Вы находитесь на странице: 1из 16

www.annuurpapers.co.

tz

Sauti ya Waislamu

ISSN 0856 - 3861 Na. 1151 MUHARRAM 1436, IJUMAA ,

NOV. 14-20, 2014

BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Majibu haya ya
dhihaka
Ni ishara ya chuki
mbaya
Uk. 2

Masheikh wanadhalilishwa
kwa Uzanzibari wao?
Ahoji Mbunge wa Konde Khatibu Haji
Mariam Msabaha asema, tunaiita laana
Mh. Mathias Chikawe alikoroga zaidi
Wazanzibar waja juu Bungeni, wazimwa

Ajabu kuwaita
Masheikh ni
'mbwa wa
Jahannamu'

Hii ni itikadi ya Uyahudi Vs ma-goyim


Tusipokuwa makini na sera za Takfiri
Mguu utaota tende na majuto ni mjukuu
Mipango ya Yahudi Oded Yinon inatimia

Waziri wa Mambo ya Ndani Bw. Mbunge wa Jimbo la Konde


Zanzibar, Mh. Khatibu Said Haji.
Mathias Chikawe.

iasi wiki moja iliyopita


kulikuwa na mjadala
usio rasmi, kule
Zanzibar, watu wakijadili
Inspekta Jenerali wa Polisi nchini, hali iliyoibuka hivi sasa ya
Ernest Mangu.
baadhi ya makundi ya Salafi
h u w a p a c h i k a Wa i s l a m u
wenzao ukafiri na kuwatia
motoni. Mwalimu mmoja wa
chuo (madrasa) akaeleza kisa
kimoja ambapo alikutana
na mmoja wa Salafi hao
na katika mazungumzo yao
akasema kuwa masheikh wote
wa Zanzibar akiwataja baadhi
kwa majina (tunayahifadhi)
-wasio kuwa Salafi wa mtizamo
wake, kwamba ni Kilabu ni
nari, kwa maana kuwa ni
mbwa wa motoni.
soma Uk. 8

Kundecha akumbusha
usia wa Ustadh Ilunga
Waislamu watafakari, wapange, watende
Si kulalamika, kuwatupia lawama viongozi

Tahariri/Habari

2
AN-NUUR

S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786


Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM.
www.annuurpapers.co.tz
E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk
Ofisi zetu zipo: Manzese Tip Top
Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

Majibu haya ya dhihaka


Ni ishara ya chuki mbaya
CHUKI ni tatizo baya na
lenye madhara makubwa
katika jamii yeyote ile.
Palipo na chuki hapakosi
dhulma na palipo na
dhulma hapakosi uadui
na faraka.
Tu n a a m i n i k a b i s a
k wa m b a c h u k i i k i o t a
mizizi katika akili ya
mwanadamu, husambaa
kila mahali na itaendelea
kurithishwa kizazi hadi
kizazi.
Sehemu kubwa ya
chuki huenda hata ikawa
imeingizwa katika mfumo
wote wa maisha katika
jamii. Iwe ni katika sekta
ya kuichumi, kiutawala, au
kihuduma nk.
Dhulma, ubinafsi,
ubaguzi na upendeleo ni
matokeo ya kushamiri
chuki katika jamii.
Kwa bahati mbaya, imani
za dini ambazo ndio dawa
ya kumfanya binadamu
asikurubie maovu haya
ya nafsi, lakini kutokana
na utofauti wa dini, dini
h i z o h i z o z i m e k u wa
zikitumika kwa utashi
wa kibinadamu, kukoleza
chuki katika jamii.
Tu n a v y o f a h a m u ,
hakuna polisi wala nguvu
ya kidola popote pale
iwezayo kuondoa chuki
ambayo imesababisha
umwagaji mwingi wa
damu katika jamii sehemu
mbalimbali duniani.
Tizama Serbia, Bosnia,
Somalia na kwingineko.
Hata hivyo, kabla ya
kutafuta utatuzi, lazima
tupate kuelewa kiini cha
visa vya chuki.
Wa p o w a n a o s e m a
kuwa chuki hujitokeza
kwa sababu ya hofu tu,
wengine wanasema kuna
chuki kwasababu ya dhana
na kuhisi tu kuchukizwa,
kuna chuki ya kuonyesha
uwezo na chuki ya
k u t o k u wa n a u we z o ,
kuna ulipizaji kisasi na
kuna chuki inayotokana
na husuda, kuna chuki
ya mwonezi na chuki ya
mwenye kuonewa.
Ni masikitiko yetu kuona
kwamba milipuko ya chuki
nchini imekuwa ikitokea
mara nyingi kwasababu
tu ya tofauti ya imani zetu.
Tu n a s e m a h i v y o
kwasababu hatudhani
kwamba mtu anaweza
kufanyiwa kitendo cha
liwati, halafu akatokea

mtu ambaye amepewa


dhamana y a kusimamia

haki za watu, ambaye


kimamlaka ndiye kimbilio
la walalamikaji, akaja na
majibu ya kushangaza kama
ya Waziri Chikawe.
Hatudhani kwamba katika
sakata hili la kudhalilishwa

Masheikh
wetu
magerezani, lingetokea
kwa mwingine asiyekuwa
wa sampuli ya kuvaa
kilemba, mamlaka husika

zingekaa kimya mpaka sasa


au pale watu wanapohoji kuja
na majibu ya dhihaka kama ya
Waziri Mheshimiwa Mathias
Chikawe.
Wala hatutarajii kwamba
wahusika wangetoa kauli
hizi za ajabu za kuchunguza
tabia ya muadhirika kabla
ya kushughulika na tukio
lenyewe.
Unaposema unachunguza
kwanza tabia ya mtuhumiwa
aliyelawitiwa, unachosema
ni kuwa kama kwa mfano
mtuhumiwa aliingia rumande
na tabia ya kuvuta bangi, basi
halali kupewa bangi na askari
magereza. Au kama alikuwa
mbwia unga, basi polisi na
askari magereza waendelee
kumpatia kokeni.

M a j i b u k a m a h a ya ,
sio dhihaka tu, bali
yanaashiria kutokujali na
kutokujali kunakuja kwa
sababu ya chuki. Ndio
maana Mbunge wa jimbo
la Konde alihoji Je, ni kwa
kuwa aliyedhalilishwa ni
Mzanzibar au ni nani?
Tuseme tu kwamba,
tusipochukua hatua za
makusudi kukomesha
chuki katika jamii yetu,
itaendelea kututafuna.
Ni ushauri wetu kwamba
kuna haja na muhimu
kuchukuliwa hatua za
makusudi kuibadili jamii
yetu kuondoa nafsi yenye
kuchochea chuki na hasa
juu ya chuki kutokana na
misingi ya kidini.
Ni kweli kwamba chuki
haiwezi kuondolewa bila
jitihada zozote, wala jambo
hili haliwezi kufanywa
kwa usiku mmoja. Lakini
linaweza kufanywa.
Misingi ya utu, hekima
na uadilifu ndio suluhisho
la kuondokana na chuki
kwa watendaji na maafisa
waliopewa dhamana ya
kuwahudumia watu. Lakini
zaidi ni kuheshimiana na
kuvumiliana katika imani
zetu.

AN-NUUR

MUHARRAM 1436, IJUMAA NOVEMBA 14-20, 2014

Kundecha akumbusha usia wa Ustadh Ilunga


Na Bakari Mwakangwale

WAISLAMU tafakarini,
pangeni na kutenda, sio
kulalamika.
Hayo yamesemwa na
Amiri wa Baraza Kuu
la Jumuiya na Taasisi za
Kiislamu (T), Sheikh Mussa
Kundecha, katika nasaha
zake za mwaka mpya wa
Kiislamu 1436 Hijiria.
Amesema, mwaka
uliopita yalijiri mengi
kwa Waislamu, lakini
Waislamu wanapaswa
kuelewa kwamba agizo la
Mwenyezi Mungu kwao
ni kutafakari kwa nini
yametokea hayo na kwa
nini kwa kiwango hicho.
Hatuwezi kutibu
matatizo tuliyonayo kwa
kunungunika, tutatibu
matatizo tuliyonayo kwa
kutafakari kwa makini na
kuyapatia ufumbuzi yale
yanayotukabili, kiwango
cha manunguniko kwa
Waislamu kimezidi, kila
mmoja anaona hana
jukumu la kuupigania
Uislamu na kudhani
kuwa jukumu hilo ni la
viongozi. Alisema Amir
Kundecha.
A l i t o a f u n z o k u wa
Mwenyezi Mungu hawezi
kubadili hali ya watu
waliyokuwa nayo, mpaka
watu hao kwanza wao
wenyewe, mmoja mmoja
watie nia ya kufanya
mabadiliko katika sababu
zilizosababisha wao kuwa
katika hali hiyo.
Amir Kundecha
alionyesha kushangazwa
na Waislamu ambao mara
kwa mara wamekuwa na
tabia ya kuwapigia simu
viongozi, wakiwalalamikia
matukio yanayowatokea
k u h u s u Wa i s l a m u a u
Uislamu kabla ya wao
kushughulikia matatizo
hayo.
Sisi viongozi kila siku
kazi yetu ni kupokea simu,
Muislamu anakwambia
kuna mtu kakojolea
Qur an hapa. Suala hilo
naambiwa mimi Amir wa
Taifa, Sasa unachotaka
nini, nikupe fatwa au
niruke nije hapo ulipo,
alijisemea Sheikh Ilunga,
badala ya kushughulika,
mtu anapiga simu, haya ni
matatizo kwa Waislamu,
mwaka huu mpya wa 1,436
tubadilike.
Aidha Sheikh Kundecha
aliielezea hali hiyo kwa
Waislamu kuwa ni kama
ugonjwa.
Kwamba mambo
ya Kiislamu ni lazima

SHEIKH Mussa Kundecha.


yafanywe na watu fulani
au kusubiri viongozi
wawaambie kufanya
jambo, hata kama lipo
ndani ya uwezo wao,
wamebaki kuwa kazi yao ni
kutoa taarifa kwa viongozi
na kulalamika.
Alisema kule kuzorota
kwa mambo ya Kiislamu ni
dalili tosha kwamba hakuna
Muislamu anayetafakari
mambo ya Kiislamu
yatakwamuka vipi,
isipokuwa anafikiria kuwa
wapo watakayoyafanya
na hao si wengine bali ni
viongozi na yeye hahusiki.
Imeelezwa kuwa mbali
ya kasumba ya kulalamika,
pia Waislamu wamekuwa
na ugonjwa wa kutoa
visingizio badala ya kuwa
watendaji.
Mambo mengi
yanayotukuta kama jamii
ya Kiislamu, katika hali
ya kawaida tumekuwa
na tabia ya visingizio,
tutafakari kwa visingizio
tumerekebisha mambo
mangapi? Alihoji Amir
Kundecha.
Alisema mwongozo
wa Kiislamu (Quran)
hauruhusu Muislamu
kuwa na visingizio, bali
unamtaka atafakari hali
aliyonayo, kwamba
atatoka vipi katika hali
inayomkabili bila ya kuwa
na visingizio.
K w a m b a Wa i s l a m u
w a m e k u w a
n a
manunguniko mengi na
kwa bahati mbaya kila

wanapotafutia ufumbuzi
jambo fulani, huwa
wanaongeza manuguniko
jambo ambalo sio dawa ya
kuondoa tatizo.
Mwaka huu wa 1436,
Waislamu wameuanza
kwa msiba, pamoja na
kwamba hatuichukii hali
hiyo, lakini Allah (s.w)
anatutaka tutafakari,
wapo wanaotangulia
mbele ya haki, wengine
bado wapo magerezani,
nani wa kufanya
h a r a k a t i ? , Wa i s l a m u
tunapaswa tutafakari.
Alitahadharisha.
Alisema kwa ujumla
mwaka uliopita wa
K i i s l a m u , u l i k u wa n i
wa matatizo ya aina ya
peke yake kwa umma
wa Kiislamu, kwani
umekamilika mwaka huo
kwa sehemu kubwa ya
viongozi wa Kiislamu
kuwekwa ndani.
Aliongeza kuwa
kuwekwa ndani ni jambo
moja, kwa nini wako ndani
ni jambo la pili na kwa
makosa gani, alisema
katika hali hiyo inawapasa
Waislamu kutafakari zaidi.
Itafakari propaganda
inayoelezwa, inaelezwa
kuwa wamefanya
uchochezi, wanasimamia
ugaidi, kwa Muislamu
unaposema unamwamini
Allah (s.w) na kukemea
dhulma, hilo linatosha
kuwa ni kosa na kupewa
adhabu wanayoitaka wao.
Alisema Amir Kundecha.

Habari

AN-NUUR

MUHARRAM 1436, IJUMAA NOVEMBA 14-20, 2014

Masheikh wanadhalilishwa kwa Uzanzibar, Uislam wao?


Na Azza Ally Ahmed

KILIO cha Waislamu juu ya


kudhalilishwa Masheikh
wanaotuhumiwa ugaidi kimefika
Bungeni.
Katika kufikisha kilio hicho,
baadhi ya wabunge wamehoji ni
kwa nini serikali imepiga kimya
juu ya tuhuma nzito kama hizo.
Katika kuonyesha uzito wake,
Mbunge wa Konde akahoji iwapo
wanafanyiwa hayo na kimya
hicho kinakuja kwa vile wale ni
Wazanzibari?
Leo hii wazee wale
wanalalamika, mzee na watoto
wake anasimama mahakamani
anasema mimi siwezi kusimama,
nimefanyiwa vitendo hivi, hivi
kweli ni amani gani iliyopo nchi
hii. Kiongozi ana wazazi, ana
wafuasi, ana watoto wake, ndugu
zake, wanakaa kwenye televisheni
na wafuasi wake wanamuona
baba yao analalamika hawezi
kusimama kwa sababu kafanyiwa
ulawiti, hiki ni kitendo kibaya
sana ambacho kinafanyika ndani
ya nchi yetu. Hakuna anayesema,
hakuna anayejali kwa nini? Kwa
sababu wale ni Wazanzibar au
kwa sababu wale ni nani? Alihoji
kwa uchungu Mbunge huyo.
Hiyo ilikuwa Jumanne wiki
hii, ambapo Mbunge wa Jimbo
la Konde Zanzibar, Mh. Khatibu
Said Haji, aliomba muongozo kwa
Naibu Spika Job Ndugai, kwamba
kwanini serikali haiwachukulii
hatua waliohusika na vitendo vya
kinyama na udhalilishwaji dhidi
ya viongozi wa dini, ambao ni
watuhumiwa wa ugaidi waliopo
magerezani.
Akiomba mwongozo huo,
alisema baadhi ya watuhumiwa
ambao ni viongozi wa dini
kutoka Zanzibar, wanafanyiwa
vitendo vya udhalilishaji vya
liwati magerezani na hakuna
anayewasikiliza.
Kuna (watuhumiwa)
ambao wamekamatwa kutoka
Zanzibar wako katika magereza
hapa, wamekuwa wakitoa
malalamiko kila siku kwamba
ndani ya magereza vitendo
wanavyofanyiwa si vitendo vya
kibinadamu, utawala bora uko
wapi katika Taifa hili.
Mhe. Mwenyekiti naomba
niyaseme haya, kuna taarifa
kwamba Masheikh wetu wale,
ndugu zetu wale, wameshitakiwa
kwa kosa la ugaidi Ok,
h a t u i n g i l i i m a s h i t a k a ya o ,
lakini hawajashitakiwa wafike
mahala pale ndani ya magereza
wakafanyiwe vitendo vya ulawiti,
tunaumia. Alisema Bw. Haji.
Aliongeza kuwa pamoja na
kulalamika, watuhumiwa hawana
watetezi na kudai kwamba, Baraza
Kuu la Waislamu Tanzania si
chombo cha kuwatetea Waislamu.
Alisema, Baraza hilo ni Jumuia
kama zilivyo Jumuia nyingine tu

MMOJA wa watuhumiwa wa ugaidi akionesha suruali yenye usaha


Salaam hivi karibuni.
za CCM na kwamba haina msaada dini, ni dalili dhahiri kwamba
wowote kwa Waislamu.
hakuna utulivu, hatuna amani
Aliongeza kuwa Bakwata ipo katika nchi hii.
kwa maslahi ya watu wachache
Alisema kila siku mawakili na
na kwamba ni Jumuia ya kinafiki. magazeti yanatoa habari juu ya
L e o h i i w a z e e w a l e udhalilishwaji wa watuhumiwa
wanalamika, mzee na watoto hao, lakini hakuna anayethubutu
wake anasimama mahakamani k u s e m a n a h a p o n d i p o
anasema mimi siwezi kusimama, alipohitimisha hoja yake kwa
nimefanyiwa vitendo hivi, hivi kuieleza Bakwata kuwa ni jumuia
kweli ni amani gani iliyopo nchi ya kinafiki huku akirejea kauli
hii. Kiongozi ana wazazi, ana hiyo mara tatu.
wafuasi, ana watoto wake, ndugu
Kwa upande wake, Mbunge
zake, wanakaa kwenye televisheni Mariam Msabaha naye aliguswa
na wafuasi wake wanamuona na udhalilishwaji wa viongozi
baba yao analalamika hawezi hao wa Kiislamu na kutoa rai
kusimama kwasababu kafanyiwa bungeni hapo, na kusema kitendo
ulawiti, hiki ni kitendo kibaya hicho kinaweza kusababisha laana
sana ambacho kinafanyika ndani mbaya.
S o t e t u n a j u a k u wa wa l e
ya nchi yetu. Hakuna anayesema,
h a k u n a a n a ye j a l i k wa n i n i ? watuhumiwa ni wanavyuoni,
Kwasababu wale ni Wazanzibar au laana itatutafuna kwa kuwafanyia
kwa sababu wale ni nani?, alihoji Masheikh vitendo vile, tunaweza
kupata laana na tusijue laana hiyo
kwa uchungu Mbunge huyo.
tumeipata wapi. Alisema Mariam
Bw. Haji alisema anachoweza Msabaha.
kusema ni kwamba, matendo
Hata hivyo siku ya Jumatano,
yale ni ya kinyama na ambayo k a t i k a h a l i ya k u s h a n g a z a
yanatakiwa yalaaniwe na yeyote. Waziri wa Mambo ya Ndani Bw.
Washitakiwe kwa tuhuma Mathias Chikawe, alitoa majibu
z i n a z o w a k a b i l i z a u g a i d i , yaliyotatanisha, kukanganya
kesi iendelee mpaka mwisho, na kuwatia hasira zaidi baadhi
lakini inatuuma sana matendo ya Wabunge, hasa wa kutoka
wanayofanyiwa Wazanzibar wale, Zazniabr.
Katika majibu yake bungeni,
leo unafikiri amani iko wapi, leo
alisema
serikali haijamchukulia
anasimama mtoto wa mzee yule
hatua yeyote katika kadhia hiyo
anapewa bomu akalipue, ataacha kwa kuwa wanachunguza kwanza
kulipua?
tabia ya nyuma (background) ya
Mbunge huyo alisema kwa anayedai kulawitiwa.
k u k i t h i r i m a t e n d o h a y o ya
Akasisitiza kuwa, serikali
udhalilishaji kwa viongozi wa h a i w e z i k u c h u k u a h a t u a

mahakamani Kisutu jijini Dar es


yoyote kwa sasa hadi tabia za
wa na o l a l a m i k i a k ul a w i t i wa
kuchunguzwa kwanza.
Majibu ambayo yanatoa ujumbe
kuwa aliyedai kufanyiwa liwati,
huenda ni tabia yake.
Wakati Chikawe anayasema
hayo, baadhi ya wabunge walikuwa
wakishangilia na kugonga meza.
Hata hivyo, wengi wa wabunge
kutoka Zanzibar walionekana
kukasirika na kutaka kupata
mwongozo kutoka kwa
Mwenyekiti.
Lakini, Mwenyekiti aliwazima
kwa kutomruhusu hata mmoja
kusema akisimama katika hoja
kuwa jambo hilo liachwe kwa
sababu lipo mahakamani.
Wa z i r i
C h i k a w e
alisema mtuhumiwa huyo
anashughulikiwa afya zake na
kwamba jitihada zinafanyika za
kumpeleka Muhimbili.
Wa k a t i h a l i i k i wa h i v y o ,
taarifa zinaeleza kuwa mmoja
wa watuhumiwa wanaodaiwa
kudhalilishwa, Salum Ali Salum,
anahitajika kufanyiwa upasuaji.
Imeelezwa kuwa mtuhumiwa
huyo ambaye alikuwa na shida ya
kutembea, sasa ameanza kutembea
lakini hospitali ya Amana Ilala
jijini Dar imeshindwa kumfanyika
upasuaji hivyo amepewa rufaa
k w e n d a h o s p i t a l i ya Ta i f a
Muhimbili.
Taarifa zilizotufikia zinasema
kuwa taratibu za Kimagereza
zinaendelea ili kumpelekea
hospitali ya Taifa Muhimbili.

Habari

AN-NUUR

MUHARRAM 1436, IJUMAA NOVEMBA 14-20, 2014

Sirajul Munir yaendelea kungara Bagamoyo


Na Athumani Shomari, Bagamoyo

SHULE ya Msingi Sirajul Munir


ya mjini Bagamoyo, imeendelea
kufanya vizuri katika mtihani wa
Taifa wa kumaliza elimu ya msingi.
Akizungumza na An nuur,
Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Haruni
Mchau, alisema katika mtihani huo
ambao matokeo yake yametangazwa
na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi hivi karibuni, wanafunzi wote
24 waliofanya mtihani katika shule
hiyo wamefaulu, ambapo wanafunzi
9 kati yao wamepata alama A na 15
wamepata alama B.
Mwl. Mchau, alisema kufuatia
matokeo hayo, shule imefanikiwa
kushika nafasi ya tatu katika wilaya
kati ya shule 122 zilizopo Wilayani
Bagamoyo, huku ikishika nafasi ya
tatu mkoa kati ya shule 520 zilizopo
mkoa wa Pwani.
Mkuu huyo wa shule alisema
matokeo hayo yamepatikana kufuatia
shule hiyo kupata wastani wa 190.791
na kushika nafasi ya 143 kitaifa kati
ya shule 15,867 zilizopo nchi nzima.
Pamoja na mafaniko hayo, Mwl.
Mchau alielezea changamoto
zinazoikabili shule hiyo katika kuinua
kiwango cha taaluma, kuwa ni tatizo
la bweni la wanafunzi, maktaba
ya shule pamoja na mashine ya
kudurufu (photocopy kwa ajili ya
mitihani ya majaribio inayofanywa
mara kwa mara shuleni hapo, kwani
kwa sasa hulazimika kutembea
umbali mrefu kutafuta huduma hiyo.
Alisema matokeo hayo ni kutokana
na mazingatio kwa wanafunzi
wake katika kile walichofundishwa
na walifanya mitihani hiyo kwa
kujiamini na kutumia uwezo walio
nao.
Akielezea kasumba na tabia ya
kuwapa majibu ya mitihani wanafunzi
kabla ya mtihani, alisema suala
hilo ni baya na halifai na ni mwiko
shuleni hapo, hasa ikizingatiwa
kuwa shule hiyo ni ya Kiislamu, na
wanafunzi wanafundishwa kuwa
wizi na kughushi, hata kama ni katika
mitihani ni haramu na ni chukizo kwa
Mwenyezi Mungu.
Wakati huohuo mwl. Mchau,
a m e wa t a k a wa z a z i n a wa l e z i
kufuatilia tabia za watoto wao katika
shule wanazosoma, ili kudumisha
tabia na maadili mema waliyopata
shuleni hapo.
Shule ya msingi na awali ya Sirajul
Munir iliyopo nje kidogo ya mji wa
Bagamoyo, inamilikiwa na Taasisi ya
Sirajul Munir Islamic Center (SIMIC),
yenye makao makuu yake eneo
Majani Mapana, Wilayani Bagamoyo.
Shule hiyo ina jumla ya wanafunzi
304 kwa sasa, ambapo tayari
imeshatoa wahitimu wa darasa la
saba kwa mara nne tangu kuanzishwa
kwake mwaka 2011.
Shule hiyo ya Kiislamu, imewahi
kupata tunzo ya ngao kutoka Wizara
ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
sambamba kupatiwa cheti cha
kufanya vizuri (Best Performing
Schools), baada ya kufanya vizuri
katika mtihani wa Taifa mwaka jana.
Katika matokea ya mtihani wa
darasa la saba mwaka jana (2013),
shule hiyo ilishika nafasi ya tatu katika
wilaya na nafasi ya tatu mkoa kwa
wastani wa 192.5625, na kufanikiwa
kuwa ya 93 Kitaifa.

Wahitimu wa darasa la saba katika Shule ya Sirajul Munir (English Medium Prymary School) iliyopo
Bagamoyo, wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufanya mtihani wao wa Taifa. (Picha. Na
Athumani Shomari).

Vijana wapatiwe ajira-Lipumba


Na Bakari Mwakangwale

SERIKALI imetakiwa kuhakisha


kwamba vijana wanaohitimu
vyuoni wanapatiwa ajira baada
ya kuhitimu mafunzo yao, kwa
kuzingatia kwamba wengi wao
wamehitimu katika taaluma ya
Ualimu.
Wi t o h u o u m e t o l e wa n a
Profesa Ibrahim Lipumba, wakati
akiongea na waandishi wa habari
katika mahafali ya Chuo Kikuu
Cha Waislamu Morogoro (MUM),
Jumamosi ya wiki iliyopita.
Alisema jambo hilo halina
budi kuzingatiwa kwa kuwa
Taifa linakabiliwa na upungufu
wa wa l i m u , j a m b o a m b a l o
ni changamoto kwa jamii na
kwamba, hiyo ni fursa kwa vijana
hao kupewa ajira ili waweze kutoa
taaluma waliyoipata na kuongeza
ufanisi katika sekta ya elimu.
Alisema katika mahafali hayo
ya saba ya chuo hicho, wengi
waliohitimu ni walimu na kwa
ujumla, katika shule mbalimbali
n c h i n i k u n a u p u n g u f u wa
walimu katika masomo yote,
hivyo aliwataja wahitimu kuwa
ni watu muhimu kupewa ajira ili
shule ziweze kupata walimu wa
kutosha.
Aidha Prof. Lipumba alikitaka
chuo hicho (MUM) kuwasiliana
na sekta binafsi ili kuwawezesha
vijana wanaohiti chuoni hapo
katika fani nyingine kuweza

Profesa Ibrahim Lipumba


kupata ajira.
Changamoto nyingine iliyopo
kama chuo, ni kuwasiliana na
sekta binafsi kuona kwamba vijana
wanaomaliza hapa wanaweza
kupata ajira katika sekta zao, ili
yale mambo wanayoyapata hapa
yaweze kukidhi mahitaji ya ajira.
Alisema Prof. Lipumba.
Alisema sehemu moja ambayo
ni muhimu kwa wahitihimu
kuelewa kuwa katika jamii ya
Waislamu, wengi bado hawana
elimu ya kutosha ya dini, hivyo

ni wajibu wao kuweka utaratibu


ambao wataweza kutoa elimu
ya dini huko watakapokuwa, ili
kuwawezesha vijana wengine
kuijua dini yao katika ngazi ya
chini.
A k i z u n g u m z i a wa h i t i m u
kujiingiza katika siasa, alisema
japo si vibaya wasomi kujihusisha
na siasa, lakini si sahihi kuingia
moja kwa moja katika siasa
ukitoka chuo na kwamba watu
wasiache taaluma zao.
Kushiriki kwenye siasa ni
sawa, lakini ni vyema kujikita
pia katika taaluma uliyoisomea
kwa kuifanya kwa weledi katika
eneo ambalo wewe unakuwa na
utaalamu nalo. Alisisitiza Prof.
Lipumba.
Alisema, vijana wenye umri
chini ya miaka 35 ni takribani
asilimia 80 ya Watanzania wote,
kwa maana hiyo alisema vijana
ndio wengi nchini na wao ndio
wanaopaswa kushiriki katika
kutafuta ufumbuzi wa matatizo
yanayoikabili jamii ikizingatiwa
wao ndio waathirika zaidi na
matatizo yaliyopo nchini.
Alisema, vijna ndani ya Taifa
hili wana kila sababu ya kuwa
mstari wa mbele kuitafuta haki
na kuhakikisha mali asili za nchi
yao zinatumiwa kwa manufaa ya
wananchi wote.

Habari za Kimataifa

AN-NUUR

MUHARRAM 1436, IJUMAA NOVEMBA 14-20, 2014

Mtuhumiwa wa ugaidi aliyeuliwa Kenya azikwa FBI iache


Polisi washukiwa kumuua
ujasusi
Maandamano yaibuka na kusababisha kifo
misikitini
Marekani
HASSAN Nasrullah Musa
"Guti ", mtuhumiwa wa ugaidi
aliyeuliwa kwa kupigwa
risasi huko Mombasa Kenya,
amezikwa mwishoni mwa
wiki iliyopita. Musa alipigwa
risasi na kuuawa wakati akiwa
kwenye gari na mkewe mjini
Mombasa, ambapo mkewe
alipigwa risasi ya mguu na
anaendelea kuuguza majeraha
ya usoni kutokana na vipande
vya vioo.
Mashuhuda wa tukio hilo
walibainisha kwamba Bw.
Musa aliuliwa kwa staili ile ile
waliyouliwa Masheikh maarufu
wa Mombasa, Aboud Rogo na
baadae nduguye Ismail Rogo
na kufuatia kuuliwa Sheikh
Makaburi, wote walidaiwa
na polisi kuwa waliuawa
na watu wasiojulikana na
wakihusishwa na ugaidi.
Mnamo mwaka huu kuna
idadi kubwa ya wahubiri wa
dini ya Kiislamu walouliwa
na watu wasojulikana na hadi
hii leo hakuna aliyekamatwa
wala kushtakiwa kwa mauwaji
hayo.
Ust. Musa alizikwa katika
makaburi ya Waislamu ya
Kikowani siku ya Jumapili,
ambapo baadae yalifanyika
maandamano makubwa ya
kulaani mauaji hayo.
Kufuatia maandamano
hayo ghasia ziliibuka kwa
waombolezaji katika eneo
la Majengo mjini Mombasa,
wakishutumu na kulaani
mauaji hayo, ambapo Mhadhiri
mmoja wa Chuo Kikuu, David
Munga aliuliwa na watu
wengine wapatao watano
kujeruhiwa, liliripoti gazeti la
Daily Nation la Kenya.
Majeruhi walilazwa katika
Hospitali Kuu ya Pwani kwa
matibabu.
Kwa mujibu wa ripoti ya
polisi, Musa anaaminika kuwa
na mafungamano na kikundi
cha magaidi mjini Mombasa
na alikuwa anakabiliwa na
mashitaka ya mauaji kwenye
Mahakama ya Mombasa,
huku ikidaiwa mawaidha ya
siasa kali ndiyo yaliyochochea
ghasia hizo, kiliripoti kituo cha
Capital FM cha Kenya.
Hata hivyo viongozi wa
dini wameendelea kukanusha
dhana za polisi kwamba
mawaidha yao ndiyo
yanayochochea ghasia, bali
wanasema hali ya usalama
imezorota sana katika jiji hilo
la pili kwa ukubwa Kenya.

Mkurugenzi Mtendaji wa
Shirika la Haki za Binadamu
la Haki Africa, Hussein Khalid,
alilielezea tukio hilo kuwa
ni "mauaji ya makusudi" na
kutoa wito serikali kuanzisha
uchunguzi ili kuwajua
wahusika.
"Mombasa leo imeshuhudia

mauaji mengine, tumemuona


kijana leo akiuawa kwa risasi
m c h a n a k we u p e k we n ye
mitaa ya Mombasa. Uko wapi
usalama? Iko wapi serikali?
Lazima tuseme kwa pamoja.
" Alisema Mkurugenzi huyo.
(sabahi)

MMOJA wa waathirika wa upasuaji wa kuzuia ujauzito India


akiwa mahututi.

Nane wafariki wakifungwa kizazi India


50 mahututi

U PA S U A J I u l i o f a n y wa wa
kuwafunga vizazi wanawake
zaidi ya 80 nchini India, umetoa
uhai wa wanawake nane na
wengine 50 wanaugua baada
ya kufanyiwa upasuaji wa
kuwafunga vizazi nchini India.
Wanawake hao wameelezea
kuhisi maumivu makali na homa
punde baada ya kupewa matibabu
hayo ya upasuaji wa kuwafunga
uzazi, katika kliniki ya kiserikali
huko eneo la katikati mwa India
Chhattisgarh.
Ta a r i f a z a i n a e l e z a k u wa
wanawake 30 kati ya wagonjwa
walionusurika waliopo hospitali
hapo, inasemekana kuwa katika
hali mahututi.
Tayari Idara ya Afya nchi India
imeamuru uchunguzi ufanyike
mara moja.
Zaidi ya wanawake 80
walishiriki katika upasuaji huo wa
kuzuia kupata uja uzito Jumamosi
ya wiki iliyopita katika hospitali
hiyo ya kijijini Pendari huko
Chattisgarh.
Baadhi ya wanavijiji wanadai
shughuli hizo za upasuaji
zilifanywa na daktari mmoja
na msaidizi wake katika muda
wa saa sita tu, hivyo wanahoji
iwapo ziliendeshwa vyema. Miili
ya waliofariki bado inafanyiwa

uchunguzi huku wanaougua


wakiendelea kupewa matibabu
katika hospitali tofauti katika
eneo hilo.
Waziri wa Afya katika jimbo hilo
ameiambia BBC kuwa wanafanya
wawezalo kuokoa maisha ya
wanaougua na wameunda jopo
litakalochunguza kilichosababisha
hali hiyo isiyo ya kawaida.
Serikali ya India imekuwa na
utaratibu wa mara kwa mara
wa kutoa huduma ya jumla
kwa wanaohitaji operesheni za
kufunga kizazi, kama njia moja
ya kujaribu kudhibiti ongezeko
kubwa la idadi ya watu nchini
humo. (BBC)

KIONGOZI Mwandamizi wa
Baraza la Uhusiano wa Kiislamu
nchini Marekani (CAIR),
ameitaka Polisi ya Marekani
(FBI) kuacha kufanya ujasusi
ndani ya Misikiti nchini humo.
Akizungumza kwa niaba ya
Waislamu, Mkurugenzi Mtendaji
wa CAIR huko Minnesota,
Lori Saroya, amesema kuwa
wafanyakazi wa FBI wamekuwa
na tabia ya kutembelea na kuingia
Misikitini katika miji ya Saint
Paul, Minneapolis na miji mingine
katika jimbo la Minnesota, kwa
lengo la kuwarubuni baadhi ya
Waislamu ili wafanye ujasusi
dhidi ya Waislamu wenzao.
S a r o ya a l i s e m a k wa m b a
wafuasi wa dini ya Kiislamu
wanaelewa majukumu yao ya
kidini na kijamii ya kutoa taarifa
kwenye vyombo vya dola, pindi
wapoona dalili za kufanyika
uhalifu na jinai.
Alisisitiza kwamba polisi
wa FBI wanapoingia kwenye
maeneo ya ibada hasa Misikitini,
husababisha hali ya hofu na
wasiwasi kwa waumini wa dini
hiyo.
Aliongeza kuwa, kitendo cha
kuwarubuni Waislamu ili kufanya
ujasusi dhidi ya Waislamu
wenzao, kinakinzana na misingi
ya kidini na kitabia.
Hayo yanajiri katika hali
ambayo, msemaji wa FBI
amekataa kutoa tamko kuhusiana
na tuhuma hizo zilizotolewa
dhidi ya Polisi ya Marekani. (irib.
ir)

TANGAZO

Taasisi ya Kiislamu iliyosajiliwa kisheria, (Almuhajirina Islamic


Foundation) inaomba msaada wa kifedha kutoka kwa Waislamu
ili kuweza kumalizia deni la ununuzi wa eneo (nyumba yenye
Madrasa ya Taasisi). Tayari Taasisi imelipa kiasi cha Tsh.
40,000,000/- (Milioni Arobaini) bado Tsh. 80,000,000/-(Milioni
Themanini).
Unaweza kutoa mchango wako kupitia A/c
No. 52 12 01 00 00 38 74 PBZ. Tawi la LUMUMBA DSM. Au
piga simu Namba:-0658 05 65 92,
0665 66 98 65 na 0655 24 12 70.

Habari

AN-NUUR

MUHARRAM 1436, IJUMAA NOVEMBA 14-20, 2014

Norway yaihimiza SMZ kuenzi maridhiano


SERIKALI ya Mapinduzi
Z a n z i b a r , i m e h i m i z wa
kuendelea kudumisha
umoja, mshikamano na

maelewano yaliyopo, ambayo


ni matunda ya kufikiwa
maridhiano ya kisiasa
yaliyozaa Serikali ya Umoja
wa Kitaifa.
Wito huo umetolewa na
Balozi wa Norway nchini, Bi.
Hanne Marie Kaarstad, wakati
alipokuwa na mazungumzo na
Makamu wa Kwanza wa Rais
wa Zanzibar, Mhe. Maalim Seif
Sharif Hamad, ofisini kwake
Migombani mjini Zanzibar.
Balozi Kaarstad amesema
kutokana na uzoefu wa hali ya
siasa siku za nyuma, hivi sasa
Zanzibar imepiga hatua kubwa
katika kudumisha amani,
maelewano na utulivu, mambo
ambayo yemejenga mazingira
mazuri kwa Serikali kujikita
kwenye maendeleo na kwa
wananchi kufanya shughuli zao
bila matatizo.
Naye, Makamu wa Kwanza
wa Rais Zanzibar, Mhe. Maalim
Seif Sharif Hamad, amesifu
ushirikiano uliopo kati ya
Zanzibar na Norway na kuahidi
kuwa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar itafanya kila jitihada
kuona ushirikiano huo unazidi
kuimarika.
Maalim Seif alisema Norway
imetoa mchango wa kipekee
katika kuhakikisha Zanzibar
inapata mafanikio makubwa
katika nyanja mbalimbali,
ikiwemo kudumishwa utulivu
wa kisiasa pamoja na kusaidia
sekta mbalimbali za kiuchumi,
maendeleo na kijamii.
Alisema mchango wa serikali
ya Norway katika kufanikisha
kufikiwa kwa Maridhiano ya
Kisiasa yaliyozaa Serikali ya
Umoja wa Kitaifa Zanzibar ni
wa kipekee na njia muafaka
ya kuuenzi ni kuhakikisha
Zanzibar hairudi tena kwenye
siasa za chuki na uhasama.
Aidha Maalim Seif, alisema
ili maridhiano hayo yaweze
kudumu, kasoro zinazojitokeza
ambazo zinaweza kurejesha
nyuma taswira na dhamira
njema ya kufikiwa kwake,
hazina budi kupatiwa ufumbuzi
kwa haraka pale zinapojitokeza,
ili kuzidi kujengwa hali ya
umoja na kuaminiana.
Maalim Seif alizitaja baadhi

ya c h a n g a m o t o z i l i z o p o
k u wa n i m a r i d h i a n o n a
maelewano hayo kueleweka
na kutekelezwa zaidi katika
ngazi za juu Serikalini, ambapo
mkazo zaidi unahitajika katika
ngazi za chini, kama vile
kwenye Shehia.
Alisema ipo haja kwa Serikali
na taasisi zote zinazosimamia
haki kutekeleza wajibu huo

na kila mtu aweze kupata


haki anayostahili, bila kujali
itikadi yake kisiasa, kabila au
dini yake.
Aliyataja baadhi ya maeneo
yanayolalamikiwa kuwa ni
baadhi ya wananchi wenye
sifa kunyimwa vitambulisho
vya ukaazi, kukoseshwa
haki za kushiriki katika
chaguzi mbalimbali pamoja
na kuwepo malalamiko
kuwa vikosi vya serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar,
baadhi ya wakati hutumika
vibaya hasa katika masuala
ya uchaguzi.
Hata hivyo, Maalim
Seif alisifu mchango wa
Norway kwa Zanzibar katika
kusaidia kukuza demokrasia,
upatikanaji wa nishati ya
umeme vijijini pamoja na
kusifu mchango mkubwa
wa nchi hiyo katika suala

Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad

la uhifadhi wa mazingira
Zanzibar.
Maalim Seif ametoa
wito kwa Noway kuzidi
kushirikiana na Zanzibar
katika nyanja za uvuvi wa
bahari kuu, sekta za elimu

na afya na kuendeleza elimu


ya uhifadhi na mazingira, ili
kuilinda Zanzibar na hatari
inayojitokeza ya eneo lake
la ardhi kuliwa na maji ya
bahari. (Habari kwa hisani
ya OMKR)

alinukuliwa akisema
Makamu wa Rais Gharib
Bilal.
Tanzania ni mwenyeji wa
Mahakama ya Kimataifa
ya Jinai ya Rwanda (ICTR),
lakini mahakama hiyo
imepangwa kufungwa
mwishoni mwa mwaka huu.
Hatima ya watu nane
waliosamehewa mashtaka
huko ICTR, na wengine
watatu waliotumikia vifungo
na sasa wanaishi kama
wafungwa katika nyumba
salama huko Arusha bado
halijatatuliwa.
Wengine 11 wameendelea
kubaki katika ulinzi
na inadaiwa wamesema
hawawezi kurudi Rwanda.
ICTR ilianzishwa
kusimamia mashtaka ya
mauaji ya kimbari ya mwaka
1994, ambapo watu wapatao

800,000 waliuawa, wengi wao


kutoka jamii ya ya Watutsi.
" M o j a ya k u s h i n d wa
kwa ICTR ambako
tunaweza kujifunza
kuhusiana na kushindwa
kwake kuwasaidia
wa l e wa l i o s a m e h e wa . . .
wakiondoka Tanzania na
kwenda kuishi maisha yao
ya kawaida," alisema msajili
wa ICTR Bongani Majola.
" N i d h a h i r i h a l i ya o
inawakilisha changamoto
kubwa za haki za binadamu
ambazo zinahusika na
msaada wa jumuiya ya
kimataifa." Aliongeza.
W a n y a r a n d w a
wa l i o k u wa n a t u h u m a
ndogo, walihukumiwa na
mahakama za Rwanda na
maelfu kadhaa ya mahakama
za chini, zinazojulikana
kama gacaca, zilizowekwa na
serikali ya Rwanda. (sabahi).

Tanzania yawaombea hifadhi Wanyarwanda


Na Mwandishi Watu

TANZANIA imetoa wito


kwa serikali za nje kutoa
hifadhi za kisiasa kwa
wale waliosamehewa
mashtaka yanayohusiana
na mauaji ya kimbari ya
1 9 9 4 h u k o R wa n d a n a
wale walioachiliwa baada
ya k u t u m i k i a k i f u n g o
gerezani, AFP iliripoti.
Wi t o h u o u m e t o l e wa
Jumamosi Novemba 8 na
Makamu wa Rais Dk. Gharib
Bilal.
"Kwa unyenyekevu
ninawaomba wawakilishi
wa serikali walio hapa
kuona namna unavyoweza
kuchukua jukumu hili la
kimataifa kwa kukubali
kuwatafutia mahali
watu waliosamehewa
n a wa l i o a c h i wa h u r u , "

Makala

AN-NUUR

MUHARRAM 1436, IJUMAA NOVEMBA 14-20, 2014

EBOLA - Janga la kuthamini zaidi faida kuliko uhai


Said Rajab.

MLIPUKO wa kirusi hatari


cha Ebola Afrika Magharibi,
ambacho kimeua zaidi ya
watu elfu tano mpaka sasa,
u m e a n z a k u wa s u a l a l a
kushughulikiwa katika ngazi
ya dunia zilipotoka tu taarifa
za raia kadhaa wa nchi za
Magharibi kuambukizwa
ugonjwa huo.
Hata baada ya hapo, bado
mwitikio wa jumuiya ya
kimataifa haujawa wa kutosha,
ambapo maafisa wa Umoja wa
Mataifa wameripoti kwamba
m a o m b i ya d o l a b i l i o n i
moja yaliyoletwa kwa ajili
ya kupambana na Ebola, ni
asilimia 25 tu ndiyo iliyotolewa.
Bwana Stephen Hall, Afisa
Mtendaji Mkuu wa kampuni
moja ya madawa anafafanua
kwanini:
" Wa we k e z a j i we t u
hawajahamasika kutoa fedha
kwa ajili ya kutengeneza chanjo
ya Ebola, ambapo mpaka
sasa, hili limekuwa ni tatizo la
ulimwengu wa tatu."
Anaongeza bwana Hall:
"Hata sasa ambapo Ebola
imeingia kwenye nchi zingine,
wawekezaji wetu bado
hawajaonyesha hamasa ya
kutosha. Wanasukumwa zaidi
na manufaa ya kiuchumi".
Kuacha kufanya utafiti
wa kutengeneza chanjo ya
Ebola kutokana na ukosefu
wa motisha za kifedha kwa
zaidi ya miaka 40, ni ushahidi
mzito kwamba makampuni
ya madawa yameweka
kipaumbele zaidi kwenye faida
kuliko maadili.
Ebola ni Kirusi hatari
sana. Kimepata jina lake hilo
kutoka mto Ebola uliopo
Congo, ambapo ugonjwa
huo ulionekana kwa mara
ya kwanza mwaka 1976.
"Ugonjwa huu ni miongoni
mwa magonjwa hatari sana
ya k u a m b u k i z a a m b a y o
yamewahi kufahamika kwa
wanadamu na kasi yake ya
kuua ni ya kutisha" anasema
Dk.Graham Fry wa 'Tropical
Medical Bureau' mjini Dublin.
Mpaka sasa hakuna tiba wala
chanjo iliyothibitishwa kwa
ajili ya kupambana na Ebola.
Hali hii haitokani na upya wa
kirusi cha Ebola kwa sababu
kirusi hiki kimekuwepo kwa

zaidi ya miongo minne.Tatizo


ni ukosefu wa fedha za utafiti
wa kutengeneza chanjo yake.
Michael Katze, Profesa wa
'microbiology' katika Chuo
K i k u u c h a Wa s h i n g t o n
nchini Marekani amesema:
" Tu m e i s o m a E b o l a k w a
takriban muongo mmoja na
wakati wote tumevutiwa na
Ebola.Imekuwa kama kirusi
mashuhuri cha virusi vyote"
anasema Prof.Katze.
Anaongeza zaidi:
"Makampuni makubwa ya
m a d a wa h a ya k o k we n ye
biashara ya hisani, mpaka
wapate fedha, bila hivyo
hawatashughulika kabisa na
chanjo ambayo siyo muhimu
katika nchi hii"
Ukizama kwa kina kwenye
tasnia ya madawa, utaelewa
kwanini chanjo ya virusi vya
Ebola haijagunduliwa mpaka
sasa. Makampuni ya madawa
duniani yanapaswa kuzingatia
kanuni kali za udhibiti
zinazojulikana kama FDA,
ambazo haziruhusu kabisa
dawa zilizoshindwa majaribio
ya kitaalamu kuingia sokoni.
Matokeo yake, makampuni
ya madawa yanalenga
z a i d i k u f a n ya u t a f i t i n a
kutengeneza dawa ambazo
zitaweza kulipia gharama zao
walizowekeza,ikiwa ni pamoja
na kuleta faida nono. Kwa
hiyo katika muktadha wa sasa,
ili kampuni ya dawa iweze
kubaki, inahitaji kugundua
d a wa i t a k a y o u z i k a k wa
gharama kubwa kila baada ya
miaka michache.Yaani,dawa
itakayoweza kuingiza mabilioni
ya dola.
Sasa magonjwa 'yatima' kama
Ebola yanaangukia kwenye
kipengele cha bidhaa zenye
masoko madogo, kwa sababu
magonjwa hayo yanawaathiri
tu watu walio kwenye nchi
masikini, ambao hawana
uwezo wa kulipia matibabu
yanayohitaji dawa za gharama
kubwa.
Isitoshe tiba kama hizo
huchukua kipindi kifupi tu, ni
wiki chache siyo miaka mingi,
hatua ambayo inamaanisha
kuna uwezekano mkubwa wa
kupata hasara kuliko faida.
Kwa hiyo hali hiyo imeondoa
rasilimali fedha kwenye utafiti
wa kirusi cha Ebola.

Kwa mujibu wa mchambuzi


wa Shirika la 'IBIS World
Healthcare' Sara Turk, mara
mtu anapotumia dawa za Ebola,
hatakuwa na sababu tena ya
kuendelea kununua dawa
hizo, hali ambayo inamaanisha
uwezekano mdogo wa mapato
kutoka kwenye dawa za Ebola.
K wa h i y o , m a k a m p u n i
makubwa ya dawa hayako
tayari kuwekeza kiasi kikubwa
cha rasilimali zinazohitajika
katika kutengeneza dawa ya
kutibu Ebola.'Model' hii ya
kibiashara inajulikana vyema
na imeleta utata mkubwa
kwa kipindi kirefu. Mfano
magonjwa kama HIV, maelfu
ya wagonjwa kutoka Afrika
walikataliwa tiba ya vidonge
kwa sababu tu serikali zao
h a z i k u wa n a u w e z o wa
kununua dawa hizo.
Hivi sasa kuna mzozo
k u h u s u u t e n g e n e z a j i wa
dawa mpya aina ya 'antibiotic'
ambayo inahitajika sana katika
kupambana na aina mpya ya
bakteria ambao ni sugu kwa
'antibiotics' zilizopo.
Andrzej Rys, Mkurugenzi
wa Mifumo ya Afya na bidhaa
wa Umoja wa Ulaya amesema:
"Jumuiya ya Ulaya inafahamu
fika kwamba miaka mingi ya
mafanikio ya kupambana na
bakteria sasa inatishiwa na
kuibuka upya na kuenea kwa
vimelea vilivyo sugu kwa dawa
hizi za msingi.Vimelea sugu
ni moja ya changamoto kubwa
za afya ulimwenguni, wakati
huo huo kuna upungufu wa
uwekezaji kwenye sekta ya
dawa katika kutengeneza
dawa mpya zenye ufanisi zaidi
katika kupambana na bakteria.
Matokeo yake ni kwamba

msingi wa kutengeneza dawa


m p ya z a k u p a m b a n a n a
bakteria haupo tena."
Bwana Klaus Dembowsky,
Mganga Mkuu wa Kampuni ya
Polythor amefafanua kwamba
u k o s e f u wa ' a n t i b i o t i c s '
mpya ni ukosefu wa mapato
yanayoletwa na dawa kama
hizo: "Sababu ya makampuni
mengi kuacha kujikita kwenye
maeneo hayo ni ukosefu wa
faida kutokana na uwekezaji
unaofanyika"
Lakini hakuna kinachoweza
kufanyika ili kubadili huu
utegemezi wa dawa kutoka
makampuni binafsi chini
ya mfumo wa Ubeberu
unaotawala dunia. Mfumo
huu unaendeshwa na mfumo
wa uchumi wa soko huria.
Nguvu ya soko na bei ndizo
zinazoendesha uchumi.
Hata Mkurugenzi wa
S h i r i k a l a A f ya D u n i a n i
(WHO) Margareth Chan pia
anashangazwa na mwenendo
huu wa makampuni ya
madawa:
"Ebola imeibuka takriban
miaka 40 iliyopita. Kwanini
mpaka leo madaktari wako
m i k o n o m i t u p u , h a wa n a
chanjo wala tiba?" Anajijibu
mwenyewe. "Kwa sababu
Ebola umekuwa ni ugonjwa,
ambao kihistoria na kijiografia,
umejikita kwenye mataifa
masikini. Sekta inayoendeshwa
kwa faida haiwekezi miradi
k we n ye m a s o k o a m b a y o
hayalipi."
Ubeberu haukubuniwa ili
utoe maamuzi kwa kuzingatia
m a a d i l i , i s i p o k u wa k wa
kuzingatia kikamilifu maslahi
Inaendelea Uk. 10

Makala

Na Omar Msangi

iasi wiki moja iliyopita


kulikuwa na mjadala usio
rasmi, kule Zanzibar, watu
wakijadili hali iliyoibuka hivi
sasa ya baadhi ya makundi ya
Salafi huwapachika Waislamu
wenzao ukafiri na kuwatia
motoni. Mwalimu mmoja wa
chuo (madrasa) akaeleza kisa
kimoja ambapo alikutana na
mmoja wa Salafi hao na katika
mazungumzo yao akasema kuwa
masheikh wote wa Zanzibar
akiwataja baadhi kwa majina
(tunayahifadhi) -wasio kuwa
Salafi wa mtizamo wake, kwamba
ni Kilabu n nari, kwa maana
kuwa ni mbwa wa motoni.
Katika mazungumzo hayo
ikabainishwa kuwa baadhi ya
Salafi hao, wamerejea masiku ya
hivi karibuni kutoka masomoni
Yemen na wanapigania kushika
uongozi wa Misikiti mbalimbali
huku wakifanya juhudi kubwa
mitaani kupata wafuasi.
Watu hawa japo wanaonekana
kuwa kundi moja, lakini
wamegawika katika makundi
mawili. Wote wanaunganishwa na
mtizamo mmoja wa kuharamisha
mambo mengi ikiwemo elimu
ya m a z i n g i r a n a k u s h i r i k i
nyingi ya shughuli za kijamii na
kimaendeleo katika jamii. Lakini
pia wanaungana katika itikadi
ya kuwatia Waislamu wengine
wote katika ukafiri na kuwaona
adui namba moja ndio wafuatie
makafiri halisi, Mayahudi na
washirikina. Kwa hiyo wanasema
kama ni kuanza kupambana, basi
wa kuanza nao ni hawa Waislamu
wasio Salafi Takfiri. Ndio pale
kijana mmoja aliyeacha shule
akiwa kidato cha tano kule Unguja
anasema kuwa bora mkewe
atibiwe na John, au kafiri yoyote,
lakini sio Muislamu asiye Salafi
kama yeye.
Wakiungana katika hayo,
lakini miongoni mwao wapo
wanaohimiza watu kushika
silaha wakidai kuwa kufanya
dawah ya namna yoyote ile
ni kupoteza muda. Hawa ndio
wanahimiza watu kuacha shule,
kuacha ajira zao, biashara na
shughuli nyingine za kimaisha,
wakapige kambi wajifue waje
kupambana na makafiri wakianza
na Waislamu wasio kuwa wao.
Yaliyojiri hivi karibuni kwa baadhi
ya vijana kuacha shughuli zao na
kujichimbia kule Kilindi, linaleta
picha hiyo.
Lakini wapo wengine ambao
wao husema kuwa hakuna haja
ya kupambana kwa silaha. Hata
kama unaishi katika serikali isiyo
ya Kiislamu, wewe huna haja ya
kuibughudhi. Usiiguse serikali/
mamlaka hata ikiwa ya kikafiri. Itii
maadhali haikubughudhi katika
kutekeleza usalafi wako.
Niliwahi kuambiwa na
Muislamu mmoja kutoka Mwanza
kuwa baadhi ya hawa Salafi
Jihadia, walikuwa wakisema katika
mmoja ya misikiti waliyokuwa
wa k i wa i d h i M wa n z a k u wa

AN-NUUR

MUHARRAM 1436, IJUMAA NOVEMBA 14-20, 2014

Ajabu kuwaita Masheikh


Ni 'mbwa wa Jahannamu'

Hii ni itikadi ya Uyahudi Vs ma-goyim


Tusipokuwa makini na sera za Takfiri
Mguu utaota tende na majuto ni mjukuu
Mipango ya Yahudi Oded Yinon inatimia

wakianza Jihad ya kupambana


na makafiri, wataanza na wale
walio katika taasisi za Kiislamu.
Wakazitaja kwa majina baadhi ya
shule za Kiislamu. Sasa ukisikia
maneno kama haya, inakujengea
wasiwasi na dhana kuwa huenda
yale yaliyokuwa yakidaiwa
kuwa kuna watu walimwagiwa
tindi kali kule Arusha kwa vile
hawakubaliani na misimamo
fulani, huenda ikawa ni kweli.
Z i p o t a a r i f a z i m e t o l e wa
kuelezea maafa yaliyokwisha
kuletwa na Boko Haram kule
Nigeria katika muda wa miaka
sita toka ilipoanza mashambulizi
ya silaha. Taarifa zinaonyesha
kuwa maelfu ya watu wasio na
hatia wameshauliwa, wakiwemo
Wakristo, Waislamu, wanawake
na watoto, polisi, wanafunzi na
hata wanajeshi. Pamefanyika
pia uharibifu mkubwa kutokana
na kulipuliwa majengo, vituo
vya polisi, maduka, shule, vyuo,
magari ya abiria na kuchoma moto
nyumba/makazi ya watu katika
vijiji mbalimbali.
Leo ukisikia mtu akisema
kuwa Boko Haram wanapigania
Uislamu au ukisikia kuwa kuna
mtu anasema kuwa Waislamu
wenzake ni mbwa wa motoni,
lazima uwe na wasiwasi kuwa
tunao Salafi Takfiri miongoni
mwetu.
Nani Salafi Takfiri

MAKAMU wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal (wa pili kulia) akikaribishwa
na mdhamini wa jumuiya ya Istiqama Sheikh Suleiman Nassor Msellem
katika hafla ya kuukaribisha mwaka mpya wa Kiislamu 1436 Hijiria katika
ukumbi wa Karimjee DSM mwishoni mwa wiki.

Labda tujiulize nani Salafi


Takfiri na nini itikadi yao na
mtizamo wao. Watafiti wengi
waliotafiti kundi hili, wanasema
Inaendelea Uk. 9

Shukri Mustafa (1942-1978)

HUKRI Mustafa alizaliwa


tarehe 1 Juni, 1942, katika
kijiji cha Abu Khurus,
kiasi kilometa 30 kusini mwa
mji wa Asyut, Misri. Mwaka
1965, wakati akisoma katika
Chuo cha Kiislamu cha Sayansi
ya Kilimo, Shukri alikamatwa
kwa kuhusishwa na harakati za
Ikhawan (Muslim Brotherhood.)
Akiwa jela, Mustafa na kundi la
wafungwa wengine, walijitenga
na wenzao na kuunda kundi
walilolipa jina la Jama'at alMuslimun (Muslim Society),
ambalo ndilo baadae lilikuja
kujulikana kama Takfir w'alHijra. Katika kujitenga kwao,
waliwashutumu Ikhwan kuwa
wanashirikiana na serikali ya
kikafiri ya Gamal Abd al-Nasser
k u p a m b a n a n a M a ya h u d i .
Msimamo wao ukawa kuwa
wapambane kwanza na Waislamu
walioitakidi kuwa ni makafiri kama
Nasser, ndio wamgeukie Yahudi.
Na alipotoka jela mwaka 1971
ndio akaimarisha zaidi msimamo
huo na kutafuta wafuasi. Hata
hivyo, wengi hawakukubaliana
naye, hasa alipokuja na mbinu
za kuuwa Waislamu na kuteka
nyara ili kupata pesa hata ikibidi

kuuwa akiitakidi kuwa kuiba


pesa, na hasa ya kafiri (wakiwemo
Waislamu wasio kuwa katika
mtizamo wake) ili itumike kwa
Jihad, sio mbaya.
Shukri na kundi lake la Jama'at
al-Muslimun, walijitenga na jamii
waliyodai kuwa ni ya kikafiri
wakaenda kuishi mbali na watu,
wakidai kuwa wanafanya hivyo
wajiandae wakipata nguvu ndio
waje kupambana na Waislamu
wa Misri waliowaita makafiri.
Kufanya hivyo, wanasema ni
kumuiga Mtume (s.a.w) aliyehama
Makkah kwenda Madina baadae
ndio akarudi akiwa na nguvu.
Ukiacha hilo, waliharamisha
karibu kila kitu wakianza na
elimu ya mazingira. Walidai kuwa
hakuna sayansi, sayansi ni Mungu
tu.
Kama nilivyosema, hawa awali
wenyewe wakijiita Jama'at alMuslimin , walikuja kuitwa alTakfir w'al-Hijra. Takfir ikitokana
na kile kitendo cha kuwatia ukafirikufr (infidel) Waislamu wenzao
na kuhama miji. Shukri akasema
hata kama Misri itavamiwa na
Mayahudi, utakuwa ni ukafiri
wa kumpeleka mtu motoni kama
atasimama pamoja na jeshi la
Abdul Nasser kupambana na

Mayahudi. Bora mtu ukimbie


uache Yahudi ateke nchi, ukipata
nguvu ndio urudi upigane na
Yahudi kumtoa ndani ya nchi.
Pamoja na kupiga marufuku
kusoma kemia, jiografia, sayansi
ya jamii na ile ya mazingira
(natural sciences), Shukri alipiga
pia marufuku kufuata fatwa za
Maimamu wanne-Shafii, Malik,
Abu Hanifa na Hanbal.
Pamoja na mkakati na mtizamo
huo wa kujitenga na jamii, ndio
warudi kupambana na Waislamu
na makafiri wengine, Shukri
hawakuweza kutimiza lengo
la kuwa na kundi la Waislamu
Salafi wa kupambana na jeshi la
serikali. Kinyume chake wakabaki
wakipora mali za watu na kuteka
watu nyara ili wapewe pesa kwa
kubadilishana. Walifanya hivi
kwa fatwah ya Shukri kwamba
kupora mali ya Muislamu asiye
Salafi kama wao au Kafiri yoyote
ni halali ilimuradi tu baadhi ya
pesa hiyo uitumie kwa Jihad.
Ni katika mwaka wa 1977
walimteka Waziri katika serikali
ya Anuwar Saadat wakitaraji
kupewa pesa na serikali, lakini
hawakupata. Shukri Mustafa
akakamatwa na kunyongwa
tarehe 19 Machi, 1978.

Makala

AN-NUUR

MUHARRAM 1436, IJUMAA NOVEMBA 14-20, 2014

Kuvunjwa kulikoandaliwa na kupanguliwa kisiasa kwa Irak:

Hatua kuelekea kuundwa na Marekani kwa dola ya Kiislamu


Dola ya Kiislamu ya Irak na Shamu: Nyenzo ya mfungamano wa kijeshi wa nchi za Magharibi

Na Profesa Michel Chossudovsky


(Global Research, Agosti 27, 2014)
RAIS Barack Obama ameanzisha
mfululizo wa Marekani kupiga
mabomu nchini Irak dhidi ya kile
kinachoitwa jeshi la uasi la Dola ya
Kiislamu (IS).
Magaidi hao wa Dola ya Kiislamu
wanaonyeshwa kama maadui wa
Marekani na nchi za Magharibi.
Kwa vielelezo vingi, imedhihirishwa
kuwa Dola ya Kiislamu ni kitu
kilichoundwa na mashirika ya ujasusi
ya nchi za Magharibi zikiungwa
mkono na CIA na Mossad ya Israel,
na kuwezeshwa kifedha na Saudia
na Qatar.
Tunachoangalia hapa ni mpango
wa kijeshi wa kudhamiria ambako
Marekani inaelekeza nguvu zake
dhidi ya jeshi la uasi ambalo linapewa
fedha na Marekani na washirika
wake. Kuingia nchini Irak kwa Dola
ya Kiislamu kuelekea mwisho wa
mwezi Juni kulikuwa sehemu ya
mpango wa kijasusi ulioandaliwa
kwa uangalifu.
Waasi wa Dola ya Kiislamu,
waliokuwa wakiitwa ISIS, walikuwa
wakipata misaada ya siri kutoka
Marekani-NATO - Israel kuendesha
vita ya kigaidi dhidi ya serikali ya
Syria ya Bashar el Assad. Uhalifu

dhidi ya binadamu uliofanywa nchini


Irak unafanana na ule uliofanywa
nchini Syria. Wafadhili wa IS akiwemo
Barack Obama wana damu mikononi
mwao.
Kuuawa kwa raia wasio na hatia na
magaidi wa Dola ya Kiislamu kunatoa
kisingizio na uhalali wa kuingilia
kijeshi kwa Marekani kwa misingi

ya kutoa misaada ya kibinadamu.


Ili tusisahau, waasi waliofanya
uhalifu huo na ambao wanalengwa
na operesheni ya kijeshi ya Marekani
wanaungwa mkono na Marekani.
M a s h a m b u l i z i ya m a b o m u
yaliyoamrishwa na Obama hayana
lengo la kuwaondoa magaidi hao, ila
kinyume chake. Marekani inalenga

Inatoka Uk. 8
imekuwa vigumu kujua lini na
nani hasa mwanzilishi wa kundi
hili, lakini historia ya hivi karibuni
inaonyesha kuwa Shukri Mustafa,
kutoka Misri, ndiye aliyelipa
uhai na kuwa kiongozi wake
akitambulika Misri na nje ya
hapo. Huyu baada ya kutoka
jela alikokuwa amefungwa,
alisema kuwa kuishi katika
jamii ya kikafiri ni ukafiri kwa
hiyo akahama akiishi mbali na
watu huku akitafuta wafuasi wa
kupigana Jihad akisema kuwa wa
kwanza kuanza nao ni Waislamu
wa Misri na serikali ya Misri kabla
ya kuwageukia Mayahudi.
Kundi lake likiitwa al-Takfir wa
al-Hijra (ATWAH), alihalalisha
vitendo vya mauwaji, uporaji na
kuteka nyara kama namna moja
wapo ya kukabiliana aliowaita
makafiri na vibaraka wa makafiri.
Katika utafiti na uchambuzi wake
aliouchapisha kwa anuwani
ya Jihad Without Rules: The
Evolution of al-Takfir wa al-Hijra
(Publication: Terrorism Monitor
Volume: 4 Issue: 13, June 29, 2006),
mwandishi Hayder Mili anasema
kuwa Mustafa:
was able to justify theft,

kidnapping, forced marriages and


even the assassination of anyone
who was not part of the group (such
as apostates). Most of these core
precepts are still loosely followed by
contemporary Takfir groups.
Kwamba Mustafa alihalalisha
wizi, utekaji nyara, ndoa za lazima
mauwaji, kuuwa yoyote asiye
katika kundi lake akidai kuwa
hao ni makafiri. Lakini zaidi
anasema kuwa mtizamo huo bado
unafuatwa na baadhi ya watu
(Waislamu) hadi hii leo.
Najaribu kuyatizama
haya anayosema Hayder,
n a k u ya l i n g a n i s h a n a ya l e
yaliyodaiwa kuhubiriwa na
baadhi ya watu hapa nchini
yakihalalisha kuuwa na kupora
mali. Nayalinganisha pia na
yale yanayodaiwa kufanywa
na Boko Haram kule Nigeria
ya kuteka watoto wa shule na
madai ya kuwaoza kwa nguvu!
Yalinganishe pia na haya madai
ya baadhi ya watu wanaodai
kuwa wakianza kazi wataanza
na hawa walio katika taasisi za
Kiislamu ambazo wanadai kuwa
zenyewe na wanaoziendesha
hawana shaksia za Kiislamu!
Katika sehemu nyingine

mwandishi Hayder anasema:


Takfir is able to legitimize criminal
activities, justifying these activities
through the theory of the fay'e (the
licit) by appropriating the goods and
property of infidels and apostates.
Criminal activities like theft and
drug trafficking are thus encouraged
if one-fifth of the proceeds are used to
fund the jihad.
Kwamba ni halali kupora mali
ya kafiri (na Muislamu asiye Salafi
Jihadia) ilimuradi tu pesa au mali
hiyo utatoa sehemu yake kwa
ajili ya Jihad! Hebu yachambue
haya anayosema ulinganishe na
yale yaliyokuwa yakisemwa kule
Mwanza kuwa ni ujinga kulala
njaa wakati kafiri ana mali! Na ile
ya kuhimiza kuwa na silaha bila
kujali unaimiliki kwa mujibu wa
sheria au la!
Ni kutokana na msimamo huo,
Shukri alianzisha vikundi vya
utekaji na mauwaji. Mwaka 1977
alimteka Waziri mmoja katika
serikali ya Misri, aliyekuwa pia
miongoni mwa Masheikh wa
kuaminika, akataka alipwe fedha
ndio amwachie. Serikali ilipokataa
kulipa, akamuuwa Waziri huyo.
Hapo ndipo serikali ikamkamata
na kumuuwa mwaka 1978.

RAIS Barack Obama wa Marekani.

rais wa kawaida na makundi ya


wapiganaji wa Irak wanaopinga
utawala ulioko madarakani.
Lengo halisi ni kupangua misingi
ya dola ya Irak kama taifa na
kuwezesha kuigawa nchi hiyo katika
vipande vitatu.
Kuundwa kwa Dola ya Kiislamu
kumetangazwa. Dola ya Kiislamu ya
Irak na Shamu (ISIOS) imebadilishwa
na kuwa Dola ya Kiislamu (IS). Dola
ya Kiislamu siyo asasi huru ya kisiasa.
Ni mradi wa kubuniwa na vyombo
vya ujasusi vya Marekani.
Vyombo vya habari vya nchi za
Magharibi vimekuwa vikielezea
mapigano yanayoendelea nchini
Irak kama "vita vya wenyewe kwa
wenyewe" kati ya Dola ya Kiislamu
ya Irak na Shamu dhidi ya majeshi
ya serikali ya Al Maliki.
Mafarakano hayo yanaelezwa
kuwa ni "vita ya makundi ya kidini"
kati ya wa-Sunni wenye siasa kali na
wa-Shia bila kuangalia "nani yuko
nyuma ya vikundi hivi." Kilichopo
dhahiri ni agenda iliyopangwa kwa
uangalifu na ujasusi wa kijeshi wa
Marekani.
Wa k i w a w a n a f a h a m i k a n a
vielelezo tele vipo juu yao, vikundi
vilivyochipua kutoka Al Qaeda
vimekuwa vikitumiwa na MarekaniNATO katika mifarakano maridhawa
kama 'nyenzo za kijasusi' tangu enzi

Inaendelea Uk. 11

Ajabu kuwaita Masheikh ni 'mbwa wa Jahannamu'

Hata hivyo, pamoja na


kuuliwa kwake, wafuasi wake
waliendeleza harakati ambapo
walisambaa katika nchi za Sudan,
Syria, Yemen, Jordan, Lebanon
na baadhi ya nchi za Afrika
Kaskazini. Ipo mifano mingi
ambapo Salafi hawa wamehusika
katika kushambulia watu mpaka
ndani ya Misikiti na kuuwa katika
nchi za Sudan, Lebanon, Morocco,
Misri na Uturuki.
Swali ambalo bado tunatakiwa
tulijibu ni hili: Hii itikadi na
mtizamo wa kuwaona Waislamu
waliotamka shahada kuwa ni
mbwa wa motoni wanaostahiki
kuuliwa inatoka wapi?
Mwandishi Jonathan Azaziah
akihitimisha utafiti wake alioupa
jina The Takfiri Gy Golem: ISIS,
Jabhat al Nusra, Their Israel
masters and the repackaged Zio ist
war on Islam, anasema ISIS should
change its name to IGGSIS: Israels
Goy Golem in Iraq and Syria.
Baada ya kuonyesha kwa
ushahidi wa nyaraka mbalimbali
kwamba ISIS na Jabhat al Nusra
zimeanzishwa na zinaendeshwa
na Mayahudi/mabeberu, anasema
kuwa itikadi inayofuatwa na
Inaendelea Uk. 11

10

Makala

AN-NUUR

MUHARRAM 1436, IJUMAA NOVEMBA 14-20, 2014

EBOLA - Janga la kuthamini zaidi faida kuliko uhai

Inatoka Uk. 7

ya kiuchumi,kama anavyobainisha

Dk.John Ashton, Rais wa Kitivo cha


Afya ya Umma nchini Uingereza:
"Lazima pia tupambane na janga
l a M a k a m p u n i ya M a d a wa
kutotaka kuwekeza kwenye utafiti
wa kutengeneza tiba na chanjo.
Wanakataa kwa sababu faida
inayopatikana, kwa mtazamo
wao, ni ndogo sana kuhalalisha
uwekezaji unaofanyika".
Mwaka hadi mwaka,
Makampuni ya Madawa
yanaogelea kwenye faida kubwa.
Kuanzia mwaka 2003 mpaka
2012,Makampuni makubwa ya
Madawa yalitengeneza faida
inayokadiriwa kufiki a Dola

Bilioni 711.4. Mwaka 2012 pekee,


Kampuni moja tu imetengeneza
faida inayokaribia Dola Bilioni
85. Kwa mujibu wa Taasisi ya
IMS Health, ambayo inaongoza
duniani kwa utafiti wa huduma
za afya, masoko ya dunia kwa
madawa yanatarajiwa kuzidi
Dola Trilioni Moja katika
mauzo ifikapo mwaka 2014.
Ungetarajia kwamba kiasi
c h a m a d a wa ya k u o k o a
maisha kingeongezeka duniani
kutokana na ongezeko hilo la
faida, lakini hali haiko hivyo.
Dawa chache sana muhimu
zimeingizwa sokoni katika
miaka ya hivi karibuni na hizo
zimetengenezwa kutokana na
utafiti uliodhaminiwa na fedha
za walipakodi.
Kama zilivyo sekta nyingine
zote kwenye Ubeberu, uchumi
wa soko huria umeruhusu
sekta ya madawa kuwa na
nguvu, msuli wa kisiasa na
ushawishi wa kijamii, na hivyo
kudhibiti kabisa maamuzi
ya serikali. Serikali za
Magharibi hazina kauli kwa
Makampuni makubwa ambayo
yanamilikiwa na matajiri.
Hili janga la Ebola
haliko tu kwenye sekta ya
madawa, lakini pia serikali
za Magharibi, ambazo
zilianza kuchukua hatua kwa
mlipuko wa ugonjwa huo,
mara tu watu wa Wamagharibi
walipoambukizwa,licha ya
ugonjwa huo kusambaa tangu
Desemba 2013, katika nchi za
Afrika Magharibi, zikiwemo
Guinea, Liberia na Sierra Leone.
Baadaye sana, ndipo
Rais Barack Obama wa
Marekani,alipoanza kuchukua
hatua za kudhibiti ugonjwa
huo ambao ni tishio kwa dunia,
kwa kupeleka wanajeshi 3000
katika maeneo maalumu barani
Afrika, ili kutoa msaada wa
matibabu na lojistiki. Uingereza

nayo ikafuata mkumbo wa


kupeleka wanajeshi, meli na
ndege katika maeneo ya Afrika
Magharibi yaliyoathiriwa na
Ebola.
Kwa hiyo, waathirika
wa v i r u s i v ya E b o l a n a
wale watakaoathirika siku
zijazo, siyo tu ni waathirika
wa ugonjwa huo, bali pia ni
waathirika wa unyama wa
Ubepari. Mimi siyo shabiki wa
falsafa za Mwalimu Nyerere,
lakini namuunga mkono sana
katika kauli yake ya "Ubepari
ni Unyama".Sasa naelewa
vizuri sana Mwalimu alikuwa
anazungumza nini.
U b e p a r i n i m f u m o wa
maisha ambao unaifunga
misaada ya kibinadamu na
maslahi ya kisiasa au faida za
kiuchumi. Hiyo ndiyo sababu
ugonjwa ambao umejulikana
kwa zaidi ya miaka 40, ambapo
tiba ingeweza kutafutwa,
ukapuuzwa kabisa.
Sasa hapo ndipo utakapoona
ubora wa Uislamu.Uislamu
unapinga kabisa kutoa misaada
ya kibinadamu ili baadaye
ujipatie manufaa ya kifedha.
Uislamu unaibana Dola ya
Kiislamu kisheria kuwasaidia
wale wanaohitaji tiba, maji,
chakula, elimu na mahitaji
mengine muhimu ya kijamii,
bila ya kujali kama ni Waislamu
au siyo Waislamu.
Sultan Abdul Majid wa Dola
ya Kiislamu ya 'Uthmaniyya'
alituma meli za misaada ya
vyakula kwenda Ireland, ambayo
ilikumbwa na janga kubwa la njaa

mwaka 1847.
Historia inaonyesha Dola ya
Kiislamu iliweka mazingira
mazuri ya kuendeleza Sayansi
n a Te k n o l o j i a , m s u k u m o
ukijikita kwenye kuhudumia
masuala yanayowahusu
watu kuliko kupata faida za
kiuchumi.
Katika fani ya Tiba,
mwanasayansi wa Kiajemi
aliyejulikana kama
I b n S i n a a u Av i c e n n a
kama anavyofahamika
katika ulimwengu wa
Magharibi,aliandika kitabu
chake mashuhuri "The Canons
of Medicine"(Misingi ya Tiba),
ambacho ndiyo kilikuwa
kitabu mashuhuri cha kiada
kinachofundishwa kwenye
vyuo vikuu vya tiba duniani
mpaka karne ya 18.
Katika kitabu hicho, Ibn
Sinna ametambulisha asili ya
magonjwa ya kuambukiza,
matumizi ya karantini kudhibiti
kuenea zaidi kwa maambukizi,

magonjwa yanayotokana na
hali ya ubongo kama kifafa,
kiharusi na kichaa, ikiwemo
dalili na matatizo ya kisukari.
Maendeleo ya Tiba
ya l i y o f i k i wa , ya l i t o k a n a
n a Wa i s l a m u k u z i n g a t i a
kikamilifu amri za Mwenyezi
Mungu kama zilivyobainishwa
ndani ya Qur'an na Sunna,
ikiwa ni pamoja na Hadith ya
Mtume inayosema: "Hakuna
ugonjwa ambao Mwenyezi
Mungu ameuumba, isipokuwa

am eleta na tiba yake"(Sahih

Bukhary).
U we p o wa t i b a k wa k i l a
u g o n j wa n a k u s h u g h u l i k i a
masuala yanayowahusu raia
waliokuwa wakiishi ndani ya
Dola ya Kiislamu, viliwasukuma
Waislamu kupiga hatua kubwa
katika utafiti wa tiba. Hiyo
ndiyo tofauti kati ya Uislamu na
Ubeberu. Uislamu unathamini
uhai wa binadamu kuliko kitu

kingine chochote.

TANGAZO
S.S.M.F

SHEIKH SHARIFF MIKIDADI MATONGO

Ni Yule aliyeanza kutangaza Dini ya Kiislamu toka akiwa mtoto


kabisa akitokea Mkoani Tabora. Baada ya safari zake za nchi
mbalimbali Afrika kwa mara nyingine tena atafanya mkutano
mkubwa JIJI DAR ES SALAAM.
Wapi: Katika viwanja vya Jangwani-DSM.
Siku: Jumamosi-15/11/2014 hadi 16/11/2014.
Muda: Saa 8:00-12:00-Jioni.
Sheikh Shariff, ataambatana na Wahadhiri mbalimbali akiwemo,
bingwa wa usomaji Qur an, Ust. Rajai Ayoub. Pia itafanyika DUA
kwa watu wenye matatizo mbalimbali.

Nyote mnakaribishwa kuwaidhika.

11

Makala ya Mtangazaji

AN-NUUR

MUHARRAM 1436, IJUMAA NOVEMBA 14-20, 2014

Hatua kuelekea kuundwa na Marekani kwa dola ya Kiislamu

Inatoka Uk. 9

za vita vya Urusi nchini Afghanistan.


Nchini Syria, kundi la Al Nusrah na
waasi wa ISIS ni askari wa miguu wa
mfungamano wa kijeshi wa nchi za
Magharibi, ambao unasimamia na
kudhibiti kusajili na kutoa mafunzo
kwa makundi ya wapiganaji. Kundi
linalotokana na Al Qaeda la Dola ya
Kiislamu ya Irak (ISI) lilitokea mwezi
Aprili 2013 likiwa na jina tofauti na
ufupisho mwingine, kwa kawaida
likiwa linaitwa Dola ya Kiislamu
ya Irak na Syria (ISIS). Kuundwa
kwa asasi ya kigaidi inayojitanua
ndani ya Irak na Syria kwa pamoja
ilikuwa sehemu ya ajenda za ujasusi
wa kijeshi wa Marekani. Ilikuwa
inaendana na mahitaji ya kimkakati
katika eneo hilo. Ilifuatana vile vile na
mwelekeo wa ushindi wa majeshi ya
serikali ya Syria dhidi ya uasi nchini
humo unaofadhiliwa na Marekani
na kushindwa kwa makundi ya Jeshi
Huru la Syria (FSA) na makundi
mengine "ya upinzani" ya kigaidi.
Uamuzi ulichukuliwa Marekani
kupeleka misaada yake (kisiri) kwa
kundi la kigaidi ambalo lingekuwa
kinafanya operesheni zake ndani
ya Syria na Irak na ambalo lina
miundombinu ya kivita katika nchi
zote mbili. Mradi wa Dola ya kiSunni wa Dola ya Kiislamu ya Irak na
Shamu inaendana na agenda ya muda
mrefu ya Marekani ya kuzigawa
Irak na Syria katika maeneo matatu
tofauti: dola ya Kiislamu ya ki-Sunni,
dola ya ki-Shia ya Kiarabu na Jamhuri
ya Kurdistan.
Wakati serikali kibaraka wa
Marekani nchini Irak inanunua
silaha za kisasa kutoka Marekani
ikiwa ni pamoja na ndege za kivita
za F-16 kutoka kampuni ya Lockheed

Martin, Dola ya Kiislamu ya Irak


na Shamu - ambayo inapigana na
majeshi ya serikali ya Irak - inaungwa
mkono kisiri na mashirika ya kijasusi
ya Magharibi. Lengo ni kuchochea
vita vya wenyewe kwa wenyewe
nchini Irak, ambako pande zote mbili
zinadhibitiwa kwa njia fulani na
Marekani-NATO.
Kinachotokea ni kuwapa silaha
na zana nyingine, pande zote mbili,
kuwapa fedha na mifumo ya kisasa
ya silaha halafu 'kuwaacha wapigane.'
Marekani-NATO inahusika katika
kusajili, kutoa mafunzo na kuwezesha
kifedha makundi ya wauaji wa ISIS
yanayoendesha operesheni zao ndani
ya Irak na Syria. ISIS inaendesha
shughuli zake kupitia njia za kificho
zenye uhusiano na mashirika ya

kijasusi ya nchi za Magharibi. Kwa


upande mwingine , unaodhihirishwa
na taarifa kuhusu uasi nchini Syria,
vikosi maalum vya nchi za Magharibi
na askari wa kukodiwa wanajiunga
ISIS.
Misaada ya Marekani-NATO
kwa ISIS inafanyika kisiri kupitia
washirika wakuu wa Marekani, Qatar
na Saudia. Kwa mujibu wa gazeti la
Daily Express la Uingereza, makundi
hayo yalikuwa na fedha na silaha
zilizotolewa na Qatar na Saudia.
"Kwa kupitia washirika kama
Saudia na Qatar, nchi za Magharibi
zimeunga mkono makundi ya waasi
ambayo baadaye yamegeuka kuwa
ISIS na makundi mengine yenye
uhusiano na Al Qaeda,: kwa mujibu
wa gazeti la Daily Telegraph la

Inatoka Uk. 9
makundi haya na yale ya Takfiri
kwa ujumla, ni ileile ya Kizayuni.
Kwa mujibu wa itikadi ya
Kizayuni, binadamu wateule
wa Mungu ni Mayahudi pekee.
Wengine ni ma-Goyim. Kama
wanyama tu mfano wa mbwa,
ngombe-ambao, Yahudi akiona
hana manufaa nao, ni haki yake
kuwauwa, kuchukua mali zao na
hata huko Akhera hawana fungu
kwa Mungu.
The best of the gentiles: kill
himHating your enemy {goyim} is
permitted, even commanded.
Hayo ni baadhi ya mafundisho
ya Uyahudi yaliyo katika kitabu
cha Talmud , ambayo yanahimiza
kumchukia na kumuuwa goyim.
(Tazama: Judaism Discovered:
A Study Of The Anti-Biblical
Religion Of Racism, Self-Worship,
Superstition And Deceit; Chapter
Talmudic Interpretation Of Scripture,
by Professor Michael A. Hoffman II,
Independent History and Research.)
Kama Uyahudi ulivyo, kwamba
watu waliosalimika ni Mayahudi
pekee, bali wengine ni ma-goyim,
ngombe tu, na hawa Salafi Takfiri

nao, huwaona Waislamu wasio


wao kuwa ni kama najisi ya
kusafishwa kwa kuuliwa.
The best of the gentiles: kill
himHating your enemy {goyim} is
permitted, even commanded.
Ya l i n g a n i s h e h a y a n a
wanayosema Salafi Jihad wetu.
Hata hivyo, wakati Uzayuni
u n a w a k u s a n y a Wa y a h u d i
wote, popote walipo duniani na
kuwafanya kundi moja dhidi ya
ma-goyim, Uzayuni ulioingizwa
katika Salafi umechakachuliwa au
kuboreshwa ili kutimiza malengo
ya Mazayuni. Katika Uzayuni wa
Kisalafi, Waislamu wanafanywa
kuwa maadui wao kwa wao wa
kushikiana panga, bunduki na
mizinga. Na katika muktadha
wa sasa hivi wa ISIS na vita dhidi
ya ugaidi, Usalafi Takfiri huu
unatumika kutekeleza mkakati
uliowekwa na Yahudi Oded Yinon
miaka ya mwanzo ya 1980s.
Mwandishi Stephen J. Sniegoski
ameandika makala akihoji ni
kwanini Israel imekaa kimya toka
ISIS ianze harakati zake za vita
na mauwaji Syria na Iraq. Katika
kujibu swali hilo baada ya kufanya

utafiti anasema:
What the Islamic State is causing
in the Middle East is perfectly attuned
with the view of the Israeli Right
as best articulated by Oded Yinon in
1982 which sought to have Israels
Middle East enemies fragmented and
fighting among themselves in order to
weaken the external threat to Israel.
Gazeti la Israel Ha'aretz tarehe
6/2/1982) liliarifu juu ya kile
kilichoitwa:. A Strategy for Israel
in the Nineteen Eighties.
Mkakati huo uliobuniwa na
Oded Yinon, unazungumzia
namna ya kuzidhoofisha nchi
za Kiarabu na kuibakisha Israel
ikiwa mtemi pekee mwenye
kutamba Mashariki ya Kati.
Gazeti hilo Ha'aretz, likasema
kuwa mkakati huo utajumuisha
kuzisambaratisha nchi za Syria na
Iraq katika vinchi vidogo vidogo
Shi'ite state, Sunni state
na nchi ya Wakurdi. Mkakati
nini? Kuwapiganisha Mashia na
Masuni na Masuni kwa Masuni
ili wauwane na kudhoofika.
Ndio kile anachosema Yahudi
Oded Yinon kuwa wapigane na
kuuwana wenyewe kwa wenyewe

WAPIGANAJI wa ISIS.

Uingereza, Juni 12, 2014.


Wakati vyombo vya habari vinakiri
kuwa serikali ya Waziri Mkuu Nuri
al-Maliki imezituhumu Saudia na
Qatar kwa kuiunga mkono ISIS,
inashindwa kusema kuwa nchi
hizo mbili zinafanya hivyo kwa
ushirikiano wa karibu na Marekani.
Chini ya bango la vita vya wenyewe
kwa wenyewe, vita ya chini kwa
chini ya kupambana na nchi hiyo
inaendeshwa ambayo inachangia
katika kuteketeza nchi hiyo, taasisi
zake, uchumi wake. Operesheni
hiyo ya siri ni sehemu ya agenda
ya kijasusi, mpango uliodhamiriwa
ambao nia yake ni kuifanya Irak iwe
ni nchi isiyo na mipaka halisi.
Wakati huo huo, maoni ya watu
ya n a e l e k e z wa k u a m i n i k u wa
kinachogomba hapa ni mfarakano
kati ya wa-Shia na wa-Sunni.
Ukaliaji kijeshi wa Marekani
nchini Irak umebadilishwa kuingia
katika njia zisizo rasmi za vita. Hali
halisi inafichwa. Kama kipingamizi
kinachouma, nchi inayohujumu
inaonyeshwa kuwa ndiyo inakuja
kuokoa jahazi la "nchi huru ya Irak."
Vita ya ndani ya "wenyewe kwa
wenyewe" kati ya wa-Shia na waSunni inachochewa na MarekaniNATO kwa kuunga mkono serikali
ya Al Maliki na pia waasi wa ki-Sunni
wa ISIS.
Kuvunjika kwa Irak kwa mpangilio
wa kidhehebu ni sera ya muda mrefu
ya Marekani na washirika wake.
"Kuunga mkono pande zote mbili"
Vita "Dhidi ya Ugaidi" kiini chake
ni kuunga makundi ya Al Qaeda kama
sehemu ya operesheni za kijasusi,
halafu kuja kuiokoa serikali ambazo
zinalengwa na uasi huo wa kigaidi.

Inaendelea Uk. 15

Ajabu kuwaita Masheikh ni 'mbwa wa Jahannamu'

(wakiamini kuwa wanapigana


Jihad kusimamisha Khilafah).
Si jambo la kudhani hivi
sasa, bali lililo na ushahidi wa
kutosha kuwa Abu Baghdad, ni
Yahudi Shimon Elliot na kwamba
kikosi chake ISIS na sasa Islamic
State, kimeundwa na Mayahudi
wakishirikiana na mabeberu wa
NATO kwa lengo la kutekeleza
ule mkakati wa Oded Yinon.
Japo hakuna ushahidi wa moja
kwa moja kuwa Shukri Mustafa
naye alikuwa Yahudi au alitumwa
kazi na Mazayuni, lakini sera na
mwelekeo wa al-Baghdadi ni ule
ule wa Shukri. Kinachojitokeza
hapa ni kuwa inavyoonekana
baada ya kuweka- A Strategy for
Israel in the Nineteen Eighties,
Mayahudi walifanya kazi kubwa
kuwaandaa akina Abu Baghdadi
na wapiganaji wengine kutoka
makundi ya Kisalafi na Waislamu
wengine. Na kazi kubwa ikawa
kuwaaminisha kuwa wanapigana
Jihad.
Laiti Israel na mabeberu
wangepanga kutekeleza
Inaendelea Uk. 15

12
UKIMYA HUU WA DOLA, MHH!
(SWADAKTA, MBUNGE WA KONDE!)

Bilhaki hukukenga, kongole nakupongeza,


Kwa kujitoa muhanga, dhulma kuiangaza,
Kwenye vya Bunge viunga, kwa ya sijini mayaza,
SWADAKTA hukukenga, KHATIB SAID HAJI.

Barua/Mashair

Kuhama Mtume (s.a.w.) ni somo na mazingatio

Mashekhe wetu wahanga, wanosota magereza,


Ni tumbi yanowasonga, pamwe na kuwatatiza,
Ashakum ulilonga, liwati kwa kudokeza,
SWADAKTA hukukenga, KHATIB SAID HAJI.
KWELI haukuitenga, kwa PUYA kuhanikiza,
Kama wasaka faranga, na vyeo kuendekeza,
Waridhiao vimbwanga, hata vya kuwamaliza,
SWADAKTA hukukenga, KHATIB SAID HAJI.
Na dubwasha la manyanga, nalo ukatudokeza,
Dhimaye kuu kuunga, mkono yanotukwaza,
Ndio mana 'watunyonga', kimya limejituliza !,
SWADAKTA hukukenga, KHATIB SAID HAJI.
KWELI tupu ulolonga, na kuntu uloeleza,
Mwenye dhamana mganga, ya janga kulimaliza,
Kinywa naye amefunga, lengole nini nawaza,
SWADAKTA hukukenga, KHATIB SAID HAJI.
Anyamaziaje janga, UTU lenye kuutweza,
Yu nani wa kuliganga, kucha kutwa ninawaza,
Bado kichwa chaniwanga, kwalo DOLA kunyamaza,
SWADAKTA nakuunga, MBUNGE kwa ulolonga,
ABUU NYAMKOMOGI-MWANZA.

BURIANI SHEKHE OTHMAN MJINGA


Abtadi kumsifu, Khaliku na Mfishaji,
Kwa wake uadilifu, wa hayati uumbaji,
Kadhalika na kwa ufu, uso na ubaguaji,
Allah mlaze peponi, Othman wa Mjinga.

Mauti hayaarifu, katika wake ujaji,


Pweke yunouarifu, ujiowe Muumbaji,
Baghtata hukhatafu, roho zetu waumbwaji,
Allah mlaze peponi, Othman wa Mjinga.
Sote kwa huo wasifu, kutufika twataraji,
Pasi kujali dhaifu, na mwenye nguvu kwa taji,
Tujiadidi kwa ufu, kwa wa Ilahi uchaji,
Allah mlaze peponi, Othman wa Mjinga.
Barzakhi tutatufu, baada ya ufishwaji,
Malaika watukufu, ndanimwe watatuhoji,
Faridi na si sufufu, kwa wa kwetu utendaji,
Allah mlaze peponi, Othman wa Mjinga.
Thuma sote tutakifu, kwa kupulizwa buruji,
Mahashari ashirafu, mbele ya Wahidi JAJI,
Kwa mizani mukawafu, tutalipwa afuwaji,
Allah mlaze peponi, Othman wa Mjinga.
Tushike ya uongofu, njia iso aawaji,
Ya Qur-an tukufu, na Sunna za muonyaji,
Kwa matendo matukufu, yaso na ubanangaji,
Allah mlaze peponi, Othman wa Mjinga.
Kaditama kualifu, wafiwa na wasomaji,
Si nudhumu ya mkufu, wala si ya wajiwaji,
Ya taazia ya ufu, na ya dua uombaji,
Muepushe na nirani, na mruzuku jinani.
ABUU NYAMKOMOGI-MWANZA.

AN-NUUR

MUHARRAM 1436, IJUMAA NOVEMBA 14-20, 2014

Na Sheikh Abdusalami
Mohamed Abdusalami
SHUKRANI zote anastahki
Mwenyezi Mungu, Mola
mlezi wa ulimwengu na
kwake tunaomba msaada na
rehema na amani zikutane
kwa Imamu wa Mitume
na Manabii Bwana wetu
Muhamad na jumaa zake na
sahaba zake na wale wenye
kumfuata kwa wema hadi
siku ya mwisho.
Ama baada ya utangulizi
h u u m f u p i . Pa m o j a n a
kuandama mwezi wa
mfungo nne, kwa kila mwaka
husimama watu wema na
wacha Mungu, ambao
huchukua mazingatio na
hufafanua maana na hutenga
masomo na huweka upya
h a r a k a t i k wa k u p a n d a
mbegu za matumaini na
kuhimiza kuzifanyia kazi
na huwaangazia njia na
huwapelekea kuyaendea yale
aliyoyaamrisha Mwenyezi
M u n g u k wa h a r a k a n a
huwarahisishia matatizo ya
dunia na ugumu wa maisha.
Kwa yakini uhamaji wa
Mtume toka Makka kwenda
Madina ndani yake kuna
masomo na mazingatio tele.
Wakati ambao ni uhai.
Na huenda somo la
kwanza tunalojifunza katika
kuhama ni kujua thamani ya
wakati, kwani wakati ndio
uhai na kuutumia katika
twaa ni njia ya kufaulu
kuliko kukubwa kutokana
na uhai uliopita, ikiwa kwa
utamu au uchungu au kwa
kheri au shari au kwa wema
au ubaya hatujui. Hayo
yatakuwa yanatutetea au
kutushitaki hivyo basi ni
wajibu tuwe kwa Mwenyezi
Mungu watu tulio na woga
kwake. Amesema Mwenyezi
Mungu, wale ambao
wanamuogopa Mola wao hali
ya kuwa hawamuoni na wao
juu ya kiama wanakiogopa.
Ambiyai (49).
Kwa hakika kwisha kwa
mwaka katika umri wetu
kunatusogeza kukutana
na Mwenyezi Mungu
hatua kwa hatua na wala
hatujui miaka mingapi
imebaki katika umri wetu.
Anasema Imamu Hassani alBiswiriyi Mungu amrehemu,
hakika ewe binadamu ni
masiku yaliyokusanyika,
itakapoondoka siku yako
basi imeondoka baadhi yako.
Ya m p a s a b i n a d a m u

atumie vizuri siku yake ya


leo kwa kumtii mwenyezi
Mungu Mtukufu, amesema
Mtume (s.a.w), yapatie
manufaa mambo matano
kabla ya mambo matano
Uhai wako kabla ya umauti
wako, afya yako kabla ya
ugonjwa wako, wakati wa
bure kabla ya kubanwa na
shughuli (bize) ujana wako
kabla ya uzee wako, utajiri
wako kabla ya umasikini
(kufilisika). ameipokea alHakim.
Thamani ya kujitolea kwa
ajili ya daawa ya Mwenyezi
Mungu Mtukufu.
Miongoni
mwa
masomo muhimu ambayo
ametufundisha Mtume
( s . a . w ) n i u t u k u f u wa
kujitolea, ambao husimama
kwa ajili ya kulingania.
Kuacha nyumba na mji
k wa a j i l i ya k u f i k i s h a
ujumbe na kutekeleza amri
ya Mwenyezi Mungu na
akautazama mji wake akiwa
anaondoka Mtume (s.a.w)
akausemesha kwa kauli
hii, Namuapia Mwenyezi
Mungu hakika mji wa Makka
ni ardhi ninayoipenda sana
na laiti kama kukosa kunitoa
watu wako nisingetoka.
Ameisahihisha al-Bani
walimfuatisha Maswahaba
juu ya njia hii ya kujitolea.
Hebu tumtazame huyu
Sayidina Ally (r.a), hakusita
kulala katika kitanda cha
Mtume (s.a.w) usiku wa
k u h a m a , a k a wa n i wa
mwanzo kujitolea katika
Uislamu. Na huyu ni
Bwana Suhaibu, mtu wa
Rum analinganisha kati
ya mali yake na kuhama
kwake kwenda Madina,
a k a wa a c h i a m a l i z a k e
washirikina na akahama
alipomuona Mtume (s.a.w)
akasema:- Amepata faida
baba Yahya kwa alichouza
na Mwenyezi Mungu
anasema, na miongoni
mwa watu wapo wanaouza
nafasi zao kwa kutaka radhi
za Mwenyezi Mungu na
Mwenyezi Mungu ni mpole
kwa watu (207) Al-Bakarat.
Miongoni mwa masomo na
faida kutoka katika Hijra.
Vyanzo vya tabia nzuri
ambavyo havigawanyiki
imethibitika katika Hijra
(kuhama), kwamba vyanzo na
tabia nzuri hazingawanyiki
na kushikamana, nazo ni
lazima kwa watu wenye
imani pamoja na matatizo
yote kwani Mtume (s.a.w)
alikuwa ni mwenye
pupa kwa kutekeleza
amana za watu kwa wale
waliomuamini, naye ndiye
aliyesema tekeleza amana
kwa aliyekuamini na wala
usimfanyie hiyana yule
anayekufanyia hiyana.
Ameipokea Abuu Daudi na
Tirmidhi.
Alimuacha Ally nyuma
yake pale Makka ili arudishe
amana za watu kwa wenyewe
na hili ni jambo la ajabu sana,
kwani wao walihalalisha
damu yake na wakataka
kumuua, pamoja na yote

hayo hawakuamini vitu


vyao vya thamani au visivyo
n a t h a m a n i i s i p o k u wa
wa k a we k e k wa M t u m e
(s.a.w) na wao wakamuita
mkweli muaminifu,
akahifadhi amana zao na
kuwarudishia zikiwa kamili
bila mapungufu, na hii ni
daraja la juu zaidi katika
kutekeleza amana.
A m e s e m a M we n ye z i
Mungu Mtukufu hakika
Mwenyezi Mungu
anakuamrisheni mtekeleze
amana kwa wenyewe na
mnapohukumu kati ya watu
muhukumu kwa usawa (58)
An-Nisaai.
Mshikamano wa jamii
na ushirikiano ni dalili ya
nguvu zake. Miongoni mwa
somo kubwa tunalopata
faida katika Hijra ni
mshikamano na umoja,
hawakuyumbayumba
katika msimamo kwa kitu
chochote na haya ndiyo
aliyoyazingatia Mtume
(s.a.w) pale alipofika Madina,
kwani aliwaunganisha kati
ya Muhajirina na Answari
na wala hawakuwanyima
Answaru juu ya kuwapa
Muhajirina kwa kitu
chochote hadi wakastahiki
k u s i f i wa n a M we n ye z i
Mungu katika mambo yao
kwa kauli yake Mwenyezi
Mungu Mtukufu, Na
wale waliofanya maskani
yaani Madina, imani zao
kabla yao wanawapenda
wale waliohamia kwao na
wala hawajali chochote
kwa kile walichokitoa na
wa n a wa t a n g u l i z a wa o
kuliko nafsi zao, hata kama
wana mahitaji nayo na
yeyote mwenye kujilinda na
ubahili wa nafsi zao hao ndio
waliofaulu.
Akawawapatanisha
M t u m e ( s . a . w ) k a t i ya
Au s i n a H a z a r a t i n a
kuyamaliza yale waliyo nayo
miongoni mwa ugomvi na
kuwaunganisha baina yao
na kuwaita (Answari), kisha
akafunga ahadi mbalimbali
na mataifa ya Kiyahudi
ambao walikuwa wakiishi
karibu na Waislamu katika
mji wa Madina na kwa hivyo
basi, ikawa jamii ya Madina
imeungana kwa mataifa
yote. Kwa hakika masomo
na mazingatio kutoka katika
Hijra (kuhama) kwa Mtume
(s.a.w) ni mapana katika
nyanja nyingi kwa hapa
hapatoshi, kwani ilikuwa
ni nusra na ukombozi kwa
Uislamu na Waislamu.
A m e s e m a M we n ye z i
Mungu Mtukufu, ikiwa
hamkumnusuru yeye
ameshanusuriwa na
Mwenyezi Mungu, pale
alipomtoa kwa wale ambao
waliokufuru, wakiwa wawili
katika pango pale aliposema
kumwambia mwenziwe,
usihuzunike hakika
mwenyezi Mungu yupo
pamoja na sisi (40) Tauba.

13

MAKALA

AN-NUUR

MUHARRAM 1436, IJUMAA NOVEMBA 14-20, 2014

QUDS- Kibla cha kwanza cha Waislamu kilichosahauliwa -1


Na Salum Bendera

MJI wa Baytul
Muqqadas ni moja
kati ya miji muhimu
ya kihistoria duniani
hususan katika
ulimwengu wa
Kiislamu kutokana
na kuwa kwake na
utambulisho wa kidini.
Baadhi ya nukuu za
historia zinaonesha
kwamba, mji huu
uliasisiwa zaidi
ya m i a k a e l f u n n e
iliyopita.
Mitume na Manabii
wengi wa Mwenyezi
Mungu walizaliwa au
kuishi katika mji huo
mtukufu. Ni kwa sababu
hii ndio maana mji
huu ukazingatiwa na
kuwavutia wafuasi wa
dini tatu za mbinguni
yaani Uyahudi, Ukristo
na Uislamu.
Wakati Nabii Ibrahim
AS alipohajiri kutoka
Misri hadi Palestina,
aliishi katika Mji wa
Quds. Kwa amri ya
Mwenyezi Mungu,
Nabii Ibrahim AS
aliujenga upya mji huo
na kukarabati eneo lake
takatifu yaani Msikiti

wa al Aqswa ili wafuasi


wa Tauhidi waweze
kumuabudu Mwenyezi
Mungu hapo.
Mji wa Quds pia ni
mtakatifu kutokana na
kuwa Nabii Mussa AS
aliona nuru ya Mwenyezi
Mungu na kuzungumza
Naye akiwa hapo.
Katika zama zake,
Nabii Mussa AS aliamua
kuihamisha kaumu ya
Bani Israel kutoka Misri
hadi Palestina kutokana
dhulma na ukandamizaji
wa Firauni, lakini kwa
sababu ya kaumu hii
kukataa kutii amri,
Mwenyezi Mungu
aliwaacha watapetape
jangwani kwa muda
wa miaka 40 na
hakuwaruhusu kuingia
Pal e s ti na . H ali h ii
iliendelea hadi mwisho
wa u m r i wa N a b i i
Mussa AS. Inaaminika
kuwa Nabii Mussa AS
alizikwa karibu na mji
wa Quds. Baadhi ya
Mitume wa Mwenyezi
Mungu ambao majina
yao yako katika Qurani
Tukufu, wamezikwa
katika ardhi ya Palestina.
Mitume hao ni pamoja
na Nabii Ibrahim AS,

Msaada

Ustadhat Mwasiti (kulia) akiwa na wanafunzi


Masjid Kadiria Mwasiti uliopo kijiji cha Kibuta wilayani
Kisarawe mkoani Pwani wanaomba msaada wa kuchimbiwa
kisima katika Msikiti huo.
Gharama za uchimbaji wa kisima hicho ni shilingi milioni
tano mpaka sasa zimepatikana milioni moja hivyo basi bado
milioni nne (4).
Shime Waislamu kutoa ni moyo, unaombwa kuchangia
chochote ulichojaaliwa na Muumba wako kwa ajili ya
kuweka akiba ya Akhera yako.
Unaweza kuchangia kupitia Akaunti ya benki na namba
za simu kwa tigo pesa:
0656 092 436 au A/c No 001340085740001 Amana Bank
Wabillah Tawfiq

Nabii Yusuf AS, Nabii


Yaaqub AS, Nabii Ishaq
AS, Nabii Daud AS,
Nabii Sulaiman AS na
Nabii Zakaria AS.
Baada ya Nabii Daud
AS kupewa Utume na
Mwenyezi Mungu,
aliamua kuupanua mji
wa Quds na kulijenga
upya eneo la ibada la mji
huo ambalo kwa mujibu
wa riwaya za kihistoria
lilikuwa limeharibiwa
na kukarabatiwa mara
kadhaa.
Kati ya matukio
mengine yaliyojiri
katika ardhi za Palestina
na hivyo kuongeza
umuhimu na utukufu
wake miongoni mwa
wafuasi wa dini za
Tauhidi ni kuzaliwa
hapo Nabii Issa AS.
Nabii Issa AS alikuwa
mbeba bendera ya
amani, utakasifu na
ucha Mungu. Nabii Issa
AS alizaliwa katika kijiji
cha Baitul Lahm karibu
na mji wa Quds. Nabii
Issa AS alianza kuhubiri
katika mji wa huo wa
Baitul Muqaddas na
hapo ndipo alipopaa na
kuelekea mbinguni. Na
mwisho kabisa Masjidul
Aqswa katika mji wa
Quds ndiyo sehemu
a m b a y o M t u m e wa
Mwisho Muhammad
al Mustafa SAW alipaa
kuelekea katika mbingu
katika tukio maarufu la
Miiraj.
Palestina na Mji wa
Baitul Muqaddas ni
muhimu kwa Waislamu
kutokana na kuwepo
maeneo matakatifu
hapo. Mwenyezi Mungu
SWT katika kitabu
Chake cha mwisho yaani
Qur'ani, ameutaja mji
huo kuwa ardhi yenye
Baraka na takatifu.
Masjid al-Aqswa
ni eneo la tatu kwa
utukufu miongoni mwa
Waislamu baada ya
Masjidul Haram huko
Makka na Masjidun
Nabii huko Madina.
Masjid al-Aqswa
ndicho kibla cha kwanza
cha Waislamu. Kwa
miaka kadhaa Waislamu
walisali kuelekea Masjid
al-Aqswa. Katika
mwaka wa pili wa Hijria,

Mwenyezi Mungu alitoa


amri kwa Waislamu
kubadilisha kibla chao
kutoka Masjid al-Aqswa
mjini Quds na kuelekea
Masjid al-Haram katika
mji wa Makka. Aya za 142
hadi 150 katika Suratul
Baqara zimezungumza
kuhusu tukio hili. Katika
sehemu moja ya aya ya
150 Mwenyezi Mungu
anamkhutubu Mtume
SAW na Waumini kwa
kusema: "Na popote
wendako elekeza uso
wako kwenye Msikiti
Mtakatifu. Na popote
mlipo elekezeni nyuso
zenu upande huo..."
Umuhimu wa pili
wa Masjid al-Aqswa
miongoni mwa
Waislamu unatokana
na kuwa Mtume
M u h a m m a d S AW
alipaa kutoka hapo na
kuelekea mbinguni
katika tukio la Miiraji.
M i i r a j i ya M t u m e
SAW ilianzia Masjid alHaram mjini Makkah
hadi Masjid al-Aqswa.
Katika safari hiyo mji wa
Quds ulipewa umuhimu
maalumu na Mwenyezi
Mungu la sivyo Miiraji
ya Mtume wa Uislamu
SAW ingeanzia huko
huko Makka na kwenda
moja kwa moja mbinguni
bila ya kupitia Baytul
Muqaddas uliko msikiti
wa al-Aqswa.
K u a n z a s a f a r i ya
kimiujiza ya Mtume wa
Mwisho SAW kutoka
Masjid al-Haram hadi
Masjid al-Aqswa ni suala
linalobainisha wazi
uhakika usiopingika
kuwa misikiti hii miwili
iko pamoja katika
utakatifu.
Aya ya kwanza ya
Suratul Israa ya Qur'ani
Tukufu imeashiria safari
hii ya kimiujiza kama
ifuatavyo:
S U B H A N A ,
A m e t a k a s i k a
aliyemchukua mja Wake
usiku mmoja kutoka
Msikiti Mtukufu mpaka
Msikiti wa Mbali,
ambao tumevibariki
vilivyouzunguka, ili
tumuonyeshe baadhi ya
Ishara Zetu. Hakika Yeye
( M we nyez i M u ngu )
ni Mwenye kusikia na

Mwenye kuona.
Mmoja wa wafasiri
wa Q u r ' a n i k a t i k a
kubainisha namna
Msikiti wa al-Aqswa
na maeneo ya pembeni
mwake yalivyojaa
baraka anaandika: "Ibara
ya 'baarakna haulahu'
yaani tumevibariki
vilivyouzunguka ina
maana kwamba, mbali
na kuwa Masjidul
Aqsa uko katika eneo
takatifu, maeneo ya
pambizoni mwake nayo
ni yenye baraka. Hii
ni kwa sababu eneo la
pambizoni mwa Baitul
Muqaddas n i la kijani
kibichi na lenye rutuba
likiwa limejaa miti iliyo
na matunda mengi na maji
yanayotiririka na hivyo
kuzidisha umaridadi wa
eneo hilo. Aidha aya hiyo
yumkini imeashiria baraka
za kimaanawi za eneo
hilo. Hii ni kwa sababu
katika historia yake, ardhi
ya Quds imekuwa kituo
cha Mitume wakubwa
wa Mwenyezi Mungu na
kitovu cha Tawhidi na
ucha Mungu."
Sayyed Qutb, mfasiri
wa Qur'ani kutoka Misri
anaandika hivi: Israa na
Miiraj inaziunganisha dini
zote za Tawhidi kutoka
zama za Manbii Ibrahim na
Ismail AS hadi Mtume wa
Mwisho SAW. Inaonekana
kuwa Mtume Muhammad
SAW katika safari yake
ya usiku alitangaza
kwamba ujumbe wake
unajumuisha risala za
Mitume waliotangulia na
utaendeleza risala hizo.
Katika historia ya
Uislamu tunasoma kuwa
Mtume SAW katika tukio
la Miiraj aliswali katika
maeneo mbalimbali kama
vile Mlima Sinai sehemu
ambayo Mwenyezi Mungu
alizungumza na Nabii
Musa AS na vile vile Baitul
Lahm sehemu aliyozaliwa

Nabii Issa AS. Baada


ya hapo aliingia katika
M a s j i d u l A q s wa n a
baada ya kusali katika
mihrabu ya Mitume
watukufu, alipaa na
kuelekea mbinguni. Hii
ndio sababu Masjidul
Aqsa ukawa msikiti
wenye umuhimu
m k u b wa s a n a k wa
Waislamu wote.

14

Na Rashid Abdallah,
MUM
MSHUKURU Mungu
sana ikiwa wewe
unapata sehemu nzuri
ya kulala hadi asubuhi
bila ya kubughudhiwa
na mtu yeyote. Ndani
ya u m a s i k i n i wa k o ,
lakini unatafuta riziki
kwa amani hadi jioni
unaporudi nyumbani
japo unakumbana na hali
ngumu katika utafutaji
wa k o wa r i z i k i k wa
kutegemeana na kazi
unayoifanya.
Ni la kushukuru mno
kama unatoka nyumbani
kwako hadi sokoni na
unakutana na watu
unaowajua na usio wajua,
kisha munasalimiana kwa
furaha. Hadi unarudi
na kapu lako nyumbani
h u j a s i k i a b o m u wa l a
kuvamiwa kwa marungu
na kupigwa pengine kwa
sababu ya kofia yako.
Usiombe ukawa myonge
kisha kukawepo mbabe
asiye na huruma ukawa
chini yake, umeumia na
utatamani dunia igeuke
ili Kusini kuwe Kaskazini
na Kaskazini-Kusini upate
kukimbia. Mshukuru
Mungu ukiwa bado upo
kwenye amani japo ndogo
inayokuwezesha kufanya
shughuli zako za kila siku.
Shirika la habari la
The Associated Press
Jumamosi ya October 25,
mwaka huu, linasema
kuwa idadi ya Waislamu
wa j am i i ya Roh in g y
wanaokimbia Mnyanmar
imefikia 100,000 tangu
mwaka 2012.
Usidhani kuwa
wanakimbia kwa
kuwa wamependa
kuondoka katika ardhi
hiyo. Hawaondoki na
kukimbia kwa makundi
makubwa makubwa
kwa sababu wanafurahia
kuhama huko. Lakini
kuna Mabudha wababe
walio juu ya Rohingy
wachache na wanyonge

Makala/Tangazo

AN-NUUR

MUHARRAM 1436, IJUMAA NOVEMBA 14-20, 2014

Rohingy jamii ndogo


inayoteseka Myanmar

ndio wanaosababisha
Waislamu hao kuyahama
makaazi yao.
Miaka miwili tangu
Mabudha waanze ukatili
dhidi ya jamii hiyo ndogo
ya watu, kumekuwepo na
vitendo vya kila siku vya
mauaji, ubaguzi, uharibifu
na ubabe usio na mipaka
dhidi ya Rohingy.
Mnyanmar nchi yenye
M a b u d h a wa n a o f i k i a
milioni 50 na Jamii ya
Rohingy milioni 1.3.
Kutokana na mashambulizi
ya Mabudha dhidi
ya Rohingy, mamia ya
watu kutoka jamii hiyo
wameuwawa na wengine
140,000 kuishi katika kambi
za wakimbizi, ambako
wanaishi bila ya kupata
huduma za kutosha za
afya, elimu n.k.
Serikali ya nchi hiyo
inawataja Rohingy kuwa
ni wahamiaji haramu
kutoka Bangladesh,
wakati mwengine Serekali
huchukua sababu hiyo
kuwakamata na kuwapiga.
Hii ndio ile ile kanuni
ya kumpa mbwa jina baya
ili ukimuua usionekane
ni mkosa. Siamini kuwa
wao ni wahamiaji haramu
kwani wapo muda mrefu
sana na hadi kufikia
milioni 1.3 inatoa tafsiri
kuwa wameishi hapo
muda mrefu sana. Hata
mtu kuwa mhamiaji
haramu bado haitoi haki
ya kumuua na kmharibia
makaazi yake.
Nadhani dini ndio
inabeba sehemu kubwa ya
dhulma wanazofanyiwa.
Uislamu wao ndio chachu
na chanzo cha wao kuuliwa,
kupigwa na kuharibiwa
mali zao yakiwemo
maduka na nyumba. Na
serekali ya nchi hiyo na
wanasiasa wasiojua utu na
ubinaadamu, hushirikiana
na makundi ya Mabudha
ili kutekeleza unyama
wao.
Wiki tatu zilizopita
serekali ya Mnyanmar
imeanzisha mpango uliouwita Rakhine Action
Pl a n . L e n g o l a k e n i
kuwalazimisha Rohingy
kuondoka nchini humo.
N i z a i d i ya R o h i n g y
milioni moja watafukuzwa
nchini humo kutokana
na mpango huo mpya
unaosimamiwa na serekali
ya Minyanmar.

Ta a r i f a z i n a s e m a
kuwa Waislamu hao wa
Myanmar pia wanaweza
kufungwa jela kwa
muda usiojulikana kwa
mujibu wa mpango huo
wa k i b a g u z i , a m b a o
u n a wa t a k a wa k u b a l i
kupangwa tena kimakabila
na kuandikishwa kuwa ni
Wabengali au kufungwa
jela.
Japo makundi ya
kutetea haki za binadamu
yameitaka jamii ya
kimataifa iishinikize
s e r i k a l i ya M ya n m a r
kufuta mpango huo na
k u u t a j a k u wa h a u n a
maana yoyote zaidi ya
kuthibitisha kuendelea
ubaguzi. Lakini hakuna
jamii ambayo imechukua
hatua yoyote.
Katibu Mkuu wa UN
amekuwa mwepesi wa
kuzungumza lakini ni
mvivu wa kutenda kwa
ajili ya kutatua matatizo.
Ni miaka 66 sasa Rohingy
wako katika dhulma lakini
hadi hi leo tatizo hilo
halijapatiwa tiba.
Ta n g u m wa k a 1 9 4 8
ambapo nchi hiyo ndipo
ilipopata uhuru, basi
Waislamu wa jamii ya
Rohingy wameendela
kuuwawa, kudhalilishwa,
kupigwa na kuharibiwa
mali zao na mabudha
wenye misimamo mikali
wakishirikiana na serekali
yao ambayo inawaunga
mkono Mabudha hao dhidi
ya unyama wanaoufanya
k w a Wa i s l a m u w a
Rohingy.
Hakuna jamii ya
Kimataifa itakayo
wasaidia, wao kazi yao
kubwa ni kuvamia nchi
za wengine na kuuwa
tu. Unadhani kubwa la
maadui Marekani anaweza
kuwasaidia Rohingy hasa
akijua kuwa ni Waislamu.
Yapo mataifa ya Kiarabu
ambayo yangekuwa ni
msaada mkubwa kwa
matatizo ya Waislamu
lakini mataifa wenyewe ni
mahatuti.
Kupitia mtandao wa
Redio Swahili Tehran
unaeleza kuwa, Gazeti
la Miyanmar Times
limeripoti kuwa, misaada
ya kibinadamu hasa ya
kitiba ilizuiwa kuwafikia
Wa i s l a m u m k o a n i
Rakhine huko Myanmar
baada ya Mabudha

wenye misimamo mikali


kushambulia taasisi za
misaada ya kibinadamu
mkoani humo. Idadi
k u b wa ya Wa i s l a m u
waliukimbia mkoa huo
kutokana na ukatili na
u n ya n ya s a j i m k u b wa
wa Mabudha wenye
misimamo ya kufurutu
ada.
Mabudha wenye
misimamo mikali
wamekuwa wakatili
mno, wanataka Rohingy
wafe njaa. Wanazuia na
kushambulia misaada
ambayo huenda
ikawasaidia kwa kiasi
kikubwa. Mtu kapewa
nguvu kuzitumia vizuri
anashindwa, jee Mungu
angekukosesha si
ungelalamika kakuonea.
Ndio binaadamu!
Ukiwa unapata wakati
wa kupumzika bila ya kero

yoyote mbali ya kelele za


watoto wako nyumbani,
basi unapaswa kuinua
mikono kumshukuru
Mungu na kuwaombea
wale ambao bado wako
katika dhiki na matatizo ya
usiku na mchana. Ukipata
wakati wa kuyafikiria ama
kuyaona baadhi ya maisha
wanayoishi binaadamu
basi ndipo utakapo
gundua kuwa kuna watu
wako katika dhiki tangu
kuzaliwa kwao hadi sasa.
Hawana uhakika wa
kukaa na kuzungumza
kisha kikao chao kikamaliza
kwa amani bila ya kusikia
mripuko wowote, ukiwa
u m e r i p u k o a c h i n i ya
miguu yao ama pembeni
yao kama si mtaa wa pili
kutoka walipo. Hayo
ndio maisha ya baadhi
yetu, yanasikitisha kupita
kiwango.

TANGAZO LA MUHADHARA WA MWEZI WA


MUHARRAM MWAKA 1436/2014 - 2015
MSIKITINI ANSWAR SUNNA KINONDONI

Uongozi wa Msikiti wa Answar Sunna


Kinondoni ulio chini ya taasisi ya Jamaat
Ansawr Sunna una yo furaha kuwatangazia
Waislamu kuwa ndugu zao wa Miskiti wa
Answari Sunna Kinondoni wameazimia kuwa
pawepo na muhadhara japo mmoja kila mwezi
katika msikiti wao. Lengo kuu ni kuwafikishia
Waislamu mafundisho ya dini yao kwa
mnasaba wa wakati na mazingira na kuwatia
hima katika kuyatekeleza mafundisho hayo.
Kwa mnasaba huo basi mnaarifiwa kuwa
mada ya mwezi huuwa Muharram Kwanini
maswahaba wa Mtume waliteua kuwa Hijra
ya Mtume iwe ndiyo msingi wa Kalenda ya
Kiislamu Na muwasilishaji wa mada hiyo
ni Sheikh Twaha Sulayman Bane, Muhadhir
katika chuo cha Al_Haramayn na kiongozi
katika Hayaa al Ulamaa ya Tanzania.
Muhadhara huo utakuwa tarehe 16 Novemba
2014 siku ya jumapili kuanzia saa 10:30 Alasiri.
Mnaombwa kufika kwa wakati
Wa billahi Tawfiq
Abdallah Salim
Imam Mkuu
Masjid Answar Sunna Kinondoni

15

HABARI

AN-NUUR

MUHARRAM 1436, IJUMAA NOVEMBA 14-20, 2014

Hatua kuelekea kuundwa na Marekani kwa dola ya Kiislamu

Inatoka Uk. 11

Shughuli hiyo inafanywa chini ya


bango la kupambana na ugaidi.
Inatoa kisingizio cha kuingilia kati.
ISIS ni mradi wa dola ya Kiislamu
ya kuunda utawala wa Kiislamu wa
ki-Sunni. Siyo mradi wa watu wa
dhehebu la Sunni nchini Irak ambao
kwa jumla wanapendelea mifumo
huria ya serikali. Mradi wa kuundwa
kwa dola ya Kiislamu ni sehemu ya
agenda ya kijasusi ya Marekani.
Ili kujibu mwendo kasi wa waasi
wa ISIS, Marekani inatazamia
kutumia upigaji mabomu kutoka
angani pamoja na mashambulio ya
ndege zisizo na rubani kuisaidia
serikali ya Irak kama sehemu ya
operesheni ya kupambana na ugaidi.
Yote hii ni kwa mkakati wenye nia
njema: kupambana na magaidi, bila
kukiri hata hivyo kuwa magaidi hawa
ni 'askari wa miguu' wa ushirika wa
kijeshi wa nchi za Magharibi. Bila
kuhitaji kuainisha, matukio haya
yanachangia siyo tu kuivuruga Irak,
lakini hata kudhoofisha harakati
za wanaopambana na serikali ya
Irak, ambayo ni moja ya malengo ya
Marekani-NATO.
Dola ya Kiislamu inaungwa mkono
kwa siri na CIA ikishirikiana na
Saudia, Qatar na vyombo vya kijasusi
vya Uturuki. Israel pia inahusika
katika kupeleka misaada kwa
makundi ya Al Qaeda nchini Syria
(kutokea milima ya Golan) pamoja na
vikundi vya kujitenga vya wa-Kurdi
nchini Syria na Irak. Kwa upana zaidi,
"Vita ya Kimataifa dhidi ya Ugaidi"
inaundwa na mantiki endelevu na
ya kiharamia: pande zote mbili, yaani
magaidi na serikali - wanaungwa
mkono na wahusika wale wale wa
kijeshi na kijasusi, yaani MarekaniNATO.
Wakati mpangilio huu unaelezea
hali ilivyo hivi sasa nchini Irak, mfumo
wa 'kusaidia pande zote mbili' kwa
dhamira ya kuchochea mifarakani ya
kidhehebu umetekelezwa mara nyingi
katika nchi tofauti. Uasi unaoendana
na Al Qaeda (na kuungwa mkono
na mashirika ya kijasusi ya nchi za
Magharibi) umeshika usukani katika
nchi kadhaa ikiwamo Yemen, Libya,
Nigeria, Somalia, Mali, Jamhuri
ya Afrika ya Kati, Pakistan. Lengo
kimalizio ni kuhujumu nchi huru na
kuzifanya ziwe za wazi (kwa ajili ya
wanaoitwa wawekezaji kutoka nje).

Kisingizio cha kuingilia ili kutoa


misaada ya kibinadamu (kwa mfano
nchini Mali, Nigeria au Jamhuri
ya Afrika ya Kati) kinategemea
kuwepo kwa makundi ya kigaidi
ya wapiganaji. Hata hivyo makundi
hayo yasingekuwepo bila misaada ya
siri ya Marekani-NATO.
Hitimisho
Hapakuwa na waasi wa Al Qaeda
kabla ya uvamizi wa Irak mwaka
2003. Isitoshe, Al Qaeda haikuwepo
nchini Syria kabla ya kuanza kwa uasi
unaosaidiwa na Marekani-NATOIsrael mwezi Machi 2011. ISIS siyo
asasi huru. Ni kitu kilichoundwa na
mashirika ya kijasusi ya Marekani. Ni
kifaa cha kijasusi, cha kufanyia vita
ambayo siyo ile ya kawaida.
Lengo kamili la mgogoro huu
u n a o e n d e l e a u l i o a n d a l i wa n a
Marekani-NATO kupinga majeshi
ya serikali ya Al Maliki kwa uasi wa
ISIS, ni kuteketeza na kuiyumbisha
Irak kama taifa halisi. Ni sehemu
ya operesheni ya kijasusi, mkakati
wa kubadilisha nchi kuwa maeneo/
Kuvunjika kwa Irak kwa misingi ya
kidhehebu ni sera ya muda mrefu ya
Marekani na washirika wake.
ISIS ni mradi wa kuunda dola ya
Kiislamu ya ki-Sunni. Siyo mpango
wa watu wa dhehebu la Sunni nchini
Irak ambao kihistoria wamekuwa
wakiunga mkono mfumo huria wa
serikali. Mradi wa dola ya Kiislamu
umeandaliwa na Marekani. Kusonga
mbele kwa majeshi ya ISIS kuna nia
ya kuwezesha kuungwa mkono na
sehemu kubwa ya wa-Sunni dhidi ya
serikali ya Al Maliki.
Kuwa kuiunga mkono kisirisiri
Dola ya Kiislamu ya Irak na Shamu,
Marekani inasimamia kuanguka
kwa utawala wa vibaraka wake
nchini Irak. Suala hapa siyo 'kubadili
serikali' au hata kumbadilisha tu
Waziri Mkuu Nuri al-Maliki.
Kugawanywa kwa Irak katika
maeneo ya kidhehebu ni lengo ambalo
limekuwa likifanyiwa kazi na jeshi la
Marekani kwa zaidi ya miaka 10.
Kinachotazamiwa na Marekani
ni kuvunjiliwa mbali kabisa kwa
utawala wa Irak na taasisi za serikali
kuu, kufikia mchakato wa kuigawa
na kuifuta Irak kama nchi. Mchakato
wa kuigawa Irak kimadhehebu
kutakuwa bila shaka na athari
kwa Syria. ambako kwa sehemu
kubwa magaidi wanaofadhiliwa na
Marekani-NATO wameshashindwa.

Inatoka Uk. 11
mkakati huu kwa kuzivamia
Syria na Iraq, pangekuwa na
ugumu kwa sababu kwanza
hiyo ingewaunganisha
Wa i s l a m u n a Wa a r a b u
k u wa l a n i n a k u p a m b a n a
nao hata kwa kuzomea tu.
Kwa hiyo wangeshindwa
japo katika uwanja wa habari
na propaganda. Lakini pia
ingekuwa vigumu kuungwa
mkono na inayoitwa Jumuiya ya

kimataifa. Lakini kwa kuwapata


akina Abu Baghdadi na Abu
Dawood, kazi inafanyika
bila ya Israel wala Marekani
kulaumiwa. Ni Waislamu
wanauwana wenyewe kwa
wenyewe kufanikisha mpango
wa Mazayuni na mabeberu.
Lakini tujue pia kuwa hawa
Takfiri wanapotumwa huku,
lengo ni lile lile. Kuchochea
machafuko na kumalizana
wenyewe kwa wenyewe na
kutoa fursa kwa mabeberu kuja

Kuyumbishwa na kugawanyika
kisiasa kwa Syria kunatazamiwa vile
vile: Nia halisi ya Marekani siyo tena
lengo finyu la "kubadili utawala"
nchini Syria. Kinachodhamiriwa ni
kuvunjwa kwa Irak na Syria kwa
misingi ya kidhehebu na kikabila.
Kuundwa kwa dola ya Kiislamu
inaweza kuwa hatua ya kwanza
kuelekea katika mgogoro mkubwa
zaidi eneo la Mashariki ya Kati,
ukichukulia kuwa Iran inaiunga
mkono serikali ya Al-Maliki, hivyo
nia ya Marekani inaweza pia kuwa
ni kutaka Iran iingilie. Kugawanyika
kunakopendekezwa kwa Irak na Iran
kunachukua mfano wa iliyokuwa
Yugoslavia ambayo iligawanywa
kuwa 'nchi huru saba' (Serbia, Croatia.
Bosnia-Herzegovina. Macedonia,
Slovenia, Montenegro, Kosovo).
Kwa mujibnu wa Mahdi Darius
Nazemroaya, kugawanywa kwa Irak
kuwa nchi tatu tofauti ni sehemu ya
mchakato mpana zaidi wa kuandika
upya ramani ya Mashariki ya Kati.
I p o r a m a n i i l i y o t a ya r i s h wa
na Luteni-Kanali Ralph Peters.
Ilichapishwa katika Jarida la Jeshi la

Marekani mwezi Juni 2006. Peters


ni kanali mstaafu na mhadhiri wa
Chuo cha Taifa cha Vita nchini
Marekani. Licha ya kuwa ramani

kutukalia. Kama alivyosema


Alex Jones katika uchambuzi
wake Obama's CIA Runs Boko
Haram, kwamba mab eberu

Joseph Mfanyakazi, Arusha.


Harakaharaka tuliambiwa kuwa
FBI wanakuja kutusaidia kufanya
uchunguzi. Kule Kenya ilipodaiwa
kuwa al Shabab wameingia
Nakumati, haraka haraka
tuliambiwa kuwa makachero
wa Mossad na wale wa kutoka
Uingereza walikuwa wa mwanzo
kufika.
Tu k i ya t i z a m a y o t e h a ya ,
tuna kila sababu ya kuchukua
tahadhari, la sivyo mguu utaota
tende na majuto ni mjukuu.

hiyo haionyeshi maoni rasmi ya


makao makuu ya Jeshi la Marekani,
imekuwa ikitumika katika programu
za mafunzo katika Chuo cha Ulinzi
cha NATO kwa maofisa wa ngazi za
juu. (Angalia 'Mpango wa Kuweka
Upya Mipaka Mashariki ya Kati:'
Mradi wa Mashariki ya Kati Mpya wa
Mahdi Darius Nazremroaya, Global
Research, Novemba 2006).
(Makala hii imefasiriwa kwa
Kiswahili na Anil Kija kutoka
makala The Engineered Destruction
and Political Fragmentation of
Iraq. Towards the Creation of a
US Sponsored Islamist Caliphate:
*The Islamic State of Iraq and alSham: An instrument of the Western
Military Alliance iliyoandikwa na
Prof Michel Chossudovsky (Global
Research, August 27, 2014))

Ajabu kuwaita Masheikh ni 'mbwa wa Jahannamu'


wa n a p a n d i k i z a k i t i s h o c h a
ugaidi, kisha wanakuja kama
wasamaria wema wanakuambia
wanakuletea makachero na
wanajeshi kupambana na magaidi
wanaokusumbua.
Bila shaka tunakumbuka
lilivyotokea tukio la kuuliwa
Padiri Zanzibar na lile shambulio
la bomu katika kanisa la Mtakatifu

AN-NUUR

16
16

16

MAKALA

MUHARRAM 1436, IJUMAA NOVEMBA 14-20, 2014

AN-NUUR

Soma
gazeti la
AN-NUUR kila Ijumaa

MUHARRAM 1436, IJUMAA NOVEMBA 14-20, 2014

Istiqaama wapongezwa kujenga shule ya kimataifa


Na Seif Msengakamba

MAKAMU wa Rais Dk.


Mohammed Gharib Bilal,
amesema amefarijika
kusikia kuwa Jumuiya
ya Kiislamu ya Istiqaama
Tanzania, tawi la Dar es
Salaam ina mpango wa
kujenga shule ya Kimataifa
huko Kigamboni.
Dk. Bilal, alionyesha
faraja yake hiyo katika hafla
ya kuupokea mwaka mpya
wa Kiislamu 1436 Hijriya,
iliyofanyika mwishoni mwa
wiki iliyopita katika ukumbi
wa Karimjee jijini Dar es
Salaam, ambako alikuwa
mgeni rasmi.
Alisema
kuwa
amefurahishwa na namna
Jumuiya hiyo ilivyofanikiwa
kutimiza malengo yake kwa
kutekeleza kwa vitendo
ujumbe wao wa mwaka
jana 1435 Hijriya, ambapo
u l i we k wa m k a k a t i wa
kujipanga, kuhamasisha na
kuboresha elimu nchini.
Mwaka jana katika hafla
kama hii iliyotukusanya hapa,
mliwasilisha ujumbe jinsi
Jumuiya yenu ilivyojipanga
kuboresha elimu nchini,
leo mmedhihirisha yale
yaliyokuwa katika ujumbe
wenu, nimefarijika sana kwa
namna mlivyotekeleza na
kusimamia mkakati mzima
wa elimu, alisema Dk. Bilal.
Aliongeza kuwa anaamini
v i j a n a wa n a o a n d a l i wa
sasa watapatiwa elimu
bora na sahihi na wale
waliochukuliwa kwa ajili
ya kuwasaidia kuwalipia
gharama na mahitaji
mbalimbali kielimu,
watakuja kuwa vijana bora
katika jamii.
Dk. Bilal alitoa wito
kwa Waislam kwa kila
aliyejaaliwa, kutoa
mchango wake bila kusita ili
kuhakikisha jambo hilo jema
linafanikiwa kwa wakati
uliopangwa.
Aidha aliwakumbusha
wana Istiqama kuhusu
k a u l i m b i u ya m wa k a
h u u wa 1 4 3 6 H i j r i y ya ,
ambayo ni UISLAMU
NA MAZINGIRA, kuwa
waitekeleze kwa vitendo
ujumbe huo muhimu kama
walivyofanya katika ujumbe

wao wa mwaka jana.


Hafla ya kuupokea
mwaka mpya 1436 Hijriyya,
ni kubainisha kuhama
kwa Mtume Muhammad
(S.A.W) kutoka Makka
kwenda Madina na hapo
ndipo kalenda ya Kiislamu
ilipoanza rasmi.
Ni tofauti na dhana
ya walio wengi, ambao
wa n a o n a k u wa m wa k a
mpya wa Kiislamu ndio
kuanza kwa Uislamu.
Akisoma risala ya taasisi
hiyo kwa mgeni rasmi,
Mdhamini wa Jumuia ya
Istiqaama, Sheikh Suleiman
Nassor Msellem, alisema
s h u l e ya k i m a t a i f a ya
Istiqaama itajengwa eneo la
Kigamboni na inatarajiwa
kuwa mfano wa kuigwa
kwa shule zote za Kimataifa
zilizopo nchini na kuleta
mafanikio ya elimu ya kisasa
kwa Watanzania.

MAKAMU wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na
viongozi wa Jumuiya ya Istiqama katika hafla ya kuukaribisha mwaka mpya wa Kiislamu
1436 Hijiria katika ukumbi wa Karimjee DSM mwishoni mwa wiki.

1,197 wahitimu shahada MUM

Na Bakari Mwakangwale

JUMLA ya wahitimu 1,197


wametunikiwa shahada
katika fani mbalimbali
baada ya kuhitimu mafunzo
yao katika Chuo Kikuu
Cha Waislamu Morogoro
(MUM), mwishoni mwa
wiki iliyopita.
Hafla ya mahafali hayo
ya saba tangu chuo hicho
kilipoanzishwa, imefanyika
katika viwanja vya chuo
hicho ambapo zoezi la
kuwatunuku wahitimu hao
lilifanywa na Mkuu wa
Chuo hicho Hajjat Mwantum
Malele.
Mkuu huyo wa chuo
amewataka wahitimu
kufuata maadili katika
kutekeleza majukumu yao
pale watakapo kwenda
kufanya kazi zao kulingana
taaluma walizosomea.
Hajjat Malale, alisema
kufanya kazi kwa uadilifu
ndio msingi bora wa
uwajibikaji na kwa
kufanya hivyo, watakuwa
wanakitangaza chuo na
kuwa mabalozi wazuri wa
chuo hicho.
Naye Makamu Mkuu wa
Chuo hicho, Alhaji Profesa
Hamza Njozi, akiongea
katika Mahafali hayo alisema
chuo hicho kimestawi na

kuchanua vyema kutokana


na Watanzania kuwaamini
kufuatia ubora wa taaluma
na malezi bora ya kimaadili
wanayoyatoa.
Ta n g u c h u o c h e t u
kuanza mpaka sasa, katika
muda huo chuo chetu
kimestawi na kuchanua
vyema, kwani Watanzania
wametuamini kutokana na
ubora wa taaluma na malezi
tunayoyatoa. Alisema Prof.
Njozi.
Alisema hali hiyo
inajidhihirisha kwa idadi
ya wanafunzi wanaoomba
kudahiliwa katika chuo
hicho, ambapo kwa mwaka
huu jumla ya wanafunzi
1,011 wenye sifa zinazo stahili
waliomba na kupewa fursa ya
kusoma katika chuo hicho.
Hata hivyo Prof. Njozi,
alisema pamoja na idadi hiyo
kuhitaji kujiunga na MUM,
baadhi yao wameshindwa
kujiunga kutokana na
kushindwa kupata mikopo,
lakini akasema hata
wale ambao mikopo yao
imekwenda katika vyuo
vingine, bado wanaendelea
kuomba mikopo yao ipelekwe
katika chuo walichojiunga
nacho (MUM).
Alisema hali hiyo
inatokana na taaluma bora
yenye maadili inayowafanya
wanaohitimu katika Chuo

hicho kukipa sifa kubwa


huko waliko kwa namna
wanavyo jipambanua katika
mambo matatu.
Kwanza kwa uadilifu
wao kwa kuamrisha mambo
mema katika jamii na
kukataza maovu, hususani
kwa watendaji wenzao
wanaokiuka maadili ya kazi
zao, pili kwa umahiri wao
na uchapakazi wao na tatu
utayari wao wa kuwatumikia
wananchi popote watakapo
p a n g i wa . A l i b a i n i s h a
Makamu Mkuu huyo wa
MUM.
Alisema Wizara ya Elimu
na Mafunzo ya Ufundi,
inawatambua katika hilo, kwa
kuwa vijana kutoka katika
Chuo hicho, wamekuwa
hawana tabia ya kusingizia
maradhi wasiyokuwa nayo
ili wabakie Dar es Salaam au
maeneo ya kwao.
Kwa maana hiyo, Prof.
Njozi alisema vijana wao
wametawanyika sehemu
k u b wa ya J a m h u r i ya
Muungano wa Tanzania.
Napenda kuchukua
fursa hii kuwapongeza
na kuwashukuru kwani
mwenendo huo ndio
utakao wasaidia wahitimu
wengine kuaminiwa na
k u t h a m i n i wa n a j a m i i
popote watakapokwenda
katika kutekeleza majukumu

yao. Alisema Prof. Njozi.


Katika hatua nyingine,
Prof. Njozi aliueleza umma
uliofika katika mahafali
h a y o k u wa C h u o c h a o
kimeondokewa na wahadhiri
wake wawili na kuwataka
wadau hao kuwaombea dua
njema wahadhiri hao.
Novemba 4, 2014, chuo
chetu kulipata msiba wa
kuondokewa na mhadhri
wetu mwl. Jafari Siraj,
ambaye pia alikuwa ni
miongoni mwa wanafuzi
wa awali walioanza kusoma
katika Chuo hiki.
Novemba 5, 2014, chuo pia
kiliondokewa na mhadhiri
mwingine mwl. Athumani
Mjinga. Tumeipokea misiba
hii na kukiri kuwa, hakika sisi
sote tunatoka kwa Mwenyezi
Mungu na kwake tutarejea.
Tunamuomba Mwenyezi
Mungu awakubalie amali
zao na awasamehe makosa
yao-Amin. Alisema Prof.
Njozi kwa huzuni.
Naye Mwenyekiti wa
Baraza la Chuo hicho, Dk.
Hassad, alisema Chuo Kikuu
Cha Waislamu Morogoro
kimeanzisha kozi za
Stashahada ya Ualimu wa
Shule za msingi.

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na POA Printing Works Limited, S.L.P. 4605 Dar es Salaam.

Вам также может понравиться