Вы находитесь на странице: 1из 18

Jarida la

Jarida la Bunge

Wizara ya Habari Utamaduni


Sanaa na Michezo
ISSN-085-6046


TOLEO LA:001/2016

MACHI - MEI, 2016

TOLEO LA: 003


NOVEMBA, 2016 HALIUZWI

Mafanikio ya Wizara ya Habari


ndani ya mwaka mmoja wa
Mhe. Rais John Pombe Magufuli
www.habari.go.tz

Jarida la Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo

Bodi ya Uhariri
Mwenyekiti
Zawadi Msalla
Msanifu Jarida
Benedict Liwenga
Wahariri
Genofeva Matemu
Raymond Mushumbusi
Wajumbe
Lorietha Laurence
Shamimu Nyaki
Anitha Jonas

Limeandaliwa na:
Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
Jengo la PSPF Golden Jubilee
Ghorofa ya 8
Mtaa wa Ohio
S.L.P 8031, Dar es Salaam-Tanzania
Faksi : (+255) 22 2126834
Simu : (+255) 22 2126826
Tovuti: www.habari.go.tz

Jarida la Wizara ya Habari

ii

Jarida la Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa


na Michezo
Jarida
la Bunge

DIRA, DHAMIRA NA MAJUKUMU YA


WIZARA
DIRA
Kuwa na Taifa lililohabarishwa vizuri, linathamini utamaduni wake na linakuwa
mahiri katika michezo ifikapo mwaka 2025.
DHAMIRA
Kuendeleza utambulisho wa Taifa kwa kuwezesha upatikanaji mzuri wa habari,
kiuchumi, kukuza utamaduni na michezo kwa umma kwa maendeleo ya
kijamii na kiuchumi.
MAJUKUMU YA WIZARA
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ina majukumu yafuatayo:
Kuandaa na kusimamia utekelezaji wa Sera za Sekta za Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo.
Kuendeleza, kuwezesha na kuratibu masuala ya kuwajengea uwezo
watumishi wa Wizara.
Kusimamia Vyombo vya Habari (Magazeti na vituo vya Redio na
Televisheni).
Kusimamia na kuratibu maendeleo ya michezo nchini.
Kusimamia na kuratibu maendeleo ya utamaduni nchini.
Kusimamia utendaji wa Taasisi, Mashirika ya Umma, Wakala, Miradi na
programu zilizo chini ya Wizara.

Jarida
Jarida
la Bunge
la Wizara
Juni
ya- Habari
August 2016

4
iii

Jarida
la Bunge
Jarida
la Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo

TAHARIRI
NI MUDA MUAFAKA KWA TAALUMA YA HABARI KUHESHIMIKA
Na Shamimu Nyaki
Taaluma ya Habari ni taaluma ambayo imebeba majukumu makubwa sana katika jamii ikiwemo kuelimisha na
kuhabarisha jamii .Ni taaluma ambayo ikitumika tofauti na ilivyokusudiwa inaweza kusababisha migogoro
mikubwa ambayo inaweza hata kusababisha uvunjifu wa amani miongoni mwa jamii.
Kwa kutambua umuhumu wa taaluma hii Serikali kupitia Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo chini
ya Mhe. Waziri Nape Moses Nnauye mapema mwezi Septemba mwaka huu uliwasilishwa Muswada wa Sheria ya
Huduma za Habari ya mwaka 2016 katika Bunge la Jamahuri ya Muungano wa Tanzania kwa mara ya kwanza
na baadaye mwezi Oktoba Mhe. Nape Nnauye aliuwasilisha tena kwa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma
ya Maendeleo ya Jamii.
Yote haya yalifanyika kwa nia nzuri ya kutaka tasnia hii iwe ni tasnia inayoheshimika na kuondoa dhana kuwa ni
taaluma ya waliokosa weledi na hata kupelekea kubatizwa majina ya ajabu kama vilekanjanja
Wakati akiwasilisha Muswada huo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma ya Maendeleo ya Jamii,Waziri
wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alieleza kuwa, Muswada huo unalenga
kuihamisha Sekta ha Habari kuwa taaluma kamili na kuweka masharti ya kukuza na kuimarisha taaluma na
weledi katika tasnia ya habari nchini.
Sheria hii inaleta mageuzi makubwa katika usimamizi wa sekta ya habari hapa nchini, ni Sheria ambayo
inakwenda kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu kuifanya sekta ya habari kuwa sekta rasmi Alisema
Mhe. Nape.
Muswada huu sasa umebaki kuungwa mkono na wadau na wanahabari kwa ujumla kwani unairejesha tasnia ya
habari kwenye heshima yake kwa kuifanya iwe miongoni mwa fani za weledi kama fani nyingine za Sheria
Udaktari na nyinginezo.
Si hayo tu, bali pia unaboresha maslahi ya ya Waandishi wa habari na wafanyakazi wote ikiwemo kulinda
maslahi ya waandishi wa habari wakiwa kazini, wanapopata majanga mengine kama kuugua kuustaafu au
kuachishwa kazi ambapo mwajiri atatakiwa kisheria kuweka bima na hifadhi ya jamii kwa kila mtu aliyeajiriwa
katika chombo chake.
Faida nyingine iliyopo katika Muswada huu ni kuanzishwa kwa Baraza Huru la Habari, Mfuko wa Mafunzo ya
Habari na kuwezesha mafunzo ya ndani na nje ya nchi kwa Wanahabari na kudhibiti utangazaji na uandishi
wenye la kuleta kashfa kwa nchi.
HAPA KAZI TU!

Jarida
Jarida
la Bunge
la Wizara
Juniya- August
Habari 2016

Jaridana
laMichezo
Bunge
Jarida la Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa
Yaliyomo

iii

Jarida la Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo

iv
5

Mafanikio ya Wizara ya Habari


ndani ya mwaka mmoja wa
JPM
Ukurasa wa 1

Muswada wa Sheria ya Huduma


za Habari wa mwaka 2016
Ukurasa wa 3

Sheria ya Huduma za Habari


kufuta Sheria ya Magazeti ya
mwaka 1976
Ukurasa wa 5

Utamaduni na Sanaa ni fursa kwa


Vijana kujipatia ajira
Ukurasa wa 7

Jitihada za Serikali katika


kuendeleza sekta ya Filamu
nchini
Ukurasa
Ukurasawa
wa299

Jarida
Jarida
la Bunge
la Wizara
Juni
ya- Habari
August 2016

16

Jarida
la Bunge
Jarida
la Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo

Mafanikio ya Wizara
ya Habari ndani ya
mwaka mmoja wa JPM
Na Genofeva Matemu

wenye macho haambiwi


tazama na anayeshindwa
kushukuru kwa jambo dogo hata
akifanyiwa jambo kubwa kwake
yeye ataliona dogo kwa sababu
amedhamiria kutokuwa na roho ya
kuridhika.
Novemba Tano mwaka 2016 ni
mwaka mmoja tangu Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
alipoapishwa kuwa Rais na Amri
Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na
Usalama wa Nchi hii ambapo
ameweza kufanya mambo makubwa
kiasi kwamba ukipingana na hali
halisi basi utaonekana kuwa mtu
usiyekuwa na shukrani kwa kila
jambo.
Hatua hii inaonyesha kuwa katika
kipindi cha mwaka mmoja wa
uongozi wake toka aingie
madarakani amekua mstari wa
mbele kuhakikisha mafanikio
makubwa yanapatikana katika sekta
ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo kupitia viongozi
wanaosimamia sekta hizo pamoja na
serikali kwa ujumla.
Baada ya kuapishwa kwake Rais wa
Serikali ya Awamu ya Tano aliona
umuhimu wa sekta ya Sanaa hivyo
kuamua kuiundia Idara ili sekta hiyo
iweze kusimamia kwa karibu kazi za
Sanaa na kuwafanya wasanii kupata
haki halali kupitia kazi za zao.
Katika hali ambayo haikutarajiwa na
watu wengi, Waziri wa Habari,

Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.


Nape Moses Nnauye hakusita
kufanya ziara ya kushtukiza kwa
wafanyabiashara wa kazi za Sanaa
maeneo ya Soko la Kariakoo akiwa
na lengo la kuwafichua
wafanyabiashara wote wa kazi za
Filamu na Muziki ambazo hazina
stika za Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) zinazoashiria uhaliali
wa kazi hizo.
Mhe. Nnauye anasema kuwa, hatua
hii ni ya mwanzo kwa kuwaonyesha
kuwa agizo la Rais wa Serikali ya
Awamu ya Tano, Mhe. Dkt. John
Pombe Magufuli la kulipa kodi kwa
bidhaa zote zilizopo sokoni pamoja
na kununua bidhaa halisi kwa kudai
risiti linasimamiwa na kutekelezwa
ipasavyo.
Ili kuua soko haramu la kazi za filamu
na muziki wito kwa watanzania
ulitolewa na Mhe. Nnauye kuwa tuwe
na tabia ya uzalendo kwa kununua
bidhaa za filamu zenye stampu ya
TRA ili kusaidia katika kukusanya
kodi na kuinua uchumi wa nchi lakini
pia kuinua kipato cha wasanii.
Sanjari na hilo Serikali ya Awamu ya
Tano kupitia Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo
imedhamiria pia kurasimisha kazi ya
sanaa kuwa shughuli rasmi ya
kiuchumi katika kipindi cha miaka
mitano ya uongo wa Rais Dkt. John
Pombe Magufuli.
Ili kuwezesha hilo Mhe. Nnauye
amewaomba wadau mbalimbali
kujitokeza kudhamini mashindano ya
kuibua vipaji vya sanaa huku akiahidi
kuendeleza sekta ya sanaa nchini ili
kuwezesha vijana wengi kutambua
Jarida
Jarida
la Bunge
la Wizara
Juniya- August
Habari 2016

vipaji vyao na kuweza kujiajiri na


kuajiri wengine kupitia kazi za sanaa.
Wakale uneni msina kwao mtumwa.
Lugha aushi na adhimu ya Kiswahili
imeongeza mawanda mapya ndani
ya mwaka mmoja wa Serikali ya
Awamu ya Tano ambapo Bunge la
Afrika Mashariki (EALA) limekubali
hoja ya kuifanya lugha ya Kiswahili
kuwa lugha rasmi katika shughuli za
bunge la Afrika Mashariki hatua hiyo
dhahiri inayounga mkono pendekezo
la mwenyekiti wa wakuu wa Jumuiya
hiyo Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Akizungumzia hoja hiyo Mbunge wa
EALA Mhe. Shayrose Banji amekiri
Bunge la Afrika Mashariki limekubali
kuifanya lugha ya Kiswahili kuwa
lugha rasmi lakini haswa kuienzi na
kuithamini lugha hii ambayo ndiyo
pekee inayozungumzwa katika nchi
zote za Jumuiya na hata nchi zilizo
nje ya Jumuiya.
Aidha, Mbunge wa EALA kutoka
Tanzania Mhe. Adam Kimbisa
amesema kuwa hapa Tanzania
Kiswahili kinatumika kwa asilimia
zaidi ya 95, Kenya zaidi ya asilimia
80, Uganda zaidi ya asilimia 50,
Rwanda zaidi ya asilimia 50 na
Burundi zaidi ya asilimia 60 hivyo ni
wakati muafaka kwa Bunge hilo
kuridhia lugha hii kuwa rasmi ndani
ya Bunge.
Katika kuunga mkono jitihada za
Serikali ya Awamu ya Tano katika
kukuza lugha ya Kiswahili, Kanisa
Katoliki nchini liliandaa Kamusi ya
Ukristo iliyoandikwa na Padre Jordan
Nyenyembe na kuzinduliwa rasmi na

Jarida la Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa


Michezo
Jarida na
la Bunge

Serikali mwezi Agosti mwaka 2016.


Uzinduzi wa Kamusi hiyo utasaidia
siyo tu uelewa wa imani na kukua
kwa lugha ya Kiswahili, bali pia
kuchochea upendo na amani nchini
kwa kutumia lugha ya Kiswahili
iliyopo ndani ya kamusi hiyo.

na masuala ya Habari alizungumza


na uongozi wa juu wa Startimes na
kuwataka kutekeleza maazimio ya
mkataba wa awali wa kukamilisha
ujenzi wa jengo la TBC pamoja na
kuboresha studio ya shirika hilo
kuifanya kuwa studio ya kisasa zaidi.

Dhahiri Serikali ya Awamu ya Tano


imeonyesha umuhimu wa lugha ya
Kiswahili kwa kukutana na manguli,
majagina na mangwiji, wakongwe na
wapenzi wa lugha ya Kiswahili
kujadili changamoto zinazoikabili
tasnia ya lugha ya Kiswahili nchini na
kupendekeza jinsi ya kuzitatua
changamoto hizo katika kukubali na
kuunga mkono juhudi za Serikali
katika kuishadidisha lugha adhimu ya
Kiswahili. Chambilecho cha Hayati
Shaaban Robert alisema maajabu
makuu mawili sintayasahau ni
Mwalimu Nyerere na Lugha ya
Kiswahili.

Sambamba na hayo uongozi huo wa


Startimes umeridhia kuanza kufanya
mafunzo ya kubadilishana uzoefu na
wafanyakazi wa TBC kwa lengo la
kuwaongezea ufanisi katika
kutekeleza kazi zao kupitia mifumo
ya teknolojia ya kisasa.

Aidha Naibu Waziri wa Habari,


Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.
Anastazia James Wambura alisema
kuwa Serikali ya Awamu ya Tano
imezingatia umuhimu mkubwa wa
kuwa na Sera ya Lugha ambayo ni
mwongozo thabiti unaosimamia
masuala yote yanayohusu Lugha
nchini ambapo kwa sasa Wizara
inaendelea na mchakato wa uandaaji
wa Rasimu ya Sera ya Taifa ya Lugha
iliyofikia hatua ya ukusanyaji wa
maoni ya awali ya wadau wa Lugha
kwani tangu tulipopata uhuru mwaka
1961 masuala yahusuyo lugha katika
nchi yetu yamezingatiwa kama
kipengele muhimu katika Sera ya
Utamaduni ya mwaka 1997.

Katika kuleta maendeleo ya sekta ya


habari serikali imekamilisha ndoto ya
wanatansia wa habari kwa kuwaletea
Muswada wa Sheria ya Huduma za
Habari wa mwaka 2016 uliokuwa
ukisubiriwa kwa zaidi ya miaka
ishirini, ambapo Muswada huo
umelenga kuirasimisha sekta hiyo na
kuifanya iweze kuheshimiwa kama
tansia nyingine tofauti na ilivyo sasa.
Muswada huo umesheheni mambo
mengi mazuri yatakayoweza
kuinyanyua sekta hiyo ikiwemo
kuanzishwa kwa Baraza Huru la
Habari ambalo litakuwa likisimamia
waandishi wote wa habari kwa
kuwasajili, pia muswada utasaidia
kuundwa kwa bodi ya ithibati ambapo
bodi hiyo itakuwa ikitoa vitambulisho
vya waandishi wa habari na kuishauri
serikali katika mambo ya elimu ya

Pamoja na hayo katika kipindi cha


mwaka mmoja sekta ya habari
imepata manufaa kwa upande wa
Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC)
ambapo Mhe. Nnauye ameutaka
uongozi wa Shirika hilo kurejea
mkataba wao na Kampuni ya
Startimes wanayoshirikiana nao
baada ya kubainika kuwepo na
upungufu hivyo kuufanyia
marekebisho mkataba huo ili kusaidia
TBC kuboresha mapato tofauti na
ilivyokuwa awali.

mafunzo ya wanahabari.
Serikali ya Awamu ya Tano katika
kipindi cha mwaka mmoja
imeanzisha mfumo wa tiketi za
elektroniki katika uwanja wa Taifa
ikiwa na lengo la kuongeza mapato
lakini pia kukidhi huduma ya haraka
kwa wananchi wote watakaotumia
Uwanja wa Taifa katika matukio
mbalimbali ya michezo.
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa
mfumo huo, Katibu Mkuu wa Wizara
ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel
alisema kuwa mfumo wa elektroniki
katika Uwanja wa Taifa ni wa kisasa
na unawawezesha watu wote kuingia
uwanjani ndani ya dakika 180 hivyo
kuokoa muda wakati wa kuingia
uwanjani.
Prof.Gabriel amesema kuwa kila
mashine inatumia sekunde mbili
kumruhusu mteja kuingia uwanjani
tofauti na awali ambapo ilimlazimu
mteja kupanga foleni kwa kutumia
tiketi za kawaida wakati wa kuingia
uwanjani lakini pia mfumo huo ni
kichocheo kikubwa katika kuongeza
mapato ya Serikali.
Rais huyu wa Serikali ya Awamu ya
Tano katika kuonyesha umuhimu wa
michezo nchini ameweza kufanya
mazungumzo mazuri na Mfalme
Mohammed VI wa Morocco ambapo
mazungumzo hayo yakaleta neema
ya kujengewa uwanja wa mpira
wenye thamani ya Dola za Marekani
milioni 80 (zaidi ya shilingi Bilioni 160)
katika Mji wa Dodoma utakaokuwa
mkubwa kuliko Uwanja wa Taifa
uliopo Jijini Dar es Salaam.
Heko Rais wetu, Mhe. Dkt. John
Pombe Joseph Magufuli, heko
viongozi wa Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa
kufanya mambo makubwa na mazuri
katika kila sekta ndani ya mwaka
mmoja. Ni ukweli usiopingika kuwa
Serikali ya awamu ya tano ipo kwa
ajili ya kuujenga uchumi wa nchi yetu.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu
Mbariki Rais wetu, Mungu wabariki
viongozi wote wa Serikali ya Awamu
ya Tano.

Aidha waziri huyo mwenye dhamana


Jarida
Jarida
la Bunge
la Wizara
Juni
ya- Habari
August 2016

38

JaridaJarida
la Bunge
la Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo

Muswada wa Sheria
ya Huduma za Habari
ya mwaka 2016
Na Cosato Chumi

atimaye, baada ya miaka zaidi


ya ishirini, Serikali imekuja
kukubali kuwasilisha Muswada wa
Sheria ya Habari, ukisomeka:
Sheria ya Huduma za Habari ya
Mwaka 2016, au kwa Kiingereza
Media Service Act, 2016.
Kwa mujibu wa taarifa za Bunge na
Serikali,Muswada huu ulichapishwa
kwenye Gazeti la Serikali Na. 36
Toleo la 97 la tarehe 26 Agosti, 2016
au kwa lugha ya kiserikali/kiingereza
ulikuwa Gazzetedtarehe hiyo.
Mpaka ninapoandika makala hii fupi,
Muswada huu unasomeka hivi
(nasema mpaka ninapoandika kwa
sababu michango ya wada, wajumbe
wa Kamati na Wabunge kwa ujumla
hupelekea kubadilika vile ambavyo
sheria itakavyosomeka) Unasomeka
hivi: Muswada wa Sheria kwa ajili ya
kuweka masharti ya kukuza na
kuimarisha taaluma na weledi katika
tasnia ya habari, kuundwa kwa Bodi
ya Ithibati ya Wanahabri, Baraza
Huru la Habari, kuweka mfumo wa
Usimamiazi wa huduma za habari;
na amsuala mengine yanayohusiana
na hayo.
Sina nia ya kuujadili muswada huu,
nia yangu na rai yangu kwa wadau
wa Habari wakiwemo Waandishi wa
Habari na Vyama vyao kama vile
Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF),
Muungano wa Vyama vya Waandishi
wa Habari Tanzania (UTPC), Umoja
wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari
(MOAT), Mashirika yasiyo ya
Kiserikali kama vile Kituo cha haki za
Binadamu (LHRC) na Taasisi ya

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kushoto)
akijibu hoja mbalimbali za wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo
ya Jamii wakati wa majadiliano ya Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari leo
Oktoba 21,2016 Mjini Dodoma kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Peter Serukamba.

Msaada wa Kisheria (NOLA).


watetezi wa Vyombo vya habari vya
habari kama vile LHRC, NOLA na
Taasisi nyingine za masuala ya
Vyombo vya habari ikiwemo MISA
Tan na Baraza la habari Tanzania.
Kwamba, baada ya miaka zaidi ya
ishirini hatimaye Serikali ikaja
kukubali kuuleta Muswada huu, ni
jambo ambalo naweza kusema kuwa
sio tu la kuunga mkono (bila kujali
yaliyomo ndani ya muswada) bali ni
suala la kufa na kupona kuhakikisha
kuwa ushiriki wa Wadau katika kutoa
maoni yao unakuwa wa hali ya juu na
wenye tija kwa tasnia na kwa pande
zote.
Nasema hivi kwa sababu,
kumejitokeza dalili kama za kusua
sua katika kuwasilisha maoni ya
wadau kwa kile walichodai kuwa
Jarida
Jarida
la Bunge
la Wizara
Juniya- August
Habari 2016

hawakupata muda wa kutosha


kuupitia muswada huo. Lakini baada
ya kusua sua huko, hatimaye Wadau
wakiongozwa na Jukwaa la Wahariri
wakatanga kugomea kutoa maoni
yao. Hawakuishia hapo, wameomba
Mhe Rais kwa Mamlaka aliyonayo
aondoe. Hoja Kuu ya Wadau ni
kwamba muda waliopewa hautoshi,
hivyo muswada uwasilhhswe katika
Bunge la Februari, 2017.
Wote tunatambua kwamba, Vyombo
vya habari ni Muhimili wa nne wa
Dola. Ni kimbilio la wanyonge na
wasio wanyonge, ni kiunganishi
baina ya matabaka katika jamii, lakini
pia ni kiunganishi baina ya Serikali na
wananchi, mwingine angependa
kusema ni kiunganishi baina ya
watawala na watawaliwa, mimi
kwangu nachukulia ni kiunganishi
baina ya Serikali na wananchi.

Jarida
la Bunge
Jarida la Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo

3
Kwa hakika, kuletwa kwa muswada
huo haikuwa kazi ya kitoto.
Kumefanyika jitihada kubwa na
msukumo mkubwa zaidi kutoka kwa
Wadau wa Vyombo vya Habari.
Mara kadhaa ilionekana kama vile
Serikali ndio inayochelewesha jambo
hili lakini hatimaye Muswada
umewasilishwa na uko katika hatua
muhimu ya wadau kutoa maoni yao.
Hata hivyo katika hali ya kushangaza,
Jumatano ya wiki iliyopita, wadau wa
vyombo vya habari waligomea
kuwasilisha maoni yao kwa Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za
Jamii kwa kile walichodai kuwa,
wanahitaji muda zaidi wa kuupitia
muswada huo.
Hoja ya wadau hao ni kuwa
hawakupewa muswada huo kwa
wakati. Madai yao tunaweza kusema
kuwa walikurupushwa, kwamba
walipewa dakika za majeruhi hivyo
hawakuwa wamejiandaa ipasavyo
kutoa maoni yao.
Hata Mwenyekiti wa Kamati Peter
Serukamba kuongeza muda kwa
muda wa takribani siku kumi, bado
wadau hawakutokea jomamosi ya
tarehe 29 Oktoba, 2016.
Ninasema katika hali ya kushangaza
kwa sababu, sikutarajia hoja hii
kutoka kwa Wadau wakati muswada
huo uliwasilishwa awali wakati wa
Bunge la Septemba, lakini pia hata
Waziri mwenye dhamana aliitisha
Mkutano na waandishi wa habari
mara baada ya kuwasilishwa. Kama
vile haitoshi Muswada huo ulikuwa
unapatikana katika tovuti za Bunge
na ile ya Wizara husika.
Bado nina mashaka na hoja hizi za
wadau, kwa mawazo yangu, hata
kama, narudia tena hata kama
ingekuwa Muswada huo haujawekwa
online kwa maana ya kwenye tovuti
za Bunge na Wizara, bado kwa jinsi
ambavyo jambo hili limesumbukiwa
kwa miaka mingi, ilikuwa ni wajibu wa
wadau kuhakikisha kuwa wanaupata
Muswada huo kwa udi na uvumba

hasa kwa kuzingatia kuwa Serikali


ilishausoma Bungeni wakati wa
Bunge la Septemba.
Ifahamike kwamba wadau
ninaowataja hapa baadhi yao ni
waandishi nguli katika habari za
uchunguzi, nina hakika hata kama
ungekuwa muswada huo umefichwa
bado waandishi na vyama vyao
wangeufukunyua popote ulipo na
kuufanyia kazi ipasavyo. Binafsi
nimeona wadau wamepoteza fursa
hii adimu. Ndio maana rai yangu kwa
wadau wa Vyombo vya Habari toka
awali ilikuwa, wasikubali kwa sababu
yoyote ile kutojitendea haki kwa
kupoteza fursa hii.
Mimi sio muumini wa kukimbilia
kutunga sheria bora tu imetungwa
kwa kuwa tuliihitaji muda mrefu,
lahasha bali hoja yangu na imani
yangu ni kuwa mchango wa wadau ni
muhimu katika kutengeneza sheria
ambayo kesho itakuwa na manufaa
kwa Taifa letu vizazi hata vizazi.
Katika kujenga hoja ya kuwa muda
hautoshi wapo wanaotaka muswada
huu usubiri mpaka Bunge la Februari.
Kusogeza mbele ni kuendelea
kujikosea haki ambayo wadau wa
Vyombo vya habari wamekuwa
wakiipigania kwa zaidi ya miaka
ishirini.
Ni kwa sababu hiyo, ninaona ilikuwa
ni ni wajibu wadau wa vyombo vya
habari kujichimbia na kuupitia
muswada huu kwa kina na kisha
kuwasilisha mapendekezo yao kwa
Kamati ya Bunge. Kinyume chake ni
kujikosea haki na kutojitendea haki,
lakini zaidi kutowatendea haki
waandishi wengi wa habari ambao
ninaamini sheria hii itakuwa
mkombozi sio tu katika kuilinda tasnia
bali pia katika kulinda maslahi yao.
Kumekuwa na kilio kikubwa cha
uwepo wa makanjanja lakini pia kilio
kikubwa cha malipo duni kwa
waandishi wa habari, kutokuwa na
mikataba ya kazi, michango yao
katika Mifuko ya jamii, huduma za
bima kama vule bima za afya, bima
za kazini.
Ni wajibu wa wadau kuyatazama
maslahi hayo kwa mapana kuliko tu
Jarida
Jarida
la Bunge
la Wizara
Juni
ya- August
Habari 2016

maslahi ya wachapishaji na wamiliki


wa vyombo vya habari. Ni wazi kuwa
wapo baadhi ya wamiliki wa Vyombo
vya habari ambao wasingependa
Sheria hii ije kupita. Hii ni kwa sababu
ya hayo niliyoyataja hapo juu.
unyonyaji uliokithiri miongoni mwa
baadhi ya wamiliki dhidi ya
wafanyakazi wao na hasa waandishi
wa habari.
Katika hali ya sasa, kwa mfano
waandishi wa kujitegemea
correspondent walio wengi hakika
wanalazimika kunyanyasika kwa
sababu tu hakuna sheria inayoweza
kuwalinda. Mwandishi wa aina hiyo
anayetegemea kulipwa kwa story,
inayopimwa kwa sentimita, na
ambaye anaweza kuwa amefanya
kazi katika chombo husika kwa miaka
isiyopungua mitano, anaposhindwa
kufanya kazi ama kwa kuugua au
kwa sababu yoyote hiyo, huo ndo
mwisho wake wa kupata kipato.
Lakini wapo wamiliki ambao
wanawafanyisha kazi waandishi sio
tu kwa malipo duni bali hata kwa
kuwakopa.
Wadau wa Vyombo vya habari,
walipaswa waione fursa hii kama
golden chance , kwa kujitendea haki
lakini pia kuwatendea haki wale
waliowapa dhamana ya
kuwawakilisha kwa kubalance
maslahi. Wakijisahau na kujikuta
wanaegemea upande mmoja,
watabaki na hoja ya kwamba
muswada upelekwe mbele na
matokeo yake fursa hii adhimu ikaja
kupotea.
Wadau wa Vyombo vya habari
wanaweza kujikuta baadhi yao
wametumiwa, naamini wapo ambao
wanaweza kutumika kwa kutambua
kuwa wanatumiwa lakini pia wapo
ambao wanaweza kujikuta pasi kujua
kama wametumiwa na nani
anayewatumia. Yeyote ambaye
anaona kwamba sheria hii itatibua
maslahi yake bila shaka atakuwa
tayari kuloby ili ikwame kwa maslahi
yake tu na sio kwa maslahi ya tasnia
ya habari.

10
5

Jarida la Wizara
Bunge ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo

Sheria ya Huduma za
Habari kufuta Sheria
ya Magazeti ya
mwaka 1976
Na Benedict Liwenga

i hekima na busara kuangalia


upya Sheria ambayo imedumu
kwa miaka takribani 40. Hii ni
sheria ya Magazeti ya Mwaka 1976
(News Paper Act, 1976).
Kulingana na mabadiliko ya
kiteknolojia na utandawazi ni dhahiri
kuwa Sheria hii imeanza kupitwa na
wakati. Wakati umefika kwa watu
wanaojitambua kuwa na Sheria
Mpya inayoendana na wakati uliopo
na ikiendelea kutumika pia kwa
wakati ujao.
Kwa sasa nachelea kuiita Sheria
kwani mchakato wa kuitunga bado
unaendela. Ni vyema ikatamkwa jinsi
ilivyo kuwa ni Muswada wa Sheria ya
Huduma za Habari (Media Services
Bill). Muswada huu unalenga
kuifanya fani ya Habari kuwa
Taaluma hivyo kuipa heshima tasnia
ya habari kwa ujumla. Haya ni baadhi
ya maneno yanayonukuliwa kutoka
kwa mdau wa habari ambaye ni
Mkurugenzi wa Idara ya HabariMAELEZO, Bw. Hassan Abbas.
Jambo ambalo ni la kupongeza
katika muswada huu na la kuungwa
mkono na wanahabari ni hli la
kuanzisha Mfuko wa Mafunzo ya
Habari ambao unalenga kuwainua
vijana wengi kitaaluma kwenye
tasnia ya habari.

Wapo vijana wengi wenye vipaji vya


uandishi na utangazaji lakini baadhi
yao hawana mafunzo ya taaluma ya
habari na pengine wangependa
kujiendeleza lakini kwa ukosefu wa
fedha wamekuwa wakishindwa
kupiga hatua na wengine kukata
tamaa kabisa na kuamua
kujishughulisha na mambo mengine
yasiyokuwa na tija kwao wala kwa
Taifa.
Mfuko huu utawawezesha kujiunga
katika vyuo vya ndani na nje ya nchi
ili kupata mafunzo ya taaluma ya
habari.
Sheria ya Magazeti ya Mwaka 1976
imepeigiwa kelele sana na kupewa
majina mengi. Wengine wameiita
Sheria Kandamizi, na wadau
wengine wakasema ni ya kizamani
sana hivyo imepitwa na wakati pia
imeitwa sheria mbovu. Kwa kuyaona
hayo yote ndio maana Serikali
imekuja na Muswada wa Sheria ya
Huduma za Habari ambao uko
kwenye hatua za mwisho baada ya
kusomwa kwa mara ya kwanza
Bungeni Septemba mwaka huu
(2016).
Wanahabari na wadau wengine wa
habari wamejitokeza kutoa maoni
yao ili kuuboresha Muswada huo.
Vipo vipengele ambavyo
vimeonekana kuwa na maoni tofauti
kutoka kwa wadau. Kipengele
Jarida
Jarida
la Bunge
la Wizara
Juniya- August
Habari 2016

ambacho kimeonyesha duku duku


kwa baadhi ya wadau ni kile cha 55
kinachozungumzia madaraka ya
Waziri. Kipengele hicho kinasema
Waziri atakuwa na mamlaka ya
kuzuia uchapishaji au utangazaji wa
maudhui yanayohatarisha usalama
wa Taifa au afya ya jamii.
Bwana Abbas anasema kuwa hata
Sheria za Kimataifa zinazoongelea
uhuru wa vyombo vya habari na
uhuru wa kuandika au kutangaza
habari zinazungumzia pia makatazo.
Mfano Sheria hizo au matamko ya
Umoja wa Mataifa yanazungumzia
kutotoa taarifa ambazo zitahatarisha
usalama wa Taifa au kumkashifu mtu.
Hivyo Waziri hawezi kuacha maasi
yanatokea watu wanauana eti
asikataze chombo husika kuendelea
kutoa matangazo ya uchochozi wa
uvunjifu wa amani. Hivyo basi
kipengele 55 kinachozungumzia
mamlaka ya waziri ni muhimu kibaki
ili kulinda usalama wa Taifa na afya
ya jamii. Masuala ya habari ni nyeti
sana hivyo yanahitaji umakini
mkubwa na usimamizi pia.
Imeonekana katika nchi jirani jinsi
vyombo vya habri hasa redio
vilivyochochea mauaji ya kimbali na
watu wengi kupoteza maisha yao,
hivyo usalama wa Taifa hauwezi
kuachwa holela lazima kuwepo na
msimamizi, Alisema Bw. Abbas.

Jarida
la Bunge
Jarida la Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo

5
Wahariri wa vyombo vya habari
wanayo maoni yao kuhusu Muswada
huu. Wengi wao wanauunga mkono
katika vipengele kadha.
Bi Scolastika Mazula ambaye ni
Mhariri Mkuu wa kituo cha Redio Efm
anasema katika muswada huo wa
Sheria ya Huduma za Habari yapo
mambo mazuri yenye tija katika sekta
ya habari kama suala la kuanzishwa
kwa Mfuko wa Mafuzo ya Habari ni
jambo jema sana kwani utasaidia
kutoa fursa za waandishi
kujiendeleza kimasomo na kuifanya
fani ya habari kuwa na wasomi zaidi
tofauti na inavyoonekana kwa sasa.
Mfuko huu upo katika ibara ya 21 ya
Muswada wa Sheria ya huduma za
Habari.
Suala la elimu kwa waandishi ni bora
liwekwe wazi kisheria kwani tansnia
hii ya habari inahitajika kuheshimika
kama ilivyo tansia nyingine badala ya
kuonekana wababaishaji, anasema
Mazula.
Licha Mfuko huu kuanzishwa na
Sheria ambayo ipo kwenye
mchakato, yapo mambo mengi
ambayo ni mazuri kwa wanahabari
na tasnia kwa ujumla katika
Muswada huu, alisema Bw. Abbas.

kuanzishwa kwa bodi ni zuri ila


ingekuwa vyema kama bodi hiyo
itakuwa na asilimia kubwa ya wadau
wa habari na ijitegemee na Waziri
mwenye dhamana ya habari na
Mwanasheria Mkuu wasiwe na
mamlaka sana katika bodi hiyo.
Muswada huu wa Sheria
umesubiriwa kwa takribani miaka 20,
kwani tangu miaka ya 80 wadau wa
habari wamekuwa na kiu ya kupata
sheria nzuri ya kusimamia masuala
ya habari hapa nchini na hasa lengo
likiwa ni kuondoa Sheria ya Magazeti
ya mwaka 1976. Kutokana na kiu hii
ndio maana wanadau wengi
wamejitokeza kutoa maoni yao
kuhusu Muswada huu. Kwa asilimia
karibu 90 ya maudhui ya Muswada
huu ni ya wadau wa habari.
Ikumbukwe kuwa mwaka jana (2015)
Muswa wa Sheria ya Huduma za
Habari uliletwa Bungeni kwa hati ya
dharula ukakataliwa na kurudishwa
kwa wadau ili kupata maoni yao
kwani ndio wataosimamiwa na
Sheria mpya endapo muswada
utapitishwa bungeni na kuwa sheria.
Hivyo ilibidi urudishwe kwa wadau na
kupata maoni yao.

11

mara ya kwanza na kuwapa wadau


fursa nyingine ya kutoa maoni yao.
Ni ukweli usiopingika kuwa Muswada
huu ukishakuwa sheria utaongeza
uhuru wa vyombo vya habari
ukilinganisha na Sheria ya Magazeti
ya mwaka 1976. Wanataaluma ya
habari wataheshimika kitaaluma na
kufanya kazi kwa weledi zaidi.
Bodi ya Ithibati nayo itakuwa na
mchango mkubwa katika
kuwatambua wanahabari na
kuwasimamia ili watimize wajibu wao
kwa uhuru na weledi.
Kwa waliotoa maoni yao watakuwa
na jambo la kujivunia endapo sheria
mpya ya Huduma za habri itapitishwa
na kuanza kazi baada ya kutiwa saini
na Mhe. Rais na kupitia taratibu zote
za kisheria.

Licha Mfuko huu kuanzishwa


na Sheria ambayo ipo kwenye
mchakato, yapo mambo mengi
ambayo ni mazuri kwa
wanahabari na tasnia kwa
ujumla katika Muswada huu,
-Hassan Abbas.

Zamu hii Muswada umeletwa kwa


mchakato wa kawaida wa kutunga
sheria ambapo umesomwa kwa

Jambo mojawapo katika hayo ni


kuunzishwa kwa Baraza Huru la
Habari. Baraza hili pamoja na kazi
nyingine litaandaa na kuidhinisha
kanuni na maadili ya taaluma ya
habari na kukuza maadili na viwango
vya taaluma baina ya wanahabari na
kampuni za habari.
Kwa kuwa hili Baraza litaundwa na
wanahabari wenyewe itakuwa rahisi
kuwekea kanuni na maadili
yanayofaa kwa wanataaluma na
kuwataka wayafuate. Hii itabadilisha
tasnia ya habari na kuifanya ya
kuheshimika. Hapa makanjanja
watakuwa hawana nafasi ya
kuichafua taaluma hii.

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura


(katikati) akisisitiza jambo kwa Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii
wakati wa majadiliano ya Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari leo Oktoba 21,
2016 Mjini Dodoma.

Pamoja na hayo Bi. Mazula


anaendelea kusema kuwa suala la
Jarida
Jarida
la Bunge
la Wizara
Juniya
- August
Habari 2016

12
7

Jarida
la Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
Jarida
la Bunge

Utamaduni na Sanaa
ni fursa kwa vijana
kujipatia Ajira
Na Lorietha Laurence

tamaduni na Sanaa ni vielelezo


vya utashi na uhai wa Taifa
ambapo pia ndio nyenzo kuu
muhimu katika kutambulisha jamii
kwa jamii kulingana na utaratibu
wa maisha.
Kwa
ekokutambua umuhimu
Wizara wa Sanaa
ya

na Utamaduni katika Taifa, Serikali ya


H
awamu ya kwanza chini ya hayati

Habari,Utamaduni,Sanaa
na
Michezo kwa kusimamia ujenzi wa
Mwalimu
Kambarage
Nyerere
mageti ya Julius
kielektroniki
katika kuboresha
mwaka
1962yatokanayo
ilianzisha rasmi
Wizara
makusanyo
na michezo
iinayofanyika
Uwanja lengo
wa likiwa
Taifa.
ya
Vijana na Utamaduni

kuanzisha sera na kuratibu shughuli


Hizo ni
zikitolewa
kwa
zote
zapongezi
sanaazilizokuwa
na utamaduni
katika
uongozi wa Wizara kutoka kwa wadau
Taifa.

wa michezo hivi karibuni mara baada ya


kuzinduliwa kwa mfumo wa kisasa wa
Katika
kipindi
hichoambayo
kilianzishwa
mageti ya
kieletroniki
hutumia
kikundi
cha ambazo
sanaa Ilala
kadi maalumu
ndiyo Sharriff
huruhusu
Shamba
ambacho kilianza
na kikundi
mageti kufunguka
na mtu
kupita.
cha
mwaka
ikifuatiwa
Hivyongoma
basi namna
hiyo1964
ya mageti
hayo
yanavyofanya
kazi ndiyo
huleta
tafsiri
na
sarakasi mwaka
1976 na
baadaye
ya mfumo wa
ya kieletroniki.
kufuatiwa
namageti
maigizo
mwaka

1974,mnamo 1981 Serikali iliamua


Akizungumza katika makabidhiano ya
kuhamisha
chuo na kukipeleka
mageti hayo ya kieletroniki yaliyoko katika
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam

Bagamoyo ambapo mpaka leo ndipo


ilipo Taasisi ya Sanaa na Utamaduni
Bagamoyo (TaSUBa).
Mwaka 1982 serikali kupitia TaSUBa
ilianzisha Tamasha la Sanaa na
Utamaduni Bagamoyo ambalo
lilikuwa likiwakutanisha wasanii wa
fani mbalimbali ili kuonyesha umahiri
wao katika sanaa na utamaduni huku
ikiwa
nyenzo ya kuendeleza
Waziri ndio
wa Habari,Utamaduni,Sanaa
na
sekta hizo
kwa wageni
vizazi
Michezo,
Mhe.Nape
Mosesna Nnauye
vijavyo.
alisema kwa kufanikisha hilo kumeifanya
Tanzania kuwa nchi ya kwanza kuwa na
Tokea
kuanzishwa
mageti ya
kisasa katikakwake
ukanda mwaka
huu wa
Afrika
1 9 8 2Mashariki.
Ta m a sNa
h ahiil ani sehemu
S a n a anzuri.
na

Utamaduni limekuwa kivutio kikubwa


Kukamilika
kwa ujenzi
wa mbalimbali
mageti hayo
kwa kujumuisha
watu
kunafuatiwa na agizo la Waziri Mkuu
kutoka ndani na nje ya nchi na ndio
Mhe.Kassim Majaliwa alipofanya ziara
Tamasha
Kongwe
la Sanaa
na
ya kikazi uwanjani
hapo mnamo
Februari
Utamaduni
nchiniWaziri
ambapo
17,2016
na hapa
kumwagiza
wa
malengo ya kuanzishwa
ni
Habari,Utamaduni,Sanaa
nakwake
Michezo
p a m o j a kuwa
n a kujenzi
u o n huo
y e sunakamilika
ha kazi
kuhakikisha
mbalimbali
sanaa
kwaniwananchi
kwa
haraka zakwa
kuwa
sehemu
ya
ujenzi
w a mkataba
B a g a mwa
oyo
n a wa
m auwanja.
eneo
yanayozunguka ikiwa ni njia ya
Pamoja
k u p i m na
a hayo
k i w aWaziri
n g o Nnauye
c h a ualieleza
sanii
kuwa mfumo huo umeandaliwa na
kilichofikiwa kwa mwaka.
Kampuni ya kizalendo ya SELCOM
Jarida
Jarida
la Bunge
Tume
la Wizara
yaJuni
Taifa
ya- Habari
August
ya Uchaguzi
2016

Malengo mengine ni pamoja ni


kuelimisha jamii kwa kutumia njia
mbalimbali za sanaa ,kutambulisha
Taifa ,kuburudisha jamii,kubadilisha
mawazo na kujenga mahusiano
miongoni mwa wasanii wa ndani na
nje ya nchi,kutoa mafunzo ya sanaa
kwa vitendo,warsha na semina
pamoja na kutoa fursa kwa
wajasilimiamali ya kutangaza na
kuuza bidhaa zao.
Kupitia tamasha hilo tasnia za Sanaa
na Utamaduni imeweza kukua nchini
na kutengeneza fursa nyingi
zinazowawezesha vijana kujiajiri na
kujipatia kipato hivyo kuleta tija katika
maisha yao na jamii kwa ujumla
kupitia vipaji vyao kwa kubuni sanaa
mbalimbali ambazo mbali na
kuongeza kipato, pia zinasaidia
kutangaza Utamaduni wa
Matanzania ndani na nje ya nchi.
Tamasha hili lina hadhi ya kitaifa na
kimataifa kwa kuwa limekuwa
likijumuisha ushiriki wa vikundi vya
sanaa vya hapa nchini na nje ya nchi

Jaridana
laMichezo
Bunge
Jarida la Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa

7
zikiwemo Kenya,Ujerumani,Norway,
Argentina na Japan.
Katika kuadhimisha Tamasha la 35
lililokuwa na kauli mbiu ya SANAA
N A U TA M A D U N I K WA
MAENDELEO YA VIJANA Naibu
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa
na Michezo Mhe.Anastazia
Wambura anasema kauli hiyo
imekuja wakati muafaka ambapo
Serikali ya Awamu ya Tano ina
ajenda mahususi ya kuhakikisha
vijana nchini wanatumia fursa zote
zilizopo katika kujipatia ajira kwa
ustawi wa maisha yao.
Mhe. Anastazia anaongeza kwa
kueleza kuwa tasnia hizo zimegusa
kona zote za Utamaduni na Sanaa
kwa kushirikisha ngoma za
asili,maigizo ,maonyesho,filamu
,sanaa za ufundi na muziki na hivyo
kuwapa vijana mwanya wa kuchagua
kazi zipi za Sanaa na Utamaduni
zinawafaa katika kujiajiri na kuchukua
hatua ya kuzitumia kwa maslahi
binafsi na taifa kwa ujumla.
Vijana huu ni wakati muafaka wa
kutumia fursa zilizopo katika tasnia
ya sanaa na utamaduni kwa
maendeleo yenu na taifa kwa jumla
huku mkiimarisha ushirikiano na
mshikamano baina yenu anasema
Mhe. Anastazia.

Pia Mhe.Anastazia aliwataka wasanii


kuimarisha umoja na mshikamano
na kuitambua sanaa kuwa ni ajira
ambayo kwa kiasi kikubwa inasaidia
katika kubadilisha hali ya maisha yao
na kupelekea kufanya mambo
makubwa na mazuri.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa
Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa
na Michezo, Prof.Elisante Ole Gabriel
amewataka wasanii kutumia kazi za
sanaa katika kuelimisha jamii
umuhimu wa kufanya kazi kwa
manufaa yao binafsi na nchi kwa
ujumla.
Wa s a n i i m k i d h a m i r i a j a m b o
hufanyika na uwezo wa kufanya
hivyo mnao,ni vizuri mkatumia
sanaa yenu kuwaelimisha wananchi
manufaa ya kufanya kazi kwao
wenyewe na Taifa kwa ujumla,
anasema Prof.Ole Gabriel.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi ya Sanaa na Utamduni
Bagamoyo (TaSUBa) Dkt.Herbert
Makoye anasema tasnia ya sanaa
na utamaduni inahitaji elimu tofauti
na vile jamii inavyoichukulia kuwa ni
kipaji peke yake ndio
kinachomuwezesha msanii kufanya
sanaa bali elimu ya sanaa inahitaji
zaidi ili kuwawezesha vijana kujifunza
kuhusu tasnia hizo kwa ajili ya zao
bora ya kazi zao.

13

Ni budi jamii kuondokana na dhana


potofu ya kuziona tasnia hizi zipo
kwa ajili ya watu waliokosa nafasi ya
kwenda shule kitu ambacho si kweli
bali muelewe kuwa tasnia hizi
zinahitaji elimu na kujifunza zaidi ili
kuwa kuifanya kazi kwa umakini na
uelewa wa kutosha anasema Dkt.
Makoye.
Dkt.Makoye anaeleza kuwa
kumekuwapo na changamoto
mbalimbali wakati wa kuandaa
maadhimisho hayo ikiwemo ukosefu
wa wafadhili wa uhakika ,ushiriki wa
wasanii wachache kwa kukosa fedha
za kuwawezesha kushiriki ,hata hivyo
aliahidi kushirikisha wadau wa tasnia
hizo mbili ili tamasha la 36 liwe la
tofauti na kipekee na kujumuisha
wasanii wengi zaidi.
Mmoja wa washiriki wa tamasha hilo
mwanamzuki,Vitalis Maembe alitoa
p o n g e z i k w a Ta S U B a k w a
kuendeleza tamasha hilo ambalo
limekuwa jukwaa pekee la
kuunganisha wasanii kutoka sehemu
mbalimbali duniani na hivyo kupata
fursa ya kuzitangaza kazi zao na
kushirikiana kimawazo.

Naibu Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo
Mhe. Anastazia Wambura (katikati)
akicheza muziki ikiwa ni ufunguzi wa
Tamasha la 35 la Sanaa na
Utamaduni lililofanyika September
26 Wilayani Bagamoyo Mkoa wa
Pwani chini ya uratibu wa Taasisi ya
Sanaa na Utamaduni
Bagamoyo(TaSUBa).

Jarida
Jarida
la Bunge
la Wizara
Juni
ya- August
Habari 2016

14
9

Jarida
la Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
Jarida
la Bunge

Jitihada za Serikali
katika kuendeleza Sekta
ya Filamu nchini
Na Shamimu Nyaki

atika kuhakikisha Filamu za


hapa nchini zinafanya vizuri
katika soko la ndani na nje ya
Tanzania Serikali imedhamiria
kusimamia kwa ukamilifu
utengenezaji na uuzaji wa kazi za
sanaa ambazo ni halisi na zenye
maadili kwa jamii.
Kupitia Wizara ya Habari,Utamaduni,
Sanaa na Michezo chini ya Waziri
wake Mhe. Nape Moses Nnauye,
ambayo ndio imepewa dhamana ya
kusimamia Sekta hiyo tayari
imeshaweka mikakati mbalimbali ya
kuhakikisha kuwa sekta hiyo
inasonga mbele zaidi katika soko la
ndani na nje.
Miongoni mwa mikakati ambayo
Serikali imeweka kwanza ni
kuhakikisha kazi za sanaa
zinatengenezwa katika ubora
unaotakiwa kwa kuwaagiza wasanii
kufanya hivyo ili iwe rahisi
kupambana na mianya yote ya
uharamia wa kazi za sanaa ikiwemo
kuuza kazi ambazo sio halisi kwa
kukosa kibali kutoka Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA),kupunguza
bidhaa za sanaa za nje zinazoingia
nchini kinyume na sheria.
Hivi karibuni Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na
Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye
alipozindua filamu ya Sikitu
iliyotayarishwa na kutengenezwa na
kampuni ya Kajala Entertainment
alitoa agizo kwa wadau wa kazi za
sanaa kutengeneza filamu ambazo
zitakuwa zina soko kubwa ndani na
nje ya nchi na ameahidi kupambana

na wale wote wanaojihusisha na wizi


wa kazi za wasanii kwa kuziuza na
kuzisambaza kinyume na Sheria
wakati wowote.
Nataka niwahakikishie wasanii na
watengenezaji wa Filamu kwamba
kazi hii nimeianza na nitaendelea
nayo na hatutoshindwa bali
tutashinda na nawaonya wanaofanya
kazi ya kuiba kazi za wasanii waache
mara mojaAlisema Mhe.Nape.
Huu ni mwanzo mzuri wa kuendeleza
Sekta hii kwakuwa ni sekta ambayo
imeajiri vijana wengi ambao watapata
maendeleo na pia kuitangaza nchi.
Mhe. Waziri aliongeza kuwa Serikali
itaendelea kujenga misingi mizuri
kwa wasanii wa tasnia ya filamu kwa
kuhakikisha wanapata soko ndani na
nje ya nchi ambapo kwa soko la
ndani amewaomba wadau wa sanaa
kushirikiana na Serikali kuangalia njia

nzuri ya kuonyesha filamu za ndani


ikiwemo kuwepo vibanda
vinanyoonyesha filamu za kitanzania
kuwa kumbi maalum kwa ajili ya
kuonyesha filamu hizo.
Ni wazo zuri la kubadilisha vibanda
kuwa kumbi maalumu kwa kuwa
itarahisisha kutangaza filamu za
wasanii kwani itakuwa rahisi kwa
mwananchi wa kawaida kuchangia
kiasi kidogo cha pesa
kitakachomuwezesha kupata elimu
na burudani na kuleta hamasa kwa
wananchi kupenda kutazama filamu
za hapa nchini.
Aidha, jitihada nyingine
zinazotekelezwa na Serikali ni
kuhakikisha kuwa kazi zote za filamu
kabla ya kwenda sokoni zinakuwa
na vibali vyote vinavyotakiwa kama
vile sheria ya Filamu na Michezo ya
kuigiza Na.4 ya mwaka 1976
inayosimamiwa na Bodi ya Filamu
Tanzania.

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi.Joyce Fisoo akitoa neno la shukrani
wakati wa ufunguzi wa mafunzo maalum ya siku mbili ya kuwajengea uwezo wasanii
na watarishaji wa filamu wa michezo ya kuigiza yaliyofanyika tarehe 21 na 22 Oktoba
mwaka huu Mkoani Morogoro,kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Bw. Michael Joseph.

Jarida
Jarida
la Bunge
la Wizara
Juniya
- August
Habari 2016

10

10

Jarida la Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo

9
Sheria ya Baraza la Sanaa Tanzania
(BASATA) Na.23 ya mwaka 1984,
Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki
Na.7 ya mwaka 1999 inayosimamiwa
na Chama cha Hakimiliki na
Hakishiriki ( COSOTA) pamoja na
Sheria ya Ushuru wa Bidhaa Sura ya
147 chini ya kanuni za stampu kwa
bidhaa za Filamu na Muziki ya
mwaka 2013 inayosimamiwa na
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Mhe. Nape alisema kuwa hatua hii ni
muhimu sio tu kwa manufaa ya
wasanii lakini pia katika kutekeleza
agizo Mhe.Rais wa Awamu ya Tano
wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania. Mhe.Dkt.John Pombe
Magufuli la kuwataka wanachi kulipa
kodi na kununua bidhaa halisi kwa
kutoa risiti na kupambana na wizi wa
kazi za sanaa nchini linasimamiwa
ipasavyo.
Hivi ndio vyombo vilivyopewa
dhamana ya kusimamia tasnia hii na
tayari vinaonesha dhamira ya dhati
kuhakikisha tasnia inasonga mbele
ambapo Kwa upande wa Bodi ya
Filamu Tanzania ambayo ina jukumu
la kutoa kibali cha kutengeneza
filamu,kukagua filamu kabla
haijaenda sokoni inasimamia kwa
ukamilifu jukumu hilo.
Katika hilo Katibu Mtendaji wa Bodi
ya Filamu Tanzania, Bibi Joyce
Fissoo alipokutana na viongozi wa
Mashirikisho ya Filamu nchini hivi
karibuni alisema kwamba Bodi yake
inahakikisha kuwa hakuna filamu
inayokwenda na itakayokwenda
Sokoni bila kufuata Sheria zote
zinazosimamiwa na Bodi hiyo
ikiwemo Sheria ya Filamu na
Michezo ya kuigiza kuigiza Na.4 ya
mwaka 1976.
Bibi Joyce ameongeza kuwa wasanii
wa filamu wanapaswa kuwa na tabia
ya kujifunza zaidi kuhusu filamu
kwakua ni sekta ambayo inabadilika
mara kwa mara kutokana na
maendeleo ya teknolojia.
Nawashauri muwe na utamaduni

wa kupenda kujiendeleza kielimu na


kupenda kujifunza mara kwa mara
kwa vile tasnia ya filamu inabadilika
mara kwa mara kutokana na
maendeleo ya sayansi na teknolojia
ili muweze kumudu soko la
duniaalisema Bibi Joyce.
Aidha,Bibi Joyce amewataka wasanii
kutengeneza filamu zenye maadili ya
kitanzania ambazo zitatangaza vizuri
Utamaduni wetu na kuepuka
kutengeneza filamu ambazo kwa
namna moja ama nyingine zinakiuka
maadili kwani endapo kutakuwa na
filamu ya aina hiyo Bodi yake
italazimika kuifungia.
Hakikisheni Filamu
mnazotengeneza zina maadili mazuri
ya Taifa letu epukeni kutengeneza
filamu ambazo hazina maadili
ikibainika mtayarishaji amefanya
hivyo hatua kali za kisheria
zitachukiliwa dhidi yake na filamu
hiyohaitaruhusiwakwenda
sokonialifafanua Bibi Joyce.
Katibu Mtendaji huyo amesema
kuwa Serikali itasimamia kwa
umakini filamu za hapa nchini kwa
kutoa mafunzo kwa vijana ili wafanye
kazi zenye ubora ndani na nje na
amewashauri kujiunga katika vyama
ili iwe rahisi kutambuliwa.
Kuwepo katika vyama ni msingi
mkubwa wa mafanikio ,fuateni katiba
kuweni na nidhamu katika kazi zenu
na pia muwe na vipaumbele bora
alisema Bibi Joyce.
Yote haya yanatekelezwa na Serikali
kwa ajili ya kuendeleza tasnia hii ili
iwanufaishe watu wengi na
maendeleo nchikwa ujumla na tayari
wadau wenyewe wa tasnia
wameipongeza Serikali kwa hatua
hiyo.
Naye Rais wa Shirikisho la Filamu
Tanzania,Bw Simon Mwakifwamba
ameishukuru Serikali kwa jitihada
inayofanya kukuza tasnia ya Filamu
kwa kutatua changamoto mbalimbali
zilipo katika tasnia hiyo ikiwemo wizi
wa kazi zao pamoja na kukahikisha
kuwa filamu za nje zinadhibitiwa kwa
kuingizwa nchini kwa njia sahihi na
haziathiri soko la filamu za ndani.
Jarida la Wizara ya Habari

Bw. Mwakifwamba pia ameishukuru


Serikali kwa kuanzisha sekta mpya
ya sanaa na kusema kuwa ni sekta
ambayo itakuwa mkombozi kwa
wasanii kwa kuwa itakuwa rahisi
kwao kutambulika na kuahidi kutoa
ushirikiano mzuri katika sekta hiyo.
Tunaishukuru Serikali kwa kuona
umuhimu wa kazi zetu na jinsi
inavyopambana kuhakikisha kuwa
kazi zetu zinatambulika na jinsi
inavopambana na wezi wa kazi zetu
Alisema Bw. Mwakifwamba.
Ili azma ya Serikali ya kuikuza tasnia
hii ifanikiwe ni vyema kwa wasanii
wenyewe kwanza kuanza
kutengeneza filamu zenye ubora
kuanzia soko la ndani mpaka nje
zenye maadili zinazopinga matendo
maovu kwa kuwa jamii ya sasa
imepanuka kimawazo kutokana na
kukua kwa teknolojia katika kila sekta
hivyo kwa kuzingatia hilo wasanii
wanayo nafasi ya kutumia sanaa yao
kuelimisha kufuata sheria zote
zinazotakiwa katika utengezaji na
uuzaji wa filamu.
Ni wakati sasa kwa wasanii
kutengeneza kazi nzuri zenye ubora
utakaofaa ndani na nje ya nchi
ambazo zitasaidia kuitangaza nchi na
wao wenyewe kupitia kazi zao
ambazo zitawaletea mafanikio
makubwa kama walivyofanikiwa
wasanii Single Mtambalike (Richie
Richie) pamoja na Elizabeth Michael
(Lulu) ambao hivi karibuni walipata
tuzo nchini Nigeria kutokana na
filamu bora walizotengeneza.

Nataka niwahakikishie
wasanii na watengenezaji
wa Filamu kwamba kazi
hii nimeianza na
nitaendelea nayo na
hatutoshindwa bali
tutashinda na nawaonya
wanaofanya kazi ya kuiba
kazi za wasanii waache
mara moja
-Mhe. Nape Nnauye

Jarida la Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo

Umuhimu wa Filamu
katika ukuzaji wa Lugha
ya Kiswahili
Na Genofeva Matemu

ugha ni kitambulisho kikuu cha


Mawasiliano katika Taifa lolote
lile. Aidha Tanzania ina zaidi ya
lugha za kijamii zipatazo 150 lakini
zaidi ya asilimia 95% ya
Watanzania wanao uweledi na
ujuzi wa kuzungumza lugha ya
Taifa yaani Kiswahili.
Kwa hivi sasa, lugha ya Kiswahili
imekuwa ya 10 duniani kwa kuwa na
wazungumzaji milioni 100.
Aidha, lugha za kijamii zimeendelea
kutoa mchango mkubwa wa
kushehenesha na kuneemesha
lugha ya Kiswahili kimsamiati. Lugha
ya Kiswahili imekuwa na kaida ya
kutohoa maneno kutoka lugha
anuwai za kigeni katika kukidhi
mahitaji ya kiistilahi ya wakati wa
maendeleo ya sayansi na teknolojia.
Filamu ni moja ya chombo
kimojawapo kilichoweza kuchangia
katika kukuza lugha adhimu na aushi
ya Kiswahili kwani ni nyenzo
mojawapo inayotumika katika
upashanaji habari, kuburudisha,
kuelimisha, kutoa mafunzo/
kuadilisha, kukosoa, kuchochea lakini
pia ni kielelezo cha utambulisho wa
mila, desturi na utamaduni wa jamii.
Filamu ni utanzu unaofumbata
tamaduni za watu wa jamii ambapo
h u tu mia lugha i na yowe zesh a
wahusika kutumia lugha faafu katika
kufikisha ujumbe tarajiwa kwa jamii
husika.
Uandaaji wa kazi za filamu unajikita
katika kufikisha ujumbe kwa hadhira

na jamii kwa lengo la kurithisha


utamaduni wa jamii na marudi huku
Lugha ya Kiswahili ikitumika kama
kibebeo muhimu sana
kinachozingatia tanzu zote za Fasihi,
ufasaha, usanifu na usahihi wa lugha,
na maudhui yanayowasilishwa kwa
jamii lengwa.
Aidha kazi za Filamu zinajinasibu,
kutengenezwa na kuoneshwa kwa
hadhira kwa lugha ya Taifa Kiswahili
na filamu zingine hutafsiriwa kwa
lugha za kigeni kwa minajili ya
kufikisha ujumbe uliolengwa kwa
hadhira kubwa yenye kuzungumza
lugha ya kigeni.
Mkurugenzi Msaidizi Lugha kutoka
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo Bibi. Shani Kitogo
anasema Filamu zimechangia kwa
kiasi kikubwa katika kukuza lugha ya
Kiswahili kutokana na matumizi ya
lugha za kijamii ambazo msamiati
wake hutumika kukuza lugha ya
Kiswahili.
Bibi. Shani anaendelea kufafanua
Filamu ya Chite ukae, Chungu,
Odama, Kinyamkera, Mwenembago,
Mzimu wa Kolelo, na nyinginezo ni
mifano inayodhihirisha kwamba
filamu hukuza msamiati wa lugha ya
Kiswahili kutoka lugha za kijamii na
kutangaza Urithi wa Utamaduni wa
Mtanzania.
Hali ilivyo kwa jamii ya kileo ni vigumu
sana kwa shwaibu na ajuza kusimulia
hadithi kwa wajukumu zao, haya ni
matokeo ya kubadilika kwa mifumo
ya maisha ya kila siku ya jamii
kutokana na maendeleo ya sayansi
na teknolojia yaliyofikiwa na jamii
zetu kwa sasa.

Jarida la Wizara ya Habari

Filamu imebeba dhima ya tambo la


hadithi ambayo ni mojawapo ya
utanzu wa fasihi simulizi
inayowasilishwa kwa njia ya picha
zilizo katika mwendo, na
inapotekeleza wajibu huu filamu
inakuwa imetekeleza wajibu
mwingine wa ukuzi na uenezi wa
lugha na kurithisha amali za jamii.
Afisa Utamaduni Bw. Simon Maqwai
amesema kuwa Lugha ya Kiswahili
imekua ikitumika sana katika kazi za
filamu hivyo kuifanya kuwa chombo
cha mawasiliano kwani baadhi ya
filamu hutengenezwa katika lugha za
kigeni na kutafsiriwa kwa lugha ya
Kiswahili.
Hadhira nyingi duniani zimekua
zikifikiwa na maudhui ya filamu za
waswahili na wengi kuvutiwa nazo na
hivyo kuweka juhudi kubwa za
kujifunza lugha ya Kiswahili hali
ambayo imesababisha lugha ya
Kiswahili kukua, kuenea na
kuendelea kushamiri duniani kote
amesema Bw. Simon.
Ni ukweli usiopingika kuwa katika
nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki
kumekuwa na wapenzi wengi wa
filamu za kitanzania. Hili lilipata
dhihiko katika Kongamano la Chama
cha Wanafunzi wa Kiswahili Afrika
Mashariki (CHAWAKAMA) lilifanyika
mwezi Septemba, 2016 Mjini
Zanzibar.
Wanafunzi kutoka Nchi za Uganda
na Burundi waliohudhuria
Kongamano hilo walikiri kwamba
wanavutiwa sana na lugha ya
Kiswahili inayotumiwa katika Filamu
zetu. Aidha, walidhihirisha kwamba
filamu za Kitanzania zinawasaidia
kujifunza lugha ya Kiswahili ambayo

10

Jarida la Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo

hutumiwa na wahusika katika filamu


kufikisha ujumbe kwa hadhira
lengwa.
Kuna baadhi ya watu hupenda
kusikiliza nahau za Bi. Rihama na Bi.
Hindu ambao wanamisemo na lahaja
za kimtangata, kiunguja ambayo
huvutia watazamaji mfano
aliyekutwika ndiye atakutua;
Nyumba hii ni ulimwengu wa
kambale; wote wanamasharubu;
Mtoto, Mama, Maba hajulikana mke
wala mume Pia ukimtazama Mzee
Majuto ambaye hutumia lugha ya
mvuto katika kufikisha ujumbe.
Hii humaanisha kuwa maudhui ya
kazi za filamu zinasawiri utajiri wa

misemo na nahau za lugha ya


Kiswahili zinazotumika katika jamii,
kwa lengo la kuvutia na kuepusha
hadhira kuchoka na kuchusha pindi
watazamapo filamu husika.
Mtaalamu wa Tehama Bw. Malekela
Maingu amesema kuwa uhifadhi wa
Filamu kwa njia ya kisasa ya
Kielektroniki husaidia katika kuhifadhi
lugha iliyotumika katika filamu husika
na kuifanya idumu kwa muda mrefu
hivyo kuifikia hadhira inayotumia
mitandao pia inawezesha uhifadhi
wa kazi za filamu inayowasilishwa na
maktaba hai kwa njia ya masimulizi
yanayoambatana na picha jongefu.

yenye staha katika kazi za filamu ili


kufikisha ujumbe kwa hadhira lengwa
na kwa kuzingatia rika, jinsi,
mandhari, itikadi, falsafa, n.k. hivyo
kutambulisha mila, desturi na
utamaduni na ustaarabu wa jamii
zetu.
Lugha ni kielelezo na kibebeo cha
utamaduni wetu. Uzingatiaji wa
ufasaha, usanifu na usahihi wa lugha
ya Kiswahili katika uandaaji na utendi
wa kazi za Filamu utawezesha
kukua, kuenea, kuendelea na
kushamiri kwa lugha aushi na adhimu
ya Kiswahili, Utamaduni na Maadili
ya Mtanzania.

Ni vyema wasanii wakatumia lugha

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura (kushoto) akipokea Kamusi kuu ya
Kiswahili kutoka kwa Katibu Mtendaji Baraza la Kiswahili Taifa (BAKITA) Dr. Selemani Sewange alipotembelea ofisi za BAKITA
kufahamu mambo mbalimbali yanayofanywa na Taasisi hiyo Machi 2016.

Jarida la Wizara ya Habari

18

Jarida la Bunge

Limeandaliwa na:
Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
Jengo la PSPF Golden Jubilee
Ghorofa ya 8
Mtaa wa Ohio
S.L.P 8031, Dar es Salaam-Tanzania
Faksi : (+255) 22 2126834
Simu : (+255) 22 2126826
Tovuti : www.habari.go.tz

Jarida la Bunge Juni - August 2016

Вам также может понравиться