Академический Документы
Профессиональный Документы
Культура Документы
Sehemu fulani za sala hii zinaweza kuimbwa; nazo ni kuanizia Ewe Mungu
Tunakuomba mpaka tujazwe kila baraka na neema ya mbinguni.
Doksolojia ya mwisho inaweza kuimbwa pia.
Anafumbua mikono CP
Ee Baba mwema, Wakoselebranti
Wanafumba
tunakusihi kwa unyenyekevu, Mikono.
na kukuomba kwa njia ya Yesu Kristu Mwanao, Bwana wetu,
uzipokee na kuzibariki dhabihu hizi takatifu,
tunakotolea pia
kwa ajili ya mtumishi wako Baba Mtakatifu wetu F.
na Askofu wetu F.
Nao wote wenye kushika imani katoliki ya Mitume.
TUNASHIRIKIANA ZA PEKEE
Noeli na oktava yake:
Epifania:
Tunashirikiana kuadhimisha ile siku takatifu,
Mwanao wa pekee aliopotokea na kuonekana mtu
kama sisi.
Ndiye Mwanao aliye milele pamoja nawe katika
utukufo wako.
Tena tunamheshimu kwanza Maria mtukufu
daima Bikira,
Mama wa huyo Yesu Kristu Mungu Bwana wetu.-
Pentekoste:
Tunashirikiana kuadhimisha ile siku takatifu ya
Pentekoste,
Roho Mtakatifu alipowatokea Mitume katika ndimi
za moto.
Tena tunamheshimu kwanza Maria mtukufu
daima Bikira
Mama wa huyo Yesu Kristu Mungu Bwana wetu.-
Maria mtakatifu
daima Bikira,
Mama wa Yesu Kristu Mungu Bwana wetu.
Halafu tunamheshimu Yosefu mwenye heri,
mume wake huyo Bikira,
na Mitume na Mashahidi wako wenye heri Petro na Paulo, Andrea,
( Yakobo, Yohane, Toma, Yakobo, Filipo, Bartolomeo,
Mateo, Simoni na Tadeo, Lini, Kleti, Klementi, Sisti,
Korneli, Sipriano, Laurenti, Krisogoni,
Yohane na Paulo, Kosma na Damiano)
na Watakatifu wako wote.
akatwaa kikombe
katika mikono yake mitukufu,
akakushukuru na kukutukuza,
akawapa wafuasi wake akisema:
Anainama kidogo. Wananyosha
Mikono ya kulia
Twaeni, mnywe wote: Kuonyesha kikombe.
Ewe Mwenyezi,
kati ya zawadi ulizotujalia
tunakutolea sadaka safi na takatifu,
yaani mkate mtakatifu wa uzima wa milele
na kikombe cha wokovu wa milele.
Ee Mungu Mwenyezi,
tunakuomba kwa unyenyekevu,
umtume malaika wako mtakatifu,
aichukue sadaka hii
na kuipeleka kwenye altare yako mbinguni,
mbele ya uso wako mtukufu.
Nasi tutakaopokea
Mwili na Damu takatifu ya Mwanao
katika altare hii,
Anainuka, anafanya ishara ya msalaba: *
C3
tujazwe kila baraka na neema ya mbinguni. Wanafumba
mikono.
(Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu. Amina. )
Anafumbua mikono:
Ee Bwana,
uwakumbuke pia watumishi wako marehemu F. na F. ,
waliotutangulia wakiwa na ishara ya imani,
wamepumzika usingizi wa amani.
Anafumba mikono anasali kimya kwa muda mfupi anafumbua mikono:
Tunakuomba, ee Bwana,
uwapatie mahali pa faraja, mwanga na amani,
hao na wote wanaopumzika katika Kristu.
(Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu. Amina. )
Anajipiga kifua: *
C4
Nasi pia watumishi wako wakosefu,
tunaotumainia wingi wa rehema zako,
utujalie nafasi
tukae pamoja na Mitume na Mashahidi wako watakatifu:
Yohane, Stefano, Matia, Barnaba,
( Inyasi, Aleksanda, Marselino, Petro, Felisita, Perpetua, Agata,
Lusia, Anyesi, Sesilia, Anastasia)
na Watakatifu wako wote.
Tunakuomba utupokee kwa huruma miongoni mwao
ingawa hatustahili.
Anafumba mikono: CP
Wote: Amina.
SALA YA EKARISTI II
Sala ya Ekaristi ya pili yafaa itumike katika Misa za juma au katika mazingira
ya aina fulani kwa ajili ya maneno yake ya pekee.
Sehemu fulani za sala hii zinaweza kuimbwa; nazo ni kuanzia Yeye alipojitoa
mpaka ...kusimama mbele yako na kukutumikia. Doksolojia ya mwisho
inaweza kuimbwa pia.
Anafumbua mikono:
Bwana awe nanyi
Awe pia nawe
Anainua mikono juu:
Inueni mioyo
Tumeiinua kwa Bwana.
Anafumbua mikono:
Tumshukuru Bwana Mungu wetu
Ni vema na haki.
UTANGULIZI
Anafumba mikono:
Anafumbua mikono:
Ee Bwana, kweli u mtakatifu na chemchemi ya utakatifu wote.
Anafumba mikono, kisha anafumbua na kuitandaza juu ya mkate na divai: *
Tunakusihi uzutakase kwa nguvu ya Roho wako dhabihu hizi,
Anafumba mikono, anabariki mkate na kikombe:
ili ziwe kwetu Mwili na Damu ya Bwana wetu Yesu Kristu.
Wananyosha
Anainama kidogo: mikono ya kulia
Twaeni, mle wote: kuonyesha hostia.
Katika Misa ya wafu, anaweza kuongeza:
Anafumbua mikono:
C2
Uwakumbuke pia ndugu zetu,
waliofariki dunia wakiwa na tumaini la ufufuko.
Uwakumbuke na marehemu wote,
uwapokee kwenye nuru ya uso wako.
Tunakuomba utuhurumie sisi sote, C3
ili tustahili kushiriki uzima wa milele
na kukusifu na kukutukuza
pamoja na Maria Bikira mwenye heri Mama wa Mungu,
Mitume wenye heri na Watakatifu wote
waliokupendeza tangu kale.
Anafumba mikono:
Tunakuomba hayo kwa njia ya Mwanao Yesu Kristu.
CP
Kwa njia yake, pamoja naye, na ndani yake,
wewe Mungu Baba Mwenyenzi
katika umoja wa Roho Mtakatifu
unapata heshima na utukufu wote,
daima na milele.
Wote: Amina.
SALA YA EKARISTI III
Sala ya Ekaristi ya tatu inawezwa kusemwa na utangulizi wo wote. Inafaa
itumike hasa katika Misa za Jumapili na za sikuku, kama vile Sala ya
Ekaristi ya kwanza (kanuni ya Kirumi) inavyotumika.
Sehemu Fulani za sala hii zinaweza kuimbwa; nazo ni kuanzia Usiku ule
alipotolewa mpaka Sadaka hii yenye uzima utakatifu. Doksolojia ya
mwisho anaweza kuimbwa pia.
Anafumbua mkono:
CP
Ee Bwana, kweli u Mtakatifu,
na kila kiumbe kilichoumbwa nawe kinakusifu kwa haki. Wakonselebranti
Wanafumba
Maana, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristu Mwanao, Mikono.
na kwa uwezo wa Roho Mtakatifu,
unatia uzima na kutakasa vitu vyote,
Wala huachi kuwakusanya watu kwako,
ili toka maawio ya jua hata machweo yake
Wakutolee sadaka safi.
Anafumba mikono nakuitandaza juu ya mkate na divai: CC
Basi, tunakusihi, ee Bwana, .
Uzibariki dhabihu hizi tunazokutolea,
Upende kuzitakasa kwa Roho wako,
Anafumba mikono:
wanaonyesha
Anainama kidogo. mikono ya kulia
kuonyesha hostia.
Twaeni, mle wote:
Huu ndio mwili wangu,
utakaotolewa kwa ajili yenu.
Anawaonyesha watu hostia, aniweka juu ya patena na kupiga goti. Wanatazama hostia;
kisha wanainama
Anafunua kikombe: sana.
Anainama kidogo.
Wananyosha
mikono ya kulia
Twaeni, mnywe wote: kuonyesha kikombe.
C3
Usikilize kwa wema
Sala za jamaa hii iliyo hapa mbele yako.
Ee Baba mwema, kwa huruma yako uwakusanye kwako
Wanao wote waliotawanyika po pote duniani.
Anafumba mikono :
Utujalie hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu
Aliye asili ya mema yote.
Anainua hostia na kikombe pamoja, akisema kwa sauti :
CP
Kwa njia yake, pamoja naye, na ndani yake,
Wewe Mungu Baba Mwenyenzi
Katika umoja wa Roho Mtakatifu
Unapata heshima na utukufu wote,
Daima na milele.
Wote: Amina.
Katika Misa ya wafu:
Anafumba mikono:
utujalie hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu,
aliye asili ya mema yote.
Wote: Amina.