Академический Документы
Профессиональный Документы
Культура Документы
Wizarayaya
Maliasili
Maliasili
nana
Utalii
Utalii
CHUMBA CHA HABARI
Wahariri:
Hamza Temba
Dorina G. Makaya
Lusungu Helela
Yaliyomo Uk
Sera ya Uhariri:
Madhumuni ya jarida hili la MALIASILI 1. Mapato ya Utalii yaongezeka kwa asilimia 5.6 ....................... Uk.4
ni:
2. Tanzania yatajwa nchi bora kwa Safari za Utalii
(i) Kuhabarisha na kuelimisha umma barani Afrika ........................................................................... Uk.5
kuhusu sekta ya Maliasili, Malikale
na Maendeleo ya Utalii. 3 . Kigwangalla aagiza msako mkali kwa walioua
Simba tisa Serengeti .............................................................. Uk.6
(ii) Kuwa jukwaa la mawasiliano la
watumishi.
4. Madhimisho ya Kimondo cha Mbozi kufanyika
Juni, 2018 ............................................................................. Uk. 7
(iii) Kufafanua na kuelezea sera za
Wizara ya Maliasili na Utalii.
5. Olduvai; Chimbuko la binadamu ............................................ Uk.8
Isipokuwa pale ambapo itakatazwa,
makala za MALIASILI zinaweza 6. Tanzania yasisitiza ujenzi mradi wa Stiegler’s Gorge .............. Uk.9
kunukuliwa kwa kutambua jarida
hili kama chanzo cha habari husika 7. Mapori Matano ya Akiba Kupandishwa hadhi ya kuwa
(Source). Hifadhi za Taifa .................................................................... Uk.10
15. Faru mwenye umri mkubwa kuliko wote Duniani ................ Uk.19
2 Jarida la MALIASILI
Tahariri Wizara ya Maliasili na Utalii
REGROW:
ikawe chachu
ya kufungua
Utalii Kanda
ya Kusini
Wizara ya Maliasili na Utalii ina dhamana ya kusimamia sekta Mwezi Novemba mwaka jana (2017) Serikali ilisaini mkopo
ya Maliasili na Malikale na Kuendeleza Utalii hapa nchini. wa masharti nafuu wa Dola za Kimarekani milioni 150, sawa
Inaelezwa kuwa katika kufanikisha utekelezaji wa jukumu hilo, na takriban Bilioni 340 za Tanzania kutoka Benki ya Dunia
Wizara kwa kushirikiana na Benki ya Dunia imeandaa mradi
kwa ajili ya kuendeleza mradi huo.
wa kusimamia maliasili na kuendeleza utalii wa kanda ya
kusini ujulikanao kama REGROW (Resilient Natural Resource
for Tourism and Growth). Tunafahamu kuwa mradi huu ni moja ya mkakati wa Serikali
kupanua wigo wa vivutio vya utalii nchini kwa kuongeza
Lengo la mradi huo ni kuongeza mchango wa sekta ya mazao mbalimbali ya utalii na kusisimua kanda zingine za
maliasili na utalii katika uchumi wa Taifa kwa kuboresha vivutio utalii ziweze kutumika ipasavyo kuleta tija katika sekta hii
vya utalii, miundombinu, usimamizi wa vivutio na kuongeza na kuongeza pato la Taifa tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo
faida za kiuchumi kwa jamii zinazoishi jirani na maeneo ya vivutio vingi vinavyotumika ni vile vya ukanda wa Kaskazini.
hifadhi katika ukanda huo wa kusini.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla
Mradi huu ambao maandalizi yake yalianza mwezi Novemba anaeleza kuwa kwa sasa vivutio vya utalii vya kaskazini
2014 ulizinduliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya vimeanza kuelemewa kwa kuwa watalii wengi hutembelea
Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan tarehe
vivutio hivyo kutokana na uwepo wa mazingira bora ya
12 Februari, 2018 katika viwanja vya Kihesa Kilolo Mjini Iringa
miundo mbinu, uwekezaji katika huduma za utalii na utangazaji
na Kauli Mbiu ya uzinduzi huo ikiwa “Utalii kwa Maendeleo
Endelevu- Karibu Kusini”. tofauti na ilivyo kwa maeneo mengine yenye vivutio ambayo
yanakabiliwa na changamoto mbalimbali.
Akizindua mradi huo, Makamu wa Rais alisema utasaidia
kupambana na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi Tunaamini kuwa REGROW itakuwa chachu ya kurekebisha
na kuchochea ukuaji wa sekta hiyo katika Nyanda za Juu changamoto zilizopo katika ukanda wa kusini ili nao uweze
Kusini kwakuwa vivutio vyake havijapewa kipaumbele cha kutembelewa na watalii wengi kama ilivyo kwa kanda ya
kutosha kama vile vya maeneo ya kaskazini mwa nchi. Kaskazini.
Taasisi zinazohusika na utekelezaji wa mradi huo ni Wizara Tunatoa rai kwa kila mdau anayehusika na utekelezaji wa
ya Maliasili na Utalii, Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania, mradi huu kutimiza wajibu wake kwa kufanya kazi kwa bidii
Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania, Tume ya na ubunifu wa hali ya juu ili matunda yaliyokusudiwa ya
Taifa ya Umwagiliaji, Ofisi ya Bonde la Mto Rufiji, Bodi ya mradi huu yaweze kupatikana kwa faida ya kizazi cha sasa
Utalii Tanzania, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania na na kijacho.
Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania kwa kushirikiana
na Halmashauri za Wilaya mbalimbali nchini. Sambamba na mradi huu tunatoa wito kwa wadau wengine
wa sekta ya umma na binafsi kutumia fursa ya mradi huo
Mradi huo utaanza utekelezaji katika maeneo ya kipaumbele kuwekeza katika ujenzi wa miundombinu ikiwemo ya hoteli za
ambayo ni Hifad hi ya Taifa ya Ruaha, Mikumi, Udzungwa kitalii na utoaji wa huduma nyingine mbalimbali za utalii.
na Pori la Akiba la Selous hususan Kanda ya Kaskazini
unakofanyika utalii wa picha. Mhariri.
Jarida la MALIASILI 3
Wizara ya Maliasili na Utalii
Mapato yatokanayo na utalii nchini na kudhibiti matukio ya ujangili na “Mfumo huo utaunganishwa na
yameongezeka kutoka Dola za matumizi yasiyo endelevu ya maliasili mfumo wa Serikali wa malipo ya
Marekani milioni 2,131.57 kwa mwaka na malikale. kielektroniki na kuhuishwa na mifumo
2016 hadi kufikia Dola za Marekani
mingine ya Serikali kama vile Uhamiaji,
milioni 2,250.3 kwa mwaka 2017 ikiwa Aliongeza kuwa, katika juhudi
ni sawa na ongezeko la asilimia 5.6. za kutangaza utalii, Wizara yake NIDA, TIRA, BRELA, TRA na NBS.
imeendelea kutekeleza mikakati Mfumo huo utaiwezesha Wizara
Hayo yalielezwa Bungeni Jijini Dodoma mabalimbali ikiwemo kuandaa kufuatilia watalii wa nje na wa ndani,
na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. utambulisho wa Tanzania Kimataifa kukusanya na kuchambua takwimu
Dkt. Hamisi Kigwangalla alipokuwa (Destination Branding). Lengo ikiwa za sekta ya maliasili na utalii kwa
akiwasilisha makadirio ya mapato na ni kuitambulisha Tanzania kama kituo
wakati, kuimarishsa utoaji wa huduma
matumizi ya wizara yake kwa mwaka mahsusi cha utalii Duniani.
wa Fedha 2018/2019. kwa wateja na kufanikisha ukusanyaji
Alisema wizara yake inashirikiana na udhibiti wa mapato,” alisema Dkt.
“Idadi ya watalii walioingia nchini Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa Kigwangalla.
imeongezeka kutoka watalii 1,284,279 na Michezo kuanzisha chaneli maalum
kwa mwaka 2016 hadi kufikia watalii katika Televisheni ya Taifa (TBC 1) kwa Mfumo huo ambao utatumiwa na
ajili ya kutangaza utalii ambapo kwa Wizara, Taasisi na wadau mbalimbali
1,327,143 kwa mwaka 2017, ikiwa
sasa Wizara kupitia TTB inaendelea unatarajia kuanza kutumika rasmi
ni ongezeko la asilimia 3.3. Watalii
na maandalizi ya kuanzisha studio mwaka ujao wa fedha.
kutoka Marekani wameongoza katika
maalum ya kutangaza utalii kwa njia ya
kuitembelea Tanzania wakifuatiwa na Kwa upande wake Mwenyekiti wa
teknolojia ya habari na mawasiliano.
nchi za Uingereza, India, Uholanzi na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,
Uswisi,” alisema Dkt. Kigwangalla. Aidha, alisema, Wizara yake imeanza Maliasili na Utalii, Mhe. Nape Nnauye
kutengeneza mfumo mmoja funganishi aliipongeza Serikali kwa kuboresha
Alisema, mafanikio hayo yanatokana na wa TEHAMA unaoitwa “MNRT Portal” miundombinu ya utalii hususan
ujenzi wa miundombinu ya barabara, kwa kutoa leseni na vibali, ukusanyaji barabara, huduma za maji na umeme
kuongezeka kwa kasi ya kuboresha na wa takwimu na mapato kutoka vyanzo ambavyo vimeendelea kuvutia watalii
kutangaza vivutio vya utalii, kuimarishwa mbalimbali vya sekta ya Maliasili na wengi kutembelea vivutio vya utalii na
kwa mifumo ya ukusanyaji maduhuli Utalii. kuongeza idadi ya watalii hapa nchini.
4 Jarida la MALIASILI
Wizara ya Maliasili na Utalii
Jarida la MALIASILI 5
Wizara ya Maliasili na Utalii
Askari wa wanyamapori wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wakikusanya miili ya simba tisa waliouwawa kikatili kwa kulishwa sumu, mmoja
kukatwa na kuchomolewa baadhi ya viungo vyake na wananchi katika kijiji cha Nyichoka, wilaya ya Serengeti mkoani Mara hivi karibuni kwa
ajili ya kuwafanyia uchunguzi kubaini chanzo cha vifo vyao.
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Mhe. Walipouawa simba wa Ruaha hivi kwanza kutokea hapa nchini ambapo
Dkt. Hamisi Kigwangalla ameagiza karibuni walikufa fisi zaidi ya 70 na mwishoni mwa mwaka jana simba
Kikosi Kazi Dhidi ya Ujangili cha ndege mbeshi zaidi ya 100, achilia wengine watano waliuawa pembezoni
Taifa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi mbali wadudu,” amesema Dkt. mwa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.
na Usalama ya wilaya ya Serengeti Kigwangalla kwa masikitiko makubwa.
kuwasaka watu waliohusika na mauaji “Mwaka huo huo mwanzoni simba
ya simba tisa katika kijiji cha Nyichoka, Amesema pamoja na faida kubwa za watatu nao walipigwa risasi kikatili
wilaya ya Serengeti mkoani Mara na simba kwa Taifa kiuchumi, Kijiji cha wilayani Serengeti huku mwaka 2015
kuwafikisha kwenye vyombo vya Nyichoka pekee walikouwawa simba simba 7 wakauwawa tena kwa sumu,
sheria. hao ni katika sehemu iliyofaidika sana huko huko Serengeti”.
na miradi ya ujirani mwema kutoka
Dkt. Kigwangalla ametoa agizo hilo Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. Akizungumzia sababu za ujangili huo
ofisini kwake Jijini Dodoma baada ya amesema mara nyingi ni kwa ajili ya
kupokea taarifa rasmi ya mauaji hayo “Wanyama hawa jamii ya paka kulipiza kisasi baada ya ng’ombe wa
ya kikatili yaliyoripotiwa hivi karibuni wakubwa ni muhimu sana kwa kuweka wananchi kuliwa na simba, changamoto
kwa simba hao kulishwa sumu kali mizania ya ikolojia sawa, maana ambayo husababishwa na wananchi
katika kijiji hicho huku mmoja akikatwa wanadhibiti idadi ya wanyama wala wenyewe kusogelea na kuweka makazi
miguu, mkia, ngozi ya juu ya mgongo nyasi kwa kuwala, bila hivyo hifadhi karibu kabisa na mipaka ya hifadhi za
na kuchukuliwa baadhi ya viungo zote zinaweza kugeuka kuwa jangwa. wanyamapori kwa lengo la kulisha
vyake ambapo amesema mauaji hayo mifugo pembezoni na wakati mwingine
hayavumiliki kwa kuwa yana athari “Hakuna mtalii atakayekuja hifadhini ndani ya hifadhi hizo kinyemela.
kubwa kiikolojia, kiutalii na uchumi wa asitamani kumuangalia simba, mfalme
Taifa kwa ujumla. wa pori. Wanapouawa maana yake Simba ambao wanakadiriwa kuwa zaidi
tunashusha hadhi ya hifadhi zetu kidogo ya 22,000, pamoja na wanyama
“Bahati mbaya sana ni kuwa kiutalii na hivyo kutishia kupoteza wengine jamii ya paka wamepungua
anapouawa simba kwa sumu hafi mapato yanayotokana na utalii” sana miaka ya hivi karibuni kiasi cha
peke yake, inakufa familia nzima ya amesisitiza Dkt. Kigwangalla. kuwekewa tishio la kutoweka hapa
simba, na mara nyingi wanakufa pia duniani. Duma nao wanakadiriwa
wanyamapori wengine wanaodowea Amesema tukio hilo la kuuwawa kwa kubaki 1,200 pekee.
nyama na wanaokula mizoga. Simba wa Ikolojia ya Serengeti sio la
6 Jarida la MALIASILI
Wizara ya Maliasili na Utalii
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga na viongozi wengine wa mkoa wa Songwe, wakiangalia Kimondo cha Mbozi.
Mkoa wa Songwe kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili riadha (Kimondo Marathon), mashindano ya netiboli na mpira
na Utalii na wadau wengine wa uhifadhi na maendeleo wa miguu (Kimondo Ligi).
utafanya maadhimisho ya siku ya Kimondo cha Mbozi kwa
mara ya kwanza katika historia kwenye Kijiji cha Ndolezi Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.
Kata ya Mlangali, wilayani Mbozi kuanzia Juni 28 hadi 30 Japhet Hasunga amesema Serikali kupitia Wizara yake
mwaka huu . itashiriki kikamilifu katika maadhimisho hayo kwa kushirikiana
na mkoa wa Songwe na wadau wengine ili kuhakikisha
Maadhimisho hayo yataenda sambamba na maadhimisho kivutio hicho cha Kimondo kinajulikana zaidi ndani na nje ya
ya siku ya Vimondo duniani ambayo yaliazimiwa kufanyika nchi na hatimaye kiongeze idadi ya watalii na mapato.
Juni 30 kila mwaka na kikao cha Umoja wa Mataifa cha
tarehe 6 Desemba, 2016. Amesema wizara yake ina mkakati maalum wa kuimarisha
kituo hicho cha utalii ambapo hivi sasa imeshajenga kituo
Pamoja na mambo mengine, kikao hicho pia kiliazimia maalum cha taarifa ambacho kimegharimu zaidi ya Shilingi
tarehe hiyo kuwa siku ya kuelimisha umma kuhusu elimu ya milioni 400 za Kitanzania.
anga na mafanikio ya tafiti mbalimbali yaliyopatikana kuhusu
elimu hiyo, kutambua juhudi zilizofanyika, kuweka sheria Aidha, amesema kupitia mkakati mpya wa wizara wa
za kimataifa na kutoa tahadhari juu ya athari zinazoweza kuimarisha na kuvijengea uwezo vituo vya malikale nchini
kutokea endapo dunia itafanya uharibifu juu ya anga. kwa kuzishirikisha taasisi za uhifadhi wa wanyamapori na
misitu, Shirika la Hifadhi za Taifa Tanapa litashirikiana na kituo
Akizungumza wakati akiwasilisha taarifa ya maandalizi ya hicho kwa kuimarisha miundombinu pamoja na utangazaji.
maadhimisho hayo kwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,
Mhe. Japhet Hasunga Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Kimondo cha Mbozi kinakadiriwa kilianguka mwaka 1840
Songwe, Herman Tesha amesema lengo la maadhimisho kutoka kwenye obiti yake huko angani huku kikikadiriwa
hayo ni kutangaza Kimondo hicho kama kivutio muhimu cha kuwa na tani 12 na mchanganyiko wa madini ya Chuma
utalii mkoani Songwe pamoja na vivutio vingine vya mkoa 90%, Nickel 8.69%, Copper 0.66%, Sulphur 0.01% na
huo kwa ujumla ili kutoa fursa ya uwekezaji kwenye sekta ya Phosphorus 0.11. Kimomdo hicho ni cha pili kwa ukubwa
utalii mkoani humo. barani Afrika na cha nane duniani kati ya vimondo 600
vilivyodondoka maeneo mbalimbali ulimwenguni, sifa yake
Amesema maadhimisho hayo yataenda sambamba na kubwa ni kuwa na ubaridi wakati wote hata mchana wa jua
kongamano la uwekezaji na sayansi ya vimondo, maonesho kali.
ya malikale, maonesho ya kiutamaduni, mashindano ya
Jarida la MALIASILI 7
Wizara ya Maliasili na Utalii
Serikali ya Tanzania kupitia Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la zamadamu wanaoitwa Zinjanthropus au Paranthropus boisei
Ngorongoro kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya imejenga na Homo habilis, zana za mawe za mwanzo zilizotumika
Makumbusho mapya ya Olduvai ambayo inaonesha (Oldowan) katika kujipatia chakula na ushahidi wa kale wa
Chimbuko la Binadamu (The Cradle of Humankind) katika ulaji wa nyama katika historia ya mabadiliko ya binadamu,
Bara la Afrika. takribani miaka million 2 iliyopita.
Makumbusho hayo mapya na Onesho la Chimbuko la Sehemu ya tatu inahusu maisha ya jamii ya Homo erectus.
Binadamu, yalifunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamii hii ilikuwa inafanana zaidi na binadamu wa sasa kuliko
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu jamii zilizotangulia. Aidha yapo pia masalia ya zamadamu
Hassan mwishoni mwa mwaka jana katika eneo la Olduvai, Homo erectus, zana za mawe (Acheulian) na ushahidi wa
ndani ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro. ulaji wa wanyama wakubwa kama vile Nyati na tembo katika
historia ya mabadiliko ya binadamu, takribani miaka million
Onesho hilo ni matokeo ya utafiti wa muda mrefu uliofanyika 1.7 iliyopita.
katika Bonde la Olduvai na Laetoli katika Wilaya ya
Ngorongoro mkoani Arusha. Sehemu ya nne inaonesha kipindi cha mwanzo cha
binadamu wa sasa (Homo sapiens) walioanza kutokea hapa
Idadi kubwa ya vioneshwa katika Makumbusho hii, vilipatikana Afrika miaka laki 2 iliyopita. Sehemu hii pia inaonesha mila na
katika bonde la Olduvai na Laetoli nchini Tanzania kupitia utamaduni wa makabila mbalimbali kama vile Wahadzabe,
utafiti wa kisayansi wa muda mrefu na vilikuwa vimehifadhiwa wamasai na Datoga. Yapo pia mavazi ya asili ya jamii hizo,
katika Makumbusho ya Taifa, Jijini Dar es Salaam. zana za kuwinda na vifaa mbalimbali wanavyovitumia katika
maisha yao ya kila siku.
Vioneshwa hivi ni pamoja na masalia ya zamadamu, zana
za mawe na masalia ya wanyama walioishi takribani miaka
milioni 4 iliyopita.
8 Jarida la MALIASILI
Wizara ya Maliasili na Utalii
Jarida la MALIASILI 9
Wizara ya Maliasili na Utalii
Baadhi ya Twiga katika mwambao wa ziwa Burigi kwenye Pori la Akiba Burigi ambalo litapandishwa hadhi kuwa Hifadhi ya Taifa.
Wizara ya Maliasili na Utalii imetangaza kuanza mchakato kwa ajili ya kuidhinishwa kuwa Sheria kamili ya kupandisha
wa kuyapandisha hadhi Mapori ya Akiba ya Burigi, Kimisi, hadhi mapori hayo.
Biharamulo, Ibanda na Rumanyika kuwa Hifadhi za Taifa.
Akizungumzia mikakati mingine mipya ya kuboresha sekta ya
Mchakato huo tayari umeungwa mkono na Rais wa Jamhuri maliasili na utalii itakayotekelezwa, Dkt. Kigwangalla alisema
ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph ni pamoja na kuanzisha mamlaka ya usimamizi na uendelezaji
Magufuli. wa utalii wa fukwe nchini, kuhuisha maeneo ya vivutio vya
Mambo ya Kale na kuviunganisha katika ‘package’ moja ya
Hayo yameelezwa bungeni Jijini Dodoma na Waziri wa Maliasili utalii na vivutio vya wanyamapori.
na Utalii, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati akihitimisha
mjadala wa bajeti wa makadirio ya mapato na matumizi ya Mikakati mingine ni kuunda mfumo mmoja funganishi
wizara yake kwa mwaka wa fedha 2018/2019. wa TEHAMA uitwao “MNRT Portal” kwa ajili ya kutoa
leseni na vibali, ukusanyaji wa takwimu na mapato kutoka
“Mheshimiwa Spika, ninaomba kulitaarifu Bunge lako tukufu vyanzo mbalimbali vya sekta ya maliasili na utalii, ambapo
kuwa Mhe. Rais ameridhia ombi letu la kupandisha hadhi utaunganishwa na mifumo mingine ya Serikali iliwemo GePG,
Mapori ya Akiba ya Burigi, Kimisi, Biharamulo, Ibanda na NIDA, TIRA, BRELA, TRA na NBS.
Chief Rumanyika kuwa Hifadhi za Taifa, kipekee namshukuru
sana Mhe. Rais kwa kuridhia ombi letu hilo” alisema Dkt. Alisema mikakati mingine ni kuanzisha Jeshi Usu, Utambulisho
Kigwangalla. wa Utalii wa Tanzania Kimataifa ujulikanao kama “Tanzania,
Unforgettable”, kufungua utalii wa kanda ya kusini, kuanzisha
Alisema kufuatia hatua hiyo, wizara yake inaanzisha mchakato mwezi wa maadhimisho ya Urithi wa Mtanzania “Urithi
rasmi wa kukamilisha taratibu za kupandisha hadhi mapori Festival” (Septemba), kuhuisha sheria za TANAPA, TAWA na
hayo ili kupanua wigo wa vivutio vya utalii katika kanda TFS, pamoja na kuunda kanuni mpya za kusimamia vizuri
ya Kaskazini Magharibi na hivyo kufikia azma ya Serikali sekta hizo.
kuongeza idadi ya watalii kufikia milioni 8 na mapato ya dola
za kimarekani bilioni 16 katika kipindi cha miaka 7 ijayo. Pori la Akiba Burigi lina ukubwa wa kilomita za mraba 2,941
katika wilaya za Karagwe, Muleba na Ngara mkoani Kagera,
Inaelezwa kuwa mchakato huo utapitia hatua mbalimbali wakati Pori la Kimisi likiwa na ukubwa wa kilomita za mraba
ikiwemo kuwashirikisha wadau husika kupata maoni yao, 1,030 katika wilaya za Ngara na Karagwe mkoani humo.
mapendekezo kuwasilishwa baraza la mawaziri kabla ya
kujadiliwa bungeni na hatimaye kuwasilishwa kwa Mhe. Rais (Inaendelea Uk. 11)
10 Jarida la MALIASILI
Wizara ya Maliasili na Utalii
Jarida la MALIASILI 11
Wizara ya Maliasili na Utalii
Eneo katika shamba la Miti Kawetire mkoani Mbeya, ilipopita Barabara ya lami ambayo ipo juu zaidi ya nyingine nchini ikiwa na urefu (Altitude)
wa mita 2961 kutoka usawa wa bahari. Serikali itaboresha mazingira ya eneo hilo ili yatumike kama kivutio cha utalii nchini.
Serikali imesema itaboresha mazingira ambayo ni lazima tuiboreshe tuweke ya kale yaliyotumiwa na wakoloni
ya kivutio cha utalii cha barabara kibao kizuri tuweke mazingira mazuri katika shamba hilo na badala yake
ya lami ambayo ipo juu zaidi kutoka pamoja na kukitangaza ili watanzania yatumike kwenye utalii wa mambo ya
usawa wa bahari kuliko barabara zote na watalii kutoka nje waweze kale sambamba na utalii wa misitu ya
nchini ili kupanua wigo wa vivutio vya kutembelea hapa,” alisema Hasunga. kupandwa inayopatikana pia katika
utalii na kuongeza idadi ya watalii na shamba hilo.
mapato. Alisema ili kufikia lengo liliwekwa na
Serikali la kuongeza idadi ya watalii Hata hivyo alisema kupitia mradi wa
Hayo yalielezwa na Naibu Waziri wa kufikia milioni mbili mwaka 2020 na REGROW wa kuendeleza utalii kanda
Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga milioni 8 mwaka 2025 vivutio vyote vya ya kusini Serikali imepokea mkopo wa
baada ya kutembelea shamba la miti la utalii vilivyopo nchini vitatambuliwa, masharti nafuu wa dola za Kimarekani
Kawetire wilayani Mbeya na kujionea kuimarishwa na kuviwekea milioni 150 sawa za zaidi ya bilioni
sehemu ya barabara ya lami inayopita miundombinu itakayowavutia watalii 340 za kitanzania kutoka benki ya
katikati ya shamba hilo katika mlima kuvitembelea. dunia kwa ajili ya kusaidia kuboresha
Kawetire kwenye safu za milima ya miundombinu ya vivutio vya ukanda
Mbeya. Aidha aliuagiza uongozi wa shamba huo.
hilo kushirikiana na wakala wa
Eneo hilo la barabara hiyo ambayo huduma za barabara –Tanroads katika Kwa upande wake Meneja wa shamba
hupitisha magari kutoka Jijini Mbeya kuboresha mazingira yanayozunguka hilo, Arnorld Shoo alisema eneo hilo
kwenda katika Wilaya ya Chunya na eneo hilo ikiwa ni pamoja na kuweka la barabara limekuwa ni kivutio cha
Mikoa ya Singida na Tabora lina urefu bango la kisasa la kutambulisha eneo kipekee cha utalii katika shamba hilo
(Altitude) wa mita 2961 kutoka usawa hilo, kujenga bustani na maeneo rafiki ambapo pia hupata mapato kupitia
wa bahari katika Latitude 08’ 35 S na ya kupumzikia kwa ajili ya kuwavutia watu na vikundi mbalimbali ikiwemo
Longitude 33’ 25 E. watalii kutembelea eneo hilo na kupiga wanakwaya na wanafunzi ambao
picha. hufika eneo hilo kwa ajili ya kupiga
“Hatutaki ule utalii wa kutegemea picha za kumbukumbu.
wanyamapori pekee, hii sasa ni Mbali na kivutio hicho aliuagiza uongozi
sehemu ya aina nyingine ya utalii wa shamba hilo kutobomoa majengo
12 Jarida la MALIASILI
Wizara ya Maliasili na Utalii
Mtendaji Mkuu wa TFS, Prof. Dos Santos Silayo (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Mihan Gas, Hamisi Ramadhan (kulia) wakisaini
mkataba wa makubaliano wa kukopesha mitungi ya gesi na vifaa vyake kwa watumishi wa Umma Jijini Dodoma hivi karibuni. Katikati
anayeshuhudia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi.
Serikali imesaini mkataba na Kampuni Pamoja na kusaini mkataba huo, TFS upatikanaji wa huduma hiyo ni
ya Gesi ya Mihan Gas kwa aijili ya na Kampuni ya Mihan Gas zilizindua jitihada za kuhakikisha matumizi ya
kukopesha mitungi ya gesi na vifaa kampeni ya kukopesha mitungi mkaa yanapungua.
vyake kwa watumishi wa umma. ya gesi na vifaa vya vyake kwa
Watumishi wa Umma. Alisema nishati mbadala ndiyo njia
pekee itakayosaidia jamii kuachana
Hatua hiyo imekuja ikiwa ni juhudi
Awali, Katibu Mkuu Wizara ya na matumizi ya mkaa na kuni.
za Serikali za kutaka kupunguza
Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Milanzi
matumizi ya mkaa pamoja na kuni akizungumza katika hafla hiyo, Kwa upande wake, Mkurugenzi
kwa lengo la kuimarisha uhifadhi wa alitoa wito kwa watumishi wa umma Mtendaji wa Kampuni ya Mihan
misitu ambayo imekuwa ikitumika kuchangamkia fursa hiyo ambayo Gas, Hamisi Ramadhani aliishukuru
kama nishati kuu. itasaidia kupunguza uharibifu ya Serikali kwa kuikubalia kampuni hiyo
misitu nchini. kusambaza gesi kwa watumishi wa
Mkataba huo ulisainiwa hivi karibuni umma.
Jijini Dodoma na Mtendaji Mkuu “Hili ni tukio kubwa hasa kwa wale
wa Wakala wa Huduma za Misitu ambao ni watunzaji wa mazingira Akizungumzia namna watumishi
Tanzania (TFS), Profesa Dos Santos katika kuiwezesha jamii kuanza watakavyonufaika na mpango huo,
Silayo na Mkurugenzi Mtendaji wa matumizi ya nishati mbadala,” Mkurugenzi huyo alisema kampuni
kampuni ya Mihan Gas, Hamisi alisema. hiyo imetenga fungu la kutosha kwa
ajili ya kuwezesha ukopeshaji wa
Ramadhan huku Katibu Mkuu wa
Naye, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa vifaa hivyo na kwamba kila Mtumishi
Wizara ya Maliasili na Utalii, Mej.
Misitu zaTanzania (TFS), Profesa Dos atapewa nafasi ya kukopa na kulipa
Gen. Gaudence Milanzi akishuhudia Santos Silayo akizungumza baada mwezi mmoja mara baada ya kuanza
tukio hilo. ya kusaini mkataba huo alisema, matumizi ya gesi hiyo.
Jarida la MALIASILI 13
Wizara ya Maliasili na Utalii
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na balozi wa Uingereza hapa nchini, Mhe. Sarah Cooke.
Serikali imefanikiwa kudhibiti vitendo vitendo hivyo kwa kuimarisha ulinzi wa Fukwe nchini ili kuimarisha utalii wa
vya ujangili hapa nchini kwa zaidi ya katika maeneo ya hifadhi nchini ikiwa ni fukwe pamoja na kutambua barabara
asilimia 50. pamoja na kuanzisha jeshi maalum la iliyokuwa ikitumika katika biashara ya
usimamizi wa Misitu na Wanyamapori, utumwa wakati wa ukoloni ili iweze
Hayo yalielezwa na Waziri wa Maliasili Sheria ya wanyamapori na za taasisi kutumika kiutalii.
na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla za uhifadhi zimeanza kufanyiwa
wakati akizungumza na Balozi wa marekebisho kuwezesha mabadiliko Akizungumzia migogoro ya mipaka
Uingereza hapa nchini, Sarah Cooke hayo. iliyopo baina ya wananchi na maeneo
ofisini kwake jijini Dodoma. ya hifadhi, Dk. Kigwangalla alisema
Katika hatua nyingine Dk. Kigwangalla Serikali itatatua migogoro hiyo kwa
Mazungumzo hayo yalilenga kujadili alimueleza balozi Cooke kuwa, Serikali kushirikisha wananchi sambamba na
mambo mbalimbali ikiwemo kuimarisha kupitia Wizara yake inaendelea kuwasaidia kutatua changamoto za
ushirikiano baina ya nchi hizo mbili kuimarisha vivutio vya utalii hapa nchini msingi ambazo ni kuimarisha maeneo
katika sekta ya uhifadhi na maendeleo kwa kupanua jeografia ya maeneo ya ya malisho ya mifugo, upatikanaji wa
ya utalii. utalii sambamba na kuongeza vivutio ili maji kwa ajili ya wananchi na mifugo,
kuongeza idadi ya watalii na mapato. mpango bora wa matumizi ya ardhi na
Dk. Kigwangalla alisema katika kipindi uendelezaji wa kilimo na ufugaji.
cha miezi sita iliyopita hakuna mauaji Alisema Serikali itajenga makumbusho
mapya ya wanyamapori yaliyoripotiwa ya Marais Wastaafu wa Tanzania Kwa upande wake balozi Cooke
na kwamba nyara zinazokamatwa hivi mjini Dodoma pamoja kuanzisha alisema nchi yake itaendelea
sasa ikiwemo meno ya tembo na ngozi makumbusho ya meno ya tembo kuimarisha ushirikiano inaoutoa kwa
za wanyamapori ni masalia ya zamani. katika miji ya Dar es Salaam, Arusha, Serikali ya Tanzania katika kudhibiti
Iringa na Dodoma. mtandao wa uhalifu wa madawa ya
Alisema mafanikio hayo yametokana kulevya, rushwa na ujangili.
na juhudi mbalimbali zinazofanywa na Sambamba na hayo alisema Serikali
Serikali kudhibiti vitendo vya ujangili itaanzisha mwezi maalum wa Alisema kwa sasa watalii zaidi ya
ikiwemo doria za mara kwa mara maadhimisho ya urithi wa Mtanzania 75,000 wa Uingereza hutembelea
za kiitelijensia ambazo zimekuwa ambao utafanyika mwezi Septemba Tanzania kila mwaka na wengine
zikishirikisha vyombo mbalimbali kila mwaka pamoja na kuendeleza wamewekeza katika sekta utalii
vya ulinzi na usalama pamoja na raia utalii wa mikutano. hapa nchini, hivyo akaiomba Serikali
wema. kurekebisha baadhi ya changamoto
Alisema Serikali pia itaanzisha chache zilizopo katika sekta hiyo
Alisema Serikali itaendelea kudhibiti Mamlaka ya Usimamizi na Uendelezaji kwenye mtiririko wa kodi.
14 Jarida la MALIASILI
Wizara ya Maliasili na Utalii
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kushoto) akizungumza na wadau wa sekta ya ufugaji nyuki nchini katika kikao
alichokiitisha kujadili maendeleo ya sekta hiyo ikiwemo marekebisho ya kanuni za ufugaji nyuki za mwaka 2017 Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Alisema mbali na kuongeza uzalishaji, 54 ya ukubwa ardhi yote ya Tanzania
Mhe. Japhet Hasunga ametoa wito mazao hayo pia yanatakiwa ambayo ikitumiwa ipasavyo na
kwa wananchi kutumia fursa kubwa kuongezewa thamani na kuwekewa wananchi itawawawezesha kujiajiri na
iliyopo hapa nchini ya ufugaji nyuki ngazi za ubora ili yaweze kuhimili kuongeza uzalisahaji wa mazao ya
na uwepo wa masoko ya ndani na nje masoko ya ndani na nje ya nchi. nyuki na mapato.
ya nchi kwa kuongeza uzalishaji wa
mazao yake na kuyaongezea thamani Aliongeza kuwa, ili kuimarisha sekta Alisema ili kulinda mazalia ya nyuki
ili kuinua uchumi wao na taifa kwa hiyo Serikali itashirikiana na wadau na kuongeza uzalishaji wa mazao ya
ujumla. kutatua changamoto zilizopo ikiwemo nyuki nchini, Serikali kupitia Wakala
kutafuta masoko, kuimarisha uwekezaji wa Huduma za Misitu Tanzania TFS,
Alitoa wito huo mbele ya wadau wa na kuanzisha viwanda vidogo vya imeanzisha hifadhi za nyuki 11 huku
sekta ya ufugaji nyuki kutoka mikoa kuchakata mazao ya nyuki ikiwemo Serikali za vijiji zikianzisha hifadhi za
yote nchini katika mkutano aliouitisha asali na nta ambayo ina soko kubwa nyuki 14.
kujadili maendeleo ya sekta hiyo nje ya nchi.
ikiwemo marekebisho ya kanuni za Wadau walioshiriki mkutano huo
ufugaji nyuki za mwaka 2017 katika Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi ambao ni wazalishaji, wachakataji na
ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma. wa Idara ya Misitu na Nyuki wa wizara wasafirishaji waliishukuru Serikali kwa
hiyo, Deosdedit Bwoyo alisema kuandaa mkutano huo na kuiomba
Alisema kwa sasa mchango wa sekta Tanzania ni moja kati ya nchi 50 duniani kusaidia katika tafiti, elimu kwa
ya nyuki katika pato la taifa bado ni zenye utajiri mkubwa wa rasilimali za wananachi wanaojihusisha na ufugaji
mdogo ukilinganisha na fursa zilizopo misitu ambazo zinatoa fursa pana ya nyuki hususan maeneo ya vijijini na
za ufugaji nyuki hapa nchini ambazo ufugaji nyuki nchini. utafutaji wa masoko ya uhakika.
zikitumiwa ipasavyo zitasaidia kuinua
pato la wananchi na taifa kwa ujumla. Alisema eneo la misitu ni takriban
hekta milioni 48.1 ambalo ni asilimia
Jarida la MALIASILI 15
Wizara ya Maliasili na Utalii
b) Matumizi ya uvunaji
Aina hii ya matumizi hufanyika kwa kuwaondoa wanyamapori katika maeneo yao ya asili, mfano
uwindaji wa kitalii, uwindaji wa kitoweo, ukamataji wa wanyamapori kwa ajili ya ufugaji na biashara
ya wanyamapori hai.
16 Jarida la MALIASILI
Wizara ya Maliasili na Utalii
Tanzania – TAWA kwa kujaza fomu ya maombi. Mwombaji aambatishe nyaraka zifuatazo kwenye
fomu ya maombi:-
i. Uthibitisho wa malipo ya ada ya maombi ya leseni yaani Stakabadhi ya Serikali (ERV),
ii. Nakala ya Hati ya Usajili wa aina la biashara /kampuni pamoja na nakala ya katiba na
mwongozo wa kampuni (Memorandum and Articles of Association),
iii. Andiko la mradi likijumuisha Mpango wa Biashara (Project Proposal and Business Plan),
iv. Uthibitisho wa umiliki wa eneo la mradi,
v. Cheti cha Tathmini ya Athari ya Mazingira (EIA Certificate),
vi. Nakala ya utambulisho wa mlipa kodi (Taxpayer Identification Number - TIN)
Muda wa kuwasilisha maombi ya leseni ni kuanzia tarehe 1 Oktoba hadi tarehe 15 Novemba katika
mwaka husika.
5. Lesseni zinazotolewa,
Ufugaji wa wanyamapori uko katika daraja tatu zifuatazo:-
i. Daraja 17: Bustani ya wanyamapori
ii. Daraja 18: Mashamba ya ufugaji wa wanyamapori
iii. Daraja 20: Ranchi za wanyamapori
7. Ada zinazotozwa
Ada kwa maombi ya leseni ya ufugaji wa wanyamapori ni kama ifuatavyo:-
i. Bustani ya wanyamapori
Dola za kimarekani 150 kwa mradi unaomilikiwa na mzawa peke yake. Dola za kimarekani
250 kwa mradi unaomilikiwa kwa ubia kati ya mzawa na mgeni.
ii. Mashamba ya ufugaji wanyamapori
Dola za kimarekani 200 kwa mradi unaomilikiwa na mzawa peke yake. Dola za kimarekani
500 kwa mradi unaomilikiwa kwa ubia kati ya mzawa na mgeni.
iii. Ranchi za wanyamapori
Dola za kimarekani 500 kwa mradi unaomilikiwa na mzawa peke yake. Dola za kimarekani
1000 kwa mradi unaomilikiwa kwa ubia kati ya mzawa na mgeni.
Sheria imetoa fursa ya kuingiza wanyamapori nchini kwa kuomba kibali cha kuingiza
wanyamapori (Import Permit).
8.2 Matumizi ya wanyamapori wanaofungwa
Matumizi ya wanyamapori wanaofugwa pia yako katika makundi mawili:-
i. Matumizi ya uvunaji na
ii. Matumizi yasiyo ya uvunaji
Matumizi hayo hufanyika kwa ajili ya utalii wa ndani na nje, kuzalisha na kusafirisha nje ya nchi,
kitoweo na kujipatia kipato.
Jarida la MALIASILI 17
Wizara ya Maliasili na Utalii
JENGO la kitega uchumi la Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo huko porini watakuwa wanaonekana “LIVE” (Mubashara)
la Ngorongoro jijini Arusha (pichani) ambalo ujenzi wake kwenye jengo hili kupitia LED Screen ambazo zitakuwa
unatarajiwa kukamilika mwezi juni mwaka huu litakuwa zimezunguka jengo hili” alisema Dk. Kigwangalla.
kivutio cha kihistoria cha utoaji wa huduma za utalii hapa
nchini. Alisema huduma nyingine zitakazotolewa katika Jengo
hilo ni pamoja na zile za kuangalia jiji la Arusha kupitia
Hayo yameelezwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dk. darubini, huduma za burudani ikiwemo kumbi za starehe
Hamisi Kigwangalla muda mfupi baada ya kukagua jengo na migahawa.
hilo ambalo linasemekana kuwa refu kuliko majengo yote
jijini Arusha likiwa na jumla ya ghorofa 18. Kwa upande wake Meneja wa Idara ya Urithi wa Utamaduni
wa Mamlaka hiyo, Mhandisi Joshua Mwankundwa alisema
Alisema jengo hilo ambalo linatizamana na Round About ya ujenzi wa jengo hilo ambalo ulianza mwezi Novemba, 2013
AICC katikati ya jiji hilo, limekusudiwa kuwa Kituo Kimoja unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi juni mwaka
(One Stop Centre) cha shughuli zote za utoaji wa huduma za huu.
utalii jijini humo kuanzia uwekezaji, utangazaji na menejimenti
kwa ujumla. Alisema jengo hilo ambalo lina uwezo wa kupaki magari
67 kwa wakati mmoja katika ghorofa za chini linagharimu
Alisema jengo hilo litatoa fursa kwa wadau mbalimbali shilingi za Kitanzania bilioni 45.
wanaotoa huduma za utalii kuweka ofisi zao ikiwemo
mabenki, watoa huduma za usafiri, mashirika ya ndege, Katika ziara hiyo ya siku moja ya ukaguzi wa jengo hilo, Dk.
mawakala wa safari za utalii na huduma, maduka ya bidhaa Kigwangalla aliongozwa na Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka
za utalii na mahoteli. ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro, Dk. Fredy Manongi na
Naibu Mhifadhi wa Huduma za Uendeshaji wa Mamlaka
“Tutapamba pia jengo hili na” live screen” (Mabango ya Video hiyo, Asangye Bangu.
Mubashara) za vivutio, hivyo wanyama wakiwa wanapita
18 Jarida la MALIASILI
Wizara ya Maliasili na Utalii
Faru huyu anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 55 anapatikana katika Hifadhi ya Ngorongoro na
alianza kuonekana mwaka 1963 akiwa angali mdogo.
Faru huyu amekuwepo tangu enzi za Faru John. Faru John alikuwa mnyama mwenye umbo kubwa,
machachari na mwenye nguvu kuliko faru wengine.
Faru John alijimilikisha karibu faru jike wote katika Kreta ya Ngorongoro na hakutoa nafasi kwa faru
dume wengine kujihusisha na faru jike yeyote.
Robo tatu ya faru weusi waliopo katika Hifadhi ya Ngorongoro kwa hivi sasa wametokana na uzao wa
Faru John.
Pamoja na wasifu wake huo mzuri, Faru John alishindwa kumzalisha Faru Fausta ambae waliishi nae
kwa muda mrefu.
Katika umri wake huo faru Fausta hakubahatika kupata mtoto mpaka leo.
Aidha, faru huyo anatumia jicho moja tu kutokana na jicho jingine kuwa bovu (Chongo).
Jarida la MALIASILI 19