Вы находитесь на странице: 1из 3

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA WAZIRI MKUU

Simu: +255-26-232-2484/232-4560 Mlimwa Kusini,


11 Barabara ya Edward Sokoine,
Nukushi: +255-26-232-1955, S. L. P. 980,
Barua-pepe: pm@pmo.go.tz 41193 – Dodoma,
Tovuti: www.pmo.go.tz Tanzania.

21 Januari , 2018

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


WAZIRI MKUU AMUAGIZA RAS MARA KUKAGUA HALMASHAURI YA BUTIAMA
*Aagiza DED, DT na Ofisa Manunuzi wachunguzwe
*Ni kutokana na matumizi yasiyoeleweka ya fedha za miradi

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa


Mara Bw. Raphael Nyanda kutuma timu ya wakaguzi kwenda kufanya ukaguzi
maalumu katika ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Butiama.

Amesema Halmashauri hiyo imekuwa na tabia ya kutumia fedha za miradi


mbalimbali ya maendeleo zinazotolewa na Serikali katika shughuli nyingine jambo
ambalo ni kinyume cha sheria.

Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana (Januari 20, 2018) wakati akizungumza na
watumishi na madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Bitiama katika ukumbi wa
chuo Kikuu cha Kilimo cha Mwalimu Nyerere cha Mara.

Pia Waziri Mkuu aliagiza kuchunguzwa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya


ya Butiama Bw Solomon Ngiliule pamoja na Mweka Hazina wa Halmashauri Bw.
Masanja Sabuni na Ofisa Manunuzi wa Halmashauri hiyo Bw. Robert Makendo.

Alisema viongozi hao wanatakiwa wachunguzwe kutokana na matumizi


yasiyoeleweka ya fedha za miradi ya maendeleo zinazotolewa na Serikali
zikiwemo sh. milioni 12 walizotumia kuandaa profile ya Halmashauri hiyo.

Waziri Mkuu alisema fedha zingine ni pamoja na sh. milioni 70 za elimu maalumu,
sh. milioni 288 za mradi wa maji Butiama ambazo zote hazijulikani zimetumikaje.
“Hatuwezi kuvumilia vitendo hivi fanyeni uchunguzi na naomba taarifa yake mara
mtakapokamilisha.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu aliiagiza Taasisi ya Kuzuzia na Kupambana


na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Mara imkamate na kumuhoji Meneja wa

1
Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) mkoani Mara, Mhandisi Peter Salim baada
ya kushindwa kutekeleza ujenzi wa mradi wa ofisi za Halmashauri ya wilaya ya
Butiama.

Waziri Mkuu alisema kuwa Serikali ilitoa sh milioni 600 Aprili, 2017 kwa ajili ya
kuanza kwa ujenzi wa ofisi za Halmashauri ya wilaya hiyo lakini hadi sasa wakala
huo haujafanya kazi yoyote.

Katika maelezo yake Mhandisi Salim alisema ujenzi wa ofisi hiyo hadi kukamilika
utagharimu sh. bilioni tatu, kati ya sh. milioni 600 zilizotolewa na Serikali sh milioni
400 zimetumika kujengea msingi, kauli ambayo ilipingwa na Mkuu wa wilaya hiyo
Bibi Anna-Rose Nyamubi.

“Mheshimiwa Waziri Mkuu siyo kweli kwamba kuna kazi inayoendelea bali
kilichopo pale ni mashimo ambayo hayajulikani ni ya nini. Pia kuna jengo moja
lilijengwa kwa mabati kama stoo na hakuna mafundi wanaoendelea na kazi"

Waziri Mkuu alisema kuwa Serikali iko katika mchakato wa kuboresha mazingira
ya wafanyakazi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa ofisi za watumishi na kwamba
haitamvumilia mtu yeyote atayekwamisha juhudi hizo.

Waziri Mkuu baada ya kuwasili wilayani Butiama akiambatana na mkewe Mama


Mary Majaliwa walizuru kaburi la Baba wa Taifa marehemu Mwalimu
Julius Nyerere, katika Kijiji cha Mwitongo na kufanya mazungumzo na mjane wa
Baba wa Taia, Mama Maria Nyerere.

Baada ya kuwasili katika eneo alilozikwa Mwalimu Nyerere, Waziri Mkuu na


Mkewe waliweka shada la maua juu ya kaburi na kisha walishirikiana na wananchi
kufanya maombi yaliyoongozwa na Chifu wa Wazanaki, Japheth Wanzagi.
Pia Waziri Mkuu alihutubia wakazi wa wilaya ya Butiama kwenye mkutano wa
hadhara uliofanyika katika uwanja wa Mwenge, ambapo alitumia fursa hiyo
kueleza juhudi mbalimbali za kuwaletea maendeleo zinazofanywa na Serikali ya
Awamu ya Tano, inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli.

(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMAPILI, JANUARI 21, 2018.

2
3

Вам также может понравиться