Вы находитесь на странице: 1из 16

www.annuurpapers.co.

tz

Facebook:annuurpapers@yahoo.com

Sauti ya Waislamu

Kundecha, Togwa wazungumzia ushiriki wao Bunge la Katiba

ISSN 0856 - 3861 Na. 1113 RABIUL THAN 1435, IJUMAA , FEBRUARI 21-27, 2014 BEI TShs 500/=, Kshs

Tupo Mwananyamala Islamic Club Kona ya Makumbusho Dar es salaam. Tunaendelea Kusajili wanafunzi wa Q.T, Reseaters O-Level, waliofeli Kidato cha Pili na Kidato cha nne. Kwa mawasiliano zaidi tutembelee Shuleni au piga simu 0767 307 607, 0783- 723 312 au 0652 010 136. Pata elimu Bora kwa Gharama Nafuu.

SEKONDARI YA JIONI ( MESS) Inatangaza nafasi za masomo 2014

Dhamana ya Sheikh Ponda yaiva


Mahakama Kuu yasubiri upande wa mashtaka Uk. Uk.10 10

Na Bakari Mwakangwale

Waislamu waitikia uteuzi wa Makadhi Waislamwatakiwakuchangia dhamana Masheikh Uamsho


SHEIKH Ponda Issa Ponda (kushoto) akiteta jambo na Mawakili wake katika Mahakama Kuu Jijini Dar es Salaam Jumatano. (Picha na Abdulkarim Msengakamba)

Na Bakari Mwakangwale

WA I S L A M U n c h i n i wametakiwa kukusanya nguvu ili kuhakikisha Masheikh wa Jumuiya

ya Uamsho, wanatimiza masharti ya dhamana waliyopewa na M a h a k a m a K u u ya Zanzibar. Wito huo umetolewa

n a N a i b u A m i r wa Taasisi na Jumuiya za Kiislamu Zanzibar, Sheikh Yusuph Khamis, akiongea na An nuur Inaendelea Uk. 6

WITO wa uwasilishaji wa wasifu (CV) kwa Waislamu wenye taaluma ya Shariah kwa ajili ya kazi ya Ukadhi katika sehemu mbalimbali nchini umeitikiwa kwa kishindo. Mratibu wa zoezi hilo, Amir wa Baraza Kuu, Alhaj Sheikh Mussa Yusuph Kundecha, amelipasha gazeti hili Ijumaa ya wiki iliyopita kwamba tokea kutangazwa kwa suala hilo amekuwa akipokea simu nyingi kutoka kwa Waislamu wakitaka ufafanuzi zaidi. Inaendelea Uk.2

2
www.annuurpapers.co.tz

Tahariri/Habari
Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM. E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk Ofisi zetu zipo: Manzese Tip Top Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

RABIUL THAN 1435, IJUMAA FEBRUARI 21-27, 2014

AN-NUUR

AN-NUUR S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786

MSIKITI ni mahali maalum kwa ajili ya Waislamu kufanya ibada mbalimbali. Msikiti kwa Wa i s l a m u , n d i k o mahali sahihi kwa ajili ya kujadili, kukupanga, na kupata muafaka wa mambo yao ya Kiislamu. Iwe ni ya kiimani, kisiasa, kiuchumi au kijamii. Katika enzi za Mtume Muhammada (saw), msikiti ulitumika kama Ofisi kuu ya Mambo ya Waislamu. (Mfano Madina State). M b a l i n a s wa l a , Mtume (SAW) alitumia msikiti wa Madina kupanga mikakati ya kiutawala, kiuongozi, Baraza la mashauri mbalimba, kujadili masuala ya kiuchumi husasi masuala ya kukusanya na kutumia kodi, na kutoa elimu kwa Waislamu. Kwa ujumla tunaweza kusema kuwa Msikiti katika Uislamu, una falsafa kubwa katika mfumo m z i m a wa m a i s h a jamii ya Kiislamu. Pamoja na somo hilo kutoka kwa Mtume (saw) kuhusu namna alivyotumia Msikiti kama chimbuko la kufanikisha ustawi wa jamii ya Kiislamu, hapa kwetu sasa hali inaonekana kuwa tofauti. Tu n a s e m a h i v y o kwasababu siku za hivi karibuni kumetokea vuguvugu la mabadiliko, hususan ya kiuongozi au kimfumo katika baadhi

Tusipokuwamakinimisikiti itapoteza hadhi yake

ya misikiti yetu. Kwa bahati mbaya, vuguvugu hili linainyemelea zaidi Misikiti ambayo inaonekana kuwa mfano mzuri wa kiuendeshaji au kiuongozi kwa jamii ya Kiislamu nchini. Kwa bahati mbaya, mabadiliko haya yanaonekanakuzua h o f u n a wa s i wa s i mkubwa miongoni m w a Wa i s l a m u , wakihofia matokeo hasi katika misikiti hii, tofauti na hali ilivyokuwa hapo awali. Mabadiliko siyo j a m b o b a ya k a m a mabadiliko yenyewe yana lengo la kuboresha zaidi kuliko kulinda maslahi ya kundi au watu fulani. W a s i w a s i unakolea zaidi kwa Waislamu kwa kuwa sehemu kubwa ya wanaopigania mabadiliko hayo, kutaka kuchukua mamlaka katika msikiti hii au kubadili umilini wa kitaasisi, wana sifa zisizoridhisha katika masuala ya uendeshaji shughuli za Waislamu huko watokako. Tu m e l a z i m i k a kukumbusha hilo kutokana na dalili zinazojitokeza siku hizi, ambapo baadhi ya Misikiti imeanza kugeuzwa kuwa mahali pa Waislamu kuswali tu na kuondoka zao. Katika siku za nyuma misikiti hiyo hiyo ilikuwa kitovu cha jamii ya Kiislamu kupata mawaidha,

darsa, na kwa hakika ilikuwa mahali sahihi pa Waislamu kuweka mikakati na mipango yao thabiti ya maendeleo. Tayari baadhi ya Misikiti imefanikiwa kufanya mabadiliko hayo na tayari ishara za misikiti hiyo kudumaa imeonekana. Kama tulivyoeleza hapo awali, mabadiliko sio jambo baya katika jitihada kusaka maendeleo ya watu au waumini au kwa lengo la kuboresha zaidi Misikiti hiyo. La k i n i ma ba di l i k o h a y o ya n a p o k u wa ni ya kurudi nyuma, yanawakwaza Waislamu na kuwatia simanzi japo waliopigania ua kufanya mabadiliko hayo, kwao inaweza kuwa si neno ilimradi tu matakwa yao yametimia. Msikiti wa Mtambani ni moja ya Misikiti inayonyemelewa na hatari ya mabadiliko haya hasi. Hofu ya Waislamu ni aina ya

Mpaka sasa hivi (Ijumaa iliyopita) kuna muitikio mkubwa kutoka kwa Waislamu ambao ni walengwa (wenye taaluma ya Sharia) kwa maana tumeshapokea simu nyingi wakiulizia mahali pa kuwasilisha. Alisema Alhaj Kundecha. Alisema, wengi wamekuwa wakiulizia kuwasilisha vyeti vya taaluma zao, lakini a l i s e m a wa m e k u wa wakiwajibu kwamba kinachohitajika kwa sasa ni wasifu tu (CV). Alisema, wasifu huo

Inatoka Uk. 1

Waislamu waitikia Uteuzi wa Makadhi


(CV) unatakiwa uwe umeonyesha umesoma vitu gani katika taaluma ya Sharia za Kiislamu na kwa sasa upo wapi kisha cheti kitafuata baadae. Alhaj Kundecha alisema baada ya hapo wataandaa mchakato wa kuwaita wale wote watakaowasilisha wasifu wa o i l i k u wa f a n y i a uhakiki kisha kufanya nao semina ya pamoja juu ya kuweka ofisi za Makadhi katika namna nzuri ambayo ni imani yao itawafaa Waislamu. N a p e n d a niwahakikishie Wa i s l a m u k w a m b a mfumo wa Kadhi ambao haswa Waislamu walikuwa wakiutaka ndio huu sasa unaandaliwa na kuratibiwa na Baraza Kuu kwa kushirikiana na Hayat. Alisema Alhaj Kundecha. K wa m a a n a h i y o , Alhaj Kundecha, aliomba ushirikiano wa kutosha kutoka kwa Waislamu i ki wa ni p a m oj a na kuwakumbusha jamaa zao waliohitimu somo la Sharia kuomba nafasi hiyo kwa ajili ya kuwatumikia Waislamu katika taaluma hiyo.

watu wanaopigania mabadiliko hayo kulingana na sifa na rekodi zao za kiutendaji katika masuala ya Kiislamu. Jamii ya Waislamu inapata mashaka makubwa ikitizama rekodi wa watu hawa. Ta ya r i u l i o k u wa msikiti maarufu wa Idrisa Kariokoo jijini Dar es Salaam, umeshafanya m a b a d i l i k o tunayoyazungumzia. Sasa tunashuhudia Msikiti ukiwa domant!, zile hutba za kiamiri hazisikiki. Habari au taarifa za matukio (Current affair) hakuna. Kutokana na ishara ambazo zimejitokeza katika misikiti hii iliyokuwa ikijitahidi kutimiza wajibu wake kwa Waislamu, kwa nia nzuri kabisa, ndio maana tunaona kwamba kuna haja ya uongozi au taasisi zinazosimamia Misikiti, kuwa makini

sana na wanaoendesha vuguvugu hili la mabadiliko yanayotia mashaka ya kudumaza waumini. Tutoe tu tahadhari kwamba iwapo umakini utakosena katika kuisimia na kuiendesha misikiti hii, tutasahau zile kazi zilizokuwa zikifanyika k a t i k a M s i k i t i wa Madina enzi za Mtume Muhamad (saw) na badala yake, itabakia m i s i k i t i ya s wa l a , dhikri na milango ya msikiti kufungwa. Kuna haja ya Waislamu kuwa macho kuhakikisha kwamba misikiti haipotezi maana yake halisi kwa Waislamu. La msingi ni kuhakikisha kuwa inalindwa barabara dhidi ya watu wachache a m b a o k wa m u d a m r e f u wa m e k u wa wakibeba sifa mbaya za kudumaza harakati za maendeleo ya Wa i s l a m u k a t i k a misikiti hapa nchini.

Habari

RABIUL THAN 1435, IJUMAA FEBRUARI 21-27, 2014

AN-NUUR

Kundecha, Togwa wazungumzia ushiriki wao Bunge la Katiba

Na Bakari Mwakangwale

MBUNGE wa k u t e u l i wa k a t i k a Bunge la Katiba kupitia Taasisi za Kidini, Sheikh Mussa Kundecha, amesema watasimamia maslahi ya Wa i s l a m u k wa hoja wakizingatia muongozo wa Qur an na Sunnah. Akiongea na An nuur, mwishoni mwa wiki iliyopita Mh. Shkh. Kundecha, alisema pamoja na kwamba maoni ya Waislamu hayakupatikana moja kwa moja hususani yale ya kiimani, kimsingi hiyo ni fursa nyingine ya kwenda kuyaongelea Bungeni, kwa hoja zaidi. Alisema, pamoja na uchache wao lakini watasimama katika misingi ya hoja kwa kuzingatia madia ya Wa i s l a m u k wa kuzingatia muongozo wa Qur an na Sunnah, na kwamba watakuwa wamekamilisha eneo lao kwa kiwango kikubwa kabisa. Ilivyo ni kwamba yapo maoni ya Wa i s l a m u a m b a y o hayakupatikana moja kwa moja haswa yale ya kiimani lakini pia yapo mambo mengine ni ya Kiislamu lakini yamekaa kijamii zaidi ambayo pia yanawahusu Waislamu moja kwa moja, tutayasimamia kwa hoja madhubuti kwa kuzingatia muongozo wa Qur an na Sunnah. Alisema Mh. Kundecha. Mh. Kundecha, alisema msingi wa kuingia katika Bunge la mabadiliko ya Katiba, una namna mbili ambazo kwanza ni rasimu ya Katiba yenyewe na la pili ni yale maoni ya tume (yenyewe) yaliyokusanywa na kusema, hizo ndizo

MBUNGE wa kuteuliwa katika Bunge la Katiba kupitia Taasisi za Kidini, Sheikh Mussa Kundecha. Mh. Tongwa, ambaye r e j e a k u u a m b a z o watakuwa wameandika hali ya sasa duniani zitajadiliwa katika Bunge historia kwamba hili kote, vikao vyote vya ni Mwenyekiti wa Baraza la Katiba. Akifafanua zaidi a l i s e m a , k wa k u wa ripoti ya Tume inakiri kwamba ilipokea maoni ya Waislamu, isipokuwa ilishindwa kuyaingiza kwa sababu ilizoziona yenyewe, na kwamba kwa kuwa mjadala wa Bunge hilo utatokana na ripoti ya Tume na rasimu i l i y o p o , wa n a i m a n i bado fursa ya maoni ya Waislamu yana nafasi. Mh. Kundecha, alisema kwa sababu bado wapo ndani ya nchi hii wanatakiwa kujipanga na kujiratibu zaidi kupitia mfano wa zoezi hili na kwamba, ikiwa (Waislamu) watajiratibu vizuri zaidi ni wazi wana nafasi ya kuingiza jambo wanalolitaka na likakubalika. Lakini pia Mh. Kundecha, alisema j a m b o l i m e k a t a l i wa na wao walisimama katika msimamo wao na hata wakati watasema hata katika kikao cha maamuzi walikifikisha, lakini hakikuzingatiwa. Alisema, kiujumla wamejipanga na wamekuwa wakikutana wote ambao wamepata fursa hiyo na wataendelea kufanya vikao vya pamoja kwa kadri ya shughuli za vikao vya Bunge vitakavyokuwa vinaendelea ili kuona ni kwa namna gani wanatumia uchach e wao vizuri zaidi kuliko uchache huo pia ukatumika kwa kutokuwa na mawasiliano ya karibu yenye tija. Akijibu swali kuhusu wao kama Waislamu kuingia katika jambo hilo lenye sura ya Kisiasa, alisema katika maamuzi vinawafikisha watu kupitia mfumo wa mlango wa siasa unaotumika na nchi husika uwe wa Kiislamu au mwingine. Na kwamba, kwa hali halisi iliyopo, ukiacha ushabiki na jazba zisizo na msingi, ukiacha kushiriki katika vikao vya maamuzi kama bungeni, we n g i n e wa t a p a n g a na kuamua kwa niaba yako na matokeo yake ni lazima mamlaka za nchi zitakulazimisha kutekeleza. Kwa upande wake, Mbunge, mteule mwingine Ustadhi Hamisi Togwa, alisema kwa kuteliwa kwake kuingia katika Bunge la katiba kwa mlango w a Wa i s l a m u , a n a imani kuwa ataweza kuwawakilisha vizuri Waislamu kwa uwezo wa Allah (sw). l a Wa ku u wa S hu l e za Kiislamu Tanzania, alisema anafahamu matakwa ya Waislamu, kutokana na kushiriki katika mchakato wa maoni ya Waislamu tokea awali. Alisema, kwa kushirikiana na wenzake ambao wana uzoefu na uoni mpana zaidi katika mustakabali wa Waislamu nchini ana imani kwamba wataweza kusimama kwa hoja ili kuyawakilisha vyema. Hata hivyo, Mh. Togwa, ambaye pia ni Mkuu wa Shule ya Kiislamu ya K i r i n j i k o , S a m e , alisema suala si kusema tu, bali ni kuratibu masuala yanayowahusu Wa i s l a m u k a t i k a utaratibu unaoeleweka ili kuweza kuyafikisha Bungeni na hatimaye kufikia lengo lililo kusudiwa.

Rehema Trust watoa matibabu ya macho Mkuranga


Na A. Msengakamba

Habari

RABIUL THAN 1435, IJUMAA FEBRUARI 21-27, 2014

AN-NUUR

MFUKO wa Urafiki na Mshikamano wa Rehema Friendship and Solidarity Trust, kwa kushir ikia na na Doctors World Turkey na Turkish Cooperation and Development Agency (TICA) pamoja na madaktari kutoka Azerbaijan wametoa matibabu ya bure ya macho kwa wakazi wa wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani. Huduma hiyo imezinduliwa mwishoni mwa wiki katika hospitali ya wilaya ya Mkuranga, Ambapo itawahusu wananchi wa maeneo ya Vianzi, Mwanambaye, Sangasanga, Mlamlezi, Njopeka na vijiji vingine vya jirani. Mkurugenzi Mtendaji wa mfuko huo Bw. Abdi Adamu, alisema kuwa taasisi yake na washirika wake wameamua kutoa huduma hiyo, kufuatia takwimu (CIAworld factbook) zinaonyesha kwamba asilimia moja kati ya watanzania wote ni walemavu wa macho au ni vipofu, kwa maana ya watanzania laki nne na themanini, ambapo nusu yao ni wagonjwa wa mtoto a jicho. Alisema kiwango cha kimataifa cha huduma ya macho kinataka wagonjwa 2,000 kati ya idadi ya watu milioni moja watibiwe kila mwaka, lakini hapa nchini wagonjwa wanaopata huduma hiyo ya matibabu ni wastani wa wa g o n j wa 5 0 0 badala ya 96,000 kwa watu milioni moja, ambao ni robo ya kiwango cha kimataifa. Alisema katika nchi

la maji. Naye daktari wa kitengo cha macho katika Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga, Dk. Halison Peter Mjema, alisema katika siku ya uzinduzi wa huduma hiyo ya macho, kwa kushirikiana na madaktari hao wa Uturuki na Azerbaijan wamepokea wagonjwa wapatao 180, kati ya hao 50 wamekutwa na matatizo ya mtoto wa jicho na watafanyiwa upasuaji. Alisema wengine 80 wamegundulika kuwa na tatizo la short sight na watapatiwa huduma ya miwani. Kwa upande wake MADAKTARI Bingwa wa macho toka Uturuki wakimpima macho Alhaj Rais mstaafu wa Ali Hassan Mwinyi, Mkuranga mwishoni mwa wiki. awamu ya pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi, aliwataka watanzania pamoja na raia wa kigeni wanaoishi nchini kushirikiana pamoja katika kufanikisha suala zima la huduma ya afya kwa Jamii yote kwa ujumla. Mzee Mwinyi ambaye alikuwa mgeni rasmi katika utoaji wa huduma hiyo ya macho, alisema ushirikiano katika kukabiliana na maradhi hayo ya macho ni wa muhimu kwa maslahi ya kijamii h a s a i k i z i n g a t i wa MGONJWA wa macho akiwa katika hatua za awali za kupimwa macho, k w a m b a h u d u m a Mkuranga mkoani Pwani.Nyuma ni foleni ya wananchi wakisubiri zamu za afya, elimu, ajira na maji bado ni yao ya kufanyiwa uchunguzi. changamoto kubwa kwa watanzania zilizoendelea, idadi ya hapa nchini, kiwango nchini. wagonjwa wanaopata c h a wa g o n j wa wa Baadhi ya huduma wengi. Aliwataka wananchi huduma ya upasuaji macho kinaongezeka ambazo hutolewa na wa Mkuranga na vijiji w a m a g o n j w a y a kutokana na gharama mfuko wa Rehema macho ni 5,000 kwa kubwa za matibabu, hapa nchini ni pamoja vya jirani kujitokeza idadi ya watu milioni ufahamu mdogo wa na kusaidia katika kwa wingi kupatiwa moja, hivyo katika nchi wagonjwa kuhusu sekta ya elimu, afya, huduma hiyo ya bure hizo hakuna upofu ugonjwa huo, umbali c h a k u l a , k u s a i d i a kutoka Mfuko huo unaosababishwa na mrefu wa kuwafikia yatima, kuwajibika kwa kushirikiana na mtoto wa jicho. wagonjwa pamoja na katika majanga na madaktari bingwa wa Bw. A d i m u uhaba wa upatikanaji maafa na kusaidia macho kutoka Uturuki aliongeza kuwa kwa wa huduma za macho wananchi katika tatizo na Azerbaijani.

Habari za Kimataifa

RABIUL THAN 1435, IJUMAA FEBRUARI 21-27, 2014

AN-NUUR

RIPOTI maalumu iliyotolewa na Umoja wa Mataifa, imeeleza kuwa mauaji dhidi ya jamii ya Waislamu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati yameongezeka. Hayo yamesemwa na Mshauri wa Shirika la Kimataifa la Amnesty International, Bi. Joanne Mariner. Alisema kuwa, mauaji ya halaiki yanaendelea kufanywa na waasi wa Kikristo wa Anti-Balaka dhidi ya Waislamu wa nchi hiyo. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, mauaji makubwa yamefanywa dhidi ya Waislamu wa Kaskazini magharibi mwa nchi hiyo. Kamishna Mkuu wa Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, alisema kuwa ameshuhudia maafa ya kibinadamu yasiyoelezeka wakati alipotembelea Jamhuri ya Afrika ya Kati hivi karibuni. Guterres ameongeza kuwa maangamizi makubwa ya kikabila na kidini yanaendelea kufanyika huko Jamhuri ya Afrika ya Kati na kwamba, ukatili wa kutisha na vitendo visivyo na kibinadamu vimegubika mauaji wanayofanyiwa Waislamu nchini humo. Hii ni katika hali ambayo Shirika la Kutetea Haki za Kibinadamu Duniani la Amnesty International, limekosoa kimya kinachopigwa na jamii ya kimataifa kuhusu mauaji yanayoendela kujiri nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati. Shirika hilo limetangaza kuwa lina ushahidi unaoonyesha kufanyika m a u a j i ya m a m i a ya Waislamu yaliyofanywa na Wakristo wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, tangu yalipofanyika Mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 2013. Naye Afisa Mwandamizi wa kundi la Madaktari Wasio na Mipaka huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, Catherine Ainsworth, amesema kuwa robo ya wananchi wa nchi hiyo wameyakimbia makazi yao kutokana na hali mbaya ya kiusalama. Catherine Ainsworth, amesema kuwa kila siku wastani wa watu 10 hupelekwa hospitalini kufuatia kujeruhiwa kwa kupigwa risasi, jambo

Wakristo waendelea kuua Waislamu kikatili CAR


linaloashiria kukidhiri maafa ya kibinadamu nchini humo. Afisa huyo ameongeza kuwa, hali bado ni tete nchini humo, hasa katika mjini mkuu wa kwani milio ya risasi bado inaendelea kusikika mjini humo. K wa u p a n d e wa k e , Mhariri mkuu wa Pan African News Wire huko Michigan Marekani, Abayomi Azikiwe, amesema kuwa kasoro kubwa za kiuongozi ndiyo chanzo kikuu cha matatizo yanayoikabili Jamhuri ya Afrika ya kati. Azikiwe alibainisha kwamba nchi za Magharibi zinajitumbukiza Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa lengo la kupora maliasili na utajiri mkubwa wa madini ya urani, dhahabu na almasi.

NAIROBI SERIKALI ya Kenya imelishutumu vikali Shirika la Misaada la Marekani USAid kuwa linafanya uchochezi na njama za kuzusha machafuko nchini Kenya. Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri wa Usalama wa Taifa ya Kenya, Francis Kimemia, amelishutumu shirika la Misaada la Marekani nchini humo USAid, kuwa linatumia fedha zake kuchochea maandamano dhidi ya serikali ya Jubilee na kudhamini harakati za siri za kuleta machafuko nchini Kenya. Bw. Kimemia alidai kuwa serikali ina habari za kijasusi zinazodhibitisha kuwa USAID imekuwa ifadhili mashirika ya s i o ya k i s e r i k a l i yanayopinga serikali ya Rais Uhuru Kenyatta, kwa kutoa maelfu ya dola kwa wanaharakati Boniface Mwangina John G, kufanikisha maandamano mjini Nairobi. Aliongeza kuwa,

Sasa Kenya yaishutumu Marekani kwa uchochezi


lengo la njama hizo za Marekani ni kusukuma taratibu malalamiko ya watu ndani ya Bunge la Kenya, ili kuwachochea wabunge wa Kenya wafanye uadui dhidi ya serikali ya nchi hiyo. K wa m u d a m r e f u Kenya imekuwa mshirika mkubwa na wa karibu wa Marekani, hasa baada ya kuletwa msamiati wa vita dhidi ya ugaidi. Umuhimu wa kijiografia wa Somalia katika Pembe ya Afrika imetajwa kuwa ndiko kunako wafanya viongozi wa Marekani waipe uzito mkubwa nchi hiyo. H a t a h i v y o , k wa upande mwingine hususan kuhusu mambo yanayohusu siasa na mamlaka ya dola ya Kenya, uhusiano baina ya n c h i h i z o m b i l i u l i d h o o f i k a m wa k a u l i o p i t a , b a a d a ya aliyekuwa Balozi wa Marekani nchini humo kuwaonya Wakenya kutowapigia kura watuhumiwa wa kesi za mauaji ya halaiki, yaani Rais Uhuru Kenyatta na Makamu wake William Ruto, katika uchaguzi mkuu uliopita. Madai hayo yalikolezwa zaidi juma lililopita na ripoti iliyo m n u k u u a l i ye k u wa kiongozi wa mashitaka katika mahakama ya kimataifa ya ICC, mjini Hague Uholanzi, Louis Moreno Ocampo, akikiri kuwa alishinikizwa na mataifa ya magharibi kuweka vikwazo ili kuwazuia wawili hao wasiwanie urais katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi Machi mwaka uliopita. Kiongozi wa Kenya Kenyatta na Makamu wake William Ruto, wamekuwa wakiyalaumu mataifa ya kigeni kushinikiza kesi dhidi yao katika mahakama ya ICC. Hata hivyo, Balozi wa Marekani nchini Kenya Robert Godec, amekanusha madai hayo akisema miradi yao yote nchini Kenya imeruhusiwa na serikali. Bw. Godec alisema serikali yake imekuwa ikichangia maendeleo na utawala bora nchini

MUUAJI wa Kikristo (Anti-Balaka) akiburuta maiti ya kijana wa Kiislamu mjini Bangui.

Kenya kwa kipindi cha miaka 50. Tamko kali la Kamati ya Usalama waTaifa ya K e n ya d h i d i ya Marekani, limekuja baada ya wanaharakati wa asasi za kijamii kufanya maandamano dhidi ya serikali mjini Nairobi. Polisi walilazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi k u w a t a w a n y a waandamanaji jijini Nairobi wiki iliyopita. Waandamanaji hao walikuwa wakiituhumu s e r i k a l i ya J u b i l e e kuwa imejaa ufisadi na ubadhirifu na kwamba, imeshindwa kupambana na umaskini, ukosefu wa kazi na ukosefu wa usalama nchini Kenya. M r a t i b u wa maandamano hayo, Boniface Mwangi, alipinga madai hayo. Mwanaharakati mwingine mashuhuri nchini Kenya Timothy Njoya, aliyeshiriki katika maandamano hayo, alisema kuwa madai ya serikali ya Kenya ni ya kipuuzi.

Waislam watakiwa kuchangia dhamana Masheikh Uamsho


Inatoka Uk. 1 katika ofisi za Imamu wa Msikiti wa Mtambani, Jumatatu wiki hii. Kufuatia wito huo, S h u r a ya M a i m a m , imeaanda Kongamano kubwa katika Msikiti wa Makukula Buguruni, Jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kufanya harambee ya michango kwa ajili ya dhamana ya Masheikh. Akiongea kwa niaba ya Amir wa Shura ya M a i m a m , I m a m wa Msikiti wa Mtambani, Abuu Rahiyan, alisema Kongamano hilo litaanza majira ya saa nne asubuhi na kuhitimishwa mara b a a d a ya s wa l a ya Adhuhuri (saa Saba). Alisema, ujumbe wa Masheikh kutoka Zanzibar, watakuwepo kuzungumza na Waislamu na kuelezea mwenendo mzima wa kesi hiyo ambayo imeweka historia kufutatia masharti ya dhamana waliyowekewa Masheikh waliopo gerezani. Alisema, mbali ya Masheikh hao kutoka Zanziba, pia watakuwepo Masheikh wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu wa Jijini Dar es Salaam, na Morogoro, ambapo kwa ujumla watazungumzia m we n e n d o wa k e s i zinazowakabili Masheikh wa Tanzania B a r a n a Wa i s l a m u wengine kwa ujumla. Aidha, Imam huyo alisema Masheikh hao pia watazungumzia uteuzi na ushiriki wa Masheikh wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu wakiongozwa na Amir wa Baraza Kuu na Shura ya Maimam, Alhaj Mussa Yusuph Kundecha, katika Bunge la Katiba. Akizungumzioa juu ya ziara yao, Amir Khamis, akiwa ameambatana na ujumbe maalum kutoka Zanzibar, alisema wamefika Jijini Dar es salaam, kukusanya n g u v u k u t o k a k wa

Makala

RABIUL THAN 1435, IJUMAA FEBRUARI 21-27, 2014

AN-NUUR

BAADHI ya Masheikh wa Uamsho wakiwa Msikitini kabla kukamatwa. Waislamu ili kuweza kukabiliana nakadhia ya dhamana ya Mashekh waliopo mahabusu kwa muda wa mwaka mmoja na miezi minne sasa. A l i s e m a , kilichowasukuma kufika Jijini Dar es Salaam, ni kukusanya nguvu kutoka kwa Waislamu wa Tanzania Bara, ili kuweza kupatajumla ya S h i l i n g i M i l i o n i miambili Hamsini, kwa ajili ya dhamana ya Masheikh. Tunawaomba Wa i s l a m u k u wa pamoja katikakuitafuta dhamana ya Masheikh wetu, kwa kuzingatia Khadithi ya Mtume Muhammad (s a w) inayosema, mwenye kumsitiri Muislamu mwenzake naye atamsitiri siku ya k i a m a , n a m we n ye kumuondoshea uzito mwenzake katika maisha ya dunia naye Allah (sw) atamuondoshea uzito katika maisha yake ya akhera, kwa hivyo kila Muislamu aweze kutoa mchango wake kutimiza jambo hilo.Alisema Amir Khamisi. Alisema, tokea kutolewa masharti ya dhamana hiyo ambayo imeelezwa masharti yake hayajawahi kutolewa popote katika t a wa l a z i n a z o f u a t a utawala wa sheria, wamekuwa wakipigania kufanikisha dhamana ya Masheikh hao ili ikiwezekana ipatikane kabla ya Februari 27, siku ambayo kesi yao itatajwa tena. Amir, Khamisi alisema, ikiwa watafanikisha kukusanya michango hiyo na kutekeleza masharti mengine, basi siku hiyo (Februari 27) wataweza kuondoka na Viongozi hao na wa t a k u wa wa k i f i k a Mahakamani hapo wakitokea majumbani mwao. Alisema, mathalani wakipatika Waislamu Stini elfu, na kila mmoja akato akiasi cha shilingi elfu tano, kwa muda mfupi watakuwa wamepata shilingi milioni mia tatu. Tu n a h i t a j i k i l a Muislamu achangie kwa uchache kiasi cha Shilingi elfu tano tu, na yule ambaye atajaaliwa z a i d i b a s i a n a we z a kutoa pia.Tunalazimika kufanya hivi kutokana na ugumu wa masharti yaliyowekwa na M a h a k a m a K u u ya Zanzibar. Alisema Shkh. Khamisi. Amir, Khamis, alisema wamewekautaratibu wa kukusanya pesa kwa njia ya mitandao yote ya simu za mkononi, kwa Muislamu mmoja mmoja na kupitia Misikitini katika mkusanyiko wa Waislamu. Alisema, kuna risiti maalum kwa wale watakao changia ambapo baada ya kuchangia atapatiwa ili kuepuka uchangiaji holela au kuwaepuka matapeli watakaoibuka kuchangisha kwa k u t u m i a a n u a n i ya mchango wa dhamana ya Masheikh. Kuna watu maalum watafanya zoezi hili na watakuwa na risiti maalum, ambazo zitatolewa na michango ya Msikitini itatolewa risiti moja kwa anuani ya Msikiti kwa niaba ya waumini wa Msikirti husika. Alifafanua Shkh. Khamisi. Amir. Khamis, alisema michango hiyo inahitajika mpaka Inaendelea Uk. 7

Waislam watakiwa kuchangia dhamana Masheikh Uamsho


Inatoka Uk. 6

Makala

RABIUL THAN 1435, IJUMAA FEBRUARI 21-27, 2014

AN-NUUR

Februari 26, 2014, kabla ya Masheikh hao kurudi

Mahakamani Februari 27, 2014, na baada ya hapo alisema, wataangalia na kuwatangazia Waislamu hali imekuwaje. Sasa hivi tumeweka zoezi hili kama awamu ya kwanza mpaka hadi Februari 26, 2014, ili kutazama tumefanikiwa kwa kiasi gani na kama michango na masharti yakiwa bado basi michango itaendelea, mpaka tufanikiwe. Alisema. Hata hivyo, alidaiJaji wa Mahakama Kuu Zanzibar, katika kesi hiyo katika kutoa kwake masharati ya dhamana amefanya u b a g u z i wa d h a h i r i , kwa kutaka wadhamini kuwa wafanya kazi wa Serikali tu, akimaanisha waliokuwa si wafanyakazi Serikalini hawana haki ya kuwachukulia dhamana Masheikh hao. Hichoni kitendo kinachokwenda kinyume na Katiba ya nchi, Mahakama ilikuwa ndio chombo ambacho kiwe cha kwanza kulinda haki za raia lakini imekuwa ya kwanza kuvunja haki na kuwabagua raia, kwa hili Jaji ametoa sharti ambalo limekwenda kinyume na Katiba.Alisema. A l i s e m a , Wa i s l a m u h a w a n a b u d i kumtanabaisha Jaji Bi. Fatma, kwamba amewanyima baadhi yao haki ya kuwachukulia dhamana viongozi wa o k wa wa l e wa s i o wafanyakazi, ambao ndio asilimia kubwa ya Wazanzibar. Wa f a n y a k a z i w a Tanzania Zanzibar ni asilimia thelathini tu, sisi tusio wafanyakazi tupo we n g i , k wa m a s h a r t i hayo mtu anashindindwa kumchukulia dhamana ndugu yake kwa sababu si mfanyakazi wa Serikali hivyo tumenyimwa haki yetu hiyo. Alisema akionyesha kusikitishwa na masharti hayo. Amir. Khamis, alisema Pamoja na ugumu huo jitihada zinafanyika kwa pamoja ikiwa ni kutafuta pesa na kuangalia uwezekano wa kuwapata hao wadhamini kutoka Serikalini, ambao

SHEIKH Farid Hadd (katikati) akiwa na Sheikh Azzan Hamdan (kulia). wameshaanza kujitokeza huku akiwatoa hofu kwa d h a n a ya k u f u k u z wa kazi kwani hiyo ni haki yakikatiba kumchukulia dhamana ndugu yake au jamaa yake. Alisema, kuna masharti kama kumi waliyopewa Masheikh hao ambapo aliyataja miongoni mwa hayokuwa ni kuwasilisha pesa tasilimu 25ml, kwa kila mmoja pia wapatikane wafanyakazi watatu wa Serikali, na wawili kati ya hao wawasilishe hati ya kitu kischo hamishika kama nyuma au shamba vyenye thamani ya Shilingi 25ml, vilivyothaminiwa na mthamini wa Serikali. Lakini pia alisema, Masheikh hao ambao ni viongozi wa Waislamu Visiwani Zanzibar na Tanzania kwa ujumla, wa m e t a k i wa wa s i t o e m a wa i d h a i s i p o k u wa kuswalisha tu sambamba nakutotoka nje ya Kisiwa cha Unguja. Haya mashari yote ni magumu sana kulingana na makosa wanayo tuhumiwa nayo na mengine yanapingana na Katiba ya nchi.Alisema Amir Khamis. Awali, Amir Khamis, alisema wanaimani k w a m b a Wa i s l a m u wa k ip a ta ta a rifa h iz i Bara na Visiwani pesa hiyo inaweza kupatikana kwa siku moja tu kama wataamua na si zaidi ya siku kumi, kubwa ni taarifa kuwafikia Waumini. A l i s e m a , Wa i s l a m u waelewe kuwa Masheikh hao ni watetezi wa haki na siku zote unaposimama katika haki katika utawala usiofuata haki, haya ni matokeo yake. Hata hivyo alisema, b a a d h i ya Wa i s l a m u Zanzibar, waliopata taarifa hizi wameitikia wito lakini wengi wametoa ahadi kulingana na hali ya kiuchumi ilivyo sasa ndio maana ikawalazimu kutoka nje ya Visiwa hivyokwani Waislamu wote ni ndugu. Ahadi zipo nyingi kutoka kwa baadhi y a Wa i s l a m u l a k i n i bado hatujafikia lengo lililokusudiwa kwa sababu t u n a i m a n i Wa i s l a m u wengi hawana taarifa na hawajahamasishwa au kupewa utaratibu wa kutoa michango yao. Alisema. Amir Khamis, alisema wa k i wa J i j i n i D a r e s Salaam, watatembelea katika Misikiti mbalimbali kuwapa taarifa hizi Wa i s l a m u , a m b a p o aliomba ikiwa kuna Msikiti au Muislamu yoyote atawahitajikwa ajili ya kuchangia wapo tayari kuwafikia. Natoa taarifa kwa Waislamu kwa ujumla wao, kila atakayepata taarifa hii ajitokeze katika kutoa mali yake au chochote alichojaaliwa kwa ajili ya kutarajia kupata malipo kutoka kwa mola wake. Alisema Naibu Amir Shkh. Yusuph Hamisi. Amir Khamis, alizitaja namba za simu za kutuma michango kwa ajili ya kukamilisha dhamana ya masheikh hao, kuwa ni EZY PESA-0773 388 080. TIGO PESA-0715 312 238. M.PESA-0757 262 585, Pamoja na AIR TEL MONEY-0785 790 485. Masheikh na viongozi hao wa Jumuiya ya Uamsho Zanzibar, walikamatwa n a k u f u n g u l i wa k e s i katika Mahakama Kuu, ambayo mpaka sasa bado haijasikilizwa, ambapo Januari 31, 2014, Mahakama hiyo ya Zanzibar iliweka wazi dhamana zao zenye masharti magumu

Makala

RABIUL THAN 1435, IJUMAA FEBRUARI 21-27, 2014

AN-NUUR

UCHAMBUZI: Kutoka Ronald Reagan na Vita ya Urusi nchini Afghanistan hadi George W. Bush na Septemba 11, 2011
Na Profesa Michel Chossudovsky Global Research, Septemba 9, 2010
MAKALA hii inaweka kwa ufupi machapisho ya awali kuhusu tukio la 9/11 na nafasi ya Al Qaeda katika sera za nje za Marekani. Kwa maelezo zaidi angalia Michel Chossudovsky, A m e r i c a s Wa r o n Te r r o r i s m , G l o b a l Research 1005. Marekani ilitumia m a m i l i o n i ya d o l a kuwapelekea watoto wa shule nchini Afghanistan vitabu vya kiada vilivyojaa picha za kikatili na mafundisho ya utumiaji nguvu ya Kiislamu . Vitabu hivyo vya kufundishia madarasa ya awali, vilivyojaa lugha ya Jihad na michoro ya bunduki, risasi, wanajeshi na mabomu ya kutegwa, vimekuwa vikitumiwa kuanzia wakati huo kama sehemu ya mafunzo muhimu. Hata utawala wa Taliban ulitumia vitabu hivyo kutoka Marekani (gazeti la Washington Post, Machi 23,2002) Matangazo ya biashara, yaliyolipwa kutoka mifuko ya CIA, yaliwekwa katika magazeti na vijarida kote duniani kuahidi vivutio na motisha kujiunga na Jihad. ( Pe r ve z H o o d b h o y , Peace Research, May 1, 2005) B i n L a d e n aliandikisha wapiganaji wa kujitolea elfu nne kutoka nchini mwake na kujenga mahusiano ya karibu na wengi kati ya viongozi wa siasa kali wa Mujahidina. Pia alifanya kazi kwa karibu na CIA,. Tangu Septemba 11 (2001) maofisa wa CIA wamekuwa wakisema kuwa hawakuwa na uhusiano wa moja kwa moja na bin Laden. (Phil Gasper, International Socialist Review, NovembaDesemba 2001) Marejeo muhimu -Osama bin Laden, m t w i s h wa j i m i z i g o mkuu wa Marekani, aliandikishwa na CIA mwaka 1979 wakati Jihad inayofadhiliwa na Marekani ilipoanza (nchini Afghanistan). Alikuwa na umri wa miaka 22 na alipewa mafunzo katika kambi ya kufunza wapiganaji porini iliyoundwa na CIA . - Wa a n z i l i s h i w a mkakati wa kificho kuunga mkono siasa kali ya Kiislamu ulioanzishwa wakati wa utawala wa Ronald Reagan ulikuwa muhimu katika kuanzisha Vita dhidi ya Ugaidi ya dunia nzima baada ya Septemba 11. -Rais Reagan alikutana na viongozi wa Islamic Jihad katika Ikulu ya Marekani mwaka 1985. - Chini ya utawala wa Reagan, sera ya nje ya Marekani ilielekea kuunga mkono bila kipingamizi na kuwakubali wapigania uhuru wa Kiislamu. Katika dunia ya leo, wapigania uhuru hao wanapachikwa jina la magaidi wa Kiislamu. -Katika lugha ya Pashtun, neno Taliban lina maana ya Wa n a f u n z i , a u wahitimu wa madrasa (vituo vya kusomea au shule za Kurani)

RAIS wa zamani wa Marekani Ronald Reagan (mwenye suti nyeusi) akiongea na viongozi wa Mujahidina wa Afghanistan Ikulu ya Marekani. zilizoundwa na wakufunzi Wahhabi kutoka Saudia, kwa msaada wa CIA. - Elimu katika kipindi kilichotangulia vita ya Urusi na Afghanistan ilikuwa zaidi ni ya kawaida. Mkakati wa siri wa elimu wa Marekani uliharibu e l i m u ya k a wa i d a . Idadi ya mashule za kidini (madrasa) yaliyofadhiliwa na CIA iliongezeka kutoka 2,500 mwaka 1980 hadi zaidi ya 39,000 miaka kadhaa baadaye. Vi t a ya U r u s i n a Afghanistan ilikuwa ni sehemu ya agenda ya siri ya CIA iliyoanzishwa wakati wa utawala wa Jimmy Carter ambayo hasa ililenga kuunga mkono na kutoa fedha kwa brigedi za Kiislamu, baadaye zikaitwa Al Qaeda. Serikali ya kijeshi ya Pakistan ilikuwa na nafasi kuanzia mwanzo katika miaka ya 1 9 7 0 m w i s h o n i , nafasi muhimu katika operesheni za kijeshi na kijasusi nchini Afghanistan z i l i z o s i m a m i wa n a Marekani. Baada ya k u m a l i z i k a k wa Vita Baridi, nafasi hii ya Pakistan katika operesheni za kijasusi za Marekani ilipewa upana zaidi katika eneo la Asia ya Kati na Mashariki ya Kati. Kuanzia mwanzo wa vita ya Urusi na Afghanistan mwaka 1979, Pakistan chini ya utawala wa kijeshi iliunga mkono kwa nguvu brigedi za Kiislamu. Ikishirikiana kwa karibu na CIA, idara ya ujasusi wa kijeshi ya Pakistan, Inter Services Intelligence (ISI) ikawa taasisi yenye nguvu, serikali ya ziada, yenye kukusanya nguvu na ushawishi mkubwa. Vita ya siri ya Marekani nchini Afghanistan , i k i t u m i a Pa k i s t a n kama jamvi la kuruka kufika Afghanistan, ilianzishwa wakati ya utawala wa Carter kabla ya uvamizi wa Urusi nchini Afghanistan. K wa m u j i b u wa historia rasmi, misaada ya CIA kwa Mujahidina ilianza mwaka 1980, kwa maana kuwa ni baada ya jeshi la Urusi kuvamia Afghanistan, Desemba 24, 1979. Lakini hali halisi, iliyokuwa imelindwa kwa siri hadi sasa, ni tofauti kabisa. Naam, ilikuwa Julai 3, 1979 ambako Rais Carter alitia saini agizo la kwanza la kupeleka misaada ya siri kwa wapinzani wa utawala wenye kukabiliana na Urusi mjini Kabul. Siku hiyo hiyo, niliandika dokezo kwa rais ambapo nilimweleza kuwa kwa
Inaendelea Uk. 9

Makala

RABIUL THAN 1435, IJUMAA FEBRUARI 21-27, 2014

AN-NUUR

Inatoka Uk. 8 maoni yangu msaada huu utasababisha Urusi iingilie kijeshi nchini Afghanistan. (Mshauri za zamani wa Usalama wa Taifa nchini Marekani, Zbigniew Brzezinski, akihojiwa na Le Nouvel Observateur, jarida la Ufaransa, toleo la Januari 15-21 1998). Katika kumbukumbu binafsi alizochapisha Waziri wa Ulinzi Robert Gates, ambaye alikuwa katika nafasi ya Naibu Mkurugenzi Mkuu wa CIA wakati vita ya Urusi nchini Afghanistan inauma, ujasusi wa Marekani ulilenga kuanzia mwanzo, kabla ya uvamizi wa Urusi, kupeleka misaada kwa brigedi za Kiislamu. Wakiungwa mkono na CIA na kupelekewa misaada mingi ya kijeshi, ISI ya Pakistan ilikuzwa na kuwa mfumo tofauti wenye nguvu katika fani zote za serikali, anasema Dipankar Banerjee, Uwezekano wa uhusiano kati ya ISI na uzalishaji wa madawa ya k u l e v ya k a t i k a jarida la India Abroad, Desemba 2, 1994. ISI i l i k u wa n a m a o f i s a wa kijeshi na kijasusi, wa t a wa l a , m a j a s u s i kificho na watoa taarifa, wanaokisiwa kufikia 150,000 kwa mujibu wa jarida hilo. Wa k a t i h u o h u o , operesheni za CIA zilikuwa zimelipa nguvu jeshi la Pakistan likiongozwa na Jenerali Zia Ul Haq: Mahusiano kati ya CIA na ISI yalizidi kuimarika baada ya (Jenerali) Zia kumwondoa (Zulfikar Ali) Bhutto na kuanza kwa utawala wa kijeshi. ..Wakati wa kipindi chote cha vita ya

UCHAMBUZI: Kutoka Ronald Reagan na Vita ya Urusi nchini Afghanistan hadi George W. Bush na Septemba 11, 2011
Afghanistan, Pakistan ilikuwa na chuki zaidi kuhusu Urusi kuliko hata Marekani. Mara baada ya majeshi ya Urusi kuvamia Afghanistan mwaka 1980. Zia (ul Haq) alimpeleka mkuu wake wa ISI kuvuruga mataifa ya Urusi ya Asia ya Kati. CIA ilikubali mpango huu baadaye mwezi Oktoba 1984, kwa mujibu wa jarida hilo hilo. ISI ikiwa inafanya kazi kama idara tanzu ya CIA, ilichukua nafasi kubwa katika kupeleka misaada kwa makundi ya kijeshi ya Kiislamu nchini Afghanistan na baadaye katika jamhuri za Kiislamu za iliyokuwa Urusi. Ikitekeleza shughuli za CIA, shirika la ISI lilijishughulisha na kuandikisha na kutoa mafunzo kwa Mujahidina. Katika kipindi cha miaka kumi kutoka 1982 hadi 1992, kiasi cha wapiganaji 35,000 kutoka nchi 43 za Kiislamu waliandikishwa kupigana katika Jihad nchini Afghanistan. Madrasa nchini Pakistan, yakifadhiliwa na vikundi vya misaada vya Saudia, vilianzishwa kwa msaada wa Marekani kwa nia ya kukuza maadili ya Kiislamu. Makambi h a y o ya k a wa v y u o vikuu vya ukereketwa wa Kiislamu huko baadaye, kwa mujibu wa A h m e d R a s h i d , katika kitabu The Taliban. Mafunzo ya wapiganaji wa porini chini ya CIA na ISI yalikuwa ni pamoja na mauaji ya kuvizia ya mtu mmoja mmoja, na mashambulio kwa kutumia bomu la kutegeshea katika gari.

GEORGE W. Bush.

Dick Chenney Trade. Angalia pia McCoy, 2003, uk. 477) Osama bin Laden Osama bin Laden, m t w i s h wa j i m i z i g o mkuu wa Marekani, aliandikishwa na CIA mwaka 1979 wakati inaanza Jihad iliyofadhiliwa na Marekani. Alikuwa na umri wa miaka 22 na alipewa mafunzo katika kambi iliyoundwa na kusimamiwa na CIA. Wakati wa utawala wa Reagan, Osama, ambaye alitokea familia tajiri ya ki-Saudi ya B i n L a d e n a l i p e wa nafasi ya kusimamia utafutaji fedha kwa ajili ya brigedi za Kiislamu. Makundi tofauti ya kusaidia wenye shida na mifuko maalum iliundwa. Operesheni hiyo ilisimamiwa na idara ya ujasusi ya S a u d i a i k i o n g o z wa na Pr i nce Tu r ki a l Faisal, akishirikiana kwa karibu na CIA. Fedha iliyotokana na mashirika ya misaada ilitumika kulipia kusajili Mujahidina wa kujitolea. Al Qaeda, au maskani kwa Kiarabu ilikuwa ni kituo cha kukusanya wapiganaji wa kujitolea walioandikishwa kupigana katika jihadi ya Afghanistan. Kituo hicho cha kuhifadhi taarifa na takwimu za walioandikishwa hapo mwanzo kiliongozwa na Osama bin Laden. Utawala wa Reagan waunga mkono siasa kali ya Kiislam Shirika la Ujasusi la kijeshi la Pakistan, ISI lilitumika kama mshenga. Misaada ya kificho ya CIA kwa Mujahidina nchini Afghanistan ilifanyika
Inaendelea Uk. 11

Silaha zilipelekwa na jeshi la Pakistan na ISI kwa makambi ya waasi katika jimbo la mpakani Kaskazini Magharibi karibu na mpaka wa Afghanistan. Gavana wa jimbo hilo ni Luteni-Jenerali Fazle Haq ambaye (kwa mujibu wa Alfred McCoy) aliruhusu m a m i a ya m i t a m b o ya kusafisha heroin kujengwa katika jimbo alilosimamia. Kuanzia mnamo 1982, magari ya kijeshi ya Pakistan yakiwa yamebeba silaha za CIA kutoka Karachi mara kadhaa hupakia heroin katika jimbo la Haq na kurudi yamejaa h e r o i n . Ya n a l i n d wa yasipekuliwe na polisi kutokana na vitambulisho vya ISI . (1982-1989: US Turns Blind Eye to BCCI and Pakistan Government Involvement in Heroin

10

Makala

RABIUL THAN 1435, IJUMAA FEBRUARI 21-27, 2014

AN-NUUR

Dhamana ya Sheikh Ponda yaiva


Na Mwandishi Wetu

MAHAKAMA Kuu K a n d a ya D a r e s Salaam, imeahirisha kesi inayomkabili Katibu wa Jumuia na Taasisi za Kiislamu nchini Sheikh Ponda Issa Ponda, hadi Februari 26, 2014, kufuatia ombi la upande wa mashtaka kutaka upewe muda kujiandaa zaidi. Kesi hiyo ilisikilizwa tena katika Mahakama hiyo Jumatano wiki hii, kwa ajili ya kusikiliza m a o m b i ya r u f a a yaliyowasilishwa na mawakili wa Sheikh Ponda Mahakamani hapo. Jaji Agustino Mwalija wa Mahakama Kuu,aliyesikiliza kesi hiyo, alikubaliana na maombi ya Wakili wa Serikali Bw. Tumaini Kweka, aliyeiomba Mahakama hiyo kuupa upande wa mashtaka muda zaidi ili wajiandae vizuri. Akiongea nje ya Mahakama h i y o , Wa k i l i J u m a Nassoro, alisema s i k u ya J u m a t a n o ilikuwa Mahakama isikilize maombi yao ya dhamana waliyowasilisha awali katika Mahakama hiyo. Kesi leo ilikuwa imekuja kwa ajili ya kutajwa kufuatia maombi tuliyowasilisha Mahakamani hapa, ili iweze kupitia mwenendo mzima wa ile kesiya Morogoro. A l i s e m a Wa k i l i Nassoro. Akifafanua zaidi Wakili Juma, alisema wa l i a m u a k u r u d i

SHEIKH Ponda Issa Ponda (kushoto) akizungumza na Mawakili wake katika Mahakama Kuu Jijini Dar es Salaam Jumatano. (Picha na Abdulkarim Msengakamba)

katika Mahakama Kuu, kufuatia kuwapo kwa mapungufu mengi na makubwa ya kisheria katika kesi aliyofunguliwa Sheikh Ponda, Mjini Morogoro. Leo ( Jumatano) kilichotokea ni kwamba upande wa Jamhuri hawajajibu bado yale maombi yetu, kwa hivyo wametakiwa wajibu ifikapo Februari 24, 2014. Na sisi kama tutakuwa na maelezo mengine tutayatoa Februari 25, hivyo kesi imeahirishwa hadi Februari 26, 2014. ( Jumatano ya wiki ijayo) ambapo tutarudi Mahakamani hapa kuendelea. Alisema Wakili Nassoro.

Hata hivyo alisema kwamba kuwapa m u d a u p a n d e wa Mashtaka ni jambo la kawaida katika taratibu za kimahakama kwasababu kesi haiwezi kuanza kusilizwa mpaka pande mbili zinazohusika ziwe zimewawasilisha vielelezo vyake muhimu na ndiyo jambo tunalolitaka. Sheikh Ponda Issa Ponda, ambaye Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, anakabiliwa na kesi ya uchochezi sambamba na kudaiwa kukiuka amri ya Mahakama ya Kisutu iliyomhukumu kifungo cha nje cha mwaka mmoja mwaka jana.

DVD, inayozungumzia umuhimu wa Elimu ya kumjua ALLAH (SWT), sasa zinapatikana. Mwasilishaji wa mada hiyo ni Sheikh Fahad Ibrahim kutoka Shule ya Alfurqaan, BuguruniMalapa. Kwa mahitaji na mawasiliano zaidi piga Simu No:- 0773 032 328, 0712 232 328, 0768 816 040.

DVD

DVD

DVD

11

Makala

RABIUL THAN 1435, IJUMAA FEBRUARI 21-27, 2014

AN-NUUR

Inatoka Uk. 9

UCHAMBUZI: Kutoka Ronald Reagan na Vita ya Urusi nchini Afghanistan hadi George W. Bush na Septemba 11, 2011
kuliongezeka kutoka tani 10,000 za bunduki na risasi mwaka1983 hadi tani 65,000 kwa mwaka, mnamo 1987. Pamoja na silaha, kutoa mafunzo, vifaa vingine muhimu vya kijeshi vilipelekwa ikiwa ni pamoja na picha za kijeshi za satelaiti na vifaa vya kisasa zaidi vya mawasiliano, kwa mujibu wa jarida la University Wire, Mei 7, 2002. Wa k a t i wa u t a wa l a wa William Casey kama Mkurugenzi Mkuu wa CIA, NSDD 166 ilielezewa kuwa operesheni ya siri kubwa kuliko zote katika historia ya Marekani. Mkusanyiko huo wa m i s a a d a u l i k u wa n a sehemu muhimu tatu utawala na miundombinu, teknolojia ya kijeshi, na msaada wa propaganda kwa kuendeleza na kuhimiza upinzani wa Afghanistan (kwa uwepo wa jeshi la Urusi nchini humo). Lakini mchango mkubwa zaidi wa Marekani ilikuwa ni kuleta watu na silaha kutoka nchi za Kiarabu na kwingineko. Wapiganaji wenye uzoefu n a d h a m i r a ya d h a t i kiitikadi walitafutwa kwa mantiki kuwa watakuwa ndiyo wapiganaji bora. Matangazo, yaliyolipiwa na fedha kutoka CIA, yaliwekwa katika matangazo na vijarida kote duniani yakiahidi motisha na ushawishi wa kujiunga na Jihad, (kwa mujibu wa Pervez Hoodbhoy, Afghanistan na Chanzo cha Jihad ya Kimataifa, Peace Research, May 1, 2005) Usisitizaji wa itikadi ya kidini Chini ya NSDD 166, misaada ya Marekani kwa brigedi za Kiislamu iliyokuwa ikipitia Pakistan, haikuwa tu ni kwa mahitaji ya kijeshi. Washington pia iliunga mkono na kutoa fedha kwa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) kuendeleza uinuaji itikadi ya dini, iliyowezesha kuangamizwa kwa taasisi za kiraia, za kawaida.

k wa kificho kupitia ISI,

hivyo CIA haikupeleka misaada moja kwa moja kwa Mujahidina. Kwa maneno mengine, ili operesheni hiyo ya siri ifaulu, Washington iliweka tahadhari ya kutokufichua lengo la msingi la Jihad hiyo, ambalo hasa lilikuwa ni kuiteketeza Urusi. Mwezi Desemba 1984, S h a r i a ( ya K i i s l a m u ) ilitangazwa kama mfumo wa sheria nchini Pakistan baada ya kura ya maoni iliyovurugwa na utawala wa kijeshi wa Jenerali Muhammad Zia ul-Haq. Miezi michache baadaye, Rais Ronald Reagan alitoa uamuzi wa Usalama wa Taifa namba 166 kutoa misaada ya siri kwa wingi zaidi kwa Mujahidina pamoja na kuunga mkono propaganda za kidini. Kutangazwa kutumika kwa Sharia nchini Pakistan na kuinuliwa kwa siasa kali ya Kiislamu ilikuwa ni sera ya makusudi ya Marekani kufikia malengo yake ya kimkakati katika eneo la Kusini ya Asia, Asia ya Kati na Mashariki ya Kati. Makundi ya hivi karibuni ya siasa kali ya Kiislamu yalipata misaada ya moja kwa moja au kwa kificho kutoka Marekani, mara nyingi ikipitia mashirika ya misaada ya ki-Saudia na nchi za Ghuba. Wakufunzi kutoka wanazuoni wa ki-Wahhabi nchini Saudi Arabia, wasiotaka lipunguzwe neno lolote katika sharia, wa l i p e wa k u s i m a m i a mpango wa madrassa yanayofadhiliwa na CIA kaskazini ya Pakistan. Chini ya amri ya NSDD 166, mfululizo wa operesheni za siri za CIA na ISI ulianza. Marekani ilitoa silaha kwa brigedi za Kiislamu kupitia ISI. Maofisa wa CIA na ISI walikuwa wanakutana katika makao makuu ya ISI mjini Rawalpindi kuwezesha misaada ya Marekani kwa Mujahidina. Chini ya NSDD 166, kupatikana kwa silaha za Marekani kwa wapiganaji wa Kiislamu

Picha: Mstari wa mbele kutoka kushoto: Meja Jenerali Hamid Gul, Mkurugenzi Mkuu wa ISI (idara kuu ya ujasusi ya jeshi la Pakistan), Mkurugenzi Mkuu wa CIA William Webster, Naibu Mkurugenzi wa Operesheni Clair George, kanali wa ISI, na afisa mwandamizi wa CIA, Milt Beearden, wakiwa katika kambi ya kufunza Mujahidina jimbo la mpakani la kaskazini magharibi ya Pakistan, mwaka 1987. (Picha na RAWA).
Marekani ilitumia mamilioni ya dola kuwapatia watoto wa shule nchini Afghanistan vitabu vya kusomea ilivyojaa picha za ukatili na shari za mafundisho ya Kiislamu, sehemu ya operesheni ya kificho ya kuinua upinzani kwa kukaliwa na Urusi nchi hiyo. Vitabu hivyo vya awali, ambavyo vilikuwa vimejaa lugha ya Jihad na michoro ya bunduki, risasi, wapiganaji na mabomu ya kutegwa, vimeendelea kutumika kama vitabu vya kiada (vya kufundishia) katika mfumo wa masomo wa Afghanistan. Hata Taliban ilipokuwa madarakani ilitumia vitabu vilivyotengenezwa Marekani. I k u l u ya M a r e k a n i ilitetea mwelekeo huo wa kidini wa vitabu, ikisema kuwa kanuni za Kiislamu zimejijenga katika utamaduni wa Afghanistan na kuwa vitabu hiyo vinaendana kabisa na sheria na sera za Marekani. Wataalamu wa sheria hata hivyo, wanauliza kama vitabu hivyo havikiuki kanuni ya kikatiba ya kupiga marufuku kutumia fedha za kodi kuhamasisha dini. Maofisa wa shirika la misaada la USAID walisema katika mahojiano kuwa waliacha vitabu hivyo bila kugusa kilichoandikwa kwa sababu waliogopa wakufunzi wa ki-Afghani watakataa vitabu ambavyo havina chembe nzito ya fikra ya Kiislamu. Shirika hilo liliondoa nembo yake na ishara yoyote kuhusu Serikali ya Marekani katika vitabu vya dini, msemaji wa USAID Kathryn Stratos alisema. "Siyo sera ya USAID kuunga mkono mafundisho ya dini," alisema. "Lakini tuliendelea na mradi huo kwa sababu dhamira muhimu ....ni kuwafundisha watoto, kitu ambacho hasa ni cha kawaida (siyo cha kidini)." ...Ikiwa inachapishwa katika lugha muhimu za Afghanistan za ki-Dari na ki-Pashtuni, vitabu hivyo vya kusomesha vilitengenezwa katika miaka ya awali ya 1980 chini ya msaada wa USAID kwa Chuo Kikuu cha Nebraska, jimbo la Omaha, na kituo chake cha utafiti juu ya

Afghanistan. Shirika hilo lilitumia dola milioni 51 katika programu za chuo kikuu hicho kuhusu Afghanistan, kuanzia 1984 hadi 1994," kwa mujibu wa gazeti muhimu la Washington Post, Machi 23, 2002. (Imefasiriwa kwa Kiswahili na Anil Kija kutoka-9/11 ANALYSIS: From Ronald Reagan and the Soviet-Afghan War to George W Bush and September 11, 2001-Hii ni sehemu ya uchambuzi wa Prof Michel Chossudovsky, Global Research, September 09, 2010.)

12

Mashairi/Makala

BUNGE LA KATIBA (ADA YA MJA HUNENA...!)


Wahenga walishanena, si leo toka zamani Ada ya mja hunena, methali kamilisheni Msibakie kuguna, mkishindwa ulizeni Yanenwayo na kupangwa, twayangoja matendoni. Si juzi wala si jana, ni Jumanne jioni Tulipoanza kuona, na kusikiza uneni Mwororo tena mwanana, wa wajumbe 'mjengoni' Yanenwayo na kupangwa, twayangoja matendoni. Yanenwayo yatafana, kwa kutiwa matendoni Bali yatavia sana, kwa kubaki 'HANSADINI' Tija na yake maana, ni kuchakatwa kazini Yanenwayo na kupangwa, twayangoja matendoni. Sioni yake maana, kuyajaza 'HANSADINI' Na kubaki 'lundikana, mithili taka jaani Si jambo la kiungwana, na ninyi tafakarini Yanenwayo na kupangwa, twayangoja matendoni. Kwa sasa nachokiona, ni viroja 'HANSADINI' Migombo na kuzozana, na misutano bungeni Kumbukumbu kujazana, kama hizi ni kwanini Yanenwayo na kupangwa, twayangoja matendoni. Kwangu hasa ya maana, 'HANSADI' ya vitendoni Katu si yenye maana, 'HANSADI' ya kaulini Kwa 'HANSADI' ya maana, utendi tuuenzini Yanenwayo na kupangwa, twayangoja matendoni. Shime mabibi, mabwana, mlo humo'mjengoni' Aula ninokiona, utendaji himizeni Si kukaa kulumbana, kwa hoja za midomoni Yanenwayo na kupangwa, twayangoja matendoni. Kaditamati kunena, kwa vina na kwa mizani Lengo ni kukumbushana, pamwe kukuusieni "Ada ya mja hunena, muungwana kitendoni" Kwaherini waungwana, twawangoja matendoni. Abuu Nyamkomogi MWANZA. Kalamu nimeishika, kuwauliza vijana Majibu yenu nataka, msijefanya khiyana Uhuni sitautaka, nijibuni kiungwana Siku hii Valentine, asiliye hasa nini?
Kathiru twaghururika, kwa huu wetu ujana Siku hii Valentine, walengwawe hasa nani?

UPOGO WA SIKU YA VALENTINE !

Kwa kweli naliwazika, kutunukiwa ujana Japo nasikitikia, utumizi wa ujana


Wapendwa mnopendeka, wapenzi wa Valentina Nipeni basi hakika, nini hasa Valentina Yu ukhti anotajika, au siku ya fitina Siku hii Valentine, muasisiwe yu nani? Arubashara 'kifika, Februari twaona Idhaani hutajika, i siku ya Valentina Hupambwa na kupambika,na kughilibu vijana Siku hii Valentina, tarehe hii kwanini?

Thuma nderemo huzuka, za mabibi na mabwana Kumbini hujumuika, na denda wakinyonyana Kwa sana 'huserebuka', wa kila rika vijana Siku hii Valentine, mseto huu wa nini? Libasi zinovalika, ahamaru tena sana Dukuduku lanishika, kunako yake maana Kwa wale mnojivika, nijuzeni yake mana Siku hii Valentine, wekundu huu wa nini? Upendo unosifika, katu si wa kuoana Kwa nduni watambulika, ya uzinifu kufana Mwishoni huathirika, kwa 'ngoma' wengi vijana Siku hii Valentine, hatimaye hasa nini? Kichwani natatizika, nahitaji mbayana Mwenye hoja za hakika, za mambo ya Valentina Wazi apate 'niweka, kwa marefu na mapana Siku hii Valentine, Lengole hasa ni nini? Vijana mlolimbuka, vipenzi wa Valentina Nyote ninawaalika, mlo na hoja mwanana Mezani hoja naweka, nangojea mbayana. Siku hii Valentine, wa kunifunda ni nani? Upambe sitautaka, uso na hoja za mana Japo utoke kwa kaka, au dada Amina Sitaupa mlahaka, nakujuzeni bayana Utata wa Valentine, wa kuutatua nani? Abuu Nyamkomogi MWANZA.

NAPENDA kutoa maelezo machache kuhusiana na michango tulioitisha kwa ajili ya matibabu ya mtoto Mansoor Hamad Saleh ambaye anahitaji matibabu baada ya kuanguka katika mnazi na kukaa hospitali kwa mwaka mzima bila ya mafanikio. Huu ni mwaka wa tatu sasa tokea Mansoor kuwa kitandani. Daktari anayemkagua Mansoor alitupa makisio ya shilingi millioni 20 ili zipatikane asafrishwe kupelekwa India. Jitihada zetu za awali hadi sasa zimefanikisha kupatikana shilingi millioni 3 na laki 4,. Alhamdulillah. Bado tunaendelea kukusanya na Inshallah tunatarajia tutafanikiwa kwa uwezo wa Allah, nia ipo ya kumsaidia. L a k i n i p i a tumewapeleka madaktari wawili mmoja kutoka Mnazi Mmoja na mwengine kutoka Dar es Salaam na wote kimsingi wametuma mawazo matatu yanayofanana. Mtaalamu wa p h i s i o t h e r a p y ametushauri kwamba kwa muda huu anahitaji k u p a t a m a t i b a b u ya k u n y o o s h wa v i u n g o vyake ili kumpunguzia maumivu anayoyapata kwa kukaa muda mrefu katika kiti hicho cha mbao. Pili, anahitaji kubadilishiwa kiti badala cha mbao apate kiti chengine kilaini. Ta t u , t u m e a m b i wa Mansoor anahitaji kupata tiba ya kisaikolojia angalau kwanza aweze kuondokana na mawazo a l i y o n a y o ya k u k a t a tamaa na kuishi kwake. Kimsingi kufuatia hayo mashauri matatu tuliopewa na wataalamu, nimeanza kuchukua khatua na khatua ya kwanza mimi kwa kushirikiana na wazazi wake Mansoor ambao h a wa n a u w e z o h a t a kidogo, tumemsafirisha kumpeleka Dar es Salaam angalau tu aondoke hapa Zanzibar na atakuwepo

Taarifa ya Mansour

RABIUL THAN 1435, IJUMAA FEBRUARI 21-27, 2014

AN-NUUR

Mansoor Hamad Saleh


hapo kwa muda fulani ili aweze kupatiwa matibabu hayo ya awali ya kumuondoshea hali aliyonayo kisaikolojia na nadhani ataweza kidogo kuchangamka kisha tutamrejesha Zanzibar na kuanza naye phisiotherapy lakini hapo alipo ameanza kupata hayo matibabu ya phisiotherapy pia. N a k h a t u a ya p i l i tumejaribu kuongea na we n z e t u k u m u a g i z i a kiti maalumu na Alhamdulillah tunavyoambiwa kimepatikana kwa hivyo we n z e t u k wa j u h u d i kubwa sana waliosaidia kwa dhati kuchangishana fedha wamekitafuta kiti ambacho naamini kitamsaidia sana kama alivyotuelekeza daktari. Na tayari tumeshampata daktari ambaye amejikubalisha atakuwa tayari kumfuatilia Mansoor pale Mnazi Mmoja kwa hali zote hivyo hilo nalo tumefarijika sana kupata mtu dhamana na atalichukulia suala hili kwa uangalifu kabisa. Alhamdulillah, tunamshukuru na tunampongeza sana daktari wetu mzalendo kwa kubeba dhamana hii. ANGALIZO: Fedha ambazo tumetumia kumsafirisha Mansoor Dar es Salaam sio zilizochangishwa, bali fedha tunazochanga ni kwa ajili ya matibabu ambayo tumeagizwa na daktari k wa s a s a t u n a t u m i a fedha zetu tunahitaji kwanza kumsaidia aweze kupata matumaini na aondokane yale madhila yanayomkabili na Inshallah atapata nafuu kwani alikuwa anasikitisha kutokana na maumivu ayapatayo. Pamoja na kuwepo h u k u D o d o m a n i k i k a b i l i wa n a k a z i ngumu ya kitaifa, lakini bado naendelea kufuatilia kwa karibu sana hali ya Mansoor inavyoendelea na pia naendelea kukusanya michango yetu ambayo wenzetu waliojitolea wamekuwa wa k i k u s a n ya k u t o k a Oman, Dubai, Turky na Kenya na huku Zanzibar pia nimemuweka mtu kwa ajili ya kukusanya michango hiyo. Na mwisho kabisa napenda nitoe pongezi zangu za dhati kabisa kwa wale wote waliojitolea na kukubali kuchukua dhamana hii ya kukusanya michango ya mtoto wetu na wale wote waliosaidia kwa njia moja au nyengine katika kumsaidia mtoto huyu kwa kutoa michango yao ya fedha na mawazo na natoa wito zaidi watu waendelee kuchangia ili kumsaidia mwenzetu huyu.

13
Na Mtume alikuwa akisema; Ewe Mola wangu mlezi! Hakika watu wangu wameifanya hii Quran ni kihame. (25:30) Aya hiyo hapo juu inaonyesha jinsi Mtume (S.A.W) a l i v y o s h i t a k i k wa Mola wake kuhusu taabu aliyoipata kwa watu wake katika kufikisha ujumbe, lakini wakaihama, kuipuuza na kuifanyia inda na uadui. Hivyo si katika wakati wa Mtume (S.A.W) tu, bali hali imeendelea hadi leo japo Waislamu wamekiri kuwa Quran ni kitabu chao. Ni sawa na mume kujitapa ana mke, kumbe alishamtelekeza miaka chungu nzima wala hajui maisha ya huyo mke yanafanana vipi! N A M N A W A I S L A M U WA L I V Y O I H A M A QUR AN Kutokuisoma Qur an: Hawakujifunza tangu utoto, h a wa k u l e l e wa n a Quran hivyo kukata tamaa kujifunza ukubwani kwa aidha kutokuona umuhimu wake, kuridhika na Uislamu wa majina (kuoa/kuzikwa). Mbinu mbovu za ufundishaji Quran husababisha watu kukata tamaa kusoma. Kujikita zaidi katika vitu vingine vya kusoma kama C o m p u t e r , T . V, magazeti, vitabu vya hadithi, tuition kwa wanafunzi nk. Ni jambo ala ajabu kidogo mtu kujipa sifa asizokuwa nazo, hakika ataonekana k u wa a n a k a s o r o k a t i k a a k i l i ya k e . Kwa hiyo ni ajabu

Tumeihama Quran!

Makala/Tangazo

RABIUL THAN 1435, IJUMAA FEBRUARI 21-27, 2014

AN-NUUR

mtu kujiita Muislamu wakati haijui Quran. Wapo waliojifunza Q u r a n l a k i n i hawaisomi. Aidha kwa uvivu, uzembe, kazi nyingi, starehe za dunia au hawaoni f a i d a ya k u i s o m a Quran hapa duniani wala akhera. Quran wameisusa nayo imewasusa. Kuisoma kwa matini. Huku ni kusoma bila kujua maana na ujumbe halisi uliokusudiwa katika kile mtu anachokisoma, japokuwa mtu anasoma vizuri kwa hukmu na sauti ya kupendeza. Quran ni maneno ya Allah (sw) kuwapa ujumbe viumbe wake ili waufahamu na wautekeleze. Hivyo kusoma kwa kelele tu ni kupoteza muda bure na kuondoa ithibati katika kusoma. Ni sawa na mtu asiyejua kiingereza akasoma novel yote bila kuelewa maana,

h u y u a t a k u wa n a kasoro akilini. Ni Waislamu wengi wamehifadhi Quran v i f u a n i m wa o a u wa n a j u a k u i s o m a vizuri na kuona kuwa Uislamu wao u m e k a m i l i k a k wa hilo, kumbe ni sawa na punda kubeba mzigo usio na faida kwake.

Kuwaachia baadhi tu ya watu. Waislamu wamekwepa kuishi katika Quran kwa kuamini kuna watu maalumu walioteuliwa kuisoma hiyo Quran, na wao hawana ulazima wowote kwa kuwa watakuwepo Mashekhe/ Maustadhi watakaosoma kwenye

swala na khafla mbalimbali kama dua, hitma, harusi, maziko n.k, kisha wao watabakia kuwa watoaji wa malipo/ gharama kwa watu hao. Makundi yote hayo matatu yanaishi mbali na lengo la kuumbwa (51:56 ), yaani kumcha Allah (sw). Hakika mtu hawezi kumcha Allah (sw) bila kufuata njia aliyoelekeza kumcha. Na njia hiyo ipo kwenye mwongozo ambao ni Quran, (2:2) na Mtume (saw). Hiki ni kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake, ni mwongozo kwa wamchao Mwenyezi Mungu Na Quran hiyo (mwongozo) mtu hawezi kuijua hadi asome. Ndugu Waislamu, tuzinduke, tutie nia tuisome na t u i e l e w e Q u r a n . Hapo tutaithamini na kuipenda Quran na hatimaye kuifanyika kazi kama inavyotakikana. Wallahu aalam. Zabibu Idd Ngonda

SHURA YA MAIMAMU

Inawatangazia Waislamu wote Kongamano kubwa litakalo hutubiwa na Masheikh kutoka Jumuiya na Taaisi za Kiislamu Bara na Visiwani. Mada: - Hatma ya dhamana kwa Masheikh wa Uamsho Zanzibar. - Mwenendo wa kesi ya Sheikh Ponda Issa Ponda. - Ushiriki wa Viongozi (Masheikh) wa Kiislamu Katika Bunge la Katiba. Mahali:- Masjidi Makukura- Buguruni. Siku:- Jumapili, Februari 23, 2014 Muda:- 4:00 (Saa nne-Asubuhi) hadi Saa 7, baada ya Swala ya Dhuhuri. Imam Masjid Mtambani K.n.y. Amir wa Shura ya Maimam.

Kongamano

14

Makala

RABIUL THAN 1435, IJUMAA FEBRUARI 21-27, 2014

AN-NUUR

TEL AVIV NAIBU Spika wa Bunge la Israel Moshe Feiglin, amesema kuwa ardhi ya Palestina inayokaliwa k wa m a b a v u n i ya Mayahudi na kwamba, Wa p a l e s t i n a w o t e wanapaswa kupelekwa Saudi Arabia. Naibu Spika huyo ametaka Wapalestina wote waondoshwe na kupewa makazi mapya nchini Saudi Arabia. Bw. Feiglin alianza kwa kuuvunjia heshima Msikiti wa Qubbat Sughra, kwa kuingia msikitini humo na viatu na kisha k u t a n g a z a k wa m b a Wa p a l e s t i n a w o t e wanapaswa kufukuzwa na kupelekwa Saudi Arabia. Aliongeza kuwa, Quds Tukufu ni ya Mayahudi na Waarabu wanapaswa kuelekea Saudi Arabia na kwamba, nafasi ya Wapalestina iko nchini humo.

Wapalestina wote wapelekwe Saudi Arabia

SANAA Habari kutoka Yemen zinaeleza kuwa, shehena kubwa ya s i l a h a k u t o k a Marekani na Saudi Arabia imekamatwa katika jimbo la Amran lililoko kaskazini mwa Yemen. Taarifa zinasema kuwa, silaha na zana hizo za kivita zimegunduliwa katika mji wa Houth, ulioko katika jimbo la Omran, baada ya kundi la wanamgambo wa al Houthi kufanya operesheni kali katika eneo la kabila la Hashid. Taarifa zinasema kuwa, uhalifu mkubwa ukiwemo k u k a t wa k a t wa n a kuuawa kinyama

Yemen yafichua silaha za Marekani, Saudi Arabia


watoto zimeshuhudiwa katika eno hilo, baada ya wanamgambo kutoka kabila la Hashid kukimbia mji wa Houth. Taarifa hizo zimeeleza kuwa, jinai hizo za kutisha zimefanywa na makundi hayo kabla ya kutoroka katika eneo hilo. Abdulkarim ar Razihi, mmoja kati ya viongozi wa eneo hilo amesema kuwa mbali ya kukamatwa kiasi kikubwa cha silaha na milipuko, makundi hayo ya wanamgambo walishafanikiwa kufanya uhalifu kubwa katika eneo hilo. Siku za hivi karibuni yameshuhudiwa mapigano makali kati ya wanamgambo wa al Houthi dhidi ya makundi ya Kiwahabi na Kisalafi ambayo yanapata misaada ya silaha na fedha kutoka Saudi Arabia.

NAIBU Spika wa Bunge la Israel Moshe Feiglin.

RAIS wa Marekani, Barack Obama.

15

Matukio

Masheikh wapata ajali

RABIUL THAN 1435, IJUMAA FEBRUARI 21-27, 2014

AN-NUUR

WA N A H A R A K AT I w a Kiislamu, Sheikh Hamisi Shemtoi (kushoto) akiwa na Ustadhi Ally Issa Dimoso, wakiwa katika hospitali ya Teule, Muheza Tanga, baada ya kupata ajali ya Pikipiki, mapema mwezi huu wakiwa katika harakati za Daawa, katika Kijiji cha Mbomole, Amani, Mkoani humo. Katika ajali hiyo Shemtoi, amevunjika mguu wa kulia mara mbili na kupasuka mdomo kwa ndani na kushonwa nyuzi nne. Naye Ust. Dimoso (pichani chini) ameumia kwa kupata majeraha makubwa kichwani na kupoteza fahamu kwa muda wa siku mbili. Kwa sasa wanaendelea vizuri. (Picha Na. Bakari Mwakangwale)

16

AN-NUUR
MAKALA

RABIUL THAN 1435, IJUMAA FEBRUARI 21-27, 2014

16

RABIUL THAN 1435, IJUMAA FEBRUARI 21-27, 2014

Soma AN-NUUR kila Ijumaa

AN-NUUR

Maimamu Dar watakiwa kujihami na fitna ya ugaidi


Na Azza A. ahmed UGAIDI na vita dhidi ya ugaidi, ni mchezo wa maadui wa Uislamu waliopania kuupiga vita Uislamu. Hiyo ni kwa sababu, ugaidi ni jambo lisilokubalika katika mafunzo ya Uislamu na kwamba wanaofungamanisha jambo hilo na Uislamu ni kutaka kuipaka matope dini ya Kiislamu kwa chuki zao. Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Kituo cha Kiislamu cha Markaz Chang`ombe Dk. Osama Ismail, katika semina elekezi ya Maimamu iliyofanyika kituoni hapo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Akiwasilisha mada katika semina hiyo, Dk. Ismail alisisitiza kuwa ugaidi ni tatizo ambalo linadhuru mtu mmoja mmoja na jamii pia na kwamba, mafunzo ya Kiislamu yanakataa kabisa jinai hiyo hivyo kuitaka jamii kamwe kutohusisha ugaidi na Uislamu. Kwa upande wake Amiri wa Shura ya Maimamu nchin iSheikh Mussa Kundecha, amewataka Maimamu hao na waliohudhuria semina hiyo kutambua kuwa ugaidi ni chanzo cha fitna hapa duniani. Alisema, ugaidi husababisha madhara makubwa kwa jamii huku wenye kuasisi jinai hiyo wakitumia fursa hiyo kutimiza malengo yao na

PICHA ya pamoja ya Maimamu wa jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza semina elekezi iliyoandaliwa na Markaz Chang'ombe mwishoni mwa wiki. kuwasukumia mzigo wa jinai Uislamu kwa propaganda na fitna. Kwa upande wake Sheikh Suleiman Amran Kilemile, ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanazuoni Tanzania amewakumbusha Maimamu hao kutambua umuhimu wao wa kulingania katika kubainisha ufahamu sahihi wa Uislamu. Aliwahimiza washiriki wa semina hiyo kuwa kulingana na nafasi yao, wao ni watu ambao wanakutana na watu wengi mara nyingi zaidi kwa siku mara tano, kwa maana hiyo wana majukumu makubwa katika mabega yao ya kuwaeleke za watu na kuwafundisha Uislamu sahihi na kuwataka waachane na yale yasiofaa katika Uislamu. Alisema, kwa kuwa Maimamu wanaongoza jamii ya watu mchanganyiko, hivyo wana dhima ya kuikumbusha jamii ya l e ya l i y o s a h i h i , kwani wapo Waislamu wanaofanya makosa kwa kufahamu na wengine kwa kutokufahamu. Naye Sheikh Swalaha Sayed Hussein Maftah, Mwalimu wa Al-Azhari, Sharif aliwakumbusha Maimamu hao kukaa na vijana na kuwaelimisha juu ya umuhimu wao katika kusimamisha dini ya Allah (s.w) na kuhitajika kwao katika jamii. Akiwasilisha mada yake katika semina hiyo, aliwataka Maimamu kuwalingania zaidi vijana kuwa wao ndio nguzo ya umma na ndio tegemeo katika kujenga tabia njema, ili kuja kupatikana kizazi kilicho na maadili bora katika jamii inayowazunguka. Alisema, vijana ndio ambao wamekuwa wakitumika vibaya bila wao kujitambua katika kuharibu amani na utulivu, kukosa maadili mema na kufanya matukio yasio sahihi na kumuudhi Allah (s.w). Wa k a t i h u o h u o , Dk. Ahmad Mahmud Abdulatif, ambaye ni Naibu Mkurugenzi wa Markaz, yeye aliwasilisha mada isemayo Uislamu u na l i nga ni a j u u ya amani na siugaidi. Katika mada hiyo alisema Dini ya Mwenyezi Mungu daima imedumu katika kuwafundisha watu mafunzo sahihi ambayo yanasisitiza amani. Katika mada hiyo, aliwaeleza Maimamu hao kuwa kwa hakika Dini ya Kiislam inaukataa ubaguzi na ugaidi wa aina yoyote na kwa kiumbe yeyote bila ya kuangalia utaifa, rangi au Imani yake.

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na POA Printing Works LTD, S.L.P. 4605, Dar es Salaam.

Вам также может понравиться

  • Annuur 1264
    Annuur 1264
    Документ20 страниц
    Annuur 1264
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1231 PDF
    Annuur 1231 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1231 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1262
    Annuur 1262
    Документ20 страниц
    Annuur 1262
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1232 PDF
    Annuur 1232 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1232 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • HOTUBA YA BAJETI OFISI YA RAIS Final
    HOTUBA YA BAJETI OFISI YA RAIS Final
    Документ15 страниц
    HOTUBA YA BAJETI OFISI YA RAIS Final
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1230 PDF
    Annuur 1230 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1230 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Press Realse 28
    Press Realse 28
    Документ4 страницы
    Press Realse 28
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • HOTUBA YA BAJETI OFISI YA RAIS Final
    HOTUBA YA BAJETI OFISI YA RAIS Final
    Документ15 страниц
    HOTUBA YA BAJETI OFISI YA RAIS Final
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1227 PDF
    Annuur 1227 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1227 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1228d
    ANNUUR 1228d
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1228d
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1228d
    ANNUUR 1228d
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1228d
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1229 PDF
    Annuur 1229 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1229 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1225
    Annuur 1225
    Документ20 страниц
    Annuur 1225
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1226 PDF
    Annuur 1226 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1226 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1219
    Annuur 1219
    Документ20 страниц
    Annuur 1219
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1218 PDF
    Annuur 1218 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1218 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Press Release - Muungano Na Mazingira
    Press Release - Muungano Na Mazingira
    Документ4 страницы
    Press Release - Muungano Na Mazingira
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1224
    Annuur 1224
    Документ20 страниц
    Annuur 1224
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1223
    Annuur 1223
    Документ20 страниц
    Annuur 1223
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1220
    Annuur 1220
    Документ20 страниц
    Annuur 1220
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Karume Shujaa
    Karume Shujaa
    Документ11 страниц
    Karume Shujaa
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1217
    Annuur 1217
    Документ20 страниц
    Annuur 1217
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1216d
    ANNUUR 1216d
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1216d
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1214
    Annuur 1214
    Документ20 страниц
    Annuur 1214
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Hotuba Ya Maalim Seif - January 9 2016
    Hotuba Ya Maalim Seif - January 9 2016
    Документ27 страниц
    Hotuba Ya Maalim Seif - January 9 2016
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1215 PDF
    Annuur 1215 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1215 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    100% (1)
  • Annuur 1212
    Annuur 1212
    Документ20 страниц
    Annuur 1212
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1213 PDF
    Annuur 1213 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1213 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1210a
    Annuur 1210a
    Документ20 страниц
    Annuur 1210a
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1209aaa
    ANNUUR 1209aaa
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1209aaa
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет