya mashambulizi ndani ya ardhi yake, ikiwemo pia utekaji nyara wageni na wafanyakazi wa mashirika ya misaada. Lakini Ben Rawlence wa shirika la kutetea haki za binaadamu la Human R i g h t s Wa t c h , h a o n i uhusiano wa moja kwa moja wa sura hizi mbili za kupambana na ugaidi. "Siwezi kusema kwamba Kenya inafuata mtindo huo wa Marekani. Hata Marekani yenyewe haiwezi kumuua raia wake nchini mwake. Na sisi hatuwezi k u j u a k u wa n i k we l i serikali imehusika, lakini mahakama na sheria za Kenya zipo. Mtuhumiwa anapaswa
kupelekwa mahakamani na kuhukumiwa kisheria. Si kuuawa mitaani." Alisema Bw. Rawlence. Kwa mujibu wa taarfa ya Jukwaa la Haki za Binaadamu kwa Waislamu, m n a m o m we z i M a c h i mwaka 2002, mhadhiri mwengine wa Kiislamu, Samir Khan, aliyekuwa pia akikabiliwa na mashitaka ya kuwa na silaha kinyume na sheria na kutoa mafunzo kwa ajili ya al-Shabaab, na rafiki yake Mohammed Qassim, walitolewa kwenye basi mjini Mombasa na watu waliojitambulisha kama polisi. Mwili wa Khan ulikuja kugundulika siku kadhaa baadaye katika mbuga ya Tsavo, ukiwa umekatwakatwa vibaya huku hatima ya Kassim ikiwa hadi sasa haijuilikani. Kwa mujibu wa Human Rights Watch, mwanzoni Polisi ya Kenya ilikuwa imewaambia waandishi wa habari kuwa Khan alikuwa ameshikiliwa na Kikosi Maalum cha Kupambana na Ugaidi, lakini baadaye wakakana kumshikilia. Mara kadhaa, wakili wa Sheikh Rogo, Mbugua Mureithi, alikuwa amesema mteja wake alilalamikia kufuatwafuatwa na polisi, na hata kumtaja afisa mmoja wa polisi ambaye alimtishia kwamba wao, polisi, wangelitafuta njia ya kumalizana naye. Al-Amin Kimathi, ambaye mwenyewe si mgeni wa kutiwa misukosuko na polisi, anasema kwamba hayo hayashangazi. Wakati Wakenya na dunia wakisubiri majibu kwa mauaji dhidi ya Sheikh Aboud Rogo na machafuko ya l i y o t o k e a b a a d a ya hapo, majibu ya kutekwa na hatimaye kutoweka kwa akina Samir Hashim Khan, Mohamed Bakhit Qassim, Sylvester Opiyo, Jacob Musyoka, Jeremiah Onyango Okumu, Stephen Mwanzia Osaka, Omar Shaib na Salim Abubakar ndani ya kipindi hicho cha mwaka mmoja, bado hayajapatikana. Kwa mujibu wa Jukwaa la Haki za Binaadamu la Waislamu nchini Kenya, matukio yote hayo yaliripotiwa kwenye vyombo vya dola. Katika mazingira yale yale, kauliwa kaka yake Aboud Rogo, Sheikh Ibrahim Omar Rogo na wenzake watatu. Mauaji ya Sheikh Ibrahim Rogo na vijana wengine watatu wa Kiislamu, ni i s h a r a t o s h a k wa m b a maisha ya walinganiaji wa Kiislamu yamo hatarini kwa mgongo wa lugha ya ugaidi, al shabab na al Qaeda.
4
Inatoka Uk. 1 hiyo? Au mazingira haya yanalingana na mafunzo ya Al-qaid au kijeshi ? Kuliko kukurupuka bila kupata maelezo ya upande wa pili wa jambo lenyewe, zaidi huishia kuwatisha wananchi tu. Hali imekuwa ya wasiwasi huku polisi wakimwagwa katika baadhi ya vijiji Wilayani N a n y u m b u b a a d a ya kuripotiwa kuwepo kwa magaidi wa Al Qaida. Taarifa zinasema, askari wamekuwa ni wengi na wanawapa tabu wananchi hasa Waislamu. Mashuhuda wanasema kuwa askari wamemwaga kila sehemu, katika mji huo na zaidi wamekuwa wakiwaandama Waislamu haswa wale wenye kajipamba na zile sifa za Kiislamu, huangaliwa ama kudhaniwa ni adui hivyo wanakuwa ni watu wa kupata misukosuko ya ajabu kwa kuwatuhumu ugaidi. Katika hali hiyo, baadhi ya viopngozi wa Dini ya Kiislamu Mkoani Mtwara, wamelaani taarifa ya Jeshi la Polisi na kushabikiwa na vyombo vya habari kuhusiana na vijana 11 kuwa walikuwa mafichoni wakipata mafunzo ya kijeshi. Vyombo mbalimbali vya vya habari mapema wiki hii, viliripoti taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Zelothe Stephen, kwamba wamewatia mbaroni vijana hao na kudai kuwa walikuwa wakipata mafunzo ya kijeshi ambayo ni hatari na yakutisha. Tukio hilo limeripotiwa kutokea katika milima ya Kijiji cha Nakopi, kilichopo kati ya Wilaya za Masasi, Nanyumbu na Newala, ambapo wanadaiwa kukutwa na CD za AlShabab, mapanga mawili na Visu. Mmoja wa viongozi hao, aliyepo Wilayani Nanyumbu, alilifahamisha gazeti hili kwa njia ya simu akidai kwamba vyombo vya habari vimep ak a matope juu ya suala hili, na kwamba anadiriki kusema kuwa vimekurupuka sana kwa kule kuripoti kuwa wamekamtwa magaidi. Akavitaka vyombo v ya h a b a r i k u t o i s h i a hapo katika kulikuza na kulishabikia suala hilo na kuwatisha wananchi hususani katika eneo la tukio, zaidi akavitaka vyombo hivyo kufika eneo la tukio kufanya uchunguzi wa kina kuliko kulishwa habari na Jeshi la Polisi. Waje wawaone watu wenyewe maana itasaidia
Habari
AN-NUUR
hata kutumia akili zao tu za kuzaliwa kulinganisha n a t u h u m a h i z o k wa kujiuliza kuwa huyu kweli alikuwa na dhamira hiyo (?) au mazingira haya yanalingana na mafunzo ya Al-qaid au kijeshi (?), kuliko kukurupuka bila kupata maelezo ya upande wa pili wa jambo lenyewe, zaidi huishia kuwatisha wananchi tu. Alisema. Kiongozi huyo akielezea tukio hilo alisema, wao baada ya kusikia vijana hao wamekamatwa na taarifa zikihusisha tukio hilo na Uislamu, waliwasiliana na baadhi ya Polisi wa kituo cha Nangaka, kama pia waliwakamata na silaha za moto, lakini akadai kwamba walijibu kuwa hawakuwakuta nazo. N i k a wa h o j i , k a m a silaha za moto hawakuwa nazo, sasa kosa lao ni lipi, ili hali pia ni wakazi wa huko huko Likokona, alinijibu kuwa hayo yote yanaendelea kuchunguzwa, kwa kuwa taarifa zao wamezipata kupitia uongozi wa kijijini kwao. Alisema kiongozi huyo. Alisema, vijana hao wamekuwa na shughuli zao za mazoezi ya mwili kila siku katika utaratibu wao waliojiwekea, lakini alidai taarifa zao zilivyoripotiwa zimegubikwa na propaganada zaidi kuliko uhalisia wa jambo lenyewe na haswa baada ya kunaswa na vyombo vya habari. Alisema, hali hiyo hawajakutwa na silaha za moto zaidi ya kuwa na panga na visu, ambavyo vitu hivyo si kosa kuwa navyo hususani kwa watu wa vijijini, kwani ndiyo vitendea kazi vikubwa katika shughuli zao. K wa u p a n d e wa k e Naibu Amir wa Jumuiya moja ya Kiislamu Mkoani humo, alisema, hajafika eneo la tukio lakini kwa m u j i b u wa m wa l i m u mmoja wa Shule ya msingi aliyeko katika Kijiji hicho, alimueleza kuwa, vijana hao walikamatwa na kufanyiwa mahojiano ya kawaida na Polisi kujiridhisha na ndio maana walipewa dhamana, kulingana na wepesi wa tuhuma zenyewe. Mwalimu huyo, alimueleza Amir huyo kuwa kadhia hiyo, ni ya wiki moja iliyopita wala si ya wiki hii kama umma
kama lilivyoripotiwa. Kilisema chanzo chetu kwa mshangao. Taarifa hizo zilieleza kuwa baada ya taarifa hizo kupitia vyombo vya habari, zilipatikana taarifa kuwa vijana hao wanatakiwa wakamatwe tena, jambo ambalo lilitekelezwa na vijana hao walikamatwa siku hiyo hiyo. Leo asubuhi (Jumatano) nilifika katika kituo hicho cha Polisi, nimekutana na ndugu wa vijana hao ambao walitokea huko Kijijni, ambao walikuwa wanafuatilia ndugu zao na kuthibitisha kweli walikamatwa na kwamba wapo ndani. Niliporudi kuwaandalia chai ili tuwapelekee pale, niliona gari za Polisi, zikiongozana moja likiwa na jamaa zetu wakiondoka nao, huku nyuma wakifuatiwa na gari ya Kamanda wa Polisi Mkoa (RPC). Kilieleza chanzo chetu cha habari. Chanzo hicho kilieza kwamba vijana hao wamechukuliwa ingawa wapo nje kwa dhamana huku sababu za msingi zikiwa hazieleweki kufutia hatua hiyo. Kufutia hatua ya kukamatwa tena vijana hao na Jeshi la Polisi, mpashaji wetu habari alisema kwamba hadhani kuwa watuhumiwa hao walivunja mashariti ya d h a m a n a , p a m o j a na kwamba hajayajua, ndio maana walipoenda kukamatwa waliwakuta katika makazi yao hapo Kijijini. Naye Ustadhi Pwirila, aliye makazi Wi l a ya n i N a n y u m b u , akizungumzia tukio hilo, aliitaka Serikali kuwa makini pindi wanapopata taarifa za aina yoyote, k wa n i a l i d a i e n d a p o watakuwa wanazichukua kwa kukurupuka bila kuzifanyia kazi, wanaweza wakawa wanawatesa watu bila kuwa na hatia yoyote. Alisema, kutokana na Jeshi la Polisi kuwakamata vijana hao kwa mara ya kwanza na kuwahoji kisha kuwafikisha Mahakamani, wa l i s h a r i d h i k a k u wa wa n a st a hi l i dhama na kulingana na tuhuma wanazowatuhumu nazo. Lakini akasema, kitendo cha kuwakamata t e n a b a a d a ya s u a l a hili kuripotiwa kupitia vyombo vya habari na kuonekana kubwa na zito kuliko uhalisia wenyewe,
wamechukua jukumu la kuwakamata tena. Huu ni uonevu wa dhahiri unaofanyika dhidi ya Waislamu, na pengine Serikali yetu inafanya kazi kwa kuongozwa na vyombo vya habari kwani suala hili walivyorilipoti limestua zaidi kuliko ambavyo lilikuwa halijaripotiwa. Alisema. Ama kuhusu Jeshi la Polisi, Ust. Pwirila, alisema linapaswa pia kuwa makini kwa sababu wanapokamata watu kwa tuhuma wawe wepesi kuwafikisha katika m i k o n d o m i n g i n e ya sheria ili waweza kujieleza kwa mujibu wa sheria kuliko kukaa nao kwa muda mrefu. Si sahihi kuendelea k u m n g a n g a n i a mtuhumiwa kwa muda mrefu sana, upande mwingi inaonekana kama ni utesaji na kuwanyima watu haki zao na suala hili limekithiri sana kwa watuhumiwa wanapokuwa ni Waislamu. Alisema. Ust. Huyo alisema, baada ya kadhia hiyo, kuripotiwa na vyombo vya habari, askari wamekuwa ni wengi na wanawapa tabu wananchi hususan Waislamu. Alisema, askari wamemwaga kila sehemu, katika mji huo na zaidi wamekuwa wakiwaandama Waislamu haswa wale wenye kajipamba na zile sifa za Uislamu, huangaliwa ama kudhaniwa ni adui hivyo wanakuwa ni watu wa kupata misukosuko ya ajabu. Mmoja wa viongozi wa M s i k i t i Wi l a ya n i Nanyumbu, aliliambia gazeti hili kuwa, amestushwa na taarifa k u p i t i a v y o m b o v ya habari siku ya Jumanne, wiki hii pamoja na kuwa watuhumiwa hao walikuwa wapo nje kwa dhamana. Sasa inasemekana Mkuu wa Polisi wa Mkoa (RPC), ameamuru vijana wale wakamatwe tena wakati Mahakama iliwaachia kwa dhamana, hivyo mpaka sasa ( Jumatano) wapo mikononi mwa Polisi tena. Alisema kiongozi huyo. Ama kuhusu CD, wanazotuhumiwa nazo, alisema mikanda hiyo ipo kwa watu mbalimbali na pengine na wao walikuwa nayo kwa ajili ya kungalia tu huwezi kusema moja kwa moja malengo yao i l i k u wa n i k u j i f u n z a ugaidi.
Habari za Kimataifa
AN-NUUR
BALI WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry, ametetea hatua ya nchi yake ya kufanya operesheni za kijeshi katika nchi za Libya na Somalia. John Kerry ambaye hivi sasa yuko kisiwani Bali, Indonesia kwa ajili ya kushiriki katika kikao cha Jumuiya ya Kiuchumi ya Asia na Pasifiki (APEC), amedai kuwa, Marekani haitaacha kampeni zake za kupambana na makundi ya kigaidi. A i d h a Wa z i r i h u y o wa Mambo ya Nje wa Marekani amejigamba
TEHRAN MKURUGENZI wa Shirika la Atomiki la Iran (AEOI), Dk. Ali Akbar Salehi, amesema kuwa vikosi vya usalama vya Iran vimewatia mbaroni watu wanne wa l i o k u wa wa n a p a n g a njama za kufanya hujuma kwenye taasisi moja ya nyuklia humu nchini. Dk. Saleh ameongeza kuwa, wahujumu hao wanne wametambuliwa. Hata hivyo imeelezwa kuwa Mkurugenzi huyo hakutoa ufafanuzi zaidi kuhusu jambo hilo kwa sababu za kiusalama. Katika miaka ya hivi k a r i b u n i , wa n a s a ya n s i kadhaa wa nyuklia wa Iran waliwahi kuuliwa nchini
humo kutokana na njama za maadui wa taifa hilo, ukiwemo utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kushirikiana na baadhi ya vibaraka wa ndani. Hata hivyo Maafisa usalama nchini Iran wamekuwa macho wakati wote katika kulinda taasisi za nyuklia nchini humo na wamefanikiwa kuvunja njama kadhaa za kuhujumu miradi hiyo. Dk. Salehi amesema kuwa, kuna nchi hazipendi kuona kadhia ya nyuklia ya Iran inatatuliwa kwa njia za amani na hivi sasa wameongeza njama zao, baada ya kuona kuwa kuna muelekeo wa suala hilo kutatuliwa kidiplomasia.
Jumuiya na Taasisi za Kiislamu (T) Inawatangazia Waislamu wote kuwa kutakuwa na Baraza la Idd. Litakalo fanyika:- Masjidi Mtambani, uliopo Kinondoni-DSM. Siku ya Idd Mosi ya Jumatano-Tarehe 16/10/2013. Muda:- 9:00 (Saa Tisa-Alasiri). Mada mbalimbali zitawasilishwa na Masheikh (Viongozi) kuhusiana na mwenendo wa masuala ya Uislamu na Waislamu kwa ujumla. Wahi mapema Kwa niaba ya Katibu
BARAZA LA IDD
Nchi za Mashariki ya Kati na jamii ya kimataifa zina wasiwasi mkubwa kuhusu hatari ya silaha za nyuklia za utawala wa Israel. H a y o ya m e s e m wa n a mkuu wa ujumbe wa Jordan katika Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) kwenye mkutano wa kila m wa k a wa wa k a l a h u o unaoendelea mjini Vienna. Husam al Husseini amesema kuwa silaha za nyuklia za Israel zinatia wasiwasi mkubwa na kwamba utawala huo unalazimika kutia saini mkataba wa kuzuia utumiaji na usambazaji wa silaha za atomiki (NPT). Al Husseini amesisitiza kuwa, maghala ya silaha za nyuklia za Israel yanapaswa kuwekwa chini ya usimamizi wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki na kusema kuwa, kujiunga Israel na mkataba wa NPT kunaweza kuimarisha amani Mashariki ya Kati na kuzihamasisha nchi mbalimbali zielekeze juhudi zao kwenye masuala ya ustawi na maendeleo badala ya k u t u m b u k i a k we n ye mashindano ya silaha. Mkutano wa kila mwaka wa 57 wa wakala wa IAEA ulianza kazi zake Jumatatu iliyopita na utamalizika kesho katika makao ya Umoja wa Mataifa mjini Vienna. Novemba 2011, taarifa ziliripoti juu ya kuongezeka jitihada za Israel za kuzalisha na kujirundikia silaha za kijeshi za nyuklia. Hii ni katika hali ambayo, fikra za walio wengi duniani zinahofia hatua hizo za Israel za kuzalisha kwa wingi silaha za nyuklia na kemikali, silaha ambazo kivitendo z i m e b a d i l i s h a Pa l e s t i n a inayokaliwa kwa mabavu kuwa ghala la silaha za mauaji
inayokaliwa kwa mabavu na nchi ya Misri na kwamba, kinajengwa kwa msaada wa madola ya Magharibi. Pia hivi karibuni ilifichuliwa kwamb a Israel imeanza kujenga kiwanda kipya cha atomiki katika eneo la an Naqab. Zaidi ya hayo mwaka huo huo 2010, Israel ilitiliana saini makubaliano mapya na Marekani ya kushirikiana katika masuala ya nyuklia. Misaada ya Marekani na madola mengine yenye silaha za nyuklia ya Magharibi kwa utawala wa Kizayuni kwa ajili ya kutengeneza silaha za nyuklia yanakiuka wazi Mkataba wa Kuzuia Uzalishaji na Usambazaji wa Silaha za Nyuklia NPT. Hii ni katika hali ambayo Israel kwa kuungwa mkono kila upande na nchi za Magharibi imekataa kutia saini mkataba wa NPT na kutoruhusu wakaguzi wa IAEA wakague viwanda vyake vya nyuklia. Hatua za Israel, Marekani na nchi nyinginezo zinazomiliki silaha za nyuklia za kuzidi kuzalisha silaha hizo, zinakiuka Mkataba wa NPT na kupingana na makubaliano ya upokonyaji silaha ya kimataifa. Makubaliano ya upokonyaji silaha yanazitaka nchi zote zenye kumiliki silaha hizo kutekeleza ahadi zao za kutokomeza kikamilifu silaha za atomiki kwa njia za wazi, kutodanganya katika ahadi hizo na kuharakisha mwenendo huo wa kimataifa. Hata hivyo dola hizo zimeendelea kuzalisha silaha za nyuklia huku yakihatarisha amani ya ulimwengu, huku zikipiga propaganda za kuzisakama nchi za Korea Kaskazini, Irani, na sasa Syria.
6
Na Omar Msangi KATIKA taarifa ya habari ya TBC1 saa mbili usiku juzi Jumanne, kulikuwa na taarifa za mambo ya ugaidi na Marekani. Taarifa ilikuwa ikieleza k a u l i y a Wa z i r i w a Mambo ya Nje, John Kerry kwamba ilikuwa halali kwa Marekani kumvizia na kumkamata mtuhumiwa wa ugaidi ndani ya Tripoli, Libya na kutoweka naye. Taarifa hiyo ilihusu lile tukio la Jumamosi iliyopita ambapo Kikosi Maalum cha Marekani kilichopo ndani ya Libya kilimkamata Nazih AbdulHamed al Ruqai, maarufu kwa jina Abu Anas al Libi. Marekani inamtuhumu mtu huyo kuwa ni al Qaida. Lakini wakati Kerry akisema hayo, Serikali ya Libya inasema kuwa huo ni sawa na utekaji nyara na kwamba hiyo ni sawa na kuidhalilisha Libya, kwamba jeshi la nje linaingia na kukamata watu ndani ya nchi huru kana kwamba hakuna Serikali. Katika kusherehesha taarifa hiyo, zilitolewa picha za video zikiwaonyesha Waislamu wakiwa katika s wa l a . Wa m e s i m a m a , wakirukuu na kusujudu huku wengine wakiwa wameshikilia bunduki. Hapana shaka habari na picha zile kilichokusudiwa kuonyeshwa ni kuwa hao wanaorukuu na kusujudu, ndio magaidi. Mtu unajiuliza, habari zinamhusu Abu Anas al Libi, kwa nini haoneshwi huyo Libi ikatosha, wanaonyeshwa na Waislamu wakiswali? Halafu wanaunganishwa na wengine waliofunika nyuso zao wakiwa na bunduki ambao mara nyingi picha hutolewa na kudaiwa kuwa hao ndio Al Shabaab. Kama ni kujenga habari ya Anas al- Libi, basi labda ingeelezwa kuwa hawa Marekani inaodai kuwa ni magaidi, ndio hao iliokuwa ikishirikiana nao na kuwapa silaha na kila aina ya msaada katika kumpiga na kumngoa Gadhafi. Wanajuana! Habari hizo za TBC zinakuja siku ambayo asubuhi yake, takribani magazeti yote yalizungumzia kukamatwa kwa vijana 11 waliodaiwa kuchukua mafunzo ya ugaidi msituni huko mkoani Mtwara.
Makala
AN-NUUR
Salam za Elbaradei
MOHAMED Elbaradei ameandika kitabu chake alichokipa jina: The Age Of Deception: Nuclear Diplomacy in Treacherous Times. Katika sehemu moja ya utangulzi wa kitabu hicho anasema, kila mara huwa anapitia ushahidi wao juu ya Silaha za Maangamzi Iraq, na kwamba hazipitii bila ya kutafakari juu ya maelfu ya askari na mamia ya maelfu ya raia wasio na hatia waliouliwa, mamilioni kutiwa vilema, kuharibiwa makazi yao na kuwa wakimbizi na nchi kuvurugwa kabisa. Anasema, anayatafakari haya kwa sababu, vita ya Iraq 2003, haikuwa na
cha kigaidi na mhariri anashangaa ni kwa nini mpaka sasa serikali haijachukua hatua. Kwa hiyo katika kuikumbusha serikali, mhariri wa RAI anasema: Wito wetu kwa Serikali ni kwamba, inapaswa s a s a k u z i n d u k a k wa kuhakikisha inazichukulia kwa uzito unaostahili t a a r i f a z o z o t e z e n ye mwelekeo wa kigaidi au kuhatarisha amani, b a d a l a ya k u z i p u u z a kama ambavyo imekuwa ikitokea.
Nazih Abdul-Hamed al Ruqai, maarufu kwa jina Abu Anas al Libi. Vijana 11 wanaswa wakijifunza ugaidi. Vijana wabambwa wakijinoa kijeshi: Walikuwa na CD za Al-Shabab. Hivyo ni baadhi ya vichwa vya habari magazeti ya Jumanne. Gazeti la Rai lenyewe liliandika: Wafuasi 11 wa Al Qaida watiwa mbaroni Mtwara.Watumia mapanga, video za Osama bin Laden kujifua. Katika para ya kwanza gazeti hilo linasema: Jeshi la Polisi mkoani Mtwara, linawashikilia watu 11 kwa tuhuma za kukutwa msituni wakifanya mazoezi ya kijeshi. Pamoja na mengi yaliyoelezwa, lakini moja muhimu kuliko yote ni kuwa: Vijana hao walikutwa na vitabu vya Kiislamu. RAI likaendeleza habari hiyo kwa tahariri ya gazeti lake la Jumatano ambapo lilisema: Serikali isipuuze taarifa za ugaidi. Katika maelezo yake likasema, Jana vyombo vya habari nchini, vilitawaliwa na habari kubwa iliyokuwa ikieleza kunaswa kwa vijana 11 waliokuwa wanafanya mazoezi ya kivita msituni kwa kutumia video za makundi ya kigaidi. Vijana hao wanatajwa kuwa wakazi wa Nanyumbu, mkoani Mtwara na walikamatwa na polisi wakifanya mazoezi kwa kutumia CD za kundi la kigaidi la Al Shabaab na Al Qaida. Likiendelea Rai l i n a s e m a , : Ta a r i f a hizi ni za kushtusha na zinatusukuma sisi wa RAI Jumatano kuamini kuwa taifa letu sasa linakabiliwa na tishio kubwa la vikundi vya kigaidi. Kisha linasema, Kukamatwa kwa vijana hao kunaturejesha miezi michache nyuma, ambapo gazeti Dada la Mtanzania Jumatano liliripoti habari ya c h u o k i m o j a ( c h a Kiislamu kwa jina la Al Jazeera) kilichoko wilayani Ukerewe ambacho
sababu. Ilikuwa ni uvamizi na uhalifu wa wazi kwa sababu Tume iliyopewa kazi na Umoja wa Mataifa kutizama madai kuwa Iraq ina silaha za maangamizi ilionyesha kuwa hakuna silaha hizo. Lakini Marekani kwa ubabe wake ikavamia tu na kupiga bila hata ya idhini ya Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa. Elbaradei alikuwa ndiye Mkurugenzi Mkuu wa International Atomic Energy Agency (IAEA) toka 1997 hadi 2009 na n d i o wa l i o p e wa k a z i ya kutizama madai ya Marekani kuwa Saddam Husein alikuwa na silaha za maangamzi (WMD).
MOHAMED Elbaradei.
Makala
kwenye kiwanda cha silaha zenyewe na kuhakiki. Kwa upande mwingine anasema, taarifa za kuwa Saddam ameagiza madini ya Uranium kutoka Niger, zilipigiwa sana debe na Marekani na Uingereza ambapo Rais George W Bush katika hotuba yake kwa taifa Januari 2003 alisema: The British government has learned that Saddam Hussein recently sought significant quantities of uranium from Africa. Kufuatia madai hayo, Elbaradei anasema walitaka serikali ya Uingereza iwape taarifa zao za ki-intelijensia ili wazifuatilie kuthibitisha jambo hilo. Anasema baada ya kudai sana walipewa nyaraka mbili ambazo hata hivyo waligundua kuwa zote ni za kughushi. Moja ilidaiwa kuwa ni barua ya Rais wa Niger Mamadou Tandja kwenda kwa Saddam. Lakini saini i l i k u wa ya k u g h u s h i na mambo mengine ya uwongo yalikuwa ndani yake. Nyaraka ya pili ilikuwa barua ya Oktoba 2000 kutoka kwa Waziri wa Mambo Nje ya Niger ikiwa na saini ya Allele Habibou. Walioghushi barua hiyo walisahau kuwa Habibou hajawahi kushika nafasi Serikalini toka mwaka 1989. Pennsylvania Ave NW, Wa s h i n g t o n , D . C . n a Downing Street, London, kwamba Saddam ana silaha za maangamzi. Anasema Elbaradei, hata walivyotoa nyaraka za kuonesha jinsi barua za Niger kwenda kwa Saddam juu ya uranium zilivyoghushiwa, vyombo v ya h a b a r i v i l i p u u z a habari hizo. D e s p i te th e on -th e ground knowledge of the UN inspectorate, we were losing the battle of information, in the Western press, and to some extent in the public eye. IAEA and UNMOVIC statements were being discounted, or
AN-NUUR
Ushahidi wa kughushi
KATIKA maelezo yake ndani ya kitabu chake, Ebaradei anasifia wanasayansi ya nyukilia na fisikia kwa ujumla waliokuwa katika Wakala huo wakiwemo kutoka Ufaransa na Marekani kwenyewe na kwamba walifanya kazi kubwa ya kuchunguza sehemu zote ambazo zilikuwa zikidhaniwa kuwa zina silaha ikiwa ni pamoja na zile walizopewa habari zake kupitia mashirika ya kijasusi ya Marekani na NATO. Hata hivyo anasema hawakuona kitu. Lakini pamoja na hayo anasema Marekani ilikuwa ikishikilia kuwa Saddam ana silaha za maangamzi na walipotaka ushahidi wa k a a m b i wa m a m b o mawili: Moja anasema Marekani lidai kuwa vyombo vyake vya kijasusi vina taarifa ya k u p a t i k a n a v i f a a fulani (tubes za bati) zinazoweza kutumika kutengenezea silaha hizo. Na pili ni taarifa kuwa Saddam Hussein alinunua madini ya Uranium kutoka Niger. Mohamed Elbaradei anasema walifuatilia madai hayo na walichogundua ni kuwa tubes zile za bati (aluminium tubes) zilikuwa za kutengenezea roketi za kawaida na walikwenda mpaka
JUZI Jumanne wakati napitia kurasa za kitabu hiki cha Elbaradei nikakumbuka tena kile kisa cha Fake BBC Video. Bado mgogoro wa Syria unazidi kutokota. Na baada ya Marekani kukwama katika namna nyingi, ilikuja na hoja kuwa Serikali ya Syria inatumia silaha za sumu katika kupambana na wapinzani. Moja ya vyombo vya habari ambacho akina
S a s a k a m a inavyoonyesha timu hii ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa juu ya masuala ya nguvu na silaha za nyukilia, IAEA, wanaonyesha hayo magazeti yanayodaiwa kuwa ya kuheshimika kwamba jamani barua inayodaiwa kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje ya Niger Allele Habibou ya Oktoba 2000 ni ya kughushi kwa sababu huyu Allele si Waziri kutoka mwaka 1989, hawasikilizi, wao wameshikilia lile l i l e wa l i l oa m b i wa na Washington kuwa Saddam kaandikiwa barua na Allele ya kupewa Uranium. Na nani kasema hivyo, Blair!
kwamba ndio jeraha baya na lenye maumivu makali zaidi kuliko jeraha lolote linalotambulika duniani. Kwa hiyo haiwezi kuwa akinamama na watoto wanaodaiwa kuwa wana majeraha ya kuunguzwa na napalm halafu wamekaa wametulizana wakimtizama mpiga picha anavyowarekodi huku wanaongea bila wasiwasi. Footage of genuine napalm victims would likely be far too horrific and
Samantha KILICHOWASHANGAZA wajumbe wa IAEA ni kuwa pamoja na ushahidi walitoa kuwa nyaraka zote hizo zilikuwa za kughushi, lakini waliokuwa wamepania kufanya vita waliendelea kushikilia msimamo wao. Lakini kilichowatisha z a i d i n i v y o m b o v ya habari. Kadiri IAEA ilivyojitahidi kutoa taarifa za kiuchunguzi zenye ushahidi na uthibitisho wa uhakika, vyombo vya habari viliendelea kupiga tarumbeta kutoka 1600
yahe huku ndio wanasema kuwa ni vya kuheshimika sana, BBC, Agosti 29, 2013 ikaja na mkanda wa Video (documentary) inayoonyesha lililodaiwa shambulio la silaha za s u m u k a t i k a m j i wa Aleppo. I n a o n y e s h wa k u n a z a h a m a k u b wa wa t u wanaoneshwa wana majeraha ya kuungua huku wakipiga kelele. Dakitari naye, ambaye ni Dr. Rola, anapaza sauti akidai kuwa anapokea majeruhi wengi wakionekana kuunguzwa na silaha za sumu. Its just absolute chaos
world-23892594) Hata hivyo, haukupita muda, barua, simu na makala mbalimbali zimeandikwa kuchambua tukio hilo kuonesha kuwa ilikuwa mchezo wa kuigiza (fabrication.) Waliohusika na kuandaa kipindi hicho ambacho sasa kinaonekana kuwa ni igizo, Ian Pannell na D a r r e n C o n wa y ( B B C cameraman), wanaambiwa na wataalamu wa silaha z a s u m u k u wa s u m u ya napalm huunguza na k u t o a j o t o ( m o t o ) unaofikia nyuzi joto 800 mpaka 1,200 (Celsius) na
distressing to broadcast and to describe the alleged injuries depicted in these scenes as napalm-like is an insult to those who have suffered the reality. Anayesema maneno haya amejitambulisha kwa jina la Robert akiwa mmoja wa watu walioiandikia BBC kulalamika kuwa wanaonyesha habari za kutunga na anawaambia kudai kuwa watu walioonyeshwa katika kipindi chao wana majeraha ya napalm, ni sawa na kuwatukana na kuwakejeli watu Inaendelea Uk. 8
Makala
magodoro nao vipi?, Umeporomoshaje jengo? Nani kalipua wakati ilishaambiwa magaidi wameondoka? Na tangu lini moto wa magodoro ukaporomosha jengo kama lililopigwa bomu zito? Hayo hutasikia wakijiuliza waandishi wetu na magazeti yetu. Sana sana utawasikia wakiandika, eti Samantha n a m a g a i d i we n z a k e walitoroka kupitia mtaro wa maji machafu ulio chini ya jengo! Wanaleta stori za yale wanayoona katika picha za Hollywood. Lakini wanaoandika habari hizo huko Marekani na Ulaya sio wajinga. Wanajua wanachokifanya. Kubwa ni kukupumbaza (age of deception) kuwa hawa magaidi al Qaida na al Shabaab, wanaorukuu na kusujudu, ni hatari sana. Ni makomandoo ambao kupambana nao ni kazi kweli! Kwa sisi huku tunaiga na kukariri tu. Zaidi ni ujinga na kuwa na akili ya kushikiwa. MHARIRI wa RAI anahimiza Serikali k u wa c h u k u l i a h a t u a watuhumiwa wa ugaidi ikiwa ni pamoja na vyuo vya Kiislamu anavyodai v i n a t o a m a f u n z o ya kigaidi. Lakini jingine linaloandamana na hilo, ni hii hali inayooekana hivi sasa ambapo ukifika mahali kama pale Mlimani City au kuingia mpirani Uwanja wa Taifa, unakuta upekuzi mkubwa. Wanapekuwa asije akapita Al Shabaab na silaha!!! Kama tunaamini kuwa Samantha na wanaodaiwa kuwa ni magaidi wenzake, waliweza kuingia Kenya wakaingiza lundo la silaha ndani ya Westgate Mall na kuondoka baada ya shambulio, basi ambalo ni la uhakika ni kuwa hakuna Polisi, mgambo, jeshi au Usalama wa Taifa wanaoweza kuzuiya magaidi wa namna hiyo. We ukipekuwa watu Mlimani City na Uwanja wa Taifa, wao wanapiga na kuuwa watu Soko la Tandika. Ukilinda Soko la Kisutu (Soko Mjinga), wao wanapiga Soko Matola Mbeya au huko Newala! Na wakifanya hivyo, utasikia Twitter imesema wanaohusika ni Al Shabaab tawi la Tanzania. Magazeti yetu yatapiga tarumbeta na kwa ujinga, tutaamini. Wala hatutajiuliza, Twitter ni nani katika zama hizi za electronic/digitali. Mtu anakwambia Twitter ya Al Qaida imesema wanahusika unaamini. Sasa katika upumbafu wa kiwango hiki, hatutasalimika. Tu k i o l a v i j a n a kukamatwa Mtwara, lilitokea kiasi wiki moja iliyopita. Vi j a n a wa k a f i k i s h wa mahakamani wakapewa dhamana. Lakini lilivyoripotiwa juzi ni kana kwamba ndio kwanza linatokea. Ndio polisi wakaenda na kuwakamata tena na kuwaweka ndani. Na walikutwa kijijini wakiendelea na shguli zao kama kawaida. Si watu waliojificha kama wahalifu. Labda la kusema hapa kwa Waislamu ni hili: Hizi ni zama za Deception. Jambo la uwongo linapigiwa zumari mpaka linaonekana kuwa kama kweli. Iraq imeangamizwa kwa mtindo huo. Hivi sasa Syria inasukiwa kitanzi. Vyombo vya habari vinatoa taarifa za kutunga. Stand By, Camera
AN-NUUR
Inatoka Uk. 7
Hatari ya uwongo
KATIKA Quran ipo aya inasema: Kama fasiki akikujieni na habari (yoyote ile msimkubalie tu), bali pelelezeni (kwanza) msije mkawadhuru watu kwa ujahili na mkawa wenye kujuta juu ya yale mliyoyatenda. (49:6) Ili kuelewa vizuri somo la aya hii, sikiliza habari hii. It turns out we were all wrong. Mohamed Elbaradei anamnukuu David Kay akitoa taarifa yake kwa Kamati ya Kijeshi ya Seneti (U.S. Senate Armed Services Committee), kwamba wote katika Marekani walisema uwongo juu ya Saddam Hussein. Anamnukuu pia Makamo wa Rais Dick C h e n e y a k i h o j i wa n a MSNBC katika kipindi Meet the Press ambapo anasema: We never had any evidence that (Saddam Hussein) had acquired a nuclear weapon. Lakini Elbaradei anasema hiyo ni Septemba 2003 na Januari 2004 wakati huo Iraq ishavamiwa maelfu kwa mamilioni ya watu washauliwa,
waliopatwa na msiba wa kweli wa kushambuliwa na sumu hiyo wakati wa vita ya Vietnam. Sasa kwa watu ambao akili zao na mawazo yao ni kuwa hawa BBC na Daily Mail ndio vyombo vya kuheshimika, haishangazi leo kuona kuwa hakuna wanachojiuliza: Inakuwaje mwanamke Samantha, atoke Mogadishu aingie nchi ya watu na lori la silaha, nchi yenye Usalama wa Taifa, yenye polisi na jeshi mpaka ateke Westgate Mall, lenye walinzi masaa 24 na kamera za ulinzi!. Na akimaliza shambulio atoroke asikamtwe huku jengo zima limezingirwa na Jeshi la Kenya! Wala hatajiuliza, hivi hawa watu wanaodaiwa kupigwa risasi mgongoni, mguuni na tumboni, mbona wanatembea wenyewe? Mbona picha haziwaoneshi hao magaidi wakivamia na kukata watu mikono au kuwapiga risasi? Na ule moto wa
John Rambo rolling, action Watu wanapigwa picha wakiwa na majeraha bandia ikidaiwa ni ya silaha za sumu. Huku kwetu napo inaonekana wana hamu s a n a ya k u p a n d i k i z a kitisho cha ugaidi. Zipo kanda nyingi zimetengenezwa kama zile zilizoonyeshwa na TBC katika taarifa ya habari wakionyeshwa watu wanaswali huku wana bunduki na unaambiwa kuwa hawa ni Al Qaida au Al Shabaab. Wa l i o z i t e n g e z e a na kuziingiza katika mtandao, wanajua wapo vijana watazi-down load, kuzirudufu na kufanya biashara. Wa n a j u a p i a k u wa wapo vijana wa Kiislamu wa t a z i p e n d a . L a k i n i wanajua pia kuwa P o l i s i wa m e a n d a l i wa kutafuta vitu kama h i v y o . Wa k i k a m a t wa nazo, vyombo vya habari vitadaka Vijana 11 wa Al Qaida wakamatwa Mtwara. Vitaandika. Swali ni je, kujifunza kareti, mpaka uwe na kanda hizo zinazodaiwa kuwa za al Shabaab na al Qaida? Kama shida yako ni kujua kareti au kuwa jitu lenye nguvu linalojua kupigana, tumia za John Rambo, Anold Schwarzenegger na Chuck Noris.au hata Jackie Chan. Na kujifunza kareti sio lazima uende porini. Hata nje ya nyumba yako au darasa la shule ya msingi mnafanya. Lakini mjue kuwa kama ilivyo ile Fake BBC Video. Wanaweza kupatikana vijana pia wa k a wa t o s a we n z a o . Watakuja na kuleta hoja k u wa wa o wa m e i va . Wanajiandaa na kitali au kupigana Somalia. Watataka ushiriki darasa
Chuck Noris. lao la harakati. Ujue hao ni washenga wa vita dhidi ya Uislamu. Ni maadui sawa na maadui wengine japo utawaona wanaswali na kusoma aya kali kali. Mohamed Elbaradei baada ya kufanya kazi kama Mkuu wa IAEA na kuona Iraq ilivyozuliwa uwongo, jinsi watu walivyotumika kuweka ushahidi bandia, anasema: This is The Age of Deception. Ni zama za uwongo, hadaa, udanganyifu, ulaghai, propaganda na kila wazimu. Na yote hayo hufanywa kwa sasa kwa lengo la kuwapiga vita Waislamu na kwa upande mwingine kutoa fursa kwa wababe kutawala dunia wakitawanya makucha yao katika kila kona. Vijana wa Kiislamu tumieni akili. Nyie ndio walengwa. Wale waliochezeshwa Fake BBC Video ni vijana na raia wa Syria. Basi mjue na nyinyi m t a c h e z e s h wa F a k e Mafunzo ya Al Qaida Nanyumbu. Sikilizeni, chambueni mjue lipi la kweli. Ipi propaganda. Upi udanganyifu. Muhimu zaidi, msinaswe mkajidhuru kwa mikono yenu wenyewe. Anayekwambia kaiva, mwambie akalime ajitosheleze kwa chakula na kingine atuuzie. Ajenge shule, hospitali na kutuondolea dhiki ya maji. A k i n g a a n g a n i a mazoezi ya kwenye kambi na darasa za ki-Al Shabaab zilizoko katika kanda za CD/DVD, ujue huyo ni kachero au mtu mjinga sana anayetumiwa bila ya kujijua. Na mtu mjinga muepuke. Mjinga wa kiwango hicho, mkimbie, la sivyo atakutosa.
wakionekana kuwa ni collateral damage! Uwongo umeangamiza roho za mamilioni ya watu na inavyoonekana hakuna anayejali-collateral damage. Anasema kilichokuwa k i k i t a f u t wa I r a q s i o silaha za maangamizi, demokrasia, kuondoa udikiteta au usalama wa Marekani na dunia. N i v i t a ya K i i t i k a d i iliyochanganyika na masilahi. Kwa baadhi ya watu usalama wa dunia ni pale wao wanapodhibiti rasilimali za kila mahali na kuwafanya wengine watwana wao.
Makala
AN-NUUR
(a.s.) alikuwa amesimama kuswali na kunyenyekea kwa Mola wake kwa nguvu zote, akimuomba Allah (s.w.t.) amuhifadhi na kumlinda mke wake na dhulma ya mfalme huyo. Mfalme alivutika sana na uzuri wa Bibi Sara wakati walipo kuwa faragha peke yao wao wawili tu. Ghafla alipo nyoosha mkono wake kutaka kumshika Bibi Sara, mkono wake ulipatwa na kiharusi akawa hawezi hata kuutikisa, akaingiwa na hofu kuu na kutetemeka. Akamuomba mwanamke huyo amuombee dua na papo hapo hali yake ikarejea katika ukawaida wake. Lakini mfalme huyu hakukoma na kwa mara ya pili tena akajaribu, akataka kuunyoosha mkono kwa mara nyingine lakini hali ikawa ni ile ile, hakupoa isipo kuwa baada ya dua ya m wa n a m k e m w e m a yule. Hatimaye alimgeukia mtumishi wake, akamlaumu sana na kudai kwamba huyo mwanamke aliye mleta si mwanadamu bali huyo ni shetani. Mfalme akaamrisha mwanamke huyo arejeshwe kwa mwenyewe na apewe binti katika wajakazi wa mfalme awe ni mtumishi wake. Baada ya mtihani huo, Nabii Ibrahim (a.s.) akarejea Sham akiambatana na mke wake na binti huyo aliyepewa na mfalme ambaye jina lake ni Hajara. Kwa vile Bibi Sara hakuwa amepata ujauzito kwa kipindi kirefu c h a m a i s h a ya o , j a m b o ambalo liliashiria huenda alikuwa tasa, bibi mwema huyu alimtaka mume wake amkubali binti huyo kama mke wake na amuingilie pengine akaruzukiwa mtoto kwake. Nabii Ibrahim na bibi Sara, pamoja na mjakazi wake Hajara akiwa kama mke wake wa pili, waliondoka Misri na kurejea Shamu. Baada ya kitambo kifupi, Nabii Ibrahim (a.s.) alijaaliwa kupata mtoto wa kiume kwa mke huyo wa pili mwenye asili ya Misri, akampa jina la Ismail. Huyo ndiye mtoto wa kwanza wa Nabii Ibrahim (a.s.) ambaye Allah (s.w.t.) alimsifu katika Qur-ani kwamba ni mkweli wa kutimiza ahadi, nabii na mjumbe wa Allah (s.w.t.). Kwa mujibu wa maumbile ya kila mwanamke, Bibi Sara baada ya muda alianza kuhisi tofauti katika nafsi yake. Alihisi upweke na huzuni kwa kujiona ni muda mrefu na yeye hakujaaliwa kupata mtoto, akatawaliwa na ghera hadi akawa anashindwa kumuangalia mtoto huyo na mama yake. Hapo ndipo Bibi Sara alipoamua kumshauri Nabii Ibrahim (a.s.) kumuhamisha mtoto huyo na mama yake, awaweke mbali na macho yake katika sehemu
ijenga ni Nabii Ibrahim na mwanawe huyo Ismail. Wa a r a b u w a k a b i l a la Jurhum walipo kuwa wakipita katika msafara wao wa kibiashara, waliiona sehemu hiyo na namna i l i v y o c h a n g a m k a k wa kuzungukwa na ndege, kwa sababu ya neema ya maji ya chemchem hiyo. Wakaenda mahala hapo na wakaomba ruhusa kwa Bibi Hajara ili na wao waweze kuishi hapo pamoja na wanyama wao. Jurhum waliishi hapo na Ismail akawa pamoja nao, akajifunza lugha yao na akaoa kwao. Baada ya kupita muda fulani, Nabii Ibrahim alikuja na akamkuta mwanawe Ismail tayari amesha kuwa ni kijana mwenye rika la mtu mwenye akili timamu. Akamwambia ya kwamba Allah (s.w.t.) amemuamrisha ajenge nyumba ya ibada, ambayo kwa hivi sasa ndio inayoitwa Al-Kaaba na hapo ilipo ndio Makka. Nabii Ismail (a.s.) akaijenga Al-Kaaba kwa ushirikiano wa mwanawe Ismail, baba anajenga na mtoto akimbebea mawe. Na kwa baraka hiyo Makka ikaanza kuimarika kidogo kidogo. Hii ndio mara ya kwanza nyumba hii kujengwa kama Qur-ani inavyo tueleza. Nabii Ibrahim (a.s.) baada ya kumaliza ujenzi wa nyumba hii, Allah (s.w.t.) akamuamrisha awatangazie watu Hijja kokote waliko duniani. Mara ya pili, Al-Kaaba ilijengwa kabla ya kudhihiri kwa Uislamu katika mji wa Makka, wakati Bwana Mtume (s.a.w.) akiwa bado ana umri wa miaka thelathini na tano. Kufuatia mvua kubwa iliyo nyesha katika mji wa Makka, mafuriko makubwa yaliingia katika eneo lenye AlKaaba na kuta za Al-Kaaba zilidhoofika na kupasuka. Makureishi wakakubaliana kuijenga Al-Kaaba na Bwana Mtume (s.w.a.) pia alipata
fursa ya kushiriki katika ujenzi huo. Mara ya tatu, Al-Kaaba ilijengwa tena katika kipindi cha Yazidu bin Muawiya, aliye kuwa kiongozi mkuu katika awamu ya pili ya dola ya Bani Umayya baada ya kushambuliwa na majeshi yake kutoka Sham. Yeye Ya z i d u n d i ye a l i ye t o a amri jeshi lake kumzingira Abdullah bin Zubeir (r.a.) kutokea nje ya Makka na akaishambulia Al-Kaaba hadi ikavunjika na kuungua. Baada ya mashambulizi hayo, Abdullah bin Zubeir akaijenga tena Al-Kaba n a a k a f a n ya b a a d h i ya mabadiliko humo. Mara ya nne, baada ya Abdullah Zubeir kuuawa kwa dhuluma, Abdul-Malik b i n M a r wa n ; k i o n g o z i wa Dola ya Bani Umayya k a t i k a a wa m u ya t a n o , naye huyu alifanya baadhi ya marekebisho katika AlKaaba. Lakini katika kipindi cha Dola ya Abbasiya, Harun Rashid akachukua uongozi wa dola hiyo katika awamu ya tano, na yeye alitaka kufanya mabadiliko katika ujenzi wa Al-Kaaba. Hasa katika yale marekebisho yaliyo fanywa na Abdul Malik bin Marwan na kuyarejesha katika hali yake ile ile kama yalivyo kuwa wakati wa Bwana huyo Abdul Malik bin Marwan. Lakini Imamu Malik bin Anas akamkataza na akamtaka awe na tahadhari Al-Kaaba isije ikawa ni mchezo wa wafalme baada yake na hatimaye heshima yake ikatoweka katika nyoyo za watu. Kuna kauli nyingine zinazo semwa kwamba Nabii Ibrahim (a.s.) sie wa kwanza aliye ijenga Al-Kaaba, bali Nabii Adam (a.s.) ndiye wa kwanza kuijenga Al-Kaaba. Na wengine wanasema wa kwanza kuijenga ni Shiyth mtoto wa Nabii Adam. Ukweli ni kwamba kauli hizo zipo na zimeandikwa katika baadhi ya vitabu, lakini si kauli sahihi. (abawaziri@hotmail. co.uk +255 767 215 998)
10
Nabtadi kuangaza, halisi yake launi Si mwingine mpendeza, mwalimu Pugu shuleni Isimuye kudokeza, Nyerere si jina geni Sura halisi ni hii, ya Julius Nyerere. Kila kona husifiwa, kwa sifa ziso kifani Na chapuo hupigiwa, ndani na ughaibuni Wa Mungu mteuliwa, yanadiwa hadharani Sura halisi ni hii, ya Julius Nyerere. Ya uasisi kasumba, imewalevya vichwani Huyumba huku wakimba, "mwasisi nambari 'wani' " Waimbaji mnoimba, 'wimbo' huu sikizeni Sura halisi ni hii, ya Julius Nyerere. Nyerere mkaribishwa, hilo nyote ng'amueni Na Bantu katambulishwa, kwa Abdul jijini Kisha akakutanishwa, na wa TAA waumini Sura halisi ni hii, ya Julius Nyerere. Ikawa mara ya kwanza, kutajika siasani Safari akaianza, yu chini ya waumini Nguvu hawakumtenza, kwa tofauti ya dini Sura halisi ni hii, ya Julius Nyerere. Kwa wema wakaamuru, aushike usukani Akajifanya 'jabaru, alipowekwa kitini Wema akaukufuru, kwa kugeuka mdini Sura halisi ni hii, ya Julius Nyerere. Kura tatu ikajiri, Tabora unyamwezini Ikatoka tahadhari, ya dalili za udini Udini ukadhihiri, na umma kuufitini Sura halisi ni hii, ya Julius Nyerere. Sheikh wetu Takadiri, muhanga nambari 'wani' Kisa kutoa indhari, kwa nduguze waumini Wakamsusa dahari, kisa eti yu mdini Sura halisi ni hii, ya Julius Nyerere. Likatimu lake lengo, Nyerere 'Bwana' udini Ukawa wake ulingo, na siriye mtimani Akaja kushika 'bingo', sitina moja mwakani Sura halisi ni hii, ya Julius Nyerere. Masaibu yakaanza, kuwazonga waumini Ni walewale wa kwanza, waanzilishi chamani Kikubwa kilowaponza,si kingine yao dini Sura halisi ni hii, ya Julius Nyerere. Masheikh wakakamatwa, na kutiwa gerezani Mongoni mwalokamatwa, ni Sharifu Adinani Kisha nyuma akafatwa, na Sheikh Komoriani Sura halisi ni hii, ya Julius Nyerere. Kisha Sheikh Nurdini, mwana mwema wa Husseni Akaongezwa kundini, na Sheikh Al-Amini Hata Bilali Rehani, yu hai muulizeni Sura halisi ni hii, ya Julius Nyerere. Mwisho akajakamatwa, Mufti wetu nchini Hassan yeye aitwa, Amir wake ubini, Ikawa mchana kutwa, mazonge kwa waumini Sura halisi ni hii, ya Julius Nyerere. Orodha ni ndefu sana, kuitaja shairini Lengo sio kulumbana, bali haki kubaini Yeyote anayekana, alete hoja mezani Sura halisi ni hii, ya Julius Nyerere. Mwisho nakuusieni, tarekh tuisomeni Iwe yetu ya nchini, au ya Ughaibuni Mengi tutayabaini, ya dhahiri na batini Huyo jama tambueni, n'do mwalimu Nyerere. ABUU NYAMKOMOGI MWANZA.
SHAIRI/HABARI
AN-NUUR
Mbali ya utoaji wa damu katika kitengo hicho cha ustawi wa jamii, Amirat huyo alisema pia hujihusisha na shughuli za mazishi k wa Wa i s l a m u , hususani kwa wale wanaokosa ndugu. Alisema, shughuli hizo ni za kujitolea zaidi kwa nguvu na mali za wanakikundi na hakuna muwezeshaji, zaidi ya kujitolea huku akitoa wito kwa Waislamu kwa ujumla kujitokeza kushiriki katika zoezi hilo endelevu.
WA N A F U N Z I wa kidato cha pili na wale wa kidato cha nne, wamehimizwa kujiandaa vyema na mitihani inayowakabili hivi sasa, ili waweze kufanya vizuri katika mitihani hiyo. Wito huo umetolewa na Mratibu wa Elimu ya Dini ya Kiislamu Wilaya ya Temeke, Ustadh Abubakar Shaaban, katika Msikiti wa Muuminina- Buza nje kidogo ya Jijini la Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita, kwa ajili ya wanafunzi wa Kiislamu wa kidato cha pili wanaofanya mitihani yao hivi sasa n a wa l e wa k i d a t o cha nne wanaotarajia kufanya mtihani wa Ta i f a N o v e m b a 4 mwaka huu. Nawasisitizia kuyafanyia kazi yale yote mliyofundishwa na walimu wenu kwa vitendo kwani kusoma ni ibada kama zilivyo ibada nyingine. Alitilia mkazo Ust. Shaaban. Alisema kuwa wanafunzi wa sasa ndio viongozi wa baade n a k wa m b a , k a m a hawatajengewa misingi i m a r a ya d i n i k wa wakati huu, isitarajiwe kupatikana viongozi wa baadae watakaomjua Allah (s.w) na watetezi wa dini yetu katika dunia hii na kwamba kitarajiwe kizazi kibovu katika jamii. Aidha wanafunzi hao wameaswa kuwa makini na mbinu mbalimbali za maadui wa Uislamu na Waislamu katika yanja mbalimbali, kwani mbinu hizo ni
m a m b o ya u s h a u r i alitoa nasaha zake kwa wanafunzi kwa kuwataka wasome sana kabla ya mtihani, lakini siku ya mtihani hawatakiwi kusoma kwa kukesha usiku mzima ikiwa siku inayofuata wana mitihani. Alisema hali hiyo inaweza kumsababishia m w a n a f u n z i kushindwa kwa sababu ya akili kuchoka sana na kutokukumbuka yale aliyosoma siku za nyuma. A m e w a t a k a watahiniwa hao kuswali rakaa mbili usiku wa kuamkia siku ya mtihani kumuomba Mwenyezi Mungu kuwafanyia wepesi katika mitihani yao. A i d h a a l i wa t a k a wanafunzi hao kuwa makini wanapopewa karatasi ya maswali kwa kuzisoma kwa umakini kila kipengele, kwani wa k i k o s e a k u s o m a maelezo (Instructions) kwa makini ndio m wa n z o wa k u f e l i mtihani. Mtaalamu huyo amewataka wanafunzi kutokujadili mtihani uliopita kwa kukaa vikundi vikundi na kupoteza muda badala yake wametakiwa kujiandaa na somo linalofuata. Kwa upande wake, Sheikh Mikidadi K h a l f a n a l i ye k u wa amewakilisha Baraza la Wazee wa Kiislamu Msikitini hapo, amewataka wanafunzi hao kuzifanyia kazi nasaha walizopewa na yote waliofundishwa na walimu wao ili kufanya vizuri katika mitihani ya o n a k u f a n i k i wa katika maisha yao ya baadae.
11
BARAZA LA VIJANA WA KIISLAMU
MKOA WA DAR ES SALAAM
KAMATI YA MAANDALIZI YA MKUTANO WA SEKRETARIETI (KAMATI NDOGO YA KITAIFA) TUNATOA SHUKRANI ZA DHATI KWA WALE WOTE WALIOSAIDIA KUFANYIKA KWA MKUTANO WA PILI TAREHE 26-29/09/2013 KWA MAFANIKIO MAKUBWA SANA. AIDHA TUNAWAPONGEZA WAJUMBE WOTE KUTOKA MIKOA YOTE YA TANZANIA KWA KUSHIRIKI VIZURI. IKUMBUKWE VIJANA WA KIISLAM HATUJAWAHI KUKUTANA KITAIFA MARA YA MWISHO ILIKUWA MIAKA 14 ILIYOPITA. TUNAWAKUMBUSHA WAPENDA MAENDELEO YA UISLAMU NA HARAKATI ZA VIJANA MKUTANO MKUBWA WA KITAIFA UTAKAOSHIRIKISHA VIJANA WOTE TOKA NCHI ZOTE ZA AFRIKA MASHARIKI UTAKAOFANYIKA MWANZA HAPO DISEMBAINSHAALLAH WAJUMBE KUTOKA KILA JUMUIYA ZA VIJANA KUTOKA KILA JIMBO, WILAYA NA MIKOA YA TANZANIA WAJIANDAE KWA MKUTANO HUO. TUNAWATAKIA MAANDALIZI MEMA YA MKUTANO HUO WA KIHISTORIA. WA S H I R I K I WA N AW E Z A K U P I G A N A M B A ZIFUATAZO: 0715/0756/0784/0772/822332 AU 0759 362888 AU 0713 495992 AHSANTENI SANA AMIR-KAMATI YA MAANDALIZI
Matangazo
AN-NUUR
12
AN-NUUR
MAKALA
12
AN-NUUR
katika kutekeleza majukumu ya serikali, ingawaje bado zipo changamoto katika ngazi za chini za uongozi. Amesema baadhi ya viongozi wa ngazi za chini wakiwemo masheha, bado wanahitaji taaluma zaidi katika kuufahamu muundo huo mpya wa serikali, ili kufikia malengo yaliyowekwa na serikali hiyo, ikiwa ni pamoja na kuwanganisha wananchi. Kuhusu mchakato wa mabadiliko ya Katiba, Maalim Seif amesema kwa sasa wananchi wa n a s u b i r i b u s a r a
za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Jakaya Kikwete ambaye ndiye aliyeasisi mchakato huo. Kwa upande wake balozi Ingunn ameelezea matumaini yake kuwa mchakato wa katiba mpya utamalizika salama na Tanzania itasonga mbele kimaendeleo. Hata hivyo amesema ipo haja kwa Tanzania kusimamia vyema zoezi hilo, ili kuhakikisha kuwa inapata Katiba itakayokidhi haja, kulingana na mabadiliko ya hali ya kiuchumi, kisiasa na kijamii.
Certificates and transcripts of the graduands will not be given at the ceremony. These can be received at another convenient day from the Office of REHEARSAL the DVC (Academic) Since the rehearsal upon signing register is an integral part books and presenting of the ceremony , all an ID card. graduands who wish to attend the graduation ceremony MUST attend DEPUTY VICE the rehearsal which is CHANCELLOR scheduled on Saturday (ACADEMIC)
Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.
13
AN-NUUR
14
AN-NUUR
15
AN-NUUR
16
AN-NUUR