Вы находитесь на странице: 1из 1

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAJI

Simu: +255 (0) 26 2322602 NBC MazengoBranch,


Tovuti: www.maji.go.tz Barabara ya Kuu,
Barua pepe:ps@maji.go.tz S. L. P. 456,
40473 Dodoma.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) ameelekeza timu ya wataalam wa maji kutoka Wizara ya
Maji kukagua miradi yote ya maji katika wilaya ya Mbulu mkoani Manyara na kuainisha changamoto za
miradi hiyo na namna ya kuzimaliza ili wananchi wapate huduma ya majisafi na salama kama Serikali
ilivyopanga.

Mhe. Aweso ametoa maelekezo hayo wakati wa ziara ya kikazi katika Wilaya ya Mbulu ambapo
amekagua mradi wa maji wa Arri, mradi wa maji Mongahay – Tumati, na mradi wa maji Dongobesh.

Mhe. Aweso (Mb) amesema miradi hiyo imechukua muda mrefu kukamilika wakati wananchi wanapata
adha ya kutokua na uhakika wa majisafi na salama kwasababu mahitaji yameongezeka. Amesema baadhi
ya miradi wamepewa wakandarasi wasio na uzoefu wa kutosha hivyo kushindwa kuikamilisha kama kwa
mujibu wa mikataba waliyopewa.

Waziri Aweso (Mb) akiongea na wakazi wa Mbulu amesema hatavumilia kuona rasilimali za serikali
zinatumika vibaya katika sekta ya maji, na kuainisha kuwa wakandarasi wanaoharibu miradi ya maji,
watachukuliwa hatua za kisheria, pamoja na kufungiwa kushiriki kazi yoyote inayohusu sekta ya maji
hapa nchini.

Pamoja na hilo, Mhe. Aweso (Mb) ameelekeza Jumuiya za Watumia Maji nchini zisajiliwe, na ziweke
mikakati ya kutunza miradi ya maji ili idumu na kuwa endelevu. Aidha, viongozi wawashirikishe waanchi
kulinda vyanzo vya maji na watoe elimu zaidi ili kuzuia kazi ya aina yoyote katika vyanzo vya maji ndani
ya umbali wa mita 60. Aidha, Mhe. Aweso (Mb) ameagiza fedha za dharura kiasi cha shilingi milioni 60
zitumike kuchimba kisima cha maji kwa wakazi wa Haydom.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini


Wizara ya Maji.
24.10.2018
1

Вам также может понравиться