Вы находитесь на странице: 1из 2

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU

Simu: 255-22-2114512, OFISI YA RAIS,


2116898 IKULU,
E-mail: press@ikulu.go.tz 1 BARABARA YA
Tovuti : www.ikulu.go.tz
BARACK OBAMA,
Faksi: 255-22-2113425
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo
tarehe 06 Januari, 2018 amewajulia hali baadhi ya wagonjwa waliolazwa katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Jijini Dar es
Salaam wakiwemo Mzee Kingunge Ngombale Mwiru na Mapacha walioungana
Maria na Consolata Mwakikuti.

Katika wodi ya Mwaisela, Mhe. Rais Magufuli amemjulia hali Mzee Kingunge
Ngombale Mwiru ambaye anatibiwa majeraha baada ya kushambuliwa na mbwa
wake, nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam.

Dkt. Ibrahim Mkoma wa hospitali hiyo amemueleza Mhe. Rais Magufuli kuwa
hali ya Mzee Kingunge inaendelea vizuri.

Mzee Kingunge amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kwenda kumuona


hospitalini hapo na amemueleza kuwa sasa anajisikia nafuu baada ya kupata
matibabu.

Pamoja na kumpa pole na kumuombea apone haraka Mhe. Rais Magufuli


amesema anatambua mchango mkubwa wa Mzee Kingunge katika siasa na
maendeleo ya nchi.

Katika wodi ya Sewahaji, Mhe. Rais Magufuli amemjulia hali Bw. Richard
Kajumulo ambaye ni Kaka wa Mbunge wa Muleba Kusini Prof. Anna Kajumulo
Tibaijuka, Bw. Said Abeid Salim, Bi. Amina Ismail Shirwa, Mzee Hamad Lila na
amempa pole Naibu Katibu Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI) Dkt. Zainab Chaula aliyefiwa na Mama yake mzazi wakati Mhe. Rais
akiwa wodini humo.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amewajulia hali mapacha walioungana
Maria na Consolata Mwakikuti ambao wamelazwa katika Taasisi ya Moyo ya
Jakaya Kikwete kwa matibabu ya moyo.

1
Maria na Consolata wamemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kwenda kuwaona na
kuwapa pole na pia wameongoza sala ya kumuombea Mhe. Rais Magufuli na
nchi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Prof. Mohamed


Janabi amesema matibabu kwa Maria na Consolata ambao ni wanafunzi mwaka
wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Kanisa Katoliki Ruaha (RUCU) yanakwenda
vizuri.

Aidha, Prof. Janabi amesema taasisi hiyo imefanikiwa kutoa matibabu kwa
wagonjwa wa moyo 1,400 katika mwaka uliopita na kwamba inashika nafasi ya
tatu barani Afrika kwa utoaji wa huduma bora za matibabu ya moyo.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amewashukuru na kuwapongeza madaktari wa


hospitali ya Taifa Muhimbili na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kwa kazi
kubwa wanayofanya kutibu wagonjwa na amesema Serikali itaendelea kutatua
changamoto zinazowakabili ili kuboresha huduma zaidi.

“Nawashukuru sana madaktari na wafanyakazi wote, mnafanya kazi


kubwa ya kuwatibu wagonjwa, pia mmeboresha hospitali na inaonekana ni
safi, mimi niwaahidi kuwa Serikali itaendelea kuboresha mazingira yenu ya
kazi ili muendelee kutoa huduma nzuri” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
06 Januari, 2018

Вам также может понравиться