Вы находитесь на странице: 1из 69

anamed team

DAWA ZA ASILI KATIKA NCHI ZA


TROPIKI

II MATIBABU

Matibabu ya magonjwa ya kawaida na matumizi ya


baadhi ya mimea muhimu katika nchi ya tropiki.
Kitabu cha Semina
Ki-suahili Numba: 119
Kitabu hiki kimeandikwa na anamed team: Dr. Hans-Martin Hirt, Dr.Peter Feleshi, Philip
Mateja, Dr. Lindsey na washiriki wengine wengi wa anamed.

Anamed Angola: Baptista Nsenda, Margarethe Roth


Anamed Congo – Kinshasa: Konda Ku Mbuta, Bindanda M´Pia
Anamed Congo South Kivu: Innocent Balagizi
Anamed Congo Prov. Equator: Dieudonne, Akuma Tande
Anamed Eritrea: Nighisti Alazar, Micele Paliaro
Anamed Ethiopia: Ralph Wiegand, Belay Bekele, Temesgen Choleyea
Anamed India: Sr. Rosita Kandathil, Kambala Subramanyam
Anamed Kenya: Roger Sharland, Rebecca Nzuki
Anamed Mozambique : Pascoal Cumbane, Myriam Wahr
Anamed Nigeria: YMCA Jos
Anamed Afrika Kusini: Margrit Hirt
Anamed Sudan: Dr. Elijah
Anamed Tanzania: Philip Mateja, Peter Feleshi, Maike Ettling
Anamed Uganda Christopher Nyakumi

na msaada wa uchunguzi wa Prof. Dr. Christoph Schäfer

Kwa toleo hili la ki-swahili tunamshukuru Emmanuel Biligeya kwa kazi yake ya utafsiri na
Mchg Hezron Shimba na Maike Ettling kwa kuhariri. Pia tunaishukuru HUYAMU (Idara ya
Afya ya AICT – Dayosisi ya Mara & Ukerewe) kwa ushirikiano wao wa karibu.

Toleo la tatu September 2015

© 2008 Hakimiliki na anamed

Anamed ingependa taarifa zilizo katika kijitabu hiki zisambazwe mahali popote zinapowezekana
kufika. Tunawahamasisha watumiaji wa kitabu hiki kukitafsiri katika lugha zao. Hata hivyo kwa
kuwa mambo yaliyomo yanaboreshwa mara kwa mara, tafadhali wasiliana na anamed kwanza.
Haki miliki ya tafsiri zote inabaki na anamed. Hakuna sehemu ya kitabu hiki inayoruhusiwa
kuchapwa na kuuzwa tena.

Mabango ya rangi (anamed No. 403) vinaonyesha mimea iliyoelezwa katika kitabu hiki.

Toleo la pili la kitabu hiki linapatikana katika lugha ya kifaransa, kireno, kijaluo, kiamharic,
kiateso na kichichewa. Baadhi ya vitabu vya anamed vinapatikana katika baadhi ya nchi za
Afrika.
Wafuatao wanaunganisha anamed na ndio wauzaji na wasambazaji wa vitabu na vifaa vya
anamed:
anamed, Schafweide 77, D – 71364 Winnenden, Germany
Email: anamedhmh@yahoo.de
Website: www.anamed.net
YALIYOMO

Sehemu I: Kuzuia magonjwa ya kawaida


Sura 1: Kuzuia magonjwa ya kawaida....................…………………………..3

Sehemu II: Tiba ya magonjwa ya kawaida


Sura 2: Vidonda, kuungua, majipu na uvimbe………………………………...5
Sura 3: Magonjwa ya ngozi……………………………………………………8
Sura 4: Kuharisha…………………………………………………………….11
Sura 5: Malaria ………………………………………………………………16
Sura 6: UKIMWI: Imarisha mfumo wa kinga mwilini………………………19

Sehemu III: Matumizi ya baadhi ya mimea


muhimu ya nchi za Tropiki
Sura 7: Allium Sativum (kitungu saumu)……………………………………21
Sura 8: Artemisia annua anamed (A – 3)…………………………………….23
Sura 9: Azadirachta Indica (Mwarobaini)…………………………………….38
Sura 10: Carica papaya (Mpapai)…………………………………………….42
Sura 11: Moringa oleifera (Mlonge)

Sehemu IV: Utengenezaji wa baadhi ya madawa


Sura 12: Mafuta na dawa za mafuta …………………………………………47
Sura 13: Jiwe jeusi……………………………………………………………49

Sehemu V: Msingi wa matumizi ya dawa za asili


Sura 14: Kazi ya kikundi – Maendeleo ni nini?...................................
Sura 15: Anzisha bustani ya mimea ya madawa……………………………...50
Sura 16: Mawazo ya ki-biblia ………………………………………54
Sura 17: Mwongozo na maadili kwa “Waganga wa asili”.……………………55
anamed

Madawa ya asili katika nchi za Tropiki: Matibabu II

Matibabu, mimea, madawa, kazi ya vikundi na maadili.

Kitabu cha maelezo kwa semina ya madawa ya asili


kwa muda wa juma moja.
Na anamed team na
Washiriki wengi wa anamed duniani kote.

anamed (Action for Natural Medicine) ni shirika la Kikristo na Muungano wa huduma


unaolenga kusaidia watu katika nchi za Tropiki kujitegemea kadri iwezekanavyo, hasa kwa
masuala ya kiafya. anamed inafanya kazi na watu wa imani zote waliojitoa kuinua hali ya afya
ya majirani zao, mkoa na taifa.

anamed inafanikisha lengo hili kwa kuwasikiliza waganga wa jadi, kufanya uchunguzi wake
binafsi, na kuboresha mchanganyiko wa madawa kwa matibabu. Tunatoa matokeo katika kitabu
kiitwacho “Dawa za asili katika nchi za tropiki.” Kwa hiyo tangu 1985, tumeweka wazi kwa
watu wote ujuzi wetu wote juu ya afya na uponyaji kwa kutumia mimea inayopatikana bure kwa
jamii nzima. Hatuna siri, na hakika hatuna sheria inayozuia kuigwa!

anamed inatoa ujuzi na uzoefu huu, hasa katika Afrika, kwa kuendesha semina za “Dawa za
asili” kwa muda wa juma moja kwa wafanya kazi wa afya, madaktari, waganga wa jadi, viongozi
wa dini, wahudumu wa jamii na kadhalika. Semina inapitia utambuzi na uchunguzi zaidi wa
baadhi ya mimea ya dawa, utayarishaji wa madawa kutokana na mimea hiyo, matumizi yake
katika tiba na matatizo ya kawaida ya kiafya na magonjwa.

Kwa kusema “dawa za asili,” anamed ina maana ya muungano wa faida za madawa ya jadi na
zile za huduma za tiba za kisasa zenye msingi wa kisayansi.

Kitabu kiki, kitabu cha pili katika mfululizo wa “Dawa za asili katika nchi za Tropiki,” ina
karibu masomo yote yanayohitajika kwa mafunzo ya semina kwa juma zima la kwanza katika
dawa za asili. Nafasi hairuhusu maelezo zaidi juu ya falsafa ya kazi yetu, ingawa jambo hili ni la
muhimu sana. Jambo hili limeelezwa katika kitabu cha kwanza, ambacho pia kinaeleza mimea
mengi zaidi na kina maelezo zaidi juu ya kujitengenezea dawa nyumbani. Kitabu cha tatu ni
msaada wenye taarifa nyingi kwa viongozi wa semina. Kitabu cha nne kimetolewa kwa ajili ya
huduma kwa wanaoishi na VVU/UKIMWI.

Sehemu I ya kitabu hiki inaelezea jinsi ya kuzuia baadhi ya matatizo ya kitabibu yaliyo ya
kawaida katika nchi za tropiki, na sehemu ya II ni juu ya kutibu. Sehemu III inaelezea mimea na
miti mitano maalumu, ambayo yote inaweza kustawi katika nchi za tropiki. Kwa miti hii mitano
tu matatizo mengi ya kiafya yanaweza kutibiwa. Kwa nyongeza, unaweza kupata chakula chenye
virutubisho, kusafisha maji, kurutubisha ardhi na kutengeneza kiuatilifu kizuri. Sehemu ya IV
inaeleza jinsi ya kutengeneza baadhi ya madawa. Na sehemu ya V inatoa baadhi ya msaada kwa
ajili ya semina, pamoja na mtiririko muhimu wa rejea kwa ajili ya waganga wa dawa za asili.
Ukishahudhuria semina ya anamed juu ya dawa za asili, tafadhali endelea kuwasiliana na
wengine katika mkoa wako na nchi yako ambao wanatibu kwa madawa ya asili. Panga
kutembeleana, endesha mafundisho, na julisha anamed International huku Ujerumani juu ya
mafanikio yako! Asante!

Sehemu I
Sura 1:
Kuzuia magonjwa ya kawaida.
Kama tukijali mtindo wetu wa maisha, lishe, afya na mazingira tunayoishi tunaweza kutoa
mchango mkubwa sana katika afya bora ya familia zetu, mimea yetu na wanyama.

1.1.Kula vizuri!
Mara nyingi ni tatizo kwamba, watu wakitajirika kidogo, ubora wa lishe yao unashuka.
Vyakula bora (angalia jedwali hapo chini) vinatujengea nguvu na mfumo wetu wa kinga
mwilini – yaani uwezo wetu kushambulia maambukizi na magonjwa. Vyakula visivyo
bora kama vile sukari nyingi, unga uliokobolewa, mkate mweupe, soda mbalimbali,
vyakula vya kwenye makopo, hupelekea ukosefu wa vitamini na protini. Kwa hiyo
tunakuwa na uwezekano mkubwa kupata maambukizi yoyote na magonjwa.

Jedwali I: Vyakula vya ki-msingi


Kwa kupata nguvu kwa Mizizi ya wanga: Mihogo, viazi vitamu, “Taro”
urahisi Matunda ya wanga: Ndizi, “breadfruit”
Kwa kupata nguvu na Nafaka na mbegu: Ngano, mahindi, mchele, mawele,
protini mtama, mkate. Kula mkate wa unga usiokobolewa na
unga wa mahindi yasiyokobolewa.
Epuka mkate uliotengenezwa kwa unga mweupe na
mahindi yaliyokobolewa!
Kwa chakula chenye protini Mbegu za mafuta: boga, tikitimaji, ufuta na alizeti.
kwa wingi Jamii ya kunde: maharage, njugu, dengu, soya zenye
kokwa, karanga, korosho, “almonds”
Mazao ya wanayama: maziwa, mayai, jibini, samaki,
kuku, na nyama yoyote.
Kwa vitamini na madini Mboga: majani ya kijani – nyeusi, majani ya mihogo,
viazi vitamu na majani ya viazi vitamu, nyanya, karoti,
maboga, majani ya mlongelonge, mbegu za amaranth na
mengine zaidi.
Matunda: maembe, machungwa, limao, mapapai, mapera,
passion fruit n.k.
Jusi ya matunda.
Kwa kinga imara ya mwili Kula vitunguu swaumu vibichi, unga wa majani ya
mlonge, mbegu za amaranth, nyama laini ya jamii la
msubili.

Lima matunda, mbogamboga na mimea ya madawa wewe mwenyewe! Siyo jambo lililopitwa na
wakati wala rahisi! Vyakula vya kujitengenezea kutokana na bustani ya nyumbani ndivyo
vyenye virutubisho bora zaidi.

Lisha watoto mara kadhaa kwa siku. Wanahitaji vyakula kidogo kidogo mara kwa mara.

Kunywa jusi ya matunda halisi – nchi za Tropiki zina wingi wa matunda !

Hatari za lishe mbaya


a) Watu wa Afrika kwa sasa wanakula sukari zaidi kuliko ilivyowahi kutokea. Soda zina sukari
nyingi, hata wanga katika mkate mweupe unabadilishwa na vimengenya kuwa sukari mdomoni.
Matokeo yake watu wengi sasa wameoza meno na kupata kisukari au matatizo mengine ya afya.
Wengi hawawezi kugharimia matibabu yake. Kwa hiyo punguza utumiajii wa sukari ya
kiwandani. Na jaribu kunywa chai na kahawa bila sukari!
b) Watoto wanaokula mkate mweupe, ugali wa mahindi na mihogo wanaweza kuingia katika hali
ya utapiamlo kwa sababu ya upungufu wa protini, vitamin na madini.
c) Kama kwa vyovyote ikiwezekana, nyonyesha mtoto kwa maziwa ya titi – usishawishiwe na
matangazo ya biashara juu ya maziwa ya chupa kwa mtoto. Uchafu na maambukizi mengine
yananywewa na mtoto kwa urahisi kupitia hizi chupa, ambapo hupelekea kuharisha na
magonjwa mengine. Vyakula vya madukani vya watoto hudhoofisha mtoto wako na uchumi wa
familia yako!
d) Matukio ya saratani na madhara ya ki-afya yanaongezeka kwa sababu ya kuongezeka kwa
idadi ya madawa ya viwandani kutengenezwa. Soda na vinywaji vitamu vingine pamoja na
bidhaa zingine za kibiashara zinakuwa na madawa na sukari ya kiwandani ambazo zinaweza
kuharibu afya yako. Vyakula vya makopo pia vinakuwa na madawa hatarishi ya kuhifadhi
chakula. Hata Blue Band ya mikate ina hayo madawa ya kuhifadhi chakula. Ni vizuri zaidi
kupaka embe mafuta kwenye mkate wako!
Madawa hatarishi ya viwandani yanakuwepo sio tu kwenye vyakula vya madukani, lakini pia
kwenye kilimo (kama mbolea ya madawa ya kuulia wadudu), katika moshi ya magari na hata
kwenye nguo na vifaa vya ujenzi.

1.2. Angalia maji yako!


Hakikisha maji unayokunywa ni salama. Kutokana na ubora wa maji yako, unaweza kutengeneza
chujio la maji kwa mchanga, unaweza kutumia mbegu za mlongelonge zilizosagwa kama
ilivyoelezwa katika sura ya 11, au unaweza kuchemsha maji katika jiko la jua.
Shirikiana na wengine kuhakikisha mto wako unabaki msafi. Toeni matakataka yote! Kama
watu wakifulia nguo zao, au hata baiskeli na magari, katika maji ambayo wengine wanakwenda
kutumia kwa kunywa, basi wanasababisha matatizo ya afya!

1.3. Rutubisha ardhi yako – kiasili.


a) Panda mimea jamii ya kunde (ambayo huongeza naitrojeni kwenye udongo). Mimea
jamii ya kunde ni pamoja na mboga kama vile maharage na karanga, miti kama vile
Lusina. Lusina inaweza kupandwa kufuata kontua kuzuia mmonyoko wa ardhi, na zikatwe
ncha zake mara kwa mara ili kutengeneza uzio. Matawi yanayokatwa yanasaidia
kurutubisha udongo.
b) Ozesha takataka za mimea, maganda yote ya matunda, majani ya mboga, takataka za
shambani (lakini epuka mbegu za magugu), samadi ya kuku na wanyama wengine
virundikwe (siyo karibu sana na nyumbani lakini). Kama vikidumishwa katika hali ya
unyevu na uvuguvugu, udongo mzuri mweusi utapatikana ndani ya miezi 3, ambao,
ukichanganywa katika shamba lako, utaweka virutubisho (naitrojeni na madini) taratibu
kwenye shamba lako.
c) Tandazia nyasi – angalia sura ya 14.
d) Epuka matumizi ya madawa hatarishi ya kilimo. Usitumie au tumia kiasi kidogo sana
cha mbolea za viwandani au dawa za kuua wadudu. Zinachafua maji, zinaua viumbe,
wanyama na mimea visivyo na madhara (na zaidi vyenye umuhimu) na zinadhuru rutuba
ya asili katika udongo.

1.4. Vyoo vya kienyeji ni visafi na ni rahisi kutumia!


Kinyesi na mkojo vinaweza kuwa vyanzo vya maambukizi mengi. Chimba shimo, jenga kijumba
juu yake. Tundu la shimo lazima lifunikwe wakati wote. Kama ukiweka dohani ambayo
huchukua hewa kutoka kwenye shimo hadi juu ya paa, choo hakitatoa harufu. Shimo likijaa,
lifunike kwa udongo na upande mwembe juu yake! Kisha tengeneza choo kingine cha kienyeji
mahali pengine. Vyoo vya kienyeji vinatunza rutuba ndani ya ardhi, wakati ambapo vyoo vya
maji vinachafua vijito na mito. Na vinatumia maji kidogo, ambayo katika sehemu nyingi
yamezidi kuwa adimu.

1.5. Tupa takataka kwa uangalifu !


Katika miji mingi unaweza kuona “moto wa milele”, ambao mara chache unazima na ambamo
takataka - ikiwa ni pamoja na plastiki na metali – vinatupwa. Moto huu una moshi mweusi mzito
wenye sumu kali zinazoitwa dioxins.
Takataka zinazozagaa hazipendezi. Vitu vyenye ncha kali vinaweza kukata watu, betari na
baadhi ya vifaa vya umeme vina sumu, ni pamoja na maji ya mvua yaliyotuama katika mifuko ya
plastik, magurudumu yaliyochakaa ambamo pia hutengeneza sehemu za mbu wa malaria
kuzaliana.
Kwa hiyo tupa takataka zako kama ifuatavyo:
Mara utakapozoea kutenganisha takataka zako namna hii nyumbani kwako, wafundishe mfumo
huu kijijini kwako au hata mjini unapoishi.

a) NDOO YA KIJANI: Tupa kila siku: Kwa ajili ya takataka za ki-mimea kutoka bustani
yako au jikoni (“0rganic waste”). Uziozeshe kupata mbolea. Au afadhali zaidi: uwalishe
kuku zako na takataka za ki-mimea ili panya na nyoka wasikaribishwe karibu na nyumba
yako
b) NDOO YA BLUE: Tupa kila wiki: Kwa ajili ya karatasi. Ukusanye kwenye ndoo na mara
moja kwa wiki choma karatasi pamoja na plastiki inayoweza kuchomwa ndani ya dakika 5.
Majivu yatupwe pamoja na metali.
c) NDOO NYEKUNDU: Tupa kila mwezi. Kwa ajili ya metali, vioo, plastiki, betari. Kama
kuna uwezekano wowote wa kuvitumia tena au kuvibadilisha kuwa vitu vingine, fanya
hivyo. Sisitiza serikali yako idai fedha za kuwekesha kwa kila mfuko wa plastiki na chupa za
vioo inayouzwa, ili kwamba ziweze kutumika tena au kurudishwa viwandani. Vikusanye
kwa uangalifu, na kama hakuna mfumo wa kuweza kuvitumia tena kila mwezi uvizike chini
sana kwenye udongo. Betari hasa zina sumu! Usipande mboga zako juu ya shimo hilo!
d) Mbao: Uchome na uweke majivu yake shambani, yana madini yenye thamani.

1.6. Mifuko ya Plastiki


Baadhi ya nchi za kiafrica sasa zinazuia matumizi ya mifuko ya plastiki. Katika miji mifuko ya
plastiki pamoja na chupa zimekuwa zikichafua mazingira na yanapochomwa yanatoa hewa za sumu.
Imekuwa ikiziba mifereji ya maji na kusababisha mafuriko mvua kubwa zinaponyesha.
Mashambani, mifuko ikiliwa na ng´ombe na mbuzi inaziba matumbo yao na wanyama wanakufa.
Hata watoto wanaweza kufa baada ya kuchezea mifuko ya plastiki au chupa zilizoathiriwa na mate
au kinyesi.

1.7.Usafi na Afya
Wakati wote osha mikono yako kwa sabuni na maji kabla ya kula au kutayarisha chakula, na baada
ya kutoka chooni. Kama huna sabuni jitengenezee, au sugua mikono yako kwa maji ya majani ya
mpapai.
Kuoga mwili mzima kila jioni hufanya mwili na kitanda kuwa safi.

1.8. Kwa upishi wa ndani, weka dohari!


Kama wakati mwingi chumba chako kimejaa moshi basi uko katika hatari kubwa ya kupata matatizo
makubwa ya macho na magonjwa ya mapafu. Ufumbuzi bora zaidi wa tatizo hili ni kutengeneza jiko
linalotumia nishati kidogo (maana yake matumizi ya kuni kidogo ) pamoja na dohani.

1.9. Mazoezi na uimara wa mwili


Watu wengi wana mazoezi mengi, mfano wanawake wanaotembea kilometa nyingi kila siku
kutafuta kuni na maji. Wengine wana mazoezi kidogo sana. Je familia yako “ina maendeleo“au
“haijaendelea”? Katika familia “zilizoendelea” mwanaume na mwanamke wanafanya kazi kwa
pamoja, hivyo wana mazoezi yanayofanana. Kwa njia hii mke hawi dhaifu sana, wala mme hanenepi
sana. Kama ukiuweka mwili katika hali inayofaa, utakuwa na kinga bora zaidi kwa magonjwa.

1.10. Zuia ajali za barbarani


Kuongezeka kwa kasi kwa idadi ya magari inaongeza matukio ya ajali zinazosababisha majeraha
makubwa na vifo katika nchi za joto. Himiza kampeni za kuangalia usalama wa magari, vidhibiti
mwendo, vipunguza moshi wa magari na njia za ziada kwa wote watembea kwa miguu na
waendesha pikipiki

SEHEMU II MATIBABU YA MAGONJWA YA KAWAIDA

SURA 2 Vidonda, kuungua, majipu na uvimbe

Tumia kitambaa kilicho safi. Wakati wa dharula, kama unahitaji huduma lakini ukawa huna
kitambaa, chukua vipande vya nguo hasa za pamba. Ili kuzifanya salama zichemshwe katika
maji kwa dakika 20 na zikaushe kwa kutumia kaushio la jua (sola) lililo safi au kama huna
kaushio la jua zikaushe kwa kuanika kwenye kamba ya nguo juani.

Muhtasari ya tiba ya vidonda, kuungua na uvimbe:


Aina ya Ugonjwa Chaguo la kwanza Chaguo la pili Chaguo la tatu
Vidonda Tibu kwa sukari Tibu kwa asali Tibu kwa papai
vipya lililoiva
Vidonda Vidonda Papai na sukari Tibu kwa papai Embwe la majani
vyenye bichi ukibadilisha ya mpera
uambukizo na tiba ya sukari
Kuungua Ute wa Aloe Maji ya chumvi Osha kwa chai ya
kupya (msubili) mpera
Kuungua Kuungua Utomvu mweupe Ute wa Aloe Dawa ya mafuta ya
kuliko na wa mpapai, maji (msubili) vitunguu
uambukizo yenye chumvi
Jipu Vitunguu saumu Dawa ya pilipili ya Dawa ya mafuta ya
lililofungwa vilivyopondwa mafuta vitunguu
Jipu pondwa
Jipi lililo wazi Papai na sukari Tibu kwa papai Embwe la jani la
bichi ukibadilisha mpera
na tiba ya sukari

A. Vidonda
Lengo kuu la tiba hii ni kuzuia kidonda kupata maambukizi, hivyo kuruhusu mchakato wa mwili
kujiponya wenyewe vizuri iwezekanavyo.
a) Kwanza osha kidonda.

Kwa Vidonda vilivyo wazi, visafi, vipya, visivyo na usaha

Tumia ama i) Maji baridi yaliyochemshwa na kuwekewa chumvi kidogo,


au ii) Chai ya mpera:
Chemsha kiganja 1 cha majani ya mpera kwenye lita 1 ya maji kwa muda wa
dakika 15. Yapoe na baadaye yachuchwe. Osha kidonda kwa kutumia maji haya.
Tengeneza upya kila unapoosha kidonda.

Kwa kidonda kinachoonesha dalili za maambukizo,


tumia maji yenye utomvu wa mapapai
Maji yenye utomvu wa mapapai: Kama kidonda ni kichafu ukioshe mara kadhaa kila siku kwa
kutumia maji yenye utomvu wa mapapai. Osha papai bichi lililopo mtini kwa kutumia kitambaa
safi na maji safi ya moto. Weka lita 1 ya maji yaliyochemshwa na kupoa kwenye chupa safi.
Ongeza kijiko 1 cha mezani cha chumvi na koroga vizuri. Kata papai na kukusanya matone 3 – 5
ya utomvu wake kwenye chupa ile (kama ilivyooneshwa kwenye picha ya kitabu hiki). Usitoe
tunda kwenye mti, kwa sababu utomvu unakauka kwa haraka papai linapovunwa. Lakini
ukiliacha kwenye mti unaweza kuendelea kulitumia mara kwa mara.
A. 1. Vidonda safi, vilivyowazi na visivyo na usaha
A.1.a. Sukari pekee
Rundika sukari kwenye kidonda. Funga kidonda kwa kitambaa ili kuzuia sukari isitoke. Sukari
huondoa unyevu kwenye vimelea vya magonjwa kwa mchakato uitwao mfyonzo (osmosi) na
vimelea hivyo hufa.
Kihudumie kidonda mara 3 kwa siku kwa kuongeza sukari, usikioshe.
A.1.b. Mchanganyiko wa asali na sukari
Hakikisha una asali halisi. Njia bora ni kununua sega la nyuki, na ukamue asali mwenyewe. Hii
inafanyika kwa namna hii: Pondaponda sega hilo. Unaweza kufanya hivyo kwa kutumia kinu
kipya au chombo cha kusagia nyama ikiwa kimeondolewa kitufe cha kusagia. Ni vizuri kufanya
hivyo usiku ili kuepuka kusumbuliwa na nyuki. Sambaza mchanganyiko huu kwenye kitambaa
safi cha pamba kilichofungiwa juu ya bakuli safi la metali. Viweke kwenye jiko la jua (solar
oven) mchana kutwa hadi asali na nta vyote vivujie kwenye bakuli. Vitaunda matabaka tofauti.
Jioni funua jiko la jua na ondoa nta, ambayo inaweza kutumika baadaye kwa kutengeneza dawa
za mafuta (angalia sura ya 12).
Sasa asali ni tayari kwa matumizi. Weka kiwango sawa cha asali na sukari. Sukari huzuia asali
kusambaa kwa urahisi. Asali huua bakteria na kuacha kidonda kikiwa safi. Kidonda kitibiwe kwa
mchanganyiko wa asali na sukari mara kadhaa kwa siku pasipo kukiosha tena.
A.1.c. Papai lililoiva (Carica papai)
Weka kipande chembamba na laini cha papai lililoanza kuiva juu ya kidonda.

A.2. Vidonda vyenye maambukizo, majipu yaliyopasuka ya siku nyingi, vidonda vya wazi
Papai (Carica Papai)
Kwa matayarisho ya papai yafuatayo, vidonda vya wazi vilivyokuwa sugu kwa miaka mingi
vimeweza kupona, kwa kawaida hata ndani ya wiki 1. Hii ni moja kati ya mifano kadhaa ambapo
dawa za asili zimekuwa bora kuliko madawa ya hospitalini.
Tumia matayarisho yafutayo ya mapapai hadi kidonda kisiwe na usaha tena. Kisha tibu kidonda
kwa sukari au mchanganyiko wa asali na sukari.
A.2.a. Sukari ya papai
Changanya gramu 10 za sukari (nusu ya kikopo cha mikanda ya picha) na matone 10 ya utomvu
wa papai bichi. Tengeneza upya kila siku. Tusemapo sukari „halisi“ tuna maana ya sukari
ambayo imechukuliwa moja kwa moja kutoka kwenye mfuko mpya kwenye kiwanda. Weka hii
sukari ya papai kwa wingi kwenye kidonda, na mara tu inapoanza kuwa na majimaji ongeza
nyingine. Kidonda kinaweza kuhitaji huduma hii mara kadhaa kwa siku.

A.2.b. Papai bichi


(i) Kipande chembamba: Weka kitambaa kwenye maji yanayochemka, wakati kikiwa bado cha
moto sana osha papai bichi vizuri ambalo bado liko mtini. Osha kisu, kiweke ndani ya maji
yanayochemka kwa dakika kadhaa, kisha kata kipande chembamba cha papai chenye unene wa
kidole kidogo cha mtoto. Kiwekwe juu ya kidonda na ukishikize kwa kukifunga kwa kitambaa.
Usikiondoe kwa masaa 8. Kama kikisababisha maumivu sana kiondoe mapema! Fanya huduma
hii mara 3 kwa siku kwa siku kadhaa hadi kusiwe na usaha tena. Endeleza tiba hii na pia tumia
tiba ya sukari kama tiba mbadala kwa hii. Baada ya kila huduma ya sukari rudi kwenye mti,
ondoa sehemu ile nyembamba ya lile papai ambayo kwa sasa itakuwa chafu, kisha kata na weka
kipande chembamba kinachofuata kwenye kidonda.
(ii) Vijiti: Vidonda vyembamba vyenye kina mara nyingine hutokea, kwa mfano, kwenye
migongo ya wagonjwa waliolazwa muda mrefu. Katika mazingira yasiyo na maambukizo,
waganga katika hospitali wanaweza kukata vipande vyembamba vya papai bichi na kuviingiza
kwenye kidonda.

A.2.c. Embwe la majani ya mpera (Psidium Guajava)


Tiba hii haina gharama yoyote. Kwa hiyo inapatikana kwa wale wasioweza hata
kununua dawa za gharama ya chini kabisa. Twanga kiganja kizima cha majani ya mpera
yaliyooshwa. Yachemche taratibu pamoja na kikombe cha maji kwenye chungu kilichofunikwa
kwa dakika 15. Iache ipoe. Weka embwe kwenye kidonda na vifunge. Rudia tiba hii asubuhi na
jioni.
A.2.d. Papai lililoiva
Weka kijiko na bakuli katika maji yanayochemka kwa muda wa dakika 10 na kisha uvitumie
kusaga nyama za papai lililoanza kuiva na kusambazia embwe lake kwenye kidonda. Fanya
hivyo kwa kufuata kila hatua, asubuhi, mchana na jioni. Jinsi kidonda kinavyoonesha kuwa na
maambukizo zaidi ndivyo unavyotakiwa kutumia papai bichi zaidi.
A.2.e. „Gel“ ya Aloe (Msubili)
Kwa vidonda vya siku nyingi vilivyo wazi na vilivyokataa kupona, kifunike kidonda kwa gel ya
Aloe iliyochukuliwa moja kwa moja kutoka kwenye jani lililo kwenye mmea mara 3 kwa siku.
A.2.f. Mafuta ya Kitunguu saumu
Tumia mafuta ya kitunguu saumu (Allium Sativum), angalia sura ya 7.5. Weka mara kadhaa kwa
siku. Kwa kutengeneza kiasi kidogo cha mafuta ya kitunguu saumu changanya kijiko 1 cha
mezani kitunguu kilichokatwakatwa vipande vidogovidogo sana na vijiko 2 vya mezani vya
mafuta ya mimea. Weka kwenye chombo cha kioo, tikisa vizuri. Yatumike ndani ya masaa 24.
A.2.g. Mafuta au dawa ya mafuta ya vitunguu maji (Allium cepa):
Angalia sura ya 12
A.2.h. Kwa vidonda na majipu yanayotoa usaha tumia jiwe jeusi (angalia sura ya 13)

B. Kuungua
B.1. Kidonda kipya cha kuungua
Kwanza poza kidonda kwa maji safi ya baridi. Kumbuka, lengo kuu la huduma hii ni kuzuia
maambukizo. Mweke mgonjwa kwenye chandarua ili kuzuia inzi kwenye kidonda.

B.1.a. Aina za Msubili (Aloe barbadensis, Aloe ferox au Aloe arborescens)


Osha jani vizuri bila kuliondoa kwenye shina. Kisha likate toka kwenye shina. Osha kisu kikali
na ukiweke kwenye maji yanayochemka. Kwa kutumia kisu hiki, kata ile sehemu iliyo wazi tena
ili kuifanya iwe safi kabisa, na pia kata na kuondoa ncha zenye miiba. Kisha ukate katikati kwa
kufuata urefu ili kuweka wazi sehemu kubwa ya „gel“ iliyokatikati, ndani ya jani. Paka sehemu
ya majimaji ya jani la msubili kwenye sehemu yote iliyoungua. Rudia mara kadhaa kwa siku.
Mweke mgonjwa ndani ya chandarua kuzuia inzi. Msubili hufanya kazi ya kuzuia maambukizo
na kuzuia kuvimba.
B.1.b. Chumvi ya mezani
Yeyusha gramu 9 (kijiko 1 cha mezani kilichojaa kabisa) za chumvi ya mezani katika lita 1 ya
maji, chemsha kwa dakika 20 na iache ipoe. Mwagie mchanganyiko huu kwenye sehemu
iliyoungua mara kadhaa kwa siku. Kama kidonda kina kina kirefu, kifunge kwa „bandaji“ au
kitambaa kisafi (kilichoondolewa maambukizo). Mwaga haya maji ya chumvi mara kadhaa kwa
siku juu ya kitambaa hicho. Matone kadhaa ya utomvu kutoka kwenye papai bichi yanaweza
kuongezwa kama kuungua kunaonekana ni hatari sana. Kwa dharula, kama huna chumvi,
chemsha mkojo wa mgonjwa na utumie! Mkojo una chumvi!
B.1.c. Chai ya mpera (Psidium guajava)
Chemsha taratibu kiganja 1 cha majani mabichi yaliyooshwa ya mpera kwenye lita 1 ya maji
katika chungu kilichofunikwa kwa dakika 15. Acha ipoe na uichuje. Baada tu ya kuchuja osha
kidonda kwa chai hii. Rudia mara 3 kwa siku. Itakayobaki uimwage – tengeneza chai mpya kila
inapohitajika.
B.1.d. Mafuta na dawa ya mafuta ya kitunguu maji: Angalia sura ya 12.
B.2. Kuungua kuliko na maambukizo
B.2.a. Maji yenye utomvu wa papai na chumvi
Kama sehemu iliyoungua ni chafu, isafishe mara kadhaa kwa siku kwa kutumia maji ya utomvu
wa papai kama iliyoelekezwa hapo juu (A). Tumia pia “Gel” ya Aloe (angalia B.1.a.) au mafuta
ya vitunguu maji (angalia B.1.d.)

C. Majipu
Jipu ni maambukizo yanayosababisha kifurushi kidogo cha usaha chini ya ngozi.
C.1. Jipu lililofungwa usaha chini ya ngozi, ni pamoja na majipu yaliyo na mdomo,
vidonda vilivyofungwa, maambukizo ya ngozi kuzunguka makucha ya vidole vya mkono
au miguu n.k.
C.1.a. Vitunguu saumu (Allium sativum)
(i) Kata vipande vyembamba vya vitunguu saumu na uvifungie kwenye sehemu iliyoathirika
(fanya hivi kwa usiku mzima kwa siku kadhaa) au
(ii) Pondaponda kitunguu saumu na upake sehemu iliyoathirika au
(iii) Tumia mafuta ya kitunguu saumu (angalia sura 7)
Vitunguu saumu vina nguvu sana kuliko vitunguu maji. Uwe mwangalifu: Mgonjwa mwenye
udhaifu wa ngozi anaweza kupata mabaka. Kufungia kitunguu saumu kwenye ngozi ndiyo njia
bora zaidi, lakini pia iletayo maumivu zaidi. Kupaka ngozi kwa mafuta ya vitunguu saumu ni
tiba dhaifu kidogo lakini pia isiyosababisha maumivu sana.
C.1.b. Dawa ya mafuta ya pilipili: Angalia sura ya 12

C.1.c. Kitunguu maji (Allium cepa)


Fuata matumizi ya vitunguu saumu hapo juu (C.1.a.). Badala ya mafuta ya vitunguu saumu tumia
dawa ya mafuta ya vitunguu maji (angalia sura ya 12). Dawa ya vitunguu maji siyo kali kama
dawa ya vitunguu saumu.
C.2. Jipu lililo wazi
Utibu kama vidonda vyenye maambukizo, angalia A.2.hapo juu.

Sura 3: MATATIZO YA NGOZI

A. Utangulizi: Matunzo ya ngozi na usafi


Tengeneza na tumia sabuni inayolinda ngozi. Kwa kufua, tumia sabuni ya kujitengenezea
iliyotengenezwa kama ifuatavyo: Chukua vipimo 4 vya sabuni ya kawaida, na kipimo 1 cha
mafuta ya mboga na kipimo 1 cha maji. Pondaponda sabuni, ichanganye na mafuta na maji.
Chemsha mchanganyiko polepole hadi sabuni itakapoyeyuka. Koroga mchanganyiko huo mpaka
utakapopoa, kisha uumwage kwenye vyombo vya chapa. Acha kwa majuma 2 kabla ya
kuutumia. Sabuni hii inaweza kuwekewa dawa kwa kudondoshea matone kadhaa ya mafuta ya
mwarobaini, au majani makavu yaliyopondwa yanayotokana na mwarobaini au mlongelonge
kabla ya kuimwaga kwenye vyombo vya chapa.

B. Matatizo mbalimbali ya ngozi


Kwa matatizo ya ngozi yasiyojulikana chanzo chake, kunywa mchanganyiko wa aina mbalimbali
za chai za dawa, hasa Rozela na Artemisia, ili kuondoa sumu mwilini. Zinasaidia kusafisha
damu, kulainisha takataka kwenye utumbo mkubwa, na kuzisaidia kutolewa nje hadi chooni.
Uchafu na takataka mwilini zinaweza kusababisha matatizo ya ngozi.

Kwa matibabu ya ngozi, tunapendekeza uanze na matibabu rahisi zaidi yanayonawirisha ngozi
(yaliyotajwa mwanzoni), na endelea kwa utaratibu hadi kwenye zile zenye nguvu - lakini pia
madhara - zaidi.

 Persea americana (avocado/ embe-mafuta)


Upakaji wa nyama ya embe-mafuta lililoiva hufanya kazi kama huduma ya msingi ya kuanzia
au dawa nzito ambayo hunawirisha ngozi yenye maambukizo au ngozi kavu. Dawa hii
inaweza kutayarishwa jioni kwa kutumiwa kwa urembo; lakini lazima itumike haraka baada
ya kutengenezwa. Changanya nyama ya embe-mafuta lililoiva na matone kadhaa ya limau na
upake kwenye sehemu iliyoathirika kwa muda wa masaa 12 kwa siku; kwa mfano usiku
mzima. Nyama ya embe-mafuta inaweza pia kutumika kama kiungo cha msingi kwa madawa
au vipodozi, mfano: kwa kuchanganya na maji ya limau, mafuta ya mbegu za mwarobaini,
nyama ya msubili n.k.
 Mafuta ya mbegu, kama vile mafuta ya mbegu za mchikichi, mafuta ya alizeti, mafuta
ya karanga. Changanya kijiko 1 cha chai cha mafuta kwa kipimo kilekile cha maji kwenye
kiganja cha mkono wako na usugue kwenye sehemu iliyoathirika.
 Nyama ya msubili: angalia sura ya 2.
 Brassica oleracea (kabeji): Tengeneza uzingo kutokana na jani la kabeji liliooshwa, na
ulizungushe sehemu iliyoathirika. Huko Nigeria, mtoto mmoja aliamka mara 4 kila usiku
akitoka damu, mwenye ngozi kavu. Kumzinga kwa jani la kabeji kulileta nafuu haraka.
 Mafuta au dawa ya mafuta iliyotengenezwa kutokana na mafuta ya mbegu na mimea kama
vile mpera, chamomila au artemisia. Kwa mchanganyiko huu angalia sura ya 12.
 Mafuta ya mbono (kutokana na Ricinus Commonis), ama iliyotengenezwa kiwandani,
iliyotengenezwa kienyeji kijijini au iliyotengenezwa kwa kutumia mchanganyiko kutoka
“Madawa ya Asili katika Nchi za Tropiki I”.
 Cassia alata (ringworm bush): Tengeneza embwe kwa kutumia majani yaliyopondwa na
mafuta.
 Azadirachta Indica (Mwarobaini): Tumia kama embwe la majani na mafuta au maji, au dawa
ya mafuta kutokana na majani, au mafuta ya mbegu za mwarobaini.
 Allium Cepa (Kitunguu maji): Tumia mafuta yake au dawa ya mafuta. Angalia sura ya 12.
 Capsicum frutescens (pilipili): Paka mafuta ya pilipili au dawa ya mafuta yake kwenye
sehemu iliyoathirika. Pilipili ina viasili vinavyoua maambukizo na mara nyingine huondoa
maumivu. Angalia sura ya 12.
 Allium Sativum (vitunguu saumu – kama mafuta ya vitunguu saumu). Angalia sura ya 7.
 “Mafuta ya upele”: Kipimo cha 50:50 cha mchanganyiko wa mafuta ya taa na mafuta ya
mbegu hautumiki kwa upele pekee, bali pia kwa matatizo mengine, k.mf. maumivu
yanayosababishwa na filaria. Angalia D.1.
 Allium Sativum (kitunguu saumu): Sugua kipande chembamba, au kifungie, kwenye sehemu
iliyoathirika.

C. Maambukizi ya mba
Maambukizi ya mba yanaweza kutokea kwenye sehemu yoyote ya mwili, lakini mara nyingi
yanapatikana katikati ya vidole vya miguu (athlete’s foot), au vidole vya mikono na katikati ya
paja. Baka (alama nyeupe ya mviringo kichwani) pia ni maambukizi ya mba. Sehemu
zilizoathirika zioshwe kila siku kwa maji na sabuni. Baadaye ziwekwe katika hali ya ukavu na
zihudumiwe kama ilivyoelekezwa hapo chini. Ikiwezekana, ukae kwenye hewa nzuri na mwanga
wa jua. Vaa nguo zilizotengenezwa kutokana na malighafi asilia, yaani pamba. Endelea na
matibabu hayo mpaka majuma 2 baada ya dalili kupotea.
C.1. Vigunguu saumu (Allium sativum)
Sugua mafuta ya vitunguu saumu (angalia sura ya 7.5) kwenye sehemu iliyoathirika. Kwa mba
wa kwenye vidole vya miguu unaweza kuweka kikonyo cha kitunguu saumu katikati ya vidole
vya miguu.
C.2. Ringworm bush (Cassia alata) na mbono au mafuta ya mawese.
Twanga majani mabichi ya Cassia alata, na uchanganye vijiko vyake 10 na kijiko 1 cha mafuta
ya mbono. Kama mafuta ya mbono hayapatikani, tumia mafuta ya mawese au mafuta mengine
ya mimea. Weka mara 3 kila siku. Tengeneza upya kila siku. Kama huna mafuta kabisa, twanga
haya majani mabichi na uyasugue kwenye sehemu iliyoathirika mara 3 kwa siku.
C.3. Ringworm bush (Cassia alata), papai na mafuta
Twanga kiganja kizima cha majani mabichi na machanga ya ringworm bush, ongeza matone 10
ya utomvu wa papai bichi na kijiko kizima cha mezani cha mafuta ya mbono au ya mawese.
Changanya na usugue kwenye sehemu iliyoathirika mara 3 kwa siku. Tengeneza dawa mpya kila
siku.
C.4. Dawa ya mafuta ya kuzuia mba. Tumia mwarobaini, melia au ringwormbush (Angalia
sura ya 12).
D. Upele (Scabies)
Upele hutambulishwa na uvimbe mdogomdogo unaowasha, ambao unaweza kutokea mwili mzima.
Katikati ya uvimbe huu kuna vipele vyeusi vidogovidogo zaidi vyenye vichwa vyenye ukubwa wa
vichwa vya sindano. Upele ni kawaida kwa watoto. Unapatikana zaidi katikati ya vidole vya
mikono, kwenye kiungo cha mkono na kitanga, kiuno, na sehemu za siri. Husababishwa na vijidudu
vidogo vinavyotengeneza njia chini ya ngozi. Unaambukiza kwa urahisi sana. Kama mtu mmoja
katika familia akiwa na upele, lazima familia nzima itibiwe. Usafi ni muhimu. Oga mwili mzima na
badilisha nguo zako kila siku. Nguo zote na matandiko lazima yafuliwe na kuanikwa juani. Njia
rahisi ni kuziweka kwenye jiko la jua. Safisha sehemu za chuma au za mbao za kitanda chako kwa
mafuta ya taa.

D.1. Mafuta ya taa na mafuta ya mboga (“Mafuta ya upele”)


Tayarisha mafuta ya upele kwa kuchanganya kikombe 1 cha mafuta ya taa na kikombe 1 cha mafuta
ya mboga. Mara 2 kwa siku na kwa siku 2 hadi 3, oga mwili mzima na upake mafuta ya upele
kwenye sehemu iliyoathirika. Mchanganyiko huu wa anamed kwa sasa unatumiwa na hospitali
nyingi. Matibabu haya ni mazuri pia kwa mwasho unaosababishwa na filariasis (minyoo
midogomidogo kwenye damu) kuzunguka kiuno. Filaria husafiri hadi sehemu nyingine za mwili.
Weka mafuta ya taa na haya mafuta ya upele mbali na moto na watoto pia.
D.2. Mafuta ya Vitunguu saumu (Allium sativum) Angalia C.1. hapo juu
D.3. Mwarobaini (Azadirachta indica). Angalia sura ya 9.
D.4. Mimea mingine
Kwa watu wazima wenye upele, na kwa upele kwenye sehemu ndogo, bila kuwa na fedha ya
kununua mafuta ya taa, na kama vitungu saumu na mwarobaini havipatikani, kuna njia tatu: Iliyo na
sumu ndogo zaidi ni Tephrosia vogelii (kibaazi). Chaguo la pili ni Rauwolfia vomitoria
(kimusukulu) na la tatu ni Nicotiana tabacum (tumbaku). Matumizi ya kila mmea ni kusugua majani
safi yaliyokomaa kwenye sehemu zilizodhurika. Mbadala ni bora zaidi kwa ngozi kuponda majani
haya na kuyachanganya na kiasi fulani cha mafuta ya mboga. Sugua mchanganyiko huu kwenye
sehemu iliyoathirika mara 3 kwa siku. Tengeneza mpya kila siku. Uwe mwangalifu, karibu mimea
hii yote ina sumu!

SURA 4: KUHARISHA

Mtu anaharisha wakati haja kubwa inapokuwa ya majimaji. Kama haja kubwa pia itakuwa na
kamasi na damu, tatizo linaitwa “kuharisha damu” (Dysentry).

Kuharisha ni ugonjwa hatari sana. Inahusika na vifo vya zaidi ya watoto millioni 3 katika nchi
zinazoendelea kwa mwaka. Karibu mara zote watoto wasingekufa – kama tu wazazi wao au hata
klinki zingejua matibabu yaliyoelezwa katika sura hii. Kuharisha ni hatari hasa kwa watoto
waliopungukiwa lishe.

Kuharisha kunaweza kuwa dalili za magonjwa mengine, ambayo pia yanahitaji matibabu,
angalia jedwali hapo chini 4.1. Kama ukienda chooni mara moja, lakini ukakaa huko siku nzima,
una kipindupindu!

Watoto wanapoharisha, wakati wote wapewe maji ya chumvi (Oral)! Watu wazima wangependa
kwanza kujaribu dawa rahisi zaidi kama vile dawa ya mkaa, matunda ya mpera mabichi n.k.,
lakini kama kuharisha kukiendelea, au kwa matatizo makubwa zaidi, maji ya chumvi ni ya
lazima kwa watu wazima pia! Mgonjwa lazima aendelee kula vyakula vinavyoongeza vitamini
na madini ya kutosha.

Mara nyingi kuharisha kunaweza kuzuiwa, hasa kwa kujali suala la usafi.

4.1. Jinsi ya kuzuia uharishaji.


a) Osha mikono yako kwa sabuni (au majani ya mpapai) na maji yanayotiririka kabla ya kula na
baada ya kutoka chooni.
b) Usitumie chupa za watoto za kunyonyeshea kwa watoto - zina uwezekano mkubwa wa
kusababisha maambukizo. Maziwa ya mama ni bora zaidi!
c) Wakati wote tupa chooni kinyesi cha watoto wachanga na wakubwa.
d) Oga kila jioni na ulale sehemu iliyo safi.
e) Watu wazima na watoto lazima watumie vyoo kwa haja kubwa na ndogo. Tundu la choo lazima
lifunikwe na kifuniko ili kuzuia inzi kusambaza maambukizo kutoka kwenye kinyesi kwenda
kwenye chakula. Pambana na mila na desturi zinazozuia matumizi ya vyoo.
f) Kula chakula kizuri, chenye lishe kamili na hamirojo (mfano: mahindi na mawele), protini
(mfano: nyama na mayai) na vitamini (mfano: mboga na matunda). Angalia sura ya 4.
g) Kula vitunguu saumu mbichi na/au kipande cha jani la mpapai chenye urefu wa sm 5 za mraba
kila siku ili kuzuia minyoo na maambukizo ya amiba. Njia hii ni msaada hasa kwa wale wenye
matatizo ya kuharisha mara kwa mara.

4.2. Jinsi ya kutibu kuharisha

A. Rudishia maji yaliyopotea, nguvu na madini kwa maji ya chumvi (Oral).


Kwa kuharisha, jambo la muhimu zaidi ni kufidia maji yaliyopotea. Kwa watu wazima na watoto,
wakati wote tumia maji ya chumvi na wakati wote jitengenezee maji ya chumvi mwenyewe.
Usitumie ya madukani (ORS) - ni gharama kubwa. Hatufurahishwi pia na viroba vya chumvi za
haya maji vinavyotolewa bure na umoja wa mataifa, maana jambo hilo linachochea hali ya
utegemezi! Kila mzazi lazima ajue jinsi ya kutengeneza maji-chumvi

A.1. Yaliyomo katika maji-chumvi.


Maji chumvi yana vitu 3: Maji, sukari, na chumvi. Maji ni muhimu kwa shughuli zote za mwili,
sukari kwa ajili ya nguvu, na chumvi kufidia chumvi iliyopotea wakati wa kuharisha.

Jedwali 4:1: Jinsi ya kutambua na kutibu kuharisha.

Dalili Sababu zinazoweza Tiba


kusababisha.
Sumu kwenye chakula. Watoto: maji-chumvi;
Wazima: maji-chumvi/ mkaa.
Hakuna damu Kuharisha Watoto: maji-chumvi,
kwenye kinyesi, kunakosababishwa na Wazima: maji-chumvi/ mkaa
virusi
hakuna homa.
Kipindupindu (kuharisha Tumia maji-chumvi kwanza kisha
kwa nguvu ambako mharo mpeleke hospitali.
wake ni kama maji ya Hakuna hospitali? Tumia antibiotic (ni
mchele). dawa za kuua bacteria).
Hakuna anti-biotic? Jaribu chai ya
anamed ya kuharisha (angalia B.3. chini)
au chai ya Artemisia.
Malaria Wakati wote tumia maji-chumvi; chai ya
mchachai wakati wote na dawa za kutibu
malaria (angalia sura ya 5).
Hakuna damu
Homa ya matumbo Maji-chumvi na antibiotic. Hakuna
kwenye kinyesi, antioitic? Jaribu maji-chumvi na chai ya
homa majani ya Azadirachta indica, au
Artemsia annua, au Vernonia amygdalina
au Melia azedarach.
Kuharisha damu sababu ya Maji-chumvi na chai ya mziwaziwa
Damu kwenye amiba. (euphorbia hirta). Kuharisha kukiendelea:
Maji chumvi na chai ya kuharisha ya
kinyesi – hakuna
anamed (angalia B.3 chini).
homa
Damu kwenye Kichocho. Maji-chumvi. Jaribu chai ya artemisia
kinyesi au mkojo. annua. Nenda kwenye Zahanati au
hospitali kwa matibabu.
Hakuna homa.
Maji-chumvi na chai ya kuharisha ya
Kuharisha kwa sababu ya anamed (angalia B.3. chini). Kama
bacteria (“Bacterial hakuna maendeleo yoyote, nenda
Damu kwenye choo
Disentery”) Hospitali.
na homa. Hakuna Hospitali? Tumia antibiotic, maji-
chumvi na chai ya kuharisha ya anamed.
Hakuna antibiotic? Tumia maji-chumvi,
na ongeza Vinca rosea kwenye chai ya
kuharisha ya anamed hadi kuharisha
kukome. Angalia B.6. chini.

 MAJI: Tumia maji mazuri, kama hakuna maji safi ya chemchemi, tumia maji
yaliyochemshwa au tengeneza chai ya majani ya mpera na uitumie badala ya maji.
 SUKARI: Hasa tumia asali, isipokuwa kwa watoto walio chini ya mwaka mmoja, ambao
kwao haishauriwi kutumia asali. Kama hakuna asali, tumia sukari ya nyumbani (baadhi
ya hospitali zinatumia glucose). Kama huna sukari au mgonjwa ana kisukari, badala ya
gramu 30 za sukari kwenye mchanganyiko ulioelezwa hapo chini (A 2), unaweza
kutumia na kuchanganya vizuri moja kati ya vifuatavyo katika lita 1 ya maji:
a) Gramu 100 za ndizi tamu zilizosagwa (kama nusu kiganja, usichemshe).
b) Gramu 100 za viazi vitamu (kama nusu kiganja, chemsha kwa dakika 10).
c) Gramu 30 (vijiko 3 vya chai vilivyojaa sana) vya unga wa ngano, mchele
uliotwangwa au mtama. Chemsha kwa dakika 5.
 CHUMVI: Hasa, tumia ile inayoitwa “chumvi ya kienyeji.” Hii inatengenezwa kwa
kienyeji kwa kuchukua majivu ya miti iliyochomwa, ongeza maji, chemsha hadi maji
yakauke kwenye chungu cha udongo (kwa sababu vyombo vya metali vinaweza
kuharibika) na kukusanya chembechembe zinazojitokeza. Hii ni nzuri, kwa sababu ina
potassium. Ama sivyo tumia chumvi ya mezani (sodium chloride).
 POTASSIUM: Ni kitu kinachopaswa kuongezwa kama chumvi ya mezani ikitumika na
kama kuharisha kutaendelea kwa siku kadhaa. Potassium inasaidia misuli ya utumbo na
matumbo kufanya kazi vizuri. Vyanzo vizuri vya potassium ni pamoja na mchicha, embe-
mafuta, ndizi, boga, maji ya nazi, karoti, soya iliyopikwa, njugu, moringa na majani ya
mboga za kijani-nyeusi yaliyochemshwa.
Kwa watoto wadogo ambao hawawezi kula chakula kingi, ongeza kijiko 1 cha chai cha
majivu safi (kutokana na miti au nyasi zisizo na sumu, au kutokana na magugu maji
yaliyokaushwa, ambayo yana potassium nyingi) kwenye lita 1 ya maji inayotumika
kutengenezea maji-chumvi (angalia chini). Baada ya dakika kadhaa, chuja maji.

Angalizo: Chumvi za potassium ziongezwe tu kama mgonjwa anaweza kukojoa.

Kama chochote kati ya vifaa vyako (maji, sukari au chumvi) siyo safi kikamilifu,
chemsha mchanganyiko huo kwa dakika chache ili kuua bacteria. Nyongeza ya rangi na
harufu havisaidii kwa lolote.

A.2. Kutengeneza maji-chumvi


Nyumbani: Ama, ongeza vijiko 4 vya mezani vya asali au vijiko 2 vya mezani vilivyojaa sana
vya sukari (gramu 30) na nusu kijiko cha chai kilichosawazishwa cha chumvi, kwenye lita 1 ya
maji. Au, kwenye kikombe kikubwa cha maji (ml 500), ongeza vijiko 2 vya mezani vya asali au
kijiko 1 cha mezani cha sukari kilichojaa sana, na mbinyo 1 wa chumvi kiasi cha chumvi laini
unachoweza kubeba kati ya kidole gumba na shahada.
Hospitalini: Kwenye lita 1 ya maji ongeza gramu 20 za glucose au gram 30 za sukari ya
nyumbani, gramu 2.9 za trisodium citrate dihydrate, gramu 3.5. za chumvi ya mezani (NaCl) na
gram 1.5 za potassium chloride.

A.3. Maji-chumvi: Kipimo cha kunywa.


Kwa siku: ml 200 (glass moja) kwa kila kilo 1 ya uzito wa mtoto wako. Kama hujui uzito wa
mtoto wako, na huwezi kupima ml, jedwali lifuatalo litakusaidia: Vikombe ni vipimo vizuri zaidi
kuliko chupa, kwa sababu ni vigumu kuosha chupa vizuri.

Jedwali 4:2: Matumizi ya kila siku ya maji-chumvi.

UMRI ML IDADI YA VIKOMBE AU CHUPA ZENYE


UKUBWA WA ………….
LITA 0.33 LITA 0.5 LITA 0.7 LITA 1
Chini ya miezi 6 700 2 1.5 1 ¾
Miezi 6 – miaka 2 1,400 4 3 2 1½
Miaka 2 – 6 2,100 6 4 3 2
Miaka 7 na zaidi 2,800 8 6 4 3
Watu wazima 3,500 10 7 5 3½
Kunywa taratibu kwa uaminifu kutwa nzima. Kwa watoto wachanga lazima uendelee
kunyonyesha maziwa ya mama.

B. Kutibu kwa chai ya mimea ya dawa au mkaa wa dawa.

B.1. Mpera (Psidium guajava)


Mpera huzuia maambukizo, huzuia mshituko wa mwili, na ina kemikali ya hudhurungi
inayosaidia usukumaji wa damu kwenye misuli. Sifa zote hizo ni nzuri kwa kutibu kuharisha.
Kutengeneza chai ya mpera, chukua kiganja (maana yake: kiasi cha majani ambayo mgonjwa
mwenyewe anaweza kuzinga katika kiganja chake) cha majani ya mpera, yachemshe katika lita 1
ya maji kwa dakika 2. Baadaye uache ikolee kwa dakika nyingine 30, chuja na tumia ndani ya
masaa 24.
a) Kuharisha kwa kawaida kwa watu wazima: Kunywa lita 1 ya chai ya majani ya mpera ya
kawaida. Hii husaidia katika 90% ya matukio yote ya kuharisha.
b) Kwa kuhara kunakodumu kwa watu wazima na watoto tumia “maji-chumvi ya mpera”
kwa kiasi kilichotolewa kwenye jedwali 4.2. Tayarisha chai ya mpera kama ilivyoelezwa
hapo juu, na ongeza sukari na chumvi kama ilivyoelezwa kwenye A.2. hapo juu.
c) Chai ya mpera inasaidia pia kwa vidonda vya tumbo: Kunywa kidogokidogo kila baada ya
saa 1.

B.2. Mziwaziwa (Euphorbia hirta)


Kama chai ya mpera haisaidii: Chemsha kiganja 1 cha
majani mabichi (kata kwa mkasi, ukiacha mizizi ili mmea
uweze kustawi tena) kwenye lita 1 ya maji kwa dakika 2
(Kama una mzani: tumia gramu 10 za majani mabichi au
gramu 2 za majani yaliyokauka) na uache ikolee kwa dakika
nyingine 30. Chuja na unywe kwa awamu kutwa nzima.
Endelea na tiba hii kwa siku 8.
Hii inafaa sana, hasa kwa maambukizi ya amiba. Ni muhimu
kuutambua mmea huu kama ulivyo. Umeenea katika nchi za
tropiki. Unakua kati ya sm 30 na sm 40 kwa urefu, na una
majani (yenye menomeno mafupi) kwenye vikonyo vifupi. Mashina yamefunikwa na
nywelenywele ngumu zilizotapakaa zenye rangi ya njano.
Unafanana na magugu mengine mengi, lakini una tofauti tatu zinazoonekana:
a) Utomvu mweupe unaovuja kutoka katika shina linapokatwa.
b) Kitita cha maua madogo madogo sana ya kijani yanakuwa kwenye shina fupi ambao
linatokeza mahali ambapo jani linaungana na shina.
c) Matunda yana mbegu zenye rangi nyekundu, ambazo zina urefu usiofikia milimeta 1 na
zenye kingo 3.

B. 3. Kuhara sana na kuhara damu. “Chai ya kuhara ya anamed”


Chai ya kuhara ya anamed inafaa sana, na imeokoa maisha ya watu wengi. Hata hivyo,
inatakiwa kutumika pale tu unapokuwa umetumia chai ya mpera na ukaona haitibu. Osha na
changanya kiganja 1 (maana yake: kiasi ambacho mgonjwa mwenyewe anaweza kushika
katika kiganja chake) cha kila vifuatavyo:
 Mziwaziwa (Euphorbia hirta – mmea mzima lakini siyo mizizi)
 Majani ya mpera
 Majani ya mwembe machanga ya kijani.

Jedwali 4:3 - Kipimo cha anamed cha dawa ya kuhara.

Umri Kipimo cha kila siku


Mwaka 1 – 3 ¼ lita kila siku
Miaka 4 – 6 ½ lita kila siku
Miaka 7 – 12 ¾ lita kila siku
Miaka 13 – watu wazima lita moja

 Chemsha kwa dakika 2 katika lita 1 ya maji, na uache ikolee kwa dakika nyingine 30.
Kama mwembe au mpera haupatikani tumia majani ya mpapai. Lakini chai hiyo itakuwa
chungu na mtoto anaweza kuikataa.
 Kunywa kiasi hiki cha chai kwa masaa 24. Endelea kwa siku 8 hata kama dalili
zimetoweka. Tiba inayoendelezwa huondoa mayai yaani amiba kutoka kwenye matumbo.
Mara nyingi inaondoa minyoo ya kwenye matumbo pia.
 Bakavu, huko Kongo, mahali ambako kumbukumbu zimetunzwa kwa uangalifu, walikuwa
na mafaniko ya 99% katika kutibu zaidi ya wagonjwa 200 wanaosumbuliwa na amiba na
kuharisha damu kwa kutumia chai ya majani ya Euphorbia Hirta, mpera na mwembe.

Dokezo kwa Mahospitali: Unaweza kupendelea kutayarisha chai hii ya kuharisha ya anamed
kutokana na majani makavu. Vuna mimea hii kwa kiwango kilicho sawa kuelekea mwisho wa kipindi
cha mvua, ikaushe vizuri na uisage. Kipimo sasa kitakuwa kuchemsha kijiko 1 kilichojaa katika lita 1
ya maji kwa dakika 2 na baadaye uache ikolee kwa dakika nyingine 30. Kama unga wa majani makavu
ukitunzwa kwenye chombo kisichoruhusu hewa kuingia, itadumu salama kwa mwaka mmoja .

B.4. Mimea mingine


Mimea iliyotajwa juu isipopatikana, chai inaweza kutengenezwa kwa kutumia majani ya
mwarobaini (angalia sura ya 9), kutokana na Artemisia annua (angalia sura ya 8) au kutokana
na majani mabichi ya kijani ya mwembe (Mangifera indica).
Majani ya mpapai (Carica papai) pia yanatibu: Chemsha kiganja 1 kilichojaa cha majani
katika lita 1 ya maji kwa dakika 1, kisha acha ikolee kwa dakika 20. Chuja na unywe kwa
sehemu sehemu kutwa nzima. Watoto hupendelea chai ya majani ya mpera kwa sababu chai
ya majani ya mpapai ni chungu. Kama hakuna kingine kinachopatikana, kunywa maji
uliyotumia kupika mchele.

B.5. Mkaa wa dawa


Mkaa unatumika kwenye matukio ya chakula chenye sumu au kwa kuhara polepole. Uwe
mwangalifu kwa watoto, hata mkaa lazima wakati wote unywewe ukiambatana na maji-
chumvi. Tengeneza mkaa kutokana na mti ambao hauna sumu. Kwa mfano, tumia matawi
yanayoota kuelekea katikati ya mwembe ambao kamwe hayazai matunda, au tumia maganda
ya karanga yaliyopondwapondwa. Yachemshe katika chombo cha chuma kilichofunikwa
hadi mti au maganda yawe mkaa. Uwe mwangalifu wakati unafunua, unga unaweza kushika
moto kwa ghafla! Ponda mkaa, uchekeche, uchemshe tena ili kuhakikisha hauna
maambukizo. Kunywa kijiko 1 cha chakula, mara 3 kwa siku katika maji. Endelea kunywa
maji mengi au maji-chumvi wakati wote (angalia A.2. juu).
B.6. Vinca rosea
Katika hali zinazotishia maisha, ambapo hata chai ya kuzuia kuhara ya anamed haisaidii,
tayarisha chai ya anamed ya kuzuia kuhara kama ilivyoelekezwa hapo juu. Kisha, mara moja
baada ya kushusha chai kutoka kwenye moto, ongeza kiganja kizima cha majani mabichi ya
Vinca rosea kwenye chai na uiache ikolee kwa dakika 30. Chuja na kunywa kwa awamu kwa
muda wa siku nzima.
Angalizo: Vinca rosea ina sumu!

SURA 5: MALARIA

5.1. Utangulizi
Katika dunia nzima karibu watu milioni 500 hupata malaria kila mwaka. Kati ya hao, millioni 1
hadi 2 hufa. Wengi kati yao ni watoto chini ya miaka 5.
Malaria huambukizwa kutoka mtu mmoja hadi mwingine na mbu wa jamii ya Anopheles.
Wanapochukua damu kutoka kwa mtu aliyeambukizwa wanachukua vimelea vya malaria
(vijidudu viitwavyo plasmodium). Kisha wanapochukua damu kutoka kwa mtu mwingine,
wanaingiza plasmodium pamoja na mate yao. Plasmodium husafiri hadi kwenye ini, na kutokea
hapo huingia hadi kwenye chembe nyekundu za damu. Mtu huugua baada ya siku 7 hadi 10
baada ya kuumwa na mbu.
Kwa kawaida mgonjwa wa malaria huhisi baridi na mara nyingine hutoka jasho. Inawezekana
lakini kwamba dalili mojawapo ikawa na nguvu zaidi, kiasi kwamba haidhihiriki haraka kwamba
mgonjwa ana malaria. Kwa njia hii malaria inaweza kujificha nyuma ya safu ya dalili za
magonjwa, mfano: kuharisha na kutapika, matatizo ya kiakili, kupoteza fahamu, upungufu wa
damu au homa.

Mimea inayotibu inaweza kuokoa maisha ya wengi. Mfano wa kushangaza unatokea Kongo
D.R.C.: Mwaka 1997 Askofu wa Dayosisi ya Bolungu–Ikela ilimbidi kuwakimbia waasi na
kujificha porini kwa majuma 4, akiwa na watu wengine 20. Hawakuwa na nyumba wala
chandarua, wala madawa. Waliishi chini ya miti! Walipopata homa walikunywa chai za dawa
zilizoorodheswa hapa chini. Askofu alisema, “Pamoja na hofu yetu, hakuna mmoja wetu
aliyekuwa mgonjwa sana kwa malaria.”

5.2. Jinsi ya kuzuia malaria


1. Punguza idadi ya mbu nyumbani kwako na katika mazingira yaliyo karibu.
 Usiwe na maji yaliyo wazi katika mapipa au matenki yote; yanahitaji vifuniko au nyavu
za kuzuia mbu.
 Kusiwe na maji yaliyosimama ya aina yoyote.
 Kusiwe na taka zinazozagaa – mfano mbu huzaliana katika taili zilizochakaa na
makopo.
 Tunza msitu wako kwa sababu huko wanaishi maadui wa asili wa mbu.
 Usiwe na mimea mirefu (mfano nyasi) karibu na nyumba, isipokuwa mimea yenye
harufu nzuri kama vile Cymbopogon citrates (mchaichai), jamii za tururu, (Tagetes
erecta, Tagetes minuta) au Artemisia annua. Inashauriwa hata kuwa na mimea hiyo
ndani ya nyumba (ikiwa imeoteshwa kwenye vyombo).
2. Punguza mgusano kati ya mbu na watu.
 Tumia chandarua, hasa wakati wa kulala na nyavu za kuzuia mbu kwenye madirisha.
Weka kiasi kidogo cha mafuta ya mwarobaini katika mafuta ya kuwashia taa.
 Weka maua ya pyrethrum yaliyokaushwa na kupondwapondwa kwenye kona ya chumba
chako.
3. Punguza idadi ya vimelea.
 Tibu wagonjwa
 Zuia vimelea kuwa sugu – tumia tiba za aina mbalimbali (angalia jedwali Na. 5).
4. Jenga kinga nzuri ya mwili
 Unapokuwa na malaria – itibu inavyopaswa.
 Kula matunda na mboga kwa wingi – ambavyo vina vitamini C.
 Weka vitunguu saumu vingi kwenye chakula chako hasa vibichi. Angalia sura ya 6.
 Epuka uvutaji sigara na pombe

Jedwali 5 Madawa ya asili kwa ajili ya kutibu Malaria

Jina la mmea Utumike hadi Sehemu Jinsi ya kutumia Nguvu ya Madhara


joto la mwili ya mmea mmea
(°C)
Cymbopogon wakati wote Majani chai (angalia point 3) + Hakuna
citratus
(mchaichai)
Allium Sativum Wakati wote Vitunguu vijiko 3 vya vitunguu ++ Maumivu ya
Vitunguu saumu tumbo
saumu vilivyokatwakatwa
(angalia sura
ya 7)
Zingiber 37.5 Mizizi kula tangawizi bichi + Hakuna
officinale kiganja 1 au chemsha
(tangawizi) kwa dakika 10.
Usichuje, kula na
kunywa kila kitu
Psidium 37.5 Majani chai (decoction) + Hakuna
guajava
(mpera)
Carica Papaya 38.0 Majani chai (infusion) ++ Kuna
(mpapai) uwezekano wa
angalia sura ya kutapika au
10 kupata allergic
readtion
Vernonia 38.5 Majani au majani: infusion ++ Haijajulikana;
amygdalina mizizi mizizi: decoction ina aina ya
(bitter leaf) (angalia sumu lakini
maelezo
No 4 na 8)
Azadirachta 38.5 Majani majani: infusion ++ Inaathiri ini
indica (angalia
(mwarobaini) – maelezo
angalia sura ya No 4 na 8)
9
Cinchona 39.0 Gome chai (decoction) +++ Mlio masikioni
officinalis (angalia Wakati
maelezo mwingine
No kichefuchefu na
5 na 8) kutapika. Dawa
ikizidishwa
kiziwi kinaweza
kujitokeza au
kutoka kwa
damu masikioni
Artemisia 39.0 Majani chai (infusion) +++ Hakuna
Annua (angalia (angalia
sura ya 8) maelezo
No 8)

5.3.Kutibu kwa mimea


Tumia mimea ya dawa ya aina nyingi ili kuzuia vimelea vya malaria kuwa sugu kwa
tiba.Tunapokwua na maambukizi, vijidudu vinasababisha homa, hasa vinapokufa na kuanza kuoza.
Vitu vyovyote vinavyosababisha homa vinaitwa “pyrogens.” Unywaji husaidia mwili kuondoa
pyrogens. Pyrogens pia hutolewa nje kupitia kwenye ngozi kwa njia ya jasho. Chai ya moto ya
mchaichai hasa husababisha mwili kutoa jasho na kukojoa sana, kwa jinsi hiyo husafisha damu na
mwili. Kutokwa jasho hasa kunaondoa sumu mwilini. Tunapendekeza kwamba mtu mzima mgonjwa
wa malaria anywe lita 2 za chai ya mchaichai kwa nyongeza kwenye lita 1 ya chai ya dawa ya
mimea iliyotajwa kwenye jedwali Na. 5. Hata hivyo, tunapendekeza kwamba mtu mzima ye yote
mwenye joto kali anywe lita 2 za mchaichai kila siku - kwa tatizo lolote.
Kila tiba ya hii mimea iendelezwe kwa siku 7. Sukari au asali inaweza kuongezwa kwenye aina zote
za chai. Malaria huharibu sukari mwilini, na kwa hiyo kufidia sukari katika damu ni jambo
linalosaidia. Pia wagonjwa wa malaria ni vyema wapewe chakula kwa kuwa mara nyingi hupoteza
hamu ya chakula na hivyo kupungukiwa lishe.

Muhtasari wa matibabu
1. Watu wazima wanatakiwa kunywa jumla ya lita 3 kwa siku. Watoto nao ni lazima pia
wanywe sana kiwango kikitegemea uzito wa miili yao.
2. Chai ya dawa inaweza kutengenezwa kwa kuchemsha dawa katika maji au kumwagia maji
ya moto.
Kumwagia maji ya moto (Infusion): Mwaga lita 1 ya maji yanayochemka kwa kiganja
kizima cha majani mabichi ya dawa, au gramu 15 ya majani makavu (kama ni Artemisa
annua au Azadirachta indica iwe gramu 5). Iache kwa dakika 10 hivi, kisha ichuje.
Kuchemsha (Decoction): Kipimo ni kama katika kumwagia maji ya moto. Chemsha
maji na mimea kwa pamoja kwa dakika kama 20 hivi. Poza na uchuje.
3. Kwa mchaichai, chemsha majani yake kwa dakika 2. Acha itulie kwa angalau dakika 10,
kisha ichuje.
4. Vernonia amygdalina. Majani yake ni machungu sana. Magamba ya mizizi yake lina nguvu
zaidi. Tumia mizizi yenye unene wa kidole, mizizi ya pembeni, siyo mzizi mkuu, ili mti
usife. Tumia kiganja 1 cha magamba ya mizizi na uchemshe kwenye lita 1 ya maji kwa
dakika 20. Chuja na unywe kwa awamu 4 kwa siku 1. Endeleza tiba hii kwa siku 7.
5. Cinchona officinalis: Chemsha gram 10 au vijiko 3 vya chai vya magamba
yaliyopondwapondwa katika lita 1 ya maji kwa dakika 10, chuja na unywe kwa awamu ndani
ya masaa 24. Watoto wanywe kiasi kidogo zaidi kufuatana na uzito wao.
6. Katika hali ambayo mimea yote hii haisaidii, endelea kutumia lita 2 za mchaichai kila siku,
na pia tumia dawa za hospitalini (k.mf. Amodiaquine au Fansidar). Hakikisha pia kwamba ni
malaria kweli inayomsumbua mgonjwa na si ugonjwa mwingine.
7. Kumbuka kuwa hakuna wagonjwa wawili wanaoweza kuwa na hali zilizo sawasawa kamwe.
Ingawa watu wawili wanaweza kuwa na dalili zile zile, wanaweza wasitibiwe na dawa ile ile
ya mmea.
8. Akina mama wajawazito wasitumie Azadirachta indica (mwarobaini) au Vernonia
amygdalina (mtukutu). Katika miezi 3 ya mwanzo ya ujauzito tumia Cinchona officinalis
(mkwinini) au Artemisia annua chini ya uangalizi wa Daktari tu.

SURA 6: UKIMWI: Imarisha mfumo wa kinga mwilini

Ili kudumu katika afya njema, kila mtu anatakiwa kuhakikisha mfumo wake wa kinga mwilini
uko imara kadri iwezekanavyo. Jambo hili ni la muhimu hasa kwa watoto wadogo, wajawazito
na watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (VVU).

Jali haya yote yafuatayo:


a) Ishi kwa matumaini, uwe na uhusiano mzuri na majirani zako na uwe karibu na Mungu.
b) Hakikisha kuwa chakula chako ni kizuri na kina lishe kamili. Kunywa maji ya matunda
na maji salama kwa wingi. Jiepushe na aina mbalimbali za soda. (angalia sura ya 1)
c) Usivute sigara, na kama unakunywa pombe, kunywa kiasi kidogo sana.
d) Fanya mazoezi ya viungo. Tembea kwa miguu, endesha baiskeli au fanya shughuli
kwenye bustani kila siku.

Mimea na mazao ya asili yafuatayo yanasaidia kuimarisha mfumo wa kinga mwilini. Vinafaa
kwetu sote. Kama unaishi na VVU, tumia mimea miwili au mitatu kati ya ifuatayo. Washiriki
wa anamed katika nchi nyingi wametoa taarifa za mafanikio mazuri katika matumizi ya kila siku
ya unga wa majani ya mlonge na chai ya artemisia – bila kujali kama wanatumia madawa ya
kupunguza makali ya VVU (ARV´s) au la.

1. Allium Sativum (kitunguu saumu)


Tia vitunguu saumu kisichopikwa (kibichi) kingi kiasi uwezacho katika chakula chako cha kila
siku. Unaweza kuvikata vipande vidogovidogo na kuvichanganya katika chakula chako
unapotaka kula.
Vitunguu saumu vina kiasili cha kuua bacteria (antiseptic, antibiotic, antiviral, antifungal na
antidiabetic). Umuhimu wake kwa UKIMWI ni kwamba vitunguu saumu vimeonekana kuzuia
jamii za ugonjwa wa mkanda wa jeshi (herpes simplex) ambao ni kirusi kinachochochea
kuzaliana kwa VVU. Watu wanaopata maumivu ya tumbo wanapokula kiasi kikubwa cha
vitunguu saumu wanashauriwa kula kiasi kidogo cha mafuta ya maji kama vile mafuta ya alizeti
au samuli ambayo hufunika ukuta wa tumbo na kusambaza viini vinavyoleta maumivu. Huko
China vitunguu saumu vinatumika kutibu vidonda vya tumbo.

2. Aloe Vera (Msubili)


Aloe ina acemannon, kiini kinachoharibu VVU kwa kubadilisha ngozi yake ya protini kiasi
kwamba hakiwezi kujishikiza kwenye T-lymphocytes, ambayo ni sehemu muhimu kwenye
mfumo wa kinga ya mwili. Kata jani kubwa lililokomaa sana la aloe kama ilivyoelezwa katika
sura ya 2, kisha parua ute wake mzito kwa kijiko. Chukua kijiko 1 hadi 2 vya mezani vya ute
mzito wa msubili. Kula kijiko 1 hadi 2 vya mezani vya ute mzito wa msubili kila siku,
ikiwezekana kabla hujala chochote.

3. Artemisia annua
Washiriki wa anamed wanaoishi na VVU walitumia chai ya artemisia kama ifuatavyo:
a) Wakati wa hali mbaya ya ayfa (acute phase): Mwaga maji ya moto kwenye gramu 5 (yaani
vijiko 4 vya chai vilivyojaa sana) za majani makavu ya artemisia, acha itulie kwa dakika 15,
chuja na unywe chai hii kwa awamu 4 ndani ya siku moja. Kutegemea hali ya mgonjwa njia hii
inaweza kuendelea kwa muda wa wiki kadhaa au hata miezi.
b) Baada ya hapo (chronic phase): Mwaga robo lita ya maji ya moto kwenye gramu 1,25 (yaani
kijiko 1 cha chai) ya majani makavu ya Artemisia, acha itulie kwa angalau dakika 15, chuja na
unywe chai hii wakati wa asubuhi. Unaweza kuendelea hivyo kwa wiki au hata miaka.
Kama una mimea ya Artemisia kwenye bustani yako unaweza kutumia gramu 25 (acute phase)
au gramu 6,25 (chronic phase) ya majani mabichi kila siku.

4. Azadirachta indica (mwarobaini)


Mradi wa permaculture huko Malawi na Kuluva Hospital huko Uganda vyote hutengeneza unga
wa majani ya mwarobaini yaliyokaushwa na huwapa wagonjwa wa UKIMWI kijiko 1 hadi 2 vya
chai kila juma.

5. Citrus limon (Limau)


Limau lina vitamin C nyingi. Kunywa maji ya limau 1 kila siku, ama katika maji vuguvugu (siyo
ya moto ili usiharibu vitamin C) au lililokamuliwa katika chakula chako.

6. Cymbopogon Citratus (mchaichai)


Chai ya mchaichai: Chemsha kiganja 1 cha majani ya mchaichai mabichi katika lita 1 ya maji
kwa dakika 2, acha ikolee kwa dakika 15 na kisha uichuje kwa chujio. Kunywa lita 2 kwa
awamu kwa siku nzima. Huko Afrika kusini kwenye Moretele Sunrise Hospice, Mpho
Sebanyoni na wenzake wamegundua kwamba wagonjwa wa UKIMWI ambao wanakunywa
mchaichai kila siku wanapata tena hamu ya chakula, wanaongeza uzito na wanakuwa na nguvu
tena.

7. Lishe: Moringa Oleifera na/ au mbegu za Amaranth


Majani ya Moringa Oleifera (mlongelonge) na Moringa Stenopetala yanajulikana sana kwa
kuwa yana kiasi kikubwa cha vitamin, protini na madini pamoja na amino acids. Kwa sababu hii
kula mlongelonge kila siku, ama mbichi iliyotayarishwa kama mboga au kama unga wa majani
(angalia sura ya 11) unaochanganywa katika chakula cha kila siku. Mlongelonge unaonesha
mafanikio makubwa kurudisha afya ya watoto walioathirika kwa kukosa lishe. Unasaidia sana
pia kwa wajawazito na kina mama wanaonyonyesha. Kutumia unga wa majani ya mlongelonge
siyo tu kwamba kunajenga upya mwili, bali mara nyingi huondoa matatizo nyemelezi kama
kuharisha na matatizo ya ngozi.
Ongeza kijiko 1 cha chai kilichojaa cha unga wa mlongelonge kwenye chakula mara 3 kwa siku.
Wagonwja wa UKIMWI wafanye hivi kila siku katika maisha yao.

Jani, mbegu na vitumba vya


Moringa oleifera, unga wa majani
ya mlongelonge unaweza pia
kunywewa kama chai.

Amaranth ni mboga inayozalisha mbegu na majani yenye virutubisho inayofanana kabisa na


mlonge. Mbegu zinaweza kusagwa kutengeneza unga na kuliwa kama uji pamoja na unga wa
ulezi au mahindi, au unaweza kutumika katika kuumua mikate, keki na biskuiti.

8. Mazao ya asili ya nyuki


Asali: anamed Bukavu huko D. R. Kongo hutibu kwa chai ya artemisia na mchanganyiko wa
asali na aloe pamoja na kitunguu saumu kwa siku 20 kila mwezi. Kila siku, changanya kijiko 1
cha chakula cha ute mzito wa msubili na vijiko 2 vya mezani vya asali na unywe katika siku
moja. Mara 3 kwa siku, kata kata vikonyo 3 vya kitunguu saumu na unywe kwa maji kiasi. Chai
ya artemisia inanywewa kama kwa malaria.

Propolis: Gundi hii ni fukizo la kiasili linalotengenezwa na nyuki katika mizinga yao, na
imeonekana kuwa ni antibiotic, anti-fungal, antiseptic na antiviral. Changanya gramu 10 za
propolis na ml 100 za kileo halisi cha kutengenezea dawa (98%) kwa matumizi ya ndani
(kunywa). Tikisa mara moja kwa siku kwa muda wa siku 30. Chuja. Kipimo: kunywa matone 20
mara 1 hadi mara 3 kwa siku.
Kwa maelezo zaidi angalia katika kitabu cha anamed “Ukimwi na madawa ya asili”
SEHEMU III: MATUMIZI YA BAADHI YA MIMEA MUHIMU
KATIKA ENEO LA TROPIKI

SURA 7: Allium Sativum (Kitunguu saumu)

7.1. Maelezo ya kibotania (asili ya mimea) Familia: Liliaceae


Vitunguu saumu ni zao linalostawi mwaka hadi mwaka. Hurefuka hadi kati ya sm
30 na 90, na shina lake huwa na vikonyo kati ya 5 na 15. Asili yake ni Ulaya na
Afrika kaskazini, lakini jamii mpya kwa sasa zinaweza kustawi katika maeneo ya
tropiki.

7.2. Ulimaji
Vitunguu saumu hupendelea udongo wenye rutuba unaopitisha maji vizuri. Pogoa kikonyo kwa
uangalifu kutoka kwenye shina la saumu, na ukipande kwenye eneo yenye kivuli kwa kina cha
sm 5, na umbali wa sm 15 mche hadi mche kwenye mstari wa sm 30 mstari hadi mstari. Kama
mmea ukianza kutoa maua likate ua kusudi nguvu ya mmea iende kustawisha shina. Vuna wakati
majani yakianza kuwa na rangi ya hudhurungi na kuanza kunyauka. Kausha vitunguu kivulini
mahali ambapo kuna hewa nzuri inayopita, na kwa uangalifu vifute udongo na majani ya juu
(ukifanya hivi wakati vitunguu vina unyevu, vikonyo vitaharibika). Vitunze katika chombo cha
udongo.

7.3. Nguvu ya uponyaji ya vitunguu saumu


Imekuwa ikisemwa kwamba kitunguu saumu ndio mfano mzuri zaidi wa falisafa inayosema
kwamba dawa yako ndiyo iwe chakula chako, na chakula chako kiwe dawa yako.
Kuna hadithi juu ya nguvu za dawa za vitunguu saumu tangu mapema miaka ya 1700. Wezi
wanne walikuwa wamegundua njia ya kujilinda dhidi ya ugonjwa wa tauni na walikuwa
wanaishi maisha mazuri kwa kuiba maiti za wahanga wa tauni. Mara alipokamatwa, wale wezi
waliokoa maisha yao kwa kufichua siri yao – walikunywa siki kingi kilichochanganywa na
vitunguu saumu. Wachunguzi wanaamini kwamba allicin ndicho chanzo kikubwa sana (lakini
siyo yote) cha nguvu ya uponyaji – ikiwa pia ndio chanzo cha harufu yake. Inatengenezwa
kutokana na muungano wa alliin na mmeng’enyo wa alliinase, ambao hutokea mara kitunguu
saumu kinaposagwa, kinapokatwa vipande vyembamba au vidogovidogo.
Kuna madai kwamba kitunguu saumu kinaweza kutumika kutibu matatizo mengi, pamoja na
kifaduro, maambukizi ya njia ya hewa na njia ya mkojo, matatizo ya uyeyushaji wa chakula na
kutapakaa kwa vidudu vibaya mwilini, matatizo ya ngozi, magonjwa yanayoshika watu wengi
kwa mara moja (epidemic) na homa. Katika vita vya kwanza vya dunia vilitumika kuzuia kuoza
kwa vidonda na damu kupata sumu sababu ya maambukizo ya kidonda. Huko China imekuwa
ikitumika kutibu kuharisha, kuharisha damu, kifua kikuu, diptheria, ugonjwa wa ini, ringworm,
homa ya matumbo na trachoma. Katika nchi za magharibi vimekuwa vikitumika kutibu
magonjwa sugu ya njia ya hewa.

7.4. Vilivyomo:
Allicin: Vitunguu saumu vinaposagwa, enzaimu alliinase inaibadilisha alliin na kuwa allicin.
Allicin ni dawa ya bakteria na fangasi yenye nguvu. Alisini pia inatibu kukaza kwa mishipa ya
moyo (Arteriosclerosis).
Ajoene: Pamoja na kuwa na asili ya kuua vidudu na fangasi (anti-bacterial na antifungal) pia
inazuia kuganda kwa damu na kupunguza uwezekano wa kutokea magonjwa ya moyo
Flavonoids: Ni vizuizi vya kupotea kwa oksijeni na inapunguza hatari za saratani, magonjwa ya
moyo na baadhi ya magonjwa ya mishipa ya fahamu.

7.5. Kujenga mfumo wa kinga


Ulaji wa vitunguu saumu wa kila siku umeonyesha kupunguza uwezekano wa kutokea
kwa:
o Magonjwa ya moyo
o Stroke (kupooza upande mmoja wa mwili)
o Saratani
o Shinikizo la damu
o Mafua

Vinafanya hivyo kwa:


o Kupunguza kiasi cha “cholesterol” katika damu
o Kuvunja fibrin ambayo ni moja kati ya vilivyomo katika vigandisha damu.
o Kupambana na vijidudu, mba na jamii za virusi. Kwa baadhi ya magonjwa
‘antiobitic’ zinaweza kuwa na nguvu zaidi, lakini mara nyingi vitunguu saumu
vina nafasi kubwa ya kutibu na vinapenya kwa urahisi zaidi katika sehemu
iliyoambukizwa. Vitunguu saumu pia vina madhara kidogo zaidi.

Wakati wa maambukizo ya watu wengi ya ugonjwa wa uti wa mgongo katika eneo fulani huko
Ethiopia, wenyeji wa eneo hilo walihamasishwa kula vitunguu saumu vibichi. Kati ya wale
waliokula hakuna aliyekufa, lakini wale wengine wengi wao walikufa. Harufu ya vitunguu
saumu katika pumzi ya mtu inaweza kupunguzwa kwa kula tangawizi kwa njia yoyote.

7.6. Kutayarisha tiba ya vitunguu saumu


 Kula vitunguu saumu vibichi. Hii ndiyo njia bora zaidi.
 Vipike katika chakula.
 Asali ya vitunguu saumu. Jaza chupa kubwa ya kioo kwa vikonyo vya vitunguu saumu
vilivyomenywa na kukatwa katwa. Taratibu mimina asali ili ijaze nafasi zote kati ya
vikonyo. Weka chupa hiyo kwenye joto la wastani na nyuzi 20ºC. Kati ya majuma 2 na
4 asali itafyonza maji ya vitunguu saumu hivyo vitakuwa tepetepe na visivyo vyeupe
tena. Vichuje. Tumia ndani ya miezi 3.
 Mchanganyiko wa kitunguu saumu na sukari.
Pondaponda kijiko 1 cha chai cha vikonyo vya kitunguu saumu. Changanya na kiwango
kile kile cha sukari au asali. Tumia haraka.
 Mafuta ya vitunguu saumu
Chukua sehemu 1 ya vitunguu saumu vlivyokatwakatwa na changanya na sehemu 2 za
mafuta ya mimea. Koroga vizuri. Kama huna fridge, tumia ndani ya wiki 1. Hatushauri
tena kuyatunza kwa muda wa mwezi 1 kutokana na hatari ya kuingilia kwa vijidudu
vinavyoweza kusababisha sumu ya botulism. Botulism inaweza kusababisha kupooza
kwa mwili.
 Saumu ya kileo (Tincture): Tumbukiza gramu 200 za vikonyo vilivyomenywa na
kukatwa katwa katika lita 1 ya mvinyo au 40% ya kileo kingine kwa siku 14 katika eneo
lililo na joto kama nyuzi 20ºC katika chupa yenye kifuniko kisichopitisha hewa. Tikisa
chupa mara kadhaa kwa siku. Chuja vipande vya vitunguu. Dawa ya aina hii inaweza
kutumika mwaka mzima.

7.7. Magonjwa ambayo vitunguu saumu vinaweza kutibu:


A. Kikohozi, mafua na koo linalouma
1. Kula kikonyo cha kitunguu saumu kutwa mara 3.
2. Kunywa kijiko 1 cha chai kilichojaa cha dawa ya asali ya vitunguu saumu kila
baada ya masaa chache.
3. Tumia kijiko kizima cha chai cha mchanganyiko wa sukari na vitunguu saumu
kila baada ya masaa machache.
4. Kunywa kijiko cha chai cha mafuta ya vitunguu saumu mara 6 kwa siku.
B. Maambukizi sugu ya ‘sinus’, maumivu ya kichwa, maumivu ya kichwa ya upande
mmoja yaumayo kwa vipindi.
Mara kwa mara dondosha tone la mafuta ya vitunguu saumu katika kila tundu la pua, au
kata ncha za vikonyo 2 vya vitunguu na uweke kikonyo 1 katika kila tundu la pua.
(Angalizo: ni muhimu kuacha ganda la kitunguu saumu, vinginevyo kitunguu saumu
kitaunguza ngozi nyepesi (mucose membrane) ndani ya pua).
C. Sprains, maumivu, maambukizo ya mba, matatizo madogo madogo ya ngozi
Sugua mafuta ya vitunguu saumu moja kwa moja kwenye eneo lililoathirika. Angalia
sura ya 3
D. Kisukari: Kula kitunguu saumu kila siku. Vitunguu saumu na vitunguu maji hupunguza
sukari kwenye damu na shinikizo la damu.
E. Shinikizo la damu: Kula vitunguu saumu vibichi, au tumia matone kati ya 5 na 25 ya
vitunguu saumu ya kileo (tincture) mara kwa mara kwa siku, kiasi kinachohitajika.
F. Malaria: Katakata kitunguu saumu vizuri. Meza kijiko 1 cha mezani cha vitunguu hivi
mara 3 kwa siku, na unywe lita 2 za chai ya mchaichai kwa siku. Endeleza tiba hii kwa
siku 5. Ikibidi ongeza tiba nyingine ya malaria.
G. UKIMWI: Changanya vitunguu saumu vingi kiasi iwezekanavyo katika chakula chako
cha kila siku ili kuimarisha mfuno wa kinga mwilini. Vitunguu saumu kwa sasa vinazidi
kutumika kama tiba ya msaada kwa malaria na UKIMWI.
H. Kuumwa na wadudu:
Wadudu wana vidudu vya maambukizo. Maambukizo au mzio vinaweza kufuata baada
ya kuumwa na mdudu. Sugua sehemu iliyoumwa kwa kitunguu saumu kibichi, au fungia
kipande bapa chembamba cha kitunguu saumu kwenye sehemu iliyoumwa kwa kutumia
plaster.
I. Maumivu ya jino
Kwa dalili ya kwanza ya maumivu ya jino (kutokana na usaha chini ya jino) weka
kipande bapa chembamba cha kitunguu saumu kwenye sehemu iliyoathirika. Kiweke kati
ya shavu na jino. Upande uliokatwa uwe upande wa jino, upande mwingine uwe upande
wa shavu. Badilisha kila siku na ukiacha kwa muda wa siku kadhaa wakati wa mchana au
usiku. Athari ya kuungua kwenye taya au ulimi itatoweka baada ya dakika chache.
Kitunguu saumu huua bacteria wanaosababisha meno kuoza kwa sababu kinaweza
kupenya katika nyama na katika tabaka gumu la juu la jino.
Pia kula vitunguu saumu vibichi mara kwa mara.
J. Majipu yasiyo na mdomo; usaha chini ya ngozi (pamoja na maumivu na usaha
kwenye vidole au kucha)
Tumia kitunguu saumu kilichosagwa au mafuta ya kitunguu saumu (angalia sura a 2).
Kitunguu saumu kina tabia ya kupambana na bacteria kupitia ngozi. Hata hivyo,
unatakiwa kuwa makini, kwa sababu kitunguu saumu kina nguvu sana na kinaweza
kuunguza ngozi na kuacha makovu ya kudumu.

SURA 8: Artemisia annua anamed “A-3” (Sweet annie)

8.1. Maelezo ya kibotania: Familia Asteraceae.


Artemisia annua anamed (A-3) ni zao la mwaka 1 linaloweza kurefuka hadi meta 3. A – 3 ni
zao la mchanganyiko wa aina za Artemisia annua, ambalo linapolinganishwa na aina zake za
porini, yenyewe ina faida nyingi zaidi:
 Inarefuka zaidi
 Ina majani mengi zaidi
 Inastawi kwa muda mrefu zaidi kabla ya kutoa maua na kufa
 Ina kiwango kikubwa cha viasili vya dawa.
 Muhimu zaidi ni kwamba inastawi katika eneo la tropiki

8.2. Ulimaji
Hifadhi mbegu zikiwa kavu na zidumu kuwa kavu.
Tumia kiasi chake kidogo sasa, na kilichobaki kwa kila mwezi. Kama zikitunzwa katika hali ya
ukavu kabisa, hazitaharibika. Kiwango cha kuota kinapungua kwa 10% kwa mwaka. Mbegu na
miche inayozaliwa ni midogo sana na dhaifu. Vinahitaji uangalizi mkubwa! Usijaribu kulima A
– 3 mpaka wewe au mtunza bustani yako awe amejitayarisha kutoa muda wake mwingi kwa
jambo hili, ni pamoja na Jumamosi na Jumapili.

Tayarisha kitalu cha mbegu.


Ni vyema kutayarisha kitalu kinachobebeka. Mfano: Ubao bapa mpana wenye ukingo wenye
urefu wa sm 6, au tumia kingo za plastiki za ndoo. Kwa mbegu 500 unahitaji kitalu cha mbegu
cha sm 50 × sm 50. Au trei chache ndogo ndogo. Kamwe usisahau kutoboa matundu ya kutosha
kwenye kitako ili maji ya ziada yaweze kutoka na ili maji yaweze kunyonywa kupitia kitako.

Weka tabaka la udongo mzuri lenye unene wa sm 3 kwenye kitako cha trei, na ufunike kwa
tabaka nyingine la mchanga la sm 3. Mchanga huu uchemshwe kwa dakika lisizopungua 5 ili
kuua mbegu za magugu ambazo zinaweza kuwemo. Mbegu zenyewe zina virutubisho vya
kutosha vinavyohitajika wakati wa hatua za mwanzo za kukua.

Hakikisha kwamba kitalu kina unyevu sana lakini hakina maji yaliyotua. Mbegu zisambazwe
kwa usawa kwenye uso wa udongo – chujio la jikoni linaweza kusaidia mchakato huu. Usifunike
mbegu.

Mbegu za Artemisia huhitaji mwanga na unyevu ili kuota na kustawi.


Weka kitalu chini ya paa ili kuzuia mvua. Kiwe mahali ambapo kitapata mwanga wa jua moja
kwa moja. Joto la kadri kwa uotaji ni kati ya nyuzi 20 na 30ºC lakini uotaji pia umefanikiwa
katika joto la chini kiasi cha nyuzi 10ºC na joto kali kiasi cha nyuzi 40ºC. Kama kuna hatari
yoyote kutoka kwa ndege, panya au kuku, funika kitalu kwa waya wa mbu.
Kuhakikisha kwamba udongo una unyevu wakati wote, mara kwa mara weka kitalu chako katika
trei kubwa lenye maji kidogo kwa dakika 10, ili maji yaingie kupitia kwenye kitako.
Majani ya kwanza ya kijani hutokeza baada ya siku 3 na 7. Artemisia annua ni “dicotyledon”,
maana yake ni kwamba inapoota majani mawili hutokea. Kwa hiyo inaweza kutofautishwa na
miche ya majani ambayo huchipua jani moja tu. Siku 8 baada ya kupanda miche iotayo karibu
karibu sana inatakiwa ing’olewe kwa kutumia kikoleo na ipandwe sehemu nyingine kwenye
kitalu cha mbegu tena.

Kuweka miche katika viroba


Kati ya wiki 1 hadi 4 baada ya kupanda, ihamishe kwenye viroba. Unaweza kutumia vyungu vya
kupandia, vifijo vya plastiki au vyungu vilivyotengenezwa kwa majani ya migomba. Udongo
huu uwe na rutuba nyingi; mchanganyiko wa sehemu zilizo sawa za mboji iliyooza vizuri ( au
udongo mweusi) na mchanga ndio bora zaidi.

Kuhamishia shambani
Mimea ikifikia urefu wa sm 15, kama majuma 8 baada ya kupanda, tayarisha
shamba lako.
Artemisia hustawi vizuri katika aina mbalimbali za udongo na hali ya hewa.
Inastawi vizuri zaidi katika udongo wa hali ya kati au wa hali ya “alkaline” kidogo,
lakini inavumilia udongo wenye hali ya acid kidogo.
Zao zuri kulima kabla ya artemisia ni viazi vitamu au viazi mviringo, kwa sababu
viazi huufanya udongo uingize hewa nzuri . Artemisia ni mmea wa jalalani, maana
yake ni kwamba inastawi vizuri kwenye udongo unaopitisha hewa vizuri ambao una
nitrojeni nyingi kama vile udongo kutoka kwenye rundo la mboji. Kwa hiyo lainisha udongo.
Kama ardhi ni ngumu sana na ina udongo wa mfinyanzi, chimba kwanza shimo ambalo ni kubwa
zaidi sana ya kipimo ulichotaka, tuseme sm 70 × sm 70 × sm 70 na ndani yake tupia vijiti na
majani mengi (lakini siyo yatakayo katika mimea yenye “acid” kama vile conifers au mkaratusi)
na kwenye udongo changanya mbolea iliyooza ambayo ina kinyesi cha ng’ombe au kuku. Kama
ukipanda miche ya artemisia kwa umbali wa sm 60 toka mche hadi mche, utapata miche 30,000
katika hekta. Kama nafasi itaruhusu panda kwa umbali wa meta 1. Kati ya miche ya artemisia
unaweza kupanda maharage au karanga, ambavyo hurutubisha udongo, au panda mpapai,
mahindi au mtama katika mistari kwa kubadilishana na mstari wa artemisia. Katika udongo
wenye rutuba artemisia itakua na kufikia upande wa meta 1 na urefu wa meta 3!
Badala ya kupanda artemisia katika shamba moja kubwa, ipande katika maeneo mbalimbali,
kwenye jua, kwenye kivuli, karibu na mlima, kwenye ardhi tambarare, ili ugundue mwenyewe ni
sehemu ipi inayofaa zaidi. Kwenye eneo lenye joto ni bora zaidi ardhi ikikaa na unyevu. Kama
joto litakuwa zaidi ya nyuzi 30º wakati wote na hakuna uwezekano wa kumwagilia wakati wote,
tengeneza kivuli. Hili linawezekana kwa kutengeneza kiunzi cha mianzi ambacho kwacho
unaweza kustawisha mimea yenye virutubisho kama maharage yanayotambaa, Passion fruit na
maboga, au kwa kubadilishana katika mistari kati ya mistari ya A – 3, na mistari ya mapapai au
mahindi.

Kama unaishi katika eneo kame sana, pandikiza miche kwenye mistari kama sm 5 chini ya uso
wa ardhi. Kama unaishi katika eneo ambalo mara nyingine maji hutua kwa siku kadhaa
mfululizo, panda miche kwenye mistari juu kidogo ya usawa wa kawaida wa ardhi.
Tumia jembe na umwagilie mara kwa mara. Ardhi lazima ikae na unyevu, hasa majuma 2 ya
kwanza baada ya kupanda. Mmea huitikia matatizo, hasa ya ukame mkali, kwa kutoa maua kabla
ya kukomaa. Mimea ikifikia sm 50 kwa urefu, unaweza kuiwekea mbolea ya asili, kama vile
kinyesi cha wanyama kilichoozeshwa vizuri. Tumia mbolea za viwandani pale tu unapokuwa
huna njia nyingine. Kwa hali hii, jaribu kutumia mbolea ya N-P-K.

Kuzalisha artemisia annua


Kama ilivyoelezwa hapo juu, A-3 ni chotara, kwa hiyo mbegu zake haziwezi kutumika. Zingine
zitaota lakini mimea yake itakuwa dhaifu, ikiwa na sura mchanganyiko na upungufu wa 30% wa
viasili vya dawa. Hii inaweza kuwa ndogo sana kiasi cha kutoweza kutibu malaria.
Kwa hiyo artemisia lazima izalishwe kwa vipandikizi! Miezi 2 au zaidi baada ya kupanda,
chagua mimea 3 yenye nguvu na afya zaidi. Kata matawi katika vipande vyenye urefu wa sm 2
hadi 3 kwa kutumia wembe. Kwa njia hii, katika mmea moja unaweza kupata vipandikizi 1,000
vyenye uwezo wa kutibu wagonjwa 5,000 na zaidi! Tengeneza vipandikizi kila mwezi. Kamwe
usitumie mimea yenye maua, au chipukizi. Ukitumia hivyo, mimea yako itaanza kutoa maua
mapema!
Ondoa majani yote makubwa katika vipandikizi hivi. Tayarisha udongo na uvipande sm 1
udongoni kwenye kitalu cha kile kilichotayarishwa kama ilivyoelezwa hapo juu lakini kikibeba
udongo ambayo ni mchanganyiko wa mchanga na mboji iliyoozeshwa vizuri.
Kila kipandikizi lazima kiwe na vifundo visivyopungua 2. Mkato wa chini lazima uwe chini

kidogo tu ya kifundo ama sehemu ya kipandikizi iliyo


udongoni itaoza. Ondoa majani yote kwenye kifundo cha chini, na kwenye kifundo cha juu.
Ondoa jani kubwa tu, na uache kichipukizi cha pembeni salama. Vichomeke vipandikizi hivi
udongoni ili mizizi iote kuanzia kwenye kifundo cha chini, na ili kipandikizi hicho kiwe kwenye
ulalo wa nyuzi 30º kutoka kwenye wima. Kama hewa ni kavu sana, funika vipandikizi kwa
plastiki ambayo umeitoboa vitundu. Lakini kama hali ya hewa ina unyevu sana, acha wazi.
Vipandikizi lazima viwe kwenye mwanga, lakini visiwekwe kwenye jua moja kwa moja. Jambo
zuri ni kuwa na vitalu 2 ambavyo unavihudumia kwa namna tofauti kidogo, ili kujifunza namna
nzuri katika mazingira yako.
Wakati watu wengine hawana tatizo kabisa katika kuzalisha kwa kutumia vipandikizi, wengine
wanaona ni vigumu sana. Kama ni hivyo, weka vipandikizi vyako, kama ilivyoelekezwa hapo
juu – katika maji ambayo yana matone kidogo ya mbolea ya viwandani au mbolea ya asili.
Mbolea ya maji ya asili inaweza kutengenezwa kwa kuchanganya maji na kinyesi cha mbuzi na
kuachwa kitulie kwa majuma 6.
Kutoka katika mimea inayokua unaweza kuchukua vipandikizi zaidi, na katika mimea mipya vile
vile, unaweza kuchukua vipandikizi kwa njia hii mwaka hadi mwaka bila kupoteza kiasi
chochote cha “artemisinin” katika mmea.

Njia mbadala (stone-method), wakati mmea ukifikia urefu wa sm 50, ni kupinda matawi ya chini
na kuzika sehemu zake za kati kwa udongo. Jiwe linaweza kuhitajika kuzuia lisifyatuke. Mara tu
tawi lililozikwa likianza kuota mizizi, likate kutoka kwenye shina mama na ulipande shambani.
Kama kawaida tumia mmea wenye afya zaidi, na mimea isiyo na maua pekee au hata vitumba.
1. Changanya vikombe kumi kumi kila kimoja cha udongo, mchanga na maji.
2. Chemsha mchanganyiko huu kuua mbegu za magugu.
3. Tengenza kitalu kinachochukulika kutokana na miti na uweke vitundu vidogovidogo kwenye kitako.
4. Weka udongo kwenye kitalu.
5. Fungua mfuko wenye mbegu – ambazo ni ndogo sana!!
6. Sambaza mbegu kwa usawa. Usizifunike, na uweke kitalu kwenye sehemu yenye mwanga. Udongo
ukianza kukauka, weka kitalu ndani ya maji.
7. Mbegu huota kati ya siku 3 hadi 7. Zinahitaji jua la kutosha.
8. Punguza mimea.

9. Juma 1 baada ya kupanda, weka kila mche kwenye kifuko chake.


10. Mara mmea ukifikisha urefu wa sm 10, ukaupande bustanini au shambani.

11. Achanisha mimea kwa umbali wa mita 1.


12. Kutoka katika mimea bora, chukua vipandikizi.
13. Au zalisha mmea kwa njia ya “stone – method.”
14. Mmea unahitaji kiasi cha kutosha cha mwanga wa jua, maji mengi, na mboji nyingi.
15. Mara tu unapochanua maua, vuna mmea mzima. Kata majani kuanzia kwenye ncha za matawi hadi kwenye
kitako.
16. Ondoa matawi yote, katakata majani katika vipande vidogovidogo, na yakaushe kwa siku 3 tu.
17. Sugua majani makavu kupitia kwenye chekecheo na mabaki uipe mifugo wako.
18. Majani ya artemisia, katika kifuko chenye maelezo, kilichozibwa, tayari kwa matumizi. Tunza sehemu
kavu.
Picha: Bindanda Tsobi, Kinshasa. Taarifa na hakimiliki: www.anamed.net.

Magonjwa na maadui wa mmea yanayoweza kujitokeza


Katika hali ya kawaida, inapopandwa katika shamba la kawaida, huwa magonjwa hayajitoezi.
Katika nyumba ya kuoteshea mimea, ugonjwa unaweza kutokea. Kama hali ni ya uvuguvugu
sana, utitiri wa majani unaweza kutokea; kama kuna baridi sana, magonjwa ya mba yanaweza
kutokea. Tibu utitiri kibaiolojia, mfano kwa unga wa pareto (mfano Sprutiz – artemisia
huvumilia dawa ya unga kuliko ya maji) au kiuatilifu kinachotokana na mwarobaini (angalia sura
ya 9). Mara kwa mara miche ya artemisia imekuwa ikishambuliwa na panzi, wadudu au ndege.
Katika hali hii ilinde kwa chandarua au nguo inayopitisha mwanga katika majuma machache ya
kwanza.

Mara nyingine mchwa huunda kiota chao kuzunguka shina la artemisia. Kama hali hii ikizidi
sana kuwa tatizo, jaza ndoo kwa majani na mashina ya mimea yenye protini, mfano: kibaazi,
tithonia, au lesena, acha vitulie kwa juma 1 na uvimwage kuzunguka shina.
Mpango unaowezekana kwa nchi za kusini.
Wakati wowote wa mwaka, siha sehemu kidogo ya mbegu halisi kutoka anamed. Kama unakaa
sehemu za milimani, lima artemisia mwaka mzima. Kama unaishi kwenye nchi zenye joto, za
bondeni, lima artemisia kivulini. Mfano: Panda katika mistari kwa kubadilisha, mstari wa
artemisia ukifuatiwa na mstari wa mahindi, kisha wa artemisia tena. Au vizuri zaidi: Siha
artemisia wakati wa mvua, ipandikize mwanzo wa kipindi cha ukame na uimwagilie!

8.3. Uvunaji
Vuna majani yote wakati vifundo vya maua vinapoanza. Artemisimin ni nyingi zaidi kabla
kidogo maua haujachania. Mabaki ya mavuno yake yanaweza kufanywa mboji au kulishwa
wanyama.

Jinsi ya kufanya:
Kwa mkono mmoja, shikilia kwa nguvu mwisho wa tawi, kwa mkono mwingine, purura majani
kutoka kwa ncha hadi kitakoni. Unaweza kupenda kuvaa kifuko cha mkono. Ondoa matawi yote
kwenye mavuno yako. Unaweza kutumia majani haya mabichi hapohapo kutibu malaria. Ama,
laza majani kwenye ubao, na kwa kisu kikali, yakatekate vipande vidogo vidogo vyenye urefu
wa sm 1 (kama jinsi Afrika tunavyokatakata mboga za majani). Yakaushe kwa makini
iwezekanavyo katika siku 3 kwa joto lisilozidi nyuzi 40ºC. Kama hewa ina unyevu, yakaushie
kwenye jua, kama ni kavu basi kaushia kivulini. Kwa vyovyote majani lazima yakaushwe ndani
ya siku 3. Wakati yanakauka ondoa vijiti vilivyosalia kwa kusugua majani kwenye chekecheo
lenye nafasi kama za waya wa kuzuia mbu madirishani. Unaweza kujitengenezea chekecheo
nyumbani kwa kutumia waya huo.
Kausha unyevu hadi kipima unyevu, kilichowekwa katika mfuko wa plastiki pamoja na majani,
kitakapoonyesha kiwango cha unyevu kisichozidi 40 % katika nchi za kusini.

Ni vigumu kukadiria mavuno ya zao jipya lililolimwa kwenye eneo jipya. Katika hali nzuri
kabisa ya hewa kwa uzalishaji, kila mmea unatoa gramu 400 za majani makavu. Kwa jinsi hiyo
mmea mmoja unaweza kutumika kutibu karibu wagonjwa 11 (gramu 35 kila mmoja).

Kuhifadhi: Hifadhi kwenye giza, kwenye chombo kisichopitisha hewa kama vile plastiki au
pipa la metali. Weka kipima unyevu katika chombo hicho. Kama kipima unyevu kikionyesha
unyevu kuwa 40%, basi majani yana maji 4% na yatadumu kwa mwaka 1. Kama ni 30%, majani
yana maji 3% na yatadumu miaka 3.

Ubora: Majani yanatengeneza chai yenye ubora kama hayana vitawi au maua, rangi ni kijani
iliyokolea sana (nyeusi) na siyo ya kijivu au hudhurungi, na yaliyokaushwa vizuri.

Upakiaji: Pakia katika vifuko vya gramu 50 visivyopitisha hewa. Kwenye label juu ya kifuko
andika tarehe ya mwisho kutumika ambayo kwa majani yaliyokaushwa vizuri na vifuko
visivyopitisha hewa (vinavyozuia unyevu pia) iwe mwaka 1 kufuatia wakati wa upakiaji.

Bei: Bei inayolingana na bei za dawa zingine za kawaida za Malaria zinakubalika.

Taarifu serikali ! Kama artemisia haijaanza kulimwa katika nchi yako, jaribu kupata kibali
maalumu cha kuistawisha. Itaarifu Wizara ya Kilimo kwamba artemisia tayari inalimwa na
washiriki wa anamed katika nchi zaidi ya 70. Kama ni muhimu mwombe Askofu wako
akuombee kibali Wizarani.

8.4. Kutibu malaria kwa artemisia annua anamed “A-3.”


Tena, tunashauri uwasiliane na mamlaka husika. Huna sababu ya kuwa na hofu, kwa sababu
unafuata vizuri sana mwongozo wa Shirika la Afya duniani (WHO). Hapo nyuma mwaka 1987
WHO ilitamka: “Nchi wanachama
a) ziwashirikishe waganga wa jadi katika huduma ya afya ya jamii.
b) zisaidie katika uchunguzi wa mimea inayotumika kutibu kwa jadi.
c) zikuze ushirikiano na nchi nyingine katika nyanja za dawa za jadi”.

Tembelea wawakilishi wa Shirika la Afya duniani (WHO) na Wizara ya Afya katika nchi yako,
waonyeshe cheti chetu na mimea yako. Hakika utasifiwa!

Neno la faraja – na tahadhari: anamed inaweza kuokoa maisha ya watu wengi zaidi kwa
artemisia kuliko kwa mmea mwingine wowote! Chai iliyotengenezwa kwa majani ya artemisia
annua imekuwa ikitumika China kutibu homa kwa zaidi ya miaka 2000. January 2006, shirika la
Swiss Pharmaceutical Company “Novartis” lilitangaza kwamba lililenga kuzalisha dozi milioni
100 za dawa ya malaria aina ya Coartem (artemether/lumefantrine) mwaka 2006 (kutoka milioni
30 za 2005). Wanadai kwamba dawa hii inatibu kwa 95%. Pamoja na hayo, ni vizuri kusisitiza
kwamba kila dawa - iwe ya kikemia au ya kibailojia - ina kipimo cha mafanikio. Itakuwa ni
makosa kwa mtu kuweka imani yote kwa aina moja tu ya dawa, iwe ya vidonge au ya mimea.
Mafanikio maalumu ya anamed yalikuwa ni kuhakikisha kwamba chai iliyotengenezwa kwa
mmea chotara maalum A-3 inafaa sana katika tiba ya malaria. Chai ya Artemisia yenyewe ni
dawa mchanganyiko, kwa sababu ina dawa 10 tofautitofauti zinazohusika na kutibu malaria.
Dozi tunazotumia zimetokana na zile zilizotajwa katika “IX Chinese book of drugs,” taarifa
zilizo katika kitabu cha Hagers na katika uchunguzi wetu kwenye Chuo Kikuu cha Tuebingen
huko Ujerumani. Tunaweza kudondoa kumbukumbu za Zahanati 3 huko Congo. Waafrika 161
walijitolea kutibiwa kwa kutumia chai ya artemisia. Baada ya siku 5 – 7, 91% kati yao
hawakuwa na vidudu vya malaria kabisa.

Kutayarisha chai ya A-3


Kwa watu wazima wenye uzito wa kilo 60 –70, mwaga lita 1 ya maji yanayochemka kwenye
gramu 5 za majani makavu ya A-3 (au gramu 25 za majani mabichi).
Acha vipoe kwa dakika 15, kisha chuja. Gawa chai hiyo katika sehemu 4 zinazolingana, na
unywe kila baada ya masaa 6. (Unahitaji mizani – au gramu 5 ni kiasi kinachojaa kwenye
kikopo cha plastiki cha mikanda ya picha ya mm 35).

Jedwali 8:1 Dozi ya kila siku ya chai ya Artemisia.

Uzito wa mgonjwa Umri Chai ya Artemisia inanywewa kwa mdomo;


(kg) ...gramu za majani katika …..ml za maji
kwa siku, kwa siku 7.
5–6 Miezi 2 – 3 0.5g / 100ml
7 – 10 Miezi 4 – 11 1g / 200ml
11 – 14 Miaka 1 – 2 1.5g / 300ml
15 – 18 Miaka 3 – 4 2g / 400ml
19 – 29 Miaka 5 – 9 3g / 600ml
30 – 39 Miaka 10 – 11 3.5g / 700ml
40 – 49 Miaka 12 – 13 4g / 800ml
50 + Mtu mzima 5g / 1000ml

Tahadhari: Usitengeneze chai ya artemisia kwenye chombo cha chuma, kwa kuwa
artemisinin huingiliana na chuma!

8.5. Tiba ya malaria kwa chai ya A-3. Ufafanuzi wa kina:


Maelezo:
A. Mapendekezo haya ni matokeo ya uchunguzi wetu kwa kujifunza na kusoma vitabu.
WHO inahimiza matumizi ya “madawa ya jadi.” Lakini ni mara chache sana
inapopendekeza dawa fulani maalumu ya jadi. Kwa hiyo unatakiwa kwanza kupata
kibali cha mamlaka ya afya kabla ya kutumia tiba hizi.
B. Mapendekezo haya hayakuandikwa kwa ajili ya watalii, bali kwa wakazi na
wahamiaji wanaoishi katika maeneo yenye malaria sugu.
C. Ukiwa mgonjwa, usisite kutafuta ushauri wa daktari wakati wowote! Kama mganga
usisite kutumia madawa yanayofaa ambayo yanapatikana hapohapo ulipo! Kama
mhudumu wa afya, zitangaze dawa hizi nchini mwako!
D. Tafadhali usichapishe mapendekezo haya bila kuwasiliana nasi kwa kuwa wakati
wote tunaendelea kuyaboresha kutokana na taarifa tunazopata kutoka kwa washiriki
wetu.
E. Kila tusemapo juu ya “artemisia,” tuna maana ya majani yanayotokana na mmea wa
Artemisia annua anamed - yenye kiasi kikubwa cha dawa, yaliyo mabichi,
yamekaushwa ipasavyo na kutunzwa katika chombo kisichoingiza hewa.
F. Kwa watu wazima wengi, tiba kwa chai ya artemisia pekee inaweza kutosha. Hata
hivyo tiba ya ziada itafaa, ama katika hali ya kujirudia kwa malaria katika majuma 4,
au kama mgonjwa asipopata nafuu ndani ya masaa 24 tangu alipoanza kutumia tiba
ya chai ya artemisia. Katika hali hii ya mwisho, kwa kawaida tatizo huwa siyo
malaria.
G. Kupima chai ya artemisia: Kausha majani ya artemisia kwa siku 3 katika joto
lisilozidi nyuzi 40ºC. Chuja kwa kutumia chekecheo la unga. Upime unga huu
kwenye mizani. Kama huna mizani, basi kikopo cha mkanda wa picha za kamera za
mm 35 kilichojazwa unga mkavu wa majani ya artemisia (bila kushindiliwa ) ni
karibu sawa na gramu 5. Kama ukisaga majani haya yakawa unga laini na ukajaza
katika kikopo kile kile utapata gramu 10 za artemisia.

Hata hivyo ni vizuri kujitengenezea mizani yako: Ning’iniza vikombe 2 vya plastiki
kushoto na kulia mwa kipande cha mti kama ilivyoelezwa katika kitabu chetu
kiitwacho “Madawa ya asili katika nchi za joto: Vikorokoro vya walimu IV, toleo
namba 113”. Kwenye kikombe cha kushoto, weka karatasi 5 za kawaida A 4 (zenye
uzito wa gramu 80 kwa meta za mraba, yaani gramu 5 kwa hizo karatasi). Kwenye
kikombe cha mkono wa kulia weka majani mabichi ya artemisia. Kama mizani
italingana, utakuwa na gramu 25 za artemisia!
H. Matayarisho ya “Chai ya artemisia ya anamed.”
Mwaga lita 1 ya maji yanayochemka kwenye gramu 5 za majani makavu au gramu 25
za majani mabichi ya artemisia. Acha itulie kwa dakika zisizopungua 15, kisha chuja.
Tayarisha chai mpya kila siku. Lazima chai itumike ndani ya masaa 24 tu.
I. Kama hupendi ule uchungu wa artemisia: Ponda majani mabichi. Kila asubuhi na
jioni changanya gramu 2,5 ya unga wake kwenye yoghurt, peanut butter au ndizi
zilizopondwa na ule unga ndani yake. Kunywa maji baadaye.
J. Sukari katika chai: Kwa kawaida tunapinga uwekaji wa sukari katika chai kwa sababu
inasababisha kuoza meno. Kwa upande wa malaria, walakini vijidudu vya malaria
huharibu sukari iliyo katika damu, kwa hiyo kwa watoto walio na umri hadi mwaka 1,
unaweza kuongeza sukari kwenye chai ya artemisia. Kwa watoto wakubwa weka
asali au sukari. Lakini weka sukari au asali pale chai hii itakapokunywewa, ama
sivyo, kwa siku hiyo, vidudu vinaweza kuzaliana katika chai.
K. Asali: Kwa kawaida tunapendekeza kuchanganya chai zetu na asali badala ya sukari.
Haishauriwi kuwapa asali watoto walio chini ya miezi 12. Kwa watoto walio zaidi ya
mwaka 1 ni vizuri sana kuchanganya majani makavu ya artemisia moja kwa moja na
asali na kumpa mgonjwa. Walakini mchanganyiko huu unatakiwa kutengenezwa
upya kila siku.
L. Kutayarisha “sukari ya artemisia ya anamed.”:
Kwa kuwa mchanganyiko utatumiwa na watoto, unatakiwa uwe na mchanganyiko
ulio safi kabisa.
Osha mikono kabla ya kuvuna, na uchukue majani kutoka kwenye sehemu ya juu ya
mmea iliyo safi zaidi. Osha majani kwa uangalifu, yakate na kuyakausha kwenye
meza safi. Yasage hadi yawe laini kabisa kwa kutumia vifaa safi. (Unaweza kutumia
kifaa cha umeme cha kusagia kama kinapatikana).
Chemsha sukari kwenye kikaangio ili kuwa na uhakika kwamba vijidudu vyote
vimekufa na sukari imekauka. Mara tu sukari inapokauka, changanya gramu 10 za
unga wa artemisia kwa gramu 90 za sukari. Kama huna mizani, hii ni sawa na
kuchanganya kikomo cha mkanda wa picha za kamera cha unga wa artemisia ulio
laini sana na vikopo 3 vya namna hiyo vya sukari. Kijiko cha chai kilichosawazishwa
cha mchanganyiko huu kina uzito wa gramu 3 na ni sawa na gramu 0.3 za artemisia
kavu.
Mwisho wa kutumika: Baada ya mwaka 1 kama imetunzwa katika chombo
kisichopitisha hewa.
M. Kuinika: Msimamie mgonjwa ili kuhakikisha kwamba dawa uliyomwinika haitoki.
Kama ikitokwa kwa kupitia njia hiyo hiyo ya haja kubwa katika dakika 30 za kwanza,
mwekee kiasi kile kile cha dawa tena.

MATIBABU
1. Mjamzito katika miezi mitatu ya kwanza
Chini ya uangalizi wa Daktari unaruhusiwa kutumia chai ya artemisia ya anamed. Au unaweza
kutumia vidonge vya quinine (mg 10 kwa kila kilo ya uzito wako, mara 3 kwa siku, kwa siku 7).
Pia kunywa lita 2 za chai ya mchaichai kila siku.
2. Mjamzito katika mwezi wa 4 – 6 au 7 – 9.
Kama kuna daktari, mwombe ushauri wake. Unaweza kutumia chai ya artemia ya anamed,”
(angalia maelezo H hapo juu). Kunywa lita 1 kila siku kwa angalau siku 7. Pia kunywa lita 2 za
chai ya mchaichai kila siku. Ikibidi unaweza kuongeza vidonge vya quinine (mg 10 za quinine
kwa kila kilo ya uzito mara 3 kwa siku, kwa siku 7).
3. Kina mama wanyonyeshao
Unaweza kutumia “Chai ya artemisia ya anamed”, (Angalia maelezo H hapo juu). Kunywa lita 1
kila siku kwa siku zisizopungua 7. Pia kunywa lita 2 za chai ya mchaichai kila siku. Ikibidi
unaweza kuongeza vidonge vya quinine (mg 10 kwa kila kilo ya uzito mara 3 kwa siki, kwa siku
7, au vidonge 3 vya SP (sulfadoxin-pyrimethamine – jina la ki-biashara: Fansidar ).
Kama mgonjwa hawezi kunywa, jaribu njia hii: Mwaga ml 500 za maji kwenye gramu 10 za
majani makavu au katika gramu 50 za majani mabichi, subiri angalau dakika 15, chuja na utumie
njia ya kuinuka (enema) (kwa kuigawa dawa sehemu 4 au zaidi). Ikibidi, unaweza kuchanganya
kwa kuyeyusha vidonge vya quinine, au quinine ya maji katika artemisia hii ya kuinikia.
Yeyusha mg. 30 za quinine kwa kila kilo ya uzito wa mtu katika ml 500 za dawa ya maji ya
kuinikia. Tumia dawa hii ya kuinikia kwa siku 7, au hadi hapo mgonjwa atakapoweza kunywa
tena, yaani wakati ambapo dawa itanywewa kama chai.

4. Watoto wenye miezi 2 – 3 (au uzito hadi kilo 6).


Toa robo ya kidonge cha SP mara moja au jumla ya dozi ya mg 150 ya chloroquine
iliyogawanywa katika siku 3, au kwa watoto wenye uzito zaidi ya kila 5 tumia ALU kidonge 1
mara 2 kwa siku kwa muda wa siku 3. Mpe mtoto kiasi kikubwa cha kunywa (maji
yaliyochemshwa, kumnyonyesha).
Kama dawa hizi hazipatikani au hazifanyi kazi tena, basi tumia artemisia. Kama mtoto anakubali
kunywa chai hii, tumia ml 25 ya “chai ya artemisia ya anamed” (angalia maelezo H hapo juu )
mara 4 kwa siku, yaani jumla ya ml 100 kwa siku, kwa siku zisizopungua 7. Kuna uwezekano
mkubwa wa mtoto kupenda kutumia “artemisia ya sukari ya anamed” (angalia maelezo ya K
hapo juu) kuliko chai ya artemisia anamed: Mpe nusu kijiko cha chai kilichosawazishwa mara 4
kila siku, yaani jumla ya vijiko 2 vya chai vilivyojaa kila siku.

Kama mtoto amepoteza fahamu, jaribu njia ifuatayo: Chukua quinine ya maji, au yeyusha katika
ml 50 za maji mg 30 za quinine vidonge kwa kila kilo ya uzito wa mtoto kwa siku, gawanya
katika sehemu 4 au zaidi na umwinike mgonjwa kwa siku hiyo moja. Acha kumwinika mara tu
mgonjwa apatapo fahamu, kisha mpe dawa inayotakiwa kwa njia ya mdomo.

Kama hakuna quinine, unaweza kujaribu kumwinika kwa kutumia artemisia. Changanya ml 50
za maji yanayochemka katika gramu 1 ya majani makavu au gram 5 za majani mabichi, subiri
dakika 15, chuja, na uache ipoe. Tumia chai hii kwa kuinika, ikiwa imegawanywa katika sehemu
4 au zaidi za dozi katika siku 1. Rudia njia hii kwa siku 7, au hadi wakati mgonjwa atakapoweza
kunywa tena. Wakati huo, nunua dawa nyingine kwa sababu artemisia pekee yawezekana
isitoshe kwa mtoto huyu.

5. Watoto wenye umri kati ya miezi 4 – 11 (au uzito hadi kg 10)

Toa nusu ya kidonge cha sulfa – pyri mara moja, au kiasi cha chloroquine mg 250
iliyogawanywa katika siku tatu, au dozi ya amodiaquine mg 250 iliyogawanywa katika siku 3 au
kidonge 1 cha ALU mara 2 kwa siku kwa siku 3. Mpe mtoto vinywaji vingi (maji
yaliyochemshwa, maziwa ya mama). Kama dawa hizi hazipatikani au hazifanyi kazi mwilini,
tumia artemisia. Kama mtoto anakubali kunywa chai hii, mpe ml. 50 za “chai ya artemisia ya
anamed” (angalia H hapo juu) mara 4 kwa siku, yaani ml 200 kwa siku, kwa siku zisizopungua
7. Mtoto anaweza kufurahia zaidi “artemisia ya sukari ya anamed“ (angalia K hapo juu). Mpe
kijiko cha chai kilichosawazishwa mara 4 kwa siku; yaani jumla ya vijiko 4 vya chai.

Kama mtoto hajitambui, jaribu yafuatayo: chukua quinine ya maji, au yeyusha vidonge vya
quinine (mg 30 za quinine kwa kilo moja ya uzito wa mwili kwa siku) katika ml 50 za maji,
gawanya dawa hii katika sehemu 4 au zaidi na umwinike mtoto kwa siku 1. Acha kumwinika
mgonwja mara tu apatapo fahamu, kisha mpe dawa inayotakiwa kupitia mdomoni.

Kama quinine haipatikani, unaweza kujaribu kumwinika kwa kutumia artemisia: Changanya ml
100 za maji yanayochemka katika gramu 2 za majani makavu, au gramu 10 za majani mabichi,
subiri kwa dakika 15, chuja, na acha ipoe. Tumia chai hii kuinika ikiwa imegawanywa katika
dozi 4 au zaidi katika siku 1. Fanya namna hii kwa siku 7, au hadi hapo mgonjwa atakapoweza
kunywa tena. Kwa wakati huu nunua dawa nyingine kwa sababu artemisia pekee inaweza
isitoshe kwa mtoto huyu.

Kwa kundi la umri huu, Artemisia annua inaweza pia kuchanganywa na proguanil au
cotrimoxazol.

6. Watoto wenye umri kati ya miaka 1 – 2 ( au uzito hadi kg 14).


Kama mtoto yuko tayari kunywa chai, tumia ml 75 za “chai ya artemisia ya anamed” (angalia
maelezo H hapo juu) mara 4 kwa siku, yaani jumla ya vijiko 5 vya chai kwa siku zisizopungua
7. Mtoto akipendelea kunywa “sukari ya artemisia ya anamed” (angalia K hapo juu): Mpe kijiko
cha chai kilichosawazishwa mara 5 kwa siku. Yaani jumla ya vijiko 5 vya chai, kwa siku
zisizopungua 7. Kwa usalama zaidi, ongeza ¾ ya SP ya kidonge, au kiasi cha dozi ya
chloroquine mg 350 kilichogawanywa kwa siku 3, au dozi ya amodiaquine mg 350
iliyogawanywa katika siku 3 au kidonge 1 cha ALU mara 2 kwa siku kwa muda wa siku 3. Mpe
vinywaji kwa vingi (chai ya mchaichai, maji ya kunywa yaliyochemshwa yakapozwa n.k.).

Kama mgonjwa hajitambui, jaribu yafuatayo: Changanya ml 150 za maji yanayochemka kwenye
gramu 3 za majani makavu au gramu 15 za majani mabichi ya artemisia, subiri kwa angalau
dakika 15, chuja na uache ipoe. Ongeza vidonge vya quinine au quinine ya maji (mg 30 za
quinine kwa kila kilo ya uzito). Mwinike, dawa igawe katika dozi 4 au zaidi na itumike kwa siku
1. Endelea kumwinika kwa muda wa siku 7. Mara tu mgonjwa atakapoweza kunywa tena, mpe
dawa zote kwa njia ya mdomo.
Kwa kundi la umri huu, Artemisia annua inaweza pia kuchanganywa na proguanil,
cotrimoxazole au malarone.

7. Watoto wenye umri wa miaka 3 – 4 (uzito wa mwili hadi kg 18).


Kama mtoto yuko tayari kunywa chai hii, mpe ml 100 za chai ya artemisia ya anamed” (angalia
H hapo juu) mara 4 kwa siku, yaani, ml 400 kwa siku, kwa siku zisizopungua 7. Mtoto akipenda
kunywa “Artemisia ya sukari ya anamed“ (angalia K hapo juu), mpe vijiko 2 vya chai
vilivyosawazishwa, mara 4 kwa siku, yaani jumla ya vijiko 8 kwa siku, kwa siku zisizopungua 7.
Kwa usalama, ongeza kidonge 1 cha SP mara moja, au dozi ya jumla ya mg 450 za chloroquine
iliyogawanywa katika siku 3, au jumla ya dozi ya mg 450 za amodiaquine iliyogawanywa katika
siku 3 au vidonge 2 vya ALU mara 2 kwa siku kwa muda wa siku 3. Mpe vinywaji vingine (chai
ya mchaichai, maji nk)
Kama mgonjwa hajitambui, jaribu ifuatavyo:
Changanya ml 200 za maji yanayochemka katika gram 4 za majani makavu au gramu 20 za
majani mabichi ya artemisia, subiri kwa angalau dakika 15, chuja na uache ipoe. Ongeza vidonge
vya quinine au quinine ya maji (mg 30 ya quinine halisi kwa kila kilo 1 ya uzito wa mwili).
Gawanya katika sehemu 4 au zaidi na umwinike katika siku 1. Rudia kuminika kwa muda wa
siku 7. Mara tu mgonjwa atakapoweza kunywa tena, mpe madawa yote kupitia mdomoni.
Katika kundi la umri huu, artemisia annua inaweza pia kuchanganywa na proguanil,
cotrimoxazol au malarone.

8. Watoto wenye umri kati ya 5 – 9 (au uzito hadi kg 29).


Unaweza kutumia Artemisia: Changanya ml 600 za maji yanayochemka, katika gramu 3 za
majani makavu ya artemisia (au zaidi ya gramu 15 za majani mabichi ya artemisia).
Subiri kwa angalau dakika 15, kisha chuja, gawa katika vikombe 4 na umpe kikombe 1 mara 4
kwa siku. Rudia kwa namna hii kwa siku zisizopungua 7. Kama mtoto akikataa kunywa chai hii,
anaweza akakubali kwa urahisi kunywa “artemisia ya sukari ya anamed”. (Angalia maelezo K).
Mpe vijiko 2 vya chai vilivyosawazishwa mara 5 kwa siku, ambayo ni vijiko 10 vya chai, kwa
siku zisizopungua 7.
Kama tiba hii pekee haitasaidia, ongeza kidonge 1 ½ cha SP mara moja, au dozi ya jumla ya mg
700 ya chloroquine ya vidonge iliyogawanywa katika siku 3, au dozi ya amodiaquine ya mg 700
iliyogawanywa kwa siku 3 au vidonge vya ALU (vidonge 2 mara 2 kwa siku akiwa na uzito hadi
kg 25, kilo zikizidi apewe vidonge 3 mara 2 kwa siku kwa muda wa siku 3). Mpe vinywaji vingi
(chai ya majani ya mchaichai, maji n.k.).
Kama mgonjwa hajitambui, jaribu yafuatayo: Changanya ml 300 ya maji yanayochemka katika
gram 6 za majani makavu au gramu 30 za majani mabichi. Subiri kwa angalau dakika 15, chuja
na uruhusu kupoa. Mwinike, igawanye katika dozi 4 au zaidi kwa siku hiyo 1. Kama ikihitajika,
unaweza kuyeyusha vidonge vya quinine (au kutumia quinine ya maji) katika kuinika huku kwa
kutumia artemisia (mg 30 za kidonge cha quinine kwa kila kilo 1 ya uzito wa mwili kwa siku).
Rudia kumwinika kwa siku zisizopungua 7. Mara tu mgonjwa awezapo kunywa tena, mpe dawa
yote kwa njia ya mdomo.

Katika hili kundi la rika, Artemisia annua inaweza pia kuchanganywa na proguanil,
cotrimoxazol, malarone, au primaquin.

9. Watoto wenye umri wa miaka 10 – 11 (au uzito hadi kg 39.)


Unaweza kutumia artemisia. Changanya ml 700 za maji yanayochemka katika gramu 3.5 za
majani makavu ya artemisia (au zaidi ya gramu 17 za majani mabichi ya artemisia). Subiri
angalau dakika 15, kisha chuja, igawe katika vikombe 4 na umpe kikombe 1 mara 4 kwa siku.
Rudia namna hii kwa siku zisizopungua 7. Kama tiba hii pekee haisaidii, ongeza vidonge 2 vya
SP mara moja au dozi ya jumla ya mg 900 ya chloroquine vidonge iliyogawanywa katika siku 3,
au dozi ya jumla ya mg 900 ya amodiaquine vidonge iliyogawanywa katika siku 3 au vidonge 3
vya ALU mara 2 kwa siku (kuanzia uzito wa kilo 35 atumie vidonge 4 mara 2 kwa siku) kwa
muda wa siku 3. Mpe vinywaji kwa vingi (chai ya mchaichai, maji n.k.).
Kama mgonjwa hajitambui, jaribu yafuatayo: Changanya ml 350 za maji yanayochemka katika
gramu 7 za majani makavu au gramu 35 za majani mabichi, subiri angalau dakika 15, chuja na
acha ipoe. Mwinike, igawe katika sehemu 4 au zaidi na itumike katika siku 1. Kama ikihitajika,
unaweza kuyeyusha vidonge vya quinine ( au quinine ya maji) katika dawa hii ya kumwina ya
artemisia (mg 30 za quinine za vidonge kwa kila kilo ya uzito kwa siku).
Rudia kumwinika kila siku kwa muda wa siku 7. Mara tu mgonjwa atakapoweza kunywa tena,
mpe dawa zote kwa mdomo. Katika rika hili, Artemisia annua inaweza pia kuchanganywa na
proguanil, cotrimoxazole, malarone, primaquin, doxycyclin au tetracycline.

10. Watoto wenye umri wa miaka 12 – 13 (au uzito hadi kg 49).


Unaweza kutumia artemisia: Changanya ml 800 za maji yanayochemka katika gramu 4 za
majani makavu ya artemisia (au zaidi ya gramu 20 za majani mabichi ya artemisia). Subiri
dakika 15, chuja, igawe katika vikombe 4 na umpe kikombe 1 mara 4 kwa siku. Rudia jambo hili
kwa siku zisizopungua 7. Kama tiba hii pekee haifai, ongeza vidonge 2 ½ vya SP mara moja tu,
au jumla ya dozi ya chloroquine mg 1,200 iliyogawanywa katika siku 3, au dozi ya jumla ya
amodiaquine mg. 1,200 iliyogawanywa katika siku 3 au vidonge 4 vya ALU mara 2 kwa siku
kwa siku 3. Mpe vinywaji vingi (majani ya mchaichai, maji n.k.).
Kama mgonjwa hajitambui, jaribu ifuatavyo: Changanya ml 400 za maji yanayochemka katika
gramu 8 za majani makavu au gramu 40 za majani mabichi, subiri kwa angalau dakika 15, chuja
na ruhusu kupoa. Mpe kwa kumwinika ikiwa imegawanywa katika dozi 4 au zaidi kwa siku.
Ikihitajika unaweza kuyeyusha vidonge vya quinine (au quinine ya maji) katika dawa ya
kumwinika ya artemisia (mg 30 za quinine kwa kila kilo ya uzito wa mwili kwa siku). Rudia
tendo hili kwa siku 7 mara tu mgonjwa atakapoweza kunywa tena, mpe dawa yote kwa mdomo.
Katika rika hili, artemisia annua inaweza pia kuchanganywa na proguanil, cotrimoxazol,
malarone, primaquin, doxycycline au tetracycline.

11. Watoto zaidi ya miaka 13 na watu wazima (uzito zaidi ya kg 50).


Unaweza kutumia artemisia: Changanya lita 1 ya maji yanayochemka katika gramu 5 za majani
makavu ya artemisia (au zaidi ya gramu 25 za majani mabichi). Subiri angalau dakika 15, kisha
chuja, gawa katika vikombe 4 na umpe kikombe 1 mara 4 kwa siku. Rudia namna hiyo kwa siku
zisizopungua 7. Kama tiba hii pekee haisaidii, ongeza vidonge 3 vya SP mara moja tu, au dozi ya
jumla ya mg 1500 ya chloroquine vidonge iliyogawanywa katika siku 3, au dozi ya jumla ya
amodiaquine mg 1500 iliyogawanywa katika siku 3 au vidonge 4 vya ALU mara 2 kwa siku kwa
siku 3. Mpe vinywaji vingi (chai ya majani ya mchaichai, maji n.k.).
Kama mgonjwa hajitambui, jaribu yafuatayo: Changanya ml 500 za maji yanayochemka katika
gramu 10 za majani makavu au gramu 50 za majani mabichi, subiri dakika 15, chuja na uache
ipoe. Mpe kwa kumwinika ikiwa imegawanywa katika sehemu 4 au zaidi kwa siku moja.
Ikihitajika, unaweza kuyeyusha vidonge vya quinine (au quinine maji) katika dawa ya
kumwinika ya artemisia (mg 30 za quinine kwa kilo kilo ya uzito wa mwili kwa siku). Endelea
namna hii kwa siku 7. Mara tu mgonjwa atakapoweza tena kunywa, mpe dawa zote kwa njia ya
mdomo.
Katika rika hili, artemisia annua inaweza pia kuchanganywa na proguanil, cotrimoxazole,
malarone, primaquine, doxycycline au tetracycline.

8.6. Matumizi mengine ya artemisia annua

A. MATUMIZI YA DAWA – KWA NDANI (KUNYWA).


Tahadhali: Kwa matumizi ya wajawazito, tafadhali soma maelekezo hapo juu.

Kwa matatizo yafuatayo, unaweza kuamua kama unakunywa artemisia katika kiwango kikubwa
kwa siku cha gramu 5 au kipimo cha chini cha gramu 1.25.
Dozi kubwa: Changanya lita 1 ya maji yanayochemka katika gramu 5 za majani makavu, au
gramu 25 za majani mabichi, na kunywa katika siku 1. Majani makavu yaliyochekechwa ya
gramu 5 ni sawa na vijiko 4 vya chai.
Kipimo cha chini: Changanya ml. 200 (kikombe kikubwa 1) cha maji yanayochemka katika
gramu 1.25 za majani makavu, au gramu 6,25 za majani mabichi, na unywe katika siku 1. Kijiko
1 cha chai cha majani makavu yaliyochekechwa ni sawa na gramu 1,25.

Kuzuia Malaria
Washiriki wengi wa anamed katika nchi za Afrika walitambua kwamba wakinywa chai ya
artemisa anamed siku kwa siku wanapata malaria mara chache sana au kama wanapata, malaria
haina nguvu kama ilivyokuwa bila kutumia chai ya artemisia anamed.
Kwa sasa kampuni mbalimbali (k.mf. katika nchi za Burundi, Cameroon, Uganda) wanawashauri
wafanyakazi wao kutumia chai ya artemisia kwa ajili ya kuzuia malaria.
a) Kwa watalii kutoka Ulaya (wasio na kinga ya Malaria) wajaribu njia ifuatayo:
Mwaga kikombe 1 (ml 200) ya maji yanayochemka kwenye gramu 1,25 ya majani makavu ya
artemisia annua anamed (sawasawa ya kijiko 1 cha chai) na ipoe kwa angalau dakika 15. Chuja
na kunywa kikombe kizima mara moja. Usigawanye kikombe hiki – kwa sababu kwa njia hii
unahakikisha kuwa na kiasi cha artemisinin kwenye damu yako ambacho ni mara 4 zaidi kuliko
kiasi kinachohitajika kuua vidudu vya malaria. Watoto wanatakiwa kutumia kiasi kidogo zaidi –
kulingana na uzito wao. Wasioweza kutumia chai ya artemisia kutokana na uchungu wake
wanaweza kuponda majani yake na kuchanganya unga wake na yoghurt au peanutbutter au asali.
Anza kutumia njia hiyo siku unapofika katika nchi ya Afrika, endelea kutumia siku kwa siku na
endelea ukiwa umesharudi nyumbani kwa angalau wiki 3.
b) Kwa waliozaliwa au wanaoishi katika nchi za Tropiki (SEMI-IMMUNES) wanaweza kutumia
chai ya artemisia ya anamed mara 1 au mara 2 kwa wiki tu. Hii inaweza kupunguza malaria kwa
asilimia 50 %.

UKIMWI:
Huduma za kusaidia kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili: Artemisinin imeishaidhinishwa
kutumika kama dawa ya kupunguza makali ya UKIMWI. Katika vituo kadhaa vya afya ambavyo
vinatumia madawa ya asili wagonjwa wa UKIMWI wanakunywa chai ya artemisia, katika dozi
ya juu au ya chini, kila siku ya maisha yao. Inapowezekana wanatumia pia chai ya mchaichai,
unga wa mlongelonge, vitunguu saumu kwa vingi au ute mzito wa msubili. Kwa taarifa zaidi juu
ya tiba ya UKIMWI/VVU kwa madawa ya asili, angalia toleo la anamed liitwalo “UKIMWI na
madawa ya asili”.

Kichocho:
Artemisinin hupunguza idadi ya vidudu vya kichocho. Jaribu kutumia dozi ile kubwa lakini pia
endelea kutumia chai hiyo kwa majuma 2 hadi 3. Ikiwezekana ongeza matibabu ya vidonge pia.
Tafadhali angalia matokeo ya tiba ya dawa hii katika maabara na ututumie matokeo yako.
Utafiti wa hivi karibuni ulionesha kwamba wanyama walioambukizwa na Kichocho na kutibiwa
kwa kutumia Artemeter, walionesha matokeo ya kupona, (Utafiti ulifanyika na Institute of
Parasitic Diseases, Shanghai, and the Swiss Tropical Institute, Basel pamoja na Ushirika wa
Afya Ulimwenguni (WHO).

Magonjwa ya njia ya hewa na koo linalowasha:


Changanya maji yanayochemka na majani machache makavu au mabichi ya artemisia na uweke
chombo kwenye joto kidogo. Vuta mvuke wake. Kwa makoo yanayowasha sukutua kooni kwa
chai ya artemisia.

Saratani: Artemisinin tayari imesajiriwa kuwa tiba ya saratani na imekuwa ikitumiwa na


madaktari kwa kutibu uvimbe. Wagonjwa, kwa msaada wa daktari, wakati wowote
inapowezekana, wanaweza kunywa chai ya artemisia kila siku na kuona kwa kiasi gani
inabadilisha hali ya ugonjwa.

Candida (fangasi) ya mdomoni:


Tafuna majani ya artemisia mchana kutwa. Watoto wanaweza kupendelea mchanganyiko wa
kijiko 1 cha chai cha asali na kingine cha unga wa majani makavu ya A-3.

Candida (fangasi) ya kwenye matumbo:


Kunywa chai ya A-3, iliyotengenezwa kama ile ya malaria, kwa siku 12.

Chikungunya na Dengue Fever: Tumia ile dose kubwa ya chai ya artemisa anamed kwa wiki 2.
Kutokana na maelezo tuliyoyapata, muda wa homa na kiasi cha maumivu kinapungua.
Homa, mafua ya kawaida:
Maambukizi yakitokea mara ya kwanza kunywa lita 3 za chai ya mchaichai kila siku. Kama joto
litaendelea au kama mafua au kikohozi kitaendelea basi kunywa lita 1 ya chai ya artemisia (dozi
kubwa) na lita 2 za chai ya mchaichai kila siku kwa siku 7 hadi 12.

Bawasiri: Hii ni kumbukumbu ya kwanza kabisa ya matumizi ya chai ya artemisia katika dawa
za jadi za ki-China. Kunywa lita 1 ya chai ya artemisia kila siku. Katika jimbo la Gamo Gofa
nchini Ethiopia watu wengi wanasumbuliwa na bawasiri sugu, na wamekuwa na mabadiliko
makubwa kwa kutumia tiba hii (kwa dozi kubwa – angalia hapo juu). Kwa bawasiri ya kawaida,
kunywa mara chache kikombe cha chai ya artemisia (dozi ya chini). Kwa matumizi ya nje pia
tumia artemisia ya mafuta (angalia sura ya 12).

Lupus erythematosus (ugonjwa unaosababisha tissue kuvimba, kuwa nyekundu, na kuumwa):


Tumia artemsia anamed (dose kubwa) kwa wiki 4. Kama hakuna mabadiliko, sitisha matumizi
ya artemisa, kama mabadiliko yanaonekana, endelea na dose ya chini

Matatizo ya tumbo na utumbo; mfano msokoto wa tumbo, Crohn’s disease, divertialitis, na


kuharisha damu, pia magonjwa ya mifupa, baridi yabisi, borreliosis nk: Kunywa chai ya
artemisia katika dozi ya juu kwa siku 7, kisha kwa dozi ya chini hadi dalili zitakapokwisha.
Artemisia husafisha mfumo mzima wa tumbo na matumbo na hurudisha mfumo wa kinga katika
hali yake ya kawaida.

Magonjwa mengine: Tumepokea taarifa za wagonjwa wenye matatizo mbalimbali kuendelea


vizuri kutokana na matumizi ya chai ya Artemsia. Matatizo hayo ni pamoja na gout, kisukari,
shinikizo la damu, vivimbe (warts), kifafa, kulainika kwa mifupa (osteoporosis), maumivu
makali ya kichwa, matatizo ya ngozi (psoriasis) na leishmaniosis. Mlango uko wazi kwa utafiti
zaidi ! Mgonjwa atumie gramu 5 au artemisa kila siku kwa wiki 1. Kama hakuna mabadiliko
matibabu yanasitishwa. Kama mgonjwa anaendelea vizuri aendelee na dozi ya gramu 5 mpaka
apate nafuu, baadaye aendelee na dozi ya gramu 1,25 kila siku.

B. Matumizi ya dawa - kwa nje.


Vidonda vyenye maambukizi/ usaha: Chemsha polepole majani ya artemisia kwa dakika 20
kwenye maji madogo, uyalaze kwenye kidonda. Kwa uvimbe wa chini ya ngozi, tumia vitunguu
saumu (angalia sura 2).

Maambukizi ya macho:
Njia ya utengenezaji A: Watu wengi katika nchi za tropic hawaoni (Trachoma) kwa sababu
wakiwa watoto, wakisumbuliwa na inzi, hawakuwa na fedha za kutumia dawa. Njia
zinazoelezwa hapo chini ni kwa ajili ya dharula tu – wakati ambapo dawa ya macho hazipatikani.
Tahadhari: watu kutoka Ulaya mara nyingine wana allergy ya maua ya artemisia. Uhakikishe
kwamba hawana allergy na pia tumia dawa tu ambayo kwa uhakika haikutengenezwa kutokana
na maua.
Tayarisha chai ya artemisia kwa kuchemsha majani kwenye maji. Chemsha gramu 5 za majani
makavu katika kikombe 1 cha maji kwa dakika 5. Chuja kwa karatasi na uache ipoe. Weka
kitambaa safi cha pamba katika chai hii na ichemshe tena kwa muda mfupi. Ikiishapoa, weka
kitambaa hiki chenye dawa katika macho yako kwa dakika 5. Rudia tiba hii mara kadhaa kwa
siku. Tibu macho yako pia kwa ute mzito wa msubili. Kata jani la msubili kwa marefu kupitia
katikati na uguse jicho kwa kutumia ute huo. Kwa wakati huo huo kunywa chai ya A-3 (dozi ya
juu) iliyotengenezwa kwa kumwagia maji katika unga wa artemisia au majani mabichi
(infusion).

Njia ya Utengenezaji B: Changanya gramu 10 za majani safi ya Artemisia (yasiyo na maua)


yaliyokaukshwa na kupondwa na ml 100 za mafuta ya zeituni na gramu 10 za nta. Chemsha
kwenye sufuria safi, ukiendelea kukoroga. Kwa kutumia kipimo joto uhakikihe joto iwe kati ya
joto ya nyuzi 95 hadi 100° C kwa dakika 15. Chuja moja kwa moja kwenye chujio la karatasi na
weka kwenye chombo kisafi (au funga gramu 5 kwenye mifuko midogo ya plastiki). Tumia
kama majaribio ya kwanza kwa macho yenye maambukizo. Fanya kazi kwa kuzingatia usafi!
Kwa njia zote 2 rudia matibabu mara kadhaa kwa siku. Tumia pia aloe gel kwenye macho yako
and kunywa chai ya artemisia anamed.

Matatizo ya ngozi, eczema na bawasiri:


Tumia mafuta ya artemisia kwa sababu ya kazi yake ya kuua wadudu. Ponda gramu 5 (kwa
bawasiri gramu 2,5) za majani ya artemisia na changanya na ml 100 ya mafuta ya mimea (mafuta
ya zeituni yanafaa zaidi, au mafuta ya karanga au alzeti) Chemsha katika fukizo-maji kwa saa 1.
Chuja kwenye kitambaa safi, ongeza gramu 10 za nta iliyoyeyushwa na weka kwenye vyombo
moja kwa moja (k.mf. makopo ya kanda za filmu). Tumia ndani ya mwaka 1. Mara zote weka
kwenye ngozi yenye UNYEVU na sugua vizuri. Kwa njia hii tuliona matokeo mazuri hata kwa
watoto wenye shida za ngozi ambapo madaktari waliona njia tu ya kumpatia cortison....

C. MATUMIZI MENGINE
Dawa ya mifugo:
Tulipata taarifa za mafanikio zilizotushangaza kutoka watu mbalimbali – mojawapo kuwa
matibabu ya saratani kwa mbwa. Kwa ujumla, baada ya kuvuna majani ya artemisia, matawi
yaliyobaki yanaweza kutumika na wanyama ili watafune kulingana na mahitaji yao. Artemisia
inatibu maambukizo ya wadudu (bacterial infections) na hata ugonjwa wa coccidiosis
unaosababisha kifo kwa wanyama.
Wanyama wengine wanaweza kupewa majani (mabichi au makavu) yaliyokatwakatwa na
kuwekwa kwenye chakula chao. Pendekezo ya dose kwa kuku, nguruwe, njiwa nk (badala ya
kutumia antibitic): gramu 10 za majani ya artemisia yaliyokaushwa kwenye kilo 1 ya chakula
chao. Watumie kwa siku 5 hadi 10.
Watafiti huko Romania waliponyesha kuku wao waliougua ugonjwa wa eimeriosis (ugonjwa
unaoathiri ngozi ya ndani ya matumbo) kwa kutumia gramu 15 za majani makavu ya artemisia
kwenye kilo 1 ya chakula chao.
Artemisia annua (sweet wormwood) pia inajulikana kwa kutibu minyoo na viroboto.

Viuatilifu vya kilimo: Wakulima katika nchi ya Tanzania waligundua kwamba wakiweka
mistari ya mahindi katikati ya mistari ya artemisia, mahindi yanapata madhara mchache zaidi
kutoka kwa wadudu na kwa hiyo hayahitaji dawa ya sumu ili kuua wadudu.

Kuzuia mbu: Ili kufukuza mbu weka miche ya artemisia au matawi ya artemisia kwenye
chombo cha maji ndani ya nyumba yako.
Nondo: Weka majani makavu ya artemisia yaliyofungwa kwenye kitambaa au kwenye mfuko
wa plastiki katikati ya nguo zako

Vinywaji: Kwa kutengeneza kinywaji ili kuepukana na matumizi ya soda, chemsha gramu 5 za
majani makavu au gramu 25 za majani mabichi kwenye lita 1 ya maji kwa dakika 10. Kwa kila
kikombe 1 cha chai hii ongeza vikombe 20 vya maji masafi na maji ya malimau 10. Tumia ikiwa
baridi sana.

SURA 9: Azadirachta Indica (Mwarobaini)


Mwarobaini asili yake ni India ambako unaheshimika sana. Wahindi wamekuwa wakienda nao
katika nchi za kigeni, kwa sababu kwao “unaashiria mwendelezo wa jadi
yao na hutimiliza hitaji la kuishi kwa uhusiano mwema na uumbaji wa
asili.” Miti 50,000 ya Mwarobaini imepandwa Meka ili kutoa kivuli kwa
watu wanaokwenda Kuhiji.

Sabuni, manukato, madawa, na viuatilifu vya kilimo vinavyotokana na


mwarobaini vinaendelea kutumika kwa wingi zaidi katika kila bara duniani
- hasa Ulaya na Amerika kaskazini.

9.1. Maelezo ya Kibotania


Familia: Meliaceae (familia mahogany)
Mwarobaini unastawi vizuri zaidi mahali ambapo mvua ni kati ya mm 250 – 2,000 kwa mwaka
na udongo wa kina kirefu, wa kichanga na unapitisha maji. Unaweza kuvumilia ukame mkali, na
kustawi katika eneo lisilostawisha mazao yoyote, kwenye udongo wa hali ya chini kabisa, ambao
baadaye utabadilishwa na kuwa udongo mzuri. Haustawi vyema kwenye ardhi yenye unyevu
mwingi. Inastawi katika joto kati ya nyuzi 4 - 40ºC, na kutoka usawa wa bahari hadi m 2000.
Majani ya mwarobaini ni ya kijani wakati wote. Unaishi hadi miaka 300 na inaweza kurefuka
hadi meta 30 juu na upana meta 20. Kwa kawaida huanza kutupa matunda kati ya miaka 3 – 5,
kuzaa kwa ukamilifu na wingi baada ya miaka 10. Katika hali nzuri ya hewa mti mmoja unazaa
kama kilo 50 za matunda kwa mwaka na kilo 350 za majani ya kijani. Kilo 50 za matunda hutoa
kilo 30 za mbegu, ambazo zinaweza kutoa kilo 6 za mafuta na kilo 24 za keki ya mbegu za
mafuta.

9.2. Uoteshaji:
Mwarobaini unaoteshwa vizuri kutokana na mbegu zake. Chukua mbegu zilizotoka mtini –
zinaota kama zina umri usiozidi miezi 3. Ondoa maganda yake na kuweka kwenye magazeti
yaliyolowana na maji. Weka mahali penye joto na hakikisha magazeti yawe na unyevu wakati
wote. Baada ya wiki 1 ondoa magazeti na weka mbegu kwenye udongo wa mchanga kwenye trei
mahali penye mwanga, pasipo na jua la moja kwa moja. Baada ya majuma 2 zipandwe moja kwa
moja katika vyombo vya kukuzia vyenye udongo uliotengenezwa kwa udongo 50% na mboji
iliooza vizuri 50%. Kisha, baada ya miezi 3, zipandwe sehemu ya mwisho zitakapoishi wakati
wote.
Kwa kuotesha kwa vipandikizi, kata kitawi na ukiondolee majani kisha kichomeke kwenye
udongo wenye unyevu. Kwa kuotesha kwa mizizi, chimba kama meta 2 kutoka kwenye shina la
mti uliokomaa, na tafuta mzizi uliolala usawa wa ardhi ulio na unene wa kati ya sm 2 na 4. Ukate
katika urefu kama wa sm 20, na uchomeke sm 5 chini.
Mwarobaini inaweza kupandwa kwenye mteremko ya juu ya milima, ardhi isiyostawisha mazao
yoyote, karibu na barabara kwenye ardhi isiyo na kina cha udongo na yenye mawe na hata
kandokando ya bahari.

9.3. Kuvuna na kuhifadhi mbegu za mwarobaini


Osha mbegu, na uzikaushe vizuri juani kwa siku chache. Zihifadhiwe kwenye vyombo
vinavyopitisha hewa kama vile magunia ya katani au vikapu. Kamwe usizihifadhi kwenye
mifuko au magunia ya plastiki ili kuzuia uwezekano wa kushambuliwa na mba wenye sumu.

9.4. Kutengeneza mafuta ya mwarobaini (yatumikayo katika dawa na kilimo).


Kwanza ondoa ngozi ya mbegu. Njia rahisi kabisa ni kuweka mbegu katika kinu kikubwa na
kuzitwanga polepole hadi ngozi kupasuka. Pepeta mchanganyiko wa ngozi na mbegu katika
kikapu. Mbegu zitadondoka kwenye kikapu na ngozi nyepesi zitapeperushwa. Endeleza tendo
hili hadi ngozi zote zimedondoka.
Ondoa mbegu zilizooza, ambazo zimepoteza rangi yake ya hudhurungi nyepesi, hizi zinaweza
kuwa na sumu. Rudisha mbegu nzuri kwenye kinu na uzitwange hadi ziwe unga wa hudhurungi
unaonata. Kanda embwe hii kwa mkono. Unatakiwa kuongeza maji kidogo ili embwe iweze
kukandwa kwa mkono. Baada ya kukanda kwa muda kidogo mafuta huanza kuvuja. Minya
embwe kwa nguvu zaidi, na mafuta zaidi yatazidi kutoka. Endelea kukanda na kuminya hadi
mafuta yatakapoacha kutoka kabisa. Kwa njia hii karibu ml 100 - 150 zinaweza kupatikana
kutokana na kilo 1 ya mbegu za mwarobaini. Mabaki magumu yanaitwa keki ya mbegu za
mwarobaini, na zinaweza kutumika kama chakula cha mifugo, mbolea na dawa ya asili ya kuua
wadudu.

9.5. Matumizi kwa dawa


TAHADHARI: Tiba ya mwarobaini, hasa kwa matumizi ya ndani (kama kunywa), isiendelee
kwa muda mrefu. Matumizi ya mwarobaini ya muda mrefu yanaweza kudhuru ini.

A. Kulinda mdomo na meno


Huduma ya meno inazidi kuwa ya muhimu. Karibu kila mahali, watu wanatumia sukari nyingi,
na kusababisha kuoza kwa meno.
Mswaki: Tumia kitawi kidogo kutoka kwenye mti. Hiki husafisha meno na kutoa dawa ya asili
ambayo hulinda meno na fizi. Magamba ya mwarobaini kwa sasa yanatumika kutengeneza dawa
za meno na maji ya kusafisha mdomo za kibiashara.
Dawa ya meno ya unga:
Osha vizuri gamba la mwarobaini, likate vipande vidogo vidogo na ulikaushe vizuri. Isage hadi
iwe unga laini. Chemsha chumvi ya mezani ili kuondoa unyevu wote. Changanya chumvi
(ambayo bado ni ya moto) kikombe 1 na kikombe 1 cha unga wa gamba la mwarobaini. Twanga
na uchekeche kupitia kwenye kitambaa cha nailoni (nylon). Tunza katika chombo kisichopitisha
hewa na weka maelezo.
Itumie kama dawa ya meno. Mwarobaini hausafishi meno tu, bali hulinda fizi pia. Ugonjwa
mbaya kabisa wa fizi uitwao kimenomeno (pyorrhoea), unaosababisha kuvimba na mara
nyingine fizi kutoa damu, unapunguzwa sana kwa kutumia unga wa gamba la mwarobaini.

B. Tiba ya ngozi
Mwarobaini ni mzuri sana katika kutibu aina nyingi za magonjwa ya ngozi kama vile chunusi,
maambukizo ya mba, psoriasis, upele na eczema. Inaweza kutumika pia kutibu mzio.
 Oga !: Kwa jadi, Wahindi walioga maji ya moto yenye majani ya mwarobaini.
 Dawa ya mafuta:
- Dawa ya mwarobaini ya mafuta isiyo kali: Changanya gramu 10 za majani makavu
na gramu 100 za mafuta ya mboga, chemsha kwa saa 1 katika fukizo–maji, chuja na
kisha uchanganye na gramu 10 za nta ya nyuki iliyoyeyushwa.
- Dawa ya mwarobaini ya mafuta iliyo kali kiasi: Changanya gramu 10 za unga wa
mbegu kavu na gramu 100 za mafuta ya kula, chemsha kwa saa 1 katika fukizo-maji,
chuja na uongeze gramu 10 za nta ya nyuki iliyoyeyushwa.
- Dawa ya mwarobaini ya mafuta iliyo kali sana: Yeyusha gramu 10 za nta ya nyuki
katika ml 100 za mafuta ya mboga. Ikikaribia kupoa, ongeza ml 10 za mafuta ya
mwarobaini.
 Dawa ya maji (tincture): Zamisha gramu 20 za majani makavu katika ml 100 za kileo
chenye 70% (Ethanol kwa matumizi ya nje, au kileo kilichotengenezwa kijijini). Baada
ya juma 1, chuja mchanganyiko huo. Ukitaka tu kuitumia, ndipo uchanganye kijiko 1 cha
chai cha tincture hii na kijiko 1 cha chai cha mafuta ya mboga na upake kwenye eneo
lililoathirika.

Baka la mba kwenye miguu (Athlete’s foot): Sugua majani kwenye eneo lililoathirika. Ama
tumia mchanganyiko wa tincture na mafuta.

Kutunza nywele: Chemsha majani katika maji na utumie hayo maji kuosha kichwa kwa
kuondoa tatizo la chawa na mba.

Kutibu ngozi iliyo na ndui au tetekuwanga.


Mafuta ya mwarobaini au tincture yake inaweza pia kuwa tiba dhidi ya virusi vya ndui au
tetekuwanga.

Vivimbe (warts): Paka mafuta ya mwarobaini kwenye ngozi moja kwa moja.

Upele: Kuna namna nyingi:


a) Twanga majani hadi yawe teketeke pamoja na maji kidogo, na usugue kwenye
sehemu iliyoathirika.
b) Sugua mafuta ya mwarobaini kwenye sehemu ya ngozi iliyoathirika.
c) Tengeneza embwe la majani mabichi ya mwarobaini na manjano kwa uwiano wa 4:1
kwa uzito ( au kiganja kizima cha majani ya mwarobaini kwa kipande cha manjano ½
ya urefu wa kidole cha shahada). Paka mwili mzima na uache ikauke.
Kuvimba matezi ya shingo, vidonda visivyo na maumivu, baka la mba.
Paka mafuta ya mwarobaini. Kama ikisababisha maumivu makali, ichanganye na mafuta ya
mboga kupunguza ukali. Chemsha kiasi cha majani katika maji ya kutosha kwa dakika 10, kisha
laza majani hayo ya moto kwenye eneo lililoathirika kwa kukandamiza kwa dakika 15 asubuhi
na jioni. Wengine wanashauri kutumia tiba hii kwa vidonda vya ukoma pia, lakini fuata ushauri
wa daktari wako.

Maambukizo katika sehemu iliyoungua:


Chemsha kiganja kizima cha majani mabichi katika lita 1 ya maji kwa dakika 20, chuja ikiwa
bado ya moto (kuepuka maambukizo), poza, na utumie hapo hapo kuosha sehemu iliyoungua
kwenye maambukizo. Tayarisha dawa hii na uitumie mara 3 kwa siku. Mweke mgonjwa kwenye
chandarua kuepuka maambukizo mengine.

Majipu: Kama majipu hayana mdomo, tengeneza kibandiko cha dawa kwa kutumia majani na
uweke.

Majipu yenye mdomo, vidonda, na upele mbaya: Majani lazima yachemshwe kwa dakika 10
kwenye maji kidogo kabla hayajatengenezwa kama kibandiko cha dawa na kutumika.

Candida: Candida ni mba kama hamira ambayo wakati wote inapatikana kwenye ute wa ngozi
za ndani, lakini inaweza isizuiwe na kinga ya mwili hadi ikasababisha madonda mdomoni,
kwenye uke na kwenye ngozi. Changanya sehemu 1 ya mafuta ya mwarobaini na sehemu 9 za
vitu vifuatavyo na utumie:
- Kwa candida ya mdomoni: asali
- Kwa candida ya kwenye ukeni: Yoghurt au mafuta ya mboga.
- Kwa candida ya kwenye ngozi: Mafuta ya mboni au mafuta yoyote ya mboga.

Vidonda sugu vinavyokataa kupona: Vitibu kwa mafuta ya mwarobaini mara 2 kwa siku.

C. Malaria
Tengeneza chai yake kwa kumwaga lita 1 ya maji yanayotokota kwenye gramu 5 za majani
yaliyokaushwa (au gramu 10 kwa malaria kali zaidi.) Kunywa kikombe 1 mara 4 kwa siku.
Kunywa vinywaji vingine kwa wingi, hasa lita 2 za chai ya majani ya mchaichai. Soma sura ya 5
juu ya malaria. Chai ya aina hii inaweza pia kutumika kutibu surua na kuharisha.
Angalizo: Kama ilivyosemwa juu, matumizi ya muda mrefu ya mwarobaini yanaweza
kusababisha madhara ya ini.
Kwa kuzuia malaria, ongeza kiasi kidogo cha mafuta ya mwarobaini kwenye mafuta ya taa ndani
ya taa ili kufukuza mbu, na tafuna majani kadhaa kila juma ili kuongeza kinga ya mwili.

9.6. Sabuni zenye dawa na sabuni ya nywele (shampoo)


Chukua gramu 100 za sabuni ya kawaida. Ivunjevunje, ongeza maji kidogo na mafuta ya
mwarobaini kati ya gramu 1 na 10. Vitwange pamoja, vitengenezee umbo na uache ikauke.
Mafuta ya mwarobaini huipa sabuni uwezo wa kuzuia bacteria kwa sababu ya viasili vya
mwarobaini vinavyozuia vijidudu.
Vipodozi vinavyotokana na mwarobaini kama vile mafuta ya usoni na shampoo (ml 99 shampoo
na ml 1 mafuta ya Mwarobaini) vinazidi kuwa maarufu huko Ulaya na Amerika Kaskazini.
9.7. Madawa ya mfugo na vyakula vya mifugo
Tumia mazao ya mwarobaini kufukuza kupe, inzi, chawa, kuhudumia michubuko na mikato na
kutibu upele. Kutegemea kiwango cha maumivu, tumia dawa ya kuchemsha majani kwa
maumivu yasiyo makali, dawa ya mbegu zilizosagwa kwa maumivu makali, na mafuta ya
mwarobaini kwa maumivu makali sana.
Tumia keki ya mwarobaini na majani kama chakula cha ziada kwa mifugo. Majani yana madini
na kiwango kikubwa cha protini (15%) na nyuzinyuzi kidogo.

9.8. Mwarobaini kama dawa ya kuua wadudu ya kupulizia: Matayarisho na matumizi ya


maji ya mwarobaini.
Mbegu hazihitaji kumenywa. Ama twanga viganja 2 vya mbegu zilizomenywa hadi liwe unga
usio laini, au twanga mbegu na ngozi yake. Fanya hivi mara 2 zaidi, na kila awamu uongeze
viganja 2 vilivyojaa. Kama hakuna mbegu, tumia viganja 10 vya majani mabichi
yaliyopondwapondwa. Changanya katika lita 10 za maji kwenye ndoo, tikisa kwa nguvu na
uache kwa siku nzima. Chuja. Kama hakuna mashine ya kupulizia, jitengenezee mfagio wa
majani makavu au kitu kinachofanana na hicho. Uchovye kwenye hayo maji ya dawa na
uupitishe kwenye kila mmea mara kadhaa, huku ukijaribu kusambaza hayo maji kwenye kila
jani vizuri iwezekanavyo. Rudia kuweka dawa kila baada ya siku 4 hadi 5. Kumbuka kwamba
siyo kila mdudu anaathiriwa kwa kiwango kilekile. Unapomwagilia mimea, mwagilia kwenye
shina la mmea ili usioshe dawa kwenye majani.

9.9 Mwarobaini katika kuhifadhi vyakula:


Changanya majani makavu ya mwarobaini na mpunga, ngano na nafaka nyingine kabla ya
kuvitunza kwa miezi ijayo. Majani ya mwarobaini, mafuta ya maji yake hufukuza wadudu kama
funza walao nafaka, dumuzi, wadudu walao mbegu za maharage, nondo washambulia viazi.
Nafaka zilizoingiliwa na wadudu zinaweza kufukizwa ili kufukuza wadudu kwa kutumia moshi
utokanao na majani makavu ya mwarobaini yanayowaka.

Kwa kutunza maharage ml 2 – 3 za mafuta ya mwarobaini zinahitajika kwa kilo 1 ya maharage.


Kwa hiyo ml 250 za mafuta zitatumika kwa gunia la kg 100. Maharage lazima yachanganywe
vizuri na mafuta ili kuhakikisha mafuta yamesambaa vizuri kwenye maharaghe. Kwa wakati
mmoja, changanya kidogo kwenye karai la plastiki. Kilo 1 ya mbegu kavu au majani
yaliyokaushwa na kusagwa vizuri, hadi kuwa unga, vinaweza pia kutumika.

Vifaa vya kuhifadhi nafaka visivyoruhusu wadudu kuingia vinaweza pia kutengenezwa kwa
kutumia mchanganyiko wa majani ya mwarobaini, udongo wa mfinyanzi na majivu.

Nguo pia zinaweza kulindwa dhidi ya nondo kwa kuweka majani ya mwarobaini yaliyokaushwa
kwenye kibindo.
Majani ya mwarobaini (Melia azadarach (kushoto) na
Azadirachta indica (kulia): mimea hii miwili ina sifa za dawa
na kiuatilifu zinazofanana. Kwa matumizi ya ndani, walakini,
tunapendekeza Azadiracta indica kwa sababu umefanyiwa
uchunguzi wa kutosha.

SURA 10: CARICA PAPAYA (PAPAI)

10.1. Maelezo ya kibotania: Family: Caricaceae


Asili yake ni maeneo ya tropiki ya Afrika. Siyo mti halisi kwa sababu hautoi mbao. Ni mmea wa
dawa ulio kama mti. Unakua haraka na kutoa matunda katika chini ya mwaka mmoja.
Unaendelea kutoa maua isipokuwa katika hali ya ukame
mbaya. Hudumu na majani wakati wote na unaweza
kuvumilia ukame. Mimea yake inaweza kuwa ya kike au ya
kiume au mara chache sana mmea unaweza kuwa wa kike
na kiume kwa wakati mmoja.
Unahitaji mvua ya kutosha au kumwagiliwa, lakini pia
unahitaji udongo tifutifu. Hauwezi kuvumilia eneo la maji
yaliyotua. Unastawi katika hali mbalimbali za joto, na
unauawa na baridi ya theluji. Unastawi hadi meta 1,500
kutoka usawa wa bahari.

10.2 Uoteshaji na utunzaji


Kutokana na mbegu: Panda sm 1 kwenda chini kwenye udongo wa mchanga katika chombo cha
kuoteshea, hamishia kwenye viriba juma 1 baada ya kuota ambayo itakuwa kati ya juma 1 na
majuma 4. Weka miche 3 pamoja. Iweke kwenye jua la asubuhi. Baada ya miezi 6 ikishachanua,
ng’oa miche ya kiume na ya kike iliyo dhaifu.
Nematodes hustawi zaidi katika eneo lililolimwa mapapai, kwa hiyo ni bora kubadilisha mazao,
na kuchanganya keki ya mwarobaini katika udongo. Uwe makini hata hivyo kwa kuwa mizizi ya
mipapai haipendi usumbufu.

10.3. Matumizi ya mpapai


A. Furahia tunda! Zuia upungufu wa vitamin A, B au C.
Kula mapapai yaliyoiva kwa wingi. Tunahitaji vitamin A kwa ajili ya kuona vizuri, vitamini B
kwa mishipa ya fahamu, na vitamini C kwa kuimarisha kinga ya mwili, ambayo huusadia mwili
kupambana na maambukizo.

B. Minyoo
Utomvu wa papai bichi mara nyingi unafaa kwa aina zote za minyoo ya tumbo. Osha kisu kwa
maji yanayotokota, osha papai bichi likiwa bado limening’inia mtini, na ulichanje mistari wima
kwa kisu. Kinga utomvu wake moja kwa moja kwenye kijiko cha chai au kikombe.
Angalizo: Utomvu hii ni hatari kwa macho.
Dawa hii inywewe asubuhi kabla ya kula chochote, pamoja na maji mengi pamoja na dawa ya
kusababisha kupata choo.
Unaweza kutumia vifuatavyo kama dawa ya kupata choo:
1. Kula maembe au mapapai yaliyoiva sana kwa wingi.
2. Mafuta ya mboni ya hospitalini.
3. Cassia Occidentalis au Cassia alata. Chemsha kijiko 1 cha chakula cha
majani makavu au magamba ya mizizi kwa dakika 10 katika lita 1 ya maji.
Kunywa lita nzima. Utaona matokeo yake kama baada ya masaa 8.
Tiba hii itolewe mara moja tu, lakini irudiwe baada ya juma 1 ili kuhakikisha kwamba minyoo
yote imeondolewa. Tiba inaweza kutolewa pia wakati mgonjwa anaharisha tayari.

Jedwali 10: Dozi ya utomvu wa mapapai kwa tiba ya minyoo ya tumbo.

Umri Kiasi
Miezi 6 – mwaka 1 ½ kijiko cha chai
Mwaka 1 – miaka 3 Kijiko cha chai 1
Miaka 4 – miaka 6 Vijiko vya chai 2
Miaka 7 – miaka 13 Vijiko vya chai 3
Miaka 14 – mtu mzima Vijiko vya chai 4

C. Kama kinga kwa minyoo na amiba.


Kila siku tafuna kipande cha jani la mpapai cha mraba kwa urefu wa sm 5 kila upande. Au,
angalau mara 1 kwa wiki, tafuna na umeze kijiko 1 cha mezani cha mbegu za mpapai. Kaskazini
mwa Msumbiji shule zote zinatibiwa kwa namna hii! Minyoo inaonekana kuchukia ladha ya
mbegu hata kuliko watu.

D. Kutosagwa chakula tumboni.


Papai lina papaine, inayosaidia uyeyushaji wa chakula tumboni. Kama una matatizo ya usagaji
wa chakula tumboni, kunywa matone machache ya utomvu wa papai, au kula kipande cha jani la
mpapai pamoja na chakula chako.

E. Kikohozi
Chimba mizizi michache ya mpapai (siyo mzizi mkuu). Osha vizuri, ikate vipande vipande na
uchemshe nusu ya kiganja katika lita 1 ya maji kwa dakika 15. Chuja.
Watu wazima wanywe chai hii katika siku 1 tu. Watoto wanywe kidogo kutokana na uzito wa
miili yao.

F. Tatizo la pumu
Vuta moshi wa majani ya mpapai! Kausha na usage majani machanga ya mpapai na uyavute
kwenye kiko au kama sigara – au choma majani haya karibu na kitanda chako na uvute mvuke
wake. Badala yake, kunywa chai iliyotengenezwa kutokana na kiganja kizima cha majani ya
mpapai au kiganja cha majani ya mziwaziwa (Euphorbia hirta.)

G. Kama sabuni:
Yasuguliwapo kwenye ngozi, pamoja na maji mengi, majani ya mpapai yanasafisha mwili kama
sabuni ya asili! Kwa jinsi hiyohiyo yanawezekana kutumika kufua nguo za rangi.

H. Kuharisha: angalia sura ya 4

I. Malaria:
Changanya maji yanayotokota na kiganja 1 cha majani mabichi yaliyo safi. Acha itulie kwa
dakika 15 na uchuje. Kunywa kwa awamu kwa siku nzima. Kwa nyongeza, kunywa lita 2 za chai
ya mchaichai. Endeleza tiba hii kwa siku 7. Angalia sura ya 5.

J. Majipu yaliyo wazi, vidonda vyenye maambukizo: Angalia sura ya 2.


K. Maambukizo ya mba: Angalia sura ya 3.

SURA 11: MORINGA OLEIFERA (MLONGELONGE)


11.1. Maelezo ya kibotania: Familia: Moringaceae
Moringa oleifera ni mti mdogo unaokua kwa haraka, unapukutisha majani, ni jamii ya miti ya
vichaka ambao hufikia mita 12 ukikomaa. Asili yake ni India. Shina lake ni laini, gamba laini na
mizizi yake huonekana kwenda chini sana. Unastawi vizuri penye joto kati ya nyuzi 26 na 40ºC,
mvua kwa mwaka ni zaidi ya mm 500 na kutoka usawa wa bahari isiwe zaidi ya m 1,000.
Unavumilia ukame. Ingawa hutoa vitumba, siyo jamii ya kunde.
Moringa Stenopetala asili yake ni Kenya na Ethiopia. Unastawi hadi m 2,000 kutoka usawa wa
bahari. Unavumilia ukame zaidi kuliko M. Oleifera. Majani, vitumba na mbegu zake ni kubwa
zaidi, na unadhaniwa kuwa na sifa zilezile. (Angalia hapa chini).

11.2. Uoteshaji
Mti huu hukua haraka kutokana na kupandwa kwa kutumia mbegu au vipandikizi, hata kwenye
udongo dhaifu. Jinsi unavyokua, utakavyozidi kuupunguza usirefuke ndivyo utakavyotoa majani
mengi zaidi.

11.3. Vilivyomo
Kwa virutubisho: Majani ni chanzo bora cha vitamini A, B na C. Yana
madini, hasa calcium, chuma na phosphorus. Pia yana protini kwa wingi, na
yamekuwa na amino acidi muhimu kama aminu asidi inayotakiwa kwa afya
bora, ambayo haziwezi kujizalisha zenyewe. Majani mabichi yana calcium
mara 4 zaidi ya ile iliyomo kwenye maziwa na vitamini A mara 4 zaidi ya
iliyomo kwenye karoti – na hizi zimeongezeka kwenye unga wa mlonge.
Kwa dawa: Moringa Oleifera ina tabia ya kupambana na bacteria
(isothiocynates). Hii pia inazuia kukua kwa chembechembe za ki-saratani.

11.4. Utumie kama mboga.


Panda miti ya mlongelonge karibu na jiko lako. Una virutubisho vingi!
Majani ya Moringa oleifera yanaliwa Ghana kama mboga, na majani ya M.
Stenopetala Ethiopia. Kila mahali yalipoanza kutumika, yalileta mafanikio
makubwa katika kupambana na utapiamlo na ukosefu wa lishe bora – hasa
kwa watoto.
Yanaweza kuliwa yakiwa mabichi. Uyavune yakiwa na hali nzuri, yakaushwe, na kutunzwa.
Yanaweza kuvunwa wakati wa kipindi cha ukame, wakati mboga nyingine hazipatikani kwa
urahisi.

Kutengeneza unga wa majani ya mlongelonge: Vuna majani, yakaushe ndani ya siku 3,


ikiwezekana kivulini. Kwenye jua kali yanapoteza vitamin A. Yatwange, yachekeche kuondoa
vitawi na yatunze kwenye vyombo visivyopitisha hewa, kwenye giza. Ikiwezekana pima
kiwango cha unyevu kwa kutumia kipima unyevu (hygrometer), ili ujue ni kwa muda gani
unaweza kuhifadhi unga huo.
Unga huu unaweza kongezwa kwenye wali, nafaka, mchuzi na kwenye chakula chochote. Wekea
watoto walio chini ya miaka 5 walio na magonjwa ya upungufu wa lishe na matatizo mengine ya
kiafya, ongeza kijiko 1 cha chai kwenye chakula chao mara 3 kwa siku. Watoto walio zaidi ya
miaka 5 ongeza vijiko hivyo 2 au 3 kwa kila mlo, kufuatana na uzito wao na umri wao.
Vitumba vinaliwa pia. Vinapokuwa vichanga sana vikatwekatwe katika vipande vidogovidogo,
vipikwe na viliwe kama maharage ya kijani. Vikikomaa kidogo, vichemshe na uondoe mbegu na
nyama ya ndani. Vinapokomaa zaidi, lakini vikiwa vya kijani, tumia mbegu pekee zinazoitwa
karanga (mbegu) za mlongelonge. Zikaange kwa mafuta na uzile kama karanga.
Maua yanaweza kuliwa kama yalivyo au yakatumiwa kutengeneza chai. Nyuki hutengeneza asali
nzuri kutokana na chavua za maua ya mlongelonge.

11.5. Mafuta ya mlonge


Kutengeneza mafuta ya mlonge usitumie mbegu za mlonge moja kwa moja kutoka
kwenye mti, bali tumia mbegu zilizokaushwa vizuri.
a) Toa maganda
b) Zikaange kwenye kikaangio.
c) Ziponde na baadaye uzisage kwa jiwe.
d) Tengeneza uji mwembamba kwa maji kidogo
e) Weka kwenye maji yanayochemka na yaendelee kuchemka. Ongeza maji
mengine ili mchanganyiko ubaki kuwa majimaji. Mafuta yatatokea juu na
yanaweza kuenguliwa.
Mabaki, ambayo ni mashudu ya mlonge, yanaweza kutumika kusafishia maji au kama mbolea.

Mafuta ya mlonge yanaweza kutumika kwa:


a) kupikia: Ina ubora kwa lishe kama mafuta ya zeituni. Mafuta haya hayachachi haraka, na
ni mazuri sana kwa saladi.
b) kwa kulainisha mashine zinazohitaji uangalifu.
c) kwa utengenezaji wa sabuni na kama kichanganyo cha msingi kwa vipodozi.
d) katika taa.

11.6. Tumia kama dawa


Sehemu nyingi za mmea huu, kama mizizi, gome, shina, jani, maua na vitumba, zina ubora wa
tiba. Una kiasi fulani cha antiobitic, kinachofanya kazi vizuri katika hatua za kwanza za
maambukizo. Tumekuwa tukiambiwa juu ya tiba zifuatazo:
a) Kula majani siyo kwamba ni lishe bora tu, bali pia kunasaidia katika maswala ya
kuharisha, kunaongeza kiasi cha maziwa ya mama, na kinatibu ukosefu wa damu na
vidonda vya juu juu.
b) Jongo, kuvurugika kwa tumbo na baridi yabisi (Rheumatism): Mafuta ya mbegu za
mlonge yanasaidia
c) Kisukari na shinikizo la damu: Mlongelonge inapunguza kiwango cha sukari katika
damu lakini pia inapunguza pressure ya damu. Kunywa chai iliyotengenezwa kwa
majani yake mara kadhaa kwa siku. Wagonjwa wengi walitoa taarifa kwamba sukari
na blood pressure ilipungua kutokana na kutumia unga wa mlonge kwa wingi.
Kutegemea ukubwa wa tatizo, walitumia kijiko 1 hadi vijikio 3 vya mezani kwa siku.
Wagonjwa wengine walipendelea kutafuna na kumeza mbegu za mlonge 1 hadi 3
mara 3 kwa siku. Wengine wanakunywa chai ya Mlonge. Ukiwa na shida ya kisukari
au shinikizo la damu hakikisha ukapimwa mara kwa mara kuona maendeleo.
d) Maambukizo ya ngozi na upele: Tengeneza embwe lake kwa kutwanga mbegu na
kuongeza maji kidogo. Chemsha mizizi au gamba la tawi katika maji, na uweke hayo
maji kwenye sehemu iliyoathirika. Twanga majani na ukamulie maji yake kwenye
sehemu iliyoathirika.
e) Maumivu ya jino: Twanga mzizi mbichi na uweke kwenye jino.
f) Vidonda: Twanga majani mabichi au vipande vya gamba, ongeza maji kidogo na
uchemshe kwa dakika 10 hadi 20, kisha uweke moja kwa moja kwenye kidonda.
g) Kwa mafua: Chemsha maua yake kwenye maji yanayotokota kwa kama dakika 5.
Kunywa kama inavyohitajika.
h) Kizunguzungu: Tengeneza mchuzi kwa kutumia majani yake na unywe.
i) Maumivu ya viungo (baridi yabisi):
Twanga mizizi mibichi na uweke kwenye sehemu iliyoathirika. Mbadala, oka kiasi
fulani cha mbegu, zitwange hadi ziwe unga, changanya na mafuta ya mboga. Uweke
kwenye sehemu iliyoathirika.
Angalizo: Maganda ya mizizi wala mizizi yenyewe ya mlongemlonge isitumiwe na
wajawazito!

11.7. Matumizi katika kilimo


a) Panda msitu: Mlongelonge ni mzuri sana kwa kuzuia upepo na kujengea boma, inakua
tena haraka baada ya kufyekwa kwa juu. Kwa kweli kufyeka juu mara kwa mara
kutaongeza uzaaji wa matawi. Kufyeka boma kwa juu inaweza kuwa ndiyo njia bora ya
kupata faida nyingi za mlongelonge kwa pamoja; mfano: Upataji wa majani kwa wingi,
kuni, kivuli, mahali pa mimea utambaayo, kuzuia upepo, kuzuia mmonyoko na kugawa
maeneo ya ardhi.
b) Chakula cha mifugo: Majani ya mlongelonge yanaweza kufikia 40% ya chakula kikavu
cha mifugo, na inaongeza uzalishaji wa maziwa.
c) Mbolea: Keki ya mbegu inayobaki baada ya kutoa mafuta au kwenye usafishaji wa maji
huwa ni mbolea nzuri au chakula kizuri cha wanyama.
d) Mlongelonge unaweza kutumika kama mbolea ya kijani: Panda kwa kuubananisha (sm
50 x sm 50) na kuchanganya na udongo kwa jembe mara ufikiapo urefu kama ½ meta.
e) Mlonge unaweza kutumika kama nyasi. Panda kwa kubananisha (sm 10 x 10) na kata
mara kwa mara ii kupata chakula cha wanyama.
11.8. Tumia kusafisha maji
Vitumba vya mbegu viachwe vipevuke vikiwa mitini na vivunwe vikikauka. Mbawa na
magamba ya mbegu yaondolewe na kuacha viini vyeupe vya mbegu. Hivi husagwa na kupondwa
vizuri kwa kutumia mchi na kinu. Kiasi cha mbegu kinachohitajika kusafisha maji hutegemea
kiasi cha tope kilichomo katika maji.
Huwa Watumiaji wa mbegu za mlonge huzoea haraka mabadiliko ya mahitaji ya maji yao kwa
kuwa kiasi cha tope hubadilika kufuata majira.
Kusafisha lita 20 ya maji (kiasi cha maji yaliyo kwenye ndoo kubwa) kama gramu 2 za mbegu
zilizosagwa zinahitajika (kama mbegu 10 za M. Oleifera). Ongeza kiasi kidogo cha maji kwenye
mbegu zilizosagwa ili kutengeneza embwe. Weka embwe hii kwenye chupa safi – kwa kawaida
tumia chupa ya soda. Ongeza kikombe cha maji (ml 200) na utikise kwa dakika 5. Tendo hili
huamsha kemikali kwenye mbegu zilizosagwa.
Chuja mchanganyiko huu kwa karatasi ya kuchujia (filter paper) au kitambaa cheupe cha pamba
katika ndoo yenye lita 20 za maji unayotaka kusafisha. Koroga kwa haraka kwa dakika 2
ikifuatiwa na kukoroga polepole kwa dakika 10 – 15. Katika wakati huu wa kukoroga polepole,
mbegu za mlongelonge hugandisha kwa pamoja chembe ndogondogo na bacteria kuwa chembe
kubwa kidogo zinazozama na kutua kwenye kitako cha ndoo. Baada ya masaa kadhaa ya usiku
mzima maji safi yanaweza kuchotwa kutoka kwenye ndoo.
Tendo hili litaondoa asilimia 90 – 99.9% ya bacteria waliojishikiza kwenye chembe chembe hizo
ngumu, pamoja na kusafisha maji. Kama maji yana taka zaidi, usafishaji zaidi unashauriwa,
kama kwa kuchemshwa (ikiwezekana katika jiko la jua /solar) au kuchujwa kwa chujio la
mchanga (simple sand filter).

Kumbuka: Mbegu za mlongelonge zinaweza kutumika kwanza kwa kutoa mafuta yake.
Makapi yake ambayo yanaweza kukaushwa na kutunzwa yana uwezo ule ule wa
kusafisha maji kama mbegu ambazo hazijakamuliwa mafuta.

SEHEMU YA IV: Utengenezaji wa baadhi ya madawa

Sura 12: Mafuta na dawa za mafuta


Mafuta na dawa za mafuta hufanya njia nzuri ya kutumia dawa za mimea kutibu matatizo ya
ngozi ya aina mbalimbali – ukurutu, kukatwa, mikwaruzo, kuteguka, kuungua, vidonda, na hata
maumivu ya viungo.
Dawa mafuta inaweza kutunzwa kwa miaka kadhaa kwa hiyo ni muhimu sana wakati mimea
hiyo haipatikani mwaka mzima.
Hospitali au Kituo cha Afya kinaweza kuwa na akiba nzuri ya dawa ya mafuta wakati wowote.
Jumuia katika jamii zinaweza kutengeneza kipato kidogo kutokana na kuzitengeneza na kuziuza.

12.1. Vifaa vinavyohitajika:


Vyungu 2 vya kupikia, kimoja kidogo, kimoja kikubwa ili kutengeneza fukizo-maji.
Kopo 1 lenye vipimo vya ujazo, au vikopo vya nyanya.
Chekecheo 1 au chujio la nguo na vigingi.
Vyombo vidogo vidogo vya kubebea kama vile vikopo vya mikanda ya picha.

12.2.Zana zinazohitajika
- Mimea iliyokaushwa na kupondwa
- Tumia mafuta yoyote mazuri ya mboga, mfano mafuta ya shea, mafuta ya mchikichi,
mafuta ya alizeti, mafuta ya karanga n.k. - USITUMIE vaciline. Kama unatumia mafua
yaliyotengenezwa nyumbani, uhakikishe maji yote yameondolewa na wadudu wote
wamekufa. Chemsha kwanza mafuta haya (kwenye joto la nyuzi 100 ° C)
- Tumia nta ya nyuki au nta ya mshumaa. Uwe mwangalifu: Siyo mishumaa yote
imetengenezwa kwa nta.

12.3. Maandalizi
a) Uandaaji wa sehemu za mmea zinazohitajika.
Kata vizuri sehemu zinazohitajika. Kausha ndani ya siku 3 kwenye kitambaa safi. Kwenye nchi
za joto kaushia kivulini. Kwenye nchi za ubaridi, au mahali palipo na unyevu mwingi, kaushia
juani kabisa. Kama baada ya siku 3 majani yatakuwa hayajakauka hata kuweza kufikichika
mkononi, kaushia kwenye jiko la jua (solar), kwenye joto lisilozidi nyuzi 40ºC. Twanga vizuri ili
kutengeneza unga mzuri.

b) Chemsha hiyo zana ya mmea kwenye mafuta.


Vingi kati ya viasili vya dawa huyeyuka katika mafuta ya kula ya moto.
Tayarisha fukizo–maji kama ilivyoonyeshwa kwenye mchoro. Vyungu vidogovidogo vya
kupikia huwekwa kwenye mafiga ili kuvishikilia. Ikiwezekana vishikio vya sufuria ya ndani
vilazwe kwenye sufuria ya nje.
Njia hii huhakikisha kwamba mafuta kamwe hayapati joto zaidi ya
nyuzi 100ºC. Kama ingekuwa mafuta na zana za mmea zinachemka
zaidi ya joto hilo, viasili vya dawa ndani yake vingeharibika. Ni
muhimu kuhakikisha kwamba hakuna maji yanayochanganyika na
mafuta. Unaweza kutunza dawa ya mafuta kwa miaka 2 au zaidi,
lakini kama kuna maji mchanganyiko huo utachacha baada ya siku
chache.

Mwaga mchanganyiko wa mmea mkavu uliosagwa na mafuta (kiasi


ni kutokana na jedwali hapa chini) katika chombo cha ndani cha
fukizo–maji. Na vyote uviweke kwenye moto. Endelea kuchemsha mafuta na zana za mmea kwa
njia hii kwa muda wa saa 1 baada ya maji kuwa yameanza kutokota. Koroga mchanganyiko kila
baada ya dakika 10 – 15. Njia bora zaidi ni kuweka hilo fukizo-maji kwenye jiko la jua (solar) na
kufuata hatua zile zile.

c) Chuja mchanganyiko huo.


Chujia mchanganyiko huo kwenye kombe au chombo safi kwa kutumia chujio la
nguo (mfano: kitambaa cha nailoni). Kamua mmea huo ili kuhakikisha unapata
mafuta yote yenye dawa yanayopatikana uliyotengeneza. Sasa mafuta yake ya
dawa yako tayari. Inaweza ikatumika kama ilivyo; kama dawa kwa matumizi ya nje.

d) Ili kutengeneza dawa ya mafuta, ongeza nta.


Yeyusha nta ya nyuki au nta ya mshumaa na ongeza kwenye mafuta mpaka ujazo ufikie 10 %.
Koroga vizuri.
Kwa haraka na kwa umakini mwaga mchanganyiko huo kwenye vyombo
vidogovidogo.

e) Andika vibandiko
Vitambulisho ni vya muhimu! Kwenye vitambulisho andika jina lako, jina la dawa ya mafuta,
tarehe ilipozalishwa na tarehe dawa itakapomaliza muda wake (kwa kawaida ni miaka 2).

Jedwali: Dawa za mafuta


Jina la Matumizi Mmea wa dawa Kwa duka la Kwa kijijini – Kwa semina –
mafuta au uliokaushwa na dawa – kupima kwa tumia ml 75 za
dawa ya kusagwa kutumia ml. makopo ya nyanya
mafuta mizani ya “puree.”
Uzito wa Ujazo wa Kiasi cha makopo
majani katika majani katika ya majani kwa
ml 1,000 za ml 1,000 za makopo 15 ya
mafuta mafuta mafuta.
Mtoto Kulinda ngozi - Usitumie mmea wo wote, bali mafuta mazuri ya
mboga tu
Urembo Kulinda ngozi Mlimau na/au Gramu 70 ml 200 makopo 3
majani ya
msubili
Bawasiri Uvimbe wo wote angalia Gramu 25 ml 75 makopo 1
unaouma maelezo 1 chini
Chamomile Maambukizi Maua ya Gramu 100 ml 300 makopo 4
yoyote chamomile
Artemisia Kulinda ngozi, Majani ya Gramu 50 ml 150 makopo 2
kuua bacteria artemisia
Mkaratusi Kufukuza wadudu, Majani ya Gramu 100 ml 300 makopo 4
au kwa maumivu ya viungo mkaratusi
kukanda
Vitunguu Kuungua, Kitunguu Gramu 50 ml 100 1½ (angalia
maji madonda, vidonda kilicho- maelezo ya 2)
kwa sababu ya katwakatwa
kulala muda mrefu.
Maumivu Maumivu ya Pilipili Gramu 100 ml 300 makopo 4
ya viungo viungo
(angalia
maelezo 3
chini)
Dawa ya Mba na upele Majani ya Gramu 100 ml 300 makopo 4
mba mbaya mwarobaini,
Melia
azedarach,
Cassia alata au
artemisia
annua

 Matumizi kwenye semina: Vipimo hivi vinatosha kujaza vikopo 35 vya mikanda ya
kamera.

Kumbuka 1: Mafuta ya bawasiri: Tumia majani baadhi au yote ya artemisia, basil na


mpera, maua ya chamomile.

Kumbuka 2: Dawa ya mafuta ya vitunguu: Haihitaji njia ya fukizo-maji. Katakata


vitunguu vipande vidogovidogo sana na uvikaushe kwa siku 1. Vikaange katika
mafuta hadi viwe na rangi ya hudhurungi ya njano. Chuja, changanya na nta ya nyuki
kwenye hayo mafuta yaliyochujwa, koroga, kisha umwage kwenye chombo safi.

Kumbuka 3: Mafuta ya maumivu ya viungo (Baridi Yabisi): kwa sababu capsaicine,


ambayo ni sehemu kubwa ya pilipili (Capsicum frutescens), ni hatari, ni lazima uandike kwenye
kibandiko: “Onyo: Weka mbali na macho. Kama ikigusa macho, osha kwa maji mengi ya
baridi”.

SURA 13: “JIWE JEUSI”

13.1. Matayarisho ya “mawe meupe.”


a) Fanya urafiki na wauza nyama ya ng’ombe! Chukua
moja ya tatu ya sehemu ya katikati ya mfupa wa paja la
ng’ombe jike. Kwa kutumia msumeno wa nyama, ukate vipande vyenye ukubwa kama
sm 2. Baadaye uvikate tena ili upate vipande 6 hivi.

b) Ondoa mafuta yaliyo ndani ya uwazi wa mifupa.


c) Chemsha vipande hivyo vya mifupa katika maji kwa dakika 10.
d) Chemsha tena mifupa kwa kutumia maji safi yenye sabuni (mfano: OMO) kwa dakika
10. NaOH ni nzuri zaidi kuliko sabuni ya kawaida. Inaondoa mafuta
yaletayo utelezi.
e) Rudia hatua d)
f) Chemsha tena kwenye maji safi kwa dakika 10 ili kuondoa sabuni.
g) Kausha juani kwa siku 5 au kwenye jiko la jua kwa siku 1.

13.2. Matayarisho ya “mawe meusi.”


a) Tumia tupa kuondoa sehemu zote zisizo laini.
b) Kunja kila kipande katika tabaka 2 au 3 za jora la Aluminium.
c) Weka vipande hivyo katikati ya jiko la mkaa, kwenye ule mkaa uliowaka na kuwa
mwekundu. Kutegemea joto la moto na ukubwa wa mawe, mchakato huu unaweza
kuchukua kama dakika 10 hadi ½ saa.
d) Inahitaji ujuzi na uzoefu kuweza kuamua wakati yanapokuwa tayari. Kanuni nzuri ni
kusubiri hadi harufu mbaya iishe. Kisha angalia mfupa mmoja, ukiwa makini sana
usiunguze vidole vyako. Jiwe linatakiwa liwe jeusi na gumu. Kama likiwa na rangi ya
kahawia kali, bado halijawa tayari, kama kuna vumbi jeupe, ujue limechemshwa kwa
muda mrefu zaidi, na limeanza kuungua na kusambaa.
e) Ondoa mawe yote kwenye moto na uyaweke kwenye chombo kilichofunikwa kwa dakika
10 ili kupoa. Sasa ondoa jora la aluminium.

13.3. Utunzaji wa “jiwe jeusi”


Tunza jiwe kwa uangalifu mkubwa. Lichunge lisipatwe vumbi, hakikisha ni kavu kabisa. Litunze
katika chombo kisichopitisha hewa.

13.4. “Jiwe jeusi” kulirudishia nguvu.


Ni vizuri zaidi kutengeneza jiwe jipya kwa matumizi mapya. Lakini ikibidi kulitumia tena,
lichemshwe kwenye maji ya sabuni kwa dakika 10, tena kwenye maji safi kwa dakika 10 na
mwisho likaushwe kwenye jiko la jua.

13.5. Matumizi ya “jiwe jeusi.”


a) Majipu, majipu madogo madogo, na vidonda vyenye maambukizo.
Vunja jiwe jeusi kufuata ukubwa wa jipu. Kufanya hivi, weka jiwe kwenye mfuko wa plastiki,
viringishe kwa nguvu na uponde kwa nyundo. Likandamize ndani ya jipu ili ligusane na
majimaji. Jiwe jeusi hunyonya jipu, kwa jinsi hii huondoa sehemu kubwa ya vijidudu.
b) Kuumwa na nyoka na wadudu wenye sumu kama nge. Likandamize kwenye kidonda ili
ligusane na majimaji. Mara tu jiwe linapogusa damu, linagandia kidonda na halitoki mpaka sumu
na majimaji yote yamefyonzwa. Jambo hili linaweza kuchukua siku nzima.

Kwa hiyo jiwe jeusi, ni kitu muhimu katika kila sanduku la huduma ya kwanza kwenye eneo la
tropiki!

13.6. Jiwe jeusi linafanyaje kazi?


Lina maelfu ya njia ndogondogo. Kwa njia ya mchakato wa kapilari, mgandamizo mdogo
unatokea katika njia ndogo hizi. Matokeo yake majimaji yanaanza kutiririka kutoka kwenye
jeraha kwenda jiwe hadi jeraha linapokauka. Ni kama kipande cha godoro (sponge) kwenye
maji.
SEHEMU V: Msingi wa shughuli za dawa za asili

SURA 14: Kazi za vikundi: Maendeleo ni nini?


Katika vikundi mlinganishe kijiji A na B (angalia michoro iliyochorwa na mchoarji wa ki-
africa) kwa kujiuliza maswali yafuatayo:
a) Kuna tofauti gani kati ya kijiji A na B?
b) Kuna mambo yo yote mazuri katika kijiji A?
c) Kama ungetumwa katika kijiji A kama Mhudumu wa Afya au Mtu wa kusaidia katika
maendelo, ungeanzaje? (vipau mbele, mikakati, mbinu, kuhakikisha kazi iwe
endelevu...)

SURA 15: ANZISHA BUSTANI YA MIMIEA YA MADAWA


Ni muhimu kutengeneza bustani ya mimea ya dawa, ili:
- Wakati wote unaweza kupata mimea inayohitajika kujitengenezea dawa.
- Mimea ya porini isipotee kwa kutumia kupindukia.
- Uwe na mali ghafi mlangoni kwa ajili ya kufundishia wengine.
Faida nyingine ni kwamba bustani ya madawa ya zahanati au hospitali inaweza kutoa ajira kwa
jamaa ya wagonjwa wasioweza kulipa gharama kufanya kazi kama malipo kwa tiba waliyopewa.

15.1. Bustani ya uzalishaji wa madawa


1. Kwanza tafuta sehemu za ardhi zinazolingana urefu (contour lines). Mara nyingi jambo hili
linafanyika kwa kutumia fito zilizoungwa kwa umbo la “A.” Panda boma la miti kufuata
mistari ya sehemu hizi za ardhi zinazolingana kwa umbali wa meta 3 kwenye mteremko au
meta 5 kwenye tambarare. Ongeza mchaichai, na mimea ambayo inaongeza rutuba kwenye
ardhi, mfano lesena, tephrosia vogelii. Miti hii ya boma huzuia mmonyoko wa ardhi wakati
wa mvua, huleta kivuli, inaongeza hali ya unyevu katika mazingira, na pia inaweza kuwa
chakula cha wanyama. Ikate mara kwa mara na kuiacha katika urefu wa meta 1.
2. Changanya majani na vijijiti ulivyovikata katika udongo, au kutandaza kwenye ardhi kuzuia
joto. Pia ozesha taka zote za mimea, na uzitumie kurutubisha bustani yako.
3. Katikati ya hiyo mistari ya boma ya miti, panda mimea ya dawa iliyo ya muhimu zaidi.
Hakikisha unajumuisha mimea yote iliyotajwa katika kitabu hiki.
4. Tengeneza sehemu ya kukuzuia miche, mahali ambapo utapanda vipandikizi vya artemisia
annua, na kukuzia miche mingine; mfano: mlongelonge, mpapai, mwarobaini na chipukizi za
msubili.
5. Ingawa mkaratusi ni mmea wa dawa wenye thamani, usiupande kwenye bustani yako.
Mkaratusi hukausha udongo haraka na kuufanya kuwa mkali, na hivyo kutofaa kwa kilimo.
6. Matunda na mboga vina umuhimu ule ule. Hivi vinaweza kuchanganywa kwenye bustani
yako ya dawa, au vikalimwa pekee.
7. Majira yote ya mwaka, punguza eneo la ardhi linalokaa wazi bila mimea. Tandaza majani na
nyasi chini; mfano: kwa kutumia majani ya migomba, majani na vijiti baada ya kusawazisha
boma au ya ngano na mchele. Hivi hutunza unyevu na kuongeza kiwango cha mboji. Pia
wakati ardhi ikiachwa wazi kwenye jua na joto lake, hupoteza rutuba kwa sababu vijidudu
muhimu huharibiwa.
8. Ozesha mimea yako yote na utumie udongo wenye rutuba, ulio mweusi, wakati unapanda.

15.2. Bustani ya maonyesho.


Andaa bustani ndogo nyingine kama bustani ya mafunzo katika sehemu ambayo watu wengi
wataiona, kwa mfano mbele ya shule, hospitali au kanisa. Tumia bustani hii kwa mafunzo.
Otesha mmea moja tu wa kila aina. Andaa vibandiko vya kila mmea. Unaweza, kwa mfano,
kutumia wino mweusi kuandika jina la ki-sayansi, la kiingerza na jina la kienyeji kwenye
kipande cha bati lililonyoshwa na kuwekwa kwenye mti.

SURA 16: Mistari ya Biblia inayohusu maendeleo.

1. MSIMAMO WA KIKRISTO
Luka 6: 9 – 10 : Yesu amponya aliyepooza siku ya Sabato.
Wafilipi 2: 5 – 8 : Uwe na nia kama ya Yesu
I Wakorintho 13:1 – 13 : Jambo muhimu kabisa ni upendo.
Mathayo 18: 18 – 20 : Enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi
wangu.
2. PAMBANA NA KUZAGAA KWA MIFUGO
Mithali 12:10 : Mwenye haki hujali uhai wa wanyama wake.
Kutoka 22:5 : Mfugaji lazima alipe fidia ya hasara iliyosababishwa na
mifugo yake.
I Samwel 16:11 : Daudi alikuwa mchungaji wa kondoo.
Yeremia 23:1 : Wachungaji wabaya hutawanya kondoo.

3. TUZUIE UCHOMAJI WA MISITU


Mwanzo 1:26, 29, 31 : Mungu akaona kila alichokifanya, na tazama,kilikuwa
chema sana.
Ayubu 22:20 : Moto huteketeza mali.
Yeremia 22:7 : Waharibifu watachoma mielezi.
Zakaria 11: 1- 4 : “….malisho mazuri yameharibika.”

4. KILA MTU APANDE MITI 10 KWA MWAKA


Luka 6: 43 – 45, Mathayo 7:16 – 20: Mti mwema huzaa matunda mema.
Ayubu 14:7 : Mti uliokatwa utachipua tena.
Ezekiel 31: 1- 9 : Uzuri wa mielezi ya Lebanoni.

5. TUTUMIE UZAZI WA MPANGO


Luka 14:29 – 30 : Ukitaka kujenga mnara kwanza angalia kama utaweza
kuugharamia.
I Timotheo 5:8 : Lazima mtu awe na uwezo wa kuwatunza watoto wake.
Mwanzo 33:13,14 : Bwana ajua kuwa watoto ni dhaifu.
6. TUSHIRIKIANE KWA KAZI WANAUME NA WANAWAKE
Mwanzo 2:17 – 19 : Mwanaume alishughulikia bustani
II Thesalonike 3:7 10 : Kama mtu asipofanya kazi na asile.
Waefeso 5:33 : Mme apende mke wake kama nafsi yake mwenyewe.
7. TUJIVUNIE MADAWA YA ASILI
I Samweli 16:14 – 23 : Muziki ulileta faraja kwa Sauli.
Marko 8:22 – 26 na Yohana 9: 1 – 12:
Yesu amponya kipofu kwa mate na mikono yake.
Luke 10:34 : Msamaria mwema aponya kwa divai na mafuta.

8. KILA FAMILA IWE NA KICHANJA NA CHOO


Kutoka 19:10 : Mungu anamwambia Musa kuwaambia watu wafue nguo
zao.
Walawi 15 : Oga na ufue nguo na matandiko unapokuwa
umetokwa na uchafu mwilini.
Kumbukumbu 23: 13 – 15: Jisaidie shimoni.

9. TUWE WAAMINIFU NA WAANGALIFU


Walawi 15 : Mwongozo wa kujamiiana kwa wana wa Israeli
Kutoka 20:14 : Usizini.
Malaki 2:14 – 15, Mithali 7: 1- 27 na Mithali 5:1 – 21: Uwe mwaminifu.
I Wakorintho 6: 12 – 20 : Kuhusu uzinzi na uasherati.

10. KUFANYA KAZI KWA PAMOJA NI FURAHA KWA WOTE


I Wakorintho 12:12-31 : Mwili wa Kristo
I Wakorintho 1:10 : Mwe na nia moja.
Waefeso 4: 3 – 5 : Kuna mwili mmoja.

SURA 17: MWONGOZO NA MAADILI KWA


“WAGANGA WA ASILI.”
Kwa kuanza kutambua na kufuata mwongozo huu, waganga wa jadi wanaweza kutibu kama
“waganga wa dawa za asili”. Kwa jinsi hii wanaweza kuepuka mwelekeo mbaya wa kazi yao, na
wataweza kushirikiana na “madawa ya kisasa”, katika njia ambayo Shirika la Afya duniani
linaiendeleza, ingawa imekwama mara kwa mara, tangu Azimio la Alma Atala 1978.
A. Waganga wa asili
1. Hawatachoma sindano.
2. Hawatachanja chale.
3. Hawatafanya upasuaji wa aina yoyote.
4. Hawatachanja kuingia ndani sana ya mwili.(Yaani : Mikato mwilini kwa lengo la
kuondoa maumivu au roho mbaya zisumbuazo (pepo). Mfano: katika maumivu ya
viungo: “kuondoa maumivu,” au kwa saratani: “kuondoa pepo wabaya”.
5. Hawatachanja chale ndogo ndogo mahali pa kuweka dawa
6. Hawatawaondolea watoto kile kiitwacho meno ya plastiki. Meno yanayotaka kuota ya
watoto wenye upungufu wa lishe mwilini hung’aa kupitia kwenye ufizi. Wengine
huamini kwamba meno ya zamani lazima yang’olewe.
7. Hawaruhusiwi kung’oa tonsills, kung’oa au kukata kimio.
8. Hawaruhusiwi kutoa mimba.
9. Hawaruhusiwi kutumia aina yoyote ya uchawi.
10. Hawaruhusiwi kutumia kinyesi.
11. Hawaruhusiwi kutumia mwili au viungo vya binadamu.
12. Hawaruhusiwi kutumia wanyama kwa njia yoyote.
13. Hawaruhusiwi kuinika – inaweza kuwa hatari – isipokuwa kwa maji kutibu kufunga
choo.
14. Kujifanya kutibu VVU/ Ukimiwi
15. Kutahiri wanawake (Hii ni kumtia mtu kilema.)

B. “Waganga wa madawa ya asili” watatafuta kuweka watu na jamii nzima katika afya
nzuri kwa:
1) Kuweka njia za kinga kwa kijiji au wilaya.
2) Kuelimisha watu katika njia za kujikinga kiafya; mfano kutotumia sabuni zenye zebaki
(“mercury”).
3) Kushiriki kikamilifu katika kikundi cha dawa za asili cha wenyeji wa mahali anapoishi.
4) Kulinda mimea ya dawa.
5) Kujifunza majina ya kisayansi ya mimea inayotumika.
6) Kuanzisha bustani ya uzalishaji wa dawa na bustani ya maonyesho ya dawa pamoja na
mimea yenye lishe bora.
7) Kutumia chai za dawa kwa njia zilizoelekezwa (angalia “Dawa za asili katika nchi za joto
I” Sura 4:2).
8) Kutumia maelekezo mengine yaliyo salama kutengenezea dawa kama dawa za mafuta,
mafuta ya dawa, maji -chumvi (ORS), dawa za unga, jiwe jeusi n.k.
9) Kushughulika na ugonjwa mmoja tu.
10) Kutoa dozi zinazotakiwa.
11) Kutumia kipima joto.
12) Kushirikiana na hospitali kuwapeleka wagonjwa ambao huwezi kuwatibu au walio na
joto kali; au walio na hali mbaya sana.
13) Kukubali malipo yanayofaa kutoka kwa wagonjwa, kutokana na jinsi wawezavyo
kujipatia kipato.
14) Kufundisha wengine juu ya dawa za asili.
15) Kuwajali kwa upendo wagonjwa wa UKIMWI, na kutibu dalili na magonjwa
yanayohusiana na ugonjwa wa UKIMWI, ili waweze kuishi maisha marefu na mazuri.
Kwa kufuata mwongozo huu kila Mganga wa Asili anaweza kuwa mfanyakazi wa afya ya
msingi. Vivyo hivyo kwa kufuata hatua zilizotajwa chini ya namba 2 hapo juu, kila mfanyakazi
wa afya ya msingi anaweza kuwa Mganga wa asili.
anamed : Matoleo mbalimbali
Schwafweide 77, 71364, Winnenden, Germany.
e-mail kwa kuagiza: anamedhmh@yahoo.com

website: www.anamed.net

Kwa kiingereza:
105: Hirt/M’pia, “Natural Medicine in the Tropics I,” toleo la pili.
106: Kitabu hiki pamoja na kipeperushi cha rangi (403).
109: Hirt/Lindsey, “Natural Medicine II - Treatments” kKitabu cha maelezo ya semina.
113: Natural Medicine: III Seminar Leaders’ Resource kit.
114: Lindsey, “Making peace: Biblical principles.”
115: “Natural Medicine: IV AIDS and Natural Medicine.”
116: Hati “Four ULOG Solar ovens and one drier: Construction plans and uses.”
117: Hati: “Neem in medicine and agriculture.”
403: “Colour poster of 60 tropical medicinal plants 70×50cm.”
- Kipeperushi cha rangi cha mimea 60 ya madawa iliyo eneo la tropiki
70×50sm.
107: Lindsey/Hirt “Use water Hyacinth.”
201: Taarifa, “Be black, stay beautiful.”
204: Hati, “Malaria: Artemisia annua” pamoja na maelezo ya jinsi ya kulima.

GERMAN
101: Hirt /M’pia “Natürliche medizin inden tropen.”
102: Kitabu hiki pamoja na kipeperushi cha rangi (401).
401: Kipeperushi cha rangi, “Heilpflanzen in den Tropen 70×50cm.”
303: Taarifa za mbegu za mimea inayoponya: kununua, kutunza.
202: Hati “Malaria: Artemisia annua” pamoja na maelezo ya mwongozo wa jinsi ya
kulima.

KIFARANSA
103: Hirt/M’pia “La medecine Naturelle I”
104: Kitabu hiki pamoja na kipeperushi cha rangi (402).
112: “La Medecine Naturelle: II Traitements” Kitabu cha mwongozo wa semina, 40
pp.
118: “La Medicine Naturelle: III Guide du Formateur.”
402: Kipeperushi cha rangi, “Plantes medicinales tropicales” sm70×50
206: Taarifa “Sabuni za zebaki: Kashifa ya siku hizi.” (kwa kifaransa)
203: Hati “Malaria: “Artemisia annua” pamoja na maelezo ya jinsi ya kuilima.

KIHISPANIA
110: Hirt /M’Pia “Medicina Natural” 160 pp.
207: Taaifa: “Malaria” “Artemisia annua” pamoja na maelezo ya jinsi ya kuilima.
121: “Medicina Natural en el Tropica: Parte B”
KIRENO
120: Hirt/M’Pia “Reme’dios Naturais nos Tropicos : I.”
111: Hirt /M’Pia “Reme’dios Naturais nos Tropicos: II Tratamentos” kitabu cha
mwongozo wa semina.
205: Taarifa “Malaria: Artemisia annua” pamoja na maelezo ya jinsi ya kuilima.
405: Kipeperushi cha rangi cha mimea 60 ya madawa, sm70×50.”

KISWAHILI
123/ "Madawa ya Asili-1", Tome 1,
119/ "Dawa za Asili-2", Tome 2, Uzoefu (Seminars)
124/ "Ukimwi na Madawa ya Asili“ Tome 4, (AIDS and Natural Medicine
406/ Colour poster of 60 tropical med.plants (70x50cm), in Swahili,
453/ “Black is beautiful” 10 Posters DIN A3 about dangerous cosmetics, Swahili

ZANA NYINGINE
400: Karatasi kubwa nyeupe ya sm 70×50 yenye gamba jembamba pande zote kwa
kufundisha kwa marker-pen.
404: Kipeperushi cha rangi chenye mimea 60 ya madawa, bila maneno ya ufafanuzi zaidi; ina
gamba laini kwa ajili ya matumizi ya markers.
408: Mkusanyiko wa mbegu za kitropiki (Tayari kwa kuota).
409: Vikorokoro vya kuanzia ulimaji wa Artemisia vikiwa na mbegu 5,000.
412: Mbegu za artemisia, kifuko cha kujaza tena kwa ajili ya 409.
419: Mbegu za Moringa oleifera na maelezo ya kiingereza; na muhtasari kwa
kifaransa.
431: Vipandikizi vya Artemisia au miche (kutokana na upatikanaji) kwa ajili ya
uoteshaji.
411: Majani ya artemisia yaliyokaushwa kwa ajili ya matumizi ya kisayansi, 250g.

Picha ya nyuma kwenye kitabu: “Watu wa mataifa mbalimbali – kufuata mistari ya biblia –
wanasaidiana kuheshimu mimea ya dawa”. (Mchoro wa Gregor Müller, St Gallen,
Switzerland).

Вам также может понравиться