Вы находитесь на странице: 1из 5

WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO

RELI ASSETS HOLDING COMPANY (RAHCO)

TAARIFA KWA UMMA


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilianzisha Kampuni Hodhi
ya Rasilimali za Reli Tanzania Reli Assets Holding Company (RAHCO)
mwaka 2007 kupitia Sheria Na. 4 ya mwaka 2002 Railway Act No. 4 of
2002 ikiwa ni matokeo ya mchakato wa ubinafsishaji wa Shirika la Reli
Tanzania (TRC) ambalo lilibinafsishwa rasmi mnamo mwezi wa
September 2007.
Sheria Na. 4 ya mwaka 2002 iliyounda RAHCO inaainisha kazi na
majukumu ya RAHCO kuwa ni 1: Kusimamia, kukuza na kuendeleza
miundombinu ya reli kwa niaba ya Serikali; 2. Kuchukua majukumu ya
lililokuwa Shirika la Reli Tanzania (TRC) ikiwa ni pamoja na kurithi mali,
haki na madeni ya TRC; na 3. Kuingia mikataba na makampuni mengine
kwa njia ya ukodishaji, ubia na ushirikishaji wa sekta binafsi katika kutoa
huduma ya usari wa reli.
RAHCO inasimamia mtandao wa Reli yenye urefu wa jumla ya kilomita
2707 nchi nzima, na inasimamia ujenzi wa miradi mbalimbali kama
ilivyoainishwa hapa chini;
1. Mradi wa kujenga reli ya kati ya kisasa Standard gauge kutoka Dar es
salaam hadi Mwanza, ujenzi wa mradi huu utaanza mapema baada ya
taratibu za kumpata mkandarasi kukamilika.
2. Mradi wa kujenga reli mpya ya Standard gauge kutoka Mtwara hadi
Mbamba Bay. Katika mradi huu, upembuzi yakinifu na usanifu wa awali
ulikamilika mwezi Februari 2016. Kazi hii ilifanywa na Kampuni ya
Ushauri ya Dong Myoung kutoka Korea Kusini.

3. Miradi ya kujenga reli ya Standard gauge kutoka Tabora hadi


Kigoma na kutoka Kaliua hadi Mpanda. Miradi hii ipo katika hatua ya
usanifu wa kina na inasimamiwa na kampuni ya ushauri ya COWI kutoka
Denmark. Inatarajiwa ikapo mwezi November 2016, usanifu wa kina
utakuwa umekamilika.
4. Miradi ya reli ya Mpanda hadi Karema na Uvinza hadi Musongati kwa
kiwango cha Standard gauge. Miradi hii ipo katika hatua ya upembuzi
yakinifu na usanifu wa awali chini ya kampuni ya ushauri ya HP Gauff
kutoka Ujerumani na inatarajiwa ikapo mwezi October 2016, hatua hizi
zitakuwa zimekamilika.
5. Mradi wa kujenga reli ya Standard gauge kutoka Tanga kwenda
Arusha mpaka Musoma. Usanifu wa kina kwa upande wa Tanga hadi
Arusha ulifanywa na kampuni ya ushauri ya COWI ya Denmark na
ulikamilika mwezi Mei 2015. Kwa upande wa Arusha hadi Musoma, mradi
uko katika hatua za upembuzi yakinifu na usanifu wa awali unaofanywa
na kampuni ya ushauri ya HP Gauff ya Ujerumani na unatarajiwa
kukamilika ifikapo mwezi December 2016.
6. Mradi wa kujenga reli mpya katika jiji la Dar es Salaam na viunga vyake
kwa ajili ya treni za abiria ili kupunguza msongamano wa abiria na
magari. Mradi huu uko katika hatua za upembuzi yakinifu na usanifu wa
awali chini ya kampuni ya ushauri ya GIBB Engineering ya Afrika Kusini.
Kazi hii inatarajiwa kukamilika mapema mwanzoni mwa mwezi Desemba
2016.
Miradi yote hii imekuwa ikigharamiwa na inagharamiwa na Serikali kwa
nia ya kutimiza azma yake ya kukuza uchumi, kuleta maendeleo kwa jamii
ya Watanzania na hasa tunapoelekea katika uchumi wa Viwanda kupitia
sekta muhimu ya usarishaji.
Serikali imeendelea kutafuta vyanzo mbalimbali vya mapato ili kuweza
kutekeleza mipango yake katika sekta ya usarishaji kwa njia za reli.

Lengo kubwa ni kuhakikisha inaboresha miundombinu ya reli iliyopo na


vile vile inaendeleza miradi mipya ya reli.
Imetolewa na
Catherine Moshi
Ofisa Uhusiano, RAHCO
Dar es Salaam
07/09/2016

Ramani inayoonyesha mtandao mzima wa reli nchini Tanzania unaosimamiwa na


kuendelezwa na RAHCO, mtandao huu unajumla ya Kilometa 2707, unajumuisha
ukanda wa kaskazini Tanga-Arusha-Musoma, Ukanda wa kati DSM-Tabora-Mwanza
na Kigoma na ukanda wa Kusini Mtwara-Mbamba bay.

Moja ya daraja jpya lililojengwa na RAHCO lililopo Km 517 Bahi-Dodoma, RAHCO


inasimamia ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya reli ikiwa ni pamoja na ujenzi
wa madaraja na makarvati mapya.

Kushoto ni daraja jipya lililojengwa Km 293 Kilosa Mkoani Morogoro na


kusimamiwa na RAHCO, daraja hili linauwezo wa kubeba mzigo mkubwa
Zaidi,kulia lenye vyuma vyuma ni daraja la zamani lililojengwa na wanajeshi wakati
wa Mafuriko makubwa mwaka 2012

Muonekano wa ndani wa daraja jipya lililojengwa Km 293 Kilosa Mkoani Morogoro


na kusimamiwa na RAHCO,ikiwa ndio wasimamizi wa miundombinu ya reli nchini.

Eneo ambalo njia ya reli imehamishiwa kabisa katika eneo liliopo Km 303 kati ya
Kilosa na Munisagara katika njia ya reli ya kati mahali ambapo reli nzito ya ratili 80
ilijengwa baada ya kukwepa mafuriko mkoani Morogoro, ujenzi huu wa kupasua
mlima na kutengeneza njia mpya ya Reli ulifanya na RAHCO

Reli Assets Holding Company Ltd Railway Street/Sokoine Drive | S.L.P 76959 |
DAR ES SALAAM | Simu: +255 (0)222112695 | Nukushi: +255 (0)222127404 | Barua
pepe: md@rahco.go.tz | Tovuti: www.rahco.go.tz

Вам также может понравиться