Вы находитесь на странице: 1из 2

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA WAZIRI MKUU

Simu: +255-26-232-2484/232-4560 2 Barabara ya Reli na


Mahakama,
Nukushi: +255-26-232-1955, S. L. P. 980,
Barua-pepe: pm@pmo.go.tz Dodoma,
Tovuti: www.pmo.go.tz Tanzania.

14 Januari , 2018

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

WAZIRI MKUU AUVUNJA MFUKO WA KUENDELEZA KAHAWA

*Amuagiza CAG kufanya uchunguzi tangu kuanzishwa kwake

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameuvunja Mfuko wa Wakfu wa Kuendeleza zao la Kahawa
(CDTF) na amemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuchunguza
mwenendo wa mfuko huo tangu ulipoanzishwa.

Ametoa agizo hilo leo (Jumapili, Januari 14, 2018) wakati akizungumza na wadau wa zao
hilo kwenye kikao cha kujadili maendeleo ya zao la kahawa alichokiitisha, mjini Dodoma.

Waziri Mkuu amechukua hatua hiyo baada ya kubaini kwamba uundwaji wa mfuko huo si
wa kisheria bali ni wadau wa zao hilo kwa kushirikiana na Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB).

“Wakati Serikali inapambana kupunguza makato ya hovyo kwa wakulima, kumbe huku
kuna chombo cha kuwachukulia fedha wakulima hii haikubaliki.”

Pia aliagiza kufungwa kwa ofisi za CDTF ili kupisha uchunguzi na baada ya CAG
kukamilisha uchunguzi na kukabidhi ripoti, kazi zote zilizokuwa zinafanywa na mfuko huo
zitafanywa na Bodi ya Kahawa.

Hata hivyo, Waziri Mkuu ameongeza kuwa majukumu ya kuundwa kwa mfuko huo
yanaingiliana na yale ya Bodi ya Kahawa, ambayo ni pamoja na kufuatilia maendeleo ya
zao hilo, hivyo hakuna haja ya kuwa vyombo viwili vinavyofanya kazi moja.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amepiga marufuku wanunuzi wa kahawa kwenda kununua
kwa wanavijiji na badala yake kahawa yote itauzwa kwa njia ya minada.

“Kahawa itauzwa katika minada tu na utaratibu wa kutoa vibali kwa wanunuzi wa kahawa
kwenda kununua kwa wananchi vijijini marufuku kuanzia sasa, kama kuna watu
wamepeleka fedha zao wazirudishe kwani hazitafanya kazi.”

Amesema Wakuu wa Mikoa na Wilaya wasimamie uuzwaji wa zao hilo na kuwachukulia


hatua wote watakaokutwa wananunua kahawa kwa wakulima. “Anayetaka kahawa
akanunue mnadani na si kwa wanavijiji lengo ni kuhakikisha mkulima anapata tija.”

1
Pia ameziagiza halmashauri zote zinazolima kahawa nchini kuanzisha vitalu vya miche ya
kahawa na kisha kuigawa bure kwa wakulima, pia Maofiza Kilimo wawaelimishe walkulima
wote wenye miti mikongwe waanzisha mashamba mapya.

Kuhusu suala la utafiti wa zao hilo, Waziri Mkuu ameiagiza Wizara ya Kilimo itumie vyuo
vyake vya kilimo ianzishe vituo vyake vya utafiti vitakavyofanya kazi ya utafiti wa zao
hilo.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Bw. Joseph Kakunda
amesema watahakikisha maagizo hayo yanafanyiwa kazi, ambapo aliwaagiza Wakuu wa
mikoa yote 16 inayolima kahawa pamoja na wakuu wa wilaya wake 52 wahakikishe wanafuta
mara moja vibali vya ununuzi wa kahawa katika vyanzo vyao vya mapato.

Kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Hazina mjini Dodoma kilihudhuliwa na Waziri
wa Kilimo Dkt. Chales Tizeba, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bw. Charles
Mwijage, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Bw. Kakunda.

Wengine ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu,, Bibi Maimuna Tarishi, Katibu Mkuu Wizara ya
Kilimo, Mhandisi Mathew Mtigumwe, Wakuu wa mikoa 16 wanaolima kahawa na wakuu wa
wilaya,Mrajis wa Vyama vya Ushirika Nchini, Dkt. Tito Haule, Makatibu tawala wa mikoa
inayolima kahawa.

Mwenyekiti wa Bodi ya Kahawa na wajumbe wa bodi hiyo,,Mkurugenzi wa bodi ya Kahawa


Tanzania, Wakurugenzi wa Halmashauri,

Imetolewa Na:

Ofisi ya Waziri Mkuu


Jumapili, Januari 14, 2017.
S. L. P. 980,
Dodomma

Вам также может понравиться