Вы находитесь на странице: 1из 17

Jarida la

Wizara ya Habari
Utamaduni, Sanaa na Michezo

DESEMBA, 2016

TOLEO LA 004

Miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara

Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa


na Ufisadi na Tuimarishe Uchumi wa Viwanda
kwa Maendeleo Yetu
ZWI

HALIU

www.habari.go.tz

Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na


Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu

Bodi ya Uhariri
Mwenyekiti
Zawadi Msalla

Wajumbe
Genofeva Matemu,
Lorietha Laurence,
Raymond Mushumbusi,
Anitha Jonas,
Shamimu Nyaki

Msanifu Jarida
Benedict Liwenga

Jarida hili hutolewa na:

Wizara ya Habari Utamaduni


Sanaa na Michezo
Jengo la PSPF (Golden Jubilee) Ghorofa ya
8Mtaa wa Ohio
S.L.P 8031, Dar es Salaam-Tanzania
Faksi : (+255) 22 2126834
Simu : (+255) 22 2126826
Tovuti: www.habari.go.tz

Jarida la Wizara ya Habari

Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na


Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu

TAHARIRI
HONGERA WAZIRI NAPE KWA KUWAKUMBUKA BLOGGERS TANZANIA
Hivi karibuni Chama cha Bloggers (Tanzania Bloggers Network) walitoa
mafunzo kwa wanachama wake ili kuwaongezea uwezo katika masuala ya
habari na matumizi ya Mitandao ya kijamii katika kuhabarisha Umma.
Mitandao ya kijamii kwa miaka ya sasa imekuwa ni njia ya haraka na rahisi
kufikisha habari Duniani na watu kwa sasa wanatumia mitandao ya kijamii
hasa Blogu katika kuangalia mambo mbalimbali yanayojiri Duniani.
Kutokana na ukuaji huu wa matumizi ya mitandao ya kijamii, Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye
aliwaeleza washiriki wa mafunzo hayo kuwa, Serikali inatarajia kuja na
mpango wa kuanzisha Tuzo za Bloggers Tanzania hapo mwakani ambapo
itakuwa ni fursa ya kuikuza tasnia ya Habari kwa njia ya Blogu.
Wakati wa Ufunguzi wa mafunzo hayo, Mhe. Nape Nnauye alisisitiza kuwa
Serikali inazitambua Blogu kuwa ni kati ya njia za usambazaji rahisi wa
habari na matukio mbalimbali yanayojiri na ndiyo njia inayokuwa kwa kasi
Duniani.
Serikali inazitambua blogu na nimeshaanza mchakato wa kuanzisha Tuzo
kwa Bloggers ili tuwe na ushindani katika hili na kukuza tasnia ya habari
kupitia Blogu, alisisitiza Mhe. Nnauye.
Kwa Bloggers sasa hii ni fursa ya kipekee ya kuikuza tasnia ya Habari
kupitia Blogu na mitandao ya kijamii, hivyo tuichukue fursa hii katika
kuitangaza nchi yetu na fursa zilizopo katika kutangaza utalii na uwekezaji
nchini.

Jarida la Wizara ya Habari

ii

iii

Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na


Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu

Uk. 1

Waandishi wa habari washauriwa kutumia Wataalam


waliopo vijijini kuelimisha Watanzania kuhusu lishe
bora.

Uk. 3

Sera itakayobadilisha Sekta ya Sanaa nchini yaja.

Uk. 5

Taaluma na weledi kiini cha ubora wa Filamu.

Uk. 7

Fahamu Azimio la kupinga matumizi ya dawa za


kuongeza nguvu michezoni.

Uk. 9

Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016 kuboresha


upya Taaluma ya Uandishi wa habari.

Uk. 11

Matukio mbalimbali katika Picha.

Jarida la Wizara ya Habari

Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na


Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu

Waandishi washauriwa kutumia


Wataalam Vijijini kuelimisha
Watanzania kuhusu lishe bora

Na Raymond Mushumbusi

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akikabidhi
zawadi ya tablet na shilingi million 1.5 kwa Bi.Tumaini Msoyowa mshindi wa kwanza wa
Shindano la mwandishi Bora wa habari zinazohusu lishe kutoka gazeti la Mwananchi
katika hafla iliyofanyika Jijini Dar es Salaam Novemba 22, 2016.

ekta ya Habari ni moja kati ya


sekta muhimu katika maendeleo
ya nchi na ikitumika vizuri inaweza
kuchangia kuleta mabadiliko na
maendeleo ya taifa kwa ujumla.
Katika kuliona hilo waandishi
wa habari nchini wameshauriwa
kutumia kalamu zao kuielimisha
jamii ya watanzania hasa katika
masuala muhimu ya kijamii
hususani suala la lishe bora
katika hafla iliyofanyika Jijini
Dar es Salaam hivi karibuni.
Ushauri huo umetolewa hivi
karibuni na Naibu Waziri wa Habari

Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.


Anastazia Wambura alipokuwa
akitoa zawadi kwa waandishi wa
habari bora wa habari za lishe
Tanzania na kusisitiza kuwa
Serikali imelitilia mkazo suala la
lishe na imeamua kutenga jumla
ya Dola za kimarekani Millioni 115
kwa ajili ya kuboresha lishe ikiwa
ni katika mpango wa maendeleo
wa miaka mitano 2016/2021
na
mkakati
wa
kuboresha
lishe kwa mwaka 2016/2021.
Mhe.
Anastazia
Wambura
aliongeza kuwa bado kumekuwa
na changamoto katika upatikanaji

wa lishe bora nchini ikiwemo


kuwepo kwa tamaduni mbalimbali
zinazonyima fursa kwa watoto na
wakina mama kupata lishe iliyo bora.
Serikali imeingiza suala la lishe
katika mpango wa maendeleo wa
taifa wa miaka mitano na katika
kulitekeleza hili Serikali ya awamu
ya Tano itatenga dola million 115 kwa
ajili ya mkakati wa kuboresha lishe
nchini alisisitiza Mhe. Anastazia.
Katika sula la kuelimisha jamii
kuhusu
lishe
bora
Serikali
imewashauri
waandishi
wa
Habari
nchini
kuwatumia
Inaendelea Uk. 2

Jarida la Wizara ya Habari

Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na


Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu

Inatoka Uk. 1

wataalamu wa vijijini kuandika


habari
zinazoelimisha
jamii
kuhusu upatikanaji wa lishe bora.
Mhe.
Anastazia
Wambura
ameongeza
kuwa
waandishi
wa habari wawatumie maafisa
Afya waganga wakuu wa wilaya
na Mikoa kupata taarifa kamili
kuhusu lishe bora na upatikani
wake ikiwemo faidia za lishe
katika ukuaji wa binadamu.
Naomba waandishi wa habari
mtumie fursa ya uwepo wa maafisa
Afya, Waganga wa Wilaya na Mikoa
kupata taarifa sahihi juu ya lishe
bora na faida za lishe bora kwa
ukuaji wa binadamu ili tupunguze
tatizo la udumavu linalotukabili,
alisisitiza Mhe. Anastazia.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mtendaji wa Jukwaa la Lishe
Tanzania (PANITA) Bw. Tumaini
Mkindo alisema kuwa hali ya
lishe imeendelea kuimarika hasa
kwa miaka mitano iliyopita hili
linadhihilisha kuwa mikakati thabiti
iliyopo imesaidia kwa asilimia
kubwa kupambana na tatizo la
ukosefu wa lishe bora nchini.

Bw. Mkindo ameipongeza Serikali


kwa juhudu inazozichukua katika
kupanga mikakati na kuitekeleza
katika suala la upatikanaji wa
lishe bora nchini ili kuondokana na
suala la udumavu linaloleta athari
kubwa katika ukuaji wa Binadamu.
Aliongeza kuwa Jukwaa la Lishe
Tanzania litaendelea kushirikiana
na Serikali na wadau wengine
katika harakati za upatikanaji wa
lishe bora na kufikia malengo
ya Shirika la Afya Dunia (WHO)
yaliyosainiwa
na
Tanzania
yahusuyo masuala ya lishe pamoja
na kupunguza udumavu kwa
asilimia 40 ifikapo mwaka 2025.
Pia Katibu wa Jukwaa la
Wahariri Tanzania Bw. Neville
Meena aliwasisitiza waandishi
kuchangamkia fursa ya kuandika
na kuelimisha jamii kuhusu
upatikanaji wa lishe bora na
kuendeleza jitihada za Serikali
za kupunguza udumavu nchini.
Niwaombe waandishi wenzangu
tuliangalie
hili
kama
fursa
ya
kuelimisha
jamii
hasa
kutangaza vyombo vyetu na sisi
wenyewe piaalisema Meena.

Aidha mmoja ya waandishi wa


Habari na mshindi wa uandishi
Bora wa Habari za Lishe Bi
Tumaini
Msoyowa
alisema
kuwa fursa hii ni adhimu kwa
waandishi wa habari kuelimisha
jamii na kuendeleza mapambano
dhidi ya udumavu Tanzania.
Aliongeza kuwa waandishi wa
Habari wanapaswa kungalia mambo
muhimu yanayogusa jamii moja
kwa moja ambayo yatasaidia sana
kuiondoa jamii yetu katika matatizo
mbalimbali yakiwemo udumavu
kwa watoto chini ya miaka mitano.
Nawashauri waandishi wenzangu
tuangalie jamii yetu kwa jicho la
tatu tutumie kalamu zetu kuisaidia
jamii yetu kuondokana na matatizo
mbalimbali yanayoikumba jamii ya
kitanzania alisisitiza Bi Tumaini.
Ni wakati sasa wa waandishi wa
habari na watanzania kwa ujumla
kuendeleza juhudi za Serikali
kupambana na suala la udumavu
ambalo limekuwa ni changamoto
katika hatua za ukuaji kwa watoto
walio chini ya miaka mitano.

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akizungumza na
Waandishi wa habari, wadau wa harakati za upatikanaji wa lishe bora nchini pamoja na Wahariri
wa Vyombo vya habari katika hafla ya kuwatunuku tuzo Waandishi bora wa masuala ya lishe nchini
iliyofanyika Jijini Dar es Salaam Novemba 22, 2016.
Inaendelea Uk. 3
Jarida
Jaridala
laWizara
Nchi Yetu
ya Habari
2016

Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na


Tuunge
Mkono
Jitihada
Kupinga
Rushwa
na Ufisadi
Tuimarishe
Uchumi
waza
Viwanda
kwa
Maendeleo
Yetu na
Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu

Sera itakayobadilisha Sekta


ya Sanaa nchini yaja

Na Shamimu Nyaki

Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia James Wambura


akiangalia baadhi ya kazi za Sanaa kutoka kwa Wasanii wakati wa uzinduzi wa Tamasha
la Siku ya Msanii Duniani lilioandaliwa na Baraza laTaifa la Sanaa (BASATA) pamoja na
Kampuni ya Haak Neel Production lililofanyika hivi karibuni Jijini Dar es Salaam.

anaa ni chombo kinachoionesha


jamii kama ilivyokama tafsiri ya
neno sanaa inavyosema kuwa ni
ufundi anaoutumia mwanadamu
katika kuwasilisha fikra au mawazo
yaliyoko ndani ya akili yake kwa
namna mbalimbali kama vile mu
ziki,ushonaji,ususi,ufinyazi,mao
nyesho,uchongaji na kadhalika.
Sanaa kama kioo cha jamii husika
hufanya mambo makubwa matatu
ambayo hueleza juhudi iliyofanywa
na jamii ya watu,hueleza matatizo
ambayo jamii inabidi ipambane
nayo yakiwemo ya kijamii,kisiasa
na hata kiuchumi pia ni chombo

ambacho jamii inatumia kuhifadhi


na
kuwasilisha
kumbukumbu
muhimu
katika
maisha.
Hapa Tanzania Sanaa ilianza
kutumika mwanzoni mwa miaka
ya
1980
ambapo
ilitumika
kuwaelimisha
wanajamii
kujitambua na kuthamini vipaji
walivyonavyo kutokana na fani
mbalimbali zilizopo katika sanaa.
Ni lazima kukubaliana na usemi
kuwa sanaa ni tasnia mojawapo
yenye uwezo wa kuleta ajira na
faida ya kipato kwa watu binafsi,jamii
na Taifa iwapo itapewa kipaumbele

na kuwekewa mipango thabiti na


mahsusi kwaajili ya kuiendeleza.
Si hayo tu bali pia ni sekta ambayo
inampa
fursa msanii kuwa na
uwezo wa kufanya biashara kupitia
shughuli mbalimbali za sanaa.
Kwa kutambua umuhimu wa sekta
hii Serikali inakusudia kuandaa
Sera Mpya ya Sanaa kwa lengo
la kuunda sheria itakayosimamia
maslahi ya wasanii hapa nchini
na kuweka wazi majukumu ya
Serikali,wasanii na wadau wote
wa sanaa kutumia kikamilifu fani
zote za sanaa na kufafanua jinsi
Inaendelea Uk. 4

Jarida la Wizara ya Habari

Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na


Tuunge
Mkono
Jitihada
Kupinga
Rushwa
na Ufisadi
Tuimarishe
Uchumi
waza
Viwanda
kwa
Maendeleo
Yetu na
Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu

Inatoka Uk. 1

umma utakavyoshirikishwa katika


shuguli za sanaa kwa kuweka
taratibu mpya za kugharamia
uendeshaji wa shughuli za sanaa.
Katika Rasimu hiyo yapo mambo
mengi muhimu yaliyoainishwa
ambayo yataleta maendeleo katika
sekta ya sanaa. Katika hatua
ya kwanza Serikali imeandaa
Rasimu ya Sera ya Sanaa
kuhakikisha kuwa mifumo thabiti
ya kuratibu shughuli za utamaduni
inaanzishwa, kuanzisha mfumo
utakaowezesha jamii kutambua,
kumiliki, kuhifadhi na kuendeleza
tunu za kitaifa, ikiwa ni pamoja
na maliasili, madini na masalia ya
viumbe au zana na vifaa vya kale.
Sio hayo tu balikuhakikisha kuwa
mfumo wa kisheria wa kulinda kazi
na maslahi ya wasanii unawekwa,
Kuhakikisha kuwa utaratibu wa
kukabiliana na utandawazi ambao
unachangia katika mmomonyoko wa
maadili unaandaliwa, Kuhakikisha
kuwa, mifumo ya kurasimisha
tasnia
zote
za
utamaduni
unaanzishwa ili kutambua mchango
wake katika kukuza uchumi.
Katika sera hiyo kutakuwa na
utaratibu wa kuwatambua na
kuwaenzi wadau wa sekta ya
utamaduni waliochangia na kuipa
heshima nchi yetu kuhakikisha
kuwa mfumo wa kisheria wa
kulinda kazi na maslahi ya wasanii
unawekwa,
kuhakikisha
kuwa
mifumo na miongozo mbalimbali ya
kusimamia burudani inaboreshwa ili
kuzingatia maadili, mila, desturi na
kuenzi utamaduni wa Mtanzania,
Kujumuisha lugha ya Alama na
Maandishi ya Nukta Nundu ambazo
hazikuzingatiwa katika Sera iliyopita;
Sera
itawezesha
utekelezaji
shirikishi utakaohusisha wadau
mbalimbali wa sekta ya utamaduni.
Pia inaweka msisitizo katika kukuza,
kuimarisha, kulinda, kuhifadhi,
kuthamini na kurithisha Utamaduni

unaoshikika

na

usioshikika.

Sera inatambua mchango wa


sekta
ya
utamaduni
katika
kuimarisha
umoja
wa
taifa
na kujenga uchumi wa nchi.
Waziri wa Habari,Sanaa na
Michezo
Mhe. Nape Mosses
Nnauye alipokuwa akizungumza
katika kipindi cha TUNATEKELEZA
kinachorushwa na Televisheni
ya Taifa (TBC) alieleza kuwa
Wizara inaendelea na mchakato
wa kuandaa sera ya sanaa
ambayo
itakuwa suluhisho
katika uundaji wa Sheria nzuri
itakayosimamia kazi za Wasanii .
Mhe. Nape alieleza kuwa Serikali
inatambua uwepo wa changamoto
mbalimbali zinazowakabili wasanii
katika uendeshaji wa kazi zao hasa
kipato kidogo kisichoendana na
kazi zao,kazi zao kuingiliwa na watu
wasiohusika ambao wamekuwa
wakijinufaisha wenyewe na uuzwaji
holela wa kazi za wasanii kutoka nje.
Sera ya Utamaduni iliyopo sasa
ina mapungufu kwani haijaeleza
vizuri namna inavyowanufaisha
wasanii
na
kusimamia
kazi
zao.Alisema
Mhe.
Nape
Alisema
kuwa
watanzania
wanapaswa kujenga utamaduni
wa kujituma kuacha tamaduni
ambazo ni kinyume na maadili
ya
mtanzania
hasa
vitendo
vya ukeketaji kwa watoto wa
kike,ndoa za utotoni,mauaji ya
watu wenye ulemavu wa ngozi
(albino),mauaji ya vikongwe katika
baadhi ya Mikoa ya Kanda ya
Ziwa,pamoja na baadhi ya wazazi
kutosomeshwa watoto wa kike.
Sera hiyo ipo katika hatua za awali
ambapo
Serikali
imeshandaa
rasimu na imeipeleka kwa wadau ili
watoe maoni yao na mapendekezo
kwa
ajili
ya
kuiboresha
kabla
ya
kuanza
kutumika.
Jarida la Wizara ya Habari

Mhe. Anastazia Wambura naye


alisema kuwa, sera itaweka
utaratibu wa kuwawezesha watoto
wa mitaani kupata elimu na kuishi
maisha ya heshima,rasimu hii
pia
itahimiza, kuelimisha na
kuhamasisha wadau kujenga,
kutunza na kuendeleza maeneo
ya burudani, sera pia inaelekeza
kuwapo elimu ya fani za utamaduni
kufundishwa
kuanzia ngazi ya
elimu ya awali hadi elimu ya juu.
Toeni maoni katika rasimu hii ili
kujenga jamii yenye nidhamu,
ujasiri, uzalendo, utii, maadili na
inayothamini na kuenzi, mila,
desturi na utambulisho wake kupitia
Sanaa, alisema Mhe. Anastazia.
Mhe.Naibu Waziri pia amewaomba
wadau wote wa Sanaa kutoa maoni
yao katika kuboresha tasnia hii
yenye kubeba maeneo kama Muziki,
Filamu, Maonyesho, Ususi, pamoja
na Uchoraji ili kuwezesha tasnia hii
kujulikana na kuboresha mapato ya
Wasanii,na akasisitiza kuwa jitihada
hizo zimeanza kuzaa matunda
kwa kuungwa mkono na wadau
mbalimbali wa kitaifa na kimataifa.
Hata hivyo utaratibu ambao
umewekwa wa kupokea maoni
ni pamoja na Idara ya Sanaa na
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA)
kukutana na wadau wote wa sekta
ya Sanaa na kupokea maoni
yao moja kwa moja,kusambaza
dondoo kwa wadau wa sanaa
ili watoe maoni yatakayosaidia
kuboresha
Sekta
hiyo.
Ni wakati sasa kwa wadau wa kazi
za sanaa kutoa maoni yao katika
Rasimu hiyo ili kuweza kuiboresha
sekta ya Sanaa kama ambavyo
baadhi ya Wadau wameanza kutoa
maoni yao ikiwemo kuhamasisha
ushirikishwaji na elimu ya uhifadhi
na uendelezaji wa urithi wa
Utamaduni katika ngazi zote.

Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na


Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu

Taaluma na weledi kiini cha


ubora wa Filamu

Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo akizungumza na wadau wa sekta ya
filamu Jijini Mwanza katika kikao cha kujadili maendeleo ya filamu nchini.

Na Loreitha Laurence

aaluma ni mafunzo ya aina


yoyote
yanayomuwezesha
mshiriki kupata uelewa na stadi
kwenye eneo mahsusi ndani
ya tasnia hau fani husika na
kumuwezesha
kufanya
kazi
iliyobora kwa manufaa yake na jamii.
Aidha, Weledi ni utendaji au
utekelezaji
wa
majukumu
uliotukuka
kwenye
eneo
mahsusi ndani ya tasnia au fani
yawezekana akawa mwongozaji

wa filamu,mtunzi,mwandishi
muigizaji.

na

Taaluma na Weledi katika tasnia ya


filamu haviwezi kutenganishwa kwa
sababu vinakwenda sambamba
kwa kuwa kabla kitu hakijafanyika
au kutekelezwa kwa weledi,mhusika
lazima awe na taaluma ya
kutosha
itakayomuwezesha
kutumia maarifa na stadi za
kutosha kukamilisha jambo hilo
mfano mzuri ni tasnia ya filamu.

Filamu nyingi zinazotengezwa bila


kufuata weledi na taaluma mara
nyingi hukosa soko ambapo Bishop
Hiluka aneleza kukosekana kwa
mafunzo ya taaluma,watengenezaji
wa filamu na wasanii wa Tanzania
wamekuwa
watu
wanaolipua
kazi,wasiojali ubora,wanaoshindwa
kubuni na kujikuta wakiishia kunakiri
kazi za nje na hata kazi zao nyingi
hazizingatii mambo muhimu kwa
kisingizio cha bajeti kuwa kubwa.
Inaendelea Uk. 6

Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na


Tuunge
Mkono
Jitihada
Kupinga
Rushwa
na Ufisadi
Tuimarishe
Uchumi
waza
Viwanda
kwa
Maendeleo
Yetu na
Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu

Inatoka Uk. 5

Bishop Hiluka anaongeza kuwa


wengi waliomo katika tasnia ya filamu
wamekuwa hawana uthubutu kwa
sababu wamejawa na wogo,jambo
ambalo
limekuwa
linarudisha
nyuma maendeleo ya tasnia hii.

ambapo wengi wao wanakuwa


na mafunzo yasiyo rasmi huku
wakisema wao wamezaliwa na vipaji
vya uandishi,uongozaji na uandaaji
wa filamu na matokeo yake ni
kuandaa kazi zilizo chini ya kiwango.

Wasanii wa Tanzania wamekuwa


wakikwepa
kuhudhuria
makongamano,warsha,mafunzo
na semina mbalimbali za filamu
zinazoandaliwa
na
serikali
kupitia Taasisi zinahusika na
mambo ya filamu ikiwemo Bodi
ya Filamu Tanzania (BFT) na hii
inaonyesha ni kutokana na hofu
, kutokujiamini na kukosekana
kwa maelewano baina yao.

Hakuna mtu asiye na kipaji


tumeona wasanii wengi maarufu
duniani wenye vipaji lakini bado
waliingia darasa kupata elimu
zaidi ili kukuza nakuendeleza
vipaji vyao, alisema Dkt. Makoye.

Mwitikio wa wasanii katika kujifunza


kupitia
warsha
na
mafunzo
mbalimbali yanayoandaliwa kwa
dhumuni ya kuwaongezea stadi na
ubunifu umekuwa ni mdogo na hivyo
kupelekea waandaaji hao kuzalisha
kazi zisizo bora na hivyo kutokukidhi
kiwango cha soko la Kimataifa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi
ya Sanaa na Utamaduni ya
Bagamoyo (TaSUBa) Dkt. Herbert
Makoye anaeleza kuwa ili sanaa ya
Tanzania iwe ya Kimataifa na yenye
ubora inahitaji kuzingatia taaluma
na weledi ikiwemo mgawanyiko wa
majukumu katika kukamilisha kazi
hiyo lengo likiwa ni kutanua soko
la nje kama ilivyo kwa wenzetu wa
Nigeria na nchi nyingine za Afrika.
Akiwasilisha Mada ya umuhimu wa
taaluma na Weledi katika filamu
wakati wa mafunzo ya siku mbili
ya kuwajengea uwezo wasanii wa
filamu yaliyofanyika Oktoba 21 na 22
mwaka huu Mkoani Morogoro Dkt.
Makoye anaeleza kuwa waandaji
wengi wanajirundikia kazi na hivyo
kushindwa kufanya kazi kwa ustadi.

Dkt. Makoye alieleza kuwa kuna


aina mbalimbali za mafunzo ya
ukuzaji na uimarishaji wa taaluma
kupitia njia zisizo rasmi kama vile
kwa kuangalia wengine wanafanyeje
au
namna
wanavyotekeleza
jambo,pia
kushiriki
kwenye
kutekeleza
kazi
Fulani
na
kushirikishwa na mwenye taaluma
katika kutekeleza kazi husika.
Kwa upande wake Dkt. Mona
Kalinga Mkufunzi kutoka Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam anaeleza
kuwa katika kazi ya filamu kuna
watendaji wakuu ili kazi hiyo
ikamilike na kuwa bora ambao ni Mt
ayarishaji,Muongozaji,Mwandishi
wa Mswada wa filamu ,Msimamizi
wa
Mswada
na
Msimamizi
wa maeneo ya kupigia picha.
Aidha, Dkt. Mona anaongeza
kwa kueleza kuwa watayarisha
wengi wa filamu nchini wamekuwa
wakijitwika majukumu mengi jambo
linalopelekea kuzalisha filamu
zilizo chini ya kiwango au kwa
lugha nyingine zisizo na ubora.

Dkt. Makoye anaongeza kuwa


wasanii wa filamu wengi hawapati
mafunzo rasmi ya taaluma hii
Jarida la Wizara ya Habari

Anazidi kufafanua kuwa ili filamu iwe


bora na kukidhi soko la Kimataifa
basi ni budi taaluma na weledi
vizingatiwe ikiwemo mgawanyiko
wa kazi
kwa kufanya hivyo
kutaondoa mlundiko wa kazi kwa
mtu mmoja na hivyo kuwa makini
zaidi katika kuandaa kitu kilicho bora.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji
wa Bodi ya Filamu Tanzania
(TFB) Bibi.Joyce Fissoo alieleza
kuwa endapo msanii wa filamu
atatengeneza kazi yenye ubora na
viwango vinavyotakiwa atakuwa
ameimarisha kipato chake
na
uchumi wa Taifa lake pia.
Katika kuhakikisha weledi na
taaluma
unazingatiwa
katika
tasnia ya filamu ,Bodi ya Filamu
nchini imeratibu mafunzo ya
kuwajengea uwezo wanatasnia
ya filamu ambapo tayari Mikoa
wa
Morogoro
na
Mwanza
imepata fursa ya mafunzo hayo.
Mafunzo hayo yanawakilishwa na
kauli mbiu ya Filamu ni uchumi na
ajira na tayari vijana zaidi ya 500
wamepata nafasi ya kuhudhuria
mafunzo hayo hatua ambayo ni
nzuri katika kuhakikisha filamu
za kitanzania zinafika katika soko
la kimataifa na kuinua uchumi
wan chi na wa mtu binafsi.

Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na


Tuunge
Mkono
Jitihada
Kupinga
Rushwa
na Ufisadi
Tuimarishe
Uchumi
waza
Viwanda
kwa
Maendeleo
Yetu na
Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu

Fahamu Azimio la kupinga


matumizi ya dawa za kuongeza
nguvu michezoni
Na Anitha Jonas
Harakati za kupinga Matumizi
ya Dawa za kuongeza nguvu
michezoni zimeanza tangu miaka
ya 776 kabla ya kristo chini ya dola
ya Ugiriki ambapo wanamichezo
mbalimbali walikuwa wakishiriki
michezo
wakiwemo
askari
walishiriki matamasha yaliyofanyika
kila mwaka katika eneo la Olympia
ambalo ndiyo chimbuko la Olympic.
Mpaka mwaka 2016 katika bara
la Afrika ni nchi saba ambazo
zilikuwa hazijaridhia mkataba huo
ambapo mnamo mwezi Juni, 2016
Bunge la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania katika kikao cha nne
Bunge la 13 lilipitishwa Azimio
la kupinga Matumizi ya Dawa za
Kuongeza
Nguvu
katika
Michezo
(International
Convention
Against
AntiDoping
in
Sports),
ambapo
kwa sasa
nchi
za
Afrika ambazo
hazijapitisha
Azimio
hilo
ni
Jamhuri
ya
Kati,
Guinea
Bissau,Mauritania,Visiwa
vya
Sao,Tome na Principe, Sierra
Leone
na
Sudani
Kusini.
Bunge la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania lilipitisha Azimio hilo

kwa kuzingatia Ibara ya 63 (3) (e)


ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania ya Mwaka 1977.

Mkataba wa Kimatifa wa Udhibiti


wa Matumizi ya Dawa na Mbinu za
kuongeza nguvu katika Michezo.

Katika

Mwaka
2003
Mjini Paris,
katika
kikao
cha
Mawaziri
wenye
dhamana
ya
Elimu
kutoka nchi 103 wanachama
wa
UNESCO
walipendekeza
kuanzisha
chombo
kisheria
kitakachotambulika
Kimataifa
kwa ajili ya kudhibiti matumizi ya
dawa na mbinu haramu katika
michezo,alisema Waziri Nnauye.

Hotuba

ya

Waziri

wa

Akiendelea kuzungumza Mhe.


Nnauye alisema Tanzania ni
Mwanachama wa Shirika la Umoja
wa Mataifa la Elimu,Sayansi
na
Utamaduni
UNESCO na Ibara
36 ya Mkataba huo
inazitaka
nchi
wanachama
kuridhia
na
kuwasilisha
hati
ya
kuridhia kwa
Mkurugenzi
Mkuu UNESCO.

Habari,Utamaduni,Sanaa
na
Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye
alipokuwa akiwasilisha azimio hilo
bungeni alisema katika Mkutano
Mkuu wa UNESCO Kikao cha 33
kilichofanyika Paris Tarehe 3-21
Oktoba, 2005 uliridhia kuandaliwa

Dawa za kuongeza
nguvu
zimekuwa
zikitumika
na
wanamichezo katika mashindano
ya Kitaifa na Kimataifa kwa
lengo ni kupata udhindi dhidi ya
wapinzani kinyume na misingi ya
kimichezo katika mashindano.
Katika kipindi cha Mwaka 1928
Inaendelea Uk. 8

Jarida la Wizara ya Habari

Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na


Tuunge
Mkono
Jitihada
Kupinga
Rushwa
na Ufisadi
Tuimarishe
Uchumi
waza
Viwanda
kwa
Maendeleo
Yetu na
Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu

Inatoka Uk. 7

kulionekana kuwepo na wasiwasi


wa kuwepo
kwa baadhi ya
wanamichezo watumiao madawa ya
kuongeza nguvu michezoni ndipo
Shirikisho la Kimataifa la Mchezo wa
Riadha (International Assosiation
of
Athletics
FederationIAAF)
kuanza kupima wanamichezo.
Mwaka
1968
huko
Glenoble,Ufaransa vita dhidi ya
Matumizi ya Dawa za kuongeza
nguvu michezoni vilianza na
upimaji wa kwanza ulifanyika chini
ya Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa
(IOC) na iliona ni muhimu kuandaa
utaratibu wa kudhibiti matumizi
matumizi ya dawa za kuongeza
nguvu katika michezo yote.
Pamoja na hayo mnamo mwezi
Februari Mwaka 1999 katika Mji
wa Lausanne,Uswisi kulipitishwa
Azimio
la
kuanzishwa
kwa
Wakala wa Dunia (World Anti
Doping AgencyWADA) ambapo
wakala hii Makao Makuu yake
yapo
Montreal nchini Canada.
Hata hivyo wakala hiyo ilianza
kufanya kazi katika Michezo ya
Ishirini na Saba ya Mashindano
ya
Olimpiki
iliyofanyika
Sydney,Australia mwaka 2000.
Aidha, mpaka sasa wakala hiyo
ya WADA imekwisha anzisha
Ofisi katika Kanda nne ambazo ni
katika Mji wa Cape Town nchini
Afrika Kusini kwa nchi za Bara la
Afrika, Tokyo (Japan) kwa nchi
za Asia na Oceania, Montevideo
(Uruguay) kwa nchi za Latin
America pamoja na Lausanne
(Switzerland) kwa nchi za Ulaya
na Mashirikisho ya Kimataifa.
Mnamo mwaka 2005 Umoja wa
Mataifa kupitia Shirika lake la
Elimu,Sayansi
na
Utamaduni
(UNESCO) iliunga mkono jitihada
za IOC na ulianda Mkataba wa
Kimataifa wa kudhibiti matumizi
ya dawa na mbinu za kuongeza

nguvu katika Michezo (International


ConventionAgainst Doping in Sport).
Mkataba huo uliyoundwa na
UNESCO ulizingatia Chimbuko
la Azimio la Lusanne linalozuia
Matumizi ya Dawa na mbinu
za
kuongeza
nguvu
katika
Michezoni (Anti-Doping) ambalo
liliridhiwa
katika
mkutano
uliofanyika Copenhagen huko
Denmark
machi
5,
2003.
Mheshimiwa
Waziri
Nnauye
alisisitiza kuwa katika Mkataba
wa UNESCO unaopinga Matumizi
ya Dawa za Kuongeza Nguvu
Michezoni Ibara ya 19 inazitaka
nchi
wanachama
kuhakikisha
zinachukua hatua za kuhamasisha
vyama vya michezo kuzuia dawa
za kuongeza nguvu katika michezo
na kuchukua hatua madhubuti kwa
wanamichezo wanaojihusisha na
matumizi ya dawa na mbinu za
kuongeza nguvu katika michezo.
Akizungumzia kuhusu dawa za
kuongeza nguvu Michezoni ni
aina gani, Kaimu Mkurugenzi
wa
Michezo
Wizara
ya
Habari,Utamaduni,Sanaa
na
Michezo Bw. Alex Nkenyenge
alizitaja
baadhi
kuwa
ni
Bangi, Kahawa, Mirungi na
kusema zipo aina nyingi zaidi.
Kupitishwa Azimio la kupinga
matumizi ya dawa hizo kutasadia
serikali kuongeza jitihada za
kusimamia vyama vya michezo na
kupitia viongozi wao kuendesha
kampeni ya kupinga matumizi
dawa hizo kwani kuwepo kwa
mwanamichezo yoyote anayetumia
dawa hizo ni kuilifedhehesha
taifa na sekta ya michezo kwa
ujumla, alisema Bw. Nkenyenge.
Kwa upande wa Katibu wa
Baraza la Michezo la Taifa (BMT)
Bw.Mohamed Kiganja toa rai
kwa viongozi wa vyama vya
Michezo kusimamia wanamichezo
Jarida la Wizara ya Habari

wake kutotumia madawa hayo


michezo
kwani
yanaathari
nyingi
ikiwemo
kusababisha
kifo,ugonjwa
wa
kisukari,
kuharibikiwa akili na Saratani.
Aidha, Katibu huyo wa BMT alisisitiza
kuwa serikali inajipanga vyema
kusimamia utekelezwaji wa azimio
hilo kwa wanamichezo kwani haliko
tayari kuingia aibu ya kupata kashfa
ya mwanamichezo kujihusisha
na matumizi ya dawa hizo.
Tumejipanga kutoa elimu kwa
wanamichezo kupitia vyama vya
michezo husiana na suala la
matumizi ya dawa hizo pamoja na
kuwaeleza athari zake,alisema
Bw. Kiganja.
Hata
hivyo
Waziri
Nnauye
alisema kuna faida nyingi zitakazo
patikana baada ya kuridhiwa
kwa azimio hilo ambazo kama
kuwezesha
wanamichezo
wa
Tanzania kuhudhuria Mafunzo
nje ya nchi, Mikutano, Vikao
vya Kimataifa na kushiriki katika
Makongamano pamoja na kupewa
nafasi ya hata kuwa mwenyeji
wa
makongamano
yenye
maamuzi mbalimbali ya azimio.
Kwa upande wa Katibu wa chama
cha Kuogelea Tanzania (TSA) Bw.
Ramadhani Namkoveka aliipongeza
serikali kwa kukubali kusimamia
Azimio hilo kwani wanatumaini
kuwa itasaidia vyama vya michezo
kupata
misaada
mbalimbali
ikiwemo ya mafunzo na vifaa vya
michezo.Pia ameahidi kusimamia
suala la kupinga matumizi ya
dawa hizo pamoja na kutoa elimu
kwa wanamichezo wa chama
chake akiwa kama kiongozi nchini.
Hivyo basi kwa wanamichezo
wote
waliyokuwa
wakitumia
dawa hizo ni vyema waache
mara moja kuepuka fedhea ya
kwao binafsi na taifa kwa ujumla.

Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na


Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu

Sheria ya Huduma za Habari ya


Mwaka 2016 kuboresha upya
Taaluma ya Uandishi wa habari
Na Benedict Liwenga

ambo ambalo ni la kupongeza


katika Muswada wa Sheria
uliosainiwa na RAIS wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Dkt. John Pombe Magufuli na
kuwa Sheria baada ya kupitishwa
na Bunge la 11 la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania katika
Mkutano wake wa Tano Mjini
Dodoma ni hili la kuanzisha Mfuko
wa Mafunzo ya Habari ambao
unalenga kuwainua vijana wengi
kitaaluma kwenye tasnia ya habari.
Wapo vijana wengi wenye
vipaji vya uandishi na
utangazaji lakini baadhi
yao hawana mafunzo ya
taaluma ya habari na
pengine
wangependa
kujiendeleza
lakini
kwa ukosefu wa fedha
wamekuwa wakishindwa
kupiga
hatua
na
wengine kukata tamaa
kabisa na kuamua
kujishughulisha
na
mambo
mengine
yasiyokuwa
na
tija kwao wala kwa Taifa.
Mfuko
huu
utawawezesha
kujiunga
katika
vyuo
vya
ndani na nje ya nchi ili kupata
mafunzo ya taaluma ya habari.
Katika Sheria ya Huduma za
Habari ya mwaka 2016 ambayo
imefuta rasmi Sheria ya Magazeti
ya Mwaka 1976 kuna mambo
mengine muhimu ambayo yana

tija katika tasnia ya habari ikiwemo


kuanzishwa kwa Bodi ya Ithibati
itakayoainisha
viwango
vya
taaluma
kwa
wanahabari
na
kutoa
vitambulisho
v
y
a
wanahabari,
Baraza
Huru la

Habari
ambalo
pamoja
na
majukumu
mengine
litasaidia
kutatua migogoro na kuandaa
Kanuni za Maadili kwa wanahabari.
Bodi ya Ithibati nayo itakuwa
na mchango mkubwa katika
kuwatambua
wanahabari
na
kuwasimamia ili watimize wajibu
wao kwa uhuru na weledi.
Sheria ya Magazeti ya Mwaka
1976 imepigiwa kelele sana na

kupewa majina mengi, wengine


waliiita Sheria Kandamizi, na
wadau wengine wakasema ni ya
kizamani sana hivyo imepitwa na
wakati pia imeitwa sheria mbovu,
hivyo Kwa kuyaona hayo yote
ndio maana Serikali imekuja na
Muswada wa Sheria ya Huduma
za Habari ambao sasa tayari
umesainiwa na kuwa Sheria.
Ikumbukwe kuwa hatua ya kupata
Sheria hii ya Huduma za Habari ya
mwaka 2016 kumetokana na kazi
nzuri ya Wabunge wa Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania baada ya kuujadili
Muswada kifungu kwa
kifungu na kuunga mkono.
Baada ya kusainiwa kwa
Muswada huo na kuwa
Sheria, Rais Magufuli
aliwapongeza
wadau
mbalimbali waliofanikisha
shughuli
hiyo
na
kusema
kuwa
kuwa
Sheria hiyo
itasaidia
kuboresha
sekta
ya
habari
kwa manufaa ya wanataaluma
wenyewe na Taifa kwa ujumla.
Mnamo Novemba 04, mwaka huu,
wakati Rais Magufuli akizungumza
na Wahariri wa vyombo vya
habari, aliahidi kwamba pindi
Muswada huo ukifika mezani
kwake atausaini mara moja huku
akiusifia kuwa ni Sheria nzuri
inayolenga kulinda maslahi ya
Waandishi wa habari na kuweka

Inaendelea Uk. 10
Jarida la Wizara ya Habari

10

Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na


Tuunge
Mkono
Jitihada
Kupinga
Rushwa
na Ufisadi
Tuimarishe
Uchumi
waza
Viwanda
kwa
Maendeleo
Yetu na
Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu

Inatoka Uk. 9

heshima katika tasnia ya habari.


Mara baada ya kupitishwa kwa
Muswada huo, Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo,
Mhe. Nape Nnauye kwa nafasi
ya pekee aliwashukuru wadau
wote walioshiriki katika kutoa
maoni juu ya Muswada huo kwani
maoni hayo ndiyo yamepelekea
kukamilisha
mchakato
mzima
wa
kupata
Sheria
hiyo.

Sheria ya Huduma za Habari


wa
mwaka
2016
imeweka
kipengele cha kuwakatia Bima
Waandishi wa habari kufanya
kazi katika mazingira hatarishi
na kuanzishwa kwa Mfuko wa
Mafunzo kwa Waandishi wa habari
ambao utakuwa unatoa mafunzo
ya muda mfupi ya kitaaluma
ambapo jambo hili pia ni muhimu.

Kwa niaba ya Serikali napenda


kuwashukuru
wadau
wote
walioshiriki kwa namna moja
au nyingine katika kuhakikisha
tunatimiza
malengo
ya
takribani miaka 20 iliyopita ya
kuifanya taaluma hii ya habari
kuheshimika kama zilivyo taaluma
nyingine, alisema Mhe. Nape.

Bila shaka, tunaamini kuwa,


Sheria ya Huduma za Habari ya
Mwaka 2016 iliyosainiwa na Mhe.
Rais Magufuli itasaidia kujenga
upya taaluma ya Uandishi wa
habari
iliyokuwa
imevamiwa
na baadhi ya watu mbalimbali
kama vile Makanjanja na hivyo
kuhatarisha usalama wa jamii kwa
kuandika matukio yasiyozingatia
maadili na yaliyojaa uchochezi.

Aidha, alisema kuwa, kwa sasa


Muswada huo umeshapitishwa
hivyo kilichobaki ni utungaji
wa Kanuni ambapo aliomba
wadau wa tasnia ya habari
kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya
kutoa maoni yatakayopelekea
kuwa na Kanuni zenye tija kwa
wanahabari na Taifa kwa ujumla.

Sheria ya Huduma za Habari wa


mwaka 2016 imesubiriwa kwa
takribani miaka 20, kwani tangu
miaka ya 80 wadau wa habari
wamekuwa na kiu ya kupata sheria
nzuri ya kusimamia masuala
ya habari hapa nchini na hasa
lengo likiwa ni kuondoa Sheria
ya Magazeti ya mwaka 1976.

Kwa upande mwingine Waziri


Nape Nnauye aliwaasa wadau
wa habari kuunganisha nguvu
kwa pamoja hasa katika kipindi
hiki ambacho Muswada huo
umepitishwa na kuwataka wadau
hao
kutoruhusu
mgawanyiko
utokee kati yao, bali washirikiane
na Serikali katika kutekeleza
wajibu wao wa kihabari kwa jamii.

Kutokana na kiu hii ndiyo maana


wadau wengi walijitokeza kutoa
maoni yao kuhusu Muswada
huo ambapo sasa ni Sheria.

Hakika Muswada wa Sheria ya


Huduma za Habari wa mwaka
2016 ni mwanzo mpya wa tasnia
ya habari nchini hivyo wadau wa
habari pamoja na Waandishi wa
habari wanapaswa kutambua kuwa
haki mara zote huendana na wajibu,
hivyo hakuna haki isiyo na wajibu.

Ikumbukwe
kuwa
mwaka
jana (2015) Muswa wa Sheria
ya Huduma za Habari uliletwa
Bungeni kwa hati ya dharula
ukakataliwa na kurudishwa kwa
wadau ili kupata maoni yao kwani
ndiyo wataosimamiwa na Sheria
hii mpya iliyopitishwa bungeni na
kuwa Sheria. Hivyo ilibidi urudishwe
kwa wadau na kupata amoni yao.
Zamu hii Muswada uliletwa
kwa mchakato wa kawaida wa
kutunga Sheria ambapo ulisomwa

Jarida la Wizara ya Habari

na baadaye Wabunge ambao


ndiyo watunga Sheria waliweza
kuujadili na kuupitisha ambapo
bila kuchelewa Mhe. Rais Dkt.
John Pombe Magufuli aliusaini
mara moja na kuwa Sheria.
Ni
ukweli
usiopingika
kuwa
Sheria ya Huduma za Habari ya
Mwaka 2016 itaongeza uhuru wa
vyombo vya habari ukilinganisha
na Sheria ya Magazeti ya mwaka
1976. Wanataaluma ya habari
sasa wataheshimika kitaaluma na
kufanya kazi zao kwa weledi zaidi.

Kwa niaba ya
Serikali napenda
kuwashukuru
wadau wote
walioshiriki kwa
namna moja au
nyingine katika
kuhakikisha
tunatimiza malengo
ya takribani miaka
20 iliyopita ya
kuifanya taaluma
hii ya habari
kuheshimika kama
zilivyo taaluma
nyingine,

-NAPE NNAUYE

Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na


Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu

11

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (kulia)


akimkabidhi Kadi ya Uanachama ya PSPF Mmoja wa Bloggers Bw. Yusuf Badi
wakati wa kufunga Mafunzo ya siku mbili kwa Bloggers yaliyofanyika hivi
karibuni Jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura


akikabidhi zawadi ya tablet na Shillingi million 1.5 kwa Bi. Tumaini Msoyowa
mshindi wa kwanza wa Shindano la mwandishi bora wa habari zinazohusu
lishe kutoka gazeti la Mwananchi katika hafla iliyofanyika Jijini Dar es Salaam
Novemba 22, 2016.
Jarida
Jarida la
la Wizara
Wizara ya
ya Habari
Habari

12

Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na


Tuunge
Mkono
Jitihada
Kupinga
Rushwa
na Ufisadi
Tuimarishe
Uchumi
waza
Viwanda
kwa
Maendeleo
Yetu na
Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA

Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole


Gabriel (kulia) akiwa na mgeni wake kutoka Chuo cha Council for East Africa
Prof. Alexandre Lyambambaje alipotembelewa ofisini kwake Novemba 21, 2016.

Waziri wa Utamaduni na Sanaa wa Afrika ya Kusini Mhe. Nathi Mthethwa


(wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Mazimbu
Campus na ujumbe kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
wakati alipotembelea eneo hilo katika ziara yake hapa nchini hivi karibuni.
Jarida la Wizara ya Habari

LIMEANDALIWA NA
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
Jengo la PSPF (Golden Jubilee)
Ghorofa ya 8Mtaa wa Ohio
S.L.P 8031, Dar es Salaam-Tanzania
Faksi : (+255) 22 2126834
Simu : (+255) 22 2126826
Tovuti : www.habari.go.tz

Tufuatilie kupitia

@Wizara_Habari

Wizara YA Habari

wizara_habari

Вам также может понравиться