Вы находитесь на странице: 1из 12

TANESCO

HAIVUNJWI
TANESCO
HAIVUNJWI
Bulletin
News
Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali
kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini
Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263
au Fika Ofsi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: badra77@yahoo.com
http://www.mem.go.tz
HABARI ZA
NISHATI &MADINI
Toleo No. 32 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Tarehe - Septemba 4 -11, 2014
nBali tunapeleka madaraka zaidi mikoani
nlengo ni kuboresha huduma na kuongeza ufanisi
Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati na
Madini Eliakim Maswi
Soma Uk. 2
2 Bulletin News
http://www.mem.go.tz
Na Mwandishi Wetu
W
akati Serikali iki-
wa katika jitihada
za kuimarisha
na kurekebisha
muundo wa Shiri-
ka la Umeme Tanzania (TANE-
SCO) lengo kuu likiwa ni kubore-
sha huduma na kuongeza ufanisi
katika sekta ndogo ya umeme baa-
dhi ya Wafanyakazi wa Shirika hilo
wamekuwa na wasi wasi au kutok-
uelewa mustakabali wao.
Hali hiyo imekuja hivi karibuni
baada ya Katibu Mkuu wa Wiz-
ara ya Nishati na Madini Ndugu
Eliakim Maswi alipofanya ziara
katika baadhi ya mikoa na kuzun-
gumza na Wafanyakazi wa Mikoa,
Wilaya na Mitambo ya kuzalisha
umeme.
Katibu Mkuu Maswi aliwa-
hakikishia na anawahakikishia
Wafanyakazi wa TANESCO
kwamba mpango wa kurekebisha
sekta ndogo ya umeme ni mzuri na
utaleta tija na hivyo Wafanyakazi
wasiwe na wasiwasi wowote kwani
lengo ni kupounguza madaraka
TANESCO Makao Makuu na
kuongeza Madaraka mikoani ili
waweze kutengeneza bajeti zao,
kufanya manunuzi ya vitu mbalim-
bali, kufanya maamuzi mbalimbali.
Hivi sasa mambo mengi yanay-
ohusu kazi mbalimbali za Mikoa ya
Kitanesco yanafanywa TANESCO
Makao Makuu na kusababisha ku-
pungua ufanisi jambo ambalo Shiri-
ka limekuwa likitupiwa lawama
nyingi na wateja wake kwa upande
mmoja na upande mwingine Wa-
fanyakazi nao wamekuwa wakiona
maamuzi yanachelewa kufanyika
kutokana na kusubiri kila kitu ki-
fanywe na Makao Makuu.
Hivi sasa Serikali kupitia Wiz-
ara ya Nishati na Madini imeanza
kufanya maandalizi ya utekelezaji
wa mpango huo kwa kuunda timu
itakayojumuisha wadau wote wa
umeme ambao ni TANESCO,
EWURA, na Wizara ya Nishati na
Madini itakayosimamia utekelezaji
huo.
Vile vile timu hiyo itafanya
tathmini ya mali za TANESCO,
rasilimali watu, kudurusu sheria,
taratibu na kanuni za umeme.
Aidha, kitakachofanyika ni
kutenganisha kazi na mapato ya-
nayotokana na uzalishaji umeme,
usafirishaji na usambazaji tofauti
na ilivyo sasa ambapo mapato na
matumizi ya uzalishaji umeme, us-
afirishaji na usambazaji huchang-
anywa na kushindwa kujulikana
nani amezalisha nini na ametumia
kiasi gani kinachotokana na shu-
ghuli hizo kuu tatu.
TAHARIRI
MEM
Na Badra Masoud
FIVE
PILLARS OF
REFORMS
KWA HABARI PIGA SIMU
KITENGO CHA MAWASILIANO
BODI YA UHARIRI
MHARIRI MKUU: Badra Masoud
MSANIFU: Essy Ogunde
WAANDISHI: Veronica Simba, Asteria Muhozya, Greyson Mwase
Teresia Mhagama, Nuru Mwasampeta
INCREASE EFFICIENCY
QUALITY DELIVERY
OF GOODS/SERVICE
SATISFACTION OF
THE CLIENT
SATISFACTION OF
BUSINESS PARTNERS
SATISFACTION OF
SHAREHOLDERS
TEL-2110490
FAX-2110389
MOB-0732999263
Mabadiliko TANESCO
hayaepukiki!!!!
W
iki iliyopita Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini
ambaye ndiye Mtendaji Mkuu wa Wizara alifanya ziara ya
kutembelea Mikoa kadhaa kukagua miradi, ofisi na kuzun-
gumza na Wafanyakazi wa Madini na wa Shirika la Umeme nchini
(TANESCO).
Katika ziara hiyo miongoni mwa mambo makubwa mbali ya
kujionea ofisi za taasisi hizo ni kuwasilikiliza Wafanyakazi ambao
miongoni mwao walio wengi walishikwa na mshangao mkubwa na
kusema kwamba hawajahi kumuona Ofisa wa juu wa Serikali kama
Katibu Mkuu kukutana nao na kuzungumza nao.
Baadhi yao wapo waliodiri kusema Maswi ni Katibu Mkuu wa
kwanza kuzungumza na Wafanyakazi mikoani na wengine wakitoa
ushuhuda kwamba wamekaa katika shirika kama TANESCO kwa
zaidi ya miaka 31 hawajawahi kumuona Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini akiwatembelea na kuzungumza nao.
Lakini Wafanyakazi hao walienda mbali zaidi ya kuomba kushi-
kana naye mikono na hata kupiga naye picha ili wapate kumbukum-
bu, lakini hilo si hoja yangu kubwa kwa wiki hii bali hoja yangu ni
kwamba miongoni mwa maswali mengi na yaliyojirudia aliyoulizwa
Katibu Mkuu ni hatma ya Shirika la TANESCO.
Shirika hili ni Shirika kubwa hapa nchini kwa sasa ambalo lina
Wafanyakazi takriban 6000 na mitandao yake ya umeme imesambaa
nchini nzima kuanzia mikoa yote, Wilaya zote na sasa mitandao hiyo
inazidi kuongezeka katika vijiji baada ya Serikali kuamua kuongeza
kasi ya kupeleka umeme vijijini ili ifikapo mwaka 2025 taifa la Tan-
zania liwe la kipato cha kati.
Ili kufikia kwenye kipato hicho lazima sekta ya umeme iboreshwe
kwa kuwa umeme ndiyo uti wa mgongo na moyo wa uchumi wa kila
taifa kwani bila umeme uchumi hauwezi kupanda.
Kwa sasa TANESCO bado linaonekana kuelemewa na madeni
ingawa Serikali inajitahidi kulisaidia kupunguza madeni hayo katika
kujiendesha ni dhahiri na ukweli uliowazi sekta ya umeme inahitaji
mabadiliko ili kuweza kutoa huduma bora na kuopngeza ufanisi ili
ikiwezakana kujiendesha kibishara kwa maslahi ya wenye mali am-
bao ni Watanzania wenyewe.
Lakini hayo hayawezi kufikiwa iwapo bado maamuzi mbalimbali
kama si yote yataendelea kufanywa kutokea juu na kushuka chini
(Makao Makuu na kwenda Mikoani) na pia ni muhimu kutengani-
sha shughuli kuu za shirika hilo kujitegemea yaani Uzalishaji umeme
peke yake, usafirishaji peke yake na usambazaji peke yake ili kila shu-
ghuli ijue inachopata na inachotumia.
Kwani kwa sasa maamuzi na manunuzi ya vitu mbalimbali yana-
fanywa Makao Makuu ya TANESCO na Mikoa wanachoweza ku-
nunua ni vifaa visivyozidi gharama ya Sh 7,500,000/= tu na kwa
shirika kama TANESCO manunuzi ya vifaa vyake vingi ni zaidi ya
fedha hizo mathalan mikoa hairuhusiwi kununua mafuta ya kuende-
sha mitambo kama kule Kigoma, Ruvuma, Rukwa, Katavi nk. la-
zima mafuta yanunuliwe Makao Makuu ya TANESCO hivyo iwapo
yatakwisha mapema TANESCO Mkoa hana mamlaka ya kununua.
Kwa kutengenisha shughuli hizi kutasaidi kuongeza ufanisi,
ushindani na kuboresha huduma kwani kila shughuli kati ya hizo tatu
itakuwa inatambua fika faida inazopata mathalani Idara ya uzalishaji
umeme itakuwa inajua inapata kiasi gani na kiasi gani watumie kwa
ajili ya kujiendesha, kwenye usafirishaji nao wataelewa ni kiasi gani
inapata kwa kusafirisha umeme kutoka kwa wanaozalisha na kupele-
ka kwa Idara ya usambazaji, usambazaji nao wataelewa ni kiasi gani
cha faida wanapata baada ya kuwauzia umeme wateja wake.
Kwa mgawanyo huo wa utendaji wa shughuli kuu tatu za TANE-
SCO ni dhahiri kila Idara itaongeza juhudi, bidii na ufanisi ili kupata
faida maradufu ambapo kwa namna moja ama nyingine itaboresha
huduma hivyo napenda kusema kwamba mabadiko TANESCO hay-
aepukiki!!!!!!
TEL-2110490
FAX-2110389
MOB-0732999263
TANESCO HAIVUNJWI
Bibiana Ndumbaro
(STAMICO) na Maliki
Munisi (TPDC)
S
hirika la Madini la Taifa
(STAMICO) linatarajia
kuanza kuchoronga mi-
amba Gombero Tanga, ikiwa ni
hatua ya awali ya utekelezaji wa
zabuni ya utafutaji wa mafuta
na gesi katika eneo hilo, iliyo-
tolewa na Shirika la Maendeleo
ya Mafuta (TPDC).
Akizungumzia zabuni ya
mradi huo wakati wa utiaji saini
mkataba mwishoni mwa wiki
iliyopita jijini Dar es Salaam,
Kaimu Murugenzi Mtendaji
wa STAMICO Mhandisi Ed-
win Ngonyani alieleza kuwa,
kazi hiyo itafanyika kitaalamu
na kwa wakati ili iwe na manu-
faa kwa mashirika yote na Taifa
kwa ujumla.
Nina wataalamu wa kuto-
sha na wenye uzoefu wa kusi-
mamia, kuratibu na kufanya
kazi za uchorongaji. Hadi sasa
hatua za kupeleka mitambo
ya kuchoronga miamba(rigs)
zimekamilika na timu ya
wataalamu itawasili katika eneo
la mradi mapema wiki ijayo ili
kuanza kazi mara moja al-
iongeza Mhandisi Ngonyani.
Naye Kaimu Mkurugenzi
wa Utafiti na Uchorongaji wa
STAMICO Mjiolojia Alex Ru-
MAONI
nNi katika Mradi wa kutafuta Mafuta, Gesi Gombero Tanga
STAMICO YAANZA UCHORONGAJI
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji
wa STAMICO Mhandisi
Edwin Ngonyani (kulia) na
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji
wa TPDC James Andilile
(Kushoto) wakibadilishana
mkataba wa uchorongaji
miamba wa mradi wa
Gombero Mkoani Tanga.

INAENDELEA UK.3
3
Bulletin News
http://www.mem.go.tz
tagwelela alieleza kuwa, Shirika
limejipanga vizuri kufanya Dia-
mond Drilling kwa kutumia
mashine za kuchoronga (rigs) za
Shirika.
Aliongeza kuwa, Uchorongaji
huo utafanyika katika mashimo
kumi yenye urefu wa mita mia
moja na hamsini kwenda chini
na inakadiriwa mita arobaini zi-
tachimbwa kwa siku ili kuweza
kumaliza kazi hiyo mapema
iwezekanavyo.
Kwa upande wake, Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC
James Andilile alieleza kuwa,
amefurahishwa sana kuona STA-
MICO imeshinda zabuni kwa
kuwa, ubia kati ya STAMICO na
TPDC utakuwa na nguvu ambayo
itakuwa na mafanikio makubwa
yenye manufaa kwa watanzania.
Aliongeza kuwa, makubaliano
kati ya STAMICO na TPDC yana
lengo la kuwanufaisha na kuwaen-
deleza watanzania, kwa sababu
mradi huo unamilikiwa na watan-
zania.
Aidha, Andilile alisisitiza
kuwa hatua hiyo ni nzuri kuona
hivi sasa Tanzania inawatumia
wataalamu wa ndani katika kufan-
ya miradi mbalimbali na kuongeza
kwamba, Shirika lake litawatumia
wataalamu watanzania katika mi-
radi mbalimbali kila inapoweze-
kana.
STAMICO imekuwa ikifanya
kazi ya uchorongaji kwa miaka
mingi na imeshinda zabuni hiyo
kutokana na kuwa na wataalamu
wa kutosha na wenye uzoefu
mkubwa. Shirika limefungua
milango kwa wadau wengine ka-
tika sekta ya madini na nishati ku-
litumia katika kazi za uchorongaji.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji
wa STAMICO Mhandisi Edwin
Ngonyani (kulia) na Kaimu Mku-
rugenzi Mtendaji wa TPDC James
Andilile (Kushoto) wakibadilis-
hana mkataba wa uchorongaji
miamba wa mradi wa Gombero
Mkoani Tanga.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi (wa tatu kushoto) akiwaeleza jambo baadhi wa watendaji watumishi wa
Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) alipowatembelea ofisini hapo.
Maswi aelezea ziara
yake Mikoani
Na Asteria Muhozya,
Dodoma
K
atibu Mkuu wa Wizara
ya Nishati na Madini Eli-
akim Maswi, ameielezea
ziara yake katika Mikoa
ya Lindi, Mtwara, Iringa, Njombe,
Ruvuma, Mbeya , Dodoma na kui-
taja kuwa ni mwanzo wa kuangalia
changamoto na fursa zilizopo katika
sekta za nishati na madini.
Maswi aliyasema hayo wakati
akitoa taarifa ya majumuisho ku-
fuatia ziara yake ya kukagua na
kutembelea miradi na shughuli zina-
zotekelezwa na Wizara ya Nishati na
Madini katika mikoa hiyo na kuwa-
taka viongozi waliopo katika sekta
hizo katika ngazi za mikoa, wilaya
na Makao makuu ya Wizara ku-
wasikiliza watumishi waliopo chini
yao kutokana na kwamba, jambo
hilo lina uhusiano wa moja kwa
moja na utendaji mzuri wenye tija.
Viongozi sikilizeni matatizo ya
watumishi wenu. Taasisi zote siki-
lizeni watumishi, msipowasikiliza,
hakuna tija katika mipango na mi-
kakati yetu tunayopanga. Tanesco
watembeleeni watumishi wenu kujua
matatizo yao, alisisitiza Maswi.
Aidha, aliongeza kuwa, zipo fur-
sa nyingi katika sekta za nishati na
madini na hivyo kuwataka watendaji
kuhakikisha kwamba, kila mmoja
anatekeleza wajibu wake kikamilifu
kwa uwazi, uadilifu ili kuweza ku-
fikia azma ya Serikali ya kuhakiki-
sha kwamba wananchi na taifa wa-
nafaidika na rasilimali asilia zilizopo
nchini ikiwemo kuzalisha ajira kupi-
tia sekta za nishati na madini.
Vilevile, Katibu Mkuu aliahidi
kuzifanyia kazi changamoto zilizopo
katika utekelezaji wa miradi mbalim-
bali ambayo bado hazijatekelezwa
kikamilifu ikiwemo utekelezaji wa
mradi wa uchimbaji Chuma Liganga
na uzalishaji umeme wa Makaa ya
Mawe Mchuchuma.
Tunataka kuufanya mradi wa
Liganga- Mchuchuma kuwa historia.
Nawaomba Shirika la Maendeleo ya
Taifa (NDC) na Shirika la Umeme
Tanzania (Tanesco) kutaneni mzun-
gumze ili mradi wa makaa ya mawe
Mchuchuma uanze haraka, tusisubi-
ri, aliongeza Maswi.
Halikadhalika, Maswi alitumia
nafasi hiyo kuwapongeza watumi-
shi wa TANESCO walioko mikoani
kwa kazi nzuri wanazofanya za
utekelezaji wa majukumu yao ka-
tika mazingira magumu, na pia
aliwapongeza watumishi wote wa-
naofanya kazi katika mabwawa ya
kuzalisha umeme nchini yakiwemo
ya Kihansi, na Mtera aliyoyatembe-
lea na kueleza kuwa, wanafanya kazi
kubwa katika kuhakikisha kwamba
nishati ya umeme inapatikana nchini
na kuchangia katika Gridi ya Taifa.
Tunduru Tanesco wanafanya
kazi vizuri sana, pamoja na kuwa
wanafanya kazi katika mazingira
magumu, alisistiza Maswi.
n Awataka viongozi kusikiliza matatizo ya watumishi
n Tanesco Tunduru wapongezwa
STAMICO YAANZA UCHORONGAJI
Kamishna Masanja
awapongeza
Muhongo, Maswi
Na Asteria Muho-
zya, Dodoma
K
amishna wa Ma-
dini Tanzania
Mhandisi Paul
Masanja, amewapongeza
Waziri wa Nishati na
Madini Profesa Sospeter
Muhongo na Katibu
Mkuu Eliakim Maswi
kwa uongozi na utendaji
wao katika kusimamia
sekta ya madini na kue-
leza kuwa, wameiwez-
esha sekta hiyo kupaa.
Kutokana na uwepo
wa viongozi hawa, wamei-
fanya kazi yangu kuwa
nyepesi. Nawapongeza
sana kwasababu wamei-
wezesha sekta ya madini
kupaa, alisisitiza Kam-
ishna Masanja.
Masanja aliyasema
hayo mjini Dodoma
wakati akitoa taarifa ya
majumuisho kufuatia zi-
ara ya Katibu Mkuu Wiz-
ara ya Nishati na Madini
Eliakim Maswi, aliyoifan-
ya hivi karibuni katika
mikoa mbalimbali nchini
kuangalia maendeleo ya
utekelezaji wa shughuli
na miradi inayosimamiwa
na Wizara katika mikoa
hiyo.
Aidha, aliongeza
kuwa, kasi ya uvunaji
madini bado ni ndogo na
hivyo, kuwataka wachim-
baji waliopewa leseni
kuyaendelea maeneo yao
na kwakueleza kuwa,
kwa wale wasioyaen-
deleza ndani ya kipindi
walichoomba watafutiwa
leseni hizo.
serikali inataka kuona
mataokeo ambayo yana
tija kwa taifa na wananchi
kupitia rasilimali hizi .
Maafisa Madini tuleteeni
taarifa za wasioendeleza
maeneo yao, tutazifuta,
aliongeza Masanja.
Vilevile, aliwataka
Makamishna Wasaidizi
wa Madini na Maafisa
Madini kusimamia uku-
sanyaji wa maduhuli ya-
nayotokana na rasilimali
hizo na kuongeza kuwa,
kwa watakaoshindwa
kufikia malengo wali-
yowekewa na Wizara,
wataondolewa katika na-
fasi zao.
Akizungumzia kuhu-
su uimarishaji biashara
ya madini nchini, alieleza
kuwa, Serikali itaimarisha
usimamizi wa biashara
hizo ikiwa ni pamoja na
uanzishaji vituo maalum
vya biashara za madini na
kuyataja baadhi ya mae-
neo yatakayojengwa vit-
uo hivyo kuwa ni pamoja
na Arusha na Dar es Sa-
laam.
Masanja aliongeza
kuwa, ili kuendana na
ukuaji katika sekta hiyo,
tayari Wizara imeanza
kuboresha ofisi mbalim-
bali za madini nchini ili
kuendana na kasi kwa
kuwa, maboresho hayo
yatasaidia kuimarisha
utendaji wa ofisi hizo ka-
tika ukusanyaji maduhuli.
Vilevile, katika ki-
kao hicho Kamishna
Masanja alitumia fursa
hiyo kuipongeza Ofisi ya
madini Mbeya kutokana
na kasi ya makusanyo wa
maduhuli na kutokana
na ushirikiano uliopo
baina ya ofisi ya Kanda
na Wakala wa Ukaguzi
wa Madini Tanzania
(TMAA) mkoani humo.
Aidha, alitumia fursa
hiyo kuipongeza Ofisi
ya Madini Nachingwea
kutokana na kazi nzuri
iliyofanyika ya ukusan-
yaji maduhuli pamoja na
uchanga wa ofisi hiyo ya
madini.
Katika ziara hiyo, Ka-
tibu Mkuu aliyeambatana
na Kamishana wa Nishati
na Madini alitembelea
mikoa ya Lindi, Mtwara,
Ruvuma, Njombe, Iringa,
Mbeya na Dodoma
n Ni kwa kusimamia sekta ya Madini
n Awasifu madini Nachingwea, Mbeya
4 Bulletin News
http://www.mem.go.tz
Na Veronica Simba -
Mwanza
W
achimbaji wadogo wa
madini nchini wametak-
iwa kuachana na utam-
aduni uliozoeleka kwa wengi wao
wa kutumia kemikali ya Zebaki
kwa kukamatia dhahabu kwani
matumizi yake yana madhara
makubwa kwa afya ya mtumiaji
na mazingira kwa ujumla.
Wito huo ulitolewa hivi ka-
ribuni jijini Mwanza na Afisa
Mazingira kutoka Wizara ya Ni-
shati na Madini, Emmanuel Shija
wakati akiwasilisha mada kuhusu
wachimbaji wadogo wa madini
na uhifadhi wa mazingira katika
semina ya mafunzo kwa Maafisa
Mazingira wa Kanda ya Ziwa
Victoria iliyofanyika Septemba 1
4, mwaka huu.
Shija alisema wachimbaji
wadogo wamekuwa wakitumia
kemikali ya zebaki kwa muda
mrefu bila kujua madhara yake
kwani kwa kawaida hayaonekani
kwa muda mfupi bali huanza ku-
jitokeza kuanzia miaka mitano na
kuendelea.
Aliwataka wachimbaji hao
kutumia vifaa vya usalama (pro-
tective gears) pamoja na kutumia
Kigida wakati wa kuchoma dha-
habu ili kujiepusha na madhara
ya Zebaki.
Aidha, aliongeza kuwa
wachimbaji wadogo wanapaswa
kutumia mialo iliyojengewa kwa
saruji ili kuepuka kemikali ya Ze-
baki kuharibu vyanzo vya maji na
pia aliwasisitiza kuepuka kutumia
Zebaki nyingi kupita kiasi kina-
chotakiwa.
Akizungumzia dalili za ma-
tatizo sugu ya athari za sumu ya
Zebaki, Shija alitaja baadhi yake
kuwa ni pamoja na kuongezeka
kwa hasira na kupoteza kum-
bukumbu, kutojiamini, kukosa
hamu ya chakula, kuathirika
kwa figo na kuumiza mfumo wa
uzazi.
Katika hatua nyingine, Nas-
sor Abdullatif, ambaye pia ni
Afisa Mazingira kutoka Wizara
husika alisisitiza umuhimu wa
kufanya tathmini ya athari za
kimazingira (Environmental Im-
pact Assessment EIA) kwa wa-
dau wa sekta za nishati na madini
kabla ya utekelezaji wa mradi
wowote, ili kuepusha madhara
mbalimbali yanayoweza kusaba-
bishwa na mradi husika kwa afya
za binadamu na mazingira kwa
ujumla.
Aliwashauri Maafisa Maz-
ingira walioshiriki semina hiyo
kutoa ushirikiano kwa Wizara ya
Nishati na Madini kuhakikisha
hakuna mradi unaotekelezwa pa-
sipo kufanya EIA.
Kufanya tathmini ya athari
za kimazingira kusichukuliwe
na wadau husika kama kikwazo
cha maendeleo bali ichukuliwe
kama nyenzo muhimu ya kuleta
maendeleo endelevu kutokana
na utekelezaji wa miradi mbal-
imbali, alisisitiza Abdullatif na
kuwashauri washiriki wa semina
kusaidia kuelimisha jamii husika
juu ya umuhimu huo.
Semina ya mafunzo kwa
Maafisa Mazingira kutoka Kan-
da ya Ziwa Victoria iliandaliwa
na Wizara ya Nishati na Madini
kupitia Kitengo chake cha Maz-
ingira ikiwa ni mwendelezo wa
utoaji mafunzo kwa Maafisa
Mazingira kutoka sehemu mbal-
imbali nchini waweze kuongeza
uelewa wa masuala ya uhifadhi
wa mazingira na hivyo washiriki-
ane na Serikali katika utekelezaji
wake hususan kwa miradi ya ni-
shati na madini.
WACHIMBAJI MADINI
WAASWA KUTOTUMIA ZEBAKI
Wizara ya Nishati na Madini Yafadhili Wanafunzi
Kusoma Shahada ya Mafuta na Gesi China
Na Asteria Muhozya,
Dar es Salaam
K
utokana na kutambua
umuhimu wa kuwaendeleza
wataalamu wazawa kufua-
tia nchi ya Tanzania kuingia katika
uchumi wa mafuta na gesi, Wizara
ya Nishati na Madini imewapa
ufadhili wa masomo wanafunzi
wanne (4) wa Kitanzania kwenda
nchini China kusoma masuala
ya mafuta na gesi katika ngazi ya
Shahada ya Uzamili Oil and Gas
Development Engineering katika
Chuo Kikuu cha China University
of Petroleum, Beijing.
Akizungumza wakati aki-
waaga wanafunzi hao, Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na
Madini Eliakim Maswi amewa-
taka kuwa mfano bora kwa kuso-
ma kwa bidii na kufaulu vizuri ili
baadaye waweze kulisaidia taifa
kutokana na utaalamu wataka-
oupata. Tunatarajia mtafanya
vizuri katika masomo yenu.
Msituangushe,tunawategemea,
amesisitiza Maswi.
Naye, Kaimu Mkurugenzi wa
Shirika la Maendeleo ya Petroli
Tanzania (TPDC), James Andilile
amewataka wanafunzi hao kuitu-
mia nafasi waliyopata kwa kuwa
mabalozi wazuri wa Tanzania na
kuongeza kuwa, fursa za ajira ka-
tika uchumi wa gesi na mafuta ni
nyingi nchini na hivyo, kuwataka
kuiwakilisha Tanzania vizuri kiel-
imu na kimaadili.
Mnakwenda kama mabalozi,
hamkutumwa na wazazi bali mme-
tumwa na nchi. Mkaweke taswira
nzuri ya Tanzania, ameongeza
Andilile.
Wanafunzi waliopata ufadhili
huo ni Swalehe Laus Makanjila,
Hijira Yassini, Amani Athmani
Masoud na Sadiki Hamis Zavallah
kufuatia maombi yao waliyowasili-
sha Wizarani mwezi Machi.
Aidha, ufadhili wa wanafunzi
hao ni mwendelezo wa juhudi za
Wizara ya Nishati na Madini ku-
hakikisha kuwa inaongeza idadi
ya wataalamu katika masomo ya
mafuta na gesi, baada ya wanafun-
zi wengine 10 kupata ufadhili wa
masomo katika ngazi ya Shahada
ya uzamili na uzamivu kupitia Seri-
kali ya China.
5
Bulletin News
http://www.mem.go.tz
Na Greyson Mwase,
Manyara
Imeelezwa kuwa katika ku-
hakikisha kuwa wataalamu wa
kitanzania wananufaika katika
soko la ajira kupitia mgodi wa
uchimbaji wa madini ya vito
aina ya tanzanite wa Tanzan-
ite One, mgodi huo umeweka
mkakati wa kuhakikisha kuwa
unaajiri wataalamu wa kitan-
zania zaidi badala ya kuingia
gharama ya kuajiri wataalamu
kutoka nje ya nchi.
Kauli hiyo imetolewa na
Mkurugenzi wa mgodi huo
Bw. Farai Manyemba mbele ya
timu ya majaji wanaoendesha
zoezi la kumtafuta mshindi wa
Tuzo ya Rais ya Huduma za
Jamii na Uwezeshaji ilipofanya
ziara kwenye mgodi huo.
Bw. Manyemba alisema
kuwa mgodi huo unaomilikiwa
kwa asilimia hamsini kwa ham-
sini kati ya TanzaniteOne na
Serikali kupitia Shirika la Madi-
ni la Taifa (STAMICO) umean-
za kuajiri vijana wa kitanzania
na kusisitiza kuwa mgodi huo
utaendelea na mkakati wa ku-
hakikisha kuwa wataalamu we-
nye taaluma na uwezo mkubwa
wanaajiriwa katika mgodi huo
na kupunguzia Serikali ghrama
ya kuajiri wataalamu kutoka nje
ya nchi.
Ugunduzi wa madini
umepelekea sekta ya madini
nchini kukua kwa kasi kubwa
sana, wawekezaji wanaongeze-
ka kila kukicha, hivyo ni juku-
mu letu kama kampuni ya ma-
dini ya vito kuhakikisha kuwa
vijana wa kitanzania wenye
uwezo mkubwa kutoka vyuo
vyetu nchini wanaajiriwa ikiwa
ni pamoja na kuwajengea uw-
ezo, alisema Bw. Manyemba
Aliendelea kusema kuwa
katika kuhakikisha kuwa sekta
ya madini inachangia ipasavyo
kwenye pato la taifa nchi zi-
lizoendelea zimewekeza kwa
kuwasomesha wataalamu wake
katika masuala ya madini am-
bapo wataalamu hao wameku-
wa na mchango mkubwa.
Alisisitiza kuwa nchi zi-
lizoendelea zimewekeza katika
teknolojia ambayo imeziwez-
esha kupiga hatua katika sekta
hiyo na kuongeza kuwa mtaji
mkubwa wa fedha unahitajika
ili kukuza sekta ya madini.
Akizungumzia juu ya
mchango wa makampuni ya
madini katika kuongeza pato
la taifa Bw. Manyemba alisema
kuwa iwapo makampuni yote
ya madini nchini yatasimamia
vyema sheria na kanuni za ma-
dini pamoja na mapato yake,
sekta hiyo ina uwezo mkubwa
wa kuiwezesha nchi kupiga hat-
ua kubwa kimaendeleo.
Akielezea mchango wa
mgodi huo katika huduma za
jamii Bw. Manyemba alisema
kuwa kwa kipindi cha mwaka
2013 kampuni yake ilitoa ufa-
dhili kwa wanafunzi 11 kutoka
katika familia maskini kusoma
katika shule za sekondari za
Msitu wa Tembo, Terrari, Nais-
inyai na Benjamin William
Mkapa zilizopo katika mkoa
wa Manyara.
Bw. Manyemba aliainisha
michango mingine kuwa ni
pamoja na ujenzi wa kituo cha
polisi cha Naisinyai kilichopo
Manyara ambapo ujenzi wake
uligharimu dola za Marekani
37,500
Aliongeza kuwa mgodi pia
ulifadhili kikundi cha waki-
namama wa kimasai kijulikana-
cho kama Ebeneza kwa ajili ya
mradi wa kutengeneza urembo
na mapambo mbalimbali.
Pamoja na kufadhili ki-
kundi cha Ebeneza, tumekuwa
tukitangaza bidhaa zake ka-
tika masoko mbalimbali nchini
Marekani. Alisisitiza Bw.
Manyemba
Bw. Manyemba alitaja
michango mingine ni pamoja na
kuanzisha kampeni ya kupanda
mlima Kilimanjaro ili kuchang-
ia kituo cha watoto yatima cha
New Vision kilichopo Mirerani
ambapo kiasi za Dola za Mare-
kani 34,000 zilipatikana.
Aliongeza kuwa katika ku-
kabiliana na mafuriko ambayo
hutokea katika kipindi cha
masika kampuni ya Tanzan-
iteOne ilijenga ukingo katika
eneo la Naisinyai ambalo ndilo
eneo linaloathirika na mafuriko
wakati wa mvua.
Akizungumzia changamoto
katika kampuni hiyo Bw. Many-
emba alisema kuwa ni pamoja
na wachimbaji wadogo wasio
waaminifu kutorosha tanzanite
na kwenda kuuza nchi za jirani
kama Kenya.
Alitaja changamoto nyigine
kuwa ni pamoja na uvamizi
kwenye mgodi huo uliosababi-
sha hasara ya dola za Marekani
milioni tano kutokana na mali
za kampuni kuharibiwa, mauaji
ya wafanyakazi na kuongeza
kuwa kwa sasa mgodi umeima-
risha ulinzi katika kila eneo.
Akielezea mikakati ya ku-
kabiliana na changamoto hizo
Bw. Manyemba alisema kuwa
mgodi utaendelea kutoa elimu
kwa jamii inayouzunguka hu-
susan wachimbaji wadogo, ku-
jenga mahusiano mazuri kwa
jamii pamoja na kuimarisha ul-
inzi kila eneo la mgodi.
TanzaniteOne kutoa ajira zaidi kwa wazawa
Wanamazingira wahamasishwa
kuwalinda binadamu, viumbe hai
Na Veronica Simba
- Mwanza
M
aafisa Mazingira
nchini kote wame-
pewa changamoto
kuhakikisha kuwa
uwekezaji mkubwa unaoendelea
hivi sasa katika sekta za nishati
na madini, hauathiri binadamu
na viumbe hai wengine.
Changamoto hiyo ilitolewa
Septemba 1, 2014 jijini Mwanza
na Kamishna Msaidizi wa Nisha-
ti Mbadala kutoka Wizara ya Ni-
shati na Madini, Leonard Ishen-
goma wakati akifungua semina
ya mafunzo kwa Maafisa Maz-
ingira wa Wilaya kutoka Kanda
ya Ziwa Viktoria, juu ya mpango
kazi wa mazingira wa sekta za ni-
shati na madini.
Akifungua semina hiyo kwa
niaba ya Katibu Mkuu wa Wiz-
ara husika, Eliakim Maswi,
Kamishna Msaidizi alisema hivi
sasa, sekta za nishati na madini
zinapata uwekezaji mkubwa sana
na kutolea mfano sekta ya nishati
ambapo shughuli za utafutaji wa
mafuta na gesi zinaendelea na
hivyo kuwataka wanamazingira
hao kutimiza wajibu wao kwa ku-
hakikisha mazingira hayaathiriwi
na shughuli husika.
Aliongeza kuwa, upande
wa sekta ya umeme, uwekezaji
unategemewa kuongezeka kwa
kiwango kikubwa pia kwa siku
za hivi karibuni ikiwa ni mi-
kakati ya Wizara kuhakikisha
inakidhi mahitaji ya nishati hiyo
kwa wananchi na hivyo alisema
uwekezaji huo utaleta changa-
moto nyingi za kimazingira, kiu-
chumi na kijamii.
Akizungumzia sababu ny-
ingine zinazochangia kuharibu
mazingira, hususan zinazohusi-
ana na sekta za nishati na madi-
ni, Ishengoma alisema matumizi
ya nishati yanachangia kwa kiasi
kikubwa kuleta mabadiliko ya
tabianchi ambayo husababisha
madhara mbalimbali kama vile
majanga ya mafuriko, ukame na
maradhi ya milipuko.
Kwa upande wa sekta ya ma-
dini, Kamishna Msaidizi Ishen-
goma alisema kwa miaka ya hivi
karibuni, sekta hiyo imekua kwa
kasi kubwa sana, hususan uchim-
baji na uzalishaji wa madini, shu-
ghuli ambazo zinachangia katika
uharibifu wa mazingira.
Vilevile, alisema wengi wa
wachimbaji wadogo na wa kati
wa madini wana mwamko mdo-
go sana katika kuhifadhi mazin-
gira katika maeneo yao ya kazi na
aliongeza kwamba hata baadhi
ya wawekezaji wakubwa wanak-
wepa kutimiza taratibu za utun-
zaji wa mazingira kwa lengo la
kupata faida kubwa.
Ni kwa sababu hiyo, Wiz-
ara ya Nishati na Madini imean-
daa Mpango Kazi wa Mazingira
Kisekta ambao utekelezaji wake
utaenda hadi ngazi ya wilaya ili
kuhakikisha shughuli za maen-
deleo zinazofanyika, haziathiri
mazingira, alisisitiza Ishengo-
ma.
Aidha, aliwahamasisha
Maafisa Mazingira kuhakikisha
wanahuisha masuala ya maz-
ingira katika mipango na bajeti
zao za wilaya kwa kuwa wana
nafasi nzuri katika uhifadhi na
usimamizi wa mazingira kwani
huko ndiko kuliko chimbuko la
maendeleo.
Semina hiyo ya Mafunzo kwa
Maafisa Mazingira, ni mwen-
delezo wa semina zinazotolewa
na Wizara ya Nishati na Madini
kupitia Kitengo chake cha Maz-
ingira ili kuongeza uelewa na
hivyo kutekeleza kwa dhati azma
ya utunzaji mazingira.
Maafisa Mazingira wana-
oshiriki katika semina hiyo ya
mafunzo ya siku tatu ni kutoka
Wilaya 18 za mikoa ya Mwanza,
Shinyanga, Geita, Mara, Kigoma
na Tabora.
6 Bulletin News
http://www.mem.go.tz
Mgodi wa North Mara wachangia
bilioni 7.5 shughuli za jamii
Na Greyson Mwase,
Tarime
I
meelezwa kuwa mgodi wa
North Mara uliopo wilay-
ani Tarime mkoani Mara
umechangia jumla ya shilingi
bilioni 7.5 katika kipindi cha
mwaka 2013 kwa ajili ya miradi
mbalimbali ya maendeleo ka-
tika vijiji saba vinavyouzunguka
mgodi huo.
Akizungumza mbele ya timu
ya majaji kwa ajili ya kumtafuta
mshindi wa Tuzo ya Rais ya
Huduma za Jamii na Uwezeshaji
chini ya mwenyekiti wake Profe-
saSamwel Wangwe Meneja Ma-
husiano wa Mgodi huyo Fatuma
Mssumi alitaja vijiji hivyo kuwa
ni pamoja na Nyangoto, Nyam-
waga, Nyakunguru, Kerende,
Kewanja, Genkuru na Matongo.
Mssumi alisema kuwa kupitia
sekta ya elimu, mgodi ulichangia
madawati 2700 yenye thamani
ya shilingi milioni 251.9 kwa aji-
li ya shule mbalimbali za msingi
na sekondari na kuongeza kuwa
mgodi ulijenga shule ya sekond-
ari ya Ingwe kwa shilingi bilioni
1.1 miradi ambayo imekamilika.
Alieleza kuwa mgodi ulifan-
ya ukarabati pamoja na ujenzi
wa shule ya sekondari ya Ke-
mambo kwa gharama ya shilingi
milioni 905.5, na shule ya msingi
ya Bongenge kwa gharama ya
shiligi milioni 827.
Aliongeza kuwa mgodi huo
katika awamu yake ya kwanza
ulichangia shilingi milioni 605.
8 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya
sekondari ya Nyamwaga mradi
ambao bado unaendelea.
Mgodi uligharamia shilingi
milioni 12.7 kwa ajili ya wa-
nafunzi waliofanya vizuri ku-
soma katika shule na vyuo mbal-
imbali, aliongeza Mssumi.
Aliongeza kuwa nia ya ku-
wekeza katika elimu katika
wilaya ya Tarime ni kuhakiki-
sha wanajenga msingi utaka-
opelekea kupatikana wataalamu
kwa ajili ya kufanya kazi katika
mgodi huo.
Akielezea mchango wa mgo-
di huo katika sekta ya afya Bi
Mssumi alitaja miradi mingine
kuwa ni pamoja na ukarabati na
ujenzi wa zahanati ya Genkuru
uliogharimu shilingi milioni
61.2, upimaji wa macho kwa
wanakijiji 3,000 kwa shilingi mil-
ioni 19 pamoja na upimaji wa
virusi vya Ukimwi kwa wanaki-
jiji 1067 uliogharimu shilingi
milioni tano.
Aliendelea kusema kuwa
mgodi huo ulitoa msaada kwa
ajili ya upasuaji kwa wanaki-
jiji 11 ambapo jumla ya shilingi
milioni 12.2 zilitumika
Akielezea sekta ya Mssumi
alisema kuwa mgodi ulichim-
ba visima katika vijiji sita kwa
thamani ya shilingi milioni 888.3
pamoja na usambazaji wa maji
katika vijiji vya Nyangoto, Ke-
wanja, Matongo na Kerende uli-
ogharimu shilingi bilioni 1.2
Halikadhalika, aliongeza
kuwa mgodi pia ulifanya ukara-
bati katika kituo cha afya cha
Nyangoto kwa gharama ya
shilingi milioni 481.7 pamoja na
usafi katika vijiji vya Nyangoto,
Kerende, Kewanja na Nyamwa-
ga uliogharimu shilingi milioni
544.4
Aidha, alisisitiza kuwa ili
kuhakikisha kuwa wachimbaji
wadogo wananufaika na sekta
ya madini kupitia kujiajiri mgodi
huo ulichangia shilingi milioni
91.4 kwa kikundi cha wachim-
baji wadogo Tarime kwa ajili ya
ununuzi wa mashine kwa ajili ya
kusaga kokoto.
Mssumi aliongeza kuwa hat-
ua iliyofikiwa sasa ni mkandara-
si kufanya kazi ya kutoa umeme
kutoka mgodi wa North Mara
hadi mashine ilipo ili ianze kazi
mara moja.
Aliongeza kuwa mgodi pia
ulifadhili miradi mbalimbali
kwa gharama ya shilingi milio-
ni 252.5 pamoja na vikundi vya
kijamii/kidini kwa gharama ya
shilingi bilioni 1.8
Akizungumzia mchango wa
mgodi huo katika sekta ya mi-
undombinu Bi Mssumi alisema
kuwa mgodi huo ulikarabati
barabara yenye urefu wa kilomi-
ta 47.9 kwa gharama ya shilingi
milioni 469 pamoja na uun-
ganishaji wa umeme kwa kush-
irikiana na Shirika la Umeme
Nchini (Tanesco) katika vijiji
vya Kerende na Matongo kwa
gharama ya shilingi milioni 472
Alitaja miradi mingine kuwa
ni pamoja na ujenzi wa kituo
cha polisi uliogharimu shilingi
milioni 555.5 na ujenzi wa ma-
hakama ya mwanzo Nyamongo
ikiwa ni pamoja na ujenzi wa
nyumba za wafanyakazi wa
mahakama hiyo kwa shilingi
milioni 182.9 mradi ambao hau-
jakamilika bado.
Akizungumzia changamoto
katika utekelezaji wa miradi
hiyo, Mssumi alisema kuwa
kumekuwepo na tatizo la wa-
navijiji kuhujumu miundom-
binu ya maji iliyowekwa hali in-
ayopelekea mgodi huo kuingia
gharama kwa ajili ya ukarabati
wa miundombinu hiyo.
Wapo wanakijiji wasio
waaminifu ambao huharibu mi-
undombinu ya maji kwa maku-
sudi ili kufanya biashara ya maji
jambo ambalo linarudisha nyu-
ma maendeleo ya vijiji hivyo
alisisitiza Mssumi.
Mwenyekiti wa Jopo la Majaji kwa ajili ya kumtafuta mshindi wa Tuzo ya
Rais ya Huduma za Jamii na Uwezeshaji Profesa. Samwel Wangwe (kushoto)
akisalimiana na Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Ingwe Bw. Alfred
Joseph mara timu hiyo ilipofanya ziara kwenye shule hiyo iliyofadhiliwa na
mgodi wa North Mara.
Afisa Uhusiano wa Kijiji cha Matongo Bw. Magesa Wanjara akionesha jinsi ya kutumia bomba la kisima cha maji kilichofadhiliwa na mgodi wa North
Mara mbele ya timu ya majaji, sekretarieti na wajumbe wengine.
Meneja Mahusiano wa Mgodi wa North Mara (mbele) akielezea shughuli za
mgodi wa North Mara mbele ya jopo la majaji waliotembelea mgodi huo ili
kuendelea na zoezi lake la kumtafuta mshindi wa Tuzo ya Rais ya Huduma
za Jamii na Uwezeshaji.
7
Bulletin News
http://www.mem.go.tz

Na Asteria Muhozya,
Dar es Salaam
W
aziri wa Nishati na Madini
Profesa Sospeter Muhongo
amewataka wamiliki na
waombaji wa leseni za kuchimba ma-
dini kuhakikisha wanayaendeleza mae-
neo yao kwa kufanya kazi katika muda
walioomba kulingana na leseni hizo la
sivyo watafutiwa leseni zao kwa mu-
jibu wa sheria ya madini.
Waziri Muhongo ameyasema hayo
wakati akisaini leseni za Kampuni
mbalimbali zilizokidhi vigezo vya ku-
patiwa leseni za uchimbaji madini
katika maeneo mbalimbali nchini na
kuongeza kuwa, kuanzia sasa Wizara
haitaruhusu wamiliki wa leseni za ma-
dini kuuza maeneo yao kwa wamiliki
wengine na kubadilisha majina ya kam-
puni kutoka kwa mmiliki mmoja kwen-
da mwingine badala yake itaruhusu en-
dapo pande mbili zitaingia ubia.
Hatutakubali wamiliki wa leseni
kuuza maeneo yao na kubadili jina
kutoka kwa mmliki mmoja kwenda
mwingine badala ya kuyaendeleza, lak-
ini kama wanaingia ubia hilo linakuba-
lika alisisitiza Muhongo.
Kauli ya Waziri imekuja baada ya
kubaini kuwa, baadhi ya wamiliki wa
leseni za uchimbaji madini kutokuy-
aendeleza maeneo yao kwa muda mre-
fu pindi wanapopewa leseni na badala
yake kuyauza na kubadili majina ya
kampuni jambo ambalo linachochea
migogoro katika maeneo husika.
Wananchi wanategemea mara
baada ya kampuni kupewa leseni
waombaji waendeleze maeneo yao la-
kini badala yake maeneo yanakaa bila
kuendelezwa jambo ambalo linaibua
migogoro, aliongeza Muhongo.
Aidha, ameongeza kuwa, hatua
hiyo inalenga kuwafanya waombaji na
wamiliki kuwajibika na kufanya kazi
kisasa badala ya kufanya kwa mazoea.
Hatutaki waombaji wafanye kazi ki-
zamani, hatutaki kupotezeana muda
katika hili, alisisitiza Waziri.
Kampuni zilizopata leseni za
uchimbaji, ni pamoja na Bafex Tanza-
nia Limited (Kanda ya Kusini Maghar-
ibi) Autrad Mining Company Limited,
Nyangwale Diamonds Limited (Kan-
da ya Kati Magharibi) na Paulo Sun-
gura na Joyce Abinel Sekwao (Kanda
ya Magharibi).
Na Bibiana Ndumbaro
(STAMICO)
S
hirika la Madini la Taifa (STAMICO) limetoa
mafunzo elekezi kwa wataalam wake mjini Dodo-
ma ili waweze kufanya kazi kulingana na taratibu
na kanuni za utumishi wa umma.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO
Mhandisi Edwin Ngonyani amesema mafunzo hayo
ni muhimu kwa wafanyakazi hao ili waweze kuendana
na ari na kasi ya STAMICO mpya, yenye lengo la ku-
peleka fedha serikalini (HAZINA).
Kwa mujibu wa Mhandisi Ngonyani, alieleza kuwa,
upelekaji fedha Serikalini (HAZINA) uko kwa njia tatu
kupitia kulipa kodi, kutoa gawio serikalini na kulipa
fedha katika taasisi zingine za serikali kupitia leseni na
ada mbalimbali.
Aidha, Mhandisi Ngonyani aliwata wataalamu
kuwa, mafunzo hayo yawe chachu ya utendaji kazi wa
kujituma na kufuata kanuni za utumishi wa umma kwa
manufaa ya Shirika na Taifa kwa ujumla.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali
Watu (STAMICO) Deusdedith Magala Alieleza kuwa,
mafunzo haya yametoa mwongozo wa utendaji kazi
kwa wafanyakazi wa Shirika hilo na kuelezwa kuwa,
mafunzo hayo hutolewa kwa kufuata sheria na kanuni.
Aliongeza kuwa, mafunzo hayo yana mchango
mkubwa kwa wataalamu wa STAMICO katika kuleta
mabadiliko ya kiutendaji na yamewawezesha kufahamu
mambo mbalimbali yanayohusu Shirika hasa STAM-
ICO mpya kanuni na maadili ya utumishi wa umma,
hali ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI eneo la
kazi, utunzaji wa kumbukumbu, usiri wa nyaraka za
Serikali na kufanyiwa upekuzi.
Akizungumzia kuhusu miradi mbalimbali ya Shiri-
ka, Kaimu Mkurugenzi wa Uwekezaji na Masoko
Aloyce Tesha aliwataka wataalamu kuwa makini na
kutumia utaalamu wao katika kazi ili kuleta matokeo
mazuri yenye tija kwa Shirika na taifa.
Aliongeza kuwa, siri kubwa ya kuweza kufikia
malengo katika miradi hiyo ni kujitolea zaidi ya muda
wa kazi ili kuweza kumaliza kazi kwa wakati unaotak-
iwa.
STAMICO imewapiga msasa wataalamu wake ili
wawe tayari kuanza kupeleka kuchangia fedha HAZI-
NA ndani ya kipindi cha miaka miwili. Aidha, mafun-
zo hayo yatakuwa yakitolewa kila mara baada ya kuajiri
wafanyakazi wapya na vilevile kuendelea kutoa mafun-
zo yanayoendana na kazi na utaalamu ili kuongeza
ufanisi katika kazi za Shirika.
STAMICO
YAWANOA
WATAALAMU
WAKE WAPYA
Wafanyakazi wa Shirika la Madini la Taifa
(STAMICO) walioshiriki kwenye mafunzo
elekezi yaliyofanyika mjini Dodoma katika
picha ya pamoja
Wamiliki, Waombaji leseni
za madini watakiwa
kufuata Taratibu
8 Bulletin News
http://www.mem.go.tz
TANZANIA DAIMA LAIKOSEA WIZARA
MOIL yaonesha nia kuwekeza mitambo
ya uhifadhi na usafrishaji mafuta
Na Teresia
Mhagama
K
ampuni ya MOIL ya
Tanzania imeonesha
ya kuwekeza katika ku-
jenga matenki ya kuhifadhia
mafuta jijini Dar es Salaam na
kujenga bomba la kusafirishia
mafuta hayo kwenda sehemu
mbalimbali nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa
kampuni hiyo, Shanif Hirani
alieleza nia hiyo jijini Dar es
Salaam wakati alipokutana na
Waziri wa Nishati na Madini,
Profesa Sospeter Muhongo
pamoja na watendaji wa Wiz-
ara katika Ofisi za makao
makuu ya Wizara ya Nishati
na Madini.
Hirani alieleza kuwa
ujenzi wa mitambo ya uhifa-
dhi mafuta na bomba la kusa-
firishia mafuta hayo utakuwa
katika awamu tatu ambapo
katika awamu ya kwanza
watajenga matenki 10 yata-
kayokuwa na uwezo kuhifa-
dhi lita milioni 120 za mafuta
na endapo mradi utapata
kibali cha serikali, utakamilika
mwishoni mwa mwaka 2015.
Alisema awamu ya pili ya
ujenzi itajumuisha ujenzi wa
bomba la kusafirishia mafuta
kutoka Kigamboni kwenda
Chalinze ambapo mradi huo
utajumuisha ujenzi wa maten-
ki manne
yenye uwezo
wa kuhifadhi
mafuta lita
milioni 50 na
endapo mradi
huu utapata
kibali, utaan-
za kuanza
mwaka 2015
na kumal-
izika mwaka
2018.
Hirani aliwaeleza wa-
tendaji hao wa Wizara kuwa
awamu ya tatu ya mradi huo
utajumuisha ujenzi wa bomba
la kusafirishia mafuta kutoka
Chalinze hadi Morogoro am-
bapo mradi huu unatarajiwa
kuanza mwaka 2019 na kuka-
milika mwaka 2021.
Kituo hicho cha kuhifa-
dhi mafuta kitakuwa na faida
nyingi kwa nchi ikiwemo uku-
sanyaji wa mapato ya serikali
kwa sababu mafuta yatakuwa
yakiingia na kusambaziwa ka-
tika kituo kimoja ambacho ki-
takuwa na mitambo ya kisasa
kitakachoonyesha jinsi mafuta
hayo yanavyosambazwa vi-
levile tutapunguza msonga-
mano wa magari jijini Dar es
Salaam kwa sababu vituo hivi
pia vitajengwa mikoani. Ali-
sisitiza Mkurugenzi Mtendaji.
Naye Waziri wa Nishati
na Madini, Profesa Sospeter
Muhongo aliwaeleza watend-
aji wa kampuni hiyo ya MOIL
kuwa nia yao ya kuwekeza
katika kujenga kituo cha
kuhifadhi mafuta na kusam-
baza mafuta hayo kwa njia
ya bomba ni nzuri kwa kuwa
Taifa linauhitaji mkubwa wa
kuwa na kituo kikubwa cha
kuhifadhi mafuta lakini lazi-
ma serikali itathmini kuhusu
mradi huo kwanza kabla ya
kuchukua maamuzi yoyote.
Waziri Muhongo aliwa-
taka watendaji hao kujadiliana
na wataalam kutoka Wizarani,
Taasisi za Serikali zinazohusi-
ka na nishati hiyo pamoja na
wadau wengine kutoka Taasisi
zizizo za kiserikali ili endapo
mradi huo utaanza uwe ush-
irikishi.
Na Mwandishi Wetu
K
atibu Mkuu wa Wizara
ya Nishati na Madini,
Eliakim Maswi amese-
ma Wilaya zote za Kitanesco
zitapatiwa magari Double
Cabin na Dianna zenye crane
ifikapo mwaka ili kuboresha
utendaji wa kazi wa Wafan-
yakazi wa TANESCO.
Katibu Mkuu aliwaeleza
Wafanyakazi wa Wilaya za
Tunduru na Songea mkoa wa
Ruvuma, Iringa na Mbeya al-
ipokutana nao wiki iliyopita
na kuzungumza nao wakati
wa ziara yake ya kukagua na
kutembelea miradi ya maende-
leo mikoani humo ili kubaini
changamoto zinazolikabili
shirika hilo.
Maswi aliyasema hayo
baada ya wafanyakazi wengi
wa TANESCO kwenye Wilaya
na Mikoa aliyotembelea ku-
lalamika kwa hawana magari
ya kutosha ya kufanyia kazi
na kwamba utendaji wa kazi
unakuwa hafifu na kushindwa
kuwahuduma wateja hususan
katika Idara za Matengenezo
na dharura (emergency) kwani
Wilaya ziko mbali na ni vigu-
mu kuzifikia kwa haraka.
Aidha, Maswi amewa-
taka viongozi wa Wizara na
taasisi zilizo chini ya Wizara
kuwasilikiliza Wafanyakazi
wa mikoani mahitaji yao hu-
susan vitendea kazi ili waweze
kutekeleza majukumu yao ina-
vyopaswa.
Huwezi kumkamua
ng`ombe kama humlishi hivyo
lazima tuwasikilize wafan-
yakazi na kuwapatia vitendea
kazi ili wazalishe na iwe rahisi
kuwaondoa wanaoshindwa
bila kuwa na visingizio, alise-
ma Maswi.
Wilaya zote TANESCO kupewa magari 2015
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati
na Madini Eliakim Maswi
(wa tano kushoto) akiwa
katika picha ya pamoja na
Wafanyakazi wa Tanesco Songea
alipowatembelea hivi karibuni.
Anayefuatia ni Kamishna wa
Madini Tanzania, Mhandisi Paul
Masanja (wa sita kushoto).
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati)
akiwa katika kikao na Watendaji wa Kampuni ya MOIL (waliokaa
upande wa kushoto) wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa
kampuni hiyo, Shanif Hirani (kulia kwa Waziri) wanaotaka kuwekeza
katika mitambo ya kuhifadhi na kusafirisha mafuta nchini.Wa kwanza
kutoka kulia ni Abbas Kisuju, Mwanasheria wa Wizara, wa pili kutoka
kulia ni Mjiolojia Mkuu katika Wizara ya Nishati na Madini, Habass
Ngulilapi, na wa kwanza kushoto ni Eng.Joyce Kisamo, Kaimu
Mkurugenzi wa Shughuli za Usafirishaji na Usambazaji Gesi asilia na
Mafuta Kutoka TPDC.
u
9
Bulletin News
http://www.mem.go.tz
Wadau watoa maoni
Sera ya Petroli
Teresia Mhagama na
Jamila Masonga, Dar
es Salaam
K
atika kuhakikisha
kuwa wananchi wana-
shirikishwa ipasavyo
katika uandaaji wa
sera mbalimbali zinazoende-
sha sekta ndogo ya mafuta na
gesi nchini, Wizara ya Nishati
na Madini mwishoni mwa wiki
iliyopita iliandaa kongamano
kubwa lililoshirikisha wadau ku-
toka sekta mbalimbali ili kuweza
kutoa maoni yatakayoboresha
rasimu ya Sera ya Petroli am-
bayo inatarajiwa kukamilishwa
ifikapo octoba 15 mwaka huu.
Kongamano hilo lilidhuriwa
na wadau mbalimbali wak-
iwemo wakuu wa mikoa amba-
ko shughuli za utafiti wa mafuta
na gesi zinafanyika, viongozi
wa dini, vyama vya siasa, sekta
binafsi, makampuni ya mafuta
na gesi, Taasisi za Serikali na zi-
sizo za Serikali na vyombo vya
habari.
Akifungua kongamano hilo
mkuu wa mkoa wa Mbeya, Ab-
bas Kandoro alisema kuwa kon-
gamano hilo ni muhimu kwa
kuwa tayari Tanzania ina uvum-
buzi mkubwa wa gesi asilia am-
bayo inafikia futi za ujazo trilioni
50.5 lakini pia kuna shughuli za
utafutaji mafuta zinazoendelea.
Alisema pamoja na Tanza-
nia kubarikiwa na rasilimali hizo
lakini itafika wakati itakwisha
hivyo katika kuhakikisha kuwa
rasilimali hiyo inawanufaisha
watanzania pale inapovunwa,
lazima kuwe na sera ambayo pia
itakuwa muongozo katika kuten-
geneza sheria, kanuni pamoja na
vyombo vitakavyosimamia sekta
hiyo nchini.
Sera ya Petroli pia itatoa
mwongozo katika kuihakikishia
nchi kuwa pato linalotokana na
sekta ya mafuta linawanufaisha
watanzania wote na ndio maana
wamealikwa wadau mbalimbali
ili maoni yao yatumike katika
kuiboresha sera hiyo. Alisisitiza
Mkuu wa mkoa wa Mbeya.
Naye Kamishna wa Ni-
shati na Maendeleo ya Petroli,
Mhandisi Hosea Mbise alieleza
kuwa kutokana na ukuaji wa
haraka wa sekta ndogo ya utafu-
taji na uzalishaji mafuta Serikali
imeona umuhimu wa kuandaa
Sera ya Petroli ambayo pamoja
kutoa miongozo mahsusi ya
kusimamia kwa ufanisi shughuli
za utafutaji wa mafuta na gesi
lakini pia itatoa miongozo ya
kuendesha biashara ya mafuta
nchini ikiwamo usafirishaji, us-
ambazaji, na matumizi ya petro-
li.
Alieleza kuwa Sera ya Petroli
vilevile itatumika kama msingi
wa kufanya marejeo ya kubore-
sha mfumo wa usimamizi katika
sekta ndogo ya utafutaji na uzal-
ishaji mafuta na gesi asilia nchini
ikiwamo sheria, kanuni,mkataba
kifani, muundo wa kitaasisi, na
mipango mkakati ili kuhakikisha
kwamba rasilimali za mafuta na
gesi zinachangia kikamilifu ka-
tika kuongeza pato la Taifa na
maendeleo ya jamii.
Akieleza kuhusu matokeo ya
uwepo wa Sera ya Petroli Kam-
ishna wa Nishati alieleza kuwa
sera hiyo italeta matokeo chanya
ikiwemo kuleta ufanisi katika
mfumo wa kisheria na kitaasisi
katika usimamizi wa shughuli
za utafutaji mafuta na gesi asi-
lia nchini, kuwepo kwa mfumo
madhubuti na utaratibu wa ku-
tunza takwimu za shughuli za
utafutaji na uzalishaji mafuta
ambazo serikali na wadau wa
sekta husika wanaweza kuziakisi
na kuzitumia kwa manufaa ya
sekta na Taifa.
Matokeo mengine yata-
kayokuwepo kutokana na uwe-
po wa Sera ya Petroli ni kuwepo
kwa uhakika wa upatikanaji wa
bidhaa za mafuta nchini, na ku-
wepo mfumo madhubuti wa ku-
kabiliana na kuelimisha umma
juu ya matarajio
halisi kuhusiana na shughuli za
utafutaji na uzalishaji rasilimali
za mafuta na gesi asilia na mapa-
to yatokanayo na shughuli hizo.
Kwa upande wake Mjiolo-
jia Mkuu kutoka Wizara ya Ni-
shati na Madini, Adam Zuberi
alisema kuwa rasimu hiyo ya
Sera ya Petroli inaeleza kuhusu
ushirikishaji wa watanzania ka-
tika shughuli za mafuta na gesi
ili kila mtanzania afaidike na ra-
slimali hiyo.
Alisema watanzania wa-
naweza kushiriki katika shu-
ghuli za mafuta na gesi kwa
njia mbalimbali ikiwemo utoaji
wa huduma katika makampuni
yanayojishughulisha na utafu-
taji na uchimbaji wa rasilimali
hizo, pamoja na kuingia ubia na
makampuni hayo ili kuendesha
shughuli hizo nchini.
Zuberi alisema kuwa Sera
ya Petroli pia inaeleza kuhusu
mapato yanayotokana na rasili-
mali hiyo kunufaisha jamii in-
ayozunguka shughuli za mafuta
na gesihuku akitolea mfano wa
halmashauri ya Kilwa inavyo-
faidika na mapato ya gesi asilia
ambayo ni asilimia 0.3 ya ma-
pato yote yanayopatikana katika
rasilimali hiyo.
Nao wadau walioshiriki
kongamano hilo waliweza kutoa
maoni mbalimbali ya kuobore-
sha sera hiyo ikiwemo masuala
ya utunzaji wa mazingira, jinsia,
uwepo wa mkakati wa mawasi-
liano, matumizi ya mapato ya-
takayotokana na rasilimali hiyo,
biashara ya petroli, na masuala
ya uwazi katika uendeshaji wa
rasilimali hiyo.
Rasimu ya Sera Petroli im-
eandaliwa na Kamati inayoju-
muisha wajumbe kutoka Wizara
ya Nishati na Madini, Ofisi ya
Rais-Tume ya Mipango, Wizara
ya Ardhi, Nyumba, Maji, na Ni-
shati ya Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar, Shirika la Maende-
leo ya Petroli (TPDC), Baraza la
Mazingira la Taifa (NEMC) na
Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA).
Serikali kuimarisha
mazingira ya Uwekezaji
Na Koletha
Njelekea,Perth
Australia
S
erikali imesema itaendelea
kuimarisha mazingira ya
uwekezaji nchini ili kupanua
kiwango cha matumizi ya rasili-
mali za taifa yakiwemo madini ili
kuongeza tija kwa taifa.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara
ya Nishati na Madini Mhandisi
Ngosi Mwihava ametoa msima-
mo huo wa Serikali jana wakati
akiwasilisha mada kuhusu mi-
kakati ya Serikali katika kuboresha
uwekezaji nchini; katika Konga-
mano la 12 la Uwekezaji katika
sekta ya Madini linalofanyika kila
mwaka katika mji wa Perth nchini
Australia.
Mwihava alieleza kuwa, maz-
ingira mazuri ya uwekezaji yak-
iwemo Sera, Sheria, Kanuni bora za
ukusanyaji kodi ikiwemo mirahaba
yameiwezesha Tanzania kuongeza
miradi ya ubia katika sekta ya ma-
dini jambo ambalo limesaidia ku-
jenga uwezo wa wataalam wake,
kuboresha kiwango cha uwajibikaji
na uzalendo kwa watanzania ka-
tika kulitumikia taifa.
Changamoto iliyopo mbel-
eyetu ni kuboresha mfumo wa
teknolojia ya habari na mawasi-
liano (TEHAMA) katika sekta zote
ili kuwawezesha wawekezaji kupa-
ta taarifa sahihi na kwa wakati
na hivyo kukuza uelewa katika
sekta wanazohitaji kuwekeza na
Tanzania, alifafanua Mwihava.
Aidha alieleza kuwa sambam-
ba na uboreshaji wa mazingira ya
uwekezaji Wizara ya Nishati na
Madini itaendelea kuharakisha
utoaji wa leseni za madini kwa
wawekezaji ili kuongeza kiwango
cha miradi mikubwa ya madini
ambayo itachangia kuimarisha
utoaji huduma za jamii katika sek-
ta mbalimbali ikiwemo vile elimu,
afya, maji, nishati, na miundom-
binu.
Misingi ya uwazi, utawala
bora, uwajibikaji na mfumo bora
ya ufuatiliaji na udhibiti wa vitendo
viovu vikiwemo vya rushwa ni si-
laha kuu ya serikali katika kudhibiti
mapato na kukuza uchumi wa
nchi kupitia uwekezaji, alisisitiza
Mwihava.
Vilevile alieleza kwamba, sekta
ya madini imechangia kwa kasi
kuliingizia Taifa fedha za kigeni
ambapo kati ya mwaka 2000 na
2013 zaidi ya dola za kimarekani
bilioni 14.29 zimepatikana kupi-
tia migodi tisa mikubwa iliyopo
nchini.
Katika kipindi hicho vilevile
jumla ya dola za kimarekani bil-
ioni 1.46 zimelipwa kama mrahaba
(royality) na makampuni ya nje ya
madini yaliyowekeza nchini jam-
bao ambalo linatia moyo kwa taifa
kuendelea kutetea mazingira bora
ya uwekezaji, aliongeza Mhandi-
si Mwihava.
Mafanikio haya katika kukuza
pato la taifa yameiwezesha Seri-
kali kuendelea kuboresha miun-
dombinu umeme, reli, bandari na
barabara hususani katika maeneo
ya migodi ili kupunguza gharama
za uzalishaji na uwekezaji katika
utafiti.
Naye Kamishna wa Madini
nchini Mhandisi Paul Massanja
alieleza kuwam pamoja na changa-
moto za mtaji zinazoikabili Tanza-
nia, kama nchi ina nafasi kubwa
ya kunufaika kupitia kongamano
hilo Kongamano kwani itaweza
kuongeza miradi mikubwa ya ma-
dini kwa ushirikiano na makam-
puni makubwa ya madini ya Aus-
tralia.
Katika miaka 15 iliyopita
Tanzania imeweza kuingia katika
uzalishaji mkubwa wa madini na
hivyo kuboresha uwezo wake ki-
taalam ikiwemo kubuni miradi
na kuindesha kwa faida chini ya
mwongozo wa wataalam wa Ki-
tanzania kwa asilimia kubwa, ali-
sisitiza Masanja.
Kongamano hilo la siku tatu
lililoanza tarehe 3 Septemba 2014
linatarajiwa kumalizika leo (tarehe
5) ambapo Mawaziri 20 kutoka ka-
tika sekta ya madini Barani Afrika
wamehudhuria Kongamano hilo.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na
Madini akiwasilisha hotuba yake katika
Kongamano la 12 la Uwekezaji katika sekta ya
Madini linalofanyika kila mwaka katika mji wa
Perth nchini Australia. Mwaka huu linafanyika
tarehe 3-5, 2014 mjini hapo.
Wadau
mbalimbali
wakiwa katika
Kongamano la
kutoa maoni
kuhusu Rasimu
ya Sera ya Petroli
lililofanyika jijini
Dar es Salaam
mwishoni mwa
wiki iliyopita
u
u
Wadau watoa maoni
Sera ya Petroli
10 Bulletin News
http://www.mem.go.tz
http://www.mem.go.tz
Matukio Katika Picha
Meneja wa Bwawa la kuzalisha Umeme Mtera, Mhandisi Athony Mushi,
akimwonesha Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi
(Katikati) kipimo kinachoonesha kiasi cha maji katika bwawa hilo. Wa
kwanza kushoto ni Meneja uzalishaji Costa Rubagumwa.
Wanafunzi waliopata ufadhili wa kupitia Wizara ya Nishati na Madini kusoma Shahada
ya Uzamili Oil and Gas Development Engineering nchini China, wakiwa katika picha ya
pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi (wa tatu kushoto),Kaimu
Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania James Andilile (wa tatu kulia) na
Mkurugenzi Msaidizi Rasilimali Watu Wizara ya Nishati na Madini, Luis Mwenda(wa kwanza
kulia)
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava (wa saba
kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Wizara na Taasisi
zilizochini ya Wizara hiyo zinazoshiriki katika Kongamano la 12 la Uwekezaji katika
sekta ya Madini linalofanyika kila mwaka katika mji wa Perth nchini Australia. Mwaka
huu linafanyika tarehe 3-5, 2014 mjini hapo na linakwenda sambamba na maonesho ya
makampuni na taasisi mbalimbali zilizowekeza katika sekta ya madini Barani Afrika.
11
Bulletin News
http://www.mem.go.tz
Matukio Katika Picha
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi (kulia) akipokea
barua ya shukrani na pongezi kutoka kwa mwakilishi wa kampuni ya
Mitusubishi Akihiko Ichikawa (kushoto) kutokana na ushirikiano mzuri
kati ya kampuni hiyo na Wizara.
Meneja wa Bwawa la kuzalisha Umeme Mtera, Mhandisi Athony Mushi,
akimwonesha Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi
(Katikati) kipimo kinachoonesha kiasi cha maji katika bwawa hilo. Wa
kwanza kushoto ni Meneja uzalishaji Costa Rubagumwa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na madini, Eliakim Maswi (wa pili kushoto),
akiangalia namna shughuli za uchambuzi wa madini aina ya Saphire zinavyofanywa
baada ya kuchimbwa na wachimbaji wadogo. Wa tatu kulia ni Kamishna wa Madini
Tanzania Mhandisi Paul Masanja na katikati ni Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya
Kusini Magharibi Julius Salota.
Katibu Mkuu Wizara
ya Nishati na Madini,
akiangalia mkaa unaoweza
kutumiwa kwa jiko la
kupikia chakula uliotokana
na makaa yam awe
katika mgodi wa Ngaka.
Anayemweleza Katibu
Mkuu ni Leah Kayombo
mwakilishi wa akina
mama katika kikundi cha
Mbalawala Women Group.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro (kushoto)
akiongea na waandishi wa habari mara baada ya
kufungua Kongamano la Wadau kutoa maoni kuhusu
Rasimu ya Sera ya Petroli, kushoto kwa Mkuu wa
Mkoa ni Mjiolojia Mkuu kutoka Wizara ya Nishati na
Madini, Adam Zuberi.
12 Bulletin News
http://www.mem.go.tz
TMAA yawanoa wachimbaji
wadogo/ wa kati Nyarugusu
Afisa Mkaaazi wa Madini Geita, Mhandisi Pius Lorbe akiongea na waandishi wa habari wakati wa warsha
hiyo.
Meneja Utafiti na Mipango Wakala wa
Ukaguzi wa Madini Tanzania Julius Moshi
akiwasilisha mada wakati wa warsha hiyo.
Teresia Mhagama
W
achimbaji ma-
dini wadogo na
wakati katika
eneo la Nyarugu-
su mkoani Geita
wamepata elimu ya masuala mbal-
imbali ikiwemo kupata uelewa
kuhusu utunzaji wa kumbukumbu
za uzalishaji na mauzo ya madini,
ulipaji wa mrabaha, pia elimu
kuhusu viwango vya kodi na Tozo
mbalimbali iliyotolewa na wataal-
am kutoka Wakala wa ukaguzi wa
Madini Tanzania (TMAA) kwa
kushirikana Ofisi ya Madini mkoa
wa Geita.
Elimu hiyo ilitolewa na wataal-
am hao kutoka TMAA na Ofisi
ya Madini mkoa wa Geita katika
warsha ya siku moja iliyojumui-
sha wadau mbalimbali wakiwemo
wachimbaji madini wadogo na
wakati, wamiliki wa leseni za
utafiti na uchimbaji madini,
wachenjuaji marudio ya madini ya
dhahabu,viongozi wa kisiasa, seri-
kali, Jeshi la Polisi na waandishi wa
habari.
Meneja wa Utafiti na Mipango
wa TMAA, Julius Moshi aliwa-
sisitiza wamiliki hao wa leseni za
madini kufuata kanuni na sheria
zinazoongoza sekta hiyo nchini
ikiwemo kutekeleza suala la utun-
zaji wa kumbukumbu za uzalishaji
na mauzo ya madini kwenye eneo
la uchimbaji au katika anuani iliyo-
tumika kuandikisha leseni kama ki-
fungu cha 100 cha sheria ya madini
ya mwaka 2010 kinavyoelekeza.
Vilevile alieleza kuwa kifungu
cha 15(1) cha kanuni za Uchimbaji
za mwaka 2010 zinamtaka mmiliki
wa leseni ndogo ya uchimbaji ma-
dini kuwasilisha taarifa za uchim-
baji huo za kila robo mwaka kwa
Afisa Madini wa Kanda.
Taarifa hizi za uchimbaji
madini katika kila robo mwaka
zinatakiwa ziwe na vielelezo mbal-
imbali ikiwemo maelezo ya leseni
yako, taarifa za wafanyakazi ul-
ionao ikiwamo idadi yao, malipo,
mishahara na posho. Vilevile ka-
tika taarifa yako ya robo mwaka
unatakiwa kueleza kuhusu kiasi
na thamani ya madini yaliyozal-
ishwa na kuuzwa, matukio ya
ajali, majeruhi na vifo pamoja na
taarifa nyingine zinazohusiana na
uendeshaji wa mgodi.. Alisisitiza
Moshi.
Moshi alitaja faida za utunzaji
wa kumbukumbu hizo kuwa ni
pamoja na kupata picha ya ma-
pato yanayoingia kwenye biashara
pamoja na kufahamu matumizi
yake, kuweka vipaumbele ka-
tika kutumia rasilimali fedha ka-
tika uendeshaji wa biashara ,kutoa
msingi wa kutengeneza taarifa ya
faida na hasara, pamoja na kuaini-
sha nguvu na udhaifu wa biashara
ikiwemo kufahamu vitu vinavyo-
gharimu zaidi, sehemu gani zi-
natumia gharama kidogo, na ku-
fahamu eneo ambalo mchimbaji
anapata faida zaidi.
Utunzaji huu wa kumbukum-
bu pia utawarahisishia kutengen-
eza bajeti ya biashara zenu, kuan-
daa taarifa (returns) zinazotakiwa
na mamlaka husika mfano Wizara
ya Nishati na Madini na Mamlaka
ya Mapato (TRA), pia kumbukum-
bu hizi zinatoa picha na uhakika
wa biashara yako kwa mwekezaji
au mbia na pia itawasaidia kupata
mikopo katika mabenki na taasisi
za fedha. Alisema Moshi.
Kuhusu mrabaha unaopaswa
kulipwa serikalini kutokana na shu-
ghuli za uchimbaji madini, Moshi
alieleza kuwa Kifungu cha 87 cha
Sheria ya Madini ya Mwaka 2010
kinaainisha viwango mbalimbali
vinavyotumika katika kukokotoa
mrabaha kwenye thamani halisi ya
madini yaliyouzwa.
Alisema kuwa madini ya urani,
madini ya vito (ghafi) na almasi
(ghafi) yanatozwa mrabaha wa
asilimia Tano, madini ya metali
ikiwemo shaba, dhahabu, fedha na
metali za kundi la platinam yanato-
zwa mrabaha wa asilimia Nne, ma-
dini ya vito na almasi iliyokatwa
yanatozwa mrabaha wa asilimia
Moja, na madini mengine ikiwemo
ya ujenzi, chumvi na madini ya vi-
wandani yanatozwa mrabaha wa
asilimia Tatu.
Pamoja na masuala mengine
kuhusu sekta ya madini, Moshi
aliwakumbusha wamiliki wa leseni
za madini kuzingatia sheria, kanu-
ni na taratibu zilizopo kuhusiana
na utunzaji kumbukumbu, uwasil-
ishaji taarifa sahihi kwa mamlaka
za serikali, ulipaji mrabaha stahiki,
na kodi mbalimbali za serikali.
Vilevile aliwataka wamiliki wa
leseni kutoa ushirikiano kwa taasisi
za serikali ili kupata elimu na ku-
jenga tabia ya kutunza kumbukum-
bu za biashara zao kwa manufaa
na ufanisi wa biashara zao.
UJUMBE WA WAZIRI WIKI HII
WATENDAJI WOTE WA WIZARA NA TAASISI ZILIZO CHINI YA WIZARA
WAZINGATIE 4US KATIKA UTENDAJI WAO.
UADILIFU, UWAJIBIKAJI, UWAZI, UBUNIFU
TMAA yawanoa wachimbaji
wadogo/ wa kati Nyarugusu
UJUMBE WA WAZIRI WIKI HII

Вам также может понравиться