Вы находитесь на странице: 1из 16

www.annuurpapers.co.

tz

Sauti ya Waislamu

Skip Estes kutoka Texas alivyosilimu Uk. 9

Tunataka kuwaona Sheikh Kundecha, MatakaBungeni


Na Bakari Mwakangwale

ISSN 0856 - 3861 Na. 1110 RABIUL AWWAL 1435, IJUMAA , JANUARI 31 - FEB. 6, 2014 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Jifunzeni kutoka kwa Waislamu


Makadhi wawapa nasaha Majaji

WAISLAMU tunataka kusikia majina ya Masheikh na wasomi wa Kiislamu wakijitosa katika chaguzi mbalimbali zijazo-Udiwani, Bunge n.k. Soma Uk. 6

Mihadhara, kelele majukwaani inatosha

Alghaithiyyah, Zanzibar MAJAJI na Mahakimu wametakiwa kujifunza kutoka mafundisho ya Quran ambapo masilahi ya kifamilia na kijamii huzingatiwa zaidi hasa katika migogoro ya kifamilia. U k a t o l e wa m f a n o wa migogoro ya ndoa a m b a p o , b a d a l a ya kungangania kutafuta nani mshindi kati ya mume na mke, mtizamo na mkazo huwa katika kuleta sulhu na

KIONGOZI WA Hizbullah, Sayyed Hassan Nassrallah (katikati). Habari Uk. 8

Unakumbuka mauwaji Njia mpya kuelekea Iran Ijumaa Jan. 26, 2001?
Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu. Inaendelea Uk. 3

Sheikh Omar Mahita:

Hizbullah Vs Sunni Salafi Maangamizi kwa Waislam Uk. 8

Prof. Lipumba alisema tusamehe lakini Baada ya u-IGP, muhimu sasa kutubia Uk. 2

2
S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786 Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM. www.annuurpapers.co.tz E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk Ofisi zetu zipo: Manzese Tip Top Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

Tahariri/Maoni
AN-NUUR

RABIUL AWWAL 1435, IJUMAA JANUARI 31-FEB. 6, 2014


N a i t o s h e n a f s i ya k e kujihesabu mwenyewe maana anajijua alichofanya siku hiyo. Watu walipowaona kundi hilo la Polisi wakiwa na silaha katika hali ya tahadhari walianza kufadhaika, wengi wakianza kuondoka taratibu na hata kukimbia kusalimisha maisha yao. Mara ikasikika amri ya kuuwa. Shoot!. Amri ikapokewa kwa kufyatuliwa risasi kutoka mmoja wa polisi wale. Ta h a m a k i I m a m n a M wa n a z u o n i c h i p u k i z i Ustadh Juma Khmais Mohammed akiwa katika umri wa miaka 30, yupo chini. Kakata roho. Bado waumini wa Masjid M we m b e t a n g a , U n g u j a , Pemba na Tanzania kwa ujumla, wanajiuliza: Nini lilikuwa kosa la Imam Juma hata kustahiki kupigwa risasi kwa lengo la kuuwa? Kwa kosa gani ameuliwa Imam Juma? Labda IGP Mstaafu Omar Mahita na mamlaka ziliowatuma polisi wale ku-shoot, wanajua, lakini hawajataka kusema hadharani. Ila lililo la uhakika ni kuwa ipo siku ya hukumu, hili litafahamika na kila aliyehusika katika mauwaji yale atabeba sehemu ya jinai hii kwa kadiri ya kushiriki kwake. Na Allah (SWT), Ni mbora wa kulipa. Na wala sio mwenye kughafilika na tunayoyafanya. Daftari la amali limehifadhi kila kitu na hiyo siku madaftari yatakapofunuliwa, kweli itadhihiri na kila mtu atalipwa kwa heri zake na shari zake.

AN-NUUR

Unakumbuka mauwaji Waislamu wakizinduka na Ijumaa Jan. 26, 2001? kuifanyia kazi zaka watafaulu N
NI ukweli usiopingika k wa m b a z a k a k a t i k a U i s l a m u , n i m o j a ya vyanzo muhimu sana vya mapato katika jamii. Mapato ambayo msingi wake ni walio na uwezo waliojaaliwa na Mwenyezi Mungu, wanalazimika kutoa sehemu ya mali zao kwa ajili ya kuwasaidia wale wasiokuwa na uwezo. Kutoa zaka ni faradhi n a n g u z o ya t a t u ya Uislamu. Amri ya kutoa zaka imebainishwa wazi k a t i k a Q u r a n 1 4 : 3 1 , pale Mwenyezi Mungu aliposema, Waambieni waja wangu walioamini, wasimamishe swala n a wa t o e k a t i k a v i l e tulivyowaruzuku, kwa siri na kwa dhahiri kabla haijafika siku isiyokuwa na (msaada unaopatikana kwa) kujikomboa wala urafiki. Waislamu tunapaswa kufahamu kwamba neno zakat ni la Kiarabu likiwa na maana ya utakaso. Katika sheria Kiislamu, zaka ni sehemu ya mali ya mwenye uwezo, kwa maana ya asilimia 2.5 ambayo anaitoa mhusika kutekeleza amri ya Allah (sw) na kuwapa wale wanaostahiki (wasio na uwezo) baada ya kwisha mwaka au baada ya mavuno au mapato iwapo mali hiyo imefikia kiwango au faida. Licha ya kuwa kutoa zaka ni ibada na nguzo katika Uislamu, laiti kama Waislamu wangezinduka, wakawa kitu kimoja na kuazimia kuitendea haki kanuni ya zaka na kuitekeleza ipasavyo, leo umma wa Kiislamu ungekuwa katika neema kubwa. Tunamaanisha kwamba zaka ni moja ya vyanzo bora na vizuri vya jamii kuwezeshana, hususan katika huduma za kijamii na kiuchumi. Baadhi tunafahamu kwamba angalao taasisi wanataamula wa K i i s l a m u ( TA M P R O ) walianzisha utaratibu huu wa kukusanya zaka na kuipeleka panapohusika, lakini bado hawajapata ushirikiano unaostahili kutoka jamii ya Kiislamu au labda tuseme, hawajaifanyia kazi vizuri. Inaonekana kama walijaribu au hawajaipa umuhimu unaostahiki. La kuwakumbusha ni kuwa kuna kazi kubwa ya elimu inatakiwa kufanyika. Pili, hii ni taasisi inayohitaji watendaji makini. Ni zaidi ya taasisi za kiserikali za kodi kama TRA. Kwa hiyo si jambo la kufanya kama part time au mradi liende. Tunachukua fursa hii kuwasihi viongozi wetu wa taasisi za Kiislamu nchini, kukutana na kujadili namna ya kuunganisha nguvu zao katika kutekeleza nguzo hii muhimu katika Uislamu. Mfuko huo unaweza kuanzishwa kwa kuwatumia wanataalama wa Kiislamu, kuweka taratibu wa kukutana na matajiri wa Kiislamu na Waislamu wenye uwezo kwa ujumla, ili kukubalina na mna ya kuuendesha na kuusimamia mfuko huo. Wenzetu katika baadhi ya majimbo nchini Nigeria, wamefanikiwa na kila mwaka hutathmini pato la zaka na kuhudimia jamii ya Kiislamu. Aidha katika ngazi za misikiti, utaratibu huo utakaoanzishwa unaweza kupelekwa misikitini, a m b a p o v i o n g o z i wa Misikiti nao watakuwa na chombo maalum cha k u k u s a n ya z a k a k i l a mwaka na kuhudumia jamii ya Kiislamu katika eneo husika. Ni mtazamo wetu kwamba, iwapo Waislamu watazinduka, wakaacha ujinga unaotokana na kuabudu hitilafu zao zisozokuwa za msingi katika dini, wakaweka U i s l a m u wa o m b e l e , watapata mafanikio makubwa kabisa ya kimaendeleo. Hatuwezi kusonga mbele kwa kutaraji sadaka za Ijumaa miskitini. Zaka inaweza kuwa suluhu ya matatizo yaliyopo, la msingi na muhimu ni busara na uadilifu katika kukusanya na kusimamia matumizi ya Zakka kwa mujibu wa sharia na kwa uadilifu.
I miaka 13 imepita toka kuuliwa kwa Imam wa Msikiti wa Mwembetanga. Inawezekana Bwana Omar Mahita, hata hakumbuki kuwa kulikuwa na kiumbe kama huyo duniani. Lakini mjane wa Sheikh Juma Khamis Mohammed anakumbuka. Ya t i m a w a l i o a c h w a , wazazi, ndugu na waumini waliokuwa wanaswalishwa na Imam Juma Khamis, hawawezi kusahau. Ndio maana kila mara wa n a m w o m b e a D u a n a k wa u p a n d e m w i n g i n e , wanamlilia Mola wao juu ya kadhia hii. Kwamba Yeye tu pekee, aliye Hakimu wa mahakimu, Maliki yaumid diin, ndiye atakayetoa hukumu ya haki juu ya waliofanya Jinai ya kumpiga risasi na kumuuwa Imam Juma Khamis. Baada ya serikali kupiga marufuku maandamano ya CUF, Polisi hawakusubiri Jumamosi ifike. Wao walianza kazi Ijumaa, wakifanyia kazi agizo la Makamo wa Rais Omar Ali Juma (Marehemu) kwamba watu wakimaliza tu swala, hakuna cha uradi, dhikri wala mawaidha. Watawanyike, la sivyo! Marehemu Ali Nabwa a l i wa h i k u t o a k a u l i ya kumtetea Makamo wa Rais Omar Ali Juma kwamba ilikuwa kauli na agizo la kuwatahadharisha Wazanzibari kwa sababu alijua kwamba kuna shari ilikuwa imeandaliwa juu yao na hakuwa na namna ya kuwatahadharisha kwa lugha nyingine. Kwa sababu ni jambo la kiserikali naye ni mtumishi wa serikali, lazima alisimamie. Ila kwa huruma ya watu wake ndio akatoa kauli hiyo kama watamwelewa, wajifungie majumbani mwao. Allah ndiye mjuzi nini kilipangwa na nini nafasi ya kiumbe huyo wa Allah, Omar Ali Juma, ambaye sasa hivi yupo Barzakh. Lakini mtekelezaji mkuu, kwa maana kuwa wakati huo alikuwa ndiye Mkuu wa Polisi (IGP), Inspekta Generali wa Polisi, Bwana Omari Mahita, bado yu hai. Na bila shaka Fadhakkir kwake bado inafanya kazi. Ndiyo inayofanyika hapa. Kama alivyosema Profesa Lipumba, ili jinai hii isisahaulike, tukajisahau tukaifanya tena, IGP Mstaafu Omar Mahita akumbuke kuwa mara baada ya swala ya Ijumaa mnamo tarehe 26 Januari, 2001, Polisi walifika Masjid Mwembetanga wakiwa na silaha za moto. Ilikuwa ni majira ya saa saba na nusu mchana siku hiyo, ndio kwanza Waislamu wanamaliza sala zao misikitini. Misikiti mingine ilikuwa imeshamaliza kusali na watu wako milangoni wakitakiana kheri na kuagana. Bila shaka wengine wa l i k u wa n j i a n i t a ya r i wakielekea majumbani kwani misikiti mingine hutangulia kusali kidogo. Kwa Msikiti wa Mwembetanga, ndio kwanza watu walikuwa wanatoka wakiwa wamechanganyika changanyika kwa kusalimiana na kutakiana kheri ya Ijumaa na kuagana. Mara Polisi waliokuwa na silaha walifika ghafla kama waliotumwa kupambana na wahalifu. Baadhi ya mashuhuda wanasema kuwa kikosi kile kilikuwa kinaongozwa na Ofisa wa Polisi, maarufu sana hapa Unguja.

Sheikh Omar Mahita:

MKUU wa Jeshi la Polisi aliyestaafu Bwana Omar Mahita.

3
Inatoka Uk. 1
maelewano baina yao. Kwamba ukienda kwa mtindo wa kutafuta mshindi, kwanza mashauri huchukua muda mrefu, lakini pia huondoa maelewano na kuharibu maslaha ya familia. Akiongea katika semina ya Majaji na Mahakimu iliyofanyika Zanzibar, Kadhi wa Kenya Mshali Khamis Mshali amesema kutatua m i g o g o r o k wa n j i a za usuluhishi ni bora zaidi kuliko kwenda mahakamani kwa kuwa k e s i z i n a z o a m u l i wa mahakamani huchukua muda mrefu. Mkutano huo wa Majaji na Mahakimu kutoka nchi tano za Afrika Mashariki ulikuwa wa kutafuta njia mbadala za usuluhishi badala ya kutegemea njia ya Mahakamani. Katika mkutano huo uliofanyika Hoteli ya Ocean View Mjini hapa, Mshali alisema kutatua migogoro kwa njia ya usuluhishi ni jambo zuri ambalo wamekuwa wanalitumia muda wote kutokana na kuwa wamekuwa wakisuluhisha migogoro mbali mbali ya kifamilia, ikiwemo ile ya kijamii, urithi, ndoa, talaka na mambo yanayohusiana na hayo. Sisi Makadhi tumeshazowea kutatua migogoro ya kifamilia kwa kutumia njia za kukaa pamoja na kutafuta ufumbuzi hasa kwa kutumia Quran Tukufu na Hadithi za Bwana Mtume (s.a.w) hivyo mafunzo kama haya yatatusaidia sana katika kuendeleza utatuzi wetu tuliouzowea, alisema Kadhi huyo. Alisema, Uislamu umefundisha wazi unapohukumu kesi na hivyo jambo la kwanza ni kusikiliza kwa makini kati ya pande mbili, mdai na mdaiwa. Mantiki ya kusikiliza pande zote mbili za mgogoro kwa makini ni kuwa katika kuhukumu basi, hukumu itolewe kwa haki. Hata hivyo, katika

Habari

RABIUL AWWAL 1435, IJUMAA JANUARI 31-FEB. 6, 2014 ilianza kutumika mwaka 1994 na imekuwa ikitumika sana lakini bado haijaingia miongoni mwa wanasheria. U s u l u h i s h i unatumika katika mashauri yote ya k a z i n a a j i r a h u wa inashughulikiwa katika suluhu mpaka ishindikane ndio inakwenda mahakamani alisema. Alisema utatuzi wa migogoro sio jambo geni katika nchi za Afrika na kutoa mfano kuwa kuna baadhi ya mabaraza ya wazee yanafanya kazi za mahakama katika jamii kwa kusuluhisha migogoro mbali mbali. Aidha alishauri mfumo huo wa utatuzi mbadala wa migogoro uanze kufundishwa vyuoni ili kuanza kujua mbinu za kutatua migogoro kwa njia mpya ya usuluhishi. Kwa upande wake Mwanasheria wa Jumuiya ya Afrika Mshariki Bi Rehema Kirefu ambaye ndio Mratibu wa semina hiyo amesema mafunzo hayo n i m u e n d e l e z o k wa Majaji na Mahakimu ambapo lengo ni kuwajengea uwezo na kuwapa mafunzo ya kutatua migogoro ikiwa ni njia ya kuisaidia mahakama katika kutatua kesi. Katika nchi zetu kuna mrindikano mkubwa na ucheleweshaji mkubwa wa kesi kwa hivyo dunia imeona kama kuna njia nyengine ya kutatua migogoro kwa hivyo wa m e o n a wa h u s i k a wa kesi wakenda nje ya mahakama itasaidia kupunguza 0kesi zilizopo mahakamani, alisema Kirefu. Mkutano huo unafanyika wakati wananchi wengi wanalalamika kuhusu utendaji wa mahakama ambapo ucheleweshaji wa kesi unahusishwa pia na kuwepo kwa rushwa na kutowajibika kwa watendaji wa Mahakamani wakiwemo Majaji na Mahakimu.

AN-NUUR

Jifunzeni kutoka kwa Waislamu

MAJAJI na Mahakimu nchi za Afrika Mashariki wakiwa katika semina Zanzibar hivi karibuni. m a s h a u r i ya n d o a , ni bora kuyarejesha kwa wanafamilia na kuwahusisha wazazi wa pande zote mbili ili kutafuta ufumbuzi utakaodumisha mahusiano mazuri na kudumisha ndoa. Urudishe utata ule kwa familia na wazazi ndio watakuwa watatuzi wa migogoro ya ndoa, na hayo ndio mafunzo ya dini yetu. Alisema. Akitoa ufafanuzi alitoa mafunzo yanayopatikana kutoka Surat Nisaa aya ya 35 ambayo inasisitiza juu ya sulhu. Aya hiyo inasema: Na kama mkiona kuwa kuna ugomvi baina ya mke na mume, basi pelekeni mwamuzi mmoja katika jamaa za mwanamume na mmoja katika jamaa za mwanamke. Kama wa k i t a k a m a p a t a n o Mwenyezi Mungu atawawezesha. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa habari za siri na habari za dhahiri. (4:35) Mkutano huo wa siku tatu umewashirikisha Majaji na Mahakimu kutoka nchi za Kenya, Rwanda, Burundi, Uganda, na wenyeji Tanzania na Zanzibar ikiwa ni njia moja ya juhudi za kutafuta njia mbadala za kutatua migogoro hiyo inayozidi kujitokeza katika jamii. Akifungua mkutano huo wa mafunzo, Jaji M k u u wa Z a n z i b a r Omar Othman Makungu alisema kumekuwepo na malalamiko ya mashitaka (kesi) kuchelewa, kwa hivyo hivi sasa majaji na mahakimu wanatafuta njia bora za kupunguza changamoto za wingi wa kesi katika mahakama zao. Alisema, ingawa Mahakimu wengi hawapendi njia ya usuluhishi na wanapendelea njia ya kuamuliwa mahakamani jambo ambalo kunakuwa na mshindi na mshindwa katika kesi, lakini mfumo h u o wa u s u l u h i s h i utasaidia sana katika jamii hasa kwa kuzingatia kesi nyingi huzorota mahakamani. Makungu alisema mafunzo hayo yatawaelimisha majaji na mahakimu katika kupunguza kesi za mahakamani pamoja na kuwafanya wafurahie suala la mahakama. S u a l a linalopendekezwa ni kutafuta njia mbadala ya usuluhishi sisi kama mahakama tunaipendelea ingawa mahakimu wengi hawaupendi utaratibu huu ambao umekuwa u k i t u m i wa n a n c h i nyingi duniani hivi sasa, tunaamini utarapunguza kesi mahakamani na pia utarahisisha upatikanaji wa haki kati ya mdai na mdaiwa, alisema Jaji Makungu. Akizungumza kando ya mkutano huo Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Robert Vincent alisema jambo la utatuzi wa migogoro sio geni kwa Tanzania umekuwa ukitumika zamani kabla ya kuja kwa ukoloni ulikuwa ukitumiwa ndani ya familia. Alisema utatuzi kwa njia mbadala uliondoka baada ya kutungwa kwa sheria za nchi lakini bado unaweza kutumika na kuondosha migogoro kwa kuwa jamii inaweza kutumia mfumo huo wa zamani kurejeshwa na kufuata utaratibu wa zamani wa kutatua migogoro ambapo sheria yake ilirekebishwa na

4
Na Mtume alikuwa akisema: Ee Mola wangu m l e z i ! H a k i k a wa t u wangu wameifanya hii Qur'ani ni kihame. (Al Furqan 25:30). Kila sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu, Swala na Amani zimfikiye Mtume Muhammad (s.a.w) na jamaa zake. Lengo la kushushwa Q u r a n n a v i t a b u vingine vyote vya Allah (Sw) ni kumuongoza mwanadamu katika njia iliyooka. Amesema Allah (Sw), Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa h u m o Q u r ' a n i k u wa ni uwongofu kwa wat u , na ho ja zilizo wazi za uwongofu na upambanuzi... ( Al Baqara 2:185). Katika kuonyesha uwezo wake wa k u m u o n g o z a mwanaadamu Quran i m e i t wa k wa m a j i n a mengi na moja kati ya majina hayo ni Al-Quran. Maana yake ni Chenye kuunganishwa pamoja au Chenye kusomwa. Yaani Quran ni kitabu kilichofumwa na herufi, silabi, maneno aya na s u r a , k i n a c h o s o m wa mara kwa mara. Kitabu hiki kimeitwa kwa jina Al-Quran kwasababu ni mkusanyiko wa mafunzo ya msingi ya maisha ambayo mtu h a n a b u d i k u ya r e j e a mara kwa mara. Quran ndio Muongozo pekee wa maisha ya mwadamu hivi sasa. Aya nyingi za Quran zinatufahamisha kuwa Q u ra n h u wa o n g o z a waumini katika njia iliyonyooka, huwanyanyua na kuwafanya watawala katika jamii, huwatatulia matatizo yao na kuwaondolea mashaka yote yanayoikabili jamii ya mwadamu kwa ujumla. Huwatoa katika maishagiza nakuwaingiza katika nuru. Amesema Allah (Sw) Hiki ni Kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake; ni uwongofu kwa wachamungu, (Al Baqara 2:2). Hakika hii Qur'ani inaongoa kwenye ya yaliyo nyooka kabisa, na inawabashiria Waumini ambao wanatenda mema ya kwamba watapata malipo makubwa. (Al Israai or Bani Israil: 17:9) Tukiwa na yakini kuwa

Makala

RABIUL AWWAL 1435, IJUMAA JANUARI 31-FEB. 6, 2014


m i t a a l a ya m a d r a s a . Huko Kenya wakaenda kwa pupa kwa balozi wa Marekani kutoa rundo la misaada ya vitabu na pesa kwa madrasa. Waislamu wakashituka na wakakataa. Makafiri hakukata tamaa walijifunza kosa lao. Hapa Tanzania, wakaamua kuwa kwanza kabisa waanze na utafiti utakaowajulisha u k we l i h a l i s i j u u ya madarsa. Nawakaona Marekani wasionekane waziwazi. Wakawatumia wa t u we n g i n e , ya a n i Shirika la Kijerumani liitwalo Konrad Adeneur Stiftung. Mwezi Mei/Juni 2003 walifanya utafiti wao walioita Quran Madrasa Baseline Survey. Yaani utafiti wenye lengo la kujua hali halisi ya Madrasa kwa Mkoa wa Dar es Salaam. Waligundua mengi, lakini kwa sasa tuseme tu kuwa baadhi ya waliyojua ni kuwa karibu ya nusu ya walimu wa madrasa wanapata mshahara wa chini ya shilingi 10000/= kwa mwezi (kwa mwaka 2003). Na wengine hawalipwi kabisa. Theluthi mbili ya madrasa zinamilikiwa na watu binafsi na zipo vibarazani. Wazazi na viongozi wa Kiislamu hawana taarifa wala hawataki kufuatilia kinachoendelea kwenye hizo madarsa. Baada ya kuupata ukweli huo Marekani ikaamua kuanza kuingilia madrasa kwa kuanzia Zanzibar. Kwa ufupi ni kuwa S e r i k a l i ya M a r e k a n i kwa kupitia Shirika l a k e L i i t wa l o U S A I D linasaidia madrasa huko Zanzibar. Hivyo Waislamu tunasaidiwa kwa kupitia mifuko mikubwa minne: Mfuko wa Rais Bush wa Elimu ya Waislamu (President Bushs Muslim Education Initiative). Mfuko wa Rais Bush wa Kupambana na Ugaidi Afrika Mashariki (President Bushs East African Counter-terrorism Initiative). Scholarship za Balozi k wa wa s i c h a n a ( T h e A m b a s s a d o r s G i r l s Scholarship Program). Mfuko wa elimu Afrika (African education initiative). Itaendelea toleo lijalo

AN-NUUR

Waislamu tumeipa mgongo Quran

BINT wa Kiislamu akitoa Da'awah kwa asiye Muislamu. Quran ni kitabu cha Allah (Subhaanahu wa Taala) kisicho na shaka ndani yake (Al Baqara 2:2), na kila tumalizapo kusoma Quran tunabwagiza kwa: Swadaqallahul-adhiim yaani, Kasema Kweli Allah Aliyemtukufu, iweje leo hii Waisamu takribani ulimwenguni kote wawe ni dhalili na wenye mashaka kinyume na aya tulizo rejea? Tatizo liko wapi? Ukichunguza kidogo utagundua kuwa tatizo liko kwenye kuiendea Quran. Ukirejea historia ya kushuka Quran amri ya: ...Na Soma Quran vilivyo (tartila) ni amri yatatu aliyopewa Mtume (Swalla Allaahu alayhi wa sallam) na Mola wake baada ya amri ya kusoma (96:1-5) na ile ya kusimama usiku kwa swala (73:2-3). Kusoma Quran vilivyo (tartila) ni kusoma kwa mazingatio katika utekelezaji hatua kwa hatua, je, amri hii ya Mola wetu tunaitekeza katika kuisoma kwetu? Ni katika msisitizo w a k u i s o m a Q u r a n kwa mazingatio, Allaah (Subhaanahu wa Taala) anatuhimiza kila isomwapo tuisikilize na tuwe kimya ili tustahili rehma zake. Amesema Allah (Sw), Na isomwapo Qur'ani isikilizeni na mnyamaze ili mpate kurehemewa. (Al-A'raaf 7:204) Tareikh inatuonyesha kuwa pale jamii ya Waislamu ilipoiendea Quran kwa mazingatio, iliweza kuja juu na kuendesha mambo yake yote ya kibinafsi na kijamii kwa mujibu wa Quran na Sunnah ya Mtume (Saw) na haikuweza kutawaliwa na matwaaghuut kirahisi. Kwa mfano historia inatuonyesha kuwa Wa i n g e r e z a wa l i p a t a ugumu sana kutawala makoloni yao yaliyokuwa akikaliwa na Waislamu. Wa l i o n y e s h a u g u m u huo katika kuitawala Misri, Uturuki na Afrika Mashariki. Mwaka 1882, Waziri Mkuu wa Uingereza, Bw. Gladstone, akiwa ameinua juu kitabu c h a Q u r a n , a l i s e m a k u wa a m b i a wa b u n g e wa Uingereza (House of Commons): So long as the Egyptions have got this book with them, we will never be able to enjoy quit of peace in that land. (Muhammed Qutb 1972: xi) Tafsiri: M a d h a l i Wa m i s r i wa n a c h o k i t a b u h i k i hatuwezi kamwe kufurahia utulivu au amani katika nchi ile. Katika miaka 1900, kauli kama hiyo ilitolewa na Waziri wa Makoloni ya Uingereza huko Uturuki pale aliposema: Muda wa kuwa Waislamu wanayo Quran, basi watakuwa kikwazo kwetu. Kwahiyo ni lazima tuiondowe kutoka maishani mwao. Mwaka 1900 Kamishina wa Makoloni huko Uganda, Sir Henry Johnson, alimwandikia D.C. wa Wilaya ya Busoga, kumfahamisha sera ya serikali ya kikoloni juu ya Uislamu pale aliposema: Haitakuwa kwa maslahi ya Serikali ya Uingereza iwapo Uislamu utapata wafuasi wengi k wa n i k wa a s i l i ya o Waislamu ni wagumu kuwatawala na katika nyoyo zao wanapinga utawala wa dola ya Kikirsto/Kitwaaghuut. Marekani kwa kupitia a l i ye k u wa Wa z i r i wa Mambo ya Nchi za Nje wa zamani Bw. Collin P o w e l l , n a Wa z i r i wa Ulinzi bw. Dolnad Rumfeld, wamesema kuwa umadhubuti wa Waislamu unatokana na wao kusoma, kufundisha, kuiamini na kuifuta Quran. Hivyo ufumbuzi wa kudumu ni kuwatoa Waislamu katika Uislamu wao kwa kuingilia mafundisho ya Quran. Na njia nzuri ni kuanzia kwenye Madrasa zao. Kampeni hiyo iwe ya dunia nzima. Hapa tutangalia tu wanayafanya Tanzania na mafnikio yao ukilinganisha na yetu sisi Waislamu (wanaharakati). Njia ya kwanza waliona ni kutoa misaada kwenye Madrasa ili iwe ni mwanya na hatimaye kubadilisha

Habari mchanganyiko

RABIUL AWWAL 1435, IJUMAA JANUARI 31-FEB. 6, 2014

AN-NUUR

UN wasema Waislamu wana hali ngumu CAR


BANGUI Umoja wa Mataifa ameonya kuhusu k u o n g e z e k a mashambulizi dhidi ya Waislamu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati. Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Navi Pillay, amesema magenge ya wanamgambo wanaharibu na kupora misikiti, maduka na nyumba za Waislamu katika maeneo kadhaa k a t i k a m j i m k u u wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui. Imearifiwa kuwa, katika siku za hivi karibuni wanajeshi wa Ufaransa walioko Bangui, wamewatimua wanamgambo Waislamu wa kundi la Seleka na hivyo kuwaacha raia Waislamu bila ulinzi. Kutokana na hali hiyo, magaidi wa Kikristo wanaojulikana kwa jina la anti-balaka, wanawashambulia kikatili raia Waislamu wakiwemo wanawake na watoto wadogo na kuwaua

Ndege isiyo na rubani yatumika kusimamia mitihani


BRUSSELS Shule moja nchini Ubelgiji imeamua kutumia ndege isiyo na rubani (drone), kusimamia mitihani baada ya kushindwa mbinu za kawaida kuwazuia wanafunzi kufanya udanganyifu katika mitihani yao. Ndege hiyo yenye kamera ya kuchukua picha za video, pia inarekodi harakati zozote zinazotia mashaka kwa mwanafunzi yeyote yule ndani ya chumba cha mtihani na kurusha matukio yote hayo yanayofanywa na mwanafunzi moja kwa moja kwenye TV kubwa. Hatua hii imerahisisha s a n a u n g a m u z i w a vitendo vya udanganyifu

kiholela. Kuna askari 1,600 wa Ufaransa na maelfu ya askari wengine wa kulinda amani kutoka nchi za Kiafrika huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, lakini wameshindwa kuzuia m a u a j i ya Wa i s l a m u yanayofanywa na magenge ya Wakristo. Mashirika ya kutetea haki za binadamu yameonya kuwa kuna uwezekano wa kutokea mauaji ya kimbari dhidi ya Waislamu katika nchi hiyo ya katikati mwa Afrika. Waziri Mkuu mpya wa n c h i h i y o A n d r e Nzapayek e, ameunda Baraza la Mawaziri 20 wa k i w e m o w a u n g a j i mkono wa Seleka na anti-balaka ili kujaribu kurejesha utulivu nchini humo. Mapigano ya ndani katika Jamhuri ya Afrika ya Kati yalianza mwezi Machi mwaka jana, baada ya kung'olewa madarakani serikali ya aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Francois Bozize.

WAKRISTO Afrika ya Kati wakishangilia kuondoka madarakani Rais Muislamu.

Ulinzi waongezwa kwa viongozi wa Ikhwanul


CAIRO Duru za habari nchini Misri zinaarifu kuwa, baadhi ya viongozi wa wa n a h a r a k a ti wa I k h wa n u l M u s l i m i n n c h i n i h u m o , wamehamishwa katika jela mpya jijini Cairo. Hayo yamethibitishwa na mmoja wa mawakili wa viongozi wa wanaharakati hao Sidi Nasr, aliposema kuwa hadi sasa haijafahamika lengo la kuwahamisha viongozi hao wa Ikhwanul Muslimin katika jela yao na kuwapeleka katika jela ya Torah ya jijini Cairo. Bw. Sidi ameongeza kuwa jela hiyo ina nyenzo na mitambo mingi ya kisasa kwa ajili ya kuwachunga wafungwa sambamba na ulinzi mkali wa usalama. Amesema kuwa, Ahmad Arif na Jihad al-Haddad, ambao ni wasemaji wa chama hicho waliotiwa mbaroni baada ya kuondolewa madarakani Rais wa nchi hiyo Mohammad Mursi, ni miongoni mwa viongozi wa wanaharakati hao waliohamishiwa katika jela hiyo. Hii ni katika hali a m b a y o v i o n g o z i wa Misri wametangaza kuwa, hatua za kiusalama ni miongoni mwa sababu za kuhamishwa wafungwa hao. Wa k a t i h a y o yakiripotiwa, duru za habari zinaeleza kuwa viongozi wa Wanaharakati hao wanaoshikiliwa na jeshi la Misri, wanazuiliwa kufanya mawasiliano na familia zao. H a t u a h i z i zinachukuliwa huku Rais wa serikali ya mpito ya nchi hiyo Adly Mansour, akitangaza kuwa uchaguzi wa Rais utafanyika kabla ya ule wa Bunge nchini humo. Tangazo hilo limezidisha tetesi kuwa Mkuu wa Jeshi, Jenerali Abdel Fattah al-Sisi, atagombea urais Misri. Jumamosi iliyopita maelfu ya watu walikusanyika katika u w a n j a w a Ta h r i r mjini Cairo wakati wa kuadhimisha miaka mitatu tangu Hosni Mubarak kupinduliwa. Umati huo ulimedaiwa kumtaka Jenerali al-Sisi agombee uongozi. Wakati huo huo, wakuu wamesema watu wapatao 49 waliuawa katika sehemu mbali-mbali za nchi hiyo, wakati askari wa usalama walipopambana na waandamanaji wanaopinga serikali.

Majeshi ya Marekani yaendelea kuua Somalia


MAREKANI imeendelea kutumia ndege zisizo na rubani (drone) kuua watu nchini Somalia, l i c h a ya m a l a l a m i k o yanayoongeza ya kimataifa dhidi ya mashambulizi hayo yanayoua idadi kubwa ya raia wasio na hatia katika maeneo mbalimbali duniani. Afisa mmoja wa jeshi la Marekani ambaye hakutaka jina lake litajwe, amesema ndege zisizo na rubani za nchi hiyo Jumapili iliyopita zilishambulia nchini Somalia. Hata hivyo afisa huyo wa jeshi la Marekani hakutoa maelezo zaidi kuhusu mlengwa na iwapo operesheni hiyo ilikuwa na mafanikio au la. Maafisa wa Marekani wanasema kuwa mlengwa alikuwa afisa wa ngazi za juu wa kundi la al Shabab n a k wa m b a , a l i k u wa akifuatiliwa na Marekani kwa miaka mingi. Afisa mwingine wa jeshi la Marekani amesema kuwa shambulizi hilo lilifanyika karibu na eneo la Barawe, lililoko umbali wa m a i l i 1 1 0 k u t o k a Mogadishu. Mwezi Oktoba mwaka jana, makomandoo wa jeshi la Marekani walifanya jaribio la kumteka nyara kiongozi wa al Shabab,

vinavyofanywa na wanafunzi wakati wa kufanya mitihani yao. (irib.ir)

Ikrima, katika mji wa Barawe lakini operesheni hiyo haikufanikiwa. Uchunguzi uliofanywa na Bureau of Investigative Journalism (TBIJ) yenye makao yake nchini Uingereza, unaonyesha kuwa ndege zisizo na rubani za Marekani zimeuwa kiasi cha watu 2,400 duniani katika kipindi cha miaka mitano tangu Rais Barack Obama achukue madaraka nchini humo.

Tunataka kuwaona Sheikh Kundecha, Mataka Bungeni A


Na Bakari Mwakangwale l-MARHUM Profesa Kigoma Ally Malima, katika uhai wake a l i wa u s i a Wa i s l a m u nchini kuwa waseme maneno machache lakini yenye uzito mkubwa. Profesa Malima, a l i w a a s a Wa i s l a m u wasibakie kuwa ni watu wa kulalamika bali wajiratibu kisha wafanye kazi na kwa kufanya hivyo shida zao zitaondoka na haki zao watazipata. Usia huu nikiutafakari, binafsi naona mpaka sasa haujafanyiwa kazi ipasavyo. Wenye wajibu wa kusimamia usia huo ambao ni viongozi wa Waislamu (Masheikh) bado hawajaamua kuufanyia kazi. N a s e m a h i v y o k wa sababu umma wowote au kundi lolote haliwezi kufanya mambo yake kwa ufanisi bila ya kuwa na viongozi wa kupanga, kuratibu na kusimamia mambo kisha kufanya tathmini. Kutokana na mfumo wa kiutawala wa nchi ulivyo, Waislamu wanatakiwa kujiratibu katika mfumo wa kisiasa na kuufanyia kazi mfumo huo kisayansi ili waweze kuingia katika mamlaka za maamuzi ya mfumo wa kiutawala. Kama zoezi hili litaratibiwa kwa umakini na viongozi wa Waislamu wa k a f a n i k i wa k a t i k a Mabaraza ya maamuzi, nadhani ndio mwanzo wa kupambana na kuwa chanzo cha kuondoa shida zao na kuzipata haki zao. Ni wakati sasa kwa Waislamu kujiratibu ili kuingia katika mabaraza ya maamuzi kuanzi ngazi ya mtaa kwani mfumo wa kudai na kuilalamikia S e r i k a l i m a j u k wa a n i umeonekana hauna tija yoyote, sana sana ni kupoteza muda muhimu wa kufanya kazi. Mpaka sasa, Waislamu wamesha wasilisha malalamiko yao kimaandishi chungu nzima Serikalini, wakieleza madai yao na kuitaka Serikali kuwatendea haki,

Makala

RABIUL AWWAL 1435, IJUMAA JANUARI 31-FEB. 6, 2014

AN-NUUR

AMIR wa Shura ya Maimamu, Sheikh Mussa Kundecha (kulia) lakini hakuna jibu sahihi lililotoka, zaidi ya lile la Mzee Benjamin Mkapa. Mzee Mkapa, akiwa Rais wa awamu ya Tatu, akijibu malalamiko na madai ya Waislamu aliyopewa ili kuyatafutia ufumbuzi, alikuja na majibu kuwa matatizo ya Waislamu nchini ni ya kihistoria! K wa s a s a s i h a b a , Jumuiya na taasisi mbalimbali za Kiislamu zimejikita katika kuanzisha na kuendesha Shule za Kiislamu bila shaka walijiratibu na kujipanga, na kwa sasa kupitia Shule hizo vijana wengi wanapata fursa ya kusoma tofauti na pale awali ambapo malalamiko ya l i k u wa wa t o t o wa Kiislamu wananyimwa elimu. Bila shaka, kupitia Shule hizo kuna vijana wengi wenye elimu ya kutosha kushika nafasi mbalimbali za kisiasa kuanzia ngazi ya mtaa mpaka Taifa, cha msingi kilichopo ni kwa viongozi (Masheikh) kuitumia rasilimali vijana hawa, kuratibu nakufanya nao kazi kwa lengo la kuwaingiza kunako maamuzi na kupigania haki za Waislamu kwa hoja. Ukiangalia hivi sasa katika idara na Taasisi za umma, kumejaa watu au watendaji wa imani ya dini moja (Wakristo) jambo ambalo linatia mashaka katika maamuzi yanayohusu Waislamu, kwani inawezekana kabisa kuwa maamuzi yao huzingatia utashi wa kiimani. Muasisi wa Chadema, Mzee Edwin Mtei, aliwahi kuilalamikia hali hiyo pale Rais Jakaya Kikwete, a l i p o t e u wa Tu m e ya kuratibu Katiba mpya baada ya majina mengi kujitokeza kuwa ni ya Waislamu. Nikihesabu Waislamu k a t i k a h i i Tu m e k wa kuzingatia majina, naona zaidi ya theluthi mbili ni wao (Waislamu). Wengine (theluthi moja) ni Wakristo au watu wasio kuwa na dini. Alisema Mtei. Muasisi huyo wa Chadema, aliongeza kwa kusema licha ya kwamba Tanzania siyo nchi inayozingatia dini katika maamuzi yake ya kisiasa, ni lazima ikubalike kuwa madhehebu ya Dini yana Influence (ushawishi) katika mchakato na hatima ya maamuzi. Ndiyo maana hata aliyekuwa Rais wa kwanza Tanzania, Mwalim Juliaus K . N y e r e r e , a l i k u wa a k i t e u w a Wa k r i s t o kwa malengo yake, hii ilibainika mwaka 1970, pale alipokuwa akieleza mikakati ya kulisaidia Kanisa Katoliki (Wakristo) nchini, kwamba ni pamoja na kuteuwa watu wenye imani thabiti ya Kikristo na kuwapa uongozi katika Chama (CCM) na Serikali. Hayo yalikuwa ni maongezi baina ya Mwalimu Nyerere (1970), alipo wakaribisha Ikulu, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu ( Ta n z a n i a E p i s c o p a l Conference-TEC) Fr. Robert Rweyemamu na mwakilishi wa Pope nchini, Mgr. Giovano Cerrano. Mikakati na mipango hiyo ya Mwalimu Nyerere, ndiyo inayowaumiza hadi leo Waislamu, kwani ni wazi alifanikiwa kuweka watu wenye Imani thabiti ya Ukristo , ambao na wa o wa m e j i e l e wa n a kuindeleza hali hiyo, a m b a c h o Wa i s l a m u wamekipa jina Mfumo Kristo. Unaweza ukajiuliza kwa nini madai ya Wa i s l a m u ya n a k u wa hayashughulikiwi ipasavyo mbali ya kuyazungumzia majukwaani lakini pia ya n a wa s i l i s h wa k wa maandishi katika mamlaka husika. Hapa ndio ukirejea kauli ya Mzee Mtei, ambaye naye alifanya kazi kwa karibu na Mwalimu Nyerere (awamu ya kwanza) na kauli ya

Nyerere, mwenyewe kwa viongozi wake wa Kanisa, unapata jibu kwa nini Waislamu mambo yao mengi yanapofika S e r i k a l i n i h u k wa m a . Lakini ya upande wa pili yanapatiwa! Kwa mtazamo huo, Waislamu hawana budi kujipanga wenyewe kuanzia ngazi ya chini kwa kujiratibu na kuangalia wanaweza vipi kuingia kwa wingi katika ngazi za maamuzi, ili japo uwiano wa viongozi uwe sawa na katika maamuzi washindane kwa hoja. Kama hushiriki au haumo katika maamuzi ya kiuongozi aidha Mtaa wako, Kata yako, Jimbo lako la uchaguzi na hatimaye Serikali yako, basi uelewe kuwa wale ambao watashiriki ndio watakaokupangia wewe uwe katika hali gani na p e n g i n e k u k wa m i s h a mambo yenu. Kwa kifupi mchakato wa kuwaondoa Waislamu katika hali waliyonayo hivi sasa kama sehemu ya jamii unaanzia katika kukamata nafasi za kisiasa, kwa lengo la kushiriki katika maamuzi kuanzia ngazi ya chini. Masheikh, pamoja na viongozi wa Kiislamu waelewe moja ya jambo ambalo wanapaswa kulishughulikia na kulisimamia wakati huu tukielekea katika chaguzi kuanzia ngazi ya Mtaa (2014). Madiwani, Wabunge na hatimaye Rais (2015) ni hili, je, Waislamu wanaingia na wanashiriki vipi katika hatua hizo. Ni vyema, viongozi wa Kiislamu wakafikiria kuwa na viongozi wa Kisiasa, ambao wana malengo ya kutetea usawa katika jamii na kuondoa dhulma, na waende huko si kwa kudai upendeleo kwa jamii ya Waislamu bali kusimamia haki kwa wote na kutahadharisha ubaya wa kukandamiza kundi moja katika jamii na kulipa nafasi kundi lingine. Ta t i z o M a s h e i k h wanashindwa kubaini kwa muda mrefu kwamba wingi wa Waislamu nchini Inaendelea Uk. 7

Makala

RABIUL AWWAL 1435, IJUMAA JANUARI 31-FEB. 6, 2014


u r a t i b u wa v i o n g o z i ( M a s h e i k h ) wa n g a z i za juu. Vipi Maimmau wanashindwa kutumia vyema nguvu kazi hii? Sheikh Kilemile, anasema Ibada ya swala ya Ijumaa itumike kuwaeleza Waislamu mustakabali wao kisiasa kila Ijumaa, viongozi (Masheikh) waratibu mada maalum k wa Wa i sl a mu ye nye ujumbe mmoja kote. Hii ndio kazi ya swala ya Ijumaa. Mnawaacha Wa i s l a m u wa n a s wa l i kisha wanatawanyika, hawaelezwi chochote, ni lazima uwepo utaratibu wa kuwa na hotuba ya aina moja yenye muelekeo na mustakabali wa Waislamu nchini. Anasema Sheikh Kilemile. Hoja kama hizi za Sheikh Kilemile, ndio Masheikh wanapaswa kukusanyana hivi sasa akiwemo yeye (Kilemile) kuratibu na kuweka mikakati hivi s a s a n a k u r u d i k wa Waislamu na kuwaeleza, kwani umma wa Kiislamu hauna tatizo, bali umekosa viongozi wa kuwaongoza tu. Uzuri wa bahati, kuna mabaraza mengi ambayo yamesheni wanazuoni wenye elimu ya mazingira na ile ya Dini, pia kuna Taasisi ya wanataaluma wa Kiislamu (TAMPRO), hawa ni wasomi watupu na wanaufahamu mzuri juu ya Uislamu na Waislamu. Sio vibaya tukasikia majina ya Mashekh au wasomo wa Kiislamu kama Maalim Bassaleh, Amir Musaa Kundecha, Ramadhani Sanze, Hashim Saiboko, Injinia Mussa N ya m s i n g wa , S h e i k h H a m i s i M a t a k a , Pa z i Mwinyimvua na wengine wengi, wakijitosa katika chaguzi mbalimbali zijazoUdiwani, Bunge n.k. Waswahili wanamsemo wao kwamba, Kanzu ya Ijumaa, hufuliwa Alhamisi. Ni vyema Masheikh na wa s o m i wa K i i s l a m u wakakutana na katumia muda huu kuratibu masuala ya chaguzi kisha wakayapeleka kwa Wa i s l a m u i l i k u a n z a kufanyiwa kazi.

AN-NUUR

Tunataka kuwaona Sheikh Kundecha, Mataka Bungeni


Inatoka Uk. 6 ni silaha na ni mtaji lakini tatizo ni kutoamua kwao kuratibu mikakati ya muda mfupi na muda mrefu ili kuweza kuleta usawa katika jamii. Siku zote Waislamu katika nchi hii kabla na baada ya Tanganyika ( Ta n z a n i a ) h u r u , wamekuwa wakijitazama kama raia wa Tanzania ( Ta n g a n y i k a ) . N a wamefanya mambo yote tokea kudai katika sura hiyo wakitaraji haki na usawa kwa makundi yote, baada ya Uhuru. Lakini nyuma ya pazia wale ambao wasiokuwa Wa i s l a m u a m b a o waliwaamini na kuwaweka mbele kabla na baada ya Uhuru, wakijitazama kwa Dini zao kwanza kisha baadaye wakajitazama sasa kama raia wa Tanzania (Tanganyika). Mfano wa hilo ni hii kauli ya Mwalimu Nyerere, katika moja ya vitabu ananukuliwa akisema, Nimeanzisha idara ya Siasa katika TANU (CCM) na nimemuweka Mkristo kuwa kiongozi wa idara hiyo, japo si mwanasiasa mashuhuri lakini nimemuweka kutokana na imani madhubuti ya Dini aliyonayo. Kwa mikakati hiyo na mingine mingi ambayo ilikuwa ikifanywa na Mwalimu Nyerere akiwa Rais, kwa kuiwekea misingi, ndio maana hutaona Bungeni Waislamu wakawazidi Wakristo kama ilivyo katika sekta zingine za Umma. Mwaka 2009, Kanisa Katoliki lilitoa nyaraka mbili kuelekea katika uchaguzi Mkuu, mmoja uliitwa Ilani na wa pili u l i i t wa M p a n g o wa Kuhamasisha huduma ya Kichungaji katika jamii kuelekea Uchaguzi Mkuu 2010. K wa h i y o t u j a d i l i pamoja na kama jumuiya za Kanisa ni lazima tujifunze kuhimiza mahitaji yetu yazingatiwe na wenye maamuzi. Maoni yetu yasikilizwe na kufanyiwa kazi, tunu za Kikristo tunazozisimamia zionekane katika sera na katika mgawanyo wa bajeti ya Serikali. Hiyo ni sehemu ya nukuu kutoka katika moja ya nyaraka hizo. Kwa hali hiyo unaweza kupata picha kuwa l o l o t e l e n ye m a s l a h i n a Wa i s l a m u k u p i t i a Bungeni linapingwa kwa nguvu zote na wapingaji wa k u b wa wa k i wa n i hao hao, rejea matukio Bungeni mathalani, sakata la Mahakama ya Kadhi, Tanzania kujiunga na OIC kisha Serikali kufuta misamaha ya kodi kwa mashirika ya Kidini! Kisha tafakari nukuu hii kutoka katika ILANI ya Kanisa Katoliki, Lazima tujifunze kuhimiza mahitaji yetu yazingatiwe na wenye maamuzi. Ni nani hao wenyewe maamuzi, ndiyo tunarudi kule kule, viongozi wa Serikali za Mitaa, Mabaraza ya Madiwani, Wabunge n.k. Lakini pia angalia idadi ya Wachungaji waliongia Bungeni katika uchaguzi wa Mkuu 2010, lakini vipi kwa Waislamu kuna Masheikh wangapi, iwe wa kuchaguliwa au kuteuliwa! Waislamu nao kuelekea uchaguzi huo walitoa kitu kinachoitwa Muongozo. Akiongea katika uzinduzi wa Muongozo huo katika Viwanja vya Mnazi mmoja, Maalim Ally Bassaleh, alisema lengo lake ni kuwaelekeza Waislamu kupiga Kura ya Maslahi. Na hili linawezekana ikiwa kama kweli Wa i s l a m u wa t a a m u a kwa kuwa Waislamu ni wengi, kinachotakiwa ni umoja na mshikamano tu. Alibainisha Maalim Bassaleh. Sijui mkakati huo uliishiaje! Katika moja ya semina za Waislamu katika kukumbushana majukumu, Sheikh Amran Kilemile, alihimiza Misikiti iwe ni vituo vya kuwaandaa wanasiasa. Misikiti tumeitoa katika kazi yake, ndio maana leo haiwezi k u a n d a a wa n a s i a s a . Alisema Sheikh Kilemile. Prof. Malima, anasema Wa i s l a m u wa j i r a t i b u kisha wafanye kazi, kama Masheikh wakijipanga wanaweza kutumia Misikiti kuweka mikakati na kuratibu mambo ya Waislamu kisha yakaleta tija katika jamii. Mfumo wa Uislamu unawaweka Waislamu kukutana mara tano, Muislamu lazima aitikie wito wa adhana na afike Msikitini. Sasa vipi Imamu, ashindwe kuongea na waumini wake, akiwa na jukumu la kufikisha

SHEIKH Illunga Hassan Kapungu akiwa katika moja ya makongamano ya Waislamu yaliyofanyika Diamond Jubilee miaka ya hivi karibuni. (Picha kutoka Maktaba yetu)

Njia mpya kuelekea Iran


Hizbullah Vs Sunni Salafi Maangamizi kwa Waislam

Makala

RABIUL AWWAL 1435, IJUMAA JANUARI 31-FEB. 6, 2014

AN-NUUR

Na Omar Msangi

IJANA mmoja mwanaharakati, kwa uchungu kabisa huku akigugumia kwa kwikwi na kushindwa kuongea, alisimama muda mfupi mara baada ya kumalizika kisimamo cha usiku na kabla ya adhana ya swalat subhi, kueleza masikitiko yake, kwa nini vita inayoendelea Somali na Syria, inaitwa Civil War (Vita ya wenyewe kwa wenyewe) badala ya kuitwa Jihad. S i s i t u n a n ya n y u a mikono tunaomba, A l l a h u m a n s u r l-mujahidina Fi Somali, Syria, mtu anapigwa risasi ya kifua kwa ajili ya dini ya Allah, halafu mtu anasema ile ni Civil War!!... Kufika hapo kijana aliishiwa nguvu kabisa akashindwa kuongea. Wa t u wa l i o k u wa wamekaa mstari wa mbele wakamsaidia kukaa. Hiyo ilikuwa katika semina moja iliyofanyika hivi karibuni mkoani Kilimanjaro ambapo pamoja na mada nyingine, ilitolewa mada juu ya tahadhari. Ilikuwa ni katika mada hiyo, ilisisitizwa kuwa watu wawe makini na wachukue tahadhari wasije wakajiangamiza kwa mikono yao wenyewe. Civil War, ni neno la Kiingereza ambalo kwa Kiswahili maana yake ni vita ya wenyewe kwa weyewe. Syria wanapigana wanajeshi wa serikali, ambao ni Wasyria wakipambana na waasi ambao ni Wasyria pia. Somalia, pamoja na k u w e p o wa l e a s k a r i wa AMISOM ambao wanawasaidia askari wa serikali, lakini kimsingi wanaopigana ni askari wa Somalia, ambao ni Wasomali na Al Shabab, ambao ni Wasomali pia. Kwa upande mwingine, Al Shabab wanapambana na Hizbul Islami na Ahlu Sunna Wal Jamaa ambao ni Wasomali pia. Hata hivyo, hilo halikuwa ndio suala la msingi. Hoja ilikuwa juu ya tahadhari katika kufanya Dawah na Jihad.

Mwaka 1971 vijana waliokuwa wamevalia k a m a Wa p a l e s t i n a , kimavazi na lugha ya Kiarabu ulikuwa huna n a m n a ya k u wa k i s i a kuwa sio Wapalestina, walijitambulisha kwa m p i g a n a j i m m o j a wa Kipalestina katika Gaza wakijitambulisha kuwa wao ni wapiganaji wa Kipalestina wa kundi la Popular Front for the Liberation of Palestine (PFLP) kutoka tawi la Kambi ya Wakimbizi wa Kipalestina Lebanon. Wakiwa na vitambulisho vya kughushi, walidai kuwa wametumwa na Kamanda Abu Seif waje Gaza kukutana na makamanda wa PFLP katika Kambi ya Beth Lahia (Kusini mwa Ukanda wa Gaza). Asubuhi iliyofuata wageni hawa kutoka Lebanon walikutana na kikosi cha watu kadhaa kutoka Beth Lahia katika nyumba moja ya siri. B a a d a ya wa t u w o t e waliokusudiwa kufika na kuchukua nafasi zao katika viti, mgeni mmoja kutoka Lebanon alinyanyua mkono na kutizama saa yake ya mkononi. Ghafla risasi zikarindima, wapiganaji wote wa Beth Lahia, wakauliwa. Ta r a t i b u n a k w a tahadhari kubwa, wageni wale wakatoka katika nyumba ile wakaingia katika vichochoro vya mitaa ya Gaza wakapita njia za panya na kuingia Israel. Jioni ile Kapteni Meir Dagan, aliyekuwa Kamanda wa kikosi maalum cha siri (secret Rimon Commando Unit) katika jeshi la Israel (IDF) akaripoti kwa Generali Ariel (Arik) Sharon kuwa Operation Chamelion (Operesheni Kinyonga), imefanikiwa. Viongozi wote wa Popular Front katika Beth Lahia, wameuliwa. Huu ni mfano tu wa m a t u k i o a m b a y o yanaonyesha nafasi ya tahadhari, na hasa katika kupigania haki na kupigania dini ya Allah a m b a y o i n a a n d a m wa na maadui wengi katika

KIJANA wa Kiislamu (mwenye kofia) akitoa Da'awah nje ya Msikiti nchini Ufaransa. Manasara na Mayahudi, inavyotokea baina ya Al ya mwaka 2009 iliyopewa tunaowajua na tusio wajua. Shabab na Hizbu Islamia, jina, "Which Path to Persia?" Labda kabla ya kwenda S o m a l i a a u b a i n a ya Ukisoma, Which Path m b e l e n i t o e n u k u u makundi ya Jihad katika to Persia: Options for a ifuatayo: Syria). new American Strategy In my opinion, there is a Wakati ule Nasrallah Toward Iran (Analysis huge campaign through the a k i t o k a m a o n i ya k e , Paper Number 20, June 2009) media throughout the world ndio zilikuwa zikipamba inaelezwa kuwa: to put each side up against the moto zile harakati za Kinachotafutwa katika other (to deliberately instigate kulipuliwa misikiti Iraq. vurugu na kelele zote juu fitna). I believe that all this is Leo unalipuliwa wa Shia, ya Syria na Iran, ni Western being run by American and wanakufa makumi ya hegemony across the Middle Israeli intelligence. watu wasio na hatia. Kesho East, with Saudi Arabia Maneno haya yalisemwa unalipuliwa wa Sunni, and Israel the principle dual na kiongozi wa Hezbullah wa n a k u f a Wa i s l a m u . benefactors. Hassan Nasrallah, mwaka Bila kutafakari kwa nini, Kwamba Marekani na 2007 wakati akifanya Waislamu wakajengeana Ulaya ziendelee kuzidhibiti mahojiano na mwandishi chuki na visasi. Leo kila nchi za Mashariki ya Seymour Hersh. uchao ni mauwaji Iraq. Kati huku Israel nayo U n a p o z u n g u m z i a Shia wanauwana na Sunni, ikinufaika. Saudi Arabia f i t n a m a a n a y a k e jambo ambalo halikuwepo n a y o i m e t a j wa k u wa kwa Kiingereza kama kabisa wakati wa Saddam i t a n u f a i k a ! ! ! ! K i v i p i ? alivyoiweka mwandishi Hussein. Labda kwa kuhakikisha Hersh katika makala yake Labda niseme kuwa kuwa ufalme unadumu na ni: kwa jinsi alivyokuwa hakuna wa kuutikisa! i n s u r r e c t i o n a n d na uchungu kijana yule Seymour Hersh akieleza fragmentation within Islam. k u t o k a Ta n g a k a t i k a kinachoendelea Syria hivi U f u p i w a m a n e n o semina ile ya Wilayani sasa, kilipotokea mwaka n i u p i n z a n i w a Same, ni wazi kuwa ule 2007 na malengo yake, k u u v u n j a v u n j a n a mpango wa George W anasema, ili kuidhoofisha kuuangamzia Uislamu Bush, umefanikiwa kwa Iran, serikali ya Bush k u t o k e a n d a n i . K wa kiwango kikubwa sana na iliamua kushirikiana na maana ya kutumia mikono unaendelea kuwanufaisha Suni wa Saudi Arabia ya Waislamu kujiangamiza maadui wa Uislamu na k u a n d a a m i p a n g o ya wenyewe. kwa upande mwingine h u j u m a ( c l a n d e s t i n e N a s r a l l a h k a m a kuwaangamiza Waislamu operations) iliyokusudiwa alivyofafanua, alituhumu na nchi za Waislamu. kuidhoofisha Hizbullah, uongozi wa Rais Bush inayoungwa mkono na k wa m b a wa k a t i h u o Kinachotafutwa Syria sio Iran. ulikuwa ukiandaa mpango Khilafah wala demokrasia Akasema kuwa katika wa fitna ambao lau K w a w a n a o p e n d a clandestine operations hizo, utafanikiwa utaleta balaa kujua ukweli wa mambo, ikawekwa mikakati ya kubwa kwa ummah wa watizame makala ya Hersh kuwatumia Mujahidina Kiislamu: katika gazeti la New Yorker wa Kisuni waliojazwa Kwanza utawafanya (2007) ikisema: f i k r a n a k u c h o c h e wa Waislamu kupambana "The Redirection: Is the kuwa hakuna namna ya wenyewe kwa wenyewe Administration's new policy kufanya mashauriano baina ya Shia na Sunni na benefiting our enemies in the na Ulaya/Marekani, ila pili hata Sunni kwa Sunni war on terrorism?" Jihad. Na kwa upande watakuwa wakipambana Watizame pia ile ripoti mwingine, mujahidina na kuuwana pia (kama ya taasisi ya Brookings Inaendelea Uk. 10

Makala

RABIUL AWWAL 1435, IJUMAA JANUARI 31-FEB. 6, 2014


Anasema siku moja mwaka 1991, kwa mara ya kwanza ndio alikuja kufahamu kuwa kumbe Waislamu wanamkubali Yesu, kuwa ni Mtume wa Mungu na kwamba alizaliwa kimiujiza bila ya Baba na kwamba Mama yake alichukua mimba kwa neno la Mungu. Anasema hiyo ilikuwa jambo la kustua kwa sababu alichojua ni kuchukia kila kitu Islam na Muslim na kwamba hawana jema lolote. Kwa upande wa baba yake, naye alikuwa mfuasi mzuri wa Ukristo na akipenda kusikiliza vipindi vya TV na mahubiri vya wahubiri kama Jimmy Swaggart, Jim and Tammy Fae Bakker, Jerry Fallwell, John Haggi na Pat Robertson. Huyu Pat Robertson, anasifika kuwa ndiye adui mkubwa kabisa wa Uislamu katika Marekani na duniani kote. Pamoja na yeye mwenyewe kusikiliza mahubiri ya watu hawa, baba yake alifanya kazi ya kuzisambaza kwa watu wengine kupitia biashara zake na kama sadaka yake. Ilitokezea kuwa mwaka h u o 1 9 9 1 b a b a ya k e alikutana na Muislamu kutoka Misri na akawa anafanya biashara naye. Akiona kuwa anawajibu wa kumuingiza katika wokovu, mzee alimwomba Skip akutane na Muislamu huyu aanze kumpa dozi kumvuta katika Ukristo. H a t a h i v y o , kilichomshangaza kulingana na matarajio ya k e , a l i p o k ut a na na Muislamu huyo, hakuwa amevaa kanzu, hakuwa na madevu wala kuonyesha dalili yoyote ya ukatili kama alivyoaminishwa. Unamuamini Mungu, alimuuliza ambapo jawabu lilikuwa ndio. Unaamini kuwa asili ya mwanadamu ni Adam na Eva? Mmisiri akajibu ndio. Kisha anasema akamuuliza juu ya manabii kama Ibrahimu, Musa, Daud, Ismail, Yacob na kisha kuja alikolenga. Unamuamini Yesu? Jibu likawa ndio. Zaidi ya majibu hayo ambayo hakuwa ameyatarajia, lakini aliona kitu cha ziada kwa Muislamu huyu. Upole, adabu, ukarimu na maadili mema kwa u j u m l a , ya l i k u wa ya Inaendelea Uk. 12

AN-NUUR

uyu ni Skip Estes mwanamuziki wa kwaya za Kanisa na mhubiri kutoka Texas. Yeye anasema, kiukweli kabisa alikuwa Mkristo mchamungu "dedicated Christian" and a good 'ole boy from Texas. Kama walivyo watu kama yeye katika Marekani, Skip anasema, alichukia kila kilichonasibishwa na Uislamu. Aliaminishwa na akaamini kuwa Waislamu hawaamini Mungu, wanaabudu Jiwe Jeusi huko jangwani, Makkah, ni magaidi wauwaji, ila tu wanabusu ardhi mara tano kwa siku kabla ya kulipua watu katika harakati zao za kufanya ugaidi na kuteka nyara watoto na wanawake. Ni kama ada kwamba ukiwa Mkristo Muamerika, n i l a z i m a u wa c h u k i e Wa i s l a m u n a u a m i n i kuwa ni magaidi, ndivyo alivyojieleza Skip. Akiwa na miaka 70 sasa, Skip Estes alioa na kutaliki, kisha akaoa tena na ana watoto 5. Kutokana na shughuli zake za mahubiri na biashara, amesafiri sana takriban majimbo yote ya Marekani na nje hapo. Nchi alizotembelea ni pamoja na Monaco, the Grand Bahamas, Canada, Mexico, France, Germany, England, Italy, Sweden, Denmark, Holland, Ireland, Germany, na Austria. Akijieleza mwenyewe alivyosilimu, Skip anasema mara nyingi watu wanamuuliza inakuwaje mhubiri na mchungaji wa K i k r i s t o k u b a d i l i dini na kuwa Muislamu, hasa ikizingatiwa jinsi Uislamu na Waislamu wanavyopakwa matope n a k u c h u k i wa k a t i k a ulimwengu wa Ulaya na Marekani unaochukuliwa kuwa ndio ulimwengu wa Wastaarabu? Skip, kwa sasa Yusuf Estes alizaliwa katika familia ya Kikristo Midwest. Kutoka enzi za mababu zake na kutokana na imani yao thabiti katika Ukristo, wamejenga makanisa na shule za Kikristo katika maeneo mbalimbali katika Jimbo lao. Akiwa katika umri wa kuanza shule ya msingi, walihamia Houston, Te x a s ( 1 9 4 9 ) a m b a p o aliendelea na masomo ya dini (Sunday school) na kubatizwa akiwa na umri wa miaka 12. Katika ujana wake, Skip anasema alijawa na kiu ya

Skip Estes kutoka Texas alivyosilimu

Skip Estes kusoma na kujua zaidi juu ya Mungu na Kanisa kwa hiyo alisoma maandiko na kuhudhuria mahubiri ya makanisa mbalimbali yakiwemo Baptists, Methodists, Episcopalians, Charismatic movements, Nazarene, Church of Christ, Church of God, Church of God in Christ, Full Gospel, Agape, Catholic, Presbyterian n.k Lakini pia alisoma na kupata ufahamu juu ya Hinduism, Judaism, Buddhism, Metaphysics na imani za Waamerika wa asili (native American beliefs). Hata hivyo anasema, pamoja na kiu hiyo ya kumjua Mungu na Neno la Mungu, lakini hakusoma juu ya Uislamu. Alipenda muziki na hivyo kuwa muhubiri na kiongozi wa kwaya na muziki wa kanisa. Katika miaka ya 1960s alikuwa akifundisha upigaji k inanda na h atimaye kuanzisha studio yake ya muziki aliyoipa jina Estes Music Studios kule Laurel, Maryland. Kwa zaidi ya miaka 30 Skip Estes alikuwa a k i f a n ya b i a s h a r a n a baba yake katika eneo la burudani, na hasa muziki pamoja na studio wakiwa na maduka ya kuuza vifaa vya muziki na kuandaa program mbalimbali za starehe kutoka Texas na Oklahoma hadi Florida. I made millions of dollars in those years, but could not find the peace of mind that can only come through knowing the truth and finding the real plan of salvation. I'm sure you have asked yourself the question; "Why did God create me?" or "What is it that God wants me to do?" or "Exactly who is God, anyway?" "Why do we believe in 'original sin?" and "Why would the sons of Adam be forced to accept his 'sins' and then as a result be punished forever. But if you asked anyone these questions, they would probably tell you that you have to believe without asking, or that it is a 'mystery' and you shouldn't ask. Anasema Skip Estes kwamba kutokana na biashara hizo, alipata faida ya mamilioni ya dola, lakini kamwe hakuwa na furaha ya maisha. Hii ni kwa sababu alikuwa akijiuliza maswali ya msingi ambayo hakuwa akipata majibu sahihi. Maswali yenyewe ni kama, nani Mungu, kwa nini nimeumbwa. Kilichomtatiza zaidi anasema ni dhambi ya asili. Kwanini dhambi ya asili. Kwa nini mtu aadhibiwe kwa dhambi ya asili? Ukiuliza sana unaambiwa hilo ni fumbo takatifu unachotakiwa ni kuwa na imani! And then there is the concept of the 'Trinity.' If I would ask preachers or ministers to give me some sort of an idea how 'one' could figure out to become 'three' or how God Himself, Who can do anything He Wills to do, cannot just forgive people's sins, but rather and had to become a man, come down on earth, be a human, and then take on the sins of all people. Keeping in mind that all along He is still God of the whole universe and does as He Wills to do, both in and outside of the universe as we know it. Hiyo tisa, kubwa yake anasema ni ile imani ya Utatu Mtakatifu. Anasema kadiri alivyouliza maaskofu, mapadiri na wachungaji, huyu Mungu mmoja, anakuwaje watatu na hawa watatu wanakuwaje mmoja, walikwama kumpa jibu la kutoshekeza akili yake. L a k i n i p i a a l i k u wa akihoji, huyu Mungu muweza wa kila kitu, Muumba wa vitu v y o t e , a n a s h i n d wa j e kuwasamehe watu wake waliomkosea mpaka alazimike kujishusha ajivike mwili wa kibinadamu (na wakati huo huo ni Mungu) ili ateswe apate uchungu wa kibinadamu, kwa dhambi ambayo haukuitenda Yeye, ili iwe ndio kafara ya watu waovu!!!

10
Inatoka Uk. 8 hao hao watumike kuwapiga Mashia huku Mashia nao wakitumika kuwapiga Sunni. Lakini wakati huo huo, Marekani wanawatangaza hawa mujadina kuwa ni magaidi na kupinga mpango wao wa kuweka serikali ya Kiislamu. Sasa Muislamu leo akisikia kila anayepigwa vita na Marekani na kuitwa gaidi, yeye anaona huyo ndiye Mujahidina, kumbe ni wakala wa proxy war. Kwa namna hiyo, Waislamu Sunni wataona makundi haya kama alNusra Front, ni Mujahidina wanaopigana Syria kuwangoa Shia-Alawites ili kusimamisha Khilafah, hivyo watawashabikia na kuwaunga mkono. (The Redirection, Seymour Hersh) Katika kutimiza lengo hilo Hersh anasema, ilikubaliwa Saudi Arabia (na Qatar ) watumiwe kuandaa wapiganaji (Mujahidina) ambao watapambanishwa na majeshi ya Rais Bashar Assad. Lakini ukifanya hivyo, utakuwa pia umewaingiza Hizbullah katika vita, kwa sababu Hizbullah (Lebanon) na Shia, Iran, wataingia vitani kuwatetea Shia, Syria dhidi ya wapiganaji Sunni wanaoandaliwa na kufadhiliwa na Saudi Arabia. Katika vita kama hii, kadiri itakavyoachwa kuchukua muda mrefu, itaidhoofisha Syria kijeshi na kidiplomasia ya kimataifa, kwa hiyo, haitakuwa tena na uwezo wa kukabiliana na Israel katika medani ya kisiasa au kijeshi. Na kweli, hivi sasa inaripotiwa kuwa Israel imeingia Syria na kutoa v i b a l i v ya u c h i m b a j i mafuta katika milima ya Golan, eneo ambalo ni la Syria. Israel imetoa vibali hivyo kwa makampuni ya Murdoch na Rothschild. "Israel has granted oil exploration rights inside Syria, in the occupied Golan Heights, to Genie Energy. Major shareholders of Genie Energy which also has interests in shale gas in the United States and shale oil in Israel include Rupert Murdoch and Lord Jacob Rothschild.

Makala

RABIUL AWWAL 1435, IJUMAA JANUARI 31-FEB. 6, 2014


ya miji na makazi ya watu. Lakini mwandishi Tony Cartalucci anasema kuwa hili ndilo lililokuwa limetarajiwa wakati Marekani, Israel na Saudi Arabia wakiweka mkakati wa kuandaa vikundi vya wapiganaji wa Kissuni na kuwatia chuki dhidi ya Mashia. Haya ndiyo yaliyotarajiwa katika hii Proxy War. Kwamba Mujahidina watauwa watu wakiamini kuwa hiyo ni vita halali ya kusimamisha Khilafah! Anasema Cartalucci kuwa leo Marekani na washirika wake kupaza sauti ya masikitiko na kulani kuwa kuna maafa ya kibindamu au uhalifu wa kivita Syria, ni unafiki mkubwa, kwa sababu nd i v y o i l i v y o p a ng wa iwe toka mwanzo. Na waliopanga walijua kuwa hayo yatatokea lakini maadhali lao linatimia, k u f a wa t u h a t a k wa mamilioni hilo kwao ni collateral damage tu. Kama ilivyotangulia k u s e m w a , kinachowashughulisha mabeberu ni udhibiti wa Mashariki ya Kati. Kwamba hadi sasa wameshafanikiwa kuifanya shamba lao la bibi. Lakini wana wasiwasi kuwa Iran ikishikamana na Syria pamoja na Hizbullah katika Lebanon, wanaweza kubadili mambo. Kwa hiyo kinachofanyika kwa sasa ni kuharibu nguvu hiyo na kuondoa kabisa uwezekano wa kuibuka nguvu ya kuweza kuhatarisha maslahi ya mabeberu katika Mashariki ya Kati. Kwa mtindo wa yule kijana kulia, akiambiwa kuwa kupigana na Bashar Assad sio Jihad, au kwa mawazo kama ya baadhi ya wasomaji kudai kuwa vita ya Syria ni Jihad ya kusimamisha Khilafah, ndio ujinga na upofu anaousikitikia Tony Cartalucci. Kwamba utaendelea kuwaangamiza Waislamu. Namna pekee ya kupata nusra, ni kutambua mchezo huu Waislamu wanaochezewa, wakawazomea na kuwakataa mawakala wanaotumiwa.

AN-NUUR

Njia mpya kuelekea Iran


Ndivyo anavyoarifu Craig Murray ( January 22, 2014). Israel kutaka kuchimba mafuta na madini katika Milima ya Golan (the occupied Golan Heights), ni kinyume kabisa na sheria za kimataifa. Awali Israel ilijaribu kufanya siasa kali na mapambano kwa vikundi vya Kiislamu dhidi ya Israel na Magharibi, kwa upande mwingine ni vikundi hivyo vinavyoitwa vya kigaidi na Marekani na Ulaya, na katika vita kama hii ya Syria; ni vikundi hivyo hivyo vinavyotumika zimetumika kuwasaliti mamilioni ya Waislamu kwa kuwatumia hawa mujahidina kufanya vita (kama ya Libya) ambayo mwisho wa yote ni kuangamzia nchi za Waislamu. Tony Cartalucci anamnukuu mmoja wa

MMOJA ya vikosi vya Kiislamu vinavyopigana Somalia. hivyo miaka 20 iliyopita, lakini serikali madhubuti ya Syria ik a pin g a na ikapata kuungwa mkono na jumuiya ya kimataifa ikashinda. Hata Marekani wakati ule haikuweza kuihami Israel katika dhamira yake ya uporaji. Lakini kwa fursa hii ambayo imepata baada ya Mujahidina kutumiwa kupigana Proxy War ya mabeberu na kudhoofisha serikali Syria, Israel inaona s a s a k u wa n i wa k a t i muafaka na fursa nzuri kwenda mbio kuanza kuvuna mafuta katika milima ya Golan. Sisi huku tunasubiri na tunatamaa kuwa akingoka tu Bashar Assad, Khilafah inasimama Syria! Katika hali ya kusikitisha Seymour Hersh anasema kuwa wakati baadhi ya nchi za Kiarabu zikijifanya zinaichukia Israel na nchi za kibeberu, kwa mlango wa nyuma nchi hizo hizo zinatumika kwa masilahi ya I s r a e l n a n c h i z a Magharibi. Anasema zinatumika kwa namna mbaya kwa sababu zinaunda vikundi vya Kijihad, zinapandikiza hisia za kupigana na jeshi la Syria kama vilivyotumika kupigana Libya. Ni hali ya kusikitisha k wa s a b a b u a n a s e m a inaleta maafa makubwa kwa Waislamu na watu wengine wasio na hatia kama ambavyo raia wa Syria hivi sasa wanateseka na vita ambayo haitanufaisha Syria bali kuiangamiza. Katika makala yake, 2007 New Yorker Article Exposed US-Israeli-Saudi Conspiracy to Overthrow Assad, mwandishi na mchambuzi Tony Cartalucci, anasema kuwa japo ni mbinu ya tangu zama iliyotumiwa na watawala kuwa ukitaka kuwashinda na kuwatawala watu, uwagawe, lakini baadhi ya nchi za Kiarabu zinatumiwa vibaya mno. K wa m b a s i a s a k a l i wanaodaiwa kuwa virusi hatari kwa ustaarbu wa Magharibi, hali iliyozaa vita dhidi ya ugaidi, waliandaliwa na wanapepewa kuendelea kuwepo kwa mpango maalum. Na kwamba baadhi ya nchi za Kiarabu m a k a c h e r o wa S a u d i Arabia akiihakikishia Marekani kuwa wasiwe na wasiwasi na hawa siasa kali na wana-Jihad. Unajua kwa nini? Anasema: Kwa sababu wameyaunda makundi hayo yanayopigana Syria na yaliyokuwa Libya na ni wao wanaoyapa fedha na silaha, hawatashindwa kuyadhibiti. Na kwamba hata kama watafanya v i t e n d o v i n g i n e v ya kigaidi wasivyotumwa na wafadhili wao, lakini ilimuradi hawa Mujahidina wanarusha mabomu kuwapiga Mashia, Hezbollah, Moqtada al-Sadr, Iran, na kwa Syria, kama itaendelea kushirikiana na Hezbollah na Iran, sio tatizo. (-The Redirection, Seymour Hersh.) Hivi sasa nchi za Magharibi, na hasa Marekani, pamoja na Umoja wa Mataifa, wanakuja juu kuishutumu serikali ya Syria kuwa inafanya mauwaji kwa raiya. Jumuiya za kimataifa nazo zinatahadharisha juu ya maafa na janga linaloadamana na mauwaji ya halaiki na maangamizi

11

ASJID Sahaba, katika jiji la Paris, Ufaransa umekuwa maarufu kwa k u p o k e a Wa i s l a m u wapya, kiasi kwamba sasa unaitwa Msikiti wa Waliosilimu (the mosque of the converts). K i l a m wa k a k a t i k a msikiti huo ulio katika eneo la Crteil, Paris, kumekuwa kukifanyika tafrija zaidi 150 za kupokea Waislamu wapya waliosilimu kutoka Ukristo. Msikiti huo uliojengwa mwaka 2008 ukiwa na mnara (minaret) wenye futi 81, ni moja ya alama kuwa Uislamu unakuwa kwa kasi Ufaransa. Inaelezwa kuwa katika mamia ya watu wanaofurika hapo siku ya Ijumaa kwa swala, ni vijana ambao awali walikuwa Wakatoliki wakasilimu. Kwa sasa wanaonekana wakiwa wamevaa kanzu na kofia. Wachambuzi wa siasa za Ufaransa wanasema kuwa hali hii ya kusilimu raia wa nchi hiyo, japo haiwezi kusemwa ni kubwa sana ikilinganishwa na idadi ya Wakristo wa nchi hiyo, lakini inatoa changamoto kubwa kutoka kwa serikali na jamii ya Ufaransa k wa u j u m l a a m b a y o imeonyesha chuki kubwa kwa Uislamu. Ni kutokana na hali hiyo, makachero wa Ufaransa walio katika kikosi cha kupambana na ugaidi, wanajaribu kutoa kitisho juu ya hali hiyo kama njia ya kuichochea serikali kuchukua hatua kali ili kuepukana na ugaidi unaodaiwa kuwa utaletwa na kuongezeka kwa idadi ya Waislamu raia. Wanajenga hoja kuwa kupambana na magaidi wa nje ni jambo jepesi kwa sababu unaweza kuwazuiya wasiingie, lakini hawa wanaozidi kusilimu watakuwa ni raia wenye hati za kusafiria za Ufaransa. M wa k a j a n a p o l i s i waliendesha operesheni waliyo dai ya kusaka magaidi walikamatwa watu 12 wakiwemo raia wawili wa Ufaransa waliosilimu siku za karibuni. Kwa upande mwingine inadaiwa kuwa magereza ya nchi hiyo yamekuwa kama shule za kusilimishia watu kutokana na rekodi ya kusilimu watu wengi wakitokea gerezani. Inadaiwa kuwa pamoja na uchache wao katika n c h i h i y o , Wa i s l a m u

Kasi ya kusilimu Ufaransa

Makala/Tangazo

RABIUL AWWAL 1435, IJUMAA JANUARI 31-FEB. 6, 2014


imeongezeka mara dufu ikilinganishwa na miaka mitatu iliyopita ambapo kwa mwaka 2012 watu 130 walisilimu. Hiyo ni kwa mujibu wa taarifa ya Abderrahmane Ghoul, a m b a ye n i I m a m wa msikiti wa Marseille na Rais wa tawi la French Council of the Muslim Faith. K wa u p a n d e wa k e Hassen Chalghoumi, I m a m wa m s i k i t i wa Drancy, moja ya viunga vya jiji la Paris, anasema zile sera na misimamo ya usekula katika kuendesha mambo ya kiserikali na kijamii, huzaa ombwe la mambo ya kiroho na hivyo kuwafanya watu kukimbilia katika Uislamu ambao unaonekana kuwa ndiyo dini inayoishi ndani ya familia na katika mambo ya kijamii. Rafaello Sillitti, mmoja wa raia wa U f a r a n s a a l i ye s i l i m u anasema changamoto kubwa inayowakabili ni kuwaonyesha Wafaransa kuwa hakuna tatizo kuwa Mfaransa na ukawa Muislamu. Hakuna mgongano baina ya Ufaransa na Uislamu bali Muislamu ndiye Mfaransa mzuri. Lazima tufute haya mawazo ya kufikirika kuwa Uislamu ni tatizo. Tuonyeshe kuwa utamaduni wa Ufaransa unaweza kuishi pamoja na Uislamu kwa amani.

AN-NUUR

Masjid Sahaba, katika jiji la Paris, Ufaransa ndio waliojazana katika magereza ikiwa ni zaidi ya theluthi ya wafungwa wote na kwamba wakiwa huko ndani hugeuza jela kuwa uwanja wa kusilimisha na kupandikiza siasa kali za Kiislamu. Hivi sasa inakadiriwa kuwa idadi ya Waislamu Ufaransa ni kiasi milioni 6 (kati ya watu milioni 65) ambapo kiasi laki moja (100,000) wanadaiwa ni wa kusilimu. Hii ikiwa ni takwimu rasmi ya kiserikali, taasisi za Kiislamu zinasema kuwa waliosilimu ni zaidi ya 200,000. Huko nyuma, watu wengi walisimu kupitia n d o a . K wa m b a k a m a ni msichana alipata mchumba Muislamu na akakubali kusilimu na kinyume chake, lakini hivi sasa wengi wanasilimu kwa kuangalia maadili na hali za maisha ya Waislamu. Anatajwa kijana CharlieLoup, wa shule ya kanisa, St.-Maur-des-Fosss, aliye na miaka 21 sasa, ambaye alisilimu akiwa na umri wa miaka 19 baada ya kugombana na mama yake. Huyu alilelewa katika Ukatoliki, lakini akiwa na marafiki wengi Waislamu akiwa shuleni. Katika maeneo mengi yenye Waislamu wengi inaelezwa kuwa vijana wenye marafiki Waislamu hufikia nao kufunga mwezi wa Rmadhani, japo si Waislamu katika kile kinachoitwa athari ya makundi (the group effect). Kwa wengi wanaMagharibi, Uislamu ndio mfumo wanaoona utawarejesha katika maadili ya kifamilia na kijamii ambapo haki za wa n a wa k e n a wa t o t o z i t a z i n g a t i wa , l a k i n i ikizingatiwa pia tofauti ya m k e n a m u m e n a majukumu yao katika familia. Katika mji wa Marseille, idadi ya wanaosilimu

MASJID Kadiria Mwasiti uliopo Kijiji cha Kibuta Wilayani Kisarawe Mkoani Pwani wanaomba msaada wa k u c h i m b i wa k i s i m a katika Msikiti huo pamoja na Jenereta kwa ajili ya kusukuma maji kwa matumizi ya Msikitini. Gharama za uchimbaji wa k i s i m a h i c h o n i Shilingi milioni tatu. Dada Mwasiti amejitahidi kuchangisha pesa kwa ajili ya kuchimba kisima hicho na mpaka sasa a m e f a n i k i wa k u p a t a milioni moja tu. Shime Waislamu kutoa n i m o y o , u n a o m b wa kuchangia chochote ulichojaaliwa na Muumba wako kwa ajili ya kuweka akiba ya Akhera yako. Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na Dada Mwasiti kupitia namba:0656 092 436. Wabillah Tawfiq

Msaada wa kuchimbiwa Kisima

DADA Mwasiti (kulia) akiwa na wanafunzi wa Madrasa katika Masjid Kadiria Mwasiti Kibuta Kisarawe.

12

Mashairi/Makala

RABIUL AWWAL 1435, IJUMAA JANUARI 31-FEB. 6, 2014

AN-NUUR

POLENI KWA MAFURIKO


Inna lillahi wa inna, ilayhi rajiuna Kauli ya Maulana, si yangu ninayenena Misibani kuinena, katuamuru Rabbana Poleni kwa mafuriko, ndugu zetu Morogoro. Rambirambi waungwana, ada yao kupeana Japo kwa neno kunena, la 'POLE' kuliwazana Adhimu na la maana, si dogo kwa Subhana Poleni kwa mafuriko, ndugu zetu Morogoro. Nami nanyi naungana, japo kwa 'POLE' kunena Wazee pamwe vijana, wa Mbigili na Mabana Aimi ! Poleni sana, kwa janga la wiki jana Poleni kwa mafuriko, ndugu zetu Morogoro. Thumma akali naona, kunenanyi budi sina Vyema tukakumbushana, Qadari ya Subhana Kwa kuwa tumeiona, kwa macho yetu bayana Poleni kwa mafuriko, ndugu zetu Morogoro. Hatupaswi kulumbana, au hata kusonona Akadirilo Rabbana, wa kuliepa hakuna Maafa ya wiki jana, yote Qadari ya Bwana Poleni kwa mafuriko, ndugu zetu Morogoro. Wapo wanaoikana, na hasa washirikina Eti ! Qadari hakuna, kwa vinywa vyao hunena Chambilecho Maulana, kweli nadhari hawana Poleni kwa mafuriko, ndugu zetu Morogoro. Adayo kushikamana, leo, kesho hata jana Na ya upogo imana, na ya Muumba kukana Kwao bora ya insana, kuliko ya Maulana Poleni kwa mafuriko, ndugu zetu Morogoro. Kwetu lisowezekana, sahali kwa Maulana Si sawia kuikana, Qadariye Subhana Apangalo Maulana, wa kupangua hakuna Poleni kwa mafuriko, ndugu zetu Morogoro. Niwombe ajimaina, ya kheri kutakiana Pamwe kuauniana, pasipo kubaguana Sote wa Adamu wana, viumbe wa Subhana Poleni kwa mafuriko, ndugu zetu Morogoro. Allahuma Rahmana, nakuomba Maulana Wajazi muuminina, pamoja waloungana Swadaka kuzitayana, Magole bila khiyana Poleni kwa mafuriko, ndugu zetu Morogoro. Lengo si mengi kunena, bali 'POLE' kupeana Thumma na kukumbushana, QADARI ya Subhana Na DUA kuombeana, kwa Rabbul-alamina Poleni kwa mafuriko, ndugu zetu Morogoro. Mazidadi mimi sina, ya kunena kwenu tena Kwa utashi wa Molina, asaa tutaonana Kuagana uungwana, kwaherini waungwana Poleni kwa mafuriko, wa Magole Morogoro. ABUU NYAMKOMOGI - MWANZA.

Skip Estes kutoka Texas alivyosilimu


Inatoka Uk. 9 kuvutia ikiwa ni kinyume kabisa na waliyojazwa vichwani kuwa Waislamu ni magaidi, wateka nyara, wauwaji na watu wasio mjuwa Mungu. Wakati huo Mmisri huyu alikuwa akikaa pamoja na familia ya Estes, kwa sababu ilikuwa yeye akifanya kazi mchana usiku anakwenda kulala Msikitini, ndio Estes akamwomba baba yake kuwa wakae naye katika nyumba yao kwa sababu ina nafasi. Estes akikaa na mkewe, baba yake na mama yake wa kambo. Kadiri walivyokaa na Mohamed na kusafiri naye katika shughuli za kibiashara, ndivyo alivyojifunza mengi juu ya maadili mema ya Kiislamu ambayo Mohamad alikuwa akiyaonyesha kwa vitendo na sio kwa kuigiza, bali ilikuwa ndio m we n e n d o wa k e wa maisha. Ilitokezea siku moja wakati Skip Estes na Mohamed wakiwa hospitali kuangalia wagonjwa walikutana na mgonjwa mmoja aliyeonyesha dalili ya kuchanganyikiwa akiwa katika kigari/baiskeli ya wa g o n j wa . B a a d a ya mazungumzo ya kumfariji ambapo Estes a limh u b iria k is a ch a Nabii Noa (Nuhu), yule mtu alimshukuru sana kwa kumfariji na kumpa matumaini ya maisha na akataka kuungama makosa yake mbele yake. Mtu yule kumbe awali alikuwa kasisi wa Kikatoliki na alifanya kazi za kanisa kwa zaidi ya miaka ya 12 Mexico na nchi mbalimbali za Amerika ya Kusini pamoja na New York, ndani ya Marekani. Alipopona, siku ya kutoka hospitali alimwomba akapumzike nyumbani kwake kabla ya kurejea kwake. Ilikuwa ni katika mazungumzo ya o ya k i d i n i , E s t e s alimwambia kasisi huyu juu ya yale aliyogundua juu ya Uislamu kupitia kwa Mohamed. Kasisi yule akamchosha zaidi alipomwambia kuwa hayo wao wanayasoma katika kozi zao katika vyuo vya kikatoliki inabidi wasome na Uislamu kujua unasema nini. Ikawa sasa mjadala ukawa juu ya mafundisho halisi ya Uislamu, U i s l a m u wa n a o u o n a k w a M o h a m e d Vs yale wanayopigwa propaganda kupitia vyombo vya habari na wachungaji. Kuwepo kwa kasisi wa Kikatoliki na Mohamed, k u l i f a n ya n y u m b a n i kwa Estes kuwa mahali pa darasa duara la kila siku. Baba atakuja na Biblia yake anayoipenda, King James Version of the Bible, wakati Yusuf yeye hupenda Revised Standard Version of the Bible. Mke wa Estes naye anakuja na yake, mara nyingi akichukua Jimmy Swaggart's 'Good News For Modern Man." Kisha Kasisi naye atakuja na Biblia ya Kikatoliki yenye vitabu 7 zaidi ya ile ya Protestanti (Catholic Bible which has 7 more books). Siku mmoja mjadala ukawa, Biblia ipi sahihi kati ya hizi zote na wakawa wanatizama zile tofauti za msingi. Wakajiuliza, kama watafanikiwa kumshawishi Mohamed kubadili dini, watampa Biblia ipi? Ya Kikatoliki, King James au Revised Standard Version of the Bible? Kufika hapo wakamuuliza Mohamed, nyinyi katika Uislamu mna aina ngapi au matoleo mangapi (version) ya Quran? Moja tu. Likawa ndio jibu. Kwamba Quran iliyopo leo ndio ile ile iliyokuwepo miaka 1,400 iliyopita, haijawahi kufanyiwa marekebisho na kufanyiwa toleo jipya. Na hata lugha haijabadilika. Ni Kiarabu kile kile alichotumia Mtume Muhammad (s.a.w) wakati akiipokea kutoka kwa Mungu. Na zaidi akawaambia kuwa hata kama zitakusanywa Quran zote zichomwe moto, kuna mamilioni ya watu wamehifadhi Quran yote harufu kwa harufu nukta kwa nukta. Kwa upande mwingine ikaoneshwa kuwa licha ya kuwepo matoleo mbalimbali ya Biblia, lakini hata ile lugha ya asili ya Yesu au ile lugha ya asili iliyoandikiwa Biblia, ilishakufa. Kwa hiyo ni vigumu kupata tafsiri ya maneno ya asili. Kasisi akawa wa kwanza kusilimu. Yeye alijenga ukaribu zaidi na Mohamed na akawa anamwomba kila akienda msikitini waende wote. Hatimaye akasilimu. Estes naye, kila alivyotafakari juu ya utata wa Utatu na dhambi ya asili akilinganisha na yale anayosoma kupitia kwa Mohamed na kisha kwa kasisi wa Kikristo, naye haikuchukua muda, akasilimu. Hiyo ilikuwa mwaka 1991. Alifuatia mkewe kisha baba yake, wote wakasilimu wakawa sasa wanaswali msikiti wa jirani badala ya kwenda kanisani walikolelewa. Akawatoa watoto wake kutoka shule ya kanisa na kuwaingiza katika shule ya K i i s l a m u a m b a p o miaka kumi baadae walishahifadhi sehemu kubwa ya Quran na kujua Uislamu kwa kuusoma. Anasema, mwishowe hata mkwewe, yaani baba wa mke wake naye alifikia akakubali kuwa Yesu hawezi kuwa Mungu Mkuu, ila Mtume mwenye hadhi kubwa kwa Mungu. Pamoja na yote aliyoeleza, lakini Estes anasema kuwa haoni kuwa hili ni jambo la kawaida kwa familia nzima ya wajenga makanisa na wachungaji p a m o j a na k a s i s i wa kikatoliki kusilimu. Sasa badala ya darasa duara la Biblia, ni darsa la Quran. Anasema hii ni Rehma ya Mwenyezi Mungu. Lakini anasema katika maisha yake amekutana na watu wengi kama yeye waliosilimu na hawa walikuwa na nyadhifa katika kanisa. Anamtaja mwanafunzi mmoja Leo kutoka Tennessee aliyekuwa katika seminari moja, Baptist Seminary College, karibu na jiji la Dallas ambaye alisimu baada ya kuisoma Quran yote. Ila anasema, wapo pia ambao pamoja na kuuona ukweli wanasita kusilimu wakihofia kazi zao na uhai wao. Anamtaja rafiki yake mmoja wa Kikatoliki Father John, ambaye baada ya kuongea naye mambo mengi juu ya Uislamu na yeye kuyakubali alimuuliza, mbona sasa husilimu umebaki katika Ukatoliki? Unataka nipoteze kazi yangu? Lilikuwa ndio jibu.

13

Makala

RABIUL AWWAL 1435, IJUMAA JANUARI 31-FEB. 6, 2014


kuwasaidia Wasomalia hivi sasa ni kuwafanya watanabahi kuwa wao ni ndugu katika Uislamu na kisha Wasomali. Wakishafahamu hilo, watasimama kama Waislamu na kama Wasomali kupambana na beberu yeyote hata awe na nguvu kiasi gani. Nguvu ya pamoja ya Waislamu, iwe kidiplomasia, kisiasa, kitaarifa za habari, kiuchumi na kila njia na juhudi itakayowezekana, inatakikana kuelekezwa kwa wadhulumiwa kama hawa Waislamu wa Burma, kule Ufilipino na Palestina. Hiyo ni katika kiwango cha kimataifa. Lakini kitaifa na kinchi, tunatakiwa pia kujitizama na kuhakikisha kuwa tunajiimarisha kama umma mmoja katika kila nyanja. Elimu lazima tuwe mbele. Uchumi tushike hatamu. Lakini pia katika huduma za kijamii na kuonyesha njia kwa vitendo katika suala zima la maadili mema. Hapo ndio tutakapoibuka kama viongozi-Makhalifah. Huwezi kuwa Khalifah kama huna manufaa wala msaada wowote kwa watu. Huna cha kutoa wala kuigwa katika elimu, uchumi, huduma za kiafya na kijamii, tabia njema, na masala ya ubinadamu kwa ujumla kama yanavyoainishwa ndani ya Quran na Sunnah. Khilafah ianze kusimama katika mioyo, familia, mitaa na miji wanamoishi Wa i s l a m u . Wa i s l a m u waonyeshe Uislamu wao katika biashara zao, kazini, katika shughuli zao za kijamii, huduma kwa watu na shughuli zao mbalimbali. Paliposimama Khilafah Muislamu akitaka huduma bora ya elimu, afya/matibabu, habari, huduma za kijamii na kibinadamu, anazipata kwa Waislamu na katika taasisi za Kiislamu. Wakati wengine wakizama katika tope la rushwa, ufisadi, wizi kazini na kutokufanya kazi vyema, Waislamu iwe ni katika polisi, jeshi, ofisi za kiserikali, binafsi na umma; daima watakuwa viongozi na watu wa kuonyesha mfano bora kwa kuchapa kazi na uadilifu. N i m a l i z i e k wa k u t o a pongezi zangu kwa wale Wa i s l a m u w a Ta n g a wanaopita katika hospitali kutoa huduma kwa wagonjwa ikiwemo hata kuwasafisha wasio kuwa na ndugu. Niwapongeze pia kile kikundi cha Akhlaqu Islam, wa n a o t o a m c h a n g o wa damu na huduma nyingine za kijamii. Bila shaka hii ni hatua muhimu katika kuendea kufanya makubwa zaidi ya kunufaisha jamii na kufanya Dawah kwa vitendo.

AN-NUUR

Na Mwandishi Wetu

AARIFA zilizokuwa zimezagaa katika vyombo vya habari Ijumaa iliyopita, ziliarifu kuwa zaidi ya Waislamu 16 waliuliwa na wengine zaidi ya 100 kutekwa ambapo wanawake walibakwa. Mauwaji na utesaji huo ulifanywa na Polisi wa Burma usiku wa Januari 14 walipovamia kijiji cha Du Char Yar Tan, usiku wa tarehe 14 Januari, 2014. Mauwaji hayo yanakuja siku chache baada ya kugundulika mauwaji ya Waislamu wengi wa Rohingya waliofukiwa katika kaburi moja. Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali za makundi ya haki za binadamu, wasichana wa Kiislamu wamekuwa wahanga wakubwa wa visa na ukatili wa jeshi na polisi kwani kila wanapovamia miji na vijiji vya Waislamu, hufanya ubakaji. Haya ndiyo yanayowakuta Waislamu wa Rohingya ndani ya nchi ya Burma ambao kilio na machozi yao hayafiki kokote. Si Umoja wa Mataifa wa l a n c h i z a K i i s l a m u zinazopeleka Jihad huko. Katika Burma, watu wa kabila la Rohingya ndiyo walio Waislamu na wengi wao wanaishi katika Jimbo la Rakhine (Rakhine state), ambapo imekuwa kana kwamba serikali ya Kibudha imeweka sera ya kuwahilikisha. Ukiacha mauwaji yanayofanywa na Polisi na wanajeshi, kumekuwa pia na makundi ya watu (Mabudha) wanaovamia vijiji vya Waislamu wakafanya mauwaji, ubakaji, uporaji na kisha kuteketeza nyumba kwa moto. Ilichoweza kufanya Umoja wa Mataifa mpaka sasa ni kusema tu kuwa Waislamu wa Rohingya, ndio watu wanaonyanyaswa na kuteswa kuliko watu wengine duniani kote. Kwa kule kuwa Waislamu, kwa sheria ya Burma ya mwaka 1982, Waislamu hao sio raiya. Wanaonekana kama wahamiaji haramu ndani ya nchi yao (illegal immigrants in their own home.) Haya si madhila yaliyoanza jana au juzi, bali ndiyo maisha ya Waislamu wa Burma miaka nenda mika rudi. Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa za Shirika la Amnesty International na Human Rights Watch, wimbi la sasa hivi lililoanza kiasi miezi 12 iliyopita, imekuwa kama mkakati wa kuhakikisha kuwa Waislamu wanamalizwa kabisa (ethnic cleansing) katika Jimbo la Rakhine. Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa z a i d i ya wa t u 1 4 0 , 0 0 0 wamekimbia mateso hayo, na hiyo ikiwa ni moja ya njama za serikali ya Burma,

Jihad ipo Rakhine, Myanmar


Waislamu wanauliwa, wanabakwa Misikiti, nyumba zinachomwa moto Ile kuwa Muislam, unavuliwa uraiya
Wa k a t i w a k i f a n y a uharamia huo, wavamzi hao walikuwa wakiimba wimbo wa Taifa wa taifa hilo na askari hawakutokea mpaka ulipofanyika uharibifu mkubwa. Iliripotiwa katika felevisheni ya taifa kuwa zaidi ya nyumba 42 na maduka 15 yaliteketezwa kabisa kwa moto. "People descended on our village with swords and spears, and sang the national anthem and began destroying shops and burned houses. Police shouted at the mob to disperse, but did not take any serious action." Anasimulia Aung San (48) Muislamu ambaye nyumba yake ilichomwa moto. Aung San, anayeishi na wazazi wake walio katika umri wa zaidi ya mika 70, anasema aliwaficha wazazi wa k e k a t i k a m a k a b u r i pamoja na dada na watoto wake, wakiangalia kwa mbali nyumba yao inavoteketezwa. Na wauwaji walipoondoka, wakakimbilia kujificha katika shule moja ya Kiislamu. Katika jitihada za kuficha uovu huo, Wizara ya Habari ya Burma ilidai kuwa uvamizi huo ulifanywa na watu wenye hasira baada ya kusambaa habari kuwa kuna Muislamu alitaka kumbaka mwanamke mmoja wa Kibudha. Hata hivyo inaelezwa kuwa huko nyuma, Mabudha na Waislamu walikuwa wakiishi pamoja bila ya bughudha, lakini kidogo kidogo chuki zikapandikizwa na sasa imefikia mahali hata serikali inashiriki badala ya kukomesha. Wakati huo huo, Serikali ya Burma, imepitisha sheria i n a y o wa p i g a m a r u f u k u Waislamu kuwa na watoto zaidi ya mmoja. Ruhsa kisheria ni kuzaa watoto wawili tu. Ukizaa mtoto wa tatu, huyo anaingizwa katika daftri jeusi na hatapewa cheti cha kuzaliwa wala huduma ya elimu, matibabu na hata kuoa au kuolewa. Sheria hiyo ya kibaguzi ni kwa miji yenye Waislamu wengi ya Buthidaung na Maungdaw, ambapo Waislamu ni zaidi ya asilimia 95. M s e m a j i wa s e r i k a l i katika Jimbo la Rakhine, kwamba mateso yakizidi, basi Waislamu watakimbia (kama wanavyofanyiwa Wapalestina na Mayahudi). Ukiacha hao wanaokimbia kutafuta makazi salama, wapo wanaokufa kwa njaa katika makambi ya wakimbizi, wanaouliwa na vijiji vinavyoangamizwa kwa moto. Kinachoitwa Jumuiya ya Kimataifa, wanampongeza Rais Thein Sein, eti kwa kuimarisha demokrasia Burma, lakini hawasemi lolote juu ya mateso na mauwaji anayowafanyia Waislamu. Kwa makusudi kabisa, serikali imekuwa ikivunja misikiti, kukamata Waislamu kwa mamia na kuwaweka ndani, kuzuiya misaada ya kibinadamu kuingia vijiji vya Waislamu na katika makambi ili wafe kwa njaa na magonjwa. Katika tukio la 23 Octoba 2012, makundi ya wavamizi kutoka kabila la Arakanese, wa k i s a i d i wa n a p o l i s i , walivamia kijiji cha Waislamu c h a Ya h T h e i , a m b a p o wakiwa na visu, mapanga na mikuki, waliuwa Waislamu 70 wakiwemo watoto 28 waliochomwa kwa miti iliyochongwa na kuwekwa kama mishikaki inayotaka kuchomwa. "The Burmese government participated, encouraged and stood by the violence [against Rohingya], including president Thein Sein, who last year called for international help to deport the Rohingya. Anyone in the country has prejudice against them. The president supports the prejudice by saying they don't belong to Burma and reinforcing those who conduct violence." Ndivyo inavyosema taarifa moja ya uchunguzi kwamba, si jambo la kuficha kuwa serikali inashiriki katika kuwaangamiza Waislamu na inasimama na kila anayevamia na kuuwa Waislamu. Katika tukio jingine mwezi Agosti mwaka jana 2013, kundi la ma-Budha lilivamia kijiji cha Waislamu, kaskazini magharibi mwa Myanmar na kuchoma moto nyumba na maduka ya Waislamu. W i n M ya i n g , a n a s e m a kuwa sera na sheria hiyo imelenga kupunguza idadi y a Wa i s l a m u a m b a y o inaonekana kuwa ndio moja ya vyanzo vya vurugu za kidini na kikabila. Lakini ambalo haliangaliwi ni kuwa japo Waislamu ni wengi katika miji inayotajwa, lakini Waislamu hao ni asilimia 4 tu (4%) ya watu takribani milioni 60 katika Myanmar (Burma). Kama ilivyoelezwa awali, serikali ya Myanmar, h a i wa t a m b u i Wa i s l a m u (Rohingya) kama moja ya m a k a b i l a ya k e m a d o g o (ethnic minorities) yapatayo 135, baada ya Mabudha. Wa i s l a m u h a d h i ya o ni wakimbizi haramu (illegal immigrants) kutoka Bangladesh. Lakini Waislamu hao wamekuwepo hapo karne na karne, hata hiyo Bangladesh hawaijui. Hivi sasa wapo watu wanakusanyana chini ya nembo ya Jihad kwenda kupigana Syria. Hawa wanafadhiliwa na Saudi Arabia na Qatar na kwa mlango wa nyuma wanafadhiliwa na kusadiwa na Marekani/NATO/Israel. Wakifika kule wanapambana na askari wa Syria, Waarabu na Waislamu. Hakuna Mzungu wala kafiri anayepigana pale. Kwa nini kama lengo ni Uislamu, hatuoni Mujahidina hawa wakiungana kwenda kuwahami Waislamu wa Burma? Kwa nini waishie kupigana proxy war ambayo mwisho wa yote ni kuwafaidisha wanaotaka kukomba mafuta ya Wa a r a b u / Wa i s l a m u , kudhoofisha nguvu na umoja wa nchi za Waislamu na hatimaye kuimarisha nguvu ya Israel, Mashariki ya Kati? Katika Somalia kuna tatizo. Mabeberu wana masilahi na hali ya ghasia inayoendelea k wa h i y o wa t a e n d e l e a kulikoroga. Ufumbuzi hapa hauwezi kuwa kupeleka zaidi wapiganaji Somalia, iwe ni upande wa Al Shabab, Hizb Islamia au Ahlu Sunna Wal Jamaa. Namna pekee ya

14

Habari

RABIUL AWWAL 1435, IJUMAA JANUARI 31-FEB. 6, 2014

AN-NUUR

Innalillah Wainaillayhr Rajuun


Na Mwaandishi wetu

Sheikh Dkt. Abdul-Karim Zaidan ametutoka


Zaidan alikuwa Profesa katika masomo ya Sharia (Islamic Law) na Kanuni za Kimataifa. Sheikh Dkt. Abdukarim Zaidan alikuwa ni mtunzi na mwandishi maarufu ulimwenguni na mpaka kufariki kwake ameandika vitabu na makala zaidi ya hamsini (50). Sheikh Dkt. Abdukarim Zaidan amekuwa muhadhiri katika vyuo vikuu mbalimbali katika ulimwengu wa Kiislamu hususan katika nchi za Iraq, Kuwait, Saudi Arabia, Yemen nk. Sheikh Dkt. Abdukarim Zaidan alizaliwa mwaka 1917 nchini Iraq na amefarika dunia nchini Yemen akiwa na umri unaofikia miaka tisini na saba (97). Sheikh Dkt. Abdukarim Zaidan amewahi kupata tunzo ya kimataifa ya utunzi bora wa kitabu katika mwaka 1997 ya King Faiswal inayotolewa nchini Saud Arabia. Sheikh Dkt. Abdukarim Zaidan amewasomesha wanazuoni wengi sana ulimwenguni na miongoni mwa wanafunzi wake

M O J A w a Wa n a z u o n i w a Kiislamu Tanzania (HAY-ATUL- ULAMAA) umepokea kwa huzuni kubwa taarifa ya kifo cha mwanachuoni mkubwa wa Kiislamu ulimwenguni Sheikh Dkt. Abdukarim Zaidan, kilichotokea asubuhi ya Jumatatu Januari 27,2014 katika mji mkuu wa Sanaa nchini Yemen. A k i t o a t a a r i f a k wa M a s h e i k h , Ta a s i s i , vyombo vya habari na watu mbalimbali nchini, Katibu mtendaji wa Hay-atu- Ulamaa Sheikh Dkt. Ibrahim Hamad, amesema kuwa Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania tayari umepeleka salamu za rambirambi kwa wahusika pamoja na uongozi wa juu wa Chuo Kikuu cha Al-imaan (ALEMAN UNIVERSITY) cha nchini Yemen, ambacho Sheikh Dkt. Abdukarim Zaidan amekuwa akikitumikia kwa muda mrefu mpaka kufariki kwake. Sheikh Dkt. Abdukarim

AL-MARHUUM Sheikh Dkt. Abdukarim Zaidan. nchini Tanzania ni: Sheikh. Ibrahim Ally Hamad, Sheikh. Ramadhan Khamis Kwangaya, Sheikh. Omar Khamis Shaame, Sheikh. Rajab Kassim Mgeo, Sheikh. Yussuf Mwilima na Sheikh. Akhfash Harun Mbwana. Tunamuomba Allah (S.W) amueke Almarhum Sheikh Dkt. Abdukarim Zaidan mahali pema Peponi Aamiyn.

Inatoka Uk. 16 tutakuwa tumemalizana. Yeye aende panapostahili, i we B a r a z a l o l o t e l a Wa i s l a m u a u Ta a s i s i inayokubalika na msikiti husika tunaweza kuwasaidiana nao katika kutatua taizo husika. Alifafanua Kamanda Kiondo. Alisema kuwa tayari Polisi temeke wana Kamati zao za kushughulikia masuala ya dini kwa kila upande. Yaani Kamati ya kushughulikia masuala ya Waislamu kuna polisi Waislamu wakiongozwa na Bw. Zuberi Mombeki ambaye ni Mweyekiti wa Kamati, kadhalika na kamati ya kushughulikia masuala ya Wakristo ina wajumbe Wakristo. Aidha Kamanda Kiondo alisema kufuatia

Muafaka Masheikh, Kamanda wa polisi Temeke wafikiwa


maridhiano yaliyofikiwa, barua juu ya maafikiano hayo zitasambaza katika mahakama za jijini kama ushahidi wa maandishi kuanzia mahakama za mwanzo, Wilaya na kuendelea. Aidha makubaliano hayo pia yatafikishwa katika ofisi za wakuu wa wilaya na mkuu wa mkoa ambao tayari wana taarifa za mkutano huo na kinachofanyika ni kitu gani. Alisema atahakikisha kwamba makubaliano yaliyofikiwa hayatakiukwa kwa kuwa yametokana na busara za Masheikh pamoja na polisi na kwamba, ikitokea hitilafu ye y o t e a t a wa i t a t e n a Masheikh na Maimamu wajadili. Kamanda Kiondo alisema lengo la kuundwa kamati hizo ni kuondoa migogoro isiyokuwa ya lazima kati ya jeshi la polisi na watu wa dini na kusababisha kuchukiwa na jamii hiyo ya kiislamu. Akizungumza katika makubaliano hayo, Imamu wa Masjid Tungi, Shaban Ibrahim, alisema kitendo alichokifanya Kamanda Kiondo ni cha kiungwana, kwani amejua kuwa utatuzi wa migogoro hiyo inafaa kufanyika kupitia kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna za Mtume (SAW). Imamu huyo aliongeza kuwa uchache wa elimu na kukosa ucha Mungu, ndio imekuwa chachu ya baadhi ya viongozi wa dini kupeleka migogoro ya misikiti yao polisi. Alisema muafaka huo umekuwa ni jambo jema kufanywa na polisi na kwamba, kwa mtindo huo,

wale wanaopendezwa na mizozo misikitini watafikia tamati. Hata hivyo alisema matendo ndio yawe yenye kufuatwa zaidi kuliko maneno katika makubaliano yaliyofikiwa. Imamu huyo amewataka Waislamu kuendelea kushikamana katika kitabu chao ili waweze kufanikiwa k a t i k a m a m b o ya o yanayowakabili. Naye Imamu wa Ve t e n a r i S h e i k h Nurdin Kishki, alisema makubaliano waliyofikiwa yanaweza kuondoa migogoro ya misikiti au kuipunguza. Alisema ni jambo la aibu kwa Waislamu kugombana na kupeleka migogoro yao polisi, kwani kwa mujibu wa Kamanda Kiondo hata

Wa k r i s t o wa m e k u wa wakigombana lakini ugomvi wao huutatua wenyewe. Wa k i j a p o l i s i , warejeshwe kwenye Mabaraza ambayo misikiti yao inayafuata ili kujadili na kupata suluhu. Kamanda

kawakumbusha wajibu wao. Alisema Sheikh Kishki. Sheikh Kishki alisema kuwa tatizo linalowasumbua Misikiti mingi pale panapotokea mizozo, ni dharau za wao kwa wao katika usuluhishi. M k u t a n o h u o wa Polisi na viongozi wa dini ya Kiislamu Temeke, umekuja kufuatia kuibuka migogoro mingi misikitini jambo linalowafanya polisi kupokea kesi ambazo kwa mujibu wa kanuni zao hawapaswi kuingilia mambo hayo ya kiibada.

15
Na Salma Said

Makala

RABIUL AWWAL 1435, IJUMAA JANUARI 31-FEB. 6, 2014


alisema Mansoor. Baadhi ya majirani wanasema maisha ya Bi. Farashuu na Mume wake Bwana Hamad Saleh ni m a g u m u wa k a t i m u m e hana kazi ya kufanya Bi. Farashuu anahangaika na kupika maandazi kwa ajili ya kuendeleza maisha yake na familia yake. Mwandishi ngoja mimi nikuambie ukweli maana yeye mwenyewe anaona aibu kusema, kwa kweli maisha yake ni magumu sana kuliko unavyomuona hapa maana ananunua unga na kukanda maandazi kila siku, ndio hayo wanauza kupata senti na hayo hayo wanafanya chakula cha siku. Alisema Sada Hamed Rashid ambaye ni jirani yake. Kufuatia hali yao ngumu ya maisha na wanataka kumtibu mtoto wao wameamua kuuza nyumba yao kwa thamani ya shilingi millioni 30 lakini tangu wameanza kutangaza bei, hadi leo hii haijanunuliwa huku baadhi ya jamaa zao wakikataa nyumba hiyo isiuzwe kutokana na kuwa watapata tabu na kukosa sehemu ya kuishi. J a m a a z a n g u we n g i wa m e n i s h a u r i t u s i i u z e nyumba yetu, wanasema tutapata tabu ya makaazi ya kujisitiri mimi na wanangu lakini hali ndio ngumu mtoto anateseka kwa hivyo lazima tutafute namna ya kutatua tatizo hili, lakini pia ni mtihani maana hiyo nyumba pia hatujapata mteja alisema Bi. Farashuu. Idadi ya watu wenye kupata ulemavu imekuwa ikiongezeka kufuatia kuanguka juu ya minazi, lakini zaidi ni wanaoanguka juu ya mikarafuu ambapo baadhi yao huvunjika viungo vya miili yao na wengine kupooza na kuwa walemavu. K w a m u j i b u Wa z i r i wa Biashara, Viwanda na Masok o Nassor Ahmed Mazrui, amesema ni kweli wapo watu ambao huanguka kwenye mikarafuu lakini idadi haifiki 200 kwani baadhi yao kati ya hao wanaotajwa, wameanguka mikarafuu, minazi na wengine wamepata ajali mbalimbali ikiwemo vespa na gari. Hivyo ndio maana idadi inaonekana ni kubwa zaidi lakini katika kipindi cha mwaka jana wizara yake imeshuhudia watu watatu walioanguka katika mikarafuu ambao wa m e p a t a m a j e r a h a n a ulemavu. Msomaji wa Makala hii kumbuka kwamba kutoa ni moyo na sio utajiri, kwa hivyo utakachoweza kutoa wewe toa tu na kitasaidia, hata kama ni shilingi elfu tano (5,000) utakuwa umemsaidia Mansoor katika matibabu yake kwani hii ni sadaka yako na utakuwa unamkopesha Mwenyeenzi Mungu na bila ya shaka utakikuta mbele ya safari Inshallah. Mtu ambaye ataguswa na matatizo ya Mansoor awasiliane moja kwa moja na Mwandishi wa Makala hii Salma Said kwa email m u f t i i y @ ya h o o . c o m a u simu+255777477101 au Tigo Pesa +255657570000 Amour Ali Muhsin.

AN-NUUR

I mwenye furaha usoni mwake, huwezi kuamini kama ni mgonjwa. Huwezi kukubali kama ana machungu ndani ya moyo wake kwa kuwa sura yake ni ya kutabasamu wakati wote na kuonesha matumaini ya kuishi kwa amani. Lakini utagundua tu, pale utakapomsikiliza kwa makini sana katika maelezo yake na ukimtulizia jicho, ndipo utakapobaini kweli kijana Mansoor Hamad Saleh (21) ana majonzi na maumivu makali anayoyapata katika kiwiliwili chake. Ni miaka mitatu sasa tangu Mansoor alipoanza kulala kitandani kutokana na matatizo ya kupooza miguu yake yote miwili, chanzo chake khasa cha ulemavu huo kilikuwa ni kuanguka juu ya mnazi huko Maangwe, Wete Pemba alipokuwa amepanda kwa ajili ya kuangua nazi kwa ajili ya matumizi ya nyumbani kwao. Mansoor ni mwanafunzi wa kidato cha pili ambaye alikuwa akijitayarisha na kufanya mitihani, lakini kwa bahati mbaya sana kabla ya kuanza tarehe za mitihani alipata mtihani mkubwa wa kuanguka kutoka juu ya mnazi hadi chini na kusababisha matatizo m a k u b wa ya l i y o m l a z a kitandani hadi leo hii, akiwa hana matumaini tena katika maisha yake. Hata hivyo Mansoor anajipa moyo kwamba iwapo atatibiwa na akafanikiwa kupata fedha za kumfikisha nchini India, ataweza kurejea katika hali yake ya kawaida. Amekuwa akiomba apate matibabu hayo ili aweze kurejea shuleni kuendelea na masomo yake kama kawaida. Awali Mansoor alipoanguka kutoka juu ya mnazi miaka mitatu iliyopita, alikimbizwa katika hospitali ya Chake Chake Kisiwani Pemba na alilazwa hapo kwa muda wa mwaka mmoja chini ya uangalizi wa Daktari Shaaban wa hospitali hiyo, kabla ya kusafirishwa na k u l e t wa U n g u j a k a t i k a Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja kwa matibabu zaidi. Lakini licha ya matibabu hayo ya mwaka mzima, hakuweza kupata nafuu na bado yupo kitandani. K wa k u wa n i k i j a n a mdogo, hapendi kulala muda wote na amekuwa akipenda sana kujishughulisha ingawa hawezi, lakini anajilazimisha kukaa japokuwa ni vigumu kwake kukaa katika kiti muda mrefu, hata hivyo amekuwa akijaribu kukaa na kulala mara kwa mara. Napenda niendelee kusoma lakini siwezi kwenda skuli na hiki kigari changu kwa sababu kila wakati naumia sana mgongo wangu, kwa hivyo inanibidi kila wakati

Muonee huruma kijana Mansoor


Sadaka yako inahitajika sana
wa kwanza. Anashukuru kuona mwanawe bado yupo hai licha ya hali mbaya na ya kusikitisha kutokana na maumivu ayapatayo mwilini mwake. M wa n a n g u a l i k u wa akijitayarisha na mitihani ya darasa la kumi na mbili lakini akapata mtihani huu maana na huu ni mtihani mwengine mkubwa zaidi ya huo mtihani wake wa darasani, alisema Mama Mzazi wa Mansoor, Bi. Farashuu. Bi. Farashuu anasema amefanya juhudi mbalimbali za kutafuta misaada kwa ajili ya kumuokoa mwanawe ili aweze kurejea katika afya yake, lakini ameshindwa kutokana na familia yao kuwa masikini sana na haina uwezo wa kuchangishana fedha kwa ajili ya matibabu ya mwanawe huyo. Jamaa zangu wanataka kunisaidia lakini jambo kubwa wamenambia wao hata familia nzima ikichangishana, haitaweza kupata hata milioni tano na ndio maana nakuwa napata wakati mgumu na wakati mwengine nachanganyikiwa nikimuona mwanangu anavyoteseka na maumivu, alisema huku akiwa na uso wa huzuni sana. Bi. Farashuu anasema mwanawe amekuwa akitaja mara kwa mara kufanya kazi iwapo atakosa matibabu na kushindwa kuendelea na kusoma hivyo angependelea kufanya kazi gereji kutengeneza magari. Mansoor anapoletewa supu kwa ajili ya kunywa ili kurejesha afya yake, amekuwa akisema bora hao kuku anaoletewa kwa ajili ya supu apewe mwenyewe aweze kuwafuga waweze kuendeshea maisha yao yeye na ndugu zake wengine. Mwanangu ameshakata tamaa kama baba yake na ndio maana nakhisi kama hatokuwa tena na akili ya kuendelea na masomo na ndio maana anakuwa anataja sana kutaka kufanya kazi gereji kutengeneza magari, alisema Bi. Farashuu. A n a p o l e t e w a s u p u anywe, basi anawaambia nileteeni hao kuku nitafuga mwenyewe kwa sababu akifuga atapata pia kuuza na watazaa wengine na hivyo atapata kuendeleza mifugo na pia atasaidia ndugu zake, alisema Bi. Farashuu na kuongeza kuwa hivi sasa kijana wake huyo ameshapata makoo wawili kwa ajili ya kufuga. Mansoor anahitaji kupata banda la kuku dogo ili aweze kuwaweka kuku wake ambao wameletewa na jamaa zake baada ya kukataa kupikiwa supu kwa ajili ya kuimarisha afya yake. Nikifuga kuku nitapata kuchinja nipate supu lakini pia nitapata pesa kwa ajili ya kuwasaidia wenzangu,

MANSOOR Hamad Saleh .


nilale kidogo ninyanyuke nikae kidogo nilale kidogo hivyo hivyo kutwa nzima na nikijilazimisha basi naumia sana, alisema huku akionesha kukunja uso kwa maumivu. Sehemu ya kiuno hadi miguu kwenye nyayo iliathirika na kutofanya kazi na vipimo vya X Rays vinaonesha kuwa ameumia maeneo ya uti wa mgongo, imesema ripoti yake ya hospitali. Licha ya matibabu a l i y o f a n y i wa M a n s o o r , alipatiwa dawa mbalimbali ya kuamsha hisia za mwili wake na kuondosha maumivu, kulazwa katika sehemu maalumu ili kunyoosha mgongo wake vile vile kufanyiwa mazoezi mepesi ya kusimamishwa ili viungo vyake viweze kufanya kazi katika kipindi chote cha kuumwa kwake, lakini matibabu hayo hayajaweza kuleta mafanikio. Mansoor baada ya k u f a n y i wa v i p i m o v ya Computer Tomography Scan (CT SCAN) vinaonesha athari aliyoipata katika mgongo wake anahitajika kusafirishwa na kupelekwa India kwa matibabu kwani ameumia katika uti wake wa mgongo. Kwa mujibu wa maoni ya madaktari, wameshauri Mansoor kupelekwa India kufanyiwa operesheni kwa k u wa o p e r e s h e n i ya k e haiwezi kufanyika hapa nchini Tanzania na kila anapoendelea kukaa madhara yanaweza kuongezeka zaidi. Kwa mujibu wa madaktari waliomchunguza, wanasema jumla shilingi millioni 20 zinahitajika kwa makisio ya matibabu yake ya kumfikisha nchini humo. Makisio ya fedha hizo ni pamoja na gharama za usafiri kutoka Zanzibar hadi India, vipimo vya uchunguzi, matibabu na gharama za malazi na fedha ya kufuatana na Daktari atakayeweza kuondoka naye hapa nchini hadi India. Matatizo yake makubwa kwa sasa ni kuwa hawezi kusimama kwa vile amepata athari katika viungo vyake vya upande wa chini (nyayo) kukosa hisia na pia hawezi kuzuwia haja kutokana na kuathirika kwenye uti wa mgongo. Wa z a z i w a M a n s o o r wa m e k u wa wa k i t a f u t a misaada mbalimbali kutoka k wa wa t u , l a k i n i b a d o hawajafanikiwa kukusanya kiasi chochote cha fedha licha ya kuandika barua kadhaa kwa wafadhili . Sisi wazee wake Mansoor, baba na mama sote ni masikini sana, hatuna uwezo wa kumsafirisha mtoto wetu kwa ajili ya matibabu, mtoto wetu anakabiliwa na ulemavu wa kudumu, tunaleta kilio chetu kwa lengo la kupata msaada wa tiba ya mtoto wetu huyu wa kwanza. Imesema moja ya barua yao ya maombi wazee hao ya hivi karibuni ambayo iliandikwa 15/9/2013. Bi. Farashuu Mansoor Mohammed, ni mama mzazi wa Mansoor mwenye familia ya watoto nane, kati yao ni wanawake wawili na Mansoor ndio mtoto wake

16

AN-NUUR
MAKALA

RABIUL AWWAL 1435, IJUMAA JANUARI 31-FEB. 6, 2014

16

RABIUL AWWAL 1435, IJUMAA JANUARI 31-FEB. 6, 2014

Polisi kutojihusisha na migogoro ya Waislamu


Na A. Msengakamba KAMANDA wa Polisi mkoa wa kipolisi Temeke RPC Engelbert Kiondo na Masheikh na Maimamu wilayani humo, wamekubaliana kwa pamoja kwamba jeshi la Polisi Wilayani humo halitashughulikia migogoro ya Misikiti inayoendelea kujitokeza sehemu mbalimbali wilayani humo, na badala yake migogoro hiyo itashughulikiwa na Waislamu wenyewe kupitia taasisi na Mabaraza ya Waislamu ambayo misikiti hiyo inayakubali. Makubaliano hayo ya pamoja yamefikiwa Jumamosi ya wiki iliyopita katika mkutano maalum uliowakutanisha maafisa wa jeshi la polisi Temeke wakiongozwa na Kamanda Kiondo pamoja na Masheikh na Maimamu wa Misikiti ya wilaya ya Temeke, uliofanyika katika ukumbi wa Polisi Chan'gombe jijini Dar es Salaam. Baada ya mjadala wa muda, kati ya Masheikh, Maimam na Kamanda Kiondo, iliridhiwa kwamba iwapo utatoteka mtafaruku wowote katika msikiti kuhusu masuala ya kiimani, basi mtafaruku huo utashughulikiwa na Mabaraza ya Wa i s l a m u k a m a v i l e Baraza Kuu, Bakwata, Jumuia ya Maulamaa au taasisi nyingine yeyote iliyoandikishwa kisheria, ambayo inakubalika na msikiti husika. Kamanda Kiondo aliongeza kuwa taarifa za maamuzi yaliyofikiwa katika mkutano huo, zitapelekwa kwa maandishi katika mahakama zote kuanzia

Muafaka Masheikh, Kamanda wa polisi Temeke wafikiwa


za mwanzo jijini Dar es Salaam, Wakuu wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa na kwa wakuu wote wa jeshi la polisi akiwemo IGP. Hata hivyo alisema kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa katika mkutano huo, lalamiko lolote litakalokuja katika kituo cha polisi linapokelewa kwa kuwa tayari jeshi hilo l i n a wa t a a l a m wa k e katika kamati zake za kushughulikia masuala ya kidini. Lakini akasema polisi h a wa t a c h u k u a h a t u a zozote kabla ya kupata maelezo ya kina kwa maandishi iwapo lalamiko hilo liliwahi kuwasilishwa katika taasisi au Baraza lolote la Kiislamu kwa ajili ya kushughulikiwa na kupata suluhu. Alisema kimsingi kazi ya kutatua kesi za kidini sio kazi ya jeshi la polisi na kwamba, kazi hiyo ni ya Mabaraza na taasisi za Kiislamu. Kwa msingi huo, Kamanda Kiondo na Masheikh wa Temeke wamekubaliana kwamba hakuna tena mzozo wa msikiti hukusu mambo ya kiimani utakaoletwa polisi kabla ya kupitia taasisi husika zinazokubalika katika misikiti. Kwa utaratibu huu wa kukutana na kujadiliana, tunaweza kufika mbali na kuboresha mahusiano yetu sisi polisi na viongozi wa Kiislamu. Sasa tumeshakubaliana kwa pamoja kwamba kuanzia sasa, hakuna a t a k a ye l e t a mg o g o r o wa msikiti polisi. Akija mtu hapa tunamshangaa kwa kuwa tayari tuna mkataba wa makubaliano yetu, tutamuonyesha na Inaendelea Uk. 14

Tupo Mwananyamala Islamic Club Kona ya Makumbusho Dar es salaam. Tunaendelea Kusajili wanafunzi wa Q.T, Reseaters O-Level, waliofeli Kidato cha Pili na Kidato cha nne. Kwa mawasiliano zaidi tutembelee Shuleni au piga simu 0767 307 607, 0783- 723 312 au 0652 010 136. Pata elimu Bora kwa Gharama Nafuu.

SEKONDARI YA JIONI ( MESS) Inatangaza nafasi za masomo 2014

AN-NUUR

KAMANDA wa Polisi mkoa wa kipolisi Temeke RPC Engelbert Kiondo (wa tatu kushoto waliokaa) katika picha ya pamoja na Masheikh na Maimamu wilayani Temeke.

Islamic Foundation wasaidia waathirika wa mafuriko


Tani za maharage, unga na nguo zatolewa
Steven Kebwe. Alibainisha Bw. Bawazir. Alieleza kuwa misaada hiyo ni sehemu ya michango waliyoikusanya kutoka kwa Waislamu na wadau mbalimbali, kwa ajili ya wananchi waliokumbwa na maafa hayo. Bw. Bawazir aliainisha aina ya misaada waliyokabidhi kwa waathirika hao kuwa ni maharage tani mbili na nusu, unga tani sita na robo pamoja na nguo. Bw. Bawaziri, ambaye p i a n i M k u r u g e n z i wa Habari wa Radio na TV Imaan, alisema bado wanaendelea na michango na Jumatatu (wiki hii) kuna timu nyingine inatarajiwa kupeleka michango mingine itakayokuwa imekusanywa. Akitoa nasaha zake kufutia maafa hayo, Bw. Bawaziri alisema Waislamu na wananchi kwa ujumla wanatakiwa kutambua kuwa maafa hayana matayarisho. Mapema wiki iliyopita iliripotiwa kuwa takribani watu 7000 katika Kata tatu

Na Bakari Mwakangwale, Morogoro


TA A S I S I y a I s l a m i c Foundation ya Mjini Morogoro, imetoa msaada wenye thamani ya shilingi milioni 11.5 kwa wananchi waliokumbwa na mafuriko katika eneo la Magole Wilayani Kilosa. Akiongea na An nuur Mjini Morogoro Jumapili ya wiki iliyopita, Mwenyekiti wa Kitengo cha Maafa katika Taasisi hiyo, Bw. Ahmed Bawazir, alisema walikabidhi misaada hiyo ikiwa ni sehemu ya awali ya misaada kwa waathirika h a o n a k wa m b a , b a d o wanaendelea kukusanya zaidi. Msaada huo ulitolewa jana ( Jumamosi wiki iliyopita) katika eneo la tukio la maafa Magole, na kumkabidhi Mkuu wa Mkoa Bw. Joel Bendera aliyekuwa na Mbuge wa Kilosa, Mustapha Mkulo na Naibu Waziri wa Afya Dk.

tofauti wilayani Kilosa, wamekosa makazi baada ya kaya zao kusombwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha milimani. Mafuriko hayo mbali na kuharibu makazi ya watu, pia yamesababisha uharibifu wa vyakula vya akiba majumbani sambamba n a m a z a o ya l i y o k u wa mashambani kwa kusombwa na maji. Islamic Foundation ni taasisi ya Dini ya Kiislamu ambayo inasimamia mambo mbalimbali ikiwemo kujenga Misikiti, kuchimba visima. Hadi sasa taasisi hiyo imeshajenga takribani Misikiti 600 na kuchimba visima zaidi ya 500 katika sehemu mbalimbali nchini. Kazi nyingine za Islamic Foundation ni kusaidia kutoa mahitaji kulingana na aina ya athari pindi panapotokea maafa, kupitia kitengo maalum kinachoitwa Kitengo cha Maafa.

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na POA Printing Works LTD, S.L.P. 4605, Dar es Salaam.

Вам также может понравиться

  • Annuur 1264
    Annuur 1264
    Документ20 страниц
    Annuur 1264
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1231 PDF
    Annuur 1231 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1231 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1262
    Annuur 1262
    Документ20 страниц
    Annuur 1262
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1232 PDF
    Annuur 1232 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1232 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • HOTUBA YA BAJETI OFISI YA RAIS Final
    HOTUBA YA BAJETI OFISI YA RAIS Final
    Документ15 страниц
    HOTUBA YA BAJETI OFISI YA RAIS Final
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1230 PDF
    Annuur 1230 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1230 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Press Realse 28
    Press Realse 28
    Документ4 страницы
    Press Realse 28
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • HOTUBA YA BAJETI OFISI YA RAIS Final
    HOTUBA YA BAJETI OFISI YA RAIS Final
    Документ15 страниц
    HOTUBA YA BAJETI OFISI YA RAIS Final
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1227 PDF
    Annuur 1227 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1227 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1228d
    ANNUUR 1228d
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1228d
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1228d
    ANNUUR 1228d
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1228d
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1229 PDF
    Annuur 1229 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1229 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1225
    Annuur 1225
    Документ20 страниц
    Annuur 1225
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1226 PDF
    Annuur 1226 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1226 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1219
    Annuur 1219
    Документ20 страниц
    Annuur 1219
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1218 PDF
    Annuur 1218 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1218 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Press Release - Muungano Na Mazingira
    Press Release - Muungano Na Mazingira
    Документ4 страницы
    Press Release - Muungano Na Mazingira
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1224
    Annuur 1224
    Документ20 страниц
    Annuur 1224
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1223
    Annuur 1223
    Документ20 страниц
    Annuur 1223
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1220
    Annuur 1220
    Документ20 страниц
    Annuur 1220
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Karume Shujaa
    Karume Shujaa
    Документ11 страниц
    Karume Shujaa
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1217
    Annuur 1217
    Документ20 страниц
    Annuur 1217
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1216d
    ANNUUR 1216d
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1216d
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1214
    Annuur 1214
    Документ20 страниц
    Annuur 1214
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Hotuba Ya Maalim Seif - January 9 2016
    Hotuba Ya Maalim Seif - January 9 2016
    Документ27 страниц
    Hotuba Ya Maalim Seif - January 9 2016
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1215 PDF
    Annuur 1215 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1215 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    100% (1)
  • Annuur 1212
    Annuur 1212
    Документ20 страниц
    Annuur 1212
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1213 PDF
    Annuur 1213 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1213 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1210a
    Annuur 1210a
    Документ20 страниц
    Annuur 1210a
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1209aaa
    ANNUUR 1209aaa
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1209aaa
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет