Вы находитесь на странице: 1из 2

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA WAZIRI MKUU

Simu: +255-26-232-2484/232-4560 Mlimwa Kusini,


11 Barabara ya Edward Sokoine,
Nukushi: +255-26-232-1955, S. L. P. 980,
Barua-pepe: pm@pmo.go.tz 41193 – Dodoma,
Tovuti: www.pmo.go.tz Tanzania.

30 Januari , 2018

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


AFRIKA YAAZIMIA KUZALISHA UMEME WA KUTOSHA-
MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassima Majaliwa amesema nchi za Bara la Afrika zimeazimia


kujiimarisha katika uzalishaji wa umeme hadi vijijini ili uweze kuleta maendeleo.

Aliyasema hayo jana (Jumatatu Januari 29, 2018) alipozungumza baada ya


mkutano wa Viongozi wa Wakuu wa Nchi za Afrika uliofanyika mjini Addis Ababa,
Ethiopia.

Katika Mkutano huo ambao Waziri Mkuu alimuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli,
alisema nchi za Afrika zimejipanga kuzalisha umeme wa kutosha mijini na vijijini.

Waziri Mkuu alisema nchi hizo zimeazimia kuzalisha umeme mwingi kwa lengo
la kuinua kiwango cha maisha ya wananchi wake na kuharakisha maendeleo ya
kiuchumi.

Alisema nchi za Afrika zinatakiwa zijitegemee kiuchumi, ambapo nchi za Jumuia


ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya nyingine za Afrika zimefikia
amapendekezo ya kuimarisha uzalishaji wa umeme.

“Tanzania iko vizuri kwa sababu ina vyanzo vingi vya kuzalisha umene na sasa
inamikakati ya kuzalisha umeme wa kutosha kuendesha viwanda vikubwa na
kukaribisha wawekezaji kwenye maeneo mbalimbali.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alisema maelengo ya mkutamo huo


yalikuwa ni kupokea taarifa za tume mbalimbali zilizoundwa katika kikao
kilichopita.

Alisema miongoni mwa taarifa hizo ni pamoja na ya tume iliyokuwa


inashughulikia masuala ya usalama na amani katika Bara la Afrika.

1
“Tume nyingine ilihusika na mapitio ya namna kuhamasisha nchi za Afrika kufikia
kwenye maendeleo na nyingine ilikuwa inahamasisha mahusiano ya nchi kupitia
kwenye Jumuia zilizopo ndani ya Bara la Afrika kama SADC.”

Pia Waziri Mkuu alisema mkutano huo ulifanya mapitio ya mapendekezo ya


namna nchi za Afrika zinavyoweza kupata mitaji kupitia michango ya nchi
mbalimbali, ambapo kanuni ziliandaliwa ili kuwezesha kila nchi kuchangia katika
mfuko mkuu wa Umoja wa Afrika.

Alisema Tanzania ilihusika kutoa mchango juu suala la amani na usalama katika
nchi za Afrika. ambapo kila nchi inawajibika kujilinda yenyewe na kulinda nchi
jirani pamoja na Jumuia zake.

(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMANNE, JANUARI 30, 2018.

Вам также может понравиться