Вы находитесь на странице: 1из 20

Tamko la Masheikh kuhusu

Mahakama ya Kadhi

Sauti ya Waislamu

ISSN 0856 - 3861 Na. 1163 RABIUL THANI 1436, IJUMAA , FEBRUARI 6 - 12, 2015 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Uk.16

Mkurugenzi TAMPRO afunguliwa kesi ya ugaidi


Asimamishwa kizimbani na mkewe
Ombi la dhamana kwa mkewe lakwama
Watuhumiwa walalamika kukosa hewa

Melody mwaka huu Zanzibar


huenda ikawa mbaya zaidi

Kauli ya Waziri Mathias Chikawe


Bundi kalia juu ya nyumba mchana

Picha Juu, Kaimu Mkurugenzi


Mtendaji wa TAMPRO, Ustadhi
Haruna Mussa Lugeye. Chini
mkewe Bi. Mwajumbe Wendu
Bakari.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mheshimiwa Mathias


Chikawe. Soma Uk. 10.

Kura ya Maoni.

Hatari tupu
kwa Zanzibar
Vereje wa-Bara wapige kura!
Ya nini hadaa na janja yote hii
Kuinyima Zanzibari sauti ya kuamua?

Soma Uk. 13

Tahariri
AN-NUUR

S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786


Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM.
www.annuurpapers.co.tz
E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk
Ofisi zetu zipo: Manzese Tip Top
Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

Jeshi la Polisi lijisafishe

MALALAMIKO
kuhusu utendaji
usioridhisha wa jeshi
letu la polisi yamekuwa
mengi. Raia wa kawaida
ndio ambao wamekuwa
wakilalamika zaidi,
lakini kwa bahati
mbaya, sauti zao hazina
msikilizaji.
Viongozi wa vyama
vya upinzani na asasi
za wanaharakati nao
wamekuwa wakipaza
sauti zao, kilio kikiwa ni
kile kile cha utendaji ulio
jaa dhulma na ukiukwaji
wa haki za binadamu wa
jeshi hilo. Nao hakuna
aliyewasikiliza.
Lakini kwa upande
mwingine, jeshi hilo
hilo la polisi limekuwa
na utekelezaji mzuri
wa amri kutoka kwa
wanasiasa walioshikilia
dola na hata wenye
fedha na ukwasi wa
mali. Vyombo vya habari
mara kadhaa vimekuwa
vikiripoti madhila kadha
wa kadha yanayofanywa
na jeshi hilo dhidi ya raia
na wanyonge, wakiwa na
matumaini labda serikali
inaweza kuguswa na
kuamua kulisafisha jeshi
hilo, ili liweze kufanya
kazi zake kiadilifu na
kwa weledi kwa mujibu
wa sheria bila kuwaonea
watu.
Pamoja na kelele za
viongozi wa vyama vya
siasa na wanaharakati
pamoja na raia ambao
kwa namna moja au
nyingine wameumizwa
na jeshi hilo, bado hakuna
hatua zozote madhubuti
zilizochukuliwa
kuliboresha jeshi letu
likawa la kistaarabu na
linalofuata sheria na haki
za binadamu.
Takwimu za taasisi
mbalimbali zimeonyesha
kuwa jeshi hilo ndio
kinara wa rusha nchini.

Pamoja na kutolewa
taarifa hizo za kitafiti,
bado serikali imepiga
kimya.
B a a d h i
y a
polisi wamekuwa
l i k i l a l a m i k i wa k wa
kubambikia watu
kesi, hakuna hatua
zilizodhihirika za
kukomesha unyama huo.
B a a d h i
y a
askari wamekuwa
wakituhumiwa
kuhusika katika baadhi
ya vitendo vya kihalifu
kama ujambazi, bado
hatusikii wala kuona
usafi ukifanyika ndani
ya jeshi hilo.
W a n a s i a s a
wamelalamika kuwa
jeshi linatumiwa kisiasa
kudhibiti wanasiasa hasa
wa upinzani, hususana
katika kutumia haki
yao ya msingi ya
kufanya mikutano
au kuandamana kwa
amani, njia mbazo
ndizo zilizozoeleka
kwa wanasiasa
kuwafikia watu wao.
Tumeshuhudia mikutano
ya k i s i a s a i k i p i g wa
marufuku kwasababu
zinazoitwa za kiusalama,
lakini kimantiki lengo
likiwa ni kuzuia nguvu
ya upinzani. Hapa ndipo
tulipolifikisha jeshi letu.
Limegeuka kuwa kama
chombo cha kulinda
maslahi ya watu kisiasa,
kugeuza vituo vyake
kuwa ofisi za kuchuma
fedha chafu kwa njia ya
rushwa, kugeuka pepo
ya wenye fedha kununua
haki za wanyonge nk.
Siku hizi kwa
upande wa walala hoi,
wakifikishana polisi
kutatuliwa mashauri yao,
kila upande utalazimika
kutoa chochote
ukitegemea kupata
haki. Muhimu si nani
kamkosea mwenzake. Ni

mfuko wako.
Kuna tetesi kwamba
hata faini za vyombo
vya moto barabarani
(Notification) nazo zipo
halisi na za kughushi.
Lakini hakuna wa
kuchunguza licha ya
tetesi hizo kusambaa kila
kona.
Watu wamejeruhiwa
kwa vipigo bila hatia.
Wa p o w a l i o p o t e z a
maisha yao, wapo
walioharibiwa mali zao,
yote hayo ni matokeo ya
kinachodaiwa kuwa ni
uozo ndani ya jeshi hilo.
Tunakumbuka mwaka
2006 kulikuwa na
mpango wa kuboresha
Jeshi letu la Polisi uliotwa
Programu ya Maboresho
ya Jeshi la Polisi.
Ilikuwa ni Programu
ya serikali ya kuboresha
utendaji wa Jeshi la
P o l i s i c h i n i Wi z a r a
ya Mambo ya Ndani
ya N c h i , i l i y o k u wa
imegawanywa kwa
awamu mbili. Awamu ya
kwanza ilielezwa kuanza
2010/2011 hadi 2014/2015
na awamu ya pili
iliahidiwa kutekelezwa
kati ya mwaka 2015/2016
hadi 2019/2020.
Programu hiyo ilianza
baada ya Jeshi la Polisi
kupokea ripoti ya timu
iliyohusisha watalaamu
wa ndani na nje ya Jeshi
la Polisi iliyofanya utafiti
na kutoa mapendekezo
yao kwa uongozi wa
Jeshi la Polisi na Wizara
ya Usalama wa Raia.
Timu hiyo iliweza
kukusanya maoni toka
kwa viongozi wa juu wa
nchi wakiwemo Marais
waliokuwa madaraakni
na wastaafu, Rais,
Mawaziri, wanachuoni,
viongozi wa vyama vya
siasa na dini, wananchi
wa kawaida na wadau
wengine.
Moja ya Mapendekezo
ilikuwa ni kuanzishwa
kwa Programu ya
Maboresho ya Jeshi la
Polisi ili kuzifanyia kazi
changamoto mbalimbali
zilizokuwa zinalikabili
Jeshi la Polisi.
Mwaka
2007
iliteuliwa timu ya
kuratibu na kusimamia
maboresho iliyohusisha

AN-NUUR

RABIUL THANI 1436, IJUMAA FEBRUARI 6 - 12, 2015


wanataaluma wa
ndani ya Jeshi la Polisi
wenye fani mbalimbali.
Programu iliidhinishwa
rasmi na Baraza la
Mawaziri tarehe
31.03.2012 na kuifanya
itambulike rasmi kama
mojawapo ya Programu
za Maboresho ya Sekta
ya Umma yanayoendelea
hapa nchini.
Baadhi ya sababu za
k u f a n ya m a b o r e s h o
ndani ya Jeshi la Polisi
z i l i k u wa n i p a m o j a
na kubadilika na
kuongezeka kwa aina,
m b i n u n a i d a d i ya
makosa makubwa ya jinai
nchini hususan mwaka
2005 na mwanzoni mwa
2006 kulikosababisha
kudorora kwa hali ya
usalama wa raia na mali
zao kote nchini.
Nyingine ilikuwa ni
kudorora kwa ufanisi
katika utendaji kazi wa
Jeshi la Polisi kutokana
na kutumia mifumo
iliyopitwa na wakati
wa kuzuia na kudhibiti
uhalifu, uchache wa
a s k a r i , u k o s e f u wa
mafunzo ya ujuzi,
uchache wa vitendea
kazi na mazingira duni
ya ofisi na makazi.
Kupungua kwa imani
ya wanachi kwa Jeshi
la Polisi kutokana na
kuongezeka kwa vitendo
vya uhalifu nchini na
kushuka kwa nidhamu
na hadhi ya Jeshi la Polisi.
Hata hivyo, kwa
mwenendo wa sasa wa
jeshi letu hili, hatudhani
kama serikali ilitilia
m k a z o u t e k e l e z wa j i
wa progaramu yake
hiyo kuboresha jeshi
hilo na kuzifanyia
kazi changamoto
zilizoanishwa hapo juu.
Ni matumaini yetu
kwamba, wabunge
kwa kutambua shida
wanazopata wananchi,
wataifanyia kazi hoja
iliyowasilishwa Bungeni
hivi sasa na Mhe. James
Mbatia, kuhusu utendaji
usioridhisha wa chombo
hiki kinachoitwa cha
usalama wa raia.
Zitizamwe sheria na
kanuni zinazosimamia
jeshi hili, ili kuondoa
sheria na kanuni

zinazotoa mwanya kwa


askari wetu kudhulumu
haki za watu badala ya
kulinda usalama wa
watu.
Tunafahamu kuwa
jeshi ni chombo cha dola
cha kudhibiti wakorofi,
wahuni na wahalifu.
Tunajua kuwa ni lazima
chombo hicho kitumie
nguvu na zana kutekeleza
wajibu wake wake huo.
Lakini pia tunafahamu
kuwa chombo hiki
lazima kitumie
utaalam, kuzingatia
sheria na kanuni
katika kukabiliana na
wa h a l i f u h a o . K wa
mfano, hatudhani mtu
kama Marehemu Daud
M wa n g o s i a l i s t a h i l i
kupigwa hadi kufa kama
mhalifu hali ya kuwa
mazingira na uhalisia
unadhihirisha kuwa
h a k u wa m h a l i f u n a
hakustahili kipigo. Wala
haitukutarajiwa kama
vijana wa Kamanda
Suleiman Kova,
wa n g e g o m b e a f u k o
la fedh a zilizokuwa

zimeibwa katika duka


moja huko Kariakoo
jijini Dar, badala ya
kupambana na kuwatia
adabu majambazi
waliokuwa wameziiba
fedha hizo na kukimbia
huku wakitupa fuko
hilo la fedha.
Kadhalika si sahihi
kummiminia marungu
mwandamanaji
aliyekamatwa na
kumweka ndani ya
himaya (gari la polisi)
kasalimu amri, halafu

polisi wakaendeleza
kipigo kwake. Matukio
ya namna hii yamekuwa
mengi na hakuna
anayewajibika.
Wananchi wanataka
ifike tamati ya mazoea
yaliyojengeka kwa
miongo kadhaa ya
watu kudhulumu kwa
kutumia Crown.
Watanzania wanahitaji
jeshi safi lenye maadili,
linalofuata sheria
na haki za binadamu
katika ukekelezaji wa
majukumu yake.
Si jambo lenye tija wala
la kujivunia kuendelea
kuwa na jeshi la polisi
lisiloaminika mbele ya
raia wake.

Habari/Tangazo

AN-NUUR

RABIUL THANI 1436, IJUMAA FEBRUARI 6 - 12, 2015

Mkurugenzi TAMPRO afunguliwa kesi ya ugaidi


Na Seif Msengakamba

WAISLAMU waliduwaa
kwa muda baada ya
juzi Jumanne wiki hii
kumuona Mkurugenzi
wa Fedha na Utawala
wa TAMPRO, Ustadhi
Haruna Mussa Lugeye,
pamoja na mkewe
wakipandishwa
kizimbani katika kesi
nyingine ya ugaidi.
Ustadh Lugeye
pamoja na mkewe Bi.
M w a j u m b e We n d u
Bakari, walipandishwa
kizimbani katika
Mahakama ya Kisutu
jijini Dar es Salaam,
mbele ya Hakimu Janet
Kaluyenda.
Hata hivyo Hakimu
Kaluyenda aliahirisha
kesi hiyo hadi Februari
16 mwaka huu kwa kuwa
Hakimu anayeisikiliza
kesi yao Mh. Moshi
hakuwepo mahakamani.
Juhudi za kumtoa
mkewe kwa dhamana
nazo zilikwama pia.
Hii ni kutokana na
H a k i m u K a l u ye n d a
kusisitiza kuwa yeye
hatoweza kutoa
dhamana kwa sababu
shauri halipo kwake.
Na hivyo kushauri
Wa k i l i w a u t e t e z i
amsubiri Hakimu
mwenye shauri hilo.
Kuhusu kesi hiyo,
wakili Salim alisema Bw.
Haruna Mussa Lugeye na
mkewe wanatuhumiwa
kwa mashitaka ya ugaidi
na Kesi yao ilianza tarehe
10/12/2014.
Alisema hiyo ni kama
mara ya tatu au ya nne
kutajwa Mahakamani
hapo.
Wakati huo huo, kesi ya
Watuhumiwa wa ugaidi
inayowakabili Waislamu
2 3 a k i we m o S h e i k h
Mselem Ali Mselem
na Waislamu wengine,
wameilalamikia
mahakama kuwa
gari linalowabeba
wakati wakipelekwa
mahakamani hapo
halifai.
Wa t u h u m i wa h a o
walidai gari walilokuwa
wamepanda lilikuwa
l i k i f u n g wa v i o o n a
kusababisha kuvuta
hewa kwa taabu.

Akizungumza
mahakamani hapo,
wakili wa upande wa
utetezi Abubakari
Salim, alisema kuwa
ameshangazwa na
kitendo hicho kwani
sio cha kiuungwana
na kuitaka Mahakama
itambue kuwa,
watuhumiwa hao ni
binadamu wanaohitaji
hewa.
Akithibitisha kutokea
kwa tukio hilo, dereva
wa gari linalowabeba
watuhumiwa hao
(jina la dereva huyo
halikufahamika mara
moja) alisema kuwa vioo
vilifungwa kwa sababu

za kiusalama kufuatia
vurugu zilizotaka
kujitokeza katika eneo
l a m a g e r e z a wa k a t i
wanajiandaa kuanza
safari ya kuelekea
mahakani.
Niliamua kufunga
vioo baada ya kuona
dalili ya vurugu,
lakini kabla sijaamua
kufunga niliwatangazia
watuhumiwa kuwa
nafunga kwasababu ya
usalama wao na wangu.
Kwa bahati mbaya
nilisahau kufungua,
lakini sikuwa na nia
yoyote mbaya", alisema
dereva huyo.
Kwa upande wake

hakimu anayesikiliza
kesi hiyo Mh. Janet
Kaluyenda, alimtaka
dereva huyo kutorudia
tena kitendo hicho na
endapo kitajirudia, basi
t a a r i f a i t o l e we k wa
mkuu wa magereza ili
atoe maamuzi, kwani
mahakama haihusiki na
masuala ya magereza.
Hakimu Kaluyenda
aliahirisha kesi hiyo hadi
Februari 16 mwaka huu.
Naye Wakili waupande
wa utetezi Abubakari
Salim, alisema kesi zote
mbili zilipangwa kwa
ajili ya kutajwa.
"Ile Kesi ya Masheikh
na Waislamu wengine

ambayo inahusu watu


23 ilipangwa kutajwa leo
lakini Serikali walisema
kupitia kwa DPP,
kuwa wameshaamua
kukata rufaa kwenda
Mahakama ya Rufaa kwa
hiyo mara ya mwisho
wametuambia wamesha
faili hati ya rufaa lakini
hatukuwa nayo.
Alisema wakili huyo.
Alisema siku ya
kutajwa kesi ndio
wamepata barua kutoka
Mahakama ya Rufaa,
ambayo inathibitisha
kwamba
kweli
wameshapeleka hati ya
kukata rufaa.

Sheikh ataka hijab iheshimiwe Kenya


KATIBU Mtendaji wa
Baraza la Maimamu na
Wahubiri nchini KenyaCIPK, ameitaka serikali
kuweka mikakati ya
kuhakikisha vazi la
hijab linaheshimiwa
kwa mujibu wa katiba
ya nchi hiyo.
Sheikh Mohamed
Khalifa, aliongeza
kuwa sharti la hijab
ni kusitiri sehemu za
mwili wa mwanamke
na bila kumuonyesha
sehemu zake za mwili na
kusababisha matamanio
kwa wanaume.
Sheikh Khalifa
aliyasema hayo katika
siku ya kimataifa
ya kuadhimisha vazi
la hijab, inayofanyika
Februari mosi kila
mwaka na kusisitiza
kwamba, serikali
ya Nairobi inapaswa
kuweka mikakati
kabambe ili kuhakikisha
va z i h i l o l i n a p e wa
heshima ipasayo kwa
mujibu wa katiba ya nchi
hiyo.
Aidha Katibu huyo
Mtendaji wa CIPK
alisema kuwa, vazi la
hijab ni ishara ya stara,
faragha na ucha Mungu
k wa m wa n a m k e wa
Kiislamu.
Hata hivyo vazi hilo la
stara kwa wanawake wa
Kiislamu linakabiliwa

na chamgamoto kadhaa
ulimwenguni hasa
mashuleni, vyuoni,
makazini na hata kwenye
sehemu za umma.

Sheikh Khalifa alisema


kuwa, changamoto
wanayokumbana nayo
wanawake wa Kiislamu
ni taasisi za binafsi

zinazohujumu haki zao,


kauli iliyoungwa mkono
na viongozi wengine wa
dini ya Kiislamu nchini
Kenya. (Sabahi).

Muhadhara wa mwezi
Rabiul Thani 1436/2015

Jihesabu Kabla Hujahesabiwa


Uongozi wa Msikiti wa Answar Sunna Kinondoni ulio chini ya taasisi
ya Jamaat Ansawr Sunna, unayo furaha kuwatangazia Waislamu kuwa
ndugu zao wa Miskiti wa Answari Sunna Kinondoni wameazimia
kuwa pawepo na muhadhara japo mmoja kila mwezi katika msikiti
wao. Lengo kuu ni kuwafikishia Waislamu mafundisho ya dini yao kwa
mnasaba wa wakati na mazingira na kuwatia hima katika kuyatekeleza
mafundisho hayo.
Kwa mnasaba huo basi, mnaarifiwa kuwa mada ya mwezi huu wa
Rabiul Thani ni Jihesabu Kabla Hujahesabiwa.
Muwasilishaji wa mada hiyo ni Sheikh Yusuf Salim, Imam wa masjid
Nurul Huda Argentina Dar es Salaam
Muhadhara huo utakuwa tarehe 8 Februari 2015 siku ya Jumapili
kuanzia saa 10: 15 Alasiri.
Mnaombwa kufika kwa wakati
Wa billahi Tawfiq
Abdallah Salim
Imam Mkuu
Masjid Answar Sunna Kinondoni

4
SI panya mnyama aishie na
watu, wala si changudoa
samaki kitoweo kizuri na
chenye bei nzuri. Hawa ni
watoto wetu, ama ni ndugu
zetu kwa nasaba au kwa
majirani. Inashtusha na
kushangaza. Dar es Salaam
ilikumbwa na taharuki
ya Dar es PANYA ROAD
(Mbwa Mwitu).
Mengi yamesemwa na
watu mbalimbali wakiwemo
watu wazito katika jamii,
l a k i n i w e n g i wa l i o o n a
kwa karibu tukio husika
wakihadithia unahisi kama
wanahadithia filamu ya
Anorld SChwatzneeger au
Sylvester Stallone.
Hofu, vicheko na mzaha
vilikuwa ndio gumzo kubwa
la kwanza la mwaka 2015
hapa Jijini Dar es Salaam.
Imesababisha mpaka wengine
kushukuru wapendwa wao
kurudi nyumbani mapema
na wengine kuhuzunika
wapenzi wao kuchelewa
kurudi nyumbani, kisa
Sekeseke la Panya Road
maeneo kadhaa ya jiji la Dar
es Salaam.
Wengi waliangukia katika
kuinyooshea vidole serikali,
hasa Jeshi la Polisi kwa
kuzembea kupata habari za
Ki-intelijensia kuthibiti hali
hilo na wengine wamehoji,
wapi zile mbwembwe za
polisi jamii katika kupambana
na uhalifu.
Nilikaa na kuangalia
nini hasa kimetokea na
wapi tunaenda. Nini nafasi
ya k i l a c h o m b o h u s i k a
katika taharuki kama hizi.
Familia, jirani, Misikiti,
Kanisa, Serikali Polisi na
walimwengu kwa ujumla.
Nakubaliana na maoni ya
watu mbalimbali juu ya Polisi
na vyombo vya usalama
kukosa taarifa za msingi juu
ya kuthibiti kilichotokea.
Lakini kwa sehemu kubwa
vyombo habari vya kijamii,
yaani social media (Whats
U p , F a c e b o o k , Tw i t e r ,
Blogs, Instagram etc) nazo
zimekuwa mtihani sana kwa
kukuza mambo kuliko hali
halisi.
Pamoja na kwamba kuna
faida, lakini hii moja ya
madhara ya vyombo hivi
katika jamii. Upokeaji wa
habari kwa vyombo hivi
u n a h i t a ji u ma k i n i sa n a
kwani nusu ya taarifa huwa
zinatengenezwa na watu
b i n a f s i we n ye m a l e n g o
tofauti.
Nadhani kuna umuhimu
wa kuongeza mtazamo wa
ziada juu ya hili, nalo ni mkao
wa jamii yetu ya Kitanzania
kwa ujumla.
Panyaroad, changudoa,
mbwa mwitu, kiboko msheli,
American etc ni vikundi
ZAO la kuporomoka kwa
maadili ya Jamii. Hawa vijana
wanatoka katika jamii zetu.
Tunaishi nao kama watoto
wetu, wadogo zetu, majirani
zetu, waumini wenzetu etc.
Nini kumetokea mpaka
tumefika hapa na nini
matumaini ya baadae kama
tutaendelea na visingizio
vya kutushughulisha na
mambo mepesi na kuacha
kushughulikia matatizo ya
msingi, ambayo sehemu
kubwa ni kuporomoka kwa
mfumo wa familia na maadili
katika Jamii zetu na kukosa
upendo kwa watu wa imani
na dini mbalimbali.
Familia ni taasisi kongwe
na kubwa, ambayo ndio ya

Makala

AN-NUUR

RABIUL THANI 1436, IJUMAA FEBRUARI 6 - 12, 2015

Panya road na changudoa

Umekwenda wapi wajibu wa dini, familia

MUFT Issa Shaban Simba.


kwanza kimajukumu katika
jamii yoyote. Taasisi ya
familia hujengwa na mifumo
imara ya ndoa katika jamii
husika. Kuwa na taasisi
imara kama ni nguzo kubwa
sana ya amani na msaada
mkubwa sana katika utulivu
na ustaarabu watu katika
nchi.
Tujiulize nini kinatokea
n d a n i ya f a m i l i a z e t u ?
Ndoa zinavunjika hovyo,
migongano ya kifamilia,
wazazi kutowajibika
kimaadili mbele ya watoto
wao, na kubwa zaidi watoto
kulelewa na mifumo ya
vyombo vya habari hususan
TV na Internet, ambapo si
ajabu kukuta mzazi amejaza
filamu zenye mambo ya ajabu
na watoto kuangalia pasi
na kufuata mila, desturi na
sheria za nchi.
Haya yote ni miongoni
mwa mengi yanayotuzalia
Panya Road.
Suala la Polisi
kuwashughulikia ni hatua
ya kutibu badala ya kuzuia.
Hatua ambayo ni ya mwisho
kabisa katika ngazi za kijamii.
Je, kuna uwezekano wa kuishi
na kuondoa Panya road na
changudoa kwa kuwa na
familia za aina hii? Watoto
wangapi wanazaliwa na baba
anaingia mitini na mama
kubaki mlezi pekee katika
makuzi ya mtoto?
Ndoa ngapi zinavunjika
kwa fitna za wana jamii
waliozunguka huku jamii
hiyo ikijua fika kuwa
kwa kufanya hivyo ndio
tunazalisha panya road
na machangudoa wengi
zaidi kwa ndoa kuvunjika.
Kuna baadhi ya jamii za
kidini, mfano Waislamu
wanaamini kuwa kuwepo
wa Mahakama ya Kadhi
kunaweza kupunguza
kusambaratika kwa familia,
kwa kuelimisha na kutoa
haki kwa wanandoa. Lakini
jamii nyingine isiyo ya imani
hiyo inapinga kwa sababu
ya chuki tu za kiimani na
kusahau kuwa familia imara
yenye maadili ya kidini ndio
mzizi mkuu wa kupambana

IGP Ernest Mangu.

POLYCARP Kadinali Pengo

na matatizo ya vijana, ambao


m w i s h o we h u t u m b u k i a
katika makundi machafu
na kufanya muendelezo
wa kuzalisha Panyaroad na
changudoa?.
Haya ni sehemu ya
Maswali ya Kujiuliza
kama jamii kwa kuangalia
mporomoko wa Taasisi ya
Familia. Mengi ya Maswali
haya Ukiangalia kwa makini
utaona kuwa serikali kama
ingekuwa inaamini kuwa si
polisi au jeshi tu peke yake
ndio linaweza kuleta amani
ila kuna mambo ya msingi
lazima yawepo na jeshi la
polisi au chombo chochote
cha usalama kinaweza fanya
kazi kwa wepesi zaidi katika
mazingira hayo ya uwepo
wa misingi ya Kifamilia
Bora, basi kungefanyika
uwekezaji mkubwa sana
hasa katika mahali pa Familia
walau kusikiliza jamii zenye
mahitaji maalum kama hayo
ya Mahakama ya Kadhi na
mengineyo ya Msingi.
Ujirani na kuvumiliana ni
moja ya misingi mikubwa ya
jamii kuendelea kwa pamoja
katika nyanja mbalimbali za
kisiasa, kijamii na kiuchumi.
Jamii zetu za zamani zilikuwa
zimeshikana sana na kuona
kuwa kila mtoto anakuwa ni
mtoto wa jamii na si mtoto
wako tu.
Hapa unakuta matatizo
kama ya utoro shuleni nk,
yanadhibitiwa na watu wa
eneo husika na kuleta amani
na utengamano katika jamii.
Kwa sasa ujirani umekuwa
ni jambo adimu sana.
Nyumba ya pili yaweza tokea
jambo kubwa kama msiba au
kupotea mtoto na nyumba
ya tatu inaweza isijue. Jamii
kama hii lazima Panya road
wawepo kwa kuwa hakuna
uthibiti wa pamoja katika
eneo husika kama jamii.
Taasisi za dini, hapa
namaanisha Misikiti na
Kanisa kwa hapa kwetu
Ta n z a n i a . H a p a n a k o

kuna matatizo makubwa


sana kwani hali ni mbaya.
Baadhi ya madhehebu ya
kidini mengi yamezongwa
na kashfa za ngono, wizi
na tama ya fedha kama
tulivyoshuhudia viongozi
wa dini katika sakata la
Escrow, madawa ya kulevya,
mifarakano ya kiuongozi nk,
uanzishwaji wa madhebu
kwa ajili ya kuvuna fedha nk.
U n a p o k u wa n a j a m i i
inayokulia na kushuhudia
aina hizi za tabia katika
imani, basi haiwezekani hata
siku moja kuiweka jamii
ikaepukana na uchafu wa
kitabia kama wa Panya road
au changudoa.
Kubwa zaidi katika jamii
ya Kitanzania kuna ongezeko
kubwa la chuki za kiimani,
makundi mbalimbali ya
kidini. Tumeshuhudia hadi
M a wa z i r i wa k i o n ye s h a
kukerwa na imani fulani
katika Bunge la Katiba,
na hivi majuzi tumeona
miongoni mwa viongozi
wa kidini akiishambulia
taasisi ya Mkaguzi Mkuu wa
Serikali kwa hisia za kidini
bila ya ushahidi.
Walau kama ni kweli,
jambo hilo lina athari gani
katika jamii ambayo inataka
kupambana na Panya road
na changudoa na sio uwepo
wa Msikiti au Kanisa sehemu
fulani.
Haya yote ni hali ileile
ya kuonyesha kuwa imani
za kidini hazina mtazamo
mmoja juu ya kupambana
na mambo ya hatari na
maovu katika jamii, kama
vitabu vyao vinavyoelekeza
zaidi ya kila mmoja kudhani
kuwa kuna kundi litakuwa
juu ya wenzake kwa raha
mustarehe, ama kundi
kukandamiza jamii moja au
hata kuiweka katika wakati
mgumu ili ionekane dhaifu.
Hili nalo ni tatizo
kubwa sana. Tumeona hao

Pa n ya r o a d wa p o a k i n a
Abdallah na John au Fatuma
na Ester. Pia katika harakati
zao za vurugu mbalimbali
tumewaona akina Ephraim
na akina Hassan wakipata
kibano.
Laiti jamii hizi za dini
zingekuwa na mtazamo
mpana wa kushirikiana
katika mambo ya msingi bila
hila, ambayo kwayo ndio
maamrisho ya vitabu vyao,
basi matatizo kama haya ya
Panyaroad yangekuwa ni
kwa nadra sana kwa kuwa
sehemu kubwa ya jamii
ingekuwa tiifu na yenye
upendo.
Kwa ujumla bado sehemu
kubwa ya jamii inainyoosha
kidole serikali, hasa jeshi
la polisi pasi na kuangalia
ukubwa wa tatizo husika.
Ukiangalia kwa makini
muelekeo wa Watanzania
wengi kwa sasa, utaona
tunashughulishwa sana na
vitu ambavyo si matatizo
ya msingi katika jamii yetu,
tunaacha kuhangaika na
matatizo halisi ambayo
yanaendelea kututafuna
tunashabikia mambo ya
kijinga.
EPA ESCROW na ujambazi
mwingine, yote hayo ni
matokeo ya kuporomoka
malezi ndani ya jamii yetu.
Tumekuwa tukiamini katika
maendeleo ya ubinafsi na
kusahau kuwa tunatengeneza
bomu zito.
Nadhani kama nchi,
tukiweza kuchunguza na
kutambua upungufu wetu,
kwa kutafakari kwa kina,
tunaweza kupata njia nzuri
ya kuondokana na ongezeko
la maovu ndani ya jamii na
kujenga jamii bora yenye
amani na utulivu wa kweli.
N a a m i n i p a n ya r o a d
na Machangudoa ni tatizo
la kijamii zaidi, kuliko
kuwaonyesha vidole vyote
Jeshi la Polisi na Serikali.
Japo nalo limekuwa jeshi la
operesheni zenye maslahi
zaidi kwao kuliko kulinda
mali na usalama wa watu kwa
ujumla kama inavyotakikana.
Kwa zile jamii zenye
madai maalum na serikali
kuyazima madai hayo kwa
nguvu au hila, basi hapa
tusishangae anguko la
kijamii likiongezeka, hasa la
kutotii mamlaka zilizopo na
kuongezeka zaidi hao panya
road.
Jamii ya Kitanzania
ikishirikiana inaweza
kuondoa mashaka mengi
ya kijamii na kiuchumi
na kuleta maendeleo ya
pamoja kama jamii moja.
Hili linawezekana, lakini
linahitaji uongozi thabiti
unaoona umuhimu wa jamii
yanye maadili kuanzia ngazi
ya familia, koo, ujirani hadi
serikalini kwa Ujumla.
Vi o n g o z i wa s e r i k a l i
wana dhima ya kulisimamia
hili na kulisema kadri
iwezekanavyo. Wao wawe
mfano wa uadilifu katika
nyadhifa zao.
Mungu ibariki Tanzania,
Mungu ibariki Afrika.
Maasalaam...

Makala

AN-NUUR

RABIUL THANI 1436, IJUMAA FEBRUARI 6 - 12, 2015

Chama hiki naona kinajiua wenyewe


Na Mwadini A. Mwadini

NDIVYO ninavyoamini kwa


uhakika kabisa mpaka hivi
niandikapo haya maneno,
kwamba chama hichi
Chama Cha Mapinduzi
(CCM) ambacho ndicho
kinachoshikilia hatamu
za uongozi wa jamhuri,
ikiwemo pia katika nchi
yetu rahimu Zanzibar
kinajiua chenyewe.
Hapa tena wala hapana
haja ya kutafutwa ni nani
mchawi anayekiangamiza:
e t i i l i m t u h u y o n d i ye
apewe huyu mwana (CCM)
amlee. Katika ule msemo
wa mchawi mpe mwana
kulea. Hayupo mtu yeyote
wa kukisaidia CCM kirudi
kwenye mstari ulionyooka
kama kilivyokuwa zamani
kama wale wenyewe
hawashughulikii mivutano
inayokitafuna.
Hadithi ya matatizo ya CCM
ni kama vile walivyosema
kikulacho kinguoni mwako.
Wa n a o k i s h a m b u l i a n a
kukihasidi chama hichi ni
makada wenyewe. Tatizo
wana majivuno yasiyo kifani.
Wakaidi. Makada wa CCM
ni watu waliolelewa katika
fitina na khiyana. Yote haya ni
maovu na mambo ya hasadi.
Na haya waliyabuni hasa kwa
ajili ya kuyatumia kusakama
wasiokuwa waumini wa
chama hichi wapinzani
kisiasa. Sasa kwa kuwa
mla nyama ya mtu haachi,
wakishakosa wa kumsakama
ndani ya chama chao, kwa
maana miongoni mwa
wanachama wenzao, makada
wa CCM huendeleza ushetani
kwa kulana wenyewe kwa
wenyewe. Hawa watu ni
mzoea vya kunyonga vya
kuchinja haviwezi. Hawawezi
kustahamili kukosa kwa
kuwa walivyolelewa ni watu
wa kupata tu, hata ikiwa
kupata kwao ni maafa kwa
wenzao.
Nenda jimbo la uchaguzi
la Uzini, Wilaya ya Kati,
Mkoa wa Kusini Unguja,
utasikia mfarakano
unaorindima kati ya viongozi
waliochaguliwa na wananchi
kwenye uchaguzi. Jimboni
kule, ambako wananchi
wake kwa zaidi ya asilimia
90 wamekuwa wakiishi kwa
kutegemea shughuli za kilimo,
ikiwemo ufugaji, Mjumbe
wa Baraza la Wawakilishi,
Mohamedraza Hassanali
Dharamsi, anavutana na
Mbunge wa Bunge la Jamhuri
ya Muungano, Muhammed
Seif Khatib. Uliza mfarakano
wao umesababishwa na kitu
gani, ndipo utapothibitisha
zaidi ninachokisema
kwamba wana-CCM
wanaishi kwa kufitiana
na kupikiana majungu
kama wanavyowafanyia
wasiokuwa CCM.
M v u t a n o wa m a k a d a

hawa nauelewa kwa upana


wake ulivyoanza. Nataka
kuwathibitishia kwamba
zipo chuki kati yao. Lakini,
chuki hizi ni matokeo ya
siasa za fitina na husda
zinazokitafuna chama
hichi. Wako baadhi ya watu
ambao wana chuki dhidi
ya Wazanzibari wasiokuwa
na rangi nyeusi, hasa hasa
wale anaoamini ni watu
waliotokana na vizazi vya
jamii za Kiarabu, Kihindi
au wale wa makabila
madogo zaidi waliokuwa
wameshika ulwa serikalini
kabla ya mapinduzi ya 1964.
Baadhi ya watu hawa ni wale
waliokuwa katika utumishi
wa serikali zilizokuwepo
chini ya hifadhi ya
Waingereza, ikiwemo serikali
mchanganyiko iliyoundwa
baada ya Zanzibar kupata
uhuru siku ya Disemba
10, 1963. Khatib anawajua
vema watu hao. Ameishi
na baadhi yao akiwa bado
kinda. Historia inaonesha
kuwa yeye alilelewa na watu
wa namna hiyo ambao leo
anawachukia mwisho wa
akili yake. Maisha ya mitaa
ya Kikwajuni aliyavaa sana
wakati ule.
Watu wazima waliokuwa
wanamuona Kikwajuni,
wanasema Khatib akifanya
biashara ndogo za vitafunwa,
huku akiwa anaenda skuli.
Alikuwa katika familia isiyo
na kipato cha kutosheleza
m a h i t a j i , h i v y o a k a wa
analazimika kusaidia
ipatikane riziki ambayo kwa
upande mwengine kujisaidia
kimatumizi.
Wakubwa wa umri hao
tuliopata kuzungumza
nao historia mbalimbali za
kimaisha na za kiharakati za
zama zile, leo wanayaeleza
mambo kuwa alipokuwa
anakua, Khatib alionekana
akichukia mno wenye ulwa.
Kwa hivyo basi, tunaambiwa
kwamba ujanani kwake
akawa ameondokea hivyo
na haikuwa rahisi kubadilika
tena kisilka na akabakia
mtu aliyejenga uchukivu
kwa watu wale waliokuwa
na kipato wakiwemo
waliowatumishi serikalini.
Khatib akaja kutokea
kupenda masomo ya historia
na lugha ambayo hatimaye
yamemfikisha katika hadhi
ya udaktari kwa kubobea
maeneo hayo mawili.
Amejaza shahada zake tatu
na kuwa mmoja wa wajuzi
wa historia na lugha. Ni
mtu mkubwa kwa tungo,
simulizi na historia. Chuki
dhidi ya Raza zilionekana
pale alipoikamata fomu ya
kuomba ridhaa ya chama
ili kugombea uwakilishi
baada ya Maalim Khamis,
aliyekuwepo kitini,
kutangulia mbele ya haki
mwaka 2012.
Raza ni Mzanzibari
mwenye asili ya Uhindi.

Ni anayetoka kizazi cha


wananchi waliotoka Ghuba
ya Uajemi Persia, eneo
ambalo lina historia ndefu
ya watu wake kuwa na
uhusiano mkubwa wa
kidamu na Wazanzibari.
Uhusiano huo ulianza
mbali. Nyakati za safari za
majahazi wafanyabiashara
wa k i f i k a Z a n z i b a r k wa
ajili ya kuleta bidhaa
mbalimbali, nao badala yake
wakinunuua zile zilizokuwa
zikizalishwa Zanzibar. Ni
watu waliojijenga kimaisha,
ingawa baadhi yao hawakuwa
na utajiri uliopitiliza
m i p a k a . Wa n a j u l i k a n a
walivyohangaika kimaisha
kama ambavyo Raza
hupenda kusema waziwazi
kuwa familia yake ilikuwa
ni maarufu kwa kazi ya
uchungaji punda.
Kwa makada wa CCM
waliojengeka kihafidhina
kama huyu gwiji wa lugha
mbunge wetu Khatib,
Raza hawezi kuwa mtu
safi, muungwana, rahim,
karim, mtulivu na mpenda
watu anayejitolea kusaidia
wasionacho. Basi aliamini
atampiku kihuduma
kwa wananchi jimboni.
Katika kundi la makada
waliosimama kidete
kujitahidi kumtilia vikwazo
asifikie kuteuliwa, wandani
wanasema alitajwa kuwemo.
Kwamba hakupenda hata
kidogo mwakilishi awe huyo
Raza. Hakupenda kabisa.
Sababu nyingine za ndani
zaidi mwenyewe anazijua.
Safari moja nilibahatika
kutembelea kijiji cha Umbuji,
moja ya vijiji maarufu katika
jimbo la Uzini na ambako
ndiko anakotoka mbunge
K h a t i b . I l i k u wa k a t i k a
kuhudhuria msiba wa mzee
Haji Hassan, aliyekuwa mtu
maarufu wa dhikri pembeni
mwa skuli ya Umbuji. Ndipo
nilipata simulizi za alivyo
Khatib. Nilipokuja kusikia
Raza anagombea uwakilishi
Uzini, Umbuji ikiwa sehemu,
haraka nikatilia nguvu yale
niloyasikia hapo kabla.
Hakika palikuwa na kishindo
si kidogo wakati makada
wakielekea kwenye upigaji
kura za maoni ili kumtafuta
mgombea wa kusimama na
mshindani kutoka Chama
c h a Wa n a n c h i ( C U F ) .
Uzuri wanakijiji wenyewe
wa Umbuji, hususan
wa rika la ujana kabisa,
mabarubaru, walisikika
wakisema hadharani kuwa
wanampigania Raza awe
ndio mwakilishi wao.
Walisema wanataka kitu
kipya baada ya kushindwa
kumfikia kwa matumaini
mbunge wa miaka mingi.
Si uongo, kura za maoni
lilikuwa ni tukio lililojaa
mvuto. Makada wahafidhina
walijenga nguvu kuhakikisha
Raza anaanguka. Walitumia
pesa na nyenzo nyingine,

Dk. Salmin Amour Juma, Rais wa Awamu ya Tano Zanzibar.


zikiwemo zile za kawaida wananchi wakati anaomba
fitina, chuki na majungu kura za wanajimbo.
kushawishi umma
Mpaka leo, machungu
umchague Athumani Ali ya fitina dhidi ya Raza,
Maulid, badala yake. Huyu yanawasononesha Umbuji,
ni kijana kindakindaki wa ambako alitoa ahadi ya
jimboni. Msomi wa kiasi
chake na mtumishi wa cheo kujenga hospitali ya kisasa;
cha kati serikalini. Nguvu ya a t a k a y o i j a z a v i f a a n a
Raza nayo haikuwa ndogo. vitendea kazi vya kisasa.
K u b wa t u k wa s a b a b u A l i a h i d i k u wa o n g e z e a
alishazunguka na kujieleza k i p a t o w a f a n y a k a z i
kuwa anataka kuwapelekea watakaokuwepo.
Wakati
Umbuji
maendeleo ya kweli wana
wakishangiria
kujengewa
wa Uzini, wakiwemo wa
k w a o K h a t i b , U m b u j i , barabara yao kwa kiwango
lami, likiwa ni jambo
ambako kuna shida kubwa cha
lililowaumiza vya kutosha
ya kituo cha afya. Kwa macho wananchi, wanaendelea
yangu, kilichomtoa Raza kunyongeka roho kwa kukosa
ni ule utashi wa wananchi tiba machoni pao. Kituo cha
wenyewe kutaka mtu mpya, afya kilichojengwa miaka ya
mwenye mvuto wa kusaidia, 1990 kati, kimekwisha. Jengo
wakiwa tayari wanamjua linavuja laisal kiasi.
vilivyo Raza ambaye historia
A k i l i ya n g u i n a n i p a
inaonesha alisaidia maeneo i m a n i k w a m b a w a l e
mengi ya nchi wakati akiwa vijana waliobeba mabango
s a h i b m k u b wa wa D k . yenye salamu nzito kwa
Salmin Amour Juma, Rais Katibu Mkuu wa CCM,
wa Awamu ya Tano Zanzibar. A b d u l r a h m a n K i n a n a ,
R a z a n i m m o j a w a alipohutubia mkutano wa
wafanyabiashara wachache hadhara wa jimbo mapema
walioanzisha biashara ya vifaa w i k i h i i , w a U m b u j i
vya michezo. Alifungua duka hawakosekani.
Wa n a i s h i h a s a n a
eneo la Majestik, na kuwa
mfarakano
wa mwakilishi
maarufu kwa ufadhili katika Raza na mbunge
Khatib.
sekta ya michezo, hasahasa Kama Kinana ndio anajua
k a b u m b u n a n e t i b o l i . leo ukorofi wa makada
Raza alishinda kwa kura wahafidhina wa aina ya
zisizo hesabu. Akateuliwa gwiji wa lugha, basi ndipo
k u g o m b e a u w a k i l i s h i nikasema mchawi wa CCM
Uzini. Si ajabu ulipokuja ni wenyewe.
uchaguzi, akachaguliwa kwa
Wajumbe wote wa Kamati
kura zisizo hesabu vilevile. Maalum ya NEC, ikiongozwa
Huyo akaingia jumba jeupe. n a R a i s w a Z a n z i b a r
M p a k a l e o m wa k i l i s h i na Makamu Mwenyekiti
Raza haivi chungu kimoja wa CCM Zanzibar, Dk.
na mbunge Khatib. Ali Mohamed Shein
Walichokishuhudisha wakazi wanajua. Wajumbe wote
wa Miwani, kinajulikana wa NEC wanajua. Viongozi
bali ni hatua ya kuonesha waandamizi na wa kati katika
wanajimbo walivyotoshwa Wilaya ya Kati wanajua.
na mfarakano wa viongozi Tatizo ni lilelile CCM
wao. Raza na Khatib, ukweli walizoea kuzitumia silaha
hawaelewani. Bali Raza zao kwa upinzani zaidi, sio
ukimuuliza, anasema hana kujikosoa wao wenyewe na
tatizo isipokuwa anajisikia kujisahihisha. Hakika ndivyo
kukosewa kwa kuzuiwa vinavyokisokomeza kuzimu
kutimiza ahadi zake kwa chama chao.

Makala

AN-NUUR

RABIUL THANI 1436, IJUMAA FEBRUARI 6 - 12, 2015

TIMAMU TEA INAWAFAA WATU WOTE! -3


Na Juma Killaghai

KATIKA kujenga hoja ni


kwa nini chai ya Haiiba
Timamu inamfaa kila
mtu, tumeshatoa makala
mbili tayari. Hoja
ya msingi iliyotawala
makala zote mbili, na
ambayo tunaiendeleza
katika makala hii ni ile
inayoelezea kuwa tiba
ya chai hii inatokana na
kumrejeshea mhusika
viini lishe mbali mbali
vilivyopungua mwilini
m wa k e , a m b a v y o n i
muhimu katika kujenga
siha bora.
Katika makala
z i l i z o t a n g u l i a
tulizungumzia viini lishe
vya vitamini na madini
lishe vilivyomo ndani
ya Haiiba Timamu Tea.
Katika makala yetu ya pili
tulizungumzia madini
lishe yote yaliyoko katika
chai ya Haiiba Timamu
isipokuwa mawili tu. Haya
ni madini ya Chromium
na yale ya Manganise.
Makala yetu ya leo
itamalizia kiporo hicho,
kisha itazungumzia kundi
la tatu la viini lishe. Hili
ni kundi la viini lishe
vinavyojulikana kama
vijenzi vya protini au
tindikali za amino (amino
acids).
Chromium: Haya ni
madini yenye faida nyingi
muhimu kiafya. Baadhi ya
faida hizi ni pamoja na:
Huratibu uchakataji wa
wanga, mafuta na protini
na kuongeza uwezo wa
homoni ya insulin kufanya
kazi yake na hivyo
kusaidia katika kudhibiti
kisukari cha ukubwani
(type II diabetes).
Husaidia kupunguza
uchu wa kutaka kula
mara kwa mara. Husaidia
kuratibu wingi wa lehemu
(cholesterol) mwilini;
na Hukinga dhidi ya
ongezeko la shinikizo la
damu.
Manganese: Haya ni
madini yenye faida nyingi
muhimu kiafya. Baadhi
ya faida hizi ni pamoja
na: Madini haya ni ya
lazima katika ujenzi wa
mifupa imara. Husaidia
sana katika kuhifadhi na
kulinda mifupa ya uti wa
mgongo. Madini haya
hufanya kazi kama kizuia
kioksidishaji chenye
nguvu na hivyo kusaidia
kulinda mwili dhidi
ya chembe zilizobeba
u m e m e c h a n ya ( f r e e
radicals) zinazozalishwa
mwilini katika mchakato
wa kawaida wa ujenzi
na uvunjifu wa kemikali
mwilini, ambazo zina
madhara makubwa
kiafya. Husaidia kuweka
kiwango cha sukari katika

damu kuwa katika hali ya


kawaida.
Ili kutekeleza jukumu
hili madini haya huweka
sawa uzalishaji wa homoni
ya insulin ndani ya mwili
na pia huzuia kuporomoka
kusikotabirika kwa
sukari mwilini kwa wale
ambao ni wagonjwa wa
sukari. Husaidia kuzuia
shambulio la ugonjwa wa
kifafa. Huamsha baadhi
ya vimengenya ambavyo
vina jukumu katika
uchakataji wa lehemu
(cholesterol), vijenzi vya
protini (amino acids) na
wanga. Aidha huhusika
k a t i k a u c h a k a t a j i wa
viini lishe vya vitamini
E na Vitamini B1 na pia
hulisaidia ini kufanya kazi
kwa weledi na ufanisi.
Husaidia kudhibiti
mfuro (inflammation) na
miteguko. Inaaminika
k wamba msaada huu
hutokana na uwezo wa
manganese kuongeza
kemikali ya superoxide
dismutase (SOD). Kemikali
hii ina uwezo mkubwa wa
kupambana na mfuro na
hivyo ni msaada mkubwa
sana kwa wagonjwa wa
jongo na baridi ya abisi.
Husaidia kukabiliana na
matatizo yanayohusiana
kukaribia kuingia kwenye
hedhi (Pre-menstrual
syndrome). Ni kiambata
muhimu cha homoni ya
thyroxine. Homoni hii
ni muhimu sana katika
kuendesha mchakato wa
ujenzi na uvunjifu wa
kemikali ndani ya mwili
(metabolism). Husaidia
sana katika ufyonzwaji wa
vitamini mwilini. Ufanisi
wa ufyonzwaji wa vitamini
muhimu mwilini kama
vitamini E na vitamini
B1 pamoja na madini ya
magnesium hutegemea
sana uwepo wa madini
ya manganese. Utendaji
kazi mwanana wa ubongo.
Manganese ni muhimu
kwa ajili ya utendaji bora
wa ubongo na pia husaidia
sana katika tiba ya matatizo
yayohusiana na mfumo wa
neva. Inaaminika kuwa hii
ni kutokana na manganese
kuchochea kuzalishwa
kwa superoxide dismutase
(SOD). Kemikali hii
hufanya kazi ya kusaka
chembechembe zenye
u m e m e c h a n ya ( f r e e
radicals) kila mahala
mwilini na kuzizimua
kabla hazijasababisha
madhara makubwa ya
kiafya. Husaidia katika
uchakataji wa glucose
na kuifanya ifanye kazi
barabara ndani ya mwili
na kuzuia ongezeko la
ziada ndani ya damu, kitu
ambacho ni hatari kwa
wagonjwa wa kisukari.
Husaidia utendaji kazi wa
mfumo wa usagaji chakula

na hivyo kuboresha
ufyonzwaji wa virutubisho
na uondoshaji wa uchafu
mwilini kwa njia ya haja.
TINDIKALI ZA AMINO AU
VIJENZI VYA PROTINI: VIJENZI
VYA PROTINI NI NINI?
Vi j e n z i v ya p r o t i n i
( tindikali za amino/
amino acids) ni molekuli
(molecule) ndogondogo
zinazotumika kama tofali
za kuundia protini. Protini
ni molekuli (molecule)
kubwa za kibaiolojia zenye
majukumu kadhaa wa
kadhaa ndani ya mwili.
Idadi kubwa ya shughuli
mbali mbali katika seli za
mwili hufanywa na protini.
Aidha protini zinahitajika
katika uratibu na utendaji
kazi wa tishu na viungo
vya mwili, ikiwa ni pamoja
na kuunda maumbo ya
tishu na viungo husika.
P r o t i n i h u u n d wa n a
m a m i a a u m a e l f u ya
molekuli za tindikali
za amino zilizoungana
katika umbile la nyororo.
Kuna tindikali za amino
20 zinazoweza kuungana
katika michanganyiko
mbalimbali (combination)
kutengeneza molekuli za
protini. Kwa kawaida
huwa tunatakiwa tupate
vijenzi vyote vya protini
tunavyohitaji kupitia
katika lishe. Hata hivyo
kutokana na mapungufu
mbalimbali yaliyoko katika
lishe zetu inatokea tukawa
na upungufu wa baadhi
ya hivi vijenzi vya protini
na hivyo kukumbwa na
magonjwa yanayohusiana
na huo upungufu.
V I J E N Z I M U H I M U V YA
PROTINI VILIVYOKO KATIKA
HAIIBA TIMAMU TEA
Baadhi ya vijenzi
m u h i m u v ya p r o t i n i
v i l i v y o k o k wa w i n g i
katika chai hii ni
Arginine, Histidine,
Isoleicine, Leucine,
Lysine, Methionine,
Phenylalanine, Threonine,
Tryptophan, na valine.
Arginine: Faida
za argininei ni nyingi.
Miongoni mwa faida hizi
ni pamoja na: Huongeza
kasi na ufanisi wa kupona
majeraha. Huongeza
ufanisi wa figo katika
kuondosha uchafu
mwilini. Huboresha kinga
za mwili na utendaji kazi
wa homoni. Huboresha
mzunguko wa damu na
hivyo huusaidia moyo
kufanya kazi kwa ufanisi
kupunguza uwezekano
wa kupata magonjwa
yanayohusiswa na
mkakamo wa mishipa ya
damu kama shinikizo la
damu, kupoteza nguvu
za kiume, shambulizi
la moyo na maumvu ya
kifua yanayosababishwa
na mzunguko dhaifu wa

damu (angina).
Histidine: Faida
za Shaba ni nyingi.
Miongoni mwa faida hizi
ni pamoja na: Huhusika na
kuimarika kwa tishu zote
ndani ya mwili, hususan
zile zinazounda utando
unaozunguka mishipa yote
ya fahamu (myelin sheath).
Hupunguza uwezekano
wa kupata ugonjwa wa
ukungu katika lenzi
za macho (carrtaracts).
Hupunguza uwezekano
wa k u p a t a b a r i d i ya
yabisi (rheumatoid
arthritis) na hupunguza
athari na maumivu
yanayoambatana na
ugonjwa huo.
Isoleucine: Faida za
Isoleucine ni nyingi.
Miongoni mwa faida hizi
ni pamoja na: Kutengeneza
chembechembe nyekundu
za damu (Hemoglobin).
Inachochea ukarabati wa
tishu baada ya upasuaji au
ajali. Inaleta unafuu kwa
magonjwa mbalimbali
ya akili kama msongo
endelevu, mfadhaiko,
kukosa usingizi,
nakadhalika. Inazuia
misuli isiharibike wakati
wa kufanya mazoezi.
Inaongeza nguvu mwilini;
na inajenga uwezo wa
mwili kuhimili kazi
ngumu.
Leucine: Hii ni miongoni
mwa tindikali za amino
ambazo hazizalishwi ndani
ya miili yetu na kwa hivyo
ni lazima kuipata kupitia
lishe. Faida za Leucine ni
nyingi. Miongoni mwa
faida hizi ni pamoja
na: Inachagiza ujenzi
wa protini zinazounda
misuli mbalimbali ya
mwili. Humsaidia mtu
anayepunguza kula ili
kupunguza uzito aunguze
mafuta yaliyolundikana
mwilini, bila kuathiri
misuli; na inachagiza
kemikali moja inayokaa
kwenye misuli inayoitwa
m-TOR (mammalian target
of rapamycin) ambayo
hufanya kazi kama swichi
ya kuwezesha uzalishaji
wa protini zinazohitajika
katika kujenga misuli
kufanya kazi kikamilifu.
Lysine: Hii ni miongoni
mwa tindikali za amino
ambazo hazizalishwi
ndani ya miili yetu na kwa
hivyo ni lazima kuipata
kupitia lishe. Faida za
Lysine ni nyingi. Miongoni
mwa faida hizi ni pamoja
na: Husaidia kuratibu
k i wa n g o c h a l e h e m u
(cholesterol) mwilini.
Ni muhimu sana katika
kulinda afya ya mifupa.
Inasaidia mwili kupokea
na kutumia madini ya
kalisi (calsium) kwa weledi
zaidi na pia husaidia
kupunguza upoteaji
wa kalisi kutoka katika

mifupa. Huzuia kuzaliwa


kwa virusi aina ya Herpes
na husaidia kuongeza
k a s i ya k u p o n a k wa
watu waliopata maradhi
yanayosababishwa na
virusi hivyo. Husaidia
kupunguza makali ya
ugonjwa wa mkanda wa
jeshi (shingles). Inachagiza
ujenzi wa protini na hivyo
ukuaji bora wa viungo vya
mwili. Humsaidia mtu
kupungukiwa na matatizo
ya msongo na mfadhaiko.
Husaidia kupunguza
maumivu ndani ya mwili;
na husaidia kuboresha
siha ya moyo na mfumo
wa mzunguko wa damu
kwa ujumla.
Methionine: Hii ni
miongoni mwa tindikali
za amino ambazo
hazizalishwi ndani ya
miili yetu na kwa hivyo
ni lazima kuipata kupitia
lishe. Faida za Lysine ni
nyingi. Miongoni mwa
faida hizi ni pamoja na:
Husaidia kuchakata na
kuondoa mafuta mwilini.
Inazuia mlundikano wa
mafuta kwenye ini na
hivyo kutoa kinga dhidi ya
ugonjwa wa ini bonge (fatty
liver disease). Inahitajika
katika utengenezaji wa
creatine. Creatine ni kiini
lishe kinachohitajika
k a t i k a u z a l i s h a j i wa
nishati inayohitajika
katika kuifanya misuli
ifanye kazi zake kwa
ufanisi. Inahitajika katika
uzalishaji wa protini aina
ya collagen ambayo ni
muhimu katika uundaji
wa ngozi, kucha na tishu
zinazounganisha misuli.
Husaidia kuimarisha
siha za watu wanaoishi
na virusi vya ukimwi.
Husaidia kupunguza
mfuro (inflammation)
wa kongosho yaani
pancreatitis. Husaidia
kupunguza dalili za
ugonjwa wa Parkinson.
Husaidia kukabiliana na
maambukizi katika njia
ya mkojo.
Phenylalanine: Faida
za Lysine ni nyingi.
Miongoni mwa faida hizi
ni pamoja na: Husaidia
kukabiliana na mfadhaiko.
Huleta utulivu kwa watu
wanaokabiliwa na ugonjwa
wa kukosa umakini na
wenye kiwango kikubwa
cha utukutu (Attention
Deficit - Hyperactivity
Disorder ). Inapunguza
dalili za ugonjwa wa
Pa r k i n s o n . H u s a i d i a
kukabiliana na maumivu
ndani ya mwili. Husaidia
kukabiliana na ugonjwa
wa baridi ya yabisi; na
husaidia kukabiliana
na ugonjwa wa vitiligo
(ugonjwa wa kuchujuka
rangi ya ngozi).
Inaendelea Uk. 7

7
Na Shaban Rajab
MWENYEZI Mungu
amemuumba mwanadamu
na kumtengenezea
mazingira ya kuishi
duniani, na akampa uwezo
wa kumudu kuishi
katika mazingira hayo na
kumwabudu hadi siku yake
ya mwisho ya uhai wake.
Binadamu aliwekewa kila
alilolihitaji katika kumudu
maisha ya duniani. Baadhi
ya vitu muhimu kabisa
vya kimaisha ambavyo
binadamu tunategemea
kuendelea kuhifadhi
mfumo wa uhai wake ni
chakula, mavazi na malazi.
Haya ni mahitaji ya asili
ambavyo binadamu hapaswi
kuyakosa.
Zaidi ya hapo binadamu
amejaaliwa kuwa na maarifa,
fikra na ujuzi, nyenzo ambazo
huzitumia katika kufanya
mambo yake mbalimbali ya
kimaisha hapa duniani, ili
kupata ufanisi na tija.
Lakini pia kuna sehemu
nyingine ya mahitaji ambayo
tunaweza kusema kuwa ni
yale yasiyokuwa ya lazima.
Katika zama hizi mahitaji
haya yasiyo ya lazima,
ndio yamegeuzwa kuwa
ya msingi katika maisha ya
mwanadamu kiasi cha kuwa
chanzo cha kuibuka fikra za
ubinafsi, chuki, tamaa na
kibri.
Mahitaji kama haya hayana
kikomo katika kuhitajika
kwake, kwani ni mengi na
wala mtu hawezi kuyapata
au kukidhi yote, ila katika
ndoto na mawazo tu. Kiu
ya kutafuta mali za ziada
ili kukidhi matumizi yake
ya kitamaa imetawala nafsi
za wengi. Na kwa hakika
udhaifu huu, ndio chanzo
cha na kumfanya binadamu
awe mpumbavu, alewe kiasi
cha kushindwa kutumia akili
yake aliyopewa na Mwenyezi
Mungu vizuri.
Kwa kuwa kudumu
na kustawi katika maisha
ya mahitaji ya tamaa
kunategemea mali zaidi,
watu siku hizi hulazimika
kudhulumu, kufisidi,
k u f a n ya u b a d h i r i f u n a
kuhakikisha kuwa anakuwa
na ubinafsi wa hali ya juu.
Kufuatana na muundo
wa kimaumbile, kwa
namna moja au nyingine
kila mtu anahitajia msaada
wa mwenzake kwa ajili ya
kustawisha, kukamilisha na
kuzalisha matunda ya vipawa
vyake. Anahitajika kuwa
na moyo wa kushirikiana
na kusaidiana kama msingi
muhimu katika kuleta
maendeleo na mafanikio.
M u u n d o wa u u m b a j i
wa binadamu umeundwa
k wa a j i l i ya m a i s h a ya
kijamii, hivyo kimaumbile
binadamu anastahili
kushirikiana na wenzake
katika kutatua matatizo yake
ya kimaisha. Kwa upande
mwingine, utajiri mwingi
mara nyingi huambatana
na kiburi, majivuno na tabia
chafuchafu. Mtu anapokuwa

Makala

AN-NUUR

RABIUL THANI 1436, IJUMAA FEBRUARI 6 - 12, 2015

Kwa chuki, ubinafsi tunaangamia

CHUKI huzaa vita na mauaji ya watu wasio na hatia.


na mali nyingi kupita kiasi,
ubinafsi na ufahari humlevya
huku tamaa zake zikiwa
hazimaliziki.
Ni lazima mtu afahamu
amekuja duniani kwa lengo
gani, ili aweze kufanya
jitihada za kutafuta ufanisi
wa kimaisha kwa kutumia
maarifa yake aliyojaaliwa
na Mwenyezi Mungu. Ni
lazima achague njia bora
inayolingana na mahitaji yake
katika maisha, ili kuepukana
na dosari zinazoweza
kuharibu ukamilifu wa roho
ya kibinadamu.
Hatudhani kwamba ni
ufanisi au uhodari mtu
kutumia njia za kitamaa
kupata mali ili kuwashinda
wenzake na kutafuta
utukufu, kwani mali si kiini
wala msingi wa maisha na
wala haifai kukiukwa mipaka
ya ucha Mungu, wema na
uadilifu kiasi cha ubinadamu
kuwekwa kando.
Maslahi binafsi
yametawala fikra za umma
wa siku hizi na kusababisha
j a m i i k u o g e l e a k we n ye
maisha ya dhulma. Dhulma
imewafanya watu wengi
kuona kwamba utajiri ndio
furaha ya maisha na ndio
mafanikio katika maisha.
Mtu ambaye hazina yake ya
roho imefurika utajiri, huwa
ni nadra sana kuruhusu roho
ya kibinadamu kutawala
maisha yake.
Tamaa au uroho ni hali
ya inayomfanya mtu daima
atafute na apate hasa kwa
dhulma, kwa maslahi binafsi
ya kidunia, na zaidi kwa ajili
ya kukidhi mambo yasiyo ya
msingi bali ya laghawi tu.
Roho ya mwenye tamaa
huwa tayari kuhalifu
utu, ilimradi anapata
anachokitaka. Kadiri
anavyozidisha juhudi
kutafuta utajiri zaidi, ndivyo
anavyozidi kuhisi uhitaji
wake zaidi. Wapo baadhi

ya watu wenye kukinahi


n a we n ye h o f u , a m b a o
wanaridhika na mali kidogo
inayokifu gharama zao za
maisha. Lakini wako watu
ambao wana mali nyingi
sana na mapato yao yanazidi
matumizi yao, lakini daima
hulalamika kutopata
matakwa yao kikamilifu.
Siku zote mwenye
tamaa hatosheki na neema
za ulimwenguni. Kadiri
anavyozidi kupata huzidi
kuwa na tamaa. Tamaa
i k i t a wa l a k a t i k a t a i f a ,
huibadili jamii kuwa uwanja
wa mapigano na mashindano,

huzuka na ugomvi kati ya


watu badala ya kuwepo
amani na uadilifu.
Jambo la msingi la
kuzingatiwa hapa ni
kwamba, suala la maendeleo
na ukamilifu katika mambo
mbalimbali ya maisha, lina
tofauti kubwa na dhana ya
kuabudu pesa au mali.
Tu n a f a h a m u k u wa
binadamu ana sababu ya
kuleta mabadiliko na
maendeleo katika jamii,
lakini ni lazima afanye hivyo
kwa haki na uadilifu, na
kwa kutumia vipawa vyake
alivyojaaliwa na Mwenyezi

Mungu bila kuwadhuru watu


wengine.
Wengi wenye tamaa kuleta
balaa na matatizo katika jamii
kwa kutaka kukidhi haja zao
za kimaisha bila ya kufuata
msingi wa uadilifu, na kuleta
masaibu kwa watu wote.
Kwa kawaida watu hawa
hupenda kuhodhi madaraka
au mamlaka, vyombo
muhimu vya uzalishaji mali
na vile vya msingi katika
huduma za kijamii, kusudi
wajichumie manufaa zaidi.
Na kwa njia hii, huzidisha
matatizo ya kiuchumi na
umaskini katika jamii husika.
Tu n a f a h a m u k wa m b a
dhiki, faraja, utajiri ni sehemu
ya maisha ya mwanadamu.
Kila mtu duniani awe maskini
au tajiri anaathirika navyo
kulingana na hali yake. Lakini
utajiri wa kupita kiwango cha
mahitaji, hausaidii katika
kumletea mtu raha au furaha.
Baadhi ya watu hawana
ukwasi wa mali, hawana
m a va z i ya f a h a r i wa l a
makasri, lakini wanaishi kwa
raha zaidi kuliko matajiri
wengi.
Mwenye tamaa ni
mtumwa wa mali, amejifunga
mnyororo usioonekana
kwenye shingo yake na
amesalimu amri mbele ya
fikra zake zisizokamilika.
Hudhani kwamba ukwasi
wake ambao ungewatosha
hata kizazi chake cha baadaye,
ni hazina ya dharura kwa ajili
ya siku ya shida!
Lakini anasahau kuwa
kuna mauti, na wakato
huo mali zake hazitamfaa
c h o c h o t e . At a b a k i a
kuzitazama kwa masikitiko
na kwa kukata tama, mali
alizozikusanya kwa taabu
na mashaka anaziacha
pasipokujua hatima yake.

TIMAMU TEA INAWAFAA WATU WOTE! -3


Inatoka Uk. 6

Threonine: Hii ni
miongoni mwa tindikali
za amino ambazo
hazizalishwi ndani ya
miili yetu na kwa hivyo
ni lazima kuipata kupitia
lishe. Faida za Lysine ni
nyingi. Miongoni mwa
faida hizi ni pamoja na:
H u r a t i b u u w i a n o wa
protini ndani ya mwili
ili kudhibiti upungufu.
Inachagiza tindikali
nyingine za amino kujenga
protini mbalimbali
zinazohitajika kwa ajili ya
tishu mbalimbali xa mwili.
Inatengeneza tindikali za
amino za glycine na serine
2 ambazo ni muhimu sana
katika uundaji wa protini
aina za collagen na elastin
ambazo ni vitu muhimu
sana kwa siha ya ngozi,
tishu zinazounganisha
misuli na mishipa ya damu.
Inatengeneza tabaka

jembamba linalozunguka
jino kwa nje (tooth
enamel). Inashirikiana na
methionine na tindikali
aina ya aspartic (aspartic
acid) kuliwezesha ini
kuondokana na mafuta.
Inafanya sukari ya damu
isiongezeke au kupungua
kiholea. Inaboresha
mfumo wa kinga za mwili.
Ina umuhimu wa kipekee
katika ukuaji wa tezi ya
thymus katika ubongo.
Ni ya lazima kwa ajili
ya siha bora ya mfumo
wa mishipa ya fahamu.
Inasaidia kupambana na
msongo na mfadhaiko.
Inawezesha mchakato
wa kikemia unaohitajika
kuzalisha nishati katika seli
(krebs cycle) kufanya kazi
kwa ufanisi unaotakiwa.
Husaidia ujenzi wa mifupa
imara; na huongeza kasi ya
kupona kwa majeraha.
Siku zote kinga ni bora

kuliko tiba. Kutokana na


faida nyingi zinazoletwa
na viini lishe vilivyoko
katika Haiiba Timamu
Tea kama tulivyozielezea
hapo juu, ni wazi kabisa
kuwa kila mtumiaji wa
Haiiba Timamu Tea, bila
kujali hali yake ya kiafya
anaweza kunufaika sana.
K WA M A E L E Z O
Z A I D I WA S I L I A N A
NA WATENGENEZAJI
WA
CHAI
HII,
YA A I N I H E R B A L
IMPACT, KWA SIMU
NAMBA: 0754281131;
0655281131; 0686281131;
NA 0779281131 AU
WATEMBELEE OFISINI
KWAO:
MOSQUE STREET,
N O . 1 5 7 4 / 1 4 4 ,
KITUMBINI, DAR ES
SALAAM (MKABALA
NA LANGO KUU LA
KUINGILIA MSIKITI
WA SUNNI)

Makala

AN-NUUR

RABIUL THANI 1436, IJUMAA FEBRUARI 6 - 12, 2015

Uhalali wa kura ya maoni uko wapi?


Na Mwandishi Wetu

NI kashfa kukuta nchi


inayojivunia demokrasia
pana na uongozi wa
sharia, ikawa ya mwanzo
kuvunja katiba ya nchi kwa
makusudi sababu tu ya
kuweka siasa mbele badala
ya kujenga heshima ya
wananchi na nchi yenyewe.
Majuzi tu tumemsikia
Wa z i r i w a F e d h a w a
Muungano, akitamka ndani
ya Bunge kwamba baadhi
ya miradi iliyoidhinishiwa
fedha na bunge katika vikao
vya bajeti, hazikupelekwa
zilipostahiki na badala
yake zikatumiwa kinyume
na maagizo ya bunge. Ni
kosa kubwa ambalo kama
lisingegunduliwa na kamati
za Bunge, sifikirii kama
kulikuwa na nia thabiti ya
kuweka uwazi huo bungeni.
Lakini kubwa ninaloliona
kama kashfa zaidi ya
Escrow ni suala la kura
ya maoni juu ya Rasimu
iliyopendekezwa (Rasimu
ya Vijisenti) ambayo zoezi
lake limekuwa likifanywa
kienyeji kinyume na katiba
ya nchi inavyotamka pamoja
na hata sheria zilizotungwa
kuendesha zoezi lenyewe.
Uongozi wa pande zote
mbili umekuwa kimya kama
vile vipengele hivi havina
nguvu ya kuharamisha
zoezi la kura ya maoni na
kuliweza kulitia taifa hili
changa katika gharka ya
matumizi makubwa ya fedha
huku faida yenyewe ikawa
haionekani.
Tutazama mambo mawili
makubwa ambayo wengi
wamekuwa wakiyapigia
kelele ambazo hazionekani
kuamsha serikali
katika usingizi wa pono
asiejitambua. Angalizo
kubwa ni uhalali wa kura
ya maoni juu ya Rasimu
pendekezwa kwa upande
wa visiwani hasa kutokana
na vifungu vya katiba ya
Z a n z i b a r v i n a v y o we k a
masharti kwa sheria yoyote
ya bunge la muungano
kuidhinishwa kwanza na
Baraza La Wawakilishi.
Pili ni suala zima la utoaji
tarehe ya kufanyika kwa
zoezi lenyewe la upigaji
kura, hasa ukizingatia sheria
iliotungwa inatoa maelezo
ya nani wa kutangaza baada
ya kutangazwa kwa suala
la kura ya Maoni na pia
muda uliowekwa kisheria
wa kutoa tangazo lenyewe.
Haya yote yamo katika sheria
ya kura ya Maoni namba 11
ya mwaka 2013.
Majuzi katika moja ya
Mijadala ya taasisi ya utafiti
visiwani (ZIRPP) suala hili
lilizungumzwa na kujadiliwa
kwa kina hasa namna ya
sheria zilivyovunjwa na
wale watetezi wakubwa wa

Mhe. Samwel Sitta (kushoto) akiwa na Mhe. Andrew Chenge.


Rasimu iliopendekezwa. Kati
ya alietufungua macho kwa
hoja nzito ni Mheshimiwa
Awadh Ali Said, (mmoja wa
wajumbe wa iliokuwa Tume
ya Warioba) ambae alitaka
wananchi kuifahamu vyema
katiba ya Zanzibar hasa
kifungu cha 132 kinachozuia
sheria za muungano
kutumika Zanzibar na
pamoja na sheria ya kura
ya Maoni ya namba 11 ya
mwaka 2013 ya muungano
ambayo ni ya muda kwa vile
uhai wake unakwisha pale
kura ya maoni inapokwisha,
tafauti na ile ya Zanzibar
namba sita ya mwaka 2010
ambayo ni ya kudumu.
Nilichokiona hapa ni
kwamba zoezi hili zima
limeharibiwa na mkuu wa
nchi kwa kutokuwa makini
katika tafsiri pana za katiba
zetu pamoja na sheria hasa
hizi zilizotungwa mahsusi
kwa zoezi la upatikanaji wa
katiba mpya nchini. Hoja hizi
bado hakuna aliezivunja kwa
kutoa ushahidi wa kupinga
yale yalioelezwa katika
kongamano la ZIRPP na
kwa hivyo inatuwia vigumu
kuamini kwamba serikali
hii sikivu imekosa weledi
wa kutambua makubwa
haya yanayoweza kabisa
kuharamisha zoezi zima la
upigaji kura ya maoni na
kutufanya kuwa kicheko cha
dunia kwa uvivu mkubwa
wa kusimami utendaji wa
majukumu yetu.
Tukianza na kifungu cha
132 (1) ya katiba ya Zanzibar
ya mwaka 1984, kinaeleza
wazi kwamba hakuna sheria
yoyote itayopitishwa na
Bunge la Muungano ambayo
itatumika Zanzibar mpaka
sheria hiyo iwe kwa ajili
ya mambo ya muungano
tu, na ipitishwe kulingana
na maelekezo yaliyo chini
ya vifungu vya katiba ya
muungano. Inaendelea

katika 132 (2) Sheria kama


hiyo lazima ipelekwe mbele
ya Baraza la Wawakilishi na
Waziri anayehusika. Mifano
miwili ya kutumika kwa
kifungu hichi cha katiba
ya Zanzibar kuzuia sheria
z i l i z o t u n g wa n a B u n g e
la Muungano kutumika
Z a n z i b a r n i S h e r i a ya
kuundwa kwa Tume ya Haki
za Binaadamu pamoja na
sheria ya Uvuvi wa Bahari
kuu.
Ukitazama kwa upana
zaidi sheria hizo mbili
z i l i z o z u i l i wa k u t u m i k a
Zanzibar, ni kwa sababu
ya k i f u n g u c h a K a t i b a
kama kilivyoeleza na pia
kwamba vyote hivyo viwili
havikuwamo katika kapu
la masuala ya Muungano.
Sasa ukitazama sheria ya
kura ya maoni ya namba
11 mwaka 2013, inatamka
kwamba itatumika kote
bara na visiwani, kulikuwa
na haja pia kwa Waziri
mhusika kwa upande wa
Zanzibar kuipeleka Baraza
la Wawakilishi kama kifungu
cha 132(2) kinavyotamka.
Hadi hii leo Baraza la
Wawakilishi halijapokea
kutoka kwa Waziri Sheria
husika kama katiba yetu
inavyotamka wala kulijadili
suala zima la sheria husika
kwa maslahi mapana ya
Zanzibar na wananchi wake.
Jee kuna uhalali wa kura hii
ya maoni kwa upande wa
Zanzibar katika mazingira
ya namna hii? Haya ndio
yale yale yaliyofanyika katika
uundwaji wa muungano kiasi
kwamba hadi hii leo hakuna
uthibitisho wa kwamba
Baraza la Mapinduzi lilijadili
uundwaji wa Muungano
au kuridhia kama ilivyo
kwa upande wa Bunge la
Tanganyika.
Tu n a r u d i k u l e k u l e
kupitisha katiba kwa
mizengwe bila ya kutafakari

athari zake siku za mbele.


Hivi hawa Wawakilishi
wanaopiga kelele kutwa
majukwaani kuwaomba
wananchi kuipigia kura ya
ndio rasimu iliopendekezwa,
tuwafahamu vipi? Kuna woga
gani kuhakikisha taratibu za
kisheria na kikatiba hapa
Zanzibar zinafanyika hata
kwa makusudi tudharau
katiba inayoweka mkazo
sheria za Muungano
kudhihirishwa na kujadiliwa
katika Baraza la Wawakilishi?
Sehemu ya pili ya hoja
kubwa inayozua gumzo juu
ya uhalali wa kura ya maoni
ni namna ya zoezi zima
lilivyotangazwa na siku yake
kutajwa bila ya kuzingatia
sheria husika inavyoeleza.
Moja ya vipengele muhimu
vilivyopuuzwa na wakuu
wetu wa nchi ni kwa
mwenye haki ya kutangaza
kura ya maoni pamoja na
tarehe husika inavyotakiwa
kuwekwa hadharani
na mwenye mamlaka ya
kutangaza zoezi lenyewe
b a a d a ya k u c h a p i s h wa
kwa suali la kura ya maoni.
Mwenye mamlaka ya
kutangaza kura ya Maoni
ni Tume ya Uchaguzi ya
Muungano na ile ya Zanzibar
(NEC/ZEC). Na kutokana
na uthibitisho uliopo ni
kwamba suali la kura ya
maoni lilichapishwa tarehe
17 October, 2014 na sheria
inatamka kwamba tarehe
ya kura ya maoni itajwe na
NEC/ZEC katika siku kumi
na nne za kuchapishwa kwa
suali la kura ya maoni. Hadi
hii leo si NEC au ZEC iliotaja
tarehe ya kura ya maoni ikiwa
zaidi ya miezi minne tokea
kuchapishwa kwa suala la
kura ya maoni. Jee, uhalali
uko wapi wa kuendelea
na zoezi hili? Hadi hivi
leo alietangaza kwa tarehe
ya kura ya maoni ni Rais
wa Jamhuri ya muungano,

tarehe 22 Oktoba mwaka


2014, kinyume na sheria
iliotoa jukumu kwa NEC/
ZEC kutangaza siku husika.
Ikiwa sheria tuliozipanga
wenyewe tunazipuuza na
kutofahamu umuhimu wa
kufuata taratibu za kisheria,
jee ikitihibitika kwamba sheria
hazikufuatwa katika zoezi
hili tutaendelea kulihalalisha
wakati tayari limezongwa na
jazba za wakuu waliojijenga
kisiasa badala ya msukumo
wa ufuataji wa sheria za
nchi? Kwa watawala sioni
hasa mantiki ya kulitia taifa
katika misukosuko isiyo na
tija wakati kwanza tayari
kulishakuwa na tamko baina
ya Mkuu wa nchi na vyama
vya siasa vya kusogeza mbele
kura ya maoni hadi baada ya
uchaguzi mkuu kutokana na
changamoto zilizokuwapo.
Mbali ya khofu ya
uvunjwaji wa sheria ya kura ya
maoni ya Muungano pamoja
na matakwa ya katiba ya
Zanzibar kutotimizwa, kuna
masuala ya kiufundi ambayo
nayo pia hayajawekwa uwazi
unaostahili. Majuzi Mkuu
wa upinzani nchini alilieleza
Bunge kwamba vifaa vya
uandikishaji na teknolojia
nzima ya mfumo mpya wa
upigaji kura haujafahamika
vizuri. Kuna khofu ya Uwezo
wa vifaa husika kuandikisha
watu 22 kwa siku katika nchi
yenye wapiga kura halali
wa zaidi ya milioni 24 huku
wakati wenyewe uliobaki
ni siku 84. Hata majibu ya
Waziri Mkuu hayakuwa
ya kuridhisha kwa vile nae
hakuonekana akijiamini kwa
maelezo yake. Yote haya
yanaashiria kwamba zoezi
hili linabebwa zaidi kwa
maslahi ya kisiasa badala
ya wananchi, nchi, sheria na
katiba za nchi zetu.
K wa u sh a h i di u l i op o
ni wazi kwamba zoezi hili
halitakuwa na uhalali ikiwa
litatendeka katika mazingira
haya haya yalivyo hasa
mazingatioa ya kupuuzwa
kwa kifungu namba 132
(2) cha katiba ya Zanzibar
ya mwaka 1984, pamoja na
sheria namba 11 ya kura
ya maoni ya mwaka 2013
ambayo kimsingi imeweka
mamlaka ya uchapishaji suala,
tarehe na muda maalum
wa kutangazwa kwa tarehe
ya kura ya maoni ambayo
v y o t e v i m e p u u z wa . N i
vyema serikali ikajitathmini
tena kabla ya uwezekano
wa mahakama kuingilia
kati mchakato mzima kwa
u s h a h i d i wa m a z i n g i r a
yaliopo yenye utata mkubwa
na weledi wa zoezi la kura ya

Makala

AN-NUUR

RABIUL THANI 1436, IJUMAA FEBRUARI 6 - 12, 2015

Kipi Kilichokwenda Kombo Zanzibar?


Na Ben Rijal

BILA ya kujiuliza pale


ulipopakosea kutaka
kujirekebisha, basi elewa
fika utakuwa unaendelea
kukosea kwa kuwa
hujajiuliza na kutaka
kujirekebisha. Mila,
utamaduni na silka ni
katika mambo muhimu
katika jamii yoyote ile
itakayo taka kuwa na
mafanikio.
Anuwani ya makala
hii ni kipi kilichokwenda
kombo? Hapa najaribu
kutafuta suluhisho la kuona
maadili ya Kizanzibari
kuwa yamekwenda
arijojo na kuna hatari
kwa kasi inayokwenda
kuja kujikuta ni kuwa
taifa lilokosa mtizamo na
muelekeo katika maadili.
Inaweza kuwa
kuna sababu tele
zinazosababisha kuona
vijana hata wazee kila
mmoja amepoteza
mwelekeo na kujiuliza
kipi kilichowasibu
Wa z a n z i b a r i ? M a r a
nyingi unapokuwa
unaliachia jambo ima
k wa k u t o k u s u d i a a u
kwa makusudi jambo
ambalo baadaye litakuja
kuwa na madhara, basi
ujuwe hakutokuwa wa
kulaumiwa isipokuwa
wewe ulilolichangia liwe
hivyo.
Zanzibar yetu ambayo
tunaililia ilikuwa ni kituo
au nchi ambayo atakayetia
mguu wake tu, anaona
ameingia katika nchi
iliyojaa nidhamu ya hali
ya juu n utamaduni wa
kupigiwa mfano kwa uzuri
wake. Ilikuwa mwiko
k u m u o n a m wa n a m k e
kavaa vazi lilokuwa sio la
stara na kupita njiani huku
akijishau na hakuna anaye
t h u b u t u k u m wa m b i a
e l e e . L e o m wa n a m k e
kuwa katika hali kama
hio ni jambo la kawaida.
Leo vijana wamekuja na
mtindo wao wa kuvaa
suruali na kuona suruali
ya ndani na akapita kijana
huyo katika kadamnasi
ya watu na hakuna
h a t a a t a k a ye t h u b u t u
kulikaripia hilo. Leo vijana
wamekuwa hata hawaoni
shida kutumia uraibu wa
sigereti mbele ya wazazi
wao na wanapoulizwa
hujibu kuwa wanaondoa
mawazo, wakati huko
nyuma hata kijana akiingia
katika dimbwi la uvutaji
sigereti, basi atahakikisha
kuwa anavuta kwa

RAIS wa Zanzibar, Dkt.


Ali Mohamed Shein.
kujificha.
Leo hata kwenye
ibada, imekuwa watu
kushambuliana yule
anajua zaidi huyu hajui,
huyu usimzikilize
almuradi kumekorogeka,
utajiuliza haya yanatokea
hata Misikitini? Iweje
kwenye Msikiti sadaka
iliyoletwa wapate kila
aliopo kwa wakati ule
Msikitini, imalizikie
sadaka ile kwa Imamu
na muadhini wake tu?
Yakiwa Msikitini yanajiri
hayo, yataweza kuvuka
penginepo?
Barabarani kulikuwa
na nidhamu ya hali ya juu
kabisa, iwe unakwenda
kwa miguu, umepanda
baskeli au umo kwenye
gari. Leo ukiwa unatoka
nyumbani kwako iwe
u m e t o k a k wa m i g u u
au umepanda chombo
chochote kile, basi
utakuwa umo kwenye
khofu kama utafika salama
huko ulipokusudia. Leo
njia ya upande mmoja tu
ambayo ndio kawaida
iliowekewa, utaona njia
hio imegeuzwa kuwa njia
ya pande mbili, utajiuliza
kwani wataalamu wa
mawasiliano kuona njia
ile iwe inakwenda na
v y o m b o k wa u p a n d e
mmoja walikosea?
Waendeshaji baskeli nao
hao hawasemeki wao
hujifanyia watakavyo,
lakini baya zaidi huwa
h a wa c h u k u i k u r u n z i
wakati wa usiku na hio sio
kama ni sheria tu, lakini
inakuwa kwa usalama wa
mwendeshaji wa baskeli na

MAKAMU wa kwanza
wa Rais wa Zanzibar, Seif
Sharif Hamad.
usalama kwa waendeshaji
wa magari.
Utajiuliza kwanini leo
watoto wanaokwenda
skuli kuwa humo njiani
wanamopita ni kelele
tupu na kusema maneno
yasiostahiki. Basi tena
usadifu kupanda daladala
n a o h a p o u t a ya s i k i a
usioyapata kuyasikia.
Wa l i m u h u k o n y u m a
ndio waliokuwa kioo kwa
wanafunzi na jamii kwa
jumla. Leo aghlabia ya
walimu mienendo yao
sio yenye maadili. Siku
h i z i k u s i k i a wa l i m u
wa madrasa baada ya
k u e l e k e z a k u t e n d wa
mwenendo mwema wao
ndio sasa wanaowaharibu
watoto, inasikitisha kusikia
humo kwenye madrasa
watoto ndio wanaharibiwa.
Hivi sasa unasikia fukuto
lilokuwa sio la chini kwa
chini lakini lishatoa moto
wala sio moshi kusikia
mapenzi yanayofanywa
na watu wa jinsia mmoja,
halafu kumsikia mtu
analizungumzia kama ni
jambo la kawaida katika
jamii. Anatamka mtu
yule mpenzi wake, huyo
anayoambiwa ni mpenzi
wake ni wote wawili
ni watu wa jinsia moja.
Hapa ndipo unapojiuliza,
hao wanaopiga zumari
kuhalalishwa matendo
hayo machafu sio
watapata mwanya
kusema yahalalisheni
kuliko kuwachia
kuwa hayatendeki na
kuwakosesha mashetani
hao uhondo?
Leo madanguro yapo na

MAKAMU wa pili wa
Rais wa Zanzibar, Balozi
Seif Idd.
unapouliza unaambiwa laa
hio ni gesti tu. Inafahamika
fika kuwa nyumba hizo
zinaruhusiwa na wamiliki
wake watu kwenda
kujifanyia watakavyo. La
kujiuliza, kweli na huo
UKIMWI utatoweka?
Siku hizi kuna maeneo
ukipita nyakati za usiku
utakutana na wale
wanaouza miili yao na
soko hilo huambiwa ni la
watalii, lakini na wenyeji
nao sio kalili.
Zamani ilikuwa mtu
akiwa na haja ya nazi
huwenda kwa mmiliki wa
shamba na kumuomba
nazi. Hapo mmiliki ama
atamgea kama zipo au
atamwambia kama
unaweza kuukwea
mnazi, basi kajichukulie
zitazokidhi haja zako.
Huko nyuma utaikuta
ndizi imekaa kwenye
mgomba kila ukipita
imekutumbulia macho.
Leo wizi wa mazao
umeshika kasi na kupamba
m o t o . M we n ye n d i z i
anaikata ingali changa
kwa kuhofia isije kuibiwa.
Leo la kusikitisha nikuona
mifugo inavyoangamizwa.
Mtu anamchinja
ngombe aliomuiba kisha
akachukua paja moja tu
na kumwacha ngombe
na sehemu zake zilizobaki
kama mzoga. Wakulima
na wafugaji kila mmoja
anafanya amali hizo kwa
kuwa ni mazoea tu, lakini
sio wenye matumaini na
kupata kipato kutokana na
kazi hizo.
Mvuvi amekuwa
mfano wa yule anawekea

kinyesi sahani anayokulia.


Inasikitisha kuwa mvuvi
anajua kuwa matumbawe
ndiyo makazi na mazalia
ya samaki na ndipo sehemu
inahitajia kuhifadhiwa
kwa hali ya juu ili aweze
kupata kuvua samaki
wakutosha. Leo mvuvi
huyo ndio anayeongoza
kuyaharibu na kuyafisidi
hayo matumbawe tena
kufanya hayo kwa
makusudi.
Wengi wetu kutokana
na hali zetu za vipato,
huenda kutibiwa katika
hospitali za serikali. Eeeh,
h a p o u t a u m wa m a r a
mbili. Unafika unaambiwa
daktari hayupo, mara yupo
lakini anaingia na kutoka.
We n g i n e wa t a k u t a j i a
vya kuchangia visivyo
na hesabu. Kwa mfano
mtu anataka kupasuliwa,
kumbe nusu ya vitu hivyo
vinakuwa mali yake na
a n a p o k u j a m we n g i n e
anamtajia hivyo hivyo
lakini atamwambia vipo
hapo alipo na kumpiga
bei atakayo. Hapo anakua
daktari anawakaanga
wagonjwa kwa mafuta yao.
Leo tukimbile wapi kwa
kufahamu daktari ndio
mtu mwenye huruma ya
hali ya juu. Leo madaktari
nao wameingia ngomani.
Ukiyachukua na
k u ya f a s i l i h a y o y o t e
niliyojaribu kuyaelezea,
u t a o n a Wa z a n z i b a r i
tumetoka katika mstari ule
tuliokuwa nao uliokuwa
wa kupigiwa mfano sio
tu Afrika ya Mashariki,
lakini kwa dunia nzima.
Unaposoma maandishi
mbalimbali utaona
tulivyokuwa tukisifiwa.
Leo anayekuja kutoka
nje hakuulizi ya karibuni
anakuuliza ya kale.
La kujiuliza, kwanini
yawe hayo? Tujiulize kipi
kilichokwenda kombo?
Tuendelee hivi hivi au
kuna haja ya kutafuta
mwaarubaini wa kuweza
kuyatatua haya machache
niliyoweza kuyanukulu?
Watu sio wale wale, sasa
kipi kilichowabadilisha
wawe sivyo kama
walivyokuwa waliopita?
Kipi kilichokwenda
kombo? Utakapoyasoma
makala hii, hebu jiulize
kisha jaribu kupata
jawabu.

10
Na Omar Msangi
WASWAHILI wana msemo
wao, siku njema huonekana
asubuhi. Lakini kwa mantiki
hiyo hiyo, hata mbaya pia.
Zipo sababu za kuwa na
wasiwasi kuwa huenda hali
ikawa mbaya katika mwaka
huu wa uchaguzi mkuu,
na hasa Zanzibar. Kama
huko nyuma kulikuwa
na melody, basi huenda
melody ya mwaka huu
ikawa mbaya zaidi. Hii ni
kutokana na yaliyojitokeza
katika mkutano na
maandamano ya Chama cha
Wanachi, CUF, yaliyokuwa
yafanyike Jan. 27, 2015 na
kuzuiwa na Polisi.
Yapo mambo matatu ya
kuongoza mjadala huu.
Moja ni ile kauli ya Waziri
w a M a m b o ya N d a n i ,
Mheshimiwa Mathias
Chikawe, pale alipoliambia
Bunge kuwa, ilibidi polisi
wazuiye maandamano kwa
sababu kuna ugaidi na
kwamba, panapokuwepo
ugaidi, basi magaidi huwa
wanatumia mikusanyiko ya
watu wengi kufanya ugaidi
wao.
Pili, ni kile kilichoonekana
watu kupigwa mpaka
kupitiliza. Taarifa ndani ya
bunge ikasema kuwa baadhi
ya polisi walitumia spana
za magari (chuma/nondo)
kupiga watu vichwani.
Ta t u , n i i l e k a u l i
iliyoripotiwa pia Bungeni
k u wa b a a d h i ya p o l i s i
walipoulizwa kwa nini
walifanya vile, walidai kuwa
ni amri kutoka juu.
Katika mauwaji ya
Vietnam, Cambodia na Laos,
ambapo mamilioni ya raia
wasio na hatia waliuliwa
na wanajeshi wa Marekani
kati ya mwaka 1969 na 1973,
Henry Kissinger, wakati
h u o a k i w a Wa z i r i w a
Mambo ya Nje, anadaiwa
kuwa msimamizi mkuu
wa m a u wa j i h a y o p a l e
alipopeleka ujumbe kwa
askari akiwaambia kuwa
anachotaka kusikia Rais
Nixon ni kuuwa, kupiga
mabomu bila kikomo na bila
huruma. Kila kinachotembea
au kutambaa, kila kilicho hai
kisiachwe. Kipigwe tu.
[Nixon] wants a massive
bombing campaign in
Cambodia. He doesn't want to
hear anything about it. It's an
order, to be done. Anything that
flies or anything that moves.
Na kweli, kutokana
na amri hii kutoka juu,
mamilioni ya watu wasio
na hatia waliuliwa. Na kwa
vile amri ilisema, chochote
kinachotembea, kipigwe
tu. Hapakuwa na msalie
kwa raia.
Kila yakitokea matukio
yanayotafsiriwa kuwa
ni ugaidi, viongozi wetu
wanatuambia kuwa
wameagiza FBI kutusaidia
kwa sababu wana uzoefu
katika mambo haya. Na hivi
sasa tumekuwa ni washirika
wao wazuri katika mambo

Makala

AN-NUUR

RABIUL THANI 1436, IJUMAA FEBRUARI 6 - 12, 2015

Melody mwaka huu Zanzibar


huenda ikawa mbaya zaidi
Taifa la Kipolisi linakuja kwa kasi
Kauli ya Waziri Mathias Chikawe
Bundi kalia juu ya nyumba mchana

HENRY Kissinger (kushoto), Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani wa Marekani.


yao mbalimbali mpaka kuwa wengine wakiandamana nje Mambo ya Nje wa Uingereza,
na mazoezi ya pamoja ya na mabango yao wakimwita Robert Finlayson "Robin"
kijeshi na hata kutunolea Kissinger kuwa ni muuwaji na Cook. Katika uhai wake
vijana wetu wa polisi wa mhalifu wa kivita, anatakiwa "Robin" Cook alisisitiza kuwa
kupambana na ugaidi. Sasa kukamatwa. Katika hali hakuna kikosi halisi cha
kama walimu wetu ndio ambayo haikufahamika watu magaidi wanaitwa Al-qaida,
hawa waliotoa amri kuwa waliingia mpaka ndani ya bali ni watu wa kuundwa
hawataki kusikia chochote kikao cha Kamati ya Bunge tu ili kukidhi matashi ya
kule Cambodia, ila kupiga na mabango yao na kuvuruga siasa za kibeberu. Kama
tu mabomu na kwamba kila kabisa kikao hicho. Wengine wanavyosema wataaalamu
kinachotembea juu ya ardhi walibeba pingu wakitaka na wachambuzi wengine,
au kupaa ngani, kisionewe wamkamate na kumtia pingu ni Intelligence Assets za
kutumiwa muda wowote.
h u r u m a , ya we z a i s i we na kuondoka naye.
jambo la kushangaza sana
Wa z i r i M h e s h i m i w a Lakini pia wakati mwingine
kusikia kuwa wanafunzi Chikawe ametuambia kuwa intelligence assets hao kama
wao, wanatumia spana za mkutano wa CUF ulizuiwa ilivyokuwa kwa Mujahidina
magari kupasua watu vichwa kwa sababu ya kuhofia ugaidi. waliopigana Afghanistan,
kutokana na amri kutoka Kwa hapa kwetu ukiuliza L i b y a n a s a s a S y r i a
nani gaidi utaambiwa Al- (wakiwemo IS), huandaliwa
juu.
Hivi sasa Henry Kissinger Qaidah au Al-Shabaab wenye na hao hao mabeberu kuwa
kama jeshi la kimataifa la
anatembea na International uhusiani na Al-Qaidah.
kutumiwa muda wowote
Hivi
karibuni
alipata
Arrest Warrant shingoni
kutoka Ufaransa na Hispania. kuhojiwa aliyewahi kuwa kama foot soldiers katika
Kinachomsaidia ni ubabe Afisa wa CIA na kamanda proxy war.
Hivi karibuni alikamatwa
wa Marekani. Hata hivyo m k u u w a k i k o s i c h a
kwa jinsi watu walivyo kupambana na Osama Bin mmoja wa makamanda wa IS.
na usongo naye kutokana Laden, kuwa nani adui Katika mahojiano kamanda
na mauwaji na mateso ya namba moja wa Marekani huyo Yousaf al Salafi alikiri
mamilioni ya watu Asia na baada ya kuwa Osama Bin kuwa wanapata pesa na
Amerika ya Kusini, Mei 8, Laden amekufa. Alichojibu silaha kutoka Marekani.
2010 alinusurika kukamatwa Michael F. Scheuer ni kuwa Hawa ni IS ambao hivi
akiwa hotelini kule Dublin A l - Q a i d a h h a wa j a wa h i sasa Barack Obama anadai
Ireland. Lakini hata ndani kuwa maadui wa Marekani, kupigana nao! Yousaf al
ya M a r e a n i k we n ye we , Osama akiwa hai wala sasa Salafi katika maelezo yake
kunaonekana si salama akiwa amekufa. Akifafanua kwa vyombo vya usalama
tena kwa Henry Kissinger. akasema kuwa adui wa vya Pakistan anasema kuwa
Januari 29, 2015 kulikuwa Marekani ni aduni wa kubuni amekuwa akipewa pesa (na
k u k i f a n y i k a k i k a o c h a ili kukidhi masilahi ya kisiasa, watu wengine wamekuwa
Kamati ya Bunge la Marekani kiuchumi na mambo kama w a k i p e w a s e h e m u
inayohusika na mambo hayo. Sasa, kama ni adui wa mbalimbali duniani) kutafuta
ya usalama kikiongozwa kubuni, maana yake ni kuwa watu wa kuwaingiza katika IS
na veteran wa vita, John hata matukio mengine katika wakiamini kuwa wanapigana
McCain. Kissinger alikuwa haya yanayoitwa ya kigaidi, Jihad. Anasema, kwa kila
mmoja wa watu walioitwa ni ya kubuni vilevile au ya mtu mmoja anayempata na
kutoa ushahidi katika kamati kupanga ili kusimika kitisho kumfikisha Syria kujiunga
hiyo. Baadhi ya wananchi cha ugaidi.
na IS, anapewa dola mia
wa l i p o j u a k a m a y u p o ,
Na hayo ndiyo aliyosema sita ($600). Biashara nono
walivamia kikao hicho huku pia aliyekuwa Waziri wa kabisa. (Tazama: The Express

Tribune, Daily Express, New


York Times, Jan. 28th, 2015)
Hili ndilo alilolisema
Robert Finlayson "Robin"
Cook kwamba, watu
hawa wanaoitwa magaidi
wamekuwa wakipewa
mafunzo na asasi za kijasusi
za nchi za NATO na wengine
kama Idara ya Usalama
ya Pakistan-Inter-Services
Intelligence (ISI), au katika
nchi yoyote linapofanyika
zoezi hili, kutumika kama
vibaraka tu.
Na hili ndilo ambalo
tumewahi kulisema katika
gazeti hili kwamba kuibuka
kwa watu wanaohubiri na
kuhamasisha watu kufanya
vitendo vya kihalifu kwa jina
la Jihad au kuhamasisha watu
kwenda kupigana Somalia/
Syria, huenda tayari tunao
akina Yousaf al Salafi nchini.
Na maadhali hii yaonekana
kuwa biashara nono, huenda
ikatupa tabu. Ila tukiifahamu
kwa sura yake hiyo halisi,
inaweza kutusadia namna ya
kuikabili kuliko kwenda na
mtizamo potofu kuwa tuna
magaidi halisi nchini.
Msamiati huu wa magaidi
tumeupokea kwa sababu
tumewajibika kutumikia
siasa za utandawazi. Kila
anayepachikwa ugaidi kutoka
Washington, sisi tunabaki
kuwa vipaza sauti. Tutamuita
gaidi hata kama hakuna lolote
tunaloweza kulithibitisha
kuwa katufanyia la kigaidi.
Tunavyozungumza hivi
sasa kuna watu kutoka
Zanzibar wapo rumande
wakituhumiwa kwa ugaidi.
Lakini katika utetezi wao
mahakamani wanadai
kuwa wao yamewakuta
kwa sababu ya msimamo
wao juu ya muundo
wa muungano na katiba
inayopendekezwa. Hayo
si ya kujadili kwa sasa kwa
sababu mahakama inafanya
kazi yake. Lakini la kusema
hapa ni kuwa ikishakuwa ni
suala la tuhuma za ugaidi,
hata kanuni za kisheria, haki
za binadamu na mahakama,
zinabadilika. Kuna watu
wapo katika Gereza la Mateso
la Kimataifa, Guantanamo
kwa zaidi ya miaka 15.
Hapo hakuna cha haki za
binadamu, haki za mfungwa
wala haki za mtuhumiwa.
K i s a ! Wa t u h u m i wa wa
ugaidi!
Mkutano na maandamano
ya l i y o p i g wa m a r u f u k u
na kusababisha vipigo,
yalikuwa ya CUF.
Tunafahamu msimamo wa
chama hicho katika Katiba
inayopendekezwa na
msimamo wake juu ya mfumo
wa muungano. Lakini tunajua
pia jinsi Tume ya Jaji Warioba
ilivyodhalilishwa kuhusu
rasimu ya Katiba Mpya
ambayo ilizingatia maoni ya
wananchi. Na tunafahamu
jinsi rasimu hiyo ilivyotupwa
ikawa mjadala ni juu ya hoja
ambazo zinadaiwa za wale
wahafidhina wanaotaka
mfumo uliopo udumu.
Chukua hali hiyo
ukizingatia kuwa
tunakabiliwa na kura ya
maoni na kisha Uchaguzi
Mkuu. Upo wasiwasi mkubwa
kuwa hiki walichofanyiwa

Inaendelea Uk. 12

11
HALI ya mambo siku
chache kabla ya upigaji
kura kwenye Bunge
Maalum la Katiba ilikuwa
ngumu sana kwa watu
saba walioamua kuikataa
katiba iliyolazimishwa na
Chama Cha Mapinduzi
(CCM). Mwandishi Salma
Said ameandika alichoita
Simulizi za Ushuhuda
wa hali waliyokuwa nayo
kwa sababu tu waliazimia
na hatimaye kupiga kura
ya HAPANA. Fuatilia
si m ul i zi zake katika
makala yake.
Ningependa niandike
simulizi za siku chache
kabla ya upigaji kura namna
ambavyo hali ngumu
ilivyotukabili sisi watu
saba tulioamua kupiga
kura ya HAPANA, tena ya
wazi, kwani Wazanzibari
wenzetu walituchukulia
kwa mtazamo tofauti
kutoka nyumbani
Zanzibar. Baadhi ya vijana
walichapisha vipeperushi
na kuvisambaza kwenye
m i t a n d a o ya k i j a m i i
wakitutaka turudi
nyumbani na kutuita
wasaliti, huku Wazanzibari
wenzetu Dodoma nao
wakitupa vitisho vya
kila namna tu maana
haikuwa kutushawishi
tu, bali mambo yalizidi na
kupindukia mipaka hadi
wengine wakitwambia
tukipiga kura ya hapana
tutakiona cha moto.
Baada ya kuonekana
wapo watakaopiga
kura za hapana, lugha
iliyokuwa ikitumika
miongoni mwa wenzetu
wa CCM wakisema
k u n a wa t u wa n a t a k a
kuharibu mchakato wa
katiba inayopendekezwa
katika dakika za mwisho
lakini waliapa kwenda na
sisi iwapo hatutaregeza
misimamo yetu ya
kuikataa rasimu hiyo.
Sio kazi rahisi kama
we n g i wa n a v y o d h a n i
kama ambavyo haikuwa
we p e s i wa l i o t o k a n j e
ya b u n g e , U m o j a wa
K a t i b a y a Wa n a n c h i
( U K AWA) k u r u d i
ndani, halikadhalika
ugumu ulikuwepo kwa
waliokuwepo ndani kutoka
nje, wengine tuliamini hata
maamuzi ya watu kutoka
bungeni wangetoka basi
naamini wangetoka watu
wachache kama watu
wa t a t u t u a u wa n n e
ambao wana msimamo
madhubuti na wengine
wangebaki na kurahisisha
mafanikio ya kupatikana
2/3 kirahisi, kutokana na
khofu miongoni mwetu.
Baadhi ya wajumbe
kutoka Zanzibar hasa wale
wanaotokana na kundi la

Makala

AN-NUUR

RABIUL THANI 1436, IJUMAA FEBRUARI 6 - 12, 2015

Katiba mpya na mfumo wa


kuwagawa Wazanzibari

MAKAMU wa kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad.


201 walikuwa na msimamo wenzangu kuikataa rasimu ya Zanzibar katiba hii ni
wa kuikataa rasimu yote lakini najiuliza kwa nini mwiba mchungu kwangu
na ndio maana kiukweli iwe kosa mimi kushawishi na ndio maana natoa
taarifa za ndani zinasema kuikataa na isiwe kosa changamoto (challenges)
waliopiga kura za hapana kwa wale wengine ambao i l i w a t u w a f u a t i l i e
rasimu nzima walikuwa walitushawishi kuikubali? hansad wataona kama
ni wajumbe sita kati ya
Wapo ambao kutokana kuna mchango wangu
waliopiga kura za siri n a u z a l e n d o w a o katika kamati kwa kuwa
na baadhi yao walikuwa walitutaka tutoke nje nilikuwa nikiamini kuwa
wamekataa baadhi ya ibara kwa maana ya kususia siri yangu moyoni ni siri ya
tu za rasimu. Naamini Bunge, lakini mimi binafsi kura yangu ya HAPANA
kwamba walikuwa wana n i l i k a t a a k w a k u w a baada ya majadiliano ya
nia njema ya kuikwamisha niliamini nina maamuzi ndani ya kamati mwisho
rasimu hii kwa kuwa yangu binafsi na siko tayari wa m c h a k a t o m z i m a
haina maslahi na Zanzibar kuchukua ushauri kutoka k u l e b u n g e n i , n a s i o
lakini walikuwa hawataki popote kwa kuwa niliamini kwenye kamati niliamini
kuonekana wabaya na sijatumwa na chama cha ndani ya kamati hakuna
wao ndio kikwazo ila siasa, wala kikundi cha n i t a k a c h o p e n d e k e z a
wanaamini katiba hii haina dini wala taasisi yoyote kikazingatiwa na hayo
maslahi isipokuwa kwa zaidi ya jumuiya yangu a m b a y o w e n z a n g u
kuwa wameshurutishwa ya Waandishi wa Habari wakiyasema hayakuwa
na misimamo ya chama za Maendeleo Zanzibar yakizingatiwa, niliamua
a m b a p o b a a d h i y a o (WAHAMAZA) ambao sina sababu ya kuongea
wengine waliendekeza kimsingi walinishauri chochote ila niwe na siri ya
khofu zao za kupiga siri t o k e a k u a n z a k w a maamuzi yangu moyoni.
wakiamini kwamba siri mchakato huo nibaki ndani
Wajumbe waliopiga
zao zitalindwa.
na nitetee nikiwa ndani kura ya HAPANA
B i n a f s i n i l i s h a o n a kwa hivyo nisingeweza
1. Adil Mohammed
m a p e m a h a r a k a t i kwenda kinyume.
Ali (Walemavu)
zilivyokuwa zikiendelea
Binafsi nilikuwa
2. Alley Soud Nassor
namna gani wajumbe naamini naweza kuizuwia (Taasisi za Elimu)
wakitushawishi tupige 2 / 3 n i k i wa n d a n i ya
3. Ali Omar Juma
kura ya siri nikajua hapa bunge na hamu yangu (Vyama vya Siasa)
kuna namna fulani ya ilikuwa niweke rekodi
4. Jamila Abeid Saleh
kuibiwa kura zetu na ndipo ili vijukuu vyangu vije (Vyama vya Siasa)
nikawashauri wenzangu kusoma kuwa Salma Said
5. S a l m a Ha m o ud
wachache tusipigeni kura alipiga kura ya HAPANA Said (Taasisi zisizo za
za siri ila kwa wale ambao kwa rasimu hii ya katiba kiserikali)
hawakutaka hatukuwa na ambayo kimsingi sikuwa
6. Mwanaidi Othman
namna ya kuwabadilisha nakubaliana nayo tokea Tahir (Vyama vya Siasa)
w a l i k u w a h u r u n a kuanza kwa majadiliano
7. Fatma Mohammed
wakapiga kura zao za ambayo yaliondosha sura Hassan (Taasisi za Dini)
siri ambazo zilistiriwa ya kwanza na sura ya
I n a s h a n g a z a
na zilistirika kwa usiri sita ambazo ndio khasa R a i s K i k w e t e n a y e
w a k e . M i m i n a s e m a kiini na roho ya katiba kajichanganya wakati
kusudi haiambiwi pole na hii. Nimetoka Zanzibar akizitaja hizi kura za wazi
walichokipanda ndicho ili kusimamia maslahi kwanza kasema kura za
walichokichuma.
ya Zanzibar na kiapo wazi ni 7 kisha kasema
Mimi kwa upande wangu changu moyoni kilibeba ni 5 nadhani alikusudia
sikuona kama nimefanya dhana hiyo. Kwa hivyo kura tano kwa maana ile
makosa kama ambavyo sikutaka kujizonga kwani ya watu wawili waliotaka
wengi wananichukulia niliamini ndani ya moyo kuitwa katika Kamati
kuwa nimewashawishi wangu nje ya maslahi ya Maridhiano ambapo

wakati Mwenyekiti wa
Bunge Maalum la Katiba
akitangaza timu yake ya
kamati hiyo wajumbe
w o t e s a b a wa l i o p i g a
HAPANA wapo njiani
kurejea Zanzibar; jee
wajumbe wangapi hao
waliotajwa kukutana na
Kamati ya Maridhiano
wakati hawakuwepo tena
Dodoma?
Wajumbe saba waliamua
kuondoka Dodoma
kutokana na dharau,
matusi ya nguoni, vitisho
walivyokuwa wakivipata
kutoka kwa wajumbe
walio wengi ambao ni wa
CCM, hawakujifanya tu
kuwa wao ndio wengi, bali
walijifanya wao ni wenye
nguvu, wenye maamuzi ya
wenzao kwa kisingizio cha
kuwa na dola eti wao ni
wenye uwezo wa kufanya
chochote katika katiba
hii kutokana na kauli
walizokuwa wakituambia.
Lakini pia ningependa
niandike namna
g a n i Wa z a n z i b a r i
walivyotumika kufanyiana
u a d u i we n y e we k wa
wenyewe; kuoneshana
ubabe, dharau, matusi ya
nguoni, kebehi na vijembe
kutokana na kuwa na
mitazamo tofauti wakati
wenziwao wa Tanzania
Bara wakikaa pamoja.
Hii Katiba itapita
mtake msitake, hii katiba
nyinyi hata mkipiga
hapana nyote mliopo
ndani ya ukumbi huu mjue
tu kwamba tutaipitisha
mnacheza na wana CCM
nyie, hii ndio chama dume,
hiki ndio chama chenye
uwezo, hiki ndio chama
tawala ..., ni maneno ya
kiongozi CCM Zanzibar.
Kauli kama hizo
zik itolewa na b aadhi
ya viongozi wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM)
na wanachama wengine
waliondoka katika nafasi
zao bungeni na kuja
pale tulipokaa sisi na
kuunga kauli za Shaka
na wenzake kama wanne
kuanza kuongea maneno
k a m a ha y o k uo ne s ha
sisi ni watu wajinga,
watu tunaotumiwa kwa
kuongozwa na kuburuzwa.
Hamtaki hata haki ya
kuishi hata mtu kuishi
hataki basi kila kitu hapana
tu, alisema mmoja wao
(jina nalihifadhi).
Wa j i n g a wa n a m j i
wao tutawaonesha hawa
wanaosema hapana ni
watu wenye kutumiwa
na wakoloni wanatumiwa
na Waarabu na wengine
hapa wala sio kwao, kwao
ni Oman lakini hii katiba
itapita mtake msitake hizo
Inaendelea Uk. 14

12

MAKALA/SHAIRI

KILIO CHA ALBINO !


(Kama si ushirikina,...)

Albino tunalia, si tu wa Mwanza jijini,


Albino tunalia, bali wa kote nchini,
Albino tunalia, mijini na vijijini,
Albino tunalia, aimi! tu majonzini,
Kama si ushirikina, tusingekuwa twalia!

Albino ninalia, kwa uchungu na huzuni,


Albino ninalia, hadharani si batini,
Albino ninalia, kwa mayowe pasi soni,
Kama si ushirikina, nisingekuwa nalia !
Albino ninalia, hofu yangu mtimani,
Albino ninalia, si na simba wa porini,
Albino ninalia, si na papa baharini,
Albino ninalia, si na chatu vichakani,
Kama si ushirikina, nisingekuwa nalia !
Albino ninalia, si na hao hayawani,
Albino ninalia, na ndugu yangu insani,
Albino ninalia, kuniwinda nje-ndani,
Albino ninalia, maisha yangu shakani,
Kama si ushirikina, nisingekuwa nalia !
Albino ninalia, siko salama nyumbani
Albino ninalia, siko salama shuleni,
Albino ninalia, siko salama kazini,
Albino ninalia, USALAMA mwafanyani?
Kama si ushirikina, nisingekuwa nalia !
Albino ninalia, si leo tangu zamani,
Albino ninalia, wa kunauni simwoni,
Albino ninalia, na kuhoji kwa huzuni,
Albino ninalia, hivi nami si insani?
Kama si ushirikina, nisingekuwa nalia !
Albino ninalia, kwa kejeli za insani,
Albino ninalia, kuninadi hadharani,
Albino ninalia, 'mimi dili tijarani'
Albino ninalia, kosa langu kwenu nini?
Kama si ushirikina, nisingekuwa nalia !
Albino ninalia, kuona ndovu nyikani,
Albino ninalia, i yake juu thamani,
Albino ninalia, kuzidi yangu jamani,
Albino ninalia, hali hii kulikoni?
Kama si ushirikina, nisingekuwa nalia !
Albino ninalia, kutengwa mamilioni,
Albino ninalia, kwa uhai wa 'yawani,
Albino ninalia, najiuliza kwanini,
Albino ninalia, kwangu kutoyumkini?
Kama si ushirikina, nisingekuwa nalia !
Albino ninalia, wa nchi yenye amani !
Albino ninalia, na ya nchini amani !
Albino ninalia, amani amani gani ?
Albino ninalia, kama si ya mdomoni?
Kama si ushirikina, nisingekuwa nalia !
Albino ninalia, kuhajiri natamani,
Albino ninalia, nondoke humu nchini,
Albino ninalia, niduru ulimwenguni,
Albino ninalia, nikaisake amani,
Kama si ushirikina, nisingekuwa nalia !
Albino tunalia, ya ILAHI ya MANANI,
Albino tunalia, twakwomba Utuauni,
Albino tunalia, hatwoni wa kutwauni,
Albino tunalia, ila wewe RAHMANI,
Kama si ushirikina, tusingekuwa twalia!
ABUU NYAMKOMOGI-MWANZA.

Melody mwaka huu Zanzibar

Inatoka Uk. 10

CUF kwa kisingizio cha


ugaidi, huenda kikatumika
katika kuhakikisha kuwa
yanayotakiwa yanapita,
na yasiyotakiwa hayapati
nafasi. Na hii maana yake ni
watu kupigwa sana spana
za magari vichwani. Huu
ni wasiwasi tu, lakini kama
nilivyosema, kama siku
njema huonekana asubuhi,
basi hata na mbaya pia.
Ila la kusisitiza hapa
ni kuwa, matesao na
mauwaji yaliyotokea mahali
mbalimbali duniani ambapo
ubeberu ulitia mguu, ilikuwa

ni kwa lengo la kusimamia


masilahi yao sio kujali
u s a l a m a wa n c h i wa l a
maendeleo yake. Na katika
zama hizi, ndio wametujia na
ugaidi wa Al-qaida, ISIS, AlShabaab na mengine kama
hayo.
Sasa hatujui hawa magaidi
anaotutahadharisha nao
M h e s h i m i wa C h i k a we ,
ndio hawa hawa wa akina
Michael F. Scheuer au nasi
tumetengeneza wa kwetu
wa kuhakikisha Kidumu na
Mapinduzi Daima!

AN-NUUR

RABIUL THANI 1436, IJUMAA FEBRUARI 6 - 12, 2015

Sheikh Mohammed Idd


amepatia kuhusu Bakwata

Ila ni gari bovu lisilofaa ukarabati

Na A.S Chachika
SHEIKH Mohammed
Idd, maarufu kama
Abuu Idd, amefungulia
m wa n g wi ili sa u ti
ambayo ilikwisha
toka kwa kupitia
vinywa anuai kuhusu
BAKWATA, kuwa ni
kikwazo kikubwa kwa
maendeleo ya Uislamu na
Waislamu. Aliyoyasema
Sheikh ni yale yale
yaliyokuwa yanasemwa
na Waislamu wote wenye
kuguswa na vikwazo
vinavyofanywa na
Taasisi inayojinasibisha
na uongozi na
uendelezaji wa Uislamu
na Waislamu nchini
Tanzania.
Amenukuliwa na
An-nuur, No. 1156
ya Desemba 2014,
akidhihirisha yale
yanayomkera, aliyataja
machache ambayo ni
Bakwata Kuhodhi mali
za waqfu na kuzitumia
kinyume na malengo
yake. Jingine alilosema ni
kuwa, Bakwata kukosa
mipango ya maendeleo,
hali inayofanya
Waislamu, wakose dira
na kuvunja umoja wa
Kiislamu kwani yule
aliyejivika ukinara wa
kuongoza, hana mpango
wa mambo ya maendeleo.
Zaidi Abuu Idd, alisema
Bakwata huwasiliana na
na Serikali siku za Idd au
kama wameletewa mbuzi
au Tende kutoka Makka.
Labda tuchukue
fursa hii kumkumbusha
Abuu Idd, kuwa hayo
aliyoyasema ni machache
miongoni mwa mengi
na mazito yaliyokuwa
yamefanywa na Waislamu
wa kada mbalimbali
na kwa nyakati tofauti
z a wa t u ( Wa i s l a m u )
walipofunuliwa na
k u e l e wa u k i r i t i m b a
wa Bwakata dhidi ya
Uislamu na Waislamu.
Hivyo haya aliyoyataja ni
mwangwi (Echo).
Moja ni ile ya Mufti
wa B a k wa t a , S h e i k h
Simba, aliyoitoa Jijini,
Tanga, mnamo Juni 30,
2007, katika sherehe
ya kutimiza miaka 50
ya Taasisi ya TAMTA.

Mufti alisema Bakwata


sawa na Gari moshi,
bovu ila alinukuliwa
akiomba msaada na dua
za Waislamu ili aweze
kulikarabati. Kwa kauli
hiyo ya Mufti wa Bakwata,
tunasema amepatia.
Labda tunaweza tu
k u t o f a u t i a n a j u u ya
namna ya kulikarabati
hilo gari bovu, maana
wengine tunaamini kuwa
h a l i k a r a b a t i k i k wa n i
ndivyo lililovyoundwa
na ndiyo ilikuwa dhamira
ya walioliunda kuwa liwe
bovu daima.
Nukta ya pili katika
maoni yake ni kuwa,
yeye akiwa ni kipenzi cha
Bakwata hawezi kuihami,
bali ni kutafuta njia ya
kuirekebisha. Amesema
kuwa yeye anaipenda
B a k wa t a , p a m o j a n a
uozo wake wote huo.
Hiyo ni fikra yake na
anadhamira ya kukaa
karibu na Bakwata ili
aweze kuirekebisha.
Dhamira yake hiyo, si
ngeni. Njia hiyo imekuwa
ikitumika tangu zama
za uongozi wa Rais Ally
Hassan Mwinyi na Mufti
Hemmed bin Jumaa.
Tutakumbuka kuwa Rais
mwinyi, alitumia fursa
yake kama Muislamu,
aligundua madhaifu
ya Bakwata, akafanya
t a r a t i b u z a k u wa i t a
viongozi waandamizi
akiwemo Mufti na
kuwanasihi namna gani
wairekebishe Bakwata
ili iwe kwa manufaa ya
Uislamu.
Katika kikao hicho,
ilifika hatua Mufti Hemed,
kumtamki Rais Mwinyi,
Mimi siji tena ofisini
kwako, yawezekana kuwa
wewe hujui sababu za
kuasisiwa kwa Bakwata.
Mh. Mwinyi, aliishia
hapo.
Lakini, alipoingia
Rais Jakaya Kikwete,
pia alipata kuwaambia
viongozi wa Bakwata,
katika Baraza la Idd,
lililofanyika Jijini Arusha,
akiwa mgeni rasmi, kuwa
Kama Taasisi yenu hii
(Bakwata) ingekuwa ya
Kisiasa, ningewaita ofisini
k wa n g u n i wa e l e k e z e
namna ya kuiboresha.
Hata hawa wote

SHEIKH Mohammed Idd.


walioanzisha Taasisi za
Kiislamu nje ya Bakwata ni
baada ya kutambua kuwa,
kuhangaika na kuirejesha
Bakwata, katika njia sahihi
ni kupoteza muda. Hali
hiyo ndiyo iliyo sababisha
kila aliyeguswa na haja
ya kusimamisha Uislamu
katika jamii akatafuta
wadau wenzake na
k uanzisha Taasisi za
Kiislamu kwa maendeleo
y a Wa i s l a m u k w a
mafanikio tunayoyaona.
Tu n a m u o m b a A l l a h
(sw) aziwezeshe Taasisi
zenye malengo mema
kuepukana na rai na
mapungufu mengine.
Tuanze na swali la
pili. Jibu lake ni wazi na
rahisi kwani kulikuwa
na Taasisi maarufu sana
ikiwaunganisha Waislamu
katika kutekeleza mambo
yao. Taasisi hiyo ni East
African Muslim Welfare
Society (EAMWS).
Taasisi hii ilijihusisha
zaidi na usambazaji wa
huduma za elimu na
afya, na iliwaunganisha
Waislamu wote. Hata hivyo
Kanisa halifurahishwi
na umoja wa Waislamu
na haswa jinsi Jumuiya
hiyo ilivyokuwa ikiratibu
shughuli zake. Kanisa
lilihofia Jumuiya hiyo
na likatamka wazi kuwa
mshikamano wa Waislamu
ni tishio kwa hatma ya
Kanisa. Yaani ili Kanisa
listawi, lazima Waislamu
wasambaratishwe.
Serikali, ilipiga
marufuku Jumuiya hii
na ikawaundia Waislamu
Jumuiya mbadala, yaani
Bakwata. Serikali pia
ikaipatia Bakwata mali na
rasilimali zote za Jumuiya
hiyo.

13
SIKU moja baada ya
kupiga kura ya hapana kila
mmoja wetu alikabiliwa
na vitisho na matusi
mbalimbali, lakini kila
mmoja alisimama imara
hadi dakika za mwisho.
Hakuna aliyetetereka na
kubadilisha msimamo
wake, zaidi ya watu 14
walikuwa na msimamo
wa kuikataa rasimu yote
lakini kutokana na khofu
wakaanza kupungua na
kuamua kupiga kura za
siri.
Kulikuwa na vikundi
vidogo vidogo vikitujadili
tuliokubali kupiga kura ya
HAPANA kwa njia ya wazi
kuwa eti si wazalendo
na nikitangazwa mimi
kuwa ndio Public Enemy
Number One, lakini hilo
katu halikunitia khofu
wala kunivunja moyo
kwa kuwa nilijua mambo
kama hayo yatanikuta na
nilijitayarisha kuyapokea
na kuyakabili kwa hali
yoyote.
Ingawa wajumbe
wengi waliotoka Zanzibar
walikuwa wana msimamo
kama wetu wa kupiga
kura ya hapana kuanzia
sura ya kwanza hadi
sura ya 19 na ibara zake
zote, lakini hawakuwa na
uwezo wa kutetea uamuzi
wao huo kwa kupiga
kura ya wazi kutokana
na ushawishi, vitisho
na khofu za kuogopa
kupoteza kazi zao, nafasi
z a o n a wa p o a m b a o
walikuwa wakiona muhali
kupiga kura ya wazi kwa
sababu tu wamekuwa na
maelewano ya karibu na
baadhi yao katika kipindi
chote cha bunge na baadhi
ya wale watu ambao wana
mitazamo tofauti.
Mimi nipo pamoja na
nyie lakini kwa kweli nikiri
kwamba siwezi kupiga
kura ya wazi kwa sababu
tumeshakaa na hawa watu
na wananiamini sana
kwamba mimi ni mwenzao
sasa nikipiga kura ya wazi
nitawavunja moyo sana
lakini niaminini kwamba
mimi sijapokea pesa na
hata kama nimepokea,
nitapiga kura ya hapana,
alisema mmoja wa
wajumbe walopiga kura
ya siri.
Kilichotokea ambacho
wengi hawakijui, wajumbe
wengi, viongozi wengi
wa l i h a d a i k a n a wa l e
wachache waliomo
katika kamati zetu 12
kukubaliana na maoni ya
wengi na hivyo kuona
idadi ya wanaopingana
na rasimu hii ni wachache,
lakini walisahau kwamba
n d a n i ya k wa m f a n o
kulikuwa na wajumbe

Makala

AN-NUUR

RABIUL THANI 1436, IJUMAA FEBRUARI 6 - 12, 2015

Siku moja baada ya kura ya HAPANA

Mh. Samwel Sitta,


aliyekuwa Spika wa
Bunge Maalum la Katiba.

Mh. Saada Salum Mkuya


aliyekuwa mjumbe wa
Bunge Maalum la Katiba.

Mh. Ismail Jusa Ladhu


aliyekuwa mjumbe wa
Bunge maalum la Katiba

watano wenye mtazamo


wa kuikataa lakini
waliokuwa wakijionesha
wazi ni wawili na watatu
wanakubaliana na wengi
na hivyo kufichika siri
ya wale wenye maoni ya
wachache. Ambapo wengi
wao walikuwa wakisubiri
kupiga kura ya HAPANA
kwenye ukumbi wa bunge
na hawajataka kujionesha
kwenye kamati.
Siku za upigaji kura
zilivyokuwa zinakaribia,
tuliitwa sisi mmoja mmoja
na kuulizwa misimamo
yetu na kwa sababu za
kuikataa rasimu hii kwa
kuwa tayari fununu
zilishaanza kusikika kama
kuna watu watapiga kura
ya HAPANA, wapo ambao
walipoitwa na kuregeza
misimamo baada ya
kutakiwa wapige NDIO
lakini wapo pia tuliokataa
nikiwemo mie mwenyewe
sikukubali na kila
nilipoitwa nilisema siwezi
kuipitisha kwa sababu tatu
tu ingawa zipo nyingi 1.
Naamini katiba hii ikipita
itakwenda kuiathiri katiba
yangu ya Zanzibar. 2.
Naamini katiba hii haina
maslahi na Zanzibar na
3. Naamini katiba hii
ikipita itaongeza orodha
ya kero za Muungano
badala ya kuzipunguza.
Hayo ndio mambo matatu
niliyoyaona ni muhimu
kwangu ingawa yapo
mengi sana.
Ni ukweli usiopingika
kwamba hakukuwa na
msimamo wa Wazanzibari
kwa kuwa aliyepaswa
kuitisha kikao ni Makamo
wa Pili wa Rais wa
Zanzibar, Balozi Seif Ali
I d d i k u wa u n g a n i s h a
Wa z a n z i b a r i i l i
kuzungumzia mahitaji
yao au madai yao ndani ya
Katiba, lakini kwa bahati
mbaya mara kadhaa licha

ya kuombwa awakutanishe
alishindwa kabisa kuwaita
Wazanzibari na kukaa nao
pamoja ingawa baadhi
yao walipenda iwe hivyo
akiwemo aliyekuwa
Mwanasheria Mkuu wa
Zanzibar, Othman Masoud
Othman na baadhi ya
wajumbe wa CCM.
Na hilo la kukaa kama
Wazanzibari lilianzia
ndani ya kikao cha Baraza
la Wawakilishi ambapo
Mwakilishi wa Jimbo la
Mji Mkongwe, Ismail Jussa
Ladhu alitaka kujua iwapo
Wazanzibari wanakwenda
kwenye bunge la katiba
wanakwenda kama nani,
Wa z i r i wa S h e r i a n a
Katiba, Abubakar Khamis
Bakary alisema yeye kama
Abubakar angependa
kuona wanakwenda
kama Wazanzibari na
sio kama CCM au CUF.
Lakini kwa bahati mbaya
sana aliposimama kuja
kufunga kikao hicho,
Balozi Seif alisema serikali
haina msimamo, na kauli
hiyo ndio iliyokwenda
kuharibu na kuathiri
m a m b o n a u m o j a wa
Wazanzibari kule bungeni.
K a b l a y a U K AWA
kutoka nje ya bunge,
juhudi za kuwakutanisha
Wa z a n z i b a r i p a m o j a
zilifanyika kupitia
wajumbe kutoka CCM na
CUF kumuendelea Balozi
Seif na kutaka wakae
pamoja kuzungumzia
maslahi ya Zanzibar,
lakini bahati mbaya zilifeli
katika hatua za mwanzo
kwa kuwa hakukuwa
na dhamira ya dhati ya
kuitetea Zanzibar ndani ya
katiba hii.
Hatimae Wazanzibari
wakawa wanakwenda
katika vikao vya kamati
hawana kitu mkononi
kama walivyojipanga
wenziwao; na matokeo yake

wakawa wanaandikiwa
baadhi ya mapendekezo
wakipewa wayasome na
wao wanayasoma lakini
wakiambiwa wayatetee
au kuyatolea ufafanuzi
h a wa we z i k wa k u wa
hawajaandika wao.
Kwa hakika ilikuwa
ni mambo ya aibu na
kujifedhehesha kama
Wazanzibari. Yalitamkwa
mengi na wenzetu wa
Bara, lakini tukistahiki
matusi hayo.
Wapo watu wengine
wa l i k u wa wa k i d h a n i
pesa ndio iliyowahadaa
Wazanzibari na kukubali
kupitisha mambo kirahisi.
Ukweli ni kwamba sio
pesa peke yake, kulikuwa
na hila na mbinu chafu na
hadaa ikifuatiwa na chuki
ndani yake ambayo kwa
kiasi kikubwa imechangia
ukubwa na ubabe wa
mkubwa dhidi ya mdogo
na hata wale waliokuwa
wana msimamo wa
kuitetea Zanzibar
walifunikwa katika
kichaka cha chama na
matokeo yake wakajiona
wanafuata mkumbo wa
kuhofia kuwajibishwa
na hivyo hisia zao za
uzalendo zikafichika ndani
ya kichaka hicho.
Sisi tulitakiwa tukae
kama Wazanzibari na
sio kama CCM na CUF
kwa sababu tushaingia
katika vikao hivyo
lakini hivyo vikao ni vya
chama bara na Zanzibar
lakini tunapotoa hoja ya
Zanzibar tu tunaonekana
kama wasaliti kama
ilivyojitokeza kwenye
Kamati ya Uongozi,
ukiongea kitu ukanukuu
Katiba ya Zanzibar unapata
upinzani mkali kutoka kwa
wenzetu, lakini ukichukua
nukuu hiyo hiyo ukaisema
itachukuliwa kama
hujaitaja Zanzibar,

alisema mmoja wa
wajumbe wa CCM ambaye
ni mjumbe wa kamati ya
uongozi.
Pia ningependa
kugusia kidogo namna
Mwanasheria Mkuu,
Othman Masoud
alivyokaangwa kuanzia
ndani ya kamati yetu na
baadae kikao cha pamoja na
mawaziri na watani wake
walivyoshiriki kummaliza,
ujasiri na msimamo
wake madhubuti juu ya
Zanzibar na hatimae kura
yake HAPANA.
Othman alianza
kupingwa ndani ya
kamati yake namba 11
ambapo Mwenyekiti
wake ni Anna Kilango
na Makamo Mwenyekiti
wake ni Hamad Masauni,
wakati Othman akitoa
mapendekezo yake,
baadhi ya wabunge kutoka
Bara walisema kimsingi
wanaona mapendekezo
yaliyotolewa na Othman
yana mantiki na baadhi
yake wanakubaliana nayo
na pia yanabeba msimamo
wa serikali, lakini mjumbe
mmoja kutoka Zanzibar,
Mbunge wa viti Maalum
CCM, alipingana na
wajumbe wenzake wa
CCM.
Othman ni mjumbe
kama wajumbe wengine
na mawazo yake
yasichukuliwe kama yeye
anaiwakilisha serikali
k wa h i v y o n a i k i wa
yeye ni mwanasheria wa
serikali, basi yeye Othman
anaunga mkono serikali
ya shirikisho haya basi
tumfateni eeeeh si mnataka
kuchukua maneno yake,
alisema Mjumbe huyo kwa
kebehi.
Ningeandika maneno
machache sana kabla ya
kumalizia yanayomkhusu
rafiki yangu wa karibu
sana asiye mwanasiasa,
ni mtu mwenye misingi,
mtu mwenye uchungu
na nchi yake, mwenye na
msimamo mzuri sana na
mwenye uadilifu wa hali ya
juu sijawahi kusikia kama
amewahi kuburuzwa au
kumfuata mtu kwa kile
asichokiamini lakini kwa
hili aaaah sikutarajia hata
siku moja kama ataweza
kwenda kinyume na
u a d i l i f u wa k e k a t i k a
utendaji wake wa kazi.
Aaaaaaah siamini sikubali
na sitaki kusikia kama
yeye ndio aliofanikisha la
kupatikana 2/3? No siamini
kama ni madaraka siamini
kama ni fedha na siamini
kama nguvu zilizomfanya
atende asichokiani. Ipo
siku nitamsuta japo sio
Inaendelea Uk. 14

14

Makala

AN-NUUR

RABIUL THANI 1436, IJUMAA FEBRUARI 6 - 12, 2015

Katiba mpya na mfumo wa kuwagawa Wazanzibari

Inatoka Uk. 11
kura zenu za hapana ni
bure tu, alisikikia akisema
m w i n g i n e a m b a ye n i
Mbunge (CCM) akihama
kutoka alipokuwa na kuja
tulipokaa sisi.
M h e s h i m i wa Ya h ya
Kassim Issa, Mbunge
wa Chwaka na wenzake
walioniomba nipige
kura ya NDIO ambapo
Dk. Mwinyihaji Makame
Mwadini aliuliza iwapo
kama hatujaona jambo zuri
hata moja katika rasimu
iliyopendekezwa hata
tupige kura ya HAPANA
lakini jibu letu lilikuwa

rakhisi, jee nyinyi mliopiga


ndio, basi hakuna baya
hata moja lililowachukiza
hata muamue kukubali
rasimu nzima?
Kwa ufupi baadhi ya
wana-CCM walitoka
sehemu zao walizokaa
na kuja tulipokaa ili
k u t u f a n y i a f u j o k wa
maneno ya dharau na
kebehi huku wakitumia
lugha za udhalilishaji ili
kuturudisha nyuma na
kutaka tupoteze muelekeo
ili tukubali kwa kupiga
kura za Ndio.
Kutokana na katiba
iliyopendekezwa

Siku moja baada ya kura ya HAPANA


Inatoka Uk. 13

kwa maneno lakini jicho


langu na lake likikutana,
basi tayari atakuwa
ameshapata ujumbe
wangu mzito.
Hebu tupitie hizi
takwimu kidogo kama
kujikumbusha tu.
Wajumbe kutoka Zanzibar
walikuwa ni 219 kati yao
waliotoka nje na UKAWA
ni 66 na kura za wazi
za hapana zilikuwa ni 7
=73. Na 2/3 ya 219 ni 146.
Sasa jaaliya Wabunge na
Wawakilishi waliokuwepo
ndani wote wawe
wamepiga NDIO wale
walopiga kura za siri wote
wawe wamepiga kura za
NDIO, pamoja na wale
wajumbe sita walopiga
kura nje ya bunge wawe
wamepiga kura ya NDIO.
Tulitakiwa kuhudhuria
katika kamati ya
maridhiano kati yetu
wende watu wawili lakini
wakati kamati inatangazwa
sisi sote watu saba wakati
huo tulikuwa njiani kurudi
zetu Zanzibar. Sasa ni
nani na nani ambao
wamekwenda katika
kamati ya maridhiano
kurekebisha kura zao za
HAPANA? Tuambiwe
tuwajue. Na wajumbe
walopiga kura nje ni
sita, kati yao wanne ndio
walikuwa Makkah (Barua
ya Ubalozi imethibitisha
kuwa kutokana na
ratiba kuwa ngumu sana
mahujaji hao hawajapiga
kura) na wawili wagonjwa.
1. A m i n a A n d r e a
Clement
2. Shawana Bukheti
Hassan
3. M a u w a A b e i d
Daftari
4. Mohammed Raza
Dharamsi

Na walopiga kura nje


ambao ni wagonjwa ni
watano. Salum Hassan
Turky (India) na wa sita
S a a d a M k u ya S a l u m
(Zanzibar) Tunaambiwa
kura mbili zilitakiwa
k wa g h a r a m a z o z o t e
wa l o l e n g wa m wa n z o
wazipige hizi kura ni
Zeudi Mavano (Chadema),
Maryam Salum Msabaha
(Chadema), Mwanamrisho
Abama (Chadema) na
Haji Ambar (NCCRMageuzi) ambaye
tayari ameshanukuliwa
na vyombo vya habari
akikanusha kupiga kura,
hizo kura mbili zilikuwa
zitokane na hawa lakini
hawa wote hawajapiga
kura. Sasa tuambiwe, jee
hao wawili wametoka
wapi na ni kina nani?
Kwa nini iwe siri wakati
kanuni zinasema wajumbe
watakaopiga kura nje
ya bunge watatajwa
majina yao na kura
zao zitafunguliwa pale
hadharani tuzione?
Lakini kwa nini mtandao
wa Bunge Maalum la Katiba
ambao uliandika matokeo
umefungwa haraka mno
kabla hatujamaliza kiu
yetu ya kujiridhisha juu
ya takwimu? Na kwa nini
kuwepo na kigugumizi
kwenye hizi takwimu?
Tu m e j i f u n z a m e n g i
katika bunge hili,
j i n s i Wa z a n z i b a r i
wanavyogawiwa na
kuona namna gani
demokrasia katika nchi
yetu inavyoendeshwa.
Nimalizie kwamba
ikiwa demokrasia ndio
i n a v o f a n ya k a z i v i l e
ilivyotokea Dodoma, basi
tuna safari ndefu kufikia
walipo wenzetu.
(Salma Said)

Mhe. Yahya Kassim Issa


kuonekana imelalia sana
upande wa Zanzibar, wapo
baadhi ya wawakilishi
na wabunge wa CCM
wa liok u wa wa k is e ma
potelea mbali wapoteze
majimbo yao lakini
wasiipoteze Zanzibar, na
walikuwa na hamasa ya
kutaka kuvikataa baadhi
ya vifungu vya rasimu
wakisema chama chao
kiliwapa muongozo wa
kuikataa sura ya kwanza
na ya sita tu lakini hakijatoa
muongozo katika sura na
ibara nyengine.
Sisi hatukupewa
muongozo wa hizi sura
n y e n g i n e , t u l i o p e wa
muongozo ni sura ya
kwanza na sura ya sita,
kwa hivyo kwa kuwa
rasimu hii haina maslahi
ya Zanzibar hatuwezi
kuvikubali baadhi ya
ibara lazima tuvikatae,
ingawa tunajua kwamba
tutapoteza nafasi zetu,
tunapoteza majimbo yetu,
lakini potelea mbali vizazi
vyetu vitakuja kuona
kwamba hatujachangia
kuizamisha Zanzibar,
walisema baadhi ya
wajumbe wa CCM.
Siku ya upigaji kura
baadhi ya wajumbe hao
walifurahi kutokana na
kauli ya Mheshimiwa
William Lukuvi ya kuwa
kila mmoja ana msimamo
wake wa kupiga kura ama
ya wazi au ya siri hivyo
wengi wao iliwapa fursa
ya kuamua watakavyo.
Lukuvi tayari
ameshasema kuwa
tutapiga kura tutakavyo,
mtu asiamuliwe, kila
mmoja achagua akitaka
kupiga kura ya wazi au ya
siri na nikisema Lukuvi
basi ujue huo ni msimamo
wa P M ( M h e s h i m i wa

Mheshimiwa William Lukuvi.


Waziri Mkuu Pinda) mimi
kura yangu nitapiga ya
siri si tumeshaambiwa
tupige kura tutakavyo,
aliniambia mjumbe mmoja
wa CCM.
Lakini muda mfupi
baada ya mjumbe huyo
kueleza kauli hiyo,
k i l i i t i s h wa k i k a o n a
kubadilishwa uamuzi huo
na ikaamuliwa kura iwe
moja tu na ni ya wazi. Hivyo
baadhi ya wajumbe hasa
kutoka Zanzibar na wale
wenye kudai Tanganyika,
wakashindwa kuonesha
misimamo yao hadharani
na wakalazimika kupiga
kura zao kwa wazi na
kukubaliana na maelezo
waliopewa.
Daaah mambo
yameshabadilika, sasa
tunatakiwa tupige kura
ya wazi lakini hii najua
ni mbinu makusudi ya
kututega lakini aaaah,
alisema mjumbe mmoja
wao aliyehiyari kukataa
baadhi ya ibara.
Mheshimiwa Salma hii
katiba inataka kupitishwa
lakini kwa ufupi haina
maslahi na Zanzibar
hata kidogo na afadhali
ile katiba ya 77 kuliko
hii maana katiba hii
itakwenda kuiathiri katiba
yetu ya Zanzibar kwa kiasi
kikubwa, nyinyi bwana
ikataeni kwani tunaamini
nyinyi ndio wakombozi
wetu, sisi tupo nyuma
yenu Inshallah maana
unajua tena sisi mazingira
yetu, alisema mjumbe
ambaye ni Waziri ila sitaki
kusema anatoka wizara
gani na katika serikali
gani.
Binafsi namheshimu
sana kutokana na taaluma
yake ambayo sina shaka
hata chembe na uzalendo

wa k e n a n d i o m a a n a
alithubutu kunikabili
n a k u n i e l e z a wa k a t i
wenzake wakiniona kama
n i a d u i wa o , i n g a wa
baadhi wanamlaumu kwa
nini na yeye asichukue
uamuzi mgumu? Wengi
hawajamfahamu lakini
mimi nimemfahamu sana
kutokana na uamuzi wake
huo.
Natamani nivute
kumbumbuku pale dakika
chache kabla ya kura ya
HAPANA siku ya kwanza
ambayo alianza kupiga
Adil Mohammed Ali
akifuatiwa na Dk. Alley
Soud, akaja Ali Omar,
Fatma Mohammed na Bi
Jamila Abeid na baadae
mimi na hatimae kura
ya mwisho ambaye
ikitarajiwa kupigwa na
Mwanaidi Othman lakini
muda mfupi aliondoka
na kwenda chooni
akitujulisha kwa simu
ya m k o n o n i k wa m b a
Siwezi kupiga kura ya
wazi nitapiga kura ya siri
na kisha aliondoka katika
sehemu ambayo alikuwa
amekaa na kwenda kukaa
kwenye kiti akiwekwa
kati kati upande mmoja
akiwa ameketi Mwana na
upande mwengine akiwa
ameketi Mahmoud Thabit
Kombo.
Lakini mwisho alipiga
kura ya wazi na kusema
HAPANA na baada ya
kura 7 za hapana hapana
zilivyoanza kujipanga
kura ya mwisho namna
ilivyopatikana katika
tundu ya shindano kwa
mikiki, vitisho, dharau,
khofu, kulazimishwa na
kutekwa nyara na matusi
ya nguoni lakini pamoja
na yote hayo kura saba
zilipiga HAPANA na
ndio mwisho wa mchezo.
(Salma Said)

15

Makala

Mwaka wa Zanzibar kuraruliwa


vipande vipande umeingia tena

AN-NUUR

RABIUL THANI 1436, IJUMAA FEBRUARI 6 - 12, 2015

Wahafidhina washatoa ilani ya hatari

Na Ally Saleh
N I M E WA H I k u s e m a
kuwa kuna haja kubwa
ya kutumika busara ili
Kura ya Maoni isifanyike
kabisa mwaka huu na
niliungana na wale
waliokuwa na fikra kama
hiyo, hadi pale wenzangu
walipobadilika.
Walibadilika kwa sababu
walikuwa na lengo la
kisiasa. Walichukulia
fursa ya kufanyika Kura
ya Maoni na ushindi
utaopatikana kama ikipita
ni sawa na kukifyagilia
njia Chama cha
Mapinduzi kwa ushindi
wa Uchaguzi Mkuu kote
Bara na Zanzibar.
Hoja yangu wakati huo
ilikuwa ni kuwa Kura ya
Maoni kwa hadhi zote ni
sawa na Uchaguzi Mkuu
maana huwa na kipindi
cha elimu ya mpiga kura,
kisha huwepo na kampeni
na kuwepo pande
zinazopingana katika
hicho kinachopigiwa kura
na kwa hili la katiba, ni
dhahiri kutakuwa na kazi
kubwa. Kazi kubwa maana
yake pande zinazotaka
katiba ipite na isipite zote
zimeshanowa visu kwa
ushindani mkali na bila ya
shaka kutapelekea kuwepo
mvutano, uhasama na
pengine hata magomvi
ambayo huambatana na
uchaguzi katika mazingira
yetu ya Kiafrika zaidi.
Wasiwasi wangu ni
kuwa kunaweza kukawa
na chaguzi nne katika nchi
kwa mwaka mmoja kwa
maana ya Kura ya Maoni
ya April 30 na iwapo
itarudiwa kwa kupigwa
H A PA N A m a r a y a
kwanza. Kisha kufuatiwa
na Kura ya Maoni ya
Wazanzibari kupitisha
hiyo Katiba Pendekezwa
na mabadiliko yake kwa
Katiba ya Zanzibar ya 1984
na kisha Uchaguzi Mkuu
wa 2015 mwezi Oktoba.
Naionea huruma sana
Zanzibar yangu ambayo
itakuwa na chaguzi zote

hizo wakati tunajua mara


nyingi chaguzi huirarua
Zanzibar vipande vipande
na tumeanza kupata
afueni hivi karibuni tu
kwa kuundwa Serikali
ya Pa m o j a b a a d a ya
mabadiliko ya Katiba ya
Zanzibar ya 2010. Na hali
imeshaanza kujitokeza
kutaka kuvunja Serikali
ya Umoja wa Kitaifa kiasi
ambacho inawezekana
kabisa wakati tukifanya
mabadiliko ya Katiba
Pendekezwa kwa mnasaba
wa Katiba ya Zanzibar,
kukawa na shindikizo
pia la kuvibadilisha
vifungu vya Serikali ya
Umoja wa Kitaifa jambo
a m b a l o wa h a f i d h i n a
ndani ya CCM wamekuwa
wakilisema jahara.
Uwepo wa Kura ya
Maoni ni jambo la kisheria
na kwa kweli ni hatua
ya lazima kupata Katiba
Mpya. Lakini si jambo la
kufa na kupona kwamba
lazima lifanywe kwa tarehe
maalum au muda lazima
uwe sasa na ndio maana
Rais Kikwete alikuwa
amekubaliana na vyama
vya siasa vilivyo chini ya
mwamvuli wa Tanzania
Democracy Council (TCD).
Na kwa kweli hicho ndicho
ambacho sasa kimejitokeza
kwamba nchi, yaani taasisi
husika na Serikali yenyewe
hazijakuwa tayari kwa
Kura ya Maoni. Kama leo
ni Februari tayari hakuna
muda wa kutosha wa
maandalizi kuanzia ya
uandikishaji wapiga kura
kwa njia ya eltroniki yaaani
BVR lakini pia mipango
mengine inayoambatana
na kura hiyo.
Muda huu ulikuwa ndio
muafaka wa kuwa na suali
la kuulizwa kwenye kura
hiyo, makundi yanayotaka
kuwa wapiga kampeni
ya HAPANA na NDIO
yawe tayari yanaelekea
kujiandikisha na pia
tuone harakati za elimu
ya wapiga kura zikianza
kuwekwa bayana na Tume
ya Uchaguzi. Hakuna

lolote linalofanyika
la kuutia umma imani
kuwa kweli kuna mambo
yanayotoka au pengine ni
kwa sababu ya usiri? Jee
umma unaweza kuwekwa
nje ya kujua jambo hili kwa
kiasi chote hiki?
Kwa sababu hizo basi,
ndio kukaanza kuzuka
kundi jengine kabisa, na
khasa Umoja wa Katiba ya
Wananchi UKAWA ambao
umekuja na mpya kuwa
wao wanasusia kabisa
mchakato kupita Kura ya
Maoni kwa sasa sababu
k u wa h a k i t a p a t i k a n a
kilichokusudiwa. Wao
wanaona, hasa kwa vile
waliukimbia mchakato
huo katika Bunge Maalum
la Katiba, kuwa hapana
liwalo na Kura ya Maoni
haina tija kwa aina ya
k a t i b a i n a y o p e l e k wa
k wa wa n a n c h i ya a n i
i l e i n a y o i t wa K a t i b a
Pendekezwa ambayo ni
shikilia la Rais Kikwete
na Chama cha Mapinduzi.
Pili, wanaona ni haramu
kitu ambacho walikikataa
katika utengejezaji wake
kisha warudi wakipigie
kura kukihalalisha.
Wanasema hiyo abadan
na tayari wamewataka
wanachama wao na
wanachi wasusie kura
hiyo. Taasisi nyengine
pia kama Kituo cha Haki
za Binadamu (HRLC)
wa m e t o k a wa z i wa z i
wakisema katiba hiyo
haifai kupigiwa kura ya
kuungwa mkono ingawa
wao wanataka wananchi
wakapige kura na waikatae
Katiba Pendekezwa.
Mimi kama Mzanzibari
nataka nijihusishe zaidi
na ubaya wa Sheria ya
Kura ya Maoni ambayo
ndio inayoongoza taratibu
nzima za kura hiyo na
a mb a y o i n a madh a r a
makubwa kwa Zanzibar.
Kwa mujibu wa Kifungu
cha 34 cha Sheria hiyo, kura
za upande wa Zanzbar,
ambapo kila upande ili
kura zipige itahesabiwa
kwa zaidi ya asilimia

RAIS Jakaya Mrisho Kikwete

hamsini, zinaweza kuwa


na mashakil makubwa.
Sheria hiyo inasema
kura za Zanzibar
zitatoka sehemu
tatu. Kwanza wapiga
kura waliondikishwa
na ZEC yaani Tume
ya Uchaguzi wa
Zanzibar, na hilo halina
mashaka na orodha
yake tunaijua, japo ina
mivutanovutano.
P i l i wa p i g a k u r a
pia watakuwa ni watu
walioandikishwa na
Tume ya Uchaguzi ya
Tanzania NEC ambao
wanaishi Zanzibar na
hapa wengi tutajiuliza
juu ya uhalali wa
Wa t a n z a n i a h a w a
kupiga kura kwa kapu
la Zanzibar na kama
Wapemba wanavyosema
vyereje?
Lakini kali zaidi
ni kifungu hicho
k u s e m a k u wa k u r a
za kapu la Zanzibar
pia zitahesabiwa kwa
Wazanzibari ambao
wa n a o s h i Ta n z a n i a
Bara na ambao
wameandikishwa

kwenye daftari la NEC.


Hapa mtu unajiuliza
ilikuwaje mpaka yafike
yote haya wakati hivi
sasa Wazanzibari hao
hao wananyimwa fursa
ya kupiga kura kwao
na hata wale walioko
kwao wanakataliwa kwa
sababu ya ukaazi?
Basi katika sakata
lote la Kura ya Maoni
hili ndilo ambalo mimi
linaniuma zaidi. Ya
nini hadaa na janja
yote hii ya kuwanyima
Wa z a n z i b a r i s a u t i
yao ya kuamua? Hivi
ndio maana wakubwa
wakawa na hakika kuwa
kura itapita tu vyovyote
iwavyo?
Na kwa kweli
itapita kama sheria
imeelekeza kama hivyo.
Na kwa sababu hiyo,
naungana na wale wote
wanaosema kuwa njia
mbadala ni kususia kura
hiyo na kama ikipita
dunia ijue kuwa sauti ya
umma imesokotwa na
maamuzi ya kura hiyo
ni ya hadaa na kijanja.
(Ally Saleh +255 777

16

Makala

AN-NUUR

RABIUL THANI 1436, IJUMAA FEBRUARI 6 - 12, 2015

TAMKO LA TAASISI 11 ZA KIISLAMU KWENYE MAENEO AMBAYO YAMEPOTOSHWA NA MATAMKO YA


BAADHI YA TAASISI ZA KIDINI NA MAGAZETI IKIWEMO MAASKOFU, BAKWATA NA GAZETI LA MIZANI
KWENYE MCHAKATO WA KUTOA MAONI JUU YA MUSWADA UNAOHUSU MAHAKAMA YA KADHI
Utangulizi
SISI Waislamu, kupitia Jumuiya
na Taasisi zetu za Kiislamu nchini,
tumepitia matamko kadhaa
yaliyotolewa na taasisi mbalimbali,
watu binafsi, viongozi wa serikali
na magezeti, hususan, maaskofu,
Jukwaa la Wakristo Tanzania, gazeti
la Mizani, Sheikh Jongo na Sheikh
Mohammed Idd kupitia kipindi cha
Ar-risala kinachorushwa na Kituo
cha TV cha Channel 10.
Matamko hayo yana malengo
ya kupotosha baadhi ya maeneo ya
maoni yaliyotolewa na Waislamu,
kupitia Jumuiya na Taasisi zao
kuhusu muswada wa marekebisho
ya sheria yanayohusu Mahakama ya
Kadhi kwenye Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala
tarehe 19/01/2015.
Muhtasari wa Maoni ya Taasisi
Kumi na moja
Kwa muhtasari maoni ya
Wa i s l a m u a m b a y o m a t a m k o
tuliyoyataja hapo juu yanalenga
kuyapotosha yalibainisha makosa,
kasoro na udhaifu mwingi ulioko
k w e n y e m u s wa d a u n a o h u s u
Mahakama ya Kadhi kiasi cha kutia
shaka juu ya uthabiti wa nia ya
Serikali wa kutaka kuleta sheria
itakayowezesha mfumo wa utoaji
haki wa sheria za Kiislamu kufanya
kazi hapa nchini kwa ufanisi zaidi
kulio mfumo wa sasa unatoa nafasi
kwa watendaji wa mahakama kama
majaji na mahakimu kuhukumu
masuala ya sheria za Kiislamu
ambapo mara nyingi maafisa hao
hawana sifa, ujuzi, maarifa na uzoefu
wa kushika nafasi ya kuhukumu
chini ya utaratibu wa sheria za
kiislamu.
Maoni hayo, ya Waislamu, kupitia
jumuiya na taasisi zao kumi na
moja, yalidhihirisha dosari kubwa
kwenye muswada huo kwenye
maeneo yanayohusu, kutokuwepo
kwa kifungu kinacho anzisha
na/au kuitambua mahakama ya
kadhi; kutokuwepo muundo wa
Mahakama ya Kadhi inayokusudiwa;
kutoelezwa sifa za kadhi; upungufu
kwenye utaratibu wa uteuzi wa
makadhi; kukosekana maelezo
ya ajira na usalama wa ajira ya
makadhi; upungufu unaoambatana
na kuweka mamlaka ya kutengeneza
kanuni za mahakama ya kadhi kwa
Mufti na ya kukazia hukumu kwa
Waziri; kukosekana kwa utaratibu
wa kudhibiti nidhamu, mwenendo
na maadili ya makadhi; upungufu
kwenye uwigo wa mamlaka wa
mahakama; hiyari kwa mdaawa
Muislamu kufungua shauri lake la
sheria ya Kiislamu katika Mahakama
ya Kadhi; upungufu wa dhana ya
Mahakama ya Kadhi kujiendesha;
mamlaka ya Waziri kutoa matamko
ya sheria za Kiislamu; na ulazima
wa Mahakama ya Kadhi kutajwa
kwenye Katiba.
Kwa hoja hizo, Waislamu kupitia

taasisi zao hizo kumi na moja,


walishauri kwa kupendekeza
muswada mbadala kwamba serikali
iuondoe muswada huo ili uboreshwe
kabla ya kuwasilishwa bungeni kwa
ajili ya mjadala.
Upotoshaji Uliofanywa na Matamko
Yaliyotolewa
U p o t o s h wa j i wa m a o n i ya
Waislamu yaliyotolewa kupitia
taasisi zao kumi na moja, uliofanywa
na matamko yaliyotolewa na taasisi
mbalimbali, watu binafsi, viongozi
wa serikali na magezeti, umejikita
kwenye maeneo haya ya fuatayo: (i)
Kuwa taasisi 11 zilizowasilisha maoni
ya Waislamu juu ya muswada wa
Mahakama ya Kadhi zinawakilisha
wachache; (ii) Kuwa asasi hizo 11
ni za Wahabi na hivyo maoni yao
hayawakilishi Waislamu wote; (iii)
Kuwa Mufti ndiye kiongozi mkuu
wa Waislamu; (iv) Kuwa Mufti
ndiye anastahiki kuteua makadhi;
(v) Kuwa BAKWATA ndiyo taasisi
baba, nyingine watoto wake; na
(vi) Kuwa Mahakama ya Kadhi
italeta hukumu za kukata mikono,
kuhukumu wasio kuwa Waislamu,
na kubagua wasio kuwa Waislamu.
M a t a m k o a m b a y o ya m e b e b a
upotoshaji huu yametolewa kwa
makusudi kwa lengo la hadaa kwa
Waislamu, wananchi na serikali kwa
jumla ili wasitilie maanani maoni
yaliyotolewa na taasisi hizo kumi na
moja ambayo kama yatafanyiwa kazi
na Serikali yatawezesha kupatikana
kwa Mahakama ya Kadhi inayokidhi
matakwa ya sheria za Kiislamu na
wajibu wake kama mamlaka ya
kutoa na kutenda haki.
Tamko Letu Dhidi ya Upotoshaji
Uliotolewa
Hivyo basi, kwa lengo la kuweka
sahihi kumbukumbu na kuondosha
uwezekano wa upotoshaji huu
kuchukuliwa kuwa ni kweli, ni
vyema tukabainisha ukweli kama
ifuatavyo:
1. Jumla ya taasisi kumi na
moja (11) ziliwasilisha maoni ya
Waislamu juu ya muswada wa
Mahakama ya Kadhi. Hizi ni pamoja
na taasisi ambazo zinatambulika,
zimesajiliwa na zenye uwakilishi
na mtandao wa kitaifa. Baadhi ya
taasisi hizo ni Baraza Kuu, TAMPRO,
BASUTA, JASUTA, IPC, HAIYAT
ULAMAA, Umoja wa Jumuiya na
Taasisi za Kiislamu Tanzania; na
Shura ya Maimam Tanzania. Maoni
juu ya muswada wa Mahakama
ya Kadhi yalipatikana baada ya
mchakato uliohusisha wanachama na
wawakilishi wa asasi hizo Tanzania
nzima. Hivyo, siyo kweli kuwa asasi
hizi kumi na moja (11) zinawakilisha
maoni ya wachache. Ni wazi pia
kuwa upotoshaji huu unadhihirisha
kuwa waliotoa kauli za upotoshaji
huu wanaona uzito wa umoja huu
wa asasi za Kiislamu na maoni yao
kweye suala hili la Mahakama ya
Kadhi.
Hawa wanaosema taasisi hizi
zinawakilisha maoni ya wachache
na ya wahabi, hawatuambii kuwa

maoni yao yanawakilisha taasisi


ngapi za Kiislamu na ya madhehebu
yepi. Ukweli ni kwamba hoja hii
inadhihirisha hofu ya mshikamano
wa asasi za Kiislamu katika kuliendea
suala hili la Mahakama ya Kadhi.
Ndiyo maana badala ya kujibu hoja
na mapendekezo yaliyotolewa na
asasi hizi, matamko hayo yamejikita
kwenye kushambulia taasisi husika
kwa hoja ambazo zina misingi ya
kuwagawa Waislamu.
2. Madai kuwa Mufti ndiye
kiongozi mkuu wa Waislamu hapa
Tanzania na kwamba ndiye anaye
stahili kuteua makadhi nchini siyo
sahihi. Inawezekana kwa taasisi
kuwa na muundo wa uongozi
ambao unamfanya Mufti kuwa
kiongozi mkuu wa Waislamu wa
taasisi hiyo na hapa huyo Mufti
atakuwa mkuu wa taasisi husika na
siyo Waislamu wote wa Tanzania.
Mfano wa taasisi ambazo kiongozi
wake mkuu ni Mufti ni BAKWATA.
Hii haina maana kuwa kiongozi
huyo ndiye kiongozi wa Waislamu
wote nchi nzima. Tulieleza kwenye
kamati ya Bunge kama tunavyoeleza
hapa kuwa zipo taasisi nyingi
za Kiislamu zilizoandikishwa na
mamlaka mbalimbali za uandikishaji
wa asasi huru na vyama vya kijamii
(NGOs) zenye viongozi wenye cheo
cha Mufti. Kwa hivyo, siyo vyema
sheria kuweka mamlaka yoyote
inayohusu Mahakama ya Kadhi
(mfano uteuzi wa makadhi) kwa
Mufti wa taasisi binafsi kwa kuwa
kunaweza kukatokea mgongano na
mgogoro mkubwa kwa kila asasi
kutaka kutumia mufti wake kuteua
makadhi.
3. Madai haya kwamba Mufti
ndiye kiongozi mkuu wa Waislamu
na anaye stahili kuteua makadhi
yanalenga kupotosha hoja ya msingi
kwamba siyo sahihi kwa sheria
kumpa Mufti mamlaka yeyote
yahayohusu Mahakama ya Kadhi
kwa kuwa mufti huyu, ama wa
BAKWATA au wa taasisi nyingine
yeyote, siyo chombo kinachoundwa
na sheria yoyote (bali katiba ya
taasis husika) na wala hakuna sheria
inayounda ofisi ya Mufti. Mahakama
ya Kadhi kuwekwa chini ya Mufti
ni kuifanya mamlaka hiyo muhimu
ya kutoa haki kuwa chombo kilicho
chini ya Taasisi binafsi, jambo ambalo
ni kinyume cha sheria. Kwa mfano,
siyo kila Muislamu wa Tanzania Bara
ni mwanachama wa BAKWATA na
yuko chini ya Mufti wa BAKWATA.
Ibara ya 20 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania inatoa uhuru
wa kujumuika na kujiunga katika
jumuiya mbalimbali. Kuwalazimisha
Waislamu wawe chini ya Mufti
wa BAKWATA au Mufti wa taasisi
nyingine yeyote ni kuvunja Katiba
ya nchi. Hivyo basi si sahihi mamlaka
ya kutoa haki kuhusishwa na MUFTI
anayetokana na Katiba ya Taasisi
binafsi.
4. Kama tulivyokwisha eleza

kwenye maoni yetu tuliyowasilisha


kwenye kamati ya Bunge juu ya
muswada wa mahakama ya kadhi,
kwa istilahi ya Kiislamu Mufti
maana yake ni alim (msomi) mwenye
upeo mkubwa wa elimu ya dini na
sheria. Ni mtu aliyebobea katika
taaluma za dini na sheria. Si afisa
wa Serikali wala hana dhima ya
utawala au uongozi. Mwanachuoni
h u t a m b u l i wa k u wa M u f t i n a
maulamaa wenzake wa eneo husika
kwa kutambua upeo wake mkubwa
katika fani za elimu ya dini na sheria.
Alim akitambuliwa na kupewa hadhi
ya mufti huchukuliwa kuwa ni
marejeo kwa ajili ya kutolea ufafanuzi
masuala ya elimu ya dini na sheria.
Kwa hiyo Mufti jukumu lake ni
kufutu masala ya dini na sheria.
Si kuwa mtawala au mpangaji wa
masuala ya utawala. Ni dhahiri kuwa
madai yaliyotolewa kuwa Mufti ndiye
kiongozi Mkuu wa Waislamu hayana
mashiko kilugha wala kiistilahi.
5. Hatuamini hata kidogo
kuwa wanaotoa madai haya na
upotoshaji huu hawajui nafasi ya
Mufti katika mfumo wa sheria za
Kiislamu na kilugha. Tunashawishika
kuamini kuwa wanafahamu ukweli
kama tulivyouweka hapo juu, bali
wanapotosha kwa malengo mahsusi
kwa sababu baadhi yao ni wasomi
wenye shahada mpaka shahada za
juu katika fani mbalimbali za dini ya
Kiislamu.
6. Madai kuwa BAKWATA
ndiyo taasisi baba na taasisi
nyingine ni watoto wake, hayana
m a s h i k o ye y o t e n d i y o m a a n a
hata Kamati ya Bunge haikutoa
mualiko kwa BAKWATA pekee,
bali kwa taasisi nyingi za Kiislamu
ikiwemo BAKWATA. Ifahamike
kuwa BAKWATA ni taasisi ya kidini
kama zilivyo taasisi nyingine, lakini
pia BAKWATA ni taasisi dhaifu na
iliyopoteza imani kwa Waislamu
wengi nchini. Jina la taasisi hiyo
haliifanyi taasisi hiyo kuwa ndiyo
kubwa na yenye hadhi kuliko taasisi
zingine za Kiislamu. Hata hivyo,
kimuundo na kiuwakilishi, taasisi
hii haina sifa ya kuwa ni taasisi
kubwa na yenye mamlaka dhidi ya
taasisi nyingine za Kiislamu kwa
sababu zifuatazo;(i) BAKWATA haina
wanachama tofauti na taasisi zingine
ambazo zina wanachama; (ii) Mara
kadhaa BAKWATA imetoa matamko
kuwa haiwakilishi Waislamu wote wa
Tanzania; (iii) Asili yake BAKWATA
haijaundwa na Waislamu kwa
umoja wao. Ndiyo maana uhalali wa
BAKWATA kuwa ndicho chombo
kikuu cha uongozi wa Waislamu
nchini umehojiwa na Waislamu mara
nyingi.
7. Kama tulivyoeleza kwenye
maoni yetu juu ya muswada wa
Mahakama ya Kadhi, tunarudia
kusema tena kuwa iwapo
Serikali itafuata upotoshaji huo
kuwa BAKWATA ndiyo chombo

Inaendelea Uk. 17

17

Makala

AN-NUUR

RABIUL THANI 1436, IJUMAA FEBRUARI 6 - 12, 2015

Kwa nini kila mahala ngoma, tunaficha nini?

Na Mohammed Ghassani

I J U M A A ya l e o , R a i s
Joachim Gauck wa
Ujerumani na ujumbe
wake wanaondoka kurejea
kwao baada ya kuwepo
ndani ya ardhi ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania
tangu usiku wa Jumatatu,
tarehe 2 Februari.
Pale uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Mwalimu Julius
Nyerere, Dar es Salaam,
ujumbe huo ulipokelewa
kwa matarumbeta na ngoma
nyengine za kienyeji. Siku
ya pili yake alipokelewa
rasmi na mwenyeji wake,
Rais Jakaya Kikwete kwenye
Ikulu ya Magogoni, ambako
mbali ya matarumbeta ya
bendi ya jeshi, gwaride na
mizinga 21 kwa heshima
ya kiongozi wa nchi,
uwanja mzima wa Ikulu
hiyo ulitanda matarumbeta
mengine.
Wa k a t i m k e w e R a i s
Gauck, Bi Daniela Gauck,
alipotembelea kituo cha tiba
cha CCBRT kilicho kando
kidogo ya kitovu cha jiji la
Dar es Salaam, wagonjwa
wa fistula wanaotibiwa
huko walikuwa na muda
pia wa kumuimbia nyimbo
mwanamke mwenzao huyo,
wakisema Sisi ni tegemeo la
akinababa, sisi ni tegemeo la
watoto. Sisi ni tegemeo.
Usiku wa tarehe 3
Februari, Rais Kikwete na
mkewe, Bi Salma Kikwete,
waliwakaribisha tena
wageni wao Ikulu kwenye
chakula cha jioni. Ndani ya
ukumbi muliporomoshwa
muziki mkali wa bendi ya
polisi. Wakati wageni hao
wanaondoka kurudi hotelini
kwao saa 4:00 usiku, nje
kulikuwa na vikundi vya
ngoma za kienyeji kuwaaga.
Wa k a t i wa n a o n d o k a
siku ya Jumatano kuelekea
Zanzibar kwa boti ya Azam
Marine, bandarini palikuwa
n a b e n d i n ye n g i n e ya
matarumbeta ikitumbuiza
kwa zogo na shangwe.
Wi m b o K i t o r o r o wa
msanii nyota wa Tanzania,
Naseeb Abdul, maarufu
kama Diamond Platinumz.
Zanzibar na Arusha
nako hali haikuwa tafauti.
Kulikuwa na ngoma wakati
wa kuwasili na ngoma
wakati wa kuondoka. Kwa
makisio tu, hadi Rais Gauck
n a w e n z a k e wa n a r u d i
Ujerumani, baada ya kuwepo
Tanzania kwa siku zisizozidi
tano, tayari walishapigiwa
ngoma zaidi ya mara saba.
Wa l a u j u m b e wa
Rais Gauck si pekee
unaokumbana na ukarimu
huu wa kukatikiwa mauno.
Ni utamaduni mkongwe
ambao sasa unahitaji
kuhojiwa kwa sababu sio tu
unaudhi, bali pia unabeba
maana kadhaa zisizosema
uhalisia ulivyo.

Rais Joachim Gauck wa Ujerumani na ujumbe wake wakiondoka kurejea kwao baada
ya kuwepo nchini. Hapa wakiwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu
Julius Nyerere, Dar es Salaam ambapo ujumbe huo ulipokelewa kwa matarumbeta
na ngoma nyengine za kienyeji.
Kitamaduni na kijamii,
nafahamu kwamba
kwetu Waafrika ngoma
si kielelezo cha mikatiko
na minyumbuliko ya miili
yetu tu, bali pia njia ya
mawasiliano. Hata hivyo,
ninaamini kuwa nyuma ya
ngoma zinazotayarishwa,
kulipiwa na kushajiishwa
na dola kuchezwa mbele ya
wageni kutoka nje, ujumbe
unaotumwa una maana
mbaya sana.
Chukulia mfano huu
halisi. Dhamira ya ziara ya
Rais Gauck nchini Tanzania
ilikuwa na dhamira mbili
kuu: moja ya kisiasa na
nyengine ya kiuchumi.
Sikiliza hotuba yake, angalia
maeneo waliyoyatembelea,
u t a j u a k u wa wa l i k u wa
wamekuja kwa lengo
maalum na lenye uzito wa
aina yake. Mikutano ya
wafanyabiashara wa pande
mbili iliyoangalia fursa za
uwekezaji, mazungumzo na
asasi za kijamii, waandishi
wa habari, wanasiasa na
wanasheria. Ujumbe huu
una ujumbe ndani yake.
Ongeza ukweli mmoja
mchungu sana pia.
Ujerumani ilikuwa mkoloni
wa Ta n g a n y i k a n a i n a
historia refu inayorudi
nyuma kwenye majilio ya
wakoloni kwenye ardhi hii
yenye wingi wa rasilimali
tangu mwishoni mwa
karne ya 19 kupitia wale
waitwao wavumbuzi na
wamishionari. Miongoni
mwa upotoshaji uliomo
kwenye historia ya
kimapokezi ni kwamba
wahenga wa Kitanganyika
waliweza kudanganywa
na wavumbuzi akina
Karl Peters wa Ujerumani
wakawapa ardhi na
rasilimali zao kwa shanga
n a s i g a r a , wa k a t i wa o
wakicheza ngoma na
kufanya matambiko.
Si lazima upotoshaji huu
uwe na ukweli wa asilimia

mia moja, hasa ikikumbukwa


kuwa baadaye wazee wa
Kitanganyika, wakiwemo
Chifu Mkwawa na Bushiri,
wa l i wa o n g o z a we n z a o
kupambana na Mjerumani
kwenye vita vya silaha na
umwagaji damu kupigania
ardhi zao na kupinga
kutawaliwa.
Hivi leo, karne nzima
baadaye, Tanganyika na
Z a n z i b a r ( s a s a z i k i wa
s e h e m u ya J a m h u r i ya
Muungano wa Tanzania)
ni huru na zina watawala

wake wazawa. Njia kuu


za uchumi na mifumo ya
kisiasa imo mikononi mwao
wenyewe, angalau kwa
maana nyepesi. Bado, hata
hivyo, nchi hii ni miongoni
mwa mataifa masikini sana
duniani, ambayo pato la raia
wengi ni chini ya dola moja
kwa siku.
Kuna hadithi rasmi ya
serikali ambayo wawekezaji
kutoka nje husimuliwa na
wao wakaisimulia kwa
wengine, kwamba ukuwaji
wa uchumi ni zaidi ya

asilimia 7 kwa mwaka. Lakini


pia kuna hadithi ya kisasa
ya deni la serikali kupanda
katika kiwango kinachotishia
kutokopesheka. Kuna
hadithi ya machungu ya
ukuwaji huo unaoongeza
idadi ya wengi wasionacho
kabisa na wengi walionacho
cha kupitiliza.
Miongoni mwa hao
wengi wasionacho kabisa,
ndio wanaoonekana mbele
ya wageni wa kimataifa
wakikatika mabuno na
kuruka wakitua chini. Ndio
wanaopiga matarumbeta
na kuimba Kitorondo,
mwendawazimu kaingiaje!
Tukiri. Tuna tatizo. Na
kama hatukujihoji, hakuna
atakayetuchukulia kwa
umakini, licha ya utajiri
tulionao. Tutakuwa watu
wa kupiga ngoma kama
fursa pekee tuliyonayo
mbele ya wageni, maana
ni huko ambako hawawezi
kushindana nasi. Lakini
tukienda mbele ya meza ya
mazungumzo na mikataba
ya kibiashara na uwekezaji,
tunaangushwa chini.
Hapo ndipo uwekezaji
unapogeuka ukwapuaji
wa rasilimali, si kwa kuwa
wageni ni wana dhati ya
wizi, bali kwa kuwa ni
wafanyabiashara wazuri
wanaojua kutengeneza faida,
nasi ni wachezaji wazuri wa
ngoma tunaojua kukatika
mabuno.

TAMKO LA TAASISI 11 ZA KIISLAMU

Inatoka Uk. 16
kikuu kinachowakilisha

Waislamu wote na hivyo


kuipa BAKWATA nafasi
ya kuwawekea Waislamu
Mahakama ya Kadhi,
itahesabiwa na Waislamu
kuwa ni hila ya Serikali
kutaka kulazimisha
mamlaka ya BAKWATA
juu ya Waislamu hata
wale wasioikubali taasisi
hiyo. Jambo ambalo
litakuwa limekiuka
haki ya msingi ya kila
Mtanzania kujumuika
kwa uhuru bila kutezwa
nguvu au kushinikizwa.
Inasikitisha kwamba,
wa k a t i m c h a k a t o wa
maoni juu ya muswada
wa Mahakama ya Kadhi
unaendelea, baadhi ya
v i o n g o z i wa j u u wa
serikali wametoa kauli
ambazo zinaoana na hoja
dhaifu kuwa BAKWATA
ndicho chombo cha
uwakilishi cha Waislamu
na kwamba serikali
imeuandaa mchakato wa
Mahakama ya Kadhi kwa
kuishirikisha BAKWATA
kwa karibu kama

chombo kinachowakilisha
Waislamu wote. Hili ni
kosa kubwa kwa kuwa
BAKWATA siyo chombo
cha Waislamu wote nchini.
8. K u n a m a t a m k o
yametolewa na taasisi
na watu binafsi ambao
wa n a t u m i a m u s wa d a
huu wa Mahakama
ya K a d h i k u l e t a h o j a
zinazokusudia kuleta
faraka za kimadhehebu
kwa propaganda ambazo
hazina msingi au ukweli
wowote katika dini ya
Kiislamu hasa suala la
kupinga Mufti kuwa ndiye
mteuzi wa makadhi na
utengenezaji wa kanuni
za Mahakama ya Kadhi.
Tunaotoa udhaifu wa
kumpa madaraka hayo
Mufti tumezingatia
hoja za kisheria, kidini
na kimantiki. Hivyo si
kweli kuwa tunapinga
Mufti kupewa madaraka
hayo kutokana na tofauti
za madhehebu ndani ya
Uislamu. .
9. Kadhalika, wapo
viongozi wa dini ambao
s i Wa i s l a m u ( m f a n o
maaskofu) wametoa
m a t a m k o ya k u p i n g a

M a h a k a m a ya K a d h i
kwa hoja kuwa italeta
hukumu za kukata
mikono, kuhukumu wasio
kuwa Waislamu, kubagua
wasio kuwa Waislamu
nk. Hoja hizo zote siyo
za kweli na watoaji wa
hoja hizo wanajua ukweli
k u wa M a h a k a m a ya
Kadhi inayokusudiwa ni
mahakama itakayotumia
sheria za Kiislamu ambazo
zinatumika kwenye
mahakama za kawaida
toka enzi za ukoloni
mpaka leo. Inajulikana
wazi kuwa Mahakama
ya Kadhi itas hughulika
na mambo binafsi ya watu
kwa mujibu wa sheria za
Kiislamu ambazo ni sehemu
ya sheria halali zinazotumika
hapa nchini, mfano mambo
kama ndoa, talaka, mirathi,
wakfu na malezi ya watoto.
Kinachofanywa na viongozi
hao wa dini wasiokuwa
Waislamu ni kuivunjia
heshima jamii ya Kiislamu
na kupotosha ukweli ambao
uko wazi.
Sheikh Abdallah A.
Bawazir
Makamu Mwenyekiti
wa Hay Atul -Ulamaa
03/02/2015

18
Na Shaban Rajab
HIVI karibuni vyombo
mbalimbali vya habari
duniani vilitangaza tukio
la kukamatwa kamanda
wa kikundi cha waasi cha
Uganda cha Lord Resistance
Army (LRA), Bw. Dominic
Ongwen. Hata hivyo
taarifa zimesema kuwa
hivi karibuni Bw. Ongwen,
alijisalimisha mwenyewe
kwa vikosi maalum vya
majeshi ya Umoja wa Afrika
vinavyosimamia amani
Jamhuri ya Afrika ya Kati
Januari 17 na Jumamosi,
alikabidhiwa kwa
Mahakama ya Kimataifa
ya Jinai za Kivita The
Hague, kwa ajili ya kusubiri
mashitaka dhidi yake.
Dominic Ongwen,
ameelezwa kuwa alikuwa
msaidizi wa Bw. Joseph
Kony, Kamanda Mkuu wa
kundi la waasi la Kikristo
linaopigania serikali
inayosimamia amri kumi za
Biblia (LRA) nchini Uganda.
Imefahamika kuwa baada
ya kujisalimisha, Bw. Ongwen
alidai aliamua kufanya hivyo
baada ya bosi wake Bw.
Kony, kubaini kuwa alikuwa
na nia ya kujisalimisha kwa
serikali ya Uganda, ambayo
awali ilitangaza msamaha
kwa wanachama wa LRA
watakaojisalimisha kwa
hiari.
Vyombo vya habari vilidai
kuwa alifanya hivyo baada ya
wapiganaji watiifu wa Kony,
kumweka chini ya ulinzi
huku wakimtesa ili abadili
nia yake ya kujisalimisha na
kwamba, iwapo angeendelea
na msimamo wake huo basi
angeuliwa.
Aidha alinukuliwa
akisema kuwa hata yeye
aliingia katika himaya ya
Kony baada ya kutekwa
akiwa mtoto ndogo.
O
n
g
w e
n
a m e s h a k a b i d h i wa T h e
Hague akisubiri kukabiliwa
na tuhuma za kutenda jinai
za kivita, mauaji ya halaiki
kwa raia, utumwa na jinai
dhidi ya binadamu. Tayari
imeripotiwa kuwa mawakili
zaidi ya 30 wamejitokeza
kutaka kumtetea katika kesi
itakayomkabili.
Mwaka 2005, ICC ilitoa hati
ya kukamatwa makamanda
watano wa kundi la LRA,
akiwemo Dominic Ongwen.
Bado operesheni za kumsaka
Joseph Kony, ambaye
anadiwa kujificha huko
Jamhuri ya Afrika ya Kati
zinaendelea.
Waasi wa Kikristo wa
Lord's Resistance Army huko
Kaskazini mwa Uganda,
ambao wamekithiri kutenda
jinai dhidi ya raia wasio na
hatia hasa watoto, awali
walianza uasi dhidi ya
serikali ya Kampala mwaka
1980.
Pamoja na kutenda jinai
za kutisha kwa muda mrefu
dhidi ya watu wasio na
hatia hasa katika maeneo
ya Kaskazini mwa Uganda,
kufanya mauaji ya halaiki kwa

AN-NUUR

Makala

RABIUL THANI 1436, IJUMAA FEBRUARI 6 - 12, 2015

Haya ya Kony sio ugaidi,


ugaidi utakuwa nini sasa?

Bw. Joseph Kony,


raia, kuwakata viungo watu
wanaowakamata, kuteka
watoto na kuwaingiza vitani,
kuchoma moto nyumba
za wanaokaidi amri zao
wakati wa utekaji nk, bado
duru za kisiasa za Afrika na
kimataifa kwa kipindi chote
hicho zimeshindwa kabisa
kubainisha utambulisho
wa kweli na malengo halisi
ya waasi hao. Hawasikiki
wakiitwa magaidi wa
Kikristo au Wakristo wenye
imani kali nk.
Kwa mujibu wa takwimu
za Umoja wa Mataifa, katika
kipindi cha miongo mitatu
iliyopita, waasi wa LRA
wameuwa karibu watu laki
moja na kuwateka nyara
watoto zaidi ya 60,000.
Watoto wanaotekwa nyara
wamekuwa wakiingizwa
vitani kupigana dhidi ya
Jeshi la serikali ya Uganda
na wale wa kike wakigeuzwa
vyombo vya starehe ya
ngono.
Dominic Ongwen, ni
m i o n g o n i m wa wa t o t o
waliokamatwa mateka na
kutumiwa na waasi wa
LRA kama askari vitani
na hatimaye kuwa mtu wa
karibu sana wa Joseph Kony,
kiongozi mkuu wa waasi
hao.
Katika miaka ya hivi
karibuni, waasi hao wa
Uganda wameweka makazi
yao katika misitu ya Jamhuri
ya Afrika ya Kati, Jamhuri
ya Demokrasia ya Kongo,
Sudan Kusini. Wakitokea
katika maficho ya nchi hizo
bado wameendelea kuua na
kufanya uporaji na utekaji.
Awali serikali ya

Bw. Dominic Ongwen.

Uganda ilitaka Domonic


Ongwen, iwapo akikamatwa
ashitakiwe na kuhukumiwa
nchini humo.
Hata hivyo kutokana na
ushawishi wa Marekani
nchini Uganda na katika
eneo la Afrika ya Kati,
imelazimika kamanda
huyo wa LRA akabidhiwe
Mahakama ya ICC.
Ongwen ambaye kutokana
na jinai zilizokubuhu za
L R A , i l i d h a n i wa k u wa
iwapo angekamatwa
angeshughulikiwa
kama kamanda wa al
Shabab, au Boko Haram,
lakini Marekani ambayo
inajinasibu kuwa kiranja wa
haki za binadamu, imetaka
kamanda huyo wa waasi wa
Uganda asibakishwe Uganda
kwa kuhofia kutotendewa
uadilifu na badala yake
akabidhiwe kwa mahakama
ya ICC, kwa madai kwamba
kuna uwezekano akafanyiwa
tofauti nchini Uganda.
Ushawishi huo wa
Marekani kuhusu Ongwen
haushangazi kwa kuwa ni
muendelezo tu wa siasa
zake za kibeberu na za
kindumilakuwili.
Kwa wanaoitizama
kwa jicho la tatu, ni wazi
kwamba wanaiona Marekani
ambayo kwa gamba lake la
nje inaonekana kama kinara
wa demokrasia na haki
za binadamu, ndiyo hiyo
hiyo ambayo ni kiranja wa
matendo ya jinai za kivita,
uporaji na mauaji duniani.
Ndiyo kinara wa kuunga
mkono utawala wa Kizayuni
wa Israel, ambao kila uchao
inakoleza umwagaji wa

damu za watu wasio na


hatia huko Palestina, Syria,
Afghanistan, Somalia na
Iraq.
I e l e we k e t u k wa m b a
Resistance Army (LRA), asili
yake ni kundi la kuvizia
ambalo limejihusisha na
kampeni za ghasia zenye
azma ya kuanzisha serikali
inyoongozwa kwa mujibu
wa Kikristo nchini Uganda.
Kundi hili kama
wanavyodai, limejengwa
kwenye misingi ya Biblia ya
Kikristo na amri kumi. Kundi
la LRA ambalo limejulikana
kwa vitendo vyake dhidi
ya wenyeji wa Uganda
Kaskazini, limeteka nyara
takribani watoto 30,000 na
kusababisha watu milioni 1.6
kukimbia makazi yao tangu
kuanza ugaidi wao mwaka
1986.
Joseph Kony, kiongozi wa
kundi hili la wanamgambo
wa LRA, alizaliwa mwaka
1961 katika kijiji cha Odek,
kinachopatikana Mashariki
mwa Gulu huko Kaskazini
mwa Uganda.
Katika ujana wake, Joseph
K o n y a l i f u n z wa k u wa
mganga wa kijiji na kakake
mkubwa, Benon Okello, na
kakake alipofariki alichukua
kikamilifu wajibu wa kuwa
mganga wa kijiji.
Baba yake alikuwa
muumini wa Kanisa Katoliki
na mama yake alikuwa
Muanglikana.
Kony alikuwa akipata
mafunzo ya Kanisa kwa
miaka kadhaa lakini baadae
aliacha kwenda Kanisani
akiwa na umri wa karibu
miaka 15. Aidha aliacha

masomo yake akiwa katika


elimu ya sekondari.
Januari mwaka 1986,
akiwa na miaka ishirini na
kitu hivi, alianza kupata
umaarufu. Kundi lake
lilikuwa moja ya makundi
makubwa yaliyoibuka huko
Acholi wakati wa vuguvugu
wa kundi maarufu la Roho
Mtakatifu lililoongozwa na
Alice Auma (Lakwena).
Shida ilianza baada
ya kuibuka mgogoro
k w a Wa c h o l i , a m b a o
walinung'unikia kupoteza
uashawishi wao madarakani
kufuatia kupinduliwa Rais
Tito Okello, aliyekuwa
Muacholi.
Mapinduzi hayo
yalifanywa na Rais wa sasa
wa Uganda Yoweri Kaguta
Museveni kupitia jeshi lake
la National Resistance Army
(NRA) baada ya mfululizo
wa vita vya msituni nchini
Uganda vilivyofikia tamati
mwaka 1986.
Awali kundi la Kony
liliitwa United Holy
Salvation Army (UHSA) na
halikuchukiliwa kama tisho
kwa NRA.
Hata hivyo ilipofikia
mwaka 1988, baada ya
mkataba kati ya NRA na
Uganda People's Democratic
Army, Kony alilazimika
kuongeza kundi la
wapiganaji ikiwa ni pamoja
na kusajili watoto kwa nguvu
na kulilifanya kundi la
United Holy Salvation Army
kuwa jeshi lililoogofya.
Askari jeshi wake
wengi walikuwa watoto.
Inakadiriwa kuwa kipindi
hicho alichukuwa watoto
zaidi ya 104.000 wakiwa
ni wavulana na wasichana
tangu LRA ilipoanza
kupigana na serikali ya
Museven mwaka 1986.
Katika mashambulizi
yake, jeshi la Kony lilifanya
mauaji ya jamaa na majirani
wa watoto hawa kabla ya
kuwateka na kuwalazimisha
wapigane katika jeshi lake.
Kamanda wa kundi jingine
la UPDA, Odong Latek,
alifanikiwa kumshawishi
Kony atumie mbinu za
kisasa za kijeshi, tofauti na
majaribio ya awali ambayo
yalihusu mashambulizi ya
msalaba na kutumia maji
matakatifu.
Mbinu hii mpya
ilifanikiwa kiasi kwa kutumia
mashambulizi madogo
madogo na kuwadhibiti
NRA Kaskazini. Kufuatia
hali hii, Museven na NRA
yake walianza kulipiza kisasi
kwa kudhoofisha kundi la
Kony kisiasa kwa kampeni
iliyoitwa Oparation North.
Mwaka 1992 Kony
alilipa kundi lake jina jipya
la Muungano wa Jeshi la
Kikristo la Demokrasia. Ni
katika kipindi hiki ndipo
alipowateka nyara wasichana
44 kutoka shule za sekondari
za Sacred Heart na St. Mary's
Girls School.
Inaendelea Uk. 19

19

Makala

AN-NUUR

RABIUL THANI 1436, IJUMAA FEBRUARI 6 - 12, 2015

Upole wa Mtume (s.a.w) ni ujumbe hai hadi zama tulizonazo

Dkt. Oukili Mohamed Oukil.


Mpenzi msomaji wa safu
hii ya makala, leo hii
tutatizama na kuizingatia
moja ya ujembe wa Mtume
(saw), ambao ni hai hadi
zama zetu hizi pale nitakapo
kubainishia utukufu wa
upole wa Mtume (saw),
pale anaposema Mwenyezi
Mungu, Na hakukuleta
wewe isipokuwa uwe ni
rehema kwa ulimwengu.
Sura Anbiyai aya ya (107).
Na unapozingatia ndugu
yangu msomaji katika aya hii
tukufu, utamkuta Mwenyezi
Mungu amemsifu Mtume
wake (saw) kwamba yeye
ni rehema kwa ulimwengu
wote na wala hakusema ni
rehema kwa waumini, jambo
ambalo linajulisha kuwa
kuletwa kwake si tu, kwa
ajili ya Waislamu pekee na
Inatoka Uk. 18
Kufuatia mtindo huu wa
utekaji na mauaji ya kundi
la Kony, Operation North
iliweza kuharibu kabisa
ushawishi wa wana mgambo
wa Lord's Resistance Army
na idai yao ikazidi kupungua
kutoka melfu hadi kufikia
mamia.
Hata hivyo, waliendelea
kuwavamia raia na washirika
wa NRA.
Mara nyingi katika
mazungumzo ya amani
yaliyoanzia mwaka 1993,
Kony na kundi lake
lililazimisha kushirikishwa
viongozi wa Kanisa.
Hata kabla ya mkutano,
a l i l a z i m i s h a wa h u s i k a
wake katika mazungumzo
kupakwa kwanza mafuta
matakatifu, akiamini kuwa
yanawakinga na risasi na
pepo mbaya.
Ilifika wakati Kony kabla
ya kundi lake kushiriki
mazungumzo na serikali,
aliweka sharti la kusaka
kwanza ushauri kutoka kwa
Roho Mtakatifu.
Mazungumzo yalipoanza
walisisitiza kwamba viongozi
wa dini washirikishwe na
walifungua mkutano kwa
maombi yaliongozwa na
Mkurugenzi wa Masuala
ya Dini wa LRA Bw. Jenaro
Bongoni.

kwa nini iwe hivyo?


Amesema Ibnu Abbasi
(ra) yeyote mwenye
kumuiga Mtume atakuwa
ni rehema duniani na akhera,
na kwa yuke asiyemfuata
h u s a m e h e wa k wa ya l e
a t a k a y o p e wa m i t i h a n i
kwa yale waliopewa
umati zilizopita kama vile
kudidimizwa na kufutwa na
kutupwa.
Kwa hivyo basi,
inatubainikia kuwa rehema
kubwa ambayo wameifanya
viumbe kutoka kwa Mola
wao mlezi ni kuletwa Mtume
mpole na muongofu, Nabii
Muhamad (saw).
A m e s e m a M we n ye z i
Mungu kuibanisha rehema
hii na kujigamba kwa viumbe
wake na waja wake, Na
hatukukutumiliza wewe
isipokuwa ni rehema kwa
ulimwengu wote. Anbi yai,
aya ya 107.
Hakuna kiumbe yeyote
hapa duniani isipokuwa
amepata fungu lake juu
ya rehema, viumbe vyote
vimefurahia ujumbe wake
Mtume (saw). Kwa hakika
uwazi wa rehema ya Mtume
(saw) imekusanywa katika
maisha yake na imejaa
katika sheria yake, na ni
kumuhurumia mdogo na
mkubwa na wa karibu na wa
mbali na adui na rafiki. Pia
rehema yake ipo hadi kwa
wanyama na vitu vingine
visivyo na roho na hakuna
njia ya kuifikia rehema ya

Mwenyezi Mungu isipokuwa


ni hii ambayo ameielekeza
Mtume (saw) kwa umma
wake, na kuwahimiza juu ya
mwenendo wake na hakuna
njia inayomuepusha mtu na
rehema ya Mwenyezi Mungu
isipokuwa imekemewa na
kuwatahadharisha nayo.
Yote hayo ni kwa ajili
ya kuwahurumia wao na
kuwafanyia upole kwao, na
hupata furaha yule mwenye
kupata fungu lake la rehema
ya Mtume (saw). Wa kwanza
wao ni Masahaba zake (ra),
ukaja moyo wake Mtume
( s a w ) , u p o l e k wa o n a
kuwahurumia wao hadi
akashuhudia hilo Mola
wake mlezi kwa neno lake,
Kwa hakika amekujieni
Mtume kutoka na nyinyi
wenyewe, ni mpenzi
kwenu, yanamgusa yale
yanayokusumbueni nyinyi,
ana pupa na nyinyi, kwa
waumini ni mpole mwenye
rehema. Tauba (128).
Na katika sahihi Bukhari
na Muslim toka kwa Anasi
(ra), Mwarabu mmoja
alikojoa ndani ya Msikiti,
wakataka baadhi yao
kumpiga akasema Mtume
(saw), Muacheni na wala
msimkatishe mkojo wake.
Alipomaliza akaita ndoo
yenye maji akamwagia juu
ya mkojo.
Imekuja katika baadhi ya
mapokezi mengine kwamba
yule Mwarabu alisema, Ewe
Mwenyezi Mungu nirehemu

mimi na Mohamed (saw) na


wala usimrehemu mwingine
k a m we . M t u m e ( s a w )
akamwambia kwa hakika
amefanya duara liwe dogo.
Mpenzi msomaji,
yatupasa sisi sote kumuiga
Mtume (saw) ili tufaulu kwa
kupata radhi za Mwenyezi
Mungu mtukufu. Na rehema
zake ni hapa duniani na
akhera. Pia Mtume (saw)
ni Mtume wa haki kutoka
kwa Mwenyezi Mungu,
haki ambayo imejengwa na
msamaha na wepesi kwa
watu na kuweka mbali na
kila linalopelekea msimamo
mkali na kuvuka mipaka
na kutumia fujo, kwani
hayo yote husababisha
kuvunja umma na jamii, na
Mwenyezi Mungu mtukufu
alichokitaka ni kuimarisha
dunia na kueneza amani
na huu ndio mwenendo wa
Mtume (saw) na muongozo
wake.
Mwenyezi Mungu
anasema, hakika imekuwa
ni kiigizo chema kwa Mtume
wa Mwenyezi Mungu
kwa yule anayemtarajia
Mwenyezi Mungu na siku ya
mwisho na akamtaja mungu
kwa wingi, Ahzab (21).
Hakika upole, uwepesi
rehema katika Uislamu ni
alama kubwa na ya wazi
inayoonekana katika imani
yake na ibada yake na kuishi
na watu vizuri na tabia zake.
Na katika sahihi kwamba
Mtume (saw), Hakupewa

Haya ya Kony sio ugaidi, ugaidi utakuwa nini sasa?

Inakumbukwa hata katika


mazungumzo ya amani ya
mwaka 1994, Kony aliingia
huku wanaume waliovaa
m a j o h o wa k i wa m b e l e
yake wakimyumyizia maji
takatifu.
Juhudi nyingi za
kimataifa za kuleta amani
na kukomesha utekaji
nyara wa watoto na mauaji
yaliyokuwa yakifanywa na
wanamgambo wa kundi
lake la Lord's Resistance
Army zilifanyika kati ya
1996 na 2001. Juhudi zote
zilishindwa kumaliza utekaji
nyara wa watoto, ubakaji,
kusajili askari-jeshi watoto,
mauji ya raia na ushambuliaji
wa kambi za wakimbizi.
Kwa kipindi chote hicho
cha uasi na kukithiri vitendo
vya jinai nchini uganda,
hakuna Jumuia ya Kimataifa
wala Taifa lolote linalojiita la
kidemokrasia lililothubutu
kulitangaza kundi la LAR
kuwa ni la kigaidi, hadi
ilipofika Agosti 28 mwaka
2008, ndipo Marekani
ilimuorodhesha Kony
miongoni mwa kundi la
magaidi wa kipekee duniani.
Hata hivyo pamoja na
kufanya hivyo, haikuchukua

hatua madhubuti kama


ilivyochukua Somalia dhidi
ya al Shaabab na Afghanistan
dhidi ya Taleban. Bado Kony
anatamba bila kizuizi cha
nguvu ya Kimataifa kama
ilivyo kwa Boko Haram
wa Nigeria. Wenye kufikiri
wameona kuwa Marekani
k u c h e l e wa k u l i t a n g a z a
LRA kundi la ugaidi na
kutochukua hatua zake
kama ilivyozoelekea dhidi
ya ugaidi huo, ilikuwa ni
kiini macho tu cha kuondoa
aibu na kuzima mashaka
kwa walimwengu.
Hazikusikika drone
kuvurumusha makombora
yake Gulu, Sudan Kusini
wala Afrika ya Kati
kuwashambulia magaidi
hao wa LRA.
Kwa umri wa ugaidi
wa LRA hadi sasa,
hazionekani hatua za kijeshi
za Marekani na washirika
wake kukabiliana vilivyo na
kundi hilo la Amri Kumi za
Mungu, kama inavyofanya
Afghanistan dhidi ya
Taliban, Somalia dhidi ya al
Shaban au dhidi ya al Qaeda.
Wakati
Zumari
likikolezwa na Fox,
CNN, BBC, kuutangazia

ulimwengu kwa mapana


matukio ya ugaidi ya Boko
Haram, Alqaeda, al Shaabab
na ISS wakichinja Wazungu.
Kwa mapana hayo hayo ni
vigumu kusikia vyombo
hivyo kukoleza habari
za mauaji, utekaji watoto
wadogo, ubakaji kutoka
LRA, Anti Balaka nk.
Kony anawaamuru
watoto anaowateka wachore
msalaba kwenye vifua vyao
na mafuta wanayopakwa
yangewakinga na risasi.
Kony anasisitiza
kwamba wana mgambo
wa Lord's Resistance Army
wanapigania Amri Kumi.
Haya hayaelezwi kama
wa n a v y o o n ye s h wa I S S
wanavyotangazwa kutetea
Islamic State.
Kony katika kuhalalisha
ugaidi wake anasema
kusimamia Amri Kumi siyo
kukiuka haki za binadamu
na amri haikutolewa na
Joseph, haikutolewa na LRA,
la, amri hiyo ilitolewa na
Mungu. " Haya ulimwengu
hauelezwi.
Oktoba 6, 2005
Mahakama ya Kimataifa
ya Uhalifu (ICC), ilitoa
vibali vya kukamtwa kwa

kuchagua Mtume kati ya


mambo mawili isipokuwa
kuwahi kuchagua lililo
jepesi zaidi, lakini lisilo na
madhambi.
Na toka kwa Abu
Harairata (ra) amesema
Mtume (saw), Hakika ya
dini hii ni nyepesi na hatoitia
ugumu yeyote isipokuwa
itamshinda. Hivyo basi
fanyeni mazuri na jisogezeni
na peaneni maneno mazuri
ya matumaini na ombeni
msaada asubuhi na jioni
na kipande cha usiku.
Ameipokea Imamu Nakhari
na maana ni kukataza juu
ya msimamo mkali katika
dini kwa kujibidisha mtu
mwenyewe katika ibada,
a m b a y o h a j a a m r i s h wa
n a h u f a n ya h i v y o k wa
k u t u m i a n g u v u k u b wa
dini haichukuliwi kwa
kushindana.
Amesema Mtume
(saw) Shakaneni na yale
niliyokuacheni nayo tu,
hakika wameangamia
waliopita kabla yenu kwa
kutofautiana na Mitume
yao, nitakapo kukatazeni
jambo jiepusheni nalo na
nitakapokuamrisheni jambo
lifanyeni kiasi muwezavyo.
Ameipokea Imam Bhukhari
na Muslim.
Wa s a l a m u a l a i k u m
warahma tullahi
Wabarakatu.
Dkt. Oukili Mohamed
Oukil ni Mwalimu wa
al- Azhari Sharif tawi la
Tanzania
wanamugambo watano wa
kundi la Lord's Resistance
Amy kwa uhalifu dhidi ya
haki za binadamu, kufuatia
kufunguliwa mashitaka.
Waziri wa Ulinzi wa
Uganda, Amama Mbabazi,
alidokeza kuwa Joseph
Kony na wenzake wa
karibu, Vincent Otti na
makamanda Raska Lukwiya,
Okot Odiambo na Dominic
Ongwen walikuwa miongoni
mwa wale ambao vibali vyao
vya kukamtwa vilitolewa.
J u m a m o j a b a a d a ye ,
O k t o b a 1 3 , a l i y e k u wa
M we n d e s h a M a s h i t a k a
Mkuu wa ICC Luis
Moreno Ocampo, alitoa
maelezo kuhusu mashitaka
yaliyomkabili Kony. Kuna
jumla ya mashitaka 33, 12
yakiwa ni uhalifu dhidi ya
haki za binadamu, ambayo
ni pamoja na mauaji,
utumwa, utumwa wa ngono
na ubakaji.
Kuna mashitaka mengine
21 ya uhalifu wa kivita
ambayo ni pamoja na mauaji,
ukatili kwa raia, ushambulizi
wa kimakusudi kwa raia,
uporaji mali, ubakaji na
kusajili watoto kwa nguvu
katika vikosi vya waasi.
Ocampo alisema kwamba
Kony aliwateka wasichana
kuwatoa kama zawadi kwa
makamanda wake.
Itaendelea toleo lijalo

AN-NUUR

20

MAKALA

20

Na Bakari Mwakangwale

AMALI
njema
kwa mwanadamu
alizochuma kabla ya
kufikiwa na umauti,
ndizo zitakazo mfaa
katika maisha yake ya
kaburini.
Hayo yamesemwa
na Ustadhi Saidi
Juma, akiwahutubia
Waislamu katika hotuba
ya swala ya Ijumaa ya
wiki iliyopita katika
Msikiti wa Taqadir,
Mwendapole, Wilayani
Kibaha.
Ust. Juma, alisema
mwanadamu anatakiwa
kutengeneza akhera
kwa kuwa ni ya kudumu
kuliko kutengeneza
maisha ya dunia,
ambayo ataiacha muda
wowote.
U s t .
J u m a
akisherehesha hadithi ya
Anas Ibn Malik, alisema
Mtume (s a w) ameeleza
kuwa atakapofariki
mwanaadamu,
atasindikizwa na
mambo matatu kwanza
ndugu zake, mali zake,
kisha amali zake.
Lakini, akasema kwa
mujibu wa hadithi hiyo,
katika hivyo vitatu,
viwili vitarudi baada ya
mwanaadamu kuzikwa
kwani havina uwezo wa
kuingia alipoingizwa
mwanaadamu huyo.
Akasema hadithi hiyo
inabainisha kuwa amali
njema alizozichuma
mtu huyo akiwa hai
ndizo atakazo baki nazo
akitiwa kaburini na
ndizo zitakazo msaidia
kwa muda wote mpaka
pale Allah (s w) atakapo
simamisha kiama.
Ndugu zetu, wake
zetu, watoto wetu hata
wakilia na kujigaragaza,
l a k i n i h a wa t a k u wa
na uwezo wa kuingia
kaburini kukusaidia,
kwani wataishia katika
kizingiti cha kaburi.
Huenda ndugu
akawa na uwezo wa
kumnufaisha ndugu
yake katika ardhi

RABIUL THANI 1436, IJUMAA FEBRUARI 6 - 12, 2015

Soma
gazeti la
AN-NUUR
kila Ijumaa

Ibada ndio masurufu


yako Akhera - Sheikh
hii, lakini safari yake
ikishaanza ya akhera,
hatakuwa na uwezo
wa kufanya chochote
pamoja na kwamba
u l i wa s a i d i a k a t i k a
maisha yao. Alisema
Ust. Juma.
Khatibu huyo,
alielezea hali ilivyo sasa
kuwa mwanaadamu
ametawaliwa na
kuitengeneza dunia

(maisha yake ya
dunia) na kusahau
(kuiandaa) akhera
yake ili hali Mwenyezi
Mungu, amemuasa
M w a n a d a m u
awe makini na
kutodanganyika na
maisha ya dunia kwani
maisha ya akhera ni
yenye kudumu.
Ewe Mwanaadamu
kuwa mwepesi katika

AN-NUUR

RABIUL THANI 1436, IJUMAA FEBRUARI 6 - 12, 2015

k u ya e n d e a m a m b o
mazuri na kuwa pamoja
na wale waendao mbio
miongoni mwa wale
wanaoipigania akhera
zaidi kwani mali na
ndugu hivyo ni amana
tu na ipo siku amana
hiyo itarudi kwa
mwenyewe. Alisema.
Ust. Juma, akawataka
Waislamu kuitumia
fursa ya uhai wao wa

maisha uliobakia katika


kuandaa akhera kwa
kufanya mambo ya
kheri kwani hakuna
a n a ye j u a k i l i c h o p o
mbele yeke.
Ust. Juma, alisema kwa
ujumla hali ya kimaadili
iliyopo sasa katika
jamii ni mbaya kwani
mema yamebadilika
na kuonekana kuwa
mabaya na mabaya
kuonekana kuwa mazuri
na jamii kuyapupia
mabaya hayo pasi ya
kumuogopa Mungu.
Akautanabaisha
umma akisema, watu
waepuke kuyaendea
mambo mabaya kwani
umauti haupo mbali
na kwamba, kwa
mujibu wa Mtume (s
a w), alama ndogo za
kiama alizoziainisha
kwa sasa zinadhihiri na
kilichobaki ni zile alama
na dalili kubwa.
Alisema, Waislamu
wanatakiwa kutumia
mafundisho ya
Mwenyezi Mungu na
Mtume wake, kwa kuwa
M t u m e , a n a wa t a k a
kufaidika na mambo
matano kabla ya matano
hayajamfika mtu, moja
katika matano hayo ni
kutumia muda vizuri.
Kwa maana hiyo,
alisema ukishindwa
kutumia muda wako
vizuri katika uhai wako
kwa kutenda mema
na kheri mbalimbali
ni wazi utambue kuna
kukwama siku ya
kiyama.

Watoto 38,000 Somalia hatarini kufa kwa njaa


ZAIDI ya watoto 38,000 wa
Somalia wako katika hatari
kubwa ya kufa kutokana na
njaa licha ya kuwa viwango
vya njaa vimeimarika kwa
takriban thuluthi moja
nchini kote, wataalamu wa
Umoja wa Mataifa walisema
siku ya Alhamisi (tarehe 29
Januari).
Tathmini hiyo inakuja
miaka mitatu tu tangu ukame
mkali na vita kusababisha
njaa nchini humo, iliyoua
zaidi ya robo ya watu milioni
moja, nusu yao wakiwa ni
watoto.

Zaidi ya watu 731,000


pamoja na watoto 203,000
ambao wana utapiamlo
mkali, wanakabiliwa na
uhaba mkubwa wa chakula,
k wa m u j i b u wa r i p o t i
iliyotolewa na Kitengo cha
Uchambuzi wa Usalama wa
Chakula na Lishe cha Umoja
wa Mataifa kwa Somalia,
Mtandao wa Mfumo wa
Kutoa Onyo la Njaa Mapema
na washirika wengine.
Jumla ya idadi ya
walioathirika inawakilisha
anguko la asilimia 29 kutoka
tathmini ya kipindi cha miezi

sita iliyopita, baada ya mvua


nzuri mwishoni mwa mwaka
2014 kuongeza mavuno.
" Wa t o t o we n g i wa n a
utapiamlo mkali, licha ya
kupungua kidogo kwa idadi
yao katika kipindi cha miezi
sita.
Makadirio ya watoto
2 0 2 , 6 0 0 c h i n i ya u m r i
wa miaka mitano wana
utapiamlo mkali, ikiwa ni
pamoja watoto 38,200 ambao
wanakabiliwa na utapiamlo
mkubwa na kukabiliana na
hatari kubwa ya maradhi na

kifo." Ilisema ripoti hiyo.


Robo tatu ya wale walio
katika mahitaji makubwa
zaidi ni wale ambao
walizikimbia nyumba zao,
sababu kubwa ikiwa ni
mapigano yanayoendelea.
"Viwango vya utapiamlo
bado ni vikubwa sana.
Mwelekeo wa mwaka 2015
unatia mashaka," alibainisha
M r a t i b u wa U m o j a wa
Mataifa wa Masuala ya
Kibinadamu kwa Somalia,
Philippe Lazzarini. (irib).

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na POA Printing Works LTD, S.L.P. 4605, Dar es Salaam.

Вам также может понравиться