Вы находитесь на странице: 1из 16

Mitawi kizimbani

Sauti ya Waislamu

ISSN 0856 - 3861 Na. 1156 SAFAR 1436, IJUMAA ,

DESEMBA 19-25, 2014

BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Uk. 2

Mtuhumiwa ugaidi kutoka


Zanzibar afanyiwa upasuaji
Ni aliyedai kudhalilishwa na Polisi
Hali yake ilikuwa inatisha, arejeshwa Segerea

SHEIKH Mohamed Idd.

Sheikh Mohammed Idd


aikosoa vikali Bakwata
Halina mwelekeo, wala mipango
Ahoji mali za Wakfu zinavyotumika
Awataka wajifunze kwa Maaskofu
Na Bakari Mwakangwale

MTUHUMIWA wa ugaidi Ust. Salum Ally.

SHEIKH Mohamed Idd, amesema BAKWATA ni


tatizo kwa mustakabali wa Waislamu.
Aidha amesema kuwa, Baraza hilo limekuwa ndio
sababu ya Waislamu kuwa nyuma nchini.
Limekuwa kikwazo katika juhudi za Waislamu
kujiletea maendeleo huku likiwa limehodhi mali za
Wakfu likizitumia kinyume na nia na malengo ya
waliozitoa.
Inaendelea Uk. 3

Tahariri/Habari

2
AN-NUUR
S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786

Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM.
E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk
Ofisi zetu zipo: Manzese Tip Top
Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

www.annuurpapers.co.tz

Sheikh kahujumu Waislamu


Sheikh Mohammed Issa, Alhad, Jongo
Kuweni makini na waandishi wa habari

S H E I KH m m o j a nc hi n i
Pakistan, ametoa kauli kali
akilani mauwaji ya watu
140 yaliyofanyika KhyberPakhtunkhwa, Peshawar.
Sheikh huyo Hafiz
Mohammad Saeed amesema
kuwa Uislamu ni dini ya
amani na hakuna namna
ambavyo inaruhusu mauwaji
kama hayo kufanyika.
Uislamu ni Dini ya amani,
hata katika Jihad hairuhusiwi
kuuwa watoto na wanawake.
Amesema Sheikh Saeed katika
taarifa yake ndefu aliyoitoa
kwa lugha ya Urdu.
Mauwaji anayozungumzia
hapa ni yale yaliyofanyika
Jumanne Desemba 16, wiki
hii ambapo ilidaiwa kuwa
magaidi saba walivamia shule
na kuuwa watu 140, wengi
wao wakiwa wanafunzi na
baadhi wakiwa walimu na
watumishi wengine wa shule
hiyo inayoendeshwa na jeshi.
Kwa upande wake serikali
katika eneo hilo nayo ikaunga
mkono kauli ya Sheikh Saeed
ikisema:
Hakuna dini inayoruhusu
kuuwa watoto. Uislamu,
kwa madhehebu yake yote,
unakataza kuwa watoto na
wanawake.
Mara tu baada ya shambulio
hilo, vyombo vya habari
vilidai kuwa waliohusika
na shambulio hilo lililouwa
watoto wasio na hatia zaidi
ya 100 ni kundi la Kiislamu
linalojulikana kwa jina la
Tehrik-e Taliban Pakistan
(TTP) maarufu Pakistani
Taliban (Taliban wa Pakistan).
Zikishatolewa habari kama
hizi, kwamba waliohusika ni
Waislamu wa kundi fulani
au Waislamu hao wamedai
katika mtandao wao,
Sheikh ukitoa taarifa kuwa
Uislamu ni Dini ya amani,
hairuhusiwi kuuwa watoto na
wanawake, japo ulilosema
ni kweli, lakini kwa upande
mwingine unathibitisha kuwa
waliofanya mauwaji hayo
ni hao Waislamu. Na hilo
ndilo wanalotafuta watu wa
propaganda iwe wanasiasa
au vyombo vya habari.
Tunachosema ni kuwa,
yanapotokea matukio
kama haya, mara nyingi
wanasiasa na vyombo vya
habari wanakimbilia kutaka
maoni ya Masheikh. Sheikh
akisema kuwa mauwaji hayo
hayakubaliki katika Uislamu
au kama Sheikh Saeed
alivyosema kuwa Uislamu
haurusu kuuwa watoto na
wanawake hata iwe katika

Jihad, atakuwa hajakosea.


Amepatia kabisa. Ni kweli
Uislamu hauruhusu mauwaji
ya namna hiyo.
Lakini la kufahamu hapa
n i k u wa m u u l i z a s wa l i
haja yake sio kuelimishwa
yeye na wasikilizaji juu ya
msimamo wa Uislamu. Iwe
ni wanasiasa au waandishi
wa habari, wote wanajua
kuwa Uislamu hauruhusu
mauwaji ya watoto au mtu
yeyote asiye na hatia, kama
ambavyo wanajua kuwa
Ukristo na hata dini za kimila
haziruhusu. Wanachotaka ni
wewe kusaidia kusambaza
propaganda/uzushi kuwa
waliohusika ni Waislamu.
Sasa wewe ukijibu huku ukitia
aya na Hadithi nyingi kutilia
mkazo jibu lako, utamwona
yeye akitikisa kichwa na
kutabasamu. Ukiona hivyo
nawe unazidi kuporomosha
aya, hasa ukijua kuwa watu
huko wanakusikiliza katika
BBC, ITV au TBC1!
Tumeshudia mara kadhaa
Spika akiendesha kikao cha
Bunge huku ma-Khatib wapo
juu ya mimbar wanahutubu
siku ya Aljumaa; mbona
waandishi hao wa habari
h a wa wa e n d e i M a s h e i k h
kuwauliza wanaonaje jambo
hilo. Ni sawa anavyofanya
Spika au la. Lakini wapo pia
mahakimu ambao wamewahi
kutoa hukumu zilizo kinyume
kabisa na Sheria ya Kiislamu
katika mambo ya Wasia,
Mirathi, Talaka na Ndoa,
mbona katika mambo kama
haya wanasiasa na waandishi
wa habari hawataki kujua
m a o n i ya M a s h e i k h n a
msimamo wa Uislamu?
Kuliwahi kuibuka wimbi
hapa la madai ya kuchomwa
m a k a n i s a , wa t u h u m i wa
wakiwa Waislamu. Jaaliya
kunatolewa habari kuwa kuna
kikundi cha wanaharakati wa
Kiislamu wamedai kuhusika
na Sheikh unaulizwa maoni
yako. Ukisema kuwa Uislamu
hauruhusu, kimantiki na
msingi uliokwishawekwa,
utakuwa umekubali kuwa
wanaochoma makanisa ni hao
wanaharakati wa Kiislamu, ila
unaongezea tu kuwa kufanya
ni kinyume na Uislamu. Sasa
hata kama utaongeza na
kusema kuwa wanaharakati
hao ni wanapotosha
Uislamu, hawana elimu
a u h a wa k u s o m a v i z u r i
Quran, haina maana yoyote.
Muhimu ni kuwa ulichosema
ni kuwa kuna Waislamu
wanachoma makanisa na

AN-NUUR

SAFAR 1436, IJUMAA DESEMBA 19-25, 2014

hivyo unahalalisha hatua


zozote zitakazochukuliwa
kupambana nao.
Ulilo na uhakika nalo
wewe Sheikh ni kuwa
Uislamu hauruhusu
ugaidi, kuuwa au kuchoma
nyumba za ibada za watu
wengine maana unaambiwa
usiwatukanie miungu yao.
Ulilo na uhakika ni kuwa
hakuna mwanaharakati wa
kweli wa Kiislamu atakaye
uwa watu ovyo au kupita
akichoma makanisa kwa
jina la Uislamu. Lakini huna
uhakika kuwa wanaodaiwa
kuchoma kanisa ni
wanaharakati wa Kiislamu.
Hata kama itasemwa kuwa
wamesambaza vipeperushi
wakidai. Kipeperushi
kinaweza kuandikwa na
kusambazwa na mtu yeyote
kama ambavyo mtu yeyote
anaweza kuandika na kutuma
habari yoyote katika mtandao
na kudai ni fulani kafanya.
Kwa hiyo, jibu lako ni lazima
ulipange kwa namna ambayo
itaonyesha kuwa mpaka sasa
muhusika hafahamiki. Na
uzuri wa Uislamu, kama
tunavyoambiwa na Masheikh
zetu, Uislamu haukusaza
kitu. Mafundisho ya Uislamu
yanatuambia kuwa lau watu
wangeaminiwa kwa madai
yao tu, wapo watu wangedai
damu na mali za wengine.
Kwa hiyo ni kazi ya mdai
kuleta ushaidi wa kuthibitisha
madai yake. Na ushahidi
hauwezi kuwa hizi kauli
kuwa kikundi cha Kiislamu

kimedai kuhusika.
Lakini hata kama mtu
atajiita ni Muislamu, na
akakiri hadharani kuhusika,
bado si hoja ya kuuhusisha na
Uislamu. Jambazi au mvuta
kokeni, hata akitambulika
kuwa ni Mkristo, kwa namna
yoyote ile, haiwezi kuwa
ujambazi wake ukahusishwa
na Ukristo halafu mnakwenda
kumtaka Askofu wake atoe
maoni!
Toka yaanze mashambulizi
ya Drone, kama njia moja
wapo ya kupambana na
ugaidi Pakistan, wameuliwa
watoto mamia kwa maelfu.
Sheikh unapoulizwa juu ya
wanaodaiwa kuuwa watoto
140, labda itakuwa vyema
kwanza uulize uelezwe, ni
kwa kosa gani wamefanya
watoto hao hata wawe shabaha
ya makombora kutoka Drone?
Muuwaji kachukuliwa hatua
gani? Anayeuwa watoto
hawa na maelfu ya watu
wengine wasio na hatia,
wala hajifichi, anauwa huku
akitamba ulimwengu mzima
ukimshuhudia, walimwengu
wanasema nini juu ya
muuwaji huyu?
Tumewataja Masheikh
Alhad, Shekh Haamid
Jongo na Mohammed Issa,
kama wawakilishi tu wa
Masheikh ambao mara nyingi
wamekuwa wakifuatwa ama
na wanasiasa au vyombo
vya habari kutakiwa kutoa
maoni yao binafsi au kueleza
msimamo wa Uislamu.
Tunachosisitiza ni kuwa
m a r a n y i n g i wa n a s i a s a

n a v y o m b o v ya h a b a r i
wanapowaendea Masheikh
au watu muhimu katika
jamii kutaka maoni yao,
huwa wanachosema sicho
walichokusudia. Na kwa
vile ni mafundi wa mambo
yao, wanauliza maswali ya
mtego ambapo usipokuwa
makini, unawasaidia katika
propaganda na jambo lao
ambalo wala wewe huna
habari nalo na wakati
mwingine la kukuhujumu
hata wewe mwenyewe na
waumini wenzako.
Bila shaka tutakuwa na
kumbukumbu ya kadhia ya
mauwaji ya Mwembechai
ambapo wanasiasa
wa l i c h u k u a v y u m a v ya
k u f u n g i a m a t u r u b a i ya
Msikiti na kudai kuwa ni
silaha zilizokuwa zimefichwa
Msikitini hapo. Tutakuwa pia
tunakumbuka jinsi wanasiasa
hao pamoja na vyombo vya
h a b a r i , wa l i v y o m t u m i a
Sheikh wetu Haamid Jongo
kukoleza propaganda ya
kuwadhuru Waislamu hadi
kuonekana kuwa Waislamu
waliouliwa kwa risasi kwa
kulengwa shabaha na polisi,
ndio wa kulaumiwa. Na
wala sio wauwaji waliovamia
Wa i s l a m u M s i k i t i n i
kwa shinikizo la Paroko
Lwambano aliyedai kuwa
Yesu anatukanwa Msikitini
hapo!
Muhimu ni kuwa makini.
Tu s i j e k u t u m i w a k a m a
viungo vya kukoleza utamu
wa propaganda ya kuhujumu
Uislamu na Waislamu.

Na Mwandishi Wetu

R u s h wa n a U h u j u m u
Uchumi Zanzibar.
Katika kosa hilo la
kwanza, ilidaiwa kuwa
mshitakiwa Hassan
Abdalla Mitawi na Mamy
James Matata kwa nyakati
tofauti mwaka 2014
katika jengo la Shirika
la Habari na Utangazaji
(ZBC ) Televisheni kwa
makusudi walifanya
bishara ya kuuza magari
bila ya kujiandikisha kuwa
walipa kodi na kulipa kodi
hizo kwa mamlaka husika.
Aidha, Mgongo alisema
kosa la pili la matumizi
mabaya ya ofisi kinyume
na vifungu vya 53 na 61
vya sheria namba moja
ya mwaka 2012 ya Kuzuia
R u s h wa n a U h u j u m u
Uchumi Zanzibar.
Katika kosa la pili
muendesha mashitaka
huyo alisema kwamba
mshitakiwa kwa nyakati
tofauti mwaka 2014 huko
jengo la ZBZ Televisheni
akiwa Mkurugenzi Mkuu
wa Shirika la ZBC alitumia

nafasi yake kwa kufanya


biashara ya kuuza magari
katika eneo la ofisi kwa
lengo la kujipatia maslahi
binafsi.
Kwa upande wake
Hakimu Ali Ameir alimtaka
mshitakiwa huyo kutojibu
lolote mahakamani
h a p o k wa s a b a b u n i
kesi inayosikilizwa na
Mahakama Kuu, hivyo
ataenda kujibu shitaka hilo
mbele ya Jaji wa Mahakama
Kuu.
Hata hivyo, mshitakiwa
amepewa dhamana ya
maandishi ya shilingi
milioni moja pamoja na
wadhamini wawili kwa
kima hicho hicho kwa kila
mmoja.
Hivi karibu serikali
i m e p i t i s h a s h e r i a ya
kuzuwia rushwa na
uhujumu uchumi ambayo
inakataza watumishi wa
serikali kujihusisha na
mipango yoyote ambayo
ni kinyume na matumizi ya
ofisi za serikali ya kisheria.,

Mitawi kizimbani

M K U R U G E N Z I
M k u u wa S h i r i k a l a
Utangazaji Zanzibar
(ZBC) Hassan Abdalla
M i t a w i a m e f i k i s h wa
mahakamani kwa makosa
kadhaa ikiwemo kosa la
matumizi mabaya ya ofisi
na ukwepaji kodi.
Mkurugenzi huyo
alipanda kizimbani majira
ya saa 5 asubuhi juzi katika
mahakama ya mkoa Vuga,
mbele ya Hakimu Ali
Ameir.
Akisoma mashitaka
mbele ya hakimu huyo,
Muendesha mashitaka
Abdalla Issa Mgongo,
alisema mshitakiwa huyo
amefikishwa mbele ya
mahakama hiyo akiwa na
mashitaka mawili.
Alisema, kosa la kwanza
linalomkabili ni kukwepa
kodi kinyume na vifungu
44 kifungu kidogo cha (1)
(e) na kifungu kidogo cha
(2) pamoja na kifungu cha
61 vya sheria ya Kuzuia

Habari

AN-NUUR

SAFAR 1436, IJUMAA DESEMBA 19-25, 2014

Mtuhumiwa ugaidi kutoka Zanzibar afanyiwa upasuaji


Na BakariMwakangwale

HATIMAE mtuhumiwa wa ugaidi


Ust. Salum Ally, amefanyiwa
upasuaji sehemu ya haja kubwa
katika hospitali ya Taifa ya
Muhimbili.
Huyo ni yule aliyedai kufanyiwa
vitendo kinyume na maumbile na
Askari Polisi.
Amefanyiwa upasuaji huo
baada ya kuwa katika maumivu
makali takribani miezi sita tokea
kukamatwa na kulalamika kuwa
amefanyiwa vitendo vibaya na
Askari Polisi baada ya kukamatwa
na kuomba apatiwe matibabu
kulingana na hali aliyokuwa nayo.
Baada ya kuona hali inazidi
kuwa mbaya, huku mamlaka
husika zikisuasua kumpeleka
hospitali kwa ajili ya matibabu,
Ust. Salum, alithubutu kuonyesha
suruali yake iliyojaa usaha
katika eneo la makalio mbele ya
Mahakama ya Kisutu, Jijini Dar es
Saalam, ikiwa ni kithibitisho kwa
kile anacho kilalamikia.
Baadhi ya ndugu na jamaa wa
mtuhumiwa huyo walieleza kuwa
hali yake ilikuwa ikidhoofu siku
hadi siku hata kufikia hali ya kutoa
harufu ikiwa ni ishara ya hali
mbaya kiafya.
Wa k i o n g e a n a A n n u u r ,
ndugu wa mtuhumiwa huyo na
Kamati ya Maafa ya Shura ya
Maimam, wamesema Ust. Salumu,
alifikishwa Muhimbili siku ya
Ijumaa na siku ya Jumamosi,
a l i f a n y i wa u p a s u a j i , l a k i n i
hapakuwa na ruhusa ya kumuona
wala kumpatia chakula.
Hata hivyo, Mjumbe wa Kamati
ya Maafa ya Shura ya Maimamu
(T), Ust. Ally Mbaruku, alisema
mtuhumiwa huyo, amerejeshwa
Mahabusu, katika Gereza la
Segerea siku moja baada ya
kufanyiwa operesheni hiyo.
Ndugu wa mtuhumiwa huyo,
alisema alibaini kuwa ndugu
ya k e y u p o M u h i m b i l i p a l e
alipompelekea chakula katika
gereza la Segerea, siku ya Jumamosi
(iliyopita) ndipo alipoelezwa
na wenzake kuwa, Ust. Salumu
kapelekwa Muhimbili toka siku
ya Ijumaa na hajarudi.
Ndugu huyo ambaye
hakutaka jina lake liandikwe
gazetini, alisema baada ya kupata
taarifa hizo alilazimika kwenda
Muhimbili kwa lengo la kujua hali
yake na kinachoendelea katika
matibabu ya ndugu yake huyo.
Alisema, baada ya kufika
Muhimbili, hakuweza kumuona
kutokana na ulinzi aliowekewa
huku akitakiwa kuwa na kibali
maalumu kutoka Gerezani
kinachomruhusu kumuona.
Alisema, akiwa hapo Muhimbili
katika kutafuta wodi aliyopo
ndugu yake, alikutana na Askari
Magereza na kuwaeleza shida
yake, ambapo walimthibitishia
kuwa mtuhumiwa huyo yupo

lakini hatoweza kumuona wala


kumpatia chakula.
Baada ya kujibiwa hivyo,
anaeleza kwamba alikumbuka
kuwa kuna Kamati ya Shura,
ambayo ina kibali cha Magereza
cha kuwaona na kuwapatia
chakula watuhumiwa hao ndipo
alipowasiliana na kamati hiyo ili
wafike Muhimbili kumuona na
kumpatia huduma ya chakula.
Kwa upande wake Mjumbe wa
Kamati hiyo ya Shura ya Maafa,
Ust. Mbaruku Ally, alisema baada
ya kupata taarifa hizo kutoka kwa
ndugu huyo wa Ust. Salimu, siku
ya Jumamosi, jioni ilimlazimu
kufika Muhimbili siku iliyofuata
(Jumapili) majira ya saa kumi na
mbili, asubuhi.
Alisema, alikwenda moja kwa
moja katika wodi ya Kibasila,
a l i m o k u wa a m e l a z wa U s t .
Salim na kukutana na askaria
Magereza akiwa na buduki, kisha
alijitambulisha na kumueleza
sababu ya yeye kuwapo
pale, ambapo Afande huyo,
alimthibitishia kuwa mtuhumiwa
huyo yupo hapo.
A f a n d e y u l e a l i m u i t a
mwenzake naye nikamueleza na
kumkabidhi kibali cha Magereza
k u wa n a h i t a j i k u m u o n a n a
kumpatia chakula Salum, pamoja
na kibali kile kukiona, akanihoji ni
nani kanieleza kuwa mtuhumiwa
huyo yupo pale, zaidi akaniambia
pamoja na hayo hakuna ruhusa
ya mtu yoyote kumuona mpaka
atakaporuhusiwa kurudi
gerezani. Alisema Ust. Mbaruku.
Awali, ndugu huyo wa Ust.
Salum, aliitaka Serikali, kuwa wazi
kuhusiana na watuhumiwa hao wa
Ugaidi, hususani katika matibabu
yao kwa kuwaeleza ndugu zao
juu ya matibabu wanayoyapata
kuliko kuwa wanaficha kama
wanavyofanya sasa kutokana na
yale waliotendewa.
Alisema, kwamba siku za
nyuma, alipata kuelezwa na Salum,
kuwa alipelekwa Muhimbili na
kufanyiwa uchunguzi na Daktari
alitoa taarifa kamili jinsi alivyo
athiriwa.
Serikali inatakiwa kulifanyia
kazi suala hili kulingana na uzito
wa jambo lenyewe kisha waliweke
wazi nawapatiwe haki yao ya
matibabu, ukifika eti wanakwambia
kama sisi tunawapenda lakini wao
wanawapenda zaidi.
Kauli hii haina ukweli wowote,
kwani haiendani na uhalisi wa hali
zao humo gerezani. Utasemaje
unampeda wakati anaathirika
lakini humpeleki hospitali ndani
ya miezi sita. Alisema ndugu
huyo. Alisema.
Hata hivyo taarifa kutoka katika
Gereza la Segerea, zimeeleza
kuwa Ust. Salum, amesharejeshwa
gerezani, Jumatatu wiki hii
siku moja baada ya matibabu
akitokea Muhimbili alikofanyiwa
operesheni.

BAADHI ya watuhumiwa wa kesi ya ugaidi wakiingia katika


Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Sheikh Mohammed Idd aikosoa vikali Bakwata

Inatoka Uk. 1
Sheikh Mohamed Idd, maarufu
kwa jina la Abuu Idd, ameyasema
hayo akiongea na Waislamu, katika
mada yake aliyoiita Bakwata ni
sababu ya Waislamu wa Tanzania
kuwa nyuma.
Alisema, suala hilo liko wazi
sana na kwamba anauhakika na
anachokisema kuwa Bakwata ni
tatizo.
Bakwata ni tatizo, na kila mmoja
anajua hilo, lakini tunatoafautiana
katika mfumo wa kuondoa tatizo,
niliwahi kusema na nitaendelea
kusema kwa kuwa nina hakika na
ninachokizungumza. Alisema
Abuu Idd.
Akifafanua ni kwa namna gani
kuwa BAKWATA ni tatizo kwa
Waislamu, alisema matarajio
ya Waislamu, ni kuona Baraza
hilo linakuwa mstari wa mbele
kutetea maslahi yao sambamba na
kuwaletea maendeleo.
Abuu Idd, alisema Waislamu
wanapoona kimya pale
wanapopata madhila ama hawaoni
mipango yoyote ya maendeleo yao
chini ya Bakwata, hali hiyo hufanya
Waislamu wakose dira na kuvunja
umoja kwani yule aliyejivika
ukinara wa kuwaongoza hana
mpango wa mambo hayo kwa ajili
ya Waislamu.
Alisema, Bakwata pamoja
na kuwa na fursa ya kuongea
na Serikali kuhusu masuala ya
Waislamu, lakini haitumii nafasi
hiyo, badala yake imekuwa
ikiwasiliana na Serikali kwa
mambo maalumu.
Akasema, Bakwata itakuwa na
mawasiliano na Serikali siku za
Idd, au kama kumeletwa mbuzi
wa Makka, ama kama kumeletwa
tende kisha zinatakiwa kugaiwa

kwa Waislamu na baada ya hapo


(Bakwata) itakuwa kimya na
endapo hapo katikati itatakiwa
kauli nzito dhidi ya Waislamu
ndipo itaibuka iongee.
Abuu Idd, alisema kuna sababu
za msingi za kuisema Bakwata, kwa
sababu jinsi ilivyo unageuka kuwa
mwanachama utake au usitake na
unapokuwa mwanachama unao
uhuru wa kukihoji chama chako.
A l i s e m a , ye ye a n a i p e n d a
Bakwata, pamoja na uoza wake
wote huo kwani alidai anaamini
kwamba moja ya njia ya kuweza
kuirekebisha, si kuikalia mbali bali
ni kwa kuwa nayo karibu.
Kwa hiyo Bakwata yangu
sitaki iwe hivyo, naona hilo ni
tatizo lazima irekebeshwe na kwa
kuwa ni ya kwetu tuangalie namna
ya kuirekebisha maana hali ni
mbaya. Alisema Abuu Idd.
Alisema, Bakwata jinsi ilivyo
haina uwezo hata wa kuwasaidia
Waislamu kiasi chochote cha
Juzuu Amma, ila ina uwezo wa
kuchapa barua kuidhinisha mtu
apewe msaada huo hata kama ni
wa Juzuu hamsini.
Kazi yao ni kuidhinisha
kwa kuandika, Kwa yoyote
anayehusika (huko Msikitini)
fulani mtajwa hapo juu, sisi
Bakwata tumemthibitisha kwamba
anashida ya juzuu, asaidiwe. Basi
hiyo ndio kazi kubwa ya Bakwata
toka kuundwa kwake. Alisema
Abuu Idd.
Kwa uthibisho wa hilo, akasema
leo ukiwapa nafasi, Taasisi moja tu
mfano ya DYCCC, waseme wana
kiasi gani cha barua za namna
hiyo kutoka Bakwata, watakuwa
na mlima wa barua hizo, ikiitaka
Taasisi hiyo asaidie.
Aidha, alisema na kama kuna
Inaendelea Uk. 4

4
BUNGE la Kenya hivi sasa linajadili
muswada unaopendekeza sheria
ya usalama kufanyiwa mabadiliko,
ili kuiwezesha serikali kuimarisha
usalama na kupambana barabara na
jinamizi la ugaidi.
Hata hivyo, mapendekezo ya
marekebisho ya sheria hiyo ya
usalama yaliyotolewa na serikali ya
Kenya, yamedaiwa kuwa yanajenga
mazingira kwa nchi hiyo kurudi tena
katika enzi za utawala wa kipolisi
ulioshuhudiwa katika miongo ya 80
na 90 chini ya utawala wa Rais wa
wakati huo, Daniel Arap Moi.
Pamoja na mambo mengine,
muswada huo unapendekeza polisi
kupewa nguvu na mamlaka zaidi ya
kuwakamata na kuwaweka kizuizini
watuhumiwa wa ugaidi. Imeelezwa
kuwa iwapo muswada huo utapita
na kuwa sheria kama ulivyo, basi
polisi watakuwa na mamlaka ya
kumshikilia mtuhumiwa wa ugaidi
kwa takriban mwaka mmoja badala
ya muda wa sasa wa miezi 3 bila
kumfikisha mahakamani.
Polisi pia watakuwa na uwezo
wa kufuatilia mawasiliano ya mtu
au watu wanaotuhumiwa kuwa
ni magaidi, ikiwa ni pamoja na
kusikiliza mazungumzo yao ya simu.
Aidha imeelezwa kuwa pamoja
na kuwepo hofu ya matatizo hayo,
vyombo vya habari navyo vitakuwa
katika wakati mgumu kwa mujibu
wa muswada huo iwapo utapitishwa
na kuwa sheria.
Katika muswada huo imebainishwa
kwamba, pale chombo cha habari
kitakachochapisha au kutangaza
habari zinazoonekana kuonyesha
aina fulani ya uungaji mkono magaidi
au kushajiisha ugaidi, wakuu wake
watakamatwa na kuhukumiwa
kifungo cha miaka isiyopungua 20
jela. Tayari inatarajiwa kwamba
wabunge wa Kenya wataidhinisha
muswada huo.
Muswada huo ambao serikali
imesema utasaidia kuimarisha
usalama, umekabiliwa na shinikizo
kali kutoka kwa makundi ya kiraia,
wanasiasa wa upinzani na mashirika
ya kutetea haki za binadamu ndani
na nje ya Kenya.
Mashirika ya Kimataifa ya Kutetea
Haki za Binadamu ya Amnesty
International na Human Rights
Watch, yametoa taarifa ya pamoja
inayokosoa vikali muswada huo na
kusema ukipitishwa kuwa sheria,
utakiuka haki za binadamu kwa
kiwango kisichokubalika.
Taarifa ya mashirika hayo imesema
kuwa kuna wasiwasi wa kurejea
tena utawala wa kipolisi nchini
Kenya. Wapinzani kwa upande
wao nao wamesema serikali ifanye
ifanyavyo, lakini hakuna jambo lolote
linaloweza kuhalalisha ukiukwaji wa
haki za binadamu.
Rais wa Kenya, Uhuru Muigai
Kenyatta alisema siku ya Ijumaa
iliyopita kwenye hotuba yake kwa
taifa kuwa, sheria hiyo ndio njia
pekee ya kuvipa nguvu vyombo vya
usalama kukabiliana na magaidi na
hali ya ukosefu wa usalama ndani
ya taifa hilo.
Hotuba ya Rais Kenyatta katika
kuadhimisha miaka 51 ya uhuru wa
Kenya ilisisitiza juu ya ulazima wa
kubana mianya ya ugaidi ili kuliweka
taifa katika hali ya amani na utulivu.
Wachambuzi wengi wanaona
kuwa, sheria hiyo inaweza
kuwafungulia polisi milango ya
kukiuka zaidi haki za binadamu
katika siku za usoni kwa kisingizio
cha kupambana na ugaidi.
Hii ni katika hali ambayo, polisi

Makala

Utawala wa kipolisi Kenya


Sheria ya kidhalimu yaja
NGO zaidi ya 500 zafungwa

ASKARI nchini Kenya wakiwa nje ya jengo la biashara la Westgate muda


mfupi baada ya kuvamiwa na wanaodaiwa magaidi.
ya Kenya imekuwa ikituhumiwa
kuwaua kiholela watu wanaoshukiwa
kuwa na mfungamano na makundi
ya kigaidi, wakiwemo viongozi wa
kidini katika maeneo ya Pwani ya
Kenya.
Serikali ya Kenya imekuwa katika
mashinikizo kubwa tangu kutokea
shambulizi la kigaidi katika jumba la
kibiashara la Westgate jijini Nairobi
mwaka uliopita, ambapo watu 67
walipoteza maisha yao na wengine
wengi kujeruhiwa.
Matukio mengine yaliyofuata
baada ya tukio la Westgate kama vile
mashambulizi ya Mpeketoni huko
Lamu, mauaji ya raia katika miji
ya Mandera, Wajir na hata Nairobi
pia ni jambo jingine linalodaiwa
kuchochea ari ya serikali ya kuja na
mapendekezo hayo ya kurekebisha
sheria ya usalama.
Hata hivyo kwa upande wa
wale wanaounga mkono serikali,
wametetea mapendekezo ya
mabadiliko ya sheria hiyo ya usalama,
wakisema kwa sasa Wakenya wengi
wanaikaba koo serikali wakitaka
ichukue hatua kwa vitendo
kukabiliana na hali mbaya ya usalama
nchini humo.
Mashirika ya asasi za kijamii
yanaelezea wasiwasi wao juu ya
mswaada wa kurekebisha sheria
ya kupambana na ugaidi ya Kenya,
wakisema ikiwa mabadiliko hayo
yatafanyika kama yalivyopendekezwa
yatabana uhuru wa kiraia wa
Wakenya.
Kwa kifupi ni kwamba Muswada
wa Marekebisho ya Sheria za Usalama
wa Mwaka 2014, unapendekeza
mabadiliko kwenye sheria 21 zilizopo,
ambao serikali inasema utaviwezesha
vyombo vya usalama kulishughulikia
tatizo la ukosefu wa usalama.
Mswada huo mpya utafanya iwe ni
kosa lenye adhabu ya faini ya ahadi
shilingi million 1 (dola 11,000) au
kifungo cha miaka mitatu jela kwa
kusambaza kile kilichoelezwa kuwa
ni "vitu vichafu, matusi au mambo
yenye kuudhi ambayo yanaweza
kusababisha hofu na wasiwasi kwa
wananchi" ikiwa utapitishwa kuwa

AN-NUUR

SAFAR 1436, IJUMAA DESEMBA 19-25, 2014

sheria.
Mswada huo pia utaipa nguvu
Idara ya Usalama wa Taifa (NIS)
kunasa na kurikodi mazungumzo

ya simu bila ya amri ya mahakama,


kitendo ambacho kwa sasa kinahitaji
idhini ya Mahakama Kuu.
Vile vile, vyombo vya habari na
waandishi wa habari wanaochapisha
au kutangaza picha za wahanga wa
matukio ya kigaidi bila ya idhini au
ridhaa ya polisi watapewa adhabu ya
kifungo cha hadi miaka mitatu jela au
faini ya hadi shilingi milioni 5 (dola
55,200), kwa mujibu wa mswada huo.
Mashirika ya habari kwa sasa yako
huru kuchapisha vitu kama hivyo,
lakini yanaongozwa na kanuni ya
madili ya Baraza la Habari la Kenya
na kanuni binafsi za vyombo husika.
Marekebisho hayo pia yanampa
nguvu kubwa Rais kumteua Mkuu
wa Polisi, jambo ambalo wakosoaji
wanasema linaifanya nafasi hiyo
kuwa ya uteuzi unaochochewa
kisiasa. Kwa sasa Kamisheni ya Taifa
ya Huduma za Polisi ndiyo yenye
mamlaka ya kumteua Mkuu wa
Polisi.
Mswada huo pia unaondoa muda
wa mwisho wa kikazi kwa Mkuu wa
Polisi, Mkurugenzi Mkuu wa Idara
ya Ujasusi na wa Mkurugenzi wa
Upelelezi wa Uhalifu, jambo ambalo
wakosoaji wanasema litaingilia
ufanisi wa kazi na pia kuhujumu
uhuru wao na kuwafanya kutumika
kirahisi na mamlaka ya uteuzi.
Tayari Wajumbe wa Bunge la
Taifa walishapangiwa kurejea
vikaoni kutoka mapumzikoni siku
ya Alhamisi (tarehe 18 Disemba) kwa
ajili ya kikao maalum na kuupigia
kura mswada huo.

Inaendelea Uk. 12

Sheikh Mohammed Idd aikosoa vikali Bakwata


Inatoka Uk. 3

Madrasa inavuja na inahitaji bati


15 tu, Bakwata pia haina uwezo wa
kukupatia bati hizo, zaidi itafanya
kazi ile ile ya kukuandikia barua
kwenda kuomba Miskitini au kwa
Taasisi fulani.
Abuu Idd, alisema kwa hadhi ya
Bakwata, ilitakiwa moja ya jukumu
lake katika kila Msikiti ipeleke Imamu
na imlipe ili awe na jukumu la kutoa
darsa na huduma za kiroho katika
eneo husika, lakini akasema Baraza
hilo halina mpango huo.
Akahoji, haya majumba ya Waqfu
kazi yake ni nini, kwani alisema ndani
ya Bakwata kuna miradi ambayo,
ukiitazama kwa harakaharaka
miradi hiyo ingelitumika kwa ajili
ya kuendeleza Uislamu ni wazi
Waislamu wangekuwa wapo mbali.
Alisema, wachamungu, waliotoa
mali zao wakaziweka Waqfu chini
ya Bakwata, walikusudia kusaidia
Uislamu uende mbele, kupitia
mapesa ya mali za Waqfu.
Badala yake Bakwata inazitumia
mali hizo ili kutengezea mazingira
ya wao kubaki kwenye uongozi,
lakini malengo ya watoaji si kuifanya
iwepo bali kusimamia huduma kwa
Waislamu na Uislamu. Alisema.
Abuu Idd, alisema hali hiyo
inasikitisha na inahudhunisha
kwani inapofikia Taasisi ya Kiislamu
ambayo inajinasibisha kuwa ndio
chombo cha Waislamu wa Tanzania,
lakini haina uwezo hata wa kutoa
Juzuu 50, ni aibu.
Alisema, kwa upande wa mabaraza
ya Kikristo, mara kwa mara utasikia
Maaskofu wakiikosoa Serikali na
kuwa wakali pale maslahi ya dini yao
yanapoguswa, lakini kwa Bakwata
huwa ni kimya.

Na kuna taarifa kuwa hao


M a a s k o f u c h i n i ya m a b a r a z a
yao, wamefungua ofisi maalumu
itakayokuwa ni kiunganishi kati ya
Serikali na Makanisa.
Hii ina maana kwamba wakitaka
kuzungumza na Serikali ofisi hiyo
ndiyo itakayotumika, hii ni mipango
na mikakati, lakini kwetu chini ya
Bakwata hilo halipo. Alisema Abuu
Idd.
M b a ya z a i d i , a k a e m a k a m a
utakwenda Bakwata kuomba mpango
kazi wa maendeleo ya Waislamu na
Uislamu hauwezi kupata zaidi ya
mpango kazi wa kuifanya Bakwata
iendelee kwepo katika hali iliyo nayo
sasa.
Lakini huwezi kupewa
maelezo ya mipango kwamba
mwaka huu tunatarajia kujenga,
Madrasa kadhaa, Shule kadhaa,
au tutasomesha Maimam kadhaa
ambao tutawasambaza katika Misikiti
tunayokusudia kuijenga. Alisema
Abuu Idd.
Alisema, kauli kubwa ya Bakwata,
siku zote utasikia tuna malengo ya
kudumisha amani, mshikamano na
utulivu wa nchini,
Alisema moja ya njia ya
kuirekebisha Bakwata ni kuwa karibu
nayo, ili uweze kukosoa na kutoa
ushauri wako ukiwa ndani yake.
Akasema, uzoefu wake
u n a m wa m b i a , wa n a o i s h i k i l i a
B a k wa t a , wa n a p e n d a k u s i k i a
Waislamu wakiilani mbali wakiwa
na imani kuwa kelele hizo huishia
hapopao kwani hawawezi kwenda
kuuliza mapato na matumizi ya pesa
za zao.

Habari za Kimataifa

AN-NUUR

SAFAR 1436, IJUMAA DESEMBA 19-25, 2014

Maandamano ya kupinga dhulma yapamba moto Marekani


Wafanyakazi wa Bunge nao waunga mkono

ZAIDI ya wafanyakazi mia moja


wa Bunge la Marekani ambao ni
jamii ya watu weusi, walitoka nje
ya Bunge hilo Alhamisi iliyopita
kupinga maamuzi ya Mabaraza
ya Mahakama katika miji ya New
York City na Ferguson, Missouri
kufuatia kutochukuliwa hatua
dhidi ya maafisa wa polisi wa
kizungu, waliohusika katika vifo
vya wanaume weusi wa Marekani
ambao hawakuwa na silaha.
Kundi la wafanyakazi wa Bunge,
wengi wao wakiwa Wamarekani
weusi takriban 150 walikusanyika
kwenye ngazi za jengo la Bunge
muda mfupi baada ya saa tisa na nusu
alasiri, kuonyesha mshikamano wao
na mamia ya waandamanaji katika
miji hiyo, katika kile kiongozi wa dini
Bungeni Barry Black, alichosema ni
Sauti ya wale wasiosikika.
Leo hii wakati watu wote katika
taifa hili wanaandamana kutetea
haki katika ardhi yetu , tusameheni
pale tuliposhindwa kupaza sauti
zetu kwa wale ambao hawakuweza
kuzungumza au kupumua wenyewe,
aliomba Bw. Black.
A l i t o a m w i t o Wa m a r e k a n i
wasisahau historia ya nchi yao,
akisema waliostahili kuchukua hatua
wameshindwa na kuomba Mungu
awafariji wale wanaoomboleza ambao
wanajua uchungu wa kupoteza
wapendwa wao.
Wabunge hao waliongeza sauti
zao katika maandamano kote nchini
wiki iliyopita baada ya maamuzi ya
majopo ya majaji walioteuliwa na
mahakama, kupinga hukumu kwa
Daniel Pantaleo, polisi mzungu wa
New York aliyehusika na mauaji ya
Julai 17 ya Eric Garner, alipokuwa
akifanya kazi yake kama mchuuzi
katika eneo la Staten Island.
Garner alikabiliwa na maafisa
kadhaa wa polisi huku Pantaleo
akimkaba koo, na kusikika kwenye
ukanda wa video akisema I cant
Breath (Siwezi kupumua) kabla ya
kupoteza maisha yake.
Maelfu ya waandamanaji
waliandamana katika barabara za
majiji ya Washington na New York
baada ya mahakama kutoa uamuzi
kuwa askari aliyemuua raia mweusi
kwa kumkaba koo hatafunguliwa
mashitaka
Punde baada ya mahakama
kutangaza uamuzi huo wa
kutomfungulia mashitaka askari
mzungu Daniel Pantaleo, aliyemuua
mwanamume kwa jina Eric Garner
mwenye umri wa miaka 43, mamia
ya waandamanaji walikusanyika
katika ukumbi wa rockefeller na
katika ukumbi wa umma wa New
York wakiimba hakuna haki hakuna
amani.
Kamishna wa polisi wa mji wa
New York, Bill Bratton, alisema
wamewakamata watu thelathini.
Makundi ya waandamanaji kutoka
sehemu mbalimbali jijini humo
walikutana kwa maandamano
makubwa katika barabara kuu ya
NewYork na gazeti la Washintgon
Post liliripoti waandamanaji 5,000
walijitokeza.
Awali taarifa iliyotolewa na
kiongozi wa kutetea haki za raia,
Al Sharpton, ilieleza kuwa Bunge

linahitaji kuchukua hatua kubadilisha


sheria na hali barabarani.
Kati ya wataohudhuria
maandamano hayo ni familia za
Michael Brown, kijana aliyeuwawa
katika jimbo la Missouri, na Eric
Garner, ambaye alikufa wakati
anakamatwa mjini New York.
Garner alikufa mikononi mwa
polisi akikamatwa kwa kuuza sigara
ambazo zilikuwa hazijalipiwa kodi
na hakuwa na silaha wakati wa tukio
hilo lililotokea mwezi Julai mwaka
huu.
Kufuatia uamuzi huo wa
mahakama, Mwanasheria mkuu wa
Marekani Eric Holder alisema ofisi
yake itaanzisha uchunguzi kuhusu
kifo cha Garner baada ya kukabwa
koo na askari.
Hata hivyo tangazo hilo la Holder,
linamaanisha kuwa kuna uwezekano
askari anayetuhumiwa akachukuliwa
hatua.
Video iliyonakiliwa wakati Garner
akikamatwa na askari kadhaa
inaonyesha akisema mara kadhaa
kuwa hawezi kupumua baada ya
kuwekwa chini na askari akiwa
amebanwa kooni.
Rais wa Marekani akizungumza
muda mfupi baada ya uamuzi wa
mahakama amesema kuuawa kwa
Garner sio tatizo la watu weusi au
weupe bali la Marekani nzima.
Kesi za askari polisi waliohusika
na vifo hivyo zilifutwa na kuzusha
maandamano kote Marekani. Hayo
yamekuja baada ya uamuzi wa
mahakama ya Fergusson katika
jimbo la Missouri kutomshitaki askari
aliyemuua kijana wa miaka 18 Michael
Brown, mwezi Agosti uamuzi ambao
ulisababisha maandamano makubwa
nchini humo kupinga ubaguzi wa
rangi.
A s k a r i wa k i z u n g u n c h i n i
humo wameshutumiwa na jamii
ya watu weusi nchini Marekani,
kwa kutumia nguvu kupita
kiasi wanaposhughulikia visa
vinavyowahusisha washukiwa Weusi
Wakati matukio haya yakijiri katika
nchi inayoitwa kuwa ni ya utawala wa
kidemorasia wenye kufuata misingi
ya usawa na demokrasia, Mwezi
Septemba mwaka huu Wizara ya
Sheria ya Marekani ilitangaza kuwa
uchunguzi mpya ulianza kuhusu faili
la mauaji yaliyofanywa na polisi ya
mji wa Ferguson dhidi ya Mmarekani
mweusi, Michael Brown.
Waziri wa Sheria wa Marekani
aliwaambia waandishi habari kuwa
uchunguzi mpya umeanza katika
kiwango cha Serikali ya Federali na
kwamba lengo lake ni kuchunguza
mwenendo wa polisi ya mji wa
Ferguson katika jimbo la Missouri.
Waziri wa Sheria wa Marekani Eric
Holder alisema, kuna sababu nyingi
za kufanyika uchunguzi ili ibainike
iwapo polisi wa mji wa Ferguson
walikwenda kinyume na Katiba ya
Marekani au la.
Mji wa Ferguson na miji mingine
ya Marekani kuanzia tarehe 9 Agosti
mwaka huu iligeuka uwanja wa
maandamano makubwa na ghasia

ASKARI polisi wa Marekani alinayetuhumiwa kumuua Mmarekani mweusi


(picha ndogo)
zilizoandamana na ukatili wa polisi
ya Marekani baada ya ofisa wa polisi
wa kizungu kumuua kwa kumpiga
risasi kijana Michael Brown mwenye
asili ya Afrika, ambaye hakuwa na
silaha ya aina yoyote.
Polisi iliwatia nguvuni
waanaandanaji wengi waliokuwa
wakipinga mauaji ya kijana huyo na
sera za ubaguzi za vyombo vya dola.
Polisi ya nchi hiyo ilitumia gesi ya
kutoa machozi, maji ya kuwasha na
magari ya kivita ambayo kawaida
hayatumiwa isipokuwa dhidi ya adui
wa kigeni katika medani za vita.
Maandamano ya kupinga ubaguzi
wa rangi yaliendelea nchini Marekani
hadi tarehe 22 Agosti na baada ya
hapo hali ya mambo ilikuwa shwari
katika mji wa Ferguson.
Baadhi ya viongozi wa Marekani
akiwemo Waziri Holder walikosoa
vikali mbinu na hatua zilizochukuliwa
na polisi katika kadhia hiyo. Vilevile
wabunge wa Congresi ya Marekani
walitoa wito wa kuangaliwa upya
ratiba ya Wizara ya Ulinzi Pentagon
ya kutuma silaha za kivita na magari
ya deraya kwa idara za polisi kote
nchini humo.
Takwimu zilizotolewa huko
M a r e k a n i z i n a z o n e s h a k u wa
kufungwa jela Waafrika wa Marekani,
tena bila ya kuambiwa makosa yao
au kufikisha mahakamani, kutiwa
mbaroni ovyo na bila sababu,
kukanyagwa haki zao za kijamii,
umasikini na ukosefu wa ajira katika
jamii ya weusi wa Marekani ni
mkubwa sana kuliko wenzao weupe.
Takwimu hizo zinaonesha kuwa
mji wa Ferguson una asilimia 65 ya
Wamarekani weusi wenye asili ya
Afrika, lakini inashangaza kuwa
raia hao wanaunda asilimia 11 tu
ya maafisa wa jeshi la polisi ya mji

huo, suala linaloonesha ukosefu wa


mlingano na jinsi Wamarekani weusi
wasivyoshirikishwa ipasavyo katika
masuala mbalimbali hata ya jamii zao
wenyewe.
Mwezi Agosti mwaka huu Waziri
wa zamani wa Mambo ya Nje wa
Marekani, Hillary Clinton, alisema
kuwa, hakuna uadilifu katika mfumo
wa vyombo vya sheria vya nchi hiyo.
Clinton ambaye anatazamiwa
kugombea nafasi ya urais katika
uchaguzi wa mwaka 2016 nchini
Marekani, ameyasema hayo
alipokuwa akiashiria tukio la mauaji
ya kijana mwenye asili ya Afrika
Michael Brown, aliyeuawa kwa
kupigwa risasi na afisa wa polisi
huko mjini Ferguson, Missouri na
kuongeza kuwa, serikali inapaswa
kuchukua hatua kali kukabiliana na
tukio hilo na mengineyo kama hayo.
Akizungumzia maandamano ya
kupinga mauaji na ukandamizaji
u l i o k i t h i r i d h i d i ya j a m i i ya
Wamarekani weusi nchini humo,
alisema kuwa, serikali haitakiwi
kufumbia macho mapungufu na
vitendo vinavyokinzana na uadilifu
katika idara za mahakama nchini.
Aliitaka serikali kufanya juhudi
kubwa kurejesha hali ya uaminifu wa
wananchi kwa serikali.
Kufuatia wimbi la maandamano
makubwa ya kupinga ubaguzi wa
rangi na ukatili vinavyofanywa na
polisi na vyombo vya sharia nchini
humo dhidi ya Wamarekani wenye
asili ya Kiafrika, Kamishna Mkuu
wa Haki za Binadamu wa Umoja
wa Mataifa Navi Pillay, aliitaka
Marekani kujiangalia yenyewe
kabla ya kuzituhumu nchi nyingine
za dunia kuwa zinakiuka haki za
binaadamu.

Makala

AN-NUUR

SAFAR 1436, IJUMAA DESEMBA 19-25, 2014

Somo gumu kufahamika au ndio ushenga wa ajali!


Rais Kenyatta afuata nyayo za Bush
Aljazeera nao waibua maswali mengi
Waislamu, Wakristo Kenya njia panda
Na Omar Msangi
KAMA ilivyokuwa kwa George
W Bush, Rais Uhuru Kenyatta
anasema kuwa, ama Wakenya
wawe pamoja naye, au watakuwa
pamoja na magaidi wa alShabaab.
"No freedoms are being curtailed
unless you are a terrorist yourself.
No part of our constitution has been
violated."
"The time has come for each and
every one of us to decide and choose
- are you on the side of an open,
free, democratic Kenya... or do you
stand with repressive, intolerant
extremists.
A m e ya s e m a h a y o U h u r u
Kenyatt a akitetea muswada
wa sheria ya kupambana na
ugaidi unaoshutumiwa kuwa
dhidi ya haki za kikatiba na za
kibinadamu kwa wananchi wa
Kenya. Akitangaza Vita dhidi
ya ugaidi kwa mara ya kwanza
ambapo aliita ni Crusade, Bush
alisema ama upo pamoja naye
(Marekani) katika vita hiyo au
upo pamoja na magaidi. Hakuna
nafasi ya ziada.
Sasa Rais Uhuru Kenyatta
naye anayasema hayo katika
kuchagiza Wabunge na Wakenya
kwa ujumla kuikubali sheria
mpya ya kupambana na ugaidi
iliyofikishwa bungeni. Sheria
hiyo imetajwa kuwa mbovu
kabisa inayokiuka katiba na
haki za binadamu. Inaelezwa
kuwa sheria hiyo inawaruhusu
maofisa wa vyombo ya dola
k u k a m a t a n a k u wa s h i k i l i a
watu kwa mwaka, bila hata
ya kuwafikisha mahakamani.
Inaelezwa kuwa muswada wa
sheria hiyo umebuniwa haraka
haraka kutokana na tukio la
kuuliwa watu 29 walioshushwa
katika gari na kupigwa risasi
baada ya kutambuliwa kuwa
ni Wakristo. Ikadaiwa kuwa
waliofanya mauwaji hayo ya
kikatili ni al-Shabaab.
Likielezea sheria hiyo, gazeti
la Daily Nation limeitaja kuwa ni
mzawa wa ile sheria maarufu ya
Marekani-US Patriot Act, ambayo
imejengwa juu ya dhana kuwa
namna bora ya kupambana na
ugaidi ni kuwa na Tifa la Kipolisi
(police state) ambapo vyombo vya
dola na jeshi vinaweza kuvunja
haki na uhuru wa yeyote bila ya
kuulizwa. Chini ya sheria hiyo,
hata kuandika habari za mtu
aliyeteswa na polisi kwa tuhuma
za ugaidi ni kosa lenye kutolewa
adhabu kali. Kama ni kuandika
mpaka upate kibali cha polisi.

Hii maana yake ni kuwa watu


watakamatwa na kuteswa hata
kuuliwa bila taarifa zao kujulikana
kwa sababu ni marufuku vyombo
vya habari kuandika habari hizo.
Hivi sasa, watu wanakamatwa
Kenya, kuteswa na hata kuuliwa
kinyume kabisa na sheria kama
ilivyoelezwa katika makala ya
Aljazeera. Watu wanajiuliza,
ikipitishwa sheria hiyo, hali
i t a k u wa j e ? Au n d i o s h e r i a
inatungwa kuhalalisha yale
ambayo yamekuwa yakifanywa
na kilichodaiwa kuwa ni kikosi
cha mauwaji kilichowauwa Sheikh
Aboud Rogo na Sheikh Makaburi?
Lakini kinachosikitisha zaidi
katika mjadala unaoendelea
Kenya juu ya sheria hii mpya
juu ya ugaidi ni kuwa, tatizo la
msingi na ambalo ndio linaitafuna
Kenya na wote waliozamishwa na
watakaokuja kuzamishwa katika
vita hii feki; halisemwi. Wabunge,
wanasheria, waandishi wa habari
na watetezi wa haki za binadamu,
wote wanachozungumzia ni juu
ya kuvunjwa haki za kikatiba
na haki za binadamu. Maswali
ya msingi ni je, sheria hizi (ziwe
zinavunja haki za binadamu au
la) na kuwa na vikosi maalum,
ndio utatuzi wa unaoitwa ugaidi
wa al-Shabaab? Je, tunamjua adui
tunayepigana naye? Ni adui wa
kweli au wa kufikirika? Adui
yetu ni nani? Au tunahangaika na
boya? Na boya hili katutupia nani
na kwa malengo gani? Kwa nini
al Shabaab wawe maadui zetu?
Je, wana uwezo huo wa kufanya
wanayodaiwa kufanya Kenya?
Al-Shabaab inapambana na jeshi
la serikali ya Somalia, al-Shabaab
inapambana na AMISOM, alShabaab inapambana na majeshi
ya Kenya yaliyoko Somalia, alShabaab inapigwa na Marekani
kutoka angani kwa kutumia
Drone. Al Sahaab hii ni dubwana
la namna gani la kushindana na
nguvu zote hizi? Je, yenyewe
inapata wapi silaha na uwezo wa
kukabiliana na nguvu zote hizo?
Uzoefu kutoka Yemen
My name is Fahd Abdullah
Ahmed Ghazy. I am a human being -a man -- who is loved and who loves.
Hayo ni maelezo ya mfungwa
wa Guantanamo-ISN 026, kijana
wa Kiyemen Fahd Abdullah
Ahmed Ghazy aliyekamatwa
mwaka 2001 akiwa na miaka 17.
Hivi sasa ana umri wa miaka 31
bado yupo jela na katika muda
wote huo hakuwahi kufikishwa
m a h a k a m a n i . M wa k a 2 0 0 7
vyombo vya usalama na vya

RAIS Uhuru Kenyatta wa Kenya.

GEORGE W. Bush, Rais wa


zamani wa Marekani.

kisheria vya Marekani, kwa


pamoja vilisema kuwa mtoto
Ghazy, hana hatia. Alikamatwa
kimakosa kwa hiyo aachiliwe.
Hata hivyo, mpaka sasa serikali
ya Barack Obama haijaweka
mipango ya kumwachia kijana
huyo na kumrejesha kwao Yemen,
kijiji cha Diwan, ambapo mkewe
mbichi kabisa aliyemwacha na
mimba, amekuwa akimlea pweke
binti yao Hafsa. Hafsa hivi sasa
ana umri wa miaka 13, hajawahi
kumwona baba yake wala baba
hajawahi kumwona mtoto wake.
Jina langu ni Fahd Abdullah
Ahmed Ghazy. Ni binadamu
-mwanaume - anayependwa na
anayependa.
Hapa, Guantanamo, sijawahi
kusikika. Napuuzwa tu. Katika
m i a k a 1 3 ya k i f u n g o b i l a
mashitaka, sijaweza kumweleza
mtu yeyote mimi ni nani hasa.
Ningependa kuwa na uwezo wa
kueleza kilichojiri katika miaka
13 ya Guantanamo. Akili yangu
inakwama ninapojaribu kufikiria
jambo hilo. Na sina maneno
yanayoweza kukufanya uelewe
kikamilifu.
Nakuasa: Uwe sauti ya wasio
na sauti - kwa ajili ya binadamu
mwingine ambaye anateseka.
Kwa vile sasa umesikia habari
yangu, huwezi kukwepa jukumu
la kunisaidia.
Hiyo ni kauli ya kijana Fahd
Abdullah Ahmed Ghazy kwa
wanasheria na watetezi wa haki za
binadamu. (Tazama: I Grew Up in
Guantanamo: Now That You Have
Heard My Story, You Cannot Turn
Away.)
I grew in Guantanamo,
nimekuliwa Guantanamo, ni
msemo anaopenda kuutumia
Ghazy akisimulia masaibu yake
kila anapoandika barua au kupata
fursa ya kuongea na watetezi wa
haki za binadamu na wanasheria.

Serikali ya Marekani inasema


kijana huyo hana hatia, lakini nani
atalipa dhulma hiyo? Kwa miaka
17 maisha na matarajio ya kijana
huyo, yamepotelea Guantanamo,
nani atamlipia hasara hiyo?
Guantanamo, ndio gereza
l a m a t e s o wa l i k o l u n d i k wa
watuhumiwa wa ugaidi kutoka
Yemen, Afghanistan, Pakistan,
Iraq n.k. Na tunaambiwa kuwa
kwa kukamatwa watu hao na
kufichwa, ni katika mikakati ya
kuondoa ugaidi. Labda tujiulize,
hali ikoje leo katika nchi hizo?
Na tukumbuke kuwa, pamoja
na kukamatwa kijana Ghazy
n a we n z a k e ( Ye m e n n d i y o
yenye wafungwa wengi zaidi
Guantanamo), Yemen iliweka
(wekewa na Marekani) mikakati
mingine ambapo ndege za
kivita za Marekani zilikuwa
zikishambulia na kuuwa watu,
halafu serikali inasema ni askari
wake wamefanya mashambulizi
hayo kukabiliana na ugaidi. Lakini
tukumbuke pia kuwa pamoja na
sheria na kuweka vikosi maalum,
Yemen ilipewa zawadi nyingine
ya kupambana na ugaidi: Ilipewa
Drone. Watu wakiuliwa kila
uchao. Lakini leo matukio ya
ugaidi ni mengi na ya kutisha
zaidi Yemen kuliko ilivyokuwa
mwaka 2001 alipokamatwa Fahd
Ghazy.
Hakuna mahali popote duniani
ambapo sheria kali na vikosi
maalum vya kupambana na
ugaidi vimefanikiwa kumaliza
tatizo. Bali uzoefu unaonyesha
kuwa kadiri unavyokokotwa na
kuingizwa katika vita hii na kadiri
unavyojizatiti kupambana, ndivyo
unavyozamishwa katika wimbi
la mashambulizi na umwagaji
damu.
Aliwahi kujisemea aliyekuwa
Waziri wa Mambo ya Nje wa
Inaendelea Uk. 7

Makala

AN-NUUR

SAFAR 1436, IJUMAA DESEMBA 19-25, 2014

Somo gumu kufahamika au ndio ushenga wa ajali!

Inatoka Uk. 6
Uingereza, Robert Finlayson
"Robin" Cook , kwamba, alQaida (A-Shabaab na wenzao) ni
magaidi wa kubuni na wa kutumiwa

na mabeberu kwa malengo yao.


Sasa labda ujiulize, vipi unaweza
kupambana na adui wa kubuni halafu
ukashinda?
Pamoja na matatizo waliyokuwa
nayo Somalia, vita vyao havikuwa
tatizo la Kenya, Uganda, Zanzibar
wala Dar es Salaam, ukiacha tatizo
la wakimbizi. Lakini tukaimbishwa
k u wa a l - S h a b a a b n i m a g a i d i
wa n a o h u s i a n a n a a l - Q a i d a h .
Tukaupokea wimbo tukaimba kwa
juhudi na mbwembwe nyingi mithili
ya zile nyimbo na ngonjera za John
Komba wa TOT, utadhani ni wetu
tulioutunga wenyewe!
Katika shambulio la Westgate
Shopping Mall, Nairobi. Tuliambiwa
magaidi kati ya 10 na 15 kutoka
Somalia waliigia Kenya wakiwa na
gari lililosheheni silaha wakaingia
katika kituo hicho maarufu cha
kibiashara na kuanza kuuwa watu.
Walivamia tarehe 21 Septemba 2013,
na kudumu katika jengo hilo hadi
24 Septemba ambapo ilidaiwa kuwa
watu 67 waliuliwa na wengine zaidi
ya 175 kujeruhiwa.
Polisi, vikosi maalum vya polisi,
Idara za Usalama za Ndani na Nje
ya Kenya na jeshi la Kenya, wote
hao walikuwa katika operesheni
ya kukabiliana na magaidi hao 15
kutoka Somalia! Vifaru na silaha
nyingine nzito za kijeshi, vikaonekana
vikiranda na kuzingira Nakumati.
Hata hivyo, vikosi vyote hivyo
havikufanikiwa japo kukamata au
kuuwa hata gaidi mmoja na kuonyesha
maiti yake! Magaidi wakafanya
waliyofanya, wakajiondokea zao
wakaacha huku nyuma wanajeshi,
serikali na wananchi wa Kenya,
wakiparurana kuwa badala ya
kupambana na magaidi, wanajeshi
walikuwa wakipora mali na kulewa.
Ta a r i f a z a k u i n g i a m a g a i d i
Nakumati, Westgate, Nairobi,
zilipambwa na kusindikizwa na
visa vyingi vilivyonogeshwa zaidi
na vyombo vya habari vikiwa vile
vilivyopigiwa zumari kuonyesha jinsi
magaidi hao al-Shabab walivyokuwa
katili kwa Wakristo. TV na magazeti
yakaandika na kupamba kwamba
magaidi hao walikuwa wakiwapa
mateka wao mtihani, anayefaulu
kuthibitisha kuwa ni Muislamu
anaachwa, anayefeli anapigwa
risasi kichwani. Lakini tukaambiwa
pia kuwa hata watoto wadogo
wakithibitika kuwa ni Wakristo,
walikuwa wakibamizwa vichwa
vyao katika ukuta au mikono yao
kukatwa ikachongwa na kufanywa
kalamu za kuandikia huku damu
ikifanywa wino. Vyombo vya habari
vikasherehesha sana habari hizi.
Mpaka tukio linamalizika,
ishawekwa ushahidi kuwa wapo
magaidi wanaoitwa al-Shabaab weye
uwezo wa kushinda polisi, Idara
ya Usalama ya Kenya na Jeshi lote
la Kenya likipewa msaada kutoka
Israel na Uingereza! Lakini maadhali
tuliambiwa kuwa walikuwepo
makachero wenye silaha nzito wa
MOSSAD na wale wa Uingereza

James Foley (iwe alichinjwa kweli au


la), akapata uungwaji mkono kutoka
ndani ya Bunge na kwa wananchi.
Kilichotangulia kupitishwa kwa
US Patriot Act, ni kilichodaiwa
kuwa ni ugaidi wa kimeta (Anthrax
Terror Attack). Watu, wakiwemo
wabunge na waandishi wa habari

MAREHEMU Ibrahim Rogo.


(na Marekani?), ni kwamba tukio
liliweka muhuri pia kuwa magaidi
hao ni hatari mno kiasi kwamba
hata wazito hao wa kidunia katika
vita na ukachero, hawana ubavu wa
kukabiliana nao!
Maadhali ushaweka msingi huo,
na maadhali ushakubali kuwa una
kitisho hicho cha ugaidi wa kiwango
hicho, katika ulimwengu huu wa Vita
dhidi ya Ugaidi, yaliyosalia au tuseme
yatakayokuja kufanyika baadae
ili kuendeleza vita ya wenyewe
mabeberu dhidi ya ugaidi, wala
hutakuwa na udhibiti nayo. Huo
ndio ukweli. Kuiga US Patriot Act na
kuifanya sheria yako ya nchi, unazidi
tu kujitosa katika balaa.
Yaliosemwa na Aljazeera
Wiki iliyopita kituo cha Aljazeera
kilitoa makala iliyodai kuwa Kenya
kuna kikosi cha mauwaji ambacho
ndicho kinachohusika na kuuliwa
Masheikh na watu mbalimbali
wa n a o t u h u m i wa k wa u g a i d i .
Wanahojiwa maofisa wa vyombo
vya usalama na kutoa ushuhuda wa
kutisha. Japo hawaonyeshwi sura,
lakini ni jambo la uhakika kwamba
serikali inaweza kupitia taratibu zake
ikawatambua watu wale. Swali ni je,
maofisa wale walipata wapi ujasiri
ule wa kuiumbua serikali? Lakini
pia pale inatajwa Israel, Uingereza
na Marekani. Na tunafahamu kuwa
Aljazeera makao yake yapo Qatar, na
Qatar inafahamika nafasi yake katika
ushirika wake na mataifa hayo katika
vita dhidi ya ugaidi. Ukiyatizama yote
haya, lazima ikupe wasiwasi kuwa
huenda haya makala yametolewa
makusudi kwa malengo maalum.
Kwa sababu kwanza hakuna namna
ambayo mwandishi wa Aljazeera
angezipata taarifa zile za siri, na kama
si kwa kuruhusiwa hakuna namna
ambayo watumishi wale wa vyombo
vya dola wangeyasema waliyosema.
Makala yanaonyesha jinsi Masheikh
na Waislamu wanavyouliwa na
vyombo vya dola. Kinachotarajiwa ni
kuwa Waislamu watapata hasira, na
ni jambo la kawaida. Wakipata hasira
kuna hatua watachukua.

MAREHEMU Aboud Rogo.


Binafsi nahisi kuwa pengine
ilitarajiwa kuwa kwa yote
yaliyokwishafanyika, sasa Kenya
kungekuwa hakukaliki. Wameuliwa
Masheikh na Waislamu mbalimbali
kikatili na hadharani. Lakini pia
wa m e u l i wa wa l i o d a i wa k u wa
Wakristo pale Nakumati ikidaiwa
k u w a Wa i s l a m u w a l i w e k w a
kando kisha Wakristo wakapigwa
risasi. Juzi pia tunaambiwa kuwa
abiria wameshushwa katika basi,
ukionekana Mkristo kwa kutokuweza
kutamka Shahada au kusoma Aya ya
Quran, unapigwa risasi. Yote haya
kwa hali ya kawaida, labda ilitarajiwa
kuwa yangetosha kuilipua Kenya.
Hivi sasa Wakristo na Waislamu
wangekuwa wanashikiana bunduki,
mikuki, panga na pinde. Sasa labda
inaonekana mambo yanachelewa.
Pengine makala hii ya Aljazera
kuwaambia Waislamu wanauliwa
na vikosi maalum vya serikali, basi
mambo yatakwenda mbio mbio
Kenya kuzama katika machafuko.
Likipatikana tukio ambapo vijana
wa Kiislamu wa uhakika, si wa
kupandikiza, wamelipua kituo cha
polisi au kanisa, na likipatikana
tukio la uhakika ambapo Wakristo
watakuwa wamevamia Waislamu na
kuwauwa wakilipiza kisasi, bila shaka
huo utakuwa mtaji wa uhakika wa
kuleta yote yale tunayosikia ya Boko
Haram, Nigeria. Yatafanyika mambo
wala hutajua anayefanya nani, ila
kama kawaida utaaambiwa magaidi
wa al-Shabaab wamekiri kufanya!
Hiki ni kitendawili na dilema kwa
Wakenya . Itabidi watafakari na
kunoa bongo zao vyema katika
kukitegua. Lililo la ukweli na uhakika
ni kuwa, njia anayotumia Rais Uhuru
Kenyatta, haitaisaidia Kenya zaidi ya
kuizamisha zaidi katika mauwaji na
umwagaji damu. Swali ni je, Rais na
vyombo vyake hawayajui haya?
Tunayo ya kujifunza
kutoka US Patriot Act
Rais Barack Obama alipotaka
kupeleka jeshi Iraq/Syria kukabiliana
na ISIS, alipata upinzani mkali. Lakini
mara baada ya tukio la kuchinjwa
mwandishi wa habari wa Kimarekani

wakatumiwa barua ndani yake


kukiwa na vimelea vya kimeta.
Miongoni mwa watu waliotumiwa
kimeta hicho ni wabunge wawili
waliokuwa wapinzani wa sheria
hiyo, Maseneta Tom Daschle
(South Dakota) na Patrick Leahy
(Vermont. A), wote wa chama
cha Democrat. Na ili ngoma
ipate wachezaji wenye sauti
yenye kupaa hadi mbali, kimeta
kikatumwa pia kwa vyombo vya
habari kama ABC News, CBS
News, NBC News, New York Post
na National Enquirer.
Baada ya watu watano (5) kufa
na wengine kuambukizwa na
kuwahi kutibiwa, huku ushahidi
wa kisanii ukiachwa kuwahusisha
Waislamu/Al-Qaida, na ugaidi
huo, upepo ukabadilika. Bunge
likaunga mkono USA Patriot
Act ikapitishwa haraka haraka,
na sisi huku tukamegewa. Pius
Msekwa wakati huo Spika wa
Bunge akachagiza Wabunge kule
Dodoma sheria ikapita.
Sasa leo gazeti la Daily Nation
la Kenya linasema kuwa Sheria
hii mpya anayokuja nayo Uhuru
Kenyatta inaletwa kutokana
na matukio ya kuuliwa watu
64 hivi karibuni halikadhalika
kuongezeka kwa ujahidina kwa
vijana wa Pwani (Mombasa),
ambapo ilibidi polisi kuvamia
misikiti minne na kuifunga kwa
muda. Likiandika habari hizo
Daily Nation lilisema:
is a response to the slaughter of
64 people by Al-Shabaab, the Somali
group in the last fortnight and the
increasing radicalizing of youths by
Jihadists at the Coast and elsewhere.
Kwa Anthrax Terror Attacks
iliyoibua US Patriot Act, ilichukua
miaka minne (Septemba 2001Aprili 4, 2005) hadi kuanza
kuvuja na kusambaa habari kuwa
kumbe kile kimeta kilichodaiwa
kutoka kwa Waislamu wa Iraq/AQaidah, kilitoka katika maabara
za kijeshi za Marekani, Fort
Detrick in Frederick, Maryland.
Hadi sasa kesi iliyofunguliwa
juu ya waliosambaza kimeta
hicho imekwama kwa sababu
mtuhumiwa mkuu Dr. Bruce
Edwards Ivins, alikufa kifo
cha kutatanisha Julai 29, 2008,
ikidaiwa kuwa alijiuwa kwa sumu
ya acetaminophen.
Hatujui itachukua muda gani
kujua ukweli juu ya tukio la
kuuliwa watu 64 linalotumiwa
kama sababu ya kupitisha haraka
haraka sheria hii ya kupambana
na ugaidi Kenya. Tusubiri!

Makala

AN-NUUR

SAFAR 1436, IJUMAA DESEMBA 19-25, 2014

Sababu za magonjwa ya meno na jinsi ya kujitibu


Na Juma Kilaghai

LEO tutazungumzia sababu


zinazopelekea tuugue
maradhi ya meno, na hatua
tunazopaswa kuchukua
kulinda afya ya vinywa
vyetu, ili kupunguza
uwezekano wa kuingia
katika mazingira ambayo
yanaweza kuwa hatarishi
kwetu.
Pamoja na mambo mengine,
hatua hizi zitatusaidia
kupunguza uwezekano wa
kupata maradhi ya meno.
Tukipunguza uwezekano
wa kupata maradhi ya meno,
tutapunguza uwezekano
wa kukutana na aina ya
matibabu ambayo yanaweza
yakatusababishia matatizo
zaidi ya kiafya.
Magonjwa ya meno,
kama yalivyo magonjwa
mengi mengine, ni dalili au
kiashiria tu (signal) kuwa
kuna tatizo katika eneo fulani
la miili yetu. Aghalabu kiini
cha tatizo kinakuwa kiko
mbali kabisa na eneo dalili
inapoibukia. Tunapoacha
kusaka kiini cha tatizo,
tukahangaika kupigana na
dalili, matokeo yake aghalabu
huwa ni mabaya zaidi. Kwa
bahati mbaya sana hii ni
falsafa ambayo imeupiga
chenga mfumo wa tiba wa
Kimagharibi. Na ni bahati
mbaya zaidi, kuwa huu ndio
mfumo tunaoutambua kama
wa kisasa, ama mfumo rasmi
wa tiba. Kwa kulitambua
hili, leo tutajikita zaidi katika
falsafa inayotumiwa zaidi
na wadau wa tiba mbadala.
Kwa wadau hawa kwao tiba
ni kuondoa kiini cha tatizo
na siyo kuhangaika na dalili.
Kwa mfano, unapoumwa
na jino na ukakimbilia
kulitoa, huko ni kuhangaika
na dalili. Utaratibu mzuri
ungekuwa ni kujiuliza hivi
ni kitu gani kimepelekea
jino hilo likaanza kuuma,
na ukishagundua kiini
cha tatizo uchukue hatua
za kuondoa kiini cha tatizo
hilo. Kwa utaratibu huu,
siyo tu kwamba utakuwa
umetibu jino linalokusumbua
kwa wakati huo, lakini pia
utakuwa umetoa ulinzi kwa
meno yako mengine ambayo
kwa wakati huo yatakuwa
bado hayajaanza kuuma.
Pamoja na kwamba ziko
sababu kadhaa zinazoweza
kumpelekea mtu kupata
maradhi ya meno, sababu
kubwa ni mbili. Sababu hizi
ni:
1. Chakula; na
2. Usafi wa kinywa.
Chakula
Kila chakula ni mjumuiko
wa viambata vya kikemikali
(chemical components)
a m b a v y o h u f a n ya k a z i
kwa pamoja vikiwa katika
hali ya mizania (balance).
Uchakatuaji (processing)
hundosha mizania iliyopo
na kuvuruga utaratibu

wa kiambata kimoja
kutegemea kingine kufanya
kazi iliyodhamiriwa
bila kusababisha athari
mbaya. Kadri kiwango cha
uchakatuaji kinavyozidi
kuwa kikubwa, ndivyo
mizania baina ya viambata
inavyozidi kupotea,
na ndivyo athari mbaya
zinavyozidi kuongezeka
kwa mtumiaji wa chakula
kilichopitia mchakato huo.

metals). Yaliyo maarufu


zaidi miongoni mwa madini
haya ni sodiumu (sodium),
potasiamu (potassium),
magnesi (magnesium), na
kalisi (calcium).
Kadri namba kwenye
kipimo cha pH inavyozidi
kuwa ndogo kuelekea 0,
ndivyo ukali wa tindikali
husika unavyoongezeka,
na kadri namba kwenye
kipimo hicho inavyozidi

Katika vyakula vya


wa n g a ( c a r b o h y d r a t e s )
vilivyochakatuliwa kwa
kiasi kikubwa, mizania ya
viambata imeegemea sana
k we n ye s u k a r i n ye p e s i
(simple sugars). Hii ni kwa
sababu katika uchakatuaji
huo viini hai (protini), mafuta
(fats), vimengenya (enzymes)
na nyuzi lishe (fibers)
kuondolewa. Hii ina maana
kwamba mtu anayekula sana
vyakula hivi huingiza kiasi
kikubwa sana cha sukari
m w i l i n i m wa k e ; s u k a r i
ambayo haina viambata
mwenza vya kuizuia
isisababishe athari mbaya
mwilini. Moja ya sukari
hizi, fructose, inatuhumiwa
kupelekea kuzaliwa kwa
kiwango kingi cha tindikali
mkojo (uric acid), wakati wa
kuchakatuliwa kwake ndani
ya mwili.
Tindikali ni kitu
chochote kile ambacho
kinapoyeyushwa kwenye
maji huongeza idadi ya
chembechembe zenye kubeba
umeme chanya. Kipimo
kinachotumika kutambua
ukali wa tindikali na vitu
vingine vilivyoyeyushwa
kwenye maji na kutengeneza
vimiminika huitwa kipimo
cha pH. Kipimo hiki
kimegawanywa katika
tarakimu kuanzia 0 hadi 14.
Kwa kawaida kimiminika
chochote ambacho pH yake
ni kati ya namba 0 na namba
7 huhesabika kama tindikali
(acid), na kile ambacho pH
yake ni kati ya namba 7 na
namba 14 huhesabika kuwa
ni alikali (alkali). Namba 7 ni
pH ya maji halisi yasiyo na
chochote kilichoongezewa
ndani yake.
Alikali ni chumvi yoyote
ile inayotokana na madini
yanayojulikana kama
madini ya alikali na yale
yanayojulikana kama madini
ya alikaline (alkaline earth

kuwa kubwa kuelekea 14,


ndivyo ukali wa alikali
husika unavyoongezeka.
Kimaumbile ukiondoa
majimaji yaliyomo katika
mfuko wa tumbo ambayo
yana pH ya kati ya 1 na
5 kutegemeana na kama
umekula, au hujala; na kama
umekula, aina ya chakula
ulichokula, vimiminika
vingine vinavyokuwemo
mwilini muda wote vina pH
kati ya 7 na 8.
Ukiondoa ukweli kwamba
tindikali mkojo inaposimama
kama yenyewe ina madhara
mengi mwilini, lakini pia
huchangia katika kuongeza
kiwango cha mkusanyiko
wa tindikali mwilini kutoka
k a t i k a v ya n z o v i n g i n e
mbalimbali. Vyanzo hivi
vingine ni pamoja na:
1. Vyakula vyote vya aina
ya protini (protein);
2. Vyakula vyote vya
aina ya wanga (hata kama
havijachakatuliwa);
3. Matunda aina ya
cranberry; na
4. Mchakato wa kuishi
(yaani kupumua, kuona,
kusikia, kufikiri, kutembea,
nakadhalika).
K u wa h a i n i k i t e n d o
kinachohitaji matumizi
makubwa ya nishati. Kila seli
za mwili zinapozalisha nishati
hii na kisha kila inapotumika,
moja ya mazao ya vitendo
hivyo ni kuzalishwa kwa
tindikali. Hii ina maana
kwamba kila sekunde
tindikali inaongezeka ndani
ya mwili. Ongezeko hili ni
hatari sana kiafya iwapo
hatua sahihi hazichukuliwi
kukabiliana nalo.
Tindikali hupoozwa
kwa alikali. Kwa sababu hii
tunahitajika tuwe tunakula
kwa wingi vyakula vyenye
madini ya alikali au yale ya
alikaline. Vyakula pekee
vinavyoweza kutupatia kiasi
kikubwa cha madini haya

ni vile vya mchanganyiko


wa mbogamboga za majani,
na vile vya mchanganyiko
wa matunda. Kwa bahati
mbaya sana wengi wetu
tunakula vyakula hivi vikiwa
chini ya kiwango halisi cha
mahitaji ya miili yetu. Hali
hii huilazimisha miili yetu
kutafuta njia mbadala ya
kujitetea dhidi ya tindikali
nyingi inayoongezeka
mwilini.
Moja
ya
hatua
zinazochukuliwa na mwili
dhidi ya ongezeko kubwa
la tindikali mwilini pale
kunapokuwa hakuna alikali
ya kutosha kutoka kwenye
lishe, ni kutoa ishara kwa
mifupa kuanza kuachia
madini ya kalisi (calcium)
kuingia kwenye mzunguko.
Kitendo hiki kinachukuliwa
kama cha dharura
kinacholenga kuusadia mwili
kufanya kazi ya kuipooza
tindikali iliyojilundika.
Hapa mwili unatatua
tatizo kwa kutengeneza
tatizo jingine, lengo likiwa ni
kujihifadhi na hatari iliyoko
usoni. Hekima ya mwili hapa
ni kuwa unaweza kuishi na
mifupa iliyodhoofika, lakini
huwezi kuendelea kuishi
na kiwango kikubwa cha
tindikali kinachojilundika
m w i l i n i ! M w i l i wa k o
unakutarajia uchukue hatua
madhubuti na za haraka
kuijiondoa katika dharura
hii. Ni kama vile pale
gari yako inapolazimika
kutembelea gurudumu la
akiba. Matarajio ni kwamba
utachukua hatua za haraka
sana kuhakikisha kuwa
kitendo hicho kinakuwa ni
cha muda mfupi. Kwa kifupi
kinachotarajiwa na mwili
wako ni kuurejeshea mwili
huo akiba ya kutosha ya
madini ya alkali au yale ya
alikaline, tena bila kuchelewa.
Meno, kama ilivyo mifupa
mingine mwilini, huathiriwa
pia na hali hii ya kupoteza
madini ya kalisi pale
tindikali inapozidi mwilini.
Dalili kubwa kwamba mtu
umeathiriwa na hali hii ni
udhaifu unaodhihirishwa na
meno yako pale yanapoanza
kukatika na kumeguka
hovyo.
Tindikali pia inapozidi
mwilini hufikia pahala
ikaanza kubadilisha pH za
vimiminika (body fluids)
mbalimbali vilivyoko
kwenye mwili. Vimiminika
hivi ni pamoja na damu,
mate, majimaji yaliyoko
katika mfuko wa tumbo,
majimaji yanayozalishwa
na ini na kongosho kwa
ajili ya uchakatuaji wa
chakula kwenye utumbo
mwembamba, majimaji ya uti
wa mgongo, manii, machozi,
nakadhalika.
Iwapo tindikali
inayozalishwa mwilini kila
sekunde na kujumuika na ile
inayotoka kwenye lishe kama
tulivyoona haitapoozwa,

basi italundikana na kuanza


kubadilisha vimiminika
mwilini kutoka hali ya
ualikali (pH 7 -8) na kuwa
katika hali ya utindikali (pH
chini ya 7).
M o j a ya v i m i m i n i k a
vya mwili vinavyoweza
kuathiriwa na hali hii ni
mate. Wingi wa tindikali
mwilini unaweza kupelekea
mate kupoteza hali yake
ya asili ambayo ni alikali
dhaifu (slightly alkaline),
na kubadilika kuwa katika
hali ya utindikali. Hili
likitokea meno yatakuwa
katika mazingira ya kupata
madhara zaidi kwa sababu
sasa yatakuwa yanaogelea
m o j a k wa m o j a k a t i k a
bahari ya mate yenye hali
ya utindikali. Hii ina maana
kwamba sehemu kubwa ya
madini ya kalisi yaliyoko
k w e n y e m e n o i t a k u wa
inayeyuka moja kwa moja
kutoka kwenye meno na
kuingia kwenye mate kwa
lengo la kupooza tindikali
kwenye mate hayo. Kwa
kuwa sehemu kubwa ya
kalisi itakayoyeyuka ni ile
iliyoko kwenye jino kwa
nje, sehemu ya ndani ya jino
itapoteza kinga yake dhidi
ya hali kama za joto, baridi
na ukakasi. Wale wote wenye
malalamiko ya meno yao
kuathiriwa na joto, baridi na
hata vitu vyenye ukakasi,
basi wajue kuwa moja ya
sababu kubwa za hali hiyo
ndiyo hiyo tuliyoielezea.
Kujilinda dhidi ya
uharibifu wa meno na mifupa
mingine unaosababishwa na
tindikali unahitaji kufanya
mabadiliko makubwa katika
l i s h e ya k o . Wa t a a l a m u
wanasema ili kuuweka mwili
katika viwango vya tindikali
ambavyo havina madhara
kiafya asilimia themanini
ya chakula chako kwenye
sahani iwe ni mbogamboga
na matunda, na asilimia 75
ya mbogamboga na matunda
hayo viwe katika hali ya
ubichi.
Usafi
Mabaki ya vyakula vya
wanga vilivyochakatuliwa
k wa k i wa n g o k i k u b wa
yanayokuwemo mdomoni
baada ya kula pia yanakuwa
na kiwango kikubwa cha
sukari kama hivyo vyakula
vyenyewe. Sukari hii ni
kivutio kikubwa mno cha
bakteria wa aina ya gram
positive. Bakteria hawa
wa n a p o i n g i a k i n y wa n i
kwa nia ya kufuata mabaki
ya vyakula, hujikuta
wakishambulia na meno
pia, hasa pale meno hayo
ya n a p o k u wa n i d h a i f u
na ambayo hayafanyiwi
usafi wa kina. Matokeo
ya mashambulizi haya ni
uharibifu zaidi kwa meno, na
hatimaye maumivu.
Wa t u w e n g i h u w a
Inaendelea Uk. 12

Makala

AN-NUUR

SAFAR 1436, IJUMAA DESEMBA 19-25, 2014

CHAI YA AJABU!

Ni kitu gani cha ajabu juu ya hii chai tuliyochagua kuiita Haiiba Timamu Tea?
Na. Juma Killaghai

PINGILI YA UTI WA MGONGO YAPONA!


Mimi nilikuwa mtu wa kwanza
kabisa kushuhudia maajabu ya hii
chai. Niilibuni hii chai kama jaribio
la kutibu pingili yangu ya mwisho
ya uti wa mgongo (karibu na kiuno)
ambayo ghafla ilikuwa imeanza
kunipa maumivu makali, haswa
mida ya asubuhi baada ya kuamka.
Siyo siri, nachukia mno dawa za
kifamasia. Kutokana na kutozipenda
dawa hizo niliamua nichukue
kwanza sheria mkononi, na iwapo
itashindikana ndipo nijisalimishe
kuzitumia! Kwa sababu kitaaluma
mimi ni mkemia mtafiti wa vitu
asili vyenye uhai (organic natural
products research chemist) niliamua
kufanya utafiti. Kama ilivyo ada
hatua ya kwanza ya utafiti wowote ni
utafiti wa nyaraka (literature review).
Kimsingi utafiti wangu uliishia katika
hatua hii, kwani kupitia nyaraka
mbalimbali stahiki niliweza kubaini
mimea kadhaa ambayo ilikuwa na
mwelekeo wa kuweza kunitatulia
tatizo langu. Baada ya tafakuri ya
kina niliamua kubuni mchanganyiko
wa mimea hii katika muundo ambao
mtumiaji angetumia kama chai.
Kama nilivyotangulia kusema,
nikawa mtu wa kwanza kabisa
kuitumia hii chai. Maajabu! Ndani ya
siku tatu za matumizi maumivu yale
ya pingili yalitoweka na hadi leo sijui
yalikopotelea. Huu ni karibu mwaka
wa tano sasa! Kufuatia matokeo haya
ya kustaajabisha niliamua kuiita chai
hii HAIIBA TIMAMU TEA
HAPA CHINI NITAELEZEA VISA VINGINE
VICHACHE VYA KWELI AMBAVYO NADHANI
VINAHALALISHA KUIITA CHAI HII KUWA NI
CHAI YA AJABU!
1. MKE WANGU APONA MAUMIVU SUGU
YA KICHWA!
Baada ya kupona maumivu ya
pingili yangu ya uti wa mgongo,
nilipata hamasa ya kuishawishi
f a m i l i a ya n g u k u t u m i a c h a i
iliyonitibu. Baada ya siku chache
mke wangu alinipa siri yake ya
muda mrefu. Alisema kuwa alikuwa
akikabiliwa na maumivu ya kichwa
ya muda mrefu na alikuwa amejaribu
matibabu mbalimbali ya hospitali
bila kuniambia lakini haikuwa
imemsaidia. Aliniambia kuwa baada
ya mimi kuwahamasisha watumie
HAIIBA TIMAMU TEA aliamua
kujaribu japo kwa shingo upande
lakini alishangaa kuwa baada ya
siku chache maumivu yote yalikuwa
yametoweka!
2. ARUDIA KULA NYAMA NYEKUNDU!
Siku moja alikuja rafiki yangu
mmoja akadai kwamba kila
alipokuwa akila nyama nyekundu
alikuwa anapata maumivu makali
kwenye viungo (joints) haswa kwenye
vifundo vya vidole. Nilimwambia
kuwa uwezekano mkubwa ni kuwa
alikuwa anakabiliwa na ugonjwa wa

jongo (gout). Kwa kuwa rafiki yangu


huyu anafahamu kuwa nafanya tafiti
za tiba mbalimbali zinazotokana
na mimea na viumbe hai vingine
aliniuliza iwapo nilikuwa na dawa.
Nilimjibu kuwa nilikuwa nimebuni
chai fulani inayoitwa HAIIBA
TIMAMU TEA ambayo pengine
ingeweza kumsaidia. Siku chache
baadaye alinifuata akaniambia kuwa
baada ya kutumia CHAI niliyompa
tatizo lake lilikuwa limekwisha
na alikuwa ameanza kula tena
nyama nyekundu bila kuathiriwa na
maumivu makali ya viungo.

3. NAONA RIZKI YANGU IMEFIKIA


UKINGONI!
Siku moja rafiki yangu mwingine,
bwana Chake Bakari Nyumba
(kaniruhusu nimtaje na nitoe namba
yake ya simu kama kuna mtu
anataka kufanya ithbati ya haya
maelezo), alinipigia simu akidai
kwamba anahisi riziki yake duniani
imekwisha. Nilipomuuliza ni kwa
nini anasema hivyo alijibu:
Wala sijui hata ninaumwa nini.
Najisikia hovyo kabisa. Siwezi kula
chochote!
Nilimwambia ajaribu chai ya
HAIIBA TIMAMU. Baada ya siku
chache nilimpigia simu kuumuliza
alikuwa anaendeleaje akanambia
kuwa alikuwa mzima kabisa! Namba
ya simu za bwana Chake Bakari ni
0754415161/0715159159
4 . H A L I N I M B AYA W A L A S I J U I
NINACHOUMWA!
Jirani na ofisini kwangu mtaa
wa Mosque, Kitumbini (mkabala
na msikiti wa Sunni) liko duka
la vyombo vya nyumbani la KD
Sundries. Duka hili liko kwenye kona
ya mitaa ya Mosque na Mshihiri.
Ni duka maarufu kwa vyombo vya
kila aina vya nyumbani. Mmoja wa
wafanya kazi wa duka hilo anayeitwa
Rajab Bakari Amani ni rafiki yangu
wa muda mrefu (kanipa ruksa
nimtaje na kutoa namba yake ya simu
iwapo kuna mtu atataka kuhakiki
taarifa hii). Siku moja, mida ya saa
4 hivi asubuhi, nikiwa ndio kwanza
nimefika mjini nilipita nje ya duka la
KD Sundries nikiwa njiani kuelekea
ofisini kwangu. Nilimkuta Rajab
akiwa ameketi nje ya duka huku
akiwa amejikunyata (mida hiyo duka
lao bado lilikuwa halijafunguliwa).
Nilisimama kumsabahi na kumuuliza
ni kwa nini alikuwa katika hali ile.
Brother, hali yangu ni mbaya
sana, wala sijui naumwa nini! Karibu
wiki ya tatu sasa
Alinambia.
Hospitali umekwenda?
Nimekwenda lakini sijaona
matokeo yoyote ya maana!
Du! Sasa mbona umekuja kazini
kama hali ndiyo hiyo?
Nilimuuliza.
Sasa kaka nitafanya nini? Si
unajua kazi zetu hizi? Muhindi
hawezi kukuelewa hata siku moja
kuwa umelala nyumbani, hasa kwa
sababu haielweki utalala mpaka lini!
Kuna dawa fulani hivi, labda
nikupe uijaribu

Nilimwambia.
Kaka utakuwa umeniokoa kaka!
Nilimpatia Rajab pakiti moja ya
chai ya HAIIBA TIMAMU nikampa
maelekezo jinsi ya kuitumia. Maajabu!
Siku iliyofuata nilikutana na Rajab
akiwa mchangamfu na akanambia
kuwa hakuwa anajisikia kuwa na
tatizo lolote!
Namba ya simu ya Rjabu ni:
0712242557
5. BABA KAWEZA KWENDA MJINI!

Kuna jamaa yangu mmoja ni


mtaalamu wa shughuli za usafi
na bustani. Huyu tumekuwa naye
kwa miaka kadhaa tukishirikiana
kila ninapopata kazi za kandarasi
zinazohusiana na shughuli za usafi na
bustani. Huyu jamaa yangu siku moja
alinifuata akaniambia kuwa alikuwa
anataka kusafiri kwa siku chache
kwenda kijijini kuwasalimia wazazi
wake. Aliniambia kuwa nimpatie chai
ya HAIIBA TIMAMU ampelekee baba
yake akaijaribu kwa kuwa kwa muda
mrefu amekuwa akisumbuliwa na
matatizo mengi ya kiafya. Nilimpatia
huyu jamaa yangu pakiti mbili za hii
chai tukaagana. Siku chache baadaye
huyu jamaa yangu alirejea kutoka
kijijini. Nilishangaa kuwa alikuwa
akitabasamu kila mara aliponiona
kinyume na kawaida yake. Siku mbili
baadaye udadisi ulinizidi nikaamua
kumuuliza kilichokuwa kinaendelea.
Baba alienda mjini!
Aliniambia.
Kwani huwa haendi mjini?
Nilimuuliza kwa mshangao.
Anakwenda lakini ni lazima
afuatane na mtu. Alishashindwa
kwenda mwenyewe siku nyingi
zilizopita!
Sasa imekuwaje?
Nilimuuliza.
Baada ya kuitumia hiyo chai
yako si kafunga safari peke yake hadi
Moshi mjini na kurudi!
Du!
Nilipigwa na mshangao. Pamoja
na kwamba miye mwenyewe ndiye
mtengenezaji wa hiyo chai nilikuwa
napata tabu kuamini nilichokuwa
nakisikia!
6. SHEMEJI USIPONISAIDIA SIJUI WAPI
PENGINE PA KWENDA!
Siku moja nilirejea nyumbani
kiasi cha saa 4 usiku huku nikiwa
nimechoka sana. Nilifadhaika
nilipoona kuna mgeni, kwani nilijua
kuwa suala la kuoga na kupumzika
mara moja halikuwepo tena. Mgeni
mwenyewe alikuwa ni rafiki ya mke
wangu ambaye alikuwa anaishi mtaa
wa tatu kutoka pale kwetu. Baada ya
kusabihiana mke wangu alinitaka
tuingie chumbani. Huko chumbani
aliniambia kuwa shoga yake alikuwa
amekaa muda mrefu akinisubiri kwa
imani kwamba ningeweza kumsaidia.
Kwani ana shida gain?
Niliuliza.
Anasema anaumwa. Naona ni
bora umsikilize mwenyewe
Sasa wewe umemwambia kuwa
mimi naweza kumtibu
Niliuliza.

Mimi sijamwambia. Ila


kangangania kwa sababu kipindi kile
ulimpa ile dawa ya jino ikamsaidia
Du! Sasa itakuwaje? Anyway
hebu ngojea nimsikilize
Nilisema.
Rafiki yake mke wangu aliniambia
k u wa a l i k u wa a n a m u d a wa
juma zima anajisikia mwili wote
unamuuma, kichwa kimekaa hovyo
hovyo kabisa na kwa ujumla hana
amani kabisa.
Sisi tunatibiwa katika vituo vya
afya vya AAR. Nimezunguka vituo
vitatu tofauti sijaona tofauti yoyote.
Shemeji usiponisaidia sijui wapi
pengine pa kwenda!
Aliniambia.
Nilimwambia asubiri nikalelekea
chumbani. Alikuwa ameniweka
kwenye mazingira magumu kweli
kwa kule kujenga kwake imani kuwa
mimi ndiye niliyekuwa msaada
pekee. Wakati natafakari cha kufanya
mke wangu aliingia.
Nilimwangalia kwa mfadhaiko.
Huyu rafiki yako ananipa mtihani
kweli! Sasa tutampa nini? Labda
jaribu kumpa hizo pakiti mbili za
TIMAMU TEA zilizobaki hapo
Nilimwambia.
Siku mbili baadaye nilimuuliza
mke wangu.
Hivi shoga yako anaendeleaje?
Bwana we! Nilisahau kukwambia.
Anakushukuru sana! Bukheri wa
afya
7. HEDHI ISIYOKATA!
Kwa kumalizia nielezee visa
vitatu vilivyoletwa na jamaa watatu
tofauti ambao walidai kuwa wake zao
wanasumbuliwa na kutokwa na hedhi
isiyokata! Niliwashauri kuwa siyo
sahihi kutafuta dawa za KIENYEJI
bila kwanza kupata vipimo vya kisasa
ikajulikana wanaumwa nini.
Kwa nyakati tofauti kila mmoja
alirejea na kuniambia kuwa wake
z a o wa m e f a n y i wa v i p i m o n a
kugundulika kuwa wana saratani za
shingo ya uzazi.
Nimesikia kuwa una dawa!
Ilikuwa ni kauli ya kila mmoja.
Kiukweli miye dawa ya ugonjwa
huo sina. Hata hivyo iko dawa moja
hivi ambayo mchanganyiko wake
pengine inaweza kusaidia. Hata hivyo
itabidi mgonjwa akubali kuitumia
kwa muda mrefu
Yalikuwa ndio majibu yangu kwa
kila mmoja.
M a a j a b u ! K i l a m m o j a k wa
wakati wake alitoa taarifa kuwa
hedhi iliyokuwa inamtoka mkewe
mfulululizo ilikuwa imekata na
maumivu yametoweka. Saratani
imepona? Hilo miye sijui. Ushauri
niliompa kila mmoja ni kuwa kama
hali ya uchumi inaruhusu mgonjwa
aendelee na matumizi ya TIMAMU
TEA kwa walau miezi sita zaidi
mfulululizo.
Ukitafakari kwa undani kunaweza
kusiwe na maajabu yoyote katika
huu uwezo wa HAIIBA TIMAMU
TEA. Magonjwa mengi ya kimfumo
yanasababishwa na upungufu wa
Inaendelea Uk. 12

10

Makala ya Mtangazaji

AN-NUUR

SAFAR 1436, IJUMAA DESEMBA 19-25, 2014

Arab League chief visits Paris to seek support for Palestine UN bid
CAIRO (Ma'an) -- Arab League
secretary-general Nabil alArabi has started coordination
with regional states over a joint
plan to recruit support for the
Palestinian UN bid setting a
2-year deadline for ending
the Israeli occupation of the
Palestinian territory.
The official Palestinian news
agency Wafa reported Monday
that al-Arabi left for Paris Monday
where he was set to meet with
Foreign Minister Laurent Fabius.
That meeting and another
with US Secretary of State John
Kerry are part of a plan in which
foreign ministers of member
states of the Arab League have
prepared recently to support the
Palestinian UN bid to end Israeli
occupation.
The plan, says Palestine's envoy
to the Arab League and assistant
secretary-general for Palestinian
affairs Muhammad Subeih, was
approved in Cairo on Nov. 29,
in the presence of President
Mahmoud Abbas.
France is also leading European
efforts to cobble together a
resolution which would require
a return to the Israeli-Palestinian
peace negotiations.
Several European parliaments
have called on their governments
to move ahead with the
recognition of a Palestinian state.

immediate investigation into the


death of Palestinian Minister Ziad
Abu Ein.
The statement said Japan was
shocked to learn about the
incident and expressed hopes that
it will not trigger more violence.
Meanwhile, Irish Foreign
Minister Charles Flanagan
condemned the murder and told
Palestines ambassador in Ireland,
Ahmad Abdul-Razeq, he had
instructed Irish ambassador to Tel
Aviv to inform the Israeli Ministry
of Foreign Affairs of Irelands

Portuguese Vote to Recognize


Palestine Supports Peace, says PLO
RAMALLAH (WAFA) - PLO
Executive Committee Member,
Hanan Ashrawi, said the
Portuguese parliaments vote in
favor of recognizing Palestine as
an independent state is a step
in the right direction for peace.
In a statement issued by the PLO
Executive Committee Department
of Culture and Information on
Sunday, She expressed hope
that the Portuguese government
would follow suit and officially
recognize Palestine on the 1967
borders with Jerusalem as its
capital.
Ashrawi said Palestinians
hope the Portuguese government
will work to end the military
occupation by holding Israel
a c c o u n t a b l e w i t h p u n i t i ve
measures for its flagrant
violations of international law
and Palestinian human rights.
On behalf of the Palestinian
leadership and the people
of Palestine, we express our
appreciation to the Portuguese
parliament for taking a principled
stand and overwhelmingly
voting to recognize the State of
Palestine, said the statement.
The Portuguese parliament is
the fifth European assembly to
recognize the State of Palestine
after the UK, Ireland, France and
Belgium.

condemnation.
Abu Ein died last Wednesday
during a peaceful Olive planting
event, during which Israeli Border
guards assaulted the protestors
and fired teargas canisters from
a close range. Abu Ein suffocated
and was no longer able to breathe
which led to his death.
A video footage released online
also showed a member of the
border guards unit pushing and
grabbing Abu Ein by the throat a
few moments before Abu Ein lost
consciousness and died.

Japan Urges Probe into Minister


Abu Eins Death
RAMALLAH (WAFA) The
Japanese Ministry of Foreign
Affairs in a statement published
on Monday called for launching

timing for membership is up to


its leaders.
Palestine secured an observer
status at a meeting of the ICC
in New York on December 8.
Palestinian President Mahmoud
Abbas had threatened that
Palestine would join the court
to sue Israel over crimes against
Palestinians.
Israel launched a 50-day war
on the Gaza Strip in early July.
About 2,140 Palestinians, mostly
civilians, including women,
children and elderly people, were

ISRAEL Soldiers

Palestinians have agreed to join


ICC to sue Israel: Official
Palestinian Ambassador to the
United Nations Riyad Mansour
says Palestinians have reached a
consensus to join the International
Criminal Court (ICC) to seek
justice against Israeli war crimes.
Addressing the 122 members
of the ICC for the first time on
Monday, Mansour said that
Palestinian have agreed to join
the tribunal in the hope of ending
Israeli crimes.
We view the ICC as the
international legal and peaceful
mechanism to combat impunity
and seek accountability and
justice, Mansour said.
It is the court where the
Palestinian people desire to seek
justice for the war crimes and
crimes against humanity being
perpetrated against them by
Israel, the occupying power, he
said.
The Palestinian official added
that Palestine may very well
be the 123rd state party to the
international tribunal but the

killed in the Israeli onslaught.


Around 11,000 others were
injured. Tens of Israeli soldiers
were also killed by the Palestinian
resistance retaliatory attacks.
On November 29, 2012,
the 193-member UN General
Assembly voted to upgrade
Palestines status to non-member
observer state.
Israeli Army Closes Highway to
Allow Settlers Rally
HEBRON (WAFA) Israeli
soldiers on Monday closed a
highway linking between the town
of Yatta and nearby small villages
to allow a rally organized by
Jewish settlers to pass, according
to local sources.
C o o r di n a t o r o f t h e A n t i Settlement Committee, Rateb
Jabour, said the Israeli army
closed Highway 60 and prevented
Palestinian drivers from using it
to allow settlers, residing illegally
in the West Bank, to organize a
provocative rally.
Highway 60 is a major intercity
road in the West Bank and links
between major central cities.
According to international
law, settlers in the Occupied
Palestinian Territories are residing
in the West Bank illegally and are
not treated as Israeli citizens.
Jewish settlers, nevertheless,
continue to harass Palestinians
and vandalize their property
in areas adjacent to the illegal
settlements.
The issue of settlement
construction and expansion in the
West Bank and East Jerusalem has
proved to be an obstacle for peace
between Palestinians and Israelis

in all rounds of negotiations, as


Israel persists on maintaining
major settlement blocs in any
future deal with the Palestinians.
Israel Arrests Seven in Jerusalem,
West Bank
JERUSALEM (WAFA) At least
six Palestinians were arrested on
Monday by the Israeli authorities
during predawn raids in occupied
East Jerusalem and the West
Bank, reported local and security
sources.
In Jerusalem, Israeli police
stormed the house of Omar
Shalabi, a Fatah official, assaulted
him and sabotaged his house
before arresting him, local sources
said.
Israeli police stormed Shuafat
refugee camp, north of Jerusalem,
and the neighborhood of Ras alAmoud, and arrested three local
residents, who were identified
as Omar Mhesen, Nasser Hadmi,
and Udai Senokrot.
Earlier at night, police arrested
Ibrahim Abu Gharbia, 39, a
member of the Fatah movement.
Meanwhile, the Israeli army
broke into the city of Jenin, in the
northern West Bank, and arrested
two Palestinians after raiding
and ransacking their homes and
sabotaging their furniture. The
two were identified as Ahmad
Darbi, 28, and Mohammad Turki,
32.
Local sources said Turki was
arrested after Israeli soldiers
blasted his houses door and used
some of his family members as
human shields.
Meanwhile in Hebron,
army forces stormed the city
of Yatta and handed summons
to three Palestinians to appear
for interrogation before Israeli
intelligence.
The Palestinian Prisoners Club
(PPC) said at least 214 Palestinians,
including six women, were
arrested by the Israeli authorities
since the beginning of December.
Israeli soldiers kill Palestinian
during Ramallah arrest raid
RAMALLAH (Ma'an) -- Israeli
soldiers shot and killed a young
Palestinian man during a dawn
detention raid in Qalandiya
refugee camp near Ramallah,
medics said Tuesday.
Mahmoud Abdullah Udwan,
21, was shot in the head while
standing on the rooftop of his
family home in the camp, medics
said.
He was hit as Israeli soldiers
ransacked homes to make arrests
at around 3 a.m.
Clashes broke out as a result
of the raid, with youths throwing
stones at Israeli soldiers.
Despite the confrontations,
Israeli soldiers managed to detain
26-year-old Mujahid Hamad,
who works with the Palestinian
football federation as a security
guard at stadiums.
Four Palestinians have been
killed by Israeli soldiers in
Qalandiya refugee camp this year
during arrest raids.

11

Makala

AN-NUUR

SAFAR 1436, IJUMAA DESEMBA 19-25, 2014

Mafunzo kutoka harakati za Mzee Mandela


Na Said Rajab

IJUMAA iliyopita, wananchi wa


Afrika Kusini waliadhimisha mwaka
mmoja wa kifo cha Rais wa kwanza
mweusi nchini humo, ambaye ana
hadhi ya baba wa taifa hilo, Mzee
Nelson Mandela. Mzee Madiba,
kama wenyewe wanavyomuita,
alifariki Desemba 05, 2014 mjini
Pretoria, akiwa na umri wa miaka
95. Kifo cha mwanaharakati huyo
wa kupinga siasa za ubaguzi wa
rangi nchini Afrika Kusini, kwa
hakika kiliutikisa ulimwengu.
Vyombo vya habari dunia nzima
vilionyesha kuhuzunishwa na kifo
hiki. Mchango wa mzee huyu, jinsi
alivyotoa muhanga maisha yake
kwa ajili ya watu wake, kusema
ukweli ulimgusa kila mtu. Mzee
Madiba aliheshimika sana duniani
na ameondoka akiwa na heshima
yake!
Nelson Mandela, kama kiongozi
wa chama cha 'The African National
Congress (ANC), alioongoza harakati
za kupinga ubaguzi wa rangi nchini
mwake kwa kutumia njia zote ustaarabu na ghasia. Leo Mandela
anaheshimika dunia nzima kwa
kazi nzuri aliyoifanya, lakini wakati
wa harakati zake za kisiasa, yeye
na chama chake cha ANC waliitwa
"magaidi".
Tunao Masheikh wa Uamsho
kutoka Zanzibar, ambao wamekuwa
mstari wa mbele kupigania haki ya
nchi yao kuwa na mamlaka kamili
katika Muungano. Masheikh hawa
na viongozi wengine wa Kiislamu,
hivi sasa wako ndani kwa tuhuma
za "Ugaidi" na uchochezi! Kama
alivyokuwa Mandela, kuna maelfu
ya watu duniani, wanaopigania
haki zao na waliojitoa muhanga
kuleta mabadiliko katika jamii zao.
Ama harakati zilizoendeshwa na
Mzee huyu wa Afrika Kusini, kwa
hakika, zinatupa mafunzo mengi ya
msingi. Funzo la kwanza tunalopata
ni kwamba fikra zina uwezo wa
kuangusha Serikali. Mandela
aliamini katika fikra kwamba
watu weusi wasibaguliwe nchini
Afrika Kusini kutokana na rangi
yao. Msukumo wa fikra hiyo ndiyo
uliomfanya achukue hatua kadhaa za
kijasiri kubadili hali hiyo katika jamii
yake. Mandela aliendesha harakati
kubwa za kufanya ubaguzi wa rangi
ushindwe nchini Afrika Kusini, na
watu Weusi wasitawalike kupitia
siasa hizo za kibaguzi. Alihamasisha
na kukusanya watu, lengo likiwa
kufichua uovu wa siasa za ubaguzi
wa rangi, na pia aliendesha vitendo
vya hujuma, vurugu na ghasia
kwa lengo la kuidhoofisha serikali
kandamizi ya makaburu.
Aliwaandaa watu, akawapika
katika itikadi ya mapambano,
akawaunganisha na kuwajengea
ujasiri na ukakamavu, ili waweze
kukabiliana vilivyo na matokeo
magumu ya kazi waliyopanga
kuifanya. Hatua hii ilihakikisha
kwamba kifo chake au kukamatwa
kwake kusingekwamisha harakati
alizoanzisha.
Harakati za kupinga ubaguzi
wa rangi zilimgharimu kwa kiasi
kikubwa Mzee Nelson Mandela
mwaka 1962 wakati alipohukumiwa
kifungo cha maisha jela. Chama cha

HAYATI Nelson Mandela.


ANC na kitengo chake cha kijeshi makaburu pia unatumiwa na serikali
'Umkhonto We Sizwe' viliendeleza zote za kisekula duniani kukandamiza
harakati za ukombozi bila ya makundi ya Waislamu wanaopigania
kutetereka. Na ilipofika mwishoni haki zao. Wanawabandika majina
mwa miaka ya 1980, utawala wa mabaya kama "magaidi" Waislamu
makaburu nchini Afrika Kusini, wote wanaopigania mabadiliko ya
uliokuwa ukitekeleza sera ya ubaguzi kuondoa dhulma na kusimamisha
wa rangi, ukatambua wazi kwamba haki.
siasa yake hiyo haiwezi tena kuwa
Hii inaonyesha kwamba siku
endelevu. Wakasalimu amri na zote mabadiliko halisi ya kuondoa
kubwaga manyanga!
mfumo kandamizi na kuleta haki na
Funzo la pili tunalopata kutoka usawa katika jamii, yatakumbana na
kwenye harakati za Mzee Madiba changamoto nzito, kwa sababu wale
ni watawala madhalimu kuhujumu wanaonufaika na mfumo kandamizi
m a b a d i l i k o h a l i s i . M a n d e l a hawataki mfumo huo uondoke.
alichukiwa na tabaka la watu Weupe Watautetea kwa gharama yoyote ile,
waliokuwa wakitawala Afrika Kusini, wengine hata kwa Aya na Hadith!
wakati alipotoa wito wa mabadiliko
Somo la tatu tunalojifunza kutoka
na kutaka watawala hao madhalimu kwenye harakati za Mzee Nelson
waondolewe.
Mandela ni kwamba kinachotakiwa
Serikali ya makaburu, Serikali ya ni mabadiliko halisi ya mfumo
Uingereza iliyokuwa ikioongozwa wa kisiasa na utawala na siyo tu
na Margareth Thatcher na Rais mabadiliko ya sura za viongozi. Kwa
Ronald Reagan wa Marekani, wote bahati mbaya sana, harakati za Mzee
walimwita Mandela "Gaidi".
Mandela ziliisha kwa maridhiano,
Mzee Mandela alichukiwa na ambayo kimsingi hayakubadili kabisa
Wazungu si kwa sababu alitaka hali mbaya ya watu Weusi nchini
m a b a d i l i k o , b a l i k wa s a b a b u Afrika Kusini.
mabadiliko aliyoyataka yalilenga
Viongozi wa makaburu, PW Botha
kung'oa mfumo kandamizi wa na FW De Klerk walifanikiwa kulinda
utawala wa Weupe uliokuwepo maslahi ya tabaka tawala la watu
wakati ule.
Weupe, hata baada ya kukomesha
Ni kutokana na shinikizo kubwa ubaguzi wa rangi nchini Afrika
aliloweka dhidi ya Serikali, kwa Kusini. Mfumo wa siasa na utawala
kuwahamasisha wananchi kupinga nchini humo havikubadilika kabisa.
ubaguzi wa rangi, ndiyo maana
Na Mzee Mandela alikumbatia
Serikali ya makaburu ikalazimika kile kilichokuwepo wakati ule kuzungumza na harakati ya Mandela Demokrasia ya Kiliberali na Soko
(ANC) mwishoni mwa miaka ya 80.
Huria. Mfumo huo umewaingiza
Mkakati huo uliotumiwa na wananchi wa Afrika Kusini katika

utumwa mpya wa mabeberu.


Baada ya miongo miwili tangu
ubaguzi wa rangi ukomeshwe nchini
Afrika Kusini, hali bado siyo nzuri
kwa watu Weusi nchini humo. Leo
hii matajiri wakubwa nchini humo,
ambao ni asilimia 10 tu wanamiliki
asilimia 58 ya utajiri wote wa nchi. Na
asilimia 5 ya matajiri hao, wanamiliki
asilimia 43 ya utajiri wote wa nchi.
Leo asilimia 70 ya ardhi yote ya
Afrika Kusini, bado inamilikiwa
na watu Weupe wanaotokana na
makaburu. Hali iko hivyo, licha ya
ahadi za ANC kugawa upya asilimia
30 ya ardhi kutoka kwa watu weupe
kwenda kwa weusi. Asilimia 50 ya
wananchi wa Afrika Kusini wanaishi
chini ya mstari wa umasikini. Yaani ni
masikini wa kutupwa.
Harakati za Mandela kung'oa
mfumo kandamizi katika jamii yake
ni funzo kwa Waislamu wote duniani,
wanaofanya harakati kama hizo.
Ofa za mazungumzo au maridhiano
kutoka kwa watawala madhalimu au
washirika wao, mara nyingi hulenga
zaidi kuzima cheche za harakati hizo,
ili kuendeleza mfumo kandamizi
uliopo.
Iwapo mazungumzo hayo
ya t a k u b a l i wa , k wa k i s i n g i z i o
chochote kile, basi matokeo yake ni
kwamba umma wa Waislamu utabaki
kama ulivyo umma wa Mandela leo.
Mzee Nelson Mandela ametumikia
kifungo cha miaka 27 jela, kwa
kupinga vikali kile alichoamini
kuwa ni ukandamizaji wa haki.
Mzee Mandela alikumbatia mfumo
uliokuwepo wakati ule nchini mwake,
na hali hii ikawatumbukiza watu
wake kwenye aina mpya ya ukoloni.
Lakini kwa Waislamu, ufumbuzi
wa matatizo yao mara zote unatoka
ndani ya Uislamu. Kazi inabaki kwa
Waislamu wenyewe kufinyanga njia
yao ya kisiasa, ambayo itawaletea
ukombozi kamili wa kweli.
Bila shaka tunaweza kuchota
mafunzo mengi ya msingi kutoka
kwa Mzee Madiba. Binafsi,
nimejifunza mengi sana kutoka kwa
Mzee Mandela. Ametufundisha
msimamo kwenye harakati,
kutopoteza 'focus' ya harakati zetu
na kuwa tayari kubeba matokeo ya
harakati tunazofanya. Hizo ni sifa
muhimu sana za mwanaharakati
aliyekamilika. Harakati za kupigania
haki zina gharama kubwa!
Mzee Mandela ametufundisha
kwa nadharia na vitendo, kwamba
msimamo katika harakati za
kupigania haki ni lazima. Hiyo
maana yake tuwaepuke kabisa watu
wanaojifanya wenzetu, kumbe ni
maadui zetu. Huku wako na kule
wako! Wamekuwa kama Popo,
hajulikani ni ndege au mnyama!
Mzee Nelson Mandela pia
ametufundisha kwamba harakati
za kupigania haki lazima ziwe
na 'focus'. Tufahamu vizuri sana
tunachopigania ili tusiyumbishwe na
mbinu mbalimbali za maadui. Tunao
wenzetu wengine wameshatekwa na
maadui, sasa wanaimba na kucheza
wimbo wa madhalimu.
Mzee Nelson Mandela vile vile
ametupa somo la vitendo kwamba
harakati za kupigania haki zina
gharama kubwa. Mtu unaweza
kupoteza maisha. Kwa maana hiyo
wanaharakati lazima wawe tayari
kupokea matokeo ya harakati zao.
Mzee Mandela ametufundisha
kwamba harakati zinahitaji ujasiri na
kwamba visingizio vya kuhalalisha
woga wa kijinga havina nafasi.

12

MAKALA

AN-NUUR

SAFAR 1436, IJUMAA DESEMBA 19-25, 2014

Ni kitu gani cha ajabu juu ya hii chai tuliyochagua kuiita Haiiba Timamu Tea?

Inatoka Uk. 9
virutubisho mbalimbali
vinavyohitajiwa na

mwi l i i l i kuimaris h a
siha. Mimea iliyotumika
kuandaa chai hii ina
utajiri mkubwa sana wa
hivi virutubisho. Orodha
kamili ya virutubisho
hivi ni: AMINO ACIDS
(VIJENZI VYA PROTINI),
Arginine; Histidine;
Isoleucine; Leucine;
Lysine; Methionine;
Phenylalanine; Threonine;
Tryptophan; na Valine.
VITAMINI NA MADINI
Carotine (Vitamin A);
Thiamin (Vitamin B1);
Riboflavin (Vitamin B2);
Niacine (Vitamin B3);
Vi t a m i n C ; C a l c i u m ;
Copper; Iron; Magnesium;

Phosphorous; Potassium;
Zinc; Chromium; na
Manganise.
VIZUIA VIOKSIDISHA JI
(ANTI OXIDANTS)
Curcumin; Catechines;
Polyphenols; Flavonoids;
na Piperine.
Viua vijiduduCinnamaldehyde.
Sasa ukisoma nyaraka
za kitafiti utabaini kuwa
viini lishe hivi vinatajwa
kuwa ni msaada mkubwa
kwa matatizo mbalimbali
ya kiafya ikiwa ni pamoja
na:
Kudhibiti maumivu ya
viungo; Kudhibiti uchovu
n a k u o n d o a h a l i ya
kujisikia homa mara kwa
mara; Kudhibiti mfuro
wa seli (inflammation);

Sababu za magonjwa ya
meno na jinsi ya kujitibu

Inatoka Uk. 8
tunafanya makosa ya
msingi kuhusiana na usafi
wa vinywa vyetu. Makosa
haya ni pamoja na kukaa
n a m a b a k i ya v ya k u l a
mdomoni kwa muda mrefu
sana kabla ya kuchukua
hatua ya kusafisha kinywa.
Watu walio wengi wamezoea
kupiga mswaki mara moja
tu ndani ya masaa 24, na hii
ni asubuhi baada ya kutoka
usingizini. Hii ina maana
kwamba mtu mwenye tabia
hiyo muda mwingi kinywa
chake ni dampo la mabaki
ya vyakula, na anatoa muda
mrefu kwa gram positive
bakteria kuweka kambi
k we n ye k i n y wa c h a k e .
Ingekuwa ni bora sana
kama mtu angepata fursa ya
kusafisha kinywa chake kila
baada ya mlo, ili kuepukana
na hali hii.
Hata hivyo, kwa sababu
katika hali halisi hili ni
gumu, basi ni bora mtu
ukahakikisha kuwa unapiga
mswaki wa hali ya juu sana
usiku kabla ya kulala. Hii
ina maana kwamba usiku
wote utakuwa umelala huku
ukiwa na kinywa kisafi, na
hivyo kutoa wakati mgumu
sana kwa gram positive
bakteria kushambulia wakati
ukiwa usingizini.
Ni vizuri pia ikafahamika
kuwa kupiga mswaki pekee
hata kama mswaki huo
utaupiga kila siku kabla ya
kulala - hakutoshi kukiacha
kinywa chako huru kwa
asilimia mia moja dhidi ya
uwepo wa gram positive
bakteria. Njia ya uhakika ya
kujihakikishia hili ni kutumia
kitakasaji cha mdomo (oral

disinfectant), kila baada


ya muda fulani. Vitakasaji
viko vya aina nyingi, lakini
vile vya asili vinavyotokana
na mimea vinaweza kuwa
bora zaidi, kwa maana ya
kutokuwa na madhara kwa
mtumiaji.
Moja ya vitakasaji bora
kabisa vya aina hii ni Haiiba
Dental Guard kutoka
Herbal Impact. Utafiti wetu
unaonyesha kuwa kati ya
watumiaji 10 wanaokitumia
kama tiba ya maumivu
ya meno, basi 9 kati yao
hupona maumivu yao moja
kwa moja. Suala la kuwepo
kwa mtumiaji 1 ambaye
hapati nafuu inavyopasa
kati ya hao watumiaji 10,
limekuwa likitusumbua
sana kwa muda mrefu.
Hata hivyo tunashukuru
kuwa hivi karibuni
tumelipatia ufumbuzi
baada ya majaribio ya muda
mrefu. Ufumbuzi huu ni
kubuniwa kwa kitakasaji
kipya kinachoitwa Haiiba
Dental Guard Plus. Baada
ya mgonjwa kutumia Haiiba
Dental Guard na kuhisi
kuwa haijamsaidia kiasi cha
kutosha, tunamshauri kuwa
afuatishe matumizi ya awali
na Haiiba Denta Guard Plus.
Tunamshukuru Mungu
kwamba hadi sasa
muunganiko wa vitakasaji
hivi viwili umetufanya
tufikie mafanikio ya asilimia
mia moja katika kuwasaidia
wale wanaokuja kwetu na
shida ya maumivu ya meno.
Kwa ushauri zaidi
unaweza kuwasiliana
nasi kwa namba: 0754281131/0655-281131.

Kuimarisha kinga za
mwili; NA Kusawazisha
k iwa n g o ch a le h e mu
(cholestrol) mwilini kuwa
cha kawaida. Mengine
n i K u d h i b i t i k a s i ya
kuzeeka; Kuboresha
usagaji wa chakula
tumboni; Kuboresha siha
ya mfumo wa damu na
utendaji wa ini; Kusafisha
ngozi na kuhifadhi
mnyumbuko wake;
Kupeleka virutubisho
muhimu kwenye ngozi;
Kuimarisha siha ya macho;
Kuzuia kuongezeka kwa
seli za saratani; Kuzuia
seli za kawaida za mwili
kubadilika na kuwa seli
za saratani; Kuuchochea
mwili wako kuangamiza
seli za saratani kabla
hazijasambaa mwilini;
Kuzuia uundwaji wa
mishipa ya ziada ya damu
kwa ajili ya kufikisha
virutubisho vya ziada
katika seli za mwili zenye
saratani na Hupunguza
shinikizo la damu.
Inasaidia pia Kupunguza
uwezekano wa kupata
shambulizi la moyo
(heart attack); Kupunguza
uwezekano wa mishipa
ya f a h a m u k u p o t e z a
utando wa nje unaokinga
sehemu ya ndani na kwa
hivyo kuifanya ifanye
kazi kwa ufanisi (multiple
sclerosis); Kuongeza
uzalishaji wa nyongo;
Kuzuia uharibifu wa
lehemu nyepesi mwilini
kutokana na mwingiliano
na oxygen; Kupunguza
madhara ya kisukari cha
ukubwani; Kupunguza
dalili za ugonjwa wa
kupoteza kumbukumbu
(Alzheimers disease);
Kuharakisha kupona kwa
majeraha; Kupunguza
madhara ya baridi ya
yabisi; Kupunguza kasi
ya ongezeko la virusi vya
ukimwi; Kukinga dhidi ya
uharibifu wa ini; Kukinga
dhidi ya sumu na makovu
kwenye mapafu; Kukinga
dhidi ya ugonjwa wa ngozi
kuchuja rangi, yaani,
vitiligo; na Kusafisha
kinywa dhidi ya bakteria
wa s i o t u m i a o k s i j e n i
(anaerobic bakteria)
Chai hii inaweza
kukusaidia pia kama
unahisi kuwa unakabiliwa
na moja wapo ya hali hizi.
Hivi sasa inapatikana Dar
es Salaam pekee, katika
ofisi zetu zilizoko Mosque
Street, No. 1574/144
(mkabala na msikiti
wa Sunni), Kitumbini.
Jitihada zinafanyika
pia ili kabla ya mwisho

wa m wa k a h u u i w e
inapatikana walau katika
miji yote iliyo makao
makuu ya mikoa Tanzania
nzima. Kwa maelezo zaidi
unaweza kuwasiliana nasi
kwa simu namba 075428
1131/0686281131/065528
1131.
KWA WALIOKO DAR ES
SALAAM
Kama unaishi Dar es
salaam unaweza kuja
hapa ofisini kwetu mtaa
wa Mosque, kwa ajili ya
kupata chai ya Timamu.
Tuko Kitumbini, mtaa
wa Mosque. Mtaa huu
unaitwa Mosque kwa
sababu kuna misikiti
miwili mikubwa
inayoongozana (Ibaadh
na Sunni); ambayo
imetenganishwa na duka
la tamu-tamu la Taj Mahal
Sweet Mart.
Mtaa huu pia ni maarufu
sana kwa MGAHAWA
WA M I A K A M I N G I
SANA UNAOITWA NEW
ZAHIR RESTAURANT
(Tazama picha. Jengo lenye
canopy yenye mistari
myekundu.). Iwapo
utalazimika kuuliza ili
ufike Mosque Street, basi
waambie hao unaowauliza
ni mtaa iliko NEW
ZAHIR RESTAURANT.
Ukiweza kufika NEW
ZAIHIR RESTAURANT
utaiona hiyo misikiti
miwili tuliyoitaja iliko.
Kama hukuiona wewe
mwenyewe uliza! Ni hapo
jirani kabisa.
Sisi tunatazamana na
huo msikiti wa Sunni
(wenye minara ya kijani).
Aidha tuko jirani kabisa na
duka maarufu la vifaa vya
usafi na bidhaa nyingine za
majumbani la ZANZIBAR
S TAT E T R A D I N G
CORPORATION. Ukiona
mabango ya TRIPLE A
TAILORING SERVICES
yafuate, utakuwa tayari
umefika. HERBAL
I M PA C T, T R I P L E A
TAILORING SERVICES
NA NEOBIZ tunachangia
eneo la ofisi.
JINSI YA KUFIKA
1. kwa wanaotokea
m a e n e o ya M b a g a l a ,
K u r a s i n i n a Te m e k e
ambao wakija mjini kituo
chao cha mwisho cha
daladala ni Stesheni, basi
waje mpaka barabara
ya Samora liliko tawi la
NBC SAMORA. Mtaa
wa Mosque unaanzia

NBC Tawi la Samora na


kupandisha kuelekea
juu hadi mtaa wa Libya.
Ili kufika ofisini kwetu,
ukitokea hapo NBC
Samora utavuka kwanza
mtaa wa India, kisha
mtaa wa Indira Gandi.
Hapo utakuta hiyo
misikiti mikubwa miwili
inayoongozana.
2. Kwa wanaokuja mjini
kwa njia za Morogoro na
Ali Hassan Mwinyi, kituo
cha basi cha kushukia
n i A K I B A . B a a d a ya
kuteremka tembea hadi
k w e n y e m a u n g i o ya
Morogoro Road, ingia
Morogoro Road na uifuate
kama vile unaelekea
Bandarini zinakoegeshwa
Boti za kwenda Zanzibar.
Endelea mbele ambapo
utavuka mitaa ya Libya
na kisha Jamhuri mpaka
utakapokutana na tawi la
benki ya NMB la Morogoro
Road likiwa mkono wako
wa kulia. Hapo kata kulia
kuingia mtaa wa Mshihiri.
Ukiendelea mbele kidogo
utakutana na mtaa wa
Mosque unakatiza na
kushoto kwako utaiona
hiyo misikiti miwili.
3 . K wa wa n a o k u j a
na barabara za Nyerere
au Uhuru hadi Mnazi
Mmoja. Ukifika mnazi
mmoja vuka mataa hadi
liliko tawi la benki ya
NBC la Mnazi mmoja.
Hapo utakuwa uko mtaa
wa Jamhuri. Shusha moja
kwa moja na huo mtaa
hadi utakapokuta kituo
cha mafuta cha Puma.
Mbele kidogo ya hicho
kituo ni mtaa wa Mosque
unakatiza. Ukifika hapo
kwenye mauongio ya
Jamhuri na Mosque,
t a z a m a k u l i a k wa k o
utaona hiyo misikiti
miwili.
4. Kama unataka kuja
na gari lako Mwenyewe ni
bora uende hadi Samora
Avenue uingie Mosque
Street kwa kutokea hapo
tawi la NBC Samora. Au
kama unatokea barabara
ya Nkrumah au Uhuru,
ukishafika Clock Tower
ingia mtaa wa India,vuka
mtaa wa Aggrey (kuna
kituo cha mafuta cha
GAPCO) na barabara
utakayokutana nayo
ikikatisha ni Mosque.
Hapo kata kushoto na
baada ya kuvuka Mtaa wa
Indira Gandi utaiona hiyo
misikiti miwili mkono
wako wa kulia.

13

Makala

AN-NUUR

SAFAR 1436, IJUMAA DESEMBA 19-25, 2014

KUMBUKUMBU YA MIAKA 53 YA UHURU WA TANGANYIKA

Haruna Taratibu muasisi wa TANU Jimbo la Kati-2


WASOMI wa Makerere, ambao
Mwangosi aliwaamini sana
katika kuunda TANU, walipopata
habari kuhusu mkasa wa Taratibu
na DC, Bwana Smith, waliogopa.
Waliamua kujiweka mbali kabisa
na mambo ya siasa na kuendelea
na kazi yao ya kufundisha.
Haruna Taratibu na Omari
Suleiman sasa waliamua kugeuza
mbinu, waliitisha mkutano wa siri
usiku nyumbani kwa Swedi bin
Athumani. Mkutano huu uliamua
kuwa Taratibu lazima aende
makao makuu ya TANU Dar es
Salaam akazungumze na Nyerere
ana kwa ana kuhusu matatizo
yaliyokuwa yakiikabili TANU
Dodoma. Mahdi Mwinchumu
aliyekuwa mwanachama wa
TANU Dar es Salaam alijitolea
kufuatana na Taratibu hadi makao
makuu ya chama Dar es Salaam
kwa kuwa alikuwa akijuana na
viongozi wa TANU. Said Mussa,
mjumbe mwingine wa ile kamati
ya siri alijitolea vilevile kufuatana
na Taratibu na Mwinchumu hadi
Dar es Salaam.
Siku ya kuondoka, Job Lusinde
alikwenda stesheni ya gari moshi
kuagana na ule ujumbe uliokuwa
ukielekea Dar es Salaam, makao
m a k u u ya TA N U . L u s i n d e
aliuambia ule ujumbe kuwa jamaa
wa Makerere wanaunga mkono
maamuzi yote yatakayoamuliwa
na ile kamati ya siri. Kwa bahati
nzuri katika gari moshi lile lile
ambamo Taratibu na wenzake
walikuwa wakisafiri kulikuwa
na wajumbe wa TANU kutoka
Kigoma, Bukoba na Mwanza
wakisafiri kwenda Dar es Salaam
kuhudhuria mkutano mkuu wa
kwanza wa mwaka wa TANU.
Wahudumu ndani ya gari moshi
walipofahamu kuwa walikuwa
na wajumbe wa TANU kwenye
gari moshi lile, waliwafanyia
heshima kubwa. Mmoja wa
wahudumu wale alijitolea kumpa
malazi Salum Mussa nyumbani
kwake Dar es Salaam. Mahdi
Mwinchumu aliwapeleka Haruna
Taratibu na Said Mussa makao
makuu ya TANU New Street,
ambako walifanya mazungumzo
na Nyerere pamoja na Rupia.
U o n g o z i wa m a k a o m a k u u
ulielezwa kwa ufupi matatizo
yaliyokuwa yakikabili Dodoma
katika kufungua tawi la TANU.
Papo hapo Nyerere alimwalika
Taratibu kuhudhuria mkutano
mkuu Hindu Mandal Hall
kama mjumbe wa Jimbo la Kati.
Mkutano ule ulimchagua Taratibu
kuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya
Taifa ya TANU.
Taratibu na ujumbe wake
walirudi Dodoma washindi,
walikwenda Dar es Salaam
watu wasiojulikana na walirudi

HAYATI Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (katikati). Kulia kwake ni Marehemu Sheikh Ramia.
n y u m b a n i wa k i f u a t a n a n a
mjumbe wa Kamati Kuu ya
Taifa wa TANU, chombo cha juu
kabisa katika chama. Nyerere
alimpa Taratibu dafari ya tasjili
ya wanachama, kadi mia moja
hamsini za uanachama wa TANU
na nakala hamsini za Bill of Rights.
Kazi ya kuwahamasisha na
kuwaingiza watu TANU alipewa
Omari Suleiman, na fundi
cherahani mwingine aliyejulikana
kwa jina la Abdu Mohamed
Mkamba. Mara tu baba mwenye
nyumba wake alipopata habari
za kuwa mpangaji wake, Haruna
Taratibu alikuwa mwanachama
wa TANU, alimfukuza kutoka
kwenye nyumba yake.
Baada ya kupata kikundi
kidogo cha wanachama, Taratibu
alipiga simu makao makuu ya
TANU na kuzungumza na kaimu
katibu, Elias Kissenge akaomba
ruhusa ya kufanya uchaguzi.
Kissenge hakuweza kutoa uamuzi
wowote wa maana kuhusu tatizo
la uongozi wa TANU Dodoma.
Taratibu alifanikiwa kumpata
Kambona ambaye aliidhinisha
uchaguzi ufanyike kwa shuruti
moja la kuwa Hassan Suleiman na
Ali Ponda waruhusiwe kushiriki
na kugombea uongozi wa chama.
Kusisitiza kwa Kambona juu
ya uongozi wa zamani wa TAA
kuongoza chama kipya huenda
kulishawishiwa na mafanikio ya
zamani ya uongozi wa Hassan
Suleiman, mbaye alimfahamu
huko Dodoma wakati Kambona
alipokuwa mwalimu akifundisha
Kikuyu Secondary School. Kwa
bahati mbaya, wanachama wa
TANU waliokuwa wanainukia
na chama pale mjini Dodoma
waliwaona Hassan Suleiman na
Ali Ponda kama wasaliti kutokana
na kutokushirikiana na wenzao
katika kuanzisha TANU.
Wakati ametatizwa na tatizo
la uchaguzi wa TANU, Taratibu

alijulishwa na makao makuu


kuwa makamo wa rais, John
Rupia, atapita Dodoma kwa
gari moshi akiwa njiani kwenda
Tabora kushughulikia mambo ya
chama. Gari moshi liliposimama
Dodoma Rupia alishangazwa
kuona kundi la wananchama wa
TANU wakimsubiri katika kituo
cha gari moshi, wakimtaka avunje
safari waende mjini kujadili na
kutatua tatizo la uchaguzi. Rupia
aliwaeleza wanachama wa TANU
wa Dodoma kuwa yeye hakuwa
na idhini kutoka makao makuu
kufanya shughuli yoyote ya chama
mjini Dodoma. Wanachama wa
TANU hawakutaka kusikia lolote
na walimwambia Rupia kuwa
wamechoshwa na makao makuu
kwa kushindwa kwake kutoa
uamuzi wa tatizo la uchaguzi.
Mizigo ya Rupia ilishushwa
chini kutoka kwenye gari moshi
na Rupia akawa hana khiyari
i s i p o k u wa k u wa f u a t a wa l e
wanachama wa TANU hadi mjini.
Ghafla mji mzima ukavuma
tetesi kuwa makamu wa rais wa
TANU, John Rupia, yupo mjini
kufungua tawi la TANU. Rupia
alimwita Hassan Suleimna na
akamtaka alete hati ya tasjili
ya TANU Hindu Mandal siku
inayofuata, mahali ambako
mkutano utafanyika. Hassan
Suleiman hakutokea mkutanoni
lakini alimtuma mtu apeleke
ile hati. Ali Ponda alihudhuria
mkutano ule. Rupia alikuwa
mwenyekiti wa mkutano na
TANU ikafanya uchaguzi wake wa
kwanza. Alexander Kanyamara
a l i c h a g u l i wa R a i s ; H a r u n a
Taratibu Makamu wa Rais, Abdu
Mohamed Mwamba, Katibu na
Omari Suleiman Mweka Hazina.
Miongoni mwa wanachama

waasisi alikuwa mwanamke


mmoja wa Kimanyema, Binti
Maftah Karenga; wengine
walikuwa Bakari Yenga, Maalim
K h a l f a n , m wa n a c h u o n i wa
Kiislamu aliyekuwa akiheshimiwa
sana, Idd Waziri na Said Suleiman.
Wale wasomi wa Makerere
hata mmoja hakujitokeza kwenye
mkutano huu wa kuasisi TANU.
Ali Ponda, mwanasiasa mkongwe
alipuuzwa na hakuchaguliwa
k u s h i k a wa d h i f a w o w o t e .
Walipoona hawakupewa wadhifa
wowote katika TANU, Ali Ponda
na Hassan Suleiman walijiunga na
UTP kuipinga TANU.
Baada ya uchaguzi huo, wale
mafundi cherahani wawili, Abdu
Mohamed Mkamba na Omari
Suleiman, walianza kuhamasisha
wananchi wazi wazi kujiunga
na TANU ili wapiganie uhuru
wa Tanganyika. Tawi la TANU
la Dodoma baada ya kujizatiti
pale mjini, lilituma wanaharakati
kuwahamasisha watu wa Kondoa
ili wafungue tawi la TANU katika
wilaya hiyo. Abdallah Jumbe
alizipenyeza kadi za TANU na
kuzipeleka kwenye wilaya hiyo
kwa siri akaanza kuandikisha
watu. D.C. wa Singida alikuwa
jeuri sana kiasi kwamba ni baada
ya Mkutano Mkuu wa Tabora
wa mwaka 1958, ndipo Abdallah
J u m b e a l i we z a k u f a n i k i wa
kufungua tawi mjini Singida.
Wakati huo TANU ilikuwa
na nguvu sana ikiwa na
wajumbe wake katika Baraza
la Kutunga Sheria. Kwa ajili hii
hakuna Mzungu aliyethubutu
kuwa fedhuli kwa TANU na
kuwabughudhi wanachama wake.
(Makala hii imekusanywa na
kuandikwa na Mohammed Said)

14
NILIWAHI kuandika makala
iliyokuwa na kichwa cha habari:
Vita vya msalaba Masheikh
wako Golgotha. Nilieleza habari
ya Rais W. Bush, na Mchungaji
Teghua. Kwa lugha ya Biblia
neno mnyama linawakilisha,
mfalme, mtawala, n.k. Hapo ni
kuwa mtawala wa Marekani
(Rais W. Bush), alijifanya ni
nabii, kwa kujifanya mlokole, na
kusoma Biblia, kabla hajatangaza
vita vya Iraq, na kuwateka kina
Teghua, na Wakristo na wasio
kuwa Wakristo, jumla mataifa
(wanyama) 32, wakaiangamiza
Iraq Afghanstan, Libiya na
sasa Siriy, n.k. Lakini wasomi
hawa hawajaona kitabu chao
walichoandika wenyewe kuwa
kinaeleza kuwa kiongozi wa
wanyama hao wawili ni Joka
jekundu (shetani mwekundu):
13:14 Kanisa hufaulu kufanya
miujiza kwa Roho Mtakatifu ili
kusudi kuwaaminisha Wakristo
imani. Hivyo mnyama wa pili
anamwiga Roho Mtakatifu kama
mnyama wa kwanza alivyo mwiga
Yesu mfufuka (13:3) Kwa hiyo Joka
na wanyama hao wawili wanaiga
Utatu Mtakatifu kwa dhihaka ya
kufuru. Biblia ya Imprimatur.
H a p a a n am a a n i s h a k uwa
Kanisa la Rumi chini ya uongozi
wa Papa na utawala wa Marekani
wanashirikiana na yule Joka
jekundu (shetani jekundu),
kuutawala ulimwenu kwa njia
ya kufuru. Aya ya 13:16-17;
inaonesha sera ya vitambulisho,
vya aina mbalimbali, vikwazo
vitakavyotumika kwa kuwabagua
watu, kuwawekea vizuizi n.k.
Si lazima uone muhuri hasa,
bali matendo yanayofanana
na kuwa na muhuri na namba
tunayaona kwani hata sasa
mambo yanayoendelea sasa
yanatumia mfumo huo. Hutibiwi
bila kitambulisho, husomi bila
kitambulisho n.k.
Ufafanuzi wa aya ya 13:18:
Tarakimu (666) hiyo ni mfano
wa Kaisari Nero. Kadiri ya
Kiyahudi kila herufi ya alfabeti
yao ni tarakimu Fulani. Jumla ya
herufi za jina la Kaisari Nero
kwa Kiyahudi ukitazama kama
tarakimu utapata herufi hii: 666.
Biblia ya Imprimatur.
ONYO LA MWISHO
K WA D U N I A M P A N G O
WA U L I M W E N G U M P YA
UNAKUJA! Hicho ni kichwa
cha habari cha Jarida la Family
Development International P.O.
Box 17 Mafinga Tanzania. Uk.1.
Chini mwisho wa ukurasa huo
kuna maandishi mekundu hivi:
Marekani- Upapa- Umoja wa
Mataifa. Picha hiyo hapo iko juu
iko juu ya Jarida hilo katika ukurasa
huo wa kwanza, ikionyesha
kuwa, Rais wa Marekani Clinton,
wa n g e k a m i l i s h a k a z i h i y o
wakishirikiana na Umoja wa
Mataifa na Papa Yohana Paulo II.
Kwa mujibu wa jarida hilo,
kazi ya kuitawala dunia kwa huo
utatu; ilitakiwa ikamilishwe na
Papa Yohana Paulo II. Viongozi
wa Ulimwengu Wanautaka. Unao

Makala

Jamani, hili ni joka


Tangu lini joka likaleta amani?

RAIS wa zamani wa Marekani, George W. Bush.


Watetezi Wengi. Ulitabiriwa miaka
elfu mbili iliyopita. Umekaribia
sana. Utauteka Ulimwenu.
Hizo ni nukta za mwanzo katika
jarida hilo. Nilieleza hapo mwanzo
k u wa , U f u n u o wa Yo h a n e ,
iwe ni Yohane aliyeandika, au
vinginevyo, umetekwa nyara na
Joka. Na ndipo joka anazalisha
haya tunayoyashuhudia, kwa
kuutumia huo utatu.
Niwazo Kubwa: mpango mpya
wa ulimwengu, wakati mataifa
mbali mbali wanaposukumwa
pamojani Marekani pekee
ambayo ina msimamo thabiti na
uwezo wa kuusukuma mbele.
George Bush, asema Katika Gazeti
la, Los Angeles, Feb 18/1991,
Chini ya uongozi shupavu wa
Papa Yohana II, makao Makuu
ya Vatikani yaidhinisha mahali
pake katika ulimwengu kama
sauti ya Kimataifa. Ni haki ya
kwamba nchi hii ya Marekani
ndio tu inayoonyesha heshima
kwa Vatikani kwa kuielewa kama
msuluhishi au mpatanishi na
kama taifa katika ulimwengu.
Dan Quayle, Mwito kwa Baraza
la Umarekani, Septemba 22, 1983.
(Yohana Paulo II) asisitiza ya
kwamba watu hawana tumaini la
kutegemewa kwa kuiunda serikali
inayojitegemea, mpaka tu iwe
chini ya msingi wa Ukristo wa
Katoliki ya Kirumi. M. Mrtini,
Key of this Blood, ukurasa wa 492.
Umoja wa Mataifa viongozi
wa Kamati ya Ulinzi wa kimataifa
walikuwapo hivi leo huko New
York katika mkutano wao mkubwa,

AN-NUUR

SAFAR 1436, IJUMAA DESEMBA 19-25, 2014

wakiwa tayari kuiweka Umoja wa


nchi za Mataifa kuwa katikati ya
mpango huu wa ulimwengu mpya
na kuyasukumia mapatano ya
umoja kuhusu kuleta amani na
ulinzi wa silaha.-(Birmingham
News, Jan. 31,1992. )
Ushuhuda umetolewa hapo juu
na Papa Yohana, kuwa, serikali,
ni lazima iwe chini ya Ukristo
wa Roma. Maelezo hayo yapo
katika ukurasa wa kwanza wa
Jarida hilo chini ya picha ya Papa
Yohana Paulo II na Rais Clinton
wa Marekani. Kwa maelezo ya
Jarida hilo, unapata ule utatu
nilioeleza. Katika uk. wa 15, wa
jarida hilo kuna picha na nembo
ya utatu.
Chini ya picha hiyo kuna
maelezo yafuatayo: Kuyeyuka
kwa ukuta Berlin 1989 Ni Nguvu
ngapi zimebakia?
Nguvu zinazoulizwa hapo,
ni zile zitakazopinga huo utatu.
Urusi ilikuwa moja wapo, lakini
imesambaratishwa; lakini, ki
dini, haikuwa tishio kwa mfumo
Kristo; hivyo nguvu ya kwanza
kusakwa ni Uislamu na Waislamu.
Ndiyo maana ikaandamwa Iraqi,
Afghanstan, Pakistan, Irani,
Libiya, Siria na wengine kama
hao.
Tukiendelea na mikakati ya
hiyo NEW WORLD ORDER.
Tunaambiwa kuwa-AMANI
duniani ni jambo lijulikanalo
sana mara moja kila mwaka
na ulimwengu wa Wakristo
washerehekeapo KrismasiVita
vya kwanza vya dunia vilipiganwa

kumaliza vita ubatili wa madai


hayo viliwekwa wazi na mteketeo
mkubwa wa vita vya pili vya
dunia. Kwa kweli vita hii vya
ulimwenu wote vilifikia mwisho
tu, wakati ule fumbuzi na utumizi
wa silaha za atomiki binadamu
amefumbua silaha zenye nguvu
za kuangamiza na za kuogofya
hivi kwamba tumehofia ya
kwamba vita vyo vyote vyaweza
kumalizia kwa maanamizi ya
kinuklia vikiwa na uwezekano
mkubwa wa kuangamiza maisha
ya watu katika sayari hii. Jukumu
la papa katika kuvunja Ukomonisti
wa Urusi, junzi imeonyeshwa
katika kuanguka kwa Berlin wall
Novemba 9, 1989.
Ikumbukwe kuwa ,katika vikao
vya wakuu wa Kanisa Katoliki
na hata makanisa mengine; adui
wao wakuu walikuwa ni wawili;
Ukomunisti na Uislamu:
Lengo kubwa la utume wa
kijamii wa viongozi wa Kanisa
Katoliki katika mwaka 1953 hadi
1956 lilikuwa kulinda nafasi ya
Kanisa katika jamii Kanisa
katika kupinga kuenea kwa
dini ya Kiislamu. Kwa kifupi,
viongozi hao waliona kuwa
walikuwepo vikwazo (maadui)
viwili (wawil) vya (wa) Kanisa
hapa Tanzania, yaani Uislamu na
Umax. Waliamua kutumia utume
wao wa kijamii kama mkakati
wa pekee kupambana na hayo
mawili. (Dr. John C. Sivalon
M.M. Kanisa Katoliki na Siasa
ya Tanzania Bara 1953 hadi 1985
uk. 24. )
Limeangushwa taifa kuu Urusi
na mshirika wake Ujerumani
Mashariki, sasa kuna adui mmoja
tu: Uislamu.
Tu j i u l i z e k u w a h i i I S
inayopambana Syiria na Iraq,
kwa nini haianzii katika zile nchi
wanazozita makafiri mutlaki
kwa nini waanzie katika nchi za
Waislamu waliotoa Shahada?
Na kwa nini wapate mafunzo,
pesa na silaha kutoka kwa nchi
zinazofahamika kama maadui wa
Uislamu?
Kwa kifupi, haya yanayoendelea
katika nchi za Kiislamu na
Waislamu, ndiyo mikakati ya huo
utatu. Waislamu wanatumiwa
kujimaliza wenyewe kukamilisha
mkakati huo.
Ukatili uliofanywa na nchi za
Ulaya chini ya utawala wa Kirumi
enzi za giza, ulizalisha watu
katili mpaka sasa, na zinaendelea
kuzalisha watu wa aina hiyo
katika mataifa yasiyokuwa ya
Ulaya. Kama vile walivyozalisha
taifa la Marekani, na la Makaburu,
mataifa hayo yalienda huko na
ukatili ule ule waliotoka nao huko
Ulaya. Wazungu waliohamia
Marekani wakawauwa na
kuwatokomeza wenyeji Wahindi
We k u n d u . M a k a b u r u n a o
wakawasaka Waafrika wa Afrika
ya Kusini.
Sasa wameusambaza ukatili
wao dunia nzima kwa visingizio
mbali mbali, na majina mbali
mbali. Eti wanadai kuleta amani
na demokrasia wakati waongo na
watu waovu kabisa. Jamani! ni lini
joka likaleta amani?
Wabillahit Tawfiiq
(K. J. Mziray: 0757 013344.
31/10/2014.)

15

Makala/Shairi

AN-NUUR

SAFAR 1436, IJUMAA DESEMBA 19-25, 2014

Je, daktari wako anakueleza kuhusu madhara ya Panadol?


Na Juma Kilaghai

WATU wengi wana mtizamo


kuwa dawa zinazouzwa
katika maduka ya dawa
b a r i d i n a m a d u k a ya
kawaida ya vyakula, yaani
zile ambazo hazihitaji agizo
la daktari ( over-the-counter
(OTC) drugs ) ni salama.
Ukweli ni kwamba hali
haiko hivyo kabisa. Nyingi
ya dawa zilizoko katika
kundi hili huko nyuma
zilikuwa ni miongoni mwa
zile zilizosimamiwa na
kuratibiwa kwa karibu,
huku zikitolewa tu kwa
agizo la daktari.
Pamoja na kuondolewa
k a t i k a k u n d i l a d a wa
zinazohitaji kutolewa kwa
agizo la daktari, bado dawa
za OTC ni kemikali ambazo
mara nyingi haziondoi
kiini cha tatizo ulilonalo,
na zinaweza kukupelekea
kupata madhara makubwa,
ikiwa ni pamoja na kifo.
Mfano mmoja wapo
ni dawa ya panadol,
ambayo pia hujulikana
kama paracetamol,
acetaminophen, tyenol,
nakadhalika. Panadol ni
dawa maarufu kweli kweli.
Ni dawa maarufu hasa
kutokana na uwezo wake
wa kutuliza maumivu na
pia kushusha homa haraka.
Watu wengi hunywa
panadol bila ya kujiuliza
chochote kuhusu usalama
wake. Kupitia kwa wazazi
na walezi wao, watoto wengi
sana pia ni wabugiaji wa
dawa hii. Hii ni kutokana na
wazazi/walezi wao kuamini
kuwa kila mtoto anapolia
basi mtoto ana maumivu, na
au kila anapopata homa, basi
kuna ulazima wa kuishusha
homa hiyo.
Kwa kiasi kikubwa tabia
hii imejengwa na madaktari
na wafamasia ambao
nao hutoa dawa hii kwa
wagonjwa bila kuzingatia
usalama wake, na hivyo bila
kutoa ushauri wowote kana
kwamba dawa hizi ni salama
kama maziwa!
Hatuna miundo mbinu
ya kubaini idadi ya watu
wanaoudhuriwa na
matumizi haya ya kiholela
ya panadol, lakini kwa
kuangalia takwimu za nchi
nyingine, bila shaka watu
hao watakuwa ni wengi sana.
Nchini Marekani utumiaji
uliopindukia wa panadol
(overdose) umetambuliwa
kuwa ndio sababu kuu ya
simu zinazopigwa kuomba
msaada katika vituo vya
udhibiti wa sumu (Poison
Control Centers) nchini
humo, kila mwaka. Panadol
pia inatuhumiwa kuwa kila
mwaka inasababisha kiasi
cha watu zaidi ya 56,000
k u p a t i wa m a t i b a b u ya
dharura, watu 2,600 kulazwa
hospitalini, na kiasi cha
watu 458 kupoteza maisha,

katika taifa hilo. Sababu ya


madhara haya inatajwa kuwa
ni kushindwa kwa kiwango
cha juu kwa ini kufanya kazi.
Taasisi ya chakula na dawa
ya Marekani (US Food and
Drug Administration (FDA))
mnamo mwaka 2009 ilitoa
maelekezo kuwa vifungashio
vya dawa hii viwekewe onyo
kuhusu uwezekano wa dawa
hii kuharibu ini la mtumiaji.
Hatua hii ilikuja miaka 32
baada ya jopo la wataalamu
kutoa ushauri kwa FDA
kuwa onyo hili lilikuwa ni
suala la lazima!
Katika hatua nyingine,
k wa n i a ya k u p u n g u z a
madhara, mnamo tarehe
14 Januari, 2014 FDA ilitoa
kauli iliyokuwa ikiwahimiza
wataalamu wa afya kuacha
kuandika maagizo ya dawa
(prescriptions) kwa dawa
mchanganyiko ambazo
miongoni mwake kulikuwa
na vidonge (au vimiminika)
vilivyokuwa na kiambata
cha panadol kilichokuwa
kikifikia kiasi cha miligramu
325.
Ni vizuri kuzingatia kuwa
baadhi ya dawa za maumivu
zinazotolewa kwa maagizo ya
daktari kama vile Vicodin na
Percocet, pia zina kiambata
cha panadol na kwa hivyo
hazipaswi kuchanganywa na
dawa zingine zenye kiambata
hiki.
Kimsingi panadol siyo
sumu kama yenyewe.
Inakuwa sumu kwa sababu
ini linaibadilisha na kuwa
kemikali ya aina nyingine
inayoitwa NAPQI. NAPQI
husababisha kifo cha haraka
sana kwa seli za ini. Bahati
nzuri ni kwamba ini lina
u w e z o wa k u u a s u m u
ya NAPQI kwa kuifanya
iungane na kemikali
inayoitwa GLUTATHIONE.
Kama siyo hivyo kila
mara tukinywa panadol
tungekuwa tunakabiliwa na
kifo muda mfupi baadaye.
Glutathione ni miongoni
mwa vizuia vioksidishaji
(anti-oxidants) muhimu sana
ndani ya mwili. Pamoja na
kwamba miili yetu itaendelea
kupata ulinzi wa kutosha
dhidi ya acetaminophen/
panadol pale itakapokuwa
ina kiasi cha kutosha cha
glutathione, ni lazima tujue
kuwa kuingiza mwilini kiasi
kikubwa cha acetaminophen/
panadol kunasababisha
uharibifu wa ini.
U T U M I A J I W A PA N A D O L
WAKATI WA UJA UZITO UNAWEZA
K U C H O C H E A U G O N J WA WA
UTUKUTU MKUBWA KWA WATOTO
(Attention Deficit Hyperactivity
Disorder ADHD)
Hivi sasa kuna kundi la
watafiti ambao wanahoji
matumizi ya panadol kwa
kina mama wajawazito.
Hoja yao ni kwamba
m a t u m i z i ya d a wa h i i
katika kipindi cha ujauzito

yanaweza kusababisha mtoto


atakayezaliwa kuwa na tabia
ya utukutu uliokithiri.
Matokeo ya utafiti
yaliyochapishwa katika
jarida la JAMA Pediatrics,
yanaonyesha kuwa panadol
ni kitibua homoni ( hormone
disruptor ), na uwepo wa
homoni usio wa kawaida
mwilini wakati wa ujauzito
unaweza kuathiri maendeleo
ya k u k u a k wa u b o n g o
wa mtoto anayeendelea
kubadilika na kukua
tumboni.
Utafiti huu ambao
ulijumuisha takwimu
zilizohusisha zaidi ya kina
mama na watoto 64,000
kutoka katika kituo cha
Taifa cha Kujifungulia cha
Denmark (Danish National
Birth Cohort), ulionyesha
k u wa z a i d i ya 5 0 % ya
wanawake waliohusishwa
walitoa taarifa za kutumia
panadol wakati wakiwa
waja wazito. Utumiaji huu
wa panadol kwa wanawake
hao ulionyesha matokeo
yafuatayo: Ongezeko la 30%
la hatari ya mtoto kukumbwa
na ADHD katika miaka saba
ya kwanza ya maisha yake.
Ongezeko la 37% la hatari
ya mtoto kukumbwa na
ugonjwa wa hyperkinetic
disorder (HKD), ambao ni
aina ya ADHD iliyopindukia
mipaka.
Utafiti pia ulibaini kuwa
kiwango cha madhara
kilitegemeana na dozi. Kadri
mama mjamzito alivyotumia
panadol kwa wingi wakati
wa ujauzito, ndivyo jinsi
ambavyo uwezekano
wa mtoto kukumbwa na
magonjwa yenye uhusiano
na ADHD ulivyoongezeka.
Aidha kwa mujibu wa utafiti
huu, watoto wa wanawake
ambao walitumia panadol
kwa majuma 20 au zaidi
wakati wa ujauzito walikuwa
na kiwango karibu mara
mbili cha hatari ya kukutwa
na ugonjwa wa HKD.

MADHARA MENGINE YA KIAFYA


YANAYOHUSISHWA NA MATUMIZI
YA PANADOL
Ukiondoa uharibifu wa ini,
panadol pia imehusishwa na
madhara mengine ya hatari
kama uharibifu wa figo pale
inaponywewa na pombe,
saratani za damu, madhara
yanayopelekea ngozi
kukumbwa na magonjwa
kadhaa kama StevensJohnson Syndrome (SJS),
toxic epidermal necrolysis
(TENS), na acute generalized
exanthematous pustulosis
(AGEP), na kuzuia chanjo
zisifanye kazi vizuri pale
vinapotumiwa pamoja..
KUDHIBITI MAUMIVU
Kwa kuwa watumiaji
wengi wa panadol, hasa
kwa watu wazima, hufanya
hivyo kwa nia ya kupambana
na maumivu, ni muhimu

wakajifunza mbinu salama


na mbadala za kuondoa
hayo maumivu. Moja ya
mbinu mujarabu sana katika
suala hili ni kuhakikisha
kuwa muda wote mwili
wako haukabiliwi na
uhaba wa maji. Mwili wako
unapokabiliwa na uhaba wa
maji, akili iliyoko mwilini
mwako inawasha mfumo
wa mgawo wa maji kidogo
yaliyoko ndani ya mwili, ili
kuzuia shughuli muhimu
zinazotakiwa kuendelea
mwilini zisije zikasimama.
Mfumo huu huratibiwa na
kusimamiwa na homoni
ya HISTAMINE, ambayo
kunapokuwa na haja ya
mgawo mwili huizalisha kwa
wingi. Kwa bahati mbaya ni
kwamba katika harakati za
kufanya kazi yake, homoni
hii pia huzalisha kiasi fulani
cha maumivu katika maeneo
mbalimbali ya mwili.
Ukiondoa uhaba wa
maji mwilini, pia viko
aina ya vyakula ambavyo
huuchochea mwili
kuzalisha kiasi kikubwa
cha HISTAMINE. Ulaji wa
vyakula hivi ni kichocheo
kikubwa cha maumivu ndani

ya mwili kwa muda wote.


Mungu tutakuja kuviongelea
vyakula hivi kwa kina.
Tatizo
lingine
linalosababisha maumivu
mwilini ni seli za mwili
kukumbwa na mfuro/uvimbe
m wa k o ( i n f l a m m a t i o n )
kutokana na baadhi ya
vyakula tunavyokula,
au kutokana na kuugua
ugonjwa wowote ule. Mfuro/
uvimbemwako ni zao la kinga
za mwili pale zinapoingia
katika mapambano na
magonjwa mbalimbali.
M f u r o / u v i m b e m wa k o
u n a p o t o k e a k wa m u d a
mfupi tu siyo tatizo sana.
Tatizo linakuwa pale ambapo
mfuro/uvimbemwako
huo umekuwa ni kitu cha
kudumu. Miongoni mwa
dawa nyingi za kifamasia
utakazopewa na daktari
wako kwa ajili ya maumivu
ni zile zinazolenga kuzuia
mfuro/uvimbemwako. Hata
hivyo kutokana na dawa
nyingi za kifamasia kuwa
na usalama unaotia shaka,
ni bora mtu ukajaribu njia
za asili (natural) za kuzuia
mfuro/uvimbemwako.

KONGOLE, JAJI WEREMA !


(WENGINE MWANGOJA NINI?)
Hongera Jaji Werema, kwa kwako kuwajibika,
Umejivua lawama, na vibaya kusemeka,
Umefanya jambo jema, dahari la kusifika,
Kongole Jaji Werema, wengine mwangoja nini?
Kwalo ya kwako adhama, umeitunza hakika,
Hukungoja kwa lazima, kitini kuja kung'oka,
Kwa RAIS muadhama, kando aje kukuweka,
Kongole Jaji Werema, wengine mwangoja nini?
Kisha ubaki lalama, na moyo kusononeka,
Ushindwe kuwatazama, watu kwa kuaibika,
Nao wadumu daima, dawamu wakikucheka,
Kongole Jaji Werema, wengine mwangoja nini?
Baidi umetazama, kwa risala kuandika,
Kwa Kikwete muadhama, kuachia madaraka,
Umefanya jambo jema, linopaswa kugezeka,
Kongole Jaji Werema, wengine mwangoja nini?
Kuchunga zao heshima, tarikayo wangeshika,
Si mui bali i njema, hiyo ya kuwajibika,
Meli ikenda mrama, zaidi wataumbuka!,
Kongole Jaji Werema, wengine mwangoja nini?
Kwa kujibakiza nyuma, si sawa kujamtwika,
Nahodha wenu lawama, kwa dhoruba kuwafika,
Wangekugeza Werema, pazuri wangejiweka!,
Kongole Jaji Werema, wengine mwangoja nini?
Jaribu nao kusema, huenda wakazinduka,
Wasisubiri nakama, wakaja kufedheheka,
Wakose pa kuegama, au hata pa kushika,
Kongole Jaji Werema, wengine mwangoja nini?
Niwombe kwa taadhima, ESCROW walohusika,
Waungane na Werema, na wao kuwajibika,
Kwa nane leo nakoma, kalamu chini naweka,
Wengine mwangoja nini, au mwangoja fedheha?
ABUU NYAMKOMOGI,
MWANZA

AN-NUUR

16
16

16

MAKALA

AN-NUUR

Soma
gazeti la
AN-NUUR kila Ijumaa

SAFAR 1436, IJUMAA DESEMBA 19-25, 2014

SAFAR 1436, IJUMAA DESEMBA 19-25, 2014

Maalim Seif
ziarani Uturuki
Na Mwandishi Maalum

MAKAMU wa Kwanza
wa Rais wa Zanzibar Mhe.
Maalim Seif Sharif Hamad,
amewasili nchini Uturuki
kwa ziara ya siku tatu ya
kiserikali.
Ziara hiyo inafuatia
mwaliko rasmi wa serikali
ya Uturuki kupitia kwa
Waziri Mkuu wa nchi hiyo
Mhe. Ahmet Davutoglu.
Kwenye uwanja wa ndege
wa Kimataifa mjini Istanbul,
Maalim Seif alipokelewa na
Waziri wa Mambo ya nje
wa nchi hiyo Mhe. Mevlut
Cavusoglu.
Mbali ya kufanya
mazungumzo na mwenyeji
wake ambaye ni Waziri
Mkuu wa Uturuki, Makamu

wa Kwanza wa Rais wa
Zanzibar pia anatarajiwa
kukutana na viongozi wa
jumuiya ya watembezaji
watalii ya nchi hiyo.
Aidha Maalim Seif
ambaye ameambatana na
Katibu Mkuu Wizara ya
Habari, Utamaduni, Utalii
na Michezo Zanzibar
Bw. Ali Saleh Mwinyikai,
anatarajiwa kuhudhuria
kwenye maadhimisho ya
sherehe kubwa za kimila
nchini humo ambazo pia
zitahudhuriwa na Rais wa
nchi hiyo Mhe. Recep Tayyip
Erdogan.
Sherehe hizo zinatarajiwa
kuhudhuriwa na wageni
kadhaa mashuhuri kutoka
sehemu mbali mbali duniani.

MASHEIKH na watoa mada walioendesha semina ya Maimamu na viongozi wa


Dini semina hiyo imefanyika katika kituo cha Kiislamu cha Markazi Chang`ombe
jijini Dar es salaam hivi karibuni.

TANGAZO LA MUHADHARA WA MWEZI WA SWAFAR MWAKA


1436/2014 - 2015 MSIKITINI ANSWAR SUNNA KINONDONI
IPO KWA HUDUMA MBALIMBALI ZA
KIBIASHARA NA MAENDELEO KAMA:
1. Kutengeneza mipango ya biashara (Business Plans)
2. Kuandaa michanganuo kwa ajili ya kuombea mikopo (Loan Documents)
3. Kuandaa maandiko ya miradi (Project Write-ups)
4. Kutengeneza mipango mkakati ya taasisi (Strategic Planning)
5. Kutengeneza miongozo ya fedha na uendeshaji katika taasisi (Financial
and Operational Manuals)
6. Kuandaa katiba kwa ajili ya usajili wa vyama na taasisi zisizo za
kiserikali (NGOs)
7. Kufanya usajili wa kampuni/Jina la biashara
8. Kufanya usaili kwa waajiriwa watarajiwa
9. Kuandaa nyaraka za zabuni (Tender documents)
10. Huduma za ushauri kwa wahitimu wa vyuo wanaosaka ajira (Coaching
services)
11. Nakadhalika.

KARIBU: MOSQUE STREET, NO. 1574/144 (MKABALA


NA MSIKITI WA SUNNI), KITUMBINI DAR ES SALAAM.

Uongozi wa Msikiti wa Answar Sunna Kinondoni ulio chini ya taasisi


ya Jamaat Ansawr Sunna unayo furaha kuwatangazia Waislamu kuwa
ndugu zao wa Miskiti wa Answari Sunna Kinondoni wameazimia
kuwa pawepo na muhadhara japo mmoja kila mwezi katika msikiti
wao. Lengo kuu ni kuwafikishia Waislamu mafundisho ya dini
yao kwa mnasaba wa wakati na mazingira na kuwatia hima katika
kuyatekeleza mafundisho hayo.
Kwa mnasaba huo basi mnaarifiwa kuwa mada ya mwezi huu wa
Swafar ni Jinsi Ambavyo Chakula Kinaweza Kumnufaisha au
Kumdhuru Mwanaadamu Na muwasilishaji wa mada hiyo ni Akhi
Pazi Semili Mwinyimvua, Muhadhiri na Mtafiti Katika chuo cha Dar
es salaam na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wataalamu wa Kiislamu
Tanzania(TAMPRO).
Muhadhara huo utakuwa tarehe 21 Desemba 2014 siku ya jumapili
kuanzia saa 10:315 Alasiri.
Manombwa kufika kwa wakati
Wa billahi Tawfiq
Abdallah Salim
Imam Mkuu
Masjid Answar Sunna Kinondoni

Вам также может понравиться

  • Annuur 1230 PDF
    Annuur 1230 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1230 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1262
    Annuur 1262
    Документ20 страниц
    Annuur 1262
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1232 PDF
    Annuur 1232 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1232 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1264
    Annuur 1264
    Документ20 страниц
    Annuur 1264
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Press Realse 28
    Press Realse 28
    Документ4 страницы
    Press Realse 28
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1229 PDF
    Annuur 1229 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1229 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1231 PDF
    Annuur 1231 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1231 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • HOTUBA YA BAJETI OFISI YA RAIS Final
    HOTUBA YA BAJETI OFISI YA RAIS Final
    Документ15 страниц
    HOTUBA YA BAJETI OFISI YA RAIS Final
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • HOTUBA YA BAJETI OFISI YA RAIS Final
    HOTUBA YA BAJETI OFISI YA RAIS Final
    Документ15 страниц
    HOTUBA YA BAJETI OFISI YA RAIS Final
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Press Release - Muungano Na Mazingira
    Press Release - Muungano Na Mazingira
    Документ4 страницы
    Press Release - Muungano Na Mazingira
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1228d
    ANNUUR 1228d
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1228d
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1228d
    ANNUUR 1228d
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1228d
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1227 PDF
    Annuur 1227 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1227 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1226 PDF
    Annuur 1226 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1226 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1224
    Annuur 1224
    Документ20 страниц
    Annuur 1224
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1225
    Annuur 1225
    Документ20 страниц
    Annuur 1225
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1223
    Annuur 1223
    Документ20 страниц
    Annuur 1223
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1213 PDF
    Annuur 1213 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1213 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1220
    Annuur 1220
    Документ20 страниц
    Annuur 1220
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1217
    Annuur 1217
    Документ20 страниц
    Annuur 1217
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1218 PDF
    Annuur 1218 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1218 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1219
    Annuur 1219
    Документ20 страниц
    Annuur 1219
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Karume Shujaa
    Karume Shujaa
    Документ11 страниц
    Karume Shujaa
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1216d
    ANNUUR 1216d
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1216d
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1214
    Annuur 1214
    Документ20 страниц
    Annuur 1214
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1212
    Annuur 1212
    Документ20 страниц
    Annuur 1212
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1215 PDF
    Annuur 1215 PDF
    Документ20 страниц
    Annuur 1215 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    100% (1)
  • Hotuba Ya Maalim Seif - January 9 2016
    Hotuba Ya Maalim Seif - January 9 2016
    Документ27 страниц
    Hotuba Ya Maalim Seif - January 9 2016
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • ANNUUR 1209aaa
    ANNUUR 1209aaa
    Документ20 страниц
    ANNUUR 1209aaa
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет
  • Annuur 1210a
    Annuur 1210a
    Документ20 страниц
    Annuur 1210a
    Anonymous x8QGwFF
    Оценок пока нет