Академический Документы
Профессиональный Документы
Культура Документы
PRESS RELEASE
Zanzibar 12. 08 .201 7
Katika vikao vya leo, Dk. Shein kwa nyakati tofauti alikutana na Uongo zi wa Wizara
ya Fedha na Mipang o, Bodi ya Wakurugenzi ya PBZ na uongozi wake pamoja na Bodi
ya Wakurugenzi ya Shirika la Bima na uongozi wake .
Aidha, Dk. Shein alieleza kuwa licha ya changamoto zilizojitokeza lakini Benki hiyo
imeweza kupata mafanikio makubwa na kusisitiza haja ya kuw epo kwa mashirikiano
ya pamoja hatua ambayo itasaidia kuiendeleza Benki hiyo.
A kitoa maelezo yake Dk. Shein alisema kuwa wafanyakazi Benki hiyo ni lazima
wafuate maadili, sheria na taratibu za kazi na kuutaka uongozi kuwapongeza kwa
wale wana ofanya vizuri .
Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Dk. Khalid Mohamed alitoa pongezi k wa Rais
Dk. Shein kwa miongozo anayoitoa kwa Wizara hiyo na kupongeza hatua zilizofikiwa
na PBZ kwa kumiliki asilimia 41 ya mikopo kwa Soko la Mabenki hapa Zanzibar kwa
mwaka 2016 ha tua ina yoonesha jinsi Benki hiyo inavyoaminiwa.
Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee
kwa u pande wake ali toa pongezi kwa hatua kubwa iliyofikiwa na Benki hiyo sambamba
na ku sisitiza haja kwa Benki hiyo kuwa Serika li ina matumaini makubwa n a chombo
hicho kwani ni chanzo kimojawapo cha kuiongezea mapato yake.